yaliyomo - home | ilala municipal council...daktari mfawidhi wa hospitali hiyo, sophinias ngonyani...

12

Upload: others

Post on 02-Feb-2021

4 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 2

    YALIYOMO

    Gazeti hili la Habari Ilala, ni gazeti la kila Mwezi

    linalotolewa na Manispaa ya Ilala, Ambapo ndani

    yake utaweza kusoma Habari mbalimbali na matukio

    yaliyojiri Ndani ya Manispaa ya Ilala kwa kipindi cha

    mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa

    Miradi ya kimaendeleo

    TAHARIRI

    UTANGULIZI

    UPULIZAJI WA DAWA YA DENGUE

    MAENEO YA KATA YA MCHIKICHINI

    MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

    HUDUMA BORA ZA AFYA ZAVUTA WENGI HOSPITAL YA MNAZIMMOJA

    JITIHADA ZA KUTOKOMEZA KIPINDUPINDU NA

    DENGUE ZAENDELEZWA ILALA

    WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI 2019

    MADIWANI ILALA WAMCHAGUA KUMBILAMATO

    KUWA MEYA MANISPAA YA ILALA

  • 3

    UTANGULIZI

    H almashauri ya Manispaa ya Ilala ni miongoni mwa Manispaa tano zinazounda jiji la Dar es salaam. Kwa mujibu wa makadirio ya watu Tanzania ya mwaka 2018, Halmashauri inakadiriwa kuwa na jumla ya wakazi wapatao 1,648,849 { wanaume

    805,003 na wanawake 843,846 }

    Idara ya Afya ni mojawapo kati ya idara 13 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Usimamizi wa shughuli za idara unafanywa na

    Bodi ya Halmashauri ikishirikiana na kamati ya uendeshaji wa Huduma za Afya { CHMT } inayoongozwa na Mganga mkuu wa

    Manispaa.

    1

    Udhibiti wa ugonjwa wa malaria umeendelea ambapo jumla ya lita 212.5 za viuwa dudu zimezimetplewa kwa ajili ya kupulizia

    kwenye mazalio yenye viluwiluwi wa mbu katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2019. Aidha kwa upande wa ugonjwa wa Dengue

    umeendelea jumla ya Wagonjwa 1,110 walilipotiwa kutoka vituo vinavyotoa huduma. Uelimishaji jamii juu ya Dengue

    umeendelea katika maeneo walipotoka wagonjwa.

    Idara ya Afya imegawanyika sehem kuu mbili za kiutendaji ambazo ni kamati ya menejimenti ya huduma za Afya { Management

    Committee } pamoja na kamati ya utendaji { Technical Committe }.Aidha idara ina jumla ya Watumishi 1104 katika vituo vya

    serikali, Vituo vinavyotoa tiba ni 313 ambapo 37 ni vituo vya serikali na majeshi na vituo 229 ni vya watu binafsi na mashirika ya

    Dini.

    Kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2019 Magonjwa 10 yaliyoongoza katika vituo vya tiba kwa wagonjwa wa nje

    UMRI CHINI YA MIAKA MITANO UMRI ZAIDI YA MIAKA MITANO

    NA. UGONJWA IDADI ASILIMIA UGONJWA IDADI ASILIM-IA

    1. Magonjwa ya njia ya hewa 30,482 20.7 Magonjwa ya njia ya hewa 42210 12.8

    2. Magonjwa ya njia ya mkojo 17,806 12.3 Magonjwa ya njia ya mkojo 53331 16.1

    3. Homa ya mapafu 12,570 8.5 Homa ya mapafu 8247 2.5

    4. Magonjwa ya Ngozi 10,407 7.1 Magonjwa ya Ngozi 14091 4.2

    5. Kuharisha 9,310 6.3 Shinikizo la damu 18,696 5.7

    6. Minyoo 6,394 4.3 Minyoo 6908 2.1

    7. Magonjwa ya matumbo 6,191 4.2 Magonjwa ya matumbo 11659 3.5

    8. Malaria 4,644 3.1 Malaria 14230 4.3

    9. Magonjwa ya masikio 3,161 2.1 Magonjwa ya kinywa cha meno 16,092 4.8

    10. Anaemia 2,941 2 Kisukari 9208 2.7

    JUMLA 103,906 70.6 194,672 58.7

  • 4

    UMRI CHINI YA MIAKA MITANO UMRI ZAIDI YA MIAKA MITANO

    NA. UGONJWA IDADI ASILIMIA UGONJWA IDADI ASILIMIA

    1. UTI 5 4.2 UTI 38 9.1

    2. Upungufu wa damu 14 11.7 Upungufu wa damu 30 7.1

    3. Homa ya mapafu 16 13.4 Homa ya mapafu 6 1.4

    4. Majeraha ya moto 2 1.6 Kuharisha 26 6.2

    5. Kuharisha 15 12.6 Shinikizo la damu 31 7.4

    6. Utapiamlo 12 10.1 Utapiamlo 30 7.1

    7. Magonjwa ya matumbo 10 7.9 Magonjwa ya matumbo 25 5.9

    8. Malaria 13 11 Malaria 59 14.1

    9. Magonjwa ya akinamama 10 2.4

    10. UKIMWI 28 6.7

    JUMLA 72.5 67.4

    2

    Kwa kipindi cha Aprili hadi Juni 2019 Magonjwa 10 yaliyoongoza katika vituo vya tiba kwa wagonjwa wa ndani

    Katika kipindi cha Aprili hadi 2019 huduma za afya kwa wagonjwa wa kifua kikuu na ukoma zinaendelea

    kutolewa kama kawaida katika vituo vyote vya afya, zahanati na Hospitali za Serikali na kwenye baadhi ya

    vituo binafsi. Jumla ya wagonjwa wapya 1408 wa kifua kikuu na 8 wa ukoma waliandikishwa, Kati yao 523

    { 37.1% } walikutwa na vimelea { bacteria } vya kifua kikuu. Wagonjwa 44 walirudiwa na ugonjwa wa

    kifua kikuu , kiwango cha uponaji wa wagonjwa { treatment rate } wa kifua kikuu ni 94.2%.

    AINA YA WAGONJWA KIFUA KIKUU UKOMA

    Walioandikishwa wote kwa ujumla wao 1408 8

    Waliopimwa na kukutwa na vimelea vya kifua kikuu { wapya } 523

    Waliorudiwa na ugonjwa 44 3

    Wagonjwa waliokutwa na ulemavu wa { WHO-DG 1 na 2 } 0

    Watoto chini ya miaka 14 walipatikana na kifua kikuu 258

    Wagonjwa wa kifua kikuu sugu 24

    UDHIBITI WA KIFUA KIKUU NA UKOMA

  • 5

    Daktari Ngonyani anaeleza kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kuhudumia watu 800 hadi 1000 na kusisitiza haitoi huduma kwa wakazi wa jiji pekee bali hata wanaotoka nje ya wilaya ya Ilala ikiwemo Wilaya ya Ki-nondoni, Mkuranga, Kisarawe, Bagamoyo, Chalinze, Pwani na Kigamboni. Anabainisha kuwa katika kuhakikisha hospitali inaendelea kutoa huduma bora za afya kwa ufanisi, vitengo mbalimbali vinafanya kazi zake kwa ufanisi kikiwemo Kitengo cha Wagonjwa wa nje, Idara ya wagonjwa wa ndani wakiwemo wajawazito wanaosubiri kujifungua, wodi ya wakinamama wanaojifungua kwa upasu-aji. Daktari Ngonyani anafafanua kuwa kitengo cha Maabara ya kisasa kinahadhi ya nyota tatu na wataalam wanafanya kazi kwa ufanisi ambapo vipimo vya damu, mkojo, homoni, pamoja na kipimo cha kuotesha wadudu kwa ajili ya tiba hutolewa (culture).

    3

    HUDUMA BORA ZA AFYA ZAVUTA WENGI HOSPITAL YA MNAZIMMOJA

    H ospitali ya Mnazi Mmoja ni hospitali iliyopo katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kabla ya kupandishwa hadhi kuwa hos-pitali ilikuwa Zahanati mwaka 1950 ikihudumia wakazi jijini humo na ilipofika mwaka 1990 ilipewa hadhi ya kuwa Kituo cha Afya. Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Sophinias Ngonyani anasema mwaka 2012 ilipewa hadhi ya kuwa hospitali ambapo iliendelea kutoa huduma kwa wakazi wa Kata za Jangwani, Mchikichini, Upanga, Kivukoni na Mchafukoge.

    Dkt. Sophinias Ngonyani Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mnazi

    mmoja

  • 6

    WAZIRI UMMY ASHIRIKI ZOEZI LA UPULIZAJI WA DAWA YA DENGUE MAENEO YA

    KATA YA MCHIKICHINI

    W aziri wa Afya ,Jinsia, wazee na Watoto Mh.Ummy Mwalimu ameshiriki zoezi la upuliziaji wa dawa ya Dengue maeneo ya Kata ya Mchikichini katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala akiongoza-

    na na Mbunge wa Ilala Mussa Hassani Zungu, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ,Mkurugenzi

    wa Ilala Jumanne Shauri pamoja na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Amini Iddi.

    Kwa mujibu Waziri Ummy amesema takwimu za kata ya Mchikichini mwezi wa 5 zinaonyesha

    idadi ya wagonjwa wa Dengu 525 lakini kutokana na jitahada za Manispaa ya Ilala kufikia mwezi

    wa 6 wagonjwa wamepungua mpaka kufikia 207.

    4

    Huduma ya kinywa na meno Hospital ya Mnazi mmoja imeendelea kutoa huduma bora za kinywa na meno ambapo kwa mwaka jumla ya wagonjwa wanaohudumiwa huweza kufikia 880 kwa mwezi. Kitengo cha Macho Mtaalamu kutoka Kitengo cha Macho Ali Nganyagwa anasema kitengo hicho hutoa huduma ya upimaji macho na utengenezaji wa miwani kwa gharama nafuu. Mtalaamu huyo anafafanua kuwa wagonjwa wanaokuja hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa tiba mbalimbali za macho hupitia hatua mbalimbali ziki-wemo za kupitia kwa mtalaam wa kuangalia aina ya tatizo linalomsumbua mgonjwa kwa vipimo maalum na baadaye hupatiwa matibabu ya miwani kwa gtharama nafuu kulingana na tatizo la mgonjwa. Huduma ya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano Daktari Mfawidhi wa hospitali hiyo, Sophinias Ngonyani anasema baada ya huduma ya wakinamama waja-wazito na watoto chini ya miaka mitano kimechangia kuongezeka idadi ya wakinamama wanaokwenda ku-pata huduma hospitalini hapo ambapo kwa wastani kwa siku wakinamama 15 hupatiwa huduma.

    Daktari Mgaya anabainisha kuwa vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano hospitalini hapo vimepungua ambapo takwimu za mwaka 2014 kulikuwa na vifo 54, mwaka 2015 viipungua hadi 33, mwaka 2016 viliku-wa 23 huku mwaka 2017 vikitokea 21. Anafafanua kuwa hata idadi ya Wakinamama wanaojifungua imeongezeka kufuatia uboreshaji wa huduma hizo ambapo kuanzia mwaka 2015 walijifungua 3,373 , mwaka 2016 wamama 3,040, mwaka 2017 ni 3,795 huku mwaka 2018 wakijifungua 3,797.

    Mbali na kitengo hicho Daktari Ngonyani anaeleza Idara ya Famasia imefanyiwa ukarabati ambao umesaid-ia upatikanaji wa dawa kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa asilimia 93%.

    Daktari Sophinias anabainisha kuwa kuna Kitengo cha Huduma ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wagonjwa wahitaji na kwamba wagonjwa wanaopata matibabu kwa bima hiyo wametengewa eneo lao lenye huduma zote ikiwemo sehemu ya mapokezi, daktari, maabara na duka la dawa. Daktari Ngonyani anasema Kitengo cha Damu Salama kinafanya kazi ya kukusanya damu kwa ajili ya wagonjwa wenye mahitaji ambapo kwa wastani hukusanya chupa 15 kwa siku.

    Pia anasema, kuna Kitengo cha Tiba ya Mionzi (Ultra Sound na X-ray) hutolewa ambapo hospitali imenunua mashine mpya ya kisasa ya Ultra sound na mashine ya X-ray ya kidigitali ya kisasa ambayo hutoa huduma kwa wagonjwa 100 hadi 150 kwa siku.

  • 7

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema

    wananchi wanapaswa kuchukua hatua wenyewe za kupambana na homa ya Dengue na

    kusafisha mazingira bila kushurutishwa na wenyeviti wa mitaa kwa wale watakaokiuka

    watachukuliwa hatua ikiwemo kulipa faini kwa mujibu wa sheria.

    Akizungumza na mwandishi wa habari katika zoezi hilo kata ya Mchikichini mkazi

    mmoja ameuomba uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwazibia mitaro ya

    maji machafu ili kuepukana na mazalia ya mbu wanaoeneza Dengue.

    5

    Aidha Waziri amesema kipimo cha Dengue ni bure na hakuna kutozwa gharama yoyote

    ile, Ummy ameipongeza Manispaa ya Ilala kwa kununua vifaa kwa ajili ya kuuwa

    mbu wa Dengue.

    Pia amewashukuru Mkoa wa Dar-es-salaam hususani Halmashauri ya Manispaa ya Ila-

    la kwa kufanya unyunyuziaji wa dawa za kuuwa mbu wa Dengue kwa kununua

    mashine za kutumia mota na viuwadudu kwa fedha zao japokuwa wizara ilitoa lita

    2000 lakini Ilala iliongeza lita 5000 na kila lita moja ni shilingi 15500.

    Pia Ummy Mwalimu ni matarajio yake ifikapo tarehe 30 mwezi wa 7 kuwe hakuna

    tena homa ya Dengue Tanzania, ambapo ametaka kila mwananchi ,wenyekiti wa mitaa

    kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huu kwa kusafisha mazingira yao.

  • 8

    JITIHADA ZA KUTOKOMEZA KIPINDUPINDU NA DENGUE ZAENDELEZWA

    K amati ya Usimamizi huduma za Afya ya Manispaa ya Ilala (CHMT) katika kuendeleza jitihada za kutokomeza ugonjwa wa Dengue na Kipindupindu leo imefanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba katika

    Kata ya Jangwani Mtaa wa Mtambani pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali katika kudhibiti magonjwa

    hayo.

    Shughuli zilizofanyika katika Kata ya Jangwani mtaa wa Mtambani kwa kutembelea kaya kwa kaya ni

    pamoja na upulizaji wa dawa ya kuua viluwiluwi { Larviciding }, upulizaji wa dawa ya Lysol katika vyoo

    kuua vimeleo vya ugonjwa wa kipindupindu, kutambua kaya walizotoa wagonjwa wa kipindupindu na ku-

    puliza dawa pamoja na kuchukua sampuli za maji kwa ajili ya vipimo vya maabara.

    Zoezi la kupulizia Dawa ya Uuwaji wa Viluwi luwi likiendelea katika maeneo mbalimbali katika mtaa wa

    Mtambani

    Pichani ni baadhi ya watumishi wa Manispaa wa Idara yaAfya-

    wakitoka nyumba moja kwenda nyingine kutoa elimu

    Baadhi ya Wajumbe wa Kamati wakitoa Elimu juu ya

    Athari ya uuzaji wa vyakula na vinywaji visivyo salama .

    Aidha timu hii imetoa elimu ya Afya juu ya tahadhali ya ugonjwa wa Dengue na Kipindupindu kwa kutumia

    gari la matangazo pamoja na kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa

    sehemu za uuzaji wa vyakula .

    6

  • 9

    7

    H almashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na wadau inaendelea na utekelezaji wa afua mbalim-bali za VVU na UKIMWI. Utekelezaji wa afua hizo umekuwa ukisimamiwa na kamati ya kudhibiti UKIM-

    WI ya Halmashauri (CMAC) na kamati za UKIMWI za kata 36 na Mitaa 159. Hadi kufika mwaka

    2015/2016 utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI katika Halmashauri ulikuwa unategemea Zaidi fedha za

    ruzuku kupitia mfuko wa NMSF Grant. Baada ya ufadhili kupitia mfuko NMSF kukoma hapo mwaka

    2015/2016, Halmshauri ilichukua jukumu la kutenga bajeti kupitia mapato yake ya ndani.

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kama zilivyo Manispaa nyingine za jiji la Dar es salaam ina kiwango

    kikubwa cha maambukizi kwa asilimia 4.7 (THIS 2016/2017)

    Kiwango hiki kimeshuka ikilinganishwa na kile cha awali cha asilimia 6.9 (THMIS 2011/2012)

    BAADHI YA HUDUMA NA SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA KWA MWAKA 2018/2019

    • Uhamasishaji jamii juu ya hudum za VVU na UKIMWI kwa kutumia maonesho 20 vikundi vya Sanaa

    ambapo watu 9,608 kati yao wanaume 4,971 na wanawake 4,637 walihudhuria.

    • Kushirikiana na Asasi za vijana kuhamasisha vijana kujitokeza ili kupata huduma rafiki za VVU na

    UKIMWI kwa vijana zinazotolewa katika vituo 13 jumla ya vijana 22.464 ( wanaume 11,073 na wana-

    wake 11,391)walihudhuria.

    • Ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU na inayotolewa katika vituo 91 na huduma mkoba, watu

    257,299 walipata huduma hii (wanaume 108,157 na wanawake 257,133) kati yao watu 8,298 (wanaume

    2,761 na wanawake 5,537) sawa na asilimia 3.2% waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU.

    • Huduma rafiki kwa vijana (YFS) imetolewa kwa vijana katika vituo 13 ambapo vijana 10,217 walifiki-

    wa.

    • Usambazaji wa kondomu

    • Huduma ya ushauri na tiba ya magonjwa ya ngono inatolewa katika vituo 28. Katika hiki kipindi jumla

    ya watu 11,185 kati yao wanaume 2,097 na wanawake 9,088 walipatiwa huduma.

    Ushiriki wa Asasi

    • Asasi zote zinafanya kazi chini ya mtandao wa asasi wa Ilala (IMCSNet) unaongozwa na Mwenyekiti

    • Asasi huwakilishwa na mwakilishi wa Asasi katika CMAC ambaye si lazima awe wadhifa katika

    mtandao na huchaguliwa kila baada ya miaka 2.6

    • Asasi hukutana katika vikao vya wadau kila miezi 6 vinavyoandaliwa na Halmashauri na Asasi ili kufan-

    ya tathimini ya UKIMWI.

    • Asasi 54 zinashiriki kutoa taarifa kupitia mfumo wa TOMSHA.

    • Uanzishaji na uendelezaji wa mpango wa VICOBA kwa WAVIU ambao hadi sasa vikundi 66 vime-

    anzishwa (huduma hii itaongelewa Zaidi katika mada yake)

  • 10

    8

    VICOBA KWA WAVIU

    • Mpango ulioibuliwa kwa pamoja katika Halmashauri na uongozi wa WAVIU na kuanza mwezi February, 2011.

    • Mwezi machi,2011 vikundi 2 vya PEACE na IDINEPHA vilianzishwa vikiwa na jumla ya wanachama 30.

    • Hadi sasa vikundi 66 vyenye jumla ya wanachama 872 vimeanzishwa (wanawake 654 na wanaume 218).

    • Jumla ya hisa ziliozochangwa na wanachama hao hadi sasa ni 422,915,000.

    • WAVIU 15 wamepatiwa mafunzo ya T.O.T ili kuweza kuanzisha vikundi Zaidi.

    • Tangu kuanza kwa mpango huu Halmashauri imechangia jumla ya Tshs 122,480,000kwa ajili ya kuanzisha na

    kuendeleza vikundi hivi.

    • Shughuli zote zinazohusu WAVIU zimekuwa zikisimamiwa na KONGA iliyo na jukumu la kuongoza WAVIU

    walio katika Halmashauri.

    • Kupitia KONGA Ilala WAVIU huchagua mwakilishi wao katika CMAC.

    • Kuwepo kwa asasi nyingi zisizo na uhakika wa vyanzo vya rasilimali umekwamisha asasi hizo kutekeleza majuku-

    mu yao (asasi za mfukoni).

    • Mahitaji makubwa ya msaada wa fedha na chakula kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI na watoto yatima.

    WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI 2019

    K atika kuadhimisha wiki ya UNYONYESHAJI duniani, Manispaa ya ILALA inaungana na duniani nzima kuha-masisha , kutoa elimu, na unasihi juu ya umuhimu wa UNYONYESHAJI wa maziwa ya mama kwa watoto wachanga

    na wadogo. Katika maadhimisho manispaa imejipanga kuifikia jamii kwa kutoa elimu hiyo katika vituo vya kutoa

    huduma za afya na watoa huduma ngazi ya jamii ili kwa pamoja iweze kufanikisha dhana nzima ya Unyonye-

    shaji.

    Kwa kuzingatia umuhimu wa maziwa ya mama taratibu sahiihi za Unyonyeshaji zinapaswa kufuatwa kama mtoto

    kuanzia kunyonya maziwa ya mama ndani ya SAA moja mara baada yakujifungua, kunyonyesha mtoto Mara kwa

    Mara na kila anapohitaji na kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya mwanzo bila kumpa maji wala

    chakula.na kuhakikisha wananyonyesha vizuri kwa muda usiopungua miaka miwili.

    Wazazi wanapaswa kutomwanzishia mtoto vyakula vya nyongeza kabla ya miezi sita ya mwanzo ilikuepukana na

    changamoto mbalimbali za kiafya hasa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano..

    Kauli mbiu kwa mwaka 2019

    *WAWEZESHE WAZAZI KUFANIKISHA UNYONYESHAJI*.

    Aliyebeba mtoto pichani ni Bibi Flora, Afisa lishe Manispaa ya Ilala

  • 11

    9

    MADIWANI ILALA WAMCHAGUA KUMBILAMATO KUWA MEYA MANISPAA YA ILALA

    B araza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala leo tarehe 31 Julai, 2019 lilifanya uchaguzi wa kuziba nafasi ya Umeya iliyokuwa imeachwa wazi baada ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala

    Bw. Charles Kuyeko kujiuzilu. Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkutano wa

    Arnatoglou wajumbe walimchagua Omary Kumbilamoto kuingoza Manispaa hiyo. Kumbilamoto ambaye

    alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala alichaguliwa baada ya kupata kura 41 kati ya kura 55 zilizopig-

    wa na kumshinda mgombea mwengine wa nafasi hiyo ya umeya Mhe Greyson Selestine aliyepata kura 14.

    Uchaguzi huo ulisimamiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Bibi Sheila Likuba

    Kabla ya uchaguzi huo kuanza majira ya saa 10:30 asubuhi wagombea wote wawili walipewa nafasi za

    kujinadi kwa wapiga kura wao ambao ni madiwani pamoja na wabunge wa Manispaa ya Ilala, mgombea

    kutoka chama cha Chadema bwana Greyson Selestini alikuwa wa kwanza kupewa nafasi ya kujinadi kabla

    ya mewnzake wa chama Chama Mapinduzi, ndugu Omary Kumbilamoto’

    Kabla ya kupiga kula wajumbe waliomba mwongozo wa kisheria baada ya msimamizi wa uchaguzi

    kutangaza kwamba ”uchaguzi huu utakuwa tofauti na chaguzi zingine badala ya kuweka tiki kwa picha ya

    mgombea basi watapaswa kuandika jina la mgombea moja kwa moja”

    Jumla ya wapiga kura wote walikuwa hamsini na tano, na hakuna kula iliyoharibika. Ndugu Greyson

    mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo alipata kula 14 sawa na asilimia 25% na ndugu Omary

    Kumbi la Moto toka CCM kupata kura 41 sawa na asilimia 74.5 hivyo Omary Kumbil la Moto toka ccm

    kutagazwa mshindi na Kutawazwa kuwa Meya mpya wa Manispaa ya Ilala.

    Baada ya uchaguzi huo wagombea wote wawili waliweza kutoa neno la shukran kwa wapiga kura wao,

    mgombea toka Chadema bwana Greyson, amesema “katika maisha mnaposhindana wawili au watatu lazima

    mmoja awe mshindi japo inauma lakini sina budi nimpongeze tu mwenzangu kwa ushindi alioupata” naye

    Meya aliechaguliwa hakusita kuonesha furaha yake nakusema, “asanteni sana kwa kuniamini nakunichagua

    katika nafasi hii nitoe pia pongezi kwa chama changu cha Mipinduzi kwa imani yao kwangu napenda ku-

    wahakikishia kwamba nitawajibika kwa nafasi yangu katika kuwatumikia wananchi wa manispaa ya Ilala”

    Meya wa Halmashauri ya Manispaa

    ya Ilala Omari Kumbilamoto akiwashukuru

    wajumbe kwa kumchagua kuiongoza Manispa

  • 12