sheria ya leseni za usafirishaji (sura ya 317) kanuni ......sheria ya leseni za usafirishaji (sura...
TRANSCRIPT
SHERIA YA LESENI ZA USAFIRISHAJI
(SURA YA 317)
_____________
KANUNI
_____________
(Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 45)
_____________
KANUNI ZA LESENI ZA USAFIRISHAJI (MAGARI YA ABIRIA), ZA MWAKA 2019
_____________
MPANGILIO WA KANUNI
Kanuni Jina
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA AWALI
1. Jina la Kanuni.
2. Matumizi ya Kanuni.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
MAOMBI NA UTOAJI WA LESENI
4. Vigezo vya kuomba leseni kwa kampuni.
5. Vigezo vya kuomba leseni kwa mtu binafsi.
6. Utaratibu wa kuomba leseni.
7. Vigezo vya kuomba leseni kwa magari ya shule.
8. Utaratibu wa kuomba leseni za magari ya shule.
9. Vigezo vya kutoa leseni.
10. Aina na muda wa leseni.
11. Leseni ya Kawaida.
12. Leseni ya Muda Mfupi.
13. Leseni Maalumu.
14. Ada za leseni na tozo nyingine.
15. Uchambuzi wa maombi na utoaji wa leseni.
16. Kukataliwa kwa ombi la leseni.
17. Yaliyomo kwenye leseni ya kampuni au mtu binafsi.
18. Kubandika leseni.
19. Mfumo wa tathmini ya ubora wa huduma.
20. Uhuishwaji wa leseni.
21. Kupotea au kuharibika kwa leseni.
22. Kibali cha Dharura.
SEHEMU YA TATU
2
MASHARTI YA LESENI
23. Masharti ya msingi kwa magari ya usafirishaji wa abiria.
24. Masharti ya leseni kwa usafirishaji wa abiria wa mijini.
25. Masharti ya leseni kwa magari ya abiria kati ya mji na mji na nchini na nchi
nyingine.
26. Masharti maalumu ya leseni kwa magari yaliyosajiliwa nje ya nchi.
27. Masharti ya leseni kwa basi ya shule.
SEHEMU YA NNE
KUSITISHA AU KUFUTA LESENI
28. Mamlaka ya kusitisha leseni.
29. Utaratibu wa kusitisha leseni.
30. Kufutwa kwa leseni.
SEHEMU YA TANO
UTOAJI WA TIKETI NA USHUGHULIKIAJI WA MIZIGO YA ABIRIA
31. Utozaji wa nauli iliyoidhinishwa.
32. Uwekeshaji wa tiketi.
33. Utoaji wa tiketi.
34. Wajibu wa kuandaa orodha ya wasafiri.
35. Haki ya mtoa huduma kutoza nauli iliyoidhinishwa.
36. Jukumu la kutoa usafiri.
37. Nauli ya mwanafunzi au mtoto.
38. Utozaji gharama za usafirishaji wa mizigo ya abiria.
39. Wajibu wa abiria kutambulisha mzigo.
40. Wajibu wa mtoa huduma kuweka utambulisho kwenye mzigo wa abiria.
SEHEMU YA SITA
MATUMIZI YA RATIBA, BATLI NA JEDWALI LA NAULI
41. Utoaji na matumizi ya ratiba, batli na jedwali la nauli.
42. Wajibu wa kuzingatia njia na ratiba zilizoidhinishwa.
SEHEMU YA SABA
MAKOSA NA ADHABU
43. Makosa na adhabu.
44. Uwezo wa kufifisha makosa.
45. Ufifishaji wa makosa.
3
46. Taarifa ya makosa.
47. Utaratibu wa malipo.
48. Kutolipa faini ya kosa lililofifishwa.
49. Kutosaini taarifa ya makosa.
SEHEMU YA NANE
MASHARTI YA JUMLA
50. Wajibu wa kutoa taarifa ya gari kusitisha utoaji huduma.
51. Wajibu wa kufunga na kutunza kifaa maalumu cha kufuatilia mwenendo wa gari.
52. Mamlaka ya kuzuia baadhi ya magari ya abiria kutoa huduma katika maeneo
maalum.
53. Mzigo uliosahaulika kwenye gari la abiria.
54. Mamlaka ya kusimamisha na kukagua gari.
55. Upakaji rangi na uwekaji matangazo kwenye gari la abiria.
56. Wajibu wa kutoa taarifa.
57. Kuhamisha umiliki au kuondoa gari kwenye huduma.
58. Mapitio ya uamuzi wa Mamlaka.
59. Masharti ya mpito na yanayoendelea.
60. Kufutwa kwa Kanuni. ____________
MAJEDWALI ____________
4
SHERIA YA LESENI ZA USAFIRISHAJI
(SURA YA 317)
_________
KANUNI
_________
(Zimetungwa chini ya kifungu cha 45)
___________
KANUNI ZA LESENI ZA USAFIRISHAJI (MAGARI YA ABIRIA), ZA MWAKA 2019
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA AWALI
Jina la Kanuni 1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Leseni za Usafirishaji (Magari ya Abiria), za
Mwaka 2019. Matumizi ya
Kanuni 2. Kanuni hizi zitatumika kwa magari yote yanayotoa huduma ya usafiri wa
abiria. Tafsiri 3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale muktadha utakapohitaji vinginevyo:
“abiria” inamaanisha mtu yeyote anayesafiri kwenye gari la abiria mwenye
tiketi halali na inajumuisha mtoto;
“ajali” inamaanisha tukio au mlolongo wa matukio maalumu yasiyofaa, ya
uzembe au yasiyokusudiwa yenye athari kwa abiria na watumiaji wengine wa
barabara;
Sura ya 317 “Sheria ” maana yake sharia ya leseni ya Usafirishaji;
“basi la shule” inamaanisha gari la abiria linalomilikiwa au kutumiwa na shule
au linalomilikiwa na mtu binafsi au linalotumika chini ya mkataba na shule hiyo
ambalo limekusudiwa kutoa huduma kwa wanafunzi kwenda au kutoka shule, au
kwa shughuli nyingine yeyote inayohusiana na shule kwa pamoja;
“basi la wafanyakazi” inamaanisha gari la abiria ambalo limekusudiwa kutoa
huduma kwa wafanyakazi au wanafunzi wa elimu ya juu; Sura ya 197 “chama cha ushirika” inamaanisha chama kilichosajiliwa chini ya Sheria ya
Vyama vya Ushirika;
“eneo la kibiashara la mji” inamaanisha eneo la jiji, manispaa au mji kama
lililovyotamkwa na mamlaka husika; “gari la abiria” inamaanisha gari linalobeba au lililokusudiwa kubeba abiria kwa
kukodishwa au kwa malipo, linalojumuisha gari inayotumika au iliyoundwa
kutumika kwa kazi hiyo au kazi nyingine; Sura ya 337 “jumuiya” inamaanisha taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Jumuiya
za Kijamii na kusajiliwa kama Mdhamini;
Sura ya 168 “kadi ya usajili wa gari” inamaanisha kadi ya usajili wa gari iliyotolewa chini
ya Sheria ya Usalama Barabarani; Sura ya 212 “kampuni” inamaanisha kampuni iliyoundwa na kusajiliwa Tanzania Bara chini
5
ya Sheria ya Makampuni; “Kifaa Maalumu cha Kufuatilia Mwenendo wa Gari” inamaanisha kifaa
kinachofungwa kwenye gari la abiria kwa ajili ya kuchukua taarifa za mwenendo
wa gari husika na kuzituma wakati huo huo kwenye mfumo maalumu wa
kufuatilia mwenendo wa gari;
“leseni” inamaanisha leseni ya usafirishaji wa abiria iliyotolewa chini ya
Kanuni hizi; “leseni maalumu” inamaanisha leseni inayotolewa na Mamlaka kwa idhini ya
Waziri kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji kwa maeneo ya mjini au maeneo
mengine kwa muda maalumu utakaopangwa; Sura ya 413 “Mamlaka” inamaanisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini kama
ilivyoanzishwa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Mamlaka ya LATRA; “mfanyakazi” inajumuisha dereva, kondakta na mfanyakazi mwingine yeyote
wa mtoa huduma anayefanya kazi kwenye gari la abiria au gari la shule likiwa
kazini; “Mfumo Maalumu wa Kufuatilia Mwenendo wa Gari” inamaanisha mfumo
unaoweza kufuatilia na kunukuu mwendo wa gari la abiria kutembea kwa kasi
iliyoidhinishwa na Mamlaka;
Sura ya 168 “Mkaguzi wa Magari” inamaanisha mtu aliyeteuliwa chini ya Sheria ya
Usalama Barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa magari; Sura ya 413 “Mkurugenzi Mkuu” inamaanisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka aliyeteuliwa
chini ya Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini;
“mmiliki” inamaanisha mtu yeyote yule ambaye jina lake linaonekana kwenye
kadi ya usajili wa gari kama mmiliki; “mtoa huduma” inamaanisha mtu, jumuiya, taasisi au kampuni iliyosajiliwa na
na Mamlaka kwa ajili ya kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria;
“mtoto” inamaanisha mtu mwenye umri wa miaka mitatu au chini yake;
“mfanyakazi gari la abiria inamaanisha, dereva, kondakta au mfanyakazi yeyote
anayefanya kazi kwenye basi la usafiri wa umma, basi la shule, linapokuwa
safarini;
“mwanafunzi” inamaanisha mwanafunzi wa shule ya awali, msingi au sekondari
anapokuwa katika sare ya shule au mwenye kitambulisho;
“ratiba” inamaanisha utaratibu wa maandishi unaotolewa na Mamlaka
unaoonesha muda wa kuondoka na kufika kwa gari la abiria katika vituo
mbalimbali kwa kila njia; Sura ya 317 “Sheria” inamaanisha Sheria ya Leseni za Usafirishaji;
“taarifa ya ukaguzi wa gari” inamaanisha taarifa ya gari inayothibitisha ubora
wake kwa matumizi ya barabarani inayotolewa na Mkaguzi wa Magari au taasisi
nyingine yeyote inayotambuliwa na Mamlaka;
“taasisi iliyosajiliwa” inajumuisha chama cha ushirika, wadhamini, jumuiya,
kampuni au ubia ambao umesajiliwa chini ya sheria husika; Sura ya 413 “tozo ya mwaka” inamaanisha tozo inayolipwa kwa Mamlaka kwa mujibu wa
kifungu cha 41 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini,
6
SEHEMU YA PILI
MAOMBI NA UTOAJI WA LESENI
Vigezo vya kuomba
leseni kwa kampuni
4.–(1) Mtu yeyote anayehitaji kutoa huduma za usafirishaji wa abiria
ataomba leseni kwa Mamlaka.
(2) Mtu yeyote: (a) hatatoa huduma za usafirishaji wa abiria bila kuwa na leseni halali;
(b) baada ya kuanza kutumika kwa Kanuni hizi, hatapewa leseni ya kutoa
huduma za usafirishaji wa abiria isipokuwa kama mwombaji huyo: Sura ya 212 (i) ni kampuni; na
(ii) anamiliki angalau idadi ya chini ya magari ya abiria kama
itakavyoelekezwa na Mamlaka kulingana na wakati; na
(iii) amekidhi viwango vilivyoelekezwa kwenye kanuni ya viwango
vya ubora na usalama wa huduma.
Vigezo vya kuomba
leseni kwa mtu
binafsi
5.-(1) Mamlaka inaweza kutoa leseni kwa mtu binafsi ili kutoa huduma
kwenye njia maalumu kwa kipindi maalumu.
(2) Mamlaka, baada ya kuanza kutumika kwa Kanuni hizi, haitatoa
leseni kwa mtu binafsi isipokuwa iwapo mtu huyo: (a) ni raia wa Tanzania;
(b) anamiliki idadi ya chini ya magari ya abiria kama ambavyo itaamuriwa
na Mamlaka kulingana na wakati; na
(c) amekidhi viwango vilivyoelekezwa kwenye kanuni ya viwango vya
ubora na usalama wa huduma
Utaratibu wa kuomba
leseni
6.-(1) Mtu anayekusudia kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria atawasilisha
maombi ya leseni kwa Mamlaka kwa kujaza fomu kwa mkono au kielektroniki
kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi. (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1), yataambatishwa na: (a) nakala ya cheti cha usajili wa kampuni; (b) nakala ya kadi ya usajili wa gari; (c) taarifa ya ukaguzi wa gari; .
(3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (2), mwombaji wa leseni maalumu,
atahitajika kuwasilisha: (a) andiko la biashara; (b) mpango wa kusimamia usalama; (c) mpango wa kushughulikia dharura; (d) taarifa ya fedha iliyokaguliwa ya kipindi cha karibuni; (e) utaratibu wa kushughulikia malalamiko;
(f) uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi kama ilivyoainishwa
katika Jedwali la Pili la Kanuni hizi; na
(g) nyaraka nyingine zozote ambazo Mamlaka inaweza kuzihitaji
wakati wowote. Vigezo vya
kuomba leseni kwa
magari ya shule
7.-(1) Mamlaka inaweza kutoa leseni kwa kutuo cha kulelea watoto, shule,
mtu binafsi au kampuni kwa ajili ya kutumia basi la shule kwa kipindi mahsusi.
(2) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (1), Mamlaka inaweza kutoa vigezo
kwa ajili ya utoaji wa leseni za mabasi ya shule kwa kuzingatia uwezo wa
7
mabasi kama itakavyoona inafaa.
Utaratibu wa
kuomba leseni za
magari ya shule
8.-(1) Mtu anayekusudia kutoa huduma ya magari ya shule atawasilisha
maombi ya leseni kwa Mamlaka kwa kwa njia ya kujaza fomu kwa mkono au
kielektroniki. (2) Maombi chini ya kanuni ndogo ya (1), yataambatishwa na: (a) nakala ya kadi ya usajili wa gari; (b) taarifa ya ukaguzi wa gari;
(c) nyaraka nyingine zozote ambazo Mamlaka inaweza kuzihitaji wakati
wowote.
Vigezo vya kutoa
leseni
9. Mamlaka, iwapo itaona ni muhimu, inaweza -
(a) kuweka vigezo vya kutoa leseni yoyote chini ya Kanuni hizi: (i) kwa kuzingatia njia na umbali utakaotumiwa na gari la abiria; (ii) kutegemeana na uwezo wa gari na idadi ya magari ya abiria; au (b) kurekebisha vigezo vya kutoa leseni yoyote.
Aina na muda wa
leseni
10. Mamlaka inaweza kutoa aina zifuatazo za leseni kwa mmiliki wa gari la
kubeba abiria kwa ajili ya kutoa huduma za usafirishaji kwa umma: (a) Leseni ya Kawaida; (b) Leseni ya Muda Mfupi; au (c) Leseni Maalumu. Leseni ya Kawaida 11.(1) Leseni ya kawaida:
(a) itatolewa kwa mwombaji ambaye amekusudia kutoa huduma za
usafirishaji kwa
a. wafanyakazi au wanachuo wa taasisi za elimu ya juu za umma au
binafsi; b. wanafunzi; c. watalii; d. abiria katika maeneo ya mijini; e. mabasi ya kutoka na kuingia vijijini na mjini; f. abiria kati ya mji na mji au mkoa na mkoa; g. abiria wanaoingia na kutoka kati ya nchi moja na nchi nyingine; h. shughuli maalumu au kukodiwa; na i. aina nyingine ya leseni kama itakavyoamuliwa na Mamlaka; na (2) itakuwa halali kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Leseni ya Muda
Mfupi
12. Leseni ya Muda Mfupi:
(a) itatolewa kwa ajili ya biashara ya msimu au utekelezaji wa kazi
maalumu; na (b) itakuwa halali kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu. Leseni Maalumu 13.-(1) Leseni Maalum:
(a) itatolewa kwa mwombaji ambaye anakusudia kutoa huduma ya
usafirishaji abiria kwa maeneo maalumu ya mjini au njia nyingine
yoyote kwa masharti na muda maalumu; (b) itakuwa kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. (2) Bila kuathiri uwezo wa jumla wa Mamlaka kutoa leseni chini ya Kanuni
8
hizi, leseni maalumu itatolewa baada ya mashauriano na Waziri.
Ada za leseni na
tozo ya mwaka
14.-(1) Mwombaji atalipa kwenye Mamlaka ada na tozo nyingine kama
ilivyooneshwa kwenye Jedwali la Pili la Kanuni hizi.
(2) Ada na tozo nyingine kwenye kanuni ndogo ya (1) zitalipwa kwenye
akaunti ya Benki ya Mamlaka kwa fedha taslimu au kwa njia ya kielektoniki na
ushahidi wa malipo utawasilishwa makao makuu ya LATRA au Ofisi za Mikoa. Uchambuzi wa
maombi na utoaji wa
leseni.
15. Mamlaka, baada ya kupokea maombi ya leseni ya usafirishaji abiria,
itayachambua na, iwapo itaridhika, itatoa leseni.
Kukataliwa ombi la
leseni 16.-(1) Mamlaka inaweza kutotoa leseni kwa mwombaji endapo atakuwa:
(a) hajatimiza mahitaji yaliyoanishwa kwenye Kanuni hizi;
(b) amewasilisha nyaraka za kughushi; au
(c) ametoa taarifa zisizokuwa sahihi kuhusiana na maombi ya leseni;
(d) ameomba njia ambayo idadi ya magari yanayotakiwa
yametosheleza; au
(e) sababu nyingine yoyote ambayo Mamlaka itaona inafaa.
(2) Endapo Mamlaka itakataa kutoa leseni, itamtaarifu mwombaji kwa
maandishi, ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya maombi ya leseni
yalipopokelewa, sababu ya kukataliwa kwa maombi hayo.
(3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) (b), Mamlaka inaweza kukataa kutoaa
leseni kwa mtu yeyote aliyewasilisha nyaraaka za kughushi mpaka zipite siku
tisini tangu siku alipokataliwa;
Yaliyomo kwenye
leseni ya kampuni au
mtu binafsi
17.-(1) Mamlaka inaweza kutoa leseni kwa Kampuni au mtu binafsi.
Leseni ya mtu binafsi itajumuisha mambo yafuatayo:
(a) jina na anwani ya la mtoa huduma;
(b) muda wa leseni;
(c) Masharti ya leseni;
(d) Namba ya leseni;
(e) Namba ya usajili wa gari;
(f) Idadi ya magari yaliyochini ya hiyo leseni;
(2) Leseni ya kampuni itajumuisha mambo yafuatayo
a. Jina na anwani ya Kampuni ya mtoa huduma;
b. Muda wa leseni;
c. Masharti ya leseni;
d. namba ya leseni;
e. namba ya usajili wa gari;
f. Idadi ya magari yaliyo chini ya leseni
Kubandika leseni 18.-(1) Mtoa huduma atabandika leseni sehemu ya wazi upande wa kushoto
wa kioo cha mbele cha gari la abiria.
(2) Ikiwa ni Kampuni, mtoa huduma atatakiwa kubandika kwenye sehemu
ya wazi kwa kila gari, nakala halisi ya leseni itakayotolewa na Mamlaka.
Mfumo wa tathmini
ya ubora wa huduma 19.-(1) Mtoa huduma, baada ya kupokea leseni yake, atazingatia vigezo vya
utoaji huduma vilivyopangwa na Mamlaka.
(2) Ikiwa ni kampuni iliyosajiliwa, mtoa huduma:
(a) atawasilisha Taarifa ya Mwaka ya Utendaji kwa Mamlaka; au
9
(b) anaweza kuandaa viwango vya utoaji huduma za usafiri wa abiria na
kuviwasilisha kwa Mamlaka kwa ajili ya kuidhishwa.
Uhuishwaji wa leseni 20.-(1) Mtoa huduma anayetaka kuhuisha leseni anaweza kuomba kwa
Mamlaka ndani ya siku thelathini kabla ya tarehe ya kuisha kwa leseni husika. (2) Maombi ya kuhuisha leseni yataambatishwa na:
(a) nakala iliyothibitishwa ya hati safi ya kodi, isipokuwa kwa maombi
ya leseni ya magari ya shule; (b) nakala iliyothibitishwa ya taarifa ya ukaguzi wa gari; na
(c) nyaraka nyingine zozote ambazo Mamlaka itazihitaji wakati
wowote.
(3) Mamlaka inaweza kutoza asilimia hamsini ya ada ya maombi ya leseni
yatakayowasilishwa siku kumi na nne baada ya tarehe ya kuisha kwa leseni na
asilimia tano kwa kila mwezi utakaofuata kwenye kiasi kinachodaiwa kwa
kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili. Kupotea au
kuharibika kwa
leseni
21.-(1) Endapo leseni:
(a) imeharibika au imechakaa, mtoa huduma ataitaarifu Mamlaka kwa
maandishi haraka iwezekanavyo pamoja na maombi ya kupewa
leseni mbadala;
(b) imepotea, mtoa huduma ataitaarifu Mamlaka haraka iwezekanavyo
kwa maandishi pamoja na kuwasilisha taarifa ya polisi ya upotevu
na maombi ya kupewa leseni mbadala.
(2) Endapo Mamlaka itaridhika kwamba leseni imepotea, imeharibika au
imechakaa, itatakiwa, baada ya mwombaji kulipa ada iliyopangwa, kutoa nakala
ya leseni kwa mtoa huduma, Isipokuwa kwamba,
(a) ikiwa leseni imechakaa, Mamlaka itatakiwa, kabla ya kutoa nakala ya
leseni, kumtaka mtoa huduma kuwasilisha leseni ya mwanzo kwa ajili
ya uhakiki;
(b) endapo leseni iliyopotea itapatikana baada ya kutolewa kwa nakala
mpya ya leseni chini ya kanuni hii, mtoa huduma atarudisha nakala ya
leseni kwa Mamlaka. Kibali cha Dharura 22.-(1) Mamlaka inaweza kutoa Kibali cha Dharura kwa mtoa huduma kwa
kipindi kisichozidi siku saba-
(a) iwapo mtoa huduma anataka kubadili gari la abiria lililoharibika ambalo
liliruhusiwa kutoa huduma ya usafirishaji wa umma; au (b) kwa ajili ya sababu nyingine ambayo Mamlaka itaamua. (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma anaweza kupata
Vibali vya Dharura kutoka Ofisi yoyote ya Mamlaka na kuviweka ofisini kwake
kwa ajili ya kuvitumia inapotokea dharura.
SEHEMU YA TATU
MASHARTI YA LESENI
Masharti ya msingi
kwa magari ya
usafirishaji wa
abiria
23.-(1) Mtoa huduma wa gari la abiria atahakikisha kuwa:
(a) gari la abiria halina hitilafu;
(b) idadi ya abiria, uzito na upakiaji wa mizigo, uzito wa gari na mwendo
haizidi viwango vilivyoainishwa kwenye Sheria nyingine za nchi;
10
(c) dereva mmoja haendeshi gari mfululizo kwa muda unaozidi saa nane;
(d) taarifa sahihi zinaandaliwa na kutolewa na kumbukumbu za biashara
ya usafirishaji wa abiria zinatunzwa;
(e) gari la abiria linakuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza
kilichowekwa mahali panapoonekana, kilicho na dawa na vifaa tiba
vilivyoainishwa;
(f) chombo cha taka kinawekwa kwenye gari la abiria na taka
zinazokusanywa zinatupwa kwenye maeneo maalum ya kutupa taka;
(g) haajiri mfanyakazi ambaye ametenda kosa lililoainishwa katika
Kanuni hizi mara tatu mfululizo katika kipindi cha uhai wa leseni;
(h) anazingatia viwango vya madaraja ya mabasi ya abiria
vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne kwenye kanuni hizi;
(i) anazingatia masharti mengine yoyote ambayo yatawekwa na
Mamlaka.
(2) Mfanyakazi wa basi la abiria atahakikisha kuwa:
(a) gari la abiria halibebi mzigo hatarishi;
(b) gari la abiri halibebi abiria zaidi ya idadi iliyoandikwa kwenye leseni;
(c) burudani itakayotolewa kwenye gari la abiria wakati wa safari
itazingatia maadili na tamaduni ya Kitanzania na kwa sauti ya ndogo;
na
Sura ya 168 (d) Sheria ya Usalama Barabarani na sheria nyinginezo za nchi
zinatekelezwa. Masharti ya leseni
kwa usafirishaji wa
abiria wa mijini
24.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya msingi kama yaliyoainishwa chini ya
sehemu hii-
(a) Mtoa Huduma wa mabasi ya usafiri wa mijini atahakikisha kuwa:
(i) dereva wa gari la abiria au gari binafsi la kukodi ana umri usiopungua
miaka ishirini na tano na usiozidi miaka sitini;
(ii) tiketi ya basi inauzwa kwa mfumo wa karatasi au kielektroniki na
inatolewa kwa abiria;
(iii) gari la abiria linapakwa rangi ya utambulisho wa njia na kwa namna
iliyoelekezwa na Mamlaka;
(iv) nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka inaandikwa karibu na mlango wa
kuingilia abiria;
(v) haajiri mfanyakazi ambaye ametenda kosa lililoainishwa katika Kanuni
hizi mara tatu mfululizo katika kipindi cha uhai wa leseni;
(vi) anazingatia masharti mengine yoyote ambayo yatawekwa na Mamlaka.
(b) Mfanyakazi wa mtoa huduma ya usafiri wa mjini atahakikisha kuwa:
(i) anavaa sare safi na nadhifu kama Mamlaka itakavyoamua;
(ii) hakuna mtu anayefanya biashara, anayehubiri, anayefanya shughuli za
siasa au kutoa burudani ambayo inakiuka kanuni ya kanuni hizi ndani ya
gari la abiria mijini;
(iii) gari la abiria linatoa huduma kwenye njia ambayo imeainishwa kwenye
leseni; na
(iv) gari la abiria halibadilishi njia au halisitishi safari kabla ya kufika
mwisho wa kituo kama ilivyooneshwa kwenye tiketi ya abiria.
Masharti ya leseni
kwa magari ya
abiria kati ya mji na
mji na nchi na nchi
25. Kwa kuzingatia masharti ya msingi kama yaliyoainishwa chini ya kanuni
ya 23-
(a) Mtoa huduma kwa gari la abiria linalofanya safari kati ya mji na mji na
11
nyingine kati ya nchi na nchi atahakikisha kuwa:
(i) dereva ana umri usiopungua miaka thelathini na usiozidi miaka
sitini;
(ii) gari la abiria lina vigezo vya madaraja ya mabasi ya abiria
vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne la Kanuni hizi;
(iii) gari la abiria limefungwa kifaa maalum kilichoidhinishwa na
Mamlaka kwa ajili ya kufuatilia mwendo wa gari;
(iv) gari la abiria lina batli iliyotolewa na Mamlaka;
(v) gari la abiria lina mikanda inayofanya kazi na safi kwa kila kiti cha
abiria;
(vi) haajiri mfanyakazi ambaye ametenda kosa lililoainishwa katika
Kanuni hizi mara tatu mfululizo katika kipindi cha uhai wa leseni;
(vii) anazingatia masharti mengine yoyote ambayo yatawekwa na
Mamlaka.
(b) Mfanyakazi wa gari la abiria linalofanya safari kati ya mji na mji na kati
ya nchi na nchi atahakikisha kuwa:
(i) anavaa sare safi na nadhifu kama Mamlaka itakavyoamua;
(ii) tiketi halali ya basi inauzwa kwa mfumo wa karatasi au
kielektroniki na inatolewa kwa abiria; na
(iii) hakuna mtu anayefanya biashara, anayehubiri, anayefanya shughuli
za siasa au kutoa burudani ambayo inakiuka kanuni hizi ndani ya
gari la abiria;
(iv) gari la abiria linazingatia batli, ratiba na chati ya nauli
iliyoidhinishwa na Mamlaka;
(v) gari la abiria lina nakala tatu ya orodha ya abiria kwa kila safari
ambapo nakala moja itabaki katika gari la abiria, nakala nyingine
itawasilishwa kituo cha polisi na nakala moja nyingine itaachwa
kwenye ofisi za mtoa huduma;
(vi) wafanyakazi wanavaa vitambulisho, vinaonekana kwa urahisi kwa
mtu yeyote na ambavyo vina:
(a) jina la mfanyakazi;
(b) jina, anwani, namba ya simu na sahihi ya mtoa huduma;
(c) cheo na sahihi ya mfanyakazi; na
(d) picha ya hivi karibuni ya paspoti ya mfanyakazi;
(vii) gari la abiria linasimama kwenye maeneo ambayo huduma za choo
na huduma nyinginezo zinapatikana;
(viii) gari la abiria linatoa huduma kwenye njia ambayo imeainishwa
kwenye leseni;
(ix) safari haikatishwi kabla ya kufika kwenye kituo cha mwisho wa
safari kama inavyoonekana kwenye tiketi ya abiria na
(x) abiria wanatangaziwa masuala ya usalama kabla ya kuanza safari na
wakati wa safari. Masharti maalumu
ya leseni kwa
magari
yaliyosajiliwa nje
ya nchi
26. Mtoa huduma na mfanyakazi wa gari linalotoa huduma kati ya nchi na
nchi lenye usajili wa nchi nyingine watahakikishwa kwamba gari hilo halitoi
huduma za usafirishaji kama gari lililosajiliwa nchini.
Masharti ya leseni
kwa basi la shule
27.-(1) Mtoa huduma wa basi la shule atahakikisha kuwa:
(a) gari la abiria halina hitilafu; Tangazo la Serikali
Na. 412 of 2014 (b) amekidhi viwango vilivyoelekezwa kwenye kanuni ya viwango vya
12
ubora na usalama wa huduma
(c) dereva wa basi la shule ana umri usiopungua miaka thelathini na tano
na usiozidi miaka sitini;
(d) basi la shule linapakwa rangi ya njano yenye namba Rgb (255,255,0)
na kuandikwa maneno “School Bus” au “Basi la Shule”;
(e) basi la shule linakuwa na kisanduku cha huduma ya kwanza
kilichowekwa mahali panapoonekana, kilicho na dawa na vifaa tiba
vilivyoainishwa;
(f) haajiri mfanyakazi ambaye ametenda kosa lililoainishwa katika
Kanuni hizi mara tatu mfululizo katika kipindi cha uhai wa leseni;
(2) Mfanyakazi wa basi la shule atahakikisha kuwa:
(a) basi la shule halibebi wanafunzi zaidi ya idadi iliyoandikwa kwenye
leseni;
(b) uwezo wa gari, upakiaji na mwendo wa gari havizidi viwango
vilivyoainishwa kwenye sheria nyingine;
(c) anavaa sare safi na nadhifu kama Shule itakavyoamua;
(d) chombo cha taka kinawekwa kwenye gari la abiria na taka
zinazokusanywa zinatupwa kwenye maeneo maalum ya kutupa taka;
na
(e) anazingatia masharti mengine yoyote ambayo yatawekwa na
Mamlaka.
SEHEMU YA NNE
KUSITISHA AU KUFUTA LESENI
Mamlaka ya
kusitisha leseni
28.-(1) Mamlaka inaweza kusitisha leseni ikiwa imeridhika kwamba mtoa
huduma:
(a) amesababisha ajali iliyopelekea vifo au majereha makubwa kwa abiria
kutokana na ukiukwaji wa masharti ya leseni;
(b) ameshindwa kufunga kifaa cha kuratibu mwenendo wa basi; (c) ameharibu kifaa maalumu cha kuratibu mwenendo wa gari; (d) ameshindwa kulipa ada na tozo za Mamlaka; (e) amekataa kutii amri halali ya Ofisa wa Mamlaka; (f) amemzuia Ofisa wa Mamlaka kufanya ukaguzi; au
(g) ametenda kosa hilohilo chini ya Kanuni hizi zaidi ya mara tatu ndani ya
mwaka mmoja.
(2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), Mamlaka inaweza kusitisha leseni
endapo ni muhimu au inafaa kwa maslahi ya usalama barabarani.
(3) Endapo ukiukwaji unahusu kushindwa kufunga au kuharibu kifaa cha
kuratibu mwenendo wa basi, usitishaji utakuwa wa siku thelathini au zaidi.
Utaratibu wa
kusitisha leseni
29.-(1) Mamlaka inaweza, kabla ya kusitisha leseni, kutoa notisi kwa mtoa
huduma ili kutoa maelezo ni kwanini leseni yake isisitishwe.
(2) Mtoa huduma atatakiwa, baada ya kupokea notisi chini ya kanuni ndogo
ya (1), kuwasilisha maelezo ya maandishi kwa Mamlaka ndani ya siku saba tangu
tarehe ya kupokea notisi akieleza ni kwanini leseni yake isisitishwe.
(3) Mamlaka inaweza kusitisha leseni na kutoa sababu za usitishwaji wa
leseni endapo:
(a) Mamlaka haikuridhishwa na maelezo yaliyotolewa kupitia kanuni ndogo
13
ya (2); au
(b) Mtoa huduma hakufanya wasilisho lolote.
(4) Bila kujali kanuni ndogo za (1), (2) na (3), Mamlaka inaweza, endapo
itaona inafaa, kusitisha leseni bila kutoa notisi kwa mtoa huduma kuwasilisha
maelezo.
(5) Endapo leseni imesitishwa chini ya kanuni ya 28, mtoa huduma ataacha
mara moja kutoa huduma za usafirishaji na kurudisha leseni kwa Mamlaka ndani
ya siku saba tangu tarehe aliyopokea notisi ya usitishwaji wa leseni.
(6) Mamlaka, iwapo leseni itakuwa hai hadi wakati wa kumalizika kwa
kipindi cha usitishwaji, itarudisha leseni hiyo kwa mtoa huduma baada ya
kumalizika kwa kipindi cha usitishwaji na kutekelezwa kwa masharti mengine
yoyote kama yatakavyoainishwa katika notisi ya usitishwaji.
Kufutwa kwa leseni 30. Mamlaka itafuta leseni iliyositishwa kwa mara ya tatu.
SEHEMU YA TANO
UTOAJI WA TIKETI NA USHUGHULIKIAJI WA MIZIGO YA ABIRIA
Utozaji wa nauli iliyoidhinishwa
31. Mtoa huduma hatatoza nauli zaidi ya ile iliyoidhinishwa na Mamlaka
kulingana na daraja la basi husika.
Uwekeshaji wa
tiketi
32. Mtoa huduma anaweza kuruhusu wekesho la tiketi kufanyika kwa mfumo
wa karatasi au kielektroniki.
Utoaji wa tiketi
33.-(1) Mtoa huduma atatoa tiketi ya basi kwa abiria baada ya kupokea
malipo ya nauli iliyoidhinishwa kwa ajili ya safari husika kama ilivyo ainishwa
kwenye Jedwali la Tano la Kanuni hizi. (2) Tiketi ya basi itolewa kwa mfumo wa kielektroniki.
(3) Bila kuathiri kanuni (2) Mtoa huduma anaweza kutoa tiketi ya karatasi
kwa ruhusa maalumu ya Mamlaka. Sifa ya tiketi ya basi ni kama ifuatavyo: (a) kama ni basi linalotoa huduma ya usafiri kati ya mji na mji: (i) jina la abiria na namba ya kiti; (ii) muda wa kuripoti na kuondoka; (iii) kituo cha kuondokea, njia ya kupitia na kituo cha mwisho wa safari; (iv) nauli ya safari; (v) anuani kamili ya mtoa huduma pamoja na namba yake ya simu; (vi) namba ya usajili wa basi la abiria;
(vii) tarehe ya kutolewa na tarehe ya kusafiri; (viii) namba ya tiketi; (ix) namba ya dharura na taarifa ya LATRA na Polisi; na
(x) namba ya LATRA ya kuuliza viwango vya nauli.
(xi) namba ya simu ya mtoa huduma; (b) kama ni gari linalotoa huduma ya usafiri mijini: (i) namba ya usajili wa gari la abiria; (ii) jina la njia ambapo gari la abiria linatoa huduma; (iii) nauli iliyoidhinishwa; (iv) jina na anuani ya mtoa huduma; (v) tarehe ya kutolewa; na (vi) namba ya simu ya mtoa huduma.
14
(3) Tiketi iliyotolewa kwa ajili ya safari kati ya mji na mji au nchi na nchi
itakuwa na nakala mbili, nakala moja itatolewa kwa abiria na nakala ya pili
itabaki kwa mtoa huduma.
(4) Mtoa huduma atatunza taarifa za tiketi zote zilizotolewa kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja kuanzia tarehe zilipotolewa.
(5) Pale ambapo abiria atafuta wekesho la tiketi yake ya safari saa ishirini na
nne au zaidi kabla ya kuanza safari, mtoa huduma, atalazimika kumrudishia
abiria nauli aliyolipa mara tu baada ya kufuta wekesho la tiketi.
(6) Pale ambapo wekesho la tiketi litafutwa kwenye muda usiozidi saa
ishirini na nne na si chini ya saa kumi na mbili kabla ya muda uliopangwa kabla
ya safari kuanza: (a) atapewa nafasi ya kubadilisha tarehe ya safari; au (b) atarudishiwa asilimia themanini na tano ya nauli aliyolipa.
(7) Bila kujali kanuni ndogo ya (5) na (6), pale ambapo tiketi ilinunuliwa kwa
mfumo wa kielektroniki, mtoa huduma atakuwa na haki ya kukata kiasi cha fedha
kutoka kwenye nauli sawa na gharama iliyotumika kutoa huduma hiyo.
(8) Mtoa huduma hataongeza taarifa yoyote kwenye tiketi ambayo ni kinyume
na Kanuni hizi na masharti ya leseni.
Wajibu wa kuandaa orodha ya wasafiri
34.-(1) Kwa madhumuni ya Kanuni hizi, mtoa huduma ataandaa orodha ya
abiria wanaosafiri kama ilivyoelekezwa na Mamlaka na kwa kuzingatia Jedwali
la Sita la Kanuni hizi. (2) Mtoa huduma atajaza orodha ya abiria wanaosafiri katika nakala tatu na:
(a) kuwasilisha nakala moja katika kituo cha jirani cha polisi ambapo gari la
abiria limeanzia safari; (b) kutunza nakala moja kwenye ofisi ya mtoa huduma; na (c) kutunza nakala moja kwenye gari husika la abiria.
(3) Mtoa huduma atahakikisha kwamba nakala ya orodha ya abiria
wanaosafiri inayotunzwa ndani ya gari inahuishwa wakati wote wa safari na
kumbukumbu zake zinatunzwa kwa kipindi cha miaka mitano.
Haki ya mtoa huduma kutoza nauli
iliyoidhinishwa
35. Mtoa huduma atakuwa na haki ya kudai malipo ya nauli halali na endapo
abiria atashindwa kulipa nauli hiyo, mtoa huduma anaweza kukataa kumsafirisha
abiria huyo. Jukumu la kutoa usafiri
36.-(1) Mtoa huduma ambaye amekwishampa tiketi abiria atawajibika
kumsafirisha abiria huyo kwa mujibu wa masharti ya leseni na ratiba ya safari
iliyoidhinishwa na Mamlaka. (2) kama mtoa huduma atashindwa kutoa huduma ya usafiri kati ya mji na mji
au nchi na nchi: (a) ndani ya saa moja tangu muda wa kuanza safari mtoa huduma
atamrudishia abiria kiwango chote cha nauli kilicholipwa isipokuwa abiria
kwa hiyari yake akubali kusubiri usafiri mbadala utakaotolewa na mtoa
huduma au; (b) gari likiharibika akiwa safarini ndani ya masaa mawili mtoa huduma
atawajibika: (i) kutoa usafiri mbadala; (ii) kurudisha nauli yote kwa abiria; au (iii)kutoa chakula na malazi, ikiwa abiria kwa hiyari yake atakubali
kusubiri usafiri mbadala wakuendealea na safari.
15
Nauli ya
mwanafunzi au
mtoto
37.-(1) Mtoa huduma atamtoza nauli mwanafunzi atakayepanda gari la abiria
linalotoa huduma ya usafiri ndani ya mji kwa kiwango cha nauli
kilichoidhinishwa na Mamlaka. (2) Mtoto anayepakatwa hatalipa nauli kwa usafiri wa mji na mji na kati ya
nchi na nchi. Utozaji gharama za
usafirishaji wa
mizigo ya abiria
38.-(1) Mtoa huduma atasafirisha bure:
(a) mzigo wa abiria wenye uzito usiopungua kilo ishirini wa abiria
anayesafiri kati ya mji na mji au nchi na nchi ambao hauzidi urefu wa
sentimita 60, upana sentimita 45 na kimo sentimita 30; (b) vifaa saidizi vinavyotumiwa mtu mwenye ulemavu wa viungo kwa ajili
ya kutembea wakati anaposafiri kwenye gari linalotoa huduma kati ya
mji na mji au nchi na nchi. (2) Mtoa huduma atapima kila mizigo wa abiria na kutoza malipo kwa uzito
unaozidi kilo ishirini na kutoa risiti. Wajibu wa abiria
kutambulisha
mzigo
39.– (1) Abiria atawajibika kutoa taarifa ya:
(a) kitu chochote cha thamani ambacho kimewekwa kwenye buti la gari;
na
(b) vitu vyovyote alivyobeba endapo atatakiwa na mtoa huduma kufanya
hivyo. (2) Endapo abiria atakataa mzigo wake kukaguliwa na mtoa huduma, mtoa
huduma anaweza kukataa kusafirisha mzigo huo. (3) Mtoa huduma atakuwa na wajibu wa kutoa taarifa ya mizigo aliobeba
kwenye gari ambao anautilia shaka kwa Afisa wa Polisi. Wajibu wa mtoa
huduma kuweka
utambulisho
kwenye mzigo wa
abiria
40. Mtoa huduma, wa gari la abiria linalotoa huduma kati ya mji na mji au
kati ya nchi na nchi, anapaswa:
(a) kuweka alama ya utambulisho wa mzigo na kumpa abiria mwenye mzigo
kadi yenye kuonyesha jina la abiria na kituo cha mwisho mzigo
unakofika; (b) kuhakikisha mzigo wa abiria unawekwa mahali salama, unalindwa na
unawasilishwa kwa abiria mara baada ya kufika kituo cha mwisho; na (c) pale mzigo wa abiria unapopotea au unapoharibika, anafidia mzigo au
analipa kiasi cha fedha kinacholingana na thamani ya mzigo kwa abiria
ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kupata taarifa ya tukio la upotevu
na kuwasilisha uthibitisho wa kupotea kwa mzigo huo.
SEHEMU YA SITA
MATUMIZI YA RATIBA, BATLI NA JEDWALI LA NAULI
Utoaji na matumizi
ya ratiba, batli na
jedwali la nauli
41.-(1) Mamlaka itatoa ratiba na batli kwa basi linalotoa huduma ya
usafirishaji abiria kati ya miji na miji au kati ya nchi na nchi.
(2) Mtoa huduma wa basi linalotoa huduma za usafirishaji abiria kati ya miji
na miji au kati ya nchi na nchi atahakikisha kuwa:
(a) ratiba, batli na jedwali la nauli zilizotolewa chini ya kanuni ndogo ya
(1) zinatumika wakati wote wa safari na kuhifadhiwa ndani ya basi;
(b) ratiba na jedwali la nauli vinawekwa mahali pa wazi ndani ya basi la
abiria; na
16
(c) mtoa huduma anawajibika kuonyesha batli kwa Ofisa wa Polisi au
Mamlaka wakati wa ukaguzi pale inapohitajika.
(3) Endapo mtoa huduma atatumia basi jingine, ahakikishe ratiba, batli na
jedwali la nauli zinazotumiwa na basi lenye leseni ya njia husika zinawekwa
kwenye basi hilo mbadala.
Wajibu wa
kuzingatia njia na
ratiba
42.-(1) Gari la abiria litatoa huduma kwa kufuata ratiba ya njia na kwa
kuzingatia ratiba iliyoidhinishwa.
(2) Endapo mtoa huduma anataka kubadilisha njia na ratiba, ataomba kwa
Mamlaka na kulipa gharama za maombi ya kubadilisha leseni au na ratiba. (3Mamlaka inaweza kutoa leseni mpya baada ya kujiridhisha na sababu za
kubadilisha njia.
SEHEMU YA SABA
MAKOSA NA ADHABU
Makosa na adhabu
43.-(1) Mtu atakaye kiuka masharti ya leseni au kifungu chochote cha Kanuni
hizi, atakuwa ametenda kosa na endapo atatiwa hatiani atawajibika kulipa faini
isiyopungua shilingi laki mbili za kitanzania na isiyozidi shilingi laki tano au
atafungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka miwili au
vyote kwa pamoja.
(2) Bila kuhathiri kanuni ndogo ya (1), mtoa huduma hataajiri mfanyakazi
ambaye ametenda kosa lililoainishwa katika Kanuni hizi mara tatu mfululizo
katika kipindi cha uhai wa leseni;
Uwezo wa kufifisha
makosa
44.-(1) Mamlaka inaweza, pale mtoa huduma atakapokiri kwa maandishi
kwamba ametenda kosa kwa Mamlaka au afisa wa Mamlaka, Ofisa wa Mamlaka
anaweza, wakati wowote kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi mahakamani,
kufifisha kosa hilo na kuamuru mtoa huduma alipe kiasi cha fedha kisichozidi
nusu ya kiasi cha faini ambayo angetozwa endapo angetiwa hatiani kwa kosa hilo
Mahakamani.
(2) Pale ambapo kosa limefifishwa na mtenda kosa akashtakiwa Mahakamani
kwa kosa lilelile, itakuwa ni utetezi mzuri kwa mtenda kosa kuthibitisha kwa
kiwango cha kuiridhisha Mahakama kwamba kosa ambalo mtenda kosa
alishtakiwa nalo lilishafifishwa na Mamlaka.
Ufifishaji wa
makosa
45. Mamlaka inaweza kufifisha makosa kwa kuzingatia Jedwali la Saba la
Kanuni hizi. Taarifa ya makosa 46.-(1) Mamlaka, baada ya kubaini kosa linalokiuka Kanuni hizi, itamtaarifu
mtoa huduma kwa mfumo wa kielektroniki au karatasi kwa kutumia Fomu ya
Taarifa iliyoainishwa kwenye Jedwali la Nane la Kanuni hizi kuhusu: (a) kosa lililotendwa; (b) adhabu ya kosa ; (c) kiasi kinachotakiwa kufifishwa; (d) tarehe na namna ya kufanya malipo kwa Mamlaka; na (e) taarifa nyingine yoyote ambayo Mamlaka itaona inafaa.
(2) Mtenda kosa anaweza kukiri au kukataa kukiri kutenda kosa linalotakiwa
kufifishwa kwa kusaini Fomu ya Taarifa ya Makosa kama ilivyoainishwa kwenye
Jedwali la Nane la Kanuni hizi.
17
Utaratibu wa malipo 47.-(1) Endapo mtoa huduma anakiri kosa lififishwe, atalipa kiasi
kinachotakiwa kufifishwa katika muda wa siku kumi na nne kwenye akaunti ya
benki ya Mamlaka kwa kupeleka kiasi hicho cha fedha au kwa kutumia njia ya
kielektroniki na kuwasilisha uthibitisho wa malipo hayo Makao Makuu ya
Mamlaka au kwenye Ofisi za Mikoa.
(2) Baada ya kuwasilisha uthibitisho wa malipo, Mamlaka itatoa stakabadhi ya
malipo. Kutolipa faini ya
kosa lililofifishwa 48. Endapo mtoa huduma anashindwa kutekeleza amri ya kulipa kiasi cha
fedha kinachotakiwa kufifishwa chini ya Kanuni hizi katika muda ulioainishwa,
Mamlaka: (a) itatoza riba ya asilimia tano na asilimia nyingine tano ya kiasi kinachodaiwa
kila baada ya siku thelathini kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja; au (b) inaweza kukazia amri sawa sawa na amri ya hukumu iliyotolewa na
Mahakama kwa ajili ya malipo ya kiasi cha fedha kilichotajwa kwenye amri.
Kutosaini taarifa ya
makosa 49.-(1) Pale ambapo mtoa huduma au dereva:
(a) hajakiri kutenda kosa, atalazimika, katika kipindi cha siku kumi na nne tangu
tarehe ya kutenda kosa hilo kuwasilisha Fomu ya taarifa ya kosa kwa
Mamlaka kwa ajili ya kufikishwa Mahakamani. (b) anashindwa kufika kwenye Ofisi za Mamlaka ndani ya muda ulioainishwa
itaamuliwa kuwa amekiri kosa na atatakiwa kulipa adhabu kama
ilivyoainishwa kwenye Kanuni hizi.
SEHEMU YA NANE
MASHARTI VYA JUMLA
Wajibu wa kutoa
taarifa ya gari
kusitisha utoaji
huduma
50. Mtoa huduma atakuwa na wajibu wa kuitaarifu Mamlaka pale ambapo
gari la abiria halitatoa huduma kwa kipindi kinachozidi siku thelathini.
Wajibu wa kufunga
na kutunza kifaa
maalumu cha
kufuatilia mwenendo
wa gari
51. Mtoa huduma wa gari la abiria atahakikisha kuwa:
(a) kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari kinafanya kazi vyema wakati
wote, kinatunzwa na kinalindwa dhidi ya mazingira hatarishi na
uharibifu wa makusudi wakati wote wa kutoa huduma; na
(b) hitilafu yoyote ya kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari inatolewa
taarifa kwa Mamlaka ndani ya saa kumi na mbili baada ya hitilafu
hiyo kutokea.
Mamlaka ya kuzuia
baadhi ya magari ya
abiria kutoa huduma
katika maeneo
maalum
52. Mamlaka inaweza:
(a) kuzuia aina fulani ya magari ya abiria kutoa huduma kwenye njia
yoyote, au maeneo ya jiji kati, manispaa au mji; na
(b) kuainisha maeneo ya jiji kati, manispaa au mji kulingana na wakati.
18
Mzigo uliosahaulika
kwenye gari la abiria 53. Endapo mzigo umeachwa na abiria kwenye gari la abiria, mtoa huduma
atahakikisha kwamba mzigo huo unahifadhiwa kwa ajili ya kuchukuliwa na
mmliki wake. Mamlaka ya
kusimamisha na
kukagua gari
54. Ofisa wa Mamlaka au Polisi anaweza:
(a) kusimamisha na kukagua gari la abiria wakati wowote au sehemu
yoyote ili kujiridhisha iwapo Kanuni hizi zinatekelezwa; au
(b) kutaka kukagua gari, kuonyeshwa leseni au nyaraka ya aina yoyote
ambayo inaweza kuhitajika kuwepo ndani ya gari la abiria. Upakaji rangi na
uwekaji matangazo
kwenye gari la abiria
55. Mtoa huduma hatapaka rangi au kuweka tangazo kwenye gari la abiria
ambalo:
(a) linaingiliana na rangi za utambulisho wa njia iliyopitishwa na Mamlaka;
au (b) linazuia abiria kuona vyema mandhari ya nje wakiwa ndani.
Wajibu wa kutoa
taarifa 56. Mtoa huduma ataitaarifu Mamlaka ndani ya siku thelathini kuhusu
mabadiliko ya anwani ya ofisi na taarifa nyingine zozote au mabadiliko ya
vigezo vyovyote vilivyotolewa wakati wa maombi ya leseni. Kuhamisha umiliki
au kuondoa gari
kwenye huduma
57. Endapo mtoa huduma anahamisha umiliki wa gari la abiria atatakiwa,
ndani ya siku saba, kutoa taarifa kwa Mamlaka.
Mapitio ya uamuzi
wa Mamlaka
58. Mtoa huduma ambaye hajaridhika na uamuzi wa Mamlaka uliotolewa
kwa mujibu wa Kanuni hizi anaweza, ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya
uamuzi, kuiomba Mamlaka ifanye mapitio ya uamuzi kwa mujibu wa Kanuni za
LATRA (Utaratibu wa Malalamiko na Mapitio). Masharti ya mpito na
yanayoendelea 59. Leseni zote, maelekezo au maelezo yaliyopitishwa au kutolewa kabla ya
kuanza kutumika kwa Kanuni hizi, yataendelea kuwa na nguvu ya kisheria hadi
pale leseni hizo, maelekezo au maelezo yatakapofutwa au kubatilishwa. Kufutwa kwa Kanuni
Tangazo la Serikali
Na. 421 la mwaka
2017.
60. Kanuni za Usafirishaji Abiria (Magari ya Abiria) za mwaka 2017
zimefutwa.
________
MAJEDWALI
________
19
_________
JEDWALI LA KWANZA
_________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6 (1))
_________
MAOMBI YA LESENI YA USAFIRISHAJI WA ABIRIA
Aina ya Maombi: Mpya Kuhuisha Kubadili njia
Muda Unaoombwa: Kubadili leseni Mwaka mmoja Muda mfupi
A. TAARIFA ZA MUOMBAJI WA LESENI
1. Jina Kamili …………...…………………………………………………………...............................................................................
(Jina/Kampuni/Wabia–kwa HERUFI KUBWA)
2. Anwani ya Posta …………………………………………………………………………………………………………………...
Namba ya Simu ya Mkononi ya Ofisi ……………………… Namba ya Simu
ya Mwombaji
……………………
Baruapepe: …………………………………………………………………………………………………………………………..
3. Anwani ya Mahali:
Mtaa: …………………………………... Namba ya Kiwanja: ………………….. Namba ya Ofisi:……........
4. Je, maombi yako ya leseni yamewahi kukataliwa/kusitishwa au kufutwa? Ndio: Hapana:
Kama ndio, eleza lini na wapi maombi yako ya siku za nyuma yalikataliwa, yalisitishwa au kufutwa…………………………..
Eleza sababu za maombi yako kukataliwa, kusitishwa au kufutwa……………………… na tarehe …………................................
5. Taarifa za Ofisa Usafirishaji au Msimamizi:
(a) Jina: ……………………………….…............................................................................................................................................
(b) Sifa ya Elimu: ……………………………………………………………………………………
(c) Namba ya Simu ya Mkononi:………………………………………………………………………
6. Taarifa ya Karakana ambapo magari yanafanyiwa/yatakuwa yakifanyiwa matengenezo:
(a) Jina la Karakana: …………………………………………………………………………………...............................
(b) Anwani ya Mahali:……………………………………………………………………………………………………
(c) Jina na sifa ya elimu ya Msimamizi wa Karakana: …………………………………………………………………………
B. TAARIFA ZA GARI LINALOOMBEWA LESENI
1. Orodha ya magari (iambatishwe endapo ni taasisi iliyosajiliwa)
2. Namba ya usajili wa gari (endapo ni mtu binafsi):…………………………………………………………………………………..
3. Aina: ……………………………………………………………………………………………………………………….............
4. Uwezo wa gari (idadi ya juu ya abiria wanaoruhusiwa) ……………………………………..……………………………………
5. Madaraja ya huduma:
Kawaida Others (specify)……………………… Daraja la Kati Chini Daraja la Kati Juu Daraja la Starehe
C. TAARIFA ZA HUDUMA INAYOOMBEWA LESENI
1. Maeneo ya njia ambayo au ambapo huduma inatarajiwa kutolewa .……………………………………...........................................
2. Jinsi/Aina ya huduma (weka ( √ ) inapostahili)
Kati ya Mji na Mji Daladala Basi la Shule Nje ya nchi
Basi la wafanyakazi Kijijini-mjini-kijijini Binafsi ya kukodi Utalii
Aina nyingine (Ainisha)………………………………………………
3. Ratiba inayopendekezwa:
Safari ya kwenda: ……………….……………………………….…... Safari ya kurudi: …………………………..…………..
Jedwali la nauli inayopendekezwa kwa huduma ya Daraja la Starehe:
Tshs. ………………… kwa kila safari
D. NYARAKA ZA KUWASILISHA WAKATI WA KUOMBA LESENI
1. Maombi ya kwanza yataambatishwa na vitu vilivyoorodheshwa chini:
(a) Kadi ya Usajili wa Gari,
(b) Cheti Safi cha Mlipa kodi,
(c) Taarifa ya Ukaguzi wa Gari, na
(d) Cheti cha Kusajiliwa (endapo ni taasisi iliyosajiliwa).
2. Maombi ya kuhuisha yataambatishwa na vitu vilivyoorodheshwa chini:
(a) Taarifa ya Ukaguzi wa Gari, na
20
(b) Cheti Safi cha Mlipa kodi.
3. Mamlaka inaweza kuhitaji taarifa zaidi au nyaraka wakati wowote.
Mimi/Sisi nina/tunatamka kuwa kwa mujibu wa ufahamu/uelewa wangu/wetu na nina/tunaamini taarifa zote
zilizotolewa kwenye maombi haya ni za kweli.
Jina Kamili: ………………………………………………………....... Saini:……...……………………................
Cheo ………………………………………………………………….. Tarehe:.…………………………...............
KWA MATUMIZI YA OFISI TU
4. Uhakiki na Uidhinishaji
(a) Hayajaidhinishwa:
Toa sababu ……………………………………………………………
(b) Yameidhinishwa:
Tarehe ya Kuanza: …………………………………………………… Tarehe ya Mwisho: …………………........
Jina kamili la la Ofisa : ……………………………………………………………………………………………………………..
Cheo: …………………………………………………………….
Saini: ………………………………………………………………….
Tarehe : ……………………………………………………………….
Kiasi kilicholipwa: ………………..………………………………….. Stakabadhi Na. …………………………..
Tarehe:...……………………………………………………………..
Saini:………………………...…………….
NAMBA YA JALADA LA MTOA HUDUMA………………... NAMBA YA LESENI …………….……..
UTAMBULISHO WA NJIA .…………………………………...
Kanuni za Leseni ya Usafirishaji (Magari ya Abiria) za Mwaka, 2019
TAHADHARI:
1. Kutoa taarifa ya uongo kwa kujua kwa ajili ya kupatiwa leseni ni kosa la jinai chini ya Sheria ya
LATRA Mwaka 2019.
2. Mabadiliko yoyote ya taarifa zilizotolewa kwenye Fomu hii yanapaswa kuwasilishwa LATRA
vinginevyo utakuwa unafanya kosa la jinai chini ya Kanuni hizi.
21
________
JEDWALI LA PILI
_________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14(1)
_________
ADA ZA LESENI ZA MAGARI YA ABIRIA
KWA HUDUMA ZA NDANI YA NCHI KWA HUDUMA ZA NJE YA NCHI
NA KWA UTALII
UWEZO WA KUBEBA
ABIRIA
ADA YA MWAKA
(TSHS)
ADA YA MIEZI
MITATU (TSHS)
ADA YA
MWAKA
(US$)
ADA YA MIEZI
MITATU (US$)
BASI LA KAWAIDA NA KATI CHINI
Watu wasiozidi 15 35,000 17,500 50 15
Watu 15 lakini wasiozidi
watu 25 70,000 35,000 80 20
Watu 25 lakini wasiozidi
watu 45 110,000 55,000 145 35
Watu 45 lakini wasiozidi
watu 65 130,000 65,000 150 40
Watu 65 na zaidi 150,000 75,000 160 45
Ada ya fomu ya maombi 10,000 10,000 10 10
Ada ya kubadilisha njia
Asilimia hamsini (50%) ya ada ya leseni
BASI LA DARAJA LA KATI JUU NA STAREHE
Linalozidi watu 25 200,000 100,000 180 60
Ada ya maombi 10,000 10,000 10 10
Tozo ya kubadilisha njia Asilimia hamsini (50%)
ya ada ya leseni
ADA NYINGINEZO
Kwa nakala ya leseni au uidhinishwaji wa leseni iliyopotea, iliyoharibika au kuchafuliwa 20,000/=
Kwa ajili ya kutoa ratiba 10,000/=
Kwa ajili ya batli 10,000/=
22
________
JEDWALI LA TATU
_________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya ……..
_________
TOZO YA UDHIBITI
1. Tozo kwa leseni ya kawaida itakuwa ni asilimia moja (1%) ya pato ghafi inayotokana na utoaji
huduma za usafirishaji abiria.
2. Tozo kwa kampuni yenye leseni
maalumu itakuwa ni
asilimia moja (1%) ya pato ghafi inayotokana na utoaji
huduma za usafirishaji abiria.
23
JEDWALI LA NNE
_________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 23(1)(h) )
_________
MADARAJA YA MAGARI
NA. VIWANGO
VILIVYOKUBALIKA
DARAJA LA
KAWAIDA
DARAJA LA KATI
CHINI
DARAJA LA KATI
JUU
DARAJA LA
STAREHE
1. Kiwango cha juu cha
urefu wa basi
14m 14m 14m 14m
2. Kiwango cha juu cha
upana wa basi
2.6m 2.6m 2.6m 2.6m
3. Kiwango cha juu cha
kimo cha basi likiwa
limejaza abiria au
likiwa halina abiria
4.6m 4.6m 4.6m 4.6m
4. Uwezo wa kubeba
abiria kwa basi lenye
urefu wa 12.5m
Kiwango cha juu cha
uwezo wa kubeba
abiria kitakuwa ni
abiria 65 ikiwa ni
pamoja na dereva
Kiwango cha juu cha
uwezo wa kubeba
abiria kitakuwa ni
abiria 60 ikiwa ni
pamoja na dereva
Kiwango cha juu cha
uwezo wa kubeba
abiria kitakuwa ni
abiria 60 ikiwa ni
pamoja na dereva
Kiwango cha juu
cha uwezo wa
kubeba abiria
kitakuwa ni abiria
51 ikiwa ni
pamoja na dereva
5. Mahitaji ya viti
Pale ambapo viti
vimepangwa kuelekea
upande mmoja na
umbali wa ulalo kwa
mbele na nyuma
haupungui 680mm viti
vya abiria havitakiwa
kurekebishwa
(a) Viti vyote vya
abiria viwe
vinaweza
kurekebishika
(b) Pale ambapo viti
vimeelekea
upande mmoja,
umbali chini wa
ulalo kati ya
sehemu ya mbele
na sehemu ya
nyuma ya kiti
lazima
usipungue 690
mm
(a) Viti vyote vya
abiria lazima
viwe katika hali
inayoweza
kurekebishika
(b) Pale ambapo viti
vimeelekea
upande mmoja,
umbalichini wa
ulalo kati ya
sehemu ya mbele
na sehemu ya
nyuma ya kiti
lazima
usipungue 690
mm
(a) Viti vyote
vya abiria
lazima viwe
katika hali
inayoweza
kurekebishika
(b) Pale ambapo
viti
vimeelekea
upande
mmoja,
umbali chini
wa ulalo kati
ya sehemu ya
mbele na
sehemu ya
nyuma ya kiti
lazima
usipungue
690 mm
6. Mpangilio wa viti kwa
ajili ya mabasi
makubwa
3x2 au 2x2 2x2 2x2 2x2
7. Mikanda ya viti Viti vyote vya abiria
ikiwa ni pamoja na kiti
cha dereva lazima viwe
na mikanda ya viti
Viti vyote vya abiria
ikiwa ni pamoja na
kiti cha dereva lazima
viwe na mikanda ya
viti
Viti vyote vya abiria
ikiwa ni pamoja na
kiti cha dereva lazima
viwe na mikanda ya
viti
Viti vyote vya
abiria ikiwa ni
pamoja na kiti cha
dereva lazima
viwe na mikanda
ya viti
24
8. Taa za ndani Idadi ya chini ya taa
tatu ndani ya basi ziwe
katika umbali sawa
sambamba na njia ya
kupita ndani ya basi
Pamoja na taa zote
zilizopo katika gari la
kawaida, kila kiti cha
abiria lazima kiwe na
taa yake
Pamoja na taa zote
zilizopo katika gari la
kawaida, kila kiti cha
abiria lazima kiwe na
taa yake
Pamoja na taa
zote zilizopo
katika gari la
kawaida, kila kiti
cha abiria lazima
kiwe na taa yake
9. Viyoyozi Hakuna kiyoyozi Hakuna kiyoyozi Muhimu Muhimu
10. Luninga Hakuna luninga Lazima kuwa na
angalao luninga mbili
(kwa mabasi
makubwa)
Lazima kuwa na
angalao luninga mbili
(kwa mabasi
makubwa)
Lazima kuwa na
angalao luninga
mbili (kwa mabasi
makubwa)
11. Redio na redio ya
muziki
Sio lazima Gari lazima iwekewe
redio na redio ya
muziki
Gari lazima iwekewe
redio na redio ya
muziki
Gari lazima
iwekewe redio na
redio ya muziki
12. Kipaza sauti Muhimu Muhimu Muhimu Muhimu
13. Mapazia ya madirisha Sio lazima Muhimu Muhimu Muhimu
14. Msalani/chumba cha
mapumziko
Hakuna huduma za
msalani
Hakuna huduma za
msalani
Hakuna huduma za
msalani
Muhimu
15. Kipasha joto Sio lazima Sio lazima Sio lazima Lazima kuwe na
kipasha joto kwa
ajili ya
kuchemshia maji
au kupasha moto
vinywaji kama
vile kahawa, chai
nk
16. Jokofu /sanduku la
baridi
Sio lazima Sio lazima Sio lazima Lazima kuwe na
jokofu na
/sanduku la baridi
17. Vinywaji baridi Sio lazima Sio lazima Sio lazima Lazima huduma
ya vinywaji baridi
itolewe
25
JEDWALI LA TANO
________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 33(1))
________
MFANO WA TIKETI YA GARI LA ABIRIA
MABASI YA MASAFA MAREFU
NEMBO YA KAMPUNI
Namba: .....................
Jina la Kampuni: ……………………………………………………………………………………………….
Anuani ya Mmiliki…………….............................................................................................................................
Namba ya Basi: ……………. Njia ya Safari: …..…………….... Tarehe ya kuandikwa tiketi ...........................
Jina la Abiria………………………………………… Kuanza safari saa…………………………………….
Namba ya kiti ……………………………………….. Kuwasili kituoni saa ………………………………....
Kituo cha kuanzia safari ni .......................................... Kuelekea ......................................................................
Tarehe ya safari………………………………………
Nauli ni Shillingi ……………………………………
Muda wa kuanza safari: …………………………….. Tarehe ya Safari: …...………………………………..
MABASI YA MIJINI
Nembo ya Kampuni/Mmiliki (kama ipo) ……………………………….………………………………………
Namba ya Usajili wa Gari ……………………….…. Jina na Anuani ya Mmiliki...…………………………
Njia…………………………………………………... Nauli iliyoidhinishwa ya Shilingi …………………..
Tarehe ya Kutolewa …………….………………….
26
JEDWALI LA SITA
________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 34(1))
________
MFANO WA ORODHA YA ABIRIA WANAOSAFIRI
NEMBO YA KAMPUNI Namba: .....................
ORODHA YA ABIRIA WANAOSAFIRI
Jina la Kampuni: ………………………………………………………………………………………………………….
Jina la Mmiliki: ………………………….............................................................................................................................
Anwani ya Mmiliki: ……………………………………………………………………………………………….……….
Namba ya Basi: …………………………. Njia ya Safari: …..……………………………………...............................
Muda wa kuanza safari: ………………… Tarehe ya Safari: …………………………………………………………..
Na. Jina Kamili la
Abiria
Uraia Namba ya
Simu ya
Mtu wa
karibu
Namba ya
Kiti
Kituo cha
kuanza
safari
Kituo
anachokwenda
Kiwango cha
Nauli
1.
2.
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
11.
12.
13.
14.
15.
16.
17.
18.
19.
20.
↓
Jumla ya Abiria: …………………………………………………………………………………………………………
Jina la Dereva (1): ….…………………….. Namba ya Leseni: ………………………… Saini: .…………………....
Jina la Dereva (2): …………..……………. Namba ya Leseni: …………………………Saini: …………………….
Jina la Kondakta: ………………………………………………………………………… Simu: ……………………..
27
JEDWALI LA SABA
_________
( Limetengenezwa chini ya kanuni ya 45)
_________
MAKOSA NA ADHABU ZINAZOFIFISHWA NA LATRA
NA. AINA YA KOSA KANUNI KIASI
KILICHOFIFISHW
A NA LATRA
MAKOSA YA JUMLA KWA AINA ZOTE ZA MAGARI
1. Kutoa huduma ya kusafirisha abiria bila kuwa na leseni
halali ya LATRA.
4 250,000/=
2. Kushindwa kubandika leseni sehemu ya wazi upande wa
kushoto wa kioo cha mbele cha gari la abiria.
18(1) & (2) 100,000/=
3. Kushindwa kuzingatia vigezo vya utendaji vilivyowekwa na
Mamlaka.
19 (1) 100,000/=
4. Kushindwa kwa Taasisi iliyosajiliwa atawasilisha Taarifa
ya Mwaka ya Utendaji kwa Mamlaka; au
19 (2) (a) 100,000/=
5. Kutumia gari jingine bila kuwa na kibali cha dharura pale
gari la abiria la njia husika linapoharibika
22 (1) 100,000/=
6. Kuendesha gari la abiria likiwa na hitilafu; 23 (1) (a) 250,000/=
7. Kushindwa kuzingatia idadi ya abiria, uzito na upakiaji wa
mizigo, uzito wa gari na mwendo kama vilivyoainishwa
kwenye Sheria nyingine za nchi.
23 (1) (b)
250,000/=
8. Dereva mmoja wa gari la abiria kuendesha gari mfululizo
zaidi ya saa nane. 23 (1) (c) 250,000/=
9. Kushindwa kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa
sahihi za biashara ya usafirishaji wa abiria. 23 (1) (d) 250,000/=
10. Kuendesha gari la abiria bila kuwa na kisanduku cha
huduma ya kwanza, kilichowekwa mahali panapoonekana,
kilicho na dawa na vifaa tiba vilivyoainishwa.
23 (1) (e) 250,000/=
11. Kushindwa kuweka chombo cha taka kwenye gari la abiria
na kushindwa kutupa taka kwenye maeneo maalum. 23 (1) (f) 250,000/=
12. Kushindwa kuzingatia viwango vya gari la abiria kama
vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne. 23 (1) (h) 250,000/=
13. Kubeba mzigo hatarishi kwenye gari la abiria. 23 (2) (a) 250,000/=
14. Kubeba abiria zaidi ya idadi ya watu iliyobainishwa kwenye
leseni. 23 (2) (b) 100,000/=
15. Kuruhusu au kuacha watu kupanda ndani ya gari la abiria
kufanya biashara, kuhubiri au siasa na kuweka burudani,
kuonyesha picha au kupiga mziki kwenye gari la abiria
wakati wa safari ambazo haziendani na maadili na tamaduni
za Kitanzania na kwa sauti ya juu.
23 (2) (c) 100,000/=
16. Kushindwa kutekeleza Kanuni hizi, Sheria ya Usalama
Barabarani na sheria nyinginezo za nchi. 23 (2) (d) 100,000/=
MAKOSA YA USAFIRISHAJI WA ABIRIA WA MIJINI
17. Kutotoa tiketi ya safari kwa abiria. 24 (1) (a) (ii) 100,000/=
18. (
a
)
Mtoa huduma kutopaka rangi ya utambulisho wa njia
iliyopitishwa na Mamlaka au kupaka rangi au kuweka
matangazo kwenye gari la abiria ambayo yanaingiliana na
rangi au inazuia abiria kuona vyema mandhari ya nje akiwa
ndani.
24(1)(a)(iii) 100,000/=
28
19. Kutoa huduma ya kusafirisha abiria bila kuandika nauli
iliyoidhinishwa na Mamlaka karibu na mlango wa kuingilia
abiria.
24 (1) (a)
(iv) 100,000/=
20. Mfanyakazi wa gari la abiria linalotoa huduma ya usafiri wa
mjini kutovaa sare safi au nadhifu kama ilivyoidhinishwa na
Mamlaka.
24 (1) (b) (i) 100,000/=
21. Mfanyakazi wa gari la abiria kuruhusu mtu kufanya
biashara, kuhubiri, kufanya shughuli za siasa au kutoa
burudani ambayo inakiuka kanuni ya 23 (2) (c) ndani ya gari
la abiria mijini;
24 (1) (b)
(ii) 100,000/=
22. Mfanyakazi wa gari la abiria kutoa huduma ya usafirishaji
abiria kwenye njia ambayo haijaidhinishwa kwenye leseni.
24 (1) (b)
(iii) 100,000/=
23. Mfanyakazi wa gari la abiria gari kubadilisha njia au
kusitisha safari kabla ya kufika mwisho wa kituo kama
ilivyooneshwa kwenye tiketi ya abiria.
24 (1) (b)
(iv) 100,000/=
MAKOSA KWA MAGARI YATOAYO HUDUMA KATI YA MJI NA MJI NA NCHI NA NCHI
24. Kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa gari ambalo
halina vigezo vya madaraja ya mabasi ya abiria
vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne la Kanuni hizi;
25 (a) (ii) 250,000/=
25. Kutoa huduma ya kusafirisha abiria kati ya mji na mji
au nchi na nchi kwa gari ambalo halijafungwa kifaa
maalum kilichoidhinishwa na Mamlaka kwa ajili ya
kufuatilia mwendo wa gari;
25 (a) (iii) 250,000/=
26. Kutoa huduma ya gari la abiria bila kuzingatia batli,
ratiba na chati ya nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka; 25 (a) (iv) 100,000/=
27. Kutoa huduma ya kusafirisha abiria bila gari kuwa na
mikanda inayofanya kazi na safi kwa kila kiti cha
abiria;
25 (a) (v) 100,000/=
28. Mfanyakazi wa gari la abiria kutovaa sare safi na
nadhifu kama ilivyoamuliwa na Mamlaka. 25 (b) (i) 100,000/=
29. Mfanyakazi wa gari la abiria kutouza tiketi halali ya
basi kwa mfumo wa karatasi au kielektroniki na
kutotolewa kwa abiria.
25 (b) (ii) 100,000/=
30. Mfanyakazi wa gari la abiria kuruhusu mtu kufanya
biashara, kuhubiri, kufanya shughuli za siasa au kutoa
burudani ambayo inakiuka kanuni ya 23 (2) (c) ndani
ya gari la abiria.
25 (b) (iii) 100,000/=
31. Mfanyakazi wa gari la abiria kutozingatia batli, ratiba
na chati ya nauli iliyoidhinishwa na Mamlaka. 25 (b) (iv) 100,000/=
32. Mfanyakazi wa gari la abiria kushindwa kuwa na
nakala tatu za orodha ya abiria kwa kila safari ambapo
nakala moja itabaki katika gari la abiria, nakala
nyingine itawasilishwa kituo cha polisi na nakala
nyingine itaachwa kwenye ofisi za mtoa huduma.
25 (b) (v) 100,000/=
33. Wafanyakazi wa gari la abiria kutoa huduma ya usafiri
bila kuvaa vitambulisho vinavyonekana kwa urahisi
kwa mtu yeyote wakati wa safari.
25 (b) (vi) 100,000/=
34. Mfanyakazi wa gari la abiria kutoa huduma kwenye
njia ambayo haijaidhinishwa kwenye leseni; 25 (b) (viii) 100,000/=
35. Mfanyakazi wa basi la abiria kukatisha safari kabla ya
kufika kituo cha mwisho wa safari kama
inavyoonekana kwenye tiketi ya abiria.
25 (b) (ix) 100,000/=
36. Mtoa huduma na mfanyakazi wa gari linalotoa huduma
kati ya nchi na nchi lenye usajili wa nchi nyingine
kutoa huduma za usafirishaji abiria kama gari
lililosajiliwa nchini na linalotoa huduma za ndani.
26 250,000/=
29
MAKOSA KWA MAGARI YA SHULE
37. Mtoa huduma wa basi la shule kutoa huduma ya
usafirishaji gari likiwa na itilafu. 27 (1) (a) 250,000/=
38. Kutoa huduma ya usafiri wa basi la shule lisilokidhi
viwango vya Usalama na Ubora wa Huduma
usafirishaji magari ya abiria
27 (1) (b) 250,000/=
39. Kutoa huduma ya usafiri wa basi la shule bila kupakwa
rangi ya njano yenye namba Rgb (255,255,0) na
kuandikwa maneno “School Bus” au “Basi la Shule”.
27 (1) (d) 100,000/=
40. Mfanyakazi wa basi la shule kubeba wanafunzi zaidi
ya idadi iliyoandikwa kwenye leseni. 27 (2) (a) 100,000/=
41. Mfanyakazi wa basi la shule kuruhusu upakiaji kupita
uwezo wa gari na mwendo wa gari kinyume na
viwango vilivyoainishwa kwenye sheria nyingine;
27 (2) (b) 100,000/=
42. Kuendesha basi la shule bila kuwa na kisanduku cha
huduma ya kwanza kilichowekwa mahali
panapoonekana, kilicho na dawa na vifaa tiba
vilivyoainishwa.
27 (1) (e) 100,000/=
43. Mfanyakazi wa basi la shule atashindwa kuvaa sare
safi na nadhifu kama Shule itakavyoamua. 27 (2) (c) 100,000/=
44. Mtoa huduma na mfanyakazi wa basi la shule
atashindwa kuweka chombo cha taka kwenye gari na
taka zinazokusanywa na zinatupwa kwenye maeneo
maalum ya kutupa taka; na
27 (2) (d) 100,000/=
MAKOSA YA JUMLA KWA MABASI YA ABIRIA
45. Mtoa huduma hatatoza nauli zaidi ya ile
iliyoidhinishwa na Mamlaka kulingana na daraja la
basi husika.
31 250,000/=
46. Mtoa huduma atarudisha kiwango cha nauli iliyolipwa
pale ambapo wekesho la tiketi litafutwa kwenye muda
usiozidi saa ishirini na nne na si chini ya saa kumi na
mbili kabla ya muda uliopangwa kabla ya safari
kuanza:
33 (6) (7) 100,000/=
47. Mtoa huduma kushindwa kuandaa orodha ya abiria
wanaosafiri kama ilivyoelekezwa na Mamlaka na kwa
kuzingatia Jedwali la Sita la Kanuni hizi.
34 (1) (3) 100,000/=
48. Kama mtoa huduma atashindwa kutoa huduma ya
usafiri kwa abiria ambaye amekwisha kupewa tiketi
atawajibika kwa mujibu wa vigezo na masharti ya
tiketi na ratiba ya safari.
36 (1) (2) 100,000/=
49. Mtoa huduma atakayemtoza nauli mwanafunzi
atakayepanda gari la abiria linalotoa huduma ya usafiri
ndani ya mji kwa kiwango cha nauli kisichoidhinishwa
na Mamlaka.
37 (1) 100,000/=
50. Mtoa huduma atakayetoza malipo ya kusafirisha mzigo
wa abiria wenye uzito usiozidi kilo ishirini. 38 (1) 100,000/=
51. Mtoa huduma atakayetoza malipo kwa vifaa saidizi
vinavyotumiwa mtu mwenye ulemavu wa viungo kwa
ajili ya kutembea wakati anaposafiri kwenye gari
linalotoa huduma kati ya mji na mji au nchi na nchi.
38 (1) (b) 100,000/=
52. Kushindwa kuweka alama kwenye mzigo wa abiria
inayotambulisha jina la abiria na kituo cha mwisho wa
safari ya abiria
40 100,000=
53. Mtoa huduma atakayeshindwa kutoa taarifa kwa
Mamlaka pale ambapo gari la abiria halitoi huduma
kwa kipindi kinachozidi siku thelathini.
51 250,000/=
54. Mtoa huduma wa gari la abiria atakaeshindwa 52 (a) (b) 250,000/=
30
kuhakikisha kuwa:
(a) kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari kinafanya
kazi vyema wakati wote, kinatunzwa na kinalindwa
dhidi ya mazingira hatarishi na uharibifu wa makusudi
wakati wote wa kutoa huduma; na
(b) hitilafu yoyote ya kifaa cha kufuatilia mwenendo
wa gari inatolewa taarifa kwa Mamlaka ndani ya saa
kumi na mbili baada ya hitilafu hiyo kutokea.
55. Mtoa huduma atakayepaka rangi au kuweka tangazo
kwenye gari la abiria linaloingiliana na rangi za
utambulisho wa njia iliyoidhinishwa na mamlaka.
57 100,000/=
56. Mtoa huduma atakayeshindwa kuitaitaarifu Mamlaka
ndani ya siku thelathini kuhusu mabadiliko ya anwani
ya ofisi na taarifa nyingine zozote au mabadiliko ya
vigezo vyovyote vilivyotolewa wakati wa maombi ya
leseni.
58 100,000/=
31
__________
JEDWALI LA NANE _________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 46) __________
HATI YA MAKOSA NA UTEKELEZAJI WAKE KWA DEREVA
SEHEMU YA I: TAARIFA YA KOSA
Kwa: .…………………………………………………………………………………
Anwani: ……………………………………………………………………………………
1. ……………………..………………………………………………… Mwenye Leseni ya Udereva Na. …………
Daraja …………… dereva wa gari la abiria lenye Namba za Usajili Na. ……………. Unatuhumiwa kwa
kosa/makosa dhidi ya kanuni namba ……………………………………………………..
Taarifa ya kosa:
Kwamba …..………… siku ya …….……………. mwaka………………………………
kwenye eneo la ………………………………. wewe (maelezo mafupi kuhusu kosa):
……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………… 2. Iwapo HUKUBALI kuwa umefanya kosa/makosa, jaza Sehemu “A” ya fomu hii ya makosa.
3. Iwapo UNAKUBALI kuwa umetenda kosa/ makosa, jaza Sehemu “B” ya fomu hii ya Makosa.
4. Kiasi cha kufifisha makosa KITALIPWA Benki kwenye akaunti ya LATRA namba ……………….
SEHEMU YA II: TAARIFA YA DEREVA
SEHEMU A: NIA YA KWENDA MAHAKAMANI
Mimi …………………………………………………..………… wa (anuani ya eneo la makazi au biashara)
…………………………………………..…..…………………….. nina nia ya kujitetea Mahakamani dhidi ya kosa
nililotuhumiwa nalo la ……………………………………………… kinyume na kanuni ya ………………….. ya
Kanuni za Leseni ya Usafirishaji (Magari ya Abiria), za mwaka 2019.
Jina: …………………………...…………………………………………………………………..
Sahihi: …………………………...…………………………………………………………………..
SEHEMU B: KUKIRI KOSA
Mimi …………………………………………………..………… wa (anuani ya eneo la makazi au biashara)
…………………………………………..…..…………………….. nakiri kosa la
……………………………………………………………… kinyume na kanuni ya ………………….. ya Kanuni za
Leseni ya Usafirishaji (Magari ya Abiria), za mwaka 2019.
Ninaomba kosa lififishwe kwa mujibu wa kanuni ya ………… ya ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji (Magari ya
Abiria), za mwaka 2019.
Nitalipa faini ya Tshs……………………..ndani ya siku kumi na nne (14) tangu tarehe ya kupokea taarifa ya kosa
kama kiasi cha kufifisha kosa.
Jina: ………………………………………………………………………………………………….
Sahihi: ………………………………………………………………………………………………….
Na. ya
Kitambulisho:
………………………………………………………………………………………………….
Imetolewa na: Mkoa: Imeshuhudiwa na:
32
______________
JEDWALI LA TISA
_________
(Limetengenezwa chini ya kanuni ya 46) ______________
HATI YA MAKOSA NA UTEKELEZAJI WAKE KWA MTOA HUDUMA
SEHEMU YA I: TAARIFA YA KOSA Kwa: .…………………………………………………………………………………
Anwani: ……………………………………………………………………………………
1. Unashitakiwa kwa kosa la …………………………………………………..
Taarifa ya kosa/makosa dhidi ya kanuni namba:
Kwamba …..……… siku ya ……………………… mwaka…………………
kwenye eneo la ……………………………… wewe (maelezo maupi kuhusu kosa):
(a) ……………………………………………………………………………………….
(b) ……………………………………………………………………………………….
(c) ……………………………………………………………………………………….
(d) ……………………………………………………………………………………….
2. 2
.
Iwapo HUKUBALI kuwa umefanya kosa/makosa, jaza Sehemu III “A” ya fomu hii ya makosa.
3. 3
.
Iwapo UNAKUBALI kuwa umetenda kosa/ makosa, jaza Sehemu III “B” ya fomu hii ya Makosa.
4. 4
.
Kiasi cha kufifisha makosa KITALIPWA Benki kwenye akaunti ya LATRA namba ……………….
SEHEMU YA II: TAARIFA YA DEREVA
Mimi …………………………………………………..………… Mwenye Leseni ya Udereva Na. ………… Daraja
…………… dereva wa gari la abiria lenye Namba za Usajili Na………………….ninayefanya biashara
kama…………………… ninakiri kupokea Taarifa ya Kosa Na. ………… kwa kosa na. ……………. Ninachukua
jukumu la kuwasilisha Taarifa hii ya kosa kwa mtoa huduma wa gari lililotajwa hapo.
Sahihi: ……………………………….……………… Tarehe: ………………………………..……………...
Jina la Shuhuda: ……………………………….…… Signature: ..………………………..………………….
Tarehe: ……………………………….……………… Mkoa: ……………………………….………………..
SEHEMU YA II: TAARIFA YA MTOA HUDUMA
SEHEMU A: NIA YA KWENDA MAHAKAMANI
Mimi …………………………., mtoa huduma wa gari lenye namba za usajili ……………………..……… wa (anuani
ya eneo la makazi au biashara) ……………………………….…..…………………….. ninakiri kupokea Taarifa ya
kosa na nina nia ya kujitetea Mahakamani dhidi ya kosa nililotuhumiwa nalo la
……………………………………………… kinyume na kanuni ya ………………….. ya Kanuni za Leseni ya
Usafirishaji (Magari ya Abiria), za mwaka 2019.
Jina: …………………………...…………………………………………………………………………...
Sahihi: …………………………...…………………………………………………………………………...
SEHEMU B: KUKIRI KOSA
Mimi ………………………………………, mtoa huduma wa gari la abiria lenye namba za usajili
…………………..………… wa (anuani ya eneo la makazi au biashara)
…………………………………………..…..…………………….. nakiri kupokea Taarifa ya kosa na nnakiri kutenda
kosa hilo …………………………………………… kinyume na kanuni ya ………………….. ya Kanuni za Leseni ya
Usafirishaji (Magari ya Abiria), za mwaka 2017.
Ninaomba kosa lififishwe kwa mujibu wa kanuni ya ………… ya ya Kanuni za Leseni ya Usafirishaji (Magari ya
Abiria), za mwaka 2017.
Nitalipa faini ya Tshs……………………..ndani ya siku kumi na nne (14) tangu tarehe ya kupokea taarifa ya kosa
kama kiasi cha kufifisha kosa.
Jina: ………………………………………………………………………………………………………..
Sahihi: ………………………………………………………………………………………………………..
Na. ya
Kitambulisho:
………………………………………………………………………………………………………..
Imetolewa na: