policy training manual

27
1 Dodoma Environmental Dodoma Environmental Network Network (DONET) MWONGOZO WA MWANANCHI JUU YA KUZIFAHAMU NA KUZIJUA SERA NA MIONGOZO KATIKA SEKTA YA MAZINGIRA, ARDHI NA MISITU N D DONET P.O. Box 1414, DODOMA Tel/Fax:026 2324750 E-mail: [email protected]

Upload: samwel-nchagwa-magoiga

Post on 03-Nov-2014

197 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

Tanzania land policy training manual

TRANSCRIPT

Page 1: Policy  Training Manual

1

Dodoma Environmental Dodoma Environmental NetworkNetwork (DONET)

MWONGOZO WA MWANANCHI JUU YA KUZIFAHAMU NA KUZIJUA SERA NA

MIONGOZO KATIKA SEKTA YA MAZINGIRA, ARDHI NA MISITU

N

D

DONETP.O. Box 1414, DODOMA Tel/Fax:026 2324750 E-mail: [email protected]

Page 2: Policy  Training Manual

2

1. UTANGULIZIa) Maana ya Neno Mazingira

Neno mazingira linajumuisha viumbe hai na visivyo hai na mfumo wa maisha ya binadamu na viumbe vinginevyo.

Kwa maana nyingine

Neno mazingira hujumuisha hewa, ardhi na maji; uhai wa mimea na wanyamaukiwemo uhai wa binadamu; hali za jamii, kijamii, kiuchumi na ustawi wa maisha ya wanadmau na jumuia zao, shughuli za wanadamu pamoja na ama sehemumoja, au mchanganyiko wa mahusiano ya vyotevilivyotajwa hapo juu.

Viumbe hai

Mfumo wa maisha ya binadamu

Viumbe visivyo hai

Page 3: Policy  Training Manual

3

b) Maana ya Neno Sera

Neno Sera linatafsiliwa kama ni matamko ya jumla ya

serikali au taasisi au chama yanayotoa mwelekeo au dira

na majukumu ya washirika au wadau. Hivyo kila sera ina

lengo kuu au lengo la jumla ambalo halina budi kuzingatiwa

wakati wa kuainisha madhumuni ya sekta inayohusika na

sera hiyo

Page 4: Policy  Training Manual

4

c) Uhusiano wa wa mazingira na watumiaji

Maisha ya watanzania wote ni yenye uhusiano wa karibu sana namazingira. Ni lazima tujitahidi kusiamamia mazingira na maliasili zake kwa namna inayotoa nafasi ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo yanayojihimili kwa vizazi vya sasa na kwa vizazi vijavyo. Watanzania hatuwezi kufumbia macho athari za kimsingi za uharibifu wa mazingira zitokanazo na shinikizo za shughuli za maendeleo. Matatizo yatokanayo na uharibifu wa mazingira ni halisi na si uzushi, na yanatuhusu sisi sote. Kuna Uhusiano tegemezi kati ya uharibifu wa mazingira na umasikini. Uharibifu wa mazingira hasa husababishwa na kuenea kwa umasikini; vivyo hivyo, umasikini mara nyingi husababisha uharibifu wa mazingira. Matatizo yatokanayo na maendeleo duni kama umasikini, afya duni, na mengineyo ambayo huikabili idadi kubwa ya watanzania, kwa kiasi kikubwa yana uhusiano na mazingira kwa maana ya kwamba ni ya kimaendeleo.

Page 5: Policy  Training Manual

5

d) Athari za binadamu katika utumiaji wa Mazingira

Shughuli za kila siku za binadamu mara nyingi hutegemea uwepo wa eneo ambalo ni sehemu moja wapo ya mazingira. Katika tafiti mbalimbali zimeonyesha ya kuwa hali halisi ya mazingira ya Tanzania inatia wasiwasi. Uchambuzi umebaini matatizo sita yanayohitaji suluhisho la haraka. Matatizo haya ni:

– Uharibifu wa ardhi (kutokana na matumizi mabaya) – Kutopatikana kwa maji safi kwa wakazi wa mijini na vijijini – Uchafuzi wa mazingira– Upotevu wa makazi ya viumbe – pori na bioanuwami – Uharibifu na makazi ya viumbe wamajini; na– Uharibifu wa misitu

Page 6: Policy  Training Manual

6

Cont….Cont….

Matatizo taja hapo huu yamebainika ya kuwa huleta madhara yafuatayo;

• Uharibifu wa ardhi wa unapunguza uwezo wa ardhi kuzalisha mazao katika sehemu nyingi nchini mwetu

• Pamoja na jitihada kubwa za kitaifa, zaidi ya nusu ya wakazi wa mijini na vijijini hawapati maji safi kwa njia ya matumizi ya nyumbani

• Uchafuzi wa mazingira mijini na vijijini unadhuru sana afya za watu wengi, na umepunguza tija ya mazingira

• Upotevu wa au kupunguza kwa makazi ya wanyamapori unatishia urithi wa taifa na unaleta mashaka katika bishara ya utalii ya siku zijazo

• Uzallishaji kutoka kweney mito, maziwa na bahari unatishiwa na uchafuzi wa mazingira na usimamizi hafifu wa rasilimali hizo

• Urithi wa Tanzania wa misitu na nyika unapunguzwa kila mwaka kutokana na ukataji wa miti kw aajiri ya kuni, kuvamiwa kwa maeneo ya hayo kwa ajili ya kilimo, na kwa matumizi mengine

Page 7: Policy  Training Manual

7

e) Jinsi maendeleo yanavyochangia Uharibifu wa Mazingira

Hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali ya Tanzania katika kuimarisha ustawi mzuri wa maisha ya wananchi wake pamoja na kuwaletea maendelea katika sekta zote za kijamii na kiuchumi.

Juhudi zinafanyika ili kuubalisha mfumo wa uchumi ili uwe uchumi wa soko huria, ambapo sekta binafsi inapewa nafasi kubwa zaidi.

Ongezeko la uwekezaji katika sekta mbalimbali za Kiuchumi yatasababisha mabadiliko ya mfumo mzima wa uchumi. Aidha yatathiri shughuli kubwa za kiuchumi, mgawanyo na matumizi, na mazingira kwa ujumla

Page 8: Policy  Training Manual

8

Cont.......

• Katika mabadiliko haya ya kiuchumi, mtazamo wa serikali utakuwa katika sekta za kilimo na viwanda, hususani Utalii,madini na miundo mbinu ya usafirishaji, kama vichocheo muhimu vya kukuza uchumi. Serikali inatambua kwamba, kuendelza sekta ya kilimo, kunaweza kuleta athari kubwa na mbaya kwa maliasili na mazingira, hivyo kudhoofisha zaidi ukuaji wa kilimo.

• Upanuaji wa kilimo unamaanisha upanuzi wa mashamba katika maeneo ambayo ni misitu na yika, maeneo ya wanyama pori; kukaushwa kwa matindiga, kupanua kilimo cha umwagiliaji unaosababisha maji yatuame na yaongeze chumvichumvi ardhinini, na ongezeko kubwa la matumizi ya madawa ya kilimo, uchafuzi wa maji yaliyo chini ya ardhi kutokana na madawa yatumiwayo vibaya mashambani, na kadhalika. Vivyo hivyo serikali inatambua kwamba “kupiga jeki” sekta ya utalii, viwanda na miundo mbinu kunaweza kusabababisha mabadiliko katika matumizi ya maliasili na kwa mazingira

Page 9: Policy  Training Manual

9

2.2. DHIMA NA MALENGO YA SERA YA DHIMA NA MALENGO YA SERA YA

MAZINGIRA- TANZANIAMAZINGIRA- TANZANIA

a) Dhima ya Sera ya Mazingira • Dhima ya sera ya mazingira inalenga kutoa mfumo

muafaka utakaofanikisha kufanya mabadiliko yanayohitajika kuhusiana na masuala ya mazingira katika maamuzi nchini Tanzania. Ikilenga kutoa miongozo na mipango ya sera, ili kufikia upatanifu miongoni mwa sekta na vikundi vya kijamii vinavyohusika, na kukuza usirikiano miongoni mwao.

Page 10: Policy  Training Manual

10

b) Malengo ya jumla juu ya Sera ya Taifa ya Mazingira

Malengo ya haya yameainishwa kama ifuatavyo: • Kuhakikisha upatikanaji, ulizi na matumizi sawa ya rasilimali

katika mahitaji muhimu ya vizazi vya sasa na vijavyo • Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea, na hewa• Kuhifadhi na kuimarisha urithi wetu wa ssili, na usio wa asili,

ikiw apaojana bioanuwani zilizo katika mfumo wa kiikolojia • Kuboresha hali na uzalishaji wa maeneoo yanayoharibiwa ikiwa

ni pamoja na makazi ya vijijini na mijini ili watanzania waishi katika mazingira safi, mazuri na yenye kuzalisha

• Kuongeza utambuzi na ufahamu wa uhusiano katika ya mazingira na maendeleo, kuendeleza ushirikishwa wa watu binafsi na jumuiya katika maswala ya mazingira

• Kukuza ushirikiano wa kimataifa katika agenda ya mazingira na kupanua ushirikishwaji na kutoa mchango kwa mashirika na programu baina ya pande mbili, kikanda, na kimataifa ikiwa ni paoja na kutekeleza mikataba iliyowekwa.

Page 11: Policy  Training Manual

11

3. HALI HALISI YA KIMAZINGIRA KATIKA SEKTA YA ARDHI NA

MISITU

Jitahadi nyingi zimefanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa sera mbalimbali katika kukabilina na matatizo yanayokabilina na mazingira, ikiwa ni pamoja na Sera ya Misitu ya Mwaka 1998, na Sera ya Ardhi ya mwka 1999. sera zote hizi zilitanguliwa na sera ya kilimo ya mwaka 1983 na ile ya mifugo ya mwaka 1984. Zote zinasisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwa na mipango na matumizi bora ya ardhi na mazingira kwa ujumla.

Page 12: Policy  Training Manual

12

a) SEKTA YA ARDHI

• Historia ya uchumi wa nchi yetu inaonyesha kuwa muda mrefu kabla na baada ya uhuru pato la wananchi wengi linaendelea kuwa dogo. Na hii imetokana na kuwa na mfumo ya kisiasa na kuchumi ambayo haikuweza kuleta maendeleo makubwa kwa jamii.

• Kutokana na dhana hiyo serikali imetayarisha sera inayoeleza masuala ya usimamizi wa ardhi. Sera hii imetayarishwa kwa kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau (washiriki) wote, ikiwemo serikali yenyewe, taasisi mbalimbali zinazojihusisha au kutumia ardhi, na wananchi wa wote wa Tanzania

Page 13: Policy  Training Manual

13

Cont………..

• Hivyo basi Sera ya Taifa ya Ardhi inalenga mambo makuu yafuatayo:

• Kuigawanya ardhi bila ya upendeleo wowoet • Kuwapatia wananchi wa hali zote Haki ya kumiliki ardhi hasa

kwa wakulima na wafugaji wadogo• Kuhakikisha wananchi wanazifahamu, wanazielewa na

kuzikubali kulingana na sheria haki za umiliki wa ardhi, na kuwa na Hati za kisheria za umiliki wa ardhi.

• Kuwa na ardhi pekee inayoweza kumilikiwa na mtu moja• Kuhakikisha ardhi inahifadhiwa hasa kwa uzalishaji ili

kuboresha maisha ya wakazi husika • Kuendeleza na kuweka mbinu madhubuti katika usimamizi

wa ardhi na kuhakikisha mingogoro inatatuliwa kwa usawa

• Kuhakikisha kuna usimamizi mzuri wa ardhi na hakuna

matumizi ya uharibifu ya ardhi.

Page 14: Policy  Training Manual

14

Cont……

Sera inasisitiza umuhimu wa ardhi ya Tanzania

kusimamiwa kama ifuatavyo:› Rais ndiye mwenye dhamana ya kujua ardhi inatumiwa

vipi na wananchi wake

› Ardhi ina thamani – ikiwa na maana unaweza kuinunua au kuiuza

› Wananchi hawana haki ya kujimilikisha ardhi bila kibali cha Serikali na kutokuwa na hati miliki, au bila kuilipia

› Halimashauri za vijiji ndio wasimamizi wa ardhi yote ya kijiji

› Mikakati inapaswa kuwekwa kwa kulinda maeneo ya uhifadhi hasa ya uvunaji maji, visiwa, pwani, misitu, mito, maliasili n.k

Page 15: Policy  Training Manual

15

b) SEKTA YA MISITU – Katika sekta ya Misitu Sera ya Taifa ya Misitu imetungwa

kwa kuzingatia mfumo wa jumla wa kiuchumi, kimazingira na kijamii. Sera ya misitu ina madhumuni yanayolenga kupiga vita umasikini na ufukara ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi. Kimazingira sera inalenga kuhakikisha upatikanaji, ulinzi, na maamuzi sawa ya rasilimali kwa ajili ya mahitaji muhimu ya vizazi vya sasa na baadae bila kuharibu mazingira na kuhatarisha afya na usalama wa binadamu.

– Neno MisituMisitu lina maana ya ardhi yote yenye uoto wa mimea na uwingi wa miti ya kimo chochote kile ivunwayo, na isiyovunwa na iliyo na uwezo wa kuota mbao na mazao mengine yenye kurekebisha hali ya hewa au mfumo wa vyanzo vya maji, au yenye kuhifadhi mifugo au wanyama pori.

Page 16: Policy  Training Manual

16

Cont………

• Manufaa ya misitu ni kuwa pamoja na – Chanzo cha mazao ya mbao (mabanzi, kuni, nguzo,

mkaa na majengo) – Chanzo cha mazao yasiyo ya mbao kama gundi, asali,

nta, dawa , matunda, uyoga, mboga za majani na wadudu

– Makazi ya wanyama pori– Kuhifadhi vyanzo vya maji na udongo– Jutekeleza masuala ya mila kama tambiko – Shughuli za utalii– Kutoa ajira katika viwanda vya misitu kama shughuli za

ukusanyaji na uuzaji wa nishati za timbao pamoja na mazao mengine kanma vile majani ya kuezekea, vinu na mitumbwi

Page 17: Policy  Training Manual

17

Lengo na Madhumuni ya Sera ya Misitu

Lengo:Lengo kuu sera ya Taifa ya misitu ni kuimarisha mchango wa sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa kuifadhi nakusimamia misitu yake kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo Madhumuni:Madhumuni ya sekta ya misitu kwa kuzingatia lengu kuu ya Taifa ni:-• Kuhakikisha upatiakanaji endelevu wa mazao na huduma ya

misitu kwa kuwa na maneno ya kutosha ya misitu iliyohifadhiwa chini ya usimamizi madhubuti

• Kupanua ajira na kuendeleza pato kutokana na maendeleo endelevu ya viwanda vilivyijikita kwenye misitu na biashara

• Kuimarisha mifumo ya ikolojia kwa kuhifadhi bionuwai ya misitu, maeneo lindimaji na rutuba ya udingo

• Kukuza uwezo wa Taifa kusimamia na kundeleza sekta ya misitu kwa wadau (washirika wengine)

Page 18: Policy  Training Manual

18

Cont………Cont………

Kulingana na madhumuni hayo Sera inaelekeza yafuatayo ili kuwa na maendeleo endelevu ya misitu na uhifadhi wa mazingira

a) Matumizi mazuri ya rasilimali za misitu na programu za upandaji wa miti ili kukidhi mahitaji ya ndani na ya nje ya nchi

b) Hifadhi ya ardhi kwa kuifanika kwa uoto itaendelezwa kwa kupanda miti

c) Usimamizi utaimarishwa na sheria zianzohusika zinazohusika zitatekezwa kwa kupanda miti

d) Misitu asilia yenye thamani kubwa za kibiolojia itahifadhiwa.

e) Wakulima, wafanyabiashara, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs/ CBOs), shule na vikundi vingine vitahamasishwa kujishughulisha na upandaji miti.

Page 19: Policy  Training Manual

19

4.4. USHIRIKI/ NAFASI YA SERIKARI, USHIRIKI/ NAFASI YA SERIKARI, VIKUNDI AU JUMUIYA ZA KIRAIA VIKUNDI AU JUMUIYA ZA KIRAIA

KATIKA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA KATIKA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA

MAZINGIRAMAZINGIRA

• Mazingira ni urithi wa kiasili na wa kiutamaduni. Kwa hiyo, vizazi vya sasa vinaweza kunufaika. Ni lazima kutambua utaratibu iliopo wa uendeshaji na kufikia njia na namna ambazo uratibu wa, na ushirikino kati ya vyombo mbalimbali vya kitaasisi vyenye majukumu yanayolingana, unavyoweza kuimarishwa. Aidha kuna haja ya kuunganisha dhamira na kazi za vyombo hivyo

• Baraza la Mawaziri ndilo kamati kuu na ya kudumu yenye jukumu la kuratibu na kutung asheria ambazo wizara mbalimbali huwasilisha malengo y aSera, mipango ya utekelezaji na vipaumbele

Page 20: Policy  Training Manual

20

a) Wizara yenye dhamana ya kusimamia Mazingira

• Wizara inashughulikia mazingira, kama mamlaka ya juu kabisa na kichocheo cha utendaji kwa niaba ya Serikali nzima, itasimamia sera nzima, mipango na utendaji wa majukumu ya usimamiaji wa shughuli za mazingira. Na itakuwa chanzo cha maelekezo yote na ushauri kuhusu kuendesha mwelekeo muhimu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutunga, kuchambua na kutathimini kwa mapana sera nzima ya mazingira, pamoja na kutunga na kupitia malengo yanayopatana na mtazamo huo.

• Wizara itatoa misimamo kuhusu sera kwa wakati unaofaa, inayowakilisha nguvu za pamoja kwa kuhakikisha kwamba matumaini y aserikali kuhusu mazingira yanawasilishwa kwa wakati. Wizara itasimamia utekelezaji wa maagizo na usimamiaji wa sera, pamoja na kupima mabo muhimu ya mazingira ikiwemo n autatuzi wa matatizo yanayojitokeza kwa nji aya kuunganisha nguvu za taasisi mablimbali, kupanua uwanja wa makubaliano na kupitisha vipaumbele vilivyokubaliwa.

Page 21: Policy  Training Manual

21

Cont......Cont......• Mkurugenzi wa Mazingira (Director of Environment)

Mkurugenzi wa mazingira ana jukumu la Kuratibu vyama, vikundi au tasisi zote, ikiwemo serikali, katika maswala yote yanayohusiana na mazingira. Kuishauri serikali katika maswala ya kisheria yahusianayo na mazingira kwa kushirikisha mahusiano ya kimataifa, na usimamizi mzima wa serikali katika mazingira.

c) Bazara la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (National Environment Management Council) NEMC

Baraza hili lina jukumu la kutoa Ushauri, na kusimamia utekelezaji wa maamuzi yanayohusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira na kufanya kazi ya usuluhishi wa kitaalamu katika kushughulikia tathimini ya athaliza uharibifu wa mazingira. Pia lina kazi ya kuaratibu na kufanya tafiti mbalimbali zihusianazo na uhifadhi wa mazingi kwa kuzishirikisha taasisi zote za umma na binafsi.

Page 22: Policy  Training Manual

22

Cont....Cont....

d) Serikali za Mitaa• Serikali za mitaa zinawakilisha sehemu yenye uwezo

mkubwa katika mfumo mzima wa serikali. Hiki ni chombo muhimu katika kuamua na kufanikisha malengo ya sera za mazingira. Zina wajibu wa kujenga, kuendesha na kuendeleza miundombinu kiuchumi, kijamii na kimazingira

• Serikali za mitaa zitawajibika kusimamia michakato y amipango na kuanzisha sera na sheria ndogondogo kuhusu mazingira kwenye maeneo yao,pamoja na kutekeleza dhima muhimu ya kuelimisha, kuhamashisha na kuitikia maoni y awatu wake kwa shabaha ya kutekeleza malengo ya mazingira.

Page 23: Policy  Training Manual

23

Cont.....Cont.....

e) Kamati za Mazingira (Mkoa, Wilaya, Kata na Kijiji)

• Kutakuwepo na kamati ya Sera ya mazingira kwenye ngazi ya mkoa ambayo itawajumuisha wakuu wa wilaya wa eneo hilo na mweyekiti wake atakuwa Mkuu wa Mkoa. Kamati hii itashughulikia mambo ambayo yanaathiri mazingira kimkoa, itatoa mwongoz wa sera au kupendekeza hatua zinazofaa kuchukuliwa katika kutekeleza sera.

• Kazi za kamati ya mkoa ya Sera ya mazningira itasaidiwa na Kamati za wilaya, Kata na Vijiji na zitafadhiliwa na mabaraza ya wilaya, kata na vijiji. Kamati hizo zitawajibika kuratibu nakutoa ushauri kuhusu vikwazo kweney utekelezaji wa Sera na programu za mazingira; kuongeza mwamko au utambuzi kuhuz mazingira, utoaji habari, ukusanyaji na utawanyaji habari zinazohusu mazingira katika wilaya, kata au vijiji vyao.

Page 24: Policy  Training Manual

24

f) Vikundi vya kijamiiVikundi vya kijamnii vinaweza saidia uhifadhi wa mazingira kwa kuwa na miradi/ shughuli kuu mbili:

– Shughuli za kiuchumi

Ambazo ni Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Usindikaji, Viwanda vidogovidogo na vikundi vya akiba na mikobo. Shughuli hizi za kiuchumi mara zote hulenga kuongeza kipato. Ambapo uzalishaji wa bidhaa hutegemewa kuwa wa juu na baadae kuzwa na kupata fedha ambazo zitatumiwa na wanakikundi.

– Shughuli za kijamii

Miradi ya kijamii hulenga kuboresha upatikanaji wa hudumu mbalimbali kwa maeneo yao (kama vile mahitaji ya viwanda, Elimu, Afya n.k) huduma zinapokuwa karibu hupelekea kupunguza gharana za upatikanaji.

Page 25: Policy  Training Manual

25

Cont.......

• Vyama vya Akiba na Mikopo

(SACCOS na MaBank)

Vikundi hivi vyaweza kuanzishwa na watu wenye kukubaliana kwa hiari yao kujiwekea akiba ya mazao, fedha au mifugo kwa lengo la kusaidiana pale mmoja wao anapokuwa na shida kwa njia kukopeshana.

Hivyo kuwa kutumia vikundi hivi kutakuwa na urashisi katika kupta mafunzo ya njia bora za uhifadhi wa ardhi, njia za matumiz bora ya rasilimali na uundwaji wa vikundi vya miradi rafiki wa mazingira

Page 26: Policy  Training Manual

26

5. HITIMISHOKutokana na kero ya umasikini wa wananchi na uharibifuwa mazingira wananchi kwa kushirikiana na serikali na taasisi/ asasi/ wadau mbalimbali wanapaswa kuamka na kuamua kwa pamoja kupambana na uharibifu wa mazingira unaopelekea umaskini katika jamii zetu.

Hivyo basi kwa kujatilia mkazo haya mkazo unatakiwa zaidi katika upangaji wa matumzi ya ardhi kwa kuwashirikisha wananchi wenyewe ili hatimaje waweze kutekeleza mipango na sera kikamilifu. Na mwongozo huu unaweka wazi mambo muhimu yakufanywa na kutekelezwa ikiwa sera na sheria zitatekelezwa ipasavyo.

Page 27: Policy  Training Manual

27

ANSTENIANSTENI

Imeandaliwa na

Lameck Batimo SebyigaProject Officer/ Liaison Officer

Dodoma Environmental Network (DONET) P.O.Box 1414

Cell: +255 713 285290/ +255 757 395662Email: [email protected]

Dodoma, Tanzania