ripoti ya ufuatiliaji na uwajibikaji kwa jamii (sam) sam... · 1.1 dhana ya ufuatiliaji wa...

36
Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma 2018

Upload: others

Post on 30-Jun-2020

12 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji

kwa Jamii (SAM)

Halmashauri yaWilaya ya MpwapwaDodoma

2018

Page 2: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM)

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

Dodoma

Novemba 2018

Page 3: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali
Page 4: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

i

Nitumie fursa hii kuwakaribisha wasomaji na watumiaji wa ripoti zetu kupokea toleo hili ikiwa ni sehemu

ya mwendelezo wa ripoti za utekelezaji wa ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii (SAM) nchini.

Ripoti hii imeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Sikika na wananchi wa wilaya ya Mpwapwa baada ya

kufanya ufuatiliaji shirikishi katika mifumo ya utoaji huduma za afya wilayani. Ufuatiliaji huu ulilenga

katika kutathimini mchakato wa mipango hususani maeneo ya mgawanyo wa rasilimali za afya,

matumizi ya rasilimali hizo na utendaji wa vyombo vya usimamizi wa utoaji huduma za afya.

Utekelezaji ulifanyika kwa kutumia mbinu shirikishi ambapo wadau mbalimbali hususani wananchi

walipatiwa mafunzo kwa vitendo yaliyowawezesha kufanya uchambuzi wa taarifa za idara ya afya na

hatimaye kufanya tathimini kwa kutumia dodoso kama lilivyoambatanishwa katika ripoti hii. Matokeo

yaliyopatikana yamechangia ushiriki wa wananchi katika kuboresha huduma za afya katika wilaya ya

Mpwapwa kupitia majadiliano baina ya wananchi na timu ya menejimenti ya afya Mpwapwa.

Vilevile, matokeo ya zoezi hili ni muhimu kwa wadau wa afya kwa kuwa yanatoa taarifa zinazo ainisha

maeneo yanayohitaji kuboreshwa na pia yanaweza kutumika kama maelezo ya msingi (baseline

information) katika kupima maboresho katika huduma za afya katika wilaya ya Mpwapwa.

Asanteni

Irenei KiriaMkurugenzi Mtendaji wa Sikika

Kutoka kwa Mkurugenzi

Page 5: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

ii

Shukrani

Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi mzima wa wilaya ya Mpwapwa. Kuanzia ofisi

ya Mkuu wa Wilaya inayoongozwa na Mh. Jabiri S. Shekimweri na Katibu Tawala wake Bi. Sarah J.

Komba. Baraza la madiwani na uongozi mzima wa Halmashauri chini ya Mwenyekiti Mh. Donath S.

Ng’wenzi na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu. Paul S. Sweya. Aidha, tunamshukuru Mganga Mkuu wa

Wilaya Dkt. Said Mawji, timu ya wataalamu ya Halmashauri - CMT na timu ya uendeshaji wa shughuli

za afya - CHMT kwa ushirikiano wao wa dhati.

Pili, shukrani zetu ziende kwa shirika la Sikika kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa wilaya yetu

katika utekelezaji wa shughuli zake hususani zoezi la Ufualiaji wa Uwajibikaji kwa Jamii. Kuendelea

kutekelezwa kwa zoezi la SAM hapa wilayani, ni kuendelea kutoa mwanga kwa wananchi na kutoa

mwelekeo chanya wa kuboresha mifumo ya afya. Zaidi, tunawashukuru wawezeshaji wa zoezi la

Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka shirika la Sikika; Lilian R. Kallaghe, Richard Msittu, Mathew

Kihulya, Nelson Lema na Khamis Hamadi kwa kutuwezesha kupata uelewa mpana kuhusu dhana ya

uwajibikaji.

Mwisho, napenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote wa wilaya ya Mpwapwa, viongozi na

watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya, maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji

na wajumbe wa timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii. Wote kwa namna moja ama nyingine

wameshiriki kikamilifu katika hatua zote hadi kukamilika kwa zoezi hili lililolenga kuboresha mifumo ya

kutolea huduma za afya wilayani Mpwapwa.

Asanteni sana,

Gabriel MnyawamiMwenyekiti, Timu ya SAM

Page 6: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

iii

Yaliyomo

Kutoka kwa Mkurugenzi...................................................................................................................i

Shukrani.......................................................................................................................................ii

Orodha ya Vifupisho.......................................................................................................................iii

Muhtasari.......................................................................................................................................iv

Sehemu ya Kwanza.........................................................................................................................1

1.0 Utangulizi...................................................................................................................................1

1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii.........................................................................1

1.2 Malengo ya SAM................................................................................................................... ...1

1.3 Mbinu za Utekelezaji wa SAM...................................................................................................2

Sehemu ya Pili................................................................................................................................3

2.0 Matokeo ya Uchambuzi wa Mipango, ripoti za utekelezaji na Uhakiki Vituoni..........................3

2.1 Tathimini ya Uandaaji wa Mipango na Utekelezaji wa Shughuli za Afya.................................3

2.1.1 Utawala na Fedha...............................................................................................................4

2.1.2 Dawa, vifaa na vifaa tiba.....................................................................................................6

2.1.3 Rasilimali watu katika afya..................................................................................................9

2.1.4 Majengo ya Afya, Mifumo ya Maji na Umeme..................................................................12

2.2 Tathimini ya Ufanisi wa Sheria, Miongozo na Taratibu za Utoaji Huduma za Afya....................15

2.2.1 Ufanisi wa sheria, miongozo na taratibu za kazi...............................................................15

2.2.2 Mamlaka, kamati za nidhamu na hatua zilizochukuliwa...................................................15

2.3 Tathimini ya Utendaji wa Vyombo vya Usimamizi wa Uwajibikaji............................................16

Sehemu ya Tatu............................................................................................................................18

3.0 Hitimisho.................................................................................................................................18

3.1 Mapendekezo.........................................................................................................................18

3.2 Mpango Kazi wa Pamoja........................................................................................................19

Viambatanisho...............................................................................................................................20

A. Orodha ya vituo na wajumbe wa timu ya SAM.........................................................................20

B. Dodoso la uchambuzi na uhakiki vituoni..................................................................................21

Page 7: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

iv

Orodha ya Vifupisho

CHF Community Health Fund / Mfuko wa afya wa jamii

CHMT Council Health Management Team / Timu ya Uendeshaji wa shughuli za Afya za

Halmashauri

CMT Council Management Team / Timu ya Menejimenti ya Halmashauri

DHSB District Health Service Board/ Bodi ya Afya ya Wilaya

HSBF Health Sector Basket Fund / Mfuko wa Pamoja wa Afya

LGBG Local Government Bloc Grant / Mfuko Mkuu wa Pamoja wa Serikali za Mitaa

KE Mwanamke

ME Mwanaume

MSD Medical Store Department /Bohari Kuu ya Dawa

NHIF National Health Insurance Fund /Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa

OC Other Charges / Matumizi mengineyo

SAM Social Accountability Monitoring / Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii

WAVIU Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi

WEO Ward Executive Officer/ Mtendaji wa Kata

Page 8: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

v

Muhtasari

Pamoja na mabadiliko yanayoimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini, sekta ya afya bado

inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo rasilimali fedha na watu. Mgawanyo wa bajeti ya

afya umeendelea kuwa chini ya kiwango kinachohitajika kukidhi utoaji wa huduma stahiki. Hali hiyo

imesababisha baadhi ya vituo kuwa na changamoto katika kutoa huduma bora za afya kutokana na

upungufu wa watumishi, vifaa tiba na miundombinu

Miongoni mwa mambo yanayosababisha uwepo wa changamoto hizo ni usimamizi hafifu katika sekta

ya afya. Hii huathiri mchakato wa mipango, ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali za afya wakati wa

utekelezaji ambapo hupelekea kuwa na mipango isiyokidhi viwango, udhibiti usioridhisha wa matumizi

ya rasilimali na ufuatiliaji hafifu. Changamoto hizi zinaweza kuzuilika ikiwa Serikali itaimarisha mifumo

ya utoaji wa huduma za afya.

Ili kuchangia jitihada za serikali katika kutatua changamoto kwenye sekta ya Afya, Sikika imekuwa

ikitumia dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii yaani Social Accountability Monitoring (SAM)

kwa kiingereza tangu mwaka 2012. Shirika limefanikiwa kutekeleza SAM 22 katika wilaya 19 hadi

mwaka 2018. Katika Wilaya ya Mpwapwa, zoezi la SAM linatekelezwa kwa mara ya tatu. Utekelezaji

wa zoezi hili, ulihusisha uchambuzi wa nyaraka kama vile Mpango Kabambe wa afya (CCHP), ripoti

za utekelezaji miradi na fedha, na kufanya ziara za uhakiki katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Katika vituo 63 vilitembelewa; vituo 55 vinavyotoa huduma za afya na vituo 8 vipo katika hatua

mbalimbali za ujenzi. Uchambuzi na ziara za vituoni viliiwezesha timu ya SAM kushuhudia mabadiliko

ya kiutendaji yaliyofanyika ukilinganisha na mazoezi ya nyuma mwaka 2012 na 2014. Maboresho

makubwa yameonekana hasa katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, mgawanyo mzuri wa rasilimali

watu katika afya na miundombinu ya afya.

Mafanikio mengine ni pamoja na uwasilishaji wa taarifa za Mpango Kabambe na Ripoti (2016/17 na

2017/18) kwa wakati ngazi ya Mkoa, utekelezaji wa usimamizi elekezi kwa kila robo, utoaji wa mafunzo

kwa kamati za usimamizi wa vituo (HFGC) na uhamasishaji jamii kujiunga na CHF mpaka kufikia

kuongoza ngazi ya Mkoa kwa asilimia 16.

Pamoja na mafanikio hayo, matokeo ya utekelezaji yamebainisha pia changamoto kadhaa hususani

katika maeneo ya uandishi wa nyaraka, uwepo wa nyaraka mbili za Mpango Kabambe wakati wa

utekelezaji, bajeti kuu kutofautiana na mchanganuo wa bajeti kwa vipaumbele, kubadili matumizi ya

fedha bila kuonekana katika ripoti za utekelezaji, shughuli kutoonekana katika ripoti za utekelezaji bila

ufafanuzi, na shughuli kuonekana kwenye ripoti za utekelezaji lakini kwenye mpango hazikubainishwa.

Changamoto nyingine zilihusisha vituo vya Kizi na Igoji-I kutopata fedha za Mfuko wa Pamoja kwa

takribani miaka 2, vituo kutomaliziwa ujenzi na vilivyokamilika kutoanza kufanya kazi, na changamoto

ya kukosekana kwa vyoo bora, mifumo ya maji na umeme, vichomea taka na mashimo ya kondo la

uzazi yanayokidhi viwango.

Page 9: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

1

Sehemu ya Kwanza 1.0 UtanguliziMoja ya mbinu shirikishi ambayo serikali ya Tanzania imekuwa ikiitumia kimkakati kuboresha utoaji wa

huduma ni kupitia mfumo wa uwajibikaji jamii. Sikika pia inaendeleza mfumo huo kwa kuwezesha jamii

kushirikiana na serikali kwa kutumia mbinu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii.

Utekelezaji wa SAM ngazi ya serikali za mitaa unakusudia kuimarisha uwajibikaji kwa jamii, ukilenga

kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma bora za afya. SAM inahimiza ushiriki wa jamii katika mchakato

wa kuandaa mipango na kufuatilia utekelezaji wa miradi katika maeneo yao. Vilevile, SAM inahimiza

wadau kufuatilia usimamizi ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kama ilivyopangwa na iwapo kuna kuna

matumizi mabaya ya rasilimali au utekelezaji usioridhisha, kuchukua hatua stahiki.

1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa JamiiSAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali za umma ili ziweze kukidhi mahitaji

muhimu ya jamii. SAM husimamia misingi ya haki za binadamu, uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa

wananchi na watoa huduma katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma. Dhana ya SAM imeundwa

kwa kuzingatia mfumo wenye hatua tano ambazo ni Mipango na Mgawanyo wa Rasilimali, Usimamizi

wa Matumizi, Usimamizi wa Utendaji, Usimamizi wa Uadilifu kwa Umma, na Usimamizi wa Uwajibikaji.

1.2 Malengo ya SAMLengo kuu la SAM kwa upande wa Sikika, ni kuimarisha mifumo ya usimamizi na uwajibikaji katika

utoaji wa huduma za afya kwa kushirikisha wananchi, watoa huduma, watendaji na wasimamizi ndani

ya wilaya.

Malengo Mahususi;

1. Kutathimini mchakato wa mipango na mgawanyo wa rasilimali afya hususani katika dawa, vifaa na

vifaa tiba, rasilimali watu na usimamizi fedha.

2. Kulinganisha mgawanyo wa bajeti na matumizi ya miradi ya afya hususan dawa, vifaa na vifaa tiba

na rasilimali watu.

3. Kutathimini usimamizi wa rasilimali fedha na watu, vifaa vya afya, dawa na vifaa tiba na miundombinu

ya afya kwa mujibu wa mpango kabambe wa afya.

4. Kutathimini usimamizi wa uadilifu kwa umma, uwezo wa kupima ufanisi na maadili ya kazi katika

usimamizi wa rasilimali afya.

Page 10: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

2

1.3 Mbinu za Utekelezaji wa SAMUtekelezaji wa SAM wilayani Mpwapwa ulianza kwa kutambulisha mradi kupitia mikutano ya Jamii,

Baraza la Madiwani na mkutano wa Wadau wa Afya. Hatua hizo ziliwezesha kuundwa kwa timu yenye

wajumbe 15 ambao walipatiwa mafunzo, kufanya uchambuzi wa taarifa za afya na uhakiki kwenye

vituo vya kutolea huduma za afya. Matokeo ya uchambuzi na uhakiki yalijadiliwa kwa pamoja na timu

ya menejimenti ya afya wilaya. Hatua hii ilitoa fursa ya kuandaa maazimio kwa ajili ya utekelezaji

ambayo yaliwasilishwa kwa wadau kupitia mkutano wa mrejesho kwa wadau wa afya.

Ufuatiliaji wa utekelezaji wa maazimio ya pamoja ni mbinu inayotumiwa kuhakikisha maboresho

yanafanyika. Hatua hii ni ya mwisho katika utekelezaji wa SAM.

Jedwali Na. 1: Uwakilishi wa wajumbe wa timu ya SAM

Kundi la Uwakilishi IdadiWananchi 6

Madiwani 2

Watendaji Kata 1

Timu ya Uendeshaji Afya/ CHMT 1

Timu ya watalamu wa Halmashauri/ CMT 1Kamati ya usimamizi wa shughuli za Afya (HFGC) 1

Bodi ya Afya (DHSB) 1Asasi za Kiraia 2Jumla 15

Page 11: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

3

Sehemu ya Pili

2.0 Matokeo ya uchambuzi wa mipango, ripoti za utekelezaji na uhakiki

2.1 Tathimini ya uandaaji wa mipango na utekelezaji wa shughuli za afya Utekelezaji wa zoezi la SAM ulifanikisha tathimini ya michakato ya uandaaji wa mipango na utekelezaji

katika maeneo ya utawala na fedha katika afya, bidhaa za afya, rasilimali watu katika afya na

miundombinu ya afya. Uchambuzi na uhakiki vituoni ulitoa matokeo yafuatayo:-

Page 12: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

4

Kielelezo Na. 1: Tathimini ya mchakato wa uandaaji mipango ya afya katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Idadi ya shughuli zilizopangwa na kutekelezwa

Jumla ya shughuli 162 zilipangwa, kati ya hizo shughuli 129 pekee ndizo ziliweza kutekelezwa. Kwa

mujibu wa CHMT, sababu ya kushindwa kutekeleza shughuli zote ni kupokea fedha chache pamoja na

kuchelewa kupata fedha.

Mgawanyo wa bajeti ya idara ya afya

Idara ilipanga kutumia shilingi 5,859,336,431/= na kupokea shilingi 3,693,139,340/= kutoka vyanzo

tofauti. Kati ya hizo, ilitumia shilingi 3,683,706,490/= kutekeleza shughuli. Hata hivyo, katika vyanzo

vyote 9 vya mapato vilivyoainishwa kwenye mpango, hakuna chanzo kilichotoa fedha zote. Idara

ilifanikiwa kupata angalau zaidi ya nusu ya fedha zilizoombwa kutoka katika vyanzo viwili pekee;

serikali kuu (LGDG) na mfuko wa pamoja wa afya (HSBF) kama inavyoonekana kwenye kielelezo Na.

2 hapo chini.

2.1.1 Utawala na fedha Uandaaji wa mipango kwa kuzingatia miongozo

Tathimini imeonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 idara ya afya ilifanikisha maandalizi ya

Mpango Kabambe wa Afya na utekelezaji wake kwa kuzingatia miongozo. Vilevile, uandaaji wa taarifa

na uwasilishaji ngazi ya mkoa ulifanyika kwa wakati. Aidha, ukiachia mbali changamoto ya idara kuwa

na mipango kabambe miwili wakati wa utekelezaji kinyume na taratibu na miongozo, idara ilifanikisha

usambazaji wa mipango ya vituo katika vituo 50 (94%) kati ya vitio 53. Mafunzo ya namna ya uandaaji

wa mipango yalitolewa katika vituo 52 (98%) angalau kwa mfawidhi na mwenyekiti wa kamati ya kituo.

Hata hivyo, mchakato wa kuandaa mpango ulihusisha kamati ya usimamizi wa kituo kwa mwaka

2017/18 na sio timu ya kuandaa mipango kama ilivyo ainishwa katika muongozo wa uandaaji mipango

ya vituo na zahanati wa mwaka 2016.

Page 13: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

5

Mabadiliko ya matumizi ya fedha

Shughuli nyingi zilitekelezwa kama zilivyopangwa; zikionesha kiasi kilichotengwa, kilichopokelewa,

kilichotumika na bakaa. Aidha, baadhi ya shughuli katika ngazi ya ofisi ya Mganga Mkuu, Hospitali ya

Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati zilionekana kufanyiwa mabadiliko bila ya kuwepo kwa ufafanuzi

katika ripoti za utekelezaji. Mfano; Ngazi ya ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) – Uchambuzi

ulionesha uwepo wa mabadiliko ya matumizi ya fedha dhidi ya mgawanyo wa fedha ulioainishwa. Mfano;

Bakaa ya shughuli ya kufanya matengenezo ya magari ya shilingi 2,909,999/= ilielekezwa kufanya

shughuli ya usimamizi shirikishi (supportive supervision). Hata hivyo, kwa mujibu wa menejimenti, hali

hii ilitokana na suala la mfumo kutokuwa na kolamu ya kuweka ufafanuzi wa ziada.

Vituo kutokupokea fedha za Mfuko wa Pamoja na CHF

Idara imejitahidi kuhakikisha vituo vingi vinasajiliwa na kuingizwa katika mfumo wa kupokea fedha moja

kwa moja. Pamoja na jitihada hizo kufanyika, timu ilibaini kuwa Zahanati za Igoji-I na Kizi hazikupata

fedha za Mfuko wa Pamoja (Basket Fund) kwa miaka miwili mfululizo jambo ambalo limezorotesha

utoaji wa huduma na kuathiri morali ya watoa huduma. Kwa upande wa fedha za CHF iliyoboreshwa,

pamoja na wanachama wengi kujiunga hadi kupelekea wilaya ya Mpwapwa kuongoza ngazi ya mkoa

kwa kufikisha asilimia 16 ya uandikishaji, ilibainika kuwa fedha za marejesho hucheleweshwa vituoni.

Kwa mfano; Zahanati ya Kizi, pamoja na kukosa fedha za mfuko wa pamoja na kuwa na wapokea

huduma karibu wote wenye kadi za CHF bado huathirika kiutendaji kutokana na kucheleweshewa

fedha za marejesho ya CHF.

Kielelezo Na. 2: Tathimini ya mgawanyo wa bajeti na matumizi kwa kila chanzo cha mapato kwa idara ya afya. Chanzo: Mpwapwa

CCHP, 2017/2018.

Page 14: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

6

2.1.2 Vifaa vya afya, dawa na vifaa tibaBajeti ya dawa na vifaa tiba

Kwa mwaka 2017/18, fedha zilizotengwa kwa kipaumbele cha dawa zimeoneka kutofautiana katika

taarifa za CCHP na ripoti za utekelezaji. Kwa upande wa CCHP, idara imeonesha kutenga shilingi

589,430,734/= tofauti na ripoti za utekelezaji zinazoonesha jumla ya shilingi 1,073,835,940/=. Hata

hivyo, ufafanuzi wa menejimenti umetofautiana na taarifa hizo ukionesha kiasi cha shilingi 907,985,209/=

ambacho ni tofauti na kiasi cha kwenye CCHP na ripoti yake ya utekelezaji. Aidha, pamoja na kuwa na

makadirio ya juu ya dawa na vifaa tiba, uhalisia umeonesha idara ilipokea shilingi 342,886,362/= na

kutumia shilingi 315,874,107/=.

Kwa upande wa tathimini ya mwenendo wa bajeti ya bidhaa za afya hususani dawa katika kipindi

cha miaka mitatu kama unavyo onekana katika kielelezo Na. 3 hapo chini, umeonekana kupanda na

kushuka hivyo kuashiria ufinyu wa fedha ambazo zinaweza kuathiri upatikanaji wa dawa vituoni.

Hali ya upatikanaji wa dawa na vitendanishi

Mpaka kufikia mwezi Novemba 2018, vituo 49 (93%)

kati ya vituo 53 vilithibitisha kuwa na dawa muhimu

vituoni ukilinganisha na asilimia 94 ya upatikanaji

kwa mwaka uliotangulia wa 2017/2018. Hata hivyo,

takwimu hizo zinakinzana na taarifa za fedha za dawa

pamoja na maoni ya watumia huduma ambao kwa

nyakati tofauti walieleza kutokuridhishwa kwao na

upatikanaji wa dawa vituoni.

Kielelezo Na. 4: Tathimini ya upatikanaji wa dawa na

vitendanishi kwa mwaka 2017/18 na 2018/19 katika

vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Kielelezo Na. 3: Tahimini ya mwenendo wa bajeti ya vifaa vya afya, dawa na vifaa tiba katika kipindi cha miaka mitatu. Chanzo: Mpwapwa CCHP, 2017/2018.

Page 15: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

7

Hali ya upatikanaji wa vifaa vya afya

Katika vituo 53 vilivyofanyiwa tathimini ya uwepo wa vifaa 6 vya afya na hali yake ya matumizi, vituo

vyote vimeonesha uwepo wa vifaa kwa zaidi ya asilimia 80 huku baadhi ya vifaa vikiwa havitumiki. Kwa

upande wa mashine za kupimia CD4, katika vituo 5 sawa na asilimia 11 ya vituo vyenye sifa ya kuwa na

mashine hizo vilikuwa nazo. Hata hivyo, kati ya vituo hivyo ni vituo 3 (6%) tu ya vituo hivyo vilivyokuwa

na mashine za kupima CD4 ambazo zilikuwa zinafanya kazi.

Hali ya upatikanaji wa vifaa vya kujifungulia wajawazito

Vituo 4 (7%) kati ya vituo 53 vimeonesha upungufu wa vifaa vya kujifungulia hususani vitanda na seti

za vifaa vya kujifungulia wajawazito. Asilimia 93 ya vituo vyote vilionekana kuwa na vifaa hivyo japo

kuna baadhi ya vifaa havikuwa katika hali nzuri.

Kielelezo Na. 5: Tathimini ya hali ya upatikanaji wa vifaa vya afya na vifaa tiba katika vituo 53 vya kutolea huduma za afya. Chanzo: Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Kielelezo Na. 6: Tathimini ya hali ya upatikanaji wa vifaa vya kujifungulia wakinamama wajawazito katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 16: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

8

Hali ya upatikanaji wa vifaa vingine vya afya

Hali ya upatikanaji wa vifaa vingine katika jedwali Na. 7 inaonesha kuwa nzuri ambapo upungufu

kwa vifaa vyote vilivyotathiminiwa umeonekana kuwa chini ya asilimia 50. Glovu ngumu zilikosekana

katika vituo 17 (32%) ikiwa ndio kiwango cha juu kabisa cha upungufu kwa upande wa vifaa (vingine)

vilivyotathiminiwa.

Hali ya mfumo wa mnyororo baridi

Vituo 52 kati ya 53 vilithibitisha kuwa na huduma ya chanjo kupitia mfumo wa mnyororo baridi. Kituo

cha Mafene hakikuwa na huduma ya myororo baridi, huduma hii kwa mujibu wa mfawidhi hutolewa

katika kituo cha jirani cha Lumuma. Kwa upande wa uwepo wa mfumo wa mnyororo baridi kituoni,

katika vituo 52 vilivyokuwa na mfumo ni asilimia 96 na 94 ya vituo hivyo vilikuwa na jokofu au deli,

ama vyote kwa pamoja kulingana na nishati zilizopo. Asilimia 91 na 94 vilikuwa na mtungi wa gesi au

umeme wa sola ama vyote kwa pamoja kama chanzo cha nishati ya mfumo wa mnyororo baridi.

Kielelezo Na. 8 (A&B): Tahimini ya uwepo wa mfumo wa mnyororo baridi katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Kielelezo Na. 7: Tathimini ya hali ya upatikanaji wa vifaa vingine vya afya katika vituo 53 vya kutolea huduma za afya. Chanzo: Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 17: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

9

2.1.3 Rasilimali watu katika afya Bajeti ya mishahara na stahiki za watumishi

Idara ya afya ilipanga kiasi cha shilingi 3,175,897,588/= kwa ajili ya watumishi waliopo na waliotarajiwa

kuajiriwa. Jumla ya shilingi 2,888,168,137/= zilipokelewa na kutumika zote. Kwa mujibu wa CHMT,

upungufu huo wa fedha za mishahara haukuathiri watumishi waliopo isipokuwa watumishi wapya

ambao walitarajiwa kuajiliwa endapo fedha hizo zingepatikana.

Hali ya upatikanaji wa rasilimali watu katika afya

Uchambuzi ulibaini kuwa, Idara ya Afya ilikuwa na upungufu wa watoa huduma kwa asilimia 48. Mpaka

kufikia mwaka 2017/18 Hospitali ya wilaya ilikuwa na upungufu wa watumishi 48 huku ngazi ya zahanati

ikiathirika zaidi kwa kuwa na upungufu wa watumishi 278. Zahanati nyingi zilikuwa na watoa huduma

kati ya 1 hadi 3 pekee. Mfano; Zahanati za Ikuyu, Mtamba, Chunyu, Kidenge, Igoji, Lukole na Wangi

zilikutwa zikiwa na mtoa huduma mmoja tu kwa kila zahanati.

Malipo ya stahiki mbalimbali za watumishi wa afya

Tathimini imeonesha kuwa stahiki za watumishi kama posho za kuwezesha watumishi kuwasilisha

taarifa wilayani ambazo zinalipwa moja kwa moja kituoni kutokana na fedha kupelekwa kituoni moja

kwa moja, zimeonekana kulipwa katika vituo 45 (85%) ukilinganisha na zile ambazo haziji kituoni moja

kwa moja kama malipo ya likizo yenye asilimia 21.

Kielelezo Na. 9: Tathimini ya hali ya upatikanaji wa watumishi wa afya kwa ngazi ya hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati. Chanzo: Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 18: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

10

Motisha za kubakiza watumishi wapya kazini

Katika vituo 53 vilivyotembelewa na timu ya SAM, ni vituo 36 (68%) tu ndivyo vilivyothibitisha watumishi

wapya walipewa magodoro kama motisha. Kituo kimoja (2%) kati ya vituo vyote 53 ndicho kilithibitisha

watumishi wake kupewa vitanda huku vituo 2 (4%) vilionesha watumishi wake walipewa motisha

nyingine kutoka kwa jamii zikihusisha kuchinjiwa mbuzi na kupewa nyumba na kijiji.

Kielelezo Na. 10: Tathimini ya malipo ya stahiki mbalimbali za watumishi wa afya katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Kielelezo Na. 11: Tathimini ya mbinu zitumikazo kutoa motisha ya kubakiza watumishi wapya kazini pindi wanaporipoti vituoni (n=53). Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018

Page 19: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

11

Utoaji wa mafunzo mbalimbali kazini

Vituo 16 (30%) kati ya vituo 53 ilithibisha kuwa watumishi wake walipatiwa mafunzo ya jinsi ya

kuhudumia wagonjwa wa TB hii ikiwa ni kiwango cha chini kabisa ukilinganisha na mafunzo mengine

kama huduma za mama na mototo amboyo yalitolea katika vituo 40 (76%).

Kielelezo Na. 12: Tathimini ya hali ya utoaji wa mafunzo kazini kwa watumishi wa afya katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 20: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

12

Hali ya mfumo wa rufaa za wagonjwa

Asilimia 100 ya vituo 53 vilivyotembelewa na

timu ya SAM vilithibitisha kutoa huduma ya

rufaa kwa wagonjwa kwa ngazi inayofuata

kwa mujibu wa taratibu. Kwa upande wa

tathimini ya uwepo wa gari la wagojwa,

vituo 5 (8%) kati ya 53 vilipaswa kuwa na

gari la wagonjwa wakati wa uhakiki. Kati ya

hivyo, vituo 3 (75%) vilikuwa na gari kituoni.

Ufafanuzi ulionesha kuwa gari la kituo cha

afya Mima na Zahanati ya Chipogolo yapo

katika hospitali ya wilaya kuhudumia wakati

gari la hospitali likiwa matengenezo.

2.1.4 Majengo ya afya, mifumo ya maji na umemeUjenzi na ukarabati wa majengo

Idara ilitenga jumla ya shilingi 128,422,450/= kutekeleza kipaumbele cha miundombinu ya afya. Kiasi

cha shilingi 77,326,506/= kilipokelewa na shilingi 79,116,450/= zilitumika ikiwa zimejumuisha na fedha

zilizovuka mwaka. Lisha ya kupokea fedha kidogo, idara imeendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali

ya afya ambapo vituo 23 (43%) ya vituo 53 vilikuwa vinaendelea na ujenzi ama ukarabati huku nyumba

za watumishi zikiwepo katika vituo 45 (85%). Jumla ya zahanati 8 na vituo vya afya viwili vipo katika

hatua mbalimbali za ujenzi. Hii ni hatua kubwa kwa serikali na ni muhimu kuhakikisha pindi tu majengo

yanapokamilika yanaanza kutumika ili kuepuka kuanza kuharibika kabla ya matumizi kama ilivyo kwa

jengo la zahanati ya Kitati.

Kielelezo Na. 13: Tathimini ya mfumo wa utoaji rufaa katika vituo 53 na uwepo wa gari la wagonjwa katika kituo kinachostahili kuwa na gari la wagonjwa. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Kielelezo Na. 15: Tathimini ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya afya hususani nyumba, vituo na miundombinu mingine katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 21: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

13

Aidha, katika zahanati ya Wiyenzele, paa la nyumba liliezuliwa na mvua miaka 7 iliyopita na

haijakarabatiwa tena. Miundombinu ya jengo la wazazi katika Hospitali ya Wilaya haikidhi mahitaji

kwa sasa nafasi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya akinamama wanaojifungua kwa siku. Hali hii

inasababisha akinamama wawili hadi watatu kulala katika kitanda kimoja. Huduma ya chumba cha

watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao pia ni changamoto kubwa. Eneo la chumba cha kuhifadhi maiti

(Mortuary) nalo halikidhi mahitaji. Hata hivyo, kwa mujibu wa mganga mfawidhi, ukarabati unaendelea

ingawa chumba kitahitaji kuongezewa majokofu ya kuhifadhia miili kwani yaliyopo matatu hayatoshelezi

kwa hospitali ya wilaya hasa inapotokea miili imekuwa mingi.

Hali ya nyumba za watumishi wa afya

Katika vituo 53 vilivyohakikiwa, vituo 45 (85%) vilikuwa na nyumba za watumishi. Kati ya hizo, nyumba

6 (13%) zilikuwa katika hali nzuiri huku nyumba 3 (6%) zikiwa hazina ubora kabisa na hazifai kwa

matumizi. Mfano; Hospitali ya Wilaya pekee ina nyumba 10 na zote zinahitaji ukarabati huku zahanati

za Tambi, Mwanakianga, Iwondo, Mlunduzi, Chipogolo, Kisima na Galigali zote zikiwa katika hali

isiyoridhisha. Kwa upande wa zahanati ya Mang’aliza nyumba ipo lakini haina choo wala bafu

Hali ya vyoo

Kwa mujibu wa CHMT, idadi ya vyoo vilivyoboreshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya Wilayani

Mpwapwa ni asilimia 87, idadi ya vyoo vya kawaida (vya asili) ni asilimia 13. Uhakiki vituoni ulithibitisha

baadhi ya vyoo kuwa katika hali nzuri japo changamoto ya ukosefu wa vyoo ilionekana katika zahanati

za Malolo, Ikuyu, Chunyu na Wangi. Pia, ukosefu wa miundombinu rafiki kwa watu wenye mahitaji

maalumu ni miongoni mwa changamoto zilizojitokeza katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za

afya. Mfano, miundombinu ya vyoo katika kituo cha afya Mima na choo cha Hospitali ya Wilaya ya

Mpwapwa sio rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu. Kwenye hospitali ya wilaya, eneo la kuingilia

lipo juu ingawa kuna mlalo wa kuingilia.

Kielelezo Na. 16: Tathimini ya hali ya nyumba za watumishi katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 22: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

14

Hali ya shimo la kondo la uzazi na vizimba vya kuchomea taka

Vituo 31 (58%) kati ya vituo 53 vilivyotembelewa vilikuwa na mashimo yasiyo na viwango (mashimo

ya asili) ya kutupia kondo la nyuma la uzazi. Mfano; zahanati ya Ipera, Kidenge, Sazima, Igoji, Lukole,

Wangi na Inzomu hutumia mashimo ya asili. Aidha, vituo 8 (15%) kati ya vituo 53 vilikuwa na vizimba

maalumu vya kuchomea taka ngumu na hatarishi. Vituo hivyo ni Hospitali ya Wilaya; vituo vya afya vya

Kibakwe, Mima, na Rudi; zahanati za Mbori, Kiyegea, na Pwaga. Vituo vingine huteketeza taka kwenye

mashimo ya kuchimba chini (mashimo ya asili). Changamoto nyingine iliyobainika ni kutokuwepo kwa

uzio katika mashimo na vizimba.

Hali ya upatikanaji wa nishati

Vituo 51 kati ya 53 ndivyo vilikuwa na nishati ya umeme. Hata hivyo, baadhi ya vituo vina changamoto ya

mifumo ya nishati ya umeme. Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ina changamoto ya jenereta kutokuwa

na nguvu ya kutosheleza Hospitali nzima. Zahanati ya Lufu na Chinyanghuku, wana changamoto ya

betri za umeme jua ambazo hazina nguvu. Changamoto kubwa ipo katika zahanati ya Igoji II na Wangi

ambazo hazina nishati ya umeme kabisa, wanatumia tochi nyakati za usiku.

Mifumo ya maji safi na salama vituoni

Vituo 20 (38%) kati ya vituo 53 vilivyo hakikiwa vilikuwa na mifumo ya maji safi inayofanya kazi. Hata

hivyo, kituo 1 (2%) ya vituo hivyo vyote kilikuwa na mifumo yenye hali nzuri huku mifumo mingine

ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo kubwa la mgawo wa maji mfano katika Hospitali

ya Wilaya ambayo hupata maji mara 2 au 3 kwa wiki. Zahanati ya Berege huchangia bomba na kijiji,

zahanati ya Kizi huchota maji mbali na kituo huku zahanati ya Igoji II ikiwa haina maji kabisa.

Kielelezo Na. 17: Tathimini ya hali ya vichomea taka na mashimo ya kutupia kondo la nyuma la uzazi katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 23: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

15

2.2 Tathimini ya Ufanisi wa Sheria, Miongozo na Taratibu za Utoaji Huduma za Afya Utoaji wa huduma ya afya huongozwa na sheria pamoja na taratibu mbalimbali. Uchambuzi na uhakiki

wa timu uliangazia tathimini ya uzingatiaji wa sheria na taratibu katika usimamizi na utoaji wa huduma

za afya wilayani kama ifuatavyo:-

2.2.1 Ufanisi wa sheria, miongozo na taratibu za kazi Uchambuzi na uhakiki ulibaini kuwa CHMT pamoja na watoa huduma vituoni hutumia miongozo

mbalimbali katika kutoa huduma. Mfano; Muongozo wa uandaaji wa mipango na utoaji wa taarifa,

muongozo wa uandaaji wa mpango kabambe, muongozo wa utoaji wa huduma kwa wateja, na

muongozo wa CHF.

Aidha, katika vituo vyote vilivyotembelewa ilibainika kuwa maandalizi ya mipango yalifanyika kupitia

Kamati za Afya kinyume na muongozo wa uandaaji unavyoelekeza (Rejea: Muongozo, Uk. 3 – 2.2)

kuwa wajumbe watokane na makundi mbalimbali ikiwepo kamati ambayo ni sehemu ya wajumbe.

Taarifa za utekelezaji hazitolewi kulingana na matakwa ya majedwali katika muongozo. Mfano; vituo

vingi havikuwa na ripoti za utekelezaji ispokuwa baadhi kama Mafene, na Hospitali ya wilaya, vilikuwa

na taarifa za fedha za kila robo.

2.2.2 Mamlaka, kamati za nidhamu na hatua zilizochukuliwa• Uhakiki ulionesha kuwa tuhuma mbalimbali ziliripotiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya

na kushughulikiwa ama na Mfawidhi au Kamati ya usimamizi ya kituo.

• CHMT walipokea tuhuma za aina mbili kuhusu uuzaji wa dawa na matumizi ya lugha mbaya kwa

wapokea huduma ambazo zote walizishugulikia kwa kuandika barua ya onyo kali pamoja na

kuwa na usimamizi wa karibu kwa ajili ya kuhakikisha changamoto iliyotokea hairudii tena.

Mifumo ya kutoa maoni na kupokea malalamiko vituoni

Tathmini ya timu katika vituo vya kutolea huduma za afya ilibaini kuwa, vituo vinatumia njia mbalimbali

kupata maoni na malalamiko kutoka kwa jamii. Kutoa malalamiko kwa Kamati za Afya za vituo ndio

iliyoonekana kutumika zaidi katika vituo 46 (87%) kati ya vituo 53 kama inavyoonekana kwenye

kielelezo Na. 20.

Kielelzo Na. 19: Tathimini ya mifumo ya maji safi na salama katika vituo 53. Chanzo; Uhakiki wa timu ya SAM, 2018.

Page 24: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

16

Njia nyingine ambayo hutumiwa ni kupitia simu kwa kuwasiliana moja kwa moja na DMO, Diwani au

viongozi wengine. Hata hivyo, pamoja na uwepo wa mbinu hizo changamoto zifuatazo zilibainika: -

• Masanduku ya maoni katika vituo vyote hayakuwa na kufuli mbili

• Uelewa mdogo wa wananchi na kamati za vituo kuhusu matumizi ya masanduku ya maoni

• Baadhi ya vituo kukosa masanduku ya maoni na mbao za matangazo. Mfano; Igoji II, Lufu, Bere-

ge, Sazima, Lukole na Iyenge.

• Masanduku ya maoni kuwekwa sehemu zisizo rafiki kwa watumiaji. Mfano; zahanati ya Winza

ilikuwa na sanduku nje kwenye matofari.

2.3 Tathimini ya Utendaji wa Vyombo vya Usimamizi wa Uwajibikaji Ushiriki wa jamii ulibainika kuwepo kwa wastani kwa kushiriki katika mikutano ya kijamii na kujitolea

kufanya usafi na nguvu kazi wakati wa ujenzi. Aidha, katika usimamizi na ufuatiliaji wa utoaji huduma

vituoni wananchi hushiriki kupitia Kamati za afya za vituo ambazo zinatambulika kupitia miongozo na

kimuundo.

Kamati za afya: Katika vituo vyote vilivyotembelewa, kamati za afya zilikuwepo na huwa zinakutana

japo kuna changamoto zifuatazo:

• Kamati zote hazijapewa mafunzo kuhusu majukumu na wajibu wao.

• Baadhi ya vituo kuwa na wajumbe wasio na sifa. Kwa mfano; Diwani au Mwenyekiti wa Kijiji

kuwa mjumbe katika kamati za afya.

Menejimenti iliahidi kuzipatia mafunzo kamati hizi na kuwaondoa wajumbe wasiostahili.

Bodi ya Afya: Kuhusu utendaji wa Bodi ya Afya ya wilaya, uchambuzi ulionesha vikao vyote vilifanyika

isipokuwa si kwa ukamilifu katika utekelezaji wa majukumu yake. Wajumbe wa Bodi hawakuwa na taarifa

kuhusu bajeti kuu ya Idara ya Afya na Mpango Kabambe wa Afya. Pia walifanyia kazi mapendekezo ya

Taasisi ya Usimamizi kwa kukutana na kupitia hoja zote.

Madiwani: Uchambuzi ulionesha kuwa Baraza la Madiwani walipokea na kujadili ripoti ya Mdhibiti na

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na ripoti ya Mkaguzi wa Ndani. Miongoni mwa

Kielelezo Na. 20: Tathimini ya mifumo ya kutoa maoni na kupokea malalamiko vituoni. Chanzo: Uhakiki wa timu ya SAM, 208.

Page 25: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

17

hoja za afya ambazo hazikupatiwa ufumbuzi ni mbili;

• Utawala wa halmashauri kukopa fedha za CHF shilingi 88,842,790/= bila kuzirejesha idara ya

afya.

• Kutowasilishwa kwa shilingi 4,000,000/= za CHF Halmashauri kutoka kwa wakusanyaji.

Page 26: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

18

Sehemu ya Tatu 3.0 HitimishoLengo kubwa la zoezi la SAM wilayani Mpwapwa, lilikuwa ni kuchangia katika kuboresha mifumo ya

utoaji wa huduma za afya. Hivyo, ni imani yetu kila mdau wa afya atakuwa chachu ya kuleta mabadiliko

chanya ya utoaji wa huduma za afya kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria, kwani uwajibikaji huanza

na mtu binafsi. Tunaamini mafunzo ya SAM yatasaidia kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma za afya

wilayani Mpwapwa.

3.1 Mapendekezo3.1.1 Kuimarisha usimamizi na kuboresha mfumo wa utunzaji wa taarifa Ni vyema menejimenti (CHMT) ikaboresha mfumo wa utunzaji wa taarifa muhimu (kieletroniki na

kawaida). Hii itarahisisha ofisi kuwa na taarifa zote muhimu za afya kwa muda wowote zitakapohitajika

kwa matumizi. Kuendelea kuimarisha usimamizi ili kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali na kuchukua

hatua kwa wakati kupitia usimamizi shirikishi na vyombo vya usimamizi katika ngazi zote.

3.1.2 Rasilimali watu katika afya Rasilimali watu katika Idara ya Afya ni miongoni mwa mahitaji ya muhimu sana katika kuboresha

mifumo ya utoaji wa huduma za afya. Hivyo, tunashauri Wizara iendelee kuweka mikakati endelevu ya

kuhakikisha idadi ya watoa huduma inaongezeka ili kuziba pengo la watumishi. Vilevile, zahanati zenye

watoa huduma mmoja mmoja ni vyema zipewe kipaumbele na Idara pindi watumishi wanapopatikana.

3.1.3 Majengo ya Afya, Miundombinu na mifumo mingineKuendelea kuboresha miundombinu na ujenzi wa majengo ya Afya hususani nyumba za watumishi

katika vituo vya kutolea huduma za afya ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele na usimamizi wa

karibu ili kuokoa rasilimali za afya.

3.1.4 Upatikanaji na utunzaji wa dawa na vifaa tibaKwa kuwa upatikanaji wa dawa umeanza kuimarika, ni vema Idara ya Afya ikaongeza jitihada katika

uhifadhi na utoaji wa elimu stahiki kwa wananchi juu ya uwepo wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya

kutolea huduma za afya ili wawe mawakili wazuri.

3.1.5 WananchiWananchi ndio msingi wa maendeleo ya jamii yoyote, hivyo basi, wanapaswa kuwajibikaji wao

wenyewe kwa kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya maendeleo ya jamii zao. Mathalan,

kushiriki kikamilifu katika mikutano ya jamii, kushiriki katika miradi ya maendeleo na kuelewa vyema

mifumo ya utoaji wa huduma ikiwemo mifumo ya afya. Ni muhimu zaidi kwa wananchi kutoa ushirikiano

kwa watoa huduma.

Page 27: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

19

3.2 Mpango Kazi wa PamojaTimu ya SAM na menejimenti (CHMT) kwa pamoja waliafikiana kufanya maboresho kwa kuanza na

maeneo yafuatayo.

NA MPANGO KAZI WA PAMOJA MHUSIKA1 Kushughulikia suala la mfumo wa mipango na bajeti (planrep) katika

utoaji wa ripoti ili changamoto za takwimu zilizojitokeza kutorudia tena katika mipango na utekelezaji wa taarifa zijazo

CHMT

Kushughulikia suala la utunzaji wa nyaraka mbalimbali hususani za Idara ya afya, kila ripoti zitokapo wajumbe muhimu wa CHMT watakuwa na nakala za mipango na bajeti, pia kuboresha eneo la utunzaji wa nyaraka

CHMT/ CMT

3. Kila mdau kukabidhiwa rasimu ya ripoti ya SAM na kuanza utekelezaji kama ilivyo bainishwa katika kila hoja

SIKIKA/ TIMU YA SAM

4 Vyombo vya usimamizi na uwajibikaji kupokea taarifa na masuala ya kimfumo kuingizwa katika vikao na kutolewa uamuzi ili kuboresha huduma za afya

CMT/ BARAZA LA MADIWANI

5 Timu ya SAM kufanya ufuatiliaji endelevu wa utekelezaji wa maazimio na mpango kazi wa pamoja na kutoa mrejesho kwa mamlaka husika na Jamii ili kuchukua hatua stahiki angalau mara moja kwa kila robo mwaka

SIKIKA & TIMU YA SAM

6 Halmashauri na wadau wote kutumia mfumo wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii, katika utendaji ili kukuza uwajibikaji kwa lengo la kuboresha huduma afya

CMT & WADAU WOTE

7 Menejimenti kufanyia kazi hoja zilizoibuliwa, maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na timu ya SAM katika kipindi cha mwaka mmoja

MENEJIMENTI YA HALMASHAURI

Page 28: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

20

ViambatanishoA. Orodha ya vituo na wajumbe wa timu ya SAM1. Orodha ya vituo vya kutolea huduma za afya vilivyotembelewa

Hospitali Vituo vya Afya ZahanatiHospitali ya Wilaya

Rudi Mazae Ng’ambi Chinyanghuku Mwanakianga

Kibakwe Lukole Chitemo Berege Mkanana

Mima Mkoleko Singonhali Inzomvu Mwenzele

Mbori Igoji-II Igoji-I Sazima

Iyenge Kisokwe Pwaga Mbuga

Wotta Wangi Mlunga Mlembule

Kizi Kidenge Chinyika Mgoma

Msagali Chunyu Kiegea Ikuyu

Lufu Luhundwa Ipera Kitati

Godegode Matonya Galigali Mafene

Kikuyu Iwondo Mlunduzi Seluka

Mtera Wiyenzele Chipogolo Kisima

Mtamba Mang’aliza Makose Winza

Chogola Malolo Nzugilo Idodoma

Gulwe Kiboriani Tambi

Timu ya SAM ilifanikiwa kutembelea jumla ya vituo 63 vya kutolea huduma za afya ambapo kati ya

hivyo 55 ni vituo vinavyofanya kazi na 8 ni vituo ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Taarifa zilikusanywa kutoka katika vituo 53 kati ya 55 vinavyofanya kazi. Taarifa hizo zilifanyiwa

uchambuzi na matokeo yake kutumika katika ripoti hii..

2. Majina ya wajumbe wa timu ya SAM

Jina Kundi la Uwakilishi KE ME1 Alfredina Rwezaula Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) KE

2 Amina A. Ramadhani Wananchi KE

3 Clemence J. Fugusa Watendaji ME

4 Fredrick Mazanda Watu wenye Ulemavu ME

5 Gabriel M. Mnyawami Kamati Ya Usimamizi Wa Kituo ME

6 Isaya R. Mgwazi Asasi Ya Kiraia ME

7 Mh. Ludo A. Boramungu Diwani ME

8 Mh. Rehema Vahaye Diwani KE

9 Milka P. Kaombwe Asasi Ya Kiraia KE

10 Nikoras P. Pama Wananchi ME

11 Ramadhani Mtinangi Mwenyekiti Wa Bodi ME

12 Robhi Kenyunko Timu Ya Uendeshaji Wa Shughuli Za Afya (Chmt) KE

13 Steveni P. Mbwani Wananchi /HFGC ME

14 Tabu N. Samila WAVIU KE

15 Witnesy J. Bwanza Wananchi/HFGC KE

Jumla 7 8

Page 29: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

21

B. Dodoso la uchambuzi na uhakiki vituoni

1. Tathimini ya Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya Ngazi ya WilayaTathimini ya Usimamizi wa Mipango

Na. Eneo la Tathimini

1 Mpango wa mwaka uliopita CCHP ulifuata mwongozo wa CCHP toleo Na. 4?

2 Bajeti kuu ya Idara ya Afya

3 Linganisha mtiririko wa gharama za matumizi kwa kila mtumiaji wa huduma ya Afya dhidi ya malengo ya kitaifa?

4 Kwa mwaka uliopita, hali ya uchangiaji katika mfuko wa CHF ilikuaje?

Tathimini ya Mtiririko wa Bajeti ya Dawa na Vifaa Tiba

Na. Eneo la Tathimini

1 Mtiririko wa Bajeti ya Dawa na Vifaa tiba kama ilivyoainishwa ndani ya CCHP

Tathimini ya Hali ya Upatikanaji wa Watumishi wa Afya

Na. Eneo la Tathimini

1 Kuna upungufu wowote kwa kila kada ambao umeainishwa ndani ya CCHP?

2 Kiasi gani cha fedha kimetengwa kupunguza upungufu huo? (Kwa kila kada na eneo)?

3 Mikakati ipi iliwekwa ili kupunguza masuala ya ukosefu wa maadili kazini? (Rushwa, utoro, wizi wa madawa n.k)?

Tathimini ya Hali ya Vyoo Safi na Salama

Na. Eneo la Tathimini

1 Kuna vyoo safi na salama katika vituo vya kutolea huduma za afya?

Tathimini ya Mgawanyo wa Bajeti na Matumizi Halisi

Na. Eneo la Tathimini

1 Kiasi gani cha bajeti kilipangwa kwa kila chanzo?

2 Kiasi gani kilipokelewa kwa kila chanzo?

3 Kiasi gani kilitumika kwa kila chanzo?

Tathimini ya Utendaji wa Vyombo vya Usimamizi

Na. Eneo la Tathimini

1 Madiwani walipokea ripoti ya CAG ya Halmashauri?

3 Je, kuna masuala ya ukaguzi ambayo hayakupatiwa ufumbuzi?

Page 30: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

22

Aina ya kituo Idadi ya vituo

Hospitali ya wilaya 1

Vituo vya Afya 3

Zahanati 49

Jumla 53

1 Tathimini ya Mpango Kazi wa Kituo 1.1 Hali ya uwepo wa mpango

1.2 Hali ya utoaji mafunzo ya uandaaji mpango

1.3 Mchakato wa uidhinishwaji mpango na kamati

2 Tathimini ya Upatikanaji wa Dawa Muhimu 2.1 Mwaka ……………….

2.2 Mwaka ……………….

3 Tathimini ya Utoaji wa Stahiki za Wafanyakazi wa Afya

3.1 Malipo ya muda wa ziada

3.2 Malipo ya motisha

3.3 Malipo ya likizo

3.4 Malipo ya sare za kazi

3.5 Malipo ya muda wa dharula

3.6 Posho ya kuwasilisha taarifa ngazi ya Wilaya (Kwa DMO)

4 Tathimini ya Hali ya Nyumba za Watumishi wa Afya 4.1 Hali ya Uwepo wa Nyumba

4.2 Nyumba ambazo hazina ubora kabisa

4.3 Nyumba ambazo zina ubora kiasi

4.4 Nyumba ambazo zina ubora wa wastani

4.5 Nyumba zenye hali nzuri

Tathimini ya Hali ya Ujenzi na Ukarabati Unaoen-delea

4.6 Vituo vinavyoendelea na ujenzi

4.7 Vituo vinavyoendelea na ukarabati

5 Tathimini ya Mbinu za Kubakiza Watumishi Wapya Kazini

5.1 Kutoa magodoro kwa watumishi

5.2 Kutoa vitanda kwa watumishi

5.3 Kutoa fedha za kujikimu

5.4 Kutoa motisha nyingine

2. Tathimini ya Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya Ngazi ya Vituo vya Kutolea Huduma

Page 31: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

23

6 Tathimini ya Hali ya Utoaji wa Huduma ya Mkoba

6.1 Hali ya utoaji wa huduma ya mkoba CTC/chanjo (2017/18 & 2018/19)

7 Tathimini ya Utoaji wa Mafunzo Kazini 7.1 Mafunzo ya CTC/PMTCT

7.2 Mafunzo ya MTUHA

7.3 Mafunzo kuhusu huduma za mama na mtoto

7.4 Mafunzo ya huduma za TB

7.5 Mafunzo kuhusu uingizwaji na utunzaji wa takwimu

8 Tathimini ya Uwepo wa Vifaa vya Mnyororo Baridi

8.1 Uwepo wa Jokofu

8.2 Uwepo wa Deli

9 Tathimini ya Uwepo wa Nishati 9.1 Uwepo wa mtungi wa gesi

9.2 Uwepo wa umeme wa sola

10 Tathimini ya Uwepo wa Vifaa Kinga vya Kuzuia Maambukuzi

10.1 Uwepo wa ndoo za kunawia mikono

10.2 Uwepo wa sabuni za maji

11 Tathimini ya Uwepo wa Vifaa vya Kujikinga na Maambukizi Watumishi

11.1 Uwepo wa “gloves” ngumu

11.2 Uwepo wa buti za kufanyia usafi

11.3 Uwepo wa ndoo za kutupia taka zenye rangi tofauti

11.4 Uwepo wa nguo kinga na maski

11.5 Uwepo wa “Chlorine”

Uwepo wa mifuko ya taka yenye rangi tofauti

Page 32: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

24

12 Tathimini ya Utoaji wa Rufaa kwa Wagonjwa 12.1 Hali ya utoaji wa rufaa kwa wagojwa

12.2 Uwepo wa gali la wagonjwa

13 Tathimini ya Uwepo wa Kichomea Taka na Shimo la Kutupia Kondo la Nyuma la Uzazi

13.1 Uwepo wa Kichomea taka

13.2 Uwepo wa shimo la kutupia kondo la nyuma la uzazi

14 Tathimini ya Uwepo wa Vifaa vya Kujifungulia 14.1 Uwepo wa vifaa vya kujifungulia

15 Tathimini ya Hali ya Mfumo wa Maji 15.1 Mfumo wa maji safi unaofanya kazi

15.2 Mifumo yenye hali mbaya

15.3 Mifumo yenye hali ya wastani

15.4 Mifumo yenye hali nzuri

15.5 Mifumo yenye hali nzuri sana

16 Tathimini ya Hali ya Vyoo Katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya

16.1 Uwepo wa vyoo safi na salama

16.2 Uwepo wa vyoo vilivyo zingatia makundi maalum

* Ujenzi wa nyumba, zahanati, chumba cha maabara/upasuaji kituoni

** Kuchinjiwa mbuzi/sherehe za mapokezi

*** Wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto

3. Tathimini ya Matumizi ya Mifumo ya Kutoa Maoni na kupokea Malalamiko Vituoni

Aina ya Mfumo Hali ya Utumiaji

Sanduku la maoni

Kamati ya Afya ya kituo

Mikutano ya jamii

Njia nyingine

NB: Njia nyingine: Fafanua

Page 33: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

25

4. Tathimni ya Hali ya Upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba

Vifaa Tiba Je kifaa kipo Je kifaa kinafanya kazi

Jokofu

Mashine za kupima BP

Vitakasa vifaa

CD4 counting Machine

Vitanda

Kabati za kuhifadhia dawa

Vifaa vingine

5. Tathimini ya Hali ya Uwepo wa Watumishi wa Afya kwa Kada 20 katika Vituo vya Kutolea Huduma za Afya

Kada Hospitali ya wilaya Kituo cha Afya Zahanati

Mahitaji waliopo Mahitaji waliopo Mahitaji Waliopo

Daktari

Daktari msaidizi

Tabibu

Tabibu Msaidizi

Afisa Muuguzi

Afisa Muuguzi Msaidizi

Muuguzi

Muhudumu wa Afya

Afisa Afya

Mtaalamu wa Dawa/Mfamasia

Mfamasia teknologia

Mteknologia msaidizi maabara

Mtaalamu wa Maabara

Afisa Lishe

Mteknologia vifaa tiba

Medical recorder

Katibu wa Afya

Dereva

Dobi

Page 34: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

26

Watumishi wengine

Page 35: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali
Page 36: Ripoti ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii (SAM) SAM... · 1.1 Dhana ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii SAM ni mbinu shirikishi ya ufuatiliaji na usimamizi wa rasilimali

Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali

Nyumba Na.69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa WaverleyS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa Kilimani S.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzTwitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika1