‘aprili mbaya’ kwa wanahabari

18
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikisha viwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji Jarida la Baraza la Habari Tanzania Toleo la 164, April, 2021 ISSN 0856-874X Uamuzi wa Samia utadumu? Watoa taarifa kuhamasishwa Wanahabari kutuzwa Z’bar Uk 5 Uk 17 Uk 8 ‘Aprili mbaya’ kwa wanahabari

Upload: others

Post on 18-Nov-2021

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu kabisa vya weledi na uwajibikaji

Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 164, April, 2021ISSN 0856-874X

Uamuzi wa Samia utadumu?

Watoa taarifa kuhamasishwa

Wanahabari kutuzwa Z’bar

Uk 5 Uk 17Uk 8

‘Aprili mbaya’kwa wanahabari

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTHamis Mzee Mhariri

MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22 27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255 22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:- www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:- www.twitter.com/mctanzania

2

TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania

Magazeti haya yafunguliweMagazeti manne hayapo

m i t a a n i k u f u a t i a uamuzi wa wenye mamlaka kuyafungia

matatu kati yao na moja kulifutia leseni.

Wakati April 6, 2021 Rais Samia Suluhu alipoagiza kufunguliwa vyombo vya habari na kuboresha mwenendo wa demokrasia nchini, hatua hiyo ilipokewa kwa furaha kubwa.

Na katika hotuba yake ya kwanza Bungeni April 22, 2021, alisisitiza kuwepo uhuru wa habari na kulegeza vizuizi vya kisiasa chini ya mfumo wa siasa za vyama vingi.

Hata hivyo kwa magazeti yaliyofungiwa, furaha ya kunufaika agizo la Rais ilitoweka kutokana na wenye mamlaka kufafanua baadaye kwamba magazeti hayakuwemo katika agizo hilo la Rais.

Watendaji wa serikali walidai kuwa agizo la kufungulia vyombo vya habari lilihusu runinga za mtandaoni na siyo magazeti ambayo walidai yalifungiwa kwa mujibu wa sheria.

Msimamo huu unaibua swali kama hizo runinga za mtandaoni zilifungiwa kinyume cha sheria?

Magazeti matatu yaliyofungiwa kwa sababu tofauti na vipindi tofauti yalifanikiwa kuishinda serikali mahakamani na mahakama zikaamuru yaruhusiwe kufanyakazi tena.

Hata hivyo maofisa wa serikali walikataa kutekeleza maelekezo ya mahakama hatua ambayo imeibua maswali kuhusu utawala wa sheria na kutokujali.

Gazeti lililofutiwa leseni, liliomba upya leseni lakini maofisa wa serikali wanasema hawaafiki orodha ya wahariri na wakurugenzi wa gazeti hilo.

Kutokana na kauli zake, ni wazi Rais anataka mwanzo mpya kuhusu uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza na siasa za vyama vingi.

Kwa hiyo, ni muhimu wenye mamlaka wakaruhusu magazeti haya yafunguliwe na kufanyakazi tena.

MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003

FREE MEDIA PIONEER

Mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Jesse Mikofu alivyokuwa baada ya kufanyiwa unynyasaji na askari Zanzibar.

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tamko la kufungua ukurasa mpya katika mahusiano ya

vyombo vya habari na serikali, uhali-sia mambo ni tofauti kabisa.

Aprili 6, 2021 Rais aliagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuvifungulia vyombo vya habari na kuwataka watendaji waepuke kuvishughulikia kwa namna ambayo inaweza kusababisha serikali kulaumiwa kwa kubinya uhuru wa habari.

Baraza la Habari Tanzania na wadau wengine wa vyombo vya habari walipokea vizuri hatua hiyo ya mkuu wa nchi kama ni hatua chanya kwa kuzingatia hali ngumu kwa vyombo vya habari iliyokuwepo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Inashangaza sana kwamba katika mwezi huo huo wa Aprili ambapo Rais alitoa agizo hilo la

kufunguliwa vyombo vya habari na kutaka kuwepo hali bora na kutobinywa uhuru wa habari, mambo yamekuwa mabaya zaidi kukiwa na matukio ya kunyanyasa wanahabari kuongezeka.

Furaha ilikuwa ya muda mfupi na mwezi huo kugeuka kuwa Aprili mbaya kwa wanahabari.

Ni kinyume kabisa na akili za kawaida kwamba mwezi huo ambao Rais amelegeza hali ngumu kwa wanahabari, vyombo vya dola ndiyo vinaonyesha umwamba kwa wanahabari.

Matukio yaliyorekodiwa katika mwezi huo ni kama ifuatavyo:- • Aprili 12, 2021 waandishi

wawili , Christopher James kutoka ITV na Radio One na Dickson Billikwija wa Island TV waliwekwa ndani kwa amri ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi, akiwatuhumu kwa kuvamia mkutano wake.

• Tukio lingine ni la April 9,

2021 mjini Mwanza ambapo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi, alitishia kuchukua hatua dhidi ya mwanahabari Mabere Makubi wa ITV ambaye alimtuhumu kuandika taarifa zinazotishia ajira yake.

• Aprili 12, 2021 mwandishi wa kujitegemea anayeandikia gazeti la The Guardian kutoka Moshi, James Lanka alikamatwa na kuswekwa rumande na polisi kwa siku tatu bila kufunguliwa shitaka lolote na polisi haikuchukua maelezo yake alipofuatilia kukamatwa ovyo wafanyabiashara.

• Tukio lingine lilitokea mkoa wa Katavi ambapo mwanahabari anayeandikia kituo cha runinga cha Channel 10, Pascal Katona ambaye alikuwa akiandika habari za uchaguzi wa Imamu wa Msikiti wa Makanyagio

3

Habari

Toleo la 164, Aprili, 2021

‘Aprili mbaya’ kwa wanahabari

Endelea Ukurasa wa 4

Wanahabari wanafanyakazi muhimu ingawa baadhi ya watendaji wa dola hupenda kuwanyanyasa.

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

alishambuliwa na baadhi ya wamuni ambao hawakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo na kuharibu zana zake za kazi.

• Aprili 21, 2021 mjini Zanzibar mwandishi wa Mwananchi , Jesse Mikofu alishambuliwa na askari wa JKU. Alikutwa na kadhia hiyo alipokuwa anapiga picha askari wakiwaondoa wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la Darajani ambao waliamriwa kuhamia eneo la Kibandamaiti. Askari hao licha ya kumtesa mwanahabari huyo na kumgalagaza kwenye dimbwi la maji walimuamuru

aiharibu simu yake aliyotumia kupigia picha.

MCT imelaani vikali tabia hii ya kuwanyanyasa wananahabari wanapokuwa kazini.

Katika taarifa ya Baraza iliyotiwa saini na Katibu Mtendaji wake, Kajubi Mukajanga na kutolewa Aprili 22, 2021, Baraza limevikumbusha vvyombo vya dola kuwa uandishi wa habari siyo tu ni kazi ya kisheria bali ni muhimu katika jamii na lazima iheshimiwe.

Mukajanga alitolea mfano agizo la Rais Samia S. Hassan kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo la kufungulia vyombo vya habari na kuacha kuvitisha.

“Ninaelewa kuwa kuna vyombo vya habari mmevifungia,

vifungulieni na kwamba vifuate sheria. Tusitoe mwanya kuhalalisha malalamiko kuwa tunabinya uhuru wa habari na kujieleza” Rais Samia aliagiza.

Baraza , taarifa hiyo iliendelea, linashangazwa na nini kinachoendelea kutokana na unyanyasaji wa wanahabari kuendelea hata baada ya agizo la Rais, kinyume cha matarajio ya watanzania wengi.

“Tunajiuliza ni wananchi ama maofisa ndiyo hawakumwelewa Rais?, Baraza limehoji katika taarifa yake.

MCT inasimamia rejista ya kurekodi matukio mbalimbali ya ukiukwaji wa uhuru wa habari.

Rejista hiyo ilianzishwa 2012. Mwaka jana jumla ya matukio 43 ya ukiukaji wa uhuru wa habari yaliorodheshwa katika kanzi data.

Kwa mujibu wa rejista hiyo, ingawa matukio ya ukiukaji uhuru wa habari ni mengi, rejista ina matukio yale tu yaliyoripotiwa kwa Baraza ama kupitia vyombo vya habari.

Ukiukaji huo ni pamoja na vitisho, mashambulizi, kunyimwa habari na kufungiwa vyombo vya habari.

4

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

‘Aprili mbaya’ kwa wanahabariInatoka Ukurasa wa 3

Waandishi wa habari wakiwa kazini.

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wetu

Rais Samia Suluhu Hassan ali-poagiza kufunguliwa vyombo vya habari, alifungua ukurasa mpya kwa tasnia.

Uamuzi wa Rais alioutangaza katika hotuba yake iliyokuwa na masuala mbalimbali Aprili 6, 2021 ilikuwa ni hatua kubwa tofauti kabisa na mtangulizi wake hayati John Pombe Magufuli, aliyesifika kwa msimamo wake mkali dhidi ya vyombo huru vya habari.

Kwa vyombo vingi vya habari ambavyo viliathirika kutokana na kukosa mauzo, matangazo na waangaliaji, agizo la Rais Samia lilikuwa ni hatua chanya ya kuvisaidia.

Ghafla, vichwa vya habari vya kusisimua vilianza kuonekana kwenye magazeti na viongozi wa

upinzani wakaanza kupewa nafasi katika kurasa za mbele za magazeti, jambo ambalo lisingefikiriwa katika kipindi cha miaka sita cha utawala wa Magufuli.

Mahusiano mabaya ya Magufuli na vyombo vya habari yalianza mara baada ya alipochukua madaraka ya kuendesha nchi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

Hatua yake ya kwanza ilikuwa ni kuzuia matangazo mubashara ya runinga ya vikao vya Bunge ambayo yalivutia watazamaji wengi.

Kashfa ya Richmond ya kuzalisha umeme ambayo ilimlazimisha Edward Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, na kashfa ya akaunti ya Escrow ya mwaka 2014, ambayo ililazimisha baadhi ya mawaziri kuachia ngazi na kuwahusisha wafanyabiashara

wakubwa , wanasiasa na majaji ni miongoni mwa masuala makubwa yaliyotangazwa mubashara kwenye runinga.

Utawala wa Magufuli awali ulizuia matangazao ya runinga ya taifa TBC na baadaye kukumba pia runinga binafsi.

Matangazo mubashara sasa yamebakia kwa vikao vya asubuhi vya Bunge kipindi cha maswali na majibu, lakini mijadala haionyeshwi tena mubashara.

Serikali ilidai kuwa matangazo ya mubashara yalikuwa ghali na gharama ya mwezi ilikuwa sh. bilioni 4.2.

Bunge lilianzisha utaratibu wake wa matangazo. Runinga zikawa zinapewa taarifa zinazochujwa kwa ajili ya kutumia katika taarifa zao za habari.

Uchunguzi kuhusu kusitishwa kwa matangazao hayo mubashara ya Bunge uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ulionyesha kuwa vituo vya runinga havikupendelea utaratibu wa kupewa taarifa na picha na kitengo cha habari cha Bunge kwa maelezo kwamba hazikuwa za kiwango.

Mhariri mmoja miongoni mwa

5

Endelea Ukurasa wa 6

Uamuzi wa Samia utadumu?

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameleta matumaini mapya kwa tasnia ya habari.

Toleo la 164, Aprili, 2021

Habari

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

kadhaa waliohojiwa katika uchunguzi huo alisema kuwa walilazimika kufanya juhudi za ziada kwa kufanya mahojiano na wabunge mwishoni mwa kila kikao nje ya Bunge ili kupata kazi yenye ubora.

Hata hivyo licha ya madai ya gharama kubwa, matangazo ya mubashara yamekuwa ni kwa ajili ya Rais pekee kwani popote alipoenda hata vijijini alitangazwa mubashara.

Baraza lilifanya uchunguzi mwingine wakati aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipovamia kituo cha runinga cha Clouds Media usiku wa Machi 17, 2017 akiwa na watu wenye silaha. Haijabainika ni watu kutoka taasisi gani ya ulinzi.

Licha ya uchunguzi huo wa MCT uliofanyika Mei mwaka huo kueleza kuwa alikiuka uhuru wa uhariri na taarifa nyinginge iliyotolewa na timu iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye, hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya Makonda na badala yake Nnauye alitimuliwa kazi.

Mwandishi Azory Gwanda, aliyekuwa akiripoti kwa gazeti la Mwananchi alitoweka Rufiji mwaka 2017 na hatma yake haijulikani hadi leo baada ya kuchukuliwa na watu wanaodaiwa hawajulikani.

Vikundi vya kutetea haki na wanaharakati walichachamaa baada ya serikali kumkamata mwanahabari Erick Kabendera kwa tuhuma zenye shaka. Baadaye alifunguliwa mashtaka ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kujihusisha na makundi ya wahalifu kabla ya kuachiwa miezi saba baadaye baada kuingia makubaliano ya kukiri na waendesha mashtaka.

Ufungaji na usimamishaji vyombo vya habari hasa magazeti ulikuwa katika hali ya juu katika utawala wa Magufuli ambapo baadhi yalisimamishwa kwa siku saba hadi miezi 24 wakati mengine yalifutiwa leseni.

Wakati wa hotuba ya Rais Samia magazeti ya Mawio, Mwanahalisi, na Mseto yalikuwa bado yamefungiwa licha kufanikiwa kushinda kesi zao dhidi serikali mahakamani ambazo ziliamuru yaruhusiwe kuendelea kuchapishwa.

Gazeti la Tanzania Daima limefutiwa leseni na juhudi za kuomba liruhusiwe kuchapishwa zimekwama.

Kwa vyombo vya habari vya

kieletroniki – runinga na redio na vyombo vya mtandaoni hali si shwari pia kwani baadhi vilitozwa faini kubwa na vingine vilisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za utangazaji.

Katika hotuba yake Rais Samia alikataza tabia ya kuvinyamazisha vyombo vya habari kwa kueleza kuwa hatua kama hizo zinatoa mwanya wa

kuibuka malalamiko dhidi ya kubinywa kwa uhuru wa habari.

“Tusiruhusu hii kutokea ”, Rais alisema kwa kauli ya muafaka.

Hata hivyo wachunguzi wanachukulia kauli ya rais kwa tahadhari wakijiuliza watendaji ambao wanapenda kubinya vyombo vya habari watatekeleza agizo hilo? Ni suala la muda tu.

6

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kuonyesha umwamba alivamia studio za Clouds Media.

Nape Nnauye aliyetimuliwa kazi ya Uwaziri wa Habari baada ya kuunda kamati kuchunguza uvamizi wa Clouds Media.

Azory Gwanda mwanahabari aliyetoweka katika kipindi cha utawala wa mtangulizi wa Rais Samia Suluhu Hassan inadaiwa alitwaliwa na watu wasiojulikana.

Erick Kabendera mwanahabari wa kujitegemea aliyeswekwa ndani kwa miezi saba kwa tuhuma za uhujumu uchumi kutokana na kazi yake.

Uamuzi wa Samia utadumu?Inatoka Ukurasa wa 5

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Vyama vya habari vimetakiwa kuchangam-kia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuvi-

fungulia vyombo vya habari. Baraza la Habari Tanza nia,

Jukwaa la Wahariri na vyama vingine vya masuala ya habari ni muhimu vichangamkie fursa kutokana na uamuzi wa Rais, mwanahabari veterani, mshauri, na mkufunzi Ndimara Tegambwage amesema.

Akizungumza katika mahojiano ya runinga moja ya mtandaoni, Tegambwage ametahadharisha kuwa fursa hii isipotee, akieleza kuwa vyombo vya habari vidai mambo zaidi ili kuweza kutelekeleza yaliyotolewa.

Kuna sheria zinazobinya vyombo vya habari na haki zingine zimekaliwa , alisema.

Pia alionya kuwa vyombo vya habari visitegemee fadhila au kukumbukwa.

“Nalichukulia agizo hili kama jambo muhimu na la maana katika mazingira yaliyopo… na kwa vyombo vya habari kama alivyosema Rais kwa usahihi kuwa vilifungiwa kinyume cha taratibu”, alisema.

Kauli ya Rais ina nguvu kubwa, Tegambwage alisema na kuongeza kuwa ina uzito wa ziada kwa kuruhusu vyombo vya habari kufanyakazi tena.

Aliwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari kuwa walipopewa fursa ya kuanzisha chombo cha habari na kinapoanza kufanyakazi, chombo hicho siyo chako tena bali ni cha umma unaokifuatilia”.

Kama mtu akifunga chombo hicho, madhila kutokana na hatua hiyo hayamsibu mmiliki wake peke yake bali pia na umma.

Unapofunga vyombo vya habari, wamiliki watafunga biashara na wafanyakazi wao watapoteza ajira na waliokuwa wakitumia chombo hicho kutoa

maoni yao watapoteza jukwaa la kufanya hivyo.

Kutokana na kauli ya Rais, Tegambwage ambaye alisisitiza umuhimu wake, alisema kuwa kuna kitu cha ziada ndani yake.. kutakuwa na uhuru wa kujieleza, uhuru wa watu kuzungumza.

Aliongeza kuwa bila vyombo vya habari watu watanong’ona na unapofunga vyombo vya habari unawaambia wanyamaze.

Alisema watu wasioongeza hawatabiriki “kama unaongoza watu kama ng’ombe unakuwa na tatizo na hata serikali haitakuwa

na taarifa”.Kutokana na agizo la

kuvifungulia vyombo vya habari, kuna uhuru na serikali itajua mahitaji ya wananchi, alisema na kuongeza kuwa vyombo vya habari vitafanyakazi bila hofu, vitatafuta na kupokea taarifa na kufikia watu wengi ambao sauti zao zitasikika.

Vyombo vya habari vichangamke, vifanyekazi bila woga na kwa weledi kwa manufaa ya watu. Waboreshe utendaji wao na kuwa na vyanzo vya kuaminika.

7

Habari

Vyama vya habari vyahimizwa kuchangamkia agizo la Rais

Mwanahabari nguli, mkufunzi na mshauri wa masuala ya Habari, Ndimara Tegambwage.

Toleo la 164, Aprili, 2021

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

8

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Watoa taarifa wahitaji kuhamasishwa - Ripoti Na Mwandishi wa Barazani

Kuhamasisha watoa habari kuhusu sheria ya Haki ya Ku-pata Taarifa na wajibu wa maofisa habari wa serikali ni

miongoni mwa mapendekezo ya ripoti kuhusu haki ya kupata taarifa na hali ya uhuru wa habari nchini.

Watoa taarifa wametajwa kwenye ripoti kufuatia utafiti ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya.

Imeelezwa kwenye ripoti hiyo wakihamasishwa viongozi hao watakuwa na uelewa kwamba wanawajibika kuwaruhusu maofisa

habari kujibu maombi ya taarifa yanayotolewa na wanahabari.

MCT imetakiwa kuandaa taratibu mbalimbali ikiwemo mafunzo na uragbishi kufanyia mapitio vifungu vya sheria hiyo ya haki ya kupata taarifa na sheria nyingine zinazohusiana na uhuru wa habari.

Baraza limetakiwa kuhakikisha wanahabari na vyombo vya habari hasa vyombo vya habari vya jamii kuelewa wajibu wao na aina gani ya msaada vinavyotaka kutoka katika Baraza vinapokabiliwa na changamoto hasa ukiukwaji wa uhuru wa habari.

Baraza pia lishauriane na serikali katika masuala ya haki ya kupata taarifa na uhuru wa habari na haja ya kuwa na uhusiano mzuri kati ya pande

hizi mbili. Pia lishauriane na wamiliki wa

vyombo vya habari kuhusu haja ya kutoa fursa za mafunzo kwa waandishi wao na vitendea kazi stahiki kama vile rekoda, kamera na makrofoni kwa sababu katika baadhi ya matukio wanahabari hukataliwa kwa kuvikosa na badala yake wanakuwa na simu za mkononi ambazo baadhi ya watoa habari huzikataa.

Kuhusu Covid-19, Baraza limetakiwa kuandaa mafunzo kwa wanahabari kutokana na mambo yatokanayo na jangwa hilo na vipi wanaweza kujiandaa vizuri kuripoti majanga mengine.

Baraza pia limetakiwa kuandaa jukwaa kuhusu uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

Neville Meena mmoja wa watafiti wa Ripoti kuhusu upatikanaji wa taarifa na uhuru wa habari kwa maagizo ya Baraza la Habari Tanzania, akielezea ripoti hiyo kwa washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza.

Picha

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Picha

UJUMBE WA MCT WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI MOROGORO

Toleo la 164, Aprili, 2021

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

9

Habari

Na Mwandishi wa Barazani

Katika muda wa wiki moja mwezi April , 2021, wana-habari kutoka mikoa 12 wamehudhuria mafunzo yali-

yoendeshwa na Baraza la Habari Tan-zania (MCT) kuhusu uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

Mafunzo ya kwanza yalifanyika Jijini Dar es Salaam kwa waandishi kutoka Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Tanga na Pwani wakati mafunzo ya

pili kwa wanahabari kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida, Mbeya, Iringa , Dodoma and Morogoro yalifanyika Morogoro.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa Uragbishi wa Data unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID). MCT inatekeleza mradi huo kwa upande wa vyombo vya habari kwa kushrikiana na Pact Tanzania na Freedom House.

Mafunzo hayo yanafuatia utafiti kuhusu uhuru wa habari na hali ya haki ya kupata taarifa nchini.

Utafiti huo ulifanyika Machi 2021 katika mikoa sita – Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza na Mtwara.

Akifungua mafunzo ya kwanza Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa MCT , Kajubi Mukajanga amesisitiza umuhimu wa uragbishi wa data kwa lengo la kurahisishwa upatikanaji taarifa.

Alisema watafiti walipelekwa mikoa sita kufuatilia utendaji wa wanahabari na kupata taarifa kwa misingi ya sheria ya Haki ya Kupata taarifa.

Aliwahimiza washiriki wa mafunzo

Ofisa Programmu wa Baraza la Habari Tanzania, Saumu Mwalimu, akiwasilisha mada katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Baraza.

Toleo la 164, Aprili, 2021

Wanahabari wa mikoa 12 wahudhuria mafunzo ya MCT

Endelea Ukurasa wa 10

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

10

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Wanahabari wa Mikoa 12 wahudhuria mafunzo

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifuatilia kwa makini wakati mafunzo hayo.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania,Kajubi Mukajanga, akifungua mafunzo ya wanahabari yaliyoandaliwa.

hayo kujadili changamoto wanazokabiliana na fursa kwa maboresho. Mukajanga pia alihimiza wanahabari kuripoti matukio yote ya ukiukaji wa uhuru wa habari kwa Baraza ili kuliwezesha kuyafuatilia kwa ufumbuzi.

Katibu Mtendaji alizungumza hayo baada ya baadhi ya washiriki kutoa maelezo yaliyoonyesha ukiukwaji wa uhuru wa habari ambao

haukuripotiwa, na alisisitiza kuwa ushahidi unahitajika katika uragbishi.

Alisema Baraza limefanya uchunguzi kwa matukio kadhaa ya ukiukwaji wa uhuru wa habari.

Baraza alisema limechunguza na kutoa ripoti wakati mwanahabari Daudi Mwangosi alipouawa, wakati aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipovamia studio ya Clouds Media, na wakati wanahabari waliponyanyaswa katika mikoa ya

Mtwara, Geita na Ruvuma. Katika mafunzo hayo maofisa

wawili wa Baraza , Saumu Mwalimu na Paul Mallimbo waliwasilisha mada kuhusu Sheria ya haki ya Kupata Habari (ATI) na Ukiukaji wa Uhuru wa Habari Neville Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri (TEF) alielezea kwa upana ripoti utafiti inayoitwa Haki ya Kujua na kusaidia na mwandishi veterani na mtafiti, David Mbulumi.

Inatoka Ukurasa wa 9

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Unaweza kufikiria kuwa mahusiano kati ya vy-anzo vya habari na waandishi wa habari ni

ya kinafiki na kwamba watoa ta-arifa hasa maofisa wa serikali wa-naona vyombo vya habari ni vibaya lakini ni muhimu kush-irikiana navyo?

Hali hii ndiyo imebainishwa na timu ya watafiti waliotumwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kufuatilia hali ya uhuru wa habari na upatikanaji habari nchini.

Utafiti ulifanyika Machi 14 hadi 18, 2021 katika mikoa sita – Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza na Mtwara.

Hata hivyo kwa wananchi wa kawaida vyombo vya habari ni daraja na njia wanayotumia

kueleza matatizo na mahitaji yao kwa wenye mamlaka.

Watafiti walitumia dodoso kukusanyia data kutoka kwa wanahabari 73 ( 43 wanaume na 25 wanawake) wa magazeti, redio, runinga na mtandaoni wenye uzoefu wa miaka miwili hadi miaka 25. Utafiti huo ulilenga kuwahoji wanahabari 60.

Utaratibu wa ukusanyaji data ulihusu majadiliano ya mtu kwa mtu, majadiliano ya kikundi lengwa na kufuatilia kwa maswali kuhusu Uhuru wa Habari, Upatikanaji Taarifa , Uchaguzi na COVID-19.

Waandishi waliohojiwa walikuwa wa vyombo vya kitaifa, mikoa na jamii. Jumla ya vyombo 56 viliwakilishwa.

Kuhusu uhuru wa habari, zaidi ya nusu ya watu waliohojiwa walidai kuwa wamewahi

kukumbwa na ukiukaji wa uhuru wa habari wakiwa kazini kati ya 2019 na 2021.

Ukiukaji huo ulijumuisha vitisho, kutekwa kwa zana za kazi, kunyimwa habari na kwa kiwango kidogo kukamatwa na polisi.

Habari za siasa na uchumi ambazo zinakosoa serikali, COVID-19, kutoa nafasi kwa vyama vya upinzani , masuala ya haki za binadamu na migongano ni aina ya habari zenye changamoto na hatari kuziripoti kwa majibu ya waliohojiwa.

Kwa Mtwara waandishi walisema walikabiliwa na changamoto kuandika habari za korosho na gesi.

Mwandishi mmoja aliyehojiwa alidai kuwa aliandika habari

11

Habari

Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki?

Endelea Ukurasa wa 12

Ofisa Programu wa Baraza la Habari Tanzania, Paul Mallimbo akiwasilisha mada kuhusu ukiukwaji wa uhuru wa habari

Toleo la 164, Aprili, 2021

Habari

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

12

kuhusu wakulima ambao hawajalipwa baaada ya serikali kuchukua korosho zao.

Alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kupata maelezo ya upande wa serikali, Mkuu wa Mkoa alitaka kujua kama mwandishi huyo anaripoti kutoka mkoa gani.

Baada ya mwandishi kumwambia kuwa yuko mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Mkoa alimwambia kama anataka kuendelea kubaki kufanyakazi mkoani humo, asitangaze habari hiyo.

Habari za kusifu serikali ikiwa pamoja na za uzinduzi wa miradi, taarifa za kiserikali na habari za kibinadamu zinapendelewa na serikali.

Majibu kuhusu mahusiano kati ya vyombo vya habari na vyanzo yalitofautiana kwa kila mkoa wakati waliohojiwa Kilimanjaro wakisema kuwa mazuri, mazuri kiasi Dodoma (asilimia 75) na hafifu Arusha( asilimia 28.5).

Mahusiano hayo, kwa mujibu wa waliohojiwa yalibadilika kwa nyakati tofauti kutegemea maudhui na jinsi ya vyanzo vinavyoripotiwa katika vyombo vya habari.

Mahusiano yanaboreka wakati vyanzo vikiripotiwa vizuri kwenye vyombo vya habari. Asilimia 75 ya waliohjiwa Mwanza walisema mahusiano ni ya kinafiki.

Katika matukio ambapo mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ni hafifu , asilimia 80 wamesema hali hiyo inatokana na hofu ya watoa habari kwamba watapoteza kazi na hivyo kuamua kutotoa habari hasa pale masuala yenyewe yakiwa nyeti na hasi.

Kiasi cha asilimia 15% ya waliohojiwa wameeleza mahusiano hafifu kwa upande wa vyanzo vya habari ni kutojua sheria ya haki ya kupata taarifa na kwa upande wa wanahabari ni udhaifu wa weledi na maadili.

Kulikuwa pia na madai kuwa

vyanzo vilipendelea zaidi vyombo vikubwa vya habari vya kitaifa badala ya vile kwenye maeneo katika wilaya na vya jamii.

Kuhusu sheria ya Haki ya Kupata Taarifa, miongoni mwa wanaojua kanuni za sheria hiyo asilimia 15 wamesema hawapendi kanuni inayowapa muda wa hadi 30 watoa taarifa kujibu maombi ya taarifa kwa maelezo kuwa taarifa itakayotolewa baada ya kipindi kirefu kama hicho itakuwa si habari tena labda pengine kwa makala na vipindi maalum.

Kuhusu upatikanaji taarifa na uhuru wa habari wakati wa uchaguzi mkuu, majibu yalitofautiana kulingana na wapi na lini habari inapotokea.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa upatikanaji wa habari katika uchaguzi mkuu wa 2020 ulikuwa mzuri wakati wa uteuzi wa ndani ya vyama na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imepongezwa kwa kuweka utaratibu mzuri ikiwa pamoja na vituo kwa wanahabari kwenda kupata taarifa kila wakati kuhusu mchakato wa uchaguzi.

Mambo yalibadilika katika kipindi cha kuelekea hatua za mwisho za kampeni, kupiga kura, kuhesabu kura na utangazaji wa matokeo ya uchaguzi. Kufungwa kwa intaneti kuliathiri zaidi vyombo vya habari vya mtandaoni ambavyo vilitegemea kupata taarifa kwa njia hiyo na kuzitoa.

Wasiwasi mwingine ulionyeshwa na watu waliohojiwa ni kuwa mwongozo wa kuripoti uchaguzi wa NEC ulibana sana.

Vyombo vya habari viliruhusiwa tu kuripoti taarifa za maofisa a NEC. Taarifa zingine zote hazikuruhusiwa.

Pia walilalamika kuwa ni waandishi wachache tu ndiyo waliruhusiwa kuripoti habari za uchaguzi tofauti na chaguzi zilizopita.

NEC iliagiza vyombo vyote vya habari kuwasilisha majina ya waandishi watakaoripoti uchaguzi wa 2020 ili wapatiwe vitambulisho.

Lakini ni baadhi tu walipewa vitambulisho , kusababisha madai kuwa zoezi hilo lililenga kuwanyima vitambulisho waandishi wanaohoji fursa ya kuripoti uchaguzi.

Baadhi ya waliohojiwa walilaumu vyama vya siasa hasa chama tawala CCM na chama kikuu cha upinzani Chadema kwa kubagua wanahabari walioripoti uchaguzi.

Walisema CCM ilikuwa na orodha ya waandishi ambao ingefanyakazi nao na ilikataa mtu mwingine yeyote asiyekuwemo kwenye orodha yao. Chadema waziwazi ilionyesha kutowaamini wanahabari kutoka vyombo vya habari vya serikali - Daily News na Habari Leo, na runinga na redio za TBC.

Hata pale vyombo hivi vilipojitahidi kupeleka waandishi kufuatana na wagombea wa Chadema kwa gharama zao, chama hicho kilikataa. Katika matukio mengine Chadema haikuwaalika waandishi kutoka vyombo hivyo kwenye mikutano ya waandishi.

Waliohojiwa walisema haikuwa rahisi kwa vyombo vyao kufanya uchambuzi wa mchakato wa uchaguzi kwa sababu maofisa wa chama tawala walikataa mialiko kushiriki vipindi kuhusu uchaguzi, zaidi kutokana na hofu.

Pia ilikuwa hatari kualika baadhi ya wagombea wakiwemo wa upinzani kwa mahojiano ya habari na uchambuzi kwa kuwa walikuwa wanatumia lugha kali wakati wa kampeni.

Aidha, waliohojiwa wengine walisema kulikuwa na hofu katika vyombo vyao kutoa muda sawa kwa wagombea wa upinzani kuhofia kuonekana na wenye mamlaka kuwa wanasaidia ama wanakampeni kwa upinzani, na hiyo inaweza kuwagharimu.

Waliohojiwa pia walitaja baadhi ya matukio ya ukiukaji wa uhuru habari wakati wa uchaguzi. Kwa mfano, wahariri wawili wa Daily News walisema walipata vitisho

Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki? Inatoka Ukurasa wa 11

Endelea Ukurasa wa 14

Waliomeremeta

Toleo la 84, September-Oktoba, 2010

Na Mwandishi wa Barazani

Wadau wa Habari wameeleza kuvutiwa na hatua ya Rais Samia Suluhu kuagiza wenye

mamlaka kuachana na tabia ya kufungia na kusimamiasha vyombo vya habari, tabia ambayo aliyoieleza ni ya “umwamba”.

“Tumefurahishwa na hatua hiyo”, Kajubi Mukajanga ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) alisema katika taarifa kufuatia hotuba ya Rais ambayo ilihusu masuala

mengi. Hotuba hiyo iliyotolewa wakati

wa kuapishwa kwa Makatibu Wakuu , Manaibu Makatibu Wakuu na wakuu wa mashirika ya umma imeinua matumaini, alisema Mukajanga.

Alisema hotuba hiyo pia inaweka maandalizi ya marekebisho ya sheria za vyombo vya habari na kanuni zao na kuzirekebisha ili taifa liwe taifa linalozungumza.

Licha ya hotuba hiyo yenye matumaini, MCT imewakumbusha wanahabari kuwa ngao yao nzuri dhidi ya ukiukwaji wa uhuru wa habari ni kuzingatia maadili ya

taaluma yaliyowekwa na tasnia yenyewe na kuendelea kuwa na mshikamano.

Uhuru unakwenda pamoja na uwajibikaji hivyo wanahabari lazima wazingatia taaluma na maadili ya uandishi, alisema Mukajanga.

Kufuatia agizo la Rais Samia , Baraza limewasihi viongozi waliopewa majukumu ya kusimamia vyombo vya habari kulitekeleza bila visingizio kama ilivyotokea kwa vyombo vya habari vilivyoishinda serikali mahakamani na kuruhusiwa kufanyakazi lakini mpaka sasa bado vimefungiwa.

Wakati Baraza linachukulia kwa uzito agizo la serikali kwa vyombo vya habari kuzingata sheria na kanuni , limewataka watendaji wa Baraza kuwashirikisha wadau katika mchakato wa kuandaa sheria na kanuni zake kuhakikisha zinakwenda sawa na

13

Habari

MCT yapongeza agizo la Rais Samia

Toleo la 164, Aprili, 2021

Endelea Ukurasa wa 14

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga.

Waliomeremeta

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

14

Jarida la Baraza la Habari Tanzania

Habari

katiba ya nchi. Sheria na kanuni mbaya

zitafifisha nia njema ya rais na vyombo vya habari vilivyofungiwa na vitafungiwa tena katika muda mfupi kutokana udhaifu wa sheria.

Baraza limeikumbusha serikali kuhusu uamuzi wa mahakama ya ya Afrika Mashariki wa Machi 28, 2019 ambao uliamuru serikali kurekebisha sheria kulingana na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika

Mashariki baada ya vifungu 16 vya Sheria ya Huduma ya Habari kuonekana kukwaza kanuni za demokrasia za uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari. Mpaka sasa, uamuzi huo haujatekelezwa.

Baraza limeitaka serikali kutekeleza uamuzi huo na limeeleza utayari wake kushirikiana na mamlaka kwa kuwa “ sote tunajenga nyumba moja”.

Baraza na washirika wake katika Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) limeahidi

kufanyakazi kwa karibu na serikali katika shughuli za ujenzi wa taifa kwa kuzingatia utawala bora na utawala wa sheria.

Washirika katika CoRI ni Twaweza, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),Chama cha Waandishi Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Wanasheria (TLS), Sikika, Policy Forum, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), MISA-Tan, TCIB, Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Jamii Forum na MCT.

kutoka kwa vyanzo vya habari wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hata hivyo hawakudhurika.

Wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi ya wabunge wa majimbo ya Tandahimba, Nanyumbu na Mtwara Mjini, waandishi wachache waliruhusiwa kuripoti.

Mjini Arusha kulikuwa na taarifa za polisi kutwaa kamera za wanahabari watatu na kufuta picha, wakati mwandishi mmoja alikamatwa kwa amri ya Kamanda wa polisi wa Mkoa.

Radio ya Sunrise FM ya Arusha pia iliathirika wakati wa uchaguzi ilipoamriwa kusimamisha matangazo wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Kulikuwa na tukio Mwanza ambapo polisi walilazimisha wanahabari waliopiga picha ya mwanamke aliyetuhumiwa kukutwa na karatasi feki za kura, kuzifuta picha zote.

Asilimia 91.4% ya waliohojiwa wote wamesema kuwa kila waliponyimwa habari hawakuona hiyo imetoka na jinsi yao.

Mtu mmoja Arusha alisema wakati mmoja alikataliwa kupewa taarifa kwa sababu ya jinsi yake

alipokuwa akijiandaa kuripoti kuhusu mila za Wamasai ambapo wazee wa kabila hilo walimwambia hawatoi habari hizo kwa mwanamke.

Mjini Mwanza, mhariri mmoja alisema siku ya uchaguzi hakuwatuma waandishi wanawake kwa sababu za kiuslama kutokana na hofu kuwa zoezi hilo lingechukua muda mwingi zaidi.

Kuhusu Covid-19, wahojiwa wengi walisema upatikanaji wa taarifa kuhusu COVID-19 ulikuwa mzuri wakati mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa huo alipobainika nchini mapema Machi, 2020.

Serikali ilikuwa inatoa taarifa kila wakati hadi mwishoni mwa Aprili 2020 iliposimama.

Hata hivyo asilimia 88 ya waliohojiwa walisema kuwa vyombo vya habari havikuweza kutimiza wajibu wao kama ilivyotarajiwa kwa sababu waandishi hawakuweza kupata taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vya kuaminika na kufanya washindwe kuandika kwa upana kuhusu ugonjwa huo, ambao ni mpya kwao.

Waliohojiwa walifikiri kwamba ingekuwa vizuri kufahamisha

umma idadi ya walioathirika katika mikoa yao ili wachukue tahadhari au kuepusha taharuki isiyo lazima.

Vyombo vya habari havikuruhusiwa kufanya uchunguzi, kuhoji kutafuta habri zaidi. Vilitakiwa kuripoti walichoambiwa na maofisa waliopewa jukumu hilo.

Waliohojiwa walitaja baadhi ya athari ya utangazaji hafifu wa COVID-19 ni kuibuka taarifa zisizo kweli na za kutatanisha kwa umma na kukana uwepo wa ugonjwa na matokeo yake kuongezeka maambukizi.

Kuhusu matokeo ya habari za COVID-19 kutolewa na watu watatu tu (Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Msemaji wa Serikali), wote waliohojiwa walisema hiyo ilikwaza upatikanaji taarifa kwa kuwa kama watu hao hawakuzungumza hakukuwa na taarifa yoyote iliyotolewa na umma uliathirika.

Kuhusu athari za COVID-19 kwa vyombo vya habari, asilimia 80% ya waliohojiwa walikubaliana kwamba tasnia ya habari iliathirika kutokana na janga hilo ambapo mishahara ya wafanyakazi ilipunguzwa na wengine kuachishwa kazi.

Mahusiano kati ya vyanzo na vyombo vya habari ya kinafiki? Inatoka Ukurasa wa 12

MCT yapongeza agizo la Rais SamiaInatoka Ukurasa wa 13

Na Mwandishi wa Barazani

Mara baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari,

kumeibuka mkanganyiko wa vyombo vipi vinavyostahili kufunguliwa.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Dk. Hassan Abbasi aliripotiwa kueleza kuwa Rais alimaanisha kufungulia runinga za mtandaoni na siyo magazeti.

Mkanganyiko ulizidishwa zaidi na kauli ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa alipoungana na mtazamo wa Dk. Abbasi.

Suala hilo lilitulizwa kiana na Waziri wa Habari Innocent Bashungwa alipoawaalika wenye magazeti yaliyofungiwa kukutana naye kujadili suala hilo.

Kwa kuamini kwamba kuna nia njema kutokana na agzio la Rais, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga amewashauri wamiliki wa magazeti yaliyofungiwa kuitikia mwito wa Waziri Bashungwa.

Mukajanga, alieleza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW,

15

Habari

Toleo la 164, Aprili, 2021

Mkanganyiko waibuka agizo la Rais la kufunguliwa magazeti

Endelea Ukurasa wa 16

Waziri wa Habari Innocent Bashungwa

16

Jarida la Baraza la Habari Tanza-nia

kuwa inashangaza kujaribu kutatua tatizo kwa kutumia sheria na kanuni zilizosababisha kuwepo tatizo hilo.

“Tunachosema hapa ni kwamba huwezi kushughulikia tatizo la kubinywa kwa uhuru wa habari kwa kutumia sheria na vifungu zilizoandaliwa makusudi kukwaza haki ya kupata taarifa na uwezo wa wanahabari kufanyakazi kwa uhuru na kitaaluma. ”

Baadhi ya vifungu, Mukajanga alisema mahakama imevieleza kuwa havifai na Mahakama ya Afrika Mashairiki imeitaka serikali kufanyia marekebisho vifungu 16 vya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016.

Kwa hiyo ,amesema , kujadili suala hili kwa kutumia kanuni hizo hizo na sheria ni tatizo.

Baadhi ya magazeti yaliyofungiwa ni Mawio, Mwanahalisi, na Mseto wakati Tanzania Daima imefutiwa leseni na Msajili wa Magazeti.

Baadhi ya magazeti haya yalifanikiwa kuishinda serikali mahakamani na kuamriwa kuwa yafunguliwe lakini serikali imekaidi.

Mmiliki wa Mwanahalisi na Mseto, Saed Kubenea tayari amekutana na Waziri wa Habari.

Mmiliki wa Mawio, Simon Mkina alisema amepanga kwenda Dodoma kukutana na Waziri.

Mkanganyiko waibuka agizo la RaisInatoka Ukurasa wa 15

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dk. Hassan Abbasi

17

Habari

Toleo la 164, Aprili, 2021

Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) wakipitia kijitabu kilichorahisisha sheria ya Haki Kupata Taarifa.

Waandishi Zanzibar kupewa tuzoNa Mwandishi wa Barazani

Wanahabari Zanzibar watapewa tuzo za umahiri na weledi wa uandishi wa habari

katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka huu.

Kwa kuwa Mei 3, ambapo siku hiyo huadhumishwa imeangukia katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Zanzibar itaadhimisha siku hiyo Mei 23, 2021.

Waandaaji wa tuzo hizo za wanahabari wamesema kuwa zitahusisha kazi katika maeneo matano yafuatayo:

• Uandishi wa habari za uchumi wa buluu

• Uandishi wahabarizaJinsia

• Uandishi wa habari za rushwa naUwajibikaji

• Uandishi wa habari za Serikali ya Umoja wa kitaifa.

• Uandishi wa habari za kulipa kodi

Kamati ya maandalizi imewaalika waandishi wa habari kukusanya kazi zao au kuandika katika maeneo hayo na kuziwasilisha kwa wakati.

Habari zitakazochukuliwa ni za uchunguzi, makala au vipindi vya redio na runinga.

Vigezo muhimu vya kuzingatia katika kazi zinazoshindanishwa ni:• Ubora wa kazi iliyowasilishwa• Upekee wa mada• Umuhimu wa kuzingatia

uwiano sawa wa jinsia.• Vyanzo vingi vya habari

vilivyojitawanya.• Ubunifu wa mada husika.

• Matokeo baada ya kutoka habari au kipindi

• Uwasilishaji wa mada husika• Mpangilio wa mada• Ufasaha na mtiririko wa lugha• Kuzingatia maadili ya uandishi

wa habari• Weledi na matumizi ya

takwimu.• Kipindi chaRedio na runinga

kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe katika ubora unaostahiki.

• Kipindi au makala iliyochapishwa au kurushwa na chombo cha habari chochote hapa Tanzania kuanzia Januari 2021 hadi Mei, 2021

Kazi ziwasilishwe katika ofisiya Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) iliopo Weles kuanzia Aprili 15 hadi Mei 1, 2021.