annuur-115

Upload: annurtanzania

Post on 22-Jul-2015

681 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Sauti ya Waislamu

TBC waomba radhiUk. 15

Madudu Baraza la MitihaniKuna mchungaji kulinda maslahi ya Wakristo Kwaya za Injili zimejaa katika komputa za Baraza Shule ya Pengo Marian yachua siri kubwa Ndalichako hawezi kujihukumu mwenyewe Huu ni mgogoro kati ya Waislamu na BarazaNa Mwandishi Wetu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1015 RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 1-7 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

tunataka Baraza la N D A L I C H A K O Mitihani litusute, hawezi kujihukumu t u n a t a k a s e r i k a l i m w e n y e w e , Inaendelea Uk. 2

Mwembechai sasa yanukia Zanzibar

IGP Mwema taaban Zanzibar Wauwaji Syria hawa hapaASKARI wa kutuliza ghasia (FFU) wakiwa mitaani Unguja mwishoni mwa wiki/ Wa i s l a m u Z a n z i b a r jiandaeni. (Soma Uk. 7)

NASHINDWA kujua, nini k i t a w a k u t a Wa i s l a m u Zanzibar baada ya karipio la Askofu Mokiwa. Wakati ule kauli tu ya paroko, Waislamu walipigwa risasi wakafa. Wanawake wa Kiislamu wakakamatwa wakiwa msikitini baada ya kupigwa sana mabomu wakatupwa rumande ambapo walidhalilishwa sana. Leo ni kauli ya Baba Askofu Valentino! Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Rais wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki!

Askofu Mokiwa amcharukia Rais Shein Waislamu wanasubiri kukatwa vichwa

ASKOFU Valentino Mokiwa.

'Wahadhina' watuhumiwa kulipua Makanisa Lengo kuvuruga agenda ya kudai nchi Atakiwa asiwabughudhi Masheikh ZNZ Mbona polisi wana adabu kwa Maaskofu ? Awashughulikie wanaomtukana Rais Muhadhara kufanyika Jumapili Lumumba Itqaaf Leo Kidongochekundu. IGP aalikwa Maandamano ya kihistoria tarehe 26

MAUAJI na uhalifu uliofanywa katika mji wa Houla tarehe 27 Mei, yanaelekea kufanywa chini ya mkakati wa mbinu za El Salvador kutumika nchini Syria. Kutokana na habari zinazovuja kutoka Houla, inaonekana wazi kuwa serikali ya Syria haikuhusika na mauaji ya watoto 32 na wazazi wao, kama inavyodaiwa na vyombo vya habari vya magharibi, na hata Umoja wa Mataifa. Mbinu za El Salvador ni mpangilio wa kigaidi wa mauaji ya watu wengi kwa vikundi vinavyoundwa na Marekani ambazo zilitumika kwanza nchini El Salvador wakati wa harakati ya kupinga utawala dhalimu wa

Robert S. Ford kijeshi, na kusababisha mauaji ya watu wanaokisiwa kufikia 75,000. (Soma Uk. 5)

2S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected] Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/HabariAN-NUUR

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

MAONI YETU

K W A m i a k a mingi kumekuwa na malalamiko, manunguniko juu ya kero za muungano ulioasisiwa tarehe 26 Aprili 1964 na aliyekuwa Rais wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage N y e re re n a R a i s w a Zanzibar Abeid Aman Karume. Katika hati ya Muungano, tunaelezwa kwamba wakuu hao walikubaliana kimsingi juu ya mambo kumi na moja ambayo ndio msingi wa Muungano waliouasisi. Hata hivyo, kadiri siku zilivyosonga mbele, ndivyo kasi ya upungufu wa muungano kati ya nchi hizi mbili ulivyojidhihirisha. Katika yale mambo kumi na moja ambayo ndio yaliyoweka msingi wa makubaliano ya kuwepo muungano, yaliongezwa moja baada ya jingine hadi kukia 23. Tunaona kwamba ongezeko la vipengele hivi vya kimuungano kutoka kumi na moja hadi kukia 23 hivi sasa, ni matokeo ya udhaifu wa kikra katika kuanzisha muungano wenyewe. Sote tunakiri kwamba kuungana ni jambo zuri, ni suala la udugu, kiutu na kijamaa. Lakini tunaona ulikosewa katika muundo wake na kimamlaka kwa pande zote mbili. Hata taratibu na njia za kuuanzisha nazo hazikuweka msingi muafaka wa kujali maslahi na haki sawa kwa pande mbili za nchi. Pamoja na makosa katika kuuasisi na hatimaye kuwepo muungano, hilo lisingekuwa tishio kubwa kwa Taifa iwapo wahusika wangetambua na mapema na kuchukua hatua muafaka kuuboresha muungano huo, kwa kufanya marekebisho mara moja na kusawazisha kasoro zinazodaiwa kuwepo. Sisi tunaona kwamba siasa nyingi na uhadhina

Muungano pasipo maridhiano ni kutafuta balaa, leo au kesho

wa viongozi kuendelea kukumbatia mfumo wa muungano wanaoutaka wao badala ya ule wanaoutaka wananchi, ndio sababu kubwa ya kukidhiri matatizo ya muungano wetu. Tumeundiwa hadi wizara maalum kwa ajili ya kushughulikia kero za muungano, lakini inavyoonekana wizara hiyo imekuwepo kama chanzo tu cha ajira kwa watu, hazionekani hatua za dhati na madhubuti za kuunusuru muungano. Pamoja na kuwepo wizara hiyo, hatuoni kero kupungua. Badala yake, ndio kwanza zimeongezeka na kuleta tafrani na kuhatarisha amani ya nchi. Leo tunaona watu wanaotaka muungano usiwepo wakizidi kuongezeka badala ya kupungua. Leo Zanzibar kunafukuta, wamechoshwa na ubutu wa kutatuliwa kero za muungano. Wakati serikali ikizungumzi suala la mchakato wa kuandikwa katiba mpya, wengine hawaoni umuhimu katika hilo. Wao wanataka kero za muungano zishughulikiwe kwanza ndipo yazungumzwe masuala ya katiba mpya. Katiba kwa sasa kwao sio suala la msingi bila kuwepo muungano wa haki kimaslahi kati ya pande mbili za nchi. Haya yote ni matokeo ya kukumbatia muungano wenye kasoro nyingi bila kuzitatua kwa wakati kwa maslahi ya pande mbili husika za nchi. Tunaona kwamba uvivu wa makusudi wa wahusika waliopewa dhamana katika kuhangaikia muungano unaokidhi maslahi ya pande zote mbili, ndio uliotukisha hapa tulipo. Lakini tunaamini kwamba iwapo utapatikana ujasiri na nia ya dhati ya kuondoa kero zinazolalamikiwa na wananchi juu ya muundo wa muungano, tunaweza kuka mahali panapostahili.

itushitaki kwamba tunasema uwongo au ikiri kwamba kuna mfumokristo ndani ya Baraza la Mitihani Tanzania unaowahujuma Waislamu. Na hili haliwezi kufanywa na Joyce Ndalichako au kwa kubadili F walizopewa Waislamu na kuwarejeshea A na B zao kimya kimya.

Madudu Baraza la Mitihanilakini Baraza hilo hilo limekataa kuajiri mtaalamu wa somo la Maarifa ya Uislamu. K w e l i tumewadhulumu, ni kauli iliyonukuliwa kutoka kwa mtumishi mmoja wa vitengo vyeti vya Baraza la Mitihani mara baada ya kuka barua ya Wakuu wa Shule za Kiislamu wakikataa matokeo ya mwaka 2012. Inaelezwa kuwa ubaridi usio tarajiwa uliwagubika wakuu wa vitengo nyeti wa Baraza hilo ambao hawakutarajia kuwa Wa i s l a m u w a n g e f i k i a mahali pa kuhoji na kukataa matokeo. Inaelezwa kuwa ubaridi huo unatokana na ukweli kuwa wamejiamini sana kiasi kwamba watafanya lolote na hakuna wa kuhoji wala kugundua hujuma inayofanywa na hata ikigundulika, hapawezi kufanywa lolote. Katika kufuatilia suala hili toka Wakuu wa Shule za Kiislamu walipoandika barua kwa Katibu Mkuu, Wi z a r a y a E l i m u n a Mafunzo ya Ufundi ya kutokuwa na imani na Baraza la Mitihani, gazeti hili limegundua madhaifu na mianya ambayo huenda ndiyo inayotumika kuwahujumu Waislamu. Aidha, gazeti hili limepata habari za kuaminika kwamba kuna ama uchakachuaji wa makusudi au udhaifu mkubwa ambapo inatokea mwanafunzi mweye alama za chini hupewa daraja la juu akapewa daraja la chini mwenye alama za juu. Wa p a s h a h a b a r i wetu wanasema kuwa, mwanafunzi mwenye kwa mfano alama 50 anaweza kupewa A na mwenye 70 kupewa F na kwamba lau utafanyika uchunguzi, yatagundulika mengi ya kushangaza na kutia hasira kwa waliohujumiwa. Hadi sasa wanaolalamikia hali hiyo wakidai kuwa wanafunzi wao alikuwa na A, B na C lakini wakaishia kupewa F, ni Waislamu. Moja ya mwanya unaotajwa ni kuwa w a s a h i h i s h a j i wakishamaliza kazi yao ya kusahihisha na kutoa

Hayo ni maoni ya baadhi ya Waislamu ambao walikuwa wakizungumzia suala la malalamiko ya Waislamu dhidi ya dhulma wanayofanyiwa na Baraza la Waislamu. Wa k i j a d i l i s u a l a hilo katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam wamesema kuwa malalamiko ya Waislamu yamekuwa ni ya muda mrefu sana na wamekuwa wakipuuzwa. Sasa maadhali malalamiko hayo yamefikishwa rasmi serikalini, kinachohitajika ni kufanyika uchunguzi huru na wa kina ijulikane nani Baraza kwa maana toka limeanzishwa limekuwa likidhibitiwa na akina nani na nini walikuwa wakifanya. Katika maoni yao Waislamu wengi wanasema kuwa, mtuhumiwa hapa ni Baraza, haliwezi kujishitaki lenyewe, likawa mwendesha mashitaka, shahidi, hakimu na askari jela. Wapo baadhi ya walimu wanasema kuwa katika komputa za Baraza la Mitihani kumejaa miziki ya Injili na hupigwa katika osi na zinasikika hata watu wakisahihisha mitihani, hili ni Baraza la Mitihani la Tanzania au Baraza la Mitihani la Kikristo? Anahoji Bwana Abdu Ismaili wa Ilala, Bungoni. Japo Ismail hakutaka kutaja jina la mwalimu aliyemsikia akilalamika, lakini zipo taarifa za kuaminika kuwa Baraza la Mitihani limeajiri mchungaji anayelipwa na serikali akisimamia maslahi ya wanafunzi Wakristo,

alama, hakuna kanuni katika Baraza la Mitihani inayoweka wazi, nani anahusika kuweka madaraja ya mwisho. Hajulikani kwa sifa wala kwa majina, lakini pia utaratibu wa kuamua nani apewe A na nani B na kwa vigezo gani haujulikani. Taarifa za awali zinasema kuwa wapo Wakuu wa Shule ambao wana taarifa za uhakika juu ya A na B walizokuwa nazo wanafunzi wao waliomaliza kidato cha sita, lakini matokeo yakachakachuliwa wakapewa F. Katika kujaribu kulitafiti suala hili, ndio An nuur imegundua kuwa anayeamua nani apate A, B, C, D, na F baada ya wasahihishaji kumaliza kazi yao na kurekodi maksi, ni jopo la siri lakini linalodaiwa kuwa ni mawakala wa kanisa. Kwa maana kuwa jopo linalokaa na kuamua shule ipewe gredi gani, shule gani zitese na zipi ziwe za mwisho, wanafunzi gani wapate darala la kwanza (Div. 1) au waambulie 0; halijulikani wajumbe wake ni kina nani, na wamepewa kazi hiyo kwa sifa gani. Imekuwa ni jopo la siri kama la Freemasons, hawa ndio humpiga kiatu mwenye A wakampa F kama Wakuu wa Shule za Kiislamu wanavyolalamika. Anasema mwalimu mmoja. Mwalimu huyo akiongea na mwandishi anasema kuwa zipo ripoti ambazo zilishawahi kutaja udhaifu huo na kupendekeza kuwa pawe na mfumo rasmi wa kupata gredi unaofahamika kwa wadau wote wa elimu na kutumika kikamilifu ili kuleta haki kwa watahiniwa. Akaongeza kuwa yapo malalamiko ya kweli pia kwamba hata uteuzi wa wasahihishaji wa mitihani ya taifa unafanyika kwa upendeleo na hivyo kupoteza umakini katika usahihishaji. Huu ni mgogoro kati ya Baraza la Mitihani na Waislamu, tunataka Rais aunde tume huru suala hili lichunguzwe, ziwekwe hadharani karatasi za mitihani toka Inaendelea Uk. 3

Madudu Baraza la MitihaniInatoka Uk. 2Baraza hili limeundwa, lakini kwanza Baraza hili llivunjwe, wakuu wake wasije wakaanza kuchoma makaratasi kuharibu ushahidi. Alisema mzazi mmoja akiongea nje ya msikiti wa TIC, Magomeni Kichangani. M z a z i h u y o aliyejitambulisha kwa mwandishi kwa jina la Hatibu Mwinshehe anasema kuwa ana taarifa kuwa kuna wakuu wa shule za Kiislamu tayari wana ushahidi madhubuti jinsi matokeo ya watoto wa Kiislamu yalivyochakachuliwa. Tunataka wakuu hao waweke ushahidi hadharani, na wasikubali kuundwa Tu m e k i j a n j a k i j a n j a bila wao kushirikishwa, vinginevyo watakuwa wamewasaliti Waislamu na hasira za Waislamu zitawashukia wao pamoja na madhalimu. Alisema. Katika kuonyesha kuwa Jopo linaloamua nani apate A na nani apewe F, w a k a t i m w i n g i n e halitizami hata alama alizopewa mwanafunzi na wasahihishaji, wapo wanafunzi Waislamu ambao hawakufanya mitihani kwa sababu ya ugonjwa na Baraza lina taarifa, lakini katika kugawa F nao wakagawiwa F. Maksi zilizowapatia wanafunzi hawa F zimetoka wapi? Wanahoji walimu na kutaka ufafanuzi kutoka Baraza la Mitihani. Wakati huo huo, baadhi ya wakuu wa shule wamehoji kigezo kinachotumika kuzitaja baadhi ya shule za seminari za Kikristo kuwa zinaoongoza na kutoa wanafunzi bora, wakati wanafunzi hao wakija katika shule nyingine hawaonyeshi kuwa na uwezo mkubwa. Ufuatiliaji wa karibu unaonyesha kuwa baadhi ya wanafunzi waliotajwa kuwa wanafunzi bora, kupata divisheni One na shule zao kuongoza katika zile kumi bora katika Dk. Joyce Ndalichako mitihani ya kidato cha 4, walipofika kidato cha 5 wanafunzi walioambulia baadhi ya walimu kuwa baadhi ya wanafunzi katika shule zisizokuwa divisheni 3. Katika kufuatilia suala waliomaliza kidato cha za Kikristo, wamejikuta w a k i t u p w a m b a l i n a hili, alifahamishwa na 4 katika shule ya Marian

3

Habari

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

Girls, Bagamoyo wakitoka na daraja la kwanza (Div. 1), walipoka katika shule hizo wameshindwa hata kuingia katika 20 bora. Baadhi ya wanafunzi walipohojiwa ina kuwajewalikuja na Div. 1, lakini wanaonekana kuwa dhaifu walisema kuwa walifaulu vizuri kwa sababu katika shule waliyotoka ya Marian kuna utaratibu wa kufanya mitihani ya kiwango cha mitihani ya taifa toka mwezi wa tano na kwamba katika maswali waliyofanya wanayakuta katika mitihani ya mwisho. Inakuwa washafundishwa mtihani bila ya kuambiwa kwa uwazi. Mwenyekiti wa Bodi ya Marian anatajwa kuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo. Lakini yapo pia madai kuwa ukiacha mtindo huo usio wa

Khutba ya mwisho ya Mtume Muhammad (s.a.wlBismillahi Rahmani anatambua matendo Raheem. yako. Allah amekataza ENYI watu niazimeni kuchukua Riba (interest), masikio yenu kwa umakini kwa hiyo vyote vyenye kwa maana najua sidhani kuhusisha riba inawajibika baada ya mwaka huu mimi nitakua mingoni mwenu kuviepuka. Rasilimali yako tena, kwa hiyo sikilizeni kwa namna yoyote yatakiwa kile ninachokisema kwenu uitunze hutopungukiwa, kwa umakini mkubwa hutotaabika katika kutaka sana, na muyachukue mtaji. maneno haya kwa wale Allah ameshahukumu wote ambao hawakuweza kwamba riba haikubaliki kuhudhuria hapa leo hii. E n y i w a t u , k a m a na Riba yote imuhusuyo muzingatiavyo kwa Abbas ibn Abdal kuutukuza mwezi huu, siku Muttalib (Mjomba wa hii na mji huu mtukufu, basi mtume Mohammad s.a.w) jitoleeni maisha yenu na iepukwe. mali ya kila Muislamu kwa Jihadharini na shetani, ajili ya sehemu hii tukufu na kwa usalama wa dini yenye kuaminika. yenu. Shetani amepoteza Rudisha kila kisichostahili matu main i n a k amw e kwako kwa wenye haki nayo, usimdhuru yeyote kwa hiyo hatokuwa na uwezo wa hakuna atakayekudhuru na kuwaongoza katika upotofu wewe. Kumbuka kwamba wa mambo makubwa, kwa kwa hakika utakutana na hiyo jihadharini kumfuata Mola wako na kwa hakika katika makosa madogo. Enyi watu, ni kweli mna haki na wake zenu, lakini nao pia wana haki juu yenu, kumbukeni kwamba mmewachukua kama wake zenu tu chini ya dhamana ya Allah na kwa ruhusa yake, kama watatekeleza haki zenu basi kwao ni haki kulishwa, kuvishwa kwa upole (wema). Wa t e n d e e n i w e m a wake zenu na muwe wapole kwao kwani wao ni washirika wenu na wasaidizi wa kweli. Na ni haki kwenu kutowaruhusu kufungamana kiurafiki na yeyote ambaye hamjamthibitisha (kumridhia) na kamwe msifanye uchafu. Enyi watu, nisikilizeni kwa makini, muabuduni Mungu, timizeni swala tano kila siku, mfunge mwenzi wa Ramadhani, mtoe zakka kutokana na mali mnazomiliki, tekelezeni ibada ya hajj kwa mwenye uwezo. Binadamu wote wametokana na Nabii Adam (a.s) na Hawaa (a.s) Mwarabu hana ubora juu ya asiye Mwarabu, na mweupe hana ubora juu ya mweusi na mweusi hana ubora juu ya mweupe isipokuwa kwa kumcha Mungu na kufanya matendo merna. Tambueni kwamba kila Muislamu ni Ndugu wa kila Muislamu na Uislamu unaunda undugu mmoja kwa Waislamu wote. Hakuna kitakacho kuwa haki kwa Muislamu ambacho ni mali stahiki ya Muislamu mwenzie mpaka kiwe kimetolewa kwa uhuru na hiyari kamwe msifanyiane yasiyo haki wenyewe kwa wenyewe. Kumbuka ipo siku utasimamishwa mbele

moja kwa moja, wanafunzi wanaonyeshwa mitihani katika shule za seminari za Kikristo. Yote haya ni mambo na madai ambayo yanahitaji kufanyiwa uchunguzi, ukweli ufahamike ili wananchi warejeshe imani kwa Baraza la Mitihani.

ya ALLAH na kutakiwa kujibu yote uliyoyatenda kwa hiyo Jihadharini msikengeuke (kupotoka) mkatoka katika njia ya haki (ya ukweli) baada ya kuondoka kwangu. Enyi watu, hakuna MTUME au NABII atakaye kuja baada yangu mimi na hakuna IMANI mpya itakayozaliwa. Tafakarini vizuri enyi watu na muyaelewe maneno yangu niliyowaeleza. Ninawaachia nyuma yangu vitu viwili. Kitabu kitukufu (QURAN) na SUNNAH na kama mkivifuata hivi viwili kamwe hamtapotoka. Nyote mnaonisikiza mimi muyakishe maneno yangu kwa wengine na hao wengine wayakishe kwa wengine tena na wa mwisho watayaelewa maneno haya vizuri zaidi kuliko waliyoyasikiza moja kwa moja.

4Na Mwandishi Wetu

MAMBO yamekuwa magumu, lakini mepesi pia, kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Generali (IGP) Said Mwema. Wepesi ni kuwa yeye anakuwa mjumbe tu aliyepewa salamu kukisha kwa Rais Kikwete kwamba hakuna sulhu Zanzibar mpaka Wazanzibari wapate nchi yao. Ugumu unaomkabili ni pamoja na shutuma zinazoelekezwa kwa Jeshi la Polisi Nchini kuwa, baadhi ya askari wake wamehusika kuchoma makanisa na uhalifu mwingine mitaani ili wapate kuwasingizia Waislamu na Masheikh wao. Lengo katika kufanya mchezo huo mchafu linaelezwa kuwa ni kutaka kuhamisha na kuvuruga agenda ya wananchi wa Zanzibar kudai nchi yao na uhuru wao. Kwa upande mwingine IGP Mwema anashutumiwa na jeshi lake la polisi kuwa ameshindwa kuwakamata na kuwachukuliwa hatua za kisheria watu wanaowatukana na kuwadhalilisha viongozi wa ngazi za juu wa serikali akiwemo Rais Ali Mohamed Shein. Pamoja na kuwatukana viongozi, watu hao wanadaiwa pia kuchochea chuki, uhasama na farka baina ya watu wa Unguja na Pemba katika hali ambayo inahatarisha amani ya nchi. Akizungumza katika muhadhara uliofanyika Msikiti wa Mbuyuni juzi Jumatano jioni, Sheikh Farid Had amesema kuwa wapo watu wamekuwa wakisambaza kauli za uchochezi na kuwatukana viongozi lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa. Alisema kuwa watu hao katika mikutano yao wamekuwa wakiwachonganisha Wapemba na Waunguja na kutoa kauli za kumwaga damu. Alisema, Rais Shein na makamo wake ni Wapemba, kwa hiyo kuwatukana na kuwadhalilisha Wapemba ni sawa na kumtukana na kumdhalilisha Rais wa Zanzibar. Japo hakuwataja kwa majina au vyama wanavyowakilisha, lakini baadhi ya wana CCM,

IGP Mwema taaban Zanzibar

Habari

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012 Lumumba. Akasema, katika kujikurubisha na kutaka msaada wa Mwenyezi Mungu, kutakuwa na Itiqaaf leo katika msikiti wa Kidongo chekundu ambapo Waislamu watakesha hapo wakimlilia Mola wao. N a w e w e tunakukaribisha maana wewe ni Said Mwema, Sheikh Farid alitoa mwaliko rasmi kwa IGP Mwema akisema kuwa Said ni katika watu wa kheri. Kwa upande wa wanawake Itiqaaf itafanyika Masjid Jibril nao wakikesha kwa ibada na dua. Kama taarifa rasmi kwa IGP na kwa serikali, Sheikh Farid alisema kuwa kutakuwa na maandamano makubwa ya amani Juni 26 ambapo ulimwengu mzima utapata habari juu ya madai ya Wazanzibari. Sheikh ahitimu Wakati huo huo, Sheikh Mussa Abdallah Juma aliyekuwa amekamatwa, amesema kuwa anashukuru kwamba amepata suna ya Mitume ya kuwekwa jela kwa ajili ya Allah. Amesema, kuwekwa kwake rumande Madema imekuwa ni kana kwamba sasa amehitimu na kupata shahada na sasa hakuna kurudi nyuma ila wembe ni ule ule katika kupigania haki ya Zanzibar. Alisema alipokuwa rumande alihojiwa na makachero wa Bara kwa jeuri. Haya ndiyo tunayopinga kwa nini wasifanye kazi hii askari wa Zanzibar. Alisema na kuhoji Sheikh Mussa. Alirejea kusema kuwa wanachotaka Wazanzibari ni nchi yao, wanataka kulinda heshma ya Rais wao na viongozi wao wa serikali na kwamba hawataki kutawaliwa kimwili. Akasema haya ya kuchoma makanisa, mabaa na kuharibu mali za watu hayafanywi na Wazanzibari bali watu wabaya wasio itakia mema Zanzibar. Kwa upande mwingine naye akaitaka serikali kuacha upendeleo ambapo imekuwa ikichunga heshma za maaskofu hata wale wanaotuhumiwa kwa madawa ya kulevya na ubakaji, lakini ikija kwa Masheikh huwafanyia vitendo vya utovu wa adabu.

AN-NUUR

WAZANZIBARI wakiwa katika kongamano la kujadili Muungano hivi karibuni. maarufu kama wahadhina vya kihalifu kama hivyo kuwa amesikia kikosi cha kama wale wa maskani ya kwa sababu ni haramu. Jeshi la Wananchi wa Kisonge na wale waliofanya Kwa upande mwingine Tanzania (JWTZ) kutoka mkutano wa hadhara hivi Sheikh Farid amesema pia Bara kimeletwa Zanzibar. karibuni kuwajibu wanaohoji kuwa kumekuwa na mazoeya Akahoji iwapo hayo ni ya polisi kuwadhalilisha mapinduzi, vita au nini. muungano. Katika mkutano huo masheikh na kuwafanyia Hata hivyo akawataka kulitolewa shutuma kali vitendo vya utovu wa J W T Z k u w a k a m a wale askari wa Misri wakishutumiwa Wazanzibari adamu. wenye asili ya Pemba Akasema, wapo maaskofu ambao walikaa pembeni kwamba ndio wanataka na viongozi wengine wa wakitizama wananchi kuvunja muungano na taasisi za Kikristo ambao wakiandamana na kupiga kwamba hawana shukrani. wamekuwa wakituhumiwa kambi hadi Husni Mubarak Lakini pia zilitolewa kauli kwa tuhuma mbaya kama alipongoka. Akasema kuwa kutoa za kuhamasisha umwagaji kuwa na madawa ya kulevya, nasaha hizo sio kwamba damu zikitumiwa baadhi ya wizi na ubakaji; lakini aya za Quran. hata kama ni kukamatwa anaogopa, ila ni katika kuhimiza amani ya nchi Katika maelezo yake hukamatwa kwa adabu. Muislamu haogopi Lakini polisi hao hao kwa kwani katika kupigania juzi, huku akimwelekea kufa IGP, Sheikh Farid alivitaka sheikh hata akaiwa hana kosa haki. vyombo vya dola kuchukua humkamata kwa ufedhuli na Sie ndio Maquraish kanda za Masheikh (wa kumvunjia hesma na kwa wenye Zanzibar yetu, Jumiki na Jumaza) waone kumdhalilisha. alisema Farid akisisitiza Sisi sio Al Qaidah, sio k u w a w a n a c h o t a k a kama kuna mahali popote wametamka neno la kuvunja magaidi, sisi Wazanzibari Wazanzibari ni Zanzibar t u n a t a k a h a k i b i l a yao hawataki muungano sheria. A l i s i s i t i z a k u w a kubaguliwa. Msinikamate kwa sababu tangu hapo na wanachopigania ni uhuru na k w a u h u n i , p a t a k u w a haukuwepo kwa sababu haki ya Wazanzibari kuwa hapakaliki wala hapatoshi. hata hiyo hati ya muungano Kama kwa taratibu, adabu na haipo. nchi huru. Si jingine. Kama wewe unayo Kuhusu tuhuma kuwa heshma nitakuja mwenyewe t u p e , Wa z a n z i b a r i huenda polisi wamehusika polisi na mahakamani. Alisema Sheikh Farid wameitafuta kote mpaka kuchoma makanisa, Sheikh Farid amesema kuwa wapo k w a m b a k a m a p o l i s i U m o j a w a M a t a i f a watu wameshuhudia polisi wanadhani watamdhuru hawajaipata. Akamalizia kwa wakipiga mabomu misikiti na hata kuwafanya watoto kumtaarifu IGP kwamba na kulipua vyombo vya wake kuwa yatima halafu hawataacha kukutana na iwe basi, wanajidanganya. usari na wamepiga picha. Watoto wangu wakibaki kufanya mihadhara kwani Katika hali hiyo akasema kuwa, yawezekana pia ndio yatima, basi na wenu sio hiyo ni haki yao kikatiba hao hao waliolipua makanisa heshma mnawapa maaskofu na kishreria. Na akatangaza kuwa sie mnatudhalilisha; ili kipatikane kisingizio. muhadhara mkubwa Alisisitiza kuwa hakuna hatukubali. Alisema. Katika kumalizia nasaha utafanyika Jumapili Juni sheikh, hakuna Muislamu anayeweza kufanya vitendo zake Sheikh Farid amesema 3 katika viwanja vya

Mbinu za El Salvador zinapotumika SyriaVikundi vya mauaji vya Marekani na NATO vinapounganisha majeshi ya wapinzaniNa Prof. Michel ChossudovskyMay 28, 2012 (Mtandao wa Kupashana Habari) IKICHUKUA mfumo wa operesheni za kificho za Marekani katika eneo la Amerika ya Kati, mkakati wa Pentagon (makao makuu ya Jeshi la Marekani) wa matumizi ya mbinu za El Salvador nchini Irak mwaka 2004 ulitekelezwa chini ya uangalizi wa Balozi wa Marekani nchini Irak, John N e g ro p o n t e ( 2 0 0 4 - 2 0 0 5 ) pamoja na Robert Stephen Ford, ambaye aliteuliwa Balozi wa Marekani nchini Syria mnamo January 2011, chini ya miezi miwili kabla ya kuanza kwa uasi wa kijeshi dhidi ya serikali ya Bashar Al Assad. Mbinu za El Salvador ni mpangilio wa kigaidi wa mauaji ya watu wengi kwa vikundi vinavyoundwa na Marekani ambazo zilitumika kwanza nchini El Salvador wakati wa harakati ya kupinga utawala dhalimu wa kijeshi, na kusababisha mauaji ya watu wanaokisiwa kukia 75,000. John Negroponte alikuwa Balozi wa Marekani nchini Honduras kuanzia 1981 hadi 1985. Akiwa balozi Tegucigalpa, alikuwa na nafasi muhimu katika kuunga mkono na kusimamia kundi la Contra nchini Nicaragua, askari mamluki waliokuwa wakishambulia kutoka Honduras. Mashambulio ya Contra mpakani kutokea Honduras yalifikia mauaji ya watu takriban 50,000. Mwaka 2004, John Negroponte aliteuliwa balozi wa Marekani nchini Irak, akiwa na mkakati maalum wa kutekeleza. Mbinu za El Salvador nchini Syria: Nafasi maalum ya Balozi wa Marekani Robert S. Ford: Balozi wa Marekani nchini Syria (aliyeteuliwa January 2011), Robert Stephen Ford alikuwa mmojawapo kati ya wasaidizi wa Negroponte katika ubalozi wa Marekani mjini Baghdad (2004-2005). Katika mazingira haya, mbinu za El Salvador nchini Irak ziliweka msingi wa kuzuka kwa uasi nchini Syria mwezi Machi 2011, ulioanzia katika mji wa kusini ya nchi ulioko mpakani, Daraa. Ukifuatilia matukio ya hivi karibuni, mauaji na uhalifu mwingine uliofanywa katika mji wa Houla ambao pia uko mpakani tarehe 27 Mei pia yanaelekea kufanywa chini ya mkakati wa mbinu za El Salvador kutumika nchini Syria. Serikali ya Russia imetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi, na kutokana na habari zinazovuja kutoka Houla, nchini Syria, karibu na mji wa Homs na mpaka wa Syria na Lebanon, inaonekana wazi kuwa serikali ya Syria haikuhusika na mauaji ya watoto 32 na wazazi wao, kama inavyodaiwa na vyombo vya habari vya magharibi, na hata Umoja wa Mataifa. Inaelekea kuwa badala yake, ni vikundi vya mauaji ana kwa ana ambavyo wanaharakati wanasema ni maharamia wanaotetea utawala au wanamgambo wakati serikali ya Syria inasema ni magaidi wa Al Qaeda wanaoshirikiana na waingiliaji kutoka nje. (Angalia Tony Cartalucci, Serikali ya Syria yalaumiwa kwa uhalifu wa vikundi vya mauaji vinavyofadhiliwa na Marekani, katika Global Research, May 28, 2012). Balozi wa Marekani Robert S. Ford alipelekwa Damascus mwishoni mwa Januari 2011 wakati harakati zinakia kilele nchini Misri. (Mwandishi wa makala hii alikuwepo mjini Damascus January 27, 2011 wakati balozi mpya wa Marekani akitoa hati zake za utambulisho kwa serikali ya Al Assad). Wakati naanza ziara ya Syria mwezi Januari 2011, nilikuwa natafakari kuhusu umuhimu wa uteuzi huu na jinsi ambavyo unaweza kutumika katika mbinu za kicho za kuvuruga utawala. Hata hivyo sikupata hisia kuwa agenda hii ya kuvuruga utawala nchini Syria inaweza kutekelezwa chini ya miezi miwili kufuatia kuanza kazi kwa Robert S. Ford kama balozi wa Marekani nchini Syria. Kurudishwa kwa Balozi wa Marekani nchini Syria, na zaidi kumteua Robert S. Ford kama balozi wa Marekani, ina uhusiano wa moja kwa moja na kuanza kwa uasi ukiambatana na vikundi vya mauaji katikati ya mwezi Machi 2011 dhidi ya serikali ya Bashar Al Assad. Robert S. Ford alikuwa ndiye anafaa kwa kazi hiyo. Akiwa namba mbili; katika ubalozi wa Marekani nchini Irak (20042005) chini ya John Negroponte, alikuwa na nafasi muhimu katika kutekeleza mkakati wa Pentagon wa Mbinu za El Salvador kwa Irak. Mkakati huo hasa ulikuwa ni kuunga mkono vikundi vya mauaji nchini Irak na wanamgambo kwa mtindo ule ule wa Amerika ya Kati. Kuanzia wakati alipofika mjini Damascus mwishoni m w a J a n u a r i 2 0 11 h a d i aliporudishwa nyumbani na serikali ya Marekani mwezi Oktoba 2011, Balozi Robert S. Ford alifanya kazi kubwa ya kuweka msingi ndani ya Syria pamoja na kuweka mawasiliano na vikundi vya upinzani. Ubalozi wa Marekani baadaye ulifungwa mwezi Februari (2012). Ford pia alishiriki katika kukusanya Mujahidina mamluki kutoka nchi jirani za Kiarabu na kuunganishwa kwao katika vikosi vya upinzani vya Syria. Tangu aondoke Damascus, Ford anaendelea kusimamia mradi huo wa Syria akiwa katika Wizara ya Mambo ya Nje (ya Marekani). Alinukuliwa akisema Kama Balozi wa Marekani nchini Syria - nafasi ambayo Waziri wa Mambo ya Nje na Rais wamenibakiza nitafanya kazi na wenzangu mjini Washington kufikia mageuzi ya amani kwa wananchi wa Syria. Sisi na washirika wetu kimataifa tunatazamia kuona mageuzi yanayowafikia na kuunganisha jamii zote za Syria na yanayowapa watu wote wa Syria tumaini la maisha bora baadaye. Mwaka wangu mmoja nchini Syria unaniambia kuwa mageuzi hayo yanawezekana, lakini siyo katika mazingira ambayo upande mmoja wakati wote unafanya mashambulizi dhidi ya watu wanaotafuta hifadhi katika nyumba zao, (kwa mujibu wa ukurasa wa Ubalozi wa Marekani nchini Syria katika Facebook). Mageuzi ya amani kwa watu wa Syria? Balozi Robert S. Ford siyo mwanadiplomasia wa kawaida. Alikuwa mwakilishi wa Marekani mwezi Januari 2004 katika mji wa Kishia wa Najaf nchini Irak, ambako ndiyo maskani ya jeshi la Mahdi. Miezi michache baadaye akateuliwa kuwa namba mbili (mshauri wa masuala ya siasa) wakati Balozi John Negroponte anaanza kazi nchini Irak (June 2004 hadi Aprili 2005). Ford baadaye alifanya kazi chini ya aliyechukua nafasi ya Negroponte, Zalmay Khalilzad kabla ya kuteuliwa kwake kuwa balozi nchini Algeria mwaka 2006. Kazi ya Robert S. Ford kama mshauri wa siasa chini ya Balozi John Negroponte ilikuwa ni kuratibu, kutoka ubalozi wa Marekani, kuunga mkono kwa siri vikundi vya mauaji na kudhoosha harakati za (kupinga uvamizi wa Marekani). John Negroponte na Robert S. Ford katika ubalozi wa Marekani walifanya kazi kwa karibu katika mradi huo wa Pentagon. Maosa wengine wawili wa ubalozi, yaani Henry Ensher (naibu wa Ford) na osa mmoja kijana katika dawati la siasa, Jeffrey Beal, walifanya kazi ya kuzungumza na makundi

5

Kimataifa

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

Robert S. Ford: Balozi wa Marekani nchini Syria tofauti ya wa-Iraki, ikiwa ni pamoja na wenye siasa kali. (Angalia gazeti la New Yorker, Machi 26, 2007). Mshirika mwingine muhimu katika kundi la Negroponte alikuwa James Franklin Jeffrey, aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Albania (2002 hadi 2004). Ni muhimu pia kukumbusha kuwa mkuu mpya wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) aliyeteuliwa na Rais Barack Obama, Jenerali David Petraeus alikuwa na nafasi muhimu katika kuweka mtandao wa kuwaunga mkono waasi wa Syria kwa siri, kuingiliwa kwa vyombo vya ujasusi vya Syria na majeshi yake, n.k. Petraeus alikuwa na nafasi muhimu katika mkakati wa El Salvador kwa Irak, ambako aliongoza kamandi ya washirika wa Marekani katika kuandaa mazingira ya kiusalama ya kuondoa majeshi ya kigeni nchini Irak, ambako alisimamia mkakati wa kupambana na ugaidi mjini Baghdad mwaka 2004 akishirikiana na John Negroponte na Robert S. Ford katika ubalozi wa Marekani mjini Baghdad. CIA inasimamia mikakati ya siri nchini Syria. Katikati ya mwezi Machi, Jenerali David Petraeus alikutana na wakuu wenzake wa mashirika ya kijasusi mjini Ankara, Uturuki, kujadili Uturuki kutoa misaada kwa Jeshi Huru la Syria (FSA) (Angalia habari Mkuu wa CIA ajadili Syria, Irak na Waziri Mkuu wa Uturuki, RTT News, Machi 14, 2012). (Habari hiyo ilisema) David Petraeus, mkuu wa CIA, alifanya mikutano na maosa wa juu wa Uturuki jana na juzi Machi 12, gazeti la kila siku la Hurriyet limefahamishwa. Petraeus alikutana na Waziri Mkuu R e c e p Ta y y i p E r d o g a n jana na mkuu mwenza Hakan Fidan, mkuu wa Shirika la Taifa ya Ujasusi (MIT), siku iliyotangulia. Osa mmoja wa ubalozi wa Marekani alisema maosa wa Uturuki na Marekani walijadili ushirikiano bora zaidi kuhusiana na masuala nyeti ya ukanda huu katika miezi ijayo. Maofisa wa Uturuki walisema Erdogan na Petraeus walibadilishana mawazo kuhusu hali ilivyo Syria na mapambano dhidi ya ugaidi. (Mkuu wa CIA atembelea Uturuki kujadili Syria na kupambana na ugaidi Atlantic Council, Machi 14, 2012). (Makala hii imefasiriwa katika Kiswahili na Anil Kija kutoka makala ya Kiingreza The Salvador Option For Syria US-NATO Sponsored Death Squads Integrate Opposition Forces iliyoandikwa Mey 28, 2012 na Profesa Michael Chossudovsky. Ilichapishwa kwanza katika jarida la Global Research, 2012)

6

Makala/Tangazo

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

Mwenye jukumu la kusimamia nyumbaWAZAZI kutokana na kutingwa na shughuli ambazo mara nyingi mno hazina ratiba wala malengo bali hukurupuka kwa kila lile linalowatokezea mbele yao liwe ni jambo lenye maslahi kwao au la, baba mwenye jukumu la kuongoza familia hana nafasi au utaratibu wa kuwaweka watoto au familia yake vikao vya mara kwa mara kuwapa maelekezo na kusikiliza matatizo yao. Hutoka kwenda kwenye mihangaiko yake al-fajiri na kurudi usiku akiwa yuko hoi. Na wale kina mama ambao hawako kwenye ajira rasmi, kila kukicha mbio mitaani kwenye ujasiriamali. Hivyo jukumu la kulea mtoto huachiwa House girl (Mtumishi wa ndani wa kike) au kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto, ambavyo wenye kuvimiliki wana malengo yao. Na wale ndugu zangu wa Pangu pakavu tia mchuzi wanawalea watoto wao kama vile kuku wa kienyeji. Kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu, wazazi ndio wenye majukumu ya kumlea mtoto wao na watawajibishwa kwa hilo kwa mujibu hadithi iliyopelekwa na Abdullah bin Omar (R.A) amesimulia kuwa Mtume (S.A.W) amesema: Nyote ni wachungaji na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. Kiongozi ni mchunga, na mume ni mchungaji juu ya mkewe, na mke ni mchungaji nyumba ya mumewe na watoto wake, kwa hiyo nyote ni wachungaji na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga. (Bukhari na Muslim) Lakini kuna dharura imejitokeza katika zama zetu ambapo mzazi hana elimu ya kuweza kuwaelimisha watoto wake au ufinyu wa muda hivyo kulazimika kuwapeleka kwenye madrasah au shule za awali. Inapotokea dharura kama hii inamlazimu mzazi kuwafahamu walimu juu ya itikadi zao na tabia zao kwani mwanafunzi huathirika kwa tabia za mwalimu wake kama anavyoathirika kwa tabia za mzazi na wanafamilia kwa ujumla. Amesema Allah (S.W): Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii: basi msife ila nayi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu ya mwanamke duniani, fursa sawa kwa wote, mfumo dume upingwe vita n.k. Uislamu haujakataza kwa mwanamke kufanya kazi lakini kufanya kazi huko kusisababishe kumfanya mwanamke kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kike. Hivyo mwanamke kujivua majukumu yake aliyoumbiwa nayo na nafasi ya kuchukuliwa na televisheni kwa kumlea mtoto na house girl au jamii. Uislamu umewaamrisha wazazi kuwafundisha watoto wao swala wakiwa na umri mdogo na pindi mzazi anapokwenda naye msikitini mtoto wake huwa anampandikiza kitu kwenye moyo wake. Badala yake wazazi wanatumia fursa ya kumpeleka madrasah, mwalimu atatekeleza wajibu wake wa kufundisha na kupandikiza fikra ya kumtambuwa Mwenyezi Mungu, taribia, itikadi na akhalaki, mtoto arudipo nyumbani hakuna mtu wa kuvisimamia vile alivyopandikizwa kimatendo. Hivyo mwalimu wa madrasah anapandikiza fikra, wazazi nyumbani wanaiondoa na kuingiza mambo ya laghawi na munkarati kwa vitendo vyao au mwalimu televisheni. (Imeandikwa na Abu Saumu Kombo Hassan, Tanga Mob: 0714 720 965)

(2:132). Wazazi wengi wa Kiislamu wanazingatia zaidi mno katika kuwapatia watoto wao mahitaji ya chakula, makazi, malazi, elimu ya sekula na mahitajio ya mambo ya laghawi tu. Hii ni fikra na matendo ya watu ambao ni Materialists, yaani ambao wamefanya lengo lao la maisha ni kuchuma vitu, kuwa na mali, kula na kunywa. Na hawashughulishwi kabisa kuhakikisha kwamba wanapatia malezi ya kiitikadi, kiakhalaki na kiimani. Na ikitokea kwa baadhi ya wazazi kuwapatia malezi hayo yanakuwa ni ya masikhara na mchezo bila kuyathamini. Kwa msingi huo watoto wanashindwa kuelewa lengo, jukumu na dhima ya kuwepo kwao hapa ulimwenguni. Hivyo kufuata dini kimazowea bila kuwa na elimu nayo. Kwenye Quran, Mwenyezi Mungu ameuelezea wasia wa mzee Luqman kwa mwanawe, haya ni mafunzo ambayo wanaelekezwa Waislamu na Mola wao ili kujifunza na kuyaingiza katika utekelezaji. Kwenye kisa hiki cha Luqman, kuna mafunzo yanayopatikana ya kiitikadi, kiakhalaki, kiimani na kitaribia n.k. Amesema Allah (S.W): Na Luqman alipomwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usishirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila shaka ni dhuluma kubwa. (Suratul Luqman 31 :13)

Ewe mwanangu! Shika sala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anayejivuna na kujifakharisha. (Suratul Luqman 31 :17-18) Wema waliotutangulia malezi ya watoto wao yalikuwa katika sehemu tatu. Nyumba, msikitini na sehemu ndogo katika jamii. Mama ambaye katika mtizamo Kiislamu

ndiye aliyebebeshwa jukumu la kutunza nyumba ikiwemo kuwalea watoto, ndio wema waliotangulia kama vile Imamu Shafii na Imamu Ahmad, daraja walizokia ni kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu kisha ni kwa juhudi iliyofanywa na mama zao kwa kuwalea katika taribia na akhalaki njema. Ikizingatiwa wao walikuwa ni mayatima. Lakini katika zama zetu hizi mwanamke anatolewa nyumbani na ikadaiwa kuwa ni maendeleo kwa kutumiwa misamiati mbalimbali kama vile azimio la Beijing, siku Bismillah Rahman Rahim

DAR ES SALAAM No. Usajili CU-112 UDAHILI (INTERVIEW) MAFUNZO YA UALIMU 2012-2013 CHUO KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO NA UDAHILI 9 June 2012 Jumamosi saa 2:00 Asubuhi. GRADE III A NA DIPLOMA KWA VIGEZO VYA WIZARA YA ELIMU NA BARAZA LA MITIHANI.Waliosoma Elimu ya dini ya Kiislami EDK na madrasa watapata kipaumbele. UDAHILI UTAFANYIKA KWENYE VITUO VYOTE VYA KUCHUKULIA FOMU VILIVYOPO MIKOANI KWA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA CHUONI UNUNIO. KWA MAWASILIANO ZAIDI: MKUU WA CHUO: 0713 022178 MSAJILI 0715 822332 0784 822332 0756 822332 Wabillah Tawq

CHUO CHA UALIMU UNUNIO

7Na Omar Msangi MWAKA 2001 waliuliwa Wazanzibari kwa uchache wasio pungua 20. Wapo wake za watu na wasichana wari waliobakwa. Wanawake waliporwa mikufu na vito vyao vya thamani. Nyumba zilivunjwa watu wakaibiwa. Hiyo ni mbali na wale wengi waliotiwa vilema vya kudumu. Katika operesheni hiyo, watu walivamiwa Misikitini, misikiti ikapigwa mabomu na Imamu mmoja akapigwa risasi mara tu alipotoka kuswalisha Ijumaa. Hawa waliouliwa hawakuwa wahalifu, wahuni, magaidi wala siasa kali. Walikuwa wananchi ambao hawakuridhika na matokeo ya kura na wakafanya maandamano ya amani kupaza kilio chao. Kwa upande mwingine, waliofanya mauwaji yale hawakuwa Uamsho, Jumiki wala Maimamu. Walikuwa polisi. Walikuwa jeshi la polisi, wengine wakiwa wametolewa Musoma, Bukoba, Moshi, Songea, Mbeya na Zanzibar kwenyewe. Hawa ndio kwa kutumia bunduki na risasi zilizonunuliwa kwa fedha za kodi za Watanzania waliowafyatulia risasi wananchi na kuwauwa na wengine kuwapa vilema vya kudumu. Wakati ule hatukumsikia Askofu Valentino Mokiwa akicharuka na kusema kuwa haridhishwi na utendaji wa polisi. Hatukumsikia akilaumu serikali ya SMZ na ile ya muungano kwamba haikuchukua hatua kwa askari waliouwa. Kinyume chake zilizosikika ni kauli za maaskofu za kuunga mkono na kushabikia mauwaji yale. Pengine anachopaswa kuelewa Askofu Mokiwa ni kuwa askari waliouwa watu wasio na hatia mwaka 2001 na serikali iliyoamuru askari kuuwa na baada ya hapo ikawalinda, ndio hiyo hiyo ambayo ipo madarakani leo japo wakati ule kwa sura na jina alikuwepo Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Amani Abeid Karume. Sasa mtu unaweza kujiuliza, leo jeshi la polisi linaonekana halifai pamoja na serikali yenyewe kwa sababu sasa ni Wakristo wanalalamika na wakati ule waliouliwa Walikuwa Waislamu na pengine akina Askofu Mokiwa walikuwa na uhakika kwamba hakuna muumini wao aliyeuliwa au kutiwa kilema? La kukumbusha hapa ni kuwa aliyekuwa akiongoza harakati za kuvamia Misikiti

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012alikwaana na kafiri mmoja kwa bahati mbaya. Yule kari akamwambia, umenigonga sasa nakukata kichwa chako, inamisha shingo. Muislamu akainamisha kichwa akisubiri akatwe kichwa. Lakini kari akajikuta kuwa hakuwa na upanga. Akamwambia yule Muislamu, nisubiri hapo hapo nakwenda kuchukua upanga nyumbani. Akaenda nyumbani mahali pa masaa kadhaa, akarudi na kumkuta Muislamu anamsubiri amkate kichwa. Akamkata na kumuulia kwa mbali. Anasema Deedat hiyo ilikuwa ndiyo hali ya udhalili wa Waislamu baada ya kuporomoka dola ya Kiislamu katika nchi nyingi. Walidhalilishwa mpaka wakafikia kukubali kuwa udhalili ni haki yao. Unaweza kuona kuwa hii ni simulizi tu na haina ukweli katika hali halisi. Hadi anaingia Wizara ya Elimu marehemu Kighoma Ali Malima, hapakuwa na shule ya Kiislamu hata moja iliyokuwa imesajiliwa na serikali wakati zilikuwepo shule nyingi za seminari za Kikristo. Ilikuwa wakati ule ukitaka kuandikisha shule unaambiwa kalete kibali cha Bakwata, ukienda Bakwata hupewi kibali. Ilikuwa ni baada ya Malima kuingia Wizara ya Elimu aliyewafungua macho Waislamu kuwa hapakuwa na sheria kama hiyo. Ndio maana Wakristo wao walikuwa hawaambiwi walete kibali cha Baraza la Maaskofu wala CCT. Ilikuwa ni Malima huyo huyo aliyegundua kuwa kulikuwa na hujuma kubwa ambapo watoto wa Kiislamu waliokuwa wamefaulu kwenda kidato cha kwanza majina yao yalikuwa yakikatwa kwa makusudi. Matokeo yake ni kuwa Waislamu wanaonekana asilimia 80 shule za msingi, lakini wakifika sekondari wanakuwa asilimia 10. Kilichokuwa kikifanyika ni kuwa watoto wanafanya mitihani kwa kutumia namba, ikishasahihishwa na kupewa maksi, namba huvishwa majina yake ndio uchaguzi wa wanaokwenda sekondari hufanyika hazichaguliwi namba. Kwa hiyo kilichokuwa kikitokea ni kuwa kwa vile jopo la waliokuwa wanachagua ni Wakristo watupu, majina ya Ali, Hassan, Aisha na Halima yalikuwa yakikatwa kama yalikuwa na alama kubwa. Wale John na Ester wakipewa kipaumbele hata kama wakiwa na alama za chini. Inaendelea Uk. 12

AN-NUUR

Mwembechai sasa yanukia ZanzibarAskofu Mokiwa amcharukia Rais Shein Waislamu wanasubiri kukatwa vichwaikihitimishwa na kuuliwa Waislamu pale Mwembechai kwa kulengwa shabaha. Piga yule, na yule, bado mwongeze. Askofu Mokiwa, hivyo ndivyo alivyonaswa kamanda mmoja akitoa amri kuuliwa Waislamu pale Mwembechai. Baba Askofu Valentino Mokiwa, hao ndio askari wetu ambao leo unawalalamikia kwamba hujaona kasi yao katika kuwakamata na kuwashugulikia watu waliochoma makanisa Zanzibar! Hiyo ndiyo serikali yetu ambayo ilituma askari kukamata Masheikh na kufikia kuuwa Waislamu kwa shinikizo la Paroko. Binafisi nashindwa kujua, nini kitawakuta Waislamu Zanzibar baada ya karipio lako na jinsi ulivyocharuka mbele ya Waziri Aboud. Wakati ule kauli tu ya paroko, Waislamu wanne walipigwa risasi wakafa, wanawake wa Kiislamu wakakamatwa wakiwa msikitini baada ya kupigwa sana mabomu wakatupwa rumande ambapo walidhalilishwa sana. Leo ni kauli ya Baba Askofu Valentino. Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Rais wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki! Wa i s l a m u Z a n z i b a r jiandaeni. Na mmesikia kauli ya Waziri wa Nchi Osi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alivyoongea kwa unyenyekevu mkubwa mbele ya Baba Askofu kama alivyofanya Yusuf Rajab Makamba mbele ya Padiri Camellius Lwambano. Na Baba Askofu Mokiwa ashamsuta Waziri Aboud, anasema hataki kusikia kuwa waliochoma makanisa ni wahuni. Pengine, anataka bila hata kufanyika uchunguzi, wakamatwe Masheikh ndio ataridhika kama ilivyofanyika baada ya shinikizo la paroko Lwambano. Labda hili niliachie hapa kwani tangu hapo haikuwa mada yangu ya leo. Almarhum Sheikh Ahmed Deedat aliwahi kusimulia kisa kimoja ambapo alisema kuwa Muislamu mmoja wakati anatembea

Askofu Mokiwa na kuamuru askari kuingia na kukemea ubaya ukifanyika, mabuti yao misikitini kupiga ukifanywa na yoyote na waumini alikuwa kamanda kufanyiwa mtu yeyote. George Kizuguto. Waulize Hawasubiri mpaka yawakute Waunguja watakuambia, nini au kumka mtu anayewahusu walifanyiwa na afande George ndio waseme na kulaani. na Wazanzibari wakati huo Mwaka 1998 alitokea wakituhumu kwamba huenda paroko mmoja wa parokia afande George alikuwa ya Mburahati jijini Dar es kaletwa rasmi kwa ajili ya Salaam na kuishutumu serikali kuwadhalilisha Waislamu kwamba imeshindwa kuwatia au pengine akifanya tu kwa adabu watu wanaomtukana ukereketwa wake wa kidini Yesu. Akatishia kwamba kama alivyokuwa afande serikali isipochukua hatua, N g o w i k u l e M o r o g o r o tena haraka iwezekanavyo, aliyetaka Allah afikishwe itabeba lawama. Kilichofuatia nini? Serikali mahakamani kwa kuandika haikutaka hata kuchunguza Quran inayosema kuwa Yesu na kujua kama ni kweli si Mungu. Hoja yangu ya msingi kuna watu wanamtukana hapa sio kuondoa uhalali na Y e s u n a k u k a s h i f u wajibu wa Askofu Mokiwa Wa k r i s t o . I l i c h o f a n y a , kulalamika na kuwatetea t e n a k w a u n y e n y e k e v u waumini wake. Hoja hapa mkubwa, ni kuwataka radhi ni kuwa yapo mambo mengi Wakristo na kuwaahidi mabaya yanatokea kufanywa kwamba wasubiri wataona na serikali pamoja na vyombo i t a k a v y o w a s h u g h u l i k i a vya dola dhidi ya wananchi. Wa i s l a m u . M a s h e i k h Kwa viongozi wa kidini na wakakamatwa na kuwekwa watu wanaosimama katika ndani, Waislamu wakapigwa haki, msimamo wao ni m a b o m u w a k i s w a l i

8Na Mwandishi Maalum WASWAHILI wanao usemi kwamba ukiona vyaelea vimeundwa, yaani kila linalojiri hutokana na chanzo na maandalizi yake, kwani jambo lolote hutegemea pia mwanzo na hata mwisho wake, pamoja na asili yake. Yaliyojiri hivi karibuni Mjini Unguja na pembezoni mwake, ni muendelezo wa hili suali gumu la kwa nini Zanzibar , na pia kwamba si bure, bali nayo yameundwa. Hapana budi kwa mwenye busara na hikma kujiuliza swali hilo kutokana na mfululizo wa yale yanayoendelea kuelemezewa Visiwa hivi vya Waislamu, katika Bahari ya Hindi, tangu asili na zama. Haya ya machafuko ya kisiasa, taharuki mitaani, mapigo ya mabomu, risasi, na hata maji ya pilipili, ambayo haiba yake haina tafauti na hali ilivyo Jerusalem au Ukanda wa Gaza , nayo ni muendelezo wa hoja ya kwa nini Zanzibar. Kabla ya jawabu ama majibu ya suali hilo kwa wale walioona mbali na kujaribu kuyaandaa hayo, yapo maswali ambayo pia huenda yangelisaidia kuona nuru ya haki na kusibu kwa wenye hikma ambao walisaidia kujibu, kwani hawa hawa Waswahili kwa upande mmoja wa mantiki na methali walinena kwamba dawa ya moto ni moto na usisikie la kuambiwa mpaka uone mwenyewe. Miongoni mwa dadisi hizo ni lipi hasa lililopelekea kuleta mzaha mzaha ambao mwishowe ukaleta karaha ya maguvu na hujuma, kwa kile kinachodaiwa kumshikilia Ust. Mussa Juma, mmoja wa wanaharakati wa Jumuiya ya Uamsho, ambapo hapana shaka hicho ndicho kilikuwa kisa na mkasa cha haya yalioisibu Zanzibar hivi karibuni na kuuamsha ulimwengu, hasa wa dhana na hisia za kila namna. Jee Uamsho walikosea kuendeleza harakati ya

Darasa la wanawake/Tangazo

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012 anza Sofala ya Mozambiki, kupitia Kilwa na Mafia, Bagamoyo mpaka Pate na Kismayu ya Somalia, lakini haina maana kwamba Waislamu Watanganyika ni Wageni kutoka Pemba na Unguja; maana kilichokuwa kikijaribu kupandikizwa hapa ni ati kwamba na Watanganyika wangeliweza kulipiza kisasi cha Misikiti iliyopo Bara kutokana na Makanisa yaliyodaiwa kuchomwa Unguja, thubutu! Muungano sio ulioleta Uislamu na Misikiti Bara kama alivyoongopa yule askofu aliyepewa kipaumbele na vyombo vya habari na kunyenyekewa sana na viongozi wenye heshma zao wa serikali na vyombo vya dola. Mbona mnajidanganya? La msingi hapa ni kurejea maneno juu ya hoja ya wenye busara wanaoona mbali, ambao wamenena juu ya ukweli kwamba kupora na kuchoma makanisa si utamaduni wa Wazanzibari. Iwapo hayo yalibainika, ni ya watu wachache, lakini zaidi waliotumwa au mapandikizi, uchunguzi wa kina ufanyike na ikibidi kuchukuliwa hatua za kisheria, ya kwamba huo si ustaarabu na jeraha la nchi nzima. Kama hoja ni haya makanisa yaliyodaiwa kuchomwa moto kupitia vurugu za hivi karibuni, kwamba inatosha ati hao ni Wapemba na Waislamu wa Uamsho, hivi ni Mzanzibari gani asiyeona na atakayedanyika tena. Wengi ni mashahidi pale ambapo vibanda vya nyasi vikitiwa moto na wenyewe kule Tunguu na Jumbi kisha wakakamatwa na kuwekwa kizuizini akina hawa hawa wanaoitwa Uamsho na Maimamu, mbona hadi sasa haukupatikana ushahidi, licha ya hilaki iliyowapata Waislamu. Hili linapelekea sasa Wazanzibari waamini na wathibitishe kwamba kila baadhi ya watu wanapotaka kujengewa Makanisa, huo ndio mtego wao, na wanafaulu k w a n i t a y a r i Wa z i r iInaendelea Uk. 9

AN-NUUR

Kwa nini Zanzibar?

HALI iliyokuwa katika mitaa mingi mjini Unguja mwisho mwa wiki. mihadhara, au Kiongozi huyo aliteleza pale kwenye muhadhara uliofanyika pale Viwanja vya Lumumba Jumamosi kabla ya siku ya heka heka, au ni namna umma wa Wazanzibari, ulivyohamasika siku hiyo juu ya ile kauli ya kukataliwa kubaya, wakisema kwa kauli moja hatutaki Muungano. Suala linarudi tena kwa nini Zanzibar? Kwa nini haya hayakuonekana pale Viwanja vya Jangwani ambapo pia Wakubwa wakitukanwa mitusi ya nguoni na pia huo Muungano wenyewe na waasisi wake wakilaaniwa katika kiwango ambacho wasemaji wamesema- laisa lkiasi yaani hapana ukomo wa idhilali hiyo. Jee, dola haikuwapo ama haikusikia hoja za pale, au ndiyo ya mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu. Wapo wanaohoji kwa nini hali ya sasa ya Uamsho na harakati juu ya taaluma ya kuuamsha Umma wa Kizanzibari, imepewa thamani ya kiasi cha watu au kikundi cha wachache hivi kwamba ati ni wafanya vurugu wachache, wakati ambapo lipo sauti la zogo la kupasua masikio kwamba Wazanzibari na watu wengine hawautaki Muungano huo. Kwa nini wakati yanajiri hayo, Kamanda Mwema na Waziri wake Nchimbi walikuja kushuhudia kwamba ni vitoto vidogo vilivyoibuka mtaani vikiwakebehi wana ulinzi kwa karaha ya mzaha wa kujitakia; jee wale walikuwa Wapemba, Waislamu, au Wazanzibari wa Uamsho? Mbona hoja imegeuziwa huko? Tunayaona Makanisa ya zama na zama kule kisiwani Pemba ambako hakuna aliyewahi kuyauliza ndewe wala sikio. Kizimbani, Mkungumalofa na kwingineko; tena haya ni makanisa ambayo yanaishi kwa rehema, subra, na ustaarabu wa Wazanzibari wenyewe tu, wasiopendelea hata siku moja wakisikia watoto wao wakiambiwa kwa Yesu kuna neema kwa Muhammad hakuna wema. Sasa imekuwaje ya wasioelewa kinachoundwa hapa Zanzibar wakiwaelemezea kikombe hiki Wapemba au Waislamu? Utashangaa yule aliyedaiwa Mtumishi wa Kanisani pale Mpendae na Uwanja wa Farasi tena usoni mwa vyombo vya habari vya Serikali ati anadai na huko kwao Vijijini Tanganyika, nako Wapemba wako na wanao Msikiti wao mmoja! Kha! Hapana shaka mdomo huo umethibitisha ya moyoni na yale tuliyosema ya kuona vinaelea vimeundwa, juu ya hisia mbaya za ulimwengu wa namna hiyo dhidi ya watu wanaoitwa Wapemba ili libakie kuwa jina baya la yule mbwa anayetafutiwa kifo, na hilo lingebainishwa tu ni jina la Waislamu wote, na popote walipo duniani. Tena kwa ufinyu wa kufikiri walioleta hoja hiyo kuwa ni harakati ya Wapemba na ya Uamsho, na sio angalau kusema n i y a Wa z a n z i b a r i kuukataa Muungano, ambayo ndiyo ilikuwa maudhui ya Mfululizo wa Mihadhara ya Uamsho, walisikika wakisema ati miongoni mwa matunda ya Muungano ni hawa Wapemba na Wazanzibari k u p el e k a M i s i k i t i n a Uislamu Tanganyika; kwa hilo wanajidanganya. Ni kweli kwamba Zanzibar ijapokuwa kwa kumbukumbu zilizofifia iliwahi kuwa na himaya za utawala katika Ukanda wa Pwani ya Tanganyika,

9Inatoka Uk. ameshawahakikishia atawajengea makanisa na hata mahekalu kama yapo yaliyotiwa moto. Tunakumbuka moja ya Mikutano ya hivi karibuni ambapo miongoni mwa watumishi wa Kanisa walipaza sauti kwamba wamekuwa hawatendewi haki na hivyo walistahiki usawa wa fursa kama kwa wananchi wengine. Madai hayo yalipelekea miongoni mwa wasomi wa kutegemewa wa Visiwani, kuibuka na kutahadharisha juu ya madai hayo aliyoyaita yasiyoona mbali, pale alipowambia wanakanisa wa Mkutano huo kwamba wasijaribu kuibua madai ya namna hiyo, wakielewa kwamba iwe iwavyo wao katika Visiwa vya Unguja na Pemba ni wageni, na kwamba kulilia fursa zisizostahili ni kuibua hamasa za watu wa asili ya Zanzibar kwamba sasa umeka wakati Wakristo wapunguziwe rehma waipatayo katika nchi ya Waislamu zaidi ya asilimia 99. Bado mfululizo wa dadisi unaendelea kuhoji sasa ni nani aliyeupiga mabomu akaubomoa Msikiti wa gharama kubwa, mpya wa Omar Ibn Khattab, wa Masumbiji, mjini Unguja, au nao pia ni wa Wapemba na Waislamu wanaotaka kujengewa mpya? Jee, ni nani ambaye akiyaunguza kwa moto maduka na mafriji majokofu yaliyopo pale Msumbiji na Amani kwa Mabata, ambapo hata majirani walipotaka kwenda kunusuru hali hiyo na kuokoa mali walielekezewa mabomu ya pilipili na mitutu ya bunduki, au hao pia ni Wazanzibari wanaowachukia Watanganyika? Inaeleweka wazi kwamba wapo wanasiasa wanaochochea hoja hizo na hivyo kupandikiza mbegu mbovu dhidi ya Waislamu, Wazanzibari, na zaidi wa Kisiwa kinachoitwa Pemba . Viongozi hao hawakujicha majukwaani na hata katika

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012 walipojaribu kutoa jawabu hata ambapo baadhi yao hawapo tena duniani. Ni nani atakayebisha k w a m b a Wa a s i s i w a Muungano huo walituachia jawabu la suali hilo gumu, kwa kila mmoja alivyoonelea? Jee Baba wa Taifa hakuunasishi utawala usoni mwa Jamii ya Kimataifa kwamba Hakuna haja ya kuwapiga mabomu Wazanzibari pindipo watakapokuja kuuchoka na kuukataa Muungano huo?. Jee hayati Mzee Abeid Amani Karume hakuuwacha wimbo ambao hadi sasa hata mtoto mdogo wa Visiwa vya Unguja na Pemba anauwimba yaani, Muungano ni kama koti likiwabana litupilieni mbali? na hatimaye kama ilivyozoeleka kwa kusema mwisho Chumbe. Hivi sasa upo ujumbe mfupi unaotembea katika simu za mkononi ukisema yafuatayo: Kaburini nako si shwari kati ya Nyerere, Karume na Thabiti Kombo. Nyerere anauliza mnasikia kelele kutoka duniani? Karume anajibu Nini tena? Nyerere anajibu, muungano. Thabiti Kombo anasema, Karume nilikwambia toka zamani hukuwashauri Wazanzibari na sisi ndio tuko huku itakuwaje? Karume anajibu, niliwaachia usia Wa z a n z i b a r i k w a m b a muungano ni kama koti likikubana utalivua. Kama hawakunifahamu shauri zao. Kwa hali yeyote, busara inahitajika ya kulijibu suala hili na pia katika kukabiliana na hali halisi ya mahitaji ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla, na wala siyo kwa kutezana nguvu juu ya Muungano Wautakao. Hili limesikika hata kwa mmoja wa Wanadiplomasia wa Chama Tawala, ambaye kwa hikma zake anakiri mamlaka zimechemsha kuubeba msala usiokuwa na asili, yaani Muungano usiokuwa na mashiko.

AN-NUUR

Kwa nini Zanzibar?

WAZANZIBARI wakiwa katika maandamano ya amani kupinga muungano.

kampeni ya kupiga kura ya hee au haspana kama walivyosikika pale watu wa Nchi hii walipochagua maridhiano ya Kisiasa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Hao wanajulikana wapo; wameonekana takriban katika majukwaa yote ya Mikutano zaidi ya Mitano iliyofanyika kabla ya kuja kwa mabomu ya hivi

SHEIKH Farid Had (kulia) majuzi, na hao wakitumia kwenye kioo cha luninga Aya na Msahafu kupinga ya Serikali? Hawa ni rahisi kauli ya Wazanzibari ya pia kuwahoji kwa nini Kuukataa Muungano huo. Zanzibar . Jee, hawa kuwapo Hayo na mengineyo ni w a l i o b e b a s i l a h a n a mengi katika hoja lakini wakauma vidole wakisema katika kujifariji wenyewe afanalek hawa akina watu wa Nchi hii hawakosi Nchimbi na Saidi Mwema kusema Muungu yuko. Tulisema wapo wametuharibia tulitaka tuendelee kuwatwanga waliobashiri kwamba haya wash. Hawa, na kisha yatakuja tu siku ikiwadia mitusi yao ikawasuta hata na hawakusema uongo

10SIKUWAna nia ya kuandika makala kama hii katika vyombo vya habari lakini hamu yangu ya kutaka nchi na jamii yetu kubaki katika hali ya amani, utulifu na kuheshimiana inapatikana imenilazimisha kufanya hivyo. Mwanafalsafa maarufu Ibnu Khal`duun anasema: mwanaadamu kimaumbile yake ni mwanajamii (ni kiumbe ambae anahitaji kimaumbile kuishi pamoja na viumbe wa aina yake) tafsiri ni yangu mimi mwandishi. Katika maisha yake mwanaadamu huyu bila shaka ataishi na watu wenye kutofautiana nae kimitazamo, rangi, kabila na hata itikati au dini, na ili mahusiano yaweze kuendelea, ni lazima kuheshimu mitazamo, rangi, kabila, dini na hata maumbile ya wale unaoishi nao ili nao waweze kuyaheshimu hayo kwa upande wako ijapo mambo hayo yanakizana kwa namna moja au nyengine. Kwani linapokosekana hili basi ni lazima jamii ya namna hiyo itasambaratika. Baada ya kuanguka Uongozi wa Kiislamu hapo mwanzoni mwa kar`ne ya 20, Waislamu katika Ulimwengu wamekuwa wakionekana wanyonge na ambao hawana wa kuwatetea. Uongozi wa Kiislamu ambao ulikuwa katika miaka yake ya mwisho ukiwakilishwa na UKHALIFA WA U`TH`MAANIYYAH (UT`MAN EMPIRE) inaonekana ndio ilikuwa kinga ya kulinda hadhi na matukufu ya Waislamu yasidharauliwe, na baada ya hapo Uislamu na matukufu yake umekuwa ukifanywa kama kichwa cha mwendawazimu kila mtu anajifundishia kunyoa. Sura hii ndio inayojitokeza katika ulimwengu wote. Ni jambo la kawaida kusikia huko nje ya nchi majeshi ya nchi kama Marekani na mfano wake yakiwadhalilisha akina mama na watoto wa Kiislamu au hata wanaume kufanyiwa vitendo viovu na vya kudhalilisha, lakini mambo hayakuishia hapo, bali wanajeshi kama hao wanasonga mbele zaidi kwa kukanyaga kupaka kinyesi au hata kuchoma moto Kitabu kitakatifu cha Waislamu

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

Ukereketwa, ubabe wa kina Prince Newton ni hatarimpya shehe yule yule binafsi niliisoma makala hio na kisha kuirejelea tena na tena na nikawataka baadhi ya Masheikh wenzangu waisome na baada ya yote hayo, nikagundua ya kwamba kile alichokiandika mwandishi huyo hakina uhusiano wowote na Masheikh na kanzu zao, ila alichokikusudia mwandishi ni kuonyesha ukereketwa wake hadharani na dharau na kejeli aliyo nayo dhidi ya Masheikh ambao ni viongozi wa Dini ya Kiislamu, dini ambayo ni moja ya dini zenye wafuasi wengi hapa Tanzania bali nathubutu kusema kwamba ndio Dini yenye wafuasi wengi zaidi hapa nchini kwani takwimu za kabla ya uhuru zilionyesha hivyo na hakuna majanga makubwa yaliotokea na kuwahusisha Waislamu peke yao katika kipindi hicho chote na kwa vile Uislamu ndio dini inayoruhusu kuoawa wake mpaka wanne na ndio hao hao ambao wanapinga kwa nguvu zao zote suala zima la kufunga kizazi isipokua katika hali za dharura kubwa tu, wakati ambapo dini nyengine yenye wafuasi wengi mwanamume haruhusiki kuoa zaidi ya mke mmoja, jambo ambalo linaonyesha wazi wafuasi wa dini hiyo kamwe hawawezi kuwa na idadi zaidi ya Waislamu. Hii ni maudhui ambayo tutakuja kuijadili pale itakapobidi. Nilichotaka kukisema ni kwamba: alichokifanya PRINCE ni kuonyesha ukereketwa, dharau na kejeli alionayo dhidi ya Masheikh ambao ni viongozi wa Dini ya Kiislamu ambayo ni moja ya dini yenye wafuasi wengi hapa Tanzania na hapa ndipo pale linapokuja suali langu, je nini kilichomsukuma PRINCE mpaka kuonyesha kejeli na dharau kwa Viongozi wa Kiislamu? Akina Terry Jones na pia wanajeshi wa Kimarekani na wengineo wanajivunia nguvu za nchi zao. Je, akina PRINCE wanajivunia nini katika nchi hii ambayo ni yetu sote? Au nyuma yao kuna SUPER POWER wanayoitegemea? Katika makala yake PRINCE pamoja na kunukuu baadhi ya vipengele katika Bibilia, lakini kamwe hakuthubutu kuwataja Viongozi wa dini ya Kikiristo na mavazi yao kupigia mfano wa maoni yake (ingawa mimi pia nisingefurahia kufanya hivyo). Hakufanya hivyo kwa sababu anatambua heshima ya viongozi hao. Sasa je, ni lipi linalomsukuma PRINCE kuwavaa bila kujali Masheikh na kanzu zao? Bila shaka yeyote ni ule ukereketwa wake pamoja na ubabe uliompa nguvu ya kutokujali hashima ya viongozi hao lakini pia kutokujali ule UMMA mkubwa uliopo nyuma ya viongozi hao, na hili kiukweli ni hatari kwa mshikamano wa jamii tunayoishi nayo ya Tanzania yenye mchanganyiko wa Imani na Itikadi tofauti. Inawezekana kulingana na Imani na Itikadi ya mtu ikawa haioni heshima ya Imani na itikadi ya mtu mwengine kutokana na kwamba Imani na Itikadi hiyo si sahihi kwa mtazamo wake, lakini inapokia hatua ya kuonyesha wazi dharau kimaandishi au kimatamko ya hadharani hili linaonyesha upeo wa uwezo mkubwa alionao alieyaonyesha hayo, na hapa ndio inabidi kutahadharisha kwani yule anaekabiliana na dharau na kejeli juu ya imani na Itikadi yake, basi ni wazi ya kwamba atatafuta njia ya kukabiliana na nguvu ya yule anaemdharau na ikifkia hatua hio hakuna tena mshikamano wa kijamii. Heshima ya mtu hasa inapofungamana na Itikadi, ni vitu vinavyopewa umuhimu mkubwa na kila mwanaadamu. Hivyo inapaswa kuwa makini ili tusije tukaisababishia jamii yetu janga ambalo thamani yake ni kubwa mnoo.. watu wasiojali kama akina PRINCE ni hatari kwa mshikmano wetu Watanzania, tunapaswa bila kujali mitazamo yetu tofauti tusiwape nafasi ya kuonyesha Ubabe na Kutojali kwao. Namalizia makala yangu kwa kumtaka PRINCE kuuomba radhi Umma wa Kiislamu kutokana na dharau alioionyesha kwa Viongozi wao, pia kulitaka Gazeti la Rai kuwaomba radhi Masheikh kwa kukubali kwake kuchapisha makala inayoonyesha dharau kwa viongozi hao. (Sheikh, Dr. Ibrahim Ghulaam, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania. Simu: 0658 88 22 12 / email : ibralhamd2000@yahoo. com)

Sheikh Alhad Mussa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam (BAKWATA), (Qur`an). Bila shaka hili linafanywa na jeshi la nchi kama Marekani kwa sababu nchi hio imekuwa ikijiona ndio hakimu wa ulimwengu kwa kuzingatia ya kuwa hakuna anaeweza kuhoji kwa lolote ambalo nchi hiyo imeamua kulifanya na atakayejaribu kufanya hivyo basi atakiona cha mtema kuni. Hivyo Marekani na mfano wake pamoja na majeshi yao tunakijua nini wanachokitegemea na bila shaka hata akina Terry Jones (Kasisi wa Kimarekeni alieamua kuichoma moto Qur`an) pamoja na ukereketwa wake wa Kikanisa lililompa nguvu za kufanya hivyo ni kilekile cha kujizingatia kwamba yeye ni mwananchi wa super power ya Ulimwengu wa leo. Nadhani Terry Jones asingesubutu kufanya hayo iwapo hana kitu anachokitegemea ya kwamba kitamlinda! Lakini matendo kama hayo ya kuyachezea Matukufu ya Kiislamu hayakuishia katika nchi kama Marekani na mfano wake tu! Bali yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mengine Ulimwenguni, mfano mkubwa ni hapa petu Tanzania (kisiwa cha amani). Imekuwa sasa ni jambo la kawaida kusikia Qur`ani imechomwa moto au Qur`ani imechanwa au Qur`ani imekojolewa au kupakwa kinyesi chengine au Qur`ani imepakwa damu ya nguruwe, au Msikiti umechomwa moto au Msikiti umeingizwa nguruwe au Muislamu kakamatwa au kadhalilishwa au Sheikh fulani ka. au au au . ukirejelea yote hayo hakuna unacho kipata, ila ni chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Katika gazeti la Dira ya Mtanzania la siku ya Jumatatu Mei 7 13, 2012 ukurasa wa sita wenye anuani ya HABARI ingawa kilichoandikwa ni makala (samahani sikusudii kuingilia utaratibu na usanifu wa gazeti) ya JICHO PA N A y a m w a n d i s h i aliejitambulisha kwa jina la PRINCE NEWTON yenye anuani ya maandishi yaliokoza Mawaziri: Kanzu

Wazanzibari wanajitambua sio wabaguziNa Nova Kambota MIAKA minne imepita tangu mwandishi maarufu wa makala nchini Bwana Hussein Siyovela alipoandika makala akihoji Wazanzibari wanategemea nini nje ya Muungano? Akiwahoji Wazanzibar kama wanafahamu athari za kuwa nje ya Muungano ama la? Naye mwandishi mwingine Bwana Prudence Karugendo ameandika akimjibu Siyovela katika makala iliyokuwa na kichwa cha habari Wazanzibari wanategemea Muungano Imara. Hawa ni waandishi wawili walioonyesha mitazamo tofauti, huku Siyovela akionyesha dalili za kuwatisha Wazanzibari mwenzake Karugendo ameonyesha jinsi Wazanzibari wanavyoelewa kile wanachokipigania. Labda ambacho Karugendo amesita kukiweka wazi ni jinsi Watanganyika walivyo kimya kwenye hoja ya muungano kiasi cha kutoa picha ama hawajui waseme nini? Au hawaujui muungano wenyewe? Nitajadili hili leo. Tu k i a c h a n a n a h a y a mazingaombwe ya watawala ya kutaka tuandike katiba mpya pasipo kuujadili muungano na porojo nyinginezo, acha niwapongeze Wazanzibari kwa msimamo wao kuhusu muungano. Nayasema haya kutokana na uzalendo mkubwa wa watu wa visiwa hivi wa kusema ukweli kutoka moyoni kwao kuwa tujadili muungano kwanza halafu mengine baadae. Hali ni tofauti kwa Watanganyika ambao wako kimya utadhani muungano hauwahusu. Hii ni ajabu sana! Nitaendelea kushangaa kutokana na ukimya wa Watanganyika huku wenzao Wazanzibari wanatamba kila jukwaa wakiichambua kwa uzuri kabisa kile kinachoitwa historia ya Zanzibar Empire, naendelea kushangazwa na ukimya huu wa Watanganyika ilihali wenzao Wazanzibar wameanza hata kupendekeza aina ya muungano wanaoutaka, huku baadhi wakitaka muungano wa kimkataba na wengine wakitaka serikali tatu. Najiuliza nani kawaziba midomo Watanganyika? Hivi huu ni ukimya au kuna la zaidi hapa? Iwapo mkimbizi mwenyewe hasiti kujitambulisha, iweje leo watu walioadhimisha miaka hamsini ya uhuru hawataki kujadili historia yao! Hivi leo ni Mtanganyika gani mwenye ujasiri wa kutueleza historia ya Tanganyika? Nasema historia huru ya Tanganyika kwa maana ninachokiona sasa ni historia ya Wazungu ndani ya Tanganyika kubatizwa na kuitwa historia ya Tanganyika, huu mzaha! Sijui utadumu mpaka lini? Labda niseme hivi, ingekuwa ni tofauti baina ya wanandoa tungewaachia wenyewe, lakini hili linahusu maslahi mapana ya taifa na watu wake, na kwa vile ni mmoja wa wananchi wa taifa hili lazima nipaze sauti katika hili. Haiwezekani tukajifanya kukataa ukweli kuwa kwa jinsi hali ilivyo sasa ni kama vile Zanzibar wana historia yao, wanajivunia, wanaiongea waziwazi, na wanajua wanachokitaka tofauti na Watanganyika ambao ukimya wao unazidi kuwaduwaza walimwengu. Kwa tuliobahatika kuka Zanzibar tunafahamu jinsi Wazanzibar wanavyodumisha utamaduni wao, nathubutu

11

Makala/Habari

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

JESHI la Polisi Zanzibar katika pilikapilika za kudhibiti ghasia, kusema isingelikuwa wahamiaji wahuni visiwani humo leo hii msamiati wizi na uchangudoa ungefutwa kwenye kamusi yao. Sasa nani hafahamu Shiva Arusha au Buguruni na Manzese nini kinatokea? Nani hajui kuwa Wazanzibar wapo tayari kujipambanua kokote kwa misingi ya tunu zao hizi au tuseme Watanganyika wamepigwa na mawimbi ya ubepari kiasi cha kupoteza tamaduni zao? Kuna nini hapa? Halafu anaibuka mtu asiyetaka kuona ukweli huu na kuwapakazia dhambi ya ubaguzi Wazanzibar. Huu ni upuuzi! Hivi nani kakataza Watanganyika kueleza historia yao? Au lini mtu kujitambulisha ikawa ubaguzi? Eti nimesikia kilio cha samaki kuwa ubaguzi ni dhambi kama baba wa taifa alivyowahi kuasa ni kweli ubaguzi dhambi! Lakini nani mbaguzi? Umefika wakati Wa t a n g a n y i k a w a a c h e kukimbia kivuli chao. Waache kumungunya maneno badala yake wajivunie historia yao kuliko kutaka kuwatisha wazalendo wa Zanzibar. Kwa nukta hii sasa, wakati nawapongeza Wazanzibar kwa uzalendo wao na historia yao tamu isiyochosha masikio, nawataka Watanganyika waache vitisho vya kusadikika kuhusu ubaguzi badala yake waiambie dunia pasipo uwoga kuwa na wao wana historia yao tena tamu kama asali. Kinyume cha hili, nitaendelea kuamini kuwa Wazanzibari wanajielewa wakati Watanganyika wanajikana wenyewe. Wanajikana au hawajitaki. (Mwandishi anapatikana kwa barua pepe [email protected], au www.novakambota. com)

Waislamu Iringa kuanza na walimuInatoka Uk. 16 katika kila Shule ya Serikali wanafika walimu kufundisha kipindi cha Elimu ya Dini ya Kiislamu. Wa m e s e m a , t a y a r i wamechanga zaidi ya shilingi milioni tatu kupitia Misikiti yao kwa ajili ya kuimarisha somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu mashuleni. Wakianisha michango hiyo kwa kutaja Misikiti na kiasi cha fedha katika mabano walisema, Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Miyomboni umeongoza kwa kuchanga zaidi ya shilingi laki saba (700,000/-), Msikiti wa Taqwa 333,000/-, Tawhiid 330,450, Dhinurayn 220,000/, Hidaya 214,650/-, Nnur 210,000/, Ilala 205,500/-, Kheir 120,000/-, Furqan 90,000/-, Ndiuka 60,000/-, Abubakar 30,000/- na Twayba shilingi 20,000/-. Wakati huo huo, mikoa ya Kanda ya Ziwa imepanga kufanya makongamano

mfululizo ili kuwaelimisha Waislamu juu ya kadhia hii. Kongamano la kwanza litaanzia Musoma Jumapili kuanzia saa 2 asubuhi mpaka dhuhri. Mada kuu ni jinsi Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) linavyo wahujumu Waislamu.

Kadhi Mkuu ahimiza umojaInatoka Uk. 16 yote, kuanzia ngazi ya elimu ya awali, Msingi na elimu ya kati. Mchakato wa ramani na michoro umekamilika. Alisema Ust. Juma. Wakati huo huo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Waislamu nchini kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutunga Katiba mpya, ili kusaidia kupata Katiba itakayolinda maslahi yao. Maalim Seif, ameyasema hayo akiongea na umma wa Kiislamu katika haa hiyo ya Maulid akiwa mgeni rasmi. Alisema, ni vyema kwa Waislamu kutumia fulsa hii kwa kutoa maoni yao kwa tume iliyoundwa na Rais (Jakaya Kikwete) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuratibu maoni ya kuundwa Katiba mpya. Waislamu kama sehemu ya Watanzania tumieni mchakato unaokuja wa mapendekezo ya Katiba kutoa maoni yenu, m k i w a k a m a Wa i s l a m u mmekuwa mkiamini katika Katiba iliyopo kuna mambo mengi yanawakandamiza. Tumieni fursa hiyo kupendekeza mambo muhimu yanayopaswa kuingizwa katika Katiba mpya, na yaliyo mabaya

lamu. Katibu huyo alisema, Munira Madrasa inaamini kwamba uwepo wa usadi, ubadhirifu, rushwa mmomonyoko wa maadili na maovu mengine, ni matokeo ya kutokuwa na elimu sahihi ya na malezi ya kiroho. Alisema, katika jumla ya malengo ya muda mrefu ya taasisi yao ni kuwa na shule ya kisasa, ambapo hadi sasa Taasisi inamiliki ardhi kwa ajili ya shughuli hiyo. Lengo la matumizi ya ardhi hiyo ni kujenga shule yenye kufundisha masomo

yatolewe ili kuweka usawa kwa makundi ya watu wote kwa ujumla. Alisema Makamu huyo wa rais. Akizungumzia Madrasa za Waislamu zinazotoa mafunzo kwa vijana wa Kiislamu kwa ujumla, Maalim Seif, aliwataka Waislamu kuziboresha ili ziwe za kisasa na kwenda na wakati. Akifafanua alisema kuwa, imefika wakati sasa Madrasa hizo ziwe vituo kwa vijana wa Kiislamu kwa kutoa mafunzo yote kwa ujumla ili kuweza kuwajengea watoto msingi bora wa masomo yote kama ilivyo kwa somo la Qur an.

12TUSEME SASA YATOSHAII] Kumi na tano kurasa, Annuri nalifungua, Kwa mikono napapasa, Nipate kujisomea, Ghafula ninaigusa, Habari iso vutia, Naomba uke muda,Tuseme sasa yatosha. [2] Kakamata wanafunzi, Hijabu akawavua, Mwalimu alo mshenzi, Ubao akafutia, Kitamfaa kitanzi, Na juu kuninginia, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [3] Hijabu vazi nadhifu, Yeye analichafua, Analitia uchafu, Kwa chaki anafutia, Hivi hakuwa na hofu, Au shari kaamua, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [4] Wasinge vaa hijabu, Angevua kitu gani? Angeliwapa adhabu, Siketi washushe chini, Kisha awatie tabu, Wamkufuru manani, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [S] Mshenzi huyu mwalimu, Ni mchafu wa tabia, Kapata wapi elimu, Chuo kipi kasomea, Ni kweli alihitimu, Mie naomba kujua, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [6] Adabu hana hekima, Hakujaliwa busara, Ndani ya wake mtaa, Akiliye taahira, Mwisilamu akihema, Yeye anakunja sura, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [7] Aliyopata adhabu, Mnadhani inatosha? Kwangu siioni tabu, Uhai akifupisha, IIi washike adabu, Na fundisho la maisha, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. [8] Ninamshukuru Mola, Yeye kwangu ni jalali, Ajuae yangu kula, Bora isiwe batili, Wachekao na fadhila, Si hofu mie sijali, Naomba uke muda, Tuseme sasa yatosha. Mwalimu Swalehe A Ndimbe Mkuu Shule ya Sekondari-Rombo, Kilimanjaro.

Mashairi/Barua

RAJAB 1433, IJUMAA MEI JUNI 1-7, 2012

AN-NUUR

Tuwe macho na elimu potofuNdugu Mhariri, Katika elimu kuna mada katika masomo ambazo haonekani kukubalika katika akili iliyo salama, kwa kuwa mada hizo zimetokana na kra ambazo si sahihi. Waislamu tumehimizwa kusoma kwani elimu ni takrima na ni amri ya kwanza kutoka kwa Allah (sw). Hatutakiwi kubagua elimu kwa kuwa elimu zote zinatoka kwa Allah (sw). Uislamu umeigawanya elimu katika sehemu mbili, elimu ya muongozo na elimu ya mazingira. Elimu ya mazingira mara nyingi inapokosa kuhusishwa na elimu ya muongozo huwa na upotoshaji. Somo la historia, ni miongoni nadharia hii uko wapi. Kutokana na udhaifu wa fikra za mwanadamu katika baadhi ya mambo, hushindwa kujua ukweli wa mambo kama alivyoshindwa mnadharia huyu wa evolution of man. Kuna sababu nyingi za kuonyesha udhaifu wa nadharia hii, lakini sababu kubwa zaidi ni maneno ya Allah (sw), muumba wa mwanadamu (aliyejua asili yake) na mazingira yote yaliyomzunguka. Allah(sw) anasema kupitia Quran: Na katika ishara zake (Allah) za kuonyesha kuwepo kwake) ni huku kukuumbeni kwa udongo kisha mnakuwa watu mnaoenea (kila mahali) (30:20). Katika somo la Kiswahili hili nasibu, lililotumika katika lugha ni wazi kuwa fasiri hiyo ya lugha humaanisha kuwa lugha imetokea katika jamii pasi na wao ama kuwepo aliyeleta lugha. Tafsiri hii ina udhaifu kulingana na sababu kadhaa lakini hoja kubwa yapatikana (yatoka) kwa Allah (sw), ambaye ndiye mwanzilishi wa yote. Kupitia Quran anasema: Na katika kuonyesha kuwepo kwake na uwezo wake ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitilafiana lugha zenu na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi (30:22). Katika Kiingereza lugha nayo hufasiriwa kwa kufanana na fasiri ya Kiswahili. A language is specic system of arbitrary, conversational and vocal or written symbols.. Lugha ni mfumo wa sauti nasibu (arbitrary) au alama zilizoandikwa. Kutokana na fasiri hizi zote mbili, kwa mujibu wa aya hiyo ya 30:22 ni wazi kuwa waliotoa fasiri hizi sio wajuzi, japokuwa leo ndio wanaoonekana kuwa ni wajuzi bobezi na kutunukiwa vyeti vya kuonyesha ujuzi wao. Si wajuzi (hawana elimu)kwa kutojua lugha inatokea wapi. Hapa tumeshachambua mada chache tu, lakini zipo nyingi, hivyo ujuzi wa kuioanisha na elimu ya muongozo wahitajika. Nasisitiza tena, si kwamba nahitaji msisome ama kutojibu maswali ya mada hizo zenye upotovu, la, someni, lakini tusizibebe mada hizo kwa mwendo wa kondoo, kwa kuzitolea hoja ili kuzikingia kifua, utapotea. Abdulkarim Mbunju S.L.P 6596, Dar es Salaam.

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie: Mhariri AN-NUUR, S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe E-mail: [email protected] masomo yenye mada zenye upotoshaji kwa kuwa zimetumika fikra ambazo si sahihi. Kwa kuanza na somo la historia, somo hili lina mada ya evolution of man. Mada na Kiingereza, nayo pia katika mada ya lugha si sahihi kulingana na mafundisho ya elimu sahihi ya dini (mfumo wa maisha wa (Kiislamu. Katika somo la Kiswahili, neon lugha hufasiriwa kuwa ni mfumo wa sauti nasibu ambazo hutumiwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano kati yao. (TUKI). Katika Tafsiri hii ndani yake kuna neno nasibu, neno hili linafanana na neon bahati, maneno haya kutokana na kuwiana katika maana yaweza kufasirika kama , kutokea au kufanyika kwa kitu au jambo pasi na kutarajia. Kutokana na maana ya neno

Sumu[l] Kwenye kiti nimekaa, Ndimbe najikilia, Akili imezubaa, Jibu halijaingia, Sasa naona fadhaa, Swali ninawaletea, Nani alionja sumu, Akajua ni tayari? [2] Ni nani aliingiza, Kinywani akagundua, Kuwa sasa inaweza, Yeyote ikamuua, Ikamuua kilaza, Ikamtoa dunia, Nani alionja sumu, Akajua ni tayari? [3] Na huyo alieonja, Hongera tele apewe, Atafutiwe kiwanja, Na nyumba tumjengee, Na kisha tumpe wanja, Mke tumtafutie, Nani alionja sumu, Akajua ni tayari? Mwalimu Swalehe. A. Ndimbe

na kubadilika hata akawa mtu kama walivyo watu hivi sasa. (hono sapiens). Sihitaji kuinyambua zaidi mada hii, bali kutaka kuonyesha tu udhaifu wa

hii hudai kwamba asili ya mwanadamu ni nyani, nyani ambaye alibadilika kidogo kidogo kwa kupitia hatua mbalimbali. Katika kupambana na mazingira yak e, nyani huyo amekuwa

Mwembechai sasa yanukia ZanzibarInatoka Uk. 7 Ili kudhibiti hali hiyo, Malima aliweka utaratuibu mpya ambapo namba hazikupewa majina mpaka limalizike zoezi la kuchagua majina ya kwenda sekondari. Mwaka huo idadi ya Waislamu waliochaguliwa kuingia sekondari iliongezeka kwa aslimia 40. Kilichofuatia nini? Malima alipigwa vita akatangaziwa udini, akadaiwa kujenga msikiti Wizarani, zogo likawa kubwa mpaka akangolewa. Utaratibu wa zamani ukarejeshwa. Toka wakati huo, miaka zaidi ya 20 Waislamu wanabamizwa. Haya ninayoandika hapa Kighoma Ali Malima aliyasema serikalini na kuyasema hadharani k u w a a m b i a Wa i s l a m u , Masheikh na Watanzania. Waislamu wamefanya nini mpaka sasa? Wana tofauti gani na yule aliyeambiwa inama usubiri nikalete upanga na kweli akasubiri? Si Malima tu, alisema Bori Lilla na ikaandikwa katika vyombo vya habari jinsi ambavyo majopo y a Wa k r i s t o w a t u p u yanavyohujumu watoto wa Kiislamu waliofaulu vizuri. Waislamu wamefanya nini? Hivi sasa Wakuu wa Shule za Kiislamu wameandika Wizara ya Elimu kulalamika kwamba hawana imani na Baraza la Mitihani. Ushahidi na vielelezo wanavyo. Kama alivyoinama yule Muislamu akisubiri kafiri akachukue upanga nyumbani aje kumkata kichwa, yawezekana Waislamu wa Tanzania nao wakainama wakisubiri Joyce Ndalichako awakate tena vichwa watoto wa Kiislamu Novemba mwaka huu na hata kuendelea mpaka atakapochoka na timu yake na kuwakabidhi timu ya mawakala wengine wa mfumokristo.

13Na Bakari MwakangwaleAPRIL 29, Mwaka huu, mfanyabiasha maarufu jijini Dar es Salaam, Bw. Mustafa Sabodo, alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), uliofanyika Jijini Dar es Salaam. Katika jumla ya mambo mbalimbali aliyoongea katika mkutano huo kuhusua chama hicho, ni suala la kukanusha kuwa Chadema, si chama cha kidini. Bw. Sabodo, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akijaribu kuondoa shutuma au dhana hiyo iliyo wazi kuwa hizo ni propaganda zinazoenezwa kuwa Chadema kina udini, akidai hazina ukweli wowote na kuwa zinafanywa na maadui wa chama hicho kwa lengo la kuwakatisha tamaa. Mimi naitwa Mustafa Sabodo nakisaidia chama, viongozi na wanachama wana dini tofauti sasa udini hapo uko wapi? Alisema na kuhoji Sabodo. Chama hicho mbali ya viongozi wake kujaribu kukanusha suala hilo, lakini pia wamekuwa wakijitahidi kuwasimamisha watu ambao kwa namna moja ama nyingine wana nasibishwa na Uislamu, na kusimama mbele ya hadhira wakijaribu kupangua hoja hiyo. Safari hii agenda hiyo ameibeba mdau wa Chadema, akijibabatua kwa kuyasema hayo aliyoyasema. Katika utetezi wake raki huyo Chadema anajaribu kuutoa hofu umma, ambao nadhani ukiwalenga zaidi Waislamu, kuwa eti yeye ni Muislamu anaitwa Mustafa Sabodo na anakisaidia chama! Na kwamba ndani ya chama hicho kuna viongozi na wanachama wa dini tofauti (wakiwemo Waislamu). Sidhani kwamba hoja hizo zinajitosheleza kuondoa dhana ya udini (Ukristo) inayoonekana na kufanywa waziwazi na wafuasi wa Chama hicho pamoja na viongozi wakuu kwa kujihusisha na mambo kadha wa kadha ambayo nitayaanisha chini. Bw. Sabodo na Waislamu waliopo ndani ya Chadema, ni haki yao na wapo huko pengine kwa maslahi yao wanayo yajua wenyewe au pengine wamekuwa kama yule anayetangatanga katika usiku wa giza totoro akitafuta njia na asiyejua anakokwenda. Au wale mashabiki wa kudandia bogi wasilojua litokako wala liendako. Mwenyezi Mungu amesema katika Qur an.Na mfano wa wale (wanaowalingania) waliokufuru (kwa inadi tu, si ujinga) ni kama mfano wa yule anayemuita asiyesikia ila sauti na kelele tu. (Wao) ni viziwi, mabubwi, vipofu kwa hivyo hawafahamu. (2:171).

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA JUNI 1 - 7, 2012hii, ufadhili ni wa CDU hata kama utasema hawatafundishwa masuala ya dini (Udini), hiyo itakuwa ni ngumu kukubalika itikadi ni itikadi tu, kamwe mafunzo hayo hayawezi kutoka nje ya malengo ambayo kwa chama hicho ni kujenga maadili ya Kikristo (Ukatoliki) katika siasa, jamii, na maisha kwa ujumla. Katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Saiasa ya Tanzania Bara 1953-1985, Padri John Sivalon, anabainisha jinsi mafundisho ya Maaskofu yalivyokuwa yakiunga mkono masuala yenye manufaa na Kanisa, hususani suala la Azimio la Arusha na hii ilikuwa mara baada ya kutoka Vatikano, katika mafundisho yao. Msimamo wa Maaskofu katika barua hii uliongozwa na mafundisho ya Vatikano II. Maaskofu walikuwa ndio kwanza wamerudi kutoka Vatikano ambako walienda kuhudhuria Mtaguso wa pili wa Vatikano. Uk.37. Zaidi imeelezwa kuwa humu nchini, Chadema itafanya kazi kwa karibu na taasisi ya Conrad Adenaure Foundation ambayo ni taasisi ya Kikristo iliyo mshirika wa chama cha CDU, chini ya Bw. Konrad H. Adenauere ambaye ni Mkatoliki, lengo lake ni kuona maadili ya Ukristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Nadhani Jamii ya Waislamu nchini, hususan Jijini Dar es Salaam, watakumbuka vizuri lile sakata la kuukataa mtaala wa Madrasa ulioandaliwa kwa ufadhili wa Conrad Adenaure Foundation, baada ya kuelewa malengo na asili ya taasisi hiyo ya Kikatoliki, kuwa lengo lake ni kuona maadili ya Ukristo yakitawala. Leo hawa ndio watafanya kazi kwa karibu na Chadema, unategemea nini! Lakini pia wale wanachama wa JUWAKUTA, watakumbuka ni kwa jinsi gani walibaini na kuitambua Conrad, baada ya kukubali ufadhili wao chini ya Sheikh Alhad Mussa, katika mkutano wao Mkuu uliofanyika pale Mjini Morogoro, kwani Masheikh na Maustadhi walishuhudia Ukristo, ulivyotaka kupenyezwa katika mkutano wao huo na kupelekea mkutano kusambaratika, baada ya wajumbe kukataa kupelekeshwa na Conrad ya Kikristo. Ama katika uchaguzi mkuu uliopita (2010), hali ilikuwa dhahiri kabisa, kwa Maaskofu kusimama kidete na kuonyesha mwelekeo wao kwa kumtetea na kumsasha dhidi ya tuhuma alizokuwa akielekezewa Padri Slaa, aliyesimama kama mgombea Urais wa Chama hicho. Jamii ilishuhudia juhudi za Maaskofu wa Makanisa mbalimbali walipo muunga mkono Padri Wilbrod Slaa na kumsasha kwa jamii kuhusu shutuma za uchafu wa kutembea

AN-NUUR

Ukristo ndani ya ChademaSabodo ajibabatua kukisasha Kauli ya Mbunge yamuumbuambalimbali sambamba na Chama hicho, likichukua nafasi yake ya maombi Kwa jina la Yesu hatua kwa hatua, kwa muda wote wa kampeni hizo. Wachungaji kutoka Makanisa mbali mbali walimuwekea mikono Joshua Nasari (Mtoto wa Mchungaji) kila tulipokuwa tunaanza mikutano yetu ya kampeni. Nawaambieni kama sio jina la Yesu tusingeshinda Arumeru. Anadhirisha Mchungaji, Mbunge Natse. Kama si cha kidini vikosi vya wanamaombi katika kampeni zao vinaashiria nini, kama anavyosema Mchungji Natse, kuwa walikuwa na kikosi kamili cha wanamaombi ambacho kilikuwa nyuma ya jukwaa wakati wote, ambao wanasiasa walikuwa majukwaani wakiendesha mikutano ya kampeni. Je, kulikuwa pia na kikosi cha Wasilat Shai? Au maombi ya Kiislamu hayahitajiki katika Chadema? Ama kwa upande wa viongozi wake wakuu wa kitaifa, Chadema pia ilibainisha wazi uraki wake wa karibu na chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU), kwa uraki huo Chadema iliahidiwa kupewa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani kwa vijana na viongozi wake kusomea maadili na uongozi. Hali hiyo ilibainika Juni mwaka jana 2011, kwa Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, baada ya kufanya mazungumzo ya siri (faragha) kati yao (Mbowe, Padri Salaa na viongozi wengine wa juu) na ujumbe wa CDU, ulioongozwa na rais wa zamani wa Ujerumani, Profesa Dk. Horts Kohler. Ndani ya mtazamo wa CDU, maadili yatolewayo ni yale ya Kikristo, kama yalivyobuniwa na muasisi wake Bw. Konrad Hermann Joseph Adenauer. Hapa inapasa utambue kwamba CDU ni chama cha Kikristo (Katoliki) haswa, kilicho anzishwa mwaka 1946, ambacho kiliwaunganisha Wakatoliki kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, jamii, na maisha kwa ujumla. Leo anasimama kiongozi anasema kupitia CDU, wanachama wake watapelekwa kupatiwa mafunzo! Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mbowe, dhamira ya mafunzo hayo kwa vijana wa Chadema, ni kuwafanya wawe viongozi wenyewe maadili mazuri kwa taifa lao! Maadili gani? Yale ya CDU, ya Kikatoliki. Unaweza ukatafakari picha

FREEMAN Mbowe, Mwenyektii wa CHADEMA.Ama ukigeukia kauli za viongozi hao wa juu wa Chadema, hukanusha vikali suala hilo na kujibu kwa kifupi sana kuwa chama chao si cha kidini, sababu eti ndani ya Chama hicho kuna wanachama na viongozi Waislamu! Chama chetu ni cha siasa na si cha kidini. Alijibu Mwenyeki wa Chama hicho. Mh. Freeman Mbowe, alipoulizwa na mwandishi wa gazeti moja hivi karibuni kwa njia ya simu kisha alikata simu. Hakika Mwenyezi Mungu anasema, wanayoyadhihirisha midomoni mwao, ni machache kuliko yalimo vifuani mwao. Hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anayajua wanayoyaficha na nwanayoyadhihirisha? (Qur an 2:77). Kauli na mwenendo sambamba na matukio ndani na nje ya chama hicho inakuwa ni vigumu kujipapatua na dhana au madai ya udini ndani ya Chama hicho, ukizingatia kauli hizo zinatolewa pia na baadhi ya wabunge wake, mfano rejea kauli za Mchungaji na Mbunge wa Karatu Mh. Israel Yohana Natse, mara baada ya uchaguzi wa Ubunge katika jimbo la Arumeru, hivi karibuni. Watu wengi wanashangilia, wamejaa furaha baada ya matokeo chanya, lakini hawajui siri kubwa iliyotuwezesha kushinda.. Siri gani hiyo, bila hofu anafafanua Mchungaji huyo kwamba waliamua kuunda kikosi cha maombi ya kutangaza vita katika Ulimwengu wa Kiroho na kuongeza kwamba Tulizindua kampeni kwa maombi na tukaendelea hivyo. Swali ni je, maombi haya yalikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu au kwa Jina la Mungu Mmoja asiye na mshirika? Je, waliambiwa Wakristo waombe kwa Mungu wao Mkuu aliye wakati huo huo mwana aliyetahiriwa baada ya siku saba za kuzaliwa na Waislamu nao wakaambiwa kuomba kwa jina la Allah, Almaliku lwaahidul Qahhaar au walikusanyana tu mchungaji na watu wake? Lakini wimbi la wachungaji lilionekana katika mikutano

Inaendelea Uk. 15

Wanaochoma Makanisa ni magaidiWasakwe, hatua kali zichukuliwemchezo tu. Na yameanza, hakuna mtu mwenye haki ya kudai haki yake na kuhujumu mali za watu wengine na kuchoma makanisa ya watu wengine. Wanaofanya vitendo hivi ni wahuni wakuu na serikali ya Zanzibar ichukue hatua kali. Uhuni wa namna hii ulitokea pale Tandahimba mwezi uliopita ambapo polisi walihusika live katika oparesheni ya kikatili ya kuchoma waziwazi maduka zaidi ya 55 ya wafanyabiashara na gari moja na pikipiki moja. Kabla hawajaanza oparesheni ushenzi hiyo, polisi walitengeneza tukio kwa kuichoma ofisi ya OCD ili wapate nafasi ya kulipiza kisasi kwa wananchi wasio na hatia (kisasi cha kutengeneza) Ujinga ulioje, aibu iliyoje? Pana makundi yanadai Zanzibari huru, yaachiwe uhuru wao, yasikilizwe. Wa j a n j a w a s i j i t o k e z e wakatumia upenyo huo ili kuyavunja makundi hayo kwa kuyabambikizia uchomaji makanisa ili kuyahusisha na hila za dini moja kuhujumu dini nyingine, tuache michezo hii ya kipuuzi. Siamini kama UAMSHO na wanaharakati wale ndio wanachoma makanisa. Naamini kuna janja nyuma ya suala hili. Labda pana wajanja wanataka kuua move ya (harakati za) mjadala wa kudai Zanzibari huru. M a j u z i Wa z a n z i b a r i waliamua kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wakapiga kura wakaamua sawia na serikali yao ikawa. Hawakutushirikisha kwa sababu peke yao wanaweza kusimamia na kuendesha mambo yao na tumeona wanaweza. Mie nasema Wazanzibari wakidai Zanzibar huru yao, tusiwapige na kuwakamata na kuwanyanyasa. Tukae nao mezani tusikilize hoja zao. Na kama wengi wao wakitaka Zanzibar huru yao, tuwape. Baba yangu mzee aliyeko kijijini hatapungukiwa na lolote iwapo Zanzibar itaendeleza muungano na Tanzania (Tanganyika) au itajitoa. Zanzibar ikijitoa katika muungano haitaongeza wala kupunguza kilo ya sukari au kilo ya mchele. Watanzania wana matatizo makubwa yanayotishia uhai wao kila kukicha kuliko muungano huku Tanganyika. Muungano ni jambo la kisiasa tu na kama mkuu wa kaya anasema usijadiliwe, lazima utavunjika tu. Hana namna ya kuuokoa maana kushindana na umma wa upande mmoja ni kazi bure. Mie nawashauri sana pia wana vikundi vya Uamsho na watu wote wanaodai Zanzibari yao kuwa watumie busara na njia za kawaida sana kudai haki yao wanayoiamini. Kwa sababu Tume ya Jaji Warioba inakwenda kukusanya maoni ya katiba waisubiri. Ikifika waioneshe na waieleze kuwa hawautaki muungano. Majority of Zanzibaris wakiwa na msimamo huo, maana yake ni kuwa katiba ya Tanzania itafeli kwa sababu lazima ipitishwe na pande zote za muungano kwa uwiano sawa. Hii ni njia nyepesi sana kuliko njia zingine. Wanaweza kuendelea kutoa elimu juu ya kuupinga muungano kwa njia ya makongamano na mikutano tu. Hii itawasaidia kutengeneza mtizamo mzuri na kuondoa uwezekano wa watu wowote wenye nia mbaya kutumia shughuli zao na kujenga taswira mbaya zinazoweza kuweka amani, usalama na mshikamano wa wananchi hatarini. Mwisho ni kwa serikali zote mbili, hii ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ile ya Rais Shein na Maalim Seif. Movement hii ya Uamusho na makundi mengine ya kijamii, kiharakati na kidini upande wa Zanzibar ya kudai kuvunja muungano, siyo jambo la kubeza na kuchezea. Ukiwatizama wale Uamsho utaona umati wa watu wanaokusanya ni mkubwa kuliko mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Hii ina maana kuwa panahitajika busara na nia thabiti katika kumalizana na wananchi hawa. Serikali zote mbili zikae nao chini na kutatua suala hili. Ni bora kuuvunja muungano kwa heri (kwa utaratibu), kuliko kuuvunja kwa nguvu. Muungano ukivunjika kwa nguvu na ghafla patatokea mpasuko mkubwa sana. Pana ma-laki ya Wazanzibari wako Tanganyika, pana mahusiano makubwa yameshajengwa. Tunahitaji mechanism na akili nyingi kulishughulikia. Nguvu na mabavu havitasaidia kuzima mawazo thabiti amba yo wananchi wanayaamini, nguvu na majeshi vinaweza kuua mwili tu lakini haviui dhamira. Hata kama wananchi hawa watapigwa na kukamatwa na kuwekwa g erezani, moto huu hautazimika. Muungano utizamwe upya. Tusikilize matakwa ya wananchi wengi. Ikiwa wengi watasema uvunjwe, basi na tuuvunje kwa amani. (Julius Mtatiro +255 717/787/ 536759, Dar es salaam, 29 Mei 2012. Haya ni maoni yangu binafsi, kwa namna yoyote ile yasihusishwe na chama changu wala uongozi wangu ndani ya chama).

14

Makala

RAJAB 1433, IJUMAA MEI 25-31, 2012

AN-NUUR

MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) akiongea na Kaimu Katibu Mkuu (Bara) wa CUF Julius Itatiro (kulia). HABARI za uchomaji wa makanisa Zanzibar katika vurugu za hivi karibuni haziungwi mkono kwa namna yoyote ile. Yeyote anayefanya vitendo hivi ni gaidi kwa sababu anafanya vitendo vya kigaidi. Serikali ya Zanzibar ichukue hatua kali za kisheria kwa yeyote aliyehusika na vitendo hivi bila kujali yeye ni nani. Kuchoma makanisa ni jambo la hatari. Sielewi anayefanya hivi yeye ni dini gani. Sijui ni dini ipi inayoruhusu uchomaji wa nyumba za ibada za din