wasemavyo wanasayansi kuhusu qur'an

12
WASEMAVYO WANASAYANSI KUHUSU QUR'AN Ibrahimu H. Kabuga ©ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH P.O.BOX 76644 Dar es Salaam Tanzania Phone: +255 712 566595 / 0763348213 E-mail: [email protected]

Upload: x-paster

Post on 30-Sep-2014

1.599 views

Category:

Documents


4 download

DESCRIPTION

Chaguo langu la Muhammad kuongoza orodha ya watu walioacha athari kubwa duniani linaweza kuwashangza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na baadhi yao, lakini ndiye mtu pekee katika historia aliyefanikiwa mno kwenye ngazi zote mbili za kisekula na kidini … yumkini nguvu na athari husika ya Muhammad kwenye Uislamu ni kubwa mno kuliko athari na nguvu ya Yesu Kristo na Mt. Paulo kwenye Ukristo zikiunganishwa pamoja… ni muungano huu usio kifani wa nguvu ya kisekula na kidini ambayo ninahisi inampa Muhammad hadhi ya kuchukuliwa kuwa mtu mwenye athari na nguvu kuliko wengine katika historia ya binadamu. (Michael Hart katika 'The 100, A Ranking of the Most Influential Persons In History,' New York, 1978).

TRANSCRIPT

Page 1: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

WASEMAVYO WANASAYANSI KUHUSU

QUR'AN

Ibrahimu H. Kabuga

©ISLAMIC CENTRE FOR RESEARCH

P.O.BOX 76644 Dar es Salaam – Tanzania

Phone: +255 712 566595 / 0763348213

E-mail: [email protected]

Page 2: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

2

Chaguo langu la Muhammad kuongoza orodha ya watu walioacha athari kubwa duniani linaweza

kuwashangza baadhi ya wasomaji na kuhojiwa na baadhi yao, lakini ndiye mtu pekee katika

historia aliyefanikiwa mno kwenye ngazi zote mbili za kisekula na kidini … yumkini nguvu na

athari husika ya Muhammad kwenye Uislamu ni kubwa mno kuliko athari na nguvu ya Yesu Kristo

na Mt. Paulo kwenye Ukristo zikiunganishwa pamoja… ni muungano huu usio kifani wa nguvu ya

kisekula na kidini ambayo ninahisi inampa Muhammad hadhi ya kuchukuliwa kuwa mtu mwenye

athari na nguvu kuliko wengine katika historia ya binadamu. (Michael Hart katika 'The 100, A

Ranking of the Most Influential Persons In History,' New York, 1978).

Page 3: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

3

Keith L. Moore

Profesa Emeritus, Idara ya Anatomia na Baolojia ya chembehai, Chuo Kikuu cha Toronto. Mwana- embriolojia mashuhuri na mwandishi wa vitabu kadhaa vya matibabu, kama vile, Clinically Oriented Anatomy (3rd Edition) na The Developing Human (5th Edition, with T.V.N. Persaud).

Utafiti wa kiinitete katika hatua ya 'alaqa.

Dr. Moore alikuwa ni Rais wa zamani wa Chama cha Canada cha wana-anatomia, na chama Amerika cha wana-anatomia wa tiba. Alitunukiwa tuzo yenye hadhi kubwa ya J.C.B. Grant Award kutoka chama cha wana-anatomia wa Canada na mwaka 1994 alipokea Tuzo ya mwanachama anayeheshimika (theHonoured Member Award) kutoka chama cha wana-anatomia wa Amerika " kwa mchango bora katika uwanja wa anatomia ya tiba".

"Kwa kipindi cha miaka mitatu, nimefanya kazi na

Kamati ya Embriolojia ya Chuo Kikuu cha Mfalme

Abdulaziz mjini Jeddah, Saudi Arabia, nikiwasaidia

kutafsiri maelezo mengi yaliyomo ndani ya Qur'an na

Sunnah kuhusu uzazi wa binadamu na maendeleo yake

kabla ya kuzaliwa. Mwanzo nilistaajabishwa mno na

usahihi na ukweli wa maelezo haya yaliyoandikwa karne

ya 7 AD, kabla sayansi ya Embriolojia haijaanzishwa.

Ingawa nilikuwa nikiifahamu historia tukufu ya

wanasayansi wa Kiislamu katika karne ya 10 AD, na

baadhi ya mchango wao kwenye tiba na madawa, sikuwa

nikijua chochote kuhusu mambo matukufu yenye

kushangaza na imani mbalimbali zilizomo ndani ya

Qur'an na Sunnah."[2]

kwenye Kongamano mjini Cairo aliwasilisha mada ya ushuhuda wa utafiti na kusema: "Imekuwa furaha kubwa kwangu kutoa mchango katika kufafanua taarifa mbalimbali zilizomo ndani ya Qur'an kuhusu maendeleo ya binadamu. Ni wazi kwangu kuwa lazima zitakuwa zimemfikia Muhammad kutoka kwa Mwnyezi Mungu, au Allah, kwa sababu sehemu kubwa ya maarifa haya hayakugunduliwa mpaka baada ya karne nyingi kupita. Hii inathibitisha kwamba lazima Muhammad

atakuwa Mtume wa Mungu, au Allah" [1]

Profesa Moore vilevile alieleza kuwa: ""…Kwa kuwa uonyeshaji wa kiinitete cha binadamu ni

Page 4: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

4

suala tata, kutokana na mchakato wa kuendelea kubadilika wakati wa ukuaji, inapendekezwa kuwa mfumo mpya wa Uainishaji inaweza kupatikana kwa kutumia masharti yaliyotajwa katika Qur'ani na Sunna. Mfumo huo unaopendekezwa ni rahisi, mpana, unaendana na maarifa ya kisasa ya Embriolojia.

" Utafiti mkubwa wa Qur'an na Hadith katika kipindi cha

miaka minne iliyopita umeonyesha wazi mfumo wa

uainishaji wa kiinitete cha binadamu ambao ni wa ajabu

kutokana na ukweli kwamba uliandikwa tangu karne ya

saba AD .. maelezo yaliyomo katika Qur'an hayawezi

kuwa yametokana na msingi wa elimu ya sayansi katika

karne ya saba ..." [1]

E. Marshall Johnson

Profesa na Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia na Maendeleo ya Baolojia, na Mkurugenza wa Taasisi ya Daniel Baugh, Chuo Kikuu cha Thomas Jefferson, Philadelphia, Pennsylvania, Marekani.

Ni mwandishi wa zaidi ya machapisho 200. Miongoni mwa kazi zake nyingine aliwahi kuwa Rais wa Chama Teratolojia. Profesa Johnson alianza kuvutiwa na miujiza ya kisayansi iliyomo ndani ya Qur'an kaika Kongamano la 7 la Tiba lililofanyika Saudi Arabia (1982), baada ya kuundwa kwa kamati maalumu ya kutafiti miujiza ya kisayansi iliyotajwa ndani ya Qur'an na Hadithi. Mwanzo, Profesa Johnson alikataa kukubali kuwa kaika Qur'an na Hadithi kuna maandiko kama hayo. Lakini baada ya majadiliano na Sheikh Zindan alianza kuvutika na hata kuufanya utafiti wake ujikite kwenye maendeleo ya ndani na nje ya kiinitete.

"...kwa ufupi, maelezo ya Qur'an sio tu kwamba yanaelezea juu

ya maendeleo muundo wa ndani, bali pia inasisitiza juu ya hatua

za ukuaji wa nje, ukuaji wa ndani wa kiinitete, uumbwaji wake

na maendeleo yake, ikisisitiza juu ya matukio makubwa

yanayotambuliwa na elimu ya sayansi ya kisasa."

" Kama mwanasayansi, ninaweza tu kushughulika na vitu

ninavyoweza kuviona kabisa. Ninaweza kuielewa embrolojia na

maendeleo ya kibaolojia. Ninaweza kuyaelewa maneno

ninayotafsiriwa kutoka ndani ya Qur'an. Kama nilivyotoa mfano

hapo awali, kama ningetakiwa kujibadilisha mimi kuwa katika

zama hizo, kwa kujua kile ninachofanya leo kuelezea vitu,

nisingeweza hata kidogo kuelezea mambo haya yaliyoelezwa…

Page 5: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

5

Sioni ushahidi wowote wa kukanusha fikra ya kwamba mtu

huyu Muhammad alikuwa akipata taarifa hizi mahali fulani …

hivyo sioni chochote kinachokinzana na fikra ya kuwa Mungu

alihusika katika kile alichoweza kukiandika…"

T.V.N. Persaud

Ni Profesa wa Anatomia, na Profesa wa magonjwa na afya ya watoto, Chuo Kikuu cha Manitoba, Winnipeg, Manitoba, Canada.

Ameandika na kuhariri zaidi ya vitabu 20, na amechapisha zaidi ya machapisho 181 ya Kisayansi. Ni mwandishi mweza wa kitabu cha The Developing Human (toleo la5, pamoja na Keith L. Moore). Alipokea Tuzo ya J.C.B. Grant Award mwaka 1991. Profesa Persaud aliwasilisha machapisho kadhaa ya utafiti.

"Kwangu inaonekana kwamba Muhammad alikuwa mtu

wa kawaida sana, hakuwa akisoma, hakuwa akiandika,

kwa hakika alikuwa mtu asiyesoma wala kuandika...

tunazungumzia miaka takriban 1400 iliyopita, unakuwa

na mtu asiyejua kusoma wala kuandika anatoa habari

nzito za kushangaza na zenye usahihi wa ajabu, za tabia

ya sayansi...

Mimi binafsi sioni kama mambo haya yalitokea kwa

bahatibahati tu, kuna mambo mengi sana ya ukweli na

kama Dr. Moore, sina shida katika akili yangu kukubali

kuwa huu ni muongozo au ufunuo wa kimungu

uliomuongoza kwenye taarifa hizi" ." [1]

Page 6: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

6

Joe Leigh Simpson

Ni Progesa na Mwenyekiti wa Idara ya ukunga (uzazi) na jinakolojia (elimuuzazi), Chuo cha Tiba cha Baylor, Houston,

Texas, Marekani.

Ni Rais wa Chama cha Uzazi cha Marekani. Amepokea tuzo nyingi, ikiwemo ya chama cha Maprofesa wanaoheshimiwa na jamii katika fani ya ukunga ya mwaka 1992 (Association of Professors of Obstetrics and Gynaecology Public Recognition Award). Kama ilivyokuwa kwa wasomi wengine wengi, Profesa Simpson alishangazwa sana alipogundua kuwa Qur’an na Hadithi vina maandiko yanayohusu fani yake. Alipokutana na Sheikh Abdul-Majeed A.Zindani, alisisitiza kuthibitisha maandiko ya Qur’an na Hadithi yaliyoletwa kwake.

"... hizi hadithi (maneno ya Muhammad) zisingepatikana kwa msingi wa

utaalamu wa kisayansi wa zama za ‘mwandishi husika’…kwa hiyo ina

maana kwamba sio tu kwamba hakuna mgongano kati ya sayansi ya

kijenetiki na dini (Uislamu) bali ni hakika kuwa dini (Uislamu) unaweza

kuiongoza sayansi kwa kuongezea ufunuo kwenye njia za kawaida za

kisayansi… Katika Qur’an kuna maelezo yaliyothibitika karne nyingi

baadaye na kuunga mkono moja kwa moja kuwa maarifa yaliyomo

ndani ya kitabu hiki yametoka kwa Mwenyezi Mungu." [1]

Alfred Kroner

Profesa katika idara ya Geosciences, Chuo Kikuu cha Mainz, Ujerumani.

Profesa Kroner ni miongoni mwa wanajiolojia maarufu duniani, akifahamika kwa wanasayansi wenzake kwa ukosoaji wake dhidi ya nadharia mbalimbali za wanasayansi wakubwa katika fani yake. Sheikh cAbdul-Majeed A. Zindani alikutana naye na kumpatia aya na hadithi kadhaa alizozifanyia utafiti na kuzitolea maoni.

"Nikitafakari mahali Muhammad alitoka... Naddhani

haiwezekani kuwa alikuwa akijua vitu kama vile asili ya

ulimwengu inayokubaliwa na kila mtu, kwa sababu ni miaka

ya hivi kwaribuni ambapo wanasayansi kwa shida sana na

kwa kutumia teknolojia ya kisasa iliyoendelea sana

wameligundua jambo hilo."

"Mtu ambaye hakuwa akijua chochote kuhusu fizikia za

nyuklia miaka 1400 iliyopita nafikiri, kwa kutumia akili

yake tu, asingekuwa katika nafasi ya kugundua mathalan

Page 7: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

7

kwamba ardhi na mbingu vina asili moja, au masuala

mengine mengi ambayo tumeyajali hapa...

Ukikusanya pamoja maelezo yote haya yaliyotolewa na

Qur’an juu ya mambo yanayohusu ardhi na mpangilio /

uumbikaji wa ardhi na sayansi kwa aujumla, kimsingi

unaweza kusema kwamba maelezo hayo yaliyotolewa ni

sahihi na ni kweli kwa namna mbalimbali, sasa yanaweza

kuthibitishwa na utafiti wa kisayansi. Unaweza kusema kwa

uwazi kabisa kuwa Qur’an ni kitabu sahihi cha sayansi kwa

mwanadamu sahihi. Na kwamba maelezo mengi

yaliyotolewa humo hayakuweza kuthibitishwa kwa wakati

huo, lakini sasa utafiti unaofanywa sasa hivi wameweza

kuthibitisha kile kilichosemwa na Muhammad miaka 1400

iliyopita"

Yushidi Kusan

Mkurugenzi wa Tokyo Observatory, Tokyo, Japan.

Sheikh Abdul-Majeed A. Zindani alimpatia aya kadhaa zinazoelezea mwanzo wa ulimwengu na mbingu, na uhusiano uliopo kati ya mbingu na ardhi. Alielezea kushangazwa kwake, akisema kuwa Qur’an inaielezea dunia kama inavyoonekana kwa mtu anayeitazama kwa upande wa juu, kila kitu kipo wazi na kipo dhahiri.

"Nasema, nimevutiwa mno na kukuta mambo sahihi

ya astronomia ya kweli katika Qur’an, na kwa sisi

wanaastronomia wa sasa tumekuwa tukichunguza

sehemu ndogo sana ya ulimwengu. Tumeziweka juhdi

zetu zote kujaribu kuisma sehemu ndogo sana. Kwa

sababu, kwa ktumia arubini, tunaweza tu kuona

sehemu ndogo sana za angabila kufikiria kuhusu

ulimwengu mzima. Hivyo, kwa kuisoma Qur’an na

kwa kujibu masuala husika, nafikiri ninaweza kupata

njia yangu ya baadaye ya kuutafiti ulimwengu."

Page 8: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

8

Profesa Armstrong

Profesa Armstrong anafanya kazi na shirika la anga la Marekani (NASA) na pia ni profesa wa masuala ya anga (Astronomy), Chuo Kikuu cha Kansas, Lawrence, Kansas, Marekani.

Prof. Armstrong aliulizwa maswali kadhaa kuhusu aya za

Qur’an zinazohusu fani yake. Aliulizwa: “Umejionea na kugundua mwenyewe maumbile halisi ya astronomia ya kisasa kwa kutumia chombo cha kisasa, roketi, satellite mbalimbali zilizotengenezwa na mwanadamu. Vilevile umeona jinsi mambo hayohayo yalivyoelezwa ndani ya Qur’an karne kumi na nne zilizopita. Sasa ni yepi maoni yako?”

"Hilo ni suala gumu ambalo nimekuwa nikilifikiria

tangu tulipoanza mjadala wetu hapa. Nimevutiwa sana

na namna baadhi ya maandiko ya zamani

yanavyoafikiana na elimuanga iliyovumbuliwa hivi

karibuni. Mimi sio mwanachuoni wa kutosha wa

historia ya binadamu kwamba nijiweke moja kwa moja

katika mazingira yaliyokuwepo miaka 1400 iliyopita.

Kwa hakika, ningependa kuliacha hilo kwamba, kile

tulichokiona ni cha ajabu, kikiwa au kisiwe na maelezo

ya kisayansi, lazima kuna kitu ambacho kitakuwa nje

ya uelewa wetu wa maarifa ya kibinadamu katika

kufafanua maandiko ambayo tumeyaona." [1]

William Hay

Profesa wa sayansi ya bahari (Oceanogprahy), Chuo Kikuu cha Colorado, Boulder, Colorado, Marekani.

Profesa Hay ni miongoni mwa wanasayansi maarufu sana wa bahari nchini Mrekani. Sheikh

cAbdul-Majeed A.

Zindani alikutana naye na kumuuliza masuali mengi kuhusu bahari, kigawanyisho kati ya bahari kuu na bahari ndogo (upper and lower sea), na kuhusu mazingira ya chini ya bahari na jiolojia ya bahari.

"Naona ni jambo la kuvutia sana kwamba taarifa

hizi zinapatikana ndani ya maandiko ya kale ya

Qur’an Tukufu, na sikuwa na njia ya kujua kuwa

yalitoka wapi. Lakini nadhani inashangaza mno

kwamba yapo na kaazi hii inaendelea

Page 9: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

9

kuyavumbua,kwa kuchunguza maana ya baadhi

ya kurasa za kitabu hiki."

Na alipoulizwa kuhusu chanzo cha Qur’an, alijibu:

"Nafikiri lazima kitakuwa kimetoka kwa

Mungu.”

Durja Rao

Profesa wa Jiolojia ya Bahari katika chuo kikuu cha Mfalime Abdulaziz , Jeddah, Saudi Arabia.

Sheikh Zindani alimpatia Prof. Rao aya nyingi zinazohusu eneo la fani yake, na kumuuliza: "Unasemaje kuhusu kuwepo kwa taarifa za kisayansi ndani ya Qur'an? Mtume Muhammad aliwezaje kuyajua mambo haya karne kumi na nne zilizopita?"

"Ni vigumu kufikiri kwamba aina hii ya maarifa

ilikuwepo zama hizo, takriban miaka 1400

iliyopita. Huwenda baadhi ya mambo walikuwa

na taarifa nayo kwa kiwango kidogo, lakini

kueleza kwa kina mambo hayo ni jambo gumu

sana. Kwa hiyo, maarifa haya hayatokani na

mwanadamu hata kidogo. Mwanadamu wa

kawaida hawezi kutoa maelezo ya kina kuhusu

maajabu haya. Hivyo, naona kuwa taarifa hii

lazima itakuwa imetoka kwa chanzo chenye

uwezo ulio juu ya uwezo wa chochote.

Page 10: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

10

Profesa Siaveda

Profesa wa Jiolojia ya Bahari, Japan.

Sheikh Zindani alimuuliza maswali kadhaa yanayohusu fani yake, na kisha akamueleza kuhusu aya za Qur’an pamoja na hadithi mambo ya kimaumbile aliyoyazungumzia. Swali moja lilikuwa likihusu milima. Sheikh Zindani alimuuliza kuhusu muundo wa milima; na iwapo ilikuwa imewekwa kama vigingi katika ardhi. "Ni yepi maoni yako kuhusu ulichokiona ndani ya Qur’an na Sunnah kuhsu siri mbalimbali za ulimwengu, ambazo wanasayansi wamezigundua leo?”

"Kwangu mimi laonekana kuwa mwujiza wa hali

ya juu, jambo la kuashangaza na la taabu

kuaminika. Nadhani kama kweli ulichosema

ndicho, kitabu hiki ni cha ajabu mno,

ninakubali."

Tejatat Tejasen

Mwenyekiti wa Idara ya Anatomia na Mkuu wa zamani wa kitivo cha tiba, Chuo kikuu cha Chiang Mai, Chiang Mai,

Thailand.

Profesa Tejasen alisoma makala mbalimbali kuhusu Qur'an na Embriolojia ya kisasa. Alitumia siku nne akiwa pamoja na wasomi kadhaa, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, wakijadili maajabu hayo yaliyomo ndani ya Qur'an na Hadithi. Wakati wa kongamano la Tiba mjini Riyadhi Saudi Arabia, alisimama na kusema

"Katika miaka mitatu iliyopita, nilivutiwa na kuisoma Qur’an...

Kutokana na uchanguzi wangu na kupitia yale niliyojifunza

katika mkutano huu, ninaamini kuwa kila kilichoandikwa ndani

ya Qura’an miaka elfu moja mia nne iliyopita lazima ni kweli,

na sayansi inaweza kulithibitisha.

kwa kuwa Mtume Muhammad hakuwa akisoma wala kuandika,

lazima Muhammad atakuwa Mtume aliyetangaza ukweli huu

ulioteremshwa kwake kama nuru kutoka kwa Muumba wa

kweli. Muumba huyu lazima atakuwa ni Allah.

Page 11: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

11

Nadhani huu ni muda muafaka wa kutamka La ilaha illa Allah,

hakuna mungu anayesathiki kuabudiwa isipokuwa Allah,

Muhammad rasoolu Allah, Muhammad ni Mjumbe wa Allah...

Kitu cha thamani zaidi ambacho nimekipata katika kongamano

hili ni La ilaha illa Allah, na kuwa Mwislamu."

Dr. Maurice Bucaille

Akiwa amezaliwa mwaka 1920, Mkuu wa zamani wa Kliniki ya upasuaji, Chuo kikuu cha Paris, kwa muda mrefu amekuwa

akijishughulisha na kufanya uchunguzi na kufanya mlinganisho baina ya mafundisho ya Maandiko Matakatifu na elimu ya kisasa ya kisekula.

Ni mwandishi wa kitabu kinachonunuliwa zaidi cha "The Bible, The Qur'an and Science" (1976). Usomaji wake wakina wa lugha za maandiko matakatifu, ikiwa ni pamoja na Kiarabu, kwa kuhusisha maarifa yake ya maandiko ya hairoglifu, umemuwezesha kufanya utafiti wa kina, ambapo mchango wake binafsi kama daktari umetengeneza hoja zenye kuondoa shaka. Kitabu chake kiitwacho, "Mummies of the Pharaohs - Modern Medical Investigations" (St. Martins Press, 1990), kilishinda Tuzo ya Historia kutoka Académie Française na tuzo nyingine kutoka Chuo cha tiba cha Ufaransa (French National Academy of Medicine). vitabu vyake vingine ni pamoja na: "What is the Origin of Man" (Seghers, 1988), "Moses and Pharaoh, the Hebrews in Egypt", (NTT Mediascope Inc, 1994); and "Réflexions sur le Coran" (Mohamed Talbi & Maurice Bucaille, Seghers, 1989)

Baada ya utafiti uliodumu kwa kipindi cha miaka kumi, Dr.

Maurice Bucaille alikihutubia chuo cha tiba cha Ufaransa mwaka 1976 kuhusu uwepo wa maelezo kadhaa ndani ya Qur’an yanayozungumzia fiziolojia na mfumo wa uzazi wa binadamu. Sababu yake ya kufanya hivyo ni:

"...maarifa yetu juu ya misingi hii ni kwamba,

haiwezekani kufafanua jinsi maandiko fulani katika

enzi za Qur’an yangeweza kuwa na mawazo

yamegunduliwa tu katika nyakati za hivi karibuni."

"Uchunguzi huo unaifanya nadharia iliyoibuliwa na

wale wanaomuona Muhammad kama mtunzi Qur’an

kuwa nadharia dhaifu isiyoweza kusadikika wala

kutetewa. Mtu amabaye hakusoma aliwezaje kuwa

mtunzi / mwandishi mkubwa, kwa uandishi

maridhawa, katika fasihi nzima ya Kiarabu? Kisha

Page 12: Wasemavyo Wanasayansi Kuhusu Qur'an

12

aliwezaje kutamka ukweli wa sayansi ya maumbile

ambayo hakuna binadamu mwingine aliyeweza

kuyavumbua wakati huo, na yote haya aliyaeleza bila

kukosea hata kidogo katika uelezeaji wa suala husika?"