mkataba wa huduma kwa mteja mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 wizara ya katiba na...

12
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Upload: others

Post on 31-Oct-2020

26 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Wakala wa Usajili Ufi lisina Udhamini

Wakala wa Usajili Ufi lisi

Mkataba wa Hudumakwa Mteja

Page 2: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

1

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Mkataba wa Huduma kwa Mteja

YALIYOMO

1.0 DIBAJI 2

2.0 DIRA, DHIMA, MAADILI YA UTENDAJI KAZI 3

2.1 Dira 3

2.2 Dhima 3

2.3 Maadili yetu 3

3.0 MADHUMUNI YA MKATABA 3

4.0 WATEJA WETU 3

5.0 HUDUMA ZETU 4

6.0 VIWANGO VYA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA 5

6.1 Mahusiano 5

6.2 Viwango vya muda 6

7.0 WAJIBU WA WAKALA KWA MTEJA 9

8.0 HAKI NA WAJIBU WA MTEJA 9

8.1 Haki ya Mteja 9

8.2 Wajibu wa Mteja 9

9.0 MREJESHO KUHUSU MKATABA 10

10.0 NJIA ZA KUWASILIANA NA WAKALA 10

Page 3: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Mkataba wa Huduma kwa Mteja2

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

1.0 DIBAJI

Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini – RITA, ulizinduliwa rasmi Tarehe 23 Juni 2006 kutoka iliyokuwa Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali ambayo ilijulikana sana kama Ofi si ya Vizazi na Vifo, Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka. Wakala umechukua majukumu yaliyokuwa yakifanywa na Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali ambayo yanajumuisha shughuli za Usajili, Ufi lisi na Udhamini.

Lengo la Mkataba huu ni kuweka bayana huduma tunazozitoa, viwango vya huduma hizo na pia utaratibu wa kutoa mrejesho kuhusu huduma zetu. Mkataba huu ni ahadi yetu kwenu kuwa tutatoa huduma zetu kwa kuzingatia maadili ya kiutendaji. Mkataba huu utaendelea kuboreshwa kulingana na mahitaji ya utoaji huduma yatakayozingatia mabadiliko ya ki-siasa, ki-uchumi, ki-jamii na ki-teknolojia kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji.

Ni matarajio yetu kuwa mtashirikiana nasi kwa kutoa mrejesho kwa njia mbalimbali ili kutuwezesha kuwapa huduma bora zaidi na kukidhi matarajio yenu.

................................................................ .................................................

Phillip G. Saliboko TareheAFISA MTENDAJI MKUU,Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Page 4: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

3

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Mkataba wa Huduma kwa Mteja

2.0 DIRA, DHIMA, MAADILI YA UTENDAJI KAZI

2.1 Dira Dira yetu ni kuwa chombo chenye ufanisi katika utoaji wa huduma za

Usajili, Ufi lisi na Udhamini nchini

2.2 Dhima Dhima yetu ni kutoa huduma za hali ya juu katika Usajili, Ufi lisi na

Udhamini ili kuchangia katika upatikanaji wa haki.

2.3 Maadili Yetu • Uadilifu • Uzalendo • Ushirikiano • Utaaluma/Ueledi • Ukarimu na Usikivu

3.0 MADHUMUNI YA MKATABA

Madhumuni ya mkataba huu ni kuweka bayana huduma tunazozitoaviwango vya huduma hizo na matarajio ya wateja. Aidha, Mkatabahuu umeweka wazi utaratibu wakutoa mrejesho utakaotuwezeshakuboresha huduma zetu.

4.0 WATEJA WETU

Tunatoa huduma mbali mbali kwa wateja na wadau wafuatao:• Wafanyakazi wa RITA• Viongozi wa Dini – Mapadre, Wachungaji, Mashehe n.k • Mawakili wa Kujitegemea• Wadhamini wa Taasisi• Warithi wa Mirathi inayosimamiwa na RITA• Mabalozi wa wakilishi wa nchi za nje• Wadeni/Wadaiwa wa Makampuni yanayofi lisiwa

Page 5: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Mkataba wa Huduma kwa Mteja4

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

• Wadai mbali mbali wa RITA• Wadeni mbali mbali wa RITA• Waombaji wa Vyeti vya Kuzaliwa• Waombaji wa Vyeti vya Vifo• Waombaji wa Vyeti vya Ndoa • Waombaji wa Vyeti vya Talaka• Waombaji wa Usajili wa Udhamini• Vizazi,Vifo, Ndoa na Talaka• Waombaji wa Leseni za kufungisha ndoa• Waombaji wa kibali cha kufungisha Ndoa sehemu maalum• Waombaji wa Shahada ya kutokuwepo na pingamizi la kufunga

Ndoa• Makatibu Tawala wa Wilaya• Waombaji wa Vyeti vya Kuasili• Wateja wa Ufi lisi • Wateja wa huduma za Wosia• Waombaji wa Ushauri wa Kisheria• Wizara, Idara zinazojitegemea, Hospitali, Zahanati, Mashirika ya

Umma, na Wakala za Serikali• Wazabuni• Wadau wa Maendeleo kama vile UNICEF, PLAN

INTERNATIONAL-TANZANIA, UNDP n.k • Waombaji wa Usajili wa Makubaliano ya kisheria (Deeds of

Arrangement)• Waombaji wa Takwimu mbali mbali zanazohusiana na kazi za

Wakala wa RITA• Wajumbe wa Bodi ya Ushauri

5.0 HUDUMA ZETU

Tunatoa huduma mbalimbali kama zilivyoainishwa hapa chini; • Kusajili Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka• Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa, Vifo, Ndoa, Talaka na Kuasili• Kutoa Shahada ya kutokuwepo na Pingamizi la kufunga Ndoa

Page 6: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

5

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Mkataba wa Huduma kwa Mteja

• Kutoa Shahada ya Muunganisho wa Wadhamini • Kuthibitisha nyaraka/nakala mbali mbali hususan zile zitolewazo

na ofi si yetu mfano vyeti vya Kuzaliwa, Ndoa, Vifo, Talaka n.k• Kutoa Shahada za Ndoa• Kutoa Leseni za kufungisha Ndoa kwa Viongozi wa Dini mfano

Mapadre, Wachungaji, Mashehe n.k• Kutoa kibali cha kufungisha Ndoa mahali maalum• Kutoa kibali cha kufunga Ndoa ya Haraka bila kutangaza siku 21• Kutayarisha na kuhifadhi Wosia• Kutoa Ushauri wa Kisheria • Kusimamia Mirathi, Mali za Wafi lisiwa na mali zisizo kuwa na

wenyewe• Kutoa taarifa na takwimu mbali mbali zinazohusiana na kazi

zetu za Wakala• Kutoa Huduma za Ufi lisi• Kulipa na kupokea malipo mbalimbali• Kujenga uwezo wa Watumishi kitaaluma• Kutoa vitendea kazi• Kujibu na kuandika barua• Kupiga na kujibu simu• Kusimamia Viapo na kuandaa nyaraka mbali mbali za Kisheria• Kuendesha mashauri Mahakamani

6.0 VIWANGO VYA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

Wakala wetu unaahidi kutoa huduma zake kupitia Idara zake kamaifuatavyo:-

6.1 MahusianoKatika kuhakikisha kuwa Wakala unaboresha mahusiano mazuri nawateja wake• Tutahakikisha kuwa taratibu za upatikanaji wa huduma

zinaeleweka kwa wateja wetu wote.

Page 7: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Mkataba wa Huduma kwa Mteja6

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

• Tutajenga mahusiano ya karibu na wateja wetu kwa kupeleka huduma zetu katika Ofi si ya Mkuu wa Wilaya.

• Tutatoa huduma zetu kwa haki, uwazi, usiri, ukweli, uadilifu, usikivu na kwa kufuata taratibu, kanuni na miongozo ya kazi katika Utumishi wa umma.

6.2 Viwango vya muda

i. Kutoa malipo mbali mbali• Tutatoa malipo ya wateja wetu wa ndani kwa muda wa siku

tatu (3) baada ya kupokea maombi sahihi ya malipo• Tutawalipa wateja wetu wa nje ndani ya siku arobaini na tano

(45) baada ya kuwasilisha/kupokea ankara zao

ii. Kujenga uwezo wa Watumishi kitaaluma• Tutatoa na kugharamia mafunzo kwa wafanyakazi kwa kuzingatia

mpango wa mafunzo katika Taasisi zinazotambulika serikalini.

iii. Kutoa vitendea kazi• Tutatoa vitendea kazi vya Usajili kwa Watendaji wetu wa

Wilayani ndani ya siku tano (5) baada ya kupokea maombi

iv. Kujibu barua na simu• Tutakiri kupokea na kujibu barua ndani ya siku nne (4) baada ya

kupokelewa • Tutapokea simu ndani ya milio mitatu (3) kwa kujitambulisha

Jina na Ofi si/Idara/Kitengo• Tutakiri kupokea na kujibu barua pepe ndani ya siku moja (1)

baada ya kutumwa na kuisoma

v. Kutoa Ushauri wa kisheria • Tutatoa ushauri wa kisheria kuhusu kazi za Wakala ndani ya siku

saba (7) baada ya kupokea maombi na kuyafanyia utafi ti

Page 8: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

7

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Mkataba wa Huduma kwa Mteja

vi. Kusimamia na Ugawaji wa mali za Warithi• Tutasimamia na kugawa mali za warithi kwa haki ndani ya miezi

sita (6) hadi miaka miwili (2) baada ya kupata barua ya uteuzi wa Mahakama kuu na kama Mirathi hiyo haina migogoro.

vii. Kuthibitisha nyaraka mbali mbali kama vile vyeti vya Kuzaliwa, Ndoa, Vifo, Talaka n.k• Tutahakiki na kuthibitisha nyaraka ndani ya siku nne (4) baada ya

kupata maombi na viambatanisho sahihi hasa kwa zile nyaraka zilizoko Makao Makuu ya RITA

• Tutahakiki na kuthibitisha nyaraka ndani ya siku kumi na nne (14) Baadaya ya kupata maombi na viambatanisho husika, Hii ni kwa maombi ambayo kumbukumbu zake bado ziko wilayani

viii. Kutoa shahada za Ndoa• Tutatoa shahada za Ndoa ndani ya siku mbili (2) tokea

kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi/husika

ix. Kutoa vyeti vya Kuzaliwa, Vifo, Ndoa, Talaka, Shahada ya kutokuwepo na pingamizi la kufunga Ndoa, Muunganisho wa Wadhamini na Kuasili• Tutatoa cheti cha Kuzaliwa ndani ya siku tano (5) tokea

kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi • Tutatoa cheti cha Kifo ndani ya siku tatu (3) tokea kuwasilishwa

kwa maombi na viambatanisho sahihi• Tutatoa cheti cha Ndoa ndani ya siku mbili (2) baada ya kupokea

maombi na viambatanisho sahihi• Tutasajili na tutatoa cheti cha Talaka ndani ya siku mbili (2)

baada ya kupokea maombi na viambatanisho sahihi• Tutasajili na tutatoa cheti cha Kuasili ndani ya siku mbili (2)

baada ya kupokea maombi na viambatanisho sahihi• Tutatoa Shahada ya kutokuwepo na pingamizi la kufunga Ndoa

ndani ya siku mbili (2) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi.

Page 9: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Mkataba wa Huduma kwa Mteja8

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

• Tutatoa Shahada ya Muunganisho wa Wadhamini ndani ya siku mbili (2) tokea kuwasilishwa kwa maombi, viambatanisho sahihi, na baada ya kukamilika taratibu za kiserikali

x. Kusajili Vizazi, Vifo, Ndoa na Talaka• Tutatoa huduma ya usajili wa Vizazi na kutoa vyeti vya kuzaliwa

ndani ya siku tatu (3) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi, kwa kizazi kinachozidi siku 90

• Tutatoa huduma ya usajili wa Vifo na vyeti vya kuzaliwa ndani ya siku tatu (3) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi, kwa Vifo vinavyozidi siku 30

xi. Tutatoa Leseni za Kufungisha Ndoa, kibali cha kufungisha Ndoa mahali maalum na kufunga Ndoa ya haraka • Tutatoa Leseni ya kufungisha Ndoa kwa Viongozi wa Dini

ndani ya siku Tatu (3) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi

• Tutatoa kibali maalum cha kufunga Ndoa ya haraka isiyotangazwa kwa muda wa siku 21, ndani ya siku moja (1) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi.

• Tutatoa kibali cha kufungia ndoa mahali maalum ndani ya siku moja (1) tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi.

xii. Kutayarisha na kuhifadhi Wosia• Tutatoa huduma ya kutayarisha Wosia ndani ya siku mbili (2)

tokea kuwasilishwa kwa maombi na viambatanisho sahihi.• Tutatoa huduma ya kuhifadhi Wosia ndani ya siku moja (1)

baada ya kupokea maombi na viambatanisho sahihi

xiii. Kutoa taarifa na Takwimu mbali mbali zinazo husu kazi za Wakala• Tutatoa taarifa na takwimu sahihi zinazohusu kazi za Wakala

ndani ya siku tatu (3) baada ya kupokea maombi

Page 10: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

9

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

Mkataba wa Huduma kwa Mteja

7.0 WAJIBU WA WAKALA KWA MTEJA

Tuna wajibu wa kutoa huduma kwa viwango vya hali ya juu. Aidha,tunatoa ahadi za utekelezaji kama ifuatavyo;

• Kutoa huduma kwa wakati, ubora, usahihi na ushirikiano.• Kutoa taarifa kwa uwazi na maelezo yote kwa lugha ya

kueleweka kwa njia ya vipeperushi, matangazo n.k• Kujenga mtandao ambao utashirikisha Umma katika kutoa

huduma na kupokea maoni. • Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kama njia mbadala

kwa mteja. • Kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa kwa haki sawa,

wanaheshimiwa na inapobidi kupewa kipaumbele kwa wateja walemavu na wazee wasiojiweza.

• Tutashughulikia malalamiko kwa haraka, uwazi na kwa uhakika.

8.0 HAKI NA WAJIBU WA MTEJA

Tumeweka ahadi za viwango vya huduma ili kukidhi matarajio yawateja wetu. Aidha, wateja wana haki na wajibu kama ifuatavyo ;

8.1 Haki ya Mteja• Kusikilizwa• Kuhudumiwa kwa heshima bila upendeleo na kwa wakati• Kutoa maoni • Kulalamika• Kufahamishwa hatua zilizochukuliwa kwenye malalamiko yake• Faragha na kutunziwa siri zinazohusu maelezo yake• Kupata taarifa sahihi na kwa wakati

8.2 Wajibu wa Mteja• Kuleta viambatanisho/taarifa sahihi kwa wakati• Kulipia gharama halisi ya huduma anayopewa

Page 11: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

Mkataba wa Huduma kwa Mteja10

Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini

• Kufi ka kwa wakati wa masaa ya kazi• Kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za kiofi si• Kumsikiliza mtoa huduma• Kumheshimu mtoa huduma

9.0 MREJESHO KUHUSU MKATABA

Maoni yako ni muhimu sana katika kuboresha huduma zetu, kwamantiki hii, tungependakupata maoni au malalamiko yako kuhusianana huduma zetu kwa njia zifuatazo;• Barua kwa kutumia njia ya mkono au sanduku la Posta• Sanduku la maoni• Barua pepe• Nukushi• Tovuti• Simu • Kuonana na uongozi au mkuu wa idara husika.

10.0 NJIA ZA KUWASILIANA NA WAKALA

Makao Makuu ya Wakala yako Dar es Salaam. Wakala pia una Ofi sikatika kila Ofi si ya Mkuu wa Wilaya Tanzania Bara. Hivyo mnawezakuwasiliana nasi kupitia anuani zifuatazo;

(i) Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini (RITA)

Mtaa wa Kipalapala Kitalu Namba.516 S.L.P 9183 Dar es Salaam, Tanzania. Simu +255 22 2153069 | Nukushi: +255 22 2153075 Barua pepe: [email protected] | Tovuti: www.rita.go.tz Saa za kazi: Saa 2.00 Asubuhi hadi saa 9.30 Mchana

(ii) Ofi si ya kila Mkuu wa Wilaya -Tanzania Bara

Page 12: Mkataba wa Huduma kwa Mteja Mkataba wa huduma kwa... · 2014. 6. 24. · 3 Wizara ya Katiba na Sheria - Wakala wa Usajili Ufi lisi na Udhamini Mkataba wa Huduma kwa Mteja 2.0 DIRA,

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA KATIBA NA SHERIA

P.O. Box 9183, Dar es Salaam, Tel: +255 22 2153069, Fax: +255 22 2153075, Email: [email protected], Website: www.rita.go.tz

WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINIREGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA KATIBA NA SHERIA

P.O. Box 9183, Dar es Salaam, Tel: +255 22 2153069, Fax: +255 22 2153075, Email: [email protected], Website: www.rita.go.tz

WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINIREGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA KATIBA NA SHERIA

WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINIREGISTRATION INSOLVENCY AND TRUSTEESHIP AGENCY (RITA)

P.O. Box 9183, Dar es Salaam | Tel: +255 22 2153069 | Fax: +255 22 2153075, Email: [email protected], Website: www.rita.go.tz