yesu katika india

133
YESU KATIKA INDIA Ikiwa ni taarifa ya kuepukana kwake Yesu na kifo juu ya msalaba na safari yake ya kwenda India Kimetungwa na: HADHRAT MIRZA GHULAM AHMAD WA QADIAN Mwanzilishi wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika Islam Kimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Bwana Mohammed Saidi Kibindu wa Dar es Salaam Tafsiri ya Kiswahili imetangazwa na: JUMUIYA YA WAISLAMU WAAHMADIYYA TANZANIA S.L.P. 376 SIMU: 2110473 FAX: 2121744 DAR ES SALAAM.

Upload: hoanganh

Post on 30-Dec-2016

960 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: Yesu katika India

1

YESU KATIKA INDIA

Ikiwa ni taarifa ya kuepukana kwake

Yesu na kifo juu ya msalaba na safari

yake ya kwenda India

Kimetungwa na:

HADHRAT MIRZA GHULAM AHMAD

WA QADIAN

Mwanzilishi wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika Islam

Kimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Bwana Mohammed

Saidi Kibindu wa Dar es Salaam

Tafsiri ya Kiswahili imetangazwa na:

JUMUIYA YA WAISLAMU WAAHMADIYYA TANZANIAS.L.P. 376

SIMU: 2110473 FAX: 2121744DAR ES SALAAM.

Page 2: Yesu katika India

2

YESU KATIKA INDIA

Mwandishi: Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s.

Mfasiri: Bwana Muhammed Said Kibindu

© Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania

Chapa ya kwanza: 2000 Nakala: 3000

Kimechapwa na

Ahmadiyya Printing PressP.O. Box 376Simu: 2110473, Fax 2121744Dar us SalaamTanzania.

Page 3: Yesu katika India

3

YALIYOMO

1. Neno la Mbele . . . . . . . . . . . . . . . . . . 4

2. Utangulizi . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7

3. Sura ya Kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21

4. Sura ya Pili . . . . . . . . . . . . . . . . . . 56

5. Sura ya Tatu . . . . . . . . . . . . . . . . . . 62

6. Sura ya Nne . . . . . . . . . . . . . . . . . . 72

I. Sehemu ya Kwanza . . . . . . . . . . . . . . . . . 72

II. Sehemu ya Pili . . . . . . . . . . . . . . . . . . 78

III. Sehemu ya Tatu . . . . . . . . . . . . . . . . . . 98

7. Viambatanisho . . . . . . . . . . . . . . . . . . 112

Page 4: Yesu katika India

4

NENO LA MBELE

"YESU NCHINI INDIA" ni tafsiri ya KISWAHILI ya "MasihiHindustan Mein" ambacho ni kitabu cha Kiurdu kilichoandikwana Mwanzilishi Mtukufu wa Jumuiya ya Ahmadiyya katika Islam,Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. (1835-1908).

Mada kubwa iliyofafanuliwa katika kitabu hiki ni kuepushwakwake na kifo cha fedheha juu ya msalaba na safari yake yakwenda India kuyatafuta makabila yaliyopotea ya wana waIsraeli ambao ilikuwa lazima awakusanye na kuwaingiza katikazizi lake kama ilivyotajwa katika Agano Jipya.

Ushahidi chungu nzima umekwisha patikana katika Maandikoya Kikristo na pia ya Kiislamu, vitabu vya zamani vya tiba na piavya historia, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu za kale za Kibuddhakatika kulifafanua jambo hili.

Akiwa ameianza safari yake kutoka Yerusalemu na akiwaamepitia Nasibus, na Iran, Yesu anaonyeshwa kuwa alifikaAfghanistan ambako alikutana na Wayahudi waliokaa pale baadaya kutolewa utumwani kwa Nebachadnezzar.

Kutoka Afghanistan Yesu alikwenda Kashmir ambako piabaadhi ya makabila ya Waisraeli yalikaa. Alipofanya mahali hapakuwa maskani yake na ndipo mahali alipofia. Kaburi lakelimetafutwa na kukutwa katika mtaa wa Khanyar, mjini Srinagar.

Kwenye sehemu inayoshughulika na ushahidi uliopatikanakatika kumbukumbu za kale za Kibuddha Hadhrat Ahmadametatua swali ambalo kutokana na hali yake ya ugumu limekuwakwa muda mrefu likiwatatiza waandishi wengi wa Kimagharibi.

Waandishi hawa wamefumbwa na kufanana kwa ajabukunakopatikana baina ya mafundhisho ya Kibuddha na yale yaKikristo na kati ya matukio ya maisha ya wote wawili Yesu naBuddha kama ilivyofunuliwa katika maandiko ya kila mmoja wao.

Baadhi ya waandishi hawa wanashikilia maoni kwamba kwavyo vyote vile mafundisho ya Kibudha ni lazima yawe yalifika

Page 5: Yesu katika India

5

Falastwini na kutumiwa na Yesu katika mahubiri yake. Lakinihakuna kabisa uthibitisho wa kihistoria wa kuunga mkono nadhariahii.

Msafiri wa Kirusi aitwae Nicolas Notovitch aliishi kwa kipindikirefu na Walama wa Tibet na wakamtafsiria vitabu vyao vitakatifu.Yeye ana maoni kwamba Yesu lazima alikuja Tibet kabla yakusulubiwa kwake na kurudi Falastwini baada ya kujifunzamafundisho ya Kibuddha. Haya pia ni matamshi tu ambayohayaungwi mkono na ushahidi wa kihistoria wenye kuaminika.

Akiyakanusha maoni hayo ya namna mbili, Hadhrat Ahmadanaandika kwamba Yesu alikuja India siyo kabla ya tukio laMsalaba bali baada yake na kwamba si yeye aliyekopa mafundishoya Kibuddha bali ni wafuasi wa Buddha wanaoonekana kuwawameichapisha upya picha ya Injili zote katika vitabu vyao.

Kulingana na Hadhrat Ahmad, Yesu pia alitembelea Tibetwakati wa safari zake nchini India akiyatafuta makabila yaliyopoteaya Israeli. Alihubiri ujumbe wake kwa watawa wa Kibuddha ambaobaadhi yao walikuwa Wayahudi waliojiunga na dini hiyo yaKibuddha. Wafuasi wa Buddha waliathirika sana na mafundishoyake na wakamchukulia yeye kuwa ni udhihirisho wa Buddha namwalimu wao Aliyeahidiwa. Wakiwa wanamwamini kama Bwanawao, wakayachanganya mafundisho yake na yale yaliyomo katikakumbukumbu zao na wakayahesabu yote kwa pamoja ni yaBuddha. Ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono maoni hayaunapatikana katika kumbukumbu za kale za Kibuddha.

'Masih Hindustan mein' kiliandikwa mnamo mwaka 1899na ni kiishilizio cha zama ambamo kwa karne nyingi Waislamuna Wakristo waliamini Yesu kupaa mbinguni. Kikiwa ni kitabu chakwanza pekee kilichoandikwa kuhusu suala hili kwa mjio wa kiakili,kitabu hiki kilileta kishindo kikubwa.

Hoja zake zilitangazwa na katika nusu karne iliyopitakimepata mafanikio ya kutosha katika kumwondolea Yesu sifaza uwongo za kiungu na kumwonyesha hadharani mbele yaulimwengu akiwa nabii mtakatifu ambavyo kwa hakika ndivyoalivyokuwa.

Page 6: Yesu katika India

6

Katika nyanja za Kiislamu kishindo cha kitabu hiki kilikuwakikubwa sana kiasi kwamba Mufti wa Chuo Kikuu cha Al-Azharjijini Cairo, alitoa Fatwa kwamba kulingana na Qur`an Tukufu Yesualikufa kifo cha kawaida. Mvuto wake wa kuzishawishi fikra zaKikristo pia ulikuwa wa kusumbua sana.

Ingawa hakuna kitabu kingine miongoni mwa maandiko yakechenye jina hili, hata hivyo Hadhrat Ahmad aliyajadili kikamilifumasuala yote haya pamoja na mengine mengi muhimu kuhusuukweli wa Islam, ukweli wa madai yake na ukweli kuhusu kifocha Yesu katika vitabu vingi tu alivyoviandika baada ya hichokilichotajwa hapo juu.

Tafsiri ya Kiingereza ilifanywa na Qazi Abdul Hamidaliyekuwa mhariri wa jarida la kila juma liitwalo: "The Sunrise" laLahore ambamo ilichapishwa kwa mfululizo katika kipindi chamiaka ya 1938 hadi 1939. Ilitangazwa kwa mara ya kwanza katikasura ya kitabu mnamo mwaka 1944 na Nashrul-Ishaat SadrAnjuman Ahmadiyya, Qadian.

Pamoja na wengine wote waliotusaidia kwa njia moja aunyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki, shukrani zetu nyingizimwendee Bwana Mauloud Ahmad Khan, aliyekuwa Imam waMsikiti wa London ambaye alijitolea sana kuzikusanya nukuuzinazohusika kutoka katika vitabu vya asili vilivyorejewa na HadhratAhmad katika kulithibitisha jambo hili. Nukuu hizozimeunganishwa na kitabu hiki kwa mpangilio wa viambatanishonamba 1 hadi namba 18.

Mei, 1962Wakilut - TabshirTahrik Jadid,Rabwah, Pakistan

Page 7: Yesu katika India

7

KWA JINA LA MWEZI MUNGU, MWINGI WA REHEMA,MWINGI WA UKARIMU. TUNAMHIMIDIA YEYE

NA TUNAMSALIA MTUME WAKE MTUKUFU S.A.W.Ee Mola! Hukumu baina ya watu wetu kwa haki.

Hakika wewe U m`bora wa mahakimu.

UTANGULIZI

Nimeandika kitabu hiki ili, kwa kuleta uthibitisho kutoka kwenyeukweli ambao umekwisha kubalika na kutoka kwenye ushuhudawa kihostoria usiokuwa na shaka na wenye kuthaminiwa, nakutoka kwenye nyaraka za kale za wasiokuwa Waislamu, niwezekuondoa mawazo potofu sana ambayo yamezagaa miongonimwa Waislamu na miongoni mwa takriban madhehebu zote zaKikristo kuhusu maisha ya mwanzoni na ya baadaye ya Yesu(amani juu yake) - mawazo potofu ambayo athari zake za hatarisiyo tu zimelidhuru na kuliteketeza wazo la kuwako kwa umojawa Mungu, bali pia ushawishi usiofaa na wenye sumu kwa mudamrefu umekuwa ukionekana katika maadili ya Waislamu wa nchihii (India). Maradhi ya kiroho, yaani utovu wa maadili mema,mawazo machafu, ukatili na utovu wa huruma vinaendeleamiongoni mwa firqa za Kiislamu na ni matokeo ya kuziaminihadithi na hekaya kama hizi zisizokuwa na msingi. Huruma yabinadamu, majuto na kupenda haki, upole na unyenyekevu - sifazote nzuri zinatoweka siku hadi siku, kana kwamba hivi karibunizitaiaga jamii hii. Ukatili huu na utovu huu wa maadili memaunawafanya Waislamu wengi waonekane kama wanyama waporini. Mfuasi wa Buddha ambaye katika dini ya Kibuddha huitwaJain huogopa na hujiepusha na kuua hata mmbu au kiroboto,lakini lo! wako wengi miongoni mwa sisi Waislamu ambao wanauamtu asiyekuwa na hatia au kufanya mauaji yasiyokuwa na mipaka,hawamuogopi Mwenyezi Mungu mwenye nguvu ambayeameyakadiria maisha ya binadamu kuwa ya daraja la juu kulikoyale ya wanyama wote. Lakini huu ukatili na dhuluma na utovuwa huruma vinasababishwa na nini? Vinasababishwa na jambo

Page 8: Yesu katika India

8

hili - kwamba tangu wakati wa utoto wao, hekaya na hadithi nafikra potofu za itikadi ya Jihadi vinaimbwa ndani ya masikio yaona kushinikizwa katika mioyo yao, matokeo yake yakiwa kwambapolepole wanakufa kiroho na kutokuhisi ubaya wa vitendo vyaovya kuchukiza; la, bali yule mtu anayemwua mtu mwingine bilakutarajiwa na hivyo kuleta maangamizi kwenye familia ya mtualiyeuawa, hudhania kwamba amefanya kitendo kinachostahili;au tuseme, kwamba ameitumia vema fursa ya kujipatiaupendeleo kutoka kwa jamii yake. Kwa vile hakuna mafundishoau hotuba zinazotolewa nchini mwetu kuzuia uovu wa namnahiyo - na iwapo kuna mafundisho yo yote ya namna hiyo yanaviini vya unafiki ndani yake - watu - wa kawaida huwa na fikra zakuviunga mkono vitendo hivyo viovu. Kwa hiyo basi, kwakuwahurumia watu wangu mwenyewe, nimetunga vitabu kadhaa,kwa Kiurdu, Kiajemi na Kiarabu ambamo nimesema kwambamaoni yanayoshikiliwa na watu wote kuhusu Jihadi ambayoyamezagaa miongoni mwa Waislamu, yaani, kusubiriwa kwaImamu mwenye kumwaga damu aliyejawa na chuki na uaduikwa watu wengine ni mfumo wa imani potofu zilizofundishwa namaulamaa wasioona mbali; vinginevyo, Islam hairuhusu utumiajiwa upanga kuieneza Imani hii; isipokuwa wakati wa vita vyakujihami au wakati wa vita zinazopiganwa ili kumwadhibumdhalimu au kutetea uhuru. Haja ya kuwepo kwa vita ya kujihamiinakuja wakati ambapo uchokozi wa adui unahatarisha maishaya mtu. Basi hizo ndizo aina tatu za Jihadi zinazoruhusiwa nasheria, na kinyume cha hizi aina tatu, hakuna aina nyingine yavita ambayo inaruhusiwa na Islam katika kuizagaza Imani. Kwakifupi nimetumia kiasi kikubwa cha fedha katika kuvichapishavitabu hivyo na nimevitangaza humu nchini, na nchini Arabia naSyria na Khurasan na kadhalika. Lakini kwa msaada wa MwenyeziMungu sasa nimegundua hoja zenye nguvu sana ambazozitatumika katika kuzifutilia mbali imani hizi potofu mioyoni mwawatu. Ninao uthibitisho ulio wazi, ninao ushahidi wa kimazingirausiokuwa na shaka, na ninao ushahidi wa kihistoria ambao nuruya ukweli wake inaleta matumaini makubwa kwamba mara baada

Page 9: Yesu katika India

9

ya kutangazwa kwa ushahidi huo patatokea mabadiliko ya ajabukatika nyoyo za Waislamu dhidi ya imani hizo potofu. Na natumainibali nina hakika kwamba baada ya mambo haya ya kwelikufahamika, zitabubujika kutoka katika mioyo ya wachamunguwana wa Islam zile chemchem tamu na safi za unyenyekevu,huruma na amani, na kwamba yatatokea mabadiliko ya kirohoambayo yatakuwa na ushawishi mzuri na wenye baraka nyingikatika nchi hii (India). Nina uhakika pia kwamba wachunguzi waKikristo na watu wengine wote wanaoutamani na wenye kiu yakuupata ukweli huu, watafaidika sana na vitabu vyangu. Na huuukweli nilioutaja hivi punde, kwamba shabaha halisi ya kitabu hikini kuzisahihisha imani potofu ambazo zimekuwa sehemu yakanuni za imani za Waislamu na Wakristo, unahitaji maelezokidogo ambayo nayatoa hapa chini.

Naifahamike kwamba takriban Waislamu na Wakristo wotewanaamini kwamba Yesu (amani ya Mungu juu yake) alipaambinguni akiwa hai; watu wote hawa waliendelea kuamini kwamuda mrefu kwamba Yesu (amani juu yake) yungali hai hukombinguni na baadaye katika siku za mwishoni atashuka ardhini.Tofauti iliyopo katika maoni yao, yaani maoni ya wafuasi waIslam na yale ya Wakristo ni hii tu kwamba Wakristo wanaaminikwamba Yesu (amani juu yake) alifia msalabani, alifufuliwa, naalipaa mbinguni akiwa na mwili wake, aliketi mkono wa kulia waBaba yake, na atakuja duniani katika siku za baadaye ili kujakuhukumu, wanasema pia kwamba Mwumbaji na Bwana waulimwengu huu ni huyu huyu Masihi Yesu na si mwingine ye yote;yeye ndiye yule ambaye katika siku za mwisho wa dunia atashukaardhini kwa mshuko wa utukufu ili kuja kutoa adhabu na thawabu;kisha, wale wote ambao hawatamwamini yeye au mama yakekama Mungu, watakokotwa na kutupwa jahanamu ambamo kaziyao itakuwa kulia na kuomboleza. Lakini firqa zilizokwisha semwaza Waislamu zinasema kwamba Yesu (amani juu yake)hakusulubiwa; isipokuwa, wakati Mayahudi walipomtia mbaroniili kumsulubu malaika wa Mungu alimchukua na kumpelekambinguni akiwa na mwili wake wa kidunia na bado yungali hai

Page 10: Yesu katika India

10

huko mbinguni - ambayo wanaiita mbingu ya pili ambako pia yukonabii Yahya, yaani Yohana. Zaidi ya hayo Waislamu wanasemapia kwamba Yesu (amani juu yake) ni nabii mashuhuri waMwenyezi Mungu, lakini si Mungu wala si mwana wa Mungu nawanaamini kwamba katika siku za akheri zamani atashuka ardhinikaribu na Mnara wa Demeshki au karibu na sehemu nyingineakiwa amebebwa juu ya mabega ya malaika wawili, na kwambayeye na Imam Muhammad Mahdi ambaye atakuwa tayari yukoulimwenguni, na ambaye atakuwa ametokana na uzao waFaatimah, watawaua wote wasiokuwa Waislamu bila kumwachaye yote hai isipokuwa wale ambao pale pale na bila kuchelewawatasilimu.

Kwa ufupi shabaha halisi ya kushuka duniani kwa Yesu(amani juu yake) isemwavyo na firqa za Kiislamu ziitwazo Ahli-Sunna au Ahli-Hadithi ambazo watu wa kawaida wanaziitaWahabii - ni hii kwamba, kama alivyofanya Mahadev wa Wahindu,ni lazima auteketeze ulimwengu wote; kwamba ni lazima kwanzaawalazimishe watu kusilimu na kisha iwapo wataendeleakutokuamini awaue wote kwa upanga; zaidi ya hayo wanasemakwamba yeye yu hai mbinguni akiwa na mwili wake wa kidunia ilinguvu za Kiislamu zitakapodhoofika ateremke na kuwauawasiokuwa Waislamu au kuwalazimisha kwa kuwatia uchungumkali ili wasilimu. Kuhusiana na Wakristo, hususan viongozi wafirqa hizo zilizokwisha tajwa, wanasema kwamba wakati Yesu(amani juu yake) atakapoteremka kutoka mbinguni atavunjamisalaba yote ulimwenguni, atafanya vitendo vingi vya kikatili kwakutumia upanga, na ataujaza ulimwengu kwa mafuriko ya damu.Na kama nilivyokwisha sema, hawa watu, yaani Ahli-Hadithi nakadhalika watokao miongoni mwa Waislamu wana jazba kubwasana kuhusu hii imani yao kwamba muda mfupi kabla yakuteremka Masihi atatokea Imam kutoka miongoni mwa BaniiFaatima ambaye jina lake litakuwa Muhammad Mahdi. Huyu ndiyeatakayekuwa Khalifa na Mfalme wa wakati ule, na kwa kuwaatatokana na Wakureshi, shabaha yake halisi itakuwa kuwauawote wasiokuwa Waislamu isipokuwa wale ambao wataitamka

Page 11: Yesu katika India

11

Kalima mara moja. Yesu (amani juu yake) atateremka ilikumsaidia huyu Imam katika kazi hiyo; na ingawa Yesumwenyewe (amani juu yake) atakuwa Mahdi, la, bali Mahdimkubwa zaidi -hata hivyo kwa kuwa Khalifa wa zama hizo lazimaawe Mkureshi, Yesu (amani juu yake) hatakuwa Khalifa wa zamahizo. Khalifa wa zama hizo atakuwa huyo huyo Muhammad Mahdi.Wanasema kwamba hawa wawili kwa pamoja wataijaza duniakwa damu ya binadamu, na watamwaga damu nyingi zaidi kulikoiliyowahi kumwagwa hapo kabla katika historia ya ulimwengu huu.Mara tu watakapojitokeza wataanza kampeni hii ya umwagajidamu. Hawatahubiri wala kumsihi mtu wala kuonyesha isharayo yote. Na pia wanasema kwamba ingawa Yesu (amani juu yake)atakuwa kama mshauri au naibu wa Imam Muhammad Mahdi,na ingawa hatamu za uongozi zitakuwa miongoni mwa Mahdipeke yake, Yesu (amani juu yake) atamchochea Hadhrat ImamMuhammad Mahdi kuua watu wote ulimwenguni na atamshaurikuchukua hatua kali, yaani atayafanyia marekebisho yalemafundisho yake ya kuhurumiana aliyoyatoa hapo kabla, yaani,usishindane na shari yo yote na maovu, na "ukipigwa shavu mojaugeuze jingine pia."

Hivi ndivyo Waislamu na Wakristo waaminivyo kumhusuYesu (amani juu yake), na wakati ambapo ni kosa kubwawafanyavyo Wakristo kumwita binadamu mnyonge "Mungu,"imani za baadhi ya wafuasi wa Islam, miongoni mwao ikiwamohii firqa inayoitwa Ahli-Hadithi ambayo pia inajulikana kamaWahabii, kuhusu Mahdi mwenye kumwaga damu na Masihimwenye kumwaga damu, zinaathiri maadili yao vibaya sana, kwakiasi hiki ambapo kutokana na ushawishi mbaya wa imani hizo,ushirikiano wao na watu wengine hauko katika misingi ya uaminifuna nia nzuri wala hawawezi kuwa watiifu kikwelikweli na kikamilifukwa serikali isiyokuwa ya Kiislam. Watu wote wenye busarawatatambua kwamba imani kama hiyo, yaani kwamba wasiokuwaWaislamu washurutishwe, kwamba imma wasilimu mara mojaau wauawe ni lazima itapingwa kwa njia zote. Kila mtu mwenyekupenda mema atakubali mara moja kwamba kabla mtu

Page 12: Yesu katika India

12

hajatambua vya kutosha ukweli wa imani fulani, na kablahajatambua uzuri wa imani hiyo na mafundisho yake safi, haifaikabisa kumshurutisha kwa njia ya kumtia machungu makali iliaikubali Imani hiyo.Kinyume kabisa cha kuchangia katika ukuwajiwa Imani hiyo, kitendo hicho kitawapatia wapinzani fursa ya kuitoamakosa. Matokeo ya mwisho ya kanuni hii ni kwamba nyoyozitakuwa zimehamwa na ile sifa ya huruma ya kibinadamu nakwamba amani na haki ambazo ni sifa kuu za maadili yakibinadamu zinamhama mtu kabla na badala yake chuki na uaduivinaelekea kuota mizizi; zinazosalia nyuma ni silika za kinyamatu zikiendelea kufutilia mbali maadili yote mema. Lakiniitatambulika kwamba fundisho kama hilo halitakuwa limetoka kwaMwenyezi Munngu, ambaye hashushi adhabu Yake isipokuwa tubaada ya kukamilisha hoja Zake.

Kwa hiyo jambo hili ni lazima lifikiriwe kwa makini: Kwambaiwapo kuna ambaye haikubali Imani ya kweli kwa sababu badoyungali mjinga na hajui ukweli wake, hajui mafundisho yake nahajui uzuri wake, je, itakuwa jambo la busara kumwua mtu wanamna hiyo mara moja? Sivyo, mtu huyu anastahili kuhurumiwa;anastahili kufundishwa polepole kwa heshima kuhusu ukweli,uzuri na faida za kiroho za imani ile; siyo akikataa basi kukataakwake kujibiwe kwa upanga au bunduki.

Kwa hiyo, itikadi ya Jihadi inayopendekezwa na firqa hizi napia ile imani kwamba wakati umekaribia ambapo patatokea Mahdimwenye kumwaga damu ambaye jina lake litakuwa ImamMuhammad, na kwamba Masihi atateremka kutoka mbinguni ilikuja kumsaidia, na kwamba hao wawili kwa pamoja watawauawatu wote wasiokuwa Waislamu iwapo wataukataa Uislam, yotehaya ni kinyume kabisa na maadili ya kiakili. Je imani hii siyo ileimani ambayo inaua sifa zote nzuri na maadili mema ya binadamuna kutilia nguvu sifa za maisha ya porini? Wale wanaoshikiliaimani kama hizi wanaishi maisha ya kinafiki kwa kulinganishwana watu wengine, kwa kiasi hiki kwamba hawawezi kuonyeshautii wa kweli kwa viongozi wa serikali wa Imani nyingine, wanaapakiudanganyifu kuwa watiifu kwa viongozi hao, ambalo ni kosa.

Page 13: Yesu katika India

13

Hii ndiyo sababu baadhi ya firqa za Ahli-Hadithi nilizozitaja hivipunde zinaishi maisha ya namna mbili chini ya serikali yaKiingereza katika India inayotawaliwa na Uingereza. Kisirisiriwanawapa matumaini watu wa kawaida kuhusu ujaji wa siku zaumwagaji damu za Mahdi mwenye kumwaga damu nakuwafundisha jinsi watakiwavyo kufanya wakati huo, lakiniwanapokwenda kwa viongozi wa serikali wanawasifu kwa sifaza uwongo na kuwahakikishia kwamba wao hawaungi mkonomawazo ya namna hiyo. Lakini kama ni kweli kwamba waohawaungi mkono mawazo ya namna hiyo, kwa nini hawatangazimsimamo wao huo kimaandishi na kwa nini wao waendeleekusubiri ujaji wa yule Mahdi na Masihi ambao kama isemwavyowako kwenye kizingiti cha mlango tu, wakiwa tayari kuja kuungananao katika kampeni zao?

Kwa kifupi imani kama hizo zimeharibu kwa kiwango kikubwasana tabia za Mashekhe hawa; hawana uwezo wa kuwafundishawatu adabu wala amani. Kwa upande mwingine, kuwaua watuwengine bila sababu ya msingi, kwao ni wajibu mkubwa wa kidini.Ningefurahi sana kama firqa yo yote ya Ahli-Hadithi ingezipingaimani hizi, lakini kwa masikitiko makubwa siwezi kujizuia kusemakwamba miongoni mwa hizi firqa za Ahli-Hadithi(1) wako waleambao kwa sirisiri wanaamini kufika kwa Mahdi mwenyekumwaga damu na dhana zilizoenea kuhusu Jihadi. Hawazikubalifikra sahihi na wanakihesabu kitendo cha kuua kwamba ni chenyekustahili pale wapatapo fursa ya kuwaua watu wanaoungamaimani zingine, wakati ambapo hizi imani za kuwaua watu wenginekwa jina la Islam, au kuziamini tabiri kama huu utabiri wa kujaMasihi mwenye kumwaga damu na kutaka kuiendeleza silsila ya___________________________________________________

(1) Baadhi ya Ahli-Hadithi wanasema isivyopasa na bila haki yo yote katikavitabu vyao kwamba kufika kwa Mahdi kumekaribia sana: Kwamba atawatiagerezani watawala wa Kiingereza wa India na kwamba mfalme wa Kikristoatakamatwa na kuletwa mbele yake. Vitabu kama hivyo bado vinawezakupatikana katika nyumba za hawa Ahli-Hadithi, kimojawapo kikiwa Iqtarabus-Sa'at cha Ahli-Hadithi aliye mashuhrui sana, ambamo katika ukurasa wa 64taarifa kama hiyo inaweza kuonekana.

Page 14: Yesu katika India

14

Islam kwa umwagaji damu au kwa vitisho, ziko kinyume kabisana Qur`an Tukufu na Hadithi zenye kuaminika. Mtume wetuMtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake) alipatamateso makali sana mikononi mwa makafiri akiwa Makka na piabaadaye. Miaka kumi na mitatu aliyokaa Makka ilikuwa miaka yausumbufu na mateso ya kila aina - kuifikiria miaka hiyokunasababisha machozi yatiririke katika macho ya mtu. Lakiniyeye hakuinua upanga dhidi ya maadui zake, wala hakuujibuuchokozi wao mpaka wengi miongoni mwa masahaba zake narafiki zake wapenzi walipouawa kinyama; na mpaka yeyemwenyewe alipotiwa katika mateso ya kila namna kama vilekutiliwa sumu mara nyingi; na mpaka majaribio mengi ya kutakakumwua yalipofanywa. Lakini ulipizaji wa Mwenyezi Munguulipowadia, ikatokea kwamba wazee wa Makka na machifu wamakabila mbalimbali kwa pamoja waliamua kwamba kwa vyovyote vile mtu huyu ni lazima auawe. Wakati ule ule, MwenyeziMungu ambaye Ndiye Msaidizi wa wapendwa Wake na Msaidiziwa wakweli na wachamungu, Alimjulisha yeye kwamba hakunakilichosalia katika mji ule isipokuwa ouvu, na kwamba watu wamji ule walikuwa wamejiandaa kumwua na kwamba ni lazimaauhame mara moja. Kisha kulingana na amri ya kimbingu alihamiaMadina, lakini pamoja na hatua zote hizo maadui zakehawakumwachilia; wakamfuata kule na wakataka kuuteketezaUislam kwa njia yo yote ile. Wakati urukaji wao mipaka ulipofikiakikomo, na walipokuwa wao wenyewe wamejihalalishia adhabukwa kuwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, ambao waliwauasiyo katika ugomvi au vita bali hivi hivi tu, kutokana na utunduwao wa kuleta madhara, na ambao waliwanyang`anya mali zao.Lakini, licha ya yote haya, wakati Makka ilipotekwa Mtume wetuMtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)aliwasamehe wote hao. Kwa hiyo ni makosa makubwa na sijambo la haki kudhani kwamba Mtukufu Mtume (amani na rehemaza Mwenyezi Mungu juu yake) au Masahaba zake waliwahikupigana kwa nia ya kueneza Imani, au kwamba waliwahikumlazimisha mtu ye yote kujiunga na silsila ya Islam.

Page 15: Yesu katika India

15

Ni jambo la kuzingatiwa pia kwamba kwa kuwa wakati ulewatu wote walikuwa na chuki dhidi ya Islam, na kwa kuwawapinzani walikuwa wanafanya mpango wa kuuteketeza Uislamambao waliudhania kuwa ni dini mpya ambayo wafuasi wake nijumuiya ndogo tu, na kwamba kila mtu alikuwa na shauku yakuona Waislamu wakiteketezwa mapema au kusambaratishwaili pasiachwe hofu ya hao kuongezeka zaidi na kujiendeleza,Waislamu wa wakati ule waliwekewa vipingamizi hata katikamambo madogo sana, na mtu ye yote kutoka katika kabila lo lotealiyeupokea Uislam na akawa Mwislamu, imma aliuawa maramoja na watu wa kabila lake au aliishi katika hatari ya kudumu.Katika wakati kama huu, Mwenyezi Mungu, Akiwahurumia walewaliojiunga na Islam, Aliwatwisha adhabu watawala wadhalimu,yaani wawe wasaidizi kwa Islam na hivyo kufungua milango yauhuru wa Islam. Hii ilikuwa na shabaha ya kuondoa vipingamizikatika njia ya wale waliotaka kuikubali Imani hii; ilikuwa ni hurumaya Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu na haikumdhuru mtu ye yote.Lakini ni jambo lililo bayana kwamba watawala wasiokuwaWaislamu wa siku hizi hawajiingizi katika masuala ya Islam;hawapigi marufuku sunna muhimu za Kiislam. HawawauiWaislamu wapya; hawawatii gerezani au kuwatesa; kwa nini basiIslam iinue upanga wake dhidi ya watu hawa? Ni dhahiri kwambaIslam haijawahi kushabikia ulazimishaji. Iwapo Qur`an Tukufu,vitabu vya Hadithi na kumbukumbu za historia vitachunguzwakwa uangalifu na pale inapowezekana iwapo vitasomwa aukusikilizwa kwa makini, itafahamika kwa yakini madai kwambaIslam ilitumia upanga ili kueneza Imani hiyo kwa nguvu ni madaiya aibu na yasiyokuwa na msingi dhidi ya Islam.

Dai kama hilo dhidi ya Islam linafanywa na watu ambao badohawajaisoma Qur`an, Hadithi na taarikhi za kuaminika za Islamkatika hali ya kujitegemea wao wenyewe, bali wameutegemeasana uwongo na kwa hiyo wakaleta madai yenye makosa dhidiya Islam. Lakini najua kwamba wakati umeisha karibia ambapowale wenye njaa na kiu ya kutafuta ukweli watatiwa nuru ya kujuaiwapo kuna ukweli wo wote katika madai haya. Je tunaweza

Page 16: Yesu katika India

16

kuielezea Imani hii kuwa ni imani ya kutumia nguvu wakati kitabukitakatifu Qur`an, kinaelekeza wazi kwamba hakuna ushurutishajikatika mambo ya dini na kwamba hairuhusiwi kutumia shuruti aunguvu katika kumfanya mtu ajiunge na Islam? Je tunawezakumshitaki Mtume yule Mkuu kwamba alitumia mabavu dhidi yawatu wengine, ambaye usiku na mchana kwa miaka kumi namitatu aliwahimiza Masahaba zake wote mjini Makka wasirejesheuovu waliotendewa na maadui, bali wavumilie na kusamehe?Lakini wakati fujo ya maadui ilipopita kiasi na wakati kila mtualipokuwa anajitahidi kuufutilia mbali Uislam, Mwenyezi Mungumwenye ghera Aliamua kwamba ulikuwa ni wakati muafaka walewatu waliopigana kwa upanga lazima wateketezwe kwa upanga.Waila Qur`an Tukufu haijaidhinisha kulazimisha. Kamakulazimisha kungeidhinishwa na Islam, Masahaba wa Mtumewetu Mtukufu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)wasingeonyesha tabia ya watu wakweli na wanyoofu, wakati wamajaribu. Lakini utiifu na uaminifu wa masahaba wa Bwana wetuMtukufu Mtume (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake)ni jambo ambalo sina haja ya kulitaja. Si jambo la siri kwambamiongoni mwao kuna mifano ya msimamo imara ambao ni vigumukupata cha kuwalinganisha nao katika taarikhi za mataifa mengine;kundi la waaminio halikutetereka katika utiifu na msimamo waoimara hata walipokuwa chini ya kivuli cha upanga. Bali wakiwapamoja na Mtume wao Mkuu na Mtukufu walitoa uthibitisho waule msimamo imara ambao hakuna mtu awezaye kwa vyo vyotevile kuuonyesha mpaka moyo wake na kifua chake viwe vimetiwanuru ya imani ya kweli. Kwa kifupi hakuna kulazimisha katikaIslam. Vita katika Islam ni vya aina tatu: (1) vita ya kujihami, yaanivita kwa sababu ya kujilinda; (2) vita ya kuadhibu, yaani damukwa damu; (3) vita ya kupata uhuru, yaani vita ya kuvunja nguvuya wale wanaowaua wale wanaojiunga na Islam.

Kwa hiyo kwa kuwa hakuna maelekezo katika Islam kwambakila mtu aingizwe huku kwa kulazimishwa au kwa kutishiwakuuawa, ni jambo la upuuzi mtupu kusubiri kutokea kwa Mahdiau Masihi ye yote mwenye kumwaga damu. Haiwezi kutokea

Page 17: Yesu katika India

17

kamwe kwamba katika ulimwengu huu atokee mtu ambayekinyume na mafundisho ya Qur`an atumie upanga kuwasilimishawatu. Hili si jambo gumu kutambua wala haliko nje ya uwezo wamtu wa kufahamu. Ni watu wajinga tu walioangukia imani hiikutokana na uchoyo wao. Kwani takriban Mashekhe wetu wotewanajihangaisha na fikra zao potofu kwamba vita atakazopiganahuyu Mahdi zitawaletea utajiri mwingi sana kiasi kwambawatakuwa hawana mahali pa kuhifadhia utajiri huo, na kwa kuwatakriban Mashekhe wote wa hivi sasa ni watu walio fukara sana,wanasubiri usiku na mchana kutokea kwa huyo Mahdi ambayewanadhani atakuja kukidhi hizo tamaa zao za kiuchoyo. Kwa hiyowatu hawa humpinga kila mtu ambaye haamini kutokea kwa Mahdiwa namna hiyo; mtu wa namna hiyo atatangazwa mara mojakuwa ni Kaafir na yuko nje ya wigo wa Islam. Kwa hiyo mimi pianimekuwa Kaafir machoni pa watu hawa; na nimepewa ukafirihuo kwa misingi hiyo hiyo. Kwani, mimi siamini kutokea Mahdimwenye kumwaga damu na Masihi mwenye kumwaga damu.La, bali nayachukia mawazo ya kipuuzi ya namna hiyo nanayadharau sana. Na nimetangazwa kuwa Kaafir siyo tu kwasababu ya kukanusha kwangu kutokea kwa huyo anayesemekanakuwa Mahdi na huyo anayesemekana kuwa Masihi ambaowanaamini, bali pia nimetangaza hadharani baada ya kujulishwajambo hili na Mwenyezi Mungu kwa njia ya ufunuo kwamba MasihiAliyeahidiwa halisi na wa kweli ambaye pia ndiye Mahdi wa kweliambaye ishara za kutokea kwake zinapatikana katika Biblia naQur`an na ambaye kuja kwake kumeahidiwa pia katika Hadithi, nimimi mwenyewe; lakini ni mimi ambaye sikupewa upanga wowote wala bunduki. Nimeamrishwa na Mwenyezi Mungu kuwaitawatu kwa unyenyekevu na upole kwa Mwenyezi Mungu Ambayendiye Mungu wa kweli, na milele na Asiyebadilika Ambaye anaUtakatifu uliokamilika, Ujuzi uliokamilika, Amani iliyokamilika naHaki iliyokamilika.

Mimi ndiye nuru ya zama hizi za giza; yule ambaye atanifuatamimi ataokolewa katika kutumbukia ndani ya shimo lililotayarishwana Shetani kwa ajili ya wale wanaotembea katika giza.

Page 18: Yesu katika India

18

Nimeletwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu waulimwengu huu kwa Mungu wa kweli kwa njia ya amani na upolena kuzifunga upya hatamu za maadili mema katika Islam.Mwenyezi Mungu amenipatia ishara za kimbingu kwa ajili yakuwaridhisha wale wenye kutafuta haki. Amefanya mambo yaajabu katika kuniunga mkono; Amenifunulia siri za mambo yaghaibu na za mambo yajayo baadaye ambayo kulingana na vitabuvitakatifu ni ishara za mdai wa kweli wa ofisi ya kimbingu, naAkanijaalia elimu safi na takatifu. Kwa hiyo, zile nafsi ambazozinachukia ukweli na zinafurahishwa na giza zikaamua kunipinga.Lakini niliamua kuwahurumia binadamu - kwa kadiri nilivyoweza.Kwa hiyo huruma kubwa zote wawezazo kufanyiwa Wakristokatika zama hizi ni kuyaelekeza mawazo kwenye Mungu wa kweliAmbaye ameepukana na zile kasoro kama vile kuzaliwa na kufana kupata mateso; Yule Mungu ambaye aliziumba sayari zoteza awali huko mbinguni katika umbo la mviringo na katika kanuniYake ya hali ya asili aliweka kigezo hiki cha mwongozo wa kirohokwamba kama vile lilivyo umbo la mviringo, kuna Umoja ndaniYake Yeye na kwamba ndani ya Yeye hakuna welekea. Hii ndiyosababu vitu vilivyomo mbinguni havikutengenezwa kwa umbo lapembe tatu, yaani vitu ambavyo Mwenyezi Mungu aliviumba hapoawali kama vile ardhi, mbingu, jua na mwezi, nyota zote na viinivya asili vya kila kitu - vyote viko katika umbo la mviringo, ambapohali yao ya asili ya kuwa mviringo inaashiria kwenye Umoja. Kwahiyo hapawezi kuwa na kuwahurumia Wakristo zaidi kulikokwamba waelekezwe kwenye Ambaye alivyoviumbavinamtangaza Yeye kuwa ameepukana na wazo la utatu.

Na huruma kubwa kuliko zote kwa Waislamu ni lazimawageuzwe kimaadili na kwamba lazima juhudi ifanywe kuondoamatumaini ya kiudanganyifu wanayoyashikilia kuhusiana nakutokea kwa Mahdi na Masihi mwenye kumwaga damu, ambayoyako kinyume kabisa na mafundisho ya Kiislamu. Na nimekwishasema hivi punde kwamba mawazo ya baadhi ya Maulamaa wasiku hizi kwamba patatokea Mahdi mwenye kumwaga damuambaye ataeneza Uislam kwa ncha ya upanga, yote hayo yako

Page 19: Yesu katika India

19

kinyume cha mafundisho ya Qur`an na ni matokeo yasiyo chochote isipokuwa uroho na uchoyo.

Ili mtu mwenye akili timamu na Mwislamu mpenda ukweliaweze kuachana na imani na mawazo kama hayo, itamtosha tukuisoma Qur`an kwa uangalifu na kutafakari, na ataona kwambaNeno Takatifu la Mwenyezi Mungu liko kinyume kabisa na utoajiwa vitisho vya kuua ili kumlazimisha mtu ye yote kuingia katikaboma la Islam. Kwa kifupi, hoja hii moja tu inatosha kabisakuyakanusha mawazo haya ya udanganyifu. Hata hivyo, kutokanana hisia za huruma nimeamua kuyakanusha mawazo hayoyaliyokwisha tajwa kwa uthibitisho madhuhuti na ulio wazi kutokakatika historia, na kadhalika. Kwa hiyo, nitajaribu kuthibitisha katikakitabu hiki kwamba Yesu (amani juu yake) hakufia msalabani,hakwenda juu mbinguni wala isidhaniwe kamwe kwamba atakujatena ardhini akitokea mbinguni, bali alikufa akiwa na umri wa miaka120 mahali paitwapo Srinagar katika Kashmir na kwamba kaburilake linapatikana katika mtaa wa Khan Yar katika mji ule. Ili kutoamaelezo kwa uwazi zaidi nimeugawa uchunguzi huu katika surakumi; na neno la mwisho ambalo linajumuisha ushahidi wa Biblia,ushahidi wa Qur`an Tukufu na Hadithi, ushahidi wa vitabu vyatiba, ushahidi wa kumbukumbu za historia, ushahidi wa mapokeoya mdomo ambayo yamerithiwa toka kizazi hadi kizazi, ushahidiwa ziada wa kimazingira, ushahidi wa hoja za kiakili na ushahidiwa ufunuo mpya kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuhusu kujakwangu. Hizi zinajumuika kuwa sura kumi. Katika sura ya 9kutakuwa na malinganisho mafupi kati ya Ukristo na Uislam nazitapangwa hoja zenye kuthibitisha ukweli wa Islam. Katika suraya 10 kutakuwa na maelezo marefu kidogo kuhusu malengo yakutekelezwa ambayo kwa ajili ya hayo mimi kuwa ndiye MasihiAliyeahidiwa na kuwa mimi nimekuja kutoka kwa MwenyeziMungu. Na mwishowe, kutakuwa na neno la mwisho ambamoyataratibiwa maagizo fulani fulani.

Natumaini wasomaji wa kitabu hiki watakisoma kwa bidii.Sitazamii kwamba watautupilia mbali ukweli uliomo humukutokana na chuki isiyokuwa na sababu. Ningependa

Page 20: Yesu katika India

20

kuwakumbusha kwamba huu sio uchunguzi wa juu juu tu; baliuthibitisho uliomo ndani ya kitabu hiki umepatikana baada yautafiti wa ndani na wa kina.

Namwomba Mwenyezi Mungu anisaidie katika jukumu hilina aniongoze kwa njia ya ufunuo na mwongozo Wake maalumna kwa njia ya Nuru kamili ya ukweli - kwani elimu ya kweli nautambuzi halisi hushuka kutoka Kwake, na kwa njia ya idhinikutoka Kwake Yeye tu, niweze kuiongoza mioyo ya watu kwenyeukweli. Amin! Amin!

MIRZA GHULAM AHMAD

Qadian, Tarehe 25 Aprili, 1899.

Page 21: Yesu katika India

21

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa ukarimu,

SURA YA KWANZA

Ifahamike kwamba ingawa Wakristo wanaamini kwambaYesu (amani juu yake) baada ya kukamatwa kwa sababu ya usalitiwa Yuda Iscariot na kusulubiwa na kufufuka alikwenda mbinguni,hata hivyo, kulingana na Biblia Takatifu inaelekea kwamba imaniyao hii ni yenye makosa moja kwa moja. Mathayo (sura ya 12aya ya 40) anasema kwamba kama vile Yona alivyokaa michanamitatu na mausiku matatu katika tumbo la samaki, vivyo hivyoMwana wa Adamu nae atakaa michana mitatu na mausiku matatundani ya tumbo la ardhi; Sasa ni dhahiri kwamba Yona hakufandani ya tumbo la samaki; sana sana kilichotokea ni kwambaalikuwa katika hali ya kuzirai au kuzimia. Vitabu vitakatifu vyaMwenyezi Mungu vinashuhudia kwamba kwa msaada waMwenyezi Mungu Yona alibakia hai katika tumbo la samaki naalitoka humo akiwa hai; na hatimae watu wake wakampokea.Iwapo basi Yesu (amani juu yake) alifia ndani ya tumbo la "ardhi",pangekuwapo na kufanana gani kati ya mtu mfu na aliye hai, naingewezekanaje kulinganisha mtu aliyekufa na aliye hai? Baliukweli ni kwamba Yesu alikuwa nabii wa kweli na kwa kuwa alijuakwamba Mwenyezi Mungu Ambaye yeye alikuwa mpendwa wakeAtamwokoa na kifo cha laana, alitoa utabiri kwa njia ya methaliiliyofunuliwa kwake na Mwenyezi Mungu ambamo alidokezahatakufa juu ya msalaba wala hatakata roho juu ya ubaouliolaaniwa; kinyume cha hayo, kama vile ilivyokuwa kwa nabiiYona, yeye atapitia katika hali ya kuzimia tu. Katika methali hiyoamedokeza pia kwamba atatoka nje ya tumbo la ardhi na kishaataungana na watu, na kama vile ilivyokuwa kwa Yona,ataheshimiwa na watu hao. Kwa hiyo, utabiri huu pia ulitimia;kwani Yesu, akiwa ametoka katika tumbo la ardhi, aliyaendeamakabila yake yaliyoishi nchi za Kashimir, Tibet na kadhalika,yaani yale makabila kumi ya Waisraeli ambao miaka 721(1)

___________________________________________________(1) Licha ya hawa, Wayahudi wengi zaidi walilazimishwa kuishi ugeninikatika nchi za mashariki kutokana na unyama wa Wababilonia.

Page 22: Yesu katika India

22

kabla ya Yesu yalitekwa nyara kutoka Samaria na Shalmaneser,mfalme wa Assur na akaondoka nayo. Hatimaye makabila hayayalikuja India na yakajifanyia maskani katika sehemu mbalimbaliza nchi hii. Na kwa vyo vyote vile ni lazima Yesu awe aliifanyasafari hii, kwani shabaha ya kimbingu ya kuja kwake ilikuwa nilazima akutane na Wayahudi waliopotea ambao walikuwawakiishi katika sehemu mbalimbali za India; sababu yake ilikuwakwamba kwa hakika hawa ndio waliokuwa kondoo waliopoteawa nyumba ya Israeli ambao hata ile imani ya mababu zaowalikuwa wameiacha wakiwa katika nchi hizi na wengi waowakawa wameingia katika dini ya Kibuddha na kurejea polepolekwenye ibada ya masanamu. Dakta Bernier, kwa kuwanukuu watukadha walio wasomi, anasema katika kitabu chake kiitwachoTravels kwamba Wakashmiri kwa hakika ni Wayahudi ambaowakati wa mtawanyiko uliotokea wakati wa zama za yule mfalmewa Assur, walihamia katika nchi hii.(1)

Ilmuradi ilikuwa ni lazima kwa Yesu (amani juu yake) kutafutamahali walikokuwa hawa kondoo waliopotea ambao, baada yakuja katika nchi hii ya India, wakachangnyika na watu wengine.Hivi punde nitatoa ushahidi kwamba kwa hakika Yesu (amani juuyake) alikuja India, na kisha, hatua kwa hatua akaenda Kashmirna kuwagundua kondoo waliopotea wa Israeli wakiwa miongonimwa watu walioungama imani ya Kibuddha na kwamba hatimaewatu hawa walimpokea kama vile watu wa nabii Yonawalivyompokea Yona. Na hili lilikuwa ni jambo la lazima, kwaniYesu alisema mara chungu nzima kwamba ametumwa kwa ajiliya kondoo waliopotea wa Israeli.

Licha ya hayo, ilikuwa lazima aepukane na kifo juu yamsalaba kwani ilikwisha semwa katika kitabu kitakatifu kwambaye yote mwenye kutundikwa juu ya mti amelaaniwa. Na ni kufruya kikatili na isiyokuwa ya haki kumnasibisha na laana mtumashuhuri kama Masihi Yesu, kwani kulingana na maoni ya wotewale wanaoijua lugha hii, neno La`nat au laana lina marejeokwenye hali ya moyo wa mtu.___________________________________________________________(1) Dr. Bernier, Travels Vol. II. Appendix I

Page 23: Yesu katika India

23

Mtu atasemekana kuwa amelaaniwa wakati moyo wake,baada ya kutenganishwa na Mwenyezi Mungu unakuwa mweusikweli kweli; unapokuwa umenyimwa amani ya kimbingu namapenzi ya kimbingu; ukiwa hauna kabisa elimu Yake; akiwaamepofushwa kama shetani, anakuwa amejazwa sumu ya ukafiri;wakati ambapo hapabaki hata chembe moja ya mapenzi na elimuya kimbingu katika nafsi yake; wakati fungamano la utii linapokuwalimevunjika, na kati yake yeye na Mwenyezi Mungu panazukachuki, dharau, kinyongo na uadui, kwa kiasi hiki kwamba MwenyeziMungu na yeye wanakuwa maadui wao kwa wao; na wakatiMwenyezi Mungu Anapochoshwa na yeye; na yeye kuwaamechoshwa na Mwenyezi Mungu; kwa kifupi wakati anapokuwamrithi wa sifa zote za Shetani - na hii ndiyo sababu Shetanimwenyewe anaitwa mlaaniwa (1). Ni dhahiri kwamba maana yaneno Mal`un yaani mlaaniwa ni chafu sana hivi kwamba haiwezikunasibishwa kwa mtu ye yote aliye mchamungu ambayehukaribisha mapenzi ya Mwenyezi Mungu katika moyo wake.Laahaula! Wakristo hawakutafakari sana kuhusu maana ya laanawalipobuni imani hii; vinginevyo wasingaliweza kutumia neno bayakama hilo kwa mtu mchamungu kama Yesu. Je, tunawezakusema kwamba moyo wa Yesu uliwahi kutengana na MwenyeziMungu, kwamba alimkana Mungu, kwamba alimchukia Munguna akawa adui Yake? Je, tunaweza kudiriki kudhania kwambaYesu aliwahi kuhisi katika moyo wake kwamba alikuwaametengwa na Mwenyezi Mungu, kwamba alikuwa adui waMwenyezi Mungu na kwamba alikuwa amezama katika giza laukafiri na ukaini? Iwapo basi Yesu kamwe hakuwa katika hali yamoyo ya namna hiyo, kwamba moyo wake ulikuwa kila maraumejawa na mapenzi na nuru ya elimu ya kimbingu, je ipo hajakwenu watu wenye hekima kutafakari iwapo tunaweza kusemakwamba si moja tu bali maelfu ya laana kutoka kwa MwenyeziMungu yalishuka katika moyo wa Yesu pamoja na maana mbayayote ya laana hizo?___________________________________________________________(1) Tazama makamusi: Lisaanul - Arab, Sihah Jauhar, Quamus, Muhit,Tajul-Arus na kadhalika.

Page 24: Yesu katika India

24

Hasha. Tunawezaje basi kusema kwamba (Mungu apishe mbali),alikuwa amelaaniwa? Ni jambo la kusikitisha kwamba mtuanapotoa matamshi kuhusu jambo fulani baada ya kuwa namsimamo kuhusu imani fulani si rahisi kuiachilia imani hiyo hatakama upuuzi wa imani hiyo utabainishwa kwa kila hali.

Tamaa ya kupata uokovu, kama imejengwa katika misingiya ukweli ni jambo la maana, lakini kuna faida gani kuwa na tamaaya uokuvu ambayo inaua ukweli na inaipendelea imaniinayosema, kumhusu nabii mtukufu na binadamu aliyekamilikakwamba alipitia katika hali ambapo alitenganishwa na MwenyeziMungu na ambamo badala ya kuwa na moyo mmoja na msimamommoja pakatokea hali ya kukaa mbali na kujitenga, uadui na chuki,na badala ya nuru giza likauzunguka moyo wake?

Ifahamike vilevile kwamba hali hii siyo tu haiendani na unabiina utume wa Yesu (amani juu yake) bali ni kinyume na madaiyake ya kuwa na umashuhuri wa mambo ya kiroho, utakatifu,upendo na elimu kumhusu Mungu ambayo ameyaeleza kwakuyakariri katika Injili. Wewe angalia katika Biblia tu; humo Yesuanadai waziwazi kwamba yeye ndiye Nuru ya ulimwengu,kwamba yeye ndiye Njia, na kwamba yeye anao uhusiano mkubwasana wa upendo kwa Mwenyezi Mungu; kwamba yeyeameheshimika kwa kuzaliwa uzazi ulio safi na kwamba yeye yuMwana mpendwa wa Mwenyezi Mungu. Inawezekanaje sasa,pamoja na husiano zote hizi zilizo safi na takatifu, laana yenyemaana zote mbaya iweze kunasibishwa na Yesu? Kamwehaiwezekani. Kwa hiyo hapana shaka kwamba Yesuhakusulubiwa, yaani hakufia msalabani, kwa sababu haiba yakehaikustahili na matokea ya kifo juu ya msalaba. Na kwa kuwahakusulubiwa aliepukana na kunasibishwa na sifa mbaya zalaana, na bila shaka hii inathibitisha pia hakupaa mbinguni, kwasababu kupaa mbinguni ni sehemu tu ya mpango wote huu na nimatokeo ya hili wazo kwamba yeye alisulubiwa. Kwa hiyoikithibitishwa kwamba hakulaaniwa wala hakukaa Jahanamu kwamuda wa siku tatu, wala hakufa, hii sehemu nyingine ya mpangohuu, yaani kwamba alipaa mbinguni, itathibitika kuwa ni ya

Page 25: Yesu katika India

25

uwongo. Kuhusu jambo hili Biblia inazo hoja zingine zaidi ambazonitaendelea kuzitaja hapa chini. Moja ya hoja hizo ni kauli ya Yesu:"Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni kwendaGalilaya". (Mathayo Sura ya 26 aya ya 32). Aya hii inaonyeshawaziwazi kwamba baada ya kutoka kaburini Yesu alikwendaGalilaya na siyo mbinguni. Na maneno ya Yesu "baada ya kufufukakwangu" hayana maana ya kufufuka kwake baada ya kufa; bali,kwa kuwa machoni pa Wayahudi na watu wa kawaida "alifiamsalabani," aliyatumia mapema yale maneno ambayoyatakubaliana na vile watakavyo mfikiria hapo baadaye. Na kwakweli mtu ambaye aliwekwa msalabani na ambaye mikono yakena miguu yake ilipigiliwa misumari mpaka akazimia kutokana nauchungu, ni kana kwamba alikuwa amekufa; iwapo mtu huyoaliokolewa kutoka katika baa hilo na kama akaweza kupata fahamutena, haitakuwa kutia chumvi kuhusiana na mtu kama huyokusema kwamba amepata uhai tena. Na hapana shaka kwamba,baada ya mateso yote hayo, kuepushwa kwake Yesu na kifoilikuwa ni mwujiza; halikuwa jambo la kawaida. Lakini kudhaniakwamba alikufa ni makosa. Ni kweli kwamba ndani ya vitabu vyaAgano Jipya maneno ya namna hii yanapatikana, lakini hili ni kosala waandishi wa vitabu hivyo, kama walivyoweza kufanya makosaya kurikodi matukio kadhaa ya kihistoria. Wafasirina waliovifanyiautafiti vitabu hivi wanakubali kwamba vitabu vya Agano Jipya vinasehemu mbili: (1) maagizo ya kiroho yaliyopokelewa na wanafunzikutoka kwa Yesu (amani juu yake) ambayo ndiyo kiini chamafundisho ya Injili; (2) matukio ya kihistoria - kama vile ukoo waYesu; kutiwa kwake mbaroni na kupigwa; kuwepo kwa kidimbwicha miujiza wakati wa zama zake na kadhalika. Haya yaliandikwana waandishi wenyewe; hayakufunuliwa; bali yaliwekwa humokulingana na mawazo ya waandishi. Katika baadhi ya sehemukuna kutiwa chumvi kulikozidi kiasi, kama pale mahalipanaposema kwamba kama miujiza na kazi zote za Yesuzingehifadhiwa katika vitabu dunia hii isingalikuwa na uwezo wakuvihifadhi vitabu hivyo. Huku ni kutia chumvi kulioje!

Licha ya hayo, si kinyume cha matumizi ya misemo

Page 26: Yesu katika India

26

kulielezea balaa kubwa lililompata Yesu kuwa ni kifo. Iwapo mtu,baada ya kupita katika hali ya kufa na kupona, hatimayeanaokolewa, msemo wa kawaida wa watu wote huielezea halihiyo kwa njia ya methali - "amepewa uhai mpya", na hakuna watuhata kama watoke nchi gani, watasita kulielezea jambo hili kwanjia hii.

Baada ya yote hayo kusemwa, ni lazima izingatiwe kwambakatika Injili ya Barnabas, ambayo ni lazima inapatikana katikaJumba la Makumbusho la Uingereza, imetamkwa kwamba Yesuhakusulubiwa wala hakufia msalabani. Sasa tunaweza kusemavizuri sana kwamba ingawa kitabu hiki si miongoni mwa vitabuvilivyomo katika Injili na kimekataliwa moja kwa moja, lakini hapanashaka kwamba ni kitabu cha kale na ni cha zama zile zile ambapoInjili zingine ziliandikwa. Je, hatuna fursa ya kukihesabu kitabuhiki cha kale kuwa ni kitabu cha historia ya zama za kale nakukitumia kama kitabu cha historia? Je, si dhahiri kutokana nakitabu hiki kwamba kwa uchache wakati wa tukio la msalaba watuhawakukubaliana kwa kauli moja kuhusu Yesu kufa juu yamsalaba? Tena, licha ya hayo, wakati ambapo katika Injili nnezenyewe kuna methali kama vile ya mtu aliyefariki kusemwakwamba, hakufa bali amelala, si jambo lisiloingia akilini kuwazakwamba hali ya kuzimia inaweza kuelezewa kama hali ya kifo.Nimekwisha sema kwamba nabii hawezi kusema uwongo. Yesualizilinganisha siku zake tatu za kukaa kaburini na zile siku tatuza Yona za kukaa ndani ya nyangumi. Hii inaonyesha tu kwambakama vile Yona alivyobakia hai kwa siku tatu katika tumbo lanyangumi, ndivyo hivyo Yesu alivyobakia hai kwa siku tatu akiwakaburini. Makaburi ya Mayahudi ya siku zile hayakuwa kamamakaburi yetu ya siku hizi; yalikuwa na nafasi kubwa na yalikuwana mlango upande mmoja ambao ulifunikwa kwa jiwe kubwa. Nahivi punde nitathibitisha nitakapofika mahali panapostahili kwambakaburi la Yesu ambalo limegunduliwa hivi karibuni mjini Srinagarkatika Kashmir ni la namna ile ile kama alimowekwa Yesu wakatiakiwa katika hali ya kuzimia.

Kwa kifupi, aya niliyokwisha inukuu hivi karibuni inaonyesha

Page 27: Yesu katika India

27

kwamba baada ya kutoka kaburini Yesu alikwenda Galilaya. NaInjili ya Mtakatifu Marko inasema kwamba baada ya kutoka kaburinialionekana katika barabara inayokwenda Galilaya, na hatimayeakakutana na wale wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa wakilachakula; aliwaonyesha mikono na miguu yake ambayo ilikuwana majeraha na wakadhania pengine yeye alikuwa kiumbe chakiroho. Ndipo akawaambia: " Tazameni mikono yangu na miguuyangu, ni mimi yule yule; nishikeni muone, kwani kiumbe chakiroho hakina nyama na mifupa kama hii mnayoniona nayo" (Luka24:39). " Akatwaa kutoka kwao samaki aliyechemshwa na kipandecha sega la asali akala mbele yao. (Luka 24:42-43).

Aya hizi zinaonyesha kwamba ni jambo la yakini kabisakwamba Yesu kamwe hakwenda mbinguni; baada ya kutokakaburini alikwenda Galilaya; - akiwa kama watu wa kawaida, akivaanguo za kawaida na akiwa na mwili wa kibinadamu. Kamaalifufuliwa baada ya kufa, ilikuwaje mwili huo wa kiroho ulikuwabado una vidonda alivyovipata msalabani? Alikuwa na haja ganiya kula? Na kama alilhitaji chakula wakati ule, ni lazima aweanahitaji chakula hata sasa.

Wasomaji kwa vyo vyote vile wasibabaishwe na jambo hili:msalaba wa Wayahudi haukuwa kama kitanzi kinachotumikakumnyongea mtu siku hizi, ambacho mtu akitiwa, takriban nijambo lisilowezekana kutoka humo akiwa hai, kwani msalaba wasiku zile haukuwa na kamba ya kuvishwa shingoni mwa mhusika,wala hakudondoshwa kutoka kwenye ubao kisha ndipoaning'inizwe; bali aliwekwa tu msalabani na mikono yake na miguuikapigiliwa misumari kwenye msalaba huo; na iliwezekana sanakwamba iwapo baada ya kumsulubisha mtu na kumpigiliamisumari iliamuliwa baada ya siku moja au mbili - kumsamehemtu yule na kuokoa maisha yake, aliteremshwa chini akiwa haikabla mifupa yake haijavunjwa, ikihesabiwa kwamba adhabualiyokwisha pata ilikuwa inatosha. Na kama iliamuliwa kumuua,alibakizwa msalabani kwa akali kwa siku tatu; maji au mkatehavikuruhusiwa kuletwa karibu naye, na aliachwa katika hali hiiakiwa juani kwa siku tatu au zaidi, ndipo mifupa yake ikavunjwa

Page 28: Yesu katika India

28

na hatimaye kutokana na mateso hayo akafa. Lakini rehema yaMwenyezi Mungu Mwenye nguvu ilimwokoa Yesu katika matesohaya ambayo yangemaliza maisha yake. Usomaji wa Injili hizikwa uangalifu utaonyesha kwamba Yesu (amani juu yake)hakubakia msalabani kwa siku tatu; hakulazimika kuumwa nanjaa au kiu kwa siku tatu; wala mifupa yake haikuvujwa. Balialibakia juu ya msalaba kwa saa mbili tu, na rehema na hurumaya Mwenyezi Mungu viliweza kuufanya usulubishaji huo ufanyikejioni ya siku ile, ambayo ilikuwa Ijumaa, na muda mfupi tu ulisaliakabla ya jua kuzama, na siku iliyofuata ikiwa ni Sabato ambayoilikuwa sikukuu ya Fasah ya Mayahudi. Na kulingana na desturiza Kiyahudi ilikuwa hairuhusiwi na lilikuwa kosa la jinai ambalokwalo mtu aliadhibiwa, kumfanya mtu ye yote abakie juu yamsalaba katika siku ya Sabato au usiku wa kuamkia siku hiyo; naMayahudi, kama walivyokuwa Waislamu, walitumia kalenda yamwezi ambapo usiku huhesabiwa kuwa upande mmoja, kulikuwana haya mazingira ambayo yalisababishwa na sababu za kidunia,na kwa upande mwingine, Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvuAlisababisha kuwepo kwa haya mazingira ya kimbingu, yaaniilipotimia saa ya sita kukatokea dhoruba ya vumbi ambayoilisababisha kuwepo giza ardhini kwa muda wa saa tatu (MarkoSura 15: aya ya 33). Saa hii ya sita ilikuwa baada ya saa sitamchana, yaani ilipokaribia magharibi. Sasa basi, Mayahudiwalishikwa na wasiwasi kutokana na giza hili nene, isije usiku waSabato ukawapita na isije kwa kunajisi utakatifu wa Sabato,wakastahili adhabu. Kwa hiyo, kwa haraka wakamwondoa Yesumsalabani pamoja na wale wezi wawili. Zaidi ya hayo yote,kulikuwa na sababu nyingine ya kimbingu, kwamba Pilatoalipokuwa akiendesha mahakama yake, mkewe alimpelekeaneno kwamba asimfanye lo lote mtu yule mchamungu (yaaniasijaribu kumpa adhabu ya kifo), kwa sababu alisema, alipatandoto usiku ule, ambayo ilimsumbua sana. (Mathayo Sura 2 ayaya 19). Kwa hiyo, huyu malaika ambaye mkewe Pilato alimwonakatika ndoto yake - atatuthibitishia sisi na watu wote wenye akilitimamu, kwa yakini, kwamba Mwenyezi Mungu hakukusudia kuwa

Page 29: Yesu katika India

29

Yesu afe msalabani. Tangu ile siku ya kuumbwa kwa ulimwenguhuu, haijatokea kwamba Mwenyezi Mungu apenyeze habari katikamoyo wa mtu kwa njia ya ndoto kwamba jambo fulani litatokeakwa njia fulani, kisha jambo hilo lisitokee. Kwa mfano, Injili yaMathayo inasema kwamba malaika wa bwana alimjia Yusufukatika ndoto na kusema, "Ondoka na umchukue mtoto pamojana mama yake na mkimbilie Misri, na mkae huko mpakanikuambie." Kwani Herod anamtafuta huyo mtoto ili amwue."Mathayo 2:13). Sasa, kuna mtu ye yote awezaye kusemakwamba Yesu angeweza kuuawa nchini Misri? Kadhalika ilendoto ambayo mkewe Pilato aliiota ilikuwa ni sehemu ya mipangoya Mwenyezi Mungu, na kamwe haiwezi kuwa kwamba mpangohuu ushindwe kufikia shabaha yake; na kama vile ambavyouwezekano wa Yesu kufa akiwa safarini nchini Misri ungekuwakinyume na ahadi maalum ya Mwanyezi Mungu, kwa hiyo haponapo, ni jambo lisiloingia akilini kwamba malaika wa MwenyeziMungu Mwenye nguvu amtokee mkewe Pilato na kumwelekezaaseme kwamba iwapo Yesu atakufa juu ya msalaba halitakuwajambo zuri kwake, lakini kutokea huku kwa malaika kuwe hakunamaana na kwamba Yesu aachiliwe kufa juu ya MSALABA. Je,kuna mfano wo wote wa namna hiyo ulimwenguni? Hakuna.Dhamiri safi ya watu wote wema, itakapojulishwa kuhusu ndotoya mkewe Pilato, bila shaka itashuhudia kwamba ni jambo la kwelikwamba shabaha ya ndoto ile ilikuwa kuweka misingi yakumwokoa Yesu. Naam, ni hiyari ya mtu kuukana hata ukweli uliowazi kutokana na husuda itokanayo na imani ya mtu; anawezakuukataa, lakini uadilifu utatulazimisha kuamini ndoto ya mkewePilato kuwa ni sehemu ya ushahidi mzito wa Yesu kuepukana namsalaba. Na Injili ya kwanza kwa daraja miongoni mwa hizi, yaaniInjili ya Mathayo imeuhifadhi ushahidi huu. Kwa hiyo, ingawaushahidi madhubuti nitakaouratibu katika kitabu hiki unafutilia mbaliuungu wa Yesu na itikadi ya kafara, hata hivyo uaminifu na kupendahaki vinatutaka tusiwe wenye kupendelea imani ya kijamii au yakijadi katika suala la ukweli. Toka siku ya kuumbwa kwa binadamuhadi leo akili fupi ya binadamu imewekeza maelfu ya vitu katika

Page 30: Yesu katika India

30

uungu na Umungu, kwa kiasi hiki kwamba hata paka na nyokawameabudiwa; hata hivyo watu wenye hekima, kwa msaada wakimbingu wameendelea kuokolewa na imani za kishirikina kamahizo.

Na miongoni mwa ushahidi wa Biblia wenye kuunga mkonokuepushwa kwa Yesu na kifo juu ya msalaba ni safari yake yakwenda mahali pa mbali ambayo aliianza baada ya kutoka nje yakaburi.

Mnamo asubuhi ya Jumapili kwanza alikutana na MariaMagdalena ambaye mara moja aliwajulisha wale wanafunzikwamba Yesu alikuwa hai, lakini hawakuamini. Kisha alionekanakwa wawili miongoni mwa wale wanafunzi walipokuwawanakwenda nje ya mji, na mwishoni akajitokeza kwa wale kumina mmoja waliokuwa wakila chakula na akawalaumu kwa ugumuwao na utovu wa imani (Mathayo 16:9 - 14), na wanafunzi waYesu walipokuwa wanakwenda kuelekea kwenye makazi yaitwayoEmmau ambayo yalikuwa umbali wa maili 33/4 kutoka YerusalemYesu akakutana nao: na walipoyakaribia makazi yale, Yesuakatangulia ili kutengana nao, lakini hawakumruhusu kwendazake, wakisema kwamba usiku ule watakuwa pamoja. Kishaakala nao chakula, na wote hao pamoja na Yesu walilala kwenyekijiji kiitwacho Emmau (Luka 24:13-31). Sasa, kusema kwambaYesu alifanya yote hayo akiwa na mwili wa kiroho (ambayo ndiyohali inayotakiwa kuwa ya mwili baada ya kifo), ambayoyaliwezekana kufanywa na mwili wa kidunia tu, - kama kwa mfanokula, kunywa na kulala na kutembea safari ndefu ya kwendaGalilaya ambao ulikuwa kwenye umbali wa maili sabini kutokaYerusalem ni kusema jambo lisilowezekana na lililo kinyume chaakili. Na, licha ya ukweli kwamba kutokana na upendeleo wakibinafsi taarifa za Injili zimehitilafiana, hata hivyo, karina zakekama zilivyo zinaonyesha waziwazi kwamba Yesu alikutana nawanafunzi wake akiwa na mwili wa kawaida wa kibinadamuuwezao kufa, na kusafiri safari ndefu ya kwenda Galilaya kwamiguu; alionyesha vidonda vyake kwa wale wanafunzi, alikula naochakula cha usiku na akalala pamoja nao. Hivi punde nitathibitisha

Page 31: Yesu katika India

31

kwamba alitumia marhamu kwa ajili ya vidonda vyake.Sasa, hapa mtu anatakiwa afikirie iwapo, baada ya kujipatia

mwili wa kiroho wenye kudumu milele, yaani, baada ya kupataule mwili usiokufa ambao ulimwepusha na ulazima wa kula nakunywa, kukaa mkono wa kulia wa Mwenyezi Mungu nakuepukana na vidonda vya aina yo yote, na maumivu, na udhaifuwa kila aina, bado ulikuwa na kasoro moja, ingawa ulikuwa nasifa za utukufu wa Mwenyezi Mungu wa Milele na wa Tangu naTangu; - na udhaifu huo ni huu ya kwamba mwili wake ulikuwana vidonda vipya vya msalaba na misumari, ambavyo vilikuwavikitoa damu na vilikuwa vichungu sana na ambavyo vilitayarishiwamarhamu, na hata baada ya kupata mwili wenye utukufu nausiokufa, mzima wa milele, usio kasoro, mkamilifu, nausiobadilika, mwili huo huo ukaendelea kupatikana na kasoro zaaina nyingi; Yesu mwenyewe aliwaonyesha wanafunzi wakenyama na mifupa ya mwili wake, na tena si hilo tu, bali yalikuwakopia mapigo ya njaa na kiu - vitu vya lazima vya mwili wenye kufa,vinginevyo palikuwa na haja gani kwake wakati wa safari yakwenda Galilaya, kufanya vitu visivyokuwa na faida kama vile kulana kunywa maji, kupumzika na kulala? Hapana shaka, katikaulimwengu huu, njaa na kiu ni vitu vyenye kuutia uchungu mwiliwenye kufa ambapo huweza kuleta kifo iwapo njaa na kiu hiyo nikali. Kwa hiyo hakuna shaka kwamba Yesu hakufa juu ya msalaba,wala hakupata mwili mpya wa kiroho; bali alikuwa katika hali yakuzimia inayofanana na kifo. Na, kwa rehema ya Mwenyezi Munguikatokea kwamba lile kaburi alimowekwa halikuwa kama makaburiya nchi hii; kilikuwa chumba chenye kuingiza hewa. Na katikasiku zile ilikuwa desturi ya Wayahudi kulifanya kaburi liwe na hewakama nyumba yenye nafasi kwa kuliwekea mlango. Makaburi yanamna hiyo yalitayarishwa mapema; na maiti ziliingizwa humokulingana na hali iliyosababishwa na tukio. Injili zinatoa ushahidiulio wazi kuhusu jambo hili: Luka anasema; "Hata ilipoingia sikuya kwanza ya wiki, mapema sana asubuhi, (yaani ilipokuwa badokuna giza - giza) hao (yaani wale wanawake) walikwenda kaburiniwakipeleka viungo vya manukato pamoja na vitu vingine

Page 32: Yesu katika India

32

walivyokuwa wametayarisha. Na wakakuta lile jiwelimebiringishwa kando ya kaburi (hebu fikiria jambo hili!) nawakaingia ndani lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu. (Luka24:13-31) Hebu yatafakari kwa muda maneno haya; "wakaingiandani." Ni dhahiri kwamba mtu anaweza tu kuliingia kaburi ambalolinafana na chumba na lina mlango. Nitaeleza ndani ya kitabuhiki, patakapofikia mahali pake maalumu, kwamba kaburi la Yesu(amani juu yake) lililogunduliwa hivi karibuni mjini Srinigar,Kashmir, lina mlango na dirisha kama kaburi hili. Hii ni dalili yetuambayokama itafikiriwa kwa makini itawaongoza wachunguzi wa jambohili kwenye uamuzi mkubwa na wa muhimu sana.

Na miongoni mwa ushahidi wa Injili ni maneno ya Pilatoyaliyorikodiwa na Mtakatifu Marko: "Hata ilipokwisha fikia kuwajioni, kwa sababu ni maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya Sabato,akaenda Yusufu, mtu wa Arimathaya, Mstahiki, mtu wa barazaya mashauri, naye mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu,akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato, akauomba mwili wakeYesu. Lakini Pilato akastaajabu iwapo tayari alikuwa amekwishakufa. (Marko 15:42 - 44). Hii inaonyesha kwamba katika kile kipindicha wakati wa kusulubiwa wenyewe kulikuwa na shaka iwapoYesu alikuwa amekufa kweli, na shaka hiyo haikutoka kwa mtumwingine isipokuwa yule aliyejua kutokana na uzoefu, kuwa nimuda gani ilimchukua mtu kufa juu ya msalaba.

Na miongoni mwa ushahidi wa Injili ni hii aya, "Basi Wayahudikwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku yasabato, (maana ile Sabato ilikuwa siku kubwa) walimwomba Pilatomiguu yao ivunjwe wakaondolewe. Basi askari wakaenda,wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili aliyesulubiwa pamojanaye. Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa,hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma mkukiubavuni; na mara ikatoka damu na maji." (Marko 15:42-44). Ayahizi zinaonyesha wazi wazi kwamba ili kuutoa kabisa uhai wamtu aliyesulubiwa ilikuwa ni desturi katika siku zile kumweka mtuhuyo juu ya msalaba kwa siku chache, halafu kuivunja miguu

Page 33: Yesu katika India

33

yake, lakini miguu ya Yesu haikuvunjwa kwa makusudi, naaliteremshwa msalabani akiwa hai kama wale wezi wawili. Hiyondiyo sababu damu ilitoka wakati ubavu wake ulipochomwa. Lakinidamu huganda baada ya kifo. Na hapa, inaelekea pia kwambayote hayo yalikuwa matokeo ya mpango maalumu. Pilato alikuwamtu mwenye kumwogopa Mwenyezi Mungu na alikuwa mtumwenye roho nzuri; asingeweza kuonyesha upendeleo bayanakwa kumuogopa Kaisari; kwani Mayahudi walikwisha mtangazaYesu kuwa ni mwasi. Haidhuru Pilato alikuwa na bahati yakumwona Yesu lakini Kaisari hakuwa na bahati hiyo.Huyu Pilato si tu alimwona Yesu bali pia alimfanyia upendeleomkubwa - hakutaka Yesu asulubiwe. Injili zinaonyesha waziwazikwamba mara kadhaa Pilato alitaka kumwachia huru, lakiniMayahudi walisema kwamba kama angemwachia huruhangekuwa mtiifu kwa Kaisari; walisema pia kwamba Yesualikuwa mwasi aliyetaka kuwa mfalme. (Yohana 19:31-34). Naile ndoto ambayo mkewe Pilato aliiona ilitia msukumo zaidi wakumwachia huru Yesu; vinginevyo Pilato na mkewe wangejitiakatika maangamizo. Lakini kwa kuwa Mayahudi walikuwa watuwakorofi waliokuwa tayari hata kumjulisha Kaisari kwa siri kuhusukitendo cha Pilato, hivyo Pilato alitumia hekima ya kumwokoaYesu: Kwanza aliipanga Ijumaa kuwa siku ya kumsulubisha,masaa machache tu kabla ya kuzama kwa jua, na usiku wasabato iliyo kubwa ulikuwa unakaribia kuingia. Na Pilato alijua vizurisana kwamba kulingana na amri za sheria zao Mayahudiwangeweza kumbakiza Yesu msalabani hadi jioni tu, na baadaya hapo ilikuwa kinyume cha sheria kumbakiza mtu ye yote juuya msalaba. Basi ikatokea vivyo hivyo; na Yesu akateremshwamsalabani kabla ya magharibi. Na haiyumkiniki kwamba walewezi waliosulubiwa wakati mmoja na Yesu wawe wamebakia hai,lakini Yesu awe amekufa katika kipindi cha masaa mawili tu. Hichokilikuwa kisingizio kilichobuniwa ili kumwokoa Yesu na utaratibuwa kuvunja miguu. Huu ukweli kwamba wezi wote wawiliwaliteremshwa msalabani wakiwa hai ni ushahidi wa kutoshakwa mtu mwenye akili; na kuwateremsha msalabani wahusika

Page 34: Yesu katika India

34

wakiwa hai ndiyo iliyokuwa desturi ya kawaida ya wakati ule;walikufa pale tu mifupa yao ilipovunjwa au walipofanywa kubakiajuu ya msalaba bila chakula au maji kwa siku kadhaa. Lakini Yesuhakukabiliwa na tajriba zo zote za namna hii - yeye hakubakiamsalabani kwa siku kadhaa wala mifupa yake haikuvunjwa; nakwa kufanya ionekane kana kwamba alikwisha kufa, Mayahudiwalifanywa walisahau jambo lote. Lakini mifupa ya wale weziilivunjwa na waliuawa mara moja. Lingalikuwa jambo tofauti kamaingesemwa kumhusu mmoja wa wale wezi kwamba naye piaalikuwa amekufa na kwamba hapakuwa na haja ya kuvunja mifupayake. Na mtu mmoja aitwae Yusufu rafiki mheshimiwa wa Pilatona mtu mashuhuri katika kitongoji kile na mwanafunzi wa kisiri-siri wa Yesu - alijitokeza katika wakati unaofaa. Ninahisi kwambayeye pia aliitwa kutokana na ushauri wa Pilato. Yesu kwakudhaniwa kwamba alikuwa amekufa, mwili wake ulikabidhiwakwake, kwa kuwa alikuwa mtu mkubwa ambaye Mayahudiwasingeweza kugombana naye. Alipofika mahali pa tukioalimchukua Yesu aliyekuwa katika hali ya kuzimia tu, kanakwamba alikuwa maiti. Na jirani ya mahali pa tukio palikuwa nanyumba yenye nafasi kubwa iliyojengwa kama kaburi kulinganana desturi za wakati ule, yenye mlango na ambayo ilijengwa mahaliambapo Mayahudi hawakuwa na shughuli napo. Yesu aliwekwakwenye nyumba hii kwa ushauri wa Pilato. Matukio haya yalitokeakatika karne ya kumi na nne baada ya kifo cha Musa; na Yesualikuwa Mujaddid (Mhuishaji) wa sheria ya Kiisraeli katika karneya kumi na nne. Na ingawa Mayahudi walikuwa wakimtazamiaMasihi Aliyeahidiwa katika karne hii hii ya kumi na nne, na tabiriza manabii waliopita pia ziliashiria kwenye wakati huu-huu kwakutokea kwake, lakini loo! Makuhani wa Kiyahudi wasiokuwa namaana hawakuutambua wakati huu na msimu huu, nawakamkamata Masihi Aliyeahidiwa kwa kumdhania kuwa nimuongo. Si hivyo tu bali walimtangaza kuwa ni kafir, wakamwitasi muumini, wakatamka hukumu ya kifo dhidi yake nawakamkokota hadi mahakamani.

Hii inaonyesha kwamba katika karne ya kumi na nne

Page 35: Yesu katika India

35

Mwenyezi Mungu alizikusanya zile tashwishi zote zilizofanyamioyo ya watu kuwa migumu, makuhani kuwa watu wa kidunia,vipofu na maadui wa haki. Hata hivyo, malinganisho kati ya karneya kumi na nne baada ya Musa na karne ya kumi na nne baadaya "mfano" wa Musa - Mtume wetu Mtukufu s.a.w. yataonyesha,awali ya yote, kwamba katika kila mojawapo ya karne hizikulikuwako na na mtu aliyedai kuwa Masihi Aliyeahidiwa; dai lakweli likiwa linategemea mamlaka ya Mwenyezi Mungu. Kisha,inaonekana pia kwamba makuhani wa watu waliwatangaza wotehao wawili kuwa ni makafiri, na kuwaita wasioamini na Madajjali,na kutoa fatwa ya kifo dhidi yao, na kuwakokotea mahakamani -mahakama ya Kirumi kwa kesi moja na ya Kiingereza kwa kesinyingine. Hatimae, wote waliokolewa; na hao makuhani - Mayahudina Waislamu - walishindwa katika hila zao. Mwenyezi Mungualikuwa Amekusudia kuanzilisha jumuiya zilizo kubwa kwa Masihiwote wawili na kuzishinda hila za maadui zao. Kwa kifupi, karneya kumi na nne baada ya Musa na karne ya kumi na nne baadaya Mtume wetu mtukufu Muhammad s.a.w. ni za majaribumakubwa kwa Masihi wake wahusika - na pia ni zenye barakanyingi kadiri muda unavyopita.

Na miongoni mwa ushahidi unaoonyesha kwamba Yesu a.s.aliokolewa Msalabani ni ule uliosimuliwa na Mathayo katika suraya 26 aya ya 36 hadi 46 ambazo zinaeleza kwamba baada yakupewa habari kwa njia ya ufunuo kuhusu kutiwa mbaronikulikokuwa kunamsubiri, Yesu alimwomba Mwenyezi Mungu usikukucha, akisujudu na kutokwa na machozi, na maombiyaliyofanywa kwa unyenyekevu wa namna hiyo, na ambayo Yesualikuwa na muda wa kutosha wa kuyaomba, hayawezi kuwayalipita bila kupokelewa; kwani kilio cha mteule wa MwenyeziMungu kinachotolewa wakati wa dhiki kamwe hakikataliwi.Ilikuwaje sasa, kwamba maombi ya Yesu aliyoyaomba usikukucha akiwa na moyo uliojawa na uchungu na akiwa katika haliya dhiki yakataliwe? Ilhali Yesu alisema; Baba aliye mbinguniananisikiliza. Kwa hiyo, iwapo maombi yake aliyoyaomba katikahali ya dhiki kama ile hayakuweza kusikilizwa, inawezaje kusemwa

Page 36: Yesu katika India

36

kwamba Mwenyezi Mungu Anasikiliza maombi? Injili zinaonyeshapia kwamba Yesu a.s. alikuwa na yakini ya kutoka moyoni kwambamaombi yake yalikubaliwa; alikuwa na matumaini makubwa katikamaombi yale. Hii ndiyo sababu alipokamatwa na kuwekwamsalabani, na alipoona kwamba mazingira yale hayakuwa sawana matarajio yake, akashindwa kujizuia kulia kwa kusema "Eloi,Eloi lama sabachtani", ikimaanisha, "Mungu wangu, Munguwangu, mbona Umeniacha?" Yaani hakutazamia kwambaangekuja kuwa namna hii - kwamba angekufa juu ya Msalaba.Aliamini kwamba maombi yake yangesikilizwa. Kwa hiyo, rejeazote hizi mbili za Injili zinaonyesha kwamba Yesu aliamini kwadhati kuwa maombi yake yangesikilizwa na kukubaliwa, kwambamaombi yake aliyoyaomba usiku kucha kwa kutokwa na machoziyasingepotea bure, wakati yeye mwenywe aliwafundishawanafunzi kwa maelezo kutoka mbinguni: "Mtakapoomba,maombi yenu yatapokelewa." Isitoshe, alisimulia pia fumbo lahakimu ambaye hakumwogopa mtu wala Mungu. Na shabahaya fumbo hili ilikuwa kwamba wale wanafunzi watambue kuwabila shaka Mwenyezi Mungu Hupokea maombi. Na ingawa Yesualijua kutoka kwa Mungu kwamba kulikuwako na mateso makubwayaliyokuwa yakimsubiri, hata hivyo, kama walivyo watu wote waliowacha-Mungu, alimwomba Mwenyezi Mungu akiamini kwambahapakuwepo na jambo lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu nakwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kukadiria iwapo tukiofulani litokee au la. Kwa hiyo, kukataliwa kwa maombi ya Yesumwenyewe kungeitikisa imani ya wale wanafunzi. Jeingewezekana kuweka mbele ya wanafunzi mfano wenyekubomoa imani zao? Kama wangeliona kwa macho yao wenyewekwamba maombi ya nabii mkubwa kama Yesu, yaliyoombwausiku kucha kwa bidii kubwa ya moyo, hayakukubaliwa, mfanohuo wenye bahati mbaya ungeleta majaribu makubwa katika imanizao. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu aliye mwingi wa rehemaAsingefanya jambo lingine isipokuwa kuyakubali maombi haya.Ni jambo la yakini kwamba yale maombi yaliyoombwa mahalipaitwapo Gethsemane yalipokelewa.

Page 37: Yesu katika India

37

Kuna kitu kingine kuhusiana na jambo hili. Kama vileilivyokuwepo njama ya kumwua Yesu, na kwa ajili hiyo makuhanina waandishi waliitisha mkutano wa pamoja nyumbani kwakuhani mkuu aitwae Caiaphas ili kutengeneza mpango wakumwua Yesu, kadhalika iliwahi kuwepo njama ya kumwua Musa,na vivyo hivyo, kulikuwa na ushauri wa kisiri-siri mjini Makka mahalipaitwapo Daarun-Nadwa ili kumwua Mtume wetu Mtukufu s.a.w.Lakini Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu aliwaokoa Mitume hawawakubwa na hila hizo mbaya. Kiwakati, njama dhidi ya Yesuilikuwa katikati ya hawa wengine wawili. Sasa kwa nini Yesuhakuokolewa ilhali yeye aliomba kwa nguvu zaidi kuliko ye yotemiongoni mwa hao wawili? Kwa nini maombi ya Yesu yaliachwakusikilizwa ilhali Mwenyezi Mungu husikiliza maombi ya watumishiwake wapendwa na kuharibu hila za waovu? Watu wote waliowacha-Mungu wanajua kutokana na uzoefu kwamba maombi yawenye dhiki na wenye kuteswa hupokelewa; la, bali saa yamateso kwa mtu aliye mcha-Mungu ni saa ya ishara. Mimimwenyewe nimewahi kuwa na uzoefu wa jambo hili. Shitaka lauwongo la jaribio la kuuwa lilifunguliwa dhidi yangu miaka miwiliiliyopita na mtu mmoja aitwae Dakta Martin Clark, Mkristo aishiyemjini Amritsar katika Punjab mbele ya mahakama katika Wilayaya Gurdaspur akidai kwamba nilimtuma mtu mmoja itwaye AbdulHamid, ili kumwua daktari huyo. Ikatokea kwamba katika kesi hiinilipangiwa na watu wachache wenye hila waliotokana na Jumuiyatatu, yaani Wakristo, Wahindu na Waislamu; waliungana nawalijaribu kadiri walivyoweza ili kuthibitisha shitaka la jaribio lakuua dhidi yangu. Wakristo walikuwa na manung'uniko dhidi yangukwamba nilikuwa najaribu - na naendelea kujaribu hata sasa -kuwaokoa watu kutoka katika fikara potofu ambazo Wakristowanazikaribisha kumhusu Yesu; na huu ndio ulikuwa muonjo wakwanza wa kile nilichotendewa na watu hao. Wahinduwalikasirishwa nami kwa sababu nilitoa utabiri kuhusu kifo chamtu mmoja aitwaye Lekh Ram, Mwanazuoni wa Kihindu, kwaruhusa yake mwenyewe, na utabiri huo ukatimia katika kipindicha wakati uliopangwa - Ishara ya kutisha kutoka kwa Mwenyezi

Page 38: Yesu katika India

38

Mungu. Kadhalika Masheikh wa Kiislamu walikasirika kwa sababunilipinga wazo la kuwepo kwa Masihi mwenye kumwaga damuna ile itikadi ya Jihadi kama inavyoeleweka na hao. Kwa hiyo,baadhi ya watu mashuhuri wa jumuiya hizi tatu walishaurianakwa pamoja kwa nia ya kuthibitisha lile shitaka la mauaji dhidiyangu ili imma ninyongwe au nitiwe gerezani. Kwa hiyo haowalikuwa watu wadhalimu mbele ya Mwenyezi Mungu, naMwenyezi Mungu Alinijulisha mimi kuhusu jambo hili kabla ya ilesaa ya mashauriano yao ya siri. Alinipa habari njema zakuachiliwa kwangu hapo mwishowe. Funuo hizi safi kutoka kwaMwenyezi Mungu zilitangazwa mapema kwa maelfu ya watu;na wakati baada ya ufunuo huu nilipoomba: Mola! niokoe mimina mateso haya, ikafunuliwa kwangu kwamba Mwenyezi MunguAtaniokoa na Ataniondolea mashitaka yaliyofunguliwa dhidi yangu.Ufunuo huu ulielezwa kwa njia ya mdomo kwa zaidi ya watu miatatu ambao wengi wao bado wangali hai. Na ikatokea kwambamaadui zangu walileta mashahidi wa uwongo mahakamani, nailibakia kidogo tu wathibitishe shitaka hilo - mashahidi wa hizoJumuiya tatu zilizotajwa hapo kabla wakiwa wanatoa ushahididhidi yangu. Kisha, ikatokea kwamba habari za kweli kuhusu kesiile zikabainishwa kwa njia mbalimbali na Mwenyezi Mungu kwayule hakimu aliyekuwa akiisikiliza kesi ile ambaye jina lake lilikuwaKapteni W. Douglas, Naibu Kamishna wa Gurdaspur. Aliridhikakwamba kesi ile ilikuwa ya uwongo. Kisha, bila kumjali huyo daktaambaye pia alikuwa m-mishionari, muono wake wa hakiulimshawishi kuifutilia mbali ile kesi, na hivyo basi yote yale ambayoniliyatangaza kuhusu kuachiliwa kwangu, kwa maelekezo yaufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa mamia ya watu, nakwenye mikutano ya hadhara, yakatokea kuwa kweli ambayoilisaidia kuimarisha imani ya watu wengi, ijapokuwa mazingirayaliyokuwapo kabla yaliashiria welekea wa hatari. Si haya tu,tuhuma nyingi za namna hii na mashitaka yenye sura ya jinaiyalipendekezwa dhidi yangu kutokana na sababu zilizotajwa hapojuu, na kesi zikapelekwa mahakamani, lakini kabla sijaitwamahakamani Mwenyezi Mungu alinijulisha mwanzo na mwisho

Page 39: Yesu katika India

39

wa jambo lote na katika kila kesi ya hatari nilipewa habari njemaza kuachiliwa.

Suala la msingi hapa ni kwamba bila shaka Mwenyezi MunguMwenye nguvu Huyapokea maombi hususan wakati watumishiWake waaminifu wanapokwenda mlangoni pake wakiwawameonewa; Hushughulikia utetezi wao na huwasaidia kwa njiaza ajabu. Kuhusu hili mimi mwenyewe ni shahidi. Kwa nini basiyale maombi ya Yesu aliyoyatoa akiwa katika hali ya uchungumkuu kama ule yawe hayakupokelewa? Hapana, yalipokelewa,na Mwenyezi Mungu Alimwokoa. Mwenyezi Mungu Alitengenezamazingira ardhini na mbinguni ili kumwokoa. Yohana, yaani nabiiYahya hakuwahi kupata muda wa kuomba kwa sababu mwishowake ulikuwa umekwisha wadia, lakini Yesu alikuwa na usikumzima wa kufanya maombi, na akautumia usiku wote huo kwakufanya maombi akiwa amesimama na kusujudu mbele yaMwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu Alikusudia kwambaYesu aonyeshe dhiki aliyokuwa nayo na aombe kuachiliwa kwakekwa Mwenyezi Mungu Ambaye kwake hakuna lisilowezekana.Kwa hiyo Mola, kulingana na desturi Yake ya tangu na tangu,Aliyapokea maombi yake. Mayahudi walisema uwongo paleambapo walipokuwa wakimsulubu Yesu walimsuta kwamba yeyealimtegemea Mwenyezi Mungu; kwa nini Mwenyezi MunguHakumwokoa? Kwa hiyo Mwenyezi Mungu Alibatilisha hila zoteza Mayahudi na kumwokoa Masihi Wake mpendwa kutokana namsalaba na laana inayoambatana na msalaba huo. Mayahudiwalishindwa.

Na miongoni mwa ushahidi wa Injili uliotufikia ni aya kutokaMathayo: "Kwamba ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagikajuu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damuya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu namadhabahu. Amin, nawaambieni, mambo hayo yote yatakuja juuya kizazi hiki (Mathayo 23:35-36). Sasa, iwapo mtazitafakari ayahizi mtagundua kwamba Yesu a.s. anasema waziwazi kwambakuuawa kwa manabii kulikokuwa kunafanywa na Mayahudikuliishia kwa nabii Zakaria, na kwamba baada ya hapo Mayahudi

Page 40: Yesu katika India

40

wasingekuwa na uwezo wa kumwua nabii ye yote. Huu ni utabirimkubwa ambao unaonyesha kwamba Yesu a.s. hakuuawakutokana na kuwekwa msalabani; bali aliokolewa kutokamsalabani, na hatimae akafa kifo cha kawaida. Kwani kama Yesua.s. angepata kifo cha kuuawa na Mayahudi kama Zakaria,angeashiria hivyo katika aya hizi kuhusu kifo chake yeyemwenyewe. Na kama itadaiwa kwamba Yesu a.s. pia aliuawana Mayahudi lakini kuuawa kwake hakukuwapatia dhambiMayahudi kwani kifo cha Yesu kilikuwa katika hali ya kafara, daihilo ni vigumu kulithibitisha kwani katika Yohana sura 19 aya ya11 Yesu anasema wazi wazi kwamba Mayahudi walitenda dhambikubwa kwa kukusudia kumwua Yesu; na kadhalika, katika sehemuzingine nyingi kuna kidokezo kilicho wazi kwamba walistahiliadhabu mbele ya Mwenyezi Mungu kama malipo ya uovuwaliomtendea Yesu (Mathayo 23:35 - 36).

Na miongoni mwa ushahidi wa Injili uliotufikia ni aya yaMathayo, yaani "Amin, nawaambieni, pana watu katika hawawasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatawatakapomwona mwana wa Adamu akija katika ufalme wake."(Mathayo 26;24). Kadhalika ile aya katika Yohana: "Yesuakamwambia: Ikiwa nataka huyu (yaani mwanafunzi, Yohana)abakie (yaani mjini Yerusalem) hata nijapo." (Mathayo 16:28). Hiiina maana: Kama nikitaka, Yohana hatakufa mpaka nije tena.Aya hizi zinaonyesha kwa uwazi mkubwa kwamba Yesu a.s. alitoaahadi kwamba baadhi ya watu wataendelea kuishi mpakaatakaporudi. Miongoni mwa hao alimtaja Yohana. Kwa hiyo ilikuwalazima ahadi hii itimie. Hivyo basi, hata Wakristo wamekirikwamba ili utabiri huo uhesabiwe kuwa umetimilizwa ni lazimakuja kwa Yesu kutokee katika wakati ambapo baadhi ya watu wazama zile watakuwa bado hai, ili utabiri huo utimilizwe kulinganana ahadi. Huu ndio msingi wa tangazo la viongozi wa kanisakwamba kulingana na ahadi yake Yesu alikuja Yerusalem wakatiwa kuteketezwa kwake na kwamba Yohana alimwona, kwa vileaikuwa hai wakati ule. Lakini ni lazima itambuliwe kwambaWakristo hawasemi kwamba Yesu aliteremka kidhahiri kutoka

Page 41: Yesu katika India

41

mbinguni akifuatana na Ishara zilizoahidiwa; bali wanasemakwamba alijitokeza kwa Yohana kama katika kashfu ili awezekutimiliza utabbiri wake uliomo katika aya ya 38 ya sura ya 16 yaMathayo. Lakini mimi nasema kwamba kuja kwa namna hiihakutimilizi utabiri ule. Hiyo ni tafsiri dhaifu sana ambayo inakwepakwa taabu lawama zitolewazo dhidi ya msimamo huu. Na tafsirihii ni dhahiri kabisa kwamba haiwezi kuthibitishwa na ni yamakosa, kwa kiasi hiki kwamba hakuna haja ya kuikanusha,kwani kama Yesu ilikuwa atokee kwa mtu ye yote kwa njia yandoto au kashfu utabiri wa namna hiyo ungekuwa kichekesho(Mathayo 26:24)1. Yesu alijitokeza kwa Paulo pia kwa namna hiyohiyo muda mrefu kabla ya tukio hili. Inaelekea kwamba utabiriuliomo katika aya ya 38 ya sura ya 16 ya Mathayo umewatiakiwewe mapadri na wamekuwa bado hawajaweza kupata maanainayokubalika akilini kulingana na imani zao wenyewe, kwani nivigumu kwao kusema kwamba Yesu wakati wa kutekwa kwaYerusalem alishuka kutoka mbinguni akiwa katika hali ya utukufu,na kwamba kama vile radi inavyolimulika anga lote na inaonekanana kila mtu, wote walimwona yeye; na pia haikuwa rahisi kwaokuipuuza ile kauli, yaani: Baadhi ya wale waliokuwa wamesimamahapa hawataonja kifo mpaka wamwone mwana wa Adamu katikaUfalme wake. Kwa hiyo, kutokana na tafsiri iliyotiwa chumviwaliamini kutimilizwa kwa utabiri ule kwa njia ya kashfu. Lakinihii siyo kweli; watumishi wacha-Mungu wa Mwenyezi Munguhujitokeza kila mara kwa wateule kwa njia ya kashfu, na kwakupata kashfu si lazima ya kwamba zitokee wakati wa ndoto tu;sivyo, zinaweza kuonekana hata katika hali ya kuwa macho; mimi___________________________________________________________________

1. Nimeona katika vitabu fulani fulani tafsiri za aya ya 24 ya sura 26 (ayaya 38 ya sura 16 - Mfasiri) ya Mathayo zilizotolewa na Masheikh ambazozimetiwa chumvi zaidi hata kuliko zile za Wakristo: wanasema kwambawakati Yesu alipoitangza kuwa ishara ya kuja kwake kwamba baadhi yawatu wa kizazi kile watakuwa bado hai na kwamba mwanafunzi mmojapia atakuwa bado yu hai wakati wa Masihi atakapotokea, ni lazimakwamba yule mwanafunzi awe ameendelea kuishi hadi sasa kwani Masihibado hajaja; na wanafikiri kwamba yule mwanafunzi amejificha mahalifulani katika baadhi ya milima akimsubiri Masihi!

Page 42: Yesu katika India

42

mwenyewe nimekwishapata tajriba ya shani kama hizo.Nimemwona Yesu a.s. mara nyingi katika kashfu (ndoto

katika hali ya kuwa macho), na nimekutana na baadhi ya mitumenikiwa macho kabisa; pia nimemwona Mkuu wetu, Bwana wetuna Kiongozi wetu, Mtume Muhammad s.a.w. mara nyingi katikahali ya kuwa macho na nimeongea naye - katika hali ya kuwamacho wazi wazi kwa kiasi hiki kwamba usingizi au kusinziahavikuhusiana kabisa na hali hiyo. Pia nimekutana na baadhi yawafu kwenye makaburi yao au sehemu zingine nikiwa macho;na nimeongea nao. Najua vizuri sana kwamba kukutana kwanamna hiyo na wafu katika hali ya kuwa macho ni jambolinalowezekana, siyo tu tunaweza kukutana, tunaweza kuongeapia, na hata kushikana mikono. Hakuna tofauti ya tajriba kati yahali hii ya kashfu na ile hali ya kuwa macho ya kawaida; mtuanajiona ya kwamba yuko katika ulimwengu huu huu, ana masikioyale yale, macho yale yale na ulimi ule ule, lakini kutafakari kwakina kutabainisha ulimwengu ulio tofauti. Ulimwengu wetu huuhauna utambuzi kuhusu tajriba ya namna hii, kwani ulimwenguhuu unaishi maisha ya kutojali. Tajriba hii ni zawadi kutokambinguni; ni ya wale waliopewa vipawa vipya vya fahamu. Hili nijambo la hakika - halisi na kweli. Kwa hiyo, wakati Yesualipojitokeza kwa Yohana baada ya kuteketezwa Yerusalem,ingawa alionwa na Yohana katika hali ya kuwa macho, na ingawayawezekana kulikuwako na mazungumzo kidogo na kushikanamikono, hata hivyo tukio hilo halihusiani kabisa na utabiri ule. Shaniza namna hiyo hutokea mara nyingi ulimwenguni; na hata sasa,iwapo nitafunga nia kidogo kuhusu jambo hili, ninaweza kwarehema ya Mwenyezi Mungu kumwona Yesu au baadhi ya Mitumewatakatifu nikiwa katika hali ya kuwa macho. Lakini kukutanakwa namna hiyo hakutimilizi ule utabiri uliomo katikaMathayo:16:38).

Kwa hiyo, kilichotokea hasa ni hiki ya kwamba Yesu alijuakwamba ataokolewa Msalabani na atahamia nchi nyingine nakwamba Mwenyezi Mungu Hatamwachilia afe wala kumwondoakatika ulimwengu huu iwapo atakuwa bado hajaona kuteketezwa

Page 43: Yesu katika India

43

kwa Mayahudi kwa macho yake mwenyewe na kwambahangekufa wakati ambapo bado yale matunda ya ufalme ambayowatu mashuhuri wa kiroho wamepewa na mbingu hayajapatikana.Yesu alitoa utabiri huu ili awahakikishie wanafunzi kwamba hivipunde wangeona ishara kwamba wale walioinua upanga dhidiyake wangeuawa kwa upanga wakati wa uhai wake na mbele yamacho yake. Kwa hiyo, iwapo ushahidi una thamani yo yotehakuna ushahidi mkubwa kwa Wakristo kuliko huu: kwamba Yesukwa ulimi wake mwenyewe anatoa utabiri kwamba baadhi yaowatakuwa bado wangali hai atakapokuja tena.

Ni lazima itambulike kwamba Injili zina aina mbili ya utabirikuhusu kuja kwa Yesu: (1) Ahadi ya kuja kwake siku za baadaye;kuja kwake ni kwa sura ya kiroho, na kunafanana na kuja kwanabii Eliya katika zama za Yesu. Kwa hiyo, kama vile alivyokuwaEliya, amesha jitokeza tayari katika zama hizi; na ni mimimwandishi; mtumishi wa watu wote, ambaye nimekuja kamaMasihi Aliyeahidiwa, kwa jina la Yesu a.s. na Yesu alitoa habariza kuja kwangu katika Injili. Amebarikiwa yule ambaye, kwa ajiliya kumheshimu Yesu anatafakari kwa uaminifu na ukweli kuhusukuja kwangu, na hivyo kujiepusha na kujikwaa. (2) Aina zingineza utabiri kuhusu kuja mara ya pili kwa Yesu zilizotajwa katikaInjili kwa hakika zimetajwa kama ushahidi wa uhai ambao kwarehema ya Mwenyezi Mungu ulibakia pasipo upungufu wakati watajriba ya msalaba. Mwenyezi Mungu Alimwokoa mtumishi Wakemashuhuri na kifo cha Msalaba; kama unavyoashiria utabiriuliotajwa hivi punde - Wakristo wamo katika makosawanapozichanganya karina hizi mbili: Kwa sababu hiiwamechanganyikiwa na wanalazimika kukabiliana na shida nyingi.Kwa kifupi, ile aya katika sura ya 16 ya Mathayo ni kipande muhimusana cha ushahidi unaounga mkono kuepukana kwa Yesu nakifo cha Msalaba.

Na miongoni mwa ushahidi wa Injili uliotufikia ni aya ifuatayoya Mathayo: "Ndipo itakapoonekana ishara ya Mwana wa Adamumbinguni; ndio mataifa yote ya ulimwengu yatakapoomboleza,nao watamwona mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya

Page 44: Yesu katika India

44

mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. (Tazama Mathayo,sura ya 24 aya ya 30). Maana ya aya hii ni: Yesu (amani juu yake)anasema kwamba wakati utafika ambapo kutoka mbinguni, yaanikutokana na uwezo wa kimbingu wa kuingilia kati zitazuka elimu,hoja na ushahidi ambao utabatilisha imani za uungu wa Yesu,kifo chake juu ya msalaba na kupaa kwake mbinguni na kuja tena;na kwamba mbingu itashuhudia dhidi ya uwongo wa walewaliomkana yeye kuwa nabii wa kweli, kwa mfano Mayahudi; nawale wa upande mwingine waliomhesabu yeye kuwa mtualiyelaaniwa kwa sababu ya kusulubiwa kwake, kwani ukweli wakutopatikana kwake na kifo juu ya Msalaba na kwa hiyo kutokuwamlaaniwa kungebainishwa wazi wazi; kwamba kisha mataifayote ya dunia ambao walitia chumvi na kupunguza sehemu yahadhi ya kweli wangeaibishwa sana na kosa lao; kwamba, katikazama zile zile ambapo ukweli huu ungebainishwa watu wangeonakuteremka kwa Yesu duniani kimethali, yaani katika siku zile zileMasihi Aliyeahidiwa angekuja katika uwezo wa sifa za Yesu,angejitokeza kwa ishara zote za kung'ara na msaada wa kimbinguna kwa uwezo na utukufu ambao ungetambulika. Aya hii - kwakuelezwa zaidi - ina maana kwamba kudra ya Mwenyezi Munguimeitengeza nafsi ya Yesu na kuyapanga matukio ya maishayake ili kuwafanya baadhi ya watu kutia chumvi, na wenginekupunguza hadhi yake, yaani wako watu ambao wanamtoakatika jamii ya binadamu kwa kiasi hiki kwamba wanasema kuwabado hajafa na amekaa mbinguni akiwa hai. Na watu ambaowamewapita hawa ni wale wasemao kwamba, baada ya kufaMsalabani na kufufuka amekwenda juu mbinguni na amepewauwezo wote wa kiungu, la bali yeye ndiye mungu mwenyewe. Nawatu wengine ni Mayahudi ambao wanasema kwamba aliuawamsalabani na kwa hiyo (najikinga kwa Mwenyezi Mungu kwakusema hivyo) amelaaniwa milele; amehukumiwa kuwa mlengwawa hasira ya kudumu; Mwenyezi Mungu Hapendezwi naye naAnamwona kama adui mwenye kuchukiwa; kwamba ni mwongona mdanganyifu - na Mungu apishe mbali - ni kaafir, msikuaminimkubwa; kwamba hakutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kutia chumvi

Page 45: Yesu katika India

45

huku na kupunguza kulikuwa kwa dhuluma kubwa kiasi hikikwamba isingekuwa isipokuwa kwamba Mwenyezi MunguAmsafishe Mtume Wake wa kweli na tuhuma hizi. Aya ya Injiliiliyotajwa hapo kabla inaashiria kwenye ukweli huu. Ile kaulikwamba mataifa yote ya dunia yataomboleza inaleta fikra kwambamataifa yote yale ambayo ainisho la neno "taifa" linahusika nayo,yataomboleza katika siku ile; watapiga vifua vyao na kulia, nakuomboleza kwao kutakuwa kukubwa. Hapa Wakristo ni lazimawaifuate aya inayohusika kwa uzingativu; ni lazima wafikiriekwamba wakati ambapo aya hii inao utabiri kwamba mataifa yoteyatapiga vifua vyao, imekuwaje wao wasihusike na maombolezohaya? Je hao sio taifa? Wakati, kulingana na aya hii haowamejumuishwa miongoni mwa wale ambao ni wapigaji wa vifua,kwa nini hawashughulikii uwokovu wao? Aya hii inasema waziwazi kwamba ishara ya Yesu itakapotokea mbinguni mataifa yoteyakaayo ardhini yataomboleza. Kwa hiyo yule mtu anayesemakwamba taifa lake halitaomboleza anamkana Yesu. Lakini walewatu, ambao idadi yao bado ni ndogo hawawezi kuwa watuwaliodokezwa katika utabiri huu; hawajafikia sifa ya kuainishwakama "taifa", na watu au taifa lile ndio sisi; la, bali yetu ndiyoJumuiya pekee ambayo iko nje ya maana na upeo wa utabiri huu,kwani Jumuiya hii bado inao wafuasi wachache tu ambao kwaoneno "taifa" na "kabila" haliwezi kutumika. Yesu kwa mamlaka yaufunuo wa kimbingu anasema kwamba ishara itakapotokeambinguni watu wote wa ulimwenguni ambao, kutokana na idadiyao watastahili kuainishwa kwa "kabila" au "taifa" watapiga vifuavyao; hapatakuwa na asiyehusika isipokuwa watu wenye idadindogo ambao kwao neno "taifa" haliwezi kutumika. Si Wakristowala Waislamu, wala Mayahudi na wala Mkanushaji ye yoteawezaye kuwa nje ya utabiri huu.

Jumuiya yetu peke yake ndiyo iko nje ya upeo wa utabiri huukwani wamepandwa kama mbegu na Mwenyezi Mungu hivipunde. Neno la nabii haliwezi kuwa la uwongo. Wakati manenohaya yana kidokezo cha wazi wazi kwamba kila taifa likaaloulimwenguni litaomboleza, ni wepi miongoni mwa watu hawa

Page 46: Yesu katika India

46

wawezao kudai kwamba wako nje ya upeo wa maneno haya?Yesu hajakiri kutokuhusika kwa ye yote katika aya hii. Lakini lilekundi ambalo bado halijafikia ukubwa wa "kabila" au "taifa" kwavyo vyote vile halihusiki yaani Jumuiya yetu. Na utabiri huuumetimilizwa waziwazi katika zama hizi, kwani ule ukweli kuhusuYesu ambao umegunduliwa hivi sasa bila shaka ndio chanzo chamaombolezo ya makabila haya, kwani umefichua makosa yaowote. Makelele yote ya Wakristo kuhusu uungu wa Yesuyanageuka na kuwa mipumuo ya huzuni; kung'ang'ania kwaWaislamu - usiku na mchana - kwamba Yesu amepaa mbinguniakiwa hai, kunageuka na kuwa kilio cha maombolezo; na Mayahudihao ndio wanaopoteza kila kitu.

Na hapa ni lazima kutaja kwamba katika kauli iliyomo katikaaya hiyo, yaani, kwamba wakati ule mataifa yote ya dunia yatapigavifua vyao, "dunia" ina maana ya Baladish-Sham (Falastin na Syria- Mfasiri) ambazo zina uhusiano na watu hawa wa aina tatu -Mayahudi kwa sababu hapo ndipo mahala pao pa asili na mahalapao pa ibada; Wakristo kwa sababu Yesu alitokea mahali hapona jumuiya ya kwanza ya dini ya Kikrsto iliinukia kutoka katikanchi ile; Waislamu, kwa sababu watakuwa warithi wa nchi hiihadi siku ya kiyama. Na kama neno "dunia" litachukuliwa kuwana maana ya kuzikusanya nchi zote, hata hivyo hakuna tatizo,kwani ukweli utakapodhihirishwa wakanushaji wote wataaibika.

Na miongoni mwa ushahidi uliotufikia kupitia Injili ni kauliinayoandikwa hapa chini kutoka katika Injili ya Mathayo: "Namakaburi yakafunguliwa, na miili mingi ya watakatifu iliyolalaikaamka na kutoka nje ya makaburi baada ya kufufuka kwake(yaani Yesu) na wakauingia mji na wakajitokeza kwa watu wengi"(Mathayo 27:52).

Hapana shaka hata ile ndogo kwamba kisa hiki kilichotajwakatika Injili, yaani, kwamba baada ya kufufuka kwa Yesuwatakatifu walitoka nje ya makaburi na kujitokeza wakiwa hai kwawatu wengi, hakitokani na uhakika wa kihistoria; kwani kamaingekuwa hivyo, siku ya kiyama ingekuwa imetendeka katikaulimwengu huu huu, na kile ambacho kilikuwa kimewekwa siri

Page 47: Yesu katika India

47

kwa maana ya kuwa kipimo cha imani na uaminifu kingebainishwakwa wote; imani isingekuwa imani, na, machoni pa kila muminina mkanushaji, hali ya ulimwengu ujao ingekuwa jambo la dhahirina bayana kama vile kuwako kwa mwezi, jua na kuhitilafiana kwausiku na mchana kulivyokuwa jambo la wazi. Katika hali kamahiyo imani isingalikuwa kitu chenye kuthaminiwa na isingalikuwakitu cha thamani ambacho kingeweza kuleta thawabu yo yote.

Kama watu na Manabii wa zamani wa Israeli ambao idadiyao ni mamilioni, walifufuliwa kweli wakati wa kusulubishwa kwaYesu na wakaja mjini wakiwa hai, na kama muujiza - kwambamamia ya manabii na mamia mengi ya maelfu ya watakatifuyalifufuliwa kwa wakati mmoja - kwa hakika ulionyeshwa kamauthibitisho wa ukweli wa uungu wa Yesu, Mayahudi walikuwa nafursa nzuri sana ya kuwauliza hawa manabii waliofufuliwa, iwapoYesu aliyedai kuwa yeye ni Mungu ni Mungu kweli au alidanganya.Na huenda hawakuipoteza fursa hii. Ni lazima waliuliza kuhusuYesu, kwani walikuwa na shauku ya kuwauliza wafu kamawangaliweza kufufuliwa. Kwa hiyo, wakati mamia ya maelfu yawatu walifufuliwa na kuja mjini na maelfu ya hao yalirudi kwenyenyumba zao, Mayahudi wangewezaje kuiachilia fursa kama hii?Ni lazima wawe wameulizia, siyo kutoka kwa mtu mmoja auwawili, bali kutoka kwa maelfu; na wale wafu kila mmoja alipoingiakatika nyumba yake ni lazima kulikuwa na msisimko katika kilanyumba, kwani mamia ya maelfu ya hao yalirudishwaulimwenguni. Katika kila nyumba lazima kulikuwa namazungumzo mengi na kila mtu ni lazima alikuwa akiwaulizawafu iwapo walijua kwamba yule mtu aliyejiita Yesu Masihi alikuwani Mungu kweli. Lakini, kwa kuwa Mayahudi hawakumwamini Yesukama ilivyotazamiwa, wala nyoyo zao hazikulainika, baliwaliimarika katika ugumu wa mioyo, inaelekea yumkini wafu haohawakuzungumza neno jema kumhusu yeye. Ni lazima walitoamajibu bila kusita kwamba mtu huyu alikuwa anatoa madai potofuya Uungu na alikuwa akisema uwongo dhidi ya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndiyo sababu Mayahudi hawakuacha utundu, ingawa mamiaya maelfu ya manabii yalifufuliwa. Baada ya "kumwua" Yesu

Page 48: Yesu katika India

48

wakajaribu kuwaua watu wengine. Mtu awezaje kuamini kwambamamia ya maelfu ya watakatifu waliokuwa wamelala makaburinimwao katika ardhi ile iliyobarikiwa, tangu zama za Adamu hadizama za Yohana Mbatizaji, wote hao wawe wamefufuliwa? -kwamba wote hao waje mjini kuhubiri, na kila mmoja waoasimame na kutoa ushahidi mbele ya maelfu ya watu kwambaYesu, Masihi hakika alikuwa mwana wa Mungu - la, bali Mungumwenyewe; kwamba yeye tu aabudiwe; kwamba watu lazimawaache imani zao za zamani vinginevyo watakwenda motoniambako watakatifu hao wamekushuhudia wao wenyewe! na badopamoja na kuwepo kwa ushahidi mzuri wa namna hiyo na taarifaza watu walioshuhudia kwa macho yao zilizotoka vinywani mwamamia ya maelfu ya watakatifu waliokufa, Mayahudi wasiachekukataa kwao! Mimi binafsi siko tayari kuamini hivyo. Kwa hiyo,iwapo mamia ya maelfu ya watakatifu na manabii na mitumekadhalika, waliokuwa wamekufa, walifufuka kweli na kuja mjinikutoa ushahidi, bila shaka walitoa ushahidi usiofaa; kamwehawakutoa ushahidi wenye kuunga mkono uungu wa Yesu. Hiiyaelekea kuwa ndiyo iliyokuwa sababu kwa nini Mayahudi baadaya kuusikiliza ushahidi wa wafu, wakaimarika katika kutoaminikwao. Yesu alitaka kuwafanya waamini uungu wake, lakini hao,kutokana na ushahidi huu, walikanusha kwamba wala hakuwa nabii.Kwa kifupi, imani za namna hiyo zina matokeo mabaya na yenyekuleta madhara sana - imani hizi, yaani kwamba mtu aseme kuwahaya mamia ya maelfu ya watu waliokufa au mtu ye yote aliyekufakabla ya zama zile alifufuliwa na Yesu; kwani, kurejeshewa uhaikwa wale waliokufa hakukuleta jambo lo lote la maana. Mtualiyetembelea nchi ya mbali na ambaye anarudi mjini kwake baadaya miaka michache ya kutokuwapo kwa kawaida huwa na shaukuya kuwaambia watu kuhusu mambo ya ajabu aliyoyaona nakuwasimulia hadithi za ajabu za nchi aliyotembelea; hatanyamazaau kuwa na ulimi uliofungwa akutanapo na watu wake baada yakipindi kirefu cha kutengana. Hasha, wakati kama huo watuwengine pia huwa na shauku ya kumkimbilia na kumwulizakuhusu nchi ile; na iwapo kwa bahati watu hawa wanafikiwa na

Page 49: Yesu katika India

49

mtu fulani aliye dhalili, mpole kwa umbile na ambaye hata hivyoanadai kuwa mfalme wa nchi ambayo mji wake mkuu umekwishaonwa na watu hawa na ambaye anasema kwamba yeye nimkubwa zaidi katika cheo cha ufalme kuliko mfalme mwinginehuyu au yule, kwa kawaida watu huhoji kuhusu wasafiri kamahao, iwapo mtu fulani anayepitapita wakati ule katika nchi yao nimfalme kweli wa nchi ile; na kisha, wale wasafiri, kulingana nayale waliyoweza kuyaona, huyajibu maswali ya namna hiyo. kwakuwa hivi ndivyo ilivyo, kama nilivyokwisha sema hapo kabla,kufufuliwa kwa wafu na Yesu kulikuwa kunastahili kuaminiwaiwapo ule ushahidi walioulizwa wafu - kuuliza ambako kulikuwahapana budi kufanywe - ulileta matokeo mema. Lakini hapa sivyoilivyokuwa. Kwa hiyo, pamoja na hiyo dhana kwamba wafuwalifufuliwa, mtu analazimika kudhani pia kwamba hao wafuhawakutoa ushahidi unaofaa kwa Yesu, ambao ungemfanya mtuauamini ukweli wake; bali walitoa ushahidi ambao ulizidishamtafaruku. Laiti kama mnyama fulani angetangazwa kuwaamefufuliwa badala ya binadamu wa kweli! Hiyo ingalitatuamatatizo mengi. Kwa mfano, kama ingalisemwa kwamba Yesualifufua elfu chache za madume ya ng'ombe - hayakuwa na ulimiwa kutolea ushahidi unaofaa au usiofaa! Lakini wafu ambao Yesualiwafufua walikuwa binadamu. Kama baadhi ya Wahinduwataulizwa hivi leo iwapo kama mababu zao wa zamani kumi auishirini wangefufuliwa na kurudishwa ulimwenguni, na kamawangesema kwamba dini kadhaa na kadhaa ndiyo dini ya kweli,bado tu wangekuwa na shaka kuhusu ukweli wa dini ile. Kamwewasingesema kuwa ni ya kweli.

Kwa hiyo, lichukulieni kuwa jambo la yakini kabisa kwambahakuna mtu ulimwenguni kote awezaye kuendelea kutoaminikwake na pia ukanushaji wake baada ya ubainishaji wa namnahii. Nasikitika kwamba katika kubuni hekaya za namna hiiMasingasinga wa nchi yetu wamefanya vizuri zaidi kulikoWakristo. Hawa Masingasinga wametoa uthibitisho wa werevuwao katika sanaa ya kutunga hekaya; kwani wanasema kwambaGuru wao, Bawa Nanak, mara moja alimfufua tembo. Sasa huu

Page 50: Yesu katika India

50

ni "muujiza" ambao haukabiliwi na upinzani uliotajwa hapo juu.Kwani Masingasinga wanaweza kusema: Huyo tembo hakuwana ulimi wa kuongelea, kwamba angaliweza kutoa ushahidi wakumwunga mkono au wa kumkanusha Bawa Nanak. Kwa kifupi,watu wa kawaida wenye akili ndogo, wanafurahishwa na "miujiza"kama hiyo lakini wenye hekima wanakuwa walengwa wa upinzaniwa watu wengine na hivyo wanakerwa na upinzani huo.Wanafedheheshwa mbele ya wale wanaohusishwa na hekayahizo za kipuuzi. Hivyo, kwa kuwa mimi ninazo hisia zile zile zaupendo na ukweli kwa Yesu kama walizonazo Wakristo, la balimimi nina fungamano la nguvu zaidi kwake, kwani Wakristohawamjui mtu huyu wanayemsifu lakini mimi namjua ninayemsifu,kwani nimemwona; kwa hiyo, naendelea kufichua hali halisi yataarifa zilizotolewa katika Injili - kama vile ile taarifa kwamba wakatiwa tukio la msalaba watakatifu wote waliokufa walifufuliwa nawakaja mjini.

Kwa hiyo, naieleweke wazi wazi kwamba taarifa kama hizizinakuwa katika hali ya Kashf, kama lile ono lililoonwa na baadhiya watu watakatifu wakati wa tukio la msalaba - kwambawatakatifu waliokufa walifufuliwa na wakaja mjini ambakowaliwatembelea watu. Na kama vile ndoto zilivyo na uaguzi wakeambao umetajwa hata katika kitabu kitakatifu cha Mungu - kwamfano ndoto ya Yusufu ilikuwa na uaguzi - ono hili pia lilitakiwaliwe na uaguzi wake; na uaguzi huu ulikuwa kwamba Yesu hakufajuu ya Msalaba; kwamba Mwenyezi Mungu Alimwokoa na kifo juuya msalaba. Na kama swali liulizwe kwamba nimeupata wapiuaguzi huu, jibu lake ni kwamba watu maarufu wenye maarifayawezayo kupokewa bila shaka kuhusu sanaa ya uaguziwanasema hivyo, na waaguzi wote wameshuhudia hivyo kutokanana uzoefu wao. Hapa nanukuu kutoka katika uaguzi wa mtu wakale aliyekuwa maarufu na mwenye maarifa kuhusu sanaa yauaguzi, yaani mtunzi wa Ta'tirul - Anam: (Tazama Kitaab Ta'tirul -Anam fi Ta'birul - Manam, kilichotungwa na Qutubuz-ZamanShaikh Abdul Ghani An-Nablisi, ukurasa 289) ambao ukitafsiriwani kwamba kama mtu ye yote anaona katika ndoto au ono lililo

Page 51: Yesu katika India

51

katika hali ya kashf, kwamba wafu wametoka makaburini nawamekwenda majumbani kwao, uaguzi wake ni kwambamfungwa ataachiwa huru kutoka kifungoni, na kwambaataokolewa kutoka katika mikono ya watesi wake. Karina hiiinaonyesha kwamba mfungwa huyu atakuwa mtu mkubwa namashuhuri. Hivyo itaonekana jinsi uaguzi huu kiakiliunavyohusikana na Yesu. Mtu anaweza kuelewa mara mojakwamba baada ya kufufuka, watakatifu waliokuwa wamefufukawalionekana wakienda mjini ili kuonyesha ukweli huu, ili wenyehekima wajue kwamba Yesu ameokolewa na kifo cha Msalabani.

Kadhalika, rejea nyingi zaidi katika Injili zinaonyesha waziwazi kwamba Yesu hakufa Msalabani; aliokolewa nacho, naakahamia nchi nyingine. Lakini, nafikiri yale niliyoyaeleza yanatoshakwa mtu asiye na upendeleo usio na sababu za kiakili.

Yawezekana baadhi wanaweza kukaribisha mioyoni mwaoule upinzani kwamba mbona Injili zinasema mara kwa marakwamba Yesu alikufa msalabani, au kisha baada ya kufufuliwaalipaa mbinguni. Upinzani wa namna hii nimekwisha ujibu kwakifupi, lakini ningeweza kusema tena kwamba kukutana kwa Yesu(amani juu yake) na wanafunzi baada ya tukio la Msalaba; kusafirikwake hadi Galilaya; kula mkate na nyama; kuonyesha vidondavya mwilini mwake; kukaa usiku mzima na wanafunzi paleEmmau; kukimbia kisirisiri kutoka kwenye mamlaka ya Pilato;kuhama kutoka mahali pale kama ilivyokuwa desturi ya manabii;na kusafiri chini ya kivuli cha woga - matukio yote hayayanathibitisha kwamba hakufa msalabani; kwamba mwili wakeuliendelea kuwa na sifa yake ya kufa; na kwamba haukupatamabadiliko yo yote.

Hakuna ushahidi katika Injili kwamba mtu ye yote alimwonaYesu akipaa mbinguni; na hata kama ushahidi kama huoungelikuwapo, usingekuwa wa kuaminiwa, kwani kutengenezamilima kwa kutumia vichuguu vya fuko na kuvikuza vitu vidogovionekane vikubwa yaonekana kuwa ni tabia ya waandishi waInjili. Kwa mfano, kama mmoja anatokea kusema kwamba Yesuni Mwana wa Mungu, mwingine anaanza kumfanya Mungu kamili,

Page 52: Yesu katika India

52

wa tatu anampa uwezo juu ya ulimwengu wote, na wa nneanasema bila kificho kwamba yeye ni kila kitu, na kwamba hakunaMungu mwingine zaidi ya yeye. Kwa kifupi, kutia chumvikunawafikisha mbali sana. Kama mtu atafikiria lile ono ambamowafu walionekana wakitoka nje ya makaburi yao na kuelekeamjini, mtu huyo atagundua kwamba ono hili lilikuwa limepewauaguzi wake wa dhahiri kiasi cha kusema, kwamba wafu kidhahiriwalitoka nje ya makaburi yao na kuja katika jiji la Yerusalemambako waliwatembelea watu. Sasa ona, jinsi "Unyoya" mmojawa kunguru ulivyofanywa kuwa "kunguru"; na si kunguru mmojatena, bali mamilioni mengi! Wakati mambo yanatiwa chumvi kiasihicho, hatuna jinsi ya kuutafuta ukweli. Vile vile yafaa kufikiria -kwamba hizi Injili, zinazoitwa vitabu vya Mungu, zina madaiyasiyosadikika - kama vile, kama kazi zote za Yesu zingewekwakatika maandishi, maandishi hayo yasingepata nafasi yakuyahifadhia ulimwenguni kote! Je kutia chumvi kwa namna hiyondiyo njia ya uaminifu na ukweli? Iwapo kazi za Yesu zilikuwahazina kikomo kama hivyo, na iwapo hazingeweza kuandikwa,ilikuwaje kwamba kazi hizo zilifanyika katika kipindi cha miakamitatu tu? Tatizo jingine kuhusu hizi Injili ni kwamba zinatoa rejeaza kimakosa kuhusu baadhi ya vitabu vya kale; hazisemi kwausahihi hata kuhusu ukoo wa Yesu. Kutokana na Injili yaelekeakwamba watu hawa walikuwa wazito wa kuelewa kwa kiasi hikikwamba baadhi yao walimchukulia Yesu kuwa ni kiumbe wakiroho.

Na hizi Injili tangu hapo mwanzoni zilikuwa zinakabiliwa natuhuma kwamba hazikuhifadhi usafi wa maandiko yake, na kwakuwa viko vitabu vingine vinavyoitwa Injili, hakuna sababbumadhubuti kwa nini taarifa zote za hivi vitabu vingine zikataliwe,na kwa nini zote zilizomo katika hizi zinazoitwa na wengi kuwaInjili zikubaliwe kuwa za kweli. Hakuna mtu awezaye kusemakwamba hizo Injili zingine zina utiwaji chumvi kama huuunaopatikana katika hizi injili nne. Inashangaza kwamba wakatikwa upande mmoja zinasema kwamba Yesu alikuwa mtumchamungu na kwamba tabia yake haikuwa na lawama, kwa

Page 53: Yesu katika India

53

upande mwingine zinaletwa dhidi yake tuhuma zisizomstahili mtuye yote aliye mchamungu. Kwa mfano, pasipo shaka kulinganana mafundisho ya Taurati, manabii wa Kiisraeli walikuwa na mamiaya wanawake kwa wakati mmoja, ili kwa kufanya hivyo wawezekuongeza kizazi cha wachamungu, lakini hungesikia kamwekwamba nabii ye yote aliwahi kuonyesha mfano wa uhuru kamahuu kwamba amruhusu mwanamke mchafu na mzinifu, malayamaarufu wa jiji, aguse mwili wake kwa mikono yake, kumruhusuampakaze mafuta kichwani mwake - ustadi wa mafanikio yauasherati wake - na kumpangusa miguu kwa nywele zake;kwamba aruhusu yote haya kufanywa na mwanamwali mzinifu,na asimwambie "Acha". Mtu ataokolewa na lawama ya kushukuambako kunajileta kwenyewe mtu aonapo jambo la namna hii -kwa kuamini wema wa Yesu. Hata hivyo, mfano huu si mzurikwa watu wengine. Kwa kifupi, Injili hizi zinayo mambo mengiyanayoonyesha kwamba hazikuhifadhi hali yao ya asili, au kwambawaandishi wake walikuwa watu wengine - sio wale wanafunzi.Kwa mfano, je inaweza, ile taarifa ya Injili ya Mathayo: "Na hililinajulikana vema miongoni mwa Mayahudi hadi leo",kunasibishwa na Mathayo? Alikuwa mtu mwingine ambaye aliishikatika wakati ambapo Mathayo alikuwa tayari amekwisha fariki?Kisha, Injili hiyo hiyo ya Mathayo inasema: "Na wakakusanyikapamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedhanyingi, wakisema, semeni ya kwamba wanafunzi wake walikujausiku na wakamwiba sisi tulipokuwa tumelala" (Mathayo 28:12-13). Yaweza kuonekana jinsi taarifa kama hizo zisivyosadikikana zisivyoingia akilini. Kwa maana ya kauli hii ni kwamba Mayahudiwalitaka kuficha kufufuaka kwa Yesu kutoka katika wafu, nakwamba waliwahonga maaskari ili kwamba mwujiza huu mkubwausijulikane kwa watu wengi, kwa nini basi Yesu ambaye wajibuwake ulikuwa kuutangaza mwujiza huu miongoni mwa Mayahudi,aliufanya kuwa siri; la bali aliwakataza watu wengine kuutangaza?Kama ikidaiwa kwamba aliogopa kukamatwa, ningesemakwamba, wakati amri ya Mwenyezi Mungu ilipomshukia, na baadaya kufariki akafufuka akiwa na mwili wa kiroho na mtukufu, hofu

Page 54: Yesu katika India

54

gani aliyokuwa nayo sasa kuhusu Mayahudi? - Bila shakaMayahudi sasa hawakuwa na uwezo wo wote juu yake; sasaalikuwa mbele na juu ya maisha yawezayo kufa. Mtu anaona kwamasikitiko kwamba, wakati kwa upande mmoja inasemekanakwamba alikutana na wale wanafunzi na akaenda Galilaya nakutoka hapo akapaa mbinguni, hata hivyo anawaogopa Mayahudikwa mambo madogo madogo tu, na pamoja na kuwa na mwiliwenye utukufu, anakimbia kisiri siri kutoka katika nchi ile, isijeMayahudi wakamgundua; anakwenda safari ya maili sabiini hadiGalilaya ili kuokoa maisha yake na mara kwa mara anawaombawatu wasiwaambie watu wengine kuhusu jambo hili. Je hizi ndizodalili na ishara za mwili wenye utukufu? Hapana! Ukweli ni kwambahaukuwa mpya wala haukuwa mwili wenye utukufu - ulikuwamwili ule ule, wenye vidonda, ambao uliokolewa katika kifo; na,kwa vile kulikuwako bado na ile hofu ya Mayahudi, Yesu aliihamanchi ile kwa kutumia njia zote za uangalifu. Mazungumzo ya jambolo lote yaliyo kinyume na maelezo haya ni upuuzi mtupu; - kamalile linalohusu Mayahudi kuwahonga maaskari ili kuwafanyawaseme kwamba wanafunzi waliiba maiti wakati hao maaskariwalipokuwa wamelala. Iwapo hao maaskari walikuwa wamelalawanaweza kuulizwa vizuri sana jinsi walivyoweza kujua wakatiwakiwa usingizini kwamba maiti ya Yesu iliibiwa. Na kutokana nahuo uhakika peke yake wa Yesu kutokuwemo ndani ya kaburi, jemtu mwenye akili timamu anaweza kuamini kuwa amepaambinguni? Je hapawezi kuwako na sababu zingine ambazo kwazomakaburi yanaweza kubakia tupu? Wakati wa kupaa mbinguniilikuwa ni wajibu wake Yesu kukutana na mamia machache yaMayahudi, na pia Pilato. Alikuwa akimwogopa nani akiwa na mwiliwake wenye utukufu? Hakujali kuwapatia wapinzani wake hatauthibitisho mdogo tu. Bali alishikwa na hofu na akakimbiliaGalilaya. Hii ndiyo sababu tunaamini kwa uhakika kwamba ingawani kweli kwamba aliliacha lile kaburi, lililokuwa kama nyumba nalenye mlango, na ingawa ni kweli kwamba alikutana kwa siri nawale wanafunzi, hata hivyo siyo kweli kwamba alipewa mwili wowote mpya na wenye utukufu; ulikuwa mwili ule ule, na vidonda

Page 55: Yesu katika India

55

vile vile na hofu ile ile moyoni mwake isije walaaniwa Mayahudiwakamkamata tena. Wewe soma kwa utulivu tu Mathayo, suraya 28 aya ya 7 hadi ya 10. Aya hizi zinasema wazi wazi kwambawale wanawake walioambiwa na mtu fulani kwamba Yesu alikuwahai na alikuwa anakwenda Galilaya, na ambao piawalinong'onezwa kwamba wawajulishe wanafunzi, bila shakawalifurahi kusikia habari hizi, lakini walikwenda wakiwa na moyowenye hofu, - walikuwa bado wanaogopa isije Yesu akashikwatena na Mayahudi waovu. Na aya ya tisa inasema kwamba wakatiwanawake hawa walipokuwa njiani kwenda kuwajulishawanafunzi, Yesu alikutana nao na akawasalimu. Na aya ya kumiinasema kwamba Yesu aliwaomba wasiwe na hofu, yaani, yakukamatwa kwake; akawaomba wawajulishe nduguze kwambawote waende Galilaya1; kwamba wataonana naye huko, yaani,hakuweza kukaa pale kwa kuwaogopa maadui. Kwa kifupi, kamaYesu alifufuka kweli kutoka katika kifo na akapata mwili wenyeutukufu, ulikuwa wajibu wake kuwapatia Mayahudi uthibitisho wamaisha kama hayo. Lakini tunajua kwamba hakufanya hivyo. Kwahiyo, ni upuuzi kuwalaumu Mayahudi kwa kujaribu kufanyauthibitisho wa kufufuka kwa Yesu ukanushike. Hapana, Yesumwenyewe hakutoa walau uthibitisho mdogo tu wa kufufukakwake; bali kwa kukimbia kwake kisirisiri, na kwa uhakika wa yeyekuwa amekula chakula, na kulala na kuonyesha vidonda vyake,yeye mwenyewe alithibitisha kwamba hakufa Msalabani._________________________________________________________

1. Hapa, Yesu hakuwaliwaza wale wanawake kwa maneno kwambaamefufuka akiwa na mwili mpya na wenye utukufu, kwamba sasa hakunaawezaye kumkamata. Hapana, kwa kuona hali yao ya udhaifu aliwaliwazakwa njia ambayo kwa kawaida wanaume huitumia kuwaliwaza wanawake.Kwa kifupi hakutoa uthibitisho wa mwili wenye utukufu; bali alionyesha nyamana mifupa yake na hivyo kuthibitisha kwamba ulikuwa mwili wa kawaidawenye kufa.

Page 56: Yesu katika India

56

SURA YA PILI

Kuhusu ushahidi wa Qur'an Tukufu na mapokeosahihi yanayothibitisha kuokoka kwa Yesu

Hoja ambazo sasa nitaziratibu zaweza kuonekana kuwahazina maana kwa vile zimekusudiwa kuwaongoza Wakristo,kwani watu hawa hawalazimiki kukubali kile kinachosemwa naQur'an Tukufu au Hadithi kuhusu suala hili; lakini ninazisema tukwa sababu ninataka Wakristo waujue muujiza wa Qur'an yetuna Mtume Mtukufu s.a.w.; kuwaambia kwamba ule ukweli ambaoumegundulika baada ya mamia ya miaka tayari umekwishatangazwa na Mtume wetu Mtukufu na Qur'an. Hivyo basi, naratibubaadhi ya ukweli huo hapa chini:-

Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu Anasema katika Qur'an:"Na kusema kwao: Hakika tumemwua Masihi Isa mwana waMariamu, Mtume wa Mungu; hali hawakumwua walahawakumfisha msalabani, bali alifananishwa kwao (kama maiti).Na kwa hakika wale waliohitilafiana kwalo, yakini wana shaka nalo,wao hawalijui hakika yake isipokuwa wanafuata dhana. Na kwayakini wao hawakumwua- Bali Mwenyezi Mungu AlimnyanyuaKwake, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima."Yaani Mayahudi hawakumwua Yesu wala hawakumfisha juu yamsalaba, hapana, walishuku tu kwamba Yesu alikufa Msalabani;hawakuwa na hoja ambazo zingeweza kuwashawishi nakuwaridhisha kwamba Yesu (amani juu yake) alikufa kwelimsalabani.

Katika aya hizi Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu Anasemakwamba ingawa ni kweli kwamba kidhahiri Yesu aliwekwamsalabani, na kwamba walikuwa wamedhamiria kumwua, hatahivyo ni makosa kwa Mayahudi na Wakristo kudhania kwambaYesu alikufa kweli juu ya msalaba. Hapana, Mwenyezi MunguAlitengeneza mazingira ambayo yalimwokoa Yesu na kifo chamsalabani.

Page 57: Yesu katika India

57

Hivyo basi, kama mtu ni mwadilifu atalazimika kusemakwamba kilichosemwa na Qur'an dhidi ya Mayahudi na Wakristohatimaye kikatokea kuwa kweli. Na uchunguzi wa hali ya juu sanahivi leo umethibitisha kwamba kwa kweli Yesu aliokolewa na kifocha Msalabani. Usomaji kwa bidii wa kumbukumbu unonyeshakwamba Mayahudi hawakuweza kamwe kulijibu hili swali: Ilikuwajekwamba Yesu alikufa katika kipindi cha masaa mawili au matatuilhali mifupa yake haikuvunjwa?

Hili likawafanya Mayahudi walete utetezi mwingine - kwambawalimwua Yesu kwa upanga, ilhali historia ya kale haionyeshikwamba Yesu aliuawa kwa upanga. Utukufu na uwezo wa dhatiTukufu ya Mwenyezi Mungu ulifanya pawepo na giza ili Yesu awezekuokolewa. Palikuwapo na tetemeko la ardhi. Mkewe Pilato alionandoto. Usiku wa sabato ulikaribia kuingia ambapo haikujuzukuruhusu mwili uliosulubiwa ubakie msalabani. Na yule hakimukutokana na ndoto ile ya kutisha, akawa amepata shinikizo lakumwachilia Yesu. Yote haya yaliletwa sawia na Mwenyezi Munguili kumwokoa Yesu. Yesu mwenyewe alifanywa azimie iliachukuliwe kuwa amekufa. Kwa njia ya ishara za kutisha kamaile ya tetemeko la ardhi, na kadhalika, ukalazimika katika nafsi zaMayahudi woga na hofu, na pia hofu ya adhabu ya kimbingu. Piakuliwako na hofu isije ile miili ikabakia misalabani wakati wa usikuwa Sabato. Tena, Mayahudi walipomwona Yesu akiwa katika haliya kuzimia walidhani kuwa amekwisha kufa. Ilikuwa giza. Nakulikuwako na tetemeko la ardhi na wasiwasi mkubwa. Piawalikuwa na wasiwasi kuhusu majumbani kwao - watoto waowalikuwa wakijisikiaje katika hali ile ya giza na tetemeko la ardhi?Pia kulikuwako na hofu kubwa katika mioyo yao kwamba kamamtu huyo alikuwa mwongo na Kaafir kama walivyomdhania, kwanini ishara zenye nguvu zimeonyeshwa wakati wa kuteswa kwake- ishara ambazo hazikuonyeshwa hapo kabla? Walikuwawamefadhaika sana kiasi kwamba hawakuwa tena katika hali yakujiridhisha wenyewe iwapo Yesu alikuwa amekufa kweli au kwahakika alikuwa katika hali ya namna gani.Lakini kile kilichotokea ulikuwa mpango wa kimbingu wa

Page 58: Yesu katika India

58

kumuokoa Yesu. Hii inadokezwa katika ile aya . . . yaani, Mayahudihawakumwua Yesu - Mwenyezi Mungu Aliwafanya waaminikwamba walikwisha mwua. Mazingira haya yanawatia moyowacha-Mungu kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwambaMwenyezi Mungu Anaweza kuwaokoa watumishi wake jinsiAtakavyo.

Na Qur'an Tukufu inayo aya hii: "Jina lake litakuwa Masihi Isamwana wa Mariamu, mwenye heshima katika dunia na Akhera,na yu miongoni mwa wale waliopewa ukaribu na MwenyeziMungu".

Hii ina maana kwamba, siyo tu hapa, ambapo Yesu atakuwana heshima na umashuhuri na kuwa na ukuu machoni pa watuwa kawaida, bali hata akhera pia. Hivyo, ni dhahiri kwamba Yesuhakuheshimiwa katika nchi ya Herod na Pilato. Kinyume chahayo, yeye alifedheheshwa. Na kuleta rai kwamba ataheshimiwawakati wa kuja kwake mara ya pili duniani ni jambo lisilokuwa namsingi. Ni kinyume na vitabu vitakatifu na kinyume na sheria yamilele ya hali ya asili. Isitoshe hakuna uthibitisho wa jambo hilo.Lakini ukweli ni kwamba baada ya kuachiliwa kutoka mikononimwa watu wale walaaniwa, Yesu alikuja katika ardhi ya Punjabna akaifanya iheshimike kutokana na ziara yake; Mwenyezi Mungualimpa umashuhuri mkubwa - hapa akayakuta makabila kumiyaliyopotea ya Israeli. Yaonekana takriban wote miongoni mwaWaisraeli hawa walikuwa wameangukia kwenye ibada yamasanamu iliyo duni sana. Lakini kutokana na kuja kwa Yesumahali hapa, takriban wote walirejea kwenye njia iliyo sawa; nakwa kuwa katika mafundisho ya Yesu mlikuwemo mawaidha yakumwamini Mtume atakayekuja, yale makabila kumi ambayoyalikuja kujulikana katika nchi hii kama Waafghani na Wakashmirihatimae yote yakawa Waislamu. Kwa hiyo Yesu alikuja naheshima kubwa katika nchi hii. Hivi karibuni imegunduliwa sarafukatika nchi hii ya Punjab, ambamo limeandikwa jina la Yesu (amanijuu yake) kwa herufi za Kipali.Sarafu hii ni ya zama za Yesu. Hii inaonyesha kwamba Yesualikuja katika nchi hii na alipokewa kwa heshima ya kifalme; sarafu

Page 59: Yesu katika India

59

hii ni lazima iwe imetolewa na mfalme ambaye alikuwa mfuasiwa Yesu. Sarafu nyingine imepatikana ikiwa na sanamu yaMuisraeli. Yaonekana kwamba hii pia ni sanamu ya Yesu.Qur'an tukufu pia inayo aya isemayo kwamba Yesu alibarikiwana Mwenyezi Mungu kila alipokwenda . . . kwa hiyo, sarafu hizizinaonyesha kwamba alipokea heshima kubwa kutoka kwaMwenyezi Mungu, na kwamba hakufa hadi alipopata heshima yakifalme. Kadhalika Qur'an Tukufu inayo aya hii: "(Kumbukeni)Mwenyezi Mungu Aliposema: Ewe Isa kwa yakini Mimi Nitakufishana Nitakuinua Kwangu, na nitakutakasa na (masingizio ya) walewaliokufuru ......

Yaani Ewe Isa! Mimi Nitakusafisha kutokana na tuhuma hizi;Nitathibitisha hali yako ya kutokuwa na hatia na Nitaziondoalawama zilizoletwa dhidi yako na hawa Mayahudi na Wakristo.Huu ni utabiri mkubwa, ambao una maana kwamba Mayahudiwalidai kuwa baada ya kusulubiwa Yesu akawa (Mungu apishembali) mlaaniwa, na hivyo akapoteza mapenzi ya Mungu,kwamba moyo wa Yesu, kama neno "laana" linavyolazimisha,ulimpa kisogo Mwenyezi Mungu; yaani akatokea kumchukia. Moyowake ukawa umefunikwa na utando mnene wa giza. Akatokeakuyapenda maovu na kujitenga na mema. Ukajitenga naMwenyezi Mungu na ukawa chini ya ushawishi wa shetani.Kukawa na uadui kati yake na Mwenyezi Mungu! Lawama hiyohiyo - kwamba alikuwa mlaaniwa - ililetwa na Wakristo, lakinizaidi ya hiyo Wakristo kutokana na ujinga wanaunganisha halimbili zinazopinzana na zilizo mbalimbali kabisa; wanasemakwamba Yesu alikuwa mwana wa Mungu, lakini pia wanamwitamlaaniwa, na baya zaidi wanakiri kwamba mtu aliyelaaniwa niMwana wa Giza na Shetani au ni shetani mwenyewe. Kwa hiyo,hizi ndizo tuhuma chafu zilizoletwa dhidi ya Yesu; lakini utabiriuliomo katika neno unaonyesha kwamba ulikuwa utokee wakatiambapo Mwenyezi Mungu Angemwondolea Yesu tuhuma zotehizi. Na huu ndio wakati ule. Bila shaka kutokuwa na hatia kwaYesu kumethibitika machoni pa watu wenye kutafakari kutokanana ushahidi wa Mtukufu Mtume s.a.w., kwani yeye na pia Qur'an

Page 60: Yesu katika India

60

Tukufu imethibitisha kwamba tuhuma zilizoletwa dhidi ya Yesu(amani juu yake) zote hazina msingi. Lakini ushahidi huu kidogoulikuwa wa kiakili na wa hali ya hoja zaidi kuweza kuwashawishiwatu wa kawaida. Kwa hiyo, haki ya kimbingu ilitaka kwambakama vile kusulubiwa kwa Yesu kulivyokuwa tukio la kuonekanawazi na la kujulikana sana, vivyo hivyo usafi wake ni lazimauonyeshwe kwa vitendo kwa namna ambayo itawafanya watuwote wauone. Na hilo likatimia. Kutokuwa na hatia kwa Yesu kumokatika misingi siyo tu ya hoja bali kumeonyeshwa kwa vitendokwa njia iliyo bayana kuliko zote. Kwani, mamia ya maelfu yawatu kwa macho yao wenyewe wameona kwamba kaburi la Yesua.s. linapatikana njimi Srinagar, Kashmir. Na kama vilealivyosulubiwa mahala paitwapo Golgotha, yaani mahali pa "Sri",vivyo hivyo na kaburi lake lake limekutwa mahali pa "Sri", yaani,Srinagar. Neno "Sri" linalopatikana katika majina ya mahali potepawili ni jambo la kustaajabisha sana. Mahali ambapo Yesualisulubiwa paliitwa Gilgit au "Sri", na mahali ambapo katikasehemu ya mwisho ya karne ya kumi na tisa kaburi la Yesuliligunduliwa pia panaitwa Gilgit, au "Sri". Na yaelekea kwambamahali panapoitwa Gilgit nchini Kashmir, panaashiria neno hilohilo "Sri". Mji huu huenda ulianzishwa katika zama za Yesu, naikiwa kama kumbukumbu ya tukio la Msalaba kwa ajili ya mahalipale, ukaitwa Gilgit, yaani "Sri"; kama vile Lhasa, ambayo inamaana ya "Mji wa anayestahili kuabudiwa"; neno hili ni la asili yaKiebrania na linaashiria kwamba mji huu pia ulianzishwa katikazama za Yesu.

Na taarifa za kuaminika katika hadithi zinaonyesha kwambaMtukufu Mtume s.a.w. alisema kuwa Yesu alikuwa na umri wamiaka 125. Isitoshe, firqa zote za Kiislamu zinaamini kwambaYesu alikuwa na sifa mbili za pekee - sifa ambazo hazipatikanikwa nabii mwingine ye yote, nazo ni:

(1) Aliishi hadi kufikia umri kamili wa uzee, yaani hadi miaka125; (2) Alitembea katika sehemu nyingi za ulimwengu na kwahiyo akaitwa "nabii mtembeaji". Ni dhahiri kwamba kamaalipaishwa mbinguni akiwa na umri wa miaka 33 tu taarifa ya

Page 61: Yesu katika India

61

"miaka 125" isingalikuwa kweli, wala asingalikuwa ametembeakwa kiasi kikubwa kama hicho ilhali alikuwa na umri wa miaka33 tu. Na siyo tu taarifa hizi zinapatikana katika vitabu vya Hadithivyenye kuaminika. Zimekuwa zikijulikana sana miongoni mwafirqa za Kiislamu hivi kwamba ni vigumu kufikiria jambo lingine lolote ambalo limepata kujulikana kwa wingi zaidi miongoni mwao.Kanzul - Ummal (Jalada la 2) ambacho ni kitabu cha Hadithichenye habari nyingi kinayo Hadithi kwenye ukurasa wa 34 kutokakwa Abu Huraira. Yaani, Mwenyezi Mungu Alimfunulia Yesua.s.., Ewe Isa! Tembea kutoka mahali pamoja kwenda mahalipengine". Yaani, nenda kutoka nchi moja hadi nyingine isijeukabainika na kuteswa. Tena, kwenye kitabu hicho hicho kamailivyoripotiwa na Jabar, ipo Hadithi Isemayo:

1Kila mara Yesu alikuwa akisafiri; alikwenda toka nchi mojahadi nyingine, na usiku ulipoingia alikuwa akila majani ya porinina kunywa maji safi po pote alipokuwa. Tena kwenye kitabu hichohicho ipo taarifa kutoka kwa Abdullah bin Umar:

2Mtukufu Mtume alitangaza kwamba wenye kupendwa sanambele ya Mwenyezi Mungu ni wale walio maskini. Aliulizwa nenomaskini linamaanisha nini? je ni wale watu ambao kama YesuMasihi walizikimbia nchi zao wakiwa na Imani zao?___________________________________________________________

1. Jalada la 2 ukurasa 712. Jalada la 2 ukurasa 51

Page 62: Yesu katika India

62

SURA YA 3

Kuhusu Ushahidi unaotokana na Vitabu vya Tiba

Kipande cha ushahidi wenye thamani kubwa kuhusiana na Yesukuepukana na Msalaba ambao mtu hawezi kujizuia kuukubali nichanganyiko la dawa lijulikanalo kama Marham-i-Isa au "Marhamuya Yesu" lililotajwa katika mamia ya vitabu vya tiba. Baadhi yavitabu hivi vilitungwa na Wakristo, baadhi na Majusi na Mayahudi,baadhi na Waislamu. Vingi vyao ni vya zamani sana. Uchunguziunaonyesha kwamba mwanzoni changanyiko hilo lilipatakujulikana kama jambo la jadi miongoni mwa mamia ya maelfuya watu. Kisha wakaliweka katika maandishi. Kwanza, wakatiwa zama zile zile za Yesu, muda kidogo tu baada ya tukio laMsalaba, kitabu cha kifamasia kilitungwa kwa lugha ya Kilatiniambamo kulikuwa na kutajwa kwa changanyiko hili pamoja nataarifa kwamba changanyiko hilo lilitayarishwa kwa ajili ya vidondavya Yesu. Kisha, kitabu hiki kikatafsiriwa katika lugha kadhaa, hadikatika zama za Mamun-al-Rashid ambapo kilitafsiriwa katika lughaya Kiarabu. Aidha ni kutokana na uingiliaji kati wa kimbingu waajabu kwamba matabibu mashuhuri wa dini zote - Wakristo,Mayahudi, Majusi na Waislamu - wote wamelitaja changanyikohili katika vitabu vyao, na wanasema kwamba lilitayarishwa nawanafunzi kwa ajili ya Yesu. Usomaji sana wa vitabu vya elimuya utengenezaji madawa unaonyesha kwamba changanyiko hilini la manufaa sana katika ajali ziletazo majeraha kutokana namapigo au mianguko, kwa kuzuia mara moja mtiririko wa damu,na kwa vile linayo "manemane" pia ndani yake, kidonda hubakiabila usaha. Marhamu haya pia yanafaa sana katika kutibu ugonjwawa tauni; ni mazuri kwa ajili ya majipu na vidonda vya tumbonivya aina zote. Lakini bado haiko wazi iwapo marhamu hayayalitayarishwa kutokana na ufunuo wa kimbingu alioupokea Yesumwenyewe baada ya kupata mateso ya Msalaba, au kwambayalitayarishwa baada ya mashauriano na baadhi ya matabibu.

Baadhi ya vichanganyizio vyake ni kama dawa halisi ya ugonjwa

Page 63: Yesu katika India

63

mmoja: hususan "manemane" ambayo pia inatajwa katika Taurati.Kwa vyo vyote vile vidonda vya Yesu vilipona kwa muda wa sikuchache tu kwa kutumia marhamu haya. Ndani ya kipindi chasiku tatu alipona vya kutosha na kupata uwezo wa kutembeamaili sabini kwa mguu kutoka Yerusalem hadi Galilaya. Hivyo basi,kuhusu nguvu ya changanyiko hili inatosha tu kusema kwambawakati Yesu aliwaponya watu wengine, changanyiko hili lilimponyayeye! Vitabu vilivyoweka kumbukumbu ya ukweli huu vinafikia idadiya zaidi ya elfu moja. Kuvitaja vyote itakuwa orodha ndefu sana.Isitoshe, kwa vile matumizi ya dawa hii yanajulikana sanamiongoni mwa matabibu wa Kiyunani (yaani wale waliobobeakatika madawa ya kale ya Kigiriki), sioni haja ya kutaja majina yavitabu vyote hivi; naorodhesha hapa chini majina ya vichache tuambavyo vinapatikana hapa.:-

Orodha ya Vitabu vyenye mtajo wa Marham-i-Isa, na taarifakwamba Marham hayo yalitayarishwa kwa ajili ya Yesu,

yaani kwa ajili ya vidonda vya mwilini mwake

Qanun; kilichotungwa ba Shaikur - Rais Bu Ali Sina, Jalada la 3,Ukurasa 133;Sharah Qanun; kilichotungwa na Allama Qutbud-Din Shirazi,Jalada la 3;Kamil-us-Sanaat; kilichotungwa na Ali Bin-al-Abbas Al-Majuusi,jalada la 3, ukurasa 602;Kitab Majmua-i-Baqai; Mahmud Muhammad Ismail, Mukhatif azKhaqan, kilichotungwa na Khitab pidar Muhammad Baqa Khan,Jalada la 2 ukurasa 497;Kitab Tazkara-i-Ul-ul-Albab; kilichotungwa na Shaikh Daud-ul-Zariirul - Antaki, ukurasa 303;Qarabadin-i-Rumi; kilichotungwa karibuni wakati ule ule wa zamaza Yesu na kutafsiriwa kwa Kiarabu wakati wa utawala wa Mamunal-Rashid, tazama Maradhi ya Ngozi;Umdat-Ul-Muhtaj; kilichotungwa na Ahmd Bin Hasan al-Rashidal-Hakim. Katika kitabu hiki, Marham-i-Isa na machanganyiko

Page 64: Yesu katika India

64

mengine yameandikwa kutoka katika vitabu mia moja, penginezaidi ya mia moja, vitabu vyote hivi vikiwa katika lugha ya Kifaransa.Qarabadin, kwa lugha ya Kiajemi, kilichotungwa na HakimMuhammad Akbar Arzani-Maradhi ya Ngozi;Shifaaul-Asqaam, Jalada la 2 ukurasa 230;Miratush - Shafaa, kilichotungwa na Hakim Hatho Shah(muswada) Maradhi ya Ngozi;Zakhira-i-Khawarazm Shahi, Maradhi wa Ngozi;Sharah Qanun Gilani, Jalada la 3;Sharha Qanun Qarshi, Jalada la 3;Qarabadin, kilichotungwa na Ulwi Khan Maradhi ya Ngozi;Ilajul-Amraz, cha Hakim Muhammad Sharif Khan Sahib, ukurasa893;Qarabadin, Unani - Maradhi ya Ngozi;Tuhfatul Mu'miniin, kwenye nafasi ya pembeni ya Makhzanul-Adwiya, ukurasa 713;Muhit Fi-Tibb, ukurasa 367.Aksir-i-Azam, jalada la 4, kilichotungwa na Hakim MuhammadAzam Khan Sahib, Al Mukhatab ba Nazim-i-Jahan, ukurasa 331;Qarabadin, kilichotungwa na Masumi-ul-Masumi bin Karamu-Din Al-Shustri Shirazi;Ijala-i-Nafiah, Muhammad Sharif Dehlavi, ukurasa 410;Tibb-i-Shibri, kwa jina jingine kijulikanacho kama LawamiShibriyya. Syed Hussain Shibri Kazimi, ukurasa 471;Makhzan-i-Sulaimani, tafsiri ya Aksir Arabi, ukurasa 599,kilichotungwa na Muhammad Shamsud-Din Sahib waBahawalpur.Shifaaul-Amraz, kilichotafsiriwa na Maulana Al-Hakim MuhammadNuur Karim, 282;Kitab Al-Tibb Dara Shakohi, kilichotungwa na Nurud-DinMuhammad Abdul Hakim, Ainul-Mulki Al-Shirazi, ukurasa 360;Minhajud-Dukan ba Dastuurul-Aayan fi Aamal wa Tarkib al-NafiahLil-Abdan, kilichotungwa na Aflatuun-i-Zamana wa Rais-i-AwanaAbdul-Mina Ibn Abi Nasrul-Atta Al Israili Al-Haruuni (Yaani Myahudi),ukurasa 86,

Page 65: Yesu katika India

65

Zubdatut-Tibba, kilichotungwa na Syedul-Imam Abu Ibrahim Ismailbin Husaini Al-Jarjani, ukurasa 182;Tibb-i-Akbar, kilichotungwa na Muhammad Akbar Arzani, ukurasa242.Mizan-ul-Tibb; kilichotungwa na Muhammad Akbar Arzani,ukurasa 152;Sadidi, kilichotungwa na Raisul-Mutakaalimin Imamul-MuhaqqiqiinAs-Sadidul-Kazruuni, Jalada la 2 ukurasa 283;Hadi Kabir, kilichotungwa na Ibni Zakariya, Maradhi ya Ngozi;Qarabadin, kilichotungwa na Ibni - Talmiz, Maradhi ya Ngozi;Qarabadin, kilichotungwa na Ibni - Abi, Sadiq, Maradhi ya Ngozi.

Vitabu hivi vimetajwa hapa kwa njia ya kielelezo. Watu waliowasomi, husuusan matabibu, wanajua kwamba vingi miongonimwa vitabu hivi, katika zama za kale vilifundishwa katika sehemumuhimu za mafunzo chini ya utawala wa Kiislamu; hatawanafunzi kutoka Ulaya walijifunza vitabu hivyo. Ni jambo lauhakika, na hakuna kutia chumvi walau kidogo tu, kwamba katikakila karne kumekuwako na mamilioni ya watu ambao walikuwawanavijua vitabu hivi; mamia ya maelfu ya watu hao wamekuwawakivisoma vitabu hivyo kwa mfululizo. Naweza kudai kwambahakuna mtu walau mmoja tu miongoni mwa wasomi wa Ulayana Asia ambaye alikuwa hajajua walau baadhi ya majina ya vitabuvilivyomo katika orodha iliyotajwa hapo juu. Wakati Hispania naQastmonia na Shantrin zilipopata vyuo vikuu, Qanun kuu ya BuAli Sina, kitabu maarufu cha tiba ambamo yamepangwa vizurimatumizi ya Marham-i-Isa, na vitabu vingine kama vile Shifaa naIsharat na Basharat kuhusu sayansi, elimu ya nyota na falsafa,vilisomwa kwa hamu na kufunzwa na Wazungu. Kadhalika, vitabuvya Abu Nasr Farabi, Abu Raihan, Israil, Thabit bin Qurrah, Hunainbin Ishaq na kadhalika - vitabu vyote maarufu vya mafunzo - tafsirizilizofanywa na watu hao kutoka Kigiriki pia zilifundishwa.Tafsiri za vitabu vyao bila shaka zitakuwa bado zinapatikana hukoUlaya hadi leo. Kwa vile watawala wa Kiislamu walikuwa wafadhilihodari wa mambo ya tiba, walitayarisha tafsiri za vitabu vizuri

Page 66: Yesu katika India

66

vya Kigiriki.Ukhalifa ambao ndio mamlaka ya juu, kwa muda mrefu ulibakimikononi mwa wafalme ambao walitamani kuipanua elimu kulikokuendeleza tawala zao. Hii ndiyo sababu siyo tu vitabu vya Kigirikivilitafsiriwa kwa lugha ya Kiarabu bali pia waliwaalika makuhaniwa Kihindu kutoka India, na wakawafanyisha kazi ya kutafsirivitabu vya tiba na vinginevyo, wakiwalipa marupurupu makubwa.Kwa hiyo moja ya madeni makubwa ambayo watafutaji elimu yakweli wanadaiwa na watu hao, ni hili ya kwamba walitayarishatafsiri za Kilatini na Kigiriki za vitabu vya tiba ambavyo vilikuwa namtajo wa "Marhamu ya Yesu", na ambavyo, takriban kamamchoro, vimeurikodi ukweli huu kwamba marhamu yaleyalitayarishwa kwa ajili ya vidonda vya Yesu. Wakati wasomi wazama za Kiislamu kama vile Thabit bin Qurrah na Hunain binIshaq ambao licha ya kuwa na elimu ya tiba, walibobea katikaSayansi na falsafa, waliitafsiri Qarabadin ambamo mlikuwa namtajo wa Marham-i-Isa, walilihifadhi kwa busara neno Shailikhakwa herufi za Kiarabu ili kuendeleza ule muashirio kwamba kitabukile kilitafsiriwa kutoka katika maandiko ya kifamasia ya Kigiriki.Hii ndiyo sababu takriban katika kila kitabu linatokea nenoShailikha.

Isitoshe, ni jambo la kuzingatia kwamba ingawa sarafu zazamani zina thamani kubwa, kama itokeavyo kwamba zinafumbuamafumbo ya kihistoria, hata hivyo, vitabu vya kale ambavyo kwanyakati zote vimekuwa vikijulikana kwa mamilioni ya watu naambavyo vimekuwa vikifundishwa kama vitabu vya mafunzokwenye vituo vikubwa vya elimu na bado vinaendelea kutekelezakusudio hilo, ni vyenye thamani mara elfu moja zaidi kuliko sarafuna michoro. Kwani, kwa upande wa sarafu na michoro upouwezekano wa udanyanyifu pia. Vitabu vya elimu ambavyo tanguwakati wa kutungwa kwao vimekuwa vikijulikana na mamilioni yawatu na vimehifadhiwa na kulindwa na mataifa yote navinaendelea kulindwa hadi leo, ni ushahidi ulio na thamani kiasihiki kwamba sarafu na michoro havina cho chote cha kulinganishiana hivyo. Naataje mtu ye yote kama anaweza, sarafu au mchoro

Page 67: Yesu katika India

67

ambao umepata kujulikana na watu wengi kama Qanun ya Bu AliSina.

Kwa kifupi, "Marham ya Yesu" yanajemga kipande cha ushahidimuhimu sana kwa ajili ya watafutaji ukweli. Kama ushahidi huuusiaminike, ushahidi wote wa kihistoria ni lazima ukataliwe, kwani,licha ya idadi ya vitabu vya namna hiyo ambavyo vina mtajo waMarham-i-Isa kuwa elfu moja au zaidi hivyo na watunzi wa hivyowanajulikana na mamailioni ya watu. Yule ambaye hataukubaliuthibitisho huu ulio bayana na ulio wazi na wenye nguvu ni lazimaauchukie uthibitisho wote utokanao na historia. Je anawezakuthubutu kupuuza kipande cha ushahidi wenye nguvu kama huu?Je tunaweza sisi kutilia shaka ushuhuda huu mzito ambaoumesambaa Ulaya na Asia na ambao ni matokeo ya kauli zawanafalsafa maarufu - Mayahudi, Wakristo, Majusi naWaislamu?

Hivyo basi, enyi wachunguzi waadilifu uangalieni ushuhudahuu: Ukimbilieni uthibitisho huu adhimu na kuutafakari. Je ushahidikama huu wenye kung'ara unastahili kupuuzwa? Je hatupendi"Uhai" kutoka katika "Jua" hili la ukweli? Ile rai kwamba Yesu awezakuwa ameyapata baadhi ya majeraha kabla ya wakati wa kuitwakwake au kwamba yaweza kuwa majeraha yaliyopatikana kipindifulani wakati wa mahubiri yake lakini si kutokana na kusulubishwa;kwamba mikono na miguu yake yaweza kuwa iliumizwa kutokanana sababu zingine; kwamba aweza kuwa alianguka kutokakwenye paa na marham yaweza kuwa yalitayarishwa kwa ajili yamajeraha aliyoyapata katika mwanguko huu, ni ya kipuuzi. Ni yakipuuzi kwa sababu kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa Mtumehakuwa na wanafunzi, ambapo sambamba na kutajwa kwamarham hayo wametajwa pia wanafunzi. Neno Shailikha, ambaloni neno la Kigiriki bado linapatikana katika vitabu hivi. Zaidi yahayo, kabla ya kutangaza utume wake Yesu hakuhesabiwa kuwamtu muhimu wa kiasi hiki kwamba matukio ya maisha yake yaweyanarikodiwa. Kazi yake ya mahubiri ilidumu kwa kipindi cha miakamitatu na nusu tu, na wakati wa kipindi hiki hakuna ajali au jerahalililoripotiwa katika kumbukumbu kumhusu yeye isipokuwa tukio

Page 68: Yesu katika India

68

la Msalaba.Lakini kama mtu ye yote ana maoni kwamba Yesu aliyapatamajeraha haya kutokana na sababu zingine, ni juu yake kuletauthibitisho kwani tukio ambalo tumelirejea linathibitika nakukubalika kwa kiasi hiki kwamba si Myahudi wala Mkristowawezao kulikana hilo tukio, yaani, la Msalaba. Lakini, wazo laYesu kuwa alijeruhiwa kutokana na sababu zinginehalijashuhudiwa na kumbukumbu yo yote ya kihistoria. Kwa hiyo,kukaribisha wazo kama hilo ni kuiacha njia ya ukweli kwa kujua.Uthibitisho ambao umekwisha tolewa si ule ambao unawezakukataliwa kwa kutegemea rai ya kipuuzi kama hiyo.

Ipo miswada ambayo inapatikana hata leo; mimi pia ninayonakala ya zamani ya Qanun Bu Ali Sina ya zama zile, iliyoandikwakwa mkono. Kwa hiyo, litakuwa jambo la dhuluma kubwa - itakuwani kuuchinja ukweli moja kwa moja - kutupilia mbali uthibitishoulio wazi kama huu. Ufikirieni tena na tena - tafakarini kwa kinakuuhusu huo - Vitabu hivi bado viko mikononi mwa Mayahudi,Majusi, Wakristo, Waarabu, Waajemi, Wagiriki, Warumi,Wajerumani na Wafaransa, na vile vile katika maktaba za kale zanchi nyingine za Ulaya na Asia. Je ni sawa kuuacha uthibitishokama huu ambao nuru yake hulitia kiwi jicho la ukanaji? Kamavitabu hivi vingekuwa vimetungwa na Waislamu tu, na kamavingekuwa mikononi mwa wafuasi wa Islam, kungeweza kuwana watu ambao wangeamua kwa pupa kwamba Waislamuwalighushi taarifa hii na kuirikodi kwenye vitabu vyao ili kuifanyaiwe shambulio dhidi ya imani ya Kikristo. Lakini hii, licha ya sababunitakazotaja hivi punde, ni fikra isiyokuwa na msingi pia kutokanana ukweli kwamba Waislamu kamwe wasingekuwa na hatia yakughushi kwa namna hii; kwani, kama walivyo Wakristo, Waislamupia wanaamini kwamba baada ya tukio la Msalaba Yesu ghaflaakapaa mbinguni. Zaidi ya hayo Waislamu hawaamini kwambaYesu aliwekwa Msalabani kwa vyo vyote vile au kwamba alipatamajeraha yo yote kutokana na kusulubiwa. Yawezekanaje sasawatengeneze kwa makusudi taarifa ya kughushi ambayo ikokinyume na imani yao? Isitoshe, Islam haikuwapo ulimwenguni

Page 69: Yesu katika India

69

wakati vitabu hivi vya tiba, kwa lugha ya Kilatini na Kigiriki,vilipokuwa vinatungwa na kusambazwa miongoni mwa mamiaya maelfu ya watu; vitabu ambavyo vilikuwa na maelekezo yamatumizi ya "marhamu ya Yesu" na pia maelezo kwambamarhamu haya yalitayarishwa na wanafunzi wa Yesu (amani juuyake). Na wale watu, yaani, Mayahudi, Wakristo, Waislamu naMajusi walikuwa wakipingana wao kwa wao katika mambo yadini. Kwa hiyo, ule ukweli kwamba wameyataja marhamu hayakatika vitabu vyao, au tuseme, ule ukweli kwamba hawazijali hatadini zao mbalimbali, ni uthibitisho ulio wazi kwamba utayarishajiwa marhamu hayo ulikuwa ni ukweli unaojulikana kwa kiasi hikikwamba haukukanwa na jumuiya au taifa lo lote. Lakini ni kweli,kwamba hadi kufikia wakati wa kutokea kwa Masihi Aliyeahidiwa,haikutokea kwa ye yote miongoni mwa watu hawa kufaidika nadawa hii ambayo imetajwa katika mamia ya vitabbu na ilijulikanakwa mamilioni ya watu wa mataifa mbalimbali. Kwa hiyo hatunanjia nyingine isipokuwa kukubali kuhusiana na jambo hili kwambaMwenyezi Mungu Alitaka - ilikadiriwa na Yeye - kwamba silaha hiiyenye kung'ara na hoja hii yenye kufichua ukweli ambayoinateketeza ile imani kuhusu msalaba ielezwe ulimwenguni naMasihi Aliyeahidiwa; kwani Mtukufu Mtume s.a.w. alitabiri kwambaImani ya Msalaba haitapungua wala maendeleo yakehayatasimamishwa hadi Masihi Aliyeahidiwa atakaptokeaulimwenguni. Ilikuwa ni Masihi Aliyeahidiwa ambaye mikononimwake ulikuwa usababishwe "Uvunjaji wa Msalaba". Kidokezokatika utabiri huu kilikuwa kwamba katika zama za MasihiAliyeahidiwa Mwenyezi Mungu Angeleta mazingira ambayoyangeweka wazi ukweli kuhusu tukio la msalaba. Kisha mwishoungekuja, na Imani ya msalaba ingekamilisha kipindi cha uhaiwake, siyo lakini, kwa njia ya vita na vurugu, bali kwa njia ya wakalaza kimbingu tu, ambazo zingejidhihirisha ulimwenguni kwa suraya hoja na ugunduzi. Hii ndiyo maana ya Hadithi iliyotajwa naBukhari na wengineo. Kwa hiyo ilikuwa lazima kwambazisizifichue thibitisho hizi na vipande hivi vya ushahidi usio nashaka mpaka zama za kutokea kwa Masihi Aliyeahidiwa. Na hivyo

Page 70: Yesu katika India

70

macho yatafunguka na watu wenye kufikiri watadadisi kuhususwali hili. Kwani Masihi wa Mwenyezi Mungu ameshatokea.Akili ni lazima sasa zinolewe; nyoyo ni lazima ziwe zingativu;kalamu zishikwe kwa nguvu, na wote ni lazima wajifungevibwebwe. Nyoyo za kiuchamungu hivi sasa zitapewa ufahamu,na kila mtu aliye tayari atapata akili. Kwani, kila king'aachombinguni huimulika dunia pia. Aliyebarikiwa na mwenye bahatinzuri ni yule ambaye anayo hisa ya nuru hii! Kama vile tundalinavyotokea kwa msimu, kadhalika Nuru nayo hushuka kwa wakatiwake uliowekwa; hakuna awezaye kuiteremsha kabla haijashukayenyewe, wala kuizuia wakati inaposhuka. Hitilafu na mabishanoni lazima yawepo. Lakini, mwishowe ukweli ni lazima utashinda,kwani hii siyo kazi ya binadamu; mwana wa binadamu hana hisahumo - unatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye hubadilishamisimu, Huzisogeza nyakati na Huugeuza usiku kuwa mchanana mchana kuwa usiku. Ameumba giza lakini Anapenda nuru.Anaiachia Shirki (Imani ya kuwepo miungu wengi) ipatikaneulimwenguni, lakini anapenda Tauhidi au Umoja Wake Mwenyewe;Hapendi utukufu wake kutolewa kwa mtu mwingine ye yote. Tangukuzaliwa kwa binadamu, na mpaka binadamu atakapotowekaulimwenguni, Sheria ya kimbingu ni hii ya kwamba MwenyeziMungu Anadumisha Tauhidi au Umoja Wake. Lengo la Manabiiwote walioletwa na Yeye lilikuwa kufuta kuabudiwa kwa binadamuna viumbe vingine na kuanzilisha kuabudiwa kwa MwenyeziMungu. Huduma waliyoitoa ulimwenguni ilikuwa kuifanya hii kanuni"Hakuna apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah" ing'areulimwenguni kama inavyong'ara mbinguni. Kwa hiyo mbora waoni yule ambaye alifanya kazi kubwa zaidi ya kuifanya kanuni hiiing'are kwa kumetameta; ambaye kwanza aliweka wazi udhaifuwa miungu ya uwongo na kuthibitisha kutokuwa cho chote kwamiungu hiyo, kwa misingi ya akili na uwezo, na kisha alipokwishathibitisha kila kitu, aliacha ukumbusho na ushindi wake dhahirikwa sura ya hii Kalima: Hakuna Mungu isipokuwa Allah, Muha-mmad ni Mtume wa Allah." Hakuitamka Kalima hii: "Hakuna Munguisipokuwa Allah" ikiwa madai matupu; bali kwanza alitoa vithibitisho

Page 71: Yesu katika India

71

na kubainisha kosa la imani za uwongo na kisha akawaita watuwaje washuhudie kwamba hakuna Mungu kinyume cha yeyeAmbaye Alizivunja nguvu zao zote na Ambaye Alikivunjavunjakiburi chao chote. Kwa hiyo, ikiwa kama ukumbusho wa ukwelihuu uliothibitika, akafundisha kalima hii iliyobarikiwa: "HakunaMungu isipokuwa Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah".

Page 72: Yesu katika India

72

SURA YA 4USHAHIDI KUTOKA KWENYE VITABU VYA HISTORIA

Kwa kuwa sura ifuatayo imehodhi ushahidi wa ainambalimbali, kwa ajili ya kuweka wazi mfuatano wa

mambo, imegawanywa katika sehemu chacheambazo zinapangwa hapa chini:

SEHEMU YA 1

Ushahidi kutoka katika vitabu vya Kiislamu kutajasafari ya Yesu.

Katika Rauzat-us-Safa, kitabu kijulikanacho sana cha historiakwenye ukurasa wa 130-135 panajitokeza taarifa kwa lugha yaKiajemi ambayo ikitafsiriwa kwa muhtasari ni kama ifuatavyo:

Isa (amani juu yake) aliitwa "Masihi" kwa sababu alikuwa msafirimkubwa. Alivaa shali ya hariri kichwani mwake, na mgolole wahariri mwilini mwake. Alikuwa na fimbo mkononi mwake; alikuwana tabia ya kutembea tembea kutoka nchi moja hadi nyingine nakutoka mji moja hadi mwingine. Usiku ulipoingia alitulia mahalaalipokuwa. Alikula mimea ya porini, na aliendelea na safari zakekwa mguu. Katika moja ya misafara yake, Masahaba zake wakatimmoja walimnunulia farasi; siku moja akampanda huyo farasi,lakini kwa vile hakuweza kuandaa masurufu kwa ajili ya kumlishafarasi huyo, akamrudisha. Akisafiri kutoka nchini mwake aliwasiliNasibain, mji ambao ulikuwa kwenye umbali wa maili mia chachekutoka nyumbani kwake. Pamoja naye walikuwepo wachachemiongoni mwa wanafunzi wake ambao aliwatuma mjini kwendakuhubiri. Lakini huko mjini kulikuwako na uvumi mpya mpyaambao ni wa uwongo na usiokuwa na msingi kuhusu Isa (amaniya Mungu juu yake) na mama yake. Kwa hiyo gavana wa ule mjialiwakamata hao wanafunzi na kisha kumwita Yesu. Yesualiwaponya baadhi ya watu kimiujiza na kuonyesha miujizamingine.

Page 73: Yesu katika India

73

Page 74: Yesu katika India

74

Kwa hiyo mfalme wa jimbo la Nasibain pamoja na majeshi yakeyote na watu wake, akawa mfuasi wake.Kile kisa cha "kuteremka kwa chakula" kilichomo ndani ya Qur'anTukufu ni cha zile zama za misafara yake.

Hii kwa kifupi, ndiyo taarifa ya Rauzat-us-Safa. Lakini, mtumziwa kitabu hicho amenasibisha kwa Yesu miujiza mingi ya kipuuzina isiyoingia akilini ambayo sitaitaja hapa, na kwa kuiachanishana uwongo na utiaji chumvi wa kipuuzi, naligeukia suala halisi lamjadala ambalo linaongoza kwenye uamuzi kwamba Isa (amanijuu yake) wakati wa safari zake aliwasili Nasibain. Hii Nasibain nimahali kati ya Mosul na Syria ambapo katika ramani za Kiingerezapameitwa Nasibus. Kama mtu anasafiri kutoka Syria kwendaUajemi, atapita Nasibain, ambao upo kwenye umbali wa maili450 kutoka Yerusalem: Mosul uko takriban maili 48 kutokaNasibain na maili 500 kutoka Yerusalem. Mpaka wa Uajemi ukoumbali wa maili 100 tu kutoka Mosul. Hii ina maana kwambaNasibain uko maili 150 kutoka mpakani mwa Uajemi. Mpaka waMashariki wa Uajemi unaugusa mji wa Herat katika Afghanistan,yaani Herat uko katika mpaka wa Magharibi wa Afghanistankuelekea upande wa nchi ya Uajemi na uko takriban maili 900kutoka mpaka wa Magharibi wa Uajemi. Kutoka Herat hadi kwenyeMlangobahari wa Khayber umbali wake ni kama maili 500 hivi.Ifuatayo hapa ndiyo ramani inayonyesha ile njia aliyoifuata Isa.

Ramani hii inaonyesha njia aliyoitumia Yesu katika safari yakeya Kwenda Kashmir. Lengo la safari hii lilikuwa kwamba awezekukutana na Waisraeli ambao mfalme Shamaneser aliwakamatamateka na kuwapelekea Media. Itaonekana kwamba kwenyeramani zilizochapishwa na Wakristo, Media unaonyshwakuelekea Kusini kwa Bahari ya Khizar (Avoz), ambapo hivi sasani Uajemi. Mpaka wa Mashariki wa Uajemi unatangamana na Af-ghanistan; kuelekea Kusini ipo bahari na kuelekea Magharibi ipoDola ya Kituruki. Kama taarifa iliyomo katika Rauzat-us-Safa nisahihi inelekea kwamba, kwa kwenda Nasibain Yesu alikusudiakuja Afghanistan kupitia Uajemi, na kuwaita kwenye ukweli.Mayahudi waliopotea ambao wakaja kujulikana kama Waafghani.

Page 75: Yesu katika India

75

Neno "Afghan" laelekea kuwa na asili ya Kiebrania; na nenolililotokana na neno jingine ambalo maana yake ni "shujaa".Yaeleeka kwamba kwenye kilele cha ushindi wao wakajichaguliajina hili1.

Kwa kifupi; Yesu alikuja Punjab baada ya kupitia Afghanistanakiwa na kusudio la asili la kwenda Kashmir baada ya kuionanchi ya Punjab na Hindustan. Itaonekana kwamba Chitral naukanda wa Punjab vinatenganisha Kashmir na Afghnistan. Kamamtu atasafiri kutoka Afghnistana kwenda Kashmir kupitia Punjab,mtu huyo atatembea umbali wa maili 80 au kiasi cha kilometa135.

Lakini kwa busara, Yesu akachagua njia ya kupitia Afghanistanili kwamba yale makabila yaliyopotea ya Israeli yajulikanayo kamaWaafghani nayo yaweze kufaidika naye. Mpaka wa Mashariki waKashmir unagusa Tibet. Kutoka Kashmir angaliweza kwenda kwaurahisi hadi Tibet na baada ya kufika Punjab hakuwa na ugumuwa kuzizungukia sehemu muhimu za Hindustan kabla ya kwendaKashmir na Tibet. Kwa hiyo inawezekana sana, kama baadhi ya

__________________________________________________________

1Katika Taurati kulikuwako na ahadi kwa Mayahudi, kwamba kamawangemwamini nabii wa "mwisho" wangepewa ufalme na utawala, baadaya kupitia kwenye mateso mengi. Ahadi ile ilitimilizwa kwa yale makabilakumi ya Israeli kuukubali Uislamu. Hii ndiyo sababu kumekuwako wafalmewakubwa miongoni mwa Waafghani na pia miongoni mwa Wakashmiri.

Ipo barua katika sehemu ya 14 ya Sura ya Kwanza ya Historiakwa Kigiriki "Imani ya Eusebio" iliyotafsiriwa na Mlondon mmoja aitwayeHeinmer mnamo mwaka 1650 kwa kalenda ya Kikristo, ambayoinaonyesha kwamba mfalme mmoja aitwaye Abgerus alimwita Yesukutoka nchi iliyo ng'ambo ya mto Euphrates, kwenye Ikulu yake. Baruailiyopelekwa na Abgerus kwa Yesu, na majibu yake, zimejawa na uwongona utiaji chumvi mwingi sana. Lakini hili moja laonekana kuwa ni la kweli,kwamba mfalme yule, baada ya kuarifiwa kuhusu ukatili wa Mayahudialimwita Yesu kwenye Ikulu yake ili ampe hifadhi. Yumkini mfalme huyoaliamini kwamba alikuwa nabii wa kweli.

Page 76: Yesu katika India

76

kumbukumbu za zamani za kihistoria za nchi hii zinavyoonyesha,kwamba Yesu aweza kuwa aliiona Nepal, Benares na sehemuzingine. Kisha hana budi alikwenda Kashmir kupitia Jammu naRawalpindi. Kwa kuwa yeye alikuwa mwenyeji wa nchi ya baridi,ni jambo la yakini kwamba alikaa kwenye majimbo haya wakatiwa kipupwe tu, na ilipofikia mwishoni mwa mwezi wa Machi aumwanzoni mwa Aprili hana budi alianza kuelekea Kashmir. Kwavile Kashmir inafanana na Shamu ni lazima awe alichaguamakazi yake ya kudumu katika nchi hii. Aidha yawezekanakwamba aweza kuwa alikaa kwa kipindi fulani nchini Afghanistan.Si jambo lisilowezekana kwamba aweza kuwa alioa katika nchiile. Mojawapo miongoni mwa makabila ya Waafghani linajulikanakama "Isa Khel" - halitakuwa jambo la kushangaza iwapo hao niwazao wa Yesu. Lakini ni jambo la kusikitisha kwamba historiaya Waafghani ipo katika hali ya vurugu; kwa hiyo ni vigumu kufikiakwenye jambo lo lote la uhakika kwa kusoma taarifa zao zakikabila. Lakini hakuna shaka, kwamba Waafghani ni Waisraelikama walivyo Wakashmiri. Wale ambao wamechukua maoniyaliyo tofauti na haya kwenye vitabu vyao wamepotezwa kupoteakwa hali ya juu; hawakulichunguza jambo hili walau kwa dakikamoja. Waafghani wanakiri kwamba wao ni wazao wa Qais; naQais ni mtu wa Israel. Lakini si lazima kuendeleza mjadala huuhapa. Nimekwisha lishuhgulikia suala hili kikamilifu katika kimojamiongoni mwa vitabu vyangu; hapa, ninatoa taarifa ya safari yaYesu kupitia Nasibain, Afghanistan, Punjab na kuendelea hadiKashmir na Tibet. Aliitwa "nabii mwenye kusafiri, la bali kiongoziwa wasafiri", kutokana na safari hii iliyo ndefu sana.

Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, yaani, Ibn-al-Walid Al-FahriAt-Tartuushi Al-Maliki, ambaye alitukuzwa kwa ajili ya kisomochake, anasema kumhusu Yesu kwenye ukurasa wa 6 wa kitabuchake Siraajul-Muluk, kilichochapishwa na Matbaa Khairiya yaMisri mnamo mwaka 1306 A.H.:

"Yuko wapi Isa, aliye Ruhullah, na Kalimatullah, ambaye alikuwakiongozi wa wachamungu na chifu wa wasafiri?" akimaanishakwamba alikuwa amekufa, na kwamba, hata mtu mkubwa kama

Page 77: Yesu katika India

77

yeye aliondoka katika ulimwengu huu. Ni lazima izingatiwekwamba msomi huyu mwenye mamlaka anamwita Yesu siyo tu"Msafiri" bali "Kiongozi wa wasafiri". Kadhalika kwenye ukurasawa 461 wa Lisaanul-Arabi imesemwa:

Yesu aliitwa "Masihi" kwa sababu alisafiri huku na huko, nakwa sababu hakukaa katika sehemu moja." Taarifa hiyo hiyoimerikodiwa katika Tajul-Urus Sharah Qamus. Humo imesemwapia kwamba "Masihi" ni yule ambaye amepewa wema na baraka,yaani amepewa sifa hizi kwa kiwango cha namna hii kwambahata mguso wake umebarikiwa; na kwamba jina hili lilitolewa kwaYesu, kwani Mwenyezi Mungu Humpa jina hili ye yote Amtakaye.Kinyume na huyu, yuko "Masihi" mwingine, ambaye mguso wakeni mwovu na wenye laana, yaani, asili yake iliumbwa kwa laanana uovu, kwa kiasi hiki kwamba mguso wake unaleta giza la uovuna giza la laana. Jina hili lilitolewa kwa yule Masihi ambaye niDajjal na kwa wale wote ambao wanafanana na yeye. Aidha hayamajina mawili, yaani Masihi mwenye kusafiri na MasihiAliyebarikiwa si yenye kupingana. Moja halilibatilishi lenzie. Kwani,ni desturi ya kimbingu kwamba Mwenyezi Mungu Humwita mtukwa zaidi ya njia moja na kwamba majina yote ya namna hiyoyanamhusu yeye. Kwa kifupi, katika hali ya kuwa msafiri, Yesuamethibitishwa vizuri sana na historia ya Kiislamu hivi kwambakama rejea zote zitanakiliwa kutoka kwenye vitabu vile nadhanizitasababisha kupatikana wa lijitabu likubwa sana. Kwa hiyoniliyoyasema yanatosha.

Page 78: Yesu katika India

78

SEHEMU YA 2

Ushahidi kutoka kwenye vitabu vya Kibuddha.

Naiwe wazi kwamba maandiko matakatifu ya Kibuddhayametupatia ushahidi wa aina mbalimbali ambao kwa jumlaunatosha kuthibitisha kwamba Yesu (amani juu yake) lazimaalikuja Punjab na Kashmir n.k. Nauratibu ushahidi huo humu iliwatu waadilifu kwanza waweze kuusoma, na kisha kwa kuupangakatika akili zao kama taarifa iliyoungana, waweze wao wenyewekufikia kwenye uamuzi uliokwisha semwa. Ushahidi huo ni huuhapa. Kwanza: majina aliyopewa Buddha yanafanana na majinaaliyopewa Yesu. Kadhalika, matukio ya maisha ya Buddhayanalingana na yale ya maisha ya Yesu. Lakini rejea ya hapainahusu Dini ya Kibuddha ya sehemu zilizopo ndani ya mipakaya Tibet, kama vile Leh, Lhasa, Gilgit na Hams n.k., ambazo ndizosehemu zilizothibitika kuwa zilitembelewa na Yesu. Kuhusianana kufanana majina, inatosha kuonyesha kwamba, iwapo kwamfano Yesu (amani juu yake) anajiita "Mwanga" katika mafundishoyake, vivyo hivyo Gautama ameitwa Buddha, ambalo kwa lughaya Sanskrit lina maana ya "Mwanga"1. Iwapo Yesu ameitwa"Bwana"2 katika Injili, vivyo hivyo Buddha ameitwa Sasta au"Bwana". Kama Yesu ameitwa "Mbarikiwa" katika Injili, vivyo hivyoBuddha ameitwa Sugt, yaani, "Mbarikiwa". Kama Yesu ameitwa"Mwanamfalme" vivyo hivyo Buddha naye ameitwa"Mwanamfalme. Yesu ameelezewa pia na Injili kama mtu ambayeanatimiliza shabaha ya kuja kwake. Vivyo hivyo Buddha nayekatika maandiko matakatifu ya Kibuddha ameitwa Siddhartha,yaani, "mtu anayetimiliza shabaha ya kuja kwake". Yesu piaameitwa na Injili "Kimbilio la waliochoka". Vivyo hivyo katikamaandiko matakatifu ya Kibuddha, Buddha ameitwa Asar Sarn,yaani "Kimbilio la wasiokuwa na mahali pa kukimbilia." Na Yesuameitwa pia "Mfalme" na Injili, ingawa yeye alilitafsiri hilo kuwa___________________________________________________________1. Kitabu cha Sir M. M. William, Buddhism, Ukurasa wa 232. Kitabu cha Sir M. M. William, Buddhism, Ukurasa wa 23

Page 79: Yesu katika India

79

na maana ya "mfalme" wa Ufalme wa Mbingu. Vivyo hivyoBuddha naye ameitwa "Mfalme". Kufanana kwa matukiokunathibitishwa na matukio kama haya: Kama vile Yesualivyoshawishiwa na shetani kwa utajiri na ufalme wa ulimwenguilmuradi tu amsujudie, kadhalika Buddha naye alishawishiwa naShetani alipomwambia kwamba atampatia fahari na utukufu wawafalme kama angeachana na maisha yake ya upweke na kurudinyumbani. Lakini, kama vile Yesu alivyokataa kumtii shetani, vivyohivyo imerikodiwa kwamba Buddha naye hakumtii. TazamaBuddhism cha T.W. Rhys Davis; na Buddhism cha Sir MonierMonier Williams.1

Hii inaonyesha kwamba majina yale yale anayojinasibisha nayoYesu katika Injili, kadhalika yamenasibishwa kwa Buddha kwenyevitabu vya Kibuddha ambavyo vilitungwa muda mrefu baadae;na, kama vile Yesu alivyoshawishiwa na Shetani, vivyo hivyo vitabuhivi vinadai kwamba Buddha naye alishawishiwa na Shetanil la,bali taarifa ya kushawishiwa kwa Buddha kama ilivyoandikwakatika vitabu hivi ni ndefu kuliko ile taarifa ya kushawishiwa kwaYesu katika Injili za Kikristo.Imerikodiwa kwamba wakati shetani alipomtangulizia kishawishicha utajiri na heshima ya kifalme, Buddha alielekea kurudinyumbani. Lakini hakuitii tamaa hii. Lakini Shetani huyo huyoakakutana naye tena katika usiku mmoja, akiwa amewaletawazao wake wote, na kumtisha kwa sura za kuogopesha. KwaBuddha mashetani hawa walionekana kama nyoka waliokuwawakitema moto kutoka kwenye midomo yao. Hawa "nyoka"walianza kumtupia sumu lakini sumu yao ikageuzwa kuwa mauana ule moto ukafanya mduara wa nuru kumzunguka Buddha.

Huyo Shetani baada ya kutofanikiwa hivyo, akawaita kumi nasita miongoni mwa mabinti zake na akawaomba wamdhihirishieBuddha uzuri wao, lakini Buddha bado hakutikisika. Shetaniakashindwa katika hila zake. Akachagua njia zingine lakinihakuweza kufanya lo lote dhidi ya usimamaji Imara wa Buddha,___________________________________________________________1. Pia, tazama Chinese Buddhism cha Edkins; Buddha, cha Oldenberg,kilichotafsiriwa na W. Hoey; Life of Buddha kilichotafsiriwa na Rickhill.

Page 80: Yesu katika India

80

ambaye aliendelea kupanda madaraja ya utakatifu ya juu na juuzaidi, na baada ya usiku mrefu, yaani baada ya majaribu makalina ya muda mrefu, alimshinda adui yake Shetani; "Mwanga" waElimu ya kweli ulimchomozea, sambamba na kufika kwa"asubuhi, yaani, mara tu baada ya majaribu yake kumalizika,akatokea kuyajua yote. Siku ambapo vita hii kubwa ilimalizikailikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa dini ya Kibuddha. Wakati huoGautama alikuwa na umri wa miaka 35; aliitwa Buddha au"Mwanga" na ule Mti ambao chini yake alikuwa ameketi wakatiule, ukaja kujulikana kama "mti wa Mwanga". Hivyo, kamamtafungua na kuiangalia Biblia mtaona jinsi kushawishiwa kwaBuddha kunavyofanana na kushawishiwa kwa Yesu kwa kiasihiki kwamba umri wa Buddha kwa wakati ule ulikuwa takribansawa na umri wa Yesu. Na, kama inavyoonekana kutoka katikamaandiko ya Kibuddha, yule Shetani hakujitokeza kwa Buddhakatika hali ya kimwili inayoweza kuonekana. Ilikuwa shaniiliyoonwa na Buddha tu; yale "mazungumzo" ya Shetani ni"ushauri mbaya uliotiwa moyoni mwa Buddha", yaani, yule Shetanialipojitokeza kwake, alitia ushauri katika moyo wa Buddhakwamba yeye (Buddha) aache njia yake, kwamba ni lazimaamfuate yeye (Shetani), kwamba Shetani atampa utajiri wote waulimwengu. Kadhalika, imani ya madaktari wa Kikristo ni kwambaShetani aliyejitokeza kwa Yesu hakuja kwake katika hali ya kimwili- hakuja kwa Yesu kama binadamu - mbele ya macho yale yaleya Mayahudi, akipita mitaani na vichochoroni akiwa katika mwiliwenye umbo la kibinadamu na akizungumza na Yesu kwa namnaambayo angeweza kusikika na wale waliokuwapo. Kinyume chahivyo, mkutano huo ulikuwa katika hali ya Kashf iliyoonwa na Yesutu; yale mazungumzo pia yalikuwa katika hali ya ushauri uliotiwamoyoni, yaani Shetani, kama desturi yake alipenyeza ushaurimbaya katka moyo wake. Lakini Yesu hakukubali - aliukataaushauri huo wa shetani.

Hivyo inafaa kutafakari kwa nini kulikuwako na kufanana kwingikati ya Buddha na Yesu? Kuhusiana na jambo hili Maaryawanasema kwamba Yesu alizijua habari za dini ya Kibuddha

Page 81: Yesu katika India

81

kutokana na safari zake nchini India, na baada ya kujipatia elimukuhusu uhakika wa maisha ya Buddha, alitengeneza Injili yakekutokana na elimu hii aliporejea kwenye nchi yake ya uzalendo;kwamba Yesu alitunga mafundisho yake kimaadili kwa kuibamafundisho ya kimaadili ya Buddha; kwamba kama vile Buddhaalivyojiita "Mwanga" na "Ujuzi" na kujipangia majina mengine -vivyo hivyo Yesu naye aliyanasibisha kwake majina yote hayo,kwa kiasi hiki kwamba hata ile hadithi ndefu ya kushawishiwakwa Buddha ikachukuliwa na yeye. Lakini huu ni uzushi wa Maarya.Si kweli hata kidogo kwamba Yesu alikuja India kabla ya tukio laMsalaba; hakuwa na haja ya kufunga safari kama hiyo wakati ule- alikuwa na haja ya kufunga safari kama hiyo wakati Mayahudiwa nchi ya Sham walipomkataa na kama walivyoamini kwambawalimwua msalabani. Lakini mpango mzuri sana wa kimbinguulimwokoa. Hivyo baada ya kumaliza juhudi zake zote za kutakakuwahurumia Mayahudi na shauku yake ya kutaka kuwahubiriana kutokana na Mayahudi kuwa na moyo mgumu sana kwasababu ya uovu wa hali yao ya asili iliyowafanya wasiweze kabisakuukubali Ukweli, Yesu, kwa kujulishwa na Mwenyezi Mungukwamba makabila kumi ya Mayahudi yalihamia upande wa India,akashika njia kuelekea kwenye majimbo hayo. Na, kwa kuwamakundi makubwa ya Mayahudi yalikuwa yameingia katka diniya Kibuddha, hapakuwa na njia nyingine kwa nabii huyu mkweliisipokuwa kuelekeza juhudi zake kwa wafuasi wa dini ya Kibuddha.Makuhani wa Kibuddha wa nchi ile walikuwa wakitazamia kutokeakwa "Masihi" Buddha. Kwa hiyo, yale majina ya Yesu na pia baadhiya mafundisho yake ya kimaadili kama vile "Mpende adui yako;usirejeshe uovu", na kama vile ilivyotabiriwa na GautamaBuddha kuhusu Yesu kuwa na ngozi yenye ung'avu, kutokana naishara zote hizi makuhani wakamchukulia yeye kuwa ndiye Bud-dha. Yawezekana pia kwamba baadhi ya majina yake namafundisho yake na mambo ya uhakika kuhusu maisha ya Yesuvyaweza kuwa vilinasibishwa kwa Buddha wakati ule kwamakusudi au bila kukusudia; kwani Wahindu kamwe hawajatoauthibitisho wa ustadi wa kutosha katika kuiweka historia kwenye

Page 82: Yesu katika India

82

kumbukumbu. Matukio ya maisha ya Buddha hayakuwekwa katikakumbukumbu hadi wakati wa Yesu.

Kwa hiyo, Makuhani wa Kibuddha walikuwa na fursa nzuri sanaya kulinasibisha kwa Buddha jambo lo lote walilotaka. Hivyoyaelekea kwamba walipokuja kuujua uhakika kuhusu maisha yaYesu na mafundisho yake kimaadili, wakayachanganya haya namambo mengine waliyoyabuni wao wenyewe na wakayanasibishayote hayo kwa Buddha1. Hivi punde nitathibitisha kwamba yalemafundisho ya kimaadili ya Biblia - yale majina "Mwanga" n.k.ambayo, jinsi yalivyo kwa Yesu yanakutwa yamerikodiwa kumhusuBuddha kama pia kilivyo kisa cha kushawishiwa na Shetani - yotehaya yaliandikwa kwenye vitabu vya Kibuddha wakati Yesualipokuja humu nchini baada ya kutungikwa msalabani.

Zaidi ya hayo kupo kufanana kwingine kati ya Buddha na Yesu:Dini ya Kibuddha imeweka katika kumbukumbu zake kwambawakati wa kushawishiwa Buddha alikuwa amefunga saumu nakwamba kufunga huko kulidumu kwa muda wa siku arobaini.Wasomaji wa Injili wanafahamu kwamba Yesu pia alifunga kwasiku arobaini.

Na, kama nilivyokwisha sema hivi punde kuwa kupo kufananakwa ajabu kati ya mafundisho ya Kimaadili ya Buddha na yale yaYesu kwa kiasi hiki kwamba kwa wale wanaoyafahamu yote mawililimekuwa kwao jambo lenye nguvu sana. Kwa mfano, Injilizinasema; usilipize maovu, mpende adui yako, ishi katikaumaskini, jiepushe na majivuno na uwongo na uchoyo. Hayo hayondiyo mafundisho ya Buddha. La, bali mafundisho ya Kibuddhayanaweka mkazo zaidi kuhusu jambo hilo kwa kiasi hiki kwambaviumbe vyote vyenye uhai - hata kuua mchwa na wadudukumetangazwa kuwa ni dhambi. Kanuni maarufu ya dini yaKibuddha ni: Huruma kwa ajili ya ulimwengu mzima; kuwatakiahali njema binadamu wote na wanyama wote; kuchochea moyo___________________________________________________________1. Hatuwezi kukana kwamba tangu zama za kale Imani ya Kibuddha ilikuwainayo mafundisho ya kimaadili ya kutosha ndani yake; lakini wakati huo huonashikilia kwamba ile sehemu ambayo ni mafundisho matupu ya Injili - yalemafumbo na nukuu zingine kutoka katika Biblia - bila shaka iliongezwa kwenyevitabu vya Kibuddha wakati Yesu alipokuwa katika nchi hii.

Page 83: Yesu katika India

83

wa umoja na upendo kwa kila mtu. Hayo hayo ndiyo mafundishoya Injili.Tena, kama vile Yesu alivyowatuma wanafunzi wake kwendakwenye nchi mbalimbali - na yeye mwenyewe akiwa amekwendakwenye nchi moja - vivyo hivyo ndivyo alivyofanya Buddha.Buddhism kilichotungwa na Sir Monier Wiliams kinarikodi kwambaBuddha aliwatuma wanafunzi wake kwenda kuhubiri, akiwaagizahivi: Enendeni na zungukeni kila mahali kwa kuuhurumiaulimwengu na kwa ajili ya ustawi wa miungu na watu. Enendenikatika pande mabalimbali. Hubirini itikadi (Dharham), kwa nasahanjema (Kalayana) mwanzoni, katikati na mwishoni, kwa maanayake halisi (artha) na jinsi ilivyoandikwa (vyanjana). Tangazenimaisha ya kujizuia kikamilifu, maisha ya utakatifu na maisha yakutokuoa (Drahmacariyam). Mimi pia nitakwenda kuihubiri itikadihii. (Mahavagga 1.11.1)1. Buddha alikwenda Benares naakafanya miujiza mingi kwenye jimbo lile; alifanya karamu yakuvutia juu ya kilima kama vile Yesu alivyofanya karamu yakemlimani. Tena, kitabu hicho hicho kinasema kwamba mara nyingiBuddha alihubiri kwa njia ya mafumbo; alielezea mambo ya kirohokwa mfano wa vitu vyenye kuonekana kwa macho ya kawaida.

Naikumbukwe kwamba mafundisho haya ya kimaadili na njiahii ya kuhubiri, yaani, kuzungumza kwa mafumbo ilikuwa njia yaYesu. Namna hii ya kuhubiri na mafundisho haya ya kimaadiliyakichanganywa pamoja na mazingira mengine, yanaashiria maramoja kwamba huku kulikuwa ni kumuigiza Yesu. Yesu alikuwahapa India; alikwenda kuhubiri kila mahali; wafuasi wa imani yaKibuddha walikutana naye, na baada ya kuona kwamba yeyealikuwa mtu mtakatifu aliyefanya miujiza, wakayarikodi mambohaya kwenye vitabu vyao; la, bali wakamtangaza yeye kuwa ndiyeBuddha kwani ni tabia ya hali ya asili ya binadamu kujaribu kujipatiajambo jema po pote litapokuwa, kwa kiasi hiki kwamba watuwanajaribu kurikodi na kukumbuka tamshi lo lote la kiakili lenyekufanywa na mtu ye yote machoni pao. Kwa hiyo inaelekea zaidi___________________________________________________________1. Buddhism, kilitungwa na Sir Monier Williams, kilichotangazwa naJohn Murray, London 1889, ukurasa 45.

Page 84: Yesu katika India

84

sana kwamba wafuasi wa imani ya Kibuddha wanaweza kuwawameinakili picha nzima ya Injili zote kwenye vitabu vyao; kwamfano kufunga kwa siku arobaini kwa wote wawili, Yesu na Bud-dha; kushawishiwa kwa wote wawili; kuzaliwa bila baba kwa wotewawili, mafundisho ya kimaadili ya wote wawili; kujiita "Bwana"na "Masahaba" zao kuitwa "wanafunzi"; kama vile Mathayo, suraya 10 aya ya 8 na 9 zinavyosema: "Msichukue dhahabu walafedha wala mapesa kwenye mishipi yenu", vivyo hivyo Buddhanaye alitoa amri hiyo hiyo kwa wanafunzi wake; kama vile Injiliinavyohimiza kuishi bila kuoa, vivyo hivyo ndivyo yafanyavyomafundisho ya Buddha; kama vile kulivyokuwako na tetemeko laardhi wakati Yesu alipowekwa Msalabani; vivyo hivyo imerikodiwakwamba kulikuwako na tetemeko la ardhi wakati wa kufariki Bud-dha. Mambo yote haya yenye kufanana yanatokana na ukweli waziara ya Yesu nchini India, ambayo ilikuwa ni kipande cha bahatinjema kwa wafuasi wa Imani ya Kibuddha, kutokana na yeye kuishimiongoni mwao kwa muda mwingi kidogo na kutokana nawafuasi wa Buddha kujipatia elimu nzuri, uhakika wa maisha yakena uhakika wa mafundisho yake yaliyo bora. Kwa sababu hiyo,ilikuwa lazima kwamba sehemu kubwa ya mafundisho hayo nasuna zake ziwe zimejipenyeza kwenye kumbukumbu zaKibuddha kwani Yesu aliheshimiwa na kuhesabiwa kuwa ni Bud-dha na wafuasi wa Buddha. Kwa hiyo, watu hawa wakazirikodihadithi zake kwenye vitabu vyao na wakazinasibisha na Buddha.

Kwa kweli ni jambo la ajabu, kwamba Buddha, kama alivyofanyaYesu, awe amewafundisha wanafunzi wake kwa njia ya mafumbo- hususan kwa njia ya mafumbo yale yanayopatikana katika Injili.Katika moja ya mafumbo hayo Buddha anasema:

"Kama vile mkulima anavyopanda mbegu lakini hawezi kusema:Mbegu hii itavimba leo, na kesho itachipua, vivyo pia ndivyo ilivyokwa wanafunzi; ni lazima atii maagizo, ajizoeze kutafakari naajifunze itikadi; hawezi kusema leo au kesho nitaokolewa".1

Hili, itakumbukwa, ndilo fumbo lile lile ambalo limekuwamo ndaniya Injili hadi leo. Buddha anasimulia tena fumbo jingine:___________________________________________________1. Sir. M. M. Williams, Buddhism, ukurasa 51

Page 85: Yesu katika India

85

"Tena kama vile kundi la kulungu linavyoishi msituni na mtuanakuja kulifungulia njia ya udanganyifu na: kulungu haowakaumia, na mwingine anakuja kulifungulia njia ya usalama nakulungu wakasitawi, vivyo hivyo wakati watu wanapoishi miongonimwa mambo ya furaha mtu mwovu anakuja na kufungua njia yauwongo yenye ncha nne. Kisha anakuja mtu mkamilifu nakufungua njia ya usalama yenye ncha nne ya imani ya kweli n.k.(P. Oldenberg 191 - 192)".

Buddha alifundidha pia:Uchamungu ni hazina iliyo salama ambayo hakuna awezaye

kuiiba. Ni hazina ambayo inakwenda pamoja na watu hata baadaya kifo: Ni hazina ambayo ni chanzo cha Elimu yote na Ukamilifuwote".1

Hivyo itaonekana kwamba mafundisho ya Injili ni yale yale.Kumbukumbu za kale za Kibuddha zenye mafundisho haya niza kipindi ambacho hakiko mbali na wakati wa Yesu - la, bali niza kipindi kile kile. Tena, kwenye ukurasa wa 135 wa kitabu hichohicho panajitokeza hadithi ambamo Buddha anazungumziakuhusu hali yake ya kutokuwa na hatia kwa vile hakuna mtuambaye angeweza kuonyesha doa katika tabia yake. Hili pia linaomfano na usemi wa Yesu. Buddhism, kwenye ukurasa wa 45kinasema:

"Mafundisho ya Kimaadili ya Buddha yana mfanano wa ajabuna yale ya Kikristo."

Nakubali; ninakiri; yote yanasema, "Usiupende ulimwengu;wala mali; usiwachukie adui zako; usitende maovu; yashindemaovu kwa wema; watendee wengine kama wewe unavyotakakutendewa" - hii inaonyesha mfanano wa ajabu kati ya Injili namafundisho ya Buddha kwa kiasi hiki kwamba si lazima kutajamambo mengine zaidi ya ufafanuzi.

Kumbukumbu za Kibuddha zinaonyesha pia kwamba GautamaBuddha alitabiri kutokea kwa Buddha wa pili ambaye aliitwaMetteyya._____________________________________________________________1. Sir. M. M. Williams, Buddhism, ukurasa 51

Page 86: Yesu katika India

86

Utabiri huu umo katika Laggawati Sutatta - kumbukumbu yaKibuddha. Imetajwa kwenye ukurasa wa 142 wa kitabu chaOldenberg. Utabiri huo unasomeka hivi:1

"Atakuwa kiongozi wa kundi la wanafunzi lenye kufikia idadi yamamia ya maelfu, kama mimi nilivyo sasa kiongozi wa makundiya wanafunzi yenye kufikia idadi ya mamia."

Itaonekana hapa kwamba neno la Kiebrania Masiha, nisawasawa na neno la Kipali Matteyya. Ni jambo la elimu yakawaida kwamba wakati neno linapohamishwa kutoka katikalugha moja kwenda kwenye lugha nyingine aghlabu linapatamabadiliko: neno la Kiingereza pia, linalochukuliwa na lughanyingine, linapata mabadiliko: kwa mfano; Max Muller, kufuatiaorodha iliyotolewa kwenye ukurasa wa 318 wa jalada la 2 la "Sa-cred Books of the East, anasema: Ile 'th' ya alfabeti ya Kiingerezainakuwa kama 's' kwenye Kiajemi au Kiarabu. Kwa kuyazingatiamabadiliko haya tunaweza kuelewa kwa urahisi kwamba nenoMessiah likawa Metteyya kwa lugha ya Kipali, ambayo ina maanakwamba Metteyya atakayekuja baadaye ambaye alitabiriwa naBuddha kwa hakika ndiye Masihi - si mtu mwingine. Hili linaungwamkono na ukweli kwamba Buddha alitabiri kwamba imanialiyoianzilisha itadumu ulimwenguni kwa zaidi ya miaka 500;kwamba wakati wa kupungua kwa kanuni na mafundisho yake,huyo Metteya atakuja nchini humu na ataziimarisha tenaulimwenguni. Sasa tunajua kwamba Yesu alitokea miaka 500baada ya Buddha, na kwamba kama vile Buddha alivyowekakikomo cha muda wa kupungua kwa Imani yake, dini ya Kibuddhailiingia katika hali ya mwanguko ulipowadia wakati uliowekwa.Kisha ndipo Yesu, baada ya kuepuka Msalabani, akasafiri kujahumu nchini; na wafuasi wa dini ya Kibuddha walimtambua nawakamtendea kwa heshima kubwa. Hapana shaka kwambamafundisho ya kimaadili na mazoezi ya kiroho yaliyofundishwana Buddha yalifufuliwa na Yesu.Wakristo wanakiri kwamba ile karamu ya Mlimani ya Injili namafundisho mengine ya kimaadili ni yale yale yaliyohubiriwa na_______________________________________________________________________1. Dr. Herman Oldenberg. Buddha.

Page 87: Yesu katika India

87

Buddha ulimwenguni miaka mia tano kabla. Wanasema piakwamba Buddha hakufundisha mafunzo ya kimaadili tu;alifundisha pia kweli nyingine zilizo kuu. Kwa maoni yao hii lakabu"mwanga wa Asia" inayotumika kumhusu Buddha inatumikamahali pake hasa. Hivyo kulingana na utabiri wa Buddha, Yesualitokea miaka mia tano baadaye; na kama wanavyokiri wanazuoniwengi wa Kikristo, mafundisho yake yalikuwa sawasawa na yalemafundisho ya Buddha. . . Kwa hiyo, hapana shaka kwambaalijitokeza katika "roho" ya Buddha. Kwenye kitabu cha Oldenberg,kwa mamlaka ya Laggawati Sutatta, imeelezwa kwamba kwakuangalia yajayo baadae, wafuasi wa Buddha walijiliwaza kwamawazo kwamba, wakiwa wanafunzi wa Metteyya, watapatafuraha na wokovu; yaani walikuwa na yakini kwamba Metteyyaatawajia na kwamba watapata wokovu kwa njia yake, kwani yalemaneno ambayo Buddha alitangaza kuhusu matumaini ya kujakwa Metteya yaliashiria kwamba wanafunzi wake wangekutananaye. Maelezo ya kitabu kilichotajwa hapo juu yanatilia nguvu iledhana kwamba kwa ajili ya kuwaongoza watu hawa MwenyeziMungu Alitengeneza seti mbili za mazingira: kwanza, kutokanana jina Asaf lililotajwa katika Mwanzo 3, aya ya 10, ambalo linamaana ya "mtu anayewakusanya watu", Yesu hakuwa na budiisipokuwa kuizuru ile nchi ambako Mayahudi walikuja kulowea;pili, kwamba kulingana na utabiri wa Buddha, ilikuwa jambo lamuhimu kwamba wafuasi wa Buddha ni lazima wamwone nawafaidike na uchamungu wake. Kwa kuzitafakari nukta hizi mbilikwa pamoja linakuwa takriban ni jambo la yakini kabisa kwambaYesu ni lazima awe ameizuru Tibet. Na ule ukweli kwambamafundisho na taratibu za ibada za Kikristo vimeathiri sana diniya Kibuddha ya Tibet unafanya liwe jambo la lazima ile imanikwamba Yesu ni lazima awe aliwahi kuwatembelea watu wa Ti-bet. Isitoshe, ule ukweli kwamba wafuasi wakereketwa wa diniya Kibuddha, kama inavyoelezwa kwenye kumbukumbu zaKibuddha hadi leo, walikuwa kila mara wakitazamia kukutananaye, unadhihirisha kwamba hii shauku yao kali ilitangazamapema ziara yake nchini humu.

Page 88: Yesu katika India

88

Kwa kuzingatia kweli hizi mbili, mtu mwadilifu hana haja yakuziepa kumbukumbu za Kibuddha ili kupata maelezo kwambaYesu alipata kuja Tibet. Kwani, kulingana na utabiri wa Buddha,kwa kuwa shauku ya kuja kwa Buddha mara ya pili ilikuwa kubwa,utabiri wenyewe utakuwa umemvuta Yesu kwenda Tibet.

Ni lazima itambulike kwamba hili neno "Metteyya" lililotajwamara kwa mara kwenye vitabu vya Kibuddha bila shaka ndiloneno "Masihi". Katika kitabu kiitwacho Tibet, Tartary, Mongolia,kilichotungwa na H. T. Prinsep, kwenye ukurasa wa 14, kuhusuMetteyya Buddha ambaye kwa hakika ndiye Masihi, imeelezwakwamba baada ya kusikia na kuona kwa mara ya kwanza halizinazopatikana nchini Tibet, wamishionari wa kwanza (Wahubiriwa Kikristo) walifikia uamuzi kwamba ndani ya vitabu vya kalevya Walama ziliweza kuonekana alama za dini ya Kikristo. Tenakwenye ukurasa huo huo imeelezwa kwamba hapana shakakuwa mamlaka hizi za kale ziliamini kwamba wanafunzi wa Yesuwalikuwa bado wangali hai wakati mafundisho ya Kikristo yalipofikamahala hapa. Kwenye ukurasa wa 171 imeelezwa kwambahapana shaka kuwa wakati ule kulikuwako na imani iliyoshikwana wengi kwamba angetokea mkombozi mkubwa ambaye kuhusukutokea kwake Tacitus anasema kwamba si Mayahudi tuwaliohusika na Imani hiyo bali dini ya Kibuddha yenyewe ilikuwainajenga msingi, yaani ilitabiri kuja kwa Metteyya. Mtunzi wa kitabuhiki cha Kiingereza anasema kwenye maelezo: Vitabu viitwavyoPitakkatayan na Atha Katha vinao utabiri ulio wazi kuhusu kutokeakwa Buddha mwingine, ambao utatimia miaka 1000 baada yawakati wa Gautama au 'Sakhiya Muni'. Gautama anaelezakwamba yeye ni Buddha wa 25 na kwamba yule 'BagawaMetteyya' bado hajatokea, yaani baada ya yeye kuondoka atakujayule ambaye jina lake litakuwa Metteya, ambaye atakuwa mng'avu.Mtunzi huyo wa Kiingereza anaendelea kusema kwamba nenoMetteyya lina mfanano wa ajabu na Masihi. Kwa kifupi, GautamaBuddha anaeleza wazi wazi kwenye utabiri huu kwambapatatokea Masihi katika nchi yake, miongoni mwa watu wake namiongoni mwa wafuasi wake.

Page 89: Yesu katika India

89

Huo ndio ulikuwa msingi wa imani ya kudumu kuhusu kuja kwaMasihi miongoni mwa wafuasi wake. Kwenye utabiri wake huyuBuddha alimwita "Bagwa Metteyya" kwa sababu kwa lugha yaSanskrit "Bagwa" ina maana ya "Mweupe" na kwa kuwa Yesualikuwa mkazi wa jimbo la Syria, alikuwa na rangi nyeupe.

Watu wa nchi inayohusika na utabiri huu, yaani, watu waMagadh, ambamo ndimo mlimokuwa na mahali paitwapoBajagriha, walikuwa weusi. Na Gautama Buddha mwenyewealikuwa mweusi. Aliwasimulia wafuasi wake ishara mbili zakuondoa shaka kuhusu Buddha atakayekuja baadaye: (1)kwamba atakuwa "Bagwa" (2) kwamba atakuwa "Metteyya", yaani"msafiri", na kwamba atakuja kutoka nchi ya kigeni. Kwa hiyo,watu hawa kila mara walikuwa wakizitafuta ishara hizi hadiwalipomwona Yesu kidhahiri. Kila mfuasi wa dini ya Kibuddha nilazima kabisa ataungama ile imani kwamba miaka mia tano baadaya Buddha, yule Bagwa (mweupe) Metteyya alitokea katika nchiyao. Kwa hiyo lisiwe jambo la kustaajabisha iwapo vitabu vyaimani ya Kibuddha vitataja kuja kwa Metteyya, yaani, Masihi nchinimwao, na kutimilizwa kwa utabiri wake. Na tuseme kwambahakuna mtajo wa namna hiyo, hata hivyo, kwa sababu kwa msingihuu wa ufunuo wa kimbingu Buddha aliwapatia wanafunzi wakematumaini kwamba Bagwa Meteyya atakuja nchini mwao, hakunamfuasi wa dini ya Kibuddha ambaye anautambua utabiri huuanaweza kukana ujaji nchini humu wa Bagwa Metteya ambayejina lake jingine ni Masihi; kwani, kutokutimilizwa kwa utabiri huokunathibitisha uwongo wa imani hiyo. Na huu utabiri ambaokutimia kwake kuliwekewa wakati maalumu na ambao GautamaBuddha aliusimulia kwa wafuasi wake mara nyingi - kama utabirihuu usingetimia katika wakati wake uliowekwa, wafuasi wa Bud-dha wangetilia shaka ukweli wake na ingalielezwa kwenye vitabukwamba utabiri huu haukutimilizwa. Hoja nyingine yenye kuungamkono kutimia kwa utabiri huu ni kwamba kunako karne ya sababaada ya kuzaliwa Yesu vilipatikana nchini Tibet vitabu vilivyokuwana neno "Masihi", yaani vilitaja jina la Yesu (amani juu yake) likiwalimeandikwa kama Mi-Shi-Hu. Mtayarishaji wa hiyo orodha

Page 90: Yesu katika India

90

iliyokuwa na hilo neno Mi-Shi-hu ni mfuasi wa dini ya Kibuddha.Tazama kitabu kiitwacho A record of the Buddhist Religionkilichotungwa na I. Tsing na kutafsiriwa na G. Takakusu. HuyuTakakusu ni Mjapani aliyetafsiri kitabu cha I. Tsing; na I. Tsing nimsafiri wa Kichina - ambaye pembezoni na kwenyekiambatanisho cha kitabu chake Takakusu anaeleza kwambakwenye kitabu kimoja cha kale linapatikana hili jina Mi-Shi-Hu(Masihi). Kitabu hiki ni cha zama takriban za karne ya saba;kilitafsiriwa hivi karibuni na Mjapani aitwaye G. Takasuku nakutangazwa na Clarendon Press, Oxford1. Kitabu hiki kwa vyovyote vile kinalo hili neno Masihi jambo linaloonyesha kwambahili neno halikuingizwa kutoka nje na wafuasi wa dini ya Buddhabali lilichukuliwa kutoka kwenye utabiri wa Buddha na maranyingine liliandikwa Masihi na mara nyingine likaandikwa BagwaMetteyya.

Na miongoni mwa ushahidi tulio nao wa kumbukumbu zaKibuddha ni kwamba kwenye kitabu kiitwacho Buddhismkilichotungwa na Sir Monier Williams, kwenye ukurasa wa 45imeandikwa kwamba mwanafunzi wa sita wa Buddha atakuwani mtu aitwaye "Yasa". Neno hili la mwisho laelekea kuwa nikifupisho cha neno "Yasu". Kwa vile Yesu (amani juu yake) alitokeamiaka mia tano baada ya kifo cha Buddha, yaani kwenye karneya sita, aliitwa mwanafunz wa sita. Ni lazima ifahamike kwambandani ya kitabu kiitwacho The Nineteenth Century, kwenye ukurasawa 517 wa toleo la Oktoba 1894, Professa Max Muller anaungamkono maelezo yaliyotolewa hapo juu kwa kusema kwambawaandishi mashuhuri wamekwishaonyesha mara nyingi kwambaYesu aliathiriwa na kanuni za dini ya Kibuddha na kwambamajaribio yanafanywa hata leo ili kugundua baadhi wa misingi yakihistoria ambayo kwayo kanuni za imani ya Buddhazitathibitishwa kuwa zilifika Falastin wakati wa siku za Yesu. Jambohili linaviunga mkono vitabu vya imani ya Kibuddha ambamoimeandikwa kwamba Yasa alikuwa mwanafunzi wa Buddha,kwani, wakati Wakristo mashuhuri kama Profesa Max Muller____________________________________________________________1. Tazama ukurasa wa 169 na 223 wa kitabu hiki.

Page 91: Yesu katika India

91

wamekiri kwamba kanuni za dini ya Kibuddha zilikuwa na atharikwa Yesu haitakuwa kukosea sana kusema kwamba hii ilikuwana maana ya yeye kuwa mwanafunzi wa Buddha.

Hata hivyo, mimi nachukulia utumiaji wa maneno kama hayokumhusu Yesu (amani juu yake) kuwa ni utovu wa heshima na niufidhuli. Na maelezo yanayopatikana kwenye vitabu vya imani yaKibuddha kwamba "Yasu" alikuwa mwanafunzi wa Buddha nimfano tu wa tabia iliyothibitika ya makuhani wa watu hawa yakutaja mtu mkubwa atakayetokea wakati ujao kana kwamba nimwanafunzi wa yule aliyetokea kabla. Licha ya hayo, kamailivyokwisha elezwa, kwa vile upo mfanano mkubwa kati yamafundisho ya Yesu na Buddha haitakuwa kukosea sanakuzungumzia uhusiano wa bwana na mwanafunzi kati ya Bud-dha na Yesu, ingawa unaweza kuwa hauendani na hisia zaheshima. Lakini mimi sikubaliani na jinsi wachunguzi wa Kizunguwanavyotaka kuthibitisha kwamba kanuni za dini ya Kibuddhazilifika Falastin wakati wa siku za Yesu. Ni jambo la bahati mbayakweli kweli kwamba wakati jina na kutajwa kwa Yesu kumo ndaniya vitabu vya kale vya dini ya Kibuddha wachunguzi hawa badowaendelee kuchukua njia iliyopinda ya kujaribu kutafuta alamaza imani ya Buddha nchini Falastin. Kwa nini wasitafute nyayozilizobarikiwa za Yesu kwenye ardhi ya majabali ya Nepal, Tibetna Kashmir? Lakini najua kwamba wachunguzi hawawasingeweza kutazamiwa kugundua ukweli ambao ulikuwaumefichika chini ya matabaka elfu moja ya giza; bali ilikuwa nikazi ya Mwenyezi Mungu - Ambaye Aliona kutoka mbingunikwamba kuabudiwa binadamu na urukaji wa mipaka yotevimezagaa ulimwenguni kote na kwamba kuabudiwa kwa Msalabana kinachodhaniwa kuwa ni kafara ya binadamu viliitenganishamioyo ya mamilioni mengi ya watu na Mwenyezi Mungu wa kweli- Ambaye ghera Yake ilimleta ulimwenguni mtumishi Wake kwajina la Yesu Mnazareti ili kuvunja imani ya Msalaba. Na kulinganana ahadi ya zamani alitokea kama Masihi Aliyeahidiwa. Kishaukaja wakati wa kuvunjwa kwa Msalaba, yaani ule wakati ambapokosa la imani ya Msalaba likadhihirishwa kama vile kukivunja

Page 92: Yesu katika India

92

kipande cha ubao katika sehemu mbili. Kwa hiyo sasa ndio wakatiambapo Mbingu imefungua njia kwa ajili ya uvunjwaji wa Msalabaili mtafutaji ukweli aweze kuangaza macho na kuutafuta ukwelihuo.

Lile wazo la Yesu kupaa mbinguni, ingawa lilikuwa kosa, hatahivyo lilikuwa na maana, yaani kwamba Ukweli wa Kimasihiulikuwa umesahauliwa na ulikuwa umefutiliwa mbali kama vilemaiti inavyoliwa na udongo kaburini - Ukweli huu wa Kimasihiuliaminiwa kuwako mbinguni katika hali ya kimwili ya binadamu.Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba Ukweli huu uteremshwe ardhinikatika siku za baadaye. Na umeteremka ardhini katika zama hizikwa sura ya binadamu aliye hai; "umeuvunja" Msalaba; na yalemaovu ya uwongo na ya kuabudu mambo yasiyokuwa kweliambayo katika Hadithi ihusuyo Msalaba Mtume wetu Mtukufuameyalinganisha na nguruwe, yamekatwa vipande vipandesambamba na "kuvunjwa" kwa msalaba, kama vile nguruweakatwavyo kwa upanga. Hadithi hii haimaanishi kwamba MasihiAliyeahidiwa atawauwa makafiri na kuvunja misalaba yaokidhahiri: bali, kuvunjwa kwa Msalaba kunamaanisha kwambawakati wa zama zile Mungu wa Mbingu na Ardhi Ataufichua huuukweli uliofichika ambao kwa ghafula utalivunja jengo lote laMsalaba. Na kuuawa kwa nguruwe hakuna maana ya kuuawakwa watu au nguruwe bali kuna maana ya kuuawa kwa tabia zakinguruwe - kama vile kudumu katika uwongo na usisitizaji wakuwasilisha uwongo huo kwa watu wengine, jambo ambalo nisawasawa na kula uchafu. Kwa hiyo, kama vile nguruwe mfuasivyoweza kula uchafu, vivyo hivyo wakati utafika - la bali tayariumeshafika - ambapo silika za uovu zitazuiliwa kula uchafu wanamna hii. Maulamaa wa Kiislamu wamepotoka katika kuutafsiriutabiri huu. Maana halisi ya "Kuvunjwa kwa Msalaba" na "Kuuawakwa nguruwe" ni hiyo niliyoieleza. Isitoshe, katika zama za MasihiAliyeahidiwa vita za kidini zitafikia ukomo; na Mbingu itazirudishazile kweli zing'aazo kiasi cha kuleta machoni pa mtu ile tofautiiliyo ang'avu kati ya ukweli na uwongo. Kwa hiyo, msidhani kwambanimekuja na upanga. Hasha, nimekuja kuziingiza panga zote

Page 93: Yesu katika India

93

katika ala zake. Ulimwengu umekuwa ukipigana vikali gizani.Watu wengi wamewashambulia wale wakweli wawatakiao mema,wameijeruhi mioyo ya marafiki wenye kuwahurumia nakuwaumiza wapenzi wao. Lakini sasa, giza halipo tena. Usikuumeondoka na hivi sasa ni mchana. Na amebarikiwa yuleambaye atabakia bila kupata hasara tena.

Na miongoni mwa ushahidi uliomo kwenye kumbukumbu zaKibuddha ni ule ushahidi uliopo kwenye ukurasa wa 419 wa kitabukiitwacho Buddhism kilichotungwa na Oldenberg. Ndani ya kitabuhiki, kwa mamlaka ya kitabu kiitwacho 'Mahavaga', ukurasa wa54 sehemu ya kwanza, imerikodiwa kwamba mrithi wa Buddhaatakuwa mtu aitwaye 'Rahula' anayeelezewa pia kamamwanafunzi; la, bali mtoto wake. Sasa hapa nasema kwa nguvukwamba lile neno 'Rahula' lililomo kwenye kumbukumbu zaKibuddha ni matamshi mabaya ya neno "Ruuhullahi" ambalo nimoja miongoni mwa majina ya Yesu. Na kile kisa kwamba huyu'Rahula' alikuwa mwana wa Buddha ambaye, baada yakumtelekeza mtoto huyu akiwa yungali mchanga alikwendauhamishoni, na ambaye akiwa na nia ya kuachana na mkewemoja kwa moja, alimwacha akiwa amelala bila kumjulisha walakumuaga, na akakimbilia nchi nyingine, wote huo ni upuuzi, nijambo la kijinga na lenye kuaibisha utukufu wa Buddha. Mtu katilina mwenye moyo mgumu wa namna hiyo ambaye hakuwa nahuruma kwa mkewe maskini, ambaye alimwacha mkewe akiwaamelala na bila kumwambia neno la kumliwaza, akayeyuka kamamwizi; ambaye alipuuza moja kwa moja wajibu aliokuwa naokwake kama mume - bila kumtaliki wala kumwomba ruhusa yakwenda safari isiyokuwa na mwisho; ambaye aliupa dharuba kalimoyo wake kwa kupotea ghafla, ambaye alimtia machungu nahakumpelekea walau barua hadi mtoto akakua na kuwa mtumzima, na ambaye hakukihurumia hicho kitoto kichanga - mtuwa namna hiyo ambaye hakuyaheshimu mafundisho ya kimaadilialiyoyafundisha yeye mwenyewe kamwe hawezi kuwamchamungu. Busara yangu inakataa kulikubali hili kamainavyokataa kukubali kile kisa kilichomo kwenye Injili kwamba siku

Page 94: Yesu katika India

94

moja Yesu hakumstahi mama yake, kwamba hakumjali alipokujana kumwita, bali badala yake akamtolea maneno ya matusi.

Kwa hiyo ingawaje hivi visa vihusuvyo kuumizwa kwa hisia zamke na mama vina aina fulani ya kufanana, hata hivyo hatuwezikuvinasibisha visa vya namna hiyo, ambavyo vinaleta maana yamchapuko kutoka kwenye viwango vya kawaida vya tabia, kwaYesu au Gautama Buddha.Kama Buddha hakumpenda mkewe, je hakuwa vile vile nahuruma juu ya mwanamke masikini na mtoto anayeteseka? Hiiina maana ya utovu mbaya sana wa tabia njema; mbaya kwakiasi hiki kwamba nimepata uchungu kwa kuufikiria baada yakupita kwa mamia ya miaka. Mtu anashindwa kuelewa kwa ninialiyafanya yote haya. Kutokumjali mke kunatosha kumfanya mtuawe mbaya- isipokuwa pale mwanamke mwenyewe anapokuwahana maadili mema, si mtiifu au mtovu wa imani na adui kwamumewe. Hivyo, hatuwezi kuinasibisha tabia mbaya yo yote yanamna hiyo kwa Buddha; hili likiwa kinyume hata na mafundishoyake mwenyewe. Kwa hiyo mazingira haya yanaonyesha kwambakisa hiki siyo sahihi. Kwa hakika 'Rahula' lina maana ya Yesuambaye jina lake jingine ni "Ruuhullahi". Neno "Ruuhullahi" kwaKiebrania linakuwa sawa na "Rahula", na huyo "Rahula", yaani"Ruuhullahi" ameitwa mwanafunzi wa Buddha kwa sababu kamanilivyokwisha eleza kuhusu Yesu kuja baada yake na kuletamafundisho ya Buddha, na kwa sababu ya wafuasi wa imani yaKibuddha kutangaza kwamba chanzo cha mafundisho yale niBuddha na kwamba Yesu alikuwa mmoja wa wanafunzi wake.Na lisiwe jambo la kustaajabisha iwapo Buddha, kutokana naufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu akamtangaza Yesu kuwa'mwana' wake.Kipande kingine cha ushahidi wa kimazingira ni kwamba ndaniya kitabu hicho hicho imerikodiwa kwamba wakati 'Rahula'alipotenganishwa na mama yake, mwanamke aliyekuwa mfuasiwa Buddha, na ambaye jina lake lilikuwa Magdaliyana alifanyakazi ya utarishi. Itazingatiwa kwamba jina Magdaliyana nimatamshi mabaya ya Magdalena, mwanamke mfuasi wa Yesu

Page 95: Yesu katika India

95

aliyetajwa ndani ya Injili.Ushahidi wote huu, ambao umepangwa kwa muhtasari

unawaongoza watu waadilifu kufikia kwenye uamuzi kwambaYesu ni lazima awe alikuja nchini humu, na licha ya ushahidi wotehuo bayana, hakuna mtu mwenye busara awezaye kupuuzamfanano unaopatikana hususan nchini Tibet, kati ya mafundishona ibada ya dini ya Kibuddha na ile ya Ukristo. La, bali kunamfanano wa kustaajabisha kati yao kwa kiasi hiki kwambaWakristo wengi wenye kutafakari wanaamini kwamba dini yaKibuddha ni Ukristo wa Mashariki, na Ukristo ni dini ya Kibuddhaya Magharibi.

Kwa kweli ni jambo la kustaajabisha sana ya kwamba kamavile Yesu asemavyo, "Mimi ni Mwanga na Njia", hayo hayoyamesemwa na Buddha; kama vile Injili zinavyomwita YesuMkombozi, Buddha pia anajiita Mkombozi (tazama LaltaWasattara). Ndani ya Injili imeelezwa kwamba Yesu hakuwa nababa, na kuhusiana na Buddha imeelezwa kwamba kwa hakikaalizaliwa bila baba, ingawaje kidhahiri, kama vile Yesu alivyokuwana baba, Yusufu, vivyo hivyo Buddha alikuwa na baba. Imeelezwapia kwamba nyota ilichomoza wakati wa kuzaliwa kwa Buddha;kipo pia kile kisa cha Solomon akitoa amri ya kukatwa mtoto katikanusu mbili na kumpa moja ya nusu hizi mbili kila mmojawapo wawale wanawake wawili, ambacho kinapatikana ndani ya kitabucha Buddha kiitwacho Jataka. Hii, licha ya kuonyesha kwambaYesu alikuja nchini humu, inaonyesha pia, kwamba Mayahudi wanchi ile waliokuja nchini humu, walianzisha mahusiano na dini yaKibuddha. Na ile hadithi ya mwanzo kama ilivyoelezwa ndani yavitabu vya imani ya Kibuddha ina mfanano mkubwa na hadithi yanamna hiyo hiyo iliyotolewa ndani ya Taurati. Kama vile kulinganana Taurati mwanamume anavyohesabiwa kuwa bora kulikomwanamke, vivyo hivyo katika dini ya Buddha mtawamwanamume anahesabiwa kuwa bora kuliko mtawamwanamke. Lakini yaweza kuonekana kwamba huyu Buddhaaliamini uhamaji wa roho, lakini "uhamaji" aliouamini yeye haukokinyume na mafundisho ya Injili. Kulingana na Buddha uhamaji

Page 96: Yesu katika India

96

uko wa aina tatu:(1) Kwamba vitendo vya mtu anayekufa na juhudi zakevinalazimisha kupatikana kwa mwili mwingine; (2) ile aina yauhamaji ambayo Watibet wanaamini itafanya kazi miongoni mwaWalama, yaani, sehemu fulani ya roho ya Buddha au BuddhaSatwa inahamia kwa Mlama kwa wakati ule; ambayo inamaanishakwamba uwezo wake, tabia yake na sifa zake za kirohozinahamishiwa kwa Mlama huyo na kwamba roho yake inaanzakumhuisha Mlama huyo; (3) kwamba katika maisha haya mtuanapitia katika uumbaji wa aina mbalimbali - unafika wakatiambapo anakuwa kama dume la ng'ombe; anapozidi kuwamchoyo na mwovu, anakuwa mbwa, lile umbile lake la kwanzalikiwa linatoweka na kujichomoza jingine linalooana na tabia navitendo vyake; lakini mabadiliko yote hayo yanatokea katikamaisha haya haya ya kidunia. Imani hii haipingani na mafundishoya Injili.

Nilikwisha eleza kwamba Buddha anaamini kuwako Shetani,kwa hiyo anaamini pia kuwako kwa jahanamu na pepo na kuwakokwa malaika na siku ya Kiyama. Na ile tuhuma kwamba Buddhahamwamini Mwenyezi Mungu ni uzushi mtupu. Buddhahakumwamini Vedanta na hakuiamini miungu ya kimwili yaWahindu. Amezikosoa vikali sana hizi Veda. Haziamini hizi Vedazilizopo. Anakihesabu kile kipindi ambapo alikuwa Mhindu mfuasiwa hizi Veda kuwa ni kipindi cha kuzaliwa kiovu. Kwa mfanoanadokeza kwamba kwa kipindi fulani alikuwa nyani; tena kwamuda alikuwa tembo; kisha akawa kulungu na mbwa; mara nneakawa nyoka na kisha akawa kinega, kisha akawa chura, akawasamaki mara mbili, mara kumi chui, mara nne kuku, mara mbilinguruwe na mara moja sungura, na kwamba wakati alipokuwasungura alikuwa akiwafundisha manyani, mbewa na mbwa - maji;tena, anasema kwamba alikuwa pepo; siku moja alikuwamwanamke, mchezaji na shetani. Vidokezo vyote hivi vina maanaya kuonyesha awamu za maisha yaliyojaa woga, za tabia za kike,za utovu wa kuogopa adhabu na ushenzi, na za ufisadi, ulafi naimani ya mambo ya uchawi. Inaonekana kwamba kwa njia hii

Page 97: Yesu katika India

97

anaonyesha wakati ambapo yeye alikuwa mfuasi wa hizo Veda,kwani, baada ya kuachana nazo hatoi kidokezo cha dalili yo yoteya maisha mabaya ambayo bado yanaendelea kumkabili. Balikinyume cha hayo, baadae anadai madai makubwa; alisemakwamba yeye amebadilika na kuwa mdhihirishaji wa MwenyeziMungu na amefikia daraja ya Nirwana.

Buddha anaeleza pia kwamba mtu anayeuhama ulimwenguakiwa amebeba vitendo vya kijahanamu anatupwa ndani yajahanamu. Walinzi wa jahanamu humkokota kuelekea kwaMfalme wa jahanamu aitwaye Yamah, na kisha mlaaniwa huyuhuulizwa iwapo hakupata kuwaona wajumbe watano ambaowalitumwa kwake ili kwenda kumuonya: Utoto - Uzee - Maradhi -Kuadhibiwa mtu kutokana na makosa yake katika maisha hayahaya ya kidunia ambao ni uthibitisho wa adhabu ya akhera - Maitiambazo zinaashiria uwezekano wa kuteketezwa kwa ulimwengu.Na huyu mtu mlaaniwa anajibu kwamba alikuwa mjinga kwa hiyohakupata kulitafakari lo lote miongoni mwa mambo haya. Kishawalinzi wa jahanamu humkokota hadi mahali pa kutolea adhabuna kumfunga kwa minyororo ya chuma ambayo iko moto kamamoto wenyewe. Zaidi ya hayo Buddha anasema kwambajahanamu ina majimbo kadhaa ambamo wenye dhambi wamakundi mbalimbali hutupwa. Kwa kifupi, mafundisho yote hayayanabainisha wazi wazi kwamba dini ya Kibuddha ina deniinalodaiwa na ushawishi binafsi wa Yesu. Lakini sikusudiikuendelea na mjadala huu. Naifunga sehemu hii hapa, kwaniwakati ambapo kuna utabiri ulio wazi, ulioelezwa ndani ya vitabuvya imani ya Kibuddha kuhusu kuja kwa Yesu nchini humu - utabiriambao hakuna mtu awezaye kuukanusha - wakati mafumbo namafundisho ya kimaadili ya Injili yanapatikana ndani ya vitabuvya imani ya Kibuddha vilivyotungwa wakati wa zama za Yesu -nadharia zote hizi mbili zikiwekwa pamoja haziachi shaka yo yotekuhusu kuja kwa Yesu katika nchi hii. Kwa hiyo, ushahidituliopanga kuufanyia utafiti kwa kutumia kumbukumbu zaKibuddha umepatikana wote - Ashukuriwe Mwenyezi MunguMwenye nguvu.

Page 98: Yesu katika India

98

SEHEMU YA 3

Kuhusu ushahidi kutoka kwenye vitabu vya historiaunaoonyesha kwamba kuja kwa Yesu kwenye jimbo

la Punjab na maeneo jirani yake lilikuwa jambo lalazima

Swali linajitokeza katika hali ya asili kuhusu kwa nini baada yakuepukana na Msalaba Yesu alikuja katika nchi hii. Ninikilimshawishi kufanya safari ndefu ya namna hiyo? Linakuwa nijambo la lazima kulijibu swali hili kwa kutoa kiasi fulani chaufafanuzi. Tayari nilikwisha sema kitu kuhusu jambo hili, hata hivyonadhani kuna ulazima wa kulijadili kikamilifu ndani ya kitabu hiki.

Kwa hiyo, naitambulikane kwamba ilikuwa ni lazima sana kwaMasihi Isa (amani juu yake), kutokana na wadhifa wake wa kuwamjumbe wa Kimbingu, kufunga safari ya kuelekea Punjab navitongoji vyake kwani, yale makabila kumi ya Israeli ambayo katikaInjili yameitwa Kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli, yalihamianchini humu, ukweli ambao haukanushwi na mwanahistoria yeyote. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima kwamba Masihi Yesu (amani juuyake) afunge safari ya kuja nchini humu, na baada ya kuwaonahao kondoo waliopotea awahubirie ujumbe wake kutoka mbinguni.

Na kama asingefanya hivyo, ujumbe wake ungekuwa badohaujatimilizwa, kwani kazi aliyotumwa ilikuwa hii ya kuwahubiriakondoo waliopotea wa Israeli; kufariki kwake dunia bila kuwatafutakondoo hawa waliopotea, na baada ya kuwaona kuwafundishanjia ya wokovu, kungekuwa sawasawa na mtu aliyetumwa namfalme wake kuliendea kabila fulani la porini ili kuwachimbia kisimana kuwagawia maji, badala yake anakwenda mahali pengine nakukaa huko miaka mitatu au minne lakini hachukui hatua yo yoteya kulitafuta lile kabila. Je mtu kama huyo atakuwa ametekelezamaagizo ya mfalme? Hapana, hata kidogo; mtu huyu halijali lilekabila; anajitafutia starehe zake tu.

Lakini, kama iulizwe ni kwa vipi na kwa nini idhaniwe kwambayale makabila kumi ya Israeli yalikuja nchini humu, jibu lake ni

Page 99: Yesu katika India

99

kwamba upo ushahidi ambao hata mwenye akili ndogo hawezikuutilia shaka: kwani inajulikana vizuri sana kwamba watu kamavile Waafghan na wakazi wa kale wa Kashmir kwa hakika niWaisraeli kwa asili. Kwa mfano, watu wa ukanda wa vilima vyaAlai ambao uko umbali wa safari ya siku mbili au tatu kutoka wilayaya Hazara, wamejiita Banii Israeli tangu zama zisizokumbukwa;vivyo hivyo wakazi wa Kala Dakah, ukanda mwingine wa vilimakatika jimbo hili, huona fahari ya kuwa wenye asili ya Kiisraeli.Kisha lipo kabila katika Wilaya ya Hazara yenyewe ambalolinanasibisha asili yao nchini Israeli. Kadhalika, watu wa eneo lamilimani baina ya Chalas na Kabul hujiita Waisraeli. Kuhusu watuwa Kashmir , maoni yaliyoelezwa na Dk. Bernier kwa mujibu wamamlaka ya baadhi ya wanazuoni wa Kiingereza kwenyesehemu ya pili ya kitabu chake kiitwacho Travels in the MoghulEmpire, yanaonekana kuwa sahihi: yaani, yale maoni kwambawatu wa Kashmir ni wana wa Israeli; mavazi yao, maumbile yaona baadhi ya mila zao zinaonyesha moja kwa moja kwenye ukwelikwamba wana asili ya Kiisraeli. Mwingereza mmoja, GeorgeForster kwa jina, anaeleza katika kitabu chake kwamba wakatiwa ukaaji wake nchini Kashmir alijidhania yuko miongoni mwakabila la Mayahudi. Ndani ya kitabu kiitwacho The Races of Af-ghanistan, kilichotungwa na H. W. Belews C.S.I., (Thacker Spink& Co., Calcutta) imetajwa kwamba Waafghan walikuja kutokaSyria. Nebuchadnezzar aliwakamata mateka na kuwakalishanchini Uajemi na Media ambapo kutoka hapo baadae walitembeakuelekea Mashariki na kulowea katika vilima vya Ghaur, ambakowalijulikana kama Banii Israeli. Katika kulithibitisha hili kuna utabiriwa nabii Idrisa (Enoch), usemao kwamba yale makabila kumi yaIsraeli ambayo yalikamatwa mateka yalitoroka kutoka utumwanina yakakimbilia katika eneo liitwalo Arsartat ambalo laelekea kuwandilo jina la sehemu iitwayo Hazara hivi leo, ambapo sehemunyingine ya jimbo hilo inaitwa Ghaur. Ndani ya kitabu kiitwachoTabaqat-i-Nasri, ambamo kuna taarifa ya kutekwa kwa Afghani-stan na Changiz Khan, imeelezwa kwamba katika zama za ukoowa kifalme wa Shabnisi paliishi kabila liitwalo Banii Israeli ambao

Page 100: Yesu katika India

100

baadhi yao walikuwa wafanya biashara hodari. Mnamo mwaka622 baada ya kuzaliwa Yesu, karibu na ule wakati ambapo Mtumewetu Mtukufu Muhammad (amani na rehema za Mwenyezi Mungujuu yake) alitangaza mwito wake, watu hawa walikalishwa katikaeneo kuelekea Mashariki mwa Herat. Chifu mmoja wa Kikuraishi,Khalid bin Walid kwa jina, aliwaletea habari njema za majilio yaMtume kwa nia ya kuwaleta chini ya bendera ya Mjumbe huyuwa Kimbingu (amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake).Machifu watano au sita walijiunga naye, ambao miongoni mwaoQais ndiye aliyekuwa kiongozi na ambaye jina lake lingine lilikuwaKish. Baada ya kuukubali Uislam watu hawa walipigana kishujaakuutetea Uislam na walipata ushindi mwingi, huku Mtukufu Mtume(amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake) akiwapa zawadinyingi walipokuwa wakirejea, akiwabarikia na kutabiri kwambawatu wale wangepata nguvu kubwa za utawala. Mtukufu Mtumealisema kwamba machifu wa kabila hili daima watajulikana kamaMalik. Alimpa Qais jina la Abdul Rashid na akampa cheo cha'Pathan'. Waandishi wa Kiafghan wanasema kwamba hili ni nenola Kisyria ambalo lina maana ya 'usukani'. Kwa kuwa huyu Qaisaliyejiunga upya na Islam alikuwa kiongozi wa kabila lake, kamavile ulivyo usukani wa meli akapewa cheo cha 'Pathan'.

Haiwezekani kusema ni katika wakati gani Waafghan wa Ghaurwalisonga mbele na kuja kulowea katika eneo lililopo kando kandoya Kandhar, ambako ndiyo maskani yao hivi leo. Hii ilitokea yumkinikatika karne ya kwanza ya Kiislam. Waafghan wanashikiliakwamba Qais alimwoa binti wa Khalid bin Walid ambaye alizaanaye watoto wa kiume watatu ambao majina yao yalikuwaSaraban, Patan na Gurgasht. Saraban alikuwa na watoto wakiume wawili walioitwa Sacharj Yun na Karsh Yun ambao wazaowao ni Waafghan, yaani Banii Israeli. Watu wa Asia - Minor, nawanahistoria wa Kiislamu wa nchi za Magharibi wanawaitaWaafghan "Wasulaimanii".

Na katika kitabu kiitwacho The Encyclopaedia of India, East-ern and Southern Asia kilichotungwa na E. Balfour, jalada la 3imeelezwa kwamba watu wa Kiyahudi wamesambaa katika

Page 101: Yesu katika India

101

majimbo ya kati, Kusini na Mashariki ya Asia. Katika siku zamwanzo watu hawa walikalishwa kwa makundi makubwa katikanchi ya Uchina; walikuwa na hekalu mahali paitwapo Yih Chu,ambapo ndiyo makao makuu ya wilaya ya Shu. Dakta Wolfalizunguka kwa muda mrefu akiyatafuta yale makabila kumiyaliyopotea ya Yahuda na Bin Yamin. Taarifa nyingine inaonyeshakwamba Mayahudi walipewa hifadhi ya ukimbizi katika nchi yaTartary; walikutwa katika makundi makubwa kwenye majimboyaliyo pembezoni mwa Bukhara, Merv na Khiva. Prester John,Mfalme wa Tartary, akiandika kuhusu milki zake katika barua kwaAlexis Comninus, Mfalme wa Constantinapole anasema kwambang'ambo ya mto huu (AMU) yapo yale makabila kumi ya Israeliambao ingawa wanadai kuwa chini ya mfalme wao wenyewe,kwa hakika ni raia wake na ni watumwa wake. Tafiti za DaktaMoore zinaonyesha kwamba makabila ya Tartar yanayoitwaChosan ni ya asili ya Kiyahudi na kwamba miongoni mwaozinapatikana alama za imani ya kale ya Kiyahudi: Kwa mfanowanashikilia desturi ya kutahiri. Waafghan wanayo simulizikwamba wao ni yale makabila kumi yaliyopotea ya Israeli. Baadaya kutekwa kwa Yerusalem mfalme Nebuchadnezzaraliwakamata mateka na kuwakalisha katika nchi ya Ghaur karibuna Bamiyar. Kabla ya kuja kwa Khalid Bin Walid waliidumishakwa uthabiti imani ya Kiyahudi.

Kimaumbile Waafghan wanafanana na Wayahudi kwa kila hali.Kama walivyo hao, ndugu mdogo huoa mjane wa kaka yake.Msafiri wa Kifaransa aitwaye L. P. Ferrier ambaye alipitia Heratanaeleza kwamba katika eneo hili kuna Waisraeli wengi ambaowana uhuru kamili wa kutekeleza desturi za imani yao. Mnamokarne ya kumi na mbili baada ya kuzaliwa Yesu, Rabbi Bin Yaminwa Toledo (Hispania) alijitosa katika kuyatafuta haya makabilakumi yaliyopotea. Anaeleza kwamba Wayahudi hawa wameloweakatika nchi za Uchina, Iran na Tibet.

Kwenye kitabu chake cha kumi na moja katika msururu wataarifa kuhusu Mayahudi waliotoroka utumwani wakiwa na mtumeEzra, Josephus ambaye aliandika historia ya kale ya Mayahudi

Page 102: Yesu katika India

102

mnamo mwaka 93 baada ya kuzaliwa Yesu, anaeleza kwambahayo makabila kumi yalikalishwa ng'ambo ya Euphrates hatawakati ule, na kwamba idadi yao haikuweza kuhesabika.

Kwa kusema "ng'ambo ya Euphrates" ina maana ya Uajemina maeneo ya Mashariki. Na Mtakatifu Jerome ambaye aliishikatika karne ya tano baada ya kuzaliwa Yesu, akiandika kuhusuMtume Hosea kuhusiana na suala hili, anasema kwenye ukingowa ukurasa kwamba tangu siku ile makabila kumi (ya Waisraeli)yamekuwa chini ya mflame Parthya, yaani Paras, na badohayajatolewa utumwani. Katika jalada la kwanza la kitabu hichohicho imeelezwa kwamba Count Juan Steram anaandika kwenyeukurasa wa 233-34 wa kitabu chake kwamba Waafghani wanakirikwamba baada ya kuteketezwa kwa Hekalu la Yerusalem,Nebuchadnezzar aliwapeleka uhamishoni kwenye eneo laBamiyan. (eneo hili linatangamana na Ghaur, na liko Afghanistan).Na katika kitabu kiitwacho A Narative of a Visit to Ghazni, Kabuland Afghanistan kilichotungwa na G. T. Vigne, F.G.S. (1840)kwenye ukurasa wa 166 imeelezwa kwamba mtu mmoja aitwayeMullah Khuda Dad alisoma kutoka kwenye kitabu kiitwachoMajma-ul-Ansab kwamba mwana mkuu wa Yakubu alikuwaYahuda ambaye mwanawe alikuwa Usrak; mwana wa Usrakalikuwa Aknur; mwana wa Aknur alikuwa Maalib; na wa Maalibalikuwa Ka-Farlai; wa Ka-Farlai alikuwa Qais, wa Qais alikuwaTalut; wa Talut alikuwa Armea na mtoto wa Armea alikuwa Af-ghan ambaye wazao wake ni watu wa Afghan ambao wanaitwakwa jina la mtu huyu. Afghan alikuwa mtu wa rika moja naNebuchadnezzar; aliitwa mzao wa Israeli na alikuwa na watotowa kiume arobaini. Wakati wa kizazi cha 34, baada ya miaka2000 akazaliwa Qais, aliyeishi katika zama za Muhammad(Mtukufu Mtume, amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake).Wazao wake waliongezeka na kufikia vizazi 64. Mwana mkuuwa Afghan aitwaye Salm alihama kutoka nyumbani kwake nchiniSyria na kulowea katika Ghaur Mashkoh, karibu na Herat. Wazaowake wakasambaa nchini Afghanistan.

Na katika Encyclopaedia of Geograpy kilichotungwa na James

Page 103: Yesu katika India

103

Bryce, F.G.S. (London, 1856) kwenye ukurasa wa 11 imeelezwakwamba Waafghan wanafuatilizia uzao wao kwa Saul, Mfalmewa Kiisraeli na wanajiita kuwa ni wazao wa Israeli. AlexanderBurns anasema kuwa Waafghan wanaeleza kwamba wana asiliya Kiyahudi; kwamba mfalme Babul aliwateka na kuwakalishakatika eneo la Ghaur ambalo liko Kaskazini - Magharibi ya Babul;kwamba hadi kufikia mwaka 622 baada ya kuzaliwa Yesuwaliendelea na imani yao wenyewe ya Kiyahudi, lakini kwambaKhalid bin Abdullah (lilikosewa badala ya Walid) alimwoa binti wachifu wa kabila hili na akawafanya waukubali Uislamu katikamwaka ule.

Na katika kitabu kiitwacho History of Afghanistan kilichotungwana Kanali G. B. Malleson na kutangazwa mjini London (1878),kwenye ukurasa wa 39 imeelezwa kwamba Abdullah Khan waHerat, yule msafiri wa Kifaransa Friar John na Sir William Jones(ambaye alikuwa mustashiriki mkubwa) wanatokana na Banii Is-raeli; wao ni wazao wa yale makabila kumi yaliyopotea. KitabuKiitwacho History of the Afghan kilichotungwa na L. P. Ferrierkilichotafsiriwa na Kapteni W. M. Jasse na kutangazwa mjini Lon-don (1858) kimerikodi kwenye ukurasa wa 1 kwamba wengimiongoni mwa wanahistoria mustashrikina wana maoni kwambawatu wa Afghan wametokana na yale makabila kumi ya Israelina kwamba maoni ya Waafghan wenyewe ni hayo hayo.Mwanahistoria huyo huyo anasema kwenye ukurasa wa 4 wakitabu hiki kwamba Waafghan wanao ushahidi kuwa wakati wakuvamiwa kwa India, Nadir Shah alipewa na machifu wa kabila laYusuf-Zai zawadi ya Biblia iliyoandikwa kwa Kiebrania mahalipaitwapo Peshawar, na pia alipewa vitu vingine kadhaavilivyohifadhiwa na familia zao kwa ajili ya kufanyia tafrija za kidiniza imani yao ya zamani. Walikuwepo Mayahudi pia kwenye kambiya Nadir Shah. Walipoviona vitu vile wakavitambua mara moja.Tena mwanahistoria huyo huyo anaeleza kwenye ukurasa wa 4wa kitabu chake kwamba kwa maoni yake maoni ya AbdullahKhan wa Herat ni ya kuaminika.

Yakielezwa kwa muhtasari maoni hayo ni kwamba: Malik Talut

Page 104: Yesu katika India

104

(Saut) alikuwa na watoto wa kiume wawili Afghan na Jalut. Af-ghan ndiye aliyekuwa mzee mheshimiwa wa watu hawa. Baadaya utawala wa Daudi na Suleiman kulikuwako na mapigano yawenyewe kwa wenyewe baina ya makabila ya Israeli ambapokutokana na mapigano hayo kila kabila likajitenga na mengine nahali hii ya mambo ikaendelea hadi wakati wa Nebuchadnezzar.Nebuchadnezzar akafanya uvamizi na kuua Mayahudi elfu sabiini.Akauteketeza mji na kuwachukua Mayahudi waliosalia hadiBabel wakiwa wafungwa. Baada ya maangamizi haya watoto waAfghan walikimbia kwa hofu kutoka Judea hadi Arabia na wakaishikule kwa muda mrefu. Lakini kwa kuwa maji na ardhi vilikuwaadimu, na watu na wanyama walikuwa wote katika dhiki kubwa,wakaamua kuhamia India. Kundi la ma-Abdali lilisalia nchini Arabiana wakati wa Ukhalifa wa Hadhrat Abu Bakar mmoja wa machifuwao alianzisha kiungo kwa ndoa kati yao na Khalid Bin Walid . . .Wakati Iran ilipotekwa na Arabia, watu hawa walihama kutokaArabia na wakajikalisha katika majimbo ya Iran ya Faras naKirman. Walikaa kule hadi ulipofanyika uvamizi na Changiz Khan.Hawa ma-Abdali hawakuweza kujisaidia dhidi ya ukatili waChangiz Khan. Wakaja India kupitia Makran, Sindh na Multan.Lakini hawakuwa na amani mahali hapa. Hatimae wakaenda KohSulaiman na kukaa pale. Wanachama wengine wa hili kabila lama-Abdali pia waliungana nao kule.Wanajumuika kufanya makabila 24 - wazao wa Afghan ambayealikuwa na wana watatu, yaani Saraband (Seraban), Arkash(Gargasht), Karlan (Batan). Kila mmoja wao alikuwa na watotowa kiume wanane ambao walizaliana hadi kufikia makabila ishirinina manne, kila kabila likiitwa kwa jina la kila mtoto wao wa kiumemmoja. Majina yao pamoja na majina ya makabila yao yanatolewahapa chini:

Wana wa Seraband Jina la kabila

Abdal AbdaliBaboor BabooriWazir Waziri

Page 105: Yesu katika India

105

Lohan LohaniBarch BarchiKhugiyan KhugiyaniSharan Sharani

Wana wa Gargasht (Arkash) Jina la kabilaKhijl KhijliKakar KakariJamurin JamuriniSaturiyan SaturiyaniPeen PeeniKas KasiTakan TakaniNasar Nasari

Wana wa Karlan Jina la kabilaKhatak KhatakiAfrid AfridiToor TooriZaz ZaziBab BabiBanganesh BanganeshiLandipoor Landipoori

Na kitabu kiitwacho Makhazan-i-Afghani cha KhawajaNimatullah wa Herat, kilichoandikwa mnamo mwaka 1018 Hijriyyakatika zama za Mfalme Jahangir, na tafsiri yake kutangazwa naProfessa Bernhard Doran wa Chuo Kikuu Cha Kharqui (London,1836) kimehodhi katika kurasa zilizotajwa hapa chini kaulizifuatazo:

Katika Sura ya 1 kuna historia ya Yakubu Israel ambayekutokana naye kinaanza kizazi cha watu hawa (Waafghan).

Katika sura ya 2 kuna historia ya Mfalme Talut, yaani uzao waWaafghan unafuatiliwa kwa Talut.

Kwenye ukurasa wa 22 na 23 imeelezwa: Talut alikuwa na wana

Page 106: Yesu katika India

106

wawili Barkhiya na Armiyah. Barkhiya alikuwa na mwana mmoja,Asaf, na Afghan alikuwa na wana 24 na hakuna mtu miongonimwa Waisraeli aliyelingana na wazao wa Afghan. Kwenye ukurasawa 65 imeelezwa kwamba Nebuchadnezzar aliitwaa nchi yoteya Sham (Syria), n.k., akayatia uhamishoni makabila ya Kiisraelina kuyapeleka kwenda kukaa Ghaur, Ghazni, Kabul na Firozambako ndiko hasa wazao wa Asaf na Afghan walikofanyamaskani yao.

Na kwenye ukurasa wa 37 na 38 wa kitabu hiki, kwa mamlakaya mtunzi wa Majma-ul-Ansab, na kwa mamlaka ya Mastaufiambaye ndiye mtunzi wa Taarikh Buzidah, imeelezwa kwambawakati wa uhai wa mtukufu Mtume (amani na rehema zaMwenyezi Mungu juu yake) Khalid Bin Walid aliwakaribisha kwenyeUislamu wale Waafghan ambao baada ya tukio la utawala naNebuchadnezzar walifanya makazi yao katika eneo la Ghaur.Machifu wa Kiafghan chini ya uongozi wa Qais ambaye alikuwamzao wa Talut katika kizazi cha 37, walikuja kwa Mtukufu Mtume(amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake). (Hapa Talut-Saul amepewa uzao wa Abdul Rashid Qais). Mtukufu Mtume(amani na rehema za Mwenyezi Mungu juu yake) aliwatunukumachifu wale cheo cha Pathan ambacho maana yake ni "usukaniwa meli". Baada ya muda kidogo machifu wale walirudi kwenyeeneo lao na wakaanza kuhubiri Uislamu.

Na katika kitabu hicho hicho Makhzan-i-Afghan kwenye ukurasawa 63 imerikodiwa kwamba Farid-ud-Din Ahmad anatoa kauliifuatayo kuhusiana na majina Banii Afghanah na Banii Afghankatika kitabu chake kiitwacho Rasalah Ansab-i-Afghaniyah: Baadaya Nebuchadnezzar, Majusi waliwateka Waisraeli na maeneoya Sham, na alipoiteketeza Yerusalem aliwakamata matekaWaisraeli na kuwapeleka uhamishoni wakiwa watumwa.Aliondoka na mengi miongoni mwa makabila yao ambayoyaliifuata Sheria ya Musa na kuwaamrisha waachane na imaniya mababu zao na wamwabudu yeye badala ya Mungu, jamboambalo walikataa kulifanya. Hatimae Nebuchadnezzar aliwauawatu elfu mbili miongoni wa watu wao waliokuwa na akili na

Page 107: Yesu katika India

107

hekima nyingi sana na kuwaamuru waliosalia wajiondoe kwenyeufalme na kwenye eneo la Sham. Baadhi yao waliondoka kwenyeeneo la Nebuchadnezzar wakiwa chini ya chifu mmoja na kwendakwenye vilima vya Ghaur. Wazao wao walikaa mahali hapa,wakazaliana, na watu wakaanza kuwaita Banii Isaraiil, Banii Asafna Banii Afghan.

Kwenye ukurasa wa 64 mtunzi huyo anaeleza kwambakumbukumbu zenye kuaminika kama vile Taarikh-i-Afghani,Taarikh-i-Ghaur, n.k. zinayo madai kwamba Waafghani takribanwote ni Banii Israiil na baadhi yao wanatokana na Wamisri asilia.Zaidi ya hayo Abdul Fazl anaeleza kwamba baadhi ya Waafghanwanajihesabu kuwa wanatokana na asili ya Kimisri, sababuwaitoayo ikiwa kwamba wakati wa Banii Israiil waliporejea Misrikutoka Yerusalem, hili kabila (yaani Waafghan) walihamia India.Kwenye ukurasa wa 64 Farid-ud-Din Ahmad anasema kuhusujina 'Afghan': Kuhusu hili jina Afghan baadhi wamerikodi kwambabaada ya kupelekwa uhamishoni (nje ya Syria) walikuwa kila mara'wakiomboleza na kulia' (faghan) katika kukumbuka nyumbanikwao. Kwa hiyo wakaitwa Waafghan. Sir John Malcom naye piaana maoni hayo hayo; tazama History of Persia, Jalada la 1ukurasa wa 101.

Kwenye ukurasa wa 63 imeratibiwa kauli ya Mahabat Khan:"Kwa vile wao ni wafuasi na ndugu wa Suleiman (amani juu yake),kwa hiyo wao wanaitwa na Waarabu Wasulaimani".

Kwenye ukurasa wa 65 imeandikwa kwamba takriban tafitizote za wanahistoria mustashrikina zinaonyesha kwamba maoniya watu walio Waafghan wenyewe ni kwamba wanatokana naasili ya Kiyahudi. Baadhi ya wanahistoria wa hivi leowameyachagua maoni hayo hayo au yawezekana sanawameyahesabu kuwa ni ya kweli.

Ama kuhusu kutumiwa kwa majina ya Kiyahudi na Waafghanikunakosemekana kuwa kunatokana na kuukubali kwao Uislamu,hakuna jambo lo lote lenye kuunga mkono maoni ya mfasiri huyuBernhard Doran.Katika sehemu za Kaskazini na za Magharibi ya Punjab yako

Page 108: Yesu katika India

108

makabila yenye asili ya Kihindu ambayo yamejiunga na Uislamulakini majina yao hayatanguliwi na majina ya watu wa Kiyahudi,jambo linaloonyesha wazi wazi kwamba kwa kujiunga na Uislamusi lazima watu wapewe majina ya Kiyahudi.

Kwa maumbile, Waafghan wana mfanano wa ajabu naWayahudi, ukweli ambao wanaukiri hata wale wanazuoni ambaohawachangii katika maoni kwamba Waafghani wana asili yaKiyahudi. Na huu waweza kuwa ndio uthibitisho pekee uliopo wakutokana kwao na Mayahudi. Kuhusiana na jambo hili manenoya Sir John Malcom ni haya:

"Asili ya makabila ya Kiafghan yanayokaa katika ukanda wamilima baina ya Khorasan na Indus inafuatiliziwa kwa njia nyingina wanahistoria mbalimbali. Baadhi yao wanadai kwambawametokana moja kwa moja na makabila ya Kiyahudi yaliyotiwautumwani na Nebuchadnezzar, na wale machifu wakuuwanasemekana kuwa wanazinasibisha familia zao kwa Daudina Saul. Ingawa haki yao ya kukubalika kwenye uzao huu wafahari ni yenye kutiliwa shaka, ni dhahiri kutokana na maumbileyao binafsi na desturi zao nyingi kwamba wao ni taifa lililo tofautina Waajemi, Watartar na Wahindi na kwamba hili peke yakelaelekea kuipa itibari ndogo ile kauli ambayo inakinzwa na kwelinyingi zenye nguvu na ambayo kuihusu hiyo hakuna uthibitishowa moja kwa moja uliokwisha tolewa."

Kama kufanana kwa maumbile kati ya watu wa aina moja nawatu wa aina nyingine kunaweza kuashiria jambo lo lote,Wakashmiri wakiwa na maumbile yao ya Kiyahudi bila shakawataonekana kuwa wenye asili ya Kiyahudi. Hili limetajwa siyona Bernier tu bali na Forster pia, na huenda na wanazuoniwengine.

Ingawaje Forster hakubaliani na maoni ya Bernier, anakirikwamba alipokuwa miongoni mwa Wakashmiri alidhani alikuwakatikati ya watu wa Kiyahudi.

Kuhusu neno"Kashmiri" yanajitokeza maneno yafutayo kwenyeukurasa wa 250 wa Kamusi ya Jiografia ya A. K. Johnston:

Kwenye ukurasa wa 250, chini ya kichwa cha habari

Page 109: Yesu katika India

109

CASHMERE: "Wazalendo wote ni watu warefu wenye mitamboya miili yenye nguvu na maumbile ya kijanadume - wanawake nivipande vya wanamama walio warembo wa sura na wenye puanyembamba na nyuso nyembamba zinazofanana na zile zaMayahudi".

Katika Civil & Military Gazette (23 Novemba, 1898 ukurasawa 4), chini ya kichwa cha habari 'Sawati and Afridi' pamenakiliwawaraka wenye thamani na wenye kuvutia sana uliowasilishwakwenye Kitengo cha Elimu ihusuyo habari zote za binadamu chaChama cha Kiingereza kwenye mmoja wa mikutano yake ya hivikaribuni, ambao utasomwa kwenye kikao cha majira ya baridimbele ya Kamati ya Utafiti wa Elimu ihusuyo habari zote zabinadamu. Waraka huo umeripotiwa hapa chini:

"Hapa chini hatutaweza kuandika maneno yote ya ule waraka wenyethamani kubwa sana na wenye kuvutia mno uliochangwa kwenye Kitengocha elimu ihusuyo habari zote za binadamu kwenye mkutano wa hivikaribuni wa Chama cha Kiingereza, na ambao bado utasomwa mbeleya Taasisi ya Elimu ihusuyo habari zote za binadamu kwenye mojawapoya mikutano yake ya majira ya baridi."

"Wakazi wa asili wa njia hizi za milimani za Magharibi mwa Indiawanatambulika katika historia ya mwanzoni sana, mengi ya makabilahayo yakiwa yametajwa na Herodotus na wanahistoria wa Alexander.Katika zama za baina ya mwaka 500 na mwaka 1500 pori chafu lisilolimwana milima waliyoikalia liliitwa Roh, na wakazi wake wakaitwa Rohilla, nakwamba mengi miongoni mwa makabila haya ya mwanzoni ya Rohillaau Pathan yalikuwa katika sehemu zao muda mrefu kabla ya hayamakabila ya Afghan yaliyotanda hayajafikiriwa. Waafghan wa aina yoyote ile hivi sasa wanahesabiwa kama ni ma-Pathan kwa sababu wotewanazungumza lugha ya ki-Pathan na ki-Pushto. Lakini hawakubalikwamba wote wanatokana na ukoo mmoja, wakijidaia wenyewe kwambawao ni Banii Israiil wazao wa yale makabila ambayo yalitekwa naNebuchadnezzar na kupelekwa utumwani nchini Babylonia. Lakini wotemiongoni mwao wamechagua kuzungumza lugha ya ki-Pushto na wotewanazitambua sheria za kimila zile zile za ki-Pathan ziitwazo Paktanwali,ambazo katika miongoni mwa vipengele vyake vinaashiria kwa njia yaajabu kwenye zama za utume wa Musa na kwenye mila za kale zamataifa ya Rajput."

Page 110: Yesu katika India

110

ALAMA ZA KIISRAELI

Kwa hiyo ma-Pathan ambao hivi karibuni tumekuwa tukijishughulishanao sana, wanaweza kugawanyika katika jamii kubwa mbili, yaanimakabila na koo kama vile Waziriyya Afridiyya, Orkzaiyya n.k. ambaowana asili ya Kihindi, na wale Waafghan ambao wanadai kwambawametokana na makabila ya Sham na ambao wanawakilisha taifa lililoeneakwa wingi katika sehemu za mpaka wetu; na kwa uchache inaonekanakuwa ni jambo linalowezekana kwamba hii Paktanwali ambayo ni sheriaisiyoandikwa na ambayo inakubalika sawasawa na wote hao inawezakuwa na asili iliyochanganyika kwelikweli. Tunaweza tukakuta ndani yakesheria za Musa zikiwa zimepandikizwa katika mila za Rajput na kufanyiwamabadiliko na desturi za Kiislamu.Waafghan ambao wenyewe wanajiita Wadurani na ambao wamefanyahivyo tangu kuanzilishwa kwa Ufalme wa Kidurani yapata karne mojana nusu iliyopita wanasema kwamba wanafuatiliza uzao wao kutokakwenye makabila ya Kiisraeli kupitia kwa babu mmoja aitwaye Kish,ambaye Mtume Muhammad alimpa jina Pathan (ambalo kwa Kisyrialina maana ya usukani wa meli), kwa sababu alikuwa awaongoze watuwake kwenye mikondo ya Uislamu. Lakini tumekwisha ona kwambautaifa wa Kipaktan au Kipathan ni mkongwe sana mno kuliko Uislam.Ni vigumu kuelezea kuenea kwa majina ya Kiisraeli miongoni mwaWaafghani bila kukiri kuwepo kwa kiasi fulani cha uhusiano wa awali nataifa la Kiisraeli.Ngumu zaidi ni kuelezea kwa uhakika maadhimisho kama vile kwa mfanokudumishwa kwa Sikukuu ya Pasaka (ambako kwa uchache kumeigizwakwa namna ya ajabu na taifa la Waafghan) au mshikilio ambao kwaoWaafghan wenye elimu chache wanaidumisha desturi hii, bila kuwa naaina fulani ya misingi ya ukweli ya asili kuhusu jambo hili. Bellew anafikirikwamba uhusiano huu wa Kiisraeli waweza kuwa ni uhusiano halisi,lakini anaainisha kwamba kwa uchache moja miongoni mwa matawimatatu makubwa ya jamii ya Kiafghan ambalo kulingana na simulizilililotokana na Kish, linaitwa kwa jina la (Sarabaur) ambalo kwa hakikandilo jina la kale la Kipushtu lililotumika kutaja taifa la jua la Warajputambao makoloni yao yanajulikana kuwa yalihamia nchini Afghnistanbaada ya kushindwa kwao na Wachandraban - taifa la mwezi katikaushindani huu mkubwa, wale Mahabharat waliotajwa katika kumbukumbuza mwanzoni za India. Hivyo Muafghan anaweza kabisa kuwa Muisraeli

Page 111: Yesu katika India

111

aliyechanganyika na makabila ya kale ya Warajput, na kwangu mimihuu ndio kila mara ulioonekana kuwa ufumbuzi mzuri zaidi wa lile tatizola asili yake. Kwa vyo vyote vile, Muafghan wa kisasa anashika msimamowake wa kuwa mmojawapo miongoni mwa lile taifa teule na mzao waIbrahimu kutokana na misingi ya simulizi na anatambua tu udugu wakena Mapathan wengine kwa njia ya kuzungumza lugha moja na kutumiasheria moja ya mila za kikabila".

Nukulu zote hizi kutoka katika vitabu vya waandishi mashuhurisana, vikifikiriwa kwa pamoja vitamshawishi mtu aliye muadilifukuamini kwamba Waafghan na Wakashmiri wanaopatikana nchiniIndia, mpakani na katika nchi za jirani, kwa hakika ni Banii Israiil.Katika sehemu ya pili ya kitabu hiki Mungu Akipenda nitathibitishakwa ufafanuzi zaidi kwamba shabaha ya msingi iliyosababishasafari ndefu ya Yesu kwenda India ilikuwa kwamba ili awezekutekeleza wajibu wake wa kuyahubiri makabila yote ya Waisraeli,ukweli ambao ameutaja katika Injili.

Kwa hiyo si jambo la kushangaza ya kwamba alilazimika kujaIndia na Kashmir. Bali lingelikuwa jambo la kushangaza sanaiwapo angepaa mbinguni bila kutekeleza wajibu wake. Na kufikiahapa naufunga mjadala wa sasa.

Amani iwe kwa wale wenye kuongozwa njia iliyo sawa.

MIRZA GHULAM AHMAD

MASIHI ALIYEAHIDIWA

Qadian, Wilaya ya Gurdaspur.

Page 112: Yesu katika India

112

KIAMBATANISHO Na. 1

P. W. Rhys Davis, M. A., Phd.Buddhism

Kilichotangazwa na: The Society for Promoting Christian Knowl-edge, Northumberland Avenue, Charing Cross W. C. 43, QueenVictoria street, London, E. C. 1887.

"Mama yake Buddha anasemekana kuwa alikuwa bikra." Ukurasawa 183. "Mama yake alikuwa mbora na mtakatifu kuliko mabinti wotewa binadamu."

Zingatia: Chini kabisa ya ukurasa wa 183 Davis anamnukulu MtakatifuJerome.

Mtakatifu Jerome anasema (Contra Sovian bk. 1). "Imepokelewakama simulizi miongoni mwa firqa ya wanafalsafa wa kale wa Kihinduwa India kwamba Buddha, mwanzilishi wa mfumo wao alizaliwa nabikra kutoka ubavuni mwake."

KIAMBATANISHO Na. 2

The Hibbert Lectures - 1831Indian Buddhism. kilichotungwa na T. W. Rhys Davis, Chapa ya 2.Kimetangazwa na: Williams & Norgate, 14,

Henrietta Street, Covent GardenLondon. 1891

Ukurasa wa 147. " Yote haya yana faida ya aina yake kutokanana mtazamo wa kimalinganisho. Ni usemi unaotokana na msimamo waKibuddha ambao unaiweka kando ile nadharia ya kuwepo kwa MunguMkuu, au wazo linalofanana sana na lile ambalo limeelezwa katikamaandiko ya kistaarabu wakati Yesu anapoonyeshwa kama Udhihirishowa Mungu lililofanywa kuwa mwili, kama Mkate wa uhai, na si suala labahati nasibu kwamba wafuasi wa dini hizi mbili wenye imani iliyo tofauti

Page 113: Yesu katika India

113

na walio wengi baadae walizitumia dhana za Buddha na Neno kamamisingi ya nadharia zao za chanzo. Ni mfano mpya tu wa njia ambayokwayo mawazo ya namna moja katika akili zinazolingana yanakujakubadilishwa kwa njia zinazofanana sana. Kwa wafuasi w a Buddhawa mwanzoni, Chakka-Vatti Buddha alikuwa kama alivyokuwa MasihiNeno kwa Wakristo wa mwanzoni. Katika kadhia zote mbili, yalemawazo ya namna mbili yanafanana, yanaingiliana na yanajalizana.Katika kadhia zote mbili mawazo hayo ya aina mbili kwa pamojayanafunika takriban uwanja ule ule kama unaoruhusiwa na misingi tofautiya mafundisho hayo ya aina mbili. Na ni mzunguko wa mawazo yaChakka-Vatti Buddha katika kadhia moja, na Masihi Neno katika kadhianyingine, ambao ndio wenye ushawishi katika kuamua kwamba maoniya maandiko ya habari za maisha ya watu ya Wakristo wa mwanzokuhusu mabwana wakubwa wao mbalimbali yalikuwa ni yale yale, nayaliongoza kwenye matokeo yanayofanana; ingawaje maelezo yakinaganaga ya maoni hayo hayafanani kwa hali yo yote ile katika kadhiahizi mbili."

KIAMBATANISHO Na. 3

Sir M. M. Williams, Buddhism (John Muray, London 1889).

Ukurasa wa 135. Alisema kujihusu yeye mwenyewe (Maha-Vagga1.6.8) "Mimi ni mtiishaji wa kila hali (Sabbabhibha) mwenye hekimakwa kila hali; sina madoa, ninayo elimu niliyopata kwa njia yangumwenyewe; sina mshindani (Patipuggalo); mimi ndiye Chifu Arhat -mwalimu mkuu. Mimi peke yangu ndiye mwenye hekima kikamilifu(Sambuddha); mimi ndiye mshindi (Jina); mioto yote ya tamaa huzimwa(Sitibhuto) katika nafsi yangu; ninayo raha ipatikanayo baada ya kifo(Nibbuto)." Ukurasa wa 126. Usiue kiumbe cho chote chenye uhai. 2.Usiibe. 3. Usifanye zinaa. 4. Usiseme uwongo. 5. Usinywe vinywajivikali. 6. Usile chakula isipokuwa katika nyakati zilizowekwa. Usitumiemaua, mapambo au manukato. Usitumie kitanda chenye miguu mirefuau kipana, bali mkeka tu uliotandikwa ardhini. Jiepushe na kuchezangoma, kuimba, muziki na matamasha ya kidunia. 10. Usimiliki dhahabu

Page 114: Yesu katika India

114

au fedha ya aina yo yote na usipokee vitu hivyo." (Maha-Vagga 1.5.6).Amri hizi kumi za Kibuddha zaweza kuwa zimeambukizwa kutoka Amrikumi za Musa."

KIAMBATANISHO Na. 4

Mtunzi: H. T. PrincepKitabu: Tibet, Tartary and Mongolia.

"Misafara ya mwanzo katika Tibet yenyewe ambayoimewasilishwa kwetu ni ile ya Mapadre wa Usharika wa Yesu, Grueberna Dorville ambao walirejea kutoka Uchina kwa kupitia njia ile mnamomwaka 1661 baada ya safari ya Marco Polo kuelekea Magharibi.Walikuwa ndio Wakristo wa kwanza kutoka Ulaya ambao wanajulikanakuwa walipenya katika sehemu zenye watu wengi za Tibet, kwanikama tulivyokwisha eleza, safari ya Marco Polo ilikuwa upande waKaskazini Magharibi kutokana na vyanzo vya Oxus. Padre Grueberalishitushwa sana na kufanana kwa ajabu alikoona na pia itikadi kamavile katika taratibu za dini za wafuasi wa Buddha walioko Lassa na zileza Imani yake mwenyewe ya Kiroma. Aligundua, kwanza: Kwambavazi la Walama linafanana na lile tulilorithishwa katika michoro ya kalekama ndilo vazi la wanafunzi wa Yesu. Pili: kwamba ile nidhamu yamajumba ya watawa na ya sharika mbalimbali za Walama au Mapadreilikuwa na mfanano ule ule kama wa Kanisa la Roma. Tatu: Kwambaile dhana ya kugeuka mtu ilikuwa ya kawaida kwa pande zote mbilikama pia ilivyokuwa ile imani ya pepo na barzakh. Nne: akanena kwambawalichagua viongozi, walitoa sadaka, walisali na kutoa dhabihu kwa ajiliya wafu kama wafanyavyo Wakatoliki wa Roma. Tano: Kwambawalikuwa na majumba ya watawa yaliyojawa na watawa na mawaliiwaliofikia idadi ya 30,000 karibu na Lassa, ambao walifunga nadhiri zaoza umaskini, utii na utaratibu kama wafanyavyo watawa wa Kiroma,licha ya nadhiri zingine. Na sita: Walikuwa na waungamaji waliopasishwana Walama wakubwa au maaskofu; na kwa hiyo walikuwa na uwezowa kusikiliza maungamo na kutoa adhabu ya kutubisha, na kutoamsamaha. Licha ya yote haya ilikutikana desturi ya kutumia maji

Page 115: Yesu katika India

115

matakatifu, ya ibada ya kuimba kwa zamu, ya kuwasalia wafu, namfanano uliokamilika kati ya mavazi ya kawaida ya Walama wakuu nawakubwa na yale ya sharika mbalimbali za jamii ya Mapadre wa Kiroma.Zaidi ya hayo wamishionari hawa wa mwanzo waliongozwa katika kufikiauamuzi kutokana na yale waliyoyaona na kuyasikia, kwamba vitabuvya kale vya Walama vilikuwa na alama za dini ya Kikristo ambayo nilazima, walifikiria, iwe imehubiriwa katika zama za wanafunzi wa Yesu."(Ukurasa wa 12 -14)

Kisha kuhusu kutokea kwa Mkombozi, mtunzi huyo H. T. Princepanaandika katika kitabu hicho hicho (Tibet, Tartary and Mongolia)kwenye ukurasa wa 171:

"Matazamio ya wengi ya kuzaliwa kwa Mtume Mkubwa, Mkomboziau Mwokozi, ambayo yametajwa hata na Tacitus kama yaliyokuwayameenea sana katika kipindi cha kutokea kwa mwanzilishi wa dini yaKikristo, hapawezi kuwa na shaka yalikuwa na asili ya Kibuddha nakamwe hayakuwa ya Wayahudi peke yao au yenye kutokana na msingiwa tabiri za maandiko yao matakatifu tu."

Yakiwa maelezo yaliyoandikwa chini ya ukurasa wa 171 mtunzi huyoaliendelea kuandika:

"Kutokea kwa Buddha mwingine miaka elfu moja baada ya Gautamaau Sakhya Muni kumetabiriwa wazi wazi katika Pitakattayan na Atha-Katha. Gautama anajitangaza mwenyewe kuwa ndiye Buddha waishirini na tano na anasema, "Bagwan Metteya bado atakuja. Hili jinaMetteya lina mfanano usiokuwa wa kawaida na neno Masihi."

KIAMBATANISHO Na. 5

Hapa kuna maneno yaliyochotwa kutoka katika kitabu kiitwacho "TheMystery of the Ages", kilichotangazwa mnamo mwaka 1887.

"Dini ya Kibuddha ni Ukristo wa Mashartiki na kwa hali hiyoimehifadhiwa vizuri zaidi kuliko Ukristo, dini ya Kibuddha ya Magharibi."

Page 116: Yesu katika India

116

Kitabbu cha Sir M. Monier Williams, ukurasa wa 541, maelezo yaliyopochini ya ukurasa.

1. Tsing. A Record of The Buddhist Religion practised in In-dia and the Malaya Archipelago. (671 - 695 A.D.).Kimetafsiriwa na J. Takakusu B. A. Ph. D. (Oxford. the ClarendonPress - 1896).

Kwenye ukurasa wa 223-224"Ni jambo la ajabu kweli kweli kulikuta jina la Masihi ndani ya maandikoya Kibuddha ingawa jina hilo limeingia humo kwa bahati mbaya sana.Kitabu hicho kinaitwa "The New catalogue of the Buddhist Bookskilichotungwa katika zama za Chiang Yuan,: (A.D. 785 - 804), katikachapa ya Kijapani ya Chinese Bhuddhist Books (Bodlerian). Library,Jap, 65 DD, p. 73). (Kitabu hiki hakimo katika Katalogi ya Nanges)

"Isitoshe, jumba la Sanghayama la Sakya na jumba la watawa la Ta-Chin (Syria) yanatofautiana sana katika mila zao, na vitendo vyao vyakidini vinapingana kabisa vyenyewe kwa vyenyewe. King-Ching (Adam)alipaswa kupokeleza mafundisho ya Masihi (Mi-Shi-Ho), naSakya Putiyiya-Sramanas aeneze maneno yenye hekima ya Buddha."

KIAMBATANISHO Na. 6

The Nineteenth Century, London, October 1894.Vol. 3 July - December.British Museum wo. P.P. 56, 39.

Kwenye ukurasa wa 517. "Katika makala iliyoandikwa na Max Mullerchini ya kichwa cha habari "Madai ya kukaa kwa Yesu nchini India"ambamo anamkosoa Nicolas Notovitch, ambaye alikwenda Tibet na kuonabaadhi ya kumbukumbu za zamani za miswada katika Jumba la watawawa Kibuddha la Himis ikizungumzia kuhusu Yesu Kristo kuwa aliyewahikuizuru nchi ya Tibet na Kashmir, na ambaye wakati wa kurejea kwakealiandika kitabu kwa lugha ya Kifaransa "Vie inconnue de Je'sus-Christ"Paris 1894. Nicolas Notovitch alikuwa Mrusi kiuraia."

Page 117: Yesu katika India

117

"Lakini ingawa Notovitch hakuileta nyumbani hiyo miswada, kwavyo vyote vile aliiona, na bila kujifanya kuwa anajua lugha ya Kitibet,maneno hayo ya Kitibet yalitafsiriwa kwa ajili yake na mkalimani naametangaza kurasa sabini za miswada hiyo kwa lugha ya Kifaransakatika kitabu chake "Vie inconnue de Je'sus-Christ". Ni dhahiri alikuwaamejitayarisha kwa ajili ya ugunduzi wa maisha ya Kristo miongoni mwawafuasi wa Buddha. Mifanano kati ya Ukristo na Dini ya Kibuddhaimekuwa ikionyeshwa mara kwa mara hivi karibuni, na lile wazokwamba Kristo alikuwa chini ya ushawishi wa itikadi za Kibuddhalimewekwa mbele ya watu zaidi ya mara moja na waandishi mashuhuri.Tatizo hadi sasa limekuwa kugundua njia yo yote ya kweli ya kihistoriaambayo kwayo dini ya Kibuddha ingeweza kufika Falastin katika zamaza Kristo. Notovitch anafikiri kwamba muswada alioukuta pale Himisunalieleza jambo hili kwa njia iliyo rahisi zaidi. Hakuna shaka, kamaasemavyo, kuna katizo katika maisha ya Kristo, tuseme kuanzia mwakawake wa kumi na tano hadi wa ishirini na tisa, wakati wa kipindi hichoMaisha ya Kristo yaliyokutwa nchini Tibet yanadai kwamba Yesu alikuwanchini India, kwamba alijifunza lugha ya Kipali ya Sanskrit, kwambaaliyasoma ma-Veda na Kanuni za Kibuddha, na kisha akarejea Falastinakipitia nchi ya Uajemi ili kuja kuhubiri Injili. Kama tunamwelewasawasawa Notovitch, maisha haya ya Kristo yamechukuliwa kutokavinywa vya baadhi ya wafanyabiashara wa Kiyahudi waliokuja nchiniIndia mara tu baada ya Kitendo cha Kusulubiwa. (ukurasa wa 237).Yalikuwa yameandikwa kwa Kipali, iliyo lugha takatifu ya Dini yaKibuddha ya Kusini; nyaraka hizo za kuviringishwa baadae zililetwaNepal na Makhada (Quaere Mazadhe) kutoka India yapata mwaka200 A.D. (ukurasa wa 236) na kutoka Nepal zikapelekwa Tibet, na hivisasa zimehifadhiwa kwa uangalifu mahali paitwapo Lhassa. Tafsiri zaKitibet za maandiko ya Kipali zinapatikana, anasema, katika majumbaya watawa mbalimbali ya Kibuddha, na miongoni mwa mengine,zinapatikana katika jumba la watawa la mahali paitwapo Himis. Nimiswada hii ya Kitibet ambayo ilitafsiriwa pale Himis kwa ajili yaN. Notovitch alipokuwa amelazwa katika jumba hilo la watawa akiwana mguu uliovunjika, na ni kutoka katika miswada hii ambamoameyachukua Maisha yake mapya ya Yesu Kristo na kuyatangaza kwa

Page 118: Yesu katika India

118

lugha ya Kifaransa pamoja na taarifa ya misafara yake. Kitabu hiki,ambacho kimekwisha pitia katika chapa kadhaa za Kifaransa, hivi pundekitatafsiriwa katika lugha ya Kiingereza."

KIAMBATANISHO Na. 7

Kitabu: Buddha; His Life, His Doctrine, His Order.

Mtunzi: Dr. Hermann Oldenberg,Kimetafsiriwa kutoka KijerumaninaWilliam Hoey, M.A., D. LitMtangazaji: Williams & Norgate, 14,

Henrietta Street, Covent Garden, W.C.London. 1882

Ukurasa wa 142. "Katika tukio la utabiri wa Buddha kumhusu Metteyya,Buddha anayefuata ambaye atatokea duniani katika siku za baadae sanainasemwa:

"Atakuwa kiongozi wa kundi la wanafunzi wenye kufikia idadi yamamia ya maelfu, kama mimi nilivyo kuwa hivi sasa kiongozi wa makundiya wanafunzi yenye kufikia idadi ya mamia". Cakkana Hisuttanta.

Ukurasa wa 149. "Kuhusu mke na mtoto wa Buddha fungu kuu lamaneno ni 'Mahauagga', 154; Rahula anatajwa mara kwa mara katikamaandiko ya Sutta kama mwana wa Buddha bila shughuli muhimukunasibishwa kwake miongoni mwa duru za wanafunzi na hadithi hiyoya kale.

Ukurasa wa 103. Rahula ni jina la mwana wa Buddha. Yeye (Buddha)anasema, "Rahula ni mzaliwa wangu, Silsila imeanzishwa kwa ajiliyangu."Kwenye maelezo chini ya ukurasa wa 103. Katika jina Rahula yaonekanakuna kutajwa kwa Raha, Jua na Mwezi kumtiisha (Kumtia giza) Shetani.

Page 119: Yesu katika India

119

KIAMBATANISHO Na. 8

Kitabu: Travels in the Moghul EmpireMtunzi: Francois BernierWatangazaji:Archibald Constable, London ............... 1891

"Lakini kuna alama nyingi za dini ya Kiyahudi zinazoweza kuonekanakatika nchi hii. Wakati wa kuingia katika Ufalme huu baada ya kuivukamilima ya Peer-Punchal, wakazi katika vijiji vya mpakani walinishtushakuwa wanafanana na Mayahudi. Nyuso zao na tabia zao na ile hali yakipekee isiyoweza kuelezeka ambayo inamwezesha msafirikuwatofautisha wakazi wa mataifa mbalimbali, yote hayo yalionekanakuwa yanapatikana kwa watu hao wa kale. Usiyachukulie hayaninayoyasema kuwa ni mawazo ya kujifurahisha tu, kwa vile kuonekanakama Wayahudi kwa wanavijiji hawa kulikwisha semwa na Padre wetuwa usharika wa Yesu na baadhi ya Wazungu wengine muda mrefukabla sijatembelea Kashmir." (Ukurasa wa 930 - 932).

KIAMBATANISHO Na. 9

Mtunzi: George Forster.Kitabu: Letters on a Journey from Bengal to England.Kimetangazwa na: R. Faulder, London, 1808

"Kwa kuwaona Wakashmiri kwa mara ya kwanza katika nchi yaowenyewe nilidhani, kutokana na vazi lao, uumbwaji wa nyuso zao ambazozilikuwa ndefu na zenye mpangilio mzuri, na aina za chakula chao,kwamba nimekuja miongoni mwa taifa la Mayahudi." (Jalada la 2,ukurasa wa 20).

KIAMBATANISHO Na. 10

Mtunzi: H. W. Bellews, C.S.IKitabu: Races of AfghanistanKimetangazwa na: Thacker Spink & Co. 1884.

Page 120: Yesu katika India

120

"Mapokeo ya watu hawa (Waafghan) yanawarudisha katika Syriakama ndiyo nchi yao ya makazi katika wakati ambapo walipelekwautumwani na Bukhtanasar (Nebuchadnezzar) na kupandikizwa kamawatu wa koloni katika sehemu mbalimbali za Uajemi na Media. Kutokamwahali humu walihama kuelekea Mashariki wakati wa kipindi fulanikilichofuatia na kufika katika nchi ya milima ya Ghor ambapo waliitwana watu majirani 'Banii Afghan' au 'Banii Israiila' yaani, wana waAfghan au wana wa Israeli. Katika kulithibitisha hili tunao ushahidi waNabii Idris ya kwamba yale makabila kumi ya Israeli ambayoyalichukuliwa utumwani, hatimae yalitoroka na kujipatia hifadhi yaukimbizi katika nchi ya Arsareth ambayo inadhaniwa kuwa inashabihianana nchi ya Hazara ya hivi leo na ambayo Ghor ni sehemu yake mojawapo.Pia imeelezwa katika Tabaqati Nasiri kwamba katika zama za ukoo wakifalme wa kizalendo wa Shan Sabi kulikuwako na watu walioitwaBanii Israiila katika nchi ile na kwamba baadhi yao walikuwawakijishughulisha sana kufanya biashara na nchi zilizowazunguka."

KIAMBATANISHO Na. 11

Balfour, Edward. Surgeon General.Kitabu: "The Cyclopaedia of India and of Eastern and Southern

Asia."Chapa: Chapa ya tatuWatangazaji:Bernard Quaritch, 15, Piccadilly, W.1Mwaka: 1885.

Chini ya Kichwa cha habari Afghanistan - ukurasa wa 31:

"Pakhtun ndilo jina la kitaifa la Waafghan halisi; lakini Waafghan naMapathan wanajiita pia Banii Israiila." Pakhtun ni mtu mmoja na Pukhtunani jina la wingi la Waafghan. Neno hili linaelezwa kuwa ni la asili yaKiebrania (Ibraniy), ingawaje baadhi yao wanasema lina asili ya Kisyria(Syrianiy) na lina maana ya kujifungua na kuwekwa huru. Neno Af-ghan pia linasemekana kuwa na maana hiyo hiyo. Simulizi moja inasemakwamba baada ya kuzaliwa kwa Afghan mama yake akasema ghafula

Page 121: Yesu katika India

121

kwa sauti kuu na mshangao, "Afghan", niko huru, na akampa jina hilo;simulizi nyingine inadai kwamba wakati wa uchungu wa uzazi aliliaAfghan, Afghan, au Fighan, Fighan, maneno ambayo kwa Kiajemi yanamaana ya huzuni, majonzi, ole! Afghan linadaiwa kuwa ni jina la wazaowa Kais tu.

"Neno Pathan linasemekana kuwa limetokana na neno Pihtan, lakabuinayodaiwa kuwa ilitolewa na Muhammad kwa Muafghan mmoja aitwaeKais.

"Asili yao imo katika utata, lakini wandishi kadhaa wanawafikiriakuwa ni wazao wa moja miongoni mwa yale makabila kumi ya Israelina haya ndiyo maoni ya baadhi ya Waafghan wenyewe. Waandishiwachache wanafikiria kwamba taifa hili halina asili ya Kiyahudi, balikwamba wale walioleta dini ya Kiislamu miongoni mwao walikuwamoWayahudi waliosilimu.

"Kisha katika ukurasa wa 34 kwa mamlaka ya kitabu cha Elphinstone'Kingdom of Caubul' (ukurasa wa 182 - 185) imeandikwa:

"Miongoni mwa hao Yusufzai hakuna mtu anayemwona mkewempaka sherehe za ndoa zikamilike, na pamoja na Burdurani zote hizokuna stara kubwa baina ya wakati wahusika wanapofungishwa uchumbana wakati wanapoozwa. Baadhi yao huishi na wakwe zao wa kiumewa baadae na kujipatia chakula chao kutokana na huduma zao, kamaalivyofanya Yakobo (alipotaka kumwoa) Raheli, bila kuona hata kidogoshabaha ya matakwa yao.

"Miongoni mwa Waafghan kama ilivyo miongoni mwa Mayahudi,inafikiriwa kuwa ni jambo linalompasa ndugu wa marehemu kumwoamjane wa marehemu huyo na ni jambo la aibu kubwa kwa ndugu huyokwa mtu mwingine ye yote kumwoa mjane wake, na ni jambo la aibukubwa kwa ndugu huyo kwa mtu mwingine ye yote kumwoa mjanehuyo bila kibali cha ndugu huyo."

KIAMBATANISHO Na. 12

Narrative of a Mission to Bokhara in the years 1843 - 1845, (kipokatika majalada mawili), Rev. Joseph Wolff D. D., LL.D.

Page 122: Yesu katika India

122

Kimetangazwa na John W. Parker, West Strand,London, 1845.Jalada la 1. Chapa ya pili.

Ukurasa wa 9."Kutokana na mazungumzo mbalimbali na Waafghan mjini

Khorassaun na kwingineko nilijifunza kwamba baadhi yao wanaonafahari ya kuwa na asili itokanayo na wana wa Israeli, lakini natilia shakaukweli wa simulizi hiyo upande mmoja."

Ukurasa wa 13."Mayahudi wote wa Turkistan wanadai kwamba Waturuki ni wazao

wa Togarmah, mmoja miongoni mwa wana wa Gomar waliotajwa katikaMwanzo 10:3."

Ukurasa wa 14.Mayahudi katika Bokhara ni 10,000 kwa idadi. Rabbi Mkuu

alinithibitishia mimi kwamba Bokhara ndiyo Habor, na Balkh ndiyo Halahiliyotajwa katika 2 Wafalme 18:11 lakini kwamba wakati wa utawalawa Changis Khan walipoteza taarifa zao zote za kimaandishi. Pale Balkhmasheikh wa Kiislamu walinithibitishia kwamba ulijengwa na mwanawa Adam, kwamba jina lake la kwanza lilikuwa Hanakh na baadaeHalah, ingawa baadae waandishi waliuita Balakh, au Balkh. Mayahudi,wote wa Balkh na Samarcand wanadai kwamba Turkistan ndiyo nchiya Nod, na Balkh ndipo mahali ilipokuwa nchi ya Nod wakati fulani."

Ukurasa wa 15."Simulizi hii ni ya zamani pale Bukhora, kwamba baadhi ya yale

makabila kumi yako nchini Uchina. Niliwatahini Wayahudi hapa kuhusunukta mbalimbali za tafsiri ya maandiko matakatifu, hususan ile moja yamuhimu katika Isaya 7:14 - bikira. Waliitafsiri kama tufanyavyo sisiWakristo na hawajui kabisa ubishani muhimu uliopo kati ya Mayahudina Wakristo kuhusu nukta hii."

Page 123: Yesu katika India

123

Ukurasa wa 16."Nilipata hati ya kusafiria kutoka kwa Mfalme baada ya ukaaji huu

wa kupendeza sana na kisha nikavuka Oxus na kuwasili baada ya sikuchache Balkh na kutoka katika jiji lile ambapo pia nilizungumza na waleWaisreali waliotawanyika, nikaelekea Muzaur."

"Baadhi ya Waafghan wanadai uzawa wenye asili ya Israeli.Kulingana na hao, Afghan alikuwa mpwawe Asaph, mwana waBerachia, ambaye alijenga hekalu la Solomon. Wazao wa huyu Afghan,kwa vile walikuwa Mayahudi, walipelekwa Babylon na Nebuchadnezzar,ambapo kutoka hapo wakaondolewa na kupelekwa kwenye mlima waGhoree nchini Afghanistan, lakini katika zama za Muhammad wakasilimu.Wanaonyesha kitabu Majma-ul-Ansab, au mkusanyiko wa vizazi,ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiajemi."

Ukurasa wa 17."Kwa hiyo nikapita hadi Peshawar. Hapa pia nikasomewa kitabu

cha ajabu cha asili ya Waafghan, kitabu cha Kipushtuu cha Khan LehaunLoote. Taarifa iliyomo katika kitabu hiki inakubaliana na ile iliyotolewakatika MSS, Teemur Nemeh na Ketaub Ansbee Muhakkek Toose.Nilidhani kwa ujumla sura zao si za Kiyahudi; lakini nilishtushwa kiajabuna kufanana na Mayahudi walikonako Yusufzai na Khalibarii, mawilimiongoni mwa makabila haya. Hawa Kaffreseeah Poosh, kama niWaafghan, basi wanatofautiana kwa mbali sana na wengine miongonimwa taifa lao. Wasafiri wengi wamewadhania kuwa ni wazao wa jeshila Alexander, lakini hawasemi hivyo."

Ukurasa wa 18."Kila mara nilidhani kwamba hawa Kaffr Seeah Poosh ni wazao wa

Israeli na baadhi ya Mayahudi wasomi wa Samarcand wana maonikama mimi."

Ukurasa wa 19 - 20Kapteni Riley, niliyeshangaa kumwona, aliwaona Waafghan kama ni

wazao wa Kiyahudi."

Page 124: Yesu katika India

124

Ukurasa wa 58."Nilikaa siku sita na wana wa Rachab (Banii Arbal). Pamoja nao

walikuwako wana wa Israeli wa kabila la Dan, ambao wanakaa karibuna Terim katika Hatramawl, ambao wanatazamia, kwa kushirikianana wana wa Rachab, kufika haraka kwa Masihi katika mawingu yaMbinguni." Jalda la 2. ukurasa 131.

"Ni jambo la ajabu sana kwamba Nabii Ezekiel katika sura ya ishirinina saba, aya ya kumi na nne anatoa maelezo halisi ya biasharailiyoendeshwa kati a Waturuki na wakazi wa Bokhara, Khiva naKhokand. Nabii huyo anasema: "Wale walio wa nyumba ya Togarmah(yaani Waturuki) walifanya biashara katika mikusanyiko yao na farasina wapanda farasi na nyumbu." Waturuki hadi leo, kama walivyo walinziwa Kiyahudi, ni mamluki na hujikodisha kwa tenga chache kwa siku.Pia ni jambo la ajabu sana kwamba nilisikia mara kwa mara Waturukiwakijiita Toghramah, na Mayahudi huwaita Waturuki Toghramah."

"Kuyaangalia makundi ya ngamia yakija na bidhaa kutoka Kashmir,Kabul, Khokand, Keetay na Orenbough kunamkumbusha mtu lile fungula maneno la Isaya 60:6 "Wingi wa ngamia utakufunika, ngamia vijanawa Midiani na Ephah, wote watakuja kutoka Sheba na wataleta dhahabuna uvumba." kwa kutaja dhahabu, nisije nikasahau kwamba karibu naSamarcand kuna machimbo ya dhahabu na feruzi."

Ukurasa wa 236."Maneno machache kuhusu wale watoto katika milima ya Kurdistan.

Watoto hawa kama alivyosema vizuri sana marehemu muombolezwaDakta Grant , wana asili ya Kiyahudi ingawa siwezi kwenda hadi kufikiamahali pa kuthibitisha kwamba wanatokana na yale makabila kumi, kwavile wao wenyewe hawaijui nasaba yao. Hivi sasa wengi wao niWakristo."

"Kwa kiasi kikubwa wanafanana na Waprotestanti wa Ujerumani naUingereza kwani hawana masanamu wala majumba ya watawa namapadre wao huoa. Lakini heshima yao ya Kiaskofu ni ya urithi na piaile ya askofu mkuu, na wakati mama wa askofu mkuu anapokuwa mja

Page 125: Yesu katika India

125

mzito anaacha kunywa mvinyo na kula nyama; na endapo mtoto wakiume anazaliwa, anakuwa Askofu Mkuu, na kama ni mtoto wa kike,analazimika kubakia bikira hadi milele."

KIAMBATANISHO Na. 13

The Lost Tribes; Kilichotungwa na Geroge Moore M. D.

Kwenye ukurasa wa 143."Tumevutwa mara moja kwenye nchi ya umuhimu mkubwa sana

katika hali ya hivi sasa ya Mashariki, na la kufurahisha zaidi kwetu, kwavile tunawakuta pale watu wanaoungama kuwa ndio Banii Israiil auwazao wa yale Makabila Kumi, yaani Afghanistan na nchi za jiraniyake."

Kwenye ukurasa wa 145."Sababu zilizo bayana kwa kufikiria kwamba tabaka fulani za watu

wa Bokhara na Afghanistan ni za asili ya Kiisraeli ni hizi: Kwanza:Kufanana kwao binafsi na familia ya Kiebrania. Hivyo, Dakta Wolffaliye m-mishionari wa Kiyahudi anasema "Nilishitushwa kiajabu nakufanana kwa wale Yusufuzai (kabila la Yusuf) na wale Khybere, mawilimiongoni mwa kabila yao, na Mayahudi." Moorcroft pia anasema kuhusuWakhyberi, "Ni warefu, na wa maumbile yenye taswira za Kiyahudikabisa." Pili: Wamejiita wao wenyewe Banii Israiil, wana wa Israelitangu wakati usioweza kukumbukwa. Tatu: Majina ya makabila yao niya Kiisraeli, hususan lile la Yusufu, ambalo linajumuisha Ephraim naManasseh. Katika kitabu cha ufunuo kabila la Yusuf linachukua mahalipa Ephraim (Ufunuo 7:6-8). Katika Hesabu 36:5 Musa anazungumziakuhusu Manasseh kama "kabila la wana wa Yusufu", hivi kwamba nidhahiri kwamba yote mawili, Manasseh na Ephraim yalikuwayakijulikana kwa jina la kabila la Yusufu. Nne: Majina ya Kiebrania yamahali na watu nchini Afghanistan yanajitokeza mara nyingi zaidi kulikoinavyoweza kuelezwa kuwa yametokana na uhusiano wa Kiislamu nanchi hiyo; na kwa hakika majina haya yalikuwapo kabla Waafghanhawajawa Waislamu.

Page 126: Yesu katika India

126

Tano: Taarifa zote zinakubaliana kwamba waliikalia milima ya Ghortangu zamani za kale za mbali sana. Ni jambo la uhakika kwamba Bintimfalme wa Ghor alitokana na kabila la Waafghan la Sooree na kwambaukoo wao wa kifalme uliruhusiwa kuhesabiwa kuwa ni wa kale ya zamanisana hata wakati wa karne ya kumi na moja. "Wanaelekea kuwawaliimiliki milima ya Soliman au Solomon tangu zamani ambayoinajumuisha yote miongoni mwa milima ya Kusini mwa Afghanistan."(Elphinstone). Sita: Afghan ni jina lililopewa taifa lao na watu wengine.Jina walilolipa taifa lao ni Pushtoon, na Dakta Garey na Marshamanwanadai kwamba lugha ya Kipushtoon ina mizizi mingi ya Kiebraniakuliko nyingine yo yote."

Ukurasa wa 147;"Kisha ukale wa jina la nchi ya Cabul au Cabool unabainishwa; na

pia inaonyesha kwamba watu fulani wa pekee wajulikanao kama'Makabila', 'Makabila Matukufu' waliishi pale wakati wa zamani sana.Kwa hiyo, kuna ushahidi mzuri kwamba wakazi wa sasa wa Cabulwanaweza kuwa na haki ya kudai kwamba tangu wakati wa mwanzokabisa wa historia, wao na mababu zao wamekuwa wakiikalia Cabulna kwamba tangu wakati usioweza kukumbukwa wamekuwawakijulikana kama 'Makabila'. Yaani, Makabila ya Kiisraeli kamawajichukuliavyo hivi sasa . . . Kulingana na Sir W. Jones watawala waUajemi - Magharibi wanakubaliana nao katika maelezo yao yahusuyoasili yao; na mamlaka kaaji na mashuhuri kama vile Sir John Malcom nayule m-mshionari Bwana Chamberlain wanatuhakikishia baada yauchunguzi mkamilifu kwamba wengi miongoni mwa Waafghan bila shakawanatokana na mbegu ya Ibrahimu."

KIAMBATANISHO Na. 14

Mtunzi : Josephus FlaviusKitabu : Antiquities.Kimetafsiriwa na: Jewish W. M. WhitsonKimetangazwa na: Hurst, Rees, Orme & Brown: London.

Page 127: Yesu katika India

127

"Nini: Je mnayafikiria matumaini yenu ng'ambo ya mto Euphrates?Je mmoja wenu ye yote anafikiri kwamba makabila yaliyo ndugu zenuyatakuja kuwasaidieni na kuwatoeni nje ya Adiabene? Isitoshe, kamayakifanya hivyo Waparthian hawatayaruhusu." (XI, V.2).

Hii ni nukuu kutoka kwa Mfalme wa Kirumi (Agrippa) akiwaambiaMayahudi kujisalimisha kwa Warumi na siyo kuwategemea Mayahudikutoka nga'mbo ya mto Euphrates.

Josephus alikuwa katika utawala wa Vespasian, katika sehemu yamwisho ya karne ya kwanza ya Kikristo.

KIAMBATANISHO Na. 15

A personal narrative of a visit to Chuzin, Cabul, in Afghanistan.

Kimetungwa na: G. T. Vigne Esq., F.R.G.S. London:Whittaker & Co. Ave maria Lane, E.C. 1840.

Ukurasa wa 166 -167."Moolah Khuda Dad, mtu aliye msomi katika historia ya watu wa

nchi yake alinisomea kutoka katika Majma-ul-Ansab (Makusanyo yaVizazi) taarifa fupi ifuatayo ya asili yao. Wanasema kwamba mwanamkuu wa wana wa Yakubu alikuwa Yudha ambaye mwanawe mkuualikuwa Osruk ambaye alikuwa baba wa Okour, baba wa Moslib, babawa Farlai, baba wa Kys, baba wa Talut, baba wa Ermiah, baba waAfghans, lilikotoka jina la Waafghan. Alikuwa wa rika moja naNebuchadnezzar, alijiita Banii Israiil na alikuwa na wana arobaini ambaomajina yao hakuna nafasi ya kuyaweka. Mzao wake wa thelathini nanne katika mstari ulionyooka, baada ya kipindi cha miaka elfu mbilialikuwa Kys. Tangu Kys ambaye aliishi wakati wa Mtume Muhammadpamekuwapo na vizazi sitini. Salum, mwana mkuu wa Afghans ambayealiishi mahali paitwapo Sam (Demeshki) aliondoka mahali hapo na kujaGhura Mishkon nchi iliyopo karibu na Herat, na wazao wakewakajisambaza polepole katika nchi ambayo hivi sasa inaitwaAfghanistan."

Page 128: Yesu katika India

128

KIAMBATANISHO Na. 16

Ukurasa wa 121

Encyclopaedia of Geography Kilichotungwa na James Brayce, M.A. LL.D; F.R.S.E. na Keith Johnson F.R.G.S.Chapa ya 2Kimetangazwa na: William Collins, Sons & Co. Ltd;

London & Glasgow.Mwaka 1880

Chini ya kichwa cha habari Afghanistan - ukurasa wa 25.

"Historia na Mahusianao ". . . " Jina Afghan halitumiwi na watuwenyewe; wao wanajiita Pooshtoon na uwingi wake ni Pooshtaunehambalo kutokana na hilo pengine ndipo likapatikana jina Puten wanaloitwanchini India. Wanafuatiliza asili yao kutoka kwa Saul, Mfalme wa Kiisraelina kujiita Israiila. Kulingana na Sir A. Burnes, mapokeo yao ni kwambawalihamishwa kutoka katika nchi Takatifu na Mfalme wa Babyloniana kuja kupandikizwa katika nchi ya Ghore iliyo Kaskazini Magharibimwa Cabul, na waliishi kama Mayahudi hadi mwaka 682 A.D.walipoingizwa katika Uislamu na Chifu wa Kiarabu Khalid ibn Abdallahaliyemwoa binti wa Chifu wa Kiafghan. Hakuna ushahidi wa kihistoriauliowahi kutolewa katika kuunga mkono asili hii, na pengine ni ubunifutu uliotokana na mambo ya hakika yaliyotajwa katika 2 Wafalme 18:11.Lakini yawezekana, wasafiri wote wanakubaliana kwamba watu hawawanatofautiana kiajabu na mataifa jirani, na wao kwa wao wanayo asilimoja inayowaunganisha wote. Wanasemekana na baadhi ya watukufanana sana na Mayahudi katika taswira na maumbile nawamegawanyika katika makabila kadhaa, yakikalia maeneo tofauti nayakibakia takriban bila kuchanganyika."

Page 129: Yesu katika India

129

KIAMBATANISHO Na. 17

History of Afghanistan. Kilichotungwa na Colonel G. Malleson, C.S.I.,W.H. Allen & Co., 13, Waterloo Place, Pall Mall, SW 1. Kimetangazwakwenye Ofisi ya India, 1878.

Ukurasa wa 39. "Sasa nawageukia watu wa Afghanistan. Nayageukiamakabila yanayoikalia nchi ile na ambayo yanazimiliki njia za milimani.Mada hii imeshughulikiwa kwa kirefu na Mountstuart Elphinstone,imeshughulikiwa na Ferrier - ambao wanamnukuu kwa wingi sanaAbdullah Khan wa Herat, imeshughulikiwa na Bellews na wengine wengi.

Kufuatia Abdullah Khan na waandishi wengine wa Kiafghan, Ferrieranashawishika kuamini kwamba Waafghan wanayawakilisha yalemakabila kumi yaliyopotea, na kuwadaia uzawa wa moja kwa mojakutoka kwa Saul, Mfalme wa Israel. Miongoni mwa waandishi wenginewanaoafiki maoni haya linaweza kutajwa jina tukufu la Sir William Jones.Kwa upande mwingine, Profesa Dorn wa Kharkov ambayeamelichunguza suala hili kwa kirefu anaikataa nadharia hii. MountstuartElphinstone anaiweka katika kundi moja na ile nadharia ya uzawa waWarumi kutoka kwa Watrojan. Pingamizi dhidi ya maoni ya AbdullahKhan zimetolewa hivi punde kwa hamaki na kwa nguvu na ProfesaDowson katika barua aliyoliandikia gazeti la 'Times'. "Iwapo", anaandikamuungwana huyo, "lilikuwa na thamani ya kuweza kufikiriwa, badohaliendani na ile fikra kwamba Waafghan ni wazao wa yale makabilakumi yaliyopotea. Saul alikuwa ni mtu wa kabila la Benjamin na kabilahilo halikuwa mojawapo miongoni mwa yale kumi yaliyopotea. Linasaliasuala la maumbile. Hili hapana shaka lina umuhimu wake, lakini haliwezikulipiku lile suala la muhimu zaidi la lugha. Kisha Profesa Dowsonanaendelea kuonyesha kwamba lugha ya Kiafghan haina alama zaKiebrania ndani yake, na akamalizia kwa kuitangaza ile dhana kwambataifa lote la Kiafghan laweza kuwa limebadilisha lugha yao kadiri wakatiulivyopita kuwa ni "jambo lisilosadikika kupita kiasi."

Page 130: Yesu katika India

130

KIAMBATANISHO Na. 18

Ukurasa wa 122

L.P. FerrierHistory of the Afghans. 1858Kimetafisiriwa na W. M. Jesse.Kimetangazwa na: John Murray, London

Ukurasa wa 4. "Wakati Nadir Shah alipowasili Peshawar, alipokuwaakienda kuiteka India, Chifu wa kabila la Yusufu Zai alimzawadia Bibliailiyoandikwa kwa lugha ya Kiebrania na vitu vingine kadhaa ambavyovilikuwa vikitumika katika ibada yao ya kale na ambavyo walivihifadhi.Vitu hivi vilitambuliwa mara moja na Mayahudi walioufuata msafarahuo wa Kijeshi."

Kwenye ukurasa wa 1 katika maelezo chini ya ukurasa anaandika:

"Mtunzi wa muswada wa historia ya Waafghan anasema kwambabaadhi hulipata jina Afghan kutoka katika maana yake ya Kiajemi'maombolezo' kwa sababu makabila haya yaliomboleza kuhamishwakwao mbali na Judea. Wengine wanasema kwamba Afghan alikuwamjukuu wa Saul na aliajiriwa na Solomon katika kulijenga Hekalu. Mtunzihuyu anazirejea historia mbili za taifa hili:Tarikh - Afghanah, na Tarikh - Ghor, yaani Historia ya Waafghan naHistoria ya Ghor. Yaelekea, anasema, kutokana na vitabu hivi viwili,kwamba Waafghan wanajihesabu kuwa kwa kiasi fulani wametokanana Wakristo walio wenyeji wa asili wa Misri, na kwa kiasi fulaniwametokana na Waisraeli, lakini hakuna ushahidi wo wote unaotolewakatika kuunga mkono dai hili.

Tunaambiwa na mmoja wa waandishi hawa kwamba baada yakuwaua wafungwa wengi, Nebuchadnezzar aliwahamishia kwenye

Page 131: Yesu katika India

131

milima ya Ghor wale waliosalia, ambako walizaliana kwa wingi sana naMayahudi kutoka Arabia; na wakati wale walipobadilisha dini yao nakujiunga na ile ya Muhammad, barua ilipokelewa kutoka kwa Myahudialiyesilimishwa aitwaye Khalid, ikiwajulisha kuhusu kutokea kwa MtumeMpya na kuwasihi wajiunge na bendera yake takatifu. Waafghanwachache walio watukufu walikwenda Arabia; mkuu wao alikuwaKais ambaye tunajulishwa na watunzi wa Kiafghan alifuatiliza uzawawake kupitia vizazi arobaini na saba hadi kumfikia Saul na kupitia hamsinina tano hadi kumfikia Ibrahimu". (History of the Afghans, Persian MSS).

"Takriban waandishi wote wa Kiislamu wanawadaia Waafghanuzawa huu na kwa wakati fulani nilikuwa na jedwali la nasaba ambamojaribio lilifanywa la kuthibitisha kuwa familia zote kuu za Afghanistan niwazao waliotokana moja kwa moja na wafalme wa Israeli."

Page 132: Yesu katika India

132

Iwapo unapenda kununua vitabu zaidi vya Dini yaKiislamu au kwa maelezo zaidi ya mafundisho yaJumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya, wasiliana naanuani iliyo karibu nawe kati ya hizi zifuatazo:

1. P. O. Box 376, Simu: 2110473 Dar es Salaam.2. P. O. Box 1, Simu: 2603477 Morogoro.3. P. O. Box 260, Simu: 2646849 Tanga.4. P. O. Box 359 Iringa. (Simu 2700633).5. P. O. Box 196, Simu: 243043 Dodoma.6. P. O. Box 94, Simu: 2600847 Songea.7. P. O. Box 10723 Arusha.8. P. O. Box 54, Simu: 2603291 Tabora.9. P. O. Box 547 Ujiji - Kigoma.10. P. O. Box 306, Simu: 2333919 Mtwara.11. P. O. Box 86, Simu: 2510082 - Masasi.12. P. O. Box 1812 Bukoba.13. P. O. Box 28, Simu 97 Kibiti - Rufiji.14. P. O. Box 391 Tarime.15. P. O. Box 605 Ifakara.16. P. O. Box 17 Kilosa.17. P. O. Box 40554, Simu: 764226 Nairobi Kenya.18. P. O. Box 97011, Simu: 492624 Mombasa Kenya.19. P. O. Box 421, Simu 40269 Kisumu Kenya.20. P. O. Box 77, Simu 52 Shianda Kenya.21. P. O. Box 552 Limbe Malawi.

Page 133: Yesu katika India

133

Jesus' escapefrom death on the cross

and journey to India

JESUS IN INDIA

This is an English version of an Urdu treatise

written by the Holy Founder of the Ahmadiyya

Movement in Islam, Hazrat Mirza Ghulam Ahmad

(1835 - 1908). The theme is the escape of Jesus

from death on the cross, and his journey to India

in search of the lost tribes of Israel. Christian as

well as Muslim scriptures, and old medical and

historical books including ancient Buddhist

records, provide evidence about this journey. Jesus

is shown to have reached Afghanistan, and to have

met the Jews who had settled there after

deliverance from the bondage of

Nebuchadnezzar. From Afghanistan Jesus went on

to Kashmir, where other Israelite tribes had

settled. There he made his home, and there in

time he died; his tomb has been found in Srinagar.