mem029

13
Bulletin News Ofi si ya Mawasiliano Serik alini inapoke a ha bari z a matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bul lettin hii na Jar ida la Wizar a ya Nishati na Madini Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 21 10389 Mob: +255 732 999263 au Fika Osi y a Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected] http://www.mem.go.tz HABARI ZA NISHATI &MADINI  To le o No. 29 Limesa mb az wa kw a Ta asisi na Id ara zote MEM  Ta re he - Ag os ti 15-21, 2014 n  Am ta ja Muhongo, Waz ir i kinara Nishati tangu Uhuru nWamteua kuwa mlezi Afrika Ku on do a uma sk in i Wizara yazidi kufungua fursa za masomo - Uk 6 MKAPA ATAKA WAJIOLOJIA AFRIKA KUTUMIA SAYANSI: Ku on do a uma ski ni S oma  h ab a ri  U k.  2 , 4 & 5 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu wa tatu, Benjamin Mkapa akihutubia katika kongamano la Wanasayansi Vijana Duniani, lililofanyika Jijini Dar es Salaam

Upload: jackson-m-audiface

Post on 11-Oct-2015

13.136 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • BulletinNews

    Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya Nishati na Madini

    Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    http://www.mem.go.tz

    Habari za nisHati &madini

    Toleo No. 29 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe - Agosti 15-21, 2014

    nAmtaja Muhongo, Waziri kinara Nishati tangu Uhuru nWamteua kuwa mlezi Afrika

    Kuondoa umaskini

    Wizara yazidi kufungua fursa za masomo-Uk6

    MKapa ataKa Wajiolojia afriKa KutuMia sayansi:

    Kuondoa umaskini Soma habari Uk. 2,4&5

    Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu wa tatu, Benjamin Mkapa akihutubia katika kongamano la Wanasayansi Vijana Duniani, lililofanyika Jijini Dar es Salaam

  • 2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzNIshATI/MAdINI

    Viongozi wanena mkutano wanasayansi vijana

    Meli yenye mitambo ya kuzamisha na kuunganisha mabomba chini ya bahari ikiwa katika bahari ya hindi nchini Tanzania.

    Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

    Vijana wanasayansi duniani wametaki-wa kutoka na njia mbadala kupitia tafiti wanazofanya

    katika tasnia ya jiolojia ili zi-saidie kuendeleza rasilimali zilizoko ardhini hususan barani Afrika na hatimaye ziweze ku-linufaisha bara hilo na kuleta maendeleo endelevu.

    Hayo yameelezwa na Maka-mu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akifungua mkutano wa tatu wa Vijana Wa-nasayansi Duniani (YES) un-aoendelea jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, vijana wa-nasayansi wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko kupitia ra-silimali mbalimbali zilizopo Af-rika yakiwemo madini, mafuta na gesi asilia.

    Utajiri uliopo ardhini uki-tumiwa vizuri, unaleta mab-adiliko makubwa kiuchumi ikiwemo kuondoa umaskini, kutoa fursa kwa wazawa kush-iriki na kuziendeleza rasilimali

    hizi, lakini zaidi na vijana wa-nasayansi wanayo nafasi kubwa ya kuchangia mabadiliko hayo, aliongeza Bilal.

    Aidha, Dk. Bilal amewataka wanafunzi nchini kupenda mas-omo ya sayansi ili kuiwezesha Tanzania kuwa na idadi kubwa ya watalamu ambao wanahitaji-ka katika tasnia ya gesi na mafu-ta katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchumi wa gesi.

    Naye Rais Mstaafu wa Seri-kali ya Awamu ya tatu, Benja-min Mkapa alizitaka serikali za Afrika kutoa kipaumbele cha elimu kwa vijana wanasay-ansi pamoja na fursa ya kutoa ufumbuzi na tafiti mbalimbali wanazofanya ili kuwezesha vi-jana hao kuendeleza rasilimali zilizopo barani Afrika.

    Leo nasisitiza mambo muhimu mawili tu, serikali za Afrika zitoe kipaumbele cha elimu kwa vijana ikiwemo kutoa fursa kwao kuonesha na kutoa ufumbuzi wa masuala mbalim-bali kupitia tafiti zao,alisisitiza Mkapa.

    Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa

    Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, Afrika ni bara la kizazi kijacho, kutokana na uwepo wa rasilimali mbalimbali zinazo-hitajika duniani kote, hivyo, ni muhimu kuwekeza kwa vijana ambao ni kiungo muhimu kati-ka kuziendeleza rasilimali hizo.

    Afrika ni bara la kizazi ki-jacho, Afrika inakua, Afrika ina badilika hivyo mabadiliko ni lazima alibainisha, Profesa Muhongo.

    Taaluma za kisayansi hu-susan gesi na mafuta zinahitaji wataalum wa kutosha na wal-iobobea katika masuala hayo ili kuziendeleza rasilimali na kukuza uchumi wa nchi husi-ka, alisisitiza Muhongo.

    Akitolea mfano wa Tan-zania alieleza kuwa, takriban asilimia 75 ya watanzania ni vijana ambao endapo serikali itawekeza kwao watakuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadi-liko.

    Aliongeza kuwa, kutokana na idadi kubwa ya watanzania iliyothibitishwa baada ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2014 inaonesha kuwa idadi yao ni takriban watu milioni 49,

    hivyo, ipo kila sababu kwa nchi kuzalisha wataalamu wengi ka-tika taaluma ya jiolojia hususani katika sekta ndogo ya mafuta na gesi.

    Muhongo alisisitiza kwam-ba, dhamira ya serikali bado ipo palepale ya kuhakikisha kwamba kufikia mwaka 2025, Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa ki-pato cha kati na hivyo, uwepo wa wataalamu waliobobea ka-tika taaluma hiyo ni jambo la muhimu.

    Kwa upande wake,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma, alieleza kuwa, mkuta-no huo wa vijana ni fursa kwao kujifunza kutoka kwa wajiolojia waliobobea Afrika na duniani, jambo ambalo litawasaidia ku-fuata nyendo za wataalam hao.

    Aidha, Mruma aliongeza kuwa, kupitia uzoefu ambao vijana hao wataupata kupitia mkutano huo, utasaidia kufa-hamu changamoto na kutoka na mapendekezo yatakayosaidia kufanikisha masuala mbalimba-li ya kiuchumi na kupitia tasnia ya jiolojia na hivyo kuchangia

    katika kuendeleza rasilimali asi-lia.

    Vilevile, alitoa pongezi kubwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kuirithisha taal-uma ya jiolojia kwa vijana wa Tanzania, Afrika na duniani kupitia nafasi mbalimbali am-bazo amekuwa kiongozi kupitia taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuongoza Wizara ya Nishati na Madini.

    Kwa upande wake Rais wa vijana wanasayansi duniani, Meng Wang, ameeleza kuwa hii ni nafasi kwao ya kuwasilisha tafiti, uzoefu, changamoto na namna ya kukabiliana nazo, pia, ni fursa kwa Afrika ikizingatiwa kuwa, mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza barani humo hivyo, Afrika na Tanza-nia ina nafasi kubwa ya kunu-faika kupitia rasilimali hizo.

    Mkutano huo umedhamini-wa na wadau mbalimbali zikiwemo kampuni za sekta za sekta za mafuta, umeme na gesi, kampuni ya BG- Tanzania inay-ofanya utafiti na uchimbaji wa mafuta ikiwa mdhamini mkuu wa mkutano huo.

    Makamu wa Rais, dk. Mohamed Gharib Bilal Rais Mstaafu wa serikali ya Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo

    nBilal aeleza umuhimu wao kiuchumi

    nMkapa aitaka Afrika kuwekeza katika elimu

    nMuhongo aitaja Afrika bara la kizazi kijacho

  • 3BulletinNewshttp://www.mem.go.tz MAoNI

    Na Greyson Mwase, Bagamoyo

    Jumla ya Dola za Marekani milioni 53.8 zimepatikana kutokana na mauzo ya vito mbalimbali ndani ya nchi kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

    Hayo yamesemwa na Mkuru-genzi wa Kitengo cha Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito, (TANSORT) kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini Ar-chard Kalugendo kwenye semina il-iyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini iliyokuwa na lengo la kujadili utendaji na uboreshaji wa shughuli za uthaminishaji wa madini ya almasi na vito nchini.

    Kalugendo alisema kuwa mauzo hayo yanatokana na usimamizi mzuri wa Kitengo hicho katika kuthamini-sha almasi na vito kwa ajili ya kukoko-toa mrabaha wa Serikali; Kutayarisha miongozo ya bei (Price Guides) ya almasi na madini ya vito inayotumika

    kukokotoa mrabaha, kutoa huduma za kijemolojia (Gemmological Ser-vices) kwa wachimbaji wadogo na wa kati, Kusimamia mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na madini ya vito.

    Kutokana na usimamizi mzuri wa mauzo na kufuatilia mwenendo wa masoko ya almasi na madini ya vito, ulipelekea wastani wa bei ya al-masi za Tanzania katika soko la dunia kupanda hadi dola za Marekani 286 kwa karati ikiwa ni ongezeko la asil-imia 13, alisisitiza Kalugendo

    Alisema masoko saba ya ki-mataifa yaliyofatiishwa ili kutambua mwenendo wa bei na masoko ya ma-dini ya vito na almasi duniani ni Bang-kok, Antwerp, Basel, London, Chang-sha, Las Vegas na Arusha.

    Kalugendo aliongeza kuwa ma-fanikio yaliyopatikana kutokana na usimamizi mzuri wa shughuli za uthamini wa almasi na madini ya vito ni pamoja na Kilo 818, gramu 269,211 na carat 40,599 za Tanzanite kuthaminiwa na kuuzwa na mgodi wa TanzaniteOne Minerals Limited (TML) wa Arusha.

    Alieleza kuwa serikali inafanyia kazi suala la kuwa na soko rasmi la kuuzia madini ya thamani kubwa hapa nchini kwa kuendelea na hatua mbalimbali ikiwemo kufanya tath-mini za mapato, kutafuta uwekezaji katika jengo litakalotumika kwa shu-ghuli hizo, kutathmini namna bora ya kuendesha soko hilo na kujifunza ku-toka nchi nyingi Kalugendo aliongeza kuwa TANSORT imejipanga kuen-delea kutoa elimu juu ya athari za vi-tendo vya udanganyifu, wizi, ukwepaji kodi, na utoroshaji wa madini ya vito.

    TANSORT ni Kitengo cha Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Ni-shati na Madini ambapo uthamini un-alenga ukokotoaji sahihi wa mrabaha wa Serikali kama ilivyoelekezwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, Vi-fungu vya 87, 88 na 89. Kitengo hiki kilichoanzishwa mwaka 1966 kina ofisi tano sehemu tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Antwerp nchini Ubeljiji, Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam) Kanda ya Kati- Magharibi (Shinyan-ga) Kanda ya Kaskazini (Arusha) na Kanda ya Kusini (Songea).

    TahaririMEM

    Na Badra Masoud

    Five Pillars oF reForms

    KWa HaBari PiGa simU KitenGo cHa maWasiliano

    Bodi ya uhariri MhARIRI Mkuu: Badra Masoud

    MsANIfu: Essy ogundeWAANdIshI: Veronica simba, Asteria Muhozya, Greyson Mwase

    Teresia Mhagama, Nuru Mwasampeta

    increase eFFiciencyQUality delivery

    oF Goods/servicesatisFaction oF

    tHe clientsatisFaction oF

    BUsiness Partners

    satisFaction oF sHareHolders

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Mliopata ufadhili msituangushe!

    Wiki hii, watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari wameshuhudia vijana 10 wa kitanzania wakikabidhiwa nyaraka mbalimbali zitakazowawezesha kwenda nchini China kwa masomo ya shahada ya uzamili na uzamivu kwenye mafuta na gesi.

    Vijana hao watakaoondoka mwezi septemba mwa-ka huu, Tisa kati yao wanaenda nchini humo katika Vyuo Vikuu mbalimbali kusomea shahada ya uzamili katika fani ya mafuta na gesi na mmoja akienda ku-somea shahada ya uzamivu katika masuala hayohayo.

    Tahariri ya leo inatoa wosia kwa vijana waliopata ufadhili wa masomo katika sekta za Nishati na Ma-dini katika nchi mbalimbali duniani kama Uingereza, Norway, China, Algeria na wale watakaoenda nchini Brazil mwaka 2015, wasituangushe watanzania kwani uendelezaji na ukuaji wa sekta hizi unahitaji wataal-am waliobobea katika fani hiyo.

    Tunaamini vijana wetu mna uwezo na mmed-hamiria kusoma ili elimu mtakayopata katika nchi am-bazo zimeshapiga hatua katika uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini mtaitumia kwa manufaa ya watan-zania.

    Nichukue fursa hii kuwapongeza viongozi wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri, Profesa Sospeter Muhongo ambao tumekuwa tukiwashuhudia wakitumia njia mbalimbali ikiwamo mikutano baina yao na wawekezaji ama viongozi wa nchi mbalimbali kusisitiza upatikanaji wa ufadhili wa masomo si katika sekta za nishati na madini pekee bali hata katika fani nyingine kama uhasibu, ukaguzi, she-ria na habari.

    Katika hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi wanaok-wenda nchini China kwa masomo, Waziri Muhongo alieleza kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa na wataal-am wasiopungua 300 katika fani ya mafuta na gesi ifi-kapo mwaka 2020 na hivyo kuwa kinara katika nchi nyingi za Afrika kwa kuwa na wataalam wengi kwe-nye fani hiyo.

    Profesa Muhongo pia ameeleza kuwa amezun-gumza na Balozi wa China hapa nchini Bw.Lu You-qing kuhusu kuongeza idadi ya wanafunzi kwenda nchini humo mwaka 2015 kwa masomo ya shahada za juu ambapo Balozi huyo aliahidi kuongeza nafasi hizo hadi kufikia 20 endapo wanafunzi wa kitanzania wali-opata ufadhili mwaka 2013 na mwaka huu watafanya vizuri katika masomo yao.

    Ni kutokana na hilo basi nazidi kusisitiza vijana wanaopata ufadhili wa masomo katika nchi mbalim-bali duniani kuzingatia masomo yao na kuelewa nini kimewapeleka huko ili waje waendeleze rasilimali am-bazo nchi yetu imejaliwa, wazidi kufungua fursa za ki-masomo kwa watanzania wengine na vilevile kufaulu kwao kutaonesha kwamba wanatambua na kuthamini juhudi zinazofanywa na serikali yao katika kuhakiki-sha kuwa wazawa wanashiriki ipasavyo katika kuen-deleza rasilimali za Nishati na Madini.

    tel-2110490FaX-2110389

    moB-0732999263

    Dola milioni 53.8 zapatikana kutokana na mauzo ya vito

    katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (pichani kushoto) akifungua semina ya kujadili utendaji na uboreshaji wa shughuli za uthaminishaji wa madini ya almasi na vito nchini. kulia akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo inayofanyika Bagamoyo.

  • 4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz nishati

    n10 kwenda China Uzamili, Uzamivun10 wengine kwenda Brazil 2015

    Teresia Mhagama na Jamilah Masonga, Dar es Salaam

    Wizara ya Nishati na Madi-ni imeendelea kufungua fursa kwa watanzania kuongeza uelewa katika fani ya mafuta na gesi

    na sasa Serikali ya China kupitia Wizara hii imetoa ufadhili wa nafasi 10 kumi za masomo kwa vijana wa kitanzania katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani hiyo.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi nyaraka mbalimbali zitakazowawezesha vijana hao kujiunga na masomo nchini China, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa wanafunzi Tisa watasoma shahada ya uzamili na mmoja atasomea shahada ya uzamivu katika mafuta na gesi.

    Nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa gesi, tulikuwa kwenye uchumi huo kwa kiwango kidogo lakini sasa tunaingia kwa gia kubwa na tunakiri kuwa wataalam wapo lakini hawatoshi, na kwa vile kazi za utafiti na utafutaji wa gesi na mafuta zinaendelea, hali inaonesha kuwa ndani ya miaka miwili au mitatu ijayo kiwango cha gesi kinaweza kuvuka futi za ujazo trilioni 150 mpaka 200 hivyo lazima watanzania tujitayarishe kusimamia rasilimali hii, alieleza Profesa Muhongo.

    Amesema usimamizi wa rasilimali gesi nchini ambayo sasa imefikia futi za ujazo trilioni 50.5 haitakiwi kusimamiwa kwa porojo au kulumbana bali wanahitajika wataalam waliobobea katika fani hiyo.

    Kutokana na hilo, Profesa Muhongo ameeleza kuwa Wizara ya Nishati na Madini iliamua kujikita katika kutayarisha wataalam wa uhakika kwa kasi kubwa katika mafuta na gesi huku akitolea mfano wa Chuo cha Madini Dodoma ambacho kina wanafunzi zaidi ya 100 wanaosomea masuala ya petroli.

    Tunahitaji wahandisi, wajiolojia, lakini pia tunahitaji wataalam wazuri zaidi katika masuala ya fedha, utawala, na upande wa sheria. Hatutafuti vijana wanaosoma upande wa shahada tu, lakini pia sekta ya Nishati na Madini inahitaji mafundi mchundo (technicians) na Chuo cha Dodoma kinafanya vizuri kwani sasa kina wanafunzi wanaosoma katika ngazi ya ufundi mchundo ambao sasa wanaingia mwaka wa pili na wanalipiwa na Wizara, vilevile katika ngazi ya chini kama ya mafundi na makenika kuna wanafunzi wa-naosomeshwa katika vyuo vya ufundi stadi (VETA) Lindi na Mtwara ambao idadi yao inazidi 390, alisisitiza Profesa Muhongo.

    Kuhusu ufadhili wa masomo wa China, Waziri Muhongo ameeleza kuwa ni wa awamu ya pili kwa kuwa mwaka 2013/2014 kuna watanzania wengine 10

    waliofadhiliwa masomo ngazi ya shahada ya uzamili katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini humo kwenye sekta za nishati na madini na serikali ya China imeahidi kuongeza idadi hiyo mwaka 2015 endapo wanafunzi waliopata ufadhili huo wata-fanya vizuri katika masomo yao.

    Ameeleza kuwa kutokana na Tanzania kuwa na spidi kubwa ya kusomesha wa-tanzania katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Norway (zaidi ya 8), Uingereza (zaidi ya 15), na wengine 10 wataenda nchini Brazili mwezi Januari mwaka 2015 kusomea shahada ya pili katika mafuta na gesi, wengine pia wataenda Uingereza hivyo Wizara imeamua kujikita katika kusomesha watanzania kutoka sekta mbal-imbali bila kubagua ili rasilimali zilizopo zisimamiwe ipasavyo.

    Waziri Muhongo ameeleza kuwa baada ya Wizara kufanya mazungumzo na serikali ya Canada na Marekani, serikali hizo zimekubali vijana wa Kitanzania waende kusoma kwenye nchi hizo mwa-kani katika shahada ya pili na ya tatu kwe-nye mafuta na gesi huku akieleza kuwa ufadhili huo pia utaanza kutolewa katika sekta ya habari hivyo amewataka vijana wa kitanzania kujiandaa vyema.

    Naomba niwaeleze watanzania kuwa katika fani ya mafuta na gesi, katika miaka michache inayokuja (kuanzia 5 hadi 6) kutoka sasa, nina imani tutakuwa na wataalam wasiopungua 300 wa kitanza-nia, ambao watakuwa wamesoma kutoka vyuo mbalimbali na nina imani Tanzania ndiyo itakuwa na wataalam wengi kwenye sekta hiyo katika nchi nyingi za hapa

    Wizara yazidi kufungua fursa za masomo

    Bi. Erasma Rutachura, mmoja wa waliopata ufadhili wa masomo nchini China,ngazi ya shahada ya uzamivu katika mafuta na gesi akipokea nyaraka zitakazomwezesha kujiunga na masomo yake mwaka huu. Anayempa nyaraka hizo ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kulia). Wa pili kulia ni katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na wa kwanza kulia ni kamishna wa Madini, Eng. Paul Masanja

    Afrika kwa sababu spidi ya kusomesha ni kubwa kwelikweli na hii ni muhimu kwa kuwa tunataka wataalam wa kusimamia rasilimali husika vizuri sana. alitanabai-sha Waziri Muhongo.

    Awali, Katibu Mkuu, Wizara ya Ni-shati na Madini, Eliakim Maswi alieleza kuwa nafasi hizo zimepatikana kutokana na jitihada za Wizara ya Nishati na Madini kuongeza uelewa katika sekta ina-zozisimamia na kwamba katika ufadhili huo wa China, katika shahada ya uzamili

    wamechaguliwa watanzania 9 kati ya 46 waliotuma maombi na katika shahada ya uzamivu amechaguliwa mtanzania mmoja kati ya wanne waliowasilisha maombi.

    Pia Katibu Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa hizi za ufadhili wa masomo pindi zinapotolewa ili kuweza kutumia elimu hiyo kwa maendeleo endelevu ya sekta za Nishati na Madini.

    Watanzania waliopata ufadhili wa masomo nchini China katika ngazi ya shahada ya uzamili na uzamivu katika fani ya mafuta na gesi wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo (katikati) na katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi (wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma) pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini mara baada ya kuagwa rasmi katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.Wengine katika picha (mstari wa mbele) ni kamishna Msadizi Nishati anayeshughulikia umeme, Eng.Innocent Luoga (wa kwanza kulia), kamishna wa Madini, Eng.Paul Masanja (wa pili kulia), kaimu Mkurugenzi utawala - Bi. Caroline Musika (wa kwanza kushoto).

  • 5BulletinNewshttp://www.mem.go.tz nishati/Madini

    Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

    Watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wam-etakiwa kusimamia sheria na kanuni katika usimamizi na uendelezaji wa sekta za nishati na madini

    Wito huo ulitolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi katika kikao kilichohusisha kampuni ya Next Generation Solar Energy na watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA); Shirika la Umeme Nchini (TANE-SCO) pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Ni-shati na Madini.

    Awali kampuni ya Next generation Solar Power kutoka nchini Marekani ilikubaliana na TANE-SCO kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa megawati tano unaotokana na jua kati-ka mkoa wa Kigoma kama mkakati wa kupunguza ukosefu wa umeme.

    Ninawaagiza kuepuka kubadilisha kanuni na sheria kwa ajili ya maslahi binafsi au kuonyesha up-endeleo kwa baadhi ya wawekezaji hali ambayo in-aweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi badala ya kupiga hatua, sheria na kanuni lazima zifuatwe kama zilivyo, alisisitiza Maswi.

    Aidha, Maswi aliipongeza EWURA kwa kusi-mamia vyema sheria na kanuni katika usimamizi wa sekta ya mafuta pamoja na udhibiti wa bei na kuongeza kuwa sekta ya umeme inahitaji kufuata mfano huo kwa kusimamia kanuni zake.

    Katika mradi huo Maswi aliagiza bei za uuzaji wa umeme kwa kampuni hiyo kuangaliwa upya ili kuona kama TANESCO inaweza kumudu ili kuliepushia taifa hasara.

    Simamieni sheria na kanuni Maswi

    Chuo cha Madini kidedea Nane Nane Na Mwandishi wetu

    Chuo cha Madini, Dodoma kimefanya vyema katika Maone-sho ya Wakulima (NaneNane) - Kanda ya Kati, yaliyofanyika viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma yakiwa na Kauli Mbiu ya Matokeo Makubwa Sasa Kili-mo na Mifugo ni Biashara.

    Chuo hicho kimefanikiwa ku-shika nafasi ya Tatu katika Taasi-si zinazotoa mafunzo na utafiti ambapo pamoja na masuala mengine, mwaka huu wataalam wa Chuo cha Madini walikuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa fomu za ku-jiunga na Chuo kwa wanafunzi 275 waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho katika mwaka wa masomo 2014/15.

    Kutokana na kuvutiwa na taaluma zinazotolewa na Chuo hicho cha Madini ambacho kime-anza kutoa elimu katika masuala ya gesi na mafuta, wanafunzi ku-toka shule za msingi na sekondari walitembelea kwa wingi katika banda la Chuo hicho ili kupata elimu na kufahamu fursa mbal-imbali za kimasomo.

    Wataalam kutoka Chuo cha Madini, dodoma (kutoka kushoto), Alen pilinga , Ramadhan singano , sunday Brown, Robert Mukunirwa na Aneth Lushara wakiwa na kikombe cha ushindi katika kundi la Taasisi za mafunzo na utafiti.

    Mkurugenzi wa kampuni ya Next Generation solar feroz kassam akisisitiza jambo katika kikao hicho

    katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akisisitiza jambo katika kikao hicho. kulia kwake ni Naibu katibu Mkuu Mhandisi Ngosi Mwihava

    u

    u

  • 6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    http://www.mem.go.tz

    Rais wa Vijana Wanasayansi duniani Meng Wang akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano la Vijana Wanasayansi duniani, Jijini dar es salaam

    Mwenyekiti wa Vijana Wanasayansi upande wa Tanzania, steven Nyagonda akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Makamu wa Rais dk. Mohamed Gharib Bilal, kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo.

    1

    Makamu wa Rais dk. Mohamed Gharib Bilal (wa nne kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani. Wengine ni viongozi waliohudhuria ufunguzi huo akiwemo Rais Mstaafu wa serikali ya Awamu ya tatu Benjamin Mkapa, (wa nne kulia), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo (wa tatu kushoto), Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie (wa kwanza kushoto), Rais wa vijana Wanasayansi duniania Meng Wang (wa pili kushoto) wengine ni Profesa Roland obehransli na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya BG- Tanzania, Adam Prince.

    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo, akimpa zawadi ya picha, Balozi wa China nchini, Lu Youqing, mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa Tatu wa Wanasayansi Vijana duniani.

    Makamu wa Rais dk. Mohamed Gharib Bilal akifurahia zawadi ya kinyago aliyopewa na Rais wa Vijana Wanasayansi duniani Meng Wang kwa niaba ya Mtandao wa Vijana Wanasayansi duniani (YEs) kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa sospeter Muhongo.

    Matukio YES Network

  • 7BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini, stephen Masele (kushoto) akiwa katika ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi duniani,wengine ni baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

    Asteria Muhozya na Jamilah Masonga, Dar es Salaam Wajiolojia Afrika wameelezwa kuwa wanao mchango mkubwa katika kuon-doa umaskini kuwezesha ukuaji uchumi utakaotokana na kutumia utaalamu wao kuendeleza rasilimali zilizo chini na juu ya ardhi barani Afrika.

    Changamoto hiyo imetolewa na Rais Mstaafu wa Serikali Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa alipokuwa akifungua kongamano la 25 la Wajiolojia barani Afrika, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwataka wajiolojia hao kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa, wanasayansi wameshindwa kuisadia Af-rika.

    Pigeni kelele itumieni sayansi na taaluma hii kuondoa matatizo ya Af-rika, tumieni taaluma yenu kulinufaisha bara hili ili dhana kwamba wanasayansi wameshindwa kuisaidia Afrika iondoke. Msipoitumia sayansi vizuri hilo ni tati-zo, alisisitiza Mkapa.

    Mkapa aliongeza kuwa, iwapo say-ansi itatumika vizuri, inaweza kwa kiasi kikubwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara hilo yakiwemo, ya kiafya, ukosefu wa maji safi na salama, matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa na matatizo ya kiasili.

    Ameongeza kuwa, wajiolojia hao wa-nayo kila sababu ya kuchangia maende-leo na mabadiliko kutokana na kwamba, kongamano hilo linawakutanisha wana-sayansi na wajiolojia wakubwa waliobo-bea katika taaluma hiyo, jambo ambalo litasaidia kuweza kujadili, kuboresha na kutoka na ufumbuzi ambao utaiwezesha Afrika kuwa na mipango na mikakati bora itakayosaidia kunufaika na rasili-mali hizo hususani wananchi wake.

    Vilevile, amewataka wataalamu hao kuisaidia Afrika kujifunza kuielewa say-

    ansi na kuwezesha kufanya tafiti bora zenye viwango ambazo zinaweza kuwa kichocheo cha ukuaji kiviwanda, kite-knolojia na kuzalisha wanasayansi.

    Jamii haielewi mchango wa sayansi katika mchango wa maendeleo. Kum-bukeni maendeleo yanahitaji rasilimali watu. Zalisheni wanasayansi na ende-lezeni rasilimali watu, zaidi wasaidieni vijana wa kike kuipenda sayansi, ali-sisitiza Mkapa.

    Aidha, aliipongeza Wizara ya Ni-shati na Madini kwa kuwezesha mku-tano huo wa Wajiolojia Afrika kufanyika nchini na kueleza kuwa, hiyo ni sifa kwa Tanzania na kuwataka wanasayansi hao, kuona namna ya kukutana na wanasiasa ili kwa pamoja wajadili na kuelewa she-ria za uwekezaji, jambo litakalosaidia kuepeusha migogoro na kuwa na uelewa wa pamoja.

    Rais Mstaafu pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Nishati na Ma-dini, Profesa Sospeter Muhongo kwa

    kuwa Waziri kinara anayesimamia vema taaluma ya sayansi hususan jiolojia, na kumtaja kuwa, Waziri makini, mchapa-kazi ambaye ameweza kuisimamia na kuiongoza vema Wizara ya Nishati na Madini Tanzania, tangu ipate uhuru.

    Kwa upande wake, Waziri wa Nisha-ti na Madini, Profesa Sospeter Muhon-go akizungumza katika mkutano huo, alieleza kuwa, wao kama wanataaluma wa jiolojia wanao wajibu wa kuona ni namna gani wanaisadia Afrika kiuchu-mi, kuinua vipato vya wananchi na kuo-na jinsi Afrika inavyoweza kunufaika na rasilimali asilia.

    Muhongo aliongeza kuwa, wakiwa wataalamu wajiolojia wanalo jukumu la kuangalia changamoto zinazolika-bili bara la Afrika zikiwemo ongezeko la watu, ukuaji wa miji na kuongezeka kwa umaskini na kueleza kuwa, kuwekeza katika sayansi hususani kwa vijana kuta-saidia kuondoa matatizo hayo.

    Wanajiolojia wenzangu, hivi sasa

    si wakati wa kusafirisha malighafi nje, ni wakati wa Afrika kuleta maendeleo, tunao vijana wengi, tunahitaji kuwaen-deleza kitaaluma, tunahitaji kuifanya Afrika kuwa na maendeleo endelevu, alisistiza Muhongo.

    Aliongeza kuwa, kama wajiolojia, wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba Afrika inazalisha nishati ya umeme ya kutosha, ya uhakika na rahisi ili kucho-chea ukuaji wa uchumi na maendeleo ikiwemo kuangalia namna ambavyo bara hilo litanufaika kupitia kilimo na kuhakikisha kuwa, Afrika inakuwa na chakula cha kutosha na wananchi wake wanapata lishe bora.

    Wakati huo huo, Waziri Muhongo ameteuliwa kuwa, mlezi wa Jiolojia Af-rika kutokana na juhudi zake katika taal-uma ya jiolojia na kutokana na juhudi za Tanzania kuwaunganisha wajiolojia hao kutoka nchi mbalimbali barani Afrika na nje ya Afrika.

    MKapa ataKa sayansi Kuondoa uMasKini

    Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Jijini dar es salaam katika picha ya pamoja na baadhi wa wawakilishi waliohudhuria mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi duniani. Waliokaa kutoka kushoto ni dk. Luca demichel, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta, (BG Tanzania), Adam Prince na Mwenyekiti wa Vijana Wanasayansi, Tanzania steve Nyagonda.

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa sospeter Muhongo akipokea tuzo ya kuwa mlezi wa Jiolojia kutoka kwa profesa Eduardo, mara baada ya ufunguzi wa kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika. Profesa Eduardo ameeleza sababu za uteuzi wa Profesa kuwa ni pamoja na juhudi zake katika kuendeleza taaluma ya jiolojia Afrika na duniani.

    Matukio YES Network

  • 8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzTANZANIA DAIMA LAIKOSEA WIZARA

    Na Veronica Simba Dar es Salaam

    Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almas na Vito (TANSORT) kinaen-deleza juhudi zake za ku-hakikisha kwamba Tan-

    zania inaingia katika ramani ya dunia kwa kuwa miongoni mwa nchi wazal-ishaji wa madini ya vito na usonara.

    Mkurugenzi wa Kitengo hicho kutoka Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo amesema kuwa matarajio hayo yata-timia kutokana na ushiriki wa nchi kati-ka maonesho ya 54 ya kimataifa ya vito na usonara yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Septemba mwaka huu nchini Thailand.

    Akizungumzia ushiriki wa Tanza-nia katika maonesho hayo, Kalugendo alisema hii ni fursa muhimu kwa nchi ambapo mafanikio yatakayopatikana ni pamoja na kutangaza madini ya vito yanayopatikana hapa nchini, kutangaza maonesho ya vito ya Arusha yatakay-ofanyika mwezi Novemba mwaka huu na kutangaza utamaduni wa Tanzania kwa kutumia madini ya Tanzanite.

    Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kukuza ushirikiano kati ya

    Tanzania na Thailand hususan katika tasnia ya vito na usonara, kutangaza na kutafuta masoko ya bidhaa za vito na usonara zinazozalishwa hapa nchini, kujifunza na kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kusimamia na kukabili-ana na changamoto za tasnia ya vito na usonara, pamoja na kuitangaza sekta ya madini ya Tanzania na kutafuta fursa za uwekezaji hususan katika tasnia ya vito.

    Kalugendo aliongeza kuwa, ushiriki wa Tanzania katika maonesho husika pia utatangaza mpango wa Serikali wa kuwa na jengo maalum kwa ajili ya kufanyia biashara ya madini ya almasi ikiwa ni pamoja na vito na madini men-gine ya thamani kubwa na pia kutafiti na kufuatilia mwenendo wa bei za vito mbalimbali kwenye soko hilo.

    Aidha, alisema fursa hii itatoa nafasi ya kuelezea mipango na tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa na zi-nazoendelea kufanywa katika sekta ya madini, ugunduzi mpya na mipango endelevu iliyopo katika tasnia husika.

    Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa Tanzania kushiriki maonesho husi-ka, Mkurugenzi Kalugendo alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kikubwa cha madini hususan vito vya usonara na mapambo ikiwemo Tanzanite inayopatikana Tanzania pe-kee hivyo ni muhimu kujitangaza ili

    kukuza soko la madini hayo na hivyo kuinua uchumi wa nchi.

    Kutokana na utajiri wa madini tulionao, ni vema kuzitumia fursa za maonesho kama haya ili kujitangaza kibiashara, kuvutia wateja, kuhimiza ubunifu wa mitindo mipya na kuvutia fursa za uwekezaji, alisisitiza.

    Kwa upande wake, Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho Teddy Goliama alisema kuwa maan-dalizi ya ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo yanakwenda vizuri na kwamba anaamini nchi itanufaika kwa kiwango kikubwa kutokana na ushiriki wake.

    Tumejipanga kuwa na ushiriki wenye tija. Tunaamini tutanufaika ipasavyo kutokana na ushiriki wetu katika maonesho hayo kwani tunao uzoefu wa kutosha kutokana na kush-iriki maonesho mbalimbali ya aina hii na hivyo safari hii tumeboresha zaidi mbinu za ushiriki, alieleza Teddy.

    Tanzania imekuwa ikipata fursa za kushiriki katika maonesho ya almasi na vito ambayo hufanyika sehemu mbal-imbali duniani kama vile Hong Kong, Tucson na Mumbai. Katika maone-sho yajayo ya Hong Kong, Tanzania itawakilishwa na Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara binafsi chini ya ura-tibu wa Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha TANSORT.

    kamati iliyoandaa Maonesho ya 53 ya Madini ya Vito na usonara Thailand

    Madini ya Vito

    Madini ya Vito, Usonara Tanzania kutambulika duniani

    Madini

    Tanzanite

    Wachina kuwekeza sekta ya madiniNuru Mwasampeta na Veronica Simba, Dar es SalaamWaziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema Wizara yake imejipanga kuhakikisha inajengwa mi-tambo ya uchakataji madini (Mineral Processing Plants) hapa nchini ili kuondokana na utaratibu wa kusafirisha madini ghafi nje ya nchi na badala yake zisafirishwe bidhaa zitokanazo na madini husika ili kuongeza thamani na hivyo kukuza pato la nchi.

    Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na ku-zungumza na Wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco ya nchini China waliokuja nchini kwa lengo la kujadiliana na Viongozi Waandamizi wa Wizara kuhusu fursa za uwekezaji hususan katika sekta ya madini.

    Tunahitaji kuwa na mitambo ya uchakataji madini hapa nchini hivyo nawashauri katika uwekezaji wenu mfikirie suala la kujenga mtambo husika kwani hatutaki kusafirisha madini ghafi nje ya nchi, alisisitiza Profesa Muhongo.

    Katika mazungumzo hayo, Waziri Muhongo aliwaeleza wawekezaji hao ambao waliambatana na Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing kuhusu fursa muhimu za uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini kuwa ni uwekezaji katika madini yaliyo katika kundi adimu (Rare Earth Elements), ma-dini ya Shaba (Copper) pamoja na madini ya Dhahabu.

    Aliwashauri wawekezaji hao kukutana na Wataalamu ku-toka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ambalo limepewa dhamana ya kusimamia maeneo yote ya uwekezaji katika sekta ya madini kwa niaba ya Serikali, ili kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuingia ubia katika uwekezaji husika ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya kina kuhusiana na uwekezaji katika sekta ya madini.

    Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi aliwaeleza wawekezaji hao kuwa Tanzania inajulikana vizuri kwa kuwa na mazingira mazuri ya kijiolojia yanayofaa kwa uwekezaji hususan kwa madini kama dhahabu, vito, shaba, nickel na cobalt na kwamba aina ya miamba inayopatikana nchini inaruhusu madini ya aina ny-ingi kupatikana akitolea mfano Tanzanite ambayo inapatikana Tanzania pekee.

    Aidha, aliongeza kuwa Tanzania inayo sera nzuri ya madi-ni, utawala bora, hali nzuri ya kisiasa (political stability) pamoja na miundombinu bora, ambazo ni miongoni mwa sababu za msingi zinazovutia uwekezaji nchini.

    Naye Kamishna wa Madini, Mhandisi Paul Masanja aliwakaribisha wawekezaji wa Kampuni ya Chinalco kuja ku-wekeza nchini na aliahidi kuwapa msaada utakaohitajika ili kufanikisha azma yao hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapa leseni ya kutafuta au kuchimba madini kwa wakati.

    Awali, Mwenyekiti wa Kampuni ya Chinalco, Bw. Xiong Weiping akiinadi Kampuni yake kwa Viongozi wa Wizara alieleza kuwa, Kampuni hiyo ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na inasimamiwa na Serikali Kuu na kwamba inajihusisha na masuala ya maendeleo ya rasilimali za madini, uchakataji wa madini ghafi na masuala ya kiufundi (technical & engineering services).

    Alisema mkakati wa kampuni hiyo ni kuendelea kupanua shughuli za uzalishaji wa madini ya Aluminum, Shaba, Rare Earth Element na uongezaji thamani madini.

    Ziara ya Kampuni hiyo nchini imekuja kufuatia ziara zi-lizofanywa awali nchini China kwa nyakati tofauti na Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ka-tika Makao Makuu ya kampuni hiyo mapema mwaka jana na kuuomba uongozi wa kampuni hiyo kupanua mipaka ya bi-ashara hadi Tanzania.

    Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika mazungumzo na ujumbe kutoka kampuni ya Chinalco kutoka China kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini hapa nchini. kushoto ni Wa-ziri wa Nishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo. kulia kwa Waziri ni Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing na kushoto kwa Waziri ni katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

  • 9BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Picha hii inaonyesha jinsi lakiri (seal) zinavyofungwa

    Ubunifu wazidi kulinufaisha TaifaTMAA

    Na Teresia Mhagama

    Kutokana na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) kubuni na kutekeleza mkakati

    wa kudhibiti mapato ya Serikali kutokana na shughuli za uchen-juaji wa marudio ya dhahabu, Wakala huo umezidi kuongeza mapato yanayotokana na shu-ghuli hizo ambapo katika kip-indi cha kuanzia Januari hadi

    Julai 2014, Wakala umewezesha Serikali kukusanya mrabaha wa kiasi cha Shilingi Milioni 861 kutokana na ukaguzi huo unao-fanyika Jijini Mwanza na katika Mji wa Geita.

    Kiasi hicho ambacho ni wastani wa makusanyo ya Shilingi Milioni 123 kwa mwezi kimetokana na ubunifu na ush-irikiano mkubwa unaofanywa baina ya Wakala, Ofisi za Ma-dini pamoja na wananchi walio-wezesha upatikanaji wa taarifa

    juu ya kuwepo kwa mitambo ya kuchenjulia dhahabu katika maeneo mbalimbali nchini.

    Taarifa kutoka TMAA im-efafanua kuwa Wakala huo uli-buni utaratibu wa kutumia lakiri ambazo zinawekwa kwenye mi-tambo ya kuchenjulia dhahabu inayojulikana kama elution plants. Lakiri hizo huwekwa kabla na baada ya kuweka kabo-ni zinazofyonza dhahabu (load-ed carbon) katika mitambo hiyo ili kuweza kuvuna dhahabu.

    uchenjuaji wa marudio ukiwa katika hatua za awali

    Mtambo wa uchenjuaji wa dhahabu (elution plant) na namna lakiri (seal) zinavyofungwa

    Wakaguzi hufungua lakiri hizo na kushuhudia mchenjuaji an-apokuwa akivuna dhahabu yake hivyo kuweza kujua kiasi cha dhahabu inayozalishwa.

    Kutokana na TMAA ku-tumia utaratibu huo wa kutumia lakiri, mmiliki wa mtambo wa kuchenjulia dhahabu analazi-mika kuwasiliana na wakaguzi wa TMAA na Ofisi ya Ma-dini husika ili kuweza kufanya uchenjuaji.

    Taarifa hiyo inaeleza kuwa ubunifu wa uwekaji lakiri katika mashine za uchenjuaji madini umekuja baada ya wachimbaji wa kati wa madini kuanza ku-tumia teknolojia ya kuchenjua marudio ya zamani yadhahabu ya wachimbaji wadogo (vat leaching) hivyo kulikuwa na changamoto kubwa ya kuweza kubaini kiasi cha dhahabu inay-ozalishwa ili kudhibiti uzalishaji huo.

    Kabla ya utaratibu huu kuanza Serikali ilikuwa

    ikitegemea takwimu kutoka kwa wachenjuaji ambazo zilikuwa za chini sana hivyo Ukaguzi huo kwa sasa unaendeshwa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara na Mbeya ambapo kuna shu-ghuli nyingi za uchenjuaji wa marudio ya dhahabu.

    Pamoja na udhibiti uliok-wisha kufanyika, Wakala kwa kushirikiana na Ofisi ya Kam-ishna wa Madini ilibuni kibali cha kusafirishia loaded carbon kutoka kwenye mitambo ya vat leaching (uchenjuaji wa awa-li) hadi kwenye Elution Plant (uchenjuaji wa mwisho). Vibali hivi ambavyo husimamiwa na Ofisi za Madini vimesaidia ku-dhibiti mapato kwa kuhakikisha kaboni zinazosafirishwa kwen-da kuchenjuliwa zimetoka kwa wachenjuaji wenye leseni halali za madini.

    Pamoja na ukaguzi huo, uk-aguzi wa kushitukiza umekuwa ukifanyika ili kuongeza udhibiti wa uzalishaji wa dhahabu. Pia, elimu imekuwa ikitolewa kwa wamiliki wa migodi na mitam-bo ya kuchenjulia dhahabu na wadau wa madini kwa ujumla

    kuhusu umuhimu wa kuzali-sha madini na kufanya bi-

    ashara ya madini kwa ku-fuata sheria na kanuni za madini ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kulipa mrabaha wa Serikali.

    Mfano wa kibali kinachotumika kusafirishia carbon kwa kanda ya Ziwa

    Na Maliki Munisi

    Mradi mkubwa wa bomba la gesi ku-toka Mtwara mpa-ka Dar es Salaam ambao unami-

    likiwa na serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kwa asilimia miamoja unaelekea ukingo ni kukamilika.

    Taarifa iliyotolewa na TPDC kupitia wataalam wake wanaosi-mamia na kuratibu ujenzi wa mra-di huo inabainisha kuwa sehemu kubwa ya shughuli mbalimbali zi-nazounda mradi huo zimekamilika kwa kiwango kikubwa.

    Shughuli ambazo zimekamilika kwa asilimia mia moja mpaka Julai, 2014 kwa mujibu wa taarifa hiyo ni usafishaji wa njia yaani Mkuza kwa ajili ya kupitisha bomba la gesi na usimikaji wa mabomba baharini kutoka Mnazi Bay hadi Madimba

    mkoani Mtwara urefu wa kilomita 4.748.

    Shughuli nyingine ambazo zimekamilika kwa kiwango kikub-wa ni pamoja na usafirishaji wa ma-bomba ya gesi kutoka kwenye ghala

    mpaka kwenye maeneo ya ujenzi ambayo tayari yamefikia urefu wa kilomita 501 kati ya 504, uungan-ishwaji na uchomeleaji wa mabom-ba umekamilika kwa urefu wa kilo-mita 491 kati ya 504, uchimbaji wa

    mtaro kwa ajili ya kulaza mabomba umekamilika kwa kilomita za urefu 430 katika maeneo ya Dar es Sa-laam, Mkuranga, Lindi naMtwara.

    Vilevile kazi ya kulaza mabom-ba na nyaya za mawasiliano yaani Fibre Optic Cables kwenye mtaro umekamilika kwa kilomita za urefu 338, ufukiaji wa mabomba na nyaya za mawasiliano ambayo yame-shawekwa kwenye mtaro umekami-lika kwa kilomita 322 za urefu.

    Pamoja na shughuli hizo, taarifa inaeleza kuwa ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na ofisi ndogo za Madimba umekamilika kwa asil-imia 99 na kituo cha kusafishia gesi Madimba kimekamilika kwa asil-imia 60.

    Ikumbukwe kuwa mradi huu wa bomba la gesi unahusisha pia ujenzi wa nyumba za wafan-yakazi, ofisi ndogo na mtambo wa kusafishia gesi huko Songosongo mkoani Lindi.

    Kazi ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi imeshakamilika kwa kiwango cha asilimia 95 na ujenzi wa kituo cha kusafishia gesi umeka-milika kwa asilimia 40.

    Kwa upande mwingine ujenzi vituo vya koki za gesi na vituo vya mapokeo ya gesi kwenye kituo cha Somanga na Kinyerezi umekami-lika kwa asiliamia 17.

    Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni wa pili kumilikiwa na Serikali kupi-tia TPDC kwa asilimia mia moja baada ya ule mradi wa bomba la gesi kutoka Ubungo mpaka maeneo ya Mikocheni uliozinduliwa tarehe 26 Julai, 2014.

    Miradi hii itakuwa chachu kub-wa ya maendeleo ya nchi kutokana na unafuu katika matumizi ya gesi kwa shughuli za uzalishaji viwanda-ni, uzalishaji wa umeme, matumizi ya nyumbani na matumizi ya kwe-nye magari.

    MRADI WA BOMBA LA GESI MBIONI KUKAMILIKA

    u

  • 10 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzKUTOKA

    Wachimbaji wadogo wajiandae kusahau uchimbaji wa kuhamahama, kuachana na watu wachache wanaowatumia kama wafanyakazi ambao huvamia maeneo ya watu na kusababisha uharibifu wa mazin-gira. sTAMICo ipo ili kuwasaidia wachim-baji wadogo kutoka kwenye mazingira ya uchimbaji duni kwenda uchimbaji wenye tija,

    Na Bibiana Ndumbaro, STAMICO

    Na Issa Mtuwa- STAMICOShirika la Madini la Taifa STAMICO lime-kabidhi msaada wa fulana mia moja zenye thamani ya Tsh. Milioni Mbili kwa Mkuu wa wilaya ya Butiama, Angelina Mabula, kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2014.Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya fulana hizo, iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya STAMICO, Kaimu Mku-rugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi Edwin Ngonyani amesema shirika hilo ni mwekezaji kama wawekezaji wengine hivyo

    linawajibika kusaidia jamii zinazozunguka miradi yake kama ambavyo mashirika na makampuni mengine yanavyofanya.

    Mhandisi Ngonyani aliongeza, STAM-ICO ipo katika hatua za utekelezaji wa mi-radi mbalimbali ukiwemo Mradi wa Ununuzi wa Madini ya Bati Kyerwa, mkoani Kagera; mradi wa Kufua Umeme wa Makaa ya Mawe Kiwira; miradi ya uzalishaji dhahabu katika migodi ya Biharamulo kupitia Kampuni yake Tanzu ya STAMIGOLD na Buckreef iliyopo mkoani Geita.

    Aidha, Ngonyani alisisitiza kuwa, dhamira ya STAMICO ni kuhakikisha kuwa

    rasilimali za madini zinawanufaisha wa-nanchi wote na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na jambo litakalowezesha shirika hilo kuchangia fedha Hazina ambazo zitaka-zochangia maendeleo ya watanzania.

    Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula aliishukuru STA-MICO kwa msaada huo, huku akiishukuru Wizara ya Nishati na Madini kwa kutekeleza ahadi ya uchangiaji wa shughuli za maende-leo ya jamii.

    Hivi karibuni Wizara ya Nishati na Ma-dini kupitia STAMICO ilitoa msaada wa Shilingi milioni mia nane kwa Wilaya ya Bu-

    tiama kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule, nyumba ya mwalimu na kituo cha afya.

    Aidha, Mabula aliiishukuru Serikali kwa kutenga maeneo ya uchimbaji madini kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika wilaya hiyo jambo ambalo limesaidia kuleta utulivu katika wilaya tofauti na awali.

    Hadi sasa tuna vikundi vitatu vya wachimbaji wadogo wadogo ambapo kila ki-kundi kina viwanja vitatu vyenye leseni kwa ajili ya wachimbaji wadogo, aliongeza Ma-bula.

    STAMICO yakabidhi msaada wa fulana wilaya ya BUTIAMA

    Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa wito kwa wachimbaji wadogo kuachana na uchimbaji wa kuhama-hama ambao hauna tija

    kwao. Wito huo ulitolewa na Kaimu

    Mkurugenzi Mtendaji wa STA-MICO Mhandisi Edwin Ngonyani alipozungumza na wananchi kupi-tia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utan-gazaji la Taifa (TBC1) mwishoni mwa wiki kikilenga kuwaelimisha wananchi kuhusu namna STA-MICO ilivyojipanga upya ikiwemo Mkakati wake wa kuwaendeleza

    wachimbaji wadogo nchini.Mhandisi Ngonyani aliongeza

    kuwa, STAMICO ipo tayari ku-wasaidia wachimbaji wadogo wa-naotaka kuongeza tija katika sekta ya uchimbaji mdogo, na kwamba tayari timu ya wataalamu imeanza kutekeleza mikakati ya Shirika kwa vitendo, ili kuwanufaisha wachim-baji wadogo.

    Wachimbaji wadogo waji-andae kusahau uchimbaji wa ku-hamahama, kuachana na watu wachache wanaowatumia kama wafanyakazi ambao huvamia mae-neo ya watu na kusababisha uhar-ibifu wa mazingira. STAMICO ipo ili kuwasaidia wachimbaji wa-dogo kutoka kwenye mazingira ya uchimbaji duni kwenda uchimbaji wenye tija, alisisitiza Mhandisi Ngonyani.

    Naye Kaimu Mkurugenzi wa

    Migodi na Huduma za kihandisi wa STAMICO Zena Kongoi alisisitiza kuwa, shirika hilo limejiandaa ku-watoa wachimbaji wadogo katika uchimbaji duni kwenda uchimbaji wenye tija.

    Aidha, alieleza kuwa, shirika litawajengea uwezo wa kitaalamu wa kutambua na kupata taarifa za mashapo, matumizi sahihi ya kemi-kali, kuwasaidia kupata vifaa bora vya kuchimbia na kuchenjulia ma-dini kwa wakati na vinavyoendana na mazingira.

    Kongoi aliongeza kuwa, shiri-ka linawasiliana na benki ya TIB kurekebisha masharti ya utoaji wa mikopo kwa wachimbaji wadogo, ili kuwawezesha wachimbaji wado-go kutekeleza taratibu za kibenki na kuandaa michanganuo ya kibiasha-ra kulingana na masharti ya benki husika ili waweze kukopesheka.

    Aliongeza kuwa, shirika pia litawasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za masoko ya ndani na nje kwa usahihi na kwa wakati ili kufuta kilio cha wachimbaji wa-dogo wengi ambao wamepoteza matumaini ya kupata masoko ya uhakika.

    STAMICO imetoa wito kwa watanzania kuachana na dhana potofu kuwa shughuli za uchimbaji mdogo hazina tija kwa kuwa shu-ghuli hizo zikiwezeshwa, zinaweza kuwa sehemu ya uchangiaji katika uchumi wa taifa.

    Ngonyani - Wachimbaji msahau uchimbaji wa kuhamahamaSTAMICO

    Mtangazaji wa shirika la utangazi la Taifa TBC1 Marin hassan (wa kwanza kushoto), akiwa katika mahojiano na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa sTAMICo Mhandisi Edwin Ngonyani (wa kwanza kulia) yaliyorushwa na TBC1 kupitia kipindi cha Jambo Tanzania, mwishoni mwa wiki. katikati ni kaimu Mkurugenzi wa Migodi na huduma za kihandisi wa sTAMICo, Zena kongoi.

    Afisa uhusiano wa sTAMICo. Issa Mtuwa akimkabidhi vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali zikiwe-mo za Miradi ya sTAMICo Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Angelina Mabula kwenye viwanja vya ofisi za sTAMICo, wanaoshuhudia ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa sTAMICo Mhandisi Edwin Ngonyani na Meneja Masoko na uhusiano kwa umma wa sTAMICo, koleta Njelekela.

    kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa sTAMICo Mhandisi Edwini Ngonyani kulia akionyesha moja ya Tshirt zilizotolewa na shirika lake kwa Ajili ya Mbio za mwenge 2014 kwa Mkuu wa Wilaya Butiama Bi. Angelina Mabula (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Makao Makuu ofisi za sTAMICo dar es salaam.

  • 11BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    Meli ya discoverer America inayohusika na kuchoronga visima kitalu 2 katika bahari ya hindi Tanzania.

    Kuwaombea watanzania fursa za masomo vyuo bora Duniani

    Muhongo akaza kamba

    Na Nuru Mwasampeta, Dar es Salaam

    Wizara ya Nishati na Madini kupitia viongozi wake waan-damizi imeendelea kusaka fur-sa za elimu katika vyuo vikuu bora duniani ili kuwawezesha

    watanzania kupata elimu bora itakayowawez-esha kusimamia rasilimali zilizopo nchini kwa umakini mkubwa.

    Hayo yamebainika wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na Prof. Wesley L. Harris toka Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) nchini Marekani aliyemtembelea ofisini kwake ambapo Waziri Muhongo alitumia fursa hiyo kuomba nafasi kwa watanzania kudahiliwa katika chuo hicho.

    Mkutano kati ya Waziri na Prof. Harris uli-lenga katika kujadili masuala ya msingi katika sekta za nishati na madini hususan mafuta na gesi, ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya-nayohusu sekta za nishati na madini, kujenga uelewa wa msingi kuhusiana na sekta pamoja na ujenzi wa mipango endelevu katika masuala ya uzalishaji wa nishati.

    Katika mkutano huo Waziri Muhongo alielezea suala la uhaba wa wataalamu katika sek-ta mbalimbali zikiwemo za jiolojia, wahandisi, wachumi, wahasibu, na wanasheria na kuiomba taasisi ya MIT kutoa nafasi za kutosha ili watan-zania waweze kwenda na kupata elimu katika tasnia hizo.

    Akizungumzia suala la uzalishaji wa nishati ya umeme Profesa Muhongo alisema kwamba mpaka sasa umeme unaozalishwa kwa wingi nchini unatokana na maji na kuongeza kuwa kwa miaka miwili hadi mitano ijayo umeme un-aozalishwa kwa maji hautapewa kipaumbele na badala yake utatumika umeme utokanao na gesi asilia, jua, makaa ya mawe, tungamotaka pamoja na jotoardhi.

    Prof Muhongo alisisitiza kuhusu nia ya seri-kali ya kuwa na programu inayojitosheleza na ita-kayotekelezeka ya kuwajengea uwezo wananchi watakaokuja kusimamia rasilimali za gesi na mafuta zilizogunduliwa nchini.

    Aidha, ameshauri uwepo wa program itakay-owahusisha watendaji wa Taasisi ya MIT kutem-belea vyuo vilivyopo nchini na kuweza kubadilis-hana uzoefu. Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Do-doma, na Chuo cha Madini Dodoma vinavyotoa kozi za mafuta na gesi kwa ngazi tofautito.

    Kwa upande wake Profesa Harris amezun-gumzia nia ya taasisi yake katika kujenga mahu-siano baina ya Tanzania na MIT katika maeneo

    Waziri wa Nishati na Madini Profesa sospeter Muhongo (kulia) akiagana na Prof. Wesley L. harris toka chuo cha Massachusetts Institute of Technology nchini Marekani mara baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala yanayohusiana na sekta za Nishati na Madini jijini dar es salaam.

    Waziri wa Nishati na Madini akiwa pamoja na watendaji wa wizara mara baada ya kutembelewa na Prof. Wesley L. harris toka chuo cha Massachusetts Institute of Technology nchini Marekani alipomtembelea ili kujadili masuala yanayohusiana na sekta za Nishati na Madini.

    uya sayansi, Tekinolojia na ubunifu.Aidha amesisitiza kuweka kipaumbele katika suala la ku-wajengea uwezo wananchi. Harris amesema suala la kuwepo kwa rasilimali si jambo kubwa, bali kuwajengea uwezo wazawa katika kusimamia rasilimali hizo ndiyo jambo la msingi.

    Profesa Harris amesema atayafanyia kazi maombi yaliyo-tolewa na Waziri Muhongo ili kuhakikisha ushirikiano baina nchi za Tanzania na Marekani hususan katika suala la kuwa-jengea uwezo wananchi linapewa kipaumbele.

    Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiwatafutia wa-tanzania ufadhili wa masomo maeneo mbalimbali duniani ili kuongeza idadi ya wataalam ambapo hivi karibuni wanafunzi 10 walipewa ufadhili wa kwenda nchini China kusomea sha-hada ya uzamili na uzamifu katika fani ya mafuta na gesi.

  • 12 BulletinNewshttp://www.mem.go.tz

    lazima watanzania tujiamini na tuaminiwe na wengine. tanzania imeingia kwenye uchumi wa gesi asilia. lazima tufanye mapinduzi

    makubwa ya uchumi kwa ajili ya kufuta umaskini miongoni mwa watanzania. uchumi imara utatoa ajira mpya, amani na usalama wa

    kudumu na matumaini mapya. tuachane na ubinafsi hakuna kukata tamaa, hakuna kushindwa.

    UJUmBe Wa WaZiri WiKi Hii

    Masele aeleza umuhimu wa sayansi Afrika

    Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wasiliana nasi kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]

    Wizara ya nishati na madini

    Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshu-ghulikia Madini, Stephen Masele amesema kuwa bara la Afrika linahitaji taaluma ya sayansi kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi.

    Masele ameyasema hayo jijini Dare es Salaam wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wa-

    nasayansi Duniani (YES), na kuongeza kuwa, Afrika inahitaji sayansi kwa ajili ya kufanya

    ugunduzi na tafiti ambazo zitachangia katika kuchochea maendeleo barani Afrika.

    Aliongeza kuwa, kutokana na umuhimu huo, Wizara ya Nishati na Madini imed-

    hamiria kuwekeza kwa vijana katika tasnia ya sayansi ikiwemo kuhamasisha Vyuo Vikuu nchini, kuanzisha masomo ya sayansi hususan katika sekta ndogo ya gesi na mafuta jambo ambalo litawezesha kuzalisha wataalam wengi zaidi watakaosaidia kue-ndeleza taaluma hiyo na rasilimali zilizopo nchini.

    Kutokana na umuhimu huo, aliutaka Mtandao wa Vijana Wanasayansi Duniani (YES), ku-hakakikisha unasaidia kuwezesha vijana kuona umuhimu wa kuingia katika taaluma ya sayansi hususan jiolojia ili kuwezesha bara la Afrika kuwa na wataalamu wengi watakaosaidia kuharakisha

    maendeleo kupitia rasilimali asilia.Mtandao wa vijana mna jukumu la kuchochea

    taaluma ya sayansi kwa vijana. Afrika inahitaji wana-sayansi wakutosha, kwa kuwa, uwepo wao utasaidia kuchochea ukuaji wa viwanda na teknolojia barani Af-rika, alisisitiza Masele.

    Aidha, alieleza kuwa, Afrika inahitaji wataalamu wanasayansi hivyo, alitoa wito kuwashirikisha vijana katika masuala ya kitaaluma ikiwemo kufanya maamu-zi.

    Nikiwa kiongozi kijana, nawataka vijana kuona umuhimu wa taaluma hii, hivyo, nawatanguliza ninyi katika hili, nendeni mkawafundishe na kuwahamasisha wenzenu waone umuhimu wa sayansi kwa dunia na kwa Afrika,alibainisha Masele.

    Aidha, aliongeza kuwa, kama kiongozi kijana, atatumia nafasi yake, kusaidia uwepo wa sera nzuri ambazo zitahamasisha ukuaji wa taaluma ya sayansi na kuwezesha vijana kisayansi.

    Kwa upande wake, Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani, Meng Wang alieleza kuwa, mkutano huo wa tatu umeacha historia kwa Tanzania na Afrika kutoka-na na kupata nafasi ya kukutana, kujadili na wanasay-ansi wakubwa waliobobea katika masuala ya Jiolojia Afrika na Duniani jambo ambalo litasaidia kuchochea ari ya vijana kuendeleza taaluma hiyo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana wengi zaidi kuingia katika sekta hiyo.

    nAtaka vijana kushirikishwa katika maamuzi

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, stephen Masele akizungumza wakati akifunga Mkutano wa Tatu wa Vijana Wanasayansi duniani, jijiji dar es salaam.

    Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, stephen Masele akimpa zawadi ya kinyago iliyotolewa na mtandao wa Vijana Wanasayansi duniani (YEs), Rais wa Wajilojia barani Afrika Profesa Aberra Mogessie.

    Rais wa Wanasayansi Vijana duniani, Meng Wang, akimkabidhi zawadi ya vinyango Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, stephen Masele mara baada ya kufunga mkutano wa tatu wa Wanasayansi Vijana duniani.