madawa ya asili katika nchi za tropiki: iv - kwa sababu ya kufa kabla ya wakati kwa wasomi na watu...
TRANSCRIPT
Madawa ya asili katika nchi za Tropiki: IV
Ukimwi na Madawa ya Asili
anamed Team
Kitabu cha msaada kwa wanaotunza wagonjwa wa
ukimwi.
Toleo la 124 la anamed
Kiswahili
UKIMWI na Madawa ya Asili.
UTANGULIZI 1
Sura 1: UKIMWI – Tumaini katika kukata tamaa ……… 3
Sura 2: Ukimwi ni nini?…………………… 7
Sura 3: Uambukizaji na uzuiaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU)… 11
Sura 4: Njia ya anamed ………………………......... 14
Sura 5: Kuishi na Ukimwi/VVU kwa matumaini …………. 17
Sura 6: Chochea mfumo wa kinga mwilini kwa madawa ya asili…. 20
Sura 7: Jinsi ya kutibu magonjwa yanayoambatana na ukimwi kwa
mimea ya madawa 23
Sura 8: Mwitikio kutoka kwa watumiaji 39
Sura 9: Mapendekezo kumi kwa serikali za nchi za kusini 42
Nyongeza 1: Mistari ya Biblia inayosaidia 44
Nyongeza 2: Mashirika yaliyochaguliwa, matoleo mbalimbali na web – site 45
Nyongeza 3: Fomu ya kumbukumbu: Dalili, tiba na maendeleo ya
wagonjwa wa Ukimwi/ wenye VVU 46
Nyongeza 4: Fomu ya taarifa - kwa kutoa taarifa kwa anamed 47
Nyongeza 5: anamed: Matoleo na vifaa 48
Toleo la pili Julai 2007.
© 2007 na anamed
Ni matumaini ya anamed kwamba taarifa zilizo katika kijitabu hiki zitasambazwa kwa umbali
iwezekanavyo. Tungependa kuwatia moyo watumiaji wa kitabu hiki kukitafsiri katika lugha zao.
Kwa kuwa mambo yaliyomo yanaendelezwa wakati wote, ni lazima kwanza kuwasiliana na anamed.
Haki zote za tafsiri zinabaki na anamed. Hairuhusiwi kuzalisha sehemu yo yote kwa kuuza.
Bango (anamed order No. 403) linaonyesha mimea iliyoelezwa katika kitabu hiki.
Vitabu vya anamed na bidhaa zake vinauzwa kutoka:
anamed, Schwafweide 77, D-71364 Winnenden, Germany.
Email: [email protected]
Internet: www.anamed-edition.com
Shukrani kwa Bindanda Tsobi wa Kinshasa kwa uchoraji wa picha za mifano. Kwa toleo hili la ki-
swahili tunamshukuru Emmanuel Biligeya kwa kazi yake ya utafsiri, Mchungaji Hezron Shimba na
Maike Ettling kwa kuhariri na kundi la Wanaoishi na VVU (Kaza Roho) lililopo Musoma kwa
ushirikiano wao wa kufanya majaribio ya kutumia madawa yaliyotajwa katika kijitabu hiki na
kushuhudia ufanisi wake.
Pia tunaishukuru HUYAMU (Idara ya Afya ya AICT - Dayosisi ya Mara & Ukerewe) kwa
ushirikiano wao wa karibu. Jalada la mbele: Wanasemina wa anamed huko D.R Congo wakijivunia madawa waliyotengeza
wenyewe.
Ukimwi na Madawa ya Asili 1
UTANGULIZI
“Wapiganapo tembo, ziumiazo ni Nyasi“.
Huu ni msemo wa kiafrika na unaelezea hali ya wagonjwa wa Ukimwi kwa sasa katika
nchi zinazoendelea.
Shirika la biashara dunia linapigania haki ya mali ya akili.
Serikali za nchi tajiri zinaziburuza nchi maskini kufuata sheria ya haki miliki za
kimataifa, wakati huo huo wao wenyewe wakizama na kupiga mbizi katika
maswala yao muhimu. Pia wanatumia fedha zaidi katika kupambana na
binadamu magaidi kuliko vimelea “magaidi” kama vile VIRUSI vya UKIMWI
na vile vya malaria “Plasmodia” viuavyo mamilioni kila mwaka.
Makampuni ya madawa yana faida kama kipaumbele chao cha kwanza na
wanalinda haki miliki zao kuvuka sheria zilizokubaliwa kimataifa.
Baadhi ya serikali za nchi masikini zinawekeza zaidi katika silaha ili
kupambana na maadui binadamu kuliko katika mahitaji ya ki-afya na madawa
yanayoshambulia vimelea kama vile VIRUSI vya UKIMWI.
Shirika la afya duniani linapigania haki lakini halina nguvu.
Wizara za afya katika nchi maskini zinashutumu makampuni ya madawa kwa
kutoza gharama zisizowezekana.
Ni tatizo gani hili! Dunia pamoja na ujuzi wake wote imeshindwa kuwasaidia
mamilioni ya watu kusini mwa jangwa la sahara walio na Ukimwi. Afya ya wagonjwa
ambao pia ni maskini ina umuhimu mdogo sana hapa duniani ukilinganisha na biashara,
na haki zilizowazi zinazolinda swala la kutengeneza faidi.
Matokeo yake ni kwamba Ukimwi unaendelea kusambaa zaidi katika Afrika na
mamilioni ya watu wanateseka. Mamilioni ya watoto wamekuwa yatima, kiuchumi
watu watenda kazi wamekufa na wanazidi kufa, na baadhi ya nchi maskini kabisa
duniani zimenaswa katika kile kinachoonekana kuwa kuanguka kusikoweza kuzuilika.
Wapiganapo tembo ziumiazo ni nyasi. Labda uwezekano pekee ni kwamba nyasi ziwe
ngumu kiasi kwamba tembo waende mahali pengine kupigana.
anamed inawatia moyo watu kujiondoa katika kuwa tegemezi wa kile ambacho
kimeelezwa kama uchumi unaonyonga dunia na kutafuta kuimarisha “uchumi hai
wenye asili ya mahali walipo” katika nyanja za afya. anamed inazitia moyo jumuiya
kutumia ujuzi ambao tayari wamekuwa nao, au hata waliokuwa nao, wa jinsi ya kula
chakula cha afya na kujitengenezea madawa, ili kujitegemea zaidi katika kukidhi
mahitaji yao ya kiafya.
anamed pia inazitia moyo jumuiya kujenga hali ya kujiamini katika kudai haki ya
huduma bora kwa ajili yao na kwa ajili ya kila mtu katika dunia hii.
Kijitabu hiki kinaelezea jinsi madawa ya asili yaani matumizi halisi ya mimea
inayostawi au inayoweza kustawishwa katika nchi za tropiki inayoweza kusaidia katika
kuhudumia mgonjwa wa Ukimwi, na kuwezesha wengi kuishi maisha mazuri zaidi.
Ukimwi na Madawa ya Asili 2
Madawa ya asili ni zaidi ya madawa
kutokana na mimea. Msingi wake ni
katika Biblia waaguzi na waganga na
madawa ya kisasa wakishirikiana na
matumizi ya mapendekezo ya shirika la
afya duniani.
HATUDAI KWAMBA DAWA ZA ASILI ZINAWEZA KUTIBU UKIMWI!
Wagonjwa wengi wa UKIMWI tayari wameinua hali za Afya zao kwa kutumia mimea
waliyonayo katika mazingira yao, na kwa kutengeneza madawa yenye gharama ndogo.
Kwa njia hii hawategemei huruma za bodi au mashirika ya nje. Silaha bora zaidi dhidi
ya Ukimwi ni kuzuia. Lazima wakati wote hilo liwe kipaumbele, na vitabu vingi
vimeongelea jambo hilo. Katika kijitabu hiki tumeleta pamoja uzoefu wa watu wengi,
na kutoa mawazo mengi ya jinsi ya kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na jinsi
magonjwa yanayohusiana na ukimwi yanavyoweza kutibiwa kwa njia za asili.
Toleo la kwanza la kitabu hiki
lilikubalika zaidi ya jinsi tulivyotegemea,
kama chanzo cha msaada kwa hospitali,
zahanati, mashirika yasiyo ya kiserikali,
vikundi vya kijamii, na watu binafsi.
Tunashukuru ukweli kwamba wizara ya
afya ya baadhi ya serikali zimeanza
kutoa miongozo kwa matibabu ya miti
shamba kwa huduma ya wagonjwa wa
ukimwi nyumbani, mfano Malawi
mwaka 1998 “Home – based care herbal
treatment guideline” National AIDS
Control Programme, Ministry of Health,
Lilongwe, Malawi, May, 1998. Kwa
bahati mbaya, matoleo hayo
yanasahihishwa na kuchapwa tena mara
chache sana mara akiba yake na fedha
inapokwisha. Kwa hiyo tunafurahia na
kushukuru msaada wa watu kutoka dunia
nzima kwa mchango wao wa msaada wa
uzoefu kutusaidia kutoa hili toleo la pili.
Tunaamini kwamba kijitabu hiki bado ni
cha kipekee katika kutoa maelekezo na
taarifa juu ya michanganyiko ya madawa
na vipimo vya madawa ya asili.
Tutathamini sana utoaji wako wa taarifa
juu ya mambo yaliyomo.
anamed ipo kwa ajili ya kuendesha
semina za dawa za asili kwa jamii zinazohitaji kupunguza kutegemea wale “tembo”
waliosemwa hapo juu.
Ukimwi na Madawa ya Asili 3
SURA I: UKIMWI: TUMAINI KATIKA KUKATA TAMAA
Upana wa tatizo.
Kutokana na Muungano wa Mpango wa Umoja wa Mataifa katika UKIMWI
(UNAIDS), mwishoni mwa 2003 takwimu za ulimwengu za UKIMWI zilikuwa kama
ifuatavyo (Kwa sehemu kubwa imechukuliwa kutoka HIV/AIDS Policy Fact sheet ya
Henry J.Kaiser Family Foundation, inayochukua takwimu zake kutoka UNAIDS, taarifa
ya ukimwi ya dunia ya 2004, July 2004.Angalia www.kff.org.).
Dunia nzima inakadiriwa watu 37.8 milioni wanaishi na Virusi vya Ukimwi au
wana UKIMWI - ni idadi kubwa isiyowahi kutokea kabla.
Kati ya hao 37.8 milioni, milioni 25 wanaishi kusini mwa jangwa la sahara,
Afrika, ambapo kulikuwa na watu milioni 3 wapya walioambukizwa mwaka
2003. 57% ya walioambukizwa ni wanawake.
Mwaka 2003, inakadiriwa watu 4.8 dunia nzima waliambukizwa virusi, ikiwa ni
pamoja na karibu watoto 630,000 (chini ya miaka 15). Hili ni ongezeko kubwa
kuliko yote tangu janga la Ukimwi lianze.
Watu milioni 2.9 walikufa kwa Ukimwi mwaka 2003. Kati ya hawa karibu nusu
ya milioni walikuwa watoto. Kati ya 15% na 40% walikufa wakiwa na
maambukizi ya ziada ya TB (kifua kikuu)
Dunia nzima watu wengi zaidi wanaoishi na VVU hawajui kwamba
wanaambukizwa.
Mategemeo ya kuishi katika nchi nyingi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara
yanaendelea kushuka kwa kasi – inategemewa kwamba mategemeo ya maisha ya
watoto wanaozaliwa katika nchi 11 hivi karibuni itakuwa zaidi kidogo tu ya miaka 30.
Kutoka: UNAIDS/WHO AIDS Epidemic Update: December 2006
Total: 39.5 (34.1-47.1) million
Watu wazima na watoto wenye Virusi vya Ukimwi mwaka 2006
Ukimwi na Madawa ya Asili 4
Kabla ya pigo la UKIMWI, kwa mfano, Botswana ilikuwa ikishamili, na wastani wa
umri wa watu wake ulikuwa karibu miaka 75. Kwa sasa ndiyo nchi yenye kiwango
kikubwa kabisa cha maambukizi duniani, na inatabiriwa kuwa mtoto atakayezaliwa
mwaka 2010 atafariki kabla hajafikia umri wa miaka 27.
Ingawa kusini mwa jangwa la Sahara ndilo eneo lililoathiriwa sana, hali ni mbaya sana
pia Ulaya Mashariki na Asia nzima, ambako kiwango cha maambukizi kiko juu.
Hizi ni takwimu za kiofisi, zinazotokana na makisio yaliyobuniwa kutokana na
uchunguzi, ambao, mara nyingine, umefanyika katika nchi ambapo vipimo vichache
sana ya VVU vilivyo sahihi vimefanyika. Katika Afrika pia, ni mara chache sana
uchunguzi wa maiti unafanyika. Kwa hiyo ni mara chache sana pia kujua sababu ya kifo
na kwa hiyo inawezekana ni waathirika wa umaskini, au wa magonjwa mengine kama
ukosefu wa lishe au kifua kikuu. Kutokana na upungufu wa lishe wanapungua uzito na
kwa jinsi hiyo kupungua kwa nguvu ya mfumo wa kinga ya mwili wanaoneka na dalili
zile zile za wagonjwa wa UKIMWI.
Matukio haya ni ya hatari pia, na madawa yote ya asili yaliyopendekezwa katika kitabu
hiki ni bora kwa matatizo hayo.
Athari kwa familia na jamii
Athari za UKIMWI zote zinaeleweka vizuri sana katika jamii zilizoathirika.
- Watendakazi katika familia na watunza familia wanakufa; yaani watu ambao kwa
kawaida wanaleta chakula kwenye familia na kutunza watoto. Kisha wanawake
ambao hufanya majukumu ya wanaume wanapata mzigo mzito zaidi.
- Familia nyingi zinabeba mayatima – desturi ya utayari wa familia za ki-afrika
kuwatunza mayatima na ndugu wengine wenye shida katika familia zao ni desturi
nzuri sana lakini inahitaji nguvu na hata fedha
- Kama matokeo ya kuwa na watu wachache wenye uwezo wa kufanya kazi, na
watu wengi wa kulisha, hatari ya upungufu wa lishe, hasa kwa watoto
inaongezeka sana.
- Wakati malipo kwa ajili ya huduma ya matibabu na madawa inapohitajika, mfugo
mara nyingi utatakiwa kuuzwa, na hivyo kuzidi kupunguza mali ya familia.
- Kwa sababu ya kufa kabla ya wakati kwa wasomi na watu wazima, elimu ya jadi
na ujuzi wa kilimo, ufundi na madawa haririthishwi kwa kizazi kingine na
vinapotea.
- Kuongezeka kwa umaskini, na hitaji la watoto yatima kufanya kazi badala ya
kwenda shule, maana yake ni kwamba kizazi kinachofuata hakitakuwa na elimu.
Kwa hiyo kuna mzunguko wa maangamizi. UKIMWI unasababisha umaskini,
upungufu wa chakula utapiamlo, upungufu wa nguvu kazi na upotevu wa elimu. Haya
yote yanawafanya wale wanaobaki kuwa rahisi kwa kuambukizwa VVU/UKIMWI.
Athari katika nchi
Uchumi wa vijiji na miji, kwa jinsi hiyo mikoa mizima na nchi zote kwa jumla,
zinaathirika vibaya sana mara wafanyakazi wanapodhoofishwa na UKIMWI. Kilimo,
viwanda na shughuli zote zinaathirika kwa kuwa haviwezi kufanya kazi kwa juhudi na
nguvu na watumishi wanakuwa na muda wa kuwa nje ya kazi kwa sababu ya
maambukizi mbalimbali, kuhudumia wagonjwa au kuzika waliokufa.
Pamoja na hayo bajeti za Taifa na huduma za Afya zinalazimika kufanya kazi ya ziada
Ukimwi na Madawa ya Asili 5
ili kupambana na janga hili kwa njia za kukinga na kutibu.
Mwitikio kwa UKIMWI
a) Vikundi vya wanakijiji, vikundi vya msingi na mashirika ya wananchi yasiyo ya
kiserikali. Mengi huunda mwitikio mzuri sana kwa rasilimali ndogo sana. Mifano
imeonyeshwa katika sura ya 8.
b) Makanisa. Kwa muda mrefu mengi yamepuuzia tatizo hili. Wahubiri wengi
walihubiri kwamba UKIMWI ulikuwa ndiyo malipo ya dhambi, vivyo hivyo
makuhani wa jadi walichukulia UKIMWI kuwa ni matokeo ya kuvunja mwiko
fulani. Kukataa kwa Kanisa Katoliki kutumia njia za uzazi wa mpango na hasa
matumizi ya kondomu, imelifanya swala hili kuwa gumu zaidi.
Leo makanisa hutambua kwamba upendo wa Mungu ni kwa wote na kwamba
huduma ya Yesu ililenga hasa watu waliotengwa na jamii, na yanashughulikia swala
hili kwa nguvu kwa niaba ya wagonjwa wa UKIMWI. Semina nyingi zaidi za
anamed zinazohusu UKIMWI. Zimeandaliwa na makanisa na misheni.
c) Mashirika ya misaada ya kimataifa. Shirika la wakala wa Maendeleo Uingereza,
Action Aid, kazi yake inaonekana kwa jamii zilizo maskini katika nchi nyingi.
Inatoa misaada ya kuwasaidia watu kujitatulia matatizo wao wenyewe. Kwa mfano,
mwaka 1987 “The AIDS support Organization” (TASO) ilianzishwa Uganda ili
kusaidia watu wenye VIRUSI/UKIMWI na familia zao, na hadi kufikia miaka ya
1990 mwishoni ilikuwa imeanzisha na kuimarisha nchi nzima vituo vinavyotoa
huduma ya ushauri nasaha, elimu ya VVU/UKIMWI, misaada ya tiba na vifaa.
d) Serikali. Taarifa ya kupambana na UKIMWI Uganda ni moja kati taarifa bora zaidi.
Hata katika siku za kwanza za UKIMWI, serikali ya Uganda ilitambua kiwango cha
tatizo kilichokuwa kinawakabiri, iliomba misaada ya kimataifa na ikaweka mikakati
yenye kueleweka. Hii ni pamoja na elimu ya afya kutahadharisha jamii kwa kutumia
radio na televisheni, ushauri kwa walioathirika, na misaada ya tiba. Walikaribisha
mashirika ya kimataifa kama Action Aid na kufanya kazi kwa kushirikiana nayo.
Jambo la kuhuzunisha, serikali nyingine nyingi zimelipuuzia au hata kutojali kabisa
tatizo hili.
e) Uchunguzi wa kisayansi – madawa. Julai 2004, Medecins Sans Frontieres (MSF)
ilitoa taarifa kwamba mchanganyiko wa dawa wenye generic antiretroviral tatu
katika kidonge kimoja imehakikishwa kwa mara ya kwanza katika uchunguzi wazi
kwenye kliniki katika nchi zinazoendelea. Ufuatiliaji wa watu 60 waliotibiwa huko
Yaounde, Cameroon, imeonyesha kufaa sana.na kuwa salama. Mchanganyiko huu
(Generic fixed – dose combinations (FDCs) za antiretrovirals ndiyo msingi mzuri
katika kuelekea kutibu maambukizi ya VVU/UKIMWI katika nchi zinazoendelea.
FDCs zina faida mbili ambazo ni urahisi wa kutumia na kuwa na bei nafuu
ukilinganisha na dawa nyingine zenye majina makubwa (MSF Press release, 2 July
2004), uchunguzi katika Maendeleo kutibu VIRUSI/UKIMWI katika nchi
zinazoendelea. Mchanganyiko wa dozi za dawa za generic antiretroviral
imehakikishwa kwenye majaribio ya kliniki) Lakini hata hivyo, hadi sasa ni 7% tu
ya watu katika nchi zinazoendelea wanaopata huduma ya antiretroviral (chanzo:
UNAIDS)
f. Shirika la Afya duniani (WHO). Mpango wa “tatu kwa tano” unalenga kuhudumia
watu milioni tatu kwa madawa ya UKIMWI hadi kufikia mwaka 2005. Ni wachache
Ukimwi na Madawa ya Asili 6
wanaoamini juu ya uwezekano huu.
g. Mpango wa “tumia kondomu”. Ni wazo zuri kabisa, kama tu kondomu za kutosha
zingepatikana katika ukubwa mbalimbali, katika bei nzuri, kutunzwa mbali na
mwanga wa jua, na kama tu wanaume wangekubali kuzitumia!
h. Ulinzi kwa wanawake. Katika nchi nyingi zinazoendelea ambapo kiwango cha
maambukizi ni kikubwa zaidi kwa wanawake, wanawake hawaruhusiwi kukataa
tendo la ngono. Uchunguzi unaendelea kufanyika juu ya dawa ya kuua vimelea
ambayo watakuwa wanajipaka kabla na baada ya tendo la ndoa ili kuua virusi, lakini
hii haielekei kupatikana baada ya miaka michache ijayo. Nyingine ambazo
zinasaidia na zinapatikana kwa sasa ni kondomu za kike na viwambo (diaphrams)
ambavyo vinazuia virusi kugusa cervix (mlango wa mfuko wa uzazi)
i. Ufadhili. Matumizi ya dunia nzima kwa UKIMWI yameongezeka toka Dola 1.2
bilioni za kimarekani mwaka 2003 hadi kisio la dola bilioni 6 mwaka 2004. Fedha
ya dunia ya kupambana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria katika bajeti yake
inapungukiwa na dola za kimarekani bilioni 1.6 ili kukidhi hitaji lililotegemewa
katika mzunguko wa tatu na ruzuku katika Oktoba 2004. Mfuko wa dunia umelipa
dola bilioni 1.5 za kimarekeni kwa ruzuku kwenye mipango 160 katika nchi 85
katika mzunguko wake wa kwanza na wa pili wa ruzuku. Marekani inatoa fedha
nyingi zaidi kwa UKIMWI kuliko nchi nyingine yoyote, lakini inapendelea
kuzitumia yenyewe bila kushirikiana na nchi nyingine kwa hiyo inakosolewa
kwamba inasaidia makampuni yake ya madawa.
j. Mpango wa kimataifa. Mpango wa kimataifa wa kutengeneza dawa inayozuia
virusi viharibifu inayotengenezwa na nchi zinazotengeneza madawa yawezayo
kununuliwa na watu katika Afrika na Asia una mafanikio kiasi fulani, hasa Afrika
kusini. Lakini, jambo la kusikitisha, ukweli unabaki kwamba hata kama bei
ingepunguzwa kwa 90% bado zisingewafikia watu walio wengi zaidi katika maeneo
ya vijijini.
Baada ya kutaja mambo yote haya, uwezekano kwamba wagonjwa wengi wa UKIMWI
wana uwezekano mkubwa wa kuwa waathirika wa umaskini na magonjwa mengine
yanayohusiana na umaskini, anamed inaamini kwamba dawa za asili ndiyo raslimali
muhimu. Madawa ya asili yanawasaidia watu wa hali ya chini kujiamini kwa sababu
wanakuwa na uwezo mkubwa wa kujitegemea kwa kutumia malighafi inayopatikana
katika mazingira yao na kwa gharama ya chini kabisa. Hatuko peke yetu katika kuamini
kwamba mimea ya madawa ni ya muhimu sana. Vyuo vikuu vingi sana duniani kote
vinafanya uchunguzi na majaribio ya jinsi ya kutumia mimea yenye dawa katika tiba ya
VVU/UKIMWI.
(Awour et al (1993), “Traditional Medicine and herbs for treatment of HIV related ailments in Kenya”
Int. Conf. AIDS June 6-11;
Burford et all (2000) “Traditional Medicine and HIV/AIDS in Africa” Journal of Alternative and
Complementary Medicine vol. 6 (5) pp 457 – 471;
Martin and Edzard (2003) “Antiviral agents from plants and herbs: a systematic review” Antirivival
therapy, vol 8 (2) pp 77 – 90)
Chuo cha “Cornell Medical College, New York, kinasema “katika yote, mimea inatoa matumaini
mazuri katika uchunguzi wa tiba ya HIV. (Chang and Kong (1996) “Meta – survey of plants and herb
material as a treatment for HIV” Int. Conf. on AIDS Canada, July 7-12, vol 11 (1) p 22) .
Ukimwi na Madawa ya Asili 7
Wanaoishi wa Virusi vya Ukiwi mara nyingi
wanaajisikia kuchoka sana
SURA 2: UKIMWI NI NINI?
Kwa ufupi UKIMWI inasimama badala ya ukosefu wa kinga mwilini. Unasababishwa
na virusi vinavyoitwa HIV au Human Immunodeficiency Virus. Kwa kuua au
kudhoofisha chembe nyeupe za mwili, zinazoitwa Lymphocytes, HIV inadhoofisha
mfumo wa kinga mwilini. Kwa jinsi hiyo mwili unapungukiwa uwezo wa kupambana
na maambukizi na baadhi ya aina za kansa.
Kwa jumla watu husemwa kwamba ana Ukimwi kama:
a) Mfumo wake wa kinga unakuwa dhaifu sana kwa sababu ya virusi wa HIV, au
b) Upungufu wa kinga yao unaohusiana na virusi vya Ukimwi unakuwa wa hatari kiasi
kwamba maambukizi yenye kutishia maisha (magonjwa tegemezi) na/au saratani
kutokea.
Mara mtu anapoambukizwa virusi vya ukimwi inamchukua wastani wa miaka 5-8
kupata Ukimwi. Watu wanaweza kuambukizwa virusi vya ukimwi lakini wakajisikia na
kuonekana wazima kwa miaka mingi, kwa jinsi mfumo wao wa kinga unavyoendelea
kupigana na virusi. Ni mpaka baadaye ambapo mfumo wa kinga hauwezi tena
kuukinga mwili, ndipo dalili za ndani na za nje zinaanza kujionyesha.
Watu walio na magonjwa sugu kama TB (kifua kikuu) au wale wanaoteseka kwa
udhaifu wa afya au wanaopata lishe ndogo, wataingia katika hatua ya kuugua ukimwi
haraka zaidi kwa sababu mfumo wao wa kinga tayari ni dhaifu.
Jinsi ya kuutambua UKIMWI
Dalili za UKIMWI ni tofauti kwa
watu tofauti. Kwa muda mrefu
inaweza isiwe wazi kama mtu
ana Ukimwi au la. Dalili ni zile
za magonjwa ya kawaida lakini,
kwa kawaida, yanakuja kwa
nguvu sana na yanadumu muda
mrefu.
Dalili nyingine za kawaida ni:
Kupungua uzito
kunakoendelea.
Kuhara kwa muda mrefu.
Homa ya muda mrefu,
ambayo inaweza kuja na kuondoka
Kikohozi kibaya cha muda mrefu, na maambukizi mengine ya mapafu.
Ukurutu.
Maambukizi ya macho.
Kujisikia uchovu mara kwa mara.
Ugunduzi wa UKIMWI bila vyombo vya maabara
Madaktari wengi wana njia zao za kugundua UKIMWI. Zote zinajumuisha uwepo wa
maambukizi nyemelezi. Panapokosekana zana halisi za kupimia UKIMWI, Shirika la
Ukimwi na Madawa ya Asili 8
Afya duniani (WHO) limependekeza mwongozo ufuatao:
Maana ya UKIMWI ya shirika la Afya duniani kwa watu wazima.
Mahali pasipo na vipimo vya virusi vya UKIMWI, mtu ataonekana kuwa ana
virusi vya UKIMWI kama akipatikana angalau na mbili kati ya dalili hizi kuu
hapa chini zikiwa pamoja na angalau dalili moja ndogo. Mgonjwa asiwe na
sababu nyingine yoyote inayosababisha kupungua kwa kinga ya mwili kama vile
saratani au upungufu mkubwa wa lishe.
Kuwepo kwa kaposis sarcoma au cryptococcal meningitis pekee kunatosha
kuonyesha uwepo wa ukimwi.
Dalili kuu:
Kupungua uzito kwa 10%
Kuharisha kunakoendelea zaidi ya mwezi mmoja.
Homa inayoendelea zaidi ya mwezi mmoja.
Dalili ndogondogo
Kikohozi kinachozidi mwezi mmoja
Kuwashwa ngozi mwili mzima
Jamii ya mkanda wa jeshi inayojirudirudia
Mtando mweupe mdomoni (Oropharyngeal candidiasis)
Maambukizi ya ngozi yanayoendelea na kusambaa mwilini
yanayosababishwa na jamii za virusi
Kuvimba matezi na mitoki (Generalised Lymphadenopathy)
Kupima UKIMWI kwa vifaa vya maabara
Ni kipimo cha maabara pekee kinachoweza kuhakikisha kama kweli mtu ana UKIMWI
au la. Kipimo ni idadi ya 200 CD4+ T-cells au pungufu kwa microlitre kukiwepo na
maambukizi ya virusi vya ukimwi. Watu wenye umri wa miaka 5 na zaidi ambao kinga
yao ya mwili inafanya kazi vizuri kwa kawaida wana CD4+T- cell kati ya cell 800—
1300 kwa microlitre.
CD4+ cell ni nini?
Virusi vya ukimwi hushambulia lympocytes, aina ya chembe nyeupe za damu zilizo na
receptor protein, zinazoitwa CD4, katika ngozi yake ya nje. Cells zenye CD4 receptor
zinaitwa CD4+cells au helper T lymphocytes.
T lymphocytes ni za muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini, kwa sababu
zinasaidia kuulinda mwili dhidi ya aina za virusi, na zinaweza kutambua na kuharibu
baadhi ya chembe za saratani.
Virusi vya UKIMWI vikiingia mwilini, huingia katika T-lymhocytes, na genetic
material za virusi huungana na zile za lymphocyte. Hapo virusi vinazaliana katika ile
chembe na hatimaye vinaiharibu. Pia inatoa virusi vingine vipya ambavyo hushambulia
lymphocytes nyingine.
Retrovirusi ni nini?
Virusi vya UKIMWI ni Retrovirusi. Retrovirusi ni aina ya virusi inayotunza taarifa za
genetic kama ribonucleic acid (RNA) zaidi kuliko inavyofanya deoxyribonucleic acid
(DNA). Virusi vikiingia katika chembe vinatoa RNA yake pamoja na kimeng’enyo
Ukimwi na Madawa ya Asili 9
(enzyme), kisha vinatengeneza DNA kwa kutumia RNA na virusi kama kielezo
(pattern). Kisha DNA ya virusi inaingizwa katika DNA ya ile chembe.
Kila mara ile chembe ikigawanyika hutengeneza nakala mpya ya DNA ya virusi iliyo
kamili pamoja na gene zake. Kwa wakati huohuo DNA ya virusi inaweza kuingilia na
kuifanya ile chembe itengeneze virusi vingine. Virusi hivi vipya humwaga nje ya
chembe iliyoathiriwa na kuvamia chembe nyingine.
Mfuatano wa magonjwa yanayohusiana na UKIMWI
Hatua ya 1: Mwili unaingiliwa na virusi vya ukimwi, na virusi vinazaliana kwa haraka
sana hadi antibodies hutengenezwa mwilini - mchakato unaoitwa “seroconversion“.
Wakati wa seroconversion , watu wengi huugua kwa kuonyesha dalili kama homa,
mwili kutokuwa katika hali yake ya kawaida, kichefuchefu, ukurutu, na vidonda
kuzunguka mdomo, mkundu na sehemu za siri.
Wakati wa kipindi chote hiki mtu ana uwezo wa kumwambukiza mtu mwingine ye yote,
ingawa kipimo cha virusi vya ukimwi huonyesha uwezo wa virusi baada ya
seroconversion kufanyika.
Hatua ya 2: Watu wengi huendelea kuwa na hali nzuri kwa miaka kadhaa wakiwa na
kiwango kidogo cha hivi virusi katika damu yao.
Hatua ya 3: Baada ya miaka 5 hivi, watu wengi huanza kupata matatizo mengi kama
matokeo ya kudhoofishwa kwa kinga ya mwili, kulikosababishwa na idadi ya chembe
za CD4 kuwa chini ya 500 kwa microlitre. Kupungua uzito kwa zaidi ya 10%
kunatokea, mtu anajisikia kutokuwa katika hali ya kawaida, na maambukizi ya nguvu
kama vile kuhara kwa kipindi kirefu kisichoelezeka hutokea.
Hatua ya 4 - UKIMWI: Mara chembe za CD4 zinapokuwa chini ya 200, mgonjwa
anapata maambukizi makuu. Wasipopata matibabu kwa kinga yao ya mwili na
maambukizi hayo, kwa kawaida hufariki katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mfuatano wa magonjwa yanayohusiana na ukimwi
Upungufu wa kinga: Mwanzoni katikati mwishoni
CD4>500 500<CD4>200 CD4<200
1000
Idadi ya
CD4
Cells
kwa 500 micro-
litre
200
0 0 Kama wiki 10 kama miaka 5 kama miaka 10
Sero-
Conversion
Illness
Kipindi kisicho
na dalili
Maambukizi yasiyo na
nguvu sana
Homa, jacho wakati
wa usiku, udhaifu wa
mwili
Magonjwa
nyemelezi
yenye
nguvu
Ukimwi na Madawa ya Asili 10
Ni tiba gani ya hospital iliyokubalika ?
Dawa zinazotumika zinaitwa anti-retroviral (ARV) drugs. Lengo lake ni kupunguza
nguvu za virusi vya ukimwi na kuvizuia kuzaliana, na jinsi hiyo kupunguza kasi ya
ugonjwa.
Kuna makundi matatu ya ARV.
a) Nucleoside reverse transcriptase inhibitors (NRTI) kama vile AZT, ddl, ddc, d4t,
3TC na abacavir.
b) Non –nucleoside reverse transcriptase inhibitors (NNRTI) kama vile nevirapine,
delavirdine na efavirenz.
c) Protease inhibitors (PI) kama vile saquinavir, ritonavir, indinavir na nelfinavir.
“Highly active antiretroviral therapy” (HAART), ni jina la matibabu lililokubaliwa na
mabingwa wa VVU (virusi vya Ukimwi) kwa kudumaza kwa nguvu kuzaliana kwa
virusi na kuendelea kwa ugonjwa
wa VVU. Mfumo wa kawaida wa
HAART unajumuisha dawa tatu
au zaidi, kama vile nucleoside
reverse transcriptose inhibitors
mbili na protease inhibitor moja,
nucleoside reverse transcriptase
inhibitors na non – nucleoside
reverse transeriptase inhibitor
moja, au michanganyiko mingine.
Mifumo hii ya matibabu
imeonekana kupunguza kiwango
cha virusi kiasi kwamba haviwezi
kuonekana katika damu ya
mgonjwa. Hasara yake ni
kwamba sehemu kubwa ya dawa
hizi husababisha madhara, hasa
kichefuchefu, kutapika, kuharisha
na maumivu ya kichwa.
Kama ukibahatika kupata dawa za
ARV, zitumie kwa kufuata
maelekezo. Kutofanya hivyo
kunatoa nafasi kwa virusi
kubadilika kimaumbile (mutate), na
dawa haitaweza kufanya kazi.
Usikose hata dozi moja, na
hakikisha kwamba unaelewa
maelekezo. Kama dawa ikikufanya
usijisikie kawaida au madhara mengine usiache kuvitumia. Mwite kwanza daktari.
Kunaweza kupatikana madawa mbadala.
Watu wengi wana hofu ya kukaa na wagonjwa
wa UKIMWI Hakuna kabisa madhara/hatari ya
kuambukizwa ukimwi kwa kuchangia choo na
mgonjwa wa Ukimwi. Lakini weka choo katika
hali ya usafi na wakati wote nawa mikono yako
baada ya hapo, kuepuka kupata maambukizi ya
aina nyingine.
Ukimwi na Madawa ya Asili 11
Ukimwi hausababishwi na wadudu.
Unaweza kulala kwa usalama karibu
na mgonjwa wa UKIMWI kwa amani
kabisa.
Sura 3: Kuambukiza na kuzuia VVU (Virusi vya Ukimwi)
Sababu za janga la VVU/UKIMWI ni nyingi na za namna nyingi . Mambo
yanayochangia ni pamoja na umaskini, ujinga, uhamiaji na kuhamahama. Kuwa na
wapenzi wengi, jambo lingine la muhimu, pia imepelekea kupata magonjwa mengine
yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana. Kusini mwa jangwa la sahara kujamiiana
kunawajibika katika 90% ya maambukizo ya VVU, kukifuatiwa na maambukizi kutoka
kwa mama hadi kwa mtoto.
Ninaambukizwa kwa namna gani?
VVU vinaweza tu kuishi katika damu, maji ya ukeni, shahawa, na maziwa ya kina
mama walioambukizwa, na vinaweza tu kupelekwa au kuambukizwa kwa njia ya
kubadilishana haya majimaji ya mwili.
Unaweza kupata VVU kutoka kwa yeyote aliyeambukizwa kwa kuwa mara nyingine
inachukua miezi au hata miaka kwa dalili za kwanza za ugonjwa kuonekana. Mtu
mwenye virusi anayeambukiza ugonjwa huu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri.
VVU vinaambukizwa kwa njia zifuatazo:
A. Kujamiiana.
Kwa kufanya mapenzi na mtu aliye na VVU. Katika Afrika sehemu kubwa ya
maambukizi ni matokeo ya kufanya ngono bila kinga.
Kufanya ngono ya mdomoni na mtu
mwenye maambukizi, hasa ukiwa na
vidonda mdomoni mwako au fizi zivujazo
damu. Maeneo mengine vijana hufanya
ngono kwa mdomo ili kulinda ubikira wao.
B. Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Wakati wa mimba.
Wakati wa kujifungua na
Wakati wa kunyonyesha kwa matiti.
C. Damu.
Kwa kutumia sindano au bomba ambalo
halikuchemshwa ili kuua vijidudu tangu
lilipotumika mara ya mwisho.
Kuongeza damu yenye maambukizi.
Kwa kutumia vifaa vya kukatia au kutobolea ambavyo havikuhudumiwa ili kuua
vijidudu. Mfano: Kutoboa masikio, kupiga chale, au kutahiri.
UKIMWI hausambazwi kwa kugusana kwa kawaida na mtu aliyeambukizwa. Tofauti na
malaria hauambukizwi kwa njia ya mdudu wa aina yeyote. Na tofauti na magonjwa ya
njia ya hewa hauambukizwi kwa kuvuta hewa yenye maambukizi.
Kwa hiyo ni salama kabisa
kuishi katika chumba au nyumba moja na mtu mwenye UKIMWI.
kuonyesha heshima au upendo kwa kushikana mikono, kukumbatiana na kubusu
kwenye shavu.
kuchangia choo kisafi na mgonjwa.
kula pamoja.
Ukimwi na Madawa ya Asili 12
Una uwezekano mkubwa sana wa kuambukizwa UKIMWI, kama:
ukifanya mapenzi na mpenzi zaidi ya mmoja.
ukianza kufanya mapenzi katika umri mdogo.
ukifanya ngono bila kinga.
ukikataa kujifunza ukweli juu ya UKIMWI.
usipotibu kwa haraka magonjwa ya zinaa.
ukishiriki katika mambo ya kitamaduni kama vile tohara katika kikundi kwa kutumia
kisu kimoja.
ukirithi mke.
ukihangaishwa na umaskini na matokeo yake:
- ukila chakula kisichotosha na kisicho bora.
- usipopata uchunguzi wa afya na matibabu.
- ukikosa hata fedha ya kununulia kondomu wakati inapohitajika.
- ukihamia sehemu nyingine kutafuta kazi, na kisha kuwa na mahusiano mengine
a kimapenzi au kufanya mapenzi na wanaofanya biashara ya ngono.
Bila chakula, mfumo wa kinga unadhoofika na maambukizi yatokanayo na upungufu
wa chakula yanapata nafasi. Chakula bora ni bora kuliko dawa ya anti-retroviral ya aina
yoyote. Kuna uhusiano kati ya VVU na njaa: VVU kusababisha njaa, na njaa kuchangia
nguvu za VVU. Msumbiji kwa mfano ilipoteza 2.3% ya wakulima wake mwaka 2000
na inategemea kupoteza 20% kufikia 2020 (The Food and Agricultrue Organisation quoted
by Rory Carroll in The Guardian “Africa’s ugly sisters leave trail of death”, 30 October 2002).
Ni wazi kutakuwa na upungufu wa uzalishaji wa chakula, hata katika miaka yenye hali
nzuri ya hewa.
Jinsi ya kuzuia UKIMWI
A. Mambo ya ngono
a) Kutofanya mapenzi kabisa.
b) Kuwa mwaminifu kwa kufanya
mapenzi na mpenzi mmoja
mwaminifu.
c) Kondomu kama wewe au
mpenzi wako akifanya
mapenzi na mpenzi mwingine,
wakati wote atumie kondomu,
na aitumie ipasavyo.
d) Kwa kutofanya mapenzi na
mtu aliye na wapenzi wengi,
hasa kama mmoja kati ya
wapenzi wao ni kahaba.
Kamwe usifanye mapenzi na
mtu afanyaye biashara ya
kuuza mwili wake.
Ukimwi na Madawa ya Asili 13
Virusi vya Ukimwi vinaambukizwa kupitia
damu. Kwa hiyo uwe mwangalifu
unapowahudumia watu waliopata ajali.
B. Damu
a) Kwa kuhakikisha kwamba vifaa vya kutahiria, kutobea masikio vinachemshwa
kila wakati kabla havijatumika.
b) Kwa vyovyote ikiwezekana jaribu kuzuia upungufu wa damu na hivyo kuepuka
kuongezwa damu. Kama ni lazima uongezwe damu uliza kama imepimwa kuona
kama ina virusi vya UKIMWI.
c) Kwa kupata Ushauri Nasaha kutoka kwa mganga wako au kliniki kwa ajili ya
huduma baada ya kugusa damu kwa bahati mbaya au majimaji ya wakati wa
ngono, kubakwa au kuchomwa kwa sindano iliyotumika au wembe.
d) Kwa kuvaa mipira wakati wa kushika damu, mfano wakati wa ajali au wa kutoa
huduma ya kwanza. Damu inaweza kuwa na VVU na vinaweza kuingia mwilini
kwa njia ya jeraha au vidonda katika mikono yako.
C. Kutibu maambukizi.
a) Kwa kutibu maambukizi yote
haraka iwezekanavyo na kwa
uhakika.
b) Kwa kuchunguza magonjwa
ya ngono (STD) vidonda vya
sehemu za siri na majimaji
yatokayo katika uume au uke,
na kuyatibu haraka
iwezekanavyo. Magonjwa ya
ngono yanaongeza uwezekano
wa maambukizi ya VVU,
lakini yanaweza kutibiwa
haraka na kwa uthabiti.
D. Kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto
Kama mama ameambukizwa VVU
uwezekano wa kumwambukiza
mtoto wake umekadiriwa kuwa kati
ya 15% na 45%. Hii imegawanyika
kama ifuatavyo: (TALC, ” HIV
Infection – virology and transmission
(Africa)”
5-10 % wakati wa mimba.
10-20 % wakati wa kujifungua
2-10 % miezi miwili ya kwanza ya kunyonyesha kwa matiti.
5-10 % wakati wa kuendelea kunyonyesha.
Katika baadhi ya nchi dawa ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya VVU toka kwa
mama kwenda kwa mtoto inapatikana. Ni muhimu pia kutoongeza uwezekano kwa
kutofanya mapenzi bila kinga. Uwezekano kwa njia ya kunyonyesha unaweza
kupunguzwa kwa kunyonyesha kwa njia ya chupa, lakini hiyo inaweza kusababisha
madhara mengine, yawezekana makubwa zaidi.
Ukimwi na Madawa ya Asili 14
Sura 4: Njia ya anamed
Kwa nini “Madawa ya Asili?”
Kwa karne nyingi waganga wa kienyeji wamekuwa ndiyo watoaji wakuu wa huduma ya
afya ya msingi kwa waafrika wengi zaidi. Hata leo, inakadiriwa na shirika la Afya
duniani (WHO) kwamba 80% ya watu walio kusini bado wanatumia huduma ya afya ya
jadi kwanza. Kwa upande wa viwanda, shirika la afya duniani linakadiria kwamba 25%
ya madawa yanayopatikana kibiashara yametokana na mimea ambapo kwanza
yalitumika kwa kienyeji.
Kwa hiyo mimea imekuwa ikichangia sehemu muhimu katika suala la afya, na kwa
watu wengi zaidi katika sehemu za vijijini Afrika, bado wanaendelea kuitumia.
Kazi ya mimea ya madawa Ulaya na Amerika kaskazini ni ya muhimu vilevile,
inaendelea wakati wote kuchunguzwa ili kugundua dawa mpya.
Kwa kawaida dunia nzima kumekuwa na tabia yenye nguvu ya watu kupendelea
kutegemea huduma za afya za kizamani maana yake ni kwamba waganga na wauguzi
kwa upande mmoja na madawa ya kujitengenezea kwa upande wa pili. Watu wameanza
hata kugundua kuwa huduma za afya za kisasa ndizo zimekuwa chanzo cha matatizo ya
afya zao kuliko hata wao wenyewe.
Huko Ulaya na Amerika ya Kaskazini leo, hesabu ya watu wanaotumia tiba za asili
inazidi kuongezeka. Kwa mara nyingine wamekatishwa tamaa na kwamba madawa
mengi ya kibiashara yana madhara mabaya sana, na wanatamani kwa mara nyingine
kuchunga maisha yao kuliko wakati wote kuwategemea waganga maalum.
Mtu kuwajibika kwa afya yake maana yake ni kujali
a) kile anachokula na kunywa – yaani kupenda vyakula vya asili (vilivyolimwa
nyumbani), maji ya matunda na maji safi ya kunywa.
b) mtindo wa maisha - mfano kwa kutumia choo ambacho kinakuwa safi wakati
wote, kwa kufanya mazoezi, kwa kunawa mikono baada ya kutoka chooni na
kabla ya kula, kwa kutokuvuta sigara n.k.
c) hitaji la watu katika jamii kufanya kazi kwa pamoja, kwa mfano kufanya
maamuzi ya pamoja katika jamii, kuanzisha miradi ya kijamii n.k
d) kutafuta huduma bora mtu akiugua
Kwa sababu ya kuwa tegemezi katika madawa ya viwandani, wengi wetu tumepoteza
ujuzi na stadi za kutumia malighafi za asili kujitibu.
Tunajuaje kuwa madawa tuliyopendekeza ni salama na yanafaa?
Wengi wameuliza jinsi anamed ilivyounda mchanganyiko wa madawa katika vitabu
vyetu. Kwa miaka 20 iliyopita tumetumia mbinu hii:
1. Tunakusanya taarifa kuhusu mmea fulani au ugonjwa kutoka katika maktaba
mbalimbali, Internet, na kwa watumiaji wa mimea au madawa ya asili.
2. Tunaamua ubora na kufaa kwa kile tunachokipokea. Kuna michanganyiko mingi
ya madawa ambayo watu wameiendeleza toka kizazi hata kizazi. Kama
tukigundua kwamba mmea ule ule umekuwa ukitumika kwa njia ileile kutibu
ugonjwa ule ule katika dawa za jadi kwa zaidi ya nchi moja, basi hii inakuwa ni
njia ya kisanyansi, isiyo ya majaribio, na tuna uhakika zaidi katika mchanganyiko
Ukimwi na Madawa ya Asili 15
huu.
3. Tunatathimini dawa kwa kuangalia jinsi inavyofanya kazi na madhara yake –
tunalinganisha faida na hasara zake.
4. Ndipo tunawashirikisha washirika wetu waliotapakaa duniani pote katika hali ya
“kushirikishana ujuzi wa jadi” ambao lazima utumiwe kwa tahadhari.
5. Tunaupandishwa “ujuzi wa jadi” hadi kuwa “mapendekezo katika dawa ya asili”
kama
a) mchanganyiko huu tayari ni sehemu ya dawa za kisasa, (mfano eucalyptus
tincture),
b) masomo ya utabibu sasa yamehakikisha uwezo wake (mf. chai ya Artemisia)
au
c) washirika wetu katika nchi za tropiki wanatupa habari za matumaini makubwa
(mfano chai a mchaichai kwa wagonjwa wa UKIMWI).
Msingi wa Kikristo kwa anamed.
Mungu Baba aliumba dunia, na uzuri wake wa aina mbalimbali za viumbe hai, mimea
na wanyama. Alituweka katika dunia iliyojaa maliasili, ili kwamba kila jamii ya
viumbe vipate kukidhiwa mahitaji yake, kuvisaidia kuishi maisha bora. Aliumba
mwanadamu awe wakili katika mali hizi kuvilinda na kuvidumisha, na kugundua
matumizi yake. Mungu Mwana alikuja kama kristo masihi kutufundisha jinsi
tunavyoweza kuokolewa katika uchoyo wetu na katika hisia za hatia kwa makosa yetu.
Alionyesha kuwajali maskini na waliotengwa na jamii na akaendelea kuponya
wagonjwa.
Mungu Roho Mtakatifu anatupa nguvu na hamasa kupita katika hatua za Yesu katika
kuwafikia watu katika hitaji lao la ndani. Hii inajumuisha huduma ya uponyaji,
msisitizo ukiwa kwa wale wasioweza kulipia matibabu ya kawaida.
Kwa njia ya “dawa za asili” kwa hiyo, anamed inalenga kusaidia watu
a) kugundua tena mimea inayoweza kuponya. Maana yake ni kujifunza kugundua na
kustawisha mazao ya madawa, kutengeneza madawa na kutibu maumivu na
magonjwa.
b) kulinda rutuba ya ardhi, usalama wa maji ya kunywa, thamani ya mazingira na
jamii zote za mimea na mazingira.
c) kushirikiana kuinua afya zao na afya za kimwili na za kiuchumi za jamii kupitia
uzalishaji wa kawaida wa vyakula, madawa na huduma mbalimbali.
d) kukuza stadi na kujiamini kunakotakiwa kujenga ushawishi wa kisiasa, ili
kwamba miundo inayoruhusu malengo haya kufikiwa iendelezwe.
e) katika yote haya kumfurahia Mungu na uumbaji wake.
anamed leo ni ushirika wa watu na makundi yaliyosambaa dunia nzima, na hasa Afrika,
ambao wanatenda kazi katika hatua za mwanzo kabisa kuwasaidia watu kujitegemea
zaidi kwa upande wa afya zao na kuboresha hali zao kijamii, kiroho, na kiuchumi.
Vikundi vya anamed vinakutania DR. Kongo, Eritrea, Ethiopia, Ujerumani, Kenya,
Malawi, Msumbiji, Myanmar, Nigeria, Afrika ya Kusini, Sudani, Switzerland, Tanzania,
Uganda na Ukraine.
Ukimwi na Madawa ya Asili 16
Maana ya dawa za Asili
Faida za dawa za kimagharibi (za kisasa) Faida za dawa za asili, za mimea.
1. Zinajali usafi 1. Inatumia mimea inayopatikana katika
mazingira ya watu.
2. Zimekubalika kisayansi na kimataifa
2. Matumizi ya mimea matokeo yake ni
kiwango kidogo sana cha takataka zenye
madhara yanayoonekana kwa sasa na
yatakayoonekana baadaye.
3. Mganga ana mafunzo mengi, hivyo
anaelewa vyema mwili na ugonjwa.
3. Hakuna tatizo la fedha za kigeni kwa
madawa ghali, wala kuchelewesha
forodhani.
4. Wagonjwa wanafanyiwa uchunguzi
kamili kwa vipimo vya maabala
4. Kuna gharama chache kwa mganga,
hivyo ni nafuu kwa mgonjwa.
5. Dozi ni sahihi kabisa 5. Huleta ajira binafsi kwa bustani za
madawa na utengenezaji wa madawa.
6. Dawa zinatunzwa vizuri
6. Fedha zinazolipwa kwa huduma zinakaa
kijijini kwa hiyo zinachochea shughuli za
kijijini.
7. Mimea inatambulishwa kwa majina yake
ya kisayansi.
7. Mganga anaangalia pia matatizo ya
familia na jamii.
8. Serikali inasimamia viwango vya
huduma za tiba. 8. Inahamasisha kujitegemea.
9. Idadi kubwa ya wagonjwa inaweza
kutibiwa (mfano katika mlipuko wa
Ugonjwa)
9. Mganga anatumia lugha ileile ya watu.
10. Kuna ujuzi katika usimamizi na uongozi.
10. Waganga wa jadi wameenea nchi nzima,
hata vijijini zaidi na maeneo yasiyofikika
kwa urahisi.
11. Inafanya kazi bila ulozi. 11. Mara nyingine ndiyo huduma pekee ya
tiba inayopatikana.
anamed inaeleza maana ya “dawa za asili” kama
mchanganyiko wa faida za dawa za jadi za mitishamba na faida za dawa za kisasa.
Kwa hiyo, dawa za asili zina faida zote zilizotajwa hapo juu.
Kwa nyongeza waganga wa dawa za asili wanahamasishwa
a) kuelewa afya kwa undani wake, na kujali ubora wa maji ya kunywa, vyoo, nyumba
nzuri (mfano dohani), elimu, utunzaji wa ardhi na utupaji wa takataka
b) kutunza mazingira, kupanda miti na kulinda miti ya dawa porini.
c) kutengeneza bustani za madawa ili kupata kiwango cha dawa kinachofaa, matunda na
mbogamboga.
Kwa njia hii, huduma ya afya inayoeleweka zaidi hata katika kiwango kidogo cha bajeti
ya afya, inaweza kutolewa.
Ukimwi na Madawa ya Asili 17
Ukiishi na VVU na
kupata mimba, lishe bora
ni muhimu sana.
Ujamiiane na mme wako
tu na hata kwa hiyo
utumie kondom.
SURA 5: KUISHI NA UKIMWI/ VVU KWA MATUMAINI
Wagonjwa wa UKIMWI wanahitaji huduma maalumu kwa hiyo wahudumie kwa
upendo, huruma na kuwatia moyo!
Paracelsus, mwanafizikia mswizi wa karne ya 16, alisema juu ya tabibu “Msingi wa
muhimu kuliko yote katika dawa ni upendo“. Kwenye Biblia, Mithali 17:22 inasema juu
ya mgonjwa “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha
mifupa”.
Kwa vitendo kumtibu mtu kwa upendo, huruma na kumtia moyo maana yake ni:
a) Kumweka mgonjwa katikati ya familia. Mkumbatie na mmfanyie mambo mengi
yanayohusisha kumgusa kimwili mwongee naye sana. Kama hawezi kuamka,
mweke katika chumba chenye shughuli nyingi nyumbani na kwenye mambo
mbalimbali na ya kumvutia kama inavyowezekana. Mpe matumaini, watu wengi
wamedumu hai wakiwa na magonjwa ya hatari sana, hata UKIMWI.
b) Wasaidie wagonjwa kujisikia wana thamani na umuhimu. Wagonjwa wanaweza
kusaidia katika bustani, kuwatunza wagonjwa wengine walio wagonjwa zaidi yao,
kutoa maelezo ya ugonjwa katika mashule na kutoa msaada na kutia moyo
wagonjwa wengine wa UKIMWI. Wakati wote kuna mambo mengi ya kufanya!
Hospitali liwe kimbilio la mwisho.
c) Tayarisha chakula bora. Wagonjwa wa UKIMWI,
kama watu wote kwa kweli, lazima wale lishe bora
ambayo ina proteini, vitamini, na madini. Matunda
na mboga za majani vina umuhimu wake katika
kumfanya mtu azidi kuwa na afya. Juice ya matunda
ya asili na chai ya mimea ya madawa (angalia sura
inayofuata) lazima vinywewe. Vinywaji vya
kibiashara vyenye sukari lazima viepukwe kabisa.
Maji salama kutoka kwenye kisima kilichotunzwa
ndiyo bora zaidi.
Fuata maelekezo yaliyotolewa katika sura I ya
“Madawa asili katika eneo la Tropiki: Tiba” Kama
una miti ya Moringa, tengeneza na utumie unga wa
majani ya moringa. Ni kirutubisho bora kabisa katika
vitamini, madini na proteini zilizomo.
Watu walio na virusi vya ukimwi wanahitaji vitamini
na madini zaidi kila siku kuliko wale wasio na virusi.
Madini muhimu ya zinki, magnesium, na chuma
yanapatikana kwenye mboga za kijani, jamii za
karanga, moringa, vitunguu saumu, uyoga na mayai n.k.
Ni bora kwa wagonjwa kula kidogo kidogo kila wakati, kuliko kutegemea kiasi
kikubwa cha chakula kinachopatikana mara chache kwa siku. Walio wagonjwa sana
wanatakiwa kupewa chakula ambacho kinayeyuka kwa urahisi kama vile supu
kuliko vyakula vigumu.
Kwa njia hizi kupoteza uzito kunaepukwa na mwili unakuwa na nguvu zaidi – na
hivyo kujikinga na maambukizi.
Ukimwi na Madawa ya Asili 18
Fanya kazi na wenzako!
Shirikishana matatizo na wengine
Someni kitabu hiki kwa pamoja
Anzisheni na msimamie bustani za mimea ya
madawa, mboga mboga na miti ya matunda.
Tengenezeni dawa za asili kwa pamoja.
d) Punguza uwezekano wa maambukizi. Tayarisha maji salama, tunza vyoo kwa
usafi, epuka hewa yenye moshi wa sigara, na epuka maambukizi toka kwa watu
wengine.
e) Fanya mazingira yawe ya kuvutia kadri iwezekanavyo. Fanya chumba kiwe cha
kupendeza, mwanga wa jua uwake ndani, na picha kwenye ukuta. Weka kitanda
kizuri. Tunza godoro kwa plastiki au shuka zilizorahisi kufua. Weka chandarua na
weka maua na majani yanayofukuza mbu chumbani. (mfano: tagetes, michaichai,
artemisia, mkaratusi).
f) Fanya massages: Tengeneza mafuta ya kuchua kwa kutumia mchanganyiko wa
majani ya mkaratusi na majani ya mlimau (angalia “maumivu ya misuli”, Sura 7)
g) Tibu magonjwa nyemelezi mara moja. Watu wachache wenye UKIMWI hufa kwa
athari za moja kwa moja za maambukizi ya VVU. Kwa kawaida kifo husababishwa
na mkusanyiko wa athari mbalimbali za maambukizi ya fursa au vimbe mbalimbali.
Viumbe au magonjwa ambayo kwa kawaida huleta tishio dogo kwa watu wenye afya
vinaweza kupelekea kifo kwa haraka kwa wale wenye UKIMWI hasa idadi ya CD4
+ lymphocyte inapopungua chembe 50 kwa microlitre ya damu.
Kwa hiyo ni muhimu kutibu maambukizi yote ya wagonjwa wa UKIMWI haraka na
kwa uhakika – angalia sura 7.
Kama una UKIMWI:
Kaa juani angalau nusu saa kila siku, ili kunufaika na miale ya nguvu za jua
inayoleta vitamini D
kwa ajili ya ngozi.
Fanya mazoezi kila
siku. Ni muhimu
kudumu na siha njema
kwa kadri uwezavyo.
Kwa hiyo kufanya kazi
kiasi fulani - kama kazi
ya bustani ndogo -
kunasaidia sana.
Uwe na matumaini. Mshukuru Mungu kwa
kila kitu katika maisha
yako ambacho ni cha
matumaini. Uone
UKIMWI kama
changamoto, ambayo
haiwezi kukushinda.
Wakati wote tumia kondomu wakati wa
kujamiiana ili
kutojiongezea
maambukizi au mwenzi wake.
Ukimwi na Madawa ya Asili 19
Mchukulie mgonjwa wa ukimwi
kama mwenzenu katika familia!
Mnaweza kula pamoja na
kuchangia vyombo mkiwa salama
kabisa. Tumieni muda wenu pamoja
naye kama ilivyokuwa kawaida
Endelea kufanya kazi! Kama ni kulima
shambani, kufanya kazi kama
seremala, au kufanya kazi ofisini - po
pote pale: endelea kufanya kazi! Fuata
maelekezo yaliyopo kwenye sura
inayofuata ili kuongeza kinga yako
kwa kutumia madawa ya asili.
Kwa ufupi: Kwa kutoa aina hii ya upendo na kujali, maambukizi makuu
yanayoambatana na UKIMWI yanaweza kupunguzwa sana. Familia nzima na jamii
vikifanya kazi kwa ushirikiano, maisha ya kiroho ya wote yananufaika.
Mwanakanisa wa kujitolea anayefanya kazi na Family AIDS Caring Trust (FACT)
Zimbabwe (HIV/ AIDS Study Pack for Community Development Workers, Tearfund, 1999)
aliandika yafuatayo:
“Walimjengea kijumba kidogo ambapo alilala mchana na usiku, akisubiri kufa. Hakuna aliyemtembelea kuongea naye, hata kuweka chakula chini tu na kuondoka. Nilienda kumtembelea lakini hakuna aliyeniruhusu kuingia katika chumba chake. Niliwasihi waniruhusu. Nilipofungua mlango ili kuingia, kulikuwa na harufu kali usiyoweza kuamini! Nilitoka nje nikatafute maji na kuyachemsha, nilimwosha nikisaidiwa na vijana wawili katika familia hiyo. Tulimweka juani - jambo ambalo alikuwa hajapata kwa miezi. Tulisafisha chumba chake na kufua nguo zake na blanketi ambazo zilikuwa zimegandamana kwa uchafu. Wakati tukisafisha chumba, uji ulikuwa ukitokota jikoni. Baada ya usafi, nilikaa pale nikimnywesha uji na kuongea naye. Kila siku nilikwenda kumwona, kumwosha na kumlisha. Ndugu na jamaa zake wakaanza kufanya hivyo hivyo. Alifariki baada ya majuma matatu, siyo tena kama aliye najisi na kutengwa bali kama aliyependwa aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Nilipomwambia Mungu anampenda na kwamba Yesu alikufa kwa ajili yake, alishikilia mkono wangu kwa nguvu. Ni kwa jinsi gani habari hii ni ya hatari ! Unafahamu matukio mengine yaliyo kama hayo? Kama tu familia hii wangechukulia sura hii ya kitabu kwa umuhimu, na wangekuwa wanajua juu ya madawa ya asili! Huyu mtu labda angeishi maisha mazuri kwa miaka kadhaa zaidi”.
Ukimwi na Madawa ya Asili 20
SURA YA 6: Chochea mfumo wa kinga mwilini kwa madawa ya asili
Kwa ujumla, dawa za ukimwi, ziwe za viwandani au za asili, zinafanya kazi ya:
1. kuzuia kuzaliana kwa VVU na |au.
2. kuua virusi vya UKIMWI na | au.
3. kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (kwa kuongeza idadi ya chembe za T-
helper) na | au.
4. kuponya dalili za UKIMWI (kwa mfano kuharisha kunakoma, uzito
unaongezeka, siku za hedhi zinandelea tena, matatizo ya ngozi yanatoweka, na
matatizo ya kiakili (kisaikolojia) yanapungua.
Kuimarisha mfumo wa kinga, njia zote zilizotajwa katika sura iliyopita lazima zifuatwe.
Hasa hakikisha kwamba chakula chako ni bora na ni mlo kamili na ukae na hali nzuri ya
mwili kadri uwezavyo, tembea, endesha baiskeli au fanya kazi yoyote ya viungo katika
shamba kila siku. Kwa nyongeza, tumia angalau moja kati ya madawa ya asili
yafuatayo:
1. Allium sativum (vitunguu saumu) Weka vitunguu saumu vingi iwezekanavyo katika chakula cha kila siku, ili kuimarisha
mfumo wa kinga.
Subhuti Dharmananda (Subhuti Dharmananda (1996) “Garlic as the central Herb therapy for
AIDS” Institue for Traditional Medicine, Portland, Oregon, USA. Habari nzima inaweza kusomwa
kwenye web-site ya Gaia Research Institute, South Africa: www.gaiaresearch.co.za/garlic.html)
anapendekeza yafuatayo;
“Mara kiwango cha CD+T-cells kinapopungua kama 200 kwa mm³, matumizi ya dawa za
anti-retroviral hamna maana tena. Kushindwa kwa namna hiyo katika mfumo wa kinga
mwilini kunaendelea kwa kasi zaidi mara ukimwi unapostawi. Kwa hiyo, kila
liwezekanalo lifanyike ili kuzuia UKIMWI usistawi zaidi, na kutibu mara moja
maambukizi yoyote yanayojitokeza, ili kutoupa mzigo mfumo wa kinga mwilini.
Idara ya dawa za jadi inapendekeza dozi ya gramu 50 za vitunguu saumu kila siku (kama
kitunguu kimoja kizima) kwa matibabu ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa
wagonjwa wa UKIMWI. Kwa lengo la kuzuia maambukizi mengine mbalimbali dozi ya
chini kidogo inashauriwa ambayo ni vikonyo vitatu kwa siku.
Vitunguu saumu vinafanya kazi kama antiseptic, antibiotic, antiviral, anti-fungal, na anti-
diabetic. Umuhimu wake kwa UKIMWI ni kweli kwamba vitunguu saumu vimeonyesha
kuwa na uwezo kuzuia herpes simplex 1, ambayo ni aina ya virusi vinavyochochea
kuzaliana kwa VVU.
Watu wanaopata maumivu ya tumbo kama matokeo ya kula kiasi kikubwa cha vitunguu
saumu, wanashauriwa kunywa kiasi kidogo cha mafuta ya maji kama vile Alizeti au siagi
ambayo hufunika ngozi za tumbo na husambaza viasili vinavyosababisha maumivu. Huko
China vitunguu saumu vinatumika kutibu madonda ya tumbo.”
Kuna mabishano juu ya matumizi ya vitunguu saumu wakati mtu anatumia dawa za
ARV. Wachunguzi wengine wanasema vitunguu saumu vinapunguza nguvu ya dawa za
ARV, wakati wengine hawakubaliani (Dr. J.M. Louw (2004) “Garlic for HIV” - unpublished
paper, MEDUNSA (Medical University of South Africa) .
2. Artemisia annua
Kutokana na vitabu mbalimbali, wagonjwa wengi zaidi wa UKIMWI wana kinga ndogo
Ukimwi na Madawa ya Asili 21
katika chembe za mwili (cellular immunity) na kinga kubwa katika majimaji ya mwilini
(humoral immunity). Maana yake ni kwamba wana kiwango kidogo cha T-helper cells,
na kiwango kikubwa cha antibodies zinazoweza kuyeyuka. Kutokana na Dharmananda
(http:/www.gpo.or.th/rdi/NetZine./V3N42/pcp.htm) pamoja na haki miliki fulani (Luo,
Xuande (1998) “Qinghaosu Derivates against AIDS” European Patent Office, EP
713877), artemisinin inaongeza kinga ya chembe na kupunguza kinga katika majimaji
ya mwili na kwa hiyo kurudisha ulinganifu katika hali hii ya mwili.
“Mganga wa madwa ya kichina katika jiji la New York (Susan Paul) amekuwa akitumia
mmea huu katika kutibu wagonjwa wa UKIMWI kwa miaka mitatu iliyopita na amedai
kuwa ni salama na yenye manufaa dhahiri” (Dharmananda).
Haki miliki iliyotajwa hapo juu inasema “Lengo la ugunduzi wa sasa ni kupata kuzuia
UKIMWI chenye kiasi kidogo cha sumu, bei ndogo …” na pia linadai kwamba, kwa
kulinganisha na dawa za retroviral za kawaida, vitu vinavyopatikana katika Artemisia
annua“vina uwezo mkubwa wa kuua VVU , wakati uleule madhara ni machache!”
Sisi katika anamed hatujui ni kwa kiasi gani hii ni kweli, lakini watu wengi wenye VVU
wamefaidika kwa kiasi kikubwa sana, kama inavyodokezwa na habari ifuatavyo:
Sister Beatrice, muuguzi katika hospitali fulani huko Afrika ya Kusini, amelima shamba la Artemisia annua. Anatumia majani yake mabichi kila wakati kwa kutibu wagonjwa wa UKIMWI, wagonjwa wa njia ya hewa, kikohozi na mafua. Alitusimulia habari ifuatavyo:
Mfanyakazi wa hospitali aliyekuwa na VVU alikuwa anaharisha na kukohoa kwa majuma matatu. Alipewa maji chumvi (ORS), lakini alizidi kuwa dhaifu. Beatrix alitengeneza chai kwa kutumia viganja viwili vya majani ya artemisia. Siku moja baadaye mgonjwa alikuwa bado dhaifu, lakini aliweza kutembea na alipata njaa. Mgonjwa aliendelea kunywa chai ya artemisia na akaaanza kujisaidia haja kubwa ya kawaida, kikohozi chake kikakoma, alikula na kuongezeka uzito na ngozi yake ikawa na hali nzuri. Alipokuwa amekonda hakuna aliyemtembelea – lakini sasa wanamtembelea.
Kwa kupata historia hii tunaendelea kupendekeza yafuatayo: Kwa siku kumi za kwanza
weka lita moja ya maji yanayotokota kwenye vijiko vitatu vya chai vya majani makavu
ya artemisia. Iache kwa angalau dakika 15, ichuje na uinywe katika siku moja tu.
Baada ya hapo, kila siku, changanya kikombe kimoja (ml 250) za maji yanayotokota
katika kijiko kimoja cha majani makavu ya A-3. Acha itulie kwa angalau dakika 15,
chuja na kunywa chai hii asubuhi.
Kijiko kimoja cha chai cha majani makavu ya artmesia ni kama gramu 1.5. Badala ya
haya unaweza kutumia pia gramu 7.5 za majani mabichi. Kwa hiyo, kama una miti ya
artmesia shambani kwako, unaweza kuvuna majani kila siku. Idara ya Mazao ya Asili
huko Punjab, India, imeorodhesha Artmesia annua kama majani ya mimea 52 ambayo
“ina nguvu sana kuhusiana na UKIMWI na inayochunguzwa juu ya UKIMWI na
madhara yake, na imeonyesha kuwa na uwezekano wa kupambana na VVU”
(Bharate sandip B(2003) “Medicinal Plants with anti HIV potential” Journal of Med.
And Aromatric Plant Sci June, vol 25 (2) pp 427-440).
3. Azadirachta indica (mwarobaini)
Uwezekano wa maambukizo ya ngozi unaweza kupunguzwa kwa kutumia wakati wote
sabuni ya mwarobaini au maji ya kuogea ya moto ambamo kumewekwa majani ya
Ukimwi na Madawa ya Asili 22
mwarobaini. The Kibisom Project (Kenya), inayoshughulika na wagonjwa wengi wa
UKIMWI, inashauri kwamba wale makapi ya mwarobaini kila siku (yanayotokana na
mabaki ya mafuta ya mwarobaini). The Permaculture Project (Malawi) na Kuluva
Hospital (Uganda) wanatengeneza unga wa majani makavu ya mwarobaini na
wanawapa wagonjwa wa UKIMWI kijiko kimoja hadi viwili vya chai mara moja kwa
wiki.
4. Cymbopogon citratus (mchaichai)
Chai ya mchaichai: Chemsha kiganja kimoja cha majani mabichi ya mchaichai kwa
dakika mbili katika lita moja ya maji, acha kwa dakika 15 kisha chuja kwa chujio la
chai. Kunywa lita 2 kwa sehemu sehemu katika siku moja. Katika Moretele Sunrise
Hospice kule Afrika ya kusini Mpho Motlhasedi na wenzake wamegundua kwamba
wagonjwa wa UKIMWI wanaokunywa dawa hii kwa kufuata kanuni hii wanapata hamu
ya chakula, wanaongeza uzito na wanakuwa na nguvu.
5. Mangifera indica (mwembe)
Chai ya majani ya mwembe: Chukua kiganja kimoja cha majani machanga ya kijani ya
mwembe, chemsha taratibu katika lita moja ya maji kwa dakika 15, chuja na unywe
kwa sehemu sehemu katika siku moja.
6. Aloe vera
The Insitute of Herbal Medicine (Nairobi, Kenya) inafanya
uchunguzi wa Aloe katika kuimarisha kinga ya mwili. Aloe ina
acemannon, kiasili kinachoharibu VVU kwa kubadili ngozi yake
ya proteini kiasi kwamba haiwezi ikajishikiza kwenye T-
lymphocites. anamed inashauri kwamba wagonjwa wa UKIMWI
watumie kijiko kimoja hadi viwili vya nyama laini ya ndani ya
aloe kila siku.
7. Mazao ya asili ya Nyuki
Idara ileile inashauri matumizi ya Propolis kwa wagonjwa wa UKIMWI. Inapatikana
katika mizinga ya nyuki na imeonyeshwa kufanya kazi kama antibiotic, antifungal,
antiseptic na antiviral. anamed Bukavu (D.R Kongo) inatoa chai ya artemisia na
mchanganyiko wa asali na aloe kwa siku 20 kila mwezi na kitunguu saumu kila siku.
Chai ya Artemisia inatumika kama kwa malaria. Nyama laini za ndani za majani matatu
ya aloe zinachanyanywa na lita moja ya asali, na dozi yake ni vijiko vitatu vya
mchanganyiko huu mara tatu kwa siku, kabla ya kula. Vikonyo 10 vya vitunguu saumu
vinakatwa vipande vidogovidogo na kunywewa kwa maji mara tatu kwa siku.
8. Dawa ya maji (tincture) ya UKIMWI.
Daktari wa Hospitali ya ki-katoliki ya Neisu, D.R.Kongo, ametengeneza mchanganyiko
ufuatao wa madawa ambao wamekuwa wakiutumia kwa miaka kumi:
Kausha na usage kiasi kilicho sawa cha majani ya baadhi au yote kati ya mimea
ifuatayo: Azadirachta indica, Artemisia annua, Ocimum basilicum na Aloe vera.
Changanya gramu 100 za unga huu na ml 700 za kileo 95 % (kinachonywewa) na ml
300 za maji yaliyochemshwa. Chuja baada ya juma moja. Kunywa matone 30 mara tatu
kwa siku.
Ukimwi na Madawa ya Asili 23
SURA 7: Jinsi ya kutibu magonjwa yanayohusiana na UKIMWI kwa
mimea ya madawa
Kumbuka 1: Katika michanganyiko hii, mkono mmoja maana yake ni kiasi ambacho
mgonjwa anaweza kubeba, au kuficha, katika kiganja chake.
Kumbuka 2: Rejea zinafanywa mahali pote katika sura hii kwa matoleo mengine ya
anamed, kama ifuatavyo:
NM I “Madawa Ya Asili Katika Nchi Za Joto I; na Hirt na Mpia,
NM II “Madawa Ya Asili Katika Nchi Za Joto II: Uzoefu”
NM III “Natural Medicine in the Tropics III: Teachers´ Resource Kit“
Kumbuka 3: Siyo michanganyiko yote ya madawa inaweza kutengenezwa nyumbani
kwa urahisi. Tunapendekeza kwamba muungane au mtengeneze kikundi chenu cha
kusaidiana. Tafuteni msaada wa muuguzi au mfamasia katika kundi lenu ili kutengeneza
dawa nzuri zaidi za asili, au dawa za “kemikali” zinazotolewa katika NM III kwa
matatizo ya ngozi.
Kumbuka 4: Katika sura hii tunaorodhesha dalili au magonjwa mengi ambayo mara
nyingine, lakini siyo wakati wote, yanahusiana na maambukizi ya VVU.
Onyo: Baadhi ya magonjwa haya yanaweza kuwa ya hatari na yanatakiwa
yachunguzwe na kutibiwa katika Kituo cha Afya, hasa kama mapendekezo yetu hayaleti
ahueni haraka.
Maumivu ya tumbo.
Sababu zinazoweza kuwa zimesababisha zimeelezewa hapa chini kama vile gastritis
au maambukizi ya minyoo, malaria au homa ya matumbo (angalia kuharisha).
Sababu zingine ni kutoyeyushwa kwa chakula tumboni, matatizo ya utumbo,
maumivu wakati wa hedhi, shida za viungo vya uzazi na appendicitis.
Tibu minyoo. Kama maumivu yakiendelea na sababu haijulikani, jaribu yafuatayo:
Zingerber officinale (tangawizi): Saga kiganja kimoja cha tangawizi kwa dakika 10
katika lita moja ya maji. Kunywa katika siku moja.
Psidium guajava (mpera): Kama maumivu ya tumbo yalifuatiwa na kuharisha,
chemsha kiganja kimoja cha majani katika lita moja ya maji kwa dakika 20. Chuja na
unywe katika siku moja
Aloe vera (shubiri): Kila siku asubuhi kula nyama laini ya shubiri pamoja na maji
kidogo na asali.
Anaemia - Upungufu wa damu.
Upungufu wa damu hutokea wakati kuna chembe kidogo sana nyekundu za damu, au
chembe hizo hazina haemoglobin ya kutosha. Inaweza kusababishwa na kutopata
lishe bora, na madawa, na chemical (kama madawa ya kulevya) ambazo
zinasababisha chembe nyekundu kufa, au inaweza kuwa imesababishwa na safura.
Upungufu wa damu unaweza kusababisha uchovu, kupoteza hamu ya chakula, ngozi
kuwa nyeupe na hata kuwa na hamu ya kula majivu au udongo mfinyanzi, ambayo
ndiyo njia ya mwili kujaribu kupata madini – chumvi zaidi.
Kula vyakula vyenye wingi wa chuma. Hivi ni pamoja na nyama (hasa ini) na
samaki, mboga za majani yenye kijani sana (kama moringa, mchicha, majani ya viazi
Ukimwi na Madawa ya Asili 24
vitamu), maharage. Kula mboga na matunda ambazo zina vitamini C kunasaidia
mwili kufyonza chuma. Kupikia katika vyungu vya chuma kunasaidia (epuka vyungu
vya aluminium kama inawezeana). Kama hakuna njia nyingine ya kupata madini ya
chuma, chomeka misumari safi ya chuma katika tunda la limau, na kunywa maji yake
baada ya siku kadhaa.
Wakati huo huo, mtibu mgonjwa kwa tiba ya minyoo kama ilivyoelezwa hapa chini.
PUMU (Asthma)
Pumu husababisha upumuaji kuwa mgumu sana, kwa sababu mirija midogo midogo
ya hewa katika mapafu inazibwa na makohozi. Mara nyingi kuna sauti kama filimbi
wakati mgonjwa anapumua. Mara nyingine hali inakuwa mbaya zaidi usiku. Mara
kwa mara pumu inarithiwa, inaweza kuwa reaction kwa kitu kilicholiwa au
kilchovutwa katika pumzi, na inaweza kuchochewa na mafua ya kawaida.
Lazima wakati wote pumu ishughulikiwe kikamilifu, kwa sababu wakati wowote
inaweza kuwa mbaya zaidi.
1. Mziwaziwa (Euphorbia hirta) (numba ANM-001)
a) Vuta kama sigara majani makavu yaliyosokotwa kama sigara, au
b) weka kichwa chako juu ya kiganja kimoja cha majani haya usiku au
c) chemsha gramu 15-30 (kiganja kimoja) za majani mabichi yaliyooshwa (au
yaliyokaushwa kama itahitajika) katika kikombe kimoja cha maji (ml 500) kwa
dakika 10. Iache itulie kwa dakika 15, kisha chuja, kunywa kwa
sehemusehemu katika siku moja. Rudia tiba hiyo kwa siku 8 mfululizo.
2. Mkaratusi (Eucalyputus globulus): Twanga kiganja kimoja cha majani mabichi
au yaliyokaushwa kisha yaweke katika ml 250 za maji yanayochemka. Vuta kwa
dakika 15 wakati bado yanaendelea kutoa mvuke wa moto, wakati kichwa na
sufuria vikiwa vimefunikwa kwa taulo (ANM – 002)
3. Papai (Carica papaya): Vuta moshi wa majani machanga mabichi yaliyokaushwa
katika kiko au yakiwa yamekunjwa kwenye karatasi kama sigara, au choma
majani hayo pembeni mwa kitanda, au katika chumba ulichokaa, na uvute moshi
wake. (ANM-003).
4. Sigara ya pumu yenye nguvu; kwa kutumia mranaa (Datura stramonium)
Sigara zenye nguvu kwa ajili ya pumu hutengenezwa kama ifuatavyo:
Majani makavu ya Datura stramonium 150mg
Majani makavu ya Eucalyptus globulus 150mg
Majani makavu ya Carica papaya 700 mg.
Yafanye kuwa sigara kwa kutumia karatasi, au yavute katika kiko. (ANM-004).
Harufu mbaya mdomoni
Safisha meno kwa kufuata kanuni, tumia kitawi cha mwarobaini au mkaratusi, au dawa
ya kusafisha meno uliyojitengenezea (angalia NM I). Kama tatizo likiendelea, tatizo
linatoka tumboni. Kwa tatizo hili tumia mkaa kidogo wa dawa. (ANM – 011)
Madonda ya kitandani
Kwa kuzuia na kutibu tumia dawa ya mafuta ya vitunguu maji (angalia NM II) (ANM –
015).
Ukimwi na Madawa ya Asili 25
Tumaini kwa wakati ujao!
Mama kutoka nchi ya Kongo
anamwonesha mtoto wake papai
ambalo lina uwezo wa kutibu
magonjwa mbalimbali.
Magonjwa ya njia ya hewa, kikohozi na mafua.
1. Vitunguu saumu (Allium sativum) (ANM – 021).
Matibabu yote ya vitunguu saumu yanaweza kuambatana na kunywa juisi ya
malimau mawili katika maji. Limau
huongeza vitamini, na husaidia mwili
kutumia vitunguu saumu.
a) Kula vitunguu saumu vibichi –
kikonyo kimoja kutwa mara tatu. Kwa
tatizo kubwa zaidi ongeza kiwango hiki
mara mbili hadi mara tatu.
b) Asali ya vitunguu saumu: Jaza chupa/
glasi kwa vikonyo vya vitunguu saumu
vilivyomenywa na kukatwa katwa
vipande vidogo vidogo. Taratibu
mwaga asali ndani yake ili ijaze nafasi
zote kati ya vitunguu saumu
zilizokatwa katwa. Weka chupa/ glasi
hiyo kwenye sehemu yenye joto kiasi
cha nyuzi 20° C. Katika majuma
mawili hadi manne asali itanyonya
majimaji ya vitunguu saumu na
vitakuwa laini na nyeusi nyeusi.
Usiichuje. Itumie katika miezi 3.
Kunywa kijiko cha chai kila baada ya
masaa kadhaa.
c) Mchanganyiko wa sukari na
vitunguu saumu: Tiba hiyo ni nzuri
kwa kikohozi. Saga vitunguu saumu
kiasi cha kijiko kimoja cha chai.
Changanya na kiasi kilekile cha sukari au asali. Tumia siku hiyohiyo. Tumia
kijiko kimoja cha chai kila baada ya masaa kadhaa.
2. Vitunguu maji (Allium cepa); (ANM – 022).
Ni kama vitunguu saumu lakini si vikali.
a) Mchanganyiko wa kitunguu maji na sukari: Katakata kitunguu maji
kibichi na nyunyizia sukari ya hudhurungi (brown sugar) juu yake, funika
kwa sahani na ukandamize kwa kitu kizito juu yake. Baada ya saa chache
hutoa maji maji mengi ya hudhurungi ambayo ni matamu na hutibu kikohozi
kwa umri wowote.
b) Kinywaji cha kitunguu maji: Changanya ½ kikombe cha kitunguu
kilichokatwa katwa na ½ kikombe cha maji, koroga, kunywa mchanganyiko
huo kwa sehemusehemu ndani ya siku moja.
3. Artemisia (Artemisia annua): (ANM – 023)
a) Chai ya artemisia. Kunywa kikombe cha chai ya artemisia kutwa mara tatu
iliyotengenezwa kwa kumwaga vikombe vitatu vya maji yanayotokota
Ukimwi na Madawa ya Asili 26
kwenye kijiko kimoja cha chai cha majani makavu ya artemisia (au mara tano
zaidi kama majani ni mabichi).
b) Kuvuta mvuke
c) Weka kijiko kizima cha majani makavu au kiganja kimoja cha majani mabichi
ndani ya maji ya moto na uvute mvuke wake.
4. Mwembe (Mangifera indica): Chukua gramu 30 (kiganja kimoja) cha majani
machanga mabichi ya kijani na uyachemshe katika lita moja ya maji kwa dakika
10. Chuja na unywe kwa sehemu sehemu katika siku moja. Usiitumie kwa
mfululizo kwa zaidi ya siku 8. (ANM – 024)
5. Mkaratusi (Eucalyptus globulus): (Siyo kwa watoto walio chini ya mwaka 1)
a) Chai ya mkaratusi: Twanga kiganja kimoja cha majani makavu au mabichi
na uyachemshe katika lita moja ya maji kwa dakika 5. Chuja na unywe kwa
sehemu sehemu katika siku moja. (ANM-025 a).
b) Mafuta ya mkaratusi: Taratibu chemsha kiganja kimoja kikavu na
kilichosagwa cha majani ya mkaratusi katika nusu kikombe cha mafuta ya
kula kwa saa moja katika fukizo – maji. Sugua kifua kwa mchanganyiko huu
mara mbili kwa siku. Usitumie kwa watoto waliochini ya mwaka 1. (ANM-
025 b)
c) Dawa ya kikohozi ya mkaratusi (Syrup): Mwaga lita moja ya maji
yanayochemka kwenye gram 65 za majani makavu, funika na weka kwenye
sehemu yenye joto kiasi kwa masaa 6. Chuja. Ongeza gramu 180 za sukari
katika kila ml 100 za chai hii, chemsha kwa muda mfupi kisha chuja. Watoto
wenye miaka 7 watumie kijiko kimoja cha chai mara tatu kwa siku, na walio
chini ya umri huo watumie kidogo zaidi kufuatana na uzito wao. Walio na
umri mkubwa zaidi pamoja na watu wazima watumie chai ya mkaratusi
kuliko hii dawa yenye sukari (syrup). (ANM-025 c)
d) Matone ya kikohozi ya mkaratusi:
Mwaga mchanganyiko wa 700 ml za kileo (chenye kileo 95% yenye ubora wa
kunywewa) na ml 300 za maji yaliyochemshwa na kuchujwa, kwenye gramu
100 ya majani makavu ya mkaratusi. Baada ya juma moja, yakamue na
kuondoa majani. Watu wazima watumie matone 30 ya hii dawa ya maji,
kutwa mara tatu (ANM-025 d).
e) Dawa ya kikohozi ya mkaratusi iliyo na kileo: Chanyanga gramu 250 za
majani makavu yaliyotwangwa ya mkaratusi katika lita tano za divai ya asali
na ukoroge vyema. Weka sehemu yenye joto kiasi, ikiwa imefunikwa lakini
bila kukoroga, kwa siku tano. Chuja na tunza katika chupa za lita moja moja
zisizoruhusu hewa kuingia. Baada ya kufungwa tunza katika sehemu isiyo na
unyevu wala mwanga. Kipimo: Watu wazima: kijiko kimoja cha chai, kutwa
mara tatu; watoto (mwaka mmoja na zaidi): matone 20-40, kutwa mara tatu
(ANM – 025 e).
f) Kuvuta mvuke wa mkaratusi: Twanga kiganjwa kimoja cha majani mabichi
au makavu, kisha chemsha katika ml 250 za maji. Vuta kwa dakika 15 wakati
bado inaendelea kutoa mvuke, kichwa chako kikiwa kimeinamishwa ndani ya
chombo hicho na vyote vikiwa vimefunikwa taulo. (ANM – 025 f)
Ukimwi na Madawa ya Asili 27
6. Limau (Citrus limon): (ANM-026)
a) Chai ya majani ya mlimau: Chemsha viganja 2 vya majani machanga
(makavu au mabichi) katika lita moja ya maji. Chuja na unywe kwa sehemu –
sehemu ndani ya siku moja. (ANM-026 a)
b) Chai ya ganda la limau: Katakata vipande vidogo vidogo vya maganda ya
limau. Changanya kiganja kimoja na lita 1 ya maji yanayochemka. Acha
kwenye sehemu yenye joto kiasi kwa dakika 15, kisha chuja. Watu wazima:
Kunywa kiasi hiki katika siku moja. Watoto: wanywe kiasi kidogo zaidi
kufuatana na uzito wao. Kumbuka limau hizi zisiwe zimepuliziwa madawa
ya kuua wadudu. (ANM-026 b)
7. Tangawizi (Zingiber officinale) (ANM – 027 )
a) Dawa ya tangawizi (Tincture): Chukua tangawizi iliyokatwa katwa na
changanya na kileo cha kutosha chenye 80% ya kileo, chenye ubora wa
kunywewa, kitakachofanya ujazo wa ml 100. Iache kwa juma moja, kisha
kamua. Kunywa matone 10-20 ya dawa hii mara 3-4 kila siku. (ANM – 027a)
b) Chai ya tangawizi: Tengeneza dawa ya kuchemsha ya mizizi ya tangawizi
mibichi au mikavu, na uchanganye na kijiko kimoja cha chai cha asali (ANM
– 027 b)
8. Embe mafuta (Persea americana): Tengeneza dawa ya kuchemsha kutokana na
majani machanga (kiganja kimoja katika lita moja ya maji) na uinywe kidogo
kidogo ndani ya siku moja (ANM-028)
9. Chungwa (Citrus sinensis): Chemsha kiganja kimoja cha majani katika lita 1 ya
maji kwa dakika 2; na unywe yote ndani ya siku moja. (ANM-029)
10. Michaichai (Cymbopogon citratus): Chemsha kiganja kimoja cha majani katika
maji kidogo na uvute mvuke wake. (ANM-030)
11. Chumvi ya mezani: Yeyusha vijiko viwili vya chai vya chumvi katika lita 1 ya
maji. Ipulizie kuelekea puani mwako na uvute hewa kwa nguvu. (ANM – 031)
“Miguu inayowaka moto”
Wagonjwa wengi wa UKIMWI hulalamika juu ya hali ya miguu kuchemka. Fuata
mapendekezo yetu kwa matibabu ya “matatizo ya ngozi”
Saratani
Angalia Kaposi´s Sarcoma (Saratani ya ngozi).
Candida ya mdomoni (Mtando mweupe mdomoni)
Ni maambukizi ya mba (fungus) yanayosababishwa na yeast candida albicans. Mba
ya aina hii inapatikana katika midomo ya watu wengi. Kwa kuwa mara kwa mara
husababisha uvimbe (inflammation) wakati kinga ya mwili ikipungua, basi ugonjwa
huu wa mdomoni hujitokeza kwa wagonjwa wenye tatizo la kinga ya mwili (mfano:
Ukimwi).
Candida inaweza kusababsiha uvimbe (inflammation) pia vijidudu ambavyo kwa
kawaida vinaishi juu ya ngozi vikikosekanawa. Hii inaweza kutokea kama mgonjwa
ametumia dawa ya antibiotic kwa muda mrefu.
Maambukizi hudhihirishwa na vidonda vidogo vidogo vyenye rangi ya maziwa au
mabaka mekundu. Dalili nyingine ni kupoteza hamu ya kula (inayosababishwa na
Ukimwi na Madawa ya Asili 28
maumivu ya mdomoni), ulimi kuwa mweupe, vidonda mdomoni na mara nyingine
kuvimba tezi. Matibabu yafuatayo husafisha mdomo na kusaidia madonda kupona.
Nyingine huchochea utoaji wa mate, ambao husaidia kufanya mdomo ukae na
unyevu.
1. Chai ya majani la mwembe (angalia juu) (ANM-040)
2. Nyonya nyanya iliyoiva sana, au kipande cha nanasi iliyoiva - mara mbili kwa
siku (ANM-041)
3. Nyonya tini pori mara mbili kwa siku (ANM-042)
4. Nyonya limau, au likamulie katika maji na chumvi (ANM-043)
5. Chai ya mchaichai (angalia huko juu) (ANM-044)
6. Kitunguu saumu na asali – tumia kijiko kimoja cha chai kila baada ya masaa
kadhaa (ANM-045)
7. Tafuna majani mabichi ya Artemisia annua masaa katikati ya milo. Watoto
wanaweza kupendelea mchanganyiko wa kijiko cha chai cha asali na kijiko cha
chai cha majani makavu yaliyosagwa ya artemisia – (ANM-046)
8. Sukutua kooni kwa chumvi na maji.( ANM-047)
9. Safisha mdomo kwa kikombe chenye maji yaliyochanganywa na kijiko kimoja
cha chai cha bicarbonate of soda. (ANM – 048)
Kama kula ni tatizo, epuka matunda jamii ya machungwa na malimau kwa muda,
kwa sababu yanasababisha maumivu. Kula chakula mara kinapopoa na ule vyakula
laini kama vile uji na viazi vilivyopondwa pondwa.
Maambukizi makali ya Candica, mfano maambukizi yanayosababsiha chakula
kutokupita kwenye mfereji wa chakula: Madaktari katika hospitali moja ya watoto
ya Afrika ya kusini, wametengeneza namna ifuatayo, ambayo imefanya kazi hata
ambapo tiba za kisasa zimeshindwa:
Menya vikonyo vya vitunguu saumu, twanga gramu 50 na uchanganye na ml 100 za
maji baridi (salama na safi). Tikisa kwa nguvu sana. (Kama kinapatikana weka
mchanganyiko huu kwenye kikorogeo cha umeme). Chuja, chukua maji na uyatunze
katika sehemu ya baridi sana uwezavyo. Kipimo: mtoto mwenye umri wa mwaka
mmoja: kunywa ml 1 kila baada ya saa 4; mtu mzima: kunywa ml 5 kila baada ya saa
4. Kama itafaa changanya na ml 50 za maji ya machungwa. (ANM-049)
Candida ukeni (maambukizi ya mba ukeni)
Dalili za maambukizi hayo ni mwasho mkali, na midomo ya uke inakuwa mikundu
sana na inauma. Inaweza kuleta maumivu wakati wa kukojoa. Osha au pulizia eneo
hilo kwa maji ya vinegar (changanya vijiko 6 vya chai vya vinegar (siki) katika lita 1
ya maji yaliyochemshwa na kupoa). Kama hakuna vinegar karibu tumia maji ya
limau yaliyochanganywa na maji. Kwa matibabu ya ndani, kunywa chai ya mchaichai
au chai ya majani ya mwembe, na utumie kitunguu saumu katika chakula chako kila
siku. Kwa nje tumia moja ya haya yafuatayo:
a) Mchanganyiko wa vitunguu saumu vilivyopondwa pondwa na mafuta, katika
uwiano wa 1:1 (ANM – 060)
b) Mchanganyiko wa vitunguu saumu viliyopondwa na Yoghurt katika uwiano wa
1:10 (ANM –061)
Ukimwi na Madawa ya Asili 29
c) Ointment ya Artemisia au mafuta ya Artemisia (ANM – 062)
Cytomegalovirus
Ni virusi viletavyo ugonjwa wa ngozi wa malengelenge ambao mara nyingi huathiri
wagonjwa wa UKIMWI. Kwa matibabu, angalia maambukizi ya ngozi na jamii ya
mkanda wa jeshi.
Kuharisha
Kuharisha kunaweza kusababishwa na maambukizi ya Ukimwi yenyewe, ukosefu wa
lishe bora, maambukizi ya amiba, malaria, salmonella, homa ya matumbo,
kipindupindu n.k. Angalia NM II kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kutibu uharishaji wa
aina mbalimbali. Tayarisha maji-chumvi (ORS) kwa kuweka vijiko viwili vya chai
vilivyojaa vya sukari na nusu kijiko cha chai cha chumvi kwenye maji
yaliyochemshwa. Wakati wote tumia hii (ORS) ukiambatanisha na matibabu
yafuatayo:
1. Chai ya mziwaziwa (Euphorbia hirta): Chemsha kiganja kimoja cha majani
mabichi yaliyooshwa katika lita moja ya maji kwa dakika 5. Chuja na unywe
kidogo kidogo ndani ya siku moja. Endelea na matibabu haya kwa siku 8
mfululizo. (ANM-070)
2. Chai ya majani ya mwembe (angalia sura 6) (ANM-071)
3. Kikombe kimoja cha chai ya mchaichai na kikombe kimoja cha maziwa (angalia
sura 6) (ANM-072)
4. Karoti: Osha karoti kubwa mbili, zikatwe vipande vidogo vidogo, vichemshe
kwa taratibu kwa dakika 5 katika lita moja ya maji na ule kila kitu. Au ule karoti
bichi mbili. (ANM-073)
5. Chai ya Artemisia: Inaamanika kwamba chai hii huondoa maambukizi ya
magonjwa kwenye matumbo na huimarisha mfumo wa kinga mwilini (ANM-
074)
6. Mchele (Oryza sativa): Kunywa maji ya mchele (maji ambamo mchele ulikuwa
umepikwa), au tengeneza mkaa wa dawa kutokana na mchele au maganda ya
karanga kwa kutumia njia iliyoelezwa katika NM I (ANM – 075)
7. Mwarobaini (Azadirachta indica): Chemsha majani 40 ya mwarobaini (yaliyo
moja moja) katika kikombe kikubwa cha maji kwa dakika 5. Chuja, poza na
unywe katika siku moja (ANM-076)
8. Kula kiasi kidogo cha chakula kwa wakati mmoja. Ndizi zilizopondwa pondwa
ni nzuri. Epuka vyakula vya mafuta. (ANM-077)
Maumivu ya sikio – maambukizi ya sikio
a) Kitunguu maji (Allium cepa): Kata kata kiganja kimoja cha vitunguu maji
vipande vidogo vidogo sana. Viweke kwenye kipande cha nguo nyepesi. Tumia
hivyo kama kikandamizo kwenye na nyuma ya sikio. Vifungie kwenye kichwa
kwa kutumia kitambaa. Badilisha vitunguu asubuhi na jioni. Hata usiku mzima
sikio lililoathirika likiwa kwenye kifuko kilichojazwa vitunguu vilivyokatwa
katwa vipande vidogo vidogo. (ANM-090)
b) Mwarobaini (Azardirachta indica): Weka matone machache ya mafuta ya
mwarobaini ndani ya sikio (ANM-091)
Ukimwi na Madawa ya Asili 30
Uchovu/ ulegevu
1. Chai ya mimea ya dawa – hasa michaichai, majani ya mwembe au chai za
artemisia (ANM-100)
2. Hewa nzuri na mazoezi (ANM-101)
3. Kula vyakula vyenye wingi wa madini ya chuma (mfano moringa) na vitamini
(hasa matunda) (ANM – 102)
Homa
Maambukizi ya UKIMWI pekee yanaweza kusababisha homa, kama uwezavyo
mlolongo wa maambukizi yanayofuatana na UKIMWI, mfano: malaria, kichomi cha
mapafu, homa ya matumbo, uti wa mgongo, surua.
1. Cymbopogon citratus (mchaichai): Kunywa lita tatu za chai ya mchaichai kila
siku. (ANM – 110)
2. Mangifera indica (mwembe) au Tamarindus indica (ukwaju): Chemsha viganja 3
vya majani katika lita 2 za maji kwa dakika 5, acha ipoe na tumia maji haya
kumwosha mgonjwa. Au ongeza maji baridi zaidi, loweka taulo ndani yake na
uweke kwenye kichwa, kifua au miguu ya mgonjwa.
Maumivu wa tumbo/ vidonda vya tumbo (Gastritis)
Ugonjwa wa tumbo unaosemwa hapo ni mwako wa tabaka la ndani la tumbo.
Inaweza kusababishwa na athari za matumizi ya asprini, au kwa hasira inayojirudia.
Vidonda vya tumbo ni madonda katika tumbo au utumbo mdogo yanayosababishwa
na tindikali. Dalili za vidonda ni tumbo kuuma sana, kuwaka kama moto na njaa.
Maumivu huonekana kutokea wakati tumbo likiwa tupu. Mara nyingi maumivu
yanaondolewa na kunywa maziwa, kula au kwa kunywa maji mengi, lakini yanaweza
kuongezeka saa moja baadaye. Ni bora kula kidogo kidogo mara kwa mara kuliko
kula kiasi kikubwa mara moja tu. Vidonda vya tumbo huonekana kupona, na
baadaye vinaanza tena.
1. Mlongelonge (Moringa oleifera) na kabeji (Brassica oleracea). Ongeza unga wa
moringa na/au kabeji mbichi katika chakula cha kila siku (ANM-120)
2. Mpera (Psidium guajava)
a) Kula matunda mabichi ya mpera (ANM-121 a)au
b) tengeneza chai ya majani ya mpera: Chemsha kiganja kimoja cha majani ya
mpera katika lita moja ya maji kwa dakika 20. Chuja. Kunywa kidogo
kidogo katika siku moja (ANM-121b)
3. Shubiri (Aloe vera (syn. Aloe barbadensis), Aloe ferox na Aloe arborescens).
Kata na uoshe vizuri jani la mmea. Osha kisu kikali kwa kukiweka ndani ya maji
yanayochemka. Kata miisho na pande za jani na uzitupe, kisha kata kupitia
katikati ili kupata eneo kubwa la ndani ya jani. Chukua nyama hizi za ndani
zisizo na rangi kwa kutumia kijiko cha chai.
Tumia kijiko kimoja cha chai cha nyama hizi mara tatu kwa siku (ANM-122).
4. Mranaa (Datura stramonium). Tumia matone 5 hadi 10 ya dawa ya maji ya
mranaa, kutwa mara 3. (Hii lazima itayarishwe na mfamasia mzoefu pekee kwa
sababu ya sumu iliyomo) (ANM-123)
5. Viazi vitamu (Ipomoea batatas). Pika viazi vitamu, vikate vipande vidogo
Ukimwi na Madawa ya Asili 31
vidogo, vikaushe na uviponde hadi kuwa unga. Kunywa kijiko kimoja cha chai
kwa maji kidogo, kutwa mara tatu (ANM-124)
Maumivu ya kichwa.
Maumivu ya kichwa yanaweza kusababishwa na uchovu, mkandamizo wa mawazo
na mahangaiko, mapigo ya moyo kuwa juu (high bloodpressure), uti wa mgongo,
ugonjwa wa macho na ukosefu wa miwani kwa matatizo ya macho, na mafua.
Kunywa lita 3 za maji safi kwa siku. Tibu chanzo cha tatizo kama kinajulikana. Kwa
maumivu makali ya kichwa, jaribu kahawa, au chai iliyotengenezwa kwa majani ya
mti wa mkahawa, au chai ya artemisia, au chai ya majani ya karanga, au majani ya
passionfruit. Kwa mbadala wa kahawa, tafuna ngongolia kama inapatikana. (NM-
130)
Herpes (Vilengelenge vya ngozi)
Herpes Zoster (Jamii za mkanda wa jeshi): Watoto duniani kote kwa kawaida
wanapatwa na maambukizi kama tetekuwanga. Kwa kawaida unatambulika kwa
malengelenge yanayouma sana ambayo yanatokeza upande mmoja wa mwili.
Herpes simplex (cold sores): Vidonda hivi mara nyingi vinapatikana vikizunguka
mdomo. Vidonda katika viungo vya uzazi vinasambazwa kupitia njia ya kujamiiana.
Jamii za mkanda wa jeshi na vidonda visivyouma vyote ni maambukizi ya virusi, na
vinaweza kutibiwa kama ifuatavyo:
1. Allium sativum (vitunguu saumu): Tengeneza mafuta ya vitunguu saumu kwa
kuweka vitunguu vilivyokatwa katwa au vilivyopondwa pondwa kwenye mafuta
mazuri ya mbegu za mimea (siyo pamba) kwa siku kadhaa. Weka mafuta haya
kwenye vidonda mara mbili au tatu kwa siku (ANM-120)
2. Plumeria regio (frangipani; msanapichi). Kamulia utomvu mweupe kutoka
kwenye kitako cha ua kwenye kidonda. Inaua vijidudu na inasababisha ganzi.
(ANM – 142)
3. Azadirachta indica (mwarobaini) (ANM-143)
i. Weka mafuta ya mwarobaini kwenye sehemu iliyoathirika hadi vilengelenge
vitakapokauka. (ANM-143a)
ii. Kunywa dawa ya maji iliyotengenezwa kwa gramu 2.5 za majani makavu
katika lita moja ya maji ya moto. Tumia katika siku moja kwa siku saba.
Tengeneza dawa mpya kila siku. (Dawa hii pia inasaidia kurudisha hamu ya
chakula.) (ANM-143 b)
Mwako wa mapafu, matumbo au macho.
Kunywa chai iliyotengenezwa ama kwa maua ya Matricaria chamomilla
(chamomile) au kwa Artemisia annua. Ili kutibu macho chuja moja ya chai hizi kwa
karatasi na uoshe macho kwa chai iliyopoa, kwa kutumia kitambaa ambacho
kimechemshwa ili kuua vijidudu vyote. (ANM – 150)
Mishtuko ya matumbo.
1. Dawa ya maji ya mranaa inaweza kutengenezwa kama ifuatavyo. Changanya:
- mbegu za mranaa (Datura stramonium) zilizokaushwa na kusagwa gramu 8
- kileo halisi chenye ubora wa kunywewa 95% ml 45
Ukimwi na Madawa ya Asili 32
- maji salama na safi ml 55
badala ya kuchanganya maji na kileo halisi unaweza kutumia kileo chenye 45%
(kati ya 40 na 50%), mfano gin au whisky.
Acha kwa juma moja, kamua na uchuje. Dawa hii ni sawa na dawa ya maji ya
belladona kwa kuzingatia kiwango cha atropine kilichomo.
Matumizi:
Watu wazima: Kiwango cha juu ni matone 30 mara 3 kwa siku.
Watoto: Tone moja kwa kila kilo ya uzito, mara 3 kwa siku. (ANM – 160)
Onyo: Dawa itengenezwe na Mfamasia tu !!
2. Mbegu za mranaa. Kama dawa ya maji ya mranaa haipatikani, ama tumia dawa
inayouzwa katika maduka ya madawa, au tafuna na kumeza kati ya mbegu 10
hadi 15 za Datura stramonium, kiwango cha juu kiwe mara tatu kwa siku hadi
mishtuko itakapokoma. Kwa kuwa mmea huu una atropine, tiba hii ina madhara
ya kukausha kinywa, mapigo ya moyo kuwa juu (high bloodpressure) na matatizo
ya usagaji wa chakula tumboni. Tumia kwa uangalifu – mmea una sumu kali
sana!
Kaposi´s Sarcoma. (Saratani ya ngozi)
Ni namna ya saratani ambayo mara nyingi inatokea kwa wagonjwa wa UKIMWI.
Kwa kawaida mara ya kwanza inatokeza kama baka lenye rangi ya pink, nyekundu,
au zambarau ambalo linaweza kuwa na umbo la duara au la yai. Mabaka haya
yaweza kutokeza sehemu yoyote katika mwili, mara nyingi usoni. Katika kipindi cha
miezi kadhaa yanaweza kutokeza katika sehemu mbalimbali mwilini, ikiwa ni
pamoja na mdomoni, katika viungo vya ndani na kwenye lymphnodes za mwilini
ambapo husababisha damu kuvujia mwilini.
Vitabu vya kisayansi vya siku hizi vinataarifu kuwa Artemisia annua inaweza
kutumika kutibu baadhi ya aina za kansa na hasa kansa ya damu na kansa ya matiti.
Kama hakuna aina nyingine za dawa ya kansa zinazopatikana, jaribu mchanganyiko
ufuatao: Mpe mgonjwa vidonge vyenye madini ya chuma (vya kuongeza damu;
Ferrous) asubuhi, na mchana mpe lita 1 ya chai ya artemisia kwa kutumia gramu 5 za
majani makavu. Endeleza matibabu haya kwa juma moja, na urudie kwa juma moja
kila mwezi. (ANM-170)
Kupoteza uzito wa mwili
Kula aina mbalimbali za vyakula vinavyopatikana katika mazingira yako. Usitumie
sukari, maziwa ya unga au vitu vilivyoingizwa kutoka nchi za nje – vyakula
tunavyozalisha ni vizuri kama siyo bora zaidi ya vile tunavyoagiza. Angalia jedwali
katika sura 1 ya NM I (ANM – 180)
Malaria
Angalia NM II kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kutibu malaria.
Yafuatao ni madawa ya asili unayoweza kutumiwa kwa kutibu malaria, kwa kuanzia
na zile za malaria isiyo kali na kumalizia na zile za malaria kali.
Cymbopogon citratus (mchaichai) (ANM –190)
Allium sativum (vikonyo vya kitunguu saumu) (ANM – 191)
Zingiber officinale (mizizi ya tangawizi) (ANM-192)
Ukimwi na Madawa ya Asili 33
Psidium guajava (chai ya majani ya mpera) (ANM-193)
Carica papaya (chai ya jani la mpapai) (ANM-194)
Cassia occidentalis (sanamaki) (ANM-199)
Azadirachta indica (chai ya mwarobaini) (ANM-195)
Vernonia amygdalina (chai ya majani au mizizi ya majani machungu) (ANM-196)
Cinchona officinalis (chai ya gamba la mwinini) (ANM-197)
Artemisia annua (chai ya majani ya artemisia) (ANM-198)
Maumivu ya misuli
Kama mgonjwa ana maumivu ya misuli, na/au anaonekana kuzidi kukonda, mchue
kila siku. Tengeneza mafuta ya kuchulia kama ifuatavyo:
Kwanza twanga majani, ambayo lazima yawe yamekaushwa vizuri. Tumia moja au
yote kati ya mimea mitatu ifuatavyo: Mkaratusi, mlimau na mchungwa. Kisha chukua
kikombe kidogo (kama ml 100) cha unga wa kila mmea na uchanganye na lita moja
ya mafuta ya kula. Chemsha mchanganyiko huu katika fukizo – maji kwa saa moja.
Chuja huo mchanganyiko, na uache mafuta ya kuchua yapoe bila kuyakoroga. Tunza
hayo mafuta katika chombo kisichopitisha hewa kwenye sehemu yenye giza. (ANM-
200)
Kichefuchefu na kutapika
Angalia pia matibabu kwa magonjwa ya tumbo.
1. Tumia unga wa tangawizi kijiko kimoja cha chai (kisichojaa) kutwa mara tatu.
(ANM-210).
2. Kunywa chai ya tangawizi kabla au wakati wa chakula. Kwa kila kikombe cha
maji chukua vipande 2 vya tangawizi vibichi vilivyooshwa, vichemshe polepole
kwenye maji ya moto kwa dakika 10 (ANM-211).
3. Kula hasa vyakula kama vile wali au mkate, na vyakula vilivyochemshwa kama
viazi, magimbi, uji. Punguza kiwango cha mafuta kinachotumika kwenye upishi,
na ule matunda jamii ya machungwa na limau kwa sababu yanasaidia mwili
kuyeyusha mafuta. (ANM – 212)
4. Kwa utapikaji wa hali ya juu, tumia Cannabis sativum (angalia chini ya
“maumivu’) (ANM-213)
Harufu ya mwili
Hii inaweza kutokea kwa sababu ya vidonda vyenye uchafu na usaha.
Tibu tatizo! Angalia matibabu chini ya vidonda. Inaweza pia kutokea kama matokeo
ya kuharisha na kukojoa kitandani. Uwe makini kwa usafi, osha mwili wakati wote
na kwa makini, fanya chumba kipate hewa vizuri, na ingiza maua yanayonukia vizuri
chumbani.
Maumivu
Kunywa chai iliyotengenezwa kwa kuchemsha majani ya Hibiscus sabdariffa
(rosella). Maua ya Hibiscus yana Vitamin B ambayo inasaidia kwa maumivu ya
mishipa ya fahamu. Inazuia pia kukua kwa bakteria za kifua kikuu. (ANM-220)
Maumivu ya kichwa mara nyingine yanaweza kuondolewa kwa kunywa kahawa.
Kwa maumivu ya matumbo, angalia kwenye vidonda yya tumbo na mishtuko ya
Ukimwi na Madawa ya Asili 34
matumbo.
Kama mgonjwa anakaribia kufa na anasikia maumivu, avute majani machanga
makavu ya Cannabis sativum (mbangi) ili kupunguza maumivu. Kwa mbadala, bangi
inaweza kutumika kama dawa ya maji (kwa kunywa) au kama tincture. Omba ruhusa
kwenye mamlaka inayohusika na madawa – katika nchi nyingi matumizi ya mbangi
hayaruhusiwi kisheria. (ANM-221)
Kichomi cha mapafu (pneumonia)
Haya ni maambukizi makali ya mapafu, na kinaweza kuanza kutokana na magonjwa
yoyote ya njia ya hewa kama vile kikohozi au magonjwa ya mirija ya hewa. Dalili
zake ni pamoja na baridi ya ghafla na kisha homa kali, kupumua kwa juu juu na kwa
haraka haraka, kukohoa, mara nyingine kikiambatana na makohozi na mara nyingi
vidonda (herpes) usoni au kwenye midomo.
Inabidi mgonjwa atafute huduma ya matibabu. Ikikosekana, tiba zilizoorodheshwa
chini ya “magonjwa ya njia ya hewa, kikohozi na mafua” ndizo zifuatwe, hasa uvutaji
wa mvuke wa mkaratusi au artemisia. (ANM-230)
Kutunza ngozi na usafi
Kwa kumwoshea mgonjwa tumia sabuni ya maji uliyojitengenezea. Inatengenezwa
kama ifuatavyo;
Vipimo vinne vya sabuni (ya viwandani au uliyojitengenezea) isiyo na rangi, kipimo
kimoja cha mafuta ya kula na kipimo kimoja cha maji. Pondaponda hiyo sabuni na
uichanganye na hayo maji na mafuta. Chemsha mchanganyiko huo taratibu hadi
sabuni iyeyuke na kuungana na maji na mafuta. Koroga mchanganyiko huo hadi
utakapopoa, na uumwage kwenye vyombo vyenye umbo unalotaka. Acha kwa
majuma mawili kabla ya kutumia. (ANM-240)
Sabuni hii inaweza “kuwekewa dawa” kwa kuiongezea matone kadhaa ya mafuta ya
mwarobaini, au majani makavu ya mwarobaini yaliyotwangwa/sagwa au
mlongelonge kabla ya kumwagwa kwenye vyombo vyenye maumbo.
Saratani ya ngozi.
Panapokuwa hakuna dawa nyingine, tumia mafuta ya mwarobaini au nyama za ndani
za jani la shubiri (Aloe vera) kupaka kwenye eneo lililoathirika mara mbili kwa siku.
Kwa nyongeza kunywa chai ya artemisia, angalia pia Kaposi´s Sarcoma. (ANM-250)
Matatizo ya ngozi.
Wagonjwa wa UKIMWI mara nyingi wanalalamika juu ya “mwako wa miguu” na
matatizo ya ngozi yasiyo na chanzo kinachojulikana, kama vile upele aina ya
“eczema”. Tunapendekeza kwamba uanze kwa kuishughulikia ngozi kwa kutumia
vitu vinavyoipa afya, na kwa makini ukiendelea kwa tiba za kuua vijidudu ambazo
pia zinaongeza ukali wa matibabu kwa jinsi athari zinavyozidi kujitokeza.
Tukianza na ile yenye nguvu za chini, tunapendekeza yafuatayo:
Persea americana (embe mafuta): Changanya nyama za embe mafuta lililoiva na
matone kiasi ya maji ya limau na upake kwenye sehemu iliyoathirika kwa masaa
12 kwa siku - mfano kwa usiku mzima (ANM-264)
Mafuta ya kula, kama vile mafuta ya mawese, mafuta ya alizeti, mafuta ya
karanga: Changanya kijiko kimoja cha chai cha mafuta haya na kimoja cha maji
Ukimwi na Madawa ya Asili 35
Washiriki wakichuana taratibu kwa
mafuta ya yabisi baridi wakati wa
Semina ya anamed huko Koritok,
Uganda.
katika kiganja cha mkono, na usugue kwenye sehemu iliyoathirika. (ANM-265)
Nyama za jani la shubiri (Aloe vera) (ANM-266)
Brassica oleracea (kabeji): Tumia jani kama kifungio (ANM-262)
Mafuta yaliyotengenezwa kutokana na mafuta ya mboga mboga na mimea kama
vile mpera, chamomile na artemisia. Kwa maelezo ya jinsi ya kuchanganya,
angalia mchanganyiko wa mafuta ya bawasiri katika NM-I (ANM-267)
Dawa ya mafuta iliyotengenezwa kutokana na mafuta haya ukiongeza 10% ya nta
ya nyuki (ANM-268)
Mafuta ya mbono (kutokana na
Ricinus communis), ama ikiwa
imetengenezwa kiwandani au kwa
kienyeji kijijini au kwa kufuata
maelezo ya jinsi ya kuchanganya
katika NM I. (ANM-269 a)
Cassia alata: Tengeneza
mchanganyiko (kama uji mzito) kwa
kutumia majani yaliyosagwa na
mafuta. (ANM-263)
Azadirachta indica (mwarobaini):
Osha sehemu iliyoathirika kwa chai
ya mwarobaini, au ifunge kwa
kitambaa ambacho wakati wote
utakilowanisha kwa chai ya
mwarobaini au sehemu iliyoathirika
ikae katika maji vuguvugu ambamo
chai ya mwarobaini imechanganywa.
Matibabu yenye nguvu zaidi ni uji-uji
wa majani yake uliochanganywa na
mafuta au maji au dawa ya mafuta
kutokana na majani, au mafuta ya
mwarobaini (ANM-261)
Allium cepa (kitunguu maji): Kama
mafuta au dawa ya mafuta (ointment).
Angalia NM I (ANM-269 b)
Capsicum frutescens (pilipili): Paka mafuta ya pilipili au dawa ya mafuta ya
pilipili kwenye sehemu iliyoathirika. Pilipili ina dawa ya kuua vijidudu na mara
nyingine huondoa mwasho. Angalia dawa ya mafuta ya yabisi baridi katika NM I
(ANM-269 c).
Allium sativum (vitunguu saumu): Mafuta ya vitunguu saumu yanatengenezwa
kama ifuatavyo: Weka vitunguu saumu vilivyomenywa na kukatwa vipande
vidogo kwenye chombo na ufunike kwa kutumia mafuta ya mzeituni (au mafuta
mazuri ya mbogamboga). Funga chombo hicho na ukiache kwenye sehemu yenye
uvuguvugu wa kama 20°C kwa siku tatu. Itikise mara kadhaa kila siku. Kisha
itunze kwenye sehemu baridi, bila kuichuja. Uitumie ndani ya kipindi cha siku
Ukimwi na Madawa ya Asili 36
tatu. (ANM-260)
Mafuta ya upele: Mchanganyiko ya nusu kwa nusu na mafuta ya taa na ya mafuta
ya kula hautumiki tu kwa kutibu upele, bali pia kwa matatizo mengine, mfano
kuwashwa kunakosababishwa na filaria. (ANM-269 d)
Allium sativum (kitunguu saumu): Menya na ukate vitunguu saumu na uvisugue
kwenye eneo lililoathirika. Kwa ajili ya tiba bora zaidi, funga kipande cha
kitunguuu saumu au vitunguu saumu vilivyopondwa pondwa kwenye sehemu
iliyoathirika wakati wa usiku. (ANM-269 e)
Maelezo zaidi juu ya matatizo ya ngozi yanaweza kupatikana katika NM I na II.
Kama kwa mfano michanganyiko yote hii haifanyi kazi, unaweza kujaribu madawa
yenye gharama zaidi ambayo yana mchanganyiko kwa mfano wa cortisone, iodine au
sulphur. Lakini pamoja na hayo huhitajiki kutumia fedha nyingi. Muulize muuguzi au
mfamasia aliye karibu nawe ili kupata mchanganyiko wa kemikali uliotajwa katika
NM III.
Uchovu
Pata mapumziko ya kutosha, kula matunda mengi, kunywa chai ya mimea ya dawa,
hasa chai ya mchaichai, majani ya mwembe na chai ya artemisia na kula chakula
chenye virutubisho vyote (angalia NM I).
Kifua kikuu (TB)
Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukizwa na unaoweza kuua. Unasababishwa na
bakteria walio katika hewa (Mycobacterium tuberculosis, M. bovis au M. africanum).
Kwa kawaida hawa bakteria wakivutwa katika hewa, kwa haraka mfumo wa kinga
mwilini unawazuia kufanya kazi. Wakati mwingine vidudu hutulia ndani ya mwili
bila kufanya kazi, kisha wakati fulani mfumo wa kinga mwilini ukiwa dhaifu, kwa
mfano kwa sababu ya UKIMWI, hao bakteria wanaanza kazi. Kifua kifuu
kinaenezwa wakati mgonjwa wa kifua kikuu akiwakohoa bakteria, ambao wanaweza
kukaa hai katika hewa kwa masaa kadhaa. Kifua kikuu kwa kawaida huanzia kazi
kwenye mapafu, lakini kinaweza kuathiri sehemu nyingine za mwili.
Dalili za kifua kikuu ni kikohozi kisichopona, hasa baada tu ya kuamka, homa kidogo
wakati wa mchana, kutoka jacho (mara nyingine kwa wingi) wakati wa usiku,
maumivu kifuani, kupungua uzito na kwa watu wenye ngozi nyeusi, ngozi kupauka.
Jinsi ugonjwa unavyoendelea unaweza kusababisha kukohoa damu.
Ugonjwa huu unazuiwa kwa kuimarisha kinga ya mwili katika njia zilizoelezwa hapo
juu. Mgonjwa wa kifua kikuu anahitaji madawa ya antibiotic na misaada mingine ya
kiuguzi. Kwa nyongeza fuata maelekezo yaliyotajwa chini ya magonjwa ya njia ya
hewa hapo juu.
Minyoo
Kuna aina mbalimbali za minyoo na viumbe wengine wadogo wadogo sana.(vimelea)
ambao wanaweza kuishi kwenye matumbo ya watu na kusababisha magonjwa.
Minyoo wakubwa zaidi, kama roundworms, threadworms na tegu inaweza kuonekana
katika haja kubwa. Hookworms (safura) na whipworms ni mara chache zinaweza
kuonekana kwenye haja kubwa, ingawa inaweza kuwa imekwishaingia katika tumbo.
Ukimwi na Madawa ya Asili 37
Kuzuia:
1. Wakati wote tumia vyoo.
2. Wakati wote vaa viatu wakati wa kulima.
3. Kula kipande cha jani la mpapai (Carica papaya) (ukubwa wa 5 x 5cm) kila siku
au baada ya siku kadhaa kula kijiko cha mezani kimoja cha mbegu za mpapai.
Minyoo inaonekana kuchukia ladha hii hata zaidi ya binadamu na itaondoka na
kukuacha. (ANM-270)
Tiba:
1. Papai (Carica papaya)
Matunda mabichi ya mpapai yana kimeng’enyo kiitwacho papaine ambacho
huondoa karibu aina zote za minyoo ya tumbo, hata tegu. Utomvu wake
unavunwa kwa kuchana tunda bichi likiwa bado mtini.
Utomvu unatumiwa mara moja, wakati wa asubuhi wakati tumbo likiwa tupu,
kwa pamoja na maji mengi na dawa ya kusababisha kuharisha. Dawa moja nzuri
ya kusababisha kuharisha ni ringworm bush (Cassia alata): Mwaga kikombe cha
maji ya moto kwenye kijiko kimoja cha chai cha majani makavu au gamba la
mzizi, chuja baada ya dakika kumi na unywe kabla ya kwenda kulala. Pia
kunywa maji mengi.
Kipimo cha utomvu wa papai kutibu minyoo:
Umri (miaka) Idadi ya vijiko vya chai.
miezi 6 - mwaka 1
mwaka 1- miaka 3
Miaka 4 - 6
miaka 7 - 13 miaka
miaka 14 na zaidi
½
1
2
3
4
Haya matibabu ya minyoo yanaweza pia kutolewa kwa mgonjwa ambaye
anaharisha. Papaine inaweza isiondoe minyoo yote kwa mara moja, kwa sababu
hiyo tunapendekeza kurudiwa kwa matibabu baada ya juma moja kama hatua ya
tahadhari. (ANM-271)
Kwa mbadala kula kijiko cha mezani kilichojaa cha mbegu za papai lililoiva kwa
siku tatu, mara tatu kwa siku. Kwa watoto iwe pungufu, kutokana na uzito wa
watoto. Kwa kuondoa minyoo iliyokufa, kunywa maji mengi. (ANM-275)
2. Mziwaziwa (Euphorbia hirta)
Osha na uchanganye:
mziwaziwa (mmea mzima bila mizizi) kiganja kimoja
majani ya mpapai kiganja kimoja
Chemsha kwa dakika 5 katika lita moja ya maji, kisha chuja. Kunywa kwa
taratibu na iishe ndani ya siku moja. Kama mtoto akikataa kunywa chai hii,
itayarishe kwa kutumia kiganja kimoja cha mziwaziwa pekee (ANM-272)
3. Lesena (Leucaena glauca) – kwa ajili ya hookworms (safura) na roundworms
Ukimwi na Madawa ya Asili 38
Kausha mbegu 30 zilizoiva, zisage na unywe unga wake kwa kikombe cha maji
ya kunywa ya moto masaa 2 baada ya kifungua kinywa. Watoto watumie kidogo
kufuatana na umri na uzito wao. Siyo nzuri kwa watoto wenye umri chini ya
miaka 7. Madhara yake: Matatizo ya tumbo, kuharisha. (ANM – 273)
4. Boga (Cucurbita maxima) – kwa tegu.
Changanya gram 100 (au vijiko vya mezani 20) za mbegu mbichi zilizosagwa
pamoja na maji na uvile pamoja na dawa ya kusababisha kuharisha kabla ya kula
chochote (asubuhi). Dawa ya kuharisha ni muhimu sana, kwa sababu minyoo
haiuawi, bali hupooza tu. Kwa dawa ya kuharisha ya asili kula mapapai yaliyoiva
mengi sana au maembe. (ANM-274)
Madonda, majipu, vidonda vyenye maambukizi
Vitibu kama ilivyopendekezwa katika NM II. Vitibu haraka mara tu vinapoonekana,
kwa sababu uponaji huenda polepole sana kwa mwili wenye kinga dhaifu.
Kwanza osha kidonda: Weka kijiko kimoja cha mezani kilichojaa chumvi katika lita
moja ya maji yaliyochemshwa au hata vyema zaidi weka katika chai ya majani ya
mpera. Kwa kuosha kidonda chenye maambukizi weka matone matatu ya utomvu wa
papai lisiloiva katika mchanganyiko huu.
Mimea na vifaa ambavyo mara nyingi vinatumika kutibu vidonda ni:
- Mchanganyiko wa asali na sukari (ANM-280)
- Kwa vidonda vinavyotoa usaha, changanya gramu moja ya sukari na tone moja la
utomvu mweupe wa papai bichi. Jaza na ufunike kidonda kwa mchanganyiko huu.
Funika kwa kitambaa na urudie tendo hilo mara moja kwa siku (ANM-286)
- Kipande cha papai (Carica papaya) kwa kuondoa usaha (ANM-282)
- Vipande vya vitunguu saumu (Allium sativum) kuondoa usaha chini ya ngozi.
Kwa hiyo vitumiwe kwa majibu yasiyo na mdomo. (ANM-283)
- Dawa ya mafuta ya vitunguu maji (Allium cepa) kwa kubandika juu ya vidonda.
(ANM-284)
- Dawa ya mkaa inaweza kuwekwa juu ya kidonda kilicho juu juu kinachotoa
usaha. (ANM-285).
Ukimwi na Madawa ya Asili 39
SURA 8: Mwitikio kutoka kwa wanaotumia
HUYAMU - (Idara ya Afya, AICT, Mara & Ukerewe Dayosisi, Tanzania)
HUYAMU ina vikundi viwili vya Wanaoishi na VVU vinavyojulikana kwa jina la
"Kaza Roho" . Pamoja na kutiana moyo, kutembeleana na kufundishana,
wanatengeneza madawa ya asili.
Madawa mengi ya ANAMED yanaonesha mafanikio ya ajabu - hasa Artemisia,
inayolimwa katika shamba kubwa nje ya Musoma. Artemisia huwa inatumiwa kwa wiki
nne mfululizo ile mara ya kwanza mtu anapokuja kwenye kundi. Baadaye inatumika
mara moja kila mwezi kwa siku 7.
Wagonjwa wengi waliokuja wakiwa wamedhoofika sana au hata wale waliotembelewa
nyumbani kwa kushindwa kutembea, walipata nafuu sana kutokana an Artemisia.
Lakini pia majani ya Mlonge yanaonesha mafanikio makubwa. Wanakikundi wote
wanatumia Mlonge katika milo yao.
Mlonge pia inaonesha mafanikio makubwa kwa watoto wanaoishi na VVU. Kwa watoto
watatu waliokuwa wadhaifu na wenye uzito pungufu, Mlonge ilileta nguvu na
wameongeza uzito sana.
Mafuta ya Artemisia pia inaonesha mafanikio makubwa kwa kila aina ya shida ya ngozi
na wengi walishuhudia msaada mkubwa kwa matatizo ya ngozi kutokana na mafuta ya
Artemisia.
Mwanakikundi mmoja alikuwa na CD4 count ya 28 alipoanza kuja kwenye kikundi.
Kutokana na Artemisia na Mlonge CD4 ilipanda kuwa 207 na pia aliongeza kilo 15 za
uzito na kuwa mwenye Afya njema.
Mifano mingi zaidi zingeweza kutajwa!
Kwa wanaotumia ARVs Artemisia na Moringa zinasaidia sana pia. Wanakikundi
wanasema zinapunguza matatizo yanayoweza kujitokeza kwa upande wa matumizi ya
ARVs lakini pia inasaidia kupata lishe bora hata kama hela hazipo.
The Moretele Sunrise Hospice, Temba, South Afrika
Mpho Sebanyoni – Motlhasedi aliacha kazi yake kama muuguzi Januari 1997 ili
kuanzisha Moretele Sunrise Hospice.
Maono ya Mpho na wasaidizi wake ni kupata jamii inayojali, iliyo na ujuzi wa mambo,
inayoendesheka, na yenye huruma. Mambo yanayoendeshwa na kituo hicho ni pamoja
na:
1. Kuwatembelea wagonjwa wa UKIMWI pamoja na familia zao majumbani mwao.
2. Kutoa elimu kuhusu utunzaji wa wagonjwa majumbani.
3. Mambo ya watoto.
4. Kusaidia vikundi vya watu wa rika mbalimbali.
5. Ushauri: Huu ni pamoja na ushauri kabla ya kupimwa, ushauri baada ya
kupimwa, ushauri wakati wa tatizo kujitokeza, na ushauri wakati wa kufiwa.
6. Kuanzisha na kuendeleza miradi ya uzalishaji.
7. Bustani ya mboga na mimea ya madawa.
8. Mpango wa kuwasaidia wanaowatunza waathirika
Ukimwi na Madawa ya Asili 40
9. Upimaji wa VVU.
10. Kuchua kwa kutumia mafuta yaliyotengenezwa nyumbani kutokana na madawa
ya mimea ya kwenye bustani ya madawa.
Watu wengi hununua mafuta, chai za dawa, na dawa za mafuta ambazo kituo
hutengeneza kutokana na mimea yake, na wengi wanakuja kwa ajili ya mafunzo.
Mpho anasema kwamba, katika kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI
chai ya mchaichai hufanya maajabu – inawapa wagonjwa nguvu na hamu ya
chakula.
chai ya majani ya mwembe ni bora sana kwa matibabu ya magonjwa ya njia ya
hewa, kukohoa, na madonda ya koo.
chai ya chamomile husaidia kutibu maambukizi ya makoo, yaani maambukizi ya
njia ya hewa kama vile ugonjwa wa kuumia kikoromeo (sehemu ya koo inayotoa
sauti) - (laryngitis)
Kibisom Women´s Group Project, Kisiwa cha Rusinga Kenya
Esther Odhiambo ameanzisha na anaendesha mradi mzuri sana unaojitegemea huko
katika kisiwa cha Rusinga. Ni mahali pazuri na pasipo na mawasiliano ambapo watu
wanateseka na umasikini mbaya mno. UKIMWI umeenea. Esther na kikundi chake cha
watu wanaojitolea wanafanya shughuli mbalimbali. Kundi hili la watu wanaojitolea,
linajumuisha vijana wenye uelewa, waliosoma vizuri lakini hawana ajira pamoja na
wajane wengi ambao wanawalea wajukuu zao.
- Wanatoa mwongozo na ushauri katika namna ambayo inaruhusu watu kueleza
hofu zao na matatizo kwa siri.
- Katika makundi wanajadili matatizo ya UKIMWI, na uhusiano wake na tabia ya
ngono, kwa wazi kabisa na bila hofu.
- Wamejenga shule ya watoto, ili kwamba watoto yatima, hata wale wa familia
maskini kabisa, waweze kupata elimu ya msingi.
- Wanatumia madawa ya asili na wanawafundisha wengine. Sabuni
walizojitengenezea zina mafuta ya mwarobaini ambayo yanasaidia kwa matatizo
mengi ya ngozi.
- Wameanzisha miradi ya uzalishaji ambayo hutoa siyo tu kipato bali pia nafasi
kwa watu kujisikia wana umuhimu na kuthaminiwa tena.
Miitikio mingine ya anamed
Sister Beatrix kutoka Afrika ya Kusini anayejishughulisha zaidi na wazee anasema
kwamba chai ya artemisia hurudisha hamu ya kula na anaitumia mara nyingi kwa
magonjwa ya njia ya hewa na kwa kuharisha. Alipewa mbegu za Artemisia annua
mapema 2001 na bado hadi leo anazalisha artemisia!
Kiongozi wa tiba wa Grace Church huko Bukavu, DR Kongo, Patrick Milabyo, aliandika: Mwaka 2003 tulizalisha kilo 17 za dawa ya mafuta ya yabisi baridi, na pia
chai ya artemisia na dawa ya mafuta ya maambukizi ya mba, yote ni kutokana na
mimea. Kwa kila dollar tuliyotumia tulirudisha dollar 3, yaani kiwango cha faida 200%
kwa ajili ya hospitali yetu.
Teresa Alajo wa CHIPS peace-making team ya kaskazini – mashariki ya Uganda
Ukimwi na Madawa ya Asili 41
anaripoti baadhi ya mambo ya kushangaza. Baada ya kuwa amefundishwa katika
semina ya anamed jinsi ya kutengeneza “dawa ya mafuta ya yabisi baridi” kutokana na
pilipili, ameweza kufanikiwa kuitumia kutibu aina mbalimbali za matatizo ya ngozi! Pia
anatumia “mafuta ya upele ya anamed” kwa upele na Carica papaya kwa minyoo.
Kwenye kambi za wakimbizi, mahali ambapo hali ya afya na usafi hayakuwa nzuri,
chai ya Euphorbia hirta (mziwaziwa) ilikuwa ndiyo iliyotumwa na Mungu kwa ajili ya
kuharisha.
anamed AIDS Care, Kinshasa, inayoongozwa na Maledi Ibanda, inaendesha semina
za kuzuia UKIMWI, na tiba yake kwa madawa ya asili, katika majimbo mengi
mbalimbali huko Kongo ya magharibi. Maledi anasema kwamba mama mmoja
mwenye miaka 25 aliyekuwa na UKIMWI alikunywa chai ya artemisia kila siku na
kuongeza unga wa majani ya mlongelonge kwenye chakula chake. Baada ya miezi
mitatu alikuwa ameongeza kg 5 kwenye uzito wake. Kwa sasa anaendesha kikundi cha
kujitegemea kwa wagonjwa wengine.
Innocent Balagizi wa Bukavu, DR Kongo aliwatibu wanakikundi wa kikundi cha
kujitegemea (“kujitegemea kwa mazao ya asili”) – kwa kutumia chai ya artemisia,
shubiri (Aloe vera), asali na vitunguu saumu. Wanane kati yao walionyesha kuongezeka
kwa uzito, ongezeko la idadi ya chembe nyeupe za damu, na kuongezeka kwa kiwango
cha kuganda kwa damu. Uchunguzi huu ulifanyika katika maabara ya hospitali huko
Goma. Tutafurahi kusikia uchunguzi zaidi kama huo kutoka kwa wasomaji wetu.
Innocent pia anasema kwamba chai ya artemisia, chai ya Vernonia amygdalina na
shubiri (aloe)/asali kwa sasa viko katika matumizi ya kawaida kwa wagonjwa wa
UKIMWI huko Kongo ya Mashariki. Mama mmoja ambaye kila siku alikula nyama za
shubiri (aloe), asali na vitunguu saumu, aliongeza uzito wake kutoka kilo 40 hadi 65
katika mwaka mmoja, na sasa ndiye mhamasishaji mkuu wa kikundi cha UKIMWI
Goma.
Ukimwi na Madawa ya Asili 42
SURA 9: Mapendekezo kumi kwa serikali za nchi za kusini
Kutokana na taarifa zote zilizo katika kijitabu hiki, anamed inaamini kwamba, kama
serikali zingechukua hatua zifuatazo, hali yao ya utoaji wa huduma ya afya
ingeboreshwa sana:
1. Zisaidie matumizi ya madawa ya asili, na kwa mahusiano ya karibu ya utendaji kazi
kati ya waganga wa jadi na madaktari. Shirika la Afya Duniani (WHO) tayari
limeendeleza mahusiano hayo tangu Azimio la Alma Ata la 1978, na limeendeleza
“Mkakati wa madawa ya jadi 2002-2005” (Angalia WHO Policy Perspectives on
Medicines, No 2, May 2002, “Traditional Medicine – Growing Needs and Potential”.)
2. Zisaidie vyama vya waganga wa jadi, siyo kutokana na madai yao bali kutokana na
jinsi wanavyofuata “Sheria ya mwongozo kwa waganga wa asili”. (Angalia Hirt and
Lindsey (2002), “Dawa za asili katika nchi za tropiki II: Tiba“, toleo la pili, anamed.
3. Zisaidie hasa zile hospitali zitumiazo malighafi inayopatikana katika mazingira ya
watumiaji, hasa mimea inayotibu. Zizitie moyo hospitali kuanzisha bustani ya
mimea ya madawa.
4. Kwa sababu ya hitaji la muhimu, fungua shule au vyuo vya madawa ya kienyeji ili
kwamba kila muuguzi, daktari na mganga wa jadi aweze kupata ujuzi mkubwa zaidi
wa mimea ya asili. Zitambue na zisaidie vile vituo vinavyojishughulisha na madawa
ya asili ambavyo tayari vipo.
5. Ziliombe Shirika la Afya duniani (WHO) liwasaidie kwa kutoa msaada wa kisayansi
kwa uchunguzi wa mimea ya kienyeji yenye dawa.
6. Zisisitize kwamba misaada ya kiganga kutoka nchi za nje zina nafasi ya kusaidia
njia za namna ya kuzuia magonjwa na uzalishaji wa madawa ya asili kuliko kuagiza
madawa kutoka nchi za nje.
7. Pinga kwa kila namna inayowezekana ule utengenezaji wa haki miliki ya ujuzi wa
jadi wa watu wako, na nchi yako juu ya mmea wowote, maumbile ya wanyama au
watu.
8. Kujiondoa katika uanachama wa World Trade Organisation (WTO) yaani Shirika la
biashara duniani sasa na kwa muda wote Shirika la biashara duniani likiendelea
a) hung’ang’ania maamuzi yake ya kuendeleza kutetea kuongeza muda wa haki
miliki kwa madawa ya viwandani kutoka kwa miaka 5 kuwa 20, ambayo itaanza
tarehe 1 January 2005. Sisitiza juu ya haki ya kupata madawa ya bei rahisi
kabisa ya kuokoa maisha bila kukabiliana na vitisho vya changamoto za kisheria
au vikwazo vya biashara. (The World Trade Organisation´s Trade Related Aspects
of Intellectual Property Rights (TRIPS) imetengeneza utaratibu wa dunia nzima wa
kanuni za kulinda haki miliki. Mfano: Sheria ya ulinzi wa haki miliki kwa miaka 20
wa aina zote za uzalishaji na utengenezaji).
b) huzuia nchi zinazoendelea katika kuendeleza viwanda vyao vya madawa.
Ujerumani ilikuwa na miaka 85 ya kuendeleza viwanda vyake vya madawa bila
sheria zozote za mikataba ya kimataifa.(yaani kutoka 1883 hadi 1968). (1883,
Mkutano wa Paris kwa ajili ya kulinda haki miliki binafsi. Hadi 1968 sheria hii
ilikuwa bado haijatumika kwa madawa huko ujerumani! Kwa hiyo kwa miaka 85
Ujerumani iliweza kuendeleza viwanda vyake vya madawa). Matokeo yake,
ujerumani ndiyo imekuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuuza madawa nchi za
Ukimwi na Madawa ya Asili 43
nje. Kwa hiyo sisitiza katika kupata nafasi kama hiyo ili kuendeleza viwanda
vyenu vya madawa!
c) hukataa kuadhibu nchi na mashirika ambayo katika jina la biashara huria,
hutengeneza au huruhusu utengenezaji wa bidhaa za hatari huko kaskazini
wakati ambapo matumizi yake au mauzo yake yamepigwa marufuku; mfano:
baadhi ya viuatilifu, sabuni ambazo zina zebaki.
9. Fanya kazi kwa ushirikiano na idara za kisayansi na makanisa ili kuunda dawa za
kibaiolojia na kikemia, na kuunda na kuendeleza benki za mbegu za mimea ya
madawa. Kuna ulazima wa kimaadili kwamba taarifa zote zinazopatikana juu ya
uzalishaji wa madawa ni lazima zipatikane kwa faida ya watu maskini kabisa.
10. Uyaunge mkono mashirika yanayozalisha mazao ya afya palepale walipo. Mzalishe
na kuuza mazao yenye ubora wa hali ya juu katika nchi yenu wenyewe, mfano dawa
za asili, sabuni na vipodozi visivyo na madhara, vyakula vilivyozalishwa kiasili bila
vinatilifu, nyama zinazofaa kwa binadamu n.k.
Kataa kuagiza bidhaa zenye thamani ya chini au ubora wa hali ya chini, na hasa
vilivyo na madhara, mfano nyama zenye vichocheo vya kukua, sabuni na vipodozi
vyenye zebaki, viuatilifu na kemikali za kilimo zilizopigwa marufuku huko
kaskazini.
Ni salama kabisa kusalimu wagonwa wa UKIMWI kwa kushikana mikono.
Vilevile, inatoa picha nzuri kwa watu wote na makundi yote kijijini, katika
wilaya, au hata katika nchi, kushikana mikono na kukaa pamoja ili kuongea.
Kwa kujadiliana, uwezekano mpya hutokea ambapo tatizo la UKIMWI linaweza
kushughulikiwa kwa pamoja.
Ukimwi na Madawa ya Asili 44
Kanisa mara nyingi iligombana na
mtazamo wa ki-mila juu ya suala
la ndoa, hasa kwa vile kanisa
lilisisitiza msimamo wa "mme
mmoja, mke mmoja"
Siku hizi, kwa sababu ya Ukimwi,
mila na desturi zingine zinabadilika,
k.mf. ndoa za wake wengi na desturi
ya kutakasa kwa wanawake
waliofiwa.
NYONGEZA 1: Mistari ya Biblia inayosaidia
(Shukrani kwa Mchungaji Sam Mugote, The AIDS Intervention Programme (TAIP), Uganda
kwenye “HIV/AIDS Study Pack for Community Development Workers” Tearfund; 1999).
2 Wakorintho 1:3-4 unatutia moyo
kuwafariji wengine kwa faraja tuliyopata
kutoka kwa Bwana.
Mathayo 22:39 inatoa taarifa ya jibu la
Yesu akituambia kuwapenda jirani
alipoulizwa ni amri ipi iliyokuwa kubwa
kati ya zote.
Mathayo 25:31-46 inaeleza mfano wa
kondoo na mbuzi ambamo hukumu ya
milele imehusishwa na jinsi tulivyo
onyesha imani yetu kwa njia ya matendo
kwa wahitaji.
Marko 1:40-45 inatuonyesha Yesu
anavyomhurumia mwenye ukoma,
ugonjwa ambao wakati wa Agano jipya
uliambatana na fedheha na kutengwa.
Yohana 8:2-11 inamwonyesha Yesu akikataa
kumhukumu mwanamke aliyekamatwa
katika uzinzi na kumruhusu “yeyote asiye
na dhambi” kwenye ule umati kuwa wa
kwanza kumrushia jiwe.
Luka 10:25-37 inatutia moyo kusaidia kwa
vitendo na kwa kujitoa, kupitia habari ya
msamaria mwema, ambaye alimhudumia
mtu fulani pamoja na kuwepo kwa chuki
ya kikabila kati ya wayahudi na
wasamaria. Alitumia chakula (divai) alichokuwa nacho kutibu vidonda - mfano
mzuri wa kutumia chakula kama dawa.
Mithali 3:5-8 inatutia moyo kutofuata njia zetu bali njia za Mungu. Kwa hiyo
tunaweza kujiuliza “Ni ipi njia ya Mungu kuhusiana na mahusiano yetu ya mambo
ya kujamiiana“?
Ukimwi na Madawa ya Asili 45
NYONGEZA 2: Mashirika, matoleo, na web-sites
Kwa kuelewa hali ya dunia na jitihada za kimataifa kupambana UKIMWI.
UNAIDS ni ungano la Programu ya Umoja wa Mataifa juu ya UKIMWI, United Nations Programme
on AIDS, na inaleta pamoja mfumo wa mashirika 8 ya Umoja wa Mataifa, yaani UNICEF, UNDP,
UNFPA, UNDCP, ILO, UNESCO na WHO na World Bank (Benki ya dunia).
Anuani: UNAIDS, 20 avenue Appia, 1211 Geneva 27, Switzerland, e-mail: [email protected]
Internet: www.unaids.org. Taarifa nyingi zinaweza kuchukuliwa kutoka katika web-site yao.
Kwa taarifa kuhusu mambo ya tiba ya VVU/ UKIWMI:
TALC - Teaching AIDS At Low Cost, P.O. Box 49, St. Albans, Herts, AL1 15TX, UK. e-mail:
[email protected]. Web.-site: www.talcuk.org. TALC inatoa vitabu vizuri, seti za slide na CD-ROMS
kuhusu tiba juu ya UKIMWI.
US Department of Health and Human Services. Taarifa juu ya uchunguzi wa kihospitali,
kutibu na kuzuia VVU, na miongozo ya huduma za kiganga kwa watumiaji na watoaji wa huduma ya
afya: www.aidsinfo.nih.gov/guidelines.
The South African National AIDS Treatment Advocacy Project: http:/www.natap.org/
Kwa ajili ya taarifa ya huduma ya madawa ya asili kwa wagonjwa wa UKIMWI: “Home – based care herbal treatment guideline”, National AIDS Control Programme, Ministry of
Health, Lilongwe, Malawi, May 1998.
Kwa taarifa kuhusu mpango wa kueneza dawa za VVU/ UKIMWI kwa gharama nafuu n.k.:
Medecines sans Frontieres: www.accessmed-msf.org/ “Campaign for access to essential
medicines” MSF International Office: Rue de la Tourelle 39, Brussels, Belgium.
Third world network briefing paper, June 2001, “TRIPS, patents and access to medicines: Proposals
for clarification and reform. Frederick M. Abbott, Commission on Intellectual Property Rights, Study Paper 2a, “WTO TRIPS
Agreement and ist implications for Access to Medicines in Developing Countries”.
The Buko Pharma-Kampagne, yenye makao yake Ujerumani, kwa miaka 20 iliyopita imekuwa
ikishughulikia shughuli za masoko ya dawa za viwandani katika nchi zinazoendelea na Ulaya
www.bukopharma.de.
“Stop AIDS Campaign“ (Mpango wa kuzuia UKIMWI) ni mpango ulioanzishwa na UK NGO AIDS Consortium, ukiletwa kwa pamoja baadhi ya vikundi vya maendeleo na VVU/ UKIMWI
www.stopaidscampaign.org.uk.
Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayojishughulisha na VVU/ UKIMWI katika nchi
zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara:
Action Aid inashauri kwamba shughuli ya kupambana na VVU/ UKIMWI lazima pia ishughulike na
umaskini. Wanatoa msaada kwa watu wenye VVU/ UKIMWI na familia zao katika nchi zaidi ya 30
katika Afrika, Asia, Latin America, na Caribbean www.actionaid.org.uk/index.asp?page id = 1195.
Afro AIDS info: Habari za VVU/UKIMWI kwa nchi za kusini mwa Afrika: www.afroaidsinfo.org
Mashirika ya msaada kwa VVU/ UKIMWI
The international AIDS/ HIV Alliance ni shirikisho la msaada, linalotoa msaada wa kiufundi na
kifedha kwa makundi ya watu yanayoshughulika na uzuiaji wa VVU, miradi ya kuwajali wenye
UKIMWI na watoto yatima katika nchi zinazoendelea. Anuani: 2 Pentonville Road, London N1 9HF,
UK. Web: www.aidsalliance.org.
Nchi nyingi zina mashirika yake ya kuratibu UKIMWI. Katika Kenya, kwa mfano, ni Kenya
AIDS NGOs Consortium (KANCO). Na nchi karibu zote zimekuwa na mashirika
mbalimbali ambayo yameanzishwa ili kuhudumia wagonjwa wa UKIMWI. Tafadhali tafuta
mashirika yanayojishughulisha na wagonjwa wa UKIMWI katika wilaya yako, na
uyaelekeze kutumia “madawa ya asili”.
anamed Nyongeza 3.
Form ya kumbukumbu: Dalili, matibabu na maendeleo ya mwenye VVU/ mgonjwa wa UKIMWI
Jina _______________________________ Jina la ukoo ____________________________________ Umri ________
Me/ke anuani ________________________________________Tarehe ya kuanza matibabu: ___________________________
Na Dalili Mwezi tangu kuanzisha matibabu
Mwezi tangu kusimamisha
matibabu
1 2 3 4 5 6 1 2 3
1 Kuharisha (idadi kwa siku)
2 Homa isiyoisha (kiwango cha joto)
3 Uzito (kg)
4 Kikohozi kisichopona (kifua kikuu/ Pneumonia) *
5 Candida alibicans (mtando mweupe mdomoni) *
6 Kansa ya ngozi (Kaposi´s sarcoma) *
7 Mkanda wa jeshi *
8 Matatizo ya ngozi *
* Tafadhali jaza kama ifuatavyo: - hakuna dalili; + tatizo la kawaida; ++ tatizo kubwa kiasi; +++ tatizo kubwa sana.
Maelezo ya matibabu yaliyotolewa
Mwezi 1
Mwezi 2
Mwezi 3
Mwezi 4
Mwezi 5
Mwezi 6
Ukimwi na Madawa ya Asili 47
Nyongeza 4: Fomu ya taarifa – Utoaji wa taarifa kwa anamed.
Tafadhali rudisha (kwa posta pekee) kwa
anamed
Schafweide 77
71364 Winnenden
Germany
Tarehe ______________________
Umegundua mchanganyiko gani wa madawa unaosaidia (tafadhali tuandikie namba
zake).
Ni dawa gani ambayo haikusaidia? (tafadhali tuandikie namba zake)
Mapendekezo mengine yoyote?
Jina _____________________________________
Anuani ________________________________________________________________
______________________________________________________________________
Email/fax _______________________________________
Maswali juu ya UKIMWI au mimea ya madawa (tafadhali andika jina la kisayansi
(scientific name) yapelekwe kwa Dr. Keith Lindsey, email: [email protected]. Tafadhali
usitutumie mimea au madawa. Maombi yoyote ya msaada wa fedha hayatajibiwa kwa
sababu sisi wenyewe hatuna fedha.
Ukimwi na Madawa ya Asili 48
Nyongeza 5: anamed: Matoleo na vifaa (hadi September 2006)
Schwafweide 77,71364 Winnenden, Germany, Tel. +497195910225. Email: [email protected]
Angalia web-site kwa ajili ya matoleo mapya na bei: www.anamed-edition.com
KIINGEREZA:
Namba kwa kuagiza/orodha ya vitu.
105 Hirt/M’Pia, ”Natural Medicine in the Tropics I”,
106 This book together with colour posters (403)
109 Hirt/Lindsey, “Natural Medicine: II Treatments” Seminar handbook
113 “Natural Medicine: III Seminar Leader's Resource Kit”
114 Lindsey, "Making peace: Biblical principles"
115 Natural Medicine IV "AIDS and Natural Medicine"
116 Document: “Four ULOG solar ovens and one drier: Construction plans and uses”
117 Document: “Neem in medicine and agriculture”
403 Colour poster of 60 tropical med. plants (folded or as roll?)
107 Lindsey/Hirt ”Use Water Hyacinth!” (inc. instructions for solar oven constr.)
201 Report ”Mercury Soaps: A Modern Day Scandal”
204 Document ”Malaria: Artemisia annua” with an illustrated cultivation guide
GERMAN
101 Hirt/M’pia ”Natürliche Medizin in den Tropen I”
102 This book together with colour poster (401)
401 Colour Poster, 70x100cm, ”Heilpflanzen in den Tropen" (folded or as roll?)
303 Information re seeds of healing plants: purchase, preservation
202 Document "Malaria: Artemisia annua" with an illustrated cultivation guide
FRENCH
103 Hirt/M’Pia ”La Medecine Naturelle Tropicale I”
104 This book with colour poster (402)
112 “La Medecine Naturelle Tropicale: II Traitements" Seminar handbook, 40pp
118 “La Medecine Naturelle Tropicale: III Guide du Formateur”
122 “La Medecine Naturelle Tropicale: IV Le SIDA et la Médecine Naturelle"
402 Colour poster, 70x100cm, ”Plantes médicinales tropicales"(folded or as roll?)
206 Report ”Mercury Soaps: A Modern Day Scandal” (French)
203 Document ”Malaria: Artemisia annua” with an illustrated cultivation guide
PORTUGUESE (KIRENO)
120 Hirt/M’Pia “Remédios Naturais nos Trópicos I”
111 ”Remédios Naturais nos Trópicos: II Tratamentos” Seminar handbook
205 Information ”Malaria: Artemisia annua” with an illustrated cultivation guide
405 Colour poster of 60 tropical med. plants (folded or as roll?)
SPANISH (KIHISPANIA.)
110 Hirt/M’Pia ”Medicina Natural I” 160pp
121 “Medicina Natural” – Part B includes extracts from NMII, III & IV. 40 pp A4
207 Information: "Malaria: Artemisia annua" with an illustrated cultivation guide
KISWAHILI
123 Hirt/M’Pia, “Madawa za asili: I”
119 Hirt/Lindsey, “Dawa za asili katika nchi za joto: II Uzoefu” Seminar handbook
124 Madawa ya asili katika nchi za Tropiki: IV Ukimwi na Madawa ya Asili
ZANA NYINGINE
400 Karatasi nyeupe, 70 x 100 cm, kwa ajili ya kufundishia/kuandikia kwa kalamu kubwa (Markers)
404 Karatasi kubwa ya rangi ya mimea 60 ya madawa, bila maelezo, kwa kutumia kalamu kubwa (Markers)
419 Mbegu za Moringa oleifera zikiwa na muhtasari wa maelezo kwa kiingereza pamoja na maelezo zaidi
kwa kifaransa.
408 Mbegu za mimea 10 tofauti ya eneo la tropiki (tayari kwa kuota).
409 Vikorokoro vya kuanzia vya mpango wa malaria wa anamed vyenye mbegu 5000.
Vikorokoro hivi vinauzwa kwa ajili ya msaada wa kibinadamu tu. Vinajumuisha mbegu na zana zote na
taarifa zote zinazohitajika kwa ulimaji na matumizi.
412 Mbegu za artemisia, kifurushi cha kujaza tena, kinapatikana kwa watu walionunua 409.
411 Majani ya artemisia makavu kwa matumizi ya kisayansi. gramu 50.
anamed pia inapendekeza matumizi ya
“Where there is no doctor: A Village Health Care Handbook for Africa
na David Werner.
Kinapatikana katika maduka mengi na kutoka TALC, P.O. BOX 49 St Albans,
Herts AL I 4AX, England.
Matoleo mengine ya anamed
“Natural Medicine in the Tropics I: Tropical plants as a source of health care.
Production of Medicine and cosmetics” (englisch second Edition 2001)
By Hans-Martin Hirt and Binanda M´Pia
Kitabu kinapatikana pia kwa kijerumani: “Natürliche Medizin in den Tropen”; kifaransa: “La Medecine
Naturelle Tropicale”, kihispania: “Medicina Natural”, kireno: “Remedios Naturais nos Naturelle
Tropicos” na urainian
Kitabu hiki kinaelezea umuhimu wa kijamii na kiuchumi wa madawa ya kienyeji, mimea 15 kwa
ufafanuzi wa kina, mimea 50 zaidi na mazao yake ya asili na jinsi ya kutengengeza chai zake, mafuta
yake, dawa za mafuta na madawa mengine.
Bango la rangi “Mimea inayotibu katika eneo la tropiki”
Picha za mimea 60 ya madawa, zinapatikana kwa kiingereza, kifaransa, kijerumani au kireno.
“Natural Medicine in the Tropics: II Treatments” Kijitabu cha semina cha anamed. Kinapatikana pia kwa kifaransa, kireno na kiswahili.
“Natural Medicine in the tropics: III Seminar Leader´s Resource Kit”
Vikorokoro kwa viongozi wa semina; mkusanyiko wa zana kwa ajili ya kazi kwa vikundi,
tafakari za biblia, na wingi wa taarifa za mshindo nyuma juu ya mada kadhaa. Pia kwa kifaransa.
Vikorokoro vya kuanzia – Malaria - artemisia. Vikorokoro hivi vinajumuisha mbegu na zana zote zinazohitajika kwa ulimaji na matumizi kwa
miaka kadhaa. Taarifa za kisayansi na maandishi, “mpango wa ulimaji”, fomu za kumbukumbu,
barua za taarifa kwa miaka miwili.
Kila box limetayarishwa na taarifa katika lugha husika.
Malaria: Artemisia annua anamed Ulimaji wa Artemisia annua na matumizi yake katika kutibu Malaria.
Kwa kiingereza, kifaransa, kijerumani, kihispania na kireno.
Mercury Soap: A Modern Day Scandal Taarifa zinaelezea tatizo la kutumia sabuni na vipodozi vyenye zebaki kwa lengo la kung’arisha
ngozi. Inajumuisha mkusanyiko wa habari kutoka kwenye magazeti, majarida ya kisayansi na
taarifa nyingine za muhimu. Anamed inatafuta kuweka sheria ya kutouza mazao hayo ya sumu
duniani.
Kwa kiingereza na kifaransa.
Making Peace: Biblical Principles Chanzo chake ni kundi la CHIPS, ambalo imeanzishwa na wakristo nchini Uganda. Kitabu hiki
kinaeleza jinsi tabibu wa dawa za asili wawezavyo kuchangia katika kutengeneza amani
anamed, Schafweide 77, 71364 Winnenden, Germany Email: [email protected]
Huu mchoro wa zamani sana kutoka Ukraine unaonyesha mtoto wa kiafrika akikimbia
kumwokoa mtoto wa kizungu aliyeanguka katika jamii ya mpungate, akiwa ameshikilia
dawa husika kwa kuua sumu.
Bado ni kweli kwamba hata leo Waafrika wana mengi ya kufundisha juu ya mimea
inayoponya. Pamoja na pigo la UKIMWI, ujuzi mwingi zaidi unazidi kupotea jinsi
wazee wanavyokufa kabla hawajarithisha elimu yao ya jadi kwa kizazi kinachofuata.
Kwa hiyo, kila siku, kazi ya kushirikishana ujuzi kuhusu UKIMWI na madawa ya asili
inaendelea kuhitajika zaidi
anamed aktion natürliche medizin
action nature et medecine
action for natural medicine