fataawa za wanachuoni (34)
DESCRIPTION
Fataawa Za Wanachuoni (34)TRANSCRIPT
1
فتاوى العلماءFataawa Za Wanachuoni
[34]
Imefasiriwa Na Kutayarishwa Na:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
©
2
Dibaji:
Hizi ni Fataawa za wanachuoni mbali mbali ambazo nimezikusanya ili
kuweza kuwasahilishia ndugu zetu Waislamu na khaswa wale watafutaji
elimu. Fataawa ni mchanganyiko kuhusiana na masuala mbali mbali ya
Tawhiyd, ´Aqiydah, Manhaj, Fiqh na mengineyo.
Hivyo, ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) ziweze kuleta faida kwa ndugu
zetu Waislamu, na ninamuomba Allaah (´Azza wa Jalla) Ajaalie kazi hii niwe
nimeifanya kwa kutafuta Radhi Zake (Subhaanahu wa Ta´ala), na Amlipe kila
Aliyeisambaza kwa ndugu mwengine na Awalipe ndugu wasomaji wote kwa
jumla.
Tanbihi: Fataawa zote hizi tumezifasiri kwa njia ya Video na zinapatikana
Youtube waweza kusoma na huku wasikiliza. Kwa mwenye kutaka hizo
Fataawa za Video aende Alhidaaya au Youtube kwa juu sehemu ya kutafuta
aandike au kukopi kichwa cha habari cha Fatwa (kama ilivyo hapo chini kwa
kila Fatwa ina kichwa chake cha habari) na atafute itajitokeza In Shaa Allaah.
Jazaakumu Allaahu Khayra
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.
3
Fataawa zilizomo:
1) Je Kuna Du´aa Maalum Ya Kumuombea Mtoto Wa Kuwaliza?
2) Inajuzu Kumuadhinia Mtoto Anapozaliwa?
3) Hukumu Ya Kumlipa Mtu Deni Msikitini
4) Ameapa Kutojichua Sehemu Za Siri Ila Kafanya, Alipe Kafara?
5) Ni Kipi Chakula Cha Majini Wa Kiislamu?
6) Mtu Akivua Soksi Alizopaka Juu Yake, Wudhuu Unatenguka?
7) Kusikiliza Qur-aan Na Kusoma Adhkaar Kwa Mwenye Janaba
8) Je Inajuzu Kutoa Zakaatul-Fitwr Pesa?
9) Inajuzu Kumpa Mtoto Jina La "Iynaas"?
10) Nasaha Za Shaykh Zayd Kwa Wale Wenye Kuangalia Filamu Za Ngono
11) Hukumu Ya Kulala Na Janaba
12) Aanze Na Swalah Ya Janaza Au ´Aswr Na Jamaa´ah Ya Pili?
13) Mama Kashika Tupu Ya Mtoto Hali Kishatawadha
14) Kundi Limechelewa Siku Ya Ijumaa, Waswali Ijumaa Au Dhuhr?
15) Je Hadiyth Dhaifu Hutumiwa Katika Fadhwaail al-A´amaal?
16) Inajuzu Kubusu Msahafu?
17) Hukumu Ya Kujitibu Kwa Tumbaku
18) Inafaa Kuwa Na Isbaal Kwa Mwenye Kuwa Na Kilemba?
19) Kijana Kila Anapotubia Anarudi Kufanya Dhambi Tena
20) Kafunga Mwezi Mzima Wa Muharram, Kapatia?
21) Kipigo Cha Kutia Adabu Kinachoruhusu
22) Kafunga Sunnah Kisha Baadae Kaamua Kula
23) Imamu Kakumbuka Kuwa Nguo Yake Ina Madhiy Ndani Ya Swalah
24) Ewe Kaka Wa Kiislamu, Mtume Wako Akuamrisha Kufuga Ndevu
25) Imamu Na Muadhini Hawatakiwi Wawe Watu Wa Bid´ah; Kama Suufiy,
Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy
26) Twawaaf Ya Kuaga Ni Wajibu Katika ´Umrah
27) Baba Hataki Kuwaozesha Mabinti Zake Kwa Kukhofia Riziki Zao
28) Hukumu Ya Kubaki Macho Baada Ya Swalah Ya ´Ishaa
29) Kuuza Katika Maeneo Ya Msikitini Kama Bustani La Msikitini
30) Mtu Anataka Kulipa Deni Katika Pesa Za Zakaah
31) Mwanaume Anaruhusiwa Kuvaa Pete?
32) Du´aa Nzuri Wakati Mwanamke Anataka Kuzaa
33) Hadiyth Ya Waislamu Kupeana Zawadi Ili Wapendane
34) Kuswali Swalah Za Sunanh Kabla Ya Swalah Ya Ijumaa
35) Mtoto Akipita Mbele Ya Mwenye Kuswali Swalah Yaharibika
36) Mwanamke Mgonjwa Anastanji Na Kujiosha Kwa Maji Ya Zamzam
37) Talaka Inatokana Na Alivyokusudia (Nia) Ya Mume
4
38) Dada Anataka Kubadilisha Rangi Ya Nywele Zake Nyeusi
39) Hukumu Ya Unyevu (Majimaji, Utoko) Umtokao Mwanamke
40) Kuna Muda Maalumu Wa Mtu Kufanya Kijicho?
41) Mwanamke Anatokwa Na Upepo Kwenye Tupu Ya Mbele, Hukumu Ya
Swalah Yake
42) Baadhi Ya Sifa Zinazopasa Kuwa Na Mke Mtarajiwa
43) Hukumu Ya Kupuuza Swalah Mpaka Ukaondoka Wakati Wake
44) Hukumu Ya Kubusu Msahafu Na Kuuweka Chini
45) Hukumu Ya Kula Daku Baada Ya Adhaana Ya Pili Ya Fajr
46) Hukumu Ya Kupuuza Swalah Mpaka Ukaondoka Wakati Wake
47) Hukumu Ya Mume Kamwambia Mke Wake Wewe Ni Kama Mamangu
48) Imefika Ramadhaan Na Ana Deni La Ramahaan Ingine
49) Inafaa Kwa Kwenye Kukaa Eda Kuangalia Jua, Mwezi, Nyota, Mbingu,
Kupika, Ndugu Zake?
50) Je Mkaaji Eda Haruhusiwi Kutoka Nyumbani Kabisa?
51) Je Salaf Waliwahi Kutofautiana Katika ´Aqiydah?
52) Kajiapiza Kutofanya Kitu Fulani Kisha Akamtaliki Mke Wake
Wanachuoni waliomo:
1) ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
2) ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
3) ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
5
Bismillaahi Rahmaani Rahiym
1) Je Kuna Du´aa Maalum Ya Kumuombea Mtoto Wa Kuwaliza?
Swali:
Je kuna Du´aa maalum ya kumuombea mtoto mpya wa kuzaliwa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Sijui kama kuna Du´aa makhsus. Ila atamuomba Allaah (´Azza wa Jalla)
Amjaalie kuwa mtoto mwema na mtiifu kwa wazazi wawili, awe ni mwenye
kumtii Allaah (´Azza wa Jalla) na mwenye kufuata Sunnah za Mtume wa
Mtume wa Allaah (´alayhis-Salaam). Na Allaah Atampokelea Du´aa yake.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2301
2) Inajuzu Kumuadhinia Mtoto Anapozaliwa?
Swali:
Ipi hukumu ya kumtolea adhaana katika masikio ya mtoto mwenye kuzaliwa?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hadiyth hii ni dhaifu. Haadhiniwi katika sikio lake la kulia wala hakimiwi
Swalah katika sikio lake la kushoto.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4870
6
3) Hukumu Ya Kumlipa Mtu Deni Msikitini
Swali:
Ipi hukumu ya kurudisha (lipa) deni Msikitini?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hakuna ubaya, kwa kuwa hili si kununua wala kuuza. Ni amana ya watu
aliokuwa nayo anairudisha kwa mmiliki. Hakuna ubaya. Lakini wasirefushe
sana hesabu na maongezi kuhusu kununua na kuuza ambayo ndio ilikuwa
sababu ya deni hili. Iwe ni kama amana alichukua sasa anamrudishia mmiliki
kisha aende zake. Hakuna ubaya kwa hilo.
Chanzo: http://youtu.be/lEhpBOGDmJE
4) Ameapa Kutojichua Sehemu Za Siri Ila Kafanya, Alipe Kafara?
Swali:
Aliapa kuwa hatojichua sehemu za siri (kupiga punyeto), halafu baadae
akafanya. Anauliza je anawajibika kutoa kafiri?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ndio. Utatoa kafara kumuadhimisha Allaah (´Azza wa Jalla) kwa kuwa
uliapa Kwake na hukuchunga ulichokiapia. Na umuombe Allaah (´Azza wa
Jalla) kwa kufanya kwako maasi haya. Ni Haramu. Ni ni juu yako kupigana
Jihaad na nafsi yako. Usijiachie kwa Shaytwaan wala kwa maasi. Ni Haramu
Haramu, na upigane Jihaad kwa hili. Huku ukifanya sababu, kama kuoa ni
katika sababu. Mwenye ada ya kufanya kitendo hiki kichafu. Kufunga pia ni
katika sababu za kuacha kitendo hiki kichafu. Tangamana na watu wema na
ukae nao, tafuta elimu pia yote haya ni katika sababu. Jitahidi kusahau
7
mambo haya na kutojishughulisha kabisa, ni katika sababu. Ama kulifikiria
sana, hii ni katika sababu ya kupelekea ukalifanya tena.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5419
5) Ni Kipi Chakula Cha Majini Wa Kiislamu?
Swali:
Je ni sahihi kuwa majini ya Kiislamu yanakula mifupa ambayo ilitajiwa Jina la
Allaah wakati wa kuitupa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Bila shaka, kumepokelewa (Hadiyth) kuhusiana na hili Hadiyth.
Chanzo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2291
6) Mtu Akivua Soksi Alizopaka Juu Yake, Wudhuu Unatenguka?
Swali:
Je Wudhuu utatenguka ikiwa aliyezivaa atazivua baada ya kupaka juu yake?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Ndio akivua soksi kwa muda maalumu, kwa mkazi ni siku (mchana) moja na
usiku wake, msafiri siku tatu - akivua soksi Twahara yake imebatilika na ni
juu yake kutawadha upya na azivae kwa Twahara kamili.
8
Chanzo: http://youtu.be/K4C8vy4Pw18
7) Kusikiliza Qur-aan Na Kusoma Adhkaar Kwa Mwenye Janaba
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza Qur-aa na kusoma Adhkaar naye yuko katika
janaba?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kusikiliza Qur-aan na kusom Adhkaar hakuna ubaya inajuzu. Ila Qur-aan
asiisome naye yuko katika janaba.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4863
8) Je Inajuzu Kutoa Zakaatul-Fitwr Pesa?
Swali:
Muulizaji kutoka Ubelgiji, je inajuzu kutoa Zakaatul-Fitwr pesa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hapana, imethibiti kutoa Zakaatul-Fitwr chakula. Na pesa zilikuwepo wakati
wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ila hakutoa yeyote katika
Maswahabah wake Zakaah pesa. Hata kama baadhi ya wanachuoni
wamejuzisha hilo, ila maneno yao yanarudishwa kwa kuwa yanakhalifu
Sunnah. Sunnah ni kutoa chakula ambacho kinapatikana katika mji huo, wala
mtu asitoe pesa.
9
Chanzo: http://youtu.be/ki4SAYRjDrI
9) Inajuzu Kumpa Mtoto Jina La "Iynaas"?
Swali:
Je inajuzu kumpa mtoto jina la "Iynaas"?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa hakuna ubaya In Shaa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4866
10) Nasaha Za Shaykh Zayd Kwa Wale Wenye Kuangalia Filamu Za
Ngono
Swali:
Ipi hukumu ya mwenye kuingia tovuti chafu za ngono kwenye Intanet, na
anaangalia Aliyoharamisha Allaah. Ipi nasaha yako kwao?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Hukumu yake ni kwamba anafanya dhambi kubwa na itamfanya nafsi yake
kuwa chafu. Allaah Anamwangalia na yeye yuko katika maasi. Ni wajibu
kwake kuwa na aibu kwa Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala) ambaye Humzidishia
mtu mwema kwa Ihsaan Zake na Humzidishia kwa fadhila Zake, na Humlipa
mtenda dhambi kutokana na ´amali yake ilivyo, kutokana na Hekima na
Uadilifu Wake. Ni juu ya watu hawa wanaotumia njia kama hizi kwa kufanya
ya Haramu na maasi, wamche Allaah. Hakika Allaah (´Azza wa Jalla) hata
10
kama bado anawaacha hajashindwa kuwakamata. Ni bora kwao kukimbilia
kuomba Tawbah maadamu roho bado ingali mwilini, waache matendo
machafu na waazimie kuacha kabisa na wasiyarudi.
Chanzo: http://youtu.be/LAnhy8aBVk4
11) Hukumu Ya Kulala Na Janaba
Swali:
Ipi hukumu ya kusikiliza Qur-aa na kusoma Adhkaar naye yuko katika
janaba?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kusikiliza Qur-aan na kusom Adhkaar hakuna ubaya inajuzu. Ila Qur-aan
asiisome naye yuko katika janaba.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4863
12) Aanze Na Swalah Ya Janaza Au ´Aswr Na Jamaa´ah Ya Pili?
Swali:
Kuna mtu aliingia Msikitini na Swalah ya Jamaa´ah imeshampita,
wakasimama watu kuswali Swalah ya janaza. Je aswali ´Aswr na Jamaa´ah ya
pili au aswali Swalah ya janaza?
´Allaamah al-Waswaabiy:
11
Aanze kwanza na Swalah ya maiti kisha ndo aswali faradhi iliyompita.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5187
13) Mama Kashika Tupu Ya Mtoto Hali Kishatawadha
Swali:
Je mama atawadhe tena ikiwa atashika tupu ya mtoto wake?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni ndio, atawadhe tena.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4874
14) Kundi Limechelewa Siku Ya Ijumaa, Waswali Ijumaa Au Dhuhr?
Swali:
Likiingia kundi siku ya Ijumaa na Imamu amekwishaswali. Je, waswali Ijumaa
au waswali Dhuhr?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa wataswali Dhuhr. Ila tu ikiwa watamkuta Imamu bado yu wima
katika Rakaa ya pili, hapo wataswali Ijumaa. Ama ikiwa kishainuka kutoka
katika Rukuu katika Rakaa ya pili, wataswali Dhuhr.
12
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5179
15) Je Hadiyth Dhaifu Hutumiwa Katika Fadhwaail al-A´amaal?
Swali:
Je wamekubaliana wanachuoni kutumia Hadiyth dhaifu katika "Fadhwaail al-
A´amaal" kama alivyosema hilo an-Nawawiy?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni hapana, hawakukubaliana. Kauli yenye nguvu ni kuwa Hadiyth dhaifu
haitumiwi. Asli ni kuegemea katika yaliyothibiti kutoka kwa Mtume wa
Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4873
16) Inajuzu Kubusu Msahafu?
Swali:
Ipi hukumu ya kubusu msahafu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Haijulikani kwa Salaf suala la kubusu msahafu. Msahafu mapenzi yake ni
ndani ya moyo na si kwa kubusu. Hatujui kwa Salaf kuwa walikuwa
wakibusu msahafu. Mtu asiubusu msahafu.
Chanzo: http://youtu.be/pUoYt3FEtzE
13
17) Hukumu Ya Kujitibu Kwa Tumbaku
Swali:
Ipi hukumu ya kujitibu kwa tumbaku?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Tumbaku nakunasihi kujiepusha nayo. Na mada yako mengi mbali na hii
tumbaku, sehemu za madawa. Pia asali ni dawa, Habbat sawdah In Shaa
Allaah na kadhalika.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4861
18) Inafaa Kuwa Na Isbaal Kwa Mwenye Kuwa Na Kilemba?
Swali:
Je kilemba kina Isbaal?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa imekuja hii pia katika Hadiyth, Isbaal katika kanzu, kikoi na
kilemba.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=5209
14
19) Kijana Kila Anapotubia Anarudi Kufanya Dhambi Tena
Swali:
Mimi ni kijana nimefanya dhambi nikatubia, kisha nikatubia kwa Allaah
lakini nikarejea tena katika dhambi hii, ipi nasaha zako kwangu?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Rejea uombe tena Tawbah yakweli na wala usikate tamaa kwa Rahmah ya
Allaah. Lakini rejea uombe Tawbah yakweli na uwe mkweli kwa Allaah
(´Azza wa Jalla). Atakusamehe Allaah dhambi yako na Ataifanya kuwa mema.
Lakini kuwa mkweli katika Tawbah yako na Allaah (Tabaaraka wa Ta´ala).
Chanzo: http://youtu.be/e7huH83HlvU
20) Kafunga Mwezi Mzima Wa Muharram, Kapatia?
Swali:
Atakayefunga mwezi wa Muharram wote au baadhi ya siku chache, je kitendo
chake hiki kapatia?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ndio ni sahihi. Muulizaji anasema kwa kuwa nimesikia katika Hadiyth:
"Swawm bora kwa Allaah baada ya Ramadhaan ni Swawm ya mwezi wa
Allaah Muharram."
Jibu ni ndio, Hadiyth hii ni sahihi.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4708
15
21) Kipigo Cha Kutia Adabu Kinachoruhusu
Swali:
Mwalimu anaweza kumpiga mwanafunzi kumuogopeshe ili arejee kufanya
jambo fulani au kuacha jambo fulani, je hili pia linangia katika tishio [la
dhuluma]?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kipigo cha kumuweka [kumtia] adabu mwalimu mnasihiaji kwa mwanafunzi,
kipigo cha kumuweka adabu kidogo halaumiwi kutokana na maslahi kwake
[mwanafunzi] na kumkinga na yatayomdhuru katika uhai wake na Mustaqbal
wake. Pia kipigo cha baba kwa mtoto wake, na kwa mleaji - kama mtu
mkubwa kwa mdogo, hali kadhalika mume kwa mke wake katika baadhi ya
hali kama jinsi Allaah Alivyotoa idhini hio. Hichi huitwa kipigo cha kuweka
adabu na kutengeneza. Atakayefanya hana makosa wala haingii katika
kufanya dhuluma. Lakini ikiwa atachupa mipaka katika kupiga, hapo
atachukuliwa amefanya dhuluma. Na ikiwa atapiga bila ya haki hata kama
kitakuwa ni kipigo kidogo, atachukuliwa ni dhalimu na siku ya Qiyaamah
Allaah naye Atamlipiza.
Chanzo: http://youtu.be/e0PZUe5gE3A
22) Kafunga Sunnah Kisha Baadae Kaamua Kula
Swali:
Kuna kanuia kufunga Swawm ya Naafil, akala wala hakutimiza Swawm yake.
Je huku ni kuharibu ´amali na kunaingia katika Kauli Yake Allaah:
أعمالكمااتبطلوااولا
16
"Wala msiviharibu vitendo vyenu." (47:33)
´Allaamah al-Waswaabiy:
Imekuja katika Hadiyth, anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Mwenye kufunga Swawm ya Sunnah na msafiri wanakhiari, wakitaka
watafunga na wakitaka watakula."
Hakuna ubaya akila na lau angelitimiza Swawm yake ingelikuwa bora.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4701
23) Imamu Kakumbuka Kuwa Nguo Yake Ina Madhiy Ndani Ya Swalah
Swali:
Akikumbuka Imamu kuwa katika nguo yake kuna madhiy, atoke katika
Swalah au aitimize?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa madhiy ni najisi. Akiweza kuvua nguo hii aivue na aendelee na
Swalah. Na akiwa hawezi atoke [ndani ya Swalah] na paingie nafasi yake mtu
mwingine.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=283
24) Ewe Kaka Wa Kiislamu, Mtume Wako Akuamrisha Kufuga Ndevu
Swali:
17
Hukumu ya kunyoa ndevu au kutoa kitu humo?
´Allaamah al-Waaswabiy:
Kufuga ndevu ni wajibu. Na kuzinyoa au kutoa kitu humo ni Haramu. Kwa
kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
"Kuweni kinyume na washirikina; fugeni ndevu kwa wingi na punguzeni
masharubu." [Muttafaq, Ibn ´Umar]
Mtume (´alayhis-salaam) anakuamrisha kufuga ndevu. Wewe zifuge na wala
usitoe humo kitu. Na anakuamrisha kuacha masharubu, usiyafanye marefu
wala usiyatoe yote.
Na Allaah Anasema:
أليم ااعذاب اايصيبهمااأواافتنة ااتصيبهمااأناأمرهااعناايخالفونااالذيناافليحذرا
"Basi nawatahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapatamsiba au
ikawapata adhabu chungu." (24:63)
Usijiamini. Kumbuka yule mtu aliyekuwa anakula kwa Mtume (Swalla
Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mkono wake wakushoto, akamwambia:
"Kula kwa mkono wakulia!". Akasema: "Siwezi". Akamwambia: "Hutoweza
kamwe."
Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi. Hakika Mtume alimuamrisha kula kwa
mkono wakulia, akasema hapana siwezi. Akamuombea Du´aa kumwambia
"Hutoweza." Wewe pia usijiamini. Akikuamrisha Allaah au Mtume Wake
(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi tekeleza. Na akikukataza Allaah au
Mtume Wake kwa kitu, basi jitenge nacho.
سولااآتاكمااوما قواافانتهوااعنهاانهاكمااوماافخذوهااالر ااوات ااإنااللا العقابااديداشااللا "
"Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho.
Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu." (59:07)
18
Chanzo:
http://www.olamayemen.net/default_ar.aspx?id=283&Name=%D8%A7%D9%
84%D9%81%D8%AA%D8%A7%D9%88%D9%89
25) Imamu Na Muadhini Hawatakiwi Wawe Watu Wa Bid´ah; Kama
Suufiy, Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy
Swali:
Muulizaji kutoka UK. Hakuna katika Msikiti wetu muadhini, vipi
tutamchangua muadhini na kwa kitu gani tutaangalia kwa mwenye kufaa
kutoa adhaana?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kwa hakika ni kwamba ni lazima kwa waliohai kuwa na Msikiti, na ni lazima
kwa Msikiti kuwepo na Imamu na muadhini, ili watu wahifadhi wakati na
waswali Jamaa´ah. Kwa Imamu anashurutishwa awe mtu mwenye ´Aqiydah
sahihi na mjuzi. Na muadhini anashurutishwa awe mtu mwenye ´Aqiydah
sahihi, iliyo salama; Asiwe Suufiy, Ash´ariy, Mu´taziliy, Jahmiy wala asiwe
mwenye ´Aqiydah (Itikadi) potofu. Bali anatakiwa awe katika Manhaj ya Ahl-
us-Sunnah wal-Jamaa´ah na awe na ´Aqiydah yao katika mlango wa Majina
na Sifa za Allaah na yanayofanana na hayo katika mambo makubwa kuhusu
´Aqiydah na Tawhiyd. Awe ni mtu mwenye kuhifadhi wakati [wa Swalah],
mtu anajua Fiqh - katika Twahara yake, usomaji wake, Swalah yake kiasi
ambacho akikwama Imamu muadhini asimame nafasi yake na aswalishe
Jamaa´ah.
Chanzo: http://youtu.be/r5C3RBFSMfY
26) Twawaaf Ya Kuaga Ni Wajibu Katika ´Umrah
19
Swali:
Twawaaf ya kuaga katika ´Umrah ni wajibu au ni Mustahaba?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ni Mustahaba. Yaani katika Hajj ni wajibu na katika ´Umrah ni Mustahaba.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4237
27) Baba Hataki Kuwaozesha Mabinti Zake Kwa Kukhofia Riziki Zao
Swali:
Ipi hukumu ya baba ambaye hataki kuwaozesha mabanati zake kwa ajili ya
riziki zao?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Huchukuliwa kuwa ni dhalimu. Na Allaah Hawapendi madhalimu. Anasema
Allaah:
الميناوا أليمااعذاباالهمااأعداالظ
"Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu iliyo chungu." (76:31)
Riziki yao iko kwa Allaah. Akimuozesha binti yake riziki yake iko kwa Allaah.
Ajitahidi kumuozesha kwa mwanamume mwema ambaye atamsaidia katika
Dini na dunia yake. Haijuzu kwake kumkatalia kwa kitu Alichomhalalishia
Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4706
20
28) Hukumu Ya Kubaki Macho Baada Ya Swalah Ya ´Ishaa
Swali:
Je inajuzu kutoka kwenda kutembea na familia baada ya [Swalah ya] ´Ishaa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kuwa macho baada ya ´Ishaa hairuhusiwi ila kwa msafiri au mwenye
kuswali, au mtafutaji elimu (mwanafunzi), au kusaidia kidogo katika mambo
ya Waislamu. Kama kwa mwenye wilaya katika wilaya ya Waislamu sawa
iwe kwa jumla au khaswa. Mbali na hayo kuwa macho inadhuru na huenda
ikawa sababu ya kukosa Swalah ya Jamaa´ah, bali hata Swalah kwa wakati
wake.
Chanzo: http://youtu.be/iYe1w1bYuvY
29) Kuuza Katika Maeneo Ya Msikitini Kama Bustani La Msikitini
Swali:
Hukumu ya kuuza katika maeneo ya Msikitini?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Pale ambapo ni maeneo ya Msikitini haijuzu kuuza, kutokana na ujumla wa
Hadiyth [inayokataza kuuza Msikitini].
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4712
21
30) Mtu Anataka Kulipa Deni Katika Pesa Za Zakaah
Swali:
Mtu ambaye mali yake imeeneza niswaab, na yeye ana madeni kwa baadhi ya
watu. Je, anaweza kulipa madeni hayo kwa kulipa Zakaah?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Fatwa za wanachuoni zinasema kuwa jambo hili halijuzu, kwa kuwa
anajihami mali yake kwa kutoa Zakaah. Lakini ampe fakiri Zakaah. Na fakiri
ikiwa ndio huyo aliyekuwa akimdai hakuna ubaya. Kwa sharti isiwe
alikubaliana naye kabla, mimi nakukopa na wewe utanirudishia. Hii ni
khiyana haijuzu.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4714
31) Mwanaume Anaruhusiwa Kuvaa Pete?
Swali:
Hukumu ya kuvaa pete kwa kijana?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hakuna tofauti kati ya kijana wala mzee, hukumu yao ni moja. Na pete
hakubainisha ni pete ipi, ikiwa ni ya dhahabu ni Haramu kwa wanaume.
Ikiwa ni ya fedha ni Sunnah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4713
22
32) Du´aa Nzuri Wakati Mwanamke Anataka Kuzaa
Swali:
Dada kutoka Ubelgiji anauliza. Ni Du´aa ipi ambayo mwanamke anaweza
kuomba wakati wa kuzaa?
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Amuombe Allaah Amuweke wepesi. Na Du´aa iliyojumuisha mengi ni yeye
aseme: "Allaahumma anta Rabbiy, laa ilaaha illa Anta. Khalaqtaniy wa ana
´abduka, wa anna ´alaa ahdika wa wa´adika mastatwa´at. A´udhubika min-
sharri maaswanaytu. Abu-ulaka bi ni´imatika 'alayyah wa abu-u bidhambi,
faghfirliy innahu laa yaghfiruu dhunuuba illa anta."
Chanzo: http://youtu.be/rKDnt34ZKX8
33) Hadiyth Ya Waislamu Kupeana Zawadi Ili Wapendane
Swali:
Hadiyth (ombeaneni Du´aa mtapendana), je makusudio yake ni watu kupeana
zawadi au ni uongofu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ni watu kupeana zawadi. Kumpa ndugu yako Muislamu zawadi, naye
akakurudishia zawadi. Zawadi inasababisha mapenzi, kama kutoleana Salaam
baina ya Waislamu pia yasababisha mapenzi baina yao.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4858
23
34) Kuswali Swalah Za Sunanh Kabla Ya Swalah Ya Ijumaa
Swali:
Je inajuzu kwa mtu kuswali kabla ya Swalah ya Ijumaa Nawaafil [Swalah za
Sunnah] kadhaa? Na je ni sahihi kuwa masuala haya yana khilafu kwa
wanachuoni, na ipi kauli yenye nguvu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kasema hili Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika taaliki yake katika
Subul-us-Salaam na pamoja na maneno ya Swan´aaniy pia katika Subul-us-
Salaam kuwa:
"Hakuna ubaya kwa Muislamu kuswali kabla ya Swalah ya Ijumaa katika
Naafil au Swalah ya Dhwuhaa apendacho."
Na Ijumaa huwa haina Sunnah za kabla, bali Sunnah zake ni baada. Kwa hiyo
anaweza kuswali kabla ya Ijumaa Swalah za Naafil, kadiri na Allaah
Atavyomuwezesha. Hakuna ubaya In Shaa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4238
35) Mtoto Akipita Mbele Ya Mwenye Kuswali Swalah Yaharibika
Swali:
Mwalimu anaweza kumpiga mwanafunzi kumuogopeshe ili arejee kufanya
jambo fulani au kuacha jambo fulani, je hili pia linangia katika tishio
[dhuluma]?
24
´Allaamah Zayd al-Madkhaliy:
Kipigo cha kumuweka [kumtia] adabu mwalimu mnasihiaji mukhlisw kwa
mwanafunzi, kipigo cha kumuweka adabu kidogo halaumiwi kutokana na
maslahi kwake [mwanafunzi] na kumkinga na yatayomdhuru katika uhai
wake na mustaqbal wake. Pia kipigo cha baba kwa mtoto wake, na kwa mleaji
- kama mtu mkubwa kwa mdogo, hali kadhalika mume kwa mke wake katika
baadhi ya hali kama jinsi Allaah Alivyotoa idhini hio. Hichi huitwa kipigo cha
kuweka adabu na kutengeneza. Ataekifanya hana makosa wala haingii katika
kufanya dhuluma. Lakini ikiwa atachupa mipaka katika kupiga, hapo
atachukuliwa amefanya dhuluma. Na ikiwa atapiga bila ya haki hata kama
kitakuwa ni kipigo kidogo, atachukuliwa ni dhalimu na siku ya Qiyaamah
Allaah naye Atamlipiza.
Chanzo: http://youtu.be/ydnNQuD5zVw
36) Mwanamke Mgonjwa Anastanji Na Kujiosha Kwa Maji Ya Zamzam
Swali:
Mwanamke ni mgonjwa, anajiosha kwa maji ya zamzam bafuni na anastanji
nayo. Je hili linajuzu?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa anajitibu kwa hili hakuna ubaya. Kwa kuwa kustanji kunachukuliwa ni
dawa. Hakuna ubaya In Shaa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4856
25
37) Talaka Inatokana Na Alivyokusudia (Nia) Ya Mume
Swali:
Ipi hukumu mume kamwambia mke wake "Nikirudi kwenye ghala mimi si
mumewe tena", kisha akajirudi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hili itatokana na nia yake. Je, makusudio yake ni Talaka kwa hili? Hili
itatokana na nia yake. Ikiwa makusudio yake ni Talaka atakuwa kamtaliki. Na
ikiwa hakukusudia Talaka, itakuwa si Talaka. Kasema Mtume (Swalla Allaahu
´alayhi wa sallam):
"Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa
kile alichokusudia."
(Akimwambia) wewe si mke wangu, wewe si mke wangu mwema, au
nimridhiae. Itatokana na anachokusudia (nia yake).
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4700
38) Dada Anataka Kubadilisha Rangi Ya Nywele Zake Nyeusi
Swali:
Dada anauliza kuhusu kubadilisha rangi ya nywele nyeusi kichwani?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa nywele za kichwani ni nyeusi hakuhitajiki kuzibadili. Tayari ziko katika
asili yake rangi nyeusi. Haifai kupoteza muda na mali katika mambo
yasiyokuwa na faida. Zinazobadilishwa ni nywele zenye rangi nyeupe (mvi),
kwa kuwa zimebadilika zilikuwa nyeusi. Mtu anabalidisha kwa rangi yoyote
26
isipokuwa nyeusi tu. Rangi nyeusi haijuzu mtu kujibadilisha kwayo.
Kutokana na Hadiyth inayokataza hilo.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4698
39) Hukumu Ya Unyevu (Majimaji, Utoko) Umtokao Mwanamke
Swali:
Anauliza kuhusu unyevunyevu (majimaji/utoko) umtokao mwanamke?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Fatwa za wanachuoni zinasema kuwa unatengua Wudhuu. Pia Fatwa ya al-
Lajnah ad-Daa´imah inasema hali kadhalika - Fatwa ya Shaykh Ibn Baaz.
Anatakiwa kustanji na aoshe sehemu ilipopatwa nguo yake na unyevu huo,
kisha atawadhe.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4857
40) Kuna Muda Maalumu Wa Mtu Kufanya Kijicho?
Swali:
Je kuna muda maalumu katika Kitabu na Sunnah ambao hutoka kijicho kwa
wale wenye vijicho?
´Allaamah al-Waswaabiy:
27
Elimu ya jambo hili iko kwa Allaah (´Azza wa Jalla), Allaah Hufanya
Atakacho. Wewe ni juu yako kujitibu nafsi yako kwa kufanya Ruqyah ya
Kishari´ah na Allaah Hufanya Atakacho. Na haya ni kama maradhi mengine
yote. Ujitibu kwa yale Aliyokuruhusu Allaah na lini maradhi yataisha, elimu
ya hili ni kwa Allaah.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4710
41) Mwanamke Anatokwa Na Upepo Kwenye Tupu Ya Mbele, Hukumu
Ya Swalah Yake
Swali:
Mwanamke katawadha kisha anatokwa na upepo wakati wa kuswali
anapoenda kwenye Rukuu na Sujuud, akaamua kuswali hali ya kuwa amekaa
ili asitokwe na upepo.
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ikiwa Swalah ni ya faradhi kusimama ni nguzo [yaani lazima]. Na ikiwa ni
Swalah ya Naafilah [Swalah ya Sunnah], akiswali hali ya kuwa amekaa
hakuna ubaya. Na kutokwa na upepo katika tupu ya mwanamke hakutengui
Wudhuu. Kitenguacho Wudhuu ni kutokwa na upepo katika tupu ya nyuma.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=4855
42) Baadhi Ya Sifa Zinazopasa Kuwa Na Mke Mtarajiwa
Swali:
28
Ipi nasaha zako kwa anayeoa kwa wale wasiyo katika jamii yake ambapo
anaishi, [mwanamke] kutoka magharibi kwa mfano?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Ndugu yetu anatakiwa kuoa mwanamke Muislamu, mwema, mtiifu, mwenye
msimamo, atakayekusaidia katika mambo ya Dini yako.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=567
43) Hukumu Ya Kupuuza Swalah Mpaka Ukaondoka Wakati Wake
Swali:
Kuna mtu alisikia adhaana ya Swalah na wala hakwenda kuswali na akaswali
baada ya wakati kuondoka, ipi hukumu?
´Allaamah a-Waswaabiy:
Anasem Allaah (´Azza wa Jalla):
الةااإنا وقوتااكتابااالمؤمنينااعلىاكانتااالص م
“Hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu.”
(04:103)
Kila faradhi ina wakati wake maalumu na mwanzo wake na mwisho wake.
Haijuzu kupuuza swalah, hakika Allaah Anasema:
ساهونااصالتهمااعناهمااالذينااللمصليناافويل ا
“Basi, ole wao wanao swali, Ambao wanapuuza Swalah zao.” (107:04-05)
Kuacha swalah ya jama´ah inachukuliwa ni katika madhambi makubwa,
mwenye kuacha swalah mpaka wakati wake ukaondoka huchukuliwa ni
29
dhambi ingine kubwa; Bali huchukuliwa ni ukafiri. Kwa kauli ya Mtume
(´alayhis-Salaam):
"Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni swalah, ataeiacha basi kakufuru."
Kuiacha yaani mpaka ukaondoka wakati wake naye kakusudia hilo. Ni wajibu
kwake kufanya tawbah na istighfaar, na ahifadhi swalah tano kwa wakati
wake tena pamoja na jama´ah. Na azidishe nawaafiyl [sunnah], nawaafiyl za
´Ibaadah kwa kuwa Allaah Anasema:
ـيئاتاايذهبنااالحسناتااإنا الس
“Hakika mema huondoa maovu.” (11:114)
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1910
44) Hukumu Ya Kubusu Msahafu Na Kuuweka Chini
Swali:
Ipi hukumu ya kuubusu msahafu na kuuweka mahala katika ardhi ambapo ni
pasafi?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kubusu msahafu kama ilivyo katika Fatwa ya al-Lajnah ad-Daa´imah ni
kwamba ni jambo halina dalili. Na kuuweka katika ardhi ikiwa ni safi hakuna
ubaya, ila bora zaidi uwe juu ya kitu kama kiti n.k.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1979
45) Hukumu Ya Kula Daku Baada Ya Adhaana Ya Pili Ya Fajr
30
Swali:
Kuna mtu kaamka kula daku katika Ramadhaan, akala na kunywa akidhani
kuwa adhaana ya pili haijafika wakati wake, na ghafla wanakimu Swalah. Ipi
hukumu ya Swalah yake?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa anachukuliwa kala siku hii. Afanye Istighfaar kwa Allaah (´Azza
wa Jalla) na ajizuie siku nzima iliobaki na juu yake ana deni [kulipa siku hii].
Ilikuwa juu yake kuharakisha wakati [wa daku].
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1909
46) Hukumu Ya Kupuuza Swalah Mpaka Ukaondoka Wakati Wake
Swali:
Mtu kasalisha watu Tarawiyh na baada ya kuwasalisha anataka kusimama
usiku kuswali, afanye nini?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Kwa kuwa aliwaongoza katika Tarawiyh, akisimama baada ya hapo [usiku]
na akaswali Rakaa mbili mbili [hakuna neno], asiswali tena Witr kwa kuwa
kishaiswali. Na katika Hadiyth:
"Hakuna [kuswali] Witr mbili katika usiku mmoja."
Aswali Rakaa mbili mbili. Pia imethibiti kutoka kwa Mtume (´alayhis-Salaam)
aliswali Witr na akaswali baada ya hapo Rakaa mbili kama ilivyo katika
Swahiyh Muslim. Ni dalili ya kuonesha katika kauli yake:
"Ifanyeni Swalah yenu ya mwisho usiku iwe Witr."
31
Imependekezwa na si wajibu.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1911
47) Hukumu Ya Mume Kamwambia Mke Wake Wewe Ni Kama
Mamangu
Swali:
Kuna mtu kamwambia mke wake "Wewe kwangu ni kama mama yangu au
binti yangu". Je, hii huchukuliwa ni talaka au Dhwihaar?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa hii ni Dhwihaar. Anawajibika kutoa kafara ya Dhwihaar, sawa
kama alisema "wewe ni kama mama yangu", au "kama binti yangu" au
mwanamke yeyote katika Mahaarim (asiyeweza kuwaoa). Na kafara ya
Dhwihaar ni kuacha mtumwa huru kabla ya kumgusa, yaani kabla ya
kumjamii (kumuingilia). Ambaye hakupata (hawezi) afunge miezi miwili
mfululizo kabla ya kumgusa; na ambaye hawezi alishe masikini sitini, pia
kabla ya kumgusa.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1973
48) Imefika Ramadhaan Na Ana Deni La Ramahaan Ingine
Swali:
Mtu ana deni la Ramadhaan, ikaingia Ramadhaan ingine na hakulipa. Afanye
nini?
32
´Allaamah al-Waswaabiy:
Atafunga Ramadhaan iliyohudhuria na baada ya Ramadhaan atalipa
Ramadhaan ya kwanza pamoja na kulipa kafara ya kulisha masikini mmoja
kwa kila siku moja ikiwa alichelewesha bila ya udhuru. Ama ikiwa
alichelewesha kwa udhuru, atalipa [atafunga] tu [bila ya kulipa kafara].
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1912
49) Inafaa Kwa Kwenye Kukaa Eda Kuangalia Jua, Mwezi, Nyota,
Mbingu, Kupika, Ndugu Zake?
Swali:
Je inajuzu kwa mwanamke aliyekufa mume katika hali ya eda yake kuangalia
mwezi na kujidhihirisha kwa Mahaarim na ndugu zake?
´Allaama al-Waswaabiy:
Jibu ni kuwa inajuzu kwake kuangalia mwezi nae yuko katika eda, pia
kuangalia jua, nyota, mbingu, ardhi, moto. Inajuzu kwake kupika chakula kwa
moto, inajuzu kwake kufanya usafi nyumbani, inajuzu kwake kuvaa nguo
zake nzuri [asitoke nazo nyumbani]. Huu ni uzushi na yanayosemwa na
wajinga wasiojua kitu. Ama kuhusu kumuangalia Mahram wake na ndugu
inajuzu, na ambaye ni ndugu lakini si Mahram usimuangalie.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1981
50) Je Mkaaji Eda Haruhusiwi Kutoka Nyumbani Kabisa?
Swali:
33
Je kwa mwenye kukaa eda kwa kufa mume wake anaweza kutoka nje ya
nyumba na mmoja katika jamaa zake?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Hakuna neno kukitokea haja [dharurah], kama kumzuru jirani yako, au katika
jamaa zako. Ila hutakiwi kubaki isipokuwa katika nyumba ya mume wako.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=570
51) Je Salaf Waliwahi Kutofautiana Katika ´Aqiydah?
Swali:
Wanasema baadhi ya watu kwamba Salaf walitofautiana katika baadhi ya
masuala ya ´Aqiydah, kwa mfano "je alimuona Mtume wa Allaah ( اعليهاللااصلى
Mola Wake Usiku wa Mi´iraaj?", na kuwa hili lilitokea zama za (وسلم
Maswahabah. Je, maneno haya ni sahihi?
´Allaamah al-Fawzaan:
Hawakutofautiana katika masuala ya ´Aqiydah ewe ndugu. Masuala ya
´Aqiydah ni kuonekana Allaah Peponi. Ni kwamba waumini watamuona
Peponi. Ama duniani hakuna yeyote atayemuona. Hakuna yeyote
atayemuona, hata Mtume ( وسلماعليهاللااصلى ) hakumuona, wala hakumuona
Muusa (´alayhis-Salaam). Alisema:
ترانيالناقالااإليكااأنظرااأرنياربااقالا
"Nionyeshe nikutazame." Allaah Akasema: "Hutoniona." (07:143)
Hili ni hapa duniani. Hawana tofauti katika ´Aqiydah. Hii ni ikhtilafu je
alimuona yeyote duniani au haikutokea. Hii sio ikhtilafu katika ´Aqiydah.
Kuonekana Allaah Peponi hili wamekubaliana wote Ahl-us-Sunnah wal-
Jamaa´ah wala hawatofautiani.
34
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2750
52) Kajiapiza Kutofanya Kitu Fulani Kisha Akamtaliki Mke Wake
Swali:
Kuna mtu alijiharamishia na akataliki, na akaapa kuwa hatofanya kitu fulani;
kisha akafanya kitu hicho, analazimika kufanya nini?
´Allaamah al-Waswaabiy:
Itarejea katika nia yake. Ikiwa nia yake [makusudio yake] ilikuwa ni Talaka,
itachukuliwa kuwa kamtaliki Talaka ya kwanza. Na ikiwa alikuwa hakusudii
Talaka bali ni yamini, hivyo atalipa kafara ya yamini ambayo
tumekwishaitaja.
Chanzo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1971
Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad , na ahli zake na
Maswahabah zake na watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya Qiyaamah.