tafsiri rahisi ya mpango kazi wa taifa wa ...duniani na siku ya mtoto wa afrika na mtoto wa kike...

13
TAFSIRI RAHISI YA MPANGO KAZI WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO TANZANIA (MTAKUWWA) DISEMBA, 2018 NITAWAELEZEA JINSI YA KUPATA FURSA AMBAZO ZITAWEZA KUWASIDIA KATIKA MAISHA YENU NA KUEPUKANA NA VITENDO VYA KIKATILI

Upload: others

Post on 24-Jan-2020

51 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

1

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO KAZI WA TAIFA WAKUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE

NA WATOTO TANZANIA (MTAKUWWA)

DISEMBA, 2018

NITAWAELEZEA JINSIYA KUPATA FURSA AMBAZO

ZITAWEZA KUWASIDIA KATIKA MAISHA YENU NA KUEPUKANA NA

VITENDO VYA KIKATILI

2 i

TAFSIRI RAHISI YA MPANGO KAZI WA TAIFA WAKUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI

YA WANAWAKE NA WATOTO TANZANIA (MTAKUWWA)

2017/18 - 2021/22

MPANGO KAZI WA TAIFA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO TANZANIA 2017/18 – 2021/22 Kimetayarishwa na: Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) Kimefadhiliwa na: Shirika la Foundation for Civil Society (FCS) Mchora Katuni: Mhidini Msamba

ii iii

YALIYOMO

Vifupisho vya Maneno ............................................................................................................................................................................. iv

Tafsiri ya Dhana za Msingi .................................................................................................................................................................... v

Dibaji ...................................................................................................................................................................................................................... vi

SEHEMU YA I: Utangulizi .............................................................................................................. 11.1 Wasifu wa Tanzania. ............................................................................................................................................................................... 1

1.2 Hali ya Kijamii na Kiuchumi ............................................................................................................................................................ 1

1.3 Tathmini ya Hali Halisi ................................................................................................................................... ..................................... 1

1.4 Jitihada za kitaifa za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ............................................. 2

1.5 Mapungufu /changamoto za kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na

watoto ................................................................................................................................................................................................................... 3

SEHEMU YA II: DIRA, DHIMA, LENGO NA SHABAHA YA MTAKUWWA ........................42.1 Dira. ...................................................................................................................................................................................................................4

2.2 Dhima.............................................................................................................................................................................................................4

2.3 Lengo. .............................................................................................................................................................................................................4

2.4 Mikakati muhimu ya MTAKUWWA ....................................................................................................................................... 5

2.5 Viashiria vya Matokeo Makuu ya MTAKUWWA ............................................................................................................ 5

2.6 Mbinu za Utekelezaji wa MTAKUWWA ............................................................................................................................... 5

SEHEMU YA III: MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA ..................................... 63.1 Matokeo ya MTAKUWWA ................................................................................................................................................................ 7

SEHEMU YA IV: GHARAMA ZA MPANGO KAZI WA MTAKUWWA ................................8SEHEMU YA V: MFUMO WA URATIBU KITAASISI WA MTAKUWWA ............................. 9SEHEMU YA VI: UFUATILIAJI NA TATHMINI YA MTAKUWWA ...................................... 146.1 Malengo ya Ufuatiliaji wa MTAKUWWA ............................................................................................................................ 14

Mpango Kazi

Kutokomeza

Ukatili dhidi ya

Wanawake

na Watoto

UKINIKUBALIAOMBI LANGU

KAZI UTAPATA

iv v

VIFUPISHO VYA MANENO

AZAKI Asasi za Kiraia

MMW Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri

FBO Asasi za Kidini

AMM Afisa Mtendaji wa Mtaa

WAMJW Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

MTAKUWWA Mpango Kazi wa Kitaifa Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake na

Watoto

NGOs Asasi zisizo za kiserikali

NPSC Kamati Kuu ya Kitaifa ya Ulinzi wa atoto

NPTC Kamati ya Ufundi ya Ulinzi wa Watoto

OWM Ofisi ya Waziri Mkuu

OR-TAMISEMI Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

RS Tawala za Mkoa

SDG’s Malengo ya Maendeleo Endelevu

TWG Kikosi Kazi cha Ufundi

AMKj Afisa Mtendaji wa Kijiji

AMK Afisa Mtendaji wa Kata

WHO Shirika la Afya Duniani

SM Sekretariati ya Mkoa

KTM Katibu Tawala wa Mkoa

Tafsiri ya Dhana za Msingi

Mtoto: Mtu yeyote chini ya umri wa miaka kumi na nane

Ukatili dhidi ya mtoto: Ukatili wa mtoto unaosababisha madhara ya kimwili na kihisia ukijumuisha vipigo, matusi, udhalishaji wa kingono, kutelekezwa na utumikishwaji.

Utelekezwaji wa Mtoto: Mzazi au mlezi wa mtoto kushindwa kutoa huduma muhimu kwa mtoto kama vile chakula, malazi, mavazi, elimu, huduma za matibabu nk.

Udhalilishaji wa Kingono kwa Mtoto: Mtu mzima kumwingilia mtoto kingono kwa kutumia udanganyifu, vitisho au nguvu.

Ajira kwa Mtoto: Ajira yenye madhara/hatarishi kwa mtoto kimwili, kimakuzi na kiakili

Familia: Baba, mama na watoto wa kuwazaa, kuwalea, kuasili au ndugu wa karibu.

Ukatili wa Kijinsia: Ni ukatili unaomwathiri mtu kimwili, kisaikolojia, kijamii na kiuchumi.

Ukatili dhidi ya Mwenza: Ukatili ndani ya mahusiano unaosababisha madhara kimwili, kimapenzi na kisaikolojia.

Ukatili wa kimwili: Unahusisha vipigo, ngumi, mateke au vitisho kwa kutumia silaha.

Mzazi: Baba au mama mzazi, baba au mama wa kuasili au mtu yeyote aliyeahidi kwa makubaliano kumtunza mtoto

Malezi: Utaratibu wa kumlea mtoto tangu utotoni hadi utu uzima.

Unyanyasaji wa kisaikolojia: Matumizi ya lugha inayolenga kumletea mtu maumivu au hofu au msongo wa mawazo

Ukatili wa Kingono: Jaribio la kupata tendo la ngono kwa kutumia nguvu na vitisho.

Msongo wa mawazo: Hutokea wakati mtu akiwa na shida kwa muda mrefu bila kuwa na ufumbuzi wa tatizo hilo.

vi 1

Dibaji

Ukatili dhidi ya wanawake na watoto umekuwa ni changamoto kubwa sana nchini na duniani kwa ujumla. Takwimu za shirika la Afya duniani (WHO) zinaonyesha kuwa moja kati ya wanawake watatu duniani amekutana na ukatili wa kimwili au kingono katika kipindi chake cha maisha. Nchini takribani wanne kati ya wanawake 10 wamepitia ukatili wa kimwili na asilimia 17 wamepitia ukatili wa kingono katika maisha yao.

Utafiti uliofanywa juu ya ukatili dhidi ya watoto (2011) unaonesha kuwa takribani mmoja kati ya wavulana saba amekutana na ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18, na kati yao 71% wamekutana na ukatili wa kimwili. Hata hivyo, utafiti huo unaonyesha kuwa kwa upande wa watoto wa kike, idadi ipo juu zaidi kwa mmoja kati ya watatu na asilimia 72.

Licha ya athari wanazopata watoto au wanawake kimwili na kisaikolojia kutokana na vitendo vya ukatili, vitendo hivyo pia vinaathari kubwa sana katika uchumi. Takwimu zinaonyesha, vitendo vya ukatili vinaugharimu uchumi wa dunia kati ya asilimia tatu hadi nane ya pato lake na kwa Tanzania, zaidi ya billioni 6.5 za kimarekani, ambayo ni sawa na asilimia saba ya pato la taifa, hupotea. Katika kutatua changamoto hizo, serikali kwa kwa kushirikiana na Wadau imeandaa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA 2017/18 – 2021/22). Mpango huu pia unalenga kuiwezesha nchi kutekeleza malengo ya Maendeleo Endelevu (2030), Ajenda ya Maendeleo ya Tume ya Umoja wa Afrika (2063) na Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025). Katika kurahisisha utekelezaji wa Mpango kazi huu, TGNP Mtandao ikishirikiana na shirika la Foundation for Civil Society (FCS), imeandaa Tafsiri rahisi ya MTAKUWWA. Kijitabu hiki pendwa kinalenga kusaidia jamii kuielewa vizuri na kuitekeleza dhana zima ya uratibu wa pamoja katika utoaji huduma bora kuzuia, kukabiliana na kutafuta ufumbuzi dhidi ya vitendo vya ukatili.

Nimatumaini yangu kuwa kitabu pendwa hiki kitakuhabarisha, na kukuwezesha kuchukua hatua ya kuwalinda wanawake na watoto wa kike dhidi ya ukatili. Kwa pamoja tunaweza kuwa na Tanzania bila Ukatili wa kijinsia. Chukua hatua-Linda wanawake na watoto.

Lilian Liundi Mkurugenzi MtendajiTGNP Mtandao.

SEHEMU YA 1

1.1 Wasifu wa Tanzania

Kwa mujibu wa Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, idadi ya wakazi nchini Tanzania kwa mwaka 2012 ilikuwa milioni 44.9. Kwa kuzingatia kiwango cha ongezeko la idadi ya watu, Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani ya wakazi milioni 50.6 ambapo milioni 24.6 ni wa kiume (48.7%) na wanawake milioni 26 (51.3%) kwa mwaka 2016. Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ni asilimia 50.1% ya watu wote ambapo wanaume ni 48.6% na wanawake ni 51.4%.

1.2 Hali ya Kijamii na KiuchumiTakribani asilimia 28.2 ya idadi ya watu waliishi chini ya kiwango cha kawaida cha umasikini mwaka 2012, ikionyesha kupungua kwa idadi ya watu hao kutoka asilimia 34% ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa Sensa hiyo, umasikini wa vijijini ulikuwa asilimia 33.3 na asilimia ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri ilikuwa asilimia 11.3%.

1.3 Tathmini ya Hali HalisiUkatili wa kijinsia ni hali halisi inayojitokeza miongoni mwa wanawake na watoto nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Ripoti ya Dunia ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2015, asilimia 35% ya wanawake duniani kote walishawahi kukumbwa na ukatili wa kimwili au wa kingono kutoka kwa wenza wao wa karibu. Nchini Tanzania, takribani wanawake wanne kati ya kumi walishakumbwa na ukatili wa kimwili na moja kati ya wanawake watano wameshawahi kufanyiwa ukatili wa kingono katika umri wa miaka 15.

Ukatili ndani ya ndoa umeshamiri zaidi kwa kiwango cha asilimia 44% kwa wanawake walioolewa. Kwa mujibu wa Utafiti wa Idadi ya Watu na Afya wa mwaka 2010, asilimia 39% ya wanawake kati ya umri wa miaka 15-49 wameshawahi kufanyiwa ukatili wa maungoni tangu wakiwa na umri wa miaka 15 na karibu theluthi moja ya wanawake (asilimia 33%) wenye umri kati ya miaka 15-49 walifanyiwa vitendo hivyo miezi 12 kabla ya utafiti.

Ushahidi unaonyesha kuwa rushwa ya ngono ni jambo linalozidi kuongezeka nchini – huku wanawake wakiombwa rushwa ili kupatiwa upendeleo katika utumishi wa umma, mahala pa kazi, shule za msingi na sekondari, vituo vya afya na ofisi za umma.

Kufanyiwa ukatili utotoni huacha majeraha ya kudumu katika ubongo wa mtoto ambao unaweza kumwathiri maisha yake yote.

Mbali na ukatili wa kimwili, kingono, na kihisia, Tanzania bado ina mila na desturi zenye madhara kwa wanawake na watoto. Wanawake wa Tanzania wanaolewa katika umri mdogo - karibu miaka mitano ikilinganishwa na wanaume. Ukeketaji nchini Tanzania umeenea kwa kiasi kikubwa na katika baadhi ya Jamii unafikia asilimia 70.8%. Inakadiriwa kuwa takribani wanawake na watoto wa kike milioni 7.9 nchini Tanzania wanakadiriwa kuwa wamekeketwa.

2 3

Pamoja na kufanyiwa ukatili, wahanga wanakabiliwa na changamoto ikiwemo kukosa huduma bora za uchunguzi wa polisi, wahalifu kutokuchukuliwa hatua, vitisho na kubaguliwa. Mfumo wa haki pia unakwamishwa na gharama, uhaba wa huduma za kisheria, rushwa na uelewa mdogo wa haki za binadamu miongoni mwa wanajamii.

1.4 Jitihada za kitaifa za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Asasi Zisizo za Kiserikali, Asasi za Kiraia na za Kidini inafanya kazi ya kupitia program mbalimbali ikiwa ni pamoja na shughuli za kukuza uelewa wa Jamii, kama vile maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Siku ya Familia Kimataifa, Siku ya Wanawake Duniani na Siku ya Mtoto wa Afrika na Mtoto wa Kike Duniani, ili kuhakikisha utekelezaji wa mikakati iliyopo katika mpango wa MTAKUWWA.

Jitihada ambazo zimefanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki za wanawake na watoto katika kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni pamoja na:

i. Kutungwa na kufanyiwa kazi sera na sheria mbalimbali zinazolenga kuboresha mifumo ya kisera, kisheria na kitaasisi;

ii. Kuweka mifumo ya ulinzi wa watoto katika Mamlaka za Serikali za Mtaa 47;iii. Kuunda timu za ulinzi na usalama wa mtoto katika ngazi za wilaya

na kijiji na kuziwezesha kupambana na ukatili dhidi ya watoto;iv. Kuhakikisha maafisa husika, kama maafisa ustawi wa jamii, polisi, na

wahudumu wa afya wanazifanyia kazi ipasavyo kesi za ulinzi wa watoto, kutunza kumbukumbu na kuzipeleka mamlaka za juu inapobidi;

v. Kuundwa kwa kamati za ajira kwa watoto katika ngazi za taifa na halmashuri kufuatilia na kuainisha mazingira ya ajira kwa watoto na kufanya uchunguzi wa aina za kazi ambazo zina madhara kwa watoto au mazingira hatarishi kwa watoto;

vi. Jeshi la Polisi Tanzania limeanza mchakato wa kuunda madawati ya jinsia na watoto nchini na kuanza kuwapa mafunzo maafisa polisi kuhusu ukatili dhidi ya watoto na ukatili wa kijinsia;

vii. Kamati ya kitaifa ya kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake iliundwa ili kumshauri Waziri mwenye dhamana ya masuala ya wanawake na watoto kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto;

viii. Kuanzishwa kwa namba za usaidizi kwa watoto wanapokumbwa na ukatili mwaka 2013, ambazo zinapatikana katika mitandao yote ya simu nchini Tanzania;

ix. Kuanzisha vituo vinne vya mkono kwa mkono (one stop centre) Mikoa ya Dar es Salaam (Hospitali ya Amana), Shinyanga (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa), Mwanza (Hospitali ya Sekou Toure) na Iringa (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa) ili kutoa huduma za afya, ushauri nasihi na msaada wa kisheria kwa wahanga wa ukatili;

x. Juhudi zinafanywa kuipitia na kufanyia marekebisho Sheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 kukataza mtoto aliye shuleni kuoa au kuolewa na Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ili kuongeza umri wa kuolewa kwa wasichana kutoka miaka 14 hadi 18; na

xi. Mfumo wa kuwa na mtu wa kufuatilia masuala ya jinsia katika taasisi ili kuhakikisha masuala ya jinsia yanazingatiwa katika kutunga sera, kupanga mipango na bajeti, na kuhakikisha masuala yote ya kimaendeleo yanafanyika

kwa kuzingatia jinsia.

1.5 Mapungufu /changamoto za kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Licha ya serikali kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, bado kuna changamoto katika ngazi ya Jamii zinazojumuisha:

● Kukosekana kwa uratibu wa pamoja miongoni mwa wadau muhimu;

● Huduma zisizokidhi kiwango kwa wahanga wa ukatili;

● Wanaume kushika hatamu katika maeneo mengi ya kiuchumi na kijamii

na hivyo kuwafanya kuwa na nguvu zaidi za kiuchumi ikilinganishwa na

wanawake;

● Matunzo duni ya watoto kutoka kwa wazazi katika ngazi ya familia;

● Uelewa mdogo wa haki za kijamii, kiuchumi na kisheria miongoni mwa

wanawake na wanaume; na

● Utamaduni wa ukimya unaotokana na unyanyapaa, hofu na kutengwa kijamii.

4 5

SEHEMU YA II

DIRA, DHIMA, LENGO NA SHABAHA YA MTAKUWWA

Wanawake na Watoto wa Tanzania wako huru dhidi ya ukatili na wanapata haki zao na usalama katika Jamii.

2.1 DiraMpango Kazi Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake

na Watoto

2.2 DhimaKuzuia na kukabiliana na aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto kwa njia ya ushirikiano wa sekta mbalimbali katika ngazi zote.

2.3 LengoKutokomeza ukatili dhidi ya

wanawake na watoto na kuboresha ustawi wao nchini Tanzania

2.4 Mikakati muhimu ya MTAKUWWA(i) Kuimarisha kaya kwa kuwawezesha wanaume, wanawake, wasichana na

wavulana katika kutafuta fursa za kijamii(ii) Kuimarisha kanuni na maadili yanayojenga uwezeshaji wa wanawake na

kulinda jamii isiyokuwa na ukatili, yenye heshima na usawa wa kijinsia.(iii) Kujenga na kudumisha maeneo salama kwa wanawake na watoto katika

jamii zetu(iv) Kukuza mahusiano mazuri ya mzazi na mtoto na kupunguza vitendo vya

kikatili vinavyofanywa na wazazi(v) Kujenga Jamii ya Kitanzania ambayo inaelewa na kuthamini mapendekezo

ya mabadiliko ya kisheria yanayotekelezwa kulinda Jamii dhidi ya ukatili(vi) Mfumo imara wa ulinzi unaoratibiwa kutoa msaada wa haraka, bora na wa

uhakika kulinda wanawake na watoto dhidi ya madhara ya ukatili(vii) Mfumo wa Kitaifa ambao ni imara na wenye ufanisi kuratibu utoaji wa

maamuzi na kuzuia vitendo vya ukatili.

2.5 Viashiria vya Matokeo Makuu ya MTAKUWWA

(i) Asilimia 50% ya wanawake wameondokana na ukatili ifikapo mwaka 2021/22

(ii) Asilimia 50 ya watoto wameondokana na ukatili ifikapo mwaka 2021/22

2.6 Mbinu za Utekelezaji wa MTAKUWWA

Mbinu zifuatazo zitatumika katika utekelezaji wa mikakati iliyoainishwa:

i. Kupata mfumo sahihi wa kisheriaii. Kuongeza uwezo wa kukabiliana na ukatili iii. Kujikita zaidi katika kuzuia ukatili

iv. Kuimarisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi na utoaji wa taarifa

6 7

SEHEMU YA III

MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MTAKUWWA

Mpango wa utekelezaji wa MTAKUWWA umeanzishwa ili kukabiliana na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto nchini Tanzania kwa kutoa, kubainisha hatua za kipaumbele, matokeo yanayotarajiwa, muda wa utekezaji, watendaji wakuu na kuweka viashiria muhimu vya kufuatilia matokeo. Muda wa utekelezaji umegawanyika katika makundi ya muda mfupi (hadi miaka miwili), ya muda wa kati (miaka miwili hadi mitano) na muda mrefu (miaka mitano na zaidi). Changamoto za kukabiliana na ukatili zitakazoshughulikiwa ni pamoja na umaskini, mazingira yasiyo salama, unyanyasaji wa watoto mashuleni na mila na desturi zenye madhara katika jamii, n.k.

Kazi zitakazotekelezwa katika kila eneo kuu la mpango huu ni zifuatazo:

I. Kuimarisha uchumi wa kaya

Ii. Kuimarisha kanuni na maadili ya jamii

Iii. Kuimarisha usalama wa wanawake na watoto

Iv. Kuboresha malezi, ushiriki wa familia na mahusiano.

V. Kushinikiza utekelezaji wa sheria

Vi. Kuboresha huduma na usaidizi kwa wakati

Vii. Kuimarisha usalama mashuleni na kukuza elimu ya stadi za kazi katika

mfumo wa elimu ulio rasmi na usiokuwa rasmi.

Viii. Kuimarisha mfumo wa uratibu, ufuatiliaji na tathmini

Shirika la Afya Duniani (WHO) liliunda mfumo uitwao INSPIRE ili kuanisha na kuchambua masuala 18 yanayohusiana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kama yanavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo.

Masuala Yaliyoibuliwa katika Mipango Kazi 8 ya Sasa

Mkakati w INSPIRE Eneo la Mpango Kazi

1. Kuwezesha familia kiuchumi.

Kuimarisha kaya kwa kuwawezesha wanaume, wanawake, wasichana na wavulana katika kutafuta fursa za kiuchumi

1. Kuimarisha Uchumi wa Kaya2. Wafanyabiashara ya ngono.

3. Kubadilisha mitizamo hasi na kulinda wanawake na watoto.

Kuimarisha taratibu za kijamii na tunu zinazowawezesha wanawake na kuunga mkono mahusiano ambayo sio ya kikatili na yenye kuzingatia usawa wa kijinsia.

2. Kuimarisha Kanuni naMaadili ya jamii

4. Uchawi na kuchoma.

5. Ndoa za utotoni na ukeketaji.

6. Wanawake na watoto wakimbizi.

Kutengeneza maeneo salama na bora kwa wanawake na watoto katika jamii

3. Mazingira salama ya sehemu za wazi

7. Mazingira salama. Mahusiano mazuri na yenye kuzingatia usawa kati ya wanaume na wanawke na kati ya watoto na walezi wao.

8. Kufundisha mbinu nzuri za ulezi.

4. Malezi, msaada wa familia na mahusiano.

9. Sheria namba Jamii ya Kitanzania inayounga mkono mabadiliko ya sheria yanayopendekezwa na kutekelezwa kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya ukatili.

5. Utekelezaji wa Sheria

10. Ndoa za utotoni.

11. Uitikiaji na utoaji huduma. Jamii ya Kitanzania inayounga mkono mabadiliko ya sheria yanayopendekezwa na kutekelezwa kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya ukatili.

6. Uitikiaji na utoaji huduma

12. Wanawake na watoto wakimbizi.

13. Watoto wa mitaani.

14. Ajira kwa watoto Kuondoa aina zote za ukatili katika mifumo rasmi na isiyo rasmi ya elimu kuwawezesha watoto wote na vijana (ikiwemo watoto wenye ulemavu) kufanikiza ndoto zao.

15. Kuwasaidia watoto kujifunza stadi za maisha na kuwa salama shuleni

16. Ufuatiliaji, utoaji taarifa, utafiti na uratibu.

Uandaaji bajeti.

Rasilimali watu na ujengeaji taasisi uwezo.

Mfumo wa uratibu wa kitaifa ambao ni madhubuti na unasaidia katika kufanya maamuzi kuhusu kuzuia na kushughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maoni na uchambuzi wa kitaalamu.

7. Shule salama na stadi za maisha

3.1 Matokeo ya MTAKUWWA

Kupitia utekelezaji wa shughuli za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa wanawake na watoto kama zilivyotajwa hapo juu, kutasaidia Tanzania kupata matokeo makuu nane kama ifuatavyo:

1. Ongezeko la kipato kwa kaya zilizo katika mazingira magumu;

2. Ongezeko la wanawake wanaomiliki mali na dhamana;

3. Utekelezaji wa kanuni na maadili yasiyoshadadia ukatili wa kijinsia;

4. Hali ya usalama kwa wanawake na watoto katika maeneo ya umma ni bora

zaidi;

5. Watoto wanapata matunzo na ulinzi dhidi ya ukatili na hivyo kutimiza ndoto

zao;

6. Wanawake na watoto wanapata ulinzi na huduma bora za kisheria;

7. Huduma bora kwa wahanga wa ukatili;

8 9

SEHEMU YA IV

GHARAMA ZA MPANGO KAZI WA MTAKUWWA

MTAKUWWA umeainisha gharama zitakazotumika katika utekelezaji wa maeneo nane ya mpango ambayo yatagharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania bilioni mia mbili sitini na saba nukta nne(Bil.267.4) katika kipindi cha miaka mitano.

Mpango huu utagharamiwa na serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na wadau wa kimaendeleo. Mpango kazi wa mwaka mmoja utaandaliwa na Idara ya Sera na Mipango ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (MoHCDGEC) kwa kushirikiana na wadau.

Jedwali 2: Gharama za Mpango Kazi (NPA-VACW) Kwa Shilingi za Kitanzania

2017/18 2018/19 2019/20 2020/21 2021/22 JUMLA

25,208,954,500 86,832,213,080 64,257,378,080 37,236,736,080 33,901,748,080 247,437,029,820

4,167,240,000 4,031,160,000 4,268,660,000 3,888,860,000 3,647,860,000 20,003,780,000

29,376,194,500 90,863,373,080 68,526,038,080 41,125,596,080 37,549,608,080 267,440,809,820

Jedwali 3: Uwiano wa matumizi ya fedha kwenye Maeneo ya Mkakati

60,923,200,000 22.8 13,404,676,000 12,983,976,000 12,603,246,000 11,118,656,000 10,812,646,000

97,704,380,000 36.5 330,300,000 49,058,320,000 28,859,500,000 11,299,860,000 8,156,400,000

2,404,642,500 0.9 381,402,500 555,200,000 627,360,000 423,640,000 417,040,000

7,127,160,000 2.7 1,283,840,000 1,332,240,000 1,532,760,000 1,367,840,000 1,610,480,000

6,441,002,000 2.4 172,040,000 1,400,166,000 2,331,696,000 1,245,464,000 1,291,636,000

27,391,620,000 10.2 5,368,356,000 5,117,356,000 5,920,716,000 5,706,996,000 5,278,196,000

34,846,992,320 13.0 213,972,000 8,827,480,080 9,047,680,080 8,449,080,080 8,308,780,080

30,601,813,000 11.4 8,221,608,00 11,588,635,000 7,603,080,000 1,514,060,000 1,674,430,000

JUMLA 267,440,809,820 100 29,376,194,500 90,863,373,080 68,526,038,080 41,125,596,080 37,549,608,080

SEHEMU YA VMFUMO WA URATIBU KITAASISI WA MTAKUWWA

Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto umepangiliwa katika ngazi kuu mbili za kitaasisi:

(i) Ngazi ya kitaifa, ambayo inahusisha serikali na taasisi zake, asasi za kiraia na

za kidini na sekta binafsi.

(ii) Ngazi ya Serikali za Mikoa, ambayo inajumuisha mikoa, wilaya, kata na vijiji.

Ngazi ya taifa

1. Kamati Elekezi za taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto

Majukumu ya kamati yatakuwa a) Kuhakikisha utekelezaji wa MTAKUWWA unaendana na mikataba ya kimataifa

na kikanda ya haki na ustawi wa wanawake na watoto, sera, sheria na miongozi

ya nchi

b) Kuhakikisha MTAKUWWA unaingizwa katika mipango na mikakati ya serikali

katika ngazi zote

c) Kuhakikisha rasilimali za kutosha zinatengwa kwa ajili ya kutekeleza

MTAKUWWA

d) Kupitia na kuidhinisha mipango ya mwaka ya MTAKUWWA

e) Kutoa miongozo ya kisera katika uratibu na utekelezaji wa MTAKUWWA

f) Kuanzisha kamati ndogo, kikosi kazi na tume pale inapohitajika na

g) Kuhakikisha shabaha zote za MTAKUWWA zinafikiwa

2. Kamati Tendaji ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto

Majukumu ya kamati yatakuwa a) Kusambaza na kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA

b) Uratibu na ufuatiliaji wa pamoja wa utekelezaji wa MTAKUWWA katika ngazi

zote

c) Kupitia na kuidhinisha mipango ya mwaka ya vikundi vya utekelezaji wa

MTAKUWWA na kutoa mwongozo kuhusu uboreshaji wa utekelezaji wake

d) Kupitia taarifa za utekelezaji wa MTAKUWWA kwenye sekta na vikundi vya

utekelezaji na kutoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho

e) Kushirikiana na wadau wa maendeleo na wadau wengine katika kuchangisha

rasilimali za utekelezaji wa MTAKUWWA

f) Kupanga na kuandaa mikutano ya kamati elekezi ya taifa mara mbili kwa

mwaka

Gharama za matumizi ya kawaida

Kuimari sha Uchumi wa Kaya

Kuimarisha Kanuni na Maadili ya jamii

Mazingira salama ya sehemu za wazi

Malezi, msaadawa familia na mahusiano

Utekelezaji wa Sheria

Uitikiaji na utoaji huduma

Shule salama na stadi za maisha

Uratibu, utuatiliaji na tathmini

Gharama za mtaji

JUMLA YA GHARAMA

10 11

3. Vikundi vya utekelezaji wa MTAKUWWA

Majukumu ya vikundi hivi yatakuwa a) Kuchambua, kujadili na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa MTAKUWWA

kulingana na maeneo ya utekelezaji

b) Kuunganisha wadau wanaotekeleza MTAKUWWA na kuimarisha mawasiliano

baina yao ili kuepeuka mgongano na mwingiliano

c) Kubaini na kuratibu wadau wote wanaofanya kazi katika maeneo ya utekelezaji

wa MTAKUWWA nchini

d) Kutoa msaada wa kiufundi kwa watekelezaji wa MTAKUWWA

4. Sekretarieti ya MTAKUWWA

Majukumu ya Sekretariet a) Watakuwa makatibu wa mikutano yote ya Kamati Tendaji na Kamati Elekezi ya

MTAKUWWA

b) Kuunganisha na kuandaa taarifa zitakazowakilishwa katika kikao cha Kamati

Elekezi na Kamati Tendaji

c) Kuratibu mapitio ya nyaraka, ufuatiliaji na tathmini ya pampja na tafiti

mbalimbali

d) Kutoa ushauri wa kiufundi kwa Kamati Tendaji ya MTAKUWWA

e) Kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha utendaji na utekelezaji

wa MTAKUWWA katika ngazi zote

f) Kuratibu utekelezaji wa MTAKUWWA wa kila siku.

Ngazi ya serikali za mikoa

1. Uratibu katika OR-TAMISEMI

OR-TAMISEMI itafanya yafuatayo: a) Kuimarisha mfumo wa utoaji taarifa na mawasiliano katika Serikali za Mitaa

b) Kuunganisha taarifa za utekelezaji wa MTAKUWWA kutoka Mamlaka za Serikali

za Mitaa na kuziwasilisha kwa Kamati Elekezi na Tendaji

c) Kuhakikisha afua za MTAKUWWA zinajumuishwa katika mipango na bajeti za

mikoa , mamlaka ya Serikali za Mtaa na za wadau kwa utekelezaji

d) Kushirikiana na wadau wa maendeleo na wadau wengine kuhusu upatikanaji

na matumizi ya rasilimali

e) Kuitisha mkutano mkuu wa wadau angalau mara moja kwa mwaka ili kutoa

mrejesho kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA

f) Kushiriki mikutano ya majadiliano ya mwaka ya MTAKUWWA

g) Kutoa msaada wa kiufundi kwa mamlaka za serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji

wa MTAKUWWA

2. Ngazi ya Sekretarieti ya Mkoa

Majukumu maalumu ya kamati ni: a) Kufuatilia na kutathimini MTAKUWWA katika halmashauri zote za mkoa

b) Kuhakikisha kuwa mipango na bajeti zote za halmashauri zinajumuisha afua

za MTAKUWWA

c) Kutoa msaada wa kiufundi kwa mamlaka za serikali za Mitaa kuhusu utekelezaji

wa MTAKUWWA

d) Kuunganisha taarifa za utekelezaji wa MTAKUWWA na kuziwasilisha kwa OR-

TAMISEMI kwa ajili ya kuhakiki zaidi

e) Kuitisha mkutano wa wadau mara mbili kwa mwaka

3. Ngazi ya Halmashauri

Majukumu ya kamati ni: a) Kufuatilia na kutathimini MTAKUWWA katika kata na kijiji

b) Kuhakikisha kuwa bajeti inatengwa kwa ajili ya uratibu na utekelezaji wa

MTAKUWWA

c) Kutoa tarifa kwa wakati kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA kwenye Sekretarieti

ya Mkoa

d) Kuwaendeleza na kuwapa mbinu mpya watumishi wanaoshughulika na

masuala ya MTAKUWWA katika halmashauri

e) Kuwezesha na kufuatila mipango ya utekelezaji ya MTAKUWWA inayoandaliwa

kila mwaka katika ngazi za halmashauri

f) Kutunza kumbukumbu za matukio, jitihada na hatua zilizochukuliwa za

kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

g) Kuwezesha usimamizi wa pamoja wa utekelezaji wa MTAKUWWA

4. Ngazi ya Kata

Majukumu ya kamati ni: a) Kufuatilia na kutathimini MTAKUWWA katika kata

b) Kubaini, kukusanya na kuboresha taarifa ya orodha za AZAKI, mashirika ya

kidini na wadau wengine katika ngazi ya kata wanaounga mkono utekelezaji

wa MTAKUWWA

c) Kuandaa na kutekeleza Afua za MTAKUWWA vijijini

d) Kuhakikisha afua za MTAKUWWA zinaingizwa katika mipango ya maendeleo

ya kijiji/mtaa

e) Kutangaza zaidi taarifa zinazohusu Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa

viongozi wa kata, vijiji na wadau wengine

f) Kuwezesha ushirikiano miongoni mwa wadau wanaohusika na utekelezaji wa

MTAKUWWA katika kata

12 13

g) Kutafuta rasilimali ili kuwezesha utekelezaji wa MTAKUWWA

h) Kutunza kumbukumbu za matukio, jitihada ba hatua zilizochukuliwa za

kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

i) Kutoa tarifa kwa wakati kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA kwa Mkurugenzi

wa Halmashauri

j) Kuwezesha usimamizi wa pamoja wa utekelezaji wa MTAKUWWA katika ngazi

ya kata.

5. Ngazi ya kijiji/Mtaa

Majukumu ya kamati ni:

a) Kubaini maeneo hatarishi katika kijiji na kupanga mikakati/mipango ya

kupunguza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

b) Kutoa taarifa na rufaa za kesi za ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

zinazotokea katika kijiji

c) Kutoa msaada wa awali kwa waathirika wa ukatili

d) Kuihamasisha jamii kuhusu athari za ukatili

e) Kuielemisha jamii kuhusu haki za wanawake na watoto

f) Kutangaza zaidi taarifa zinazohusu Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa

viongozi wa vijiji na wadau wengine

g) Kuwezesha ushirikiano miongoni mwa wadau wanaohusika na utekelezaji wa

MTAKUWWA katika Kijiji/Mtaa pamoja na shule

h) Kuwezesha utekelezaji wa shughuli za MTAKUWWA katika maeneo yao

i) Kutafuta rasilimali ili kuwezesha utekelezaji wa MTAKUWWA

j) Kutunza kumbukumbu za matukio, jitihada na hatua zilizochukuliwa za

kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto

k) Kutoa tarifa kwa wakati kuhusu utekelezaji wa MTAKUWWA kwa Mtendaji wa

Kata

l) Kuwezesha usimamizi wa pamoja wa utekelezaji wa MTAKUWWA katika ngazi

ya Vitongoji.

Mpangalio katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Kitaifa hadi Kijiji umeainishwa katika Umbo Na. 1 la mfumo wa uratibu wa kitaasisi wa mpango wa MTAKUWWA hapo chini.

Umbo namba 1: Mfumo wa uratibu wa kitaasisi wa Mpango Kazi wa MTAKUWWA

14 15

SEHEMU YA VI

UFUATILIAJI NA TATHMINI YA MTAKUWWA

Eneo la uratibu, ufuatiliaji na tathmini litaboresha mifumo yote ya kitaifa na ngazi ya mtaa katika kupanga, kutekeleza na kutoa taarifa juu ya MTAKUWWA. Ufuatiliaji na tathmini ya MTAKUWWA utahakikisha kuna kuwepo na ufanisi katika utekelezaji kamilifu wa kazi zilizoainishwa katika ngazi zote.

6.1 Malengo ya Ufuatiliaji wa MTAKUWWA

Lengo kuu la ufuatiliaji wa MTAKUWWA ni kutoa wigo wa majadiliano na utoaji wa maamuzi unaotokana na uthibitisho wa takwimu zilizokusanywa kutokana na utekekelezaji wa programu.

Malengo mahususi ya ufuatiliaji wa MTAKUWWA ni:

● Kuhakikisha kunakuwepo takwimu za uhakika kwa wakati Kuhusu MTAKUWWA;● Kufanya tafiti na mapitio ili kutoa taarifa zenye uthibitisho wa kitakwimu;● Kuhuisha uhifadhi, uchukuaji, upatikanaji na matumizi ya takwimu kwa

matumizi ya serikali na wadau wengine-● Kukuza uandaaji, utekelezaji na utoaji wa taarifa wa mpango unaojengwa na

taarifa zenye● uthibitisho wa kitakwimu.

Ili malengo haya yatimie, mifumo ya sasa ya ufuatiliaji inahitaji kuimarishwa na kuendana na mipango mikakati ya wizara, taasisi, idara na serikali za mitaa, ikiwemo kuiweka pamoja na mifumo ya ufuatiliaji ya kisekta.

16

S.L.P 821, MabiboDar es Salaam - TanzaniaSimu: +255 754 784 050Barua pepe: [email protected]: www. tgnp.org