sifa tukufu za allaah (ta´ala) - kauli za wanachuoni wa salaf

73
1 Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) Imetayarishwa na kufasiriwa na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush ©

Upload: wanachuoni

Post on 13-Apr-2015

150 views

Category:

Documents


10 download

DESCRIPTION

Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

TRANSCRIPT

Page 1: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

1

Sifa Tukufu

Za Allaah

(Ta´ala)

Imetayarishwa na kufasiriwa na:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

©

Page 2: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

2

KUSTAWAA KWA ALLAAH JUU YA ´ARSHI............................................................................................ 4

Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? I .............................................................. 4

Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? II ............................................................. 6

ad-Daarimiy Kuwa Juu Kwa Allaah.............................................................................................................. 8

al-Ajurriy Kuhusu Kuwa Juu Kwa Allaah ................................................................................................. 10

Ibn Zamaniyn Kuhusu Kuwa Juu Kwa Allaah .......................................................................................... 11

Ahmad bin Hanbal Kuhusu Kuwa Juu Kwa kwa Allaah ........................................................................ 11

KUONEKANA ALLAH AAKHIRAH ........................................................................................................... 13

Haiwezekani Kumuona Allaah Katika Maisha Haya ............................................................................... 13

al-Muzaniy Kuhusu Kumuona Allaah ........................................................................................................ 13

Hutoniona Kamwe Au Hutoniona? ............................................................................................................ 15

Ibn-ul-Qayyim Dalili Ya Tano Ya Kuonekana ........................................................................................... 16

Ibn-ul-Qayyim Dalili Ya Sita Ya Kuonekana .............................................................................................. 17

USO WA ALLAAH ........................................................................................................................................... 19

Maimamu Ambao Wamefasiri Uso Wa Allaah Mwelekeo ...................................................................... 19

Ibn Uthaymiyn Kuhusu Uso Wa Allaah ..................................................................................................... 19

at-Twabariy Kuhusu Uso Wa Allaah .......................................................................................................... 21

Dalili Ya Uso Wa Allaah I ............................................................................................................................. 22

Dalili Ya Uso Wa Allaah II ............................................................................................................................ 25

Salaf Kuhusu Kuonekana Kwa Allaah Na Uso Wa Allaah ...................................................................... 26

Ibn Khuzaymah Kuhusu Uso Wa Allaah ................................................................................................... 28

VIDOLE VYA ALLAAH .................................................................................................................................. 30

Vipi Salaf Walikuwa Wakiamini Vidole Vya Allaah?............................................................................... 30

Vidole Vya Allaah .......................................................................................................................................... 31

Kidole Kidogo Cha Allaah ............................................................................................................................ 32

Dalili Ya Vidole Vya Allaah .......................................................................................................................... 35

MGUU WA ALLAAH ....................................................................................................................................... 37

Dalili Ya Mguu Wa Allaah ............................................................................................................................ 37

KHASIRA ZA ALLAAH .................................................................................................................................. 40

Mapenzi Na Khasira Za Allaah Kwa Mtu .................................................................................................. 40

MIKONO YA ALLAAH ................................................................................................................................... 41

Mkono Wa Kulia Wa Allaah ......................................................................................................................... 41

Allaah Kamuumba Aadam Kwa Mkono Wake ......................................................................................... 42

Allaah Ana Mikono Miwili Na Yote Ni Ya Kulia ...................................................................................... 44

Page 3: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

3

KUJA KWA ALLAAH ...................................................................................................................................... 45

Kuja Kwa Allaah Kunatoa Ushahidi Kushuka Kwake ............................................................................. 45

at-Twabariy Kuja Kwa Allaah ...................................................................................................................... 45

Na Akaja Mola Wako Na Malaika Safu Safu ............................................................................................. 46

SAUTI YA ALLAAH ......................................................................................................................................... 48

Allaah Huongea Kwa Sauti Ya Kusikika .................................................................................................... 48

Hadiyth Zilizo Swahiyh Kuhusu Sauti Ya Allaah ..................................................................................... 49

SURA YA ALLAAH .......................................................................................................................................... 51

Allaah Kamuuumba Aadam Kwa Sura Yake ............................................................................................. 51

KUCHEKA KWA ALLAAH ............................................................................................................................ 53

Ibn Maajah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah ................................................................................................. 53

Ibn Khuzaymah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah ......................................................................................... 53

Ibn Battah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah ................................................................................................... 54

Ibn Abiy 'Aasim Kuhusu Kucheka Kwa Allaah ........................................................................................ 56

ALLAAH KUWA NA PAMOJA NA VIUMBE VYAKE ............................................................................. 58

Allaah Kuwa Na Viumbe Vyake Haina Maana Anachanganyika Nao Kimwili .................................. 58

Ni Nani Mtu Wa Kwanza Aliyesema Kuwa Qur-aan Imeumbwa? ......................................................... 61

Allaah Huongea Kwa Kutaka Kwake Na Kwa Uwezo Wake ................................................................... 63

SUBIRA KAMILIFU YA ALLAAH ................................................................................................................ 64

Uvumilivu Wa Allaah Wa Kikamilifu ......................................................................................................... 64

KUSHUKA KWA ALLAAH KILA USIKU KWENYE MBINGU YA DUNIA ....................................... 65

Je, Allaah Huacha ´Arshi Yake Wakati Anashuka? ................................................................................... 65

ad-Daaraqutniy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah ......................................................................................... 65

Ahmad Na Ibn Raahuuyah Kuhusu Kushuka Kwa Allaah ..................................................................... 66

Mfano Wa Uongo Wa Ibn Batuutah kuhusu Ibn Taymiyah .................................................................... 66

Uongo Dhidi Ya Ibn Taymiyyah Na Kushuka Kwa Allaah ..................................................................... 67

al-Barbahaariy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah ........................................................................................... 68

Abu Daawuud Kuhusu Kushuka Kwa Allaah .......................................................................................... 69

Abul-Hasan al-Ash'ariy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah ........................................................................... 69

at-Tirmidhiy Kushuka Kwa Allaah ............................................................................................................. 70

Abu Bakr al-Ismaa'iyliy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah ........................................................................... 71

UMILELE WA ALLAAH NA WA VIUMBE ................................................................................................. 72

Tofauti Kati Ya Umilele Wa Allaah Na Umilele Wa Peponi Na Motoni ................................................ 72

MIOYO YA WAJA IKO BAINA YA VIDOLE VIWILI VYA ALLAAH .................................................. 73

Mioyo Ya Waja Kuwa Baina Ya Vidole Viwili Katika Vidole Vya Allaah Haihitajii Kugusana .. 73

Page 4: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

4

KUSTAWAA KWA ALLAAH JUU YA ´ARSHI

Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? I

1) Hammaad bin Zayd kasema:

"Nilimsikia Ayyuub as-Sikthiyaaniy akisema kuwa Mu'tazilah wamesema:

"Mtazamo wao umezunguka kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu ya

mbingu.'"

2) al-Awzaa'iy kasema:

"Tuliishi wakati wa Taabi'uun walikuwa wengi kabisa na tulikuwa tukisema:

"Allaah ('Azza wa Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake na tunaamini Sifa zimezotajwa

katika Sunnah.”"

3) Imaam Ibn Qudaamah kasema:

"Nilipata khabari kwamba Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) kasema: "Yule

ambaye anakanusha ya kwamba Allaah Yuko juu ya mbingu amekufuru.""

4) Maalik kasema:

"Allaah Yuko juu ya mbingu, na elimu Yake iko kila mahali."

Kasema pia:

Page 5: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

5

"Kuwa kwake juu kunajulikana na namna yake haijulikani. Ni wajibu kuamini

hilo na ni Bid´ah kuulizia hilo.”

5) Hammaad bin Zayd kasema kuhusu Jahmiyyah:

"Wanachotaka kusema ni kwamba hakuna mungu yeyote juu ya mbingu.”

6) ´Aliy bin al-Hasan bin Shaqiyq kasema:

"Nilimuuliza Ibn-ul-Mubaarak: “Vipi tutamjua Mola Wetu?" Akasema:" [Ya

kwamba Yeye Yuko] juu ya mbingu saba juu ya ´Arshi Yake. Hatusemi kama

wanavosema Jahmiyyah: "Yuko hapa duniani.”"

7) 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy kasema:

"Jahmiyyah wanataka kukataa kwamba Allaah alizungumza na Muusa na

kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi. Naona wanatakiwa kutubia. Aidha watubie

la sivyo wanyongwe".

8) Imaam ash-Shaafi'iy kasema:

"Sunnah tunayofuata sisi na ambayo nimeona Ahl-ul-Hadiyth wanaifuata kama

Sufyaan, Maalik na wengine ni kuthibitisha hapana mola apasaye kuabudiwa kwa

haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah... " ... mpaka

aliposema: " ... na kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake.

Anawakurubia viumbe Vyake vile Apendavyo, na kushuka kwenye mbingu ya

chini vile Apendavyo."

9) 'Aasim bin 'Aliy – mwalimu wa al-Bukhaariy - kasema:

"Nilijadiliana na Jahmiy na kukuta kuwa haamini ya kwamba kuna mola juu ya

mbingu."

Yahyaa bin Ma'iyn kasema:

Page 6: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

6

"´Aasim alikuwa bingwa wa Waislamu."

10) al-'Abbaas ad-Dawriy kasema:

"Nilimsikia Abu 'Ubayd al-Qaasim bin Sallaam akisema baada ya kutaja Suurah

inayozungumzia kuhusu kuonekana kwa Allaah, Kursiy, Kucheka kwa Mola

Wetu na wapi Alipokuwa Mola Wetu [kabla ya uumbaji]: "Hadiyth hizi ni

Swahiyh. Wanachuoni katika Hadiyth na Fiqh wamezielezana wao kwa wao. Sina

shaka yoyote kwamba ni za kweli. Lakini ikiwa tutaulizwa, "Vipi Ameweka

Miguu Yake [kwenye Kursiy]? Vipi Anacheka" "tunasema ya kwamba hatufafanui

wala hatujasikia mtu yeyote anafafanua.””

Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744)

Chanzo: al-Istiwaa´ alaal-´Arsh, uk. 50-52

Hawa Hapa Wanaume Wetu – Wako Wapi Wanaume Wenu? II

1) Sa´iyd bin ´Aamir adh-Dhab'iy (d. 208) - Imaam wa Basrah - kasema:

"Jahmiyyah wana mtazamo mbaya zaidi kuliko Mayahudi na Wakristo. Dini zote

ikiwa ni pamoja na Waislamu wamekubaliana ya kwamba Allaah Yuko juu ya

´Arshi. Lakini Jahmiyyah wanasema: "Hakuna mungu yeyote juu ya ´Arshi.'"

2) 'Abbaad bin al-' Awaam (d. 185) kasema:

"Niliongea na Bishr al-Mariysiy na wafuasi wake na mwishowe nikaja kujua ya

kwamba wanasema hakuna mungu yeyote juu ya mbingu. Naonelea ya kwamba

mtu asichanganyike nao katika kuoana wala mtu asiwarithi.”

3) al-Asma'iyl (d. 213) kasema:

Page 7: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

7

"Mke wa Jahm alikuja wakati mtu alimwambia kuwa Allaah Yuko juu ya ´Arshi.

Alisema: "Ni Mwenye mpaka juu ya kitu chenye mpaka?" Mwanamke huyu ni

kafiri (Kaafirah) kwa sababu ya kauli hii."

4) Muhammad bin Mus'ab (d. 228) kasema:

"Yule anayedai ya kwamba Husemi na kwamba hutoonekana siku ya Qiyaamah

basi hakuamini. Nashuhudia ya kwamba Uko juu ya ´Arshi, juu ya mbingu hizi

saba, na si kama wazushi wanavyosema."

5) Wahb bin Jariyr (d. 206) kasema:

"Kaa mbali na maoni ya Jahm! Wao wamejadiliana na mimi kwamba hakuna

mungu juu ya mbingu. Huo ufunuo kutoka kwa Ibliys. Hilo si kitu jengine zaidi

na kutokuamini (Kufr). "

6) Swaalih bin Adh-Dhuray kasema:

"Kuna mtu mmoja alifungwa kwa kuwa alikuwa na ´Aqiydah ya Jahmiyyah.

Baada ya muda, akatubu. Wakampeleka kwa Hishaam bin ´Ubaydillaah ili

kumjaribu. Akasema: “Je, unaamani ya kwamba Allaah Yuko juu ya ´Arshi

Yake?” Akasema: “Sijui ni nani ambaye ametoka katika uumbaji wake.” Hivyo

akasema Hishaam "Mrudisheni gerezaki. Hakutubia."

Hishaam bin 'Ubaydillaah alikuwa ni mmoja katika wanachioni anaefuata

madhehebu ya Abu Haniyfah.

7) Abu Ma'mar Qatiy'iy (d. 236) kasema:

"Maoni ya Jahmiyyah yanaishia kwa kusema kwamba hakuna mungu yeyote juu

ya mbingu."

8) Bishr al-Haafiy (d. 227) kasema:

Page 8: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

8

"Tunamuamini ya kwamba Allaah Kastawaa juu ya ´Arshi Yake vile Apendavyo

na kwamba Anajua kila kitu."

9) Yuusuf bin Muusa kasema:

"Kulisemwa kuambiwa Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal "Je, Allaah Yuko juu

ya mbingu hizi saba, juu ya ´Arshi na katoka katika uumbaji Wake wakati nguvu

na elimu Yake viko kila mahali?" Akasema: "Ndiyo."

10) 'Abdul-Wahhaab bin ´Abdil-Hakam (d. 251), mwalimu wa Abu Daawuud,

kasema:

"Yule ambaye anasema kuwa Allaah Yuko hapa ni Jahmiy. Hakika Allaah Yuko

juu ya ´Arshi Yake na elimu Yake imekizunguka kila kitu katika maisha haya na

maisha baada ya haya."

Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn bin ´Abdil-Haadiy al-Maqdisiy (d. 744)

Chanzo: Al-Istiwaa' 'alaal-'Arsh, uk. 57-66

ad-Daarimiy Kuwa Juu Kwa Allaah

"Mlango wa 3: Kustawaa kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) juu ya ´Arshi na

kupaa Kwake mbinguni na kujitenga kutoka na uumbaji.

Hili pia wamelipinga ilihali Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) kasema:

ش توى على الأعرأ ام ثم اسأ ة أي ض في ست رأ ماوات والأ هو الذي خلق الس

“Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha Akalingana sawa

juu ya ´Arshi.” (57 : 04)

تـوى ـن على المعرمش اسم الرحم

Page 9: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

9

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya‘Arsh Istawaa (Yuko juu kwa namna

inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). (20 : 05)

يا عيسى إني متـوفييك ورافعك إل

“Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha

Kwangu.” (03 : 55)

عد المكلم الطييب والمعمل الصالح يـرمفـعه إليمه يصم

“Kwake hupanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw)

Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35 : 10)

هو المقاهر فـومق عباده

”Naye ni Al-Qaahir (Mwenye Kuteza Nguvu, Mwenye Kudhibiti) juu ya waja

Wake” (16 : 18)

علون ما يـؤممرون يافون ربـهم مين فـومقهمم ويـفم

”Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.”

(16 : 50)

سين ألأف سنة داره خمأ م كان مقأ ه في يوأ وح إليأ رج الأملئكة والر تعأ

”Malaika na Roho hupanda kwendea Kwake katika siku ambayo kadiri yake ni

miaka khamsini elfu!” (70 : 04)

لمون كمأ حاصبا ف ستعأ سل عليأ ماء أن يرأ ن في الس ض فإذا هي تمورأمأ أمنتم م سف بكم الرأ ماء أن يخأ ن في الس أأمنتم م

ف نذير كيأ

”Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na

tahamaki hiyo inatikisika! Au mnadhani mko salama kwa alioko juu ya kuwa

Yeye hakupelekeeni kimbunga chenye changarawe? Mtajua vipi maonyo

Yangu?.” (67 : 16-17)

Page 10: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

10

Mwandishi: Imaam ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy (d. 280)

Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 40-41

al-Ajurriy Kuhusu Kuwa Juu Kwa Allaah

Kwa upande mwingine, wanasema wanachuoni ya kwamba Allaah ('Azza wa

Jalla) Yuko juu ya ´Arshi Yake juu ya mbingu Zake. Elimu Yake imekienea

(imekizunguka) kila kitu. Ana ujuzi wa kila kitu Alichokiumba mbinguni, katika

ardhi na kati ya hivyo viwili. Ana ujuzi wa vya siri na vilivyojificha. Ana ujuzi wa

matakwa na mawazo. Anasikia na Anaona. Hivyo, Yeye (Subhaanahu) Yuko juu

ya ´Arshi Yake. Kwake hupanda matendo mema ya waja.

Yanayotoa ushahidi wa hilo katika Kitabu Chake, miongoni mwa dalili hizo ni

Kauli Yake:

ض فإذا هي تمور سف بكم الرأ ماء أن يخأ ن في الس أأمنتم م

”Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na

tahamaki hiyo inatikisika!” (67 : 16)

عد المكلم الطييب والمعمل الصالح يـرمفـعه إليمه يصم

“Kwake hupanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw)

Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35 : 10)

يا عيسى إني متـوفييك ورافعك إل

“Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha

Kwangu.” (03 : 55)

بل رفـعه اللـه إليمه

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04 : 158)

Mwandishi: Abu Bakr Muhammad bin al-Husayn al-Ajurriy (d. 360)

Chanzo: ash-Shari'ah, uk. 292

Page 11: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

11

Ibn Zamaniyn Kuhusu Kuwa Juu Kwa Allaah

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah ni kuamini kwamba Allaah ('Azza wa Jalla)

Kaumba ´Arshi na Anajulikana kuwa Yuko juu ya kila kitu Alichokiumba. Kisha

Akastawaa juu yake (´Arshi) vile Apendavyo. Hii limeelezwa na Yeye Mwenyewe

wakati Aliposema:

تـوى ـن على المعرمش اسم الرحم

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya‘Arsh Istawaa (Yuko juu kwa namna

inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). (20 : 05)

ها وما رج منأ ض وما يخأ رأ لم ما يلج في الأ ش يعأ توى على الأعرأ ام ثم اسأ ة أي ض في ست رأ ماوات والأ هو الذي خلق الس

ملون بصير بما تعأ ن ما كنتمأ وللا رج فيها وهو معكمأ أيأ ماء وما يعأ ينزل من الس

“Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha Akalingana sawa

juu ya ´Arshi. Anayajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na

yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda humo. Naye yupamoja nanyi

popote mlipo. Na Allaah ni Mwenye kuyaona mnayoyatenda.” (57 : 04)

Ametakasika Yeye ambaye yuko mbali kabisa akawa haonekani hata hivyo akawa

karibu kwa ujuzi Wake na nguvu hivyo Anasikia siri zinazofanywa.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin 'Abdillaah al-Andalusiy – mwenye

kujulikana kama Ibn Zamaniyn (d. 399)

Chanzo: Usuul-us-Sunnah, uk. 88

Ahmad bin Hanbal Kuhusu Kuwa Juu Kwa kwa Allaah

Page 12: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

12

Allaah Ametueleza ya kwamba Yeye Yuko juu ya mbingu. Kasema:

ض فإذا هي تمور سف بكم الرأ ماء أن يخأ ن في الس أأمنتم م

”Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na

tahamaki hiyo inatikisika!” (67 : 16)

عد المكلم الطييب والمعمل الصالح يـرمفـعه إليمه يصم

“Kwake hupanda neno zuri (dhikru-Allaah), na kitendo chema (cha ikhlaasw)

Hukipa hadhi (Hukitakabali).” (35 : 10)

يا عيسى إني متـوفييك ورافعك إل

“Ee ‘Iysaa, hakika Mimi ni Mwenye kukuchukua na Mwenye kukupandisha

Kwangu.” (03 : 55)

بل رفـعه اللـه إليمه

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04 : 158)

تـوى ـن على المعرمش اسم الرحم

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah) juu ya‘Arsh Istawaa (Yuko juu kwa namna

inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah). (20 : 05)

بل رفـعه اللـه إليمه

”Bali Allaah Alimnyanyua Kwake.” (04 : 158)

علون ما يـؤممرون يافون ربـهم مين فـومقهمم ويـفم

”Wanamkhofu Mola wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa.”

(16 : 50)

Haya ni Maneno ya Allaah. Anatwambia ya kwamba Yuko juu ya mbingu.

Mwandishi: Imaam Ahmad bin Hanbal (d. 241)

Chanzo: ar-Radd 'alaa az-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah, uk. 146-147

Page 13: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

13

KUONEKANA ALLAH AAKHIRAH

Haiwezekani Kumuona Allaah Katika Maisha Haya

Kuhusu kuwa yawezekana kuonekana kwa Allaah katika maisha haya,

wamesema baadhi kwamba kuna kauli mbili katika suala hili wakati wengine

wanasema ya kwamba kuna uwezekano wa kuonekana kwa Allaah katika maisha

haya. Maoni yote haya mawili ni upotofu. Maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-

Jamaa'ah wamekubaliana ya kwamba hakuna yeyote awezae kumuona Allaah

katika maisha haya kwa macho. Wametofautiana tu ya kuwa Mtume wetu (Swalla

Allaahu 'alayhi wa sallam) alimuona [Allaah Mi´raaj] au hapana. Kumepokelewa

kutoka sehemu mbalimbali kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam) kuwa amesema haiwezekani kumuona Allaah katika maisha haya.

Miongoni mwao, amepokea Muslim katika "as-Swahiyh" yake ya kwamba Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema wakati alipomtaja ad-Dajjaal:

"Jueni ya kwamba hakuna mtu yeyote katika nyinyi ambaye atamuona Mola

Wake mpaka pale atapokufa."

Wakati Muusa bin ´Imraan ('alayhis-Salaam) alipomuomba Allaah kuweza

kumuona, Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Akamjibu:

تراني لن

“Hutoniona!”1

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah

Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 122

al-Muzaniy Kuhusu Kumuona Allaah

1 (al-A´araaf 7 : 143)

Page 14: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

14

Siku ya Qiyaamah [waumini] watamuona Mola Wao. Hawatopata usumbufu

wowote kwa hilo na wala hawatoweka shaka. Himidi ni Zake kwa neema Yake

nyuso zao zitang´ara na watamwangalia. Watabaki katika neema ya daima:

ال يمسهم فيها نصب وما هم منها بمخرجين

“Haitowagusa humo machofu nao humo hawatotolewa (watadumu milele).”2

افرين النارالنهار أكلها دآئم وظلها تلك عقبى الذين اتقوا وعقبى الكمثل الجنة التي وعد المتقون تجري من تحتها

"Mfano wa Jannah ambayo wameahidiwa wenye taqwa, (Pepo) inapita chini yake

mito. Matunda yake ni ya kudumu, na (pia) kivuli chake. Hiyo ndiyo hatima

(njema) ya wale waliokuwa na taqwa. Na hatima (mbaya) ya makafiri ni Moto.”3

Wakanushaji watazuiliwa kumuona Mola Wao. Wataunguzwa Motoni:

ونخالد هم العذاب وفي عليهم للا سخط أن أنفسهم لهم قدمت ما لبئس كفروا الذين يتولون منهم كثيرا ترى

“Utawaona wengi miongoni mwao (Mayahudi katika mji wa Mtume)

wanawafanya marafiki wale waliokufuru. Ubaya ulioje kwa yale

waliyotanguliziwa na nafsi zao, (nayo ni) kuwa Allaah Amewaghadhibikia, na

katika adhabu wao watadumu milele.”4

ي كل كفوروالذين كفروا لهم نار جهنم ال يقضى عليهم فيموتوا وال يخفف عنهم من عذابها كذلك نجز

"Na wale waliokufuru watapata (adhabu ya moto wa)

Jahannam. Hawatahukumiwa (mauti) ili wafe, na wala hawatakhafifishiwa

adhabu yake. Hivyo ndivyo Tunavyomlipa kila mwenye kukufuru mno.”5

Isipokuwa tu wale ambao Atataka kuwarehemu miongoni mwa wale waliokuwa

wakimuabudu.

Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Yahyaa al-Muzaniy (d. 264)

Chanzo: as-Sunnah, uk. 43

2 (al-Hijr 15 : 48) 3 (ar-Ra´d 13 : 35) 4 (al-Maaidah 05 : 80) 5 (Faatwir 35 : 36)

Page 15: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

15

Hutoniona Kamwe Au Hutoniona?

Allaah (Subhaanah) Anasema:

ولما جاء موسى لميقاتنا وكلمه ربه قال رب أرني أنظر إليك قال لن تراني

"Na alipokuja Muwsaa katika miyqaat (pahala pa miadi) yetu, na Mola wake

Akamsemesha, (Muwsaa) alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”

(Allaah) Akasema: “Hutoniona!"."6

Anaeleza (Ta´ala) kwamba baada ya Muusa ('alayhis-Salaam) kuja katika miadi ya

Allaah (Ta´ala) na Akazungumza Naye (Ta´ala), akamuomba ajionyeshe kwake ili

amtazame Yeye. Akasema:

“Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.”

Wanachuoni wengi wamekutana na matatizo na neno "Lan" na kuwa

linamaanisha "kamwe" au hapana. Mu'tazilah wamelitumia kwa kuthibitisha

kuwa Allaah hatoonekana si katika maisha haya wala maisha baada ya haya. Hata

hivyo, haya ni maoni dhaifu. Kumepokelewa [mapokezi mengi] kutoka kwa

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ya kwamba waumini

watamuona Allaah siku ya Qiyaamah. Dalili nyingine ya hilo ni Kauli Yake

Allaah kuhusu makafiri:

كل إنهم عن ربهم يومئذ لمحجوبون

"Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa kumuona Mola Wao".7

Ili kuoanisha Aayah pamoja na Hadiyth zisemazo ya kwamba Allaah ataonekana

siku ya Qiyaamah, baadhi yao wamesema kwamba "Lan" inamaanisha ya

kwamba Allaah kamwe hatoonekana katika maisha haya [ya duniani].

Wengine wamesema maneno katika hali hii ni kama maneno katika Kauli Yake

(Ta´ala):

الخبيرال تدركه البصار وهو يدرك البصار وهو اللطيف 6 (al-A´araaf 7 : 143)

7 (al-Mutwaffifiyn 83 : 15)

Page 16: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

16

"Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho; Naye Al-

Latwiyful-Khabiyr (Mwenye Kudabiri mambo kwa utuvu, Mjuzi - Mjuzi wa undani

na ukina wa mambo)."8

Maelezo yake yameshatajwa tayari katika Suurat "al-An'aam". Katika maandiko

ya kale yasemekana ya kwamba Allaah (Ta´ala) alimwambia Muusa ('alayhis-

Salaam):

"Muusa! Hakuna mtu yeyote atakayeniona mpaka afe kwanza."

Mwandishi: Imaam Isma´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy

Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-'Adhwiym (2/325-326)

Mu'assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Ibn-ul-Qayyim Dalili Ya Tano Ya Kuonekana

Dalili Ya Tano: Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:

ا يشاؤون فيها ولدينا مزيد لهم م

”Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.”9

at-Twabaraaniy kasema:

"´Aliy bin Abiy Twaalib na Anas bin Maalik wamesema:

"Yaani ni kutazama Uso wa Allaah (´Azza wa Jalla).”

Limesemwa pia na waliokuja baada yao (Taabi´uun) kama Zayd bin Wahb na

wengineo.

8 (al-An´aam 6 : 103)

9 (Qaf 50 : 35)

Page 17: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

17

Mwandishi: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah (d. 751)

Chanzo: Haadiyl-Arwaah ilaa Bilaad-il-Afraah, uk. 236

Ibn-ul-Qayyim Dalili Ya Sita Ya Kuonekana

Dalili ya sita: Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:

بي وهو اللطيف الم بمصار رك الم بمصار وهو يدم ركه الم ل تدم

“Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho; Naye Al-

Latwiyful-Khabiyr (Mwenye Kudabiri mambo kwa utuvu, Mjuzi - Mjuzi wa undani

na ukina wa mambo).”10

“Dalili hii ni ya ajabu, kwa sababu inatumiwa pia na wale wanaopinga kuonekana

[kwa Allaah]. Shaykh wetu (Ibn Taymiyyah) kaonyesha jinsi Aayah hii inatoa

dalili [ya kuonesha] kwa njia nzuri iwezekanavyo na akanambia:

"Naamini ya kwamba hakuna mtu Bid´ah yeyote anayejadili na Aayah au Hadiyth

Swahiyh, isipokuwa kwa hakika inakuwa ni dalili dhidi ya maoni yake."

Miongoni mwazo ni Aayah hii inayotoa dalili yenye nguvu ya kwamba

watamuona [Allaah (Ta´ala)] kuliko kutomuona [kama wanavyodai Ahl-ul-

Bid´ah]. Allaah Kataja Aayah hii wakati Amejisifia Yeye Mwenyewe. Ni jambo

lenye kujulikana ya kuwa kujitakasa kunatokea wakati tu Sifa zinapothibitishwa.

Ama kuhusiana na kitu kinachokataliwa tu, haichukuliwi kuwa ni ukamilifu wala

Kujitakasa kwa Mola ('Azza wa Jalla).

Kauli ya Allaah "Macho hayamdiriki (hayamfikii)” inathibitisha ukuu Wake

usiokuwa na kifani na kwamba Yeye ni Mkubwa na Mwenye nguvu zaidi kuliko

kitu kingine chochote. Hii ndio sababu ya kutodirikiwa (kutofikiwa).

Ibn 'Abbaas kasema:

""Macho hayamfikii Yeye... " ina maana kwamba hayamzunguki Yeye [macho ya

waja]."

10 (al-A´aam 6 : 103)

Page 18: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

18

Qatadah kasema:

"Yeye ni Mkubwa mno kwa kufikiwa na macho."

'Atiyyah kasema:

"Watamwangalia Allaah bila ya macho yao kuweza kumdiriki kwa sababu ya

ukuu Wake. Hata hivyo, macho Yake huwadiriki (huwafikia) wao. Hivyo Kasema

Allaah (Ta´ala):

“Macho hayamdiriki (hayamfikii) bali Yeye Anayadiriki macho.””

Ina maana waumini watamuona Allaah siku ya Qiyaamah kwa macho yao bila ya

kumzunguka Yeye kwa macho yao.

Mwandishi: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah (d. 751)

Chanzo: Haadiyl-Arwaah ilaa Bilaad-il-Afraah, uk. 236-238

Page 19: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

19

USO WA ALLAAH

Maimamu Ambao Wamefasiri Uso Wa Allaah Mwelekeo

al-Buutwiy anamnasibishia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengine ya

kwamba wao wamefasiri Uso wa Allaah kama mwelekeo, Qiblah au kiini.11

Ameona mwenyewe kwamba huku ni kuharibu (kupotosha) Uso ambao ni moja

katika Sifa ya Allaah za Dhati.

Fikra hii bila ya shaka yoyote ni ya makosa. Maimamu hawa hawakumaanisha

hivi anavyoona. Neno Wajh, Uso, linaweza kuwa na maana nyingi. Inaweza

kumaanisha kiini cha sifa, Dini, nia, mwelekeo na njia. Ni muktadha wa neno

ndio hutoa maamuzi wa nini (neno) linamaanisha. Ikiwa neno Wajh litafasiriwa

kwa kuzingatia baadhi ya maana hizi kutokana na muktadha sahihi au nyingine,

basi ni sahihi na si kuharibu. Hakika ni kwamba, (haya) ni maelezo tu ya neno

hili.

Hili linathibitisha kuwa Dr. Kakosea kabisa pindi anaposema kwamba

inaruhusiwa kuelewa Aayah na Hadiyth za Sifa za Allaah kama (kwa njia ya)

mafumbo na si (kwa njia ya) halisi. Hana hata dalili yoyote ya hilo kutoka kwa

Salaf. Aliyoyataja kutoka kwa baadhi yao aidha ni kwamba hayakuthibiti au ni

kwamba hayamaanishi kabisa hivyo anavyoona yeye.

Mwandishi: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

Chanzo: al-Bayaan li Akhtwaa' Ba´dhw-il-Kuttaab, uk. 144-145

Ibn Uthaymiyn Kuhusu Uso Wa Allaah

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema:

11 Kitu muhimu sana

Page 20: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

20

"Kitu pekee ambacho mtu huomba kwacho Uso wa Allaah ni Pepo."12

Hapa kunathibitishwa Uso wa Allaah ('Azza wa Jalla). Limethibiti katika Qur-aan,

Sunnah na Ijmaa´. Katika Qur-aan miongoni mwazo kuna:

إال وجههكل شيء هالك

“Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.”13

والذين صبروا ابتغاء وجه ربهم

”Na ambao wamesubiri kutaka Uso wa Mola wao.”14

Kuna Aayah nyingi mfano wa hizi.

Ama kuhusu Sunnah, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) anasema:

"Naomba kinga kwa Uso wako."

Watu wametofautiana juu ya Uso ambao Allaah Amejithibitishia Kwake

Mwenyewe. Je, ni kweli au ni muelezo wa Chake kwa vile hana Uso au ni usemi

wa kitu ambacho mtu anataka kukipata kwa ajili ya Uso Wake, au ni mwelekeo

Wake au ujira? Kuna Ikhtilaaf, lakini Allaah Kawaongoza waumini waliosema

kuwa Uso ni wa halisi kwa sababu Allaah (Ta´ala) Kasema:

ويبقى وجه ربك ذو الجلل واإلكرام

"Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”15

Kasema pia:

تبارك اسم ربك ذي الجلل واإلكرام

"Limetukuka Jina la Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”16

ni Sifa ya Uso na si ya Bwana. Ikiwa ni Uso ذو .ni Sifa ya Mola (Allaah) na si jina ذي

ndio umeelezwa kwa ukuu na utukufu, hivyo haiwezi kuwa na maana ya

thawabu, mwelekeo au kiini tu kwa vile Uso sio kiini.

12 Abu Daawuud (2/309). Hasan amesema al-´Iraaqiy, kama ilivyotajwa katika al-Munaawiys "Faydh-ul-

Qadiyr" (6/4).

13 (al-Qaswas 28 : 88) 14 (ar-Ra´d 13 : 22) 15 (ar-Rahmaan 55 : 27) 16 (ar-Rahmaan 55 : 78)

Page 21: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

21

Wanaokanusha wanasema kwamba Uso unamaanisha kiini, mwelekeo au

thawabu. Wanasema kwamba ikiwa mtu atamthibitishia Uso halisi, itakuwa na

maana ya kwamba Allaah ana mwili na miili yote inafanana. Kwa hivyo, itakuwa

na maana kwamba mtu anafanana na Allaah wakati Allaah ('Azza wa Jalla)

Anasema:

ليس كمثله شيء وهو السميع البصير

"Hapana kitu kama mfano Wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.”17

Kusema kwamba kuna mtu kama Allaah ina maana Qur-aan inadanganya.

Isitoshe wanasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tunasema kwamba yule

anayemfananisha Allaah ni kafiri. Wanarapigwa Radd namna hii:

Kwanza: Mnamaanisha nini kwa "mwili" mnaoukimbia [kuuthibitisha]? Je,

mnamaanisha mwili uliojumuisha miguu, mifupa na damu vinavyohitajiana

baadhi yavyo? Ikiwa ni hili ndio mnalomaanisha, tunakubaliana na nyinyi ya

kwamba Allaah Hayuko namna hiyo. Ni jambo lisilowezekana Yeye kuwa namna

hiyo. Na kama mnamaanisha Dhati halisi (iliyo) na Sifa kamilifu, hakuna ubaya

kwa hilo.

Pili: Ikiwa mnasema ya kwamba miili yote inafanana, basi huu ni uongo mkubwa

sana. Je, mwili wa dubu na mdudu chungu vinafanana? Kuna tofauti kubwa kati

ya hivyo viwili tunapokuja katika kipimo, uzito, wembamba, n.k. Ikiwa hoja hii

imeanguka, basi hali kadhalika matukio pia yameanguka, nayo ni kuwa Allaah

Anafanana na viumbe Vyake.

Isitoshe, tunaona jinsi hata binadamu wana nyuso tofauti. Huwezi kupata watu

wawili na nyuso za kufanana kabisa hata kama watakuwa ni mapacha.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn

Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/357)

at-Twabariy Kuhusu Uso Wa Allaah

17 (ash-Shuraa 42 : 11)

Page 22: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

22

Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:

كل من عليها فان ويبقى وجه ربك ذو الجلل واإلكرام

"Kila kilioko juu yake kitatoweka. Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye

utukufu na ukarimu.”18

Allaah (Ta´ala) Anasema ya kwamba majini yote na wanadamu duniani

watatoweka, lakini Uso wa Mola Wako, Muhammad, utabaki katika ukuu na

utukufu wake. Ukuu na utukufu ni Sifa ya Uso. Kwa sababu Dhuu (ذو) ni

nominative. Yasemekana kuwa katika usomaji wa ´Abdullaah kuko Dhiy (ذي)

ambalo kwa hivyo itakuwa ni Sifa za Mola.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Jariyr at-Twabariy (d. 310)

Chanzo: Jaami´-ul-Bayaan (27/166)

Dalili Ya Uso Wa Allaah I

Allaah (Jalla wa 'Azz) Anasema:

كل شيء هالك إال وجهه له الحكم وإليه ترجعون

"Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake. Ana Hukumu (ya mambo yote)

na Kwake Pekee mtarejeshwa.”19

Hali kadhalika, Anasema Allaah ('Azza wa Jalla):

ويبقى وجه ربك ذو الجلل واإلكرام

"Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”20

18 (ar-Rahmaan 55 : 26-27) 19 (al-Qaswas 28 : 88) 20 (ar-Rahmaan 55 : 27)

Page 23: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

23

Pia kumetajwa ambayo ni sahihi yamethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu

'alayhi wa sallam), ambayo yanaonesha ya kuwa ni ya uhakika ['Alaa Haqiyqati

dhaalik].

Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Anasema (katika maana):

"Bustani ya Firdaws ni nne; mbili ni za dhahabu – vipodozi vyake na usaidizi na

vile vilivyomo katika hivyo, na mbili ni za fedha – vipodozi vyake na vile

vilivyomo humo. Kitu pekee ambacho kipo kati ya watu na uono wa Mola wao, ni

pazia ya enzi kwenye Uso Wake katika Bustani ya Edeni".21

Suhayb amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

kafasiriwa Aayah:

للذين أحسنوا الحسنى وزيادة

"Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-Husnaa (Pepo)

na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).”:22

"Watapata kuona Uso wa Mola wao (Azz wa Jalla)."23

Ibn Mas'uud (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema katika "al-Musnad":

"Watapata kuona uso wa Allaah (Azza wa Jalla)."

Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu) kasema:

"Watapata kuona Uso wa Allaah (´Azza wa ´Alaa)."24

Hali kadhalika amefasiri Hudhayfah bin al-Yamaan.25

Jaabir amesema (katika maana):

"Sema: “Yeye ni Al-Qaadir (Muweza daima) wa Kukuleteeni adhabu kutoka juu

yenu... " ilipoteremshwa, akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): 21 al-Bukhaariy na Muslim. 22 (Yuunus 10 : 26) 23 Muslim 24 ash-Shari'ah, uk. 257, na al-Aajurriy.

25 Ibid. uk. 265

Page 24: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

24

"Najikinga kwa Uso Wako" na “... au kutoka chini ya miguu yenu... "26 yeye

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam): "Najikinga kwa Uso Wako.'"27

Ibn Mas'uud akasema:

"Mola Wenu hana usiku wala siku yoyote. Mwanga wa mbingu unatoka kwenye

nuru ya Uso Wake."

'Abdullaah bin Ja'far kasema:

"Wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alipokwenda Twaa'if, aliomba

(katika maana): "Allaah, naomba kinga kwa nuru ya Uso Wako inayoangaza

mbingu.”"

Hadiyth hii inatoa dalili kuonyesha maana ya Maneno ya Allaah (Ta´ala):

للا نور السماوات والرض مثل نوره كمشكاة فيها مصباح

"Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi. Mfano wa Nuru Yake kama shubaka (lenye

kuwekwa) taa ndani yake. Taa hiyo iko katika gilasi (tungi)."28

Ibn 'Umar kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

kasema kuhusu nafasi ya juu watu wa Peponi watafikia (katika maana):

"Yule ambaye ana nafasi bora katika wao ni yule ambaye anaangalia Uso wa

Allaah (´Azza wa Jalla) mara mbili kwa siku."29

Allaah ('Azza wa Jalla) Kasema:

وجوه يومئذ ناضرة إلى ربها ناظرة

"Zipo nyuso siku hiyo zitaong'ara, zinamwangalia Mola Wao."30

Wafasiri wa Qur-aan kama Ibn 'Abbaas31, na Maswahabah wengine na Taabi'uun

kama Muhammad bin Ka´b, ´Abdur-Rahmaan bin Saabit, al-Hasan bin Abiyl-

26 (al-An´aam 06 :65). 27 Ibn Jariyr (9/222-223).

28 (an-Nuur 24 : 35) 29 at-Tirmidhiy (7/268).

30 (al-Qiyaamah 75 : 22-23)

31 al-Lalakaa'iy (63-64).

Page 25: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

25

Hasan32, 'Ikrimah33, Abu Swaalih, Sa´iyd bin Jubayr na wengine wamekubaliana

kwamba nyuso hizi zitaangalia Uso wa Mola Wao.

Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda

Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 94-103

Maktabah al-Ghurabaa al-Athariyyah, 1414/1994.

Dalili Ya Uso Wa Allaah II

Jaabir kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

kasema:

"Kitu pekee ambacho mtu anaomba kwacho kwa Uso wa Allaah ni Pepo."34

Hadiyth hii ni moja ya dalili nyingi katika Qur-aan na Sunnah zinazothibitisha

Uso wa Allaah (Ta´ala). Ni Sifa ya ukamilifu na kuikanusha kunaonyesha

upungufu uliokithiri na njia ya kumfananisha Yeye na vipungufu. Hali kadhalika

kunaingia humo kwa kukanusha zote, au baadhi, Sifa zingine. Matukio yake ni

kuwa wameanguka katika kitu ambacho ni kibaya zaidi kuliko kile

wanachokikimbia – Ametakasika Allaah kutokana na yale madhalimu

wanayoyasema.

Njia za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wote wanaamini yale ambayo Allaah

Kajielezea Mwenyewe katika Qur-aan na yale ambayo Mtume Wake (Swalla

Allaahu 'alayhi wa sallam) Kamuelezea Yeye kwa njia inayolingana na utukufu na

ukuu wa Allaah.

Hivyo wanamthibitishia Yeye yale Aliyojithibitishia Mwenyewe katika Kitabu

Chake na yale ambayo Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

Kamthibitishia Yeye. Hata hivyo, wanapinga ya kwamba hakuna kiumbe

32 Ibn Jariyr (29/192).

33 Ibid. (29/192).

34 Abu Daawuud (2/309).

Page 26: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

26

kinachofanana na Yeye. Kama ambavyo Dhati Yake haifanani na dhati za viumbe,

vile vile hazifanani Sifa Zake na sifa za viumbe. Atakayezipinga amepinga

ukamilifu Wake.

Mwandishi: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Hasan Aal ash-Shaykh

Chanzo: Fath-ul-Majiyd, uk. 412

Salaf Kuhusu Kuonekana Kwa Allaah Na Uso Wa Allaah

Ama kuhusu Taabi'uun (waliokuja baada ya Maswahabah) na waumini katika

maimamu wa Hadiyth, Fiqh, Tafsiyr na Taswawwuf, wanamjua Allaah tu ('Azza

wa Jalla) kwa maneno mangapi walizofanya kuhusu qadhiya hii. Sa´iyd bin al-

Musayyab kasema kuhusu:

ن وزيادة سم سنوا الم ليلذين أحم

”Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-

Husnaa (Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).”

(Yuunus 10 : 26):

"Zaidi maana yake ni kutazama Uso wa Allaah."

Imepokelewa na Maalik kupitia kwa Yahyaa.

al-Hasan al-Baswriy kasema:

"Zaidi maana yake ni kutazama Uso wa Allaah."

Imepokewa na Ibn Abiy Haatim kwa njia yake.

'Abdur-Rahman bin Abiy Laylaa kasema:

"Zaidi maana yake ni kutazama Uso wa Allaah (Ta´ala)."

Imepokelewa na Hammaad bin Zayd kupitia Thaabit.

Page 27: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

27

Hali kadhalika kasema hivi 'Amir bin Sa'd al-Bajliy, ambayo kapokea Sufyan

kupitia kwa Abu Ishaaq. Hali kadhalika kasema hivi 'Abdur-Rahmaan bin Saabit,

ambayo at-Twabariy kapokea kupitia kwa Layth. Hali kadhalika yamesemwa na

'Ikrimah, Mujaahid, Qataadah, as-Suddiy, adh-Dhahhaak na Ka´b.

'Umar bin 'Abdil-'Aziyz alimuandikia mmoja wa wafanyakazi wake:

"Nawasihi kumcha Allaah na muendelee kumtii na kujisalimisha Kwake na kwa

amri Zake. Shikamana na mkataba Aliyouchukua kwako na kukutaka

kushikamana na Kitabu Chake. Kwa kuwa na uchaji Allaah huepuka marafiki

Zake wa karibu khasira Zake. Pamoja na hilo watakuwa pamoja na Mitume na

kwa hilo zitakuwa nyuso zao ziking´ara wakati wanapomwangalia Muumbaji

wao. "

al-A'mash na Sa´iyd bin Jubayr kasema:

"Mbora Peponi ni yule ambaye atapata kumwangalia Allaah (Tabaaraka wa

Ta´ala) asubuhi na jioni."

Hishaam bin Hassaan kasema:

"Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Atajionyesha (jihidhirisha) Mwenyewe kwa watu

wa Peponi. Watapomuona, watasahau zawadi za Peponi."

Taawuus kasema:

"Wale walioshikamana na maoni (rai) na kulinganisha watakuja kufanya hivyo

mpaka pale watakapokanusha Muono (wa Allaah) na kwenda kinyume na Ahl-

us-Sunnah."

Abu Ishaaq as-Sabiy'iy kasema kuhusu:

”Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (jazaa ya ihsaan; nayo ni) al-

Husnaa (Pepo) na zaidi (ya hayo ni kupata taadhima ya kumuona Allaah).”:

"Zaidi maana yake ni kuangalia Uso wa Mwingi wa Rahmah."

Page 28: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

28

'Abdullaah bin al-Mubaarak kasema:

"Yule ambaye anataka kumwangalia Allaah, Uso wa Muumba Wake, afanye

´amali njema mema na asimueleze yeyote kuhusu hayo."

Mwandishi: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah (d. 751)

Chanzo: Haadil-Arwaah ilaa Bilaad-il-Afraah, uk. 268-270

Ibn Khuzaymah Kuhusu Uso Wa Allaah

Mlango: Yanayothibitisha Uso wa Allaah ambao Ameuelezea kwa enzi na

utukufu:

ويبقى وجه ربك ذو الجلل واإلكرام

"Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”35

Amethibitisha kwamba Yeye Atabaki wakati vyengine vyote atavyoaumua

vitatoweka, kuangamia. Ametakasika Yeye katika utukufu Wake ambaye hakuna

chochote katika Sifa Zake kitachotoweka. Anasema (Jalla wa ´Alaa):

ويبقى وجه ربك ذو الجلل واإلكرام

"Na utabaki Uso wa Mola Wako Mwenye utukufu na ukarimu.”36

Kasema:

كل شيء هالك إال وجهه

"Kila kitu ni chenye kuhiliki isipokuwa Uso Wake.”37

Anasema (Ta´ala) kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

واصبر نفسك مع الذين يدعون ربهم بالغداة والعشي يريدون وجهه

35 (ar-Rahmaan 55 : 27)

36 (ar-Rahmaan 55 : 27) 37 (al-Qaswas 28 : 88)

Page 29: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

29

"Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao asubuhi na

jioni, wanataka Uso Wake.”38

Kasema (Ta´ala):

وهلل المشرق والمغرب فأينما تولوا فثم وجه للا

"Na ni (milki) ya Allaah Mashariki na Magharibi; basi popote mnapogeuka

kuna Uso wa Allaah.”39

Kwa hivyo, Kajithibitishia Yeye Mwenyewe Uso na Kaueleza kwa enzi na

utukufu. Kathibitisha kwamba Uso Wake utabakia na kukanusha kuwa

vitatoweka.

Sisi na wanachuoni wengine wote wa Hijaaz, Tuhaamah, Yemen, Iraaq, Shaam na

Misri tunamthibitishia Allaah yale Aliyojithibitishia Yeye Mwenyewe.

Tunathibitisha hilo kwa ndimi zetu na kuuamini hilo kwa mioyo yetu.

Tunatakiwa kufanya hilo bila ya kufananisha Uso wa Muumba Wetu na viumbe.

Ametakasika Allaah kwa kufanana na viumbe Vyake. Ametakasika Allaah kuwa

kama jinsi wakanushaji wanavyosema. Ametakasika Allaah kwa kutokuwa kitu,

wasemalo waongo. Kwa kuwa kinachokosa sifa si lolote si chochote. Ametakasika

Allaah kwa yale wayasemayo Jahmiyyah. Wanakanusha kabisa Sifa za Mola Wetu

Alizojithibitishia Yeye Mwenyewe katika maandiko Yake na kupitia Mtume Wake

Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam).

Mwandishi: Imaam Abu Bakr bin Khuzaymah (d. 311)

Chanzo: Kitaab-ut-Tawhiyd (1/24-26)

38 (al-Kahf 18 : 28) 39 (al-Baqarah 02 :115)

Page 30: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

30

VIDOLE VYA ALLAAH

Vipi Salaf Walikuwa Wakiamini Vidole Vya Allaah?

Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Kasema:

ماوات مطمويات بيمينه م المقي امة والس يعا قـبمضته يـوم رمض ج ره والم بل اللـه فاعمبدم وكن مين الشاكرين وما قدروا اللـه حق قدم

”Bali Allaah (Pekee) mwabudu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru. Na

hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote Ataikamata

(Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake

wa kulia.”40

Padiri mmoja wa kiyahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

na kusema:

“Muhammad, katika Tawrat tunapata ya kwamba Allaah siku ya Qiyaamah

Atakuja kuziweka mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, milima katika

Kidole, nyota katika Kidole na baki ya viumbe katika Kidole. Halafu Atawatikisa

na kusema: “Mimi ndiye Maalik!.”” Hivyo akacheka Mtume wa Allaah (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) kiasi ambacho meno yake ya magego yakaonekana

ishara ya kuonesha kuwa padiri huyu kasema kweli. Kisha akasoma:

"Kwa hakika, wanajisalimisha kwa Allaah! Siku ya Qiyaamah dunia Ataibana na

mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia."41

Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy

Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (4/79)

Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001

40 (az-Zumar 39 : 66-67) 41 al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Jariyr.

Page 31: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

31

Vidole Vya Allaah

262 - 'Abdullaah bin 'Amr (Radhiya Allaahu 'anhumaa) amesimulia kwamba

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mioyo ya waja (binaadamu) iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Ar-

Rahmaan."42

263 - Bishr bin al-Haarith kasema:

"Jahmiyyah wanazikabili Hadiyth hizi kwa kiburi."

264 - 'Abdullaah bin Mas'uud kaelezea kwamba kuna Myahudi alikuja kwa

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kusema:

“Abul-Qaasim! Kwa hakika Allaah Atabeba viumbe katika Kidole, mbingu katika

Kidole, ardhi katika Kidole, bahari katika Kidole na nyota katika Kidole.” Hivyo

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka dalili ya kuthibitisha

kiasi ambacho meno ya magego yakaonekana. Na Allaah (´Azza wa Jalla)

Akateremsha:

وما قدروا للا حق قدره والرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينه

"Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote

Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa

Mkononi Mwake wa kulia."43

265 - Yahya bin Sa´iyd kasema:

42 Muslim (2654), Ahmad (2/168), Ibn Hibban (902) na wengineo. 43 (az-Zumar 39 : 67); al-Bukhaariy (4811), Muslim (2786), at-Tirmidhiy (3238) na wengineo.

Page 32: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

32

"Hapa ameweka (ongezea) Fudhayl bin ´Iyaad kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa

Ibraahiym, kutoka kwa ´Abiydah, kutoka kwa 'Abdullaah ambaye kasema:

"Alicheka kama ishara ya kuthibitisha (kukiri).""

266 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) amesimulia kwamba Mtume wa

Allaah (Salla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

"Siku ya Qiyaamah Allaah ('Azza wa Jalla) Atazikamata. Mbingu Atazikunja

katika Mkono Wake wa kulia. Kisha atasema: "Mimi ndiye Maalik! Wako wapi

wafalme wa duniani?"'44

267 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kasimulia kwamba Mtume (Swalla

Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Hakuna mtu anaetoa thawabu nzuri - na Allaah ('Azza wa Jalla) ni mzuri na

Hakukubali isipokuwa tu vizuri – isipokuwa Mwingi wa Rahmah (Tabaaraka wa

Ta´ala) Huichukua kwa Mkono Wake wa kulia, hata kama itakuwa ni tende moja.

Kisha Huikuza katika Kitanga cha Mkono wa Mwingi wa Rahmah hadi inakuwa

kubwa kuliko mlima".45

Mwandishi: Imaam Abu Bakr al-Ajurriy

Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 321-327

Daar al-Kitaab al-´Arabiy

Kidole Kidogo Cha Allaah

Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) Kasema:

44 al-Bukhaariy (4812), Muslim (2787), Ahmad (2/374) na wengineo.

45 al-Bukhaariy (1410), Muslim (1014), at-Tirmidhiy (661) na wengineo.

Page 33: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

33

ا فـلما تلى ربه للمجبل جعله دك

“Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye

kuvurugika vurugika... ”46

Abu Ja'far at-Twabariy kasema kuhusu Aayah hii:

"Ahmad bin Suhayl al-Waasitiy katueleza: Qurrah bin 'Iysa katueleza: al-A'mash

katueleza kutoka kwa mtu, kutoka kwa Anas ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu

'alayhi wa sallam) kasema:

"Hivyo Allaah Akajidhihirisha katika jibali, Akaashiria kwa Kidole Chake na

ikavurugika vurugika kuwa kifusi cha ardhi.”

Abu Ismaa´iyl alionesha hilo kwa kidole chake kidogo."

Katika isnadi hii kuna mpokezi asiejulikana. Kisha akasema at-Twabariy:

"al-Muthannah katueleza: Hajjaaj bin Minhaal katueleza: Hammaad katueleza

kutoka kwa al-Layth, kutoka kwa Anas." Njia maarufu ni ya Hammaad bin

Salamah kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, ambayo Ibn Jariyr amesema:

"al-Muthannah kanieleza: Hudbah bin Khaalid katueleza: Hammaad bin Salamah

katueleza kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambaye kasema:

"Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alisoma “Basi Mola Wako

Aliopojidhihirisha katika jabali, Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika",

akaweka kidole gumba karibu na kidole kidogo na kusema:

"Jabali lilididimia (liliangamia)."

Humayd alimwambia Thaabit: "Je, kasema namna hii?" Hivyo akanyanyua

Thaabit mkono wake, akampiga Humayd kwenye kifua na kusema, "Je, nifiche

hilo baada ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Anas

wametusimulia?"

Kwa njia hii imepokelewa pia Imaam Ahmad katika "al-Musnad" yake:

"Abul-Muthannah Mu'aadh bin Mu'aadh al-'Anbariy katueleza: Hammaad bin

Salamah katueleza: Thaabit al-Bunaaniy katueleza kutoka kwa Anas bin Maalik,

kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye amesema 46 (al-A´araaf 07 : 143)

Page 34: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

34

kuhusiana na Aayah “Basi Mola wako Aliopojidhihirisha katika jabali,

Alilijaalia kuwa lenye kuvurugika vurugika",

"Namna hii" yaani ni kwamba Alionesha sehemu ya kidole kidogo."

Ahmad kasema:

"Mu'aadh alituonesha hilo sisi. Hivyo akasema Humayd at-Tawiyl kumwambia:

Una maanisha nini kwa hilo?" Akampiga pigo la nguvu kwenye kifua na kusema:

"Wewe ni nani, Humayd? Wewe ni nini, Humayd? Anas bin Maalik kanieleza hili

kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na wewe unanambia nini

ninachomaanisha kwa hili?"

Namna hii pia imepokelewa na at-Tirmidhiy kutoka kwa 'Abdul-Wahhab bin al-

Hakam al-Warraaq, kutoka kwa Mu'aadh kwa isnadi iliyobaki. Vilevile alipokea

kutoka kwa 'Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daarimiy, kutoka kwa

Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah kwa isnadi iliyobaki.

Kisha akasema at-Tirmidhiy:

"Hii ni Hadiyth Hasan na Swahiyh ambayo tunaijua pekee kaipokea kupitia kwa

Hammaad."47

Vile vile, kapokea al-Haakim katika 'al-Mustadrak' yake kupitia kwa Hammaad

bin Salamah kwa isnadi iliyobaki na kusema:

"Hii ni Hadiyth Swahiyh inayoeneza masharti, si al-Bukhaariy wala Muslim

hawakuipokea."

Imepokelewa pia na Abu Muhammad al-Hasan bin Muhammad bin 'Aliy al-

Khallaal, kutoka kwa Muhammad bin 'Aliy bin Suwayd, kutoka kwa Abul-

Qaasim al-Baghawiy, kutoka kwa Hudbah bin Khaalid, kutoka kwa Hammaad

bin Salamah. Kasema:

"Ni isnadi Swahiyh isiyokuwa na kasoro yoyote.”

47 Imaam al-Albaaniy akasema:

"Swahiyh." (Dhilaal-ul-Jannah (480-485)

Page 35: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

35

Chanzo: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy

Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhiym (2/326-327)

Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Dalili Ya Vidole Vya Allaah

´Abdullaah bin Mas'uud katueleza kwamba kuna mtu mmoja alikwenda kwa

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kumwambia:

“Abul-Qaasim, kwa hakika Allaah Atabeba viumbe katika Kidole, mbingu katika

Kidole, ardhi katika Kidole, bahari katika Kidole na nyota katika Kidole.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka dalili ya kuthibitisha

kiasi ambacho meno ya magego yakaonekana na Allaah (´Azza wa Jalla)

Akateremsha:

ات بيمينهوما قدروا للا حق قدره والرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطوي

"Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote

Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa

Mkononi Mwake wa kulia."4849

Ibn Mas'uud kasema pia:

“Padiri wa kiyahudi alikuwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na

kusema: “Muhammad, katika Tawrat tunapata ya kwamba Allaah siku ya

Qiyaamah Atakuja kuziweka mbingu katika Kidole, ardhi katika Kidole, milima

katika Kidole, nyota katika Kidole na baki ya viumbe katika Kidole. Halafu

Atawatikisa na kusema: “Mimi ndiye Maalik.”” Hivyo akacheka Mtume wa

Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kiasi ambacho meno yake ya magego

yakaonekana ishara ya kuonesha kuwa Padiri kasema kweli. Kisha akasoma:

قدروا للا حق قدره والرض جميعا قبضته يوم القيامة والسماوات مطويات بيمينهوما

48 (az-Zumar 39 : 67) 49 al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Khuzaymah, ad-Daaraqutniy na al-Bayhaqi.

Page 36: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

36

"Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote

Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa

Mkononi Mwake wa kulia."5051

Wanachuoni wamekubaliana kwamba Hadiyth hii ni Swahiyh.

Wahb bin Munabbih alisema:

"Viumbe vyote na ardhi vitaenda sambamba katika Kitanga cha Mkono wa Allaah

si lolote zaidi kuliko mbegu ya haradali."

an-Nawwaas bin Sam'aan alisimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu

'alayhi wa sallam) kasema (katika maana):

"Hakuna moyo isipokuwa uko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah

('Azza wa Jalla); Akitaka kuziweka sawa, Anaziweka sawa. Na Akitaka

kuzipotosha, Anazipotosha.” Kisha akasema: “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo,

uthibitishe moyo wangu katika Dini Yako.”52

Jaabir kasema:

"Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema mara nyingi (katika

maana): “Ewe Mwenye kuzigeuza nyoyo, uthibitishe moyo wangu katika Dini

Yako.” Kukasemwa: “Ewe Mtume wa Allaah, je una khofu juu yetu ilihali

tumekuamini na yale uliyokuja nayo?” Hivyo akasema (katika maana): “Kwa

hakika, mioyo iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Mwingi wa Rahmah

(´Azza wa Jalla) na Anazigeuza na kuzipeleka namna hii”” – Sufyaan ath-

Thawriy kalieleza kwa kidole cha kuashiria (cha shahada) na kidole kirefu na

akavitikisa.53

Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda

Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 83-93

Maktabah al-Ghurabaa’ al-Athariyyah, 1414/1994.

50 (az-Zumar 39 : 67) 51 al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Jariyr. 52 Ahmad, Ibn Mâdjah na Ibn Khuzaymah. 53 at-Tirmidhiy (6/349) na akasema: "Hadiyth hii ni Hasan na Swahiyh."

Page 37: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

37

MGUU WA ALLAAH

Dalili Ya Mguu Wa Allaah

Mlango: Kauli Yake (Ta´ala):

يوم نقول لجهنم هل امتألت وتقول هل من مزيد

"Siku tutapoiambia Jahannamu: ”Je! Umejaa?” Nayo itasema: “Je! Kuna ziada?"54

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema (katika maana):

"Allaah ('Azza wa Jalla) Ataweka Mguu Wake juu ya Moto ambao utasema:

"Inatosha, inatosha."

Abu Hurayrah kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam) kasema (katika maana):

"Pepo na Moto vitashindishana. Moto utasema: "Mimi ni nafasi (ya watu wenye)

kiburi na jeuri." Pepo nayo itasema: "Ndani yangu mimi hakuingii yeyote

isipokuwa wale madhaifu na watu wa chini." Ndipo Allaah (Jalla wa 'Azz)

Akasema kuambia Moto: "Wewe ni adhabu Yangu ambayo mimi Namuadhibu

kwayo nimtakaye katika waja Wangu.” Na Akauambia Pepo: “Wewe ni Rahmah

Yangu ambayo Mimi Namrehemu kwayo yule Nimtakaye katika waja wangu.

Nyote wawili mtajazwa. Wote mtashiba." Ama kuhusiana na Moto, haitojaa

mpaka hapo Allaah Atakapoweka Mguu Wake juu yake na hivyo utasema:

“Inatosha, inatosha...”55

Anas kapokea kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

kasema (katika maana):

54 (Qaf 50 : 30) 55al-Bukhaariy (8/595), Muslim (4/2186) na Ahmad (2/214).

Page 38: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

38

"Ataweka Mguu Wake juu ya Moto ambao utasema: “Inatosha, inatosha."56

Wanachuoni wamekubaliana kwamba Hadiyth hizi ni Swahiyh. Shujaa´ kasema

kwamba alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu tafsiri ya

Allaah Neno Lake (´Azza wa Jalla):

وسع كرسيه السماوات والرض

"Imeenea Kursiyy Yake (Kiti) mbingu na ardhi."57

na hivyo akasema (katika maana):

"Kursiy Yake ni kiti Chake cha Miguu (Fotpall) na ´Arshi Yake haiwezi

kupimwa."58

Namna hii ndio alivyopokea Shujaa´ bin Makhlad kutoka kwa Mtume (Swalla

Allaahu 'alayhi wa sallam) wakati Ishaaq bin Yasaar kasema katika Hadiyth yake

kutoka kwa Abu 'Aasim kwamba ni maneno ya Ibn 'Abbaas59. Hali kadhalika

wamepokea maswahibu wa ath-Thawriy kutoka kwake60 na pia imepokelewa

kutoka kwa 'Ammaar ad-Dihniy kwa njia ya Mawquuf.

Abu Muusa al-Ash'ariy kasema:

"Kursiy ni mahali pawili pa Miguu."61

Kinachoonesha kuwa upokezi wa Ibn 'Abbaas na Abu Muusa kuhusu Kursiy ni

Swahiyh, ni yale aliyotaja ar-Rabiy' bin Anas kutoka kwa Maswahabah wa Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na kwamba walisema kumwambia Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam):

"Kursiy imeizunguka mbingu na ardhi, lakini vipi kuhusu ´Arshi?" Kisha Hivyo

ndio Allaah ('Azza wa Jalla) Akateremsha:

56 al-Bukhaariy (8%594) na Muslim (4/2187).

57 (al-Baqarah 02 : 255) 58 ad-Daaraqutniy katika "Kitab al-Asmaa was-Swifaat" (3).

59 Tafsiyr Ibn Jariyr (3/10).

60 Ibid. (3/11).

61 Ibid. (3/10). Akielezea mnyororo ni nzuri [Hasan] na taarifa kupitia 'Aliy bin Muslim bin Sa´iyd at-

Tuusiy.

Page 39: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

39

وما قدروا للا حق قدره

"Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa.”6263

Mwandishi: Imaam Abu ´Abdillaah bin Manda

Chanzo: ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah, uk. 41-46

Maktabah al-Ghurabaa al-Athariyyah, 1414/1994.

62 (az-Zumar 39 : 67) 63 Tafsiyr Ibn Jariyr (3/10).

Page 40: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

40

KHASIRA ZA ALLAAH

Mapenzi Na Khasira Za Allaah Kwa Mtu

Allaah (Ta´ala) Anampenda mtu kunapokuwa na sababu ya kumpenda na

Anamchukia kunapokuwa na sababu ya kumchukia. Kutokana na hili, Allaah

Anaweza kumpenda mtu siku moja na Akamchukia siku nyingine. Kwa sababu

hukumu inategemea sababu. Ama kuhusiana na matendo, Allaah Hupenda

daima wema, uadilifu na mfano wa hayo.

Ahl-ut-Ta'wiyl wanakanusha Sifa hizi. Wanafasiri mapenzi na radhi kuwa ni

thawabu au kutaka kwa thawabu wakati wanafasiri khasira kuwa ni adhabu au

kutaka kwa adhabu. Wanasema linatokana na upungufu na kumfananisha na

viumbe kumthibitishia sifa hizi.

Sahihi ni kwamba zinathibitishwa kwa Allaah ('Azza wa Jalla) kwa njia

inayolingana na Yeye kama jinsi tu sifa nyinginezo zote ambazo zimethibitishwa

na Ahl-ut-Ta'wiyl. Ni jambo la wajibu kuwa na uhusiano ufuatao kwa Sifa

ambazo Allaah Amejithibitishia Yeye Mwenyewe:

1 - Ni lazima kuzithibitisha kama za kweli na za halisi.

2 – Haitakiwi kabisa kuzifananiza wala kuzifikiria.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn

Chanzo: al-Qawl al-Mufiyd (2/122)

Page 41: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

41

MIKONO YA ALLAAH

Mkono Wa Kulia Wa Allaah

Mkono wa Allaah wa kulia ni Sifa iliyothibitishwa. Ana Mikono miwili halisi.

Katika moja ya upokezi wa Muslim kumethibitishwa yote miwili Mkono wa

Allaah wa kulia na wa kushoto. Kuna wanachuoni wanaosema kwamba khabari

hii haijathibitishwa na kwamba khabari iliyothibitishwa ni "Mkono Wake

mwingine" badala ya "wa kulia".

Kwa hali yoyote, khabari hii haipingani na khabari hii:

"Mikono yote ya Mola Wangu ni ya kulia."64

Wanachuoni wamefafanua makusudio ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam) kwa Hadiyth hii, yaani ili mtu asifikirie ya kwamba kuna upungufu katika

Hadiyth hiyo nyingine. Baadhi ya watu wanaweza kufikiria ya kwamba huyo

Mkono wa kushoto au mwingine sio mkamilifu kama wa kulia.

Mkono wa Allaah wa kulia umethibitishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah

(Ta´ala) Kasema:

ركون عما يشم م المقيامة والسماوات مطمويات بيمينه سبم حاه وتـعا يعا قـبمضته يـوم رمض ج ره والم وما قدروا اللـه حق قدم

“Na hawakumthamini Allaah inavyostahiki kuthaminiwa; na ardhi yote

Ataikamata (Mkononi Mwake) Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa

Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’ala (Ametakasika na Ametukuka

kwa ‘Uluwwa) kutokana na yale (yote) wanayomshirikisha.”65

Katika Aayah hii wanaradiwa Mu'attwilah ambao wanasema kuwa Mkono wa

kuthibitishwa unapelekea katika kufananisha na viumbe. Vipi mtu wa busara

ambaye atazingatia Aayah hii na kusoma jinsi Mkono wa Allaah umeelezwa kwa

njia hii kubwa na kamilifu (anaweza) kusema kwamba maana yake ni

kufananisha na viumbe mtu akithibitisha Mkono wa Allaah kama mkono halisi?

64 Muslim (1827).

65 (az-Zumar 39 : 67)

Page 42: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

42

Isitoshe, jina zinazoendana sambamba kwa mambo mawili haina maana kuwa

uhakika wake ni sawa. Ikiwa hali ni hivyo kati ya viumbe, tofauti ni kubwa zaidi

kati ya Muumba na kiumbe.

Mwandishi: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad

Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 41-42

Allaah Kamuumba Aadam Kwa Mkono Wake

271 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Allaah ('Azza wa Jalla) Kamuumba Aadam ('alayhis-Salaam) kwa Mkono Wake

siku ya Ijumaa. Akampulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika

wamsujudie."66

272 – Inatakiwa kuwaambia Jahmiyyah ambao wanapinga kwamba Allaah ('Azza

wa Jalla) kamuumba Aadam kwa Mkono Wake:

"Nyinyi hamuamini Qur-aan. Mmeikanusha Sunnah na mmekwenda kinyume na

Ijmaa´. "

273 – Ambayo Qur-aan imethibitisha, Kaamrisha Allaah ('Azza wa Jalla) Malaika

kumsujudia Aadam. Wote wakafanya isipokuwa tu Ibliys. Allaah ('Azza wa Jalla)

Kasema kuhusu Ibliys:

قال يا إبليس ما منعك أن تسجد لما خلقت بيدي أستكبرت أم كنت من العالين

“(Allaah) Akasema: “Ee Ibliys! Nini kilichokuzuia usimsujudie Niliyemuumba

kwa Mikono Yangu? Je, umetakabari, au umekuwa miongoni mwa

waliojitukuza?”67

66 Muslim (845), Maalik (1/108), Abu Dawuud (1046) na wengineo.

67 (Swaad 38:75)

Page 43: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

43

274 – Ibliys akaingiwa na wivu kwa kuwa (Allaah) Alimuumba Aadam kwa

Mikono Yake tofauti na yeye.

275 - Wakati Muusa alikutana na Aadam na wakaanza kujadili, akasema Muusa

kumwambia Aadam:

"Wewe ndiye Aadam, baba yetu. Allaah Kakuumba kwa Mkono Wake,

Akakupulizia roho kutoka Kwake na Akaamrisha Malaika kukusujudia."

Hapa anaongelea Muusa kupitia hatua ambazo Allaah Alikuwa nazo hususan na

Aadam, tofauti na wengine. Yule anayekanusha hili, ni kafiri. Kisha akamjibu

Aadam na kusema:

"Je, ni wewe Muusa, ambaye Allaah Kakuchagua kwa ujumbe Wake na kwa

Maneno Yake (kwa kuongea nawe), Kakuandikia Tawraat kwa Mkono Wake na

ambaye umesoma Tawraat?"

276 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Aadam na Muusa walijadiliana. Muusa akamwambia: "Aadam, Allaah

Kakuumba kwa Mkono Wake, Akakupulizia roho kutoka Kwake, Akaamrisha

Malaika wakusujudie na akakuacha ueshi Peponi."68

277 – Hoja ya Muusa kwa Aadam ilikuwa ni kwamba Allaah Kamuumba kwa

Mkono Wake. Kwa upande mwingine, hoja ya Aadam kwa Muusa kwamba

Allaah Kaandika Tawraat kwa Mkono Wake.

278 - Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhumaa) Kasema:

"Allaah ('Azza wa Jalla) Kamteua Ibraahiym kwa urafiki wa karibu (Khullah),

Muusa kwa kuongea naye na Muhammad kwa muono – Swalah na salaam ziwe

juu yao."

Mwandishi: Abu Bakr al-Ajurriy

Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 331-334

Daar al-Kitaab al-´Arabiy

68 al-Bukhaariy (6614), al-Humaydiy (1116), Ibn Abiy 'Aasim (153) na wengineo.

Page 44: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

44

Allaah Ana Mikono Miwili Na Yote Ni Ya Kulia

268 - Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhumaa) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Kitu cha kwanza Allaah ('Azza wa Jalla) Kuumba, ni kalamu. Aliichukua kwa

Mkono Wake wa kulia - na Mikono Yake yote miwili ni ya kulia – Akaandika

kuwepo kwa dunia, ´amali za wenye kutenda, ya uchaji Allaah na ya uasi."

269 - 'Abdullah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume wa

Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Siku ya Qiyaamah, wale ambao ni waadilifu watakuwa upande wa Mkono wa

kulia wa Allaah ('Azza wa Jalla) - na Mikono Yake yote ni miwili - juu ya mimbari

ya nuru."69

270 - 'Abdullaah bin Salaam (Radhiya Allaah 'anhu) kasema katika Hadiyth yake

ndefu:

"Kisha akasema: "Aadam, chagua!" Akasema: "Mola, nachagua Mkono Wako wa

kulia na Mikono Yako yote ni ya kulia.” Akaunyoosha na huko akaona watoto

wake katika watu wa Peponi. Akasema: "Mola, ni kina nani hawa?" Akasema: “Ni

watoto wako hadi Siku ya Qiyaamah ambao Nimeamua Kuumba kwa watu wa

Peponi.””

Mwandishi: Imaam Abu Bakr al-Ajurriy

Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 329-330

Daar al-Kitaab al-´Arabiy

69 Muslim (1827), Ibn Hibban (4484), Nasa'iy-(8/221) na wengineo.

Page 45: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

45

KUJA KWA ALLAAH

Kuja Kwa Allaah Kunatoa Ushahidi Kushuka Kwake

Kuna Hadiyth nyingi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

kuhusu kuja kwa Allaah siku ya Qiyaamah. Hali kadhalika kuja Kwake kwa watu

wa Peponi siku ya Ijumaa. Ni moja ya hoja ambayo Salaf walikuwa wanatumia

dhidi ya wale wanaokanusha Hadiyth [ya kushuka]. Wakawafafanulia kwamba

Qur-aan inathibitisha maana ya Hadiyth. Kwa njia hii, alijadiliana nao kwa mfano

Ishaaq bin Raahuuyah dhidi ya Jahmiyyah walipokuwa kwa mtoto wa mfalme

Khuraasaan 'Abdullaah bin Twaahir. Abu 'Abdillaah ar-Ribaatwiy alisema:

"Siku moja nilikaa katika kikao cha 'Abdullaah bin Twaahir na Ishaaq bin

Raahuuyah alikuwepo. Akaulizwa kuhusu Hadiyth ya kushuka kama ni Swahiyh.

Akasema: "Ndiyo." Hivyo, wakasema baadhi ya wanaume wa 'Abdullaah: "Abu

Ya'quub! Je, unamaanisha ya kwamba Allaah Hushuka kila usiku?” Akasema:

“Ndio." Hivyo akasema: “Hushuka vipi?” Akajibu: “Thibitisha kwanza kuwa

Yuko juu. Kisha baada ya hapo nitakueleza kushuka." Mtu yule akasema:

"Nathibitisha kuwa Yuko juu." Ishaaq akasema: "Allaah (Ta´ala) Kasema:

وجاء ربك والملك صفا صفا

”Na akaja Mola Wako na Malaika safu safu.”70

Hivyo akasema prince ´Abdullaah bin Twaahir: "Hii ni siku ya Qiyaamah." Ishaaq

akajibu: "Allaah Akuthibitishe prince! Kipi kitachomzuia Yeye Anayekuja siku ya

Qiyaamah kutokuja leo?"

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah

Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 39-40

at-Twabariy Kuja Kwa Allaah

70 (al-Fajr 89 : 22)

Page 46: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

46

Allaah ('Azza wa Jalla) Kasema:

وجاء ربك والملك صفا صفا

”Na akaja Mola Wako na Malaika safu safu.”71

Allaah (Ta´ala dhikruh) Kasema:

"Wakati Mola Wako Akaja, Muhammad, na Malaika Wake katika safu safu, safu

baada ya safu."

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Jariyr at-Twabariy (d. 310)

Chanzo: Jaami´-ul-Bayaan (30/232)

Na Akaja Mola Wako Na Malaika Safu Safu

Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Kasema:

وجاء ربك والملك صفا صفا

”Na akaja Mola Wako na Malaika safu safu.”72

Yaani (Akaja) kuwahukumu viumbe Wake. Hili litafanyika baada ya viumbe

kumuomba kiongozi wa wanaadamu, Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam), kumuomba Allaah (asimamishe Qiyaamah). Kabla ya hapo, waliwaomba

Mitume wengine wanne wakubwa. Wote wataomba radhi na kusema:

"Sina haki ya hilo."

Hatimaye, wataenda kwa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye

atasema:

71 (al-Fajr 89 : 22) 72 (al-Fajr 89 : 22)

Page 47: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

47

"Mimi ndiye mwenye haki ya hilo! Nina haki ya hilo!"

Atamuomba Allaah (Ta´ala) ili aje (ya'tiy) kuwahukumu [viumbe]. Namna hii

ndivyo Allaah Atamruhusu suala hili.

Hii ndio itakuwa Shafaa´ah (uombezi) ya kwanza na huitwa "cheo kinachosifika"

(al-Maqaam al-Mahmuud). Hapo ndipo Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Atakuja

(yajiy') Kuhukumu vile Apendavyo. Wakati wa tukio hili, Malaika watakuja

(yaji´uun) mbele Yake safu safu.

Mwandishi: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy

Chanzo: Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (4/657-658)

Mu’assasah ar-Risaalah, 1422/2001

Page 48: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

48

SAUTI YA ALLAAH

Allaah Huongea Kwa Sauti Ya Kusikika

Kuhusiana na Sauti ya Allaah, imepokelewa na 'Abdullaah bin Unays kutoka kwa

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

"Ataita kwa Sauti inayosikika na wote walio karibu na mbali: “Mimi ndiye Maalik

(Mfalme)! Mimi ndiye Maalik!””73

Imepokewa na Ahmad na maimamu wengine. al-Bukhaariy kataja hii kama dalili

yenye nguvu.

Ibn Mas'uud kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Wakati Allaah Anatamka kwa Wahyi, wakaazi wa mbinguni wanasikia Sauti

Yake kama mnyororo dhidi ya jiwe74 na wanasujudu."75

Kusema kwamba herufu na sauti hutoka kwa nje ya njia tu ni batili na

haliwezekani. Allaah (Ta´ala) Kasema:

يوم نقول لجهنم هل امتألت وتقول هل من مزيد

”Siku tutapoiambia Jahannamu: ”Je! Umejaa?” Nayo itasema: “Je! Kuna ziada?””76

Kaeleza kwamba mbingu na dunia vimesema:

أتينا طائعين

“Njooni mkiwa mmetii (kwa khiari) au kukirihika.”77

73 al-Bukhaariy (13/453) na al-Adab al-Mufrad (970) na Khalq Af'aal-il-'Ibad, uk. 131 na Ahmad (3/495).

Hasan kasema hivyo al-Mundhiriy katika "at-Targhiyb wat-Tarhiyb". al-Hakim kasema: "Isnadi ni

Swahiyh." adh-Dhahabiy kakubaliana nae.

74 Jiwe gumu sana 75 al-Bukhaariy (13/453), Abu Dawuud (4738) na Ibn Khuzaymah katika Kitaab-ut-Tawhiyd, uk. 95.

Swahiyh kasema al-Albaaniy katika "Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah" (1293).

76 (Qaf 50 : 30) 77 (Fusw-Swilat 41 : 11)

Page 49: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

49

Maneno haya hayatoki si nje ya njia wala si kwenye eneo. Vile vile, imepokelewa

kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwamba ule mguu wa

sumu ulizungumza naye78 na kwamba jiwe79 na mti vilimtolea Salaam80.

Mwandishi: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan

Chanzo: Qatf-uth-Thamar, uk. 84-85

Hadiyth Zilizo Swahiyh Kuhusu Sauti Ya Allaah

Katika mlango "ar-Radd 'alaa al-Jahmiyyah" wa "as-Swahiyh" yake kataja kwamba

al-Bukhaariy na mnyororo wa kupunguzwa:

"Ataita kwa Sauti inayosikika na wote walio karibu na mbali: “Mimi ndiye Maalik

(Mfalme)! Mimi ndiye Maalik!””81

Alikusanya mchanganyiko wa Hadiyth zote za Sauti. Mbali na kauli za

Maswahabah na waliokuja baada yao, ni zaidi ya Hadiyth kumi kutoka kwa

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Nilizifuatilia na kuzikusanya. Iliyosahihi zaidi

ni ile al-Bukhaariy kasimulia baada ya Hadiyth hii:

'Umar bin Hafs kanieleza: Baba yangu katueleza: al-A'mash katueleza: Abu

Swaalih katueleza, kutoka kwa Abu Sa'iyd al-Khudriy ambaye kasema kuwa

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam ) kasema:

"Allaah Atasema: "Aadam!" Hivyo atajibu: "Ninakuitikia." Kisha Ataita kwa Sauti:

“Allaah Anakuamrisha utoe nje kundi katika Ummah wako Motoni."82

78 al-Bukhaariy (6/272).

79 Muslim (2276).

80 at-Tirmidhiy (3703).

81 al-Bukhaariy na Fath-ul-Baari (13/452).

82 al-Bukhaariy (7483).

Page 50: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

50

Mwandishi: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy

Chanzo: Kitaab-ul-´Arsh (2/95)

Page 51: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

51

SURA YA ALLAAH

Allaah Kamuuumba Aadam Kwa Sura Yake

256 - Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Ikiwa mtu katika nyinyi atapiga [mtu mwengine], basi aepuke uso. Kwa hakika,

Allaah (Ta´ala) Kamuumba Aadam kwa sura Yake."83

257 - Abu Hurayrah akasema:

"Kwa hakika Allaah ('Azza wa Jalla) Kamuumba Aadam kwa sura Yake."

258 – Mapokezi haya Muislamu analazimika kuyaamini, na haitakiwi kusema

"Vipi?" au "Kwa nini?". Ni wajibu kuzipokea kwa kujisalimisha na kuzithibitisha,

bila ya kuzifanyia utafiti. Haya yamesemwa na maimamu wa hapo kabla.

259 - Abu Bakr al-Marwaziy kasema:

"Nilimuuza Abu 'Abdillaah Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) juu ya

Hadiyth kuhusu Sifa na Majina (ya Allaah), kama Kuona na kuhusu historia ya

´Arshi, ambazo zinapingwa na Jahmiyyah. Akasema: “Wanachuoni

wamezikubali. Makadirio yanakubaliwa vivyo hivyo kama yalivokuja.”"

260 - Abu Bakr al-Marwaziy alisema:

"Abu Bakr bin Abiy Shaybah na 'Uthmaan bin Abiy Shaybah walimuomba

Ahmad bin Hanbal idhini ya kupokea Hadiyth hizi wanazokanusha Jahmiyyah.

Akasema: "Zitangazeni! Kwa hakika wanachuoni wamezikubali.'"

261 – Nilisikia Abu 'Abdillaah az-Zubayriy aliulizwa kuhusu maana ya Hadiyth

hii. Akasema: "Tunaziamini kwa Imani ya kweli, bila ya kuziulizia. Hata hivyo,

tunasimama pale waliposimama. Hivyo, tunasema katika suala hili yale mpokeaji

aliyosema."

83 al-Bukhaariy (2559), Muslim (2612), Ahmad (2/244) na wengineo.

Page 52: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

52

Mwandishi: Imaam Abu Bakr al-Ajurriy

Chanzo: ash-Shari´ah, uk. 319-320

Daar al-Kitaab al-´Arabiy

Page 53: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

53

KUCHEKA KWA ALLAAH

Ibn Maajah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah

Mlago: Waliyokanusha Jahmiyyah

181 - Abu Bakr bin Abiy Shaybah katueleza: Yaziyd bin Haaruun katueleza:

Hammaad bin Salamah katueleza, kutoka kwa Ya'laa bin ´Atwaa, kutoka kwa

Wakiy´ bin Hudus, kutoka kwa mjomba wake Abu Raziyn ambaye alieleza kuwa

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mola Wetu Anacheka kwa maelezo ya waja Wake wakati kubadilika Kwake kwa

kweli kuko karibu." Nikasema: “Je, Mola Wetu Anacheka ewe Mtume wa Allaah?"

Akasema: "Ndiyo." Kisha akasema: "Basi Mola Ambaye Anacheka hatotunyima

kamwe kitu kizuri."84

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Yaziyd bin Maajah al-Qazwiyniy (d.273)

Chanzo: as-Sunan (181)

Ibn Khuzaymah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah

49 – Mlango: Uthibitisho wa Kucheka Kwa Mola Wetu ('Azza wa Jalla)

Hili litafanyika bila mtu kuelezea kucheka Kwake au kufananisha [kucheka

Kwake] na kucheka kwa viumbe. Tunaamini ya kwamba Anacheka kama

ambavyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alivyotufunza. Tunakaa

84 al-Albaaniy kasema:

"Hasan." (as-Sahiyhah 2810)

Page 54: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

54

kimya kuhusu namna85 Anavyocheka (Jalla wa ´Alaa). Allaah ('Azza wa Jalla)

Kalificha hilo kwetu [Ghayb] na Hakutueleza namna Anavyocheka.

Sisi tunasema yale ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) aliyosema

na tunaamini hilo kwa mioyo yetu na tunanyamazia yale ambayo hatukupata

kuyajua katika yale ambayo Allaah Kayafanya Ghayb Kwake Mwenyewe.

329 - Ibn Mas'uud kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)

kasema:

"Je, hamniulizi kwa nini nacheka? Namcheka mtu ambaye Mola wa viumbe

(´Azza wa Jalla) Alimcheka wakati alisema Kumwambia Yeye: ”Je, unanitania?"

Kisha Akasema: ”Sikutanii, mambo yote yako katika mamlaka Yangu.” Baada ya

hapo Akamuingiza Peponi.”

Mwandishi: Imaam Abu Bakr bin Khuzaymah (d. 311)

Chanzo: Kitaab-ut-Tawhiyd (2/563)

Ibn Battah Kuhusu Kucheka Kwa Allaah

Shikamaneni na elimu yenu – Allaah Awarehemu – ya kwamba ni katika sifa ya

watu wa haki kumthibitishia na kukubali mapokezi sahihi bila ya kupinga kwa

kulinganisha na maoni na matamanio. Imani ni kuthibitisha na muumini

anathibitisha. Allaah ('Azza wa Jalla) kasema:

ليما ويسليموا تسم نـهمم ث ل يدوا ف أفسهمم حرجا ميا قض يم موك فيما شجر بـيـم فل وربيك ل يـؤممنون حت يكي

”Basi Naapa kwa Mola wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu

(mwamuzi) katika yale wanayotofautiana baina yao, kisha wasione katika nyoyo

zao uzito katika uliyohukumu na wajisalimishe kwa unyenyekevu.”86

Katika sifa ya waumini ni kwamba wanamsifia Allaah kama jinsi Allaah (Swalla

Allaahu 'alayhi wa sallam) Alivyojisifia Yeye Mwenyewe na kama jinsi Mtume

85 Kayfiyyah 86 (an-Nisaa 04 :65)

Page 55: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

55

Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomsifia kupitia yale ambayo

yamesimuliwa na wanachuoni na kupokelewa na wapokezi waaminifu. Wanatoa

dalili kwa yale waliyopokea kwa yale mazuri na yasiokuwa mazuri, ya mila na

mapokezi. Hakusemwi kwa yale ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa

Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) "Vipi?" au "Kwa nini?". Wanafuata na

hawazushi. Wanajisalimisha na hawana kipingamizi. Wametosheka na hawana

shaka.

Katika mambo ya sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu

'alayhi wa sallam) kupitia wapokezi waaminifu na ambayo waumini ni lazima

wayaamini na ni Haramu kwenda kinyume chake, ni [kuamini kwamba] Allaah

(Ta´ala) Anacheka. Linakanushwa na analikanusha tu mtu wa Bid´ah ambaye hali

yake imehukumiwa na wanachuoni. Huyu ni katika yale mapote yaliyopotea na

maoni kutelekezwa na maoni yaliyokataliwa – Allaah Atulinde sisi na nyinyi na

Bid´ah zote na upotevu.

67 - Abu Raziyn al-'Uqayliy (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mola Wetu Anacheka kwa maelezo ya waja Wake wakati kubadilika Kwake kwa

kweli kuko karibu." Nikasema: “Je Mola Wetu Anacheka ewe Mtume wa Allaah?"

Akasema: "Ndiyo." Kisha akasema: "Basi Mola Ambaye Anacheka hatotunyima

kamwe kitu kizuri."87

68 - Abu Muusa al-Ash'ariy (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mola Wetu Atajidhihirisha kwetu siku ya Qiyaamah Akicheka.”88

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kaeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu

'alayhi wa sallam) kasema:

"Allaah (Ta´ala) Anawacheka watu wawili. Mmoja wao anamuua mwenzake na

wote wawili wanaingia Peponi. Yule aliyeuawa anapigana katika njia ya Allaah

na yule aliyeua Atasamehewa na ('Azza wa Jalla). Kisha atapigana yule aliyeua

katika njia ya Allaah na kufa shahidi".89

87 al-Albaaniy kasema: ”Hasan.” (as-Swahiyhah 2810) 88 al-Albaaniy kasema: ”Swahiyh.” (as-Swahiyha 755) 89 al-Bukhaariy (2826), Muslim (1890), Ibn Maajah (191) na wengineo.

Page 56: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

56

Mwandishi: Imaam ´Ubaydullaah bin Muhammad bin Battah al-´Ukbariy (d.

387)

Chanzo: al-Ibaanah al-Kubraa (3/3/91)

Ibn Abiy 'Aasim Kuhusu Kucheka Kwa Allaah

Mlango 118: Yaliyotajwa kuhusu kucheka kwa Allaah ('Azza wa Jalla)

554 - Hudbah bin Khaalid katueleza: Hammaad bin Salamah katueleza, kutoka

kwa Ya'laa bin ´Atwaa´, kutoka kwa Wakiy´ bin Hudus, kutoka kwa Abu Raziyn

ambaye kaeleza ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mola Wetu Anacheka kwa maelezo ya waja Wake wakati kubadilika Kwake kwa

kweli kuko karibu." Nikasem: “Je Mola Wetu Anacheka ewe Mtume wa Allaah?"

Akasema: "Ndiyo." Kisha akasema: "Basi Mola Ambaye Anacheka hatotunyima

kamwe kitu kizuri."90

555 - Ibn Musaffaa katueleza: Baqiyyah bin al-Waliyd katueleza: az-Zubaydiy

katueleza, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa 'Atwaa' bin Yaziyd, kutoka kwa

Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ambaye

amesema kuwa mtu wa mwisho ambaye ataingia Peponi atasema:

"Eeh Mola! Usiniache nikawa kiumbe Chako chakuangamia.” Atamuomba mpaka

hapo Allaah (Ta´ala) Atapomcheka na kumuingiza Peponi.”91

90 al-Albaaniy kasema:

"Hasan." (as-Swahiyhah 2810)

91 al-Albaaniy kasema:

"Isnadi yake ni Hasan na Swahiyh." (Dhilaal-ul-Jannah, uk. 256).

Page 57: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

57

Mwandishi: Imaam Abu Bakr bin Abiy ´Aasim ash-Shaybaaniy (d. 287)

Chanzo: as-Sunnah (554-555)

Page 58: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

58

ALLAAH KUWA NA PAMOJA NA VIUMBE VYAKE

Allaah Kuwa Na Viumbe Vyake Haina Maana Anachanganyika Nao Kimwili

Hanbal bin Ishaaq kasema katika kitabu "as-Sunnah":

"Nilimwambia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal: "Nini manaa ya Maneno ya

Allaah:

وهو معكم أين ما كنتم

"Naye yupamoja nanyi popote mlipo.”92

دسهم ألم تر أن للا يعلم ما في السماوات وما في الرض ما يكون من نجوى ثلثة إال هو رابعهم وال خمسة إال هو سا

وال أدنى من ذلك وال أكثر إال هو معهم أين ما كانوا ثم ينبئهم بما عملوا يوم القيامة إن للا بكل شيء عليم

"Kwani huoni kwamba Allaah Anajua vilivyomo katika mbingu na vilivyomo

katika ardhi? Hauwi mnong'ono wa watu watatu isipokua Yeye huwa ni wanne

wao, wala wa watano isipokuwa Yeye huwa ni wa sita wao. Wala wa wachache

kuliko hao, wala walio wengi zaidi, isipokuwa Yeye yu pamoja nao popote pale

walipo. Kisha Siku ya Qiyaamah Atawaambia waliyoyatenda. Hakika Allaah ni

Mjuzi wa kila kitu.”93

Akajibu:

"Ni elimu yake. Anajua yaliyofichikana na ya dhahiri. Anajua na kushuhudia

yote. Anajua yale yaliyofichikana. Mola Wetu Yuko juu ya ´Arshi bila ya mpaka

wala namna gani. Kursiy Yake imeizunguka mbingu na ardhi."

Imaam Ahmad akafafanua maana ya “Ma'iyyah” [kuwa Kwake pamoja na viumbe

Vyake], kwa ufafanuzi katika " ar-Radd 'alaa al-Jahmiyyah". Ma´iyyah imetajwa

katika Qur-aan kwa njia ya jumla, kama ilivyo katika Aayah hizi mbili, na kwa

njia maalum, kama ilivyo katika Aayah ifuatayo:

إن للا مع الذين اتقوا والذين هم محسنون

92 (al-Hadiyd 57 : 04) 93 (al-Mujadilah 58 : 07)

Page 59: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

59

"Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao

ni Muhsinuwn (wema).”94

أسمع وأرىقال ال تخافا إنني معكما

“(Allaah) Akasema: “Msikhofu; hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na

Naona.”95

معنا للا إن تحزن ال

"Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”96

Ingekuwa maana yake kwamba Yeye yuko pamoja na kila kitu kwa Dhati Yake,

sura hii ya jumla ingegongana na ile ya maalum. Ni jambo linalojulikana ya

kwamba Kauli ya Allaah:

معنا للا إن تحزن ال

"Usihuzunike, hakika Allaah Yu Pamoja nasi.”97

ni maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Abu Bakr kinyume

na maadui zao makafiri. Hali kadhalika Kauli Yake:

إن للا مع الذين اتقوا والذين هم محسنون

"Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao

ni Muhsinuwn (wema).”98

ni maalum kwa wale watendao mema na mazuri kinyume na madhalimu na

wafanyao madhambi.

Neno Ma'iyyah si katika kiarabu wala Qur-aan halina maana ya kuchanganyika

kimwili kati ya dhati mbili. Mfano wa hilo ni Kauli ya Allaah:

محمد رسول للا والذين معه

" Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na waliopamoja naye... "99

فأولئك مع المؤمنين

94 (an-Nahl 16 : 128) 95 (Twaaha 20 : 46) 96 (Tawbah 09 : 40) 97 (Tawbah 09 : 40) 98 (an-Nahl 16 : 128) 99 (al-Fath 48 : 29)

Page 60: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

60

"Basi hao watakuwa pamoja na Waumini... “100

الصادقين مع وكونوا للا اتقوا

" Mcheni Allaah na kuweni pamoja na As-Swaadiqiyn (wakweli)!"101

Na kuna dalili nyingi mfano wa hizi. Ndio maana ni jambo lisilowezekana Kauli

ya Allaah:

وهو معكم أين ما كنتم

" Naye yu pamoja nanyi popote mlipo.”102

ikawa na maana ya kwamba Dhati Yake imechanganyika na dhati ya viumbe.

Isitoshe, Kaanza Aayah kwa kuongelea kuhusu elimu na kaimalizia kwa

kuongelea kuhusu elimu. Hivyo basi, muktadha unathibitisha ya kwamba

Anamaanisha ya kuwa ana elimu ya viumbe Vyake.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah

Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 127

100 (an-Nisaa 04 : 146) 101 (Tawbah 09 : 119) 102 (al-Hadiyh 57 : 04)

Page 61: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

61

Ni Nani Mtu Wa Kwanza Aliyesema Kuwa Qur-aan Imeumbwa?

630 - Ibn Shawdhab kasema:

"Yeye - yaani Jahm – hakuswali kwa muda wa siku arubaini kutokana na shaka

[ya kuwepo kwa Allaah]. Baadhi ya Sumaniyyah103 walijadiliana na yeye na hivyo

akawa ameacha Swalah kwa muda wa siku arubaini."

631 - Yaziyd bin Haaruun kasema:

"Qur-aan ni Maneno ya Allaah. Ghadhabu ya Allaah iwe juu ya Jahm na wale

ambao wanaona na kufikiri kama yeye. Alikuwa ni mkanushaji Kaafir aliyeacha

Swalah kwa muda wa siku arubaini kwa kuwa alikuwa na mashaka ya Uislamu."

Yaziyd alisema:

"Ibn Ahwaz kamnyonga yeye Asbahaan kutokana na tamko hili."

632 - 'Ubayd bin Haashim kasema:

"Mtu wa kwanza kusema kwamba Qur-aan imeumbwa ni Jahm. Banu ´Umayyah

walimwita ili wamnyonge kisha kukawa kimya tena. Kisha kukajitokeza mtu

Kuufah na kusema kwamba Qur-aan imeumbwa. Wakati Ibn Abiy Laylaa alipata

khabari hiyo, alikwenda kwa ´Iysa bin Muusa na kumwambia hilo. Kisha

akamwandikia Abu Ja'far na Abu Ja'far akamwandikia na kusema:

"Muache atubie. Ikiwa hakufanya hivyo akatwe kiichwa chake."

Mtu huyo akatubia na kukawa kimya tena.”

633 – Sa´iyd bin Rahmah kasema:

103 Dhehebu la kihindi.

Page 62: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

62

"Jahm, ghadhabu za Allaah ziwe juu yake, alijitokeza mwaka 130 H na kusema

kwamba Qur-aan imeumbwa. Hivyo wakakubaliana wanachuoni ya kwamba

maoni yake ni kufuru (Kufr) – na hili ndilo waliloeleza watu kutoka kwao".

634 - Khalaf bin Sulaymaan al-Balkhiy kasema:

"Jahm alikuwa ni mwenye kutoka Kuufah. Alikuwa ni mwenye ufaswaha wa

kuongea lakini hakuwa msomi. Alikutana na watu wawili kutoka Sumaniyyah

waliomwambia: "Tueleze yule unayemwabudu." Hivyo akasema: "Nipe muda

kidogo." Kisha akawaendea nje na kusema: "Ni huyu upepo, na kila kitu na katika

kila kitu.”"

Abu Mu'aadh bin Sulayman bin Khalaf al-Balkhiy kasema:

"Adui wa Allaah kadanganya. Kwa hakika, Allaah Yuko juu ya mbingu juu ya

´Arshi na Yuko kama jinsi Alivyojielezea Yeye Mwenyewe."

636 - Hishaam bin 'Abdil-Malik alimwandikia Ibn Ahwaz kumuua Jahm popote

atapokutana nae. Ibn Ahwaz alikuwa ni gavana wa Marw.

Mwandishi: Imaam Hibatullaah Laalakaa'iy

Chanzo: Sharh Usuul I'tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa'ah (3/421-425)

Mukhtasari na footnotes: Maktabah Daar-ul-Hadiyth.Com

Page 63: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

63

Allaah Huongea Kwa Kutaka Kwake Na Kwa Uwezo Wake

Watu wa kwanza katika Uislamu waliokanusha kuwa Allaah Huwakurubia waja

Wake ilikuwa ni Jahmiyyah na Mu'tazilah wanaokubaliana nao. Walikanusha

hata Sifa na kustawaa juu ya ´Arshi. Kisha akaja Ibn Kullaab na kuwapinga na

akathibitisha Sifa na kustawaa juu ya ´Arshi. Hata hivyo akakubaliana nao ya

kwamba Allaah Hajisifii kwa sifa za khiyari. Hivyo akazua maoni yake kuhusu

Qur-aan na kusema kwamba Qur-aan ni ya milele na kwamba Allaah Haongei

kwa uwezo Wake. Ni jambo lisilojulikana ya kwamba kuna mtu yeyote katika

Salaf aliyesema hivyo. Kwa hakika, kumepokelewa [mapokezi mengi] kutoka

kwao [Salaf] kwamba Qur-aan ni Maneno ya Allaah na kwamba haikuumbwa na

kwamba Allaah Aliitamka kwa kutaka na Uwezo Wake, jambo ambalo limetajwa

katika vitabu vingi.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam bin Ahmad Taymiyyah

Chanzo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 105

Page 64: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

64

SUBIRA KAMILIFU YA ALLAAH

Uvumilivu Wa Allaah Wa Kikamilifu

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema katika Hadiyth Swahiyh :

"Hakuna ambaye ni mvumilivu kuliko Allaah. Wanamsifia kuwa na mtoto wakati

Anawaponya na kuwapa riziki.”104

Sifa zote kamilifu zilizotimia zinamstahiki Allaah (Ta´ala). Hili ni jambo

limethibitishwa na Shari'ah na akili. Ukamilifu huu kunaingia Majina Yake yote

na Sifa Zake. Katika ukamilifu huu kunaingia Subira. Subira iliyotajwa na

Mjumbe (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) haifanani na subira ya chengine

chochote. Subira Yake ni kamilifu yenye nguvu na yenye nguvu za kuogofya.

Inakabiliana na matusi ya viumbe waovu.

Hawawezi kuepuka nguvu Zake. Maneno yao yote, riziki zao na mahitaji yao

vinatokana na Allaah. Hawachumi chochote isipokuwa kwa ukarimu Wake.

Anawaponya na kuwapa riziki. Hakupiti wakati isipokuwa wamezungukwa na

ukarimu Wake.

Amewafungulia milango ya Tawbah, Akawasahilishia kwalo na Akawaita kwalo.

Amewaambia ya kwamba Atawasamehe na madhambi yao makubwa na

kuwaingiza katika furaha ikiwa tu watatubu.

Himidi zote ni Zako eeh Allaah, Mwenye Uvumilifu.

Mwandishi: Imaam 'Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa'diy

Chanzo: al-Fataawa as-Sa'diyyah, uk. 22

'Aalam-ul-Kutub, 1415/1995

104 Muslim (2804)

Page 65: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

65

KUSHUKA105 KWA ALLAAH KILA USIKU KWENYE MBINGU YA DUNIA

Je, Allaah Huacha ´Arshi Yake Wakati Anashuka?

Swali: Ipi kauli yenye nguvu kuhusiana na kushuka kwa Allaah; je Huacha ´Arshi

Yake au hapana?

Jibu: Kauli sahihi ni mtu kutojiingiza katika suala hilo. Tunaamini ya kwamba

Yuko juu ya ´Arshi Yake, na tunaamini ya kwamba hushuka. Hatusemi kuwa

huacha au haachi. Hiyo ina maana kujiingiza katika Kayfiyyah [kueleza namna

ilivyo – jambo ambalo ni Bid´ah kuuliza].

Mwandishi: 'Allaamah ´Abdur-Razzaaq 'Afiyfiy

Chanzo: Fataawa wa Rasaa'il (1/162)

ad-Daaraqutniy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Mapokezi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuhusu

kwamba Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) hushuka kila usiku mbingu ya chini na

huwasamehe wale wanaomuomba msamaha na huwapa wale wanaomuomba:

1 - 'Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhu) kaeleza kwamba Mtume

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Wakati inapofika theluthi ya usiku, hushuka Allaah ('Azza wa Jalla) kwenye

mbingu ya chini na kubaki hapo mpaka alfajiri inapoingia na kusema: "Je, kuna

mtu anayeniomba ili Nimpe? Je, kuna mtu anayenihitaji kwa haja Nimkidhie haja

yake? Je, kuna ambaye ni mgonjwa ili Nimponye? Je, kuna ambaye ni mwenye

madhambi aombae msamaha ili nimsamehe?"

105 Kushuka au Kuteremka

Page 66: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

66

Mwandishi: Imaam Abul-Hasan ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutniy (d. 385)

Chanzo: Kitaab-un-Nuzuul (1)

Ahmad Na Ibn Raahuuyah Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Nilimuuliza Ahmad (d. 241 - Radhiya Allaahu 'anhu) kuhusu [Hadiyth]:

"Mola Wetu hushuka kila usiku mbingu ya chini wakati kunabaki theluthi ya

mwisho ya usiku."

"Watamuona Mola Wao ('Azza wa Jalla)."

"Usilaani uso, kwa hakika Allaah ('Azza wa Jalla) Kamuumba Aadam kwa sura

Yake."

"Moto utalalamika kwa Mola Wake ('Azza wa Jalla) mpaka hapo Allaah

Atapoweka Mguu Wake juu yake."

"Muusa ('alayhis-Salaam) akampiga Malaika wa mauti (' alayhis-Salaam)."

Imaam Ahmad akasema:

“Zote ni Swahiyh.”

Ishaq [d. 238 - bin Raahuuyah] kasema:

"Zote ni Swahiyh na hazikanushwi ispokuwa tu na mtu wa Bid´ah au mtu

ambaye ana maoni dhaifu.”

Mwandishi: Imaam Ishaaq bin Mansuur al-Kawsaj (d. 251)

Chanzo: Masaa'il-ul-Imaam Ahmad bin Hanbal wa Ishaaq bin Raahuuyah

(2/535)

Mfano Wa Uongo Wa Ibn Batuutah kuhusu Ibn Taymiyah

Page 67: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

67

Ikiwa kama kusikia kwa Allaah si kama kusikia kwetu, kuona Kwake si kama

kuona kwetu, kutaka Kwake si kama kutaka kwetu hali kadhalika kuhusu elimu

na uwezo Wake, pia kunasemwa vile vile kuridhia Kwake si kama kuridhia

kwetu, khasira Yake si kama khasira yetu, furaha Yake si kama furaha yetu na

kushuka Kwake si kama kushuka kwetu na kulingana kwetu sawa.

Mwandishi: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah

Chanzo: Sharh Hadiyth-un-Nuzuul, uk. 24

Uongo Dhidi Ya Ibn Taymiyyah Na Kushuka Kwa Allaah

Ahl-us-Sunnah wanasema kwamba Allaah hushuka kwenye mbingu ya chini

kama alivyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) bila ya

kufikiria hilo. Hawaelezei namna ya Sifa za Allaah kama zilivyo sifa za viumbe.

Hawafikirii hata Sifa za Allaah.

Mu'attwilah wanaokanusha Kushuka walifanya hivyo baada ya kulifikiria hilo.

Wakaona kuwa kushuka kwa Allaah ni kama kushuka kwa viumbe. Kutokana na

hili, wakawashutumu Ahl-us-Sunnah ya kwamba wanamfananisha Allaah na

viumbe kwa kuthibitisha kwao Kushuka.

Baadhi yao wakazusha uongo dhidi ya Shaykh-ul-Islam Ibn Taymiyyah na

kwamba alishuka [teremka] mimbari na kusema:

"Allaah hushuka kama jinsi ninavyoshuka mimi."

Hili limesemwa na Ibn Batuutah. Huu ni uongo dhidi yake (Rahimahu Allaah).

Ibn Taymiyyah alifungwa wakati Ibn Batuutah alipokwenda Damaskus. Yule

ambaye anataka kujua ´Aqiydah aliyokuwa nayo Ibn Taymiyyah asome kitabu

chake "Sharh Hadiyth-in-Nuzuul". Humo amekataza kufanana kwa kushuka kwa

Allaah na viumbe. Sababu ya kumsingizia Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na

wengine kwa hili, ni kwa sababu Kushuka wanakokuelewa tu ni kushuka kwa

viumbe. Walipoona kuwa Ahl-us-Sunnah wanathibitisha Kushuka,

wakawatuhumu kumfananisha Allaah na viumbe. Ametakasika Allaah kwa hili.

Page 68: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

68

Mwandishi: Shaykh 'Abdur-Razzaaq bin 'Abdil-Muhsin al-'Abbaad

Chanzo: at-Tuhfah as-Saniyyah, uk. 50

al-Barbahaariy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Mapokezi haya yote ambayo umesikia lakini hayaingii akilini mwako, ambayo

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kasema:

"Mioyo ya waja iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (´Azza wa

Jalla).”

"Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka chini kwenye mbingu ya

chini."

"Hushuka siku ya ´Arafah."

"Hakutoachwa kutupwa [watu na mawe] Motoni mpaka hapo Allaah (´Azza wa

Jalla) Atapoweka Mguu Wake juu yake.”

Kauli ya Allaah (Ta´ala) kwa waja Wake:

“Ukinijia Mimi, ntakujia kwa kasi.”

"Kwa hakika Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka siku ya 'Arafah."

"Kwa hakika Allaah Kamuumba Aadam kwa sura Yake."

“Nilimuona Mola Wangu kwa sura nzuri kabisa.”

Na Hadiyth mfano wa hizo, ni lazima kwako kujisalimisha, kuzithibitisha,

usijiingize katika namna na uwe ni mwenye kuzifurahia na kutosheka nazo.

Usizifasiri kwa matamanio yako. Kwa hakika ni lazima kuamini hili. Yeyote yule

ambaye atafasiri chochote katika hizo kwa matamanio yake au kuzikataa, ni

Jahmiy.

Page 69: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

69

Mwandishi: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (d.

329)

Chanzo: Sharh-us-Sunnah, uk. 74-76.

Abu Daawuud Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

"Mlango: Radd kwa Jahmiyyah: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam) kasema:

"Mola Wetu (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka kila siku katika mbingu ya chini

wakati kunabaki theluthi ya usiku na kusema: "Je, kuna mtu anayeniomba ili

Nimpe? Je, kuna mtu anayenihitaji kwa haja Nimkidhie haja yake? Je, kuna

ambaye ananiomba msamaha ili Nimsamehe?”

Mwandishi: Imaam Abu Daawuud Sulayman bin al-Ash'ath as-Sijistaaniy (d.

275)

Chanzo: as-Sunan (4716)

Abul-Hasan al-Ash'ariy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Kinachothibitisha ya kwamba Allaah Kastawaa juu ya ´Arshi na si vinginevyo, ni

yale yaliyopokelewa kuhusu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa

sallam) kasema:

"Mola Wetu (Tabaaraka wa Ta´ala) Hushuka kila siku katika mbingu ya chini na

kusema: "Je, kuna mtu anayeniomba ili Nimpe? Je, kuna ambaye ananiomba

msamaha ili Nimsamehe?” Mpaka kunapopambazuka.

Page 70: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

70

Mwandishi: Imaam Abul-Hasan ´Aliy bin Ismaa´iyl al-Ash'ariy (d. 330)

Chanzo: al-Ibaanah, uk. 99

at-Tirmidhiy Kushuka Kwa Allaah

Ama kuhusiana na mapokezi kama hii Hadiyth na Sifa zingine kama Allaah

(Tabaaraka wa Ta´ala) Kushuka katika mbingu ya chini, wamesema wanachuoni

ya kwamba ni Swahiyh. Inatakiwa kuziamini bila ya kuzifikiria au kuziulizia. Hili

limepokelewa kutoka kwa Maalik bin Anas, Sufyaan bin ´Uyaynah na 'Abdullaah

bin al-Mubaarak ambao wamesema:

"Zipitisheni Hadiyth hizi bila ya kuzifikiria.”

Hili limesemwa na wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Ama kuhusiana na Jahmiyyah, wanakanusha mapokezi haya na kusema ya

kwamba zinamaanisha kufananisha (Tashbiyh). Allaah Kataja mara nyingi katika

Kitabu Chake Mkono, Kuona na Kusikia. Allaah Kaeleza hili kwa njia nyingine

kuliko njia ambayo wanachuoni wameielezea - yaani wa Jahmiyyah - wamesema:

"Allaah Hakumuumba Aadam kwa Mkono Wake. Mkono unamaana ya nguvu."

Ishaaq bin Ibraahiym [bin Raahuuyah] kasema:

"Ni kufananisha tu ikiwa mtu atasema mkono ni kama mkono au unafanana na

mkono au kusikia ni kama kusikia au kunafanana na kusikia. Huku ni

kufananisha. Hata hivyo, sio kufananisha ikiwa mtu atasema kama jinsi Allaah

Amevyosema "Mkono", "Kusikia" na "Kuona" bila ya kufikiria au kusema kuwa

Mkono unafanana na Mikono mingine au ni kama mikono mingine. Huku ni

kufananisha. Ambalo Allaah (Ta´ala) Kasema:

ميع البصير ء وهو الس له شيأ س كمثأ ليأ

“Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.” (ash-

Shura 42 : 11)

Page 71: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

71

Mwandishi: Imaam Abu Iysa Muhammad bin Iysa at-Tirmidhiy (d. 279)

Chanzo: al-Jaami' (659).

Abu Bakr al-Ismaa'iyliy Kuhusu Kushuka Kwa Allaah

Ahl-ul-Hadiyth wanaamini kwamba Allaah ('Azza wa Jalla) Hushuka katika

mbingu ya chini kutokana na Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Hii haitakiwi kulifikiria.

Mwandishi: Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym al-Ismaa'iyliy (d. 371)

Chanzo: I'tiqaad A'immah Ahl-il-Hadiyth, uk. 403

Page 72: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

72

UMILELE WA ALLAAH NA WA VIUMBE

Tofauti Kati Ya Umilele Wa Allaah Na Umilele Wa Peponi Na Motoni

Kwamba Pepo na Moto vyote na wakaazi wavyo watabaki milele halikwenda

kinyume kwamba ('Azza wa Jalla) ndie wa Mwisho ambaye hakutanguliwa na

mtu wala kitu. Kwa kuwa Allaah ('Azza wa Jalla) umilele Wake ni Dhati Yake

muhimu. Ama kuhusiana na watu wa Peponi na Motoni na umilele wao, ni wa

milele tu kwa kuwa Allaah Amewaacha wawe hivyo. Wangelisitizwa pia

ingelikuwa Allaah Hakuwaacha hivyo.

Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad

Chanzo: Qatf-ul-Jannah ad-Daaniy, uk. 128-129

Page 73: Sifa Tukufu Za Allaah (Ta´ala) - KAULI ZA WANACHUONI WA SALAF

73

MIOYO YA WAJA IKO BAINA YA VIDOLE VIWILI VYA ALLAAH

Mioyo Ya Waja Kuwa Baina Ya Vidole Viwili Katika Vidole Vya Allaah Haihitajii

Kugusana

Mfano mwingine wa pili ni Hadiyth:

"Mioyo ya waja (binaadamu) iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Ar-

Rahmaan."106

Hadiyth hii ni Swahiyh. Iko katika "Swahiyh Muslim" katika mlango "al-Qadr" na

imesimuliwa na 'Abdullaah bin 'Amr bin al-´Aasw.

Salaf, Ahl-us-Sunnah, wanaifahamu Hadiyth hii kwa udhahiri wake (Dhwaahir-

ul-Hadiyth). Wanasema kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika

Vidole vya Allaah (Ta´ala) kwa njia ya kweli (halisi). Tunathibitisha hilo kwa njia

ile ile kama jinsi Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Alivyovithitisha

Kwake. Kwamba mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya

Allaah, haihitajii kwamba (mioyo) inavigusa (Vidole vya Allaah) mtu akaelewa

kwamba Hadiyth ina pantheism (Huluul) na matukio yake ikaja kuwa ufahamu

wa kimakosa. Mwezi uko baina ya mbingu na ardhi, bila ya kugusa chochote

katika hivyo. (Mlima wa) Badr uko baina ya Makkah na al-Madiynah ilihali kuna

umbali mrefu kati yavyo.

Hali kadhalika mioyo ya watu iko baina ya Vidole viwili vya Mwingi wa Rahmah

kwa njia ya ukweli (halisi) na haihitajii kugusana wala pantheism107.

Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn

Chanzo: al-Qawaa´id al-Muthlaa, uk. 50-51

´Aalam-ul-Kutub, 1406/1986

106 Muslim (2654), Ahmad (2/168), Ibn Hibban (902) na wengineo.

107 http://en.wikipedia.org/wiki/Pantheism