wizara ya afya na ustawi wa jamii (mohsw...3. utoaji wa taarifa za idadi ya wagonjwa na kiasi cha...
TRANSCRIPT
-
MWONGOZO WA
USIMAMIZI WA DAWA ZA
KUTIBU KIFUA KIKUU NA
UKOMA
JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
(MOHSW)
MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI KIFUA
KIKUU NA UKOMA
(NTLP)
-
2
SHUKRANI
Mwongozo huu umetayarishwa kama sehemu ya msaada wa kitaalamu wa mradi wa Supply Chain
Management System (SCMS) kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Tanzania) kupitia Mpango wa Taifa
wa Kudhibiti kifua kikuu na ukoma (NTLP) kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa mfumo wa ugavi wa
dawa za kutibu kifua kikuu na ukoma. SCMS ni mradi unaodhaminiwa na Shirika la Misaada ya
Kimaendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na kutekelezwa na John Snow Inc (JSI) kwa mkataba
namba GPO-I-00-05-00032-00.
-
3
YALIYOMO
VIFUPISHO NA MAANA YA MANENO YA KITAALAMU ............................................................................................ 5
SURA YA 1: UTANGULIZI .................................................................................................................................... 6
A: MADHUMUNI YA MWONGOZO HUU .................................................................................................................... 7
B: DAWA ZINAZOSIMAMIWA KUPITIA MFUMO HUU ................................................................................................ 7
C: NANI ANAPASWA KUUTUMIA MWONGOZO HUU? .............................................................................................. 9
D: MWONGOZO HUU UTAKUSAIDIAJE? .................................................................................................................... 9
E: UTARATIBU WA MTIRIRIKO WA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA NA TAARIFA KATIKA MFUMO WA
USIMAMIZI WA DAWA HIZO ................................................................................................................................... 11
F: MUHTASARI WA MFUMO .................................................................................................................................... 12
SURA YA 2: FOMU ZA KUMBUKUMBU NA TAARIFA ZINAZOTUMIKA KATIKA MFUMO WA UGAVI WA DAWA ZA
KIFUA KIKUU NA UKOMA .................................................................................................................................... 13
SURA YA 3: UWAJIBIKAJI KATIKA USIMAMIZI WA UAGIZAJI NA USAMBAZAJI WA SHEHENA ZA DAWA ZA KIFUA
KIKUU NA UKOMA ............................................................................................................................................... 14
A. MAJUKUMU KATIKA KITUO CHA TIBA ............................................................................................................ 14
B. MAJUKUMU KATIKA NGAZI WILAYA .............................................................................................................. 15
C. MAJUKUMU KATIKA NGAZI YA MKOA ........................................................................................................... 17
D. MAJUKUMU YA BOHARI KUU YA MADAWA (MSD) ........................................................................................ 17
E. WIZARA YA AFYA (NTLP) ................................................................................................................................ 18
SURA YA 4: UTUNZAJI WA HESABU ZA BIDHAA ZINAZOTOLEWA ..................................................................... 19
SURA YA 5. UAGIZAJI.......................................................................................................................................... 20
A: KUHAKIKISHA KIASI CHA KUTOSHA CHA SHEHENA ............................................................................................. 20
B: TATHMINI YA KIASI CHA SHEHENA ...................................................................................................................... 20
C: NAMNA YA KUTAMBUA MWEZI WA MATIBABU ATAKAOKUWA MGONJWA .................................................... 24
D: UTOAJI WA TAARIFA WA VITUO VYA TIBA .......................................................................................................... 25
E: JINSI WILAYA INAVYOAGIZA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA ....................................................................... 27
F: MAOMBI YA DHARURA ........................................................................................................................................ 27
G: UGAWAJI WA DAWA KUTOKA MSD KWENDA WILAYANI ................................................................................... 28
H: UGAWAJI WA DAWA KUTOKA WILAYANI KWENDA VITUONI ............................................................................. 29
SURA YA 6: KUHIFADHI DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA ........................................................................... 31
A: HESABU YA MKONO ............................................................................................................................................ 31
B: UKAGUZI WA BIDHAA KWA MACHO ................................................................................................................... 32
C: KUHARIBU MALI ISIYOFAA KWA MATUMIZI ........................................................................................................ 32
SURA YA 7: FOMU ZINAZOTUMIKA KATIKA MFUMO WA USIMAMIZI WA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA
NA UFAFANUZI WAKE .......................................................................................................................................... 33
-
4
A. UFAFANUZI A: UJAZAJI WA DOZI ZILIZOGAWIWA/TOLEWA KWA MGONJWA KATIKA KADI YA WA KIFUA
KIKUU ...................................................................................................................................................................... 34
B. FOMU YA TAARIFA YA KITUO YA MWEZI YA DAWA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU NA UKOMA ............................. 38
C. UFAFANUZI B: UJAZAJI WA FOMU YA TAARIFA YA MWEZI YA KITUO ............................................................ 39
D. FOMU YA TAARIFA YA KITUO YA MWEZI YA DAWA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU NA UKOMA ............................. 43
E. UFAFANUZI C: KUHAKIKI TAARIFA KWENYE FOMU YA MWEZI YA KITUO NAKUKOKOTOA KIASI CHA DAWA
CHA KUGAWA ......................................................................................................................................................... 46
F. UFAFANUZI D: UJAZAJI WA TAARIFA NA MAOMBI YA ROBO MWAKA YA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA
YA WILAYA............................................................................................................................................................... 53
G. FOMU YA KUNAKILI KIASI CHA DAWA KILICHOTOLEWA VITUONI ................................................................. 59
H. FOMU YA TAARIFA NA MAOMBI YA ROBO MWAKA YA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA YA WILAYA ...... 60
-
5
VIFUPISHO NA MAANA YA MANENO YA KITAALAMU
UFUPISHO KIINGEREZA KISWAHILI
AMC Average Monthly Consumption. Wastani wa matumizi kwa mwezi
ARV Antiretroviral drugs Dawa za kupoza makali ya UKIMWI
CHMT Council Health Management Team Timu ya Halmashauri ya Usimamizi wa Afya
DTLC District Tb and Leprosy Coordinator Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya
DMO District Medical Officer Mganga Mkuu wa Wilaya
DOT Directly observed therapy
EOP Emergency order point Uwepo wa shehena inayoashiria kuwa ni lazima
uagizaji wa dharura ufanyike
FDC Fixed Dose Combination Kidonge cha dawa mchanganyiko
FEFO First to Expire, First Out Tumia kwanza zinazokaribia kwisha muda wake
wa matumizi
GOT Government of Tanzania Serikali ya Tanzania
JSI John Snow Inc. John Snow Inc.
LMIS Logistics Management Information System Mfumo wa Taarifa za uagizaji na usambazaji.
MDR-TB Multdrug Resistant Tubeculosis Kifua kikuu sugu
MOS Months of Stock Shehena Inayotosheleza (kwa miezi)
MSD Medical Stores Department Bohari Kuu ya Madawa
MOHSW Ministry Of Health and Social Welfare Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
NTLP National Tuberculosis and Leprosy
Program
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua kikuu na
ukoma
R&R Report and Request forms Fomu za Taarifa na Maombi
RTLC Regional Tb and Leprosy Coordinator Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa mkoa
SDP Service Delivery Point Kituo cha kutolea Huduma
SOH Stock on hand; stock in good condition that
can be given to patients or used with clients.
SOH does not include any damaged or
expired stock.
Shehena iliyopo Mikononi – Ni bidhaa iliyo katika
hali nzuri na inayoweza kutolewa kwa mteja.
SOH haihusu shehena iliyoharibika au kwisha
muda wa matumizi
SCMS Supply Chain Management System Mfumo wa usimamizi wa Ugavi
USG United States Government Serikali ya Marekani
-
6
SURA YA 1: UTANGULIZI
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti kifua kikuu na ukoma utafanikisha malengo yake
kutokana na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuratibu mipango inayohakikisha
kuwa mahitaji ya dawa ya wagonjwa yanatimizwa. Juhudi hizo ni pamoja na
kuhakikisha ya kuwa na dawa zinazohitajika na vitendanishi sahihi vya kupimia
vinapatikana katika kiasi cha kutosha, ziwe katika hali sahihi, zihifadhiwe na
kufikishwa mahali sahihi,kwa wakati sahihi na gharama sahihi. Ili malengo ya
mpango huo yaweze kufanikiwa ni sharti mfumo mahususi wa ugavi na usimamizi
utumike. Utaratibu huo wa ugavi hauna budi uhakikishe kuwa shehena za bidhaa
zinapatikana katika vituo vyote na kwamba hapatokei matatizo ya kulundikana kwa
shehena, upungufu, kuishiwa wala ufujaji wa bidhaa hizo.
Mfumo mzuri wa usimamizi wa dawa za kutibu kifua kikuu na ukoma utasaidia katika
kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana muda wote katika vituo vya kutolea tiba na
hivyo kuokoa maisha. Upatikanaji wa uhakika wa dawa za kifua kikuu na ukoma
utawafanya wagonjwa kuwa na imani na mfumo wa tiba na kuwafanya waendelee
kufika vituoni kwa ajili ya kupata matibabu na pia kusaidia kupunguza tatizo la usugu
wa vimelea vya ugonjwa na ubora wa tiba.
Izingatiwe kuwa mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma una fanana
na mifumo mingine ya usimamizi wa bidhaa za afya mfano Integrated Logistics
System (ILS) katika mambo mbalimbali mfano upokeaji wa bidhaa, utunzaji wa
bidhaa,ukaguzi wa macho,matumizi ya kitabu cha leja ya mali. Mambo kama haya
hayajaelezewa kwa undani katika mwongozo huu isipokuwa yametajwa tu.
Zipo tofauti muhimu kati ya mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma
na mifumo mingine kama vile ILS. Tofauti hizo ni kama; katika mfumo huu vituo
haviagizi dawa kama ilivyo kwenye ILS isipokuwa vinatoa taarifa tu na jukumu la
kuagiza ni la mfamasia wa wilaya. Katika mfumo huu pia kiasi cha dawa
zinazohusika ni kidogo ukilinganisha na bidhaa katika mfumo wa ILS. Pia idadi ya
wagonjwa ni ndogo ikilinganishwa na ile inayohudumiwa na mfumo wa ILS.
-
7
A: MADHUMUNI YA MWONGOZO HUU
Madhumuni ya mwongozo huu ni kutoa utaratibu wa namna dawa za kifua kikuu na
ukoma zitakavyokuwa zikipatikana katika vituo vinavyotoa huduma kwa wagonjwa
wa kifua kikuu na ukoma na namna ambavyo wilaya zitakuwa zikiagiza dawa hizi.
Mwongozo utaainisha hatua zinazohitajika katika kukamilisha shughuli zifuatazo:
1. Kuhakikisha kuna kiasi cha shehena kinachotakiwa kuwepo MSD, Wilayani
na katika vituo vya tiba ili kuepusha ukosefu wa dawa na kulundikana
kunakoweza kusababisha dawa kuisha muda wake wa matumizi kabla ya
kumfikia mteja.
2. Uagizaji wa dawa kutoka MSD na kutoka wilayani
3. Utoaji wa taarifa za idadi ya wagonjwa na kiasi cha shehena katika kituo cha
tiba
4. Utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa katika ngazi ya wilaya na ya
kituo cha tiba
5. Ufuatiliaji mbalimbali katika mfumo katika ngazi ya wilaya na ya vituo vya
kutolea tiba
Mwongozo huu unaelezea majukumu na kazi za wadau mbalimbali wanaohusika
na utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma.
Izingatiwe kwamba mwongozo huu siyo mbadala wa mwongozo wa matibabu
ya kifua kikuu na ukoma
B: DAWA ZINAZOSIMAMIWA KUPITIA MFUMO HUU
Mwongozo huu ni kwa ajili ya usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma na wala
hauhusishi dawa zinazosimamiwa kupitia mifumo mingine kama vile ILS.Pia mwongozo
huu hauhusishi usimamizi wa dawa za kutibu kifua kikuu sugu (multi-drug resistant
treatment - MDR)
-
8
Dawa zinazohusika ni kama zinavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:
Dawa Ukubwa wa
kifungashe
RHZE = Rifampicin 150mg + Isoniazid 75mg + Pyrazinamide 400mg +
Ethambutol 275mg
Blista ya vidonge 28
RH = Rifampicin 150mg + Isoniazid 75mg Blista ya vidonge 28
RHE = Rifampicin 150mg + Isoniazid 75mg + Ethambutol 400mg Blista ya vidonge 28
Streptomycin 1g injection Vial
Water for injection Boksi la vial 100
RH Rifampicin 60mg + Isoniazid 30mg Blista ya vidonge 6
RHZ = Rifampicin 60mg + Isoniazid 30mg + Pyrazinamide 50mg Blista ya vidonge 6
Ethambutol 100mg Boksi la vidonge 500
Ethambutol 100mg Boksi la vidonge 100
Isoniazid 100mg Box la vidonge 100
Isoniazid 300mg Blista ya vidonge 28
Presdnisolone 5mg Boksi la vidonge 1000
Pyrazinamide 400mg tabs Boksi la vidonge 1000
Pyrazinamide 400mg tabs Blista ya vidonge 28
PB (adult) Rifampicin 300 + Dapsone 100 Blista ya kutumia siku
28
PB (peds) Rifampicin 150 + Dapsone 50 Blista ya kutumia siku
28
MB (adult) Rifampicin 300 + Clofazimine 100 + Dapsone 100 Blista ya kutumia siku
28
MB (peds) Rifampicin 150 + Clofazimine 50 + Dapsone 50 Blista ya kutumia siku
28
Clofazimine 50mg Boksi la vidonge 1000
Clofazimine 100mg Boksi la vidonge 500
Pyridoxine tabs 50mg P/100 tabs
-
9
C: NANI ANAPASWA KUUTUMIA MWONGOZO HUU?
Walengwa wa mwongozo huu ni watumishi wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma,
bohari kuu ya madawa, watumishi wa afya katika ngazi ya mikoa na wilaya (wafamasia na waratibu wa
kifua kikuu na ukoma), RHMT,CHMT, vituo vya tiba na wadau wote wanaotoa msaada katika mradi wa
kudhibiti kifua kikuu na ukoma
D: MWONGOZO HUU UTAKUSAIDIAJE?
Madhumuni makuu ya mwongozo huu ni kuelezea utaratibu madhubuti na wenye ufanisi unaopaswa
kufuatwa kuhakikisha vituo vinavyotoa huduma ya utoaji dawa kwa wagonjwa wa kifua kikuu na ukoma
vinapata mahitaji yake ya dawa na kutoa taarifa:
Kwa kuhakikisha kuwepo kwa shehena ya kutosha ya dawa za kifua kikuu na ukoma
Kwa kuhakikisha kuwepo kwa hifadhi na usafirishaji wa uhakika wa dawa
Watoaji huduma za afya wanaelewa wajibu wao katika mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua
kikuu na ukoma
Kupunguza uwezekano wa dawa kuisha muda wake wa matumizi zikiwa kwenye stoo au vituo
vya tiba, ufujaji na upotevu.
Kuhakikisha uagizaji na usambazaji wa shehena unafanyika kwa kufuata mfumo uliosahihi.
Lengo la mwongozo huu wa utoaji taarifa uagizaji na usambazaji kama ulivyoelezwa ni kuhakikisha
kwamba wateja na wagonjwa wanapata dawa kila wanapohitaji. Kwa kutekeleza yaliyopo katika
mwongozo huu basi lengo kuu la mfumo wa usimamizi na usambazaji wa dawa za kifua kikuu na
ukoma yatafikiwa
Lengo la mwongozo huu ni kuhakikisha kuwa kuna;
Bidhaa Sahihi
Katika Mahali Sahihi
Kwa Kiasi Sahihi
Kwa Wakati Sahihi
Katika Ubora Sahihi
Na kwa Gharama Sahihi
Haya ndio mambo muhimu yanayopaswa kutekelezwa katika mfumo wa uagizaji na usambazaji ili
kuweza kukidhi mahitaji ya wateja.
-
10
Hivi vikimaanisha:
Shehena Sahihi inapatikana: Dawa za kutibu kifua kikuu na ukoma zinazotakiwa kupatikana,
zinanunuliwa, kusambazwa na kutumiwa ipasavyo.
Mahali Sahihi: Dawa zinafikishwa katika vituo vilikoagizwa na kwamba kuna watendaji waliofunzwa
kuhusu matumizi yake.
Kiasi Sahihi: Kituo cha tiba kina shehena ya kutosha ya dawa. Kiasi cha kuepusha kuishiwa kabla ya
kupokea shehena mpya, lakini sio nyingi kiasi cha kukosa nafasi ya kuihifadhi.
Wakati Sahihi: Wateja na wagonjwa wanatakiwa wapate mahitaji yao kila wanapokwenda kwenye
kituo cha tiba.
Ubora Sahihi: Shehena iko katika hali nzuri, haijaharibika, kuchafuka wala kwisha muda wa matumizi.
Gharama Sahihi: Hii ni gharama ya utaratibu mzima, ikiwa ni pamoja na uchukuzi, uhifadhi, nguvukazi,
n.k. hata kama shehena imetolewa na wahisani au mteja amechangia gharama. Ni lazima mpango
mzima kudhibiti kifua kikuu na ukoma uendeshwe kwa gharama zinazoeleweka. Hii hasa ni muhimu
kwa dawa za kifua kikuu na ukoma ni za ghali.
-
11
E: UTARATIBU WA MTIRIRIKO WA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA NA
TAARIFA KATIKA MFUMO WA USIMAMIZI WA DAWA HIZO
Mtiririko wa taarifa
Mtiririko wa dawa
Gari la MSD
Taarifa ya kila mwezi ya dawa
na idadi ya wagonjwa
Wateja
Vituo vya tiba
DTLC hupokea nakala ya taarifa na
maombi yanayopelekwa MSD kila
robo mwaka kutoka kwa mfamasia
DTLC hupokea taarifa za mwezi za
vituo,kukokotoa kiasi cha kugawa,
kuidhinisha na kisha kupeleka fomu
hizo kwa mfamasia
Mfamasia wa wilaya humpa
DTLC nakala ya R&R
Mfamasia wa Wilaya
Kutoa dawa kwa vituo baada ya
kupokea taarifa zilizoinishwa na
DTLC
Kuandaa taarifa na maombi ya
robo mwaka na kupeleka MSD
Medical Stores
Department
(MSD)
Taarifa na Maombi
ya robo waka
Taarifa za kiasi cha kununua kutoka NTLP kwenda MSD
MSD kutoa taarifa za matumizi ya dawa na
salio kwa NTLP
RTLC- hupokea nakala ya taarifa na maombi
yanayopelekwa MSD kila robo
mwaka kutoka kwa DTLC
National Tuberculosis and leprosy Program
(NTLP)
Taarifa mbalimbali za Utekelezaji wa mpango
DTLC humpa mfamasia fomu
ya kituo baada ya kukokotoa
na kuidhinisha kiasi cha kutoa
-
12
F: MUHTASARI WA MFUMO
Mtiririko wa dawa: Kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro hapo juu mfumo wa ugavi wa dawa za
kifua kikuu na ukoma una ngazi tatu; Ngazi ya MSD, Ngazi ya wilaya na Ngazi ya vituo vya tiba.Kiasi
cha juu cha shehena kwa ngazi ya MSD ni dawa za matumizi ya miezi 9 wakati kisi cha chini cha
shehena ni miezi 6 ya matumizi. Katika ngazi ya wilaya kiasi cha juu cha shehena ni miezi 6 ya
matumizi na kiasi cha chini ni miezi 3. Wilaya itaagiza dawa moja kwa moja kutoka MSD na mkoa
hautahifadhi shehena kama ilivyokuwa awali. Katika ngazi ya kituo, kituo kitapata mahitaji ya dawa ya
kutosheleza wagonjwa kilionao kwa mwiezi miwili
Majukumu ya uagizaji wa dawa za kifua kikuu na ukoma yamehamishwa toka kwa DTLC na sasa
yatafanywa na mfamasia wa wilaya. Wilaya itatunza shehena ya vituo vyote wilayani na mfamasia
atakuwa akigawa dawa kwa kila kituo kila mwezi baada ya kupata taarifa ya mwezi ya kituo husika
iliyoidhinishwa na kuhakikiwa na DTLC.
ZINGATIA: Katika kuandaa taarifa ya mwezi kituo kitatumia kadi za matibabu za wagonjwa ili
kujua kila mgonjwa atakuwa kwenye mwezi wa ngapi wa matibabu kisha kujaza jumla ya
wagonjwa watakaokuwa kwenye mwezi husika wa matibabu katika fomu ya taarifa ya mwezi:
Taarifa ya mwezi ya kituo itaonyesha pia salio la kila dawa kituoni na kiasi cha dawa
kilichoharibika au muda wake wa matumizi kuisha.
-
13
SURA YA 2: fomu za kumbukumbu na taarifa zinazotumika katika mfumo wa ugavi wa dawa za kifua
kikuu na ukoma
Fomu za kumbukumbu na taarifa zinatakiwa kutumika na watendaji wanaosimamia shehena za dawa.
Nakala za fomu hizi na maelekezo ya namna ya kuzijaza na kuzitumia zinapatikana Sura ya 7 ya
mwongozo huu.
Jina la Fomu Matumizi Mtumiaji Mkuu Mahali
itumikapo
Fomu ya mwezi ya
taarifa ya dawa na
wagonjwa ya kituo
Kutoa taarifa ya salio la dawa,kiasi
cha dawa zilizoharibika na idadi ya
wagonjwa katika miezi mbailmbali ya
matibabu katika mwezi unaofuata ule
unaotolewa taarifa.
DOT Nurse au
Mtumishi
aliyeteuliwa
kujaza fomu.
Vituo
vinavyotoa tiba
ya kifua kikuu
na ukoma
Fomu ya taarifa na
maombi ya robo
mwaka ya dawa za
kifua kikuu na ukoma
Kutoa taarifa ya kiasi cha dawa
zilizopo wilayani,matumizi ya wilaya
nzima,kiasi cha upotevu na
marekebisho na maombi ya dawa
kwa robo mwaka inayofuata
Mfamasia wa
wilaya au
mtumishi
aliyeteuliwa
kujaza fomu
Ngazi ya wilaya
Fomu ya kunakili
kiasi cha dawa
kilichotolewa vituoni
kila mwezi
Kuweka kumbukumbu ya kiasi cha
dawa kilichotolewa kwa kila kituo
wilayani na jumla yake. Fomu hii
inasidia kurahisisha uandaaji wa
taarifa ya robo mwaka
Mfamasia wa
wilaya au
mtumishi
aliyeteuliwa
kujaza fomu
Ngazi ya
wilaya)
Kadi ya mgonjwa ya
matibabu ya kifua
kikuu na ukoma
Kuweka kumbukumbu ya huduma
anazopata mgonjwa pamoja na aina
ya dawa anazopatiwa.
Kadi hii inasaidia kutambua mwezi wa
matibabu wa mgonjwa wakati wa
kujaza taarifa ya mwezi ya kituo
DOT Nurse Kituo
Fomu nyingine zinazotumika kwenye mifumo mingine ya usimamizi wa bidhaa za
afya zitatumika pia katika mfumo huu kwa kuzingatia matumizi yake. Fomu hizo ni;
issue voucher, goods received note (grn), verification and claim form, leja ya mali
-
14
SURA YA 3: UWAJIBIKAJI KATIKA USIMAMIZI WA UAGIZAJI NA
USAMBAZAJI WA SHEHENA ZA DAWA ZA KIFUA
KIKUU NA UKOMA
Kulingana na kazi au wajibu wako ndani ya mfumo wa usimamizi wa uagizaji na usambazaji wa dawa
za kifua kikuu na ukoma, mwongozo huu umeandaliwa kukusaidia kutekeleza shughuli zifuatazo kwa
ufanisi na kwa wakati.
A. MAJUKUMU KATIKA KITUO CHA TIBA
Wajibu wa watendaji katika vituo vya tiba katika usimamizi wa mfumo wa uagizaji na usambazaji wa
dawa za kifua kikuu na ukoma ni kama yalivyoainishwa hapa chini;
1. Majukumu ya mtunza stoo/bohari ya dawa na vifaa
Kuhifadhi kwa usahihi shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma ili kudumisha ubora na
usalama kwa matumizi na usalama wa mali.
Kufanya hesabu kwa mkono mali iliyopo kila mwisho wa mwezi.
Kuhakikisha kwamba ubora wa shehena unadumishwa.
Kutunza kumbukumbu ya dawa za kifua kikuu na ukoma zinazoingia na kutoka stoo kwa
kujaza leja mali
Kupokea shehena ya dawa kwa mujibu wa utaratibu uliopo.
Kutoa dawa stoo kwa kuzingatia utaratibu wa FEFO na FIFO
Kutoa taarifa ya dawa zilizoharibika
2. Majukumu ya DOT Nurse
Kutunza hesabu za kila siku za dawa walizopewa wagonjwa kwa kujaza kadi za matibabu ya
mgonjwa
Kujaza fomu ya Taarifa ya mwezi na kumpa mkuu wa kituo kuidhinisha.
Kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa
Kufuatilia idadi ya wagonjwa wanaotumia IPT wakati wa kujaza fomu ya mwezi (taarifa hii
inapatikana kwa CTC incharge)
-
15
3. Majukumu ya mkuu wa kituo
Kuhakikisha kuwa katika kituo kuna dawa za kutosha kulingana na idadi ya wagonjwa na
mwezi mmoja wa ziada katika hatua zote za matibabu (intensive na continuation phases)
Kuwasiliana na mfamasia wa wilaya iwapo dawa zitapungua na zitahitajika kwa dharura.
Kurudisha dawa zilizokaribia kuisha muda wa matumizi kwa mfamasia wa wilaya.
Kurudisha dawa za ziada au zisisohitajika kituoni (mfano wakati kinakuwa na dawa lakini
hakina wagonjwa) kwa mfamasia wa wilaya.
Kuteua mtu wa kufanya kazi za ujazaji wa taarifa zihusuzo usimamizi wa dawa za kifua kikuu
na ukoma kituoni kama mhusika hayupo (kuhakikisha zoezi hili linakuwa shirikishi)
Kuidhinisha fomu ya taarifa ya kila mwezi ya kituo
Kupeleka taarifa ya mwezi ya kituo wilayani katika kipindi kisichozidi tarehe 5 ya mwezi
unaoanza
Kusimamia matumizi sahihi ya dawa
Kutoa taarifa za madhara ya dawa na dawa duni
Kuratibu upokeaji dawa na vifaa tiba
Kuratibu utoaji elimu juu ya matumizi ya dawa kwa watumishi na wagonjwa
B. MAJUKUMU KATIKA NGAZI WILAYA
Wajibu wa watendaji katika ngazi ya wilaya katika usimamizi wa mfumo wa uagizaji na usambazaji wa
dawa za kifua kikuu na ukoma ni kama yalivyoainishwa hapa chini;
1. Majukumu ya Mfamasia wa Wilaya
Mfamasia wa wilaya ana kazi kubwa kuhakikisha hakuna ukosefu wa dawa za kifua kikuu na ukoma
katika wilaya yake.Hivyo majukumu yake ni;
Kuhakikisha kuwa kila mwezi vituo vinapata dawa za kifua kikuu na ukoma
Kufanya majumuisho ya taarifa za dawa alizotoa kwa kila kituo na kuandaa taarifa na maombi
ya dawa kwa kila robo mwaka ambayo itapelekwa MSD. .
Kuandaa taaarifa na maombi ya robo mwaka ya dawa za kifua kikuu na ukoma kwa msaada
wa DTLC pale inapohitajika na kuipeleka MSD.
Kupeleka taarifa na maombi ya dawa za kifua kikuu na ukoma kwa DMO kwa ajili ya uthibitisho
Kumpatia DTLC nakala ya taarifa na maombi ya dawa za kifua kikuu na ukoma inayoenda
MSD
-
16
Kuhakikisha kuwa wilaya inatunza kiasi cha juu cha shehena kisichozidi miezi 6 na kiasi cha
chini cha shehena kisichopungua miezi 3.
Kuhakikisha kuwa kumbukumbu za mahesabu ya dawa zinahuishwa kila wakati (leja ya mali
nk).
Kufanya heasabu ya mkono/kila mwezi
Kuratibu usimamizi shirikishi
Kufanya usimamizi shirikishi na mafunzo kazini (On-the-Job training) kwa watoa huduma ili
kuwajengea uwezo wa kusimamia vizuri dawa za kifua kikuu na ukoma na hivyo kupunguza
ukosefu wa dawa vituoni
Kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa vituo visivyotoa taarifa na vinavyochelewesha taarifa zao.
Kuhifadhi kwa usahihi wa shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma ili kudumisha ubora na
usalama kwa matumizi na usalama wa mali.
Kukusanya taarifa ya dawa zilizoharibika na zinazokaribia kuharibika vituoni na kuandaa
taarifa
Kutunza taarifa za mwezi za vituo zilizoletwa wilayani
Kuratibu usambazaji wa dawa za ziada au ambazo hazitumiki kutoka kituo kimoja kwenda
kingine au kuzirudisha wilayani.
Kuomba na kusambaza nyenzo za usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma
Kuingiza dawa za kifua kikuu kwenye eLMIS
Kupokea dawa kutoka MSD
Kufanya maombi ya dharura ya dawa
Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti za usimamizi wa dawa
2. Majukumu Ya Mratibu Wa Kifua Kikuu Na Ukoma Wa Wilaya (Dtlc)
Kupokea na kupitia taarifa za kila mwezi kutoka vituoni na kuangalia kama zimejazwa kikamilifu
na kwa usahihi; kujumlisha idadi ya wagonjwa katika miezi mbalimbali ya matibabu na
kukokotoa kiasi cha dawa cha kutoa kwa kila kituo
Kuidhinisha kiasi cha dawa za kutoa kwa kituo
Kumsaidia mfamasia wa wilaya katika kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea tiba wilayani
vinapata dawa za kifua kikuu na ukoma.
Kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa vituo visivyotoa taarifa na vinavyochelewesha taarifa zao.
Kushiriki katika usimamizi shirikishi
-
17
Kupokea nakala ya taarifa na maombi ya robo mwaka ya dawa za kifua kikuu na ukoma na
kuipeleka kwa mratibu wa mkoa.
Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti za usimamizi wa dawa
Kusambaza miongozo na vipeperushi vituoni
Kuratibu utoaji elimu juu ya matumizi mazuri ya dawa
Kusimamia matumizi mazuri ya dawa
3. Majukumu ya Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO)
Kuidhinisha taarifa na maombi ya dawa za wilaya
Kusaidia katika mikakati ya kuhakikisha dawa za kifuakikuu na ukoma zinapatikana muda
wote katika wilaya yake
C. MAJUKUMU KATIKA NGAZI YA MKOA
1. Majukumu ya Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa (RTLC)
Kupokea nakala za taarifa na maombi ya robo mwaka zinazopelekwa MSD kutoka kwa DTLC,
kuzikagua na kutoa ushauri kwa kadri inavyohitajika.
Kumshirikisha mfamasia mkoa taarifa za kila robo mwaka anazozipata kutoka wilaya
Kushiriki katika usimamizi shirikishi
2. Majukumu ya Mfamasia wa Mkoa
Kupitia taarifa za robo mwaka za dawa za wilaya kwa kushirikiana na RTLC na kubaini mambo
yanayohitaji kuangaliwa au kufuatiliwa kwa karibu
Kuratibu usimamizi shirikishi
D. MAJUKUMU YA BOHARI KUU YA MADAWA (MSD)
Wajibu wa watendaji Bohari Kuu ya Madawa katika usimamizi wa mfumo wa uagizaji na usambazaji wa
shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma ni pamoja na:
Kufanya manunuzi ya shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma
Kupokea na kuhifadhi kwa usahihi wa shehena za dawa ili kudumisha ubora, usalama kwa
matumizi.
Kutunza hesabu za shehena iliyopo na ile ambayo iko hatarini kwisha muda wake wa matumizi
au kuharibika au haitumiki tena MSD.
-
18
Kujaza Leja ya Mali na kujaza fomu zingine zote zinazohusu ugavi.
Kufanya hesabu kwa mkono ya mali iliyopo katika wakati uliopangwa.
Kuhakikisha kwamba ubora wa shehena za dawa unadumishwa.
Kupokea na kushughulikia maombi ya dawa kutoka wilayani
Kuandaa na kusambaza shehena wilayani kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa maombi
yaliyopokewa kupitia fomu za maombi na taarifa kwa ajili ya dawa.
Kuwasilisha NTLP taarifa za matumizi na kiasi cha shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma
katika bohari za MSD kila baada ya miezi 3.
Kuwasiliana na wilaya ambazo zinashindwa kuwasilisha maombi yake kwa muda muafaka
Mfumo huu unaitaka MSD kuwa uwezo wa kuhifadhi kiasi cha shehena kinachoweza
kutosheleza mahitaji ya vituo vyote vya tiba ya kifua kikuu na ukoma. Kiasi cha chini cha
shehena ni kile kinachoweza kutosheleza mahitaji ya miezi sita, na kiasi cha juu ni kile
kinachoweza kutosheleza mahitaji ya miezi tisa.
E. WIZARA YA AFYA (NTLP)
Wajibu wa watendaji NTLP katika usimamizi wa mfumo wa uagizaji na usambazaji wa shehena
za dawa kifua kikuu na ukoma ni pamoja na:
Kutathmini taarifa zilizopokewa kutoka wilayani kupitia MSD ili kuweza kuandaa makadirio ya
mahitaji ya kiasi cha shehena ya dawa za kifua kikuu na ukoma na kuwasilisha makadirio hayo
kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kupata fedha za kununua mahitaji hayo.
Kuratibu upatikanaji wa fedha au dawa kutoka kwa washirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na
serikali ya Tanzania (GOT) kwa ajili ya ununuzi wa shehena za dawa
Kuratibu mipango ya manunuzi kwa wakati na ratiba ya usafirishaji wa shehena za dawa ili
kuhakikisha uwepo wa dawa za kiwango cha juu wakati wote.
Kupeleka taarifa MSD kuhusu kiasi cha dawa kinachotakiwa kununuliwa.
Kupokea taarifa kutoka MSD kuhusu ununuzi na upokeaji wa shehena.
Kufuatilia shughuli za uagizaji na usambazaji wa shehena na kuwasimamia watekelezaji.
Kutoa taarifa mrejesho na taarifa za mpango kwenye vituo vya tiba na watendaji wengine
ikiwamo MSD
Kutoa taarifa mbalimabali zihusuzo dawa za kifua kikuu na ukoma (mfano kuchelewa kufika
nchini kwa shehena nk.)
-
19
Kukusanya taarifa kutoka MSD kuhusu kiasi cha shehena ambazo zimesambazwa kwenye
wilaya mbalimbali.Pia taarifa za shehena iliyopo. Taarifa zipatikanozo hutumika kuainisha
mahitaji ya kitaifa, manunuzi ya dawa
SURA YA 4: UTUNZAJI WA HESABU ZA BIDHAA
ZINAZOTOLEWA
Ni muhimu kwa watendaji katika vituo vya tiba wanaohusika na ugawaji wa dawa za kifua kikuu na
ukoma kuweka kumbukumbu ya matumizi ya dawa hizi. Matumizi hayo yanapaswa kujazwa kwenye
Rejista ya DOT ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu hivyo haijaingizwa kwenye mwongozo
huu. Kumbukumbu pia ziingizwe katika kadi za wagonjwa kama inavyofanyika hivi sasa. Kadi hii pia
haijaingizwa kwenye mwongozo huu kwani imekuwa ikitumika kwa muda mrefu.
Kadi ya matibabu ya mgonjwa iliyotajwa hapo juu hutoa taarifa muhimu ambazo hutumiwa na kituo cha
tiba kujaza idadi ya wagonjwa walio katika miezi mbalimbali ya matibabu wakati wa kujaza fomu ya
taarifa ya mwezi ya kituo.
-
20
SURA YA 5. UAGIZAJI
A: KUHAKIKISHA KIASI CHA KUTOSHA CHA SHEHENA
Moja ya kazi kuu za msimamizi wa bidhaa ni kuhakikisha kwamba daima kuna shehena ya kutosha
kukidhi mahitaji ya mteja. Izingatiwe ya kuwa katika mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na
ukoma mfamasia wa wilaya pekee ndiye anayeagiza dawa kutoka MSD. Hii ina maana ya kuwa
mfamasia wa wilaya atatoa shehena ya kutosha kukidhi mahitaji ya vituo vya tiba kulingana na taarifa
za kila mwezi anazoletewa na vituo .Kwa vituo vya tiba hii ina maana ya kuwa daima vinatakiwa kuwa
na bidhaa za kutosha kuwapa dawa wagonjwa wote wanaotumia dawa.
Moja ya maswali makuu kwa wasimamizi wa bidhaa ni “Kiasi gani cha shehena kinatosha?” MSD na
wilaya zimekwishawekewa kiasi kinachohakikisha kuwa kuna shehena ya kutosha kukidhi mahitaji ya
wateja wao na wakati huo huo kutokuwa na shehena kubwa kupindukia na kuwa hatarini kuharibika au
kwisha muda wa matumizi. Katika kituo cha ugavi (MSD) shehena inapaswa kuwa kati ya kiasi cha
chini cha kutosheleza miezi sita na kiasi cha juu cha miezi tisa. Katika wilaya shehena inapaswa kuwa
kati ya kiasi cha chini cha kutosheleza miezi mitatu na cha juu cha miezi sita.
Pia kwa wilaya kuna utaratibu wa uagizaji wa shehena ya Dharura (Emergency Order) ikiwa shehena
kwenye ngazi ya wilaya itapungua chini ya shehena ya kutosheleza mwezi mmoja na nusu.
B: TATHMINI YA KIASI CHA SHEHENA
Utaratibu wa kuwa na viwango vya kiasi cha juu na chini cha shehena ni kuhakikisha kwamba daima
shehena inakuwepo ndani ya kiwango maalum — cha juu na cha chini. Ili kufahamu iwapo shehena
yako imo ndani ya viwango hivyo, itakulazimu kufanya tathmini ya shehena.
Unapofanya mapitio ya kiasi cha shehena yako unabainisha ni kiasi gani cha kila dawa ya kifua kikuu
au ukoma inapatikana katika wilaya yako/ghala lako na kwamba kila moja ya dawa hizo itatosheleza
kwa muda gani. Unaweza kufanya mapitio ya kiasi cha shehena yako kwa kuhesabu shehena iliyopo,
kama unavyofanya wakati ukifanya Hesabu kwa mkono. (. Kwa kufanya hivyo utahakikisha unajua kiasi
halisi cha shehena iliyopo. Lakini ni muhimu zaidi kufahamu shehena hiyo itadumu muda gani na
kama una kiasi cha kutosha kukidhi mahitaji hadi kuwasili kwa shehena mpya. Hiyo inajulikana kama
Miezi ya kipindi cha Shehena (Months of Stock-MOS).
-
21
Miezi ya kipindi cha Shehena(MOS) ni idadi ya miezi ambapo shehena ya dawa itachukua hadi
kumalizika kwa kulinganisha na kasi ya matumizi kwa sasa. Unapofanya mapitio ya kiasi cha shehena
yako inakubidi ubainishe kwamba kituo chako kimesaliwa na miezi mingapi kabla ya bidhaa kuisha.
Miezi mitatu ya kipindi cha shehena ina maana kwamba shehena itadumu kwa miezi mitatu, alimradi
kasi ya matumizi iendelee kuwa kwa viwango vya sasa.
Kwa kufanya tathmini ya shehena yako utaweza kubaini iwapo kituo chako kimepungukiwa, kimezidiwa
au kimetoshelezwa. Iwapo utajikuta umepungukiwa na bidhaa mojawapo, na unafahamu kwamba
shehena ambayo umeiagiza hivi karibuni bado muda wa kuwasilishwa, huenda ukalazimika kuchukua
hatua za uagizaji wa dharura (Tazama Sehemu E kwa jinsi ya kuchukua hatua ya uagizaji wa dharura).
Iwapo utakuwa na ziada ya bidhaa, huenda ukalazimika kugawia wilaya za jirani kinachohitaji.
NAMNA YA KUBAINI MIEZI YA KIPINDI CHA SHEHENA
Kwa kukokotoa miezi ya kipindi cha shehena, kituo kinaweza kubaini iwapo kina kiasi cha kutosha cha
dawa. Ili kubaini shehena itadumu kwa muda gani, kanuni nyepesi ifuatayo inaweza kutumika:
Tuna kiasi gani?
(Shehena Iliyopo) =
Shehena itadumu muda gani
(Miezi ya kipindi cha Shehena
iliyoko) Tumetumia kiasi gani?
(Wastani wa Matumizi ya Mwezi)
Kabla ya kukokotoa Miezi ya Kipindi cha Shehena Iliyopo, kuna vitu viwili ambavyo unapaswa
kufahamu — Shehena Iliyopo na Wastani wa Matumizi kwa Mwezi
Ili kubaini Wastani wa Matumizi kwa Mwezi (Average Monthly Consumption - AMC), jumulisha matumizi
ya miezi mitatu iliyopita ya dawa fulani halafu gawanya kwa tatu.
Tumia kanuni ifuatayo kubaini AMC:
Matumizi ya mwezi huu + matumizi ya miezi 2 iliyotangulia =
Wastani wa
Matumizi kwa Mwezi 3
Zingatia: Unapokokotoa kutafuta Wastani wa Matumizi ya Mwezi, daima andika namba kamili ya juu
inayofuata. Mfano uki pata 43.6 jibu litakuwa 44 na ukipata 44.2 jibu litakuwa 44
-
22
Matumizi ya robo mwaka ya hivi karibuni zaidi yanaweza kupatikana kwenye nakala za Taarifa na
Maombi ya dawa za kifua kikuu na ukoma au kwenye worksheet ya ukokotozi inayoonyesha kiasi cha
dawa kilichogawiwa katika vituo. Kwa kila dawa ambayo unataka kutathmini kiasi cha shehena, chukua
taarifa za matumizi za miezi mitatu kamili iliyopita. (Dawa zilizotolewa kwa kituo zinahesabiaka kuwa
zimetumiaka zote hivyo kwenye mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma jumla ya
dawa zilizotolewa kwa vituo kwa miezi mitatu ndiyo jumla ya matumizi kwa kipindi hcho) Iwapo
katika kipindi chochote cha robo mwaka kulitokea kwisha kwa dawa, basi rekebisha taarifa za kwisha
kwa mali kwa kutumia kanuni za marekebisho ya ugavi, au usitumie kabisa taarifa hizo bali utumie
taarifa zingine kamili za robo mwaka ya karibu ambapo hapakutokea kwisha kwa mali. Iwapo utakosa
taarifa kamili kwa miezi mitatu, basi tumia taarifa zozote zitakazopatikana mfano taarifa za kipindi kama
hicho mwaka uliopita. Kokotoa kupata wastani wa matumizi kwa mwezi, kisha gawanya shehena
Iliyopo (inapatikana kwa Hesabu kwa mkono) kwa wastani wa matumizi kwa mwezi (AMC) uliyokokotoa
kupata Miezi ya Kipindi cha Shehena Iliyopo. Tumia kanuni ifuatayo kubaini shehena iliyopo ya kila
bidhaa itadumu kwa muda gani:
Shehena Iliyopo
= Miezi ya Kipindi cha Shehena Iliyopo Wastani wa Matumizi kwa Mwezi
Zingatia: Ukishakokotoa idadi ya miezi ya Kipindi cha Shehena, tumia tarakimu moja tu baada ya
desimali!!
Iwapo namba ambayo ingefuata baada ya namba hiyo ni 4 au pungufu, punguza kwenda namba
kamili iliyotangulia, iwapo ni 5 au zaidi, ongeza kwenda namba kamili ya juu inayofuata. Mfano kama
jibu ulilopata ni 3.23 miezi ya shehena itakuwa 3.2 au kama jibu ulilopata ni 4.36 miezi ya shehena
itakuwa 4.4
Tathmini ya Kiasi cha Shehena ifanyike lini?
Kiasi cha shehena ya katika wilaya kinapaswa kufanyiwa tathmini wakati wowote utakapokuwa na
wasiwasi kwamba huenda viwango vya shehena haviko ndani ya viwango vya juu na chini vya kituo
chako. Hali hiyo inaweza kutokea iwapo palitokea upotevu wa shehena kutokana na kuharibiwa, kwisha
muda wa matumizi au wizi, au kama patatokea ongezeko au upungufu wa ghafla wa matumizi.
Wilaya zinapaswa kufanya tathmini ya kiasi cha shehena wakati wa kujaza sehemu ya maombi katika
fomu za R&R ya wilaya, watendaji wakague hali ya shehena za dawa za kifua kikuu na ukoma:
-
23
Iwapo kiasi kinachoombwa ni namba hasi, basi ina maana kwamba shehena imejaa mno wilayani na
kuna haja ya kufanya tathmini ya hali ya sehena. Huenda shehena zikalazimika kugawiwa wilaya
nyingine iwapo kuna uwezekano wa kwisha kwa muda wa matumizi kabla hazijaweza kutumika.
Iwapo maombi ya kiasi cha shehena ni makubwa mno kuliko kiasi cha kawaida basi huenda wilaya ina
upungufu wa shehena na ishauriwe kufanya tathmini ya shehena ya mara kwa mara kuepusha haja ya
kuchukua hatua za uagizaji wa dharura.
Iwapo wilaya inawasilisha maombi ya mara kwa mara ya hatua za uagizaji wa dharura, zifanyike juhudi
za kubaini sababu za uagizaji wa dharura na kuchukua hatua zingine kama itakavyohitajika.
-
24
C: NAMNA YA KUTAMBUA MWEZI WA MATIBABU ATAKAOKUWA MGONJWA
Mfumo wa usimamizi wa dawa za kifua kikuu na ukoma una changamoto katika utekelezaji wake hasa
katika katika ngazi ya kituo. Changamoto inayouutofautisha mfumo huu na mifumo mingine ni
mabadiliko ya dawa zinazotumika na wagonjwa wa kifua kikuu kulingana na muda. Katika matibabu ya
kifua kikuu wagonjwa hutibiwa katika hatua mbili zinazojulikana kama intensive phase na continuation
phase na kisha humaliza matibabu. Kila hatua inatumia dawa tofauti na hivyo kama utaratibu wa
kutumia matumizi ya miezi mitatu iliyopita kuagizia dawa ungetumika kama ilivyo katika mifumo ya ILS
na ARVs basi hatari iliyopo ni kuwa kituo kinaweza kupelekewa dawa ambazo hazihitajiki kwani
wagonjwa watakuwa wamebadili hatua ya matibabu na hivyo kukosa dawa stahiki na kupelekea
kukosekana kwa dawa na pia mrundikano wa dawa usiohitajika kituoni. Katika mfumo wa usimamizi wa
dawa za kifua kikuu na ukoma utaratibu umewekwa kukiwezesha kituo kupata dawa kulingana na idadi
ya wagonjwa kilionao ikizingatiwa hatua ya matibabu waliyopo. Kufanikisha hili kituo kinatakiwa kutoa
taarifa ya idadi ya wagonjwa kitakaokuwa nao katika kila mwezi unaofuata na miezi ya matibabu
watakayokuwa. Kwa mantiki hii jambo muhimu hapa ni kujua namna gani nayeandaa taarifa ya mwezi
ya kituo atakavyoweza kutambua mwezi wa matibabu atakaokuwa mgonjwa katika mwezi unaofuata
ule anaotolea taarifa. Hili linawezekana kufanyika kwa kutumia kadi ya matibabu ya mgonjwa.
i. Kwa wagonjwa wa kifua kikuu mwezi wa matibabu unabainishaji wa mwezi wa matibabu
atakaokuwa mgonjwa unafanywa kama ifuatavyo;
a. Bainisha idadi ya dozi zilizokwishatolewa kwa mgonjwa hadi mwisho wa mwezi unaotolewa
taarifa
b. Kisha bainisha mwezi wa matibabu atakao kuwa kwa kufuata utaratibu ufuatao
Na Aina ya Mgonjwa Dozi alizokwishapewa mgonjwa
hadi mwisho wa mwezi
unaotolewa taarifa
Mwezi wa
matibabu
atakaokuwa
1 Mtoto & Mkubwa & Retreatment Chini ya 28 1
2 Mtoto & Mkubwa & Retreatment 28 na zaidi lakini chini ya 56 2
3 Mtoto & Mkubwa &Retreatment 56 na zaidi lakini chini ya 84 3
4 Mtoto & Mkubwa &Retreatment 84 na zaidi lakini chini ya 112 4
5 Mtoto & Mkubwa & Retreatment 112 na zaidi lakini chini ya 140 5
6 Mtoto&Mkubwa & Retreatment 140 na zaidi lakini chini ya 168 6
7 Mtoto & Mkubwa 168 Amemaliza
-
25
Na Aina ya Mgonjwa Dozi alizokwishapewa mgonjwa
hadi mwisho wa mwezi
unaotolewa taarifa
Mwezi wa
matibabu
atakaokuwa
8 Retreatment 168 na zaidi lakini chini ya 196 7
9 Retreatment 196 na zaidi lakini chini ya 224 8
10 Retreatment 224 Amemaliza
ii. Kwa wagonjwa wa ukoma mwezi wa matibabu atakaokuwa mgonjwa unabainishwa unafanywa
kama ifuatavyo;
a. Bainisha idadi ya mahudhurio ya mgonjwa hadi mwisho wa mwezi unaotolewa taarifa
b. Mwezi wa matibabu wa mgonjwa utakuwa ni tarakimu inayofuata ile inayoonyesha idadi ya
mahudhurio ilivyobainishwa. Mfano kama idadi ya mahudhurio ni 2 inamaanisha mgonjwa huyu
atakuwa mwezi wa 3 wa matibabu au kama idadi ya mahudhurio ni 1 inamaanisha atakuwa
mwezi wa 2 wa matibabu, nk.
Izingatiwe kuwa wagonjwa wa PB (watoto na wakubwa) matibabu yao ni ya miezi sita (6) tu
ilihali matibabu ya wagonjwa wa MB (watoto na wakubwa) matibabu yao ni ya miezi 12.
D: UTOAJI WA TAARIFA WA VITUO VYA TIBA
Kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu na ukoma kinatakiwa kutoa taarifa kila mwezi
kwa kutumia fomu maalumu ya utoaji taarifa ya mwezi. Fomu hii ni rahisi na huchukua muda mfupi
kuijaza.
Kama kituo hakina wagonjwa kinatakiwa kutoa taarifa kwa kuweka sifuri kwenye visanduku
husika katika fomu ya kutolea taarifa. Hii ni muhimu ili DTLC ajue kwamba kituo hakina
wagonjwa.
Hata kama kituo hakina dawa kabisa kinatakiwa kutoa taarifa kwa kuweka sifuri kwenye
visanduku mbele ya dawa husika.
Hata kama kituo hakina dawa na hakina wagonjwa kinatakiwa kutoa taarifa pia.
Kama kituo hakitatoa taarifa DTLC wa wilaya hatoweza kujua hali ya kituo.
-
26
Taarifa zinazotakiwa kwenye fomu zinapatikana kwa namna mbili;
1. Tumia kadi za matibabu za wagonjwa kujua idadi ya wagonjwa watakaokuwa kwenye miezi
tofauti tofauti ya matibabu mfano mwezi 2,3,4, na kadhalika. Katika mwezi wa 1 andika idadi ya
wagonjwa ambao hawajamaliza mwezi mmoja wa matibabu hadi mwisho wa mwezi wakati
unaandika taarifa ya mwezi pia jumuisha wagonjwa wapya wanaotarajiwa kuanza dawa katika
mwezi unaofuata ule unaotolea taarifa (mfano kama taarifa ni ya Januari idadi ya wagonjwa
wapya ni wale watakaoanza matibabu Februari. Pia kama kituo kina wagonjwa wa ukoma
kitatakiwa kuwaweka kwenye sehemu husika katika jedwali la wangonjwa kulingana na idadi
yao na miezi yao ya matibabu katika mwezi unaofuata ule unaotolewa taarifa.
2. Fanya hesabu kwa mkono kujua kiasi cha kila aina ya dawa kilichopo mwisho wa mwezi na
kukionyesha kama salio kwenye sanduku husika kwenye fomu ya taarifa. Izingatiwe kwamba
salio ni dawa zinazoweza kutumika tu kama dawa zimeharibika au muda wake wa matumizi
kuisha idadi yake iainishwe kwenye kisanduku husika kwenye fomu ya taarifa.Kiasi kiandikwe
katika vipimo vya ugawaji tu na siyo maboksi.
3. Uwasilishaji wa fomu ya taarifa ya mwezi wilayani.
DTLC atapokea fomu za taarifa za mwezi zilizojazwa kutoka vituo vyote wilayani hadi kufikia
tarehe 5 ya kila mwezi.
DTLC atazikagua taarifa kuangalia kama zimekamilika na kama ni sahihi na kama atahitaji
ufafanuzi anaweza kuwasiliana na mtoa huduma katika kituo husika.
Kisha DTLC atakokotoa kiasi cha dawa kinachohitajika kituoni katika mwezi husika
kuidhinisha na kisha kumpa mfamasia fomu ya kituo.
Mfamasia wa wilaya atagawa dawa kwa kituo kama ilivyoidhinishwa na DTLC.
Mfamasia atatumia issue vocha kama nyaraka husika katika kuonyesha dawa zimetolewa
kwa kituo lakini pia ataingiza kumbukumbu katika leja ya mali ya stoo ya wilaya.
Vituo havifanyi ukokotozi wowote wakati vikiandaa taarifa ya
mwezi.Kazi yao ni kuweka idadi ya wagonjwa watakaokuwa kwenye
matibabu katika miezi mbalimbali, salio la kila dawa na kiasi cha
dawa kilichoharibika au muda wake wa matumizi kuisha. DTLC
atafanya mahesabu kujua kiasi cha kuwapa.
Hii ni tofauti na mfumo wa ILS na wa ARVs ambapo vituo
hufanya ukokotozi wa kiasi cha kuagiza
-
27
Izingatiwe kuwa: Ni rahisi kukokotoa kiasi cha kutoa kwa kituo kwa kuzingatia taarifa zilizoletwa na
kituo katika fomu ya taarifa ya mwezi. Kituo kitapewa mara mbili ya dawa za kutosha wagonjwa wake
walio katika matibabu. Kama kituo kina shehena ya dawa itatolewa kwenye kiasi kinachohitajika na
tofauti ndiyo itakayopewa kwa kituo.
E: JINSI WILAYA INAVYOAGIZA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA
Maombi ya wilaya yanafanyika kila baada ya miezi mitatu (robo mwaka). Mfamasia wa wilaya ndiye
mwenye jukumu la kuagiza dawa za kifua kikuu na ukoma kwa ajili ya wilaya yake. Kiasi chaa dawa
atakachoagiza mfamasia wa wilaya kitatokana na kanuni ya ukokotozi inayoonekana kwenye fomu ya
taarifa na maombi ya robo mwaka ya dawa za kifua kikuu na ukoma. Mfamasia wa wilaya atampatia
DMO fomu ya taarifa na maombi ya robo mwaka aliyokwisha ijaza kwa uthibitisho. Baada ya
kuthibitishwa mfamasia ataipeleka fomu hii MSD.Fomu iwe imefika MSD ifikapo tarehe 14 ya mwezi wa
kwanza war obo mwaka iliyoanza. Fomu ya taarifa na maombi ina nakala tatu halisi moja na zingine
mbili. Nakala halisi ndiyo inayotumwa MSD moja atapewa DTLC ambaye huituma kwa RTLC na moja
hubaki kwenye kitabu.
Hapo MSD, watendaji watashughulikia maombi yako ipasavyo na kubaki na nakala yako halisi kwa ajili
ya kumbukumbu zao.
Fomu ya kutolea taarifa na maombi ya dawa za kifua kikuu na ukoma pia imewekwa kwenye
mfumo wa ki electronic (eLMIS). Wilaya inaweza kutumia mfumo huu kuagiza dawa za kifua
kikuu na ukoma kutoka MSD
F: MAOMBI YA DHARURA
Kama katika wakati wowote kiasi cha shehena ya dawa yoyote katika stoo ya wilaya kitakuwa mwezi
mmoja na nusu wa matumizi au chini ya hapo na hakuna shehena yoyote inayotarajiwa kufika wilayani
katika siku mbili zinazofuata maombi ya dharura yanatakiwa kufanywa na mfamasia wa wilaya.
Wakati wa kuandaa maombi ya dharura mfamasia,
Ajaze visanduku vyote katika mistari husika wa dawa na aagize shehena inayotosheleza
kufikisha kiwango cha juu (miezi 6 ya matumizi)
Aandike neno “maombi ya dharura” (EMERGENCY ORDER) kwa herufi kubwa juu kulia katika
ukurasa wa fomu ya taarifa na maombi.
-
28
Apeleke maombi hayo MSD kwa njia ya haraka ili kusaidia pasiwepo na ukosefu wa dawa
vituoni
G: UGAWAJI WA DAWA KUTOKA MSD KWENDA WILAYANI
Dawa za kifua kikuu na ukoma za wilaya zitatumwa kutoka ofisi ya MSD ya kanda iliyo karibu na wilaya
husika. Gari la MSD ndilo litakalo husika na kusafirisha shehena hiyo hadi wilayani na kutoka wilayani
dawa zitapelekwa vituoni.
Zifuatazo ni taratibu zinazofuatwa wakati wa kugawa dawa kutoka MSD kwenda wilayani;
1. MSD kupokea maombi na taarifa kutoka wilayani
Maombi kutoka wilayani yanatakiwa yawe yamefika MSD mwishoni mwa juma la pili (Tarehe 14) la
mwezi wa kwanza wa robo mwaka inayofuata ile inayotolewa taarifa.
2. MSD Kukagua usahihi wa maombi na taarifa kwenye fomu
Fomu zinapowasili MSD hukaguliwa kubaini usahihi wa taarifa zilizomo na kuangalia kama kiasi
kilichoombwa kipo .
3. MSD kufungasha shehena
Mfanyakazi wa MSD atachukua na kufungasha shehena tayari kwa ajili ya kupelekwa wilayani. Pamoja
na dawa katika shehena kutakuwa na nyaraka mbalimbali zinazoambatana na shehena kama ilivyo
katika mifumo mingine ya usimamizi wa bidhaa. Nyaraka hizo ni pamoja na Fomu namba 4 (MSD Sales
Invoice) na Fomu namba 7 (Verification and Claims Form). MSD pia wataambatanisha Fomu namba 6:
Goods Received Note (GRN) itakayotiwa sahihi wakati wa upokeaji wa shehena wilayani.
Uhamishaji wa dawa kutoka wilaya moja kwenda nyingine
Katika mazingira magumu mfano umbali mkubwa kutoka MSD, uharibifu wa miundombinu
kama wakati wa mvua nk. Ni vigumu kupata dawa haraka kwa dharura kutoka MSD hivyo
wilaya inaweza kuazima kutoka wilaya nyingine yenye kiasi cha kutosha cha dawa .Kiasi
kilichoazimwa kiingizwe kama marekebisho chanya katika leja ya mali ya wilaya
iliyoazimishwa na marekebisho hasi katika leja ya wilaya iliyoazimisha..
-
29
4. MSD kupeleka shehena wilayani
Shehena ya dawa za kifua kikuu na ukoma italetwa wilayani kwa kutumia gari la MSD. Shehena
inatakiwa kuwa imefikishwa wilayani inapofikia mwisho wa wiki ya kwanza ya mwezi wa pili wa robo
mwaka iliyoanza. Shehena hii itakuja pamoja na dawa nyingine zinazosimamiwa kupitia mifumo
mingine . Kama shehena haitafika kwa muda unaotarajiwa mfamasia anaweza kuwasiliana na MSD
kujua ni lini shehena italetwa.
5. Upokeaji wa shehena ya dawa wilayani
Mfamasia wa wilaya au mtumishi yeyote aliyeteuliwa atapokea shehena na kuikagua kujiridhisha kama
kiasi kilicholetwa ni sahihi.
Izingatiwe kuwa taratibu za upokeaji wa dawa za kifua kikuu na ukoma hazina tofauti na taratibu
za upokeaji wa dawa nyingine.
H: UGAWAJI WA DAWA KUTOKA WILAYANI KWENDA VITUONI
Mfamasia wa wilaya atapokea taarifa za kila mwezi kutoka kwa DTLC na atatoa dawa kwa kituo
kulingana na kiasi kilichokokotolewa na DTLC kwenye fomu ya taarifa ya mwezi ya kituo husika. Vituo
vingi vitapata dawa siku ya kupeleka taarifa wilayani baada ya kufanyiwa ukokotozi na DTLC na fomu
kupelekwa kwa mfamasia. Pale inapohitajika mfamasia kwa kushirikiana DTLC atashughulikia usafiri
wa kuzipeleka dawa katika kituo husika.
Dawa za kifua kikuu na ukoma zitolewe kwa blisters/maboksi au makopo na kama kutokana na
ukokotozi kituo kitahitaji dawa/vidonge pungufu ya blisters basi makadirio yafanyike kutoa blister nzima.
Mfano kituo kinahitaji blista 10.5 basi kipewe blisters 11 vivyo hivyo kwa makopo au maboksi. Kutokana
na uchache wa wagonjwa wa kifua kikuu na ukoma mara nyingi kituo kitahitaji kiasi kidogo cha dawa.
Mtunza stoo au mfamasia wa wilaya atatumia issue vocha kunakili kiasi cha dawa alichotoa kwenda
kituoni na wakati wa kutoa dawa atazingatia utaratibu wa FEFO na FIFO
Upokekeaji wa shehena ya dawa kituoni
Kituo cha tiba kinatakiwa kuwa kimeshapata dawa za kifua kikuu na ukoma hadi ifikapo tarehe 15 ya
kila mwezi. Wakati wa kupokea mtumishi anayefanya kazi hiyo atafanya ukaguzi kujiridhisha kuwa
dawa zilizoletwa ziko kwenye hali nzuri na zinafaa kwa matumizi. Kama kuna zilizoharibika zirudishwe
wilayani. Wakati wa kupokea mtumishi anayepokea ataweka sahihi yake kwenye issue vocha
iliyoandaliwa na mtumishi wa wilayani kuthibitisha kuwa amepokea shehena. Kisha atafanya ingizo
kwenye leja ya mali ya kituo.
-
30
Ugawaji wa dawa ndani ya kituo cha tiba
Mara nyingi katika kituo kuna sehemu moja tuu ya kugawia dawa za kifua kikuu na ukoma kwa
wagonjwa.Mtunza stoo anashauriwa agawe kiasi cha dawa kinacho tosheleza matumizi ya juma moja
kwenda sehemu ya utoaji wa dawa. Kila anapofanya hivyo azingatie kufanya ingizo kwenye leja ya mali
ya kituo na pia kutumia issue vocha itakayowekwa sahihi na yule anayepokea dawa.
-
31
SURA YA 6: KUHIFADHI DAWA ZA KIFUA KIKUU NA UKOMA
Mazingira ya kuhifadhi huathiri ubora wa dawa. Ili kuhakikisha ubora na usalama, ni lazima masharti
stahili ya uhifadhi wake yazingatiwe kabla ya kuzisambaza: Taratibu za uhifadhi wa dawa za kifua kikuu
na ukoma hazitofautiani na taratibu za uhifadhi wa dawa zingine. Taratibu za uhifadhi wa bidhaa za
afya zimejadiliwa kwa kina katika miongozo ya usimamizi wa dawa katika mfumo wa ILS na ARVs.
Mwongozo huu hautarudia kuelezea taratibu hizo.
A: HESABU YA MKONO
Ufanyaji wa hesabu ya mkono wa dawa za kifua kikuu na ukoma unafanana na ule wa dawa au bidhaa
nyingine za afya ambao umeelezewa kwa kina katika mwongozo wa mifumo ya ILS na ARV. Hesabu
kwa mkono ni kitendo cha kuhesabu kwa mkono idadi ya kila mali iliyopo kwenye kituo. Hesabu kwa
mkono ni moja ya shughuli ambazo hufanyika kila mwezi katika zahanati, vituo vya afya na hospitali na
wakati wowote inapohitajika.
Hesabu kwa mkono inapaswa kujumuisha taarifa ya hesabu kutoka sehemu zote ambapo mali ipo, kwa
mfano:
1. Kiasi kilichopo kutoka shelfu au kabati za bohari
2. Kiasi kilichopo eneo la kugawia dawa kituoni hapo.
Kwa mfano: kama kuna maboksi manne (4) ya RHZE stoo na kila boksi lina vidonge 672 na
sehemu ya kugawia dawa kuna blista 4 ambayo ni sawa na vidonge
4 * 28= 112. Hivyo jumla ya hesabu kwa mkono iliyopo kituoni ni vidonge 672+ 112 =
784
Kama hesabu ilifanyika mwisho wa mwezi ndiyo itakayo tumika kuandaa taarifa ya mwezi ya kituo
itakayopelekwa wilayani.Dawa zilizo sehemu ya kugawia zisipohesabiwa zinaweza kusababisha kituo
kikaletewa dawa zaidi ya kinazozihitaji.
Kiasi cha mali kilicho kwenye shelfu kinaweza kupatikana kwenye Leja ya mali. Hata hivyo, katika zoezi
la kuhesabu kwa mkono, kiasi kilichoko kwenye shelfu kinalinganishwa na hesabu iliyoingizwa kwenye
kitabu (Leja ya mali). Iwapo kiasi kilicho kwenye shelfu hakilingani na kile kilichoandikwa kwenye Leja,
basi Leja ihuishwe (Updated) kwa kufanya marekebisho.
-
32
Mali iliyopo eneo la kugawia dawa kituoni hapo pia itahitaji kuhesabiwa. Mtu anayefanya hesabu
asiziguse dawa kwa mkono kwa sababu si lazima kuhesabu dawa kwa kuzimwaga kwenye chombo
cha wazi, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuziharibu. Kitakachofanyika ni kukadiria ujazo wa chupa
kwa robo iliyo karibu. Kwa chupa ya vidonge 1,000, robo ni vidonge 250 na kwa chupa ya vidonge 500
robo ni vidonge 125.
Unapofanya Hesabu kwa mkono zingatia yafuatayo;
B: UKAGUZI WA BIDHAA KWA MACHO
Taratibu za ukaguzi wa macho zinazoelezewa kwenye miongozo ya mifumo ILS na ARV ndizo hizo
hizo zinazotumika kwenye mfumo wa dawa za kifua kikuu na ukoma Ukaguzi wa Macho unapaswa
kufanywa kila kunapokuwa na shughuli yoyote ihusuyo bidhaa hiyo kama vile: wakati wa kupokea,
wakati wa kutoa au wakati wa kufanya hesabu kwa kwa mkono.
C: KUHARIBU MALI ISIYOFAA KWA MATUMIZI
Kila liwezekanalo linapaswa kufanywa ili kuepusha kwisha kwa muda wa matumizi au kuharibika kwa
dawa na bidhaa zingine. Fuata utaratibu wa FEFO kupunguza tatizo hili. Hata hivyo, ikitokea kuna
dawa zilizoharibika au muda wake wa matumizi kuisha ziharibiwe kwa kufuata taratibu na kanuni
zilizowekwa na mamlaka za udhibiti (WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII, TFDA). Zoezi la
kuharibu linatakiwa lifanyike mapema ili kutoa nafasi kwa dawa zinazofaa kutunzwa na kuepusha
zisitumike kwa bahati mbaya.
Kama kuna mali iliyokwisha muda wa matumizi au imeharibika, itenge na kuiwekea
“karantini” mara moja ili isiweze kugawiwa au kutumika. Kwenye Leja ya mali (Leja), jaza
kiasi kilichoisha muda wa matumizi au kuharibika kama ni marekebisho hasi (negative
adjustments).
-
33
SURA YA 7: FOMU ZINAZOTUMIKA KATIKA MFUMO WA
USIMAMIZI WA DAWA ZA KIFUA KIKUU NA
UKOMA NA UFAFANUZI WAKE
Sehemu hii ina ufafanuzi wa utendaji wa shughuli ambazo zimetajwa katika mwongozo huu, nazo ni:
S/N JINA LA FOMU
1 Leja ya Mali
2 Hati ya Kutolea Shehena (Local Issue Voucher)
3 Kadi ya matibabu ya mgonjwa
4 Fomu ya Taarifa ya Mwezi ya Kituo
5 Fomu ya kunakili kiasi cha dawa kilichotolewa vituoni
8 Fomu ya Taarifa na Maombi ya robo Mwaka ya dawa za kifua kikuu na ukoma ya wilaya
Ufafanuzi Kinachofafanuliwa
A Kujaza dozi zilizogawiwa kwa wagonjwa katika kadi ya mgonjwa wa kifua kikuu
B Kujaza taarifa ya mwezi ya kituo
C Kuhakiki fomu ya taarifa ya kituo na kukokotoa kiasi cha kugawa
D Kujaza Fomu ya Taarifa na Maombi ya robo Mwaka ya dawa za kifua kikuu na ukoma ya
wilaya
-
34
A. UFAFANUZI A: UJAZAJI WA DOZI ZILIZOGAWIWA/TOLEWA KWA
MGONJWA KATIKA KADI YA MATIBABU YA KIFUA
KIKUU
SEHEMU A
KAZI: KUJAZA DOZI ZILIZOGAWIWA/TOLEWA KWA MGONJWA KATIKA KADI YA
MATIBABU YA KIFUA KIKUU
INAFANYWA NA: DOT Nurse
SABABU: Kutunza kumbukumbu ya dozi za dawa zilizokwishatolewa kwa mgonjwa
LINI INAFANYWA: Kila dawa zinapotolewa kwa mgonjwa
NYENZO
ZINAZOHITAJIKA:
Kadi ya mgonjwa na kalamu
SEHEMU B
Hatua Cha kufanya Zingatia
1. Visanduku vya idadi ya dawa kwenye
intensive phase: Jaza idadi ya vidonge
ambavyo mgonjwa atakuwa akitumia katika
kisanduku mahususi kulingana na aina ya
mgonjwa.Idadi ya vidonge inaendana na
uzito/umri wa mgonjwa kulingana na
mwongozo wa matibabu ya kifua kikuu
(NTLP manual); Mfano kama ni mgonjwa
mpya mwenye makohozi yaliyoonekana na
kifua kifua (smear positive) na atatumia
vidonge 3 vya RHZE andika 3 katika
kisanduku cha kwanza, chenye maelezo ya
New case AFB+ juu na RHZE chini yake
Kama mgonjwa ni wa retreatment ingiza
taarifa zake kwenye kisanduku cha tatu na
kwenye kisanduku kidogo chenye S kwa chini
andika milligram za Streptomycin ambazo
mgonjwa atakuwa akichomwa.
Kwa wagonjwa watoto waliokatika umri/uzito
wa kutumia dawa za watoto ingiza taarifa zao
katika kisanduku cha nne (Children). Kumbuka
kuwa hawa wanatumia RHZ na Ethambutol.
Hivyo kumbuka kujaza idadi ya vidonge vya
Ethambutol (E) na RHZ katika visanduku
vidogo kama inavyoongozwa.
2. Mwezi na Mwaka Intensive phase: Jaza
mwezi na Mwaka ambapo matibabu
yanatolewa katika nafasi zilizopo
Kwa kadiri matibabu yanavyoendelea mwezi
utakuwa ukibadilika na hivyo kila mwezi ingiza
jina na mwezi na mwaka. Mwaka pia unaweza
kubadilika kulingana na lini mgonjwa kaanza
matibabu
3. Dozi zilizotolewa/alizopewa mgonjwa
katika intensive phase; Andika namba ya
dozi unazompa mgonjwa kwa kuanzia na
tarehe uliyoanza kumpa. Mfano kama
mgonjwa alianza kupewa dozi ya kwanza 10
namba moja inapaswa kuandikwa ndani ya
kisanduku cha kwanza chini ya tarehe 10.
Kisha namba ya dozi zinazofuata zitaendelea
Kama mgonjwa ananywea dawa zake
kituoni (FACILITY DOT) kila siku namba ya
dozi aliyopewa itaandikwa. Mfano kwa
mgonjwa aliyetajwa hapo kushoto dozi ya pili
itakuwa tarehe 11, ya tatu tarehe 12 ya nne
tarehe 13 nk.
Kama mgonjwa anakunywa dawa zake
nyumbani (HOME BASED DOT) iandikwe
-
35
Hatua Cha kufanya Zingatia
katika tarehe zinazofuata namba ya dozi aliyonywea kituoni kisha mstari
uchorwe kuonyesha siku dawa alizopewa, na
andika namba ya dozi atakayokunywa siku ya
kurudi kuchukua dawa. NB.
Mara nyingi wagonjwa wanaotumia
dawa kupitia utaratibu wa HOME
BASED DOT katika intensive phase
hunywa dozi moja kituoni na kisha
hupewa dawa za wiki moja (siku saba)
ikijumuisha dozi watakayonywea
kituoni siku ya kurudi kuchukua dawa.
Mfano kwa mgonjwa aliyeanza dozi ya
1 tarehe 10 Nov namba 1 itaandikwa
kwenye tarehe 10 Nov kisha mstari
utapigwa hadi tarehe 16 Nov.
Mgonjwa anatarajiwa kurudi tarehe 17
Nov na atanywea dozi ya 8 kituoni,
hivyo namba 8 iandikwe kwenye
tarehe 17. Tarehe hiyo 17 Nov
atapewa dozi 7 za kutumia hadi tarehe
24 Nov ambapo atarudi kituoni na
kunywa dozi 15 hivyo mstari upigwe
kuanzia tarehe 18 Nov hadi tarehe 23
Nov na namba 15 iandikwe kwenye
tarehe 24 Nov
Katika miezi ambayo ina siku pungufu
ya 31 weka alama ya X katika
visanduku vya tarehe hizo ili kuepuka
mkanganyiko unaoweza kujitokeza.
Hivyo siku zenye X hazitahesabika
kama siku ambazo mgonjwa
ametumia dawa.
Matibabu ya wagonjwa wapya wa
kifua kikuu katika intensive phase
huchukua dozi 56
Matibabu ya wagonjwa wa retreatment
wa kifua kikuu katika intensive phase
huchukua dozi 84
4. Visanduku vya idadi ya dawa kwenye
continuation phase: Jaza idadi ya vidonge
ambavyo mgonjwa atakuwa akitumia katika
kisanduku mahususi kulingana na aina ya
mgonjwa.Idadi ya vidonge inaendana na
Kama mgonjwa ni wa retreatment ingiza
taarifa zake kwenye kisanduku cha pili
chenye maelezo Retreatment juu na RHE
kushoto
-
36
Hatua Cha kufanya Zingatia
uzito/umri wa mgonjwa kulingana na
mwongozo wa matibabu ya kifua kikuu
(NTLP manual); Mfano kama ni mgonjwa
mpya na atatumia vidonge 3 vya RH andika
3 katika kisanduku cha kwanza, chenye
maelezo ya New case juu na RH kushoto
kwake
Kwa wagonjwa watoto walio katika
umri/uzito wa kutumia dawa za watoto
ingiza taarifa zao katika kisanduku cha
tatu chenye maelezo Children juu na RH
kushoto.
5. Mwezi na Mwaka katika continuation
phase: Jaza mwezi na Mwaka ambapo
matibabu ya continuation phase yanatolewa
katika nafasi zilizopo
Kwa kadiri matibabu yanavyoendelea
mwezi utakuwa ukibadilika na hivyo kila
mwezi ingiza jina na mwezi na mwaka.
Mwaka pia unaweza kubadilika kulingana
na lini mgonjwa kaanza matibabu.
6. Dozi zilizotolewa/alizopewa mgonjwa
katika contunuation phase; Andika namba
ya dozi unazompa mgonjwa kwa kuanzia na
tarehe uliyoanza kumpa.
Kwa wagonjwa wapya na watoto dozi ya
kwanza ya continuation phase itakuwa
dozi namba 57 (mwendelezo wa idadi
kutoka intensive phase). Hivyo katika
kujaza kadi hili lizingatiwe. Kwa wagonjwa wa retreatment dozi ya
kwanza ya continuation phase ni namba
85 kwa kufuata mwendelezo kutoka
intensive phase.
Kama ilivyokuwa kwenye intensive phase
Kama mgonjwa ananywea dawa
zake kituoni (FACILITY DOT) kila
siku namba ya dozi aliyopewa
itaandikwa. Mfano kwa mgonjwa
mpya aliyeanza kutumia dawa za
continuation phase tarehe 10 Nov
ambayo ni dozi ya 57, dozi ya 58
itakuwa tarehe 11 Nov, ya 59
tarehe 12 Nov ya 60 tarehe 13
Nov nk.
Kwa wagonjwa wa retreatment dozi
ya kwanza ya continuation phase
itaanza na 85 kisha mwendelezo
ufafuata kila siku mf, 86,87,
88…….. (kwa kuzingatia tarehe)
Kama mgonjwa anakunywa dawa
zake nyumbani (HOME BASED
DOT) iandikwe namba ya dozi
-
37
Hatua Cha kufanya Zingatia
aliyonywea kituoni kisha mstari
uchorwe kuonyesha siku dawa
alizopewa na andika namba ya
dozi atakayokunywa siku ya kurudi
kuchukua dawa.
Mara nyingi wagonjwa wanaotumia
dawa kupitia utaratibu wa HOME
BASED DOT katika continuation
phase hunywa dozi moja kituoni na
kisha hupewa dawa za wiki mbili
(siku 14) ikijumuisha dozi
atakayonywea kituoni siku ya
kurudi kuchukua dawa.
Mfano kwa mgonjwa aliyeanza dozi
ya 57 tarehe 10 Nov namba 57
itaandikwa kwenye tarehe 10 Nov
kisha mstari utapigwa hadi tarehe
23. Mgonjwa anatarajiwa kurudi
tarehe 24 na atanywea dozi ya 71
kituoni, hivyo namba 71 iandikwe
kwenye tarehe 24. Tarehe hiyo 24
Nov atapewa dozi 14 za kutumia
hadi tarehe 8 Dec ambapo atarudi
kituoni na kunywa dozi 85 hivyo
mstari upigwe kuanzia tarehe 25
Nov hadi tarehe 7 Dec na namba
85 iandikwe kwenye tarehe 8 Dec.
Tarehe 31 itawekewa X kwa kuwa
Nov ina siku 30
NB.
Dozi ya mwisho ya continuation phase kwa
wagonjwa wapya wa kifua kikuu ni ya 168
Dozi ya mwisho ya wagonjwa wa retreatment
ni ya 224.
KAZI HII INAKUWA IMEKAMILIKA BAADA YA:
Idadi ya vidonge ambavyo mgonjwa atakuwa akitumia itakuwa imejazwa katika kisanduku husika.
Namba ya dozi zilizokwishatolewa kwa mgonjwa kuwa zimeandikwa kwa wagonjwa walio kwenye
FACILITY DOT
Namba ya dozi aliyokwisha kunywa mgonjwa na mstari unaoonyesha kiasi cha siku ambazo tayari
mgonjwa amepewa dawa za kutumia kwa wagonjwa walio kwenye HOME BASED DOT
-
38
B. FOMU YA TAARIFA YA KITUO YA MWEZI YA DAWA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU NA UKOMA TB 01
INTENSIVE PHASE : Laboratory Results
Indicate number of tablets per dose Month Smear Lab. No.
Body Weight
New Case AFB+ New Case AFB-/EP Retreatment Children Date Result
0
RHZE RHZE S RHZE RHZ E 1
2
3
5
RHZE: Rifampicin, Isoniazid, Pyrazinamide, Ethambutol (4FDC) S: Streptomycin RHZ: Rifampicin, Isoniazid, Pyrazinamide 7/8 For patients on health-facility DOT, write the number of dose on the date of DOT. For patients on home-based DOT, draw a horizontal line to indicate the number of days supply given to supporter, and then write number of dose on return date Month Year 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31
CONTINUATION PHASE Indicate number of
tablets per dose New case Retreatment Children
RH (4 Months) RHE (5 Months, daily) RH (4 Months)
For patients on health-facility DOT,write the number of dose on the date of DOT. For patients on home-based DOT, draw a horizontal line to indicate the number of days’ supply given to supporter, and then write number of doses on return date Month Year 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31
Treatment outcome Date : ____/____/__________
Cure
Treatment Completed
Treatment Failure
Died
Default
Transfer out
Remarks ______________________________________________________________________________________________________________
-
39
C. UFAFANUZI B: UJAZAJI WA FOMU YA TAARIFA YA MWEZI YA KITUO
Fomu hii ni rahisi kujaza na kituo kinatakiwa kujaza fomu hii hata kama hakina wagonjwa au dawa za
kifua kikuu na ukoma.
SEHEMU A
KAZI: Kujaza FOMU YA TAARIFA YA MWEZI YA KITUO
INAFANYWA NA: Mtumishi wa afya anayetoa dawa za kifua kikuu (DOT Nurse)
SABABU: Kutoa taarifa za idadi ya wagonjwa walio kwenye tiba, salio la dawa na kiasi cha
dawa zilizoharibika au muda wake wa matumizi kuisha.
LINI INAFANYWA: Mwishoni mwa kila mwezi
NYENZO
ZINAZOHITAJIKA:
Kitabu cha taarifa ya mwezi ya dawa za kifua kikuu na ukoma, hesabu ya mkono
ya dawa ya mwisho wa mwezi, kalamu (Bluu, nyeusi), hesabu ya kiasi cha dawa
zilichoharibika au muda wa matumizi kuisha
SEHEMU B
Hatua Cha kufanya Zingatia
1. Jaza namba ya utambulisho ya kituo:
Namba hii inatolewa na Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii..
2. Jaza jina la Kituo: Jaza jina la kituo
chako
3. Aina ya Kituo: Jaza aina ya kituo. Vituo vinaweza kuwa:
(GOV) Serikali
(NGO) Asasi zisizokuwa za kiserikali
(FBO) Mashirika ya Dini
Vingine
4. Jina la (Halmashauri) Wilaya: Jaza jina
la wilaya ambako kituo kinawajibika.
5. Kipindi cha Taarifa: Jaza mwezi na
mwaka unaohusika katika taarifa hii.
Hiyo itakuwa ni kipindi cha mwezi ambao ndio
kwanza umekamilika. Mfano taarifa ya Januari
itaandikwa siku ya mwisho ya Januari au
mwanzoni mwa Februari.
6. Tarehe ya kuwasilishwa: Andika tarehe
ambapo taarifa imewasilisha kwa DTLC
Hakikisha fomu inajazwa na inafika wilayani kabla
ya siku ya 5 ya mwezi unaofuata. Mfano taarifa ya
Januari ifike wilayani ndani ya kipindi kisichozidi
tarehe 5 ya February.
Kituo kipeleke wilaya nakala mbili za taarifa hii
(halisi na nakala moja). Nakala moja ibaki kwenye
-
40
kitabu kituoni. Kituo kisibebe kitabu chote na
kupeleka wilayani, ispokuwa kama kimeombwa
kufanya hivyo.
7. Miezi ya matibabu. Katika visanduku
vyenye miezi ya matibabu andika idadi ya
wagonjwa watakaokuwa kwenye mwezi
husika wa matibabu ya kifua kikuu na
ukoma katika mwezi unaofuata ule
unaotolea taarifa.
Katika kujaza jedwali hili kadi za wagojwa
ziatatumika kutambua kila mgonjwa
atakuwa kwenye mwezi wa ngapi wa
matibabu katika mwezi unaofuata.
Ni vizuri kama unayeandaa taarifa
ukachora jedwali kama hili pembeni na
kisha kuwa anaweka tick kwenye mwezi
husika pale anapobaini kuwa mgonjwa
atakuwa kwenye mwezi huo wa matibabu
baada ya kupitia kadi yake.
Baada ya kupitia kadi zote jumlisha idadi
ya tick kwenye kila kisanduku kasha
jumla yake iandike kwenye fomu
unayoandikia taarifa
Tumia sehemu hii pia kuonyesha idadi ya
wagonjwa wanaotumia Isoniazid kama kinga
tiba na miezi yao tiba hii katika visanduku
husika.
Katika mwezi wa 1 pia andika idadi ya
wagonjwa wapya wanaotarajiwa kuanza dawa
katika mwezi unaofuata (mfano kama taarifa
ni ya Januari idadi ya wagonjwa wapya ni
wale watakaoanza matibabu Februari kama.
Hii ifanyike kama kituo kina taarifa za kuwepo
kwa wagonjwa hao wapya.
Kwa wagonjwa wapya wa kifua kikuu na
watoto kama ulikuwa na wagonjwa kwenye
mwezi wa 6 wa matibabu mwezi ulioisha na
hukuwa na mgonjwa kwenye mwezi wa 5 wa
matibabu kwenye mwezi ulioisha hii
inamaanisha utakuwa huna mgonjwa kwenye
mwezi wa 6 wa matibabu na hivyo unatakiwa
uandike 0. Ikumbukwe kuwa matibabu ya
kawaida ya kifua kikuu ni ya miezi 6.
Wagonjwa wapya ambao hali yao ya
makohozi haibadiliki baada ya matibabu ya
miezi miwili huendelea na matibabu ya
intensive phase kwa mwezi mmoja zaidi
hivyo kama kituo kina mgonjwa wa aina hii
wakati wa kuandika taarifa ya mwezi
ahesabike kama atakuwa mwezi wa 2
katika mwezi unaofuata na atakapomaliza
marudio haya ataendelea kuhesabika
kama mwezi wa 3 katika mwezi unaofuata.
Pia izingatiwe kuwa
Matibabu ya wagonjwa wa retreatment ni
ya miezi 8
Matibabu ya wagonjwa wa ukoma wa MB
ni miezi 12
Matibabu ya wagonjwa wa ukoma wa PB
ni miezi 6
8. Salio la dawa: Jaza jumla ya
-
41
vidonge/kapsuli zilizopo baada ya
kufanya hesabu kwa mkono hadi kufikia
mwishoni mwa mwezi
9. KIasi kilichoharibika au kuisha muda
wa matumizi: Jaza idadi ya
vidonge/kapsuli ambazo
zimeharibika(hazifai kwa matumizi) au
ambazo muda wake wa matumizi
umeisha
Wasiliana na mfamasia kuhusu uwepo wa dawa
zilizoharibika au muda wake wa matumizi kuisha
ili mkubaliane namna zitakavyorudishwa wilayani
10. Maelezo:
Andika maelezo ya za uharibifu wa dawa
kama kuna kiasi chochote kimeandikwa
kwenye safu B mf expiry, kumwagikiwa
mafuta nk. Sehemu hii pia inaweza
kutumika kuitaarifu wilaya juu ya uwepo
wa dawa ambazo muda wake wa
matumizi utaisha ndani ya miezi mitatu
ijayo.
11. Maelezo muhimu:
Andika taarifa za wagonjwa wanaohitaji
dawa nyingine tofauti na zile
zilizoorodheshwa kwenye fomu mfano
predinisolone nk. Ili DTLC ajue namna
ya kusaidia.
12. Imeandaliwa na: Mtumishi wa kituo cha
tiba aliyeandaa taarifa hii anaandika jina
lake, saini na tarehe.
Jaza fomu ya taarifa siku ya mwisho ya mwezi au
siku ya kwanza ya mwezi unaofuata. Fomu hii
inatakiwa ifike wilayani katika muda usiozidi
tarehe 5 ya mwezi unaofuata.
13. Imepitiwa na: Mganga mkuu wa kituo
aipitie na kuipitisha taarifa kwa kuweka
sahihi na tarehe
14. Imeidhinishwa na: DTLC Mtumishi wa
wilaya aliyeteuliwa kupitia, kuhakiki na
kukokotoa kiasi cha dawa cha kugawa
ataidhinisha baada ya kuandika kiasi cha
dawa kinachopaswa kugawiwa kituoni
anaandika jina lake, saini na tarehe.
-
42
KAZI HII INAKUWA IMEKAMILIKA BAADA YA:
Namba ya kituo, Jina la Kituo na kipindi cha taarifa kujazwa.
Visanduku vya idadi ya wagonjwa katika miezi ya matibabu kujazwa
Safu za Salio la Mwisho kwa kila bidhaa
Safu ya kaisi cha dawa kilichoharibika au muda wa matumizi kuisha kujazwa
Fomu ya taarifa imesainiwa na mtayarishaji
Fomu imesainiwa na mkuu wa kituo
-
43
D. FOMU YA TAARIFA YA KITUO YA MWEZI YA DAWA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU NA UKOMA
TAARIFA YA KITUO YA MWEZI YA DAWA ZA KUTIBU KIFUA KIKUU NA UKOMA
Namba ya Kituo: Jina la Kituo: Aina ya Kituo (GOV/NGO/FBO/NYINGINE): ____________ Jina la Halmashauri Kipindi cha Taarifa-- Mwezi/Mwaka: Tarehe iliyowasilishwa: ___ Andika kwenye nafasi chini idadi ya wagonjwa unaokisia kuwa watakuwa kwenye matibabu kwa mwezi unaofuata. Andika sifuri (“0”) kwa kila mwezi ambao unadhani kuwa hakutakuwa na wagonjwa walio kwenye matibabu. Soma maelezo hapo chini. Mwezi wa wa Matibabu 1 2 3 4
5
6
7 8 9 10 11 12
Kifua Kikuu Idadi ya watu wazima
(Wapya)
Idadi ya watoto (Wapya)
Idadi ya watu wazima
(Retreatment)
Idadi ya watu wazima (IPT)
Idadi ya watoto (IPT)
Ukoma Idadi ya watu wazima (MB)
Idadi ya watu wazima (PB)
Idadi ya watoto (MB)
Idadi ya watoto (PB)
Hesabu idadi ya dawa zilizopo kwenye kituo. Andika kiasi kwa kipimo, kama blister, ulizonazo kwa kila dawa kwenye visanduku chini. Usijumuishe dawa zilizo kwisha muda wa matumizi au dawa zilizoharibika. Andika sifuri (“0”) kwenye nafasi kama dawa haipo. Soma maelekezo kwenye mwongozo wa ujazaji taarifa ya mwezi ya dawa za kutibu Kifua Kikuu na ukoma
-
44
Na SEHEMMU HII IJAZWE NA KITUO SEHEMU HII IJAZWE NA DTLC SEHEMU HII IJAZWE NA MFAMASIA
Jina la Bidhaa
Kipimo cha kugawa
Kiasi kilichosalia
Kiasi kilichoharibika/expire
Idadi ya wagonjwa watakaotumia dawa
mwezi ujao
Mahitaji ya mwezi kwa
mgonjwa mmoja
Mahitaji ya wagonjwa
wote
Mahitaji ya kituo
Kiasi cha kutoa
kiasi kilichopendekezwa kutolewa
Kiasi Kikichotolewa
Maelezo
U A B C D E = C*D
F=E*2 G= F-A G/U
1 RHZE 150/75/400/275
Blista/28 112
2 RH 150/75 Blista/28 112
3 RHE 150/75/400
Blista/28 112
4 Streptomycin 1g Kichupa(Vial)
Chupa 28
5 Water for injection
Kichupa (Ampoule)
Chupa 28
6 MB (adult) Blista Blista 1
7 PB (adult) Blista Blista 1
8 RHZ 60/30/150
Blista/6 112
9 RHZ
60/30/150
Blista/3 112
10 Ethambutol 100mg
Boksi/500 84
11 RH 60/30 Blista/6 112
12 RH 60/30 Blista/3 112
13 MB (Peds) Blista Blista 1
14 PB (Peds) Blista Blista 1
-
45
Na SEHEMMU HII IJAZWE NA KITUO SEHEMU HII IJAZWE NA DTLC SEHEMU HII IJAZWE NA MFAMASIA
Jina la Bidhaa
Kipimo cha kugawa
Kiasi kilichosalia
Kiasi kilichoharibika/expire
Idadi ya wagonjwa watakaotumia dawa mwezi ujao
Mahitaji ya mwezi kwa mgonjwa mmoja
Mahitaji ya wagonjwa wote
Mahitaji ya kituo
Kiasi cha kutoa
kiasi kilichopendekezwa kutolewa
Kiasi Kikichotolewa
Maelezo
U A B C D E = C*D
F=E*2 G= F-A G/U
15 Isoniazid 100mg
Boksi/100 56
16 Isniazid 300mg Blista/28 28
MAELEZO MUHIMU:___________________________________________________________________________________________________________
_________________________________________________________________________________________________________________________
IMEANDALIWA NA:______________________________________ SAHIHI:____________________________ TAREHE:________________
IMEPITIWA NA:_________________________________________ SAHIHI:____________________________ TAREHE: _______________
IMEIDHINISHWA NA:_____________________________________ SAHIHI:____________________________ TAREHE:________________
-
46
E. UFAFANUZI C: KUHAKIKI TAARIFA KWENYE FOMU YA MWEZI YA
KITUO NAKUKOKOTOA KIASI CHA DAWA CHA
KUGAWA
KAZI: Kuhakiki taarifa kwenye fomu ya mwezi ya kituo nakukokotoa kiasi cha dawa
cha kugawa
INAFANYWA NA: DTLC
SABABU:
Kudhibiti ukosefu wa dawa kituoni
Kuhakakiki kuwa vituo vinavyotoa dawa za kifua kikuu na ukoma vinatoa
taarifa
Kuangalia usahihi wa taarifa zinazotolewa
Kuhakikisha kuwa kituo kinapewa kiasi sahihi cha dawa
LINI INAFANYWA: Ndani ya kipindi kisichozidi tarehe 10 ya mwezi unaofuata mwezi wa
taarifa ya kituo
NYENZO
ZINAZOHITAJIKA:
Taarifa ya mwezi ya dawa za kifua kikuu na ukoma ya kituo,kalamu,kikokotozi,
na worksheet ya ukokotozi
SEHEMU B
Hatua Cha kufanya Zingatia
A: Kuhakiki kama vituo vyote vimetuma taarifa zao
1. Kuthibitisha kama vituo vyote vimeleta
taarifa.
Hesabu idadi ya fomu za taarifa ya mwezi ya dawa za kifua kikuu na ukoma zilizoletwa wilayani. Idadi inatakiwa kulingana na idadi ya vituo vinavyopaswa kuleta taarifa.
Kama kituo hakijaleta taarifa wasiliana na kituo
husika au kitembelee ili upate taarifa yake. Au
wasiliana na kituo kujua idadi ya wagonjwa
watakaokuwa katika matibabu katika miezi
mbalimbali, salio la kila dawa na kiasi cha
dawa kilichoharibika au kuisha muda wake wa
matumizi. Tumia taarifa hizo kubainisha kiasi
gani kituo kina hitaji na kwa kuandaa maombi
ya wilaya lakini pia fanya jitihada kuhakikisha
kituo kinaleta taarifa yake wilayani mapema
iwezekanavyo
-
47
Hatua Cha kufanya Zingatia
B: Kuhakiki ukamilifu na usahihi wa taarifa
2. Pitia taarifa za juu ya fomu na uone kama
zimejazwa kwa ukamilifu na usahihi
Taarifa zinazotakiwa ni;
Namba ya kituo
Jina la kituo
Aina ya kituo
Jina la halmashauri/ wilaya
Kipindi cha taarifa
Tarehe ya kuwasilisha
3. Angalia idadi ya wagonjwa iliyoandikwa
kujiridhisha kama ni ya kweli na inaleta
mantiki. Haijaongezeka wala kupungua
sana.
Pale unapokuwa na mashaka ni vizuri
kujiridhisha kwa kuangalia taarifa za miezi
iliyopita. Mfano kama imeonyeshwa kuwa
hakuna mgonjwa kwenye mwezi 4 wa
matibabu lakini wapo 13 kwenye mwezi wa 5
wa matibabu unaweza kuangalia taarifa ya
mwezi uliopita kama kulikuwa na wagonjwa 13
kwenye mwezi wa 4 wa matibabu. Kama kuna
utata wowote wasiliana na kituo husika
4. Angalia pia kiasi cha vidonge
vulivyoandikwa kama salio la mwisho wa
mwezi.
Salio la dawa linatakiwa kuendana na uhalisia
wa wagonjwa waliokuwepo kituoni katika
mwezi unaotolewa taarifa . Kama kuna
ongezeko au upungufu unaotia shaka basi
hapo kuna changamoto inayohitaji kufuatiliwa.
5. Angalia pia kiasi cha dawa zilizoharibika au
kuisha muda wake wa matumizi.
Kama kituo kina dawa zilizoharibika au kuisha
muda wake wa matumizi ratibu zoezi la
kuzirudisha wilayani.
6. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa
uhakiki wa taarifa
Taarifa inaonyesha kuna
wagonjwa lakini hakuna dawa.
Wasiliana na kituo kwa haraka
kuthibitisha na kama ni kweli hatua
-
48
Hatua Cha kufanya Zingatia
za haraka za kupeleka dawa
zichukuliwe
Taarifa inaonyesha kuna dawa lakini
hakuna wagonjwa: Wasiliana na kituo
kuthibitisha na kama ni kweli angalia
uwezekano wa kuzirudisha wilayani ili
ziweze kutumika na vituo vingine. Kituo
kibakiwe na dawa inayotosheleza mahitaji
ya mwezi mmoja ya mgonjwa mmoja
katika kila hatua ya matibabu (Initiation na
continuation phase). Na kama dawa hizo
zitakaa sana chukua hatua kutambua
muda wake wa matumizi unaisha lini na
kama kuna hatari ya kuexpire ratibu zoezi
la kuzihamishia kituo kingine
zitakakotumika kabla ya kuexpire
C: Kukokotoa kiasi cha kugawa kituoni
7 Idadi ya wagonjwa: Jumlisha idadi ya
wagonjwa watakao kuwa wakitumia
dawa ya aina moja katika mwezi
unaofuata ule uliotolewa taarifa na
kuandika jumla yao kwenye safu C ya
fomu taarifa ya mwezi ya kituo mbele
ya dawa husika
Kwa wagonjwa wapya wa kifua kikuu
watakao kuwa kwenye miezi ya 1 na 2 ya
matibabu watakuwa wakitumia dawa ya
aina moja (RHZE) na watakaokuwa
kwenye miezi ya 3 hadi 6 ya matibabu
watakuwa wakitumia dawa aina moja (RH).
Wagonjwa wa retreatment walio mwezi wa
1, 2 na 3 wa matibabu wanatumia pia
RHZE. Hivyo jumla ya wagonjwa watakao
tumia RHZE= Jumla ya wagonjwa wapya
wakubwa watakaokuwa mwezi wa 1 na 2
wa matibabu kujumlisha idadi ya wagonjwa
wa retreatment watakaokuwa mwezi wa 1,
2 na wa 3 wa matibabu.
Jumla ya watakaotumia RH 150/75mg =
Jumla ya idadi ya wagonjwa wakubwa
-
49
Hatua Cha kufanya Zingatia
wapya kwenye miezi ya 3,4,5 na 6 ya
matibabu
Jumla ya wagonjwa watakaotumia RHE=
jumla ya idadi ya wagonjwa wa retreatment
watakaokuwa kwenye miezi ya 4 hadi 8 ya
matibabu
Jumla ya wagonjwa watakaotumia
Streptomycin na water for injection ni jumla
ya idadi ya wagonjwa wa retreatment
watakaokuwa miezi ya 1 na 2 ya matibabu.
Jumla ya wagonjwa watakaotumia MB
adult ni jumla ya wagonjwa watu wazima
watakaokuwa kuwa kwenye matibabu ya
MB kuanzia mwezi wa 1 hadi wa 12 wa
matibabu.
Jumla ya wagonjwa watakaotumia PB
adult ni jumla ya wagonjwa watu wazima
watakaokuwa kuwa kwenye matibabu ya
PB kuanzia mwezi wa 1 hadi wa 6 wa
matibabu.
Jumla ya wagonjwa watakaotumia RHZ ni
jumla ya wagonjwa watoto watakaokuwa
kuwa kwenye matibabu mwezi wa 1 na 2
wa matibabu.
Jumla ya wagonjwa watakaotumia
Ethambutol(100mg) ni jumla ya wagonjwa
watoto watakaokuwa kuwa kwenye
matibabu mwezi wa 1 na 2 wa matibabu
Jumla ya wagonjwa watakaotumia RH
60/30 ni jumla ya wagonjwa watoto
watakaokuwa kuwa kwenye matibabu
-
50
Hatua Cha kufanya Zingatia
mwezi wa 3 hadi wa 6
Jumla ya wagonjwa watakaotumia MB pd
ni jumla ya wagonjwa watoto watakaokuwa
kuwa kwenye matibabu ya MB ped kuanzia
mwezi wa 1 hadi wa 12
Jumla ya wagonjwa watakaotumia BP pd
ni jumla ya wagonjwa watoto watakaokuwa
kuwa kwenye matibabu ya PB ped kuanzia
mwezi wa 1 hadi wa 12
Jumla ya wagonjwa watakaotumia
Isoniazid 300mg ni jumla ya wagonjwa
wote watu wazima watakaokuwa kwenye
miezi yote ya IPT
Jumla ya wagonjwa watakaotumia
Isoniazid 100mg ni jumla ya wagonjwa
wote watoto