ripoti ya ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii...

28
Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ) Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

Upload: others

Post on 10-Jul-2020

36 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)

Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)
Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)

Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro2012

Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Hakimiliki © 2013Shirika la Sikika, Haki zote zimehifadhiwa Imechapishwa 2013Imeandaliwa na Timu ya UUJ Simanjiro na Shirika la SikikaImechapishwa na: Digitall Ltd.

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

YaliyomoOrodha ya vifupisho iiShukrani iiiMuhtasari 1

1.0 SEHEMU YA KWANZA 2

1.1 Mchakato wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ) 21.2 Uundwaji wa Timu ya UUJ 21.3 Nyaraka za Halmashauri zilizochambuliwa 21.4 Maeneo yaliyotembelewa naTimu ya UUJ 31.5 Mpangilio wa ripoti 3

2.0 SEHEMU YA PILI 4

2.1 Mgawanyo wa Rasilimali (Mpango mkakati, CCHP na MTEF) 42.2 Usimamizi wa Matumizi 52.3 Usimamizi wa Utendaji 92.4 Usimamizi wa uadilifu 112.5 Usimamizi wa Uwajibikaji 13

3.0 SEHEMU YA TATU 16

3.1 Sauti za Wadau 163.2 Changamoto 183.3 Tuliyojifunza 184.0 SEHEMU YA NNE 194.1 Mapendekezo 194.2 Hitimisho 19

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

II

Orodha ya vifupisho3Us Uhalalisho, Ufafanuzi na Uthibitisho.

CAG Controller and Auditor General – Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

CCHP Council Comprehensive Health Plan – Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri.

CHF Community Health Fund - Mfuko wa Afya ya Jamii.

CHMT Council Health Management Team - Timu ya Menejimenti ya Halmashauri kwa Idara ya Afya.

CMT Council Management Team – Timu ya Menejimenti ya Halmashauri

DMO District Medical Officer – Mganga Mkuu wa Wilaya.

MTEF Mid – Term Expenditure Framework

SAM Social Accountability Monitoring – Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii.

UUJ Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

III

ShukraniAwali napenda kumshukuru Mungu kwa kutupatia afya njema katika kipindi chote cha zoezi zima la SAM. Napenda kutumia nafasi hii kulishukuru Shirika la Sikika kwa kuratibu zoezi la SAM tangu kuundwa kwa Timu, hadi maandalizi ya ripoti hii. Shirika la Sikika limekuwa msaada mkubwa kwani limewezesha jamii yetu kupata elimu na kutujengea uwezo wa kushiriki na kufanya ufuatiliaji kuanzia hatua ya mipango hadi matokeo.

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na DAS Ndugu Elias R. Ntirihungwa, Baraza la Madiwani, kupitia Mwenyekiti wake Ndugu Peter P. Tendee, pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Muhammad S. Nkyakwa. Ushirikiano na msaada wao mkubwa kwa Timu ya SAM tangu Shirika la Sikika lilipofika wilayani hadi kufanikishwa kwa zoezi. Aidha Ofisi ya Mkurugenzi na DMO imetoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha upatikanaji wa nyaraka mbalimbali zilizotumika kwenye mafunzo na ufuatiliaji katika kipindi chote cha zoezi. Chachu na ari hii tungependa iwe endelevu kwa timu yetu wilayani hapa.

Pia, vyombo kama CMT, CHMT na watoa huduma ya afya, kwa ngazi ya vituo vya afya kwa pamoja, wameonesha ushirikiano mkubwa kwa timu. Ushirikiano wao umewezesha kupatikana kwa 3Us ambazo kimsingi zimeweza kuongeza uelewa wa masuala mbalimbali ya afya pamoja na kupatikana kwa vkwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.

Kipekee Timu inawashukuru wawezeshaji wa zoezi la SAM; Richard Msitu, Fredrick Ngao, Norah Mchaki na Hope Lyimo kutoka Sikika kwa juhudi, maarifa na uvumilivu walioonesha wakati wote wa mafunzo, uhakiki na vikao vya mrejesho.

Shukrani za jumla tunazitoa kwa makundi yote ya kijamii na wananchi wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamewezesha kufanikiwa kwa zoezi hili. Ushiriki wao ni wa muhimu sana kwani ndivyo mfumo wa SAM unavyohitaji. Hivyo basi, tunawahamasisha waendelee kushirikiana na Timu ya SAM kwenye masuala tofauti yahusuyo afya na yale ya idara nyingine za halmashauri.

Mwisho, sisi wajumbe wa Timu ya SAM hatutakuwa tumetenda haki ikiwa hatutajipongeza kwa uvumilivu, utulivu, uelewa, mshikamano na kujituma kwetu. Tumekuwa washiriki wa mfano katika kipindi chote cha zoezi. Katika hali hiyo ni wazi kuwa tunapaswa kuendelea kuitumia elimu tuliyo nayo na pia kutekeleza majukumu yetu kwa jamii yetu.

Asanteni sana.

………………………………Mh. Diana KuluoMwenyekiti – Timu ya SAM

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

1

MuhtasariUfuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ) ni mfumo shirikishi wa uwajibikaji unaowataka watendaji wa serikali kutoa taarifa za kina kwa watumia huduma wakati zinapohitajika. Mfumo huu unatoa fursa kwa watendaji na wananchi kuwajibika na kuwajibishana pale inapodhihirika kuwa kuna ukiukwaji wa misingi ya utendaji serikalini bila shaka yoyote. Utekelezaji wa mfumo huu unahusisha hatua tano za msingi ambazo ni: Mipango na mgawanyo wa rasilimali, Usimamizi wa matumizi, Usimamizi wa utendaji, Usimamizi wa uadilifu na Uangalizi. Hatua hizi ni muhimu sana kwani zinategemeana na ni shirikishi, utekelezaji wa hatua hizi kwa kila hatua moja huhitai mambo makuu matatu ambayo ni Ufafanuzi, Uthibitisho na Uhalali kwa kila jambo linalofanyika.

Kama ilivyo kwa mashirika mengine ya kijamii, Shirika la Sikika linafanyakazi ya kuboresha huduma za afya kwa kufanya ushawishi na utetezi wa utawala bora kwa kutumia mfumo wa SAM. Utekelezaji wa dhima hii kwa Wilaya ya Simanjiro uliambatana na uundwaji wa Timu hii ya SAM ambayo ina uwakilishi wa watoa huduma na wananchi toka makundi mbalimbali ya jamii. Baada ya Timu kuundwa kwenye kikao cha wadau cha tarehe 11/10/2013, tulifanikiwa kupatiwa mafunzo ya mchakato mzima wa SAM na hivyo kuweza kufanya uchambuzi wa nyaraka za halmashauri, uhakiki na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali ili kufanya maboresho.

Timu ilifanikiwa kufanya mkutano wa ndani na watoa huduma (CMT na CHMT), ili kupata ufafanuzi wa kina wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa kwenye nyaraka na zile zilizo thibitishwa kwenye maeneo yaliyotembelewa. Ufafanuzi huo uliwezesha Timu kufanya mkutano wa mrejesho na wadau na waliridhia masuala mbalimbali na mengine kukubaliana kufanya ufuatiliaji zaidi ili kuboresha huduma za afya wilayani.

Timu imeridhishwa na ushirikiano uliooneshwa na halmashauri kwa kipindi chote. Kwa kuwa zoezi hili ni endelevu, Timu inaamini kuwa ushirikiano huu utaendelea kudumishwa kwa kipindi chote. Pia imeridhishwa na ushiriki wa wadau mbalimbali waliofanikisha shughulli zote hadi kwenye uandaaji wa ripoti hii ambayo kwa kiasi kikubwa imesheheni masuala yote ya msingi hasa mafanikio yaliyofikiwa na halmashauri, changamoto na maazimio ya pamoja kwa ajili ya ufuatiliaji zaidi.

Kwa muhtasari hoja zilizo ibuliwa awali ni 42 ambapo baada ya kikao na Utawala pamoja na wadau, zilibaki hoja 27. Aidha katika uchambuzi wa Mpango mkakati na Mpango kabambe wa afya, Timu iliridhishwa na miundo na uzingatiaji wa miongozo ya uandaaji wa nyaraka hizo. Baadhi ya masuala ambayo Timu ilishauri kufanyiwa marekebisho ni pamoja na uainishwaji wa taarifa za kina, kutumika kwa lugha rahisi ya Kiswahili, kufanyika

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

2

kwa tathmini ya kina na upembuzi yakinifu. Pia Timu inashauri kuwa halmashauri iongeze ushiriki wa wananchi wakati wa uaandaaji wa mipango na wakati wa utekelezaji wake.

Mwisho tunaamini kuwa ripoti hii ni chachu kwa halmashauri na wadau wakiwamo wananchi kujitathmini na kuwajibika kwa kila nafasi ili kuongeza ufanisi kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya. Mchakato wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ), kama ulivyochambuliwa kwenye ripoti hii ni muhimu sana kwa wadau wote kuuelewa kwa kina na kuongeza ushiriki wa ufuatiliaji masuala ya afya hapa wilayani. Kwa ujumla masuala yote yamelenga kuboresha utoaji wa huduma ya afya wilayani hapa hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake.

1.0 Sehemu ya Kwanza

UtanguliziRipoti hii ni majumuisho ya shughuli zote zilizofanywa na Timu ya UUJ kwa kipindi chote cha Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii kwa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro. Zoezi hili lilijikita kwenye tathmini ya shughuli zilizopangwa na kutekelezwa katika kipindi cha mwaka 2011/2012, ambapo kwa sehemu kubwa makabrasha ya utekelezaji yamekamilika na kutathminiwa na vyombo vya ukaguzi mfano, CAG. Sambamba na kujikita katika mwaka wa fedha 2011/2012, Timu ilifanya uianisho wa mipango na utekelezaji wake kwa mwaka huo, mwaka uliopita na mwaka uliofuata ili kupata uhalisia kwa wakati huu. Mchakato wote huo ulihusisha hatua zote za UUJ ikiwa ni pamoja na kutoa utambulisho wa UUJ kwa madiwani na wadau, kuundwa kwa Timu ya UUJ, Timu kupatiwa mafunzo, kufanya uchambuzi wa nyaraka za halmashauri, kufanya kikao cha ndani na CHMT ili kufafanua hoja, kufanya kikao cha wadau ambacho kiliridhia masuala ya ufuatiliaji zaidi.

1.1 Mchakato wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Mchakato wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ) ni mfumo shirikishi wa uwajibikaji ambao hutoa fursa kwa serikali na jamii kusimamia mipango, matumizi, utendaji, uadilifu na uwajibikaji. Mfumo huu kupitia hatua zake tano huitaka jamii kusimamia shughuli zote kikamilifu ili kuhakikisha kuwa huduma zinaifikia jamii husika kwa

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

3

ufanisi na ubora. Mchakato wa UUJ unahusisha wadau mbalimbali, hivyo kwa Halmashauri ya Simanjiro mchakato huu ulishirikisha wadau wote wa afya na hatimaye kujikita katika kuijengea uwezo Timu ambayo ilitekeleza zoezi zima kwa kuzingatia misingi yake mitano pamoja na 3Us.

1.2 Uundwaji wa Timu ya UUJ

Zoezi la uundaji Timu za UUJ kwa mfumo wa SAM, huusisha wananchi moja kwa moja. Kwa Halmashauri ya Simanjiro, Timu iliundwa ikihusisha makundi tofauti ambapo kundi la kwanza ni la wananchi sita wa kawaida ambao walipatikana kwa kuchaguliwa kwenye mikutano ya jamii kutoka kata tofauti, kundi la pili ni wawakilishi wawili wa maafisa utendaji wa kata (WEOs), waliochaguliwa miongoni mwao ikiwa mmoja ni wa kike na mwingine wa kiume, kundi la tatu ni wawakilishi wa madiwani ambao nao walichaguliwa kutoka kwenye kikao chao ikiwa mmoja ni wa kike na mwingine wa kiume, kundi la nne ni la viongozi wa dini ambapo alichaguliwa mwakilishi mmoja toka miongoni mwao, kundi la tano ni la watu maalumu (WAVIU), ambapo anapatikana mwakilishi mmoja, kundi la sita lilitokana na wawakilishi wa asasi za kiraia ambapo walimchagua mwakilishi mmoja.

Aidha wawakilishi wengine ni pamoja na mjumbe mmoja kutoka CHMT na mwingine kutoka CMT – Ofisi ya Mipango. Uundwaji wa Timu hii huzingatia jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ndani ya jamii husika. Muundo huu huiwezesha jamii kuiwajibisha Timu na kwa kiasi kikubwa ni kuijengea jamii husika uwezo wa kujisimamia kikamilifu.

1.3 Nyaraka za Halmashauri zilizochambuliwa

Timu ya UUJ baada ya kupata mafunzo ilifanikiwa kufanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashauri kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 ikiwemo; Mpango Mkakati wa Wilaya, Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri (CCHP), Ripoti ya Mkaguzi wa Ndani na wa Nje (CAG), Ripoti za Baraza la Madiwani, Ripoti za UKIMWI na Ripoti za Utekelezaji wa CCHP. Katika uchambuzi huo, Timu ilibaini masuala mengi, baadhi yakiwa ni mazuri na mengine yalitokana na udhaifu ama changamoto zilizokuwa nje ya uwezo wa halmashauri. Tunaishukuru halmashauri kwa ushirikiano wao hasa Ofisi ya Mkurugenzi ambaye kwa kiasi kikubwa alifanikisha upatikanaji wa nyaraka zote za umma tulizohitaji kwa kipindi chote cha zoezi.

1.4 Maeneo yaliyotembelewa naTimu ya UUJ

Baada ya mafunzo na uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashauri, Timu ilibaini hoja mbalimbali ambazo baadhi zilihitaji uhakiki. Timu ilitembelea jumla ya vituo 19 vya huduma ya afya. Vituo vilivyotembelewa ni Loiborsiret, Naberera, Sukuro, Narakauo, Namalulu, Ngage, Lemkuna, Nyumba ya Mungu, na Lengasit. Maeneo mengine ni Terrati, Engonongoi, Oiborkishu, Losinyai, Nadonjukin, Okutu, Kitwai A, Kitwai B, Olerumo na Orkesumet. Timu ilijiridhisha kwa baadhi ya vituo na kwa baadhi ilihitaji ufafanuzi wa ziada toka kwa Utawala. Baadhi ya majibu ya Utawala yalikidhi haja huku mengine yakihitaji ufuatiliaji zaidi ambao utaendelea kufanywa na Timu ya UUJ.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

4

1.5 Mpangilio wa ripoti

Ripoti hii ina sehemu kuu nne ambapo sehemu ya I inatoa utangulizi, sehemu ya II inaelezea hoja zilizoibuliwa, majibu ya Utawala na maoni ya Timu. Sehemu ya III inafafanua juu ya changamoto na mambo ambayo Timu imejifunza, huku Sehemu ya IV ikibainisha mapendekezo na hitimisho.

2.0 SEHEMU YA PILI

Mafunzo na uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashuri kwa Timu ya UUJTimu ilipatiwa mafunzo na kufanya uchambuzi wa nyaraka kwa vitendo kwa kipindi cha wiki mbili. Mafunzo hayo yaliyotolewa chini ya uratibu wa Shirika la Sikika yaliiwezesha kupata fursa ya kuelewa masuala mbalimbali yahusuyo halmashauri na sekta ya afya kwa ujumla. Uelewa kwa washiriki ulifanikisha zoezi la uchambuzi wa nyaraka ambao ulifanywa kwa umakini mkubwa. Miongoni mwa nyaraka muhimu zilizochambuliwa ni pamoja na:-

2.1 Mgawanyo wa Rasilimali (Mpango mkakati, CCHP na

MTEF)

Hoja ya 1: Katika uchambuzi wa muundo na uandaaji wa CCHP, Timu ilibaini kuwa halmashauri imezingatia kwa kiasi kikubwa hatua zilizoainishwa kwenye muongozo wa uandaaji wa CCHP (CCHP Guideline), isipokuwa baadhi ya taarifa zilizoainishwa si za kina na nyingine hazina uhalisia. Mfano: Kupunguzwa kwa kutoka asilimia 0.4 hadi asilimia 0.4 kwa matatizo yanayotokea baada ya kujifungua.

Pongezi: Kwa kiasi kikubwa Timu inaipongeza halmashauri kwa juhudi wakati wa uandaaji wa CCHP. Lakini pia inashauri kuwa wakati wa uandaaji wa CCHP ni muhimu kuongeza umakini na

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

5

rasimu kupitiwa na baadhi ya wataalam ili kupunguza makosa ya kiuandishi na takwimu. (Rejea CCHP Uk. V)

Hoja ya 2: Wakati wa uchambuzi wa thathmini ya ndani kwenye muundo wa CCHP, Timu iliridhishwa na tathmini ya ndani kwani imefanywa kwa kufuata taratibu na kuzingatia miongozo. Mfano: Kwenye Mpango Mkakati imebainika kuwa kata zilizotambuliwa ni 15 wakati uhalisia umeonekana kwenye CCHP kuwa ni kata 18.

Pongezi: Timu inaipongeza halmashauri, aidha inashauri kuwa wakati wa O&OD tathmini ifanyike kwa kina ili kuepuka makosa yanayoweza kuathiri upatikanaji wa huduma. Pia uhusianisho wa nyaraka ufanywe kitaalamu na ikibainika kuna upungufu ni vema nyaraka husika ikarejewa (revised).

Hoja ya 3: Katika uchambuzi wa muhtasari wa vyanzo vya mapato ya Halmashauri, Timu imebaini kuwa vyanzo hivyo vimeainishwa isipokuwa mchanganuo wa bajeti kuu haukufanywa kwa umakini kwani baadhi ya vifungu vya fedha vilitofautiana na kiasi kilicho onekana kwenye chanzo cha fedha; Mfano CDG – chanzo ni 110,000,000/= CDG – mchanganuo ni Sh. 120,000,000 tofauti ya 10,000,000. Aidha, Timu imebaini mchanganuo wa kila mfuko/chanzo cha mapato haukufanyika, ni mifuko miwili tu iliyochanganuliwa; BG na BF – Sh. 401,622,100 (Rejea: CCHP – Uk. 4).

Majibu ya CHMT: Wakati wa kikao cha ufafanuzi wa hoja baina ya Timu na CHMT, utawala ulifafanua kuwa “Fedha zilizoongezeka Sh. 10,000,000 ni za Zahanati ya Kitwai B ambazo zililetwa baada

ya maandalizi ya bajeti hivyo ilisahaulika kurekebishwa kwenye muhtasari wa bajeti wakati wa uandaaji”

Moni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu ya utawala hivyo inashauri kuwa wakati mwingine idara iwe makini zaidi ili kuwa na kumbukumbu sahihi na kuepuka makosa yanayoweza kuepukika.

Hoja ya 4: Timu ilibaini kuwa tathmini ya rasilimali watu kwa upande wa idara ya afya imeainishwa vizuri kwa kuzingatia jinsia na kubainisha tatizo kubwa la upungufu wa watumishi 135 kati ya 281mahitaji halisi. (Rejea CCHP Uk. Vii - XXi)

Majibu ya CHMT/CMT: “Tatizo la watumishi ni la kitaifa tumejitahidi kuanisha mahitaji na kuwasilisha Utumishi lakini tunapata idadi ndogo tofauti na mahitaji. bado tatizo hili ni kubwa kitaifa”

Maoni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu ya Utawala kwa kiasi, hivyo inaishauri halmashauri kuwa na mpango madhubuti wa kupunguza tatizo ikiwezekana kuundwa timu itakayoonana na Waziri Mkuu kufanya maombi maalumu ya dharura kama halmashauri nyingine zinavyofanya.

Hoja ya 5: Timu ilibaini kuwa shughuli ya ukarabati wa zahanati ya Nyumba ya Mungu haikuwepo kwenye mpango isipokuwa ilionekana kwenye ripoti ya utekelezaji. Hivyo timu ilihitaji kujiridhisha na utekelezaji wa shughuli ambayo haikupangwa kwenye CCHP, na pia, je fedha hizi zilipatikana vipi? (Rejea: CCHP - Uk. 16 - 17)

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

6

Uhakiki Vituoni: Timu ilihitaji kujiridhisha na ujenzi kwa kufanya uhakiki ambapo ilibaini kuwa utekelezaji wa shughuli umefanyika kwa ufanisi, lakini haikupata ufafanuzi kuhusu fedha zilipatikana wapi hivyo kuhitaji majibu ya Utawala.

Majibu ya CMT/CHMT: Utawala ulieleza kuwa “Fedha hizo ni za GRF ambazo zilikuwa hazijapokelewa tangu mwaka 2005/2006 hadi 2007/2008, tukazipata fedha hizo 2010/2011 hivyo hatukuweza kuzipanga tena 2011/2012 na badala yake zilipelekwa kwenye shughuli moja kwa moja”

Maoni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu na tunaipongeza halmashauri kwa kutekeleza shughuli hii. Pia timu inashauri kuwa shughuli kama hii itolewe ufafanuzi kumrahisishia msomaji kwani kwenye CCHP shughuli haikuonekana isipokuwa kwenye ripoti ya utekelezaji tu. (Rejea: CCHP – Uk ? Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 32; Shughuli Na. 80)

2.2 Usimamizi wa Matumizi Masuala yaliyobainika na mapendekezo

Hoja ya 1: Timu ilibaini kuwa kwa shughuli ya mkutano wa awali wa kuandaa bajeti posho ya kujikimu (per diem) iliyopangwa na kutumika ni Sh. 65,000 kinyume na miongozo kwa ngazi ya halmashauri, pia timu ilibaini kuwa ukumbi kwa idadi ya watu wanne uligharimu Sh 80,000 hivyo Timu ilihitaji ufafanuzi kwa Utawala (Rejea: CCHP - Uk. 26, Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 22; Shughuli Na. 2).

Majibu ya Utawala: CMT ilieleza kuwa “Vikao hivyo vilifanyikia Mkoa wa Arusha kwa kuwa wadau wengi wanatokea huko. Lakini pia suala la watu wanne kutumia ukumbi wa Sh. 80,000 ni kwamba uliotumika awali haukubadilishwa”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri kuwa vikao hivi vifanyikie Wilaya ya Simanjiro badala ya Arusha. Lakini pia halmashauri ibane matumizi kwa kutumia kumbi za bei nafuu pale ambapo kuna watu wachache kama ilivyokuwa kwa watu wanne (4).

Hoja ya 2: Wakati wa uchambuzi Timu ilibaini kuwa halmashauri ilifanya ununuzi wa jenereta hivyo ilihitaji kujiridhisha kama imenunuliwa na ipo kituoni Orkesumet (Rejea: CCHP – Uk. 29, Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 26; Shughuli Na. 18).

Uhakiki Vituoni: Timu ilibaini kuwa jenereta ipo isipokuwa haijaanza kutumika hivyo kuhitaji majibu ya Utawala juu ya hoja hii.

Majibu ya Utawala: Utawala ulieleza kuwa “Kwanza kulikuwa na tatizo la kibanda cha kuhifadhia lakini kwa sasa tumekamilisha, Pili halijaanza kufanya kazi kwani tunasubiri wataalamu waje kuunganisha mfumo wa automatic, na kwa kuwa ni gharama hili litatekelezwa kwenye bajeti ya mwaka 2013/2014”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri kuwa pindi tu fedha zitakapoingia jenereta liunganishwe mara moja ili lianze kutumika kwa maslahi ya wagonjwa. Kwa mujibu wa makubaliano na utawala, timu itafanya ufuatiliaji kwenye utekelezaji wa suala hili.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

7

Hoja ya 3: Timu ilibaini kuwa Idara ilinunua vifaa kwa ajili ya zahanati hivyo ilihitaji kujua ni zahanati zipi zilipelekewa vifaa, pia iliomba maelezo juu ya uhalali wa pesa iliyotumika (300,000/= kwa kila kituo kununua, beseni, stand ya simtank, soap bucket na ndoo) kwani ni tarakimu tu imeonekana – zahanati 20 (Rejea: CCHP UK. 30, Ripoti ya utekelezaji – UK. 28; Shughuli Na. 23).

Uhakiki Vituoni: Wakati wa uhakiki kwa vituo vilivyotembelewa, Timu ilibaini kuwa ni Kitwai A tu ndio iliyokutwa na vifaa vilivyonunuliwa hivi karibuni, vingine vilikutwa vimechakaa kati ya vituo vyote vilivyo tembelewa. Hivyo Timu ilipenda kujua ni wapi vifaa hivyo vilipelekwa, na nini uhalisia wa gharama hizo kwa kila kituo.

Majibu ya Utawala: Utawala ulifafanua kuwa “Hivyo vifaa vilinunuliwa na kusambazwa kwenye zahanati 25 tofauti na 20 kama ilivyoonekana kwenye ripoti ya utekelezaji kimakosa. Zahanati hizo ni Lobosoit B, Ruvuremit, Ngage, Nyumba ya Mungu, Ngorika, Magadini, Msitu wa Tembo, Orchoronyori, Kambi ya Chokaa, Lengast, Naisinyai, Mirerani HC, Landanai, Namalulu, Naberera, Sukuro, Narakauo, Loiborsiret, Kimotorok, Loiborsoit A, Terrat, Oljoro 5, Orkesumet HC na Orkesumet Zahanati”

Maoni ya Timu: Timu iliridhishwa na majibu ya Utawala na inaipongeza halmashauri kwa kufikisha vifaa hivyo kwenye vituo husika. Vielelezo vilivyo wasilishwa na Utawala kwa Timu vimeithibitishia bila shaka kuwa vifaa vilifika katika kila zahanati tajwa. Hata hivyo, Timu inaishauri halmashauri kuainisha vituo

ambavyo wanapeleka huduma kama hizi ili kupunguza maswali. Suala la matumizi ya Sh. 300,000 halikupatiwa ufafanuzi, hivyo timu itafanya ufuatiliaji zaidi kujua thamani ya fedha hiyo.

Hoja ya 4: Uchambuzi ulibainisha kuwa Sh 4,000,000 zilitumika kununua vifaa vya tiba ya meno bila kuainishwa ni wapi vilipelekwa. Hivyo Timu ilihitaji ufafanuzi (Rejea: CCHP- UK. 30, Ripoti ya Utekelezaji – UK. 38; Shughuli Na. 26).

Uhakiki Vituoni: Timu ilibaini kuwa katika vituo vyote vilivyotembelewa hakukuwa na vifaa hivyo. Hivyo ilishindwa kujua ni wapi vilipelekwa.

Majibu ya Utawala: Utawala ulieleza kuwa “Kwa kuwa halmashauri haina hospitali ya wilaya na huduma hiyo huwa haitolewi kwenye ngazi ya zahanati, Utawala uliamua kuvipeleka kwenye kituo cha KKKT ambacho kimepandishwa hadhi kuwa hospitali na ipo katika mchakato wa kufanywa hospitali teule ya wilaya. Lakini pia, Utawala umeshawasiliana na hospitali hiyo kwa ajili ya kupunguza gharama za kutoa huduma ili wananchi waweze kumudu. Utawala pia unatarajia kupeleka mtaalam wa meno Mirerani pale ambapo mtaalam atapatikana”

Maoni ya Timu: Timu iliridhishwa na majibu ya Utawala na pia inaipongeza halmashauri kwa jitihada ya kuboresha huduma ya meno wilayani.

Hoja ya 5: Timu ilibaini kuwa zahanati zilizowekewa umeme jua hazikusainishwa, hivyo ingependa kujua ni zahanati zipi ziliwekewa

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

8

nishati ya jua. Aidha Timu imebaini Sh 11,810,000 zilizopangwa kununua mfumo wa umeme jua zilitumika kwa asilimia mia. Timu inahitaji ufafanuzi, ni kwa jinsi gani makadirio yaliweza kutumika yote (Rejea: CCHP – Uk. 30, Ripoti ya utekelezaji – Uk. 28; Shughuli Na. 27).

Uhakiki Vituoni: Wakati wa uhakiki, Timu ilibaini kuwa, kati ya vituo ilivyotembelea, ni kweli ilikuta mfumo wa umeme jua katika kituo kimoja cha Sukuro na unafanyakazi. Timu pia ilikuta baadhi ya vituo vikiwa na nishati ya jua ambazo hazifanyi kazi zikiwa chini kwa takribani miaka mitatu.

Majibu ya Utawala: Utawala ulifafanua kuwa “Tumenunua umeme jua kwa ajili ya kituo cha Sukuro na Loiborsoit A. Lakini pia, sola zilizokutwa chini ni sola paneli ambazo ziling’olewa kutoka halmashauri na kusambazwa kwenye zahanati na shule mbalimbali zikiwa hazijakamilika, hivyo hatujapata fedha ya kununua vifaa vingine vya kukamilisha mfumo. Vilevile halmashauri itazingatia mpango wa REA wakati wa kununua sola hizo ili kuepuka kupata hasara”.

Maoni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu ya swali la msingi isipokuwa inahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu matumizi ya fedha zote kama zilivyopangwa. Pia inashauri vifaa hivyo vinunuliwe haraka ili kuvinusuru vilivyopo visiharibike.

Hoja ya 6: Uchambuzi ulibainisha kuwa halmashauri ilifanya usafirishaji wa sampuli za wagonjwa toka vijijini, lakini viwango vya malipo ya posho (per-diem) vilionekana kuwa na utata, ambapo

dereva alilipwa posho (per-diem) ya Sh 25,000 wakati aliyehusika kusafirisha alilipwa Sh 65,000 kwa siku (Rejea: CCHP – Uk. 32, Ripoti ya utekelezaji – Uk. 34; Shughuli Na. 37).

Majibu ya Utawala: “Viwango vya posho Sh. 65000 ni kwa ajili ya DSM ambako sampuli hupelekwa. Posho ya Sh. 25,000 ni ya dereva kumpeleka mganga Hedaru kwa ajili ya kupanda basi kwenda DSM. Mafuta yaliyoandikwa ni kwa ajili ya ukusanyaji wa sampuli hizo vituoni na kumfikisha mganga Hedaru”.

Maoni ya Timu: Timu iliridhishwa na majibu yaliyotolewa. Inashauri taarifa kama hizi ziainishwe kwenye mipango na utekelezaji kuondoa utata.

Hoja ya 7: Timu ilibaini kuwa shughuli ya uendeshaji ofisi ilikuwa na fungu lake (OC) lakini zikaonekana tena Sh 26,504,908 kwenye shughuli kama hiyo ya kuendesha ofisi (support office running cost) (Rejea: CCHP – Uk. 48, Ripoti ya utekelezaji – Uk. 27: Shughuli Na. 65)

Majibu ya Utawala: “Hoja hiyo ni matumizi tu ya maneno yaliyotumika kwa shughuli za kiofisi hivyo ni gharama za umeme, maji n.k”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri kuwa vifungu hivi viandikwe kwa uwazi zaidi na kuchanganua matumizi ya fedha hizo.

Hoja ya 8: Timu ilibaini kuwa gharama zilizotumika kwa ajili ya shajala moja ni Sh 120,000, hivyo ingependa kujua uhalisia

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

9

wa fedha hizo za shajala kufanana na hata kutumika zote kwa asilimia mia (Rejea: CCHP – Uk. 31, Ripoti ya utekelezaji – Uk 33; Shughuli Na. 31).

Majibu ya Utawala: “Suala la shajala haliepukiki isipokuwa mfumo wa PLANREP unataka shughuli iwe na fedha za mkupuo (lampsum) hivyo tunaandika kulingana na mfumo. Aidha kama kwenye utekelezaji fedha zinaonekana kutumika zote, hapo kuna tatizo kwani kwa kawaida shughuli kama hiyo fedha inaweza kupungua au kuongezeka – lakini tukumbuke shughuli kama hii hufanywa kwa zabuni, hivyo fedha kubaki itategemea na mtu wa zabuni kuweza kuwasilisha vitu vyote”.

Maoni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu. Na kwa kuwa tulikubaliana kufuatilia uthibitisho wa akiba, hivyo itafanya ufuatiliaji. Lakini pia endapo kuna akiba ni vema wakati wa kupanga halmashauri izingatie akiba ila kusiwe na mpango unaofanana kwa kila mwaka.

Hoja ya 9: Timu imebaini pesa zilizotumika kwenye utekelezaji wa ujenzi Nadonjukin ni Sh. 23,400,000 wakati kwenye mpango ilikua Sh. 20,000,000. Hivyo Timu ingependa kujua pesa za ziada zilitoka fungu lipi? Rejea (CCHP- Uk. 51, Ripoti ya Utekelezaji- Uk. 30 - Shughuli: CCHP 88, Ripoti ya Utekelezaji 133)

Uhakiki Vituoni: Timu ilibaini kuwa ujenzi unaendelea vizuri.

Majibu ya Utawala: Tunaomba muda ili tuweze kujiridhisha na taarifa ya tofauti ya fedha kati ya Sh 23,400,000 na 20,000,000 kisha tutatoa majibu sahihi.

Maoni ya Timu: Timu inaipongeza halmashauri kwa kufikia hatua nzuri ya ujenzi huo. Hivyo imeridhia kushirikiana na serikali kupata taarifa za uhakika.

Jengo la Zahanati ya Nadonjukini linaloendelea kujengwa

2.3 Usimamizi wa Utendaji

Masuala yaliyobainika na mapendekezo ya Timu

Hoja ya 1: Uchambuzi ulibainisha kuwa ujenzi wa maabara na mfumo wa uvunaji maji Naberera ulifanyika kwa asilimia 40, hivyo Timu ilipenda kujiridhisha juu ya thamani ya fedha iliyotumika na uhalisia (Rejea: CCHP – Uk. 29, Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 26; Shughuli Na. 16).

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

10

Majibu ya Utawala: Utawala ulitoa ufafanuzi kuwa “Ujenzi wa maabara bado unaendelea isipokuwa kwa upande wa tanki bado halijaanza kukarabatiwa lakini tumeingia mkataba na mkandarasi hivi karibuni”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri ukarabati wa tanki ufanyike mapema kwa usimamizi wa karibu kwani lililopo ni hatari kwa watoa huduma na wagonjwa kwa kuwa linaweza kuvunjika wakati wowote. Aidha, usimamizi ufanyike kurekebisha makosa yaliyoonekana kabla ya kukabidhiwa jengo, na Placenta pit ijengwe kama wataalam walivyo shauri.

Tanki la Maji Naberera likiwa na ufa mkubwa kama inavyoonekana pichani

Hoja ya 2: Timu ilibaini utekelezaji wa ujenzi wa jengo la madawa Orkesumet umefanyika kwa asilimia 38 (Sh 11,484,450), hivyo Timu ilitaka kujiridhisha na utekelezaji uliofanyika (Rejea: CCP – Uk. 29, Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 26; Shughuli Na. 17).

Majibu ya Utawala: “Jengo limekamilika isipokuwa halijaanza kutumika kutokana na kutokamilika makabati (shelves) ya kuhifadhia dawa na mfumo wa mnyororo baridi kutokamilika. Pia grili za milangoni bado zinaandaliwa ili kukamilisha shughuli”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri halmashauri iongeze kasi kuhakikisha jengo hilo linakamilika na linaanza kutumika ili huduma ziweze kupatikana kwa ubora.

Hoja ya 3: Timu ilihitaji kujiridhisha na utekelezaji wa shughuli ya ukarabati wa zahanati na ujenzi wa kichomea taka Loiborsiret (Rejea: CCHP – Uk ??, Ripoti ya Utekelezaji – Uk. 32; Shughuli Na. 79).

Uhakiki Vituoni: Timu iliridhishwa na hatua ya utekelezaji wa shughuli ya ujenzi wa shimo la kutupa kondo la nyuma la uzazi, kichomeo taka na ukarabati wa zahanati.

Maoni ya Timu: Timu inaipongeza halmashauri na uongozi wa kijiji kwa kusimamia ufanisi wa utendaji wa shughuli hii.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

11

Shimo la kutupia kondo la nyuma la uzazi na kichomeo taka kwa nyuma

katika Zahanati ya Loiborsiret ambavyo vimekamilika ujenzi.

Hoja ya 4: Uchambuzi wa Timu ulibainisha kuwa mradi wa ukamilishaji wa Zahanati Kitwai B ulipata Sh. 16,689,736 bila kutumika kati ya 23,000,000/= zilizo pangwa, hivyo Timu ilihitaji kujiridhisha na hali halisi ya mradi (Rejea: CCHP- UK 50, Ripoti ya Utekelezaji- Uk. 31; Shughuli Na. 81).

Uhakiki vituoni: Timu ilibaini kuwa mradi upo katika hatua nzuri, ila Timu haikupata majibu ya Sh. 16, 689, 736 zilitumika kwa mwaka upi.

Majibu ya Utawala: “Fedha hizo zilichelewa kufika, hivyo zikatumika 2012/2013”

Maoni ya Timu: Timu imeridhika na majibu ya Utawala kwa kupata vielelezo. Aidha inashauri kuwa Sh. 6,315,264 zilizobaki zitumike kumalizia jengo la zahanati ili wananchi waanze kupata huduma.

2.4 Usimamizi wa uadilifu Masuala yaliyobainika na mapendekezo ya Timu

Hoja ya 1: Timu ilihitaji kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi Engonongoi, ambao ulibainika kupangiwa Sh 10,000,000 lakini kwenye utekelezaji zilitumika Sh. 25,000,000, hivyo timu ilihitaji kujua pesa za ziada zilitoka wapi?(Rejea: CCHP- Uk. 51, Ripoti ya Utekelezaji- Uk. 29: Shughuli namba; CCHP 83, Ripoti ya utekelezaji 127)

Uhakiki vituoni: Timu ilibaini kuwa ujenzi haujakamilika kwa asilimia 100. Pia timu ilikuta baadhi ya fremu za milango hazifai. Vilevile milango ya choo kilichojengwa haifungi kama inavyostahili.

Majibu ya Utawala: “Tunaomba muda ili tuweze kujiridhisha na taarifa hizo za ujenzi wa zahanati za Engonongoi, Losinyai, Nadonjukin, Okutu na Lerumo kabla hatujatoa majibu.”

Maoni ya Timu: Timu imeridhia, hivyo itashirikiana na Utawala kupata majibu.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

12

Jengo la Zahanati ya Engonongoi ambalo fremu za milango zimelika kabla ya kukabidhiwa kwa halmashauri.

Hoja ya 2: Kwa hoja mbalimbali za CAG, Timu ilibaini kuwa halmashauri ilizingatia kwa kiasi kikubwa ushauri wa CAG hivyo kufanikiwa kuongeza mapato ya ndani kwa kiasi. Aidha, ilibaini kuwa mafuta ya Sh. 14,500,200 yalitolewa na hayakuoneshwa kwenye kitabu cha kumbukumbu (log book).

Majibu ya Utawala: “Vielelezo vya mafuta yaliyotumika bila kurekodiwa kwenye ‘log book’ vimepatikana na kuwasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Kanda”.

Maoni ya Timu: Timu inapongeza halmashauri kwa kuzingatia maoni ya Mkaguzi Mkuu kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, inashauri kuwa vielelezo vya matumizi yote vihifadhiwe vizuri na kuwasilishwa kwa mkaguzi pale vinapohitajika. (Rejea: CAG Ripoti 2010/2011 Uk. 2 na 7).

Hoja ya 3: Timu ilibaini kuwa vifaa vyenye thamani ya Sh. 28,484,985 vilinunuliwa bila kuzingatia Sheria ya Manunuzi kwani havikuwa na vielelezo na inawezekana kuwa havikufika kwenye vituo vilivyo kusudiwa.

Uhakiki Vituoni: Timu ilibaini kuwa kiasi cha Sh. 1,980,000 cha makusanyo toka kwa wakala hakikukusanywa kinyume na mkataba wa makusanyo hayo.

Majibu ya Utawala: CMT ilieleza kuwa “angekuwepo DMO angeweza kutoa majibu sahihi, hivyo tunaomba muda wa kupitia taarifa kabla ya kutoa majibu ya hoja hiyo.Maoni ya Timu: Timu inashauri utawala kuzingatia ushauri wa CAG, pia itaendelea kufuatilia.

Hoja ya 4: Uchambuzi ulionesha kuwa mkandarasi alilipwa fedha zaidi (Sh. 10,123,198) na hakuna mahali palipoonesha kama fedha hizo zilirudishwa. (Rejea: CAG Ripoti 2011/2012 Uk. 9).

Majibu ya Utawala: “Fedha zilikatwa wakati wa malipo yake ya mwisho. Hizi ni fedha zilizokuwa kwenye miradi vijijini, hivyo zilipobaki kamati ya kijiji ikaamua kumuongezea mkandarasi

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

13

kazi bila kupitia bodi ya ugavi ya halmashauri, kwani kila mradi ukipitia kwenye bodi ya ugavi unaweza kuchelewesha utekelezaji wa miradi vijijini”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri uwazi wa malipo ya wakandarasi uwepo ili kupunguza maswali. Pia ni muhimu Sheria ya Ugavi izingatiwe, na kuwe na namna rahisi ya kufanya maamuzi haya ili kusiwe na ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi vijijini.

2.5 Usimamizi wa Uwajibikaji Masuala yaliyobainika na mapendekezo ya Timu

Hoja ya 1: Wakati wa uchambuzi, Timu ilibaini kuwa hakukuwa na mchango wa wananchi (nguvu za wananchi) kwenye ujenzi wa Zahanati ya Okutu, hivyo Timu kuhitaji kupata ufafanuzi zaidi kwani maoni ya taarifa yalionesha kushindwa kuendelea kwa mradi kutokana na changamoto hiyo (Rejea: CCHP – Uk. 31, Ripoti ya utekelezaji – Uk. 29; Shughuli Na. 29).

Uhakiki Vituoni: Timu ilipotembelea mradi, ilibaini kuwa shughuli zinaendelea vizuri na wananchi wanashirikiana na uongozi japokuwa mchango wa wananchi ulihamishiwa kwenye mradi wa maji hivyo kufanya utekelezaji kusuasua.

Maoni ya Timu: Timu inaipongeza halmashauri, uongozi wa kata na kijiji kwa kuondoa tofauti zilizo kuwepo awali kati ya wananchi.

Hoja ya 2: Uchambuzi ulibainisha kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Losinyai uliogharimu Sh. 35,000,000

haukuwa sawia na mpango, ambapo kiasi kilichopangwa kilikuwa Sh 25,000,000 pungufu, Timu ilihitaji kujiridhisha na utekelezaji pamoja na kujua fedha za ziada zilitoka fungu lipi? (Rejea: CCHP- Uk. 51, Ripoti ya utekelezaji – Uk. 29; Shughuli namba; CCHP 87, Ripoti ya Utekelezaji 129).

Uhakiki Vituoni: Wakati wa uhakiki Timu ilibaini kuwa ujenzi hauendelei, msingi una nyufa nyingi, takribani (9) na mkandarasi amejaribu kuziba lakini bado inapasuka licha ya fedha za utekelezaji kutolewa nyingi kuliko iliyoombwa.

Majibu ya Utawala: “Uhalisia ni kwamba taratibu za kiufundi kutokana na ukubwa wa jengo hazikuzingatiwa. Mfano, udongo wa eneo hilo ulipaswa kuondolewa ila mkandarasi hakufanya hivyo. Pia, matundu ya kupumulia jengo hayakuwepo hivyo mkandarasi itabidi arekebishe nyufa na kazi atapewa mkandarasi mwingine ambaye atainua jengo kwa kuwa fedha imeshapatikana”.

Maoni ya Timu: Timu imeridhishwa na majibu ya Utawala kwa kiasi, kwa kuwa tulikubaliana kufanya ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa shughuli hii, Utawala hauna budi kutoa ushirikiano ili kuboresha huduma za afya.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

14

Nyufa katika msingi wa jengo la Zahanati Losinyai.

Hoja ya 3: Uchambuzi ulibainisha kuwa fedha zilizopangwa kwa ujenzi wa Kitwai A Sh 10,000,000 zilitofautiana na zile za ripoti ya utekelezaji ambazo ni Sh. 25,000,000 hivyo Timu ilihitaji kujua pesa za ziada zilitoka fungu lipi? Sambamba na hoja hii, Timu ilibaini kuwa salio la kufunga robo ya kwanza Julai-Septemba, 2011 sio sawa na salio anzia robo ya pili ya Oktoba – Disemba, 2011 (Rejea: CCHP- Uk. 56, Ripoti ya Utekelezaji, Uk. 22,29,30, robo ya I Uk. 1, robo II Uk. 3).

Majibu ya Utawala: “Tunaomba muda wa kujiridhisha na taarifa kisha tutatoa majibu sahihi”

Maoni ya Timu: Timu itaendelea kufuatilia ili kufanikisha kuboreshwa kwa huduma za afya kama Utawala ulivyo eleza.

Hoja ya 4: Timu imebaini kuwa mkaguzi alionesha upungufu kwenye mradi, mfano: mtendaji ametakiwa kutohusishwa katika usimamizi wa fedha na kutia saini, kukosekana kwa nyaraka muhimu za manunuzi na kusababisha wakaguzi kutolinganisha thamani ya fedha na kazi iliyofanyika. Aidha, Timu ilibaini kuwa mkandarasi alivunja mkataba kwa kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati na fedha alishalipwa. Pia Timu ilibaini kuwa mkandarasi huyo aliyevunja mkataba kwa kushindwa kukamilisha mradi ndani ya muda wa makubaliano alipewa tena mradi mwingine ndani ya halmashauri.

Majibu ya Utawala: “Moja ya sababu zilizosababisha mkandarasi kupewa kazi zaidi ya moja ni kutokana na uhaba wa wakandarasi

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

15

wilayani na pia tuliwapa kamati ushauri wa kutafuta mkandarasi mwingine lakini ikaleta mkandarasi yuleyule. Hivyo, ili kuzuia fedha zisikae muda mrefu bila kutumika na huduma kutopatikana, tukalazimika kushauri apewe kazi mkandarasi huyo”.

Maoni ya Timu: Timu inashauri kuwa ni muhimu sheria na taratibu za ugavi zifuatwe na kuzingatiwa.

Hoja ya 5: Kwa vituo vilivyotembelewa ilibainika kuwa watumishi hawalipwi posho ya muda wa ziada kwa wakati, vituo vyote vilivyotembelewa vinakosa mfumo bora wa uwasilishaji wa taarifa kwa umma na malalamiko kwani matangazo mengi hubandikwa ukutani, vituo vingi havina matabibu vinasimamiwa na wauguzi wasaidizi kinyume na utaratibu. Pia kuna ukosefu mkubwa wa maji vituoni, pamoja na kwamba ni tatizo la wilaya lakini tungependa kuona suala hili linapewa kipaumbele cha pekee vituoni ili kuepuka vituo kuwa sehemu ya kuambukizwa magonjwa badala ya tiba. Suala la wanachama wa CHF ni tatizo kubwa kwani Timu ilibaini kuwa hakuna wanachama wengi wa CHF katika vituo vingi.

Maoni ya Timu: Timu inashauri kuwa Utawala uweke mkakati madhubuti wa kukabiliana na changamoto tajwa ili kufanikisha utoaji bora wa huduma za afya kwa kila mwananchi na kuwapa ari watoa huduma za afya vituoni.

3.0 SEHEMU YA TATU

3.1 Sauti za Wadau

Huduma ya Meno:

• Daktari wa Meno – “Baadhi ya vifaa vya huduma ya meno vipo ofisini kwa DMO na vingine vipo hospitali ya KKKT, tutaomba mtaalamu aliyeko Mirerani asaidie kutoa huduma hiyo kwani hatuna vifaa vya kutosha kwa ajili ya huduma zote za meno. Vifaa vilivyonunuliwa ni vya kuziba na kun’golea tu na kwa vile ni bei ghali haviwezi kununuliwa vyote kwa mwaka mmoja. Hivyo tutaendelea kutoa rufaa mpaka pale vifaa vyote vitakaponunuliwa. Kuhusu suala la gharama, nachelea kusema kuwa matibabu ya meno ni ghali kutokana na vifaa vinavyotumika, hivyo matibabu hayawezi kutolewa bure hata kama yangetolewa katika kituo cha umma, ila halmashauri ina inandaa mpango wa kutoza kiasi cha wastani ili huduma hiyo iwe endelevu badala ya kusubiri fedha za kujiendesha kutoka halmashauri”

• Mgeni Rasmi (DAS) –“Kwa suala hili nashauri Timu iende ikathibitishe kama vifaa vilivyopo vilinunuliwa mwaka husika/tajwa wa fedha na sio manunuzi ya miaka iliyopita (miaka ya nyuma)”

Ujenzi na Ukarabati wa Zahanati:

• Mh. Diwani – Engonongoi – “Timu inapompa Mkurugenzi

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

16

muda wa kujibu kwa nini msimuulize ajibu hapo hapo? Tulitegemea mnapotuletea hoja na majibu ya Utawala pasingekuwa na sehemu ya kusubiri. Pia ili kuweka taarifa vizuri ieleweke kuwa ujenzi wa Zahanati ya Okutu haukuanza mwaka 2011 ila mwaka huo ndio fedha zilikuja na ujenzi ulianza mwaka 2013”

• Mjumbe wa SAM – “Mh. Diwani, napenda nitoe ufafanuzi kuwa Timu na Utawala kwa pamoja tuliridhia kuwa baadhi ya hoja zitolewe majibu ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa, kwani tunatambua kuwa baadhi ya taarifa zinahitaji muda kuzihakiki ili kujiridhisha, vinginevyo jamii inaweza kupewa majibu ambayo si sahihi. Tumekubaliana kufanya ufuatiliaji wa hoja zote zinazohitaji muda”.

• Katibu wa Afya – “Kwa suala la mkandarasi kulipwa bila kukamilisha ujenzi, nifafanue kuwa mkandarasi aliyeondoka pesa zake hazijalipwa zote, anadai retention hivyo Mkandarasi wa Wilaya anafanya mawasiliano ili arekebishe nyufa na asipo kamilisha, hatalipwa pesa zake badala yake zitatumika kuziba nyufa”

• Mgeni Rasmi (DAS) – “Napenda kujua huyo Mkandarasi alichukuaje pesa, na nani alimpa cheti ili alipwe hadi ibaki retention? Naomba muhusika atakayejibu aje na majibu yanayoeleweka maana hali inatisha na mimi mwenyewe nitakwenda huko kujiridhisha.

Vifaa vya kujifungulia:

• Katibu wa Afya – “Kwa suala la kitanda cha kujifungulia Terrati, kulikua na matatizo ya mawasiliano tu, kwani tulifanya mkutano na kila mtendaji aliagizwa awasilishe matatizo yaliyopo katika eneo lake lakini tatizo lililoletwa kwa zahanati hii lilikua ni nyumba ya mtumishi. Kuna vitanda viwili hapa Orkesumet na kesho kitanda kimoja kitapelekwa terrati” Ni kweli Timu ilithibitisha kupelekwa kwa kitanda Zahanati ya Terrat.

Kitanda cha kujifungulia kilichozuiliwa na mawe katika Zahanati ya Terrat

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

17

Maoni ya jumla:

• Kaimu Mkurugenzi – “Nawapongeza sana Sikika kwa kuleta mtazamo wa pamoja ili kuboresha huduma za afya, kwani mmetusaidia kuona na kutupanua uelewa wetu kuwa zahanati inapokuwepo kunahitajika vitu vingi. Pamoja na taarifa nzuri mnazotoa hasa kwenye changamoto za miundombinu, tunaomba mjaribu kupendekeza njia mbadala za vyanzo vya mapato ili kuzitatua, pia tuchague kituo kimoja ili kiwe cha mfano. Lakini naipongeza Timu, napenda kuwajulisha kwamba haya yote nimeyapokea na nitayafikisha kwa Mkurugenzi.

• Mh. Leshule – Nashukuru Shirika la Sikika na SAM, isipokuwa napenda vikao kama hivi vingefanyika kabla ya vikao vya madiwani ili viingizwe kwenye maamuzi yao kwani inasikitisha kwa jinsi tulivyopigia kelele suala la afya lakini kumbe bado kuna nyumba za watumishi na zahanati mbovu.

• Mh. Diwani – Shambarai – Viongozi tuliopewa dhamana tunashindwa kutekeleza wajibu wetu, mpaka msingi unapasuka viongozi wa vijiji wapo. Wenzangu ambao hatukufikiwa tujipime na haya yaliyotokea kwani haiwezekani mpaka hali iwe mbaya na kusubiri uletewe taarifa, uwe mtumishi wa serikali au wa kuchaguliwa, uwajibikaji unatuhusu wote, naomba kila mtu akajipime yeye katika eneo lake kuna hali gani na tukaibue matatizo yetu wenyewe. Nawapongeza Sikika kuchunguza afya, naomba itokee shirika la kuchunguza idara zingine kwani tukipata taasisi isiyo ya kiserikali inayofanya shughuli kama hizi zitatusaidia kusahihisha matatizo.

• Mwenyekiti wa Timu – “Tunashukuru kwa ushirikiano kutoka halmashauri na kukubali kufanyia kazi hoja zote tulizoziibua”

3.2 ChangamotoBaadhi ya changamoto ambazo Timu ilikumbana nazo wakati wa utekelezaji wa zoezi la SAM ni pamoja na:-

Miundombinu mibovu, kwani baadhi ya maeneo hayafikiki kirahisi

Muda ni mfupi kuelewa kila kitu na kukifanyia kazi wakati huo huo

3.3 TuliyojifunzaMasuala ambayo Timu imejifunza wakati wa utekelezaji wa zoezi la SAM ni pamoja na:-

Mfumo wa SAM ni mzuri kwa kuwa ni shirikishi na unakwenda hatua kwa hatua kwa kuzingatia misingi ya Ufafanuzi, Uthibitisho na Uhalalisho.

Tumepata ushirikiano mzuri kutoka kwa watumishi wa halmashauri na madiwani.

Ufuatiliaji unapaswa kufanyika muda wote na zoezi liwe endelevu linalopaswa kufanywa na watendaji, madiwani na wananchi.

Baadhi ya shughuli ni za kisera na hutekelezwa kwa muongozo wa Serikali Kuu hivyo kuathiri utekelezaji wa shughuli za ngazi ya halmashauri.

Fedha kutoka Serikali Kuu huchelewa kufika hivyo miradi mingi huchelewa kuanza utekelezaji.

Wadau wote tukishirikiana udhaifu unapungua kwa kiasi kikubwa.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

18

4.0 SEHEMU YA NNE

4.1 MapendekezoBaada ya mchakato wote wa zoezi la SAM, Timu inapendekeza mambo yafuatayo ili kuboresha huduma ya afya wilayani hapa.

1. Baraza la Madiwani lisiishie kupokea taarifa tu bali kamati zihakiki shughuli mara kwa mara ili kujiridhisha na utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

2. Ofisi ya Mkurugenzi izingatie ripoti za mkaguzi wa ndani na wa nje ili kupunguza hoja.

3. Wananchi kwa ujumla washiriki kikamilifu kwenye utekelezaji wa shughuli kwa ngazi ya jamii ili kuboresha huduma.

4. Watendaji wanapaswa kuzingatia maadili ya kazi na kufuata taratibu.

5. Mafunzo kwa watumishi yatolewe ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kwenda na na wakati

6. Kuundwa kwa kamati za UKIMWI na kuimarishwa kwa kamati za vituo vya afya

7. Halmashauri kuwawajibisha wakandarasi wote waliohusika kuhujumu majengo ya serikali.

8. Uelewa kuhusiana na suala la CHF uongezwe miongoni mwa wanajamii na uwekwe mkakati maalumu.

9. Changamoto za kisekta kama maji, watumishi na fedha zitatuliwe kwa pamoja ili kuboresha huduma za afya.

10. Timu inashauri uwazi uwepo zaidi ili kuimarisha utawala bora hasa vijijini

4.2 HitimishoKukamilika kwa zoezi la Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ) ni mwanzo wa kuimarika kwa uwajibikaji jamii ndani ya Halmashauri ya Simanjiro. Timu imebainisha maeneo mbalimbali ambayo kwa uhakiki yamefanywa vizuri na kwa sehemu nyingine yaliyoonekana kuwa duni tumekubaliana kuyaboresha kwa kufanya ufuatiliaji. Timu inaamini kuwa ushirikiano uliooneshwa na halmashauri katika kipindi hiki ni endelevu na wa kujivunia katika kuimarisha mfumo na hatimaye kuboresha huduma za afya wilayani.

Ni matumaini ya Timu kuwa wadau wote pamoja na Shirika la Sikika wataendelea kusimamia uwajibikaji kwa nafasi zao. Tunaiomba halmashauri kupitia Baraza la Madiwani kuchukua hatua za haraka pale inapobainika kuwepo kwa uzembe ili kuinusuru Idara ya Afya na halmashauri kwa ujumla. Mapendekezo yote yaliyotolewa ni vema yakafanyiwa kazi haraka ili kuziondoa changamoto zilizo jitokeza.

Timu itaendelea kufuatilia kwa ukaribu yote tuliyokubaliana kushirikiana, lakini pia Timu itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha masuala yote yaliyoibuliwa hayajirudii tena kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha huduma za jamii hasa afya zinakuwa bora na zinawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)
Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (UUJ)sikika.or.tz/images/content/mp3/Simanjiro_report_[3].pdfRipoti ya SAM Simanjiro 1 Muhtasari Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii (UUJ)

Ripoti ya SAM Simanjiro

20

Sikika inafanya kazi kuhakikisha usawa katika

upatikanaji wa huduma bora za afya, kwa kutathimini

mifumo ya uwajibikaji katika ngazi zote za serikali.

Nyumba Na.69Ada Estate, KinondoniBarabara ya TunisiaMtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.

Nyumba Na. 340Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970Dodoma, Tanzania.Simu: 0262321307Faksi: 0262321316

Simu: +255 22 26 663 55/57 Ujumbe mfupi: 0688 493 882Faksi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected]: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.comTwitter: @sikika1Facebook: Sikika Tanzania