maambukizo ya virusi vya ukimwi na ulishaji wa watoto wachanga

36
Maswali na Majibu Mwongozo kwa Wanasihi Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na Ulishaji wa Watoto Wachanga Majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara na wanawake, familia na jamii

Upload: doanthuy

Post on 16-Dec-2016

386 views

Category:

Documents


9 download

TRANSCRIPT

Maswali na Majibu Mwongozo kwa Wanasihi

Maambukizo ya Virusivya UKIMWI na Ulishajiwa Watoto Wachanga

Majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwamara na wanawake, familia na jamii

i

Maswali na Majibu Mwongozo kwa

Wanasihi

Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na Ulishaji wa Watoto Wachanga

TFNC

ii

Hiki kijitabu cha Maswali na Majibu Mwongozo kwa Wanasihi kuhusu maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na ulishaji wa watoto wachanga ni sehemu ya vitendea kazi iliyotokana na utafiti uliofanyika katika hospitali ya Rufaa ya Msamaria Mwema (K.C.M.C.) iliyopo Moshi, Tanzania. Kimetengenezwa na kugharamiwa na Quality Assurance Project (QAP) kikisimamiwa na University Research Co., LLC (URC), chini ya mkataba wa Marekani U.S. Agency for International Development (USAID), namba GPH–C–00–02–00004–00.

Kimechapwa: March 2005

iii

Jinsi ya Kutumia Kijitabu Hiki

Kijitabu hiki cha maswali na majibu kimetengenezwa kutokana na mahitaji ya watu kama nyinyi wafanyakazi wa afya, hususani wanasihi ambao wanahitaji vitendea kazi vya kuwezesha kuelezea mambo magumu yanayohusu Virusi vya UKIMWI na ulishaji wa watoto wachanga. Kimetayarishwa kwa namna ambayo kitamsaidia mnasihi aweze kutoa taarifa na kuwasaidia wanawake wajawazito na watoto wao kujikinga na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU).

Japo kijitabu hiki kimetengenezwa ili kitumike katika kliniki za wajawazito, kinaweza pia kutumiwa na wanawake katika maeneo mengine, na vilevile wanaume, wazee, vijana, viongozi na watu wengine katika jamii.

Mwongozo huu umelenga kutumiwa na wanasihi kama rejea ya haraka. Unatoa majibu sahihi na rahisi kueleweka, kwa maswali yanayoulizwa mara kwa mara na wanawake, familia zao na jamii kuhusu Virusi vya UKIMWI na ulishaji wa watoto wachanga. Majibu yaliyopo kwenye kijitabu hiki yametumia mapendekezo ya kimataifa ya hivi karibuni kuhusu Virusi vya UKIMWI na ulishaji wa watoto wachanga. Kitendea kazi hiki hakijitoshelezi chenyewe na wala sio badala ya mafunzo. Wanasihi wanaotumia kitendea kazi hiki wanatarajiwa wawe wamekwishapata mafunzo maalumu yanayohusu Virusi vya UKIMWI na ulishaji wa watoto wachanga. Zana nyingine za kufundishia na kujifunza zinahitajika pia ili kusaidia katika kufanikisha mawasiliano kati ya mtu na mtu na utoaji unasihi.

Tunatarajia kijitabu hiki kitafanya kazi ya mnasihi kuwa rahisi na yenye mafanikio. Kama una maswali kuhusu namna ya kutumia au maoni ya kuboresha kijitabu hiki wasiliana na Wizara ya Afya, Programu ya Taifa ya Kuzuia Maam-bukizo ya Virusi vya UKIMWI Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto (PMTCT), TFNC, Ofisi za USAID, UNICEF au WHO.

iv

Shukrani

Kijitabu hiki cha Maswali na Majibu cha Wanasihi kimetokana na kumbukumbu za rejea za Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Makao Makuu. Kamati ya Uzuiaji wa Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto (PMTCT). Shirika limepata mchango wa mawazo kutoka UNICEF, WHO, UNAIDS, IBFAN na mashirika ya binafsi machache (NGO na CBO). Pia rejea imefanyika katika mwongozo wa WHO/UNICEF HIV na Infant Feeding Counseling Tool. Kufuatia maoni ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya, PMTCT/Tanzania, UNICEF/Tanzania, WHO/Tanzania, USAID/Tanzania, Tanza-nia Food and Nutrition Centre (TFNC), Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), AXIOS Foundation, COUNSENUTH, Muhimbili College of Health Sciences (MUCHS), Chuo Kikuu cha Bergen/Norway, Quality Assurance Project (QAP) University Research Co., LLC (URC), The Academy for Educational Development na mengineyo mabadiliko yalifanyika kutokana na maoni ya wadau. Matokeo ya utafiti uliofanyika Moshi, Tanzania vile vile yamejumuishwa.

Orodha ya wataalamu waliopitia kijitabu hiki:

AMREF Tanzania: Bernedicta MdumaAXIOS Foundation/Tanzania: Hores Isaack Msaky na Amanda GibbonsCOUNSENUTH: Mary Materu, Margaret Nyambo, na Restituta ShirimaEGPAF: Christy Gavitt, Anja Giphart na Illuminata NdileHospitali ya Msamaria Mwema (KCMC): John Shao, Mark Swai, Raimos Olomi na Olola Oneko LINKAGES/AED: Ellen Piwoz, Jay Ross, Kim Winnard na Maryanne Stone-JimenezShirika la Chakula na Lishe Tanzania (TFNC): Godwin Ndossi, Hilda Missano na

Monica NgonyaniWizara ya Afya: Angela RamadhaniUNICEF/Tanzania: Bertha MlayUNICEF: Joan Mayer, Arjan de Wagt na Miriam LabbokChuo Kikuu cha Muhimbili (MUCHS): Deborah Ash, Asia Hussein, Sebalda Leshabari

na Zohra LukmanjiChuo Kikuu cha Bergen/Norway: Karen Moland na Marina de PaoliChuo Kikuu cha California, Berkeley na Davis: Kiersten Israel-Ballard na Caroline ChantryURC/QAP: Peggy Koniz-Booher na Raz Stevenson, URC/QAPUSAID/Tanzania: Patrick Swai, John Dunlop, René Berger na Susan MonaghanWHO/Tanzania: Theopista John na Feddy MwangaWHO: Peggy Henderson, Constanza Vallenas, Philippe Gaillard na Chessa Lutter (PAHO)

Utayarishaji wa UNICEF-Infant Feeding Tool, Shari Cohen (Mshauri)Utayarishaji wa Rasimu: Design of the WHO/UNICEF HIV and infant feeding counseling

flipchart (cards and flowchart): Elizabeth Thomas na Ellen Piwoz, Academy for Educational Development, and Infant Feeding and Newborn Health team, Department of Child and Adolescent Health and Development, WHO

Mratibu: Peggy Koniz-Booher na Deborah Ash, URC/QAPMtafiti: Sebalda Leshabari, Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUCHS) na Chuo Kikuu cha

Bergen/Norway Tafsiri: Mary Materu, Margaret Nyambo, na Restituta Shirima, COUNSENUTH; na

Sebalda LeshabariMichoro: Victor Nolasco, URC/QAPUtayarishaji wa michoro: Peggy Koniz-Booher na Kurt Mulholland, URC/QAP

Shukrani za pekee ziwaendee wanasihi kutoka hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa kushiriki katika kufanyia

v

Yaliyomo

Maswali Yaulizwayo Kuhusu Kuwakinga Watoto Dhidi ya Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)

1: Mwanamke anaweza kufanya nini kujikinga na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI au magonjwa mengineyo yatokanayo na ngono? ............................................1

2: Je, mwanamke yeyote anaweza kumuambukiza mtoto wake virusi vya UKIMWI? ..........2

3: Je, ni namna gani mtoto anaweza kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama yake? ..................................................................................2

4: Je, kuna uwezekano gani kwa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye Virusi vya UKIMWI kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI? ......................................2

5: Je, inakuwaje watoto wengine wanaozaliwa na wanawake wenye Virusi vya UKIMWI hupata maambukizo na wengine hawapati? ....................................3

6: Utajuaje kama mtoto amepata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI? ..............................4

7: Je, kuna kitu kinachoweza kufanyika kupunguza maambukizo kutoka kwa mama mwenye Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto? .........................................4

Maswali Yaulizwayo Kuhusu Njia Mbalimbali za Ulishaji wa Watoto Wachanga

8: Kwa nini kunyonyesha maziwa ya mama pekee ndiyo njia unayoshauriwa kumlisha mtoto iwapo mama hana Virusi vya UKIMWI au hajui hali yake ya maambukizo? ................................................................................5

9: Ikiwa mama ana Virusi vya UKIMWI ni njia zipi bora za kumlisha mtoto ili kupunguza maambukizo? ..........................................................................................6

10: Je, nini maana halisi ya misemo hii; “Kunyonyesha maziwa ya mama pekee,” “kutumia maziwa mbadala” na “kunyonyesha maziwa ya mama pamoja na kumpa mtoto vyakula au vinywaji vingine”? ..................................................................6

11: Je, katika wanawake wenye Virusi vya UKIMWI, unaweza kutambua ni yupi anaweza kumuambukiza mtoto wake Virusi vya UKIMWI kwa kunyonyesha? .................7

12: Je, ni nini maana ya misemo Ifuatayo: “Yenye kukubalika,” “Uwezekano,” “Kumudu gharama,” “Endelevu,” na “Salama” .............................................................8

13: Kwa vile kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusababisha maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto, je, si ingekuwa vyema kumpa mtoto maziwa mbadala? ..........................................................................................................9

14: Je, ni kwa nini unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee, ni mojawapo ya njia inayopendekezwa pia kumlisha mtoto wakati mama ana Virusi vya UKIMWI? ..............10

vi

Maswali Kuhusu Faida na Hasara za Njia Mbalimbali za Ulishaji Watoto Wachanga

15: Je, ni nini faida na hasara za kumnyonyesha mtoto mchanga maziwa ya mama pekee? .........................................................................................................11

16: Je, kuna faida na hasara gani za kutumia maziwa mbadala yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga? ...............................................................................12

17: Je, kuna faida na hasara zipi kwa kutumia maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa kama maziwa mbadala? ...................................................................14

18: Je ni nini faida na hasara ya kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa? .........................................................................................................16

Maswali Kuhusu Unyonyeshaji Salama na Afya ya Mama

19: Je, kuna mambo yanayoweza kuongeza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama mwenye Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto wake kupitia maziwa yake? ...............................................................................17

20: Je, kuna mambo yanoweza kupunguza uwezekano wa kumuambukiza mtoto Virusi vya UKIMWI kupitia maziwa ya mama? ..............................................................18

21: Je, kuna kitu chochote maalumu ambacho mama mwenye Virusi vya UKIMWI anashauriwa kufanya ili kuyaweka matiti na chuchu zake katika afya njema? ................20

22: Mwanamke mwenye Virusi vya UKIMWI anashauriwa kufanya nini iwapo matiti au chuchu zake zitakuwa na matatizo? ..............................................................21

23: Je, kuna mahitaji maalumu ya kilishe kwa mjamzito mwenye Virusi vya UKIMWI aliyeamua kumnyonyesha mtoto? ..................................................................21

24: Je zipo huduma maalumu kwa mjamzito aliye na Virusi vya UKIMWI wakati wa mahudhurio ya kliniki? ................................................................................22

25: Ni wakati gani mtoto anayenyonya au anayepewa maziwa mbadala aanzishiwe chakula cha nyongeza na alishwe vipi? ......................................................23

1

Maswali Yaulizwayo Kuhusu Kuwakinga Watoto Dhidi ya Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (VVU)

Mwanamke anaweza kufanya nini kujikinga na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI au magonjwa mengineyo yatokanayo na ngono?

Ni muhimu kwa kila mwanamke aweze kujikinga mwenyewe na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na magon-jwa yatokanayo na ngono. Wanawake wanaweza kuepuka maambukizo kwa aidha; kuacha ngono au kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja ambaye naye hana Virusi vya UKIMWI au magonjwa yatokanayo na ngono (yeye mwenyewe akiwa pia mwaminifu kwa mpenzi huyo huyo mmoja) au kwa kutumia kondomu kwa usahihi kwa tendo la kwanza la ngono na kila mara afanyapo ngono.

Ni muhimu sana kwa wale wote ambao wanashiriki ngono kufahamu hali zao za maambukizo ya Virusi vya UKIM-WI. Wanawake na wanaume wote kwa pamoja wanapaswa kupata ushauri nasaha kuhusu UKIMWI na kisha kupimwa kwa hiari ili kujua hali halisi za afya zao kuhusu maambukizo ya Virusi vya UKIMWI. Kufahamu hali zao za maambukizo ya Virusi vya UKIMWI itasaidia wanawake na wapenzi wao au wenzi kuchagua kuzaa watoto au kuacha na kufanya maamuzi mengine muhimu yanayohusu uzazi.

Wakati wa ujauzito na pia kipindi cha kunyonyesha ni muhimu sana sana kwa mwanamke na mwenzi wake kujikinga na maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na magonjwa mengine yatokanayo na ngono isiyo salama. Iwapo kuna mashaka, wasiwasi au kutoaminiana kwa mume na mke, au mwenzi wake, ni vyema wawili hawa kutumia kondomu kila wakati wafanyapo ngono. Hatua hii itawakinga wapenzi wawili hawa. Kumkinga mama asipate maambukizo ya Virusi vya UKIMWI ndiyo njia ya uhakika ya kuzuia Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, kujif-ungua au kupitia maziwa ya mama.

1

2

Je, mwanamke yeyote anaweza kumuambukiza mtoto wake Virusi vya UKIMWI?

Hapana. Mwanamke ambaye hana Virusi vya UKIMWI hawezi kumuambuki-za UKIMWI mtoto wake wakati wa mimba, kujifungua au wakati wa kunyonyesha.

Kama mwanamke hajapimwa hali yake ya uambukizo wa Virusi vya UKIMWI sio rahisi ku-fahamu kama ana Virusi vya UKIMWI. Inawezekana tu kujua kama mwanamke ana maambukizo ya Virusi vya UKIMWI pale tu kipimo cha virusi vya UKIMWI kimeonyesha virusi viko “changa” au anapoonyesha dalili za UKIMWI. Hii ni sababu nyingine inayomfanya mama mjamzito na mama anayenyonyesha apime UKIMWI ili kutambua hali yake na kupata ushauri wa jinsi ya kuzuia mambukizo kwenda kwa mtoto wake.

Je, ni namna gani mtoto anaweza kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama yake?

Damu na maziwa ya mama yanakuwa na Virusi vya UKIMWI. Virusi vinaweza kwenda kwa mtoto wakati wa mimba au kujifungua kama mtoto akigusishwa na damu au maji maji ya mwili wa mama yake. Ikiwa mama ananyonyesha mtoto anaweza kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kupitia kinywani au tumboni.

Je, kuna uwezekano gani kwa mtoto aliyezaliwa na mama mwenye Virusi vya UKIMWI kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI?

Siyo watoto wote wanaozaliwa na wanawake wenye Virusi vya UKIMWI wanapata maambukizo. Fikiria watoto 100 (mia moja) wanaozaliwa na wanawake wenye Virusi vya UKIMWI ni watoto ishirini (20) hupata maambukizo wakati wa ujauzito na kujifungua kama hatua yoyote haikuchukuliwa. Watoto kumi na watano (15) wengine huweza kuambukizwa wakati wa kunyonyeshwa kama mama hachukui tahadhari ya kunyonyesha kwa usalama au akinyonyesha kwa muda mrefu. Hivyo wale 65 waliobaki hawapati maambukizo hata kama wakiendelea kunyonyeshwa kwa muda mrefu bila hatua yoyote kuchukuliwa.

3

4

2

3

Je, inakuwaje watoto wengine wanaozaliwa na wanawake wenye Virusi vya UKIMWI hupata maambukizo na wengine hawapati?

Mpaka sasa haijafahamika ni kwa nini watoto wengine wapate maambukizo na wengine wasipate. Labda hutegemea afya na lishe ya mama zao, au namna wanavyowalisha watoto wao. Sasa hivi inafahamika kwamba kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi mitatu ya mwanzo humpa mtoto kinga dhidi ya uambukizo. Wanawake wengine huwa na Virusi vingi vya UKIMWI katika maziwa yao, hivyo kushinda nguvu ya kinga ya asili zilizopo kwenye maziwa ya mama. Vile vile matatizo ya matiti kama mipasuko, michubuko, majipu, vidonda na kadhalika huchangia kuongeza uwezekano wa maambukizo; kadhalika uwezekano wa maambukizo huwa mkubwa zaidi kama mwanamke amepata maambukizo hivi karibuni, au ana ugonjwa wa UKIMWI (CD4 ziko chini). Sababu nyingine inaweza kuhusishwa na afya ya mtoto. Kinywa na utumbo wa mtoto vikiwa na michubuko au mikwaruzo kutokana na kupewa vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama kabla ya miezi sita huwezesha Virusi vya UKIMWI kupenya na kuingia mwilini kwa urahisi.

5

4

Utajuaje kama mtoto amepata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI?

Kwa bahati mbaya ni vigumu kutambua kama mtoto amepata maam-bukizo ya Virusi vya UKIMWI au la. Vipimo vya kawaida vinavyotumika kugundua antibodi za Virusi vya UKIMWI haviwezi kutumika kwa watoto hadi wafikapo umri wa miezi 15 hadi 18. Vipimo vingine vya watoto wa umri mdogo vipo lakini ni vya ghali sana.

Je, kuna kitu kinachoweza kufanyika kupunguza maambukizo ya virusi kutoka kwa mama mwenye Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto?

Ndiyo. Awali ya yote ni muhimu kwa wajawazito wote na wazazi kupimwa ili kufahamu hali zao za maambukizo. Kama mjamzito au mzazi akiwa na maam-bukizo kuna mambo anayoweza kufanya yeye au mtoa huduma ya afya kuzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto. Kwa wajawazito wanaotam-bua hali zao, zipo dawa maalum za kurefusha maisha (ARVs) wanazopewa wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua. Dawa hizo hupewa pia watoto mara tu baada ya kuzaliwa ili kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Njia maalum ya kumzalisha mama hupunguza kiasi cha damu ya mama inayomgusa mtoto wakati wa kujifungua. Vilevile njia mbalimbali za kuwalisha watoto hupunguza maambukizo ya virusi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Wazazi mara nyingi huhitaji msaa-da kutoka kwa wanasihi au watoa huduma za afya ili waweze kupata dawa hizo maalum. Watahitaji ushauri kuhusu njia bora ya kumlisha mtoto ku-tokana na hali halisi.

Walioambukizwa Virusi vya UKIMWI mara nyingi wanahitaji pia msaada na taarifa muhimu mara kwa mara. Wanasihi wanatakiwa kujibu maswali ya wateja na kuwashauri jinsi ya kujikinga wao wenyewe na watoto wao.

6

7

5

8

Maswali Yaulizwayo Kuhusu Njia Mbalimbali za Ulishaji wa Watoto Wachanga

Kwa nini kunyonyesha maziwa ya mama pekee ndiyo njia inayoshauriwa kumlisha mtoto iwapo mama ana Virusi vya UKIMWI au hajui hali yake ya maambukizo?

Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto, na ndicho chakula na kinywaji pekee anachohitaji mtoto mchanga katika miezi sita ya mwanzo. Maziwa ya mama yana virutubi-shi vyote anavyohitaji mtoto mchanga na yana kinga dhidi ya maradhi. Kolostramu (maziwa majimaji ya rangi ya man-jano yatokayo siku ya kwanza hadi ya pili baada ya kujifun-gua) humpa mtoto mchanga kinga maalumu. Hata baada ya kolostramu kuisha maziwa ya mama humpatia mtoto vitamini mbalimbali, virutubishi vingine na zindiko (antibodies) na vyote kwa pamoja humfanya mtoto awe na nguvu na uwezo wa kupambana na maradhi.

Vyakula vingine kama uji, wali, chai na maziwa yato-kanayo na wanyama, maziwa ya kopo kwa watoto wachanga na hata maji vinaweza kumuumiza mtoto na kumrahisishia kupata maambukizo na magonjwa kama havikutayarishwa sawa sawa. Vinywaji na vyakula vingine huweza kuleta mzio. Bakteria na mzio huweza kuumiza kinywa, tumbo na utumbo wa mtoto na kusababisha kuhara, vichomi (pneumonia) na magonjwa men-gine ya hatari. Kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee bila kumpa kitu kingine cho chote katika miezi sita ya mwanzo huweza kuzuia mimba na hivyo kumsaidia mama asipate mimba mapema. Mtoto afikishapo miezi sita anahitaji chakula cha nyongeza wakati maziwa ya mama yanaendelea kuwa chakula muhimu kwa watoto wengi duniani hadi kufikia miaka miwili.

Kwa vile maziwa ya mama pekee hupunguza maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wanawake walio katika hatari ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI na wale wasiofahamu hali zao za maambukizo ya Virusi vya UKIMWI wanashauriwa kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo.

6

Ikiwa mama ana Virusi vya UKIMWI ni njia zipi bora za kumlisha mtoto ili kupunguza maambukizo?

Zipo njia mbalimbali za ulishaji wa watoto zinazoweza kutumika na wan-awake wenye Virusi vya UKIMWI ili kupunguza maambukizo ya virusi kwa watoto wao. Njia hizi ni pamoja na kunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo au kutumia maziwa mbadala ambayo mtumiaji anaweza kumudu gharama yake, yanayokubalika na yanayopatikana kwa muda wote yanapohitajika na vile vile ni salama. Mfano: Maziwa ya kopo maalumu kwa watoto wachanga na maziwa halisi ya ng’ombe yaliyorekebishwa yanaweza kutumika kumlisha mtoto.

Wanawake wenye Virusi vya UKIMWI pia wana njia nyingine mbili ambazo japo hazikubaliki sana, lakini jamii mbalimbali Afrika zimekwisha kuzitumia. Hii ni pamoja na kukamua maziwa ya mama na kuyachemsha ili kuua Virusi vya UKIMWI kabla ya kumpa mtoto. Njia nyingine ni kuwatumia wanawake ambao hawana Virusi vya UKIMWI kuwanyonyesha watoto badala ya mama zao.

Je, nini maana halisi ya misemo hii; “Kunyonyesha maziwa ya mama pekee,” “kutumia maziwa mbadala” na “kunyonyesha maziwa ya mama pamoja na kumpa mtoto vyakula au vinywaji vingine?”

Ni muhimu kwa mnasihi kufahamu njia mbalimbali za kum-lisha mtoto iwapo mama hana au ana Virusi vya UKIMWI, au hajui hali yake ya maambukizo.

Kunyonyesha maziwa ya mama pekee: maana yake ni kwamba mtoto ananyonya titi la mama tu au maziwa yaliyokamuliwa kutoka matiti ya mama na hapewi kitu kingine zaidi kama chakula au kinywaji kwa mfano, maji, chai, uji, wali n.k. Inashauriwa kunyonyesha maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo.

Maziwa mbadala: Hii inamaanisha kwamba mtoto hatumii kabisa maziwa ya mama bali anapewa aina nyingine ya maziwa kama maziwa ya kopo maalumu kwa watoto wachanga, maziwa halisi ya ng’ombe yaliyorekebishwa au maziwa mengine yanayopatikana.

Maziwa mbadala yanapaswa kuandaliwa na kutayarishwa kwa namna ambayo yatakidhi mahitaji ya kilishe ya mtoto kwa miezi sita ya mwanzo. Kipindi hiki mtoto hutakiwa kupewa maziwa ya mama pekee.

9

10

7

Ulishaji wa mtoto unaochanganya maziwa ya mama na vyakula au vinywaji vingine: Maana yake ni kwamba mtoto hupewa maziwa ya mama pamoja na vyakula au vinywaji vingine kama maji, chai, maziwa ya kopo, maziwa ya-tokanayo na wanyama, uji, n.k. Kwa wale wanawake ambao wana Virusi vya UKIM-WI, haishauriwi kabisa kumlisha mtoto kwa njia hii kabla mtoto hajafikisha miezi sita kwa vile kufanya hivyo kunamuongezea zaidi uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI.

Je, katika wanawake wenye Virusi vya UKIMWI, unaweza kutambua ni yupi anaweza kumwambukiza mtoto wake Virusi vya UKIMWI kwa kunyonyesha?

Haiwezekani kutambua ni mama yupi atakayemuam-bukiza mtoto wake Virusi vya UKIMWI kwa kumnyonyesha. Ndiyo maana ni muhimu sana kwa wale wanawake walio na Virusi vya UKIMWI kuchukua tahadhari wakati wa ujauzito na wakati wa kuli-sha watoto wao.

Wanawake wenye Virusi vya UKIMWI wanashauriwa ku-nyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo, au kuwapa watoto maziwa mbadala kama maziwa ya kopo maalumu kwa watoto wachanga, maziwa halisi ya ng’ombe yaliyorekebishwa au maziwa mengine yaliyokubalika. Maziwa mbadala yanatakiwa yapatikane kwa urahisi na wakati wo wote, yakubalike na jamii na yawe salama. (Angalia swali linalofuata.) Maziwa mbadala yanat-akiwa yawe na virutubishi vya kutosha, yatayarishwe kwa usahihi na kwa usalama kuepuka magonjwa na vifo. Haishauriwi kabisa kumpa mtoto maziwa ya mama pamoja na vyakula au vinywaji vingine kwa sababu kufanya hivyo huongeza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto. Wanawake mara nyingi huhitaji msaada wa ushauri wa kutambua hali zao na kuchagua njia bora inayofaa kumlisha mtoto.

11

8

Je, ni nini maana ya misemo ifuatayo: “Yenye kukubalika,” “Uwezekano,” “Kumudu gharama,” “Endelevu,” na “Salama”

Mwanamke ambaye anajua kwamba ana Virusi vya UKIMWI kuna mambo muhimu anayoshauriwa kuyazungumza na mnasihi, mwenzi wake na pia familia kabla ya kuchagua njia bora ya kumlisha mtoto wake. Mnasihi anaweza kutumia misemo hii kuongoza majadiliano baina yake na mama wa mtoto na familia, kuona uwezekano wa kutumia maziwa mbadala wakizingatia hali halisi ya mama.

Kukubalika: Maana yake ni kwamba mama hana kizuizi chochote kwa chaguo alilofanya kutoka kwa jamii au kwa kuogopa unyanyapaa na ubaguzi.

Uwezekano: Mama au familia ina muda, uwezo, maarifa na vifaa vyote vitakavyohitajika kwenye kutayarisha maziwa ya kumlisha

mtoto. Pia mama anaweza kusaidiwa kuhimili misukumo au misuko-suko itokanayo na familia, jamii n.k.

Kumudu gharama: Mama, familia na pia jamii inayom-zunguka, pamoja na mfumo wa huduma ya afya waweze kumu-

du gharama zote zinazohitajika katika matayarisho na ulishaji kwa kutumia maziwa mbadala. Vinginevyo zoezi hili lita-

onekana kuwa ni mzigo katika familia na kuweza kuathiri afya na hali ya lishe ya familia.

Endelevu: Mama na familia yake waweze kuendeleza njia waliyochagua kwa kupitia mfumo unaoeleweka, utakaompatia vifaa

vyote vinavyohitajika kwa kumlisha mtoto kwa njia

iliyochaguliwa, kwa muda wote mtoto atakapohitaji.

Salama: Vyakula na vinywaji mbadala vina-tunzwa na kuhifadhiwa kwa usahihi na kwa usalama. Vimetengenezwa kwa viwango vilivyokubaliwa kilishe na vile vile mtoto analishwa na mikono na vyombo safi. Inashauriwa kutumia kikombe.

12

9

13

Hii ina maana kwamba mama wa mtoto au yaya:

✤ Ana uhakika wa kupata maji safi bila shida (kutoka kwenye bomba au kisima kisafi).

✤ Anatengeneza chakula chenye virutubishi vyote am-bavyo mtoto anahitaji katika hali ya usafi.

✤ Anaweza kunawa mikono na kuosha vyombo vita-kate vizuri kwa sabuni, na pia kuchemsha vyombo mara kwa mara kuua vijidudu.

✤ Anaweza kuchemsha maji angalau kwa dakika mbili kwa ajili ya kutengenezea kila mlo wa mtoto.

✤ Anaweza kutunza chakula katika hali ya usafi kabla ya kupikwa kwenye chombo chenye mfuniko ili

kuzuia panya, inzi na hata wadudu wengineo.

Iwapo ni vigumu kukubalika, kupatikana, kuendeleza, kumudu gharama na kuhakikisha usalama wa maziwa mbadala, basi kumpa mtoto maziwa ya mama pekee ndiyo njia bora kwa mama na mtoto.

Kwa vile kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusababisha maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto, je, si ingekuwa vyema kumpa mtoto maziwa mbadala?

Maziwa mbadala yanaweza kuwa bora zaidi kwa mtoto ambaye mama ana Virusi vya UKIMWI pale ambapo uchunguzi wa hali halisi ya mama, familia na jamii ume-baini kuwa chaguo hili linafaa. Hii ina maana kuwa wa-naweza kumudu gharama, wanaweza kutekeleza, maziwa hayo yanakubalika na yanapatikana wakati wo wote na pia ni salama.

Mahitaji yanatakiwa yafikiriwe na kuchunguzwa kwa uangalifu kwa kila mwanamke. Maziwa mbadala hayashauriwi pale ambapo:

10

14

✤ Mama hawezi kupata kirahisi au kumudu gharama ya maziwa ya kopo, au maziwa yatokanayo na wanyama au maziwa mengine yaliyokubalika.

✤ Kama hawezi kupata maji safi na salama na nishati ya kuchemshia maji yatakayotumika kutengeneza maziwa mbadala.

✤ Kama familia haipo tayari kumsaidia kufanikisha chaguo lake

✤ Kama hana muda wa kutosha wala fedha, nishati au msaada wa kutosha kwa angalau miezi sita.

✤ Kama ataathirika kimwili na kisaikolojia kwa sababu ya unyanyapaa katika familia na jamii kwa jumla kwa kutokunyonyesha.

✤ Ikiwa hakuna mfumo mzuri wa afya na tiba ambapo mtoto anaweza ku-patiwa matibabu iwapo atahara sana au kupata magonjwa mengine yanay-oweza kusababishwa na ulishaji wa maziwa mbadala.

Je, ni kwa nini unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee, ni mojawapo ya njia inayopendekezwa pia kumlisha mtoto wakati mama ana Virusi vya UKIMWI?

Kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo ndiyo chaguo zuri zaidi kwa watoto wale ambao mama zao wana Virusi vya UKIMWI na ambao hawawezi kutumia maziwa mbadala kwa usalama. Pekee ina maana ya kumpa mtoto maziwa ya mama tu bila kitu kingine cho chote.Unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee humpatia mtoto kinga dhidi ya maradhi. Uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto kupitia maziwa ya mama huweza kuwa mdogo ikiwa kweli mtoto amepewa maziwa ya mama pekee bila kitu kingine zaidi cha kunywa wala kula. Siyo tu kwamba vyakula au vinywaji vingine havihitajiki kwa mtoto mchanga ila huweza kuumiza utumbo wa mtoto na bakteria huweza kuingia na kusababisha magonjwa ya kuhara au ya kifua.

11

Maswali Kuhusu Faida na Hasara za Njia Mbalimbali za Ulishaji wa Watoto Wachanga

Je, ni nini faida na hasara za kumnyonyesha mtoto mchanga maziwa ya mama pekee?

Zipo faida muhimu kadhaa na hasara za kumpa mtoto maziwa ya mama pekee (kumpa mtoto maziwa ya mama tu).

Faida za kunyonyesha maziwa ya mama pekee:

✤ Maziwa ya mama ndicho chakula bora kwa mtoto mchanga, na humkinga dhidi ya magonjwa mengi hu-susani ya kuharisha na kichomi (pneumonia).

✤ Maziwa ya mama yana gharama kidogo, yapo wakati wote na hayahitaji matayarisho maalumu.

✤ Kunyonyesha maziwa ya mama pekee huweza kupun-guza hatari ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto.

✤ Kwa kawaida wanawake wengi hunyonyesha watoto wao, hivyo watu wengine hawatashangaa wanaponyonyesha.

✤ Mama anaponyonyesha maziwa yake pekee, humsaidia kurudia hali yake ya kawaida ya kabla ya uzazi, pia huweza kumlinda asipate mimba nyingine mapema mno.

Hasara za kunyonyesha maziwa ya mama pekee:

✤ Mama anaponyonyesha, mtoto anakuwa katika hatari ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI vilivyopo katika maziwa ya mama. Hatari ni kubwa zaidi iwapo mama ataanza kupata dalili za UKIMWI wakati ananyonyesha au kama atapata maambukizo mapya ya Virusi vya UKIMWI wakati ananyo-nyesha.

✤ Mama hawezi kumnyonyesha na kumlisha mtoto aliye chini ya umri wa miezi sita vyakula au vinywaji vingine kwa sababu hii huongeza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI.

15

12

✤ Watu wengine huweza kumlazimisha mama kumpa mtoto maji au vinywaji vingine anaponyonyesha na hii inaweza kuwa vigumu kwa mama kusema “hapana.”

✤ Kwa mwanamke ambaye inambidi wakati mwingine kuwa mbali na mtoto, kama kazini, inaweza kuwa vigumu kwake kuendelea kumpa mtoto maziwa ya mama pekee

✤ Mama ambaye ni mgonjwa sana, inaweza kuwa vigumu kumnyonyesha mtoto wake.

Je, kuna faida na hasara gani za kutumia maziwa mbadala yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga?

Zipo faida muhimu kadhaa na hasara pia za kutumia maziwa mbadala yali-yotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga.

Faida za maziwa haya:

✤ Hakuna hatari ya kumwambukiza mtoto Virusi vya UKIMWI kupitia maziwa haya.

✤ Maziwa haya yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wachanga yamesha-ongezwa virutubishi vingi anavyohitaji mtoto.

✤ Mtoto anaweza kulishwa na mlezi mwingine badala ya mama.

Hasara za maziwa haya:

✤ Maziwa haya mbadala hayana kinga mwili za kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa, kama zile zilizopo katika maziwa ya mama.

✤ Mtoto anakuwa katika hatari ya kupata magonjwa kama yale ya kuhara, kifua na utapiamlo, hasa kama maziwa haya hayatayarishwi ipasavyo.

✤ Maziwa haya ni ghali, na mama au mlezi wa mtoto anahitaji kuwa nayo ya kutosha wakati wote. Kwa miezi sita ya mwanzo, mtoto mchanga anahi-taji kiasi cha makopo arobaini (40) yenye uzito wa gramu 500 au makopo arobaini na nne (44) yenye uzito wa gramu 450, ambayo yatagharimu wastani wa shillingi 150,000/= (2005) kutegemea aina ya maziwa na soko. Watoto waendelee kupewa maziwa ya kopo mpaka wafikie umri wa miezi 12. Kuanzie umri wa miezi 12 hadi 24, watoto waendelee kupewa maziwa yoyote kila siku.

16

13

✤ Maziwa mbadala huchukua muda kutayarisha, na inabidi yatayarishwe upya kila wakati kama hakuna jokofu.

✤ Mama akishaanza kumpa mtoto wake maziwa mbadala, hawezi tena kum-nyonyesha, kwani kufanya hivyo huzidisha uwezekano wa kumuambukiza mtoto Virusi vya UKIMWI.

✤ Mtoto anahitaji kulishwa kwa kikombe safi badala ya chupa kwa vile ni vigumu kuziweka chupa katika hali ya usalama. Hata watoto wachanga hujifunza kunywa kwa kikombe. Kumlisha mtoto kwa kikombe huchukua muda zaidi.

✤ Mama anahitaji kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji safi yaliyochemka kwa dakika mbili, nishati na sabuni.

✤ Watu wengine wanaweza kumshangaa mama kwa nini anatumia maziwa mbadala badala ya kum-nyonyesha mtoto. Hii husababisha watu kumhisi mama huyu kuwa ana Virusi vya UKIMWI na hivyo kusababisha unyanyapaa na ubaguzi.

✤ Wanawake wanaowalisha watoto kwa maziwa mbadala hawapati ile faida ya kuzuia mimba inay-opatikana wakati wa kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee.

14

17 Je, kuna faida na hasara zipi kwa kutumia maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa kama maziwa mbadala?

Zipo faida muhimu kadhaa na hasara kwa kutumia maziwa halisi ya ng’ombe yaliyorekebishwa kama maziwa mbadala.

Faida hizo ni:

✤ Hakuna hatari ya kumuambukiza mtoto Virusi vya UKIMWI kupitia maziwa haya.

✤ Gharama ya maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa inaweza kuwa ndogo kuliko ile ya maziwa yaliyotengenezwa maalumu kwa watoto wa-changa. Kama mama au familia inafuga ng’ombe wa maziwa, maziwa haya yanaweza kupatikana muda wote kwa urahisi zaidi.

✤ Mtoto anaweza kulishwa na mlezi mwingine badala ya mama.

Hasara hizo ni:

✤ Maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa hayana kinga mwili kama zile zilizopo kwenye maziwa ya mama ambazo humkinga mtoto dhidi ya magon-jwa.

✤ Ni vigumu kwa tumbo la mtoto kumeng’enya maziwa halisi ya wan-yama, pia hayana virutubishi vyote muhimu anavyohitaji mtoto kwa afya yake, kama vitamini, madini na chembechembe za mafuta (fatty acids). Kutokana na hili, maziwa mabichi ya ng’ombe yanahitaji kurekebishwa. Inabidi maziwa haya yachemshwe, yaongezwe kiasi sahihi cha maji yaliyo-chemshwa na sukari. Mtoto apewe pia vitamini za nyongeza.

✤ Mtoto anayepewa maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyorekebishwa anakuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya kuhara , kifua na utapiamlo, hasa kama njia sahihi za kutayarisha maziwa haya hazikufuatwa.

15

✤ Maziwa mabichi ya ng’ombe huchukua muda kutayarisha, na yanatakiwa yatengenezwe upya kila mara mtoto anapohitaji kulishwa kama hakuna jokofu.

✤ Mtoto huhitaji kama lita 15 kwa mwezi katika miezi sita ya mwanzo. Mama atahitaji pia kununua sukari na vitamini za nyongeza. Vitu vyote kwa pamoja vitagharimu wastani wa shilingi 55,000/= (2005) kwa miezi sita ya mwanzo kutege-mea na soko. Mtoto pia anahi-taji maikronutrienti au maltivitamini za nyongeza ambazo hupatikana kwa shida katika soko na ni za gharama kubwa.

✤ Mama hawezi kumnyonyesha mtoto wake, kwani kwa kufanya hivyo huongeza uwezekano wa kumuambukiza Virusi vya UKIMWI.

✤ Mtoto anatakiwa kunywa kwa kikombe na siyo kwa chupa. Hata hivyo watoto hujifunza kwa haraka kutumia kikombe hata kama ni wachanga.

✤ Mama anahitaji kuwa na uhakika juu ya upatikanaji wa maji safi yaliyochemka kwa dakika mbili, nishati na sabuni.

✤ Watu wengine wanaweza kumshangaa mama kwa nini anatumia maziwa mbadala badala ya kumnyonyesha mtoto. Hii husababisha kumhisi mama huyu kuwa ana Virusi vya UKIMWI na hivyo kusababisha unyanyapaa na ubaguzi.

✤ Wanawake wanaowalisha watoto kwa maziwa mbadala hawapati ile faida ya kuzuia mimba inayopatikana wakati wa kunyonyesha.

16

Je ni nini faida na hasara ya kutumia maziwa ya mama yaliyokamuliwa na kuchemshwa?

Zipo faida muhimu kadhaa na hasara za kutumia maziwa ya mama yaliyo-kamuliwa na kuchemshwa hasa kipindi cha mpito cha kuacha kunyonya maziwa ya mama pekee na kutumia maziwa mbadala.

Faida za kukamua na kuchemsha maziwa ya mama.

✤ Kuchemsha maziwa huua Virusi vya UKIMWI.

✤ Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa watoto wachanga na virutubishi vingi haviharibiki kwa kuchemsha.

✤ Maziwa ya mama yapo wakati wote na hayahitaji gharama.

✤ Mtoto anaweza kulishwa na mlezi mwingine badala ya mama yake.

Hasara za kukamua na kuchemsha maziwa ya mama.

✤ Ijapokuwa kuchemsha maziwa ya mama huua Virusi vya UKIMWI maziwa haya hayana ubora sawa na yale ambayo hayajachemshwa kwa vile kinga mwili dhidi ya maradhi huon-doka. (Hata hivyo ni bora kuliko maziwa ya kopo au ya wan-yama yaliyorekebishwa.)

✤ Inachukua muda kukamua na kuchemsha ukizingatia kwamba tendo hili litafanyika mara kwa mara usiku na mchana hasa wakati mtoto ni mchanga. Inaweza kuwa vigumu kufanya hivyo kwa muda mrefu.

✤ Mtoto anahitaji kulishwa na kikombe na siyo chupa. Watoto wachanga hujifunza haraka kunywa kwa kikombe bali huchu-kua muda zaidi kulisha.

✤ Maziwa yaliyokamuliwa yanahitaji kuwekwa sehemu ya ubaridi na yatumike katika muda wa saa moja baada ya kuchemshwa la sivyo yataharibika.

✤ Utahitaji uhakika wa maji safi, nishati na sabuni wakati wote.

✤ Watu wengine wanaweza kumshangaa mama kwa kukamua na kuchemsha maziwa yake. Hii husababisha watu kumhisi mama huyu kuwa na Virusi vya UKIMWI na hivyo kusababisha unyanyapaa na ubaguzi.

✤ Wanawake wanaokamua na kuchemsha maziwa hawapati ile faida ya kuzuia mimba inayopatikana wakati wa kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee.

18

17

Maswali Kuhusu Unyonyeshaji Salama na Afya ya Mama

Je, kuna mambo yanayoweza kuongeza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama mwenye Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto wake kutokana na kunyonyesha?

Ndiyo, kuna mambo mbalimbali ambayo huongeza uwezekano wa maam-bukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto kupitia maziwa ya mama. Mambo haya ni pamoja na kiasi cha Virusi vya UKIMWI alivyonavyo mama, ulishaji wa mtoto una-ochanganya maziwa ya mama na vinywaji au vyakula vingine; muda mtoto atakaon-yonya maziwa ya mama, utandu au vidonda kinywani kwa mtoto; matatizo ya matiti kwa mfano chuchu zilizochubuka, matiti yaliyovimba na kuuma (engorgement) na matatizo mengine kama uambukizo wa matiti (mastitis).

Kiasi cha Virusi vya UKIMWI alivyonavyo mama: Kama mama ndiyo tu amepata maambukizo au ameshafikia hali ya kuwa na UKIMWI, kuna uwezekano mkubwa wa kumuambukiza mtoto wake Virusi vya UKIMWI. Hii ni kwa sababu damu yake na maji maji ya mwili pamoja na maziwa yake huwa na virusi vingi wakati wa mwanzo wa maambukizo, na wakati mama anapofikia hali ya kuwa na ugonjwa wa UKIMWI na kiasi cha seli za CD4 kuwa chini.

Kumpa mtoto maziwa ya mama pamoja na vinywaji au vyakula vingine: Kumpa mtoto maziwa ya mama pamoja na maji, chai, uji, wali au hata maziwa ya kopo ya watoto wachanga, maziwa halisi ya

wanyama yaliorekebishwa au maziwa mengine mbadala hupunguza kingamwili inayopatikana katika maziwa ya mama pekee. Kumpa mtoto mchanga vinywaji au vyakula vingine zaidi ya maziwa ya

mama huweza kuumiza utumbo wa mtoto. Hali hii huweza ku-ruhusu Virusi vya UKIMWI kuingia katika mwili wa mtoto

kwa urahisi. Unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee huweza kupunguza maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto kwa sababu

maziwa ya mama yana kingamwili na viru-tubishi maalumu.

Muda mtoto atakaponyonya maziwa ya mama: Kadiri mtoto anavyonyonya maziwa ya mama kwa kipindi kirefu ndivyo uwezekano wa kupata maambukizo ya Virusi vya UKIMWI unavyoongezeka kwa sababu wakati huo wote hukutana na Virusi vya UKIMWI kupitia maziwa hayo. Hivyo wanawake wenye

19

18

Virusi vya UKIMWI hushauriwa kunyonyesha kwa kipindi kifupi na kuacha kabisa wakati mtoto ana umri wa miezi sita. Kitu muhimu cha kukumbuka ni kwamba mama anashauriwa awe na njia nyingine ya kumlisha mtoto ambayo atamudu gharama yake, inayotekelezeka, inayokubalika na iliyo endelevu. Vile vile iwe salama. Ni muhimu mama azingatie mambo hayo anapom-wachisha mtoto kunyonya, vinginevyo mtoto anakuwa katika hatari ya kupata magonjwa na hata kifo.

Utando mweupe au vidonda kinywani kwa mtoto: Kama mtoto ana utando mweupe au vidonda kinywani Virusi vya UKIMWI huweza kupenya ngozi yake kwa urahisi zaidi na kuingia kwenye mwili wa mtoto. Ni muhimu kutibu utando mweupe au vidonda kinywani mara moja.

Matatizo ya matiti kama chuchu zilizochubu-ka, matiti yaliyovimba na kuuma au yenye uambukizo: Kama mama hamnyonyeshi mtoto wake kila anapohitaji au mara kwa mara usiku na mchana; au hamweki mtoto wake vizuri kwenye titi wakati wa kunyonyesha, chuchu za mama huweza kuumia, au matiti huweza kuvimba na kuuma. Mata-tizo haya huweza kufanya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto kuwa rahisi zaidi. Ili kupunguza hatari ya maambukizo, mama mwenye matatizo yo yote ya matiti ata-fute msaada wa matibabu hospitalini mapema iwezekanavyo. Ushauri na msaada juu ya unyonyeshaji unaotolewa husaidia kuzuia matatizo hayo kwa kiasi kikubwa.

20

Virusi vya UKIMWI, magonjwa yatokanayo na ngono isiyo salama na maambukizo mengine wakati wa ujauzito na kunyonyesha. Ni muhimu sana kwa wanawake wote kuhakikisha hawapati maambukizo mapya (au kuendelea

Je, kuna mambo yanoweza kupunguza uwezekano wa kumuambukiza mtoto Virusi vya UKIMWI kupitia maziwa ya mama?

Ndiyo, kuna mambo yanayoweza kupunguza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto kupitia maziwa ya mama. Mambo hayo ni pamoja na:

Kuchukua tahadhari kuepuka kuambukizwa

19

kuambukizwa) Virusi vya UKIMWI wakati wa ujauzito au kunyonyesha, kwani maambukizo mapya huweza kuongeza kwa kiwango kikubwa uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua na kupitia maziwa ya mama.

Magonjwa yatokanayo na ngono isiyo salama na maambukizo mengine yanaweza pia kuongeza uwezekano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwa mtoto kupitia maziwa ya mama. Hivyo ni muhimu sana wanawake wote wajawazito na wale waliojifungua karibuni, waume zao au wenzi wachu-kue tahadhari kwa kutokujamiana kabisa au kutumia kon-domu kwa usahihi mara zote wanapofanya ngono wakati wa ujauzito na kunyonyesha.

Kutumia maziwa ya mama pekee. Hii inamaani-sha kwamba mtoto apewe maziwa ya mama pekee bila kupewa kitu kingine cho chote kama maji, chai au uji. Kumpa mtoto maziwa ya mama pekee husaidia kupunguza uweze-kano wa maambukizo ya Virusi vya UKIMWI, na kuhara, pia humpatia mtoto lishe bora.

Kuepuka kumpa mtoto maziwa ya mama pamoja na vyakula au vinywaji vingine. Kuchanganya maziwa na vyakula na vinywaji vingine kwa mtoto mchanga si ushauri unaofaa kwani huongeza uwezekano wa mtoto kuhara, kupata kichomi (pneumonia) na magonjwa mengine. Pia humpatia mtoto lishe hafifu. Mama mwenye Virusi vya UKIMWI aliyeamua kunyonyesha, anashauriwa kumpa mtoto maziwa yake pekee kwani humkinga mtoto wake na pia hu-punguza uwezekano wa kumuambukiza Virusi vya UKIMWI.

Kufupisha muda wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama inapowezekana. Mama mwenye Virusi vya UKIMWI aliyeamua kunyonyesha maziwa ya mama pekee, huweza kubadili na kutumia maziwa mbadala wakati wowote ambapo maziwa mbadala yanakubalika, mama anaweza ku-mudu gharama yake na kuyatumia kwa usalama. Pia maziwa haya yanapatikana bila kukosekana wakati wote yanapohita-jika. Hii husaidia kupunguza muda ambao mtoto anakutana na Virusi vya UKIMWI vilivyo katika maziwa ya mama, lakini humpa nafasi ya kufaidika na unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Mtoto aliyewekwa vizuri kwenye titi

Mtoto aliyewekwa vibaya kwenye titi

Mtoto amemaliza kunyonya

Kunyonyesha

20

Kutibu vidonda kinywani mwa mtoto mapema. Mama ampeleke mtoto hospitali mapema kutibiwa anapoona utandu mweupe au vidonda kinywani au mdomoni mwa mtoto.

Kutunza matiti sawasawa. Iwapo mama ananyonyesha anashauriwa kutunza matiti yake kwa kuhakikisha mtoto wake anaponyonya amewekwa kwenye titi sawasawa. Mama anyonyeshe mara kwa mara, usiku na mchana na kila mtoto anapoonyesha anataka kunyonya.

Mama apewe ushauri na msaada ili kuzuia matatizo yanayoweza kujitokeza. Mama anashauriwa kwenda kwenye matibabu mapema iwapo atapata matatizo yo yote ya matiti.

Je, kuna kitu chochote maalumu ambacho mama mwenye Virusi vya UKIMWI anashauriwa kufanya ili kuyaweka matiti na chuchu zake katika afya njema?

Wanawake wote wanaonyonyesha bila kujali hali yao ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI wanashauriwa wajilinde dhidi ya michubuko au mipasuko ya chuchu, kuvimba kwa matiti kunakoambatana na maumivu au uambukizo wa matiti. Mwanamke mwenye Virusi vya UKIMWI aliyeamua kunyonyesha, anashauriwa kujua kama matiti yake yakipata matatizo yo yote, hali hiyo huweza kuruhusu Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto kwa urahisi. Hivyo, ni muhimu sana wanawake wenye Virusi vya UKIMWI, kuyatunza matiti yao, kunyonyesha kwa usahihi na kuomba msaada mapema pale matatizo yanapojitokeza. Matatizo mengi ya matiti yana-

sababishwa na kutokumpakata na kumweka mtoto vizuri kwe-nye titi wakati anaponyonya. Matatizo mengi ya matiti yanahi-taji antibiotiki au dawa nyingine Ili yaweze kupona. Pia iwapo mama anatengana na mtoto wake kwa kipindi kirefu sana au kuchelewa kunyonyesha mchana au usiku, husababisha matiti kuvimba na kuuma.

Wanawake wote wanaonyonyesha inabidi wahakiki-she watoto wao wananyonya mara kwa mara mchana na usiku. Wakati mtoto akiwa mchanga anyonyeshwe kila ana-potaka na isiwe chini ya mara 10 kwa siku (saa 24). Si lazima kuwanyonyesha watoto wenye umri mkubwa mara nyingi sana lakini inabidi wanyonyeshwe angalau mara sita hadi nane au zaidi kwa siku (saa 24).

21

21

Mwanamke mwenye Virusi vya UKIMWI anashauriwa kufanya nini iwapo matiti au chuchu zake zitakuwa na matatizo?

Endapo mwanamke mwenye Virusi vya UKIMWI amepata mchubuko au chuchu kupasuka, vidonda au matiti yake yakitoa majimaji au kitu kingine inabidi atafute msaada wa matibabu haraka. Iwapo matiti yake yamevimba na kuuma, am-nyonyeshe mtoto wake mara kwa mara ili kuona kama kuvimba kutapungua au kuisha. Kama matiti yake yatapata uambukizo (mastitis) inabidi atafute msaada wa matibabu haraka. Kama in-awezekana, mama akamue matiti yake na kuyamwaga maziwa yale yanayotoka kwenye titi lenye uambukizo au ayachemshe kabla ya kumpa mtoto. Mama aendelee kumnyonyesha mtoto titi ambalo halina matatizo. Mama anashauriwa kumnyonyesha tena mtoto mara tu titi litakapopona.

Endapo chuchu zote zimechubuka, zina vidonda au zinatoa majimaji au kitu kingine au matiti yote yakiwa yamevimba, mama atafute msaada na matibabu haraka. Kama kuna uwezekano, amwachishe mtoto kunyonya na ampe maziwa mbadala. Inashauriwa mama akamue maziwa yote kwenye matiti na kisha ayamwage. Matiti yakipona anaweza kuamua kuanza tena kumnyonyesha mtoto au kuendelea kumpa maziwa mbadala, iwapo yanakubalika, anamudu gharama yake, anaweza kuyatumia, yanapatikana wakati wote na ni salama.

Ni muhimu kwa wanawake wote kukagua vinywa vya watoto wao mara kwa mara ili kuona kama kuna utando mweupe na kutafuta msaada wa matibabu mapema.

Je kuna mahitaji maalumu ya kilishe kwa mjamzito mwenye Virusi vya UKIMWI aliyeamua kumnyonyesha mtoto?

Ikumbukwe kwamba mwanamke yeyote mjamzito au anayenyonyesha awe na Virusi vya UKIMWI au la, anatumia nishati na virutubishi vingi ambavyo huhitajika kuvirudisha mwilini ili mama huyo awe na afya nzuri. Kama ana Virusi vya UKIMWI mahitaji yake ya nishati yanaongezeka zaidi japokuwa mama hupoteza hamu ya kula. Mama mwenye Virusi vya UKIMWI ahimizwe kula chakula cha mchanganyiko na cha kutosha. Atumie pia vitamini na madini ya nyongeza (iron and folic acid) kama ikipendekezwa na mtoa huduma ya afya.

22

23

22

Ikiwa mjamzito ana utapiamlo afya yake huathirika na ukuaji wa mtoto kimwili na akili huchelewa. Mtoto anaweza kuathirika maisha yake yote.

Kusaidia kuhakikisha mjamzito ana afya nzuri akiwa na Virusi vya UKIMWI au la anashauriwa ale chakula cha ziada. Chakula kikuu kiongezwe angalao kwa kiasi cha kiganja kwa siku. Wakati wa kunyonyesha aongeze mlo mmoja kwa siku. Wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha wanashauri-wa kula matunda, mboga mboga, aina za mikunde na vile vyakula vitokanavyo na wanyama kila siku. Vile vile atumie vitamini na madini kama ikipendekezwa na daktari.

24

✤ Kuhudhuria kliniki ya wajawazito mara kwa mara, achunguzwe afya yake, apate ushauri na huduma za kisaikologia.

✤ Kupata tiba ya malaria katika kipindi cha pili na cha tatu cha mimba ili kuzuia malaria na upungufu wa damu. Mjamzito anashauriwa kutumia chandarua chenye dawa.

✤ Kuzingatia usafi wa mwili, matayarisho ya chakula na watupe kinyesi kwa usalama kuzuia mambukizo ya magonjwa ya kuhara ambayo yataongeza mahitaji ya chakula.

✤ Kujaribu sana kupunguza kazi ngumu na nzito na kupumzika angalao saa moja mchana hasa miezi mitatu ya mwisho ya mimba.

✤ Kuacha kuvuta sigara, kunywa pombe, madawa ya kulevya na dawa nyingine ambazo hazikutolewa na mtoa huduma ya afya

✤ Kutumia dawa ya kinga ya kifua kikuu (Isoniazid) kwa miezi sita ikiwa anaishi na mtu mwenye kifua kikuu kama atakavyoshauri-wa na mtoa huduma ya afya.

Je zipo huduma maalumu kwa mjamzito aliye na Virusi vya UKIMWI wakati wa mahudhurio ya kliniki?

Mimba hupunguza kinga ya mwili kwa wajawazito wote, na Virus vya UKIMWI hufanya hivyo zaidi. Upungufu wa kinga mwili humfanya mwanamke apate maambukizo ya magonjwa kwa urahisi zaidi na hasa yale magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu na fangasi. Mjamamzito aliye na Virusi vya UKIMWI ashauriwe:

23

✤ Kutumia dawa za kuzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (ARV) kwenda kwa mtoto kama atakavyoshauriwa na mtoa huduma ya afya

✤ Kutumia kondomu wakati wa ujauzito na kunyonyesha kuzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kwenda kwa mtoto.

Ni wakati gani mtoto anayeyonya au anayepewa maziwa mbadala aanzishiwe chakula cha nyongeza na alishwe vipi?

Mtoto apewe chakula cha nyongeza afikishapo umri wa miezi sita. Kiasi atakachohitaji hutegemea kama mtoto anaende-lea kupewa tena maziwa au la. Ikiwa mama ana Virusi vya UKIMWI anashauriwa kumwachisha mtoto ziwa afikapo umri wa miezi sita na kumpa mtoto maziwa mengine kila siku mpaka atimize miaka miwili.

Mtoto anavyokua mahitaji ya chakula huongezeka na aina mbalimbali za chakula huhitajika ili mtoto aweze kupata mahitaji yake kilishe.

25

✤ Mtoto aanzishiwe chakula kidogo kidogo, kijiko cha chai kimoja au viwili mara mbili kwa siku na ongeza vyakula vya aina mbali mbali taratibu.

✤ Mtoto umri wa miezi 6 hadi 8 anahitaji kula mara mbili au mara tatu kwa siku iwapo pia anapewa maziwa. Kama mtoto hapewi maziwa alishwe mara 5 au 6 kwa siku, na chakula kiwe laini.

✤ Umri wa miezi 9 hadi 11 anahitaji kula mara 3 au 4 kwa siku na pia apewe asusa (snack) katikati ya mlo.

✤ Umri wa miezi 12 hadi 24 mtoto alishwe mara 3 au mara 4 kwa siku na pia apewe asusa. Katika umri huu mtoto anaweza kula vyakula vinavyoliwa na familia.

Epuka kuwapa watoto wadogo vinywaji visivyo na virutubishi kama chai, soda na vinywaji vingine vyenye sukari. Maziwa mabichi anayopewa mtoto inabidi yachemshwe kwanza. Vile vile wakati wa kutayarisha chakula au kumlisha mtoto inashauriwa kunawa mikono na pia mtoto anawishwe mikono kabla ya kula.

24

25

Sehemu ya Kuandika

26