mbiu ya afya magazin - sailvega.com projects/pdf/mbiu ya afya magazin.pdf · halo, hapo ni kwa...
TRANSCRIPT
GAZETI HILI LIMETENGENEZWA NA MRADI WA CHANJO WA TAIFA (EPI), WIZARA YA AFYA TANZANIA, AFRICA VISION TRUST NA WASANI WA KINGO
TAHARIRIMwezi uliopita ulikuwa na kazi nyingi! Pamoja na
kampeni ya siku za chanjo kitaifa na maandalizi yakampeni ya surua kwa hakika kulikuwa hakuna hata
dakika ya kufikiri!.Lakini hiki ni kipindi cha mwaka nilichokifurahia.
Nadhani kwa kazi zote hizi utajihisi umepata mafanikiofulani. Hata hivyo hiyo haitufanyi tuweze kupumzikamiezi mingine ya mwaka. Chanjo za kawaida nimuhimu zikiendelea.
Usalama ni jambo muhimu ambalo limekuwa kati-ka mawazo yangu hivi sasa. Katika wiki chache zilizo-pita tumekuwa na matatizo na sterilaiza yetu na imeni-pa hofu sana kama utoaji wa sindano ulikuwa salamana kwa kiasi gani. Kwa bahati nzuri tulikuwa na TSTspots mpya, hivyo tungeweza kuthibitisha kamailikuwa inafanya kazi vizuri. Hakika hatutaki kabisakusababisha hatari kwa watoto!
Lakini hiyo siyo hatari pekee ninayoihofia. Niliwahikujichoma na sindano nilipojaribu kurudishia kifunikochake mara baada ya kuitumia. Mbali ya kuwa na jer-aha baya kuna hatari kubwa ya kuambukizwamagonjwa kama vile ukimwi, hivyo nina himiza asiwe-po mtu yeyote wa kituo cha afya anayerudishia vifu-niko vya sindano. Sasa tuwe tunazitupa moja kwamoja kwenye maboksi ya usalama.
Maboksi ya usalama ni muhimu sana! Kama hatu-na maboksi maalumu ya EPI, tutengeneze yetu. Nirahisi na salama zaidi. Nimewahi kushuhudia baadhiya wafanyakazi wa afya wakiacha sindano zilizotumi-ka zikizagaa nje ya vituo. Fikiria! kama tunaishi jiranina kituo cha afya tunapaswa kuwa wangalifu zaidi kwakuhifadhi vizuri sindano zilizotumika katika maboksi ndani ya kliniki hadi tunapokuwa tayari kuya-choma moto. Watoto wangu wamekuawakubwa na hupenda kuchezea vitu mbalimbali zikiwemo sindano zilizotumika!. Niathari gani itakayowapata? Siku zote kati-ka kazi zetu tujaribu kuboresha usalamakwa watoto wetu na jamii nzima.
yal iyomo
HADITHI ZA
PICHA NA
KATUNI
Usalama Kwanza uk. 2Bastola ya Maji uk. 13Katuni uk. 24
HabariNjemauk. 12
MAKALA naSIMULIZI
Ujue ugonjwa waHepatitis B uk. 10
Tupa Salama uk. 20
VICHEKESHO uk. 9
BBC uk. 22
JISHINDIEREDIO uk. 22-23
Chemcha Bongo uk. 24
JJIISSHHIINNDDIIEE
RREE
DDIIOO
!!!!!!
USALAMA KWANZA2
Mama Tobi, itabidi umrudishe mtotobaada ya wiki nne kwa sindano
nyingine.
Sofia, vipi tena? Ah, nasikia kichefuchefu nakizunguzungu.
Furaha ya wanakijiji wa “MWEMBE TAYARI” ilikamilika mwaka juzi pale Serikali ilipowajengea kituo cha afya na kuon-dokana na adha ya kutembea maili 15 kufuata huduma za afya.Pamoja na kituo hicho bado kuna tahadhari inayopaswa
kuchukuliwa.
USALAMA KWANZA...
USALAMA KWANZA 3
Hebu lete hiyo sindano niiweke kwenyemaji. Vipi unajisikiaje?
Nasikia kizunguzungu na kichefuchefu. Watu ni wengi na sindanozimetuishia. Itabidi tuahirishe kutoa chanjo mpaka kesho.
Inabidi tuanze
kuziandaa
sindano
sasa hivi.
Unaona!, unoaji wa sin-dano unaweza kukus-ababishia maambukizi!
Mtuwie radhi kina mama. Tumeishiwa sindano zilizochemshwa.Tafadhali njooni kesho tutaendelea kutoa chanjo.
Sindano zimeanza
kuwa butu. Ngoja nzi-
noe kidogo.
Sofia ngoja,usi........
Ni rahisi kujikwangua au kujichoma wakati
unaponoa sindano na hivyokuhatarisha afya yako kwa
maambukizi ya maradhi tokakwa mtu aliyedungwa na sin-
dano hiyo.
U S I N O E S I N D A N O ,N I H ATA R I !
AAAAUU UU UU CC HH !!
USALAMA KWANZA4
...na kama ndivyo, basi tutawatu-
mia mara moja.
Zaidi ya mwaka, una uhakika? Ngoja niangalie kwenye lejaya vifaa.
Kituo cha afya cha MWEMBE TAYARI tumeishiwa - hatujaletewa sindano na akiba ya vifaa kwa zaidi ya mwaka sasa.
Halo, hapo ni kwaDCCO?
Ndio, nikusaidie nini?
Pamekuwa na uhaba wa vifaa katika nchi nzima kwa kipindikilichopita. Hata hivyo Serikali imejitahidi sana kumaliza tatizo
hilo. Pamoja na hayo ni jukumu lako kuhakikisha vifaa vyakuchemshia sindano viko kwenye hali nzuri. Endapo kifaa fulani
ni kibovu toa taarifa kwa DMO haraka!
TA H A D H A R I K A B L A YA WA K AT I !
USALAMA KWANZA 5
Halafu hii sindano yako haina kipimo cha dozi inayohitajika.
Sawa, lakini unahakika gani kama
sindano uliyonunua mtaani
ni salama?
Aka babu wee, sindano zenu ni butu. mwezi uliopita mliniumiziamwanangu. Leo nimeleta sindano yangu.
Usiogope tumeletasindano mpya.
Mna bahati, juzi tu tumepokea shehena mpyaya vifaa toka mkoani!, saini hapa!
USALAMA KWANZA6
Kwa hiyo ni rahisi kutoa zaidi au pungufu yakipimo kinachohitajika.
Alaaa kumbe!
Mwingine!
Mara hii umerudi, nilikuambiaumrudishe mtoto baada ya wiki
nne.
Angalieni sehemu mliyomchoma, sindanoilivyovimba na
kubadilika.
Du!, labda kapata ambukizo,tumpeleke kwa mganga.
Sasa naogopa, mara ya pili hii tunaletewa uvimbe wa sin-dano katika mwezi huu, pengine sterilaiza yetu ina kasoro,
ikague.
USALAMA KWANZA
Tubadilishe vyote,gasketi na valvu
mara moja.
Aah, ndio maana, hebu ona mpira wasterilaiza ulivyochakaa.
Umesahau kwenye she-hena ya vifaa vipya kuna
lebo za TST. Funguatubandike moja.
Lebo ya TST?
Weka kidogo, akiba yamafuta
imepungua. Inabidituagize Wilayani
mapema.
Ha ha ha, hata wewe msomaji hujui lebo za TST kama Sofia!TST ni lebo ya doa dogo lenye
rangi ya njano ambayo hubandikwa ndani ya sterilaiza kabla ya uchemshaji wa sindano. Kazi yake ni kuhakik-
isha mzunguko wa mvuke na joto ndani ya sterilaiza. Kama mzun-guko umefanyika sawa sawa katika dakika 20 za uchemshaji wa
sindano, doa hilo hubadilika rangi na kuwa rangi ya zambarau.
RRiiiiiiNNGG!!!!!!BBRRRRRRiiNNGG!!!!!!
7
USALAMA KWANZA8
Naona umevutiwa na habari zausalama wa sterilaiza.
Haa, mwanangu, miezi michache ijayo utakuwa mikononi mwangu. Sote tuhakik-ishe Mariam anavyotupa sindano salama.
Haaa, rangi ya TST-spot imebadilika toka njano hadi zam-
barau!Tena hizi lebo tuwe tunazibandika kwenye hiki kitabu ili kufuatilia utendaji
wa sterilaiza.
Safi, ikiharibika,
isitushitukize.
Vichekesho!! 9
NILIYOYASIKIAYANANITOSHA:
Bibi yetu mzaa Baba,yaani Lusia, amezee-ka sana kiasi kwambaanaanza kuwa kiziwi.
Madaktari walipen-dekeza afanyiwe upasuaji
wa masikio lakini yeyealipinga vikali wazo hilo.“Tangu nizaliwe sasa ninaumri wa miaka 94, halafubado mnataka nini?, kwaumri huu niliyoyasikia
yananitosha”, alijibu Bibi.
KWA JINSI NINAVYOKOHOA:
Siku zote nimekuwa najiuliza ni kwa vipi
Kaka yangu ambaye ni daktari hawashawishi
wagonjwa wake waache kuvuta sigara. Yeye
huvuta pakiti mbili za sigara kwa siku na nil-
iamini ushauri wake hauwezi kuzingatiwa.
“Hawataacha kuvuta kwa sababu ya
kuwashauri”, aliniambia.
“Wataacha kutokana na jinsi ninavyokohoa
wakati nawaambia”.
KIJOGOO:Akiwa kwenye genge la walevi,jamaa mmoja alianza kutamba;“Habari za wanawake wote wa
mtaa huu niulizeni mimi. Mfanoyule Fatuma unene wa bure tu,kiuno chake saizi inchi 23 tu...,
anashindwa hata na ka-Chausiku.Kenyewe bwana kanavaa inchi30!”, walevi wote kwenye baawaligeuka kumsikiliza jamaa.
“Lakini mtaa mzima kwa kiunokikubwa ni Mama Kidawa
anaongoza, halafu kwa maziwamakubwa Mama Cheupe
anashika namba moja; sidiriayake saizi....”. Kufikia hapo
kundi la welevi wenye hasiralikamzunguka na chupa za bia
mikononi.“Kumbe wewe ndiye kijogoo chawake zetu tunapokuwa makazinisio!, sasa tuambie umejuaje?”.
Huku jamaa akinyoosha mikonojuu, akasema;
“Aka mwaya, tusiuane bure,mimi ni fundi cherehani.Nitawashoneaje nguo bila
kuwapima?”.
AMEKWENDA KUUZIMAULE MSHUMAA:
Mke na mume walikuwa na shauku yakupata mtoto, hivyo wakaenda kwa Kasisi
ili wakaombewe.“Nina safari ya kwenda Roma kwa ajili ya
hija, hivyo nikiwa huko nitawawashiamshumaa wa baraka nanyi mtapata watoto
lukuki”, alisema Kasisi. Miaka mitatubaadaye Kasisi aliporudi kutoka Roma
aliwatembelea mke na mume huyo nyum-bani kwao na kumkuta mwanamke akiwa
mjamzito na huku anawahudumiamapacha wake.
“Yuko wapi mumeo, nataka niwapehongera”, alisema Kasisi.
“Ooho!, mmepishana, amekwenda Romakuuzima ule mshumaa uliotuwashia, ali-
jibu mwanamke.
ASINGEKUWA WANGU
NISINGEKUWA
NAMPELEKA
NYUMBANI:
Askari polisi mmoja alis-
hangazwa na kitendo cha
mwanamke mmoja aliyem-
beba mtoto wake aliyekuwa
analia na kupiga makelele.
Akiwa ameingiwa na huru-
ma, yule polisi akamuuliza
huyo mwanamke.
“Mama huyo ni mtoto
wako kweli?”,
“Asingekuwa wangu,
nisingekuwa nampeleka
nyumbani”, alijibu huyo
Mama.
KAZI YA WITO:Kwa kawaida nesi mmoja ait-
waye Salama huwachoma sin-
dano wagonjwa kumi tu kwa siku
na kuondoka kazini akiacha watu
wakilalamika. Lakini juzi aliweza
kuwachoma sindano wagonjwa
arobaini bila kulalamika kuwa
mkono wake unauma.
Dokta John alishangaa sana na
alipomuuliza kwanini anajituma
sana siku hiyo, Salama alimjibu;
“Tangu nianze kazi miaka kumi
iliyopita, leo nimetambua kuwa
uuguzi ni kazi ya wito!”.
VIC
HEKESH
O!!
Hepatitis B10
UGONJWA WA INIWENYE VIRUSI VINAVYOUA
Hepatitis B ni ugonjwa hatari wa ini unaoenezwa na virusi
vijulikanavyo kama Hepatitis B’.Virusi hivi vina nguvu
kubwa ya kushambulia mara 100 zaidi ya virusi vya
ukimwi!. Mtu anapopata uambukizo, virusi huvamia na kuanza
kuathiri chembe chembe hai za ini na
matokeo yake ni dalili kama ugonjwa wa
mafua, kuumwa kichwa, homa, kuhara,
kutapika na ugonjwa wa ngozi. Aidha
macho hubadilika na kuwa ya man-
jano.Hali hii inaweza ikaendelea kwa
muda wa wiki tatu au miezi kadhaa.
Ugonjwa huu wa Hepatitis B mara nyingi
huenezwa kati ya mtu na mtu kwa kugusana
na damu ya mtu aliyeambukizwa. Lakini
virusi hivi hupatikana pia kwenye mate,
shahawa, majimaji yatokayo kwenye sehe-
mu ya siri ya mwanamke, jasho na hata
kwenye machozi. Njia kuu ya uambukizaji
hasa ni damu, shahawa, na majimaji katika
uke.
Maambukizo mengi hutokea kwa watoto
wenye umri chini ya miaka mitano hasa
watoto wanyonyao. Watu wazima hasa wale
ambao wanafanya kazi kwenye mazingira
ya kugusana na damu au maji-maji ya
mwilini ya watu wengine kwenye
shughuli za sherehe kama vile michezo hasa
ile ya kugusanagusana na kushikana,
wanaweza kuambukizwa.
Maambukizo haya hupatikana
tangu utotoni na yanazuilika kwa
chanjo ya mama mjamzito karibu
ya mtoto kuzaliwa. Baadhi ya watu
huwa hawaponi kutokana na
ugonjwa huu na virusi vinaweza
kuendelea na kuathiri ini na hata
kuleta sarakani ya ini na hatimaye
kifo. Maambukizo ya Hepatitis B ni
janga kwa watoto kwa sababu
wazazi wao wengi hufariki na
kuwaacha wakiwa wadogo kiasi
cha kutoweza kujitegemea.
Watu wengi huwa hawana dalili
za ugonjwa huu na hata hawafa-
hamu kwamba wana ugonjwa huo hali ambayo husababisha
kuambukiza wengine wengi bila ya wao kujua.
Dalili za ugonjwa wa Hepatitis B zaweza kujitokeza wakati
wowote kati ya wiki sita na miezi sita tangu mtu apate ambukizo
la virusi, lakini kwa wastani huchukua muda wa miezi mitatu.
Kwa kuwa ugonjwa huu hauna tiba , njia muhimu ya kujikinga
ni kutumia chanjo. Moja ya chanjo dhidi ya ugonjwa huu ni
mchanganyiko wa chanjo ya DPT na chanjo dhidi ya ugonjwa wa
ini (HB). Chanjo hiyo ni DPT-HB.
Njia za kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na kuepuka matu-
mizi ya damu isiyopimwa virusi vya Hepatitis B, kutotumia
mabomba na sindano zisizotakaswa na kuepuka uasherati.
Ugonjwa huu ni hatari sana na umeenea karibu dunia nzima
ingawa idadi kubwa ya wagonjwa wapo katika mabara ya Afrika,
Asia, na Amerika ya kusini. Matarajio ya chanjo ya Hepatitis B
katika Afrika ni makubwa sana. Lakini kukosekana kwa mpango
wa chanjo maeneo mengi, mamilioni ya watoto wanaweza kufa
kutokana na ugonjwa huu ambao hujitokeza kwa kasi ukubwani.
Hepatitis B 11
LISEMWALOLIPO..!J
ohn na Sara ni marafiki wapenzi wa muda mrefu. Siku zote
wamekuwa makini sana katika uhusiano wao. Wamekuwa
wakitumia njia zote muhimu za kujikinga na magonjwa na
hasa ukimwi ambao wamekuwa wakiuchukulia kuwa ndio
ugonjwa ulio hatari zaidi ya magonjwa mengine. Matarajio yao ni
kufunga ndoa wakiwa salama.
Siku moja walihudhuria mazishi ya jirani yao mmoja ait-
waye Rose ambaye ilivumishwa alikufa kwa ukimwi. Rose
alikuwa ameolewa na aliacha mume na watoto wawili. Wakati
wa mazishi, ilitolewa historia fupi ya marehemu kuanzia
kuzaliwa kwake hadi kifo. Kilichowagusa watu wengi ni historia
ya ugonjwa wake. Marehemu Rose alianza kuumwa mafua
kwa mudamrefu na kisha kuharisha. Halafu macho yake
yalibadilika rangi yakawa ya manjano.
Alipopimwa akagundulika kuwa alikuwa
anaumwa ugonjwa wa ini unaojulikana
kwa jina la kitalaamu “hepatitis B”. Kwa
kuwa Rose alikuwa amekonda sana
watu walidhani alikuwa na ukimwi.
Msemaji wa wafiwa aliendelea kusema
kuwa, ugonjwa huo wa ini huambuk-
izwa kwa njia kama zile zile za ukimwi
na kupitia mate, jasho, hata machozi na
hasa kujamiana.
Waliporudi nyumbani,
John na Sara walijawa
na mawazo mengi.
Habari za ugonjwa huo
wa ini (hepatitis B) zili-
wanyima raha kabisa.
Sio tu kwamba
hawakuwahi kupata
chanjo ya ugonjwa huo bali pia hawakuwahi hata kusikia
habari zake kabla. Sasa walimua kwenda hospitali kupimwa ili
wajue mapema kama wanao ugonjwa huo au la. Walifurahi
sana majibu yalipoonyesha kuwa hawakuwa na ugonjwa huo.
John na Sara ni mfano wa wanajamii wote wanaopenda kuishi
maisha ya kujihami ambayo ni bora zaidi hasa kwa magonjwa
yasiyokuwa na tiba kama Hepatitis B.
Habari njema12
HA
BA
RINN
JJEEMM
AA!!!!
!!Habari njema 1● Shukurani kwa msaada maalum kutokaGAVI (Ushirika wa Kimataifa wa Chanjona Kinga ). Tanzania inatarajia kuanzishachanjo dhidi ya ugonjwa wa Hepatitis Bkatika mpango wa utoaji chanjo unaotaraji-wa kufanywa kwa watoto wachanga wotekuanzia mapema mwaka ujao (2001).
Habari njema 2● Wakati chanjo hii mpya itakayokuwaimechanganywa na DPT italeta mabadilikoyenye unafuu kwa wafanyakazi wa afyakina mama na watoto. Chanjo mpyaitakayochanganywa DPT/Hepatitis Bitakuwa inatolewa katika utaratibu ule uleunaotumiwa kwa chanjo ya DPT. Isitoshe,chanjo hii mpya itatoa kinga madhubutizaidi kwa watoto wachanga wote dhidi yavirusi hivi hatari.
Habari njema 3● Pamoja na uanzishwaji wa chanjompya, Tanzania imeamua kufanyamabadiliko kwa kuacha kutumia mabombana sindano za kuchemsha na kuanzakutumia bomba maalum ‘linalojifunga’baada ya kutumika kwa ajili ya chanjo zotezinazotumia sindano. Unaweza ukawaunalifahamu bomba la aina hii lililowahikutumika kwenye kampeni za ugonjwa wa
surua.
Watumishi wengi wa afya tulioongea naowameyapokea mabadiliko haya ya kutu-mia bomba hili la ‘kujifunga’. “Uchemshajiwa sindano ni kazi ndefu na hatuwezikumudu kuwa na vifaa vya kutosha sikuzote. Lakini sindano hizi mpya ni rahisikuzitumia na kisha unaziweka moja kwamoja ndani ya boksi la usalama. Ni rahisina salama zaidi!”, alisema Muuguzi mmojawa MCH kutoka Zanzibar.
Utajulishwa mabadiliko haya na mafunzomaalum yatatolewa karibu na kipindihicho.
BOMBA LENYE MTUTU UNAOJIFUNGA
B omba lenye mtutu unaojifungabaada ya kutumika ni salama. Maratu mtutu unaposukuma dawa
hauwezi kurudishwa nyuma tena. Hiiinafanyaisiwezekane kutumika tena, nahivyo kunakuwa hakuna hatari ya maam-bukizo kutoka kwa mgonjwa mmojakwenda kwa mwingine.
I sitoshe bado kuna hatari ya kujichomana sindano. Unapaswa uzitupe zotekwa usalama! Maboksi maalum ya
usalama yametolewa kwa kusudio hili.Tupa bomba na sindano iliyotumika mojakwa moja ndani ya boksi la usalamamara tu baada ya kuitumia. Weka boksimahali pa usalama ndani ya kliniki hadiutakapokuwa tayari kwa kulichoma moto.
BASTOLA YA MAJI 13
BASTOLA YA MAJI
BASTOLA YA MAJI14
BASTOLA YA MAJI 15
BASTOLA YA MAJI16
BASTOLA YA MAJI 17
BASTOLA YA MAJI18
BASTOLA YA MAJI 19
TUPA SALAMA20
Hatua za utupaji salama wa bomba na sindano lililokwisha/zilizokwisha tumika
Utengenezaji wa boksi la kuhifadhia bomba na sindano zilizokwisha tumika Kama utakuwa hujapata boksi maalum la EPI.
2. Usirudishie kifuniko chake kwenye
sindano kabla ya kutupakwenye
boksi
3. Tunza boksikwenye sehemu
ambayo ni salama mpaka likijaa robo tatu.Hakikisha hujazi boksi
mpaka juu
4. Likishajaa kufikia robo tatu lipelekekwenye eneo lililotengwa
kwa uteketezaji wa sindano hizo.Choma mara moja boksi likiwana sindano ndani yake na
uchafu mwingine
uliopo
5. Simamia zoezi hilola uchomaji. Usimwachie
kazi hii muhimu
mhudumu wa
usafi
6. Mara moto ukizima fukia
mabaki kwa udongo
Tafuta boksi lenyekuta nene
Funga boksi kwausalama. Funga juu na
chini kwa kutumia gundiau tepu au pini imara
Tengeneza kishimokidogo juu ya boksikitakachowezesha
sindano na bomba lake kupita bila
matatizo
1. Tumbukiza sin-dano iliyokwisha tumika
kwenye boksi mara baada ya kutumia
TUPA
SSAA
LLAAMM
AA!!
Ikiwezekana weka uzio ( mfano wa miti) kuzunguka shimo hilo la taka.
Choma boksi hilo natakataka zingine zilizopo
mara kwa mara. Unawezaukahitaji kiasi kidogo chamafuta ya taa kwa ajili ya
kuwashia moto.Moto ukisha
zima fukia mabaki kwa
udongo
TAH
AD
HA
RI
TUPA SALAMA 21
TUPA
SSAA
LLAAMM
AA!!
Na kama hunasehemu maalumya kuteketezeabomba, sindanona vifaavilivyokwishatumika basi:
Kama boksi ni jembamba kuna hatari ya sindano kuchomoza kupitiakwenye kuta za boksi hilo.
Hivyo zingatia:
● Zuia ubebaji wa boksi hilo usio wa lazima. Tafuta sehemu maalum katika chumba cha sindano ambapo unaweza ukalihifadhi boksi hilo. Hakikisha liko karibu na sehemu unayotolea sindano.
● Litunze boksi katika sehemu hiyo mpaka litakapokuwa tayari kuliteketeza kwa moto.
● Uwe mwangalifu unavyolibeba boksi kwenda kwenye eneo lililotengwa kwa uteketezaji.
● Usimwachie mhudumu wa usafi afanye kazi hii.
Tafuta na chaguasehemu kwenye eneo
hilo hilo la hospitali lililombali kidogo na majengo
ya hospitali kadiri inavyowezekana
Chimba shimoangalau lenye urefu wamita moja kwenda chini
Hakikisha uchafu unatupwa ndani
ya shimo na sio pembenimwa shimo
Tupa boksi, bila kutoasindano kutoka kwenye
boksi
hilo.
BBC/JISHINDIE REDIO!!!22
Ningependa kuanza kwa kuwafa-hamisha kuwa tuna makala maalum
juu ya afya ambayo imeanzishwa mapemamwaka huu. Makala hii hurushwa hewanikila jumatatu jioni ili kuwafahamishawasikilizaji wetu juu ya masuala yahusuyoafya katika mitazamo tofauti.
Kila inapowezekana tunazungumza nawataalam wa afya kutoka Afrika, hasa
tukizingatia kuwa wasikilizajitunaowatangazia ni kutoka barani humo.Na mada ikiwa juu ya suala linalohusianazaidi na nchi zilizoendelea au inapokuwavigumu kumpata mtaalam wa Kiafrika wamasuala hayo basi huwa tunawatumiawataalamu wa hapa hapa Uingereza.
Mara nyingi huwa tunazungumziamasuala ambayo ndio kwanza yana-
jitokeza na huwa tunafuatilia taarifa hizokwa karibu. Kwa mfano, tuliwafahamishawasikilizaji wetu wakati zilipotolewa taari-
fa juu ya athari za matumizi ya simu zamikononi, au wakati ilipotolewa taarifa juuya utafiti kuhusiana na uyoga unaowezakusaidia katika tiba ya maradhi ya mifupa,au kwa lugha ya kigeni arthritis na kadhali-ka.
Wakati mwingine huwatunazungumzia matatizo ya afya
yanayojitokeza katika maeneo ambakomatangazo yetu yanasikika. Kwa mfano,tuliweza kutangaza kuhusu operesheni yakuwatenganisha watoto mapacha waTanzania waliozaliwa huku wakiwa wame-unganika kwenye uti wa mgongo, upasuajihuo uliofanyika huko Afrika Kusini. Nahivi karibuni tu tuliweza kutangazamakala mbili kuhusiana na kampeni inay-oendelea nchini Tanzania ya kukabilianakuudhibiti na kuutokomeza kabisa ugonjwawa macho wa Trakoma, au kama unavyofa-hamika na wengi Ugonjwa wa Vikope,makala yaliyotayarishwa na kutangazwa na
mwenzangu Vicky Ntetema aliyetembeleamaeneo yaliyoathirika zaidi na maradhihaya katika mkoa wa Dodoma.
Kwa hakika ningependa kuongezakuwa BBC ina uwezo wa kuzipata
habari hizo muhimu za afya kutoka popotepale duniani, iwe kutoka kwenye mikutanoya kimataifa juu ya afya, utafiti juu yamaradhi na tiba mpya au kuzuka kwamaambukizo ya magonjwa mbali mbali.
Hivi karibuni tuliweza kuwatangaziawasikilizaji wetu kwa undani sana juu
ya mkutano wa kimataifa kuhusu janga laugonjwa wa UKIMWI uliofanyika DUR-BAN, nchini Afrika kusini..
Ni matarajio yangu kuwa Makala hayaya AFYA, kutoka Idhaa yetu ya
Kiswahili ya BBC yatakuwa na upeo waaina yake katika kukuelimisha na kukufa-hamisha mengi juu ya afya yako wewe najamii kwa ujumla.
Unaweza kusikiliza kipindi hicho cha Afya, kila siku ya Jumatatu jioni, kwenye mita bendi 19, 25 na 41. Vile vile kwenyemasafa ya FM - Dar es salaam 101.4 FM, Radio 5 Arusha kwenye 105 FM na Radio Free Africa katika 89.8 FM.
IDHAA YA KISWAHILI YA BBC YAKULETEA MAKALA YA AFYA NA MTAYARISHI - HAFSA MOSSI
JJIISSHHIINNDDIIEE
RREE
DDIIOO!!!!!!
Tunataka kujua kwa yakiniunafikiri nini kuhusu jarida hili. Endelea kuwa mwaminifu!
Maoni na mapendekezo yakoyatatusaidia kubuni jarida
bora zaidi siku zijazo.
Kama hutataka kuliharibu jaridaunaweza kunakilimajibu yako kwenyekaratasi na kutuma kwetu.Unaweza pia kututumia kivuli
chake (photocopy).Lakini kama unataka kushinda zawadi usisahau kuandika
jina na anuani yako!
Redio IsiyotumiaBetri !!!
JISHINDIE REDIO!!! 23
1. UNALIFIKIRIAJE JARIDA?
■n a. Nimefurahishwa nalo sana.
■n b. Nimefurahishwa nalo kabisa.
■n c. Ninadhani liko sawa.
■n d. Sikufurahishwa nalo.
2. NI RAHISI KULIELEWA?
■n a. Ndio, yote yaliyokuwemo yalikuwa rahisi kueleweka.
■n b. Mengi kati ya hayo yalikuwa rahisi kueleweka
■n c. Baadhi yake yalikuwa rahisi kueleweka
■n d. Sidhani kama yalikuwa yanaeleweka kwa urahisi
3. HATUA ZIPI ULIZOANZA KUCHUKUA BAADA KUSOMA JARIDA HILI?
.........................................................................
.........................................................................
4. NAKALA NGAPI ZA JARIDA HILI ULIZOPOKEA KATIKA KITUO CHAKO CHA AFYA?
Moja ■n ❙ Mbili ■n ❙ Tatu au zaidi ■n
5. WANGAPI MMESOMA JARIDA HILI?
1 ■n ❙ 2 ■n ❙ 3 ■n ❙ 4-nazaidi ■n6. UNAHUSIKA MOJA KWA MOJA NA ZOEZI LA CHANJO?
■n Ndio ❙ ■n Hapana
7.UNGEPENDAKUSOMA NAKALA YATOLEO LIJALO?
■n Ndio ❙ ■n Hapana
8. UNAFANYA KITUO KIPI CHA AFYA?
■n Dispensari
■n Kituo cha afya
■n Hospitali ya Wilaya
■n Hospitali ya Mkoa
■n Kliniki ya binafsi / hospitali
9. Ipi ni kazi yako?
■n Auxilliary/assistant ❙ ■n Muuguzi wa kituo cha afya
■n Muuguzi / mkunga ❙ ■n Cold chain Officer ❙ ■n MCH aide
■n Meneja au Msimamizi ❙ ■n Nyingine (tafadhali fafanua)
.........................................................................
10. Mapendekezo mengine yoyote?
.........................................................................
.........................................................................
.........................................................................
Ni m
akal
a ga
ni
3 ul
izof
urah
ishw
a
nazo
?
Ni m
akal
a 3
zipi
ziliz
okuf
urah
isha
kido
go?
Mak
ala
3 zi
pi
ziliz
okup
asha
haba
ri z
aidi
?
Mak
ala
3 zi
pi
ziliz
okuw
a na
upun
gufu
?
Kumbuka zawadi zitapatikana kwakuchezesha DRAW. Baada ya
DRAW hiyo majina mananeya kwanza yatapewa
ushindi.
11. 12. 13. 14.
a. Usalama kwanzab. Vichekeshoc. Hepatitis Bd. Lisemwalo lipo!e. Habari njema!f. Bastola ya majig. Tupa salamah. Makala ya afya ya BBCi. Maswali ya kushindania/uthibitishoj. Chemsha bongok. Wanasemaje kuhusu chanjo?
ANDIKA JINA NA NWANI KAMILI ILI UWEZEKUJISHINDIA REDIO........................................................................................................................................................................................................................................................................................
FOMU YA KUTHIBITISHA
Wasiliana na: “JISHINDIE REDIO”, EPI, World Health Organization, P.O.Box 9292, Dar es Salaam
CHEMSHA BONGO24
KEHOMAKYTNDUIK
AIJANUZIUAOJIM
OTFTKIBOFUUCAB
YUZUORWOAUHNPK
ASMOABOMHWAAIO
KOAWRKKJAAWCWK
DIYFAUOIPTHEUA
SCDDUKDOSOEHTV
EUNOJRLAMUANSI
DORHNIAIFRKJDP
DFGUODZBIIIAUE
UKOMAYASDPKMRA
KIFAFAHCUEUGUI
MLTOMALARIAOHE
Ndani ya jedwali hili kuna majina yamagonjwa hatari ya kuambukizayanayoleta athari kwa watoto wadogo.Yanasomeka kwa mielekeo ya pandembali mbali:Tafadhali yaonyeshe yalipo kishauyaandike hapa chini:
(a) ..............................................(b) ..............................................(c) ..............................................(d) ..............................................
C H E M S H A B O N G O N a . 1 C H E M S H A B O N G O N a . 2
Katika chemsha bongo hii, jaribu kutambua kama maelezo yaliyoandik-wa hapo chini ni ya kweli au siyo ya kweli. Kama ni kweli chukua heru-fi iliyoko upande wa “ndio” kulingana na namba za pembeni na kuiandi-ka sehemu ya “uchaguzi wako”.Kama siyo kweli fanya vivyo hivyo kwakuchukua herufi iliyoko upande wa “hapana” na kuiandika upande wauchaguzi wako.Ukimaliza kujaza kwa usahihi, utapata neno lenyeujumbe maalum.
1. Siyo vibaya kuichomoa sindano kwenye bomba lake kwa mkono baada ya kutumika.
2. Je, kabla ya kuzitupa sindano zilizotumika ni lazima kuziweka kwenye maboksi maalum?
3. Ugonjwa wa pepopunda huwapata watu wa rika zote na huambukizwa kwa njia ya hewa?
4. Kurudisha kifuniko cha sindano ni hatari kwani mtu anaweza kujichoma na kuambukizwa ugonjwa.
5. Ni kweli kwamba dalili mojawapo ya ugonjwa wa kifua kikuu ni kuvimba mwili?
6. Mabomba ya sindano yaliyotolewa sindano yanaweza kutupwa kama takataka nyingine zinavyotupwa.
7. Sindano iliyochemshwa vizuri haiwezi kumdhuru mchomwaji.
8. Siyo vibaya kumdunga mgonjwa sindano isiyo chemshwa kama kuna haraka ya kuokoa maisha ya mgonjwa.
9. Ugonjwa wa ini (Hepetitis B) hauna tiba. Isipokuwa unaweza kuuzuia kwa dawa ya chanjo tu.
10.Mtu hawezi kupata ugonjwa wa pepopunda kwa kuchomwa na sindano iliyotumika.
Na. Ndio Hapana Uchaguziwako
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10
P
E
T
O
C
H
D
N
N
O
K
A
O
A
M
E
A
P
J
A
MAJIBU: *Chemsha bongo na. 1:(a)Surua (b)Polio (c)Dondakoo (d)Kifaduro. *Chemsha bongo na. 2: “PATACHANJO”