mpya

15
TAMKO LA NDUGU VICTOR TESHA KUWANIA UTEUZI WA CCM KUGOMBEA UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI 2015 Utangulizi Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote, Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kunijalia afya njema kuifikia siku hii ya leo ambayo nilikuwa nikiiota kwa siku nyingi. Pili niwashukuru wazazi wangu, ndugu zangu, Marafiki zangu na watu wote walioniwezesha na kunisaidia kufika hapa nilipo leo. Katika mazingira yote niliyopitia kama si Mwenyezi Mungu na nyie mlionizunguka kama wazazi ndugu jamaa na marafiki nisingeweza kufikia hapa nilipo na nisingekuwa na ujasiri wa kuja kuwaambieni jambo hili zito la kutaka kuwatumikia kama mbunge wenu katika kipindi kijacho cha uongozi. Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote, Si vizuri kuwaambieni moja kwa moja nia na madhumuni yangu kwenu leo kabla sijawaeleza historia yangu kwa ufupi. Nilizaliwa mwaka 1981 hapa hapa jimbni katika kijiji cha Njari-Rononi, nilisoma shule ya msingi Moshi primary 1989-1995 baada ya kuhitimu shule ya msingi nilifanikiwa kujiunga na Seminari ya Mitume wa Yesu- Uru (apostles of Jesus-Uru Seminary) 1996-1999. Baada ya kuhitimu elimu yangu Uru Seminari nilijiunga na elimu ya kidato cha tano na sita Majengo Secondari 2000-2002. Nilijiunga na chuo kikuu Dar-esalam 2003-2006 na kupata shahada yangu ya kwanza katika Sayansi ya Jamii (bachelor degree in Arts and Social Science). Mwaka 2007- 2006 Nilijiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kusoma shahada ya Uzamili katika Masuala ya Usimamizi wa Biashara (Masters of Business Administration). Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote,

Upload: jackson-m-audiface

Post on 10-Sep-2015

47.449 views

Category:

Documents


5 download

TRANSCRIPT

TAMKO LA NDUGU VICTOR TESHA KUWANIA UTEUZI WA CCM KUGOMBEA UBUNGE WA MOSHI VIJIJINI 2015

Utangulizi Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote,

Kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kunijalia afya njema kuifikia siku hii ya leo ambayo nilikuwa nikiiota kwa siku nyingi. Pili niwashukuru wazazi wangu, ndugu zangu, Marafiki zangu na watu wote walioniwezesha na kunisaidia kufika hapa nilipo leo. Katika mazingira yote niliyopitia kama si Mwenyezi Mungu na nyie mlionizunguka kama wazazi ndugu jamaa na marafiki nisingeweza kufikia hapa nilipo na nisingekuwa na ujasiri wa kuja kuwaambieni jambo hili zito la kutaka kuwatumikia kama mbunge wenu katika kipindi kijacho cha uongozi.

Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote,

Si vizuri kuwaambieni moja kwa moja nia na madhumuni yangu kwenu leo kabla sijawaeleza historia yangu kwa ufupi. Nilizaliwa mwaka 1981 hapa hapa jimbni katika kijiji cha Njari-Rononi, nilisoma shule ya msingi Moshi primary 1989-1995 baada ya kuhitimu shule ya msingi nilifanikiwa kujiunga na Seminari ya Mitume wa Yesu- Uru (apostles of Jesus-Uru Seminary) 1996-1999. Baada ya kuhitimu elimu yangu Uru Seminari nilijiunga na elimu ya kidato cha tano na sita Majengo Secondari 2000-2002. Nilijiunga na chuo kikuu Dar-esalam 2003-2006 na kupata shahada yangu ya kwanza katika Sayansi ya Jamii (bachelor degree in Arts and Social Science). Mwaka 2007-2006 Nilijiunga na Chuo Kikuu Mzumbe kusoma shahada ya Uzamili katika Masuala ya Usimamizi wa Biashara (Masters of Business Administration).

Ndugu viongozi, wazazi, jamaa, marafiki, wadau wa maendeleo na wananchi wote,

Baada ya safari yangu hiyo kielimu nilianza kuitumikia jamii yangu ya kitanzania ambapo nilifanya kazi katika taasisi Mbalimbali kama ifuatavyo:-

Kuanzia mwaka 2006-2008 nilifanya kazi International Commercial Bank kama Retail Credit Analyst and Credit Executive officer.

Kuanzia 2008-2011nilifanya kazi Nbc Ltd kama Consultant Corporate Credit and Manger wholesale Credit.

Kuanzia 2011- March 2011- August nlifanya kazi United Bank of Africa kama Acting Head Corporate Banking

Kuanzia 2011 October 2014 Nilirudi tena kufanya kazi Nbc ltd kama Manager Business Support, product manager Retail Assets and Mortgage-Retail banking.

Kwa hiyo nimelitumikia Taifa langu na jamii yangu katika nafasi mbaimbali na sasa nimewiwa kuja kwenu kuwaambia nia Yangu hii ya kutaka kuwatumikia wana Moshi vijijini katika nafasi hii nyingine kama Mbunge wenu.

Ndugu wanajimbo,

Ninayo imani kwamba siku ya leo itafungua ukurasa mpya kwangu binafsi, familia, ndugu, marafiki na wadau wengine, lakini sana kwa jimbo letu zuri na lenye rasilimali nyingi.Nikijitazama nilikotoka, nilikopita na nilikofikia, naona wazi kwamba nawiwa sana kwa walionisaidia kwa hali na mali, waliolia nami katika shida.Kuwiwa huko kumenifanya nirudi nyumbani, ambako siwezi daima kukusahau na baada ya elimu mliyonipa, maarifa mliyonijaza, ujuzi mnionirithisha, sasa niseme nipo tayari kwa kazi ya kuwashika mikono wananchi na kulipatia maendeleo jimbo letu.Walionitangulia katika jimbo hili wamefanya kazi kwa kiwango walichoweza; tuwapongeze. Ni imani yangu thabiti kwamba sasa umefika wakati wa mimi pia kushiriki kwenye maendeleo ya Moshi Vijijini kama mwakilishi wa wapiga kura wa hapa.Mungu amenijalia kupata elimu, nguvu na talanta mbalimbali ili nitumie kwa ajili ya wengine na si kutia mfukoni au kuvitumia kibinafsi kujineemesha mwenyewe au na familia inayonizunguka.

Changamoto Zilizonisukuma kuomba Ridhaa hii

Ndugu wanajimbo,

Kabla sijaja hapa kuwaambia nia Yangu hii kwa kushirikiana na wataalamu Mbalimbali tulifanikiwa kufanya upembuzi yakinifu changamoto na matatizo ya msingi ya jimbo letu. Kama kiongozi wenu Mtarajiwa kama mkinipa ridhaa yenu hapo baaadaye ya kuwatumikia niliona ni vizuri kuyafahamu matatizo\ chanamoto na hata mafanikio ya viongozi wetu walionitangulia ili kufahamu ni nini hasa napaswa kukishughulikia pindi nipatapo ridhaa ya kuwatumikia.

Ndugu wanajimbo,

Wataalamu mbali mbali kwa kushirikiana pamoja nami tulipita kata zote 16 za jimbo hili na kugundua matatizo ya msingi ya jimbo letu ambayo kwa imani yangu naamini yakitatuliwa yataboresha maisha ya wanajimbo wa Moshi vijijini. Matatizo ya msingi kabisa yaliyogunduika kwenye jimbo hili ni haya yafuatayo:-

i) Kipato kidogo cha wanajimbo kilichochangiwa na kufa kwa zao la Kahawaii) Tatizo la Maji iii) Kiwango cha elimu Kuendelea kushukaiv) Afyav) Miundombinu Mibovu.

Changamoto hizi ndizo zilizonisukuma hasa kuja kuzitatua kama mtanipa ridhaa ya kuwatumikia kwani naamini mimi ndiye mwarobaini wa matatizo haya.

Ndugu wanajimbo,

Tatizo la kipato cha mtu mmoja mmoja kwenye jimbo letu ni tatizo kubwa sana na linalotufanya wanajimbo kuwa tegemezi kwa kiwango kikubwa mno kwa serikali yetu. Kufa kwa zao la kahawa kwenye jimbo letu kumetufanya wanajimbo kuwa omba omba na kuisubiri serikali iwaatulie kila kitu jambo ambalo linaipa serikali yetu mzigo mkubwa na kuishia kuilaumu serikali yetu. Viongozi waliotangulia pamoja na mazuri waliyoyafanya walishindwa kuja na Mbinu mbadala wa kuinua kipato cha wananchi wa jimbo hili, sitaki kuwa sehemu ya kulalamika nimekuja na mwarobaini wa kuokoa uchumi wetu uliokufa na hiki ndicho kipaumbele changu cha kwanza kama mkinipa ridhaa

Ndugu wanajimbo,

Pamoja na kuwa Jimbo letu ni mojawapo ya majimbo yaliyojaliwa vyanzo vingi vya maji ila bado wananchi wake hawanufaiki na Baraka hizi walizojaliwa na mwenyezi Mungu. Wananchi wa jimbo hili wengi hasa maeneo ya Tambarare, Old Moshi, Uru Kusini, Uru Mashariki, Mbokomu na baadhi ya vijiji vya Kata ya Kindi tatizo ni Kubwa zaidi. Sisemi kuwa maeneo mengne ya Jimbo yana huduma hii ya kutosha ila hali ni mbaya zaidi katika maeneo niliyoyataja.

Wataalamu nilioshirikiana nao walifanikiwa kufika hadi kwa mhandisi wa Halmashauri wa wilaya yetu na alithibitisha kuwa vyanzo vilivyopo vinatosha kuhudumi jimbo hili bila matatizo kabisa, tatizo kubwa lililopo ni uchakavu wa miundombinu ya maji ambayo inasababisha maji kuvuja kwa kiasi kikubwa ambapo asilimia 40% huishia kuvuja na ni asilimia 60% huwafika wananchi. Pamoja na hayo visima na matanki ya kuhifadhia maji jimboni ni michache sana. Kuna maeneo mengine yanahitaji miradi mipya kabisa ya maji ili kutatua tatizo la maji katika maeneo hayo maeneo haya ni yale maeneo ambayo hayajawahi kupata miradi ya maji kabisa.

Ndugu wanajimbo,

Elimu ndio urithi pekee ambao kwa sasa tunawaza kukirithisha kizazi hiki na kizazi kijacho. Kwa kufahamu umuhimu wa elimu katika jamii yetu na kwa taifa letu nimeamua kwa makusudi kuliweka katiaka kipaumbele changu pind mtakaponipa ridhaa ya kuwatumikia. Wataalamu wa elimu waliozunguka kwa shule zote za jimbo letu walibaini kuwa tatizo ni kubwa zaid kwa shule zetu za kata za jimbo hili. Shule zetu nyingi za kata kwa miaka mitatu toka 2012 hadi mwaka 2014 hakuna shule hata moja iliyoweza kufaulisha kwa zaidi ya zaidi ya aslimia 50%. Shle nyingi ufaulu wake ni chini ya Asilima 40% kutokana na takwimu hizi ni dhahiri kuwa taitizo ni kubwa sana na huko mbeleni tutaenda kukosa wataalamu wa kutumikia taifa hili katika Nyanja mbali mbali.

Tatizo ni kubwa zaidi kwa masomo ya sayansi ambayo wanafunzi wetu wameuwa wakiyafeli sana. Mfano somo la Fizikia lenyewe limeendelea kufanya vibaya kwa miaka yote toka 2012. Kwa kuthibitisha ukubwa wa tatizo hili zifuatazo ni baadhi ya shule za na faulu wake toka 2012-2014 katika somo la fizikia tu.

Shule201220132014

Satpass%satpass%satpass%

Msiriwa 3425.91642513538

Mawella 7222.83538271037

Meli37133532103142921.4

Masoka 14428.5221009--

Mangi sabasi38615.83372119315.8

Mangi sina361644.4241250361336

Kirima 423719210.5381026

Mkombole 15853186331516.6

Dr Cyril Chami2393917741251352

Sungu 26135015960251560

Okaoni56244225624441636

Mnini2412502283620630

Shimbwe38615.8221001--

Kisarika 52122325197647817

Kindi Kati4451119315.820420

Maringeni 826754193535822.8

Mabogini 11797.632412.5512650.9

Mpirani 4361432721301240

oria168501165466100

Manushi 4471634514.73438.9

Ndugu wanajimbo hizi ni badhi ya shule zetu na hali halisi ya ufaulu kwa somo hilo. Ndugu waajimbo,

Bila afya tunajua watu hawawezi kufanya kazi, hivyo lazima kipaumbele kiwekwe hapo, kwani ndio msingi wa maendeleo. Hospitali zetu ziwe na dawa na vifaa tiba vya kutosha. Majengo na miundombinu mingine viwe katika hali nzuri na nidhamu ya watumishi iwe juu. Bila ufuatiliaji wa mbunge ni ndoto.Ifike mahali tuwe na hospitali ya wilaya ya kueleweka; mambo ya kubahatisha kwa kupewa rufaa isiyoeleweka mara Hospitali Teule ya Kibosho Hospitali, mara Hospitali Teule ya Saint Joseph na wakati mwingine mgonjwa anatolewa Mawenzi anapelekwa huku, wakati mwingine kutoka KCMC, hakuna utaratibu mwafaka.Ifike mwisho sasa kusikia mtoto anazaliwa akiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na hakuna sababu ya mwenye VVU kufariki dunia kwa Ukimwi. Kwa nini? Tunazo dawa za kutosha na utaalamu wa kuzuia mama kumwambukiza mtoto na dawa za kurefusha maisha, ilimradi wahusika wanafuata masharti.

Ndugu wanajimbo,

Tunashukuru serikali ya awamu ya nne kwa kulikumbuka jimbo letu kwenye ilani yake ya 2010-2015, Mbunge aliyenitangulia kwa nafasi yake alifanikiwa kufuatilia kwa namna moja au nyingine ahadi za raisi kwa barabara za Kibosho road- Kindi Manoshi, Barabara ya Kibosho kirima Central na Barabara ya Rau-Njari. Kuna maeneo mengine ambayo hayajabahatika kupata huduma hii ya barabara ya lami kama maeneo ya Mbogini , Old Moshi Magharibi na Old Moshi Mashariki, Uru Mashariki na Shimbwe. Hali ya barabara katika maeneo hayo ni mbaya sana hasa kipindi cha Mvua.

Malengo na mipango ya kutatua changamoto hizo

Pamoja na kwamba najua ilani ya chama changu haijatoka lakini haininyimi fursa kuweka vipaumbele vyangu ninavyoona ni matatizo ya msingi na namna nitakavyovishughulikia katika kuvitatu kwa kushirikiana nanyi pamoja na serikali itakayokuwa madarakani. Kwa hiyo ndugu wanajimbo nimedhamiria kufanya haya pindi mtakaponipa ridhaa naamini kwa kuwa chama changu huandaa ilani yake kulingana na matatizo ya wananchi hivyo naamini kuwa matatizo niliyoyaainisha hayattofautiana sana na yatakayokuwepo katika ilani.

Hivyo nitatilia mkazo na kuishauri serikali yangu kwa pamoja kutatua matatizo haya bila kukaa pembeni na kulaumu tu. Kwa maana hiyo ndhamiria kufanya haya:-

Katika kutatua tatizo la Elimu na Kupandisha kiwango cha ufaulu hasa kwa masomo ya science nitakuwa na Mipango ya muda mfupi na mrefu. Katika kupandisha kiwango cha ufulu kwa masomo haya nimeshaanza Mchakato wa kuandaa waalimu wanaohitimu masomo ya science kutoka chuo kikuu cha Mwenge ili wabaki baadhi kuhudumia wanafunzi wetu katika jimbo letu, Ikumbukwe kuwa whitimu hawa hukaa mtaani takribani karibu mwaka mzima wakisubiria Ajira hivyo kwa kushirikiana na wazazi pamoja na wadau mbalimbali tutaandaa utaraibu wa kuwapatia posho waalimu hawa ni nimeshaongea nao wamekubali kuifanya kazi hiyo. Mipango ya Muda mrefu ni kuendelea kupeleka ushawishi serikalini kuendelea kutupatia waalimu wengi kadri iwezekanavyo na kujenga mazingira rafiki ya kuwavutia waalimu hawa kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo vyao vya kazi kuepuka kupoteza waalimu wanaohamahama.

Katika swala la Afya nimedhamiria kuhakikisha angaau kila kata mbili zinakuwa na kituo kimoja cha Afya chenye sifa zote na kitokachotoa huduma bora. Sitalenga kujenga kituo kipya cha Afya bali ni kufanya upanuzi wa zahanati zetu kwa kila kata Mbili itachaguliwa zahanati moja yenye eneo la upanuzi kwa ajili ya kupandishwa hadhi kuwa kituo ch afya. Kilichokosekana kwa wananchi ni dhamira ya dhati ya kiongozi anayeweza kuwaunganisha na serikali katika kulitatua hili. Kama wananchi hawa waliweza kujijengea kila kata kuwa na shule yake nadhani haiakuwa jambo gumu sana kwa wananchi wa kata mbili kwa kushirikiana na serikali yetu sikivu kupandisha hadhi zahanati moja. Kilihokosekana ni msukumo wa kiongozi mwenye dhamira ya dhati kulisimamia hilo.

Swala la maji nitalishughulikia kwa awamu mbili, yaani kwa mipango ya muda mrefu na muda mfupi. Katika kulitatua kwa muda mfupi nimeandaa mpango wa kila kijiji kupata angalau storage tank ya lita 25 elfu ili kuhifadhi maji. Mipango ya kupata matanki imeshaanza kufanyika kwa kupeleka maombi katika makampuni mbalimbali na mengine yameshaanza kuonyesha nia ya kutuung mkono katika hili. Kama kiongozi sitaki kuwa sehemu ya malalamiko nataka kuwa sehemu ya utatuzi na ndio maana mchakato ya awali imeshaanza kufanyika. Katika mkakati wa Muda mrefu nitahakikisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeanzisha mpango wa kufanya ukarabati ya miundombinu ya maji kuepuka upotevu huo wa maji. Kuendelea kushawishi kampuni la KFW Kutoka ujerumni ambalo lilifnya upembuzi yakinifu kwa miradi mipya ya maji kwenye jimbo kuendelea na nia yao njema ya kuianzisha miradi hiyo. Ni imani yangu kuwa kama kampuni hili litaendelea kutupatia miradi hii tatizo la maji kwenye jimbo hili litabaki Historia. Kwa kushirikiana na mhandisi wa wilaya nitaweza kujua tatizo la miradi hii iliyotolewa na kampuni hili kwa nini ilisitishwa ili kwa kushirikiana na serikali yangu sikivu kuiendeeza.

Ndugu zangu, Tunapoingia katika zama hizi mpya tunaingia na mikakati kamambe kwa ajili ya kuhakikisha tunainua uchumi wa mtu mmoja mmoja, lakini pia wa taasisi na jimbo kwa ujumla.

Ile biashara ya kuhangaikia shamba mwaka mzima halafu unaishia kubeba na kuuza debe zima na ndizi mbivu kwa shilingi 500 au hata 1,000 inafikia kikomo na awamu hii.

Wananchi wangu, Tunakuja na mambo makubwa, ambapo ndizi zinaweza pia kusindikwa kitaalamu na kutengeneza crisps, lakini pia mahindi tunayolima kwa wingi kisha kulanguliwa na wajanja wachache sasa tunaingia kwenye mkakati wa kusindika unga wake na kuuza ndani na nje ya nchi. Mimi mwenyewe na wasaidizi wangu tutaratibu kazi hiyo.

Kilimo Cha Matunda

Wapendwa, lazima tuanzishe kilimo cha mazao na matunda mapya na yenye kutengeneza fedha na kuinua uchumi wetu. Hayo ni pamoja na mapasheni, miwa, mboga mboga kwa wingi, machungwa, ilikii, mdalasini, pilipili hoho, pilipili manga, pilipili kali, alizetu na mengine yenye bei kubwa ndani na nje ya nchi.

Ufugaji kuku wa nyama na wa mayai sambamba na ufugaji wa ngombe na mbuzi bora zaidi wa maziwa kwa kutumia madume bora kabisa na nguruwe watakaotuvusha tulipo kwa mauzo yake na bidhaa zake.

Wana Jimbo, je, mlishafikiria juu ya ufugaji wa samaki kwa ajili ya afya zetu na biashara? Nakuja na fursa hiyo na wataalamu wataonesha mbinu za kutumia, namna ya kuchimba visima, jinsi ya kuotesha samaki, kipi wale na wakati wa kuvuna na kusafisha visima. Hili ni zao linalotufaa na litaboresha sana afya zetu na za wazee wetu, hasa wale wenye magonjwa ya shinikizo la damu wasiotakiwa kula nyama nyekundu, lakini litatuingizia fedha nyingi.

Mkishauza bidhaa hizi mtakuwa na uwezo wa kununua nyingine mnazohitaji pamoja na kulipia huduma, ziwe za elimu, afya na pia kujiwekea miundombinu mizuri na nyumba nzuri.

SACCOS ya Mbunge

Nikiwa mtaalamu wa masuala ya fedha, nimeshafanya mchanganuo kwa ajili ya kuanzisha miradi endelevu ya vyama vipya vya kuweka na kukopa Saccos za Mbunge, lakini pia zile za zamani zitawezeshwa zaidi na zilizochoka kukarabatiwa na zilizokufa kufufuliwa ili turuke pamoja na ndege yetu ya maendeleo.

Matunda

Jimbo hili ni maarufu kwa matunda ya maparachichi lakini wenye miti hiyo wameishia kuwa mafukara kwa sababu wanarubuniwa na watu ambao hununua matunda yote yakiwa mtini kwa kati ya shilingi 10,000 na 20,000 tu. Biashara hiyo sasa basi.

Kila mwenye mti wa parachichi au wa matunda mengine aelewe kwamba ana kitegauchumi na kwa Saccos za Mbunge, akiwa na shida ataweza kukopa na kutumia mti wake kama dhamana, ili akishauza mazao yake kwenye soko jipya ninaloleta alipe fedha kidogo alizokopa na si kurubuniwa na matapeli wachache.

Benki za vijijini zinakuja kutuongezea kasi kwenye kazi yetu hii na huu ndio muda uliopangwa kwa ajili ya kuagana na umasikini kiasi kwamba hata wale waliokimbilia mijini wataamua kurudi kujenga jimbo letu na kufaidi matunda ya uhuru.

Katika kuongeza ufanisi, lazima tukubali kwamba kuna kwenda na wakati miti ya zamani ya kahawa mingine hata kabla ya Uhuru, lazima sasa tukubali kuingoa na kupanda mipya kwa nafasi stahiki kuendana na maelekezo ya maofisa ugani.

Miti hii, mbunge wenu atahakikisha kwamba mnagawiwa bure na vyama vyenu vya msingi vya ushirika pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) pamoja na wawekezaji wakubwa walio jimboni mwetu.

Nimekuja kwa ajili ya kuwatafutia masoko mapya ya kahawa ili mnufaike na kilimo hiki na si kutegemea bei mnayopewa na KNCU pekee. Tupo na marafiki wengi na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi.

Ndugu zangu,

Tunakwenda kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika unga na ndizi mbichi zilizokaushwa. Thamani ya mazao haya itapanda, kwa hiyo mwisho wa kudharau ndishi, malalali, mananamba na kadhalika unakaribia. Ulaya wanapenda sana ndizi hizi na wanatoa fedha nzuri tu, wamekosa wa kuwapelekea kutoka kwetu, na sasa nimeingia.

Viwanda vingine vidogo vidogo pia vitajihusisha na utengenezaji wa wanga (starch) kutoka kwenye mimea ya asili kama magimbi.Tutarudia enzi zile za kutengeneza nguo na dawa; ni muhimu na litakuwa suala la faida kubwa sana.

Byogas

Mama zangu kwa namna ya pekee,

Mmehangaika na kuni za kuwashia moto vya kutosha. Nafahamu akina mama wengi na hata watoto wameugua vifua na macho kwa sababu hii. Sasa tunakuja na suluhu tofauti na rahisi, maana gesi asilia bado itachukua muda, umeme ni ghali na ninachokuja nacho ni wataalamu wa kutusaidia kuwa na biogas.

Mitambo yake inakuja na kwa gharama ndogo ya kinyesi cha wanyama tutaweza kufanya shughuli za mapishi katika hali ya usafi na afya. Tutatumia hii pia kuwashia taa na kuepuka gharama kubwa za umeme. Lengo pacha la mradi huu ni kuondoa kabisa matumizi ya kuni na uharibifu wa misitu na mazingira, eti kwa ajili ya kupikia. Mbunge mwenyewe nitaratibu hili ikiwa mtanipa ridhaa ya kuwaongoza.

Ndugu zangu,Wakati pia umefika wa kuanzisha vikundi na viwanda vya kufyatua matofali kwa kutumia udongo, mchanga kidgo na saruji kidogo. Hii kazi inawafaa wajasiriamali vijana na itasaidia kila mtu awe na nyumba nzuri kwa bei rahisi.

Katika kilimo ndugu zangu, lazima niwaambie kwamba tumeshaona jinsi ya kupanga jimbo letu; ukanda wa juu wenye hali ya hewa ya ubaridi tutakuwa na mazao ya asili kama kahawa, migomba, maharage, mahindi (kwa ajili ya kula mabichi).Ili kuwakomboa kiuchumi, tutaenda sambamba na mazao mapya yanayokubali kama iliki, mdalasini, pilipili na mboga mboga na maharagwe yanayovunwa machanga yakiwa kijani na yanauzwa sana nje ya nchi.

Mahindi mabichi nayo yatafungashwa vizuri kabisa na kuuzwa kwenye maduka makuu supermarkets bahati nzuri zimeanza kuongezeka hata hapa Moshi, lakini pia zipo mikoa mingine na nje ya nchi. Tutaenda sambamba na mapasheni na miwa ambayo itatutoa.

Kwenye ukanda wa chini kati wenye joto kidogo tuna mazao ya asili ya kahawa, migomba, mahindi na maharagwe. Sasa ili kuboresha maisha ya watu hawa wa ukanda wa chini kati, tutakuwa na mazao mapya katika maharage machanga, alizetu, matikiti maji yenye bei kubwa sokoni sambamba na mapasheni na miwa.

Ukanda wa chini wenye hali ya joto tumekuwa na mazao ya mpunga, mahindi na maharage. Tunawaongezea ukuaji uchumi kwa kuja na alizeti, maharage machanga, mananasi, mapasheni na matikiti maji ili kwenda na hali ya kuboresha maisha ya watu na kuwawezesha kiuchumi.

Tutaanzisha vikundi vya kuboresha mazingira kwa maana ya uoto wa asili na vyanzo vya maji. Kadhalika vitatumika kutatua migogoro ya maji kati ya wawekezaji na wananchi, kwa sabau wananchi nao wana haki ya kutumia maji ya mito na mifereji kumwagilia. Mifereji iliyokuwa imekufa sasa inafufuliwa yote na mbunge mpya!

Utaratibu unakuja pia kuanzisha vikundi vya ulinzi jimboni ili kuhakikisha wadokozi wachache, vibaka na wasiotakia mema wengine wanakomeshwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tutawatambua wadau wa maendeleo ya jimbo kwa namna ya pekee; wawe ndani au nje ya jimbo. Tutasajili wataalamu wenye ujuzi mbalimbali jimboni Moshi Vijijini, mfano mafundi waashi, mafundi momba, mafundi seremala, mafundi umeme ili kuwatumia hao hao kwenye miradi yetu jimboni na si kuleta wageni.

Tunakwenda kuanzisha vikundi vya michezo mbalimbali kuanzia ngazi za vitongoji hadi jimbo. Tunakuja na mashindano ya Kombe la Mbunge katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono na riadha, hasa mbio fupi na za nyika.

Tutaanzisha seminama za mafunzo hapa kwetu pamoja na zile za kuburudisha nyakati za jioni baada ya kazi ngumu ya siku.

Real Estate development

Litatengwe eneo la Moshi vijijini kwa ajili ya ujenzi wa apartment kwa ajili ya kuimarisha utalii wetu. Jimbo letu lipo chni yam lima Kilimanjaro hivyo nimelenga kuongea na bank zilizo tayari ndani na njee ya Tanzania kutujengee Gorofa maalumu na kutupatia vifaa vya kisasa ambavyo kwa yeyoe atakaye kuwa kwenye jingo hilo anaweza kuuona mlima Kilimanjaro bila kuupanda. Ikumbukwe kuwa mimi sitaki kwenda kuilalamikia serikali bali naenda kuisaidia serikali yangu hivyo mchakato wa kuomba eneo na fedha hizi toka kwenye taasisi nilizozitaja umeshaanza kufanyika na mazungumzo yanaendelea vizuri. Kwa kulifanikisha hili tutaweza kuinua pato la halmashauri yetu kwa kiwango kikubwa sana na vijana wetu kujipatia ajira. Ujenz wa jengo hili utaenda sambamba na uanzishwaji wa Utalii waasili-vyakula kahawa, mavazi na historia ya eneo na kabila la wachaga.

Haya yote sitaitegemea serikali kuatatua bali juhudu zangu kwa kushirikana nanyi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo naamini kuwa nitafanikisha haya. Serikali yangu inaenda kupata mbunge wa mfano ambaye hatakwenda kulalamika ali kuisaidia serikali yake kutatua kero za wananchi. Nawaombeni wanajimbo mnitume kuifanya kazi hii ningali na umri huu kwa kuwa nina imani nitaweza kukimbizana na kasi ya maendeleo yenu.

UBUNGE WA UWAJIBIKAJI KWA TAIFA

Ndugu zangu,Pamoja na kazi nilizoainisha hapo juu kwa ajili ya Jimbo la Moshi Vijijini, nadhamiria kuchukua nafasi ya uwakilishi wa wananchi bungeni ili kuimarisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo ni Mhimili wa Taifa.Natumia haki yangu ya kikatiba, lakini nalenga kuliwezesha Bunge kuwa na wabunge vijana zaidi, wenye uwezo wa kutekeleza majukumu kwa umahiri, uadilifu, pasipo woga wala upendeleo.Najua wapo wengine wanaoweza kujitokeza, baadhi wanatajwatajwa na wengi, lakini naamini Victor Tesha ni mtu sahihi zaidi kwa matakwa ya nyakati hizi mwenye mbinu na mikakati sahihi kwa wananchi wetu.Matatizo ya wananchi wa Moshi Vijijini ni yangu, nayabeba na kuahidi kuanza kuyafuta mengine kwa mpigo na mengine moja baada ya jingine, lakini kwa kasi ya uhakika, ari mwafaka, nguvu kubwa na kiwango cha kimataifa.Mungu Ibariki, Tanzania,Mungu Ibariki Kilimanjaro,Mungu Ibariki Moshi Vijijini.Asanteni sana._________Victor Tesha