ustawi wa wanyama - education for africa animal welfare · 2019. 4. 8. · toleo la 1, februari...

4
Toleo la 1, Februari 2019 Ustawi Wa Wanyama Wapendwa Wadau na Wanajamii Dear Partners and Community Members Mpendwa msomaji na wanadau wote, tunapenda kutambulisha kwenu jarida la Ustawi wa wanyama na mazingira. Jarida hili ni toleo la kwanza linalotolewa na shirika la Education for African Animals Welfare kwa kifupi EAW. Hii ni moja ya njenzo muhimu itakayotumika katika kufikisha ujumbe, na kutoa elimu kwa jamii na tunatalajia kufikia watu zaidi ya milioni 3.5 Jarida hili litabeba ujumbe muhimu, utakaowafahamisha wadau juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika nyanja nzima ya ustawi wa wanyama, ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya ustawi wa wanyama na utunzaji wa mazingira kwa ujumla. Kwa mantiki hiyo, jarida hili litakuwa likichapishwa kwa lugha mbili, ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wadau wote. Lugha itakayotumika ni Kiswahili, na Kiingereza huku tukiwa na maana moja kwa yote yatakayochapishwa humu. Tunaamini kuwa kupitia utaalamu utakaotumika, uzoefu, na kushirikishana uzoefu na wadau wa makundi yote katika nyanja ya ustawi wa wanyama, jarida hili litakuwa na maana kubwa, na kuleta mabadiliko katika eneo la ustawi wa wanyama, kwa kuwa na namna nzuri ya utunzaji wa wanyama. Kuna pengo kubwa katika eneo zima la utunzaji wa wanyama na mazingira. Tunaamini kuwa kwa kushirikiana na wadau na mashirika mengine, pengo hili linaweza kuondoka, na kufanya ustawi wa wanyama na mazingira kuwa bora zaidi. Katika kuhakikisha hilo linafanyika, tunahitaji kuangalia namna bora ya usafirishaji wa wanyama, chanjo na matibabu kwa wanyama, pamoja na kuelimisha jamii namna bora ya kuepuka kusababisha mateso na maumivu kwa wanyama. Kama ilivyo kwa viumbe wote, wanyama pia wanastahili kupendwa na kutunzwa. Kwa pamoja tuungane katika kuwatetea. Tuungane pamoja kwa ajili ya ustawi wa wanyama na mazingira. Kwa niaba ya EAW nawashukuru wote, na ninawatakia kila la kheri, mfurahie yale yote mtakayosoma ndani ya toleo hili. Dr. Honoratha Francis Mwenyekiti wa EAW We are pleased to introduce to you Animals Welfare Magazine under Education for African Animal Welfare Organisation(EAW). This is one of the important tools that will be used to disseminate information and to educate our community at the same time. The magazine, will carry important information that will update our partners, at the same time to inform our community on various issues regarding care and protection of animals and environment We are expecting to reach more than 3.5 people through this magazine. In this regards, the magazine will be published in two different languages to easier communication and to bring both parties in common understanding. We hope that, through expertise, sharing experience with different group of people in animal welfare arena, the magazine will make sense to the targeted group, and after sometimes there will be changes on how animals are cared and protected. There are gapes in addressing animal’s issues. In partnering with other organisation these gapes can be filed, hence the betterment of animals and environment. We need to address the humane transportation issues, proper vaccination and treatments to all groups of animals, educate all groups on how they can avoid and eliminate torchers to the animal’s. As any other creatures, animals need love and care. Let’s speak for them, lets act for them. Let’s join our hands, for the better animal situation. Thank you each and every one. Do enjoy the read and on behalf of EAW I wish you all the best in protecting animal and environment. Dr. Honoratha Francis EAW Chairperson EAW, P.O.Box 16504, Dar es Salaam, Email: [email protected], Web: www.animalswelfareafrica.org 1 st Edition, February 2019 Picture EAAW Animal Welfare and Environmental Magazine free copy Haliuzwi

Upload: others

Post on 02-Feb-2021

3 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • Toleo la 1, Februari 2019

    Ustawi Wa Wanyama

    Wapendwa Wadau na Wanajamii

    Dear Partners and Community Members

    Mpendwa msomaji na wanadau wote, tunapenda kutambulisha kwenu jarida la Ustawi wa wanyama na mazingira. Jarida hili ni toleo la kwanza linalotolewa na shirika la Education for African Animals Welfare kwa kifupi EAW. Hii ni moja ya njenzo muhimu itakayotumika katika kufikisha ujumbe, na kutoa elimu kwa jamii na tunatalajia kufikia watu zaidi ya milioni 3.5

    Jarida hili litabeba ujumbe muhimu, utakaowafahamisha wadau juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika nyanja nzima ya ustawi wa wanyama, ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii juu ya ustawi wa wanyama na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

    Kwa mantiki hiyo, jarida hili litakuwa likichapishwa kwa lugha mbili, ili kuweza kufikisha ujumbe kwa wadau wote. Lugha itakayotumika ni Kiswahili, na Kiingereza huku tukiwa na maana moja kwa yote yatakayochapishwa humu.

    Tunaamini kuwa kupitia utaalamu utakaotumika, uzoefu, na kushirikishana uzoefu na wadau wa makundi yote katika nyanja ya ustawi wa wanyama, jarida hili litakuwa na maana kubwa, na kuleta mabadiliko katika eneo la ustawi wa wanyama, kwa kuwa na namna nzuri ya utunzaji wa wanyama.

    Kuna pengo kubwa katika eneo zima la utunzaji wa wanyama na mazingira. Tunaamini kuwa kwa kushirikiana na wadau na mashirika mengine, pengo hili linaweza kuondoka, na kufanya ustawi wa wanyama na mazingira kuwa bora zaidi.

    Katika kuhakikisha hilo linafanyika, tunahitaji kuangalia namna bora ya usafirishaji wa wanyama, chanjo na matibabu kwa wanyama, pamoja na kuelimisha jamii namna bora ya kuepuka kusababisha mateso na maumivu kwa wanyama.

    Kama ilivyo kwa viumbe wote, wanyama pia wanastahili kupendwa na kutunzwa. Kwa pamoja tuungane katika kuwatetea. Tuungane pamoja kwa ajili ya ustawi wa wanyama na mazingira.

    Kwa niaba ya EAW nawashukuru wote, na ninawatakia kila la kheri, mfurahie yale yote mtakayosoma ndani ya toleo hili.Dr. Honoratha FrancisMwenyekiti wa EAW

    We are pleased to introduce to you Animals Welfare Magazine under Education for African Animal Welfare Organisation(EAW). This is one of the important tools that will be used to disseminate information and to educate our community at the same time.

    The magazine, will carry important information that will update our partners, at the same time to inform our community on various issues regarding care and protection of animals and environment We are expecting to reach more than 3.5 people through this magazine.

    In this regards, the magazine will be published in two different languages to easier communication and to bring both parties in common understanding.

    We hope that, through expertise, sharing experience with different group of people in animal welfare arena, the magazine will make sense to the targeted group, and after sometimes there will be changes on how animals are cared and protected.

    There are gapes in addressing animal’s issues. In partnering with other organisation these gapes can be filed, hence the betterment of animals and environment.

    We need to address the humane transportation issues, proper vaccination and treatments to all groups of animals, educate all groups on how they can avoid and eliminate torchers to the animal’s.

    As any other creatures, animals need love and care. Let’s speak for them, lets act for them. Let’s join our hands, for the better animal situation.

    Thank you each and every one. Do enjoy the read and on behalf of EAW I wish you all the best in protecting animal and environment. Dr. Honoratha FrancisEAW Chairperson

    EAW, P.O.Box 16504, Dar es Salaam, Email: [email protected], Web: www.animalswelfareafrica.org

    1st Edition, February 2019

    Picture EAAW

    Animal Welfare and Environmental Magazinefree copyHaliuzwi

  • Punda: Rafiki wa ajabu Donkey: Amaizing friendPunda ni moja wapo ya wanyama wafugwao, ambao kwa kiasi kikubwa wanahimili kuishi sehemu kame, hasa kwa nchi za Afrika. Hawa ni wanyama kazi, ambao wanastahimili kwa kiasi kikubwa kufanya kazi ngumu, huku wakivumilia mazingira magumu.

    Haitakiwi kuchukulia hali hiyo kuwa ya kawaida na kuwapuuza wanyama hawa. Wanahitaji kujaliwa na kupatiwa haki zao kama vile chakula, maji, chanjo na matibabu kama ilivyo kwa wanyama wengine wote. Tuungane kwa pamoja, ili kupaza sauti kwa wanya hawa kupata haki zao.Je unafahamu mzunguko wa maisha ya Punda?Kama ilivyo kwa viume hai wengine maisha ya punda yana mzunguko kamili. Mzunguko huo hugawanyika katika hatua mbalimbali.Maisha: Kwa kaiwada maisha ya punda kwa ujumla hukadiriwa kuwa kati ya miaka 25-40.

    Mtoto wa punda huhitaji kunyonya kwa kipindi cha mwaka mmoja.

    Kuzaliana: Punda hukomaa na kuwa na uwezo wa kuzaliana kuanzia anapokuwa na umri wa miaka miwili.

    Kazi: Punda ni kundi la wanyama kazi. Punda anaweza kuanza kufanya kazi akiwa na umri wa miaka mitano(5). Kulinda na kutunza afya ya punda tangu akiwa na umri 0 mpaka miaka 5 ni muhimu sana ili aweze kuwa mwenye afya, imara na kuwa na maisha marefu zaidi.

    Endapo punda wataanza kufanyishwa kazi wakiwa wadogo sana, wanaweza kuwa na matatizo mengi kiafya, na kusababisha kufa wakiwa bado na umri mdogo.Matunzo: Punda wanahitaji ukaguzi wa mara kwa mara wa kwato, na kukata inapohitajika. Kwato za punda zinahitaji kukatwa kila baada ya miezi sita(6), labla ionekane kuwa kuna ukuaji wa haraka na usiokuwa wa kawaida, ambao unahitaji ukataji kabla ya kipindi hicho.Chakula: Punda wamezoea kula nyasi kwa kiasi kikubwa. Hakikisha malisho ya punda hayapati vumbi wala matope. Maji: Punda wanahitaji kupata maji safi na salama wakati wote, ili waweze kunywa kila wanapohitaji.Malazi: Punda wanahitaji malazi salama, yatakayowakinga dhidi ya jua, mvua na wanyama wanaoweza kuwashambulia. Kununua na kuuza: Punda wanaweza kuuzwa au kununuliwa, baada ya kukaguliwa na wataalamu wa mifugo, ili kubaini endapo wapo katika hali njema kiafya na hawana majeraha.Kumbukumbu: Punda wana uwezo wa kukumbuka sehemu maalumu, kumkumbuka mtu maalumu na mambo mazuri waliyotendewa kwa miaka mingi.

    Yapo mengi kuhusiana na maisha ya punda na ustawi wake, tutaendelea kukudondolea zaidi katika toleo lijalo.Makala hii imatayarishwa na kuchapishwa kwa ushirikiano na shirika la MAWO

    Donkey is one of the domestic animals, that highly survive in dry areas especially in Africa. Donkeys is the hard working animal, while tolerates the harsh condition. We don’t have to take this for granted. Donkeys should be cared and treated like most important animal.

    We need to join our hands to shout for the right of this animals. They should be provided with water, food, shelter, vaccination and treatment where needed.

    EAAW is there to shout for the rights of this animals.Do you know life cycle of a donkey?Like any other creatures, donkey have life cycle that needs to be supported. They also have needs that should be met for them to survive.Life Span: The life span for wild donkeys is generally esti-mated to be between 25-40 years.Age: A young foal is considered to sexually matured after 2 years and can then produce offspring of its own. Work: Donkey can begin working after they 5year old. Pro-tecting the health of donkey from age 0-5 is a worthwhile investment for growing a valuable, healthy, strong well tem-pered and long living donkey. If they work too young, they can develop health problem problems and die younger. Routine Care: A donkey will need routine grooming, check-ing and hoof care. This also allows the donkey to be checked over for sings of poor health. The donkey’s hooves need to be trimmed every 6 months, unless there is visible over grown which should be trimmed sooner.Food: Donkeys are adopted to eat a high fiber diet. Keep food free from dust, mud and mold. Water: Donkeys need clean water to be available whole day so they can drink when they need. Shelter: Donkey need a safe shelter from rain, extreme sun and predators. Buying and Selling: Donkey should be bought or sold after examination. This can be done by a vet to confirm that they are in good health and not injured. Memory: Donkeys can remember special places, special people and their companions for many years.

    There are so many more things to tell about donkeys and their welfare. We shall continue providing important tips on donkeys in the next edition.

    This article is prepared and published in collaboration with MAWO

    Toleo la 1, Februari 20191st Edition, February 2019Toleo la 1, Februari 2019

    Picture EAAW

  • Fahamu ugonjwa wa kichaa cha mbwa Do you know about rabies?

    Familia nyingi nchina Tanzania na Afrika kwa ujumla, hufuga mbwa bila kuzingatia chanjo muhimu na matibabu kwa ujumla.

    Kicha cha mbwa ni ugonjwa ambao husababishwa na virusi. Ugonjwa huu huwapata wanyama na binadamu kutokana na kung’atwa na mnyama mwenye virusi vya ugonjwa huo. Ugonjwa huu hauna tiba, ila unazuilika kwa njia ya chanjo.Jinsi ugonjwa huu unavyoeneaNjia kuu ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa kuenea ni kwa kung’atwa na mbwa au mnyama mwenye ugonjwa. Dalili za ugonjwa kwa mbwa

    • Kubadilika tabia, kuwa mpole, au mkali zaidi.• Kuhangaika hangaika, kushtuka au kukimbia ovyo.• Kutembea masafa marefu.• Kutokwa mate mengi.• Kushambulia kwa kung’ata vitu ovyo kama vile vijiti na

    vyuma.• Kushindwa kula na kunywa maji.• Kudhoofu, kupooza na hatimae kifo.

    Kwa wanyama wengine kama mbuzi, ng’ombe. Paka, nguruwe, na wengineo, dalili zinaweza kujitokeza kulingana na aina ya wanyama.Dalili za ugonjwa kwa binadamuNi muhimu kuangalia kwa makini dalili zifuatazo, hasa pale inapotokea umeng’atwa na mbwa au mnyama unaehisi kuwa na ugonjwa huu. Hata hivyo ni muhimu kuwahi kupata matibabu inapotokea umejeruhiwa na mnyama.Ugonjwa wa kichaa cha mbwa kwa binadamu huonekana kwa dalili hizi:

    • Homa.• Kuumwa kichwa.• Kuogopa.• Kuchanganyikiwa.• Maumivu ya mwili.• Kuwashwa sehemu yenye jeraha.• Kuweweseka, kushtuka mara kwa mara na kuogopa.• Kuogopa kunywa maji, mwanga na upepo.• Kupooza.• Kutokwa mate.

    Mambo muhimu ya kuzingatia• Unapoanza chanjo ya kwanza ya kichaa cha mbwa,

    hakikisha unapata chanjo zote, kadri utakavyoshauriwa na mtoa huduma ya afya.

    • Toa taarifa juu ya mbwa aliyekung’ata, anaehisiwa kuwa na kichaa kwa mtaalamu wa mifugo. Hii itasaidia hatua za haraka kuchukuliwa kumfuatilia mbwa huyo.

    • Hakikisha mbwa na paka wako wanapata chanjo kila mwaka ili kutokomeza kichaa cha mbwa.

    • Hakikisha unamfungia mbwa wako kwenye banda kuanzia saa 12 asubuhi na kumfungulia saa 4 usiku.

    • Choma moto, au mfukie mbwa aliyekufa kwenye shimo lenye urefu usiopungua mita moja kwenda chini.

    Mpende mbwa wako, mtunze kwa afya na usalama wako.

    Rabies is a viral disease. The disease is spread through animal’s bites, that is infected by the rabies virus. Rabies affects both animals and human. There is no treatment for this disease, but it can be prevented through vaccination.Spread of RabiesRabies virus is spread through the saliva of infected animals. Infected animals can spread the virus by biting another animal or a person. Symptoms to animals

    • Fever.• Attacks.• Paralysis.• Hydrophobia.• Inability to swallow.• Change in tone of bark.• Muscular lack of coordination.• Unusual shyness or aggression.• Excessive emotionality.• Constant irritability/changes in attitude and behaviour.• Excessive salivation or frothy saliva.

    Symptoms of rabies to human beingThe first symptoms of rabies may be very similar to the flu and may last for days. Later signs and symptoms may include:

    • Fever• Headache• Nausea• Vomiting• Agitation• Anxiety• Confusion• Hyperactivity• Difficulty swallowing• Excessive salivation• Fear of water (hydrophobia) because of the difficulty in swallowing• Hallucinations• Insomnia• Partial paralysis

    Prevention

    To reduce your risk of coming in contact with rabid animals:• Vaccinate your pets. Cats and dogs can be vaccinated against

    rabies. Ask your veterinarian how often your pets should be vaccinated.

    • Keep your pets confined. Keep your pets inside early at 6am and let them outside at 10pm. This will help keep your pets from coming in contact with wild animals.

    • Protect small pets from predators. Keep rabbits and other small pets, such as guinea pigs, inside or in protected cages so that they are safe from wild animals. These small pets can’t be vaccinated against rabies.

    • Report stray animals to local authorities. Call your local animal control officials or other local law enforcement to report stray dogs and cats.

    • Consider the rabies vaccine if you’re traveling. If you’re traveling to a country where rabies is common and you’ll be there for an extended period of time, ask your doctor whether you should receive the rabies vaccine.

    • This includes traveling to remote areas where medical care is difficult to find.

    STOP RABIES: Join EAW in educating our community, and providing vaccination to our animals especially dogs to avoid rabies spread.

    Toleo la 1, Februari 2019 1st Edition, February 2019

    Picture EAAW

    Picture EAAW

  • Mazingira safi ya Ukanda wa Bahari ni muhimu

    Clean sea shoe environment is important for sea creatures

    Ni nani anaweza kutusaidia?

    Who can help us?

    Tunahitaji mazingira safi. Tunahitaji kutunza mazingira ya ufukweni mwa bahari, na bahari yenyewe kwa ujumla, ili kusaidia viumbe hai wa majini waweze kuendelea kuishi na kuwa na afya. Tunapaswa kuepuka matumizi ya plastiki, na kuzisambaza ovyo. Tunapaswa pia kuepuka kusambaa na kumwaga kemikali baharini.

    Ungana na kusaidiana na EAAW kupaza sauto na kukuza uelewa kwa jamii yetu, katika suala zima la utunzaji wa mazingira nchini Tanzania, kwa ajili ya ustawi wa wanyama na viumbe hai wote. Ungana nasi kutokomeza uchafuzi wa mazingira.

    We need clean environment. We have to take care of the sea shore environment and the sea zone in general, to increase the surviving rates of sea creatures. We have to avoid plastic and chemical emissions to the sea.

    Help EAAW in raising voice and awareness towards environmental conservation in Tanzania, for the welfare of animals. Education is needed to our society. Join us Now. End environmental pollution.

    Toleo la 1, Februari 2019

    Ni kama mbwa hawa na paka walikuwa wakiuliza. Ni pale tulipowakuta wakiwa wanazurura huku wakilalamika kwenye baridi usiku wa manane, wakiwa hawana tumaini.

    Tunapaswa kuifahamisha jamii yetu juu ya wajibu wao wa kuwatunza wanyama hawa wasiokuwa na hatia.

    Hawapaswi kutelekezwa. Wanahitaji kupatiwa

    Its like this pretty pet and cat asking! We found them in the cold at mid night, tired and sleeping in the sand hopelessly. They were just groaning showing that they are hungry and tired. We need to let our

    chakula, maji na mahala pa kulala. Pia wanahitaji matibabu, na chanjo pale inapohitajika.

    Ungana na EAAW kupaza sauti ili wanyama hawa wasiokuwa na hatia waweze kutunzwa na kupata haki zao. Wanyama hawa wanatutegemea sisi kuishi, lakini tunawahitaji kwa kiwango kikubwa pia.society knows their responsibility in taking care of this innocent pet’s and cats.

    They should not be ignored. They need food, water, and good shelter. They also need treatment and vaccination where needed.

    Help EAAW to shout for the innocent animals. They disserve love and care.

    EAW, P.O.Box 16504, Dar es Salaam, Email: [email protected], Web: www.animalswelfareafrica.org

    Picture EAAW

    Picture EAAW

    Picture EAAW

    1st Edition, February 2019

    Tunakaribisha watu wote kusaidia uchapishaji wa jarida hili. Unaweza kutusapoti na ukapata nakala kwa ajili ya shirika lako, na wadau unaofanya nao kazi. Halikadhalika inaweza kuwa kwa kuunga mkono kazi hii. Tutakutambua na kuwekwa katika orodha ya wanaotusaidia na kuchapishwa katika jarida hili endapo utapenda.Jichagulie Daraja lakoDhahabu-$ 1500 na kuendeleaFedha -$ 1000 na kuendeleaShaba. -$ 500 na kuendeleaWasiliana nasi sasa: [email protected]

    EAAW Welcomes all well-wishers to support the printing and distribution cost of this magazine. You can support and get some copies for your organization and other stakeholders from your working areas. Also you can support just for community to be educated. We shall list you as one of our supporters in this page if you wish, but also you can remain anonymous.Your support can be in one of this category or beyond. Choose and contact us.Gold-$1500 and moreSilver-$1000 and moreBronze-$500 and moreContact us: [email protected]

    Unaweza kutusapoti You Can support us

    EAAW is open for collaboration with all animals and environmental lovers. we can collaborate in different angles. You can donate to facilitate our activities,contact us for more information