mchungaji afanyaye watu kuwa wanafunzi - davidservant.com filehekaya za kisasa kuhusu vita ya kiroho...

34
www.shepherdserve.org Unaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza haya kwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukata chochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Haki zote zimehifadhiwa 2006 David Servant Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi David Servant Sura Ya Thelathini Na Moja Hekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa sana, lakini ya makosa, kuhusu Shetani na vita ya kiroho. Hatimaye tutatazama kinachosemwa na Maandiko kuhusu vita ya kiroho inayotakiwa kutendwa na kila mwamini. Hekaya Ya Tano: “Tunaweza Kuangusha Ngome Za Mapepo Katika Anga Kwa Vita Ya Kiroho.” Kulingana na Maandiko, hakuna shaka kwamba Shetani anatawala juu ya majeshi ya pepo wabaya ambao wanakaa katika anga la dunia, na wanaomsaidia kutawala ufalme wa giza. Biblia pia inaonyesha kwamba katika hao pepo, wapo wenye kutawala eneo fulani kijiografia (ona Danieli 10:13, 20, 21; Marko 5:9, 10). Maandiko pia yanaonyesha kwamba Wakristo wana mamlaka ya kutoa pepo katika watu wengine, na wana wajibu wa kumpinga Shetani (ona Marko 16:17; Yakobo 4:7; 1Petro 5:8, 9). Lakini je, Wakristo wanaweza kuangusha mapepo walioko juu ya miji? Jibu ni kwamba, hawawezi, na kujaribu kufanya hivyo ni kupoteza muda wao. Kwa kuwa tunaweza kutoa pepo katika watu si sababu ya kudhani kwamba tunaweza kuangusha pepo wanaotawala juu ya miji yetu. Ipo mifano mingi sana ya watu kutolewa pepo katika Injili na kitabu cha Matendo, lakini, unaweza kukumbuka mfano hata mmoja wa mtu kuangusha pepo aliyekuwa anatawala mji au eneo la kijiografia katika Injili au Matendo ya Mitume? Huwezi kwa sababu mifano hiyo haipo. Je, unakumbuka fundisho au ushauri hata mmoja katika nyaraka, kuhusu wajibu wetu kuangusha mapepo wabaya kutoka angani? Hakuna. Basi, hatuna msingi wa KiBiblia kuamini kwamba tunaweza au tunapaswa kupambana katika “vita ya kiroho” dhidi ya mapepo wabaya katika anga. Kulazimisha Mifano Izidi Maana Yake Mara nyingi Wakristo hufanya kosa la kupata maana nyingine zaidi ya iliyokusudiwa na Mungu katika vifungu vya Maandiko vinavyotumia lugha ya mfano. Mfano mzuri ni jinsi wengi wanavyoelewa vibaya maneno ya Paulo kuhusu “kuangusha ngome” yafuatayo. Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili. (Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangushya ngome;) tukiangusha mawazo na kila

Upload: others

Post on 08-Sep-2019

38 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

www.shepherdserve.orgUnaruhusiwa kuchapa, kunakili, kugawa au kusambaza hayakwa njia yoyote ile, mradi tu usibadili chochote wala kukatachochote. Vile vile hairuhusiwi kuuza maelezo haya. © Hakizote zimehifadhiwa 2006 David Servant

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa WanafunziDavid Servant

Sura Ya Thelathini Na MojaHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2

Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa sana,lakini ya makosa, kuhusu Shetani na vita ya kiroho. Hatimaye tutatazamakinachosemwa na Maandiko kuhusu vita ya kiroho inayotakiwa kutendwa na kilamwamini.

Hekaya Ya Tano: “Tunaweza Kuangusha Ngome Za Mapepo Katika Anga KwaVita Ya Kiroho.”

Kulingana na Maandiko, hakuna shaka kwamba Shetani anatawala juu ya majeshi yapepo wabaya ambao wanakaa katika anga la dunia, na wanaomsaidia kutawala ufalme wagiza. Biblia pia inaonyesha kwamba katika hao pepo, wapo wenye kutawala eneo fulanikijiografia (ona Danieli 10:13, 20, 21; Marko 5:9, 10). Maandiko pia yanaonyeshakwamba Wakristo wana mamlaka ya kutoa pepo katika watu wengine, na wana wajibuwa kumpinga Shetani (ona Marko 16:17; Yakobo 4:7; 1Petro 5:8, 9). Lakini je, Wakristowanaweza kuangusha mapepo walioko juu ya miji? Jibu ni kwamba, hawawezi, nakujaribu kufanya hivyo ni kupoteza muda wao.

Kwa kuwa tunaweza kutoa pepo katika watu si sababu ya kudhani kwamba tunawezakuangusha pepo wanaotawala juu ya miji yetu. Ipo mifano mingi sana ya watu kutolewapepo katika Injili na kitabu cha Matendo, lakini, unaweza kukumbuka mfano hata mmojawa mtu kuangusha pepo aliyekuwa anatawala mji au eneo la kijiografia katika Injili auMatendo ya Mitume? Huwezi kwa sababu mifano hiyo haipo. Je, unakumbuka fundishoau ushauri hata mmoja katika nyaraka, kuhusu wajibu wetu kuangusha mapepo wabayakutoka angani? Hakuna. Basi, hatuna msingi wa KiBiblia kuamini kwamba tunaweza autunapaswa kupambana katika “vita ya kiroho” dhidi ya mapepo wabaya katika anga.

Kulazimisha Mifano Izidi Maana Yake

Mara nyingi Wakristo hufanya kosa la kupata maana nyingine zaidi ya iliyokusudiwana Mungu katika vifungu vya Maandiko vinavyotumia lugha ya mfano. Mfano mzuri nijinsi wengi wanavyoelewa vibaya maneno ya Paulo kuhusu “kuangusha ngome”yafuatayo.

Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili. (Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezokatika Mungu hata kuangushya ngome;) tukiangusha mawazo na kila

Page 2: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukitekanyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatilizamaasi yote, kutii kwenu kutakapotimia (2 Wakor. 10:3-6).

Kutokana na maneno hayo – “kuangusha ngome” – ambayo ni lugha ya mfano,fundisho zima limejengwa ili kutetea wazo la kufanya “vita ya kiroho” kwa ajili ya“kuangusha ngome” za mapepo katika anga. Lakini ni vizuri tuelewe kwamba Paulo hapohasemi juu ya mapepo katika anga, bali ngome za imani za uongo ambazo zimo katikamawazo na akili za watu. Paulo anaharibu fikra, si mapepo wabaya katika ulimwengu waroho!

Hili linakuwa wazi zaidi tunaposoma maandiko hayo kulingana na mantiki yake.Paulo alisema hivi: “tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu yaelimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo” (maneno mepesiyameongezwa ili kukazia). Vita ambayo Paulo anaizungumzia kwa lugha ya mfano nivita dhidi ya mawazo au fikra ambazo ziko kinyume na maarifa ya kweli ya Mungu.

Kwa kutumia mifano ya kijeshi, Paulo anaeleza kwamba tuko vitani, vita ili kupatamawazo ya watu walioamini kweli za Shetani. Silaha yetu kubwa katika vita hii niukweli, na ndiyo sababu tumeagizwa kwenda duniani kote na kuhubiri Injili, tukivamiaeneo la adui kwa ujumbe unaoweza kuwaweka mateka huru. Ngome tunazoharibuzimejengwa kwa matofali ya uongo, na kuunganishwa na sementi ya udanganyifu.

Silaha Kamili Za Mungu

Fungu lingine katika maandiko ya Paulo linalotafsiriwa vibaya mara kw amara niWaefeso 6:10-17, mahali ambapo aliandika juu ya wajibu wetu kuvaa silaha kamili zaMungu. Ingawa fungu hili linahusu mapambano ya Mkristo dhidi ya Shetani na mapepowabaya, hakuna popote panaposema kuhusu kuangusha mapepo wanaotawala miji.Tunapojifunza fungu hilo vizuri sana, inakuwa wazi kwamba Paulo alikuwa anaandikakuhusu wajibu wa kila aaminiye binafsi kupingana na mipango ya Shetani katika maishayake mwenyewe, kwa kutumia ukweli wa Neno la Mungu.

Tunaposoma fungu hilo, ona pia kwamba kuna lugha ya mifano. Ni wazi kwambaPaulo hakuwa anazungumza juu ya silaha halisi zinazoshikika ambazo Wakristowanapaswa kuvaa kwenye miili yao. Badala yake, anazungumza juu ya silaha kwa lughaya mfano. Kila sehemu moja ya silaha inayotajwa ni mfano wa kweli mbalimbali zakiroho ambazo Wakristo wanapaswa kutumia kwa ajili ya ulinzi dhidi ya Shetani na pepowabaya. Kwa kujua, kuamini na kutenda Neno la Mungu, Wakristo, kwa lugha ya mfano,wanakuwa wamevaa silaha za Mungu zinazowalinda.

Basi, tutazame fungu hilo katika Waefeso mstari kwa mstari, huku tukijiuliza hivi: Je,Paulo alikuwa anajaribu kutuambia nini hasa?

Asili Ya Nguvu Zetu Kiroho

Kwanza: Tunaambiwa tuwe “hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake”(Waefeso 6:10). Mkazo ni kwamba tusipate nguvu zetu kutoka kwetu wenyewe, balikutoka kwa Mungu. Hili linatokea zaidi katika tamko la pili, kwamba, “Vaeni silaha zoteza Mungu” (Waefeso 6:11a). Hizo ni silaha za Mungu, si zetu. Paulo hasemi kwambaMungu naye huvaa silaha, bali kwamba tunahitaji silaha ambazo Mungu ameandaa kwaajili yetu.

Mbona tunahitaji silaha ambazo Mungu ametupa? Jibu ni hili: “Mpate kuzipinga hilaza Shetani” (Waefeso 6:11b). Silaha hizi ni kwa ajili ya kujilinda, si za kushambulia.

Page 3: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Kusudi lake si kutufanya tutoke na kuangusha mapepo wabaya juu ya miji. Ni ili tuwezekuzipinga hila za Shetani.

Tunajifunza kwamba Shetani ana mipango miovu ya kutushambulia, na kamahatutakuwa tumevaa silaha ambazo Mungu anatoa, tutawezwa. Vile vile, ona kwamba niwajibu wetu kuvaa silaha hizo, si wa Mungu.

Tuendelee.

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu yafalme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepowabaya katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:12).

Hapa mambo yanakuwa wazi kabisa kwamba Paulo hasemi juu ya vita ya kimwili,dhidi ya vitu vinavyoweza kuonekana na kushikika, bali ya kiroho. Tunapambana dhidiya mbinu na mipango ya pepo waovu wa ngazi mbalimbali, kama zinavyotajwa na Paulo.Wasomaji wengi hudhani kwamba Paulo aliorodhesha hao pepo kulingana na udogo waohadi ukubwa wao, “falme na mamlaka” wakiwa ndiyo cheo cha chini, na “majeshi yapepo wabaya katika ulimwengu wa roho” wakiwa ndiyo wa cheo cha juu kabisa.

Swali: Tunawezaje kupambana na viumbe wa kiroho? Tunaweza kulijibu hivi:Viumbe wa kiroho wanawezaje kutushambulia? Rahisi kabisa! Wanatushambulia kwamajaribu, mawazo, mapendekezo na fikra zenye kupingana na na Neno la Mungu namapenzi ya Mungu. Basi, silaha yetu au ulinzi wetu ni kulijua, kuliamini na kulitii Nenola Mungu.

Kwa sababu hiyo, twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuwezakushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama(Waefeso 6:13).

Hapa tena, ona kwamba kusudi la Paulo ni kutuwezesha sisi kupingana na kusimamadhidi ya mashambulizi ya Shetani. Kusudi lake si kutuwezesha tutoke na kwendakumshambulia Shetani na kuangusha pepo kutoka angani. Katika fungu hili, Pauloanatuambia tusimame imara mara tatu. Nafasi yetu sisi ni kujitetea, si kupambana.

Silaha Yetu Kubwa – Ukweli

Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni (Waefeso 6:14a).

Kinachoshikilia silaha zetu ni hiki: ukweli. Kweli ni kitu gani? Yesu alimwambiaBaba Yake hivi: “Neno lako ni kweli (Yohana 17:17). Hatuwezi kufanikiwa kusimamadhidi ya Shetani mpaka tujue ukweli ambao tunaweza kuutumia kukabiliana na uongowake. Yesu alionyesha jambo hilo vizuri kabisa wakati alipojaribiwa huko nyikani.Alijibu kila wazo la Shetani hivi: “Imeandikwa.”

Paulo anaendelea hivi:

Na kuvaa dirii ya haki kifuani (Waefeso 6:14b).

Tunapaswa kujua kuhusu aina mbili za haki, kama Wakristo. Kwanza: Tumepewahaki ya Kristo kama zawadi (ona 2Wakor. 5:21). Wale wanaomwamini Yesuwamehesabiwa haki Yake, Yeye aliyechukua dhambi zao msalabani. Msimamo huo wakuwa na haki umetukomboa kutoka utawala na kifungo cha Shetani.

Page 4: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Pili: Tunapaswa kuishi katika haki, tukitii amri za Yesu. Pengine hicho ndicho Pauloanalenga anaposema juu ya dirii ya haki. Kwa kumtii Kristo, hatumpi Shetani nafasi yaaina yoyote (ona Waefeso 4:26, 27).

Msimamo Thabiti Katika Viatu Vya Injili

Na kufungiwa miguu utayari tuupatao kwa Injili ya amani(Waefeso 6:15).

Kujua, kuamini na kutendea kazi kweli ya Injili hutupa sisi msimamo thabiti dhidi yamashambulizi ya Shetani. Viatu vilivyovaliwa na askari wa Kirumi vilikuwa na vyumaupande wa chini, vilivyowafanya wasimame imara katika uwanja wa mapambano. Yesuanapokuwa Bwana wetu, tunao msimamo thabiti dhidi ya uongo wa Shetani.

Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtawezakuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu (Waefeso 6:16).

Hapa tena, ona mkazo wa Paulo: Ni sisi kujilinda. Hazungumzi juu ya kuangushamapepo walioko juu ya miji. Anasema kuhusu kutumia imani yetu katika Neno la Munguili kupingana na uongo wa Shetani. Tunapoamini na kufanyia kazi kile ambacho Munguamesema, inakuwa sawa na kuwa na ngao yenye kutulinda na uongo wa Shetani, ambaokimfano unawakilishwa na “mishale yote yenye moto, ya yule mwovu.”

Neno La Mungu – Upanga Wetu Wa Roho

Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao nineno la Mungu (Waefeso 6:17).

Biblia inasema kuhusu wokovu kwamba ni pamoja na ukombozi wetu kutoka utumwawa Shetani. Mungu “ametukomboa kutoka ufalme wa giza, na kutuhamisha kutuingizakatika ufalme wa Mwana wa pendo Lake (Wakolosai 1:13). Kujua hilo ni sawa na kuwana kofia yenye kulinda akili zetu zisiamini uongo wa Shetani kwamba bado tuko chini yautawala wake. Shetani si bwana wetu tena – Yesu ndiye Bwana wetu.

Tena, tunapaswa kuchukua “upanga wa Roho” ambao, kulingana na maelezo yaPaulo, ni mfano wa Neno la Mungu. Kama tulivyokwisha ona, Yesu ndiye mfano borawa askari wa kiroho ambaye alitumia kwa ustadi mkubwa upanga Wake wa kiroho.Wakati wa kujaribiwa Kwake huko nyikani, kila mara alimjibu Shetani kwa kumtajiaNeno la Mungu moja kwa moja. Vivyo hivyo na sisi, kama tunataka kumshinda Shetanikatika mapambano ya kiroho, tunapaswa kujua na kuamini kile ambacho Mungu kasema,tusije tukadanganyika na uongo wa Shetani.

Ona pia kwamba Yesu alitumia “upanga wa Roho” katika kujilinda. Kuna wanaopendakuonyesha kwamba, sisi tunaodai kwamba silaha zinazotajwa na Paulo ni za kujilinda,lakini upanga ni silaha ya kushambulia. Basi, wanajaribu kujenga hoja na dhana – japodhaifu – kwamba, fungu hili katika Waefeso 6:10-12 linafaa kutumiwa kutuonyeshawajibu wetu wa kushambulia na “kuangusha ngome” za pepo wabaya katika ulimwenguwa roho.

Ni wazi kwamba kutokana na kusoma sababu ya Paulo mwenyewe kwa nini Wakristowavae silaha za Mungu (ili wapate “kuzishinda hila za Shetani”), tunajua hapoanazungumzia matumizi ya kujilinda ya silaha hizo. Tena, japo upanga unaweza

Page 5: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

kudhaniwa kuwa silaha ya kushambulia, unaweza vile vile kutumika kama silaha yakujilinda, maana unaweza kutumika kuzuia na kulinda shambulizi la upanga wa adui.

Tena, inabidi tuwe makini sana tusiharibu maana ya mfano mzima, katika juhudi zetuza kutafuta maana ya kila sehemu ya hiyo silaha, ambayo hata haipo wakati mwingine.Tukianza kubishana kuhusu kazi ya upanga, kwamba ni ya kujilinda au kushambulia,“tunakwenda mbali” kuliko maana ya mfano wenyewe, katika kukata-kata mfano rahisitu ambao haukukusudiwa kugawanywa vipande vipande kiasi hicho.

Je, Yesu Hakutuagiza “Kumfunga Mwenye Nguvu”?

Katika Injili, tunasoma mara tatu Yesu akitaja kuhusu “kumfunga mwenye nguvu.”Lakini, hakuwaambia wanafunzi Wake kwamba “kumfunga mwenye nguvu” ni kituwanachotakiwa kufanya. Hebu tutazame maneno halisi ya Yesu katika mantiki yake.

Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, AnaBeelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo. Akawaita,akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani? Naufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezikusimama; na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyohaiwezi kusimama. Na kama Shetani ameondoka juu ya nafsi yake,akafitinika, hawezi kusimama, bali huwa na kikomo. Hawezi mtukuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vituvyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipoatakapoiteka nyumba yake. Amin, nawaambia, Dhambi zotewatasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hatamilele; ila atakuwa ana dhambi ya milele, kwa vile walivyosema,Ana pepo mchafu (Marko 3:23-30. Maneno mepesi kukazia).

Ona hapo kwamba Yesu hakuwa anawafundisha wafuasi Wake jinsi ya kufungawenye nguvu. Alikuwa anajibu lawama za waandishi wa Yerusalemu kwa hoja nzito namfano dhahiri kabisa.

Wao walimshtaki kwa kutoa pepo akitumia nguvu za kipepo. Akawajibu kwa kusemakwamba Shetani angekuwa kichaa kujipinga. Hakuna mtu awezaje kujibu hoja hiyo kwanamna yoyote!

Sasa – Kama Yesu hakutumia nguvu za Shetani kutoa pepo, alikuwa anatumia nguvuza nani? Lazima ilikuwa nguvu kuliko ya Shetani. Ilibidi iwe nguvu ya Mungu, nguvu yaRoho Mtakatifu. Basi, Yesu akazungumza kimfano kuhusu Shetani, akimlinganisha namtu mwenye nguvu anayelinda vitu vyake. Anayeweza kuchukua mali za huyo mwenyenguvu lazima awe mwenye nguvu kuliko yeye – ambaye ni Yesu Mwenyewe. Hayondiyo maelezo ya kweli kuhusu jinsi alivyotoa pepo.

Hili fungu lenye kumtaja mtu mwenye nguvu, pamoja na yale mengineyanayopatikana katika Mathayo na Luka, hayawezi kutumiwa kuruhusu “kufungwa kwawenye nguvu katika miji”. Tena, tunapotazama Agano Jipya lote, hatupati mifano yoyoteya mtu awaye yote akifanya kazi ya “kuwafunga wenye nguvu” katika miji, wala hatuonimaelekezo yoyote kwa mtu yeyote kufanya hivyo. Basi, kwa usalama kabisa tunasema,kujaribu kufunga na kukosesha nguvu “pepo mwenye nguvu” katika eneo lolotekijiografia au mji, si kitu kinachoruhusiwa kwa Mkristo KiBiblia.

Page 6: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Vipi Kuhusu “Kufunga Duniani Na Mbinguni”?

Tunasoma mara mbili katika Injili, maneno ya Yesu yafuatayo: “Lolotemtakalolifunga duniani litafungwa mbinguni, na lolote mtakalofungua duniani litakuwalimefunguliwa na mbinguni.” Maneno hayo yameandikwa katika Injili ya Mathayo, marazote mbili.

Je, Yesu alikuwa anatufundisha kwamba tunaweza, na tunapaswa “kufunga” mapepoyaliyoko angani?

Kwanza – Tutafakari maneno kufunga na kufungua. Yesu anapotumia maneno hayo nikwa lugha ya mfano, maana hakumaanisha kwamba wafuasi Wake wachukue kamba aunyuzi na kufunga chochote au kufungua chochote kilichofungwa na kamba au nyuzi zakimwili. Basi, alimaanisha nini?

Ili tupate jibu, tunapaswa kutazama matumizi Yake ya maneno kufunga na kufunguakatika mantiki husika wakati aliposema maneno yenyewe. Je, alikuwa anazungumziaswala la pepo wachafu? Kama ndivyo, tunaweza kusema maneno Yake kuhusu kufungayanahusiana na kuwafunga pepo wachafu.

Basi, tutazame fungu la kwanza, ambapo Yesu alitaja kuhusu kufunga na kufungua.

[Yesu] Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? SimoniPetro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliyehai. Yesu akajibu akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-Yona; kwakuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliyembinguni. Nami nakwambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwambahuu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na loloteutakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na loloteutakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni (Mathayo16:15-19. Maneno mepesi kukazia).

Sababu ya fungu hili kufasiriwa kwa njia nyingi sana ni kutokana na kuwa na ainatano za mifano, kama ifuatavyo: (1) “damu na nyama”, (2) “mwamba”, (3) “milango yakuzimu”, (4) “funguo za ufalme wa mbinguni,” na (5) “kufunga na kufungua.” Yote hayoni maneno ya mfano, yanayozungumza kuhusu kitu kingine.

Milango Ya Kuzimu

Pamoja na maana hasa ya mifano hiyo, unaweza kuona kwamba katika fungu hili,Yesu hakutaja pepo waovu. Kitu alichosema ni “milango ya kuzimu,” ambayo ni lughaya mfano tu, maana hakuna chochote kinachoweza kufanywa na milango halisi yakuzimu ili kulizuia kanisa.

Je, “milango ya kuzimu” maana yake nini? Pengine inawakilisha nguvu za Shetani, naYesu alimaanisha kwamba nguvu za Shetani zisingezuia kanisa Lake kujengwa. Aupengine alimaanisha kwamba kanisa ambalo angejenga, lingewaokoa watu kutokana namaisha ya kufungiwa na milango ya kuzimu.

Ona kwamba Yesu alitaja milango ya aina mbili – milango ya kuzimu na milango yambinguni – anapomwambia Petro kwamba atampa “funguo za mbinguni.” Mlinganishohuo unaunga mkono hoja kwamba maneno ya Yesu juu ya milango ya kuzimu ni mfanowa kazi ya kanisa kuwaokoa watu wasiende kuzimu.

Hata kama Yesu alimaanisha kwamba “nguvu zote za Shetani zisingezuia kanisaLake,” hatuwezi kuamua kwamba maneno aliyosema juu ya kufunga na kufungua ni

Page 7: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

maagizo Yake kuhusu tunachopaswa kufanya na pepo wabaya walio juu ya miji. Hii nikwa sababu hatupati mifano yoyote katika Injili au Matendo, ya mtu yeyote akifungapepo waovu juu ya miji, wala hatupati maagizo ya aina hiyo katika nyaraka. Vyovyotetutakavyotafsiri maneno ya Kristo juu ya kufunga na kufungua, tafsiri yetu lazimaikubaliane na sehemu zingine za Agano Jipya.

Kwa kuwa hakuna mfano wowote kimaandiko kuhusu jambo hilo, inashangaza jinsiambavyo mara nyingi Wakristo wanasema, “Ninamfunga Shetani katika jina la Yesu,” au“Ninafungua malaika wawe juu ya mtu huyo” na kadhalika. Humkuti mtu yeyoteakisema hivyo mahali popote katika Agano Jipya. Mkazo katika Matendo na nyaraka sikuzungumza na Shetani au kufunga na kufungua pepo waovu, bali mkazo ni kuhubiriInjili na kumwomba Mungu. Kwa mfano: Wakati Paulo alipokuwa anateswa mara zotena mjumbe (au malaika) wa Shetani, hakujaribu “kumfunga”. Alimwomba Mungukuhusu jambo hilo (ona 2Wakor. 12:7-10).

Funguo Za Mbinguni

Hebu tutazame zaidi mantiki husika ya maneno ya Yesu juu ya kufunga na kufungua.Ona kwamba, kabla ya kutaja kufunga na kufungua, Yesu alisema angempa Petro“funguo za ufalme wa mbinguni.” Petro hakupewa funguo yoyote halisi ya lango lambinguni, hivyo, maneno ya Yesu lazima yawe ya mfano. Je, “funguo” zinawakilishanini? Funguo zinawakilisha njia ya kufikia kitu ambacho kimefungwa. Mtu mwenyefunguo ana jinsi au njia ya kufungua milango fulani, ambayo wasiokuwa na funguohawana.

Sasa – tunapotazama huduma ya Petro kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo,ni kitu gani tunachomwona akifanya, kinachoweza kuhesabika kuwa ni kufunguamilango ambayo imefungwa kwa wengine?

Kimsingi, tunamwona akitangza Injili – ile yenye kufungua milango ya mbinguni kwawote watakaoamini (ambayo pia hufunga milango ya kuzimu). Kwa hali hiyo, sisi sotetumepewa funguo za ufalme wa mbinguni, maana sote ni mabalizi wa Kristo. Basi,funguo za ufalme wa mbinguni ni Injili tu ya Yesu Kristo, ambayo ni ujumbe unaowezakufungua malango ya kuingia mbinguni.

Kufunga Na Kufungua

Mwisho – baada ya kuahidi kumpa Petro funguo za ufalme wa mbinguni, Yesu alitoatamko Lake kuhusu kufunga na kufungua – la tano katika fungu tunalotazama sasa.

Kulingana na mantiki ya matamko tuliyokwisha tazama, Yesu alimaanisha nini?Kufunga na kufungua kwa Petro kunahusikaje na Yesu kulijenga Kanisa Lake –kuwaokoa watu kutoka Kuzimu, na kutangaza Injili?

Uwezekano ni mmoja tu kwa kweli. Maana ya Yesu ilikuwa hii: “Ninakuruhusu wewekuwa mwakilishi wa mbinguni. Timiza wajibu wako duniani, na mbingu itakuungamkono.”

Kama mwajiri atamwambia mfanya kazi wake muuzaji hivi: “Chochote utakachofanyaArusha kitakuwa kimefanyika ofisi kuu”, anapaswa kuelewaje maneno ya mkuu wake?Bila shaka angechukulia kwamba ameruhusiwa kuwakilisha kampuni yake huko Arusha.Maana ya Yesu ni kwamba, Petro alikuwa ameruhusiwa kumwakilisha Mungu wambinguni hapa duniani. Ahadi hiyo kwa Petro ingetia nguvu imani yake, wakati wakuanza kutangaza ujumbe wa Mungu huko Yerusalemu, mbele ya macho makali yawaandishi na Mafarisayo – watu ambao walidhani wao ndiyo wawakilishi walioruhusiwana Mungu, na watu ambao zamani Petro aliwaheshimu hivyo.

Page 8: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Hii tafsiri ya maneno ya Yesu inakubaliana vizuri na sehemu ya pili ya tamko Lake,inayopatikana sura mbili baada ya hii, katika Injili ya Mathayo.

Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeyepeke yenu; akikusiia, umempata nduguyo. La kama hasikii, chukuapamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vyamashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Naasipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia,na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. Aminnawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwayamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua dunianiyatakuwa yamefunguliwa mbinguni. Tena nawaambia ya kwamba,wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolotewatakaoliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwakuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, naminipo papo hapo katikati yao (Mathayo 18:15-20. Maneno mepesikukazia).

Katika fungu hili la pili lenye kutaja kufunga na kufungua, hakuna chochote katikamantiki chenye kutusababisha tuamini kwamba Yesu alikuwa anazungumzia kufungapepo wabaya. Hapa, Kristo alitaja juu ya kufunga na kufungua moja kwa moja baada yakusema swala la nidhamu kanisani.

Hii inaonyesha kwamba, kwa habari ya kufunga na kufungua katika fungu hii, Yesualimaanisha hivi: “Ninakuwa wewe wajibu wa kuamua nani awe kanisani, na nani asiwe.Ni kazi yako. Utakapotimiza wajibu wako, mbingu itakuunga mkono.”

Kwa maana pana zaidi ni kwamba, Yesu alikuwa anasema hivi: “Mmeruhusiwa kuwawawakilishi wa mbinguni duniani. Mna wajibu, na mtakapokuwa mnazitimiza duniani,mbinguni mtaungwa mkono kila mara.”

Mantiki Ya Kufunga Na Kufungua

Tafsiri hii inakubaliana na mantiki iliyopita na mantiki kubwa ya Agano Jipya kwaujumla.

Kwa habari ya mantiki iliyoko, tunaona kwamba mara tu baada ya tamko Lake kuhusukufunga na kufungua, Yesu alisema hivi: “Tena nawaambia ya kwamba, wawili wenuwatakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Babayangu aliye mbinguni” (Mathayo 18:19. Maneno mepesi kukazia).

Hapo tena ile mada ya “mtakachofanya duniani kitaungwa mkono mbinguni”inaonekana. Sisi hapa duniani tumeruhusiwa na tuna wajibu wa kuomba. Tunapofanyahivyo, mbingu itajibu. Maneno ya Yesu, “Tena nawaambia …” yanaonyesha kwamba nikama anatoa ufafanuzi zaidi kuhusu tamko Lake la kwanza juu ya kufunga na kufungua.

Tamko la mwisho la Yesu katika fungu hili – “Kwa kuwa walipo wawili watatuwamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” – linaunga mkono piaile mada ya “mbinguni mtaungwa mkono”. Waamini wanapokusanyika katika jina Lake,Yeye akaaye mbinguni hutokea.

Hata kama hukubaliani kabisa na tafsiri yangu ya fungu tunalotazama, utapata kazikubwa kutoa hoja inayoungwa mkono na Maandiko kwamba Yesu alikuwaanazungumzia juu ya kuwafunga pepo wachafu wanaotawala na kuwa juu ya miji!

Page 9: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Mpango Wa Mungu Unamhusisha Shetani

Shetani na malaika zake ni jeshi lililoasi, lakini haimaanishi haliko chini ya mamlakaya Mungu. Liliumbwa na Mungu, (japo hawakuwa waasi walipoumbwa mara yakwanza). Paulo aliandika hivi:

Kwa kuwa katika Yeye [Kristo] vitu vyote viliumbwa, vilivyombinguni na viliyvo juu ya nchi, vinavyoonekana navisivyoonekana – ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, aumamlaka – vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake(Wakolosai 1:16. Maneno mepesi kukazia).

Yesu aliumba kila roho ya kimalaika ya kila ngazi, na Shetani pia. Je, alijua kwambawengine wangeasi? Bila shaka. Basi, mbona akawaumba? Kwa sababu, angetumia hizoroho zilizoasi kusaidia kutimiza mpango Wake. Kama hakuwa na mpango wowote kwaajili yao, angewafunga tu, kama tunavyoambiwa kwamba tayari amefanya hivyo nawengine (ona 2Petro 2:4), na kama atakavyofanya hivyo na Shetani siku moja (onaUfunuo 20:2).

Mungu ana sababu za kumwacha Shetani na pepo wote wabaya kufanya kazi duniani.Angekuwa hana, wasingefanya kitu. Je, sababu za Mungu kumruhusu Shetani kufanyakazi duniani ni zipi? Sidhani kama kuna yeyote anaye-elewa sababu zote, lakini Munguamefunua baadhi yake katika Neno Lake.

Kwanza – Mungu anamruhusu Shetani kufanya kazi kwa mipaka duniani ili kutimizampango Wake wa kuwapima binadamu. Shetani anakuwa chaguo lingine kwawanadamu. Watambue wasitambue, binadamu ni watumishi, aidha wa Mungu au waShetani. Sasa, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Adamu na Hawa – watu wawiliwaliokuwa na hiari ya kuamua ambayo walipewa na Mungu – ili kuwajaribu. Wotewenye hiari lazima wajaribiwe ili kudhihirisha kilicho mioyoni mwao – ama utii, aukutokutii.

Pili – Mungu humruhusu Shetani kufanya kazi kwa mipaka hapa duniani, kamawakala wa ghadhabu Yake juu ya watenda maovu. Tumekwisha thibitisha jambo hilimapema kwa kuonyesha matukio halisi katika Maandiko ambapo Mungu alileta hukumujuu ya wanaostahili kupitia pepo wabaya. Ukweli kwamba Mungu amemruhusu Shetanikutawala watu wasio-okoka wa dunia hii ni alama ya gadhabu Yake juu yao. Munguhuhukumu makundi ya watu waovu kwa kuwaruhusu binadamu waovu kuwatawala, napia kwa kuruhusu viumbe waovu wa kiroho kuwatawala. Hilo linafanya maisha yaokuwa mabaya zaidi.

Tatu – Mungu anamruhusu Shetani kufanya kazi kwa mipaka hapa duniani ilikujitukuza Mwenyewe. “Kwa sababu, Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziharibu kaziza Ibilisi” (1Yohana 3:8). Kila mara Mungu anapoharibu kazi moja ya Shetani, tukio hilohutukuza uwezo na hekima Yake.

Yesu Ni Mkuu Juu Ya Falme Na Mamlaka

Sisi kama Wakristo, wajibu wetu KiMaandiko ni kushungulika na Shetani na pepowabaya kwa namna mbili: kuwapinga katika maisha yetu wenyewe (Yakobo 4:7), nakuwatoa katika wengine wanaotaka kufunguliwa na kuwekwa huru (Marko 16:17).Mkristo yeyote mwenye uzoefu wa kutoa pepo anajua kwamba, kwa kawaida, kama yule

Page 10: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

mwenye pepo hataki kuwekwa huru, haiwezekani kumtoa huyo pepo.1 Munguanaheshimu hiari ya kila mtu, na kama mtu anataka kujitolea kwa mapepo, Munguhatamzuia!

Hii nayo ni sababu nyingine tena ya sisi kutoweza kuangusha pepo wanaotawala eneola kijiografia. Hao pepo wanaowashikilia mateka watu wa hapo wanafanya hivyo kwakibali chao. Tunapotangaza Injili kwao, tunawapa nafasi ya kuchagua. Wakichaguavizuri, watawekwa huru kutokana na Shetani na mapepo. Lakini wakichagua vibaya –yaani, wakiamua kutotubu – Mungu atamruhusu Shetani kuzidi kuwashikilia mateka.

Katika Maandiko, Yesu anatajwa kwamba ni “kichwa cha enzi yote na mamlaka”(Wakolosai 2:10). Ingawa maneno ya Kiyunani arche (kutawala) na exousia (mamlaka)hutumiwa wakati mwingine kusema juu ya viongozi wa kisiasa wa kibinadamu,yanatumika pia katika Agano Jipya kama majina kwa ajili ya viongozi pepo wa kiroho.Fungu maarufu kuhusu mapambano ya Mkristo dhidi ya wafalme (arche) na mamlaka(exousia) katika Waefeso 6:12 ni mfano mmoja.

Kimantiki, tukisoma kile ambacho Paulo aliandika kuhusu Yesu kuwa kichwa juu yaenzi yote na mamlaka katika Wakolosai 2:10, inaonekana wazi kabisa kwamba anasemajuu ya nguvu za kiroho. Kwa mfano: Katika fungu hilo hilo, mistari minne baadaye,Paulo anaandika hivi juu ya Yesu: “Akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwamkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” (Wakolosai 2:15).

Kama Yesu ni kichwa juu ya watawala wa kiroho na mamlaka, basi ana enzi juu yao.Huu ni ufunuo mzuri sana kwa Wakristo wanaoishi katika tamaduni za kipagani, zenyekutawaliwa na ushirikina, waliokuwa wanaabudu sanamu zamani kwa sababu yakuogopa uwezo wa mapepo waliojua kwamba wana mamlaka juu yao.

Njia Pekee Ya Kuepuka

Njia pekee ya kupona utumwa wa mapepo ni kutubu na kuiamini Injili. Hiyo ndiyonjia ya kupona ambayo Mungu ameipanga. Hakuna awezaye kuzifunga nguvu za mapepojuu ya mji na kukuweka huru, au hata uhuru kidogo. Bila mtu kutubu na kuiamini Injili,bado anakaa katika ghadhabu ya Mungu (ona Yohana 3:36), na hiyo ni pamoja nakushikwa mateka na nguvu za kipepo.

Ndiyo sababu hakuna mabadiliko yanayoweza kupimika katika miji ambayo mikutanomikubwa ya vita za kiroho imefanyika, maana hakuna chochote kilichotokea ambachokimeathiri mamlaka ya kipepo yenye kutawala maeneo hayo. Wakristo wanaweza kupigakelele kwa mamlaka na falme hizo mchana kutwa na usiku kucha. Wanaweza kujaribukumtesa Shetani kwa vitu vinavyoitwa “lugha za mapambano”. Wanaweza kusema,“Tunafunga pepo wabaya juu ya mji huu” mara milioni na zaidi. Wanaweza hata kufanyamambo hayo yote wakiwa ndani ya ndege au wakiwa kwenye magorofa ya juu kabisa yamajengo marefu sana (kama wengine wanavyofanya); na kitu kipekee kitakachowaathiripepo hao wabaya ni kwamba watapata nafasi ya kuwacheka hao Wakristo wajinga.

Basi, tufikie hekaya ya sita ya siku hizi, kuhusu vita ya kiroho.

Hekaya Ya Sita: “Vita Ya Kiroho Dhidi Ya Pepo Zinazotawala Eneo HufunguaMilango Ya Uinjilisti Wenye Matokeo.”

Kinachowasukuma Wakristo wengi wanaojihusisha sana katika vita ya kiroho dhidi yapepo zinazotawala eneo, ni shauku yao kuona ufalme wa Mungu ukipanuka. Kwa hilo, 1 Tofauti katika kanuni hii ni matukio ambapo wahusika wamepagawa mno na mapepo kiasi cha kwamba hawana njia yakujieleza kwamba wanapenda kufunguliwa. Kwa hali hiyo, karama maalum za Roho lazima zitumike ili kuletaukombozi, na hizo karama hutenda kazi kama Roho apendavyo Mwenyewe.

Page 11: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

wanastahili pongezi. Kila Mkristo anapaswa kutamani kuona watu wengi wakiokokakutoka kwenye utumwa wa Shetani.

Lakini, ni muhimu pia kwamba tutumie mbinu za Mungu kujenga ufalme Wake.Mungu anajua kitakachofanya kazi, na kinachopoteza muda tu. Ametuambia wazi waziwajibu zetu ni nini kuhusu kuongezeka kwa ufalme Wake. Kudhani kwamba tunawezakufanya kitu kisichopatikana katika Maandiko, kitakachozidisha fanaka ya uinjilisti wetu– kitu ambacho Yesu, Petro wala Paulo hawakufanya katika huduma zao, ni upumbavu.

Kwa nini Wakristo wengi wanadhani kwamba vita ya kiroho inaweza kufunguamlango wa uinjilisti wenye mafanikio? Mara nyingi hoja zao ni kama ifuatavyo: “Shetaniamepofusha akili za watu ambao hawajaokoka. Basi, lazima tupigane vita ya kiroho dhidiyake ili kumzuia asiwapofushe. Kile kinachowapofusha kikiondolewa, watu wengi zaidiwataiamini Injili.” Lakini je, huo ni ukweli?

Hakika Shetani amepofusha akili za watu ambao hawajaokoka. Paulo aliandika hivi:

Lakini, ikiwa Injili yetu imesitirika, imesitirika kwa haowanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofushafikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wakeKristo aliye sura yake Mungu (2Wakor. 4:3, 4).

Swali ni hili: Je, Paulo aliwapa Wakristo wa Korintho habari hizi kwa kusudila kuwahamasisha wajihusishe na vita ya kiroho ili kuangusha mapepowanaosimamia eneo, ili watu wasio-okoka wawe wasikivu zaidi?

Jibu ni Hapana, kwa sababu kadhaa zilizo wazi.Kwanza: Paulo hakuendelea hivi: “Basi ndugu Wakorintho. Kwa kuwa Shetani

ameipofusha akili ya wasioamini, ninataka mwingie katika vita ya kiroho nakuangusha pepo wote wanaosimamia maeneo, ili vinavyowapofusha wasioaminiviondolewe.” Badala yake, kinachofuata ni kusema juu ya yeye kumhubiri Kristo,ambayo ndiyo njia pekee ya kuondoa upofu wa kiroho.

Pili – Hakuna popote katika barua zake ambapo Paulo aliwaagiza waamini wowotekuhusika na kuangusha ngome juu ya miji yao, ili matokeo ya uinjilisti yaongezeke.

Tatu – Tunajua kutokana na kusoma barua zote za Paulo, kwamba, hakuaminiupofushwaji unaofanywa na Shetani ulikuwa sababu ya msingi ya wasioamini kudumukatika hali yao. Kweli, upofushwaji unaofanywa na Shetani unachangia kwa kiwangofulani, lakini si sababu pekee au iliyo kubwa. Sababu ya msingi yenye kuwafanya watuwasiokoke ni ugumu wa mioyo yao. Hili ni wazi kutokana na sababu rahisi tu kwambaShetani hawezi kumfanya kila mtu kuwa kipofu. Watu wengine wanaposikia ukwelihuamini, na hukataa uongo wote ambao waliamini hapo kwanza. Si kupofushwa naShetani kunakosababisha kutokuamini kwao, bali ni kutokuamini kwao kunakosababishaShetani kuwapofusha.

Mioyo Migumu

Katika barua yake kwa Waefeso, mtume Paulo alieleza vizuri kabisa sababu yawasiokuwa Wakristo kubakia katika kutokuamini kwao.

Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasamsienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao;ambao; akili zao zimetiwa giza [pengine ndiyo kupofushwa naShetani], nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu yaujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao;

Page 12: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadiwapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani (Waefeso4:17-19. Maneno mepesi kukazia).

Paulo anasema, wasio-okoka wamefarakanishwa na uzima wa Mungu kwa sababu ya“ujinga uliomo ndani yao.” Mbona ni wajinga? “Kwa nini “akili zao zimetiwa giza”? Jibuni, “kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.” Wame”kufa ganzi”. Hiyo ndiyo sababu yamsingi ya watu kuendelea kutookoka.2 Lawama wanabeba wao wenyewe. Shetanianachotoa ni ule uongo ambao wanataka kuuamini.

Mfano wa Yesu kuhusu mpanda mbegu na aina za udongo huonyesha hilo pia.

Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwaakizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa,ndege wa angani wakazila… Na huo mfano, maana yake ni hii:Mbegu ni neno la Mungu. Wale wa karibu na njia ndio wasikiao,kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasijewakaamini na kuokoka (Luka 8:5, 11, 12).

Ona hapo kwamba ile mbegu, ambayo ni mfano wa Injili, ilianguka kando yanjia, na kukanyagwa. Haikuweza kupenya udongo mgumu ule ambaounakanyagwa na watu wanapotembea. Basi ikawa rahisi tu kwa ndege, ambao nimfano wa Shetani, kuziiba zile mbegu.

Hoja kuu ya mfano huo mzima ni kulinganisha hali za mioyo ya watu (na jinsiwanavyopokea Neno la Mungu) na aina mbalimbali za udongo. Yesu alikuwa anaelezakwa nini watu wengine huamini na wengine hawaamini – ni uamuzi wao.

Shetani anaingiaje hapo? Yeye ana uwezo wa kuiba Neno kutoka kwa wale wenyemioyo migumu tu. Ndege katika mfano huu ilikuwa sababu ya pili ya mbegu kutochipua.Sababu ya msingi ni udongo – yaani, ugumu wa udongo ndiyo ulifanya iwezekane ndegekuzipata mbegu.

Ndivyo ilivyo kwa habari ya Injili. Tatizo hasa ni mioyo migumu ya watu ambao wanahiari. Watu wanapokataa Injili, wanafanya uchaguzi wa kuendelea kuwa vipofu.Wangependa kuamini uongo badala ya ukweli. Yesu alisema hivi juu ya hilo: “Nuruimekuja ulimwengu, lakini watu wamependa giza kuliko nuru, maana matendo yao nimaovu” (Yohana 3:19. Maneno mepesi kukazia).

Biblia haitufanyi tuamini kwamba watu ni wazuri, wenye mioyo safi, ambaowataiamini Injili bila shida yoyote, mradi tu Shetani aache kuwapofusha. Kinyume chakeni kweli. Biblia inaonyesha picha mbaya sana juu ya tabia na hali ya mwanadamu, naMungu atamwajibisha kila mtu kwa ajili ya uchaguzi wake wa dhambi. Akiwa kwenyekiti chake cha enzi cha hukumu, Mungu hatakubali kujitetea kwa mtu yeyote kwamba,“Shetani alinifanya nitende nilivyotenda.”

Jinsi Shetani Anavyopofusha Akili Za Watu

Shetani anapofushaje akili za watu? Je, ana nguvu fulani za ajabu za kirohoanazomimina ndani ya vichwa vya watu ili kuwazubaisha katika ufahamu wao? Je, pepohutia makucha yake katika akili zao, na kwa njia hiyo kuwafanya washindwe kabisakufikiri vilivyo? Hapana! Shetani hupofusha akili za watu kwa kuwapa uongo wakuamini.

2 Hata maelezo ya Paulo kuhusu wasioamini katika Warumi 1:18-32 yanaunga mkono hoja hii.

Page 13: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Ni hivi: Kama watu wangeamini kweli kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyekufakwa ajili ya dhambi zao, na kama kweli wangeamini kwamba siku moja watasimamambele Zake na kutoa hesabu ya maisha yao, basi wangetubu na kuwa wafuasi Wake.Lakini hawaamini hayo yote. Ila, kuna kitu wanachokiamini. Wanaweza kuaminikwamba hakuna Mungu, au kwamba hakuna maisha mengine baada ya kufa. Wanawezakuamini kwamba mtu akifa anarudi kuishi tena, au kwamba Mungu hawezi kumtupayeyote jehanamu. Wanaweza kudhani kwamba matendo yao ya kidini yatawafikishambinguni. Lakini – chochote wanachoamini – kama si Injili, jina lake kwa kifupi ni:uongo. Hawaamini ukweli, hivyo, Shetani anawaweka katika hali ya upofu kwa njia yauongo. Lakini, wakijinyenyekeza wenyewe na kuamini ukweli, Shetani hatawezakuwapofusha tena.

Uongo Wa Giza

Katika Maandiko, ufalme wa Shetani unaitwa “utawala wa giza” (Wakolosai 1:13).Giza ni mfano wa kutokuwepo na ukweli – kutokuwepo na nuru au kuangaziwa.Unapokuwa gizani, unakwenda kwa mawazo yako na mwishowe unaumia. Ndivyo ilivyokatika ufalme wa Shetani wa giza. Wale waliomo humo wanaishi maisha yao kwakuwaza kwao, na mawazo yao yamejazwa uongo wa Shetani. Wako katika giza la kiroho.

Maelezo mazuri kuhusu ufalme wa Shetani ni kwamba, si ufalme wa kijiografiawenye mipaka dhahiri, bali ni ufalme wa imani – yaani, kuamini katika uongo. Ufalmewa giza uko mahali pamoja na ufalme wa nuru. Wale wenye kuiamini kweli wanaishipamoja na wale wenye kuamini uongo.3 Kazi yetu kubwa ni kutangaza kweli kwa watuambao wanaamini uongo tayari. Wakati mtu anapoamini ukweli, Shetani anapoteza raiawake mmoja – hawezi kumdanganya tena!

Basi tunawaweka huru watu wasio-okoka, si kwa “kufunga” pepo waovu juu yao, balikwa kutangaza kweli. Yesu alisema hivi: “Mtaifahamu kweli, nayo kweli itawawekahuru” (Yohana 8:32. Maneno mepesi kukazia). Upofu wa kiroho huondolewa kwaukweli.

Katika fungu hilo hilo la Maandiko katika Injili ya Yohana, Yesu aliwaambia watuambao hawajaokoka hivi:

Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizompendazo kuzitenda. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; walahakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeyeni mwongo, na baba wa huo. Nami, kwa sababu nasema iliyokweli, hamnisadiki (Yohana 8:44, 45. Maneno mepesi kukazia).

Ona tofauti ambayo Yesu anaonyesha kati Yake na Shetani. Yeye husema ukweli,Shetani ni mwongo wa mwisho.

Ona pia kwamba, ingawa Yesu aliwaambia wasikilizaji Wake kwamba baba yao niIbilisi, na ingawa alimweka Shetani wazi kama mwongo, bado aliweka wajibu wakuamini kweli aliyowaambia juu yao. Halikuwa kosa la Shetani kwamba waowamepofushwa – kosa lilikuwa lao. Yesu aliwawajibisha. Shetani huwasaidia watu“wanaopenda giza” kuendelea kukaa gizani kwa kuwapa uongo ambao wanawezakuuamini. Lakini, Shetani hawezi kumdanganya yeyote atakayeamua kuiamini kweli.

3 Ila – ni kweli kwamba katika maeneo fulani kijiografia, kuna kuzidiana wingi kwa watu wa falme hizo.

Page 14: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Kwa kuwa mambo ndiyo hayo, njia ya msingi ya kusukuma nyuma ufalme wa giza nikwa kueneza nuru – kweli ya Neno la Mungu. Nidyo maana Yesu hakutuambia,“Enendeni duniani kote na kumfunga Ibilisi.” Alituambia hivi: “Enendeni duniani kote nakuihubiri Injili.” Alimwambia Paulo kwamba kusudi la mahubiri yake lingekuwakufungua “macho yao ili watoke katika giza na kuingia katika nuru, na watoke katikautawala wa Shetani na kumjia Mungu” (Matendo 26:18. Maneno mepesi kukazia). Nikitu kilicho wazsi kabisa kwamba watu huepuka utumwa wa Shetani wanapojulishwakweli ya Injili, kisha wafanye uamuzi wa kugeuka kutoka gizani na kuja nuruni, nakuamini ukweli badala ya uongo. Ngome pekee za “kuangushwa” ni ngome za uongoambazo zimejengwa katika akili za watu.

Huu Ni Mpango Wa Mungu

Usisahau kwamba Mungu ndiye alimtupa Shetani kutoka mbinguni mpaka duniani.Angeweza kumweka popote pengine katika ulimwengu, au kumfunga milele. Lakini,hakufanya hivyo. Kwa nini? Kwa sababu alitaka kumtumia Shetani kutimiza lengo Lakehatimaye – lengo la kuwa na familia kubwa siku moja, ya watu wenye hiari, ambaowangempenda kwa uamuzi wao wenyewe na kumtumikia.

Kama Mungu alitaka familia ya watoto watakaompenda, vitu viwili vilitakiwa.Kwanza – Ilibidi aumbe watu wenye hiari, kwa sababu msingi wa upendo ni hiari.Mashine na mitambo haviwezi kupenda.

Pili – Ilikuwa lazima kuwajaribu katika mazingira ambayo wangekabiliwa nauchaguzi wa kutii au kutokutii – kumpenda au kumchukia. Watu wenye hiari lazimawajaribiwe. Na kama kutakuwepo na kipimo cha uaminifu, lazima kuwepo na jaribu lakutokuwa mwaminifu. Basi, tunaanza kuelewa sababu ya Mungu kumweka Shetaniduniani. Shetani angekuwa chaguo mbadala kwa habari ya uaminifu wa binadamu.Angeruhusiwa (na mipaka fulani fulani) kumshawishi yeyote ambaye angetaka kusikilizauongo wake. Kila mtu angekabiliwa na uchaguzi huu: Je, nimwamini Mungu au Shetani?Je, nimtumikie Mungu au Shetani? Watu watambue wasitambue, wote wamekwishafanya uchaguzi tayari. Kazi yetu sisi ni kuwatia moyo watu ambao wamefanya uchaguziwa makosa watubu na kuiamini Injili, na kufanya uchaguzi sahihi.

Je, hayo si ndiyo yaliyofanyika katika Bustani ya Edeni? Mungu aliweka mti wa ujuziwa mema na mabaya pale, kisha akamkataza Adamu na Hawa wasile matunda yake.Kama Mungu hakutaka wasile, mbona aliuweka hapo? Jibu ni kwamba, ulikuwa kipimo.

Vile vile tunaona kwamba Shetani aliruhusiwa na Mungu kumjaribu Hawa. Hapo tenani kwamba – ukitaka kupima uaminifu, lazima kuwepo na jaribu la kutokuwamwaminifu. Shetani alimdanganya Hawa naye akamwamini, na wakati huo huo akaamuakutokuamini yale ambayo Mungu alikuwa amesema. Matokeo yake? Watu wa kwanzakuwa na hiari wakadhihirisha kutokuwa waaminifu kwao katika mioyo yao.

Vivyo hivyo, kila mtu mwenye uwezo wa kuamua hupimwa katika maisha yake yote.Mungu amejifunua kwa njia ya uumbaji Wake, hivyo, kila mtu anaweza kuona kwambayupo Mungu mkuu (ona Warumi 1:19, 20). Mungu ametupa sote dhamiri, na ndani yamioyo yetu tunajua kilicho sawa na kilicho kosa (ona Warumi 2:14-16). Shetani namapepo yake wameruhusiwa, kwa kiwango fulani, kudanganya watu na kuwajaribu.Matokeo ni kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kuamua anapimwa.

Ukweli wa kusikitisha ni kwamba kila mwenye uwezo wa kuamua ameasi na“kuibadili kweli ya Mungu kwa uongo” (Warumi 1:25). Lakini, Mungu ashukuriwe kwasababu ametoa malipo kwa ajili ya dhambi zetu, na njia ya sisi kuzaliwa katika familiaYake. Kifo cha Yesu cha kujitoa dhabihu ndiyo jibu la pekee lenye kutosheleza tatizoletu kabisa tatizo letu.

Page 15: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Uongo Wa Shetani Sasa, Na Baadaye

Sawa – Sasa tunaelewa angalau sababu moja kwa nini Shetani na jeshi lake la waasiwameruhusiwa kufanya kazi hapa duniani: Ni kwa kusudi la kuwadanganya walewanaopenda giza.

Kweli hii inathibitishwa zaidi tunapogundua kwamba kulingana na kitabu cha Ufunuo,Shetani siku moja atafungwa na malaika mmoja na kukaa gerezani kwa miaka elfu moja.Sababu ya hilo ni nini? “Ili asiwadanganye mataifa tena” (Ufunuo 20:3). Wakati waMiaka hiyo Elfu Moja, Yesu Mwenyewe atatawala dunia akiwa Yerusalemu.

Lakini baada ya hiyo miaka elfu, Shetani atafunguliwa kwa kitambo kidogo.Matokeo? “Atatoka ili kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za dunia” (Ufunuo20:8).

Kama Mungu hataki Shetani awadanganye watu wakati huo, mbona atamwachilia?Tena ukizingatia kwamba kusudi la Mungu la kumfunga ni ili “asiwadanganye mataifatena”?

Ni kweli kwamba Mungu asingependa Shetani adanganye mtu yeyote. Lakini anajuakwamba watu pekee wanaoweza kudanganywa na Shetani ni wale wasioamini manenoYake Mungu. Shetani anaweza kuwadanganya wale tu ambao wanakataa ukweli, nandiyo sababu Mungu anamruhusu kufanya kazi sasa, na atamruhusu kufanya kazi wakatihuyo pia. Shetani anapowadanganya watu, hali za mioyo ya watu hudhihirika, na ndipoMungu anapoweza kuchambua “ngano kutoka kwenye magugu” (ona Mathayo 13:24-30).

Hayo ndiyo yatakayofanyika mwishoni mwa Miaka Elfu wakati Shetaniatakapofunguliwa. Atawadanganya wote wanaopenda giza, nao watakusanya majeshi yaokuzunguka Yerusalemu katika juhudi za kuangusha utawala wa Kristo. Mungu atajuaanayempenda Yeye na anayemchukia Yeye. Basi, atatuma “moto kutoka mbinguni” maramoja, utakao”waangamiza” (Ufunuo 20:10). Shetani atatimiza makusudi ya Munguwakati huo, kama tu anavyofanya wakati huu. Sababu hiyo miongoni mwa zingineinatosha kutufanya tuone kwamba ni ujinga kuwaza kwamba tunaweza “kuangusha pepowanaotawala maeneo”. Mungu anawaruhusu wafanye kazi kwa sababu Zake Mwenyewe.

Uinjilisti KiBiblia

Ukweli halisi kabisa ni kwamba Yesu na mitume wa Agano Jipya hawakufanya vitahiyo ya kiroho ambayo wengine wanadai ndiyo kinachokosekana katika uinjilisti wenyemafanikio siku hizi. Hatumkuti Yesu, Petro, Yohana, Stefano, Filipo au Paulo“wakiangusha ngome” au “kuwafunga wenye nguvu” katika miji waliyohubiri. Badalayake tunaona kwamba walifuata uongozi wa Roho Mtakatifu kwa habari ya mahalialipowataka wakahubiri. Tunawaona wakitangaza Injili rahisi tu – kuwaita watu watubuna kumwamini Kristo – na tunaona wakifurahia matokeo ya ajabu sana. Na, katikanyakati ambapo waliwahubiria watu wasiotaka kusikia, waliokataa Injili, hatuwaoniwakiingia “kufanya vita ya kiroho ili Shetani asiendelee kupofusha akili za watu.” Badalayake tunawaona “wakikung’uta mavumbi ya miguu yao” kama Yesu alivyowaamuru, nakwenda mji mwingine (ona Mathayo 10:14; Matendo 13:5).

Ni ajabu kwamba mtu anaweza kudai kuwa “kuangusha ngome” na “kuwafungawenye nguvu” ni sharti la kufanikiwa katika uinjilsti wakati ambapo kuna mifano maelfuya uamsho mkubwa tu katika historia ya kanisa, ambapo “vita ya kiroho” aina hiyohaikutendwa.

Mtu atasema, “Sawa – lakini mbinu yetu inafanya kazi. Tangu tulipoanza kufanya ainahiyo ya vita ya kiroho, watu wameokoka kuliko wakati mwingine wowote.”

Page 16: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Kama huo ni ukweli, sababu ni hii. Yamekuwepo maombi zaidi kufuatana naMaandiko pamoja na kufanyika kwa uinjilisti, au ni kwa sababu ghafula, kundi la watufulani limekuwa wasikivu kwa Injili.

Ungesemaje kama mwinjilisti mmoja angekwambia hivi: “Jioni hii kabla ya kuhubirikwenye mkutano, nilikula ndizi tatu. Nilipohubiri, watu kumi na sita waliokoka!Hatimaye nimegundua siri ya uinjilisti wenye mafanikio! Tangu sasa, nitakuwa ninakulandizi tatu kabla ya kuhubiri!”?

Bila shaka ungemwambia huyo mwinjilisti, “Kula kwako ndizi tatu hakuhusiani nahao watu kumi na sita kuokoka. Siri ya mafanikio yako ni kwamba, ulihubiri Injili, nawatu hao kumi na sita waliokusikiliza walikuwa tayari kupokea.”

Mungu huliheshimu Neno Lake. Kama Mungu akitoa ahadi, na mtu atomize mashartiya hadi hiyo, Mungu atatunza ahadi Yake, hata kama huyo mtu anafanya mambomengine ambayo si ya KiBiblia.

Ndiyo ukweli kuhusu matendo ya vita ya kiroho siku hizi. Ukianza kugawa vikaratasivyenye ujumbe wa Injili na “kumfunga mwenye nguvu” juu ya mji wako wakati huo huo,kiasi fulani cha watu watakaokoka. Vivyo hivyo – ukianza kugawa vikaratasi vyenyeujumbe wa Injili bila ya kumfunga mwenye nguvu, kiasi kile kile cha watu wataokoka.

Jinsi Ya Kuombea Mavuno Ya Kiroho Kulingana Na Maandiko

Sasa basi – tuwaombeeje watu ambao hawajaokoka? Ni vizuri tutambue kwambahakuna mafundisho katika Agano Jipya yenye kutuambia kwamba tuombe namna hii iliMungu aokoe watu, wala hatuna taarifa zozote za watu katika Agano Jipya kuombahivyo. Sababu ni kwamba, kwa mtazamo wa Mungu, Yeye amekwisha fanya kila kitukinachohitajika kwa watu duniani kuokolewa. Yeye alitaka sana watu waokoke kiasi chakumtoa Mwana Wake afe msalabani.

Lakini, mbona watu wote hawajaokoka mpaka sasa? Sababu ni kwamba si wotewalioiamini Injili? Kwa nini hawakuamini? Kwa sababu mbili: (1) Ama hawajawahikusikia Injili, au (2) Wameisikia, wakaikataa.

Ndiyo sababu, njia ya kuwaombea wasio-okoka kulingana na Maandiko ni kuombawapate nafasi za kusikia Injili. Kwa mfano: Yesu alituambia “Mavuno ni mengi, baliwatenda kazi ni wachache. Basi, mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazikatika mavuno Yake” (Luka 10:2. Maneno mepesi kukazia). Ili watu waweze kuisikiaInjili na kuokoka, lazima mtu awaambie. Ndiyo sababu tunapaswa kuomba ili Munguatume watu kwenda kwao.

Kanisa la kwanza lilipo-omba juu ya mavuno kiroho, waliomba hivi: “Ukawajaliewatumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya;ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu, Yesu” (Matendo 4:29,30. Maneno mepesi kukazia).

Aidha walikuwa wanaomba (1) nafasi za kutangaza Injili kwa ujasiri, au (2) ujasiri wakuitangaza Injili katika nafasi ambazo walijua wangepata. Pia walitazamia Munguathibitishe hiyo Injili kwa uponyaji, ishara na maajabu. Hayo ni maombi ya KiBibliakabisa, na uone kwamba lengo lilikuwa kutoa nafasi kwa watu wasikie Injili. Mungualijibu maombi yao, hivi: “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali palewalipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungukwa ujasiri” (Matendo 4:31).

Paulo alishauri Wakristo waombeje kuhusu kupatikana kwa mavuno ya kiroho? Je,aliwashauri wamwombe Mungu aokoe watu zaidi? Hapana! Hebu tusome maneno yake.

Page 17: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Hatimaye ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee nakutukuzwa, vile vile kama ilivyo kwenu (2Wathes. 3:1. Manenomepesi kukazia).

[Ombeni] Pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwakufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hatanipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena(Waefeso 6:19, 20. Maneno mepesi kukazia).

Kama watu wataokoka au hapana kwa wakati huu ni swala lao, si swala laMungu. Basi, maombi yetu yawe kwamba watu wasikie Injili na Mungu atusaidiekuitangaza. Mungu atajibu sala zetu, lakini hiyo bado si uhakikisho kwamba mtuataokoka, maana Mungu anawapa watu haki ya kufanya maamuzi yao wenyewe.Wokovu wao unategemea jinsi watakavyoitikia Injili.

Hekaya Ya Saba: “Mkristo Anapotenda Dhambi, Anafungua Mlango Kwa PepoKuja Kukaa Ndani Yake.”

Ni kweli kwamba Mkristo anapotenda dhambi, yaweza kuwa ni kwa sababuamekubali jaribu la pepo. Kukubaliana na ushawishi wa pepo haumaanishi kwamba huyopepo anaweza kumwingia mwamini. Tunapofanya dhambi kama Wakristo, tunavunjaushirika wetu na Mungu kwa sababu tumeacha kumtii (ona 1Yohana 1:5, 6). Tunajisikiahatia. Lakini si kwamba tumevunja uhusiano wetu Naye, maana sisi bado ni watotoWake.

Tukiziungama dhambi zetu, “Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atusamehe dhambizetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:9). Hapo, ushirika wetu Nayeunarejeshwa. Ona kwamba Yohana hakusema tunahitaji kusafishwa pepo zozotezinazokaa ndani wakati tunapokuwa na hatia ya dhambi.

Kila Mkristo anakabiliwa kila siku na majaribu kutoka duniani, mwilini na kwaShetani. Paulo aliandika kwamba kweli tunapambana na mapepo wa aina mbalimbali(ona Waefeso 6:12). Basi, kwa kiwango fulani, kila mwamini anasumbuliwa na mapepo.Hiyo ni kawaida , na ni wajibu wetu kumpinga Shetani na mapepo yake kwa imani katikaNeno la Mungu (ona 1Petro 5:8, 9). Tunapoamini na kutenda kulingana na yalealiyosema Mungu, huko ndiko kumpinga Shetani.

Kwa mfano: Kama Shetani ataleta mawazo ya kuvunja moyo, tunapaswa kufikiriaandiko lenye kupingana na hali hiyo, na kutii Neno la Mungu kwamba “furahinisikuzote” (1Wathes. 5:16) pamoja na “shukuruni kwa kila jambo” (1Wathes. 5:18). Niwajibu wetu kutenda kulingana na Neno la Mungu na kubadili mawazo yaliyoletwa naShetani kwa kutia mawazo ya Mungu.

Lazima tutambue kwamba, kama watu wenye hiari, tunaweza kufikiri kuhus chochotetunachotaka. Ikiwa mwamini ataendelea kuchagua kusikiliza na kukubaliana na mashauriya pepo wabaya, anaweza kufungua mawazo yake yagandamizwe au kuonewa na pepo,ambayo ni hali ya kupokea na kutawaliwa zaidi na zaidi na mawazo mabaya. Akiamuakujitoa zaidi, atatawaliwa na aina fulani ya mawazo isiyo nzuri, kitu ambacho si rahisikwa Mkristo, lakini huweza kutokea. Ila, hata na hapo, huyo Mkristo akitaka kuwa huru,anachohitaji kufanya ni kuamua kufikiri na kujitolea kwa Neno la Mungu, na kumpingaShetani, naye anakuwa huru.

Lakini je, atafikia mahali pa kupagawa? Ndiyo, kama kwa hiari yake mwenyeweataamua kutoka moyoni, bila kusukumwa, kumkana Kristo na kumwacha kabisa. Hapo

Page 18: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

hatakuwa Mkristo tena4 na yawezekana akapagawa – akizidi kujitolea kwa huyo pepoaliyekuwa anamgandamiza au kumwonea. Lakini hilo liko mbali sana na wazo lakufungua mlango kwa ajili ya pepo ili aingie kwako kwa sababu ya dhambi moja tu.

Ni kweli kwamba hakuna mfano hata mmoja katika Agano Jipya wa Mkristo yeyotekupagawa na pepo. Wala hakuna onyo lolote litolewalo kwa Wakristo kuhusu uwezekanohatari huo wa wao kupagawa na pepo. Wala hakuna fundisho lolote litolewalo juu yajinsi ya kutoa pepo kutoka kwa Wakristo wenzetu.

Ukweli ni kwamba, kama Wakristo, hatuhitaji pepo zitolewe kwetu – tunachohitaji niakili zetu kufanywa upya kwa Neno la Mungu. Hiyo inakubalika na Maandiko. Pauloaliandika hivi:

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwakufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Munguyaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu (Warumi 12:2).

Nia zetu zikiisha safishwa kutokana na taratibu za kizamani za kufikiri na kufanywaupya na kweli ya Neno la Mungu, tunapata ushindi juu ya tabia za kale na kuishi maishaya kufanana na Kristo. Ukweli ndiyo hutuweka huru (Yohana 8:32). Tunabadilikatunapofanywa upya katika nia zetu, si kwa kutolewa pepo wote tulio nao!

Mbona basi kuna Wakristo wengi tu wenye kushuhudia kwamba wametolewa pepo(au mapepo)? Uwezekano mmoja ni kwamba, pengine walidhani tu kwamba wana pepoambalo limetolewa. Wakristo wengi ni wepesi kudanganywa na hawajui sana Neno laMungu. Basi, wanakuwa rahisi kutekwa na “watumishi wa ukombozi” ambaowanawashawishi watu kwa ujanja sana wanadhani kwamba wana pepo. Watu wakiishashawishika kwamba wana pepo ndani yao, watashirikiana kirahisi tu na mtu yeyoteanayeonyesha kujiamini kwa habari ya kutoa pepo ndani ya walio nazo.

Uwezekano mwingine ni kwamba watu kama hao ambao wametolewa pepohawakuwa waamini halisi wa Kristo wakati wa kufunguliwa kwao, ingawa waowalidhani ni waamini. Injili ya kisasa ambayo iko tofauti kabisa na ile Injili ya Biblia,imewadanganya wengi sana kufikiri kwamba wao ni Wakristo, ingawa hawana tofautiyoyote na wasiokuwa Wakristo. Tena, Yesu si Bwana maishani mwao. Tunaona katikaMaandiko kwamba, watu walipoamini Injili na kuzaliwa upya, pepo waliokaa ndani yaowalitoka wenyewe (ona Matendo 8:5-7). Pepo hawawezi kumpagaa mtu mwenye RohoMtakatifu ndani, na Roho Mtakatifu hukaa ndani ya watu wote walizaliwa mara ya pili.

Hekaya Ya Nane: “Kwa Kujifunza Historia Ya Mji, Tunaweza Kutambua PepoZinazotawala Hapo, Na Kufanikiwa Sana Katika Vita Ya Kiroho, Na HatimayeKatika Uinjilisti.”

Hekaya hii imejengwa juu ya mawazo kadhaa, ambayo hayana msingi katikaMaandiko. Wazo moja ni kwamba pepo wanaotawala eneo hukaa kwa muda mrefu sana.Yaani – waliokuwepo katika eneo kwa miaka mia kadhaa bado ndiyo wale wale. Hivyo,tukigundua kwamba mji ulianzishwa na watu wachoyo, tunaweza kuamua kwamba ziporoho au pepo za choyo juu ya mji huo hata leo. Kama mji ulikuwa kijiji cha Kihindi hapokwanza, basi tuamue kwamba pepo za uchawi na uaguzi bado zinatawala mji huo mpakaleo. Na kadhalika na kadhalika.

4 Wale wanaosema “ukiisha okoka, umeokoka milele” bila shaka watapinga. Hebu wasome Warumi 11:22; 1Wakor. 15:1,2; Wafilipi 3:18, 19; Wakolosai 1:21-23 na Waebrania 3:12-14. Kila wanapokuta neno “kama”, wazingatie kinachofuata aukinachotangulia hapo!

Page 19: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Lakini je, ni kweli kwamba mamlaka zile zile ovu na falme zilizokuwa zinatawalaeneo fulani kijiografia kwa miaka mia nyingi, bado zipo hata leo? Labda, lakini si lazimaiwe hivyo.

Hebu tufikiri kisa tulichotazama mapema, kutoka sura ya kumi ya kitabu cha Danieli.Yule malaika asiyetajwa, aliyesaidiwa na Mikaeli kupigana na “mkuu wa Uajemi”alimwambia Danieli hivi: “Sasa nitarudi kupigana na mfalme wa Uajemi; na tazama,mkuu wa Uyunani naye atakuja” (Danieli 10:20. Maneno mepesi kukazia). Tunasomakatika historia kwamba Dola ya Uajemi ilishindwa na Wayunani kupitia mapigano naIskanda Mkuu. Lakini, huyu malaika asiyetajwa jina alifahamu kuhusu mabadilikoyaliyokuwa yanakuja katika ulimwengu war oho – kwamba “mkuu wa Uyunani” alikuwaanakuja.

Je, mkuu wa Uyunani alipokuja, alitawala katika ulimwengu wa roho juu ya Dola yaUyunani kama mkuu wa Uajemi alivyofanya katika ulimwengu wa roho juu ya Dola yaUajemi? Pengine, na kama ndivyo, basi pepo kadhaa wa vyeo vya juu walibadilishanamaeneo maana, Dola ya Uyunani ilitawala eneo lote lililokuwa Dola ya Uajemi. Wakatiyanapotokea mabadiliko kisiasa hapa duniani, yawezekana kunakuwa na mabadiliko piakatika ufalme wa giza. Ila ukweli ni kwamba hatuwezi kujua, labda kama Munguatatufunulia.

Vyovyote vile – haileti tofauti yoyote kwamba ni aina gani ya pepo wanaotawala juuya eneo fulani kijiografia maana hakuna chochote tunachoweza kufanya juu yake kwahabari ya “vita ya kiroho”, kama tulivyokwisha ona mapema.

Kuwaweka Pepo Katika Makundi Kuliko Ilivyo

Tena, wakati mwingine, sisi hudhania tu kwamba wapo pepo wanaotawala aina fulaniya dhambi. Dhana nzima kwamba kuna “roho ya choyo,” “roho ya ashiki ya mwili,”“roho za dini,” “roho za ugomvi” na kadhalika, haina msingi katika Maandiko, licha yawazo kwamba aina hizo mbalimbali za pepo hupatikana katika ngazi za juu za pepowabaya wanaotawala katika ufalme wa giza.

Cha kushangaza kwa wale ambao hawajawahi kujifunza zile Injli nne kwa ukaribu,kuna aina tatu tu maalum za pepo ambazo Yesu alitoa. “Pepo bubu” anatajwa mara moja(Luka 11:14), na tunasoma mara moja juu ya “pepo bubu na kiziwi” (Marko 9:25), nazaidi ya mara moja tunasoma juu ya “pepo wachafu” ambao ni kama mchanganyiko wapepo wote Yesu aliotoa, pamoja na yule “bubu na kiziwi” (ona Marko 9:25).

Je, haiwezekani kwamba huyo “pepo bubu na kiziwi” alikuwa na uwezo wakumfanyia mtu kitu zaidi ya hayo? Bila shaka, maana yule mvulana katika Marko 9alikuwa anapata kifafa pia. Basi, “pepo bubu na kiziwi” pengine si aina ya pepo, bali nimtajo kuhusu jinsi pepo huyo alivyokuwa anamdhuru mtu fulani. Wengine wetu ni kamatunaehuka kwa habari ya “kupanga” mapepo mpaka tunakwenda hata zaidi ya mafunuoya Biblia.

Pepo wanaotajwa katika Agano la Kale ni “pepo wa udanganyifu” (1Wafalme 22:22,23), “pepo wa kupotosha” (Isaya 19:14), na “pepo wa ukahaba” (ktk Hosea 4:12; 5:4).Kwa habari ya aina ya kwanza na ya pili, hakika pepo wote wanaweza kuitwa “rohozidanganyazo” na “roho za kupotosha”. Kwa habari ya aina ya tatu, neno “pepo waukahaba” si lazima kuwa pepo mchafu maalum. Inaweza kuwa ni hali ya moyo iliyopo.5

5 “Pepo wa wivu” anayetajwa katika Hesabu 5:14-30 na “roho ya kutakabari” katika Mithali 16:18 ni mifano mizuri yaneno roho kutumika kuelezea hali fulani ya moyo ya kudumu, badala ya kusema juu ya pepo halisi. Tunasoma katikaHesabu 14:24 kwamba Kalebu alikuwa na “roho tofauti”, ambayo bila shaka maana yake ni hali njema ya moyo waKalebu.

Page 20: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Katika kitabu chote cha Matendo, wakati pekee ambapo pepo mchafu anatajwa nikatika Matendo 16:16, tunaposoma juu ya msichana aliyekuwa na “pepo wa utambuzi.”Na katika nyaraka zote, aina pekee ya pepo wanaotajwa hao ni “roho zidanganyazo” (ktk1Timo. 4:1), ambazo zinaweza kuwa pepo aina yoyote ile.

Basi, kutokana na mitajo michache kuhusu aina fulani za pepo katika Biblia,inashangaza kusoma orodha za siku hizi za mapepo, zenye majina mia nyingi ya ainambalimbali za pepo wanaoweza kuwapagaa watu au kutawala miji.

Hata hivyo, hatupaswi kudhani kwamba kuna mpangilio wowote, kwa dhambimaalum, wa pepo wa vyeo vya juu. Ni dhana tu kusema kwamba, “Kwa sababu kunawingi wa kamari katika mji ule, lazima kuna pepo wa kamari juu yake.”

Kuna Pepo Wa Uvutaji?

Hebu fikiri jinsi ambavyo mtu angeonekana mjinga kama angesema hivi: “Kuna pepowengi sana wa uvutaji katika mji huo, maana watu wengi humo wanavuta sigara.” Je, hao“pepo wa uvutaji” walikuwa wanafanya nini kabla ya miji hiyo kuwepo? Walikuwa wapisiku hizo? Walikuwa wanafanya nini kabla tumbaku haijajulikana na kutumiwa kwa ajiliya uvutaji? Je, sababu ya watu wavutao kupungua siku hizi ni kwa kuwa baadhi ya hao“pepo wa uvutaji” wa zamani wanakufa, au ni kwa sababu wanahamia katika maeneomapya?

Unaona ujinga wenyewe tunaposema vitu kama, “Mji huo unatawaliwa na pepo zaashiki ya mwili, maana ndiyo sababu kuna ukahaba sana pale”? Ukweli ni huu: Popoteambapo watu hawamfuati Kristo, kuna ufalme wa giza. Pepo wengi hufanya kazi katikaeneo hilo la giza, wanaoshawishi watu wao kutenda dhambi na kuendelea katika uasi waodhidi ya Mungu. Hizo pepo zitawajaribu watu katika kila eneo la dhambi, na mahalipengine, watu watakubali dhambi moja zaidi ya zingine. Tumaini lao ni Injili, ambayondiyo tumeitwa kuitangaza.

Hata kama kuna aina fulani za mapepo ambao ni mafundi katika dhambi fulani, naambao wanatawala maeneo fulani ya kijiografia, haitusaidii kujua juu yake kwa sababuhakuna tunachoweza kufanya kuwaondoa pale. Wajibu wetu ni kuomba (kulingana naMaandiko) kwa ajili ya watu walioko pale, waliodanganywa, na kuwahubiri Injili.

Uzuri pekee wa kugundua dhambi zinazotawala mji fulani ni ili tuweze kuhubirijumbe zinazowagusa watu wasio-okoka wanaokaa pale – kwa kutaja dhambi zilezinazowafanya kuwa na hatia mbele za Mungu. Lakini hakuna haja ya kufanya utafiti wahistoria ya mji ili kujua hilo. Mtu anahitaji kutembelea mji huo kwa muda mfupi tu nakutazama kwa makini na kusikiliza kwa makini. Dhambi kuu hapo zitadhihirika tukirahisi.

Mwisho – Hakuna mfano wowote katika Agano Jipya wa mtu yeyote kufanya“matembezi ya kiroho” kama namna ya kujiandaa kwa ajili ya vita ya kiroho, au uinjilisti.Wala hakuna maagizo yoyote katika Nyaraka kuhusu hilo. Katika Agano Jipya, mitumewalimfuata Roho Mtakatifu kwa habari ya mahali pa kuhubiri, kisha wakatangaza Injilikwa uaminifu na kuwaita watu kutubu, na wakamtumaini Bwana kulithibitisha Neno kwaishara. Njia yao ilifanikiwa sana!

Hekaya Ya Tisa: “Kuna Wakristo Wanaohitaji Kuwekwa Huru Kutokana NaLaana Za Ukoo Au Za Kishetani.”

Dhana nzima ya “laana za ukoo” hutokana na mafungu manne ya Maandiko katikaAgano la Kale, yenye kusema kitu kimoja yote. Hayo ni Kutoka 20:5; 34:7; Hesabu14:18 na Kumbukumbu la Torati 5:9. Tutazame Hesabu 14:18.

Page 21: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

BWANA ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenyekusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwahana makosa kwa njia yoyote ile, mwenye kuwapatiliza wana kwauovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne (manenomepesi kukazia).

Sasa – tunatafsiri vipi Maandiko haya? Je, maana yake ni kwamba Mungu atamlaanimtu au kumwadhibu kwa sababu ya dhambi za wazazi wake, au babu zake, au babu wababu, au mababu wakuu? Je, ni sawa kuamini kwamba Mungu anaweza kumsamehe mtudhambi zake anapomwamini Yesu, kisha amwadhibu kwa sababu ya dhambi za wazaziwake na babu zake?

Si hivyo kamwe, la sivyo, Mungu angeshtakiwa kwa kutokuwa na haki, na kwaunafiki mkubwa. Yeye Mwenyewe alisema kwamba kumwadhibu mtu kwa sababu yadhambi za wazazi wake ni kosa.

Lakini ninyi [Waisraeli] mwasema, Kwani yule mwana asiuchukueuovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali nahaki, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, hakika ataishi. Rohoitendayo dhambi, ndiyo itakayokufa. Mwana hatauchukua uovu wababa yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe. Haki yakemwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovuutakuwa juu yake (Ezekieli 18:19, 20. Maneno mepesi kukazia).

Tena, kulingana na Torati ya Musa, Mungu aliamuru kwamba baba wala mtotowasichukue adhabu kwa ajili ya dhambi za yeyote kati yao.

Mababa wasiuawe kwa aili ya watoto wao, wala watoto wasiuawekwa ajili ya baba zao; kila mtu na auawe kwa ajili ya dhambi yakemwenyewe (Kumbu. 24:16).

Haiwezekani kwamba Mungu mwenye upendo na haki atoe laana au adhabu kwa mtukwa sababu ya dhambi za wazee wake.6 Basi, nini maana ya Maandiko kusema kwambaMungu “hataacha kuwahesabia hatia wenye hatia, naye atapatiliza maovu ya baba juu yawana wao, mpaka kizazi cha tatu na cha nne”?

Bila shaka maana yake ni kwamba Mungu anawawajibisha watu kwa ajili ya mifanoya dhambi wanayo-onyesha mbele ya uzao wao, na kwa njia hiyo anawahusisha kwakiasi fulani na zile dhambi ambazo watoto wao wanazifanya kwa sababu ya mfano wao.Mungu anawawajibisha watu kwa sehemu, kwa sababu ya mifano yao miovu, kwa ajiliya dhambi za wajukuu zao! Mungu ni mtakatifu kiasi hicho. Na hakuna awezaye kusemakwamba anaonea mtu anapofanya hivyo.

Ona fungu tunalotazama, kwamba linasema, Mungu “atawapatiliza wana maovu yababa zao.” Yanayopatilizwa ni maovu ya baba kwa watoto wao.

6 Hii haimaanishi kwamba watoto hawateseki kwa sababu ya dhambi za wazazi wao – wanateseka. Ila, wanapoteseka, siishara kwamba Mungu anawaadhibu watoto hao kwa dhambi za wazazi wao. Ni ishara kwamba watu ni waovu kiasikwamba wanatenda dhambi fulani ambazo wanajua zitawaletea watoto wao shida. Ni wazi pia kutoka Maandikokwamba Mungu – kwa huruma Zake – aweza kuzuia hukumu kwa mtu mmoja na baadaye akaimimina juu ya mzaoafuataye, mwovu zaidi au anayestahili zaidi. Vivyo hivyo, anaweza kuzuia hukumu Yake juu ya kizazi kiovu, nakuimimina juu ya kizazi kingine kinachofuata ambacho ni kiovu zaidi au chenye kustahili (ona Yeremia 16:11, 12). Hiyoni tofauti na kumwadhibu mtu kwa ajili ya dhambi za babu zake!

Page 22: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Basi, dhana nzima ya “laana za ukoo” ni potofu na mbaya, maana inamfanya Munguaonekane asiye haki.

Laana Za Kishetani Je?

Lakini, vipi kuhusu “laana za Kishetani”?Kwanza – Hakuna kitu katika Biblia nzima chenye kuonyesha kwamba Shetani

anaweza “kumlaani” mtu, wala hakuna mifano yoyote kuonyesha akifanya hivyo. Kwelitunamwona akiwatesa watu katika Biblia, lakini hatumkuti “akilaani” familia ambayobaada ya hapo, inaendelea na balaa au maisha mabaya pamoja na vizazi vinavyofuata.

Kila Mkristo husumbuliwa na Shetani na mapepo wabaya (kwa kiwango fulani)maisha yake yote, lakini hii haina maana kwamba tunahitaji “kuvunja laana ya Kishetani”juu yetu ambayo imetoka kwa wazazi wetu. Tunachohitaji kufanya ni kusimama kwenyeNeno la Mungu na kumpinga She tani kwa imani, kama tunavyoambiwa na Maandiko(ona 1Petro 5:8, 9).

Katika Biblia, Mungu ndiye mwenye uwezo wa kubariki na kulaani (ona Mwanzo3:17; 4:11; 5:29; 8:21; 12:3; Hesabu 23:8; Kumbu. 11:26; 28:20; 29:27; 30:7; 2Nyakati34:24; Zaburi 37:22; Mithali 3:33; 22:14; Ombolezo 3:65; Malaki 2:2; 4:6). Wenginewanaweza kutulaani kwa midomo yao, lakini laana zao hazina nguvu – haziwezikutudhuru.

Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, na kama mbayuwayukatika kuruka kwake; kadhalika laana isiyo na sababu haimpigimtu (Mithali 26:2).

Balaamu alikuwa sahihi baada ya kuajiriwa na Balaki kuwalaani wana wa Israeli.Alisema hivi: “Nimlaanije yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje yeyeambaye BWANA hakumshutumu?” (Hesabu 23:8).

Wakristo wengine wamepita kiasi kwa wazo la watu kuwalaani wengine, kutokana namaneno ya Yesu katika Marko 11:23. “Amin nawaambia, Yeyote atakayeuambia mlimahuu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake ila aamin kwambahayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.”

Ila, ona kwamba hakuna nguvu katika kusema maneno tu, bali, katika kusema manenoya imani kutoka moyoni. Hakuna jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani kwamba laanayake dhidi ya mtu fulani inaweza kumdhuru huyo, kw sababu imani ni uhakika thabiti(Waebrania 11:1), na imani hutokana na kusikia Neno la Mungu tu (Warumi 10:17). Mtuanaweza kutazamia kwamba laana yake kwa mtu italeta balaa, lakini hawezi kuaminihivyo, kwa sababu Mungu hajatoa ahadi yenye kuleta imani hiyo kuhusu kuwalaani watu.

Tofauti pekee ni kama Mungu atampa mtu “karama ya imani” pamoja na “karama yaunabii” (ambazo ni mbili katika zile tisa za Roho) ili atamke kitu kama baraka au laana.Tunaona hayo mara kwa mara katika maisha ya watu fulani katika Agano la Kale (onaMwanzo 27:27-29, 38-41; 49:1-27; Yoshua 6:26. Pia 1Wafalme 16:34; Waamuzi 9:7-20,57; 2Wafalme 2:23, 24). Hata katika nyakati kama hizo, baraka au laana zilitoka kwaMungu, si kwa mtu. Basi, dhana nzima ya mtu kuweka “kumlaani” mwingine ni potofu.Ndiyo sababu Yesu hakutuagiza “tuvunje laana ambazo zimetamkwa kinyume chetu,”bali “kuwabariki wanaotulaani.” Hatupaswi kuogopa laana ya mtu yeyote. Kuogopa laanaya mtu ni kuonyesha utovu wa imani kwa Mungu. Ila – kwa bahati mbaya sana –nakutana na wachungaji mara nyingi ambao wanaamini zaidi nguvu za Shetani kuliko zaMungu. Pamoja na safari zangu nyingi kila mwezi katika nchi tofauti tofauti ili kuharibuufalme wa Shetani, siogopi hata kidogo kwamba nitatupiwa laana, wala simwogopiShetani kwamba atanilaani. Hakuna haja ya kuogopa.

Page 23: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Laana Za Kichawi Je?

Je, yawezekana kupata laana za Kishetani kwa sababu ya kujihusisha katika uchawisiku za nyuma?

Tusisahau kwamba tunapozaliwa mara ya pili, tunakombolewa kutokana na nguvu zaShetani na ufalme wa giza (ona Matendo 26:18; Wakolosai 1:13). Shetani hana nguvutena juu yetu, isipokuwa tukimpa ruhusa. Japo Biblia inaonyesha kwamba Wakristo waEfeso walikuwa wanahusika sana katika mambo ya uchawi kabla ya kuokoka kwao (ktkMatendo 19:18, 19), hakuna taarifa yoyote ya Paulo kuvunja “laana za kishetani” juu yao,au kufunga nguvu za Shetani juu yao, baada ya wao kuzaliwa mara ya pili. Sababu nikwamba waliwekwa huru kutokana na utawala wa Shetani mara tu walipomwamini Yesumara ya kwanza.

Tena – Paulo alipowaandikia Waefeso, hakutoa maagizo yoyote kwao kuhusukumweka mtu huru kutokana na laana za kishetani au za ukoo. Alichowaambia ni hiki:“Msimpe Shetani nafasi” (Waefeso 4:27), na “vaeni silaha zote za Mungu” ili kuweza“kuzipinga hila za Ibilisi” (Waefeso 6:11). Huo ni wajibu wa kila Mkristo.

Lakini, mbona mara zingine kuwa Wakristo ambao walisaidiwa baada ya mtu fulanikuvunja “laana ya ukoo” au “ya kishetani” kwao? Pengine ni kwa sababu huyo mtualiyehitaji msaada aliamini kwamba Ibilisi atakimbia baada ya “laana” hiyo kuvunjwa.Imani humfukuza Shetani, na kila Mkristo anaweza na anapaswa kuwa na imani kambaanapompinga Shetani, atakimbia. Ila, hakuna haja ya kumwita “bingwa wa ukombozi” ilikumfanya Shetani akimbie.

Mwisho – Biblia inatuambia kwamba Kristo “alifanyika laana kwa ajili yetu,” na kwakufanya hivyo, “akatukomboa na laana ya Torati” (Wagalatia 3:13. Maneno mepesikukazia). Sote tulikuwa chini ya laana ya Mungu kwa sababu ya dhambi, lakini kwakuwa Yesu alichukua adhabu yetu, tumewekwa huru kutokana na laana hiyo. Sifa kwaMungu! Kwa kuwa hatuna laana tena, tunaweza kufurahi kwamba sasa tumebarikiwa“kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo” (Waefeso 1:3).

Hekaya Ya Kumi: “Tunaweza Kuvunja Vifungo Vya Mapepo Kwa Kufunga.”

Wakristo wengine wanahesabu kufunga kuwa ni sehemu kubwa sana katika maisha yaKikristo, na jukumu muhimu sana. Inashangaza sana, hasa ukizinga tia kwamba katikanyaraka zote za Agano Jipya, hakuna fundisho hata moja kuhusu kufunga litolewalo kwaWakristo. Wala Wakristo hawatiwi moyo kufunga katika nyaraka za Agano Jipya.Ukweli ni kwamba hakuna chochote kuhusu kufunga kinachotajwa katika nyaraka,isipokuwa Paulo anataja mara chache ambazo ilibidi ashinde na njaa – mfungo bilakupanga!

Katika kitabu cha Matendo, kuna mifano miwili tu ya kufunga kwa hiari.

Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,Roho Mtakat ifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kaziile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweakmikono yao juu yao, wakawaacha waende zao (Matendo 13:2, 3.Maneno mepesi kukazia).

Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, nakuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono yaBwana waliyemwamini (Matendo 14:23. Maneno mepesi kukazia).

Page 24: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Hapo tunajifunza kwamba faida ya msingi ya kufunga katika agano jipya ni kutupamuda zaidi wa kuomba kwa dhati. Hii ni muhimu sana wakati tunapomtafuta Mungu ilikujua mwelekeo fulani maalu, au tunaposubiri maongozi Yake kuwa dhahiri katika rohozetu.

Kama kila Mkristo ajuavyo, kitu kigumu sana kuhusu kuwa na wakati mrefu katikamaombi ni kupata nafasi ya kufanya hivyo. Wakati mwingine njia pekee ya kupata masaakadhaa ya kuomba ni kuondoa kitu kingine. Pengine hii ndiyo sababu Yesu wakati fulanialiomba usiku kucha (kumbuka ilikuwa kabla hajawachagua mitume Wake), na ndiyosababu aliamka asubuhi na mapema ili aombe. Ndiyo sababu Paulo aliwaandikiaWakristo wenye ndoa kwamba wasinyimane tendo la ndoa, “isipokuwa mmepatana kwamuda ili mpate faragha kwa kusali” (1Wakor. 7:5. Maneno mepesi kukazia). Ili kuwezakupata muda wa kutosha wa maombi, itabidi tuache kwa muda baadhi ya starehe halalikabisa za maishani, kama vile chakula, usingizi na kushirikiana kimwili katika ndoa.

Ni Kufunga, Au Ni Kugoma Kula?

Ni vizuri kujua kwamba kufunga hakumbadilishi Mungu. Tusije tukadhani kwambakwa kuwa tunajitesa kwa kufunga, Mungu atatusikiliza kirahisi zaidi tunapoomba.Mambo yakiwa hivyo, huko ni kugomea chakula.

Kufunga hakutupi nguvu zaidi kiroho, wala mamlaka juu ya pepo. Kama viungokatika mwili wa Kristo, tayari sisi tumeketi “katika ulimwengu wa roho, juu sana kulikofalme na mamlaka na nguvu na utawala, na kila jina litajwalo” (Waefeso 1:21). Tayarituna mamlaka ya kutoa pepo kulingana na ahadi ya Yesu katika Marko 16:17 kwamba,“Na ishara hizi zitafuatana na waaminio. Kwa jina Langu watatoa pepo.”

Lakini, vipi kuhusu maneno ya Yesu kuhusu pepo mmoja aliyemtoa, kwamba, “Ainahii haitoki isipokuwa kwa kuomba na kufunga” (katika Mathayo 17:21)?

Kwanza: Biblia yangu inaonyesha kwamba nakala za mwanzo kabisa za Injili yaMathayo hazina mstari huo. Maana yake ni kwamba, yawezekana Yesu hakusema hivyo.

Katika maelezo ya Marko ya tukio hilo hilo, Yesu anasema hivi: “Namna hii haitokiisipokuwa kwa maombi” (katika Marko 9:29), na hapo pembeni kuna maelezo kwamba,nakala nyingi za kale huongeza “na kufunga” mwishoni mwa mstari wenyewe.

Sasa je – Yesu alisema kufunga ni kitu muhimu katika kutoa pepo aina fulani? Jibu nikwamba hatujui. Tena, kama Yesu alisema hivyo kweli, basi huo ndiyo wakati pekeeambapo Yeye na waandishi wengine wa Agano Jipya walipounganisha kufunga na kutoapepo katika watu.

Pengine itafaa kujiuliza jinsi ambavyo kufunga kunaweza kuwa msaada katika kutoapepo. Hakika kufunga hakuongezi mamlaka ya mtu juu ya mapepo. Kama Munguamempa mtu mamlaka ya kutoa pepo, anayo tu. Kitu pekee kinachoweza kufanywa kwakufunga ni kumpa mtu huyo muda zaidi wa kutafakari juu ya ahadi ya Mungu kwa habariya mamlaka yake, na kwa njia hiyo kuongeza imani yake katika kile ambacho Munguamesema. Imani ni swala muhimu sana katika kuleta ukombozi.

Katika hili tukio husika, wanafunzi walikwisha pewa mamlaka ya kutoa pepo wachafu(katika Mathayo 10:1), lakini wakashindwa kutoa pepo katika kijana mmoja. Yesualiposikia juu ya kushindwa kwao, alisikitishwa sana na kutokuamini kwao (ona Mathayo17:17), na walipomwuliza kwa nini wameshindwa, alijibu hivi: “Kwa sababu ya uhabawa imani yenu” (Mathayo 17:20). Mistari michache baadaye ndipo tunakuta tamko laYesu kuhusu kufunga.

Basi, twaweza kusema kwamba sababu ya kushindwa kwao ni kati ya hizi mbili: Amahakuwakuwa na imani katika mamlaka yao waliyopewa na Mungu, pamoja na hawakuwa

Page 25: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

wameomba na kufunga kabla, au, hawakuwa na imani katikamamlaka yao waliyopewana Mungu, na muda ambao wangeweza kutumia katika kufunga na kuomba kungesaidiakukuza imani yao. Afadhali la pili, maana linaleta maana. La kwanza linamfanya Yesuajipinge. Kumbuka kwamba yote mawili yamejengwa juu ya dhana kwamba Yesualisema maneno hayo kuhusu kufunga.

Pamoja na hayo, hatupaswi kusahau kwamba mitajo yote juu ya vita ya kiroho nakukombolewa kutoka mapepo haitaji kuhusu kufunga. Kufunga hakutajwi kabisa kwahabari ya via yetu binafsi dhidi ya Shetani na mapepo wabaya. Hivyo, kusema kwambalazima tufunge ili kupata ushindi binafsi juu ya Shetani ni kinyume cha Maandiko.

Mfungo Mungu Anaochagua

Maandiko mengine yanayotumika vibaya mara kwa mara kuthibitisha kwambakufunga kunaweza kuvunja mamlaka ya mapepo yanapatikana katika Isaya 58:6.

Je! Saumu niliyoichagua siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vyauovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, nakwamba mvunje kila nira?

Je, mstari huu unafundisha kwamba tunaweza kuvunja vifungo vya mapepo juu yawatu kwa kufunga? Labda, kama utatolewa katika mantiki yake. Hebu tumshinde Shetanikwenye mchezo wake mwenyewe (kutoa maandiko katika mantiki yake) na kusomasehemu kubwa ya sura ya 58 ya Isaya, ili tujue Mungu alikuwa anasema nini hapo.

Piga kelele, usiache. Paza sauti yako kama tarumbeta; uwahubiriwatu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao (58:1)

Hapo, Mungu alikuwa anazungumza na Isaya, akimwagiza kuwatangaziaIsraeli dhambi zao. Katika mstari unaofuata, Mungu akaanza kuorodhesha dhambizenyewe.

Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kamavile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutakakwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu (58:2).

Ni wazi kwamba Waisraeli walidai kuwa wenye haki, lakini dini yao ilikuwamfano tu. Walikuwa wanaigiza ibada. Wnamwuliza Mungu hivi:

Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu,lakini huangalii? (58:3a).

Mungu akajibu hivi:

Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe,na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyimwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwangumu ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sautiyenu juu. Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je!Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kamaunyasi, na kutanga nguo za magunia na majivu chini yake? Je!

Page 26: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA? (58:3b– 5).

Inaonekana kwamba Waisraeli walikuwa wanafunga ili kumfanya Mungu awaone aukupata upendeleo fulani Kwake, nao wakashangaa maana hali zao hazikubadilika. Munguakawajibu kwa kuwakumbusha juu ya maisha yao ya kibinafsi, yaliyokuwayanaonyeshwa hata siku za kufunga kwao. Hata sababu zao za kufunga zilikuwa zakibinafsi tu, na kufanya kufunga huko kusikubalike kwa Mungu. Kisha akawaambia ainaya kufunga anayotafuta – mfungo usiotokana na ubinafsi.

Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungovya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa,na kwamba mvunje kila nira? Je! Siyo kuwagawia wenye njaachakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbanikwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo, wala usijifichena mtu mwenye damu moja nawe? (58:6, 7).

Je, Mungu alikuwa anasema tendo la kufunga litawaweka watu huru wasifungwe napepo? Hapana. Mungu aliwataka waache ubinafsi, si chakula. Alitaka wawapende jiranizao kama nafsi zao. Alitaka wavunje nira, “kuwaacha huru walioonewa,” kugawanachakula chao na wenye njaa, kuwaingiza maskini wasio na makao nyumbani mwao, nakuwavika nguo walio uchi. Tendo la kuacha kula pekee halitaleta mambo hayo. Hayo nimambo ambayo watu lazima wafanye.

Tafsiri hii inakuwa dhahiri tunapoendelea kusoma. Kama Waisraeli wangeanzakufunga bila kufuata maisha yao ya ubinafsi, ahadi ya Mungu ni hii:

Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokeamara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyumaukulinde. Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimihapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyoshakidole, walakunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, nakuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani,na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri (58:8-10. Maneno mepesikukazia).

Mstari wa 9 unaweka wazi kabisa kwamba Mungu hakuwa anasema juu YakeMwenyewe kuondoa nira ya kipepo kama itikio la kufunga kwao. Badala yake, alikuwaanasema kwamba wao ndiyo walitakiwa kuondoa vifungo vya kibinadamu – si vyakipepo – kutoka kwa watu, kama vile kutowatendea haki na umaskini.

Mungu alikuwa anajali zaidi Waisraeli wajiepushe na ubinafsi na choyo, kulikoalivyojali kujiepusha kwao na chakula. Bila shaka huo ndiyo ukweli hata kwetu sisi.Amri ya pili iliyo kuu ni “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe” (Marko12:31), siyo “Hakikisha kwamba unafunga mara nyingi”!

Wazo kwamba tunaweza kuwafungua watu kutoka vifungo vya Shetani kwa tendo lakufunga ni kosa. Njia ya msingi ya kuwafungua watu kutokana na kufungwa kwao naShetani ni kuwaambia habari njema – Injili. Wakipokea kwa imani, watawekwa huru.Ndipo tunapoweza kuuwafundisha jinsi ya kumpinga Shetani kwa imani katika Neno laMungu.

Page 27: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Vita Ya Kiroho Ya Kimaandiko

Tumetaja hekaya nyingi za kisasa zinazohusiana na vita ya kiroho mpaka hapa. Lakinitujiulize: Je, kuna aina ya vita ya kiroho ambayo ni ya kimaandiko? Jibu ni ndiyo, natutashughulika na hilo wakati huu.

Pengine kitu cha kwanza tunachohitaji kufahamu kuhusu vita ya kiroho ni kwamba,haipaswi kuwa kiini cha maisha yetu ya Kikristo. Tunatakiwa kumtazama Kristo,kumfuata na kumtii Yeye, kadiri tunavyoendelea kukua na kufanana Naye. Ni sehemundogo sana ya Maandiko ya Agano Jipya yenye kusema juu ya vita ya kiroho, na hilolinatuonyesha kwamba kinapaswa kuwa kitu chenye kupewa mtazamo mdogo katikamaisha yetu ya Kikristo.

Cha pili tunachohitaji kujua ni kwamba Biblia inatueleza kila tunachohitaji kufahamujuu ya jambo hilo. Hatuna haja ya utambuzi wa kpekee (au mhubiri mwenye kudaikwamba ana utambuzi wa kipekee) kuhusu “mambo ya ndani sana ya Shetani.” Vita yakiroho KiBiblia ni rahisi tu. Mbinu za Shetani zinafunuliwa vizuri katika Maandiko.Wajibu zetu zimeainishwa vizuri kabisa. Ukiisha fahamu na kuamini yote aliyosemaMungu, unahakikishiwa ushindi katika mapambano hayo ya kiroho.

Kurudi Mwanzo

Hebu turudi mpaka mwanzo – katika kitabu cha Mwanzo – mahali tunapokutana naShetani kwa mara ya kwanza. Katika sura za mwanzo hapo, Shetani anatokea katikaumbo la nyoka. Kama kuna mashaka kwamba ni Shetani, Ufunuo 20:2 inaondoa mashakahayo, hivi: “Akamshika yule nyoka, yule joka wa zamani, yaani Ibilisi na Shetani”(maneno mepesi kukazia).

Mwanzo 3:1 inasema hivi: “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wamwitu aliowafanya BWANA Mungu.” Unapofikiri juu ya werevu wa baadhi ya viumbewa Mungu wanaposhindana katika kuishi na wanapowinda wenzao, utatambua jinsiShetani alivyo mwerevu. Ila kwa upande mwingine, Shetani hajui kila kitu wala simwenye hekima yote kama Mungu. Basi, hatupaswi kudhani kwamba katika kukabiliananaye, tunazidiwa akili. Yesu alitushauri sisi kuwa “wajanja kama nyoka” (Mathayo10:16. Maneno mepesi kukazia). Paulo anadai kwamba sisi hatukosi kuzijua hila zaShetani (ktk 2Wakor. 2:11) na kwamba sisi tunayo “nia ya Kristo (1Wakor. 2:16).

Shetani alitupa mshale wake wa kwanza wa moto ulioandikwa katika Biblia kwakumwuliza Hawa maswali juu ya alichosema Mungu. Jibu lake lingemfunulia kamaalikuwa na nafasi ya kumdanganya asimtii Mungu. Shetani hana njia yoyote yakumdanganya mtu anayemwamini na kumtii Mungu kwa alichosema. Ndiyo sababumkakati wake wote umejengwa kwenye mawazo yenye kupingana na Neno la Mungu.

Shetani akamwuliza, “Kwa hiyo Mungu amesema, ‘Msile matunda ya mti wowotekatika bustani’?” (Mwanzo 3:1). Utadhani ni swali tu la kawaida kutoka kwa mtuanayeuliza kitu kidogo, lakini Shetani alijua lengo lake.

Hawa akaitika hivi: “Tunaweza kula matunda ya miti yote bustanini, isipokuwa ule wakatikati. Mungu alisema, ‘Msile matunda yake wala msiuguse, msije mkafa’!” (Mwanzo3:2, 3).

Hawa alikaribia. Ukweli ni kwamba Mungu hakuwakataza kuugusa mti wa ujuzi wamema na mabaya. Aliwakataza kula matunda yake tu.

Hawa alijua ukweli kiasi cha kutosha kutambua uongo wa jibu la Shetani, kwamba,“Hakika hamtakufa!” (Mwanzo 3:4). Maneno hayo yalikuwa kinyume kabisa na kilealichosema Mungu, na isingewezekana Hawa aamini. Hivyo, Shetani akatia sukari uongowake, kwa kuongeza ukweli kidogo, kama ilivyo kawaida yake ili kurahisisha kumeza.

Page 28: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Aliendelea hivi: “Maana, Mungu anajua kwamba siku mtakayokula matunda yakemtafunguliwa macho na kuwa kama Mungu, wenye kujua mema na mabaya” (Mwanzo3:5).

Shetani alisema mambo matatu ambayo yalikuwa ya kweli, baada ya kusema uongo.Tunajua kwamba baada ya Adamu na Hawa kula lile tunda, macho yao yalifunguliwa(Mwa. 3:7) kama Shetani alivyokuwa amesema. Tena, Mungu Mwenyewe baadayealisema kwamba huyo mtu amekuwa kama Mungu na kwamba alikuwa anajua mema namabaya (Mwanzo 3:22). Angalizo: Shetani huchanganya kweli na uongo mara kwa maraili kuwadanganya watu.

Ona vile vile kwamba Shetani alikashifu tabia ya Mungu. Mungu hakutaka Adamu naHawa wale tunda lililokatazwa kwa faida yao na furaha yao, lakini Shetani akaligeuzaikawa kana kwamba Mungu anawaficha kitu kizuri. Sehemu kubwa ya uongo wa Shetanihumkashifu Mungu kuhusu tabia Yake, nia Yake na makusudi Yake.

Bahati mbaya ni kwamba wanandoa wa kwanza duniani walikataa ukweli ili waaminiuongo, nao wakapatikana na matokeo ya hilo. Lakini, ona vipengele vyote vya vita yakiroho ya kisasa katika kisa chao: Silaha pekee ya Shetani ilikuwa uongo,uliochanganywa na ukweli. Wanadamu hao walikabiliwa na uchaguzi kati ya kuaminikilichosemwa na Mungu au kilichosemwa na Shetani. Kuamini ukweli ingekuwa “ngaoya imani” kwao, lakini wao hawakuichukua wala kuishika.

Vita Ya Kiroho Ya Yesu

Tunaposoma juu ya mapambano ya Yesu na Shetani wakati wa kujaribiwa Kwakehuko nyikani tunapata kuona upesi kwamba Shetani hajabadilisha mbinu zake kwa miakaelfu nyingi. Njia yake ya kushambulia ilikuwa kukashifu alichosema Mungu, naye alijuanjia pekee adui ni kumwondoa kwenye kuamini au kutii kweli ya Mungu. Hapa tena,kiini cha mapambano ni Neno la Mungu. Shetani akatupa uongo wake, na Yesuakausukumia pembeni kwa ukweli. Yesu aliamini na kutii yale ambayo Mungu alikuwaamesema. Hiyo ndiyo vita ya kiroho kulingana na Biblia.

Yesu alikabiliwa na hali kama ya Hawa, Adamu na sisi wengine wote. Ilibidi aamuekama atamsikia Mungu au Shetani. Yesu alipigana vita Yake ya kiroho kwa “upanga waRoho” ambao ni Neno la Mungu. Hebu tuone tunachoweza kujifunza kutokana namapambano ya kiroho na Shetani.

Akisimulia jaribu la pili la Yesu, Mathayo anasema hivi:

Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu yakinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu,jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake;na mikononi mwao watakuchukua; usije ukajikwaa mguu wakokatika jiwe. Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, UsimjaribuBwana Mungu wako (Mathayo 4:5-7).

Hapo tena jambo kuu lilikuwa Mungu kasema nini. Shetani alikariri mpaka maandikoya Zaburi ya tisini na moja, lakini aliyageuza ili kuyafanya yamaanishe kitu tofauti namaana ya Mungu.

Yesu akajibu kwa kutaja andiko lingine lililofanya ahadi ya Mungu kuhusu ulinzikatika Zaburi 91 ieleweke vizuri. Mungu atatulinda, ila, hatafanya hivyo tukitenda kwaujinga, - yaani, “kumtia majaribuni”.

Ndiyo sababu ni muhimu sana kwamba hatuondoi mistari ya Biblia katika mantikiyake. Kila andiko lazima lilinganishwe na kinachosemwa na Maandiko mengine.

Page 29: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Kupindua Maandiko ni mbinu ya kawaida kabisa ya Shetani katika vita ya kiroho, nainasikitisha kwamba amefanikiwa sana kuwapata Wakristo wengi walionaswa katikakundi la vita ya kiroho ya kisasa kwa njia hiyo. Mfano mzuri wa hilo ni jinsialivyopindua neno la KiBiblia kabisa – “kuangusha ngome” – ili kuunga mkono dhana yakuwaangusha mapepo kutoka katika anga. Kama tulivyokwisha ona mapema, manenohayo, yakisomwa katika mantiki yake, hayahusiani na kuangusha mapepo katika angahata kidogo. Ila, Shetani angependa sana tudhani hivyo, ili tupoteze muda wetu tukipigakelele dhidi ya falme na mamlaka angani.

Tunasoma hivi katika maelezo ya Mathayo kuhusu jaribu la tatu la Yesu,

Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno,akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. NdipoYesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maanaimeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye pekeyake (Mathayo 4:8-10).

Hilo lilikuwa jaribu la kupata uwezo. Kama Yesu angemwabudu Shetani, na kamaShetani angetimiza ahadi yake, Yesu angepata umakamu katika ufalme wa giza.Angetawala juu ya kila mwanadamu ambaye hajaokoka, na juu ya mapepo wote, naangekuwa na mamlaka duniani kote, sawa tu na Shetani alivyokuwa nayo. Ni kitukisichofikirika kwamba nini kingetokea, kama Yesu angekubali jaribu hilo.

Ona tena hapa kwamba Yesu alipingana na mawazo ya Shetani kwa Neno la Mungulililoandikwa. Katika kila jaribu kati ya majaribu yale matatu, Yesu alishinda kwakusema hivi: “Imeandikwa.” Sisi pia, lazima tulijue Neno la Mungu na kuliamini, kamatunataka kuepuka kudanganywa na kutumbukia katika mitego ya Shetani. Hayo ndiyomambo ya vita ya kiroho.

Uwanja Wa Vita

Kwa sehemu kubwa ni kwamba, nguvu pekee Shetani na pepo zake waliyo nayo niuwezo wa kupanda mawazo katika mioyo na akili za watu (na hata katika hilowamewekewa mipaka na Mungu – ona 1Wakor. 10:13). Hebu basi tutazame Maandikomachache, yafuatayo:

Petro akasema, Anania! Kwa nini Shetani amekujaza moyo wakokumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu yathamani ya kiwanja? (Matendo 5:3. Maneno mepesi kukazia).

Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtiaYuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti … (Yohana13:2. Maneno mepesi kukazia).

Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwishowengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, namafundisho ya mashetani … (1 Timo. 4:1. Maneno mepesikukazia).

Page 30: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Lakini nachelea, kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwahila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu nausafi kwa Kristo (2Wakor. 11:3. Maneno mepesi kukazia).

Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faraghakwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwakutokuwa na kiasi kwenu (1Wakor. 7:5. Maneno mepesi kukazia).

Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalitumamtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabuyetu ikawa haina faida (1Wathes. 3:5. Maneno mepesi kukazia).

...ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zaowasioamini, isiwazuikie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliyesura yake Mungu (2Wakor. 4:4. Maneno mepesi kukazia).

Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwayeIbilisi na Shetani, audanganye ulimwengu wote; akatupwa hatanchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye (Ufunuo 12:9.Maneno mepesi kukazia).

Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, na tamaa za baba yenbu ndizompendazo kuzitenda. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; walahakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeyeni mwongo, na baba wa huo (Yohana 8:44. Maneno mepesikukazia).

Maandiko hayo na mengine yanaweka wazi kabisa kwamba uwanja wa vita wa msingikatika vita ya kiroho KiBiblia ni mioyo yetu na akili zetu. Shetani hutushambulia kwamawazo – ushauri mwovu, mawazo mabaya, misimamo ya uongo, majaribu, udanganyifumbalimbali na kadhalika. Njia pekee yetu ya kujilinda ni kujua, kuamini na kutendakulingana na Neno la Mungu.

Ni muhimu sana sana uelewe kwamba kila wazo unalowaza halitoki ndani yako.Shetani ana wasemaji wengi sana wanaomsaidia kupanda mawazo yake katika akili zawatu. Anafanya kazi ya kutushawishi kwa njia ya magazeti, vitabu, televisheni, majarida,redio, marafiki na majirani, na hata kupitia wahubiri. Hata mtume Petro kuna wakatialitumiwa kama msemaji wa Shetani bila kujua, akimshauri Yesu kwamba haukuwampango wa Mungu Kwake afe msalabani (ona Mathayo 16:23).

Ila, Shetani na pepo wachafu hufanya kazi ya kushambulia mawazo na akili zabinadamu moja kwa moja, bila ya kutumia mwanadamu mwingine, na Wakristo wotewatakutana na hali hiyo wakati fulani. Hapo ndipo vita huanza.

Namkumbuka mwanamke mmoja Mkristo – mpendwa sana – aliyekuja kwangukutubu tatizo alilokuwa nalo. Yeye alisema kwamba kila anapoingia katika sala, alijikutaanawaza mawazo ya kufuru na maneno ya kulaani. Alikuwa mama mpole, mwema,mkarimu, muungwana, mzuri sana na aliyejitoa katika wanawake wote kanisani, lakinialikuwa na tatizo hilo la mawazo mabaya.

Nilimweleza kwamba hayo mawazo mabaya si yake, bali alikuwa anashambuliwa naShetani, aliyekuwa anataka kumharibia uombaji wake. Ndipo akaniambia kwamba

Page 31: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

ameacha kuomba kwa sababu alikuwa anaogopa sana kwamba atawaza mawazo hayomabaya. Shetani akawa amefanikiwa.

Nikamwambia ni vizuri aanze kuomba tena, na mawazo hayo ya kufuru yakimjia,ayapinge kwa ukweli kutoka Neno la Mungu. Wazo likimjia kwamba, “Yesu alikuwa ------,” yeye alipinge kwa kusema, “Hapana! Yesu alikuwa na bado ni Mwana wa Mungu.”Wazo likimjia ambalo ni neno la kufuru, alibadilishe kwa kuwaza sifa kwa Yesu, nakadhalika.

Nikamwambia vile vile kwamba kwa kuogopa kwamba atawaza makosa, alikuwaanayakaribisha, maana hofu ni imani kinyume – ni kumwamini Shetani. Kwa kujaribukutowaza kitu, inabidi tukiwaze ili tuache kukiwaza (asomaye na afahamu!)

Kwa mfano: Nikikwambia, “Acha kufikiri kuhusu mkono wake wa kuume,” maramoja utaanza kufikiri juu yake unapojaribu kunitii. Kadiri utakavyojitahidi kutowaza,ndivyo utakavyozidi kuwaza. Njia pekee ya kutowaza juu ya mkono wako wa kuume nikuamua kufikiri juu ya kitu kingine, kama, viatu vyako. Ukisha fikiri kuhusu viatu vyako,hutafikiri juu ya mkono wako.

Nilimtia moyo yule mama “asiogope”, kama Biblia inavyotuagiza. Na kilaalipotambua wazo kinyume na Neno la Mungu, nilimshauri alibadilishe na linginelililokubaliana na Neno la Mungu.

Nafurahi kusema kwamba alifuata ushauri wangu, na ingawa alishambuliwa marakadhaa tena katika vipindi vya maombi, alipata ushindi kamili juu ya tatizo lake. Aliwezakushinda vita ya kiroho.

Vile vile nilishangaa kugundua baada ya kufanya utafiti katika makanisa kadhakwamba tatizo lake lilikuwa kawaida ya wengi. Zaidi ya nusu ya Wakristo ambaoniliwahoji wanaonyesha kwamba wakati mmoja au mwingine wamewahi kuwa namawazo ya kufuru wakati wakiomba. Shetani hagundui mbinu mpya – anatumia zile zile.

“Jihadhari Unasikiliza Nini”

Hatuwezi kumzuia Shetani na pepo wabaya kushambulia akili na mawazo yetu, lakinisi lazima turuhusu mawazo yao yawe mawazo yetu. Yaani – hatupaswi kufikiri mawazoya kipepo na ushauri wao, na kuyafanya yawe yetu. Kama inavyosemekana, “Huwezikuwazuia ndege kuruka juu ya kichwa chako, lakini unaweza kuwazuia wasijenge kiotakatika nywele zako.”

Tena – tuwe makini tusiruhusu akili zetu kupata ushawishi mwovu kila tunapoweza.Tunapoketi mbele ya televisheni kwa saa nzima, au kusoma gazeti, tunakuwa tumetoanafasi kwa akili zetu kushawishiwa na kuingiwa na mawazo ya kishetani. Mara tu baadaya kusimulia mfano wa mpanzi na mbegu, Yesu alitoa onyo lifuatalo: “Angalienimsikialo” (Marko 4:24). Yesu alijua matokeo mabaya ya kusikiliza uongo – yakumruhusu Shetani apande “mbegu” zake katika mioyo na akili zetu. Mbegu hizozinaweza kukua na kuwa “miiba na michongoma” ambayo mwishoni italisonga Neno laMungu katika maisha yetu (ona Marko 4:7, 18, 19).

Asemavyo Petro Kuhusu Vita Ya Kiroho

Mtume Petro alielewa vita ya kiroho ya kweli, kulingana na Biblia. Hakuna popotekatika nyaraka zake anapowashauri Wakristo waangushe ngome za falme na mamlakakatika miji. Ila, aliwashauri wakabiliane na mashambulizi ya Shetani katika maisha yaobinafsi, na aliwaambia jinsi ya kufanya hivyo.

Page 32: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kamasimba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwamateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani(1Petro 5:8-9).

Ona kitu cha kwanza anacho-onyesha Petro ni kwamba sisi kazi yetu ni kujilinda, sikushambulia. Shetani ndiye mwenye kuzunguka-zunguka, siyo sisi. Yeye ndiyeanayetutafuta, sisi hatumtafuti. Kazi yetu si kushambulia, bali ni kupinga mashambulizi,au kuyakabili.

Pili: Ona kwamba Shetani, kama simba, anatafuta wa kummeza. Anawezaje kumezaWakristo? Je, Petro alimaanisha kwamba Shetani anaweza kula nyama yao, sawa nasimba? Sivyo hata kidogo. Njia pekee ya Shetani kummeza Mkristo ni kwa kumdanganyakuamini uongo ambao utaharibu imani yake.

Tatu – ona kwamba Petro anatuambia tumpinge Shetani kwa kupitia imani yetu.Mapambano yetu si vita ya mwili, na hatuwezi kupigana na Shetani kwa kutumia ngumizetu kupiga hewani. Yeye hutushambulia kwa uongo, nasi tunapinga uongo huo kwakusimama imara katika imani yetu kwenye Neno la Mungu. Hiyo tena ndiyo vita yakiroho kulingana na Maandiko.

Wakristo ambao Petro aliwaandikia walikuwa wanapitia mateso makali mno, nawalikuwa katika jaribu kubwa la kuikana imani yao. Mara nyingi tunapokuwa katikati yamazingira magumu, Shetani hushambulia kwa mashaka yake na uongo wake. Huo ndiyowakati wa kusimama imara katika imani yako. Hiyo ndiyo “siku ya uovu” ambayo Pauloaliandika habari zake, unapohitaji “kuvaa silaha zote za Mungu, ili uweze kusimamaimara kinyume cha hila za Shetani” (Waefeso 6:11. Maneno mepesi kukazia).

Asemavyo Yakobo Kuhusu Vita Ya Kiroho

Mtume Yakobo pia alisema kitu juu ya vita ya kiroho katika waraka wake. Je,aliwaambia Wakristo kwamba sala zao zingeamua matokeo ya vita za malaika? Hapana.Je, aliwaambia waangushe pepo wa ashiki, kutokujali na ulevi walio juu ya miji yao?Hapana. Je, aliwaambia wajifunze historia ya miji yao ili waweze kujua aina za pepowaliokuwepo tangu mwanzo wa mji? Hapana!

Yakobo aliamini kuhusu vita ya kiroho kulingana na Maandiko. Basi, aliandika kamaifuatavyo:

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia (Yakobo4:7. Maneno mepesi kukazia).

Hapo tena ona kwamba nafasi ya Mkristo ni kujilinda – tunapaswa kupinga, sikushambulia. Tukifanya hivyo, Yakobo anatuahidi kwamba Shetani atakimbia. Hanasababu ya kukaa karibu na Mkristo ambaye hatashawishiwa kuamini uongo wake, walakufuata ushauri wake, au kukubaliana na majaribu yake.

Vile vile ona kwamba Yakobo kwanza anashauri tumtii au kumyenyekea Mungu.Tunafanya hayo kwa kulitii Neno Lake. Kumpinga kwetu Shetani kumejengwa kwenyekulitii na kulinyenyekea Neno la Mungu.

Page 33: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Asemavyo Yohana Kuhusu Vita Ya Kiroho

Hata mtume Yohana aliandika kuhusu vita ya kiroho katika waraka wake wa kwanza.Je, alituambia tupande juu ili kuangusha ngome za Shetani? Hapana. Je, alituambia tutoepepo wa hasira kutoka kwa Wakristo ambao hukasirika mara kwa mara? Hapana!

Badala yake, Yohana – sawa na Petro na Yakobo – aliamini katika vita ya kirohokulingana na Maandiko. Basi, ushauri wake unafanana na wenzake, hivi:

Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwambazimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengiwametokea duniani. Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kilaroho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokanana Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Nahii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja;na sasa imekwisha kuwako duniani. Ninyi, watoto wadogo,mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeyealiyendani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. Hao ni wadunia; kwa hiyo wanena ya dunia na dunia huwasikia. Sisitwatokana na Mungu. Yeye amjuaye Mungu atusikia; yeyeasiyetokana na Mungu hatusikii. Katika hili twamjua Roho wakweli, na roho ya upotevu (1Yohana 4:1-6).

Ona kwamba hoja nzima ya Yohana katika mistari hii inahusu uongo wa Shetani nakweli ya Mungu. Tunapaswa kuzipima roho ili tuone kama zinatoka kwa Mungu, nakipimo kimejengwa kwenye kweli. Pepo hawatakiri kwamba Yesu Kristo alikuja katikamwili. Wao ni waongo.

Pia, Yohana alituambia kwamba tunapaswa kuwashinda pepo wachafu. Yaani, kamaraia wa ufalme wa nuru, hatuko chini ya utawala wao tena. Aliye mkuu zaidi – Yesu –anakaa ndani yetu. Watu walio na Kristo ndani yao hawapaswi kuogopa pepo.

Tena Yohana akasema kwamba dunia huwasikiliza pepo wabaya, kitu kinacho-onyesha kwamba pepo bila shaka huzungumza. Tunajua hawazungumzi kwa sauti, lakiniwanapanda uongo ndani ya mawazo ya watu.

Kama wafuasi wa Kristo, hatupaswi kusikiliza uongo wa mapepo. Yohana anasemakwamba wale wanaomjua Mungu wanatusikiliza sisi, kwa sababu tunayo kweli. TunaloNeno la Mungu.

Hapa tena ona kwamba mkakati wa Shetani ni kuwashawishi watu kuamini uongowake. Shetani hawezi kutushinda kama tunajua na kuiamini kweli. Vita ya kirohokulingana na Maandiko iko hivyo.

Ufunguo Ni Imani

Kulijua Neno la Mungu tu hakutoshi kushinda vita ya kiroho. Siri ni kuamini kweli nakwa dhati kile ambacho Mungu amesema. Hiyo ni kweli katika kumpinga Shetani nakukemea pepo. Kwa mfano: Hebu tazama tena mfano ambao tumekwisha utazamamapema, wakati Yesu alipowapa wanafunzi Wake kumi na mbili “mamlaka juu ya pepowabaya, kwamba wawatoe” (Mathayo 10:1). Sura saba baadaye, tunawakuta wakiwawameshindwa kutoa pepo katika mtoto aliyekuwa na kifafa.7 Yesu aliposikia juu yakushindwa kwao, alisikitika sana na kusema hivi:

7 Tuwe makini – tusidhani kila tukio la kifafa linatokana na pepo kuwa ndani ya mtu.

Page 34: Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi - davidservant.com fileHekaya Za Kisasa Kuhusu Vita Ya Kiroho – Sehemu Ya 2 Tunaendelea na sura hii kwa kutazama mafundisho mengine yanayopendwa

Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hatalini? Nitachukuliana nanyi hata lini? (Mathayo 17:17. Manenomepesi kukazia).

Yesu alisikitishwa na kutokuamini kwao. Tena, baadaye wakati wanafunzi Wakewalipomwuliza sababu ya wao kushindwa kumtoa huyo pepo, Yesu aliwajibu hivi: “Kwasababu ya upungufu wa imani yenu” (17:20). Basi tunaona kwamba mamlaka yao yakutoa pepo hayakufanya kazi bila ya imani yao.

Kufaulu kwetu katika kutoa pepo na kumpinga Shetani kunategemeana na imani yetukatika Neno la Mungu. Kama kweli tunaamini alichosema Mungu, basi tutazungumzahivyo na kutenda kulingana na hivyo. Mbwa huwafukuza watu wanaowakimbia. Shetaninaye yuko hivyo hivyo. Ukikimbia, Shetani atakukimbiza. Ukisimama thabiti katikaimani yako, yeye ndiye atakukimbia (ona Yakobo 4:7).

Bila shaka kutokuwa na imani kwa mitume kungedhihirka kwa kila mtazamaji,walipojaribu bila kufanikiwa kutoa pepo katika yule mtoto. Kama pepo huyo alifanyavituko vile vile alivyofanya mbele za Yesu – kumwangusha mtoto chini “akitetemekasana” (Luka 9:42) na kumfanya atoke povu mdomoni (Marko 9:20), yawezekana imaniya wanafunzi iligeuka kuwa hofu. Bila shaka walipigwa na butwaa kwa mambowaliyokuwa wanaona.

Ila, mtu mwenye imani, hatishwi na mambo anayoyaona, bali anaguswa na kileambacho Mungu amesema. “Maana tunaenenda kwa imani, si kwa kuona” (2Wakor. 5:7.Maneno mepesi kukazia). Mungu hawezi kudanganya (ona Tito 1:2). Hivyo basi, hatakama mazingira yetu yataonekana kama yenye kuwa kinyume na kile ambacho Munguamesema, tunapaswa kusimama imara katika imani.

Ona kwamba Yesu alimweka huru yule mtoto katika muda mfupi sana. Alifanya hivyokwa imani. Yeye hakupoteza wakati “akikemea.” Walio na imani na mamlakawaliyopewa na Mungu hawana haja ya kutumia masaa wakitoa pepo.

Tena – hakuna taarifa kwamba Yesu alimpigia kelele yule pepo. Wenye imani hawanahaja ya kupiga kelele. Wala Yesu hakumwamuru huyo pepo kumtoka kwa kurudia-rudia.Amri moja tu ilitosha. Amri ya pili ingekuwa kukiri mashaka.

Hitimisho

Mtumishi mwenye kufanya wengine kuwa wanafunzi hufundisha vita ya kirohokulingana na Maandiko kwa mfano wake mwenyewe na kwa maneno yake. Kusudi ni iliwanafunzi wake waweze kusimama imara dhidi ya mbinu za Shetani na kuenenda katikakutii maagizo ya Kristo. Hawaongozi wanafunzi wake kufuata “kila upepo wa mafundisho”ya kisasa yenye kuendeleza njia zisizo za Biblia za vita ya kiroho, maana anajua kwambawale wanaozitumia na kuzifuata wamepotoka kimtazamo, na ukweli ni kwambawamedanganywa na huyo huyo Shetani wanayedai kwamba wanapambana naye kwaushindi na kumweza.