ripoti ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa jamii (sam)sikika.or.tz/images/content/mp3/kilwa report...

28
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Lindi Mei 2017

Upload: others

Post on 07-Feb-2020

18 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Lindi

Mei 2017

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Lindi

Imeandaliwa na Timu ya SAM

Mei 2017

Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa
Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

i

Mafanikio ya zoezi la Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM), kwa lugha ya Kiingereza ikijulikana

kama Social Accountability Monitoring (SAM) katika Halmashauri ya Kilwa yametokana na ushirikiano

wa hali ya juu kutoka kwa wadau wote wa Afya hapa Wilayani. Sisi, Timu ya SAM Kilwa tunatambua na

kuthamini jitihada zilizofanywa na wadau wote katika kukamilisha zoezi hili kwa mafanikio makubwa.

Tunapenda kuishukuru Sikika, hususani kwa wawezeshaji wa mafunzo haya ambao ni Maria Kay-

ombo, Clemence Mombeki na Richard Msittu, juhudi zao na maarifa yamewezesha mchakato wote wa

utekelezaji wa zoezi la SAM kufanikiwa kwa weledi mkubwa.

Shukrani za dhati ziende Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mh. Christopher Ngubiagai kwa kutambua

umuhimu, kuthamini na kusimamia utekelezaji kuanzia mwanzo hadi mwisho. Aidha, Timu inamshuku-

ru kwa kukubali kuwa mlezi wa Timu ya SAM Kilwa, jukumu ambalo analitekeleza kwa vitendo. Pia

timu ya SAM inatoa shukrani kwa Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji wa Hal-

mashauri ya Kilwa. Utayari wao na ushirikiano mkubwa waliotuonesha uliijenga Timu na kuiimarisha

kwa kiasi kikubwa. Jitihada zao ziliwezesha kujenga na kukuza mahusiano na Idara za Halmashauri

hususani idara ya Afya, ushirikiano wao uliwezesha kupatikana kwa nyaraka mbalimbali muhimu kwa

ajili ya uchambuzi. Kwa ngazi zote za Halmashauri, Timu ya SAM inapenda kuwashukuru watendaji

wote hasa wa kata na vituo vya huduma za afya vya Halmashauri ya Kilwa kwa kutoa ushirikiano

wakati wa hatua ya uhakiki vituoni.

Shukrani za pekee ziwaendee wajumbe wa Timu ya SAM wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa

kushiriki kikamilifu katika zoezi zima la SAM.

Nugu Ruki JamadariMwenyekiti – Timu ya SAM Kilwa

Shukrani

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

ii

Yaliyomo

SHUKRANI i

YALIYOMO ii

ORODHA YA VIFUPISHO iii

MUHTASARI iv

SEHEMU YA KWANZA 1

1.0 Utangulizi 1

1.1 Lengo la mchakato wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii 1

1.2 Muundo wa Timu ya SAM 1

1.3 Mafunzo na Uchambuzi wa Nyaraka 2

1.4 Uhakiki, Ufafanuzi na Uthibitisho wa Hoja za SAM 3

1.5 Taarifa ya zoezi la SAM na Maazimio ya Wadau wa Afya 3

SEHEMU YA PILI 5

Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali 5

2.0 Utangulizi 5

2.1 Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali 5

2.2 Usimamizi wa Matumizi 7

2.3 Usimamizi wa Utendaji 10

2.4 Usimamizi wa Uwajibikaji 16

SEHEMU YA TATU 19

3.0 Mapendekezo na Maazimio ya Kuboresha Huduma 19

3.1 Kiambatisho Na. 1: Majina ya wajumbe wa Timu ya SAM 20

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

iii

Orodha ya Vifupisho

CAG Controler and Auditor General (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali)

CCHP Council Comprehensive Health Plan (Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri)

CHF Community Health Fund (Mfuko wa Afya ya Jamii)

CHMT Council Health Management Team (Timu ya utawala ya afya ya Halmashauri)

DMO District Medical Officer (Mganga Mkuu wa Wilaya)

HFGC Health Facility Governing Committee (Kamati ya Usimamizi ya Kituo cha Afya)

MSD Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa)

MTEF Medium-Term Expenditure Framework (Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya

Serikali)

NHIF National Health Insurance Fund (Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya)

OC Other charges (Matumizi Mengine)

SAM Social Acountability Monitoring (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii)

WAVIU Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

WEO Ward Executive Officer (Afisa Mtendaji wa Kata)

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

iv

Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring” (SAM) ni zoezi lenye lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kuchambua utekelezaji wa mipango kuan-zia ngazi ya jamii mpaka halmashauri. Lengo kuu la SAM ni kuhimiza ushirikishwaji, ufuatiliaji na uwajibikaji wa watendaji/watoa huduma ikiwemo huduma za afya ili kuwapa wananchi haki zao za msingi kama ilivy-oainishwa katika sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Sheria na mikataba hiyo ni pamoja na; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara za (11), (12), (14) – (28), Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni unaofa-hamika kwa lugha ya Kiingereza kama“International Covenant for Economical, Social and Cultural Rights (ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

Tangu mwaka 2012, Sikika imekuwa ikishirikiana na Halmashauri mbalimbali katika kuendesha zoezi la SAM kwa kuunda timu katika halmashauri hizo. Timu hizi za SAM zinajumuisha wananchi wa makundi yote, wajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa dini na wa madiwani. Timu ya SAM hujengewa uwezo wa kushiriki katika kupanga na kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. SAM pia inalenga kuiwezesha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji, chakula na makazi.

Sikika imekuwa ikiendesha zoezi katika wilaya zaidi ya 10 zikiwemo Mpwawa, Kondoa, Ilala, Kibaha, Singi-da vijijini, Lindi, Kilolo, Simanjiro, Kiteto, Temeke na Kinondoni na wilaya hizo zimewezeshwa kuwa na timu ya SAM, ufuatiliaji na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma za afya umeongezeka, ikiwemo uboreshaji wa miundombinu katika vituo vya huduma za afya na vilevile katika kupanga bajeti yenye kufuata vipaum-bele sambamba na matumizi yenye tija.

SAM katika wilaya ya Kilwa imefanyika mwezi Aprili, 2017, ikiwa ni moja ya Wilaya mpya ambazo Sikika imeanza kutekeleza mpango mkakati wake wa mwaka 2016 -2020.

Baadhi ya matokeo ya uchambuzi yaliyotokana na zoezi hili ni pamoja na Halmashauri kushirikisha wadau wa Afya katika kupanga mpango kabambe wa Afya jambo ambalo ni jema kwa maendeleo ya sekta katika Wilaya. Kwa upande mwingine, imeonekana kuwa kuna upungufu wa wafanyakazi katika vituo vya kutolea huduma, ukosefu wa vifaa tiba ikiwemo vitanda, magodoro, vitendanishi, mikasi, mashine za kupima BP na vitakasa vifaa (sterlilizer).

Pia imeonekana kuwa kuna ukosefu mkubwa wa maji safi na salama katika vituo, majengo ni chakavu na upungufu wa nyumba za wafanyakazi na vilevile kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, vituo 10 havina kabisa vichomea taka, na vituo 5 vimeonekana kuwa na vichomea taka vibovu visivyotumika kwa sasa. Aidha, vituo 4 pekee kati ya vituo vyote vilivyotembelewa vilionekana kuwa na shimo la kutupia kondo la nyuma linalokidhi viwango.

Kutokana na matokeo hayo, Timu ya SAM na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa umeweka mkakati wa kuhakikisha masuala hayo muhimu yaliyoibuliwa yanafanyiwa kazi kwa ushirikiano na wadau wa Afya wilayani na wananchi kwa ujumla.

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

1

1.0 UtanguliziMchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii ni mbinu shirikishi ya uwajibikaji inayohusisha watoa

huduma za Umma na wapokea huduma. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, zoezi hili limetekele-

zwa katika sekta ya afya ili kutathmini na kuiwezesha Halmashauri kuboresha utoaji wa huduma za

kijamii, hususani huduma za afya ikiwa ni sehemu ya haki za Binadamu.

Sikika iliiwezesha Timu ya SAM iliyokuwa na jumla ya wajumbe 15, kufanya ufuatiliaji kwa kufuata

miongozo sahihi ya sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Sheria na mi-

kataba hiyo ni pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara za (11), (12), (14)

– (28), Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa haki za kiuchumi, kijamii na kiutama-

duni unaofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama “International Covenant for Economical, Social and

Cultural Rights (ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji ili

kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

1.1 Lengo la mchakato wa ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamiiMadhumuni ya utekelezaji wa mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii “Social Accountability

Monitoring - SAM” ni kuwajengea uwezo watoa huduma na Jamii kushiriki kikamilifu katika kupanga,

kutekeleza na kufuatilia miradi mbalimbali katika ngazi husika. SAM pia inalenga kuiwezesha jamii

kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma zinazokidhi

mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii.

1.2 Muundo wa Timu ya SAM Timu ya SAM huundwa baada tu ya utambulisho wa mradi kwa Serikali na ngazi ya Jamii. Ngazi za

utambulisho wa mradi ambazo hutoa wawakilishi ni pamoja na Baraza la Madiwani, Mkutano wa wa-

dau wa Afya, na Mikutano ya Jamii. Kwa Halmashauri ya Kilwa, Baraza la Madiwani lilitoa wawakilishi

wawili (2) (ME & KE) ambao walichaguliwa na

kuidhinishwa na Baraza.

Mkutano wa wadau ambao huongozwa na

Mkuu wa Wilaya uliwezesha kupatikana kwa

wajumbe kutoka CHMT (1), CMT (1), Bodi ya

Afya ya Wilaya (1), Viongozi wa dini (1), Kama-

ti ya Usimamizi wa Kituo (1), Asasi za Kiraia

(1), Watendaji wa Kata (1), Makundi maalu-

mu (WAVIU - 1) na watu wenye ulemavu (1).

Aidha kwa kundi la wananchi ambao huwakili-

sha Jamii hupatikana kupitia mikutano ya Jamii

Sehemu ya Kwanza

Muundo wa Timu ya SAM ya Wilaya ya Kilwa 2017Wananchi 4Wananchi - Watu Wanaoishi na VVU 1Viongozi wa Dini 1Wananchi-Watu wenye Ulemavu 1Madiwani 2Watendaji wa kata 1Kamati ya usimamizi wa kituo /HFGCs 1CHMT 1CMT 1Asasi za Kiraia 1Bodi ya afya ya Wilaya 1Jumla 15

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

ambayo hufanywa katika ngazi za kata. Katika zoezi hili, wawakilishi wa wananchi walipatikana kupitia

mikutano ya Jamii kutoka kata za Pande (1), Kivinje (1), Njinjo (1) na Somanga (1). Jumla ya wajumbe

wote wa Timu ya SAM ni 15.

1.3 Mafunzo na Uchambuzi wa Nyaraka Hatua ya mafunzo huanza mara baada ya Timu ya SAM kuundwa. Hatua hii iliikutanisha Timu na

wawezeshaji wa Sikika kwa mara ya kwanza kwa pamoja. Mafunzo yalianza kwa kuijengea uwezo

Timu kuelewa dhana ya Uwajibikaji kwa Jamii na haki za msingi za binadamu, ambapo Timu iliweza

kupata uelewa kuhusu nguzo kuu tano za mchakato wa SAM ambazo ni Mipango na Mgawanyo wa

Rasilimali, Usimamizi wa Matumizi, Usimamizi wa Utendaji, Usimamizi wa Uadilifu, na Usimamizi wa

Uwajibikaji.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakifanya uchambuzi wa nyaraka.

Diwani wa Kata ya Miteja Mh. Ibrahim Msati akichangia jambo katika kikao cha baraza la Madiwani.

2

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

3

Katika kila hatua ya mafunzo, Timu iliweza kupata uelewa wa kina kuhusu nyaraka mahususi kwa kila

hatua. Mafunzo na uchambuzi wa nyaraka kwa vitendo uliambatana na kuchambua kwa kina nyaraka za

Mpango Mkakati wa Halmashauri (2012/2013-2016/2017), Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri

(CCHP) 2015/2016, Ripoti za utekelezaji za mpango kabambe wa afya wa Halmashauri kwa kila robo

mwaka 2015/2016, Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya Serikali (MTEF) 2013/2014-2017/2018,

Mihtasari ya taa-

rifa za vikao vya

baraza la Madiwani

2015/2016, Ripo-

ti za ukaguzi za

mkaguzi wa ndani

2015/2016, Barua

ya Menejimenti

toka kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) 2015/2016. Taarifa zote hizi zilisaidia kuijenga

timu kwa kila hatua ya mchakato wa SAM. Uchambuzi wa kina uliofanywa na timu uliiwezesha kujenga

hoja mbalimbali ambazo ziliweza kuimarishwa kwa kupatiwa ufafanuzi, uhakiki na uthibitisho.

1.4 Uhakiki, Ufafanuzi na Uthibitisho wa Hoja za SAMTimu ilijengewa uwezo kuhakikisha kila hoja inapitia hatua kuu tatu za ufafanuzi, uhakiki na utibitisho

ili kuweza kufikia uboreshaji wa huduma za afya Wilayani. Hivyo, baada ya mafunzo na uchambuzi wa

nyaraka, timu ya SAM iliandaa dodoso lenye hoja zilizotokana na uchambuzi wa nyaraka ili kwenda ku-

hakiki katika vit-

uo vya huduma

za afya. Jumla

ya vituo 34 vi-

litembelewa na

timu kwa uhakiki

na kupata ufafanuzi wa taarifa zilizopatikana katika uchambuzi wa nyaraka. Hatua hii iliipelekea Timu

kufanya majumuisho ya awali na kukutana na watendaji (CHMT & CMT) ambao baada ya kupitia hojaji

waliweza kutoa ufafanuzi kwa kila hoja. Mkutano huu wa ndani wa pamoja uliipa Timu fursa ya kuhoji

kwa kina na kuafikiana maeneo ya maboresho.

1.5 Taarifa ya zoezi la SAM na Maazimio ya Wadau wa AfyaMkutano wa wadau wa afya wa mrejesho ni mahususi kwa Timu kuwasilisha majumuisho ya hoja na

ufafanuzi wa menejimenti ili kujadili na kupitisha maazimio ya pamoja kwa ajili ya utekelezaji. Hatua

hii ilifikiwa kwa mafanikio makubwa kwa Timu kutoa mrejesho wenye jumla ya hoja 33 ambapo jumla

ya hoja 23 kati ya 33 wadau waliazimia ziingizwe katika mkakati wa maboresho na hoja 10 zilipewa

baraka ikiwa ni pongezi na mafanikio kwa Halmashauri.

Vyanzo vikuu vya hoja za SAM ni pamoja na:-• Changamoto ya nyaraka za Halmashauri kuwa katika lugha ya Kiingereza na mapungufu ya mfu-

Nyaraka Zilizo Chambuliwa na Timu• Mpango Mkakati wa Halmashauri 2012/2013-2016/2017• Mpango Kabambe wa Afya kwa Halmashauri (CCHP) 2015/2016• Ripoti za Utekelezaji wa Mpango wa Afya kwa kila robo mwaka 2015/2016• Mihtasari ya Vikao vya Baraza la Madiwani 2015/2016• Barua ya Menejimenti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) 2015/2016• Ripoti za Mkaguzi wa Ndani 2015/2016

Timu ya SAM ilifanya zoezi la uhakiki kwa kutembelea vituo 34 kati ya 55Hospitali ya Kinyonga, na Vituo vya afya vya Masoko, Tingi, Njinjo na PandeZahanati za Zinga, Singino, Mavuji, Nakingombe, Migulue, Mitole, Lihimalyao, Mikoma, Mbwemkuru, Kilanjelanje, Kiwawa, Mtandi, Migelegele, Mandawa, Lushungi, Kikole, Hoteli 3, Darajani, Luhatwe, MT. Kimwaga, Chumo, Malendegu, Mingumbi, Kisiwani, Mpala, Nangurukuru, Matandu, Somanga, Miteja.

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

4

mo wa uandaaji na utunzaji wa nyaraka

• Uwezo mdogo wa kupanua wigo na kutumia rasilimali za ndani

• Upungufu wa rasilimali za kuendesha kitengo cha ukaguzi wa ndani na kamati ya ukaguzi

• Tatizo la upungufu wa watumishi wa sekta ya Afya, dawa na vifaa tiba

• Changamoto ya miundombinu ya afya (Maji, Umeme, Majengo, Barabara)

Aidha, utekelezaji wa maazimio unaanza mara tu baada ya uwasilishaji wa ripoti ya SAM kwa wadau

na utaendelea katika kipindi chote cha mwaka wa fedha 2017/2018. Katika kipindi chote cha utekeleza-

ji, Timu ya SAM itaendelea kufanya ufuatiliaji kwa ushirikiano wa karibu na Halmashauri, ofisi ya Mkuu

wa Wilaya, ofisi ya M/Kiti wa Baraza la Madiwani pamoja na Sikika ambao wataendelea kuwa waratibu.

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

5

Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali

2.0 UtanguliziSehemu hii inafafanua kwa kina uchambuzi na matokeo kulingana na nyaraka pamoja na hali halisi

kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma za afya ambapo Timu ya SAM ilifanya ziara ya uhakiki. Hivyo,

itatoa picha halisi ya majumuisho ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa na ufafanuzi uliotolewa na mene-

jimenti. Mtiririko wa hoja na ufafanuzi umegawanywa katika hatua tano za SAM kama ilivyoainishwa

katika vipengele vinavyofuata.

2.1 Mipango na Mgawanyo wa RasilimaliHatua hii ni ya kwanza katika mfumo wa uwajibikaji kwa jamii ambayo ni mahususi kwa kutathmini na

kuboresha mchakato wa mipango na mgawanyo wa rasilimali. Hutoa fursa kwa Timu za SAM ama

Jamii kujifunza na kuchambua nyaraka hususan za mipango na bajeti ambayo hutoa picha halisi ya

mahitaji ya Jamii na mgawanyo wa rasilimali kulingana na vipaumbele.

Kwa ustadi mkubwa, Timu ya SAM ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ilijifunza dhana nzima ya mi-

pango na mgawanyo wa rasilimali na hatimaye kufanya uchambuzi wa kina wa nyaraka za mpango

mkakati wa Halmashauri, Mpango kabambe wa Afya wa Halmashauri, na Mpango wa muda wa kati

wa matumizi wa Halmashauri. Matokeo ya uchambuzi huo yaliwezesha Timu kufanya majumuisho ya

hoja zifuatazo:-

2.1.1 Uandaaji wa Nyaraka na Lugha ItumikayoHoja ya TimuTimu inaipongeza sana Halmashauri kwa juhudi na uandishi makini wa Mpango Mkakati ambao umeai-

nisha bayana masuala ya msingi kama Dira, Dhamira, Vipaumbele na Malengo makuu ya mpango.

Aidha, Timu inashauri kuwa Idara ya Mipango izingatie uandishi wa nyaraka kwa kutumia lugha ya

KISWAHILI ambayo ni rafiki kwa wananchi wengi.

Majibu ya Menejimenti Miongozo inahitaji Mpango wa CCHP na ripoti za kila robo mwaka zitaandaliwa kwa lugha ya Kiin-

gereza ambapo vitabu hivyo hutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kulingana na mahitaji; mfano, nyaraka

zinapowasilishwa kwenye Baraza la Madiwani. Hata hivyo, kuanzia mwaka ujao mipango ya vituo vya

huduma za afya itaandaliwa kwa lugha ya Kiswahili. Pamoja na hayo, ushauri utazingatiwa kwa mab-

oresho hayo.

2.1.2 Mpangilio wa Taarifa Hoja ya TimuTimu inaipongeza Halmashauri kwa kuainisha shughuli katika mipango kwa uwazi, kushirikisha wadau

Sehemu ya Pili

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

6

na kuzingatia vipaumbele. Isipokuwa, Timu inashauri kuwa wakati wa uandaaji wa Mipango ni vyema

uchambuzi wa bajeti ukabainishwa. Mfano; Mpango Mkakati wa miaka mitano uliochambuliwa hauku-

wa na mchanganuo wa bajeti ya miaka mitano tofauti na mpango kabambe ulioainisha bajeti ya mwaka

kwa idara ya afya!

Majibu ya MenejimentiMpango Mkakati huwa unatoa mwelekeo wa Bajeti kwa muda wa miaka 5, ila bajeti HALISI huonekea-

na katika mipango ya utekelezaji, mfano CCHP.

2.1.3 Mchanganuo wa Shughuli Hoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa mpangilio wa shughuli kati ya mpango kabambe na ripoti

za utekelezaji haulandani hivyo kusababisha ugumu kwa watumiaji wakati wa mafunzo na uchambuzi.

Timu iliomba kupata ufafanuzi ni kwa nini mpangilio wa shughuli za mpango kabambe wa afya hauna

mtiririko unaofanana na ripoti za utekelezaji?

Majibu ya MenejimentiShughuli hutekelezwa kwa kuzingatia umuhimu, uhitaji na ugumu wa utekelezaji kwa wakati husika

na si kwa mujibu wa shughuli zilivyo katika mpangilio wa kitabu cha mpango, kwa mfano shughuli za

manunuzi, ukarabati, ujenzi huanza kutekelezwa kwanza ikilinganishwa na zile za mafunzo na vikao.

Hata hivyo, licha ya miongozo ya ukomo wa bajeti kwa kila robo mwaka na uzito wa shughuli, Idara

itatekeleza kwa mujibu wa Mpango wa CCHP kwa siku zijazo.

2.1.4 Muhtasari Mkuu - Hali ya Utekelezaji wa Shughuli Hoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa baadhi ya shughuli hazikutekelezwa (2014/2015 – 28%

& 2015/2016 – 12%) hivyo kulazimika kuhoji idadi kamili ya shughuli ambazo hazikutekelezwa kwa; 1)

Kutopatiwa fedha 2) Kupatiwa fedha kwa kuchelewa 3) Kupatiwa fedha na kushindwa kutumika.

Majibu ya MenejimentiKwa mwaka wa fedha 2014/2015 kwa mikoa ya Lindi, Manyara, na Rukwa fedha hazikufika kwa wakati

hadi robo ya nne hivyo kwa kiasi kikubwa shughuli hazikutekelezwa kwa wakati. Pia fedha za wadau

(mfano – EGPAF) zinaonekana kwenye CCHP lakini utekelezaji wake uko kwenye Akaunti ya Maende-

leo hivyo taarifa zake hazikuripotiwa kwenye vitabu vya taarifa za utekelezaji.

2.1.5 Muhtasari Mkuu – Shughuli Zinazotarajiwa KutekelezwaHoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa Muhtasari Mkuu umeainisha taarifa muhimu isipokuwa taarifa ya idadi ya shughuli zinazotarajiwa kutekelezwa kipindi cha mwaka 2015/2016 kama mwongozo wa CCHP unavyoelekeza (Uk. XIV). Aidha Timu haikuweza kupata mchanganuo halisi wa shughuli zilizovuka mwaka toka 2014/2015.

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

7

Majibu ya MenejimentiMenejimenti imehesabu shughuli za mpango, hivyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 shughuli zilizopang-

wa ni 176 (Uk. 145) ambapo shughuli zilizovuka mwaka ni 111 na hivyo kufanya jumla ya shughuli kuwa

287.

2.1.6 Muhtasari wa Bajeti Kuu Hoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa Halmashauri ilitaraji kupokea jumla ya shilingi bilioni 5.1

ikiwa ni sawa na Tzs. 29,910/= kwa kila kichwa. Timu haikuweza kujua ni kanuni ipi iliyotumika kupa-

ta kiasi hicho kwa kila kichwa. Aidha timu haikuweza kufahamu ni kwa nini Bajeti ya Mahitaji Halisi

haikulingana na makadirio ya wastani kwa kila kichwa kwa viwango vya World Health Organization

(Shirika la Afya Duniani) ambayo ni takribani $49 sawa na Tzs. 98,000/=?

Majibu ya MenejimentiMfumo wa Planrep 3 ambao hutumika kwa ajili ya kuandaa bajeti ya Afya ulifanya mahesabu kwa kuan-

galia mapato yote bila kuainisha mishahara na fedha za huduma na kupata Tzs. 29,910/=. Kiwango

cha WHO (Shirika la Afya Duniani) (Dola 49) na Azimio la Abuja (15% ya bajeti ya nchi) hakijafikiwa

kwa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara (Tanzania ikiwamo) hivyo ni vigumu kuandaa kwa kuzingatia

viwango hivyo.

2.2 Usimamizi wa Matumizi2.2.1 Mchanganuo wa MatumiziHoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa (kiambatisho Na. 10 Jedwali la 1 kwa kila robo mwaka)

Idara ya Afya ilipokea kiasi cha Tzs. 2,515,731,401/= kati ya Tzs. 5,140,008,336/= zilizoidhinishwa.

Ukijumlisha na salio la Tzs. 110,152,286/= Idara ilikuwa na Jumla ya Tzs. 2,625,883,688/= ikiwa ni kiasi

pungufu kwa takribani nusu ya bajeti iliyoidhinishwa. Hata hivyo, Timu ilijiridhisha kuwa Idara ilitumia

Tzs. 2,397,921,251/= tu na kuwa na salio la Tzs. 227,962,437/=. Timu ilipenda kujua kwa nini, pamoja

na Idara kupokea fedha nusu ya bajeti bado ilitumia pungufu ya kiasi kilichopokelewa?

Majibu ya MenejimentiFedha zilizopokelewa zilikuwa ni nusu ya bajeti kwa kuwa sehemu kubwa ilikuwa ni Mishahara ya waa-

jiriwa wapya ambapo ajira hazikutolewa kabisa kwa mwaka huo 2015/16. Aidha, kuhusu kutumia kiasi

pungufu cha fedha, hii ilitokana na kuchelewa kuingizwa kwa fedha ya robo ya nne hivyo kusababisha

kufunga mwaka na salio tajwa hapo.

2.2.2 Utekelezaji wa Bajeti kwa kila Robo MwakaHoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa Halmashauri imebainisha utekelezaji wa bajeti kwa kila

robo mwaka isipokuwa kipengele cha salio anzia na ishia hakikulandana kwa robo zote nne, ambapo

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

8

salio ishia la robo ya pili (93,502,494/=) haliendani na salio anzia la robo ya tatu (92,074,928/=). Timu

ilihitaji kupata ufafanuzi ni kwa nini kuna utofauti wa viwango vya fedha vilivyoainishwa?

Majibu ya MenejimentiUkurasa uliochapishwa haukuwa sahihi, usahihi wa kufunga na kufungua mwaka ni Tzs. 93,502,494/=

rejea kiambatisho.

2.2.3 Kutoa mafunzo ya uzazi wa mpango kwa watoa huduma wa afya 4, kwa siku sita kwenye vituo 4. Hoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa katika kitabu cha CCHP, fedha elekezi ni Tzs. 1,560,000/=

lakini kwenye ripoti ya utekelezaji imeonesha shughuli ilitekelezwa kwa Tzs. 2,040,000/= ambapo to-

fauti ni Tzs. 480,000/=. Timu ya SAM iliomba ufafanuzi wa ongezeko la kiasi hicho cha fedha.

Majibu ya MenejimentiKatika kitabu cha CCHP Ukurasa wa 1 na ripoti ya robo ya 4 ya mwaka Ukurasa wa 12 shughuli hii ili-

pangiwa kiasi tajwa, lakini hakuna fedha iliyotolewa kwa kazi hiyo na maoni ya utekelezaji yameeleza

waziwazi kuwa “haikutekelezwa”

2.2.4 Mafunzo ya unasihi wa lishe na huduma kwa siku 6 kwa washiriki 15 kutoka hospitali ya wilaya. Hoja ya TimuTimu ya SAM katika uchambuzi ilibaini shughuli hii ilipangiwa kiasi cha Tzs. 7,420,000/= ingawa katika

ripoti ya utekelezaji inaonesha shughuli hii haikutolewa kiasi chochote cha pesa kwenye robo ya 3 ya

mwaka, wakati huohuo shughuli inaonesha kufanyika kwa 100%. Timu ya SAM iliomba ufafanuzi wa

pesa iliyotumika takribani Tzs. 11,847,034/= kutekeleza shughuli kwa 100% ilitoka chanzo gani?

Majibu ya MenejimentiShughuli na kiasi kilichotajwa cha 11,847,034 ni kwa ajili ya kulipa mishahra ya watumishi wa shirika la

EGPAF (Rejea Kitabu cha robo ya 2 ya mwaka ukurasa wa 7) na si ya mafunzo ya unasihi kama timu

ya SAM ilivyosema.

2.2.5 Kuendesha kikao cha bodi ya afya cha watu 12 kwa kila robo mwakaHoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu umebaini kuwa namba ya shughuli katika kila robo mwaka imetumika

kwa shughuli mbili tofauti na mpango ulivyoainisha. Aidha, Timu imeshindwa kujua ni kwa nini Kikao

cha bodi hakikufanyika katika kila robo mwaka kama mwongozo unavyoelekeza. Timu ilipenda kupata

ufafanuzi juu ya mkanganyiko huo, pia Idara iliweza vipi kupitisha maamuzi ya kila robo mwaka bila

kufanyika kikao cha bodi ya afya?

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

9

Majibu ya MenejimentiTimu ya SAM ilipata mkanganyiko wa namba za shughuli tajwa hapo juu, mfano Ukurasa wa 13 robo

ya 2 CO1SO1 ni shughuli ya Simamizi Elekezi (mwaka 2014/15), ambapo shughuli namba CO1SO1

(2015/16) Ukurasa wa 14 ni Kikao cha Bodi ya Afya ambapo hakuna fedha iliyopokelewa wala kutu-

mika. Aidha kwa kipindi cha robo ya 1 hadi ya 3, Bodi ya Afya haikuwa hai (ilimaliza muda wake) hadi

ilipochaguliwa na kuzinduliwa upya katika robo ya 4 ya mwaka. Kwa kipindi hicho Timu ya CHMT iliku-

wa inafanya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za Afya Wilayani.

2.2.6 Kununua mashine atamizi (incubator) 1 kwa Hospitali ya Wilaya Hoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa Idara ilipokea Tzs. 1,500,000/= lakini haikutekeleza shu-

ghuli hii. Timu ilipenda kufahamu ni kwa nini Idara haikununua mashine atamizi (incubator) ikiwa fedha

zilipokelewa?

Majibu ya MenejimentiShughuli hii ilipangwa kutekelezwa katika robo ya 4 ya mwaka ambapo fedha zake ziliingia kwa

kuchelewa sana hivyo kusababisha kuvuka hadi mwaka mpya wa fedha 2016/17.

2.2.7 Ununuzi wa Hot Air Oven 1 katika Hospitali ya WilayaHoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu ulibaini kuwa Idara ilitenga kiasi cha Tzs. 3,159,475/= na kupokea fedha

zote robo ya 4 ya mwaka, hata hivyo timu inaipongeza Idara kwa kutekeleza shughuli kwa 100%. Timu

ingependa kufahamu ni kwa namna gani idara iliweza kununua kifaa tiba bila kutumia fedha hizo?

Majibu ya MenejimentiTatizo ni la kiuandishi kwani ilionesha imetekelezwa kwa 100% lakini kwenye salio pesa bado iliku-

wepo (Uk. 8 taarifa ya robo ya 4) ambayo ilivuka mwaka mpya wa fedha 2016/17 kwa hatua zaidi za

manunuzi ya kifaa hicho.

2.2.8 Ununuzi wa seti 80 za vifaa tiba kwa Hospitali ya WilayaHoja ya TimuUchambuzi uliofanywa na timu umebaini kuwa shughuli hii haikuainishwa kwenye mpango japokuwa

imeonekana katika ripoti za utekelezaji, ambapo robo ya 1 imepokea fedha na kutumia zote bila salio.

Robo ya pili imeonesha 50% ya mafanikio tofauti na Robo ya 4 iliyoonesha 100%. Timu ilipenda kujua

kwa nini shughuli hii haikuainishwa kwenye mpango na kwa nini robo ya 2 na 4 zinaonesha mafanikio

tofauti?

Majibu ya MenejimentiShughuli zilizovuka mwaka kwa kawaida huwa hazionekani katika Mpango wa CCHP, Matumizi ya

fedha zilizovuka mwaka hutofautiana kulingana na ununuzi wa vifaa kufanyika kwa awamu.

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

10

2.2.9 Ununuzi wa shuka 150 kwa ajili ya Hospitali ya WilayaHoja ya TimuUchambuzi ulioffanywa na timu umebaini kuwa Robo ya 2 imeonesha ununuzi wa seti 80 za vifaa

tiba-meno kinyume na mpango. Hata hivyo, Robo ya 4 imeonesha kupokea Tzs. 2,340,000/= na ku-

tumia sifuri na kuwa na salio la Tzs. 3,395,166/=. Timu iliomba ufafanuzi ni kwa nini shughuli ya ununu-

zi wa vifaa tiba-meno haikuainishwa kwenye mpango, na Je tofauti ya salio (1,055,164/=) kwa robo ya

nne inatokana na nini?

Majibu ya MenejimentiHaya ni manunuzi ya kupitia MSD – Shughuli za manunuzi kupitia MSD (Receipts in Kind) hazioneka-

ni kwenye mpango wa CCHP kwa kuwa chanzo chake ni bajeti nje ya Halmashauri (Out of Council

Budget) - Tofauti ya salio inatokana na maotea madogo ya Halmashauri ikilinganishwa na fedha zilizo-

pokelewa kupitia nyaraka za MSD.

2.3 Usimamizi wa Utendaji 2.3.1 Usimamizi ElekeziHoja ya TimuKatika vituo vilivyotembelewa na timu, uhakiki umeonesha kuwa changamoto nyingi ni za kiusimamizi

ama kiutendaji. Hivyo, Timu ilipenda kujua kwa mwaka 2015/2016 CHMT ilifanya usimamizi elekezi

mara ngapi kwa kila robo mwaka?

Majibu ya MenejimentiNi kweli tulifanya usimamizi elekezi lakini tutahitaji kujiridhisha kwenye vitabu japo ukweli ni kwamba

fedha mara nyingi huchelewa na ni vigumu kufanya kwa asilimia mia moja. Tutatoa uthibitisho kupitia

nyaraka za mratibu wa usimamizi elekezi.

2.3.2 Stahiki za watumishiHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo vyote 34 vilivyotembelewa hakuna kituo hata kimoja ambapo wa-

tumishi wamelipwa stahiki zao zote ikiwemo muda wa ziada, fedha za kusafirisha taarifa za kila mwezi,

likizo na fedha za uhamisho. Aidha, katika kipindi cha 2015/2016 malipo kiasi fulani yalifanyika na

2016/2017 hakuna malipo yoyote yaliyofanyika. Timu ilipenda kujua ni kwa nini watumishi wa vituo

vyote hawajakamilishiwa malipo yao na kuna mkakati gani wa kuhakikisha changamoto hiyo haijirudii?

Majibu ya MenejimentiStahiki za watumishi huwa zinapangwa kwenye Mpango na zinalipwa kwa kila robo mwaka kwa wa-

tumishi tofauti tofauti, ingawa madeni ni mengi sana. Aidha madeni ya watumishi wengi yalihakikiwa

na Serikali Kuu kupitia Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani (Takwimu zipo Ofisi ya Ukaguzi Wilaya). Pamoja na

hilo, Idara inaendelea kulipa madeni ya watumishi kadiri ya upatikanaji wa Other Charges, kwa mfano

waliostaafu (kufunga mizigo), nauli za likizo, gharama za mazishi, na uhamisho). Changamoto ni fedha

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

11

za On Call allowance ambazo hazijaingia kwa muda mrefu. Mkakati wa idara ni kulipa madeni kwa

kadiri fedha zinavyoingia idarani na kupitia mapato ya ndani.

2.3.3 Mafunzo KaziniHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo vilivyotembelewa, ni Hospitali ya Wilaya tu iliyopatiwa mafunzo ya

uandaaji wa mpango kazi. Vituo 31 havikupatiwa mafunzo hayo isipokuwa kushiriki katika kikao kazi

cha awali kuhusu uandaaji wa mpango kazi wa kituo. Timu ilipenda kujua ni kwa nini watumishi wa

vituo 31 hawakupatiwa mafunzo hayo?

Majibu ya MenejimentiWatumishi wa vituo wamekuwa wakifundishwa kila mwaka juu ya uandaaji wa mipango, na kila kituo

kina kitabu cha mwongozo wa Kiswahili kama dira ya kuandaa mipango ya vituo. Vitabu vya vituo vipo

katika Ofisi ya Wilaya na kuanzia mwezi Julai kila kituo kitakuwa kinatekeleza Mpango wake wa Kituo

(Facility Plan). Mkakati wa Idara ni kuwa kila kanda imepatiwa walezi wake hivyo katika uandaaji wa

mipango watatumika kama wawezeshaji wa uandaaji wa mipango ya vituo.

2.3.4 Uchangiaji wa Mifuko ya Pamoja ya Fedha za AfyaHoja ya TimuTimu imegundua kuwa vituo vyote vilivyotembelewa vimeonesha kuwa na vyanzo vya ndani vya map-

ato japo ni duni na imethibitika kutokuwepo kwa marejesho ya CHF kwa wakati toka Halmashauri,

kutokuwepo kwa kadi na mawasiliano hafifu kati ya kituo na wakusanyaji kutoka kwenye Jamii. Timu

ilipenda kujua ni mfumo upi unaotumiwa na Halmashauri kupokea na kurejesha fedha kwa kituo husi-

ka, na ni kwa nini fedha hazirejeshwi kwenye akaunti ya kituo husika kwa wakati? Pili, je Halmashauri

iliwajengea uwezo watumishi na Kamati ya usimamizi wa kituo juu ya uandaaji wa dokezo na utaratibu

wa malipo?

Majibu ya MenejimentiMfumo utumikao ni Makusanyo kupitia Watendaji wa Vijiji (VEOs) ambao huingizwa kwenye akaunti

mama ya CHF, kisha marejesho hufanywa kwa kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa kufuata

sheria za manunuzi na kugawiwa vituoni (Mrejesho hutegemea kiasi ambacho kituo kimekusanya).

Halmashauri imewajengea na inaendelea kuwajengea uwezo wa kuandaa madokezo na malipo wa-

tumishi na kamati za vituo vya huduma wilayani.

2.3.5 Ikama ya WatumishiHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo vilivyotembelewa, ni zahanati za Somanga (5), Nangurukuru (6),

Chumo (4), Lihimalyao (3), na Mtandi (3) tu ndivyo vimeonesha kuwa na watumishi zaidi ya wawili.

Kwa vituo vya Masoko (22), Njinjo (8), Pande (12), Tingi (20) havikuweza kufikia kiwango cha chini

kinachohitajika kwa mujibu wa mwongozo. Timu ilipenda kujua ni kwa nini hakuna mgawanyo sawia

wa watumishi katika vituo, na kuna mkakati gani maalumu wa kuomba watumishi kutoka serikali kuu?

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

12

Majibu ya MenejimentiChangamoto ya watumishi ni kubwa kwa nchi nzima, ikiwamo na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Taarifa iliyotolewa na Timu ya SAM ni sahihi kabisa. Kuna tofauti kubwa ya uwiano wa watumishi wa

afya katika vituo ikilinganishwa na IKAMA ya Wizara ya Afya ambapo kila Zahanati inatikiwa iwe na

watumishi kati ya 15-20, Kituo 39-52 na Hospitali 312.

Mkakati wa Idara – Kuendelea kugawa watumishi waliopo kwenda kwenye vituo ambavyo vina uhaba

mkubwa wa watumishi, Kusubiri ajira mpya ili kuziba mapengo ya watumishi wanaokosekana vituoni.

Aidha, changamoto kwa sasa ni matokeo ya uhakiki wa vyeti ambao umeathiri sana idara ya afya

kwani hadi sasa umegusa watumishi zaidi ya 28 katika vituo vya huduma na ikizingatiwa uhakiki bado

unaendelea kufanyika. Mgawanyo sawia hauwezi kufikiwa kwa sasa, kwani sababu mbalimbali huathi-

ri vituo vya huduma. Juhudi za idara zinafanyika kusawazisha ikama za watumishi vituoni, ingawa

changamoto ni kubwa sana.

2.3.6 Dawa na Vifaa TibaHoja ya Timu Timu imegundua kuwa kati ya vituo vilivyotembelewa hakuna kituo hata kimoja kilichokuwa na dawa

na vifaa tiba vinavyojitosheleza ikiwemo vitanda, magodoro, vitendanishi, mikasi, mashine za BP na

vitakasa vifaa (sterlilizer). Aidha watumishi hutumia majiko binafsi ya mkaa na mafuta ya taa kutakasa

vifaa ikiwa ni kwa kugharimia wo binafsi. Pia, vituo vingi vimeonekana kuwa na vyumba vidogo vya

maabara (mapokezi na kutoa damu salama vitenganishwe), na chumba cha dawa hususan Hospitali

ya Kinyoga imeonekana kuwa na chumba kidogo kupita kiasi. Timu ilipenda kujua ni kwa nini vituo vingi

havina dawa za kutosha na vifaa tiba? Je Idara imefanya jitihada zipi za kukabiliana na changamoto

hizo?

Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya ukaguzi wa dawa katika zahanati ya Mitole.

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

13

Majibu ya MenejimentiHalmashauri kwa sasa ina dawa na vifaa vya kuridhisha, hii inatokana na mgao wa dawa na vifaa

tiba kupitia mfuko wa pamoja wa wafadhili, pesa kutoka serikali kuu kuimarika katika mwaka wa fed-

ha 2016/2017. Pale ambapo dawa moja haipatikani mbadala wake huwa unapatikana kiasi cha ku-

hakikisha huduma za afya zinapatikana. Idara imekuwa inatoa maelekezo kwa vituo kutopokea dawa

zinazokaribia kuharibika isipokuwa pale ambapo kituo kina uhakika wa kutumia dawa zote kabla ya

kuharibika.

Watumishi wa idara wameelekezwa kutumia sehemu ya mapato yao ya uchangiaji kusaidia gharama

za usafiri na pia idara kwa kupitia chanzo cha fedha za wafadhili hutoa fedha kama nauli pale watumi-

shi wanapowasilisha taarifa wilayani.

2.3.7 Miundombinu ya Barabara Hoja ya TimuUhakiki uliofanywa na timu vituoni umebaini kuwa barabara nyingi ukiondoa barabara kuu ni mbovu

sana isipokuwa barabara ya Lushungi. Timu ilipenda kujua mkakati uliopo kukabiliana na changamoto

hiyo.

Majibu ya MenejimentiPamoja na Timu kuona barabara ya Lushungi ina nafuu, tukumbushane tu kuwa marekebisho kwa

kiwango cha changarawe yamegharimu zaidi ya Bilioni 7 na ni fedha za mfadhili. Tuna changamoto

kubwa ya Barabara na tumekuwa tukitenga fedha kupitia Baraza la Madiwani lakini mapato hayatoshi.

2.3.8 Ubovu wa Vifaa TibaHoja ya TimuTimu imegundua kuwa katika Hospitali ya Kinyonga kuna changamoto za kipekee hasa ubovu wa

mashine ya X-ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, ukosefu wa jenereta kwa ajili ya maabara, na hali ya

uchakavu katika wodi na maeneo ya kufulia nguo. Timu ilipenda kujua kwa nini changamoto hizi haz-

itatuliwi na Idara?

Majibu ya MenejimentiIdara inatambua matatizo haya na imeweza kupanga fedha kwa ajili ya matengenezo ya mashine ya

X ray, manunuzi ya Jokofu la kuhifadhia maiti yamepangiwa fedha kwenye mpango kabambe wa Afya

2017/2018, idara pia inafanya matengenezo ya jenereta ili iweze kutumika kwenye maeneo yote mu-

himu nyakati ambapo umeme umkatika. Kwa kutambua hali ya uchakavu wa wodi na sehemu ya ku-

fulia nguo Idara imeweka shughuli ya ukarabati wa sehemu hizi kwenye mpango wake wa utekelezaji

2017/2018.

2.3.9 Uhaba wa Wodi za WagonjwaHoja ya Timu Timu ilishuhudia uhaba wa wodi za wagonjwa katika hospitali na vituo vya afya (wagonjwa huchang-

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

14

anywa – wale wa upasuaji na wenye magonjwa ya kawaida). Timu ilihitaji kujua ni kwa nini Hospitalli

haiongezewi wodi kulingana na mahitaji?

Majibu ya MenejimentiKwa mujibu wa kanuni hospitali ya wilaya inatakiwa iwe na angalau wodi 14 (wodi 2 za upasuaji, na 1

ya upasuaji wa watoto, wodi 2 za kutenga wagonjwa, wodi 1 ya akina mama baada ya kujifungua, wodi

1 ya dharura watoto wachanga, wodi 2 za dharura, wodi 1 ya uzazi, wodi 2 za magonjwa ya kawaida,

wodi 1 ya watoto magonjwa ya kawaida, Grade II – wodi 1 ya Bima, na wodi 2 za magonjwa ya akili.

Hospitali ya Wilaya Kinyonga ina wodi 7 ambazo ni wodi ya wazazi, watoto waliozaliwa (post natal),

watoto, wanaume, wanawake, bima, na kutenga).

2.3.10 Nyumba za WatumishiHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, ni vituo 28 tu ambavyo vimeonesha kuwa na

nyumba za watumishi. Timu ilihitaji kujua ni kwa nini Idara haikarabati nyumba za watumishi na kuweka

mazingira bora kwa watumishi wa vituo hivyo?

Majibu ya MenejimentiNyumba zinakarabatiwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha za maendeleo, ambapo ki-

paumbele ni maeneo ambayo uharibifu ni mkubwa. Idara pia hushauri kamati za uendeshaji wa vituo

kufanya ukarabati mdogo mdogo kwa kutumia pesa za uchangiaji ili kukabiliana na tatizo hili.

2.3.11 Vichomea taka na shimo la kondo la uzaziHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, vituo 10 havina kabisa vichomea taka, na

vituo 5 vimeonekana kuwa na vichomea taka vibovu visivyotumika kwa sasa. Aidha, vituo 4 pekee

kati ya vituo vyote vilivyotembelewa vilionekana kuwa na shimo la kutupia kondo la uzazi linalokidhi

viwango. Hivyo, Timu iliomba ufafanuzi kwa nini vituo hivyo havina vichomea taka na shimo la kutupa

kondo la uzazi.

Majibu ya MenejimentiMenejimenti inaelewa umuhimu wa vichomea taka na shimo la kutupa kondo la uzazi na imeshauri

vituo hivi kwa kushirikiana na kamati zao na serikali kuhakikisha miundombinu hii inakuwepo na kutu-

mika ipasavyo.

2.3.12 Mfumo wa Maji Safi Hoja ya Timu Timu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa hakuna kituo hata kimoja chenye mfumo ka-

mili wa maji safi na salama. Vituo vichache vina mfumo mzuri wa kuvuna maji ya mvua japokuwa vingi

havina kabisa aina yoyote ya mfumo wa maji safi na salama. Aidha, katika hali ya kushangaza Jamii

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

15

imeshutumiwa kuharibu mifumo ya maji katika vituo vya Nakingombe, Zinga na Masoko. Ambapo koki

zimeibwa na matanki yametobolewa. Timu ilihitaji kujua ni hatua zipi zimechukuliwa na Halmashauri

kukabiliana na vitendo hivyo viovu vya Jamii dhidi ya watumishi na vituo?

Majibu ya Menejimenti Ni kweli kabisa sehemu kubwa ya vituo vyetu vya kutolea huduma ya Afya vina changamoto ya ku-

kosa mifumo thabiti ya maji safi na salama, pamoja na ukweli huu juhudi za makusudi zinafanywa na

Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuendelea kuboresha mifumo ya maji kwa ku-

wekeza kwenye uvunaji maji ya mvua. Halmashauri hukabidhi miundombinu kwa viongozi wa serikali

ya kijiji na kamati husika na pale uharibifu unapotokea hatua stahiki inabidi ichukuliwe na uongozi wa

kituo, serikali na kamati husika.

2.3.13 Hali ya Vyoo VituoniHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, ni vituo vya Nangurukuru, Masoko, Kilan-

jelanje, na Mbwemkuru pekee vilionekana kuwa na vyoo safi tofauti na vituo vingine vilivyo-tembelewa.

Timu ilipenda kujua ni kwa nini hali ya vyoo si nzuri katika vituo vingi, na kuna mkakati gani wa kumal-

iza suala hilo?

Majibu ya MenejimentiMiundombinu ya vyoo inaendelea kujengwa, kukarabatiwa na kupitia mradi wa WASH elimu inaende-

lea kutolewa juu ya ujenzi na matumizi sahihi ya vyoo.

Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya ukaguzi wa kichomea taka katika zahanati ya Zinga Kibaoni.

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

16

2.3.14 Nishati ya UmemeHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, vituo 7 havikuwa na nishati ya aina yoyote ya

umeme. Baadhi ya vituo kama Nakingombe, Pande, MT. Kimwaga na Kisiwani vimekuwa na changa-

moto ya wizi wa vifaa vya nishati ya umeme. Pia, changamoto ya Umeme Hospitali ya Kinyonga im-

eonekana hasa katika eneo la maabara ambayo inapaswa kuwa na umeme muda wote. Timu ilihitaji

kujua ni kwa nini idara haijahakikisha uwepo wa nishati ya umeme katika vituo vyote vilivyotajwa?

Majibu ya MenejimentiJiografia ya Kilwa ina mazingira tofauti tofauti na vituo vya huduma viko katika maeneo mbalimbali,

vipo vituo vinavyopata umeme wa Gridi ya Taifa na vipo vinavyotumia umeme wa jua.

Mkakati wa Idara – Kupanga bajeti ya kulipia gharama za umeme (LUKU), Kuhusu Hospitali ya Wilaya,

Idara imetenga fedha kwa ajili ya kutenganisha jengo la hospitali na nyumba za watumishi wanaoishi

ndani ya eneo la Hospitali ya Wilaya, Jenereta ya dharura ipo kwa ajili ya kukabili ukatikaji wa umeme

katika Hospitali ya Wilaya.

2.4 Usimamizi wa Uwajibikaji2.4.1 Hati ya Ukaguzi na Vyombo vya Ukaguzi Hoja ya TimuTimu ingependa kujua Halmashauri imepata hati gani ya ukaguzi kwa mwaka 2015/2016? Na, Je

kamati ya ukaguzi na idara ya ukaguzi wa ndani zimeimarishwa kwa kiwango gani?

Majibu ya MenejimentiKwa sasa Halmashauri imepata hati safi. Kamati imepitia mlolongo wa maboresho mpaka sasa, tu-

mepata mafunzo kuhusu kamati ya ukaguzi isipokuwa hatujapata waraka kuhusu muundo na utend-

Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya ukaguzi wa vyoo katika zahanati ya Zinga Kibaoni.

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

17

aji wake. Aidha, pamoja na maboresho Kitengo kimepata gari na kina bajeti ndogo sana ambayo ni

changamoto kubwa sana.

2.4.2 Makadirio ya Bajeti Kuu kwa Baraza la Madiwani Hoja ya Timu Uchambuzi uliofanywa na Timu ulibaini kuwepo mchanganyiko wa kiasi halisi cha bajeti kuu ya Hal-

mashauri kwa mwaka 2015/2016 katika nyaraka za Baraza la Madiwani 2015/2016 ikiwa ni kati ya

milioni 23 au bilioni 23. Timu ilipenda kujua Baraza lilipitisha kiasi gani cha makadirio ya bajeti?

Majibu ya MenejimentiNi kweli nyaraka zinaonesha mkanganyiko, lakini itoshe kujiridhisha kuwa kulikuwa na tatizo la uchap-

aji. Pia bajeti hupitia ngazi nyingi ndiyo maana katika kitabu cha bajeti kuu ya Halmashauri kiasi halisi

ni zaidi ya Bilioni 25.

2.4.3 Kamati za Usimamizi wa VituoHoja ya TimuTimu imegundua kuwa vituo vyote 34 vilivyotembelewa vimeonesha kuwa na kamati za usimamizi wa

kituo isipokuwa baadhi zinachangamoto ya kiutendaji. Kamati za vituo 10 tu ndizo zimebainika kupati-

wa mafunzo kuhusu wajibu na majukumu yao kutoka AghaKhan Foundation.

Timu ilipenda kujua ni kwa nini Idara haikutoa mafunzo kwa kamati zilizobaki na kuna mkakati gani wa

kuimarisha utendaji wa kamati za usimamizi wa vituo?

Majibu ya MenejimentiKamati 10 za Usimamizi wa Vituo vya huduma zilipatiwa mafunzo na AghaKhan Foundation, mafunzo

yaliendelea kutolewa kupitia Shirika la JICA kwa kushirikiana na RHMT waliofundisha Kamati 3 za Vi-

tuo vya Afya (Tingi, Njinjo na Ande). Kupitia Shirika la GIZ lililotoa mafunzo kwa HFGC za vituo 3 vya

huduma vya Mchakama, Kiwawa na Mandawa. Idara haikutoa mafunzo kutokana na ukosefu wa fedha

za kuendeshea mafunzo hayo kwa kamati zilizobakia. Mkakati wa Halmashauri ni kuendelea kufundis-

ha HFGC zilizobakia kwa awamu kupitia vyanzo vya fedha vya CHF katika vituo 10.

2.4.4 Mifumo ya Kutoa Maoni WananchiHoja ya TimuTimu imegundua kuwa kati ya vituo 34 vilivyotembelewa, vituo vya Kisiwani, Migelegele, Luhatwe,

Kikole, Zinga (kamati imekaa kikao kutengeneza), Naking’ombe, Lushungi, na MT. Kimwaga havi-

kuonekana kuwa na masanduku ya maoni na mbao za matangazo. Vituo vingine vimeonesha kuwa na

angalau mfumo mmoja unaoonekana wa kutoa maoni, malalamiko na kuhabarishana japokuwa kuna

changamoto kubwa ya uelewa wa matumizi na maeneo mifumo hiyo ilipowekwa. Timu ilipenda kujua

ni kwa nini vituo vingi havina mifumo hii ya mawasiliano?

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

18

Majibu ya MenejimentiMifumo ya mawasiliano ipo na inatumika ingawa watumiaji hawajui kama wanatumia mifumo hiyo

mfano; kwa njia ya kuonana na viongozi wa Kamati ya Zahanati, Serikali za Vijiji kutoa malalamiko na

hoja mbalimbali za huduma. Pia kwa njia ya simu kwa Viongozi wa ngazi za juu mfano Kwa Mkuu wa

Wilaya, Mkurugenzi, Mganga Mkuu wa Wilaya na kwa wajumbe wa CHMT.

Kuhusu Masanduku ya maoni, Kamati zilizopata mafunzo zimeelekezwa namna ya kuandaa na ku-

tumia masanduku hayo, aidha wanajamii wa Kiwawa, Mandawa na Mchakama wamefundishwa nam-

na ya kutumia masanduku ya maoni. Timu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) Wilaya ilipitia vituo vyote

na kuelekeza uwekaji na matumizi ya masanduku ya maoni.

Sanduku la kutolea maoni katika Zahanati ya Njinjo.

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

19

Sehemu ya Tatu 3.0 Mapendekezo na Maazimio ya Kuboresha Huduma

• Timu inashauri kuwa Idara ya Mipango izingatie uandishi wa mipango kwa kutumia lugha ya

KISWAHILI ambayo ni rafiki kwa wananchi wengi.

• Timu inashauri kuwa wakati wa uandaaji wa mipango ni vyema uchambuzi wa bajeti ubainishwe

hususani mpango mkakati.

• Timu inapendekeza mpangilio wa shughuli kati ya mpango kabambe na ripoti za utekelezaji ubore

shwe ili kuonesha mahusiano kati ya shughuli moja na nyingine katika nyaraka zote mbili ili kura-

hisisha ufuatiliaji na ushiriki wa jamii katika utekelezaji.

• Timu inaipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi, pia inashauri kuanza kuimarisha kitengo cha

ukaguzi wa ndani na kamati ya ukaguzi.

• Timu inashauri Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato na kutekeleza shughuli zote kama

zinavyoainishwa na kupatiwa fedha.

• Timu inashauri kuimarishwa kwa usimamizi elekezi na mahusiano kati ya Jamii na vituo vya ku

tolea huduma za afya.

• Kuhusu idadi ya shughuli, Timu inashauri kuwa idadi ya shughuli iainishwe katika mpango na

ziripotiwe kwa mujibu wa mpango kama miongozo inavyoelekeza

• Timu inapendekeza Halmashauri ihakikishe vikao vya bodi vinafanyika kwa wakati kama miongozo

inavyoelekeza.

• Timu inashauri kuwa mkakati wa sasa wa malipo kwa watumishi utekelezwa kwa haraka ili

kuongeza motisha ya kazi.

• Timu inashauri kuangaliwa upya kwa mfumo wa utoaji wa mafunzo ya kuandaa mipango na kujen-

gea uwezo kamati za usimamizi wa vituo.

• Timu inashauri mawasiliano yahimizwe kati ya kamati ya kituo na mtendaji ili kuhakikisha taarifa

muhimu za CHF zinakuwepo pande zote kwa wakati.

• Timu inashauri utoaji wa elimu kwa Jamii uimarishwe hususani kuhusu mahusiano na vituo ili ku-

punguza visa vya uharibifu na hujuma.

• Timu inapendekeza mgawanyo sawia wa watumishi uzingatiwe wakati wote ili kupunguza mzigo

kwa baadhi ya vituo.

• Timu inapendekeza mfumo wa uagizaji na manunuzi ya dawa na vifaa tiba upitiwe upya na

kuongeza ubunifu.

• Timu inapendekeza Halmashauri itumie ripoti ya SAM kuboresha hali ya miundombinu ifuatayo:-

a) Miundombinu ya Barabara

b) Majengo ya Huduma za Afya zikiwemo nyumba za watumishi na wodi

c) Vichomea Taka na Shimo la kondo la uzazi

d) Mfumo wa maji safi na salama na mfumo wa nishati ya Umeme

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

20

3.1 Kiambatisho Na. 1: Majina ya wajumbe wa Timu ya SAMNa JINA JINSI UWAKILISHI01 Ruki A. Jamadari KE Diwani02 Mahadi H. Mandondo ME Mwananchi03 Mwanaidi Madadi KE Mwananchi04 Michael Maqway ME HFGC05 Salima Munda KE Mwananchi06 Said A. Mbawala ME CHMT07 Said A. Kiunjira ME Kiongozi wa Dini08 Shaweji Suwedi ME Mwananchi09 Mkenda S. Dayann ME Diwani10 Sarart M. Mwakalago ME CMT11 Ibrahim S. Sota ME CSO12 Tatu M. Kamtande KE WEO13 Adinani S. Kopakopa ME Mwananchi14 Anastansia B. Lai KE Mwananchi15 Abdallah M. Matajiri ME DHSB

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)sikika.or.tz/images/content/mp3/Kilwa report 2017pg.pdfwajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa

“Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali”

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.com Twitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika Tanzania