ripoti ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa jamii (sam) report... · 2020-01-08 · valence kihwaga na...

28
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Iringa Agosti 2016

Upload: others

Post on 26-Apr-2020

7 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

Iringa

Agosti 2016

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo

Iringa

Imeandaliwa na Timu ya SAM Agosti 2016

Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda
Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

i

Timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Wilaya ya Kilolo imekamilisha utekelezaji wa zoezi

la SAM kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni jitihada za timu pamoja na wadau mbalimbali wa afya. Ni imani ya

timu kuwa ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa shirika la Sikika ulifanikisha uratibu bora wa mafunzo

kwa timu na hivyo kufikia mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ripoti hii.

Kwa dhati kabisa napenda kuwashukuru Sikika kwa umahiri waliouonesha katika kuijengea uwezo

timu ya SAM. Mafunzo tuliyopatiwa yalituwezesha kutekeleza zoezi la SAM kwa ufanisi na ukamilifu

kama ilivyotarajiwa.

Pia napenda kuwashukuru viongozi wa Mkoa; Katibu Tawala Mkoa Ndg. Nuhu Mwasumilwe na Mgan-

ga Mkuu wa Mkoa Dk. Robert Salim kwa ushirikiano wao. Aidha, kipekee napenda kuwashukuru vi-

ongozi wa Wilaya na Halmashauri; Mkuu wa Wilaya, Mh. Asia Abdallah, Mwenyekiti wa Baraza la

Madiwani Mh. Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa

kuwa pamoja na Timu muda wote. Ushirikiano wao kwa pamoja ulifanikisha upatikanaji wa wajumbe

wa timu ya SAM pamoja na taarifa mbalimbali muhimu zilizosaidia kufanyika kwa zoezi. Jambo hili ni

la kujivunia kwa Halmashauri yetu.

Kwa moyo mkunjufu nawashukuru wajumbe wa timu ya SAM kwa umakini waliouonesha na kufanya

kazi kwa bidii bila kuchoka hatimaye kuwezesha zoezi zima kufanyika kwa ufanisi.Ni rai yangu kwetu,

kuwa elimu na ujuzi huu utakuwa endelevu katika maeneo yetu na hasa kwa wananchi wenzetu.

Kwa kuwa si rahisi kumshukuru kila mmoja nachukua fursa hii kuwashukuru wote walioshiriki kwa nam-

na moja au nyingine katika kuwezesha timu kukamilisha zoezi la SAM. Naomba ushirikiano huo udumu

hata katika ufuatiliaji wa maeneo tuliyokubaliana kati ya timu na Halmashauri ili kuhakikisha uwepo na

upatikanaji wa huduma bora za afya katika wilaya yetu ya Kilolo.

Ahsanteni,Ndugu John KasugaMwenyekiti – Timu ya SAM

Shukrani

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

ii

Yaliyomo

Shukrani i

Orodha ya Vifupisho iii

SEHEMU YA KWANZA 1

1.0 Utangulizi 1

1.1 Lengo la Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii 1

1.2 Uchaguzi wa Wajumbe wa Timu ya SAM 1

1.3 Mafunzo ya Utekelezaji wa SAM 2

1.4 Uchambuzi wa Nyaraka 2

1.5 Njia Zilizotumika Kupata Ufafanuzi 2

1.6 Taarifa ya Zoezi la SAM kwa Wadau wa afya 3

SEHEMU YA PILI 4

Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali 4

2.0 Utangulizi 4

2.1 Mikutano ya Wadau (Baraza la Madiwani na Wadau wa Afya) 4

2.2 Mafunzo na Uchambuzi wa Taarifa za Halmashauri 5

2.3 Ziara ya Uhakiki Vituoni 5

2.4 Kuwasilisha Matokeo ya Awali kwa Halmashauri na Idara ya Afya 6

2.5 Hoja zitokanazo na uchambuzi wa nyaraka na maazimio ya CMT & CHMT 6

2.5.1 Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali 6

2.5.2 Usimamizi wa Matumizi 7

2.5.3 Usimamizi wa Utendaji 8

2.5.4 Usimamizi wa Uwajibikaji 11

SEHEMU YA TATU 13

3.1 Changamoto Zilizobainika Vituoni 13

3.2 Changamoto katika Utekelezaji wa Zoezi la SAM 14

3.3 Hitimisho 15

VIAMBATANISHO 16

Kiambata Na. 1 Mapendekezo 16

Kiambata Na. 2 Timu ya SAM 18

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

iii

Orodha ya Vifupisho

CAG Controller and Auditor General (Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali)

CCHP Comprehensive Council Health Plan (Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri)

CHF Community Health Fund (Mfuko wa Afya wa Jamii)

CHMT Council Health Management Team (Timu ya Menejimenti ya Halmashauri kwa Idara ya

Afya)

CMT Council Management Team (Timu ya Manejimenti ya Halmashauri)

HBF Health Basket Fund (Mfuko wa Afya wa Pamoja)

HFGC Health Facility Governing Committee (Kamati ya Usimamizi wa Kituo cha Afya)

MSD Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa)

MTEF Medium Term Expenditure Framework (Mpango wa Kati wa Matumizi)

OC Other Charges (Fedha za matumizi ya kawaida)

SAM Social Accountability Monitoring (Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii)

PLHIV People Living with HIV (Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi)

WEO Ward Executive Officer (Afisa Mtendaji Kata)

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

iv

Muhtasari Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii au “Social Accountability Monitoring” (SAM) ni zoezi

lenye lengo la kuiwezesha jamii kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kuchambua utekelezaji wa mip-

ango kuanzia ngazi ya jamii mpaka halmashauri. Lengo kuu la SAM ni kuhimiza ushirikishwaji, ufuatil-

iaji na uwajibikaji wa watendaji/watoa huduma zikiwamo huduma za afya ili kuwapa wananchi haki

zao za msingi kama ilivyoainishwa katika sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania

imeridhia. Sheria na mikataba hiyo ni pamoja na; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)

Ibara za (11), (12), (14) – (28), Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiu-

chumi, Kijamii na Kiutamaduni unaofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama “International Covenant

for Economical, Social and Cultural Rights (ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha

uwajibikaji katika kufikia upatikanaji na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

Tangu mwaka 2012, Sikika imekuwa ikishirikiana na halmshauri mbalimbali katika kuendesha zoezi la

SAM kwa kuunda timu katika halmashauri hizo. Timu hizi za SAM zinajumuisha wananchi wa makundi

yote, wajumbe wa kamati za afya, mashirika ya kiraia, wawakilishi wa viongozi wa dini na madiwani.

Timu ya SAM hujengewa uwezo wa kushiriki katika kupanga na kufanya uchambuzi wa taarifa mbal-

imbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.

SAM pia inalenga kuiwezesha jamii kuhoji uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili

waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji,

chakula na makazi.

Sikika imekuwa ikiendesha zoezi katika wilaya zaidi ya 10 zikiwamo Mpwawa, Kondoa, Ilala, Kibaha,

Singida vijijini, Lindi, Simanjiro, Kiteto, Temeke na Kinondoni na katika wilaya ambazo zimewezeshwa

kuwa na timu ya SAM, ufuatiliaji na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma za afya umeongezeka,

ikiwamo uboreshaji wa miundombinu katika vituo vya huduma za afya na vilevile katika kupanga bajeti

yenye kufuata vipaumbele sambamba na matumizi yenye tija.

Katika utekelezaji wa zoezi la SAM wilayani Kilolo uliofanyika mnamo 05/08/2016 hadi 26/08/2016,

Sikika ilipitia hatua kuu tisa (9) za utekelezaji ambazo ni (1) Kupanga na kuandaa utekelezaji wa SAM

(2) Uchaguzi wa wajumbe wa Timu ya SAM (3) Kufanya mikutano na wadau wakuu likiwamo baraza

la madiwani (4) Kufanya mafunzo ya SAM kwa timu ya SAM ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu kuhusu

uchambuzi wa nyaraka mbali mbali za mipango na bajeti (5) Kutembelea maeneo ya utekeleza wa

miradi/mipango (6) Kuwasilisha matokeo ya awali kwa CHMT na kujadiliana (7) Kuendesha Mkutano

wa pili wa wadau (kuwasilisha taarifa kwa wadau) na (8) Kuandaa mpango wa ufuatiliaji.

Zoezi la SAM lilibaini kuwa hatua zote tano za uandaaji na utekelezaji wa mipango na bajeti ya afya

ya halmashauri ya wilaya ya Kilolo zilikidhi vigezo vyote muhimu. Hata hivyo kulikuwa na mapungufu

kwenye upatikanaji wa nyaraka sahihi zilizoidhinishwa na wilaya baada ya taarifa kutofautiana kati ya

zile za Timu ya SAM na zilizokuwapo halmashauri. Hii ni kutokana na halmashauri kuwa na nyaraka

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

v

nyingi zilizofanyiwa marekebisho.

Katika zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa bajeti na mpango kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya,

timu ilibaini baadhi ya mapungufu ikiwamo, (1) Kutokukamilika kwa miradi ya ujenzi wa vituo, maabara,

jengo la upasuaji na wodi kwa wakati (2) Kupokelewa kwa dawa toka MSD zinazokaribia kumalizika

muda wake (3) Suala la mipaka ya vituo vya kutolea huduma za afya kutotambuliwa na kusababisha

uvamizi wa maeneo hayo (4) Upungufu wa watumishi hasa wa kada za matabibu na waganga wasaid-

izi (5) Vituo kutokuwa na vichomea taka na mashimo bora ya kutupa kondo la uzazi (6) Changamoto

ya Jiografia ya wilaya inayoleta ugumu kwa watumishi kuwasilisha taarifa za vituo za kila mwezi (7)

Changamoto ya upatikanaji wa maji katika vituo.

Kila hoja ilijadiliwa na kuwekewa mikakati ya pamoja ya utekelezaji kwenye kikao cha ndani kati ya timu

ya SAM na timu ya utekelezaji wa shughuli za wilaya (CMT na CHMT). Pia hoja hizi ziliwekwa bayana

katika kikao cha mwisho cha wadau na mikakati iliboreshwa.

Pamoja na mafanikio makubwa ya zoezi, kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo (1) Nyaraka za

uchambuzi kuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo si rafiki kwa baadhi ya wajumbe wa Timu ya SAM

(2) baadhi ya nyaraka za uchambuzi zilichelewa kupatikana (3) Baadhi ya nyaraka za uchambuzi haz-

ikuthibitishwa hivyo kuleta mkanganyiko wakati wa uwasilishaji wa taarifa.

Mwisho timu ya SAM ilitoa mapendekezo ya kuboresha utendaji na utekelezaji wa mipango na bajeti ya

Afya, ikiwamo (1) Kuandaa nyaraka zote kwa lugha ya Kiswahili ili ziwe rafiki kwa wananchi (2) Kuon-

doa nyaraka zote ambazo hazitumiki (zisizo thibitishwa) (3) Kuboresha mfumo wa kuandaa taarifa za

fedha ili kuleta ulinganifu wa taarifa za vyanzo mbalimbali vya fedha mfano Mfuko wa Afya wa Jamii

(CHF) na papo kwa papo (4) Kuboresha uandaaji wa bajeti na taarifa za utekelezaji kwa kuonyesha

kila shughuli iliyopangwa na kutekelezwa pasipo kuunganisha shughuli zaidi ya moja katika taarifa (5)

Timu ilipendekeza halmashauri kuwa na mipango ya kutatua changamoto zilizojitokeza katika vituo

kama upatikanaji wa maji, dawa zilizokaribia kumalizika, suala la watumishi, ujenzi wa vichomea taka

na ukamilishaji wa miradi mbalimbali.

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

1

Sehemu ya Kwanza 1.0 UtanguliziMchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii ulikusudia kuiwezesha Halmashauri ya Kilolo kubore-

sha utoaji wa huduma za kijamii, hususani huduma za afya ili wananchi wanufaike na huduma hizo

kama haki zao za msingi. Sikika iliiwezesha Timu ya SAM kufanya ufuatiliaji kwa kufuata miongozo

sahihi ya sheria za nchi na mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhia. Sheria na mikataba hiyo

ni pamoja na; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara za (11), (12), (14) – (28),

Mkataba wa Banjul (Afrika) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni un-

aofahamika kwa lugha ya Kiingereza kama “International Covenant for Economical, Social and Cultural

Rights (ICESCR, 1976)”, ambayo yote imejikita katika kuhakikisha uwajibikaji katika kufikia upatikanaji

na utoaji wa haki za binadamu na mahitaji ya msingi ya jamii.

1.1 Lengo la Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa JamiiLengo la Mchakato wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii “Social Accountability Monitoring - SAM” ni

kuijengea uwezo jamii kufanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali pamoja na kufuatilia utekelezaji wa

mipango na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali. SAM pia inalenga kuiwezesha jamii kuhoji

uwajibikaji wa wasimamizi na watoa huduma za umma ili waweze kutoa huduma zinazokidhi mahitaji

muhimu na ya msingi kwa jamii kama vile afya, elimu, maji, chakula na makazi.

1.2 Uchaguzi wa Wajumbe wa Timu ya SAMUtekelezaji wa mchakato wa SAM katika Halmashauri ya Kilolo ulifuata hatua mbalimbali. Hatua za

mwanzo kabisa zilikuwa kutoa ufafanuzi kwa viongozi wa Halmashauri, madiwani pamoja na wadau

wengine wa afya juu ya dhana ya uwajibikaji jamii. Hatua hii pia ilihusisha uchaguzi wa washiriki wa

timu ya SAM uliofanywa kupitia mikutano mbalimbali.

Mikutano ya awali ni ile ya wananchi katika kata, ambapo ililenga kutoa elimu kwa wananchi juu ya

SAM na kisha kupata uwakilishi kutoka pande mbalimbali za Halmashauri ya Kilolo. Katika mikutano

hii walipatikana wawakilishi wa wananchi wanne (4).

Mkutano wa pili ni ule wa Baraza la Madiwani, ambao ulichagua wajumbe wawili kwa ajili ya timu ya

SAM. Mbali na kupata wawakilishi kutoka katika kundi la waheshimiwa madiwani, mkutano huu wa

Baraza la Madiwani ulilenga kutoa elimu ya SAM kwa waheshimiwa madiwani ili waweze kuitumia

katika mchakato wa mipango na bajeti katika ngazi ya halmashauri pamoja na kusimamia uwajibikaji

wa watoa huduma.

Mkutano wa tatu ulifanyika katika ngazi ya Halmashauri ambao ulijumuisha viongozi na watendaji

wakuu wa Halmashauri wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Katibu Tawala, Timu ya Uendeshaji wa

Shughuli za Afya za Halmashauri (CHMT), Watoa Huduma za Afya Vituoni, Watendaji wa Kata, Bodi

na Kamati za Afya, wawakilishi wa wananchi (wananchi waliochaguliwa kutoka katika Kata), wawakil-

ishi wa wananchi Waishio na Virusi vya UKIMWI (WAVIU), wawakilishi wa Asasi za Kiraia pamoja na

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

2

viongozi wa dini). Katika mkutano huu wawakilishi wengine wa timu ya SAM walichaguliwa kuwakilisha

makundi mbalimbali ya wadau wa afya na kufanya jumla ya wajumbe wa timu ya SAM kuwa 15. Hivyo,

timu ya SAM ya Halmashauri ya Kilolo iliundwa na wawakilishi kutoka katika makundi ya Wananchi,

Madiwani, CHMT, Bodi na Kamati za Afya pamoja na Watendaji wa Kata.

Aidha, ripoti hii inafafanua kwa kina hatua ambazo mchakato wa SAM umepitia tangu kuanza rasmi

kwa zoezi tarehe 05/08/2016 hadi tarehe 26/08/2016 katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, na hivyo

kutoa fursa kwa shughuli za ufuatiliaji wa matokeo na utekelezwaji wa maazimio ya pamoja katika

mkutano wa wadau na Timu.

1.3 Mafunzo ya Utekelezaji wa SAMMafunzo yalianza mara baada ya mkutano wa tatu kuisha kwa wawezeshaji kutoka Sikika kutoa ufa-

fanuzi wa kina kuhusu SAM, sambamba na kuijengea uwezo Timu ya SAM ya Halmashauri kwa kuipa

mafunzo maalum yaliyojikita katika nguzo kuu tano za mchakato wa SAM ambazo ni Mipango na

Mgawanyo wa Rasilimali, Usimamizi wa Matumizi, Usimamizi wa Utendaji, Usimamizi wa Uadilifu, na

Usimamizi wa Uwajibikaji.

Baada ya mafunzo, timu ilichambua taarifa mbalimbali za Halmashauri na baadaye kufanya uhakiki

kwa kutembelea vituo vya huduma za afya ili kupata ufafanuzi, lengo likiwa ni kujiridhisha iwapo yali-

yomo kwenye ripoti yanaendana na hali halisi vituoni.

1.4 Uchambuzi wa NyarakaTimu ilichambua nyaraka mbalimbali zikiwemo Mpango Mkakati wa Halmashauri (2012/2013-

2016/2017), Mpango Kabambe wa Afya wa Halmashauri (CCHP) 2014/2015, Ripoti za utekelezaji za

CCHP kwa kila robo 2014/2015, Mpango wa Muda wa Kati wa Matumizi ya Serikali kwa Kiingereza

‘Medium- Term Expenditure Framework’ (MTEF) 2014/2015-2018/2019, mihutasari ya taarifa za vikao

vya Baraza la Madiwani 2014/2015, Ripoti za Ukaguzi za Mkaguzi wa Ndani 2014/2015, Ripoti ya

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2014/2015. Taarifa zote hizi zilisaidia kuijenga timu kwa

kila hatua ya mchakato wa SAM. Timu ilitakiwa kupitia taarifa ambazo zinaendana na hatua husika

ili kupata mtiririko mzuri wa mchakato mzima wa SAM. Na mwisho, timu iliandaa taarifa kwa kufuata

mtiririko wa hatua tano za mzunguko wa SAM kama ilivyoainishwa katika sehemu ya pili ya ripoti.

1.5 Njia Zilizotumika Kupata UfafanuziMara baada ya mafunzo na uchambuzi wa nyaraka, timu ya SAM iliandaa dodoso lenye hoja zilizoto-

kana na uchambuzi wa nyaraka ili kwenda kuhakiki katika vituo vya huduma za afya. Jumla ya vituo 12

vilitembelewa na timu kwa uhakiki na kupata ufafanuzi wa taarifa zilizopatikana katika uchambuzi wa

nyaraka. Baada ya kumaliza ziara vituoni, timu iliandaa taarifa yenye hoja za vituo pamoja na ucham-

buzi wa nyaraka na kuipeleka katika Ofisi ya Mkurugenzi ili kupata ufafanuzi wa maandishi. Baada ya

Halmashauri kutoa ufafanuzi wa hoja hizo, timu ilikutana na CHMT katika mkutano wa ndani ili kutoa

taarifa ya zoezi la SAM pamoja na kupata ufafanuzi wa kina wa taarifa zilizochambuliwa kutoka katika

nyaraka, pamoja na taarifa ya ziara katika vituo vya huduma za afya.

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

3

1.6 Taarifa ya Zoezi la SAM kwa Wadau wa AfyaBaada ya Timu ya SAM kupata ufafanuzi kutoka CHMT wa mambo yaliyoibuliwa katika uchambuzi wa

nyaraka pamoja na ziara za vituo vya huduma za afya, ilikutana na wadau wa afya wa Halmashauri ili

kutoa mrejesho wa zoezi zima la SAM. Mkutano ulijumuisha Watendaji wakuu wa Halmashauri wakiwamo

Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala, Madiwani, CHMT, Watendaji wa Kata, wawakilishi wa Bodi na Kamati za

Afya, wawakilishi wa wananchi (wananchi wa kawaida, WAVIU, asasi za kiraia pamoja na viongozi dini).

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

4

Matokeo ya Uchambuzi wa Nyaraka Mbalimbali

2.0 UtanguliziSehemu hii imejadili kwa undani uchambuzi wa nyaraka mbalimbali zilizotumika katika mafunzo kwa

timu ya SAM ya Halmashauri. Zaidi ya hayo, sehemu hii imejumuisha hoja zilizoibuliwa wakati wa

uchambuzi wa nyaraka na hali halisi iliyoonekana katika vituo vya huduma za afya pamoja na ufafanu-

zi uliotolewa na Timu ya Uendeshaji wa Shughuli za Afya ya Halmashauri juu ya hoja hizo. Mtiririko

wa hoja na ufafanuzi umegawanywa katika hatua tano za SAM kama ilivyoainishwa katika vipengele

vinavyofuata.

Sikika iliratibu uundwaji wa timu ambao ulifanywa na makundi husika. Katika hatua hii wananchi wali-

pata fursa ya kuielewa Sikika, kufahamu maana na lengo la SAM, manufaa yake kwa ustawi wa jamii

na kukubali kushiriki katika utekelezaji wa zoezi zima.

2.1 Mikutano ya Wadau (Baraza la Madiwani na Wadau wa Afya)Baraza la Madiwani ndicho chombo kikuu cha ushauri na maamuzi kwa Halmashauri, hivyo Sikika ilifa-

nya mkutano na Madiwani katika kutambua umuhimu huo. Aidha, katika kikao hicho Madiwani walipata

fursa ya kuifahamu Sikika na kujadili kwa kina kuhusu zoezi la SAM. Vilevile, Baraza lilitoa baraka zao

kuwa zoezi lifanyike na kuchagua wawakilishi wawili miongoni mwa Madiwani waliojumuika kuunda

timu ya SAM.

Mchakato wa SAM uliendelea pia kwa kufanyika mkutano wa wadau wa Afya ambao ulihusisha

wananchi, watendaji wa Halmashauri, Madiwani, Waganga Wafawidhi pamoja na Wenyeviti wa Kamati

za Usimamizi wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya. Wadau walipata fursa ya kujadili kwa kina zoezi

la SAM na kuitambulisha timu rasmi tayari kwa kuanza mafunzo.

Sehemu ya Pili

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

5

2.2 Mafunzo na Uchambuzi wa Taarifa za HalmashauriTimu ilipata mafunzo na uchambuzi wa taarifa katika maeneo yafuatayo; Mipango na Mgawanyo wa

Rasilimali, Usimamizi wa Matumizi, Usimamizi wa Utendaji, Usimamizi wa Uadilifu na Usimamizi wa

Uwajibikaji. Pia, timu iliweza kupatiwa mafunzo ya kina kuhusu dhana ya Uwajibikaji katika Mtazamo

wa Haki za Msingi za Binadamu hususan haki ya kupata afya. Mafunzo haya yaliiwezesha timu kupata

maarifa na ujuzi wa kuchambua taarifa mbalimbali kwa umakini mkubwa na hivyo kuweza kuainisha

hoja kutokana na taarifa hizo.

2.3 Ziara ya Uhakiki VituoniMara baada ya kuainisha hoja zilizopatikana katika uchambuzi wa nyaraka, timu ilitembelea vituo vya

kutolea huduma ya afya ili kuhakiki iwapo

taarifa za ripoti zinaendana na hali halisi

katika vituo. Kwa sababu ya vituo kuwa

vingi, ziara za uhakiki zilifanyika kwa siku

mbili; Tarehe 21/08/2016 timu ilitembelea

vituo vifuatavyo: Kidabaga, Kimala, Itonya,

Idete, Idegenda, Masisiwe, Ikula, Nyanz-

wa, Irole, Ibumu, Lyasa Image, Mtandika,

Udekwa, Lugalo, Kipaduka na Mlafu. Zoe-

zi lilimalizika 22/08/2016 kwa kutembelea

vituo vya kutolea huduma za afya vya Uk-

wega, Kising’a, Utengule, Itimbo na Kilolo.

Baadhi ya wajumbe wa timu ya SAM wakifanya uchambuzi wa nyaraka mbalimbali za halmashauri.

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

6

2.4 Kuwasilisha Matokeo ya Awali kwa Halmashauri na Idara ya AfyaBaada ya zoezi la uhakiki vituoni kukamilika, timu ilipata fursa ya kukutana na watendaji wa Hal-

mashauri hususani timu ya menejimenti (CMT) na timu ya afya (CHMT) ili kujadili hoja zilizotokana

na uchambuzi wa nyaraka pamoja na uhakiki vituoni. Mara baada ya majadiliano ya kina kati ya timu

pamoja na wajumbe wa CMT & CHMT maazimio ya pamoja juu ya utekelezaji wa maeneo yaliyojadil-

iwa yaliainishwa.

2.5 Hoja zitokanazo na uchambuzi wa nyaraka na maazimio ya CMT & CHMT

2.5.1 Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali

2.5.1.1 Hoja ya Timu: Muhtasari – Uchambuzi wa Mpango Kabambe wa Afya (CCHP) Uk. VIII na Ripoti ya Utekelezaji Robo mwaka ya kwanza -Uk.1Uchambuzi wa CCHPya mwaka 2014/2015 Uk.VIII, umeonesha salio ishia la mwaka 2013/2014 kwa

mwezi Machi (TSh. Milioni 219,837,768.16) haliendani na salio anzia katika ripoti ya utekelezaji ya

Robo ya I Uk 1 mwaka 2014/2015 (TSh. Milioni 249,289,408.40). Hivyo, timu iliomba ufafanuzi kujua

kiasi halisi cha salio anzia kwa mwaka 2014/2015.

Majibu ya MenejimentiNi vema ikafahamika kuwa mpango uliandaliwa na kuwasilishwa kabla robo ya mwisho haijafungwa

hivyo kusababisha kutumia takwimu za robo ya tatu. Kwa mujibu wa muongozo wa uandaaji wa Mpan-

go Kabambe wa Afya, mpango huandaliwa kwa kutumia taarifa za matumizi mpaka mwezi Machi, hivyo

utofauti unaoonekana unatokana na taarifa kuishia Machi. Hivyo ni wazi kuwa salio anzia 2014/2015

litaonekana bayana katika taarifa ya robo ya mwisho ya 2013/2014.

Pia ifahamike kuwa, salio ishia la mwezi Machi linaandikwa ili Serikali iweze kujua ni kiasi gani cha

fedha kimetumika hadi robo ya tatu katika fedha zilizokwisha tolewa tangu robo ya kwanza.

Maoni ya TimuPamoja na timu kuridhishwa na majibu ya menejimenti itafuatilia taarifa sahihi ili kuthibitisha ulinganifu

wa salio ishia 2013/2014 na salio anzia 2014/2015.

2.5.1.2 Hoja ya Timu – CCHP Uk. Xna Ripoti ya Utekelezaji robo ya 4 Uk. 22Uchambuzi wa timu ulionesha kuwa kiasi kilichoidhinishwa katika Mpango Kabambe cha Tsh. Bilioni

3,066, 340, 400.00 hakifanani na jumla ya kiasi kilichoidhinishwa kwa kila robo ya ripoti za utekelezaji

– Majumuisho ya Robo ya 4 Uk. 22 yanaonesha kiasi chaTsh. Bilioni 2,968,286,199.00. Timu iliomba

ufafanuzi kuhusu utofauti huo.

Majibu ya MenejimentiChangamoto hii hutokana na kubadilika mara kwa mara kwa ukomo wa bajeti wakati wa kuaandaa

mipango, hivyo huweza kusababisha kuwepo kwa tofauti. Hata hivyo, tunaichukua hoja kama changa-

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

7

moto ili kufanya maboresho huko mbeleni.

Maoni ya TimuTimu iliridhishwa na ufafanuzi wa menejimenti hasa kupokea hoja na kukubali kuifanyia maboresho

katika utekelezaji wa mipango ya sasa na ijayo. Timu itaendelea kushirikiana na menejimenti kufuatilia

utekelezaji wake.

2.5.2 Usimamizi wa Matumizi2.5.2.1 Hoja ya Timu – Ripoti ya Utekelezaji Robo ya 1-4 Uk. 1 Katika uchambuzi wa jumla kuu ya matumizi kwa ripoti za kila robo, timu ilibaini kuwa salio ishia

(bakaa) la robo ya pili (2) TSh. 235,091,352.40 Uk. 1 haliendani na salio anzia la robo ya tatu (3)

TSh. 231,478,852.40 Uk. 1. Takwimu hizo zimejirudia katika robo ya tatu ambapo salio ishia TSh.

318,238,412.40 Uk. 1 halikulingana na salio anzia katika robo ya nne (4) TSh. 266,031,431.40 Uk 1.

Timu iliomba ufafanuzi juu ya utofauti huo.

Majibu ya MenejimentiMenejimenti ilikiri uwepo wa utofauti wa takwimu katika nyaraka ilizotoa na kutumiwa na timu, hata

hivyo vithibitisho vinavyoonesha marekebisho yaliyofanyika baada ya nyaraka za utekelezaji kufika

mkoani vilikuwapo. ‘Tunapenda kuwafahamisha timu kuhusu hili na tunaomba ziingizwe takwimu hizi

kwa usahihi’.

‘Aidha, ni rai kwetu sasa kama CHMT kuwa tunapaswa kuondoa nyaraka hizo katika matumizi na

kubakiwa na ambazo ni sahihi ili kuondoa mkanganyiko kwa watumiaji wa nje na hata sisi wenyewe’

alimalizia kusema Katibu wa Afya Wilaya Bi. Helen Chisanga.

Maoni ya TimuTimu imeridhishwa na ufafanuzi pamoja na uthibitisho wa menejimenti. Aidha inawapongeza CHMT

kwa kuchukua hatua za kukubali kuondoa nyaraka zote zinazoleta mkanganyiko.

2.5.2.2 Hoja ya Timu – Ripoti ya Utekelezaji Robo ya 2 na 3 Uk. 15 na 16 Shughuli Na. C02S04

Uchambuzi umeonesha kuwa shughuli ya kufanya vikao vya Bodi ya Afya ya Wilaya kila robo ya

pili ifikapo Juni 2015 ilitumia Tsh. 2,142,000/= Uk.16 kwa asilimia 100 kinyume na matumizi ya Tsh.

5,200,000/= katika robo ya 3 Uk. 15 kwa asilimia hiyo hiyo 100. Timu ilipenda kufahamu kwanini kuna

tofauti ya gharama kwa zaidi ya mara mbili?

Majibu ya MenejimentiKatika robo ya 3, kikao cha bodi kilihusisha pia ziara ya wajumbe kutembelea vituo vya huduma ku-

toa ushauri elekezi. Hivyo kusababisha gharama ya kikao katika robo ya 3 kuwa kubwa mara mbili

ya gharama iliyotumika robo ya 2. Ili kuondoa shaka katika taarifa CHMT imeridhia kuwa siku zijazo

itatenganisha shughuli mbili tofauti zinapofanyika kwa wakati mmoja.

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

8

Maoni ya TimuTimu inashauri shughuli za aina hiyo pia zionekane katika mpango pamoja na ripoti za utekelezaji ili

kuonesha uwazi na mtiririko mzuri.

2.5.2.3 Hoja ya Timu – Ripoti ya Utekelezaji (RU) Robo ya 1-4 Uk. 12,15&16 Shughuli Na. C02S02Uchambuzi wa shughuli ya uwasilishaji wa taarifa katika ofisi ya Mganga Mkuu (W) kutoka katika vituo

55 vya huduma za Afya ifikapo Juni 2015 ulibainisha kuwa kiasi cha fedha kilichopokelewa katika robo

ya 3 ni Tsh. 2,500,000.00 (RU Uk 15), ambapo matumizi ni Tsh.2,764,000.00 na kusababisha ziada ya

matumizi ya takribani Tsh. 264,000.00.

Vile vile timu ilibaini kuwa katika robo ya 4 ilipokelewa Tsh. 2,632,000.00 (RU: Uk 16), ambapo ilitumika

Tsh. 2,600,000.00, lakini kwenye safu ya bakaa inaonesha Tsh. 2,268,000.00. Timu iliomba ufafanuzi

wa kiasi kilichozidi katika matumizi na chanzo chake.

Majibu ya MenejimentiKumekuwa na changamoto ya fedha za ‘Basket Fund’ kuchelewa kuingia Halmashauri hivyo kusa-

babisha ucheleweshaji wa malipo. Athari hiyo husababisha kutokea kwa ziada katika malipo ambayo

hutokana na fedha kuingia katikati ya robo ya utekelezaji na hivyo madai yote kulipwa kwa mkupuo.

Maoni ya TimuTimu ilitaka kuthibitisha juu ya kiasi kilichoingizwa katika kipindi hicho na pia kama watoa huduma

wanapatiwa hizo fedha.

2.5.2.4 Hoja ya Timu – Ripoti ya Utekelezaji Robo ya 2-4 Uk.15 & 16 Shughuli Na. C03C07Uchambuzi wa timu ulibaini kuwa shughuli ya watumishi wa afya kutoa huduma za dharura kwa wag-

onjwa baada ya saa za kazi kila mwezi ifikapo Juni 2015 ilitakiwa itekelezwe kwa robo zote nne lakini

imetekelezwa robo ya 1, 2 na kubaki Tsh. 1,204,000.00. Katika robo ya 3 (RU – Uk. 15) imeonesha

imepokea Tsh. 8,000,000.00 na imetumia Tsh. 4,000,000.00 na bakaa inaonesha Tsh. 5,204,000.00.

Katika robo ya 4 ilipokelewa TSh. 4,630,000.00 bila kutumika na kuwa na bakaa ya 7,434,000.00.

Timu iliomba kupata ufafanuzi juu ya utofauti wa bakaa, na je, katika robo ya nne watumishi hawakutoa

huduma za dharura kwa wagonjwa?

Majibu ya MenejimentiShughuli za dharura kwa wagonjwa hutolewa wakati wote. Changamoto hiyo ilitokana na fedha

kuchelewa ambapo ziliingia mara moja kwa robo mbili kitu ambacho kilisababisha malimbikizo ya mal-

ipo na malipo ya mkupuo. Aidha, utofauti wa nyaraka zilizotumika kufanya uchambuzi pia umepelekea

kuwapo kwa utofauti wa bakaa.

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

9

Maoni ya TimuTimu iliridhishwa na uthibitisho wa nyaraka halisi lakini inaendelea kusisitiza umakini uzingatiwe zaidi

katika matumizi ya nyaraka za umma ili kuondoa mkanganyiko katika taarifa.

2.5.3 Usimamizi wa Utendaji2.5.3.1 Hoja ya Timu – Ripoti ya Utekelezaji Robo ya 1-3 Uk. 8 Shughuli Na. C05C03Uchambuziwa timu ulibaini kuwa shughuli ya ufuatiliaji wa vifo vitokanavyo na uzazi ifikapo June 2015

haikutekelezwa kwa robo zote 4 pamoja na kuwa ufuatiliaji huu ni muhimu katika kupunguza vifo vito-

kanavyo na uzazi. Timu ilipenda kupata ufafanuzi kwa nini shughuli hii haikutekelezwa na kama kuna

mikakati/hatua zilizochukuliwa.

Majibu ya MenejimentiNi vema ikafahamika kuwa shughuli ilifanyika na inaendelea kufanyika, japokuwa fedha hazikuingia.

Uthibitisho wa utekelezaji unapatikana katika taarifa za utekelezaji wa huduma ya afya ya uzazi na

mtoto.

Maoni ya TimuTimu inashauri kuwa Halmashauri ibadilishe chanzo cha fedha za shughuli hii ili kuwe na uhakika wa

upatikanaji wake kuepuka kuathiri shughuli nyingine kwani chanzo cha sasa cha Other Charges (OC)

kinaruhusu kubadilisha matumizi tofauti na chanzo cha Health Basket Fund.

2.5.3.2 Mfumo wa Vichomeo Taka Uhakiki vituoni ulionesha kuwa vituo vingi kati ya vilivyotembelewa havikuwa na mfumo wa vichomeo

taka na uhifadhi wa kondo la nyuma la uzazi. Timu iliomba ufafanuzi kujua mpango wa ujenzi wa vi-

chomea taka na shimo la kondo la nyuma la uzazi vyenye uwezo wa kuteketeza taka hatarishi katika

vituo vya kutolea huduma za afya.

Majibu ya MenejimentiMapendekezo yatawasilishwa kupitia mradi wa WARIDI ili kuboresha eneo hili. Aidha, watashirikiana

na Serikali za Vijiji kuhakikisha eneo hili linaboreshwa.

2.5.3.3 Miradi ya Afya Kutokamilika kwa WakatiUhakiki wa timu ulibaini hali ya kutokukamilika kwa wakati miradi mingi ya afya hivyo kuhoji juu ya

jitihada za makusudi zinazofanywa ili kukamilisha umaliziaji wa miradi ya afya. Kwa mfano wodi ya

akina mama katika zahanati ya Ikula, jengo la Zahanati ya Kipaduka na Lugalo kwa manufaa ya jamii.

Baadhi ya vituo vilivyotembelewa na timu havikuwa na mfumo wa maji safi, hili lilipelekea timu kuomba

ufafanuzi juu ya jitihada za kusogeza huduma ya maji kwenye zahanati ikiwa ni pamoja na kuweka

matanki ya kuvuna maji ya mvua.

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

10

Majibu ya MenejimentiSuala hili limezingatiwa katika bajeti ya 2016/2017, hata hivyo bajeti imekuwa ikitengwa bila mafanikio

kutokana na fedha ndogo zinazopokelewa. Uhalisia huo umetokana na mwitikio mkubwa wa wananchi

kwa sera kwani nguvu za wananchi zimekuwa mbele ya kasi ya Serikali. Kwa upande mwingine Hal-

mashauri inaandika maandiko ya miradi kwa wafadhili ili kupata msaada. Pia tunashauri mabadiliko ya

sera na miongozo ya uchangiaji wa miradi ya afya ili kuwawezesha wananchi kukamilisha miradi yao

pasipo kutegemea misaada ya wafadhili na Serikali tofauti na ilivyo sasa wananchi wanapaswa kuanza

jengo na ukamilishaji ni juu ya Serikali.

Aidha, kupitia mradi wa WARIDI, Halmashauri inategemea kuweka mpango wa kuboresha huduma za

maji katika zahanati zenye shida ya maji. Mradi unategemewa kuanza mwezi Septemba 2016.

2.5.3.4 Dawa Kupokelewa Vituoni Zikiwa Zinakaribia Kuisha Muda wa MatumiziTimu ilibaini baadhi ya dawa kutoka MSD zilipokelewa wakati muda wa matumizi ukikaribia kumalizika,

ambapo baadhi zikiwa na muda usiozidi mwezi mmoja. Timu ilipenda kupata ufafanuzi ni kwa jinsi gani

Halmashauri inahimiza na kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mara kwa mara vituoni ili kuondoa tatizo la

kupokelewa kwa dawa zinazokaribia kuisha muda wa matumizi toka MSD.

Majibu ya MenejimentiMaelekezo yametolewa kwa watoa huduma kufanya ukaguzi wa dawa wakati wa mapokezi ili kubaini

kama zinazokaribia kuisha muda. Pia kwa vituo vyenye dawa hizo vitatembelewa ili zipelekwe vituo

vingine vinavyohitaji au kurudishwa MSD.

2.5.3.5 Jamii Kuingilia Maeneo ya Vituo vya Kutolea Huduma za AfyaChangamoto ya mipaka ya maeneo ya vituo vya kutolea huduma ilidhihirika wakati wa uhakiki kwani

wananchi na watoa huduma walibainisha namna jamii ilivyo athiri shughuli za afya kwa kuingilia mip-

aka ya vituo kwa shughuli binafsi. Mifano ya vituo vilivyokuwa na changamoto hiyo ni pamoja na Za-

hanati ya Kilolo. Timu ilipenda kufahamu mipango na mikakati ya Halmashauri kuhusu kuwekamipaka

katika zahanati zote na vituo vya afya ili kuepusha migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.

Majibu ya MenejimentiKupitia mpango wa afya wa mwaka huu 2016/2017 zahanati 4, zitapimwa na kuwekwa bikoni. Pia

Halmashauri inasisitiza uwekaji wa mipaka ya asili uzingatiwe na tunaiomba timu ya SAM itusaidie

kuhimiza hilo pia.

2.5.3.6 Upungufu wa WatumishiUpungufu wa watumishi wa afya ni miongoni mwa masuala makubwa yaliyobainika vituoni hasa kwa

kada ya maafisa tabibu na waganga wasaidizi. Timu iliomba ufafanuzi kujua mikakati madhubuti ya

ndani kutatua tatizo hilo.

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

11

Majibu ya MenejimentiHalmashauri imekuwa ikiomba kibali cha kuajiri kulingana na upungufu uliopo, hata hivyo serikali kuu

imekuwa ikitoa kibali cha kuajiri watumishi wachache. Hata hivyo kwa mwaka huu 2016/17 hatujaajiri

kutokana na agizo la Serikali la kusitisha ajira kwa muda. Halmashauri itaendelea kufuatilia.

2.5.3.7 Watu Wenye Mahitaji MaalamuKatika uchambuzi wa mipango, kipaumbele cha masuala ya walemavu wa ngozi kama ilivyo kwa makundi mengine mfano WAVIU hakikupata akisi sawia katika uhalisia kutokana na kutokuwapo hudu-ma maalumu angalau katika kituo cha afya. Timu ilihitaji kujua mipango ya Halmashauri katika eneo hilo.Majibu ya MenejimentiMpango wa afya kwa mwaka 2016/2017 umezingatia makundi yote katika jamii.

2.5.3.8 Uwepo na Utendajikazi wa Kamati za Afya za VituoKatika kila kituo kilichotembelewa, timu ilihoji juu ya uwepo na utendaji kazi wa kamati za usimamizi

wa vituo. Vituo vyote isipokuwa zahanati ya Ibumu hakukuwa na kamati ya usimamizi ya kituo. Timu

ilipenda kujua Halmashauri ina mkakati gani kuhakikisha kamati inaundwa na kuanza kufanya kazi kwa

mujibu wa miongozo.

Majibu ya MenejimentiKamati itaundwa baada ya kuundwa kwa Bodi ya Afya ya Wilaya, ambapo mchakato wa uundwaji wake

upo katika hatua za mwisho.

2.5.3.9 Bajeti kwa ajili ya Usafi wa Vituo vya Kutolea HudumaPamoja na timu kuipongeza Halmashauri na watumishi wa afya kwa jitahada za kufanya usafi. Timu

ilihoji juu ya kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya kugharamia huduma za usafi katika zahanati ili kuwa-

punguzia mzigo mkubwa watoa huduma za afya ambao pamoja na shughuli za kitabibu kuwa nyingi

kutokana na uchache wao wanalazimika pia kufanya usafi wa kituo.

Majibu ya MenejimentiItahakikisha wanajamii wanashiriki katika kutunza na kufanya usafi katika mazingira ya vituo vya hudu-

ma za afya. Mkurugenzi atawaandikia watendaji wa Kata ili kulisimamia hili.

2.5.3.10 Changamoto ya Jiografia ya WilayaTimu iliona changamoto ya kijiografia hasa mtawanyiko wa maeneo ya wilaya. Kutoka eneo moja la

kituo kumekuwa na mzunguko mkubwa unaopelekea vituo kuwa katika mazingira magumu kufikika.

Hali hii ilipelekea timu kuomba ufafanuzi wa jitihada za Halmashauri kutatua changamoto hiyo.

Majibu ya MenejimentiHalmashauri imepanga kununua pikipiki 5 katika mwaka huu wa fedha 2016/2017 kupitia Mfuko wa

Afya wa pamoja (Basket Fund). Kwa kuanzia vituo vitakavyonufaika ni Ilambo, Idegenda, Ikula, Kimala

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

12

na Itonya.

2.5.4 Usimamizi wa Uwajibikaji2.5.4.1 Mkanganyiko wa Taarifa za Baraza la MadiwaniUchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa na Kamati ya Elimu, Afya na Maji (Uk. 2 katika taarifa ya Kamati)

katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani 23/12/2014, ilionekana taarifa ya utekelezaji wa

shughuli kwa kipindi cha Julai, Agosti na Septemba pekee lakini haikuonekana ya Oktoba na Novem-

ba. Timu iliomba kufahamu ni kwa nini taarifa za Oktoba na Novemba hazikuwasilishwa katika kikao

cha 23/12/2014.

Majibu ya MenejimentiTaarifa husika hazikuweza kuoneka kutokana na vikao vya Baraza la Madiwani kufanyika kabla ya

kukamilika kwa robo. Hata hivyo utaratibu umerekebishwa ambapo vikao vitakuwa vinafanyika baada

ya kukamilika kwa robo ya 4 na hivyo taarifa zote husika zitaonekana.

Maoni ya TimuTimu iliridhishwa na kuipongeza menejimenti kwa kufanya maboresho hayo, aidha itaendelea kufanya

ufuatiliaji ili kuhakikisha uendelevu wa mabadiliko hayo.

2.5.4.2 Upungufu wa Taarifa za Kina Uchambuzi wa Timu ulibaini kuwa taarifa ya Baraza la Madiwani katika jedwali la yaliyomo (Uk. 1-42) imeainishwa mada pamoja na ukurasa lakini uchambuzi umeonesha hakukuwa na uwiano sawia kati ya jedwali la yaliyomo na kurasa za ripoti ya Baraza la Madiwani. Timu iliomba kupata ufafanuzi kuhusu mkanganyiko wa uandaaji wa taarifa hizo.

Timu ilibaini kuwa kumekuwa na mkanganyiko wa upangaji wa ripoti za kamati mfano, taarifa ya Kamati ya Fedha, Mpango na Utawala imeanza Novemba 2014 ikafuatia Oktoba hivyo kutokuwa rafiki kwa mtumiaji. Timu ilishauri uandaaji wa taarifa uboreshwe ili ziwe rafiki kwa watumiaji. Vile vile, timu ilibaini kuwapo kwa ushauri na mapendekezo kutoka kwa madiwani lakini ukosekana kwa mjadala/maoni. Hii inaonekana katika muhtasari wa kikao cha kawaida cha Kamati ya Elimu, Afya na Maji 22/10/2014. Timu iliomba ipatiwe ufafanuzi wa hoja hiyo.

Majibu ya MenejimentiTunakiri kuona hayo mapungufu na tunaahidi kuyafanyia kazi kwa kuyarekebisha katika nyaraka zinazokuja.

Maoni ya TimuTimu iliridhishwa na utayari wa menejimenti kushughulikia mapungufu ya uandishi wa nyaraka muhimu

za vikao vya Baraza la Madiwani.

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

13

Sehemu ya Tatu 3.1 Changamoto Zilizobainika Vituoni3.1.1 Suala la usafi wa vituo na mazingiraTimu iliona usafi wa mazingira ni mzuri na watumishi wanajitahidi sana kufanya usafi. Hata hivyo timu

inapendekeza kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya kugharamia huduma za usafi katika zahanati ili kuwa-

punguzia mzigo mkubwa watoa huduma za afya.

3.1.2 Vichomea taka/ shimo la kutupia kondo la uzaziTimu imebaini kutokuwapo kwa vichomea taka pamoja na shimo la kutupia kondo la uzazi katika za-

hanati nyingi. Mfano, kondo la uzazi kutupwa katika shimo la choo au mashimo ya kawaida kinyume

na maadili yetu. Timu inapendekeza kujengwa vichomea taka vyenye uwezo wa kuteketeza taka na

kondo la uzazi.

3.1.3 Posho za muda wa ziadaTimu imebaini ucheleweshaji wa malipo ya posho za muda wa ziada, hivyo kushusha morali ya watumi-

shi kiutendaji. Timu inapendekeza malipo malipo yafanyike kwa wakati.

3.1.4 Umaliziaji wa miradi ndani ya vituo (Wodi, Maabara, na Jengo la Upasuaji)Timu ibaini miradi ya kuboresha huduma katika zahanati haijakamilika; mfano jengo la wodi ya kinama-

ma zahanati ya Ikula halijakamilika tangu mwaka 2013. Timu inapendekeza jitihada za dhati zifanyike

ili kukamilisha miradi hii kwa manufaa ya jamii ya Kilolo.

3.1.5 Kumaliza ujenzi wa ZahanatiTimu imebaini kuwa zipo Zahanati ambazo ujenzi wake haujakamilika tangu 2012 pamoja na wananchi

kufanya jitihada kubwa; mfano Zahanati za Kipaduka na Lugalo; Timu inashauri halmashauri izipe

kipaumbele Zahanati hizi ili kuwapa wananchi moyo wa kujitolea katika miradi ya maendeleo na pia

kuwasogezea karibu huduma za afya.

3.1.6 Upatikanaji wa MajiZahanati nyingi zinakabiliwa na uhaba wa maji safi hivyo kuwafanya watoa huduma za afya kufuata

huduma ya maji umbali mrefu: Mfano Zahanati ya Itimbo, Kimala. Timu inapendekeza jitihada zifanyike

kusogeza huduma ya maji kwenye Zahanati ikiwa ni pamoja na kuweka matanki ya kuvuna maji ya

mvua.

3.1.7 Usafiri kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya hadi HalmashauriZahanati nyingi zipo mbali na makao makuu ya wilaya, hii inasababisha watoa huduma za afya kutumia

gharama kubwa kuleta taarifa za kila mwezi katika ofisi ya Mganga Mkuu wilayani: mfano Ilambo, Ide-

genda, Ikula, Kimala na Itonya. Timu inapendekeza vituo hivyo vya mbali vipatiwe usafiri wa pikipiki au

timu ya CHMT iweke utararibu wa kufuata taarifa hizo kila mwezi.

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

14

3.1.8 Kupokelewa kwa dawa zinazokaribia kuisha muda wa matumiziImebainika kuwa Zahanati ya Ikula ilipokea dawa za kupunguza makali ya VVU ambazo muda wake

wa matumizi umekaribia kuisha (Septemba 2016), hivyo timu inapendekeza ukaguzi na ufuatiliaji wa

dawa ufanyike wa mara kwa mara vituoni.

3.1.9 Mipaka ya ZahanatiTimu iligundua kuwa zahanati zote zilizotembelewa hazina mipaka iliyo wazi, hivyo timu inapende-

keza Halmashauri iweke mipaka katika zahanati zote na vituo vya afya ili kuepusha migogoro ya ar-

dhi isiyo na ulazima; Mfano zahanati ya Kilolo ambayo imekuwa na changamoto ya wafanyabiashara

kuingilia eneo la Zahanati.

3.1.10 Upungufu wa Watumishi

Zahanati nyingi zinaendeshwa na wauguzi, hivyo timu inapendekeza Halmashauri iwe na mkakati

madhubuti wa kutafuta matabibu na kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma za afya.

3.2 Changamoto katika Utekelezaji wa Zoezi la SAM

3.2.1 Kutopata nyaraka kwa wakati kiasi ambacho nyaraka zingine zilipatikana baadae wakati zoezi likien-delea hivyo kuathiri mwenendo wa utekelezaji wa zoezi kwa wakati.

3.2.2 Nyaraka zote zilikuwa katika lugha ya Kiingereza hivyo hazikuwa rafiki kwa wanatimu ambao wengi wao hawakuwa na ujuzi wa lugha hiyo. Ombi la timu ya SAM ni kuandaa nyaraka kwa lugha ya Kiswahili.

3.2.3 Katika kipindi ambacho zoezi la SAM lilifanyika kulikuwa na baridi sana hivyo kipindi kijacho ni vyema

likafanyika mwezi wa kumi (10) ambapo hali ya hewa ni nzuri na hakuna shughuli za kilimo.

3.2.4 Timu ilipatiwa baadhi ya nyaraka ambazo hazikuwa zimekamilika na kuidhinishwa baada ya mabore-sho hivyo kupelekea mkanganyiko.

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

15

3.3 HitimishoKazi ya ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii iliyotekelezwa na timu ya SAM imeibua hoja mbalimbali

ambazo tunaamini ni chachu ya mabadiliko katika Halmashauri ya Kilolo, hususan Idara ya Afya. Timu

inaamini kuwa, mchakato huu wa SAM una manufaa makubwa kwa jamii na Halmashauri kwa ujumla,

kwani pamoja na kutoa mafunzo maalumu na kuwajengea uwezo wananchi wa kushiriki katika kubore-

sha huduma za afya, bado mchakato huu umeweza kubainisha changamoto zinazoikabili Halmashau-

ri, jambo ambalo ni msaada mkubwa katika kuleta mabadiliko, hususan kwenye Idara ya Afya na utoaji

wa huduma za afya kwa ujumla.

Maazimio na mapendekezo yatatekelezwa kwa kuanzia mara tu baada ya Timu kuwasilisha ripoti

kwa wadau. Yale yanayohitaji kuingizwa katika bajeti yataanza kutekelezwa katika kipindi cha mwaka

2017/2018. Timu ya SAM itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maazimio kwa kushirikiana na

Halmashauri pamoja na shirika la Sikika ambao wataendelea kuwa waratibu wa ufuatiliaji.

Ni imani kubwa ya timu kuwa ili Halmashauri iweze kuwajibika ipasavyo kwa jamii, ni muhimu kwa zoe-

zi hili kufanyika kwa idara zote mara kwa mara. Hivyo basi, kwa imani hiyo, timu inashauri Halmashauri

kushirikiana na Sikika na wadau wengine kuiwezesha timu iwe endelevu na iweze kufuatilia uwajibikaji

kwa jamii katika idara nyingine zote za Halmashauri, lengo likiwa moja tu, kufikia haki za binadamu na

kukidhi mahitaji ya jamii.

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

16

Viambatanisho

Kiambata Na. 1 Mapendekezo

Na Hoja Maazimio1 Changamoto ya

uandaaji wa nyaraka za Halmashauri na Lugha inayotumika

• Halmashauri imeupokea ushauri huo itaanza kuzingatia hilo katika bajeti ijayo ya 2017/2018

• Kuboresha nyaraka za fedha ili kuweka ulinganifu katika mchanganuo wa bajeti

• Idara ya Afya kuondoa nyaraka ambazo hazitumiki katika mzu-nguko wa nyaraka za Halmashauri ili kuondoa mkanganyiko wa taarifa kwa watumiaji.

• Idara ya Afya kutenganisha shughuli mbili au zaidi zinapofanyi-ka kwa wakati mmoja ili kujua gharama halisi kwa kila shughuli husika na hivyo kuondoa mkanganyiko kwa msomaji.

• Ukomo wa Bajeti na mabadiliko ya kibajeti yanayofanyika wakati wa utekelezaji yaingizwe kwenye ripoti za utekelezaji.

• Nyaraka za Baraza la Madiwani ziboreshwe li kuweka mtiririko wa taarifa unaoendana na jedwali la yaliyomo (lenye mada na kurasa husika) na kurasa za ripoti

• Uandaaji wa mihutasari ya Baraza la Madiwani uendane na mzunguko wa vikao vya kila robo mwaka (miezi 3) ili kurahisi-sha rejea kwa watumia taarifa.

• Ushauri na mapendekezo ya Madiwani ni vyema yakaainishwa sambamba na chanzo cha mjadala/maoni ili msomaji afahamu ushauri au mapendekezo yalianzia wapi na yalikuwa na msingi gani

• Halmashauri iweke baya katika mpango na bajeti masuala ya walemavu wa ngozi kama ilivyo kwa makundi mengine kama WAVIU

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

17

2 Baraza la Madiwani kutoka kwa wakati kulingana na mion-gozo na kanuni

• Utaratibu wa vikao umesharekebishwa miezi kadhaa iliyopita kabla ya zoezi la SAM kufanyika hivyo katika nyaraka za mwa-ka huu changamoto hiyo haitajitokeza.

3 Kutenganisha Vy-anzo vya Mapato ya Halmashauri katika nyaraka za Baraza la Madiwani

• Mapato/makusanyo yanayotokana na CHF, papo kwa papo na bima ya afya katika taarifa za Baraza la Madiwani yatolewe taarifa kipekee ndipo jumla itokane na mchanganuo wake.

4 Changamoto ya Ukosefu wa vi-chomea taka na shi-mo la kutupia kondo la uzazi

• Timu ilipendekeza kuwa kuwe na ujenzi wa vichomea taka vyenye uwezo wa mzuri wa kuteketeza taka.

5 Changamoto ya mi-undombinu ya afya, barabara, mfumo wa majina nishati ya umeme.

• Timu ilipendekeza kuwa jitihada ya mahususi zifanyike ili ku-hakikisha ukamalishaji wa miradi ya ujenzi (mfano: Wodi ya kina mama zahanati ya Ikula, jengo la zahanati ya Kipaduka na Lugalo kwa manufaa ya jamii).

• Timu ilishauri jitihada za dhati zifanyike ili kusogeza huduma za maji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Hii ni pamoja na kuweka matanki ya kuvuna maji ya mvua.

• Timu ilijiridhisha juu ya ukubwa wa wilaya na kushauri vituo vyenye mazingira magumu kupatiwa usafiri wa pikipiki, hii ita-rahisisha kutuma taarifa za kila mwezi Halmashauri au timu ya CHMT iweke utaratibu wa kufuata taarifa hizo kila mwezi.

6 Changamoto ya kutofanyika kwa usimamizi elekezi kikamilifu na kwa wakati katika vituo

• Kutekeleza kaguzi elekezi wa mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuondoa tatizo la kupokelewa kwa dawa zinazokaribia/zilizoisha muda wa matumizi toka MSD.

7 Migogoro ya ardhi na maeneo ya vituo ku-ingiliwa na wananchi

• Timu kwa kutambua uwepo wa migogoro ya Ardhi ilipendekeza Halmashauri kuweka Mipaka katika vituo vya kutolea huduma vyote ili kuepusha migogoro ya ardhi isiyo na ulazima.

8 Upungufu wa rasili-mali watu katika afya

• Timu ilipendekeza Halmashauri iwe na mkakati madhubuti wa kutafuta matabibu na kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

18

9 Kamati za usimamizi wa vituo vya kutolea huduma kutokuwa na uwezo

• Kuundwa kamati ya usimamizi wa kituo katika Zahanati ya Ibu-mu kulingana na miongozo na taratibu ambapo ilibainika kuwa zahanati imekosa kamati ya usimamizi wa kituo toka Mei 5, 2016.

• Kamati zitenge bajeti kwa ajili ya usafi vituoni ili kuwapunguzia mzigo watoa huduma za afya.

• Kamati kupatiwa mafunzo kuhusu wajibu na majukumu yao.

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

19

Kiambata Na. 2 Timu ya SAM

Na Jina Jinsi Kundi la Uwakilishi1 John Kasuga ME HFGC

2 Rehema Msola KE WAVIU

3 Hilkia Nyalusi KE Wananchi

4 Anna Masasi KE Walemavu

5 Yusta Msigwa KE CMAC

6 Mickness Mlowe KE CHMT

7 Scholastica Gibore KE CMT

8 Visise Mtengela KE Wananchi

9 Getruda Magelanga KE Wananchi

10 Fabiola Nzasule KE Madiwani

11 Hemed Mbena ME Madiwani

12 Shukuru Malenda ME Wananchi

13 Ally Juma ME Viongozi wa Dini

14 Amos Luhwago ME Asasi za Kiraia

15 Upendo Mponzi KE WEO

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) report... · 2020-01-08 · Valence Kihwaga na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Aloyce Kwezi kwa kuwa pamoja na Timu muda

“Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi katika ngazi zote za serikali”.

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzBlog: www.sikika-tz.blogspot.com Twitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika Tanzania