annuur 1208

20
Uk. 17 Magufuli akomeshe uhuni katika siasa! Walioshindwa Zanzibar wakae pembeni Vinginevyo ni aibu kwa nchi. Atakwama KKK waunda kikosi kuchinja Waislamu RAIS John Magufuli. PROF. Ibrahim Lipumba. PROF. Kitila Mkumbo. HAWA wapo katika swala ya Ijumaa. Msaada wako unahitajika. Soma Uk. 19 ISSN 0856 - 3861 Na. 1208 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , DESEMBA 18-24, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Soma Uk. 10 www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Wahafidhina munatupeleka wapi? Turejee katika msimamo wa Mzee Karume…

Upload: zanzibariyetu

Post on 15-Feb-2016

636 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1208

Uk. 17

Magufuli akomeshe uhuni katika siasa!

Walioshindwa Zanzibar wakae pembeniVinginevyo ni aibu kwa nchi. Atakwama

KKK waunda kikosi kuchinja Waislamu

RAIS John Magufuli.

PROF. Ibrahim Lipumba. PROF. Kitila Mkumbo.

HAWA wapo katika swala ya Ijumaa. Msaada wako unahitajika. Soma Uk. 19

ISSN 0856 - 3861 Na. 1208 RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA , DESEMBA 18-24, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

Soma Uk. 10

www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Wahafidhina munatupeleka wapi?

Turejee katika msimamo wa Mzee Karume…

Page 2: ANNUUR 1208

2 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Aal Imran: 97Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Fethullah-Gulen

“NA ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu k u i k u s u d i a n y u m b a mwenye kuweza njia ya kuiendea”. [Aali-Imran 97]

K i l a i b a d a inayotekelezwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ibada hiyo ni shukrani katika mkabala wa neema nyingi ambazo amezieneza juu yetu na huenda zikawa ni mkabala wa vitendo kwa neema hizo kwa kiwango fulani mkabala ambao haupatikani isipokuwa katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili yake. Ni hivyo hivyo ibada ya Hijja, ibada hiyo ni shukrani katika mkabala

wa neema ya uzima wa mwili na neema ya mali ambayo imetolewa. Kwa msingi huo, anasema yule anayenuia kuhiji: “Nina hiji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” kwa sababu hiyo inasema Qur’an tukufu katika jambo hili: “Na haki ya Mwenyezi Mungu juu ya watu”. Na (Lam) katika tamko “ALLAH” ni ya kustahiki. Ama herufi ALA katika ALA-NNA si herufi hiyo ni ya kulazimisha ama LAM ya kuarifisha katika tamko ANNAS hiyo ni ya Ahadi. Ni kama hivyo ulikuwa mwanzo kwa kuutumia msemo ‘ALA – NNAS’ ni namna ya ufasaha ya kuanza maneno, na kuashiria yale yatakayofuatia katika vifungo maana: hakika, t amko “ALA-NNAS” linaashiria kwa baadhi ya watu ni k inanani watu hao? Hao ni wale ambao wamekamilika kwao gharama za njiani na chakula na uwezo wa kusafiri, kwa kuongezea kupatikana mahramu kwa upande wa wanawake.

Ni kutokana na kutaja kwetu herufi ya Jarri

“ALA” katika aya “ALA-NNAS” kwa undani huu: Hija ni ibada ngumu sana kuliko swala na kuliko swaumu kwa kuongezea taabu ya safari mtalazimika kutoa kiwango kikubwa cha mali na mnaacha kazi zenu, mnakuwa mbali na nchi zenu na jamaa zenu na kadhalika. Herufi ya Jarri “ALA” ambayo inatumiwa na Qur’an inaashir ia kwa mbal i kwenye haya mashaka maalumu kwa sababu ya Hijja katika ujumla wa faradhi nyingine.

Zaidi ya hayo kwa hakika “Uwezo” una maana ya kuitekeleza amri kwa radhi ya moyo na kwa njia ya kunyenyekea na kufuata, kwa njia iliyo nzuri na bora sana na hilo linafungamana na kutaka uwezo, uwezekano, maana ni kwamba uweza umetumiwa hapa na hali pa sehemu zake ambazo ni nguvu, uwezo, uwezekano na ulikuwa upana wa maana ya tamko hili ndilo chimbuko na sababu ya kutofautiana tafsiri mbele z a M a i m a m u we n ye kujitahidi na sababu ya wepesi na upana.

Jee Unajua?

MASUALA1.Mtaje Shahidi wa mwanzo katika Uislamu. Jawabu: Sumaya2.Sahaba aliokuwa na jina la Rum/Roman. Jawabu: Sohaib3.Makabila mawili Mtume (SAW) aliwakuta Madina wakiwa kwenye

ugomvi mkubwa akawasuluhisha. Jawabu: Khazraj, Aws4.Masahaba wawili watoto wao waliolewa na Mtume (SAW). Jawabu:

Abubakar, Umar5.Kipando alichokipanda Mtume (SAW) alipokwenda Miraj. Jawabu:

Buraq6.Vitabu 4 vitakatifu walivyoteremshiwa Mitume. Jawabu: Injil, Zaboor,

Tawrat, Quran7.Aya ya kwanza kuteremshwa. Jawabu: Iqra8.Muadhini wa mwanzo katika Uislamu. Jawabu: Bilali9.Nyenzo ilio muhimu katika kutia Udhu. Jawabu: Maji10.Harufu 3 za mwanzo katika Suratul Baqara. Jawabu: Alif, Lam, Mim

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 30

CHEMSHA BONGO: 31Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA1.Mwaka aliozaliwa Mtume Muhammad (SAW).2.Mwaka aliohama Mtume Muhammad (SAW) kwenda Madina.3.Mwaka aliofariki Muhammad (SAW).4.Ukoo wa Mtume Muhammad (SAW) 5.Mamake Mtume Muhammad (SAW) alimpa jina gani? Mohammed, Adam, Abass.6.Muhammad (SAW) alivyokwenda Syria alifwatana na nani katika ukoo wake? Abu Talib, Abdul Mutalib, Abubakar.7.Kwanini Bibi KHadija alitaka aolewe na Mtume Muhammad (SAW) Uzuri, Uaminifu, Umaarufu.8.Majina aliokuwa akijulikana Mtume Muhamad (SAW. 9.Mtume Muhammad (SAW) kabla ya kupewa Utume akijitenga katika eneo gani?10.Idadi ya Waislamu wa mwanzo kusilimu walikuwa wangapi?

BAADHI ya Masheikh wakiwa katika picha ya pamoja katika Kongamano lililozungumzia Athari za ugaidi katika jamii kongamano hilo liliandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Misri cha Jijini Dar es Salaam lililofanyika katika ukumbi wa Msikiti wa Hudhaifa Bin Al- Yamani mkoani Tanga mwishoni mwa wiki.

Kongamano lililozungumzia Athari za ugaidi, Tanga

1.Mito 10 ilio mirefu zaidi Afrika ni Mto wa Nile ndio mto ulio mrefu katika bara la Africa ukiwa na masafa ya urefu wa Kilomita 6,853, ukifwatiwa na mto Congo, mto Niger, White Nile, Zambezi, mto Orange, Kasai, Luluaba, mto Senegal: http://www.afrikanfacts.com/top-10-longest-river-in-africa/3/

2.Mlima ulio mrefu koliko yote duniani ni mlima Andes : https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_longest_mountain_chains_in_the_world

3.Ziwa lilo na kina kirefu duniani ni Caspian Sea – 371,000 km2 (143,000 sq mi) : http://10mosttoday.com/10-largest-lakes-in-the-world/

4.Uwanja wa ndege ulio na harakati nyingi duniani : Hartsfield–Jackson Atlanta International Airport: https://en.wikipedia.org/wiki/List_of_the_world%27s_busiest_airports_by_passenger_traffic

5.Bandari ya mizigo inayoongoza kuwa na harakati nyingi duniani ni badari ya Shanghai: https://en.wikipedia.org/wiki/World%27s_busiest_port

6.Nchi ya Malta ni nchi inayoongoza kuwa na watu wavivu, inakadiriwa asilimia 71.9 ni watu waliokua hawana harakati: http://www.forbes.com/pictures/eihg45gjhg/swaziland-4/

7.Mji uliokuwa na usafi wa hali ya juu kabisa duniani ni Singapore: http://ohtopten.com/top-10-cleanest-countries-world/

8.Nchi 7 ambazo zinatoa elimu ya Chuo Kikuu bure ni Brazil, Ujerumani, Finland, Ufaransa, Norway, Slovenia na Sweden: http://www.salon.com/2014/11/02/7_countries_where_college_is_free_partner/

9. Katika Afrika ya Mashariki nchi inayoongoza kuwa na matatizo ya akili ni: http://www.rightdiagnosis.com/m/mental_illness/stats-country.htm

S B A Q L A M Y M Z Q B K

U I L A A L I A U A U U H

M L I F A Q M S Z B R R A

A A F N M A S I A O A A Z

Y L B U N H A N M O N Q R

A I A N A A M S I R T I A

H I Q R A F N U L T A H J

A T A U R A T R I N J I L

W A B U B A K A R M A J I

S O H A I B U M A R Y A A

A L A M E E N 40 50 60 70 80 100 200

U A M I I F U S A H A B A I

A L S A D I Q U M A Y A A A

A B A S I M U A W I Y A U I

A W S K H A R J I H I J R A

P A N G O L A H I R A I S H

A L F A J R I S H A A S R I

B A N I H A S H I M H I S H

A M I N A B I N T W A H A B

570 A H M A D 576 635 632 621 767 555 622 435

Page 3: ANNUUR 1208

3 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Magufuli akomeshe uhuni katika siasa!HAKUNA mgogoro wa kisiasa Zanzibar, bali ni uhuni na ujanja ujanja usio na tija kwa nchi unafanyika.

Walioshindwa katika uchaguzi mkuu hawataki kuachia madaraka. Hilo ndio tatizo.

Hayo yamesemwa na Profesa Kitila Mkumbo pamoja Profesa Ibrahim Lipumba na kusisitiza kuwa ni jukumu la Rais Mheshimiwa John Pombe Maguful i kukomesha ujanja ujanja huo unao aibisha nchi.

Wakiongea mapema wiki hii katika kipindi kinachorushwa na Azam TV (TWO) wamesema kuwa, k i l ichofanyika Z a n z i b a r n a k a m a hakitatafutiwa utatuzi wa haraka, ni aibu kwa taifa na sio kwa Zanzibar pekee.

A i d h a w a k a s e m a kuwa Mheshimiwa Rais Magufuli kama hataingilia n a k u l e t a u f u m b u z i unaofaa, itamkwaza hata yeye kutekeleza yale aliyokusudia.

Hii ni kwa sababu hali ya Zanzibar ikiachwa kwa muda kama ilivyo hivi sasa au kuja na ufumbuzi ambao utazua mgogoro zaidi, itabidi Rais atumie muda mwingi kushugulika na mgogoro wa kujitakia Zanzibar.

Katika maelezo yake Profesa Mkumbo alisajili masikitiko yake kwamba maamuzi ya wananchi wa Zanzibar yanadharauliwa huku ikijulikana wazi kuwa nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi na hairudi nyuma.

A l i s i s i t i z a k u w a wananchi wana akil i , wanajua wanachokitaka na maamuzi yao ya kuchagua viongozi wanaowataka yaheshimiwe.

Prof. Mkumbo amesema kuwa inachofanya CCM ni kuleta ujanja ujanja na kukataa kuondoka baada ya kuwa imeshindwa kama ambavyo hivi sasa inafanya ujanja ujanja wa kuleta wapiga kura kutoka Zanzibar ili wasaidie katika chaguzi za kupata Meya katika Wilaya za Dar es Salaam, ambapo imezidiwa idadi ya Madiwani, wengi wakiwa ni wa upinzani.

Katika kulisemea hili Prof. Mkumbo akasema k u wa R a i s M a g u f u l i

Na Mwandishi Wetu a t a j i j e n g e a i m a n i kwa wananchi iwapo atakomesha ujanja ujanja huu wa CCM.

Kwa upande wake Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema kuwa hakuna s a b a b u ya k u r u d i wa uchaguzi kwa sababu kura zilipigwa, zikahesabiwa na matokeo ya majimbo mengi yakatolewa na Tume ya Jecha.

A k a s e m a , k a t i k a majimbo 23 yaliyosalia kutangazwa matokeo y a k e , m a j i m b o 1 4 yalishahakikiwa matokeo yake kutoka Majimboni ikisalia kutangazwa tu huku 9 yakiwa ndiyo hajahakikiwa.

A k a s e m a k u w a , ha ta hayo 9 ambayo hayajahakikiwa na Tume ya Jecha, matokeo yake yalishatolewa katika ngazi za Jimbo na washindi wa Uwakilishi kupewa vyeti vya ushindi kama ilivyokuwa kwa wabunge.

Ndio katika hali hiyo Prof. Lipumba akasema k u w a Z a n z i b a r n a Watanzania wanaonekana viroja na wenye kufanya mambo ya aibu.

Kwamba wapiga kura hao hao, wasimamizi hao hao, vituo hivyo hivyo, kura za Rais wa Jamhuri na Wabunge ziwe halali, lakini za Rais wa Zanzibar na Wawakilishi ziwe haramu.

Maprofesa hao, wasomi na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, wakitoka vyama t o f a u t i v y a k i s i a s a w a m e h i t i m i s h a k w a kusema kuwa hivi sasa Rais Magufuli ana nguvu ya kupendwa, lak in i itafika mahali (kama hata fanya kile wanachotarajia wananchi), nguvu hiyo itaondoka.

Kwa hivyo wakasisitiza k u wa k a m a ye ye n i msema kweli na mwamini katika demokrasia kama a n a v y o t a m b a , b a s i aikwamue Zanzibar kwa njia ya haki.

Na hakuna haki zaidi ya kuhakikisha kuwa aliyeshindwa anakubali k u s h i n d w a a s i w e king’ang’anizi kinyume na kura za wananchi.

P r o f e s a L i p u m b a akakomelea kwa kusema k u wa R a i s M a g u f u l i anajinadi kuwa ni “Msema kweli Mpenzi wa Mungu”, basi aonyeshe kuwa si katika wale wenye kusema wasiyotenda.

Na akifanya hivyo,

i t a m u i m a r i s h a n a k u j i j e n g e a h e s h m a Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

K i n y u m e c h a k e , akienda kwa msukumo w a w a h a f i d h i n a ‘ving’ang’anizi’ wasio

heshimu matakwa ya wananchi, hata agenda nyingine za “hapa kazi tu” zitakwama.

Habari

Mufti Zubeir awakosoa Masheikh wa BakwataNa Mwandishi Wetu

K I O N G O Z I WA w a Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mufti Abubakar Zuberi, a m e wa k o s o a b a a d h i ya M a s h e i k h a m b a o wameshindwa kuwajibika na kusema watu kama hao wanawatia Waislamu aibu.

Aidha Mufti Zuberi amewataka viongozi wa BAKWATA katika ngazi mbalimbali nchini, kubadili fikra na mienendo yao katika utendaji ili taasisi hiyo iweze kuwa dira kwa Waislamu wote.

Mufti Zubeir alieleza hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati akiwa katika mkakati wa kuanza safari ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu nchini na kujionea hali ya utendaji ya baraza hilo nchini.

Hata hivyo Mufti Sheikh Abubakar Zuberi alisema Bakwata ina sura mpya na malengo makuu ni kuwaunganisha Waislamu.

Alisisitiza kuwa, umoja wa Waislamu utawasaidia kuwa na nafasi muhimu katika masuala mengi ya

kitaifa.Aidha alisema Bakwata

itaanzisha kitengo cha m a s u a l a y a u c h u m i kitakachoongozwa na

wataalamu watakaokuwa na jukumu la kuiandaa jamii ya Kiislamu kushiriki barabara katika kukuza uchumi wa nchi.

MUFTI Sheikh Abubakar Zuberi.

PROFESA Kitila Mkumbo.

Page 4: ANNUUR 1208

4 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Tahariri/Habari

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

NECTA yadaiwa kukwamisha wahitimu wa Al-haramainWAHITIMU wa Shule ya Kiislamu ya Al-Haramain, kitengo cha dini, Jijini Dar es Salaam, wamedai kuwa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), linawakosesha fursa ya kujiunga na vyuo Vikuu vya ndani ya nchi.

W a n a f u n z i h a o wa m e b a i n i s h a h a y o k a t i k a m a h a f a l i ya o ya kuhitimu elimu ya Thanaw, kwa maana ya Upili (sekondari) kwa mwaka 2015, yaliyofanyika Jumapili ya wiki iliyopita Shuleni hapo, wakielezea baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, muhitimu Haroun Kondo Matambo, amesema NECTA ilikuwa ikitambua vyeti vyao lakini hali hiyo imebadilika katika miaka ya hivi karibuni.

“Uwepo wa urasimu katika Baraza la Mitihani kwa baadhi ya watendaji wake kwa kukataa kutoa ulinganishi, bila sababu za msingi kunawakosesha wanafunzi kujiunga na elimu ya juu ndani ya nchi.” Amesema Matambo.

“Katika mafanikio m a k u b w a n a y a kihistoria ni ile hatua ya kutambuliwa vyeti vya Al-Haramain kitengo cha Dini na kufanyiwa ulinganishi na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Kwa kuwa Shule hii inafundisha kwa kufuata mtaala wa Chuo Kikuu

cha Kiislamu Cha Madina, ambacho Ser ika l i ya Tanzania inakitambua”. Alisema.

M a t a m b o a l i s e m a hatua hiyo ya kukubalika kufanyia ulinganishi vyeti vya chuo hicho kulitoa fursa kwa wanafunzi wake kukubaliwa na kujiunga na elimu ya juu ndani ya nchi kupitia TCU.

Akifafanua alisema, mfano kati ya mwaka 2010 na 2012, mwanafunzi mmoja aliweza kujiunga na Chuo Kikuu cha St. John, na mwaka 2011, w a n a f u n z i w e n g i n e waliomba kujiunga na masomo ya elimu ya juu na walikubaliwa katika vyuo mbalimbali ndani ya nchi.

Alivitaja baadhi ya Vyuo ambavyo wanafunzi kutoka Shule hiyo ya dini waliweza kujiunga navyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro (MUM) pamoja na Chuo cha Ualimu cha C h u k wa n i k i l i c h o p o Zanzibar.

Mbali ya Vyuo hivyo V i k u u , p i a a l i s e m a w a n a f u n z i w e n g i n e kutoka katika shule yao wa m e we z a k u j i u n g a katika vyuo vya kwa ngazi ya Diploma na wamekuwa wakifanya vizuri tu.

Hata hivyo akasema N E C T A h i v i s a s a wamebadili utaratibu. Hawatambui vyeti vya Alharamaini kitengo cha Dini.

Kwa upande wake

Sheikh Twalib Ahmed, akiwanasihi wahitimu hao wa Thanawi, katika Shule hiyo ya Markazi Al-Haramain Islamiyah, Dar es Salaam, alisema kwa hatua hiyo wasidhani kuwa ndio wamemaliza elimu bali watambue kuwa wamepewa ufunguo ili waanze kufungua nyumba na waingie katika vyumba mbalimbali vya elimu.

“ M s i j e m k a d h a n i a hapo mlipo sasa tayari mmeshakuwa maulamaa, bali nyinyi mnaelekea kat ika huo uulamaa, ufunguo huo muutumie kuingia katika mlango wa tafsiri, hadithi, na nyanja mbalimbali za elimu.” Alisema Shkh Twalib.

Shkh Twalib, alisema k u f i k i a k i w a n g o walichohitimu wahitimu hao ni bahati kubwa kwa sababu Ulimwengu wa sasa ni kwamba, Usheikh u n a p e n d wa s a n a n a unatakiwa sana.

Akawataka kutumia njia sahihi za ufikisha ujumbe, kwa kuzingatia kuwa wao ni wasomi na wana elimu ya namna ya ufikishaji ujumbe.

Shule ya Al-Haramain kitengo cha Dini ni Shule i n a y o j i s h u g h u l i s h a na utoaji wa elimu ya mazingira na elimu ya dini ya Kiislamu kwa kiwango cha Thanaw.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1978, ikiwa na malengo ya kuandaa Walinganiaji, Makhatwib, Maimam na Walimu.

Na Bakari Mwakangwale

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dkt. Charles Msonde.

IJUMAA ijayo Desemba 2 5 , Wa k r i s t o k o t e duniani, kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea za kusherehekea sherehe zao za kidini, ni siku ya kuzaliwa Bwana wao Yesu Kristo.

K w a W a k r i s t u , u m e k a r i b i a w a k a t i wa kununua mt i wa Kr ismas i . kuupamba k wa m a d o i d o ye n ye kung’ara na kumetameta, utasimamishwa karibu na dirisha.

Maduka yanajazana wa n u n u z i wa k i s a k a z a w a d i n a w a t o t o wanasubiri kwa hamu kubwa zawadi ya Baba Krismasi Santa huku n y i m b o z a M a r r y Christmas zikishika kasi.

H a t a h i v y o y a p o maandiko ndani ya Biblia, “Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi y a k e , w a n a u p a m b a kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4).

W a k a t i W a k r i s t o wakiwa katika hekaheka za kusherehekea sikukuu yao, wapo baadhi ya Waislamu ambao kwa namna moja au nyingine wamepanga na kujiandaa barabara kusherekea sikukuu hii japo si yao.

Imepokelewa toka kwa Abu Said Al-Khudhriy (Ra) kwamba Mtume (Saw) amesema:

“Mtafuata nyendo za watu waliokuwa kabla yenu, kiganja kwa kiganja, mkono kwa mkono, hata wakiingia kwenye shimo la kenge mtawafuata. Tukasema: Ee Mjumbe wa Allah, ‘Je, Unamaanisha Mayahudi na Manaswara?’ Akasema: Kwani nani zaidi ya wao?” [Al-Bukhari na Muslim].

Tunakaribia kuingia mwaka mpya wa Kikristo (wa kalenda ya Papa Gregory ijulikanayo kama ‘Gregorian Calendar’),

Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu

n a k u n a Wa i s l a m u wengi wanaosherehekea mwaka huo mpya kama wanavyofanya Wakristo, jambo ambalo halimo katika mafundisho ya Kiislamu.

Imekuwa ni kawaida Waislamu kujiunga na wafanyakazi wenzao au marafiki zao au majirani zao na kusherehekea sherehe hizi na kuwa na tabia isiyoendana na mwendo na mafundisho ya dini yetu tukufu.

Hivyo tumeona n i m u h i m u t u wa t u m i e Waislamu ujumbe huu kwamba washikamane na yaliyoruhusiwa katika Dini yao huku wakiwaacha w a n a n c h i w e n z a o Wakristo nao wakifanya yao yaliyoruhusiwa na Dini yao.

Upendo, umoja na m s h i k a m a n o k a t i k a nch i hau jengwi kwa M k r i s t o k u f a n ya l a Kiislamu au Muislamu kufanya la Kikristo, bali kuheshimiana, kufanyiana insafu na kuvumiliana.

Tunafahamu kwamba wapo majirani, marafiki na jamaa zetu ambao wanahusika na sherehe hizi za Christmas na Mwaka mpya. Lakini Waislamu wana wajibu wa kujichunga kufanya mambo ya shirki wakati huu.

Katika siku hiyo, basi ni kama siku yoyote nyingine katika maisha yetu bila ya kuwa imehusishwa na lolote. Kama mfano ulivyo kwa watu wa Vitabu wasivyokuwa wakisherehekea wala kuzifanya siku zetu za Idd kuwa ni haswa (maalum) kwao.

La msingi ni kuchunga k u h e s h i m i a n a n a kuvumiliana katika tofauti za imani zetu.

Kanuni ya Uislamu ni “Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu.”

Page 5: ANNUUR 1208

5 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015Habari za Kimataifa

K I O N G O Z I w a u p i n z a n i w a Myanmar, Aung San Suu Kyi, Jumapili i l i y o p i t a a l i va a glovu na kuokota taka katika tarafa yake.

Majuzi Bi. Suu Kyi, aliwaomba wabunge wa chama chake waliochaguliwa hivi karibuni, waokote t a k a t a k a k a m a sehemu ya kampeni ya kufanya usafi nchini humo.

Chama cha Suu Kyi cha NLD kilishinda vit i vingi katika uchaguzi uliofanywa m w e z i u l i o p i t a nchini Myanmar.

Serikali ya sasa ya kijeshi nchini humo, i m e t e u a k a m a t i kusimamia shughuli y a k u k a b i d h i madaraka chama cha Bi Suu Kyi.

Aung San Suu Kyi aiga usafi wa Magufuli

Kiongozi wa upinzani wa Myanmar, Aung San Suu Kyi.

Uchafu ni tatizo l a t a i f a n c h i n i M ya n m a r , Ta i f a a m b a l o h a l i n a mfumo kamili wa kukusanya taka na kuzitupa.

Rais wa Tanzania J o s e p h P o m b e Magufuli, alitawala vichwa vya habari s e h e m u m b a l i d u n i a n i p a l e alipochukua jukumu la kutangaza siku ya uhuru kuwa ni siku ya kufanya usafi nchi nzima, ambapo siku hiyo yeye, Makamu wake Samia Suluhu Hassan na Waziri M k u u K a s s i m Majaliwa, walikuwa m f a n o k w a kuokota na kuzoata takataka jijini Dar n a k u wa o n g o z a w a t a n z a n i a k u s a f i s h a m i j i sehemu mbalimbali nchini.

RIPOTI iliyotolewa na kiongozi wa dini ya Kiislamu nchini Urusi, Sheikh Salam Taju Diin, imeeleza kuwa kwa kipindi chote cha utawala wa Rais wa Jamhuri ya Urusi Vladimir Putin, imejengwa Misikiti 7500 nchini humo.

H a l i i n a o n y e s h a kuwa katika muda wa utawala wa serikali ya Vl a d i m i r P u t i n nchini humo, wafuasi wa d in i tukufu ya Uislamu wamefanikiwa kujenga Misikiti mingi nchini humo, ambapo imefunguliwa Misikiti 7500 na kutumika rasmi katika taifa hilo.

K a t i k a i d a d i y a Misikiti hiyo, baadhi alianza kujengwa wakati wa zama za utawala wa Rais Mikhail Gorbachev na kufunguliwa katika

Misikiti 7,500 yajengwa Urusi

UJENZI wa Misikiti nchini Urusi.kipindi cha Rais wa sasa.

Ripoti hiyo imetolewa na kiongozi wa dini ya Kiislamu nchini humo S h e i k h I s l a m Ta j u Din, ambaye ni katika wanazuoni wakubwa wa nchi hiyo.

A i d h a b a a d a y a kubainisha ripoti hiyo

Sheikh Din alipinga vikali kuwepo fikira ya kigaidi katika Uislamu na mwisho akawataka Waislamu wa nchi hiyo kuungana na kuwa k i tu k imoja kat ika kupambana na vikundi vya kigaidi ikiwemo kile cha Daesh.

RAIA wa Saudi Arabia wameweka historia katika u c h a g u z i u l i o f a n y i k a nchini humo Jumamosi m w i s h o n i m w a w i k i iliyopita, ambapo kwa mara ya kwanza, mwanamke wa kwanza amechaguliwa kuwa mwakilishi katika uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi ya Saudia Arabia ilimtangaza Salma bint Hizab al-Oteibi, kuwa ameshinda uwakilishi na kuwa mwanamke wa kwanza mwakil ishi wa wilaya katika jimbo la Mecca.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanawake nchini Saudi Arabia kushiriki kugombea

Wanawake washinda uchaguzi Saudi ArabiaNi mara ya kwanza mwanamke kushiriki

na kupiga kura kat ika uchaguzi nchini humo.

Katika Uchaguzi huo wa kihistoria katika taifa hilo la kifalme uliofanyika siku ya Jumamosi Desemba 12, 2015, kwa mara ya kwanza wamechaguliwa Madiwani wanawake.

Karibu wanawake 13 wameshinda viti katika uchaguzi wa Baraza la Manispaa nchini Saudi Arabia.

Uchaguzi huo unakuwa wa kwanza wa wazi kwa wapiga kura na kuwepo wagombea wanawake.

Bi. Al-Oteibi aliwashinda wanaume saba na wanawake wengine wawili katika nafasi

hiyo mjini Madrakah karibu kilometa 150 Kaskazini mwa Makka.

Mitandao yenye uhusiano na serikali na mashirika ya habari ya kujitegemea yameashiria kuwa wananchi wa Saudi Arabia wamechagua karibu wanawake 17.

M a a f i s a wa S e r i k a l i walisema kuwa wanawake 130,000 wali j iandikisha kupiga kura, ikiwa ni sehemu moja kwa kumi ya wapiga kura wanaume.

Kulikuwa na wagombeaji zaidi ya 1,000 waliokuwa wakiwania viti mbalimbali katika uchaguzi huo.

I m e e l e z w a k u w a wa n a wa k e wa l i o k u wa wakigombea katika uchaguzi huo, walikuwa wakifanya kampeni zao huku wakiwa wamesimama nyuma ya pazia au wakati mwingine wakiwa wamewakilishwa na wanaume.

Wanawake kadhaa wa Saudi Arabia wamepongeza uchaguzi huo kama hatua muhimu kwa demokrasia nchini humo.

Hata h ivyo wengine wal i sema kuwa hauna umuhimu wowote kwa sababu bado maisha yao yana vizuizi vingi, kama vile kutoruhusiwa kuendesha magari.WANAWAKE wakipiga kura, Saudi Arabia.

Page 6: ANNUUR 1208

6 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015Hoja ya Juma Kilaghai

NYUKI ni mdudu mdhaifu sana. Nyuki akiwa

peke yake unaweza ukamnyanyasa unavyotaka. Amebeba mshale mmoja tu kama silaha na akishautumia, basi tena! Hata hivyo, nyuki wanaujua udhaifu wao, na hivyo ni mara chache mno kuwakuta wakiwa mmoja mmoja. Mara nyingi wanatembea na kufanya shughuli zao katika makundi makubwa yanayojumuisha nyuki malaki kadhaa au hata mamilioni.

Wanatambua kuwa nguvu iko kwenye wingi na mshikamano. Wanapokuwa kwenye makundi yao nyuki wanaweza kuwa mahasimu wa kutisha iwapo watachokozwa. Kundi moja la nyuki linaweza likasababisha watu wote mtaani kujifungia ndani!

Wanadamu tunapaswa kuuiga mfano huu wa nyuki. Nguvu ya pamoja ndiyo silaha pekee inayoweza kumhakikishia kila mmoja wetu maisha bora na ya uhakika. Kwa mfano wewe peke yako ukiwa na shilingi mia moja mfukoni utaifanyia nini? Ni vigumu kusema kwa uhakika kwa sababu, kwa thamani ya sasa ya shilingi yetu, shilingi mia ni kama haina kitu cha kununua. Je, mkiwa watu 1,000,000 na kila mmoja na shilingi mia yake? Mhh, sasa hapa ni hadithi tofauti. Mambo yanaanza kuonyesha sura nyingine. Yaani katika kundi la watu 1,000,000 kila mmoja akitoa shilingi 100, tayari kuna kitita cha shilingi milioni 100!

Tanzania inakisiwa kuwa na watu wazima 20,680,000. Tunaambiwa kuwa 36% ya hawa ni masikini sana, yaani watu 7,444,800. Hili ni kundi la watu wanaofanya kazi za vibarua, wachuuzi wa karanga, wachuuzi wa maji ya chupa barabarani, waokota chupa za plastiki zilizotumika, na kadhalika. Pamoja na umasikini wao wote hawa kila mmoja kila

Nguvu ya wingi (Strength in numbers) ndiyo silaha pekee ya wanyonge!Unamjua nyuki?

siku anaweza akachanga shilingi 100 kwenda kwenye kapu la pamoja na isimnyime usingizi. Yaani kundi hili kila siku linaweza kujichangia mtaji wa pamoja wa shilingi milioni 745! Hii ni kwa siku! Kwa mwaka ni shilingi milioni 745 x 365, sawa na shilingi bilioni 272! Wow!

Sasa hebu tuchukulie kwamba tunahitaji kuanzisha mfuko wa umoja ambao kazi yake itakuwa ni kukusanya hizi shilingi 100 za kila mmoja kila siku. Itachukua siku ngapi kuwasajili hawa watu 7,444,800 kuwa wanachama wa huu mfuko?

Tuchukulie kwamba wamepatikana waasisi 100 wa huu mfuko. Tuchukulie pia kwamba tumekubaliana kila mwanachama muasisi atafute wanachama wawili kila siku, na wale wanachama wapya nao kila mmoja atafute wanachama wapya wengine wawili kila siku.

Hii ina maana kwamba katika siku ya kwanza watapatikana wanachama 100 x 2, sawa na wanachama 200! Siku ya pili watapatikana wanachama 200 x 2, sawa na wanachama 400! Siku ya tatu wanachama 400 x 2 , sawa na wanachama 800! Siku ya tatu wanachama 800 x 2 sawa na wanachama 1,600! Siku ya nne wanachama 3,200! Siku ya tano wanachama 6,400! Siku ya sita wanachama

12,800! Siku ya saba wanachama 25,600! Siku ya saba wanachama 51,200! Siku ya nane wanachama 102,400! Siku ya tisa wanachama 204,800! Siku ya tisa wanachama 409,600! Siku ya kumi wanachama 819,200! Siku ya kumi na moja wanachama 1,638,400! Siku ya kumi na mbili wanachama 3,276,800! Siku ya kumi na tatu wanachama 6,553,600! Siku ya kumi na nne, wanachama 13,107,200!

Hata hivyo kwa kuwa lengo ni wanachama 7,444,800, ina maana kuwa siku ya kumi na nne kuna wanachama wengi tu watakuwa hawana watu wa kuwaingiza kwenye mfuko. Hebu fikiria ndani ya siku 14 tu, tayari watu 7,444,800! Haya ni maajabu ya kanuni moja ya hisabati inayoitwa GEOMETRIC PROGRESSION.

Ukweli ni kwamba katika hali ya kawaida ni vigumu sana kujenga mtandao ambao utajumuisha watu wote. Hata hivyo kwa kutumia kanuni hiyo ya hisabati tuliyoitaja hapo juu, ni rahisi kujenga mitandao inayoweza kuwa na wanachama mathalani 10,000 mpaka 100,000. Watu 10,000 wanaojichangia shilingi 100 kwa siku, ni sawa na shilingi 1,000,000.00 kila siku au shilingi 365,000,000.00 kwa mwaka. Hebu chukulia hawa watu 10,000 ni

jumuia inayoishi ndani ya kata fulani humu nchini na wanataka kujiletea maendeleo. Kwa mtaji wa shilingi 365,000,000 kwa mwaka, ndani ya miaka 10, bila shaka kata hii itakuwa imepata maendeleo ya kustaajabisha.

Je, tunaweza kujipanga?!

Dhana ya matumizi ya nguvu ya wingi katika kuondoa udhaifu wa mtu mmoja mmoja inaweza pia kutumika katika mazingira mengine. Tuchukulie kwa mfano tofauti iliyoko baina ya vijana wa Kiganda na wale wa Kitanzania katika masuala ya kijasiriamali.

Ukienda Kampala na miji mingine ya Uganda, ni jambo la kawaida kuingia kwenye duka na kukuta vijana watano au sita wote wanauza. Bila kudadisi unaweza ukadhani kuwa vijana hao ni waajiriwa tu, na mwenye mali hapo hayuko. Dhana yako hiyo itakuwa siyo sahihi hata kidogo. Ukweli ni kwamba wenye mali ndio hao walioko mbele yako na hawana 'BOSI' mwingine zaidi yao wenyewe.

Kimaumbile vijana wa Kiganda hawana tofauti yoyote na vijana wa Kibongo. Tofauti pekee iko katika jinsi makundi haya mawili yanavyofikiri. Vijana wa Kiganda wanaelewa kuwa ili kuweza kufanya biashara nzuri, ni lazima biashara zao ziwe katika yale maeneneo

yanayojulikana kama ya kibiashara (business districts). Tatizo la maeneo haya ni kwamba kodi za pango ziko juu sana. Na mara nyingi vijana hawa hawana uwezo wa kuzimudu wakiwa mmoja mmoja. Ili kuondoa kadhia hii wanakubaliana kuungana watano au sita na kupanga chumba cha biashara kwa pamoja. Wanakubaliana pia kukata leseni moja, na kuwa na faili moja la kulipia kodi ya mapato. Ambacho kila mtu anamiliki kivyake ni bidhaa zilizomo. Kwa makubaliano maalum wanakubaliana kugawana aina ya bidhaa za kuuza ili kusije kuwa na mkanganyiko. Kwa kutumia ujanja huu, vijana hawa wanafanya biashara kubwa huko katika maeneo murua kabisa ya kibiashara, huku wakiwa kwa pamoja wanatumia gharama ndogo.

Tofauti na vijana wa Kiganda, vijana wa Kibongo ni kila mtu kivyake. Ni mara chache sana kutembelea maeneo murua ya kibiashara na kukuta vijana wa kibongo wakiwa wamiliki wa biashara zilizomo zaidi ya kuwa ni waajiriwa. Kijana wa kibongo pale anapojijengea uwezo kidogo biashara yake inawekwa USWAHILINI kwa sababu kule anaweza kumudu gharama za pango peke yake na bado akabaki na mtaji wa kununulia bidhaa. Hata hivyo biashara hizi mara nyingi hazidumu (labda kama mhusika anajihusisha pia na kununua na kuuza mali za wizi), kwa sababu bei za USWAHILINI ziko chini, na pia wateja wa USWAHILINI hawafanyi manunuzi makubwa.

Vijana wa kibongo wanahitaji kubadili jinsi wanavyofikiri. Wanahitaji kujua kuwa ili waweze kufanya biashara katika maeneo ya jijini kati na kushindana na WAHINDI, ni lazima wajenge tabia ya kushirikiana. Wanahitaji kujifunza kwa Waganda!

(Kwa maoni, mawasiliano 0754 281 131)

Nyuki wakiwa katika sega lao.

Page 7: ANNUUR 1208

7 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015MAKALA

TUNAISHI katika ulimwengu ambao umegubikwa na

kila aina ya mazonge. Ulimwengu ambao mambo mengi ya kustaajabisha yanatokea kila uchao. Ulimwengu ambao propaganda, uwongo na mfanowe vinaonekana kama ndio njia pekee ya kufikia malengo mbali mbali. Ulimwengu wa Akhir Zaman (zama za mwisho).

Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo hazikuachwa nyuma katika masuala ya propaganda na uwongo. Mtaji huu umetumika vyema mno katika kipindi cha uchaguzi na wengi wanafahamu bila shaka. Lakini ifahamike kwamba, mambo haya hayafanyiki kwa bahati mbaya, bali kwa lengo maalum. Yanafanyika kwa bahati nzuri kabisa. Yanapofanyika haya, wapo wanaonufaika na wapo wanaodhulumiwa.

Katika gazeti la An-nuur toleo nambari 1205 la Novemba 27 hadi Desemba 03, 2015, ukurasa wa mwanzo kabisa lilisomeka: “Mtihani wa kwanza kwa Rais Magufuli”. Yakafuata maneno; dini sasa kufundishwa kama taaluma, yadaiwa ‘ibada’ hazijengi mshikamano, masheikh wasubiriwa kupitisha muswada. Maelezo ya kina yanapatikana ndani ya gazeti na natumai wengi wamefanikiwa kuyapitia kwa undani.

Kutokana na uzito na ukakasi wa habari hii, nikaamua nami niseme kidogo kwa kuwa tunatofautiana uwezo wa kufikiri na kuelewa mambo. Tuitizame kadhia hii kupitia makala ya mwandishi J. Mihangwa

Katika Gazeti la Raia Mwema toleo nambari 432 la Novemba 18-24, 2015, ukurasa wa 15, kichwa cha makala kinasomeka hivi: “Rais Magufuli, epuka viatu vya waliokutangulia utaharibikiwa”. Mwandishi wa makala hii anaitwa Joseph Mihangwa.

Mwandishi ameanza

Tuchague vya kurithi, siyo uwongo na propaganda!

RAIS John Magufuli.makala yake kwa kusema; ‘tumejionea na kuthibitisha wenyewe wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita, jinsi umma wa Kitanzania ulivyoonesha mori ya kutaka Mabadiliko kwa kuondokana na Mfumo wa sasa unaowafukarisha, mithili ya mfumo wa utawala wa Mfalme Louis wa XVI wa Ufaransa’. Mwandishi pia amegusia kwa uchache msukumo uliopo wa kutaka mabadiliko kupitia Katiba mpya ambayo itatokana na maoni ya wananchi wenyewe, Katiba ambayo ipo kwenye Rasimu ya Mapendekezo ya Jaji Joseph Sinde Warioba.

Lakini akaendelea kusema kwamba, endapo serikali ya sasa itapuuza ‘mihemko, hii, tuendako, amani itapata msukosuko mkubwa kwa kuzuka mapambano kati ya kikundi cha watawala wachache wanaojitajirisha kwa kujigawia fedha na mali za nchi pamoja na kutajirisha wawekezaji kutoka nje ya nchi, wanaovuna mali za nchi hii kama vile ni ‘shamba la bibi’, huku wananchi wakiendelea kufukarika kwa kufukarishwa na hao wachache.

Msingi mkuu na ambao ndio maudhui ya makala ya mwandishi huyu, kwamba kukosekana uadilifu kati ya serikali na makundi jamii ndio chimbuko la misukosuko, vurugu, kukosekana amani na mfano wa hayo. Kupendelewa kundi moja dhidi ya jingine ndiko kunakopelekea yote haya ya kukosekana amani. Watu kutaka mabadiliko, ni kwa sababu ya namna serikali inavyowafanyia. Lakini serikali iliyopo madarakani chini ya chama tawala CCM, haikutaka na pengine niseme haiko tayari kupokea mabadiliko haya. Nasema hivi kwa sababu msingi mkuu wa mabadiliko ni kwa kupitia Katiba Mpya ambapo CCM hawaitaki. Wameikataa!

Turejee maudhui ya Makala yetu, kuhusiana na pendekezo la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) katika ufundishaji wa somo la dini kama taaluma, kama njia ya kuleta upendo, amani na mshikamano. Wanachotaka kutuaminisha hapa ni kwamba, hakuna namna yoyote ile ya kuleta amani, utulivu, upendo na mshikamano

ila kwa kufanya hichi walichotuwekea mezani. Ni kama vile umefika nyumbani ukaambiwa chakula kimeisha imebaki tu ukoko, kama upo tayari kula nikutengee! TET sasa wametutengea ukoko! Lakini kwetu sisi Waislamu, bora hata huo ukoko! Sisi Waislamu ni kama tumetengewa machicha ya pombe!

Serikali yetu na watendaji wake wanataka kujifanya hawaelewi chanzo cha mpasuko uliopo nchini leo hii. Wanataka wananchi wake waamini kwamba, dini ndio chimbuko la matatizo ya uvunjifu wa amani, kukosekana upendo na mshikamano!!? Sasa ndugu yangu msomaji hebu safari na historia fupi ya Ufaransa ya kale uone kipi kilikuwa chanzo cha haya ambayo yanaogopewa na serikali yetu ya Tanzania.

Mwandishi, J. Mihangwa ameeleza kwa urefu kidogo sababu za mazonge tuliyonayo hapa kwetu hivi leo. Akaionya serikali ya sasa kuachana na ulaghai wa sasa wa kutaka kujenga tabaka la watu wenye mitaji na ubunifu kwa ulaghai wa “kubadilisha mazingira ya uzalishaji duni na kuwa uzalishaji maridhawa”. Sasa tuangalie mfumo katili wa Ufaransa ya kale ulivyoendeshwa na kuzua ghadhabu ya wananchi wakapindua serikali, tumithilishe na yale tunayoyashuhudia leo.

Wakati akichukua madaraka mwaka 1774, Mfalme wa Ufaransa, Louis wa XVI, alikuta nchi imetopea katika lindi la uozo kijamii na kiuchumi, kutokana na Uongozi mbovu wa Wafalme waliomtangulia. Kenneth Martin, katika kitabu chake kiitwacho, ‘French Liberal Thought in the Eighteenth Century’, anaielezea hali hiyo na hii tuliyomo kama ifuatavyo:

“Ni jamii iliyochakaa na kulika kwa kutu ya maovu na ufisadi; ni jamii iliyooza na kunuka kwa uozo, yenye migongano ya kitabaka, rushwa na uonevu, huku Taasisi

zikiporomoka na mawazo kinzani yakichipuka kama magugu kwenye shamba lenye rutuba lililotelekezwa”.

Ingawa orodha ndefu ya kero kwa wananchi, maarufu kama ‘cahiers’, ilikuwa imewasilishwa serikalini, Mfalme Louis hakuzifanyia kazi kero hizo, akaziba masikio na kundelea kula nchi na wateule wake, hadi hapo nguvu ya umma ilipomshukia.

Bunge lilikuwa la kitabaka, likiwakilisha matakwa ya walio nacho na matakwa ya Mfalme mwenye kauli isiyopingwa, aliyejiaminisha kuwa yeye ndiye alikuwa Ufaransa na Ufaransa ilikuwa ndio yeye.

Raia waligawanywa katika matabaka matatu yenye hadhi tofauti kisiasa, kijamii, kiuchumi na katika kutendewa haki. Tabaka la kwanza lilikuwa la Makasisi wa Kanisa [The Clergy], lililojumuisha Maaskofu, Maparoko, Mapadri na wengineo kama ilivyo hapa kwetu Tanzania. Wakati wengine wakinufaika na Memorandum of Understanding, wengine wametwezwa, kudhalilishwa, licha ya kuwa wanatozwa kodi.

Tabaka hili la kwanza halikutozwa kodi na ndio walikuwa wakimiliki ardhi huku wakipumua juu ya sheria.

Tabaka la pili lilikuwa la watu wenye nasaba bora [the nobility], ambao idadi yao ilikuwa ndogo isiyozidi watu milioni moja. Hili lilihusisha pia matajiri na lilihodhi nafasi ya ushawishi kanisani, serikalini na jeshi na siyo msikitini. Kila Askofu na kila Afisa wa Jeshi isipokuwa askari dhalili wa vikosi vya mizinga, alitoka katika tabaka hili. Kwa bahati “nzuri” pia hapakuwa na Sheikh, Imamu wala Ustadh kwenye tabaka hili la kibaguzi.

Mwandishi akafananisha tabaka la pili na kikundi kidogo cha matajiri, mafisadi walioteka mfumo wa serikali pamoja na uchumi wa nchi, na

Inaendelea Uk. 8

Page 8: ANNUUR 1208

8 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015Makala

Khabari ya Israel ‘Taifa teule’-4Na Khatibu J. Mziray

Tuchague vya kurithi, siyo uwongo na propaganda!Inatoka Uk. 7wameweza kupenyeza watu wao katika sehemu nyeti za utawala wa nchi kama vile Jeshi, Bunge na sehemu nyingine muhimu za serikali kuhakikisha kwamba utawala wa nchi unacheza kwa mdundo wa muziki wao. Mfumo huu, tunaweza kuumithilisha na Mfumo Kristo hapa kwetu Tanzania, ambapo wakristo ndio ambao wamehodhi sehemu nyeti serikalini.

Kama kweli Rais huyu anataka kuwatumikia Watanzania na asivae viatu hivi kama alivyosema mwandishi J. Mihangwa, basi na avunje mfumo kristo. Vinginevyo itakuwa ni kama danganya toto, kwa kuwa aliahidi kwenye kampeni kwamba hatakuwa mbaguzi.

Tabaka la tatu na la mwisho, lilikuwa la makabwela, lililojumuisha wakulima wadogo wadogo, wachuuzi, wafanyabiashara na wasomi wasio na ajira serikalini. Hawa hawakuwa na fursa ya kuyafikia matabaka mawili ya juu hadi kufa. Hawa ndio walioonja adha ya mfumo huo wa kidikteta wa Ufaransa

ya kale. Walitozwa kodi kubwa kwa kanisa iliyoitwa “the tithe”, kwa maana ya moja ya kumi ya kipato chao kiduchu. Walitozwa pia kodi ya ardhi, kodi ya kichwa, kodi ya mapato kwa ujumla, chumvi, kodi ya kusaga nafaka na zinginezo. Wakati haya yakifanyika, tabaka la kwanza na la pili halikutozwa kodi, na inapotokea mmojawao amefanya kosa basi hujichagulia Hakimu au Jaji wa kusikiliza kesi yake.

Tabaka hili linawafikiana zaidi na Waislamu nchini Tanzania kuliko hata hilo tabaka la pili. Tabaka la pili limechukua sehemu ndogo sana. Hali ya Waislamu nchini, madhila, udhalilishaji na mfano wa hayo yaliyowakuta na yanayoendelea kutokea yako wazi hatuna sababu ya kuyarudia. Kwa mtu mwenye akili salama, mwenye uwezo wa kufikiri atabaini tatizo la haya yanayotokea ya kukosekana amani, vurugu na mfano wa hayo.

Muislamu anaweza kukamatwa na kubambikiziwa kesi na kufanyiwa kila ubaya kama tunavyoona kwa Sheikh Ponda. Lakini

cha ajabu tukisema tunaonekana wakorofi, tunataka kuvunja amani! Matokeo ya kudai haki zetu tunapewa majina ya siasa kali, al-shabab, al-qaida n.k.

Kodi zote walizotozwa tabaka la mwisho, ziliishia kwenye mifuko ya watawala na wapambe wao; hivyo serikali ikalazimika kukopa kutoka nje. Mwandishi anamshauri Rais huyu, JPM asijaribu kamwe kuvaa viatu hivi walivyovaa watangulizi wake ataharibikiwa. Nami namuasa atekeleze ahadi ya kutokuwa mbaguzi. Kama Memorandum of Understanding itaendelea kuwepo, basi

na Waislamu nao wapate mgawo huo.

Wakati haya yakiendelea kufanyika nchini Ufaransa, kama yanavyotokea hapa kwetu leo, waandishi na wanafalsafa wa tabaka la tatu walisema, kuonya na kuandika mengi dhidi ya mfumo huo kandamizi na wa kihujuma. Francois Marie Arouet, maarufu kama “Voltaire” [1694-1778] aliandika kushambulia Ukabaila wa Kanisa. Ukilisema hili kwetu Tanzania utaambiwa unaleta uchochezi, utakamatwa, utawekwa ndani!

Moyo mgumu wa Mfalme Louis katika kuridhia maslahi mapana ya walio wengi kwa

kuruhusu mabadiliko haukumsaidia siku ya “kiyama” ilipowadia, Julai 1789; pale umma wa walala hoi wa Kifaransa, kwa kuchoshwa na “sikio la kufa”, ulipofanya mapinduzi kwa njia ya maandamano yaliyotikisa mitaa na Jiji la Paris, kisha kusambaa hadi vijijini. Magereza yalivunjwa, na wafungwa kufunguliwa, Ikulu [the bastille] ikavamiwa. Louis na mkewe wakajaribu kutoroka, lakini wakakamatwa mpakani mwa nchi kurejeshwa Paris na kunyongwa kwa usaliti wa Taifa.

Ni kazi ya serikali mpya iliyopo madarakani kuwabaini wachawi wa amani, vurugu ambao wanavunja umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi. Rais aliangalie hili kwa jicho pevu ili kuvunja ukabaila uliopo ndani ya nchi yetu hii. Atoe semina elekezi kwa TET katika namna ya kuwasaidia kufikiri vema zaidi kwa mustakbali mwema wa nchi yetu, na siyo kufundisha dini kama taaluma.

(Mwandhishi wa Makala hii ni msomaji wa siku nyingi wa An nuur-Juma Jumanne wa Katesh, Manyara. 0659 789 468.)

RAIS John Magufuli.

YAKOBO ajipatia mali kwa hila (uchawi). Hicho ni kichwa cha habari za jinsi Yakobo alivyomlaghai mkwewe, ambaye pia ni mjombaye, aliyeowa binti zake wawili, mtu na mdogo wake. Msomaji atasema ninamkashifu Yakobo, na hasa akijua kuwa mimi ni Muislamu, lakini kwa maneno hayo ya ‘ulozi’ nasema Astaghfirullah, Msamaha wa Allah uwe n a m i ; k w a n i Ya k o b o ninayemfahamu katika Uislamu, ameepukana na sifa zote mbaya na amekamilika na sifa zote nzuri. Lakini sikusema mimi, bali ni Biblia iliyoandikwa hayo. Inasema:

“Yakobo akatwaa fito za mlubna mbichi, na mlozi, na mwaramoni, akazibambua maganda, mistari myeupe ionekane ndani ya hizo

Yakobo ajipatia mali kwa hila (uchawi)fito. Akazisimamisha fito hizo alizozibambua katika mabirika ya kunyweshea maji, pale walipokuja wanyama wa n y w e ; wa k a c h u k u a mimba walipokuja kunywa. Wanyama wakapata mimba mbele ya hizo fito, wakazaa wanyama walio na milia, na madoadoa, na marakaraka.” (Mw. 30:37-39.)

Ulozi, ni uchawi, mlozi, ni mchawi, fimbo za mlozi, ni fimbo za mti unaotumika kwa kuchawia. Ndiyo maana miti hiyo mitatu ikichanganywa kwa pamoja ilizichawia-iliziloga zile kondoo, mbuzi na ng’ombe zikazaa ndama za mabaka n.k. Hiyo inamaana kuwa Yakobo alijua uchawi. Hata hivyo ukisoma habari hizo kuanzia Mw. 30:1-

43, utapata kisa kizima na vituko vyake; na jinsi watoto wa Labani yaani shemejie Yakobo, walivyo lalamika kutokana na huo ulaghai wa kimazingaumbwe wa Yakobo.

Lakini kwa imani ya wana wa Israeli na Wakristo, huo ni ufunuo, na hiyo ni sifa kwa wana wa Israeli. Ndiyo maana ukisoma Biblia ya Kiswahili cha Mvita ya mwaka wa 1937, inaanza kwa kichwa cha habari kisemacho: Werevu wa Yakobo wa kujipatia mali nyingi. Mw. 30:25.

Kuloga, kuroga, kuchawia, kunasifiwa kuwa ni werevu. H u y o n d i y e B a b u wa wana wa Israeli; ambaye sera za imani ya mila na dini inayotokana na yeye,

kwao haramu ni halali, na halali ni haramu, na ndio wanaoongoza sheria za dunia hii; na ndio washauri wakuu wa baba la vita duniani, na baba la ghilba na dhuluma na mauwaji duniani (Marekani).

Maisha ya Yakobo na majirani zakeKama tunavyoona, jinsi

wana wa Israeli walivyo, na wanavyokuwa mahodari wa kutengeneza matukio ya vita na mauaji, ndio urithi wa Yakobo (Israeli) mwenyewe alivyokuwa, na alivyowarithisha. Kuna imani iliyojengwa kwa waumini wa Kikristo na hata wasiokuwa wao, kuonesha ubaya wa Wafilisti, au wenyeji wa Kanaani, ambapo hao ndio watu wa asili kutokana na

maandishi ya Biblia: “Wana wa Hamu ni

Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani…Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori. Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi, na Myebusi , na Mwamori , na Mgirgashi, na Mhivi, na Mwarki, na Msini,….Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyika. Na mpaka wa Wakanaani ul ianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha. Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.” (Mw.10:6-20.)

“Yakobo a l ikuwa na binti yake, akiitwa Dina, akaenda kuona michezo ya Wakanaani, akakutana na mwana wa mfalme, aliyeitwa Shekemu mwana wa Hamori, Mhivi, akamchukua akalala

Inaendelea Uk. 13

Page 9: ANNUUR 1208

9 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015Makala

KUELEWA kinachotokea nchini Syria hivi sasa, inabidi uelewe mbinu na kinachowatuma Marekani na washirika wake wa NATO, nchi zinazofuata malengo sawia katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. Wakati watu wa nchi za Ulaya na Marekani wanalishwa propaganda mbichi kuhusu malengo ya kikanda yanayohusika, hali halisi ni tofauti kabisa.

Wakati propaganda inasema madikteta hapa na pale wameondolewa, au kuwa demokrasia ndiyo lengo, hakuna mojawapo kati ya hayo inayoendana na kinachotokea sasa au kilichotokea katika ukanda huo.

Kwa wanaoanza, tunafahamu wote kuwa kama maeneo ya kuchimba mafuta yasingekuwepo, nchi za Magharibi zisingejali chochote kuhusu kinachotokea katika eneo hilo.

Lakini makundi tofauti ya kimaslahi ya nchi za nje yanajali. Na malengo yao ni wazi ni pamoja na kukamata raslimali muhimu za nishati za eneo hilo. Kuna wasiwasi mkubwa kama Russia au China wanaweza badala yao wakaingia na kushikilia maeneo haya, ambayo ndiyo akiba muhimu zaidi ya mafuta duniani. Halafu, tunaweza kuachana na dhana kuwa Marekani na washirika wa NATO wana dhamira yoyote ya haki za binadamu katika suala hili. Kama wangekuwa wanajali, basi ingebidi wakubali kuwa mikakati yao na mbinu zao zimesababisha kuteseka kwa mamilioni ya watu, pamoja na kuweka mazingira ya watu wengi wengine kuingia katika majanga. Lakini itakuwa ujinga kujadili au kuelewa dhamira ya wanachofanya katika eneo hilo kwa darubini ya haki za binadamu au uhuru wa mtu binafsi -kwani hakuna kinachohusika hapa.

Mauaji na majanga Mashariki ya KatiNa Chris Martenson

Wagawe uwatawale

Sera zinazofuatwa katika eneo la Mashaiki ya Kati na Afrika Kaskazini, zina mizizi yake katika kugawa eneo hilo ili kulidhibiti kwa urahisi zaidi. Ni mbinu kongwe; kwanza ilitumiwa kwa kiwango kikubwa na Waingereza kuanzia miaka ya 1700. Gawa na kuteka: Kuna sababu ambayo ni kibwagizo cha karne nyingi.

Lakini kupata mashiko ya unyama unaohusika, nadhani inasaidia kutathmini kilichotokea Libya mwaka 2011 wakati NATO ilipomuondoa Muammar Gaddafi na kuiacha nchi ni gamba lililovunjika - kama ilivyotakiwa.

Siwezi kukupa sababu nzuri kwa NATO kushiriki katika kumwondoa Gaddafi. Ninazo sababu mbaya tu.

Sababu rasmi ilikuwa kwamba baada ya harakati za Uamsho wa kiangazi chepesi nchi za Kiarabu mapema mwaka 2011 (ambako kuna ushahidi mkubwa wa nchi za Magharibi kuchochea miali hiyo ya moto), mambo yaligeukia pabaya na waandamanaji wakapigwa risasi. Hii iliruhusu Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa inahitaji kuwalinda raia, na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa kumshtaki Gaddafi kwa jinai dhidi ya binadamu, ikisema anahitaji kusimamishwa

KIONGOZI wa zamani wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.

kizimbani. Hivi ndivyo

ilivyokuwa: Hapo 27 Juni, ICC (Mahakama ya Jinai ya Kimataifa) ilitoa hati za kukamatwa kwa Gaddafi, mwanae Seif al-Islam na mkwewe Abdullah Senussi aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa, kwa mashitaka yanayohusu jinai dhidi ya binadamu. Maofisa wa serikali ya Libya waliikataa ICC, wakidai kuwa "haina uhalali wowote" na kuainisha kuwa "shughuli zake zote zinalenga viongozi wa Kiafrika."

Mwezi huo, shirika la utetezi wa wafungwa wa kisiasa, Amnesty International lilichapisha taarifa ya uchunguzi wake, ambako lilisema tuhuma nyingi za uhalifu dhidi ya binadamu zilizoundwa dhidi ya majeshi ya Gaddafi zilikuwa hazina ushahidi wa kuaminika, na badala yake ni madai ya kutunga ya majeshi ya wapinzani ambayo yalichukuliwa na kukubalika kwa vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.

Baada ya kutolewa hati ya mashitaka ya ICC, ilikuwa ni mchezo wa kuruka na kuchupa hadi kufikia kutangazwa kwa eneo la kutorusha ndege chini ya amri ya NATO juu ya Libya kuwalinda raia.

Kutoka hapo ilikua ni mruko wa moja kwa moja hadi NATO kuelekezea mtutu chochote kinachohusiana

na serikali ya Gaddafi. NATO ilikuwa imechagua upande wake na ilikuwa inasaidia uasi moja kwa moja.

Mpangilio hapa ni ule ule nyakati zote: matukio yanayochaguliwa kwa kutengenezwa kwanza na kutumika kama kisingizio cha kuunga mkono upande unaotaka kuipindua serikali iliyopo hivyo kuacha jangwa la mifarakano ya kidhehebu kushamiri katika ombwe la utawala litakalotokea bila shaka yoyote.

Kama unafanana na watu walio wengi nchi za Magharibi, unajua kidogo sana au hujui kitu kuhusu masuala haya. Haifuatiliwi vizuri na vyombo vya habari. Na Libya haiko katika habari mara nyingi licha ya kuwa inapitia wakati mgumu.

Niligundua hotuba iliyotolewa na Gaddafi miezi michache kabla hajauawa nikaona ina mvuto wa kipekee na kufichua yaliyojificha. Nitaitoa kama ilivyo hapa. Nanukuu:

“Kwa miaka 40, au ni kitambo zaidi, siwezi kukumbuka, nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu nyumba, hospitali, mashile na wakati wakiwa na njaa, niliwapa chakula. Niliweza hata kubadili Benghazi kutoka jangwa hadi ukanda wa kilimo. Nilisimama dhidi ya mashambulio ya yule cowboy,

Reagan, pale alipomwua binti yangu wa kufikia, akijaribu

kuniua mimi, badala yake akamwua yule mtoto mdogo asiye na hatia. Halafu nikawasaidia ndugu zangu na dada zangu wa Afrika kwa fedha kwa ajili ya Umoja wa Afrika.

Nilifanya nilichoweza kuwasaidia watu kuelewa maana ya demokrasia halisi, ambako kamati za wananchi zinaendesha nchi yetu. Lakini hiyo haikuwahi kutosha, kama walivyoniambia baadhi, kwa vile ni wabinafsi walitaka zaidi. Waliiambia Wamarekani na wageni wengine, kuwa wanataka 'demokrasia' na 'uhuru' bila kujua kuwa ni mfumo wa kila mtu na lwake, ambako jibwa kubwa zaidi linawala waliobaki, lakini walikuwa wamelainishwa na maneno hayo, katu wasifahamu kuwa nchini Marekani hakuna dawa bure, hospitali bure, nyumba ya kuishi bure, elimu bure na chakula bure, ila pale watu wakipiga magoti au kwenda kuunda milolongo mirefu kupata supu.

Hapana, hata ningefanyaje, haikuwa inatosha katu kwa baadhi ya watu, lakini kwa wengine, walifahamu kuwa mimi ni mwana wa Gamal Abdel Nasser, kiongozi pekee wa Kiarabu na Kiislamu ambaye tumekuwa naye tangu Salahuddin, alipoutaka mfereji wa Suez kwa watu wake, kama nilivyoitaka Libya, kwa watu wangu, ilikuwa ni nyayo zake nilizojaribu kufuata, kuwaweka watu wangu huru na kudhibitiwa na wakoloni - kutoka kwa wezi ambao wangetuibia.

Sasa nashambuliwa na jeshi kubwa zaidi katika historia ya vita, mwanangu kijana wa Afrika, Obama anataka kuniua, kuuondoa uhuru wa nchi yetu, kuondoa ukazi bure katika nyumba, tiba bure, elimu bure, chakula bure, kubadilisha na kuweka wizi mtindo wa Marekani, unaoitwa 'ubepari,' lakini sisi sote katika nchi zinazoendelea tunajua maana yake

Inaendelea Uk. 15

Page 10: ANNUUR 1208

10 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

KKK wakisimika Msalaba.

WANACHAMA wa KKK na mavazi yao rasmi.

KKK akisoma maelekezo 'mwongozo wao' KLOBAN.

Makala

KU KLUX KLAN (KKK) kundi ambalo

limeuwa zaidi ya Wamarekani Weusi 2000, sasa limegeuzia hasira zake kwa Waislamu.

Kundi hilo katika Jimbo la Alabama limetoa ilani kuwa linaandaa kikosi cha kupambana na Waislamu likilenga kuzuiya Uislamu kuenea Marekani.

Katika kutafuta wanachama shujaa wa kufanya kazi hiyo, kundi hilo limesambaza vipeperushi vikitoa wito kwa walio tayari kujisajili.

“The KKK wants you! Help us fight the spread of Islam in our country. To join call the hot line or visit our website.”

Ndivyo unavyosomeka ujumbe katika vipeperushi ambavyo vimekuwa vikisambazwa katika mitaa na nyumba za watu.

Chuki dhidi ya Waislamu inaelezwa kuwa kubwa sana katika Marekani hasa baada ya matukio mawili ya hivi karibuni yaliyodaiwa kuwa ya kigaidi.

Matukio hayo ni lile la Paris, Ufaransa na San Bernardino, California Marekani.

Katika matukio yote mawili, ilidaiwa kuwa kuna watu waliuliwa na wauwaji ni wanaodaiwa kuwa magaidi wa IS (Waislamu).

Sambamba na tangazo hili la "the Klan" anayetarajiwa kuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican, Donald Trump anasema

KKK waunda kikosi kuchinja WaislamuNi baada ya marufuku ya Donald Matunda ya propaganza za chuki

Hata hivyo, hasira na chuki zilipelekwa pia kwa Wayahudi na Wakatoliki, hasa wahamiaji wapya.

Kufikia mwaka 2012 ilikisiwa kwamba KKK wana wanachama kati ya 5,000 na 8,000.

Katika harakati zao za kupinga haki sawa pamoja na Wamarekani Weusi, KKK walitumia njia ya vitisho na mauwaji, wakiuwa viongozi wa harakati za kupigania haki za Weusi.

Kwa upande mwingine, walikuwa wakiuwa watu Weusi tu bila ya sababu hata kama sio kiongozi.

Walilipua mabasi ya watoto wa shule na ‘kampasi’ za vyuo vikuu vyenye idadi kubwa ya watu Weusi hasa katika Majimbo na miji ya Pontiac, Michigan, Louisiana, Vanderbilt, Georgia, Mississippi, na Southern California.

Pamoja na mauwaji ya kikatili ambayo yamekuwa yakifanywa na KKK, lakini hata pale wanapokamatwa watuhumiwa na kesi kufikishwa mahakamani, hutolewa adhabu kidogo au hata watuhumiwa kuachiwa baada ya kuhukumiwa.

Mfano ni katika ‘Tennessee shooting’ ambapo mwaka 1980, wanachama watatu wa KKK waliwapiga risasi na kuwauwa wanawake wanne, Wamarekani Weusi Viola Ellison, Lela Evans, Opal Jackson na Katherine Johnson katika mji wa Chattanooga, Tennessee.

Wawili katika watuhumiwa, Bill Church na Larry Payne, waliachiwa wakati Marshall Thrash

Inaendelea Uk. 11

kuwa umefika wakati Waislamu kupigwa marufuku kuingia Marekani.

Trump anasema kuwa Waislamu wamekuwa ni watu hatari wenye chuki isiyo na sababu dhidi ya Wamarekani na kwamba inakuwa vigumu kumtofautisha ISIS na Muislamu wa kawaida.

"Until we are able to determine and understand this problem and the dangerous threat it

poses, our country cannot be the victims of horrendous attacks by people that believe only in Jihad and have no sense of reason or respect for human life."

Anasema mfanyabiashara billionea Donald Trump akidai kuwa Marekani haiwezi kukubali kuwa muhanga wa ‘mujahidina’ wenye chuki, wasiotumia akili wala kujali maisha ya binadamu.

Ku Klux Klan (KKK),

aka "the Klan", ni kundi la Wazungu wenye msimamo mkali wanaoamini katika ubora na utukufu wa Wazungu (white supremacy).

Kwa msimamo huo, wanataka Marekani isafishwe kutokana na ‘taka’ za Weusi, Wahindi, Waarabu na watu wengine wasio kuwa Wazungu.

Mwanzo wake ilikuwa kupinga harakati za kupinga utumwa na kuwapa haki watu Weusi.

Page 11: ANNUUR 1208

11 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 201511 AN-NUUR

Inatoka Uk. 10

KKK waunda kikosi kuchinja Waislamu

MWAKA mmoja uliopita waziri katika Mamlaka ya Palestina, Ziad Abu Ein, aliuawa na vikosi vya Israeli , kufuatia kipigo na kuvuta hewa chafu iliyosababishwa na mabomu ya machozi wakati wa maandamano katika eneo la Ukingo wa Magharibi nchini Palestina.

Abu Ein aliyekuwa na umri wa miaka 55, a l i k u w a a k i o n g o z a kundi la Wapalestina katika kupanda miti ya Mizeituni, karibu na kijiji cha Turmusayya Kaskazini Mashariki mwa mji wa Ramallah, alishambuliwa na askari wa Israeli na kupelekea kifo chake mnamo Desemba 10, 2014.

Abdullah Aburahmah ambae ni mwanaharakati wa kipalestina akiwa ni mmoja wa waandamanaji hao, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Abu Ein akaanguka baada ya kukosa fahamu, kufuatia afisa wa usalama wa Israeli kumpiga kwa kofia yake ya kujikinga ijulikanayo kwa jina la Helmet.

" Y a l i k u w a n i maandamano ya amani; askari wa Israel hawajui jinsi ya kukabiliana na hali kama hiyo,jambo lililowafanya kutumia

nguvu kututisha" alisema.Mashahidi wa tukio

hilo akiwemo mwandishi wa habari wa Israel na mpiga picha wa shirika la habari la Reuters , alisema Abu Ein alipigwa na wanajeshi wa Israeli wakati wa maandamano, huku wengine wakisema alipigwa kichwani na kuanguka.

Wakati wote huo wa hali tete, ulinzi uliimarishwa zaidi nchini Israeli na katika makazi ya walowezi wa kiisraeli nchini Palestina, h u k u m a a n d a m a n o yakiendelea katika ukingo wa Magharibi kwa wiki kadhaa.

Aidha Abu Ein, alikuwa ni baba wa watoto wanne na Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na ukuta wa kibaguzi na Makazi ya kilowezi nchini Palestina, vilevile aliwahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri wa Mambo ya wafungwa wa kipalestina.

Alihukumiwa kifungo cha maisha jela na Israeli mnamo mwaka 1982, lakini alitolewa katika zoezi la kubadilishana wafungwa mnamo mwaka 1 9 8 5 , h a t i m a e k u wa mwanachama wa Baraza la Mapinduzi la chama cha Fatah.

W a n a h a r a k a t i

waliokuwa pamoja Abu E in wal i sema kuwa. Walikuwa wakipanda miti ya mizeituni katika makazi haramu ya Adey, wakati ndipo maafisa wa jeshi la Israeli walipotu tushambulia kwa kiasi

kikubwa cha mabomu ya machozi.

R a i s wa Pa l e s t i n a Mahmoud Abbas amelaani vikali mauaji ya Abu Ein, na kukiita kuwa ni "kitendo cha kinyama ambacho hakiwezi kuvumiliwa",

huku akiishutumu Israeli kwa mauaji hayo ya waziri wake. Nae Mkuu wa Upatanishi wa Palestina ‘Saeb Erekat” amelaani kile alichokiita "mauaji."

Amesema Serikali ya Inaendelea Uk. 18

Makala

akitiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela miezi 8 (kwa kosa la kuuwa watu 4!!!).

Hata hivyo baada ya kukaa jela kwa miezi mitatu tu, aliachiwa huru!

Kutokana na malalamiko ya watu juu ya mwenendo huo wa kidhalimu na mahakama kutokujali haki za Weusi, mwaka 1982 mahakama ilipitisha hukumu kwamba itolewe fidia ya Dola 535,000 kwa wale wanawake waliouliwa.

Mwaka jana 2014 mwezi wa Aprili mwanachama mmoja wa KKK, Frazier Glenn

kuchoma moto msalaba mbele ya nyumba yao au katika eneo lenye kukaa watu ‘wasio wataka’.

Lakini inaelezwa pia kuwa KKK wakati mwingine wanatumia njia mbaya ya kuuwa kwa kuchoma moto.

Inakisiwa kwamba zaidi ya watu Weusi 400 wamechomwa moto wakiwa hai na KKK nchini Marekani

Sasa hawa ndio Ku Klux Klan aka “The Klan” ambao wametangaza kuwa sasa wanaandaa kikosi maalum cha kushughulika na Uislamu na Waislamu.(Habari na Mashirika ya Habari ya Kimataifa)

WANACHAMA wapya wa KKK wakipata Darsa.Cross, akijulikana pia kwa jila la Glenn Miller alifyatua risasi katika kituo kimoja cha Wayahudi Kansasi City na kuuwa watu watatu.

Hata hivyo, hutasikia

washambuliaji na wauwaji hawa wa KKK wakipachikwa ugaidi.

Katika tukio hilo la Kansasi polisi walisema kuwa hilo ni kosa la jinai inayotokana na

chuki (hate crime.)Inaelezwa kuwa

namna moja wanayotumia KKK kupeleka ujumbe wa kitisho kwa watu wanaowalenga, ni

Uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya Palestina

Page 12: ANNUUR 1208

12 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 201512 Safu ya Ben Rijal

Ijue Bunduki ya AK 47 na athari zake -2

MIKHAIL Kalashnikov mtengenezaji na mvumbuzi wa bunduki AK47.

Nani mbunifu wa AK-47 au tuite Kalashnikov?

BUNDUKI ya Kalashnikov au kwa jina jengine kwa ufupi huitwa AK-47 ni bunduki ilio mjarab na ndio bunduki inayotumiwa sehemu nyingi duniani kutokana na ubora wake. Wengi hatujiulizi ni nani ambaye alibuni bunduki h i i n a s a b a b u g a n i zilizompelekea afanye hivyo?

A l i k u w a M i k h a i l Kalashnikov mwanajeshi wa Kirusi ambaye ndio alioiasisi bunduki hii, na kilichompelekea kuiunda b u n d u k i h i i n i k u l e kujeruhiwa kwake kwenye vita na kumpitikia kuwa aina ya bunduki ambayo jeshi la Urusi wanazozitumia ni dhaifu. Akiwa anauguza jereha la bega kutokana na risasi aliyopigwa, Mikhail K a l a s h n i k o v a l i k u wa akifikiria vipi ataweza

kuiunda bunduki hiyo, i l imchukuwa muda wa miaka 6 kuweza kufikia ukomo wa kuunda silaha hii.

Mikhail Kalashnikov alikuwa mwenye majuto siku zake za mwisho wa maisha yake ingawa mwanzo alijilabu kuwa wakulaumiwa ni wanasiasa lakini katika siku zake za mwisho wa maisha yake kabla ya kufariki alifika kunena yafwatayo “Wakati nikitengeneza silaha hiyo, lengo langu halikuwa kuua mtu, bali i l ikuwa kulinda taifa langu. Kama baadaye imeanza kutumiwa na magaidi kuua watu, hilo

halikuwa lengo langu.” I l ikuwa ki la s iku ya

Mungu anaposikia habari au anavyotizama habari huona mauaji katika sehemu mbalimbali za dunia ambayo mauaji hayo yamefanyika kutokana na matumzi ya AK-47.

"Hata hivyo, kusema ukweli ningefurahi zaidi kama ningeweza kubuni kifaa ambacho kingetumiwa na wakulima kwa namna ile ile ambayo AK 47 imetumika duniani kote. pengine kwa namna hiyo ningeisaidia zaidi dunia.” Alisema.

Kitu kimoja ambacho kinaipa ubora bunduki hii ni silaha unayoweza kuisafisha kwa muda mfupi kuliko silaha nyingi kwahio haihitaji gharama kubwa katika usafishaji na kuifanyia matengenezo.

Aliwahi kusikika mara mmoja Mikhail Kalashnikov akisema kuwa “AK 47 si silaha bora kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na kuwa ana imani ya kuwa ipo siku, itakuja silaha nyingine k u b wa k u l i k o h i y o . ” Unapoyasoma maneno na misemo mingi ambayo M i k h a i l K a l a s h n i k o v aliokuwa akiyatamka ni utaona alikuwa anajutia kwanini ametengeneza silaha hio.

Jee Mikhail Kalashnikov amefaidika na uvumbuzi wake?

Majaribio yake ya silaha hii , i l imtia maradhi ya uziwi pamoja na majirani waliokuwa wakiishi karibu naye. Uziwi ulimpa tabu na hakuwa anapendelea k u t u m i a c h o m b o c h a kumsaidia kusikia. Akiona b o r a u m s e m e s h e k wa kumsogelea karibu na shikio na kisha ukapiga makelele. Wajuzi kama hawa ndio huwa na mambo ya kiajabu ajabu. Uvumbuzi wake haukumtarajirisha zaidi ya kupewa tunzo za juu kwa

nchi yake.Bunduki iliyoua marais

wengiBunduki hii haikumwacha

wa l a k u m b a g u wa i we Rais au mwananchi wa kawaida kat ika kuleta athari zake. Katika mwaka wa 1 9 8 1 R a i s A n wa r Saadat akiwa anapokea gwaride la heshima, askari wa jeshi la Misri ambao wa k i f wa t a m i s i m a m o thabiti walichupa kwenye gari yao nakufika kwenye jukwaa na kummiminia risasi Rais Anwar Saadat na kufariki hapo hapo. Mwaka wa 1972 Kapteni wa Jeshi la Wananchi, Homoud Barwany naye aliitumia bunduki hii kumuua Rais wa mwanzo wa Zanzibar baada ya Mapinduz Abeid Amani Karumei. Aidha mwaka uliofwatia mwaka wa 1973 Rais wa Cape Verde, Amilcar Cabral naye alikuwa ni muhanga wa AK-47. Mwaka huo huo Rais wa Chile, Salvador Allende aliuwawa kwa bunduki ya AK-47.

Msomaji wa makala hii unamuhukumu vipi Mikhail Kalashnikov? Unaweza ukamwita shujaa au subiyani aliochangia na kuendelea kuchangia kupotea kwa roho nyingi za watu duniani aidha na kupatikana vilema wengi kutokana na matumizi ya bunduki alioiasisi?

SHEIKH Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy alizaliwa Barawa tarehe 15 Mfungo sita mwaka wa 1250 (1854) akafika Unguja akiwa kijana mdogo kabisa. Ingawa aliwasili visiwani humu akiwa ni kijana mdogo, lakini alikuwa ameshajifunza vitabu vingi vya dini na lugha ya Kiarabu na kuweza kuwa na maarifa mapana katika uga wa dini na lugha.

Huko alikotokea alijifunza kwa maulamaa wakubwa wa nyakati hizo katika maeneo ya Barawa akiwemo Syd Abubakar Mihdhar, Sheikh Haji Ali bin Abdulrahman. Aidha alisoma kwa Sheikh Ahmad Al-Madhriby. Inaelezwa kuwa Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy alikuwa ni kiongozi wa dhikiri yeye na Sheikh

Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija-8KATIKA makala ya mwanzo ya Masheikhe waliopita visiwani, nilimuandika Sheikh Muhydin bin Sheikh ambaye alikuwa mmoja kati ya wasomi wakubwa waliopata kukuwepo Zanzibar. Katika makala hii ya leo, nitawazungumzia wanafunzi wake wawili kati ya wanafunzi wake wengi aliowasomesha na kufanya kazi kubwa ya kueneza dini nao ni Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija.

Sahuri Al-Shirazi wa Donge. Masheikhe hawa wawili baada ya kuwa na wanafunzi wengi katika kuwafunza elimu ya dini, waliigeukia dhikiri na humu kwenye dhikiri wakitumia nafasi ya kusomesha Fiqhi. Alioweza kumshajiisha Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy kuivamia dhikri na kuzama alikuwa Syd Ahmad Al-Madhriby.

Baada ya kuondoka kwao Barawa na kuwasili Unguja, alifikia mikononi mwa Sheikh Muhydin bin Sheikh akasoma

hapo kwa muda mrefu na kuelimika vya kutosha. Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy inasemekana kuwa katika masuala ya Sheria na Hukumu za Kiislamu alikuwa gwiji na alikuwa mwenye kujuwa lipi ndilo na lipi alipeleke kwenye kiasi.

Alipofika umr wa miaka 16 Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy alikuwa ameshailimika vya kutosha na hapo Sheikh Muhydin alivyomuona kuwa umri wake ni mdogo lakini upeo wa elimu yake

ni mpan, akamchagua katika wanafunzi wake kumpeleka Kilwa kuongoza mas’ala ya dini. Watu wa Kilwa walimpokea na hawakuona wala kumjadili juu ya umri wake lakini walimkubali kutokana na uwezo wa elimu yake. Sheikh Abdul Aziz alikubalika vya kutosha na darsa zake zilikuwa kubwa na zikitajika hapo Kilwa.

Sheikh Abdul Aziz aliandika vitabu vingi lakini bahati mbaya vitabu vyake hivyo vyote havijulikani vimepotelea wapi, isipokuwa vitabu viwili kimoja kati ya hivyo kilikuwa na anuwani An Nawamisi-s-Samadaniya kikiwa ni kitabu cha Dua ambacho alikiandika mwaka wa 1280 AH (1863). Aidha kwa watoto wake kilipatikana kitabu cha Tawhidi alichokimaliza

kukiandika katika mwaka wa 1883. Kitabu hiki alikiita Ikdul-La-ali ambacho baadaye akakifanyia sherehe na kuita Sherehe hio jina la Takrib Ikdi La-ali. Inasemekana kuwa aliandika kitabu juu wa wafalme wa Kibusaidi wa Zanzibar na kilipata kuonekana na alikiandika kwa ufundi mkubwa kabisa nacho kitabu hicho hakijulikani kilipotelea wapi? Aidha kulikuwa na mijadala yake na Mapadri ambayo wengi walifaidika katika hoja zake alizokuwa anapambana na Mapdri. Bahati mbaya maandiko aliyoyafanya na kuwa kitabu nayo yamepotea.

Zanzibar ilibahatika kuwa na Mapadri 3 ambao waliisoma dini ya Kiislamu na kuielewa vya kutosha na ukitaka kupambana

Inaendelea Uk. 13

Page 13: ANNUUR 1208

13 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015Safu ya Ben Rijal

Sheikh Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy na Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija-8Inatoka Uk. 12nao ilikuwa sio rahisi. Mapadri hao walikuwa Bishop Tozer, Bishop Steere na Padre Dale. Kati ya hao wote Bishop Tozer akiwaadhibu sana Masheikhe ila alikuwa hapendi kukutana na Sheikh Abdul Aziz. Bishop Tozer aliwahi kusikika akisema kuwa “Wangekuwa Abdul Aziz bin Abdul Ghany Al-Amawy wachache katika kisiwa cha Zanzibar, kazi yetu ingekuwa haifanyiki.”

Dhikiri ilikuja ikamvaa akawa saa zote yeye na muridi na akiwasomesha Muridi zaidi ya Tasawuf na Tawhidi na wanafunzi wake walikuwa wakimfwata na kuwa naye kwa karibu. Wengine wanasema lau kama asingegeukia Dhikiri, basi Sheikh Abdul Aziz angeweza kupaa zaidi alivyopaa.

Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija

Sheikh Fadhil bin Ali Mngazija ni mzaliwa wa visiwa vya Ngazija na alipowasili Unguja hajasimama ila alifikia kwa Sheikh Muhydin bin Sheikh, na alikuwa mmoja kati ya wanafunzi waliokuwa wakisoma kwa jitihada ya hali ya juu na kutopoteza wakati wake bure. Alikuwa akisoma darasa za vijana wa hirimu yake na vilevile alikuwa akijumuika katika darasa za watu wazima. Natija ya juhudi zake zilimpelekea kwa kipindi kifupi kuonekana kama ni mwanachuoni aliobobea. Alipofariki Sheikhe wake alikuwa na darsa kubwa ambazo zikihudhuriwa na wengi wa wakaazi wa mjini Unguja na kuonekana Sheikh Muhydin kilichoondoka ni kiwiliwili chake lakini ilimu alioisomesha ilikuwa haikupotea.

Sheikh Fadhil alikuwa akisomesha darasa zake katika Msikiti Gofu na akikaa kando na Msikiti Gofu. Kwa hio saa zote yeye alikuwa na Msikiti na Msikiti kuwa na yeye kutokana na kuwa anaishi pembezoni

mwa Msikiti Gofu. Aliweza kuwavutia wale wanafunzi wa Sheikhe wake kuhamia katika darasa zake kati ya hao ni Syd Muhammad bin Ahmad bin Salim, Syd Ahmad bin Salim, Sheikh Abdalla bin Wazir ambaye naye alikuwa kati ya wasomi walioisoma Bibilia vya kutosha na akipenda kuendesha mijadala na Mapadri hata watu wakimstaajabu. Mapadri wa Kizungu walioletwa miaka hiyo walikuwa wamebobea katika lugha ya Kiarabu na mafuzo dini ya Kiislamu kwa jumla na walikuwa wakipenda kuwafwata Masheikhe kwa mijadala, lakini kinyume chake, Sheikh Sheikh Abdalla bin Wazir akiwafwata wao na ikisemekana mara nyingi wakimkwepa kwani alikuwa na lugha ya kejeli nakuwa tayari kufanya mijadala hata kwa siku nzima. Alipokuwa anakwenda kufanya mijadala watu wakipenda kumfwata kusikiliza namna alivyokua akijadiliana nao. Alikuwa na ufundi wa kucheza na lugha ya Kiarabu na Kiengereza ambao haikuwa rahisi kwa masheikhe wa siku hizo kuwa na kuzimudu lugha mbili hizo.

Katika zama za Syd Barghash kulitokea ugomvi mkubwa baina ya wakazi wenye asili ya visiwa vya Comoro ambao walikuwa wakiishi Unguja na kujigawa katika mapande mawili nayo ‘Inyamwatsa Pirusa” na “Inya Fuambaa.” Hakuwa Mngazija alioishi visiwani kutokuwa kwenye mmoja wa mrengo huo ulioingia katika malumbano na kuwa na baa na belwa. Vijana wanaotokana na wazee waliotoka katika visiwa vya Comoro walikuwa na Sheikh Fadhil na walikuwa wanataka mabadiliko na kuwataka wazee wao waache kufwata utamaduni na wafwate misingi halisi ya dini ilivyo. Sheikh Fadhil alijitenga na makundi hayo yote mawili

Kati ya wale

waliokuwa wakijiweza na kina enhe kati ya wakazi wa Kingazija waliokuwa wakiishi Zanzibar walikuwa karibu na Syd Barghash na walikuwa wakihudhuria majlisi yake kwa hio wakapata fursa ya kumchongea Sheikh Fadhil kuwa ni mwanaharakati anayoleta fitna katika mji, kwa lugha ya leo angeitwa Muislamu mwenye siasa kali. Sheikh Fadhil mawazo yake na alivyokuwa fasaha kwa kuelezea Uislamu na tarekhe yake uliwavutia wengi na kuwa kama tishio kwa watawala kwa hivyo naye akapewa Persona non Grata na kuwa Prohibited Immigrant yaani mhamiaji asiotakiwa na kupakiwa meli na kurejeshwa Comoro. Ilikuwa ni pigo kwa wakazi wa Unguja lakini

ndio tuseme lilokuwa liwe haliwezi kuwa lisiwe.

Baada ya kuwasili kwake Comoro wakaazi wa Moroni walifarajika na akawa anasomesha darsa mbalimbali. Aliuwona mji wa Moroni upo karibu na Unguja akajihisi fitna zitaendelea kumwandama kwa hio akahama Moroni mji mkuu akaelekea Ndzuwani ambako alipofika tu akapewa Ukadhi na alikuwa kila mmoja katika mji akihakikisha kisima hicho kilicho na kina kirefu na kilicho jaa maji yasiokauka, ni vyema kwenda kuchota maji yaani elimu.

Sheikh Fadhil alifunga macho mwaka wa 1302 (1885) na kuwacha pengo kubwa lilokuja kuzibwa baada ya miaka mingi kupita.

Sheikh Fadhil akipenda kuona kuwa kuna umoja wa Waislamu na kupinga kwa nguvu zake zote za watu kugawanyika na alikuwa akisimamia vilivyo miongozo ya Qur’an na Suna za Mtume Muhammad (SAW). Yaliomkuta Sheikh Fadhil ni yale kwa yale yanakwenda na kujirejea hadi hii leo. Fitina wanazozipika Waislamu kutokana na tafauti baina yao, zinarindima na kufanya kuwa Waislamu siku zote wapo katika Misuko suko.

Tumuombe Allah atupe fahamu za masheikhe kama Sheikh Fadhi na atupe misimamo kama aliyokuwa nayo ya kuona Umoja wa Kiislamu unasimama siku zote, “Ameen”.

(Kwa mawasiliano, maoni, maswali tumia namba 0777436949)

Khabari ya Israel ‘Taifa teule’-4Inatoka Uk. 8naye, asubuhi akamwambia b a b a y a k e , k u w a , amempenda binti huyo hivyo anapenda awe mkewe; baba yake akamwendea Yakobo, akamweleza habari ya binti huyo kuolewa na kijana wake, hata hiyo Yakobo akamwambia anasubir i wa t o t o wa k e wa j e , n a walipokuja wakamwambia Yakobo baba yao kuwa d a d a ya o a m e f a n y i wa vibaya, wakafanya hila na babayao, wakamwambia yule mfalme kuwa, akitaka kuwa mwanawe amwoe Dina akubali kuwa raiya zake wanaume wote watahiriwe maana binti yake hataolewa na mume mwenye govi (zunga). Hamori Mhivi akamwambia Yakobo kuwa kuliko mwanawe akose kumwoa Dina amekubaliana na kutahiriwa raiya zake nayeye mwenyewe.

Akaitisha kikao cha raiya zake akawaelezea, nao wakakubali, wakatahiriwa siku moja wote; watoto wa Yakobo wakasubiri siku tatu, wakijua kuwa vidonda vya tohara vimefikia upeo wa maumivu wakawavamia wanaume wote wakawauwa pamoja na yule mvulana na baba yake; na waka wachukua wanawake na watoto na mali zote na kuteketeza makazi yao yote. Na baada ya hapo mungu wa Israeli wakawapongeza na kuzidi kuwabariki.” Kisa

hiki utakipata vizuri katika, Mw.34:1-35.

Huyo ndiye Israeli, babu wa wana wa Israeli. Huo ni mfano mmoja tu wa majirani wa Israeli (Yakobo) alivyo ishi nao. Sasa ili tuone jinsi Biblia ilivyo watukuza wana wa Israeli ; tuone wosia (wasia-usia) Yakobo aliowa-achia wanawe. Biblia ya mwaka wa 1937, imeanza kwa kichwa cha habari: Yakobo ana wabariki wanawe wote, Biblia ya Imprimatur, imeanza na Mibaraka ya Yakobo. Kulingana na urefu wa hiyo mibaraka, nitanukuu sehemu, na msomaji akitaka kuiona yote nitaonesha aya zote; Biblia ninayotumia ni toleo la Union version.

“Yakobo akawaita wanawe , akasema, Kusanyikeni ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo, Msikilizeni Israeli, baba yenu. Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, Nguvu zangu, na milimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipanda kitanda changu.” (Mw.49:1-4.)

Reubeni, alizini na mama yake, mama mdogo, mke wa nne wa Yakobo, aliyeitwa Bilha; sasa hiyo ni mibaraka?

“Ikawa Israeli, alipokuwa akikaa nchi ile, Reubeni

akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari.” (Mw. 35:22.)

H a t a h i v y o Ya k o b o hakusema kitu; kusema kwake ni huko akitoa mibaraka, hata hivyo waandishi wa Biblia za nyuma hata hii ninayonukuu, hawakuwa na hiyana; waliweka rejea hivi:

“Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na waseme, Amina.” (Kumb 27:20; Nyakati 5:1.)

Sasa hiyo ndiyo mibaraka; nilisema hapo juu kuwa, kwa wana wa Israeli na wale wanaowatukuza, kwao haramu inakuwa halali na halali inakuwa haramu.

Ukisoma B ib l ia kwa m t a z a m o h u r u ; b i l a kuegemea upande, hutaweza kumwamini mfuasi wa dini ya Kiyahudi na ya Kikristo anapokwambia kuwa ana hubiri amani katika nchi anakoishi; au katika dunia hii. Ukimwona anayezungumzia amani, hiyo ni katika ulimi, si katika imani iliyofundishwa na waasis i wa dini ya Kiyahudi. Ukitaka kujua hilo soma Biblia, kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka mwisho wa ufunuo wa Yohana, alafu weka mizani ya amani na vita jinsi ilivyofundishwa na kusisitizwa, utakuta kuwa haya machafuko tunayoyaona hapa duniani yanatokaka na mafundisho yaliyoasisiwa na wana wa Israeli wakishirikiana na watawala wa enzi hizo na hizi.

Page 14: ANNUUR 1208

14 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

TUSOMENI AN-NUUR (1)

Na Sheikh Mohamed al- Amiri Othmani

Jihadi ni kwa ajili ya kukingauadui katika dini sio kuua

MAKALA/MASHAIRI

TULIDURUSU IMAAN (1)Wito nakutoleeni, kuhusu letu IMANI,Gazeti jipya makini, kwa ya dunia na dini,Kwa sasa li mitaani, shime na tulisomeni,Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.

ARUSHA nakuiteni, pamwe na zenu jirani,Wito uzingatieni, na MANYARA wajuzeni, Na KILIMANJARO ndani, na TANGA waubaini,Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.

DAR ninakuiteni, pamwe na zenu jirani,Wito uzingatieni, kikoa MORO na PWANI,Muwe pamoja safuni, kwa kulisoma IMANI,Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.

GEITA nakuiteni, pamwe na zenu jirani,Wito uzingatieni, SIMIYU ufikisheni,Na SHINYANGA mkoani, lipate somwa IMANI,Tulidurusu IMANI, kwa habari za yakini.

ABUU NYAMKOMOGI,MWANZA

Mhariri muadhamu, nipokee hodi hodi, Janibu japo nikumu, ya gazetilo suudi, Ndaniye abra nikimu, nitoe wito saidi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Naibtadi nudhumu, kwa Allah kumhimidi, Thuma swala na salamu, kwa rasuli Muhammadi, Kadhalika taadhimu, kwa swahaba murshidi, Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Baada ya taadhimu, sina budi kulinadi,Gazeti letu adhimu, ndani lenye irishadi,Kadhalika taalimu, na mzomzo suudi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR. Limesimama kawimu, pamwe na kutabaradi, Lengole hasa ikumu, ya Ilahi Tauhidi,Na zende zote kuzimu, za rajimu itikadi,Kwa habari zenye nuru, tusomeni AN-NUUR.

ABUU NYAMKOMOGI,MWANZA.

KWA hakika Uislam pale u l i p o w e k a

sheria ya vita na jihadi imewekwa k w a a j i l i y a k u k i n g a u a d u i ambao utatokea na kupigana na wale ambao wanaopigana na waislam na wala haikuletwa kwa ajili ya kuwaua wanao tofautiana katika d i n i n a m a o n i au kutofautiana madhehebu.

A n a s e m a Mwenyezi Mungu m t u k u f u , “ N a p i g a n e n i k a t i k a njia ya Mwenyezi Mungu na wale w a n a o k u p i g e n i wala msipindukie mipaka mkawapiga w a s i o k u p i g e n i kwani Mwenyezi Mungu hawapendi warukao mipaka” ( 1 9 0 ) S u r a t u l Bakarat.

A m e s e m a I b n kathiri amesema Abuu Jafari Razi toka kwa Rabi Bin Anas i toka kwa A b i - A l - A a l i ya katika kauli yake Mwenyezi Mungu, “Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na wale

wanaokupigeni”. A k a s e m a h i i n i a ya ya m wa n z o i l i y o t e r e m s h w a katika vita hapo M a d i n a n a p a l e i l i p o t e r e m s h wa , a l i k u wa M t u m e (s.a.w) akipigana na yule anayepigana naye na al ikuwa hapigani na yule asiyepigana naye hadi ilipoteremshwa Surat Bakaratu.

Tafs i r i ya Abi i Suudi, “na piganeni k a t i k a n j i a y a Mwenyezi Mungu” kwa maana piganeni kwa ajili ya kushinda dini yake Mwenyezi Mungu na kutangaza neno lake, ni kwa k u t a n g u l i a j u u ya mtendewa wa wazi kwa ajili ya kuonyesha ukamilifu k w a m a m b o y a k u t a n g u l i a “ w a l e a m b a o w a n a o k u p i g e n i n y i n y i ” m a a n a yake ambao wanao kuchokozeni kwa v i t a n a k u we z a k u s i m a m i s h a v i ta h ivyo watu wasiokuwa nyinyi miongoni mwa watu wazima na vijana na viongozi wa dini na wanawake “wala msivuke mipaka” kwa kudhihirisha vita au kwa kupigana na wanaoishi kwa mkataba na kwa njia ya ghafla bila ya kuwalingania au kwa kisasi na pia haifai kuwaua wale mliokatazwa kuwaua miongoni m wa wa n a wa k e na watoto na wale wanofanana na wao.

“Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipaka” kwa maana ya kwamba hataki kwao nako ni kutiia ila katazo na inabainisha aya hii kwamba lengo la vita katika Uislam katika mambo yafuatayo:-

(1) Kuzuia uadui na kuondoa madhara ya nafsi

(2) K u i n u s u r u haki na uadilifu pia kunainisha kwamba miongoni mwa sharti ni vidhibiti vita.

(1) K u b a i n i s h a uzuri wa vitendea kazi na lengo

(2) H a i r u h u s i w i k u p i g a n a n a e i s i p o k u w a Y u l e anayepigana na wewe na hakuna uadui kwa wanaofanya ibada pia inabainika kwetu kwamba jihadi katika uislam imekaa vizuri m w i s h o wa k e n a vitendea kazi kwa pamoja na tunafupisha athari hizi katika nukta zifuatazo:-

(1) K u i l e a n a f s i katika kujitolea

(2) Kukubali uadilifu na uhuru kwa watu wote kwa imani zao zote

(3) K u t a n g u l i z a hukumu kuu kuliko maslahi maalum ya mtu mmoja hakika yale yanayotokea katika u l i m w e n g u w e t u wa kiislam ni sasa kutokana na ufahamu uliochanganyika juu ya maana ya vita na jihadi na kuteremshwa kwa aya hizi kwa waislam wanaotofautiana maoni huo ni upotevu wa wazi huporomoka kwa mwenye fikra hizi mbovu na kuteketea, t u n a m u o m b a Mwenyezi Mungu amani na ufahamu mzuri katika dini yake.

Page 15: ANNUUR 1208

15 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

MAKALA

Mauaji na majanga Mashariki ya KatiInatoka Uk. 9

ni nini. Ina maana makampuni au mashirika makubwa yanaendesha nchi, yanaendesha dunia, na watu wanataabika. Hivyo hakuna mbadala kwangu, lazima nichukue msimamo. na Allah akipenda, nitakufa kwa kufuata njia Yake, njia ambayo imefanya nchi yetu kuwa na utajiri wa maeneo ya kilimo, kwa chakula na afya, na hata kuturuhusu kuwasaidia ndugu zetu na dada zetu wa Afrika na Uarabuni kufanya kazi pamoja nasi, katika Jamahiriya ya Libya.

Sipendelei kufa, lakini kama itafikia hapo, kuiokoa nchi hii, watu wangu, wale maelfu ambao wote ni wanangu, basi iwe hivyo.

Agano hili liwe sauti yangu kwa dunia, kuwa nilisimama dhidi ya mashambulio ya makruseda wa NATO, nilisimama dhidi ya ukatili, nilisimama dhidi ya usaliti, nilisimama dhidi ya nchi za Magharibi na dhamira zake za kikoloni, na kuwa nilisimama pamoja na ndugu zangu wa Kiafrika, ndugu zangu wa kweli wa Kiarabu na Kiislamu, kama mhimili wa mwanga.

Wakati wengine wakijenga majumba ya kifahari, niliishi katika nyumba ya kawaida, na katika hema. Sikuwahi kusahau ujana wangu katika mji wa Sirte, sikutumia hazina ya nchi kipuuzi, na kama Salahuddin, kiongozi wetu shujaa wa Kiislamu, ambaye aliiokoa Yerusalemu kwa Uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu mwenyewe.

Katika nchi za Magharibi, baadhi wameniita 'kichaa,' 'hamnazo,' lakini wanajua ukweli na wanaendelea kusema uwongo, wanajua kuwa ardhi yetu iko huru, haiko katika makucha ya ukoloni, kuwa taswira yangu, njia yangu, na imekuwa wazi na kwa watu wangu na ambayo nitaipigania hadi pumzi yangu ya mwisho kutubakiza huru, Allah Suhanna atusaidie kubaki na imani, na huru.” (Mwisho wa kunukuu.)

Uhalifu mkubwa wa Gaddafi ni kuwa anatoa sehemu kubwa mno ya

utajiri wa mafuta kwa watu wake. Alikuwa mtu wa mabavu? Ndiyo, ila inabidi uwe hivyo ili utawale katika eneo lile hivi sasa. Alikuwa ndiyo mtu mbaya zaidi wa mabavu? Hapana, hata kwa udi na uvumba.

Awe mbaya alivyokuwa, hakuua wa-Irak milioni moja kwa tuhuma za kutengeneza za silaha za maangamizi ambazo hazikuwepo. Wala hakuwa anakata vichwa 50 kila wiki na kupiga mawe hadi kufa wanawake kwa kuzini kama ilivyo kwa Saudia hivi sasa.

Lakini pia, kama aliua waandamanaji au hapana, au alifanya uhalifu wa kivita au hapana, haina umuhimu kwa wanaohodhi mamlaka. Cha msingi ni kuwa alikuwa amezuia nchi za Magharibi kupata maslahi yao, na badala yake akatumia utajiri wa mafuta wa nchi yake kutoa bure au kwa malipo kidogo sana tiba , elimu na nyumba kwa sehemu kubwa ya wananchi wa Libya.

Hivyo, twende sasa kuona mauaji yake. Hivi ndivyo ilivyokuwa: Majira ya saa mbili asubuhi saa za Libya hapo Oktoba 20, Gaddafi na mkuu wake wa majeshi Abubakr Yunus Jabir, mkuu wake wa usalama Mansour Dhao, na kundi la askari wanaoumuunga mkono walijaribu kutoroka kwa kutumia magari 75. Ndege ya kivita ya upelelezi ya Uingereza iliona msafara huo ukienda kwa kasi kubwa, baada ya majeshi ya NATO kudaka simu ya

MAREHEMU Kanali Muammar Gaddafi.

satellite iliyopigwa na Gaddafi.

Ndege za NATO zilipiga magari 11, zikateketeza moja. Ndege ya kivita ya Marekani isiyo na rubani, Predator ikiongozwa kutoka boma la kijeshi karibu na Las Vegas, ilipiga makombora ya kwanza dhidi ya msafara huo, ikapatia takriban kilometa tatu kutoka Sirte. Dakika chache baadaye, ndege za kijeshi za Ufaransa zikaendeleza kupiga mabomu.

Mabomu ya NATO yalikwamisha msafara huo na kuua dazeni kadhaa za wapiganaji watiifu kwa Gaddafi. Baada ya shambulio la kwanza, magari takriban 20 yalitoka katika kundi kubwa na kuendelea kwenda kusini. Pigo lingine la mabomu ya NATO liliharibu au kuteketeza magari 10 kati ya hayo. Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Financial Times, vikosi vya wapiganaji wanaompinga Gaddafi vya Free Libya vikiwa katika eneo hilo pia viliupiga msafara huo.

Kwa mujibu wa taarifa yake, NATO ilikuwa haina habari wakati wa shambulio hilo kuwa Gaddafi alikuwa katika msafara. NATO ilisema kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka 1973, hailengi watu ila vitu vinavyoleta hatari katika uwanja wa vita. NATO baadaye ilisikia "kutoka vyanzo huru na taarisa za kijasusi za washirika" kuwa Gaddafi alikuwa katika

msafara huo na kuwa shambulio hilo ni wazi lilichangia kukamatwa kwake.

Kuiamini NATO, ilikuwa haina habari kuwa Gaddafi alikuwa katika msafara huo, lakini bado ikawa ina ndege isiyo na rubani inangoja hapo kando pamoja na ndege kadhaa za kivita za kulenga vitu vilivyoko ardhini (na siyo makombora ya kutungua ndege kama ambavyo ungetazamia kwa vikosi vinayodhibiti anga ndege zisiruke). Ilipita tu magari hayo mara kadhaa katika juhudi ya kuua kila aliyekuwa humo kwa sababu walikuwa "vifaa vya kijeshi vinavyoleta hatari."

Kwa sababu unaishi katika ulimwengu halisi, unajua kuwa NATO ilikuwa inafahamu ni wapi hasa alipo Gaddafi wakati wote na kuwa alikuwa katika msafara huo akijaribu kukimbia mashambulizi ya NATO. Zaidi, unaweza kushangaza kidogo kufahamu kuwa mengi kati ya magari hayo yalikuwa ni aina ya pick up ambayo hayawezi kuleta hatari yoyote ile kwa vikosi vya NATO. Suala lilikuwa ni kumwua Gaddafi, na vifaa mbalimbali vilikusanywa kwa lengo hilo.

Kuuawa kwa Gaddafi kulikuwa ni kupangwa kifo cha kiongozi wa nchi nyingine na washikadau wa nchi za Magharibi. Kwa hali hiyo, Gaddafi alikuwa ni mlengwa tu mwingine katika mlolongo wa viongozi waliouawa wakijaribu

kuzuia washikadau hao hao wasifikie malengo yao.

Baada ya NATO kumaliza uharibifu nchini Libya kwa kumwondoa Gaddafi na kuacha bonge la ombwe katika dola ya nchi hiyo, iliondoka papo hapo, kuiacha nchi hiyo ijitegemee iwezavyo. Libya ilitumbukia, bila shaka, katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na imebakia hapo tangu wakati wimbi la utumiaji nguvu kuleta serikali ya kidini lilipoanza na kuongeza uwepo na udhibiti wa ISIS (Dola ya Kiislamu Irak na Shamu).

Kama NATO/Marekani wangefuata kanuni ya kwanza ya Pier "ukikivunja, unakinunua," bado wangekuwa nchini Libya wakitoa fedha na misaada wakati nchi hiyo ikirudi katika utulivu na kuanza safari ndefu ya kujijenga upya.

Lakini hapakuwa na bahati kama hiyo. Siyo hata kidogo jinsi wanavyojiendesha. Ni ubepari maafa unaofuatwa. Dhana elekezi ni kubomoa nchi na kutengeneza pesa kwa kutumia vipande vyake. Siyo kuwasaidia watu. Vinginevyo, unawezaje kuelezea uharibifu unaoendelea katika nchi kama Irak, Libya, Yemen na Syria?

Licha ya kuwa na mapungufu ya kiutawala kwa viwango vya nchi za Magharibi, nchi zote hizo zilikuwa zimetulia na kuwa na maendeleo mazuri tu kabla maslahi ya nje hayajaingia na kuzigeuza kuwa majinamizi halisia.

Ni hali hii ambayo inaelezea kwanini makundi ya kiharamia na kupinga maendeleo kama ISIS yalizuika. Ni jibu la kiasili tu la watu walioingiliwa wakihitaji kurudisha udhibiti juu ya maisha yao ambayo bila hivyo hayana matumaini na hata maana. Sitaki kuihalalisha, ila kueleza mazingira ambayo yamefikia kuzuka kiwake.

(Hii ni sehemu ya kwanza ya Makala Murder And Mayhem In The Middle East iliyoandikwa na Chris Martenson na kutafsiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija.)

Page 16: ANNUUR 1208

16 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

MAKALA

BAADA ya kupatikana kwa Serikali mpya ya John Pombe Magufuli, ambayo ni awamu ya Tano ya uongozi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), siku zinasonga mbele na maisha yanaendelea baada ya uchaguzi.

Kwa ujumla kila raia katika makundi ya kijamii yanatafakari mustakabali wao chini ya uongozi huu mpya, ni vipi watakuwa katika faraja ya matarajio ya kuweza kutoka pale walipoachwa na utawala uliopita. Miongoni mwa makundi hayo ya kijamii lipo kundi la Waislamu, kundi ambalo naweza kusema kuwa ni ‘wahanga’ wa awamu zote chini ya Chama Cha CCM, na kutokana na madhila wayapatayo, inaonesha kama vile kundi hilo limekata tamaa na utawala wa CCM, chini ya kiongozi yoyote anayetoka katika Chama hicho.

Lakini kundi hili sina shaka kuwa linafahamu kuwa kisiasa, Rais atakaye shinda anakuwa ni Rais w a Wa t a n z a n i a w o t e waliompigia kura na wasio mpigia kura, kinachofata ni kuangalia ni namna gani wanaweza kwenda naye sawa. Ni vyema kujipa moyo kuwa anaweza kuwatendea haki , kwani Muis lamu hapaswi kutaka tamaa. Katika hili, ipo mifano mingi ni kwa namna gani Mitume wa Mwenyezi Mungu na Maswahaba wao waliweza kuishi katika tawala za mbalimbali na wakaweza kupata yao.

Rais Magufuli ameingia madarakani na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu’ kauli ambayo mara baada ya kuapishwa i m e a n z a k u j i o n y e s h a kivitendo kwa kufanya maamuzi ambayo katika tawala zilizopita ilikuwa ni nadra kufanywa.

Lakini Rais Magufuli, katika kampeni zake wakati akiomba ridhaa ya kuongoza nchi , al ikuwa aki j inadi kuwa yeye ni mwadilifu, mtu wa watu, mchapa kazi na mfuatiliaji wa mambo. Mh. Magufuli ameingia madarakani na kudhihirisha yale aliyokuwa akijinadi nayo, hivi sasa kwa watumishi wa Serikali, hususani kwa wasio waadilifu hakuna asiye na hofu juu ya mustakabali wake, na kasi hiyo sasa imekuwa ni faraja kubwa kwa wananchi wanyonge. Rais Magufuli amekuwa kivutio kwa makundi mbalimbali

Magufuli afikishiwe madai ya WaislamuLakini kwa kauli iliyo laini huenda…Akaona haki Sheikh Msellem wakasalimika

Na Bakari Mwakangwale

RAIS John Magufuli.ya Watanzania, hususani wanyonge miongoni mwao ni wale ambao walikuwa upande wa pili ambao ndio wapiga kura, ndani ya kipindi hiki kifupi tokea kuapishgwa kwake, kutokana na utendaji wake wa kazi.

Katika moja ya hotuba zake Rais Magufuli, amesikika akiorozesha kero sugu mbalimbali zinazowasumbua wananchi, miongoni mwa kero hizo ni kubambikiwa kesi, na kuahidi akisema, “ K e r o h i z i n i l a z i m a tutazishughulikia kwa nguvu zote.” Katika kudhihirisha msimamo wa Rais Magufuli, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, Novemba 29, 2015, akifungua maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Jijini Dar es Salaam, a l i wa t a k a Wa t a n z a n i a waiombee Serikali ya awamu ya Tano, ili iweze kuongoza k wa h a k i n a u a d i l i f u kwa lengo la kuwaletea Watanzania maendeleo. Kutokana na hali hiyo, napenda kulizungumzia kundi la moja katika jamii la Waislamu, ambalo linaamini kwa mifano iliyo hai kuwa ni wahanga na ni wadhulumiwa katika mambo mbalimbali ya kijamii chini ya tawala zilizopita.

Kwa kawaida binadamu unapoandamwa na mitihani, na katika kuikabili mitihani h i y o u k a wa u n a m l i l i a Mwenyezi Mungu kwa njia ya kukata tamaa, si rahisi ukapata ujasiri wa kukabiliana na mitihani zaidi na zaidi. Ni bora kundi hili likajipanga, kwenda

kumkabili Rais Magufuli, na kumueleza madai yao. Rais Magufuli amekuwa akinadi kuwa ‘Hii ni Serikali ya Magufuli’ na hata katika kampeni mara kwa mara alikuwa akisema ‘Chagua Magufuli’ mara chache alikuwa akisema chagua CCM, hizi kauli huenda mwenyewe aligundua kitu.

Katika Qu ran: 20:24. M w e n y e z i M u n g u anamwambia Nabii Mussa, “Nenda kwa Firauni, bila shaka yeye amepindukia mipaka.”

Nabii Mussa, alihofu baada ya amri hiyo akasema, “Ewe Mola wangu nipambanulie (nikunjulie) kifua changu (niweze kustahimili balaa zitakazonifika). Qur’an 20:25. Na katika Qur’an 20:46, Allah anajiubu, (Mungu) akasema: msiogope bila shaka mimi ni pamoja nanyi, nasikia na naona.

Baada ya hapo Mwenyezi Mungu alitoa mwongozo kwa Nabii Mussa, ambapo katika Qur an, 20:44, Allah (s.w) anasema “Kamwambieni maneno laini huenda atashika mawaidha au ataogopa.”

Aya hii inatufundisha siasa nzuri ya kuwafikishia watu mawaidha, nayo ni kutumia lugha nzuri na katika hali ya upole . Upole na maneno laini humvuta asiyetaka kusikiliza akasikiliza, lakini pia hata asiye ‘Minkum’ naye anastahili kufikishiwa nasaha, ikiwa ni mtawala basi atawale kwa misingi ya haki na uadilifu.

Lilokubwa na linalowatesa n a k u w a u m i z a z a i d i Waislamu kwa sasa, ni kadhia ya uwepo wa Waislamu na

Masheikh ndani (Mahabusu) ambao wamedhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vichafu. Rais afikishiwe hili. Aelezwe kuwa yeye sasa ndiye Amiri Jeshi Mkuu, aliangalie hili kwa misingi ya haki na sheria.

Ni kweli anaweza akawa anajua, lakini kujua kwake ni kule kwa misingi ya dhulma zilizopelekea kuwepo wao ndani lakini zipo hoja nyingi za kumdhihirishia kuwa Waislamu na Masheikh hao ni wahanga tu kwa tuhuma zisizo na ushahidi wowote.

Mbali na hilo, Rais huyu ‘mfatiliaji’ (Mh. Magufuli) aelezwe kwamba Waislamu hawataki kupendelewa, bali wanataka haki na usawa siku zote, kama hawa Masheikh na Waislamu wana hatia, basi sheria ifuate mkondo wake na ieleweke kama wana makosa wahukumiwe kwa mujibu wa sheria na kama hawana, basi waachiliwe warudi uraiani washiriki katika kazi ya ujenzi wa Taifa lao.

Rais Magufuli, aelezwe kwamba kama kuna raia w a n a o o n g o z a k a t i k a kubambikiwa kesi, hakuna katika raia wake kama Waislamu. Na kwa sababu ameahidi kuifanyia kazi kero hii, basi ni vyema akashajihishwa kulifanyika kazi kwa haraka.

Bila shaka akilivalia njuga suala hili la kubambikiwa kesi atabaini madudu mengi kuliko anavyofikiria na atabaini kuwa waathirika wakubwa ni Waislamu.

Nimalize kwa kuweka orodha ya Waislamu katika magreza mbalimbali kufatia

utafiti usio rasmi ambao gazeti la An nuur, umebaini kuwa Waislamu hao ni wale ambao wanatuhumiwa kwa tuhuma za ugaidi, uvamizi wa kutumia silaha.

Ndani ya gereza la Segerea kuna Waislamu wapatao 130, wanaohusishwa na kesi za Ugaidi katika idadi hiyo wapo katika mafungu ya kezi zipotazi 13, ikiwemo ile maarufu ya Sheikh Mselem Ally na Farid Had. Kesi hizo kwa ujumla zimekuwa zikiahirishwa siku baada ya siku yapata mwaka wa pili sasa.

K a t i k a g e r e z a l a Morogoro, wapo Waislamu wenye tuhuma kama hizo. Waislamu hawa wapo katika makundi mawili, kwanza ni wale wenye kesi namba 17 ya mwaka 2015 na kesi namba 16 ya mwaka 2015. Hawa wanahusishwa na lile sakata la Msikiti wa Kidatu Wilayani Kilombero, jumla wapo Waislamu 26 na kesi zao zimekuwa zikipigwa d a n a d a n a t u , h a k u n a kinachoendelea na mpaka sasa wanasota mahabusu.

Jijini Mwanza kuna kesi ya Waislamu nane, ambao wanatuhumiwa kwa tuhuma za Ugaidi, ambao wapo mahabusu katika Gereza la Butimba, hao ni kama hawa wafuatao, Amini Msharaba, Nassoro Muhammad, Sensei Kioka, Omari Awadhi, Abdi Shariif, Mohammad Ibrahiim na wenzao wawili, hawa wapo gerezani yapata miezi s i ta tangu wakamatwe. Lakini kuna kesi ya Imam Hamza, ambayo inaendelea kuunguruma kwa muda mrefu sasa.

J i j i n i A r u s h a , k u n a kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili Imam Hambali na Waislamu wengine zaidi ya 61, ambao pia wamewekwa kwa makundi nao hakuna kinachoendelea zaidi ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa mashitaka kisha kupigwa tarehe. Ama mkoani Kagera, katika Wilaya ya Muleba , yupo Ustadhi Yusuph na Abdul-Hamiid, (Wakazi wa Buseresere, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita).

Kwa ujumla hiyo ndio hali halisi ilivyo. Ni wakati sasa wa Serikali kuangalia inaweza kuiondoa vipi dhulma hii si katika kupendelewa, bali kupewa haki si kuachiwa tu. bali hata kuzipeleka kesi hizo kwa misingi ya sheria na endapo wakakutwa na hatia wakihukumiwa pia ni haki yao vile vile.

SHEIKH Msellem. SHEIKH Farid Hadd.

Page 17: ANNUUR 1208

17 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

MAKALA

MJENGA nchi ni mwananchi mwenyewe

na mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe pia. Ninavyoona ni kweli kabisa mjenga nchi ni mwananchi, lakini kwangu mvunja nchi anaweza pia kuwa mlowezi na mvamizi au adui yoyote kutoka nje, hasa wenye masilahi ya kukomba mali kama walivyokuwa Waingereza, Wafaransa na Wajerumani na sasa Wamarekani.

Raisi wa kwanza wa Zanzibar licha ya ukereketwa wake wa kimapinduzi, hakuwa na uzembe wa kuwakumbatia wale ambao walionekana hawana uchungu na nchi kwa kuwambia"Huwezi kuwa mwananchi kama huna machungu ya nchi".

Maneno haya kwa lugha ya kisasa tunaweza kusema kuwa ni maneno msumari kabisa na muda huu tuliwonawo Wazanzibar tunaweza kuyatafakari maneno haya na tukifanya hivyo tutawaelewa wale ambao sio wananchi kwani wapo ambao hawana uchungu na nchi.

Wahafidhina wa Zanzibar wengi wao hawana uchungu na nchi au wanajaribu kuupiga chenga kuzidi kufanikisha walichokusudia. Kutokuwa na uchungu wa nchi ndio kutapelekea kuvunja nchi kutokana na tamaa zao na uchu walionao wa madaraka huku wakijua wanachokifanya lakini zaidi wakilinda maslahi ya tumbo.

Kulichumia tumbo kwa kuwaangamiza wananchi na nchi,

Wahafidhina munatupeleka wapi?Turejee katika msimamo wa Mzee Karume…Na Rashid Al-Ghafri

RAIS wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.ni dhulma hivyo inawapasa muelewe kuwa dhuluma munazowafanyia Wazanzibar hazitokufa na badala yake mutalipwa uovu wa dhuluma hizo kesho mbele ya hukumu. Wahafidhina kutokana na tabia yenu hii ya kuipindisha haki kuona batili na batili kwenu kuiona haki kwa maslahi tu ya matumbo yenu, itafika siku mchana muone usiku na kutamani usiku uwe mchana.

Wahafidhina nini hasa mulichokikusudia kwa wananchi wa visiwa hivi vilivobarikiwa kila aina ya neema kuanzia bahari hadi ardhi, au ndio tuwaelewe kuwa munatupeleka kule ambako Mwalimu Nyerere alikusudia na nyinyi ndio munatekeleza hilo au kuna wasia aliwaachia.

Kwa makusudi kabisa mumethubutu kuivunja na kuisigina katiba ya Zanzibar ili muwakomoe Wazanzibar kwa kile walichoamua

kukifanya kwa mujibu wa katiba hiyo.

Kuivunja katiba hamjui kwamba munaiingiza nchi kwenye giza. Hebu tuwekeeni wazi, ni wapi hasa mnatupeleka?

Ni mwezi na siku kadhaa sasa tokea kujiongezea muda wa kuwepo madarakani kwa kisingizio cha ufutwaji wa uchaguzi mumekuwa mukikalia nafasi hizo bila ridhaa nyengine ya wananchi huku hali zao zikiendelea kudidimia. Kila huduma kwa sasa ni shida kupatikana sio tu kwa taasisi za serikali pekee ambazo zimezorota kwa kutokuwepo usimamizi wa kweli, bali hata wenye kuendesha huduma binafsi wengi wao wamejipa likizo bila kutarajia lakini likizo hilo ambalo hatujui litamalizika lini limewalazimi kulingana na hali tuliyonayo sasa.

Bidhaa nyingi zimekumbwa na mfumko mkubwa wa bei hivyo wananchi

wanyonge wakizidi kuelemewa na mzigo wa maisha. Mzigo huu walitarajia kupata nafuu baada ya uchaguzi lakini wapi. Bado tunapelekwa kule ambako wao wanaona tukishiba sisi hakuna mwingine mwenye njaa.

Tafakarini kuwa dhima kubwa ya Wazanzibar ipo mikononi mwenu popote mutakapo waingiza ni nyinyi mutakao beba lawama na kama kuna nguvu nyuma yenu inawatia mkazo kuendeleza dhamira zenu, mjue kuwa mwisho watakugeukeni na kujirusha mbali kabisa na hilo.

Uchumi wa nchi yetu ya Zanzibar kwa uhalisia kabisa umekufa na hii yote ni mipango ya zamani ya wahafidhina ambayo wanaiendeleza kwa matakwa yao. Vijana wengi hawana ajira na wenye kujiajiri wenyewe vikwazo kila kukicha. Tuangalie eneo la darajani wote walokuwa wakijishughulisha walitimuliwa kwa kisingizio kuwa ni eneo la kujenga bustani, iko wapi hiyo bustani ilojengwa na miaka kadhaa imepita sasa.

Licha ya rasilimali za mafuta na gesi zilizogunduliwa katika visiwa hivi, ninaamini hata kama uchimbaji wake utafanyika chini ya usimamizi wa hawa wahafidhina, hakuna la maana litakalopatikana kwa nchi.

Ninayasema haya kwa ushahidi unaojidhihirisha wenyewe katika zao maarufu la karafuu hususani kisiwani Pemba kwani siku za msimu kila unapopita barabarani kuna vizuizi vimeekwa ili

rasilimali ya karafuu ambayo wakubwa wameitumbulia macho kwa kuiweka kwenye udhibiti wao. Zao hili bado halijawanufaisha wakulima licha ya kazi kubwa wanayopata na wengine ulemavu wa maisha au hata kupoteza maisha kabisa wakati wa harakati za uokowaji wa zao hili walilotegemea kuwainua kiuchumi lakini wapi yao kazi faida ya wakubwa.

Harakati zote za upatikanaji wa zao hili ni za wakulima wenyewe lakini zao likiwa tayari ni la wakubwa na ndio vizuizi vikawekwa mabarabarani kila baada ya kilomita kadhaa na hili ni sawa na ule usemi wa Kishihiri "Mbuzi wa Salimini lakini maziwa ya bwana wake Salimini". Na ndio ukaona wakubwa wanajipangia bei watakayo wenyewe na kama wewe mkulima hutaki bei hiyo, basi huna pengine pakuuza.

Bei wanayopewa wakulima bado hayo hayajawa malipo halisi ya zao hilo badala yake wanachopewa ni kifuta jasho tu cha kazi ngumu wanayoifanya kwani malipo halisi ni kuboreshewa hali nzuri ya nchi yenye miundombinu imara kwa kila nyanja na hapo itakuwa kweli rasilimali hiyo imewafaidisha.

Tuangalie hali ilivo katika barabara zinazopita maeneo yanayozalisha zao hili zikoje ukilinganisha na thamani ya zao husika katika soko la dunia. Mfano barabara ya Mkoani Chake Chake ni mbovu na ya hatari kabisa haimithiliki kuambiwa ni barabara inayounganisha bandari na sehemu ya kuu ya biashara katika

Inaendelea Uk. 19

Page 18: ANNUUR 1208

18 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

Israeli ni lazima ibebe j u k u m u k wa m a u a j i ya Waziri Abu Ein na uhalifu wake unaofanya dhidi ya wananchi wa Palestina wasio na hatia, huku mauaji hayo mapya yakitarajiwa kuwa na madhara makubwa.

Mauaji ya Abu Ein yal ikuwa ni tukio la kipekee, Kwa kweli ni miongoni mwa hatua za ukandamizaji na uhalifu wa kivita, unaofanywa na Israel wanaomiliki vikosi wakati wote dhidi ya Palestina inayokaliwa kimabavu.

Mwaka mmoja tangu mauaji ya Abu Ein, ni hasara kubwa ikiongezeka k w a W a p a l e s t i n a waliochukua hatua mpya tangu mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu.

Hiyo ndio hali tete iliyopo mjini Jerusalemu ya Mashariki na maeneo mengine yanayokaliwa k i m a b a v u n c h i n i Palestina,kufuatia uvamizi dhalimu na vitendo vya kinyama vya Israel i , pamoja na msimamo mkali wa walowezi wake dhidi ya wapalestina.

M a t o k e o y a k e n i mvutano unaoendelea na mateso ya kila siku kwa wapalestina wakiwemo w a t o t o , k u t o k a n a n a u k a n d a m i z a j i n a uchokozi wa Israeli,hali inayopelekea mauaji ya kila siku kwa wapalestina wasio na hatia.

Tunachokiona hasa upinzani usio na vurugu, k wa k u wa s h i r i k i s h a maelfu ya Wapalestina kwenye maandamano , kuelekea kwenye vituo vya ukaguzi vya Israeli, kwa lengo la kudai uhuru na haki zao.

M a r a k w a m a r a m a a n d a m a n o h a y o y a n a k u m b a n a n a mashambulizi ya jeshi l a I s r a e l i , a m b a l o h u t u m i a r i s a s i z a moto ili kuwatawanya waandamanaji hao wa k i p a l e s t i n a . H a t u a iliyopelekea kupoteza maisha ya wapalestina wasiopungua 108 tokea mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.

I s r a e l i i n a f a n y a ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu kwa wapalestina,hasa pale wanapowawekea vikwazo hata kuingia Msikiti wa Aqswa,huku jeshi hilo likijikita zaidi kimakazi mj in i J e rusa lemu ya mashariki na kufunga k a m e r a k a d h a a i l i k u f u a t i l i a i b a d a z a

wapalestina msikitini humo na eneo zima husika.

H i v y o t a t i z o n i kwamba asilimia 95 ya Wapalestina ni marufuku kufika Jerusalemu, Daktari mmoja alizaliwa huko na akafanya kazi ya udaktari kwa miaka 15, hata hivyo, tangu mwaka 2005, Israel inakataa kumruhusu aende huko , ingawa yeye ni mwanachama wa kuchaguliwa wa bunge Palestina.

Wakati huo huo kuna ongezeko kubwa la vurugu zinazofanywa na walowezi wa I s r a e l i d h i d i ya Wapalestina,zilizopelekea mauaji ya Mohammed Abu Khudeir akiwa na umri wa miaka 16, ambapo tukio hilo l i l i fanyika mnamo mwezi Julai 2014; baada ya kutekwa nyara na kuchomwa moto akiwa hai na walowezi wa Israeli.

Kwa mfano huu ni dhahiri kwamba,ukatili wa Israeli hauheshimu k a b i s a u h a i w a wapalestina wasio na hatia,wakitekwa,kupigwa na hata kuuwawa katika maeneo mbalimbali hasa Jerusalemu ya mashariki.

Mauaj i mengine ni yale ya Dawabshy akiwa na umri wa miezi 18, yaliyofanywa na walowezi wa k i ya h u d i k i j i j i n i Duma,mnamo tarehe 31 Julai 2015. Ambapo wal irusha mafuta ya petroli ndani ya nyumba ya familia yao usiku, hatua iliyopelekea kuchomwa mota hadi kufa,huku wazazi wake wakijeruhiwa vibaya na baadae baba yake kufariki dunia.

Mauaji haya mawili ni ujumbe tosha kwa jumuiya ya kimataifa na kwamba wananchi wa Palestina wanadai haki yao ili kujiokoa na ukandamizaji huu na mateso haya,yaliyopelekea kuuwawa wapalestina zaidi ya 108,wakiwemo watoto 24 ,wanawake 5,tangu mwanzo mwa mwezi Oktoba mwaka huu wa 2015.

Aidha, katika kipindi hiki zaidi raia wa Palestina 12,000 wameuwawa na wengine kujeruhiwa, kufuatia matumizi ya nguvu ya Israeli, ambapo s i l a h a m b a l i m b a l i hutumika zikiwemo risasi za moto, mabomu na kadhalika.

Mtu anaweza kuuliza: Kwa nini hii inatokea? B a a d a ya m i a k a 2 2 y a m a z u n g u m z o , Wapalestina waligundua kuwa barabara ya amani imefungwa na Israeli, inayotumia mwanya huo

katika kupanua makazi yake ya kilowezi, huku uvamizi huo wa Israeli ukidumu kwa zaidi ya miaka 48.

W a p a l e s t i n a w a l i l a z i m i s h w a k u k u b a l i y a l i y o j i r i katika makubaliano ya Os lo mnamo mwaka 1993 chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, lakini kwa bahati mbaya hakuna kilichowanufaisha wapalest ina zaidi ya maonevu, ukandamizaji na kuvunjiwa utu wao, kunakofanywa na Israeli ikisaidiana na walowezi wake waishio nchini Palestina.

Kwa upande mwingine idadi ya walowezi hao wa Israeli waliopo katika ardhi ya Palestina imeongezeka sana ndani ya muda wa miaka 22,ambapo wamefikia kutoka 115,000 hadi 650,000.

Wa z i r i M k u u w a Israeli Netanyahu anadai

k w a m b a , m a p i g a n o yanayoendelea hivi sasa ni matokeo ya uchokozi k u t o k a u p a n d e w a Palestina,hivi ndivyo walivyo madikteta na viongozi wa kimabavu daima hufanya hivyo badala ya kutafuta mizizi na chanzo cha mgogoro.

Chanzo cha mgogoro ni Israeli kujitangazia umiliki wa sehemu ya ardhi ya Palestina kuwa ni yake,hasa Jerusalemu ya Mashariki tokea miaka 48 iliyopita,hali iliyopelekea k u we k a v i z i w i z i i l i kutenganisha mji huo na Ukingo wa magharibi ili kuhodhi ardhi yote ya Palestina.

Dola ya Palestina tayari imekabidhi ushahidi wake wa uhal i fu wa kivita, unaofanywa na Israeli dhidi ya Palestina na wananchi wake kwa Mahakama ya Uhalifu ya K i m a t a i f a ( I C C ) , i l i kuongeza kasi ya

uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na Israeli.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Mheshimiwa “Riad Maliki” alisema: "Suala la Palestina ni mtihani kimatai fa . . . m t i h a n i h u o d u n i a ikiushindwa itakuwa ni hasara si kwa Palestina tu bali kwa Ulimwengu mzima, kwani Palestina imeamua kutafuta haki, si kisasi."

Kama hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini aliyepambana na ubaguzi wa rangi alisema, suala la Palestina ni ukweli na haki kuliko suala tulilonalo ".

Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road – Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 E m a i l : p i c t @ p a l - t z .orgWebsite: www.pal-tz.org

MAKALA/HABARI

Chuki dhidi ya Waislamu inakolea MarekaniInatoka Uk. 20zaidi ya asilimia 57 ya wananchi wa Marekani wanapinga matamshi hayo ya chuki za kidini ya Donald Trump.

Mamia ya wanaharakati wa k i j a m i i n a h a k i z a b i n a d a m u n c h i n i Marekani, walikusanyika Alhamisi iliyopita mbele ya hoteli moja kubwa inayomilikiwa na Trump, ili kuonesha hasira zao dhidi ya mwanasiasa huyo mwenye chuki za kidini.

K u n a u w e z e k a n o Donald Trump akateuliwa na chama cha Republican k u g o m b e a u r a i s wa Marekani.

Waliojumuika mbele ya hoteli hiyo kulaani matamshi ya chuki za kidini ya Trump ni pamoja na kutoka Jumuiya ya Waislamu wa Marekani, Taasisi ya Kulinda Haki ya Uhuru na Katiba, Kanisa la Marekani na Maveterani wa Vita wa Marekani.

W a c h a m b u z i w a mambo wanaamini kuwa, mashambulio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni mjini Paris Ufaransa, yametoa fursa kwa maadui wa U i s l a m u k u p a t a kisingizio cha kuzidi kuonesha chuki zao dhidi ya Waislamu.

Lakini bado duniani wapo watu wenye fikra

huru, ambao wanaelewa vyema kuwa vitendo vya kigaidi vinavyofanywa kwa jina la Uislamu, havina mfungamano wowote na dini hiyo tukufu.

Wakati ubaguzi dhidi ya Waislamu ukikolea, Mwanafalsafa maarufu n c h i n i h u m o N o a m Chomsky, ameilaumu Marekani kwa kukithiri hali hiyo.

M c h a m b u z i h u y o mashuhuri wa masuala ya kisiasa nchini Marekani, amesema ser ika l i ya Washington na washirika wake wanafaa kulaumiwa kutokana na mashambulio ya kigaidi ya mwezi uliopita yaliyoitikisa Paris, mji mkuu wa Ufaransa.

C h o m s k y , a m b a ye pia ni mwanafilosofia a l i s e m a h a t u a y a

Marekani kuzivamia Iraq na Afghanistan imekuwa chanzo na chimbuko la harakati za ugaidi duniani.

Katika mahojiano na televisheni ya PressTV ya Iran, msomi huyo wa Marekani alisema serikali ya Washington na washirika wake wana chaguo la kuutokomeza ugaidi duniani iwapo watakuwa na irada ya kisiasa.

A m e o n g e z a k u wa , u g a i d i n a h u s u s a n kama unaoendelezwa n a k u n d i l a D a e s h , hauwezi kumalizwa kwa mashambulizi ya kijeshi tu.

Katika tukio la kigaidi la Novemba 13 mjini Paris, Ufaransa watu zaidi ya 130 kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa.

DONALD Trump.

Uhalifu wa kivita wa Israeli dhidi ya PalestinaInatoka Uk. 11

Page 19: ANNUUR 1208

19 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

MAKALA

KAMA kuna sehemu a m b a y o K a n i s a limefanikiwa kubatiza Wais lamu, bas i n i W i l a y a y a S a m e . Majina kama Marry O m a r i , E l i e w a h a Kathimu, Natujwa Emanuel Mohammed, Yohane Mathayo Saidi, Nthembia Kathibeti Rajabu, ni ya kawaida kabisa kuonyesha kuwa awali baba na babu wa vijana wa sasa walikuwa Waislamu, lakini watoto na wajukuu, wameishia kubatizwa.

Unapofanya utafiti kidogo unachogundua ni kuwa japo Uislamu ulikuwa wa mwanzo kuingia, lakini baada ya watu kuingia katika U i s l a m u k u p i t i a Maulidi na Muridi wa Twarika, hapakuwa na mwendelezo wa kuwasomesha. Kwa hiyo wengi wakabaki Waislamu wa majina. N a h a t a b a a d a e i l ipoku ja Bakwata , h a i k u s h u g h u l i k a n a k u w a e l i m i s h a W a i s l a m u , i l a kudumisha ukiritimba wa umiliki wa Misikiti na kuhakikisha hakuna anayeingia kusomesha b i l a k i b a l i c h a o wakati wao wenyewe h a w a k u w a t a y a r i kupeleka mwalimu.

K i n y u m e c h a k e , walipoingia Wakristo walikuja kama watu wenye ‘misheni’ maalum ya kufuta Uis lamu wakianzia milimani na kumalizia tambarare. Pamoja na kujenga makanisa, walijenga shule na hospitali, lakini pia kila aliyebatizwa walihakikisha kuwa anausoma Ukristo na kukomazwa kiimani kupitia taratibu zao za Kikanisa.

Same Milimani wakati awali katika miaka ya 1940s mpaka 1960s, i l ikuwa Mkris to ni wa kutafuta, hivi sasa i m e k u wa k i n y u m e chake. Kuna baadhi ya vijiji kama utauguwa uambiwe kwamba dawa ni kumpata Muislamu wa eneo hilo, akushike kichwani, basi itabidi ufe tu.

Ukiingia katika milima ya Vudee unakutana na

Hali ya Uislamu Vudee

HUU ni msikiti wa Ndolwa /Mjingo kama unavyo onekana katika picha juu. Hapa ni waumini wakisikiliza hotuba ya Ijumaa. Imam ni Mwalimu wa shule aliyehamia kijijini hapo karibuni. Anajaribu kuokoa jahazi kwa anachokijua.

vimsikiti viwili, chakavu vilivyoachana

k w a m a s a f a yasiyopungua kilomita 4 0 . M s i k i t i m m o j a ukiitwa Breni ambao uko njiani na ulinyanyuliwa mwaka 1998 baada ya kuachwa kwa muda mrefu na kuanguka. Idadi ya waumini wake ni 50 chini ya Imamu Salim.

Msikit i mwingine ni ule wa Ndolwa /Mjingo ukiwa chini ya Mwenyekiti Omari Danieli na Imamu akiwa

Mwalimu Ali Hamad Ali. Waumini katika msikiti huu ni 36. Pamoja n a k u p i g i wa m b i u kwamba kungekuwa na ugeni, siku tuliyofika msikitini hapo waumini walioswali siku hiyo ni wanaume 9 wanawake 4 watoto wa kike 3 na wavulana 3.

Kama nilivyotangulia kusema, tat izo kuu katika eneo hili ni Elimu. Idadi ya Wais lamu inapungua siku hadi siku kwa kubatizwa. Ikichangiwa na hali

ngumu ya kiuchumi ambapo Kanisa hutumia fursa hivyo kugawa chakula cha msaada na msaada wa masomo kwa watoto, basi ndio kabisa masalia ya Waislamu, yanazidi kukombwa.

Msikiti wa Ndolwa amejenga Mzee Omari Danieli na familia yake, lakini ndio uwezo wake u m e f i k i a m w i s h o . Wamepiga matofal i lakini hawajayachoma. Waumini wanaosali h a p o I j u m a a k w a Ijumaa, ni familia yake na majirani na Waislamu wa Kijiji cha Mjingo.

Msikiti wa pili Imamu wake anasema kuwa Waislamu wa eneo hilo ni kiasi cha hamsini. Kuhusu kuritadishwa, anasema kuwa hilo l imekuwa ni jambo la kawaida na ni kwa s a b a b u Wa i s l a m u hawana elimu ya msingi ya dini yao. Na hata yeye mwenyewe anasema hana elimu ya kutosha, lakini imebidi awe ndio kuiongozi.

Ombi la Waislamu wa Vudee na Same milimani kwa ujumla, ni kuwa wasaidiwe kusomesha

vijana wa pale pale wanaume na wanawake angalau elimu ya msingi ya dini ya Kiislamu ili waje kuwa walimu. Jingine ni kusaidiwa kujenga hiyo misikiti iwe na hadhi ya Msikiti pamoja na udogo wake.

Kwa vile ibada na Uislamu pekee katika maeneo hayo ni swala ya Ijumaa na Eid, watu wakishamaliza kuswali, virago (madathi), au t u s e m e m i s w a l a hukunjwa na kuwekwa juu ya dari ili isiliwe na mchwa.

M w e n y e k u t a k a kupeleka msaada huko, akiwa ana gari barabara ni nzuri ila gari iwe na uwezo wa kupanda milima na dereva awe mzoefu wa kupanda milima. Hata gari za Noah zinapanda huko. Wanaweza kupeleka misaada moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Msikiti Mzee Omari Danieli, Kwa namba 0674 045 986/0787 134 554.

Au kama unatuma v i f a a t u m a K w a Amiri wa Kamati ya Kuendeleza Uislamu (W), Same, Khatibu Juma Mziray Juhudi Studio, Box 62, simu, 0757 013 344. Same.

Wahafidhina mnatupeleka wapi?Inatoka Uk. 17kisiwa hicho.

Barabara ya Chake Chake- Wete maarufu njia kongwe, licha ya kuwa nayo ipo katika maeneo yanayotoa utajiri huo, ni barabara yenye mashimo matupu utafikiri ni shamba ambalo mkulima amelitayarisha kwa ajili ya kupanda migomba.

Katika hali ya barabara hizi mgonjwa anaweza kufika akiwa huko hali gani, kwenye yale majengo ambayo yanayoitwa spitali kama sio hoi bin taabani licha ya maradhi aliyonayo na hivo ukifika huko ni majengo yasiyokuwa

na hata panadoli licha ya fedha nyingi zinazoingia kwa zao hili.

Zitoweni faida za rasilimali za visiwa vyetu kwani hii ni haki ya wote tunahitaji jasho letu liimarishe huduma za afya, elimu maji na huduma nyinginezo na sio kujinufaisha matumbo yenu pekee.

Kwa hali inavoelekea ni mbaya isiyopigika mfano au kufikirika kabisa hasa kwa visiwa vyenye ustaarabu wa hali ya juu, yaani visiwa vyetu vya Zanzibar na hapo ndio ninapowauliza wahafidhina ni wapi hasa mnakotupeleka?

Page 20: ANNUUR 1208

20 AN-NUURRABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 201520 MAKALA AN-NUUR

20

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RABIUL AWWAL 1437, IJUMAA DESEMBA 18-24, 2015

HAIIBA TIMAMU TEA CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)

UGONJWA WA MOYO KIHARUSI JONGO (GOUT) MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM) MAUMIVU SUGU YA KICHWA BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS) MAGONJWA YA INI SARATANI MBALIMBALI UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY INCONTINENCE)

ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI PUMU UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI KASI YA KUZEEKA MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU

MKAKAMO WA NGOZI; UDHAIFU WA MACHO KUPOTEZA KUMBUKUMBU KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA MAKOVU KWENYE MAPAFU UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI, YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA INAPATIKANA

HERBAL IMPACT

MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI, DAR ES

SALAAM

TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU NAMBA:

0754281131/0655281131/0686281131/0779281131

UVIMBE KWENYE MATITI WAYEYUKA NDANI YA SIKU 3!

Na. Rahma Rashidi

Miezi michache iliyopita niligundua kuwa matiti yangu yalikuwa yameota mauvimbe kadhaa ndani. Niliogopa sana. Nilimweza mume wangu na kumwambia apapase ili aweze kujihakikishia. Alipofanya hivyo alitoa macho kwa woga. Aliniambia nifanye subra atafakari ni nini kifanyike. Jioni aliporudi alikuja na kibokisi kimoja kilichokuwa kimeandikwa ‘Haiiba Timamu Tea’. Aliniambia kuwa niitumie hiyo chai kwa sababu alikuwa ameambiwa kuwa inaweza kunisaidia. Niliitumia hiyo chai kwa siku tatu na ghafla nikakuta yale mauvimbe yametoweka! Imepita miezi kadhaa sasa sijaona mauvimbe yale yakirudi. Hata hivyo kama tahadhari nimeamua niwe natumia hii chai mara kwa mara.

https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

VITENDO vya chuki d h i d i ya Wa i s l a m u vimeongezeka nchini Marekani.

Watu wenye chuki za kidini wameuchoma moto Msikiti mwingine huko California.

Wakuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Marekani walisema Ijumaa iliyopita kuwa, watu wenye chuki za kidini walitupa bomu la chupa ndani ya Msikiti wa Coachella, California na kusababisha msikitini humo kuwaka moto.

Polisi wa Marekani wameanza uchunguzi k u b a i n i s a b a b u z a kuchomwa Msikiti huo na kuchunguza kama jinai hiyo inatokana na chuki za kidini au la.

C h u k i z a k i d i n i zimeongezeka nchini M a r e k a n i b a a d a ya mkwasi wa mali Donald T r u m p , a n a ye wa n i a kuteuliwa na chama cha

Chuki dhidi ya Waislamu inakolea MarekaniMisikiti inachomwa moto

Republican kugombea urais nchini humo, kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu.

Siku moja baada ya kutoa matamchi yake ya kutotakiwa Waislamu k u i n g i a M a r e k a n i , yaani siku ya Alhamisi, maadui wa Uis lamu waliuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa mji wa Philadelphia huko Marekani.

Vile vile Ijumaa hii iliyopita, ofisi za Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uis lamu la mj ini Washington, zilifungwa baada ya kuenea habari kwamba maadui wa U i s l a m u w a l i t a k a kuzil ipua kwa bomu baada ya kupatikana kifurushi cha kutatanisha katika ofisi hizo.

Awali Maafisa wengi wa usalama wa Marekani walionya kuwa, matamshi ya kichochezi ya Donald

Trump, yataongeza chuki na mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo.

T r u m p a m e i t a k a serikali ya Marekani ipige marufuku kuingia Waislamu nchini humo bila ya kujali wanatokea wapi.

Matamshi hayo ya

kichochezi yanaendelea k u l a a n i w a k o t e ulimwenguni.

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Ikulu ya Marekani White House na Mashirika mbalimbali kutoka pembe zote za d u n i a wa m e e n d e l e a kulaani matamshi hayo

ya chuki za kidini ya mwanasiasa huyo wa chama cha Republican cha Marekani.

Hata hivyo uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya NBC News na gazeti la Wall Street Journal unaonesha kuwa,

Inaendelea Uk. 18

Changia damu okoa maisha kwani sote ni wagonjwa watarajiwa.

Tunaomba watu wote kuchangia damu kwa hiari siku ya Jumamosi tarehe 19/12/2015 katika Hospitali za Temeke na Mbagala Rangi tatu iliyopo Zakheem kuanzia saa 1:00 asubuhi.

Nyote mnakaribishwaLimetolewa na Jumuiya ya JAE-Temeke.

JAE JAE JAE