ushuhuda wangu

7
1 Ushuhuda wangu JINSI NILIVYOWEKWA HURU Ni jambo gani la kufarahisha na lenye matumaini kama kuwa na uwakika na kitu ulichonacho katika maisha yako, kitu ambacho ulitamani kuwa nacho? Kitu ambacho hujali kama watu wengine wanakidharau au la? Hamna maisha mazuri katika dunia hii tunayo ishi kama maisha ya kumatumikia Mungu katika Roho na kweli. Labda huja pata ‘baahati’ ya kumtumikia Mungu katika Roho na kweli na ndio maana unaweza kushangaa ninacho kisema. Utangulizi Mwanzoni nilikuwa mtu wa namna gani? Mimi Christian Nicolaus nilitamani sana kuishi maisha ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli na kumshuhudia kwa matendo, maneno yangu na kila sehemu katika maisha yangu. Nikitafakari maisha yangu yalivyokuwa mwanzoni nakumbuka jinsi ambavyo nilishindwa mara nyingi zaidi kufanya maamuzi yenye kuwa na msimamo katika kila nilichokuwa nikikifanyia maamuzi. Hata marafiki zangu walitambua kuwa mimi ni mtu wa kufuata mawazo ya wengine na kushawishika kirahisi. Hivyo katika hali hii nilikosa kujiamini, nilidharaulika, roho ya uoga iliniingia na kutokujiamini kwa kila kitu nilichokifanya. Nilifanya maisha yangu yawe ya sirini zaidi na matendo niliyokuwa nikiyafanya yaliongeza hali ya huzuni na masononeko kila wakati. Siyo rahisi kwa mtu anayenifahamu kuamini kila ninachokisema kwasababu ya unafiki ambao ulijaa moyoni mwangu. Mpendwa msomaji ninaposema mnafiki nina maanisha kufanya mambo ya uovu na machafu katika hali ya sirini

Upload: kisalii

Post on 27-Apr-2015

448 views

Category:

Documents


22 download

TRANSCRIPT

Ushuhuda wanguJINSI NILIVYOWEKWA HURUUtanguliziNi jambo gani la kufarahisha na lenye matumaini kama kuwa na uwakika na kitu ulichonacho katika maisha yako, kitu ambacho ulitamani kuwa nacho? Kitu ambacho hujali kama watu wengine wanakidharau au la? Hamna maisha mazuri katika dunia hii tunayo ishi kama maisha ya kumatumikia Mungu katika Roho na kweli. Labda huja pata baahati ya kumtumikia Mungu katika Roho na kweli na ndio maana unaweza kushangaa ninacho kisema.

Mwanzoni nilikuwa mtu wa namna gani?Mimi Christian Nicolaus nilitamani sana kuishi maisha ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli na kumshuhudia kwa matendo, maneno yangu na kila sehemu katika maisha yangu. Nikitafakari maisha yangu yalivyokuwa mwanzoni nakumbuka jinsi ambavyo nilishindwa mara nyingi zaidi kufanya maamuzi yenye kuwa na msimamo katika kila nilichokuwa nikikifanyia maamuzi. Hata marafiki zangu walitambua kuwa mimi ni mtu wa kufuata mawazo ya wengine na kushawishika kirahisi. Hivyo katika hali hii nilikosa kujiamini, nilidharaulika, roho ya uoga iliniingia na kutokujiamini kwa kila kitu nilichokifanya. Nilifanya maisha yangu yawe ya sirini zaidi na matendo niliyokuwa nikiyafanya yaliongeza hali ya huzuni na masononeko kila wakati. Siyo rahisi kwa mtu anayenifahamu kuamini kila ninachokisema kwasababu ya unafiki ambao ulijaa moyoni mwangu. Mpendwa msomaji ninaposema mnafiki nina maanisha kufanya mambo ya uovu na machafu katika hali ya sirini

1

hali ukijifanya wewe ni mwema na mtakatifu mbele za watu na katika nuru. Ndivyo nilivyo ishi. Mimi Christian Nicolaus Mara nyingi kila mtu huwa anapenda kuishi katika maisha yenye mfumo unaompendeza nafsini mwake na usiokuwa na masononeko wala huzuni. Inapotokea unayatimiza zaidi tamaa ya moyo siku zote utaishi maisha usiyoyataka na zaidi sana utaishia kujilaumu bila kuwa na majibu ya lawama zako. lakini tamaa ilyopo moyoni mwa mtu siku zote mwanzo wake ni mzuri na wa kupendeza moyo lakini kadri unavyo timiza tamaa ya moyo ndivyo roho inavyozidi kuwa katika hali ya ukiwa na sononeko la uchungu; angalia kwa mfano mzinzi anapoanza kupangilia mipango yake ya uzinzi anakuwa katika hali ya shangwe moyoni mwake lakini baada ya kutimiza haja yake anabaki na huzuni, masikitiko na uchungu huku akijishauri nafsini mwake hatarudia tena na hivi na vile lakini bila Yesu hata afanye nini kesho atajikuta palepale. Kwakua uzinzi ni dhambi iliyozaliwa na tamaa moyoni baada ya kuifanya moyo unaridhika ila roho inabaki imejeruhiwa na jeraha ilo linasababisha maisha ya mtu yote yawe na majeraha. Nimetoa mfano wa uzinzi kama moja ya dhambi ambazo zinazaliwa moyoni kama tamaa ila kuna mengi sana ambayo ni dhambi, siyo kwamba uzinzi ndio dhambi pekee kama watu wengi wanavyoijali na kuitaja mara nyingi lakini hata uchoyo ni dhambi, chuki ni dhambi, uongo ni dhambi, ulafi ni dhambi na mengi tunayoyaona madogo. Swali ambalo nimeuliza mwanzoni nilikuwa mtu wa namna gani? hakuna anayeweza kutoa jibu zaidi ya yeye anawezaye kusoma kurasa za mawazo yetu katika miyoyo yetu pamoja na mimi niliyejitambua baada ya kuwekwa huru. UNAFIKI ni tabia ambayo ina ubaya MBAYA kwa sababu unapokuwa mnafiki unapoteza muda wako mwingi ukisumbuka na mambo ambayo hutayafaidi kabisa, utawaridhisha wengine kwa maneno wakati wewe binafsi unaumia na kudharauliwa na wengi na mwisho wa siku unabaki mwenyewe. Mimi Christian Nicolaus nilikuwa mnafiki kwa Mungu, nimelijua hilo na ndio maana ninao ujasiri wa kulitamka bila uoga. Nilionekana mwema machoni pa watu lakini moyoni mwangu nilikuwa mwenye dhambi za siri (unafiki), pia nilipata masononeko kwa siri bila ya

2

kuwa na wa kumweleza. Nilihudhuria kanisani siku nyingi lakini sikupata suluhisho la shida zilizonisibu, hata katika mikutano ya injili nilihudhuria lakini haikunisaidia. Ndugu yangu sisemi kwamba kufanya haya ni bure lakini mimi sikupata faida kwasababu nilitaka kuwatumikia mabwana wawili na ndipo nillipojikuta mwenye kukosa yote kila wakati. Kwa nini ninasema kuwatumikia mabwana wawili? Moyoni ndipo palipo na chemichemi za uzima pamoja mauti. Shetani ambaye watu wengi wamempandisha cheo cha juu sana katika shida zao ndiye mpandaji wa begu za tamaa katika mioyo yetu na Bwana Yesu aliyeteseka kwa ajili yetu sisi, aliyetupenda sisi kwanza, siku zote utuhurumia jinsi tunavyoishi maisha ya upotevu bila kujalii kwamba kuna siku tutaviacha vyote tunavyovitamani wakati tukiwa na afya tele. Hivyo mimi hali nikijua kama kuna mwenye mamlaka katika uhai wangu (Bwana Yesu) nilizitimiza haja za moyo wangu tena bila kufaidi ipasavyo kwasababu ya unafiki nilikuwa nao. Unajua heri uwe baridi au moto na wala siyo vuguvugu kwa maana hamna faida katika hili la kuwa vuguvugu Ninamshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo amelifanya katika maisha yangu lakini moja niliilojaa moyoni mwangu ni kwamba alinichagua kabla sijazaliwa. Nasema hivyo kwasababu hii; Mungu aliongozana nami katika mambo yote niliyoyafanya, hakunionea hasira, alinisamehe mara nyingi sana, akauficha uso wake asizitazame dhambi zangu na akanilinda na umauti mpaka hivi sasa ninavyomkiri kuwa bwana na mokozi wa maisha yangu. Nakumbuka hata siku ambayo mama yangu alipomaliza muda wake duniani akaniacha bila ya kuwa na mtegemezi ndipo katika hali hiyo hiyo ya unafiki nikamkumbuka Mungu naye akaniitikia na kunisaidia hali ya huzuni iliyonikuta katika kipindi ambacho nilikuwa nikifanya mitihani ya kidato cha nne. Katika safari yangu yote toka nilipopata ufahamu katika maisha yangu nilipendelea kusoma Bibilia na baadhi ya maneno niliyahifadhi moyoni katika hali ya kuyakariri bila kuwa na uelewa nayo,na maneno ambayo yalinikaa sana moyoni mwangu ni kutoka katika kitabu cha wafalme wakanza 18:21 pamoja na ufunuo wa Yohana 22: 11-12. Kutokana na hali ya kutamani kuishi maisha ya uhuru na msimamo, kila nilipokuwa nikitafakari maneno haya yalizidi kunichoma sana na ndipo nilipojigundua bado sijawekwa huru na dhambi; bado sijawa na msimamo; bado sijaona mwelekeo wa maisha yangu ni upi

3

an mengi ambayo yalinifanya niwe mwenye msongamano wa uchungu moyoni mara kwa mara, stressed and tensioned life.

Niliishi kwa jinsi ya mwilini, lakini tangu sasa na hata milemile YESU ameniweka huru kweli kweli, nami sitarudi nyuma wala kukata tamaa bali nitajipa moyo mkuu katika kumfuata Yeye.Kweli niliishi kwa jinsi ya mwilini nikizitimiza tamaa za mwili na kuendenda kanakwamba nitaishi milemile duniani walakini ninaishi tu kwa kupita kama maua ya bustani yachanuavyo asubuhi na kunyauka jioni. Mbali na kwamba niliishi kinafiki Sikupenda tabia yangu, kwa maana nilifahamu kuwa mimi ni mnafiki hivyo nilifanya majaribio mengi ya kuokoka na hata nilihudhuria mikutano mbalimbli ya injili lakini sikufanikiwa kuwa huru na maisha ya dhambi na zaidi sana kila nilipokupanga mikakati ya kuacha maovu ndivyo yalivyozidi kujitokeza mengi zaidi na nikawa nakubaliana hata na hali ambayo mwanzoni, utotoni, sikutegemea kwamba ningeishi hivyo. Nakumbuka mara ya mwisho kabisa nilihudhuria mkutano wa injili wa mwalimu Christopher Mwakasege uliofanyika kwenye viwanja vya bihafra mwaka 2008 kwaajili ya kuokoka, nakumbuka kabisa siku hiyo tulikuwa na kipindi cha pascal programming lakini nikakiacha kwa ajili ya kwenda kuokoka. Basi nilifika kwenye mkutano huku moyoni nikiwa na wazo moja tu kwamba leo nitampa Yesu maisha yangu yote. Ilipofika saa ya wale wanaotaka kumpa Yesu maisha yao nami nilipita mbele wa kwanza na kwa ujasiri nikatamani nipokee nguvu mpya katika maisha yangu. Mtumishi wa Mungu Christopher Mwakasege alituongoza sala ya toba na bado akatuombea baada ya hapo nikarudi chuoni. Cha ajabu na cha kuhuzunisha niliporudi hosteli ( udsm campansi) nilisikia hali ya kushindwa na kuhisi maamuzi niliyoyafanya hayakutoka moyoni mwangu, kwa kweli

4

siwezi kuelezea vizuri jinsi wimbi la dhambi lilivyokamata maisha yangu baada ya hapo. Nilitekwa mara dufu ya mwanzo na baadaye nikatambua kile nilichokifanya Mwanzoni hakikutoka moyoni na nilikuwa sijaridhika kupoteza yote ya dunia nimfate Yesu na ndio maana sikupokea toba ye yote baada ya kuombewa na maisha yangu yakawa ya kushindwa mara zote kwa kila nilichokifanya kwa mikono yangu. Hata katika masomo nilifeli sana. Pamoja na hali hii mbaya niliyokuwa nayo sikufanya tena jambo lolote kuhusu uhusiano wangu wangu na Mungu nikawa ninahudhuria kanisani kwa huzuni, mchungaji akihubiri moyoni huzuni inanishika; ikafikia hatua nikajishauri niache kuhudhuria kabisa ibada zote ili niepuke vikwazo vya moyo. Namshukuru Mungu kwa maana aliendelea kuwa pamoja nami katika hali ile ya kukata tamaa na kuishiwa nguvu rohoni kwani alinitia moyo nisivyojitambua.

...... lakini tangu sasa na hata milemile YESU ameniweka huru kweli kweli. Ilikuwa ni siku ambayo katika kumbukuzangu imejificha na ninachoweza kukumbuka katika moyo wangu tena nakumbuka vizur bila kusita ni maamuzi ambayo niliamua kwa moyo wangu wote kwamba wewe YESU utakuwa katika maisha yangu yote katika yote, nitakutegemea wewe kwa moyo wangu wote, akili zanlgu zote, nguvu zangu zote na kwa kila kitu ambacho kitatokana na mimi kitakutumikia wewe, sitajali mtu ye yote, wala kup oteza maisha wala kutukanwa wala kupwa. Nikaamini kwamba Bwana Yesu yupo na nikamkiri katika moyo wangu na akili zangu na matamanio yangu yote. Nilipomaliza kutamka maneno haya kwa kukusudia kupata hasara duniani lakini niwe na Yesu katika maisha yangu amini usiamini nilihisi wepesi namna ya utofauti moyoni na pale pale nikatamani kila niliyekutana naye nimweleze abari iliyonitokea kwa maana hali ambayo ilinitokea haikuwahi kunitokea kabisa katika maisha yangu. Namshukuru Mungu siku zote za maisha yangu kwasababu ameniokoa kwenye makucha ya samba dunia, asante Bwana Yesu. Yamkini utajiuliza ni kwanini nilifanya uamuzi wa namna hii, labada nilikuwa na dhiki sana katika maisha yangu au nilikuwa nahitaji Yesu aniwezeshe katika masomo yangu au anisaidie niishi maisha ya starehe zaidi au kuna kitu nilichokuwa nakitaka lakini nikaona kwa

5

Yesu ndipo kinapopatikana kwa urahisi zaidi? La asha, nitamtumikia Yesu siku zote za maisha yangu kwasababu ninahitaji nimwone yeye bila kujali watu watasemaje juu yangu; maana kama shetani aneweza kuwaibisha watu mchana peupe nami nitamwaibisha kwa Damu ya Yesu mchana peupe, tena sitarudi nyuma kamwe wala kukata tamaa katika hali ye yote ile ya maisha ya mwili huu wa tamaa. Ndugu unaye soma Ushuhuda huu kama hujadhamiria kuacha maisha ya dhambi moyoni mwako kwa kulia na kuona uchungu na unayoyafanya, kwamba siku moja utayaacha, na kumpa Yesu atengeneze maisha yako upya yakupasa usipoteze muda wako kwa kitu ambacho huna faida nacho ni heri kufaidi upande mmoja ipasavyo kuliko kukosa yote na bado ukatumikia mateso ya mile mile. Yesu alikutana na Yohana katika kisiwa cha patmo akamonyesha mambo yatakayotokea siku za mwisho. Namshukuru sana tena sana kwamba Bwana Yesu hakusahahu kumwambia Yohana maneno yaliyopo katika ufunuo 22:1112 ambayo yanatupa uhuru wa kuishi jinsi tupendavyo sisi (na hivyo ndivyo walio na mafanikio wanavyoenenda) siyo kwa mchanganyo! Maneno kama haya katika bibilia yanatoka katika kitabu cha 1 wafalme 18:21. Ukipata muda soma maneno haya yote kwa kutafakari jinsi maisha yako yalivyo na yalinganishe na maneno ya Yesu. Ndugu yangu chagua kundi lako ambalo kwa hilo utatambulikana. Ana heri mtu Yule amchaguaye Bwana kuwa fungu lake tena akaona kupata hasara ya dunia siyo kitu cha kuhesabu! Namshukuru sana Mungu kwa yote aliyonitendea na ninaguswa kukuambia yafuatayo: Usipoteze muda wako kwa kuwa mnafiki, heri walio moto au baridi; hasante Yesu umenifanya wako nilikuwa mnafiki tena vuguvugu lakini sasa sina hofu mbele zako. kuwa moto au baridi ni kutenda ya upande mmoja bila kuyachanganya yalio baridi na yaliyo moto, na hapo ndipo utakapofaidi vema katika ule upande uliopo. Mtumikie Mungu kila mtu aone kweli unamtumikia yeye au fanya mapenzi ya moyo wako (ya dunia) kila mtu akufahamu ulivyo! Unajua kinacho umiza ni pale unapotaka kuwa pande zote mbili halafu unakosa yote. Heri wale walio upande wa Yesu, mwanakondoo wa Mungu maana hao watafanishwa na chemichemi ya maji

6

jangwani. Ole wao waliojitoa kutumika kwa ibilisi maana hao fungu lao ni huzuni na uchungu wala hawatakula kazi ya mikono yao! Kuna siku utakayoacha yote unayoyathamini na kuyasumbukia tena hutapata nafasi ya kugusa au kuona hata moja kwa mara ya mwisho. Je, siku hiyo ubishi wako utakusaidia, elimu uliyonayo kweli itafanya chochote? Au pesa ulizonazo zitanunua tena uhai wako? Basi unamuhitaji Yesu siyo kidogo, sana! Tena sana! Usijali wasiokujali, usiwaogope wanaokudharau maana hao wote hawana mbingu ya kukupeleka wala uwezo wa kukuokoa na uwaribifu, zaidi sana watakucheka na watakusema na mwisho watakuacha peke yako na uchungu wako. Christian Nicolaus [email protected] +255715276275 S. L. PO BOX 237 USA RIVERNitamtumikia yesu bila kujali watu wanasema nini juu yanguDigitally signed by CHRISTIAN NICOLAUS DN: cn=CHRISTIAN NICOLAUS, o, ou, [email protected], c=TZ Date: 2010.04.24 14:53:21 +03'00'

7