لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya qiyâma, malipo mema,...

200
ليـــم ال قـــيا لSWALA ZA USIKU, QIYAM NA TARAWIH Kutoka katika Vitabu vya: ايو ا ا ر ىاّ ه الشيخSheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI [Na Wanavyuoni wengine] MKUSANYAJI: تـا ر اّ ه الشيخSheikh Muhammad al-Jibaly MFASIRI: خ ا أة فسيرة رّ ه اد ةاسAbu Farida Muhammad Awadh Salim Basawad

Upload: others

Post on 23-Sep-2019

106 views

Category:

Documents


2 download

TRANSCRIPT

Page 1: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

لقـــيام الليـــ

SWALA ZA USIKU, QIYAM NA TARAWIH

Kutoka katika Vitabu vya:

الشيخ حمهر ىارص ادليو األبلاينSheikh Muhammad Nasir ud-Deen al-AlbaanI

[Na Wanavyuoni wengine]

MKUSANYAJI:

الشيخ حمهر اجلتـايل

Sheikh Muhammad al-Jibaly

MFASIRI:

ادحمهر فسيرة أة األخ ةاسAbu Farida Muhammad Awadh Salim Basawad

Page 2: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Haki Ya Uchapishaji

© HAKI YA UCHAPISHAJI

Uchapishaji wa kitabu hiki ni milki ya kiufundi ya “THE QURAN AND SUNNAH SOCIETY OF EAST AFRICA”. Kila kilichomo ndani, kwa ujumla, ni hifadhi ya qssea. Hairuhusiwi kuiga kwa njia yoyote iwayo kutoka kwa wachapishaji asili; hivyobasi uchapishaji wa kitabu hiki utahitaji ridhaa kutoka kwa muandishi. Iwapo chochote kutoka kwenye kitabu hiki kitatumiwa kama sehemu ya shirika jengine la kiufundi ama isokuwa hivyo, basi ruhusa kutoka QSSEA itahitajika.

Ruhusa inaweza kuombwa kutoka kwa: The Qur‟an and Sunnah Society of East Africa, P. O. Box 85477, Mombasa, Kenya. Ama kwa Barua Pepe (e-mail)- [email protected] web-site – www.qssea.net Chapa ya Kwanza: Nakala 1000 [2014 / 1435] ISBN: 978-9966-1824-3-2

JUMUIYA YA QUR’AN NA SUNNAH YA AFRIKA YA MASHARIKI

Page 3: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

MEZA YA YALIYOMO

UTANGULIZI ......................................................................................................... XV

UTANGULIZI WA MFASIRI ............................................................................... XVII

DIBAJI .................................................................................................................... 1

Da‟wa Na Malengo Yetu .....................................................................................3

MWANZO ................................................................................................................ 9

KITABU HIKI .........................................................................................................9

KAZI ILIYOFANYIKA KWENYE KITABU HIKI ..................................................10

SHUKRANI ..........................................................................................................12

MLANGO 1 ............................................................................................................ 14

UTANGULIZI WA MUANDISHI ............................................................................. 14

FITNA YA UJINGA .............................................................................................14

SABABU YA KUANDIKA KITABU HIKI .............................................................16

MADA KUBWA ....................................................................................................16

IDADI YA RAK‟ĀT ..............................................................................................16

MADA NYENGINEZO .........................................................................................18

UJUMBE WENYE MALIPO MAKUBWA ............................................................18

MLANGO 2 ............................................................................................................ 20

QIYĀM .................................................................................................................. 20

Page 4: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

QIYĀM, TARĀWĪH NA WITR ............................................................................... 20

UFAFANUZI .........................................................................................................20

KUTOELEWEKA .................................................................................................21

TARĀWĪH.............................................................................................................21

FADHLA ZA QIYĀM .............................................................................................. 22

SWALA BORA YA SUNNAH ..............................................................................23

KUHIFADHIWA KUTOKAMANA NA UCHAWI WA SHEITWĀN .....................24

ISHARA ZA SHUKRANI ......................................................................................24

ISHARA YA WEMA .............................................................................................25

SABABU YA KUINGIA PEPONI .........................................................................25

KUKUBALIWA MAOMBI .....................................................................................25

KUJIKURUBISHA KWA ALLĀH .........................................................................27

REHMA KUTOKA KWA ALLĀH.........................................................................27

MIONGONI MWA WATU WEMA ZAIDI .............................................................27

AMALI ZA KUDUMU HUDHAMINI MALIPO MARIDHAWA .............................28

FADHLA ZA QIYĀM KATIKA MWEZI WA RAMADHĀN ....................................... 29

MSAMAHA WA MADHAMBI ...............................................................................30

MIONGONI MWA WATU WEMA .......................................................................30

KUAMKA KWA AJILI YA QIYĀM ......................................................................31

KUTAWADHA NA KUPIGA MSUAKI .................................................................... 31

Page 5: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

KUMTAJA ALLĀH ..............................................................................................31

KIWANGO CHA SAUTI ......................................................................................34

MLANGO 3 ............................................................................................................ 35

LAYLAT UL-QADR ............................................................................................... 35

MAANA YAKE .....................................................................................................35

UTUKUFU WAKE ...............................................................................................35

NI USIKU GANI? .................................................................................................38

RAI NA RIWAYA MBALIMBALI .........................................................................38

NYUSIKU KUMI ZA MWISHO ZA RAMADHĀN ................................................38

USIKU WA ISHIRINI NA MOJA .........................................................................39

USIKU WA ISHIRINI NA SABA ..........................................................................40

KWA MUKHTASARI ...........................................................................................41

JINSI YA KUITAFUTA LAYLAT UL-QADR ......................................................41

KUSWALI QIYĀM ...............................................................................................41

KUOMBA DU‟Ā‟ .................................................................................................42

KUJITENGA NA ANASA ZA KILIMWENGU KWA AJILI YA KUFANYA

IBĀDAH ...............................................................................................................42

ALAMA ZA LAYLAT UL-QADR ............................................................................ 43

ALAMA ZILIZOSWIHI .........................................................................................43

HADITHI ZA NGANO ZISIZO NA MSINGI .........................................................44

Page 6: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

MLANGO 4 ............................................................................................................ 46

KUSWALI TARĀWĪH KWA JAMĀ‟AH .................................................................. 46

SUNNAH YA MTUME .........................................................................................46

KUJUZISHA KWA MTUME ................................................................................46

KITENDO CHA MTUME .....................................................................................47

HIMA YA MTUME ...............................................................................................52

SABABU ZA KUTOENDELEZA QIYĀM KWA JAMĀ‟AH....................................... 54

„UMAR AHUISHA SUNNAH .................................................................................. 54

KITENDO CHA „UMAR .......................................................................................54

UFAHAMU WA „UMAR ......................................................................................56

UAMUZI WA MAKOSA KUTOKANA NA KITENDO CHA „UMAR....................57

KUELEWA KIMAKOSA 1....................................................................................57

KUELEWA KIMAKOSA 2....................................................................................57

WANAWAKE KUHUDHURIA JAMĀ‟AH ............................................................... 60

MLANGO 5 ............................................................................................................ 62

IDADI YA RAK‟ĀT ZA QIYĀM .............................................................................. 62

UTANGULIZI .......................................................................................................62

KUISWALI TARĀWĪH KWA JAMĀ‟AH ................................................................62

IDADI YA RAK‟ĀT ALIZOSWALI MTUME (صلى اهلل عليه وسلم) ...................63

Page 7: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

RIWAYA YA „Ā‟ISHAH .......................................................................................63

RIWAYA YA JĀBIR .............................................................................................65

RIWAYA YA IBN „ABBĀS ILIYO DHA‟ĪF ..........................................................66

RIWAYA KUTOKA KWA ‟UMAR .......................................................................69

„UMAR AAMRISHA WATU KUSWALI RAK‟ĀT KUMI NA MOJA ....................69

UDHAIFU WA RIWAYA ZA RAK„ĀT ISHIRINI .................................................71

Riwaya ya „Abd ur-Razzāq ...............................................................................71

Riwaya ya Ibn Khusayfah .................................................................................72

Riwaya ya Ibn Abī Dhubāb ...............................................................................75

Riwaya ya Yazīd Bin Rūmān ............................................................................76

Riwaya ya Yahyā Bin Sa„īd: .............................................................................76

MSIMAMO WA ASH-SHĀFI‟Ī NA AT-TIRMIDHĪ ...............................................77

RIWAYA DHAIFU ZISIZOWEZA KUTILIANA NGUVU .....................................79

UWEZEKANO WA MAPATANO ........................................................................81

RIWAYA KUTOKA KWA MASWAHABA WENGINE .............................................. 82

RIWAYA KUTOKA KWA „ALĪ ............................................................................... 82

Riwaya ya Abū al-Hasnā‟ .................................................................................82

Riwaya ya Hammād Bin Shu‟ayb ....................................................................83

RIWAYA KUTOKA KWA UBAYY BIN KA‟B .......................................................... 84

Riwaya ya „Abd ul-„Azīz Bin Rafī‟ ...................................................................84

Page 8: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

Riwaya Ya Abū Ja‟far Ar-Rāzī .........................................................................85

RIWAYA KUTOKA KWA IBN MAS‟ŪD ................................................................. 86

MASWAHABA WALIAFIKIANA VIPI? ................................................................... 87

IDADI YA RAK‟ĀT YA TARĀWĪH YENYE KURUHUSIWA ................................. 90

SUNNAH ZA MTUME NA MASWAHABA ZAKE ...............................................90

JEE, “ZIYADA” NI NZURI KILA MARA ? ........................................................92

SWALA ZA NAFL ZILIZODHIBITI ......................................................................... 94

MAANA YA BID‟AH ............................................................................................96

BAADHI YA MATAMSHI YA KI-UWANACHUONI ............................................97

KUBAINISHA BAADHI YA SHAKA ZILIZOWEKWA .........................................99

IKHTILAFU MIONGONI MWA WANAVYUONI .................................................99

HAKUNA MAANDIKO YENYE KUKATAZA NYONGEZA .............................. 102

TEGEMEO JUU YA KAULI ZA UJUMLA ....................................................... 103

KUWADHARAU (KUWATWEZA) WANAVYUONI WAKUBWA .................... 105

USALAMA KATIKA KUSHIKAMANA NA SUNNAH ............................................. 107

Kuswali Kwa Rak‟āt Chache Kuliko Kumi Na Moja ................................ 108

MLANGO 6 .......................................................................................................... 111

JINSI YA KUSWALI QIYĀM ................................................................................ 111

DU‟Ā‟ YA KUANZIA QIYĀM ................................................................................. 111

RIWAYA YA IBN „ABBĀS .................................................................................. 111

Page 9: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

RIWAYA YA „ĀISHAH ....................................................................................... 113

RIWAYA YA ABŪ SA‟ĪD .................................................................................... 114

USOMAJI KATIKA QIYĀM .................................................................................. 115

MAFUNDISHO YA MTUME ............................................................................. 115

MAFUNDISHO YA „UMAR .............................................................................. 117

UREFU WA SAWA KATIKA USOMAJI........................................................... 117

USOMAJI KATIKA RAK‟ĀT TATU ZA WITR ................................................ 118

WAKATI WA QIYĀM ........................................................................................... 118

NJIA MBALIMBALI ZA KUITEKELEZA (SWALA YA) QIYĀM ............................. 120

SAMPULI YA KWANZA ................................................................................... 120

SAMPULI YA PILI ............................................................................................ 123

SAMPULI YA TATU ......................................................................................... 124

SAMPULI YA NNE ........................................................................................... 125

SAMPULI YA TANO ........................................................................................ 126

SAMPULI YA SITA ........................................................................................... 127

SAMPULI NYENGINE ...................................................................................... 128

RAK‟ĀT TATU ZA MWISHO ............................................................................... 129

ZINAZOTAFAUTIANA NA MAGHRIB ............................................................ 129

UFAHAMU WA IBN NASR .............................................................................. 129

KUPATANISHA BAINA YA RIWAYA MBILI ................................................... 132

Page 10: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

HATIMA KUHUSU QIYĀM .................................................................................. 133

QUNŪT ............................................................................................................. 133

YAKUPASAYO KUSEMA MWISHONI MWA WITR ........................................ 133

RAK‟ĀT MBILI BAADA YA WITR ................................................................... 134

MAS‟ALA ANUWAI (TAFAUTI TAFAUTI) YANAYOHUSIANA NA WITR .......... 135

WITR MOJA KATIKA KILA USIKU MMOJA .................................................. 135

KUIKOSA SWALA YA WITR ........................................................................... 136

KUISWALI WITR JUU YA WANYAMA ........................................................... 137

MLANGO 7 .......................................................................................................... 138

QUNŪT ............................................................................................................... 138

MAANA YA QUNŪT ............................................................................................. 138

SABABU HASWA ZA KULETA QUNŪT .............................................................. 140

KUTOKEAPO MIKASA .................................................................................... 140

MATUKIO MUHIMU YENYE KUWAATHIRI WAISLAMU .............................. 142

QIYĀM NA WITR ............................................................................................. 143

NI SWALA ZIPI ZA FARADHI? ....................................................................... 143

SWALA ZOTE .................................................................................................. 143

SUNNAH ILIYOHAMWA .................................................................................. 143

WAKATI WA FAJR? ........................................................................................ 144

KABLA AU BAADA YA RUKŪ‟? ..................................................................... 146

Page 11: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

BAADA YA RUKŪ‟ .......................................................................................... 146

KABLA YA RUKŪ‟ ........................................................................................... 146

QUNŪT YA WITR ............................................................................................ 147

HATIMAE ......................................................................................................... 148

MAS‟ALA ANUWAI. (MENGINEO) ..................................................................... 148

KUISOMA QUNŪT KWA SAUTI ..................................................................... 148

KUITIKIA ĀMĪN ................................................................................................ 149

KUINUA MIKONO ............................................................................................ 149

Yanayopaswa Kusemwa Wakati Wa Qunūt Ya Witr .............................. 150

UZUSHI NA UPOTOFU ....................................................................................... 152

KUPANGUSA USO ........................................................................................... 152

KUITANGULIZA QUNŪT KWA TAKBĪR ........................................................ 153

QUNŪT NDEFU ............................................................................................... 153

KUOMBOLEZA NA KULIA .............................................................................. 153

MLANGO 8 .......................................................................................................... 155

I‟TIKĀF ............................................................................................................... 155

UFAFANUZI ........................................................................................................ 155

HUKMU ............................................................................................................ 155

RIWAYA DHA‟ĪF .............................................................................................. 157

HIKMA NA ADABU ZA I‟TIKĀF .......................................................................... 158

Page 12: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

HIKMA .............................................................................................................. 158

ADABU KATIKA WAKATI WA I‟TIKĀF ......................................................... 159

WAKATI WA MWAKA ..................................................................................... 159

MAHALI PA KUFANYA I‟TIKĀF ..................................................................... 160

MSIKITI WA IJUMAA ...................................................................................... 160

MSIKITI MITATU MITAKATIFU ...................................................................... 161

NYUMBANI? ..................................................................................................... 162

MASHARUTI YA I‟TIKĀF ................................................................................ 162

Kukaa Mumo-Humo Msikitini ........................................................................ 162

KUFUNGA (SWAUM) ...................................................................................... 163

Nyakati Za Kuanza Na Kumaliza ................................................................ 163

Siku Zake Kwa Uchache .............................................................................. 164

MAMBO YANAYORUHUSIWA WAKATI WA I‟TIKĀF ......................................... 164

Kuondoka Msikitini Kwa Haja ..................................................................... 164

Kutawadha Ndani Ya Msikiti ......................................................................... 165

Kusimamisha Hema Ndani Ya Msikiti........................................................ 165

Kutumia Godoro ............................................................................................ 166

MAMBO YASIYORUHUSIWA WAKATI WA I‟TIKĀF........................................... 166

Kuondoka Msikitini Pasi Na Haja ............................................................... 166

Kuingiliana Kimapenzi ................................................................................. 166

Page 13: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

Kujishughulisha Na Malimwengu ............................................................... 167

I‟TIKĀF YA WANAWAKE ................................................................................... 167

MLANGO 9 .......................................................................................................... 170

KATIKA KUITIMIZA SWALA KIKAMILIFU .......................................................... 170

UNYENYEKEVU KATIKA SWALA .................................................................. 170

RIWAYA ZITOKAZO KWA MTUME NA MA-SALAF ..................................... 170

UNYENYEKEVU ULIOPOTEA ........................................................................ 172

MITAZAMO YA MUANGAZA .......................................................................... 173

HADĪTH ZINAZOHUSIANA NA KUIMARIKA KWA SWALA ................................ 173

HATIMA .............................................................................................................. 177

MLANGO 10........................................................................................................ 179

MUKHTASARI ..................................................................................................... 179

NUKTA MUHIMU ................................................................................................ 179

Kuswali Tarāwīh Kwa Jamā‟ah Ni Sunnah.................................................. 179

Idadi Ya Sawa Katika Sunnah Ni Kumi Na Moja ......................................... 179

Maoni Yetu Juu Ya Wale Wanaopinga ......................................................... 180

Sunnah Ni Bora Kuliko Nyongeza ................................................................. 180

„Umar Aliihuisha Sunnah ............................................................................... 180

Maswahaba Hawakuswali Ishirini ................................................................. 180

Hakuna Ruhusa Kwa Kuongeza .................................................................... 180

Page 14: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Yaliyomo Qiyâm ul-Layl

Wanavyuoni Wapinga Nyongeza .................................................................. 181

Msimamo Kutoka Kwa Wanavyuoni Wakubwa ........................................... 181

Kupoteza Unyenyekevu ................................................................................. 181

Kuswali Kwa Uchache Kuliko Kumi Na Moja .............................................. 181

Sampuli Mbali Mbali Za Kuswali Qiyām ...................................................... 181

MWISHO KABISA ................................................................................................ 182

Page 15: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Utangulizi

UTANGULIZI

“Neno La Awali”

Kila aina ya shukrani zamstahiki Allâh (سبحانه وتعاىل) kisha swala

na salamu zimfikie mtukufu wa daraja, Mtume Muhammad ( صىل اهلل .pamoja na aqraba zake na Maswahaba wote ,(عليه وسلم

KITABU JALILI HIKI KINATOKA

KISICHO MITHALI YA KUKADIRIKA

TAFSIRI JAMILI ILIYO JAMILIKA

Ndugu zangu wapendwa, nimebahatika kukisoma kitabu hiki cha tafsiri ya “SWALA ZA USIKU, QIYÂM NA TARAWÎH”, kutokana na vitabu viwili vilivyoandikwa na Mwanachuoni mwema, Al-Imâm

Nâsirud Dîn al-Albânî (رحمه اهلل), mjuzi aliye na utaalamu mpana

katika zama hizi zetu katika fanni ya hadithi na fiqhi. Nimekiri ni kitabu kilichojaa faida tele kwa umma wetu wa ki-Islamu, na ni muhimu tukisome siku zote, sio Ramadhani peke yake. Tukirejelee kila tunapoinuka usiku wa manane kutekeleza ibada ya Qiyâm ul-Layl.

Nataraji kitawafaa mno wanaounga mkono msimamo wa al-„Allâmah al-Albânî kuhusu swala za usiku, na pia watanufaika zaidi walio na maoni tafauti na Sheikh ili warudie na kuhakikisha mategemeo yao mara kwa mara.

Page 16: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Utangulizi

Allâh ( وتعاىل سبحانه ) aibariki Jumuiya ya (QSS YA EAST-AFRICA) na

amtakabalie ndugu mpendwa, Abu Farida Muhammad Basawad na wenzake, nawashukuru kwa kunipa fursa hii, si kwa sababu yoyote, bali tu nami nishiriki katika amali hii ya kheri.

MWISHO MOLA AUMBAO NAMUOMBA KIMALIZA

ATUSAFISHE MASIKIO YAWE MEMA KUSIKIZA

MANHAJI TUAMBIWAO SHIRIKIANE KUYATIMIZA.

Abu Hâmid Shariff „Abdallah Juma

Ustâdh – Markaz Tawhîd, Mombasa

4th Sha‟bân, 1435 A.H

2nd June, 2014 A.D

Page 17: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Utangulizi

UTANGULIZI WA MFASIRI

Kila sifa njema zinamstahiki Allâh ( وتعاىل سبحانه ), muumba wa

Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake, tunamsifu yeye, tunamuomba msaada wake na tunamuomba msamaha. Tunajilinda kwa Allâh kutokana na uovu wa nafsi zetu na uovu wa vitendo vyetu.

Yoyote ambaye aliyeongozwa na Allâh, basi hapana yoyote awezae kumpotoa na yoyote ambaye Allâh amemuacha atokomee basi hapana awezae kumuongoa. Nashuhudia yakwamba hapana aliye na hakki ya kuabudiwa isipokuwa Allâh peke yake, pasi na mshirika wa aina yoyote. Na nashuhudia yakwamba Muhammad ni mtumwa na Mtume wa Allâh.

Amma ba‟d:

Kitabu hiki ni tafsiri ya mfumo ulio swahīh ya vitabu viwili vilivyoandikwa na Al-„allâmah (mwanachuoni mkubwa) Muhammad Nâsir ud-Dîn al-Albānî kiitwacho Swalāt ut-Tarawêh na Qiyām Ramadhān. Malengo ya vitabu hivyo ni kuwazindua watu wa kawaida katika kuifahamu Sunnah ya swala za usiku, na walillahi-l-hamd, natija yake imedhihirika kwenye Misikiti mingi. Kitabu hiki kimebeba uzani mkubwa sana wa „ilmu ya hadîth na kumbukumbu za wapokezi wa hadîth wakiwa juu ya mizani za ahlul-hadîth.

Utakuta kwenye tafsiri hii, nimejitahidi kubakisha baadhi ya matamshi ya kiarabu katika asili yake mtu anapoyasoma, kwa mfano - herufi ya kiarabu ya madda nimeiwekea alama ndogo juu ya herufi hiyo – badala ya (aa) nimeandika (â); na alama ya sukun („) nimeitumia ili neno lenyewe likurubiane na la kiarabu, kwa mfano; I‟tikâf. Vilevile, jina la Allâh nimelitumia badala ya Mwenyezi Mungu, nikiamini yakwamba hivyo ni bora zaidi, ingawa siwezi kuwakosoa wenye kulitumia jina hilo.

Page 18: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Utangulizi

Sina budi kutoa shukrani zangu za dhati kwa mkusanyaji wa kitabu hiki, Sheikh Muhammad al-Jibâly, kwa juhudi zake kubwa katika kukipanga kitabu hiki na kukifasiri kwa lugha ya ki-Ingereza akisaidiwa na Abu Khalīl al-Amriki na „Abdullāh al-Jibāli.

Vilevile Allâh amjazi kheri nyingi al-Ustâdh Abu Luqmân Shariff Nasîb, kwa mchango wake katika tafsiri hii. Na hatimae, Ustâdh wangu, Abu Bilâl Athman Bin Na‟mân, namuombea Allâh amzidishie kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka na kuwafaidisha Ummah.

Mwisho kabisa, nawashukuru wote waliojitolea kukigharimikia

kitabu hiki na namuomba Allâh ( وتعاىل سبحانه ), awalipe wema na awabariki

katika vizazi vyao na mali zao, Âmîn.

Tunamsifu Allâh, na tunamuomba aifanye juhudi hii ndogo iwe ni yenye kuwafaidisha Waislamu, na atuongoze kwenye njia iliyo nyo-

oka, njia ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), Maswahaba zake na wanavyuoni

waliopita. Twamuomba Allâh aija‟aliye shughuli hii itakasike kwa ajili ya uso wake, kwani kwa hakika yeye ndiye mjuzi, na mwenye kusikiya.

Abu Farida Muhammad Basawad

Rais wa QSSEA, Mombasa.

2nd Sha‟bân, 1435

31st May, 2014

Page 19: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

1

DIBAJI

Alhamdulillaah. Kwa yakini hapana shaka yakwamba, Shukrani zote na kila aina ya sifa njema zinamstahiki Allâh. Sisi tunamtukuza na kumsifu Yeye na daima tunamtaka msaada na msamaha. Kwake Yeye (Allâh) ndipo sisi tunampotafuta hifadha kutokana na maovu ya nafsi zetu na matendo yetu mabaya. Yoyote aliyeongozwa na Allâh hawezi kupotoshwa na mtu yoyote, na yoyote aliyepotoshwa [na Allâh] hapana wa kumuongoza.

Mimi nashuhudia yakwamba hapana mungu (wa kweli) isipokuwa Allâh, Peke yake pasi na mshirika, na nashuhudia

yakwamba Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم) ni „Abd1 Wake na Mtume

“Enyi Mlioamini! Mcheni Allāh kama ipasavyo kumcha; wala

msife isipokuwa mmekwishakuwa Waislamu kamili.”2

1 ‘Abd: Mja wa kujitolea katika mambo ya kheri ya Ibada.

2 Āl ‘Imrān 3:102

Page 20: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

2

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu ambaye amekuumbeni katika nafsi (asili) moja. Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile. Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika

wawili hao. Na mcheni Allāh ambaye kwaye mnaombana. Na (mwatazame) jamaa. Hakika Allāh ni mlinzi juu yenu

(anayaona kila mnayoyafanya).”1

“Enyi Mlioamini! Muogopeni Allāh na semeni maneno ya haki. Atakutengenezeeni vizuri vitendo vyenu na atakusameheni madhambi yenu; na anayemtwi‟i Allāh na Mtume wake, bila

shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.”2

Kwa hakika, maneno yaliyo bora ni maneno ya Allâh (سبحانه وتعاىل); uongofu ulio bora ni wa Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم); mambo mabaya

1 An-Nisā’ 4:1

2 Al-Ahzāb 33:70-71

Page 21: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

3

[katika aqida ya Muislamu au Ibada] ni yale yenye kuzuliwa [na watu], kwani kila jambo mfano wake lilozuliwa ni bid‟ah1, na kila bid‟ah ni kitendo cha upotofu kinachomstahiki mwenye kukitenda kuingizwa motoni2.

Da‟wa Na Malengo Yetu

Malengo yetu katika kitabu hiki na vitabu vyetu vyengine ni

kuilingania Da‟wa ya haki itokayo kwenye kitabu cha Allâh ( سبحانه Ulinganizi wa Da‟wa .(صىل اهلل عليه وسلم) na Sunnah za Mtume Wake (وتعاىل

hii ni jukumu ambalo kila Muislamu anatakiwa kulitunza.

Amesema Allâh (سبحانه وتعاىل):

“Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wakakataza maovu na

hao ndio watakaotengenekewa.”3

Da‟wa hii inaweza kufupishwa kwa maneno mawili: tasfiyah

(usafishaji na utakaso) na tarbiyah (uvunaji na „ilmu). Allâh ( سبحانه :ameyataja mas‟ala hayo katika yafuatayo (وتعاىل

1 Bid’ah: Uzushi katika Aqida au katika vitendo vya Ibada.

2 Vifungu hivi vya ufunguzi ni tafsiri ya khutbat ul-Hâjah (Khutba ya Haja) ambayo

kwayo alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiisoma pindi alipokuwa akianza khutba zake

na ambayo alipendelea sana kuwafundisha Maswahaba zake. 3 Āli ‘Imrān 3:104

Page 22: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

4

“Yeye ndiye aliyeleta Mtume katika watu wasiojua kusoma, anayetokana na wao, awasomee Aya zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na Hikima, (ilimu nyinginezo). Na kabla ya

haya walikuwa katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri.”1

Kwahivyo ulinganizi wa Da‟wah ya kweli ni lazima ufuatiliwe kwa Uislamu uliotakaswa kutokamana na mafunzo na itikadi zisizokuwa na msingi, na kufanya kazi kwa subira katika kuwasaidia Waislamu waliojifungamanisha na Dini Takatifu ya kweli. Ni lazima jambo hili litekelezwe kwa viwango mbali-mbali:

1. Ni lazima tuwe thabīti juu ya Qur‟an Tukufu na Sunnah zilizo swahīh za Mtume, na kuwa na ufahamu (kufahamu viwili hivyo) kulingana na ufahamu na utekelezaji wa Salaf wema. Ameamrisha

tena Allâh ( وتعاىل سبحانه ) kwa mara nyengine. Kwa mfano, amesema:

“Na anayemwasi Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu na akafuata njia isiyokuwa ya Waislamu, tutamgeuza alikogeukia

1 Al-Jumu’ah 62:2

Page 23: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

5

mwenyewe na tutamwingiza katika Jahannam; napo ni pahali pabaya kabisa pa mtu kurudia.”1

Na akasema Allâh ( وتعاىل سبحانه ):

“Basi wakiamini hao (Manaswara na Mayahudi) kama mnavyoamini (nyinyi)2, itakuwa kweli wameongoka.”3

2. Ni lazima tuwaangazie na kuwaelimisha Waislamu, tuwasisitize na kuwahimiza wajisalimishe kikamilifu na Dini ya Haki, watekeleze kulingana na mafundisho yake, na wajipambe nafsi zao na fadhla zake pamoja na mfumo mzima wa maadili. Hili ndilo litakalo kutuhakikishia sisi kutakabaliwa na Allâh, kwa kupitia hapo ndipo watakapofahamu na kutambua furaha na utukufu, kama jinsi ilivyoashiriwa katika yafuatayo:

“Naapa kwa zama (zako ewe Nabii Muhammad) kuwa Binadamu yuko katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri, na wakausiana (kushikamana) na

subira (kustahamiliana).”4

1 An-Nisā’ 4:115

2 Maneno haya hapa wanâmbiwa Maswahaba wa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ).

3 Al-Baqarah 2:137

4 Al-‘Asr 103:1-3

Page 24: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

6

3. Ni lazima tuwatahadharishe Waislamu na kuwasihi wajiepushe maisha yao na kila aina ya Shirk (ushirikina), na mambo ya Bid‟ah (uzushi), filosofia, au fikra nyengine za aina yoyote zilizo ngeni katika misingi iliyotakasika ya itikadi za Uislamu. Huu ni uwajibikaji ambao

Allâh ( وتعاىل سبحانه ) aliotuamuru kwa kusema:

“Na saidianeni katika wema na taqwa, wala msisaidiane katika dhambi na uadui.”1

4. Ni lazima tusaidie katika kuisafisha Sunnah na riwaya za kuzuliwa na zilizo dhaifu. Riwaya dhaifu na itikadi zisizokuwa na misingi mizuri zimeuchafua ubainifu wa Uislamu, na kuzuiya Waislamu wasiendelee mbele. Uwajibikaji huu ni wenye uhai uliokamilika kiasi

cha kwamba Mtume ( يه وسلمصىل اهلل عل ) aliwasifu wale wenye kuutekeleza

kwa kusema:

النيح , » ريفح الغح تح ي يفنح عح لف عدول , يح ا العلمح نو ك خح ذح ح هل يحلنيح ويلح الحا

تحأ الح الهتطلنيح , وح «وحاىتحح

“Itabebwa „Ilmu hii na watu walio waaminifu wa kila zama (vizazi) - wataondoa kutoka ndani yake mabadiliko yaliyoletwa na wale wenye kupindukia mipaka, madai ya batili ya warongo,

na tafsiri potofu za wajinga.”2

5. Ni lazima tupambane katika kuhuisha fikra za ki-Islamu zisizopingika ndani ya mipaka ya misingi ya Uislamu, tupinge kujifungamanisha na madh-hab kwa njia ya ukaidi, na tupinge

1 Al-Mā’idah 5:2

2 Swaheeh - Imepokewa na Ibn ‘Adiyy na wengineo.

Page 25: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

7

utwi‟ifu uliojengwa juu ya chuki za upendeleo katika vyama. Kutoyajali haya katika siku zilizopita kumesababīsha kutu kuishi kwenye nyoyo na fahamu za Waislamu, na kuwapoteza kutoka asili iliyotwahirika ya Uislamu, na kuwasababīsha kupotoka kwenye undugu wa kikweli wa Uislamu uliolinganiwa na Allāh

:(سبحانه وتعاىل)

“Na shikamaneni kwa kamba (dini) ya Allāh nyote, wala msiachane.”1

Na vilevile na Mtume wake (صىل اهلل عليه وسلم):

‹ Na kuweni ni wenye kumuabudu Allāh, ndugu moja2 ‹

6. Ni lazima tusaidie katika kupatikana suluhisho la kihakika katika matatizo yanayokabīli hizi zama zetu, na tujitahidi kurudisha tena njia ya hakika ya maisha ya ki-Islamu na kuthibitisha jamii iliyo imara inayo ongozwa na Sheriya ya Allāh.

Amesema Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Na wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allāh, wala usifuate matamanio yao.”3

Ulinganizi wetu ni kwa waislamu wote watusaidie sisi katika kuitumikia amana hii tukufu. Kwa hakika jambo hili litakuwa ni lenye kuwainua daraja zao na kuwapa hadhi na waweze

1 Āli ‘Imrān 3:103

2 Al-Bukhārī na Muslim.

3 Al-Mā’idah 5:49

Page 26: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Dibaji

8

kuusambaza ujumbe wa milele wa Uislamu katika ulimwengu mzima, kama ilivyo ahadi ya kweli ya Allāh:

“Yeye ndiye aliyemtuma (aliyemleta) Mtume wake (Nabii Muhammad) kwa uongofu na kwa dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa washirikina watachukiwa.”1

1 As-Swāff 61:9

Page 27: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mwanzo Kitabu Hiki

9

MWANZO

Kwa Ukarimu wake na Baraka zake Allāh ( وتعاىل سبحانه ), mfumo

wetu umekuwa ni kuwaletea wasomaji mambo yenye kuibainisha Sunnah katika njia iliyo swahīh, tena yenye usahali. Pamoja na hayo, tumeligusia katika kitabu hiki somo ambalo lililofahamika vibaya na watu wengi sana, ingawaje linahitajika mno na Waislamu, katika nyakati zote mbili, nao ni wakati wa Ramadhān na katika msimu wa mwaka mzima: Somo lenyewe si jengine ila ni Swala za Sunnah za Usiku.

KITABU HIKI

Kitabu hiki ni, katika sehemu yake kubwa, tafsiri ya mfumo ulio swahīh ya vitabu viwili vilivyoandikwa na „allaamah (mwanachuoni mkubwa) Muhammad Naasir ud-Deen al-Albāni kiitwacho Swalāt ut-Tarawêh na Qiyām Ramadhān.

Amesema al-Albāni katika utangulizi wake kwenye kitabu chake cha pili yakwamba sehemu yake kubwa ilikuwa ni mukhtasari wa kilichotangulia:

“Kitabu chetu Swalāt ut-Tarawêh kilichapishwa kitambo kidogo, na sasa hivi kuna haja ya kuchapishwa tena. Kulingana na mpangilio wake ulivyoandikwa, kitabu hicho kimetekeleza malengo yake - ndilo jambo muhimu, kuwazindua watu wa kawaida katika kuifahamu sunnah kuhusiana na swala ya Tarawêh, na kuwakosoa wenye kuipinga. Kwa hilo, sunnah hii imeenea sasa kwenye misikiti mengi iliyoko Syria, Jordan, na miji mengine ya ki-Islamu. Kila sifa njema ni zenye kumthubutukia

Allāh (سبحانه وتعاىل), ambae kwa baraka zake mambo mema yote

hutimizika. Kwahiyo, mimi nikakatikiwa kukifupisha kitabu hicho kwa mpangilio msafi wa kitaalamu (ki-Uwanachuoni), bila ya kuingiza ukosoaji wowote, kulingana na msemo, „Toa salamu

Page 28: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mwanzo Kitabu Hiki

10

uwende zako‟. Niliandika kwa mukhtasari mawazo yote ya kitaalamu (ki-Uwanachuoni) katika kitabu asili, na kuweka nyongeza kwa faida

zaidi. Ni Allāh ( وتعاىل سبحانه ) tunayemuomba awafaidishe watu nalo, kama

alivyofanya katika kilichotangulia na anilipe nami kheri kwa kazi hiyo, Yeye ndiye Mwenye huruma wa kuombwa.

Lakini hatahivyo, kuna majadiliano mengi yaliyo muhimu na mawazo yaliyokuwemo kwenye kitabu cha kwanza lakini yakawachwa katika kitabu cha baadae. Kwahiyo, imezingatiwa kuwa ni muhimu kumletea msomaji wa lugha hii ya kiswahili1 kitabu kitakachokusanya, kuyahifadhi majadiliano kutoka katika vitabu vyote viwili, na kuweka kando - kiasi kikubwa kadiri ya itakavowezekana - majadiliano ambayo yasiyohitajika baina yake, au, katika sehemu nyengine, hata katika sehemu chungu nzima za kitabu cha kwanza.

Kwahiyo, kitabu hiki ni chenye kukabidhi uhasibu ulio swahīh wa mazungumzo ya al-Albāni yaliyo kwenye vitabu vyake viwili, na kuhifadhi maneno yake mengi ya asili, na kuyapanga hayo kwa mtiririko bora wa mawazo.

Zaidi ya hayo, kazi ya al-Albāni iliongezewa na mambo ya ziada kutoka kwa watunzi mbalimbali, hususan kwenye milango au vifungu ambavyo majadiliano yake yalipokuwa ni kwa ufupi sana au yenye upungufu.

KAZI ILIYOFANYIKA KWENYE KITABU HIKI

Kutokana na hayo ya hapo juu, ni dhahiri yakwamba kitabu hiki kina malengo mawili muhimu:

1 Asili ya neno hapa ilikuwa ni ki-Ingereza, lakini kwa munasaba wa kitabu chetu hich

kuwa ni kwa lugha ya Kiswahili ndio nikaonelea kuibadilisha kutoka kwa ki-Ingereza

kwa Kiswahili. (Mfasiri)

Page 29: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mwanzo Kitabu Hiki

11

a. Kuandaa kitabu kamili cha muongozo juu ya Madda ya qiyām na mas‟ala yanayohusiana nayo.

b. Kuwaandalia wasomi wa lugha hii ya kiswahili na vitabu viwili muhimu vya Mwanachuoni mkuu, al-Albāni.

Ili kuyatimiza malengo yote mawili, na wakati huohuo kukifanya kitabu kiwe na mfumo wa kupendeza na kuonekana ni rahisi kukifahamu na wenye kukisoma, hatua zifuatazo zimechukuliwa:

1. Vitabu vyote viwili vya al-Albāni vimefasiriwa kikamilifu. Hii ilikuwa ni juhudi makhsusi inayohusiana na kitabu cha kwanza, kwa sababu ya mijadala yake mengi iliyopanuka ya kitaalamu kwenye mas‟ala ya hadīth.

2. Milango iliyokusudiwa kama ukosoaji wa ubinafsi wa mtu makhsusi au kundi la watu imewachwa kando.

3. Vitabu vyote viwili vimekusanywa pamoja.

4. Kurasa zimewekwa kwenye mfumo mwengine ili zipate kutiririka kwa njia ya ki-mantiki. Katika mfumo huo, vichwa vyingi vipya na vichwa vidogo vilibuniwa ili kuwasaidia wasomaji waipate kwa haraka madda yoyote makhsusi waipendayo.

5. Mawazo ya ziyada, majadiliano, au riwaya zimewachwa - isipokuwa katika baadhi ya hali fulani, ambapo marudio yalipozingatiwa na kuidhinishwa. Katika hali za aina nyingi, marejeo yametumika kwenye riwaya zilizotokeza kwenye sehemu nyingi za kitabu hiki.

6. Uchunguzi wa kuswihi kwa riwaya umesongezwa kutoka kwenye maandiko asili hadi kwenye maandiko ya chini. Hili halikuwa ni jambo la kawaida, kwa vile baadhi ya milango inahusika na utafiti wa aina hiyo peke yake. Kwa upande mwengine, maneno yote ya maelezo yenye ufafanuzi yalisongezwa kutoka kwenye maneno ya chini hadi kwenye maandiko asili.

Page 30: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mwanzo Kitabu Hiki

12

7. Maneno ya chini na sherehe yameongezwa ili kuyafafanua matamshi maalum kutoka kwenye „Ilm ul-Hadīth au matamshi na mawazo ya ki-Islamu.

8. Kurasa kutoka kwenye asili nyenginezo ziliongezewa ili kujaliza kurasa kwenye vitabu hivyo viwili. Hatahivyo, kuvitenga vitabu vya al-Albāni, maandiko ya chini yenye kutanabahisha yamewekwa kando ya Madda za Milango au vifungu ambavyo sehemu zake kubwa zilijalizwa - kwa majina, Mlango 2, 3, 7 na 8 na sehemu za kwanza na mwisho za Mlango No. 6. Asili za misingi zilizohitajika kwa shauri la kurasa za ziyada zilikuwa ni:

Ahkām ul-Qunūt cha Adnaan „Ar‟ur.

Al-Insāf fī Ahkām il-I‟tikāf cha Ali al-Halabī

Al-Jāmi‟u li-Ahkām il-Qur‟ān cha al-Qurtubee

Bughyat ul insān fī Wazā‟ifi Ramadhān cha Ibn Rajab al-Hanbalī

Fat-hul Bārī cha al-Hāfidh Ibn Hajar.

Irshād us-Sārī (v.3) cha Muhammad Ibraahim Shaqrah

Irwā ul-Ghalīl cha al-Albāni.

Lisān ul-„Arab cha Ibn Mandhūr

Mishkāt ul-Maswābī h cha al-Khattwāb ut-Twabrīzi/al-Albāni

Swifāt Swaum in-Nabī cha Salim al-Hilāli na Ali al-Halabī.

Zaad ul-Ma‟ād cha Ibn ul-Qayyim.

SHUKRANI

Kila sifa njema na shukrani ni zenye kumstahiki Mola wetu ( وتعاىل سبحانه )

kwa kutuafikia kuikamilisha kazi hii. Tathmini ya dhati na shukrani zinawastahili idadi kubwa ya Waislamu waliojitolea kusaidia na kuipa

nguvu juhudi hii kwa njia tafauti, twamuomba Allāh ( وتعاىل سبحانه ) awape

Page 31: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mwanzo Kitabu Hiki

13

malipo mema. Khususan, ningelipenda kudhihirisha furaha za usaidizi mkubwa uliotolewa na watu wawili:

a) Abu Khalīl al-Amriki, aliyejitolea kufasiri sehemu kubwa ya kitabu cha pili cha al-Albāni, akapitia kwa umakinifu sana kurasa zenye maandiko ya kitabu hicho, na akachangia mawazo yaliyokuwa na umuhimu mkubwa.

b) „Abdullāh al-Jibāli, aliyesaidia kwa upande wa utengenezaji na mpangilio wa kitabu chenyewe, akachapisha maandiko yote ya kiarabu, na kutengeneza gamba la kitabu1.

Namuomba Allāh ( وتعاىل سبحانه ) aifanye juhudi hii ya „Ibādah iwe

ni yenye usaidizi na yenye mazao mema kwa Waislamu, atusamehe madhambi yetu, atakase kazi zetu kutokamana na unafiki na kiburi, na aitakabali kutoka kwetu.

Mola wetu, tusamehe sisi na waumini wote, na umswalie na

kumtakia amani Mtume wetu Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم).

Muhammad al-Jibaly

10 Rajab 1417 H

21 November 1996

1 Makusudio hapa ni kitabu cha ki-Ingereza (Mfasiri)

Page 32: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

14

MLANGO 1

UTANGULIZI WA MUANDISHI

FITNA YA UJINGA

Amma kwa hakika Ibn Mas‟ud alikuwa ni mkweli pindi aliposema:

“Utafanyaje pindi fitnah (bahati mbaya; upotofu) itakapokukuviringa, ikamsababīsha barobaro akazeeka, na mtoto mdogo akawa ni barobaro? Watu wataichukulia kuwa ni sunnah; na lau mmoja wao atakapoipuuza sehemu yake yoyote, ataambiwa, „Wewe umeipuuza Sunnah!‟”

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliulizwa, “Mambo hayo yatatokea lini?” Nae

akajibu:

“Mambo hayo yatatokea pindi ma‟ulamā‟ wenu watakapokuwa wameshakufa; mutakuwa na wasomaji wengi, lakini ma-fuqahā‟ watakuwa ni wachache (watu wenye ufahamu wa kweli wa Uislamu); mutakuwa na viongozi wengi, lakini watakaokuwa waaminifu watakuwa wachache; mapato ya kilimwengu yatatafutwa kwa amali za akhera; na watu watatafuta „ilmu, lakini isiwe ni kwa ajili ya Dini.”1

1 Imepokewa na ad-Dârimi kwa isnâd mbili, ambapo mojawapo ilikuwa ni swaheeh na

nyengine ilikuwa ni hasan (nzuri, lakini ikawa si yenye nguvu kuliko riwaya swaheeh). Vilevile imepokewa na al-Hâkim na ibn ‘Abd il-Barr katika Jâmi’ul Bayân il-‘Ilm.

Page 33: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

15

Riwaya hii, hata kama ni mawqūf1, imepata daraja ya marfū‟2 kwa sababu imetaja mas‟ala ya ghayb3 ambayo yasiyoweza kujulikana isipokuwa kwa njia ya wahyi.

Katika hadīth hii, tunaweza kuona alama za Utume wa Muhammad na ukweli wa ujumbe wake. Bid‟ah zimesambaa kila mahali, na Waislamu wengi wamehamasika kuziandama na kuwalingania wenzao washikamane nazo. Wale waliokuwa na bidii wakashikamana na Sunnah na kupambana na bid‟ah wakabandikwa majina kuwa ni wafuasi wa bid‟ah na wasiopenda sunnah! Uhalifu wao wa kipekee ni kwamba wao wamepinga mambo ya uzushi na wakakataa kuhusika kwenye mambo ya upotofu!

Hayo ndiyo yaliyotutokea sisi, wafuasi wa sunnah, kwenye sehemu nyingi za ulimwengu. Sisi tulihuisha sunnah za kuswali rak‟āt kumi na moja katika swala ya Tarawêh, tukadumisha, kadiri iwezekanavyo, kwa njia ya „Ibādah iliyo wazi, na kuleta dhikr (utajo wa Allāh) zilizo swahīh - yote hayo ambayo yaliyopuuzwa na watu wengi wenye kuswali rak‟āt ishirini.

Suala hili likasababisha taharuki kubwa na ghadhabu miongoni mwa wale waliolelewa na kufunzwa juu ya mfumo wa taqleed (ufuasi wa ki-upofu). Wao hutushambulia mno kwenye vikao vyao, khutbah zao, na vitabu vyao - yote hayo ambayo kwa kawaida ni mambo yasiyokuwa na ‟ilmu yenye manufaa na dalili za kutegemewa, na la‟na kwa wingi na lugha za ukosefu wa adabu. Mambo kama hayo ndiyo tabia za watu wapotofu wanapojitokeza dhidi ya watu walio katika haki.

Haya hayatokoma au kutuvunja nyoyo zetu kutokana na kuyaendeleza malengo yetu mazuri ya kuisambaza Sunnah kwa marefu na mapana, katika nyanja zote za Uislamu, in shaa‟a „Llaah.

1 Riwaya “inayokoma” kwa swahabi, na inayo-onekana kana kwamba ni maneno yake

mwenyewe au maoni yake, pasi na kufungamanishwa na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) 2 Riwaya “iliyonyanyuliwa” hadi kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ).

3 Mas’ala yaliyovuka utambuzi wa ki-binadamu.

Page 34: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

16

SABABU YA KUANDIKA KITABU HIKI

Waandishi wengi wameandika vitabu wakidai yakwamba kuswali rak‟āt ishirini kwenye swala ya Tarawêh ni sunnah iliyothubutu miongoni mwa Waislamu, na kwamba, isipokuwa Abu Bakr as-Siddīq

ma-Khulafâ‟ wote waongofu (warathi wa Mtume) walikuwa ,(رضي اهلل عنه)

na msimamo huohuo wa kuziswali idadi hiyo. Wakazidi kuielekeza sifa

ya uzushi katika Dini kwa „Umar (رضي اهلل عنه) kwa sababu yeye

aliwakusanya watu waswali Tarawêh kwa jamā‟ah.

Kwahivyo, sisi tumejiandaa kuthibitisha yakwamba „Umar hakuzua katika swala hii - si kwa idadi ya rak‟āt wala kwa kuwakusanya watu kwa hilo. Bali, yeye alikuwa ni mfano bora kwa mu‟min aliyejifungamanisha karibu zaidi na Sunnah za Mtume wake

Hatuna budi sisi kubainisha ukweli huu kwa watu, ili .(صىل اهلل عليه وسلم)

wasipotezwe kwa madai ya uwongo dhidi ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

amiri jeshi wa Waumini „Umar ( عنه اهلل رضي ), au wengineo miongoni mwa

Salaf wetu waongofu.

MADA KUBWA

Mjadala kwenye kitabu hiki unazunguka kwenye mviringo wa swala ya qiyām kwa ujumla, na hususan idadi ya rak‟āt zake .

IDADI YA RAK‟ĀT

Kulingana na idadi ya rak‟āt za qiyām, sisi tutathibitisha yafuatayo:

1. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kuswali zaidi ya rak‟āt kumi na

moja katika qiyām (kumi na tatu iwapo tutahesabu rak‟āt mbili fupi za kuanzia).

Page 35: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

17

2. „Umar ( na Tamīm (رضي اهلل عنه) aliwaamrisha Ubayy Bin Ka‟b ( عنهرضي اهلل

ad-Dārī (رضي اهلل عنه) wawaongoze watu katika swala ya Tarawêh kwa

rak‟āt kumi na moja, kulingana na Sunnah iliyo swahīh.

3. Riwaya zote yakwamba watu katika zama za „Umar (رضي اهلل عنه), au

yoyote miongoni mwa ma-Swahaba watukufu, waliswali rak‟āt ishirini si swahīh na zinakwenda kinyume na riwaya za kweli zilizothibitishwa. Vilevile, madai yote yakwamba kuna ijmā‟ ya

(muafaka wa) ma-swahaba ( عنهم اهلل رضي ) yakwamba waliswali rak‟āt

ishirini hayana msingi wowote.

4. Hata kama riwaya iliyo dhaifu imezingatiwa kuwa ni swahīh na baadhi ya watu, inampasa mtu kufuata riwaya swahīh iliyothibitishwa, kwa sababu inakubaliana na idadi iliyothubutu kwenye sunnah. Haifai kwa mtu yoyote kuiwacha sunnah kwa ajili ya ufahamu au vitendo vya mtu yoyote.

5. Kwa yakini tuliyonayo yakwamba vitendo vya msimamo thabiti vya

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndivyo bora, inakuwa ni dhahiri yakwamba

inampasa mtu ajifungamanishe na idadi iliyothubutu katika sunnah, na ajiepushe na kuiongezea chochote. Huu ndio uliokuwa msimamo wa ma-„ulamā‟.

6. Na hata kama tutakubali hoja ya maneno yanayonukuliwa mara kwa mara yenye kufahamika vibaya na kunukuliwa ki-makosa yakwamba, “Kuna bid‟ah (uzushi) nzuri,” ni lazima tujifungamanishe na muafaka wa wanavyuoni yakwamba kufuata

Sunnah ni bora kuliko uzushi wowote. „Abdullāh Bin Mas‟ūd ( اهلل رضي :amesema (عنه

Page 36: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

18

“Kufanya kichache kulingana na Sunnah ni bora kuliko kufanya kingi katika njia ya bid‟ah.”1 .

MADA NYENGINEZO

Vilevile tutathibitisha katika kitabu hiki yakwamba Sunnah ya Mtume

ni kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah, kuiswali rak‟āt kumi na (صىل اهلل عليه وسلم)

moja, na kwamba Maswahaba waliihuisha na wakaifuata sunnah katika hilo.

Zaidi ya hayo, tumeonyesha sampuli tafauti za jinsi Mtume ( صىل اهلل alivyokuwa akiswali witr, umuhimu wa kufanya „Ibādah yako (عليه وسلم

kwenye swala, na vidokezo vyengine vingi vyenye manufaa na tanabuhi chungu nzima kwenye kitabu chote.

Twamuomba Allāh ( وتعاىل سبحانه ) atuongoze kwenye haki katika

tuliyoyaandika hapa na mahali pengine, aifanye shughuli hii kuwa na utakaso na unyofu kwa ajili ya Uso wake Mtukufu, na iwasababishe ndugu zetu waumini wafaidike nayo - kwa hakika Yeye ni Mwenye Rehma na ni Mwenye kurehemu.

UJUMBE WENYE MALIPO MAKUBWA

Sisi tunathibitisha hayo yaliyo hapo juu kwa dalili zilizo wazi kutoka kwenye Sunnah iliyo swahīh na riwaya za kuaminika. Kwa haya, tunatarajia kufikiliza mafundisho ya Sunnah kwa watu, emma kuhusiana na mas‟ala haya au mengineyo, tukitekeleza kwa hilo amri

ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ):

“Fikiliza („ilmu) kutoka kwangu – hata kama ni aya moja, ...”2

1 Hii ni riwaya swahīh iliyonukuliwa na ad-Dārimī, al-Bayhaqī na al-Hākimi. Al-Hākimi

akaithibitisha kuwa ni swahīh – ambayo adh-Dhahabī akaiafiki. 2 Al-Bukhārī na Muslim

Page 37: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 1 Utangulizi Wa Muandishi

19

Kwa wale walioridhika na haya, na kushikamana nayo, watafaulu na kufurahi kwenye maisha yote kuwili; nasi tutakuwa ni wenye kupata malipo mema mara nyingi, in shā‟a „Llāh, kwa

sababu amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Yoyote mwenye kuanzisha jambo zuri katika Uislamu, malipo mema kwa hilo, na malipo sawa na hayo ya kila mtu kumfuata juu ya jambo hilo – mpaka siku ya malipo - pasi na kupunguza chochote katika malipo yao.”1

Kwa wale ambao hawakuridhika, kwa sababu ya shaka fulani ambazo hawakuweza kuzibainisha, basi hapana lawama juu yao, kwa sababu yanayowapasa wao vilevile yanawapasa wanavyuoni wengi wakubwa kuhusiana na mas‟ala haya.

Ama kwa wale wenye kuipinga kwa kutegemea hawā (matamaniwa ya nafsi) zao, au hisia zao kali wakajifungamanisha na njia za wazazi wao na mababu zao, basi Allāh ndiye hakimu wao.

Kwa hali zote hizo, sisi tunaomba usaidizi wake Allāh ( سبحانه atusahilishie na atuafikie - Yeye ndiye Mwenye kusikiya na ,(وتعاىل

Mwenye kujibu.

1 Muslim na wengineo.

Page 38: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

20

MLANGO 2

QIYĀM1

QIYĀM, Tarawêh NA WITR

UFAFANUZI

Maana ya Qiyām ni “kisimamo”; na maana ya qiyām ul-layl ni “kisimamo cha usiku”. Katika muktadha ya shar‟ (sheriya ya ki-Islamu), maneno yote yanahusu kitu hicho-hicho kimoja, kwa jina, “Swala ya Sunnah ya Usiku, ambayo muda wa wakati wake ni kuanzia baada ya swala ya „ishā2 mpaka wakati wa alfajiri.” Imesifiwa kwa istilahi hii (kisimamo), kwa sababu inahusisha kisimamo kirefu ambacho ndani yake sehemu kubwa za Qurān husomwa.

Majina yake mengine maarufu ni: Swalāt ul-layl (swala ya usiku), tahajjud (kutoka kwenye neno hajada: kukesha usiku), witr (idadi isiyokuwa na mwenzi), Tarawêh (kustarehe).3

Witr hususan ina maana mbili tafauti katika Sunnah, na zote zitatumika kwenye kitabu hiki. Mara nyingi inahusiana na rak‟āt moja au tatu za mwisho za qiyām. Lakini mara nyengine ina maana ya

1 Kwa sehemu kubwa zaidi, mlango huu si katika kitabu kilichofasiriwa cha al-Albānī,

lakini imeingizwa humu kwa min-ajil ya ukamilifu. Marejeo yaliyotumika kwa kurasa hizi yametajwa kwenye utangulizi. 2 Swala ya mwisho katika swala tano za faradhi. Wakati wake umerefuka kuanzia

kupotea kwa muangaza mwekundu mawinguni mpaka katikati ya usiku. 3 Ufafanuzi kutoka kwenye: Lisān ul-‘Arab chini ya “Hajada” na “Rawaha”.

Page 39: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

21

swala ya usiku mzima, kwa sababu yote kwa pamoja idadi yake ni ambayo isiyokuwa na mwenzi.

KUTOELEWEKA

Baadhi ya watu hudhania yakwamba tahajjud ni swala ya usiku iliyo tafauti na qiyām au Tarawêh. Baadhi yao hudhania yakwamba swala za nafl (Sunnah) za usiku hupendekezwa kuswaliwa katika wakati wa Ramadhān peke yake.

Kwahiyo, ni muhimu kuyapambanua maelezo haya yasiyoeleweka vyema na kutilia mkazo yaliyotajwa hapo juu; yaani, yakwamba kuna swala ya nafl moja peke yake katika wakati wa usiku, yenye majina tafauti yanayotumika kuieleza. Hata kama Tarawêh ndilo jina litumikalo sana kuieleza swala yenyewe wakati wa Ramadhān, hili halitoifanya hii kuwa ni swala tafauti.

Zaidi ya hayo, katika baadhi ya miji na misikiti, tena sana ifikapo nusu ya pili ya mwezi wa Ramadhān, watu huswali Tarawêh usiku wa mapema, na kisha huswali swala nyengine wanayoiita tahajjud wakati wa mwishoni mwa usiku. Hiki ni kitendo cha bid‟ah kwa sababu kitendo hicho hakina msingi wowote katika Sunnah.

TARAWÊH

Tangu zamani, Waislamu walikuwa wakitumia hili neno “Tarawêh” kumaanisha swala za usiku katika mwezi wa Ramadhān. Wanavyuoni wengi wameliruhusu neno hili kutumika hivyo, lakini wengine wakasita kidogo kwa sababu neno hilo limebeba kidokezi yakwamba ni lazima mtu ajipumzishe kila baada ya rak‟āt nne za Tarawêh, jambo lisilo na msingi wowote katika Sunnah. Kulinganana na Muhammad Shaqrah:

“Sababu ya jina hili ni kwamba, kutokana na kisomo kirefu, watu walikuwa wakijipumzisha kila baada ya rak‟āt nne. Mapumziko haya yakawa ni kitu cha lazima katika swala ya

Page 40: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

22

Tarawêh, hata kama itaswaliwa kwa visomo vifupi. Jambo hili likawapelekea watu wakadhania yakwamba hili ni jina la sawa

lililoteremshwa kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Ni muhimu kubainisha yakwamba jina hili ni makosa kwenye maandiko na hata kwenye maana. Ama kwa upande wa maandiko,

hata haijulikani yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndie aliyeipa jina hili,

wala Maswahaba zake ... Na ama kwa maana, hata haijulikani

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwafundisha Maswahaba zake

wapumzike kila baada ya rak‟āt nne.

Kwahiyo, hapana budi ibainishwe kwa watu wapate kutanabahi yakwamba hili ni jina la tamthiliya. Ni bora kutumia jina ambalo

alilotumia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa swala hii: Qiyām ...

Huwenda mtu akauliza, „Jee, ni makosa mtu kupumzika baada ya kumaliza rak‟āt mbili au nne?‟ Jawabu langu ni, „Iwapo imām (kiongozi) atachoka, au akahisi yakwamba wanaoswali nyuma yake wamechoka kutokana na kisimamo na kisomo kirefu, basi anaweza kuruhusu mapumziko kidogo ...‟”1

FADHLA ZA QIYĀM

Kuna āyāt nyingi zenye kubainisha fadhla za qiyām na malipo yatakayostahiki kwa wenye kudumu katika kuitekeleza. Kwa mfano,

Allāh (سبحانه وتعاىل) amewasifu waumini wenye kustahili kupata Jannah

(pepo) kama ifuatavyo:

1 Irshād us-Sārī (uk. 75-77)

Page 41: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

23

“Huinuka mbavu zao kutoka vitandani wakati wa usiku ili kumuabudu Mola wao kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo; na

hutoa (Zaka na Sadaka) katika yale tuliyowapa.”1

“Walikuwa (watu wema) wakilala kidogo tu usiku.”2

Juu ya hayo, kuna āhādīth chungu nzima kuhusiana na madda hii. Katika yafuatayo tunawaletea chaguo la zilizo maarufu zaidi.

SWALA BORA YA SUNNAH

Amesimulia Abu Hurairah (رضي اهلل عنه) yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل :(عليه وسلم

“Swala iliyo bora, baada ya swala za faradhi, ni ile ya katikati ya usiku.”3

„Abdullāh Bin „Amr (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba

amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Swala iliyopendekeza zaidi kwa Allāh ilikuwa ni ya Dāwūd. Alikuwa akilala nusu ya usiku, akiamka (na kuswali) kwa thuluthi

moja, kisha akilala kwa sudusi moja (iliyobaki).”4

1 As-Sajdah 32:16

2 Adh-Dhāriyāt 51:17

3 Muslim na Ahmad.

4 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 42: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

24

KUHIFADHIWA KUTOKAMANA NA UCHAWI WA SHEITWĀN

Amesimulia Abu Hurairah ( عنه اهلل رضي ) yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل :(عليه وسلم

“Anapokwenda kulala mmoja wenu, Sheitwān hufunga mafundo mafundo matatu kwenye kishogo chake, na akavuvia kwenye kila fundo, „Nakutakia usiku mrefu, endelea kulala.‟ Atakapoinuka (atakapoamka) mmoja wenu na akamtaja Allāh, fundo moja hufunguka. Atakapotawadha (kwa ajili ya kuswali), fundo jengine hufunguka. Na anaposwali, fundo la tatu hufunguka, ili apate kuwa na nashati (uchangamfu) na hali njema; au kinyume chake, atainuka akiwa taabani na uvivu tele.”1

ISHARA ZA SHUKRANI

Amepokea al-Mughīrah (رضي اهلل عنه) yakwamba Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه )

alikuwa akisimama akiwa kwenye swala kwa muda mrefu sana mpaka miguu yake ikifura. Aliwahi kuulizwa, “Ni kwanini basi ufanye hivi, Ewe Mjumbe wa Allāh, haliyakuwa madhambi yako yote, yaliyopita na yatakayokuja mbeleni, umeshasamehewa?” Akamjibu:

“Basi nami sifai kuwa ni mja mwenye kushukuru?”

Vilevile Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimpa jawabu kama hiyo Bibi

„Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ), alipo-ona yakwamba kisimamo chake kirefu

kwenye swala kikisababisha miguu yake kuvimba, naye akamuuliza, “Basi ni kwanini ufanye hivi, Ewe Mjumbe wa Allāh, haliyakuwa madhambi yako yote, yaliyopita na yatakayokuja mbeleni, umeshasamehewa?”2

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 43: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

25

ISHARA YA WEMA

„Abdullāh Bin „Umar (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Kwa hakika „Abdullāh (Bin „Umar) angelikuwa ni mtu mwema lau kama angeliswali usiku.”

Ikapokewa kutoka kwa mwanae „Abdullāh wa kiume, Sālim,

yakwamba baada ya Mtume ( لمصىل اهلل عليه وس ) kusema hayo, babake

hakuwa ni mwenye kulala usiku isipokuwa kwa muda mchache tu.1

SABABU YA KUINGIA PEPONI

„Abdullāh Bin Salām (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba amesema Mtume

:(صىل اهلل عليه وسلم)

“Enyi watu! Peaneni (maamkuzi ya) Salām, toeni vyakula (kwa wenye kuhitaji), na muswali usiku haliyakuwa watu wamelala - ndipo nanyi mutakapoingia Peponi kwa amani.”2

KUKUBALIWA MAOMBI

Amesimulia Abu Hurairah ( عنه اهلل رضي ) yakwamba amesema Mtume ( اهلل صىل

وسلم عليه ):

“Mola wetu (سبحانه وتعاىل) hushuka katika kila usiku mpaka

kwenye uwingu wa chini kabisa, pindi ibakiapo thuluthi moja tu ya usiku. Naye husema, „Ni nani atakaenilingania Mimi, ili nami

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 Imepokewa na at-Tirmidhī. Ikaswahihishwa na al-Albāni.

Page 44: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

26

nipate kumjibu? Ni nani atakaeniomba Mimi, ili nami nipate kumpa? Ni nani atakaeniomba msamaha Wangu, ili nami nipate

kumsamehe.‟”1

Katika mojawapo ya riwaya, ameongezea:

“Kisha Allāh ( وتعاىل سبحانه ) hunyoosha Mkono wake akasema, „Ni nani

atakae kuekeza („amali njema) na Yule ambae si mbadhirifu wala dhalimu?‟ Huendelea kusema hivyo hadi ufike wakati wa mapambazuko.‟”2

Jābir (رضي اهلل عنه) amepokea yakwamba alimsikiya Mtume ( صىل اهلل عليه :akisema (وسلم

“Kuna muda katika usiku wa Saa Moja nzima ambao, hapana mtu yoyote aliye Muislamu atakaepambana nao na akaomba jambo jema

katika maisha ya hapa duniani au ya Akhera, isipokuwa Allāh humtakabalia na kumpa. Jambo hili hutokea katika kila usiku.”3

Abū Umāmah ( عنه اهلل رضي ) amepokea yakwamba Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )

aliulizwa, “Ni wakati gani du‟ā‟ hutakabaliwa sana?” Nae akajibu:

“Ni katika kina cha mwisho cha usiku, na mwishoni mwa swala za faradhi.”4

Mu‟ādh Bin Jabal (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba amesema Mtume

:(صىل اهلل عليه وسلم)

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 Muslim

3 Muslim.

4 Imepokewa na at-Tirmidhī. Ni Hasan kulingana naye na vilevile al-Albāni.

Page 45: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

27

“Kila Muislamu anapokwenda kulala akiwa katika hali ya twahara (akiwa na wudhū‟), akachukuliwa na usingizi huku

akimtaja Allāh, kisha akaamka usiku, akamuomba Allāh ampe jambo lolote zuri, Allāh humpa jambo hilo.”1

KUJIKURUBISHA KWA ALLĀH

Amesimulia „Amr Bin „Abasah (رضي اهلل عنه) yakwamba amesema Mtume

:(صىل اهلل عليه وسلم)

“Ukaribu alo nao mja mbele ya Allāh upo kwenye sehemu ya mwisho ya usiku. Lau kama unaweza kuwa ni miongoni mwa

wenye kumkumbuka Allāh katika wakati huo, basi fanya hivyo.”2

REHMA KUTOKA KWA ALLĀH

Amepokea Abu Hurairah ( عنه اهلل رضي ) yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل :(عليه وسلم“Allāh na amrehemu mume mwenye kuamka usiku, akaswali, na akamuamsha mkewe naye aswali; na lau (mkewe) atakataa, humnyunyizia maji usoni mwake. Na Allāh amrehemu mwanamke mwenye kuamka usiku, akaswali, na akamuamsha mumewe naye aswali; na lau (mume) atakataa, humnyunyizia maji usoni mwake.”3

MIONGONI MWA WATU WEMA ZAIDI

1 Imepokewa na Ahmad na Abū Dāwūd; imethibitishwa kuwa swahīh na al-Albāni

2 Imepokewa na at-Tirmidhī. Ni swahīh kulingana na al-Hākim, adh-Dhahabī na al-

Albānī. 3 Imepokewa na Abū Dāwūd na an-Nasā’ī. Ni swahīh kulingana na al-Hākim, adh-

Dhahabi na an-Nawawī. Al-Albāni amesema kuwa isnād yake ni hasan.

Page 46: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

28

Wamepokea Abū Sa‟īd al-Khudhrī (رضي اهلل عنه) na Abū Hurairah ( عنه اهلل رضي )

yakwamba amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Pindi mtu anapomuamsha mkewe usiku, kisha wakaswali rak‟āt mbili pamoja, wao watasajiliwa miongoni mwa wanaume na wanawake wenye kumkumbuka kila mara.”1

„Abdullāh Bin „Amr (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba amesema

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ):

“Yoyote mwenye kuswali qiyām akasoma āyāt kumi, hatosajiliwa miongoni mwa wavivu. Yoyote mwenye kuswali qiyām akasoma āyāt mia moja, atasajiliwa miongoni mwa wenye kujitolea. Na Yoyote mwenye kuswali qiyām akasoma āyāt elfu moja, atasajiliwa miongoni mwa wenye „amali njema nyingi sana.”2

AMALI ZA KUDUMU HUDHAMINI MALIPO MARIDHAWA

„Ā‟ishah ( ارضي اهلل عنه ) amesimulia yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema:

“Amali zinazopendekeza zaidi mbele ya Allāh ni zenye kudumu daima, hata kama ni chache.”3

Vilevile, Masrūq amesimulia yakwamba alimuuliza „Ā‟ishah ( رضي اهلل ”?(صىل اهلل عليه وسلم) Ni amali gani zilizopendwa zaidi na Mtume“ ,(عنها

Akajibu („Ā‟ishah), “Zenye kudumu.” Akauliza, “Na aliamka wakati

1 Imepokewa na Abū Dāwūd na Ibn Mājah. Ni swahīh kulingana na al-Hākim, adh-

Dhahabi, al-Irāqī, an-Nawawī na al-Albāni. 2 Imepokewa na Abū Dāwūd. Al-Albāni ameithibitisha kuwa hasan.

3 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 47: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

29

gani (kuswali) usiku.” Akajibu („Ā‟ishah), “Alikuwa akiamka pindi anapomsikiya jogoo akiwika.”1

„Abdullāh Bin „Amr ( عنه اهلل رضي ) amesimulia yakwamba Mtume

:alimwambia (صىل اهلل عليه وسلم)

“Ewe „Abdullāh, usiwe kama fulani na fulani. Alikuwa na mazoweya ya kuamka na kuswali usiku, kisha akawacha kufanya hivyo.”2

„Ā‟ishah (رضي اهلل عنها) amesema:

“Usiwache kuswali qiyām kabisa. Mtume ( سلمصىل اهلل عليه و )

kuiswali. Na pindi alipokuwa mgonjwa au alipodhoofika, aliiswali haliyakuwa amekaa.”3

Pia akasema:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipozeeka na kuanza kudhoofika,

alikuwa sana akiswali (usiku) haliyakuwa amekaa.”4

FADHLA ZA QIYĀM KATIKA MWEZI WA RAMADHĀN

Kuna ahādīth nyingi zenye kueleza sifa za utukufu wa qiyām hususan katika usiku wa Ramadhān. Katika yafuatayo tunawaletea baadhi chache.

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 Al-Bukhārī na Muslim.

3 Imepokewa na Abū Dāwūd; ni swahīh kulingana na al-Albāni.

4 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 48: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

30

MSAMAHA WA MADHAMBI

Amepokea Abū Hurairah (رضي اهلل عنه): Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwahimiza

watu, pasi na kulifanya hilo kuwa ni amri, waswali qiyām katika usiku wa Ramadhān. Alikuwa akisema:

“Yoyote mwenye kusimama (katika qiyām) katika mwezi wa Ramadhān kutokana na Imani na matarajio (ya malipo ya Allāh), atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.”

Jambo hilo liliendelea mpaka Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akafa, na kisha

katika khilāfah1 ya Abū Bakr (رضي اهلل عنه) na katika sehemu ya „Umar ( رضي 2”.(اهلل عنه

MIONGONI MWA WATU WEMA

Amesema „Amr Bin Murrah al-Juhanī:

“Mtu mmoja kutoka katika kabila la Qudā‟ah alimuuliza Mtume ( صىل اهلل Ewe Mjumbe wa Allāh, jee iwapo mimi nikishuhudia„ ,(عليه وسلم

yakwamba hapana mungu (wa kweli) isipokuwa Allāh na kwamba wewe ni Mtume wa Allāh, nikaswali swala tano, nikaufunga mwezi (wa Ramadhân), nikasimama kwa qiyām katika mwezi wa Ramadhān,

na nikalipa zakāh?‟ Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamjibu:

“Yoyote atakaekufa katika hali hiyo atakuwa ni miongoni mwa siddīqīn (watu wema mno) na ma-shuhadā‟.”1

1 Khilāfah: Muda wa utawala wa Khalīfah (mrathi), mwenye kumrithi Mtume ( اهلل صىل

وسلم عليه ) katika kuwaongoza Waislamu. 2 Imepokewa na Muslim. Maneno ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) katika hadīth hii vilevile

yako kwenye Al-Bukhārī.

Page 49: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

31

KUAMKA KWA AJILI YA QIYĀM

KUTAWADHA NA KUPIGA MSUAKI

Kitambo kidogo tu anapoamka, Mtume ( alikuwa akisafisha ( عليه وسلمصىل اهلل

meno yake kwa kutumia siwāk2 na kutekeleza wudhū‟. Idadi ya riwaya

kama hizo, zilizopokewa na „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها) na Ibn „Abbās ( رضي اهللرضي اهلل ) zitadondolewa katika Mlango wa 6. Zaidi ya hayo, „Alī ,(عنه :(صىل اهلل عليه وسلم) amepokea yakwamba amesema Mtume(عنه

“Anapoinuka mmoja wenu kwa ajili ya kuswali wakati wa usiku, basi na atumie siwāk (kusafisha meno yake), kwa sababu anaposoma akiwa kwenye swala, Malaika hushikanisha mdomo wake na mdomo wake, ili hapana kitokacho kwenye mdomo wake isipokuwa kitaingia kwenye mdomo wa Malaika.”3

KUMTAJA ALLĀH

Kuna ahādīth nyingi zenye kusimulia mambo ambayo aliyokuwa

akiyasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipokuwa akiamka kutoka usingizini

wakati wa usiku. Katika yafuatayo tumepanga machache miongoni mwayo.

„Ubbādah Bin as-Sāmit (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba

amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

1 Imepokewa na Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbān, na wengineo kwa sanad (msururu wa

wapokezi) iliyo swahīh. 2 Kigongo kilichokatwa kutoka kwenye mizizi ya mti wa Jangwani uitwao arāk, na

hutumiwa kwa kusafishia meno; vilevile unaitwa miswāk. Kitendo cha kusafisha meno kwa siwāk kinaitwa tasawwuk. 3 Imepokewa na al-Bayhaqī, ad-Diyā’, na wengineo. Imethibitishwa kuwa ni swahīh

na al-Albāni katika as-Swahīhah No. 1213.

Page 50: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

32

“Yoyote atakayeamka kutoka usingizini wakati wa usiku kisha akasema:

« ء ال إل إال الل لع ك ش هر و يم ل ل الهلم ول ال وحره ال شل ، كب ، وال ح

أ والل وستحان اهلل ، وال إل إال الل هر لل كريس وال

، رب اغفس يل ة إال ةالل « وال ك“Lā ilāha illallāhu wahdahu lā sharīka lahū, lah ul-mulku wa-

lah ul-hamdu wa-huwa „alā kulli shay‟in qadīr. Wa-subhān allāhi, wal-hamdu lillāhi, wa-lā ilāha illāllāhu, wallāhu akbaru,

wa-lā hawla wa-lā quwwata illā billāh.Rabbigh fir lī.” –

“Hapana mola apasae kuabudiwa (kwa haki) isipokuwa Allāh Peke yake bila ya mshirika yoyote. Ufalme ni wake Yeye; na

kila sifa njema ni zake Yeye; na Yeye ni muweza wa kila kitu. Himdi zote na kutakasika ni kwa Allāh; na hapana mola apasae kuabudiwa (kwa haki) isipokuwa Allāh; Allāh ni Mkubwa zaidi; Hapana uweza au nguvu isipokuwa kutoka kwa Allāh,” kisha

akasema, Rabbigh fir lī – Mola wangu! Nisamehe.”

Yoyote mwenye kusema hivi kisha akaomba Du‟ā‟, atajibiwa; na atakapotawadha na kuswali, basi swala yake itatakabaliwa.”1

Amesimulia Rabī‟ah Bin Ka‟b al-Aslami (رضي اهلل عنه):

“Nilikuwa na mazoeya ya kulala kwenye nyumba ya Mtume ( صىل اهلل ,Alipokuwa akiamka wakati wa usiku (kwa ajili ya kuswali) .(عليه وسلم

nilikuwa nikimsikiya akirudia rudia kwa muda mrefu:

ستحان » «هي رب العال

1 Al-Bukhārī

Page 51: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

33

“Subhāna rabb il-„ālamīn - Kutakasika ni kwake Mola wa walimwengu.”

Kisha alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akirudiarudia kwa muda mrefu:

وبهره » « ستحان الل

“Subhān allāhi wa bihamdih - Kutakasika ni kwake Allāh, kila sifa njema ni zake Yeye.”1

Amepokea Ibn „Abbās:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliketi alipotoka kwenye usingizi wake

katika thuluthi ya mwisho ya usiku, akaangalia mawingu, kisha akasema:

„Inna fī khalq is-samāwāti wal-ardhi wakhtilāf il-layli wannahāri la āyātilli ulil-albāb ...

“Katika kuumbwa Mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana, ziko hoja (za kuonyesha kuwapo Allāh mmoja), kwa

wenye akili ...>2

mpaka akaikamilisha Sūrah.”3

1 Imepokewa na an-Nasā’ī, at-Tirmidhī, Abū ‘Uwānah na Muslim (kwa sehemu).

Imeswahihishwa na al-Albānī. 2 Āl ‘Imrān 3:190-200

3 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 52: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 2 Qiyâm, Tarawêh Na Witr

34

KIWANGO CHA SAUTI

Mtu anaweza kuswali qiyām kwa sauti ya chini au kwa sauti kubwa, lakini ni bora apandishe sauti yake kwa kiyasi. Amepokea Abū

Qatadah (رضي اهلل عنه) yakwamba katika usiku mmoja, Mtume ( صىل اهلل عليه akiswali kwa sauti ya chini. Kisha (رضي اهلل عنه) alimuona Abū Bakr (وسلم

akamuona „Umar (رضي اهلل عنه) akiswali kwa sauti kubwa. Baadae, Mtume

akamwambia Abū Bakr, „Ewe Abū Bakr! Mimi nilikupitia (صىل اهلل عليه وسلم)

kando yako ulipokuwa ukiswali, nawe ukashusha sauti yako chini.‟ Akamjibu, „Ewe Mjumbe wa Allāh! Mimi nimeshasikiwa na Yeye,

niliyekuwa nikizungumza nae,” Kisha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akamwambia „Umar, „Ewe „Umar! Mimi nilikupitia kando yako ulipokuwa ukiswali, nawe ukapandisha sauti yako juu.‟ Akamjibu, „Ewe Mjumbe wa Allāh! Hapo, nilikuwa nikimuamsha aliyelala na

kumfukuza Sheitwān!” Basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema:

“Ewe Abū Bakr, nyanyua sauti yako kidogo. Na wewe „Umar, punguza sauti yako kidogo.”1

Amesimulia Ibn „Abbās ( عنه اهلل رضي ): “Kisomo cha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

(katika qiyām) kilikuwa ni kiasi cha kwamba mtu aliweza kumsikiya nje ya chumba (chake cha kulala) alichokuwemo yeye.”2

1 Imepokewa na Abū Dāwūd na at-Tirmidhī. Imethibitishwa kuwa ni swahīh na al-

Albāni. 2 Imepokewa na Abū Dāwūd; al-Albāni ameithibitisha kuwa hasan.

Page 53: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

35

MLANGO 3

LAYLAT UL-QADR1

MAANA YAKE

Maana ya qadr na qadar ni makataa (makadirio aliyoyapanga Allâh

,vilevile maana ya qadr ni utukufu au taadhima.2 Kwahiyo ;((سبحانه وتعاىل)

Laylat ul-Qadr, au Usiku wa Qadr, wenye maana ya Usiku wa Makataa, au Usiku wenye Utukufu.

UTUKUFU WAKE

Laylat ul-Qadr ni usiku uliobarikiwa sana. Ni usiku ulio bora katika mwezi wa Ramadhān, bali mwaka mzima. Malipo ya Ibādah katika wakati huo huzidishwa hadi kufikia miezi elfu moja. Ni usiku ambao Allāh aliouchagua kuiteremsha Qur‟ān mpaka kwenye uwingu wa chini, kutoka ambako ilipoteremshwa kwa sehemu ndogo ndogo

kwake Mtume Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم).

Ni usiku ambao Allāh (سبحانه وتعاىل) anapotoa makataa ya maagizo

yake ya hikma, kwa kupanga mas‟ala yanayohusiana na maisha,

1 Katika sehemu kubwa, mlango huu hautoki katika kitabu kilichofasiriwa cha al-

Albāni, lakini kiliingizwa hapa kwa min-ajil ya ukamilifu. Maregeo yaliyotumika kwenye kurasa hizi yametajwa kwenye utangulizi. 2 Lisān ul-‘Arab

Page 54: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

36

kifo, kupata riziki, maafa, na kadhaalika; na Malaika hushuka na maagizo hayo.

Amesema Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Hakika Tumeiteremsha (Qur‟ān) katika Laylatul-Qadr (usiku wenye heshima kubwa), (usiku wa mwezi wa Ramadhān). Na jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini huo usiku wa Laylatul-Qadr? Usiku wa heshima (huo) ni bora kuliko

miezi elfu. Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo. Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya

alfajiri.”1

Na akasema (سبحانه وتعاىل):

1 Al-Qadar 97:1-5

Page 55: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

37

“Kwa yakini tumeteremsha (Qur‟ān) katika usiku uliobarikiwa – bila shaka sisi ni waonyaji. Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima. Ndiyo hukumu inayotoka kwetu; kwa hakika sisi ni waletao (Mitume ili wawaongoe viumbe). Ni

rehema itokayo kwa Mola wako. Bila shaka Yeye ndiye Mwenye kusikiya (na) Mwenye kujua.”1

Inataka ifahamike hapa yakwamba kuiteremsha Qur‟ān siku ya Laylat ul-Qadr haimaanishi yakwamba iliteremshwa

Qur‟ān yote kwa mara moja kwa Mtume Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم).

Kulingana na wanavyuoni, iliteremshwa katika usiku huo kutoka al-Lawh ul-Mahfūdh (kurasa zilizohifadhiwa) hadi kwenye wingu wa chini kabisa. Kisha ndio ikateremshwa kwa sehemu ndogo ndogo, kama ilivyobidi, kwa muda wa miaka ishirini na tatu ya

maisha ya Utume wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)2.

Mambo kama hayo vilevile yanafanana na Qadar za Allāh. Hazikadiriwi katika usiku huo makhsusi kila mwaka. Bali, Allāh

( حانه وتعاىلسب ), pamoja na „ilmu yake kunjufu, alikuwa akijua yote

yatakayotokea, na akayahifadhi yote katika al-Lawh ul-Mahfūdh. Katika usiku wa Laylat ul-Qadr ndipo Allāh anapotoa Qadari zake kuhusiana na mwaka mzima unaofuata (maisha, mauti, ugaavi wa riziki, n.k) kwa Malaika, baada ya kuwa kwenye al-Lawh ul-Mahfūdh.3

1 Ad-Dukhān 44:3-6

2 Haya yamehifadhiwa katika vitabu vya Tafsīr kutoka kwa Ibn ‘Abbās, Qatadah, Ibn

Zayd, na wengineo. Rudi uangalie, kwa mfano tafsiri za Ibn Kathīr na al-Qurtubī. 3 Mâna haya yamehifadhiwa kwenye vitabu vya tafsīr kutoka kwa Ibn ‘Abbās,

Qatādah, Mujāhid, al-Hasan, na wengineo. Rudi utizame, kwa mfano tafsiri za Ibn Kathīr na al-Qurtubī.

Page 56: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

38

NI USIKU GANI?

RAI NA RIWAYA MBALIMBALI

Kuna hadīth zilizo swahīh chungu nzima ambazo Mtume ( مصىل اهلل عليه وسل )

alizoashiriya yakwamba Laylat ul-Qadr hutokea kwenye usiku1 wa ishirini na moja, ishirini na tatu, ishirini na tano, ishirini na saba, ishirini na tisa, au katika usiku wa mwisho wa Ramadhān. Kwa ajili hii, wanavyuoni wamekhitilafiana pakubwa kuhusu uhakika wa huo usiku wenyewe inapoangukia. Al-Hāfidh al-„Irāqi aliandika kijitabu kuhusu madda hii kiitwacho, “Sharh us-Sadr bi-Dhikr Laylat il-Qadr.” Ambacho ndani yake amegusia rai za wanavyuoni wote kuhusiana na

mas‟ala haya. Amesema Imām ash-Shāfi‟i ( اهلل رحمه ):

“Mimi naona kana kwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akijibu

kulingana na suala lilivyo. Kwahiyo, ikiwa mtu atamuuliza, „Jee, tuitafute katika usiku kadhaa na kadhaa?‟ Yeye alikuwa akijibu, „Ndio itafute katika usiku kadhaa na kadhaa.‟2

NYUSIKU KUMI ZA MWISHO ZA RAMADHĀN

Riwaya nyingi zina-ashiriya yakwamba Laylat ul-Qadr huangukia bila ya shaka yoyote katika nyusiku kumi za mwisho za Ramadhān, na mara nyingi katika nyusiku saba za mwisho, kama ilivyo kwenye

riwaya ya Ibn „Umar yakwamba amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Itafuteni katika nyusiku kumi za mwisho. Lau kama mmoja wenu ni mtu dhaifu, basi (angalau) na asikose nyusiku saba za mwisho.”3

1 Mâna ya “Usiku wa ishirini na moja”, ni usiku unao-itangulia siku ya ishirini na moja

ya Ramadhān. 2 Imepokewa na al-Baghawī katika Sharh us-Sunnah (6:388).

3 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 57: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

39

Maarifa ya usiku wenyewe ambao inapoangukia yamefichwa

kwa Waislamu. Amepokea „Ubbādah Bin as-Sāmit (رضي اهلل عنه) yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliingia msikitini (msikiti wa

Mtume) na akawakuta watu wawili wakigombana. Akasema:

“Mimi nilikuwa nimekuja kuwaeleza kuhusu (wakati wa) Laylat ul-Qadr; walipogombana fulani na fulani, maarifa hayo yalipaazwa (yalichukuliwa); na jambo hili huwenda likawa ni bora kwenu. Kwahiyo utafuteni katika usiku wa tisa, saba, na tano (baada ya ishirini).”1

USIKU WA ISHIRINI NA MOJA

Katika riwaya nyengine, Abū Sa‟īd al-Khudhrī (رضي اهلل عنه) amesimulia

yakwamba idadi ya Maswahaba walifanya i‟tikāf pamoja na Mtume ( صىل wakati wa siku kumi za katikati ya Ramadhān. Katika (اهلل عليه وسلم

asubuhi ya ishirini ya Ramadhān, walipokuwa wakijitayarisha

kuondoka, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwapa mawaidha na kuwaambia:

“Mimi nimepashwa habari (na Allāh) kuhusu (ni lini hiyo) Laylat ul-Qadr. Lakini mara nikasahaulishwa. Kwahiyo, itafuteni katika kumi za mwisho, tena kwenye usiku wa idadi isiyogawika kwa mbili. Vilevile nimepashwa habari yakwamba mimi nitasujudu2 (kwa swala ya asubuhi yenye kuifuata) ndani ya maji na matope.”

Kwahiyo, wale walioanza i‟tikāf pamoja na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na

warudi (msikitini kwa siku kumi zaidi za i‟tikāf).”

1 Al-Bukhārī.

2 Sujūd: Kupomoka ukiwa kwenye swala, ni jambo lenye kuhusisha kuweka bapa la

uso na pua juu ya ardhi. Hii imetokana na kitendo sajada. Na kutokana na hili ni tamko la Masjid vilevile, lenye mâna ya mahali pa kusujudu au kufanya ibada.

Page 58: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

40

Kisha Abū Sa‟īd akaendelea:

“Watu wakarudi msikitini (kuendelea na i‟tikāf). Hatukushuhudia Hatukushuhudia hata kijiwingu chembamba cha mvua kwenye mawingu. Lakini mara, likaja wingu kubwa; na kukanyesha katika usiku ule. Paa la msikiti, lililoezekwa makuti, likawa linavuja pale

pale mahali alipokuwa akiswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika usiku wa

wa ishirini na moja. Kukaswaliwa swala (ya alfajiri); na Mtume ( صىل اهلل akasujudu ndani ya matope na maji, mpaka mimi (صىل اهلل عليه وسلم)

nikayashuhudia matope kwenye pua yake na bapa lake la uso.”1

USIKU WA ISHIRINI NA SABA

Ahādīth nyengine zinaashiriya yakwamba Laylat ul-Qadr huangukia katika usiku wa ishirini na saba wa Ramadhān. Kwa mfano, Zirr Bin Hubaysh amesimulia yakwamba Ubayy Bin Ka‟b aliambiwa yakwamba amesema Ibn Mas‟ūd, “Yoyote atakaesimama kwa mwaka mzima (akiswali), hapana shaka atapambana na Laylat ul-Qadr.” Juu ya

kuyasikiya hayo, Ubayy (رضي اهلل عنه) akasema:

“Allāh na amrehemu yeye, hakutaka watu wawe na uvivu (lau kama wangelizidi kujua ni lini itokeapo). Naapa kwa Yule ambaye hapana mola apasae kuabudiwa isipokuwa Yeye, kwa hakika ni katika mwezi wa Ramadhān. Mimi naapa kwa jina la Allāh mimi naujua ni

usiku upi huo: ni katika usiku ambao Mjumbe wa Allāh (صىل اهلل عليه وسلم)

alipotuamrisha tusimame (katika swala); ni katika usiku unao-itangulia asubuhi ya ishirini na saba (ya mwezi wa Ramadhān). Alama yake ni kwamba Jua linakucha (linapanda juu) katika asubuhi ifuatayo likiwa jeupe na halina miyale.”2

1 Al-Bukhārī.

2 Muslim na wengineo.

Page 59: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

41

KWA MUKHTASARI

Kwahivyo, Laylat ul-Qadr huangukia katika usiku wa witr wa nyusiku kumi za mwisho za Ramadhān; ina uwezekano mkubwa kuwepo katika nyusiku saba za mwisho, na kuzidi uwezekano katika usiku wa katikati ya nyusiku hizo, ambao ni usiku wa sihirini na saba.

Wanavyuoni wamekhitilafiana kama iwapo hutokea daima usiku maalum, kwa jina, usiku wa ishirini na saba1, ama kuhusiana na hadīth ya Zirr, au hubadilika kutoka katika mwaka mmoja hadi mwengine baina ya nyusiku hizi2. Kwa mtazamo wa sahali ni kufuata hadīth zenye kutuamrisha tuitafute kwa uchache katika nyusiku za witiri za nyusiku kumi za mwisho. Wakati huohuo, uangalifu maalum ungelipewa ule usiku wa

ishirini na saba, kwa sababu ni usiku ambao Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliowakusanya jamii yake yote, na akawapitisha katika hali ya swala na kufanya ibada, kama itakavyokuja katika hadīth itakayokuja ya Abū Dharr (Uk. 55)

JINSI YA KUITAFUTA LAYLAT UL-QADR

Laylat ul-Qadr ni usiku uliobarikiwa zaidi. Mwenye kuukosa usiku huo, basi huyo amekosa kiwango kikubwa sana cha kheri. Iwapo mu‟min ni mwenye raghba ya kumtwi‟i Mola wake na kuongeza amali njema kwenye daftari lake, basi hana budi kujipinda aupate usiku huu na autumie katika kufanya „Ibādah na matendo mema. Kama atarahisishiwa kutekeleza hayo, atakuwa ni mwenye kusamehewa madhambi yake yote yaliyopita.

KUSWALI QIYĀM

1 Hii ni rai iliyo-elezwa na al-Albāni katika Qiyām Ramadhān.

2 Hii ni rai ya ash-Shawkāni katika Nayl ul-Awtwār.

Page 60: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

42

Imependekezwa kuswali Qiyām kirefu wakati wa nyusiku ambazo pana uwezekano wa Laylat ul-Qadr kuangukia. Haya yameashiriwa kwenye ahādīth nyingi, kama hadīth itakayokuja ya Abū Dharr (Uk. 55). Zaidi ya hayo ni kuwa amepokea Abū Hurairah yakwamba amesema Mtume

:(صىل اهلل عليه وسلم)

“Yoyote mwenye kusimama ( qiyām) katika usiku wa Laylat ul-ul-Qadr [na akarahisishiwa]1kutokana na Imani na matarajio (ya malipo ya Allāh), atasamehewa madhambi yake yote.”2

KUOMBA DU‟Ā‟

Vilevile imependekezwa kufanya maombi marefu katika usiku huu.

Amepokea „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها) yakwamba alimuuliza Mtume ( صىل اهلل عليه ,Yaa Rasūlallāh! Ikiwa nitaujua usiku wa Laylat ul-Qadr ni lini“ ,(وسلم

nisemeje mimi nikiwa katika usiku huo?” Nae akamuamrisha aseme:

فاخف خن » تب العف م إىم خف «الل

“Allāhumma innaka „afuwwun tuhibb ul-„afwa fa‟fu‟annī –

YĀ ALLĀH! Hakika wewe ni Mwenye kusamehe, na unapenda kusamehe. Basi nisamehe mimi.”3

KUJITENGA NA ANASA ZA KILIMWENGU KWA AJILI YA KUFANYA IBĀDAH

1 Nyongeza hii imepokewa na Ahmad kutoka katika riwaya ya ‘Ubādah Bin as-Sāmit;

mâna yake ni kwamba ameruhusiwa kuwa ni miongoni mwa wanyenyekevu wenye kufanya ‘Ibādahwakati wa usiku uliobarikiwa. 2 Al-Bukhārī na Muslim.

3 Imepokewa na Ahmad. Ibn Mājah na at-Tirmidhī. Imethibitishwa kuwa swahīh na al-

Albānī.

Page 61: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

43

Imezidi kupendekezwa kutumia wakati mwingi kufanya „Ibādah katika nyusiku zenye uwezekano wa kuwepo Laylat ul-Qadr. Mwito huu ni wa kuwalingania watu wajitenge na anasa nyingi za kilimwengu kwa min-ajili ya kujipatia wakati na fikra katika kumuabudu Allāh peke Yake.

Amepokea „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها):

“Pindi zilipoanza kumi (za mwisho), Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akijifunga Izār1 yake, akakesha usiku kucha akiwa macho (kwa kuswali), na kuwaamsha jamii yake.”2

Na akasema tena:

“Mtume ( alikuwa akijitahidi zaidi (katika ibādah) ( اهلل عليه وسلمصىل

katika kumi la mwisho kuliko katika nyusiku nyengine.”3

ALAMA ZA LAYLAT UL-QADR

ALAMA ZILIZOSWIHI

Kuna alama, zilizotajwa kwenye riwaya swahīh, ambazo mtu huweza kusema iwapo usiku makhsusi ulikuwa ni wa Laylat ul-Qadr au laa. Ni jambo la kushangaza kuona yakwamba alama hizi hujitokeza baada ya usiku kupita. Baadhi ya wanavyuoni wameashiriya yakwamba hikma

iliyoko nyuma ya matukio hayo ni kwamba mtu hatotegemea ujuzi fulani ili apate kuweka kiwango cha „Ibādah zake kuwa kwa usiku mmoja tu katika mwaka mzima. Ufahamu huu umeungwa

mkono na maneno ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwenye hadīth

iliyotangulia ya „Ubbādah, “na jambo hili huwenda likawa ni bora kwenu.”

1 Hii ina mâna yakwamba alijiepusha na wakeze ili apate wakati zaidi wa kufanya

ibada. 2 Al-Bukhārī na Muslim.

3 Muslim.

Page 62: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

44

Katika hadīth iliyotangulia ya Ubayy, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alisema, “... alama yake ni kwamba Jua linakucha (linapanda juu) juu) katika asubuhi ifuatayo likiwa jeupe na halina miyale.” Vilevile

Vilevile amepokea Abū Dharr yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل عليه :(وسلم

“Katika asubuhi inayofuata Laylat ul-Qadr, jua linakucha (linapanda) pasi na miyale, likiwa mfano wa bunguu, mpaka lipande juu.”1

Hadīth iliyotangulia ya Abū Sa‟īd inaashiriya yakwamba hali ya hewa ilikuwa ni usiku wenye unyevunyevu au usiku wa mvua. Hadīth iliyopokewa na Ibn „Abbās inatujulisha kuwa ulikuwa ni usiku uliotulia, haukuwa na joto wala baridi.2

Kulingana na baadhi ya wanavyuoni, hayo maelezo mawili ya

mwisho yalipatikana kwenye miaka makhsusi ambayo Mtume ( صىل اهلل عليه .alipoyazungumza maneno hayo (وسلم

HADITHI ZA NGANO ZISIZO NA MSINGI

Hekaya nyingi zimezoeleka kuzungumzwa miongoni mwa watu wa kawaida, zenye madai ya kushangaza yanayotokea wakati wa Laylat ul-Qadr. Madai haya ya hekaya yakwamba ati miti husujudu, wanyama hufanya vituko, wakhalifu na majambazi waliowahi kuamka kwa sekunde chache wakaomba utajiri hubadilika na kuwa ma-milionia, n.k ... (na kadhālika).

Yote hayo ni upuzi! Laylat ul-Qadr ni usiku uliobarikiwa ambao unahitaji kutumiwa kwa „Ibādah na utwi‟ifu, sio kwa kughafilika na kufanya ma‟asiya. Wenye kutenda mema peke yake katika wakati

1 Muslim.

2 Imepokewa na Ibn Khuzaymah na wengineo. Isnād yake ni hasan

Page 63: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 3 Laylat ul-Qadr

45

huo, kulingana na Sunnah, kama ilivyotangulia kuelezwa, ndiwo wanaoweza kupata taufiki ya Allāh na Baraka zake.

Page 64: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

46

MLANGO 4

KUSWALI TARAWÊH KWA JAMĀ‟AH

SUNNAH YA MTUME

Imependekezwa kuswali qiyām cha Ramadhān kwa jamā‟ah; na ni

bora kuliko kuiswali mtu peke yake. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), yeye

mwenyewe aliithibitisha hiyo; akaithibitisha (صىل اهلل عليه وسلم) vilevile kwa

ma-Swahaba zake, akaifanya yeye mwenyewe, na kutilia mkazo kuhusu fadhla zake.

KUJUZISHA KWA MTUME

Kujuzisha huku kumeashiriwa kwenye hadīth ya Tha‟labah Bin Abū Mālik al-Qurazī, aliyesema:

“Katika usiku mmoja wa mwezi wa Ramadhān, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alitoka (kuelekea msikitini); akaona baadhi ya watu kwenye kipembe cha msikiti wakiswali. Akauliza, “Wanafanya nini wale?” Baadhi yao wakamjibu, „Yaa Rasūlullāh, wale hawaijui Qur‟ān nyingi; Ubayy Bin Ka‟b anawasomea; nao wako nyuma yake wakifuata swala yake.‟ Nae

”.akawajibu kwa suala hilo, “Wamefanya vyema kabisa (صىل اهلل عليه وسلم)

Page 65: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

47

Au alisema, “Wamefanya sawa.” Na wala hakukataza kitendo hicho chao.1

KITENDO CHA MTUME

Kuna ahādīth nyingi zenye kuashiriya yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliswali Tarawêh kwa jamā‟ah.

1. An-Nu‟mān Bin Bashīr (رضي اهلل عنه) amesimulia:

“Tulisimama (tukiwa kwenye swala) pamoja na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

katika usiku wa ishirini na tatu wa Ramadhān mpaka kufikia thuluthi ya kwanza ya usiku; kisha tukasimama nae katika usiku wa ishirini na tano mpaka kufikiya katikati ya usiku; kisha akatuongoza kwenye usiku wa ishirini na saba (kwa muda mrefu) mpaka tukahofia kuikosa falāh (kufaulu) ... tulikuwa tukiita suhur2: falāh.”3

Katika kuisherehesha hadīth hii, al-Hākim akasema:

“Hii imebeba dalili ya wazi yakwamba kuswali Tarawêh kwenye misikiti ya Waislamu ni Sunnah iliyothubutu; „Alī Bin

Abī Twālib (رضي اهلل عنه) aliendelea kumshawishi „Umar (رضي اهلل عنه) aihuishe tena, mpaka hatimae akafanya hivyo.”4

1 Imepokewa na al-Bayhaqī (2:495). Ni mursal (hapakuwa na jina la swahaba

lililotajwa kwenye upokezi) Tha’labah, akiwa ni tābi’ī (mwanafunzi wa ma-Swahaba; kwa wingi tābi’īn au tābi’ūn). Lakini imepokewa kwa isnād nyengine kutoka kwa Abū

Hurayrah ( عنه اهلل رضي ) na Ibn Nasr al-Marwazī (katika Qiyām ul-Layl), Abū Dāwud na al-

Baihaqī. Riwaya hii inakubalika kama riwaya yenye kusaidia. 2 Chakula chepesi kinacholiwa na wenye kufunga muda mchache tu kabla ya alfajiri.

3Imepokewa na Ibn Abī Shaybah (katika al-Musannaf), Ibn Nasr, an-Nasā’ī, Ahmad, al-

Faryābī (katika Kitāb us-Siyām), na al-Hākim, isnād yake ni swahīh. 4 Al-Mustadrak 1:440

Page 66: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

48

2. Amesimulia Anas ( عنه اهلل رضي ):

“Mtume ( مصىل اهلل عليه وسل ) alikuwa akiswali katika mwezi wa

Ramadhān. Mimi nikenda kusimama na yeye; kisha akaja jamaa mwengine, kisha akaja mwengine - mpaka kikatimu kikundi

kidogo. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipotambua yakwamba sisi sote

tulikuwa tukiswali nyuma yake, aliifupisha swala yake, kisha akaingia ndani ya nyumba yake. Akiwa ndani ya nyumba yake,

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akaendelea kuswali swala iliyokuwa ndefu

zaidi kuliko ile aliyokuwa akiswali na sisi. Asubuhi, kulipopambazuka, tukasema, „Yaa Rasūlullāh, jana usiku ulitambua kuwepo kwetu?‟ Akajibu, „Na‟am, na hii ndiyo sababu ya kufanya nilivyofanya.‟”1

3. Amesimulia „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Watu walikuwa wakiswali wakati wa nyusiku za Ramadhān

katika msikiti wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwenye makundi

mbalimbali. Kwahiyo, mtu aliyekuwa na ujuzi wa baadhi ya Qur‟ān alikuwa na watu watano au sita wakiswali nyuma yake.

Katika usiku mmoja kama huo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akaniamrisha

mimi nimuwekee mkeka (msikitini) kando ya mlango wa nyumba

yangu; nami nikafanya hivyo. Baada ya kuswali „ishā‟, Mtume ( صىل اهلل عليه akenda kwenye ule mswala (ili akaswali). Watu wote waliokuwa (وسلم

msikitini wakakusanyika nyuma yake; naye (صىل اهلل عليه وسلم) akawaongoza

kwenye swala kwa kiasi kirefu cha usiku; kisha Mtume ( عليه وسلمصىل اهلل )

akaondoka na kuingia (chumbani kwangu), na kuuwacha ule mkeka palepale ulipokuwa.

1 Imepokewa na Ahmad, Ibn Nasr kwa mapokezi mawili yaliyo swahīh na at-

Twabarāni katika al-Āwswat

Page 67: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

49

Kulipopambazuka, watu wakawaeleza wenzao yakwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwaongoza baadhi ya watu kwenye swala

katika usiku uliopita. Basi usiku huo, wakaja watu wengi, mpaka

msikiti ukajaa. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akatoka katika usiku wa pili

na akaanza kuswali; nao wakamfuata kwenye swala hiyo.

Asubuhi iliyofuata, watu wakawa wanayazungumza. Kwahiyo, katika usiku wa tatu, idadi ya watu ikaongezeka msikitini [ukajaa msikiti mpaka ukafurika watu]. Kwa mara nyengine tena, Mtume

.akatoka; nao wakamfuata kwenye swala (صىل اهلل عليه وسلم)

Katika usiku wa nne halaiki kubwa ya watu ikaujaza msikiti.

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akaswali nao swala ya „ishā‟, alipomaliza

akenda zake nyumbani kwake. Lakini watu wakabakia; basi

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akaniuliza, „Ewe „Ā‟ishah, hawa watu

wanataka nini?‟ Nikamjibu, „Yā Rasūlallāh! Watu walisikiya kuhusu swala yako ya jana, na sasa wamekusanyika wapate

kuswali na wewe.‟ Akaniambia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), „Ukunje

mkeka wako,‟ Nami nikafanya hivyo.

Usiku huo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akijua kuhusu watu

waliokuwa kwenye nafasi zao, wakimungoja yeye. Baadhi ya watu miongoni mwao walikuwa wakiita kwa sauti, „Swalāh!‟

Asubuhi kulipopambazuka, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akatoka kwa

ajili ya kuswali alfajiri1. Baada ya kumaliza kuswali, aliwageukia watu, akasoma shahādah2, kisha akasema:

1 Swala ya alfajiri, ambayo ndiyo swala ya kwanza katika swala tano za faradhi.

Wakati wake ni kuanzia mwanzo wa mapambazuko hadi kucha kwa jua. 2 Sunnah ya Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) ilikuwa ni kuanza mazungumzo yake kwa Khutbat

ul-Hājah (khutba ya Hājah). Mara nyengine hii inaitwa tashahhud (kuitamka shahada) kwa sababu shahada (kukiri yakwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki na Muhammad ni Mjumbe wake) ni sehemu yake muhimu.

Page 68: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

50

“Enyi watu, naapa kwa jina la Allāh, na kila sifa njema zinamstahiki Yeye, sio kwamba nilikuwa sijui kuhusu kuwepo kwenu katika usiku wa jana, lakini khofu yangu ni kwamba niliwachelea isije swala ya usiku (qiyām) ikafaradhishwa kwenu, jambo ambalo hamutoliweza kulitekeleza. Kwahiyo jitoleeni kufanya amali ambazo mutakazoweza kuzitekeleza peke yake, kwa sababu Allāh hatochoka (kutokamana na amali yako) mpaka uchoke wewe.”

Katika mojawapo ya riwaya za hadīth hii, az-Zuhrī1 akasema:

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikufa na watu walikuwa wakiendelea

kulingana na hali hiyo (wakiswali Tarawêh kwenye makundi tafauti). Hili pia liliendelea wakati wa khilafah ya Abū Bakr na katika sehemu ya khilafah ya „Umar.”2

Kulingana na al-Hāfidh Ibn Hajar:

“Matamshi yasemayo „watu walikuwa wakiendelea kulingana na hali hiyo‟ inawahusu wasiokuwa wakiswali Tarawêh kwa jamā‟ah.”

Hatahivyo, ni bora kuyafasiri matamshi hayo kuwa, “Waliendelea kuswali Tarawêh kwa makundi tafauti,” kama unavyoashiriya mwanzo wa hadīth hii. Kwahiyo, wanaendelea kuswali nyuma ya ma-Imām mbalimbali, kama itakavyozidi kuthibitishwa kwenye riwaya za „Umar

( عنه اهلل رضي ).

Hadīth hizi zinaonyesha dalili za wazi za kuiswali Tarawêh kwa

jamā‟ah, kwani Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliziswali kwenye nyusiku hizo.

Uamuzi huu haukhitilafiani na kukoma kuswali kwake katika usiku wa nne, kwa sababu alieleza sababu za kitendo chake hicho, „niliwachelea isije swala ya usiku (qiyām) ikafaradhishwa kwenu.‟

1 Huyu ni tābi’ī aliyepokea kutoka kwa ‘Ā’ishah.

2 Al-Bukhārī, Muslim, Abū Dāwud, an-Nasā’ī, al-Faryābī, Ibn Nasr na Ahmad. Mândishi

ya hapo juu yanakubaliana zaidi na riwaya za wawili wa mwisho.

Page 69: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

51

Na hapana shaka yakwamba ufahamu huu ulisambaa kufuatia

kufa kwake (صىل اهلل عليه وسلم) baada ya Allāh (سبحانه وتعاىل) kuikamilisha

Dini. Kwahiyo, sababu ya kutoswali Tarawêh kwa jamā‟ah

imeshapita, na kuirudisha hukmu ya awali yakwamba imesisitizwa kuiswali kwa jamā‟ah. Hii ndiyo sababu ya „Umar Ibn al-Khattāb

( عنه اهلل رضي ) akaihuisha, na kama ilivyo rai ya wanavyuoni wengi.

4. Hudhayfah Bin al-Yamān ( عنه اهلل يرض ) amesimulia:

“Katika usiku mmoja wa Ramadhān, Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )

alisimama kwenye kijumba cha makuti. Akajimwagia ndoo nzima ya maji, kisha akasema, „Allāhu Akbar – Allāh ni Mkubwa [mara tatu]; Dhal malakuti, wal jabarūti, wal kibrīyā‟i, wal „adhamah - Wewe Ndiye Mwenye Ufalme, Utukufu, Majivuno na Ukubwa.‟ Kisha akasoma al-Baqarah; kisha akarukū‟ rakā‟ inayofanana (kwa muda) na kisimamo chake. Aliporukū‟ alisema, „Subhāna rabbiyal „adhīm, Subhāna rabbiyal „adhīm - ametakasika Mola wangu Mkubwa, ametakasika Mola wangu Mkubwa.‟ Kisha akainua kichwa chake kutoka kwenye rukū‟, akasimama (kwa muda) unaofanana na kurukū‟ kwake, akisema, „Lirabbīyal hamd - kwa Mola wangu ni kila sifa njema.‟ Kisha akasujudu, na sijda yake ilikuwa ni sawa (muda wake) na kisimamo chake (cha mwisho). Alikuwa akisema katika sijda yake, „Subhāna rabbiyal a‟lā - ametakasika Mola wangu Aliye juu.‟ Kisha akainua kichwa chake kutoka kwenye sijda na akaketi kitako; na akasema baina ya sijda mbili: „Rabbighfir lī, Rabbighfir lī - Mola wangu nisamehe, Mola wangu nisamehe.‟ Na akaketi kwa muda ulio sawa na sijda yake. Kisha akasujudu (mara ya pili) akasema, „Subhāna rabbiyal a‟lā, sawa (kwa muda) na kikao chake. Kwahiyo aliswali rak‟āt nne, akasoma ndani yake al-Baqarah, Āl-„Imrān, an-Nisā‟, al-Mā‟idah

Page 70: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

52

na al-An‟ām mpaka alipokuja Bilāl kutangaza wakati wa swala (ya fajr).”1

HIMA YA MTUME

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliashiriya fadhla za kuswali Tarawêh kwa

jamā‟ah. Kwa mfano, Abū Dharr (رضي اهلل عنه) alipokea yafuatayo:

“Tulifunga swaum pamoja na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika mwezi

wa Ramadhān. Hakuwahi kutuswalisha sisi (katika qiyām) mpaka zilipobaki (nyusiku) saba (za Ramadhān). Kisha akasimama na sisi (usiku huo - kwa swala) mpaka ikapita thuluthi moja ya usiku. Hakuswali na sisi katika usiku wa sita. Katika usiku wa tano, aliswali na sisi mpaka nusu ya usiku ikapita. Kwahiyo tukasema, „Yâ Rasūlullāh! Kwani wewe hutoswali na sisi usiku kucha?‟ Akajibu:

“Yoyote atakaesimama kwenye swala pamoja na imām mpaka (imām) atakapomaliza swala, huandikwa kwake yeye yakwamba ameswali usiku kucha.”

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakutuswalisha katika usiku wa nne (katika

nyusiku zilizobaki). Katika usiku wa tatu2, aliwakusanya jamii yake, wake zake na watu. Akatuongoza kwenye swala (kwa muda mrefu) – mpaka tukahofia kuikosa falāh. Hakuwahi tena kuswali na sisi katika mwezi huo.”

1 Imepokewa (katika sehemu mbalimbali na kupatikana na bâdhi ya mageuzi) na

Muslim, Ahmad, Abū Dāwud, an-Nasā’ī, at-Tirmidhī, Ibn Mājah, Ibn Abī Shaybah, Ibn Nasr, al-Hākim, at-Twahāwī katika (al-mushkal), at-Tayālisī, al-Bayhaqī na al-Baghawī. 2 Mâna yake ni usiku wa ishirini na saba, ambao ni usiku wa Laylat ul-Qadr kulingana

na riwaya nyingi. Hii ndiyo sababu kwanini Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuwakusanya jamii

yake yote na wanawake, jambo lenye kupendekeza kwamba wanawake nao wahudhurie katika usiku huu.

Page 71: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

53

Abū Dharr aliulizwa, “Ni nini falāh?” Akajibu, “Sahūr.”1

Dalili kutoka katika hadīth hii ni matamshi ya Mtume ( يه صىل اهلل عل ,”... Yoyote atakaesimama kwenye swala pamoja na imām“ ,(وسلم

ambayo ni ishara iliyo wazi yakwamba ni bora kuswali qiyām cha Ramadhān pamoja na imām. Hili limethibitishwa kwa aliyoyataja Dāwud:

“Nilimsikiya Ahmad akiulizwa, „Unapendezwa wewe na mtu kuswali pamoja na watu au aswali peke yake katika mwezi wa Ramadhān?‟ Akajibu, „Aswali pamoja na watu.‟ Vilevile nilimsikiya akisema, „napendelea mimi mtu aswali (qiyām) pamoja na imām na vilevile aswali naye witr, kwani amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم): “Mtu anaposwali pamoja na imām mpaka akamaliza,

inahifadhiwa yakwamba aliswali usiku huo kucha.”2

Vilevile Ibn Nasr amepokea kutoka kwa Ahmad. Abū Dāwud pia nae alisema:

“Aliulizwa Ahmad, na mimi nilikuwa nikisikiza, „Jee inafaa mtu kuchelewesha qiyām, kwa maana ya Tarawêh, hadi katika sehemu ya mwisho ya usiku?‟ Akajibu, „Laa, Sunnah ya Waislamu inapendekeza zaidi kwangu mimi.‟”3

Kwa hayo amemaanisha yakwamba kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah, katika nyakati za usiku wa mapema, ni bora kuliko kuiswali peke yako baadae usiku. Hata kama kuichelewesha ina fadhla zake, lakini kuiswali kwa jamā‟ah ni bora kwa sababu

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliithibitisha katika nyusiku hizo aliposwali

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah, Abū Dāwud, at-Tirmidhī (aliyeiswahihisha), an-

Nasā’ī, Ibn Mājah, at-Twahāwī (katika Sharhu Ma’ān il-Āthār), Ibn Nasr, al-Faryābī na al-Bayhaqī. Isnād yao ni swahīh. 2 Al-Masā’il

3 Al-Masā’il

Page 72: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

54

pamoja na watu, kama ilivyo kwenye ahādīth za „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها) na

wengineo. Hiyo ndiyo sababu Waislamu wanaendelea kuifanya kuanzia katika zama za „Umar mpaka sasa.”

SABABU ZA KUTOENDELEZA QIYĀM KWA JAMĀ‟AH

Kama ilivyoashiriwa katika hadīth ya „Ā‟ishah ( اعنه اهلل رضي ) katika

swahīh mbili na nyenginezo, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuswali pamoja na

Maswahaba kwa siku zilizobaki za mwezi, wakikhofiya yakwamba swala ya qiyām katika mwezi wa Ramadhān itafaradhishwa kwao, faradhi ambayo hawatoweza kuitekeleza.

Khofu hii ilitoweka na kifo chake (صىل اهلل عليه وسلم) baada ya Allāh

( وتعاىل سبحانه ) kuikamilisha Dini. Kwahiyo, sababu ya kutoswali qiyām ya

Ramadhān kwa jamā‟ah ilitoweka, ingawa hukmu ya hapo awali ya fadhla zake imebaki salama.

Kitendo cha kuiswali kwa jamā‟ah kikahuishwa na „Umar ( اهلل رضي .kama ilivyoelezwa hapa chini ,(عنه

„UMAR AHUISHA SUNNAH

KITENDO CHA „UMAR

Kama ilivyogusiwa hapo juu, baada ya kifo cha Mtume ( مصىل اهلل عليه وسل ),

watu waliswali Tarawêh misikitini kwa vikundi mbalimbali , nyuma ya ma-imām tafauti. Hayo yalifanyika wakati wa khilāfah ya Abū Bakr

( عنه اهلل رضي ) na sehemu ya khilāfah ya „Umar ( عنه اهلل رضي ). Baadae, „Umar

akawakusanya watu nyuma ya imām mmoja. Amesimulia (رضي اهلل عنه)

Abd ur-Rahmān Bin Abd al-Qārī:

Page 73: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

55

“Nilitoka na „Umar Bin al-Khattāb (رضي اهلل عنه) katika usiku mmoja

wa Ramadhān kuelekea Msikitini; tukawaona watu wakiswali katika makundi mbalimbali: palikuwa na mtu aliyekuwa akiswali peke yake, au mtu mmoja akiswalisha kikundi cha watu. Basi

akasema „Umar (رضي اهلل عنه), „Naapa kwa Jina la Allāh (سبحانه وتعاىل), mimi naamini ingelikuwa bora iwapo nitawakusanya hawa watu wote nyuma ya msomaji mmoja tu.‟ Baadae, akakatikiwa kufanya hivyo, na akawakusanya nyuma ya Ubayy Bin Ka‟b.

Nikatoka nae katika usiku mwengine na huku watu wakiwa

wanaswali nyuma ya msomaji mmoja. „Umar (رضي اهلل عنه) akasema,

„Ama kwa hakika kitendo hiki kipya ni kizuri, hata kama sehemu ya usiku waliyokuwa wameilala ni bora (kwa swala) kuliko sehemu ambayo wanayoswali sasa.‟ Kwa kusema hivyo, amemaanisha sehemu ya mwisho ya usiku, kwa sababu watu walikuwa wakiswali usiku wa mapema.”1

Hii ina riwaya nyengine ambayo „Umar (رضي اهلل عنه) alisema:

“Kama jambo hili limezuliwa, basi kwa hakika ni uzushi ulio mzuri.”2

1 Haya yamepokewa na Mālik (katika al-Muwattā’) na, kutoka kwake al-Bukhārī na al-

Faryābī. Vilevile imepokewa na Ibn Abī Shaybah bila ya matamshi yake, “Jambo hili jipya ni zuri.” 2 Imepokewa na Ibn Sa’d na al-Faryābī. Wapokezi wa riwaya hii wote ni watu

wâminifu, isipokuwa Nawfal Bin Iyās, ambaye aliyetajwa na al-Hāfidh (katika at-Taqrīb), “Mkubaliwa,” kwa mâna yakwamba anapoungwa mkono na wapokezi wengine; kwa upande mwengine, yeye ni mtu dhaifu, kama alivyosema al-Hāfidh mwenyewe katika utangulizi.

Page 74: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

56

UFAHAMU WA „UMAR

Kwahiyo, kama ilivyoashiriwa hapo awali, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliwaongoza Maswahaba katika Tarawêh kwa muda wa nyusiku tatu; kisha akasimama kwa kuhofia yakwamba swala hii itafaradhishwa kwa Waislamu. Kisha watu wakaendelea kuiswali kwa vikundi vidogovidogo, kama walivyokuwa wakifanya hapo awali, mpaka „Umar

alipowakusanya, twamuomba Allāh (سبحانه وتعاىل) awe radhi naye na

amlipe kheri nyingi kwa juhudi zake katika Uislamu. Hatimaye, Ibn ut-Tīn na wanavyuoni wengine wakawa na haya ya kusema:

“Kutokana na ithbati iliyopo, „Umar (رضي اهلل عنه) aliwajibika kufanya

hivyo kutokana na ruhusa ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) wakati wa nyusiku

hizo. Alipokuja kukirihishwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) baadae na jambo

hilo, sababu yenyewe ya pekee ilikuwa ni kukhofia isije ikafaradhishwa kwa watu. Yamkinika ni kwa sababu hii kuwa al-Bukhārī, baada ya kutaja kitendo cha „Umar, akaidondoa hadīth ya

„Ā‟ishah (iliyotangulia) ili aitolee hoja. Baada ya kufa kwa Mtume ( صىل akatambua (رضي اهلل عنه) tishio kama hilo lilikoma, na „Umar ,(اهلل عليه وسلم

umuhimu wa kuwakusanya watu, kwa sababu kuswali mbalimbali huonyesha taswira ya utengamano, na kwa sababu kuswali nyuma ya imām mmoja huwasaidia watu kuhimili urefu wa swala. Kitendo hiki cha „Umar kimekubaliwa na wanavyuoni wengi (kuwa ndio ukweli).”1

Kuhusiana na matamshi ya „Umar (رضي اهلل عنه), “sehemu ya usiku

waliyokuwa wameilala ni bora,” al-Hāfidh Ibn Hajar akasema:

“Huu ni uthibitisho kutoka kwake yakwamba kuswali wakati wa mwisho wa usiku ni bora kuliko kuswali mapema. Lakini hatahivyo, haimaanishi yakwamba kuswali swala ya usiku (Tarawêh) kwa mtu peke yake ni bora kuliko kuiswali kwa jamā‟ah.”

1 Fat-hul Bārī 4:203-204

Page 75: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

57

Kwa hakika, kuiswali kwa jamā‟ah katika wakati wa mapema bila ya shaka ni bora kuliko kuiswali mtu kando peke yake katika wakati wa kuchelewa, kama ilivyobainishwa hapo awali.

UAMUZI WA MAKOSA KUTOKANA NA KITENDO CHA „UMAR

Mazoeya ya kawaida miongoni mwa watu wa zama zetu ni kuyafasiri

ki-makosa matamshi ya „Umar (رضي اهلل عنه), “Nī‟mat il-bid‟atu hādhih -

Ama kwa hakika kitendo hiki kipya ni kizuri.” Watu wengi hutumia kama msingi katika kuelewa mambo visivyo kwa njia mbili:

KUELEWA KIMAKOSA 1

“Kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah ni bid‟ah ambayo haikujulikana

wakati wa zama za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).”

Makosa ya kutoeleweka huku yako wazi, kama ilivyothibitishwa katika ahādīth zilizotolewa hapo awali. Mtume

aliswali pamoja na watu kwa jamā‟ah kwa muda wa (صىل اهلل عليه وسلم)

nyusiku tatu katika mwezi wa Ramadhān; na akakoma kufanya hivyo kwa sababu tu ya kukhofiya yakwamba huwenda ikafaradhishwa.

KUELEWA KIMAKOSA 2

“Baadhi ya bid‟ah (mambo ya uzushi) zinastahili kusifiwa; na

matamshi ya ujumla ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), kama vile, “Kila

bid‟ah ni kitendo cha upotofu.” Inatakiwa kuwa chini ya mipaka ya matamshi haya ya „Umar.”

Jambo hili vilevile halifai. Maana yake ya ujumla na hadīth mfano wake imesimama pasi na mipaka.

Katika matamshi yake, „Umar hakukusudia maana ya bid‟ah kwa upande wa shar‟ī (kisheriya), ambayo ni kuzua katika

Page 76: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

58

Dini. Ni wazi yakwamba hakuzua kitu chochote, bali lakini alihuisha

sunnah chungu nzima za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Yeye alimaanisha bid‟ah kulingana na mojawapo ya maana zake za kilugha, ambayo ni kitu kipya au hekaya ambazo hazikuwa zikijulikana kwa kawaida kabla ya asili yake. Hapana shaka yakwamba kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah nyuma ya imām mmoja halikuwa ni

jambo la kawaida wakati wa khilāfah ya Abū Bakr ( عنه اهلل رضي ) na

sehemu ya khilāfah ya „Umar (رضي اهلل عنه), kama ilivyotangulia hapo

awali. Kwa ufahamu huu, linakuwa ni jambo jipya. Lakini kwa vile

linalingana na kitendo cha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), inakuwa ni sunnah na

wala si bid‟ah. Kuieleza kuwa ni nzuri ni kwa sababu hii tu; na huu ndio ufahamu wa wanavyuoni wakubwa katika kuyafahamisha haya matamshi ya „Umar. Kwa mfano, amesema Abd ul-Wahhāb as-Subkī:

“Amesema Ibn „Abd ul-Barr, „„Umar hakuweka sheriya isiyokuwa

sheriya iliyowekwa na Mtume ( na alichokipenda na ,( اهلل عليه وسلمصىل

kukikubali. Hakuna kilichomzuiya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na kuendelea

(kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah) isipokuwa alikhofiya isije ikafaradhishwa kwa Ummah wake (taifa au wafuasi), kwa sababu

alikuwa ni mkarimu na mwenye huruma kwa waumini. „Umar ( رضي اهلل na akafahamu ,(صىل اهلل عليه وسلم) alijifunza hayo kutoka kwa Mtume (عنه

yakwamba haifai mtu kuongeza katika uwajibikaji au kupunguza kitu

baada ya kufa kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Kwahivyo, yeye akaithibitisha

kwa watu kwa mara ya pili, akaihuisha, na kuiamrisha; alifanya haya katika mwaka wa kumi na nne wa Hijriya. Hilo lilikuwa ni jambo (zuri)

ambalo Allāh alimuhifadhia yeye makhsusi aje alifanye; Allāh ( سبحانه kulifanya, hata kama alikuwa ni (رضي اهلل عنه) hakumzindua Abū Bakr (وتعاىل

bora kuliko yeye, na kwa ujumla alikuwa ni mwepesi zaidi katika kuyatekeleza kila mazuri. Kila mmoja kati ya hawa wawili alikuwa na fadhla ambazo mwenzake hakuwa nazo.‟

Page 77: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

59

Lau kama Tarawêh haingelikuwa ni sunnah iliyoshurutishwa, ingelikuwa ni uzushi wa kukataliwa, kama ilivyo kuhusu hali ya ya ar-Raghā‟ib katika usiku wa katikati ya mwezi wa Sha‟bān na katika Ijumaa ya kwanza ya Rajab. Lau kama hali ingelikuwa ni basi ingelibidi kuikataza; lakini hilo halikufanywa, kama ijulikanavyo wazi katika Dīn.”1

Mwanachuoni mkubwa Ibn Hajar al-Haithamī amesema:

“Kuwafukuza Mayahudi na Manaswara nje ya Bara-Arabu, na kupigana na ma-Turki si mambo ya bid‟ah - kwani haya

yalitekelezwa kwa amri ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), hata kama

hayakufanywa katika uhai wake. Na katika matamshi ya „Umar

( نهرضي اهلل ع ) kuhusu swala ya Tarawêh, „kwa hakika hii ni bid‟ah

nzuri.‟ Alimaanisha maana ya bid‟ah ya ki-lugha, ambayo ni kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa, kama alivyosema

Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Sema: „Mimi sikuwa mtume wa mwanzo kuja ulimwenguni.”2

Hii haiashirii bid‟ah katika mtazamo wa shar‟ī (kisheriya), kwa sababu bid‟ah kama hiyo itakuwa ni kitendo cha upotofu, kama ilivyoashiriwa

na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Wanavyuoni wenye kuziorodhesha bid‟ah kwenye vigawanyo vya “nzuri na mbaya” huwa wanakusudia tu maana za ki-lugha za bid‟ah; na wale wenye kusema yakwamba kila bid‟ah ni upotofu humaanisha bid‟ah kwa mtizamo wa shar‟ī.

1 Ishrāq ul-Maswābīh fī swalāt it-Tarāwīh (1:168).

2 Al-Ahqāf 46:9

Page 78: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

60

Hebu tizama jinsi Maswahaba (رضي اهلل عنهم), pamoja na waliowafuata

wao kwa wema, wamepinga kuadhini kwa ajili ya swala zisizokuwa swala tano za kila siku, kama vile swala ya „Īd, hata kama hakuna makatazo ya waziwazi kuhusiana na mas‟ala hayo. Vilevile, wamechukizwa na watu kushikamana na pembe mbili za Shāmī1 za ka‟bah, na pia kuswali baada ya sa„ī2 kwa vipimo vya kulinganisha na kuswali baada ya twawāf (kulizunguka al-ka‟bah).

Zaidi ya hayo ni kwamba, kuna mambo ambayo Mtume ( صىل اهلل عليه alijiepusha nayo licha yakuwa na haja na uwezo wa kuyafanya (وسلم

katika uhai wake. Kujiepusha na mambo kama hayo kwahivyo ni sunnah, na kuyafanya ni uzushi unaostahiki lawama. Kwa msemo wetu, „licha yakuwa na haja na uwezo wa kuyafanya‟, hatukusudii kuwafukuza Mayahudi, ukusanyaji wa Mus-haf, na mambo mengine

ambayo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuyafanya kwa ajili ya sababu

zilizozuiya yasifanyike.

Kwahiyo, palikuwa na haja ya kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah, lakini

pia kulikuwa na sababu zilizomzuiya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) asiendelee

kuiswali kwa jamā‟ah.”3

WANAWAKE KUHUDHURIA JAMĀ‟AH

Wanawake wanaruhusiwa kuhudhuria swala ya qiyām, kama ilivyoashiriwa katika hadīth iliyotangulia ya Abū Dharr. Vilevile imeruhusiwa kumuwakilisha imām makhsusi kwao. Imethubutu

yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) aliwakusanya watu kwa qiyām, na

kumchagua Ubayy Bin Ka‟b awaongoze wanaume, na Suleimān Bin Abī

1 Hizi ni pembe mbili katika upande wa kaskazini mwa al-Ka’bah, ambako ndio njia ya

kuelekea ash-Shām (Syria, Lebanon, Jordan na Palestine) 2 Kukimbia baina ya as-Swafā na al-Marwah wakati wa Hajj.

3 Al-Ibdā’ fī Madārr il-ibtidā’

Page 79: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 4 Kuswali Tarawêh Kwa Jamâ’ah

61

Hathmah awaongoze wanawake. Vilevile „Arfajah ath-Thaqafī amesema:

“„Ali Bin Abī Twālib (رضي اهلل عنه) aliwaamrisha watu waswali

qiyām katika mwezi wa Ramadhān; alichagua imām mmoja kwa wanaume na mmoja kwa wanawake. Mimi ndiye niliyekuwa imām wa wanawake.”1

Jambo hili limependekezwa ikiwa msikiti ni mkubwa kiyasi kwamba ma-imām wawili hawatoharibiana utulivu (kwa usomaji wao).

1 Riwaya hizi mbilizimepokelewa na al-Bayhaqī, ‘Abd ul-Razzāq (katika al-Musannaf)

Page 80: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

62

MLANGO 5

IDADI YA RAK‟ĀT ZA QIYĀM

UTANGULIZI

Idadi ya rak‟āt za Qiyām ni Kumi na Moja (11). Hii imetokamana na

Sunnah ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Haruhusiwi mtu kuongeza zaidi ya

idadi hii, kwani Yeye (صىل اهلل عليه وسلم) hakuiongezea chochote kwenye

maisha yake yote.

Ingawaje, mtu anaweza kupunguza idadi ya rak‟āt hizi; anaweza mtu hata kuswali rak‟ah moja peke yake ya witr. Hii inaungwa

mkono na vitendo vya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na maneno yake.

KUISWALI Tarawêh KWA JAMĀ‟AH

Imependekezwa kuswali Qiyām katika mwezi wa Ramadhān kwa

Jamā‟ah ; na ni bora kuliko mtu kuiswali peke yake. Mtume ( صىل اهلل عليه yeye mwenyewe aliithibitisha: akaipendekeza: akaiafiki kutoka ,(وسلم

kwa Maswahaba zake (رضي اهلل عنهم), akaitekeleza yeye mwenyewe, na

akaisisitiza kuhusu fadhla zake.

Page 81: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

63

IDADI YA RAK‟ĀT ALIZOSWALI MTUME (صىل اهلل عليه وسلم)

RIWAYA YA „Ā‟ISHAH ( عنها اهلل رضي ):

Abu Salamah Bin „Abd ur-Rahmān alisimulia yakwamba alimuuliza

„Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) kuhusu alivyokuwa akiswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Nae [„Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي )] akamjibu:

“Iwapo ni katika mwezi wa Ramadhān au mwezi mwengine

wowote, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kuswali zaidi ya rak‟āt

kumi na moja. Alikuwa akiswali rak‟āt Nne1 - na usiulize kuhusu uzuri au urefu wake. Kisha akaswali tena Nne - na usiulize kuhusu uzuri au urefu wake. Kisha akaswali rak‟āt Tatu.”2

Imaam An-Nawawī akaeleza katika sherehe ya Swahīh Muslim, “Hii inaashiriya ruhusa ya kufanya hivyo (kuswali rak‟āt Nne na kutoa salaam moja). Ingawaje ni bora kutoa salaam baada ya kila

rak‟āt mbili, kama ilivyokuwa kawaida ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

na inayokubaliana na amri ya kuswali swala ya usiku kwa jozi (mbili-mbili).

Msimamo katika madh-hab ya Shaafi‟ī, kama ilivyoashiriwa katika “al-Fiqhu ‟alal Madhaahib il-Arba‟ah”, sherehe ya al-Qastalāni ya al-Bukhārī na wengineo ni kwamba, “Inamlazimu mtu atoe taslīm baada ya kila jozi ya rak‟āt ; na iwapo mtu ataswali Nne kwa taslīm moja, swala yake haitokubaliwa.” Msimamo huu unapingana na hadīth hii iliyo swahīh, pamoja na ufahamu wa kisawasawa uliotangulia wa An-Nawawī, ambaye ni mmojawapo wa wanavyuoni wakubwa wa madh-hab hiyo. Kwahiyo, hakuna yoyote anayeruhusiwa kutoa fatwā iliyo kinyume cha haya.

1 Mâna yake akitoa salamu moja.

2 Imepokewa na al-Bukhārī, Muslim, Abu Uwânah, Abu Dâwud, at-Tirmidhee, an-

Nasâ’ee, Mâlik, al-Baihaqee na Ahmad.

Page 82: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

64

Katika riwaya nyengine, amesema „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) aliswali wakati wa usiku, katika mwezi wa

wa Ramadhān na miezi mengine, rak‟āt Kumi na Tatu, ambamo ndani ndani yake palikuwa na rak‟āt Mbili za Fajr.”1

Na vilevile katika riwaya nyengine, „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) amesema:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali rak‟āt Kumi na Tatu wakati wa

usiku. Kisha baada ya kusikiya muadhini wa al-Fajiri, alikuwa akiswali rak‟āt mbili fupi.”2

Kuhusu ikhtilafu iliyodhihiri baina ya riwaya mbili za mwisho, al-Hāfidh Ibn Hajar akasema:

“Pana uwezekano yakwamba, katika riwaya hii, „Ā‟ishah alijumlisha katika swala ya usiku pamoja na rak‟āt mbili za

baada ya „ishā‟ ambazo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alizoziswali

nyumbani, au rak‟āt mbili fupi ambazo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alizozianzilishia Qiyām. Imethubutu katika swahīh Muslim

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akianza swala zake za

usiku kwa rak‟āt mbili fupi. Mimi naonelea hili lililotangulia baadae kuwa na uwezekano wa usawa, kwa sababu riwaya ya Abu Salamah, ambayo yenye kuiwekea mipaka idadi kuwa Kumi na Moja, inaeleza hayo, ‟Aliswali Nne kisha Nne kisha Tatu.‟ Haikutaja marejeo yoyote kuhusu rak‟āt mbili fupi zilizotajwa katika riwaya ya Mālik. Hili laruhusiwa, kwa sababu nyongeza kwenye riwaya inayofanywa na mpokezi aliye muangalifu (Hāfidh) inakubalika. Jambo hili limezidi kuthubutu kutokana na riwaya iliyopokewa na Ahmad na Abū Dāwūd kutoka kwa ‟Abdullāh Bin Abī Qays kutoka kwa „Ā‟ishah aliyesema:

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah, Muslim na wengineo.

2 Imepokewa na Mâlik na kutoka kwake, al-Al-Bukhārī na wengineo.

Page 83: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

65

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiswali witr kwa rak‟āt Nne

na Tatu, ..., au Kumi na Tatu. Hakuwa akiswali witr kwa zaidi ya Kumi na Tatu au kupungua chini ya saba.”1

Hii ndiyo riwaya iliyo swahīh mno niliyoipata kwenye mas‟ala haya, na kwa (riwaya) hiyo, mtu anaweza kuitatua ikhtilafu iliyodhihiri baina ya riwaya kutoka kwa „Ā‟ishah.”

Ufafanuzi huu wa al-Hāfidh vilevile umethibitishwa na riwaya ya Mālik kutoka kwa Zayd Bin Khālid al-Juhanī aliyesimulia:

“Katika usiku mmoja niliamua kumfuatilia kwa makini Mtume

.alivyokuwa akitekeleza swala yake ya usiku (صىل اهلل عليه وسلم)

Kwahiyo akaswali rak‟āt mbili fupi.

Kisha akaswali rak‟āt mbili ndefu sana.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali witr (rak‟āt moja).

Hizo zikawa ni rak‟āt Kumi na Tatu.”2

Linalojitokeza hapa ni kwamba hizi rak‟āt mbili fupi ni Sunnah za „ishā‟, kwa sababu hakuna riwaya zenye kuzitaja pamoja na rak‟āt Kumi na Tatu.

RIWAYA YA JĀBIR

Amesimulia Jābir Bin Abdillāh (رضي اهلل عنه):

1 Hadīh hii itatajwa mbeleni kwenye Mlango huu.

2 Imepokewa na Mâlik, Muslim, Abu Uwânah, Abu Dâwud, na Ibn Nasr.

Page 84: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

66

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alituongoza sisi (usiku mmoja) katika mwezi

wa Ramadhān, kwa kutuswalisha rak‟āt Nane na witr. Katika usiku uliofuata, tulikusanyika msikitini, tukitarajia yakwamba atakuja tena (kutuongoza kwenye swala). Tulibakia hapo (tukimungoja) mpaka asubuhi. Kisha tukaingia (mpaka katikati ya msikiti) tukaanza kusema, „Ewe Mjumbe wa Allāh! Usiku wa jana tulikusanyika msikitini tukitarajia yakwamba utatuongoza kwenye swala.‟ Ndipo nae alipojibu kwa kuwaambia: “Kwa hakika mimi nilikhofia yakwamba mutafaradhishiwa.”1

RIWAYA YA IBN „ABBÂS ILIYO DHA‟ĪF

Katika kuizungumzia hadīth iliyotangulia ya „Ā‟ishah , al-Hāfidh Ibn Hajar amesema:

“Ama kuhusu yaliyopokewa na Ibn Abī Shaybah, kutoka katika hadīth

ya Ibn „Abbās (رضي اهلل عنه) yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa

akiswali katika mwezi wa Ramadhān rak‟āt ishirini na witr‟, ina isnād iliyo dha‟īf; zaidi ya hayo inakhalifiana na hadīth ya „Ā‟ishah iliyopokewa kwenye swahīh mbili. Na („Ā‟ishah ) ni mjuzi zaidi kuliko

watu wengine kuhusiana na hali na shughuli za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

katika wakati wa usiku.”2

Kabla ya Ibn Hajar, al-Hāfidh az-Zayla‟ī nae akaeleza ufahamu kama huo.3

Kwa ujumla, hadīth hii ya Ibn ‟Abbās ni dha‟īf sana, kama

1 Imepokewa na Ibn Nasr, na at-Twabarâni katika al-Mu’jam us-Swagheer. Isnâd yake

ni hasan kwa sababu ya hadeeth iliyotangulia. Katika Fat-hul Bāri na at-Talkhees, al-Hâfidh aliashiriya uswahīh wake, na akayafanya marejeo yake kwa Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbān katika swahīh zao]. 2 Fat hul-Bāri 4:205.

3 Nasb ur-Râyah 2:153.

Page 85: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

67

ilivyosemwa na as-Suyūtī.1 Tatizo lake limechipuka kutoka kwa Abū Shaybah Ibrāhim Bin ‟Uthmān, ambaye riwaya zake zimekataliwa, kama yalivyosemwa na al-Hāfidh Ibn Hajar katika at-Taqrīb. Riwaya zote za hadīth hii zina mpokezi huyu katika isnād zake.2

Kwa hakika huyu Abū Shaybah ni dha‟īf mno, kama alivyoashiriya Ibn Hajar. Pia Ibn Ma‟īn akasema, “Si muaminifu.” Al-Jawzajānī akasema, “Aliuzulishwa (aliondolewa madarakani).” Shu‟bah alimzingatia kuwa ni mrongo kwenye kisa alichosimulia. Na Al-Bukhārī akasema, “Wao (wanavyuoni wa hadīth) hawazitangazi riwaya zake.” Kulingana na al-Hāfidh Ibn Kathīr:

“Pindi Al-Bukhārī akisema kumuhusu mtu yakwamba kutangaza riwaya zake (sakatu „anh), maana yake ni kwamba amemuorodhesha kwenye daraja mbaya ya chini kabisa.”3

Kwa ajili hii hadīth hii na izingatiwe kuwa ni ya kuzua, hususan kwa vile imekhalifiana na hadīth swahīh zilizotangulia za „Ā‟ishah na Jābir. Al-Hāfidh adh-Dhahabī ameijumuisha hadīth hii pamoja na za munkar (zilizokataliwa), na Ibn Hajar al-Haithamī akasema:

1 al-Hâwee lil-Fatâwee 2:73.

2 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah katika al-Musannaf, ‘Abd Bin Hameed katika al-

Muntakhab min al-Musnad, at-Twabarâni katika al-Mu’jam ul-KAbī r na al-Awsat, pamoja na ukusanyaji kutoka katika al-Mu’jam ul-Awsat na adh-DhahAbī, na toleo la muungano wa al-Kabī r na al-Awsat na wegineo. Vilevile imepokewa na Ibn Adiyy katika al-Kâmil, al-Khateeb katika al-Moowdih, na al-Baihaqee katika as-Sunan. Riwaya zote hizi ndani ya isnâd zake kuna huyu mtu aitwae Ibrâhim, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Muqsim, kutoka kwa Ibn ‘Abbâs. Amesema at-Twabarâni, “Hadīth hii haikupokewa kutoka kwa Ibn ‘Abbâs isipokuwa kwa isnâd hii.” Na al-Baihaqee akasema, “Hii imepokewa kutoka kwa Abu Shaybah; nae ni mtu dha’eef (katika kupokea kwake).” Vilevile al-Haythamee akasema (katika al-Mu’jam 3:172) yakwamba ni mtu dha’eef. 3 Ikhtisāru ‘Ulum il-Hadīth.

Page 86: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

68

“Ni dha‟īf sana. Ma-Imām (wanavyuoni wa hadīth) walikuwa ni wakali katika kuwashutumu na kuwakosoa mmojawapo wa wapokezi wao. Alikuwa akipokea hadīth ya kuzua, kama vile ‟Hakuna Taifa lililoangamizwa isipokuwa katika mwezi wa March,‟ na ‟Kiyama hakitosimama isipokuwa katika mwezi wa March,‟ Hadīth hii kuhusiana na Tarawêh ni miongoni mwa munkar zake. As-Subki ametangaza yakwamba, sharuti la kuikubali hadīth iliyo dha‟īf ni kwamba udhaifu wake na usiwe ni wa kupita kiyasi. Na adh-Dhahabī akasema: ‟Yoyote ambaye Shu‟bah atamzingatia kuwa ni mrongo, hadīth yake na isizingatiwe kabisa.‟”1

Tanabahi hapa yakwamba, al-Haithamī, katika kuthibitisha hoja kutoka kwa as-Subki imehusu ishara kwa mukhtasar yakwamba rai yake (al-Haithamī) ni kwamba mtu hawezi kuswali rak‟āt ishirini.

Baada ya kudondoa hadīth ya Jābir Bin Abdillāh, iliyopokewa na Ibn Hibbān, as-Suyuti amesema:

“Sisi tumefikia mapatano yakwamba kuswali rak‟āt ishirini

haikuthibitishwa kwa kitendo chake (صىل اهلل عليه وسلم). Hadīth iliyopokewa

na Ibn Hibbān inaunga mkono kikamilifu msimamo wetu wa kushikamana na aliyoyapokea Al-Bukhārī kutoka katika hadīth ya

„Ā‟ishah yakwamba Mtume ( hakuswali, ema katika mwezi ( اهلل عليه وسلمصىل

wa Ramadhān au mwezi wowote mwengine, zaidi ya rak‟āt Kumi na Moja. Nayo (hadīth ya Ibn Hibbān) imeafikiyana nayo yakwamba aliswali Tarawêh rak‟āt Nane zikifuatiwa na rak‟āt Tatu za witr, zikitimia jumla ya rak‟āt Kumi na Moja.

Yenye kuunga mkono haya, vilevile, ni kwamba Mtume ( صىل اهلل عليه alikuwa ni mwenye kuthibiti katika vitendo vyake, kama (وسلم

alivyoshikilia kuswali rak‟āt mbili baada ya ‟Asr, licha ya uhakika yakwamba ni wakati ambao swala imekatazwa. Lau kama angeliwahi kuswali rak‟āt ishirini, basi hangeliwacha kufanya kitendo hicho. Na

1 al-Fatâwee al-Kubra 1:195.

Page 87: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

69

kama lingelifanyika hilo, basi halingelifichika kwa „Ā‟ishah ( رضيعنها اهلل ) aliyesema yaliyotangulia.”1

Hii ni ishara ya nguvu yakwamba Imaam as-Suyuti amekubali kuswali rak‟āt Kumi na Moja, na kukataa kuswali ishirini kama ilivyo kwenye hadīth iliyo dha‟īf sana ya Ibn ‟Abbâs.

RIWAYA KUTOKA KWA ‟UMAR

„UMAR AAMRISHA WATU KUSWALI RAK‟ĀT KUMI NA MOJA

„Umar ( عنه اهلل رضي ) aliwaamrisha watu waswali rak‟āt Kumi na Moja.

Amesema as-Sā‟ib Bin Yazīd ( عنه اهلل رضي ):

“‟Umar Bin al-Khattāb alimuamrisha Ubayy Bin Ka‟b na Tamīm ad-Dārī kuwaswalisha watu katika Qiyām kwa rak‟āt Kumi na Moja. Msomaji alikuwa akisoma ayāt Mia Moja (katika kila rak‟āt ), mpaka ikatubidi kuzielemea fimbo kwa sababu ya kisimamo kirefu. Hatukuwa tukimaliza isipokuwa kwa kuwasili alfajiri.”2

1 [al-Hāwī lil-Fatāwī].

2 Imepokewa na Mâlik katika al-Muwattâ’ kutoka kwa Muhammad Bin Yusuf kutoka

kwa as-Sâ’ib Bin Yazeed. Isnâd hii ni swahīh mno kwa sababu Muhammad Bin Yusuf alizingatiwa kuwa muaminifu na wanavyuoni; na Masheikh wawili (Al-Bukhārī na Muslim) wamezikubali riwaya zake. As-Sâ’ib Bin Yazeed ni Swahaba aliyefanya Hajj

katika ujana wake pamoja na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل )].

Hii vilevile imepokewa na: a) Ibn Abī Shaybah (katika al-Musannaf) kutoka kwa Yahyâ Bin Sa’eed al-Qattân. b) An-Naysâburee kutoka kwa isma’eel Bin Umayyah, Usâmah Bin Zayd na

Muhammad Bin Is-hâq. c) Ibn Khuzaymah kutoka kwa Ismâ’eel Bin Ja’far al-Madanee. Na wote hao waliipokea kutoka kwa Muhammad Bin Yusuf kama ilivyokuja hapo awali.

Page 88: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

70

Yafaa kuzingatiwa yakwamba katika riwaya yake, idadi aliyokuwa nayo Ibn Is-hāq ni “Rak‟āt Kumi na Tatu”. Ibn Nasr ameipokea hivyohivyo katika “Qiyām ul-Layl”, na akaongezea:

“Ibn Ishāq amesema, ‟Kuhusiana na haya sijasikiya chochote kinachofaa na kukubalika kwangu kuliko riwaya ya as-Sā‟ib; na

sababu ni kwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiswali rak‟āt

Kumi na Tatu usiku.‟”

Idadi hii (Kumi na Tatu) ilikuwa ikitajwa na Ibn Is-Hāq peke yake. Imeafikiyana na mojawapo ya riwaya zilizotangulia kutoka kwa

„Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) kuhusu swala ya Mtume ya usiku, ambapo

aliashiriya yakwamba rak‟āt mbili ya hizo rak‟āt zilikuwa ni Sunnah za al-Fajr. Riwaya ya Ibn Is-Hāq inaweza kufasiriwa hivyohivyo, ikawa inakubaliana na wapokezi wengine.

Kutokamana na yaliyotangulia, tumetambua makosa ya wazi katika matamshi ya Ibn Abdul Barr, “Mimi simjui yoyote aliyepokea rak‟āt Kumi na Moja isipokuwa Mālik.” Al-Mubaarakfuri akazungumza kuhusu matamshi haya, “Huku ni kuelewa vibaya kusikofaa.”1 Vilevile az-Zarqānī aliyakosoa matamshi ya Ibn Abdul-Barr kwa kusema:

“Matamshi haya si sawa! Riwaya (kuhusiana na „Umar) imepokewa kwa isnād tafauti, kutoka kwa Sa‟īd Bin Mansūr, kutoka kwa Muhammad Bin Yūsuf, aliyesema, ‟Rak‟āt Kumi na Moja,‟ sawa na aliyoyahifadhi Mālik.”2

1 Tuhfat ul-Ahwâthee.

2 Sherhe ya al-Muwattâ’. Isnâd ya riwaya hii ni swahīh isiyo na shaka yoyote, kama

ilivyoelezwa na as-Suyuti katika al-Masâbīh. Hii peke yake inatosha kuikatâ kauli ya Ibn Abdul-Barr; Jee iwapo tutaongezea juu yake riwaya nyengine zenye kuunga mkono zilizotangulia kutajwa hapo awali?

Page 89: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

71

UDHAIFU WA RIWAYA ZA RAK„ĀT ISHIRINI

Kuna riwaya nyingi sana zenye kasoro zenye kudai yakwamba „Umar

( عنه اهلل رضي ) aliwaamrisha watu kuswali rak‟āt ishirini au ishirini na

mbili kwa swala ya Tarawêh. Riwaya kama hizo hazifai kutumiwa katika kupambana na riwaya zilizo swahīh yakwamba yeye ndiye aliyeamrisha watu kuswali rakāt kumi na moja, kama ilivyothibitishwa hapo awali.

Ni jambo la kusikitisha kuona yakwamba kuna watu wanaodai yakwamba:

“Riwaya ya rak‟āt ishirini imethibitishwa kwa isnād iliyo swahīh kutokana na njia nyingi.”

Hao wenye kuleta madai kama hayo huwa kwa kawaida hawaonyeshi uswahīh wa njia yoyote kati ya madai hayo! Katika yafuatayo, sisi tunawaletea na kukosoa zilizoeleweka zaidi katika riwaya hizo pungufu.

1. Riwaya ya „Abd ur-Razzāq

Amesimulia „Abd ur-Razzāq, kwa upokezi tafauti kutokamana na hiyo ya hapo juu iliyo swahīh, kutoka kwa Muhammad Bin

Yūsuf, yakwamba „Umar ( عنه اهلل رضي ) aliwaamrisha watu waswali,

“Rak‟āt ishirini na moja.” Mpangilio sampuli hii wa matamshi una makosa kutokana na sababu mbili:

a) Haikubaliani na riwaya iliyotangulia, iliyopokewa na wapokezi waaminifu, ya rak‟āt kumi na moja.

b) „Abd ur-Razzāq ndiye mpokezi wa pekee aliye na matamshi ya sampuli hii.

Hata kama tukichukulia yakwamba wapokezi baina yake na Muhammad Bin Yūsuf ni wenye kusadikika, yeye mwenyewe ana kasoro kwa sababu hata kama yeye ni hāfidh muaminifu na mkusanyaji maarufu wa hadīth, na hivyo hivyo akawa kipofu kufikia mwishoni mwa maisha yake, akifanya upokezi wake ukiwa na makosa. Haya yametajwa na al-Hāfidh Ibn Hajar katika “at-

Page 90: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

72

Taqrīb”. Vilevile, aliyekuwa hāfidh Abū „Amr Ibn us-Swalāh alimdondoa yeye kuwa kama mfano kwa wale ambao riwaya zao zikawa ni zenye kuchanganyikiwa kufikia mwishoni mwa maisha yao. yao. Akasema:

“Ahmad Bin Hanbal ametaja yakwamba „Abd ur-Razzāq alipofuka mwishoni mwa maisha yake; kwahiyo alikuwa akipata riwaya (zisizokuwa na uhakika kutoka kwa wengine). Kwahiyo, mapokezi yoyote kutoka kwake baada ya kupofuka hayana thamani yoyote. Amesema an-Nasā‟ī, „Riwaya zitokazo kwake ni zenye shaka - kwa wale waliopokea kutoka kwake kufikia mwishoni mwa maisha yake.‟”1

Vilevile amesema Ibn us-Swalāh:

“Hukmu inayohusiana na wale wenye kuchanganyikiwa katika mapokezi yao ni kwamba: riwaya zinakubalika kutoka kwa wapokezi waliopokea kutoka kwao kabla ya kuchanganyikiwa; na wanakataliwa kutoka kwa wale waliopokea baada ya kuchanganyikiwa, au katika wakati usojulikana iwapo ni kabla au baada.”2

Riwaya hii ya „Abd ur-Razzāq ni ya sampuli ya tatu; yaani; haijulikani iwapo aliipokea kabla au baada ya kuchanganyikiwa kwake, kwahivyo haiwezi kukubalika. Haya yamesemwa kwa kuamini kuwa riwaya hii imehifadhika na matatizo kuwa ni ya kushangaza au ikiwa inakhitilafiana na riwaya nyengine. Basi itawezekanaje kukubalika na matatizo haya yaliyo-ongezeka?

2. Riwaya ya Ibn Khusayfah

Riwaya hii (ya „Abd ur-Razzāq) vilevile imepokewa na al-Faryābī3 na al-Bayhaqī4, kutoka kwa Yazīd Bin Khusayfah, kutoka kwa as-Sā‟ib Bin Yazīd, kama ifuatavyo:

1 Muqaddimatu ‘Ūlūm il-Hadīth Uk. 407

2 Muqaddimatu ‘Ūlūm il-Hadīth Uk. 391

3 As-Swiyām 1:76

4 As-Sunan 2:496

Page 91: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

73

“Walikuwa wakisimama kwenye swala pamoja katika mwezi

wa Ramadhān katika zama za „Umar ( عنه اهلل رضي ) kwa rak‟āt

ishirini; walikuwa wakisoma ma-miya (ya āyāt); na mpaka wakawa wanajiegemeza kwenye bakora zao katika zama za

„Uthmān ( عنه اهلل رضي ) kutokana na kisimamo cha muda mrefu

katika swala.”

Riwaya hii ndiyo dalili ya kimsingi kwa wale wenye kudai yakwamba inaruhusiwa kuswali rak‟āt ishirini. Kwa uchunguzi wa kina inaonekana kana kwamba isnād yake ni swahīh. Kwa ajili hii, baadhi ya wanavyuoni wameizingatia kuwa ni swahīh. Lakini hatahivyo, inayo vijikasoro vyingi vya udhaifu, vilivyoifanya hadīth yenyewe kuwa na ila na kukataliwa:

a) Ibn Khusayfah ni mpokezi muaminifu; lakini hatahivyo, kama ilivyoashiriwa na Imām Ahmad, upokezi wake ni munkar (umekataliwa). Kwa sababu hii, adh-Dhahabi alimuingiza kwenye Kitabu chake cha “al-Mīzān”.1

Matamshi ya Imām Ahmad yanaashiriya yakwamba mara nyengine Ibn Khusayfah husimulia mambo ambayo hayajawahi kuhadithiwa na wapokezi wengi walio maaminifu2. Riwaya za mpokezi wa sampuli hiyo hukataliwa pindi zinapopingana na riwaya za wanavyuoni walio wengi wenye sifa ya kuwa ni waangalifu sana kwenye mambo madogomadogo, na huzingatiwa kuwa ni Shādh (kioja) – kama ilivyothibitishwa katika „ilmu ya “Misingi ya Hadīth.”

Riwaya ya Ibn Khusayfah ni miongoni sampuli hii. Wote wawili, yeye na Muhammad Bin Yūsuf wameipokea kutoka kwa as-Sā‟ib Bin Yazīd. Wawili hawa wametafautiana kuhusiana na idadi, Ibn Yūsuf akisimulia kuwa ni kumi na

1 Katika kitabu hiki, adh-Dhahabi aliyahifadhi majina ya wapokezi waliokosolewa na

wanavyuoni wa hadīth 2 Angalia kwenye ar-Raf’k wat-Takmmil fil-jahri wat-Ta’dīl cha Abū al-Hassanāt al-

Laknawī. Uk. 14-15

Page 92: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

74

moja na Ibn Khusayfah akisimulia kuwa ni ishirini. Riwaya ya Ibn Yūsuf ni yenye kuzidi kukubalika kwa sababu yeye alikuwa ni mtu muangalifu sana kwenye mas‟ala madogo madogo; al-Hāfidh alimsifu kuwa ni, “Muaminifu aliye na uangalifu wa kina,” haliyakuwa alichosema kumuhusu Ibn Khusayfah ni, “Muaminifu”. Tafauti hii ni miongoni mwa mambo yenye kutia uzani pindi ipatikanapo tafauti kwenye riwaya, kama ijulikanavyo na watu waliobobea kwenye fanni hii tukufu ya utaalamu wa hadīth („Ilm ul-Hadīth).

b) Ibn Khusayfah hakuwa na msimamo katika idadi aliyoisimulia. Ismā‟īl Bin Umayyah amepokea yakwamba Muhammad Bin Yūsuf alimsimulia riwaya inayofanana na ile iliyopokewa na Mālik (iliyotangulia). Kisha Ibn Umayyah akamuuliza, “Kwani wewe hukukusudia kuwa ni ishirini na moja (kuliko hiyo ya kumi na moja)?” Akamjibu Ibn Yūsuf, “Ibn Khusyafah nae pia aliisikiya kutoka kwa as-Sā‟ib Bin Yazīd.” Akauliza Ibn Umayyah, “Kwani wewe unamkusudia Yazīd Bin Khusayfah? Lakini yeye alisema, „Mimi nadhani yakwamba as-Sā‟ib alisema, “Ishirini na moja!”‟”1

Matamshi yake, “Ishirini na moja” katika riwaya hii inatafautiana na, “Ishirini” katika riwaya iliyotangulia. Matamshi ya Ibn Khusayfah, “Mimi nadhani” yanaashiriya kutokuwa na msimamo katika kutaja kwake idadi, na kwamba hakuyahifadhi vilivyo. Haya peke yake yanatosha kuikataa riwaya yake – hususan tunapofahamu yakwamba inatafautiana na riwaya ya aliyekuwa akitegemewa zaidi kuliko yeye.

c) Muhammad Bin Yūsuf ni mtoto wa nduguye as-Sā‟ib Bin Yazīd. Kutokana na uhusiano huu, yeye alikuwa na ustadi na ujuzi zaidi kuhusu riwaya za as-Sā‟ib kuliko watu wengine. Kwahiyo, idadi aliyoipokea ni yenye kukubalika zaidi kuliko ile ya Ibn Khusayfah. Haya yamezidi kuthibitishwa kwa uhakika yakwamba yanakubaliana na riwaya iliyotangulia ya „Ā‟ishah

1 Riwaya hii ina isnād iliyo swahīh.

Page 93: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

75

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuzidisha kuswali zaidi ya

rak„āt kumi na moja. Kwa hakika sisi tungelitarajia kitendo

cha „Umar kifanane na Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), kuliko

kuchukulia yakwamba kitendo chake kimekwenda kinyume na Sunnah.

3. Riwaya ya Ibn Abī Dhubāb

Amepokea Ibn „Abd ul-Barr:

“Al-Hārith Bin „Abd ur-Rahmān amepokea kutoka kwa Ibn Abī Dhubāb kutoka kwa as-Sā‟ib Bin Yazīd, „Qiyām katika zama za „Umar ilikuwa ni rak„āt ishirini na tatu.‟”1

Isnād ya riwaya hii ni dhaifu kutokana na kumbukumbu mbaya ya Ibn Abī Dhubāb. Amesema Ibn Abī Hātim:

“Babangu alisema, „Ad-Dārawardi alikuwa akipokea hadīth zilizokataliwa kutoka kwake (Abū Dhubāb); yeye hana nguvu hivyo; yeye anahifadhi hadīth (kutoka kwa wapokezi walio kwenye daraja ya chini ya uaminifu).‟ Na Abū Zar‟ah akasema, „Ni mwenye kupitikiwa.‟”2

Hiyo ndiyo sababu kwa nini Mālik hakupokea riwaya zake, kama ilivyotajwa na al-Hāfidh Ibn Hajar3. Vilevile Ibn Hajar amesema, “Yeye ni mkweli, ingawa alikuwa na taqsiri (ila).”4

Mtu hawezi kukubali riwaya za mpokezi kama huyo, kwa sababu ya uwezekano wa makosa yake kama hayo, hususan kwenye riwaya hii iliyojiri, yenye kukhalifiana na ile ya mpokezi muangalifu na aliye muaminifu, aitwae, Muhammad Bin Yūsuf, aliyepokea, rak„āt kumi na moja.,” kama ilivyotangulia.

1 ‘Umdat ul-Qārī 5:357.

2 Al-jarhu wat-Ta’dīl 1:2:80

3 At-Tahdhīb

4 At-Taqrīb

Page 94: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

76

La zaidi ni kwamba, hali za wapokezi wengine kwenye isnād ya riwaya hii hazijulikani, kwa sababu hatuna uwezo wa kukipata kitabu cha Ibn „Abd ul-Barr ili tupate kuangalia isnād na kuwapekua wapokezi wake.

4. Riwaya ya Yazīd Bin Rūmān

Amepokea Yazīd Bin Rūmān:

“Watu walisimama kwenye qiyām katika zama za „Umar kwa rak„āt ishirini na tatu.”1

Katika “al-Ma‟rifah”, al-Bayhaqī aliashiriya udhaifu wa riwaya hii kwa kusema:

“Huyu Yazīd Bin Rūmān hakukutana na „Umar.”

Al-Hāfidh az-Zayla„ī ameyaafiki haya.2 Vilevile an-Nawawī amesema, “Imepokewa na al-Bayhaqī, lakini ni mursal (kwa isnād iliyo pungufu), kwa sababu Yazīd Bin Rūmān hakukutana na „Umar.”3

Hali kadhaalika, ameashiriya al-„Aynī udhaifu wake kwa kusema, “Isnād yake ni munqati‟ (iliyokatika).”4

Kwahiyo, riwaya hii ni dha‟īf kwa sababu ya kukatika baina ya Yazīd Bin Rūmān na „Umar, na kwahivyo ndio ikashindikana kuchukuliwa kama dalili, hususan kwa vile imekhalifiana na riwaya iliyo swahīh kutoka kwa „Umar yakwamba waliwaamrisha watu kuswali rak„āt kumi na moja.

5. Riwaya ya Yahyā Bin Sa„īd:

Amepokea Wakī‟, kutoka kwa Mālik, kutoka kwa Yahyā Bin Sa„īd, yakwamba:

“„Umar Bin al-Khat tāb alimuamrisha mtu awaongoze watu

1 Imepokewa na Mālik, al-Faryābī, na al-Bayhaqī (wote wawili katika as-Sunan na al-

Ma’rifah) 2 Nasb ur-Rāyah 2:154

3 Al-Majmū’ 4:33

4 ‘Umdat ul-Qārī 5:357

Page 95: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

77

kwenye swala kwa rak„āt ishirini.”1

Isnād ya riwaya hii, vilevile imekatika. Mwanachuoni mkubwa al-Mubārakfūrī amesema:

“Amesema an-Nawawī katika Āthār us-Sunan, „wapokezi waaminifu; lakini Yahyā Bin Sa„īd al-Answārī hakukutana na Hii ni kweli; na kwahivyo, riwaya hii imekatika, na haiwezi kuchukuliwa kuwa ni dalili. Kwa ujumla, inakhalifiana na

yaliyopokewa kwa isnād iliyo swahīh yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) alimuamrisha Ubayy Bin Ka„b na Tamīm ad-Dārī wawaongoze kwa rak„āt kumi na moja. Vilevile imekhalifiana na yaliyothubutu

kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa isnād iliyo swahīh.”2

MSIMAMO WA ASH-SHĀFI‟Ī NA AT-TIRMIDHĪ

At-Tirmidhī aliashiriya yakwamba idadi ya rak„āt ishirini

iliyonasibishwa na „Umar (رضي اهلل عنه) na Maswahaba wengine si swahīh.

Amesema, “Imepokewa kutoka kwa „Umar (رضي اهلل عنه) na Maswahaba

wengine wa Mtume.”3 Ash-Shāfi‟ī amesema kama hayo kuhusiana na

rak„āt ishirini iliyonasibishwa na „Umar (رضي اهلل عنه).4

Mapatano ya uwiyano baina ya wata‟alamu wa Hadīth, wakizingatiwa miongoni mwao ash-Shāfi‟ī na at-Tirmidhī, wamesema yakwamba (ruwiya - imepokewa) ni ishara ya udhaifu wa riwaya hiyo. Amesema an-Nawawī:

“Wata‟alamu waliobobea katika ta‟aluma ya hadīth na vitagaa vyengine vya ki-ilimu wamekubaliana yakwamba kwa hadīth iliyo dhaifu, mtu hawezi kusema, „Mjumbe wa Allāh amesema,

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah katika al-Musannaf (2:89:2)

2 Tuhfat ul-Ahwādhī 2:85

3 Sunan ut-Tirmidhī.

4 Imepokewa na al-Muzanī kwenye Mukhtasar 1:107.

Page 96: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

78

amefanya, ameamrisha, amekataza, au matamshi mengine yoyote yenye kuashiriya uhakika.” Vilevile, mtu hawezi kusema kwa sampuli hii ya hadīth, „Amepokea Abū Hurairah, amesema, ametaja, alizungumza, amesimulia, amehukumu, au mambo mengine mfano wake.‟ Misemo inayoshabihiyana na hayo haifai kutumiwa katika kuwakusudia tābi‟īn au wale waliokuja baada yao. Katika hali zote kama hizo, mtu na aseme, „Ruwiya „anhu – imepokewa kutoka kwake; imesimuliwa kutoka kwake; imesimuliwa kumuhusu yeye; tumepashwa kumuhusu yeye; husemwa; imetajwa; imesimuliwa; imepokewa; imehadithiwa;‟ au matamshi mengine yanayofanana nayo yenye kuashiriya udhaifu, na yasiyoashiriya yakini au uhakika.

Vilevile wanavyuoni wamesema yakwamba matamshi yenye uhakika yanapaswa kutumika kwenye riwaya zilizo swahīh na hasan peke yake, haliyakuwa matamshi yenye kuashiriya udhaifu ndiyo yanayopasa kutumika kwenye riwaya zote nyengine. Sababu yake ni kwamba kudhihiri kwa uhakika wa jambo hudokeza ukweli wa lenye kunasibishwa na mwenye kuhusika; kwahivyo hayafai kutumiwa isipokuwa kwa yaliyo ya kweli, asije mwenye kuyasimulia akatumbukia kwenye urongo.

Hukmu hii imekiukwa na muandishi (wa al-Muhadh-dhab) na kundi kubwa la wanavyuoni miongoni mwa wenzetu na wengineo. Bali, yamekiukwa na idadi kubwa sana ya wanavyuoni kutoka kwenye vitagaa chungu nzima vya ilimu, isipokuwa wenye ujuzi zaidi miongoni mwa wanavyuoni wa hadīth. Kwa hakika huku ni kuzembea kubaya, kwa sababu utawakuta wengi wa wenye mazoweya ya kusema, „Imepokewa kutoka kwake,‟ kuhusiana na riwaya iliyo swahīh. Au husema, „Amesema,‟ au „amepokea‟ kwa riwaya iliyo dhaifu. Jambo hili huchangia kupotoka kutoka kwenye njia ya sawa.”1

1 Al-Majmū’ 1:63

Page 97: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

79

RIWAYA DHAIFU ZISIZOWEZA KUTILIANA NGUVU

Huwenda mtu akahoji, “Sisi tunakubali yakwamba riwaya hizi ni dha‟īf zikisimama katika hali ya upweke. Lakini, kwani haziwezi kutiliana nguvu zikiwekwa pamoja?”

Jawabu la suala hili ni, “Laa,” kwa sababu mbili zilizojadiliwa katika yafuatayo.

1. Tafauti za riwaya hizi zimedhihiri na wala si za kweli, kwa sababu riwaya tuliyo nayo ya kipekee iliyoshikana (ambayo haikukatika) ni ile ya as-Sā‟ib Bin Yazīd. Riwaya za Yazīd Bin Rūmān na Yahyā Bin Sa„īd al-Answārī, zote mbili hizo zimekatika; na inaelekea kana kwamba zote hizo mbili zilikatikia kwa mmojawapo wa wapokezi kutoka katika riwaya ya kwanza. Vilevile kuna uwezekano mwengine. Kuwepo kwa uwezekano huo kunatangua nafasi ya kupatikana kwa dalili yoyote kutoka katika riwaya hizi.

2. Tumethibitisha hapo awali yakwamba riwaya ya Mālik kutoka kwa Muhammad Bin Yūsuf kutoka kwa as-Sā‟ib ya rak„āt kumi na moja ndiyo iliyo swahīh, na kwamba yoyote mwenye kutafautiana na Mālik au Muhammad Bin Yūsuf atakuwa amekosea. Kwahiyo, riwaya za Ibn Khusayfah na Ibn Abī Dhubāb, zote hizo mbili ni Shādh (isiyo ya kawaida); na imethibitishwa katika fanni ya Hadīth yakwamba riwaya ambazo ni Shādh (zisizo za kawaida) zinafaa kukataliwa kwa sababu zina makosa; na kwamba chenye makosa hakifai kutumika katika kutilia nguvu, kama ilivyoelezwa na Ibn Abū Salāh:

“Iwapo mpokezi atakuwa pekee katika kusimulia riwaya iliyo geni, na kama riwaya hii itakhitilafiana na riwaya za wapokezi walio waangalifu na wenye kukubalika, riwaya yake itazingatiwa kuwa si ya kawaida na itakataliwa. Hatahivyo, ikiwa riwaya yake haikukhitilafiana na nyenginezo, lakini ikawa ina taarifa tu ambayo haikupokewa na wao, na lau kama yeye alikuwa ni

Page 98: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

80

mpokezi muadilifu, muaminifu na anayekubalika, basi riwaya yake hiyo geni nayo itakubalika.”1

Hapana shaka yakwamba riwaya zilizojiri ni za sampuli ya kwanza, kwa sababu wapokezi wao wanagongana na riwaya za waliokuwa na uangalifu na ubora kuliko wao. Kwahivyo wao wamekataliwa.

Ni jambo la dhahiri yakwamba sababu za kukataa kwa wanavyuoni kuhusu riwaya zilizo geni ni mgongano wao na riwaya zilizo swahīh. Kwahiyo, haina maana kutumia mithili ya riwaya zilizo na kasoro kama hizo ili kuzitilia nguvu riwaya nyengine. Jambo hili linathibitisha yakwamba riwaya geni na munkar hazifai kutumiwa kama dalili au ushuhuda kwa riwaya nyengine: kuwepo kwake hakuleti „ilmu yoyote ya ziyada.

La zaidi ni kwamba, haiwezekani kusema yakwamba riwaya mbili zilizokatika za Yazīd Bin Rūmān na Yahyā Bin Sa„īd kuwa zitasaidiana na kutiliana nguvu, kwa sababu sharuti yake ni kwamba wapokezi waliotupilia mbali isnād iliyobaki ni watu tafauti.2

Sharuti hili halifai katika hali hii, kwa sababu pana uwezekano mkubwa yakuwa wapokezi hawa wawili, wote wakiwa ni kutoka al-Madīnah, walipokea pamoja kutoka kwa Sheikh (mwalimu, mpokezi) huyo huyo mmoja; na pia pana uwezekano yakwamba huyo Sheikh wao mmoja ni mtu dhaifu au asiyekubalika. Pia inawezekana yakwamba hao mashekhe wao wawili ni Ibn Khusayfah na Ibn Abī Dhubāb, wakiwa wote wawili ni kutoka al-Madīnah, na wote wakiwa na makosa kwenye riwaya hii, kama ilivyotangulia – wakazifanya riwaya za Yazīd Bin Rūmān na Yahyā Bin Sa„īd kuwa na makosa pia. Yote haya yanawezekana; na uwezekano ukasababisha ushahidi

ukaporomoka. Amesema Ibn Taymiyyah (رحمه اهلل): “Wamekhitilafiana wanavyuoni iwapo riwaya mursal zinakubalika

1 Al-Muqaddimah Uk. 86

2 Angalia katikaNatā’ij ul-Afkār cha as-San’ānī 1:288. Sharuti hili vilevile limejadiliwa

kwa kina na al-Albānī katika Nasb ul-Majānīq.

Page 99: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

81

au zinakataliwa. Rai iliyo ya sawa ni kwamba baadhi zao zinakubalika, na nyenginezo zinakataliwa, na baadhi nyengine ni mawqūf (kuwa ni maneno ya mpokezi peke yake) ... Riwaya mursal inayogongana na riwaya za wapokezi waaminifu inakataliwa. Na iwapo riwaya mursal inapokewa na wapokezi wawili ambao mashekhe wao ni tafauti, hili linathibitisha ukweli wake, kwa sababu mtu hawezi kuwatarajia kwa kawaida kufanya makosa yenye kufanana.”1

Kutojali kwa sharuti hili muhimu kumewapelekea baadhi ya wanavyuoni waswahihishe riwaya ambazo waziwazi hazifai, kama vile kisa cha Gharānīq2!

UWEZEKANO WA MAPATANO

Baadhi ya watu hujaribu kuleta upatanishi baina ya riwaya dhaifu zilizotangulia na riwaya iliyo swahīh kutoka kwa „Umar. Wao husema, “Katika zama za „Umar, mwanzo watu walikuwa wakiswali rak„āt kumi na moja; kisha baadae wakaswali rak„āt ishirini na witr tatu.”

Lakini hata hivyo, kwa vile tushathibitisha udhaifu wa riwaya hizi kutoka kwa „Umar, hapana haja ya kujaribu kuleta mapatano ya sampuli hiyo – ambayo ndiyo njia yake ya pekee katika kutumika iwapo riwaya zitaelekea kuwa swahīh. Bali, uwezekano upo katika kuukosoa upatanishi kama huo, kama alivyosema al-

Mubārakfūrī (رحمه اهلل): “Inawezekana mtu kusema yakwamba mwanzo waliswali

rak„āt ishirini, na kisha wakaswali kumi na moja. Hili ni lenye

1 Kutoka katika kurasa ambayo haijachapishwa ya Al-Hāfidh Ibn ‘Abdulhādī katika al-

Maktabat uz-Zāhiriyyah, Damascus. 2 Mâna ya Gharānīq ni masanamu. Kisa hicho kinadai eti Allāh ( وتعاىل سبحانه ) aliteremsha

bâdhi ya āyāt kutoka katika sūrat un-Najm akiwasifu masanamu wa ki-Qureysh na akathibitisha thamani ya maombezi yao! Kisa hiki kinapatikana kwenye bâdhi ya vitabu vya tafsīr!

Page 100: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

82

kutosheleza zaidi kwa sababu linakubaliana na lilothibitishwa kutoka

kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), haliyakuwa kitendo cha kwanza kilikwenda

kinyume nacho.”1

RIWAYA KUTOKA KWA MASWAHABA WENGINE

Kuna riwaya kutoka kwa Maswahaba wengine zinazoashiriya yakwamba waliswali rak„āt ishirini. Hata hivyo, hakuna riwaya yoyote kati ya hizo iwezayo kuhimili ukosoaji wa kitaalamu. Lakini, kwa vile watu wengi wamedanganyika nao, ni muhimu kuuthibitisha udhaifu wao na kuzibainisha hali zao.

RIWAYA KUTOKA KWA „ALĪ

1. Riwaya ya Abū al-Hasnā‟

Abū al-Hasnā‟ amepokea yakwamba „Alī ( عنه اهلل رضي ) alimuamrisha mtu

awaongoze katika mwezi wa Ramadhān kwa rak„āt ishirini.2

Amesema al-Bayhaqī, “Isnād ya riwaya hii ni dha‟īf.” Udhaifu wake umetokamana na Abū al-Hasnā‟, aliyewahi kutajwa na adh-Dhahabī kuwa, “Mtu huyu hajulikani.” Na al-Hāfidh akasema, “Hajulikani (na wanavyuoni).”

Riwaya hii ina matatizo mengine vilevile, ambayo ni i‟dāl3 baina ya Abū al-Hasnā‟ na „Alī. Al-Hāfidh akasema kumuhusu yeye, “Amepokea kutoka kwa al-Hakam Bin „Utaybah, kutoka kwa Hanash, kutoka kwa „Alī kuhusiana na udh-hiyah (kuchinja).”4 Kwahiyo, katika riwaya iliyojiri, wapokezi wawili wamekosekana baina ya Abū al-

1 Tuhfat ul-Ahwadhī 2:76

2 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah katika al-Musannaf (2:90:1) na al-Bayhaqī (2:497).

3 Kukatika kunapotokea pindi wapokezi wawili au zaidi wanapokosekana kwenye

isnād. 4 At-Tah-dhīb.

Page 101: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

83

Hasnā‟ na „Alī.

2. Riwaya ya Hammād Bin Shu‟ayb

Amepokea Hammād Bin Shu‟ayb kutoka kwa „Atā‟ Bin as-Sā‟ib, kutoka kwa Abī „Abd ir-Rahmān as-Sulamī:

“„Alī ( عنه اهلل رضي ) aliwaitisha wasomaji Qur‟ān katika mwezi wa

Ramadhān, na akamuamrisha mmoja wao awaongoze watu kwa rak„āt ishirini. Kisha „Alī aliwaongoza kwenye swala ya witr.”1

Riwaya hii ni dhaifu kwa sababu tatu:

a) Riwaya za „Atā‟ Bin as-Sā‟ib hazikuwa na uwiyano (kutokana na umri wake wa uzee) – wakati Hammād Bin Shu‟ayb alipokuwa akipokea kutoka kwake.

b) Hammād Bin Shu‟ayb ni mtu dhaifu mno, kama alivyoashiriya al-Bukhārī, “Mtu huyu nina shaka naye.” Na akasema:, “Riwaya zake zinakataliwa.” Al-Bukhārī kwa kawaida huwa hatamki maneno kama hayo isipokuwa kwa watu ambao riwaya zao zote ni lazima ziepukwe. Kwahiyo, riwaya hii haiwezi kuchukuliwa kama ushahidi au dalili.2

c) Muhammad Bin Fudhayl, ambaye ni mpokezi muaminifu, alikhitilafiana na Hammād katika upokezi huu. Ibn Abī Shaybah alipokea riwaya hiyo hiyo kutoka kwa „Atā‟, kwa njia ya ufupisho, akasema, “„Alī aliwaongoza kwenye swala ya qiyām katika Ramadhān.” Riwaya hii haikutaja idadi ya rak„āt. Kwa vile Muhammad Bin Fudhayl ni mtu muaminifu,

1 Al-Baihaqī

2 Angalia hii katika Tadrīb ur-Rāwī cha as-Suyūtī, Mukhtasaru ‘Ulūm il-Hadīth cha Ibn

Kathīr, at-Tahrīr cha Ibn ul-Hammām, ar-Raf’u wat-Takmīl cha Abū al-Hasanāt, Tuhfat ul-Ahwadhī cha al-Mubārakfūrī, na kadhâlika. Wote wamekubaliana yakwamba hii ndiyo mâna anayokusudia al-Bukhārī anaposema hivyo.

Page 102: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

84

yeye hakusimulia kama alivyosimulia Ibn Shu‟ayb, riwaya ya huyu Ibn Shu‟ayb imezingatiwa kuwa ni dhaifu kulingana na hukmu za wanavyuoni wa hadīth.

RIWAYA KUTOKA KWA UBAYY BIN KA‟B

1. Riwaya ya „Abd ul-„Azīz Bin Rafī‟

Ibn Abī Shaybah amenukuu kwenye al-Musannaf kwa mapokezi swahīh yakwamba amesema „Abd ul-„Azīz Bin Rafī‟:

“Ubayy Bin Ka‟b aliwaongoza watu kwenye qiyām ya Ramadhān katika mji wa al-Madīnah kwa rak„āt ishirini ikifuatiwa na witr tatu.”

Lakini hatahivyo, isnād ya riwaya hii ilikatika baina ya „Abd ul-„Azīz Bin Rafī‟ na Ubayy Bin Ka‟b, tafauti ya muda baina ya vifo vyao ilikuwa takriban miaka mia moja au zaidi.1 Mwanachuoni mkubwa wa kihindi, an-Nīmawī, amesema, “Huyu „Abd ul-„Azīz Bin Rafī‟ hakuwahi kuonana na Ubayy Bin Ka‟b.” Al-Mubārakfūrī alinukuu maneno haya na akasema:

“Aliyoyasema an-Nīmawī ni ya kweli. Riwaya hii kutoka kwa Ubayy imekatika; na zaidi ni kwamba, imekhalifiana na yaliyothubutu kutoka kwa „Umar yakwamba aliwaamrisha Ubayy Bin Ka‟b na Tamīm ad-Dārī wawaongoze watu kwa rak„āt kumi na moja. Vilevile imekhalifiana na yaliyothubutu kutoka kwa Ubayy yakwamba aliwaongoza baadhi ya wanawake nyumbani kwake kwenye qiyām ya Ramadhān kwa rak„āt nane na witr.”

Kwa haya alikuwa akikusudia aliyoyataja kwenye ukurasa uliotangulia wa kitabu chake:

“Dalili ya rai hii ya Mālik, yaani; rak„āt kumi na moja, ndiyo yaliyopokewa na Abū Ya‟lā kutoka katika hadīth ya Jābir Bin

1 Angalia kwa mfano Tahdhīb ut-Tahdhīb.

Page 103: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

85

„Abdillāh yakwamba Ubayy Bin Ka‟b alimwambia Mtume ( صىل اهلل ‟.Jana usiku (wa Ramadhān) mimi nilifanya kitu„ ,(عليه وسلم

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamuuliza, <Na ni jambo gani hilo

ulolifanya, ewe Ubayy ?> Akajibu, „Baadhi ya wanawake nyumbani kwangu waliniomba, “Sisi hatujui kusoma Qur‟ān, sasa waonaje utuongoze kwenye swala?” Basi, mimi

nikawaongoza kwa rak„āt nane zikifuatiwa na witr. Mtume ( صىل hakusema kitu, jambo ambalo lililoifanya hiyo kuwa (اهلل عليه وسلم

ni Sunnah ya kuidhinishwa. Al-Haythamī akasema kuhusu riwaya hii, „Isnād yake ni hasan.1‟”

2. Riwaya Ya Abū Ja‟far Ar-Rāzī

Amepokea Abū Ja‟far Ar-Rāzī, kutoka kwa ar-Rabī‟ Bin Anas, kutoka kwa Abī al-„Āliyah, kutoka kwa Ubayy Bin Ka‟b yakwamba „Umar alimuamrisha awaongoze watu kwenye qiyām ya Ramadhān, akisema,

“Watu walifunga wakati wa mchana na hawawezi kuisoma (Qur‟ān) kisawasawa; sasa wasemaje, utawasomea Qur‟ān wakati wa usiku?” Akajibu, “Ewe kiongozi wa Waumini! Jambo hili halijawahi kufanywa kabla!” „Umar akamwambia, “Mimi najua, lakini hili ni bora.” Basi akawaongoza kwa rakāt ishirini.2

Isnād ya riwaya hii ni dhaifu. Jina la Abū Ja‟far Ar-Rāzī ni „Īsā Bin Abī „Īsā Bin Māhān. Adh-Dhahabī alimuingiza kwenye kitabu chake adh-Dhu‟afā‟ (Watu Madhaifu) kisha akasema, “Amesema Abū Zar‟ah, „Huyu hufanya makosa mara kwa mara.‟ Ahmad alimueleza huyu kama, „Si mtu hodari.‟ Na wakati mmoja alisema, „Mtu huyu hupitikiwa.‟ Al-Fallās akasema, „Hukosea-kosea katika upokezi wake.‟ Haliyakuwa mtu mwengine akasema, „Huyu ni mtu muaminifu.‟”

1 Vilevile imepokewa na Ibn Nasr

2 Imepokewa na adh-Dhiyā’ ul-Maqdisī katika al-Mukhtārah (1:384)

Page 104: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

86

Vilevile adh-Dhahabi alimuingiza kwenye kitabu chake, “al-Kunā”, na akasema, “Huyu alilaumiwa na Wanavyuoni wote wa hadīth.” Na Ibn ul-Qayyim akasema, “Ni maarufu kwa riwaya zake munkar. Hapana hata mmoja miongoni mwa wanavyuoni wa hadīth awezae kukubali riwaya zake za upweke.”

Mtafiti yoyote katika hadīth anaweza kwa urahisi kujionea mpangilio wa kimakosa wa Abū Ja‟far Ar-Rāzī, kwa sababu riwaya zake mara kwa mara hugongana na zile za wapokezi walio waaminifu.1

Katika riwaya iliyojiri, huyu Abū Ja‟far alikhitilafiana na riwaya

swahīh iliyotangulia na kuthibitishwa ya „Umar (رضي اهلل عنه) akimuamrisha Ubayy awaongoze watu kwa rak„āt kumi na moja. Mtu hawezi kumdhania Ubayy awachane na amri iliyo swahīh ya „Umar,

ambayo ni yenye kukubaliana na Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Shida nyengine ya riwaya hii ni kwamba Ubayy alisema, “Jambo hili halijawahi kufanywa kabla!” Hawezi mtu kumdhania Ubayy kusema mambo kama hayo, wala „Umar kuyaafiki hayo, hali ya kuwa

haya ndiyo mafundisho ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) yakwamba ni lazima

wote hao wawili wawe na mashahidi au wajulikane.

RIWAYA KUTOKA KWA IBN MAS‟ŪD

Amepokea Zayd Bin Wahab (رضي اهلل عنه), “„Abdullāh Bin Mas‟ūd alikuwa

akituongoza sisi kwenye swala katika Ramadhān, akimaliza swala na

1 Mfano mwengine ni riwaya yake yakwamba, “Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) aliendelea

kuleta qunūt kwenye swala za fajr mpaka alipoondoka kwenye maisha ya hapa

duniani.” Hii inakhitilafiana na riwaya iliyo swahīh ya Anas ( عنه اهلل رضي ) yakwamba:

“Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) hakuwa akileta qunūt isipokuwa anapowaombea bâdhi ya

watu au akiwâpiza bâdhi ya watu.”

Page 105: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

87

bado ikawa kumebaki sehemu ya wakati katika usiku.”Al-„Amash1 akaongezea, “Aliswali rak„āt ishirini na witr tatu.”2

Al-Mubārakfūrī akazungumzia kuhusu riwaya hii, “Hata hii pia imekatika kwa sababu Al-„Amash hakukutana na Ibn Mas‟ūd.”3

Matamshi ya Al-Mubārakfūrī ni ya sawa, kwani, hata kama ya riwaya hii ni swahīh mpaka kwa Al-„Amash4, kuna emma wapokezi wawili au watatu waliokosekana baina yake na Ibn Mas‟ūd.”

MASWAHABA WALIAFIKIANA VIPI?

Kutokana na mjadala uliopita, imedhihirika yakwamba Maswahaba hawakuswali rak„āt ishirini katika swala ya Tarawêh. Kwahiyo, hakuna msingi wowote katika kudai kwao yakwamba, “Maswahaba walikuwa wameafikiana yakuwa swala ya Tarawêh inatakiwa iswaliwe rak„āt ishirini5.” Kwa ajili hii, mwanachuoni Mkubwa, al-Mubārakfūrī alisema, “Madai haya hayafai.”6

Vilevile, hakuna msingi wowote katika kudai kwao yakwamba, “Kuna riwaya mutawātir7 yakwamba Maswahaba, ma-

1 Jina lake ni Suleimān Bin Mahrān. Alikuwa ni miongoni mwa wanazuoni wa hadīth

na vitagâ vyengine vya ‘ilmu. Alikufa katika mwaka wa 147H. 2 Imepokewa na Ibn Nasr al-Marwazī katika Qiyām ul-Layl (Uk. 91). Hiki ni kitabu

chenye thamani kubwa, ambacho mtunzi wake amepokea riwaya nyingi ambazo ni tabu kupata kwenye mitungo mengine. Kitabu hiki kimefupishwa na al-Maqrīzī, aliyezitupa Isnād za riwaya nyingi (ikiwemo hii iliyojiri), akaipunguzia thamani yake, na kuifanya kuwa ni vigumu kuihukumu riwaya kama hiyo. Kitabu kilichapishwa India. 3 Tuhfat ul-Ahwadhī 2:75

4 Al-‘Aynī ameitia Isnād ya riwaya hii, kutoka kwa Ibn Nasr, katika ‘Umdat ul-Ahkām

(5:357) 5 Kama ilivyo, kwa mfano katika ‘Umdat ul-Ahkām (5:357), Mirqāt ul-Mafātīh (2:175),

na kadhālika. 6 Tuhfat ul-Ahwadhi 2:76

7 Riwaya zenye isnād nyingi zilizo swahīh.

Page 106: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

88

tābi‟ūn, na wale waliowafuata wao mpaka kwenye zama zetu hizi, wote hao walikuwa wakiswali qiyām, rak„āt ishirini.” Kama ilivyothibitishwa hapo juu, haya ni madai ya urongo, kwa sababu idadi idadi hii haiwezi kunasibishwa, kwa njia iliyo swahīh, kwa swahaba swahaba yoyote; bali, inagongana na amri ya „Umar ya kuswali rak„āt rak„āt kumi na moja.

Jambo hili linapasa kuwatanabahisha wanavyuoni watahadhari, na wasikubali madai ya ijmā‟ (maafikiano) bila ya kufanya utafiti wa kisawasawa. Madai mengi ya sampuli hiyo yamethibitishwa ukosoaji wake baada ya kuchunguzwa. Amesema Siddīq Hasan Khān:

“Watu wamekuwa hawajali kabisa katika kusimulia ijmā‟ (maafikiano). Kwahiyo, twawaona wale wenye ilimu chache katika rai za wanavyuoni wakidhania yakwamba yaliyokubaliwa katika madh-hab zao (katika mas‟ala ya ki-fiqh) au nchini mwao ndiyo ijmā‟. Kwa hakika hii ni hatari kubwa. Kwa madai kama hayo yaliyokosa muelekeo, ambayo hayakuegemezwa juu ya utafiti wa ki-ilimu na ucha-Mungu, yanasababisha madhara ya ujumla kwa Waislamu.

Ama kuhusu wafuasi wa madh-hab Manne, wao huzingatia jambo lolote waliloliafiki miongoni mwao kuwa ndiyo ijmā‟. Hili zaidi limedhihiri kwa wanavyuoni wa baadae miongoni mwao, kama vile an-Nawawī kwenye ufafanuzi wake katika Swahīh Muslim.

Hii sio ile sampuli ya ijmā‟ inayochukuliwa na wanavyuoni kuwa kama dalili. Zama (Qarne) zilizokuwa bora: za mwanzo (Maswahaba), kisha zilizofuata, kisha nyengine zilizofuata, zilikuwepo kabla ya kujitokeza kwa madh-hab. Pia, katika zama za kila mmojawapo wa ma-Imām Wanne, palikuwa na wanavyuoni wasiohesabika ambao waliokuwa wakifanya ijtihād.1 Yakaendelea haya kwenye vizazi vilivyo pokezana. Yote haya ni dhahiri kwa mtu yoyote wa kisawasawa aliye na ilimu. Lakini ni kwa bahati mbaya tu yakwamba usawa ndicho kikwazo kikubwa, kisichoweza kushindwa isipokuwa na wale ambao

1 Asili au chimbuko la hukmu iliyotokamana na ushahidi unaopatikana.

Page 107: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

89

waliofunguliwa mlango na Allāh (سبحانه وتعاىل) na kuelekea kunako

ukweli. Amesema Imām ash-Shawkāni katika „Wabal ul-Ghamām, Hāshiyatu Shifā‟ il-Awām‟:

„Mas‟ala ya muafaka yaliyopokewa kwenye vitabu yakazuka kutoka kwenye hali ambazo mpokezi hakuwa na ufahamu wa kuhusiana na mas‟ala makhsusi. Kuwa katika hali ya kutolifahamu jambo fulani hakumaanishi yakwamba hapakuwa na ikhtilafu. Jambo bora liwezalo kusemwa ni kwamba mtu huwenda akadhania yakuwa palikuwa na muafaka (maafikiano). Na mambo ya mtu kuwa na dhana hayatoshelezi kuwa ndio msingi au dalili ya kupatikana kwa muafaka. Wale wenye kuchukulia muafaka kuwa ndio dalili hawawezi kuchukuwa dhana kama hizo, kutoka

kwa mtu mmoja wa Ummah huu. Allāh (سبحانه وتعاىل) hahitaji hilo

kutoka kwa viumbe vyake. Kama mwanachuoni atasema yakwamba yeye hajui dalili yoyote kutoka kwenye Qur‟ān au Sunnah kuhusiana na mas‟ala fulani, matamshi yake hayatochukuliwa na mwanachuoni yoyote aliye msomi kuwa ndiyo dalili. Sasa lau kama utayafahamu haya, itakuwa ni rahisi kwako kuihukumu taarifa kama hii kuhusu muafaka.‟”1

Vilevile, al-Imām Abū Mūhammad Bin Hazm ameyazungumza mas‟ala haya kwa kina katika kitabu chake chenye thamani kubwa, “Ihkām ul-Ahkām fī Usūl il-Ahkām”, kilichochapishwa kwa juzū Nane. Kwa atakae kufanya uchunguzi wake kuhusu madai ya mas‟ala tafauti yanayohusiana na ijmā‟ na arudie kwenye kitabu hicho, kwa sababu ni mojawapo ya vitabu bora vya misingi ya fiqh, juu ya dalili zilizo swahīh kutoka katika Kitāb na Sunnah.

1 As-Sirāj ul-Wahhāj, min Kashfi Matwālibi Swahīh Muslim Bin al-Hajjāj 1:3

Page 108: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

90

IDADI YA RAK‟ĀT YA Tarawêh YENYE KURUHUSIWA

SUNNAH ZA MTUME NA MASWAHABA ZAKE

Tumeshathibitisha yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na Maswahaba zake

waliswali rak‟āt Kumi na Moja katika Qiyām. Hii ndiyo (رضي اهلل عنهم)

idadi swahīh ambayo waliopokewa kuiswali, pasi na kuzidisha kitu, katika Ramadhani na nyakati nyengine katika mwaka mzima.

Hakuna riwaya iliyo swahīh yenye kuthibitisha yakwamba palikuwa na Swahaba yoyote aliyeswali rak‟āt ishirini za Tarawêh.

Bali, imethubutu yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) aliwaamrisha watu

waswali rak‟āt Kumi na Moja, muafaka na kitendo swahīh

kilichopokewa cha Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ). Kwahivyo, ni waajib

kushikamana na idadi hii, bila ya kuongezea kitu, kufuatia amri yake

:(صىل اهلل عليه وسلم)

“... Wale miongoni mwenu watakaoishi baada yangu wataona ikhtilafu nyingi. Kwahiyo, shikamana na Sunnah zangu, na Sunnah za Makhalifa waongofu; shikamaneni nazo kisawasawa, ziumeni kwa meno (magego), na mujihadhari na mambo ya kuzua (katika Dini), kwa sababu kila jambo la kuzua ni bid‟ah, na kila bid‟ah ni kitendo cha upotofu.”1

Kwenye haya matamshi ya mwisho, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akaongezea katika hadīth nyengine:

“Na kila kitendo cha upotofu, mwisho wake ni motoni.”2

1 Imepokewa na Imām Ahmad, Abū Dāwud, at-Tirmidhī, Ibn Mājah na al-Hākim, kwa

mapokezi mbalimbali kutoka kwa al-‘Irbādh Bin Sāriyah ( عنه اهلل رضي ). Ilihukumiwa kuwa

ni swahīh na at-Tirmidhī, al-Hākim, adh-Dhahabi, na wengineo; nasi twawâfiki katika hukmu zao. 2 Imepokewa na an-Nasā’ī, Abū Nu’aym (katika al-Hilyah) na al-Bayhaqī (katika al-

Asmā’u was-Sifāt), kwa isnād iliyo swahīh kutoka kwa Jābir Bin ‘Abdillāh. Tambua

Page 109: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

91

Ni jambo maarufu sana yakwamba wanavyuoni wamekhitilafiana kwenye mas‟ala mengi ya fiqh, miongoni mwayo ikiwemo haya mas‟ala ya idadi ya rak‟āt za Tarawêh. Twaona kwenye suala hili rai sampuli nane zilizo tafauti:

“Rak‟āt arubaini na moja, thalathini na sita, thalathini na nne, ishirini na nane, ishirini na nne, ishirini, kumi na sita na kumi na moja.”1

Hadīth hiyo iliyotangulia hapo juu inaashiriya njia ya kutatua ikhtilafu yoyote inayotokea baina ya Waislamu. Kwa vile suala hili ni jambo ambalo watu walilokosana kwalo, tulitatue kwa kuregea

kwenye Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), ambayo si chochote

isipokuwa ni kuswali rak‟āt Kumi na Moja. Kwa hakika ni waajib kufuata hilo, na kutupilia mbali lolote lenye kwenda kinyume chake - hususan iwapo Sunnah za Makhalifa waongofu (Khulafâ) inaafikiyana nayo vilevile.

Lau kama idadi ya nyongeza, juu ya riwaya swahīh ya Kumi na Moja, ingelikuwa imethubutu kutoka kwa miongoni mwa Makhalifa waongofu na wengineo katika wanavyuoni wa Maswahaba, basi tungelishindwa ikatubidi tukubali kuruhusu kwao. Sababu ya haya ni kwamba sisi twaamini ilimu yao na fadhla zao, kukataa kwao mambo ya kuzua katika Dini, na kuhusika kwao kukubwa katika kuwakataza watu kuzua. Hatahivyo, kwa vile hapana chochote katika haya kilichothubutu kutoka kwao, kama ilivyothibitishwa hapo juu, sisi hatuzingatii nyongeza yoyote kuwa ni yenye kuruhusiwa. Hili, twataraji litaleta ukumbusho kwa wale wenye kudai yakwamba wanawapenda Maswahaba na kupendelea kulinda mafunzo yao. Mlinzi wa kweli wa Maswahaba ni yule mwenye kuzifanyia utafiti

yakwamba bâdhi ya watu huizingatia ki-makosa sehemu hii na kudhania yakwamba ni katika sehemu ya hadīth iliyotangulia ya al-‘Irbādh. 1 Al-’Ayni amepokea rai hizi (5: 356-357), na kisha akataja yakwamba idadi ya mwisho

ndiyo ambayo iliyochaguliwa na Imām Mālik, na vilevile Abu Bakr Bin al-’Arabī .

Page 110: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

92

riwaya zitokazo kwao, na kisha ashikamane nazo.

JEE, “ZIYADA” NI NZURI KILA MARA ?

Sisi tunaamini yakwamba kuongezea kitu kwenye idadi ya sawa ya Tarawêh kunakhalifiana na Sunnah, kwa sababu vitendo vya ibādah ni lazima viambatane na mafundisho ya Qur‟ān na Sunnah, bila ya kumruhusu mtu kuzifanyia ziyada au kuzibadilisha juu ya makisio na uzushi.

Mtu na atafakari yakwamba kwenye mas‟ala mengi, “Ziyada ya kupita kiyasi ni mbaya kama ilivyo pungufu kupita kiyasi.” Riwaya yenye kupendeza inayohusiana na mas‟ala haya imepokewa kutoka kwa Mujāhid, aliyesema:

“Alikuja mtu mmoja kwa Ibn „Abbās akamwambia, „Mimi nilikuwa kwenye safari na mmojawapo wa marafiki zangu; nikaswali swala kamili, na rafiki yangu akaswali qasr (swala fupi).‟ Ibn „Abbās akamjibu, „Bali, ni wewe uliyekuwa na swala fupi, haliyakuwa swala ya mwenzako ndiyo iliyokuwa kamili!‟”1

Hii inaonyesha ufahamu mkubwa wa Ibn „Abbās, pindi alipoashiriya yakwamba ukamilifu wa ki-hakika na kutengea upo

kwenye kufuata Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na upungufu wa ki-

hakika na kukosa muelekeo ni kwenye lolote lenye kwenda kinyume chake, hata kama litakuwa ni kubwa katika idadi yake. Jambo hili si

la kustaajabisha kutoka kwake, kwa sababu Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alimuombea du‟ā‟ aliposema:

“Yā Allāh! Mpe huyu ufahamu wa Dīn, na umfahamishe „ilmu ya Qur‟ān.”2

Kwa hakika, mtu yoyote mwenye ufahamu wa kweli hawezi kuyakengeuka maneno haya ya Ibn „Abbās, bali atakuwa ni mwenye

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah katika al-Musannaf (2:110:2)

2 Al-Bukhāri na wengineo.

Page 111: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

93

kuyakubali kuwa ndiyo hukmu inayohusiana na kila jambo katika Uislamu. Jambo lolote lenye kwenda kinyume cha haya kunakompa sifa za upungufu na kasoro Muumba Mwenye Hikmah (Allāh); na kwa hakika:

“Mola wako si Mwenye kusahau.”1

Katika mdahalo wake na m-Shi‟ah mmoja aitwae Ibn ul-Mutwahhar, Ibn Taymiyyah alisema:

“Wewe umedai yakwamba „Alī alikuwa akiswali rak‟āt elfu moja kila mchana na usiku. Haya si madai ya kweli. Mtume

wetu ( وسلم صىل اهلل عليه ) hakuwa akiswali usiku zaidi ya rak‟āt kumi

na tatu. Vilevile, haikupendekezwa kuswaliwa usiku mzima;

bali, imekirihishwa, kwa sababu Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alimwambia „Amr Bin al-„Ās, “Mwili wako una haki juu yako.”

Na zaidi ni kwamba, Mtume ( alikuwa akiswali ( اهلل عليه وسلمصىل

takriban rak‟āt arubaini katika kila mchana na usiku. „Ilmu ya „Alī

kuhusiana na Sunnah za Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), na kujihusisha

kwake kukubwa katika kushikamana nazo, hakukumruhusu yeye kubadilisha muelekeo wake apotoke kutoka kwenye Sunnah hizo - lau tutachukulia yakwamba patakuwepo na uwezekano wa upotofu kama huo.

Lakini hatahivyo, kuswali rak‟āt elfu moja ni jambo lisilowezekana pamoja na kwamba mtu atekeleze majukumu yake yote mengine; yeye mwenyewe huwa na majukumu yake: anahitaji kulala, chakula, kinywaji, kwenda kukidhi haja, kutawadha, kuingiliana na wake zake, kuwahudumikia jamii yake

1 Maryam 19:64

Page 112: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

94

na yenye kumpasa yeye na kadhaalika, yote hayo yatakuwa ni yenye kujaza nusu ya wakati wake.

Katika sehemu ya nusu iliyobaki, itambidi aswali takriban rak‟āt rak‟āt thamanini kwa saa moja. Hakuna mtu awezae kuswali rak‟āt rak‟āt thamanini kwa saa moja isipokuwa iwe ni kwa kuisoma Fātiha

Fātiha peke yake, tena hiyo ni bila ya kuwa na utulivu. „Alī (رضي اهلل عنه) ni bora zaidi kuliko kuiswali swala ya wanafiki, inayofanana na kudona kwa ndege, na ambamo ndani yake hawamkumbuki Allāh isipokuwa kwa uchache mno - kama ilivyopokewa kwenye swahīh mbili.”1

Tanabahi jinsi Ibn Taymiyyah alivyomuinua daraja „Alī ( عنه اهلل رضي )

juu ya uwezekano wa nyongeza katika Sunnah za Mtume ( عليه اهلل صىل) kwa kusema, “„Ilmu ya „Alī kuhusiana na Sunnah za Mtume (وسلم اهلل صىل

وسلم عليه ), na kujihusisha kwake kukubwa katika kushikamana nazo,

hakukumruhusu yeye kubadilisha muelekeo wake apotoke kutoka kwenye Sunnah hizo.”

SWALA ZA NAFL ZILIZODHIBITI

Kwa swala za nafl, kama vile sunnah za kawaida, istisqā‟ (kuomba mvua), na kusūf (kupatwa kwa jua/mwezi) utakuta yakwamba Mtume

.ametuwekea idadi ijulikanayo ya rak‟āt za kuswaliwa (صىل اهلل عليه وسلم)

Mafundisho hayo yanazingatiwa na wanavyuoni kuwa ni dalili iliyothubutu yakwamba mtu hafai kuongeza idadi hizo. Kwa mfano, chini ya Mlango wa “Rak‟āt mbili kabla ya Dhuhr”, Imām al-Bukhāri amepokea hadīth iliyopokewa na Ibn „Umar yakwamba:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali rakāt mbili kabla ya dhuhr.”

1 Al-Muntaqā min Minhāj il-I’tidāl Uk. 169-170

Page 113: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

95

Akaifuatanisha hii na hadīth ya „Āishah ( عنها اهلل رضي ) yakwamba:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakupuuza kuswali rak‟āt nne kabla ya

dhuhr.”1

Katika Fat-h ul-Bārī, al-Hāfidh amefafanua yakwamba al-Bukhārī alidokeza yakwamba rak‟āt hizo mbili kabla ya dhuhr si kiwango kilichofungwa kikawa hakiwezi kuongezeka. Matamshi ya al-Hāfidh yanaashiriya waziwazi yakwamba yeye anaamini kuwa hafai mtu kuongeza (bila ya dalili iliyo wazi) idadi ya rak‟āt

zilizowekwa na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).

Vilevile, mtu hafai kuzidisha idadi iliyopokewa ya rak‟āt katika swala ya Tarawêh. Mtu yoyote atakaedai kinyume cha hivyo atahitajika kutoa dalili kwa madai yake; na hilo haliwezekani!

Swala ya Tarawêh si swala ya nafl ambayo haikuwekewa mipaka, na haifai mtu kuiswali kwa idadi yoyote apendayo yeye mwenyewe. Bali, ni swala ya Sunnah iliyothubutu na kudhibitiwa. Amesema mwanachuoni Ibn Hajar al-Haythamī:

“Tafauti iliyoko baina ya swala za nafl ambazo hazikuwekewa mipaka na swala nyengine ni kwamba, hizo za mwanzo hazikudhibitiwa kwa idadi maalum, na kuziwacha wazi kwa wenye kufanya „Ibādah wazitekeleze nyingi iwezekanavyo apendavyo mtu.”2

1 Kulingana na ma-Shāfi’ī, sunnah iliyo sawa kabla ya dhuhr ni rak’āt mbili. Kulingana

na ma-Hanafi, ni nne. Sasa kwa vile idadi zote hizi mbili zimethubutu kutoka kwa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), uwiyano baina ya hadīth hizo unaweza kufanywa kwa kusema

yakwamba kwa uchache wa swala hiyo ya Sunnah ni rak’āt mbili, na kwamba hizo

nne, ambazo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakudumu kuziswali, zilikuwa ni zenye

kupendekezwa. 2 Al-Fatāwī al-Kubrā 1:193

Page 114: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

96

Kwa vile swala ya Tarawêh imefungwa (au imeekewa mipaka)

kwa idadi maalum (ya kumi na moja) ambayo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

hakuzidisha, kwahivyo inakuwa ni swala ya nafl iliyodhibitiwa (iliyo wekewa mpaka), na mtu hawezi kuwa na chaguo la kuongeza. Kulingana na Imām an-Nawawī:

“Swala ya Tarawêh inafanana na swala ya faradhi juu ya kwamba inaruhusiwa kuswaliwa kwa jamā‟ah. Kwahiyo, haiwezekani kubadilishwa kutoka katika njia ilivyothibitishwa.”1

MAANA YA BID‟AH

Hata kama tutakubali yakwamba swala ya Tarawêh ni swala ya nafl isiyokuwa na mipaka, hatutoruhusiwa kuiwekea vikwazo juu ya idadi maalum (kama vile ishirini), kwa sababu hairuhusiwi kushikamana juu ya vitendo vya „Ibādah kwa desturi maalum ambayo haikuwahi

kutekelezwa na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Amesema Mullā Ahmad ar-Rūmī:

“Lau kama kitendo chochote hakikupangiwa kutumika (na Mtume

na Maswahaba zake) katika zama za kizazi cha (صىل اهلل عليه وسلم)

kwanza, hiyo itakuwa na maana mojawapo katika yafuatayo:

1. Hapakuwa na haja ya kuwepo.

2. Kitu kiliwazuiya wasiweze kutekeleza.

3. Hawakujua kuhusu umuhimu wake.

4. Walikuwa ni wavivu au hawakuwa na hamu ya kulitekeleza.

5. Lilikuwa haliruhusiwi.

Uwezekano katika sampuli mbili za mwanzo hazina mashiko katika hali ya „Ibādah ya utakatifu wa kiwiliwili, kwa sababu haja ya

1 Imepokewa kutoka kwa an-Nawawī na al-Qastalānī katika Sharh al-Bukhāri (3:4) na

al-Haythamī katika al-Fatāwī (1:193)

Page 115: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

97

kujikurubisha zaidi kwa Allāh ( تعاىلسبحانه و ) haikomi; na baada ya Uislamu

kupata nguvu, hapakuwa na chochote cha kuzuiya utekelezaji wake.

Vilevile, mtu hawezi kutarajia yakwamba Mtume (صلى اهلل عليه وسلم)

alikuwa hajui au alifanya uvivu kutekeleza kitendo cha „Ibādah. Hii ni mojawapo ya fikra mbaya, yenye kupelekea kunako ukafiri. Kwahiyo uwezekano wa pekee uliobaki ni kwamba kitendo kama hicho ni cha makosa na hakiruhusiwi.

Jambo lenye kulingana nalo linaweza kusemekana kuhusiana na vitendo vya „Ibādah ambavyo havikutekelezwa na Maswahaba.

Iwapo kitendo cha uzushi kingelikuwa kikizingatiwa kuwa ni bid‟ah nzuri kwa sababu tu yakwamba ni kitendo cha „Ibādah, basi hapangelikuwepo na bid‟ah yoyote mbaya katika „Ibādah! Na zaidi ni kwamba, katika hali hiyo, hapatokuwa na sababu yoyote kwa wanavyuoni kuwaonya watu dhidi ya vitendo mbalimbali vya uzushi katika „Ibādah, kama vile swala ya Raghā‟ib, kuimba wakati wa Khutbah, adhān, na usomaji wa Qur‟ān, kupaaza sauti za dhikr wakati wa kubeba Jeneza, na kadhaalika.

Yoyote mwenye kudai kuwa vitendo kama hivyo ni vizuri na aambiwe yakwamba vitendo vizuri pekee ni vile ambavyo uzuri wake uliothibitishwa kwa dalili kutoka katika shar‟ – na kwahivyo hayatohesabika kama mambo ya bid‟ah.”1

Pia katika mas‟ala haya, Amesema „Abdullāh Bin „Umar ( رضي :(اهلل عنه

“Kila bid‟ah ni kitendo cha upotofu, hata kama watu watakiona kuwa ni kizuri.”

BAADHI YA MATAMSHI YA KI-UWANACHUONI

Idadi ya wanavyuoni wakubwa wameshikilia msimamo yakwamba

1 Imepokewa na ‘Alī Mahfūdh, katika al-Ibdā’ fi Madhārr il-ibtidā’ (Uk. 21-22)

Page 116: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

98

hairuhusiwi kuswali zaidi ya rak‟āt Kumi na Moja. Miongoni mwao ni Imaam Mālik (katika riwaya mojawapo itokayo kwake). Amesema As-Suyuti:

“Al-Jūrī1, mmojawapo wa marafiki zetu, amepokea yakwamba Mālik alisema, “Idadi ya rak‟āt ambazo ‟Umar Bin al-Khattaab alizowakusanya watu juu yake inapendekeza zaidi kwangu - ambayo

ni rak‟āt Kumi na Moja. Vilevile ilikuwa ndiyo swala ya Mtume ( صىل اهلل ,Aliulizwa, Rak‟āt Kumi na Moja ikiwemo witr?‟ Akajibu ‟.(عليه وسلم

‟Na‟am: na rak‟āt Kumi na Tatu ni karibu na hiyo (katika usawa)2. Kisha akaongezea, ‟Na mimi sifahamu ni kutoka wapi watu walizua hizi rak‟āt nyingi namna hii.‟”3

Imām Ibn ul-‟Arabī amezitaja riwaya zenye kukhitilafiana kutoka kwa ‟Umar, na rai yakwamba hakuna idadi maalum katika rak‟āt za Tarawêh. Kisha akasema:

“Msimamo wa sawa ni kuswali rak‟āt Kumi na Moja, ambao

ndiyo njia ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alivyoswali Qiyām.Idadi zote

nyengine hazina dalili au msingi wowote. Lau kama tungeliweka kiwango, basi iwacheni iwe ni idadi aliyoiswali

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمص ) hakuwahi kuswali

katika Ramadhān au katika miezi mengine zaidi ya rak‟āt Kumi na Moja. Hii ndiyo swala ya Qiyām; na mtu analazimika

kumfuata Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika kuiswali.”4

Imām Muhammad Bin Ismā‟īl as-San‟āni alithibitisha yakwamba idadi ya ishirini katika Tarawêh ni bid‟ah. Kisha akasema:

1 Kuna idadi ya wanavyuoni wa ki-Shâfi’ee wenye Jina hili la ukoo. Haieleweki ni yupi

miongoni mwao as-Suyuti aliyemkusudia hapa. 2 Hapa alikuwa akikusudia bâdhi ya riwaya swahīh kutoka kwa ‘Ā’ishah zilizotajwa

hapo awali, zikiwemo ndani yake rak’āt mbili za ‘ishā’. 3 Al-Maswābīh fī Swalāt it-Tarāwīh (Al-Fatāwī 2:77).

4 Sharh at-Tirmidhee (4:19).

Page 117: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

99

“Na hakuna chenye kustahiki kusifiwa katika bid‟ah. Bali, kila bid‟ah ni kitendo cha upotofu.”1

KUBAINISHA BAADHI YA SHAKA ZILIZOWEKWA

Mara nyengine shaka huvurumizwa kuhusu baadhi za nukta katika majadiliano ya hapo juu. Katika yafuatayo, tunawaletea zilizo maarufu miongoni mwazo, zikifuatwa na ubainifu wetu.

1. IKHTILAFU MIONGONI MWA WANAVYUONI

Kama ilivyotajwa hapo juu, wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu idadi ya rak‟āt za Tarawêh. Huwenda mtu akasema yakwamba ikhtilafu hii ni ishara yakwamba hakuna maandiko yaliyo wazi yenye kuifunga idadi hiyo. As-Suyūtī akaieleza shaka hii kama ifuatavyo:

“Wanavyuoni wamekhitilafiana kuhusu idadi (katika Tarawêh). Iwapo hayo yalithibitishwa kutokamana na kitendo cha Mtume

( وسلم عليه اهلل صىل ), basi hapangelikuwepo na ikhtilafu kama hiyo -

kama ilivyo kuhusiana na hali ya witr na swala za kawaida za Sunnah.”2

Jawabu la suala hili ni kwamba sababu ya kukhitilafiana si kawaida kuwa hakuna maandiko yaliyothubutu kutoka kwa Mtume

Miongoni mwa asili nyenginezo za ikhtilafu ni .(صىل اهلل عليه وسلم)

yafuatayo:

Maandiko swahīh hayakumfikia mwanachuoni, ikamsababisha kutoa fatwā yake ambayo ni kinyume chake.

Maandiko swahīh yalimfikia mwanachuoni kwa isnād aliyoiona kuwa isiyokubalika.

1 Subul as-Salâm.

2 Al-Hāwī (1:74)

Page 118: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

100

Mwanachuoni aliyafahamu maandiko ki-vyengine kutokamana na wanavyuoni wengine.

Na kadhaalika.1

Kwahiyo, si kawaida kuwa ikhtilafu husababishwa kwa ukosefu wa maandiko yaliyo swahīh. Kama ijulikanavyo, wanazuoni wamekhitilafiana kuhusiana na mas‟ala mengi licha ya kuwepo kwa hadīth swahīh katika yenye kuhusika.

Mfano mmoja ulio wazi ni ule wa kuinua mikono wakati wa swala kabla na baada ya rukū‟. Wanavyuoni wote wamekubaliana yakwamba hiki ni kitendo kilichopendekezwa, isipokuwa ma-Hanafī. Ikhtilafu hii ilikuwepo licha ya ukweli yakwamba kuna takriban hadīth ishirini zilizo swahīh zenye kuithibitisha. Baadhi ya hadīth hizo zimepokewa

na baadhi ya watangulizi wetu waongofu kama vile „Alī (رضي اهلل عنه). Na

katika mojawapo ya hadīth hizo, Abū Humayd as-Sā‟idī (رضي اهلل عنه) akaieleza swala ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiwa pamoja na Maswahaba

kumi, na pakawemo ndani yake kuinua mikono. Alipomaliza,

wakamwambia, “Umesema ukweli; hivi ndivyo alivyoswali Mtume ( صىل 2”.(اهلل عليه وسلم

Katika majadiliano mashuhuri mno yaliyowahi kutokea baina ya Abū Hanīfah na mmojawapo wa wanavyuoni wa hadīth, kama ilivyonukuliwa katika vitabu vya ki-Hanafi, aliulizwa Abū Hanīfah ni kwanini yeye huwa hakubali kuinua mikono yake; akajibu, “Ni kwa

sababu hakuna hadīth swahīh kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu

suala hili.”

Basi Abū Hanīfah hangelisema haya lau kama angelizijua hadīth

1 Sababu nyingi zilizowasababisha wanavyuoni kukhitilafiana zimejadiliwa kwa kina

na ma’ulamā’ mbalimbali, akiwemo Ibn Taymiyyah, waliyy Ullāh ad-Dahlawī na al-Hamīdī. 2 Al-Bukhārī.

Page 119: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

101

nyingi zilizo swahīh tulizozieleza hapo juu. Hii ni dalili iliyo dhahiri yakwamba ikhtilafu katika suala hili haikusababishwa na ukosefu wa maandiko yaliyo swahīh, lakini ni kwamba haikumfikia Imām kutoka katika asili swahīh.

Kwahiyo, sawa na ukweli yakwamba ikhtilafu katika suala hili haileti ishara ya ukosefu wa maandiko swahīh, basi ndivyo ilivyo katika suala la swala ya Tarawêh. Kwa hakika, hapo awali tulithibitisha kuwepo kwa maandiko yaliyo swahīh, na wala si sawa kutia shaka kwenye maandiko haya kwa sababu ya ikhtilafu. Bali, uwajibikaji wetu ni kuondoa ikhtilafu kwa kuregea kwenye

maandiko yaliyo swahīh, kama alivyoamrisha Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Naapa kwa (haki ya) Mola wako. Wao hawawi wenye kuamini (kweli kweli) mpaka wakufanye (wewe ndiye)

hakimu (mwamuzi) katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa, na

wanyenyekee kabisa.”1

Na akaamrisha Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Na kama mkikhitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Allāh na Mtume, ikiwa mnamwamini Allāh na siku ya

1 An-Nisā’ 4:65

Page 120: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

102

mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo ina matokeo bora kabisa.”1

Basi tena, ni ipi sababu ya ki-hakika ya ikhtilafu ya wanavyuoni katika idadi ya rak‟āt za Tarawêh? Jawabu letu ni kwamba ni mojawapo katika uwezekano sampuli mbili, ya kwanza ikiwa ndio yenye uzito na kuzoeleka:

a. Kutofahamu vizuri kuhusu maandiko swahīh katika kuswawirisha idadi ya sawa. Mwenye kuwa na udhuru huu atasamehewa kwa kutojisalimisha na maandiko, kama itakavyofahamika kutoka katika hadīth itakayokuja ya „Amr Bin al-„Ās.

b. Kuelewa visivyo au kutafsiri vibaya maandiko. Kwa mfano,

baadhi ya wanavyuoni wameifasiri hadīth ya „Ā‟ishah, “Mtume ( صىل اهلل hakuwa akiswali zaidi ya rak‟āt kumi na moja,” kumaanisha (عليه وسلم

witr peke yake. Hapana shaka, hii ni tafsiri ya ki-makosa, kwa sababu aliyasema hayo kwenye jawabu la suala, “Ilikuwaje swala ya Mtume

katika mwezi wa Ramadhān ?” Inayoashiriya yakwamba (صىل اهلل عليه وسلم)

jawabu lake lilikuwa limefungamana na swala zote za usiku, na wala siyo witr peke yake. Mbali na hayo, tafsiri hii itamaanisha yakwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiswali swala za usiku sampuli mbili,

swala ya witr yenye idadi ya kikomo cha rak‟āt kumi na moja, na qiyām yenye idadi isiyokuwa na idadi maalum ya kikomo cha rak‟āt! Hakuna mwanachuoni atakaekubaliana na uainishaji kama huu.

2. HAKUNA MAANDIKO YENYE KUKATAZA NYONGEZA

Huwenda baadhi ya watu wakasema, “Tumeshatambua uhakika

wa hadīth yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali rak‟āt kumi na

moja kwa swala ya Tarawêh. Vilevile tumeshatambua udhaifu wa

1 An-Nisā’ 4:59

Page 121: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

103

hadīth za rak‟āt ishirini. Lakini hatuoni ni kwanini mtu hawezi

kuongezea kwenye rak‟āt kumi na moja, kwani Mtume ( عليه صىل اهللhakukataza hilo.”

Jawabu la shaka hiyo ni kwamba vitendo vya „Ibādah haviwezi kuthibitishwa bila ya kuwepo dalili makhsusi (kutoka katika Qur‟ān na Sunnah). Hii ni hukmu ya ki-msingi iliyoafikiwa miongoni mwa wanavyuoni; na hatuwezi kumtarajia Muislamu aliye elimika kuikataa.

Lau kama si kwa hukmu hii, basi pangelikuwa na uwezekano kwa Muislamu yoyote kuongeza, kwa mfano, kiasi chochote apendacho katika idadi ya rak‟āt za swala za sunnah na faradhi, hata ingawa idadi hizi zimethibitishwa kwa kitendo cha

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Kisingizio chake ni kwamba Mtume ( صىل اهلل عليه hakukataza kuongezea katika hilo! Hii ni hoja isiyofaa, na (وسلم

wala hatuoni haja yoyote ya kuijadili kwa kina.

3. TEGEMEO JUU YA KAULI ZA UJUMLA

Baadhi ya watu ni wenye kutegemea kauli za ki-ujumla zenye kuhimiza kuswali pasi na kutaja idadi makhsusi za rak‟āt. Kwa mfano,

wao hutaja amri ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kwa Rabī‟ah Bin Ka‟b ( رضي اهلل :(pindi alipomuomba awe pamoja naye Peponi) (عنه

“Nisaidie nami dhidi yako kwa (kutekeleza) sujūd kwa wingi.”1

Au wanaitaja hadīth ya Abū Hurayrah:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akiwahimiza watu waswali qiyām

katika Ramadhān.”

Basi watu hutaja hadīth kama hizo na nyengine zinazofanana nazo,

1 Muslim na Abū ‘Uwānah.

Page 122: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

104

ambazo ni zenye kuzungumzia kwa ujumla. Zinaashiriya mapendekezo ya kuswali, pasi na kudhihirisha idadi.

Hii ni hoja iliyo nyonge sana, kwa sababu panaweza kutumika maandiko ya ujumla katika hali za ujumla peke yake iwapo hapatokuwa na maandiko mengine yenye kuyawekea vikwazo. Idadi ya rak‟āt katika swala ya Tarawêh imewekewa vikwazo na maandiko

yaliyo wazi kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Hairuhusiwi kubatilisha

vikwazo hivyo, kwa madai yakwamba ati Tarawêh inafuata mapendekezo ya ujumla. Mtu yoyote mwenye kudai jambo kama hilo anaweza vilevile kuswali swala ya adhuhuri rak‟āt tano kwa mfano, au akafanya sujūd mbili au rukū‟ tatu katika kila rak‟āt, kwa sababu kuna maandiko ya ujumla yanayoeleza juu ya fadhla za vitendo hivyo vyote!

Mwanachuoni mkubwa „Alī Mahfūdh amesema:

“Ni makosa kufuata maandiko ya ujumla, bila ya kuregea kwenye

ubainifu wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kupitia kwenye vitendo vyake au

kujiepusha. Hii inahusisha hata kufuata mambo yenye utata, ambayo yaliyokatazwa na Allāh.

Iwapo sisi tutategemea maandiko ya ujumla, tukapuuza ubainifu

(wa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)), tutafungua kwa hilo mlango mkubwa

sana wa bid‟ah usiowezekana kufungika, na kuwacha upenyo wa mambo ya kuzua katika Dīn bila ya mipaka!

Kwa mfano, amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), “Swala ni somo zuri

mno. Yoyote awezae kuongezea kitu, na afanye hivyo.”1 Sasa iwapo tutashikilia kwenye maana ya ujumla katika hadīth hii, hatutoweza kuikataa bid‟ah mbovu ya swala ya ar-Raghā‟ib au swala ya Sha‟bān ...

1 Imepokewa na at-Twabarānī katika al-Awswat kwa mapokezi yaliyo hasan kutoka

kwa Abū Hurayrah

Page 123: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

105

Kama mtu atapenda kuadhini kwa ajili ya „Īd, kusūf, au swala ya Tarawêh, hapo tutawezaje sisi kumkataza, tukasema yakwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwahi kufanya hivyo katika maisha yake

yote, na jawabu likawa ni kwamba adhān ni kitendo cha Da‟wah na dhikr, yote hayo mawili ni mambo yaliyopendekezwa katika Uislamu? ...

Kwa hakika, kila ambalo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliloliwacha, licha

ya kuwa na haja na uwezo wa kulifanya, basi kujiepusha nalo ni sunnah, na kulifanya ni bid‟ah.”1

4. KUWADHARAU (KUWATWEZA) WANAVYUONI WAKUBWA

Tunapotia mkazo katika kushikamana na idadi ya Tarawêh iliyothubutu kwenye Sunnah, hii haimaanishi hata chembe kuwa sisi twawadharau wanavyuoni wenye kukubali idadi za ziyada, au kwamba twawanasibisha na mambo ya uzushi.

Kama ilivyofafanuliwa hapo juu (chini ya Shaka-1), sisi hatuamini yakwamba wanavyuoni wakubwa wameegemeza rai zao juu ya matamanio ya nafsi, lakini wameegemeza rai zao juu ya uwanachuoni wa kihakika na kupambana kwa kusubiri kufikiya kwenye haki. Kwahiyo, wao watakuwa ni wenye kulipwa katika hali zote (Inshaa-Allāh) kama alivyosema ‟Amr Bin al-‟Ās

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) amesema:

“Atakapohukumu hākim2 kwa Ijtihād3, na akafikiya kwenye Ukweli, atapata malipo mara mbili. Na iwapo atahukumu kwa

1 Al-Ibdā’ Uk. 25

2 Hākim ni mtu mwenye uwezo na mamlaka kutoa hukumu katika suala moja au

mengi. Kwa kawaida hili huwa linamuhusu kiongozi, hakimu, au mwanachuoni. 3 Mâna ya Ijtihād ni kutumia juhd (juhudi kamili ipasavyo) katika kufikia uamuzi wa

sawa kutokana na ushahidi unaopatikana.

Page 124: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

106

Ijtihād, na akakosa kupata ukweli, atapata malipo mara moja.”1

Sisi hatuwezi kuzikataa fadhla alizonazo mwanachuoni juu yetu; wao ndiwo waliotuongoza sisi kupitia kwenye njia ya ilimu, na wakatufundisha umuhimu wa Kitāb na Sunnah, na kwamba inatupasa kuvithamini vitu hivyo kuliko rai zozote zenye kwenda kinyume nazo. Kwa mfano Imām ash-Shāfi‟ī amesema:

“Wameafikiyana Waislamu yakwamba itakapomdhihirikia mtu

yoyote Sunnah kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), basi haifai kwake

kuiwacha Sunnah hiyo kwa ajili ya rai ya mtu yoyote.”2

Zaidi ya hayo ni kwamba kukhitilafiana na baadhi ya wanavyuoni kwenye mas‟ala haya haimaanishi yakwamba sisi tunajizingatia kuwazidi wao kwa ilimu na ufahamu. Hayo si kweli, bali ni dhana zisizofaa.

Sisi twajua kwa yakini yakwamba ma-Imām wanne wana ilimu kuliko wanafunzi wao na wale waliokuja baada yao. Na juu ya hayo, wanafunzi wao walikhitilafiana nao kwenye mas‟ala mengi. Na jambo hili ni lenye kuendelea kutokeza katika kila vizazi vinavyofuatana; wanavyuoni waliokuja baadae wakikhitilafiana na wanavyuoni wa zamani - maadamu kunaendelea kuwepo wanavyuoni wenye ‟Ilmu miongoni mwa Waislamu. Wanafunzi hawa wanapokhitilafiana na waalimu wao, hapana anaefahamu yakwamba wao wanadai kuwa ni bora kuliko wao.

Kwa hakika, msimamo wetu na ma-Imām hawa ni kama alivyosema ‟Āsim Bin Yūsuf3, aliyeambiwa, “Kuna mas‟ala mengi ambayo wewe umekhalifiana na Abu Hanīfah.” Nae akajibu:

“Abu Hanīfah amepewa (katika ‟Ilmu na ufahamu) katika ambayo sisi hatukupewa. Ufahamu wake ulifikia kiwango ambacho sisi hatuwezi kufikia. Ama kutuhusu sisi, ufahamu wetu hauwezi

1 Al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

2 Ar-Risālah.

3 Alikuwa ni mwanafunzi wa wanavyuoni wawili wakubwa, Muhammad na Abū Yūsuf.

Page 125: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

107

kupita zaidi ya kiwango chetu. Na sisi hatuwezi kutoa fatwā kulingana na maneno yake mpaka tuweze kufahamu msingi wake wa aliyoyasema.”1

Hapa ‟Āsim alikuwa akikusudia maneno mashuhuri ya Abū Hanīfah:

“Hairuhusiwi kwa yoyote kuchukuwa rai zetu mpaka ajue tumeitegemeza juu ya nini.”

Kwahiyo, ukweli wa mambo ni kwamba, yeye alikuwa akijiegemeza kwa Abū Hanīfah, hata kama anakhitilafiana nae!

Sisi tunasema hayo ya hapo juu haliyakuwa, wakati huo huo tunathibitisha yakwamba Rehma za Allāh ni kunjufu kuliko kuifungamanisha ‟Ilmu na fadhla zake kwa hawa ma-Imām wanne

peke yao. Kwa hakika, Allāh (سبحانه وتعاىل) ana uwezo wa kuumba

(watu wengine) baada yao wenye ‟ilmu kuliko wao kwenye baadhi ya mas‟ala. Pia mtu wa hali ya chini anaweza kuwa na ‟Ilmu asokuwa nayo mtu aliye na hali bora. Hili ni jambo maarufu

miongoni mwa wanavyuoni, na akasema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Taifa langu ni kama mvua; hapana uwezekano wa kueleza iwapo uzuri wake upo mwanzoni au mwishoni mwake.”2

Usalama Katika Kushikamana Na Sunnah

Pasi na kujali kuhusu majadiliano yatakayoletwa kuhusiana na kuunga mkono au kupinga nyongeza ya kwenye idadi iliyopokewa ya rak‟āt, hakuna Muislamu awezae kusitasita katika kuthibitisha yakwamba

idadi bora ya kuswali ni ile iliyothubutu kutoka kwa Mtume ( صىل اهلل عليه

1 Imepokewa na Fillānī katika ‘Iqādh ul-Himâm (Uk. 51-52 kutoka kwa mwanachuoni

Abū al-Layth as-Samarqandī). 2 [Imepokewa na at-Tirmidhee (aliyeithibitisha kuwa hasan), al-’Uqailee, na

wengineo, kwa isnād mbalimbali.

Page 126: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

108

:alisema (صىل اهلل عليه وسلم) kwa vile yeye Mtume ,(وسلم

“Uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم).”1

Hakuna cha kuwazuiya Waislamu leo kutokana na kushikamana na

sunnah hii, ili wapate kutekeleza maamrisho ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Wachana na ulilo na shaka nalo, kwa ambalo usokuwa na shaka shaka nalo.”2

Jambo hili linastahili kutiliwa mkazo zaidi tunapofahamu yakwamba Waislamu wengi wanaotekeleza swala ya Tarawêh kwa rak‟āt ishirini huitekeleza vibaya swala hii kwa kuiswali kwa haraka mno kiasi cha kwamba wanapoteza aina zote za khushū‟ na utulivu. Kwa hilo, wanaifanya swala yao yote kuwajibika na kustahili kukosa malipo na kukataliwa. Lau kama wangelichagua kuiswali kwa idadi ya sawa kama ilivyothubutu kwenye sunnah, wakatumia muda huohuo kuitekeleza, basi swala yao ingelikuwa ni ya sawa na yenye

kukubaliwa na hukmu ya mwanachuoni yoyote. Jābir ( عنه اهلل رضي )

amepokea kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuwa amesema:

“Swala iliyo bora ni ile yenye qunūt (kisimamo3) ndefu.”4

Kuswali Kwa Rak‟āt Chache Kuliko Kumi Na Moja

Mpaka hapa tumeshathibitisha yakwamba haifai kuswali qiyām kwa zaidi ya rak‟āt kumi na moja. Suali muhimu lililobaki kujibiwa ni iwapo inajuzu kuswali rak‟āt chache kuliko kumi na moja. Jawabu ni,

1 Muslim.

2 Imepokewa na Ahmad, at-Tirmidhī na wengineo, kwa isnād iliyo swahīh.

3 Hii ni mojawapo ya mâna ya qunūt. Regelea kwenye Mlango wa 7 kwa maelezo

yenye kuhusika zaidi. 4 Muslim na wengineo.

Page 127: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

109

“Ndio,” kama mafundisho ya Mtume ( اهلل عليه وسلمصىل ) na vitendo vyake

yanavyoashiriya.

Ama kuhusu vitendo vyake, „Abdullāh Bin Abī Qays

amesimulia yakwamba alimuuliza „Āishah ( عنها اهلل رضي ), “Mtume ( صىل :aliswali witr (rak‟āt) ngapi?” Āishah akajibu (اهلل عليه وسلم

“Aliswali witr (rak‟āt) nne1 na tatu, au sita na tatu, au kumi na tatu; hakuwa akiswali witr chini ya saba, wala zaidi ya kumi na tatu.”2

Hii hadīth ya „Āishah inaashiriya yakwamba yaliyopokewa

kutoka kwake katika riwaya nyengine – yakwamba Mtume ( صىل اهلل aliswali witr kwa rak‟āt tatu - maana yake ni tatu (عليه وسلم

zilizotanguliwa na nne. At-Twahāwī amenukuu kutoka kwake kwa isnād iliyo swahīh yakwamba („Āishah) alisema, “Ilikuwa witr ni (rak‟āt) saba, au tano, au tatu zilizopungua.” Akaeleza At-Twahāwī:

“Alikuwa hapendi kuswali (rak‟āt) tatu peke yake za witr, zisizotanguliwa na nyenginezo.”

Na kuhusu matamshi ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), Abū Ayyūb al-

Answārī (رضي اهلل عنه) amepokea yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل عليه :(وسلم

“Witr ni Haq (kuwa ni kitendo cha „Ibādah kilichopendekezwa). Yoyote atakae anaweza kuiswali (rak‟āt) tano; na yoyote atakae anaweza kuiswali tatu; na yoyote atakae anaweza kuiswali

1 Rak’āt mbili za mwanzo zilikuwa ni swala za sunnah za bâda ya ‘ishā’, au rak’āt mbili

hafifu alizokuwa akiziswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kabla ya qiyām. Hii vilevile ni rai ya

al-Hāfidh Ibn Hajar. 2 Imepokewa na Abū Dāwud, Ahmad na wengineo kwa mapokezi mazuri.

Imeswahihishwa na al-Hāfidh al-‘Īrāqī katika takhrīj ul-Ihyā.

Page 128: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 5 Idadi Ya Rak’ât Za Qiyâm

110

moja.”1

Hili ni andiko la wazi lenye kuruhusu kuipunguza swala ya witr kwa rak‟ah moja tu. Mara nyengine ma-Salaf walikuwa wakiyafanya haya, kama ilivyoashiriwa na al-Hāfidh Ibn Hajar:

“Imeswihi kupokewa yakwamba idadi ya Maswahaba waliswali rak‟ah moja tu kwa witr, pasi na kuswali nafl yoyote kabla yake. Imenukuliwa katika kitabu cha Muhammad Bin Nasr na wengineo, kwa isnād iliyo swahīh kutoka kwa as-Sā‟ib Bin Yazīd, yakwamba „Uthmān alisoma Qur‟ān katika usiku mmoja kwa rak‟ah moja peke yake; na wala hakuswali swala nyengine yoyote. Vilevile tutataja katika Mlango wa al-Maghāzī riwaya ya „Abdullāh Bin Tha‟labah yakwamba Sa‟d aliswali rak‟ah moja ya witr, na katika al-Manāqib, riwaya yakwamba Mu‟āwiyah aliswali rak‟ah moja ya witr, iliyopasishwa na Ibn „Abbās.”2

Hii inakosoa waziwazi madai ya baadhi ya ma-Hanafī yakwamba Waislamu wamekubaliana bila ya pingamizi yoyote yakwamba witr inatakiwa iwe ni rak‟āt tatu.”3

1 Imepokewa na at-Twahāwī, al-Hākim na wengineo. mapokezi ya hadīth hii ni

swahīh, kama ilivyohakikishwa na al-Hākim, adh-Dhahabī, Ibn Hibbān, na wengineo. 2 Fat-hul Bārī

3 Angalia katika Fat-hul Bārī (2:385), na Nasb ur-Rāyah (2:122).

Page 129: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

111

MLANGO 6

JINSI YA KUSWALI QIYĀM1

DU‟Ā‟ YA KUANZIA QIYĀM2

Kuna aina nyingi za du‟ā‟ na adhkār za kuanzia swala zilizopokewa

kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم). Hususan, kuna baadhi nyengine

alizokuwa akipenda kuzisoma mwanzoni mwa qiyām. Imependekezwa angalau kusoma mojawapo. Kuzisoma zaidi kutaruhusu kujizoezesha Sunnah kwa njia bora kwa kuzisoma katika nyakati mbalimbali. Katika yafuatayo, twawaletea riwaya tatu kama hizo.

1. RIWAYA YA IBN „ABBĀS

Amepokea Ibn „Abbās (رضي اهلل عنه) yakwamba pindi Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه )

alipoamka kwa ajili ya kuswali katika usiku wa manane, alikuwa akisema:

و « رض ونو ذيات واأل ه ىج ريم الس

هر أ م لم ال هر الل ولم ال

و رض ونو ذيات واأل ه ىج ىر الس

ات أ ه ىج ملم الس

هر أ ولم ال

1 Sehemu ya kwanza na ya mwisho kuhusiana na Mlango huu si katika kitabu

kilichofasiriwa cha Sheikh al-Albānī, lakini uliingizwa humu kwa min-ajil ya ukamilishaji. Kumbukumbu zilizotumiwa kwa kazi hii zimetajwa katika utangulizi. 2 Tizama kwenye nukta ya chini ya hapo juu.

Page 130: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

112

رض و واأل ق وللاؤك حق ونو ذي ق ووعرك ال ىج ال

هر أ ولم ال

ر يث حق وانلار حق وانلبين حق وحمه لم حق واجل اعث وك حق والسج وإل ك سلهج وبم آنيج وعليم ح

م لم أ جتج وبم حق الل

م أ

رت سست ونا أ د

نج ونا أ داصهج وإلم حانهج فاغفس يل نا كر

عليج نن ونا أ علم ة

ىج أ

س ال إل إال ونا أ ىج الهؤد

م وأ ىج الهلر

أ

ىج و ال إل ديك « أ

Allāhumma lak al-alhamdu, anta qayyim us-samāwāti wal ardh waman fīhinn, walak al-hamd, anta nūr us-samāwāti wal-ardh waman fīhinn, walak al-hamdu, anta Mālik us-samāwāti wal

ardh wamann fīhinn, walak al-hamdu, ant al-Haqqu, wa-wa‟duk al-Haqqu, wa-liqā‟uka haqqun, wa-qawluqa haqqun, wal-

Jannatu haqqun, wan-nāru haqqun, wan-nabiyyūna haqqun, wa Muhammadun haqqun, was-sā‟atu haqq.

Allāhumma laka as-lamtu, wa-bika āmantu, wa-„alayka tawakkaltu, wa-ilayka anabtu, wa-bika khāsamtu, wa-ilayka hākamt. Faghfir lī mā qaddamtu, wa-mā akh-khartu, wa-mā asrartu, wa-mā a‟lantu, wa-mā anta a‟lamu bihī minnī. Anta al-Muqaddimu, wa-ant al-mu‟akh-khiru, lā ilāha illā anta, ,

walā ilāha ghayruk-

“Ewe Mola,Wewe ndiye unayestahiki kuhimidiwa. Wewe ndiye Muumba Mbingu na Ardhi, na vilivyomo ndani yake. Na shukrani

zote ni zako Wewe. Wewe ndiye Nuru ya Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake. Na shukrani zote ni zako Wewe. Wewe

ndiye Mfalme wa Mbingu na Ardhi na vilivyomo ndani yake. Na shukrani zote ni zako Wewe. Wewe ni Mola wa Hakki na Ahadi yako ni Hakki (ya kweli), na kukutana na Wewe ni Hakki, na Neno lako ni Hakki, na Pepo ni Hakki, na Moto ni Hakki, na Mitume ni Hakki, na Muhammad ni (mtume wa) Hakki, na

Qiyama ni Hakki (ni khabari ya kweli). Ewe Mola, kwako Wewe

Page 131: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

113

nimejisalimisha, na nimekuamini Wewe, na nakutegemea Wewe, na kwako Wewe nitaregea. Na nitateta kwa ajili yako

Wewe, na Kwako Wewe nitajihukumu kwa hukmu zako, nisamehe mimi madhambi yangu yaliyopita, na yatakayokuja,

na yale niliyoyafanya kwa siri na kwa dhahiri, na yale ninayoyajua. Wewe ndiye wa Mwanzo, na Wewe ndiye wa

mwisho. Hapana Mola apasae kuabudiwa kwa Hakki isipokuwa Wewe, na wala hapana Mola mwengine asiyekuwa Wewe.”

2. RIWAYA YA „ĀISHAH

„Āishah (رضي اهلل عنها) amesimulia yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alipoamka usiku (kwa ajili ya kuswali), alifungua swala yake kwa kusema:

م » رض علم رب جب اللات واأل ه اذيل فاطس الس يل ونيكئيل وإس

ىج تكم بي ادة أ رن الغيب والش يخلفن ا ا ذي عتادك ذيها كى

رى نو تشاء إل رصاط مسخليم ق ةإذىم إىم ت نو ال لها ادخلف ذي»

Allāhumma rabba Jibrīla wa-Mīkā‟īla wa-isrāfīl. Fātir as-samāwāti wal-ardh, „ālim al-ghaybi wash-shahādah, anta tahkumu bayna „ibādika fīmā kānū fīhi yakhtalifūn. Ihdinī

lima‟khtulifa fīhī min al-haqqi bi-idhnika, innaka tahdī man tashā‟u ilā swirātin mustaqīm –

“Ewe Mola wa Jibrīl na-Mīkā‟īl na isrāfīl, Muumba Mbingu na Ardhi, Mjuzi wa mambo yaliyofichikana na yanayo onekana,

Wewe ndiye mwenye kuhukumu kati ya waja wako katika yale wanayokhitilafiana, niongoze mimi katika yale

wanayokhitalifiana katika njia ya Hakki kwa idhni yako, hakika yako Wewe ni mwenye kumuongoza umtakaye katika njia iliyo

nyooka.”

Page 132: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

114

3. RIWAYA YA ABŪ SA‟ĪD

Abū Sa‟īd al-khudhrī‟ (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba Mtume ( صىل اهلل عليه alipoamka kwa ajili ya qiyām, alianza swala kwa kusema Allāhu (وسلم

akbar, kisha kabla ya kuanza kuisoma Qur‟ān, alikuwa akisema:

ك ، وال إل ديك » م وبهرك وتتارك اسهم ، وتعال جر ستحاىم الل ،، ال إل إال الل ، ال إل إال الل كب نتيا .ال إل إال الل

أ كب ، الل

أ الل

كب نتيا ، نتيا ، أ يطان السجيم الل هيع العليم نو الش الس ذ ةالل ع

أ

، وجفث هشه ، وجفذ « نو Subhānak allāhumma wa-bihamdika, wa-tabārak asmuka, wa-

ta‟ālā jadduka, wa-lā ilāha ghayruk.

Lā ilāha illallāh. (Mara Tatu)

Allāhu akbaru kabīrā. (Mara Tatu)

A‟ūdhu billāh is-samī‟ il-„alīmi min ash-shaytwān ir-rajīm, min hamzihi wa-nafkhihi wa-nafthih –

Kutakasika ni kwako Wewe Mola wetu, na sifa zote ni zako Wewe, limetukuka Jina lako na umetukuka Utukufu wako. Na hapana Mola apasae kuabudiwa kwa Hakki isipokuwa Wewe. Hapana mola Apasae kuabudiwa kwa Hakki isipokuwa Wewe, mara tatu. Allahu Akbar Kabira, mara tatu. Najilinda kwa

Allâh, mwenye kusikia, Mjuzi kutokamana na Sheitwani muovu, kutokana na wazimu wake na kibri chake na shari yake.”

Page 133: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

115

USOMAJI KATIKA QIYĀM

MAFUNDISHO YA MTUME

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuweka kipimo cha urefu wa kisomo katika

qiyām. Kisomo chake kilikuwa kikibadilika katika urefu wake; katika baadhi ya nyakati kilikuwa ni kifupi, kwa mara nyingi kilikuwa ni kirefu, na mara nyengine katika baadhi ya matukio kilikuwa ni kirefu

mno. Amesema Ibn Mas‟ūd (رضي اهلل عنه):

“Katika usiku mmoja niliwahi kuswali pamoja na Mtume ( صىل Alisimama (alipokuwa akisoma) kwa muda mrefu sana .(اهلل عليه وسلم

mpaka nikaelekea kutaka kufanya makosa.” Aliulizwa, “Ulielekea kutaka kufanyaje?” nae akajibu, “Nilielekea kutaka kuketi chini nimuache aswali peke yake.”1

Hudhayfah Bin al-Yamān akasimulia:

“Katika usiku mmoja niliwahi kuswali pamoja na Mtume ( صىل اهلل .akaanza kusoma sūrat ul-Baqarah (2) ;(عليه وسلم

Nikajinong‟oneza nafsi yangu, „Atarukū‟ baada ya āyāt mia moja. Lakini akaendelea; basi nikadhani, „ataimaliza (hiyo sūrah) kwa rak‟āt mbili.‟ Lakini akaendelea; basi nikadhani, „atarukū‟ atakapoimaliza.‟ Lakini akaanza sūrat un-Nisā‟ (4) na akaisoma yote; kisha akaanza sūrat Āl-„Imrān (3) na akaisoma yote. Alikuwa akiisoma polepole; alipofika kwenye āyah ambayo ndani yake muna Utukufu wa Allāh, alikuwa akimtukuza; pindi āyah ilipokuwa ikilingania kwenye kumuomba (Allāh), alikuwa akimuomba; pindi āyah ilipokuwa ikilingania kwenye kutafuta hifadha (kwa Allāh), alikuwa akitafuta hifadha. Kisha akarukū‟ ...”2

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 Muslim na an-Nasā’ī.

Page 134: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

116

Katika usiku mmoja, Mtume ( ,alikuwa ni mgonjwa ( عليه وسلمصىل اهلل

akasoma (صىل اهلل عليه وسلم) sūrah saba ndefu: al-Baqarah (2), Āl-„Imrān (3),

an-Nisā‟ (5), al-Mā‟idah (4), al-An‟ām (6), al-A‟rāf (7) na at-Tawbah (8).1

Vilevile, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa mara nyengine akisoma

mojawapo ya sūrah hizi katika kila rak‟ah2. Alikuwa (صىل اهلل عليه وسلم) mara

nyengine akisoma kwenye rak‟ah moja kipimo cha sūrat ul-Muzzammil (73), ambayo ni āyāt ishirini3; mara nyengine alikuwa akisoma

takriban āyāt hamsini au zaidi4. Na akasema Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمص ):

“Yoyote anayeswali akasoma āyāt mia moja katika usiku mmoja, hato-orodheshwa miongoni mwa watu walioghafilika.”5

Katika riwaya nyengine:

“Yoyote anayeswali akasoma āyāt mia mbili, ataorodheshwa miongoni mwa wanyenyekevu na wenye ikhlās.”6

1 Imenukuliwa na Abū Ya’lā na al-Hākim. Ikathibitishwa uswahīh wake na waliokuja

bâdae, adh-Dhahabī na al-Albānī (katika Sifat us-Swalāh). 2 Imepokewa na an-Nasā’ī na Abū Dāwud. Ikathibitishwa uswahīh wake na al-Albānī

(katika Sifat us-Swalāh). 3 Imepokewa na Ahmad na Abū Dāwud. Ikathibitishwa uswahīh wake na al-Albānī

(katika Sifat us-Swalāh). 4 Al-Bukhārī na Abū Dāwud.

5 Imenukuliwa na ad-Dārimī na al-Hākim. Ikathibitishwa uswahīh wake na waliokuja

bâdae, adh-Dhahabī na al-Albānī (katika Sifat us-Swalāh). 6 Imenukuliwa na ad-Dārimī na al-Hākim. Ikathibitishwa uswahīh wake na waliokuja

bâdae, adh-Dhahabī na al-Albānī (katika Sifat us-Swalāh).

Page 135: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

117

MAFUNDISHO YA „UMAR

Kama ilivyothibitishwa hapo awali, wakati „Umar (رضي اهلل عنه) alipomuamrisha Ubayy Bin Ka‟b awaongoze watu kwenye swala katika wakati wa Ramadhān kwa rak‟āt kumi na moja, Ubayy alikuwa akisoma ma-miya ya āyāt, mpaka wale waliokuwa nyuma yake wakawa wanazielemea fimbo zao kwa sababu ya urefu wa kisimamo ; na walikuwa hawamalizi isipokuwa kwa kukurubia alfajiri.1

Vilevile imethubutu yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) aliwakusanya

wasomaji wa Ramadhān na akawaamrisha wepesi miongoni mwao wasome āyāt thalathini (katika rak‟ah moja), wastani wasome āyāt ishirini na tano, na wapole wasome āyāt ishirini.2

UREFU WA SAWA KATIKA USOMAJI

Kadiri ya qiyām kiwapo kirefu, ndio bora. Kwahiyo, mtu anaposwali peke yake, anahimizwa akirefushe kisomo chake kiasi cha inavyowezekana. Inatakiwa kama hivyo mtu anaposwali na wenzake wasio-ona uzito kuhusu usomaji mrefu. Kikwazo cha kipekee kwenye hali kama hizo ni kwamba haifai mtu kuswali usiku mzima isipokuwa kwenye matukio adimu (mara chache sana). Hii ni kulingana na

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliyesema:

“Uongofu ulio bora ni uongofu wa Muhammad.”3

Kwa upande mwengine, mtu anaposwali kama imām (kiongozi), atatakiwa arefushe kisomo kiasi cha kutowapa uzito

wale wenye kuswali naye. Amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

1 Imepokewa na Mālik, na imeshajadiliwa hapo awali kwenye kitabu.

2 Hadīth hii, iliyopokewa na ‘Abd ur-Razzāq na al-Bayhaqī vilevile imeshajadiliwa hapo

awali. 3 Muslim na an-Nasā’ī.

Page 136: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

118

“Anapowaongoza watu mmoja wenu kwenye swala, atatakiwa aifupishe swala yake; miongoni mwao kuna watoto, wazee, watu dhaifu, wagonjwa na wale wenye kutaka kukidhi mahitaji yao. Na pindi asimamapo peke yake, basi na airefushe swala yake kadiri apendavyo.”1

USOMAJI KATIKA RAK‟ĀT TATU ZA WITR

Sunnah (njia) ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika rak‟āt tatu za witr ilikuwa

ni kusoma sūrat ul-A‟lā (87) katika rak‟ah ya kwanza, sūrat ul-Kāfirūn (109) katika rak‟ah ya pili na sūrat ul-Ikhlās (112) katika rak‟ah ya tatu. Mara nyengine alikuwa akiongezea : sūrat ul-Falaq (113) na

sūrat un-Nās (114). Siku moja Mtume ( اهلل عليه وسلم صىل ) alisoma āyāt mia

moja kutoka kwenye sūrat un-Nisā‟ (3) katika rak‟ah ya mwisho ya witr.2

WAKATI WA QIYĀM

Wakati wa qiyām ni kuanzia ba‟dal „ishā‟ mpaka wakati wa swala ya

fajr. Abū Basrah (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema:

“Kwa hakika Allāh amewaongezea swala: nayo ni witr3; kwahivyo, iswalini baina ya „ishā‟ na fajr.”4

1 Al-Bukhārī na Muslim.

2 An-Nasā’ī na Ahmad kwa isnād swahīh.

3 Mâna ya witr ni idadi isiyogawanyika kwa mbili. Kama ilivyofafanuliwa hapo awali,

mara nyengine swala nzima ya usiku huitwa witr kwa sababu jumla ya rak’āt zake ni idadi isiyogawanyika kwa mbili. 4 Imepokewa na Ahmad na wengineo. Imethibitishwa kuwa ni swahīh na al-Albānī

katika as-swahīhah (no.108) na Irwā’ ul-Ghalīl (2:158)

Page 137: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

119

Lakini hata hivyo,inatakiwa mtu ajaribu kuiswali katika wakati wa usiku wa kuchelewa, kwa sababu hivyo ni bora kuliko kwenye wakati

wa mapema, kama alivyosema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Yoyote mwenye kuhofia yakwamba hatoamka katika wakati wa usiku wa kuchelewa, basi na aitekeleze witr katika wakati wake wa mwanzo. Na yoyote anayetarajia kuamka katika wakati wa usiku wa kuchelewa, basi na aiswali. Kwa hakika swala katika wakati wa usiku wa kuchelewa hushuhudiwa (na Malaika), na hilo ni bora.”1

Iwapo mtu atakuwa na chaguo la kuiswali katika wakati wa usiku wa mapema kwa jamā‟ah au wakati wa usiku wa kuchelewa akiwa peke yake, basi kuiswali na jamā‟ah ni bora. Kuiswali na jamā‟ah itahesabiwa kana kwamba ameiswali kwa usiku mzima, kama ilivyothibitishwa hapo awali (Uk.55).

Hivi ndivyo walivyokuwa wakifanya Maswahaba katika

zama za „Umar ( عنه اهلل رضي ), kama ilivyonukuliwa hapo awali

kutokana na riwaya ya „Abd ur-Rahmān Bin „Abd al-Qārī (Uk.58). Vilevile, Zayd Bin Wahb amesema:

“„Abdullāh Bin Mas‟ūd alikuwa akituswalisha katika mwezi wa Ramadhān; na alikuwa akimaliza haliyakuwa bado tuko kwenye

usiku.”2

Kama ilivyotajwa hapo awali, aliulizwa Imām Ahmad, “Jee tucheleweshe qiyām hadi kwenye sehemu za mwisho wa usiku?” katika majibu yake, alieleza ufahamu wake wa riwaya hii na iliyopita hapo awali kwa kusema, “Laa Sunnah ya Waislamu inapendekeza zaidi kwangu.”3

1 Muslim na wengineo.

2 Imepokewa na ‘Abd ur-Razzāq kwa isnād swahīh.

3 Abū Dāwud katika kitabu chake Masā’il.

Page 138: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

120

NJIA MBALIMBALI ZA KUITEKELEZA (SWALA YA) QIYĀM

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali qiyām na witr kwa njia sampuli nyingi.

Vitabu vyingi vya fiqh havina mas‟ala haya – si kwa mukhtasar wala kwa kina. Ni muhimu kuifafanua sunnah hii kwa watu, ili vipenzi vyake wapate fursa ya kuifuata, na wale wenye kuikanusha (sunnah hiyo nzima) kutokana na ujinga watalitilia suala hili maanani.

Twamuomba Allāh (سبحانه وتعاىل) atuwezeshe kumfuata Mtume Wake ( صىل اهلل kwa njia iliyo bora, na tuyaepuke mambo ya uzushi ambayo (عليه وسلم

aliyotuonya kwayo.

Kwahivyo, katika milango ifuatayo, tunawaletea njia mbalimbali

alizotuletea Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) za jinsi ya kuiswali swala ya qiyām,

kama zilivyothibitishwa kwa riwaya swahīh.

Baada ya Ibn Khuzaymah kutaja idadi ya hadīth zinazoeleza

jinsi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alivyoswali qiyām, alimalizia kwa kusema:

“Anaruhusiwa mtu kuswali idadi yoyote miongoni mwa sampuli za

rak‟āt ambazo alizoziswali Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), tena kulingana na

kama alivyotekeleza yeye mwenyewe. Hapana mtu atakaelaumiwa iwapo atajichagulia kuswali kulingana na sampuli hizi.”1

SAMPULI YA KWANZA

SWALI RAK‟ĀT KUMI NA TATU KWA JOZI, UKIANZA KWA JOZI FUPI, IKIFUATWA KWA JOZI NDEFU SANA, KISHA JOZI FUPI KULIKO HIYO, KISHA JOZI FUPI KULIKO HIYO, KISHA JOZI FUPI KULIKO HIYO, KISHA JOZI FUPI KULIKO HIYO, KISHA RAK‟AH MOJA YA WITR.

Kuna riwaya tatu kuhusiana na mas‟ala haya:

1. Amepokea Zayd Bin Khālid al-Juhanī:

1 Swahīh Ibn Khuzaymah 2:194

Page 139: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

121

“Katika usiku mmoja, niliamua kumchunguza Mtume ( صىل اهلل عليه .kwa umakinifu jinsi alivyokuwa akiswali swala zake za usiku (وسلم

Kwahiyo aliswali rak‟āt mbili fupi.

Kisha akaswali rak‟āt mbili ndefu sana.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali rak‟āt mbili fupi kuliko mbili zilizotangulia.

Kisha akaswali (witr) moja.

Ikawa ameswali jumla ya rak‟ā kumi na tatu.”1

2. Amepokea Ibn „Abbās (رضي اهلل عنه):

“Nilikuwa kwenye nyumba ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika

usiku mmoja alipokuwa kwa Maymūnah. Baada ya kupita thuluthi moja ya usiku au nusu yake, aliamka. Akenda kwenye kiriba cha maji kilichoangikwa na akatawadha; nami pia nikatawadha na yeye. Kisha akasimama na kuanza kuswali; nami nikasimama kwenye upande wake wa kushoto. Akanisongeza katika upande wake wa kulia; kisha akaniwekea mkono wake kwenye kichwa changu, kana kwamba alikuwa akinishika sikio langu kutaka kunitanabahisha. Akaswali rak‟āt mbili fupi, akasoma kwenye kila rak‟ah Umm ul-Qur‟ān2; kisha akatoa salām3. Kisha, akaswali, akakamilisha rak‟āt kumi na moja, ikiwemo witr. Kisha akalala mpaka alipokuja Bilāl na huku akisema, „Swalāh ewe Mjumbe wa

1 Imepokewa na Mālik, Muslim, Abū ‘Uwānah, Abū Dāwud na Ibn Nasr.

2 Hili ni mojawapo la majina ya Qur’ān – mlango wa kwanza wa Qur’ān.

3 Taslīm: kutoa salām imalizikapo swala.

Page 140: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

122

Allāh!‟ Basi akainuka, akaswali rak‟āt mbili, kisha (akatoka nje, kwenda) kuwaongoza watu katika swala (ya fajr).”1

3. Amepokea „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Alipoamka usiku, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akianza swala

zake kwa rak‟āt mbili fupi, kisha alikuwa akiswali rak‟āt nane, kisha witr.”

Katika riwaya nyengine, alisema („Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي )):

“Alikuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiswali „ishā‟, akifuatiza kwa

rak‟āt mbili fupi. Alikuwa akitayarisha msuaki wake na maji kwa ajili ya wudhū‟. Kila wakati alipokuwa Allāh akipenda kumuamsha, alikuwa akifanya hivyo; kwahiyo alikuwa akiamka, akisafisha meno yake kwa siwāk, akitawadha, akiswali rak‟āt mbili, kisha akisimama na kuswali rak‟āt nane na kusoma kwa vipimo vya sawa kwenye swala nzima; kisha alikuwa akiswali witr kwenye rak‟ah ya tisa. Pindi

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipoanza kuzeeka, na kuongeza uzito wa mwili,

alizigeuza hizo nane na kuwa rak‟āt sita, akaswali witr kwenye rak‟ah ya saba, na kisha alikuwa akiswali rak‟āt mbili haliyakuwa amekaa, ambamo ndani yake alikuwa akisoma al-Kāfirūn (109) na az-Zalzalah (99).”2

1 Imepokewa na Abū Dāwud, na kutoka kwake Abū ‘Uwānah katika swahīh yake. Asili

ya hadīth hii inapatikana kwenye swahīh mbili (al-Bukhārī na Muslim). Ufahamu yakwamba Ibn ul-Qayyim ameikosa riwaya hii kwenye Zād ul-Ma’ād, pale aliposema,

“Ibn ‘Abbās hakutamka yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alianza kwa rak’āt mbili fupi,

kama alivyotamka ‘Ā’ishah, …” 2 Riwaya zote mbili zimepokewa na at-Twahāwī kwa isnād swahīh. Nusu ya mwanzo

ya riwaya ya kwanza vilevile imepokewa na Muslim na Abū ‘Uwānah. Kila aliyepokea kutoka kwa Hasan al-Basrī kwa njia ya ‘an’anah (pasi ya kubainisha waziwazi yakwamba ameisikiya yeye mwenyewe, na pasi na kuwepo wapokezi wa kati, kutoka kwa wapokezi waliotangulia). Lakini hatahivyo, an-Nasā’ī na Ahmad, wote wawili waliipokea riwaya ya pili kutoka kwa al-Hasan, ambapo alipodhihirisha kusikiya.

Page 141: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

123

SAMPULI YA PILI

SWALI RAK‟ĀT KUMI NA TATU, UTOE SALĀM UMALIZAPO KILA JOZI MOJA YA RAK‟ĀT NANE ZA MWANZO, KISHA USWALI WITR KAMA RAK‟ĀT TANO, BILA YA KUKAA WALA KUTOA SALĀM ISIPOKUWA KWENYE RAK‟AH YA MWISHO.

Amepokea „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها):

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akenda kulala; kisha

husafisha meno yake kwa siwāk na akatawadha. Kisha alikuwa akiswali rak‟āt nane, kwa kukaa na kutoa salām kila baada ya kumaliza jozi moja ya rak‟āt; kisha alikuwa akiswali witr kwa tano, bila ya kukaa wala kutoa salām mpaka afikapo rak‟ah ya Kisha kukiadhiniwa (kwa swala ya fajr), huinuka akaswali rak‟āt fupi.”1

Hadīth hii iko wazi yakwamba jumla ya rak‟āt ni kumi na ukiongezea kwenye rak‟āt mbili za fajr. Jambo hili huenda likaonekana kana kwamba linagongana na hadīth iliyotajwa hapo

awali kutoka katika matamshi ya „Ā‟ishah (Uk.66), “Mtume ( اهلل صىل hakuswali zaidi ya kumi na moja ...” Lakini hatahivyo, sisi (عليه وسلم

tumeyatatua mas‟ala haya ya hapo juu kwa kudokeza yakwamba katika matamshi haya, yeye (bibi „Ā‟ishah) hakuzitia rak‟āt mbili

fupi ambazo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alizozianzia qiyām.

1 Imepokelewa na Ahmad kwa isnād swahīh kulingana na masharuti ya al-Bukhārī na

Muslim. Vilevile imepokewa kwa njia ya mkato (bila ya kutaja taslīm kila bâda ya jozi moja) na Muslim, Abū ‘Uwānah, Abū Dāwud, at-Tirmidhī, ad-Dārimī, Ibn Nasr, al-Bayhaqī na Ibn Hazm (katika al-Muhallā). Na zaidi ni kwamba, ash-Shāfi’ī, at-Twayālisī na al-Hākim, wote hao wamepokea sehemu tu ya hadīth hii kuhusu kuswali witr kwa rak’āt tano.

Page 142: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

124

SAMPULI YA TATU

SWALI RAK‟ĀT KUMI NA MOJA, UTOE SALĀM MWISHONI MWA KILA JOZI, NA UMALIZIE KWA RAK‟AH MOJA YA WITR.

Amepokea „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Kuanzia wakati alipomaliza kuswali „ishā‟ mpaka fajr, Mtume

Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمص ) aliswali rak‟āt kumi na moja, akitoa salām kila

kila amalizapo jozi moja, na akiswali witr kama rak‟ah moja. Alikuwa Alikuwa akibaki kwenye sujūd, kabla ya kuinua kichwa chake, kwa kwa kiasi cha muda wa mmoja wenu kusoma āyāt hamsini. Kisha, baada ya muadhini kumaliza adhān ya fajr, na yakamdhihirikia Mtume

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) mapambazuko, mwenye kuadhini alimjia

(kumtanabahisha). Hapo alikuwa akiswali rak‟āt mbili fupi, kisha akajinyosha (akalala) kwa upande wake wa kulia, mpaka mwenye kuadhini alipomjia (kumlingania) kwa iqāmah (ulinganizi wa kuanza kwa swala).”1

Tambua yakwamba hadīth hii imeleta dalili ya wazi kabisa ya kulala (kujinyosha) chini kwa upande wa kulia baina ya Sunnah na faradhi ya fajr. Hatahivyo, hakuna riwaya yoyote kuwahusu Maswahaba kuwa walifanya hivyo msikitini – Bali, baadhi yao hawakupenda kulifanya hilo hapo, wakajizuiya na kulifanya

majumbani mwao, kama ilivyokuwa ni katika mazoweya ya Mtume ( صىل .(اهلل عليه وسلم

Sampuli hii ya kuiswali swala ya qiyām imezidi kuthibitishwa na hadīth iliyopokewa na Ibn „Umar yakwamba mtu mmoja alimuuliza

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu swala ya usiku. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akamjibu:

1 Imepokewa na Muslim, Abū ‘Uwānah, Abū Dāwud, at-Twahāwī na Ahmad. Muslim

na Abū ‘Uwānah pia waliipokea kutoka kwa Ibn ‘Umar, na Abū ‘Uwānah akaipokea kutoka kwa Ibn ‘Abbās.

Page 143: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

125

“Swala ya usiku ni jozi moja kwa jozi moja. Na lau kama mmoja wenu atahofia kupambazukiwa, (basi na aswali) rak‟ah moja ili aipwekeshe (aifanye witr) swala yake.1

Kisha Ibn „Umar ( عنهما اهلل رضي ) akaulizwa, ni nini maana ya „jozi

moja kwa jozi moja‟?” Nae akamjibu, “Toa salām baada ya kila jozi.”2

Ibn „Umar ( عنهما اهلل رضي ) alikuwa na tabia ya ufahamu wa aina

hii, kama ilivyopokewa yakwamba:

“Alikuwa akitoa salām kabla ya rak‟ah ya mwisho ya witr, jambo lililomuwezesha kuomba chochote alichokuwa akihitaji.”3

SAMPULI YA NNE

SWALI RAK‟ĀT KUMI NA MOJA, NNE KWA TASLĪM MOJA TU, KISHA NNE NYENGINE KAMA HIZO, KISHA TATU.

Dalili ya hii ni hadīth iliyopokewa na al-Bukhārī na Muslim kutoka kwa

„Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) iliyotajwa hapo awali (Uk.66).

Ufahamu uliodhihiri wa hadīth hii ni kwamba Mtume ( صىل اهلل ,alikuwa akikaa kwa tashahhud1, bila ya kutoa salām (عليه وسلم

1 Imepokewa na Mālik, al-Bukhārī, Muslim na Abū ‘Uwānah

2 Imepokewa na Muslim na Abū ‘Uwānah. Fahamu yakwamba ufafanuzi huu wa Ibn

‘Umar umepokewa na Imām Ahmad kuwa ulitamkwa na Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), na

ukatiwa kwenye mândiko yaliyopokewa kwenye hadīth. Lakini mmojawapo wa wapokezi wake ni ‘Abd ul-‘Azīz Bin Abī Ruwād, ambae kawaida yake ni mkweli, lakini mara hufanya makosa, kama ilivyosemwa kwenye at-Taqrīb. Pana uwezekano

mkubwa yakwamba aliinasibisha sehemu hii ki-makosa kwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل );

na Allāh ( وتعاىل سبحانه ) Ndiye Mjuzi bora. 3 Imepokewa na Mālik na al-Bukhārī.

Page 144: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

126

baada ya jozi ya kwanza ya hizo rak‟āt tatu na nne. Huu ndio ufafanuzi wa an-Nawawī, kama ilivyotajwa hapo awali. (Uk.67).

SAMPULI YA TANO

SWALI RAK‟ĀT KUMI NA MOJA, UZITEKELEZE NANE ZA MWANZO BILA YA KUKAA (KWA TASHAHHUD) ISIPOKUWA KATIKA RAK‟AH YA NANE, NA KISHA BILA YA KUTOA SALĀM, USWALI WITR RAK‟AH MOJA UMALIZIE NA KUTOA SALĀM. KISHA USWALI RAK‟ĀT MBILI KWA KUKAA.

Sa‟ad Bin Hishām Bin „Āmir amesimulia yakwamba alikuja kwa Ibn

„Abbās na akamuuliza kuhusu alivyokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiswali

swala ya witr. Ibn „Abbās akamjibu, “Kwanini nisikuongoze wewe kwa mtu aliye mtaalamu zaidi katika ulimwengu huu kuhusiana na swala

ya witr ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)?” Sa‟ad akasema, “Na ni nani huyo?”

Akasema Ibn „Abbās, “Ni „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ); sasa wewe nenda kwake

ukamuulize.” Akenda kwake, na akamwambia, “Eeh Mama yao

waumini! Hebu nieleze nami kuhusu jinsi alivyokuwa Mtume ( صىل اهلل عليه :akiswali swala ya witr.” „Ā‟ishah akamjibu (وسلم

“Tulikuwa tukimtayarishiya msuaki wake na maji; Kisha Allāh

alikuwa akimuamsha kila apendapo Yeye kwenye nyakati za (سبحانه وتعاىل)

usiku. Akiamka hupiga msuaki na kutawadha, kisha alikuwa akiswali rak‟āt tisa bila ya kukaa isipokuwa afikapo ya nane, ambapo humtaja

Allāh na kumtukuza Yeye, akamswalia mtume Wake (صىل اهلل عليه وسلم), na

kumuomba Yeye. Kisha alisimama bila ya kutoa salām, akaswali rak‟ah ya tisa, akakaa, akamtaja Allāh na kumsifu Yeye, akamswalia

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), akamuomba Allāh, na akatoa salām kwa sauti

1 Vikao vya kwenye swala ambamo mtu huitamka shahadah, akamswalia Mtume ( صىل

وسلم عليه اهلل ).

Page 145: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

127

kubwa kiasi cha kutusikizisha sisi. Kufuatia hayo, aliswali rak‟āt mbili haliyakuwa amekaa. Hivyo, ewe mwanangu, itakuwa ameswali jumla ya rak‟āt kumi na moja.

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipoanza kuzeeka na mwili wake kuwa

mzito, aliswali witr, rak‟āt saba, na kisha akaziswali hizo rak‟āt mbili kama alivyofanya awali, akakamilisha jumla ya tisa – ewe mwanangu.”1

Uchunguzi muhimu kutokamana na hadīth hii ni kwamba

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akijiswalia mwenyewe, na kwamba

alisema (alijiswalia) katika tashahhud ya kwanza na vilevile ya mwisho. Kwahivyo Waislamu inawabidi wafuate sunnah hiyo badala ya kufuata amri za baadhi ya madhāhib kukirihisha vikali kumswalia Mtume kwenye rak‟ah ya kwanza. Imethubutu pasi na shaka yoyote miongoni mwa wanavyuoni yakwamba hapana utofautishaji katika mfumo wa utekelezaji baina ya swala za sunnah na faradhi – isipokuwa tu iwapo itapatikana dalili makhsusi. Na katika hali hii hapana (dalili hiyo).

Rak‟āt hizi mbili za baada ya witr zitajadiliwa karibu na mwishoni mwa mlango huu.

SAMPULI YA SITA

SWALI RAK‟ĀT TISA, UZITEKELEZE SITA ZA MWANZO BILA YA KUKAA (KWA TASHAHHUD) ISIPOKUWA KATIKA RAK‟AH YA SITA, NA KISHA BILA YA KUTOA SALĀM, USWALI WITR RAK‟AH MOJA IKIMALIZWA KWA SALĀM. KISHA USWALI RAK‟ĀT MBILI KWA KUKAA.

Dalili ya haya ni hadīth ya „Ā‟ishah katika mlango uliotangulia.

1 Imepokewa na Muslim, Abū ‘Uwānah, Abū Dāwud, an-Nasā’ī, Ibn Nasr, al-Bayhaqī

na Ahmad.

Page 146: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

128

SAMPULI NYENGINE

SAMPULI NYENGINE ZINAWEZA KUHITIMIKA KUTOKANA NA ITHBATI ILIYOPO KWA KUPUNGUZA IDADI YA RAK‟ĀT KWENYE SAMPULI ZA AINA YOYOTE ZILIZOTANGULIA, KWA MIGAWO YA RAK‟ĀT MBILI MBILI, NA KUSHUKA CHINI KWA UCHACHE WA RAK‟AH MOJA PEKE YAKE.

Hili limetokamana na matamshi yaliyotangulia ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

(Uk. 121):

“Anaweza mtu kuiswali kama rak‟āt tano, tatu au moja.”

Hadīth hii inaonyesha dalili ya wazi yakwamba inaruhusiwa kuswali witr kwa idadi hizi tatu, hata kama hakuna yoyote miongoni

mwazo iliyopokewa kutokamana na vitendo vya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) –

Bali, „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) amethibitisha kwenye riwaya iliyodondolewa

hapo awali (Uk.121), yakwamba yeye hakuwahi kuswali witr kwa idadi iliyopungua chini ya rak‟āt saba.

Anaweza mtu kuswali rak‟āt hizi tano au tatu:

a. Kwa kikao kimoja na kutoa salām, kama ilivyo kwenye sampuli ya pili hapo juu,

b. Kukaa bila ya kutoa salām kila baada ya jozi moja ya rak‟āt, kama ilivyo kwenye sampuli ya nne hapo juu (hii haiwezekani kutekelezwa katika hali ya rak‟āt tatu, kama itakavyoelezwa hapo chini),

c. Au toa salām kila baada ya jozi moja ya rak‟āt, kama ilivyo kwenye sampuli ya tatu na sampuli nyengine hapo juu – ambayo ndiyo njia bora.

Page 147: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

129

RAK‟ĀT TATU ZA MWISHO

ZINAZOTAFAUTIANA NA MAGHRIB

Hakuna katika mafundisho ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) lenye kuthibitisha

kuswaliwa rak‟āt tano au tatu zenye kikao cha katikati baada ya kila jozi moja (kama ilivyotangulia katika (b)). Isitoshe, hii inaweza kupatikana kutoka kwenye maandishi ya hapo juu ya ujumla. Lakini

hili haliwezekani katika hali ya rak‟āt tatu, kwa sababu Mtume ( صىل اهلل amekataza kuzifananisha na swala ya Maghrib. Abū Hurayrah (عليه وسلم

:(صىل اهلل عليه وسلم) amesimulia yakwamba amesema Mtume (رضي اهلل عنه)

“Musiswali witr kwa rak‟āt tatu ikafanana na swala ya Maghrib.”1

Kuna njia mbili za kuswali rak‟āt tatu kwa mfumo unaotafautiana na swala ya Maghrib.

1. Kwa kutoa salām baina ya shaf„ (igawanyikayo kwa 2) na witr (isiyogawanyika kwa 2). Mfumo huu unapendekeza zaidi kwa sababu umethubutu juu ya msingi wa sunnah.

2. Bila ya kukaa baina ya shaf„ na witr.

UFAHAMU WA IBN NASR

Amesema hāfidh Muhammad Bin Nasr al-Marwazī:

“Tunayopendekeza kwa mwenye kuswali qiyām wakati wa Ramadhān na mwengine ni kutoa salām kila baada ya jozi moja ya rak‟āt. Pindi anaposwali rak‟āt tatu (za mwisho), na asome al-A‟lā (87) katika ya kwanza na al-Kāfirūn (109) katika ya pili. Kisha na akae tashahhud na kutoa salām, kisha na asimame na

1 Imepokewa na at-Twahāwī, ad-Dāraqutnī’ na wengineo kwa isnād swahīh.

Page 148: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

130

aswali rak‟ah moja, ambamo atasoma al-Fātihah, al-ikhlās (112), na mu‟awwidhāt mbili (113, 114) ...

Inaruhusiwa kumuiga Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika mifumo hii

(alivyoswali qiyām). Lakini, chaguo bora ni hilo tulilolitaja hivi punde, kwa sababu alipoulizwa kuhusu jinsi ya kuswali qiyām,

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alijibu, “Swala ya usiku ni rak‟āt mbili kwa

rak‟āt mbili.”

Kwahiyo sisi twachukuwa chaguo alilowachagulia Ummah huu, na kwa wakati huohuo tunatoa ruhusa ya kumuiga yeye katika aliyoyafanya, kwa sababu hakuna makatazo yaliyopokewa kutoka kwake kuhusu mas‟ala haya.”1

Na akasema:

“Rai yetu ni kwamba inaruhusiwa kutekeleza kulingana na riwaya hizi sampuli mbalimbali. Riwaya zimepokewa namna nyingi kwa sababu qiyām, zote mbili witr na rak‟āt nyengine, ni swala ya

khiyari. Qiyām na witr alizokuwa akiswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

ziko sampuli nyingi kama tulivyoeleza; mara nyengine alikuwa akiswali kwa sampuli moja, na mara nyengine sampuli nyengine. Sampuli hizi zote zinaruhusiwa na ni nzuri.

Lakini hata hivyo, hatukuweza kupata riwaya

iliyothubutu yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali witr kama

rak‟āt tatu zilizoungana, bila ya taslīm (kutoa salām) isipokuwa kwenye (riwaya) ya mwisho – kama tulivyopata kwenye hali ya rak‟āt tano, saba na tisa. Riwaya za kuswali kwake witr kama rak‟āt tatu hazikutaja kuhusu taslīm. Kwa mfano, ... yakuwa

amepokea Ibn „Abbās (رضي اهلل عنه) yakwamba, „Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alikuwa akiswali witr kwa rak‟āt tatu, akisoma ndani mwake al-A‟lā, al-Kāfirūn na Qul huwallāhu ahad.‟

1 Qiyām ul-Layl (Uk. 119)

Page 149: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

131

Chini ya madda hiyohiyo, kuna riwaya za kutoka kwa „Imrān Bin Husayn, „Ā‟ishah, „Abd ur-Rahmān Bin Abzā na Anas Bin Mālik. Riwaya zote hizi hazina uhakika, zinazoleta uwezekano

yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alitoa salām kwenye rak‟āt ya pili

katika rak‟āt tatu za witr ...”1

Na akasema:

“Na rai yetu ni kwamba mtu anaweza kuswali witr kama moja, tatu, tano, saba au tisa. Hayo yote ni mazuri na yanaruhusiwa

kulingana na riwaya tulizozijumuisha kutoka kwa Mtume ( صىل اهلل عليه na Maswahaba zake baada ya kufa kwake. Lakini chaguo letu (وسلم

ni kama tulivyotaja hapo awali.

Kwahiyo, iwapo mtu atataka kuswali witr kama rak‟ah moja pasi na kuswali chochote kabla yake, sisi tutampendekezeya aitangulize na rak‟āt mbili au zaidi, na kisha aswali rak‟ah moja ya witr. Iwapo hakufanya hivyo, na akaswali witr kama rak‟ah moja peke yake, hilo linaruhusiwa. Sisi tumepokea yakwamba idadi kubwa miongoni mwa Maswahaba wa

Muhammad (صىل اهلل عليه وسلم) walifanya hivyo. Ingawaje, hata kama

Mālik na wanavyuoni wengine walilichukiya hilo, Maswahaba wa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ndiwo wenye kustahiki zaidi kufuatwa.2

1 Qiyām ul-Layl (Uk. 121)

2 Qiyām ul-Layl (Uk. 123)

Page 150: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

132

KUPATANISHA BAINA YA RIWAYA MBILI

Vilevile amesema Ibn Nasr:

“Baadhi ya riwaya zisizoidhinisha kuswali witr kwa rak‟āt tatu

zimenasibishwa kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), Maswahaba zake na

ma-tābi‟īn ...”1

Riwaya hizi ni dhaifu, isipokuwa kwa sehemu ya hadīth ya Abu Hurayrah iliyotajwa hapo awali kwenye Mlango huu. Hii huwenda ikaonyesha kuwa pana mgongano na riwaya ya Abū Ayyūb (Uk.121). Lakini zinaweza kupatanishwa kwa kusema yakwamba hayo makatazo (katika hadīth ya Abu Hurayrah) yanatumika kwenye swala ya witr itakayokuwa na tashahhud mbili, itakayoifanya swala yenyewe ifanane na Swala ya Maghrib. Lakini iwapo mtu hatokaa, basi hazitokuwa ni zenye kufanana. Al-Hāfidh Ibn Hajar ameutaja ufahamu huu katika Fat hul Bārī, uliokubaliwa na as-San‟ānī katika Subul us-Salām.

Kufanana huko kutazidi kufifiya iwapo mtu atatenganisha rak‟āt mbili kutokana na rak‟ah ya mwisho ya witr. Imām Ahmad aliulizwa, “Msimamo wako ni upi kuhusiana na witr, unatoa salām baada ya rak‟āt mbili?” Akajibu, “Na‟ām, ndio.” Kisha akaulizwa, “Ni kwa nini?” Akajibu, “Kwa sababu ahādīth zenye kuunga mkono hayo ni zenye nguvu na ni swahīh zaidi.” Katika matukio mengine, alisema

Imām Ahmad (رحمه اهلل): “Mtu na atoe salām baada ya rak‟āt mbili za mwisho. Na kama hatotoa salām, natumai yakwamba hata juu ya hayo, itakubaliwa. Lakini kutoa salām imethubutu zaidi kutoka kwa

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).”2

1 Qiyām ul-Layl (Uk. 125)

2 Masā’il ul-Imām Ahmad imesimuliwa na mwanafunzi wake Ibn Hāni.

Page 151: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

133

HATIMA KUHUSU QIYĀM

QUNŪT

Qiyām inahatimika kwa rak‟ah moja ya mwisho, ambayo ndani yake anaweza mtu kuisoma qunūt, kabla au baada ya rukū‟. Haya yamefafanuliwa kwenye mlango unaofuata.

YAKUPASAYO KUSEMA MWISHONI MWA WITR

Imependekezwa katika sunnah kusema mwishoni mwa witr, emma kabla au baada ya kutoa salām:

ذ » عذ ةسضاك نو سذطم وبهعافاحم نو خلبخم وأ ع

م إن أ الل

ثنيج لع جفسم ىج نها أ

حص ثياء عليم أ

«ةم نيم ال أ

<Allāhummā innī a‟ūdhu biridhāka min sakhatika wa bimu‟āfatika min „uqūbatika, wa a‟ūdhubika minka; lā uhsī thanā‟an „alayka anta, kamā athnayta „alā nafsik –

“Ewe Mola, hakika yangu mimi, najilinda kwa radhi zako kutokamana na hasira zako, na (kutarajia) msamaha wako

kutokamana na adhabu yako, na najilinda kwako wewe kutokamana na hasira zako. Siwezi kuzihesabu sifa zako wewe

kama utakavyojisifu nafsi yako.”

Alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akitoa salām anapomaliza

swala ya witr, alikuwa akisema:

وس » «سبحان الملك القد

<Subhānal Malik il-Quddūs – kutakasika ni kwa Mfalme Mtukufu>

Page 152: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

134

Alikuwa akiikariri hii kwa mara tatu, akiivuta sauti yake, na kuipaaza juu katika mara ya tatu.1

RAK‟ĀT MBILI BAADA YA WITR

Anaweza mtu kuswali rak‟āt mbili baada ya witr. Tumenukuu hapo

awali riwaya ya „Āishah (رضي اهلل عنها) (Uk.140) yakwamba Mtume ( صىل اهلل عليه alishikilia kuziswali daima. Na zaidi ni kwamba alipendekeza (وسلم

watu kuziswali aliposema:

“Kwa hakika safari hii (ya ki-maisha) ni mapambano na uzito kwenu; kwahiyo anaposwali witr mmoja wenu, basi na aifuatize kwa rak‟āt mbili. Iwapo ataamka (katika usiku mkubwa baadae) au laa, hizo zitakuwa (zimehifadhiwa) kwa ajili yake.”2

Rak‟āt hizi mbili baada ya witr zinaonekana kana kwamba

zimekhalifiana na maneno ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Ifanyeni swala yenu ya mwisho katika usiku iwe ni witr.”3

Wanavyuoni walijaribu kupatanisha kwa njia mbalimbali baina ya hadīth hii na riwaya mbili zilizotangulia hapo juu. Tumekuta yakwamba ufahamu ulio bora katika mas‟ala haya ni ule wa Ibn Nasr aliyesema yakwamba amri iliyokuja katika hadīth ya pili ni “amri ya khiyari, na wala si jambo la lazima.”

Na Sunnah ni kusoma katika rak‟āt hizi mbili: sūrat uz-Zalzalah (99), na sūrat ul-Kāfirūn (109).4

1 Abū Dāwud; swahīh.

2 Imepokewa na Ibn Khuzaymah, ad-Dāraqutnī na wengineo. Imethubutu uswahīh

wake kwenye Silsilat ul-Ahādīth is-Swahīhah. 3 Al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

4 Imepokewa na Ibn Khuzaymah kwa riwaya zitokazo kwa ‘Ā’ishah na Anas zenye

silsila zinazotiliana nguvu zenyewe kwa zenyewe. Angalia katika Sifat us-Swalāh.

Page 153: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

135

MAS‟ALA ANUWAI (TAFAUTI TAFAUTI) YANAYOHUSIANA NA WITR1

WITR MOJA KATIKA KILA USIKU MMOJA

Mtu akitaka, anaweza kuswali witr moja pekee kwa kila usiku mmoja. Haya yametokamana na riwaya nyingi zilizotangulia. Kwa ujumla, amepokea Talq Bin „Alī kutoka kwa babake yakwamba alimsikiya

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akisema:

“Haifai mtu kuswali witr mbili katika usiku mmoja.”2

Akitoa maoni yake kuhusu hadīth hii, at-Tirmidhī alisema:

“Wanavyuoni miongoni mwa Maswahaba wa Mtume ( صىل اهلل عليه na wale waliokuja baada yao walikhitilafiana kuhusiana na (وسلم

mwenye kuswali witr katika wakati wa usiku wa mapema, kisha baadae akaamka.

Baadhi yao wakachukuwa msimamo yakwamba atapaswa kuibatilisha witr yake ya kwanza kwa kuiongezea rak‟ah moja, kisha aswali kwa kadiri apendavyo, na kisha aimalizie kwa witr, kwa sababu haifai mtu kuswali witr mbili katika usiku mmoja. Hii ni rai ya Abū Is-hāq.

Wengine wakachukuwa msimamo yakwamba anaweza kuswali kwa kiasi apendacho, pasi na kuibatilisha witr yake. Hii ni rai ya Sufyān ath-Thawrī, Mālik Bin Anas, Ahmad na Ibn ul-Mubārak.

Rai ya sawa ni hiyo ya pili, kwa sababu imepokewa kwa

mapokezi mbalimbali yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali

baada ya witr.”3

1 Tizama katika mândishi ya chini katika mwanzoni mwa Mlango huu.

2 Imepokewa na Abū Dāwūd na at-Tirmidhī; ikathibitishwa kuwa ni swahīh na al-

Albānī 3 Sunan ut-Tirmidhī

Page 154: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

136

KUIKOSA SWALA YA WITR

Kuna ahādīth nyingi sana zenye kumruhusu mtu aliyekosa swala ya

witr ailipe wakati wa asubuhi. Kwa mfano, Abū Sa‟īd (رضي اهلل عنه) amepokea yakwamba amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Iwapo mtu atakosa kuiswali swala ya witr kwa sababu ya kulala au kusahau, basi na aiswali pindi atakapokumbuka au atakapoamka.”1

Na Zayd Bin Aslam amepokea kutoka kwa babake yakwamba

amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Iwapo mtu ataikosa swala ya witr kwa sababu alikuwa amelala, basi na aiswali wakati wa asubuhi.”2

Kwa upande mwengine, kuna ahādīth nyingi zenye kuthibitisha yakwamba haifai kuswali witr asubuhi. Kwa mfano, imepokewa

kutoka kwa Ibn „Umar (رضي اهلل عنه) yakwamba amesema Mtume ( صىل اهلل عليه :(وسلم

“Kukianza kupambazuka, swala zote za usiku na witr humalizika. Kwahiyo swalini witr kabla hakujapambazuka.”3

Upatanishi ulio bora katika ahādīth hizi ni kusema yakwamba mwenye kukosa kuswali witr kwa kusudi hana haja ya kuilipa, kinyume cha mwenye kuwa na niya ya kuamka ili aiswali witr lakini akalala usiku mzima bila ya kuamka.

1 Imepokewa na Ibn Mājah na at-Tirmidhī; imethibitishwa kuwa swahīh na al-Albānī.

2 Imepokewa na at-Tirmidhī aliyesema, “Hii imeswihi zaidi kuliko hiyo iliyotangulia.”

Yâni hadīth ya Abū Sa’īd. 3 Imepokewa na Abū Dāwūd na at-Tirmidhī; imethibitishwa kuwa swahīh na al-Albānī.

Page 155: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 6 Jinsi Ya Kuswali Qiyâm

137

KUISWALI WITR JUU YA WANYAMA

Sa‟īd Bin Yasār (رضي اهلل عنه) amepokea yakwamba alikuwa

akisafiri na Ibn „Umar. Walipokuwa safarini, yeye alibaki nyuma kwa muda mchache, kisha akajiunga nae tena. Ibn „Umar akamuuliza, “Ulikuwa wapi wewe?” akamjibu, “Nilisimama kuswali witr.”

Kisha akasema:

“Basi si ungelichukuwa mfano bora kutoka kwa Mtume

akiswali witr (صىل اهلل عليه وسلم) Mimi nilimuona Mtume ?(صىل اهلل عليه وسلم)

juu ya mnyama wake.”1

Hii inaashiriya yakwamba msafiri anaweza kuswali witr haliyakuwa amekaa juu ya mnyama anayetembea au, katika zama zetu hizi, ndani ya magari, ndege, n.k (na kadhaalika). Katika hali kama hizo, mtu na ajitahidi kadiri ya uwezo wake angalau aelekee Qiblah (kibula) mwanzoni mwa swala yake.

1 Al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

Page 156: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

138

MLANGO 7

QUNÛT 1

MAANA YA QUNŪT

Neno hili, Qunūt, limetokamana na kitendo katika lugha ya kiarabu qanata. Kulingana na Ibn Mandhūr:

“Maana ya Qunūt ni kukoma kuzungumza, maombi kwenye swala, „ibādah, kujisalimisha, kutekeleza vitendo vyema vya heshima, na kusimama. Tha‟lab amedai yakwamba maana ya pili ndiyo ya asili. Kulingana na wengine, maana yake ni kisimamo kirefu ...

Amesema Abū „Ubayd, „Qunūt inahusisha mambo mengi, likiwemo miongoni mwayo kisimamo. Hii ndiyo maana iliyokusudiwa kwenye ahādīth zinazohusiana na qunūt wakati wa swala, kwa sababu mwenye kuitekeleza (hiyo qunūt) huomba haliyakuwa amesimama. La kudhihirika zaidi kuliko hayo ni hadīth ya Jābir, pindi alipomuuliza

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) kuhusu sampuli bora ya swala, naye akamjibu,

“(Ni swala) yenye qunūt ndefu.” Maana yake ni kisimamo kirefu.‟

Mwenye kuswali huelezwa kuwa ni qānit (mwenye kutekeleza qunūt); na kwenye hadīth, “Mfano wa Mujāhid (mpiganaji katika njia ya Allāh) ni kama ule wa qānit na aliyefunga,” Maana yake ni „kuswali‟ ...

1 Kwenye sehemu kubwa, mlango huu si katika kitabu kilichofasiriwa kutoka kwenye

makala ya Sheikh Al-albānī, lakini imeingizwa humu kwa min-ajil ya ukamilishaji. Kumbukumbu zilizotumika katika makala haya yametajwa kwenye utangulizi.

Page 157: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

139

Neno Qunūt limetajwa mara kwa mara kwenye ahādīth. Lina maana nyingi, kama vile kujisalimisha, swala, du‟ā‟, „Ibādah, kisimamo, kisimamo kirefu, na kukoma kuzungumza. Kisha ikapokewa yakwamba maana iliyo makhsusi miongoni mwa maana hizi kulingana na muktadhaa katika hadīth inamojitokeza ndani yake.

Amesema Ibn ul-Anbārī, Qunūt ni sampuli nne: swala, kisimamo kirefu, kuwa na msimamo wa kuendelea na utwi‟ifu, na kuwa kimya.‟ Na akasema Ibn Sayyid, „maana ya Qunūt ni Hii ndiyo maana yake ya asili, na kulingana nayo amesema Allāh

,Al-qānitīna wal-qānitāti.>>1 Kutokana na haya>> :(سبحانه وتعاىل)

kisimamo cha ndani ya swala kimeitwa qunūt, na vilevile qunūt katika swala ya witr.‟

Maana ya Qanata kwa ajili ya Allāh ni kumtwi‟i Yeye ... Maana ya Qānit ni kuwa mtwi‟ifu; na maana yake ni mwenye kuendelea kumkumbuka Allāh; na baadhi wanasema yakwamba maana yake ni „mwenye kufanya „Ibādah‟ ... ni maarufu katika lugha yakuwa maana ya qunūt ni du‟ā‟.

Maana swahīh ya qānit ni mtu aliyesimama (yaani; mwenye kujisalimisha) na amri za Allāh. Mtu anapo-omba haliyakuwa amesimama, sifa makhsusi anayopewa huwa ni qānit

kwa sababu huwa anamtaja Allāh (سبحانه وتعاىل) akiwa amesimama

kwa miguu yake.

Kwahivyo, maana swahīh ya qunūt ni „Ibādah na kuomba

du‟ā‟ kwa Allāh (سبحانه وتعاىل) akiwa katika hali ya kusimama. Vilevile

inaweza kutumika katika vitendo vyengine vya utwi‟ifu kwa sababu hata kama hawakuhusisha kisimamo chenyewe cha miguu, lakini huwa bado wanahusisha kisimamo (cha „Ibādah) kwa niya zao.”2

1 Al-Ahzāb 33:35

2 Lisān ul-‘Arab

Page 158: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

140

Maana ya qunūt hususan inayotuvutia kwenye mlango huu ni: “kuomba du‟ā‟ wakati wa swala ukiwa katika kisimamo.”

SABABU HASWA ZA KULETA QUNŪT

Kushikamana kwa uhakika na Sunnah kunaamuru kumfuata Mtume ( صىل katika aliyoyafanya, na pia kujiepusha na aliyojiepusha (اهلل عليه وسلم

nayo. Hii ni hukmu ya ujumla inayotumika kwenye qunūt vilevile. Kwahiyo, haikuwachwa huru kwa watu wajiamulie ni katika swala zipi au ni lini wanapostahiki kuleta qunūt. Sunnah ilikwisha tanguliza uamuzi huo, na ikahifadhiwa katika vitabu vya hadīth – kutokamana

na vitendo vya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) na Maswahaba zake. Katika

mlango huu, tunadhihirisha msimamo wa sawa unaompasa mtu aitekeleze du‟ā‟ hii.

1. KUTOKEAPO MIKASA

Imeamrishwa katika Sunnah kutekeleza qunūt pindi litokeapo tukio la mkasa au maafa kwa Waislamu, kama vile vita, mitetemeko ya ardhi, mifuriko, ukame, n.k (na kadhaalika). Dalili ya haya ni hadīth ya Anas

:(رضي اهلل عنه)

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliwatuma watu sabiini waliokuwa wakijulikana

kama Al-qurrā‟ (wasomaji), kwa shughuli fulani. Mapote mawili kutoka katika kabila la Sulaym, yaitwao Ri‟l na Dhakwān, wakawasimamisha njiani karibu na kisima cha Ma‟ūnah. Wakawaambia, „Wallāhi, sisi hatukuja kupigana na nyinyi; sisi tuko

katika utumishi wa Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ) tu. Juu ya kuambiwa kote

huko, waliwauwa. Na Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ) akaomba du‟ā‟ kwa muda

wa mwezi mzima katika swala za asubuhi. Hivyo ndivyo qunūt ilivyoanza, kwa sababu hatukuwahi kuifanya kabla ya hapo.”1

1 Al-Bukhārī, Muslim.

Page 159: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

141

Utumishi wa hao wasomaji ulielezwa katika riwaya

nyengine na Anas (رضي اهلل عنه):

“Baadhi ya watu walikuja kwa Mtume ( وسلم عليهصىل اهلل )

awapelekee watu wanaoweza kuwafundisha Qur‟ān na Sunnah.

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akawatumia watu sabiini kutoka katika kabila

al-Answār (wanati Waislamu wa mji wa al-Madīnah) waliokuwa wakijulikana kwa jina la Al-qurrā‟ (wasomaji). Miongoni mwao alikuwemo mjombangu aitwae „Harām‟. Watu hao walikuwa wakiisoma Qur‟ān, wakiitafakari na kuizingatia wakati wa usiku. Uingiapo mchana, walikuwa wakileta maji msikitini, wakikusanya kuni, wakiziuza, na kwa pato hilo wakawa wanajinunulia vyakula wao pamoja na masikini waliokuwa msikitini. Kwa hivyo, Mtume

akawapelekea watu hao, lakini wakawashambulia na (صىل اهلل عليه وسلم)

kuwauwa kabla hata hawajafika walikokuwa wanakwenda ...”1

Mauaji ya hao Maswahaba wema yalimuhuzunisha sana

Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمص ) kama alivyohadithia Anas:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya qunūt kwa muda wa mwezi

mzima, walipouwawa ma-qurrā‟; na sijawahi kumuona Mtume

akiwa na huzuni kiasi hicho.”2 (صىل اهلل عليه وسلم)

Amesema an-Nawawī:

“Mfumo wa sawa na ulio mashuhuri ni kwamba kunapotokea mikasa, kama vile maadui, njaa, maradhi ya tauni, ukame, maafa ya dhahiri kwa Waislamu, na mfano wake, wao hufanya qunūt kwenye swala zote (za faradhi).”3

1 Muslim.

2 Al-Bukhārī, Muslim.

3 Sharhu swahīh Muslim.

Page 160: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

142

2. MATUKIO MUHIMU YENYE KUWAATHIRI WAISLAMU

Vilevile qunūt imeamrishwa kutekelezwa kwenye matukio ya dharura pindi Waislamu wanapokuwa katika haja kubwa sana ya usaidizi na

ulinzi wa Allāh (سبحانه وتعاىل) katika mas‟ala makhsusi. Abū Hurairah ( رضي (صىل اهلل عليه وسلم) wamepokea yakwamba Mtume (رضي اهلل عنه) na Anas (اهلل عنه

alifanya qunūt kwa muda wa mwezi mzima, baada ya rukū‟, akisema:

<Yā Allāh! Mnusuru al-Walīd Bin al-Walīd.

Yā Allāh! Mnusuru „Ayyāsh Bin Abī Rabī‟ah.

Yā Allāh! Wanusuru Waumini waliodhulumiwa.

Yā Allāh! Wakazie kibano (kabila la) Mudar.

Yā Allāh! Wateremshie miaka ya njaa, kama yale ya Yūsuf.1

Hadīth hii vilevile ilipokewa na Ibn Hibbān, aliyesherehesha:

“Taarifa hii inaashiriya waziwazi yakwamba qunūt wakati wa swala imeamrishwa pindi yanapotokea mambo muhimu peke yake, kama vile ushindi wa maadui wa Allāh dhidi ya Waislamu, dhulma za dhalimu, kumkandamiza mtu, watu wanaohitaji kuombewa du‟ā‟, Waislamu waliotekwa wakiwa kwenye mikono wa washirikina, au hali nyengine zenye kufanana na hizo.”2

Abū Hurairah pia amepokea:

“Pindi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipokuwa akitaka kumuombea mtu

du‟ā‟, au kumuapiza mtu, alikuwa akileta qunūt baada ya rukū‟.3

Na Abū Salamah (رضي اهلل عنه) amepokea yakwamba amesema Abū

Hurairah (رضي اهلل عنه):

1 Al-Bukhārī, Muslim.

2 Swahīh Ibn Hibbān, No. 1986

3 Al-Bukhārī, Ahmad na wengineo.

Page 161: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

143

“Wallahi nitawaswalia mbele yenu swala inayofanana na

swala ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم).”

Katika kuainisha kwake jinsi alivyoswali Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

Hurairah akaleta qunūt katika swala za Dhuhr, „Ishā‟, na Fajr, kwa waumini, na kuwalaani makafiri.1

3. QIYĀM NA WITR

Haya yatajadiliwa kwa kina hapa chini.

NI SWALA ZIPI ZA FARADHI?

SWALA ZOTE

Sampuli mbili za mwanzo za qunūt katika mlango uliotangulia zinafaa kutekelezwa kwenye swala za faradhi. Haya yamethubutu kutokana na baadhi ya riwaya za hapo juu na vilevile riwaya ifuatayo ya Ibn

„Abbās (رضي اهلل عنه):

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alitekeleza qunūt kwa mwezi mzima

mfululizo, katika swala za dhuhr, „asr, Maghrib, „ishā‟ na fajr. Aliileta mwishoni mwa swala, katika rakā‟ah ya mwisho, baada ya kusema Sami‟allāhu liman hamidah. Aliwalaani vitagaa miongoni mwa kabila la Sulaym: Ri‟l, Dhakwān, na „Usayyah; na waliokuwa wakiswali nae nyuma yake wakiitikia, āmīn.”2

SUNNAH ILIYOHAMWA

1 Al-Bukhārī, Muslim.

2 Imepokewa na Abū Dāwūd, Ahmad na wengineo. Isnād yake ni hasan.

Page 162: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

144

Kutokana na riwaya nyengine zilizo swahīh, baadhi yake zikiwa

zimetajwa hapo juu, hakuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akileta qunūt kila

mara katika swala za kila siku. Mara nyengine alikuwa akileta wakati wa dhuhr, „ishā‟ na fajr; mara nyengine katika wakati wa Maghrib na fajr1; na mara nyengine katika wakati wa fajr peke yake. Hii yaonekana kuwa inategemea juu ya uzito na umuhimu wa hali yenyewe inayohitaji qunūt hiyo.

Sunnah hii imepotea sana miongoni mwa Waislamu. Wengi wao hawaleti qunūt wakati wa swala za faradhi, wakiwa kwenye hali za mikasa au vyenginevyo. Wengine huleta qunūt kwa mfululizo kila wakati wa swala ya fajr. Miondoko yote hii miwili ni ya makosa, kama ilivyoelezwa hapo awali, na yatajadiliwa hapa chini kuhusiana na swala ya fajr.

Katika zama zetu hizi tulizonazo, Waislamu wako kwenye mikasa ya kuendelea ya kivita, maafa, na kadhaalika. Lakini hilo halijuzishi kuithibitisha qunūt kudumu kuwepo kwake kila siku, kwenye swala zote.

Qunūt kwa matukio yasiyo ya kawaida itawajibika kwenye hali ambazo maafa yenyewe ni ya ghafula na hayakuwa yametarajiwa, yakasababisha huzuni na ghadhabu kwa njia isiyo ya kawaida. Chini ya hali kama hizo, imependekezwa kuleta qunūt kwenye baadhi ya swala au swala zote za kila siku – kwa kutegemea uzito wa ile hali yenyewe.

Hali zinapobadilika, au zikawa ni za kawaida, basi Waislamu wanatakiwa kwa utaratibu au kwa mara moja wawache kuleta qunūt katika swala za faradhi.

WAKATI WA FAJR?

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) hakuwa na kawaida ya kuleta qunūt katika swala

ya fajr au swala nyengine za faradhi. Taarifa za hapo juu zinaashiriya

1 Muslim na wengineo kutoka kwa Barā’ (رضي اهلل عنه).

Page 163: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

145

waziwazi yakwamba alifanya kwa muda wa mwezi mzima au zaidi kidogo. Riwaya nyengine zinaashiriya yakwamba aliwalaani makafiri kwenye qunūt baada ya vita vya Uhud, au kwenye matukio mengine, mpaka Allāh alipomkataza (Āl-„Imrān 3:128).1

Kwahiyo, haikupendekezwa kuleta qunūt khususan katika swala ya fajr, wala isiwe ni ya kawaida na kudumu kwenye swala nyengine yoyote ya faradhi. Amesema Ibn ul-Qayyim:

“Ni dhahiri shahiri yakwamba, lau kama Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

angelikuwa ni mwenye kudumu katika qunūt kila alfajiri, akiwa na Maswahaba wakiitikia āmīn nyuma yake, hili lingelisambazwa na Ummah mzima – kama walivyosambaza habari zinazohusu kuisoma Qur‟ān kwa sauti wakati wake (swala hiyo), idadi ya rak‟āt zake, na wakati wake. Ikiwa wao wangelipuuza kusimulia kuhusu qunūt, basi vilevile wangelipuuza baadhi ya habari nyengine ...

Katika mafunzo yake, Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akileta

qunūt khususan panapotokea mambo yasiyokuwa ya kawaida, na penginepo kuiwacha.”2

Kwa hakika, kuna riwaya zilizo swahīh kutoka kwa Maswahaba (wakiwemo Ibn „Umar, Ibn Mas‟ūd, Ibn „Abbās, Anas na Abū Hurairah) wakieleza waziwazi yakwamba hawakuleta qunūt wakati wa swala ya fajr, na nyenginezo ambapo wameithibitisha yakuwa jambo hilo ni bid‟ah. Kwa mfano Abū

Mālik al-Ashja‟ī (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba alimuuliza

babake:

“Ewe Babangu! Wewe uliswali nyuma ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم),

Abū Bakr, „Umar, „Uthmān na „Alī. Jee hao walileta qunūt?”. Babake akamjibu, “Ewe mwanangu, huwo ni uzushi!”1

1 Al-Bukhārī na Muslim kutoka kwa Abū Hurairah na Ibn ‘Umar (رضي اهلل عنهم)

2 Zād ul-Ma’ād 1:272.

Page 164: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

146

Ama kuhusu riwaya yakwamba, “Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

aliendelea kuleta qunūt wakati wa fajr mpaka kuondoka kwake ulimwenguni,”2 hiyo ni dha‟īf, na haiwezekani kutumika kuikosoa riwaya ya hapo juu iliyo swahīh.

KABLA AU BAADA YA RUKŪ‟?

Iwapo mtu atapendelea kuleta qunūt, basi na ailete kwenye rak‟ah ya mwisho ya swala, kabla au baada ya rukū‟. Rai zote mbili zinaruhusiwa kulingana na wanavyuoni wengi.

BAADA YA RUKŪ‟

Kwa qunūt ya swala za faradhi, riwaya nyingi zinaunga mkono kuileta baada ya rukū‟. Baadhi ya riwaya hizi zimetangulia. Kwa ujumla, Ibn Sīrīn amehadithia yakwamba aliulizwa Anas Bin Mālik, “Jee, Mtume

”.alileta qunūt katika swala ya fajr?” akajibu, “Ndio (صىل اهلل عليه وسلم)

Akaulizwa, “Ilikuwa ni kabla au baada ya rukū‟?” akajibu, “Ilikuwa baada ya rukū‟, kwa muda mchache.”3

KABLA YA RUKŪ‟

„Āsim Bin al-Ahwal amesimulia yakwamba alimuuliza Anas (رضي اهلل عنه) iwapo qunūt inafaa itekelezwe kabla au baada ya rukū‟. Anas akamjibu, “kabla ya rukū‟.” Akasema, “Lakini mtu fulani wa fulani aliniambia yakwamba ati wewe ulisema, „Baada ya rukū‟.‟”

1 Imepokewa na Ahmad, an-Nasā’ī na wengineo, kwa upokezi mbalimbali ulio swahīh.

Angalia katika Ahkām ul-Qunūt. 2 Imepokewa na Ahmad, ad-Dāraqutnī na wengineo kutoka kwa Anas. Riwaya hii ni

dhaifu kwa sababu ya mmojawapo wa wapokezi katika upokezi wake, Abū Ja’far ar-Rāzī, anayezingatiwa kuwa dhaifu na wanavyuoni wa hadīth. 3 Al-Bukhārī, Muslim.

Page 165: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

147

Akamjibu, “Huyo mtu amekosa. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alileta qunūt

baada ya rukū‟ kwa muda wa mwezi mmoja peke yake ...”1

Katika riwaya nyengine, amesema Anas (رضي اهلل عنه): “Qunūt huwenda ikaletwa kabla au baada ya rukū‟.”2

Al-albāni alileta mapatano baina ya riwaya mbalimbali kusema yakwamba riwaya hizo zenye kuizungumza qunūt baada ya rukū‟, zinazungumzia qunūt wakati wa matukio na maafa (na huletwa kwenye swala za faradhi), haliyakuwa riwaya zenye kuizungumza qunūt kabla ya rukū‟ zinazungumzia kuhusu hali nyengine, iitwayo, qunūt katika witr.3

Hatahivyo, kuna riwaya zilizo swahīh zilizopokewa na Ibn Abī Shaybah4 na at-Twahāwī5 kutoka kwa ‟Umar, Ibn „Abbās na wengineo yakwamba walileta qunūt wakati wa fajr kabla ya rukū‟.6

QUNŪT YA WITR

Ubayy Bin Ka‟b (رضي اهلل عنه) amesimulia yakwamba:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akileta qunūt katika witr kabla ya

rukū‟.”7

1 Al-Bukhārī, Muslim. Nyongeza ya hadīth hii ilinukuliwa hapo awali kwenye mlango

huu. 2 Imepokewa na Ibn Mājah. Al-Hāfidh amesema katika Fat hul-Bārī yakwamba isnād

yake ina nguvu. 3 Irwā ul-Ghalīl 2:168

4 Al-Musannaf, kuanzia Na.7012

5 Al-Mushkal 1:147

6 Angalia kitabu cha Sheikh ‘Adnān ‘Ar’ūr kiitwacho “Ahkām ul-Qunūt.” Uk. 45

7 Imepokewa na an-Nasā’ī, Ibn Mājah na wengineo. Imethibitishwa kuwa ni swahīh

na al-Albānī katika Irwā’ ul-Ghalīl Na. 426

Page 166: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

148

Ibn ul-Qayyim amesema:

“Hakuna kilichopokewa kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

yakwamba alileta qunūt katika witr isipokuwa hadīth hii (ya Ubayy).”

Juu ya hayo, kuna riwaya kutoka kwa Maswahaba kuhusiana na kuhusiana na haya. Amesimulia „Alqamah, “Ibn Mas‟ūd na Maswahaba Maswahaba wengine yakwamba walikuwa wakileta qunūt katika witr witr kabla ya rukū‟.”1

HATIMAE

Kutokana na yaliyopita, tunahatimika yakwamba qunūt inaweza kuletwa kabla au baada ya rukū‟. Lakini hatahivyo, inapendekezwa kuletwa baada ya rukū‟ kwenye swala za faradhi na kabla ya rukū‟ kwenye swala ya witr.

MAS‟ALA ANUWAI (MENGINEO)

KUISOMA QUNŪT KWA SAUTI

Ni dhahiri kutokamana na riwaya zilizotangulia yakwamba Sunnah ni kuileta du‟ā‟ ya qunūt kwa sauti. Jambo hili huwawezesha waumini waisikize du‟ā‟ ya Imām wakapata kushirikiana naye.

Amesema al-Hāfidh Ibn Hajar:

“Inanidhihirikia mimi yakwamba hikma iliyoko katika kuleta qunūt (ya mikasa) ukiwa kwenye kisimamo badala ya sujūd, hata kama du‟ā‟ hupendekezwa zaidi kujibiwa katika sujūd, ni kwamba inahitaji kujumuika pamoja na wale wenye kuswali nyuma ya Imām, angalau kwa kuitikia āmīn. Kwa ajili hii,

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah (Na, 6911) kwa isnād iliyo swahīh. Angalia katika

“Ahkām ul-Qunūt.”

Page 167: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

149

wanavyuoni wamekubaliana yakwamba inafaa kusomwa kwa sauti.”1

KUITIKIA ĀMĪN

Imependekezwa kwa wenye kuswali nyuma ya Imām waitikie āmīn wakati wa du‟ā‟ ya qunūt. Kuhusiana na suala hili, tumeshatangulia hapo nyuma kuitaja hadīth ya Ibn „Abbās (Uk. 159).

KUINUA MIKONO

Katika mojawapo ya taarifa za riwaya ya Anas, alisema:

“... sijawahi kumuonapo Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akiwa na huzuni

kiasi hicho. Kwahiyo, wakati wa swala ya asubuhi, aliinua mikono yake na kuwalaani ...”2

Al-Bayhaqī alitaja riwaya mbalimbali, zikiwemo baadhi yake swahīh, kuhusu kuinua mikono kwa Maswahaba. An-Nawawī akathibitisha uswahīh wa riwaya nyengine kutoka kwa Maswahaba zilizotajwa na al-Bukhārī.

Haya vilevile yanahusu qunūt ya witr. Imethubutu

yakwamba „Umar (رضي اهلل عنه) aliinua mikono yake kwenye qunūt

hii.3

Vilevile, imependekezwa kwa wenye kuswali nyuma ya Imām wamfuate kuinua mikono yao pindi anapoinua yake wakati wa qunūt,

kwa sababu ya maelekezo yake (صىل اهلل عليه وسلم) ya ujumla:

“Imām amewekwa ili afuatwe.”1

1 Fat-hul Bārī 2:570

2 Imepokewa na Ahmad, al-Bayhaqī na wengineo, kwa isnād iliyo swahīh. Angalia

“Ahkām ul-Qunūt.” 3 Imetajwa na al-Albānī katika Irwā ul-Ghalīl 2:181

Page 168: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

150

Yanayopaswa Kusemwa Wakati Wa Qunūt Ya Witr

Baada ya kumaliza kusoma Qur‟ān kwenye rak‟ah ya mwisho ya witr, na kabla ya rukū‟, mara nyengine mtu anaweza kuomba du‟ā‟ ambayo

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliyomfundisha mjukuu wake al-Hasan Bin „Alī

( عنه اهلل رضي ):

ريج » رن ذيهو م ا ج ،وعفن ذيهو عذيج ،الل ل لن ذيهو ح ،وحخطيج

إىم تلض وال حلض ،وكن ش نا كضيج ،وبارك ل ذيها أ

ال ي ،عليم تتاركج ربيا ،وال يعش نو عديج ،زل نو والج وإى نيم إال إلم ،وتعالج

«ال ملجأ

<Allāhumma „Ihdinī fīman hadayt; wa-„āfinī fīman „āfayt; wa-tawallanī fīman tawallayt; wabāriklī fīmā a‟tayt; wa-qinī

sharra mā qadhayt; fa-innaka taqdhī walā yuqdhā „alayk; wa-innahū lā yadhillū man wālayt; walā ya‟izzu man „ādayt;

tabārakta rabbanā wa-ta‟ālayt; lā manjā minka illā ilayk –

“Ewe Mola, niongoze mimi pamoja na wale uliowaongoa, na uniafu mimi pamoja na wale ambao uliowaafu, na unifanye

mimi kuwa ni rafiki yako pamoja na wale ambao uliowafanya kuwa ni rafiki zako. Na unibariki mimi katika kile ulichonipa. Na uniepushe mimi na shari uliyoihukumu, kwani wewe ndiye mwenye kuhukumu, wala huhukumiwi. Na hakika yako wewe, humdhalilishi yule ambaye unayempenda. Wala humpi nguvu unayemchukia. Utukufu ni wako wewe, Ewe Mola wetu, na Umetukuka. Hapana uokofu isipokuwa kwa kupitia kwako.”

1 Al-Bukhārī.

Page 169: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

151

Kwa mara chache, mtu anaweza kuongezea kumswalia Mtume ( صىل اهلل Pia inapowadia nusu ya pili ya mwezi wa Ramadhān, anaweza .(عليه وسلم

mtu kuongezea katika kuwalaani Makafiri, kumswalia Mtume ( صىل اهلل عليه na kuwaombea du‟ā‟ Waislamu. Jambo hili lilikuwa likifanywa na (وسلم

ma-Imām katika zama za „Umar ( عنه اهلل رضي ), kama alivyotuhadithia

„Abd ur-Rahmān Bin „Abd al-Qārī:

“Na wakawalaani ma-Kuffār katika nusu (ya pili) ya mwezi (wa Ramadhān):

لح ةنح رسلحكح وح ذ يكح ، وح بيلكح و سح ونح عح يوح يحصد ةح ال رح فح م كحاتحل الكح الل حم، وحأ ه الف بحنيح كح ، وحخح حعدكح لق يؤنينح ة

ح، وحأ م الرعبح لق ف كلب

ح الحق ، إلح اةحكح ذح م رجزحكح وحعح يلح عح

<Allāhumma qāil „lkafarata „lladhīna yasuddūna „an sabīlik, wayukadh-dhibūna rusulak, walā yu‟minūna biwa‟dik, wakhālif

bayna kalimatahum, wa-„alqi fī qulūbihim ur-ru‟b, wa-„alqi „alayhim rijzaka wa „adhābak, ilāha „lhaqq –

“Ewe Mola, wapige makafiri wenye kuwazuiya watu katika Dini yako, na wenye kuwakadhibisha Mitume wako, na wasoamini ahadi zako. Tenganisha baina ya maneno yao na utie ndani ya

nyoyo zao, khofu. Na uwapatilize na adhabu yako. Ewe Mola wa Hakki.”

Kisha wakamswalia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), wakawaombea

Waislamu kwa kila mazuri waliyoyapendelea, na wakawaombea waumini maghfira (msamaha). Na kufuatia hayo wakasema:

حكح ل عتد ، وح م إياكح نح ىحرج الل فد ، وح نح حسعح وح كح ن إلح حسجد ، وح ن ل وح ىصحدحيتح ملحق و عح اةحكح لهح ذح د ، إن عح اةحكح ال ذح حاف عح نح بيحا ، وح رحححتحكح رح

Page 170: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

152

<Allāhumma iyyāka na‟bud, walaka nuswallī wanasjud, wa-ilayka nas‟ā wanahfidh, wanarjū rahmataka rabbanā,

wanakhāfu „adhābaka „ljadd, inna „adhābaka liman „ādayta mulhaq –

“Ewe Mola, wewe peke yako twakuabudu, na twaswali kwa ajili yako, na twakusujudia (peke yako). Na kwa ajili yako tunakwenda mbio na kujitahidi (kutafuta radhi zako), na

twataraji Rehma zako Mola wetu, na twaiogopa adhabu yako iliyo kali. Hakika adhabu yako, kwa mwenye kukufanyia uadui,

hapana shaka itakuwa ni yenye kumpata.”

Kisha huitamka takbīr na wakapomoka kwa kusujudu.”1

UZUSHI NA UPOTOFU

KUPANGUSA USO

Hakuna riwaya zilizo swahīh zenye kuthibitisha yakwamba Mtume ( صىل aliwahi kuupangusa uso wake kwa mikono yake baada ya (اهلل عليه وسلم

kuomba du‟ā‟ kwa ujumla, au baada ya qunūt khususan. Kwa ajili hii, amesema an-Nawawī:

“Hii haikupendekezwa, kulingana na alivyosema al-„Izz Bin „Abd us-Salām ... Hapana afanyaye hivyo isipokuwa mtu mjinga.”2

Na akasema al-Bayhaqī:

“Ama kuhusu kujipangusa uso kwa mikono baada ya kuomba du‟ā‟, mimi sijui yakuwa palikuwa na mwenye kufanya hivyo miongoni mwa Salaf.”3

1 Imepokewa na Ibn Khuzaymah; imeswahihishwa na al-Albānī (Qiyāmu Ramadhān).

2 Al-Majmū’

3 As-Sunan 1:212

Page 171: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

153

KUITANGULIZA QUNŪT KWA TAKBĪR

Hakuna riwaya zilizo swahīh zenye kuunga mkono kuinua mikono wakati wa kupiga takbīr (kutamka allāhu akbar) kabla ya kuanza qunūt. Kwahiyo, kufanya hivyo ni jambo la uzushi na ni lazima liepukwe.

QUNŪT NDEFU

Jambo la uzushi lililoanza kwenye Misikiti mitukufu ya ki-Islamu, na kusambaa kwenye miji mbalimbali ya ulimwengu wa ki-Islamu, ni lile la kuleta qunūt ndefu kupita kiasi, hususan baada ya nusu ya Ramadhān.

Utawakuta ma-Imām wakileta du‟ā‟ ndefu sana, wakirudia-rudia baadhi ya maana, wakichokesha mikono yao na ya wafuasi wao, wakifungua mitiririko ya fikra za wafuasi kuzurura katika hali za kuchanganyikiwa – wakimungoja Imām amalize msururu wake wa fikra na matakwa yasiyokuwa na muelekeo!

Uzushi huu hauna msingi wowote katika mafunzo ya

Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) au Maswahaba zake, ambao qunūt zao

zilikuwa ni za vipimo wastani na zenye muelekeo, kama zilivyobainishwa katika mlango uliotangulia.

KUOMBOLEZA NA KULIA

Kuongezea katika uzushi wa qunūt ndefu, vilevile imekuwa ni desturi, ambazo ma-Imām huongoza tamthilia mbele ya wafuasi wao, kwa vilio vya dhati vya sauti na kwikwi, wakiwavutia wengi wa wanaoswali nyuma yao wawafuate wao na kuwa umati unaolia kwa pamoja. Sasa inaonekana kana kwamba jambo hili ni miongoni mwa yenye kuhitajika kufanywa katika kuswali swala ya tarawīh – kiasi cha kwamba ma-Imām wanashindana kulia; na watu wa kawaida

Page 172: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 7 Qunût

154

wanadhani yakwamba Imām aliye bora zaidi ni yule mwenye kulia sana, na akawasababisha umati mkubwa wa watu walie naye!

Huu ni uzushi mwengine usiokuwa na msingi wowote katika Sunnah au mafundisho ya watu wema waliowahi kuishi katika zama bora.

Hapana makosa katika kulia kwa kumuogopa Allāh. Lakini Sunnah imewapa fadhla kubwa wale wenye kufanya hivyo wanapokuwa peke yao, wakiwa mbali na kuchunguzwa na watu. Ucha Mungu wa mtu na kutafakari juu ya madhambi yake kunaweza bila ya shaka yoyote kumfanya aangue kilio kikubwa, hata akiwa mbele ya watu. Lakini hili latakikaniwa liwe ni nadra, wala sio kawaida.

Page 173: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

155

MLANGO 8

I‟TIKĀF1

UFAFANUZI

Katika lugha ya kiarabu, maana ya nomino ya kinadharia i‟tikāf ni “kifungo”. Imetokana na kitendo „akafa, yenye maana ya “kuishi au kukaa mahali fulani”. Kutokana na maana hii vilevile limetoka neno ma‟kūf, lenye maana ya “kuwa kifungoni”.2

Katika shar‟ ya ki-Islamu, maana ya i‟tikāf ni kukaa au kuwa kwenye faragha msikitini kwa muda maalum, kutafuta kwa kufanya hivyo radhi za Allāh3. Mwenye kufanya i‟tikāf huitwa mu‟takif au „ākif.

HUKMU

I‟tikāf ni kitendo kilichopendekezwa cha „Ibādah katika mwezi wa Ramadhān, na nyakati nyengine katika mwaka mzima. Hili

1 Katika sehemu kubwa, mlango huu hautokani na kitabu kilichofasiriwa cha Sheikh

al-Albānī, lakini umeingizwa humu kwa min-ajil ya ukamilishaji. Kumbukumbu zilizotumika katika kitabu hiki zimetajwa katika dibaji. 2 Kutoka katika Hulyat ul-Fuqahā’ cha Ibn Fāris (110), Jāmi’ ul-Usūl (1:337), na al-

Misbāh ul-Munīr (2:424). 3 Kutoka katika Tar hut-Tathrīb cha Ibn ul-‘Irāqī (4:166) na al-Mufradāt cha ar-Rāghib

(343).

Page 174: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

156

limethibitishwa na Qur‟ān, Sunnah, walivyofanya ma-Salaf na ijmā‟.

Katika Qur‟ān, Allāh (سبحانه وتعاىل) amesema:

“Wala msichanganyike nao (musiwaingilie), na hali mnakaa Itikafu misikitini.”1

Katika Sunnah, kuna idadi kubwa ya ahādīth zilizo swahīh zenye

kuieleza i‟tikāf ya Mtume (صىل اهلل عليه وسلم), ambazo baadhi yake

zitanukuliwa hapa chini. Vilevile kuna riwaya chungu nzima

zinazoeleza jinsi zilivyokuwa i‟tikāf za Salaf2. Kwa mfano, „Umar ( رضيعنه اهلل ) alimwambia Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ), “Mimi nilikula kiapo wakati

wa Jāhiliyyah3 kufanya i‟tikāf kwa siku moja katika al-Masjid ul-

Harām (Msikiti Mtukufu wa Makkah).” Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

akamwambia:

“Basi tekeleza kiapo chako.”

Kwahiyo, „Umar alifanya i‟tikāf kwa siku moja.4

Ama kuhusu ijmā‟, ilibainishwa na Ibn al-Mundhir1, na kuthibitishwa na Ibn Qudāmah2.

1 Al-Baqarah 2:187.

2 Nyingi ya riwaya hizi zimepokewa na Ibn Abī Shaybah na ‘Abd ur-Razzāq katika

Musannaf zao. 3 Jāhiliyyah: Ni hali ya ujinga (jahl) na ukafiri iliyokuwa imetawala Arabuni kabla ya

Uislamu. 4 Al-Bukhārī, Muslim na Ibn Khuzaymah. Bâdhi ya riwaya zimetaja “usiku” badala ya

“mchana”. Kwa pamoja, riwaya hizo mbalimbali zinamânisha siku kamili, mchana na usiku wake, amabyo ndiyo uchache wa muda wa I’tikāf kama ilivyothibitishwa hapo chini.

Page 175: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

157

RIWAYA DHA‟ĪF

Baadhi ya riwaya zisizo swahīh mara nyingi hunukuliwa kuzidi kuwahimiza watu wafanye i‟tikāf. Twazitaja hapa kwa ajili ya kutahadharisha dhidi ya kuzitumia.

1. Kutoka kwa al-Husayn Bin „Alī (رضي اهلل عنه) yakwamba Mtume

amesema, “Yoyote mwenye kufanya i‟tikāf kwa (صىل اهلل عليه وسلم)

muda wa siku kumi katika mwezi wa Ramadhān, itahesabiwa kwake kuwa ametekeleza Hajj na „Umrah3 mara mbili.” Hadīth hii imezuliwa.4

2. Kutoka kwa „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) yakwamba amesema

Yoyote mwenye kufanya i‟tikāf akiwa na imani, na“ ,(صىل اهلل عليه وسلم)

kutarajia malipo kutoka kwa Allāh, atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.” Hadīth hii ni dha‟īf.5

3. “Yoyote mwenye kufanya i‟tikāf kwa siku moja, akitarajia Uso wa Allāh, Allāh atamuwekea mahandaki matatu baina yake na moto, na kila handaki litakuwa na upana mkubwa kuliko umbali wa baina ya Mashariki na Magharibi.” Hadīth hii ni dha‟īf.6

1 Katika al-ijmā’ (47)

2 Katika al-Mughnī (3:183)

3 Hajj ndogo inayotekelezwa katika msimu wa Hajj na nyakati nyengine katika mwaka

mzima. 4 Imepokewa na al-Baihaqī katika Shu’ab ul-Īmān. Angalia katika adh-Dha’īfah (Na.

518) na Dha’īf ul-Jāmi’ (5451) cha al-Albānī. 5 Imepokewa na ad-Daylamī. Angalia kwenye Dha’īf ul-Jāmī’ (5452) cha Sheikh al-

Albānī. 6 Imepokewa na at-Twabarānī na wengineo. Hadīth hii na tatizo la kutoeleweka,

lililofafanuliwa katika adh-Dha’īfah (Na. 5347) cha al-Albānī.

Page 176: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

158

HIKMA NA ADABU ZA I‟TIKĀF

HIKMA

I‟tikāf ni fursa ya Muislamu kumuelekea Allāh ( وتعاىل سبحانه ), katika

mojawapo ya nyumba zake za „Ibādah, kwa kuabudu na kujisalimisha, pasi na kuwepo pingamizi au ushawishi wa shughuli za kilimwengu.

Amesema Ibn ul-Qayyim ( اهلل رحمه ):

“Wema na ukakamavu wa moyo katika safari yake kuelekea kwa

Allāh ( وتعاىل سبحانه ) hutegemea jinsi unavyojidhalilisha kwake;

kushawishika kwake hutokomezwa kwa kuelekea kwake kikamilifu ...

Kwa ajili hiyo, Allāh ( وتعاىل سبحانه ) ameshatoa amri ya

i‟tikāf. Lengo lake na mvuto wa ki-roho ni kwa moyo ugeuke

kikamilifu na utakatifu kumuelekea Allāh ( وتعاىل سبحانه ), kuishi na

yeye katika faragha, kujiepusha kabisa kushughulika na viumbe wengine, na badala yake ukawa unashughulika na yeye tu. Pamoja na haya, kumkumbuka yeye, kumpenda na kumnyenyekea huchukuwa nafasi ya babaiko na fikira za moyo, ukachukuwa nafasi yao ndani yake, na ikawa ndiyo shughuli yake ya pekee. Kisha fikira zikashughulika kwa kumkumbuka yeye na kuyazingatia yale yenye kumridhisha yeye zikamkurubisha mtu karibu naye. Kisha, furaha ya mtu hupatikana kwa kuwa pamoja naye kuliko kuwa na viumbe, na hapo ndipo anapojitayarisha nafsi yake kwa siku ya upweke ndani ya kaburi, atakapokosa ushirika au furaha isipokuwa kuwa na yeye. Hili ndilo lengo kubwa kabisa la i‟tikāf.”1

1 Zād ul-Ma’ād (2:86-87).

Page 177: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

159

Na Ibn Rajab ( اهلل رحمه ) amesema:

“Maana na uhakika wa i‟tikāf ni pale mtu anapokata mafungamano yote na viumbe ili apate kujitolea kwa dhati kumtumikia muumba. Kila „ilmu ya mtu kumuhusu Allāh, kumpenda yeye, na kupenda kuwa pamoja naye kunapozidi, yeye

huipata „Ibādah nzima iliyokamilika kwa Allāh ( وتعاىل سبحانه ) katika

hali zote.1

ADABU KATIKA WAKATI WA I‟TIKĀF

Mu‟takif hafai kuisahau hikma kubwa na lengo la i‟tikāf iliyobainishwa hapo juu. Anapaswa kuzipitisha siku za i‟tikāf kwa utulivu na „Ibādah,

ajitolee kwa dhati wakati wake kwa Allāh ( وتعاىل سبحانه ), na autumie

katika kutekeleza vitendo vitakatifu vya „Ibādah, kama vile swala, kuisoma Qur‟ān, kuleta dhikr, kutafuta „ilmu ya Uislamu katika madda za tafsīr, Hadīth, n.k. Azungumze kwa sauti ya chini, ajiepushe na ugomvi, na ajiepushe na mazungumzo ya upuzi na mijadala.

Kwahiyo, mtu mwenye kufanya i‟tikāf na ajipinde na kufaidika kutoka katika makaazi yake msikitini ili awe bora katika „Ibādah na kuwa mtwi‟ifu, pasi na kujishughulisha nafsi yake na ushawishi wowote wa kilimwengu.

WAKATI WA MWAKA

I‟tikāf inaweza kutekelezwa wakati wowote wa mwaka. „Ā‟ishah ( رضي

عنها اهلل ) amesimulia yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya i‟tikāf kwa

siku kumi katika mwezi wa Shawwāl.2

1 Latā’if ul-Ma’ārif (Uk. 203)

2 Imepokewa na al-Bukhārī, Muslim na Ibn Khuzaymah.

Page 178: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

160

Lakini hatahivyo, imependekezwa sana kufanya i‟tikāf katika mwezi wa Ramadhān. Pendekezo hili limefuata kutokamana na hadīth ya Abū Hurairah:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akifanya i‟tikāf kwa siku kumi kila

kila ifikapo Ramadhān. Katika mwaka aliokufia, alifanya i‟tikāf kwa kwa siku ishirini.”1

Masiku bora ya kufanya i‟tikāf ni masiku kumi ya mwisho ya Ramadhān, kwa sababu haya ndiyo masiku ambamo inaposhuka Laylat

ul-Qadr. Amepokea „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akifanya i‟tikāf katika masiku

kumi ya mwisho ya Ramadhān mpaka Allāh ( وتعاىل سبحانه )

alipochukuwa uhai wake.”2

MAHALI PA KUFANYA I‟TIKĀF

MSIKITI WA IJUMAA

I‟tikāf inaweza kufanywa msikitini peke yake. Kama ilivyoashiriwa katika āyah ya hapo juu kutoka katika sūrat ul-Baqarah (2:187).

Vilevile, amesema „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Imependekezwa kwa mwenye kufanya i‟tikāf asiondoke (msikitini) isipokuwa kwa dharura isiyoweza kuepukika, asende kumtembelea mgonjwa, na asimguse wala asilale na mkewe. I‟tikāf inaweza kufanywa kwenye msikiti wenye kuswaliwa swala za jamā‟ah [au ambapo Jumu‟ah (swala ya Ijumaa) inaposwaliwa]. Na imependekezwa kwa mwenye kufanya i‟tikāf afunge.”3

1 al-Bukhārī na Ibn Khuzaymah.

2 al-Bukhārī, Muslim na Ibn Khuzaymah.

3 Imepokewa na al-Bayhaqī kwa silisili ya wapokezi iliyo swahīh, na Abū Dāwūd kwa

silisili nzuri. Sehemu iliyo baina ya mabano ya mraba imetoka kwa Abū Dāwūd.

Page 179: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

161

Kwahiyo, ni lazima i‟tikāf ifanywe kwenye msikiti unaoswaliwa Ijumaa. Jambo hili ni katika kumlinda mtu asiwe na haja ya kutoka nje (ya msikiti) kuhudhuria swala ya Ijumaa, ambayo ni wajibu juu yake.

MSIKITI MITATU MITAKATIFU

Hadīth ya wazi iliyo swahīh inazidi kuweka masharuti ya misikiti kwenye āyah ya hapo juu (2:187) kuwa ni mitatu peke yake: al-Masjid ul-Harām (Msikiti Mtukufu wa Makkah), al-Masjid un-Nabawī (Msikiti wa Mtume ulioko al-Madīnah), na al-Masjid ul-Aqswā (Msikiti wa Mbali ulioko Jerusalem).

Kundi la watu walifanya i‟tikāf kwenye msikiti uliokuweko baina ya nyumba za „Abdullāh Bin Mas‟ūd na Abū Mūsā al-Ash‟arī

katika mji wa al-Kūfah. Basi, Hudhayfah ( عنه اهلل رضي ) akamuuliza

Ibn Mas‟ūd ( عنه اهلل رضي ): “Wewe umeshikilia rai yakwamba

inaruhusiwa kufanya i‟tikāf (katika msikiti) baina ya nyumba yako

na ya Abū Mūsā? Wewe wajua yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema:

“I‟tikāf haifai kufanywa (mahali popote) isipokuwa kwenye Misikiti mitatu.”

Ibn Mas‟ūd (رضي اهلل عنه) akamjibu:

“Huwenda labda wewe ukawa umesahau (maana yake), na wao (wenye kufanya i‟tikāf kwenye msikiti mwengine) wakawa wamekumbuka. Au huwenda ukawa wewe umekosea, na wao wakawa sawa!”1

1 Imepokewa na at-Twahāwī katika Mushkal ul-Āthār (4:20), adh-Dhahabī katika

Siyaru A’lām in-Nubalā’ (15:81), al-Ismā’īlī na al-Bayhaqī katika as-Sunan (4:316), kwa silisili iliyo swahīh kutoka kwa Hudhayfah Bin al-Yamānī (رضي هللا عنه);

Page 180: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

162

Jawabu la Ibn Mas‟ūd linaashiriya yakwamba yeye hakatai uswahīh wa hadīth hii, lakini alikuwa hana hakika tu ya maana yake ya sawa. Ukweli katika hali hii ni kujinatisha na maana iliyo dhahiri ya hadīth hii.

Idadi kubwa ya wanavyuoni miongoni mwa Salaf wamejinatisha na maandiko (matn) ya hadīth hii; wakiwemo miongoni

mwao Hudhayfah Bin al-Yamān (رضي اهلل عنه), Sa‟īd Bin al-Musayyib na

„Atwā‟ (ingawaje Atwā‟hakutaja al-Aqswā‟). Wengine miongoni mwa Salaf wameshikilia rai yakwamba i‟tikāf inaweza kufanywa kwenye msikiti wowote unaoswaliwa al-Jumu‟ah.

NYUMBANI?

Baadhi ya wanavyuoni wamesema yakwamba hata mtu anaweza kufanya i‟tikāf kwenye sehemu ya nyumba yake iliyotengwa makhsusi kama mahali pa kuswali.

Ni jambo la wazi yakwamba mtu na afuate rai iliyo bora

inayokubaliana na hadīth swahīh. Na Allāh (سبحانه وتعاىل) Ndiye Mjuzi bora.

MASHARUTI YA I‟TIKĀF

Kukaa Mumo-Humo Msikitini

Kama ilivyoashiriwa hapo juu katika ufafanuzi wa i‟tikāf pamoja na

hadīth ya „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها), mu‟takif hafai kuvuka mipaka ya

msikiti, isipokuwa inaposimama dharura ya ki-binadamu, kama vile kula au kwenda kukidhi haja (chooni).

imeswahihishwa na adh-Dhahabī na al-Albānī katika silsilat ul-Ahādīth is-Swahīhah (Na. 2786).

Page 181: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

163

KUFUNGA (SWAUM)

Ni jambo lililopendekezwa kwa mwenye kufanya i‟tikāf afunge, kama

ilivyoelezwa hapo awali kutoka kwa „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها). Wanavyuoni

wengi wamezingatia kufunga kuwa ni miongoni mwa masharuti ya

i‟tikāf, ambapo ikosekanapo haitofaa. Amesema Ibn ul-Qayyim ( رحمه :(اهلل

“Hakuna riwaya yoyote yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya

i‟tikāf bila ya kufunga; bali alisema „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ): „Haifai

kufanya i‟tikāf bila ya kufunga.‟

Vilevile Allāh ( وتعاىل سبحانه ) aliitaja i‟tikāf peke yake na kufunga;

na Mtume ( ىل اهلل عليه وسلمص ) hakuwahi kufanya i‟tikāf isipokuwa

alikuwa amefunga. Kwahivyo rai iliyo na sauti kuu, iliyoshikiliwa na kundi kubwa la Salaf, ni kwamba: Kufunga (saumu) ni katika sharuti za i‟tikāf. Hii ndiyo rai ambayo Shaykh ul-Islām Abū al-„Abbās Ibn Taymiyyah aliyojichagulia.”1

Nyakati Za Kuanza Na Kumaliza

Imependekezwa kuanza i‟tikāf wakati wa asubuhi, punde tu baada ya

swala ya fajr. Amepokea „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Pindi Mtume ( سلمصىل اهلل عليه و ) alipoazimia kufanya i‟tikāf,

alikuwa akiswali swala ya fajr kisha huingia ndani ya sehemu yake ya i‟tikāf.”2

Vilevile imependekezwa kumaliza i‟tikāf wakati wa asubuhi. Al-Bukhārī aliweka kichwa cha mojawapo ya milango

1 Zād ul-Ma’ād.

2 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 182: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

164

katika swahīh yake kwa jina “Mlango kuhusu kuondoka kwenye i‟tikāf wakati wa asubuhi.” Kisha akainukuu hadīth ya Abu Sa‟īd al-Khudhrī

( عنه اهلل رضي ):

“Tulifanya i‟tikāf pamoja na Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) baada ya siku

kumi za kati na kati (za Ramadhān). Katika mapambazuko ya siku ya ishirini, tuliondoa vitu vyetu.”1

Siku Zake Kwa Uchache

Kutokana na ya hapo juu, ni dhahiri yakwamba mtu anatakiwa akae kwa uchache wa mchana mmoja na usiku mmoja katika i‟tikāf. Kwahiyo, kama ilivyothibitishwa na Ibn Taymiyyah, hairuhusiwi kwa mwenye kuingia msikitini kwa ajili ya kuswali aazimie kufanya i‟tikāf katika wakati wa kukaa kwake hapo (msikitini).

MAMBO YANAYORUHUSIWA WAKATI WA I‟TIKĀF

Kuondoka Msikitini Kwa Haja

Inaruhusiwa kwa mwenye kufanya i‟tikāf kuondoka msikitini ili akidhi haja yake, kama vile kwenda kukidhi haja (chooni), au kuoga josho la kulazimika. Anaruhusiwa pia kutoa kichwa chake nje au sehemu ya kiwiliwili chake nje ya mipaka ya msikiti bila ya kubatilisha i‟tikāf

yake. Amesema „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ):

“Wakati Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alipokuwa msikitini kwenye i‟tikāf,

alikuwa akileta kichwa chake (nje ya Msikiti) ndani ya chumba changu (pambizoni mwa Msikiti), ili nipate kumchana [na kumuosha] nywele zake. Baina yetu palikuwa na kizingiti cha mlango tu, nami nilikuwa kwenye ada yangu ya mwezi. Wakati

1 Al-Bukhārī na Muslim.

Page 183: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

165

alipokuwa akifanya i‟tikāf yake, hakuwa akiingia ndani ya nyumba (kikamilifu) isipokuwa kwa dharura ya ki-binadamu.”1

Kutawadha Ndani Ya Msikiti

Inaruhusiwa kwa aliye kwenye i‟tikāf atawadhe ndani ya msikiti2. Mtu

aliyekuwa akimtumikia Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alisema:

“Mtume ( يه وسلمصىل اهلل عل ) alitawadha wudhū‟ mwepesi ndani ya

msikiti.”3

Kusimamisha Hema Ndani Ya Msikiti

Aliye kwenye i‟tikāf anaruhusiwa asimamishe hema dogo nyuma ya msikiti apate kujipumzisha na kufanya ibādah zake kwa faragha4.

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alimtaka „Ā‟ishah (رضي اهلل عنها) amsimamishie hema

la ngozi pindi alipokuwa kwenye i‟tikāf5. Vilevile Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

alifanya i‟tikāf chini ya kivuli cha mkeka na busati lenye kuziba mlango wake.6

1 Al-Bukhārī, Muslim, Ibn Abī Shaybah na Ahmad.

2 Utambue yakwamba hili haliwezekani kwenye misikiti mengi ya kisasa, kwa sababu

yamejengewa kwa marumaru na mazulia, kinyume cha msikiti wa Mtume ( عليه اهلل صىل

.uliokuwa na sakafu ya mawe na ardhi kavu (وسلم3 Imepokewa na al-Bayhaqī kwa isnād nzuri na Ahmad kwa isnād iliyo swahīh.

4 Kama ilivyo kwenye tanabuhi ya hapo juu, vilevile hili haliwezekani kwenye misikiti

mengi yetu ya leo, kwa sababu ya jinsi yalivyojengwa. Lakini hatahivyo, mtu anaweza kujihifadhia kipembe mâlum cha msikiti atakapotumia wakati wake mwingi katika I’tikāf. 5 Al-Bukhārī na Muslim.

6 Muslim na Ibn Khuzaymah.

Page 184: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

166

Kutumia Godoro

Mu‟takif anaweza kujiwekea godoro au jamvi kwenye kipembe cha

msikiti kwa ajili ya kujilaza. Ibn „Umar (رضي اهلل عنه) amesimulia

yakwamba alipokuwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akifanya i‟tikāf, alikuwa

akiwekewa godoro au kitanda nyuma ya nguzo ya at-Tawbah.1

MAMBO YASIYORUHUSIWA WAKATI WA I‟TIKĀF

Kuondoka Msikitini Pasi Na Haja

Kama ilivyoashiriwa hapo juu, kuondoka msikitini pasi na haja

kunakhalifu msingi wa ufafanuzi wa i‟tikāf, na jinsi Mtume ( صىل اهلل عليه :alivyoifanya. Kwahivyo, inaibatilisha; Amesema Ibn Hazm (وسلم

“Wanavyuoni wameafikiana yakwamba mu‟takif yoyote anayetoka msikitini pasi na haja, dharura, au kitendo chema kilicho waajib, basi i‟tikāf yake inabatilika.”2

Kuingiliana Kimapenzi

I‟tikāf hubatilika kwa kujamiiyana (kimapenzi), kama alivyosema

Allāh (سبحانه وتعاىل):

“Wala msichanganyike nao (musiwaingilie), na hali mnakaa Itikafu misikitini.”3

1 Imepokewa na Ibn Mājah na al-Bayhaqī. Isnād yake ni hasan (Sifatu Sawm in-Nabī).

2 Marātib ul-Ijmā’ (Uk. 48)

3 Al-Baqarah 2:187.

Page 185: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

167

Amesema Ibn „Abbās ( عنه اهلل رضي ):

“Ikiwa mu‟takif ataingiliana na mkewe kimapenzi, ataibatilisha i‟tikāf yake, na itambidi aianze tena.”1

Hatahivyo, hakuna maandiko yaliyo swahīh yenye kuhitaji kaffārah makhsusi kwa mtu mwenye kubatilisha i‟tikāf yake namna hiyo.

Kujishughulisha Na Malimwengu

Kujishughulisha na mambo ya kilimwengu kunakhalifu uwezo wa kiroho na maana ya i‟tikāf , ambapo mtu anatakiwa ajitenge kando kwa niya ya kumuabudu Allāh peke yake bila ya kupata vipingamizi.

Mu‟takif mwenye kupoteza wakati wake kwenye mazungumzo ya upuzi na majadiliano, matusi na kulaani, au vitendo vyengine mfano wake, hupunguza na kuharibu malipo na thamani ya i‟tikāf yake. Amesema Ibn ul-Qayyim:

“Lengo la (adabu njema) hii ni kukamilisha madhumuni na niya nzuri ya kiroho ya i‟tikāf. Haya ni kinyume cha wanavyofanya wale watu wajinga, wanaofanya sehemu zao za i‟tikāf kuwa ni mahali pa mikutano ya kutembeleana, kupiga domo, na kusengenyana. Kwa hakika kufanya hivyo ni kinyume cha i‟tikāf ya ki-Utume.”2

I‟TIKĀF YA WANAWAKE

Inaruhusiwa kwa mwanamke kumtembelea mumewe akiwa kwenye i‟tikāf, na kwake kumshindikiza mpaka kwenye mlango wa msikiti.

Amesema Swafiyyah ( عنها اهلل رضي ):

1 Ibn Abī Shaybah na ‘Abd ur-Razzāq kwa silisili iliyo swahīh ya wapokezi.

2 Zād ul-Ma’ād.

Page 186: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

168

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alikuwa akifanya i‟tikāf Msikitini katika siku

kumi za mwisho za Ramadhān. Katika usiku mmoja nilikwenda kumtembelea. Alikuwa na baadhi ya wake zake, na wakaondoka muda mchache baadae. Nilizungumza nae kwa muda kidogo, kisha nikasimama ili nirudi zangu nyumbani; akaniambia, <Hebu subiri, niache nikushindikize.> Na akatembea na mimi (hadi kwenye makaazi yangu kwenye nyumba ya Usāmah Bin Zayd). Tulipofika katika mlango wa Msikiti ulio karibu na mlango wa nyumba ya Umm Salamah, watu wawili kutoka katika kabila la

Answār wakapita pambizoni; walipomuona Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

wakaanza kukaza mwendo; na Mtume ( ,akawaita ( اهلل عليه وسلمصىل

<Hebu punguzeni mwendo! Huyu ni mke wangu Swafiyyah Bint Huyayy.> Wakamjibu, “Subhānallāh (Ametakasika Allāh)! Yaa

Rasūlallāh1!” Basi Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akasema:

<Sheitwān anasambaa ndani ya mwili wa mwanadamu kama damu inavyosambaa ndani ya mishipa. Nilikhofia asije akawanong‟oneza maovu kwenye nyoyo zenu.>”2

Hata inaruhusiwa pia kwa mwanamke afanye i‟tikāf na mumewe, au

yeye peke yake. „Ā‟ishah ( عنها اهلل رضي ) amesema:

“Mmojawapo wa wakeze Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) [katika riwaya

moja: Umm Salamah] alifanya naye i‟tikāf akiwa katika istihādhah ambapo alipo-ona athari nyekundu au manjano; na mara nyengine tulikuwa tukimuwekea kitasa chini yake alipokuwa akiswali.” 3

1 Walishangao yakuwa Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) angeliwatarajia wao wasije wakapitwa

na fikra zenye shaka kumuhusu yeye. 2 Al-Bukhārī, Muslim, Abū Dāwūd.

3 Imepokewa na al-Bukhārī na Sa’īd Bin Mansūr.

Page 187: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 8 I’tikāf

169

Vilevile alisema:

“Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) alifanya i‟tikāf katika siku kumi za mwisho

za Ramadhān mpaka Allāh alipomchukuwa; kisha wake zake wakafanya i‟tikāf baada yake.”1

Hii inathibitisha yakwamba wanawake wanaruhusiwa kufanya i‟tikāf. Lakini hatahivyo, jambo hili lina masharuti mawili:

1. Ruhusa ya kwanza kutoka kwa walī (msimamizi wake).

2. Kuwe na matumaini yakwamba mwanamke mwenye kufanya i‟tikāf msikitini hatosababisha fitnah au khulwah (faragha) na wanaume.

Iwapo katika sharuti hizi mbili hazitowezekana, basi i‟tikāf haitoruhusiwa kwa mwanamke, kama msingi wa fiqh unavyodokeza:

“Kuondoa jambo ovu ni muhimu zaidi kuliko kufanya jambo zuri.”

1 al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

Page 188: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

170

MLANGO 9

KATIKA KUITIMIZA SWALA KIKAMILIFU

UNYENYEKEVU KATIKA SWALA

RIWAYA ZITOKAZO KWA MTUME NA MA-SALAF

Muislamu anahitajika wakati wowote ajitahidi kuwa ni kielelezo kizuri cha mu‟min aliye mwema: mtwi‟ifu kwa Mola wake, na mwenye kujifungamanisha na Sunnah za Mtume wake. Hii ni hukmu ya ujumla, yenye kustahiki kutumika kwenye swala ya qiyām vilevile. Katika

suala hili, amesema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Yoyote mwenye kusimama katika swala wakati wa Ramadhān kwa Imān na matarajio (ya malipo kutoka kwa Allāh), atasamehewa madhambi yake yote yaliyopita.”1

Mapema katika kitabu hiki, tumeyajadili maelezo mengi kuhusiana na

qiyām cha Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) katika wakati wa Ramadhān, pamoja

na nyakati nyengine. Tumeelezea jinsi swala yake ilivyokuwa ndefu mno yenye unyenyekevu, kama ilivoyokuja katika riwaya ya „Ā‟ishah:

“... Alikuwa akiswali rak‟āt nne, na wala usiulize kuhusu uzuri wake na jinsi zilivyokuwa ndefu ...”

1 Imepokewa na al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

Page 189: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

171

Na riwaya yake:

“Alibaki kwenye sujūd kwa kiasi cha muda wa mmoja wenu kusoma āyāt hamsini.”

Na riwaya ya Hudhayfah:

“... kisha akasoma al-Baqarah (katika rak‟ah ya kwanza); kisha aka-rukū‟; na rukū‟ yake ilikuwa ni yenye kufanana (kwa muda) na kisimamo chake ...”

Kisha Hudhayfah akaelezea kisimamo kirefu cha Mtume baada ya rukū‟ na sujūd yake ndefu baada ya hapo.

Zaidi ya hayo, katika zama za „Umar, Salaf walikuwa wakisoma vipande virefu vya Qur‟ān katika swala za Tarawêh.Wakati „Umar alipowakusanya wasomaji kwa mashauri na kuwaamrisha wawaongoze watu kwenye swala ya Tarawêh, ndipo akawaamrisha wasomaji wa haraka wasome āyāt thalathini, na wa kati na kati wasome āyāt ishirini na tano, na wasomaji wa taratibu wasome āyāt ishirini.”1

Kwahiyo walikuwa wakisoma kiyasi cha āyāt mia tatu – mpaka ikawabidi baadhi ya watu waliokuwa nyuma yao wajiegemeze kwenye fimbo (bakora) zao kwa sababu ya muda mrefu wa swala. Na hawakumaliza swala zao mpaka ulipokurubia wakati wa fajr.

Jumla ya hayo, walikuwa wakizifanya sehemu mbalimbali za swala zifanane kwa urefu na usomaji. Walikuwa wakifanya rukū‟ na sujūd ndefu, wakisoma ndani yake sampuli mbalimbali za dhikr na du‟ā‟, kulingana na Sunnah.2

1 Imepokewa na Ibn Abī Shaybah (2:89:2) na al-Faryābī (2:76) kwa isnād iliyo swahīh.

2 Kwa maelezo zaidi kuhusiana na haya, angalia katika Sifatu Salāt in-Nabī cha al-

Albānī.

Page 190: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

172

Jambo hili linapasa kututia sisi moyo tupate kuliiga kwenye swala zetu kiyasi cha uwezo wetu, kuifanya kuwa ndefu, na kusoma tasbīh kwa wingi („subhānallāh – kutakasika ni Kwake Allāh) na dhikr wakati wa rukū‟, sujūd na katikati yake. Kwa hayo, tunatarajia kujipatia, angalau, baadhi ya khushū‟ (unyenyekevu), ambayo ndiyo roho na kiini cha swala.

UNYENYEKEVU ULIOPOTEA

Wengi wa Waislamu wamekata tamaa na khushū‟ katika swala za qiyām, katika kubadilishana na upindanifu wao wa kuswali rak‟āt

ishirini, walizozinasibisha kimakosa kwa „Umar ( عنه اهلل رضي ). Wao

wamejishughulisha sana na kuidumisha idadi hii kuliko kuwa na khushū‟ na umakinifu katika swala!

Twawaona ma-Imām wengi wakifupisha visomo katika Tarawêh kwa kiyasi cha kwamba huwa hawasomi chochote baada ya al-Fātihah. Na hata kwa hiyo al-Fātihah yenyewe, wanaisoma kwa haraka, mpaka wakaipotezea uzuri na utamu wake. Katika kutafuta kwao haraka, vilevile wanaisoma kwa pumzi moja, kinyume cha

yaliyothubutu kutoka kwa Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) yakwamba alikuwa na

mazoweya ya kuisoma āyah moja baada ya nyengine.

Na ukiona miongoni mwa ma-Imām hao baadhi wanaosoma ndefu kidogo, utawakuta wakiendelea kuzipuuza Sunnah za kuzifanya sehemu tafauti za swala zilingane na urefu wa kisomo, kama ilivyo kwenye hadīth ya Hudhayfah iliyotangulia. Wote husoma kama kudona kwa Jogoo, au gea na mashini zikipanda na kushuka kwa njia za ki-ufundi, wakishindwa kuzingatia au kutafakari katika maneno ya

Allāh ( وتعاىل سبحانه ) wanayosikiya. Hata ikawa ni vigumu kwa mtu

kuwafuatilia pasi na uzito mkubwa sana!

Waandishi wengi wanaoshughulika na madda ya Tarawêh hata hawajaribu kuzivuta tanabuhi za Waislamu kunako umuhimu wa khushū‟, kana kwamba ni suala lisilohusika. Wamepindana kuelekeza

Page 191: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

173

juhudi zao katika kuthibitisha rak‟āt ishirini, bila ya kujali jinsi zinavyotekelezwa, na kiwango cha mkuruba na swala ya Mtume.

MITAZAMO YA MUANGAZA

Sisi hatutaki kupuuza, hatahivyo, idadi inayo ongezeka ya waandishi na ma-Imām waliotambua mtazamo wa kushtua ambapo jinsi swala ya Tarawêh inavyotekelezwa kwa kawaida, hapohapo wakaregea kuziswali rak‟āt kumi na moja kwa utulivu na khushū‟- twamuomba

Allāh ( وتعاىل سبحانه ) awazidishe idadi zao, na awape thabāt katika

uongofu, kushikamana na Sunnah, na uvumilivu katika kuihuisha.

HADĪTH ZINAZOHUSIANA NA KUIMARIKA KWA SWALA

Katika yafuatayo, tumedondoa idadi ya hadīth zilizo swahīh za kuwalingania Waislamu watekeleze swala kwa njia nzuri, na kuwatahadharisha na kupuuza hayo. Kwa haya, twataraji kuwakumbusha wasomaji kuhusu umuhimu wa kuimarisha swala zao zote kikamilifu –fardh na nafl, qiyām au nyengineyo.

1. Amepokea Abū Hurairah:

“Mtu mmoja aliingia msikitini akaswali wakati Mtume ( صىل اهلل عليه alipokuwa amekaa kwenye kipembe cha msikiti. Baada ya (وسلم

kumaliza, mtu huyo akenda kwa Mtume ( ليه وسلمصىل اهلل ع ) akampa

Salām. Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) akamjibu: “Wa „alayk as-Salām; rudi

ukaswali, kwa sababu bado wewe hujaswali!.” Basi huyo jamaa

akarudi, akaswali, kisha akarudi na kumpa tena Salām Mtume ( صىل) Mtume .(اهلل عليه وسلم وسلم عليه اهلل صىل ) akamjibu: “Wa „alayk as-Salām;

rudi ukaswali, kwa sababu bado wewe hujaswali.” [Jambo hili likarudia kwa mara tatu]. Baada ya mara ya tatu, yule jamaa

Page 192: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

174

akasema, “Mimi sijui kuswali vizuri, kwahivyo nifundishe, Ewe

Mjumbe wa Allāh.” Mtume ( وسلم صىل اهلل عليه ) akamwambia:

“unapotia niya ya kuswali,

Tawadha kikamilifu;

Kisha uelekee Qiblah (maelekeo ya Makkah), useme

„Allāhu Akbar‟, na usome kiyasi uwezacho cha Qur‟ān; kisha u-rukū‟ mpaka upate utulivu katika ku-rukū‟;

Kisha inua kichwa chako mpaka usimame wima;

Kisha u-sujudu mpaka upate utulivu katika ku-sujudu;

Kisha keti mpaka ustawi katika kuketi;

Kisha u-sujudu mpaka upate utulivu katika ku-sujudu;

Kisha usimame mpaka uwe wima katika kusimama kwako;

Kisha ufanye tena kama hivyo ulivyofanya katika swala yako iliyobaki.”1

2. Amepokea Abū Mas‟ūd al-Badrī ( عنه اهلل رضي ) yakwamba amesema

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Hakubaliwi mtu swala yake mpaka asimamishe uti wake wa mgongo wakati wa ku-rukū‟ na ku-sujudu.”2

3. Amepokea Abū Hurairah ( عنه اهلل رضي ) yakwamba amesema Mtume

:(صىل اهلل عليه وسلم)

1 Imepokewa na al-Bukhārī, Muslim na wengineo.

2 Imepokewa na Abū Dāwūd, an-Nasā’ī, at-Tirmidhī, Ibn Mājah, ad-Dārimī, at-

Twahāwī (al-Mushkal 1:80), at-Twayālisī, Ahmad, ad-Dāraqunī’ aliyesema, isnād yake imethubutu na swahīh. Hakika, ni kama alivyosema kwa sababu al-A’mash (mmojawapo wa wapokezi) alibainisha kusikiya (kutoka kwa mpokezi aliye juu yake)), kama ilivyo kwenye riwaya ya at-Twayālisī.

Page 193: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

175

“Mwivi aliye muovu zaidi miongoni mwa watu ni yule mwenye kuiba kutoka katika swala yake.”

Aliulizwa, “Ataibaje mtu kutoka katika swala yake, Ewe Mjumbe wa Allāh?” Akajibu, “Kwa kutotimiza rukū‟ na Sujūd.”1

4. Viongozi wa jeshi la Waislamu, „Amr Bin al-„Ās, Khalid Bin al-

Walīd, Sharhabīl Bin Hasanah, na Yazīd Bin Abī Sufyān ( اهلل رضي alimuona (صىل اهلل عليه وسلم) wote wamepokea yakwamba Mtume ,(عنهم

mtu ambaye hakuwa akikamilisha rukū‟ zake, na alikuwa akidona

katika sujūd alipokuwa akiswali. Akasema Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ):

“Lau mtu huyu atakufa katika hali hii aliyonayo, basi atakufa katika Dini isiyokuwa ya Muhammad – anadona katika swala yake kama kunguru anavyodona damu! Mfano wa asiyekamilisha rukū‟ na anayedona kwenye sujūd yake ni kama wa mtu mwenye njaa, akala tende moja au mbili zisizotosheleza njaa yake kwa uchache wake..”2

5. Talq Bin „Alī ( عنه اهلل رضي ) amepokea yakwamba Mtume (صىل اهلل عليه وسلم)

amesema:

1 Imepokewa na al-Hākim anayeizingatia kuwa ni swahīh, na adh-Dhahabi

akakubaliana nae. Inaye shahidi aliyepokewa na al-Hākim kutoka kwa Abū Qatādah

( عنه اهلل رضي ), na shahidi mwengine aliyepokewa na Mālik kutoka kwa Nu’mān Bin

Murrah, mwenye isnād iliyo swahīh, ingawa ni mursal; vilevile inaye shahidi

mwengine wa tatu aliyepokewa na at-Twayālisī kutoka kwa Abū Sa’īd al-Khudhrī ( رضي

عنه اهلل ), iliyoswahihishwa na as-Suyūti katika Tanwīr ul-Hawālik. 2 Imepokewa na al-Ājirī (katika al-Arba’īn) na al-Bayhaqī. Isnād yake ni hasan. Vilevile

amesema al-Mundhirī, “Imepokewa na at-Twabarānī (katika al-Kabīr) na Abū Ya’lā kwa isnād iliyo hasan, na pia Ibn Khuzaymah kwenye swahīh yake.

Page 194: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

176

“Kwa hakika Allāh ( وتعاىل سبحانه ) haiangalii swala ya mtu ambaye

asiye unyo-osha uti wake wa mgongo baina ya rukū‟ na sujūd.”1

6. „Ammār Bin Yāsir (رضي اهلل عنه) alisema yakwamba alimsikiya Mtume

:akisema (صىل اهلل عليه وسلم)

“Hakika mja ataswali swala ambayo, haandikiwi chochote (kutokana na Swala hiyo) isipokuwa „Ushur (1/10), tus‟u (1/9), thumun (1/8), subū‟ (1/7), sudus (1/6), khumus (1/5), rubu‟ (1/4), thuluth (1/3) au nusu yake (1/2).2

Maana ya hadīth hii, “Malipo ya watu hutafautiana kulingana na khushū‟ zao, unyenyekevu, na adabu nyengine zinazofuatana na ukamilishaji wa swala.”3

7. „Abdullāh Bin ash-Shikh-Khīr ( عنه اهلل رضي ) amesema:

“Nilimjia Mtume ( وسلم عليه اهلل صىل ) pindi alipokuwa akiswali, na

kifua chake kilikuwa kikitoa sauti ya mvumo kama ile ya chungu kinachochemka (kutokana na kilio).”4

1 Imepokewa na Ahmad, at-Twabarānī (katika al-Kabīr), na adh-Dhiyā’ ul-Maqdisi

(katika al-Mukhtārah); isnād yake ni swahīh. Vilevile ina shahidi katika al-Musnad na wapokezi wanaokubalika, ikahukumiwa kuwa swahīh na al-Hāfidh al-Irāqī katika takhrīj ul-Ihyā’, na al-Mundhiri akasema yakwamba isnād yake ni nzuri. 2 Imepokewa na Abū Dāwūd, al-Baihaqī na Ahmad kwa silisili mbili tafauti, ambazo

mojawapo imehukumiwa kuwa swahīh na al-Hāfidh al-Irāqī. Vilevile imepokewa na Ibn Hibbān katika swahīh yake, kama ilivyodokezwa kwenye at-Targhīb. 3 Fayd ul-Qadīr cha al-Manāwī.

4 Imepokewa na Abū Dāwūd, an-Nasā’ī, al-Baihaqī na Ahmad, kwa isnād iliyo swahīh

inayopatana na sharuti za Muslim. Vilevile imepokewa na Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbān kwenye swahīh zao, kama ilivyoelezwa katika at-Targhīb.

Page 195: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

177

HATIMA

Hadīth hizi tukufu zinahusu swala zote kwa ujumla, ziwapo ni za fardh au za nafl, na ziwapo ni swala za usiku au mchana. Wanavyuoni wameangazia haya kuhusiana na swala za Tarawêh khususan; kwahiyo amesema an-Nawawī:

“Mpangilio halisi wa utekelezaji wa Tarawêh unafanana na yaliyofafanuliwa hapo awali kwa swala nyenginezo; adhkār zote zilizotangulia zinahusiana nazo, kama vile du‟ā‟ za ufunguzi na nyenginezo, ukamilishaji wa tashahhud na du‟ā‟ zenye kuifuata, na mengine yaliyowahi kudokezwa. Hata kama hili laonyesha kuwa ni jambo lililo wazi na maarufu, mimi naligusia hapa kwa sababu watu wengi hudharau na kupuuza sehemu kubwa za dhikr wakati wa Tarawêh. Na ukweli ni yaliyokwisha elezwa hapa.”1

Al-„Āmirī amesema;

Suala husika zaidi hapa linalohitaji mazingatio ni kwamba idadi kubwa ya ma-Imām wenye kuwaongoza watu kwenye swala za Tarawêh wamejizoelea kwenye mfumo wa kufupisha usomaji, na kukatiza sehemu mbalimbali, na kuziepuka dhikr. Wamesema wanavyuoni, „Mfumo wa utekelezaji wake ni sawa na ule wa swala nyengine kulingana na masharuti, mitindo mbalimbali, na dhikr zote, kama vile du‟ā‟ za ufunguzi, dhikr za katika kila sehemu, du‟ā‟ baada ya tashahhud n.k [na kadhaalika].‟

Baadhi ya ma-Imām hao vilevile wanajaribu kuzisoma āyāt zenye kutaja Rehma za Allāh, wakikisiya visomo vyao ili wapate ku-rukū‟ pindi wanapozifikiya [āyāt hizo]; na kwa kufanya hivyo huwa wameziepuka adabu muhimu sampuli mbili za usomaji wa Qur‟ān wakati wa swala: Mara nyengine huwa wanaifanya rak‟ah ya pili kuwa ndefu kuliko ya kwanza; na husimama (au hukoma) baina ya āyāt zenye mafungamano ki-maana.

1 Al-Adhkār; mlango unaohusu “Adhkār za swala ya Tarāwīh.”

Page 196: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 9 Katika Kuitimiza Swala Kikamilifu

178

Sababu ya haya yote ni kwamba Sunnah zimetupiliwa mbali, zikawa zimefutika sehemu kubwa sana, kiyasi cha kwamba sasa mwenye kujifungamanisha nazo huzingatiwa kuwa ni mjinga na watu wengi kwa sababu ya kukhitilafiana na wengi; hii imesababishwa na kusambaa kwa uovu katika zama zetu, kama

alivyosema Mtume (صىل اهلل عليه وسلم):

“Kiyama hakitowasili mpaka (kabla ya hapo) la sawa litakapokuwa ni kosa, na kosa kuwa la sawa.”1

Kwahiyo hakikisha kujifungamanisha na Sunnah: ilazimishe kutoka kwako wewe binafsi, na uwaamrishe nayo wale wenye kukutwi‟i wewe. Kwa kufanya hivyo, utaokoka, uhifadhike na ufurahike. Mheshimiwa, mwanachuoni al-Fudhayl Bin „Iyyādh

( اهلل رحمه ) amesema: “Usijione mnyonge katika njia ya uongofu kwa

sababu ya uchache wa wasafiri wake; na usitiwe khofu na maangamivu ya makundi ya watu‟.”2

1 Maana hizi zinaonekana kwenye hadīth nyingi, imepokewa na at-Twabarānī katika

al-Awsat. Abū Nu’aym katika al-Hilyah, Ibn Waddāh, Ibn Mājah na wengineo. Bâdhi ya riwaya zimehukumiwa kuwa ni swahīh na al-‘Asqalānī, al-Haythamī na wengineo. 2 Karibu na mwishoni mwa kitabu cha al-‘Amirī, “Bahjat ul-Mahāfil wa-Bughyat ul-

Amāthil fī Talkhīs is-Siyari wal-mu’jizāti wash-shamā’il.”

Page 197: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 10 Kwa Mukhtasari

179

MLANGO 10

MUKHTASARI

Majadiliano katika kitabu hiki yamerefuka kupita matarajio yetu. Hili ni jambo lililokosa uwezo wa kuepukika, kwa sababu limeshurutishwa na mtazamo wa sawa wa kitaalamu. Kwa ajili hii, tumeamua kuwaletea wasomaji wetu tunaowathamini kwa mukhtasari katika mlango huu, utakaorahisisha kumbukumbu ya upesi na matumizi yake – in shā‟a „Llāh.

NUKTA MUHIMU

1. Kuswali Tarawêh Kwa Jamā‟ah Ni Sunnah

Kuswali Tarawêh kwa jamā‟ah ni Sunnah na wala si bid‟ah.

Mtume ( سلمصىل اهلل عليه و ) aliiswali kwa jamā‟ah katika nyusiku

nyingi; na sababu ya kuwacha kuendelea kuiswali kwa jamā‟ah ilikuwa ni kwa sababu tu ya baadhi ya watu miongoni mwa Ummah wake huwenda wakadhani yakwamba ni swala ya wājib lau kama angeliendeleza kuiswali bila ya kukosa. Khofu

hii ilimalizika kwa kukamilika kwa sharī‟ah pale Mtume ( صىل اهلل .alipoaga duniya (عليه وسلم

2. Idadi Ya Sawa Katika Sunnah Ni Kumi Na Moja

Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) aliswali rak‟āt kumi na moja za Tarawêh.

Hadīth yenye madai yakwamba aliswali Tarawêh ishirini ni dha‟īf sana.

Page 198: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 10 Kwa Mukhtasari

180

Hairuhusiwi kuswali zaidi ya rak‟āt kumi na moja, kwa sababu jambo hilo linakwenda kinyume na mafundisho yake na amri zake, “Swalini kama mulivyoniona mimi nikiswali.” Kwa sababu ya haya, hairuhusiwi kuiongezea Sunnah ya fajr au nyenginezo, kitu chochote.

3. Maoni Yetu Juu Ya Wale Wanaopinga

Kwa wenye kuswali zaidi ya rak‟āt kumi na moja za Tarawêh, sisi hatuwazingatii kuwa ni wazushi wala wapotofu – iwapo misimamo yao ni matokeo ya kukosekana kwa ubainifu wa Sunnah kwao, na wala si kwa sababu wamefuata matamanio ya nafsi zao.

4. Sunnah Ni Bora Kuliko Nyongeza

Hata kama mtu atakiri yakwamba inaruhusiwa kuongezea kwenye idadi ya Tarawêh, hapana shaka yakwamba ni bora

kujifungamanisha na idadi ambayo aliyoiswali Mtume ( صىل اهلل عليه kwa sababu alisema, “Uongofu ulio bora ni ule wa ,(وسلم

Muhammad.”

5. „Umar Aliihuisha Sunnah

„Umar (رضي اهلل عنه) hakuzua katika swala ya Tarawêh; bali aliihuisha

Sunnah ya kuiswali kwa jamā‟ah; na akadumisha idadi ya rak‟āt zake kulingana na Sunnah. Kila kilichopokewa tafauti kutoka kwake si swahīh katika silisili zake zote; na silisili hizo ni kiasi cha kwamba hazitiliani nguvu zenyewe kwa zenyewe.

6. Maswahaba Hawakuswali Ishirini

Haikuthibitishwa yakuwa swahaba yoyote aliswali Tarawêh, rak‟āt ishirini. Kwahivyo, inampasa mtu ajifungamanishe na idadi ya rak‟āt zilizothibitishwa katika Sunnah na kuthibitishwa na

„Umar (رضي اهلل عنه), Mtume (صىل اهلل عليه وسلم) ametuamrisha sisi kufuata

Sunnah zake na Sunnah za Khulafā‟ waongofu.

7. Hakuna Ruhusa Kwa Kuongeza

Page 199: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 10 Kwa Mukhtasari

181

Hata kama tutachukulia yakwamba imeswihi kupokewa kuongezea kwenye idadi ya sawa ya rak‟āt kutoka kwa baadhi ya Maswahaba (ambapo hali si hiyo), itatubidi kuzingatia yakwamba ilikuwa ni kwa ruhusa makhsusi ambayo leo hii haipo tena.

8. Wanavyuoni Wapinga Nyongeza

Kuswali zaidi ya kumi na moja kumepingwa na Mālik, Ibn al-„Arabī na wanavyuoni wengine wengi. Zaidi ya hayo, hakuna ijmā‟ kabisa (muafaka) kwa rak‟āt ishirini miongoni mwa Maswahaba wala wanavyuoni wakubwa.

9. Msimamo Kutoka Kwa Wanavyuoni Wakubwa

Kukataa rak‟āt za nyongeza haimaanishi kuwakataa wanavyuoni mashuhuri walioziruhusu. Kutokubaliana nao katika suala hili haimaanishi, kwa hali yoyote, kuwatweza na kudharau „ilmu zao na ufahamu wao.

10. Kupoteza Unyenyekevu

Katika kusisitiza nyongeza juu ya idadi zilizopokewa kumewasababisha watu kuswali kwa mtindo wa haraka haraka, kupoteza khushū‟ na, kwa mara nyingi, usahihishaji wa swala.

11. Kuswali Kwa Uchache Kuliko Kumi Na Moja

Hata kama hairuhusiwi kuswali zaidi ya rak‟āt kumi na moja, inaruhusiwa kuswali chache kuliko hizo, kushuka chini mpaka kiyasi cha rak‟ah moja. Hii imethibitishwa katika Sunnah na mwenendo wa Salaf.

12. Sampuli Mbali Mbali Za Kuswali Qiyām

Sampuli mbali mbali ambazo Mtume ( وسلمصىل اهلل عليه ) alizoswali

qiyām na witr, zote zinaruhusiwa. Mfumo bora ni kuswali rak‟āt kumi na moja kwa kisomo kirefu, kutoa taslīm mwisho wa kila jozi moja ya rak‟āt.

Page 200: لـــيللا مايـــق - qssea.net · kwenye mizani yake ya siku ya Qiyâma, malipo mema, kwa hima aliyonipa na juhudi mpaka kuhakikisha yakwamba Chapa ya kitabu hiki imetoka

Mlango 10 Kwa Mukhtasari

182

MWISHO KABISA

Yafuatayo ni maneno ambayo kwayo Sheikh al-Albānī alihitimisha kitabu chake Swalāt ut-Tarawêh:

“Hii ndiyo hatima ya yale ambayo Allāh ( وتعاىل سبحانه ) aliyoniwezesha

katika ukusanyaji juu ya madda ya swala ya Tarawêh. Lau kama

nimepata, basi ni kutokana na Baraka za Allāh ( وتعاىل سبحانه ), ambaye

Ndiye mwenye Utukufu wote na Ukarimu. Na kama ni uwezekano mwengine, basi nawaswihi kila mmoja atakayekuta kosa

anionyeshe; na Allāh ( وتعاىل سبحانه ) atamlipa wema.

Kutukuka ni kwako, Yâ Allāh; kila Sifa njema zinakustahiki Wewe; Mimi nashuhudia yakwamba hapana mola wa haki isipokuwa Wewe; Mimi nakuomba msamaha; na natubia kwako.

Namuomba Allāh amfikilizie swala zake na amani, Mtume aliyekuwa hajui kusoma wala kuandika, na Ahli zake wote na Maswahaba. Na hatima ya mwito wetu ni, al-hamdu li „Llahi rabb il-„ālamīn...