utangulizi · web viewkupandikiza miche kutoka katika kitalu kwenda shambani hufanyika baada ya...

22
SEMINA YA KILIMO BORA CHA GREENHOUSE IMEANDALIWA NA YETU MICROFINANCE PLC KWA KUSHIRIAKIA NA GREENTEK GROUP COMPANY LIMITED

Upload: others

Post on 15-Feb-2020

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

SEMINA YA KILIMO BORA CHA GREENHOUSE

IMEANDALIWANA

YETU MICROFINANCE PLCKWA

KUSHIRIAKIANA

GREENTEK GROUP COMPANY LIMITED

UTANGULIZI

Greenhouse ni nini?

Greenhouse ni jengo maalumu linalojengwa kwa chuma na kufunikwa na karatasi maalumu kwa ajili ya kilimo zinazosaidia kuchuja jua kwa asilimia kadhaa ili kuupa mmea mazingira rafiki kwa uzalishaji, pia inafunikwa na wavu maalumu unaotumika katika kilimo ili kuzuia vihatarishi vya mimea na mazao pamoja na kuongeza mzunguko wa hewa katika shamba kitalu.

Manufaa ya greenhouse Ongezeko la mavuno kwa zaidi ya mara 10 zaidi ya kilimo cha eneo la

wazi Matumiza mazuri na sahihi ya ardhi Huongeza ubora wa mazao Matumizi ya maji ni kwa kiasi kidogo sana Uwezo wa kudhibiti magonjwa ni mkubwa Gharama ya usimamizi ni ndogo kulinganisha na mbinu nyingine za

kilimo

Uchaguzi wa eneoGreenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua, lililo tambarare na halina upepo mkali.

Aina za greenhouseGreenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo;

I. Aina ya greenhouse kwa kigezo cha sura au umbile (shape)Zipo aina zaidi ya nne za greenhouse, hapa nitataja kulingana na majina yake ya kitaalamu

Single tunnel greenhouse

Saw tooth greenhouse

Multi tunnel greenhouse

Double layer warm keeping greenhouseII. Aina ya greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)

Greenhouse zinazoongeza joto (maalumu kwa maeneo yenye baridi kali)

Greenhouse zinazopunguza joto (maalumu kwa maeneo yenye joto)

III. Aina ya greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake Greenhouse za miti (Wooden framed structure) Greenhouse zinazotumia chuma (hot galvanized steel)

MFUMO WA UZALISHAJIMimea ikipewa mazingira rafiki huwa na uwezo wa kuzalisha mazao kwa wingi na katika ubora wa hali ya juu. Kutengeneza mazingira sahihi ya uzalishaji mzuri wa mazao unahusisha matumizi sahihi ya greenhouse na mahitaji ya zao husika.

MAZINGIRA YA UKUAJI MMEAMahitaji ya mmea katika ukuaji wake hutofautiana kutokana na aina (variety) ya mmea na steji ya ukuaji ilipofikia. Kwa mfano; joto linapoongezeka, mahitaji ya unyevuunyevu katika mmea huongezeka. Pia mwanga ukiongezeka, joto

huongezeka pia na kufanya mahitaji yam mea kuongezeka sio tu kwenye unyevuunyevu lakini pia madini kusaidia katika ukuaji.

Mwanga; Kuna vitu vitatu vinavyoathiri ukuaji wa mmea vinavyohusiana na mwanga navyo ni kiwango cha mwanga, muda na ubora wa mwanga. Kiwango cha mwanga, ikimanisha mwanga mmea hupokea kwa siku, muda ikiwa na maana ya masaa ambayo mmea hupata mwanga kwa siku.

Kiwango cha joto; Iwapo joto ni kali sana huathiri ukuaji wa mmea haswa katika majani na mizizi. Hali ya hewa, media ya kuoteshea miche na maji yanayotumika katika umwagiliaji wa matone huathiri moja kwa moja joto la mmea.

Unyevuunyevu; maji ni dereva nambari moja katika ukuaji wa mmea. Yanahusika

na kusafirisha madini kutoka katika udongo kwenda kwenye mmea.

Unyevu; ni vema kuhakikisha mmea unapa unyevunyevu kwa kiasi, ikitokea mmea umepata unyevunyevu sana ukiambatana na joto basi uwezo wa mmea kusafirisha maji kutoka kwenye mizizi kwenda katika majani yake hupungua, hivyo kupunguza mzunguko wa madini yanayohitajika na mmea.

Madini; haya ni malighafi (raw material) ya mmea hivyo kiwango na uwekaji wa haya madini na mkulima (grower) ni muhimu sana katika mafanikio ya ukuaji sahihi wa mmea.

Oxygen; Hewa ni muhimu katika ukuaji wa kiumbe hai chochote, hususani mmea. Katika greenhouse mzunguko wa hewa ni muhimu katika kuhakikisha mmea unapata hewa vizuri na kupelekea ukuaji sahihi.

UDONGO WA KUKUZIA (GROWING MEDIA)Udongo huu hutengeneza mazingira sahihi ya kusapoti mmea na katika usafirishaji wa madini na maji kwenda kwenye mmea. Ipo njia ya kulima kwa kutumia udongo na kulima bila kutumia udongo.

KULIMA KWA KUTUMIA UDONGOKwa mazao yanayolimwa moja kwa moja katika udongo, uwepo wa matuta ni muhimu na muda mwingine kuwekewa karatasi maalumu la kuhifadhi unyevunyevu. Matayalisho ya matuta huambatana na uwekwaji wa mbolea ya kuku au mboji ya ng’ombe iliyo kavu.

UMWAGILIAJI WA MATONEIkitokea kiwango cha maji kimezidi katika ardhi hutengeneza upenyo wa fungus, hivyo kusababisha kuoza kwa mizizi na kupunguza au kusimamisha kabisa ukuaji wa vinyweleo katika mizizi vyenye kazi ya kunyonya madini. Pia unyevunyevu ukizidi hupelekea kiwango joto kushuka na ukipungua ni mbaya zaidi kwa mmea.

Hivyo ni muhimu kufanya vipimo vya ardhi ili kufahamu ni kiwango gani cha maji kinahitajika katika ardhi husika. Na kupitia umwagiliaji wa matone katika greenhouse mmea hupata kiwango cha maji kinachohitajika.

MAZAO NA UCHAGUZI WA AINAIngawa wakulima wengu hufahamu ni aina gani ya zao wanahitaji kulima na katika ukubwa gani wa greenhouse lakini inashauriwa mkulima kufanya uchaguzi sahihi wa zao na aina (variety) kulingana na hali ya eneo husika alipo lakini pia hitaji la soko.

Aina za mbegu ziko nyingi na nyingine zinaendelea kugundulika kila siku lakini chagua mbegu ambazo ni hybrid.Sifa za hybrid ni;

Uimara Kupata mazao yaliyo katika hali moja ya ukuaji Kupata matunda yenye ukubwa mzuri Mmea huwa na urefu mpaka wa 3.5m kwenda juu Mavuno ya muda mrefu Huzuia baadhi ya magonjwa

Tunashauriwa kununua mbegu kutoka katika makampuni yanayotambulika kwa ubora. Pia kuna mbegu maalumu kwa greenhouse na nyingine maalumu kwa kilimo cha nje.

PROPAGANDA ZA MBEGUMazao mazuri huanzia katika miche. Hatua muhimu za kufuata katika uandaaji wa miche ni;

Piga hesabu ya idadi kamili ya mbegu unazohitaji kupanda katika eneo la greenhouse husika, bila kusahau kuongeza kidogo kiwango cha mbegu za ziada kufidia zile ambazo zitashambuliwa na wadudu, kugoma kuota au kupatwa na ugonjwa.

Andaa trei za kupandia na udongo maalumu wa kuoteshea miche Jaza udongo wa kupandia katika kiwango sawa ndani ya mashimo yote ya

trei kisha weka mbegu moja kwa shimo moja na kurudishia udongo kwa juu

Mwagia maji kwa utaratibu kuepusha kusafisha mbegu zilizooteshwa Weka miche katika eneo lenye nyuzi joto 24 – 29 Usiruhusu udongo katika trei kukauka na kila baada ya siku 7 ipatie miche

mchanganyiko wa starter kuiongezea chakula

MAZINGIRA SAHIHI YA UOTESHAJI WA MICHEKiwango cha joto na siku mpaka kuanza kuchomoza micheZAO NYUZI JOTO SIKUNyanya 26 3 – 6Hoho 25 10 -14Matango 24 3 – 5

Uhifadhi wa trei za miche ufanyike ndani ya greenhouse kuepusha wadudu wa haribifu na miche kushambuliwa na magonjwa.

UPANDIKIZAJIKupandikiza miche kutoka katika kitalu kwenda shambani hufanyika baada ya siku 21 (wiki 3) kwa nyanya na siku 29 – 30 kwa hoho ambapo mmea huwa na urefu wa 10 – 15 cm (4 – 5 inch tall) na una majani angalau 3 – 4. Hakikisha mimea unayopandikiza mizizi yake iko katika hali nzuri na imefunga vizuri pia hamisha mche bila kuharibu udongo ulioshikana na mizizi.

VIPIMO VYA UPANDIKIZAJIIkiwa unalima ndani ya greenhouse, ni muhimu kutumia njia bora ya upandikizaji ili kuepusha msongamano wa mazao (planting density). Kwa mfano; kwa matokeo mazuri nyanya inahitaji 40 – 60 cm kutoka mche mmoja kwenda mche mwingine na kwa mtindo wa zigzag.

Ikitokea kukawa na mrundikano wa miche katika upandikizaji hupelekea mavuno kidogo kwa mche kutokana na mche mmoja kusababisha kivuli kwa mche mwingine. Pia huvutia wadudu na usaambaaji wa magonjwa kirahisi.

UCHAVUSHAJI, UFUNGAJI KAMBA NA UPOGOAJI (PRUNING)Katika kilimo cha greenhouse uchavushaji, ufungaji kamba na upogoaji ni kazi kubwa tatu ambazo huongeza uzalishaji na ubora wa mazao mengi yalimwayo ndani ya greenhouse.

Uchavushaji hupaswa kufanywa na mkulima ndani ya greenhouse kuhakikisha chavua inasambaa ndani ya greenhouse kutokana na ukweli kwamba nyuki na wadudu kama vipepeo hawana nafasi ya kuingia ndani ya greenhouse na kufanya uchavushaji.

Ufungaji wa kamba miche hufanywa ili kuepusha miche kuangusha chini na kushindwa kukua kama inavyotakiwa. Mkulima anaweza kutumia kamba au vipini maalumu kwaajili ya kushikilia miche yake isianguke.

Upogoaji ni kitendo cha kuondoa majani yaliyozidi ambayo hayana umuhimu katika ukuaji wa mmea na huongeza kivuli na kuvutia wadudu.

USIMAMIZI WA MADINIMadini muhimu katika ukuaji wa mmea ni kama yafuatayo;

Nitrogen (N)

Phosphorus (P) Potassium (K) Calcium (Ca) Magnesium (mg)

Surfur (S) Copper (Cu) Iron (Fe) Chlorine (Ci) Manganese (Mn) Zinc (Zn)

Madini yanatumika katika mmea kwa kiwango tofauti; nitrogen, phosphorus na potassium zinatumika kwa kiasi kikubwa na hutambulika kama virutubishi msingi. Kuna baadhi ya madini ambayo hutumika kwa kiasi kidogo, madini hayo ni kama surfur, copper, chlorine, manganese and zinc.

AINA ZA MBOLEA NA MATUMIZIUpandikizaji wa awali; mbolea inaweza kuwekwa ardhini kabla ya kupandikiza miche, haswa mboji ya kuku au ng’ombe hutangulizwa kabla ya kupandikiza miche.

Kulisha foliarNi kitendo cha kuchanganya mbolea zilizo katika hali ya kimiminika katika maji na kupulizia majani ya mmea moja kwa moja kwani husaidia mmea kula chakula moja kwa moja kupitia majani na sio kupitia mizizi. Ni vema kuwa muangalifu kulisha mmea kutumia njia hii kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuzidisha chakula kwa mmea endapo utakua unafanya marudio ndani ya muda mfupi.

FertigationHiki ni kitendo cha kuweka mbolea au lishe katika mmea kupitia mfumo wa umwagiliaji. Mfumo huu unaweza kutumika kwa mazao yanayozalishwa juu ya matuta au kwa kutumia mfumo wa kilimo cha bila udongo. Mfumo huu ni mzuri kwani huwezesha kila mmea kupata kiwango sahihi cha mbolea/lishe, hupunguza usimamizi na nguvu kazi.

NJIA ZA UCHANGANYAJI MBOLEAKuna njia kuu mbili za uchanganyaji wa mbolea, kwanza ni kupitia tank kubwa la greenhouse na pili ni kupitia solo.Kupitia ripoti ya maji kutoka maabara mkulima ataweza kufahamu viwango vya mbolea vya kuchanganya.

UBORA WA MAJIUbora wa maji ni moja ya kiungo muhimu katika ushalishaji ndani ya greenhouse. Kabla ya kuanza taratibu zozote mkulima anashauriwa kupima maji kwa sehemu husika, kusudi afahamu ubora wa maji.

UPIMAJI WA UDONGOIkiwa kilimo kinachokwenda kufanyika kitatumia udongo, ni vizuri kufanya vipimo vya udongo ili kujiridhisha na rutuba iliyopo katika udongo. Kupitia majibu ya udongo, njia sahihi ya matumizi ya mbolea na madini huweza kutolewa.

UFUATILIAJI WA UKUAJINi muhimu kwa mkulima kufuatilia ukuaji wa mimea yake na kuweza kutambua dalili yeyote ambayo si njema katika mmea. Mkulima anatakiwa kukagua greenhouse yake kila siku ili kujiridhisha na hali ya mimea inavyoendelea. Ukosefu wa madini katika mimea hupelekea yafuatayo;

NJIA ZA KUJIKINGA NA WADUDU NA MAGONJWAWadudu husababisha uharibifu kwa kula kupitia mimea na wengine husambaza magonjwa katika mimea.Wadudu na utitiri ni kama;

Vidomozi Nzi weupe Tomato bugs Funza wa matunda Utitiri

Magonjwa ni kama; Uvimbe wa backteria, matone na madoa Mnyauko bakteria Mnyauko fusaria Bakajani tangulia Bakajani chelewa Ubwiri poda Minyoo fundo Magonjwa ya virusi Mwozo wa nja (Blossom-end rot)

JINSI YA KUJIKINGA NA WADUDU NA MAGONJWA Osha mikono yako kila uingiapo ndani ya greenhouse Vaa viatu maalumu kwaajili ya kuingilia ndani ya greenhouse ikiwezekana

jengea kijumba kidogo nje ya mlango wa ndani maalumu kwa kuhifadhia mavazi ya kuvaa ukiwa unatoa huduma ndani ya greenhouse

Hakikisha mlango wa greenhouse yako umefungwa muda wote wa kutoa huduma ndani ya greenhouse na wakati ambao hakuna huduma inaendelea ndani

Ni marufuku kuvuta sigara maeneo ya karibu na greenhouse

UTAMADUNI WA MAZAOIkiwa unafanya kilimo cha greenhouse ni vizuri mkulima akafahamu sifa na utamaduni wa zao husika ili kuweza kufanikiwa. Mazao ambayo hufanya vizuri ndani ya greenhouse ni pamoja na nyanya, pilipili hoho, lettuce na matango. Katika dodoso letu tutaongelea nyanya na pilipili hoho.

NYANYANyanya ni moja ya zao maarufu sana zinalozalishwa kupitia greenhouse. Ikiwa misingi sahihi ya kilimo cha nyanya imefuatwa, mche mmoja wa nyanya una uwezo wa kuzalisha kwa zaidi ya miezi tisa mpaka mwaka mmoja.

Zipo mbegu kwaajili ya greenhouse na mbegu kwaajili ya kilimo cha wazi, pia kuna mbegu fupi ambazo huishi muda mfupi na mbegu ndefu ambazo hukua na kuishi muda mrefu.

Kuna aina nyingi za nyanya kama nyanya mshumaa (oval shape), nyanya mviringo (round shape), nyanya pori (cherry tomato). Pia zimegawanyika hybrid na ambazo sio hybrid.

Pilipili HohoHoho ni familia moja na nyanya, viazi na bilinganya.

Zipo aina nyingi za hoho lakini nyingi zinalimwa katika greenhouse ni hoho za kijani, hoho za njano, hoho nyekundu na orange. Pia hufanya vizuri zaidi kwenye greenhouse.

Hoho zinapolimwa nje ya greenhouse ni vema kutozipogoa na ndani ya greenhouse ni vizuri zikafungiwa kamba ili kuongeza uzalishaji.

Hoho hufanya vizuri katika kiwango cha nyuzi joto 20 – 24 na kiwango cha juu ni nyuzi joto 27. Hoho huweza kuvumilia kiwango cha nyuzi joto 30 mchana na nyuzi joto 21 – 24 kwa usiku.

Magonjwa ya nyanya na hoho hayatofautiani.

Mwisho!