unasihi wa chakula na lishe kwa watu ...counsenuth-tz.org/sites/default/files/unasihi wa chakula...1...

39
COUNSENUTH Information series No. 10 Toleo la Kwanza, August, 2006 UNASIHI WA CHAKULA NA LISHE KWA WATU WANATUMIA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA UKIMWI Kitendea kazi kwa wanasihi na watoa huduma Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Upload: hoangdan

Post on 09-Mar-2018

543 views

Category:

Documents


21 download

TRANSCRIPT

COUNSENUTHInformation series No. 10Toleo la Kwanza, August, 2006

UNASIHI WA CHAKULA NALISHE KWA WATU WANATUMIADAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI

YA UKIMWI

Kitendea kazi kwa wanasihi na watoa huduma

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI

UNASIHI WA CHAKULA NA LISHE KWA WATUWANAOTUMIA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA

UGONJWA WA UKIMWI

Kitendea kazi kwa wanasihi na watoa huduma

ISBN 9987-8936-5-1

©COUNSENUTH, 2006

Kitabu hiki kimetayarishwa na:Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)

S. L. P 8218, Dar es Salaam, TanzaniaSimu/Faksi: +255 222 152 705

Barua pepe: [email protected]

Kimefadhiliwa na:Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE)

P. O. Box 1559Dar es Salaam, Tanzania

WahaririTuzie Edwin

Mary G. MateruDonald Naveta

Waliosimamia uboraProf. Joyce Kinabo (Sokoine University of Agriculture)Dr. Rowland Swai (National AIDS Control Program)

Agosti, 2006

Sehemu yeyote ya kitabu hiki inaweza kunakiliwa kwa ajili ya matumizi yasiyo ya kibiashara ilimradiionyeshwe kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye kitabu hiki kilichoandikwa na COUNSENUTH.

ii

YALIYOMO

Shukrani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . iii

Farahasa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . iv

1.0 Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1

2.0 Matumizi ya kitabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 2

3.0 Matayarisho ya kipindi cha unasihi kuhusu lishe na dawa za kupunguza makali ya

ugonjwa wa UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 4

4.0 Kutoa unasihi kwa mteja kuhusu mwingiliano kati ya chakula, lishe na dawa za

kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5

5.0 Kumsaidia mteja kutayarisha ratiba ya matumizi ya chakula na dawa . . . . . . . . . . . . . . 8

6.0 Kumsaidia mteja kufuatilia ulaji unaoshauriwa na ratiba ya dawa na chakula . . . . . . . . 11

7.0 Kumsaidia mteja kuwa na uzito unaofaa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12

8.0 Vidokezo vingine vya kumsaidia mteja anayetumia dawa za kupunguza

makali ya ugonjwa wa UKIMWI . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15

9.0 Kutoa unasihi wakati wa kumtembelea mteja nyumbani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17

10.0 Viambatanisho

Kiambatanisho Na. 1: Baadhi ya dawa na athari zinazoweza kujitokeza . . . . . . . . . . . . 19

Kiambatanisho Na. 2: Ushauri wa chakula kwa baadhi ya dawa . . . . . . . . . . . . . . . . . . 20

Kiambatanisho Na.3: Ushauri wa chakula kwa baadhi ya athari . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

Kiambatanisho Na. 4: Baadhi ya virutubishi, umuhimu, vyanzo na dalili za ukosefu . . . 23

Kiambatanisho Na. 5: Mlo kamili na makundi ya vyakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27

Kiambatanisho Na. 6: Mbinu za kuboresha chakula . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28

Kiambatanisho Na. 7: Baadhi ya vidokezo vya kuboresha lishe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29

Kiambatanisho Na 8: Mfano wa ratiba ya kula chakula na kumeza dawa . . . . . . . . . . . 30

11.0 Orodha ya vitabu vilivyotolewa na COUNSENUTH . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31

12.0 Bibliografia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 32

iii

SHUKRANICOUNSENUTH inatoa shukrani za dhati kwa Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE) kwaufadhili uliowezesha kitabu hiki kutayarishwa na kuchapishwa.

Shukrani za pekee kwa Taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwa namna moja au nyingine katika hatuambalimbali za utayarishaji wa kitabu hiki. Taasisi hizo ni pamoja na National AIDS ControlProgram (NACP) - MoH, Tanzania Network of Women Living Positive with HIV/AIDS (TNW+),Ilala Municipal Council, Muhimbili National Hospital (MNH), na Tanzania Food and NutritionCentre (TFNC).

Shukrani pia kwa uongozi na wafanyakazi wa vituo vilivyotumika katika kujaribu kitabu hiki nawatu binafsi ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika hatua mbalimbali zakutayarisha kitabu hiki. Vituo hivyo ni pamoja na MNH, Morogoro Regional Hospital na InfectiousDisease Centre (IDC)- Dar es Salaam.

COUNSENUTH inapenda kuwatambua wafuatao kwa mchango wao katika utayarishaji wa kitabuhiki:

1. Mary Materu (COUNSENUTH)

2. Tuzie Edwin (COUNSENUTH)

3. Emma Lekashingo (NACP - MoH)

4. Gelagista Gwarasa (Ilala Municipal Council)

5. Mwanahamisi Mhando (TNW+)

6. Belinda Liana (COUNSENUTH)

7. Merida Mtanda (Muhimbili National Hospital - CTC)

8. Julieth Shine (TFNC/COUNSENUTH)

9. Clara Mashio (COUNSENUTH)

10. Restituta Shirima (COUNSENUTH)

11. Dr. Lunna Kyungu (COUNSENUTH)

12. Toligwe Kaisi (Bagamoyo District Council)

Watu wengi wamechangia kwa namna mbalimbali katika kufanikisha utayarishaji wa kitabu hikihata hivyo si rahisi kumtaja kila mmoja wao. COUNSENUTH inatoa shukrani nyingi kwa wote nainawahakikishia kwamba inathamini sana mchango wao.

iv

FARAHASAAsusa - Kiasi kidogo cha chakula ambacho sio mlo kamili, kinachoweza kuliwa bila

matayarisho makubwa. Mara nyingi huliwa kati ya mlo mmoja na mwingine.

CTC - Vituo vinavyotoa huduma na matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI

ikiwa ni pamoja na dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI.

Kafeini - Kiini cha kikemia kilichoko kwenye vinywaji kama vile chai, kahawa na soda

ambacho huchangamsha mwili; lakini huweza kuathiri ufanisi wa baadhi ya

virutubishi mwilini.

Virutubishi- Viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo mwili hutumia kufanya kazi mbalimbali.

Nishati-lishe- Nguvu inayouwezesha mwili kufanya kazi mbalimbali.

Sibiko - Kuingiliwa na vimelea vya maradhi (contamination).

1

1.0 UTANGULIZI

Hali bora ya lishe ni muhimu sana kwa watu wote kwani husaidia kuboresha na kuimarisha kinga ya

mwili dhidi ya maradhi mbalimbali. Aidha kwa wale wanaoishi na virusi vya UKIMWI, hali bora ya

lishe husaidia kurefusha kipindi cha kuishi tangu kupata uambukizo wa virusi vya UKIMWI hadi

kuugua UKIMWI. Hali bora ya lishe pia huweza kupunguza makali ya magonjwa nyemelezi, husaidia

dawa kufanya kazi vizuri mwilini na huboresha hali ya maisha kwa ujumla.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa

mpango wa kutoa huduma na matibabu kwa watu wenye uambukizo wa virusi vya UKIMWI. Kama

sehemu ya huduma hiyo, dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zinatolewa kwa wale

ambao vipimo vimeonyesha kuwa wanahitaji kupewa dawa hizo.

Kitabu hiki kimetayarishwa ili kuwajengea uwezo wanasihi na watoa huduma ili waweze kutoa

maelekezo sahihi juu ya lishe na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI,

kwa lengo kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya

ugonjwa wa UKIMWI.

Kitabu hiki ni kitendea kazi kinachotoa maelezo ya hatua kwa hatua kwa mnasihi na mtoa huduma

ili kumsaidia kufanya unasihi kuhusu lishe na virusi vya UKIMWI kwa watu wanaotumia dawa za

kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI.

Kwa kutumia kitabu hiki wanasihi na watoa huduma wataweza kuwasaidia watu wanaotumia dawa

za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI:

v Kuelewa uhusiano wa lishe na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI

v Kutambua taratibu za kilishe katika:

• Kuongeza ufanisi wa matibabu

• Kuhakikisha utaratibu wa kutumia dawa na chakula unazingatiwa

• Kukabiliana na athari mbaya za dawa, na

• Kupunguza athari za dawa kwenye hali ya lishe ya mtumiaji

v Kuelewa kuhusu ulaji bora

11

2

MATUMIZI YA KITABU HIKI

Mlengwa wa kitabu hiki ni nani?

Mlengwa wa kitabu hiki ni mnasihi na mtoa huduma kwa watu wanaotumia dawa za kupunguzamakali ya ugonjwa wa UKIMWI. Kitabu hiki pia kinaweza kutumiwa na wafamasia katikakuwaelekeza wagonjwa namna ya kutumia dawa na chakula.

Wakati gani kitabu hiki kitumike?

Kitabu hiki kinaweza kutumika:

• Kumtayarisha mteja kwa ajili ya matibabu ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa waUKIMWI.

• Kutoa unasihi wa lishe kwa watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa waUKIMWI.

• Mteja anapokuja kwenye ufuatiliaji wa matibabu na maendeleo ya afya yake.

• Wakati mtoa huduma anapomtembelea mteja anayetumia dawa za kupunguza makali yaugonjwa wa UKIMWI nyumbani.

• Katika mafunzo ya wanasihi na watoa huduma kwa watu wanaotumia dawa za kupunguza makaliya ugonjwa wa UKIMWI.

Jinsi ya kutumia kitabu hiki

• Soma kitabu chote ili uweze kuelewa yaliyomo.

• Kabla ya kuanza unasihi, soma kwa uangalifu kipengele kinachomlenga mteja uliyenaye.Hakikisha una vitabu au vipeperushi na nyenzo nyingine zinazohitajika wakati wa unasihi.

• Tumia kitabu hiki wakati wa kipindi cha unasihi iwapo kitahitajika.

• Rejea kwenye kitabu ili kujadili kuhusu mwingiliano wa dawa na chakula na njia sahihi zakukabiliana na mwingiliano huo.

• Toa nakala ya kitabu kwa kila mshirikia iwapo kitahitajika wakati wa mafunzo ya watoa huduma.

22

3

Maelezo ya jumla kwa mtumiaji wa kitabu hiki• Toa ushauri maalumu kwa kila dawa. Kuna baadhi ya kanuni za jumla

zinazotumika kwenye mwingiliano wa chakula na dawa. Hata hivyo aina

tofauti za dawa zina mwingiliano tofauti na chakula. Ushauri utolewe baada ya

kuelewa wazi mahitaji maalumu ya dawa anayotumia mteja.

• Tafuta taarifa mpya na sahihi kuhusu dawa zinazotumika na mwingiliano

wake na chakula. Jumuisha katika unasihi taarifa mpya.

• Jifunze kutokana na uzoefu wa mteja wako kuhusu kinachofaa katika

kukabili athari za dawa ili kuwezesha dawa kufanya kazi kwa ufanisi. Ni

muhimu kujua kwamba kila mteja huweza kuwa na mapokeo au hisia tofauti.

• Mteja anapobadilisha dawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI,

mpe taarifa kuhusu mwingiliano unaoweza kutokea kati ya chakula na dawa

hiyo, athari za dawa na ushauri unaohitajika. Msaidie mteja katika kipindi

hicho cha mabadiliko pamoja na kutambua njia ambazo zitamuwezesha

kukidhi mahitaji yake kilishe.

• Pamoja na kumsaidia katika masuala ya lishe, mpe mteja rufaa kwa ajili ya

huduma za matibabu kila inapohitajika. Kwa mfano:

- Kama mteja ana athari zilizo mbaya au zinazoendelea.

- Kama mteja ana magonjwa nyemelezi.

- Kama dawa anayotumia mteja itashindwa kufanya kazi iliyokusudiwa.

• Unasihi umlenge mteja. Sikiliza kwa makini na kisha andika muhtasari wa

maelezo kutoka kwa mteja.

4

MATAYARISHO YA UNASIHI KUHUSULISHE NA DAWA ZA KUPUNGUZA

MAKALI YA UGONJWA WA UKIMWIKabla ya kuanza unasihi, hakikisha vifuatavyo vipo kwenye chumba au eneo la unasihi:

• Chati inayoonyesha ushauri kuhusu chakula na dawa za kupunguza makali ya ugonjwa waUKIMWI (angalia kiambatanisho na. 1).

• Chati inayoonyesha athari za dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zinazojitokezamara kwa mara (angalia kiambatanisho na. 2).

• Chati inayoonyesha ushauri wa chakula wa kukabiliana na athari zinazojitokeza mara kwa mara(angalia kiambatanisho na. 3).

Zingatia mwingiliano kati ya aina za dawa na chakula au virutubishi vyanyongeza

Tumia taarifa iliyotolewa na daktari, maelezo yaliyoambatanishwa na dawa, na vitabu vya rejea au

vipeperushi vyenye taarifa sahihi vinavyopatikana. Hakikisha una taarifa kuhusu:

• Aina ya dawa anayotumia mteja, na mwingiliano uliopo kati ya dawa hiyo na chakula.

• Vyakula, virutubishi vya nyongeza au taratibu za ulaji zinazotakiwa kubadilishwa,

kuongezwa, kupunguzwa au kuachwa.

• Athari za dawa ambazo zinaweza kuhitaji ushauri wa lishe.

• Aina nyingine za dawa anazotumia mteja ambazo si dawa za kupunguza makali ya ugonjwa

wa UKIMWI.

• Athari nyingine zozote zilizosababishwa na dawa anazotumia mteja.

33

5

UNASIHI KWA MTEJA KUHUSUMWINGILIANO KATI YA CHAKULA, LISHE

NA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YAUGONJWA WA UKIMWI

Kabla au wakati wa kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwawa UKIMWI1. Mueleze faida za lishe bora kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI ambaye anatumia dawa

za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI. Lishe bora:

(a) Huimarisha uwezo wa mwili kupambana na maradhi, hivyo huweza kupunguza magonjwanyemelezi na kuchelewesha kuugua UKIMWI.

(b) Husaidia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI kufanya kazi kwa ufanisizaidi mwilini.

(c) Husaidia kuboresha matibabu na kukabiliana na athari zitokanazo na matumizi ya dawa.

2. Mueleze namna virusi vya UKIMWI vinavyoathiri hali ya lishe ya mtu:

(a) Virusi vya UKIMWI huongeza matumizi na mahitaji ya nishati-lishe (nguvu) mwilini.

(b) Virusi vya UKIMWI husababisha magonjwa nyemelezi kama vile kutapika na kuharishaambayo mara nyingi husababisha chakula kisitumike vizuri mwilini na hivyo kusababishaongezeko la mahitaji ya chakula na virutubishi mwilini.

(c) Baadhi ya dawa zinazotumiwa na watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI zinaweza kuletaathari kama vile kichefuchefu, kukosa hamu ya kula au kutapika. Athari hizo huwezakupunguza ulaji wa chakula na hivyo kusababisha upungufu wa virutubishi mwilini yaaniutapiamlo.

3. Mueleze uwezekano wa mwingiliano kati ya chakula na dawa za kupunguza makali ya ugonjwawa UKIMWI.

(a) Baadhi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI huweza kuwa na atharizinazoweza kupunguza ulaji wa chakula, ufyonzwaji na utumikaji wa virutubishi mwilini napia huweza kuvuruga utaratibu wa kutumia dawa.

(b) Baadhi ya vyakula vikitumika na dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWIhuweza kupunguza ufanisi wa dawa na/au kuongeza athari za dawa.

(c) Kuchagua vyakula kwa makini, na kupanga utaratibu mzuri wa kutumia dawa na chakulakunaweza kupunguza athari za dawa na kuboresha ufanisi wake.

44

6

4. Mueleze mteja faida za kufahamu dawa anazotumia. Kufahamu dawa anazotumia husaidia:

(a) Kuhakikisha mteja anafuata utaratibu wa kumeza dawa na kufuata dozi inayoshauriwa.

(b) Kutambua mwingiliano unaoweza kutokea kati ya chakula na kila aina ya dawa.

(c) Kupanga utaratibu wa kutumia dawa na chakula ili kuongeza ufanisi wa dawa, nakupunguza athari zake.

5. Toa ushauri kuhusu chakula anachoweza kutumia kwa kuzingatia dawa anazotumia.

Ikumbukwe kuwa dawa zote zinahitaji:

(a) Kunywa maji mengi yaliyo safi na salama, angalau glasi 8 (lita 1.5) kwa siku.

(b) Kuepuka kutumia pombe.

(c) Kula mlo kamili (tumia kiambatanisho na. 4).

USHAURI MAALUMU WA CHAKULA KWA BAADHI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA UGONJWA WA UKIMWI

Stavudine: Haina masharti ya chakula hivyo inaweza kutumika na chakula au bila chakula.

Lamivudine: Haina masharti ya chakula hivyo inaweza kutumika na chakula au bila chakula.

Nevirapine: Haina masharti ya chakula hivyo inaweza kutumika na chakula au bila chakula.

Efavirenz: Inaweza kutumika na chakula au bila chakula. Iwapo itatumika na chakula,mteja apunguze kiasi cha mafuta kwenye mlo.

Zidovudine: Ni vyema imezwe wakati tumboni hakuna chakula, angalau saa moja kabla yamlo au saa mbili baada ya mlo. Endapo mteja atapata tatizo la kuumwa tumbo,dawa hii inaweza kumezwa na chakula. Iwapo itatumika na chakula, mtejaapunguze kiasi cha mafuta kwenye mlo.

Abacavir: Haina masharti ya chakula hivyo inaweza kutumika na chakula au bila chakula.

Didanosine: Inatakiwa kumezwa wakati tumboni hakuna chakula yaani saa moja kabla yakula au saa mbili baada ya kula kwani chakula hupunguza ufyonzwaji wake.Mteja asinywe pombe.

Lopinavir: Haina masharti ya chakula hivyo inaweza kutumika na chakula au bila chakula.

Nelfinavir: Inatakiwa kutumika pamoja na chakula au asusa. Vyakula au vinywaji vyenyeuchachu husababisha dawa hii kuwa chungu.

Ritonavir: Inapowezekana itumike pamoja na chakula.

Saquinavir: Inatakiwa kutumika pamoja na chakula au asusa. Ni vyema imezwe baada yakula chakula chenye mafuta au kalisiamu kwa wingi kama vile maziwa, dagaa nasoya. Mafuta na kalisiamu hufanya dawa hii ifyonzwe vizuri tumboni. Mtejaaepuke kutumia vitunguu saumu kwa wingi.

7

6. Sisitiza umuhimu wa kunywa maji safi na salama.

(a) Virusi vya UKIMWI huongeza hatari ya mtu kupata maambukizo mbalimbali. Kunywamaji safi na salama ni muhimu katika kuzuia maambukizo yanayosababishwa na vimeleavilivyoko kwenye maji.

(b) Dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zinahitaji kunywa maji mengi ilikupunguza athari. Kwa mfano, Indinavir inapotumika, mtu anapaswa kunywa maji safi nasalama angalu lita moja na nusu (glasi 8) kwa siku, ili kuepuka matatizo ambayo yanawezakuathiri viungo muhimu kama figo.

Ni vyema kutumia maji kumeza dawa na si vinywaji kama juisi, soda, chai,kahawa au maziwa

7. Mueleze mteja kuwa, utumiaji wa baadhi ya dawa unaweza kusababisha athari ambazo zinawezakuathiri ulaji wa chakula (angalia kiambatanisho na. 2). Baadhi ya athari hizo zinawezakukabiliwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za ulaji (tumia kiambatanisho na. 3).

8. Mueleze mteja umuhimu wa kumwambia mtaalamu wa afya dalili zinazojitokeza wakatianapotumia dawa. Baadhi, zinaweza kuwa ni dalili za magonjwa nyemelezi au matatizo mengineyanayohitaji matibabu.

9. Mtaarifu mteja kuwa inawezekana kutopata athari yoyote kati ya zilizotajwa katikakiambatanisho na. 2, kwani sio kila mtu hupata athari hizo. Kwa kawaida mtu akipata atharihizo huisha baada ya wiki 6, wakati mwili utakapozoea dawa hizo.

10. Mueleze kwamba athari nyingi za dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI huwezakupunguza ulaji wa chakula na utumikaji wake mwilini. Hii huweza kudhoofisha hali ya lishe yamtu.

11. Mueleze pia kwamba, kwa baadhi ya wateja wanaotumia dawa hizo, hamu yao ya kulahuongezeka na hivyo huweza kusababisha kuongeza ulaji wa chakula na kuongezeka uzito wamwili. Ongezeko hilo la uzito linaweza kuhitajika au kutohitajika kutegemeana na uzito wamwili wa mteja.

12. Jadili njia rahisi za ulaji zinazoweza kutumika ili kuepuka au kukabiliana na baadhi ya dalili naathari zinazojitokeza mara nyingi. Kwa mfano kula chakula kidogo na mara kwa mara wakatianapokua na kichefuchfu au kutapika.

13. Mueleze mteja kwamba inawezekana sio dalili zote atakazozipata zinasababishwa na dawaanazotumia:

(a) Kuwepo kwa baadhi ya dalili kunaweza kusababishwa na uambukizo wa virusi vyaUKIMWI au magonjwa nyemelezi. Pamoja na ushauri wa chakula na lishe, huduma yamatibabu itafutwe mapema.

(b) Ushauri wa chakula katika kukabili dalili hizo si kwa ajili ya kuponyesha; bali husaidiakupunguza ukali wa tatizo.

8

KUMSAIDIA MTEJA KUTAYARISHARATIBA YA MATUMIZI YA CHAKULA NA

DAWA

Kabla au wakati wa kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwawa UKIMWI1. Chunguza ulaji wa mteja, kwa kudodosa yafuatayo:

(a) Watu wanaohusika kufanya maamuzi kuhusu vyakula anavyokula na utayarishaji wakeikiwa ni pamoja na mnunuzi na mpishi.

(b) Vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika eneo lake na anavyotumia zaidi.

(c) Aina ya vyakula na vinywaji katika mlo na jinsi vinavyotayarishwa.

(d) Milo, vinywaji na asusa (vitafunwa) alizotumia katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

(e) Vyakula na vinywaji anavyopendelea, asivyopendelea, vyenye miiko na sababu zake.

(f) Virutubishi vya nyongeza anavyotumia.

(g) Namna vyakula (vilivyopikwa au freshi) vinavyohifadhiwa kwa mfano matumizi ya jokofu.

(h) Aina ya nishati inayotumika kupikia kwa mfano kuni, mkaa, gesi au umeme.

(i) Masuala mengine ambayo mteja ataeleza.

2. Jadiliana na mteja ili kufahamu tabia za ulaji ambazo zinaweza kuendelezwa au kuboreshwa ilikumsaidia kuwa na lishe bora, kufuata maelekezo ya kutumia dawa na kupunguza athari zake.Jadili namna ya kukabili mwingiliano kati ya dawa na chakula ambao utakuwa na madhara kwakuzingatia uchaguzi wa vyakula mbalimbali, utayarishaji na muda wa kula chakula.

3. Mfahamishe mteja vyakula anavyotakiwa kuepuka au kuongeza kwa kuzingatia aina za dawaanazotumia. Sisitiza matumizi ya vyakula vinavyopatikana katika mazingira ya mteja.

4. Jedwali na. 1 linaonyesha baadhi ya vyakula vinavyoshauriwa kuepukwa wakati wa kutumiadawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI.

55

9

Jedwali na. 1: Baadhi ya vyakula ambavyo, mtu anayetumia dawa za kupunguzamakali ya ugonjwa wa UKIMWI anashauriwa kuviepuka

5. Jadiliana na mteja vikwazo anavyokutana navyo katika kupata chakula au kufuata ulajiunaoshauriwa kwa kuzingatia aina ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWIanazotumia. Angalia vigezo vifuatavyo:

• Kipato

• Mabadiliko katika msimu

• Mgawanyo wa chakula katika kaya

• Maamuzi kuhusu uchaguzi wa vyakula na utayarishaji

• Kupungua kwa uwezo wa kula chakula kutokana na maambukizo mbalimbali

• Kupungua kwa uwezo wa kutayarisha chakula kutokana na maambukizo mbalimbali

• Ufahamu kuhusu mahitaji ya kilishe kama vile milo ya kutosha na inayofaa

10

• Sababu za kisaikolojia kama mfadhaiko au wasiwasi

• Miiko, mila na desturi zinazohusiana na ulaji wa vyakula

• Unyanyapaa

• Ugomvi, vita, vurugu ndani ya nyumba au sababu nyingine za kimazingira

• Vikwazo vingine mteja anavyokumbana navyo

6. Baada ya kujadili, msaidie kutambua njia zitakazomuwezesha kupata chakula anachohitaji na piakutambua ulaji unaowezekana na unaokidhi mahitaji ya dawa anazotumia:

(a) Jadili na mteja njia zinazowezekana kukabiliana na vikwazo vilivyotambuliwa hapo awali.

(b) Jadili vyakula mbadala na mabadiliko ya tabia ambayo yanaweza kufanywa na mtu binafsiau katika ngazi ya kaya, ili kukidhi mahitaji ya chakula yanayotakiwa wakati wa kutumiadawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI.

(c) Mfahamishe kuhusu huduma zilizopo zinazoweza kumsaidia kuboresha lishe yake. Mperufaa kila inapohitajika.

Kulingana na hali ya mteja, mfahamishe na muunganishe na hudumanyingine kama vile programu za msaada wa chakula, programu za kuongezakipato, huduma za kuboresha maisha, huduma za unasihi na makundi rika

ya kusaidiana

7. Tambua na jadili pamoja na mteja umuhimu wa kubadili taratibu za ulaji kila inapobidi, ilikuongeza ufanisi wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI. Kwa mfano:

(a) Kuongeza idadi ya milo kama kula asusa (vitafunwa), kati ya mlo na mlo. Msaidie mtejakufahamu asusa zilizo bora kilishe.

(b) Kuzingatia muda wa kula chakula na kumeza dawa.

(c) Kurekebisha utayarishaji wa chakula kama vile kupunguza kiasi cha mafuta paleinapohitajika.

8. Msaidie mteja kupanga ratiba ya muda wa kula chakula na kumeza dawa.

(a) Tengeneza mpangilio wa kula chakula na kumeza dawa wa kila siku. Mpangilio huounatakiwa kuonyesha aina ya dawa, vyakula na muda wa kutumia (tumia kiambatanishona. 8 kama mfano).

(b) Jadili na mteja namna ya kufuata ratiba na kuidumisha.

(c) Ni vyema kumshauri mteja kuteua mwanafamilia ambaye ataweza kuhusishwa katikautayarishaji wa ratiba ya chakula na dawa pamoja na kufuatilia ratiba hiyo nyumbani.

9. Ruhusu muda wa kujadili maswali au masuala yoyote kutoka kwa mteja.

11

KUMSAIDIA MTEJA KUFUATARATIBA YA CHAKULA NA DAWA

1. Dodosa namna mteja anavyofuata maelekezo ya utumiaji wa dawa na ulaji wa chakulaunaoshauriwa.

(a) Muulize mteja muda anaomeza dawa na kula chakula. Tathmini kama mteja anafuataratiba ya kumeza dawa na kula chakula. Muelekeze iwapo atahitajika kufanya hivyo (tumiakiambatanisho na. 8 kama mfano).

(b) Rejea maelezo ya mwingiliano kati ya chakula na dawa na toa ushauri unaohitajika.

(c) Mpe mteja muda wa kujadili matatizo yoyote yaliyojitokeza au masuala mengineyanayomhusu.

(d) Kumbuka kwamba athari za dawa hutofautiana kati ya mteja mmoja na mwingine.

2. Mpe mteja muda wa kueleza matatizo aliyokumbana nayo katika kufuata ushauri wa chakulaikiwa ni pamoja na ushauri wa chakula ambao haujaonyesha mafanikio. Kama itahitajika,jadiliana na mteja vyakula mbadala kwa ushauri wowote ambao mteja ameshindwa kuufuata.

3. Uliza kuhusu dalili au athari zozote zilizojitokeza, hatua zilizochukuliwa na matokeo yake.

(a) Muulize mteja hatua alizochukua ili kukabiliana na athari hizo. Kama itakavyohitajika,shauri ulaji wa chakula kwa kutumia kiambatanisho na. 3.

(b) Tathmini kama athari za dawa zimechangia kwa namna yoyote mteja kushindwa kufuatamaelekezo ya kutumia dawa.

(c) Uliza iwapo mteja alipata matibabu kwa ajili ya athari yoyote ya dawa. Kama hapana naathari hizo zinaendelea, mshauri mteja kupata ushauri wa daktari.

4. Tathmini iwapo dalili au athari zilizojitokeza zimesababishwa na magonjwa nyemelezi na siathari za dawa kwa mfano kuharisha kunakoendelea kwa muda mrefu.

(a) Kama ndivyo, mpe rufaa mteja kwa uchunguzi wa afya na matibabu.

(b) Mshauri mteja kuendelea kukabiliana na athari hizo kwa kufuata ulaji unaoshauriwa nakupata matibabu.

5. Sisitiza umuhimu wa kufuata maelekezo ya utumiaji wa dawa kwa usahihi, pamoja na ulajiunaoshauriwa. Hata kama mteja atakuwa anajisikia kuwa na afya nzuri, ni muhimu kuendeleana utaratibu wa matibabu.

6. Ruhusu muda wa kujadili maswali au masuala yoyote kutoka kwa mteja.

66

12

KUMSAIDIA MTEJA KUWA NA UZITOUNAOFAA

Kabla au wakati mteja anaanza kutumia dawa za kupunguza makali yaugonjwa wa UKIMWI au wakati wa ufuatiliaji1. Pima uzito wa mteja kwa kutumia mzani uliosahihi.

(a) Linganisha uzito wake wa sasa na uzito wa mara ya mwisho alipopima.

(b) Wateja wenye uzito pungufu, wanaopungua uzito bila kukusudia, ambao wanatakakuongezeka uzito rejea kipengele na. 2 hadi 8 hapo chini.

(c) Wateja wenye uzito uliozidi na ambao wanaongezeka uzito bila kukusudia, rejea kipengelena. 9 hapo chini.

2. Endapo mteja anapungua uzito bila ya kukusudia au haongezeki uzito, muulize chakulaanachokula kila siku. Chunguza kama mteja anatumia vyakula vinavyoupa mwili nishati-lishe(nguvu) kwa kiasi cha kutosha [tumia kiambatanisho na. 4: kipengele cha (a) na (c)].

Vidokezo vya jumla vinavyoashiria kuwa mteja anapata chakula cha kutosha:

(i) Ulaji wa angalau milo mitatu kwa siku.

(ii) Ulaji wa milo iliyo na aina mbalimbali za vyakula. Hii inajumuisha vyakula kama vilevinavyoupa mwili nishati-lishe (vyakula vya nafaka, mizizi, ndizi, mafuta na sukari),vyakula vinavyojenga mwili (vyakula vya jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyama),vyakula vinavyolinda mwili (matunda na mboga-mboga), maji na juisi halisi kwa wingi(tumia kiambatanisho na. 5).

(iii) Ulaji wa asusa (vitafunwa) kati ya milo hususan zenye nishati-lishe kwa wingi.

(iv) Kiasi cha chakula kinacholiwa.

Pambanua hilo kwa kulinganisha ulaji wa sasa na uliotangulia kwa kuzingatia kiasi, aina za vyakulana idadi ya milo au asusa katika siku.

Wateja ambao hawana dalili za UKIMWI (asymptomatic) wanahitajinishati-lishe kwa asilimia 10 zaidi ya kiasi cha nishati-lishe kinachohitajika

kwa watu wasio na VVU wenye umri na jinsi sawa, na wenye shughulizinazofanana. Wateja wenye dalili za UKIMWI (symptomatic) wanahitaji

nishati-lishe kwa asilimia 20 hadi 30 zaidi ya kiasi kinachohitajika kwa watuwasio na VVU wenye umri na jinsi sawa, na wenye shughuli zinazofanana.

77

13

3. Iwapo ulaji wa vyakula vyenye nishati-lishe hautoshelezi mahitaji, chunguza:

(a) Iwapo hali hiyo imesababishwa na athari za dawa kama vile kichefuchefu na kukosa hamuya kula, jadiliana na mteja kama ushauri wa chakula unaweza kusadia kukabiliana na atharihizo (rejea kiambatanisho na. 3). Endapo itahitajika, boresha ratiba ya chakula na dawa ilikuongeza ulaji wa chakula.

(b) Iwapo ushauri wa chakula wa kukabiliana na athari za dawa haukumsaidia mteja na atharihizo zinaendelea, mpe mteja rufaa ya kumuona daktari.

(c) Iwapo athari zitokanazo na matumizi ya dawa sio tatizo, na chakula katika kayakinapatikana, ila ulaji wa chakula hautoshelezi, toa unasihi kuhusu:

(i) Kuongeza kiasi cha chakula kinacholiwa.

(ii) Kuongeza idadi ya milo na asusa ili ifikie angalau milo kamili mitatu na asusa angalaumara mbili kwa siku.

(iii) Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye nishati-lishe (nguvu) kwa wingi.

(iv) Namna ya kuboresha chakula kwa kutumia njia mbalimbali (tumia kiambatanishona. 6).

(v) Vyakula ambavyo mteja anapendelea, vinavyopatikana na anavyoweza kumudugharama yake (tumia kiambatanisho na. 5).

(vi) Kuboresha ratiba ya chakula na kumeza dawa ili kuongeza kiasi cha chakulakinacholiwa kama itahitajika.

(d) Endapo mteja hawezi kupata chakula cha kutosha, msaidie kutambua njia mbadala zakuongeza upatikanaji wa chakula (angalia mada ya 5: kipengele cha 5 na 6). Inaweza kuwani muhimu kumuunganisha mteja na programu zinazotoa msaada wa chakula, mahitaji nahuduma nyingine.

4. Endapo mteja anapata chakula cha kutosha na anafuata maelekezo na ratiba ya kutumia dawakwa usahihi, lakini uzito wake bado ni mdogo, chunguza uwezekano wa athari za dawa,magonjwa nyemelezi au maradhi mengine ambayo huweza kuathiri ufyonzwaji wa virutubishi aumatumizi ya virutubishi mwilini.

(a) Kama kuna athari zitokanazo na dawa, magonjwa nyemelezi au maradhi mengine, toaunasihi kuhusu namna ya kukabiliana na hali hizo kilishe (tumia kiambatanisho na. 3) natoa rufaa ya kumuona daktari.

(b) Kama hakuna magonjwa nyemelezi au maradhi mengine na sababu za kupungua uzitohazijulikani, toa rufaa ya kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

5. Iwapo ulaji wa chakula unakadiriwa kutosheleza na hakuna magonjwa nyemelezi au athari zadawa zinazoweza kuathiri ufyonzwaji wa virutubishi, inawezekana kupungua uzitokumesababishwa na mabadiliko katika umetaboli au matatizo mengine. Katika hali hiyo mpemteja rufaa ya kumuona daktari. Kumbuka kumpa pia maelezo kuhusu kula chakula chenyemchanganyiko wa vyakula mbalimbali na cha kutosha (tumia kiambatanisho na. 5).

14

6. Toa unasihi kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi (mara 3 hadi 4 kwa wiki) kila inapowezekana.Kufanya mazoezi husaidia katika kujenga misuli na kuupa mwili nguvu. Iwapo mteja anapataugumu wa kufanya mazoezi, mpe rufaa ya kumuona mtaalamu wa tiba maungo (physiotherapist)kama anapatikana.

7. Iwapo uboreshaji wa mlo baada ya unasihi haujafanikiwa kumuongezea mteja uzito, mpe rufaaya kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.

8. Vigezo mbalimbali vitumike katika kutathmini hali ya lishe ya mteja. Kigezo kimojawapo nikutumia uwiano wa uzito na urefu {Body Mass Index (BMI)} ambapo BMI ikiwa chini ya 18.5inaashiria hali duni ya lishe (tumia kiambatanisho na. 9). Kigezo kingine ni kuchunguza iwapomteja amepungua uzito mwingi katika kipindi cha muda mfupi (kilo 6 hadi 7 katika kipindi chamwezi mmoja) bila kukusudia. Iwapo mteja ana utapiamlo mkali, mpe rufaa kwa matibabu zaidi.

9. Kwa wateja wenye unene uliozidi na wale wanaoongezeka uzito bila ya kukusudia:

(a) Muulize mteja kuhusu ulaji wa chakula wa kila siku. Kama mteja anakula vyakula vyenyemafuta na/au vyakula vingine vyenye nishati-lishe kwa wingi kuliko inavyoshauriwa,msadie mteja kutambua njia za kupunguza matumizi ya vyakula vyenye mafuta na nishati-lishe kwa wingi, hususan vile ambavyo havina virutubishi vingine kwa wingi.

(b) Mhimize mteja kula vyakula vya aina mbalimbali, hasa mboga-mboga na matunda.

(c) Mhimize mteja kufanya mazoezi mara kwa mara kama kutembea na kufanya shughulizinazotumia viungo vya mwili kama vile kazi za nyumbani.

(d) Iwapo ongezeko la uzito limetokana na mabadiliko ya mfumo mzima wa shughuli za mwili(umetaboli); kwa mfano uzito umeongezeka kwa haraka licha ya mabadiliko kidogokwenye ulaji, mpe mteja rufaa ya kumuona daktari kwa uchunguzi na matibabu.

10. Ruhusu muda wa kujadili maswali, au masuala yoyote kutoka kwa mteja.

15

UNASIHI WAKATI WA KUMTEMBELEAMTEJA NYUMBANI

Wakati mteja anaanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa waUKIMWI au wakati wa ufuatiliaji wa mteja ambaye anatumia dawa1. Hakikisha umejiandaa vyema kwa somo ulilopanga kujadili wakati wa kumtembelea mteja

nyumbani.

2. Chunguza na dodosa hali zilizopo katika kaya ambazo huweza kuathiri ulaji wa chakula nautumiaji wa dawa kwa kutumia vigezo vifuatavyo:(a) Hali ya usafi(b) Uzalishaji au upatikanaji wa chakula(c) Uhifadhi wa chakula(d) Chanzo na kiwango cha kipato(e) Ufahamu wa wanakaya kuhusu masuala ya chakula(f) Utayarishaji wa chakula(g) Nani anatayarisha chakula(h) Nani anafanya maamuzi yanayohusu chakula(i) Mgawanyo wa chakula katika kaya (j) Masuala ya unyanyapaa(k) Masuala ya kisaikolojia na kijamii

3. Jadili na wanakaya umuhimu wa lishe bora na mahitaji maalum ya chakula na lishe kwa mteja.Jadiliana nao pia aina mbalimbali za vyakula ambazo zitamsaidia mteja kuboresha afya nakuongeza ufanisi wa matibabu (tumia kiambatanisho na. 5).

4. Endapo kuna hali ambazo zinazuia mteja kufuata utaratibu wa kutumia dawa na chakulaunaoshauriwa, jadiliana na mteja pamoja na wanakaya ili kutambua mbinu za kukabiliana nahali hizo. Kwa mfano:

(a) Iwapo kufuata ratiba ya chakula ni tatizo jadili na wanakaya kuhusu njia zitakazowezeshakufuata ratiba hiyo.

(b) Iwapo hali ya usafi wa mteja, chakula chake na maji si ya kuridhisha, pendekeza njia zakuboresha usafi kama vile usafi wakati wa kutayarisha chakula, usafi na usalama wa maji yakunywa, usafi binafsi wa mteja na watayarishaji wa chakula.

(c) Iwapo kuna ugumu katika upatikanaji wa vyakula vinavyohitajika, jadiliana nao kuhusukuanzisha bustani ndogondogo pale inapowezekana au vyanzo vingine vya uzalishaji wachakula cha ziada.

88

16

(d) Iwapo kipato duni ndicho kinachosababisha kaya kutopata chakula cha kutosha, kamainawezekana mshauri mteja kwenda kwenye huduma za msaada wa chakula kama zipo nakujiunga na shughuli za kuinua kipato.

(e) Endapo unyanyapaa ndani ya kaya unaathiri hamu ya kula au mgawanyo wa chakula kwamteja, toa unasihi kupunguza unyanyapaa. Sisitiza wajibu wa wanakaya katika kumsaidiamteja wako. Pendekeza kuwa kula pamoja na wanakaya wengine kunaweza kusaidiakuongeza hamu ya kula ya mteja.

5. Kwa kupitia majadiliano na mteja pamoja na wanakaya, pendekeza njia zinazoweza kuboreshamlo wa mteja ili kukabiliana na mwingiliano wa chakula na dawa iwapo itahitajika.

(a) Washirikishe wanakaya taarifa kuhusu mahitaji ya chakula na utumiaji wa dawa kwa mteja.

(b) Wanakaya wengine wanaweza kuwa na wajibu muhimu katika kumsaidia mteja. Kwamfano, mwanakaya (ikiwa ni pamoja na mtoto mkubwa) anaweza kuchukua wajibu wakuhakikisha mteja anafuata kwa usahihi maelekezo ya kutumia chakula na dawa.

(c) Jadili njia kama vile:

i) Kurekebisha muda wa kula chakula kwa kufuata muda wa kumeza dawa na kuruhusumteja kula milo mara kwa mara.

ii) Kubadili utayarishaji wa chakula iwapo itahitajika ili kuandaa milo ambayo inafaa narahisi kuyeyushwa.

iii) Kutumia rasilimali zilizopo katika kaya kwa ajili ya chakula ili kukidhi mahitaji yakilishe ya mteja.

6. Ruhusu muda wa kujadili maswali au masuala yoyote kutoka kwa mteja au wanakaya wengine.

17

VIDOKEZO VINGINE MUHIMU WAKATIWA UFUATILIAJI

Wakati wa ufuatiliaji wa mteja anayetumia dawa za kupunguza makali yaugonjwa wa UKIMWIWakati mteja anatumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI, sehemu mbalimbali zamwili huweza kuathirika kutokana na matumizi ya dawa hizo. Inashauriwa kufanya vipimombalimbali pale inapowezekana ili kuweza kugundua iwapo kuna tatizo lolote lililojitokeza na hivyokuchukua hatua zinazohitajika.

1. Pale itakapohitajika, mpe mteja rufaa ya kumuona daktari ili kupima athari za dawa zakupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zinazohusiana na lishe.

a) Endapo anatumia Zidovudine au Lamivudine, atahitajika kupima kiasi cha wekundu wadamu (Hb)

b) Mteja anayetumia Efavirenz au dawa ambazo ni protease inhibitors anaweza kuhitaji kupimakiasi cha mafuta (cholesterol & triglycerides) kwenye damu pale inapowezekana.

c) Mteja anayetumia Stavudine au Zidovudine anaweza kuhitaji kupima afya ya mifupa paleinapowezekana.

d) Kwa mteja anayetumia aina nyingine za dawa za kupunguza makali ya ugonjwa waUKIMWI, tumia kiambatanisho na. 2 na ushauri wa daktari kutambua madhara mengineambayo yatahitaji vipimo.

2. Endapo mteja ana upungufu wa damu, chunguza iwapo upungufu huo unahusiana na ulaji duniwa vyakula vyenye madini ya chuma au ulaji wa vyakula vinavyozuia ufyonzwaji wa madini yachuma kama kunywa chai au kahawa wakati wa mlo.

a) Kama ulaji wa mlo wenye upungufu wa madini ya chuma unaweza kuwa ni sababu yaupungufu wa damu:

i) Mshauri mteja kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama maini, nyama,samaki, kuku, mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi kama vile matembele,mchicha na spinachi, na matunda yenye vitamini C kwa wingi kama mapera,machungwa, maembe, ukwaju, na ubuyu.

ii) Mshauri mteja kutumia virutubishi vya nyongeza vya madini ya chuma na vitaminiya foleti kama atakavyoshauriwa na mtaalamu wa afya.

b) Iwapo mlo una madini ya chuma ya kutosha, mpe mteja rufaa ya kumuona daktari kwauchunguzi zaidi. Baadhi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI zinawezakusababisha upungufu wa damu kutokana na matatizo mengine zaidi ya ufyonzwaji duni wavirutubishi au upungufu wa virutubishi mwilini.

99

18

c) Ni muhimu kutibu mapema malaria na minyoo kwani pia husababisha upungufu wawekundu wa damu mwilini.

Jedwali lifuatalo linaonyesha viwango cha wekundu wa damu (haemoglobin)vinavyoashiria upungufu wa damu

Jedwali na. 2: Kiwango cha wekundu wa damu (haemoglobin) kinachoashiria upungufu wadamu

Kundi la watu Kiwango cha haemoglobin chini ya:

Watoto kati ya miezi sita na miaka 5 11.0g/dl

Watoto kati ya miaka 5 na miaka 11 11.5g/dl

Watoto kati ya miaka 12 na 14 12.0g/dl

Wanawake wajawazito 11.0g/dl

Wanawake wasio wajawazito zaidi ya miaka 15 12.0g/dl

Wanaume watu wazima zaidi ya miaka 15 13.0 g/dl

Chanzo: WHO, 2003

3. Endapo mteja ana kiasi kikubwa cha mafuta kwenye damu:a) Chunguza kuhusu ulaji wa mafuta:

i) Chunguza iwapo mteja anapata nishati-lishe (nguvu) ya kutosha.ii) Kama mteja anapata nishati-lishe ya kutosha, na anaweza kupata nishati ya kutosha

kutoka kwenye vyakula ambavyo havina mafuta mengi hasa yatokanayo na wanyamakama siagi, samli, jibini, kiini cha yai au nyama yenye mafuta. Mshauri pia apunguzevyakula vilivyopikwa kwa kutumbukizwa kwenye mafuta kama chipsi, sambusa,kababu, maandazi, au vilivyoongezwa mafuta mengi kama vitumbua na chapati.

b) Mshauri mteja kufanya mazoezi mara kwa mara ambayo anaweza kumudu kulingana na haliyake ya afya na mazingira anayoishi. Ni muhimu pia kupata hewa safi ili kusaidia mfumowa hewa kufanya kazi vizuri.

c) Kama ushauri wa chakula na mazoezi hautaweza kupunguza kiasi cha mafuta kwenye damu,mpe rufaa ya kumuona daktari. Mteja anaweza kuhitaji ushauri wa kutumia dawa zakupunguza mafuta au kubadili aina ya dawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI

4. Kama mteja anapata mabadiliko ya umbile la mwili, kama kupoteza mafuta katika sehemuyoyote ya mwili zaidi ya tumbo, kuongezeka ukubwa wa matiti, au kuwepo kwa mgawanyiko wamafuta katikati ya mabega (buffalo humps):

a) Toa unasihi kwa mteja kuhusu uwezekano wa kutopata tiba ya hali hiyo.

b) Mhimize mteja kufanya mazoezi.

c) Mpe mteja rufaa ya kumuona daktari.

5. Ruhusu muda wa kujadili maswali au masuala yoyote kutoka kwa mteja.

19

VIAMBATANISHOKiambatanisho na.1: BAADHI YA DAWA ZA KUPUNGUZA

MAKALI YA UGONJWA WA UKIMWINA USHAURI WA CHAKULA1010

20

Kiambatanisho na. 2: BAADHI YA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA

UGONJWA WA UKIMWI NA ATHARI ZINAZOWEZA KUJITOKEZA

21

Kiambatanisho na. 3: BAADHI YA ATHARI NA USHAURI WACHAKULA

22

23

Kiambatanisho na. 4: BAADHI YA VIRUTUBISHI, UMUHIMU,VYANZO VYAKE NA DALILI ZA UKOSEFU

24

25

32 27

Kiambatanisho na. 5: MLO KAMILI NA MAKUNDI YA VYAKULAMlo kamili ni ule uliotayarishwa kutokana na vyakula mchanganyiko kutoka katika makundimbalimbali. Mlo huo unatakiwa kuwa na angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi lavyakula. Ni muhimu kula angalau milo mitatu iliyo kamili kila siku.

Umuhimu wa mlo kamili• Huwezesha mwili kupata virutubishi vyote vinavyohitajika.• Huboresha kinga ya mwili dhidi ya maradhi mbalimbali.• Huupa mwili nguvu za kufanya shughuli mbalimbali.• Huuwezesha mwili kutumia virutubishi mbalimbali

Makundi vya vyakulaVyakula vya nafaka, mizizi na ndiziVyakula hivi ndivyo vinavyochukua sehemu kubwa ya mlo na kwa kawaida ndiyo vyakula vikuu.Vyakula katika kundi hili ni pamoja na mahindi, mchele, mtama, ulezi, ngano, uwele, viazi vikuu,viazi vitamu, mihogo, magimbi, viazi mviringo na ndizi.

Vyakula vya jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyamaVyakula vilivyoko katika kundi hili ni pamoja na maharagwe, njegere, kunde, karanga, soya, njugumawe, dengu, choroko, mbaazi na fiwi. Vile vyenye asili ya wanyama ni pamoja na nyama, samaki,dagaa, maziwa, mayai, jibini, maini, figo, senene, nzige, kumbikumbi na wadudu wenginewanaoliwa.

Mboga-mbogaKundi hili linajumuisha aina zote za mboga-mboga zinazolimwa na zinazoota zenyewe. Mboga-mboga ni pamoja na mchicha, majani ya maboga, kisamvu, majani ya kunde, matembele, spinachi,mnafu, mlonge, mgagani, mlenda, mchunga, pia aina nyingine za mboga kama karoti, pilipili hoho,biringanya, matango, maboga, nyanya chungu na bamia, bitiruti, kabichi na figiri.

MatundaKundi hili linajumuisha matunda ya aina zote kama papai, embe, pera, limau, pesheni, nanasi, peasi,chungwa, chenza, zambarau, fenesi, stafeli, ndizi mbivu, pichesi, topetope, parachichi n.k. Vilevile“matunda pori” kama ubuyu, ukwaju, embe ng’ong’o, mikoche, mavilu, n.k.

Mafuta Mafuta ni muhimu ingawa yanahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. Mafuta yanaweza kupatikanakutoka kwenye mimea kama mbegu za alizeti, ufuta, karanga, mawese, mbegu za pamba, kweme, n.kna kutoka kwa wanyama kama siagi, samli na nyama ya mafuta, samaki wenye mafuta mengi kamasato, sangara, n.k.

SukariSukari ni muhimu lakini inahitajika kwa kiasi kidogo mwilini. Sukari inaupa mwili nishati-

lishe tu bila virutubishi vingine muhimu. Sukari pia huongeza ladha ya chakula na hivyohuongeza hamu ya kula. Vyakula vyenye sukari nyingi ni pamoja na miwa, asali, sukari,

kashata na jamu.

MajiMaji kwa kawaida hayahesabiwi kama kundi la chakula, lakini yana umuhimu mkubwa

katika afya na lishe ya binadamu. Inapaswa kunywa maji ya kutosha, angalau lita moja nanusu (glasi nane) kwa siku au hata zaidi. Inashauriwa kunywa maji zaidi wakati wa joto kali

ili kuzuia upungufu wa maji mwilini. Vilevile mtu anaweza kuongeza maji mwilini kwakunywa vinywaji kama supu, madafu na juisi za matunda mbalimbali.

3328

Kiambatanisho na. 6: MBINU ZA KUBORESHA CHAKULA

a) Kuponda au kusaga chakula• Hurahisisha ulaji, uyeyushwaji wa chakula na matumizi ya virutubishi mwilini.• Ni vyema vyakula kwa ajili ya mgonjwa vipondwe au kusagwa.• Nyama huweza kusagwa au kupondwa kwenye kibao au kinu kabla ya kupikwa.

b) Kuongeza vyakula vyenye virutubishi kwa wingi• Ni vyema kuongeza vyakula kama karanga, maziwa, siagi, kweme, korosho, tui la

nazi au jibini kwenye chakula cha mgonjwa.• Vyakula hivyo husaidia kuongeza ubora wa chakula na upatikanaji wa

virutubishi mbalimbali.

c) Kutumia viungo vya vyakula• Husaidia kuongeza hamu ya kula na uyeyushwaji wa chakula.• Inashauriwa kuongeza viungo kama mdalasini, vitunguu saumu, iliki,

au tangawizi kwenye vyakula au vinywaji mbalimbali.

d) Kuotesha mbegu za vyakula• Vyakula vilivyooteshwa huyeyushwa kwa urahisi na husaidia uyeyushwaji wa vyakula

vingine • Virutubishi vilivyoko kwenye vyakula hivyo huchukuliwa na mwili kwa wingi zaidi. • Nafaka kama mahindi, mtama, ulezi au uwele huweza kuoteshwa, kukaushwa na

kusagwa unga • Vyakula kama choroko, kunde, maharangwe au njegere huweza kuoteshwa na kupikwa

kama kitoweo

e) Kuchachusha vyakula• Mgonjwa atumie vyakula kama maziwa ya mgando au togwa.• Vyakula hivyo huyeyushwa na kufyonzwa kwa urahisi mwilini.• Husaidia uyeyushwaji wa vyakula vingine• Virutubishi vilivyoko kwenye vyakula hivyo huchukuliwa na mwili kwa wingi

na kwa urahisi zaidi.

f) Kupika kwa mvuke• Vyakula mbalimbali hasa mboga za majani vipikwe kwa kutumia

mvuke.• Husaidia kuhifadhi ubora wa chakula kwa kiasi kikubwa.

MTINDI

KUMBUKA

• Ili kuhifadhi virutubishi, mboga za majani zioshwe kabla ya kukatwa,kisu chenye makali kitumike kukata mboga. Mboga ipikwe mara baadaya kukatwa na kwa muda mfupi na iliwe mara baada ya kupikwa.

• Nyama ioshwe kabla ya kuikata.

34 29

Kiambatanisho na. 7: BAADHI YA VIDOKEZO MUHIMU VYAKUBORESHA LISHE

Kula vyakula vya aina mbalimbaliUlaji wa vyakula mbalimbali husaidia mwili kupata virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe naafya bora kwani hakuna chakula kimoja pekee kinachotosheleza mahitaji yote ya mwili. Vyakulavina virutubishi vya aina mbalimbali na kwa kiasi tofauti.

Kula chakula cha kutoshaUlaji wa chakula cha kutosha huuwezesha mwili kukidhi ongezeko la mahitaji ya virutubishi. Hasapale mtu anapokabiliwa na maradhi ya aina mbalimbali. Inashauriwa kula milo miwili hadi mitatuiliyo kamili na asusa kati ya mlo na mlo kila siku. Endapo mtu hawezi kula chakula cha kutosha kwamara moja, inashauriwa kula milo midogo midogo mara nyingi kwa siku.

Kunywa maji safi na salamaMaji husaidia mwili kufanya kazi zake kwa ufanisi. Inashauriwa kunywa maji yaliyo safi na salamaangalau glasi nane kwa siku. Vinywaji kama juisi za matunda halisi, maji ya madafu na vinywaji vyaviungo vinaweza pia kutumika kuongeza maji mwilini.

Matumizi ya virutubishi vya nyongeza (nutrient supplements)Virutubishi vya nyongeza huweza kutumika iwapo kuna upungufu ambao hauwezi kukidhiwa kwakula chakula. Ni vyema kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya kabla ya kuvitumia ilikufahamu ni aina gani inahitajika na kwa kiasi gani. Virutubishi vya nyongeza visitumike badala yachakula na visichukuliwe kama dawa ya kutibu UKIMWI.

Mazoezi ya mwiliMazoezi ya viungo huboresha matumizi ya chakula na husaidia kujenga misuli ya mwili. Aina yamazoezi hutegemea hali ya mgonjwa. Mazoezi ni pamoja na kutembea au kukimbia taratibu, kufanyashughuli mbalimbali zinazotumia viungo vya mwili kama kazi za bustani, kufyeka na kazi nyingineza nyumbani.

Kuepuka matumizi ya pombePombe huingilia uyeyushwaji wa chakula, ufyonzwaji, uwekaji akiba na utumikaji wa virutubishimbalimbali mwilini. Pombe huchangia kupunguza kinga ya mwili na huongeza hatari ya mtu kupatamagonjwa sugu kama saratani hasa za kinywa, koromeo na ini.

Kuepuka matumizi ya sigara au tumbakuSigara na tumbaku hupunguza hamu ya kula, huchangia kudhoofisha kinga ya mwili na huongezahatari ya mtu kupata kifua kikuu na saratani za njia ya hewa.

Kuepuka kutumia vyakula au vinywaji vilivyosindikwaVyakula vilivyosindikwa kama soda, juisi, vyakula vya kwenye makopo au vinginevyo havina uborasana na pia vina kemikali ambazo sio nzuri kwa afya hasa kama mtu ni mgonjwa.

Kuendelea kujielimisha kuhusu afyaNi muhimu kwa mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI au UKIMWI kuishi kwa matumaini nakuendelea kujifunza na kutafuta habari zilizo sahihi kuhusu afya yake na jinsi ya kuishi na virusi vyaUKIMWI.

3530

Kiambatanisho na. 8: MFANO WA RATIBA YA KULA CHAKULA NAKUMEZA DAWA

Doto ameanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI. Dawa hizo ni Abacavir,Didanosine na Lopinavir/Ritonavir. Ushauri aliopewa ni kama ifuatavyo:• Dawa ya Abacavir imezwe mara mbili kwa siku, na haina masharti yoyote ya chakula • Dawa ya Didanosine, imezwe mara mbili kwa siku, na inatakiwa kumezwa wakati tumboni

hakuna chakula (kabla ya kula)• Dawa ya Lopinavir/Ritonavir imezwe mara mbili kwa siku, na inatakiwa kumezwa wakati

tumboni kuna chakula (baada ya kula).

Ufuatao ni utaratibu wa kula chakula na kumeza dawa ambao Doto ameamua kuufuata baadaya unasihi:

• Doto ameamua kumeza dawa ya Didanosine saa 1 asubuhi na saa 1 jioni, na dawa yaLopinavir/Ritonavir na Abacavir ameamua kumeza saa 2 asubuhi na saa 2 usiku. Hii ni kwasababu dawa ya Didanosine na Lopinavir/Ritonavir haziwezi kumezwa pamoja kwani mashartiyake ya chakula yanatofautiana, na dawa ya Abacavir inaweza kumezwa wakati wowote kwanihaina masharti ya chakula.

• Doto atameza dawa ya Didanosine saa moja asubuhi kabla ya kula chochote na hatakula kituchochote mpaka saa 1 ipite.

• Saa 2 asubuhi Doto atapata kifungua kinywa, na atameza dawa ya Lopinavir/Ritonavir naAbacavir. Hii ni kwa sababu dawa ya Lopinavir/Ritonavir inashauriwa kumezwa baada ya kula(wakati tumboni kuna chakula); na dawa ya Abacavir haina masharti ya chakula. Dotoameamua kumeza dawa hizi kwa pamoja kupunguza kumeza dawa mara nyingi.

• Kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni, Doto anaweza kula vyovyote anavyopenda.

• Kuanzia saa 11 jioni Doto anatakiwa asile chakula chochote, kwani atameza Didanosine saa 1jioni wakati tumboni hakuna chakula.

• Saa 1 jioni Doto atameza dawa ya Didanosine, na ataendelea kukaa bila kula hadi saa 2 usiku,yaani ipite angalau saa moja kabla ya kula.

• Saa 2 usiku Doto atakula chakula, na kumeza Lopinavir/Ritonavir na Abacavir mara baada yakula.

• Kuanzia saa 2 usiku hadi saa 11 alfajiri, Doto anaweza kula anavyopenda.

• Kuanzia saa 11 alfajiri, Doto anatakiwa asile chakula chochote hadi atakapomeza dawa yaDidanosine hapo saa moja asubuhi. Kumbuka dawa hii inashauriwa kumezwa wakati tumbonihakuna chakula.

Kumbuka dawa ya Abacavir haina masharti ya chakula, hivyo Dotoangeweza kuchagua kumeza dawa hiyo pamoja na dawa ya Didanosine

36 31

Mchoro wa ratiba ya matumizi ya dawa na chakula wa Doto

3732

ORODHA YA VITABUVILIVYOTAYARISHWA NA COUNSENUTH

1. Ulishaji wa Mtoto Aliyezaliwa na Mama Mwenye Virusi vya UKIMWI: Vidokezo Muhimu kwaWashauri Nasaha

2. Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Vidokezo Muhimu

3. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Majibu ya MaswaliYanayoulizwa Mara kwa Mara

4. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Vyakula vinavyoboreshauyeyushwaji wa chakula na ufyonzwaji wa virutubishi mwilini

5. Unyonyeshaji Bora wa Maziwa ya Mama: Vidokezo Muhimu kwa Jamii

6. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Matumizi ya Viungo vyaVyakula katika Kuboresha Lishe na Afya

7. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Vidokezo Muhimu katikaUnunuzi na Usalama wa Chakula

8. Ulishaji Bora wa Mtoto kuanzia umri wa miezi sita: Vidokezo Muhimu

9. Lishe kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Kitabu cha Mafunzo na Rejea

10. Kadi ya kutathmini hali ya lishe kwa kutumia uwiano wa urefu na uzito

11. Zijue Haki za Uzazi katika Sheria Mpya ya Kazi Tanzania

12. Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI: Kitendea Kazi kwa MtoaHuduma Nyumbani

1111

38

BIBLIOGRAFIA1. Anaemia Prevention and Control: What works, tools and resources. The Population, Health and

Nutrition Information, 2003.

2. COUNSENUTH, Lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI: Kitabu cha Mafunzo naRejea. Novemba, 2004.

3. COUNSENUTH, Lishe na Ulaji Bora kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI: VidokezoMuhimu katika Ununuzi na Usalama wa Chakula: COUNSENUTH information series No. 7.Juni, 2004.

4. COUNSENUTH, Lishe na Ulaji Bora kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI. KitendeaKazi kwa mtoa Huduma Nyumbani. 2005.

5. FAO, Food and Nutrition Division. Family Nutrition Guide. Rome, 2004.

6. FAO/WHO, Living well with HIV/AIDS: A manual on nutritional care and support for people livingwith HIV/AIDS, Rome, 2002.

7. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), Food and Nutrition Implications of AntiretroviralTherapy in Resource Limited Settings. Academy for Educational Development, Washington DC,August, 2003.

8. Food and Nutrition Technical Assistance (FANTA), HIV/AIDS: A Guide for Nutrition, Care andSupport. 2nd Edition. Academy for Educational Development, Washington DC, 2004.

9. Family Health International (FHI), HIV/AIDS Care and Treatment. A Clinical Course for PeopleCaring for Persons Living with HIV/AIDS

10. Nutrient Requirements for People Living with HIV/AIDS. Report of the Technical ConsultationGeneva, 2003.

11. RCQHC, Food and Nutrition Counselling for PLWHA on Antiretroviral Therapy. A job aid forcounselors and anti-retroviral therapy (ART) service providers. October, 2004

12. RCQHC/FANTA/LINKAGES, Nutrition and HIV/AIDS: A Training Manual, October 2003

13. The Republic of Uganda, Nutritional Care and support for PLHA: Guideline for Service Providers.

14. The Republic of Zambia, Ministry of Health. Nutrition Guidelines for Care and Support of PeopleLiving with HIV/AIDS. November, 2004

15. The United Republic of Tanzania Ministry of Health, A National Guide on Nutritional Care andSupport for People Living with HIV/AIDS, TFNC December, 2003.

16. The United Republic of Tanzania, Ministry of Health. National Guidelines for the ClinicalManagement of HIV and AIDS. 2nd Edition. April, 2005.

ISBN 9987-8936-5-1

Kimefadhiliwa na:

Rapid Funding Envelope for HIV/AIDS (RFE)

Kitabu hiki kimetayarishwa na: Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH)

432 United Nations Road • S.L.P. 8218, Dar es Salaam, TanzaniaSimu/Fax: +255 22 2152705 au 0744 279145

Barua pepe: [email protected]

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi MtendajiKituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya

(COUNSENUTH)

Designed & Printed by:

DeskTop Productions LimitedP.O. Box 20936, Dar es Salaam, Tanzania

Contact: 0784 387899, Email: [email protected]

Printed: August 2006

Kuhusu COUNSENUTH

Kituo cha Ushauri Nasaha, Lishe na Afya (COUNSENUTH) ni asasiisiyo ya kiserikali yenye makao yake Dar es Salaam.

Dhumuni la COUNSENUTH ni kuboresha Afya na Lishe yaWatanzania kwa kutoa huduma mbalimbali za lishe na unasihi kwakushirikiana na asasi na vikundi mbalimbali vilivyoko katika jamii