utungaji/uandishi - kiswahili 1...mwalimu nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni...

55
UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017 Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1 UTUNGAJI/UANDISHI Utungaji ni neno linalotokana na kitenzi “tunga”. Kitenzi hiki kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004:414) linamaanisha “toa mawazo kutoka ubongoni na kuyakusanya, kisha kuyadhihirisha kwa maandishi, kwa kusimulia, kwa kuyaimba au kwa muziki. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa, utungaji ni kutoa mawazo binafsi kutoka akilini mwa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali katika jamii, kisha kuyaweka wazi kwa njia ya mdomo au maandishi.Kile kilichotungwa na mtunzi kinaweza kudhihirishwa kwa mitindo mbalimbali, kama vile riwaya, mashairi, tamthiliya, insha na barua. Dhima ya Utungaji Utungaji huwezesha watu kutoa maelezo, mawazo au maoni kwa njia ya maandishi au mazungumzo. Utungaji huwezesha utumiaji wa lugha fasaha, sanifu na uwezo wa kujieleza kwa njia ya maandishi au mazungumzo. Utungaji huwezesha utumiaji wa mantiki, mpangilio mzuri wa mawazo, mtiririko na matumizi sahihi na fasaha ya lugha na kanuni za fasihi. Utungaji huwezesha kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maisha yetu ya kila siku. Kupitia njia ya utungaji, watu hupata taarifa kuhusu vitu mbalimbali vinavyozunguka maisha yao ya kila siku. Utungaji hutumika kuelimisha, kukosoa na hata kuonya. Maandishi au mazungumzo (masimulizi) yanayotokana na utungaji huweza kuakisi hali halisi ya maisha ya jamii, na hivyo ikawa ni kama kioo cha kujitazama na kujirekebisha. Utungaji, hususan unaotokana na kazi za fasihi hutumika kuburudisha jamii. Hadithi na tanzu nyingine za fasihi zinazotokana na utungaji huburudisha, huliwaza na kufurahisha jamii. Utungaji hutumika kukuza lugha kwa njia ya mazungumzo au maandishi. Mzungumzaji na msikilizaji hupata ufundi wa kujieleza zaidi kupitia

Upload: others

Post on 08-Nov-2020

36 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 1

UTUNGAJI/UANDISHI Utungaji ni neno linalotokana na kitenzi “tunga”. Kitenzi hiki kwa mujibu wa

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004:414) linamaanisha “toa mawazo kutoka

ubongoni na kuyakusanya, kisha kuyadhihirisha kwa maandishi, kwa kusimulia,

kwa kuyaimba au kwa muziki.

Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa, utungaji ni kutoa mawazo binafsi kutoka akilini

mwa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali katika jamii, kisha kuyaweka wazi kwa

njia ya mdomo au maandishi.Kile kilichotungwa na mtunzi kinaweza

kudhihirishwa kwa mitindo mbalimbali, kama vile riwaya, mashairi, tamthiliya,

insha na barua.

Dhima ya Utungaji

Utungaji huwezesha watu kutoa maelezo, mawazo au maoni kwa njia ya

maandishi au mazungumzo.

Utungaji huwezesha utumiaji wa lugha fasaha, sanifu na uwezo wa kujieleza

kwa njia ya maandishi au mazungumzo.

Utungaji huwezesha utumiaji wa mantiki, mpangilio mzuri wa mawazo,

mtiririko na matumizi sahihi na fasaha ya lugha na kanuni za fasihi.

Utungaji huwezesha kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu maisha yetu ya

kila siku. Kupitia njia ya utungaji, watu hupata taarifa kuhusu vitu

mbalimbali vinavyozunguka maisha yao ya kila siku.

Utungaji hutumika kuelimisha, kukosoa na hata kuonya. Maandishi au

mazungumzo (masimulizi) yanayotokana na utungaji huweza kuakisi hali

halisi ya maisha ya jamii, na hivyo ikawa ni kama kioo cha kujitazama na

kujirekebisha.

Utungaji, hususan unaotokana na kazi za fasihi hutumika kuburudisha

jamii. Hadithi na tanzu nyingine za fasihi zinazotokana na utungaji

huburudisha, huliwaza na kufurahisha jamii.

Utungaji hutumika kukuza lugha kwa njia ya mazungumzo au maandishi.

Mzungumzaji na msikilizaji hupata ufundi wa kujieleza zaidi kupitia

Page 2: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 2

utungaji, hali kadhalika mwandishi na msomaji hupata ufundi wa kujieleza

zaidi kupitia njia ya utungaji.

Kanuni za Utungaji bora

Utungaji bora ni lazima uzingatie kanuni zifuatazo:

Matumizi mazuri ya nyakati: mfano, wakati uliopo, ujao na uliopita au hali

timilifu.

Matumizi mazuri ya lugha fasaha (lugha inayoeleweka).

Mpangilio mzuri wa mawazo na mantiki, yaani kutochanganya mawazo,

kutorudiarudia mawazo au kutosahau mawazo.

Matumizi bora ya vituo na alama za uandishi.

Matumizi bora ya sarufi ya lugha inayohusika.

Utungaji bora hugawanyika katika sehemu kuu zinazobainisha muundo wa

kazi yenyewe mf. Insha hugawanyika sehemu nne ambazo ni: Kichwa cha

insha, Utangulizi, Kiini na Hitimisho

Utungaji bora huwa na mifano ya kutosha.

Uandishi wa Insha

Insha ni utungo wenye sentensi nyingi zilizopangwa katika aya, zenye

kuzungumzia mada moja. Kwa mfano, insha zinaweza kuwa zinazungumzia

mada zifuatazo: Umuhimu wa Chakula Bora, Tiba Kutokana na Vyakula;

Ujamaa ni Imani au Jamii Inakwenda Kombo.

Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa Insha.

Bila kujali aina ya insha inayoandikwa, yapo mambo kadhaa ya kuzingatia

wakatiwa kuandika insha. Mambo hayo ni pamoja na:

(a) Kubaini mada ya kuandikia insha na kuielewa vyema.

(b) Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki

(c) Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la insha. Kwa mfano, mtindo wa

masimulizi, unafaa kwa hadithi au insha zingine za kisanaa.

(d) Kutumia lugha fasaha na inayoeleweka

(e) Kufuata kanuni za uandishi. Kwa mfano, matumizi ya alama za uandishi,

aya, herufi kubwa na ndogo, n.k

(f) Kupanga insha katika muundo wake, yaani kichwa, utangulizi, kiini na

Page 3: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 3

hitimisho.

Muundo Wa Insha Insha hugawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:

Kichwa cha Insha

Kichwa cha insha huandikwa kwa herufi kubwa, katikati, juu ya

insha. Hakipaswi kuzidi maneno matano na hupigiwa mstari.

Utangulizi (Mwanzo)

Katika sehemu hii inampasa mwandishi atoe maelezo mafupi na

maana ya habari aliyopewa.

Kiini cha insha (Kati)

Inamlazimu mwandishi afafanue kwa mapana mada

anayoishughulikia huku akitoa mifano hai inayoendana na hali halisi.

Hitimisho (Mwisho)

Inampasa mwandishi kutoa mapendekezo (maoni) ya msingi au

kusisitiza kwa ufupi yale aliyoyaelezea katika habari yenyewe.

NB: Hitimisho sio ufupisho wa hoja zilizojadiliwa katika sehemu ya insha

yenyewe.

Aina za Insha Aina ya insha au jina la insha hujulikana kutokana na mawazo ya

mwandishi. Kuna aina nyingi za insha lakini tunaweza kuziweka aina hizo

katika makundi makuu mawili ya insha za hoja na insha za wasifu. Kila

kundi kati ya makundi haya mawili kuna insha za kisanaa na insha zisizo za

kisanaa.

Zingatia kielelezo kifuatacho

Insha za Kisanaa

Hoja

Insha zisizo za Kisanaa

Insha Insha za Kisanaa

Wasifu

Insha zisizo za Kisanaa

Page 4: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 4

Insha za kisanaa hutumia vipengele mbalimbali vya fasihi katika kuwasilisha

ujumbe - mfano nahau, methali, ,misemo au tamathali za semi huweza

kutumika. Insha zisizo za kisanaa hazitumii lugha ya kifasihi katika

kufikisha ujumbe.

Insha za wasifu huelezea sifa (uzuri au ubaya) za kitu, hali au mtu fulani.

Insha za hoja ni insha ambazo hutetea mawazo ya aina fulani na kupinga

mengine kwa uthibitisho uliodhahiri. Mfano wa insha za wasifu ni Uzuri wa

bahari ya Hindi, Fahari ya Mlima Kilimanjaro, n.k. mfano wa insha za hoja

ni: Ukimwi ni Ugonjwa Hatari, Uhuru wa Bendera, n.k.

Mfano wa Insha ya Wasifu

Atukuzwe Nyerere wa Tanzania

Nyerere wa Tanzania, kiongozi shujaa wa dunia – amepata kutukuka pande zote za

dunia. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani

Mara. Alisoma elimu ya msingi katika shule ya Mwisenge – mojawapo ya shule za

zamani sana hapa nchini. Alipata elimu ya sekondari huko Tabora. Alijiunga na

Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda kabla ya kwenda huko Uingereza

kusomea shahada ya M.A.

Baada ya uhuru toka Uingereza, Mwalimu Nyerere alishughulika sana na suala la

ukombozi wa Tanganyika na Afrika kwa ujumla. Alionesha jitihada za wazi

kupambana na mabeberu wa Kiingereza hadi uhuru wa Tanganyika ukapatikana

tarehe 9/12/1961. Tanganyika ikawa ya kwanza kupata uhuru wake ukilinganisha

na nchi zote za Afrika ya Mashariki na kati – sifa kuu kwa Nyerere wa

Tanganyika.

Nyerere alishirikiana na Karume kuziunganisha nchi hizo na kuzaa Tanzania – jina

lililotumika na kuheshimiwa kote ulimwenguni. Wakati Nyerere akichanganya

udongo wa Tanganyika na Zanzibar alitamka maneno ya hekima yafuatayo:

“Tumeamua kuziunganisha nchi zetu ili kuimarisha umoja wa Afrika. Naamini

kuwa maadui wetu watachukia na kuhuzunika kwa kitendo hiki cha kishujaa

Page 5: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 5

tulichokifanya, lakini daima hatutaogopa chochote. Muungano wetu utadumu

milele na milele. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika. Amina!”

Sifa ya pekee inayomtofautisha Mwalimu Nyerere unapomlinganisha na

wanafalsafa wengine duniani kama vile Karl Marx na Mao ni kwamba yeye

aliwapigania wanyonge wote kote ulimwenguni bila kujali ubaguzi wa rangi,

kabila, taifa au bara. Aliwatetea wanyonge wa Afrika. Aliwapigania wanyonge wa

Ulaya na Mashariki. Aliwapigania wanyonge wa bara la Asia. Hali kadhalika

aliwapigania na kuwatetea wanyonge wa bara la Amerika ya Kusini. Hivyo ni sifa

ya pekee inayofaa kumtofautisha na wanafalsafa wengine waliomtangulia.

Nyerere atatukuzwa daima kwa ushujaa wake. Alikuwa si kiongozi wa

kujikombakomba kwa mataifa mengine ya kibeberu. Alipotishiwa au kuwekewa

vikwazo/vitisho, alivunja mara moja uhusiano wa kidiplomasia na taifa

linalohusika. Kwa mfano mwaka 1965 alivunja uhusiano wa kidiplomasia na nchi

ya Uingereza baada ya nchi hiyo kuitangaza nchi ya Zimbabwe kama koloni lake

la kudumu la Walowezi. Kitendo hiki kilimpatia sifa na heshima kubwa hapa

Afrika na duniani kote – kwa wapenda amani.

Ingawa ni vigumu kuzitaja sifa zake mpaka mwisho, lakini sifa ya kupiga makelele

katika majukwaa ya kimataifa haitaweza kusahaulika. Hakuwa msomi mkimya

kama wasomi wa enzi hizi. Alitumia elimu yake ipasavyo kuitetea falsafa yake ya

Haki na Usawa kwa Binadamu Wote katika majukwaa ya kimataifa.

Wananchi wa Uganda daima humkumbuka na kumtukuza kwa jinsi alivyotumia

nguvu za kijeshi kuung‟oa utawala wa kidikteta wa Nduli Idd Amini Dada.

Wakikumbuka mateso waliyoyapata enzi za utawala huo, humtukuza na kumuenzi

Nyerere usiku na mchana.

Nyerere hataweza kusahaulika kwa jinsi alivyopinga kitendo cha viongozi

wachache wenye hila kuendelea kung‟ang‟ania kwenye madaraka. Alikuwa

kiongozi wa kwanza hapa Afrika na pengine duniani kote kung‟atuka kwenye kiti

cha Urais. Alifanya hivyo kwa hiyari ili kutoa nafasi kwa wananchi wengine

washike wadhifa huu nyeti hapa nchini kwetu.

Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa

letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa hekima na

Page 6: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 6

busara. Kinywa chake daima kilinena maneno ya hekima na busara. Fikra zake

zitadumu milele kwenye vichwa vya wakulima, wasomi, wanafalsafa, mapadri,

masheikh, wachungaji, watawa na hata kwenye bongo za waovu wa Tanzania

daima watamkumbuka.

Kifo cha Mwalimu Nyerere kimeleta pengo kubwa kwa jamii yote ya wapenda

amani kote ulimwenguni. Ingekuwa mbegu ya mmea tungeipanda sote tuendelee

kuhekimika kutokana na hekima na busara zake.

Kifo cha Mwalimu Nyerere ni kama mwindaji asiye na silaha kwenye mwitu wenye

wanyama wakali kama fisi, simba, ngiri, tembo, nyoka, nyati, n.k. Je, mwindaji

atafanya nini?

Daima sifa na hekima za Mwalimu Nyerere zitukuzwe Tanzania, Afrika na

ulimwenguni kote.

Mfano wa insha ya hoja

Kijana wa leo nina balaa!!

Kilio, kilio, kilio kwa kijana wa leo, Afrika! Wakati vijana wengine wanapoombwa

kujiunga na jeshi ili kujenga na kulinda nchi yao, siyo kwangu. Kwangu

naburutwa msituni, kujiunga na jeshi kuendeleza vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Napigana na ndugu zangu ndani ya taifa moja ili matumbo machache yafaidi

almasi, dhahabu, mafuta na maliasili nyingine. Naingizwa katika vita isiyo na

maana yoyote kwangu.

Nikitaka kutafuta elimu, hakuna madarasa. Upepo umeezua paa la nyasi la shule

yetu! Nikibahatika kupata kaelimu kadogo; chini ya mti, nazuiwa kufikiri zaidi.

Naambiwa kuwa, Afrika hakuna kufikiri! Mtu mweusi hana fikra ila mtu mweupe

ndiye mwenye fikra. Natakiwa nifuate fikra zake!

Nikitaka ajira, naambiwa uzoefu miaka mitano au kumi na zaidi. Uzoefu nitaupata

wapi? Nikitamani kujiajiri mazingira hayaniruhusu: Umasikini, umasikini tena

umasikini umenikumbatia!

Nikijiunga na siasa, wimbo maarufu kote ulimwenguni ni demokrasia. Demokrasia

ina mizengwe, umajimbo, ukabila, udini, ubabe, rushwa, ubabaishaji, utapeli na

Page 7: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 7

kushindana bila kukubali kushindwa. Siasa barani kwetu ni kiini macho na

matokeo yake ni „demoghasia‟ isababishayo vifo. Ubinafsi umejaa! Kujipitishia

marupurupu kibao! Ubaguzi! Majigambo! Dharau…..!

Nikitaka kusema, naambiwa mjinga, Nikidai haki, naambiwa madai yangu ni ya

kijinga. Nalazimishwa kuandika barua ya kuomba msamaha na kuahidi kuwa

sitadai haki tena! Nalazimishwa kuwa bubu. Kijana msomi nanyimwa uhuru wa

kutoa mawazo yangu mbele ya jumuiya yangu. Kijana msomi nafungwa mdomo.

Kijana msomi kukaa na kunyamaza kimya ni usaliti. Usaliti kwa jamii ya walipa

kodi ambao pesa zao zimenisomesha hadi kuitwa msomi. Kijana msomi, kutofikiri

ni dhambi nyekundu pyuuu!- isiyosameheka. Msomi kutofikiri ni kifo cha kifikra

kwangu mimi kijana wa Kiafrika.

Chochote ninachotaka kufanya kinanikatisha tamaa. Nikiwa „deiwaka‟ mpiga

debe, kila siku nitaamkia korokoroni! Nikitaka kujiburudisha na gongo au viroba -

ni kifo cha ajabu. Nikibugia unga – kwangu ni kifo cha mende wekundu!

Nikijiingiza kwenye ukahaba, natozwa kodi ya maendeleo! Nikitaka kuwa

“changudoa”, UKIMWI unaniwinda kama mamba awindavyo viumbe baharini!

Sasa nifanye nini? Balaa kubwa kwangu!

Nikiamua kuokoka, wokovu hauonekani. Nimebaki njia panda. Mchungaji

amekuwa mwongo, katu hasemi ukweli. Ananilaghai kuwa wokovu upo karibu

kuingia badala ya kuniambia kweli wokovu umekwishatoweka. Naambiwa kuwa

nijiwekee hazina mbinguni ambako kutu na wadudu hawataharibu mali

yangu…Huu ni utapeli.

Ingekuwa vizuri kama ningeelezwa wazi jiwekee akiba tumboni mwa sheikh au

tumboni mwa mchungaji au tumboni mwa padre! Naambiwa kuwa toeni

ulichonacho utabarikiwa badala ya kuambiwa kuwa kitayabariki matumbo ya

wachache!

Nakumbuka wakati mama yangu alipokuwa mwalimu katika shule ya msingi ya

Mabonde Kuinama, aliniambia kwamba, urithi wa utamaduni wetu ni mila na

desturi za Afrika. Lakini siku hizi sivyo. Siku hizi naambiwa kuwa urithi wa kizazi

kipya ni bia aina ya “Safari Larger”.

Page 8: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 8

Kijana wa sasa naangalia wizi wanaofanyiwa watu maskini lakini sisemi chochote.

Najinyamazia kimya. Wizi umo makanisani, misikitini, Ikulu, mahakamani na hata

bungeni. Lengo ni kuwanyanyasa, kuwadhulumu, kuwaonea, kuwanyonya na

kuwadhalilisha wanyonge. Hakika kunyamaza kwangu ni usaliti. Nimeitambua

nafasi yangu. Naahidi kupambana hadi kufa na kupona.

Uandishi wa barua na kadi za mialiko

Kuna aina mbalimbali za barua. Aina hizo hugawanywa katika makundi

makuu mawili ambayo ni Barua za kirafiki/kindugu na Barua rasmi.

(a) Barua za Kirafiki/Kindugu

Hizi ni barua zinazoandikwa kwenda kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa

madhumuni mbalimbali kama vile:

- Kusalimiana

- Kujulishana maisha yetu ya kila siku

- Kuomba msaada au kutoa shukrani kwa kutimiziwa maombi yetu.

- Kutoa hongera, rambirambi, pongezi, n.k.

Sehemu za Barua za Kirafiki/Kindugu

Anuani ya Mwandishi

Huandikwa kwenye pembe ya kulia ya karatasi. Anuani hii ndiyo

hutumiwa na mwandikiwa wakati wa kujibu barua aliyoipokea na pia

hutambulisha maskani ya mwandishi wa barua kwa wakati huo. Kwa

hiyo, ni wajibu wa mwandishi kuandika anuani yake vizuri. Ni lazima

iandikwe waziwazi.

Tarehe

Hii huandikwa mara baada ya anuani ya mwandishi. Huandikwa ili

kumjulisha mwandikiwa barua imeandikwa lini na kama imefika kwa

wakati au imechelewa. Zipo njia mbalimbali za kuandika tarehe, nazo ni:

- 20.9.2017

- 20/9/2017

- 20-9-2017

- 20 Septemba, 2017

- Septemba 20, 2017

Page 9: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 9

Mwanzo wa barua

Barua za kirafiki/kindugu huanza kama ifuatavyo:

- Baba mpendwa,

- Mpendwa baba,

- Mwanangu mpendwa,

- Mama mpenzi, n.k.

Barua yenyewe

Hii ni sehemu muhimu sana. Sehemu hii ndiyo inayomfanya

mwandikiwa aelewe kusudi la mwandishi. Sehemu hii iandikwe vizuri ili

barua ieleweke kwa urahisi.

Mwisho wa barua

Mwisho wa barua ni sehemu inayostahili kuandikwa vizuri. Njia

zifuatazo ni baadhi ya zile zitumikazo kumalizia barua ya kindugu.

- Mwanao akupendaye.

- Wako wa moyoni.

- Rafiki yako akupendaye.

- Wako akupendaye.

- Wasalaam, baba yako, n.k.

Jina la Mwandishi

Ni vizuri kuandika jina lako mwishoni mwa barua ili yule

unayempelekea afahamu barua imetoka kwa nani.

Page 10: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 10

Mfano wa barua ya kirafiki

Shule ya Sekondari Mbezi Beach,

S.L.P 60213,

Dar Es Salaam.

03/07/2017.

Mpendwa,

Salaam sana. Natumai u mzima pamoja na jamaa na marafiki wa hapo

nyumbani. Nami ni mzima na ninaendelea na masomo yangu vizuri hapa

shuleni. Napenda kukujulisha kuwa maendeleo yangu kimasomo hapa

shuleni ni mazuri sana. Katika mtihani wa kumaliza mwaka wa pili

nimeshika nafasi ya pili kati ya wanafunzi 195 wa kidato cha tano.

Nimeamua kusomea mchepuo wa biashara ili hatimaye niwe mchumi wa

nchi yetu hivyo naomba tuzidi kuombeana heri.

Pamoja na mafanikio hayo yote, kuna tatizo kubwa sana ambalo linazidi

kuniandama hapa shuleni. Tatizo hili linanikosesha kabisa raha, kila

wakati huwa ninahuzunika. Tatizo hili huwa ni la umasikini. Sina hata

shilingi tano ya kununulia kipande cha muhogo. Hivyo, naomba uuze

yule jogoo mkubwa unitumie pesa haraka iwezekanavyo.

Wasalimie wote wanaonifahamu hapo kijijini. Msalimie sana shangazi

wangu Lilian Joackim.

Wako akupendaye,

Haidari Hamisi.

(b) Barua Rasmi

Kwa kawaida barua rasmi huandikwa kwa makusudi mbalimbali kama

vile, kutoa taarifa za tukio fulani, kuomba kazi, kuagiza vifaa au vitu,

kumwalika kiongozi katika shughuli maalumu, kutoa taarifa ya

kushindwa kufika mkutanoni, n.k.

Barua rasmi zipo za aina nyingi, lakini zinaweza kugawanywa katika

makundi matatu makubwa yafuatayo:

Page 11: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 11

- Barua za kuomba kazi

- Barua za kutoa taarifa

- Barua za kuagiza au kupokea bidhaa/vitu.

Sehemu za barua rasmi

(i) Anuani ya mwandishi

Anuani hii huandikwa pembe ya juu kulia ili kutambulisha maskani ya

mwandishi na pia hutumiwa na mwandikiwa wakati wa kuijibu barua husika

inapobidi.

(ii) Tarehe

Huandikwa chini ya anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa kama

barua hiyo imefika mapema au imechelewa.

(iii) Kumbukumbu namba

Barua rasmi huwa na kumbukumbu namba. Huu ni utambulisho maalumu

wa barua husika. Kumbukumbu namba aghalabu huwa ni kifupi cha jina la

taasisi inakotoka barua hiyo, kule inakokwenda, hiyo ni barua ya ngapi na

mwaka husika. Mf: Mbss/crdb/02/17

(iv) Anuani ya mwandikiwa

Anuani hii hutanguliwa na cheo cha mwandikiwa na huwekwa upande wa

kushoto chini ya kumbukumbu namba. Nafasi ya mstari mmoja au zaidi

huweza kurukwa baina ya kumbukumbu namba na anuani ya mwandikiwa.

(v) Mwanzo wa barua

Sehemu hii huandikwa chini ya anuani ya mwandikiwa. Ni heshima kutaja

cheo cha mwandikiwa mwanzoni mwa barua ya namna hii, kwa mfano

Ndugu Katibu, Ndugu Ofisa Mifugo, n.k.

(vi) Kichwa cha barua

Kichwa cha barua hutaja kwa ufupi jambo linalohusu barua hiyo. Kichwa

cha barua huandikwa waziwazi katikati ya barua mara baada ya mwanzo wa

barua. Ni muhimu kiwe kifupi na chenye kueleweka waziwazi. Hufaa zaidi

Page 12: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 12

kikiandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Hakipaswi kuzidi

maneno matano.

(vii) Barua yenyewe

Sehemu hii huandikwa mambo yote muhimu kuhusu barua yenyewe. Barua

yenyewe iwe fupi na yenye taarifa za lazima tu. Uanzaji wa barua yenyewe

umrejeshe msomaji kwenye mada ili kufupisha maelezo mengi kama vile

kwa kusema:

- Mada tajwa hapo juu inahusika

- Rejea barua yako ya tarehe…..yenye Kumb. Na….

- Husiana na mada tajwa hapo juu, n.k.

(viii) Mwisho wa barua

Mwisho wa barua huwa ni tamko la heshima la kumalizia barua. Mara

nyingi mwisho unaotumika katika barua rasmi ni kama vile:

- Wako mtiifu,

- Wako katika ujenzi wa taifa,

- Wako katika kazi, n.k.

(ix) Saini na jina la mwandishi

Mwisho wa barua mwandishi hupaswa kutia saini na jina lake kama

utambulisho wake juu ya kilichoandikwa. Saini hupaswa kutiwa kwa

mkono.

(x) Cheo cha mwandishi

Baada ya jina mwandishi hupaswa kuandika cheo chake. Cheo kinaweza

kuwa:

- Mwanakijiji

- Muombaji

- Mwalimu Mkuu

- Afisa Mtendaji, n.k

Page 13: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 13

Aina za Barua Rasmi

1. Barua ya Kuomba Kazi

Barua ya kuomba kazi inahitaji uangalifu sana katika sehemu ya barua

yenyewe. Barua hii inatakiwa iandikwe kwa umakini na ujuzi mwingi.

Katika barua hii kuna mambo makuu manne ambayo ni: kutaja kazi

unayoomba, jinsi ulivyopata taarifa, elimu, ujuzi na uzoefu, maelezo binafsi

na wadhamini.

Mfano wa barua ya kuomba kazi:

Kijiji cha Mto wa Mbu,

S.L.P 4507,

Arusha.

04/7/2017

Meneja wa Kiwanda,

Kiwanda cha Kusindika Matunda,

S.L.P 0717,

Iringa.

Ndugu,

YAH : OMBI LA KAZI YA UKARANI

Husika na kichwa tajwa hapo juu. Ninayo heshima kuomba kazi ya ukarani katika

kiwanda chako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la “Sanifu” Uk. 3 la tarehe

20/6/2017.

Mimi nilisoma katika kituo cha Elimu ya Watu Wazima huko Mufindi. Baadaye

nilijiunga na masomo kwa njia ya posta na kuhitimu kwa ufaulu wa masomo ya

Kiswahili, Siasa na Kiingereza.

Nina umri wa miaka 45, nimeoa na nina watoto wanne. Mimi ni mwanakijiji wa

kijiji cha Magadini. Napendelea michezo na kazi za mikono. Ninaweza kusoma na

kuandika vizuri na ninayo hati nzuri.

Page 14: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 14

Mwalimu Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Mufindi na msimamizi

wa masomo kwa njia ya posta anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya uwezo wangu.

Nitashukuru sana iwapo ombi langu litafikiriwa na kupokelewa vema.

Wako mtiifu,

(Saini)

Matatizo Hayaishi

Mwombaji

Barua ya kupitia kwa:

Iwapo barua itapaswa kupitishwa na mtu zaidi ya mmoja kutokana na mamlaka za

kiutawala na utambuzi mwandishi atapaswa kuandika anuani za wale wanaopaswa

kuiona barua hiyo kwa kuanza na anuani ya yule atakayeiona mwisho.

Mfano:

Kijiji cha Mto wa Mbu,

S.L.P 4507,

Arusha.

04/7/2017

Meneja wa Kiwanda,

Kiwanda cha Kusindika Matunda,

S.L.P 0717,

Iringa.

K.K

Afisa Rasilimali Watu,

Kiwanda cha Kusindika Matunda,

S.L.P 0717

Iringa Ndugu,

YAH : OMBI LA KAZI YA UKARANI

Page 15: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 15

Husika na kichwa tajwa hapo juu. Ninayo heshima kuomba kazi ya ukarani katika kiwanda

chako kama ilivyotangazwa kupitia gazeti la “Sanifu” Uk. 3 la tarehe 20/6/2017.

Mimi nilisoma katika kituo cha Elimu ya Watu Wazima huko Mufindi. Baadaye nilijiunga na

masomo kwa njia ya posta na kuhitimu kwa ufaulu wa masomo ya Kiswahili, Siasa na

Kiingereza.

Nina umri wa miaka 45, nimeoa na nina watoto wanne. Mimi ni mwanakijiji wa kijiji cha

Magadini. Napendelea michezo na kazi za mikono. Ninaweza kusoma na kuandika vizuri na

ninayo hati nzuri.

Mwalimu Mkuu wa Kituo cha Elimu ya Watu Wazima cha Mufindi na msimamizi wa masomo

kwa njia ya posta anaweza kutoa taarifa zaidi juu ya uwezo wangu.

Nitashukuru sana iwapo ombi langu litafikiriwa na kupokelewa vema.

Wako mtiifu,

(Saini)

Matatizo Hayaishi

Mwombaji

2. Barua ya kutoa taarifa

Barua hizi huandikwa kwa lengo la kutoa taarifa juu ya jambo, tukio au mtu.

Taarifa huweza kutolewa kwenye taasisi fulani kama kituo cha polisi au ofisi

yoyote ya umma.

Mfano wa barua ya kutoa taarifa

Kijiji cha Jangwani,

S.L.P 1045,

Mto wa Mbu

10/7/2017.

Bwananyama wa Wilaya,

Wilaya ya Monduli,

S.L.P 1045,

Arusha.

Page 16: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 16

Ndugu,

YAH: TATIZO LA SIMBA KIJIJINI

Husika na mada tajwa hapo juu. Ninasikitika kukutaarifu kuwa, hapa kijijini kwetu

amezuka simba anayewinda watu. Ni simba jike na watoto watatu na ameonekana

mara tatu hapa kijijini.

Simba huyo huingia hapa kijijini kutoka katika msitu wa hifadhi ya taifa ambapo si

ruhusa kuweka mitego.

Nashukuru ikiwa utatushauri haraka jambo la kufanya mara upatapo barua hii.

Wako katika kazi,

(Saini)

Rogathe Kimario

Mtendaji wa Kijiji

3. Barua ya Mwaliko

Barua za aina hii huandikwa kwa viongozi mbalimbali kwa lengo la

kuwaalika katika shughuli mbalimbali kama mahafali, uzinduzi, ufunguzi,

n.k

Mfano wa barua ya mwaliko

Shule ya Sekondari Manyara,

S.L.P 46,

Arusha.

15/7/2017.

Mkuu wa Wilaya,

Wilaya ya Monduli,

S.L.P 12,

Arusha.

Ndugu,

YAH: MWALIKO WA KUKABIDHI VYETI

Page 17: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 17

Husika na kichwa cha barua hapo juu. Ninakualika uwe mgeni rasmi katika

mahafali ya kidato cha sita yatakayofanyika hapa shuleni siku ya tarehe 20/7/2017

kuanzia saa saba za mchana hadi saa 12 jioni. Pia utatunuku vyeti vya kuhitimu

kwa wahitimu 600 katika sherehe hiyo.

Nitashukuru sana iwapo ombi letu litakubaliwa.

Wako katika ujenzi wa taifa,

(Saini)

Gambuzi Peter

Mkuu wa Shule

4. Barua ya kuagiza/kupokea bidhaa (Barua za kibiashara)

Barua hizi huandikwa kwa lengo la kuagiza bidhaa au kukiri kupokea bidhaa

zilizotumwa.

Mfano wa barua ya kuagiza bidhaa

Kijiji cha Mkwawa,

S.L.P 20,

Iringa.

12/7/2017

Meneja wa Kiwanda,

Kiwanda cha Zana za Kilimo Mbeya,

S.L.P 44,

Mbeya.

Ndugu,

YAH: AGIZO LA ZANA ZA KILIMO

Husika na kichwa cha barua hapo juu. Tunaomba ututumie zana za kilimo, kwani

tunakusudia kuanzisha mradi wa kilimo cha mahindi hapa kijijini. Zana

tunazohitaji kwa ajili ya mradi huu ni :

Page 18: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 18

- Majembe – 6

- Mapanga – 10

- Mashoka – 6

- Slesha – 20

- Toroli – 2

Tunaomba utume kwa basi la Simama Trans linalofanya safari zake kila siku hapa

Iringa. Kabla ya kutuma, tuandikie kutuarifu tarehe utakayotuma. Malipo

yatalipwa kwa hundi.

Wako katika ujenzi wa taifa,

(Saini)

Nyanya Kitunguu

Mratibu wa Mradi

5. Kadi ya Mwaliko

Kadi ya mwaliko huandikwa kwenye karatasi maalumu inayoitwa kadi. Kadi

ya mwaliko huwa na mambo yafuatayo:

- Jina la mwalikaji na anuani

- Jina la mwalikwa

- Lengo la mwaliko

- Mahali pa tukio

- Muda wa kukutana

- Mawasiliano kwa ajili ya majibu

Familia ya Bw. & Bibi Majaliwa Maisha wa S.L.P 007 Dar es Salaam, wanayofuraha

kukuali/kuwaalika Bw. & Bibi./ Bw./ Bi./ Prof./ Dkt./ Mch./ Sheikh./……………. kwenye

mahafali ya kijana wao mpendwa ………….yatakayofanyika shuleni kwao siku ya tarehe

10/7/2017 na baadaye kwenye tafrija fupi nyumbani kwao kuanzia saa 8:00 mchana hadi

saa 12:00 jioni.

Kufika kwako ndiyo mafanikio ya tafrija yetu.

Majibu kwa wasiofika

SIMU: 0717104507

Page 19: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 19

ZINGATIA: Kadi ya mwaliko huweza kujibiwa kwa kutumia muundo wa barua ya

kirafiki au barua rasmi.

6. Barua ya gazetini

Barua za magazetini ni zile zinazoandikwa na wasomaji wa magazeti fulani

fulani kwa mhariri. Barua hizi huwa na madhumuni anuai ambayo huwa na

nia mbalimbali kama vile:

- Kutoa pongezi

- Kufichua maovu

- Kutoa maoni na mapendekezo

- Kupinga madai ya barua ya awali iliyoandikwa gazetini humo

kuhusiana na mada fulani

- Kuunga mkono madai ya barua fulani iliyoandikwa gazetini

- Kulalamikia hali fulani, kwa mfano usalama wa nchi

- Kuwafahamisha wasomaji kuhusu jambo fulani, kwa mfano

umuhimu wa kompyuta katika shule za sekondari, n.k

Muundo wa barua ya gazetini

- Kichwa cha barua - huandikwa mwanzoni kabisa na huandikwa kwa

herufi kubwa na kupigiwa mstari au wino mzito

- Mwanzo wa barua – mf: ndugu mhariri

- Barua yenyewe – huwa na ufafanuzi wa hoja zenye ukweli na

ushahidi wa kutosha.

- Mwisho wa barua – mara nyingi mwisho wa barua za magazetini

huwa na ombi, maoni au mapendekezo.

- Jina la mwandishi na anuaini – huandikwa chini, upande wa

kushoto.

- Tarehe – huandikwa baada ya jina na anuani (japo si lazima)

Page 20: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 20

Mfano wa barua ya gazetini:

Nakerwa na Uchafuzi Dar es Salaam

Mhariri,

Miongoni mwa mambo yanayonikera katika Jiji la Dar es Salaam ni uchafu

uliokithiri huku viongozi wake wakionesha kushindwa kabisa kukabiliana na hali

hiyo.

Ndugu mhariri, nimekuwa nikitembelea maeneo ya Kinondoni shamba, Kariakoo,

Tandale, Manzese, Buguruni pamoja na Vingunguti kutokana na shughuli zangu za

kutembeza bidhaa lakini maeneo haya kwa kweli yanatia mashaka.

Kumekuwepo na maji machafu yanayotiririka kutoka kwenye vyoo pamoja na

lundo la takataka barabarani. Jambo hili kwa kweli inaharibu taswira ya Jiji hili.

Kwa bahati mbaya viongozi wa mitaa pamoja na wajumbe wamekuwa

hawawajibiki katika kuhakikisha mazingira haya yanaboreshwa na kuwa masafi.

Matokeo yake kumekuwepo na ongezeko la watu wanaopata maradhi ya

kuambukiza ikiwa ni pamoja na kuumwa tumbo, ukurutu na kuenea kwa harufu

mbaya.

Nakumbusha mamlaka husika kwamba, kukosekana kwa afya njema ni miongoni

mwa sababu ya kushindwa kuzalisha na hivyo kudhoofisha uchumi wa nchi.

Viongozi wa serikali za mitaa pamoja na wasaidizi wao ambao ni wajumbe

wanapaswa kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.

Kwa kufanya hivyo wanaweza kuaminika kwa wananchi na hivyo kuheshimiwa

kama viongozi na hiyo ndiyo kazi ya uongozi inavyopaswa kuwa.

Ni wajibu si kwa viongozi serikalini pekee lakini hata kwa wananchi ili

kuhakikisha mazingira wanayoishi yanakuwa safi jambo litakalowezesha kusaidia

kuepuka maradhi na mambo mengi yanayotokana na uchafu.

Pamoja na hivyo, halmashauri zinapaswa kutunga sheria ndogo ndogo zinazolenga

kutunza usafi wa mazingira na kuzisimamia.

Page 21: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 21

Rashi S. Mbonde

[email protected]

Ilala, Dar es Salaam

(Kutoka gazeti la MAWIO, Alhamisi, Agosti 6-12, 2015 Uk.14)

7. Simu ya Maandishi

Simu za maandishi ni mojawapo ya mawasiliano ya haraka baina ya watu.

Waandikiwa hupata taarifa haraka iwezekanavyo ukilinganisha na barua za

kawaida. Taarifa ya simu ni fupi lakini huwa na ujumbe ulio wazi na

unaoeleweka. Ufupi wa simu za maandishi unatokana na gharama kubwa za

malipo kwa sababu gharama za simu hulipwa kulingana na idadi ya maneno

yanayoandikwa.

Barua za simu zipo za aina mbalimbali kama vile:

Barua za simu ya kawaida

Barua za simu ya haraka

Barua za simu ya kupeleka fedha

Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa barua za simu

(i) Anuani ya anayepelekewa taarifa

Anuani ya simu ya maandishi lazima iwe kamili na ya waziwazi ili kuiwezesha

barua hiyo kupelekwa haraka iwezekanavyo bila ya matatizo. Anuani ya mji ni

lazima iwe na jina la mtaa na kama inawezekana namba ya nyumba. Vilevile jina

la ofisi ya simu iliyo karibu na mahali simu hiyo inakopelekwa.

(ii) Taarifa au ujumbe wenyewe

Hapa ndipo penye kiini cha simu. Habari ielezwe kwa ufupi sana lakini ieleweke

vizuri. Epuka mambo yasiyo ya lazima.

(iii) Jina la mwandishi au mtuma simu

Jina la mwandishi huandikwa kwa ukamilifu wake ili kumjulisha mwandikiwa

barua imetoka kwa nani.

Page 22: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 22

Kumbuka: Ni muhimu kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha

usomaji. Barua ya simu hutumika hasa kwa ajili ya mambo ya haraka sana na

muhimu. Simu huandikwa kwenye karatasi maalumu. Karatasi hizo hupatikana

posta.

Hakuna barua ya simu ya aina yoyote ambayo itasafirishwa bila ya kulipiwa

gharama ya kuipeleka simu hiyo. Hivyo, barua ya simu huwa fupi ili kuepuka

gharama za utumaji.

Mfano wa simu ya maandishi

8. Uandishi wa Matangazo

Uandishi wa matangazo ni shughuli ya kampuni, serikali au mtu binafsi ya

kusambaza habari. Kampuni huweza kutangaza bidhaa zake, nafasi za kazi,

mabadiliko fulani katika kampuni au shughuli muhimu katika kampuni.

Matangazo ni habari zinazowekwa wazi kwa nia ya kupitishwa kwa hadhira

fulani. Matangazo huhusu jambo fulani kama vile mkutano, mashindano,

harambee, n.k.

Vyombo vya habari kama vile magazeti, televisheni hutumiwa. Matangazo

pia huweza kuwekwa kwenye mabango. Matangazo huweza kuwa na habari

za kutoa onyo au kufahamisha. Kwa mfano kampuni huweza kuwatangazia

wanunuzi wake kuhusu hatari ya kununua bidhaa zisizo na chapa ya

kampuni hiyo. Tahadhari, onyo, ilani na notisi ni aina za matangazo

yanayotekeleza majukumu mbalimbali.

JUMA ALI SLP 20 MAKUYUNI

FIKA HARAKA BABA MAHUTUTI

FARIDA BAKARI

Alama za uandishi hazitumiki isipokuwa kama nazo ni sehemu ya neno.

Page 23: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 23

Sifa za matangazo

Matangazo hudhamiriwa kuwanasa wasomaji/wasikilizaji. Kwa hiyo,

mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:

Yawe mafupi – matangazo marefu huchosha na kusahaulika haraka.

Yatumie lugha yenye mvuto na sahihi inayoeleweka.

Yabandikwe sehemu za wazi ili watu wayasome kwa urahisi

Kwa kawaida huandikwa kwa herufi kubwa au wino mzito unaoweza

kuvuta makini ya watu.

Huweza kuwa na picha ili kuongeza mvuto.

Matangazo huweza kuwa ya aina mbalimbali kulingana na majukumu yake.

Zifuatazo ni baadhi ya aina za matangazo:

Matangazo ya biashara

Matangazo ya tahadhari

Matangazo ya taarifa za habari

Shughuli za kampuni

Shughuli za serikali

Kuenea kwa magonjwa, n.k

Mfano:

KAMPUNI YA KAMBI YA UUZAJI WA MASHAMBA

MASHAMBA YANAUZWA BEI NAFUU!! SHILINGI 200,000

KWA EKARI MOJA! SEHEMU CHACHE ZIMESALIA

NAMBA YA SIMU : 0717104507

CHAKUBANGA

DHIMA YA MATANGAZO KATIKA JAMII

(a) Kutangaza bidhaa mbalimbali ili kukuza soko la bidhaa hizo.

(b) Kutangaza ni njia mojawapo ya kuwasiliana na njia hii inaashiria ustaarabu wa

Page 24: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 24

kupeana taarifa mapema kabla ya tukio linalokusudiwa kutekelezwa siku za

usoni.

(c) Kuelimisha jamii, matangazo hutumika kama vitanabaishi vyenye kutoa

tahadhari, maarifa, ujuzi na stadi mbalimbali. Tumepata kusikia na kusoma

matangazo yanayohusu UKIMWI, malaria, wizi wa nyaya za simu na umeme.

Hii ni mifano ya matangazo ambayo dhima kubwa ni kuelimisha jamii juu ya

hayo yaliyotajwa.

(d) Kutangaza husaidia kuboresha shughuli za kiuchumi kama vile kufahamisha

jamii juu ya bidhaa mpya zilizotoka, huduma mbalimba zinazotolewa, mahali

wanapoweza kupata bidhaa au huduma hizo na mengineyo mengi yanayohusu

masoko na ongezeko la ziada kutokana na biashara. Kwa ujumla, lengo la

kutangaza ni, kushawishi, kuburudisha, kuonya, kutoa taarifa, kuuza bidhaa au

kutoa huduma, n.k

Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa matangazo

(a) Kichwa cha habari, kiandikwe kwa herufi kubwa

(b) Kutaja aina ya biashara (matangazo ya biashara)

(c) Kutaja aina ya bidhaa (matangazo ya biashara)

(d) Kutaja mahali inapopatikana hiyo bidhaa au huduma

(e) Kutaja njia za mawasiliano.

Uandishi wa matangazo ya biashara magazetini

Tangazo linapaswa kuwa na mambo yafuatayo:

(a) Kichwa cha tangazo ambacho huandikwa kwa herufi kubwa

(b) Kutaja aina ya biashara inayotangazwa

(c) Kutaja aina ya bidhaa unazouza na bei zake

Page 25: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 25

(d) Kutaja mahali inapotolewa huduma husika

- mji

- mtaa

- kijiji

- kata, n.k

(e) Kutaja njia za mawasiliano

- kwa barua

- kwa simu

- kwa nukushi

- kwa wavuti, n.k

Mfano

9. Uandishi wa Hotuba

Hotuba ni maelezo ambayo hutolewa na mtu mbele ya watu. Hutolewa kwa

madhumuni maalumu. Kwa mfano, hotuba inaweza kutolewa kwa madhumuni

ya kuhimiza kazi, kufanya kampeni fulani au kutoa taarifa fulani kwa watu.

Page 26: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 26

Sifa za hotuba

Ukweli wa jambo linaloelezwa

Ufasaha wa lugha

Nidhamu ya mzungumzaji mbele ya watu

Mantiki nzuri

Sauti ya kusikika

Aina za hotuba

Mahubiri: hizi ni hotuba za mafundisho ya kidini, hutolewa kanisani,

msikitini au kwa njia ya redio na televisheni.

Hotuba za kisiasa na Kiserikali: hizi ni hotuba za matangazo ya taarifa za

kiserikali na chama, za kisiasa, kuhimiza na kualika watu kutenda jambo

fulani, n.k

Mihadhara au masomo ya darasani: hizi ni hotuba au mafundisho ya

mwalimu shuleni hasa anapofundisha kundi kubwa la wanafunzi na hasa

wanafunzi wa vyuo vikuu.

Muundo wa hotuba

Muundo wa hotuba huwa na mwanzo, utangulizi, kati na mwisho.

Mfano:

Mwanzo – Mwanzo wa hotuba huwa na salamu.

Mzungumzaji: - Vijana safiiii!

Wasikilizaji: - Safiii!

Mzungumzaji: - Elimu juuuu!

Wasikilizaji : - Juuu!

Hii ni sehemu muhimu sana kwa ajili ya kuwaandaa wasikilizaji kuwa makini ili

waweze kusikiliza yale yatakayotolewa kwenye hotuba na mzungumzaji.

Utangulizi

Huwa na utambulisho kulingana na vyeo. Mfano: “Mheshimiwa mgeni rasmi,

ndugu wananchi, mabibi na mabwana…….”

Page 27: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 27

Licha ya utambulisho, utangulizi huwa na shukrani pamoja na muhtasari wa

hotuba itakayotolewa.

Kati

Baada ya utangulizi, kiini cha hotuba hufuata. Kiini ndicho hutoa ujumbe kwa

wasikilizaji na ndiyo sehemu muhimu sana katika hotuba. Sehemu hii mtoa hotuba

hueleza yale yote yaliyomsukuma kutoa hotuba hiyo.

Mwisho

Hapa huwa ni hitimisho, muhtasari wa yaliyoelezwa kwa ajili ya kusisitiza,

shukrani na maagizo.

Mfano wa hotuba

HOTUBA YA MGENI RASMI, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MHE. CHARLES M. KITWANGA, MB AKIFUNGUA KIKAO CHA KAZI

CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI UKUMBI WA

„JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE‟, DAR ES

SALAAM TAREHE 18 – 19 FEBRUARI 2016

Inspekta Jenerali wa Polisi, Ndugu Ernest Jumbe MANGU,

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdurahman KANIKI,

Makamishna wa Polisi,

Naibu Makamishna wa Polisi,

Wajumbe wa Mkutano,

Waandishi wa Habari,

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Page 28: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 28

Habari za asubuhi!

Heri ya Mwaka Mpya!

Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya

njema na kutuwezesha kukutana hapa leo hii. Pili, natumia fursa hii kumshukuru

Inspekta Jenerali wa Polisi ndugu Ernest Mangu kwa kunipa heshima hii ya kuwa

Mgeni Rasmi katika Kikao hiki muhimu. Kupitia hafla hii ninapata fursa ya

kuzungumza na viongozi wote waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa

mikoa na vikosi ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za Polisi. Ninawapongeza

sana kwa utaratibu huu mliojiwekea wa kukutana kila mwaka kwa ajili ya kufanya

tathimini lakini pia kuweka mikakati ya namna ya kuboresha huduma zenu kwa

jamii pamoja na jinsi ya kuzidi kuboresha Jeshi la Polisi nchini.

Ndugu Wajumbe,

Ni matumaini yangu kuwa kikao hiki kitakuwa tofauti na vikao vilivyopita

kutokana na kasi kubwa ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.

Dkt. John Pombe Magufuli kwa Falsafa yake ya „HAPA KAZI TU‟. Ni lazima

mbadilishe mtazamo na kufanya kazi kwa kasi inayoendana na Serikali hii.

Fanyeni tathimini ya tulikotoka, upungufu, changamoto na fursa zilizopo ili

kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Ni muhimu kupanga mikakati mipya ya

kupambana na uhalifu kwa kuzingatia changamoto zilizopo na upungufu mliouona

kwa mustakabali wa amani na usalama wa taifa letu. Kukiwa na usalama, shughuli

za kiuchumi zitafanyika kikamilifu na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na

taifa kwa ujumla. Aidha, usalama wa nchi yetu utazidi kuwavutia wawekezaji

katika sekta mbalimbali nchini na kuongeza ajira nchini.

Ndugu Wajumbe,

Kwa kuangalia tu aina ya wajumbe wa kikao hiki, nimeridhika kuwa Kikao Kazi

hiki ni muhimu sana kwa kuwa nyinyi ndiyo msingi na dira ya utendaji kazi wa

Jeshi la Polisi nchini. Maamuzi yenu mtakayoyafanya kwenye kikao hiki na

mkiamua kuyatekeleza kwa dhati taifa litakuwa limepiga hatua kubwa katika

kukabiliana na wimbi la uhalifu nchini. Nimeambiwa kuwa kaulimbiu ya kikao

hiki ni „Badilika kifikra, acha kufanya kazi kwa mazoea‟. Kaulimbiu hii ni nzuri na

Page 29: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 29

ya maana kama mtaamua kuitekeleza kwa vitendo. Malalamiko ya Wananchi

dhidi ya utendaji kazi wa Askari Polisi yatapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Ndugu Wajumbe,

Kwa kuwa hiki ni kikao changu cha kwanza kukutana na viongozi wote wa Jeshi la

Polisi wa nchi nzima, nitumie fursa hii kutoa pongezi za dhati kwenu kwa kazi

kubwa na nzuri mliyoifanya katika kipindi chote cha Uchaguzi Mkuu. Mlisimamia

kwa weledi wa hali ya juu sana Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani

katika muda wote wa mchakato. Mlisimama imara kabla, wakati na baada ya

Uchaguzi Mkuu na kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano kwa

watanzania wote. Hongereni sana kwa kazi nzuri.

Ndugu Wajumbe,

Pamoja na pongezi hizo, nafahamu kuwa zipo changamoto kadhaa za kiuhalifu

ambazo ziliripotiwa katika kipindi kilichopita. Takwimu zinaonesha kuwa kwa

kipindi cha mwaka 2015 makosa makubwa yaliyoripotiwa yalikuwa 68,814

ukilinganisha na makosa 70,153 yaliyoripotiwa mwaka 2014 ambayo ni pungufu

ya makosa 1,339 sawa na asilimia 1.9 %. Kwa upande wa makosa madogo mwaka

2015 yaliripotiwa makosa 450,389 ukilinganisha na makosa 458,422

yaliyoripotiwa mwaka 2014 ambayo ni upungufu wa makosa 8,033 sawa na

asilimia 1.8%.

Kutokanana takwimu hizo niwapongeze sana kwa kazi nzuri mliyoifanya kwa

kipindi cha mwaka jana, na niwasihi muongeze nguvu zaidi katika kupambana na

uhalifu huku tukijikita katika kuzuia zaidi kuliko kusubiri uhalifu utokee.

Aidha, nawakumbusha kuwa katika kuhakikisha kuwa hili linafanikiwa ni lazima

kujenga mahusiano mazuri na jamii kwani wao ndio hasa wahusika na waathirika

wa uhalifu na wanawafahamu wahalifu kwa kuwa ni sehemu ya jamii. Mahusiano

mazuri na jamii yatasaidia upatikanaji wa taarifa kwa wakati na hivyo kuwezesha

askari wetu kushughulikia matukio ya kihalifu kwa wakati, weledi na ufanisi.

Ndugu Wajumbe,

Naelewa changamoto zinazotokana na upungufu wa vitendea kazi, nyumba,

maslahi yasiyotosheleza kwa maafisa na askari, uhaba wa taaluma katika mafunzo

Page 30: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 30

na askari kuishi nje ya kambi. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia kwamba

Serikali itaongeza jitihada ya kuliwezesha Jeshi la Polisi na askari kwa vitendea

kazi vya kisasa kwa kadri uwezo wa bajeti utakavyoruhusu. Tutaendelea

kuwajengea uwezo na maarifa ya kiutendaji kwa kuwaelimisha watendaji ili

waendane na wakati wa sasa wa sayansi na teknolojia. Ni matarajio yangu kwamba

mtatumia fursa zilizopo katika kutatua matatizo yanayolikabili Jeshi letu la Polisi,

wakati jitihada kama nilivyoeleza hapo juu zinafanyiwa kazi kulingana na uwezo

wa kifedha wa serikali. Aidha, napenda kusisitiza kwamba hatuna budi kutunza

vizuri vifaa vilivyopo ili hivi vichache tulivyonavyo tuvitumie kwa muda mrefu

zaidi. Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha matumizi bora ya magari,

nyumba, vifaa vya ofisini, matumizi ya umeme na maji katika makazi na ofisi. Ni

muhimu sana kulisimamia hili ili kuepusha gharama zisizo za lazima. Kwa hiyo

nawataka makamanda wote msimamie hili kwa dhati na kwa nguvu zenu zote.

Pia lipo suala la ajali za barabarani ambalo limekuwa likikua siku hadi siku hasa

ajali zinazohusisha pikipiki maarufu kama boda boda. Ninaunga mkono harakati

zinazofanywa na kitengo cha usalama barabarani katika kutoa elimu ya usalama

barabarani, lakini nawataka nguvu kubwa pia ielekezwe huko kama mlivyoelekeza

nguvu kubwa kukabiliana na ajali za barabara kwa mabasi na malori yaendayo

mikoani. Kwa mfano kwa Jiji la Dar es Salaam pekee, karibu kila siku kumekuwa

kukiripotiwa ajali zinazohusisha bodaboda na nyingi zinasababisha vifo au

ulemavu kwa madereva na hata abiria wao na wakati mwingine hata kwa

watumiaji wengine wa barabara. Ajali hizi zidhibitiwe.

Mbali na kuhusika katika ajali za barabarani, bodaboda pia zimekuwa zikihusika

sana katika matukio ya kihalifu hasa unyang‟anyi wa kutumia silaha. Ni rai yangu

kwenu kuwa baada ya mkutano huu mtoke na suluhisho kwa tatizo hili hasa

uhalifu wa kutumia silaha kwa kutumia pikipiki jijini Dar es salaam.

Ndugu Wajumbe,

Yapo malalamiko kadhaa juu ya baadhi ya askari na maafisa wachache

wanaotumia beji ya polisi vibaya kwa kuwabambikia kesi wananchi, kuomba na

kupokea rushwa, kuchelewa kufika eneo la tukio hata kama ni umbali mfupi tu,

kula njama na watuhumiwa na hivyo kuharibu vielelezo vya kesi, kuchelewesha

upelelezi wa kesi, kutokuwajali wateja (huduma bora kwa mteja) na mengi

Page 31: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 31

mengineyo ambayo yamekuwa ni kero kubwa sana kwa jamii. Natambua kuwa

mmekuwa mkiwashughulikia askari na maofisa waliotuhumiwa kujihusisha na

tabia hizi kwa mujibu wa sheria, lakini nitoe rai kwenu viongozi kuongeza jitihada

zaidi katika kushughulikia matatizo haya kwa kuwasimamia ipasavyo askari wenu

kuanzia ngazi ya chini kabisa. Nawahakikishia kuwa Serikali haitafumbia macho

askari au Afisa yeyote atakayefanya mambo haya ya hovyo bila kujali cheo chake.

Tutachukua hatua kwa faida ya Watanzania.

Ninaimani kuwa kila kiongozi akijiepusha katika kulinda na uendekeza mambo ya

hovyo na akiwasimamia anaowaongoza ipasavyo na kuhakikisha kuwa

wanawajibika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi na za

nchi, malalamiko ya aina hiyo yatapungua sana kama si kumalizika kabisa.

Ndugu Wajumbe,

Mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu ndiyo jjukumu la msingi la Jeshi la

Polisi. Ninawataka makamanda wote wa mikoa kuweka mikakati ya kuimarisha

mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu katika himaya zenu ili kupunguza

uwezekano wa wahalifu kukimbilia maeneo mengine pindi wanapofanya uhalifu.

Aidha mafunzo kazini yaimarishwe ili kuwajengea askari uwezo wa kukabiliana

nauhalifu.

Mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni jukumu la kila mmoja wenu, tunasikia

taarifa za kukamatwa mirungi na bangi kwa wingi lakini dawa za kulevya za

viwandani hatuzikii zikikamatwa. Nawakumbusha kudhibiti mitandao ya madawa

ya kulevya ya viwandani. Tutapima ufanisi wenu kwa kuangalia uhalifu wa aina

zote hasa eneo hili la madawa ya kulevya. Ni wazi kuwa hii ni vita kubwa na

inahitaji umakini wa hali ya juu katika kukabiliana nayo kutokana na namna

biashara hii inavyoendeshwa. Ninawasihi katika mkutano huu mtoke na mkakati

wa namna ya kushughulika na wote wanaojihusisha na biashara hii haramu ili

kuikomesha kabisa.

Ndugu wajumbe,

Kwa kumalizia niseme tena kuwa ni matumaini yangu kikao hiki kitaleta tija kwa

taifa zima na maazimio mtakayotoka nayo ndiyo yatakuwa dira katika njia

Page 32: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 32

mtakayopita mwaka huu katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku na

kuhakikisha kuwa amani tuliyonayo inadumishwa.

Ndugu IGP, Makamanda na Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi,

Mwisho ingawa si mwisho kwa umuhimu, natumia nafasi hii kuwapongeza

Makamishna Albert Nyamhanga, Nsato Marijani na Simon Sirro kwa

kupandishwa vyeo na kupewa nafasi za juu za kuwatumikia Watanzania mkiwa

Makamishna wa Polisi. Nafasi hizo ni mzigo mzito kwenu. Nawatakia kila la

kheri katika utumishi wetu. Nitoe tena shukrani za dhati kwa Inspekta Jenerali wa

Polisi kwa kunialika kusema nanyi na kufungua Kikao hiki muhimu.

Baada ya kusema hayo sasa ninatamka rasmi kuwa kikao kazi cha Maafisa

Waandamizi wa Makao Makuu ya Polisi na Makamanda wa polisi wa Mikoa na

Vikosi cha Mwaka 2016 kimefunguliwa rasmi.

ASANTE SANA KWA KUNISIKILIZA

(Imechotwa katika mtandao wa https://www.moha.go.tz/sw/blog/2016-02-19/hotuba-ya-mgeni-

rasmi)

10. Uandishi wa Risala

Maana ya risala Risala ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la watu hasa hasa wanafunzi, wafanyakazi, washiriki, wanachama, mafundi n.k ili kutoa maelezo ya haja zao mbalimbali na mahitaji yao au kuonesha msimamo wa kundi hilo kwa kiongozi. Muundo wa risala

Utangulizi

Cheo cha kiongozi anayehusika Kundi linalowakilishwa

Kiini

Maelezo ya hali halisi ya maswala na msimamo wa kundi linalowakilishwa.

Page 33: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 33

Mapendekezso na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.

Hitimisho Huwa na shukrani, msimamo pamoja na hitimisho.

Tanbihi: Kama vilivyosemwa awali risala ni hotuba fupi lakini inachukua mambo muhimu tu na kuyaeleza. Hivyo risala yenyewe huwa ni maelezo ya muhtasari kwa jambo linalohitaji maelezo marefu Katika hotuba. Utungaji wa risala unahitaji uangalifu sana na lugha ya heshima iliyo wazi kueleweka kwa kiongozi. Mfano wa risala:

Ndugu Mgeni rasmi, Walimu, Wanafunzi wenzetu, Wazazi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana. Kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne, tunayo heshima na furaha kubwa , kukukaribisha ili ushiriki nasi katika siku hii muhimu na kusikia mafanikio mbalimbali kwa kipindi chote cha masomo yetu hapa shuleni. Shukrani zetu za pekee na za dhati ziende kwa uongozi mzima wa Shule na walimu wetu wote kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa kutufundisha, hivyo tumefundishika vyema; kwasababu tupo tofauti sana na tulivyokuja hapa mwezi januari 2009. Ndugu mgeni rasmi, tulianza kidato cha kwanza tukiwa wanafunzi 120; wasichana 60 na wavulana 60. Mpaka leo tunapohitimu tupo wanafunzi 90; kati yao wavulana ni 43, na wasichana 47. Wengine wameshindwa kuhitimu nasi siku ya leo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ujauzito na kuhama shule. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema wa Baraka kwa ulinzi wake kwetu hadi leo hii tunahitimu kidato cha nne. Ndugu mgeni rasmi, elimu hii ya kidato cha nne imetupatia msingi mzuri wa kujiunga na Elimu ya juu, pia imetujengea uwezo mzuri wa kujitambua na kufikiri, kufanya kazi vizuri na kufanya maamuzi sahihi; pia imetuwezesha sisi wanafunzi kupata elimu ya mambo mbalimbali kupitia masomo tunayo fundishwa hapa shuleni, mfano; tumepata elimu ya uraia, historia ya mambo mbalimbali katika nchi yetu na dunia kwa ujumla, pia tumeweza kupata uelewa kuhusu afya na magonjwa, usalama katika mazingira yetu, Kilimo, Maumbile ya nchi, hali ya hewa, misitu, na viwanda. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali kwa lengo la kupata ujuzi wa kuinua uchumi wetu wa taifa. Ndugu mgeni rasmi, mafanikio hayo yamepatikana kwasababu ya ushirikiano mzuri kati yetu na walimu wetu. Tangu tujiunge na shule hii tukiwa kidato cha kwanza tumefanya majaribio na mitihani ya mara kwa mara jambo lililo tusaidia kuinua taaluma yetu.Tunawashukuru sana walimu wetu, tuna waahidi kufanya vizuri katika mitihani yetu ya Taifa ya kidato cha nne mwaka huu, na Mungu awabariki sana.

Page 34: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 34

Ndugu mgeni rasmi, tumepata changamoto mbalimbali wakati wa maisha yetu ya kielimu hapa shuleni, kama ifuatavyo; Ndugu mgeni rasmi, tuna changamoto ya upungufu wa vitabu vya kiada na ziada; hii imepelekea kushindwa kujisomea vizuri, kwani kitabu kimoja kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya ishirini (20). Ndugu mgeni rasmi, changamoto nyingine ni upungufu wa vifaa vya maabara, hii inapelekea kuchangia kifaa kimoja, hivyo tuna tumia muda mwingi sana kujifunza na kumuelewa mwalimu. Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi; hii imepelekea kutomaliza ‘syllabus’ kwa wakati. Ndugu mgeni rasmi, pia kuna changamoto ya upungufu wa samani za shule, kama vile; madawati kwa ajili ya wanafunzi, viti na meza kwa ajili ya walimu; hii imepelekea baadhi ya wanafunzi wenzetu kukaa wawili kwenye dawati moja. Ndugu mgeni rasmi, maji ni changamoto hapa shuleni, kwani shule haina kisima cha maji, hii imepelekea shule kununua maji kwa gharama kubwa, ambayo hayatoshelezi mahitaji ya shule, kama vile usafi; hususani kwa upande wa vyoo, bila kuwa na maji ya kutosha tutapata magonjwa ya mlipuko, kama vile kipindupindu. Ndugu mgeni rasmi, changamoto ya vifaa vya michezo; kama unavyojua kuwa michezo ni afya, shule yetu ina upungufu mkubwa wa vifaa vya michezo kama vile; mipira ya miguu, pete na mikono, pia hatuna milingoti ya chuma kwaajili ya magoli ya viwanja vya michezo yote tunayocheza hapa shuleni. Ndugu mgeni rasmi, tunashukuru uongozi wa shule hii, walimu na wazazi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya shule yetu; kwa upande wa masomo ya sayansi; shule imeweza kutenga chumba kimoja cha darasa kitumike kama maabara japo kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa. Ndugu mgeni rasmi, tunayo matumaini kwamba maombi yetu umeyasikiliza na utayaatekeleza, maana tunajua kwamba wewe unaweza kupitia Hlimashauri unayo isimamia, asante sana. Mwisho tunaomba msamaha wa dhati toka moyoni mwetu kwa Walimu, Wanafunzi wenzetu na Wazazi pale tulipoenda kinyume na matazamio yenu, kwani watu wakiishi pamoja tofauti lazima ziwepo, tunatumaini mtapokea msamaha wetu, nasi hatuna jambo lolote baya kwenu.

Page 35: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 35

Ndugu mgeni rasmi, tuna kushukuru sana kwa kufika katika Mahafali yetu, kwani tunatambua kuwa unamajukumu mengi ambayo umeyaacha na kuwepo hapa kwaajili yetu.

11. Uandishi wa Mdahalo

Mdahalo ni majibizano yenye utaratibu maalumu. Ni kichocheo cha utafiti na

njia ya kuelimishana. Mdahalo hufanywa kwa mashindano, ambapo upande

mmoja hutoa hoja za kutetea jambo linalozungumziwa na upande mwingine

hutoa hoja za kupinga. Kila upande hujitahidi kutetea msimamo wake mpaka

mwisho.

Katika mdahalo, kunaweza kuwepo watu wa kati ambao hawafungamani na

upande wowote. Hawa huweza kutetea upande fulani wakati fulani na kupinga

uande huo huo wakati mwingine.

Mdahalo hugawanyika katika sehemu kuu tatu:

Utangulizi: huwa na maneno ya kuvuta makini ya wasikilizaji na ndimo

ufafanuzi wa mdahalo hutolewa kwa ufupi.

Mdahalo wenyewe: katika sehemu hii, mzungumzaji huonesha msimamo wake

kuhusu mada ya mdahalo, hutoa hoja za kutetea msimamo wake kwa kutoa hoja

zenye ushahidi na mifano.

Hitimisho: huwa na muhtasari wa mawazo makuu ya mdahalo. Mzungumzaji

huonesha msimamo wake kwa kutumia lugha ya kuvuta wasikilizaji.

Mambo ya kuzingatia katika kufanya mdahalo

Mzungumzaji anapaswa kuelewa mdahalo kabla ya kuanza kupinga au

kuetetea.

Mzungumzaji apange na kuandaa hoja zake za kutetea au kupinga

mdahalo. Hoja hizo zinaweza kuandikiwa maelezo mafupi.

Katika hoja za mzungumzaji, achague zilizo nzito zaidi na awe

mwangalifu asichague hoja zisizohusiana na mada.

Mzungumzaji asikilize kwa makini hoja za wengine na kati ya hizo

achague anazokubaliana nazo.

Hoja zote zipangwe kimantiki na ziwasilishwe kwa kuzingatia lafudhi

sahihi na uteuzi mzuri wa maneno.

Page 36: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 36

Mzungumzaji atumie lugha ya kimazungumzo katika uwasilishaji wake.

Kwa nini tunafanya midahalo?

Kwa kujitayarisha na kushiriki katika midahalo wanafunzi wanajifunza kutumia

taarifa kuunga mkono hoja zao. Wanajifunza namna ya kuwasilisha mawazo yao

kwa uwazi na kwa ushawishi mkubwa.

Kwa kushiriki katika midahalo, wanajifunza kuelewa mawazo ambayo ni tofauti na

yao kwa sababu, wakati wa kufanya mdahalo, wanaweza kujadiliana kwa kutoa

hoja kwa jambo ambalo hawakubaliani nalo kikamilifu, na wanapaswa kuelewa

mawazo ya wenzao wa timu ya wasiokubali hoja zao.

Matayarisho ya mdahalo

Wafanya midahalo wazuri hujitayarisha vizuri. Mdahalo unaofanywa darasani

unaweza usiwe rasmi, lakini unaweza kuwajenga wanafunzi katika hali

inayowafanya wanafunzi wafanye mdahalo rasmi katika mashindano.

Kabla ya kuandaa mdahalo, wafanya midahalo wanakusanya taarifa nyingi kwa

kadri iwezekanavyo, kutoka katika maktaba, magazetini, na kwa kujadiliana na

watu.

Wanafikiria hoja zote zinazounga mkono mada yao, na zile zinazopinga hoja yao.

Kwa maana nyingine ni kuwa, wanaelewa hoja za wapinzani wao pamoja na hoja

zao. Wanajitayarisha kwa maswali yoyote wanayoweza kuulizwa na wapinzani

wao, na changamoto zozote zinazoweza kutolewa.

Wafanya midahalo wazuri hutayarisha hoja zao katika muundo mzuri wa

ushawishi. Wanawasikiliza watu wengine wanaofanya mdahalo, ili wajifunze

ufundi na stadi za kufanya mdahalo. Wanajiunga na vyama vya kufanya midahalo,

na kufanya midahalo mara kwa mara.

Mchakato wa mdahalo

Kuna timu mbili, kila timu ina wazungumzaji wawili au watatu. Timu moja

(chanya) inaafiki hoja, na timu nyingine (hasi) inapinga hoja.

Kuna mwenyekiti, ambaye anaendesha utaratibu.

Page 37: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 37

Mdahalo na muda wa mdahalo huo unagawanywa sawasawa kwa timu zote mbili.

Kila mzungumzaji anatoa mdahalo kama upande wake umeandaa kuunga mkono

hoja zao. Pande zinazungumza kwa zamu, wakianza na anayependekeza hoja

(chanya, hasi, chanya, hasi). Kila mzungumzaji ana muda maalum wa kuzungumza

(k.m. dakika tatu au tano)

Baadaye mdahalo unaweza kufunguliwa kwa washiriki wengine, kwa wasemaji

kusimama na kutoa hoja zao za kuunga mkono au kupinga mada ya mdahalo. Kila

mzungumzaji kutoka upande wa wasikilizaji anapewa muda maalum wa

kuzungumza ( k.m. dakika moja au dakika tatu).

Kila timu inaweza pia kuzungumza kwa kujibu hoja za wapinzani wao, baada ya

kila timu kupewa muda kidogo wa mashauriano. Hii ina maana kuwa wana nafasi

ya kupinga hoja dhidi ya hoja zilizotolewa na wapinzani wao. Kila timu inaweza

kupewa nafasi ya kupinga hoja dhidi ya hoja zilizotolewa na wenzao mara moja au

zaidi. Nafasi ya kwanza ya kupinga hoja wanapewa wale wanaopinga mjadala na

nafasi ya mwisho inatolewa kwa wanaounga mkono mjadala.

Kanuni muhimu za mdahalo

Timu inayounga mkono mjadala haitakiwi kubadili hoja zao. Aidha, ile

inayopinga mjadala nayo pia hairuhusiwi kubadili hoja zao. Wanapaswa kupinga

kabisa mjadala licha ya maoni yao binafsi.

Ikiwa mzungumzaji anatoa tamko, wanatakiwa kutoa ushahidi au sababu za

kuunga mkono tamko hilo.

Taarifa zinazotolewa katika mdahalo lazima ziwe sahihi.

Wazungumzaji hawaruhusiwi kuleta hoja mpya wakati wa kujibu/kupinga hoja za

wenzao.

Hoja ya utaratibu na hoja ya taarifa

Yeyote anayehusika na mdahalo anaweza kuingilia kati wakati msemaji

akizungumza kwa kunyoosha mikono na kusema kuwa „anataka kutoa hoja‟. (Hii

ni „hoja ya utaratibu‟). Hii ina maana kuwa anataka kueleza kuwa moja ya kanuni

Page 38: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 38

za mdahalo imevunjwa (k.m. mzungumzaji amezidisha muda wake wa maongezi,

au hana ushahidi wa kuthibitisha hoja zake).

Wana-mdahalo wanaweza pia kunyoosha mikono yao wakitaka kutoa „hoja ya

taarifa‟ (swali au taarifa za ziada wanazoweza kutoa). Msemaji anaweza kuamua

kumruhusu mshiriki kuzungumza, lakini halazimiki.

Uamuzi

Timu inayoshinda katika mdahalo inaamuliwa na jaji au majaji kwa kutegemea

ubora wa mjadala.

Aidha inaweza pia kuamuliwa kwa kupigiwa kura.

Mfano wa mdahalo

Asante Mwenyekiti,katibu,mtunza muda na washiriki wote. Nipo mbele yenu

kuunga mkono mada isemayo Pesa ni chanzo cha maovu yote kwa hoja zifuatazo.

Hoja ya kwanza,………

Hoja ya pili,………

Hoja ya tatu,………..

Hoja ya nne,………..

Hoja ya tano,……..

Kwa hoja hizo nahitimisha kwa kusema kuwa ni kweli kabisa kuwa pesa ndio

chanzo cha maovu yote kwa wanadamu.

12. Taarifa za kikao

Kumbukumbu za kikao ni muhtasari wa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa

katika kikao. Ni muhimu kuandika kumbukumbu za kikao ili kusaidia na

kurahisisha utekelezaji wa mambo yaliyoamuliwa. Pia kumbukumbu za kikao

hutumika kwa ajili ya marejeleo kwa vizazi vya baadaye.

Page 39: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 39

Namna ya kuandika kumbukumbu za kikao

Katika kuandika kumbukumbu mwandishi hana budi kuzingatia mambo

yafuatayo:

(a) Kichwa cha kumbukumbu

Kichwa cha kumbukumbu kioneshe kuwa kikao kinahusu nini, kilifanyikia

wapi na tarehe gani.

(b) Mahudhurio

Mwandishi anapaswa kuandika orodha ya majina ya watu waliohudhuria kikao

na wasiohudhuria. Kama kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza

mahudhurio yatakuwa na majina ya waliohudhuria tu.

(c) Uteuzi wa viongozi

Iwapo kikao kinahudhuriwa kwa mara ya kwanza wajumbe hupaswa kuteua

viongozi wa kikao hicho ambao ni Mwenyekiti na Katibu kabla ya kuanza kwa

kikao. Kikao hakiwezi kuanza pasipo viongozi wa kusimamia mijadala yote

katika kikao husika.

(d) Ufunguzi wa kikao

Baada ya kuteua viongozi, Mwenyekiti aliyeteuliwa hufungua kikao rasmi na

kuanzisha mijadala ya kikao cha siku hiyo na siku zijazo hadi itakapokuwa

vinginevyo

(e) Ajenda

Hapa huandikwa ajenda zilizojadiliwa kwenye kikao. Mambo yaliyojadiliwa

katika kila ajenda yaandikwe kwa muhtasari. Kwa kila ajenda kauli ya

kukubaliwa au kukataliwa itamkwe wazi.

(f ) Mengineyo

Hapa huandikwa ajenda ambazo hujitokeza katika kikao lakini hazikupitia kwa

Mwenyekiti na zinastahili kujadiliwa kama ajenda.

(g) Yatokanayo

Hapa huandikwa mambo ambayo yamejitokeza katika kikao na hayana

uhusiano na ajenda za kikao. Kwa mfano masuala mtambuka kama mjumbe

Page 40: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 40

kulipia gharama za kikao,taarifa ya dharura inayoweza kumfanya mjumbe

aondoke kabla ya kikao kuahirishwa, n.k

(h) Kuahirisha kikao

Baada ya majadiliano ya ajenda, Mwenyekiti huahirisha kikao. Mwandishi wa

kumbukumbu azingatie muda kikao kilipoahirishwa.

Baada ya kikao mwandishi apitie tena kumbukumbu hizo na aziandike vizuri na

kuzihifadhi kwa ajili ya marejeleo ya kikao kijacho. Kumbukumbu hizo zitiwe

saini na Mwenyekiti na Mwandishi (katibu) kisha wakati wa mkutano mwingine

zisambazwe na kusomwa na wajumbe wa mkutano. Baadaye zithibitishwe na

wajumbe na Mwenyekiti na atie saini ya kuthibitishwa huko.

Ufuatao ni mfano wa kumbukumbu za kikao kinachofanywa kwa mara ya

kwanza:

KUMBUKUMBU ZA KIKAO CHA KWANZA CHA WANAFUNZI WA

KIDATO CHA TANO KUHUSU MAHAFALI KILICHOFANYIKA

TAREHE 5/4/2017 KATIKA UKUMBI WA SHULE KUANZIA SAA 4:00

ASUBUHI HADI SAA 6:00 MCHANA.

(a) Mahudhurio

Waliohudhuria (orodhesha majina yao)

-

-

-

-

-

-

-

-

-

Wasiohudhuria (orodhesha majina yao)

Page 41: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 41

-

-

-

-

-

-

-

-

-

(b) Uteuzi wa viongozi

Kiranja wa darasa aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kikao na katibu wake ni

kiranja msaidizi. Wajumbe wote walikubaliana na uteuzi huo.

(c) Kufungua kikao

Kiranja wa darasa ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho

alifungua kikao mnamo saa 4:00 asubuhi kwa kuwaeleza wajumbe madhumuni

ya kikao hicho.

(d) Ajenda

- Siku na mahali pa mahafali

- Mgeni rasmi

- Zawadi

- Michango ya sherehe

- Uteuzi wa kamati

Siku na mahali pa mahafali

Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kwa pamoja kuwa mahafali yafanyike

jumamosi ya pili kabla ya kuanza kwa mitihani ya kitaifa ili kuwawezesha

waalikwa wote kuhudhuria lakini pia kutoa muda wa kutosha kwa wahitimu

kujiandaa kwa mitihani yao.

Page 42: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 42

Kuhusu mgeni rasmi

Wajumbe walikubaliana kuwa jukumu la kutafuta mgeni rasmi apewe mkuu wa

shule.

Kuhusu zawadi

Wajumbe walijadiliana na kukubaliana kuwa zawadi zitapangwa na kuamuliwa

na kamati itakayoundwa.

Michango ya sherehe

Kikao kiliazimia kwa pamoja kuwa ili kupata pesa za kufanikishia mahafali kila

mjumbe apewe fomu maalumu itakayoandaliwa ili kuchangisha toka kwa

ndugu, jamaa na marafiki kiasi chochote atakachoguswa mtu kuchangia.

Uteuzi wa kamati

Wanafunzi wafuatao walichaguliwa ili wafanye mipango ya kuandaa na

kusimamia sherehe ya mahafali yao. Wanafunzi hao ni;

- Mtungi

- Baraka

- Mujuni

- Byoma

- Shukuru

- Sikudhani

- Kachacha

- Stumai

- Tamasha

- Kaitaba

Wajumbe hao walikubaliana na uteuzi huo na wakaahidi kupeana majukumu.

(f) Mengineyo

Wajumbe walisisitiza kwamba kamati ifanye mipango kwa kuzingatia kwamba

muda uliobaki ni mfupi. Walipendekeza kwamba kufanyike mkutano wa

kuwapatia wajumbe taarifa kuhusu mgawanyo wa majukumu.

Page 43: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 43

(g) Yatokanayo

Mjumbe mmoja aliwaburudisha wajumbe kwa vinywaji na nyama choma ya

mbuzi katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.

(h) Kuahirisha kikao

Mwenyekiti aliahirisha kikao kwa kuwaomba wajumbe wengine wawe na

ushirikiano kwa wenzao katika kufanikisha mahafali hayo. Kikao liahirishwa

saa 6:00 mchana. Kikao kijacho kitakuwa 12/4/2017 kuanzia saa 9:00 mchana

hadi saa 12:00 jioni.

Mwenyekiti…………………….Tarehe…………………………........

Katibu………………………….Tarehe……………………………….

Ikiwa kikao kinafanyika kwa mara ya pili:

Kikao cha pili na kuendelea huwa na muundo ufuatao:

1. Kichwa cha kikao

2. Mahudhurio

3. Kusomwa na Kuthibitishwa taarifa za kikao kilichotangulia

4. Kufungua kikao

5. Ajenda

6. Mengineyo

7. Yatokanayo

8. Kuahirisha kikao

9. Majina & saini za viongozi

13. UANDISHI WA RIPOTI

Ripoti ni maelezo kuhusu mtu, kitu au jambo fulani lililotokea. Ni aina ya

kumbukumbu ambazo huandikwa kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Ripoti

inaweza kuwa ya uchunguzi wa utafiti kuhusu jambo fulani, inaweza kuwa ya

polisi, daktari au ya tume fulani.

Page 44: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 44

Namna ya kuandika ripoti

Kabla ya kuandika ripoti lazima kuwe na ushahidi unaohusu suala au jambo

linaloandikiwa ripoti hiyo. Kwa hiyo, ni lazima mtunzi afanye uchunguzi kwanza.

Pia mtunzi anapaswa kufahamu kiwango cha elimu na uwanja wa mtu

anayemwandikia ripoti hiyo. Kwa mfano kama ni polisi, daktari, mwanasheria,

mfanyabiashara n.k. Lugha atakayoitumia mwandishi au mtunzi izingatie

muktadha wa matumizi. Lugha itegemee aina ya ripoti.

Hatua za uandishi wa ripoti

(a) Kichwa cha ripoti

Mtunzi aandike kichwa cha ripoti ambacho kinaonesha; kiini cha ripoti- ripoti

inahusu nini, tarehe ya tukio au jambo linaloandikiwa ripoti na mahali palipotokea

jambo hilo.

(b) Utangulizi wa ripoti

Katika hatua hii mtunzi hueleza kwa muhtasari madhumuni ya ripoti

(c) Kiini cha ripoti

Mtunzi aeleze mambo aliyoyaona, chanzo chake na madhara au faida yake

(d) Hitimisho

Katika kuhitimisha ripoti mtunzi aoneshe msimamo na mapendekezo yake. Baada

ya hitimisho mtunzi aandike au aoneshe ripoti imeandikwa na nani, cheo chake

(nafasi yake hasa katika ripoti hiyo) na tarehe ripoti hiyo ilipoandikwa.

Ufuatao ni mfano wa ripoti ya mkutano wa wanafunzi

Ripoti ya kikao cha wanafunzi wa kidato cha tano uliofanyika katika ukumbi wa

shule mnamo tarehe 10/4/2017 kuhusu mahafali yao.

Page 45: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 45

Mnamo tarehe 10/4/2017 saa 4:00 asubuhi, wanafunzi wa kidato cha tano

walifanya mkutano kuhusu mahafali yao yatakayofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Mambo yaliyojadiliwa siku hiyo ni pamoja na :

(i) Kuwakaribisha wazazi wao

(ii) Kuandaa michezo mbalimbali: mpira wa miguu, mpira wa

kikapu, ngonjera, nyimbo, igizo, mashairi na muziki.

(iii) Kuandaa zawadi kwa ajili ya walimu wao wa madarasa, wa

masomo na Mkuu wa shule.

(iv) Kutoa mchango wa kununulia zawadi hizo.

Wanafunzi walitoa mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na kumwomba kiranja

wao wa darasa awaeleze walimu kwamba siku hiyo wanafunzi wanaomba wasivae

sare za shule na pia waruhusiwe kuwakaribisha wanafunzi wa shule nyingine kwa

ajili ya kucheza nao dansi na wakati wa muziki pawekwe ulinzi mkali ili

wasiingiliwe na watu wa nje.

Mwisho wanafunzi wote walikubaliana kuchanga Tshs. 2000/= kila mmoja ili

kufanikisha shughuli hiyo.

Mkutano huo uliodumu kwa saa mbili ulifungwa saa 6:00 mchana na kiranja wa

darasa.

Imetayarishwa na. Saini………………………..

Jina………………………...

Tarehe………………... Cheo…………………….....

Page 46: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 46

14. Uandishi wa Wasifu

Wasifu ni insha inayosimulia maisha ya mtu fulani tangu kuzaliwa kwake, elimu

yake, kazi, ujuzi wake n.k. Anayeandika wasifu ni tofauti na anayezungumziwa

katika wasifu huo.

Kuna aina tatu za wasifu:

Wasifu wa Kawaida

Tawasifu/Wasifu binafsi Wasifu-Kazi

Wasifu wa kawaida.

Wasifu wa kawaida ni masimulizi ya maisha ya mtu fulani yanayosimuliwa na mtu

mwengine.

Katika insha, mwanafunzi anaweza kuambiwa aandike wasifu wa mtu mashuhuri-

anayejulikana kama vile Nelson Mandela, Julius Nyerere au Mzee Jomo Kenyatta

n.k. mtu yeyote anayemjua - kama vile mzazi, rafiki, mwalimu wake n.k. au

kumhusu mtu wa kubuni - mwanafunzi anaweza kubuni mtu na asimulie maisha

yake.

Mfano wa wasifu wa kawaida

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI RAIS

WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

1.0. MAISHA YAKE

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha

Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi

Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana

mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii

na kero zao zinaondoka.

Page 47: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 47

2.0. ELIMU NA MAFUNZO

Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake

iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya

Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa kikosi cha

Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.

Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya

Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha

Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI

Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani

Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.

Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa

Kagera. Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2000. Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la

Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005.

Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa. Baada ya uchaguzi,

Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka

2010.

Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne kuwa Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato. Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi

mwaka 2015.

Page 48: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 48

Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri

wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

4.0. UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa

Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya,

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia

kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi. Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa

Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua

Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania. Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

5.0. UFANISI KATIKA UONGOZI

Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa

wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini.

Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa

Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na

kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba. Akiwa Waziri

Page 49: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 49

wa ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya

barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha,

alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi

zake. Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote. Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini

William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”. Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini.

Wakati akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo, kama vile samaki, ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa

wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”.

Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi

michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya

watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli

anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 –

2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI

Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza

vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20

Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:

Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili

Page 50: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 50

alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.

Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;

Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;

Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;

Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;

Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;

Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;

Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.

Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;

Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.

HITIMISHO

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii

inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati unaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Page 51: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 51

Tawasifu/Wasifu binafsi

Katika tawasifu, mwandishi huwa anasimulia maisha yake mwenyewe. Hivyo basi,

tawasifu huandikwa na kusimuliwa katika nafsi ya kwanza.

Katika insha, mwanafunzi anaweza kuulizwa asimulie: maisha yake binafsi,

maisha yake miaka kadhaa ijayo, maisha ya mtu fulani kama yake binafsi k.m

ajifanye kuwa Rais wa Tanzania, halafu asimulie maisha yake tangu kuzaliwa hadi

alipo. k.m 'Umekuwa Rais wa nchi yako kwa muda wa miaka mitano, andika

tawasifu kuhusu maisha yako itakayowasaidia wananchi wako kukuelewa vyema zaidi maisha ya mhusika wa kubuni, kama yake binafsi

Kwa mfano, katika riwaya ya Siku Njema, mhusika Kongowea Mswahili

anaandika tawasifu akisimulia maisha yake tangu kuzaliwa, maisha ya nyumbani,

elimu yake, kazi alizozifanya, maono yake n.k.

Mfano wa wasifu binafsi

Katika maisha yangu, nimekuwa ni mtu wa kukata tama mara nyingi. Hali hiyo

inaponitokea hunifanya niwe kama moto uliomwagiwa maji. Nakumbuka siku

moja, nikiwa mjini katika hali ileile ya kukata tama, nilikutana na Chopeko. Ni

Chopeko tuliyekuwa tukimwita “njiti” shuleni kwa vile alikuwa mwembamba kama kamba. Pia, siku zote alikuwa ni mtu wa mwisho katika mitihani.

Basi nilihisi mtu ananigusa begani; kugeuka macho yangu yalipamia bonge la

mtu aliyekuwa na uso wa mviringo kama tikitimaji. Hatimaye, baada ya kitambo

alijitambulisha kuwa yeye ni Chopeko baada ya mimi kuwa wa mwisho katika mtihani wa kumkumbuka.

Chopeko alinieleza kuwa hivi sasa yeye ni mfanyabiashara anayesafiri kufuata

bidhaa China na Dubai. Tulizungumza mengi, kasha tukaagana baada ya kuwa

tumepeana namba za simu.

Kuanzia siku hiyo niliazimia moyoni mwangu kuwa kukata tama kwangu tena mwiko!

Wasifu-Kazi

Wasifu-kazi (Resume/Curriculum Vitae) ni stakabadhi inayotumiwa kuorodhesha

mambo muhimu katika maisha ya mtu kama vile elimu, kazi, ujuzi n.k

Page 52: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 52

inayotumiwa sanasana katika kuomba kazi. Kinyume na wasifu na tawasifu

ambazo hutumia lugha natharia (ya masimulizi), wasifu-kazi hutumia muundo

fulani wa orodha na/au jedwali kuwasilisha mambo muhimu tu. Isitoshe, wasifu

kazi huwa mfupi - aghalabu ukurasa mmoja.

Tunapoorodhesha mambo fulani katika wasifu, tunaanza na yale ya hivi karibuni

hadi yale ya kitambo. Kwa mfano, anza na shule uliyosomea mwisho, iliyokuwa

imetangulia hiyo n.k hadi shule uliyoenda kwanza.

Muundo wa Wasifu-Kazi

Katika wasifu-kazi unahitajika kuonesha:

1. Jina lako

2. Namna ya mawasiliano (simu, anwani, barua pepe)

3. Elimu

orodhesha shule zote ulizozisomea kutoka shule uliyosomea mwisho

hadi shule ile uliyoihudhuria kwanza.

katika kila shule, onesha miaka uliyohudhuria k.m 1996-2000

onesha shahada (degrees) na diploma ulizozipata

4. Kazi

orodhesha kazi zote ulizozifanya kutoka kazi ya hivi karibuni hadi

kazi ulizozifanya mwanzoni

onesha cheo ulichokuwa nacho katika kazi hiyo na majukumu yake

onesha kampuni au mahali ulipofanya kazi hiyo

onesha miaka ambayo ulikuwa katika kazi hiyo

taja ujuzi au taaluma uliyoipata katika kazi hiyo

5. Ujuzi / Taaluma - taja ujuzi maalumu ulionao, taaluma au talanta zozote

ulizonazo.

6. Mapato/Mafanikio/Tuzo - taja mafanikio yoyote au tuzo zozote ulizozipata

katika maisha

7. Mapendeleo - Nini kinakupendeza katika maisha? unapenda kutumiaje muda

wako wa likizo usiokuwa wa kazi

8. Maono ya Kazi - una maono gani katika kufanya kazi? ungependa kufanya

nini?

Page 53: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 53

Mfano wa Wasifu-Kazi

Taarifa binafsi

Majina: TAFUTA MAISHA USICHOKE

Utaifa: MTANZANIA

Mahali pa kuzaliwa: ARUSHA

Tarehe ya kuzaliwa: 26/11/2017

Jinsi: ME

Hali ya Ndoa: SIJAOA

Anwani ya Posta:

MBEZI BEACH

S.L.P 60213

DAR ES SALAAM

Simu: 0717104507

Barua pepe: [email protected]

Sifa za kitaaluma

2006-2009: Shahada ya Sanaa katika Elimu. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

2004-2006: Cheti cha Elimu ya sekondari ya juu. Chuo cha Taifa cha Usafirishaji

2000-2003: Cheti cha Elimu ya sekondari ya kawaida. Shule ya Sekondari

Manyara

1993-1999: Elimu ya Msingi. Shule ya Msingi Mto wa Mbu

Page 54: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 54

Uzoefu na historia ya kuajiriwa

2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications

Ltd

Ujuzi na weledi

Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia

warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi

unaoweza kukusaidia kuzalisha, kukuza, kubuni, kuanzisha, kusababisha,

kubadili, kuchangia mabadiliko na kuwezesha.

Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa

kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.

Machapisho na utafiti

Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano

ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi

kuzifanya na kuziandika.

Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa.

Lengo ni kuonesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto

zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.

Tuzo au heshima

Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonyesha namna jitihada zake

zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi

kutambuliwa katika ajira zilizopita.

Siyo lazima iwe kazini tu, inawezekana kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti

na zile tuzo za kitaaluma moja kwa moja.

Maneno kama, nilishinda, nilituzwa na nilitambuliwa, kwa sababu ya shughuli,

majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.

Page 55: UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1...Mwalimu Nyerere ni mwenzetu, ni rafiki yetu, ni mtu wa watu, ni baba wa taifa letu, ni babu yetu mwenye hekima na busara. Paji lake la uso lilijaa

UTUNGAJI/UANDISHI - KISWAHILI 1 2017

Maeda, T.S 0717104507 www.mwalimuwakiswahili.co.tz Uk 55

Orodha ya wadhamini

Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako.

Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na

wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya

kazi nawe.

Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo

wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba wakuandikie barua ya

utambulisho ukazitumia inapolazimika.

MWISHO