fataawa za wanachuoni (32)
DESCRIPTION
Fataawa Za Wanachuoni (32)TRANSCRIPT
1
فتاوى العلماءFataawa Za Wanachuoni
[32]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizo:
1) Lini Mtu Anaomba Du´aa Ya Istikhaarah?
2) Kutoka Katika I´tikaaf Na Kwenda Kuswali Tarawiyh Msikiti Mwingine
3) Kuinua Kidole Wakati Wa Kusema "Laa ilaaha Illaa Allaah"
4) Inafaa Kumuuliza Mtu, Vipi Imani Yako?
5) Yule Asiyewafanyia Tabdiy´ Watu Wa Bid´ah
6) Vijana Wanavyowekwa Mtegoni Kwa Mawaidha Ya Visa
7) Wale Wanaosema Kuwa Shaykh al-Albaaniy Ni Murji´iy
8) Uwajibu Wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Na Jamaa´at-ut-Tabliygh
9) Mume Anataka Mke Avae Suruwali
10) Mtoto Wa Baba Mdogo Ni Mahram?
11) Mbinu Za Hizbiyyuun Kumbadiy´ Imaam Ibn Hajar Na an-Nawawiy
12) Makatazo Ya Kumuacha Mke Na Mtumishi Mwanamume
13) Majumba Yaliyojengwa Kwenye Makaburi Ya Mawalii
14) Kuuza Manukato Ambayo Yana Alcohol
15) Kusoma al-Mu´awidhaat Mchana Wakati Wa Kulala
16) Kusikiliza Mikanda Ya ´Aa´idh al-Qarniy Na Twaariq as-Swaydaan
17) Kusherehekea Mwaka Wa Hijriyah Na Kuzaliwa Na Kupeana Pongezi
18) Kumkosoa Mtawala Juu Ya Minbar
19) Kujumuisha Swalah Wakati Wa Mvua, Upepo Na Barafu
20) Je Kuna Kundi Linaitwa Jaamiyyah? Na Ni Nani Shaykh Muhammad al-Jaamiy?
21) Ipi Tofauti Kati Ya ´Aqiydah Na Manhaj?
22) Inajuzu Kula Samaki Maiti Ambayo Haikuchinjwa?
23) Hukumu Ya Mwenye Kumtukana Allaah Na Mtume Wake
24) Shaykh Fawzaan Kuhusu Radd Kwa Sayyid Qutwub
25) Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalah Ya Dhuhaa
26) Kabla Ya Kutumwa Mtume Watu Walikuwa Katika Dini Ya Nani?
27) Je Sigara Inavunja Wudhuu? Na Ipi Hukumu Ya Sigara Na Bangi?
28) Nasaha Kwa Dada Wapya Waliyoingia Katika Uislamu -1-
29) Nifuturu Nyumbani Kwangu Au Msikitini Nikaapo I´tikaaf?
30) Nasaha Kwa Dada Wapya Waliyoingia Katika Uislamu -2-
31) Mume Kamlaani Mke Wake, Je Mke Katalikika?
32) Mavazi Yenye Picha Za Watu Na Minyama Na Maneno Mabaya
33) Kuna Aina Tatu Kwa Wenye Kuyatembelea Makaburi
34) Kutabaruku Kwa Mabaki Ya Mtume ( وسلم عليه هللا صلى )
35) Jinsi Ya Kuweka Nia Unapotaka Kuanza Kukaa I´tikaaf
36) Inajuzu Mume Kumkabili Mke Wake Usoni?
37) Hukumu Ya Mtu Mwenye Kuitukana Dini
38) Inajuzu Kwa Mwanamke Kufanya Kazi Ya Uuguzi Katika Mji Wa Kikafiri?
39) Muislamu Kupenda Nchi Ya Kikafiri
40) Mambo Gani Yanayofanya Mwanamke Akawa Na Msimamo Katika Dini?
41) Kuwa Na Subira Katika Da´wah Kwa Kupewa Mitihani
42) Kuna Mpaka Wa Mtu Kukaa Itikaaf Msikitini?
4
43) Ipi Faradhi Ya Kwanza Kubwa?
44) Hukumu Ya Kuhudhuria Janaza Na Kuwasalia Watu Wa Bid´ah
45) Amevaa Soksi Kisha Akazivua, Vipi Wudhuu Wake?
Wanachuoni waliomo:
1) ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
2) ´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad
3) ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
4) ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
5) ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
6) ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
7) ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
8) Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1) Lini Mtu Anaomba Du´aa Ya Istikhaarah?
Swali:
Lini mtu anasoma Du´aa ya Istikhaarah, je inasemwa ndani ya Swalah au
baada ya Swalah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni baada ya kutoa Salaam.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5485
2) Kutoka Katika I´tikaaf Na Kwenda Kuswali Tarawiyh Msikiti
Mwingine
Swali:
Nataka kukaa I´tikaaf kwa sharti niswali Tarawiyh katika Msikiti mwingine
kutokana na kisomo cha Imamu huyo, je inajuzu kwangu kufanya hivyo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Inajuzu kwako, ila kuacha ni bora zaidi. Bora kwako ni wewe kuswali
Tarawiyh katika Msikiti ambao unafanyia I´tikaaf. Hili ndo bora ili ubakie
Msikitini ambapo wewe unafanyia I´tikaaf.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2658
6
3) Kuinua Kidole Wakati Wa Kusema "Laa ilaaha Illaa Allaah"
Swali:
Je kunyanyua (kuinua) kidole cha Shahadah wakati wa kusema "laa ilaaha illa
Allaah" ni katika Sunnah?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kumepokelewa katika hili Athaar, kunyanyua kidole wakati wa Tashahhud
na kukitikisa kumepokelewa Hadiyth hata kama [baadhi yazo] ni dhaifu. Ama
kukitikisa ni wakati wa Du´aa. Atakayeshahidilia laa ilaaha illa Allaah na
akapandisha kidole hakuna ubaya kwake.
Chanzo: http://youtu.be/Ey6xPqior08
4) Inafaa Kumuuliza Mtu, Vipi Imani Yako?
Swali:
Je ibara hi ni nzuri "Vipi Imani yako"? Na je ni katika Sunnah?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kutasaahul huku hakuna faida, [kumuuliza mtu] "vipi Imani yako?" Imani
anaijua Allaah (´Azza wa Jalla) ndani ya moyo, [kinachotakiwa] ni
kunasihiana. Wakikutana Waislamu wawili, kinachojulikana ni kila mmoja
kumpa nasaha mwenziwe kwa kuwa na subira katika Dini na kuwa na
uthabiti na kuwalingania watu kwayo. Na imepokelewa kuwa Salaf
(Maswahabah) walikuwa hawaachani wanapokutana mpaka wasome kwanza
Suurat al-´Aswr:
7
"Naapa kwa Zama! Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara, Ila
wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na
wakausiana kusubiri.” (103:1-03)
Chanzo: http://youtu.be/8XzIxfQ3TDI
5) Yule Asiyewafanyia Tabdiy´ Watu Wa Bid´ah
Swali:
Ulisema jana kuwa yule ambaye hambadiy´ mtu wa Bid´ah haingii katika
mkumbo wa watu wa Bid´ah na si lazima amfuate yule anayembadiy´. Na
baadhi ya wanachuoni wanasema yule ambaye hambadiy´ mtu wa Bid´ah
anaingia katika mkumbo wao. Je, tofauti katika hili ni ya lafdhi tu?
´Allaamah ´Abdul-Muhsin al-´Abbaad:
Kuna watu wa Bid´ah ambao Bid´ah zao na mambo yao yako wazi. Wako
mbali kabisa na Ahl-us-Sunnah na si hata katika Ahl-us-Sunnah bali
wanaiharibu hata Sunnah. Sunnah iko huko na wao wako kule. Watu hawa
yule asiyewabadiy´ bila shaka naye ni Mubtadiy´. Ama watu ambao ni katika
Ahl-us-Sunnah na wakaanguka katika kitu kama kosa au ufahamu wa
makosa, watu hawa si kama wale wa kwanza. Hapa mtu hawezi kusema yule
asiyemfanyia Tabdiy´ huyu ni Mubtadiy´.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127855
6) Vijana Wanavyowekwa Mtegoni Kwa Mawaidha Ya Visa
Swali:
8
Ipi nasaha yako kwa vijana wengi ambao wamejishughulisha sana kusambaza
mikanda ya wapiga visa na watoa mawaidha na wanapuuza kusambaza
mikanda ya kielimu (ya wanachuoni)?
´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy:
Yule anayejishughulisha na mikanda hii, mikanda ya watoa mawaidha ambao
naamini wamewawekea daraja watu wa Bid´ah na mapote... Watu wa Bid´ah
na mapote wanapata nguvu kwa sura ya watu hawa. Wanawawinda vijana.
Wanaanza kwa mawaidha, kulia, unyenyekevu. Wanajidhihirisha namna hii
mbele ya vijana. Pindi wanapojisikia salama na hakika kwao, wanawaweka
katika nafsi zao utata na wanawatuma kwa hao ambao wamewapa kazi hio ya
kuwawinda [hawa] vijana. Na ndo maana utaona hawa watoa mawaidha
wamejidhatiti ima kwa pote potofu au makundi maangamivu. Hukuti Salafiy
humo, na wala hawana uhusiano na Salafiyyuun. Bali wanawafanyia shere na
hila Salafiyyuun na wanatahadharisha kupita njia yao. Wanasema wanakaza
sana, matusi na kadhalika. Na wanawasahilishia watu kutumbukia na watu
wa Bid´ah.
Mimi ninawanasihi vijana Masalafiy kujishughulisha na elimu sahihi na
Manhaj ya Salaf sahihi. Ikiwa wanataka mawaidha, yapo katika Kitabu cha
Allaah, kama wanataka elimu ipo katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kama mlivosikia katika
Hadiyth ya al-´Irbaadh Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa
anapotoa mawaidha, nyoyo zinatetemeka na macho yanatiririka machozi. Na
wakati mwingine walikuwa wakilia sana. Atakayesoma kwa mfano Riyaadh-
us-Swaalihiyn ataona kuwa kuna yakutosheleza katika Sunnah za Mtume wa
Allaah ili mtu asiwe na haja ya kuwasikiliza watu kama hawa.Na mawaidha
yao unakuta yamejaa Bid´ah, ukhurafi na Hadiyth dhaifu na za kuundwa.
Yote ni kwa kuwa hawa Madu´aat si maulamaa. Na Salaf walikuwa
wakiwadharau hawa wapiga visa, wakitahadharisha watu dhidi yao na uongo
wao. Kwa masikitiko makubwa ni hivyo! Kwa hali yoyote Manhaj ya Salaf iko
wazi. Na tunawanasihi vijana kama kweli wanataka mawaidha na mafunzo,
yapo ya kutosha katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
9
Aliulizwa Abuu Haatim kuhusu vitabu vya al-Haarith al-Muhaasibiy.
Alikuwa ni mjuzi, mchaji Allaah kuliko watu hawa watoa mawaidha. Na
alikuwa mbali kabisa na Bid´ah kuliko watu hawa. Kulipatikana katika vitabu
vyake kitu kama Taswawwuf ambayo haiwezi kukosa katika mawaidha ya
watu hawa.
Aliulizwa Abuu Zur´ah, Imaam mkubwa wa Sunnah kuhusu vitabu vya al-
Haarith.
Akasema: "Viacheni. Ni vitabu vya upotofu na Bid´ah." Wakasema vina
mafunzo.
Akasema: "Yule ambaye hakupata mafunzo katika Kitabu cha Allaah, hawezi
kamwe kupata mafunzo kwa hivyo."
Ndugu! Hii ndo Manhaj ya Salaf! Walikuwa wakitahadharisha vitabu vya
watu wa Bid´ah na mtu kuviangalia. Na walikuwa wakitahadharisha falsafa
kwa kuwa ni Bid´ah na upotofu. Shikamaneni na Kitabu cha Allaah na Sunnah
za Mtume Wake na Manhaj ya Salaf-us-Swaalih. Wallaahi naapa yule ambaye
kaanguka kwa watu hawa atakuja kupotea. Na mwenye kufaulu ni yule
mwenye kuchukua funzo kwa makosa ya wengine. Chukueni funzo kwa
vijana waliopotea waliokuwa katika Manhaj ya Salaf. Mwisho wao uliishia na
taawili potofu na propaganda za batili mpaka hapo walikuja kuwa maadui
wakubwa wa Ahl-us-Sunnah.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=123813
7) Wale Wanaosema Kuwa Shaykh al-Albaaniy Ni Murji´iy
Swali:
Kuna baadhi ya watu wanasema kuwa Shaykh al-Albaaniy ni Murji´iy.
Unasema nini kuhusu hili?
´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy:
10
al-Albaaniy ni mwanachuoni katika maulamaa wa Sunnah, na Imaam
mkubwa katika maimamu wa Sunnah. Katumia maisha yote kulingania katika
Sunnah. Katumia zaidi ya miaka sitini kwa kutumikia Sunnah za Mtume
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ana vitabu kuhusu ´Aqiydah, na ana
vitabu vinavyosafisha Sunnah za Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam) katika Hadiyth dhaifu na zilizoundwa. Ni nyingi sana. Na ana
vitabu vya Hadiyth Swahiyh na ni mijaladi mikubwa. Pia katumikia Sunnah
kwa njia zingine. Isitoshe alihakiki vitabu vingi vya Salafiyyah. Ana vitabu
kuhusu ´Aqiydah, [kwa mfano] "Tahdhiyr-us-Saajid min Ittikhaadh-il-Qubuur
Masaajid, "at-Tawassul-Anwaa´uh wa Ahkaamuh", "al-Aayaat al-Bayyinaat"
na sherehe na taaliki zake katika al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah". Alihakiki
vitabu vingi vya Iymaan, kama kitabu cha Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin
Sallaam, Ibn Abi Shaybah na Ibn Taymiyyah (Rahimahumu Allaah).
Kaitumikia Sunnah kwa kitabu "Manzilat-us-Sunnah Fiyl-Islaam", "Difaa´
´anal-Hadiyth an-Nabawiy" na "al-Hadiyth Hujjah fiyl Nafsih fiyl´-´Aqaa´id
wal-Ahkaam". Ni Radd kwa watu wa Bid´ah. Katika vitabu hivi kuna Ruduud
kwa Murji-ah na wengineo. Alikufa baada ya kuupiga vita Uirjaa´ na Murji-
ah. Yule anayesema kuwa ni Murji´iy, yeye ndo Khaarijiy mpotofu. Wamche
Allaah watu hawa na waseme ukweli. Waache kumsema vibaya mtu huyu na
mfano wake. Wahifadhi ndimi zao. Ni katika maimamu wa Sunnah. Sijawahi
kuona yeyote katika karne hizi za mwisho akipigana na Bid´ah kama yeye.
Vitabu vyake vingi kama "Swifah Swalat-in-Nabiyy" na "Hajjat-un-Nabiyy" na
vinginevyo, anahitimu kwa kuwashambulia watu wa Bid´ah. Kweli mtu
anaweza kusema kama huyu mtu ni wa Bid´ah na Murji´iy? Kamwe maishani.
Chanzo:
http://www.sahab.net/forums/index.php?s=912150d01f48950f1dec3ef1af7c98ab
&showtopic=127805
8) Uwajibu Wa al-Ikhwaan al-Muslimuun Na Jamaa´at-ut-Tabliygh
Swali:
11
Ulisema katika darsa iliopita kuwa kundi la al-Ikhwaan al-Muslimuun na
Jamaa´at-ut-Tabliygh si katika makafiri, bali ni katika Ahl-ul-Bid´ah. Je, ni
katika makundi mapotofu yatayoangamia kama ilivyokuja katika Hadiyth ya
mgawanyiko?
´Allaamah al-Fawzaan:
Sikumbuki kama nilisema kauli hii, ila maana yake [kauli hii] ni sahihi. Si
makafiri In Shaa Allaah. Lakini wako na wanaenda kinyume kutokana na
Manhaj ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Da´wah, wako na
mambo wanaenda kinyume. Ni wajibu kwao kusahihisha makosa yao na
wawe katika Manhaj sahihi - Manhaj ya Da´wah na walinganie katika
Tawhiyd na wakataze Shirki. Huu ndo wajibu. Lakini hatujawahi kusikia
wakikataza Shirki, na wala hatujawahi kusikia wakilingania [watu] katika
Tawhiyd. Huu ni upungufu mkubwa na Da´wah haiwezi kuwa sahihi kwa
mfumo huu.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127630
9) Mume Anataka Mke Avae Suruwali
Swali:
Ipi hukumu ya kuvaa suruwali mbele ya mume kwa lengo la kumpambia tu
na si [kwa lengo] la kujifananisha [na makafiri]?
Shaykh Dr. ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy:
Haya ni maneno yako wewe. Makusudio hayahalalishi kilichokatazwa. Kuvaa
suruwali mbele ya mume au wengine, huku ni kujifananisha na makafiri.
Isitoshe si hata nzuri kwa kuwa inadhihirisha uchi wa mwanamke au nusu ya
uchi wake, jambo ambalo ni baya. Na si katika ada ya wanawake wa Kiislamu,
si wa mama wa Waislamu wala baada yao kutokana na tunayojua. Na wala
12
sijasoma kama kuna mwanachuoni katoa Fatwa ya kujuzisha hilo. Mwanamke
anatakiwa kuvaa vazi la wasaa. Ni kweli mbele ya mume hahitaji kuwa na
mtandio, hahitaji Jilbaab. Anaweza kudhihirisha baadhi ya ´Awrah
anapokwenda huku na kule. Hili si katika mapambo hata kama baadhi ya
watu wajinga watamtaka asifanye hivyo, ima kwa ujinga au kwa Taqliyd kwa
baadhi ya watu wamakosa ambao wanafuata kichwa wana-askari wa kikafiri
wa mashariki na magharibi. Sisi tunawanasihi mabanati wetu wa kiislamu
wajifananishe na Waislamu wa kwanza katika wamama wa Waislamu (wake
za Mitume), Maswahabah wa kike, waliokuja baada yao na wa baada yao. Iwe
kwenu, kwetu na katika kila kona ya Kiislamu hata walioko nje kuwa na
wanawake wazuri wanaoelewa Sunnah na waipende. Hivyo wasije kuwaiga
makafiri.
Muulizaji:
Shaykh ikiwa mume atamuomba hili, na kuwa jambo hili analichukulia
pambo kwake [mume].
Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
Huyu kageuzwa nyuma na mbele. Huyu kapinda na ni mjinga. Na nadhani ya
kwamba kakuzwa kwa musalsalaat (series) na programu za uchi
zinazorushwa kwenye Video na nyinginezo. Mimi namnasihi amche Allaah
(´Azza wa Jalla) kwa mke wake na amsaidie kwa kumcha Allaah. Wala
asimtii. Kwa kuwa hakuna utiifu kwa kiumbe kwa kumuasi Muumba.
Kujifananisha na makafiri ni jambo limekatazwa.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127839
10) Mtoto Wa Baba Mdogo Ni Mahram?
Swali:
13
Je, mtoto wa mama yangu mdogo ni katika Mahram wangu, na inajuzu
kukabiliana naye uso?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ndio, kwa kuwa ni katika Mahram wako. Maadamu ni Mahram wa baba yake
basi atakuwa Mahram wake [huyo mwanaume pia].
Chanzo: http://youtu.be/lha0R_pgG7M
11) Mbinu Za Hizbiyyuun Kumbadiy´ Imaam Ibn Hajar Na an-Nawawiy
Swali:
Hizbiyyuun wanasema, kwa nini mnatahadharisha watu dhidi ya vitabu vya
Qutbiyyuun na Suruuriyyuun na hamtahadharishi dhidi ya vitabu vya Ibn
Hajar na an-Nawawiy kwa kuwa nao walikosea katika masuala ya ´Aqiydah?
´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy:
Maneno ya ajabu kabisa ya kuchekesha. Ni kweli enyi ndugu. Hivi kweli
tunaweza kulinganisha vitabu vya Sayyid Qutwub, au Muhammad Suruuriy
na mtu kama Imaam an-Nawawiy, Ibn Hajar? Kamwe maishani! Hawa ni
wapotofu masikini, na wale ni maimamu wakubwa wenye hadhi kabisa na
waaminifu. Ibn Hajar ni mwanachuoni wa Hadiyth na sidhani kama kutakuja
baada yake ambaye anaweza kuchukua nafasi yake. Hali kadhalika an-
Nawawiy ambaye ni mwanachuoni katika Fiqh na ana ufahamu mkubwa sana
fani hii. Ahl-us-Sunnah walibainisha makosa ya Ibn Hajar na an-Nawawiy
katika vitabu maalum, Allaah Awajaze maulamaa wetu kheri. Ama nyinyi
hamna hadhi hio ya watu kujishughulisha na vitabu vyenu. Ni kina nani
nyinyi? Karibu Uhizbiyyah utaisha hivi punde.
14
Chanzo: http://aloloom.net/show_sound.php?id=8677
12) Makatazo Ya Kumuacha Mke Na Mtumishi Mwanamume
Swali:
Ikiwa [mume] siniko nyumbani na kuko mke wangu na watoto wake wadogo,
inajuzu kwa mtumishi kuingia nyumbani kwa ajili ya kufanya usafi
nyumbani?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Nyumba ikiwa imejaa wanawake hakuna ubaya kuingia. Ama ikiwa ni baina
yake [mtumishi] na huyo mwanamke haijuzu kwake kuingia. Haijuzu kwa
mume kuridhia hili.
Muulizaji:
Mke wangu yuko nyumbani na watoto wadogo.
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Sio Mahaarim wake [hao watoto wadogo].
Chanzo: http://youtu.be/DQt3tcsOIyY
13) Majumba Yaliyojengwa Kwenye Makaburi Ya Mawalii
Swali:
15
Katika mji wetu kuna majumba ambayo yamejengwa kwenye makaburi ya
mawalii. Lakini hakuna anayeswali hapo wala kufanya chochote,
yamefungwa. Miaka kadhaa ya nyuma walikuwa wakiyafanyia ziara, ila kwa
sasa imesimama. Je, ni wajibu kuyabomoa au kuyaacha?
´Allaamah al-Fawzaan:
Ni wajibu kuyabomoa na wala haijuzu kuyaacha, lakini wasiyabomoe ila
wenye mamlaka, mtawala. Haijuzu kwa watu wa kawaida kuyabomoa, kwa
kuwa hili litapekelea katika fitina na shari. Yabomolewe na mtawala wa
Waislamu baada ya mashauriano na wanachuoni.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127695
14) Kuuza Manukato Ambayo Yana Alcohol
Swali:
Ipi hukumu ya kuuza (manukato yaitwayo) "Kaaloniyaa" kwa ajili ya
kuitumia wakati wa kunyoa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Tumeshataja Hadiyth kuhusiana na kaaloniyaa na kwamba inakuwa na
chembe za pombe, hivyo haijuzu kuuza pombe kwa hali yoyote. Na ni juu ya
mtu kujiepusha na vitu vyote vya Haramu na afanye yale ambayo ni Halali
yako wazi, na ajiepushe na mambo yenye utata.
Chanzo: http://youtu.be/yVNbbDlRRd4
16
15) Kusoma al-Mu´awidhaat Mchana Wakati Wa Kulala
Swali:
Je mtu anasoma al-Mu´awidhaat (al-Ikhlasw, al-Falaq na an-Naas) wakati wa
kulala tu usiku au wakati wowote anapolala mtu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Akisoma mtu wakati wa kulala kwake mchana, hakuna ubaya kwako kwa
kuwa ni kinga kwa Allaah kutokana na Mashaytwaan wa kijini na wa
kibinaadamu. Na ni jambo zuri kwa Muislamu.
Chanzo: http://youtu.be/ymlV774xPpU
16) Kusikiliza Mikanda Ya ´Aa´idh al-Qarniy Na Twaariq as-Swaydaan
Swali:
Yapi maoni yako kusikiliza mikanda yote ya ´Aa´idh al-Qarniy na Twaariq as-
Swaydaan?
´Allaamah Ahmad an-Najmiy:
Sionelei na wala siwezi kumpa Fatwa yoyote ya kujuzisha kusikiliza mikanda
ya ´Aa´idh al-Qarniy wala Twaariq as-Swaydaan.
Chanzo: http://youtu.be/SqjXLIElqQs
17) Kusherehekea Mwaka Wa Hijriyah Na Kuzaliwa Na Kupeana
Pongezi
17
Swali:
Ipi hukumu ya kusherehekea sikukuu za mwaka mpya wa Kiislamu na
sherehe za kuzaliwa?
´Allaamah Zayd al-Madhkhaliy:
Sikukuu hizi hazina asili katika Shari´ah ya Kiislamu. Bali katika Shari´ah ya
Kiislamu kuna sikukuu (´Iyd) mbili, ´Iydi al-Fitwr na ´Iyd al-Adhwhaa.
Sikukuu zisizokuwa hizo hazina asili bali ni katika Bid´ah, kutahadharishwe
kwazo na Muislamu atahadhari kutozishiriki.
Muulizaji:
Hukumu ya kupeana pongezi kwa kuzaliwa na kwa mwaka mpya?
´Allaamah Zayd al-Madhkhaliy:
Hapana, wasipeane watu pongezi ila tu kwa ´Iyd al-Adhwhaa na ´Iyd al-
Fitwr.
Chanzo: http://youtu.be/-emr5Gww6cY
18) Kumkosoa Mtawala Juu Ya Minbar
Swali:
Je ni katika Manhaj ya Salaf kumhukumu mtawala, kusema makosa yake na
kumsengenya katika mimbar? Ni vipi Manhaj Salaf katika kuwanasihi
watawala, na inakuweje?
Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz:
18
Swali hili limeulizwa zaidi ya mara moja. Si katika Manhaj ya Salaf kutaja
makosa ya mtawala katika minbar. Kwa kuwa hili linapelekea katika migomo
na watu kuacha kutii katika mambo mema. Hili linapelekea katika madhara
na halinufaishi. Njia ya Manhaj ya Salaf ni kumnasihi kisiri, kumwandikia au
unawasiliane na maulamaa kisha watamwasilia hivyo ili wamuelekeze katika
kheri. Madhambi yatajwe bila ya kumtaja mtendaji. Zinaa, pombe na Ribaa
vikatazwe bila ya kumtaja mtendaji, maasi yakatazwe bila ya kumtaja
mtendaji - bila kujali sawa ni mtawala au mwingine yeyote. Fitina ilipopamba
moto wakati wa ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhu), walisema baadhi ya
watu kumwambia Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anhu):
"Je humkatazi ´Uthmaan?" Akasema [Usaamah]: "Nimkataze mbele ya watu?
Nitamkataza kisiri baina yangu mimi na yeye bila ya kufungua mlango wa
shari kwa watu."
Jambo ambalo lilipelekea katika fitina baina ya ´Aliy na Mu´aawiyah.
´Uthmaan na ´Aliy waliuawa kwa sababu hiyo. Maswahabah wengi (Radhiya
Allaahu ´anhum) na watu wengi waliuawa kwa sababu hili la kuhukumiana
hadharani. Lilipelekea watu kumchukia mtawala wao mpaka wakumuua.
Chanzo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=127880
19) Kujumuisha Swalah Wakati Wa Mvua, Upepo Na Barafu
Swali:
Muulizaji kutoka Amerika anauliza. Kwetu kuna mvua [kali] na barafu, je
tunaweza kujumuisha Swalah?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Mvua ikinyesha wakati wa Swalah ya Maghrib na ´Ishaa, wanaweza
kujumuisha katika hali hii mvua na barafu na upepo mkali wenye baridi.
Wanaweza kujumuisha baina ya Maghrib na ´Ishaa ili isiwapite Jamaa´ah.
19
Ama ikiwa mtu kujumuisha Swalah ndo ada yake, au kwa mvua ndogo tu ni
wajibu kuswali Swalah kwa wakati wake tena Msikitini.
Muulizaji:
Kipi kipimo cha kujumuisha, yaani kujumuisha kuna muda maalumu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hapana hakuna muda maalumu maadamu udhuru wa kufanya hilo upo. Mtu
atajumuisha maadamu udhuru upo, mvua nyingi ya kulowanisha nguo,
barafu nyingi mtu hawezi kutembea katika giza, ni sahihi kwao kujumuisha
na waswali Jamaa´ah. Wajumuishe tu bila ya kufupisha. Baina ya Maghrib na
´Ishaa na ´Aswr na Dhuhr.
Chanzo: http://youtu.be/8ttnGcH4-pE
20) Je Kuna Kundi Linaitwa Jaamiyyah? Na Ni Nani Shaykh Muhammad
al-Jaamiy?
Swali:
Tumesikia kundi la Jaamiyyah ulilotahadharisha dhidi yalo, je kundi hili kweli
lipo na ni nani Shaykh Muhammad (Amaan) al-Jaamiy?
´Allaamah al-Fawzaan:
Muhammad al-Jaamiy ni ndugu yetu na kipenzi chetu, alihatimu katika Chuo
Kikuu hiki (Madiynah) na akaenda kuwa mwalimu katika Chuo kikuu cha
Kiislamu na (mwalimu) katika Msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa
sallam) na alikuwa ni mlinganiaji katika njia ya Allaah (Subhaanahu wa
Ta´ala). Hatujui kwake ila kheri tu. Na hakuna kundi linaloitwa Jaamiyyah,
hili ni uongo na udanganyifu. Haya ndo tunayoyajua kwa Shaykh
20
Muhamamd Amaan al-Jaamiy (Rahimahu Allaah). Lakini kwa kuwa alikuwa
akilingania katika Tawhiyd na akikemea Bid´ah na fikra za kipotofu, hivyo
(watu wa Bid´ah) wakawa wanamjengea uadui na kumpachika majina ya
bandia kama haya.
Chanzo: http://youtu.be/s9JIRTSAF9s
21) Ipi Tofauti Kati Ya ´Aqiydah Na Manhaj?
Swali:
Ipi tofauti baina ya ´Aqiydah (itikadi) na Manhaj (mfumo)?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
´Aqiydah na Manhaj vinaenda sambamba, tofauti tu ni katika matendo.
´Aqiydah ni ibara ya Imani, mtu kuamini nguzo zake sita (za Imani). Na
Manhaj ni yale matendo ya Kiislamu, kutekeleza wazi zile nguzo tano za
Kiislamu. Navyo ni vitu viwili vinaenda sambamba. Ni lazima Muislamu awe
na ´Aqiydah sahihi na Manhaj Sahihi. Viendane sambamba kama ilivyo katika
Manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hawatofautishi kati ya ´Aqiydah na
Manhaj katika matendo.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2632
22) Inajuzu Kula Samaki Maiti Ambayo Haikuchinjwa?
Swali:
Muulizaji kutoka Ireland anauliza, je inajuzu kula nyama ya samaki ikiwa ni
maiti?
21
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Maiti ya baharini inajuzu, ama maiti ya bara ni lazima kwanza kuichinja ima
kwa mfano bunduki na mfano wa hayo.
Chanzo: http://youtu.be/W_2CK1vmbQg
23) Hukumu Ya Mwenye Kumtukana Allaah Na Mtume Wake
Swali:
Je atatakiwa atubie yule mwenye kumtukana Allaah na akamtukana Mtume
Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na kuna tofauti baina ya haya
mawili?
´Allaamah al-Fawzaan:
Maulamaa wamesema kuwa atauawa wala hakuna cha kutakiwa kutubia.
Mwenye kumtukana Allaah na Mtume atauawa wala hatatakiwa kutubia, kwa
kuwa hii ndo adhabu yake inayofaa kumpa.
Chanzo: http://youtu.be/olZtrSblZ6s
24) Shaykh Fawzaan Kuhusu Radd Kwa Sayyid Qutwub
´Allaamah al-Fawzaan:
Sayyid Qutwub ni mjinga hana elimu wala maarifa. Wala hana dalili kwa
ayasemayo. Kumlinganisha Imaam Ahmad [bin Hanbal] na Sayyid Qutwub ni
dhuluma.
22
Chanzo: http://youtu.be/z3A6nSGyclg
25) Umuhimu Wa Kuhifadhi Swalah Ya Dhuhaa
Swali:
Je, kuna Hadiyth inayosema mwenye kuhifadhi Swalah ya dhuhaa,
atasalimishwa na khofu kubwa [ya siku ya Qiyaamah]?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa mimi sijui hili, lakini mtu huyo atakuwa katika al-Awwaabiyn,
yaani wenye kutubia, wenye kurejea kwa Allaah (´Azza wa Jalla).
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5210
26) Kabla Ya Kutumwa Mtume Watu Walikuwa Katika Dini Ya Nani?
Swali:
Je, dini sahihi kabla ya kutumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni
Haniyfiyyah Dini ya Ibraahiym au ni Shari´ah ya ´Iysa (´alayhis-Salaam)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Kwa nisba ya waarabu ni Dini ya baba yake na Ismaa´iyl, Dini ya Ibraahiym.
Ama kwa nisba ya mayahudi na manaswara, walikuwa katika Dini ya Muusa
na ´Iysa. Na kuna miongoni mwa waarabu walioathirika na Uyahudi na
Unaswara, wakifuata Dini ya Ibraahiym.
23
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2734
27) Je Sigara Inavunja Wudhuu? Na Ipi Hukumu Ya Sigara Na Bangi?
Swali:
Je kuvuta bangi kunavunja Wudhuu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa haivunji Wudhuu, lakini ni Haramu. Inachukuliwa ni katika
madhambi makubwa. Kuvuta sigara, bangi ni katika madhambi makubwa.
Kwa kuwa yanasababisha kujiua mwenyewe na kuua wengine walioko karibu
nawe, uuaji wa kidogo kidogo. Tunamuomba Allaah afya na usalama. Ni
wajibu kwa Muislamu kujiepusha na kuvuta sigara, bangi na aina zote za
sigara. Na ajiepushe na yote yanayompelekea kumuua. Hakika ni katika
uchafu, madhara yenye kuua na kuangamiza.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5207
28) Nasaha Kwa Dada Wapya Waliyoingia Katika Uislamu -1-
Swali:
Tunamuomba Shaykh kuwapa nasaha ya kijumla wanawake ambao ni wapya
wameingia katika Uislamu, huenda Allaah Akawafaa kwa hilo.
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
24
Kwanza tunawapa hongera dada zetu wa Kiislamu ambao kawakirimu Allaah
(Tabaaraka wa Ta´ala) kuingia kwao katika Uislamu na kuacha dini zenye
kwenda kinyume, ni kuokoka kutoka katika moto kwa uwezo na nguvu za
Allaah. Na wale waliong´ang´ana kubaki katika dini zao batili na wakafa
katika dini hizo hawana kwa Allaah isipokuwa Moto tu na ni makazi mabaya
sana na hawatotoka humo. Ama kwa wale Aliowakirimu Allaah katika
wanaume na wanawake, hakika hii ni katika Tawfiyq ya Allaah kwa wote.
Ni juu ya aliyeingia katika Uislamu akimbilie kujifunza nguzo za Uislamu,
kwanza aanze kuisafisha ´Aqiydah, ampwekeshe Allaah (´azza wa Jalla)
katika Uluuhiyyah - hivyo asiwe ni mwenye kumuabudu yeyote zaidi ya
Allaah Pekee. Na katika Rubuubiyyah - awe mwenye kukiri kuwa Allaah
ndiye Muumba, Mwenye kuruzu daima, Mwenye kuendesha yote. Na katika
Sifa Zake - Mwenye Kusamehe, Kurehemu, Kusikia, Kuona, Kujua, Mwenye
Hekima na mengine yote katika Majina Mazuri na Sifa Zake Kuu. Aamini yote
hayo, na atekeleze faradhi zilizofaradhishwa; kama Swalah tano - kwa jumla
kama nguzo za Uislamu tano na nguzo za Imani sita na nguzo ya Ihsaan. Na
ajitahidi kujua Halali na Haramu. Na ajilazimishe kuwa na adabu za Kiislamu
na aendelee kujifunza daima mpaka awe imara mwanaume na mwanamke
katika kuhakikisha Uislamu sahihi ambao Kawachagulia Allaah (Tabaaraka
wa Ta´ala) kwa watu wote binaadamu na majini. Kinachotakiwa ni kuendelea
baada ya Uislamu kujifunza nguzo zingine zote za Kiislamu.
Chanzo: http://youtu.be/p275UYtTbPg
29) Nifuturu Nyumbani Kwangu Au Msikitini Nikaapo I´tikaaf?
Swali:
Nyumba yangu iko karibu na Msikiti ambao nataka kukaa I´tikaaf. Je, ni bora
kwangu wakati wa futari nikafuturu nyumbani kwangu halafu nioge wakati
wa haja au ni bora kwangu kuhudhuria [kwa ajili ya futari] katika Msikiti
ambao uko karibu nami?
25
´Allaamah al-Fawzaan:
Bora ni wewe kubakia mahali ulipo, futuru Msikitini na usiende nyumbani.
Kwa kuwa hili si dharurah, na tumesema mtu anatoka tu kama kuna haja
dharurah, kama kutatua haja fulani, kutawadha. Ama hili kufuturu nyumbani
kwako si dharurah, futuru Msikitini na hili ndo bora kwako. Kwa kuwa futari
ni ´Ibaadah na ikiwa Msikitini ndo bora zaidi.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2662
30) Nasaha Kwa Dada Wapya Waliyoingia Katika Uislamu -2-
Swali:
Dada kaingia katika Uislamu naye anataka nasaha kutoka kwa Shaykh
kuhusiana na jinsi atatangamana na mamake kafiri ambaye alikata
mawasiliano naye kwa kuingia kwake Uislamu kwa kuwa [mamake]
anamfanyia kejeli kwa Hijaab yake ya Kishari´ah?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Huyu [dada yetu] tunampa hongera kwa kuingia kwake katika Uislamu,
hakika Allaah Atamuepusha na Moto ikiwa atakuwa thabiti na akafa katika
Uislamu na Imani, ambao Allaah Kawaahidi Pepo Yake yenye neema.
Tunamnasihi kuwa na ufahamu (kuielewa) Dini, nguzo za Uislamu tano,
vigawanyo vya Tawhiyd vitatu, nguzo za Imani sita, Ihsaan, kujua Halali na
Haramu, kuelewa yale mambo ambayo ni wajibu kwake na aliyoharamishiwa.
Ama mama yake atangamane nae muamala mzuri huku akimlingania kuingia
katika Uislamu, amuwekee mtumishi na aongee nae vizuri lakini amchukie
ndani ya moyo maadamu bado angali katika ukafiri wake. Na Allaah (´Azza
wa Jalla) Anasema:
نيا في وصاحبهما بع معروفا الد إلي أناب من سبيل وات
26
"Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anayeelekea
Kwangu." (31:15)
Wala usimtii kwa kitu ambacho ni Haramu. Na uendelee kumlingania huenda
Allaah Akamtoa katika ukafiri, sawa ikiwa [yuko katika dini] ya kinaswara,
kiyahudi, kiwathaniyyah; Atamuokoa kwa kumuingiza Kwake katika
Uislamu. Fanya sababu.
Chanzo: http://youtu.be/VhhE9FDNjL4
31) Mume Kamlaani Mke Wake, Je Mke Katalikika?
Swali:
Mwenye kumlaani mke wake ni kama vile kampa Talaka?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hapana, si kama aliyemtaliki. Ila akidhihirisha kuwa kakusudia kumtaliki
[itakuwa imepita]. Kumlaani ni Haramu kwake [mume], kumlaani ni Haramu
kwake.
Chanzo: http://youtu.be/l_SxS32XeMA
32) Mavazi Yenye Picha Za Watu Na Minyama Na Maneno Mabaya
Swali:
Anauliza kuhusu mavazi ya watoto ambayo yanakuwa na mapicha ya
minyama na watu?
27
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa haijuzu kununua mavazi kama haya, sawa ikiwa ni mavazi ya
watoto, wanaume au wanawake. Lazima ziwe hazina picha zenye viumve
vyenye roho na maneno mabaya.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5486
33) Kuna Aina Tatu Kwa Wenye Kuyatembelea Makaburi
Swali:
Kwetu kuna wanaoenda kuzuru makaburi na wanaamini kuwa yananufaisha
na kudhuru. Je, watu hawa ni washirikina au ni lazima kwanza
kuwasimamishia hoja?
´Allaamah Zady al-Madkhaliy:
Kuzu makaburi kumegawanyika sehemu tatu:
- Ziara ya Kishari´ah Nayo ni pale mwenye kuzuru anaenda kuzuru kwa nia
ya kuwasalimia. Atawasalimia kisha aende, atasema: "Salaamun ´alaykum
daara qaumil mu-uminiyn, wa inna In Shaa Allaahu bikum lahaaikun,
yarhamu Allaahu mustaqdimiyna minna wa minkum wal mustaakhiriyn."
Kisha anasema: "Allaahumma laa tuhrimaa ajrahum." Kisha ende. Hii ndio
ziara ya Kishari´ah."
- Na kuna ziara ya Shirki. Nayo ni pale mtu anazuru makaburi ya watu wema;
atafuta Shafaa´ah kutoka kwao, awachinjie huku akiamini wananufaisha na
kuzuia madhara. Anawaomba wafikishe haja zake kwa Allaah (´Azza wa
Jalla), huku akiamini wananufaisha au kuzuia madhara. Hii ni ziara ya
kishirki, mwenye kufanya hivi kafanya Shirki kubwa. Kwa kuwa kachinja
kwa asiyekuwa Allaah, na kawaomba maiti wamtatulie haja zake, hivyo
katumbukia katika Shirki kubwa.
28
- Na kuna ziara za Bid´ah. Nazo ni pale mtu anapomzuru aliyemo ndani ya
kaburi, kisha amuombe Allaah hapo kwenye kaburi huku akiitakidi kuwa
mahala hapo kuna baraka. Anatafuta baraka sehemu hio anamuomba Allaah
kwa mtu huyo aliyemo ndani ya kaburi akiitakidi baraka. Ni juu ya Muislamu
kutofautisha baina ya aina hizi tatu; ziara za Shirki, ziara za Bid´ah na ziara za
Sunnah.
Chanzo: http://youtu.be/WLQm_MM4wyU
34) Kutabaruku Kwa Mabaki Ya Mtume ( وسلم عليه هللا صلى )
Swali:
Muulizaji kutoka Spain, je inajuzu kutabaruku (kuitakidi baraka) kwa athari
ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Athari imegawanyika sehemu mbili, inayojuzu kutafuta kwayo baraka na
isiyojuzu.
- Yanayojuzu kutafuta kwayo baraka ni yale yaliyothibiti kuwa ni katika
mabaki yake; kama damu yake, nguo na yote yanayohusiana na yeye. Haya
inajuzu kutabaruku kwavyo.
- Ama yaliyokatazwa ni kutabaruku kwa kumuomba, kutawassul kwa jaha
yake. Haya hayajuzu kwa hali yoyote. Kukipatikana nywele, damu n.k. vya
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inajuzu kutabaruku kwavyo, kwa
kuwa hilo limethibiti wakati wa uhai wake. Yasiyokuwa hayo katika
kutabaruku kwa jaha yake, kumuomba Allaah kwa jaha yake (Mtume) na
makubwa kuliko hayo - kumuomba na kumchinjia ni Shirki kubwa inayomtoa
mtu katika Uislamu ikiwa mfanyaji ni Muislamu.
Chanzo: http://youtu.be/BSz34STSOzUp
29
35) Jinsi Ya Kuweka Nia Unapotaka Kuanza Kukaa I´tikaaf
Swali:
Je ni lazima kuitamka nia pindi mtu anapotaka kufanya I´tikaaf, au inatosha
nia ndani ya moyo?
´Allaamah al-Fawzaan:
Inatosha nia yako ndani ya moyo. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi
wa sallam):
"Vitendo vinategemea [vinalipwa kwa] nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa
kile alichokusudia."
Akinuia kukaa I´tikaaf na akanuia kutoka kwa baadhi ya mambo [wakati wa
dharurah], hii ndo sharti hata kama hakuyatamka. Na Allaah Anajua
yaliyomo ndani ya moyo na Anajua nia yako na makusudio yako hata kama
hukuyatamka.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2661
36) Inajuzu Mume Kumkabili Mke Wake Usoni?
Swali:
Je mume akimkabili mke wake uso anapata dhambi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa hapati dhambi, mlango uliopo baina ya mume na mke ni mpana.
30
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5194
37) Hukumu Ya Mtu Mwenye Kuitukana Dini
Swali:
Ipi hukumu ya kuitukana Dini katika Shari´ah ya Kiislamu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Laa hawla walaa Quwwata illa biLlaah. Kuitukana Dini ni ukafiri na kuritadi,
mwenye kuitukana Dini ya Kiislamu basi huyo karitadi katika Uislamu.
Anatakiwa kuingia [upya] katika Uislamu. Akiafikishwa na kurejea - akaomba
Tawbah ya kweli kabisa, atakubaliwa. Na ikiwa atakufa na yeye ni mwenye
kuutukana Uislamu atakuwa kafiri aliyeritadi.
Chanzo: http://youtu.be/8oWf0rFVDVg
38) Inajuzu Kwa Mwanamke Kufanya Kazi Ya Uuguzi Katika Mji Wa
Kikafiri?
Swali:
Muulizaji kutoka Spain, je inajuzu kwa mwanamke wa Kiislamu kufanya kazi
ya muuguzi (nurse) Hospitali katika mji wa kikafiri?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ikiwa atajisitiri vizuri kwa Hijaab, na akawa anawauguza wanawake tu,
kutakuwa hakuna neno. Kwa kuwa Hospitalini ni sehemu pa mchanganyiko
31
baina ya wanaume na wanawake. Kwa sharti hizi inajuzu, awe amejisitiri
vizuri kwa Hijaab na awe sehemu ya wanawake tu.
Chanzo: http://youtu.be/24d59c38gSk
39) Muislamu Kupenda Nchi Ya Kikafiri
Swali:
Muulizaji kutoka Spain, inajuzu kwa Muislamu kupenda nchi yake ya
kikafiri?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Muislamu nchi ya kikafiri sio nchi yake, bali nchi ya Kiislamu ndio nchi yake.
Ni juu yake kufanya juhudi kuhama katika nchi ya Kiislamu, ama nchi ya
kikafiri sio yake. Alihama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na
Muhajiruun katika Maswahabah na wakaiacha Makkah na wakapenda
kuhamia Madiynah na hawakurejea Makkah ila baada ya al-Fath (kutekwa
kwa Makkah na Waislamu).
Chanzo: http://youtu.be/W8s3uitAGCs
40) Mambo Gani Yanayofanya Mwanamke Akawa Na Msimamo Katika
Dini?
Swali:
Ni mambo gani yanayomthibitisha (yanampa msimamo) mwanamke katika
Dini ya Allaah?
32
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Amuogope Allaah (´Azza wa Jalla) na Imani ya kuwa Allaah Kamuumba kwa
ajili amuabudu na atamuhesabu kwa hilo. Akiyajua mambo haya hivyo
ajitahidi katika kumtii Allaah na kuacha maasi na ajikurubishe kwa Allaah
(´Azza wa Jalla) kwa yatakayomfaa katika Dini na dunia yake.
Chanzo: http://youtu.be/rXSou8HREOI
41) Kuwa Na Subira Katika Da´wah Kwa Kupewa Mitihani
Swali:
Kuna watu wanaomsema Shaykh Muhammad bin Haadiy [al-Madkhaliy] na
Shaykh ´Abdullaah al-Bukhaariy?
´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy:
Kusemwa Mashaykh sio tu Shaykh Muhammad bin Haadiy na Shaykh
´Abdullaah al-Bukhaariy. Mitume nao walisemwa. Waliwatuhumu kwa
uchawi, ukuhani, uongo na kadhalika. Wamewapiga vita maimamu wa
Uislamu kwa hila na chuki zao, hii ni Sunnah ya Allaah. Hii ni Sunnah ya
Allaah kwa waja wake yule ambaye atashikamana na njia ya haki na akapita
njia iliyonyooka, lazima apate maadui na Shaytwaan anawachochea watu
kama hawa na kuwaita waje kuipiga vita haki na watu wake. Mitume
(´alayhimus-Salaam) waliudhiwa, waliambiwa:
"Nyinyi si chochote ila ni wanaadamu kama sisi." (14:10)
"Mitume wao wakawaambia: "Sisi kweli si chochote ilani wanaadamu kama
nyinyi. Lakini Allaah Humfanyia hisani amtakaye katika waja wake." (14:11)
Kuna nini akitukanwa Muhammad bin Haadiy, Bukhaariy, Rabiy´ na
wengineo? Watu wamezowea kuongea kwa batili, dhuluma na uongo.
33
Hawakumsalimisha Muhammad bin Hanbal, Ibn Taymiyyah, [Muhammad
bin] ´Abdil-Wahhaab na wengineo katika maimamu wa Uislamu. Vipi kweli
mnaweza kusahau haya mpaka mkauliza swali kama hili? Sisi tunawanasihi
watu hawa wanaomzungumzia fulani na fulani, wamche Allaah katika nafsi
zao. Watu hawa wanaomtukana Muhammad bin Haadiy, al-Bukhaariy
wanadai Salafiyyah, nao wako mbali na Salafiyyah na msingi wake na mfumo
wake. Na wanajificha nyuma ya pazia la Salafiyyah ili wapate kupoteza waja
wa Allaah (Tabaakara wa Ta´ala) na wawapoteza katika njia ya Allaah iliyo
nyooka.
Chanzo: http://youtu.be/BIxUv8f1owg
42) Kuna Mpaka Wa Mtu Kukaa Itikaaf Msikitini?
Swali:
Je uchache wa kukaa I´tikaaf ni usiku mbili au siku moja kama ilivokuja katika
Hadiyth ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu)?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hakuna mpaka. Wanachuoni wanasema mtu anaweza kukaa hata saa moja
kwa kuwa hapakuja mpaka katika Shari´ah.
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2651
43) Ipi Faradhi Ya Kwanza Kubwa?
Swali:
Faradhi ipi kubwa aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
34
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Faradhi kubwa ni kumpwekesha Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) - Tawhiyd na
kuacha kumshirikisha. Nayo ndio Da´wah ya kila Mtume na Nabii. Na ndio
faradhi ya kwanza kubwa na iliyofaradhishwa.
Chanzo: http://youtu.be/6QPuhsXXHVw
44) Hukumu Ya Kuhudhuria Janaza Na Kuwasalia Watu Wa Bid´ah
Swali:
Ipi hukumu ya kuhudhuria janaza kukikithiri Bid´ah?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Watu wa Bid´ah wanasuswa sawa waliohai na waliokufa, na wala
hawahukumiwi ukafiri ila tu ikiwa Bid´ah zao ni za kukufurisha. Kama wale
wanaoabudu makaburi, na wale wanaowaomba maiti na kuwaomba msaada,
hizi ni katika Bid´ah za kukufurisha. Muislamu asishuhudie janaza zao na
wala asiwasalie bali wao ni katika watu wa Motoni. Ama Bid´ah chini ya
ukafiri na Shirki, hawahukumiwi wanaozifanya kwa ukafiri. Bali tu Salaf-us-
Swaalih walikuwa hawawaswalii kabisa watu wa Bid´ah wala hawahudhurii
katika janaza yao kwa ajili watu wachukue funzo kwa kutoka katika Bid´ah
walizoangukia humo.
Chanzo: http://youtu.be/UB_nHlso_AY
45) Amevaa Soksi Kisha Akazivua, Vipi Wudhuu Wake?
35
Swali:
Nikipaka juu ya soksi halafu nikazivua na kuvaa soksi zingine bila kuweka
Wudhuu upya, je Wudhuu wangu utatenguka?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ndio akizivua utatenguka, akivua moja au mbili upakaji utakuwa
umebatilika. Na ni juu yake kutawadha upya na azivae kwa Twahara kamili.
Chanzo: http://youtu.be/wcVPthHGelA
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
36