taarifa ya mwaka 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. huu ulikuwa mwaka wa...

3

Upload: others

Post on 29-Feb-2020

17 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 1

TAARIFA YA MWAKA 2017Kuwezesha wananchi kupitia uimarishaji wa asasi za kiraia (AZAKI)

Page 2: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 20172

Page 3: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 1

YALIYOMO

Mwaka 2017 katika picha

Kuunga mkono kazi ya Taasisiya Mifupa ya MOI

Wajumbe wa jukwaa la hakiardhi la wanawake huko Oldoinyo Sambu, Arusha

#JumanneYaUtoaji mwaka 2017 katika Taasisi ya Mifupa ya MOI

Kuhusu Foundation for Civil Society 2

Ujumbe wa Mwenyekiti wa Bodi 3

Ujumbe wa Mkurugenzi Mtendaji 5

Ripoti ya Miradi 7

Matokeo ya Kujenga Uwezo 24

Ripoti za Fedha 30

Utawala 33

Tunahitaji kuwalinda watotowenye ulemavu

Page 4: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 20172

Historia Yetu Foundation for Civil Society (FCS) ni taasisi huru ya maendeleo ya Kitanzania ambayo inatoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa asasi za kiraia nchini Tanzania. FCS ilisajiliwa mwezi Septemba 2002 na kuanza kufanya shughuli zake mwezi Januari 2003. Kwa miaka 15 FCS imeziwezesha zaidi ya asisi 5,000 za kiraia kwenye mikoa yote ya Tanzania, Bara na Zanzibar, kwa kuzijengea uwezo na rasilimali za kuwafikia zaidi ya wananchi milioni 31. Hivi sasa, FCS ni mojawapo wa vyanzo vikuu na vikubwa vya utoaji wa fedha kwa Asasi za Kiraia za Tanzania. Utoaji huu ni miongoni mwa ufadhili mkubwa kabisa wa aina yake kusini mwa Jangwa la Sahara.

Falsafa YetuFCS ina maoni kwamba umasikini, ukosefu wa haki na makundi ya jamii kukosa uwezo wa kupata haki, rasilimali na fursa kama adui kubwa zaidi wa binadamu leo. Tunaamini kuwa ushirikiano wa umma wenye ufanisi katika kuleta maendeleo na utaratibu wa utawala ni muhimu katika kuiondosha jamii kuondoka na na mateso hayo. Kwa hiyo tunawekeza katika kuwawezesha watu kuwa na sauti kubwa zaidi kwenye masuala ya washiriki muhimu, wakiwa ndio msingi wa kuleta maendeleo yao ya kiuchumi. Hasahasa tumejitoa katika kuhakikisha kuwa watu wanakuwa ndiyo lengo, wala si watumishi wa maendeleo yao wenyewe. Tunashiriki na kuchangia kwenye uimarishaji jamii na serikali, kama mojawapo ya njia za uhakika za jumuiya ya kiraia kuharakisha na kuchochea maendeleo na kushughulikia mifumo na miundo inayozuia ustawi wa binadamu.

KUHUSU FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Tunu Zetu1. Ushiriki2. Uadilifu3. Kujifunza na Ustadi4. Uwajibikaji5. Usawa wa Jinsia

Wito WetuKuchangia kwenye kuleta maendeleo endelevu nchini Tanzania kupitia uimarishaji wa asasi za kiraia, ushawishi wa sera na kuimarisha utamaduni wa kujielimisha.

Maono YetuKwamba Watanzaniawaliowezeshwa na wanaowajibikawanapata haki za kiuchumi nakijamii na maisha bora.

Page 5: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 3

Mwaka 2017 ulitawaliwa na maboresho ya utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada zetu na kujitoa kwetu katika kuimarisha jamii za kiraia nchini Tanzania, nafurahi kutambua kwamba tunaendelea kujenga jamii ya Kitanzania yenye nguvu na haki ambayo imewezeshwa. Kimsingi, lengo letu ni kuboresha maisha ya watu wote. Mtazamo wetu wa mwaka ujao utakuwa kuimarisha mafanikio ya miaka miwili iliyopita baada ya kuvuka hatua za kati za mkakati wetu.

Utendaji wetu mwaka wa 2017 ulipewa msukumo mkubwa na utaratibu wetu thabiti wa uteuzi wa wapokea ruzuku, usimamizi wa karibu, ufuatiliaji na uhakiki wa matokeo, na muhimu zaidi, uhusiano mwema, utendaji kazi kwa ushirikiano na Mamlaka za Serikali za mitaa, AZAKI na jumuiya tulizounga mkono mipango yao ya maendeleo. Tumepiga hatua kubwa katika kuimarisha ushiriki wa wananchi katika utawala wa kidemokrasia, uwajibikaji na ufuatiliaji wao wa sekta muhimu za kijamii kama vile maji, elimu na kilimo pamoja na uwazi kwenye Halmashauri na jamii mbalimbali.

Uhusiano na serikali Mwaka uliopita, tumeshuhudia uwepo wa asasi

za kiraia zilizo makini zaidi, hali iliyochangia kwenye utendaji wa AZAKI za hapa nchini. Kama kawaida, FCS iliendelea kutoa usaidizi usioelemea upande wowote ili kufanikisha ushiriki mkubwa zaidi na majadiliano miongoni mwa wadau wa serikali na wale wasiokuwa wa serikali (asasi za kiraia), pamoja na mikakati yao ya maendeleo.

Kulingana na mazingira haya, FCS inaendelea kuziweka wazi shughuli zake na kufanya kazi bega kwa bega na serikali. Ofisi ya Msajili wa Asasi za Kiraia inafahamu vema shughuli za FCS na mara nyingi imealikwa kwenye ziara zote za kutembelea miradi.

Mabadiliko kwenye Bodi na Utawala Prof Honest Ngowi, alikamilisha kazi yake kama Mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi mnamo Agosti 2017. Kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika Agosti 2017, wanachama wapya wawili waliteuliwa kujaza nafasi za Prof Ngowi na Modesta Lilian Mahiga.

Bibi Joyce Kafanabo alijiunga na Bodi ya FCS ili kuleta uzoefu wake wa miaka mingi kwenye sekta ya umma, asasi za kiraia na mashirika ya kimataifa. Kujiunga kwake kuliimarisha usawa wetu wa kijinsia kwenye Bodi. Vilevile, Bw Frederick Msigallah aliyechaguliwa kujiunga na Bodi kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama

UjUMbE wA MwENYEKITI wA bODI

Bw. Sosthenes Sambua MWENYEKITI WA BODI

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 3

Page 6: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

wa Agosti 2017, anaongeza uzoefu wa masuala ya miradi na kufanya kazi na watu wenye ulemavu.

Bw. Stephen Shayo amekamilisha mihula yake miwili ya miaka mitatu kila mmoja. Amekuwa mfuatiliaji wa kina na mwenye ujuzi bora katika kupitia ripoti za kifedha na kuona iwapo matumizi yamefanyika ipasavyo. Pia, Bibi Margareth Chacha aliyeshika wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi baada ya Prof Ngowi alijiuzulu mnamo mwezi Februari kwa sababu binafsi, ambazo zingeweza kuathiri ufanisi wake kwenye Bodi. Zaidi ya hayo, Dk. Ayoub Rioba ambaye alikuwa kwenye mwaka wake wa mwisho wa kipindi cha kwanza, aliiomba Wanachama wasimwongezee kipindi kingine cha ujumbe kwa kuwa alitaka kuweka kipaumbele kwenye kazi yake ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la utangazaji la serikali, nafasi aliyoteuliwa baada ya kujiunga na Bodi ya FCS.

Bodi na Utawala wa FCS wanapenda kuitumia fursa hii kuwashukuru kwa bidii isiyotetereka na kwa utaalamu uliotumika ili kuhakikisha kwamba FCS inatekeleza vema majukumu yake, kwamba inawajibika na kuendeshwa kulingana na viwango vya kisheria, kifedha na kimataifa. Tunawatakia afya njema na mafanikio katika jitihada zao.

Utawala na Utimizaji wa Wajibu Kwenye masuala ya kiufundi, FCS iliendelea kuimarisha mafanikio yaliyopatikana kwenye mwaka wa kwanza wa kutekeleza mpango wa 2016-2020. Wakati huo huo, tuliendelea

kuimarisha mifumo ya utawala na ufuatiliaji. Mikutano yote ya Bodi ilifanyika kama ilivyopangwa. Zaidi ya hayo, kaguzi za ndani zilizochelewa zilikamilika, zilipitiwa na kamati ya ukaguzi na uhakiki na ripoti kupelekwa kwenye Bodi kwa maamuzi. Kaguzi zote za ndani zilizopangwa zilifanyika. Kamati zote za Bodi zilikutana jinsi inavyotakiwa, huku Kamati ya Ukaguzi na Uhakiki ikifanya mikutano mingi. Kufuatia kuondoka kwa wajumbe wawili wa Bodi, Wanachama wa Bodi waliosalia walifanya kazi kwa bidii kwenye Kamati nyingine za Bodi ili kuziba pengo lililoachwa na Wajumbe wa Bodi walioondoka. Napenda kuwashukuru wote kwa uthabiti na utendaji wenu wa kazi.

Wakati huo huo, zimefanyika kaguzi kadhaa za ndani na nje, ukiwemo ukaguzi maalum wa thamani ya fedha kama ilivyoombwa na Wadau wa Maendeleo, ambazo zilifanyika kama ilivyopangwa. Napenda kumshukuru kila mjumbe wa Bodi, Uongozi na wafanyakazi, jitihada za pamoja ndio ufunguo wa mafanikio. Najivunia na kushukuru kwa kazi nzuri iliyofanywa na makundi yote; na mafanikio yaliyopatikana katika kazi kubwa zilizofanywa na AZAKI, kipekee ninawashukuru washirika wote wa maendeleo. Kwa kweli, mafanikio hayo yalitokana na ushirikiano.

Mwaka uliopita, kulikuwa na mabadiliko kwenye uongozi wa Bodi. Hayo hayawakuzuia wajumbe katika kutekeleza wajibu wao. Nawashukuru wajumbe wenzangu wa bodi. Zaidi ya hayo, Meneja wa Fedha na Utawala alihamia kwenye majukumu mengine ya huduma za umma. Hata

hivyo, timu iliyobaki kwenye idara ilishikamana chini ya uongozi wa muda wenye mafanikio hadi tulipompata Meneja mwingine kuiongoza idara.

Mwaka ujao, Bodi na Uongozi wa FCS wanaelekeza nguvu zao kwenye masuala matatu. Kwanza, kuimarisha taratibu za manunuzi. Tumeanzisha utaratibu wa kuboresha sera zetu za manunuzi ili tupate thamani ya fedha kwenye manunuzi yote. Jambo la pili ni kuchukua hatua za ujasiri kuhusu uimarishaji wa hali ya fedha kwa kutekeleza baadhi ya mapendekezo yaliyopelekwa kwenye Mkutano wa Mwaka wa Wajumbe kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi na kutolewa mwongozo. La tatu ni kuendelea kuimarisha uhusiano wa FCS na Washirika wa Kimaendeleo waliopo na kutafuta wengine.

Nachukua fursa hii kuwashukuruni nyote Wanachama, Washirika wa Maendeleo, Asasi zinazopokea ruzuku kutoka FCS na wadau wote.

Asanteni kwa msaada wenu na ushirikiano.

Bw. Sosthenes Sambua MWENYEKITI WA BODI

FCS Taarifa ya Mwaka 20174

Page 7: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 5

Francis Kiwanga Mkurugenzi Mtendaji

UjUMbE wA MKURUgENzI MTENDAjI

2017 ulikuwa mwaka wa kwanza kamili kwa sisi kutekeleza mkakati wetu wa 2016-2020 kupitia dhana yake ya mabadiliko, nadharia ya hatua, ufuatiliaji, tathmini na mfumo wa kujifunza. Tuliongozwa na yafuatayo: Malengo ya ngazi ya juu yanayohusiana na

mipango yote Mfumo wa kujenga uwezo Mfumo bora wa utawala bora Mfumo wa kipato cha maisha na masoko Mfumo wa uendelezaji wa taasisi unaoweka

vigezo vya ukuaji wa FCS

Tulifanya mabadiliko machache yaliyojitokeza kwenye muundo wa bajeti, mbinu za kupanga na kutoa ripoti. Hivi sasa, tunayo ripoti ya matokeo na nyingine mahsusi kwa minajili ya uwajibikaji, ili tuweze kuwasilisha vizuri zaidi habari zetu kwa washirika wetu wa maendeleo na wadau. Kimpangilio, mabadiliko haya yameboresha jinsi tunavyofanya kazi. Tumeanzisha dhana ya vitendo inayoainisha jinsi programu yetu inavyoweza kupangwa vizuri zaidi kwa lengo la kukuza ubunifu, na kuleta mahusiano bora zaidi na ushirikiano baina ya asasi zinazofadhiliwa na usimamizi wake. Utaratibu huu utatusaidia kupima matokeo ya kazi yetu kwa urahisi zaidi.

Mpango wetu, ambao sasa umepangiliwa katika mafungu manne, umewezesha kuwapo kwa ushirikiano mkubwa wa AZAKI na ushiriki wa

wananchi kwenye mchakato wa utawala wa kidemokrasia ngazi ya serikali za mitaa. Kwenye utoaji wa ruzuku, tulizifadhili AZAKI 146, hasa zilizopo maeneo ya vijijini ili kuboresha maisha ya wananchi kwa kufuatilia uwajibikaji kwenye jamii, kupambana na mazoea ya mila hatarishi, kutafuta ujumuishaji mkubwa zaidi wa vikundi vilivyo kwenye mazingira hatarishi, pamoja na haki za wanawake, na kusimamia amani na utatuzi wa migogoro kote nchini.

Kutokana na uimarishaji wa ufuatiliaji wa huduma za umma, miradi ya umma yenye thamani zaidi ya TZS 7.9 bilioni (takriban dola za kimarekani milioni 3.6) ilifuatiliwa na miradi ya FCS. Taarifa ya FCS pia yaonyesha kuwapo kwa uwezo mkubwa wa kuwakutanisha watu ili watafute suluhisho la matatizo yao. Mabadiliko mengine muhimu yaliyotajwa mwaka huu ni pamoja na: Kuimarisha ushiriki wa wananchi kwenye

michakato ya utawala Mabadiliko mazuri ya mtazamo wa jamii

juu ya haki za makundi yaliyotelekezwa na yaliyo kwenye mazingira hatarishi

Wananchi kudai kuwajibika kwa viongozi wao Serikali kuwa wazi zaidi na kuongeza

usambazaji wa taarifa Serikali iendelee kuwa jumuishi zaidi

na kujali mahitaji ya makundi ya watu waliotelekezwa na walio kwenye mazingira hatarishi.

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 5

Page 8: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 20176

Kujenga UwezoFCS iliendelea kuchukua hatua za kujenga uwezo kwa kutumia muundo wa pande tatu unaohusisha vipimo vya maendeleo, kama vile uwezo wa kuwa, ambao unahusiana na uimarishaji wa taasisi, uwezo wa kutenda, unaohusiana na uimarishaji wa utekelezaji wa programu, na uwezo wa mahusiano, ambao unatokana na nguvu inayounganisha sekta kwa njia ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha mahusiano ya ndani pamoja na sekta binafsi na serikali. Jumla ya kozi maalum nane zilifanyika mwaka huu, zilikilenga AZAKI 168. Tathmini zetu za awali na za kina

zilizofanywa baada ya mafunzo zaonyesha ukuaji wa uwezo wa AZAKI katika nyanja mbalimbali za miradi yao. Zaidi ya nusu (61%) ya AZAKI zote zilionyesha ongezeko la kiwango cha chini cha uwezo wa angalau pointi moja, ambayo ni alama iliyowekwa na FCS kudhihirisha ongezeko la uwezo wa kutosha. Vilevile, FCS imewekeza kwenye kuwezesha tathmini za ndani za AZAKI na asasi 6 zimefaidika na kujengewa uwezo kupitia mfumo huu.

Mwaka 2017, matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii, sanaa na tamasha yaliongeza ufanisi wa uhamasishaji wa vijana na jamii.

Kwa hiyo mnamo mwaka 2018, tutafanya marekebisho muhimu ili kuhakikisha kuwa hatua zetu zinazingatia baadhi ya mambo muhimu tunayojifunza. Kwa ujumla, licha ya 2017 kuwa mwaka wenye changamoto, tuliweza kutumia mifumo na njia mpya, ilitoa matokeo yaliyoweka misingi imara, si tu katika utendaji wetu wa mkakati mpya, bali pia kwa ufahamu wa upana wa mamlaka yetu ndani ya sekta ya asasi za kiraia (AZAKI) nchini.

Francis KiwangaMkurugenzi Mtendaji

Jedwali 1: Muhtasari wa wapewa ruzuku wa 2017 Eneo la matokeoa Lengo la Mpango wa Mwaka Waliopata RuzukuUtetezi Dhidi ya Mauaji ya Watu Wenye Ualbino 13 8Utetezi wa Haki za Watu Wenye Ulemavu 20 10Utetezi Dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia 20 31Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii na Matumizi ya Rasilimali za Umma kwenye Kilimo 18 15Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii na Matumizi ya Rasilimali za Umma kwenye Elimu 17 19Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii na Matumizi ya Rasilimali za Umma kwenye Maji 14 10Kutengeneza Bajeti, Mipango na Ushawishi wa Sera 17 16Haki za Ardhi kwa Wanawake 14 12Ushiriki wa Vijana 7 15Usimamizi wa Amani na Migogoro 10 10Jumla 150 146

Page 9: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 7

Na Matokeo Eneo la Matokeo Matokeo ya awali Tulipofanya kazi Ruzuku Jumla ya Fedha (Tsh)Robo ya 1 2017

Jumla ya Fedha (Tsh)Robo ya 2 2017

Ruzuku yote2017

Idadi ya watu waliofikiwa Robo ya 1

Idadi ya watu waliofikiwa Robo ya 2

Jumla ya watu waliofikiwa kupitiakwenye miradi (000)

Me Ke Jumla Me Ke Jumla Me Ke Jumla

1 Serikali za Mitaazinatoa hudumabora zaidi

UFUATILIAJI WAUWAJIBIKAJI WAKIJAMII

Kuunga mkonoushiriki wa watukwenye mipangona bajeti

Dar es Salaam, Iringa,Pwani, Mbeya, UngujaMjini Magharibi

13 540,661,290 287,524,196 828,185,486 12,251 10,377 22,628 15,655 12,620 28,275 26,896 27,100 53,996

Ufuatiliaji wa uwajibikaji namatumizi ya fedha zaumma (PETS/SAM)kwenye, elimu, maji,kilimo

Lindi, Mtwara,Manyara, Tanga, Morogoro,Kilimanjaro, Iringa,Manyara, Geita

44 1,382,500,458 880,095,240 2,262,595,698 36,960 38,255 75,215 33,284 34,638 67,922 70,244 72,893 143,137

Ushawisi wa sera Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Kagera, Iringa

3 151,080,000 91,820,000 242,900,000 671 334 1,005 569 426 995 1,240 760 2,000

2 Ufanyaji wamaamuzi namichakato yakidemokrasiainayodhihirishavema haki za raia

MILAZENYEUHARIBIFU

Uanzishwaji wamajukwaa yavijana

Dar es Salaam, Arusha,Mwanza,Tanga

15 449,717,070 238,379,363 688,096,433 174,357 262,321 436,678 13,401 11,315 24,716 461,394 273,636 735,030

Utetezi dhidi ya mila mbaya

Manyara, Kilimanjaro, Dodoma, Singida

31 1,174,043,510 823,120,642 1,997,164,152 90,835 88,483 179,318 56,685 61,861 118,546 147,520 150,344 297,864

Kampeni na utetezidhidi ya watu wenyeulemavu wa ngozi

Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara na Rukwa

8 290,371,040 245,192,745 535,563,785 6,267 6,072 12,339 28,608 29,848 58,456 34,875 35,920 70,795

Utetezi wa watuwenye ulemavu

Kigoma, Geita, Kagera, Mwanza, Singida, Dar es Salaam

10 338,050,600 303,048,815 641,099,415 27,097 25,812 52,909 9,411 8,139 17,550 36,508 33,951 70,459

Pigania upatikanaji wa ardhi na hakinyingine za umiliki

Arusha,Manyara,Morogoro, Singida,Pwani na Iringa

12 464,204,603 376,464,073 840,668,676 10,616 12,841 23,457 2,985 4,440 7,425 13,601 17,281 30,882

3 Usimamizi wa amani na migogoro

UTATUZI WAMIGOGORO

Usimamizi wa amani na migogoro

Dar es salaam, Pwani,Morogoro, Dodoma,Lindi

10 367,579,199 319,728,239 687,307,438 1,211 621 1,832 9,134 8,981 18,115 10,345 9,602 19,947

JUMLA 146 5,158,207,770 3,565,373,313 8,723,581,083 360,265 445,116 805,381 169,732 172,268 342,000 802,623 621,487 1,424,110UTOAJI WA FUNGU LA PILI LA MWAKA 2016 KWAWAFADHILIWA ULIFANYIKA MWAKA 2017

98 2,132,794,460

JUMLA YA RUZUKU 244 10,856,375,543

RIPOTI YA MIRADIJedwali 2: Muhtasari wa AZAKI zilizofadhiliwa

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 7

Page 10: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 20178

Ufunguo wa ramaniSekta husika

Utoaji huduma wa Serikali za Mitaa

Majukwaa ya Vijana

Mapambano dhidi ya mila potofu

Utetezi dhidi mauaji ya albino

Utetezi wa haki za walemavu

Haki za kumiliki ardhi kwa Wanawake

Ramani ya Miradi

Kilimanjaro

Arusha

Shinyanga

MaraMwanza

Kagera

KIgoma

Singida

Dodoma

Iringa

Mbeya

Rukwa

GeitaTanga

Manyara

Pwani

Zanzibar

Mtwara

Lindi

Morogoro

Dar es Salaam

FCS Taarifa ya Mwaka 20178

Page 11: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 9

Wananchi wanatakiwa washiriki katika kufuatilia uwajibikaji kwa jamii kwenye jamii zaoMwaka 2017, ushiriki wa wananchi kwenye Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii na Mfumo wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma, ulihusu miradi ya umma ya elimu, maji na kilimo ya takriban shillingi 7.9 bilioni za Tanzania (kama dola za Marekani 3.6 milioni) na kuweza kuokoa kiasi cha shilingi za Tanzania 55, 800,000 (Dola za Marekani 25, 022) ambazo aidha zilitumika kwa shughuli nyingine au kutumiwa vibaya na maofisa wa serikali.

Mafanikio: MBENGONET, huko Wilaya ya Chunya, Kamati ya Ufuatiliaji iliokoa shilingi za Tanzania 15,000,000 zilizochotwa kwenye vyama vidogo vya ushirika, ambazo zilitokana na akaunti ya wakulima wa SACCOS ya Makolongosi. Kutokana na ufuatiliaji uliofanywa na Kamati ya Ufuatiliaji na uwajibikaji, fedha hizo zilirejeshwa.

Shilingi za Tanzania 2,262,595,698Jumla ya Kiasi cha Ruzuku iliyotolewa

44Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

143,137 Idadi ya wanufaika

70,24472,893

Utoaji wa Huduma wa Serikali za Mitaa

Utoaji huduma kwa Serikali za Mitaa FCS inapenda kuhakikisha kuwa maofisa wa serikali za mitaa wanafanya kazi kwa ufanisi na umahiri kwa kutoa huduma za hali ya juu kwenye maeneo wanayoishi wananchi. Hili litafanikiwa iwapo wananchi wanashiriki kwenye ufuatiliaji wa utendaji wa maofisa wa serikali za mitaa kwenye maeneo yao. FCS imeyafadhili mashirika 44 ili kufanya Ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii, kufuatilia matumizi ya fedha umma kwenye sekta za maji, elimu na kilimo. Vilevile, FCS ilizisadia AZAKI 13 ili kuwezesha ushiriki wa wananchi kwenye ushawishi wa mipango, utengenezaji wa bajeti na ubunifu wa sera kwenye mikoa kadhaa nchini na kuziwezesha AZAKI 3 kushiriki katika kujenga ushawishi wa sera za umma kwenye ngazi ya taifa.

Ongezeko la ufuatiliaji wa wananchi

Yasin Lijani, Mjumbe wa Kamati ya Kufuatilia Matumizi ya Fedha za Umma anakagua darasa kwenye Shule ya Sekondari ya Narung’ombe.

Page 12: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201710

Mafanikio: Mtandao wa Usimamizi wa Misitu Kanda ya Kitapilimwa na Kituo cha Wanafunzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania kwenye wilaya za Iringa Vijijini wanaripoti kwamba hatua zilizochukuliwa na Kamati ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma umeainisha kwamba ulikuwapo udanganyifu uliofanywa na mawakala wa pembejeo za kilimo waliouza pembejeo hizo kwa bei za kubwa zikilinganishwa na zile zilizowekwa na serikali. Kwenye kijiji cha Itwaga, mbolea ilikuwa iliuzwa shilingi 60,000 kwa kilo badala ya shilingi 52,500. Kutokana na hatua zilizochukuliwa na Kamati ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma, serikali za mitaa ziliingilia kati ili kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa. Zaidi ya hayo, Kamati kama hiyo ya Wilaya ya Kilolo ilifichua ubadhirifu wa shilingi 129, 580, 000 zilizotengwa kuwawezesha wakulima 1,084 kununua pembejeo.

Wananchi wa Kilombero wanatatua changamoto zao wenyewe kupitia asasi ya KOCD

Mafanikio: Mbagala, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam: Mkakati wa Maendeleo ya Jamii Endelevu uliobuniwa na Shirika la SCORDIA, ambalo ni Shirika la Mkakati wa Maendeleo ya Jamii Endelevu, uliwawezesha wananchi kutambua kwamba viongozi wa serikali za mitaa waliweka kipaumbele kwenye ujenzi wa ofisi yao. Wananchi waliukataa mradi huo, badala yake wakaamua uwepo mradi wa usimamizi mzuri wa taka kama kipaumbele.

Mafanikio: Huko wilayani Kilombero Mkutano wa Kijiji uliwachukulia hatua Mtendaji wa Kijiji na Baraza la Kijiji kwa kukodisha hekta 300 za ardhi ya kijiji lakini wakatoa taarifa ya hekta 85 pekee.

Uwajibishaji wa Viongozi

Uwazi zaidi Serikalini Imethibitika katika maeneo ya miradi ya AZAKI kuwa viongozi wamekua na uwazi zaidi. Huko wilayani Ulanga, imeripotiwa kuwa kwa mara ya kwanza kabisa Watendaji 13 wa Vijiji katika Kata ya Vigoi waliitisha mikutano na kusoma mipango na bajeti zao kwa wanakijiji. Watendaji zaidi wa vijiji maeneo ya Dodoma, Iringa na Songea kwa sasa wanatoa taarifa kuhusu mipango na bajeti za vijiji kwenye mbao za matangazo.

Ushiriki wa Raia Ulioimarishwa

Asasi ya Tree of Hope imetoa taarifa kwamba uwepo wa Kamati ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma na Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii umeongeza imani ya wananchi kwa viongozi wao, na kuwahamasisha kushirikiana na viongozi katika utekelezaji wa miradi inayofanyika kwenye maeneo yao, mathalani ujenzi wa madarasa kwenye shule za msingi za Komsanga, Msocha na Kabuku, na vyoo kwenye shule za msingi za Kwedizinga na Msocha, na uzio kwenye Shule ya Msingi ya Michungwani mkoani Tanga. Mafanikio hayo yalionekana pia Morogoro kama ilivyoeleza taarifa ya Kikundi cha Maigizo cha Dira kwenye Kata ya Lumbiji huko Kilosa, inayoainisha kwamba kila mwananchi alichanga shilingi 1,500, matofali 5, na mfuko mmoja wa mchanga kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Lumbiji B na choo kwenye Kata ya Mabula.

Page 13: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 11

Majukwaa ya vijana yaliyoundwa Jumla ya majukwaa ya vijana 160 kwenye ngazi za kata na wilaya yameshaundwa. Sasa yamekuwa kama njia muhimu ya kuwepo kwa mdahalo baina ya serikali za mitaa na mitandao

Kuwezesha Vijana Ruzuku zilizotolewa na FCS kwa AZAKI kwa uundaji wa majukwaa ya vijana kwenye ngazi za wilaya na wilaya ndogo inalenga kuongeza sauti ya vijana na ushiriki wao kwenye uendelezaji wa sera za umma na mikakati ya utekelezaji. Serikali ya Tanzania imeweka utaratibu kwenye ngazi za serikali za mitaa ambapo mamlaka hizo zinapaswa kutenga angalao asilimia 4 ya mapato yao ya ndani ili kuwawezesha vijana. Kwa hiyo, majukwaa ya vijana yanayoundwa yatakuwa njia ya mahusiano baina ya Serikali na vijana tena yataimarisha ujenzi wa harakati, ambapo vijana watakuwa na jukwaa la kuimarisha ushiriki wao kwenye mikakati ya sera na utoaji wa maamuzi.

Shilingi za Tanzania 688,096,433Jumla ya Fedha za Ufadhili

15Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

461,394 Idadi ya wanufaika

187,758273,636

Uwezeshaji Vijana

Mwanamuziki Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye jukwaa la vijana

ya vijana. Kwa hiyo kuundwa kwa majukwaa hayo ya vijana siyo lengo la mwisho, bali yamethibitika kuwa ni muhimu kabisa katika kuwezesha ushiriki wa vijana kwenye mikakati ya utawala.

Page 14: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201712

Vijana washughulikia ustawi wao wa kiuchumi Hivi sasa yaonekana wazi kwamba kipaumbele cha vijana ni ustawi wao wa kiuchumi. Licha ya kwamba miradi yao ina sura ya kiutawala, wakati wowote ule wanapokutana, vijana wanaiona haja ya kusaidiana kwenye shughuli za kuleta kipato.

Mafanikio: Huko Mwanza, majukwaa 14 yamehamasishwa kuwa na mifuko yao wenyewe wakianza na shilingi 1,848,000 mnamo mwezi Octoba 2017. Ilipofika Januari 2018, walifanikiwa kuzalisha shilingi 5,660,000. Wanatumia fedha hizo kuchukua mikopo ili kuendesha mradi wa kilimo cha mbogamboga.

Serikali inaitika zaidiKwenye baadhi ya maeneo ya miradi, serikali imedhihirisha kuwa sikivu kwa mahitaji ya vijana. Vijana wa Mkuranga, Mkoa wa Pwani waliunda vikundi vitatu vya kuongeza kipato na kununua ardhi kwa ajili ya shughuli za jumuiya yao. Huko Mwanza, majukwaa matatu ya vijana yamepata mikopo. Kikundi cha vijana 25 kilipata mkopo wa shilingi milioni 3 nao tayari wameshaanza kutekeleza miradi ya kuingiza kipato.

Ushiriki wa Vijana kuitathmini Sera ya Vijana ya Mwaka 2007Ushirikiano wa kimkakati na Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana umeanzishwa kutokana na juhudi za chama cha umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) kinachoongoza kikundi cha mradi wa vijana. Chama cha Umoja wa Mataifa kimekuwa sehemu ya kikundi cha

nguvu kazi kinachoandaa rasimu ya kwanza ya sera ya vijana. Hii ni hatua kubwa katika kushughulikia masuala ya vijana nchini Tanzania. Tayari mapendekezo ya rasimu mpya yameshapelekwa kwenye Idara ya Vijana ya Ofisi ya Waziri Mkuu, inayoratibu tathmini hiyo.

Vijana wa asasi ya Kijana Paza Sauti ya Ubungo, Dar es Salaam

Ushiriki mkubwa zaidi wa vijana kwenye miundo ya utawala Vijana wanaanza kujumuishwa kwenye vyombo vya kufanya maamuzi, kama vile mikutano ya Kamati za Mendeleo za Kata, Vijiji na Mitaa. Mathalani, huko Mbeya, mikutano ya kuihamasisha jamii iliwawezesha Hamad Mbeyane na Daines Patrick kuchaguliwa kuwa wawakilishi wa vijana kwenye Kamati za Maendeleo za kata za Ilembo, Mbeya na Itete huko Kyela. Vilevile, huko Arusha kata 4 za Orgorok (Sakala), Soitsambu (Mondoros), Enguserosambu (Orkiu Juu) na Ololosokwan (Njoroi) zimewajumuisha vijana kama sehemu ya ajenda muhimu ya mikutano ya Kamati za Maendeleo za Wadi. Huko Mwanza na Pwani, vijana 13 wameteuliwa kushiriki kwenye mikutano ya WDC kutoka kwenye majukwaa 9 ya vijana.

Vijana wakijitolea kwenye #JumanneYaUtoaji 2017 kwenye taasisi ya MOI Muhimbili

Uhamasishaji mkubwa zaidi wa vijanaUhamasishaji wa vijana una mchango mkubwa kwenye kutoa majawabu yanayohusu wananchi kuhusu matatizo yaliyopo kwenye ngazi za chini za jamii.

Mafanikio Wanakijiji wa Mlimani, Monduli walihamasishana kutengeneza barabara inayounganisha kijiji chao na kijiji jirani cha Rasharasha. Barabara hiyo ya pekee inayowaunganisha zaidi ya wananchi 10,000 na makao makuu ya Wilaya ya Monduli ilikuwa kwenye hali mbaya, ikisababisha uharibifu wa magari na pikipiki. Hivi sasa, barabara hiyo inapitika vizuri zaidi kwa vile iko kwenye hali bora zaidi.

Page 15: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 13

Mabango ya kulaani ndoa za utotoni kwenye Kijiji cha Engalaaoni huko Arusha wakati wa kampeni zilizoongozwa na Kituo cha Wanawake na Maendeleo ya Watoto

Mkakati jumuishi umeundwa Mkakati wa wadau mbalimbali ulioanzishwa na wafadhiliwa wa FCS umetoa ripoti kwamba jumlaya kesi 897 za ukatili dhidi ya wanawake na ukeketaji wa wanawake ziliripotiwa kwenye serikali za mitaa na wananchi, ambapo migogoro 537 ilitatuliwa. Mathalani, huko Shinyanga mashauri 24, zikiwamo ndoa za utotoni, mimba za utotoni na visa vya uonevu, yaliwasilishwa serikalini. Kesi 14 bado ziko mikononi mwa polisi kwa ajili ya uchunguzi na 10 nyingine ziko mahakamani. Kwa kiasi kikubwa, kuongezeka kwa taarifa za kesi kumetokana na ongezeko la ufahamu wa jamii juu ya ukatili unaofanywa dhidi ya wanawake pamoja na ukeketaji wa wanawake.

Wasichana 247 wameopolewa toka ndoa za utotoni. Changamoto ya ndoa za utotoni imedhihirika zaidi miongoni mwa jumuiya za wafugaji na jamii ya wakulima-wafugaji. Mathalani, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, wasichana watatu (3) walikuwa wamenasa kwenye mtego wa ndoa za utotoni wameokolewa. Hata hivyo, baada ya kuingilia kati kwa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake na

Watoto (CWCD) kuliwezesha uokoaji wa watoto 160 kutoka kwenye dhahama ya ndoa za utotoni, ubakaji na ukeketaji.

Mapambano dhidi ya mila potofu Uungaji mkono wa FCS wa hatua za kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia ni sehemu ya jitihada za kuondoa mazoea ya jadi yenye madhara. Hii ni kwa sababu, licha ya hatua mbalimbali za kimataifa, kikanda, na ndani ya nchi zilizowekwa ili kukabiliana na vitendo hivi vibaya, ufanisi wa taratibu uimeathiriwa sana na ukweli kwamba zimewekwa kwa msingi wa kanuni za kitamaduni na kidini. Changamoto iko katika kutafuta njia za kuheshimu tamaduni mbalimbali bila kuruhusu kupunguzwa kwa haki za binadamu za wanawake kutokana na mazoea ya kidini na maadili ya sehemu wanazoishi.

Shilingi za Tanzania 1,997,164,152Jumla ya Fedha za Ufadhili

31Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

297,864 Idadi ya wanufaika

147,520150,344

Mapambano Dhidi ya Mila Potofu

Page 16: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201714

Kwenye kipindi cha ripoti hii, watu 11 wanaochochea ukeketaji wa akina mama kwenye mikoa ya Singida na Kilimanjaro waliachana na mila hizo. Hivi sasa wanawaelimisha wengine kuhusu athari kwa vijana wadogo.

Sheria ndogo za kuwalinda wanawake na watoto zimeanzishwa. Wilayani Arusha, Kituo cha Kuwaendeleza Wanawake na Watoto (CWCD) kimeshirikiana na serikali za mitaa kwenye utunzi wa sheria ndogo kwenye kata 10 za mradi ambazo ni Musa, Olkokola, Mwandeti, Lemanyata, Kisongo, Laroi, Oljoro, Sambasha, Ilkidinga na Matevesi.

Mafanikio: Kwenye Kata ya Mwandeti, kufuatia kuanzishwa kwa sheria ndogo, waliweka mabango ya kupiga marufuku ukeketaji wa wanawake kwenye maeneo yote ya kata. Waliendesha pia kampeni ya kutamka kuwa “Iwapo mtu atakutwa anafanya ukeketaji, basi atakwenda jela.”

Kituo cha Maendeleo cha Tusonge, bingwa wa kampeni ya kupinga ukeketaji wa akina mama

Mkutano wa wananchi uliandaliwa na SMCCT mjini Singida. Kuwahusisha wanaume ni muhimu kwenye mapambano dhidi ya mila potofu

Mabango ya kulaani ndoa za utotoni kwenye Kijiji cha Engalaaoni huko Arusha wakati wa kampeni zilizoongozwa na Kituo cha Wanawake na Maendeleo ya Watoto

Wasichana mara nyingi wanataabika wakati wa kujifungua kwa kuvuja damu nyingi. Yaumiza kuona jinsi wanavyoteseka. Baada ya kuelimishwa kuhusu athari za ukeketaji, niliamua kuwaelimisha ngariba na jumuiya nzima kuhusu athari ya ukeketaji. Twaweza kuwafikia wanawake na familia nyingi kadiri tuwezavyo kupitia majukwaa yaliyoanzishwa

anasema Bi. Maria Narsis, balozi wa kupinga ukeketaji kwenye kijiji cha Kintuntu, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.

Page 17: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 15

Mapambano dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino

Shilingi za Tanzania 535,563,785Jumla ya Fedha za Ufadhili

8Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

70,795 Idadi ya wanufaika

34,87535,920

Mapambano dhidi ya mauaji ya albino

Mateso ya walemavu wa ngozi yamekuwa yakitokea, haya yanatokana na imani kwamba viungo vyao vina nguvu ya uponyaji. Imani za ushirikina kama hizo zimeenea kwenye baadhi ya maeneo ya Maziwa Makuu. Watu wenye imani za ushirikina hutumia viungo vya walemavu wa ngozi kama viungo vya ibada, kuchanganya madawa na uganga kwa madai kuwa uganguzi wao utaleta utajiri kwa mtumiaji. Rukwa, Katavi, Simiyu, Tabora, Geita na Shinyanga ni mikoa ambayo mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yamesheheni.

Zaidi ya hapo, kina baba mara nyingi huwatilia shaka kina mama wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi kuwa ndiyo chanzo cha ulemavu wa ngozi. Wengine huwaona watoto hao kama wenye kuleta mkosi, balaa na wasiotakiwa na jamii. Walemavu wa ngozi wengi huuawa utotoni kutokanana na fikra hizo za ushirikina. Uungaji mkono wa FCS kwa utetezi wa haki za walemavu wa ngozi unalenga katika kuhakikisha kwamba upo uelewa wa kutosha wa umma kuhusu ulemavu wa ngozi, kupinga sera na desturi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyo kwa binadamu wengine. Mzungumzaji wakati wa Jukwaa la AZAKI

zinazoshughulikia walemavu

Hatua muhimu zilizoungwa mkono: • Kampeni za kuongeza uelewa (kupitia

vituo vya redio, makala za uelimishaji kwenye magazeti, utoaji na usambazaji wa machapisho pamoja na majukwaa ili kuhamasisha uelewaji wa jamii.

• Kukutana kimkakati na wadau muhimu, viongozi wa serikali, waganga, mawakala wa mabadiliko kwenye jamii, polisi, madiwani na watu wenye ulemavu.

• Mafunzo ya kujenga uwezo, uchangiaji mkubwa na maigizo ili kuongeza uelewa wa watu wenye ulemavu na wale wanaowatunza kuhusu changamoto za kiafya na kijamii zinazowakabili watu wenye ulemavu.

Page 18: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201716

Kupungua kwa dhuluma dhidi ya walemavu wa ngoziTwaona mwelekeo unaopata nguvu kuanzia mganga mmoja wa kienyeji hadi mwingine. Tumebaini mabadiliko ya mwelekeo kutoka mganga mmoja mwaka 2016 na sasa waganga wa kienyeji 30 wameweka sahihi kukubaliana na maofisa wa serikali za mitaa kwamba wanaacha shughuli za uganga. Matukio haya yalitokea Bukombe na Tabora ambapo Chama cha Walemavu wa Ngozi Tanzania na Caritas wanatekeleza mradi huo.

Washiriki wa shughuli ya kuhamasisha ulinzi kwa watu wenye ualbino

Kuongozeka kwa huduma kwa walemavu wa ngozi Kwenye wilaya ya Busega, mahitaji na madai ya walemavu wa ngozi yaliyopuuzwa kwa miaka kadhaa, sasa yamejumuishwa kwenye mipango na bajeti ya mwaka 2018/2019. Kata 15 kwenye wilaya ya Busega zimeashiria kwenye bajeti zake kuwa zitawapatia walemavu wa ngozi miwani ya kuzuia jua, kofia na mafuta ya ngozi

ili kupunguza athari za mionzi ya jua, kuwaunga mkono na kuwawezesha kupata mafunzo ya ufundi wa fani mbalimbali.

Mafanikio: Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe imetenga shilingi Tzs 9.4 milioni ili kukidhi mahitaji ya walemavu wa ngozi na ya bajeti ya mwaka 2017/ 2018. Kiasi hicho kimetengwa kwa ununuzi wa mafuta ya kupakaa ya watu wenye ulemavu. Kwenye hospitali ya mkoa Tabora, ofisi ya ustawi wa jamii imeidhinisha matibabu ya bure kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Vilevile, majukwaa ya wilaya yaliyoanziswa yameongeza upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu.

Mafanikio: Huko Busega, jukwaa la watu wenye ulemavu limeishawishi serikali kutoa shilingi milioni 11 ili kuyaunga mkono makundi yaliyo kwenye hali hatarishi (wakiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi). Kwenye wilaya hiyo, shilingi milioni 2 zitatumika kuwapatia watu wenye ulemavu wa ngozi mafuta ya kuwakinga dhidi ya mionzi ya jua.

Washiriki kwenye mdahalo unaohusu watu wenye ualbino

Watu wenye ulemavu wa ngozi wahusishwe kwenye michakato yote ya maendeleo

Tunahitaji kuwalinda watoto wenye ulemavu wa ngozi

Page 19: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 17

Utetezi kwa watu wenye ulemavu Uungaji mkono wa FCS wa haki za walemavu unatokana na ukweli kwamba watu hao ndio wanaoongoza kwa kukosa fursa na kutengwa na jumuiya. Picha hii inatokana na changamoto kadhaa, kama vile kiwango cha chini cha kujua kusoma na kuandika (asilimia 47.6 ya watu wenye ulemavu), ambacho kinawakosesha fursa ya kupata taarifa na kufurahia miundombinu, kuathirika na mitazamo hasi na kudharauliwa na jamii na familia. Hali inakuwa mbaya zaidi pale watoto wenye ulemavu wanaponyimwa haki yao ya kupata elimu. Takwimu zadhihirisha kwamba kuanzia asilimia 0.1 hadi 0.5 tu ya watoto wenye ulemavu ndio wanaosajiliwa kwenye shule za msingi za Tanzania, ambapo idadi kubwa ya watoto wenye umri wa kwenda shule aidha wanafichwa au wananyimwa fursa na wazazi wao wenyewe, ndugu au walezi. Mnamo mwaka 2017, AZAKI 10 zilifadhiliwa na FCS kwenye maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kutekeleza miradi mbalimbali, lengo kuu likiwa kuhamasisha utekelezaji kamili wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za watu wenye ulemavu na Sheria ya Walemavu ya Mwaka 2010 ya Tanzania.

Shilingi za Tanzania 641,099,415Jumla ya Fedha za Ufadhili

10Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

70,459 Idadi ya wanufaika

36,50833,951

Utetezi kwa watu wenye ulemavu Kuongezeka kwa mwitikio wa Serikali katika kushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu

Utetezi wa haki za watu wenye ulemavu

Page 20: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201718

Mamlaka za Serikali za Mitaa za Dodoma, Kwimba na Biharamulo zimefanya sensa ya watu wenye ulemavu ili kutambua idadi yao halisi na kufanikisha uandaaji wa mipango ya serikali za mitaa. Wakati wa sensa, ilibainishwa kwamba wengi wa watoto wenye ulemavu ambao tayari wana umri wa kusoma shule bado hawajaaandikishwa. Kuongezeka kwa utetezi kumeongeza kuandikishwa shule kwa watoto wenye ulemavu hata kwenye wilaya nyingine kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini:

Na Wilaya Idadi ya walemavu

2015/2016

2016/2017

2017/2018

1 Biharamulo 72 192 224

2 Kwimba 196 413 698

Kufuatia uwepo wa ongezeko kubwa la kuandikishwa kwa watoto wenye ulemavu, Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilianzisha darasa la watoto wenye mahitaji maalum kwenye Shule ya Msingi Budishi ili waweze kuhudumiwa kwa haraka zaidi. Vilevile, shule hiyo ilipatiwa mwalimu mwenye ujuzi wa lugha ya ishara wa kuwafundisha wanafunzi viziwi.

Mwelekeo kama huo ulionekana pia kwenye Mkoa wa Mara kufuatia kuwapo kwa mkutano wa kimkakati na watu wenye ulemavu, ambapo Mkuu wa Mkoa Adam Malima aliwaagiza Wakurugenzi wa Wilaya ya Mara na Mabaraza ya Mkoa wa Mara kuunda kamati za watu wenye ulemavu

zitakazokuwa kama jukwaa la kujadili na kupata suluhisho la matatizo yanayowaathiri watu wenye ulemavu.

Kwenye mikoa ya Mara na Mwanza, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetoa nafasi za ofisi bila malipo kwa watu wenye ulemavu ili kuimarisha shughuli zao na kuwakilisha maslahi yao inavyofaa. Ofisi hizi zimeongeza uwezo wa watu wenye ulemavu kutetea haki zao wakiwa kwenye mazingira mazuri zaidi.

Miundombinu bora zaidi kwa walemavu

Mabadiliko zaidi na marekebisho yalifanywa kwenye miundombinu ili kurahisisha upitaji wa watu wenye ulemavu. Huko Kibaha, Kongowe, Biharamulo na Kwimba, wakuu wa wilaya waliamrisha kufanywa marekebisho kwenye milango na mapito ili kukidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu. Tayari, shule, vituo vya afya, mabenki, maduka, makanisa na vyoo vya umma kwenye vituo vya mabasi vimebuniwa upya ili kuwahudumia vyema zaidi watu wenye ulemavu.

Miundombinu imeboreshwa kwa walemavu wa Biharamulo, Kagera

Miundombinu imeboreshwa kwa walemavu wa Kwimba, Mwanza

Page 21: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 19

watu wenye ulemavu wapata manufaa ya kiuchumi na kijamii Mkoani Morogoro, wanachama 20 wa CHAVITA wamepata bima ya afya bila malipo kutoka kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF). Sasa wataweza kupata huduma za bure kutoka kwenye vituo vya afya vinavyomilikiwa na manispaa.

Kutokana na harakati za CHAVITA, Manispaa ya Mji wa Arusha imeajiri mkalimani wa lugha ya ishara ili kuwavuta watu wenye ulemavu ndani ya jamii na kutekeleza Sera ya Watu wenye Ulemavu (2004) na Sheria ya Watu wenye Ulemavu (2010). Mtafsiri wa lugha ya ishara ana wajibu wa kurahisisha mawasiliano baina ya viongozi wa serikali na jamii ya viziwi kwenye mazingira yote rasmi ya Manispaa ya Arusha. Mkalimani wa lugha ya ishara huripoti kwenye Idara ya Ustawi wa Jamii.

Manispaa ya Arusha, Halmashauri za Wilaya za Tarime na Serengeti zimetenga asilimia 2 ya bajeti yao kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Aidha, wajasiriamali 6 ambao ni viziwi wameboresha biashara zao ndogo baada ya kupata mikopo ya ujasiriamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza. Wajasiriamali wanashughulikia useremala, ushonaji na saluni ya wanawake. Hayo yanazingatiwa pia katika Halmashauri ya Jiji la Tarime ambapo Ofisi ya Ustawi wa Jamii imepanga bajeti ya shilingii milioni 7 kwa makundi ya watu wenye ulemavu ili wapate mkopo kwa kiwango cha chini cha riba.

Hapaswi kusahaulika mlemavu yeyote

Musa Method Kidiga, mlemavu wa macho na mwalimu wa ushonaji wa asasi ya Child Support Tanzania iliyopo Mbeya

Watu wenye ulemavu wakishiriki kwenye mkutano wa kusherehekea Miaka 15 ya FCS

Page 22: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201720

wanawake wazidi kuifahamu haki yao ya kumiliki ardhi Hati za Jadi 54 za Kumiliki Ardhi zimetolewa Kiteto, Arumeru na Iringa kwa msaada wa asasi ya Ujamaa Community Resource Team ya Kiteto na Women and Children Development Foundation (TARWOC) huko Iringa; na Chama cha Wanasheria Wanawake wa Tanzania (TAWLA) kwenye Wilaya ya Arumeru. Hii inafikisha idadi ya hati za kimila za kumiliki ardhi 316 zilizotolewa kwenye kipindi cha mwaka 2017.

Haki za wanawake kumiliki ardhi FCS inazisaidia AZAKI kwenye eneo hili la matokeo, kwanza kwa kupinga sera na sheria zilivyo hivi sasa ili ziboreshwe na kuwa zenye manufaa kwa wengi ambao ni maskini na wanawake, hususan haki yao ya kumiliki ardhi. Msimamo huu unatokana na ukweli kwamba ardhi ndiyo rasilimali muhimu kabisa kwa wanawake waishio vijijini nchini Tanzania. Hata hivyo, licha ya mamlaka yaliyotolewa na Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 (Kifungu Na. 4 na 5, 2002) ya kuwapa wanawake haki

Mabaraza ya viongozi wa jadi ya Oldonyosambu ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Wilaya za Kiteto na Arumeru yamekubaliana kuacha tabia za jadi za kibaguzi ambazo huzuia umiliki wa ardhi kwa wanawake na ushiriki kwenye masuala yanayoathiri ustawi wao. Takwimu za utekelezaji zaonyesha kuwa juhudi za kuhamasisha mabadiliko zimewafikia jumla ya wanufaika 19,947 (wanaume 10,345 na wanawake 9,602).

Shilingi za Tanzania 840,668,676Jumla ya Fedha za Ufadhili

12Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

30,882Idadi ya Walionufaika

13,60117,281

Hakiardhi za Wanawake

sawa za umiliki ardhi, bado wanawake wengi waishio vijijini wanakabiliwa na matatizo kadhaa linapokuja suala la kupata, kumiliki, kudhibiti na kuuza ardhi.

Harakati muhimu zinazoungwa mkono na FCS juu ya haki za ardhi ni pamoja na:• Mafunzo na uimarishaji wa majukwaa ya

haki za ardhi za wanawake• Mafunzo na majadiliano juu ya haki za ardhi

za wanawake na stahiki zao• Programu za uelewa kupitia mipango ya

radio jamii• Mikutano ya kuhamasisha mahakama za

ardhi, wanawake na jamii kuhusu masuala ya ardhi

• Usambazaji wa vifaa vya IEC (vipeperushi, nakala za sheria za ardhi, miongozo ya migogoro ya ardhi n.k

Wanawake wa Kimaasai wa Kiteto wakiwa wameshika mkononi hati zao za jadi za kumiliki ardhi

Page 23: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 21

Mwitikio wa Serikali za Mitaa kwenye umiliki wa ardhi kwa wanawake Mojawapo ya changamoto kubwa zinazowakabili wanawake wa vijijini ni ukosefu wa wosia ulioandikwa na waume zao, kwani kifo kinapotokea, hushindwa kurithi mali. Kuwapo kwa changamoto hii kumewafanya wenyeviti wa mabaraza ya ardhi ya kata wa Wilaya ya Arumeru waruhusu uandikaji wa hati za urithi za kimila kama njia ya kupunguza migogoro ya kifamilia inayohusiana na mali na masuala ya ardhi.

Hadithi ya Elizabeth Malunde

Kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwamilikisha ardhi

Mnamo mwaka 2010, mume wa Elizabeth, Mangalami Mdanganya Masegese, alimpa mke wake kipande cha ardhi kutokana na upendo aliokuwa nayo kwa mama huyu wa watoto wake wanne.

Mangalami alitaka mkewe ajenge nyumba yake mwenyewe. Hivyo alimmilikisha kipande cha ardhi ili amudu maisha ya kujitegemea baada ya kifo cha mumewe. Eneo hilo lilikuwa na minazi, michungwa na chokaa. Rasilimali hizo zilimwezesha kuingia mkataba na soko la matunda.

Elizabeth alipanua matumizi ya ardhi kwa kupanda mchicha kwa ajili ya chakula cha nyumbani na ziada akaipeleka kwenye masoko ya maeneo jiranii. Mnamo mwaka 2016, Elizabeth alianza kujenga nyumba yake. Majirani waliokuwa wakipita walizungumza naye kuhusu eneo lake. Elizabeth aligundua kwamba hati aliyokuwa nayo iliandikwa kwa jina la mumewe. Alishauriwa kuhamisha umiliki ili kuepuka kuwepo kwa hali mbaya. Marafiki walioshiriki kwenye mradi unaofadhiliwa na FCS wa Kukuza Usawa wa Jinsia huko Zanzibar wakampeleka kwenye ofisi za Jumuiya ya Maendeleo ya Wanawake , tawi la Mkoa wa Kaskazini Unguja, iliyoanzishwa na chama cha waandishi wa habari wanawake wa Tanzania, yaani TAMWA.

Elizabeth alikwenda Tume ya Ardhi na kuchukua fomu ya maombi, ambapo alilipa shilingi 50,000 (Shilingi nyingine 30,000 alilipa kwenye Ofisi ya Ardhi ya Wilaya na 20,000 kwa Sheha). Mara baada ya kuwasilisha fomu ya maombi kwenye Tume ya Ardhi, kesi yake ilirekebishwa Jumamosi iliyofuata. Maafisa wanne waliotoka wilayani walichunguza na kupima kipande chake cha ardhi. Akakabidhiwa hati ya umiliki tarehe 14 Februari 2018.

Hivi leo, kipande hicho humletea faida ya TZS 100,000 / - kwa mwezi wakati wa msimu wa mavuno na chochote kati ya TZS 30,000 hadi 50,000 wakati wa msimu mdogo. Elizabeth anajiona yu salama kwa kuwa anamiliki kipande cha ardhi kinachompa kipato na hapohapo kutumika kama ngazi ya kumfanikisha zaidi na zaidi.

Wanachama wa Jukwaa la Hakiardhi kwa Wanawake wa Oldoinyo Sambu, Arusha

Page 24: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201722

Ujenzi wa amani na utatuzi wa migogoro Mbinu iliyonayo FCS kwa sasa ni kujumlisha mkakati wa ujenzi wa amani na usimamizi wa migogoro chini ya eneo pana zaidi la Utawala Bora. Dhana hii inasimama juu ya ukweli kwamba licha ya kuwapo kwa migogoro yote hiyo, Tanzania bado inafurahia amani, utulivu wa kisiasa, umoja wa taifa, na mshikamano wa kijamii tena imeboresha mazingira yake ya kidemokrasia na kisiasa pamoja na uvumilivu wa kisiasa. Hata hivyo, kwa miaka mingi Tanzania pia imekabiliwa na migogoro inajitokeza kwenye ngazi tofauti za kijamii—nyumbani, kiutamaduni, kidini, kijamii na kiuchumi. Vichocheo vikubwa vya migogoro hii ni ushindani wa kisiasa, haki za kibinadamu na kijamii, kubanwa kwa vyombo vya habari, migogoro inayohusiana na ardhi na rasilimali asilia na kiwango cha juu cha uzazi. Sababu nyingine ni tofauti za kidini na siasa kali, tofauti za kikabila, ubaguzi/ukosefu wa kupata haki na kadhalika. Mradi wa FCS kwenye jambo hili ni jaribio la kuyashughulikia mambo yote haya.

zilipewa mafunzo juu ya majukumu na wajibu wao katika kuimarisha amani kwenye maeneo yao.

Mijadala baina ya dini mballimbali FCS ililiunga mkono Baraza Amani la Dini mbalimbali katika kutathmini hali ya siasa ndani ya nchi kwa kushirikiana na Kamati za Amani na Usalama za serikali za mitaa na viongozi wa dini wa mikoa ya Lindi na Mtwara. Shirika lilifanya utafiti uhusu Kuielewa Amani: mambo yanayowavutia watu waishi kwenye eneo fulani na yanayowasukuma kuondoka kwenye eneo hilo, huku matokeo yakionyesha kwamba 84% ya watu 241 waliohojiwa kwenye mikoa hiyo miwili walielewa umuhimu wa kudumisha amani na utengamano kwenye maeneo yao.

Ailimia 85.7 ya waliohojiwa wanatambua kwamba wananchi shurti wawajibike kuhusu udumishaji wa amani kwenye maeneo yao. Utafiti ulionyesha kwamba vitendo vya kufanya fujo kama kuchoma maduka, nyumba na

Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba kwenye mojawapo ya mijadala ya amani ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Shilingi za Tanzania 737,200,000Jumla ya Fedha za Ufadhili

10Idadi ya Miradi Iliyofadhiliwa

19,947Idadi ya Walionufaika

10,3459,602

Ujenzi wa amani na usimamizi wa migogoro

Takwimu za utekelezaji zaonyesha kwamba hatua zilizochukuliwa zimewanufaisha watu 19,947 (wanaume 10, 345 na wanawake 9,602). Jumla ya Kamati za Amani 120 ziliimarishwa na mijadala shirikishi 48 kuhusu ujenzi wa amani ilifanyika. Kamati hizi

Page 25: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 23

Migogoro ya rasilimali

Wakulima na Wafugaji wakijadiliana huko Morogoro

Kwenye Wilaya ya Mvomero, Mkoa Morogoro, TISER, yaani Taasisi ya Mkakati wa Kuleta Shwari ya Kijamii na Kiuchumi, ilisaidia kuweka utaratibu wa kuweka mipaka baina ya wakulima, wafugaji na mbuga za akiba. Shirika hilo lilizisaidia serikali za mitaa kutunga sheria ndogo zilizojumuisha udumishaji wa sheria na utengamano kwenye vijiji na uanzishwaji wa mabaraza ya ardhi.

Huko nyuma, Baraza la Ardhi la Kata ya Milama lilikuwa likipokea kesi 75 za migogoro ya ardhi kwa mwaka, lakini baada ya kuingia kwa TISER, kiwango cha kesi kama hizo kwa mwaka kilishuka hadi 23 tu. Asasi hiyo pia iliziwezesha jamii za Mvumero kutunga sheria ndogo za kijiji kama njia ya kudumisha amani miongoni mwa wakulima na wafugaji kwenye maeneo hayo.

Kwenye Wilaya ya Mkuranga, Mkoa Pwani, Asasi ya Amani Foundation inayofadhiliwa na FCS, iliendesha mafunzo ya utatuzi wa migogoro yaliyowezesha kuwapo kwa majadiliano baina ya wawekezaji na jumuiya mbalimbali ili kutatua matatizo mawili makubwa kwenye wilaya hiyo—Mgogoro wa kijiji cha Dundani kuhusiana na moshi wa tanuru la kuchoma takataka na mgogoro kuhusu moshi wa kiwandani uliowagonganisha wanavijiji wa Kisemvule na kampuni ya kutengeneza saruji ya Rhino kutokana na kutimka kwa vumbi Asasi hiyo pia ikaanzisha kamati tatu za utatuzi wa migogoro za vijiji vya Dundani, Kisemule na Mwandege kama sehemu ya masuluhisho yawezayo kuleta suluhisho la kudumu la migogoro iliyokuwapo.

majengo ya ibada vimeongezeka kwenye mikoa hiyo miwili tena upo uwezekano wa kuzuka mgogoro baina ya vijana (kama waendesha bodaboda na wazururaji) na polisi.

Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mtwara

Baada ya kuorozesha viini vyote vya uvunjifu wa amani kwenye mikoa hiyo, Baraza Amani la Dini Mbalimbali lilizikutanisha Kamati za Amani ili ziandae toleo la pili la chapisho la utafiti wao lililoitwa “Mwongozo wa Uanzishaji na Uimarishaji Kamati za Dini Mbalimbali nchini Tanzania, 2018.” Yaliyomo kwenye kitabu hiki yatawakilishwa kwa viongozi wote kitaifa ili kusambaza ufahamu wa kuishi pamoja na kuimarishwa kwa uvumilivu baina ya dini na imani mbalimbali.

Sauti za wananchi ni muhimu katika kufanikisha usuluhishi wa migogoro

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 23

Page 26: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201724

Jedwali 3: Muhtasari wa kuzijengea uwezo AZAKI Kazi Maelezo Asasi

Mijadala ya AZAKI

Jukwaa la wakurugenzi wa AZAKI Mkutano pia ulihudhuriwa na maafisa wanne kutoka Ofisi ya Msajili wa AZAKI Bw. Katemba

Wakurugenzi wa asasi 64

Maafisa 4 kutoka Ofisi ya Msajili wa AZAKI

Mjadala wa kitaaluma wa AZAKI

Wakurugenzi 30 walihudhuria

Uhakiki wa AZAKI AZAKI 3168 zilihakikiwa kupitia mitandao ya FCS

Jukwaa la Uziduaji Tanzania 2017 lililojadili fursa za sekta za mafuta, gesi na madini nchini

Zaidi ya AZAKI 60 zilishiriki

MATOKEO YA KUzIjENgEA UwEzO AzAKIKuanzia mwaka 2017, FCS ilianza kutumia mfumo wa Pande Tatu wa Kujenga Uwezo wa AZAKI, ambao umeonyesha dalili za mafanikio zaidi kufikia mabadiliko yanayotarajiwa kwenye programu za FCS. Hii ni kulinganisha na mfumo wa mwanzo wa kujenga uwezo uliokuwa unalenga mradi mmoja mmoja tu. Katika kipindi hiki cha utekelezaji, AZAKI wafadhiliwa wa FCS wamefaidika kwa kiasi kikubwa sana na juhudi za kuwajengea uwezo za FCS moja kwa moja pamoja na zile zilizotekelezwa na taasisi viongozi za makundi ya sekta za miradi. Juhudi hizi za taasisi viongozi zililenga zaidi usaidizi wa kiufundi katika maeneo husika, yakiwemo mifumo ya ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii, uwazi na matumizi ya rasilimali za umma (PETS na SAM). Maeneo mengine ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, miradi ya watu wenye ulemavu na watu wenye ualbino, haki za kumiliki ardhi na ujenzi wa amani na utatuzi wa migogoro. Kwa upande wa FCS, juhudi zake za kujengea uwezo AZAKI zililenga zaidi kuboresha miundo na ufanisi wa AZAKI kitaasisi pamoja na uwezo wao wa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika maeneo yao. AZAKI wafadhiliwa waliwezeshwa kijitathmini uwezo wa asasi zao pamoja na uwezeshaji kwenye maboresho ya maeneo yaliyokuwa na mapungufu katika kufanikisha mabadiliko chanya ya sekta wanazosimamia.

Katika kipindi cha mwaka 2017 pia, FCS iliwekeza kikamilifu juhudi zake katika uratibu wa taarifa, takwimu na ujuzi katika miradi na sekta ambazo AZAKI zinashughulikia. Hii ilitokana na tathmini ya awali kuonyesha kuwa ujenzi wa uwezo kupitia mafunzo pekee ulileta mabadiliko na matokeo chanya kidogo sana. AZAKI wafadhiiwa walipatiwa mafunzo ya aina mbali mbali yakiwemo ya uso kwa uso, mifano hai ya weledi na wanataaluma waliobobea, mabadilishano ya uzoefu na utaalamu baina yao pamoja na majadiliano na ziara za kwenye maeneo ya miradi. Lengo hasa lilikua ni kusimika tabia ya kujifunza kwa AZAKI na pia kuhamasisha mfumo wa kujifunza kupitia wengine wakati wa kubadilishana utaalamu na uzoefu na kuwezesha ujuzi wa mtu mmoja mmoja kuwa chachu ya kujifunza kwa taasisi nzima.

Page 27: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 25

Kujenga uwezo wa mitandao ya asasi na mashirika miavuli kwenye utawala, utetezi na sera

FCS kwa kushirikiana na WAJIBU waliunga mkono mkutano wa wadau unaowawezesha washirika wa maendeleo kutafakari na kutathmini umuhimu wa mapendekezo kwenye ripoti ya Mwaka 2015/2016 ya CAG

120 idadi ya washiriki kutoka kwenyeAZAKI, Bunge, sekta binafsi, Wadau wa Maendeleo na taasisi za utafiti

Mahusiano ya AZAKI na Bunge

Kupitia HakiRasilimali tuliunga mkono mahusiano ya asasi za kiraia na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya kutoa maoni kuhusu miswada ya umiliki wa taifa wamali asili iliyopelekwa bungeni kwa hati ya dharura -2017

15 AZAKI zilizoshiriki

Kusaidia mikutano ya mwezi ya wanawake wenye ulemavu

Lengo lilikuwa kuzipa nguvu sauti za watu wenye ulemavu na wanawake wanapotetea masilahi yao

120 washiriki

Tuliwezesha uundwaji wa mtandao wa asasi za wanawake wenye ulemavu

Mtandao huo ni kituo/jukwaa ambapo wanawake wenye ulemavu wanaweza kukutana, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maishayao kisiasa, kiuchumi na kijamii na kupaza sauti zao

80 washiriki

Tuliwezesha mkutano wa wadau wa asasi za kiraiawa kujifunza na kujitathmini jifunza na kujitathmini

Mkutano huo ulikuwa fursa kwa AZAKI kujitathmini kwa undani kuhusiana na kuwapo siku za usoni kwa asasi za kiraia nchini kulingana na maono na ujumbe.

250 idadi ya washiriki

Tuliwezesha mkutano wa mwaka wa wadau wa AZAKI wa kufanyika

Tathmini ya uwezo wa asasi na uboreshaji wa utendaji kama mbinu ya AZAKI kujitathmini zenyewe na kujijengea uwezo

111 viongozi wa asasi, kiongozi wa serikali wadau wa maendeleo walishiriki

Tathmini za Kitaasisi na Kuzijengea Uwezo AZAKITathmini za ndani na maboresho1 Biashara na Haki za Binadamu Tanzania (BHRT), asasi yenye makao

yake Jijini Dar es Salaam. 2 Vijana wa Kujitolea kwenye Masuala ya Afya na Maendeleo

(VOYOHEDE), asasi hii ipo Mtwara.

Jedwali 4: Matokeo ya mafunzo kwa AZAKI

0% 20% 40% 60% 80% 100% 120%Mafunzo ya Utetezi

Usimamizi wa Miradi na Fedha (1H)Utetezi wa Watu Wenye Ulemavu

Unyanyasaji wa KijinsiaHaki za Ardhi kwa wanawake

Miradi ya VijanaMiradi ya PETS

Usimamizi wa Miradi na Fedha (2H)

Nakubali kidogo Nakubali kiasi

Page 28: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201726

Kwa ujumla, washiriki walitoa taarifa ya kupata maksi 4.42 baada ya kupata mafunzo, ikilinganishwa na maksi 3.11 kabla ya mafunzo, zikiwakilisha mabadiliko chanya ya pointi 1.31 kwenye maksi za uwezo wa wastani wenye maeneo 8 ya uwezo.

Jedwali la 5: Wastani wa alama za uwezo (kulingana na mizania 1-5) wa AZAKI zilizosaidiwa

Na MafunzoAlama Zote (Kabla ya mafunzo)

Alama Zote (Baada ya mafunzo)

1 Mafunzo ya utetezi 1.95 4.05

2 Usimamizi wa miradi na fedha 3.76 4.82

3 Utetezi wa watu wenye Ulemavu 3.35 4.56

4 Unyanyasaji wa kijinsia 3.37 4.46

5 Haki Ardhi kwa wanawake 3.34 4.50

6 Miradi ya Vijana 2.98 4.71

7 Ufuatiliaji rasilimali za Umma 2.95 4.35

8 Usimamizi wa miradi na fedha (2H) 3.18 3.93

Kwa upande mwingine, mafunzo ya utetezi kwa asasi za kiraia za Zanzibar yamerekodi mabadiliko makubwa kwenye alama za uwezo. Hili linahusishwa na ukweli kwamba kwa AZAKI nyingi za Zanzibar, uhamasishaji ni eneo jipya, na ndiyo chaanzo cha alama za chini ya uwezo zilizotolewa kabla ya mafunzo. Maeneo mengi ya mafunzo yaliona ongezeko la pointi 1 kwenye alama ya kujiripoti ya mwanafunzi mwenyewe. Mbali na mafunzo ya utetezi kwa AZAKI za Zanzibar ambazo zimeonyesha ongezeko la kiwango cha 2.10 kwenye uwezo, vingine vya nje vilijumuisha mafunzo kwenye miradi ya vijana na PETS ambayo ilirekodi mabadiliko ya pointi 1.74 na 1.40 kwenye awamu za baada ya mafunzo.

Ni muhimu kutambua kwamba mfumo mpya wa kuendeleza uwezo

unachukulia ongezeko la hatua 1 kama alama ya chini ya mafanikio ya kuimarisha uwezo. Kutoka kwa washiriki 168 kwenye awamu za mafunzo 8, wakiwakilisha mashirika 168, karibu 2 kati ya 5 (39%) waliandika ongezeko la uwezo chini ya alama 1. Vilevile, karibu theluthi moja (33%) walidhihirisha ongezeko la kuridhisha kati ya pointi 1 na 2, wakati karibu 1 kati ya 4 (asilimia 24 ) waliongeza pointi 2 hadi 3. Kiwango kidogo kabisa (1 katika 25, au 4%) kilirekodi ongezeko la alama za uwezo zaidi ya 3.

Jedwali 6: AZAKI zilizoboreshwa Na Mafunzo Chini

ya 11-2 2-3 Zaidi 3 Jumla

1 Mafunzo ya utetezi 4 11 20 4 39

2Miradi ya usimamizi wa fedha 5 9 1 - 15

3 Utetezi wa wenye ulemavu 6 5 1 - 12

4 Ukatili wa kijinsia 14 12 2 - 28

5 Haki Ardhi kwa Wanawake 9 4 1 - 14

6 Miradi ya Vijana 5 5 5 1 16

7 Ufuatiliaji rasilimali za Umma 14 9 9 2 34

8Miradi + Usimamizi wa Fedha 8 1 1 - 10

Idadi ya washiriki wa mafunzo 168

Idadi ya mashirika yaliyodhihirisha angalao ongezeko la pointi 1 kwenye mafunzo

103

Asilimia ya mashirika yanayoonyesha angalao ongezeko la pointi 1 la uwezo wa jumla kwenye maeneo yaliyofundishwa

61%

Page 29: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 27

Jedwali 7: Mabadiliko ya desturi za kazi baada ya kupata mafunzoEneo la Mafunzo

% ya asasi ambazo zilipata maudhui maalum

% zile ambazo zina-tumia utaratibu mpya

% asasi ambazo hazitumii utaratibu mpya

% zile zinazo-tumia

% zisi-zotumia

Tathmini ya wadau

114 65 49 57% 43%

Mkakati 56 32 24 57% 43%Kubuni mbinu za ufuatiliaji

96 56 40 58% 42%

Kubuni njia za kufuatilia mradi

70 46 24 66% 34%

Kutumia mbinu za ubunifu

36 17 19 47% 53%

Kutumia mbinu za ufuatiliaji

10 6 4 60% 40%

Kufanya ulinganifu

10 6 4 60% 40%

Weka miongozo ya maudhui

10 6 4 60% 40%

Uangaliaji wa kina wa takwimu waonyesha kwamba ubunifu wa zana za ufuatiliaji wa miradi ulikuwa mojawapo wa ujuzi uliokuwa rahisi zaidi kueleweka, ambapo theluthi mbili za wale waliopitia mafunzo walitumia mbinu hizo. Kwa upande mwingine, matumizi ya njia za ubunifu yaelekea kupokelewa kwa kasi ndogo na kiwango kidogo zaidi, ambapo chini ya nusu ya washiriki waliopewa mafunzo ya hatua za kujenga uwezo kwenye eneo eneo hili wanatoa taarifa kwamba wametumia kila aina ya mbinu za ubunifu kwenye utendaji wao wa kazi.

Mafanikio: Kikundi cha Kinamama Wajane

“Ni kweli kwamba FCS ilitupa fursa ya kupata ujuzi kwenye aina za ujuzi wa kuendeleza shirika kama usimamizi wa miradi na utoaji wa tarifa, usimamizi wa rasilimali, usimamizi wa fedha na mbinu za kutoa taarifa na uwezeshaji ambazo tutaendelea kuzitumia hata baada ya mradi huu ambao unafadhiliwa na FCS kumalizika,” anaeleza Rehema wa kundi la Akina Mama Wajane. Kabla ya kupewa mafunzo, Akina Mama Wajane hawakuwahi kupeleka ripoti zao kwenye Manispaa ya Temeke zikapokelewa kama ilivyosibu baada ya kupata mafunzo ya kunolewa. “Ikawa rahisi kwetu kuwahamasisha viongozi wa jamii na wasichana na wavulana kwa kutumia mbinu tulizopata kwenye mafunzo ya kujenga uwezo wa waelimishaji wa rika ambao hivi sasa wanawafikia mamia ya vijana wenzao huko mitaani na kuwapa elimu ya mbinu za maisha,’’ anakiri .

Kutokana na ufahamu wa mbinu za ujuzi wa maisha, jukwaa la jamii na vyombo vya habari, Akina Mama Wajane waliweza kuanzisha klabu nne kwenye kila shule ndani ya kata nne. Wakufunzi 40 wa elimu ya rika walifaulu kuendeleza elimu ya mbinu za maisha kwa zaidi ya wasichana na wavulana 1,200 kwenye kata zilizo kitovu cha mradi kati ya mwaka 2016 na Machi 2017.

Utetezi, sera shirikishi na mafunzo Mnamo mwaka 2017, FCS ilizisaidia AZAKI kufuatilia zoezi la uhakiki wa utaratibu wa kuboresha kandidata za AZAKI na kuzitathmini shughuli za asasi kama hizo kwa lengo la kuunda sekta thabiti ya AZAKI. Shughuli hizo ziliongozwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.

Page 30: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201728

Kupitia THRDC na NaCONGO, FCS ilifadhili uwepo wa mikutano kadhaa ya ushauri na wakurugenzi wa AZAKI na Msajili wa AZAKI ili kutafuta njia bora zaidi za kuendesha zoezi hilo. Kufuatia hatua zilizochukuliwa na asasi za kiraia, serikali ilikubali kuongeza muda wa uhakiki kutoka siku 10 hadi 30. Hatua hii iliziwezesha AZAKI kupata fursa ya kwenda kwenye ofisi za kanda kwa uhakiki. Zoezi hili pia liliboresha uhusiano baina ya serikali na asasi za kiraia hapa nchini.

miaka 15 tangu ilipoanzishwa. Ikiwa mfadhili mkubwa kabisa asasi za ngazi za chini nchini. FCS imechangia sana kwenye kujenga uwezo wa asasi za kiraia hapa Tanzania na kuziwezesha AZAKI na wananchi kuwa nguvu ya kusukuma ushawishi wa utawala wa kidemokrasia hapa nchini na kuwapo kwa maisha bora zaidi.

Kumbukumbu hiyo ilichukuliwa kama fursa kwa wadau wa FCS kuyatathmini kwa undani masuala ya siku za nyuma, sasa na baadaye ya asasi za kiraia hapa nchini na kumulika mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 15.

Mkutano huo ambao dhana yake ilikuwa “Kuzungusha magurudumu ya asasi za kiraia,” ulihimiza kuwapo kwa mifumo ya uwajibikaji kwenye sekta, kutafuta fursa za kuimarisha uhusiano na sekta binafsi na serikali kulingana na maono na ujumbe wa FCS.

Mkutano huo wa kilele ulihudhuriwa na wadau 350 kutoka kwenye asasi za kiraia, taasisi za elimu na utafiti, sekta binafsi, wawakilishi wa serikali na vyombo vya habari.

Mh. Waziri Jenister Mhagama (katikati) akizindua majarida ya FCS mwaka 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS akifanya mazungumzo na Waziri Jenister Mhagama wakati wa Maadhimisho ya miaka 15 ya FCS

Nafurahi sana kwani mafunzo yameugeuza mtazamo wangu wa kufanya uchambuzi na ushawishi wa sera. Vilevile, niliwezeshwa kujiamini zaidi katika kuzungumza hadharani na kutoa maoni kwa niaba ya jumuiya.

Ushuhuda

Mshiriki kutoka Jozani Environmental Conservation Association (JECA)

Taarifa ya Matukio Maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa FCS Mnamo mwaka 2017, FCS ilitimiza msafara wa

Page 31: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 29

Mtandao wa Asasi za Wanawake wenye Ulemavu

Kiongozi wa SHIVYAWATA wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa Wanawake wenye Ulemavu

FCS ilifadhili uundaji na uzinduzi wa Mtandao wa Wanawake wenye ulemavu kupitia SHIVYAWATA. Mtandao huo ni jukwaa la wanawake wenye ulemavu watakapoweza kujadili masuala mbalimbali ya ustawi wao na jinsi ya kuwa na sauti moja. Wanawake 80 wenye ulemavu walishiriki kwenye uzinduzi huo.

Kupitia jukwaa hili, mafanikio kadhaa yamepatikana: • Kuwaunganisha wanawake wenye

ulemavu na taasisi za fedha na ushirika ili kuhakikisha kwamba wanawezeshwa kifedha. Mathalani, wanawake wenye ulemavu wameunganishwa na Dar es Salaam Community Bank (DCB) ili kupata mikopo yenye riba ndogo kwa ajili ya kuanzisha biashara.

• Vilevile, wanawake hao wameunganishwa na mafunzo ya ufundi jijini Dar es Salaam.

• Uelewa uliopatikana kupitia mtandao huo umefanya akina mama wajiamini zaidi na

kupata uelewa. Isitoshe, umewapa moyo kujiunga na Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi. Majukwaa haya huwapa akina mama mafunzo ya ujasiriamali. Mathalani, wanawake wenye ulemavu sita (6) kutoka kata za Temeke na Mburahati wamejiunga na Jukwaa la Kuwawezesha Wanawake kwenye ngazi ya kata.

• Mtandao huo umeongeza mwonekano na utambuzi wa wanawake wenye ulemavu miongoni mwa asasi za wanaharakati wa jinsia na wanawake/ AZAKI kama Mfuko wa Wanawake (Women Fund), Mtandao wa Mpango wa Kijinsia Tanzania (TGNP) na Wanawake wa Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF).

Tumefadhili mikutano ya kila mwezi ya wanawake wenye ulemavu Jumla ya wanawake 266 wenye ulemavu na wawakilishi wa serikali walishiriki kwenye mikutano sita (6) ya kila mwezi mnamo mwaka 2017. Baadhi ya masuala muhimu yaliyojadiliwa yalikuwa Ukatili wa Jinsia, ushiriki wa wanawake walemavu kwenye siasa, ujasiriamali na uendelezaji wa biashara. Mipango mkakati iliandaliwa na kushirikishwa kwa viongozi wa serikali. Mikutano hiyo pia ilisaidia kuongeza ushirikiano baina ya watu wenye ulemavu, serikali za mitaa na Dawati la Jinsia la Polisi. Wanawake Wenye Ulemavu hivi sasa wanapata ushauri wa kisheria na msaada wa haki zao kutoka kwenye vyombo vya serikali kama jeshi la polisi.

Kuwezesha chapisho lenye sheria, sera, taratibu na miongozo yote ya AZAKI

Asasi za kiraia za Tanzania zilisherehekea miaka 30 ya shughuli zao mnamo mwaka 2017. Kwenye tarehe 13 na 14 mwezi Oktoba 2017, zaidi ya asasi za kiraia 70 zilizopo Tanzania zilikutana Arusha kwa ajili ya kufanya tafakari ya siku mbili. Kwenye mkutano huo, wakurugenzi wa AZAKI, wawakilishi wa serikali, wasomi na wadau wengine walifanya tafakari ya pamoja ya kutathmini sekta ya asasi za kiraia baada ya kuendesha shughuli zao kwa miaka 30.

Mojawapo ya mapendekezo ilikuwa kuandaa mkusanyiko wa sheria zote, sera, taratibu na miongozo inayoongoza shughuli za asasi za kiraia nchini Tanzania.

Mkutano wa Mwaka wa Asasi za Kiraia za Zanzibar Lengo ni kurahisisha mchakato wa kujiendeleza na kuwa na kuleta uelewa miongoni mwa AZAKI mbalimbali kuhusu baadhi ya vipengele vya kisheria ambavyo vinaelekeza taratibu za usajili na kuendesha shughuli ambazo asasi za kiraia zatakiwa kufanya.

Mkutano ulifanyika tarehe 23 na 24 Septemba, 2017 nao ulijumuisha washiriki 111 ( Wanawake 32, Wanaume 79) kutoka asasi za kiraia za Unguja na Pemba. Uliwajumuisha watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na wazee, waandishi wa habari na wadau wengine wa asasi za kiraia za Zanzibar. Lengo la mkutano lilikuwa kuhamasisha utii kwa masuala ya utawala bora kuhusu mgawanyo wa madaraka, haki za binadamu, na mifumo ya utekelezaji wa sheria.

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 29

Page 32: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201730

TAARIFA zA FEDHA

Page 33: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 31

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETYSTATEMENT OF PROFIT OR LOSS AND OTHER COMPREHENSIVE INCOME FOR YEAR ENDED 31 DECEMBER 2017

NOTES 2017 2016

TZS’000 TZS’000

REVENUEAccountable grants 5 17,913,249 10,322,247

Other income 6 312,902 284,846

Total income 18,226,151 10,607,093

Grants disbursements 7 11,568,235 4,200,554Other grants expenses 8 4,126,145 3,527,937FCS anniversary expenses 9 199,882Administrative expenses 10 2,636,945 2,915,797

Total expenditure 18,531,207 10,644,288

Deficit for the year (305,056) (37,195)Other comprehensive income - -

Net deficit for the year (305,056) (37,195)

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETYSTATEMENT OF FINANCIAL POSITION AS AT 31 DECEMBER 2017

NOTES 2017 2016

TZS’000 TZS’000

ASSETS

Non- current assets

Property and equipment 11 1,606,558 1,590,557

Intangible assets 12 56,333 –

1,662,891 1,590,557

Current assets

Cash and cash equivalents 13 1,133,368 4,170,328

Prepayment 14 214,224 227,192

Trade and other receivables 15 1,470,165 –

2,817,757 4,397,520

TOTAL ASSETS 4,480,648 5,988,077

EQUITY AND LIABILITIES

EQUITY

Revaluation reserve 212,204 252,401

Accumulation surplus 1,283,225 1,542,146

1,495,429 1,794,547

Page 34: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201732

FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETYSTATEMENT OF CASH FLOW FOR THE YEAR ENDED 31 DECEMBER 2017

2017 2016TZS’000 TZS’000

Cash flows from operating activitiesSurplus/Deficit for the year (305,056) (37,195)Adjustments for:Depreciation 70,362 72,062Amortization 28,161 -Interest income (561) (5,119)Loss on disposal 7,277 -

(199,817) 29,748

Changes in:Receivables (1,470,165)Prepayments 12,968 21,254Trade and other payables 19,551 281,726Deferred income (1,227,862) 2,077,065Net cash flows generated from operating activities (2,865,325) 2,409,793

Investing activitiesPurchase of furniture and equipment (120,014) (19,843)Purchase of intangible assets (84,494) -Purchase of office infrastructure (35,583)Proceeds from Disposal of assets 32,312Bank Interest received 561 5,119Net cash used in investing activities (171,635) (50,307)

Financing activitiesLoan repayments - (562,491)Net Cash used in financing - (562,491)Net changes in cash and cash equivalent during the year (3,036,960) 1,796,995

Cash and Cash equivalent at start of the year 4,170,328 2,373,333Cash and Cash equivalent at the end of the year 1,133,368 4,170,328

LIABILITIES

Non- current liabilities

Employee Long Term Service Award 16 177,112 310,359

177,112 310,359

Current liabilities

Trade and other payables 17 877,229 724,431

Deferred income 18 1,930,878 3,158,740

2,808,107 3,883,171

Total Income 2,985,219 4,193,530

Total equity and liabilities 4,480,648 5,988,077

The financial statement were approved for issue by the board of directors on________ 2018 and were signed on behalf by:

______________________Sosthenes SambuaActing Chairperson

Page 35: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 33

UTAwALA

Bw Alais MorindatMwanachama

Wanachama

Bodi ya Wakurugenzi

Dk Stigmata TengaMwanachama/Rais

Bi Margareth ChachaMkurugenzi

Bw Stephen ShayoMkurugenzi

Bw Sosthenes SambuaMkurugenzi/Mwenyekiti

Bi Mary RusimbiMwanachama

Prof Samwel WangweMwanachama

Bi Olive LuenaMwanachama

Bw Salum ShamteMwanachama

Bw Rakesh RajaniMwanachama

Bw Francis KiwangaKatibu wa Wanachama

Bi Nesia MahengeMkurugenzi

Bw Francis KiwangaKatibu wa Bodi

Prof Honest NgowiMkurugenzi

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 33

Page 36: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201734

Menejimenti

Bw Francis KiwangaMkurugenzi Mtendaji

Bi Martha OlotuMeneja wa Maendeleo, Biashara na Ushirikiano

Bw John AswileMeneja wa Fedha na

Utawala

Bi Edna ChilimoMeneja wa Kujengea

Uwezo AZAKI

Bw Guesturd HauleMkuu wa Ufuatiliaji, Tathmini, Tafiti na

Mafunzo

Bw Francis UhadiMeneja Miradi

Sekretarieti

Nasim Losai

Rosemary Mjule

Bertha Ngwada

Eveline Mchau

Nemes Maro

Nicholaus Mhozya

Karin Rupia

Imran Sherali

Neil Ngala

Georgina Lund

Rehema Malongo

Bartholomew Mbiling’i

Evanerda Minja

Boniphace Makene

Basil Lema

Yonah Lyimo

Maria Chang’a

Tusekile Anangisye

Shamsia Manu

Page 37: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 35

Mh Florence Tinguely Mattli, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania akihutubia maadhimisho

MATUKIO KwENYE PICHA

Wilson Mwakafyula akitengeneza samani kwa ajili ya watoto wa kituo cha CST kutokana na mabaki ya karatasi

Wajumbe wa AZAKI Moja ya mijadala wakati wa maadhimisho

Moja ya darasa katika kituo cha Child Support Tanzania (CST) mkoani Mbeya

Ziara ya Pamoja kukagua shule ya sekondari kwa ajili ya wasichana wilayani Kyela

Mjadala wa Mashirikiano kati ya Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia

Musa Method Kidiga akitengeneza viti vya bustani kwenye kituo cha Child Support Tanzania (CST)

Maadhimisho ya Miaka 15 ya Foundation for Civil Society

ziara ya Pamoja ya Miradi ya AzAKI mkoani Mbeya

MwAKA 2017

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 35

Page 38: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

Wadau wetu wa maendeleo mwaka 2017

Page 39: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 2017 37

Page 40: TAARIFA YA MWAKA 2017 - thefoundation.or.tz · utekelezaji wa mkakati wetu. Huu ulikuwa mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu (2016- 2020). Ninapofakari juu ya jitihada

FCS Taarifa ya Mwaka 201738

7 Madai Cresent, Ada Estate, Kitalu Na. 154, KinondoniSLP 7192, Dar es SalaamSimu: +255 22 2664890-2

Baruapepe: [email protected]: www.thefoundation.or.tz