mwongozo wa mratibu wa mafunzo ya walimu …...mwongozo wa mratibu wa mafunzo ya walimu kazini ngazi...

48
MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III Moduli ya Saba: UTAMBUZI WA SAUTI Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Upload: others

Post on 25-Jan-2020

185 views

Category:

Documents


3 download

TRANSCRIPT

Page 1: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

MAFUNZO YA WALIMU KAZINI NGAZI YA SHULE KWA MWALIMU WA DARASA LA I-III

Moduli ya Saba: UTAMBUZI WA SAUTI

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Page 2: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

Moduli hii imetayarishwa kwa ushirikiano na:

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya UfundiO�si ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Taasisi ya Elimu TanzaniaChuo Kikuu cha Dodoma

Chuo cha Ualimu MorogoroChuo Kikuu cha Dar Es SalaamChuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu MkwawaEQUIP-Tanzania

Moduli hii imewezeshwa kwa ushirikiano na:

C.C.U ButimbaC.C.U BustaniC.C.U TaboraC.C.U NdalaC.C.U Kasulu

C.C.U KabangaC.C.U BundaC.C.U Tarime

C.C.U ShinyangaC.C.U Mpwapwa

Page 3: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

1Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DIBAJI

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta ya elimu ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii. Lengo la Dira ya Maendeleo ni kuwa na taifa la watu waliolelimika na jamii iliyo tayari kujifunza ku�kia 2025. Serikali ya Tanzania imethibitisha kwa vitendo kuwa Elimu ni kiambato muhimu katika kupunguza umaskini na kuimarisha maendeleo ya taifa. Kwa muda mrefu serikali imetambua kuwa “Ubora wa Elimu yoyote hauwezi kuwa bora kuliko mwalimu mwenyewe” hivyo imetilia mkazo mafunzo kazini kwa walimu kupitia mikakati mbalimbali ili kuimarisha umahiri wa walimu katika ufundishaji na ujifunzaji darasani.

Katika kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji darasani, Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na EQUIP-Tanzania, wameandaa moduli hii ambayo imesheheni kazi mbalimbali ambazo waalimu mtazitenda katika vikundi wakati wa mafunzo kwa kutumia mbinu ya Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule. Mbinu hii inatambua umuhimu wa walimu kujifunza pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili ili kupata suluhisho la changamoto za ufundishaji na ujifunzaji kwa pamoja.

Moduli hii ya Mafunzo ya Walimu Kazini, imeandaliwa ili kusaidia juhudi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhakikisha kuwa mbinu fanisi zinatumika darasani wakati wa ufundishaji na ujifunzaji. Moduli hii pia inawasaidia walimu kushirikishana uzoefu na umahiri katika ufundishaji na ujifunzaji darasani. Vilevile Moduli inatoa mafunzo ya ziada ikitarajiwa kuwa walimu watakuwa wamekwisha pata Mafunzo Kabilishi ya utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa wa kuimarisha ufundishaji wa KKK kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili.

Taasisi ya Elimu Tanzania inatarajia kuwa moduli hii itawasaidia walimu kuimarisha umahiri wa ufundishaji na ujifunzaji ili kuwasaidia wanafunzi waweze kujenga uwezo unaokusudiwa wakati wa kujifunza.

Changamoto iliyo mbele yetu ni kuhakikisha kuwa tunaonyesha kwa vitendo matokeo mazuri yanayotokana na maudhui ya moduli hii wakati wa ufundishaji na ujifunzaji darasani ili kuimarisha ubora wa elimu ya shule ya msingi.

Dr. Leonard AkwilapoKaimu Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Elimu Tanzania.

Page 4: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

2 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Maelezo Muhimu kwa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

Mwongozo huu utatumika sanjari na moduli ya saba ya mwalimu ili kumsaidia mratibu wa mafunzo kuwa na mpangilio mzuri wenye kufuata hatua kwa hatua ili kuwafanya walimu

washiriki kikamilifu katika kujifunza maudhui ya moduli ya saba.

Mwongozo huu umegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ambayo ni upande wa kushoto wa mwongozo unabeba maelezo ambayo mratibu wa mafunzo ya walimu kazini ngazi ya

shule atatakiwa kuyafuata wakati wa kuratibu kipindi cha kujifunza maudhui ya moduli. Sehemu ya pili ambayo ni upande wa kulia wa mwongozo unabeba maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu

ambayo watayasoma wakati wa kipindi cha kujifunza.

Wakati wa kipindi cha kujifunza, unatakiwa kufuata maelezo yanayokuongoza yaliyo upande wa kushoto wa mwongozo

huu na kuyahusianisha na maudhui yaliyo kwenye moduli ya mwalimu ambayo yapo upande wa kulia wa mwongozo huu

kama yanavyosomeka kwenye moduli ya mwalimu.

Page 5: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

3Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO NA TASWIRA KATIKA MODULI

Kuna picha na michoro mingi katika moduli. Baadhi zinajirudia mara nyingi kwa sababu zinamaanisha jambo mahususi linalotokea. Zifuatazo ni mifano ya taswira mbalimbali ambazo zinapatikana katika moduli pamoja na kile ambacho zinawakilisha:

Jadili na mwenzako: Wakati wote wa kusoma moduli, walimu wataelezwa kufanya kazi pamoja na mwalimu mwingine juu ya maswali au kazi.

Fikiri– Wawili wawili – Shirikishana: Kama ilivyo katika maelezo ya hapo juu, hapa vilevile walimu wanafanya kazi wakiwa wawili wawili. Japokuwa, hapa walimu wanatafakari mmoja mmoja kwanza juu ya swali au tatizo, halafu mwalimu anafanya kazi na mwenzake na mwishoni wanawasilisha katika kundi lote.

Jadiliana katika kikundi: Wakati mwingine walimu wataelekezwa kutafakari au kujadili maswali mbalimbali katika kikundi.

Soma: Katika kila moduli kuna “dhana kuu” ambayo kwa kawaida huwasilishwa kwa kirefu katika maelezo.

Andika: Moduli itawahamasisha walimu kuchukua maelezo na kuandika �kra zao na majibu.

Igizo: Baadhi ya mazoezi yatahitaji walimu kuigiza kazi ya kufundisha wakati wengine watapaswa kuigiza kama wanafunzi.

Page 6: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

4 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MAELEKEZO KWA MRATIBU WA MAFUNZO YA WALIMU KAZINI

Kabla ya kuanza moduli hii, angalia ‘maelekezo muhimu’ na hakikisha kuwa wewe na walimu mnayazingatia.

Tafadhali waambie walimu wajiorodheshe na kusaini hapa chini.

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma utangulizi wa moduli hii. Tutasoma matini kwa sauti na kwa kupokezana. Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma aya ya kwanza, atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata.”

JINA LA MWALIMU ME / KE SAHIHI: DARASA1

2

3

4

5

6

7

8

Tarehe: Shule: Wilaya: Mkoa:

Muda wa kuanza: Jina la Mratibu na sahihi yake:

Muda wa kumaliza: Jina la Mwalimu Mkuu na sahihi yake:

Page 7: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

5Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MODULI YA 7: UTAMBUZI WA SAUTI

MAUDHUI YA MODULIModuli hii inahusu utambuzi wa sauti, au uwezo wa mwanafunzi kusikia, kutambua na kutumia sauti za lugha inayozungumzwa. Ni muhimu kuwafundisha watoto ujuzi wa utambuzi wa sauti ili wajifunze kusikia sauti za lugha na namna zinavyotumika katika maneno tofauti. Kwa mfano wanaweza kusikia ‘mtu’ na ‘mti’ zinaanza na sauti moja na kumalizika na sauti tofauti.

DHANA KUU• Sauti ya heru� – sehemu ndogo ya sauti ambayo inatengenezwa na heru� katika neno

linalotamkwa. Sauti za heru� zinaandikwa ndani ya mistari mshazari kama hivi / / (kwa mfano, sauti ya heru� ‘m’ inaandikwa /m/)

• Kuachanisha Sauti – kutenganisha sauti kutoka kwa nyingine katika kila neno (/m/ /t/ /i/ = mti)• Silabi – sehemu kubwa ya sauti ambayo hutengenezwa kwa kuunganisha konsonanti na irabu.• Kutenganisha sauti – Kutenganisha neno kwa aidha sehemu ndogo za sauti (sauti za heru�) au

sehemu kubwa (silabi).

MALENGO YA MODULIMwisho wa moduli hii, walimu watakuwa na uwezo wa:• Kuelewa kwa nini utambuzi wa fonemiki (sauti) unasaidia kusoma• Kutathmini kiwango cha uelewa wa fonemiki kwa wanafunzi• Kutumia kazi na mikakati kuimarisha ujuzi wa fonemiki kwa wanafunzi• Kutengeneza kadi za picha kusaidia mikakati ya ufundishaji wa utambuzi wa sauti

MAELEKEZO MUHIMU 1. Mara zote njoo na moduli ya mafunzo ya walimu kazini na kalamu2. Unaweza kuja na chakula au kitu cha kutafuna na maji kama mtapanga kukutana mchana

baada ya masomo 3. Penseli na kifutio4. Karatasi 4-5 za manila zenye ukubwa wa A4 kwa kila mwalimu (au vipande 6 vya bodi kadi

ambazo ni kubwa kuliko kiganja chako) 5. Kalamu ya kuweka alama au mkaa6. Mkasi7. Kalamu za rangi (kama zipo)8. Utando fomeka (kutoka kwenye kivunge cha vifaa vya kufundishia cha EQUIP-T – kama vipo)

TARATIBU ZA KUJIFUNZA KWA KILA KIPINDI• Kutana katika sehemu tulivu yenye ubao kama

inavyoonekana katika picha• Panga madawati/meza ili kuwezesha washiriki

wote waonane na kuongea pamoja • Kuwa huru kuuliza maswali kama hujaelewa• Kuwa wa msaada kwa wenzako • Kuwa mbunifu na �kiria jinsi dhana unazojifunza

zinahusiana na darasa lako • Weka simu yako katika hali ya mtetemo

Page 8: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

6 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

WAAMBIE WALIMU:

“Tangu moduli ya 6, umefanyia mazoezi shughuli mbili kwenye kipindi cha kujifunza kusoma na kuandika. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa kufundisha maudhui ya moduli hiyo darasani kwako

Una dakika 5 kwa ajili ya kazi hii.”

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa –tutajadiliana pamoja mafanikio na changamoto katika kikundi. Kwa kila changamoto ambayo imewasilishwa tufakari kwa pamoja kuhusu namna ya kukabiliana nayo. Kumbuka kuandika ufumbuzi ambao unaweza kukabiliana na changamoto zilizojitokeza. Tutatumia dakika 10 kwa majadiliano.”

Page 9: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

7Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

TAFAKARI

Kipindi kilichopita tulijifunza sauti ya heru�, jina la heru� na silabi. Orodhesha mafanikio uliyoyaona pamoja na changamoto ulizokabiliana nazo wakati wa kufundisha maudhui ya moduli hiyo darasani kwako.

ANDIKA PEKE YAKO (DAKIKA 5) Tafadhali andika kwenye visanduku mafanikio na changamoto ulizokutana nazo wakati wa kutekeleza mikakati hii katika darasa lako.

JADILIANA KATIKA KIKUNDI (DAKIKA 10) •Shirikishawenzakokwenyekundikuhusumojawapoyauzoefuhuo. •Kwakilachangamoto,pendekezanamnayakukabiliananayo. •Wakatiwamajadiliano,andikaufumbuziunaoendananachangamotoulizobainisha.

Mafanikio(Elezea utaratibu uliotumia na fafanua jinsi ulivyofanikiwa)

Changamoto (Elezea utaratibu uliotumia na fafanua changamoto zake)

Njia Muhimu za Ufumbuzi(Mawazo muhimu mahususi kwa wenzetu)

Page 10: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

8 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

WAAMBIE WALIMU:

“Leo tena tutacheza Mchezo wa Kulala kama zoezi la kutuchangamsha. Lakini muda huu mtasikiliza sauti tofauti. Kumbuka:

1. Kuinamisha kichwa juu ya mikono yako ukiwa umefumba macho ili uonekane kama vile umelala.

2. Nitatoa sauti mbili.3. Uamue kama una�kiria sauti mbili zinafanana au hazifanani.4. Kama sauti mbili zinafanana, inua mkono wako (ukiwa umeinamisha kichwa kwenye dawati).5. Kama sauti mbili hazifanani, usiinue mkono.

Baada ya kucheza mchezo, tutapitia majibu sahihi. Usiwe na wasiwasi kama hautayajibu vizuri. Haya, tuanze!

Piga kelele zifuatazo. Tulia kila baada ya jozi moja ili walimu waweze kunyoosha mikono.

1. Piga Ko� – Piga Ko� (Jibu Sahihi: Sauti Zinafanana)2. Kanyaga Chini – Gonga Dawati (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)3. Kohoa – Kanyaga Chini (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)4. Gonga Kalamu Juu Ya Dawati (Jibu Sahihi: Sauti Zinafanana)5. Kohoa – Gonga Dawati (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)6. Gonga Dawati – Gonga Kalamu Juu Ya Dawati (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)7. Kohoa – Kohoa (Jibu Sahihi: Sauti Zinafanana)8. Gonga Dawati – Kanyaga Chini (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)9. Piga Ko� – Gonga Dawati (Jibu Sahihi: Sauti Hazifanani)10. Kanyaga Chini – Kanyaga Chini (Jibu Sahihi: Sauti Zinafanana)

Baada ya kutengeneza sauti hizo, pitia majibu sahihi na wafanye walimu wakuangalie wakati unatengeneza sauti hizo).

WAAMBIE WALIMU:

“Kwakuwa tumeshamaliza, tafadhali soma maswali peke yako na �kiria utakavyojibu. Jadili majibu yako na mwenzako. Kisha utashirikisha mawazo yako kwenye kikundi.”

Jibu 1: Tumeshiriki ujuzi wetu wa kusikiliza.Jibu 2: Wanafunzi lazima wawe na uwezo wa kusikiliza sauti za heru� tofauti, na kuzioanisha na heru� zinazoandikwa. Kama wanaweza kufanya hili, wanaweza kuanza kutamka maneno yanayoandikwa ambayo hawayafahamu.

Page 11: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

9Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTANGULIZI

ZOEZI LA KUCHANGAMSHA (DAKIKA 10) Leo tutacheza Mchezo wa Kulala tena kama zoezi la kutuchangamsha. Lakini muda huu mtasikiliza sauti tofauti. Kumbuka:

1. Kuinamisha kichwa juu ya mikono yako ukiwa umefumba macho ili uonekane kama vile umelala. Tafadhali usifumbue macho!

2. Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini atatoa sauti mbili.

3. Uamue kama una�kiria sauti mbili zinafanana au hazifanana.

4. Kama sauti mbili zinafanana, inua mkono wako (ukiwa umeinamisha kichwa kwenye dawati).

5. Kama sauti mbili hazifanani, usiinue mkono.

Baada ya kucheza mchezo, tutapitia majibu sahihi. Usiwe na wasiwasi kama hautayajibu vizuri. Haya, tuanze!

FIKIRI - WAWILI WAWILI - SHIRIKISHANA (DAKIKA 10) Baada ya mratibu kupitia majibu, jadili maswali yafuatayo kwa kushirikiana na mwenzio:

1. Ujuzi gani umeshiriki katika zoezi hili? 2. Una�kiri ni namna gani ujuzi huu unahusiana na kusoma?

Page 12: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

10 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma maudhui muhimu. Tutasoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.

Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma sehemu (kwa mfano, aya au maelezo), atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome sehemu inayofuata. Wakati wa kusoma weka alama zifuatazo kwenye matini unayosoma.

Weka alama ya mshangao (!) kwenye wazo ambalo unadhani ni muhimu.

Weka alama ya kiulizo (?) Kuonesha kutokukubaliana na dhana hiyo.

Weka alama ya duara (o) kuonesha kuwa dhana hiyo ni mpya kwako.”

Page 13: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

11Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Kujifunza kusoma kunaanza kwa kusikia. Watoto wengi wanaanza shule wakijua Kiswahili cha kuongea (au lugha yao ya kwanza). Ili wanafunzi waweze kusoma Kiswahili kilichoandikwa, wanapaswa kuelewa kwamba:

Moduli hii inajikita katika hatua namba 1 – kusaidia wanafunzi kusikia na kutofautisha sauti zinazozungumzwa katika Kiswahili. Katika kufanikisha hili ni kuanza kwa kuwasaidia wanafunzi kusikia na kutofautisha sauti katika mazingira. Hiki ndicho mlichofanya katika mchezo wa kuchangamsha – mlitakiwa kujielekeza katika sauti na kuamua kama ziko tofauti.

Zoezi la kusikia, kutofautisha, na kutenganisha sauti linaitwa utambuzi wa sauti. Mara tu wanafunzi wanapoweza kutambua tofauti ya msingi kati ya ko� , kukanyaga au kugonga, watakuwa na uwezo wa kutambua tofauti ya sauti za msingi kwenye maneno kama vile amani/imani, saa/zaa au mamba/namba.

Kuwa na uwezo wa kutambua sauti baina ya maneno yanayotamkwa kunaitwa utambuzi wa sauti ya heru� (pia inajulikana kama utambuzi wa fonetiki). Umejifunza kuhusu sauti za heru� katika kipindi cha mwisho. Kumbuka, sauti ya heru� siyo sawa na jina la heru� au silabi. Hapa chini kuna kumbukizi ya vipengele vitatu vya kusoma katika Kiswahili:

UMUHIMU WA UTAMBUZI WA SAUTI (DAKIKA 30)

/m/ /a/ /m/ /a/

Sauti ya heru� ni sehemu ndogo ya sauti ambayo inasikika katika neno linalotamkwa. Tamka neno taratibu sana (kama vile ‘mama’ hapo chini) na weka umakini namna midomo yako, na ulimi vinavyobadilika wakati wa kutamka heru� tofauti. Mabadiliko haya yanaonesha kuwa unatamka sauti tofauti za heru� .

1. Manenoyanayotamkwa

yanaundwa na sautimbalimbali

2. Sauti hizi zinahusiana na

heru� zinazoandikwa

3. Heru� zinaundamaneno

yanayoandikwa

4. Manenoyanayoandikwa

yanaweza kutamkwakwa kutumia sauti

zinazofanana na heru�

1. Mwalimu mmoja aanze kusoma kwa sauti. Baada ya kukamilisha sehemu (kwa mfano, aya au maelezo) amwite mwalimu mwingine kwa jina asome sehemu inayofuata.

2. Wakati unaposoma zingatia alama zifuatazo: • Weka alama ya mshangao (!) katika sehemu ambayo unaona ni muhimu • Weka alama ya kuuliza (?) katika sehemu ambayo huelewi au hukubaliani nayo • Weka mduara katika (o) maneno ambayo ni mapya.

Page 14: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

12 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“ Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 15: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

13Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Ni rahisi kubainisha na kutamka sauti ndefu za heru� kwa sababu unaweza kuzirefusha kwa sekunde kadhaa, kama vile /m/ na /a/. Na kumbuka, kuonesha sauti ya heru� katika kuandika, mistari mishazari inawekwa namna hii: /m/

Sauti ya heru� ni tofauti na jina la heru�. Jina la heru� ni namna ambavyo unarejea heru� (kama ambavyo unasema alfabeti au kutamka neno). Majina ya heru� za Kiswahili yanakuwa kama vile yameundwa kwa kuongeza ‘e’ katika konsonati. Mfano : be, che, de, fe. Hata hivyo, majina ya heru� za irabu yanafanana na sauti za heru� zake : a, e, i, o, u.

Kwa hiyo, ni lazima kutamka heru� za Kiswahili kama hivi:a, be, che, de, e, fe, ge, he, i, je, ke, le, me, ne, o, pe, re, se, te, u, ve, we, ye, ze

Kwa hiyo, jina la heru� ‘m’ linatamkwa kama silabi ‘me’ tofauti kuliko sauti ya heru� inayotokea ukitamka ‘mtu’ au ‘mti’ au ‘mto’. Na kumbuka, kama unaandika jina la heru� tumia funga na fungua semi (‘ ’).

Unapounganisha sauti za konsonanti na sauti za irabu, unatengeneza silabi (/m/ + /a/ = ma). Kutenganisha neno kuwa silabi kunawasaidia wanafunzi kusoma na kutamka maneno marefu.

Ili kuelewa zaidi zoezi la utambuzi wa sauti, angalia picha ifuatayo na �kiria kuhusu majibu ya maswali. Kama kikundi, hebu tujadili majibu kwa kila swali.

1. Hii ni picha ya nini?2. Sauti ya mwanzo ya neno hili ni ipi? (Litamke polepole na sikiliza sauti)3. Ni sauti za heru� ngapi unazisikia katika neno hili? (zitamke polepole

na sikiliza kwa sauti tofauti) 4. Ni Silabi ngapi unazisikia katika neno hili?

YAFUATAYO NDIYO MAJIBU:

Swali la #1: Kama umesema, ‘nazi’, uko sahihi.

Swali la #2: Kama umesema sauti ya mwanzo ni /na/ au /ne/, hauko sahihi. Kama umesema, /na/ hiyo ni kwasababu umeunganisha sauti /n/ na sauti /a/. Matokeo ni muunganiko wa zote mbili. Kama umesema, /ne/ hiyo ni kwa sababu ulikuwa una�kiria kuhusu jina la heru� ‘n’. Jibu sahihi kwa swali la #2 ni sauti /n/.

Swali la #3: Kama umesema kulikuwa na sauti mbili kwenye neno ‘nazi’, hauko sahihi. Kila heru� katika neno ina sauti yake. Ukiyavunja maneno kuwa sauti, lazima usikilize sauti za kila irabu na konsonanti. Sauti hizi moja moja ni sauti za heru�. Kwa hiyo, neno hili lina sauti za heru� nne: /n/ /a/ /z/ /i/.

Swali la #4: jibu sahihi ni silabi mbili. Silabi katika neno ni: /na/ na /zi/

Page 16: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

14 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

WAAMBIE WALIMU:

“Tafadhali soma maswali peke yako na �kiria utakavyojibu. Jadili majibu yako na mwenzako. Kisha utashirikisha mawazo yako kwenye kikundi. Kama kuna mwalimu atakayekosa mwenzake, mratibu atashirikiana na mwalimu huyo.”

Baada ya dakika 5, uliza kila kundi la wawiliwawili kutoa majibu yao. Halafu pitia majibu sahihi pamoja na kundi husika.) Jibu la 1: Kama umesema, ‘bata’, uko sahihi.Jibu la 2: Kama umesema sauti ya mwanzo ni /ba/ au /be/, hauko sahihi. Kama umesema, /ba/ hiyo ni kwasababu umeunganisha sauti /b/ na sauti /a/. Matokeo ni muunganiko wa zote mbili. Kama umesema, /be/ hiyo ni kwa sababu ulikuwa una�kiria kuhusu jina la heru� ‘b’. Jibu sahihi kwa swali la 2 ni sauti /b/.Jibu la 3: Kama umesema sauti kwenye neno ‘bata’, hauko sahihi. Kila heru� katika neno ina sauti yake. Ukiyavunja maneno kuwa sauti, lazima usikilize sauti za kila irabu na konsonanti. Sauti hizi moja moja ni sauti za heru�. Kwa hiyo, neno hili lina sauti za heru� nne: /b/ /a/ /t/ /a/.Jibu la 4: jibu sahihi ni silabi mbili. Silabi katika neno ni: /ba/ na /ta/

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa kila mwalimu anaweza kushirikisha wengine kitu ambacho ameona kama ni muhimu, hakieleweki au ni kipya. Kisha tunaweza kujadili kwa nini ni muhimu kwa wanafunzi kuwa na uwezo wa kuachanisha sauti katika neno.”

Jibu la 4: Ni muhimu kwa wanafunzi kujua namna ya kuachanisha sauti kwa sababu itawawezesha kuanza kuunganisha sauti hizi kwenye maneno yaliyoandikwa. Kutamka sauti za maneno yaliyoandikwa ni utaratibu wa kusoma kwa sauti.

Page 17: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

15Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

DHANA KUU

Maswali haya yamekupitisha katika hatua za kuachanisha sauti, ambazo ni kuachanisha sauti tofauti katika neno (swali la 2 na la 3). Swali la 4 lilikuwa linahusu kutenganisha sauti, ambayo ni Kutenganisha sauti kwa aidha sehemu ndogo za sauti (sauti za heru�) au sehemu kubwa za sauti za (silabi). Vyote, kuachanisha na Kutenganisha sauti ni vipengele vya utambuzi wa sauti.

Kumbuka kuwa hatukuongelea kuhusu heru� ambazo zinaunda neno, tumeongelea sauti tu. Ni muhimu kwa wanafunzi kujua namna ya kuachanisha sauti kwa sababu wanaweza kuanza kuunganisha sauti hizi kuwa heru� zinazoandikwa. Kutamka sauti za heru� zilizoandikwa ni utaratibu wa kusoma kwa sauti. Uwezo wa kuhusianisha sauti na heru� unajulikana kama foniki, na utajifunza katika moduli ya 8.

FIKIRI - WAWILI WAWILI - SHIRIKISHANA (DAKIKA 10) Ili kuelewa zoezi la utambuzi wa sauti, angalia picha hizi hapa chini na jibu maswali na mwenzio. Kama kuna mwalimu atakayekosa mshirika, mratibu atashirikiana na mwalimu huyo.

1. Hii ni picha ya nini?2. Sauti ya mwanzo ya neno lake ni ipi?3. Unazisikia sauti za heru� ngapi katika neno hili?4. Ni silabi ngapi unazisikia katika neno hili?

Mara tu ukishajibu maswali na mwenzio, waeleze majibu hayo wana kikundi wote.

JADILIANA KATIKA KUNDI KUBWA (DAKIKA 5)

1. Ni mawazo gani muhimu uliyawekea alama ya mshangao (!)?

2. Ni mawazo gani hayaeleweki uliyoyawekea alama ya kuuliza (?)?

3. Ni mawazo gani mapya uliyoyazungushia duara(o)?

4. Kwa nini ni muhimu kwa wanafunzi kuwa na uwezo wa kuachanisha

sauti katika neno?

Page 18: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

16 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutaanza kusoma sehemu inayofuata kwa sauti. Baada ya mwalimu wa kwanza kukamilisha aya, anaweza kuita jina la mwalimu mwingine ili aendelee kusoma aya inayofuata.”

Page 19: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

17Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

Utafanyaje ikiwa kuna heru� nyingi sana na hakuna vidole vya kutosha?!

Baadhi ya maneno yana zaidi ya sauti za heru� nne (idadi ya vidole katika mkono wako). Usiwe na wasiwasi! Ukisha� kia kidole chako cha mwisho, anza tena na kidole chako cha mwanzo. Ukitamka

sauti ya heru� haraka, kimbiza kidole gumba chako kwenye vidole vyako vinne tu.

Hakikisha unasema kila neno polepole sana. Fanya hivyo walau mara mbili. Mara ukishamaliza kusema neno hilo polepole ni lazima urudie tena, lakini safari hii haraka zaidi. Kimbiza kidole gumba chako kwenye vidole vingine wakati ukitamka kila sauti haraka. Fanya hivyo mara mbili. Mwisho, sema neno hilo kama vile unaongea kwa kawaida na kunja ngumi kuashiria neno limetamkwa hadi mwisho.

IGIZO (DAKIKA 20)

Binya vidole: Njia moja ya kuwahimiza wanafunzi kushiriki katika mazoezi ya kuachanisha sauti, ni kupitia katika mbinu iitwayo “Kubinya vidole”. Kubinya vidole ni njia ya kubinya kidole gumba chako kwenye kidole kingine kwa kila sauti utakayoisikia katika neno. Unapaswa kusema kila sauti polepole sana wakati unabinya vidole vyako. Angalia katika picha ili kuona mbinu hii.

HATUA YA 1: binya vidole kwa neno “soko” (sema kila sauti polepole)

/s/ /o/ /k/ /o/

Ni muhimu kwa wanafunzi kujua namna ya kuachanisha sauti kwa sababu wanaweza kuanza kuunganisha hizi sauti na heru� zilizoandikwa. Kutamka sauti za heru� zilizoandikwa ni utaratibu wa kusoma kwa sauti.

/s/ /o/ /k/ /o/

Hatua ya 2: Tamka kila sauti haraka zaidi wakati unakimbiza kidole gumba kwenye vidole vingine

“soko”

Hatua ya 3: Tamka neno katika kasi ya uongeaji wa kawaida (kunja ngumi)

Page 20: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

18 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

(Chagua mtu mmoja aanze kufanya zoezi hilo kwa vitendo)

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutaanza kusoma sehemu inayofuata kwa sauti. Baada ya mwalimu wa kwanza kukamilisha aya, anaweza kuita jina la mwalimu mwingine ili aendelee kusoma aya inayofuata.”

Page 21: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

19Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

SASA, TUANZE KUSHIRIKI ZOEZI LA KUBINYA VIDOLE.

1. Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini atamchagua mwalimu mmoja kuanza. Mwalimu huyo atapaswa kusoma neno kutoka kwenye orodha iliyoko hapa chini, tumia mchezo wa “kubinya vidole” ili kuachanisha sauti za neno polepole. Atafanya hivyo mara mbili.

2. Baada ya kutamka sauti za heru� polepole, mwalimu huyo atapaswa kuzitamka haraka mara mbili. Safari hii akikimbiza kidole gumba kwenye vidole vingine vinne.

3. Mwisho, mwalimu huyo anapaswa kutamka neno kama vile anaongea kwa kawaida. Kunja ngumi kuashiria neno limekamilika.

4. Baada ya mwalimu wa kwanza kufanya hivyo, kundi zima linapaswa kurudia kwa kutumia utaratibu uleule – binya vidole polepole wakati unatamka neno mara mbili, haraka sana binya vidole wakati ukitamka sauti mara mbili, halafu tamka neno kwa kawaida.

5. Halafu mwalimu anayefuatia anapaswa kusoma neno linalofuatia kwenye orodha kwa kufuata utaratibu uleule.

6. Akishamaliza, kundi zima lirudie zoezi hilo kama alivyolifanya.

7. Rudia hadi maneno yote yawe yamefanyiwa mazoezi.

Binya Vidole: Maneno ya Kufanyia Mazoezi

Hapa

Sawa

Maziwa

Ndege

Sungura

KUPIGA MAKOFI KWA SILABI:

Mbinu moja kuwasaidia wanafunzi katika Kutenganisha sauti, ni kuwataka wanafunzi wapige mako� kwa kila silabi watakayoisikia katika kila neno. Kama unafundisha darasa la kwanza na wanafunzi wako bado hawajaelewa silabi ni nini, hiyo haina shida. Bado wanaweza kusikia mfuatano wa sauti ya neno na kupiga mako� kwa kila “mdundo’ katika neno. Kwa mfano:

Page 22: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

20 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa nitasoma baadhi ya maneno kwa sauti na kundi zima litafuata, tutapaswa kusema neno kwa sauti wakati tunapiga mako� kwa kila silabi:”

1. JIKO (mako� 2= silabi 2 ) (Maneno mapya: jiwe, jiji na lako, soko)2. KAKA (mako� 2 =silabi 2) (Maneno mapya: kata, kama na paka)3. VIDOLE (mako� 3 = silabi 3) (Maneno mapya: vita, visa na mkale, mchele)4. NDANI (mako� 2 =silabi 2) (Maneno mapya: ndoo, ndiyo na ndogo, sokoni)5. SALAMA (mako� 4 =silabi 4) (Maneno mapya: saa, sasa na sema, hema)6. DARASANI (mako� 4 = silabi 4) (Maneno mapya: dada, dala na nani)

Page 23: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

21Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

KUPIGA MAKOFI KWA SILABI:

Katika mfano huu neno “paka” linahitaji mako� mawili na kwa hiyo lina silabi mbili. Kwa wanafunzi ambao wamesoma kuhusu silabi darasa la 2 au la 3, hii ni njia nzuri kwa ajili yao kutambua sauti za silabi katika neno. Ni muhimu kwa wanafunzi kujua namna ya kutenganisha na kutambua sauti hizi kwa sababu wanaweza kuanza kuziunganisha sauti hizi na silabi zilizoandikwa. Vilevile wanafunzi wanaweza kuanza kuweka silabi mpya pamoja na kutengeneza maneno mapya.

SASA NI ZAMU YAKO KUANZA ZOEZI HILI:

Kupiga Mako� kwa kila silabi:

1. Mratibu wa Mafunzo ya walimu atasoma neno kwa sauti.2. Kama kundi, rudieni neno kwa sauti wakati mkipiga mako� kwa kila silabi mnayoisikia.3. Wekeni mkazo ni mara ngapi mnapiga mako�4. Halafu shikilieni vidole kuwakilisha namba ya silabi katika neno hilo. Kwa mfano kwa

neno “baba,” mtashikilia vidole viwili.5. Kisha ongeza silabi mpya katika silabi ya kwanza ya neno ili kuunda neno jipya.

Mfano; /ba/ + /ta/ = “bata”6. Kisha ongeza silabi mpya katika silabi ya awali katika neno ili kuunda silabi mpya.

Mfano, /si/ + /ta/ = “sita”

Page 24: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

22 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

WAAMBIE WALIMU:

“Tafadhali soma maswali peke yako na kisha �kiria majibu yako. Jadili majibu yako na mwenzako. Kisha shirikisha mawazo yako katika kikundi.”

Jibu la 1: Mbinu hizi zinawasaidia wanafunzi kuachanisha sauti na silabi katika maneno yanayotamkwa. Hii inaweza kusaidia kusoma kwa sababu wanafunzi wanaweza kuanza kuunganisha sauti hizi na heru� zilizoandikwa. Kutamka sauti za heru� zilizoandikwa ni utaratibu wa kusoma kwa sauti.

Jibu la 2: Kila unapofundisha neno jipya unaweza kubinya vidole kuachanisha sauti au “kupiga mako� kwa kila silabi”.

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutasoma kuhusu kuandaa kipindi cha kusoma na kuandika. Tutasoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.

Baada ya mwalimu wa kwanza kusoma sehemu (kwa mfano, aya au maelezo), atamwita mwalimu mwingine kwa jina ili asome aya inayofuata. “

KUPANGA MKAKATI

Page 25: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

23Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

ZOEZI

FIKIRI - WAWILI WAWILI - SHIRIKISHANA (DAKIKA 10) Baada ya mratibu kusoma maneno yote, jadili maswali yafuatayo na mwenzio:

1. Ni jinsi gani mbinu hizi zinahusiana na kujifunza namna ya kusoma? 2. Ni jinsi gani unaweza kutekeleza mbinu hizi katika masomo yako?

KUPANGA MKAKATI

KUANDAA ‘KIPINDI CHA KUSOMA NA KUANDIKA’ (DAKIKA 30)

Katika kuimarisha umahiri wa wanafunzi kujifunza kusoma na kuandika, ni muhimu mwalimu awe na mpango unaomwezesha kutumia maarifa mapya aliyojifunza wakati wa mafunzo ya walimu kazini kwa vitendo. Aidha, ni muhimu kwa wanafunzi kupata muda zaidi wa kujifunza kusoma na kuandika.

Kurasa zifuatazo zimesheheni mifano ya somo kazi wa jumla kwa ajili ya kazi mbili ambazo pamoja na mshirika mwingine unaweza kujaribu wakati wa vipindi vya kusoma na kuandika (au unaweza kujaribu wakati wa kipindi cha kawaida cha Kiswahili).

1. Soma kila mwongozo wa somo2. Jaza nafasi zilizo wazi katika kila mwongozo wa somo3. Halafu jaribu mikakati wakati wa kipindi cha kusoma na kuandika.

MWONGOZO WA SOMO NAMBA 1: Binya Vidole

UMAHIRI MKUU: Kubainisha sauti za heru�

LENGO KUU: Mwanafunzi aelewe sauti za heru�

LENGO MAHSUSI: Mwanafunzi aweze kutenganisha kwa vitendo sauti za heru� katika maneno

UMAHIRI MAHSUSI: Kutenganisha sauti za heru�

ZANA ZA KUFUNDISHA: Orodha ya maneno

VITABU VYA REJEA: Moduli ya 7

Page 26: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

24 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka uangalie kama walimu wanahitaji msaada)

Page 27: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

25Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI VITENDO VYA KUJIFUNZA

UTANGULIZI 51. Kabla ya somo, andaa orodha ya wanafunzi wako ambao

wameshajifunza/ au orodha ya maneno mapya yaliyo katika ngazi yako. Kwa mfano maneno haya yanatoka katika mtaala wa Kiswahili.

MAARIFA MAPYA

52. Waambie wanafunzi kwamba tutakuwa tunajifunza mchezo

uitwao ‘Binya Vidole’.3. Mchezo huu unahusu kubinya kidole gumba kwenye kidole

kingine kwa kila sauti ambayo unaisikia katika neno4. Uliza wanafunzi kama wanaweza kukupa mifano ya sauti

mbalimbali za heru�.

Kusikiliza maelezo ya

mwalimu kuhusu ‘Binya

Vidole’.

KUIMARISHA MAARIFA

105. Omba mwanafunzi mmoja ajitolee kusema neno (Nani

anaweza kunipatia neno fupi?) na tumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’.

6. Kwanza, anza na ‘Ninafanya’: Tumia neno hilo kuelekeza nam-na unavyobinya kidole chako kwa kila sauti kwenye neno.

7. Hakikisha unasema kila neno polepole.8. Halafu kimbiza kidole gumba kwenye vidole vingine kwa

haraka wakati ukisema kila sauti haraka zaidi.9. Mwisho, sema neno hilo kama vile unaongea kwa kawaida na

kunja ngumi kuashiria neno limetamkwa hadi mwisho.10. Kisha, endelea na ‘Tunafanya’: Himiza darasa lifanye zoezi hilo

kwa pamoja na wewe.11. Mwisho, maliza na ‘Mnafanya’: Himiza darasa lifanye zoezi

wenyewe.12. Endelea kufanya zoezi hili hadi uone kuwa wengi wa wa-

nafunzi wanaweza kulifanya.

Kuigiza mwalimu

wakati anatumia

mkakati wa ‘Binya Vidole’.

Kuzingatia sauti

mbalimbali za heru� katika

neno

MCHAKATO WA UFUNDISHAJI

Maneno ya darasa la. 1

Maneno ya darasa la. 2

Maneno ya darasa la. 3

MamaBabaMimiJina

KitabuKalamu

MezaVikombe

Ko�aKoti

ViatuVijiko

WanyamaWadudu

BaridiMrefu

SokoniSingiziaJengaKatili

UlimboHurumaKalendaMizani

Page 28: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

26 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka uangalie kama walimu wanahitaji msaada)

Page 29: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

27Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI VITENDO VYA KUJIFUNZA

KUTUMIA MAARIFA

1512. Kama utaona baadhi ya wanafunzi wanaelewa polepole

sana, himiza wanaoelewa waendelee kwa kutumia maneno watakayoyachagua wenyewe wakiwa wawiliwawili au katika makundi madogo (waweke wanafunzi katika makundi kwa namna wanavyokaa katika madawati). Halafu anzisha kundi maalum kwa ajili ya wale wanafunzi wanaoelewa polepole na endelea kufanya nao zoezi la Binya vidole mara nyingine na polepole.

13. Waelekeze wanafunzi wachague maneno yao wenyewe na kubinya wakiwa na washirika wengine. Hii inaweza kuwa neno au kitu ambacho wanaona darasani, chakula wanachokipenda n.k

14. Kila wakati ukiwa unafundisha neno jipya darasani, uliza ikiwa mtu mwingine anaweza kubinya vidole kwa neno hilo. Halafu simamia darasa lirudie zoezi hilo.

Kufanya mazoezi

ya kusema maneno

mbalimbaliKutenganisha

sauti mbalimbal za heru� katika

maneno

UPIMAJI 1015. Waambie wanafunzi wafungue madaftari yao na waeleze

kwamba utasoma maneno tofauti matano (Tumia maneno 5 kutoka orodha iliyopo hapo juu au �kiria mengine mapya).

16. Waeleze wanafunzi kwamba ukishasema neno wanapaswa kutumia Binya Vidole kuhesabu idadi ya sauti za heru� zilizopo kwenye neno.

17. Baada ya hapo wanapaswa waandike idadi yake katika madaftari yao

18. Kama wanafunzi hawawezi kutenganisha sauti za heru� katika maneno, rudia somo ukitumia mifano mingine ya maneno.

Kutenganisha sauti za heru� katika maneno

mbalimbali

MCHAKATO WA UFUNDISHAJI

Tathmini:

Maoni:

Page 30: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

28 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka uangalie kama walimu wanahitaji msaada)

Page 31: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

29Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

MWONGOZO WA SOMO NAMBA 2: Kupiga Mako� kwa Silabi

UMAHIRI MKUU: Kutambua sauti za heru�

LENGO KUU: Mwanafunzi aelewe namana ya kutenganisha sauti za silabi katika neno

LENGO MAHSUSI: Mwanafunzi aweze kutenganisha na kuhesabu silabi za neno analosikia

UMAHIRI MAHSUSI: Kusikiliza na kutenganisha sauti za silabi katika neno

ZANA ZA KUFUNDISHA: Orodha ya maneno

VITABU VYA REJEA: Moduli ya 7

HATUA MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI VITENDO VYA KUJIFUNZA

UTANGULIZI 10

1. Kabla ya somo, andaa orodha ya wanafunzi wako ambao wameshajifunza/ au orodha ya maneno mapya yaliyo katika ngazi yako. Kwa mfano maneno haya yanatoka katika mtaala wa Kiswahili.

MAARIFA MAPYA

52. Waambie wanafunzi kwamba tutakuwa tunajifunza mchezo

uitwao ‘Kupiga Mako� kwa Silabi’.3. Mchezo huu unahusu kupiga mako� kwa kila silabi

watakayoisikia katika kila neno 4. Kama wanafunzi wako tayari wameshajifunza silabi, waulize

watoe mifano ya silabi wanazozifahamu. 5. Kama wanafunzi wako bado hawajajifunza silabi, waeleze

kwamba silabi inapatikana kwa kuunganisha sauti mbili za heru�. Mfano, /m/ + /a/ = ma

Kusikiliza maelezo ya

mwalimu kuhusu kupiga mako� na

silabi

MCHAKATO WA UFUNDISHAJI

Maneno ya darasa la. 1

Maneno ya darasa la. 2

Maneno ya darasa la. 3

MamaBabaMimiJina

KitabuKalamu

MezaVikombe

Ko�aKoti

ViatuVijiko

WanyamaWadudu

BaridiMrefu

SokoniSingiziaJengaKatili

UlimboHurumaKalendaMizani

Page 32: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

30 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka uangalie kama walimu wanahitaji msaada)

Page 33: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

31Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI VITENDO VYA KUJIFUNZA

KUIMARISHA MAARIFA

5

6. Omba mwanafunzi mmoja ajitolee kusema neno (Nani anaweza kunipatia neno fupi?) na tumia mbinu ya ‘Ninafanya – Tunafanya – Mnafanya’.

7. Kwanza, anza na ‘Ninafanya’: Tumia neno hilo kuelekeza namna unavyopiga mako� kwa kila silabi kwenye neno.

8. Halafu shikilieni vidole kuwakilisha namba ya silabi katika neno hilo.

9. Kisha, endelea na ‘Tunafanya’: Himiza darasa lifanye zoezi hilo kwa pamoja na wewe.

10. Mwisho, maliza na ‘Mnafanya’: Himiza darasa lifanye zoezi wenyewe.

11. Endelea kufanya zoezi hili hadi uone kuwa wengi wa wa-nafunzi wanaweza kulifanya.

12. Wanafunzi wakishaweza kupiga mako� kutokana na idadi ya silabi katika neno, waambie watengeneze maneno mapya kwa kuchanganya silabi tofauti pamoja.

13. Mfano, piga mako� kufuatana na silabi za “paka”. Kisha sema, silabi ya kwanza ni /pa/. Uliza darasa kama kuna silabi nyingine ambayo unaweza kuongeza kutengeneza neno jipya. Mfano, /ta/. Kisha unapata /pa/ + /ta/ = pata

14. Kisha piga mako� kwa kufuata silabi za “baba”. Uliza silabi ya kwanza ni ipi na kama kuna silabi nyingine ambayo unaweza kuitumia kutengeneza neno jipya. Mfano, /ba/ + /ta/ = “bata”

15. Fanya hivi tena, lakini vilevile onesha jinsi ya kuongeza silabi mwanzoni mwa neno. Mfano, /be/ + /ba/ = “beba”

Kuiga mwalimu

anapotumia mkakati wa

‘Kupiga Mako� ‘.

Kuzingatia silabi

mbalimbali katika

maneno.

KUTUMIA MAARIFA

10

16. Kama utaona baadhi ya wanafunzi wanaelewa polepole sana, himiza wanaoelewa waendelee kwa kutumia maneno watakayoyachagua wenyewe wakiwa wawiliwawili au katika makundi madogo (waweke wanafunzi katika makundi kwa namna wanavyokaa katika madawati).

17. Viambie vikundi vihesabu idadi ya silabi katika orodha ya maneno uliyowapa.

18. Kisha waambie watoe maneno mengine mapya kwa kuongeza silabi mpya mwanzoni na mwishoni katika maneno yaliyopo kwenye orodha.

19. Halafu anzisha kundi maalum kwa ajili ya wale wanafunzi wanaoelewa polepole na endelea kufanya nao zoezi la Kupiga Mako� mara nyingine na polepole.

20. Kila wakati ukiwa unafundisha neno jipya darasani, uliza ikiwa mtu mwingine anaweza kupiga mako� kwa neno hilo. Halafu simamia darasa lirudie zoezi hilo.

Kutenganisha silabi zote

katika maneno.

Kutumia silabi mbalimbali

kuunda maneno

MCHAKATO WA UFUNDISHAJI

Page 34: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

32 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

(Zunguka uangalie kama walimu wanahitaji msaada)

Page 35: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

33Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUPANGA MKAKATI

HATUA MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI VITENDO VYA KUJIFUNZA

UPIMAJI10 20. Waambie wanafunzi wafungue madaftari yao na waeleze

kwamba utasoma maneno tofauti matano (Tumia maneno 5 kutoka orodha iliyopo hapo juu au �kiria mengine mapya).

21. Waeleze wanafunzi kwamba baada ya kusema neno wata-paswa kupiga mako� kuhesabu idadi ya silabi katika neno hilo.

22. Wanapaswa kuandika idadi hiyo katika madaftari yao.23. Kwa darasa 2-3, waambie waandike maneno mapya kwa

kuongeza silabi mwanzoni au mwishoni mwa silabi katika neno.

24. Kama wanafunzi wako hawawezi Kutenganisha silabi kwa usahihi, rudia somo kwa kutumia mifano ya maneno tofauti.

Kutenganisha silabi katika

maneno tofauti.

Kutengeneza maneno mapya

kwa kunyumbulisha

silabi.

Tathmini:

Maoni:

Page 36: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

34 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

WAAMBIE WALIMU:

“Sasa tutaanza sehemu ya utengenezaji wa vifaa vya kufundishia katika moduli hii. Tutapokezana kusoma kwa sauti sehemu inayofuata. Baada ya mwalimu wa kwanza kukamilisha, anaweza kuita jina la mwalimu anayefuata aendelee kusoma aya inayofuata.”

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

Page 37: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

35Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

KUTENGENEZA KADI ZA PICHA (DAKIKA 45)

Kwa sababu utambuzi wa lugha umejikita zaidi kwenye sauti ambazo wanafunzi wanasikia (siyo kuhusu heru� au maneno wanayoona), utumiaji wa picha bila maneno ni njia nzuri ya kutumia ujuzi kama Binya Vidole na Kupiga Mako� kufuatana na Silabi. Leo, utatengeneza seti ya kadi za picha ili kuwakilisha kila sauti ya heru� kwenye alfabeti. Kukamilisha kadi ya picha yako, utahitaji vifaa hivi hapa chini:

VIFAA VYA KADI YA PICHA

√ Karatasi ya A4 au karatasi kama kadi bodi kutoka kwenye boksi (karatasi itakatwa ketengeneza kadi ndogondogo)

√ Penseli

√ Viweka alama au Mkaa

√ Mkasi

√ Utando fomeka (kama vipo)

√ Kalamu za rangi (kama zipo)

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

Kadi unazotengeneza zitakuwa na picha zinazowakili-sha sauti za heru� 24 za alfabeti za Kiswahili. Ili kurahisisha kazi, mnaweza kugawana heru� ili kila mmoja atengeneze baadhi tu ya kadi na mwisho zikamilike 24. Katika darasa unaweza kutumia kadi ya picha uliyotengeneza kwa Binya Vidole au Kupiga Mako� kwa Silabi.

HATUA YA 1: Kata kadi zako Kama unatumia karatasi ya A4, ikunje katika nusu upana. Halafu, fungua ukurasa na kata kwa kufuata mstari wa sehemu iliyokunjwa. Kama unatumia karatasi kubwa zaidi, kata mistatili ambayo ni mikubwa kuliko ukubwa wa mkono wako (jaribu kuifanya kuwa nusu ya ukurasa wa A4)

Page 38: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

36 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

(Baada ya walimu kusoma maelekezo, waeleze waanze kutengeneza picha kadi zao)

Page 39: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

37Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

HATUA YA 2:

Chora picha kwenye kadi zako Chora picha moja katika kila kadi kwa ukubwa utakaoona unafaa, lakini usijumuishe heru� au maneno yoyote kwenye kadi. Picha ziwe kitu cha pekee kinachoonekana kwenye kadi. Mfano wa michoro inaoneshwa hapa chini. Unaweza kunakili picha zilizopo au kuzitumia kama mfano tu. Vilevile, andika heru� ya jina nyuma ya kadi zako.

VIATU WALI YAI ZABIBU

ANDIKA BATA CHUNGWA DUKA EMBE

FAGIO GARI HELA IMBA JUA

KISU LIA MTI NANASI OGELEA

PAKA RULA SAA TAA UA

Page 40: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

38 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

(Kagua ili kuona kama walimu wana matatizo ya kufomeka kadi za picha zao. Wape msaada kwa sababu ni rahisi zaidi ikifanywa na watu wawili).

Page 41: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

39Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

HATUA YA 3:

Fomeka kadi zako Kama umepokea Kivunge cha Vifaa vya Kufundishia kutoka kwa EQUIP – Tanzania, utaona misokoto ya utando wa kufomeka ambao una gundi tayari. Hapa kuna hatua za kukusaidia kufomeka kadi zako:

1. Chora mistari kuonesha umbo la kadi ya picha nyuma ya utando wa kufomeka. Acha nafasi ya ziada kidogo kuzunguka kadi husika. Fanya hivyo kwa upande wa mbele na nyuma ya kadi ya picha.

2. Kata kwa kufuata mistari uliyochora

3. Tumia ukucha kuondoa utando wa kufomeka kutoka kwenye karatasi.

4. Pachika utando wa kufomeka katika upande mmoja wa kadi ya picha kufuatana na mistari uliyochora awali na bonyeza chini ili gundi ikamate vizuri.

5. Fanya hivyo hivyo kwa upande wa pili wa kadi ya picha.

6. Kata utando fomeka uliozidi kuzunguka mipaka ya kadi ya picha.

Page 42: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

40 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

WAAMBIE WALIMU:

“Ukikamilisha kadi za picha zako, jaribu kufanya igizo na mwenzio. Jifanye unamfundisha mwanafunzi wako zoezi la binya vidole”

WAAMBIE WALIMU:

“ Tunaendelea kusoma matini kwa sauti na kwa kupokezana.”

Page 43: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

41Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

UTENGENEZAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA – KADI ZA PICHA

IGIZO (DAKIKA 10)

Ukiwa na mwenzio, jifanyeni kuwa mwalimu na mwanafunzi. Fanya mazoezi ya kumfundisha mwanafunzi kazi tofauti za utambuzi wa sauti (kama vile “Binya Vidole” pamoja na kadi picha):

1. Onesha kadi. Uliza hilo ni neno gani.

2. Mwanafunzi atasema neno. Muoneshe namna ya kugusisha vidole kwenye kidole gumba kwa kila sauti ya heru� katika neno.

3. Fuata hatua tatu za ufundishaji wa “binya vidole”

4. Fanya mazoezi kuhusu picha tofauti na aina mbalimbali kwakupokezana wajibu. Ambaye alikuwa mwalimu awe mwanafunzi na kinyume chake. Unaweza pia kutumia kadi za picha kuuliza sauti za mwanzo/mwisho na idadi ya silabi.

UFUATILIAJI

Baada ya kujifunza moduli hii, mratibu elimu kata, a�sa elimu wa wilaya, pamoja na wakaguzi watafuatilia kuona jinsi unavyotumia ujuzi uliopata katika ufundishaji wako darasani. Ni vizuri uwe tayari kwa ufuatiliaji huo kwa kuandaa

• Maelezo kuhusu uelewa wako wa dhana ya utambuzi wa sauti• zana kama kadi za picha• matumizi ya mikakati kama binya vidole• mojawapo ya masomo uliyoandaa kwa kutumia ujuzi wa moduli

Page 44: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

42 Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

WAAMBIE WALIMU:

“Walimu, tume�ka mwisho wa moduli yetu, tumia dakika kumi kutafakari somo letu la leo. Jaza fomu kurekodi tathmini yako ya moduli. Baada ya kukamilisha chomoa ukurasa huo unipatie. Tafadhali uwe mkweli katika majibu yako kwa sababu yatasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazini ngazi ya shule hapo baadaye.” Kusanya fomu za tathmini zilizokamilishwa na walimu na uwe nazo wakati wa mkutano mwingine katika kundi la kata.

Wakati walimu wanaendelea kujaza fomu za tathmini, tafadhali tafakari kwa ujumla juu ya mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha siku hiyo na jaza visanduku vinavyofuata. Haya utaweza kuyajadili pamoja na Timu ya Wilaya ya Mafunzo Walimu Kazini na Waratibu wengine wa Mafunzo Walimu Kazini wa mkutano unaofuata katika kundi la kata.

MAFANIKO YA JUMLA YA KIPINDI HIKI: CHANGAMOTO ZA JUMLA ZA KIPINDI HIKI:

Shule: ______________________ Wilaya: ____________________ Mkoa:____________________

Tafakuri za Moduli # ________ Mada ya Moduli: _______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki : ________ Mwalimu Mkuu alishiriki : Ndiyo/Hapana

Page 45: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

43Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule

MWISHO

MWISHO (DAKIKA 10)

Binafsi jaza fomu ifuatayo kuweka rekodi ya tathmini ya moduli ya leo. Baada ya kukamilisha, chomoa ukurasa huu na umpe Mratibu wako. Tafadhali uwe mkweli kwa vile mrejesho wako utasaidia kuboresha Mafunzo ya Walimu Kazi ngazi ya shule hapo baadaye.

JEDWALI LA KUTATHMINI Alama 0:

Sikubaliani kabisa na usemi huu

Alama 1: Kwa kiasi Sikubaliani

na usemi huu

Alama 2:Nakubaliana kwa kiasi na usemi huu

Alama 3: Nakubaliana Kabisa

na usemi huu

FOMU YA TATHMINI

Shule: ______________________ Wilaya: ___________________ Mkoa:_____________________

Tathmini ya Moduli: ________ Mada ya Moduli: ______________________________________

Idadi ya walimu walioshiriki: ________ Mwalimu Mkuu alishiriki: Ndiyo/Hapana

Mratibu alikuwepo kuwezesha: Ndiyo/Hapana

Soma semi zifuatazo kisha weka alama ya vema katika kisanduku husika kuonesha jibu lako:

0 1 2 3

1. Dhana kuu ya moduli ya leo ilikuwa inaeleweka.

2. Moduli hii ina mikakati mingi mizuri na yenye manufaa ambayo nitaitumia darasani kwangu.

3. Muda uliotumika kukamilisha moduli hii unafaa. Sikuhisi kwamba ni muda mrefu sana.

4. Moduli hii iliibua mjadala wa kufurahisha na tafakuri ya hali ya juu sana.

5. Violezo vya kipindi cha kusoma na kuandika vilisaidia sana. Natarajia vitakuwa rahisi kuvitumia ndani ya darasa langu.

6. Zana tulizotengeneza leo zitakuwa za manufaa sana (kama inahusika).

7. Mratibu amejiandaa kwa kipindi – amesoma vizuri moduli na ameandaa vifaa vyote vya kufundishia.

8. Mratibu anasimamia vizuri majadiliano – anajua jinsi ya kuwafanya watu wajieleze na namna ya kupata majibu.

9. Mratibu anajua namna ya kusimamia makundi – anahakikisha kuwa walimu wanatoa ushirikiano, wanashirikiana na wana hamasika.

10. Mratibu anajua jinsi ya kuwahamasisha walimu – anafuatilia kujua waliokosa vipindi au kuchelewa na kutukumbusha kwanini Mafunzo ya Walimu Kazini ni muhimu kwetu.

Page 46: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta
Page 47: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta
Page 48: Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu …...Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule 1 DIBAJI Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, imetoa kipaumbele katika sekta

Mwongozo wa Mratibu wa Mafunzo ya Walimu Kazini Ngazi ya Shule