morogoro - jica...jarida la afya morogoro – na.5 5 kwa miaka 4 iliyopita tayari usugu wa ugonjwa...
TRANSCRIPT
JARIDA LA
MOROGORO
MMAAEELLEEZZOO YYAA UUJJUUMMLLAA YYAA TTAATTHHMMIINNII YYAA MMWWIISSHHOO YYAA PPAAMMOOJJAA MMRRAADDII WWAA AAFFYYAA MMOORROOGGOORROO
asomaji Wapendwa,
HONGERA!!
Baada ya Taarifa ya Tathmini ya Mwisho ya Pamoja
hapo Oktoba 2005 Mradi wetu wa Afya Morogoro
umefanikiwa kukubaliwa na Shirika la Ushirikiano la
Kimataifa la Japan (“JICA”) kuongeza muda wa
mwaka mmoja; hadi 2007 Machi.
Mradi wa Afya Morogoro (“MHP”), unaofadhiliwa
na Japan ulipokea Timu ya Tathmini ya Mwisho ya
Pamoja kati ya Tanzania na Japan (ikiongozwa na Bibi
Harumi Kitabayashi, Makao Makuu ya JICA, Tokyo,
Japan) kwa kusudi la kupitia maendeleo ya mradi
tangu uanze 2001 Aprili. Kwa kuwa hapo awali mradi
ulipangwa kumalizika baada ya miaka 5 ya utekelezaji,
yaani 2006 Machi, huu ni wakati muafaka kufikiria
mradi utaendeshwaje siku zijazo.
Timu ya Tathmini, iliyokuwa na Bingwa wa nje wa
kujitegemea kutoka Makao Makuu JICA, Japan,
aitwaye Bibi Minako Nakatani na wawakilishi 2
kutoka Makao Makuu Wizara ya Afya, Tanzania,
ilipitia mafanikio ya Mradi. Walifanya hivyo kwa njia
ya mahojiano ya kina, kutumia dodoso (questionnaire)
kwa watendaji wa Kitanzania (Counterparts), wao
wenyewe kutembelea wilaya (zote) kusikofungamana
na upande wowote, na kwa kuhudhuria mikutano
mbalimbali muhimu iliyofanyika wakati wa tathmini
hapo 2 Oktoba hadi 23 Oktoba2005: kwa mfano
“Project Final Internal Evaluation Workshop”,
“Morogoro Health Stakeholders Conference” na
“Tanzania – JICA Project Review Workshop”.
Mwishoni Timu ya Tathmini ilijadili taarifa ya
tathimini kwa pamoja na mamlaka za ngazi ya juu
kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Sekretariati ya Mkoa na Halmashauri za
Wilaya za Mkoa wa Morogoro.Katika majadiliano
hayo walifikia muafaka kuwa mafanikio ya mradi
katika kujenga uwezo wa uendeshaji kiafya na baadhi
ya matokeo katika utoaji na utumiaji wa huduma za
afya ni yale ambayo yangetazamiwa kupatikana
kutegemea hali halisi katika Mkoa wa Morogoro.
Tathmini hiyo ilihitimisha kwa kusema, “Wakati wa
kazi ya kutathmini mabadiliko mbalimbali ya
mwenendo wa wajumbe wa Timu za Afya za
Uendesahji ya Mkoa na za Wilaya yalitambuliwa
kuwa yanaelekea katika uendeshaji wenye ushahidi .
Mabadiliko hayo yana thamani katika kusaidia
W
ISSN 0856-9517 Toleo Na.5 Desemba 2005
Picha ya pamoja ya washiriki wa Tathmini ya Mwisho
ya Mradi wa Afya Morogoro
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
2
mchakato wa kuondoa madararka toka ngazi za juu
kuyapeleka chini kwa jamii kwa mujibu wa
Mabadiliko Katika Serikali za Mitaa na Mabadiliko
Katika Sekta ya Afya, na yana umuhimu katika
kuhakikisha ubora wa huduma za afya wilayani.
Kwa manufaa ya watoa huduma walio mstari wa
mbele na mwishowe kwa watumiaji huduma za afya
Mkoa wa Morogoro ni lazima katika siku zijazo
juhudi zifanywe na wadau wote, ili kuimarisha
mabadiliko hayo ya mwenendo katika uwezo wa
uendeshaji wa wajumbe wa Timu za Afya za
Uendeshaji ya Mkoa na za Wilaya” – (Ikumbukwe
kuwa hakuna tafsiri yeyote ya Kiswahili ya Taarifa ya
Tathmini inayoelezewa hapa: hii ni tafsiri ya
mwandishi tu, ya nakili ya Kiingereza).
Ili kuimarisha mafanikio ya Mradi katika Timu za
Afya za Uendeshaji ya Mkoa na za Wilaya na kueneza
uzoefu na masomo yatokanayo na Mradi kwa mikoa
mingine, Timu ya Tathmini ya Mwisho ilipendekeza
kuwa kipindi cha mradi kiongezwe kwa mwaka
mmoja; kutoka Aprili 2006 hadi 2007 Machi na JICA
itoe msaada kamili. Katika siku zijazo mradi unaweza
kuwa mfano wa kujenga uwezo wa uendeshaji katika
mifumo ya afya Tanzania. Tanzania na Japan hazina
budi kufanya kazi zaidi kwa pamoja ili kuleta ubora
na usawa katika huduma za afya Tanzania.
Mradi wa Afya Morogoro ungependa kuwashukuru
Wadau wote kwa juhudi endelevu na unaridhia
kutenda zaidi ndani ya Mradi.
Ukitaka taarifa zaidi kuhusu Taarifa ya Mwisho ya
Tathmini inapatikana ofisi ya Mradi wa Afya
Morogoro, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Ofisi
za Waganga Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Morogoro.
Asanteni sana kwa ushirikiano na kujali kwenu.
Hatuna budi kutumikia ili tufikie maisha mazuri kwa
Watanzania wakati ujao.
Dk. T. Sugishita
Mshauri Mkuu
Mradi wa Afya Morogoro
- Yaliyomo -
Tathmini ya Mwisho ya Pamoja Mradi wa Afya Morogoro 1 Tahariri 3 Tabia na Mila Zinazodhuru Meno 4 Dawa Mpya ya Kutibu Malaria 4 Wachuuzi wa Chakula: Taarifa Utafiti 6 Kuboresha Mazingira kwa Kuhusisha Jamii 7 Huduma ya Wagonjwa Nyumbani 8 Utafiti wa Kiafya Kiutendaji Unavyoendeshwa 9 Matukio Muhimu : Agosti - Desemba 2005 11 Vichekesho 12
BODI YA UHARIRI
Mwenyekiti:
Bw. N. Masaoe Afisa Afya Mkoa
Katibu:
Bi. C. Maro Mratibu wa Huduma za Afya ya
Uzazi na Mtoto Wilaya Morogoro
Msaidizi wa Katibu:
Bi. N. Ahmed Afisa Muuguzi Manispaa Morogoro
Wajumbe:
Bw. J. Mankambila Katibu wa Afya Mkoa
Dk. G. Mtey Mganga Mkuu Manispaa Morogoro
Dk. O. Mbena Mganga wa Meno Wilaya Mvomero
Bw. J. Bundu Afisa Afya Wilaya Kilosa
Bw. D. Dia Katibu wa Afya Wilaya Kilombero
Bw. W. Mkessey Afisa Afya Wilaya Ulanga
Bi. M. Tsuda Mshauri, MHP*
Mshauri Mkuu:
Dk. M. Massi Mganga Mkuu Mkoa
Mjumbe Mshiriki:
Dk. F. Fupi Mshauri, MHP*
Kamati ya Ushauri:
Bw. H. Mohamed Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo, Morogoro
*MHP: Mradi wa Afya Morogoro (Morogoro Health Project),
JICA
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
3
JARIDA LA AFYA MOROGORO Wasomaji wetu wapendwa,
Kwa niaba ya bodi ya uhariri ya hili jarida,
napenda kuwakaribisha kwa Toleo la tano la hili
jarida.
Leo napenda kukazia mambo mbalimbali. Jamii
inatakiwa kufahamu kwamba, ugonjwa wa Malaria
ambao ni tatizo linaloongoza katika afya ya jamii,
sasa hautibiki kikamilifu na dawa aina ya
Sulfadoxine - Pyrimethamine (SP). Tiba mseto ya
huu ugonjwa itaanza kutolewa mwaka 2006. Jamii
inashauriwa kuweka kwa pamoja mikakati ya mseto
ya kupambana na mbu wanaoeneza Malaria kwa:
kila mtu kutumia chandarua chenye viuatilifu,
kuharibu mazalia yote ya mbu katika makazi,
kuweka nyavu za kuzuia mbu kwenye nyumba,
kuwa na silka ya kutafuta tiba mapema na kadhalika.
Bodi ya Uhariri inapongeza kwa dhati kwa
uongozi wa Serikali Kuu na halmashauri zote za
mkoa wa Morogoro kwa kuthamini hili jarida na
hivyo kutenga, katika bajeti za mwaka, fedha za
kuchapisha hili jarida. Moyo huu umefurahisha sana
Shirka la JICA ambao ndio wafadhili wa Mradi wa
Afya Morogoro (“MHP”), kwa kuwa ni dhahiri
kwamba jarida litakuwa endelevu, hata baada ya
Ufadhili wa Mradi kuhitimishwa.
Wajumbe tisa wa hii Bodi wamepatiwa mafunzo
ya “type setting” na “computer skills” ya siku nne
katika Chuo Kikuu Mzumbe. Mafunzo yalikuwa
muhimu na hii ni hatua ya maana katika kujenga
uwezo wa bodi kumudu shughuli za kitaalamu za
kuhariri na kuchapisha hili jarida. Bodi inatoa
shukrani kwa Mradi wa Afya uliolipia haya
mafunzo.
Kikundi cha wataalamu 4 wa nje: Ms. Harumi
Kitabayashi, Prof. Ichiro Okubo, Mr. Ikuo Takizawa
na Ms. Minako Nakatani waliofanya Tathmini ya
Mwisho ya Mradi wa Afya Morogoro tarehe
1-10-2005 hadi 23-10-2005; walitembelea
halmashauri zote sita za mkoa huu. Katika vituo vya
huduma ya afya walivyotembelea, walikuta makala
za hili jarida. Baadhi ya watoa huduma walitumia
makala ya jarida hili kutoka elimu ya afya. Hili
limewafurahisha sana. Bodi inawapongeza sana
wale wote wanaosoma na kutumia hili jarida
kuelimisha umma. Wengine wanashauriwa kuiga.
Timu ya Tathmini iliridhika na utehelezaji wa
Mradi na iliona kuwa makusudio ya “MHP” ya
kujenga uwezo wa uendeshaji wa Timu za Afya
Mkoani Morogoro yamefanikiwa kwa kiasi
ambacho kilitazamiwa kutegemea hali halisi.
Bodi inazidi kuomba wasomaji wa hili jarida
kutuma habari na maoni ya kuchapishwa, ili kukidhi
adhma ya kuanzishwa kwa jarida hili, yaani
kubadilishana uzoefu na maoni baina yawatendaji
wa afya na jamii kwa ujumla.
Nachukua nafasi hii kuwaarifu wasomaji wetu
kwamba, mwaka 2006 katikati ya Januari nitastaafu
rasmi na hivyo, uenyekiti wangu kwa Bodi unafika
ukingoni 2005 kati ya Desemba. Namtakia
mwenyekiti ajae Dk. G. Mtey kazi na afya njema na
kumuahidi msaada na kujitolea thabiti kwa
maendeleo ya hili Jarida.
Aidha nashukuru wajumbe wote wa Bodi ya
Uhariri na wasomaji kwa ushirikiano, msaada na
kujituma kwao, kuliowezesha kufanikisha malengo
ya hili jarida. Tutaonana Mungu akipenda.
Nawatakia wasomaji wote Krismasi njema na
Mwaka Mpya.
Bw. N. Masaoe
Mwenye Kiti
Bodi ya Uhariri
Bw. N. MasaoeMwenyekiti
Bodi ya Uhariri
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
4
TTAABBIIAA NNAA MMIILLAA ZZIINNAAZZOODDHHUURRUU MMEENNOO
Meno ya binadamu ni kiungo muhimu katika
mwili wake, yanaweka uzuri wa uso, ulinzi hasa
kama silaha na kutafuna vyakula na matunda.
Hivyo yanatakiwa kutunzwa yasiharibike kwa
kutibiwa na kukaguliwa maramara.
Walakini baadhi ya watu wamekuwa wakifanyiwa
urembo wa meno wa kimila katika baadhi ya nchi,
kulingana na tamaduni. Urembo huo umefaywa
maarufu na mataifa mengi. Katika karne kadhaa
zilizopita. Urembo wa meno kimila ulikuwa na
maana mbalimbali ikiwemo alama wakati wa vita na
sifa hasa kwa wanawake.
Meno pia yalikuwa yanatolewa kwa manufaa ya
tiba kuondoa maumivu. Wakati mwingi ilikuwa ni
tiba ya imani tu na mara chache ilikuwa tiba sahihi.
Urembo wowote ule wa meno unaharibu kinywa na
meno yenyewe.
Siku hizi urembo hauna faida kwa Mtanzania.
Hatuna budi kusisitiza kuwa watu wasirembe meno
au kuyang’oa bila sababu ya kufaa.
Baadhi ya mila na desturi zinazostahili kupingwa
ni:
• Kuchonga au kukwangua meno. Hii inaondoa
ganda la juu linalolinda jino.
• Kung’oa meno ya chini ya mbele.
• Kutoa meno ya juu na kutoboa mdomo wa juu
na kuweka “ndonya” (kitu mviringo) ambacho
ni alama ya urembo kwa wanawake wazima.
• Kung’oa meno ya utotoni mara yanapoanza
kulegea huumiza mtoto na kuchelewesha kuota
meno ya kudumu. Uvumi wa meno ya “plastic”
au “nylon” si kweli.
• Kutumia meno kufungulia vizibo vya chupa,
kukata kamba, kutafuna mifupa na kunyanyua
vitu vizito.
• Kukwangua meno kwa kutoa rangi iliyoganda
kwa mfano “fluorine”.
Hasara ya kuchonga meno:
• Kuumwa kwa jino wakati wa kula kitu moto au
baridi.
• Kufanya jino lioze kwa urahisi.
• Meno kulegea kwa urahisi na hatimaye
kungoka.
Kwa hiyo tuzingatie masharti ya miongozo ya
kulinda meno kwa afya njema.
Dk. O. Mbena
DDO Mvomero
DDAAWWAA MMPPYYAA YYAA KKUUTTIIBBUU MMAALLAARRIIAA
Malaria bado ndiyo ugonjwa hatari kupita yote
katika Dunia ya Tatu. Malaria inaongoza kwa maana
ya kuugua na vifo, hasa kwa watoto chini ya umri wa
miaka mitano na akina mama wajawazito. Serikali
imetoa mwongozo wa ugunduaji na tiba ya ugonjwa
wa Malaria ili kuwa na utabibu unaofanana nchi
nzima. Msingi wa mwongozo wa sera ya dawa ya
Malaria ni kuongeza usalama, ufaaji, ubora, gharama
nafuu, upatikanaji, kukubalika kwa tiba ya Malaria na
kupunguza ustawi wa usugu wa dawa.
Hapo Agosti 2001 nchi yetu ilibadilisha mwongozo
wa sera ya tiba ya Malaria kutoka tiba moja ya
“Chloroquine” kwenda “Sulfadoxine – Pyrimethamine
(SP)” tiba ya mchanganyiko kama tiba ya dawa ya
mstari wa kwanza kwa ugonjwa wa Malaria. Walakini
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
5
kwa miaka 4 iliyopita tayari usugu wa ugonjwa wa
Malaria kwa kutumia dawa aina ya SP umeripotiwa
kuongezeka. Tafiti zilizofanyika nchini Tanzania hivi
karibuni (2004) zimeonyesha kuwa tiba ya SP
imeshindikana kwa wastani wa asilimia 25.5 %.
Usugu wa SP (molecular markers) umeonyesha
kiwango kikubwa cha viini vya Malaria kubadilika
(mutation). Tiba ya “Amodiaquine”, iliyokuwa mstari
wa 2 kwa tiba ya Malaria, iliyoonyesha kushindwa
kwa wastani wa asilimia 12 %. Matokeo haya yana
onyesha kuwa kuna haja ya kubadili mwongozo wa
tiba.
Kutokana na hatari ya kuongezeka usugu wa
wadudu wa Malaria kwa dawa moja. Hivi sasa duniani
kote kuna mwelekeo wa kutumia tiba ya dawa
mchanganyiko. Sababu nyingine ni kwamba dawa
mchanganyiko zina faa zaidi na kuna uwezekano wa
kuchelewesha ueneaji wa usugu wa dawa.
Tiba iliyopendekezwa:
• Mchanganyiko ulipendekezwa ni dawa aina ya
“ARTEMETHER / LUMEFANTRINE (ALU)”
kama tiba ya mstari wa kwanza kwa ugonjwa wa
Malaria. (Tazama Jedwali-1)
• Endapo ALU ikishindwa kutibu au kwa sababu
yeyote mgonjwa atumie dawa iliyopo mstari wa
pili ambayo ni “Quinine”.
• Dawa iliyopendekezwa kwa tiba ya Malaria kali
ni Quinine.
• Hata hivyo dawa iliyo katika mstari wa kwanza
kwa tiba ya Malaria kwa wanawake na watoto
chini ya uzito wa kg 5 (chini ya miezi miwili) ni
Quinine.
• Dawa aina ya SP itaendelea kutumika tu kwa
akina mama wajawazito kwa kuzuia Malaria
(Intermittent Presumptive Treatment – IPT). Dozi
ya kwanza pale wanapokuwa na ujauzito wa wiki
20 - 24 na dozi ya pili (IPT) wanapokuwa na
wiki 28 - 32.
Utumiaji wa SP kwa mama wote wajawazito
utazuia hatari ya vimelea kwenye damu na vimelea wa
Malaria kwenye kondo la nyuma; kwa sababu vimelea
vilivyo kwa mama mjamzito mara nyingi havionyeshi
dalili mapema.
Dawa ya SP hupewa mama wajawazito na kumeza
mbele ya wahudumu afya (“DOT”) katika clinic zao.
Ridhaa ya mgonjwa kutumia sahihi dawa aina ya
ALU ni muhimu sana kwa sababu ALU siyo dozi
moja. Maelezo sahihi kuhusu dawa ni muhimu sana
kwa wateja. Mama wajawazito wote wanahimizwa
kutumia vyandarua vyenye dawa (ITNs) licha ya tiba
ya kuzuia (IPT).
Kitabu cha: Rejea Malaria namba 10
Bi. C. Maro
DRCHCo Morogoro
Jedwali-1 Utaratibu wa dozi za ALU – Dozi ya vidonge Artemether 20 mg & Lumefatrine 120 mg (ALU)
Uzito (Kgm)
Umri Siku 1 Siku 2 Siku 3 Msimbo
Dozi 1 2 3 4 5 6 Masaa 0(“) 8 24 36 48 60 vidonge vidonge vidonge vidonge vidonge vidonge 5-14 Miezi 3 hadi
Miaka 3 1 1 1 1 1 1 Njano
15-24 Miaka 3 hadi Miaka 7
2 2 2 2 2 2 Buluu
25-34 Miaka 7 hadi Miaka 12
3 3 3 3 3 3 Nyekundu
35 na zaidi
Miaka 12 na zaidi
4 4 4 4 4 4 Kijani
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
6
WWAACCHHUUUUZZII WWAA CCHHAAKKUULLAA:: TTAAAARRIIFFAA UUTTAAFFIITTII WWAA EELLIIMMUU NNIIAA NNAA DDEESSTTUURRII
Biashara ya uuzaji vyakula inayofanywa na
wachuuzi wa chakula, inashamiri haraka mijini na
kando ya miji. Hii biashara inayofahamika kwa jina
la fumbo (nick name) kama “mama/baba lishe” licha
ya kupatia chakula wateja kwa bei nafuu, imepatia
ajira akina mama na baba wengi wa umri wa kati na
wengineo. Vikundi vingine hutoa huduma ya
chakula katika sherehe kama harusi mazishi nk.
ambapo watu wengi hushiriki kula.
Usindikaji wa matunda, achali, na hata mvinyo
kwa matumizi ya binadamu hutayarishwa na baadhi
ya hivi vikundi.
Usafi wa hawa “mama/baba lishe” (food vendors)
siyo wa kuridhisha. Hivyo watumiaji wa hivi
vyakula huwa katika hatari isiyojulikana ya kupata
maradhi yanayotokana na chakula kilichochafuliwa.
Kutokana na hali hii, utafiti wa Elimu, Nia na
Desturi wa “mama/baba lishe” umeendeshwa katika
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Matokeo, hitimisho na Ushauri wa huu utafiti unafaa
sana kwa uimarishaji wa biashara ya mama/baba
lishe nchini kote.
Washiri 175 walidodoswa kwa dodoso la
maandishi katika eneo lililofanyiwa utafiti.
Walio dodoswa walikuwa na sifa zifuatazo:
• Umri kati miaka 18 hadi 48.
• Jinsi: 154 [88%] wanawake, 21 [12%]
wanaume.
• Elimu: 150 [86%] msingi, 13 [7%]
sekondari/ufundi na 12 [7%] hawana darasa.
• 172 [98%] wamepata mafunzo kuhusu usalama
wa chakula na 3 [2%] hawakuwa na ufahamu.
Mazingira chakula kilipoandaliwa na kuuzwa:
• Mabaki ya vyakula na plastiki zilizotumika
zimezagaa ovyo.
• Vyombo vya kulia vichafu, huhifadhiwa kwa
mifuko ya plastiki iliyotumika.
• Hakuna dawa za kutakasa ama sabuni ya
kunawa mikono.
• Uondoshaji mbaya wa maji taka na taka
ngumu.
• Baadhi ya vibanda ni chakavu, vibovu sana na
havina huduma muhimu kama: maji, sehemu ya
kujisaidia, [vyoo] vifaa vya kuzolea taka
ngumu na majitaka.
Mambo mazuri yaliyoonekana:
• Chakula kuuzwa kingali cha moto kwa wateja
wa awali.
• Bei wanazimudu wateja.
• Maji moto kwa kuoshea vyombo na kunawia
mikono, yapo katika baadhi ya sehemu.
Desturi mbaya kwa mama/baba lishe wengi
wakiwa kazini:
• Kuzungumuza.
• Kuchokonoa puani ama meno kwa vidole.
• Kujikuna mwili.
• Kupiga chafya bila tahadhari.
• Kukohoa ovyo.
• Kuvuta sigara wakipika au kupakua chakula.
• Kutopimwa afya zao kabisa au kupimwa bila
utaratibu.
• Kutokuwa na sare na zana za kujikinga.
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
7
Hitimisho na mapendekezo:
Shughuli za wachuuzi wa chakula inakua haraka
na kutoa ajira kwa akina mama na baba wa umri
mbalimbali. Wateja wengi hujipatia mlo kwa bei
nafuu.
Mamlaka husika ina wajibu wa kusimamia na
kuidhibiti kwa mujibu wa sheria zilizopo kwa:
• Kutambua, kusaili na kutoa vibali kwa mama
na baba lishe wote.
• Kutambua uongozi wao na kuwa na mdahalo
na mikutano mara kwa mara ya kuboresha
shughuli zao.
• Kuwahusisha wadau wote katika kuweka
viwango vinavyokubalika.
• Kuwapatia mafunzo na mafunzo rejea kuhusu
usalama wa chakula. Mafunzo yangeweza
kulipiwa kutoka Mipango Kabambe ya Afya ya
Halmashauri (CCHP).
• Kuwasaidia kupata mikopo ya kuimarisha
shughuli zao.
• Kuwa na ratiba ya kuchunguza afya zao.
• Kuhakikisha kila mama na baba lishe anavaa
sare na zana za kujikinga awapo kazini.
• Kuto waweka watoto wadogo/wachanga karibu
na maeneo ya biashara.
Bi. L. F. Temu
Afisa Afya [Mazoezini]
Morogoro
KKUUBBOORREESSHHAA MMAAZZIINNGGIIRRAA KKWWAA KKUUHHUUSSIISSHHAA JJAAMMIIII MMAANNIIPPAAAA YYAA MMOORROOGGOORROO
Manispaa ya Morogoro ni kati ya Manispaa zenye
mandhari na mazingira yanayovutia ya milima ya
Uluguru na mito mingi inayotiririka. Uzuri huu
umekuwa ukiporomoka kila mwaka kutokana
sababu zifuatazo:
• Wakazi wengi hawathamini usafi. Hawashiriki
kikamilifu katika mikakati ya kusafisha
Manispaa yao.
• Taka ngumu na taka mimina hulundikana
kwenye makazi bila kuondolewa.
• Baadhi ya nyumba za kuishi hazina:
○ Vyoo vinavyokubalika
○ Mashimo ya maji machafu ya kufaa
○ Karo za kuoshea vyombo na kufulia
○ Vifaa vya kuhifadhia taka za nyumbani
• Chupa za plastiki na mifuko iliyotumika
huzagaa ovyo kwenye maeneo yote ya
Manispaa.
• Baadhi ya wakazi hufugia kwenye maeneo ya
watu wengi, hivyo kusababisha kero na adha
kubwa kwa majirani.
Manispaa ya Morogoro kwa mara tatu mfululizo
imekuwa ya 12 kati ya Manispaa 13 za Tanzania
bara, katika mashindano ya usafi wa mazingira
yanayoendeshwa na Wizara ya Afya. Kutokana
sababu zilizotajwa na nyingine kama: machinjio na
chakavu, makaburi yasio na uzio, soko kuu
lisilokarabatiwa, barabara mbaya, mifereji ya maji
ya mvua isiyotunzwa na kuwepo kwa makazi mengi
yasiyopimwa (squarters).
Wakazi wa Manispaa wanatakiwa kuwajibika
kikamilifu kwa afya na usafi wa manispaa yao, kwa
kuingia ubia na uongozi ya Manispaa ili kubadili
hali hii.
Mwaka 2003, Manispaa kwa msaada toka Ubalozi
wa Denmark kupitia shirika la DANIDA wamebuni
mkakati mpya kwa kuanzishwa kwa mpango
endelevu wa “Sustainable Morogoro Project”
(SUMO). Mpango huo ukiungwa mkono utakuwa
Daima sisitiza uuziwe chakula cha moto, kilichoandaliwa kwa usafi
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
8
sehemu ya utatuzi wa tatizo hili.
Mojawapo ya malengo ya SUMO ni
kushughulikia tatizo la taka ngumu katika manispaa
kwa mbinu shirikishi inayotekelezeka na makini
kwa kutupa taka ngumu unaofahamika kama
“Sustainable Solid Wastes Program” ambao
umeanza kutekelezwa tangu Julai 2005. Programu
hiyo inatekelezwa na jamii ikishirikisha akina mama
na vijana “Community Based Organizations”
(CBOs) wanaoondoa taka ngumu wakishirikiana na
manispaa.
Huu mpango unatarajiwa, licha ya kuwapa CBOs
sauti ya kuumiliki pia unawawezesha kiuchumi na
hivyo kuchangia katika Mpango wa Kupunguza
Umaskini (MKUKUTA).
Hawa CBOs wanatarajiwa kukusanya malipo ya
uzoaji taka ngumu toka kwa makazi na kuendeleza
usafi wa mitaa na mitaro ya maji machafu na
maeneo ya wazi. Pia kuwasaidia Maafisa Afya
katika kutekeleza kanuni za afya katika maeneo yao.
Watazolea taka kwa mapipa maalumu “Skip Bucket”
na kulipa kwa manispaa gharama za kusafirisha
hayo mapipa maalumu hadi “dampo”. Akaunti
maalumu itafungliwa ili kufanya huu mpango kuwa
endelevu kwa kugharamia utunzaji wa “dampo” la
manispaa na ununuzi wa vifaa vipya.
CBOs watachaguliwa kwa nia ya zabuni katika
ngazi ya kata, kwa kupitia Kamati ya Maendeleo ya
Kata (WDC). Watakaofanikiwa, wataidhinishwa na
kamati ya zabuni ya “Manispaa Council Tender
Board”, wataazima vifaa muhimu vya kuanzia kazi.
Usimamizi na ufuatiliaji utafanyika katika ngazi
ya kata yaani WDC. Katika ngazi ya Manispaa, hili
litafanyika katika Kata na mfuko wa kusafirisha
“Skip Bucket”.
Habari hii inalenga kuamsha hamasa kwa wadau
wote ili kupata ushirikiano wao katika utekelezaji
wa huu mpango, na pia mchango wa maoni wa
kuboresha mpango wenyewe.
Imani yetu ni kwamba “Tunaweza kuleta
mabadiliko tukiiunga na pamoja”.
CHMT
Manispaa ya Morogoro
HHUUDDUUMMAA YYAA WWAAGGOONNJJWWAA NNYYUUMMBBAANNII WWIILLAAYYAA YYAA KKIILLOOSSAA
Wilaya ya Kilosa imeanzisha mpango wa huduma
ya wagonjwa nyumbani kwa wanaoishi na virus vya
UKIMWI na wenye magonjwa ya kusendeka.
Magonjwa hayo ni:
UKIMWI, Kisukari, Kifafa, Saratani, Kifua kikuu,
Magonjwa ya akili na Magonjwa ya moyo.
Sababu za kuanzisha huduma hii ni:
• Kuongezeka kwa magonjwa ya UKIMWI na ya
kusendeka. Asili mia 50 – 60% ya vitanda vya
hospitali hutumiwa na wagonjwa wa UKIMWI
na ya kusendeka.
• Kuwawezesha Wafanyakazi wa Afya kusaidia
kufundisha Familia zenye wagonjwa wa
UKIMWI pamoja na magonjwa sugu kuweza
kuwahudumia wagonjwa wao nyumbani.
Malengo mahususi ya huu mpango ni:
• Kupunguza maumivu sugu kwa wagonjwa
wanaoishi na virus vya UKIMWI.
• Kuelimisha na kusaidia wanaohudumia
Saidia magonjwa ya akili katika jamii kwa huduma ya nyumbani
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
9
wagonjwa wanaoshi na virus vya UKIMWI au
UKIMWI na magonjwa sugu ili aweze kutoa
huduma ya kitaalam kwa wagonjwa wao
nyumbani.
• Kutoa ushauri nasaha kwa wagonjwa pamoja na
ndugu zao jinsi ya kupunguza maumivu, msongo
unaotokana na UKIMWI na magonjwa sugu.
• Kusambaza vifaa vya kitaalamu, dawa na
vitendea kazi kwa wahudumu wa huduma ya
wagonjwa nyumbani.
• Kuelimisha jamii na kushauri kuanzisha huduma
hii na kuelewa kuwa njia hii itawasaidia.
• Kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na
maambukuzi na namna ya kuhudumia wenye
magonjwa ya kusendeka nyumbani.
Maafisa tabibu 14 na Wauguzi wa afya ya jamii 28
walipatiwa mafunzo ya siku 21, kuhusu huduma ya
wagonjwa nyumbani. Hawa walianza kutekeleza huu
mpango katika vituo vyao vya kazi.
Wizara ya Afya kupitia Tume ya Kudhibiti Ukimwi,
imetoa baiskeli 14 kwa watoa huduma hii, na pia
kununua dawa kwa vituo 14 vya huduma, ikiwepo
hospitali moja, vituo vya afya 5 na zhanati 8. Fedha
zilipokelewa pia za kununua chakula (unga na sukari)
kwa hivyo vituo 14 vinavyo tekeleza huu mpango.
Faida zitakazotokana na huduma hii ni pamoja na:
• Jamii inahamasika hivyo kutowanyanyapaa
wanaoihi na virus vya UKIMWI.
• Itapunguza wingi wa wagonjwa wanaolazwa
hospitalini.
• Itapunguza maambukizo mapya ya virus vya
UKIMWI kwa jamii.
• Wanaotunza wagonjwa kwa huu utaratibu
watapata nafasi ya kufanya shughuli nyingine za
kuzalisha kipato.
Huduma hii itamsaidia mgonjwa vitu vifuatavyo:
• Kuzuia magonjwa nyemelezi kwa kutoa
matibabu.
• Kuwapatia huduma muhimu km. vyakula vyenye
virutubisho na nyumba zene mwanga wa
kutosha.
• Kuendeleza usafi wa mwili na usafi wa
mazingira.
• Kuwapatia mazoezi mara kwa mara.
• Kujenga uwezo wa wahudumu wa huduma ya
wagonjwa nyumbani.
• Kuwapatia burudani na michezo.
• Huduma za kiroho.
• Msaada wa kisheria.
• Msaada wa kifedha.
• Kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya dawa za
kurefusha maisha kwa wenye UKIMWI.
Kwa kupitia huu utaratibu wa “Home Based Care”
(HBC) wagonjwa wa UKIMWI hupatiwa
Antiretroviral (ARV) kufuatana na mwongozo wa
World Health Organization (WHO). Wilaya inalenga
kusambaza hii huduma kwa vtuo 49 vya huduma ya
afya vilivyobaki katika miaka mitatu ijayo.
Dk. W. Munuo
Mratibu wa magonjwa ya kusendeka nyumbani
Kilosa
MMAAEELLEEZZOO YYAA UUJJUUMMLLAA KKUUHHUUSSUU UUTTAAFFIITTII WWAA KKIIAAFFYYAA KKIIUUTTEENNDDAAJJII UUNNAAVVYYOOEENNDDEESSHHWWAA KKWWAA
PPAAMMOOJJAA TTAANNZZAANNIIAA NNAA JJAAPPAANN KKAATTIIKKAA MMRRAADDII WWAA AAFFYYAA MMOORROOGGOORROO
Hivi karibuni Mkusanyo (Corpus) wa Kwanza wa
Taarifa za Utafiti wa Kiafya Kiutendaji (“Health
Operational Research”) ulitolewa ukiwa ni matokeo
ya mafunzo ya vitendo kwa Timu za Afya za
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
10
Uendeshaji (Health Management Teams - CHMTs), ya
Mkoa na za Halmashauri za Wilaya, Mkoani
Morogoro. Mafunzo hayo yameendeshwa na Mradi
wa Afya Morogoro (“Morogoro Health Project -
MHP”) ambao kusudi lake kubwa ni kuboresha uwezo
wa kuendesha huduma za afya za wilaya Mkoa wa
Morogoro.
Uanzishwaji wa Mabadiliko Katika Sekta ya Afya,
Tanzania, unawataka mameneja wa afya kufuata
mipango yenye misingi ya ushahidi. Mipango ya
namna hiyo huhitaji michakato (processes) ya
kutambua na kuchambua matatizo ya kiafya ya mahali
husika na kuyaingiza katika Mipango Kabambe ya
Afya ya Halmashauri ya Wilaya (Comprehensive
Council Health Plans - CCHPs). Kutokana na hali
hiyo ufanyaji wa “Operational Research (OPR)” kwa
kusudi la kupata ushahidi umekuwa ni shughuli ya
pekee lakini muhimu inayofanywa na hizo Timu za
Afya za Uendeshaji. Mtindo na fikira zinazozingatia
uchambuzi (“analytical attitude and thinking”),
ambazo zinaweza kujengeka kwa njia ya uendeshaji
“OPR”, ni vitu vya lazima kwa mameneja wa afya ili
waweze kuyamudu mazingira mageni
yanayotazamiwa katika Mabadiliko ya Jamii kwa
Ujumla (Public Sector Reforms - PSR) yanayofanywa
na Serikali.
Kwa sababu ya madai thabiti kutoka kwa mameneja
wa afya “MHP” umesaidia, tangu Septemba 2004,
uendeshaji wa “OPR” halisi unaofanywa na Timu za
Afya za Uendeshaji za Halmashauri na ya Mkoa
katika wilaya husika. Zaidi ya hayo Mradi unatoa
ujuzi stadi muhimu kwa mameneja hao wa Wilaya na
Mkoa; mradi unahusisha pia jamii na wafanyakazi wa
afya walio mstari wa mbele. Baada ya matokeo ya
utafiti (“OPR”) mipango ilifanywa (pale
panapohusika) na kuingizwa kwenye “CCHPs”.
Topiki (“Topics”), (timu husika katika mabano)
hizo, na mipango hiyo kwa mwaka 2005/6 ni kama
ifuatavyo:
1) Vifo vingi vya Watoto wachanga Manispaa ya
Morogoro (Timu Mkoa) - Mipango: Kuimarisha
Wodi ya watoto wachanga ya mfano
2) Mambo yanayoshawishi utumiaji wa vyandarua
vilivyowekwa dawa miongoni mwa watoto chini ya
miaka 5 Morogoro Mjini (Timu Manisipaa)
- Mipango: Mikutano ya uhamasishaji viongozi wa
vitongoji
3) Uchunguzi wa mkondo wa huduma za afya
zinavyotumiwa na mama wajawazito wakati wa
kujifungua wilaya ya Morogoro (Timu Morogoro)
- Mipango: Kuelekeza watoa huduma wa mstari wa
mbele kuweka mkazo katika uzingatiaji wa huduma
salama kwa wajawazito kabla ya kujifungua
4) Mambo yanayoleta usambazaji duni wa
vyandarua vyenye dawa katika udhibiti wa
malaria Wilaya ya Mvomero (Timu Mvomero)
- Mipango: Uhamasishaji wa Sekta Binafsi kuuza
vyandarua vyenye dawa
5) Uchunguzi wa i sababu zinazolleta mlipuko wa
magonjwa ya kuhara miongoni mwa familia katika
Tarafa 3 Wilaya ya Kilosa (Timu Kilosa)
- Mipango: Uhamasishaji wa jamii kuhusu udhibiti wa
kipindupindu
6) Kuchunguza utendaji wa Mipango ya Afya
katika kudhibiti milipuko ya kipindupindu Tarafa
ya Ifakara Wilaya ya Kilombero (Timu Kilombero)
- Mipango: Kutoa mafunzo ya “Participatory Hygiene
and Sanitation Transformation (PHAST)” kwa jamii
na wasaidizi wa afya
7) Uchunguzi wa mambo yanayoleta uwingi wa
kuugua na vifo kwa watoto chini ya miaka 5 katika
Tarafa ya Mwaya, Wilaya ya Ulanga (Timu
Ulanga) - Mipango: Mafunzo juu ya “Intergrated
Management of Childhood Illness (IMCI)” kwa Jamii
Hapo Novemba 2004 “MHP” ilianzisha Kundi la
Kazi (“Working Group - WG”), lililoundwa kutokana
na mjumbe mkutanishi (contact person) kutoka kila
Timu ya Afya ya Uendeshaji ya Wilaya na ya Mkoa.
Kwa njia ya majadiliano ya kina mara kwa mara
katika mikutano ya “WG” wajumbe wamejijengea
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
11
uelewano (“rapport”) miongoni mwao na kukubali
mapendekezo na ukosoaji wa kujenga kutoka kwa
watu wengine kwa nia ya kuboresha usahihi wa utafiti.
Kutokana na hali hiyo wajumbe wanaboresha ujuzi
wao wa mawasiliano na wa kufanya kazi kama timu,
ambao moja kwa moja unatumiwa na kila Timu ya
Afya ya Uendeshaji anapotoka mjumbe wa “WG”.
Wajumbe wa “WG” ndio chombo muhimu cha
kuchochea uendeshaji wa utafiti.
Kwa kifupi, uendeshaji wa “OPR” umejenga,
miongoni mwa mameneja wa afya, hali ya “kujiamini”,
ambayo ni muhimu katika kufanikisha kukabiliana na
changamoto ya kazi yao ya uendeshaji kwa kutumia
ujuzi unaotakiwa. Mwisho Tunaweza kuhitimisha kwa
kusema kuwa uendeshaji wa “OPR” ni miongoni mwa
njia zinazofaa kuimarisha uwezo wa uendeshaji wa
mameneja wa afya mkoani na wilayani katika
mchakato wa kuipelekea jamii madaraka utokanao na
Mabadiliko ya Jumla Katika Sekta ya Jamii (PSR),
Tanzania.
Kutokana na umuhimu wa kufahamishana matokeo
ya utafiti miongoni mwa mamlaka mbalimbali ngazi
husika ili kuufaidi vizuri utafiti, Timu za Afya za
Uendeshaji Mkoa na Wilaya zimeamua, kwa
kushirikiana na wadau, kupanga shughuli za kueneza
taarifa za matokeo ya utafiti kwa kutumia njia
zinazofaa kikamilifu katika kila wilaya husika. Kundi
la Kazi la Utafiti (OPR WG) linatambua kuwa Jarida
la Afya Morogoro ni mojawapo ya njia zinazofaa
kikamilifu kueneza taarifa na linashukuru kupewa
nafasi katika jarida hili kwa shughuli za utafiti.
Shukrani zinatolewa kwa wafuatao. Timu za Afya
za Uendeshaji Mkoa na Wilaya kwa kujitolea kwao,
mamlaka za Utawala ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa
msaada na ushirikiano wakati wote wa zoezi la utafiti,
kwa wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele na
jamii katika wilaya zote kwa ushirikiano wakati wa
ukusanyaji takwimu.
Inaamainiwa kuwa mameneja wa afya Mkoa wa
Morogoro wataendelea kustawisha uwezo wao wa
uendeshaji kwa kuendeleza utekelezaji wa “OPR”
ambao utaleta matokeo mazuri kwa njia mbalimbali
kadiri inavyowezekana, ili kufanikisha kikweli
huduma bora zaidi na hivyo kuleta hali ya afya bora
zaidi kwa watu wa Mkoa wa Morogoro na kwa
Watanzania kwa ujumla.
Bi. E. Fukushi
Mtaalamu Mshauri na Kundi la Kazi La Utafiti
Mradi wa Afya Morogoro
MATUKIO MUHIMU : Agosti - Desemba 2005 AGOSTI 1 - 5, 2005 Mkutano wa Waganga Wakuu wa Mkoa
Kauli mbiu: “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza: changamoto ya Watanzania” Mahali: Mtwara
AGOSTI 8, 2005 Nane Nane (Siku ya Wakulima)
Kauli mbiu: “Kilimo bora ni nyenzo muhimhu ya kuondoa aina zote za umaskini”
Mahali: Mbeya (Kitaifa) na Morogoro (Kikanda)
OKTOBA 2 - 23, 2005 Tathmini ya Mwisho ya Mradi wa Afya Morogoro (“MHP”) Taarifa ilionyesha mafanikio mazuri; Mradi umeongezewa kipindi cha mwaka mmoja hadi 2007 Machi
OKTOBA 14, 2005 Siku ya Nyerere NOVEMBA 18, 2005 Ufunguzi wa Maktaba ya Afya Kilosa DESEMBA 1, 2005 Siku ya UKIMWI Duniani Kauli mbiu: “Tokomeza UKIMWI: timiza ahadi” Mahali: Songea, Ruvuma
DESEMBA 9, 2005 Siku ya Uhuru DESEMBA 14, 2005 Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jarida La Afya Morogoro – Na.5
12
VICHEKESHO Umuhimu wa Usalama wa Chakula kwa Jamii Mtungaji/Mchoraji : Bw. N. Masaoe & Bw. J. Bundu
Makala au barua za maoni zitumwe kwa anuani zifuatazo:-
Mhariri, Jarida la Afya Morogoro S.L.P. 110, MOROGORO au, S.L.P. 1193, MOROGORO FAX 023 - 2614148
Au
Yapelekwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya husika:-
S.L.P. 166, Morogoro Manispaa S.L.P. 1862, Morogoro S.L.P. 14, Kilosa S.L.P. 47, Ifakara, Kilombero S.L.P. 4, Mahenge, Ulanga
• Tunawaomba wasomaji wetu watoe maoni yao kuhusu jina litakalofaa kuitwajarida hili.
• Aidha tunaomba wasomaji wetu watume makala za kuchapisha kwenye toleo la Julai 2006: zenye maneno yasiyozidi 400, zinazohusiana na afya ama maonikuhusu huduma za afya zinazotolewa katika mkoa wa Morogoro.
LIMECHAPISHWA NA BODI YA UHARIRI JARIDA LA AFYA MOROGORO
S.L.P. 110, MOROGORO
M H P
Morogoro Health Project
Chakula ni cha leoleo tena cha moto.
Mbona unapenda kula chakula kwa mamantilie, pesa yako ndogo nini? Hapo ndiyo tatizo …
Unakula kila kitu.
Je usafi wake vipi?