annuur 1167a.pdf

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1167 JAMADIUL AWWAL 1436, IJUMAA , MACHI 6-12, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu Mpenzi msomaji ANNUUR linapatikana kwa Shs 800/= tu AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST (1) KAMILISHA NGUZO ZA DINI YAKO! Ewe Muislamu, Hija ni nguzo ya Dini; mwenye kuisimamisha amesimamisha Dini. Thibitisha Uislamu wako kwa vitendo upate radhi za Mola wako! Bila kuhiji hujawa Muislamu kamili. Mali inaongezeka kwa kuhiji, haipungui! Muda unakwisha Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437. Zanzibar inabeba lawama kubwa Piganieni haki zenu Bungeni Sio barabarani na Mwembeyanga tu Pamoja na fitna ya Sitta... PICHA juu, Spika Anna Makinda alipotembelea Oman mwaka jana 2014. Picha chini Marehemu Salmin Awadh Salmin. Uk. 8 na 20. Hata hili tuseme Eemen! HATA hili? Tuseme Eemen! Ndivyo anavyouliza mwendesha kipindi katika televisheni. Anauliza swali hilo akichambua mahubiri ya Askofu David Olaniyi Oyedepo wa Kanisa la Living Faith Church World Wide,akidai kuwa yeye ni Mtume wa Mungu aliyepewa agizo la kupambana na ‘mashetani wa Kiislamu’. Soma Uk. 6 Askofu Olaniyi Oyedepo.

Upload: zanzibariyetu

Post on 24-Dec-2015

4.954 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1167a.pdf

ISSN 0856 - 3861 Na. 1167 JAMADIUL AWWAL 1436, IJUMAA , MACHI 6-12, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya WaislamuMpenzi msomaji ANNUUR linapatikana kwa Shs 800/= tu

AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST(1) KAMILISHA NGUZO ZA DINI YAKO!Ewe Muislamu, Hija ni nguzo ya Dini; mwenye kuisimamisha amesimamisha Dini. Thibitisha Uislamu wako kwa vitendo upate radhi za Mola wako! Bila kuhiji hujawa Muislamu kamili. Mali inaongezeka kwa kuhiji, haipungui! Muda unakwisha Gharama zote kwa Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0765462022;0782804480; 0717224437.

Zanzibar inabeba lawama kubwa

Piganieni haki zenu BungeniSio barabarani na Mwembeyanga tu Pamoja na

fitna ya Sitta...

PICHA juu, Spika Anna Makinda alipotembelea Oman mwaka jana 2014. Picha chini Marehemu Salmin Awadh Salmin. Uk. 8 na 20.

Hata hili tuseme Eemen! HATA hili? Tuseme Eemen!

Ndivyo anavyouliza mwendesha kipindi katika televisheni.

Anauliza swali hilo akichambua mahubiri ya Askofu David Olaniyi Oyedepo wa Kanisa la Living Faith Church World Wide ,ak ida i kuwa yeye ni Mtume wa Mungu aliyepewa agizo la kupambana na ‘mashetani wa Kiislamu’.

Soma Uk. 6 Askofu Olaniyi Oyedepo.

Page 2: ANNUUR 1167a.pdf

2 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Makala

KATIKA siku za hivi k a r i b u n i , v y o m b o mbalimbali vya habari nchini viliripoti kuhusu m k a s a w a v i j a n a waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT), ambao walitaka kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo jijini Dar es Salaam, kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete na kumweleza matatizo yao wanayowakabili ya ukosefu wa ajira baada ya kufuzu mafunzo yao.

Februali 15 mwaka huu, wahitimu hao walifanya m k u t a n o w a o k u l e Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wao, George Mgoba, alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba kukutana na Rais Kikwete, ili kupata f u r s a y a k u m p a s h a habari kuhusu matatizo wanayowakabili likiwemo la kukosa ajira baada ya kuhitimu mafunzo, lakini wakiishia kupewa ahadi za uongo na Katibu Mkuu wa Rais.

Kutokana na kukosa nafasi ya kuonana na Rais Kikwete kwa njia ya kiungwana, wakafikia kutumia njia nyingine ya shinikizo la kidemokrasia, ili kujaribu kushinikiza kuonana na mkuu huyo wa kaya.

Paral Kiwango ambaye alikuwa ndiye Makamu Mwenyekiti wa vijana hao, alisema suala la wao kupatiwa ajira linaonekana kuwa na upendeleo kwani w e n z a o w a u p a n d e w a Z a n z i b a r , w o t e waliomaliza mafunzo ya JKT wanapatiwa ajira lakini huku bara wameachwa tu.

Kimsingi tukio hili licha ya kwamba limetokea siku za nyuma kidogo, lakini kwa kiasi fulani limegusa hisia za Watanzania wengi. Pia limezua hofu kwamba, k a m a v i j a n a w e n y e mafunzo ya kijeshi, ambao wamehitimu mafunzo na wakawa na matarajio a u m a wa z o k wa m b a

Wahitimu mafunzo JKT wawe funzo kwa serikali

wakihitimu watapatiwa ajira na serikali, halafu w a k a i k o s a , n i w a z i kwamba raia wataingiwa na hofu iwapo vijana hawa watatumia mafunzo yao kinyume na makusudio yake. Na hatima yake haiwezi kuwa nzuri hasa ikizingatiwa kwamba idadi ya vijana wanaomaliza mafunzo hayo ya JKT ni wengi na huzalishwa kila mwaka.

Kwa mtazamo wetu, sisi hatukatai hoja zilizotolewa na vijana wetu hawa, wala hatutaki kuwa mawakala wa kuitetea serikali katika sakata hili l inalohusu mustakabali wa vijana wetu wengi tu, achilia mbali wahitimu wa mafunzo JKT, ambao wamekuwa majeruhi wa kukosa ajira hapa nchini.

Ni jambo linalofahamika kwamba ni wajibu wa s e r i k a l i k u h a k i k i s h a k w a m b a i n a b o r e s h a mazingira ya maisha ya watu wake, likiwemo suala la kuzalisha ajira kwa watu wake au kuboresha mazingira ya watu kujiajiri.

Tunakumbuka baadhi ya ahadi za Rais Jakaya Kikwete, wakati anawania nafasi ya kutuongoza tangu awamu ya yake ya kwanza ilikuwa ni kuongeza soko la ajira nchini. Hata hivyo, bado tunashuhudia soko dogo la ajira nchini, huku Rais wetu akibakiwa na muda mchache wa kuhitimisha kipindi chake cha uongozi wake.

Hutokea Jeshi la Polisi, au Idara ya Usalama wa Taifa au hata JWTZ na Magereza wakahi ta j i kuajiri watu, basi ni vyema wahusika katika majeshi h a y o wa k a wa c h u k u a k u t o k a k w a v i j a n a waliohitimu mafunzo ya JKT na kuwaajiri katika majeshi hayo. Bila shaka watafanya hivyo kwa k u w a i n g i z a k w a n z a katika vyuo vya mafunzo zaidi vya majeshi hayo na kuwaajiri kulingana na matakwa ya jeshi husika.

Tunafahamu kwamba

n i v igumu kuwaa j i r i wahitimu wote wa JKT. Lakini ni vyema ukajengwa utamaduni wa kuwapa kwanza kipaumbele vijana wanaohitimu mfunzo ya JKT, kuliko kukimbilia mitaani kusaka vijana waliomaliza kidato cha nne, sita na vyuo bila kupituia JKT.

Na hapa ndipo ambako w a h i t i m u w a J K T wangesimamia. Kwamba wamehitimu na uwepo utaratibu unaozingatiwa na kufuatwa, kwamba zikitokea ajira za majeshi, basi wahitimu mafunzo ya JKT wapewe kipaumbele. Lakini kwa kutaka kila anayehitimu, basi serikali inalazimika kumpatia ajira

iwe ni jeshini au mahali pengine, hilo kimsingi haliwezekani.

Lakini moja la msingi tuliseme hapa kwamba, mo ja ya ma l e n g o ya kurejeshwa mafunzo ya JKT kwa vijana wetu ni kujaribu kujenga kizazi cha watu wazalendo, wakakamavu na wachapa kazi katika Taifa, hasa katika umri wa ujana ambao ndio unaotegemewa kwa nguvu kazi ya Taifa.

Lakini pia mafunzo y a J K T k w a v i j a n a wetu, huwasaidia kuwa wabunifu wa ajira, hasa ikizingatiwa kuwa huko JKT, hufunzwa kujitemegea k w a k u f u n d i s h w a s t a d i m b a l i m b a l i z a

maisha, ujasiria mali , u juz i mbal imbal i , i l i watakafuzu mafunzo, kirejea uraiani wawe na ujasiri wa kubuni ajira zao na kujiajiri. Na kubwa zaidi, kuwa wazalendo. Kuwa Watanzania, na sio wa kabila/dini fulani au tabaka fulani. Hayo ndiyo malengo makuu ya vijana wetu kwenda mafunzo ya JKT.

Sasa kama vijana hawa wahitimu wa JKT, wanalilia ajira na wanafikia mahali pa kutaka kuandamana kushinikiza waambiwe ajira zao ziko wapi, hapana shaka hizo ni salamu kuwa mafunzo wanayopewa, kwa maana ya mtaala unaotumika kuwafunda wakiwa katika kambi za JKT, utizamwe upya.

SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa viumbe vyote na tunamtakia zawadi ya rehema na amani zimfikie bwana wa Manabii na Mitume, Bwana wetu Muhamad na jamaa zake na Sahaba zake na wale wote wenye mwisho. Ewe Mwenyezi Mungu tufundishe yale yenye manufaa na utunufaishe kwa yale tuliojifunza na utuongeze elimu na utupe ujuzi wa dini, Mwenyezi Mungu tukubalie.

Baada ya utangulizi huo mfupi, Uislamu umepangilia mahusiano ya kibinadamu katika dunia hii na kufanya mahusiano hayo n i ya aina mbili, mahusiano kati ya mtu na Mungu wake, nayo ni kumuabudu Mola wake mlezi peke yake na bila ya kumshirikisha na kitu chochote. Mahusiano kati ya viumbe sisi kwa sisi na Uislamu umehimiza na kuushughulikia uhusiano kati ya mtoto na wazazi wake wawili.

Laiti tukiiangalia Qur’ani tukufu tungeona sehemu nyingi zilivyojipanga juu ya mahusiano ya kibinadamu na kuyafanya mahusiano ya m wa n z o k a b i s a n i

Kuwatii wazazi wawili ni muhimu kuliko jihadi katika dini

kati ya mja na Mola wake mlezi. Kisha anataja hapo hapo mahusiano ya wazazi wawili kama i l ivyokuja katika Surat Nisai, inasema Mwenyezi Mungu mtukufu “Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote, na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali na rafiki wa ubavuni na mpita njia na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia, hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifaharisha”. Surat Nisai aya ya (36).

Na katika Surat Al-an-aami (151), amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Sema njooni nikusomeeni aliyo kuharamishieni Mola wenu, nayo ni kuwa msimshirikishe yeye na chochote na wazazi wenu wafanyieni wema, wala msiwaue watoto wenu kwa sababu ya umasikini, sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao wala msikaribie mambo machafu yanayoonekana na yanayofichikana, wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi M u n g u a m e i h a r a m i s h a kuiuwa ila ikiwa kwa haki hayo amekuusieni ili myatie akilini.”

N a k a t i k a S u r a t a l -Israi amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu “Na Mola wako mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote isipokuwa yeye tu na wazazi wawili muwatendee wema, mmoja wao akifikia uzee naye yuko kwako au wote wawili usiwakemee na sema nao maneno mazuri” (Israi, aya ya 23).

Na katika aya hizi tukufu na nyinginezo, tunafahamu kwamba kuwatii zawazi wawili na kuwafanyia ihsani na wema na kuishi nao vizuri ni muhimu sana kuliko

wajibu mwingine wowote mwengine. Na haya ndio mahusiano ya mwanzo kabisa kuliko hata mahusiano ya mtu mwingine katika maisha haya ya dunia, na sisi tunajua mambo yaliyopo katika jihadi ya Mwenyezi Mungu.

Kutoka na daraja ya juu katika Uislam na ina ubora kiasi gani na pamoja na yote hayo, lakini kuwatii wazazi wawili ni bora sana kuliko jihadi na hasa pale wanapokuwa wazazi hao hawana mtu yeyote wa kuwahudumia, isipokuwa mtoto huyo huyo wa pekee.

Toka kwa Abdallah bin Masoud ( ra ) amesema, “Nilimuuliza Mtume (saw) ni amali gani anayoipenda sana Mwenyezi Mungu? Akasema, “Kuswali katika wakati wake,”. Nikasema kisha nini?, Akasema “Kuwafanyia wema wazazi wawili”. Nikasema kisha nini? Akasema jihadi katika dini ya Mwenyezi Mungu”.

A m e i p o k e a I m a m u Bukhari, akasema Mtume (saw) kwamba, kuwatii wazazi wawili ni bora baada ya swala ya faradhi, ambayo ndiyo mahusiano kati ya binadamu na Mola wake mlezi, nayo ni nguzo muhimu katika Uislamu na akapangilia hayo kwa neno “kisha” ambalo humaanisha juu ya utaratibu na akaitanguliza twaa ya wazazi wawili kwanza kabla ya j ihadi katika dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Na alikuja mtu mmoja kwa Mtume (saw) akasema, “Ninachukua ahadi juu ya kuhama na jihadi, ninahitaji malipo toka kwa Mwenyezi Mungu, akasema Mtume (saw), “Je unao wazazi wawili au mmoja wapo yupo hai,? Akasema “ndiyo” bali wote

Inaendelea uk. 4

Page 3: ANNUUR 1167a.pdf

3 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Piganieni haki zenu BungeniW A I S L A M U wametakiwa kuweka m s i n g i wa k u p a t a h a k i z a o s a wa n a wa n a n c h i we n g i n e kwa kuhakikisha kuwa kwanza wanapata nafasi yao katika serikali za mitaa na bungeni.

P a m o j a n a n j i a n a m i h a d h a r a , m a k o n g a m a n o n a maandamano kupaza saut i kunadi madai yao, lakini wametakiwa k u h a k i k i s h a k u w a wanajishughulisha na siasa za nchi kwani kutokuwepo kwao katika nafasi za maamuzi , inaweza kuwa moja y a s a b a b u k u b w a inayofanya kilio chao katika makongamano kisifike mbali.

Wito huo umetolewa na Ustadhi Said Ayoub, akiongea na Waislamu Ijumaa ya wiki iliyopita katika Msikiti wa Tungi, Temeke Jijini Dar es Salaam.

U s t a d h A y o u b amesema, siasa ni njia mojawapo ya ufumbuzi wa matatizo yanayo ikabili jamii yoyote, hivyo Waislamu hawana budi kurejea katika Siasa kwani inaweza kuwa n i n j ia mbadala ya ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili kwa miaka mingi.

Ust. Ayoub, alisema kuwa kabla ya Uhuru Waislamu walikuwa mstari wa mbele katika h a r a k a t i z a S i a s a kwa kudai Uhuru wa Tanganyika, hata hivyo walijikuta wanawekwa k a n d o b a a d a y a kupatikana Uhuru.

Alisema, inadaiwa k u w a W a i s l a m u hawakuwa na elimu ya kuingia Serikalini na kushika nyadhifa za kisisa hivyo kumlazimu Rais Julias Nyerere, kuwajaza watu wa imani yake ambao walikuja kuwabagua Waislamu.

Na Bakari Mwakangwale Ust. Ayoub alisema k w a s a s a h a k u n a kisingizio cha elimu, bali ni juhudi za Waislamu wenyewe zinatakiwa.

Alisema, uwepo wa kundi moja kuhodhi nafasi katika vyombo vya maamuzi, hakuna n a m n a a m b a v y o u n a w e z a k u t a r a j i a kutendeka haki.

“ I l i k u p a t a h a k i kwa makundi yote ni kuhakikisha makundi hayo yanakuwa na uwakilishi sawa kuanzia ngazi ya Mtaa, Bunge na hata katika Serikali Kuu.” Alisema Ust . Ayoub.

Wa k a t i h u o h u o , Waislamu wametakiwa k u j i t o k e z a k w a wingi katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Hayo yameelezwa na kiongozi mwandamizi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Juma Ramadhani, akiongea na An nuur, kufuatia madai kuwapo kwa viongozi wa Dini na Siasa wanaowapotosha w a n a n c h i k u h u s u u s h i r i k i w a o a m a k u w a t a k a kutojiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa lengo la kususia Katiba mpya.

Sheikh Ramadhani a m e s e m a v i o n g o z i wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini , w a n a w a h i m i z a W a i s l a m u w o t e k u j i a n d i k i s h a k wa wingi katika daftari hilo wakilenga maeneo mawili muhimu yaliyo mbele yao.

Al iya ta ja maeneo hayo kuwa ni kushiriki katika zoezi la kuchagua viongozi katika uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais, lakini pili ni kubakia na msimamo wao wa kupiga kura ya hapana kuikataa Katiba mpya, kutokana na Mahakama ya Kadhi

kutokuwemo katika Katiba mpya.

“Huenda viongozi wa kuu wa Serikali wanapewa taarifa zisizo sahihi kuhusu Waislamu na msimamo wao wa ushiriki katika kura ya maoni, ukweli ni kwamba Waislamu hawatogomea kujiandikisha katika hilo daftari.

Msimamo wao n i kupiga kura ya hapana

siku hiyo itakapofika, kwa kuwa suala la Mahakama ya Kadhi halimo katika Katiba pendekezwa.

Alisema, zoezi hilo l a k u r a y a m a o n i linalotarajiwa kuanza mwezi wa nne, 2015, kwa Waislamu kila kona ya nchi watahamasishana na mazungumzo yao ya t a k u wa n i s u a l a la Kat iba mpya na Mahakama ya Kadhi.

“Tukifanya hivyo kwa wingi na utakapofika muda wa kuipigia kura rasimu hiyo ya Katiba k w a u p a n d e w e t u tutakwenda kwa azima moja tu ya kuikataa rasimu hiyo kwa kupiga kura ya ‘Hapana,’ na msimamo huu utabaki hivyo ikiwa suala la Mahkama ya Kadhi litakuwa limebaki katika sura ilivyo sasa”. Alisema Sheikh Ramadhani.

PICHANI juu na chini, baadhi ya watuhumiwa wa kesi ya Ugaidi wakiwa mahakama ya Kisutu juzi Jumatano. (Picha na Seif Msengakamba)

Page 4: ANNUUR 1167a.pdf

4 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Kuwatii wazazi wawili muhimuInatoka uk. 2wawili wapo hai. Akasema, “Je wewe unataka malipo t o k a k wa A l l a h ( s w ) , akasema “ndio”. Akasema “rudi kwa wazazi wako wawili kisha ishi nao vizuri kama walivyokulea wewe ulipokuwa mdogo.”

Na alikuja mtu mmoja kwa Mtume (saw) akasema “Nimekuja kuchukua ahadi ya kuhama na jihadi na nimewaacha wazazi wangu wawili wanalia,” Mtume akasema “Rudi kwa wazazi wako ukawachekeshe kama ulivyowaliza.” Tirmidhiyi.

Na alihama mtu mmoja miongoni mwa watu wa Ye m e n , a k a h a m a n a Mtume (saw) akamuuliza, j e k u n a y e y o t e h u k o Yemen? Akasema,“Wazazi wangu wawili,” Akasema “Wamekurusu? Akasema, “Hapana”, akamwambia rudi kwao ukawaome ruhusa na kama utaruhusiwa, basi nenda kat ika j ihadi na kama hawajakuruhusu, basi wafanyie wema.

Na pale wazazi wako wanapokukataza jambo au kukuamrisha japo kwa ishara kwa sababu wao ni wenye kukunasihi zaidi wewe kuliko wewe unavyojinasihi, hata kama utakuwa na marafiki au ndugu lakini sikiliza maneno ya wazazi na maelekezo yao, tena uwatii katika mambo mema na useme nao kwa upole na adabu na utake ushauri katika mambo yako na wala usiwakate mazungumzo yao, na wala usiinue sauti yako kwao na usiwatazame kwa hasira, wala kwa dharau

na wala usiinue mkono wako wakati wa kuongea nao wala kuonyesha kidole, wala usijadiliane nao, na usiwaongopee na wala usiwaambie waongo na usisafiri isipokuwa kwa ruhusa yao, kukubali kwao na ndio ihsani yao.

Kutoka kwa muawia, Assalami (ra) amesema, n i l i m w e n d e a M t u m e n i k a m wa m b i a , “ M i m i nimejiandikisha niende vitani pamoja na wewe kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na pepo yake”, akasema “Ole wako je, yu hai mama yako? Nikasema “Ndiyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,” akasema “Sikia shikamana na miguu yake kwani hapa ipo pepo,”. Ameipokea Ibnu Maja . Maana ya kushikamana na miguu ya mama ni “Mtii na umnyenyekee kwani kufanya hivyo ni sababu ya kuingia peponi.

Tumuombe Mwenyezi M u n g u a t u j a a l i e t u we m i o n g o n i m w a w a l e wanaowatii wazazi wao na kuwaridhisha mama zao, na atufufue pamoja na Manabii na Mitume na watu wema na tuwe na urafiki mwema nao.

Ewe Mwenyezi Mungu, mpe rehema na amani Bwana wetu Muhammad na jamaa zake na Sahaba zake kwa wingi, na shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa Ulimwengu.

Makala hii imeandaliwa na Sheikh Salah Sayed Huseni Miftah.

Mwalimu wa Al-Azhari Sharif, Tawi la Tanzania.

Pamoja na fitna ya Sitta...Zanzibar inabeba lawama kubwaF I T I N A n y e n g i n e i n a p a n d w a d h i d i y a Wa z a n z i b a r i n a dhidi ya Zanzibar. Na mpandikizaji wa mara hii ni Samuel Sit ta , Wa z i r i m wa n d a m i z i k we n ye s e r i k a l i ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye dhamana ya Mawasiliano na Uchukuzi, na ambaye ndiye aliyekuwa pia Spika wa Bunge Maalum la Katiba lililomazika kwa kutoa kile kiitwacho R a s i m u y a K a t i b a I n a y o p e n d e k e z w a inayotazamiwa kupigiwa kura mwishoni mwa mwezi Aprili 2015.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VoA) juu ya bunge hilo aliloliongoza kutopitisha kipengele cha katiba kinachowaruhusu Watanzania kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja, Sitta alisema yafuatayo:

“Ukumbuke historia, h u s u s a n h i s t o r i a ya Zanzibar, na Watanzania takriban zaidi ya laki mbili walioko Oman ambao walivyotoka kama 20,000 mwaka ule wa 1964, sasa ni kundi zito ambalo lina uwezo kifedha ambalo lipo pale Oman. Ukikaribisha uraia pacha, kwa maana ya papo kwa papo, maana yake wale wote wanakuwa ni raia wa Tanzania pia. Lakini wengi wao wana nia ya kuipindua serikali. Kwa hivyo, ukileta sura hiyo (kipengele hicho cha katiba) inaleta tabu kidogo – kumpa uraia mtu ambaye kwa matamshi yake na tabia yake na uwezo alionao ana lengo la kupindua serikali.”

A n g a l i a v i d i o kamili ili kupata chote a l i c h o k i z u n g u m z a k w e n y e s u a l a h i l i . Tusiangalie mapungufu ya hoja dhidi ya uraia wa zaidi ya nchi moja kwa Watanzania wanaoishi nje kwa sasa, ingawa si kweli kuwa ilitokana na khofu ya kupinduliwa kwa serikali. Dunia ya leo haimuhitaji mtu kuwa raia wa nchi fulani kuweza kuupindua utawala wa nchi hiyo. Wamarekani wanaokwenda kupindua s e r i k a l i z a m a t a i f a mengine hawana uraia wa nchi hizo, bali wana nguvu, sera na teknolojia ya kufanya hivyo.

Fitina ya makusudi.Tuangalie fitina hii dhidi

ya Zanzibar hasa katika

Na: Mohammed Ghassany

wakati ambapo, kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 50 na pamoja na udhaifu wake wa ndani, Zanzibar imeweza kuianika aibu ya kutawaliwa na Dodoma k u p i t i a M a b a d i l i k o ya 10 ya Katiba yake na mchakato wote wa kupatikana Katiba Mpya unaoendelea sasa.

K w a m f a n o , k i l e k i l i chotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba ambalo liliongozwa na yeye, S i t ta , k imsingi k i l i m z u w i a m t a wa l a kuandika rasimu ya katiba mpya hadi alipolazimika kutumia nguvu, hila na mizengwe kuifanya hiyo Rasimu inayopendekezwa.

Msikilize Mheshimiwa Waziri William Lukuvi, a m b a y e n a y e k a m a alivyo Sitta ni kiongozi mwandamizi kwenye serikali ya Rais Jakaya K i k w e t e , a k i m wa g a sumu Kanisani dhidi ya Zanzibar. Hapo utabaini k i w a n g o a m b a c h o Zanzibar ndani Bunge hilo Maalum la Katiba iliivuruga kabisa akili ya mtawala na mawakala wake.

L u g h a ya S i t t a n a ya Lukuvi zinafanana. Dhamira zao zinaoana. Njia yao ni moja kwa kuwa lengo lao pia ni moja – lengo la mtawala, ambalo ni kuiadhibu Zanzibar kadiri inavyoyumkinika kutokana na uthubutu wake.

Ni staili inayotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina – adhibu vikali kadiri

i n a v y o w e z e k a n a i l i l iwe fundisho na iwe mwisho. Wakati mtoto wa Kipalestina anapokirushia mawe kifaru cha kijeshi cha Israel ambacho kimeivunja nyumba yao na kuikalia kwa nguvu ardhi yao, hupigwa, akakamatwa na kufungwa jela, kama si kurushiwa risasi na kuuliwa kabisa.

Kila kombora moja la Hamas, ambalo hata hal iwahi kutua chini kwenye ardhi ya Israel kabla ya kutunguliwa huko huko angani, hujibiwa k w a k u a n g u s h i w a bomu la kilogramu 500 katikati ya makaazi ya watu, linalouwa makumi kwa mamia ya watoto, wanawake na wazee wa Kipalestina.

Ndivyo anavyofanya m t a w a l a d h i d i y a m t a w a l i w a w a k e anayethubutu. Fuatilia mwenendo wa mambo visiwani Zanzibar tangu mchakato wa ka t iba mpya uanze – kesi za viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho, watu wanaochukuliwa na kupelekwa korokoroni Bara, na kile kinachoitwa “matukio na kes i za ugaidi” utajua Zanzibar iliyothubutu inaelekezwa wapi.

Nadharia dhahanifu ya khofu dhidi ya Waarabu: K u n a k i t u k i n a i t wa “ c o n s p i r a c y t h e o r y ” kwa Kizungu, ambacho Kiswahili chake kinaweza k u w a n i “ n a d h a r i a

Samuel Sitta.

Inaendelea Uk. 18

ILALA ISLAMIC SECONDARY USAJILI S.2401

KIDATO CHA TANO NA KURUDIA MITIHANI

KWA WASICHANA TUIPO: ILALA-AMANA-MTAA WA ARUSHA: MASJID SHAFII

SHULE YA BWENI NA KUTWA

MASOMOMath, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce,

B/keeping Islamic, Arabic na Tahfidhul Qur’anCOMBINATION

PCM,PCB,CDG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEAUFAULU 2014

KIWILAYA 3/76, KIMKOA 10/191, KITAIFA 118/2322Kwa shule za kiislam KIWILAYA (1) KIMKOA (2) KITAIFA (5)

Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, VMAWASILIANO

Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822, 0714 381964

KWA WAVULANA TUIpo Ilala-Bungoni: Masjid Taqwa

DAR ES SALAAM ISLAMIC SEC.

MASOMOMath, Phy, Chem, Bios, Geo, Civ, Eng, Kisw, Commerce, B/

keeping Islamic, Arabic na Tahfidhul Qur’an

COMBINATIONPCM,PCB,CDG,HGL,HGK,HGE,HKA,HEA

UFAULU 2014Kama Ilala Islamic, imetenganishwa toka Ilala Islamic

Zipo nafasi za kuhamia kidato cha II, III na IV, VMAWASILIANO

Simu: 0713 007586, 0715 187515, 0714 393822, 0714 381964Ada ni nafuu na inalipwa kwa awamu nne

MLETE MWANAO APATE ELIMU NA MALEZI BORA

USAJILI S.4384

Page 5: ANNUUR 1167a.pdf

5 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Habari za Kimataifa

KAMANDA wa kundi la wapiganaji wa ISIL, Abu Bakr Baghdadi, amedaiwa kuwa hivi sasa anapata matibabu katika hospitali moja nchini Israel baada ya kujeruhiwa vitani nchini Iraq Ijumaa usiku, wiki iliyopita.

Vyanzo vya habari nchini Iraq vimethibitisha kuwa Abu Bakr al -Baghdadi , ambaye amepewa wadhifa wa Ukhalifa ndani ya kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria, amepelekwa Israel kwa ajili ya matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya kufuatia mashambulizi ya ndege dhidi ya msafara wake katika mji wa Al Qaim, katika jimbo la Al-Anbar mpakani mwa Iraq na Syria.

Ta a r i f a k u t o k a I r a q zimeeleza awali Baghdad alipata matibabu ya awali katika hospitali ya muda katika miinuko ya Golan inayodhibitiwa kwa mabavu na Israel na baada ya hapo, alipelekwa katika hospitali maalumu mjini Tel Aviv kwa matibabu zaidi.

Wazir i wa Ulinzi wa Iraq , Khaled a l -Abadi , amethibi t i sha Jumapi l i iliyopita katika mtandao wake wa Facebook kwamba Bw. Abu Bakr al-Baghdadi alijeruhiwa katika shambulizi hilo usiku wa kuamkia Ijumaa, ambapo Naibu wake alipoteza maisha.

Katika shambulio hilo, wapiganaji wengine 17 wa ISIL waliuliwa.

K a t i ya m a k a m a n d a w a a n d a m i z i w a I S I L waliouawa katika shambulio hi lo ni pamoja na Abu Muslim Turkmani, Thamer Mohammad, Abu Muslim Checheni, Abu Mujahid ar-Russi na Abu Ubaidah al-Azzawi.

M t u a n a y e a m i n i w a kuwa ndiye msemaji wa ISIL, Abu Muhammad Al-Adnani, Jumapili iliyopita katika mtandao wa Twitter amedaiwa kuthibi t i sha kujeruhiwa kwa Kamanda Baghdad kufuatia shambulio hilo la ndege za Marekani na jeshi la Iraq na kudai kuwa, labda wapo watu wanaoaminikuwa huo ndio mwisho wa Khalifa. Lakini anawahakikishia mataifa ya Kiislamu kuwa Amir Abu Bakr al-Baghdadi yuko salama na anamshukuru M w e n y e z i M u n g u n a kumtakiwa apone haraka.

Falah Al Essawi, Naibu Mkuu wa Baraza la Mkoa wa Al Anbar nchini Iraq, alisema ndege za kivita za nchi hiyo kwa kushirikiana na ndege za Marekani siku ya Alhamisi zilishambulia kambi za ISIL katika mji wa Al Qaim mkoani humo, ambapo wapiganaji kadhaa waliuawa.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, mwezi uliopita wa Februari watu wasiopungua 1,100 waliuawa katika machafuko nchini Iraq huku wengine 2,280 wakijeruhiwa.

Kamanda wa IS apelekwa Israel kupata matibabu

Mwezi Januari watu 1,375 waliuawa katika machafuko nchini humo huku idadi kubwa wakiwa wamepoteza m a i s h a k u t o k a n a n a mashambulizi ya ISIL.

N i c k o l a y M l a d e n o v , mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amelezea wasiwasi wake kutokana na kuongezeka idadi ya watu wanaouawa katika mapigano hayo.

Alisema karibuni hivi atachapisha idadi kamili ya waliouawa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na ISIL nchini Iraq.

Wakati hali ikiwa hivyo, Spika wa Bunge la Iraq Salim al Jabouri, Jumapili alitoa mwito wa kufanyika mazungumzo ya maelewano ya kitaifa ili kuwepo umoja k a t i k a k u k a b i l i a n a n a makundi ya kigaidi nchini humo.

ISIL waliukalia mji wa Mosul tangu mwezi Juni mwaka jana.

Kwa muda mrefu serikali ya Syria imekuwa ikisema kuwa wapiganaji waasi wamekuwa wakipata msaada kutoka nchi za Magharibi na hasa Marekani na marafiki zake hususan Israel, Uturuki, Qatar na Saudi Arabia.

Itakumbukwa mwaka jana mwezi wa Agosti, jasusi wa Marekani aliyeasi na kukimbil ia uhamishoni Urusi, Edward Snowden, alifichua siri nzito kwamba, Bw. Abu Bakr Al Baghdadi, ni mtu aliyepatiwa mafunzo na taasisi ya ujasusi ya Mossad.

Aidha alidai kuwa taasisi za kijasusi za Uingereza na Marekani pamoja na Mossad ya Israel zilifanya kazi pamoja kuunda kundi la Islamic State nchini Iraq na Syria.

Snowden alisema kazi

za kijasusi za nchi hizo tatu zilisaidia kuundwa kwa makundi ya kigaidi ambayo yaliwavuta wahafidhina wote duniani katika sehemu

moja kwa kutumia mpango ulioitwa ’the hornet’s nest’.

Bw. Snowden alibainisha katika nyaraka aliyoifichua akisema, NSA documents refer to recent implementation of the hornet’s nest to protect the Zionist entity by creating religious and Islamic slogans.

Kwa mujibu wa nyaraka alizofichua jasusi huyo aliyeasi, ilielezwa kuwa “suluhu ya pekee ya usalama wa dola la Kiyahudi ni kuunda adui jirani na mipaka yake”.

T a a r i f a z i l i z o v i j a zilibainisha kuwa kiongozi wa sasa wa ISIS Abu Bakr A l B a g h d a d i , a m b a ye alionekana kiongozi makini wa kidini alipewa mafunzo ya kijeshi kipindi cha mwaka mzima chini ya MOSSAD, licha ya mafunzo ya teolojia na utaalam wa kuhutubia.

Ripoti zimeshabainisha kuwa jina halisi la Abu Bakr al-Baghdadi na ambaye a m e p e wa U k h a l i f a n a kiongozi wa ISIL lina asili ya

kiyahudi.Kwa mujibu wa Mtandao

wa habari wa Veterans Today, jina halisi la al-Baghdadi ni Simon Elliot au Elliot Shimon na alizaliwa na wazazi Wayahudi na kupata mafunzo ya saikolojia ya vita dhidi ya Waarabu na Jamii za Kiislamu chini ya maofisa wa MOSSAD.

Ili kusaidia kufahamika vizuri ripoti yake, Veteran Today ilitoa kwa tafsiri ya Kiingereza kutoka Radio ajyal.com na Egy-press.

Kwa mujibu wa Veterans Today, mpango wa ISIS chini ya uongozi wa al-Baghdadi ni kuzivuruga nchi zote zinafahamika kuwa ni tishio kwa Israel, ili baada ya hapo dola la Kizayuni lidhibiti eneo la Mashariki ya Kati na hatimaye kustawisha kile kilichoitwa “Greater Israel."

N a d h a r i a h i z i z a ku ionyesha IS IS kama sehemu ya Uzayuni, zinaweza kuonekana vyema kutoka ripoti za awali zilizohusiana n a E d wa r d S n o w d e n , kwamba Taasisi za kijasusi za Uingereza, Marekani na Wazayuni walitengeneza ISIL, sasa wakiitwa zaidi kwa jina la Islamic State Iraq and the Levant.

AFRICA MUSLIMS AGENCY TANZANIA OFFICE The Africa Muslims Agency is an humanitarian, development and Dawah organization based in Kuwait with offices across Africa. The agency has established itself within 32 countries of Africa, including Sierra Leone, Mali, Mozambique, Madagascar, Zimbabwe, Angola, Gambia, United Republic of Tanzania and particularly South Africa. The Agency’s goals are to strengthen Islam by spreading the teachings of the Quran, as well as to build hospitals, schools and mosques. To accomplish its set goals it looks forward to recruit intellectuals in the field of education to fill the available vacancies.

Job Title: Education SupervisorJob Station: Tanga and Moshi Available Positions: 2 postsRoles and Responsibilities

• Complies with state administrative regulations and Board of Education policies • Adheres to school and local school system procedures and rules • Demonstrates timeliness and attendance for assigned responsibilities • Maintains accurate, complete, and appropriate records and files reports promptly• Preparing weekly and monthly reports and ensure timely submission of reports to the administration• Assist in recruitment and in service training of teachers• Evaluate teaching techniques and suggest means of improving them• Visit classrooms to see effectiveness of teaching and teaching materials.• Conduct seminars and workshops to teachers to demonstrate new teaching methods, teaching materials and teaching.• To provide to teachers teaching materials and all necessary equipments for teaching process.

Qualifications

• A holder of degree in education with any specification• Has at least five years in teaching or similar position with good track record• Must be willing and available to work in Tanga or Moshi• Strong leadership, communication, interpersonal, and organizational skills • Computer application skills.• Experience in working with donor funded projects.

• Excellent written and oral communication skills in English and Kiswahili, including report writing.• Excellent networking and organizational skills• Self motivated person

Mode of ApplicationSend your Application including application letter, CV and copies of certificates to:The Director Africa Muslims AgencyP o Box 9214Dar es Salaam

KAMANDA wa kundi la wapiganaji wa ISIL, Abu Bakr Baghdadi.

Page 6: ANNUUR 1167a.pdf

6 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

KAMA alivyotumia j u k wa a l a K a n i s a kupiga mbiu kuwa tatizo la Tanzania ni Waarabu na Waislamu, Mheshimiwa Waziri Samuel Si t ta naye ameibukia katika VoA akidai kuwa Waarabu wanatishia kuivamia na kuipindua Zanzibar.

Akasema, hiyo ndiyo imekuwa sababu ya k u o n d o l e wa s u a l a l a u r a i a w a n c h i mbili katika Katiba inayopendekezwa.

A k i h o j i w a n a Idhaa ya Kiswahil i ya Sauti ya Amerika (VoA) hivi karibuni, Sitta amesema kuwa wengi wa Wazanzibari waliokimbilia Oman baada ya Mapinduzi 1964, hivi sasa wana pesa za kutosha na hawajaondokana na nia ya kuipindua serikali ya Zanzibar.

“Wengi wao wana nia ya kuipindua serikali. Kwa hivyo,... inaleta tabu kidogo – kumpa uraia mtu ambaye kwa matamshi yake na tabia yake na uwezo alionao, ana lengo la kupindua serikali.”

Alisema Mheshimiwa Samwel Sitta akisisitiza kuwa ni hatari kuruhusu uraia wa nchi mbili ambao utawapa pia uraia wa Zanzibar idadi kubwa ya Waarabu wanaoishi Oman.

Mwaka 2009 baada ya kuibuka mgogoro baina ya serikali na Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, Shir ika la Umeme, TANESCO, chini ya Mkurugenzi wake Dr. Idris Rashid, lilitoa pendekezo kwa serikali kuwa serikali inunue

Sitta hana jipya…Ni yale yale ya Dowans, Symbion

Tatizo Wazanzibar wenyewe hawajitambuiHata hili tuseme, kwa Jina la Yesu Eemen?

Na Omar Msangi

na tatizo la umeme na kwamba i tachukua muda mrefu kuanza kutafuta ‘Richmond’ au ‘Dowans’ nyingine kuingia nayo mkataba. Lakini kwa mitambo a m b a y o t a ya r i i p o nchini , n i suala la kuingia mkataba wa u n u n u z i , m i t a m b o inawashwa. Pili ni kuwa, kwa kununua mitambo yetu, tungeepukana na gharama kubwa za kulipa kinachoitwa ‘ C a p a c i t y C h a r g e ’ a m b a y o TA N E S C O inalazimika kuwalipa wazalishaji binafsi wa nje kila siku. Na si pesa ndogo.

N i M h e s h i m i w a Samwel Sitta na baadhi ya wabunge, walioongoza ‘Crusade’ ya kupinga wazo la TANESCO kununua mitambo ya Dowans, zikitolewa hoja mbalimbali, moja ikiwa kwamba mitambo hiyo ni chakavu.

M k u r u g e n z i w a TANESCO wakati huo Dr. Idris Rashid, alionya kuwa nchi itaingia kizani iwapo hatua za haraka

HATA hi l i? Tuseme E e m e n ! N d i v y o anavyouliza mwendesha kipindi katika televisheni moja ya Nigeria. Anauliza swali hilo akichambua mahubiri ya Askofu David Olaniyi Oyedepo wa Kanisa la Living Faith Church World Wide, likijulikana pia kwa jina la Winners' Chapel, akidai kuwa yeye ni Mtume wa Mungu aliyepewa agizo la kupambana na ‘mashetani wa Kiislamu’.

“If you catch anyone that looks like them – kill him! Kill him and pull out his neck. I will spill his blood on the ground. What nonsense! What Islamic demons. God has anointed me to lead a revolution against Islamic jihadists”.

A n a s e m a A s k o f u O y e d e p o k a t i k a mahubiri yake ambayo yamekuwa yakitolewa katika televisheni na k u s a m b a z wa k a t i k a mitandao kutoka mwaka

Hata hili tuseme Eemen! jana.

Katika video ambayo i n a p a t i k a n a k a t i k a i n t e r n e t , A s k o f u Oyedepo anaonekana akiongea kwa hasira na kufoka huku Wakristo waliofurika katika kanisa wakimshangi l ia kwa nguvu na kupiga kofi kila akiwahimiza kuuwa Waislamu au kutaja neno “What devi l s ! , what Islamic demons!”

Ilikuwa ni pale Askofu h u y o a l i p o s e m a , “ I f you catch anyone that looks like Boko Haram”, ikiwa na maana kuwa ukimkamata, ukimuona mtu anayefanana na (looks like) Boko Haram, muuwe. Kata shingo yake, mwaga damu yake; mchambuzi huyo anauliza-jamani, hata hili tuseme Eemen?

Aliuliza hivyo kwa sababu kila Askofu David Oyedepo, akitoa wito huo, waumini hushangilia na kusema Eemen!, kama ishara ya kusikia na

kukubali wanayoagizwa.Askofu David Oyedepo

haishii hapo. Anasikika akiwaambia wafuasi wake kuwa wakishamuuwa mtu ambaye “looks like”, anayefanana na Boko Haram, wala wasipate tabu ya kutoa ripoti polisi.

I n a v y o e l e k e a maelekezo ya Maaskofu kama Oyedepo ndiyo s a s a ya n a y o f a n y i wa kazi na jeshi la Nigeria pamoja na Wakristo wa Nigeria. Katika mauwaji ya Baga, kwa siku nne m f u l u l i z o a m b a p o watu wasiofahamika, wakiwemo wanajeshi, w a k i w a w a n a u w a Waislamu na kuchoma nyumba zao moto, serikali haikushughulika kabisa kupeleka vyombo vya ulinzi kuzuiya mauwaji hayo. Maadhali watu wa mji huo wote ni Waislamu, basi wote wanaingia katika lile kundi la “looks

Inaendelea Uk. 7 Inaendelea Uk. 7

mitambo ya Dowans. Na ikawasilisha taarifa ya kitaalamu kuonyesha uzuri wa mitambo hiyo na unafuu serikali/nchi itakaopata kwa kuwa na mitambo yake badala ya kutegemea makampuni binafsi tena ya nje. Ilikuwa mitambo hiyo inunuliwe kwa Dola mil ioni 38 sawa na Shilingi bilioni 60.

U c h u n g u z i unaonyesha kuwa baada ya serikali kusitisha mkaba wake na Dowans, kampuni hiyo ilikuwa ikilazimika kuhamisha mitambo yake kutoka n c h i n i k u p e l e k a kwingine. Kwa upande mwingine, TANESCO nao wal ikuwa ama wa t a f u t e k a m p u n i

nyingine ya kuingia nayo mkataba iingize mitambo izalishe na kuwauzia umeme au iagize mitambo yake.

TA N E S C O b a a d a ya kuifanyia tathmini mitambo ya Dowans kupitia kampuni za kimataifa, ilijiridhisha kuwa mitambo hiyo ingeweza kufanya kazi kwa miaka 30 bila ya ta t izo , na kwamba matengenezo ambayo yangehitajika (service) ni ya kawaida ambayo mafundi wazalendo wangeyamudu. Aidha kwa upande wa bei, pia ilionekana kuwa ni nzuri ikilinganishwa na thamani ya mitambo hiyo au kuagiza mingine kutoka nje.

Hoja ya TANESCO ilikuwa namna mbili. Moja ni kuwa tayari nchi ilikuwa kizani kutokana

SAMWEL Sitta.

Page 7: ANNUUR 1167a.pdf

7 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Ni yale yale ya Dowans, SymbionInatoka Uk. 6

hazitachukuliwa. Lakini wapi. Namna yake, akina Sitta wakasema, bora kuwa kizani kuliko k u n u n u a m i t a m b o mtumba ya Dowans. Na kweli, nchi ikakaa kizani kwa takriban miaka miwili, wanasiasa wakilumbana.

Ghafla kimyaaa!

G h a f l a k i m ya a a ! M i t a m b o i m e k u wa ‘ m i p ya ’ i n a s i f i wa . Ilipofika 2011, mitambo hiyo hiyo ya Dowans i k a n u n u l i w a n a Kampuni ya Kimarekani Symbion Corporation, kwa thamani ya Dola milioni 100 ($100m), mara tatu zaidi ya bei a m b a y o TA N E S C O ingelipa.

Wakitoa taarifa ya ununuzi wa mitambo h i y o , v i o n g o z i wa Symbion, wakis i f ia mitambo hiyo kwa uzuri na uwezo wake, walisema w a n a w a s h a n g a a Wa t a n z a n i a k u k a a kizani kwa miaka miwili wakati mitambo hiyo ikishika kutu badala ya kuinunua na kuiwasha kupata umeme! Rais wao Barack Obama akaja Novemba 2011 kuizindua mitambo hiyo naye akaisifia kwa uzuri wake.

Akina Samwel Sitta kimyaa!!! Hawakusikika wa k i f u n u a m d o m o kusema serikali isiingie mkataba na Symbion kwa sababu mitambo yake ni ule ule ‘mtumba wa Dowans’.

S y m b i o n s a s a wanazalisha umeme, wanatuuzia kwa bei wanayotaka. Na zaidi tunalazimika kuwalipa Dola 150,000 ($150,000) sawa na Shilingi milioni 246 kila siku, kama ‘capacity charges’, iwe wamezalisha umeme au la!

Hapo ndipo akili zetu zilipoishia! Hao ndio wanasiasa wetu ambao leo wanatuambia kuwa Waarabu wa Oman, wanataka kuja kupindua Zanzibar!

Ukiangalia kwa undani sakata hili la Dowans na akina Samwel Sitta, unachogundua ni kuwa kinachotekelezwa hapa

ni kile kilichosemwa na John Perkins katika kitabu chake Confessions

of an Economic Hit Man .

Katika kitabu hicho

P e r k i n s a n a e l e z a j insi nchi za dunia y a t a t u , i k i w e m o

A f r i k a ( Ta n z a n i a ) z i n a v y o c h e z e w a mchezo mchafu na mabeberu ili kutiwa kat ika utumwa wa kudumu wa kiuchumi (economic colonization). Na njia kuu ya kupitia ni katika makampuni kama haya ya umeme.

Kutoka ke le le za akina Samweli Sitta juu ya Dowans hadi kimya chao baada ya Symbion, ni kielelezo tu kuwa wapo washenga na madalali miongoni mwetu wanaotumika k u h a k i k i s h a k u wa m i p a n g o ya h a wa ‘economic hit men’ inafanikiwa.

Lakini tukitaka kujua uzito wa tatizo hili, tuliunganishe na hili linalopigiwa kelele hivi sasa juu ya ugaidi.

Mzaha wa ‘Jihad John’W i k i i l i y o p i t a ,

m a g e z e t i k a d h a a yalishupalia mzaha (hoax) wa ‘Jihad John’. N a i l e k u wa z i p o habari kuwa aliwahi kuja Tanzania, ikawa ni habari kubwa ya kutisha ikijengwa picha kwamba Wakristo wa Tanzania wanakabiliwa na kitisho cha ‘Jihad John’. Gazeti moja likisherehesha habari hiyo likasema:

“Makanisa ya dunia y a t o a t a m k o k a l i dhidi ya mauwaji ya Wakristo. Yasema ndiyo wanaoshikilia amani ya dunia. Yataka itikadi za dini zisitumike kuchinja watu.”

H a b a r i h i y o ikasindikizwa na picha ya anayedaiwa kuwa Jihad John, ikiwa na maelezo yafuatayo:

“Gaidi Mohammed Emwazi (kushoto) wa Dola la Kiislamu (IS) aliyewahi kuja Tanzania, akijiandaa kumchinja M m a r e k a n i B wa n a James Foley.”

M we z i N o ve m b a mwaka 2004 askari wawili wa Uingereza, ‘walimbaka’ msichana wa Kitanzania Conjesta U l i k a y e n a k i s h a kumuuwa ji j ini Dar es Salaam. Askari hao waliokuwa wakishiriki uvamiz i na kuuwa watu wasio na hatia Iraq, walikuja Tanzania

Hata hili tuseme Eemen! Inatoka Uk. 6

like”. Kwa hiyo waliuliwa sawiya.

Na hiyo haikuwa mara ya kwanza. Mwaka juzi 2013, jeshi pia lilivamia mji huo na kuuwa takriban watu 200 na kuchoma moto nyumba zao. Taarifa z inafahamisha kuwa katika shambulio hilo zaidi ya asilimia 40 ya nyumba za wakazi wa Baga zilichomwa moto.

Katika kujitetea jeshi wakasema kuwa walikuwa wakipambana na Boko H a r a m . A k i s i m u l i a m k a s a wa A p r i l 1 6 , 2013, Mohammed Bella Sani ambaye ni mvuvi katika mji huo wa Baga anasema kuwa walikuja watu wawili ndani ya gari wakawa wanarusha risasi ovyo huku wakisema “Allahu Akbar”.

G h a f l a n d i o j e s h i

likavamia ikidaiwa kuwa wanawasaka Boko Haram. Na hapo kila Muislamu akastahiki kuuliwa kwa sababu kila Muislamu “Looks like” Boko Haram. Wal io barabarani na mitaani wanapigwa risasi huku walio ndani nyumba zinachomwa moto kwa kumwagiwa petroli.

“ J e s h i l i n a p o u w a raia na kuchoma moto

Inaendelea Uk. 10

Inaendelea Uk. 10RAIS wa Nigeria, Goodluck Jonathan (kushoto) akiwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo, Olesegun Obasanjo.

MHESHIMIWA Mbowe (kushoto) na Spika Anne Makinda (kulia) wakiwa na wenyeji wao Oman.

Page 8: ANNUUR 1167a.pdf

8 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

K A T I K A n d e g e waliotajwa kwenye kitabu kitukufu cha Q u r a n i , k u n g u r u yasemekana yumo. Kwa kawaida vitu au viumbe vilivyotajwa humo vina umaizi mkubwa na mafunzo makubwa tunayopaswa s i s i w a n a d a m u tujifunze kupitia kwao.

U t a f i t i m d o g o t u u l i o f a n y wa n a wanazuoni walioko T a n z a n i a b a r a u m e g u n d u a k u wa kunguru amepewa uwezo mkubwa wa macho. Inasadikiwa kuwa jicho la Kunguru lina uwezo wa kuona mara nne zaidi ya jicho la mwanadamu. Lakini je, hiyo tu ndiyo hekima aliyonayo kunguru hadi kufikia kutajwa kwenye Qur-ani? La, siyo hiyo na wala sababu hasa hatuijui sisi waja wa kawaida. Tubakie tu kusema ‘Allahu a-alam!’

S i s i w a t u w a kawaida, tusiosoma, t u n a m k u m b u k a kunguru sana kwa ule mlio wake ambao kwa wafasiri wa milio ya ndege – iwe kiutani au kiudhati, basi anapolia k u n g u r u h u s e m a maneno yanayokaririka – ‘ D u n i a H a d a a , yaghilibu shujaa!’ Na ni maneno hayo hasa ndiyo yanayonipa kifungu na uwezo mwembamba w a k u a n d i k a ukurasa huu leo, kwa w a t a k a o b a h a t i k a kuusoma!

L e n g o , n i a n a madhumuni yangu ni kuonyesha jinsi gani cheo au uluwa, pesa na nguvu zinavyoweza k u m p o t e z a n j i a m wa n a d a m u a l i ye dhaifu mbele ya Allah hadi akafikia hatua ya kukufuru na kutakabari kul ikopi t i l iza ada . Na basi bi la kujua m wa n a d a m u h u y o dhai fu kuwa kuna nguvu kubwa zaidi i n a y o m w e n d e s h a y e y e , h u e n d e l e a kutakabari hadi akafikia kupatilizwa na Mola wake akaishia kupata hasara ya milele!

Tuna mifano mingi ya viongozi waliokubuhu n a k u f u r u t u a d a . Wakatakabari kiasi ya

Kikata utamu hakina hodi‘Dunia hadaa, yaghilibu shujaa’

Na: Mwandishi Maalum

kuvaa joho la Mungu. Matokeo yake wakafikia pabaya. Mfano mzuri wa hayo ni firauni wa Misri ambaye kwa jinsi alivyotaraghani ujeuri wake, alifikia kusema; ‘Mimi ndiye Mungu wenu mkubwa kabisa!’ Wanaweza wakawepo miungu wengine, lakini “Anaa rabbukumul a’alaa”.

Basi alipofikia kipeo hiki, Muumba wa haki akajitokeza akamdaka kwa kumgharikisha hata asipate kauli ya kwi! Seuze shahada!

Kwetu sisi, yaweza kuwa mfano wa Fira-uni, ni jambo la mbali sana ki-wakati na mahali (time and space). Kwa hiyo lisituguse sana. Lakini hebu tuangalie mifano iliyo karibu nasi ambayo inaonyesha kutakabari kule kule na kwa bahati mbaya wanaingia wanasiasa z a i d i k u l i k o wa t u wengine. Mfano wa karibu tutauanza kwa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye kwa j ins i Tanzania ilivyomtukuza, alifikia hadhi ya utume na kwa wengine hata uungu haukuwa mbali naye –astaghfirulaah! Naye kwa kupata kichwa, akabweteka, akawa jimbi anayewika.

S i k u m o j a k a m a sikosei mwaka 1998

au mwanzoni mwa mwaka 1999, katika moja ya vikao vyake m w a l i m u a l i s e m a kuwa anashangaa sana kwanini mtoto mchanga hufa. Hilo lisitoshe. Akasema yeye ana tamaa ya kuishi hadi amuone Rais wa Awamu ya Nne (wakati huo haijajulikana kwamba atakuwa JK).

Akiyasema hayo , a l i k u w e p o M z e e Ruksa , Al i Hassan Mwinyi ambaye ama kwa dhihaka au kwa h i v y o k u m t u k u z a Mwalimu, alimwambia, “Nakuongeza miaka m e n g i n e m i t a n o , mwalimu!” Jumla ikawa wamepeana miaka 85 kama hivyo ya kuishi kama kwamba wao ndio Miungu. Mwaka ul iofuata Mwalimu Nyerere akafa! Ikawa ndio mwisho wake huo na hakuna aliyeweza kumwombea asife!

Yupo Bwana mkubwa mmoja alikuwa Mkuu w a M k o a k a t i k a m o j a ya m i k o a ya Pemba. Huyu aliwahi k u u n ya y u a m k o n o akasema kama kuna Mungu nauonyoosha huu mkono , naaukunje huyo mungu! Mwenyezi Mungu kwa vile ana u w e z o m k u b w a , a k a u k u n j a m k o n o wa bwana mkubwa h u y o . A k a z i k w a vipande vipande hadi

a k a m a l i z i k a . B i l a shaka tukilitaja tukio hilo, haraka haraka tutamkumbuka pia yule aliyekuwa kinara wa uharamia kule gereza l a B a m k we K i i n u a Miguu. Yaliyomkuta h a t a a n a z i k w a kipande kipande hadi akamalizika, inatisha hata kusimulia hapa. L a k i n i n d i o A l l a h anasema, Fadhakkir, tunakumbushana ili tuwaidhike turudi kwa Mola wetu.

Wapo wengine ambao walivuka mipaka ya kejeli, jeuri na dharau dhidi ya wapemba. Wakawa wanaj iona kama wao na Mungu wa n a m k a t a b a wa pamoja wa kufanya watakavyo. Hawajafa, lakini yameshawakuta ya kila aina. Ya aibu na fedheha. Ya udunifu na udhalilifu. Hatima yao hatujaijua kama tulivyokuwa hatujazijua hatima zetu sote, kila mmoja na yake.

M w a n a d a m u n i mnyama aliyetukuzwa lakini mjinga hata kuliko baadhi ya wanyama kwa sababu hajifunzi kwa waliomtangulia. Muda si mrefu, wapo tuliokuwa nao wakiwa na nguvu tele inayotokana na shibe ya marupurupu na mafao ya kuwa katika siasa za nchi hii, ghafla tunapata habari k u wa wa m e s h a a g a

dunia wakati siku tatu tu zilizopita walikuwa wakijinadi na kujilabu kwa madebusi kuwa nchi hii, CCM hawatoi.

W a p o w a t u wanasikika wakinadi kauli za kwamba nchi haitatolewa kwa kura, labda imwagike damu. Hapa ni Mapinduzi D a i m a . K i l a m t u anajua kuwa CCM nchi hawatoi. Ila hakuna haja ya kuropoka na kupitisha mipaka hadi kufika kutishia kuuwa w a t u k w a s a b a b u ya vyeo na uluwa. Huwezi kujua, kama ambavyo waliotangulia hawakujua. Kauli mbaya na za kufru kama hizo, zaweza kuwa za kuagia dunia.

H a k i k a Z a n z i b a r h a i h i t a j i v i f a r u k u i w e z e s h a C C M kutawala . Inahi ta j i ‘wembe ule ule’ tu wa kuinyolea CUF ambayo haina ubavu wa kugoma kutia maji nywele zake zisinyolewe na CCM. CCM wakiwa na wembe tu hujinyolea tu kila siku na hakuna liwalo. Hakuna haja ‘Wana-CCM nyie kindakindaki’, wengine wakikuiteni wahafidhina, kupayuka na kumpa nafasi Malaika wa dhambi kuharibu wino bure.

Nyie subirini uchaguzi ukifika watu wapige kura kisha mtangazwe washindi. CUF kama kawaida yao watalia siku mbili kisha wataunda u o n g o m w e n g i n e w a k u w a a m b i a w a n a c h a m a w a o kwanini hawakushinda uchaguzi. Hili halina shaka. Ndio mazoea yao wala sio geni tena! Hamna haja kutishia kumwada damu au kutoa maneno ya kufru!

W a l i k u w e p o waliokuwa na nia ya kuirudisha Zanzibar kwenye fujo za kisiasa kwa kuvunja Serikali ya Umoja wa Kitaifa, h a w a k u f a n i k i w a . Wametangulia mbele ya Haki. Mwenye pupa, hadiriki kula tamu!

N a h a p o n d i p o tukasema, tujihadhari na dunia. Dunia hadaa, yaghilibu shujaa! Mungu a wa s i t i r i w e n z e t u waliotangulia na sisi atupe mwisho mwema.

Amen!( Imenukul iwa na

kuhaririwa kwa hisani ya mtandao wa Mzalendo)

ALIYEKUWA Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Marehemu Salmin Awadh Salmin.

Page 9: ANNUUR 1167a.pdf

9 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala/Tangazo

Ubungo Islamic High School imeandaa mafunzo maalum kwa wanafunzi wa Kiislamu wanaorudia Mitihani ya Kidato cha Nne 2015 ambao wanatafuta sifa ‘Credit’ za kujiunga na Kidato cha Tano, 2016.

Masomo yanayofundishwa ni: Elimu ya Dini ya Kiislamu, Arabic, Kiswahili, Kiingereza, Civics, History, Geography, Basic Mathematics, Physics, Chemistry, Biology, Commerce na Book-Keeping.

Muda wa masomo: Jumatatu – Ijumaa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.Kuanzia Machi 1, 2015 hadi Septemba 30, 2015. (Kwa muda wa miezi SABA)

Uandikishaji umeanza Fika ofisi ya Mkuu wa Shule Ubungo Islamic High School kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 8:30 mchana. Fomu zinapatikana BURE.

Kwa mawasiliano zaidi: 0687 820895, 0657 350172, 0714 888557

Wahi Mapema nafasi hii adhimu

Wabillah Tawfiiq

MKUU WA SHULE

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Ubungo Islamic High SchoolMafunzo maalum ya wanaorudia Mitihani

ya Kidato cha Nne 2015

NATAMANI enzi z i le zingerudi na zama hizi zikapotea na kuwa ni historia kwetu hasa katika suala zima la uongozi wa chama chetu (CCM). Mimi kama mimi sikubuhatika k u p a t a e l i m u n z u r i , lakini pia ninashukuru ya kwamba nilijaaliwa kupata fursa muhimu ya kujifunza mambo mengi n a u l i m w e n g u k w a ujumla. Lakini kwa kiasi funzo kubwa na ambalo najivunia nalo ni jitihada za Wazee wangu kwa kule kuniasa sana juu ya kukaa kwa wema na watu na la muhimu ni kuheshimu yale mazuri yao huku nikiaswa pia kuvumilia mabaya yao kwani hakuna mkamilifu kwa vile sote ni binaadamu.

B i n a a d a m u t o k e a kuzaliwa kwake hupitia nyakat i tofauti z i le za uchanga wake lakini pia za kupevuka kwake. Katikati ya nyakati hizi, hupatikana ule wakati mjarabu na kipekee katika maisha ya Binaadam. Inawezekana kipindi hichi cha mpito kwa muhusika kikawa na faida kubwa kwake na jamii iliomzunguka au ikawa ni hasara kubwa hata kwa ile jamii mzima iliomkuza na kumlea kiumbe yule. Lakini tukumbuke tu ya kwamba falsafa hii sio tu kwa Mwaanadamu, lakini hata kwa kitu chochote kile ambacho hupitia nyakati tofauti kama Binaadam.

Wanafalsa mashuhuri walifikia mahali wakasema k w a m b a k a t i k a i l e n y a k a t i y a m w a n z o , yaani uchanga baada ya yote yatakayotendeka , kinachofuatia ni kipindi cha kati na mwishowe kufikia tamati, yaani uzee. Hapa tena tunaambiwa kiumbe yule hurejea katika ile hali ya mwanzo. Kwa lugha nyepesi ni kusema kutoka uchanga na ile hatua ya mwisho ya uzee ni kurudia tena uchanga. Wanafalsafa hao walienda mbali na kusema kwamba baada ya yote yaliopita, basi kiumbe huyu hurejea katika hali yake ya uchanga hata kimaumbile na uhalisia wake. Katika hatua hizi zote, mara nyingi hujitokeza faida pamoja na hasara zake.

U k w e l i w a f a l s a f a h i i i m e n i p a f u r s a kukipima chama changu ninachokipenda sana yaani C.C.M hasa katika suala la uongozi tokea Mapinduzi ya n a y o i t wa m a t u k u f u ambayo mimi nayaheshimu sana kwani nafuata nasaha za wazee kwamba heshimu mazuri na vumilia maovu. Hii ni kusema ovu kwako ni jema la mwenzako kwa mtazamo wake. Hata hivyo inafika wakati unajiuliza, hivi hizi fikra na mawazo yangu yana ukweli au ndio hivyo funika kombe…apite.

Hapa nakumbuka Enzi zile, zama hizi na uongozi wa chama changu. Ni

Zanzibar ya zamani imepoteaHivi sasa ni shari na balaa tupuYote hii kwa sababu ya CCM yetuInaongozwa kimagubegube tu!

MZEE Abeid Aman Karume (kushoto), Mwalimu Julius K. Nyerere (katikati) na Hassan Moyo.

Na B. OLE,

miaka hamsini na ushei sasa tokea Mapinduzi kwa wenye umri unaonizidi mimi wataelewa jinsi mapinduzi yalivyotokea, jinsi viongozi walivyopania kuyatumia Mapinduzi yale kama silaha ya kuleta umoja, usawa na maendeleo Visiwani. Uchanga ule wa Mapinduzi yale tulishuhudia mambo mengi ndani ya Serekali tokea Wananchi na viongozi wake. Enzi ile tulikuwa na Serikali madhubuti, viongozi imara, vijana waliosoma na kuelimika, heshima na adabu kwa wote. Lakini hata sheria zilikuwa madhubuti na zikifanya kazi kwa kila mmoja pindipo akipindisha sheria.

W a l e w a z e e w e t u w a t a k u m b u k a h a t a Mavalantia walivyokuwa wakifanya kazi zao kwa uaminifu mkubwa.

Waswahil i wanasema kuishi sana ni kuona mengi. Falsafa hii mimi naikubali licha ya kwamba sina Elimu lakini ifike mahala tukubali kwamba Chama changu ninachokipenda kimepoteza dira na muelekeo. Yale y o t e y a l i y o a c h w a n a k u we k e wa m i s i n g i n a maadili yamepotea. Leo chama changu kimekuwa cha kihafidhina, kubaguana, rushwa, ufitinishaji kwa sisi wenyewe kwa wenyewe. Lakini zaidi ni kuona chama

chama changu kinaendeshwa kimagubegube tu.

Zama hizi chama changu k i m e k a b i d h i wa Vi j a n a ambao hata wao wenyewe wanashindwa kujiongoza. Lakini kama hilo halitoshi, h a o t u n a o a m b i w a n i Wazee wa chama wenye vyeo vya juu, hata busara hawana sikwambii Elimu ya Kuongoza watu. Silaha zao kubwa ni matusi yenye kugombanisha Wanajamii. Hivi tu j iul ize , ni wapi tunaelekea zama hizi?

Kilichokuja kunishangaza zaidi ni kuona kiongozi wangu mmoja Mheshimiwa sana, kiongozi mwenye nyadhifa nyeti katika serikali ya Zanzibar akizungumza pumba na kuwakashifu wapiga kura wake katika jimbo ambalo lilimchagua kwa kuwapa vitisho kuwa atawafanya kitu kibaya kama walivyofanyiwa Masheikh wa Uamsho. Hivi zama hizi Zanzibar inaongozwa na akina nani? Watu kamahawa i n a k u w a j e z a m a h i z i wanakuwa viongozi !

Zama hizi tunashuhudia mengi, Zanzibar ya zama z i le imepotea . Leo h i i mgeni kutoka Mrima ndio anaeonekana ndie Binaadam kamili lakini masahibu zangu kutoka kisiwa cha mbali hawa ni wahaini na wana mji wao. Hivi tujiulize Wazanzibar tunaelekea wapi? Hii ni aibu na fedheha kwa chama changu na Serikali tunayoiongoza. Mimi kama mimi sioni fahari kuona Viongozi wangu wanapanda kwenye majukwaa huku wakihubiri matusi ya kashifa tokea mwanzo hadi mwisho. N a t a m a n i m wa k a h u u nibadilike na kwa akili yangu fupi niwaunge mkono wale wanaohubiri umoja, upendo na maendeleo.

changu ninachokipenda kimekosa muelekeo wa ushindani kidemokrasia na kimaendeleo. Lakunisikitisha ni kuona kwamba chama

changu hakina mtetezi hapa Visiwani. Viongozi hawana Elimu lakini pia wamekosa muelekeo na kutokana na hali hii ni dhahiri kwamba

Page 10: ANNUUR 1167a.pdf

10 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Ni yale yale ya Dowans, SymbionInatoka Uk. 7kupumzika baada ya kufanikisha uvamizi huo na ukaliaji kimabavu Iraq kinyume na Haki na Sheria zote za Kimataifa pamoja na Maazimio ya Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama.

David Moffett (23) na Brett Richard Mallinson (20), walifikishwa katika Mahakama ya Kisutu, ikidaiwa kuwa November 10 katika Hoteli ya- Silver Sands Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, wawili hao walimpa Ms Ulikaye Paundi 37 ili alale nao wote, akiahidiwa kuwa watamuongezea pesa baadae, lakini wakaishia kumuuwa.

Sasa uliza, nini ilikuwa hatma ya kesi ya Mtanzania mwenzetu huyo Conjesta Ulikaye! Ilikuwa sawa n a i l e ya Wa z u n g u wengine waliomlazimisha msichana wa Kitanzania, kunajisiwa na mbwa wao. “Dismiss case”-Hakuna kesi. Waliachiwa wakarudi makwao.

Mheshimiwa Samwel S i t t a , u k i s i k i a I r a q i l i va m i wa , n i k we l i ilivamiwa na watu wasio na hat ia kuul iwa na mpaka sasa inakaliwa n a w a t u w a n a z i d i kuuliwa. Wamarekani na Waingereza waliovamia I r a q n a k u m p i n d u a S a d d a m H u s s e i n , hawakuwa na uraia wa Iraq na Marekani.

Ukisoma kuwa Nigel David Moffett na Brett R i c h a r d M a l l i n s o n , walikuja Tanzania na kumuuwa Mtanzania m we n z e t u , n i k we l i C o n j e s t a U l i k a y e , aliuliwa na askari hao wa Uingereza. Lakini ukisikia ‘Jihad John’ amchinja James Foley, alijisemea M h e s h i m i w a R a i s Kikwete, akili ya kupewa, changanya na yako. Soma pia na: ISIS actor: Jihadi John, crudely constructed propaganda videos, designed to start a new war at home, and abroad. 2. Jihad John Hoax. 3. The Destabilization Doctrine: ISIS, Proxies and Patsies., kabla ya kuamini unachoambiwa kuwa kilifanyika.

Nimalizie kwa kusema kuwa nakubaliana na h o j a ya M o h a m m e d Ghasani kuwa njama na mbinu chafu kama hizi z inazowaki l ishwa na kauli za Mheshimiwa Samwel Sitta, zisingeweza k u f a n i k i w a k a m a

kusingekuwa na ujinga na kutojifahamu kwa walengwa.

Na Ghasani ametoa

Hata hili tuseme Eemen! Inatoka Uk. 7

nyumba zao na maduka yao, unachotarajia nini? Unachotafuta nini?

Al i sema na kuho j i Kole Shettima, ambaye n i m w e n y e k i t i w a taasisi i l iyopo Abuja inayojulikana kwa jina la Center for Democracy and Development. (Tazama: Nigeria accused of killing 185. HRW: Satellite images reveal 'Nigerian Army abuse' in Baga. 2013 Baga massacre)

Z i p o t a a r i f a z inasambazwa kuwa B a g a n i k a t i k a m i j i inayodhibitiwa na Boko Haram, na ndio sababu jeshi lilifikia kufanya mauwaji hayo, japo wenyewe jeshi wanasema kuwa idadi ya waliouliwa haikufikia 200, ila wanakiri kuuwa na kuchoma moto nyumba, i l a z a B o k o H a r a m . Lakini wanasema hivyo kwa sababu watu wote ni Waislamu na Khamsa Swaaalt. Labda waseme walikuwa wakifanyia kazi ile ‘amri ya kidini’ ya Askofu Oyedepo ya kuuwa na kumkata shingo kila anayefanana, “looks like”, na Boko Haram. Kwa maana hiyo kila Imamu wa Misikiti na kila Sheikh wa Baga, atakuwa “looks like” Abubakar Shekau (kwa mavazi na ndevu)!

Lakini swali moja bado linawatatiza kujibu: Kama Baga inadhibitiwa na Boko Haram, na kama wakazi wa Baga ni Boko Haram, kwa nini sasa Boko Haram hao waue watu wa Baga? Hiyo si sawa na kusema kuwa wamejiuwa wao wenyewe?

Inawezekana taarifa hizi zikaonekana kuwa za mbali. Ni za Nigeria. S io Tanzania . Lakini u k i t i z a m a k a s i y a mambo yanavyokwenda

tunakoelekea ni huko huko. Ilipoibuka ile kadhia ya Amboni, magazeti mengi yakijitahidi kupaka picha kuwa waliokuwa wakipambana na polisi ni Waislamu, Wasomali au Waarabu kwa mwonekano. Kwa hiyo, “looks like” Al-Shabaab. “Looks like magaidi.”

Hebu soma maelezo haya kutoka NIPASHE ya Februari 17, 2015 ukurasa wa 25. Yanasema:

“Watu hao walikuwa

wakipendelea mashati ya mikono mirefu, suruali za jeans zilizokatwa chini na kanzu.”

“Hawa bwana walikuwa wanavaa short jeans, yaani wamekaa ki-jihad zaidi na yeboyebo chini. …mashati yao ni ya mikono mirefu na kanzu. Wakati mwingine walikuwa wanavaa na kofia juu ya balaghashia.”

A n a c h o t u a m b i a mwandishi huyu wa N I PA S H E n i k u w a

Inaendelea Uk. 11

mfano mzuri na hai. Ile hali ya kuhasimiana, kupigana vijembe na kutukanana

kule Dodoma wakati wa Bunge Maalum la Katiba. Watu hawajui wanadai

nini, wala kipi ni katika masilahi ya Zanzibar na watu wake.

Mhe Spika akiwa na wenyeji wake pamoja na sehemu ya ujumbe wake. Wa kwanza kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe, Waziri Mhe William Lukuvi. Wa kwanza kushoto ni Mhe Ally Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman. Mhe Spika alipokuwa katika ziara rasmi ya kibunge ya siku sita mwaka jana.

WANAWAKE wa Kiislamu wa Nigeria wakiw nje ya nyumba yao baada ya kubomolewa na majeshi ya Nigeria kwa madai ya kupambana na Boko Haram.

Page 11: ANNUUR 1167a.pdf

11 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 201511 AN-NUURMakala

Inaendelea Uk. 14

Hata hili tuseme Eemen! Inatoka Uk. 10

utawatambua wahalifu (magaidi) waliokuwa wakipambana na polisi na JWTZ kule Amboni Tanga, kwa balaghashia, suruali fupi na kanzu (alisahau kutaja ndevu).

N d i o ya l e ya l e ya “anyone who looks like” ya Askofu David Olaniyi Oyedepo.

Mara kadhaa yakitokea m a t u k i o ya k i h a l i f u yanayotakiwa kutiwa nakshi ya ugaidi, lazima utas ikia kaul i kama, w a l i o n e k a n a w a t u w a l i o v a a k a n z u n a vibandiko au ‘Waarabu”. Yote hii ni ile ile “Looks like” ya Askofu David Olaniyi Oyedepo.

Picha sasa ipo wazi

Katika Nigeria, picha sasa ipo wazi kabisa. Kwamba jinamizi la Boko Haram lilipandikizwa kwa makusudi na wala sio Waislamu wanaodaiwa kutaka kus imamisha S h a r i a h . B a a d a y a kusimika kit isho cha ugaidi ul iodaiwa wa Boko Haram, wakidaiwa kuwa ni Waislamu na ikakubalika hivyo ndani na nje ya Nigeria, waliofanya mchezo huo kupitia “false flag terror attacks”, kwa maana ya mauwaji ya kigaidi ya kupanga kisha kusingizia Waislamu, sasa wanatumia ugaidi huo wa Boko Haram waliotengeneza wenyewe, kuwa sababu na kisingizio cha kuuwa Waislamu.

K u p i t i a u g a i d i wa kupanga, k i t i sho kimekuwa kikubwa sana, kiasi sasa Askofu David Olaniyi Oyedepo anasema k u wa a m e t u m wa n a Mungu ili aiokoe Nigeria na Afrika kwa ujumla kutoka na ugaidi wa Waislamu.

“God has anointed me to lead a revolution against Islamic jihadists”.

Anasema askofu huyo anayetajwa kuwa tajiri k u l i k o m a a s k o f u n a wachungaji wote Nigeria. Ana ndege binafsi nne (4). Anasema, imebidi Mungu amtume kuiokoa Nigeria kutokana na Uislamu k wa s a b a b u s e r i k a l i imeshindwa. Na katika mahubiri hayo, ambapo pia alichukua fursa hiyo kumpigia kampeni Rais G o o d l u c k J o n a t h a n , anasema kuwa Kanisa halitaruhusu Muislamu kutawala Nigeria.

“What a mess…Must

the North continue to rule? What devils!”

A l i s e m a A s k o f u Oyedepo akiwafananisha W a i s l a m u k u t o k a Kaskaz in i mwa nchi hiyo kuwa ni mashetani “devils”, na kuahidi kuwa hataruhusu mtu kutoka Kaskazini kuwa Rais Nigeria katika uchaguzi ujao. Katika kulitilia mkazo hilo, alisema kuwa yeyote a t a k a ye m p i n g a R a i s Jonathan, atamfungulia mlango wa Jahannamu.

“We Will Open The Gate Of Hell On Those Who Oppose You”.

A l i s e m a P a s t o r Oyedepo, akiwaambia waumini wake kuwa maneno hayo alimwambia

Rais Goodluck Jonathan alipomtembelea katika k u w e k a m i k a k a t i k u h a k i k i s h a k u w a a n a s h i n d a k a t i k a u c h a g u z i m k u u ambapo anakabil iana na Mohammed Buhari, m g o m b e a M u i s l a m u kutoka Kaskazini.

Maneno ya Askofu huyo kwamba atawafungulia milango ya Jehennamu w a t a k a o m p i n g a Jonathan katika kupiga kura, yamepelekea Rais wa zamani Olusegon Obasanjo kuhoji:

“My question is, How and Why does a man of God have the key to hell and not Heaven. Is that his home?”

Kwamba, kama huyu

ni mtu wa Mungu, kwa nini awe na ufunguo wa Jehannam badala ya Mbinguni (Peponi). Je, Jehannam ndio nyumbani kwake?

Lakini habari haishii hapo . Askofu David Olaniyi Oyedepo anadai kuwa hata sensa zimekuwa zikisema uwongo maana y e y e a n a o n a k u w a Kaskazini kuna vichaka tu vilivyojaa wanyama, hakuna binadamu.

“Where are the human be ings? I wouldn’t be surprised if all the North is equal to Lagos! We have never had a successful census in this country.”

Ufupi anachosema ni kuwa Nigeria ni nchi ya

Wakristo, kwani hata huko Kaskazini kunakodaiwa kuwa kuna Waislamu wengi zaidi ya Wakristo, si kweli. Anasema, huko Kaskazini ni vichaka vitupu na kama wapo Waislamu, basi idadi yao (Nigeria nzima, waweza kuwa sawa na wakazai wa Lagos pekee).

Ya Biafra yanarudi

“Tulia, s iki l iza hii ! M a a n a h a p a A s k o f u a n a t a k a k u a n g u s h a bomu zito zaidi”. Ndivyo anavyosema mchambuzi katika televisheni iitwayo Dunamis TV inayomilikwa na Mchungaji Dr. Paul Enenche wa Abuja.

“I decree the curse of God upon them (Muslims in the North). Lord, if it is Your will to break up Nigeria – break it now!”

“Laana ya Mungu iwe juu yao (wananchi wa Kaskazini-Waislamu wa Nigeria). Mungu, kama ni katika mapenzi yako kuwa Nigeria ibeguke mapande, ivunjilie kwa mbali sasa.”

Waumini wanashangilia na kuruka ruka wakisema “Eemen!”

“Jamani, na hili tuseme E e m e n ? ” A n a u l i z a mchambuaji huyo katika televisheni ya Kikristo. A k i f a f a n u a z a i d i mchambuzi huyo anasema kuwa anachofanya Askofu Oyedepo, kwanza ni kuhamasicha mauwaji holela na machafuko katika nchi. Pili, anahimiza na kuwafitisha wananchi wa Nigeria katika kiwango cha kutaka nchi igawike-Kaskazini na Kusini. Cha kushangaza ni kuwa, watu wanashangilia na kuitikia Eemen!

Lakini cha kut isha anasema kuwa haionyeshi kuwa kuna hatua zozote z i n a z o c h u k u l i wa n a serikali dhidi ya uchochezi na uhaini huo. Bali la kutisha zaidi na kwa hakika kustaajabisha na ambalo halieleweki kabisa kwa wengi, ni kuwa Askofu Oyedepo, ni katika watu wa karibu sana wa Rais Goodluck Jonathan kama alivyo Mchungaji Ayodele Joseph Oritsejafor. Hawa ni watu ambao huingia Ikulu bila ya miadi. Na amekuwa aki fuatana na Rais Jonathan katika kile kinachoitwa ‘Hija’, kwenda Israel kuzuru sehemu muhimu za kidini.

K a m a i l i v y o m c h a n g a n y a mchambua habari wa

ASKOFU David Olaniyi Oyedepo akishuka kwenye ndege yake Nairobi mwaka 2013.

NDEGE ya Askofu David Olaniyi Oyedepo ikitua kwenye uwanja wa ndege Nairobi, Kenya.

Page 12: ANNUUR 1167a.pdf

12 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 201512 MAKALA

M W E N Y E Z I M u n g u kamuumba mwanadamu na akamjaalia uwezo wa kufikiri (akili), ili kuweza kubainisha jema, zuri na baya. Kutambua lenye madhara na lisilo na madhara, kujua ni lipi lenye faida na maslahi kwake na kwa viumbe wanaomzunguka na lisilofaa. n.k

A i d h a M w e n y e z i M u n g u a m e m j a a l i a mwanadamu utawala wa ulimwengu juu ya viumbe wengine na kumfanya kuwa kiumbe bora kabisa. Akili hung'azwa na fikra. Uwezo wa kufikiri kwa binadamu ni sehemu ya maarifa ambayo yanajikita katika kutumia akili . Hazina hii ni adimu kwa viumbe wengine. Madhara ya duniani wanayopata binadamu husababishwa na binadamu wenyewe, h a s a w a l i o s h i n d w a kutumia hazina yao ya akili kuepusha majanga.

M w a n a d a m u k w a kutumia uwezo wa akili yake (tafakur), anastahili kutenda mambo kwa weledi na kwa yakini, ili kupata matokeo bora na yenye maana kwake tofauti na viumbe vingine.

Nimelazimika kuanza na maneno machache juu ya sifa na ubora wa mwanadamu, kufuatia kasumba i l iyoki thir i kwa baadhi yetu sisi Waafrika kujibadili rangi ya ngozi na kuvaa viungo bandia. Huwa najiuliza pamoja na kuwa na sifa kwa nini Waafrika h u s u s a n w a n a w a k e wanajibadilisha rangi? Kwanini weupe unapewa maana zaidi miongoni mwa jamii ya watu Weusi?

Wanawake wengi barani Afrika wanaj ichubua n a k u t u m i a v i u n g o bandia kama nywele bandia, wakiamini kuwa kufanya hivyo ni kuwa na mvuto zaidi na angalau k u s t a a r a b i k a k a m a Wazungu! Kasumba ya kutaka kufanana na watu Weupe imeharibu akili za watu wetu. Wakishindwa kufikir i , nini t i ja ya kutumia pesa nyingi kuharibu maumbile ya asili kwa kemikali na

Kalamu i mkononi, ukweli kuukashifu,Japo mchungu moyoni, jarima kuukhalifu,Mashekhe sikilizeni, pamwe na Maaskofu,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani itongoeni, kwa mizani adilifu,Viongozi wambieni, ukweli pasi na hofu,Huru utakuwekeni, kwa insi na kwa RAUFU,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani hapa nchini, imekuwa mausufu,Si Bara si Visiwani, viongozi huisifu,Kwa kauli za kinywani, vitendo iso sadifu,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani ya mdomoni, kathiru 'ishatukifu', Twataka ya matendoni, yenye tutumbi sharafu,Ninyi hilo maizini, na wao muwaarifu,Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani itazameni, kwa uyuni yakinifu,Mashekhe jihadharini, na wa fikara upofu,Ushenga uepukeni, kuridhi 'Watakatifu',Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani ichungueni, kwa mapana na marefu,Ukweli mtabaini, wenye nayo maarufu,Muhali wao sijini, kuwekwa kwa uhalifu!Penye dhulma muhali, amani kustakiri.

Amani gani ambeni, haswa mnoisharifu?'Wasota' wenzenu 'ndani', dhamana si yao kufu!Wangapi jiulizeni, 'lupango' Maaskofu?Amani kustakiri, penye dhulma muhali.

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

KONGAMANO LA UWAWAMWA(PENYE DHULMA, AMANI CHANGA LA JICHO!) Huu ni ukoloni dhidi ya akili zetu

Na Shaban Rajab uchafu. Faida yake ni ili tu, afanane na watu Weupe na kwa kufanana huko, basi atakuwa amestaarabika na kuheshimika!

Wanawake na hata baadhi ya wanaume wa Kiafrika wanaangalia uwezekano wa kubadili rangi za ngozi, pamoja na kuthibitika kwamba rangi zetu za ngozi ni Nyeusi na nzuri, wengine ngozi ni angavu na kukoleza huo uzuri.

Ajabu ni kwamba kuna wanawake na hata baadhi ya wanaume wenye ngozi nyeupe, lakini bado wanataka kuongezea zaidi ya rangi waliyonayo. Kumekuwa na kasumba kuwa na ngozi nyeupe kumeonekana kuwa kwa kipekee zaidi kwenye jamii ya watu wengi walio na ngozi nyeusi. Ni jambo linalofahamika kwamba bara la Afrika limekumbwa na matatizo mengi sana tangu ujio wa wakoloni na hata baada ya wakoloni kuondoka.

Lakini kusema kweli, t a n g u u l i p o o n d o k a ukoloni wa vi tendo, Wa a f r i k a wa m e b a k i na mateso makubwa ya ukoloni wa kifikra. Ukoloni umekuwa mbaya zaidi , na huu ndiyo unaofanya yote haya yatukute. Naona huu ndio ukoloni wenye nguvu kubwa kuliko hata wakati wakoloni walipokuwa wamekalia ardhi yetu.

Waafrika tunaonekana sasa kama hatuna uwezo wetu wa kufikir i na kufanya maamuzi yetu bila ushawishi wa sera za Kimagharibi. Ukitizama kwa undani jinsi mambo yanavyokwenda katika nchi zetu za Afrika, ni dhahiri kabisa kwamba wakoloni waliondoka ila ukoloni bado upo. Nikisema hivyo sina maana ya kubeza juhudi za wazee wetu waliotoa maiasha yao na gharama kubwa kutetea kwa nguvu zote uhuru na heshma za nchi zetu, la hasha!

Ta t i z o n i k wa mb a kizazi cha wapigania uhuru, watu waliokuwa na dhamira ya dhati ya kuikomboa Afrika kifikra na dhidi ya dhuluma za mabeberu na kujitawala wenyewe, kizazi hicho

kimekwisha na wachache waliobaki hawana nguvu wala ushawishi wowote j u u ya m a a m u z i ya msingi ya kujenga hatima ya mataifa yetu na bara letu kwa ujumla. Sasa tumebaki na kizazi cha watu wasiojali, wasiojua uchungu hasa wa gharama za uhuru tuliopewa. Kizazi ambacho hakioni shida kushawishika kuvuruga misingi ya uhuru na kujitawala kwa ajili ya ustawi wetu. Pamoja na kwamba bado tunateswa na ukoloni mambo leo wa kiuchumi na kisiasa, lakini ukoloni wa kitamaduni umeingia kwa kasi kubwa zaidi hasa katika karne za 20 na 21 kwa tiketi za ustaarabu na utandawazi na waathirika wakubwa wakiwa watoto na vijana.

Ni dhahiri kwamba vijana wengi wa Kiafrika hawaelewi maana halisi za dhana za ustaarabu na utandawazi. Akili wanazo, lakini bila kutafakari kwa akili hizo. Wanaona ni jambo lililo sawa kuiga kila kinachofanywa na watu wa mataifa yaliyoendelea.

M a t o k e o y a k e t u m e p o t e z a m i s i n g i mizuri ya kimaadili na asili yetu kama Waafrika k w a k u f i k i r i k u w a ni ushamba. Huo ni utumwa! Hili ni janga! Tunakoelekea si kuzuri, na kabla hatujajuta, ni vyema tukumbuke kuwa hakuna vita mbaya kuliko vita vinavyoharibu watu akili. Hivi ni vita ambavyo vinalenga kuvunja msingi wa kistaarabu vya kila taifa na kuondoa uwezo wa watu kufikiri.

Tunaposoma makala h i i t u t a f a k a r i k w a kina, tunatumia vizuri akili zetu kwa maslahi yetu au tunavamia na kukurupukia tu mambo kama mkia. Nadhani, wakati umefika Waafrika tujitambulishe kama watu tuliokomaa na mataifa mengine yatutambue hivyo! Tutathibitika hivyo endapo tutaweza kutumia uwezo wa kuchambua na kuchukua mazuri tu katika mambo yanayoletwa na watu wengine.

Tukatae kwa dhati ustaarabu na utandawazi u n a o l e n g a k u o n d o a uwezo wetu wa kufikiri. La sivyo, tukubali kuendelea kuwa watumwa kwa vizazi vyote. Na hilo ni janga!

Naandiliza kusema, kwa Raufu jina lake,Swala nyingi na Rehema, zende kwa Mtume wake,Duwa ziwafike hima, wote Maswahaba zake,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Leo nimekuja tena, na swali langu lifike,Kwenu malenga vijana, busara mzipeleke,Fanyeni bahathi sana, jawabu bora litoke,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Hili jambo lanitanza, sipati undani wake,Tena linanishangaza, linanitia makeke,Mwili nina uuliza, nini hasa raha yake,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Ukenda kufanya kazi, wataka upumzike,Bora ufanye ajizi, kutwa ukaghururike,Unanitia simanzi, niupe nini ushike,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Mwili wataka kulala, daima usiamke,Hautaki hata swala, kheri ukaadhibike,Hueza sahau Mola, kuwa ndo Muumba wake,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Kila nikijitahidi, alau ukurupuke,Unafanya ukaidi, lala chini upweteke,Hautimizi miadi, kwenda mahali ufike,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Hayo machache yatosha, mradi yafahamike,Yanotia mshawasha, majibu muyaandike,Nyote nawakaribisha, awezae kazi kwake,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Sasa napiga tamati, jambo jengine nishike,Japo mwili hautaki, uwache ukukurike,Usubiri umauti, uone jeuri yake,Mbona haueleweki, mwili raha yake nini.

Zainab Mtima Chuo cha Afya, MbweniZanzibar0777 357 031

Mwili una raha gani

Page 13: ANNUUR 1167a.pdf

13 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala ya Mtangazaji

Israeli soldiers urge dogs to attack Palestinian childBETHLEHEM (Ma'an) -- A video circulating on social media on Monday showed two Israeli soldiers urging two dogs to attack a Palestinian child, who they claimed threw rocks at them.

The video, which was first uploaded Sunday evening, shows the child, pleading for help, after being bit by one of the two dogs which were held by their leashes by the soldiers who continue to incite them to attack him. The child was detained before the dogs attacked

him, and he posed no threats to the soldiers.

One of the soldiers in heard clearly ordering the dog in Hebrew to

maul the child more than once, as he told the child "now who's the coward." The child then began screaming in terror.

RAMALLAH (AFP) -- The PLO is to lodge its first complaint against I s r a e l f o r a l l e g e d war c r imes a t the International Criminal Court on April 1, a senior official told AFP on Monday.

"One of the f i rs t important steps will be filing a complaint against Israel at the ICC on April 1 over the (2014) Gaza war and settlement activity," said Mohammed Shtayyeh, a member of the executive committee of the PLO.

On Jan. 2, the PLO moved to formally join the Hague-based court in a process which is due to take effect on April 1, setting the scene for potential legal action against Israeli officials for alleged war crimes.

I s r a e l r e a c t e d furiously, and quickly m o v e d t o c u t o f f millions of dollars in monthly tax payments it collects on behalf of the Ramallah-based Palestinian Authority, exacerbating an already severe financial crisis.

T h e r e w a s n o immediate response from Israel, with foreign

PLO to file ICC case against Israel in Aprilministry spokesman Emmanuel Nachshon refusing to react to a declaration which he described as "speculative and hypothetical."

O n J a n . 1 6 , t h e I C C a n n o u n c e d " a p r e l i m i n a r y e x a m i n a t i o n " i n t o Israel's actions over a

period beginning in June which included last year's war in Gaza in which about 2,200 Palestinians were killed.

UN figures indicate most of the victims were civilians.

T h e P L O i s a l s o planning to sue Israel o ve r i t s p o l i c y o f

settlement building on land they want for a future state.

Under international l a w , a l l I s r a e l i construction on land s e i z e d d u r i n g t h e 1967 Six-Day War is viewed as illegal and a major stumbling block to efforts to end the decades-long conflict.

BETHLEHEM, (WAFA) – The Israeli army flooded sewage into a Palestinian-owned olive-planted land in the village of Tekoa near Bethlehem, according to a local source.

The village’s mayor, Tayseer Abu Mfarreh, said army soldiers and settlers broke into an area near the village and proceeded to conduct military exercises, during which they flooded sewage into olive-planted fields.

Israeli Army Floods Sewage into Olive Fields

JERUSALEM (Ma'an) – Israeli authorities o n Sunda y o r der ed 83-year-old Palestinian g r a n d f a t h e r A y y u b Shamasnah and his family to voluntarily evacuate their home in the East Jerusalem neighborhood of Sheikh Jarrah before next Sunday in compliance with a final supreme court decision.

Shamasnah lives with his wife, 75, children and grandchildren in a two-room, 65-square-meter house targeted by Jewish settlers who have already evicted several Palestinian families.

The family moved to Sheikh Jarrah after they were displaced from Qatanna village

Israel orders Palestinian family to evacuate Sheikh Jarrah house

in northwest Jerusalem d u r i n g t h e c r e a t i o n of Israel in 1948. They init ial ly paid rent to Jordanian authorities, who were responsible for East Jerusalem until 1967 when Israel occupied the city.

Since 1968, the family has paid rent to Israeli authorities as protected leaseholders.

In 2011, the Israeli government's Custodian for Absentee Property started legal proceedings to evict the Shamasnah family, claiming their rental contract expired in 2008. In May 2013, an Israeli court postponed the eviction until further discussions.

The court suggested during a hearing in May

that the family could remain in the property until the elderly parents die, but settlers who are targeting the property once the family is evicted refused the proposal, according to the owner's son Muhammad.

Speaking to Ma'an Sunday, Muhammad said that the Israeli supreme court decided in August 2013 that his family should evacuate the property before Jan. 3, 2015 to be delivered to the Israeli settlers.

" T h u s , t h e f a m i l y received a letter last Thursday from the settlers' lawyer demanding that they comply with the court decision, or otherwise they will be evacuated by force."

Israeli navy opens fire at Gaza fishing boatsGAZA CITY (Ma'an) -- Israeli naval boats on Monday opened fire at fishermen off the coast of northern Gaza, residents said.

The incident occurred near the neighborhood of al-Sudaniyya, with the fishermen returning to shore for fear of arrest or having their vessels confiscated.

A n I s r a e l i a r m y spokeswoman said she was looking into the incident.

On Sunday, residents said Israeli boats opened fire at fishermen in the ear ly morning . No injuries were reported.

There are around 4,000 Palestinian fishermen in the coastal enclave, 90 percent of whom are poor according to a 2011 report by the International Committee of the Red Cross.

The Aug. 26 ceasefire agreement between Israel and Palestinian m i l i t a n t g r o u p s stipulated that Israel would immediately expand the fishing zone off Gaza's coast, allowing fishermen to sail as far as six nautical miles from shore, and would continue to expand the area gradually.

Since then, there have been widespread reports that Israeli forces have at times opened fire at fishermen within those new limits, and the zone has not been expanded.

Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road – Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email : pict@pal-tz .orgWebsite: www.pal-tz.org

Page 14: ANNUUR 1167a.pdf

14 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Inatoka Uk 11 Hata hili tuseme Eemen! Dunamis TV, ndivyo a m b a v y o M t a n z a n i a yeyote leo anavyosoma habari hizi za Askofu Oyedepo atashindwa kuelewa inakuwaje mtu kama huyu anayehimiza mauwaji na kugawika nchi, anakuwa ndiye rafiki wa karibu wa Rais wa nchi na wakati huo huo anapambwa na vyombo v ya h a b a r i n a h a t a kutetewa.

U k i i n g i a k w e n y e mtandao, tafuta mada hizi: Africa: U.S. Military Holds War Games on Nigeria, Somalia. US Army Prepares For Nigeria’s Possible Break-up (2015). Nigeria: U.S. Speaks On Nigeria’s Break-up. Obama To Visit Ghana- All About AFRICOM? N i g e r i a Ta r g e t e d F o r Destruction: Gordon Duff, US . "Unified Quest 2008" by the Rand Corporation and Booz-Allen.

Ukisoma yaliyoandikwa katika makala hizi na n y i n g i n e n y i n g i z a namna hiyo, kisha rejea sasa usome na kusikiliza haya anayosema Askofu Oyedepo: “Lord, if it is Your will to break up Nigeria – break it now!”

U k i y a c h a n g a n y a hayo, ukiunganisha na mizaha ya “Bring Back Our Girls”, na mengine kama hayo ya ‘mzaha wa Boko Haram’, unaweza kuelewa kazi anayofanya Askofu Oyedepo. Lakini kwa upande mwingine, utajua ni kwa nini inafikia leo mzaha (hoax) wa Abubakar Shekau kuteka kambi ya jeshi unaaminika kuwa ni jambo la kweli. Ni katika mlolongo ule ule wa akina “Jihad John” na Osama Bin Laden.

Ujumbe wa Redio One, ITV

Kinachojitokeza hapa ni kuwa tatizo la Nigeria ni kubwa mno na kwa bahati mbaya Wanigeria wenyewe (baadhi wenye kauli, wenye mamlaka), waliopo serikalini na s e h e m u m b a l i m b a l i muhimu, inavyoonekana wamehiyari kuchuuza nchi yao na kujichuuza wenyewe kwa mabeberu.

I la hapa n imal iz ie kwa kusema jambo moja muhimu. Redio One, wana ujumbe wao ambapo kwa kutumia watu mbalimbali w a k i w e m o m a - R a i s wastaafu, wakuu wa vyombo vya usalama, wasomi, viongozi wa dini na hata watoto wadogo wa shule, ambapo wanaeleza umuhimu wa kulinda

amani iliyopo na kutaka wanaojaribu kuiharibu, wafichuliwe haraka na kuchukuliwa hatua. Ni ujumbe mzuri.

Lakini kama tutakuwa tunaitikia ‘Eemen’ kwa maneno kama yale ya Askofu Oyedepo, ujumbe mzuri kama huu wa Redio

One, pamoja na kutolewa na watu wazito katika nchi, bado hautakuwa na maana yoyote.

Wa p o k w a m f a n o

v i o n g o z i w a d i n i walithubutu kuwahimiza waumni wao kushika mapanga, visu, mikuki na mishale, kupambana na watu wal iodaiwa kuchoma makanisa. Lakini ukitizama hao wanaodaiwa k u c h o m a m a k a n i s a , hakuna ushahidi wowote u n a o w e z a k u t o l e wa hadharani kuwa walitenda j ina i h iyo . K inyume chake, inaonekana kama n i mambo ya kuzua tu , kupandikizwa i l i kupandikiza kitisho kama kile cha Boko Haram, Nigeria.

K a u l i k a m a h i z i zinapofumbiwa macho, i taf ika mahal i , wapo Wakristo wataamini kuwa Waislamu wanachoma moto makanisa yao na kuuwa viongozi wao. Ikifika hapo, wakiibuka wale wachungaji ambao leo wanahimiza wafuasi wao kujihami kwa visu na sime, wakiwaambia wafuasi hao kwamba wakimwona mtu “anayefanana na wachoma makanisa”, hapana shaka b a l a a l a k e l i t a k u wa kubwa. Wala huu ujumbe unaotolewa na Redio One, hautatusaidia kitu.

RAIS Gooluck Jonathan (wa pili kushoto), Askofu David Olaniyi Oyedepo (mwenye tai) wakiwa ziarani Israel.

H A K U N A K a n i s a lililochomwa Yombo Dovya kama walivyodai baadhi ya Maaskofu.

Uchunguzi wa gazeti hili pamoja na ule wa Serikali za Mitaa, eneo hilo, umebaini kuwa taarifa hizo ni urongo na uzushi mtupu.

Awali Maaskofu chini ya Umoja wao unaojulikana

k a m a B a r a z a l a Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) walitoa taarifa wakisema kuwa wa m e g u n d u a m p a n g o ulioandaliwa na Waislamu wa kuchoma makanisa nchi nzima.

K a t i k a m a d a i h a y o wakasema kuwa tayari kikosi maalum cha Waislamu cha kutekeleza hujuma hiyo kilikuwa kimetua Mbeya.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Katibu

Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota a k a w a t a k a Wa k r i s t o kujihami kwa visu, mishale na mikuki” ili kupambana na Waislamu.

Baada ya kueleza na kunukuu kwa urefu yale yaliyosemwa na Katibu Mkuu wa PCT, Askofu David Mwasota, gazeti la

Maaskofu Pentekoste waongoHakuna Kanisa lililochomwa moto Yombo

Msema Kweli likamalizia kwa kudai kuwa wakati “likielekea mitamboni, bado uchomaji moto makanisa Jijini Dar es Salaam ulikuwa unaendelea, ambapo Kanisa la Kipentekoste la Faraja International Yombo Dovya lilikuwa likiteketea, huku jingine la KKKT Yombo Dovya nalo likinusurika k u t e k e t e z wa n a wa t u wanaojiita wanaharakati wa Kiislamu. (na kwamba) Mlinzi wa Kanisa hi lo aliripotiwa kujeruhiwa.”

Katika taarifa yake mbele ya waandishi wa habari, Askofu David anasema kuwa kwa kushika mikuki, visu na mishale, huenda ser ikal i i taz induka na kuwashughulikia Waislamu, kwani anasema kuwa haoni kama serikali inafanya vya kutosha kukabiliana na kitisho cha Waislamu kuchoma makanisa.

Kufuatia taarifa hizo, An nuur ilipiga hodi Yombo ili kujua ukweli wa madai hayo.

K a t i k a u f u a t i l i a j i ikabainika kuwa hakuna k a n i s a l i l i l o c h o m w a moto Yombo Dovya bali habari hizo ni uzushi na uchochezi mtupu, unaolenga kuwafarakanisha Waislamu

na Wakristo na wakati huo huo ukilenga kuwachongea Waislamu kwa serikali.

“ K w a k w e l i s i s i h a p a Yo m b o D o v y a tumeshtushwa na habari hizi, makanisa yaliyotajwa kuchomwa tunayafahamu, si kweli kwamba kuna kanisalililochomwa na ni vyema umekuja mwandishi ukayaona”.

Alisema Bw. Shamte Mwegiro mkazi wa Yombo Dovya.

Alisema kuwa baada ya kusikika habari za kuchomwa makanisa hayo hapo Dovya, taarifa ziliwafikia Wenyeviti wa S e r i k a l i z a M i t a a minne ya Yombo Dovya ambayo ni mitaa ya Uwazi, Makangarawe, Dovya na Msalakala.

B a a d a y a k u p a t a taarifa hizo viongozi hao waliwafuata viongozi wa makanisa yaliyotangazwa kuchomwa moto pamoja na kutizama hali ya makanisa yenyewe.

Taarifa zinabainisha kuwa baada ya kufika mtaa wa Uwazi lilipo kanisa la Faraja International, walikuta lipo salama.

Walipomhoji muhusika juu ya kuripotiwa kuchomwa

moto kanisa hilo, walijibiwa kuwa kanisa hilo halijaungua bali inaonekana kulikuwa na dalili za kuwepo hitilafu ya umeme.

Viongozi hao walikwenda katika Kanisa la Walokole

lililopo mtaa wa Njia Panda kwa Kombo, ambalo nalo liliripotiwa kuchomwa moto.

Kanisa hilo lililojengwa kwa mabati na kuzungushiwa pazia, nako walilikuta ni salama.

Wa l i p o h o j i k u l i k o n i kuenea habari za kuchomwa k a n i s a h i l o , m a j i b u yalikuwa ni moto uliokuwa umewashwa kuchoma taka zilizokuwa jirani na kanisa hilo, uliruka na kuchoma moja ya

pazia la kanisa, lakini uliwahiwa na kuzimwa na haukuleta madhara kanisani.

Kufuatia uzushi huo, tayari viongozi wa misikiti

Yombo Dovya hususan Masjid Swabrina, wametoa tahadhari kwa Waislamu kuwa makin i kufuat ia kuwepo propaganda za kuwapaka matope Waislamu kwa kuwazulia uhalifu. (Habari hii ilitolewa kwa mara ya kwanza katika An nuur Namba 1044 la Novemba 9, 2012. Soma makala uk. 18)

Page 15: ANNUUR 1167a.pdf

15 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

Na Ben Rijal

Na Ben Rijal

MAKALA hii itajaribu kuondosha dhana ambayo walimwengu wamekuwa n a y o k w a m i a k a n a mikaka, dhana ambayo watu wanaamini kuwa tupa baharini ukitakacho bila yakuwa na wasiwasi kwani bahari haiathiriki na uchafu. Makala mbili mfululizo italiangalia suala hili. Makala ya kwanza itazielezea aya zilizomo kwenye Quran zinazoielezea bahari na dondoo juu ya bahari na makala ya pili itaiangalia dhana potofu ya kutupa uchafu baharini na atahari zake.

“ N a t u l i p o i p a s u a b a h a r i k wa a j i l i ye n u n a t u k a k u o k o e n i , t u k a w a z a m i s h a w a t u wa F i r a u n i , n a h u k u mnatazama.” (Surah Al-Baqara, 50)

“Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi , na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara

Jee, Bahari ni Jaa Mwaga Ukitakacho Bahari Itameza?

kwa watu wanao zingatia.” (Surah Al-Baqara, 164)

“Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini n a k u v i l a , k wa f a i d a yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wa n ya m a wa b a r a maadamu mmeharimia Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu a m b a ye m t a k u s a n y wa kwake.” (Surah Al-Ma’ida, 96)

“Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha.” (Surah Al-An‘am, 59)

« Sema: Ni nani anaye kuokoeni katika giza la nchi kavu na baharini? M n a m w o m b a k w a unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa m i o n g o n i m wa wa n a o shukuru." (Surah Al-An‘am, 63)

“Na Yeye ndiye aliye k u w e k e e n i n y o t a i l i

mwongoke kwazo katika kiza cha bara na bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao jua.” (Surah Al-An‘am, 97)

“Basi tuliwapatiliza, tuka- wazamisha baharini kwa sababu walizikanusha Ishara zetu, na wakaghafilika nazo.” (Surah Al-A‘raf, 136)

“Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, wakafika kwa watu wanao abudu masanamu yao. Wakasema: Ewe Musa! Hebu tufanyie na sisi miungu kama hawa walivyo kuwa na miungu. Musa akasema: Hakika nyinyi ni watu msio jua kitu.” (Surah Al-A‘raf, 138)

“Na waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu w a l i k u w a w a k i f a n y a upotovu.” (Surah Al-A‘raf, 163)

“ Ye y e n d i y e a n a y e k u e n d e s h e n i b a r a n a

baharini. Hata mnapo kuwa ma jahaz in i na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkal i ukawazukia , na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo h u m w o m b a M we n ye z i Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.” (Surah Yunus, 22)

“Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!” (Surah Yunus, 90)

“Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akateremsha maji kutoka mbinguni. Na kwa hayo akatoa matunda kuwa ni riziki yenu. Na akafanya yakutumikieni majahazi yanayo pita baharini kwa amri yake, na akaifanya mito ikutumikieni.” (Surah

İbrahim, 32)“Yeye ndiye aliye ifanya

bahari ikutumikieni, i l i kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayo yavaa. Na unaona marikebu zikikata maji humo, i l i mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.” (Surah An-Nahl, 14)

“ M o l a w e n u M l e z i ndiye anaye kuendesheeni marikebu katika bahari ili mtafute katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kukurehemuni nyinyi. “ (Surah Al-Isra’, 66)

“Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo k u v u e n i m k a f i k a n c h i kavu, mnageuka . Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha.” (Surah Al-Isra’, 67)

“Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku v i t u v i z u r i v i z u r i , n a tumewafadhi l i sha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba. “. (Surah Al-Isra’, 70)

“Na pale Musa alipo mwambia ki jana wake: Sitoacha kuendelea mpaka nifike zinapo kutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu.” (Surah Al-Kahf, 60)

Inaendelea Uk. 16

KATIKA makala iliopita ikiwa ni utangulizi wa maudhui ya Mchango wa Waislamu katika maendeleo ya dunia, nilitoa ufafanuzi kuwa Waislamu sivyo w a n a v y o o n e k a n a n a kunasibishwa na ugaidi katika nyakati hizi. Lakini Waislamu huko nyuma wameweza kutoa michango mikubwa ya kuifanikisha dunia hii tunayoishi kuwa k a t i k a m a e n d e l e o n a mafanikio.

Kati ya vigogo mbalimbali w a K i i s l a m u a m b a o wamefanya kazi kubwa ambao wataelezewa katika mfululizo wa makala hizi ni pamoja na: Muhammad Ibn Musa Al-Khwarizm (780 – 850), Ibn Battuta (1304 – 1369), Ibn Rushd (1126 – 1198), Omar Khayyam (1048 – 1131), Thabit Ibn Qurra (826 – 901), Abu Bakr Al-Razi (865 – 925), Jabir Ibn Haiyan (722 – 804), Ibn Ishaq Al-Kindi (801 – 873), Ibn Al-Haytham (965 – 1040), Ibn Zuhr (1091 – 1161), Ibn Khaldun (1332 – 1406), Ibn Al-Baitar (1197 – 1248), Abu nasr Al-Farabi (872 –

Mchango wa Waislamu katika maendeleo ya Dunia950), Al-Battani (858 – 929), Ibn Sina (980 – 1037).

M s o m i n a g w i j i wa maendeleo ya teknolojia Al-Khwarizmi

Mjuwe Muhammad Ibn Musa Al-Khwarizmi (780 – 850)Muhammad ibn Mussa Al-

Khawarizmi Mfursi aliobobea katika fani nyingi za kitaluma ikiwa pamoja na Hesabati, Elimu ya nyota, Jiografia na elimu nyenginezo, hizo nilizokwisha kuzinukulu ndizo alizozifanyia kazi kwa kiwango kikubwa.

Al-Khawarizmi amezaliwa huko Uajemi katika mwaka wa 780 AD. Katika historia t u n a m s o m a K i o n g o z i Haroun Rashid ambaye k a t i k a u o n g o z i w a k e aliusukuma na kupeleka Uislamu mbele katika fani ya elimu na ndio nyakati hizo zikijulikana kama nyakati za dhahabu kumanisha kuwa ni nyakati ambapo Waislamu walifanikiwa na kutekeleza mengi katika elimu na maendeleo au kwa kifupi tunaweza kuita ni wakati wa mafanikio na maendeleo makubwa kwa Waislamu. Kujulikana kwake Al-Khawarizmi na kuweza kufanya kazi zake kwa upana ni pale alipohamia Baghdad katika Nyumba ya Hekima (House of wisdom) chini ya

M s o m i n a g w i j i wa maendeleo ya teknolojia Al-Khwarizmi

Kiongozi Al-Mamun, huyu akiwa ni mwana wa Kiongozi Haroun Rashid.

Kubakia kwake Baghdad, Al-Khawarizmi aliweza kuja na nadharia mbalimbali za hesabati na ufanyaji wa hesabu kwa njia rahisi kabisa kwa kutumia Logarithm. I n a e l e w e k a k u wa A l -Khawarizmi alibobea mno katika fani hii ya Algorithm a m b a y o f a n i h i i n d i o inayotumika katika masuala

yote ya Computer kuwezesha kufanya kazi kwa kirahisi. Baadhi ya wasomi hupenda kumwita Al-Khawarizmi kuwa ni Babu wa somo la Computer kwa kuwa dhana nzima inayotumika katika Computer miz iz i yake imetokana na yeye.

Katika moja ya kazi za Al-Khawarizmi

J u u ya k a z i k u b wa iliofanywa na Al-Jabir katika somo la Algebra, naye Al-Khawarizmi amefanya kazi kubwa ndani ya fani hii hasa unaposoma kitabu kinachojulikana Hisab al-Jabr wa-al-Muqabala.

Kitabu hiki katika taaluma ya sayansi kilibidi kufasiriwa mara mbili kwa lugha ya Kilatino, lugha ambayo huko nyuma ikijulikana kama ni lugha ya taaluma. Walikuwa Gerard wa Cremona na Robert wa Chester katika karne ya 12 walipoifanyia tafsiri kazi yake hiyo ya kukitafsiri kitabu hichi muhimu Hisab al-Jabr wa-al-Muqabala.

Al-Khwarizmi aliidhibiti taaluma ya utambuzi wa hesabu zijulikanazo kama Quadratic Equations ambazo alitoa mifano zaidi ya 100 katika kuweza kupata jawabu u n a p o f a n ya Q u a d r a t i c Equations. Aidha aliweza

k u f a h a m i s h a s o m o l a Geometry na kuweka mifano mbal imbal i ya kuweza kulielewa somo hilo. Fani hizi mbili ambazo nimezielezea, aliweza kurahisisha kugawa mirathi kwa njia ya kirahisi k a b i s a k w a k u t u m i a Quadratic Equations na mifano yake ya Geometry ndio yalioleta chimbuko la upimaji wa ardhi ambao hadi hii leo njia alizozipita ndizo zinazotumika.

Bahat i mbaya kat ika taa luma tunazoz isoma jina lake huwa haliguswi kwa uchoyo wa watu wa nchi za Magharibi. Uchoyo huu sio kwa Waislamu tu walifanyiwa, bali hata watu wa jamii nyengine waliokuwa sio Waislamu walifanyiwa uchoyo huo. Kwa mfano V. N. Sukachov akiwa ni Mrusi katika mwaka wa 1910 alikuwa ni mtu wa mwanzo ambaye alielezea kuwa kila kiumbe kina mwahali pake anapoishi na hapo ndipo panakuwa na maingiliano ya maisha na mazingira yaliokizunguka kiumbe hicho nadharia ya kisomi inajulikana kama Ecosystem, akiwa Sukachev alioasisi neno hilo na kuwa anayasomesha na kuyaelezea katika vyuo vya Urusi wakati

Inaendelea Uk. 16

Page 16: ANNUUR 1167a.pdf

16 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala/Tangazo

Mchango wa Waislamu katika maendeleo ya DuniaInatoka Uk. 15nchi za Magharibi hawana habari au waliibeza kazi hii mpaka alipokuja A. G. Tansley mwaka wa 1935 na kuielezea suala zima la ecosystem na kubatizwa kuwa Tansley ni muanzilishi wa dhana nzima ya ecosystem, na katika makala hizi msomaji utapata fursa kuona kuwa hata yale majina ya wasomi wa Kiislamu yanaojitambulisha kuwa ni watu wa maeneo g a n i y a m e b a d i l i s h w a na kufanywa majina yao yatamkwe Kizungu, mfano Al-Khawarizmi anatamkwa k a m a A l g o r i t m i a u Algaurizin.

A l - K h wa r i z m i a i d h a amefanya kazi kubwa katika elimu ya nyota na kuandaa kalenda, kufanya hesabu na kujua kwa dhati sehemu ya jua mwezi na sayari zinapokuwa, wanasema kuwa huyu ndio muasisi wa table kwa wasomi wa hesabu za sine na tangents. Katika kitabu chake cha Zij al- sindhind ambacho kimejikita

katika elimu ya nyota, Al-Khawarizmi alichukua rejea nyingi kutoka Uhindini na kwengineko kuweza kukifanikisha kitabu chake, Al-Khawarizmi alikuwa na akili ya ajabu ya uchunguzi na upambanuzi.

Al-Khawarizmi akiwa amefanya hesabu kwa njia ya Alogarithm miaka 200 iliopita, hii leo ndio taaluma hii inatumika kwa kiwango k i k u b wa . N i ye ye A l -Khawarizmi alizozijulisha nambari za Kiarabu kutumika katika nchi za Magharibi na kuifanya Zero nayo itumike katika kujumuisha ingawa wengi wanasema kuwa Zero iliasisiwa katika Bara la Uhindi na Al-Khawarizmi alisoma maandiko mengi ya Uhindini lakini kujulikna kwa Zero huko Ulaya ilitokana na maandiko yake.

Al-Khawarizmi amefanya kazi nzito katika somo la Jiografia, pale aliporekebisha kazi ya Ptolemy ya utafiti wa Jiografia juu ya umbo la dunia katika kazi yake

maarufu ijulikanayo Surat a l -Ardh. Kazi yake hi i haijachapishwa ilikuwa kazi iliyoandikwa kwa mkono, na ramani alizozichora bahati mbaya nazo zilipotea. Lakini maelezo yake yaliwawezesha wa n a t a a l u m a we n g i n e kuunganisha na kupata sura kamili ya ramani hizo a l izoz i taar i sha . Akiwa anasomesha katika elimu ya juu aliweza kuwasimamia wasomi kama 70 katika somo la Jiografia katika kutekeleza kazi h io i l iomwezesha kutengeneza ramani ya dunia ambayo ndio hii inayotumika sasa, kazi zake zilipotafsiriwa kwa lugha ya Kilatino ilitia msukumo mkubwa wa sayansi kusonga mbele katika nchi za Magharibi.

Al-Khawarizmi ameweza kusaidia katika kuifanikisha kazi ilioanzwa na wataalamu wengine kujua nyakati kwa kutumia chombo kinachoitwa Sundial , chombo hicho ambacho hutumika kujua wakati katika siku wakati jua linawaka. Al-Khawarizmi alikitengeneza chombo hichi kwa njia nyengine kinyume na watangulizi wake wa

Kihindi na Hellenistic. Kazi hii ya Sundial imetumika katika kujua nyakati za sala na huko nyuma kilikuwa chombo hicho kinawekwa juu ya Misikiti. Al-Khawarizmi katika kazi yake mmoja yenye kutambulika ni alisaidia katika kuifanikisha kuiandaa kalenda ya Kiyahudi hayo yanaonekana katika kitabu kinachojulikana Istikhraj Tarikh al-Yahud.

Baadhi ya kazi zake n i p a m o j a n a k i t a b u a l i c h o k i a n d i k a k w a Kiarabu na kutafsiriwa kwa lugha ya Ki lat ino katika karne ya 12 kitabu hicho ni Kitab al-Jam'a wal- Tafreeq bil Hisab al-Hindi, kitabu hichi lau ingekuwa hakijafanyiwa tafsiri kwa Kilatino kingepotea wala kisingezungumzwa kwani maandishi ya awali ya Kiarabu yalipotea. Kitabu chake cha Algebra kijulikanacho kama Al-Maqala fi Hisab-al Jabr wa-al- Muqabilah hichi kimesaidia sana wasomi wa nyakati zake nacho kilitafsiriwa kwa Kilatino kikiwa kimetoa mchango

mkubwa wa sayansi kwa nchi za Magharibi. Msomi huyu aliweza kutengeneza Jadweli ya nyota na mwenendo wake na kutafsiriwa kwa lugha mbalimbali za nchi za Magharibi na kufanyiwa tafsiri hata kwa Kichina, bila ya kusahau kazi ya S u n - d i a l s a l i p o a n d i k a kitabu kijulinacho Kitab al-Rukhmat.

Ukitaka kumuelewa Al-Khawarizmi na kuwafanya wasomaji wamuelewe, itabidi kwa uchache uandike kitabu kisichopunguwa kurasa 2,000 ndipo utapoweza kumuelezea akafahamika, juu ya hayo azma ya makala hizi ni kutoa mwanga na kueleza kwa mukhtasari Waislamu na michango yao katika maendeleo ya dunia yetu hii.

Makala i takayofwata itamuangalia Ibn Battuta na mchango wake katika m a e n d e l e o ya S a ya r i y e t u h i i . ( M c h a n g o maoni, yanakaribishwa-MOBILE:0777 436 949 , [email protected])

Jee, Bahari ni Jaa Mwaga Ukitakacho Bahari Itameza?

Inatoka Uk. 15

“Basi wawili hao walipo fika zinapo kutana hizo bahari mbili walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kaporonyokea baharini.” (Surah Al-Kahf, 61)

“Akasema (kijana): Waona! Pale tulipo pumzika penye jabali basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hapana aliye nisahaulisha nisimkumbuke ila Shet'ani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.” (Surah Al-Kahf, 63)

“Ama ile jahazi ilikuwa ya masikini za Mungu wafanyao kazi baharini . Nil i taka kuiharibu, kwani nyuma yao a l ikuwako mfalme anaghusubu majahazi yote.” (Surah Al-Kahf, 79)

“Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea.” (Surah Al-Kahf, 109)

“Na tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja wangu, na uwapigie njia kavu baharini. Usikhofu kukamatwa, wala usiogope.” (Surah Ta Ha, 77)

“F i rauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini kilicho wafudikiza.” (Surah Ta Ha, 78)

“(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya

baharini atawanyike.” (Surah Ta Ha, 97)

“Je ! Huoni kwamba M w e n y e z i M u n g u amevidhali l isha kwenu viliomo katika ardhi, na marikebu zipitazo baharini kwa amri yake, na amezishika mbingu zisianguke juu ya ardhi ila kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma kwa watu, Mwenye kurehemu.” (Surah Al-Hajj, 65)

“Au n i k a m a g i z a katika bahari kuu, iliyo funikwa na mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza. Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. Na ambaye Mwenyezi Mungu hakumjaalia kuwa na nuru hawi na nuru.” (Surah An-Nur, 40)

“Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.” (Surah Al-Furqan, 53)

“Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.” (Surah An-Naml, 61)

“Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka

pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi M u n g u ? A m e t u k u k a Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.” (Surah An-Naml, 63)

“Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?” (Surah Al-Qasas, 40)

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” (Surah Ar-Rum, 41)

“Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na ikaongezewa juu yake bahari nyengine saba, maneno ya Mwenyezi Mungu yasingeli kwisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (Surah Luqman, 27)

“Kwani huoni kwamba marikebu hupita baharini z i k i c h u k u a n e e m a z a M we n ye z i M u n g u , i l i kukuonyesheni baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri, mwenye kushukuru.” (Surah Luqman, 31)

“Na bahari mbili haziwi sawa; haya ni matamu yenye ladha, mazuri kunywa. Na haya ni ya chumvi,

machungu. Na kutokana na bahari zote mnakula nyama mpya (isiyo chacha). Na mnatoa mapambo mnayo yavaa. Na unaona ndani yake marikebu zinakata maji ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.” (Surah Fatir, 12)

“Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyo kwenda na kurejea baharini kama vilima.” (Surah Ash-Shura, 32)

“Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.” (Surah Ad-Dukhan, 24)

“ M we n ye z i M u n g u ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite marikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.” (Surah Al-Jathiyya, 12)

“Bas i tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.” (Surah Adh-Dhariyat, 40)

« Anaziendesha bahari mbili zikutane. » (Surah Ar-Rahman, 19)

“Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.” (Surah Ar-Rahman, 20)

“Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.” (Surah Ar-Rahman, 24)

“Na bahari zitakapo pasuliwa” (Surah Al-Infitar, 3)

Takriban unapozisoma aya hizi nyingi zinakuonyesha namna Qur’an ilivyoieleza m a u m b i l e n a s a ya n s i kwa ndani kabisa. Aidha, Q u r’a n h a k u n a p a h a l i kunaposhajiishwa kufanya ufisadi wa kumwaga uchafu ndani ya bahri.

Tuangalie maelezo ya kitaalamu kwa ufupi kabisa juu ya bahari: Inakisiwa kuwa bahari ina kilomita za mraba milioni 362 (362million sq km). Bahari imechukua sehemu ya asilimia 71 ya dunia tunayoishi. Zaidi ya asilimia 97 ya maji yaliopo duniani hutokana na bahari. Asilimia 10 tu ya viumbe vilivyohai baharini, ndivyo vilivyoweza kutambuliwa n a k u p e wa m a j i n a n a mwanadamu.

Sehemu ya bahari ya Antratic ambayo huyayuka barafu yake kila mwaka, ujazo wake ni sawa na masafa ya nchi ya Marekani. Zaidi ya robo tatu ya miji mikuu duniani, imejengwa karibu na bahari. Hivi sasa inaaminika kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watu, wanaishi ndani ya kilomita 100 za ufukwe. Kila mwaka hufariki ndege laki mmoja wa baharini na baadhi ya wanyama wanaoishi baharini kwa kumeza mifuko ya plastiki.

Zaidi ya mapipa milioni 21 ya mafuta huvuja katika bahari kutokana na viwanda na meli zinazosafirisha mafuta.

Asilimia 90 za bidhaa zinazosafirishwa duniani, k u t o k a n c h i m o j a kwenda nchi nyengine, husafirishwa kwa kupitia njia ya meli. ((Mchango maoni, yanakaribishwa-MOBILE:0777 436 949 , [email protected])

Page 17: ANNUUR 1167a.pdf

17 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015

Makala

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:• KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – SAME – KILIMANJARO • NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL – MWANZA • UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L – DAR ES SALAAM

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE• P.O Box 55105,Phone: 0222450069, 0784 267762, 0755 260087 & Fax 022 2450822, Dar es Salaam website :www.ipctz.org

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO – 2015/20161. Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu.2. Shule hizi ni za bweni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana .3. Zipo tahasusi za masomo (Subject Combinations) ya SAYANSI, ARTS na BIASHARA. 4. Wanafunzi wote wanafundishwa Islamic Knowledge,Introduction to Arabic na matumizi ya compyuta pamoja na kutumia mtandao (internet)

katika kujifunza.5. Muombaji anatakiwa awe na sifa za kujiunga na kidato cha tano kwa mujibu wa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. 6. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

• Arusha - Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni : 0783552414/0762817640.

• Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha :712 216490 - Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757 013344. - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 - Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. - Ugweno – Kifula Shopping Centre- Yusuph Shanga : 078458776.

• Tanga - Twalut Islamc Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111- Uongofu Bookshop: 0784 982525 - Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008. - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533. -Handeni –Mafiga -0782 105735/0657093983• Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685.- Ofisi ya Islamic Education Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770/0714097362. • Musoma - Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623• Shinyanga - Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0752180426 - Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi : 0753 993930/0688794040

• Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172 - Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531

• Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380.

• Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992

• Singida - Ofisi ya Islamic Education. Panel – karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039.

• Manyara - Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid Rahma: 0784491196

• Kigoma - Msikiti wa Mwandiga: 0714717727 - Kibondo – Islamic Nursery School: 0766406669. - Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802.

• Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.

• Mtwara - Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.

• Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264/0683670772. - Mkuzo Islamic High School :0717 348375.

• Mbeya - Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini – 0785425319.

- Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319. .• Rukwa - Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike 0717082 072.

• Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0787237342

Nzega -Dk Mbaga-0754 576922/0784576922.

• Iringa - Madrastun – Najah: 0714 522 122.

• Pemba -Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.

• Unguja - Madrasatul – Fallah: 0777125074.

- PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa Lumumba• Mafia - Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!MKURUGENZI

WABILLAH TAWFIIQ

Page 18: ANNUUR 1167a.pdf

18 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015

Makala/Tangazo

MAASKOFU wametoa taarifa rasmi wakidai kuwa Waislamu wana mkakati wa kuchoma makanisa nchi nzima. Na kwamba katika hatua za awali za kutekeleza mkakati huo, wamepata h a b a r i k w a m b a “kundi la Waislamu lilishushwa Mbeya kwa ajili ya kuchoma moto makanisa.”

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste nchini Tanzania (PCT), Askofu David Mwasota amewataka Wakristo k u j i h a m i k wa v i s u , mishale na mikuki” ili kupambana na Waislamu waliodhamiria kuchoma makanisa.

A s k o f u D a v i d a n a s e m a k u wa k wa kushika mikuki ,visu na misha le , huenda serikali itazindukana k u w a s h u g h u l i k i a W a i s l a m u , k w a n i anasema kuwa haoni kama serikali inafanya vya kutosha kukabiliana na kitisho cha Waislamu. Katibu Mkuu huyo wa PCT anamshutumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekuwa akitoa matamk o mepes i tu badala ya nguvu na hasira zote za dola kuwaangukia Waislamu.

Zilipotokea vurugu za Mbagala baada ya lile tukio la Qur’an kunajisiwa, i l ida iwa kuwa kuna makanisa yalichomwa moto. Kwa vile waliotoka kuandamana walikuwa Waislamu na kwa kuwa Waislamu ndio waliokuwa n a h a s i r a k u f u a t i a kitendo cha kukojolewa Qur’an, wakawa ndio watuhumiwa namba moja kuwa ndio waliohusika kuharibu makanisa hayo.

Lakini ukiacha taarifa hiyo, uongozi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu August ino, Mwanza, umedai kuwa Paroko wake, Padiri Andreas Buhembo ametumiwa ujumbe wa kumtangazia kifo. Kwamba, wakati kimbunga cha kuchoma makanisa kinaendelea, s a s a W a i s l a m u wanatangaza mpango wa kuuwa Mapadiri . Padiri Buhembo anasema kuwa yeye amekabidhiwa u j u m b e u n a o t i s h i a kumuuwa na Mapadiri wengine na kwamba ujumbe huo umeandikwa kwa Lugha ya Kiarabu.

Padiri Andrea Buhembo anadai kuwa akitumia mbinu za ‘kikomandoo’

Wachoma Makanisa Mbeya!!!Wakristo watakiwa kujihami kwa mikuki

kwa kuvaa sawa na mavazi ya wahudumu wa Kanisani kwake, mtu (Muis lamu) mwenye ujumbe huo ulioandikwa Kiarabu, a l i ingia na kumkabidhi mkononi w a k a t i a k i e n d e s h a ibada bila kushtukiwa na waumini . Kat ika maelezo yake Padir i B u h e m b o h a k u e l e z a iwapo anajua Kiarabu kwa hiyo aliposoma, alifahamu kilichoandikwa au alikwenda kutafuta mkalimani baadae baada ya kumaliza Misa. Ila

anachosema ni kuwa walimkamata na kumhoji l a k i n i wa k a m u a c h a a k a o n d o k a b i l a y a kumdhuru!

Kama hiyo haitoshi, uongozi huo wa Kanisa Katoliki Mwanza ukadai t e n a k u wa wa l i k u j a mabinti wawili waliovalia H i j a b u n a k u t a k a kuingia kanisani lakini wakazuiwa.

Ukitizama madai ya Askofu David Mwasota

na haya ya Padir i Andreas Buhembo, kubwa

w a n a c h o f a n y a n i

k u p i g a p r o p a g a n d a ya kuwapakazia uovu Wa i s l a m u n a h a s a kujaribu kuisimika ikae na ikubalike kuwa nchini kuna

kitisho cha Boko Haram k a m a i l i v y o k w i s h a kutajwa katika baadhi ya magazet i . Uki jua kuwa mengi ya makanisa haya ni yale yaliyoanzia Marekani au kufadhiliwa na taasisi za Kimarekani, matamshi ya Maaskofu hawa hayakupi shida sana.

L a k i n i n i s e m e

yafuatayo , kab la ya k u p i t i s h a s h e r i a ya Pat r io t Act , k i l ip i ta kwanza kitisho cha kweli cha shambulio la kimeta (Anthrax Terror Attack), wakafa watu saba wasio na hatia. Kitisho cha

Al Qaida na Usama Bin Laden, kimeonekana kweli baada ya Septemba 11 ambapo watu takriban 4,000 walikufa. Uganda ilikuwa hivyo hivyo. Watu kama 70 hivi walikufa ili kitisho cha Al Shabab kionekane kuwa ni cha kweli. Hapa hoja sio kama kweli waliopiga Kampla walikuwa Al Shabab au la. Ila tu tusisahau kuwa katika “Anthrax Terror Attack”, walituambia kuwa n i Al -Qaidah . Lakini haukupita muda wakashikana uchawi wenyewe kwa wenyewe.

Sasa labda kwa wale Watanzania wenye hamu ya kuona kitisho cha ugaidi kinakuwa cha kweli katika nchi hii, watuambie, wapo tayari kutoa gharama kiasi gani? Wapo tayari kuona watu wangapi wasio na hatia wakiuliwa? Na kwa vile propaganda hapa ni Boko Haram, ni Al-Shabaab, ni Waislamu, Swali ni je, Askofu Mwasota na Padiri Andreas, wapo tayari kuona Wakristo wangapi wakiuliwa ili hilo wanalotamani litimie?

Labda tuseme hapa k u w a w a t a k a o u w a Wakristo na watakaolipua M a k a n i s a i l i k u d a i kuwa ni Waislamu, ni hawa hawa wanaodai kuwa kuna “Waislamu walioshushwa Mbeya kulipua Makanisa…ni hawa hawa wanaodai k u w a w a m e t u m i w a ujumbe wa kifo. Nasema h i v y o k w a s a b a b u wanayodai ni urongo mtupu. Ni uchochezi. Ni usanii. Na wanafanya hivi bila ya wasiwasi k w a s a b a b u w a n a uhakika hawatakamatwa k w a i d h i l a l i k a m a wanavyofanyiwa akina Ponda, Sheikh Msellem na

viongozi wengine wa Kiislamu.

L a b d a t u j i u l i z e , Muislamu anaingiaje kanisani anakupa ujumbe wa kukutishia kifo, halafu humkamati na kumpeleka polisi?

Imekuwa kama ule usanii tulioambiwa kuwa kuna vijana wametekwa na wanaharakat i wa Kiislamu

Arusha wakateswa na mmoja wao akakatwa masikio, lakini katika p i c h a w a l i y o p i g w a wote wana masikio yao yakiwa mazima! (Habari hii ilitolewa kwa mara ya kwanza katika An nuur Namba 1044 la Novemba 9, 2012)

dhahanifu”. Fasili yake ni kuwa haya ni maelezo yanayomtuhumu mtu au kundi la watu, taasisi au jumuiya kwa aidha kupanga, kuficha, au kufanya jambo ambalo ni kinyume cha sheria na lenye madhara kwa wengine.

K u i t w a k w a k e “dhahanifu” kunaeleza ukweli mmoja muhimu – kuwa hii ni dhana ya kudhania tu, lakini ukweli mwengine muhimu zaidi ni kuwa mara kadhaa ni dhana hizi za kudhanika tu ndizo ambazo huumba mitazamo ya wengi wetu, badala ya zile dhana zilizofanyiwa utafiti na kujengewa ushahidi wa kihistoria, kisayansi na kimantiki.

Hata hivyo, “nadharia dhahanifu” ina msingi wake; na kwa hakika ni msingi huo ndio unaoipa n g u v u z a k u i f a n y a ikubalike miongoni mwa waumini wake, na kufikia mahala ya kuzichukulia hatua, hata kama mbunifu wake haiamini . Kwa mbunifu, hii huwa ni nyenzo yake ya kisaikolojia, kijamii au kisiasa wa jamii inayohusika nazo.

Waziri mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa Oman , Mhe. Sayyid Fahad Mahmoud El Said kabla ya mazungumzo yao rasmi ya kiserikali kwenye Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu wa Oman mjini Muscat Oktoba 28, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

H a p a n d i p o inapotuwama hii fitina ya mtawala, kupitia sasa akina Lukuvi na Sitta. Mtawala anajuwa vyema anachokifanya kwenye nadharia hii dhahanifu ya Tanzania kuwaogopa

Zanzibar inabeba lawama kubwaInatoka Uk. 4 ‘Waarabu wa Zanzibar’.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – kwa sera na muelekeo wake – haina la kukhofia kutoka kwa “Watanzania hao 200,000″ walioko Oman.

Kinyume chake ndicho inachokifanya hivi sasa. Kwa siku za karibuni, serikali nzima ya Rais Kikwete imekuwa haishi kiguu na njia kwenda k u o m b a m i s a a d a n a u s h i r i k i a n o w a kimaendeleo na Oman, ikiwatumia Watanzania hao hao wenye asili za Oman na Waomani wenye asili za Tanzania.

K h o f u h a l i s i y a ‘ Ta n g a n y i k a ’ k w a Zanzibar: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, i n a k h o f i a e n d a p o Z a n z i b a r i t a s i m a m a kwa miguu yake katika masuala kadhaa ya kisiasa na kiuchumi, ndani na nje ya mipaka yake. Ile fursa ya Zanzibar kuwa “Cuba ya Afrika” i l iyowahi kuwatisha Wamarekani katika miaka ya ’60 kufikia umbali wa kuchochea kuisakamiza Zanzibar k w e n y e k a b a r i z a Tanganyika, ndiyo fursa ile ile ambayo miaka 50 baadaye Zanzibar inayo.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam kutokea baharini ukiakisi ukuwaji wa u c h u m i , a m b a o unaweza kufikiwa na kupitwa na Zanzibar iliyothubutu.

Hata baada ya kuzikwa kwenye shimo kwa nusu karne, Zanzibar bado ina nafasi ya kuwa “Dubai ya Afrika” na hivyo i n a m t i s h a m t a wa l a , ambaye sasa anafikia umbali wa kuiandalia hujuma kubwa. Miaka m i t a n o i n a y o k a t i k a sasa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa

ya Zanzibar, licha ya mapungufu yake kadhaa, imedhih i r i sha kuwa ndoto hiyo ya Zanzibar i n a we z a k u j a k u wa kweli, lau uhuru zaidi wa kisiasa na kiuchumi utakuwa mikononi mwa Wazanzibari wenyewe.

Hapo ndipo penye chimbuko la fitina hii, ambao huenda mtawala anaamini ha i takuwa n a m a d h a r a k wa k e , zaidi tu ya kuiadhibu na kuidhuru Zanzibar vile inavyostahiki kwa kuonesha kiburi mbele yake. Zanzibar inapangiwa kuadhibiwa na vijenzi vya adhabu hiyo vinaendelea kujengwa kwa utaratibu na mkakat i maalum ambao unadhihir ika kwenye kauli na hatua kama hizi za kina Sitta na Lukuvi.

Hata hivyo, kufanikiwa na kutofanikiwa kwa hujuma hii kutatokana, kwa kiasi kikubwa, na udhaifu wa Zanzibar na Wazanzibari wenyewe na s io tu nguvu za mtawala pekee. Na tukiwa wakweli wa nafsi zetu, sisi Wazanzibari wenyewe tumeuonesha udhaifu huo tangu kwenye vikao vya Bunge Maalum la Katiba na tunaendelea kumuonesha hadi sasa.

Tuligawika Dodoma kwenye Bunge h i lo , tumeendelea kugawika Zanzibar nje ya bunge hilo. Hatujasimama pamoja kwa maslahi ya nchi yetu, bali tumesimama kwa maslahi ya makundi na vyama vyetu. Na hapo laz ima tubebe sehemu yetu ya lawama. Tunalaumika.

Page 19: ANNUUR 1167a.pdf

19 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 2015Makala

'PUNGUZA sana matumizi ya chumvi, au ikiwezekana wacha kabisa'!

H u u n i u s h a u r i wa kawaida kabisa unaopewa na madaktari pale inapobainika kuwa shinikizo lako la damu liko juu kuliko inavyopaswa.

S h i n i k i z o l a d a m u hupimwa kat ika ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni shinikizo la juu. Hili hutokea pale misuli ya moyo inapokikaza kusukuma damu iliyosheheni oksijeni kutoka kwenye mapafu kuisambaza mwilini. Ngazi ya pili ni shinikizo la chini. Hili hutokea pale misuli ya moyo inapojiachia kuruhusu damu irejee kwenye mapafu il i kuachia hewa chafu kutoka katika seli za mwili - hewa ukaa - itolewe ndani ya mwili

Shinikizo la juu la kawaida la damu ni 110 - 120 mmHg; na la chini la kawaida ni chini ya 80 mmHg. mmHg ambayo kirefu chake ni 'millimeters of mercury' ndiyo kipimo kinachotumika kwa kawaida kuelezea k iwango cha shinikizo la damu.

DAWA UGONJWA UNAOTIBIWA1 HAIIBA DENTAL

GUARDM a u m i v u ya meno

Maambukizi ya gram positive bakteria kwenye kinywa Harufu mbaya kinywani

2 HAIIBA DENTAL GUARD COMBO

M a u m i v u ya meno

Maambukizi ya gram p o s i t i v e b a k t e r i a kwenye kinywa

H a r u f u m b a y a kinywani

Magonjwa ya fizi Kujenga upya meno yenye matundu

3 HAIIBA IG Kuongeza kinga za mwili Vidonda vya tumbo Kurekebisha athari za kisukari cha ukubwani

4 H A I I B A I G COMBO

Hupunguza mzigo wa virusi vya ukimwi mwilini

5 HAIIBA TIMAMU TEA

Maumivu ya viungo

Kusawazisha Cholesterol

K u h i f a d h i m n y u m b u k o wa ngozi

K u p u n g u z a shinikizo la damu

Hupunguza madhara ya kisukari cha ukubwani

Hukinga dhidi ya uharibifu wa ini

Uchovu Kupunguza k a s i y a kuzeeka

K u i m a r i s h a siha ya ngozi

K u p u n g u z a u w e z e k a n o w a k u p a t a shambulio la

Hupunguza makali ya maradhi ya kupoteza k u m b u k u m b u (Alzheimer’s disease)

Hukinga mapafu yasipate makovu

Homa za mara kwa mara

Usagaj i wa c h a k u l a tumboni

K u i m a r i s h a siha ya macho

H u b o r e s h a s i h a y a m i s h i p a ya fahamu

Huharakisha kupona majeraha

Hukinga dhidi ya ugonjwa wa ngozi kuchuja rangi (vitiligo)

Mfuro (Inflammation)

Kusafisha ini Kinga dhidi ya saratani

H u o n g e z a Alkali mwilini

Hupunguza makali ya ugonjwa wa baridi ya yabisi (Arthritis)

Husafisha kinywa dhidi ya bacteria wasiotumia oxygen (anaerobic bacteria)

Kinga za mwili K u b o r e s h a m z u n g u k o wa damu

Kuharibu seli z a s a r a t a n i z i l i z o k o mwilini

H u z u i a c h o l e s t e r o l mbaya (LDL) k u i n g i l i a n a n a o x y g e n n a k u l e t a madhara

Hupunguza kasi ya ongezeko la virusi vya ukimwi

Ni kinga dhidi ya utapiamlo

DAWA UGONJWA UNAOTIBIWA6 HAIIBA GLUCOMASTER

PROGRAMMEHutibu Kisukari cha ukubwani Kurekebisha athari za kisukari cha

ukubwani

7 HAIIBA P & B Kuziba mkojo Kibofu kilicholegea8 HAIIBA C CLEAN Malaria sugu Maambukizi ya njia ya

mkojoKuondoa bacteria wabaya tumboni

Saratani mbalimbali

9 H A A I B A F A M I L Y BUSINESS

Kuondoa ukhanithi Kuimarisha sana uwezo wa tendo la ndoa

Maumivu ya kiuno na mgongo

10 HAIIBA CLEAN UP Kusafisha tumbo na njia ya haja kubwa

Kurekebisha mfumo wa usagaji chakula Nguvu za kiume

11 HAIIBA MLONGE PACK Kinga imara dhidi ya utapiamlo Huimarisha kinga za mwili Huondoa uchovu

Sukari ni kichocheo kikubwa zaidi cha Shinikizo la Damu (Hypertension) kuliko hata chumviChumvi ina tabia ya

kufyonza maji. Inapoingia m w i l i n i n a k w e n y e m z u n g u k o w a d a m u huvuta maji na kusababisha ongezeko la wingi wa maji kwenye damu. Ongezeko hili hupelekea shinikizo la damu kuongezeka. Hili huwa ni ongezeko la muda tu mpaka pale kiasi cha maji kwenye mzunguko wa damu kitakapopungua. Dawa za kifamasia za kushusha shinikizo la damu hufanya kazi kwa kuzingatia kanuni hii. Dawa hizi hulazimisha mhusika akojoe sana, kitendo ambacho hushusha kiasi cha maji kwenye mzunguko wake wa damu.

Tofauti na chumvi ambayo husababisha shinikizo la damu kuongezeka kwa muda mfupi tu, sukari hujenga mazingira ya mwili kuwa na shinikizo la damu la kudumu. Unapokula sukari ya mezani (sucrose), mchakato ufuatao hutokea ndani ya mwili. Molekuli ya sucrose huvunjwa na sukari mbili tofauti zilizomo ( f r u c t o s e n a g l u c o s e )

zinazounda molekuli hii huachiwa huru, kila moja na hamsini zake.

Wa t a f i t i w a n a s e m a kuwa Fructose (moja ya hizi sukari) huchochea seli za mwili kuchoma nishati (ATP) iliyohifadhiwa humo kwa kasi ya kutisha na matokeo yake seli husika hukumbwa na 'shock'! Shock hii hupelekea DNA katika hizi seli kusambaratika! Watafiti hawa wanaongeza kuwa DNA iliyosambaratika hujiunda katika kemikali zinazojulikana kama purines, a m b a z o n a z o h u i s h i a kujiunda kuwa tindilkali ya urea, yaani uric acid!

T i n d i k a l i y a u r e a inasababisha seli za mwili k u k u m b wa n a m f u r o endelevu, na huzuia mwili kuzalisha kemikali ya Nitric oxide inayosaidia kuta za mishipa ya damu kutanuka na kusinyaa kwa wepesi. K u s h i n d wa k u t a n u k a kwa mishipa ya damu pale inapohitajika huzaa ongezeko la shinikizo la damu. Ulaji uliopindukia wa sukari hupelekea miili

yetu kuzalisha kiasi kikubwa cha uric acid muda wote hali ambayo husababisha uharibifu wa mishipa ya damu kutokea muda wote.

Ni muhimu kujua kuwa shinikizo la damu ni ugonjwa hatari sana kwa sababu kila kiungo cha ndani cha mwili huwa kinakabiliwa na shinikizo kubwa. Viungo nyetu vinavyopitiwa na mishipa mingi ya damu, mathalani macho na figo huathirika sana. Watu wengi wamepata ulemavu wa macho kwa sababi ya kile kinachoitwa shinikizo la damu la macho. Watu wengi pia wamepoteza maisha kutokana na maradhi ya figo ambayo kimsingi chimbuko lake ni shinikizo kubwa la damu. Kama unataka kujifunza zaidi, zifuatazo ni hatua mbalimbali za tatizo la shinikizo la damu ambazo mtu anaweza akapitia.

AINA1. SHINIKIZO LA JUU

(Systolic) mm Hg 1.1. Kawaida: 110 - 120

mmHg1.2 Kuelekea kuwa na

tatizo la shinikizo la damu (Prehypertension):

120 – 139 mmHg 1.3. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 1 : 140-149

mmHg1.4. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 2: 160 au zaidi

mmHg1.5. Shinikizo la damu

lililopindukia mipaka (Hypertensive Crisis):

Zaidi ya 180 mmHg2. SHINIKIZO LA CHINI

(Diastolic) mmHg2.1. Kawaida: Chini ya 80

mmHg2.2 Kuelekea kuwa na

tatizo la shinikizo la damu (Prehypertension):

80 – 89 mmHg 2.3. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 1: 90-99 mmHg2.4. Tatizo la shinikizo la

damu (Hypertension) Hatua ya 2: 100 au zaidi

mmHg2.5. Shinikizo la damu

lililopindukia mipaka (Hypertensive Crisis):

Zaidi ya 110 mmHg

Page 20: ANNUUR 1167a.pdf

20 AN-NUURJAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 201520 MAKALA AN-NUUR

20 JAMAADIUL AWWAL 1436, IJUMAA MACHI 6-12, 20152015

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na POA Printing Works LTD, S.L.P. 4605, Dar es Salaam.

LEO naanza na neno hili: Inna lillahi waina ilayhi rajiuun. Hakika sote ni wa Mwenyeenzi Mungu na kwake tutarejea.

Aya hii huwa inasomwa sana panapotokea msiba. Amefariki mtu na kurejea kwa Mola wake katika malazi yake ya daima milele, wale wanaopokea taarifa za msiba huwa wanatakiwa kusoma aya hii. Kwa leo nami naileta kutokana na msiba wa aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin ambaye alifariki Febuari 19 wakati mwenzake John Damiano Komba aliaga dunia Febuari 28 mwaka huu wa 2015 .

Taar i fa za v i fo h iv i zimekuja kwa mshituko m k u b wa k u t o k a n a n a m a r e h e m u w e n y e w e w a l i f a r i k i g h a f l a n a hivyo kuwashitua wengi walipopata taarifa za msiba. Hawa wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wote ni watu wanaotegemewa k a t i k a c h a m a h i c h o kutokana na ujasiri wao na wanavyoweza kujenga hoja wanapochangia jambo. Lakini pia kujiamini kwao na kutetea kile wanachokiamini ndiko kulikowafanya wapate umaarufu mkubwa hasa kupitia Bunge la Katiba ambalo kwa kiasi kikubwa wameonekana misimamo y a o s i o t u k u u t e t e a Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini pia kupingana na dhana ya uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyopo Zanzibar ambayo sasa inamalizia mwaka wa tano katika uongozi.

K w a u p a n d e w a J o h n K o m b a a m e p a t a umaarufu zaidi kutokana na kutumia fani yake ya usanii katika kukiimarisha chama wakati mwenzake akitumia ukakamavu na ujasiri wake wa kijeshi katika kukiimarisha chama. Wote hao walionekana kama ni mwiba mkali kwa watu ambao wana mtazamo na itikadi tofauti na wao.

Tukio la misiba hii miwili ni fundisho tosha kwa wanaadamu ambao wapo katika ardhi hii na bado wanasubiri siku yao ifike kwa kuwa kifo ni lazima kwa kila mmoja. Mwanadamu anayeishi hapa ulimwenguni kuna siku ataiwacha dunia na kupelekwa kaburini, awe mtawala au mtawaliwa, kiongozi au mwananchi wa kawaida. Kifo hakina ujasiri wala hakina rushwa kama alivyojisemea Remmy Ongala.

L a k u s i k i t i s h a n i kuwa tukio la kifo cha S a l m i n l i m e s h i n d w a kuwaunganisha Wazanzibari kuwa kitu kimoja kama ambavyo imezoeleka khasa katika suala la huzuni. Ni kwa nini? Salmini alifariki

Ni Msiba!

dunia muda mfupi baada ya kutoka ndani ya kikao cha ndani kilichofanyika katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui ambapo kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai anasema Marehemu amefariki akiwa Shujaa. Mtu angependa kujua ushujaa wa Marehemu ni upi? Lakini jibu ni kwamba alisimamia kidete hoja yake ya kuimarisha Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa nguvu zote, kuutetea na kuulinda kama ambavyo wa m e k u wa wa k i s e m a katika wimbo wao maarufu unaoongozwa na vijana wa chipukizi wa chama hicho. “Tutaulinda na tutaitetea potelea mbali”

Vuai anasema Salmin kabla ya kifo chake alikuwa ndani ya kikao akiwa na afya yake nzuri na hakuonesha dalili ya ugonjwa na moja ya hoja zake alizokuwa akichangia katika kikao hicho ni kuudumisha Muungano hoja ambayo ilifurahiwa na wajumbe wote waliomo ndani na baadae akatoka nje hali ya kuwa akiwa mzima wakati akielekea ofisini kwake ambapo alikuwa na vikao viwili kwa siku hiyo ndipo alipoanguka ghafla na kukimbizwa hospitali k u u ya M n a z i M m o j a ambapo muda mfupi taarifa zikaanza kuenea kwamba ameshafariki dunia.

Nil ikuwa maeneo ya Darajani ndani ya duka maarufu kwa Eddy Calipso kando ya Duka kubwa la vifaa vya Electroniki maarufu kwa Muzammil. Wakati nikiwa pale alipita m t u m m o j a a k i s e m a kwamba Salmin Awadh ameanguka Kisiwandui akiwa kwenye kikao na kukimbizwa hospitali Mnazi Mmoja chumba za wagonjwa Mahatuti (ICU). Lakini muda usiozidi dakika 20, tukapata ujumbe wa simu kwamba Sa lmin ameshatutoka , ujumbe ambao kwa hakika uliwashitua watu wengi lakini uliopokewa kwa hisia tofauti.

N a k a m a k a w a i d a unapopatwa na msiba au taarifa za kifo jambo la kwanza litakalokujia mdomoni ni maneno ambayo tumefunzwa katika imani zetu huwa tunasema Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun.

Lakini ni kwa nini watu wasiungane kama ambavyo waliungana wakati ule ambapo Zanzibar iliambiwa sio nchi? Bila ya kujali itikadi za kisiasa, Wazanzibari kwa sauti moja walighadhibishwa na kauli ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda aliyoitoa Bungeni kwamba Zanzibar sio nchi. Kila Mzanzibari alionesha hisia zake kutokana na kauli hiyo.

N a u m o j a h u o w a Wazanzibari ndio ulizipa

ari mamlaka zinazosimamia s h e r i a n a k u l a z i m i k a kufanyika mabadiliko ya kumi cha sheria ya Zanzibar ambayo pamoja na mambo mengine imeweka bayana kwamba Zanzibar ni nchi na ni sehemu tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa bila ya Zanzibar hakuna Tanzania.

Mabadi l iko hayo ya k a t i b a n d i o a m b a y o tunayashuhudia leo hii kwa takriban miaka minne imeweza kuongozwa chini ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mfumo a m b a o W a z a n z i b a r i wengi wanauunga mkono ingawa wapo baadhi yao wa n a u p i n g a a k i we m o marehemu.

Katika tukio jengine kubwa lil i lotokea hapa Zanzibar na kuwaunganisha Wazanzibari wote, ni lile la ajali ya Meli iliyotokea ambapo Wazanzibari bila ya kujali itikadi zao za chama au kidini waliunganisha nguvu kusaidiana na kuwa pamoja katika msiba huo jambo ambalo haikuwa rahisi kutambua huyu ni kutoka chama gani au itikadi gani. Kwa mfano huo huo mtu anaweza kujiuliza, ikiwa tukio hilo la msiba la watu wengi watu waliweza kuungana na kuficha hisia zao, jee imekuwaje watu wasiweze kuungana katika msiba huu? Jee, kuna kitu

gani kikubwa hapo? Haya na mengine ni masuali ambayo tunapaswa kujiuliza.

Sio jambo la kawaida hata kidogo kwa tabia na mila za Wazanzibari jinsi walivyolelewa kwa mafundisho ya kidini kuweza kutokea kauli ambazo sio nzuri kwa aliyefariki, lakini katika msiba huu tumeyaona mengi na tumeyasik ia mengi yakisemwa jambo ambalo linapaswa kutupa mazingatio makubwa.

I l a w a k a t i tukikumbushana kuwa Dini inatutaka tuseme yale mema na mazuri ya maiti na marehemu wetu, tukumbushane pia kwamba kila dakika na kila sekunde tunatakiwa tujiandae kwa aji l i ya kifo. Tuchunge kauli na vitendo vyetu, isije ikawa kauli zetu zikawa za kuwaudhi binadamu wenzetu au kumkufuru Mungu.

Ya p o m a m b o ye n ye maslaha na watu walio wengi, binadamu viumbe wa Allah, mfano kwa hapa Zanzibar hili la Serikali ya Umoja wa Kitaifa, watu wamejaa makovu ya hali za huko nyuma. Leo mtu ukawa kinara wa kushadidia kuvunjil iwa kwa mbali mfumo huu, kwa hakika unachofanya ni kutaka watu wadumu katika tabu na mashaka. Sasa mambo kama haya, si ushujaa.

H a t a k a t i k a D i n i tunaambiwa tuwe katika jamaa, wala tusi tafute mambo ya kuwafarakanisha watu. Sasa unaweza kuja na jambo kama hi l i la kutaka kuvunja udugu na umoja wa Wazanzibari, ukawafurahisha wachache lakini ukawaudhi walio wengi kutokana na kuwa kila mmoja anafahamu jinsi ambavyo Wazanzibari walivyoishi katika maisha ya maumivu na mateso kupitia chaguzi z inazofanyika hadi hapo kuamul iwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa kiasi kikubwa mfumo huo umesaidia kutuliza hali. Leo mtu anaposimama akaongea kutaka kuvunja mfumo huo, ni jambo lisilo na maslaha kwa watu.

B i n a f s i k i n a c h o n i h u z u n i s h a zaidi, sio tu kwamba watu wanasema hili na lile, lakini kauli ambazo zikitamkwa na watu kuhusiana na marehemu ambapo katika uhai wake akizitumia sana na kuzisema hadharani.

Ni ukweli usiopingika kwamba kifo ni haki na kila mmoja ataondoka, lakini cha kuzingatia hapa na kutupa fundisho, ni vipi utaondoka. Waswahili “ h u s e m a u n a p o o n g e a mengine ubakishe”.

ALIYEKUWA Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Marehemu Salmin Awadh Salmin.