na ukimwi - usaid assist project | applying science … rika - vvu na ukimwi (expert patient’s...

26
KIONGOZI CHA MUELIMISHAJI RIKA VVU UKIMWI N A VVU UKIMWI N A

Upload: vuongnhi

Post on 09-Mar-2018

475 views

Category:

Documents


7 download

TRANSCRIPT

KIONGOZI CHA MUELIMISHAJI RIKA

VVU

UKIMWINA

VVU

UKIMWINA

Muelimishaji Rika - VVU na UKIMWI(EXPERT PATIENT’S POCKET GUIDE)

SWALI JIBU

�. Kuna tofauti gani kati ya VVU na UKIMWI?

VVU (Virusi vya Ukimwi) ni vimelea vinavyoshambulia kinga ya mwili UKIMWI (Upungufu wa Kinga Mwilini) ni mchanganyiko wa magonjwa nyemelezi yanayotokana na udhoofika kwa kinga ya mwili unakosababishwa na mashambulizi ya VVU.

2. VVU huambukizwaje?

VVU huambukizwa kwa njia ya:- - Ngono isiyo salama- Kuchangia vifaa vyenye ncha

kali na mtu mwenye VVU- Kuongezewa damu isiyo

salama- Toka kwa mama mwenye

maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto

- Mila potufu

3. Je, mtu kiambukizwa VVU atapitia hatua gani hadi kuwa mgonjwa?

Hatua za VVU/UKIMWI�. VVU huingia kwenye mwili

wa mtu kwa kuambukizwa2. Kipindi cha mpito ambapo

VVU huwa ndani ya mwili wa mtu lakini havionekani katika kipimo (miezi 0-3 ya mwanzo)

2

3. Kipindi cha ukimya ambapo mtu haonyeshi dalili zozote lakini anaweza kuambukiza VVU watu wengine, na akipimwa, VVU huonekana katika kipimo.

Kuzuia maambukizi kwa njia ya damu• Kupima damu • Tumia njia mbalimbali za

kuzuia maambukizi katika vituo vya afya

• Epuka kushika damu kwa kuvaa mipira mikononi na apron

• Vitu vyenye ncha kali kama vile sindano, wembe, vilivyo tumika vitupwe kwa utaratibu sahihi

Kuzuia maambukizi yatokanayo na matumizi ya vitu vyenye ncha kali kama Sindano, wembe• Tokomeza mila potofu za

kukeketa wasichana.• Epuka kuchangia sindano,

nyembe• kutochangia vifaa vya kutogea,

kutahiria nk na wengine.

4. Kipindi cha dalili kuanza ambapo ingawa mtu anaone kana kama mwenye afya, tayari baadhi ya dalili za kuathirika huonekana, ingawa hutibiwa, huchukua muda mrefu kupona

3

4. Je, VVU hupatikana kwa wingi wapi?

5. UKIMWI ni ambapo mtu hushambuliwa na magonjwa nyemelezi ambayo ni vigumu kupona na kinga ya mwili hupungua sana.

VVU hupatikana kwa wingi kwenye majimaji ya mwilini:- Shahawa,Shahawa,- Majimaji ya ukeni,- Damu,- Majimaji wakati wa kujifungua,- Maziwa ya mama

5 VVU huleta madhara gani baada ya kuingia mwilini?

Hushambulia kinga ya mwili na kudhoofisha uwezo wake wa kupambana na magonjwa.

6. Je, nitajizuiaje na maambukizi ya VVU?

Kuzuia maambukizi ya VVU kwa njia ya kujamiiana • Kutokufanya ngono kabisa

(kugunga)• Kuwa mwamiinifu kwa mpenzi

mmoja asiyeambukizwa• Matumizi sahihi ya kondomu• Kufanya ngono salama siku

zote na mara zote• Kutibiwa magonjwa ya

ngono mapema na kwa ukamilifu pamoja na mwenzi

• Kupata ushauri na kupima VVU kwa hiari pamoja na mwenzi.

4

7. Mtu utamtambuaje kama ana VVU au Ukimwi?

• Huwezi kumtambua mwenye VVU kwa kumuangalia !

• Maambukizi ya VVU hupimwa kwenye damu ya mtu na kuchunguzwa kwenye maabara / vituo vya kutolea huduma.

• Kumbuka si rahisi kumjua mtu mwenye VVU bila kupima katika maabara / vituo vya kutolea huduma / maalum

• UKIMWI ni pale ambapo mtu mwenye VVU ameanza kuugua au kuonyesha dalili za magonjwa nyemelezi.

Je, unawezaje kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto? • Kuzuia mimba zisizo

tarajiwa• Kupima VVU kabla ya

kuamua kubeba mimba• Kuanza kliniki ya ujauzito

mapema wakati wa mimba• Kuwa na msaada wa

kifamilia• Kupewa huduma na

matibabu ya UKIMWI wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua

• Kujifungulia katika kituo cha afya kwa ajili ya usalama

• Unyonyeshaji salama –kunyonyesha maziwa ya mama tu kwa miezi sita bila kumpa mtoto chakula kingine chochote au kumyonyesha maziwa ya ng’ombe/kopo.

• Kuzuia na kutibu magonjwa ya matiti ya mama

• Kufuatilia afya ya mama na mtoto mara kwa mara

5

8. Kuna uhusiano gani kati ya lishe bora na VVU/UKIMWI

• Lishe nzuri huimarisha kinga na kinga ikiwa juu hupunguza kasi ya kuongezeka kwa VVU

9. Mwenye maambukizi ya VVU / UKIMWI afanye nini ili aweze kuishi kwa muda mrefu akiwa na afya nzuri?

• Kula mlo wenye virutubisho

• Awe mfuasi mzuri wa dawa za ARV iwapo ameanza. Na nyingine atakazo andikiwa

• Awe anafanya mazoezi mara kwa mara

• Ajipangie muda wa kutosha kupumzika/kulala

• Kuepuka tabia hatarishi (pombe ya kupitiliza, sigara, ngono zembe n.k.)

• Kuepuka/ kupunguza msongo

• Zingatia usafi binafsi

�0. Nini maana ya mlo kamili?

Mlo kamili ni mlo unaojumuisha mafungu makuu manne ya vyakula ambavyo ni: - • Vyakula vya kuleta

nguvu mwilini • Vyakula vya kujenga

mwili • Vyakula vyenye vitamini • Sukari na mafuta

Maji ni muhimu katika kila mlo

6

�� Nini faida za kula mlo kamili (lishe bora)?

• Huboresha na kuharakisha kupona magonjwa yanayohusiana na VVU (magonjwa nyemelezi)

• Huimarisha kinga ya mwili na hivyo kuongeza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa.

• Huzuia kupungua uzito na utapiamlo

• Huuwezesha mwili kuhimili baadhi ya maambukizi

• Huongeza Uwezo wa mwili kuzipokea dawa vizuri na kupunguza athari za dawa za ARV

• Kuboresha maisha

�2. Je, maji yana umuhimu gani mwilini?

• Maji ni muhimu kwa kusafirisha virutubisho, kuondoa masalia/uchafu na kurekebisha joto la mwili.

7

�3. Je, mlo kamili unahusisha vyakula vya aina gani?

Mlo kamili umewegawanyika katika mafungu yafuatayo: -• Nafaka, jamii ya ndizi za

kijani, vyakula vya miziziMahindi, mchele, mtama, ngano, uwelemagimbi, mihogo, viazi, huongeza nguvu na kuufanya mwili ufanye kazi vizuri.

• Vyakula vya protini:Jamii ya maharage na kunde, jamii ya karanga, nyama, maziwa na mazao ya maziwa, samaki, mayai, senene na kumbikumbi. Protini ni muhimu kwa kujenga, kutengeneza na kuimarisha mwili.

• Matunda:Kama mapapai, maembe, machungwa, machenza and mananasi, ubuyu, mabungo na ukwaju ni vina vitamini na madini kwa wingi. Husaidia kujenga kinga ya mwili, na kuimarisha kingo za mapafu na matumbo zisishambuliwe na vimelea kirahisi.

• Mboga za majani:Mchicha, Matembele, Kisamvu, majani ya maboga, bamia, karoti, bamia, maboga, nyanya, mlenda, mchunga, figiri, mnafu hutoa vitamini na madini.

8

• Sukari, asali na mafuta:Mafuta kama siagi, jibini, mafuta ya nazi, mafuta yatokanayo na mbegu za mimea, miwa na asali huongeza nguvu, huongeza ladha na kuamsha hamu ya kula.

Kumbuka! ulaji wa sukari, mafuta na chunvi kwa wingi unahusishwa na magonjwa ya moyo, kisukari na mapigo ya moyo kuwa juu, kwa hiyo viliwe kwa kiasi.

�4. Je, ni muhimu kutumia virutubishi vya nyongeza?

Baadhi ya dawa huongeza mahitaji ya virutubishi ndani ya mwili kwa hiyo kuna wakati virutubishi vya ziada vinahitajika. Lakini virutubishi hivi visichukue nafasi ya mlo kamili bali ni nyongeza. Vilevile, virutubishi vya nyongeza visichukuliwe kama dawa ya kutibu UKIMWI. Ni vizuri kuomba ushauri kwa mtaalam wa afya.

�5. Je, kuna muingiliano wowote kati ya dawa za ARV na chakula?

Ndio, upo muingiliano kwa baadhi ya dawa za ARV na chakula hasa chenye mafuta mengi. Cha muhimu zingatia ushauri wa mtoa dawa.

9

�6. Je, pombe ina madhara yoyote kwa mtu aliyeambukizwa VVU?

Mtu aliyeambukizwa VVU anashauriwa kuacha kutumia pombe kwani matumizi ya pombe huzuia uyeyushwaji na ufyonzwaji wa vyakula na virutubishi ambavyo ni muhimu katika kuimarisha kinga. Pia pombe huathiri uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi.

�7. Ninawezaje kuzuia au kuhimili msongo?

• Epuka kujitenga na wenzako

• Shiriki katika shughuli mbalimbali za kifamilia/ kijamii

• Jisomee hadithi, magazeti na vitabu mbalimbali

• Shiriki kwenye michezo• Sikiliza mziki, kwaya n.k.• Jiunge na vikundi

vya wanaoishi na au wanaowasaidia wenye VVU

• Ongea na watu wako wa karibu au unaowaamini kuhusu hisia zako

�8. Nini maana ya magonjwa nyemelezi?

Ni magonjwa ambayo husababishwa na vimelea ambavyo vinatumia nafasi ya kudhoofika kwa kinga kushambulia mwili. Vimelea hivi huenda visingeweza kuleta madhara kwa mtu mwenye kinga madhubuti

�0

�9. Je, magonjwaagonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea mara kwa mara ni yapi?

Magonjwa nyemelezi:• Kuharisha • Malaria• Kifua kikuu (TB)• Vichomi

vinavyoambatana na kifua kubana na kikohozi kikavu

• Homa ya Uti wa mgongo ikiambatana na kuumwa sana na kichwa, homa na shingo kukakamaa

• Utando mweupe mdomoni ambao unafutika kwa urahisi

• Magonjwa ya ngozi• Magonjwa ya ngono• Mkanda wa jeshi• Kansa ya ngozi

20. Nini faida ya mpango wa kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto?

�. Kupata huduma za kuzuia maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto mapema

2. Hupata taarifa na elimu kuhusu kuzuia maambukizi kwa wengine.

3. Atapewa rufaa kwa huduma zaidi kwake na familia yake (dawa, kufuatiliwa watoto)

4. Kufanya maamuzi kuhusu tabia au jinsi ya kuishi baadae

��

2�. Je, maambukizi huweza kutokea katika kipindi gani?

Maambukizi huweza kutokea: �. wakati wa uja uzito2. Wakati wa uchungu/

kujifungua 3. Wajkati wa

kunyonyesha

22. Je, mwanamke anayeishi na VVU anaweza kubeba mimba na kuzaa salama?

Ndio, lakini kabla ya kuamua kubeba mimba ni vizuri kumuona muhudumu wa afya ili uelimishwe jinsi gani utaweza kupunguza au kuzuia kujifungua mtoto mwenye VVU. (to add more information, from DAC)

23. Nitawezaje kuzuia maambukizi toka wkwa mama kwenda kwa mtoto?

Kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto • Kuzuia mimba zisizo

tarajiwa• Kupima VVU kabla ya

kuamua kubeba mimba• Kuanza kliniki ya ujauzito

mapema wakati wa mimba• Kuwa na msaada wa karibu

kutoka kwa familia• Kupewa huduma na

matibabu ya UKIMWI wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua

• Kujifungulia katika kituo cha afya kwa ajili ya usalama

• Unyonyeshaji salama – kunyonyesha maziwa ya mama tu kwa miezi sita bila kumpa mtoto chakula kingine chochote au kumyonyesha maziwa ya ng’ombe/kopo.

�2

• Kuzuia na kutibu magonjwa ya matiti ya mama

• Kufuatilia afya ya mama na mtoto mara kwa mara

24. Nini faida za kiafya za kufanya mazoezi kwa mtu anayeishi na VVU?

Faida za kiafya za kufanya mazoezi kwa mtu anayeishi na VVU zinajumuisha:• Kujenga mwili na kupunguza

uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo, kisukari na kansa.

• Inaboresha afya ya mwili ,yanaimarisha mifupa,hupunguza dalili za sonona na msongo wa mawazo.

• Inamsaidia mgonjwa kupata usingizi

• Inapunguza mafuta kwenye tumbo na kurekebisha uzito.

• Inasaidia kinga ya mwili isishuke

• Inawezesha mfumo wa chakula kufanya kazi vizuri na kuongeza hamu ya kula.

25. Kwa siku natakiwa kufanya mazoezi kwa muda gani ili kuweka mwili wangu katika Afya nzuri?

Unatakiwa kufanya mazoezi kila siku kwa muda usiopungua nusu saa, kumbuka usifanye mazoezi kama haujisikii vizuri.

�3

26. Je, unauelewa gani kuhusu yanyapaa, ubaguzi na kujikana kwa mtu anayeishi na VVU?

• Unyanyapaa ni mtazamo au fikra za kumwona mtu hastahili heshima wala hana thamani katika jamii na kuweza kumpa jina au sifa mbaya zinazomlenga na kuonekena ni fedheha au aliyegeuka maadili ya jamii

• Ubaguzi ni kitendo kinachotokana na dhana ya unyanyapaa kwa watu wenye VVU au wanaodhaniwa kuwa na VVU

• Kujikana/kukana ni kwa mtu mwenye VVU kukataa kwamba ana maambukizi ya VVU tayari

27. Je, unafikiri ni nini chanzo cha unyanyapaa na ubaguzi ?

Unyanyapaa na ubaguzi unaweza kusababishwa na mambo yafuatayo :

• Kutoelewa au kuwa na uelewa mdogo juu ya VVU na UKIMWI

• Ukweli kwamba VVU/UKIMWI hauna tiba

• Dhana potofu ya namna VVU vinavyoambukizwa

• Uelimishaji hafifu katika vyombo vya habari

�4

• Hofu ya jamii kutoa elimu ya ngono

• Hofu ya kuugua na kufa

28. Je, unajua matokeo ya unyanyapaa na ubaguzi ?

Matokeo ya unyanyapaa na ubaguzi ni :

• Kuongezeka kwa maambukizi mapya ya VVU

• Kutengwa na jamii• Kupunguza utayari wa

mgonjwwa kufika kituo cha huduma kupata huduma

• Kifo

29. Je, ninawezaje kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi ?

Njia zifuatazo zinaweza kusaidia kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi :

• Kuwa na elimu/uelewa sahihi juu ya VVU na UKIMWI hasa njia za kujikinga na maambukizi

• Kujitangaza kuhusu hali ya kiafya kwa wenye maambukizi ya VVU kwa watu walio karibu nao

• Kujitangaza kwa wenye maambukizi ya VVU kwa jamii

• Kuwahusisha wenye VVU katika utoaji wa huduma

�5

30. Ufuasi ni nini?

• Kushiriki katika shughuli mbalimbali za kifamilia, kijamii, kidini na mashirika mbalimbali

• Kushirikiana na ASASI za kijamii zinazojihusisha na shughuli za VVU na UKIMWI

Ni makubaliano kati ya mgonjwa na mtoa huduma na mgonjwa kuelewa na kukubali kufanya mabadiliko ya muhimu kuboresha afya yake.

3�. Unaelewa nini Ufuasi wa dawa za ARV?

Kumeza dawa sahihi, kwa kipimo sahihi , kwa muda sahihi na kwa njia sahihi. Bali siyo kufuata maelekezo tu ila inahitaji kujitoa na uelewa wa matibabu.

32. Nini umuhimu wa ufuasi?

Ni ya muhimu sana kwa WAVIU kwa sababu VVU vinazaliana kwa haraka pasipo kutumia dawa za ARV.

33. Athari za kutokuwa mfuasi mzuri wa ARV

• Inachangia kuongeza usugu wa vimelea kwa ARV

• Inaongeza wingi wa Virusi mwilini

• Mabadiliko ya aina ya virusi (VVU)

�6

34 Tutafanyaje kuzuia VVU visiwe sugu kwa dawa za ARV?

• Kudorora kwa maisha• Kuongezeka magonjwa

nyemelezi• Kuongezeka ugumu wa

matibabu baadae

Kuwa mfuasi mzuri wa dawa kwa kumeza dawa sahihi, kwa kipimo sahihi , kwa muda sahihi na kwa njia sahihi

35 Taja njia za kupima ufuasi mzuri wa dawa.

• Taarifa binafsi• Hesabu/ idadi ya

vidonge• Rekodi za kutolea

dawa• Kunywa dawa chini ya

uangalizi • Kutumia vifaa vya

elektroniki• Kufuatilia vipimo vya

maabara , mfano wingi wa virusi na kuongezeka kwa CD4

• Uamuzi/ tathmini ya mtoa huduma

36 Taja njia za kukumbushia/ kusisitiza ufuasi wa dawa

• Kumtayarisha mtumiaji kutumia ARV

• Vifaa vya elektroniki mfano, saa, simu za mkononi.

• Kutumia wasaidizi wa matibabu kama; rafiki, ndugu, WAVIU na mgonjwa mwenye uzoefu wa kutumia ARV

�7

37 Ni zipi faida za kuwa mfuasi mzuri wa dawa?

• Kalenda ya kumbukumbu ya matumizi ya dawa

• Vikundi vya kusaidiana vinaweza kusisitiza ufuasi wa dawa kwa kuwaka mazingira ambayo yanaruhusu majadiliano na WAVIU.

• Chati za dawa zinazoonyesha majina ya dawa za ARV na kiwango cha matumizi.

• Inapunguza wingi wa virusi mwilini, huongeza CD4 , hupunguza hatari ya kutoka kwenye VVU kwenda kwenye UKIMWI

• Inasaidia kugundua madhara mapema

• Inasaidia kukinga magonjwa nyemelezi

• Inajenga uhusiano chanya kati ya mgonjwa na mtoa huduma

• Kupunguza athari usugu wa dawa hivyo kuboresha matibabu ya baadae

�8

39. Taja visababishi vinavyosaidia ufuasi wa kutumia dawa za ARV

• Utayari wa kuanza dawa

• Uelewa wa dawa• Kuwa na imani na

utendaji kazi wa dawa ya ARV

• Mfumo wa maisha wa WAVIU ( kutotumia madawa ya kulevya , pombe , mpangilio wa kazi, ugumu wa maisha)

• Kutokuwa na msongo wa mawazo

• Kushirikisha kuhusu hali yako ya maambukizi ya VVU.

38. Nini visababishi vinavyozuia ufuasi mzuri wa dawa ya ARV

• Adha ya kunywa dawa• Matatizo ya kifedha • Mfumo wa maisha

– utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe

• Matatizo ya kifamilia• Kutokufuata miadi ya

kuhudhuria kliniki• Imani za kidini• Aina ya ajira• Unyanyapaa• Umbali mrefu kutoka

kituo cha afya• Madhara makubwa ya

dawa• Matatizo ya

mawasiliano- vipangamizi vya lugha, tofauti ya mila, viwango vya elimu etc.

�9

• Upatikanaji wa chakula bora, hali ya maisha, uwezo wa kupata nauli

• Kutokuwa na hofu• Kutojitenga na jamii• Msaada wa kijamii-

WAVIU wanatakiwa wapate msaada kutoka kwa wanaowaangalia ili waweze kuwa wafuasi wazuri wa kutumia ARV

• Matokeo mazuri ya dawa

Dhana Potofu

40. Kula nyama ya nguruwe kunatibu VVU na UKIMWI

Hapana, Kula nyama ya nguruwe hakutibu VVU na UKIMWI

4�. Kuokoka na maombi kunatibu UKIMWI

Hakuna uhakiki juu ya jambo hili, ila pamoja na maombi, unashauriwa kuendelea kutumia huduma za afya.

42. Mila za Utakaso zinatibu UKIMWI

Hapana, mila ya utakaso hazitibu UKIMWI wala VVU

43. Kuumwa na wadudu kama mbu au kunguni kunaambukiza VVU

Kuumwa na wadudu kama mbu au kunguni hakuwezi kuambukiza VVU

20

44. Kupeana mikono, kushikana, kukumbatiana, kucheza pamoja, kufanya kazi au kwenda shule na mgonjwa mwenye VVU huambukiza VVU

Kupeana mikono, kushikana, kukumbatiana, kucheza pamoja, kufanya kazi au kwenda shule ana mgonjwa mwenye VVU hakuambukizi VVU

45. Kuchangia vyoo, simu, vyombo, bafu na mabwawa kunaambukiza VVU

VVU haiwezi kuambukizwa kwa kuchangia vitu mbalimbali mfano vilivyotajwa.

46. VVU inaweza kuambukizwa kwa kukohoa, kupiga chafya au kupiga busu kavu.

VVU haiwezi kuambukizwa kwa kukohoa, kupiga chafya au kupiga busu kavu

47. Uchawi unaweza kutumika kuambukiza VVU

Sio kabisa,uchawi hauwezi kutumika kuambukiza VVU

48. Kwamba, Kondomu inatengenezwa ndogo . zinapasuka sana, zinatoka na kuingia kwenye uke na sio za kuaminika

Si kweli, kondomu zinaweza kuvutika kufikia ukubwa wa kichwa cha mtu na hivyo zinaweza kutumika na wanaume wote, zinafanyiwa majaribio ya ubora. Zinapasuka mara chache kama zikihifadhiwa vizuri na kutumiwa katika muda muafaka.

2�

49. Kondom zina VVU

Ili kuzuia kondom kuingia kwenye uke inatakiwa kuvuliwa wakati uume ukiwa umesimama.Ikitokea kuingia kwenye uke inaweza kutolewa kwa kidole kimoja.

Kondomu hazina VVU kwa kuwa haviwezi kuishi nje ya chembechembe hai za damu za binadamu.( Check out on the fact, Dr. Bigawa) Kinyume chake kondomu inasaidia kuzuia maambukizi ya VVU na magonjwa ya Ngono endapo itatumika vizuri

50. Kondomu hupunguza raha ya tendo la ndoa, na kuwashwa sehemu za siri.

Kondomu haipunguzi raha ya tendo la ngono. Wachache wanaopata madhara ya kuwashwa sehemu za siri wanashauriwa kupata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya.

5�. UKIMWI unawapata Malaya na waasherati tu

Hii si kweli kwa kuwa mtu yeyote anaweza kuambukizwa VVU akipatwa na damu au majimaji yenye maambukizi.

52. Ukiugua kifua kikuu na homa ya mapafu tu una UKIMWI.

Si kweli, ingawa baadhi ya wenye kifua kikuu wanaonyesha dalili za kuambukizwa UKIMWI

22

53. Kila mwenye VVU amevipata katika uasherati.

Hapana, maambukizi yanaweza kupatikana kwa njia nyingine kama vile kuongezewa damu.

54. Watu wenye umri zaidi ya miaka 50 awaambukizwi VVU

Hapana, watu wote wanaweza kuambukizwa VVU bila kujali umri.

55. Watu wanaoishi na VVU na wanandoa wenye maambukizi ya VVU hawapaswi kujamiiana tena

Hii siyo kweli wanaweza kujamiiana, lakini wanashauriwa kutumia kondomu kuzuia maambukizi mapya.

56. Dawa za kienyeji na maji matakatifu ni tiba ya UKIMWI

Baadhi ya tiba mbadala ( to check out from Tiba mbadala, Ministry of Health and Social Welfare)

Hadi sasa UKIMWI hauna dawa, hata hivyo watu walio na maambukizi ya VVU na wale wanaoumwa UKIMWI wanashauriwa kutumia dawa za ARV kwa ushauri wa wahudumu wa afya ili kuongeza umri wa kuishi.

57. Kupima na kugundua kuwa umeathirika ni sawa na hukumu ya kifo*Siku hizi sio common

Hii si kweli kwani watu wenye VVU wanaweza kurefusha maisha kwa kutumia dawa za ARV vizuri na kuchukua tahadhari zinazotakiwa.

23

58. Huduma na madawa ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI ni kwa ajili ya matajiri tu.*Siku hizi sio common

Hapana, huduma za afya na dawa za ARV ni kwa ajili ya watu wote na dawa hizi hutolewa bure.

59. Mtu anayetumia dawa za kupunguza makali ya VVU akijisikia vizuri tu, basi amepona UKIMWI.

Watu wanaotumia ARV hawajapona hata kama wanajisikia vizuri ,wanatakiwa waendelee kutumia dawa hizo

60. Mwanamke liyeambukizwa virusi vya Ukimwi hawezi kuzaa mtoto

Kauli hii sio sahihi kwani anaweza kupata mtoto lakini anatakiwa kupata maelekezo ya wataalam ya jinsi ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

6�. Mgonjwa anaweza kutumia ARV zake na watu wengine ndani ya familia.

Hapana, mgonjwa haruhusiwi kutumia dawa za ARV na watu wengine ndani ya familia.

62. Mgonjwa anaweza kuacha kutumia dawa kama akijisikia afya yake imeimarika

Hapana, asiache kutumia dawa hata kama afya yake imeimarika.

24

63. Kufanya ngono na mtoto mdogo au wanyama wanaofugwa nyumbani hutibu UKIMWI

Hapana, kufanya tendo la ngono na mtoto mdogo au wanyama wanaofugwa nyumbani hakutibu UKIMWI

KIONGOZI CHA MUELIMISHAJI RIKA

VVU

UKIMWINA

VVU

UKIMWINA