kutambua mamlaka ya biblia - storage.googleapis.com · habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii...

160
KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA Na Roy C. Deaver Hakimiliki na: BIBLICAL NOTES PUBLISHING Haki Zote Zimelindwa HAKIUZWI

Upload: others

Post on 12-Jul-2020

44 views

Category:

Documents


7 download

TRANSCRIPT

Page 1: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

KUTAMBUA MAMLAKA YA

BIBLIANa

Roy C. Deaver

Hakimiliki na:BIBLICAL NOTES PUBLISHING

Haki Zote Zimelindwa

HAKIUZWI

Page 2: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga au kunakili au kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki au sehemu yake

kwa njia yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka kwa Publishing Designs, Inc., isipokuwa kwa kunukuu

pekee.

Page 3: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- iii -

DIBAJI

Kwenye dibaji ya toleo la mwaka 1997 la kazi hii, tulirejea ukweli kwamba maandishi mengi yaliandaliwa kwa ajili ya mihadhara na pia

yalitumika mwaka 1971 kwenye mihadhara ya Biblia katika Shule Kuu ya Dini, Memphis, Tennessee. Ujumbe mkuu wa mihadhara hiyo ulikuwa “Uvuvio na Mamlaka ya Biblia”. Mihadhara yote iliyowasilishwa ilichapwa katika mfumo wa kitabu, lakini katika uandishi huu, kitabu hiki hakipatikani tena. Ulikuwa ni mhadhara mzuri sana na kitabu ni kizuri sana.Kichwa cha habari niliyochopewa kilikuwa: “Kuimarisha Mamlaka ya Biblia”. Katika kuweka tayari vifaa vya kufundishia vitakavyotumika katika darasa la Hermeneutics la Shule ya Mafunzo ya Wahubiri ya Brown Trail, ndipo nikabadilisha kichwa cha habari cha kitabu na kuwa “Kuyatambua Mamlaka ya Biblia.” Hata hivyo ni sahihi kusema kuwa mwanadamu hawezi kuanzisha mamlaka ya Biblia. Ni jukumu letu kugundua hayo mamlaka (kwa kuzingatia mtazamo na mwenendo unaotakiwa), kuyaheshimu na kuongozwa nayo.Darasa la Hermeneutics (kanuni za kutafasiri Biblia, au Jinsi ya Kujifunza Biblia) ni sehemu muhimu sana katika maisha na kazi za watu wote ambao wanatamani kujua na kufundisha kile ambacho Mungu anataka tufanye. Ni lazima tukusudie kuwa na mamlaka ya Biblia kwa kile tunachofanya.

Page 4: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- iv -

Hili ni toleo jipya na liliokuzwa la Kuyatambua Mamlaka ya Biblia. Kazi hii toka imechapishwa ni mwaka mmoja sasa, na watu wengi sana wameendelea kukiagiza. Tuna furaha sana kwa hili. Ni kwa sababu ya maombi maalumu kutoka kwa William S. Cline, Mhariri wa Wakifu wa Firm, ndipo tumeweza kuandaa vifaa vitakavyotumika katika masomo ya Biblia. Kitabu hiki kina jumla ya sura kumi na tatu na orodha ya maswali ya kujifunza yanafuata kwa kila sura. Tunapenda kuwatia moyo walimu na wanafunzi kujifunza haya yaliyoandikwa kwa makini sana, kwa kufikiri, kwa maombi, daima ukiweka akilini mwako umakini na umuhimu wa suala lenyewe. Ni lazima tuelewe jinsi Mungu anavyotoa Mamlaka.Baraka za Mungu ziwe pamoja nasi kadri tunavyojitahidi sana kuwa wanafunzi wazuri wa neno Lake.

Ni wako katika Ufalme,

Roy Deaver

Page 5: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- v -

TABARUKUKwa Dr. Thomas B. Warren(Ni mtu ambaye hana haja ya kukisoma) – Rafiki Mpendwa na Askari wa Yesu, tukiwa pamoja kwa miaka mingi, mingi sana ya ajabu.

Page 6: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- vi -

Page 7: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- vii -

YALIYOMOSOMO LA KWANZA I. UTANGULIZI SOMO LA PILI II. FUNDISHO LA BIBLIA JUU YA UVUVIO

(Sehemu ya Kwanza) SOMO LA TATU III. FUNDISHO LA BIBLIA JUU YA UVUVIO

(Sehemu ya Pili) SOMO LA NNE IV. NI LAZIMA TUTAMBUE KWAMBA AGANO

JIPYA HUWEKA KIELELEZO KITAKATIFU SOMO LA TANO V. MAANA YA IMANI YA BIBLIA SOMO LA SITA VI. JE INAWEZEKANA SISI KUFAHAMU? SOMO LA SABA VII. KAULI YA MSINGI VIII. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Kwanza) SOMO LA NANE IX. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Pili) SOMO LA TISA X. TENDO NA MAJUKUMU

1

9

17

25

35

45

57

59

69

77

Page 8: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- viii -

XI. MUNGU HATAVUMILIA KILE AMBACHO HAKIKUAMRIWA

XII. NI LAZIMA TUBAKI KATIKA KILELE CHA MLIMA WA MAMLAKA YA BIBLIA

XIII. TUNAPASWA KUJUA JINSI AMBAVYO MUNGU HARUHUSU

XIV. LAKINI VIPI KUHUSU UKIMYA WA MAANDIKO?

SOMO LA KUMI XV. MAMALAKA YANATHIBITISHWA KWA

MFANO SOMO LA KUMI NA MOJA XVI. MAMLAKA YANATHIBITISHWA KWA

KUDOKEZA XVII. MAMLAKA YANATHIBITISHWA KWA

KAULI YA MOJA KWA MOJA SOMO LA KUMI NA MBILI XVIII. MAMLAKA YA BIBILIA

YANATHIBITISHWA KWA MANUFAA BINAFSI

SOMO LA KUMI NA TATU XIX. JE MAMLAKA YANANUKULIWA NA

KAMUSI? KIAMBATISHO A KIAMBATISHO B KIAMBATISHO C

78

79

80

81

87

97

100

105

115130141144

Page 9: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 1 -

1

SOMO LA KWANZA

1. UTANGULIZI

Page 10: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 2 -

Katika somo letu la KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA tunashughulika katika misingi ya kauli tatu muhimu: (1) Mungu YUPO, (2)

Biblia ni Neno la Mungu, na (3) Mungu alitupatia Biblia kutuongoza katika maisha haya na kutupeleka mbinguni baada ya maisha haya yatakapokwisha. Kauli zote hizi tatu zinaweza kuthibitishwa, lakini hii haipo katika mawanda ya somo hili kuonesha huo uthibitisho. Kwa sasa tutashughulikia zaidi kauli namba 3. Biblia mara kwa mara huzungumzia juu ya asili yake ya miujiza – UVUVIO WAKE – na namna nzuri ya kuitumia ili iwe Maandiko yaliyovuviwa. Kwa wazee wa Efeso Paulo alisema: “Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.” (Matendo 20:32). Kama hivi ndivyo na tunasadiki kwa uthabiti kabisa kwamba ndivyo, basi ni dhahiri tutakuwa tunaguswa kuhusu vile Biblia inavyotoa mamlaka. 1. Wakolosai 3:17 inaunganisha, “Lo lote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika Yeye”. “Katika jina la Bwana” humaanisha kwa mamlaka ya Bwana, kama Bwana alivyoamuru. (Matendo 4:7-10)Wakristo wanalazimika (na wana fursa) ya “kutembea

anaongozwa nacho ni kipimo cha imani. Katika Warumi kwa imani” (2 Kor. 5:7). Kipimo ambacho mkristo

10:17 Paulo anasema kwamba “Basi, imani chanzo chake nikusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.” Ni

Page 11: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 3 -

dhahiri kwamba, mkristo huenenda kwa kusikia neno la Mungu. Kama imani huja kwa kusikia neno la Mungu basi pale pasipokuwa na neno la Mungu hapawezi kuwa na imani. Na pale pasipo na imani hakuna kumpendeza Mungu. (Waebrania 11:6). Ni lazima tuguswe na kuhusu mamlaka ya Biblia na jinsi ya KUYATAMBUA mamlaka ya Biblia.Ni kazi yangu kujifunza na wewe wakati huu juu ya suala la Kuyatambua mamlaka ya Biblia. Ni jukumu langu kuelezea, kufafanua, kuthibitisha, namna Mungu anavyoamuru. Ni lazima nioneshe kwa uwazi, kwa kukazia, kwa maelezo rahisi, kwa usahihi, na kimaandiko namna ambavyo mamlaka ya Biblia yanavyothibitishwa.2. Naomba nipendekeze kwamba suala hili ni la muhimu sana. Tusipojua namna Mungu (au Biblia) inavyoamuru, hatuwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu chochote tunachofanya au kusema katika muktadha wa dini. Kijana mmoja alikuwa anahubiri kwa ajili ya kanisa la Bwana huko magharibi mwa Forth Worth. Alikuwa ameonesha shauku ya kufundisha pamoja nasi katika Chuo cha

ajili ya usaili. Nilimdokezea kwamba kuna uvumi umeenea kuwa hana uhakika kuwa matumizi ya ala za muziki kwenye ibada ya kikristo ni dhambi. Tulijadili

Ni wazi kwamba alikuwa anaelekea kutetea matumizi ya ala za muziki katika ibada. Hatimaye nikamwambia: “Ukiacha mambo mengine, uko radhi kukubali kwamba hakuna mamlaka yanayoamuru matumizi ya vyombo vya

Page 12: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 4 -

muziki kwenye Idada ya Kikristo?” Akajibu: “Ndugu Deaver, sina uhakika juu ya namna Mungu anavyotoa mamlaka”. Jibu langu lilikuwa: “Kama ndio hivyo hakika hatuwezi tukakutumia. Maana kama hujui jinsi Mungu anavyotoa mamlaka, basi huwezi kuwa na uhakika juu ya kitu chochote.” Haikuchukua muda huyu kijana akawa kwenye mstari wa dhehebu "Kanisa la Kikristo".

3. Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza

alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova. Musa alijenga hema kama alivyooneshwa mlimani. Wana wa Israeli wa Agano la Kale walimkaribia Mungu kupitia makuhani wa kabila la Lawi.

kwenda Yerusalemu kumwabudu Mungu mara tatu kwa mwaka. Daudi aliamuru matumizi ya muziki wa ala katika kumwabudu Mungu. Katika nyakati za Agano la Kale kulikuwa na desturi za ndoa za mitara na uchomaji wa ubani. Kama alivyofanya Abeli, ni lazima nami nitoe kafara ya mnyama ili nimpendeze Mungu? Kama Nuhu, ni lazima

Mungu katika madhabahu ya kidunia kwa kutoa kafara za wanyama? Kama Musa, ni lazima nijenge hema? Ni lazima nimwendee Mungu kupitia Kuhani wa kabila la Lawi? Ili ibada yangu ikubaliwe na Mungu, ni lazima niende Yerusalemu mara tatu kwa mwaka? Kama alivyofanya Daudi, je na mimi naweza kutumia vifaa vya muziki katika kumwabudu Mungu? Je, na mimi niwe na ndoa za mitala?

nijenge safina? Kama Ibrahimu, na mimi nimwabudu

Page 13: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 5 -

Kama alivyofanya Abeli, je ni lazima nitoe sadaka ya kuteketeza ili nimpendeze Mungu? Kama Nuhu, je

nitengeneze madhabahu ya kidua na nimtolee Mungu sadaka za kutekeza katika hiyo? Kama Musa na mimi leo

kupitia kuhani wa kabila la Lawi? Ili nimuabudu Mungu kwa namna inayokubalika, je napaswa kwenda Yerusalem mara tatu kwa mwaka? Je naweza kama Daudi, kutumia ala za muziki katika kumuabudu Mungu? Je naweza kushiriki katika tabia ya kuoa wake wengi? Je nitakuwa nipo sahihi nikimchomea Yehova ubani?Kama naweza kufanya vitu hivi na kama ni lazima nivifanye – nawezaje kujua kwamba naweza na ninawezaje kujua kwamba ni lazima? Kama siwezi kufanya vitu hivi na kama sio lazima nifanye vitu hivi – nitajuaje kwamba

waliwahi kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi? Je, si lazima Je, Daudi au Musa au Ibrahimu au Yakobo

Daudi au Ibrahimu, au Musa waliwahi kushiriki Meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya juma? 4. Alhamisi moja usiku, Bwana alikutana na wanafunzi wake, akashiriki Sikukuu ya Pasaka, akaanzisha Meza ya Bwana, na akawanawisha wanafunzi miguu. Kuhusiana na kuwanawisha wanafunzi wake miguu, Bwana alisema, “Kwa hiyo, ikiwa Mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi.” (Yohana

Page 14: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 6 -

13:14,15). Kama Wakristo, tunashiriki Meza ya Bwana. Hatuadhimishi sikukuu ya Pasaka, na katika ibada yetu hatunawishani miguu. Kati ya mambo haya matatu, tunaamuaje kwamba tunawajibika kutunza moja tu?5. Zaidi ya hapo, wakati Meza ya bwana inaanzishwa Bwana na wanafunzi wake walikuwa “orofani.” Wakati Paulo anakutana na ndugu wa Troas ili “kumega mkate” walikuwa “wamekusanyika pamoja” katika “chumba cha orofani” na kulikuwa kuna “mianga mingi.” Ili na sisi tuweze kufuata maandiko katika kushiriki Meza ya Bwana, ni lazima tuifanyie kwenye “chumba cha orofani”? Ni lazima kuwepo na “mianga mingi”? Tunaamuaje?6. Katika Warumi 16:16, Paulo anasema: “Salimianeni kwa busu takatifu.” Ili na sisi tuweze kumpendeza Mungu ni lazima tusalimiane kwa busu takatifu? Kama ni hapana, kwa nini? Na kama ndiyo kwa nini hatufanyi hivyo? Vyovyote vile, je tunaamuaje?Ni lazima idhihirike kuwa, ni muhimu sana kwetu, kutafakari kwa makini sana na kwa maombi katika suala la namna ya kuyatambua mamlaka ya Biblia.

Page 15: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 7 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Jadili Yeremia 6:16-19

2. Je wanadamu “wanathibitisha” mamlaka ya Biblia? Angalia Dibaji. Jukumu letu ni nini? Angalia Dibaji.

3. Nini maana ya “Hermeneutics”? Angalia Dibaji

4. Tunafanyia kazi misingi ya kauli tatu muhimu. Ni zipi hizi?

5. Kariri Matendo 20:32

6. Kulingana na Wakolosai 3:17 tunapaswa kufanya vitu vyote kwa namna gani?

7. Ni somo gani kuu tunalojifunza katika 2Wakorintho 5:7?

Ni somo gani kuu tunalojifunza katika Warumi 10: 17?

Page 16: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 8 -

Ni somo gani kuu tunalojifunza katika Waebrania 11:6?

8. Jaza: Kama hatujui namna Mungu anavyotoa mamlaka, basi ……………………

9. Ni lazima nitoe sadaka ya kuteketeza ya wanyama? Ni lazima tujenge safina? Ni lazima tujenge hema? Ni lazima kumwendea Mungu kupitia kuhani wa kabila la Lawi? Ni lazima twende Yerusalemu kuabudu?

10. Je, Daudi au Musa au Abrahamu au Yakobo waliwahi kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi?

11. Ni lazima Wakristo waadhimishe sikukuu ya Pasaka?

12. Ni lazima Wakristo washiriki Meza ya Bwana katika “chumba cha orofani”?

13. Ili kumpendeza Mungu ni lazima tusalimiane kwa “busu takatifu”?

14. Ni muhimu sana kwetu kutafakari kwa makini na kwa maombi juu ya suala gani?

Page 17: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 9 -

SOMO LA PILI

2. FUNDISHO LA BIBLIA KUHUSU UVUVIO

(Sehemu ya Kwanza)

2

Page 18: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 10 -

UTANGULIZI

Katika 2 Timotheo 3:16, 17 Paulo anathibitisha uvuvio wa maandiko (Kila andiko, lililovuviwa na Mungu…..) hii inarejelea juu ya matumizi

ya maandiko yaliyovuviwa (“….lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki…..”) na inaonesha matokeo ya uvuvio huu na matumizi yake (“…ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.”). Kuna mafungu mengi sana yanayoonesha dai la Biblia kuwa imevuviwa na Mungu. Lakini Biblia ina maana gani kuweka dai hili? Maana ya “uvuvio” ni nini kama neno linavyotumika kwenye Biblia? Ni muhimu sana kuwa makini katika kujibu swali hili. “Uvuvio” ni istilahi ambayo kwa sasa inatumika katika dhana tofauti tofauti. Mwanausasa wa cheo cha juu anadai kuamini katika Mungu. Lakini haamini katika Mungu wa kwenye Biblia, Anadai kuamini Kristo, lakini haamini katika Kristo wa kwenye Biblia. Vivyo hivyo anadai kuamini katika uvuvio wa kwenye Biblia lakini hamaanishi kwa “uvuvio” ambao Biblia inafundisha. Anaamini kwamba maandiko ya Paulo yalikuwa yamevuviwa kwa maana ile ile kama yalivyo maandiko ya Shakespeare, Milton, Tennyson, na Poe. Wala hasiti kuchambua uzuri wa kitabu cha Warumi kwa misingi ya kwamba “Paulo siku hiyo alikuwa anajisikia vizuri!”Nadharia nyingi za uongo zinasumbua ulimwengu wetu. Hebu tuangalie chache tu.

Page 19: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 11 -

(1) Kuna baadhi ya watu ambao wanadai kwamba hakuna kitu chochote cha maana kuhusiana na Biblia. Kwao Biblia ni kitabu tu kama vitabu vingine – kitabu kizuri pengine lakini ni kitabu kilichoandikwa ya mwanadamu. (2) Usasa unadai kwamba Biblia ni mkusanyiko wa kumbukumbu zilizopita za wanadamu waliowahi kuishi zamani, zilikusanywa pamoja na kuhaririwa na Goerge – George Redactor, ni hivyo tu! (3) Baadhi wanasema kuwa Biblia imevuviwa kimiujiza katika baadhi ya sehemu au kwa kiwango fulani au kwa kiasi fulani tu. Sasa tunauliza: katika maeneo gani? kwa kipimo gani? kwa kiasi gani? nani anayeamua? Hii inapinga waziwazi uvuvio wa Biblia. (4) Baadhi wanashikilia wazo la kwamba Mungu (kwa namna fulani) aliwapa watu mahususi mawazo yasiyokuwa na mipaka na akawaruhusu hawa watu kuweka “mawazo hayo kwa maneno yao wenyewe.” Sasa tunauliza Biblia inasemaje kuhusiana na uvuvio wake?

AHADI NA UTIMILIFUBwana aliahidi kutoa uvuvio wa kimiujiza. Bwana alisema: “…..nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili Yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na mbele ya watu wa Mataifa. Lakini watakapowapeleka,

mtapewa la kusema wakati huo. Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu” (Math. 10:18-20). Akaendelea kusema: “Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili Yake mwenyewe, bali atanena yale

Page 20: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 12 -

yote atakayoyasikia, naye atawaonesha mambo yajayo. Atanitukuza Mimi, kwa maana atayachukua yaliyo Yangu na kuwajulisha ninyi.” (Yohana 16:13,14)Bwana alitimiza ahadi yake. Siku ya Pentekoste ya Matendo 2, watu awa hawa ambao walipewa ahadi “…Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia” (mstari wa 4). Katika mstari wa 39 Petro alisema: “Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu na kwa wale wote walio mbali na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.’’ Andiko hili ni mfano mzuri wa uvuvio wa kimiujiza ambao Petro aliuzungumza. Umuhimu wake kwa hakika unahusisha wokovu wa Wamataifa. Lakini bado Petro yeye mwenyewe kwa wakati huo, hakuamini kuwa injili ilikuwa ni kwa ajili ya Wamataifa pia. Katika Matendo ya Mitume sura ya 10, Mungu alilazimika kufanya miujiza mara tatu ili kumwezesha Petro aelewe kuwa alipaswa kuhubiri injili kwa Wamataifa. Hivyo Mungu alimsaidia kuelewa maana ya kile alicho kihubiri takribani miaka kumi kabla! Ni Petro ambaye baadae alitangaza uwezo mtakatifu wa Mungu “…umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu….” Paulo anafafanua suala hili: “Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu. Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.” (Wagalatia 1:11-12). Kwa uwazi kabisa, waandishi wa Agano Jipya wanathibitisha kwamba Bwana alitimiza ahadi yake.

Page 21: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 13 -

MUNGU NA MAMLAKAMamlaka yote ya asili yako ndani ya Mungu Baba. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1). “Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu” (Zab. 95:5). Na ni “…Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo” (Matendo 14:15). Ni “Mungu aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, Yeye ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.” (Matendo 17:24). Ni Muumba wetu na mhuishaji wetu. Ni kupitia yeye ndipo tunaweza kutembea na kuwa watu. Kwa sababu yeye yupo hivyo alivyo, mamlaka yote ya asili-na chanzo chake yanatoka kwake.

MWANA NA MAMLAKAVitabu vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana viliandikwa ili kuwashawishi watu waamini kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Kristo, mwana wa Mungu anayeishi – Masihi ambaye ujumbe wa Agano la Kale ulimzungumzia. Mungu alisema kwamba Yesu alikuwa ni Mwana wake. Yesu alidai kwamba Mungu alikuwa ni Baba yake. Waandishi hawa walitoa ushahidi usiopingika kuthibitisha madai yake. “Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, wakaogopa wakasema, “Hakika huyu alikuwa ni Mwana wa Mungu!”(Math.27:54)

Page 22: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 14 -

Lakini kuna nini cha muhimu sana kuhusiana na ukweli huu? Kwanini kuthibisha kuwa ni Mwana wa Mungu? Jibu ni: Alikuwa (na yupo) katika nafasi ya kuwa mrithi wa mamlaka yote kutoka kwa Baba. Alikutana na wanafunzi wake katika mlima Galilaya na kwa kujiamini

duniani” (Mathayo 28:18). Mungu alitoa mamlaka kwaakatamka “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Mwana – mamlaka ya kushughulikia dhambi za wanadamu.

Page 23: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 15 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Ni hoja gani tatu za msingi zinazopatikana katika 2Timotheo 2:16, 17?

2. Nini anachofikiria mwanausasa pale anapozungumza juu ya “uvuvio”?

3. Ni zipi dhana potofu, angalau nne, kuhusu “uvuvio”?

4. Mathayo 10:18-20 na Yohana 16:13,14 zinaonesha wazo gani la msingi kuhusu uvuvio?

5. Kulingana na Matendo 2:4, Bwana alifanya nini?

6. Fafanua jinsi Matendo 2:4 inavyoonyesha kwa namna ya pekee uvuvio wa kimiujiza aliousema Petro.

7. Kwa kuhusianisha na Matendo 2:39 Mungu alifanya nini katika Matendo 10?

Page 24: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 16 -

8. Katika 2Petro 1:3, Petro alitangaza nini?

9. Kwa mtazamo wa Wagalatia 1:11,12, ni kwa jinsi gani ujumbe mtakatifu ulimjia Paulo?

10. Ni hoja gani inayojengwa waziwazi kwa kuzingatia Mwanzo 1:1; Zaburi 95:5; Matendo 14:15 na Matendo 17:24?

11. Mathayo, Marko, Luka, na Yohana viliandikwa kwa makusudi gani mahususi?

12. Liwali alisema nini kuhusu Bwana (Mathayo 27:54)?

13. Kuna umuhimu gani juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

14. Madai gani makubwa aliyodai Bwana kama ilivyooneshwa katika Mathayo 28:18?

Page 25: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 17 -

SOMO LA TATU

3. FUNDISHO LA BIBLIA KUHUSU UVUVIO (Sehemu ya Pili)

3

Page 26: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 18 -

MITUME NA MAMLAKA

Bwana alijua kwamba maisha yake ulimwenguni yangekuwa ni mafupi, lakini ujumbe wake kwa mataifa ungeendelea. Aliita, akachagua,

akafundisha, akalea, akatoa mafunzo, na kuendeleza kikundi kidogo cha watu ambao katika mabega yao, aliweka jukumu la kupeleka habari ya injili ulimwenguni mwote. Aliahidi kuwa pamoja nao katika kazi yao, na alikuwa pamoja nao. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni habari takatifu ya jinsi Bwana alivyotembea nao katika kupeleka injili kwa kila kiumbe ulimwenguni mwote (Mk. 16:19, 20). Walihubiri injili kwa uvuvio wa miujiza, neno lao lilithibitishwa kwa matendo ya miujiza. Hawa watu walidumisha uhusiano wa pekee na Kristo, Mfalme. Kimsingi, walikuwa ni “mabalozi” wa Mfalme. Paulo anasema, “Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo…” (2 Kor. 5:20). Neno ‘mabalozi’ kama lilivyotumika hapa huhusisha “ubalozi ” mtakatifu na huu “ubalozi” mtakatifu ni lazima utakuwa umehusisha mamlaka maalumu. Mitume walikuwa ni wawakilishi rasmi wenye mamlaka ya Mfalme. Mfalme alitawala akiwa mbinguni, lakini alikuwa na ubalozi miongoni mwa watu–mitume ambao aliwapa mamlaka kufunga na kufungua duniani yale yaliyo fungwa na kufunguliwa mbinguni.

KARAMA YA UNABIIKatika kanisa la awali, kulikuwa na karama za kimiujiza–karama za kiroho. Watu wa kipindi hicho hawakuwa na Agano Jipya lililokamilika katika mfumo wa maandishi, lakini kulikuwa na uhitaji mkubwa wa uongozi na

Page 27: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 19 -

maelekezo matakatifu. Ili kukidhi haya mahitaji, Mungu aliweka karama za pekee katika kanisa la awali. Mjadala wa pekee kuhusiana na karama hizi za kiroho unapatikana katika 1 Wakorintho, sura za 12, 13 na 14. Katika sura ya 12, Paulo anajadili karama tisa za miujiza. Kwa kuzingatia Matendo 8:14-21 tunasema kwa kujiamini kwamba ni Mitume pekee ndio wangeweza kutoa miujiza ya Roho Mtakatifu kwa kuweka mikono yao juu ya mtu mwingine. Ushahidi wa wazi ni kwamba ni mitume tu waliokuwa na hizi karama tisa za miujiza na kwamba ni mitume tu –kulingana hitaji walioweza kutoa vipawa hivi vya kiroho.

Moja ya karama muhimu sana za roho ilikuwa ni karama ya Roho Mtakatifu. Katika 1 Wakorintho 14 Paulo anasisitiza ukuu wa karama ya unabii. Ni muhimu kuielewa karama hii. “Kutoa unabii” hakuna maana ya “kutabiri mambo yajayo.” Maana yake hujumuisha kipengele hiki cha mambo yajayo, lakini maana yake ni zaidi ya hapa. Neno unabii maana yake ya moja kwa moja ni “kusema kwa ajili ya, au niaba ya.” Manabii (wa Agano la Kale au wa Agano Jipya) walisema kwa niaba ya Mungu. Mungu alizungumza kupitia wao. Katika Kutoka 7:1 Mungu alimwambia Musa: “…huyo ndugu yako, Haruni, atakuwa nabii wako. Musa angeweza kuzungumza kupitia Haruni. Hii ndio maana ya neno hili. Manabii wakati mwingine walishughulika na mambo ya zamani; na wakati mwingine walishughulika na mambo ya wakati uliopo (kwa wakati huo); na wakati mwingine walishughulika na mambo ya wakati ujao. Lakini walikuwa ni Manabii kwa sababu Mungu alisema kupitia wao.

Page 28: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 20 -

Kwa hiyo, karama ya unabii, ni mamlaka yaliyomo katika kila neno kwenye Biblia. Kila neno (kila neno halisi) ni neno liliotokana na miujiza ya karama ya unabii. Iwapo Luka ni miongoni mwa waandishi wa Agano Jipya, na ikiwa Luka hakuwa mmoja wa mitume, hivyo Luka alikuwa ni nabii katika kanisa la awali – ambaye kupitia yeye Mungu alifunua mapenzi yake.Ni lazima isisitizwe kwamba hakuna unabii bila (1) ufunuo

.azijuimik aw oivuvu )2( an ajomap ,ajom awk ajom awMungu alifunua, kisha mtu ambaye alipata huo ufunuo alizungumza au aliandika ujumbe uliofunuliwa kwake. Uzungumzaji au uandikaji ulifanywa chini ya uvuvio. Kulikuwa na walimu waliovuviwa wakati wa kanisa la awali lakini hawakuwa sawa na manabii. Walimu walishughulika na ujumbe uliofunuliwa kwa manabii. Andiko muhimu linalothibitisha hilo ni 1Wakorintho 14:30 – “Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.”

MAANDIKO YA KUFAAMoja kati ya maandiko ambayo yako wazi na rahisi juu ya uvuvio wa Biblia ni 1 Wakorintho 2, mstari wa 9 -13. Katika mstari wa sita Paulo anarejelea “mambo” fulani ambayo Mungu amewaandalia wale wanaompenda. Katika mstari wa 10 anasema: “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho…” Katika mstari wa 12 Paulo anasema: “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.” Zingatia: Mungu kupitia Roho alifunua “mambo.” Ufunuo ulikuja kwa watu

Page 29: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 21 -

waliomo kwenye neno “sisi.” Mimi na wewe hatumo kwenye neno “sisi”. Hatupati ufunuo wa moja kwa moja. Swali sasa: Ni kwa jinsi gani ujumbe uliovuviwa hutoka kwa wale waliohusishwa kwenye neno “sisi” na kuja kwa wengine tuliosalia? Jibu: Paulo anasema – “Nayo twayanena si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayo fundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa manemo ya rohoni” mstari wa 13). Hii inafanya suala hili liwe wazi vya kutosha! Mungu alifunua mambo kwa watu fulani (watu wenye karama ya unabii), ambao baadae waliyanena na waliyaandika kwa maneno yaliyochaguliwa na roho Mtakatifu. Hii ni fasili ya Biblia juu ya uvuvio: Huu ni ukusanyaji mzuri sana wa mambo yaliyofunuliwa, yaliyofundishwa kwa maneno yaliyochaguliwa na Roho Mtakatifu.Uthibitisho na ufafanuzi mzuri unaofanana na huo hupatikana katika Waefeso 3:1-5. Mungu kupitia Roho Mtakatifu alimfunulia Paulo siri, kwa kutumia maneno, ili kumsaidia Paulo kuelewa siri hizo. Paulo aliandika (kwa maneno) siri ambazo Mungu alimfunulia kwa ajili ya Waefeso (na wengine), ili kuwasaidia kusoma na kuelewa uelewa wa Paulo wa siri za Mungu – injili ya Kristo.

HITIMISHOMpendwa wangu, hili ndilo fundisho la Biblia kuhusu uvuvio. Inatakiwa tukumbuke kwamba uvuvio wa kimiujiza huhusiana na maneno halisi ya kitabu cha Mungu – maneno ya Kiebrania katika Agano la Kale

Page 30: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 22 -

Mungu alitoa mamlaka kwa Mwana. Mwana akatoa mamlaka kwa mitume. Mitume (na wengine waliowekewa mikono na mitume) walikuwa na karama ya unabii. Karama ya unabii ilikuwa ni njia ambayo kwayo Mungu alifunua ujumbe wake. Wale walioupata ufunuo waliusema na waliuandika “…si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu bali yanaoyofundishwa na Roho.” Walijumuisha “mambo ya kiroho” – mambo yaliyofunuliwa kwa maneno ya kiroho – maneno yaliyochaguliwa na Roho Mtakatifu.Shukrani kwa Mungu kwa ajili ya neno lake lililovuviwa, lisilopotoka, lisilo na makosa na linalojitosheleza!

na maneno ya Kiyunani katika Agano Jipya. Wafasiri au wakalimani hawavuviwi, lakini maneno hayo halisi yametoka kwa Mungu. Ni maneno yale yale yaliyochaguliwa na Roho Mtakatifu. Yana maanisha kile alichotoa Mungu yamaanishe; Na yananena kile Mungu alichotaka yanene.

Page 31: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 23 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Ili kupeleka injili ulimwenguni kote, Bwana alifanya nini?

2. Umuhimu wa Marko 16:19,20 ni nini?

3. Mitume walikuwa “mabalozi” wa Mfalme. Umuhimu wa ukweli huu ni nini?

4. 1Wakorintho sura ya 12, 13, na 14 ni mjadala mzuri wa nini?

5. Kipimo cha miujiza ya Roho Mtakatifu (karama ya roho) kingeweza kupewa kwa mtu mwingine kwa njia gani?

6. Mitume wanahusianaje na “karama za roho”?

7. Katika 1Wakorintho 14, Paulo anajadili nini?

Page 32: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 24 -

8. Maana ya “unabii” ni nini?

9. Ni kwa jinsi gani karama ya “unabii” inahusiana na mamlaka ya Biblia?

10. Ieleweke kwamba hakuna unabii bila nini?

11. Je“Manabii” katika kanisa la awali walikuwa sawa na “walimu waliovuviwa”?

12. Tafadhali andika muhtasari wa 1Wakorintho 2: 9-13.

13. Tafadhali andika muhtasari wa Waefeso 3: 1-5

14. Uvuvio wa kimiujiza kwa umahususi huhusiana na neno gani?

15. Tafadhali andika muhtasari wa fundisho la Biblia kuhusu Uvuvio.

Page 33: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 25 -

SOMO LA NNE

4. NI LAZIMA TUTAMBUE KWAMBA

AGANO JIPYA HUWEKA KIELELEZO

KITAKATIFU

4

Page 34: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 26 -

MJADALA

Kama ilivyoandikwa katika Mwanzo 6, Mungu alimwagiza Nuhu kuhusiana na ujenzi wa safina. “Uovu wa mwanadamu uliongezeka duniani”

na Mungu akaamua kumwangamiza mwanadamu na wanyama na mimea na ndege wa angani. “Lakini Nuhu alipata rehema machoni pa Bwana.” Kwa kutazamia kuja kwa gharika, Mungu alimkabidhi Nuhu majukumu ya kujenga safina. Safina ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahifadhi wenye haki, Mungu alitoa maelekezo juu ya vifaa vitakavyotumika kujengea safina, na akaorodhesha vipimo vyake. Kwa hiyo Mungu alimpatia Nuhu kielelezo mahsusi cha namna Safina itakavyojengwa. Katika Mwanzo 6:22, maandiko matakatifu yanasema: “Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.”Katika Kutoka 25, Mungu alimwelekeza Musa kujenga hema takatifu. Mlolongo wa maelekezo ya jinsi ya kujenga yalitolewa kwa Musa. Musa alionywa na Mungu: “Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake ulioonyeshwa mlimani” (Kutoka 25:40). Katika Waebrania 8:5 Roho Mtakatifu hurejelea maonyo ya Mungu kwa Musa, “…alipokuwa tayari kuifanya ile hema, maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.” Katika kutoka 40:16 andiko linasema: “Musa akafanya hayo yote, kama BWANA alivyoagiza ndivyo alivyofanya.”Kama Mungu alivyompa Nuhu kielelezo cha kujenga safina, na kama pia Mungu alivyompa Musa kielelezo cha kujenga

Page 35: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 27 -

hema, vivyo hivyo Mungu amempa mwanadamu kielelezo kwa ajili ya kujenga maisha yake. Mungu ametoa kielelezo juu ya tabia ya Kikristo (tabia na matendo) na kielelezo kwa kanisa (taasisi, jina, ibada, malengo ya wokovu, utume).

kielelezo, na pia kama vile Musa alivyowajibika kujenga hema kulingana na kielelezo, ndivyo na sisi tunavyowajibika kujenga kulingana na kielelezo kitakatifu. Mungu, ambaye alimuumba mwanadamu na ambaye anamjua mwanadamu vizuri, na ambaye anajua kitu ambacho ni bora kwa mwanadamu, siku zote amejiwekea haki ya kumwongoza mwanadamu. Na kitabu kitakatifu ambacho kupitia kwacho anatafuta kumwongoza mwanadamu sasa ni Agano Jipya la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo. Agano Jipya ni kielelezo.Kielelezo ni kitu kinachofaa kuigwa na ni kitu kinachokusudiwa kuigwa. Ni usanifu, mwongozo, kitu cha kuigwa. Mungu alipompa Nuhu kielelezo kwa ajili ya

alielewa vizuri kwamba Mungu alipompa kielelezo kwa ajili ya kujenga hema, alikuwa hatoi maoni au mapendekezo.Kuna ndugu fulani (pengine watu “wasiosadikika” lingekuwa neno zuri) miongoni mwetu ambao wanapinga kabisa kwamba Agano Jipya ni kielelezo chetu. Tafakari yafuatayo kutoka kwa Victor L. Hunter, “Some Thoughts on Theology and Mission,” Mission Magazine, March, 1972: “Tatizo la theolojia ya urejeshwaji hujikita katika kauli kwamba utume wa kanisa ni kuunda kanisa la kweli ambalo kwalo kielelezo cha maisha ya kanisa ni sawa kabisa na

Page 36: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 28 -

yale ya ulimwengu wa karne ya kwanza. Hujikita katika dhana kwamba kuna kielelezo katika Agano Jipya ambacho kanisa linatakiwa kukiiga kwa kila kizazi. Theolojia ya namna hii inafanya utume wa kanisa kuwa wa kibinafsi na wenye mtazamo wa kale kuliko kuwa wa kuangalia mbele na yenye mtazamo wa maisha ya baadae.”Inatakiwa ieleweke kuwa mtazamo ulioshuhudiwa katika nukuu ya hapo juu (Mtazamo wa Mission Magazine) ndio tabia halisi ya Kanisa la Kikristo (Wanafunzi wa Yesu). Katika ukosoaji wa Ndugu J.D . Thomas We Be Brethrean, Dr. A.T DeGroot anasema: “Katika kitabu kizima kuna dhana imejengwa kwamba Agano Jipya ni njia au kibebeo cha kielelezo cha maelekezo ya kanisa” (Alfread T. DeGroot, The Restoration Principle, St. Louis, Misouri, The Bethany Press, ukurasa 159). DeGroot anaendelea kusema: “Kutokana na uzoefu wa Wanafunzi wa Kristo na Kanisa la Kristo, tunaweza tukahitimisha kwamba kwa umahususi zaidi, kadri madai ya urejeshwaji yalivyofasiliwa katika mtazamo wa kiuongozi, kitaasisi na muundo wa tabia na taratibu za kidini ndivyo imekuwa na mafanikio madogo kama nguvu itendayo kazi katika ulimwengu wa Kikristo” (ukurasa 160).Hebu ieleweke hapa kwamba muundo wa Agano Jipya uko ndani ya ukweli kwamba hilo ni Agano Jipya la Bwana. Katika Mathayo 28:28 Bwana alisema: “Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” Katika Waebrania 9:15 tuna: “Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya…” Paulo anatangaza: “Ndugu zangu,

Page 37: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 29 -

nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno” (Wagalatia 3:15). Kauli hii ni jambo la kuchukuliwa kwa umakini. Haiwezi kubadilishwa inapokuwa imethibitishwa. Haitakiwi kupuuzwa. Masharti yake ni lazima yazin-gatiwe. Agano la Bwana (au mapenzi yake) huhusiana na baraka za ajabu na faida ambazo hutolewa kwa watu fulani pale ambapo watu hawa wanakidhi vigezo fulani.

Ukweli kwamba Agano Jipya liliwekwa ili kuwa kielelezo chetu umesisitizwa katika maandiko kadhaa: (1) “Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo hana Baba na Mwana pia” (2 Yohana 9). (2) “Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutopita yale yaliyoandikwa…. ” (1 Kor. 4:6). (3) “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo. Na kugeukia injili ya namna nyingine: Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri nyinyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri na alaaniwe.” (Wagalatia 1:6-8). (4) “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yali-yoandikwa katika kitabu hiki; na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu,

Page 38: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 30 -

ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” (Ufunuo 22:18,19).Mungu anatarajia kuona tunatembea na kuishi kulingana na kielelezo kitakatifu. Bwana alisema: “…na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” (Math. 28:20). Katika Waefeso 5:11 Paulo anasema: “…bali msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza bali myakemee.” Yohana anasema: “Mtu akija kwenu naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu; maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mwovu” (2 Yohana 10).Katika hotuba kuu tatu ambazo zinaunda kitabu cha Kumbukumbu la Torati, Musa aliwassitizia Waisraeli wa Agano la Kale kwamba ni kwa sababu Mungu aliwapenda ndio maana aliwapa sheria yake si kwa sababu aliwachukia; na kwamba upendo wao kwa Mungu ungesababisha wao kuitii sheria ya Mungu. Vivyo hivyo, ni kwa sababu ya Upendo wa Mungu kwetu ndio maana akatupatia Agano Jipya na upendo wetu kwake utatusukuma kutii hilo Agano Jipya. Bwana alisema: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15). Akaendelea kusema:

(Yohana 15:14). Yohana anasema: “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake, wala amri zake si nzito.” (1 Yohana 5:3).Mungu atusaidie kutambua kadri tunavyojifunza na kutambua ukweli kwamba Agano Jipya ni kielelezo , na Mungu atusaidie tuishi kulingana na kielelezo. Amina.

Page 39: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 31 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Jadili jukumu ambayo Mungu alimpatia Nuhu (Mwanzo 6), na jinsi Nuhu alivyoitikia.

2. Jadili jukumu ambayo Mungu alimpatia Musa (Kutoka 25), na jinsi Musa alivyoitikia.

3. Kulingana na Agano Jipya, ni kielelezo gani ambacho Mungu ametupatia?

4. Jukumu letu ni nini kuhusiana na kielelezo kitakatifu?

5. Nini maana ya “kielelezo”?

6. Ni nini mtazamo wa watu wengi miongoni mwetu kuhusiana na dhana ya “kielelezo”?

Page 40: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 32 -

7. Kwa muktadha wa sasa, ni nini umuhimu wa Mathayo 26:28; Waebrania 9:15; Wagalatia 3:15?

8. Ni nini umuhimu wa 2 Yohana 9; 1 Wakorintho 4:6; Wagalatia 1:6-8; Ufunuo 22:18,19?

9. Kulingana na Mathayo 28:20, Waefeso 5:11, na 2 Yohana 10, Mungu anatarajia nini kutoka kwetu?

10. Katika hotuba tatu kuu (katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati) Musa alikuwa anasisitiza kitu gani kwa wana wa Israeli?

11. Kwa nini Mungu aliwapa wanadamu Agano Jipya? Upendo wetu kwake utatuongoza kufanya nini?

12. Tafadhali kariri Yohana 14:15 na Yohana 15:14 na 1 Yohana 5:3.

Page 41: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 33 -

NUKUU MUHIMU KUTOKA KWA G.K.

WALLACE

Kanisa linaweza kurejeshwa kwa kuchukua Biblia na kuifuata kama mwongozo wake. Kanisa linaweza kuwa leo kama lilivyokuwa wakati

uliopita kwa kufuata kielelezo cha mitume. Agano Jipya linafunua kielelezo cha ibada na kielelezo cha mafundisho ambacho hakiwezi wala hakitakiwi kupuuzwa. Hebu tutafute kundi la watu wanaojiita Wakristo (Mdo.11:26). Hebu tutafute kundi la watu ambao wanaheshimu mpangilio wa Agano Jipya wa kanisa, wanaohubiri mafundisho ya kweli, wanaoabudu kulingana na Biblia inavyoelekeza, na kuishi na kuabudu kulingana na Biblia inavyoelekeza. “Injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu” (Warumi 1:16). Neno injili hubeba ujumbe wote na kamili wa Kristo katika nyakati hizi. Injili ni njia ya Mungu; kwa hiyo tuitafute, na tutembee katika hiyo. Kama hatutatembea katika njia sahihi, tutatembea katika ukingo na kuangukia katika shimo refu lisilokuwa na mwisho.

Page 42: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 34 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 43: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 35 -

SOMO LA TANO

5. MAANAYAIMANIYAKIBIBLIA

5

Page 44: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 36 -

Swali: Maana ya Kibiblia ya neno imani ni nini? Je imani humaanisha kuwa na mashaka au kutokuwa na uhakika? Je humaanisha kukubaliana na wazo bila kuwa na ushahidi? Je ni kutokuwa na ufahamu?

baraka na rehema za Mungu) humaanisha kusikiliza neno Jibu:Imani yenye manufaa (imani ambayo humpa mtu

la Mungu, kufuata kielelezo kitakatifu, kufanya kile Mungu alichoagiza, kwa kuwa Mungu kasema kifanye, kwa namna ambayo Mungu ameelekeza, kama Mungu ametoa kielelezo mahususi, na kwa kusudi ambalo Mungu ametaka ulifanye. Imani haimaanishi kuwa na mashaka au kutokuwa na uhakika. Haimaanishi kukubaliana na wazo au mtazamo bila kuwa na ushahidi. Sio kutokuwa na ufahamu.Katika Waebrania 11:1 Paulo anasema: “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, bayana ya mambo yasiyoonekana.” Andiko hili linarejelea mambo yatarajiwayo. “Mambo” ni yale yaliyo ndani ya pazia (Waebrania 6:19). – mbingu yenyewe, yote ambayo ni mbingu, na yote ambayo ni ya mbingu. Kwamba ambayo yatatufunga kwa usalama kwa hayo yaliyomo kwenye pazia ndilo tumaini letu, “tulilonalo kama nanga ya roho, yenye salama yenye nguvu” (Waebrania 6:16). Tumaini letu ni zao la, na lililozungukwa na imani yetu. Imani yetu ni zao la neno la Mungu. “Basi imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rum. 10:17). Kwa hiyo ni dhahiri, pale ambapo hakuna neno la Mungu hapawezi kuwa na imani.Lakini imani yangu ambayo huja kwa kusikia neno la Mungu, imejikita kwa nguvu juu ya ushahidi

Page 45: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 37 -

matumizi ya Biblia ya neno hili. Ndugu mmoja alisema, Neno “imani” mara nyingi linatumiwa kinyume na

“Hakuna namna ya kuthibitisha kwamba Mungu yupo. Tunalazimishwa kukubali wazo kwamba Mungu yupo kwa imani.” Mwingine akasema, “Hoja hizi zitakupeleka kwenye jambo hili…lakini kuanzia hapo unatakiwa usonge mbele kwa misingi ya imani.” Hawa ndugu wote walikuwa wanasisitiza juu ya wazo kwamba, ushahidi utamsogeza mtu mbele kidogo lakini kuanzia hapo mtu atatakiwa asonge mbele kwa kukubaliana na jambo bila kuwepo na ushahidi. Na kutumia neno “imani” kwa maana ya kwamba kusonga mbele pasipokuwa na ushahidi, ni kulitumia neno hili kinyume na matumizi ya Biblia.Watu wengine wana hatia ya kutumia vibaya neno “imani.” Ndugu mmoja katika kusisitiza kwamba hatuwezi kujua

unaojitosheleza na wenye ushawishi mkubwa kwamba Biblia ni kile ambacho inadai kuwa ndicho – neno la Mungu aliye hai lililovuviwa, lisilokuwa na mashaka, lisilokuwa na makosa na linalojitosheleza. Ukweli huu (huu wa kudai hivyo ulivyo) unapokuwa unapothibitishwa, wenyewe na katika maeneo mengi huwa ushahidi wangu. Na ninakubali mafundisho mengi si katika msingi mwingine isipokuwa tu kama Biblia isemavyo. Neno linakuwa ni “ngao” yangu (Efe. 6:16). Tunaitetea imani na imani inatutetea. Imani yangu sio imani ya bila ushahidi. Ni imani inayojikita katika ushahidi unaojitosheleza na wenye ushawishi mkubwa. Mambo, tumaini, imani, neno, ushahidi.

Page 46: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 38 -

Maana ya “imani” katika Biblia ni nini? Neno hili linatumiwaje? Imani (kwa maana ya Kibiblia), Je

bali tunaweza kukisia, anadai kwamba mtu mwenye imani anafanya mambo “kana kwamba anajua.” Tungependa kuuliza swali; Kama mtu wa imani anatenda kama vile anajua, Kwa nini huyu mtu wa imani asiwe mnafiki? Na kwa nini huyu mtu wa imani asiwe agnostiki? Nukuu zifuatazo zinatoka kwa watu ninaowapenda na ninaowaheshimu – watu wenye elimu zao kubwa, watu wanaompenda Mungu na neno lake, watu ambao ni marafiki wa mwandishi wa kitabu hiki. Ninaorodhesha hapa kauli zao si kwa kuwafedhehesha bali kwa kutaka kuthibitisha hoja kwamba wengi wanatumia neno “imani” kwa maana ambayo ni kinyume na maandiko. Zingatia kwa makini: “Kama ilivyoelezwa mwanzo, hakuna ushahidi wa kutosha mahali popote pale kuweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, lakini kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha dhana au imani kwamba Mungu yupo.” “Uchaguzi huu au msimamo huu ni suala la hisia binafsi, hakika, kwa sababu linavuka mipaka ya uhalisia, na kitu ambacho kinaweza kuthibitishwa waziwazi na kwa hiyo ni ’mruko wa imani tu!’” “Kwa hiyo ni vema kuchukua mruko mfupi wa imani inayotakiwa katika imani ya Kikristo, kuliko kuchukua mruko mrefu wa imani inayotakiwa katika upagani. Ushahidi kamili usiokuwa na shaka mara nyingi haiwezekani kuupata, lakini imani thabiti inaweza kuelezeka.” “Wanaoamini katika nadharia ya mgeuko, wana imani nami pia nina imani. Ninaamini kwamba imani yangu ni imani sahihi zaidi.” Matumizi ya namna hii ya neno “imani” ni hatari na yanasikitisha kwa kweli!

Page 47: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 39 -

humaanisha “mambo ya kukisia” Je ni sawa na neno lisilohakikishwa? Je inakuwepo tu pasipo ushahidi? “Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini…” (Waebrania 11:4). “Kwa imani…Nuhu alijenga safinakuokoa nyumba yake…” (Waebrania 11:7). “Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi…” (Waebrania 11:8). “Lakini kwa kuiona ahadi ya Mungu, hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani akimtukuza Mungu, huku akijua hakika Mungu anaweza kufanya yale aliyoahidi” (Warumi 4:20,21). Maneno “kwa imani” yana maana gani katika kauli hizi? Je Habili, Nuhu na Ibrahimu walikuwa wanakisia? Je, walikuwa wanafanya waliyoagizwa kwa kukisia tu? Je walikuwa wanatenda pasipo ushahidi? Biblia inasema: “Basi imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Kwa hiyo imani ya kwenye Biblia inahusisha: (1) ukweli wa uwepo wa Mungu (2) ukweli wa uwepo wa mwanadamu (3) uwezo wa Mungu wa kumfunulia mwanadamu (4)uwezo wa mwanadamu kumsikiliza Mungu (5) ushuhuda wa Mungu kwa mwanadamu (6) na mwitikio sahihi wa mwanadamu kwa ushuhuda.Tunasisitiza tena kwamba “imani” – kwa maana ya Biblia ni kutenda kama Mungu alivyoagiza. Hakuna imani ya Kibiblia ambayo haina ushuhuda kutoka kwa Mungu.Imani haimaanishi kukosekana kwa ushahidi. Ukweli ni kwamba imani inahitaji kuwepo na ushahidi, na hakuwezi kuwa na imani pale pasipo na ushahidi. Mungu anahitaji tuwe na ushahidi. Uwepo wa Biblia yenyewe

Page 48: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 40 -

ni ushahidi. Yohana anasema: “Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina lake” (Yohana 20:31).Hatuwezi tukakosoa tabia ya Tomaso (Yohana 20:24,25). Bali tunaheshimu sana tabia yake. Tabia yake ilikuwa ni: “Bila ushahidi, sitaweza kuamini. Nipatie ushahidi nami nitaamini.” Bwana alimpatia Tomaso ushahidi. Tomaso alipoona ushahidi akasema: “Bwana wangu na Mungu wangu.” Dkt. Luka mwanasayansi pekee aliyefunzwa miongoni mwa waandishi wa Agano Jipya, alifanya uchunguzi wa suala zima na akaandika kama ifuatavyo: “Kwa kuwa, watu wengi wametafuta ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu, kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale ambao walikuwa mashahidi walioona na watumishi wa Bwana, mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari

ukweli kuhusu yale uliyofundishwa” (Luka 1:1-4).Imani kwa namna yoyote ile haimaanishi kukosekana kwa vitu tunavyoweza kuviona kwa macho. Wakati mwingine imani hutofautishwa na kuona vitu (kama ilivyo katika 2 Kor. 5:7), lakini kunaweza kuwa na imani pale tunapoweza kuona. Bwana alimwambia Tomaso: “…Wewe kwa kuwa umeniona, umesadiki..” (Yohana 20:29). Wasamaria wengi walimwamini Yesu kwa sababu ya neno lake (Yohana 4:41). Ukweli kwamba walikuwa wanamwona hakukuhusisha imani yao kwake. Kuna imani pale ambapo huwezi ukaona kitu. Bwana

Page 49: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 41 -

akamwambia Thomaso: “…wa heri wale wasioona, wakasadiki.”Wala imani haimaanishi kutokuwepo kwa maarifa. Inapaswa tupaze sauti kwamba imani ya Biblia iliyothibitishwa haiondoi kukosa maarifa. Paulo alisema: “Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana”. (2 Kor. 5:6) Paulo alijuaje? “Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona” (2 Kor. 5:7). Haya

ignew airamasaW .inami al oaz in oyabma afiraam oidnwalioamini katika Bwana walimwambia mwanamke: “Sasa tunaamini wala si kwa maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua hakika huyu ndiye mwokozi wa ulimwengu.” (Yohana 4:42). Walisema, “Tunaamini” na “Tunajua.” Imani haiondoi maarifa wala maarifa hayaondoi imani. Petro alimwambia Yesu: “Nasi tumesadiki, tena tumejua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu” (Yohana 6:69). (Katika Agano Jipya la Kiyunani vitenzi vyote viwili [“kuamini” na “kujua”] ni vitenzi vya hali timilifu. Nguvu ya ukweli huu ni kwamba, kwa tafsiri ya moja kwa moja Petro anasema: “Tumeamini, sasa tunaamini, na tutaendelea kuamini; tumejua, sasa tunajua, na tutaendelea kujua.” Kuamini na kujua ni vitu vinavyokwenda pamoja.) Paulo anasema: “….kwa maana namjua yeye niliyemwamini…” (2 Tim.1:12).Mungu atusaidie tuwe makini katika usemi wetu. Tukusudie kwa upya kwamba tutaanza kutumia maneno ya kwenye Biblia kwa jinsi yalivyotumika kwenye Biblia. “Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu…” (1 Pet. 4:11).

Page 50: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 42 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Imani yenye manufaa humaanisha nini?

2. Je imani ya Biblia ina maana ya mashaka au kutokuwa na uhakika?

3. Kwa kuzingatia Waebrania 11: 1, tafakari kwa makini uhusiano uliopo kati ya maneno “mambo,” “tumaini,” “imani,” “neno” na “ushahidi.”

4. Imani yangu, ambayo huja kwa kusikia neno la Mungu imejengwa kwenye nini?

5. Biblia inadai kuwa ni nini?

6. Pale ambapo ukweli kwamba neno la Mungu limethibitishwa, basi neno lenyewe linakuwa nini?

7. Je, imani ya Kikristo ni “imani isiyokuwa na ushahidi?”

8. Kutumia neno “imani” kwa maana ya kusonga mbele bila kuwa na ushahidi ni sawa na kufanya nini?

9. Je ni sawa (yaani, sawasawa na maandiko) kutumia neno “imani” kumaanisha “makisio?” ni sawa kuzunguma juu ya “mruko wa imani?”

Page 51: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 43 -

10. Kwa kuzingatia Warumi 4:20,21 imani ya Ibrahimu ilikuwa ni kazi ya kukisia?

11. Je, Habili, Nuhu, na Ibrahimu walikuwa wanatenda kutokana na makisio?

12. Kulingana na Warumi 10:17, imani ya Biblia angalau inahusisha mambo sita. Ni yapi hayo?

13. Ukweli wa uwepo wa Bibilia huthibitisha ukweli kuhusu nini?

14. Kariri Yohana 20:30, 31

15. Elezea juu ya tabia ya kupendeza ya Tomaso.

16. Elezea kauli ya Luka katika Luka 1:1-4.

17. Je, inawezekana kuwepo na “imani” pale unapoweza “kuona” kitu?

18. Je “imani” humaanisha kukosekana kwa ushahidi?

19. Je “imani” humaanisha kukosekana kwa maarifa?

20. Je “imani” huondoa “maarifa?” Je “maarifa” huondoa “imani?”

21. Ni kwa jinsi gani tunatakiwa tuwe makini katika kutumia maneno ya kwenye Biblia?

Page 52: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 44 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 53: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 45 -

SOMO LA SITA

6. JEKUNAUWEZEKANOWASISI

KUFAHAMU?

6

Page 54: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 46 -

Swali: Katika masuala ya kiroho, je tunaweza kufahamu? Je tunaweza kujua kwamba Biblia ni neno la Mungu? Tunaweza kuelewa kwamba sisi ni Wakristo? Je kufahamu huondoa imani?Jibu: Hakika, inawezekana sisi kufahamu. Tunaweza kufahamu kwamba Mungu yupo. Tunaweza tukafahamu kwamba Biblia ni neno la Mungu. Tunaweza kufahamu kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Kufahamu hakuondoi imani, na wala imani haindoi ufahamu.

TATIZONeno la Kiyunani “ginosko” linalomaanisha “ninafahamu.” Kiambishi “a-“ (alpha ya Kiyunani) kina dhana hasi. Hivyo, “aginosko” humaanisha “kutokujua.” Neno hili ndicho chanzo cha neno la Kiingereza “agnostic.” Agnostiki ni mtu ambaye anadai kuwa hakuna ushahidi wa kuhalalisha hitimisho. “Muagnostiki ni mtu anayedai kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kujua Mungu yupo au kuna ulimwengu wa kiroho. Neno hili lina asili ya Kiyunani, likiwa na maana ya kutokujua. Muagnostiki hasemi kwamba hakuna Mungu. Anasema tu kwamba hawezi kujua. Imani kwamba mtu anatakiwa akubali kile tu ambacho kinaweza kufahamika kwa kupitia uzoefu halisi huitwa Uagnostiki”. (World Book, ukurasa wa 85).Inasikitisha sana kwamba kuna ndugu miongoni mwetu, ambao wanafundisha kwamba haiwezekani sisi kujua kwamba Mungu yupo, na kwamba Biblia ni neno la Mungu. Tafakari haya yafuatayo:

Page 55: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 47 -

1. “Ndio, hatuwezi kujua kwamba Mungu yupo. Hakuna namna tunayoweza kuthibitisha kwamba Mungu yupo. Tunalazimika kukubali wazo la kwamba Mungu yupo kwa njia ya imani.”

2. “Mjadala huu utakupeleka kwenye hoja hii…lakini kuanzia hapo itakubidi usonge mbele kwa kutumia imani. Hakuna namna kwa kweli ya kuweza kufahamu.”

3. “Hata hivyo, imani ya namna yoyote ile imejikita katika uwezekano…mambo ya kufikirika kabisa, ni dhana tu ya kinadharia.”

4. “Mtu wa imani hufanya mambo ‘kana kwamba’ alikuwa anafahamu…Watu wote wanaishi maisha yao kwa kufuata imani, kitu kinachowafanya waone ni kiwango cha juu cha uwezekano.”

5. “Kama ilivyoelezwa mwanzo, hakuna ushahidi wa kutosha mahali popote pale kuweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, lakini kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha dhana au imani kwamba Mungu yupo.”

6. “Uchaguzi huu au msimamo huu ni suala la hisia binafsi, hakika, kwa sababu linavuka mipaka ya uhalisia, na kitu ambacho kinaweza kuthibitishwa waziwazi na kwa hiyo ni ’mruko wa imani tu!’”

7. “Kwa hiyo ni vema kuchukua mruko mfupi wa imani inayotakiwa katika imani ya Kikristo, kuliko kuchukua mruko mrefu wa imani inayotakiwa katika upagani. Ushahidi kamili usiokuwa na shaka mara nyingi haiwezekani kuupata, lakini imani thabiti inaweza kuelezeka.”

Page 56: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 48 -

8. Mwamgeuko, ana imani, nami pia nina imani. Ninaamini kwamba imani yangu ni imani sahihi zaidi.”

9. “…Hakuwezi kuwa na imani ya kweli bila ukweli, ushahidi na maarifa…hata hivyo hawathibitishi kwamba hoja imekubaliwa.”

10. Mwandishi mmoja anazungumzia “Nyanja mbili za ukweli – wa kimwili na metafizikia.” Anasema kwamba katika uwanja wa kuonekana kwa vitu halisi, kunaweza kuwa na maarifa fulani lakini “….hata hivyo mambo ya kufikirika hayawezekani katika uwanja wa metafizikia.” Ni kutokana na hoja hii ndipo anasema “kiwango fulani cha kuthibitika, ambacho kinaweza kupelekea kiwango kikubwa cha uwezekano. ” Anaendela kusema: “Ikiwa Ukristo na mafundisho yake yote yanaweza kuthibitishwa, basi kusingekuwa na haja ya kuwa na imani.”

MAANA YA MAARIFATunaweza kufahamu kwamba Mungu yupo? Tunaweza kufahamu kwamba Biblia ni neno la Mungu? Swali la msingi lililopo kwenye maswali haya ni: Je, tunaweza kujua kitu chochote kile? Na je kama tunaweza kujua chochote, je tunaweza kujua kama Mungu yupo? Kujibu swali hili ni lazima tujue “kufahamu” maana yake ni nini. (Maswali mengine ya kufurahisha: Hivi inawezekana mtu kuwa na maarifa juu ya maana ya “kufahamu?” Hivi inawezekana mtu kufahamu kwamba haiwezekani mtu kufahamu?)

Page 57: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 49 -

Jibu kwa swali hili (Je tunaweza kufahamu kitu chochote?) huhusisha uwanja wa taaluma unaoitwa “epistemolojia.” “Epistemolojia” ni uwanja wa taaluma unajihusisha na chanzo, asili, mbinu na mipaka ya maarifa. Epistemolojia, au nadharia ya maarifa ni tawi la falsafa linaloshughulika na asili na mawanda ya maarifa, madhanio na misingi yake, na mategemeo ya jumla ya madai yake juu ya maarifa”. (Saikolopedia ya Falsafa, Juzuu ya 3, ukurasa wa 8). Mwanadamu anapata maarifa kupitia njia mbili. Tunapata kufahamu (kujifunza) kwa kupitia uzoefu na tunapata kufahamu (kujifunza) kwa kutafakari. Au tunapata kufahamu kwa miguso ya hisia, na tunapata kufahamu kwa kufikiri. Lengo langu sio kuleta mjadala juu ya namna “hisia” inavyohusiana na “Epistemolojia,” lakini kwa kusisitiza hilo tunapata kufahamu kwa njia za msingi mbili. Maarifa ambayo huja kwa kupitia mguso wa hisia au uzoefu halisi huwekwa ya uga Sayansi. Maarifa ambayo huja kwa njia ya kutafakari huwekwa uga wa Falsafa. Maarifa ambayo huja kupitia uzoefu, yanaweza: kihisabati, kifizikia, kibiolojia au kijamii. Ikiwa kutafakari kunahusiana na ulimwengu, basi huwekwa chini ya uga wa metafizikia. Ikiwa kutafakari kunahusiana na mwenendo, basi huwekwa chini ya uga wa maadili. Ikiwa kutafakari kunahusiana na urembo basi, huwekwa chini ya uga wa ujumi. Ikiwa kutafakari ni kujenga hoja kwa usahihi, basi huwekwa chini ya uga wa mantiki.

Page 58: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 50 -

USHAHIDI KWAMBA TUNAWEZA KUFAHAMUWanafalsafa Jarabati wanasisitiza kuwa maarifa ya kweli hupatikana kwa msaada wa kuhisi vitu vinavyoshikika. Wanafalsafa wa Maisha wanasisitiza kwamba, haiwezekani mtu kufahamu kitu chochote. Tunasisitiza katika hoja hii kwamba, ingawa kuna maarifa yanayopatikana kutokana na vitu vinavyoshikika, pia ni kweli kwamba kuna maarifa yanayotokana na kutafakari. Tunasisitiza kwamba inawezekana mtu kufahamu na kujua kwamba anajua kwa kufanya kazi (kwa bidii) kutokana na matakwa ya kanuni za ujengaji hoja kwa usahihi. Inafahamika kuwa 7 mara 7 jibu lake ni 49. “49” ni hitimisho lililofikiwa baada ya kutafakari. Lakini inawezekana sisi kufahamu (na kufahamu kwamba tunafahamu) kwamba 7 mara 7 jibu ni 49. Vilevile mtu akiweka sarafu kwenye bahasha, halafu akaiweka bahasha sandukuni – tunaweza kujua sarafu ilipo. Tunaweza kujua kwamba ipo sandukuni, na ufahamu huu tunakuwa nao kwa kutafakari, sio kwa kuhisi. Ikiwa wanadamu wote ni viumbe wanaokufa, na kama Socrates alikuwa ni mwanadamu, kwa hiyo tunafahamu kwamba Socrates alikuwa ni kiumbe anayekufa. Nilisema kitu hiki kwa wanafunzi wangu: “Kama ni kweli kwamba alama ya lafudhi inaweza kukaa kwenye silabi tatu za mwisho katika neno la Kiyunani, na kama ni kweli kwamba lafudhi ya “sakamfleksi” inaweza kukaa kwenye silabi mbili za mwisho katika neno la Kiyunani, na ikiwa

Page 59: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 51 -

ni kweli kwamba lafudhi ya “grevu” inaweza kukaa kwenye silabi ya mwisho tu ya neno la Kiyunani – kwa hiyo ni kweli kwamba silabi ya tatu ya neno la Kiyunani linakuwa na alama ya lafudhi. Na unaweza ukafahamu hili, na unaweza ukafahamu kwamba unafahamu.” Sheria ya mantiki inasema kuwa “tunatakiwa kuthibitisha hitimisho kwa ushahidi.” Ushahidi unaofaa hakika unahitaji hitimisho fulani. Hatuzungumzi juu ya makisio. Hatuzungumzi juu ya kuhisi au kubuni au uwezekano. Tunazungumza juu ya hitimisho linalohitaji ushahidi mkononi. Na hilo hitimisho linalohitaji ushahidi ni suala la maarifa. Ni maarifa sawa kama tunavyozungumzia suala la utambuzi wa hisia.Ni aina hii ya maarifa tuliyonayo akilini pale tunaposisitiza kwamba Mungu yupo, kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba Biblia ni neno la Mungu. Ni aina hii ya maarifa ambayo husukumwa na kuchunguza ukweli: haiwezekani kuwa na athari bila kuwepo sababu, haiwezekani kuwepo na sheria bila kuwepo mtoa sheria, haiwezekani kuwepo picha bila kuwepo mchoraji, hakuna shairi bila mshairi, hakuna usanifu bila msanifu, hakuna mawazo bila kuwepo na muwazaji, hakuna uhandisi bila kuwepo mhandisi, hakuna kemia bila kuwepo mkemia na hakuna hisabati bila kuwepo mwanahisabati. Sio lengo la sehemu hii ya kitabu hiki kujadili kwa kina namna tunavyoweza kufahamu kwamba Mungu yupo bali ni kusema kwa msisitizo kwamba ni ukweli kwamba tunaweza kufahamu kwamba Mungu yupo.

Page 60: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 52 -

MAFUNDISHO YA WAZI YA BIBLIAPengine inatakiwa ifahamike kwamba, kwa wale wanaopenda, kuamini, na kuiheshimu Biblia, kutakuwa hakuna tatizo kwenye hoja hii. Maana Biblia imekuwa ikisisitiza mara zote kwamba tunaweza na ni lazima tumfahamu Mungu. Tafakari yafuatayo:1. Bwana alisema: “Nao uzima wa milele ndio huu,

wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3); “Mtu ye yote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho Yangu yanatoka kwa Mungu au ninanena kwa ajili yangu mwenyewe” (Yohana 7:17); “Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).

2. Petro alisema: “Tumeamini na kujua kwamba wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.”

3. Luka mwanasayansi msomi alisema: “…mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo ewe mtukufu Theofilo, ili upate kujua ule ukweli kuhusu yale uliyofundishwa” (Luka 1:3,4).

4. Paulo alisema: “Kwa maana twajua kwamba kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu” (2 Kor.5:1).

5. Paulo akaendelea kusema: “Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, kwa maana

Page 61: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 53 -

twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana.” (2 Kor.5:6-8)

6. “…Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni haya kwa maana ninamjua Yeye niliyemwamini na kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hadi siku ile” (2Tim. 1:12)

7. Wasamaria walimwambia yule mwanamke: “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi wa ulimwengu.” (Yohana 4:42).

8. Yohana alisema: “Nimewaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo…” (1Yohana 2:13,14); “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake” (1 Yohana 2:3); “Kama mkijua ya kwamba yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye” (1 Yohana 2:29). Kimsingi, katika kitabu cha Waraka wa Kwanza wa Yohana, mwandishi anatumia neno “kujua” mara ishirini na nne. Wale wanaosisitiza kwamba hatuwezi “kujua” inatakiwa wafanye bidii katika kusoma kwa makini maandishi ya Yohana.

HITIMISHOWapendwa, tulitaka kusisitiza juu ya madai yanayotolewa kwamba eti hatuwezi kujua kwamba Mungu yupo, na kwamba Biblia ni neno la Mungu – kwamba hatuwezi kuthibitisha kuwa Mungu yupo, na kwamba Biblia ni neno la Mungu – ni madai ambayo hayana ukweli

Page 62: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 54 -

wowote. Kuna maarifa yanayopatikana kutokana na vitu vya kuonekana, na kuna maarifa yanayopatikana kwa njia ya kutafakari. Na hayo maarifa yanayopatikana kwa njia ya kutafakari (ikiwa huko kutafakari kunafuata njia sahihi ya kujenga hoja) yanakuwa ni kweli, na ya thamani, na yenye mamlaka kama ambavyo maarifa yapatikanayo kwa njia ya hisia za utambuzi. Mtu yeyote aliyewahi kupata jibu ambalo si sahihi kwenye mahesabu ya aljebra anajua kwamba inawezekana mtu kukosea – yaani kupata jibu ambalo sio sahihi. Na inawezekana mtu kuthibitisha na kujua jibu sahihi lilikuwa ni lipi.Hoja inayoongelewa hapa ni hoja yenye umuhimu mkubwa sana. Mungu atusaidie ili wote tuwasaidie wapendwa wetu na dunia kwa ujumla kujua kwamba tunaweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo, kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba Biblia ni neno la Mungu.“Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima wa milele…Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba…Sisi twajua kuwa tu watoto wa Mungu na ya kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.Nasi twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi akili ili tupate kumjua Yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani Yake Yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele” (1 Yohana 5:13, 15, 19,20)

Page 63: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 55 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Kama ilivyoonyeshwa mwanzo kwenye maswali na majibu, malengo ya sura hii ni nini?

2. Tafakari kwa makini: agnostiki ni mtu wa aina gani?

3. Kama ilivyoonyeshwa kwenye nukuu kumi, wapend-wa wengi wanafundisha kwamba haiwezekani sisi KUJUA vitu gani muhimu?

4. Ikiwa mtu anadai kwamba hatuwezi KUJUA vitu hivi muhimu, anakuwa yupo katika nafasi gani?

5. Hivi inaleta maana mtu kudai kwamba ANAJUA kwamba mwanadamu hawezi KUJUA kitu chochote?

6. Inawezekana sisi KUJUA kile kinachomaanishwa na KUJUA?

7. Ni nini maana ya neno “epistemolojia”?

8. Mwanadamu anapata maarifa kwa njia gani mbili muhimu?

9. Msimamo wa Wanafalsafa Jarabati ni upi?

10. Msimamo wa Wanafalsafa wa Maisha ni upi?

Page 64: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 56 -

11. Katika somo letu, “49” inawakilisha hitimisho la namna gani?

12. Ikiwa mtu ataweka sarafu kwenye bahasha na kisha akaiweka bahasha kwenye sanduku, je ninaweza ku-jua kwamba bahasha imo kwenye sanduku?

13. Je inawezekana sisi kujua kwamba Socrate alikuwa ni kiumbe anayekufa?

14. Tafadhali, kariri “sheria ya mantiki.”

15. Hitimisho LINALOTAKIWA kuwa na USHAHIDI ni nini?

16. Chunguza kwa makini: Yohana 17:3; Yohana 7:17; Yohana 8:32; Yohana 6:69; Luka 1:1-4; 2 Wakorintho 5:1; 2 Wakorintho 5:6-8; 2 Timotheo 1:12; Yohana 4:42; 1 Yohana 2:13, 14; 1 Yohana 2:3; 1 Yohana 2:29

17. . Mungu atusaidie ili wote tuwasaidie wapendwa wetu na dunia kwa ujumla KUJUA kwamba tunawe-za KUTHIBITISHA kuwa _______,______ kwamba ___ ni ______wa Mungu, na kwamba _______ ni _____ la Mungu.

Page 65: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 57 -

SOMO LA SABA

7. KAULIYAMSINGI

7

Page 66: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 58 -

Tumeshaona kwamba ni jukumu la Mkristo “kuenenda kwa imani.” Tumeona kwamba imani huja kwa kusikia neno la Mungu. Tumeweka

msisitizo katika hoja kwamba pale pasipokuwepo neno la Mungu hakuwezi kuwepo na imani. Na bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Katika 1 Wakorintho 4:6, Paulo anasema: “Basi ndugu zangu, mambo haya nimeyafanya kuwa mfano wa mimi binafsi na Apolo kwa faida yenu, ili muweze kujifunza kutoka kwetu maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine.” Katika Wagalatia 1:6-9 Paulo anasema: “Nashangaa kwamba mnamwacha upesi hivyo Yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata injili nyingine, ambayo kwa kweli si injili nyingine kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo. Lakini hata ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo mtu na alaaniwe! Kama vile tulivyokwisha kusema kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!” Katika Ufunuo 22:18,19 Bwana alisema: “Namwonya kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu ye yote akiongeza chochote, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kama mtu ye yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Ni dhahiri

Page 67: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 59 -

kwamba hukumu ya Mungu ipo kwa mtu yeyote na wote watakaoongeza, watakaopunguza, watakaobadilisha, watakaopuuzia, au watakaojaribu kufanya mabadiliko katika neno lake.Kutokana na mafungu haya, tunatengeneza kauli ambayo haiwezi kupingwa: Maandiko yanafundisha kwamba katika kazi ya Kikristo na ibada tunapaswa kufanya yale tu ambayo yameamuliwa na Mungu. Matokeo ya kauli hii ni kusema: Inawezekana kwa mwanadamu kuyakinisha yale yaliyoamriwa na neno la Mungu. Na kwa kuongezea hapo ni kusema: Inawezekana kwa mwanadamu kufanya kazi za Kikristo na kuabudu yale tu yaliyoamriwa na neno la Mungu.Agano Jipya mara zote husisitiza kwamba tunatakiwa kusikiliza sauti ya Mungu, vile anavyoongea nasi kupitia Mwana wake. Tunamsikia Mwana wake kwa kusikiliza neno lake. Kila kitu ambacho Mkristo anafanya ni lazima kiwe kimeamriwa na Agano Jipya. Hatutakiwi kuongeza zaidi ya mafundisho yake. Hatutakiwi kuyapunguza. Hatutakiwi kuyabadilisha. Hatutakiwi kuhukumu kile ambacho Mungu ameruhusu. Hatutakiwi kukiuka sheria ambazo Mungu kaziweka. Hatutakiwi kutunga sheria ambazo Mungu hajaziweka.

VII. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Kwanza)Katika “kuenenda sawa na neno la kweli” – katika kujitahidi kuelewa suala la kutambua mamlaka ya Biblia, kuna tofauti fulani muhimu zinazotakiwa kueleweka na kuheshimika.

Page 68: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 60 -

1. Agano la Kale/Jipya. Tunatakiwa tuelewe kwa usahihi tofauti iliyopo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Biblia yenyewe inaweka wazi tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Katika Mathayo 26:28 Bwana alisema: “Kwa maana hii ndio damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” Katika Waebrania 9:15 inasema: “Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele, Yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka katika dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza.” Na katika mistari ya 16 na 17 ya Waebrania 9 inasema: “Kwa habari ya wosia, ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeufanya, kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu akishakufa, kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yungali hai.” Katika Waebrania 8:8 Paulo anamnukuu Mungu akisema, “Siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda…” Halafu kwenye mstari wa 13 Paulo anasema: “Kwa kuliita agano hili “Jipya” Mungu amelifanya lile agano la kwanza kuwa kuukuu, lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa kikaribu na kutoweka.”Zaidi ni muhimu kutambua kwamba Mungu amejishughulisha na mwanadamu katika mifumo mitatu tofauti ya kidini, na kwamba tunaishi katika mfumo wa tatu wa dini. Ni ukweli kwamba Biblia inaweka mifumo mitatu tofauti ya kidini. Kuwa na maarifa ya ukweli huu ni muhimu sana katika kuielewa Biblia. Katika kurejelea hii mifumo ya kidini tunatumia

Page 69: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 61 -

neno “vipindi vya dini.” Kulikuwa na kipindi cha dini cha wazee. Kulingana na kumbukumbu za Agano la Kale kipindi hiki hujumuisha matukio kuanzia kipindi cha Adam hadi wakati wa kutoa sheria ya Musa. Kulikuwa na kipindi cha dini ya Kiyahudi. Kipindi hiki hujumuisha matukio kuanzia wakati wa kutoa sheria kwenye mlima Sinai hadi kipindi cha msalaba. Kuna Ukristo. Kipindi hiki huanzia wakati wa Pentekoste ya Matendo 2 hadi siku ya Kuja Bwana mara ya pili. Kipindi hiki ni wakati ambapo tunatakiwa kumsikia Kristo akizungumza nasi kupitia Agano Jipya.

2. Imani/Maoni. Ni muhimu sana kutofautisha waziwazi kati ya imani na maoni, kati ya imani na akili ya kibinadamu. Najua kwamba Biblia inasema Nikodemu alikwenda kwa Bwana wakati wa usiku. Ninaamini kwamba Nikodemu alikwenda kwa Bwana wakati wa usiku. Biblia haituambii kwa nini Nikodemu alikwenda kwa Bwana wakati wa usiku, na kwa hiyo chochote tutakachosema kuhusiana na hili itakuwa ni maoni tu. Sitakuwa na haki ya kumlazimisha mtu mwingine kukubali maoni yangu, na wala yeye hatakuwa na haki ya kunilazimisha mimi kukubali maoni yake. Hakuwezi kuwapo na umoja katika suala la maoni, na wala Biblia hailazimishi kuwepo na umoja katika suala la maoni.Walipokuwa wakitafakari juu ya safari ya pili ya utume, Barnaba alitaka kumchukua Yohana Marko, na Paulo alikuwa anapingana kabisa na wazo la kumchukua Yohana Marko (Matendo 15:36-41). Kukatokea “ukinzani mkali” baina yao. Wakagawanyika na

Page 70: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 62 -

kila mtu akaenda njia yake. Ninapata furaha kubwa kutokana na ukweli kwamba Mungu anaweza kutumia udhaifu wa wanadamu kutimiza kazi kubwa. Kwa sababu ya huu ukinzani, sasa tuna safari mbili za utume badala ya moja, na sasa tuna watenda kazi wanne badala ya wawili au watatu. Ninaridhika sana katika somo kwamba kama wahubiri wawili wazuri kabisa ambao kanisa liliwahi kuwa nao wamekinzana vikali katika maoni ya kibinadamu, hata sisi siku zote tutakuwa na kutofautiana katika maoni ya kibinadamu. Na wala Biblia hailazimishi kuwepo na umoja katika suala la maoni.

3. Muda mfupi/Kudumu. Lazima tuwe na uwezo wa kutofautisha kati ya muda mfupi na wa kudumu.Kulikuwa na mitume katika kanisa la awali – watu ambao Mungu aliwaahidi miujiza ya Roho Mtakatifu, na watu ambao Mungu aliwatimizia ahadi yake. Kuna watu ambao walikuwa na karama za roho, na ambao walipewa nguvu na uwezo wa kutoa karama za miujiza kwa watu wengine. Kulikuwa na watu wengine katika kanisa la awali waliokuwa na karama fulani za miujiza. Kulikuwa na watu ambao mitume waliwawekea mikono, na wakatoa miujiza ya kiroho. Hakika, ni kweli kwamba sasa tunaona faida ya kazi na mafundisho ya mitume, na kwamba bado yana ushawishi mkubwa katika kanisa la Bwana wetu. Lakini, ukweli unabaki kwamba hatuna mitume walio hai wenye nguvu za miujiza katika kanisa letu leo. Pia ni kweli kwamba hakuna mtu kanisani leo ambaye ana nguvu za kufanya miujiza. Mitume walio hai, miujiza, karama za roho – vitu hivi vilikuwa vya

Page 71: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 63 -

lazima katika kanisa changa, lakini vilikuwa vya muda mfupi tu katika asili na tabia; havikukusudiwa kuwa sehemu ya Ukristo wa kudumu. Kulikuwa hakuna neno la Mungu lililotimilika katika maandishi wakati wa kanisa la awali. Kulikuwa na uhitaji mkubwa wa mwongozo na maelekezo matakatifu. Kwa hiyo Mungu aliwaweka manabii katika kanisa la awali, na kupitia hawa alifunua ujumbe wake. Kulikuwa kuna “nabii” katika kanisa la awali na kulikuwepo kupata ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna nabii anayeishi katika kanisa la leo, na hakuna vitu kama mtu kupokea ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu..Katika siku ya Pentekoste ya Matendo 2, Mungu aliweka wazi kwamba alitaka ujumbe wa injili uhubiriwe kwa Kiyahudi. Kimsingi, katika mstari wa 39, Petro kwa uvuvio alitangaza kuwa ujumbe wa injili ulikuwa kwa ajili ya wamataifa pia. Lakini Petro yeye mwenyewe hakujua maana kamili ya kile Mungu alichosema kupitia yeye. Ni baada ya takribani miaka kumi baadaye ndipo Mungu akafanya miujiza ili kumshawishi Petro kuwa injili ilikuwa ni kwa ajili ya Wamataifa na Wayahudi pia. Hii ilihusisha uongokaji wa Kornelio na nyumba yake yote ambapo Mungu aliowaonesha waziwazi Wamataifa na Wayahudi kwamba injili ya Kristo ilikuwa ni kwa ajili ya Wamataifa na Wayahudi. Katika kipindi cha kuanzia miaka baada ya Pentekoste hadi kuongoka kwa Kornelio na nyumba yake, kanisa lilikuwa limekataa kuhubiri injili kwa Wamataifa. Kwa hakika,

Page 72: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 64 -

hakukuwa na dhambi kukataa. Hoja yetu hapa ni kwamba kukataa huku kulikuwa ni kwa muda mfupi, na wala haikuwa sehemu ya Ukristo wa kudumu.Hatufikii hitimisho hili bila kuwa na mantiki bali kwa kuzingatia mafundisho ya jumla ya Biblia kuhusiana na masuala haya. Kama ningekuwa namwambia mtu: Ni jukumu lako “kutafuta kwa bidii zote karama za kiroho” na kutoa nukuu katika 1 Wakorintho 14:1 kama uthibitisho, nitakuwa ninatenda na kufundisha kinyume na mafundisho ya Biblia, hata kama maneno haya yanapatikana katika 1 Wakorintho 14:1. Tunatakiwa kutofautisha kati ya mambo ya muda mfupi na yale ya kudumu.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 73: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 65 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Tumeshaelewa kweli gani nne za msingi?

2. Tafadhali kariri 1 Wakorintho 4:6

3. Elezea umuhimu wa Wagalatia 1:6-9

4. Tafadhali kariri KAULI YA MSINGI

5. “Matokeo” ya kauli hii huweza kuwa?

6. Na kuongezea katika kauli hii inaweza kuwa nini?

7. Tunatakiwa kusikiliza sauti ya ________, anayezungumza nasi kupitia______. Mwana huzungumza nasi kupitia________, ______. Kila kitu anachofanya Mkristo ni lazima kiwe _______________ kwa njia ya________.

Page 74: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 66 -

8. Hatutakiwi kuruhusu kile ambacho Mungu ________hatutakiwi________kile ambacho Mungu ameruhusu.

9. Hatutakiwi __________sheria ambazo Mungu ___________; hatutakiwi __________ sheria ambazo Mungu ______________.

10. Mathayo 26:28, Waebrania 9:16, 17, Waebrania 10:9, na Webrania 8:8-13 huonesha waziwazi kwamba tunatakiwa tuelewe hoja gani?

11. Mungu amejishughulisha na mwanadamu katika __________________tofauti ya kidini. Tunaishi katika kipindi cha mfumo wa ____________________.

12. Katika kurejelea “mifumo ” hii tunatumia neno gani?

13. Kipindi cha “Ukristo” huanzia wapi hadi wapi?

14. Pia tunatakiwa tuwe waangalifu katika kutofautisha kati ya __________na _______.

Page 75: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 67 -

15. Je biblia inatulazimisha kuwa na umoja katika masuala ya “maoni?”

16. Tumesisitiza hoja gani kuhusiana na Barnaba na Paulo?

17. Pia tunatakiwa tuwe na uwezo kwa kutofautisha kati ya ____________na ________.

18. Mitume hai, miujiza, karama za kiroho, mambo haya yalikuwa ni ya________________kwa asili na tabia; kamwe hayakukusudiwa kuwa sehemu ______ya Ukristo.

19. Leo hakuna ___________wanaoishi kanisani, na hakuna mafunuo ya ____________ kwa mwanadamu kutoka kwa Mungu.

20. Itakuwa ni sawa kwa Wakristo leo kukataa kuhubiri injili kwa Wamataifa?

21. Kwa masuala yote ya Biblia tunatakiwa kutafakari kwa makini juu ya _______________ya _____________ ____________juu ya masuala haya.

Page 76: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 68 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 77: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 69 -

SOMO LA NANE

IX.TOFAUTIMUHIMU(SehemuyaPili)

8

Page 78: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 70 -

4. MAZINGIRA/MASHARTI. Katika kujitahidi kujifunza kuhusu majukumu, wajibu na tabia zetu tunapaswa kutofautisha kwa wazi kati ya mazingira na masharti. Matendo 16:13-15 inaonesha mazungumzo kati ya Lidia na nyumba yake. Mazungumzo yalikuwa: “Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando ya mto, mahali ambapo tulitarajia tungepata mahali pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika huko. Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mfanya biashara wa nguo za zambarau, mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu. Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa Paulo. Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa nyumbani mwake, alitukaribisha nyumbani mwake akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini Bwana, karibuni mkae nyumbani mwangu.’’ Naye akatushawishi.” Siku ya Sabato, mahali pakufanyia maombi, kukaa chini, kukutana kwa wanawake – haya yalikuwa ni mazingira. Kuhubiri, kusikiliza, kuamini, kubatizwa – hizi zilikuwa ni masharti. Mazingira hubadilika; masharti hayabadiliki. Matendo 16 pia huonesha kubadilika kwa askari wa gereza pamoja na nyumba yake na kumfuata Kristo. Kufungwa kwa Paulo na Sila, kusali na kuimba usiku wa manane, wafungwa kusikiliza, tetemeko kubwa la ardhi, kuta kutetemeko, milango kufunguliwa, mikono kufunguliwa – haya yalikuwa ni mazingira. Kuhubiri, kusikiliza, kuamini, ubatizo – haya yalikuwa ni masharti, yalikuwa msingi wa wokovu wa askari wa gereza. Tunasisitiza kwamba sio vigumu

Page 79: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 71 -

kutofautisha kati ya mazingira na masharti, na katika hili akili ya kuzaliwa inaweza kutumika.

5. TUKIO/LAZIMA.Vilevile ni lazima tuweze kutofautisha kati ya tukio na ulazima. Tunajua kwamba katika eneo hili huwa kuna kuchanganya na suala la hali ya mambo na mazingira. Katika baadhi ya mambo tukio linaweza kuhusishwa na mazingira lakini “lazima” haiwezi kuwa hali.Katika Matendo 16:10 tunaona wito mkuu wa kwenda Makedonia. Mungu aliweka wazi kwamba alitaka Paulo kuhubiri injili huko Makedonia. Luka anasema: “Baada ya Paulo kuona maono haya, mara tulijiandaa kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kwa sababu tuliona kwa hakika kwamba Mungu ametuita kuhubiri habari njema huko. Tukasafirikwa njia ya bahari kutoka Troa na kwenda moja kwa moja mpaka Samothrake, kesho yake tukafika Neapoli. Kutoka huko tukasafirihadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia sehemu walipokuwa wanakaa Warumi, nasi tukakaa kwenye mji huo kwa siku kadhaa.” Katika Safari ya Kwenda Makedonia, Paulo na wenzake walichagua kusafirikwa kutumia mashua. Wangeweza kutumia njia za nchi kavu. Kitu cha lazima kilikuwa ni kwenda Makedonia. Kusafirikwa kutumia mashua kulikuwa ni tukio tu.Kulingana na Matendo 20:7-9 ndugu wa Troa walikutana ghorofa ya tatu kwa ajili ya kuabudu. Ukweli kwamba sehemu ya kukutania ilikuwa ni ghorofa ya tatu hakumaanishi kwamba ndiyo ibada inayokubaliwa. Wangeweza kufanyia ibada katika

Page 80: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 72 -

ghorofa ya kwanza, au ghorofa ya pili, au ghorofa ya tano. Kitu cha lazima kilikuwa ni kumwabudu Mungu kama alivyoagiza. Suala la tukio lilikuwa ni ghorofa ya tatu.

6. NJIA/KANUNI. Tunapaswa kutofautisha kati ya njia na kanuni. Wakati mwingine tunakuwa tunajihusisha zaidi na njia kiasi cha kushindwa kuiona kanuni.1 Wakorintho 14:26-40 ni sehemu ya mjadala mkubwa wa Paulo juu ya “Karama za Roho,” na ambapo mjadala umeanzia katika sura ya 12 mstari wa 1. Kujaribu kujifunza 1 Wakorintho 14:26-40 bila kuzingatia muktadha husika, kumesababisha matokeo ya kusikitisha sana miongoni mwa wapendwa wetu. Kimsingi watu wengi wamekuwa wakinukuu mstari wa 34 bila kujua kile kilichoandikwa mstari wa 26. Katika mistari hii Paulo anazungumzia mkutano maalumu wa wapendwa huko Korintho. Ulikuwa ni mkutano mahususi kwa ajili ya kupokea karama za roho; ulikuwa ni mkutano kwa ajili yao tu. Paulo anatoa maelekezo mahususi kuhusiana na wale watakaokuwa wanatumia karama ya kunena kwa lugha, kuhusu wale ambao watakuwa wanafasiri lugha, kuhusu wale ambao wangeweza kuwa na karama ya unabii, na kuhusu mwenendo wa wake za manabii. Kwa kuzingatia mkutano huu, Paulo anataja kwa uwazi kabisa masharti mawili ambayo kwayo watu waliambiwa kuwa kimya; lakini pia anatoa maelekezo: “Mwanamke na anyamaze kanisani….” Paulo anafafanua: (1) hawajaruhusiwa kuzungumza; (2) ni aibu mwanamke kuzungumza kanisani.

Page 81: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 73 -

Lakini sasa hivi, katika mkusanyiko wetu wa kawaida, wanawake wanaruhusiwa na wanahimizwa kuimba. Wanapoimba wanakuwa wanazungumza. Na wanapozungumza wanapokuwa wanaimba, wanafundisha. Wanawake wanaruhusiwa “kuja mbele,” kusimama mbele ya watu na kukiri imani yao kwa Kristo ili waweze kubatizwa. Wanaruhusiwa kuungama dhambi zao ili waweze kusamehewa. Haya yote hufanyika na wala hakuna dhambi na wala aibu. Kwa uhalisia mikutano yetu sio mikutano inayozungumziwa katika 1 Wakorintho 14:26-40.Je hii ina maana kwamba 1 Wakorintho 14:26-40 haitumiki katika kanisa la leo? Haimaanishi hivi kabisa. Kanuni zilizowekwa zitadumu kama zilivyokuwa; njia (mazingira, masharti) ambamo Paulo aliweka hizi kanuni hazipo katika ulimwengu wa leo. Kanuni takatifu za kudumu ni: (1) vitu vyote vifanyike kwa kusudi la kujenga; (2) Mungu sio Mungu wa machafuko, bali wa amani; (3) wote wawe watiifu; (4) mambo yote yafanyike kwa heshima na kwa mpangilio.

7. DESTURI/SHERIA. Pia tunapaswa tuwe makini kati ya kutofautisha desturi za wanadamu na sheria takatifu. Naamini hii ndio njia ya kuelewa 1 Wakorintho 11:2-16. Mengi yaliyosemwa katika mistari hii huhusiana na desturi zilizokuwepo Korintho, juu ya wanawake kuvaa utaji. Nashawishika kuamini kwamba Paulo, katika mistari hii, hafundishi kwamba wanawake Wakristo, muda wote na sehemu zote ni lazima wavae utaji. Paulo katika mistari hii kwa kuzingatia desturi husika, anasisitiza kanuni fulani muhimu ambazo

Page 82: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 74 -

zinadumu sasa kama ilivyokuwa hapo mwanzo. Kutokana na mistari hii tunajifunza: (1) Kichwa cha Kristo ni Mungu; kichwa cha kila mwanaume ni Kristo; kichwa cha kila mwanamke ni mwanaume; (2) Mwanaume hatakiwi kufanya jambo lolote ambalo litamkosea heshima Kristo; (3) Mwanamke hatakiwi kufanya kitu chochote ambacho kitamkosea heshima mwanaume; anatakiwa adumishe tabia ya heshima na kujinyenyekeza; (4) Ni sahihi na ni vema kuzishikilia desturi ambazo ni nzuri, hatupaswi kuwahukumu watu wengine kwa kukiuka hizi desturi; (5) Hatupaswi kuleta malaumu kanisani kwa kukiuka desturi ambazo ni nzuri (6) Hatutakiwi kuvaa mavazi ambayo yatatufanya tuonekane kama watu wachafu; (7) Hatupaswi kuvaa mavazi ambayo tutakuwa tunamkufuru Mungu na malaika (waliopo wakati wa ibada); (8) Mavazi yetu yanapaswa yaonyeshe heshima na usafi wetu. Tazama kiambatisho A.

Page 83: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 75 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Tunapaswa kuwa makini katika kutofautisha kati ya ___________ na _________.

2. Siku ya sabato, mahali pa kufanyikia maombi, kukaa chini, mkutano wa wanawake haya yote yalikuwa ni nini?

3. Kuhubiri, kusikiliza, kuamini, ubatizo – haya yalikuwa ni nini?

4. Kwa kurejelea kuongoka kwa askari wa gereza na familia yake, jadili mazingira yake.

5. Kwa kurejelea kuongoka kwa askari wa gereza na familia yake, jadili masharti yake.

6. Tunapaswa kuweza kutofautisha kati ya ___________ na _________.

7. Katika baadhi ya mambo tukio linaweza kuhusishwa na _________ na katika mambo mengine lazima ______________.

8. Rejea Paulo kwenda Makedonia, kitu cha lazima kilikuwa ni nini? Na tukio lilikuwa ni nini?

Page 84: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 76 -

9. Kwa kuzingatia ibada iliyotajwa katika Matendo 20:7-9, kitu cha lazima kilikuwa ni nini? Na tukio lilikuwa ni nini?

10. Tunapaswa kutofautisha kati ya ___________ na _________.

11. 1 Wakorintho 14:26-40 ipo katikati ya mjadala wa Paulo kuhusu kitu gani?

12. Ni mkutano wa aina gani ambao Paulo anajadili katika 1 Wakorintho 14:26-40 ?

13. Je mikutano yetu ya ibada ya kila siku hufanana na mikutano hii?

14. ______________ zilizowekwa katika 1 Wakorintho 14:26-40 zinadumu kama ilivyokuwa mwanzo; ____________ ambamo Paulo ameziweka hizi kanuni _______ katika ulimwengu wa leo.

15. Orodhesha kanuni kuu nne zilizowekwa katika 1 Wakorintho 14:26-40.

16. Tunapaswa kuwa makini katika kutofautisha kati ya ______________ za wanadamu na _____________ takatifu.

17. Kanuni nane takatifu zililizowekwa katika 1 Wakorintho 11:2-16 ni zipi?

Page 85: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 77 -

SOMO LA TISA

X.TENDONAMAJUKUMU

9

Page 86: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 78 -

Tunapotafakari juu ya “mamlaka ya Biblia” wakati huu, akilini tunakuwa na mamlaka ya kimaandiko yanayoongoza matendo yetu na tabia zetu kama

Wakristo. Matendo yetu ni matokeo ya tabia zetu; matendo yetu hukua kutokana na majukumu yetu. Majukumu yetu

Hili jukumu la msingi la kuokoa roho hujumuisha majukumu mengine ya jumla ya (1) kupeleka injili ulimwenguni, (2) kuwasaidia wahitaji, na (3) kujenga maadili ya kanisa. Kutekeleza majukumu haya ya jumla, huhusisha kazi nyingi mahususi.Ni lazima tuyatimize majukumu haya, kama tunataka kumpendeza Mungu – hatuna uchaguzi. Lakini, kwa kuangalia namna ambavyo tunaweza kuyatekeleza majukumu haya, kuna maeneo ambayo tunaweza kufanya uchaguzi.Lakini, ni kwa jinsi gani mamlaka ya Biblia yanathibitishwa kwa kuzingatia kile ambacho ni wajibu wetu ? Ni kwa jinsi gani mamlaka huthibitishwa kwa kuangalia namna tunavyopaswa kuyatekeleza majukumu haya?

XI. MUNGU HATAVUMILIA KILE AMBACHO HAKIKURUHUSIWAChochote kinachotolewa kama ibada kwa Mungu, ambacho hakijaamriwa na Agano Jipya, hakitakubalika machoni pake. Ukweli kwamba kitu hicho KIMEKUSUDIWA kuwa ibada kwa Mungu, haimaanishi

kama watoto wa Mungu, huhusiana na hoja moja ya msingi; uokoaji wa roho. Huu ndio utume Mungu alioutoa kwa kanisa lake – uokoaji wa roho za watu.

Page 87: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 79 -

kwamba kitampendeza Mungu. Ibada ya Kaini (Mwanzo 4:2-5) haikukubalika machoni pa Mungu. Mungu kupitia Malaki, alitafuta kuwarekebisha kuhusiana na jitihada zao katika kufanya ibada. Mungu aliwaelezea kwamba sadaka zao hazikukubalika machoni pake. Kimsingi Mungu alisema: “…Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu!...” (Malaki 1:8). Bwana alitumia unabii wa Isaya kwa Mafarisayo na Waandishi, akisema, “Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Mathayo 15:9).Biblia mara nyingi hutumia neno “geni” kwa maana ya “haikubaliki kwa sababu haijaamriwa.” Nadabu na Abihu “….wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana, ambao yeye hakuwaagiza” (Lawi 10:1). “Kisha moto ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa mbele za Bwana” (Lawi 10:2). Mfalme Suleimani alioa “mwanamke wa kigeni” ambaye Mungu hakuruhusu amwoe. Dhambi kama hii lilikuwa ni tatizo kubwa sana katika kipindi cha Nehemia (Neh. 13:27). Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka “wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili” (Yuda 7). Tumeonywa juu ya “kuchukuliwa na mafundisho ya kigeni” (Waebrania 13:9).

XII. NI LAZIMA TUBAKI KATIKA KILELE CHA MAMLAKA YA BIBLIAKanisa la Bwana limekuwa likipata mapigo ya matatizo ya (1) ukatazaji na (2) Ulegezaji. Ukatazaji ni kutengeneza sheria ambazo Mungu hakuweka. Ulegezaji hupuuzia sheria ambazo Mungu ameziweka. Ukatazaji

Page 88: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 80 -

huchukulia mambo ya maoni kana kwamba ni mambo ya imani. Uliberali huchukulia mambo ya imani kama vile ni mambo ya maoni. Ukatazaji hutafuta kufunga pale ambapo Mungu hakufunga. Ulegezaji hutafuta kulegeza pale ambapo Mungu amefunga. Mara nyingi watu wanapojaribu kutoka katika hali hii ya ukatazaji wanajikuta wapo katika hali ya Ulegezaji. Tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunakuwa makini kubaki katika kilele cha mamlaka ya Biblia. Tuhakikishe kwamba hatuangukii upande wowote kutoka kileleni – kuna kifo na uharibifu katika pande zote!

XIII. TUNAPASWA KUJUA JINSI AMBAVYO MUNGU HARUHUSULakini, ili tuweze kubaki katika kilele cha mamlaka ya Biblia tunapaswa kujua (1) JINSI MUNGU ASIVYORUHUSU NA, tunapaswa tujue, (2) JINSI MUNGU ANAVYORUHUSU. Hebu tuangalie angalau JINSI MUNGU ASIVYORUHUSU. Ni lazima nijikumbushe wakati wote kwamba Mungu haruhusu:

1. Kwa kuangalia vile ninavyovipenda na nisivyovipenda;

2. Kwa kuangalia kile kinachonifurahisha;3. Kwa kuangalia hitimisho lenye makosa ninaloweza

kufikia4. Kwa kuangalia maoni yangu au maoni ya watu

wengine;5. Kwa kuangalia kile ambacho ni maarufu sana;

Page 89: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 81 -

6. Kwa kuangalia kile ambacho kinaweza kuwa muafaka katika mhadhara wa mtu fulani;

7. Kwa kuangalia mtu fulani anayefahamika au anayeheshimika katika jamii au kile anachofundisha;

8. Kwa kuangalia tamaduni za wanadamu;9. Kwa kuangalia uwezo wa mtu kutoweza “kuona

hatari yoyote katika hiyo”;10. Kwa kuangalia desturi zilizodumu kwa muda

mrefu;11. Kwa kuangalia ukimya wa maandiko.

XIV. LAKINI VIPI KUHUSU UKIMYA WA MAANDIKOWatu wengi sasa wanasema kuwa ala za muziki katika ibada ya Kikristo zimeruhusiwa kwa ukimya wa maandiko. Wanasema hivi kwa kumaanisha kwamba, Agano Jipya halisemi chochote kuhusu hili, na kwa hiyo zimerusuhusiwa kutumika katika ibada ya Kikristo. Inashangaza sana kuona kwamba watu hawa hawa wanaosema kwamba ala za muziki zimerusuhusiwa katika ibada ya Kikristo kwa sababu maandiko yapo kimya, pia wanasema sio lazima kitu kiruhusiwe ndipo kimpendeze Mungu, na hivyo kinaweza kuruhusiwa kutokana na ukimya wa Maandiko!Dhana hii ya mamlaka ya Biblia ni kinyume kabisa na kanuni ya msingi ya mamlaka ambayo tumekwishajifunza. Biblia huruhusu kwa KILE INACHOSEMA – NA SIO

Page 90: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 82 -

KILE AMBACHO HAISEMI! Biblia haisemi chochote kuhusu kuhesabu rozari katika ibada ya Kikristo, lakini ukweli huu haumaanishi kuruhusu kuhesabu rozari katika ibada ya Kikristo. Ikiwa kila kitu ambacho Biblia imenyamaza basi kinawekwa kwenye ibada ya Kikristo, na ikiwa kuhesabu rozari ni kitu ambacho Biblia imenyamaza; kwa hiyo kuhesabu rozari ni kitu ambacho kinaweza kujumuishwa katika ibada ya Kikristo! Hoja ya kipuuzi kiasi gani! Halafu hii ndio hoja ambayo watu wengine wanaisimamia wanaposema kwamba ala za muziki zimeruhusiwa kwa ukimya wa Maandiko. Maandiko yanasema kwamba Bwana mwenyewe asingefanya kazi kama kuhani baada ya mfumo wa sheria ya Musa. Kwa nini? Kwa sababu hakukuwa na mamlaka kwa ajili ya hilo! Zingatia hili andiko: “Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka Yuda, kabila ambayo MUSA HAKUNENA LO LOTE juu yake katika mambo ya ukuhani” (Waebrania 7:14).Akiwa Yeriko, Bwana aliwafundisha Israeli mafundisho makuu na ya kushangaza; moja wapo lilikuwa ni umuhimu wa ukimya wa Maandiko. Mungu aliruhusu “kelele za kupaza sauti” mahususi. Yoshua yeye alitaka watu wapige kelele kwa namna tofauti tofauti, katika wakati ambao sio sahihi, na sehemu ambayo sio sahihi. Kwa hiyo Yoshua alifafanua jambo lenyewe. Bwana alisema: (1) baada ya kusonga mbele katika siku ya sita, na (2) baada ya kusonga mbele siku ya saba, na (3) baada ya makuhani kubeba sanduku la agano na tarumbeta saba, na (4) baada ya makuhani kupiga tarumbeta na watu kusikia sauti ya tarumbeta. NDIPO watu wangeweza kupiga kelele

Page 91: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 83 -

kuu. Yoshua alisisitiza kulingana na majukumu yaliyopo mambo ambayo hayakuruhusiwa ni (1) kupiga kelele nyakati fulani, (2) au kusikika sauti wakati fulani, (3) au kutoa sauti ya aina yoyote ile. Yoshua alisema: “Msipige kelele wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lolote lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele” (Yoshua 6:10). Ni somo gani ambalo Mungu na Yoshua waliwafundisha Israeli kuhusu ukimya wa ufunuo wa Mungu? Mungu alisema, na Yoshua akalifafanua vizuri.Kumbukumbu zinasema: “Wakati baragumu zilipopigwa, watu walipiga kelele, kwa sauti ya baragumu, wakati watu walipopaza sauti, ukuta ukaanguka, hivyo kila mtu akasonga mbele moja kwa moja kutokea pale alipokuwa kutokea kila upande na kuuteka mji” (Yosh. 6:20).Kwa kuzingatia jukumu lililokuwa mbele ya Wana wa Israeli (kupaza sauti) kungekuwa na ubaya gani kama wangepaza sauti muda mwingine wowote ule wakati wa kusonga mbele? Kungekuwa na kosa gani endapo hata wangetoa sauti yoyote hata wakati ambao ulikuwa ni wa kupaza sauti? Jibu: Wangekuwa wanafanya jambo ambalo halikuruhusiwa na mamlaka takatifu. Wangekuwa wanafuata ukengeufu wao na hisia zao tu, na sio KILE AMBACHO MUNGU AMEKWISHASEMA!

Page 92: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 84 -

MSWALI YA KUJIFUNZA

1. Akilini tunakuwa na mamlaka ya kimaandiko yanayoongoza ______ yetu na _______ zetu.

2. Matendo yetu ni matokeo ya _________ zetu; matendo yetu hukua kutokana na ____________ yetu.

3. MAJUKUMU yetu huhusiana na hoja gani ya msingi?

4. Kwa kuhusiana na JUKUMU LETU LA MSINGI, tuna MAJUKUMU YA JUMLA mengine matatu. Ni yapi hayo?

5. Kutekeleza majukumu haya ya jumla kunahusisha ________________ nyingi.

6. Kwa kuangalia namna tunavyotekeleza majukumu haya, kuna maeneo ya _______.

7. Mungu hatavumilia kitu gani?

Page 93: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 85 -

8. Kweli au Si kweli. Kuwa na NIA ya kufanya ibada kwa Mungu ni uthibitisho kwamba ibada yako imekubaliwa mbele za Mungu.

9. Tunajenga hoja gani tunaponukuu Mwanzo 4:2-5; Malaki 1:8 na Mathayo 15:9?

10. Maana ya “geni” ni nini?

11. Kanisa limekumbwa na matatizo gani mawili ya msingi?

12. Elezea juu ya asili ya “ukatazaji” dhidi ya asili ya “Ulegezaji”

13. Kwa kuzingatia haya tunatakiwa tuamue nini?

14. Kwa kurejelea JINSI AMBAVYO MNGU HARUHUSU, tulitaja hoja kumi na moja. Tafadhali elezea kila hoja.

15. Ni kitu gani ambacho watu wanabishana kuhusu “Ukimya wa Maandiko?”

16. Dhana hii (mamlaka kwa kunyamaza) ni kinyume na nini?

Page 94: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 86 -

17. Je Biblia inazungumzia kuhusu habari ya kuhesabu rozari wakati wa ibada?

18. Je, “ukimya” huu unaruhusu kuhesabu rozari wakati wa ibada?

19. Tafakari na jadili umuhimu wa Waebrania 7:14 na Bwana kuweza kuhudumu kama kuhani (kwa mujibu wa sheria za Musa).

20. Pamoja na mambo mengi, ni somo gani kubwa ambalo Mungu alilitoa kwa Waisiraeli pale Yeriko?

21. Kuhusu “kupaza sauti” kwa Waisraeli, Yoshua alikuwa anaangalia kitu gani zaidi?

22. Yoshua alifafanua kwamba kuruhusu “kupiga kelele” HAKUKUJUMUISHA angalau vitu vitatu. Ni vitu gani hivyo?

23. Kungekuwa na ubaya gani kama wangepiga kelele muda mwingine wowote ule wakati wa kusonga mbele? Kungekuwa na kosa gani endapo hata wangetoa sauti yoyote hata wakati ambao ulikuwa ni wa kupiga kelele?

Page 95: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 87 -

SOMO LA KUMI

XV.MAMLAKAYANATHIBITISHWA

KWAMFANO

10

Page 96: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 88 -

1. Neno “mfano” kwa mujibu wa kamusi, ni “kitu ambacho kinatakiwa kufuatwa au kuigwa: ni kielelezo.” Tumetaja fasili hii ili kuonesha kwamba “mfano” unatakiwa ufuatwe au uigwe. Mfano “unashurutisha.” Kwa miaka mingi swali hili limekuwa likiulizwa: “Ni wakati gani ambapo mifano inakuwa inashurutisha?” Kwa maoni yangu swali hili sio sahihi. Ni dhahiri kwamba, kama ni mfano, unashurutisha na kama haushurutishi basi huo sio mfano.Swali lingeweza kuwa: Ni wakati gani ambapo Biblia inahesabu tendo fulani kuwa ni mfano? “Lakini” unaweza kuuliza, “hivi ndugu Thomas Warren, si ana kitabu kizuri kabisa kinachoitwa ‘Wakati ambapo Mfano Hushurutisha?’’ Ndio, anacho. “Hajui kuwa swali hili sio sahihi?” Ndiyo, anajua! Anajua vizuri kuliko mtu yeyote. “Sasa kwa nini anatumia jina hili?” Kwa sababu swali hili kila mtu alikuwa analiuliza, na aliweka neno MFANO katika alama za nukuu kwa umakini kabisa.

2. Kwa hoja hii natakiwa kufafanua maana ambayo natumia neno “kushurutisha” kwa kuhusiana na mifano. Akilini mwangu nina wazo kwamba (1) vitu fulani vinashurutisha (na kwa hiyo ni mifano) kwa maana kwamba ni lazima vifanyike (hivi vinatakiwa; hakina kuchagua – ukweli huu unafafanuliwa vizuri kwa kuzingatia mafundisho ya Biblia juu ya suala hili) na (2) vitu fulani vinashurutisha (na kwa hiyo ni mifano) kwa maana kwamba vinaweza kufanyika (Hivi vimeruhusiwa; vinaweza kufanyika, lakini vinaweza kuachwa bila kufanyika).

Page 97: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 89 -

3. Kwa mfano, nimeamriwa kuazimisha Meza ya Bwana, 1 Kor. 11:24, 25. Nimeelekezwa (kwa mwongozo na mfano) kuiazimisha siku ya kwanza ya kila juma, Matendo 20:7; 1 Kor. 16:2. Hakuna uchaguzi hapa. Nimeamriwa kwa mfano kushiriki meza ya Bwana katika “chumba cha ghorofani” kikiwa na “taa nyingi.” Hili linashurutisha ikiwa tu nimerushusiwa kulifanya. Ni hiari. Nimejifunza kutoka katika maandiko mengine kwamba eneo sio kitu cha muhimu, na kwa hiyo, nikahitimisha kuwa “chumba cha ghorofani” ni suala la hiari.

4. Zaidi, nimeamriwa kutoa kadri nilivyobarikiwa. Hili ni suala la lazima. Sitakiwi kuacha kutoa wakati nimebarikiwa. Lakini, katika 2 Wakorintho 8:1-5, ninafundishwa kwa mifano kwamba ninaweza kuzidi kutoa kadri ninavyobarikiwa. Ndugu wa Makedonia walitoa “zaidi ya uwezo wao.” Je Paulo aliwaonyesha hawa ndugu kama mfano, kwa ndugu wa Korintho? Je huu ni mfano kwangu? Tendo hili linanishurutisha? Kama ni hivyo, linanishurutisha kwa namna gani? Je linanifundisha kuwa kila siku ya Bwana ni lazima nitoe zaidi ya uwezo wangu? Au linanifundisha kuwa ninaweza kutoa zaidi ya uwezo wangu? Ni kwa jinsi gani mfano huu unaenda na amri?

5. Kama Agano Jipya linasema “kwenda” ndilo jambo la lazima na kwamba njia ni uchaguzi, na kama Agano Jipya linaonyesha Paulo alisafiri kwa merikebu, kwa hiyo naweza kuhitimisha kuwa, Paulo kusafiri kwa merikebu ni mfano kwangu (inanishurutisha) kwa maana kwamba naweza kusafiri kwa merikebu. Lakini ninaweza kusafiri kwa ndege.

Page 98: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 90 -

6.

7. Kwa kuzingatia Matendo 11:29,30, naamini kwamba inashurutisha, (kwa maana kwamba mfano huo umeruhusiwa, na kwa hiyo unaweza kuigwa) kwa washiriki kuchagua watu wawili na kutoka kwenda kupeleka baraka kwa watu wengine.

Ikiwa mfano unashurutisha kwa maana kwamba ni lazima ufanyike, au kwa maana kwamba unaweza kufanyika, inatakiwa iangaliwe kwa kutazama mafundisho ya Biblia yanasema nini kuhusiana na hoja hii. Pia tunapaswa kuwa makini na mifano isiyofaa. Mungu ameonesha kwa ajili ya kutufundisha MAMBO AMBAYO HATUTAKIWI KUFANYA NA MAMBO TUNAYOTAKIWA KUFANYA. Thayer, akifafanua neno TUPOS anasema, “mifano ya kugeuza mawazo, ni kielelezo ya maonyo kwa wengine.” Ananukuu 1 Wakorintho 10:6, 11 (ukurasa 632 wa kitabu chake). Thayer anaendelea kusema: “…matukio ya kuanguka yanachukua nafasi ya maonyo kwa watu wengine.”

Kwa kuzingatia 1 Timotheo 1:3 naamini kwamba inashurutisha, (kwa maana kwamba umeruhusiwa, na kwa hiyo unaweza kuigwa) na mhubiri wa injili kufanya kazi kwenye kanisa ambapo kuna wazee. Lakini pia ninaamini (1) kanisa likiwa na wazee tu linaweza kuendelea kuwepo; (2) kwamba mhubiri wa injili anaweza kufanya kazi kwenye kanisa ambalo halina wazee wa kanisa; na (3) washiriki ambao hawana wazee wa kanisa au mchungaji wanaweza kuendelea kuwepo.

Page 99: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 91 -

8. Ukweli pekee kwamba Biblia imeonyesha tendo fulani, sio lazima iwe na maana kwamba Biblia kuonesha tendo hilo ilikusudia liwe mfano. Ni muhimu sana kutafakari juu ya “matendo yaliyopewa uzito.” Agano Jipya linazungumza kuhusu….(1) Matendo ambayo yalikuwa ni dhambi. Yuda

alimsaliti Bwana, Math. 26:47-49. Anania na Safira walisema uongo mbele ya Roho Mtakatifu, Matendo 5:1-11. Petro alisujudu mbele ya watunga sheria wa kibinadamu, Wagalatia 2:11-14.

(2) Matendo yaliyokuwa sahihi wakati yalipofanywa, lakini ambayo yangekuwa sio sahihi ikiwa tutayafanya hayo matendo leo. Kanisa la awali kwa takribani miaka 10, lilikuwa limekataa kuhubiri injili kwa Wamataifa. Paulo (Matendo 21) alikuwa anafanya mambo kuonesha kwamba alikuwa anatembea katika njia sahihi, “kushika sheria.”

(3) Matendo ambayo yalikuwa ya muda mfupi na ya lazima. Wakristo wa awali waliambiwa “kutafuta kwa bidii karama za roho,” lakini karama za roho zilikuwa ni za muda mfupi. Mitume walithibitisha neno kwa ishara, lakini miujiza ilikuwa ni ya muda tu.

(4) Matendo ambayo yalikuwa ni ya muda mfupi na hiari. Paulo alimtahiri Timotheo “…kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua kwamba baba yake alikuwa ni Myunani,” Matendo 16:3. Mitume walikuwa wanahubiri kila siku hekaluni, Matendo 5:42.

Page 100: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 92 -

(5) Matendo ambayo yalikuwa ni ya kudumu lakini ya hiari. Ndugu wa Makedonia “walitoa zaidi ya uwezo wao” 2 Wakorintho 8:3. Hii haikutakiwa kufanyika, lakini iliruhusiwa kufanyika na kanuni yao ya kwenda “maili nyingine zaidi” ni sehemu ya kudumu ya Ukristo.

(6) Matendo ambayo yalikuwa ni ya kudumu na ya lazima. Wakristo wa awali walitakiwa kutoa walichonacho. Walitakiwa kuiazimisha meza ya Bwana.Ni dhahiri kwamba, matendo yale tu ambayo yalikuwa ni ya hiari na/au ya kudumu na ya lazima na ya kudumu ndiyo tunaweza kuyahusisha na Ukristo wa leo. Tunapopata sababu ya tendo lililofanyika katika Agano Jipya (1) ambalo limeshuhudiwa kuwa ni sahihi, (2) ambalo ama lilikuwa ni la hiari au lazima na (3) ambalo linahusiana na kipengele cha kudumu cha Ukristo – hivyo tuna mamlaka ya kuiga tendo hilo. (ZINGATIO BINAFSI: Makala hii “matendo yaliyoainishwa” ilitokana na uchunguzi niliovutiwa nao nikiwa na Dkt. Thomas B. Warren, miaka mingi iliyopita, uzoefu wangu kuhusu hili ni kwamba umuhimu wa hoja hii hautambuliwi).Pengine inatakiwa ioneshwe kuwa mfano haubagui. Mfano unaoruhusu kusafiri kwa boti, lakini haubagui kusafiri kwa gari. Matendo 20:7 inaruhusu kushiriki Meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya juma. Hoja kwamba ni dhambi kushiriki Meza ya Bwana siku ya alhamisi usiku,

Page 101: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 93 -

ni kwa sababu hakuna mamlaka juu ya jambo hilo. Maandiko mengi yanaonyesha wajibu wetu wa kuimba wakati wa Ibada ya Kikristo. Jambo linalofanya uimbaji kwa kutumia ala za muziki ni makosa, ni ukweli kwamba hakuna mamlaka juu ya kufanya jambo hilo. Kanuni takatifu ya “kuenenda kwa imani” inahusisha kuheshimu ukimya wa Maandiko. Angalia Kiambatanisho B na Kiambatanisho C. Kuamua kwamba kitendo ni mfano kunahitaji; (1) matumizi sahihi ya kanuni za sayansi ya kufasili Biblia, (2) matumizi ya kanuni za MANTIKI, na (3) kuangalia UJUMLA wa mafundisho ya Biblia kuhusiana na mada inayojadiliwa.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 102: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 94 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka ya Biblia huthibitishwa na _____________.

2. Maana ya “mfano” ni nini?

3. Mtu anapouliza: “Ni wakati gani ambapo mfano unashurutisha?” je hili ni swali sahihi?

4. Swali sahihi ni nini?

5. Jadili maana mbili tofauti ambazo tunazitumia kwa neno “shurutisha”

6. Kushiriki meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya kila juma ni “lazima” kwa maana ipi?

7. Kushiriki meza ya Bwana kwenye chumba cha ghorofa ni “lazima” kwa maana ipi?

8. Kutoa kadiri nilivyofanikiwa ni suala la LAZIMA. Lakini kwa kuzingatia 2 Wakorintho 8:1-5, je ni sahihi kutoa zaidi ya nilivyofanikiwa? Mfano huu unahusianaje na “amri?”

9. Paulo kusafiri kwa Merikebu, ni mfano kwangu kwa maana gani?

Page 103: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 95 -

10. Je 1 Timotheo 1:3 inatoa mamlaka kwa wahubiri wa injili kwenye kanisa ambalo lina wazee wa kanisa? Ni kwa maana gani fungu hili “linashurutisha?” Je, ni sawa kulingana na maandiko mhubiri kufanya kazi kwenye kanisa ambalo halina wazee?

11. Je ni sahihi washiriki kuchagua watu wawili ili kuunganisha nguvu ya kuwafikia wengine? Je ni sahihi kwa washiriki kutumia mfumo wa posta kuwafikia wengine?

12. Je tunajuaje kwamba mfano unashurutisha kwa maana kwamba ni LAZIMA ufanyike, au kwa maana kwamba UNAWEZA kufanyika?

13. Katika waraka wetu tuliangalia “matendo yaliyoainishwa”. Hakikisha, unajifunza, unajadili, unaelewa aina sita tofauti za matendo.

14. Ni vitu gani vinavyotakiwa viwe kweli ili kwamba sisi tujue kwamba tuna mamlaka ya kuiga matendo yaliyoandikwa kwenye Biblia?

15. Tumesema kwamba “mfano” haubagui . Tafadhali fafanua hili.

16. Ili kujua kwamba tendo lililofanyika linahusisha mfano kunahitajika nini?

Page 104: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 96 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 105: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 97 -

SOMO LA KUMI NA MOJA

Mamlaka haitegemei kwa sababu nimeyasoma, bali ni kutokana na ukweli kwamba Mungu ameyaandika; sio kwa sababu nilitafakari kwa

usahihi, bali ni kwa sababu Mungu alidokeza hivyo.

XVI. MAMLAKA YAMETHIBITISHWA KWA KUMAANISHA Mara nyingi watu wanazungumza juu ya “dokezo,” lakini “dokezo” huhusiana na “kumaanisha.” Ufahamu huhusika na kufikirikwa usahihi, lakini kufikirikwa usahihi(katika muktadha huu) kulingana na kile Mungu alichomaanisha. Kila kitu ambacho Biblia inafundisha, hufundisha ama kwa wazi au kwa kudokeza. Na kile inachokifundisha kwa kudokeza ni cha kweli, kinashurutisha, chenye mamlaka kama kile inachofundisha kwa wazi. Tunatakiwa kufikirikwa usahihi kulingana na kile ambacho Mungu anamaanisha kwenye matamko yake ya wazi. Na mamlaka yanakuwapo sio kwa sababu nimeyasoma, bali ni kutokana na ukweli kwamba Mungu ameyaandika; sio kwa sababu nilitafakari kwa usahihi, bali ni kwa sababu MUNGU ALIMAANISHA HICHO!Kuna tofauti kubwa sana kati ya “ufahamu” na “makisio.” Vitu vingi vinaitwa “dokezo” ambavyo hata sio “dokezo” lakini ni makisio tu. Matendo 16:15 inasema kwamba Lidia na nyumba yake walibatizwa. Mara nyingi

Page 106: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 98 -

inadaiwa kuwa, kwa hiyo Lidia alikuwa ameolewa, kwamba alikuwa na watoto, na kwamba baadhi ya hawa watoto walikuwa ni watoto wachanga, na kwa hiyo imeruhusiwa na maandiko kubatiza watoto wachanga. Hapa kuna kiwango kikubwa cha “makisio” lakini sio “dokezo.” Kuhusiana na hili hebu ieleweke kwamba sio lazima kuzungumza juu ya ufahamu “wa lazima.” Kama ni “dokezo” basi ni “lazima.” Na kama si “lazima” basi sio dokezo. Mantiki ni “sayansi ya kufikia dokezo halali.” Pale ambapo tendo, ukweli, au fundisho LINADAI taarifa za Kibiblia bila kutajwa kwa umahususi, hivyo hilo tendo, huo ukweli, au hilo fundisho ni suala la KUMAANISHA. Kwa mfano, nimepewa mamlaka kufundisha kwamba baada ya Sauli wa Taso kuwa Mkristo, aliungama dhambi zake. Lakini hatuna tamko la wazi linaloonyesha kwamba aliungama dhambi zake. Tunajenga hoja kama ifuatavyo: Ikiwa (A) ni kweli kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa Mkristo bila kuungama dhambi zake; na ikiwa (B) ni kweli kwamba Sauli wa Taso alikuwa Mkristo; hivyo, (C) ni kweli kwamba Sauli wa Taso, alipotaka kuwa Mkristo, aliungama dhambi zake. Tunakubaliana na (A) na tunaweza kutoa uthibitisho, Tunakubaliana na (B) na tunaweza kutoa uthibitisho. Hii inaweza kutupatia ukweli tunapounganisha (A) na (B). Kwa hiyo, (C) – ni kweli kwamba Sauli wa Taso, alipotaka kuwa Mkristo, aliungama dhambi zake. Lakini ukweli huu hufundishwa kwa KUDOKEZWA, sio kwa WAZI.Jiometri inapowekwa kwa WAZI ukweli kwamba “kitu chochote kizima ni jumla ya sehemu zake,” hivyo jiometri

Page 107: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 99 -

imewekwa kwa KUDOKEZA (1) kwamba kitu chochote kizima ni kikubwa kuliko sehemu zake, na (2) sehemu ya kitu chochote ni ndogo kuliko kitu kizima kinachohusiana nacho. Na hiki kinachofundishwa hapa kwa KUDOKEZA ni cha kweli kama kitu ambacho kingefundishwa kwa WAZI. Ndivyo ilivyo hata katika neno la Mungu. Katika kushughulika na “dokezo” tunashughulika na kumaanisha. Biblia inatoa mamlaka kwa KUDOKEZA.Hebu turudi tena kwenye darasa la Jiometri. Tuchukulie kwamba tunajishughulisha na umbo la kijiometri, umbo ambalo ni mraba, na upande mmoja una urefu wa inchi 6. Hebu tuangalie huu ukweli kama hoja tofauti. (A) tunajishughulisha na umbo la kijiometri. (B) Umbo hili ni mraba. (C) Upande mmoja wa umbo hili ni inchi 6. Kwa kuwa tunaelewa haya mambo matatu, tunajua mambo gani mengine KWA SABABU TUNAJUA HAYA MAMBO MATATU? Au, swali hilo hilo kwa namna tofauti, “Ni nini maana ya haya mambo matatu?” Ni vitu gani VINADOKEZWA na SENTENSI VIUNGO zilizoundwa na VIUNGO (A) na (B) na (C)? Tunajua (D) kwamba kuna pande zingine tatu ambazo kila upande una inchi sita. Tunajua (E) mzingo wa umbo hili ni inchi ishirini na nne. Tunajua (F) eneo la umbo hili ni inchi za mraba sitini na sita. Na tunajua (G) kwamba kuna pembe mraba nne katika umbo hili. SENTENSI VIUNGO zilizoundwa na VIUNGO A na B na C humaanisha (D) na (E) na (F) na (G). Hiki ni kielelezo cha MDOKEZO. Kwamba kile tunachofahamu kwa MDOKEZO kinakuwa ni kweli, chenye mamlaka kama kilivyo tunachofahamu kwa WAZI. (katika hali hii ni kile tulichopewa)

Page 108: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 100 -

XVII. MAMLAKA YAMETHIBITISHWA KWA KAULI YA MOJA KWA MOJASio sahihi kabisa kwa mtu kusema: “Mfano uliothibitishwa, ufahamu wa lazima, na amri.” Tatizo langu lipo kwenye neno “amri.” Haitoshi kukidhi hali nzima. Badala yake, “amri” ni sehemu ya eneo kubwa la kujifunza ambapo katika kujifunza hilo, hapa tunatumia maneno ya “kauli ya moja kwa moja.”Katika suala la kujifunza mamlaka ya Biblia ni muhimu sana kuweka msisitizo katika eneo la “kauli ya moja kwa moja.” Baadhi ya kauli za moja kwa moja ni amri, lakini kauli nyingi za moja kwa moja sio amri. Hizi kauli za moja kwa moja zinaweza kuainishwa katika msingi wa HALI, na katika msingi wa ASILI ZAKE. Uainisho huu haukufanywa bila hoja ya msingi, bali umefanywa kwa msingi wa Agano Jipya la Kiyunani. Ni suala tu la kutambua kile tulichonacho katika Agano Jipya la Kiyunani. Sarufi ya Agano Jipya la Kiyunani ina hali nne: hali ya kuarifu, hali ya kuamuru, dhamira tegemezi na hali ya uchaguzi. Kimsingi hali humaanisha: uhusiano wa TENDO unaoneshwa na kitenzi katika ulimwengu wa UHALISIA. Kama tendo ni HALISI basi hali ni ya kuarifu. Kama tendo ni UWEZEKANO WA KUTOKEA, basi hali ama ni ya kuamuru, au dhamira tegemezi, au ya uchaguzi. Kauli katika hali ya KUARIFU inaweza kuwa: (1) katika hali ya kutangaza, kama katika Marko 16:16; au (2) ya kuuliza, kama ilivyo katika Warumi 6:1. Kauli katika DHAMIRA TEGEMEZI inaweza kuwa (1) ya kuonya,

Page 109: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 101 -

kama ilivyo katika Waebrania 6:1; (2) masharti, kama ilivyo katika Wakolosai 3:1 (kuna aina mbalimbali za masharti); (3) makatazo, (4) ya kufanya shauri, au (5)hitimisho. Kauli katika hali ya KUAMURU inaweza kuwa: (1) lazima (amri), kama ilivyo katika matendo 16:31; (2) lazima-ya kuruhusu, kama ilivyo katika Matendo 2:38; au (3) makatazo. Kauli katika hali ya UCHAGUZI huonesha matakwa au matamanio, kama ilivyo katika Warumi 6:2 (“Mungu amekataza,” kwa kawaida: haiwezi kuwa hivyo!). Kauli hii katika hali ya uchaguzi inanipa mamlaka ya kufundisha kwamba hatutakiwi kufundisha kwamba tunatakiwa kuendelea katika dhambi ili neema izidi.Hii hutupatia kauli saba tofauti. Kauli ya “lazima” (amri) ni MOJA tu kati ya hizi KUMI NA MOJA. Kwa hiyo, neno “amri” huhusiana na eneo ambamo kuna aina tofauti KUMI NA MOJA za matamko, kwa hiyo linakuwa ni tamko moja tu kati ya MATAMKO KUMI NA MOJA! Sina haki ya kupuuzia haya kumi na moja mengine.Ni kweli kwamba kuna “matamko ya moja kwa moja” mengine mengi kwenye Biblia ambayo hatuyaangalii ili kuthibitisha mamlaka ya Biblia kuhusiana na wajibu wetu. Lakini, ukweli unabaki kwamba, kuna matamko ya moja kwa moja yanayoweka mamlaka ya Biblia. Ni dhahiri kwamba sijaruhusiwa kufundisha kuwa mtu ambaye Bwana alimponya, alizaliwa na dhambi, eti kwa sababu, Wayahudi walisema hivyo (Yohana 9:34).

Page 110: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 102 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka yanathibitiswa na_____________.

2. “Dokezo” huhusiana na nini?

3. Kila kitu ambacho Biblia inafundisha, hufundisha ama kwa ____________ au kwa___________.

4. Tunajihusisha na kufikiri ______________ kwa kuzingatia kile ambacho Mungu ___________ katika kauli zake za wazi.

5. Mamlaka yaliyomo kwenye kile ambacho KINAMAANISHWA katika kauli za Mungu za WAZI yamejikita katika ukweli gani?

6. Jadili na fafanua tofauti kati ya “dokezo” na “makisio.”

7. Mantiki ni nini?

8. Je nimeruhusiwa kufundisha kuwa Paulo wa Taso aliungama dhambi zake pale alipotaka kuwa Mkristo?

9. Toa hoja zilizojengwa hapa kwa kumbukumbu zako.

10. Kuungama kwa Sauli ni suala la nini?

Page 111: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 103 -

11. Usemi “Kitu kizima chochote kile ni jumla ya sehemu zake,” hutuambia kitu kingine kipi kwa KUDOKEZA?

12. TUNAJUA nini kutokana na sababu kwamba TUNAJUA kuwa tunajishughulisha na umbo la kijiometri, ambalo ni mraba, ambalo kila upande ni inchi 6?

13. Mamlaka huthibitishwa na _____________.

14. Kwa muktadha huu, neno “amri” linajitosheleza kukidhi hali yote?

15. “Amri” ni sehemu ya eneo kubwa la kujifunza tunaloliitaji?

16. “Matamko ya moja kwa moja” yameainishwa katika msingi gani?

17. Uainisho huu hufanywa kwa kuzingatia nini?

18. Sarufi ya Agano Jipya la Kiyunani ina hali nne. Ni zipi hizo?

19. Maana ya msingi ya HALI ni nini?

20. Tendo lina weza kuwa _________ au ni _______.

21. Ikiwa tendo ni HALISI, hivyo hali ni nini?

Page 112: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 104 -

22. Ikiwa tendo lina UWEZEKANO WA KUTOKEA, hivyo HALI inaweza kuwa nini?

23. Kauli katika HALI YA KUARIFU inaweza kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

24. Kauli katika DHAMIRA TEGEMEZI inaweza kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

25. Kauli katika HALI YA KUAMURU inaweza kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

26. Kauli katika HALI YA UCHAGUZI inaweza kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

27. Hii inatupatia jumla ya aina ngapi za kauli?

28. Kauli ya “lazima” (amri) ni nini?

29. Kwa hiyo, neno “amri” ni kauli moja tu kati ya kauli ngapi?

30. Tafadhali rejea tena “kauli ya moja kwa moja – ilivyoainishwa kama HALI, na kama ASILI.”

Page 113: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 105 -

SOMO LA KUMI NA MBILI

XVIII.MAMLAKAYABIBLIA

YAMETHIBITISHWAKWAKUFANYAJAMBO

LINALOFAA

12

Page 114: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 106 -

Katika kutekeleza majukumu yetu kuna eneo la kufanya jambo linalofaa. Kila jukumu ambalo Mungu ameshawahi kutoa, limehusisha kufanya

jambo linalofaa. Kwa kuhusianisha na majukumu ambayo Mungu alishawahi kutoa, inawezekana kweli kabisa (kuhusiana na kutekeleza majukumu) Mungu alisema NAMNA ya kuyatekeleza, na hapo hapo HAKUSEMA NAMNA ya kuyatekeleza.Jambo linalofaa huhusisha hekima za kibinadamu. Ikiwa Mungu anaainisha Majukumu, lakini hajatoa maelekezo ya namna ya kuyatekeleza, basi tumeruhusiwa kuhusisha hekima za kibinadamu. Katika majukumu ya kuongoza washiriki, wazee wa kanisa ndio wenye mamlaka katika eneo la kufanya jambo linalofaa.Manufaa binafsi ni yale ambayo yanahimiza. Hakuna manufaa binafsi pale ambapo hakuna faida. Ndivyo ilivyo katika majukumu ya kanisa la mahali, jambo lenye manufaa ni lile ambalo linaendana na maandiko, ambalo lina faida ya asili, na ambalo linaweza kuchaguliwa na wazee wa kanisa katika kutekeleza jukumu lolote lile la kanisa – jukumu hilo ni lazima liwe limetokana na mifano iliyothibitishwa, kwa mdokezo, au kauli ya moja kwa moja.Inatakiwa pia tuelewe kwamba HAKUNA MANUFAA BINAFSI pale ambapo HAKUNA JUKUMU. Sina nia ya kulithibitisha hili kwa hiyo kwa haraka haraka tutaita “jambo la manufaa.” Kushindwa kutambua na kuuheshimu ukweli huu, kulitengeneza matatizo makubwa katika Harakati za mwanzo za Urejeshwaji.

Page 115: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 107 -

Pia inatakiwa isisitizwe kuwa tunapothibitisha kwamba kitu fulani ni cha manufaa – kulingana na fasili ya Biblia ya manufaa – kwa hiyo tunakuwa tunathibitisha kwamba hicho kitu kina mamlaka matakatifu, na kwa hiyo linakuwa ni suala la imani, kama kweli ni “jambo la manufaa,” basi linakuwa suala la imani.Pengine umakini unapaswa uwekwe kwenye suala la “mambo ya hiari” katika uhusiano wa “mambo ya manufaa.” Tofauti, kama ipo, ni nini? Katika kutekeleza majukumu tuliyopewa kuna “mambo ya hiari” na kuna “mambo ya manufaa.” Tafakari juu ya majukumu yetu kupata sehemu ya kukutania. Jukumu hili linafanya SEHEMU ya kukutania kuwa LAZIMA. Sehemu ya kukutania ni MUHIMU. Kuhusiana na sehemu ya kukutania kunaweza kuwa na uchaguzi wa aina nne: kununua jengo, kukodisha jengo, kujenga jengo, kukutana nyumbani. Jambo la manufaa linaweza kuwa ni kukodisha jengo. Katika mazingira tofauti, jambo la manufaa linaweza kuwa ni kujenga jengo. Ni wazi kwamba kitu hicho hicho kinaweza kuwa cha hiari na cha manufaa kwa wakati huo huo. Sio mambo yote ya hiari yanaweza kuwa ya manufaa, lakini mambo yote ya manufaa ni ya hiari. Lakini katika jambo la manufaa, kuna faida ya asili ndani yake.Ni lazima tuoneshe tofauti kwa ufupi kati ya “jambo la manufaa” (msaada) na “nyongeza.” Kitu chochote ambacho hakikuruhusiwa na Maandiko, lakini kinatumika, ni nyongeza. Msaada wa kweli, yaani jambo la manufaa, limeruhusiwa na maandiko.

Page 116: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 108 -

Mungu ametupatia jukumu la “enendeni.” Tunaweza kwenda kwa KUTEMBEA kwa miguu, na tunaweza KUENDESHA CHOMBO. Kutembea na kuendesha chombo ni njia mbili tofauti za kuenenda. Njia hizi zina uhusiano wa moja kwa moja na jukumu la “Enendeni”.Lakini hazihusiana. Kutembea sio msaada – sio jambo la manufaa, na kuendesha sio jambo la manufaa kwa kutembea. Fimbo ya kutembelea, inahusiana na kutembea, inaweza kuwa ni jambo la manufaa, ni msaada. Ni sawa na suala la utambuzi, tunatambua kwa KUSIKIA na tunatambua kwa KUTAZAMA. Kusikia sio jambo la manufaa kwa kuona, na kuona sio jambo la manufaa kwa kusikia. Hizi ni njia mbili tofauti za utambuzi. Hivi ni “viungo.” Miwani ya macho inaweza kuwa ni jambo la manufaa (msaada) kwa kuona, na kifaa cha kusikilizia kinaweza kuwa jambo la manufaa (msaada) kwa kusikia.Kwa suala la kufanya muziki – hii inaweza kufanyika kwa kuimba; inaweza kufanyika kwa kutumia ala za muziki. Kuimba na kupiga ala za muziki kuna uhusiano. Iwe ni kuimba au kupiga ala za muziki, kimoja kinaweza kufanyika bila kingine. Kuimba sio msaada kwa kupiga ala za muziki, na kupiga ala za muziki sio msaada kwa kuimba. Kitabu cha nyimbo ni msaada kwa kuimba. Kuwa na mtu anayeongoza watu kuimba ni “msaada” na jambo la manufaa. Tunapotumia kitabu cha nyimbo katika kuimba, tunakuwa TUNAIMBA TU. HATUIMBI NA KUFANYA KITU KINGINE TOFAUTI.Matumizi ya jambo la manufaa ni mapana sana. Huu ndio msingi ambapo tunalinda (1) majengo yetu ya kanisa, (2)

Page 117: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 109 -

visima vyetu vya ubatizo, (3) mafundisho yetu katika madarasa ya Biblia, (4) shule za uimbaji, (5) vitabu vyetu vya nyimbo, (6) viongozi wetu wa nyimbo, (7) kuimba wimbo wa kualikwa, (8) kutumia vikombe vya jumuia, (9) vikapu vya kuekea changizo, (10) mtu kuongoza kundi katika maombi, (11) mbao zetu za kuandikia, (12) mfumo wa kuongea na umma (13) na kadhalika.Wapendwa fulani wameshikilia msimamo sana katika mtazamo wao juu ya suala la jambo linalofaa. Wanalitambua na kuliheshimu katika baadhi ya maeneo, lakini wanashindwa kulitambua na kuliheshimu katika maeneo mengine. Wanajua kwamba jengo la kanisa ni jambo la manufaa, ni jukumu walilopewa kulijenga, lakini wanashindwa kutambua kuwa darasa la Biblia ni jambo la manufaa, linalohusiana na jukumu la kujifunza, kukua, kulisha kondoo na kuwatii wazee. Wanakubali kwamba shule ya kuimba ni jambo la manufaa, linalohusiana na jukumu la kuimba, lakini wanashindwa kutambua kwamba darasa la Biblia ni jambo la manufaa linalohusiana na jukumu la kufundisha. L.W. Hayhurst alipoacha msimamo wa kupinga-Jumapili alisema: “Nimeamua kwamba nitakapojenga jengo la kanisa nitafanya kitu kile kile kwa kuzingatia kanuni wanazozifuata pale wanapokuwa na darasa la Biblia. Nitawezaje kufanya kitu kile kile wanachofanya wao, halafu kuwahukumu kwa kile wanachofanya? ”Ni kanuni ya msingi ya kufasili Biblia kwamba kama na wakati ambapo Mungu ameainisha NAMNA ya kutekeleza jukumu lolote lile, hiyo NAMNA inakuwa

Page 118: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 110 -

ni ya lazima kama lilivyo jukumu lenyewe; lakini kama na wakati Mungu HAONYESHI NAMNA, basi njia na mbinu huachwa chini ya hekima za kibinadamu, katika suala la kufanya jambo lenye manufaa .

CHATI YA MAMLAKA !

!

"#$%#!&#'(&'$')&*!+,*!!

-."'/*$0!

1.+#(0+23*!

4.!+*#5'!6*!"07*!+,*!"07*!

8.!7*"90!5*!"*$#/**!!

&*5'!

-.!6:!;<:=>?<!

1.!(@:A>=:!BCDCACE>!

4.!6:!;<:A<=<!

8.!6:!<F@:D<E>!

*)'5'! -.!+<B:GD:E:!

1.!+<<H>E:!

4.!+<IGJ:!

8.!":K@:=B>!

L.!+:B:EI!

M.!"N>K@I!

O.!6:!+<?:GJ:!K@:<=>!

P.!+:B:EI!

Q.!5:E>A:!

-R.!5:E>A:S>G:JI=<@<K<!

--.!":B:A:G>I!

Page 119: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 111 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa na nini?

2. Kwa kuhusianisha kila jukumu ambalo Mungu alishawahi kutoa kwa mwanadamu, kuna eneo la ____.

3. “ Jambo la Manufaa ” linahusisha nini cha lazima?

4. Kuhusiana na jukumu la washiriki, ni nani ambaye anafanyaka kazi katika eneo la jambo la manufaa – mwenye mamlaka ya kufanya na kutekeleza maamuzi?

5. “Jambo la Manufaa ” ni yale ambayo _________. Hakuna “ jambo la manufaa ” pale pasipo na ________.

6. Jifunze kwa makini fasili ya “ jambo la manufaa ” (kwa kuhusianisha na kanisa la mahali pamoja).

7. Inatakiwa tuzingatie hoja gani muhimu (kuhusiana na jambo la manufaa)?

Page 120: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 112 -

8. Tunapothibitisha kwamba kitu fulani kweli ni cha “manufaa” kwa wakati huo huo tunakuwa tunathibitisha nini?

9. Je kuna tofauti kati ya “mambo ya hiari” na “mambo ya manufaa?”

10. Tafadhali fafanua, “Sio mambo yote ya hiari ni ya manufaa, lakini mambo yote ya manufaa ni ya hiari.”

11. Lakini katika mambo ya manufaa kuna kitu gani cha asili?

12. Msaada wa kweli (jambo la manufaa) _________ na Maandiko.

13. Kitu chochote ambacho HAKIJAIDHINISHWA na Maandiko, lakini ambacho kinatumika, ni nini?

14. Jadili: kwenda, kutembea, kuendesha, na fimbo ya kutembelea.

Page 121: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 113 -

15. Jadili: utambuzi, kusikia, kutazama, miwani ya macho, na vifaa vya kusikilizia.

16. “Kutengeneza muziki” kunaweza kufanywa kwa kutumia nini?

17. Kuimba na kupiga ala za muziki ni njia mbili tofauti za kufanya nini?

18. Kuimba sio ___________ kwa kupiga vyombo vya muziki, na kupiga vyombo vya muziki sio ____________ kwa kuimba.

19. Kitabu cha nyimbo (kinapotumika katika ibada yetu) ni nini?

20. Kwa kiwango ambacho Mungu anaainisha NAMNA ya kufanya jambo, hali inakuwaje?

21. Ikiwa Mungu anatoa jukumu lakini HAAINISHI NAMNA ya kuyafanya, hali inakuwaje?

Page 122: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 114 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 123: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 115 -

SOMO LA KUMI NA TATU

XIX.JEMAMLAKAINAAMULIWANA

KAMUSI?

13

Page 124: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 116 -

SWALI “Mamlaka ya Biblia inaweza kuamuliwa kwa kutumia kamusi? Ninaambatisha makala kwa ajili ya jarida, nikiomba kwamba uipitie, kama inawezekana, na iwe mapema kadri iwezekanavyo.”

JIBUMbele yangu nina makala ya jarida la Kanisa, nikiombwa kwamba niweze kuipitia. Kwa kutambua (1) umuhimu wa mada ambayo makala inaishughulikia, na (2) hatari iliyopo katika mtazamo ulioonyeshwa na mapendekezo yaliyofanywa, ninaendelea kuvuta umakini kwenye makala hii. Nitanukuu kila aya ya makala, na nitatoa maoni muafaka.

AYA YA KWANZAInaonekana siku hizi kuna maandishi mengi sana kuhusiana na suala la Mamlaka ya Biblia kwa ajili ya desturi ndani ya kanisa. Kwa kuwa ni vizuri kwamba wengi wanapenda kufanya yale ambayo ni sahihi machoni pa Mungu, suala la “mamlaka” siku zote huwa haliko wazi sana.1. Ndio mengi yameandikwa kuhusiana na mamlaka

ya Biblia. Kuna wapendwa wengi wenye uwezo, waaminifu, wanaojituma, waliojitolea ambao wamedhamiria kushikilia “mstari wa ukweli” na kupinga makosa yote. Hawa wanaonesha na kusisitiza kile ambacho Biblia inasema kuhusiana na mamlaka ya Biblia (na kuhusiana na mada yoyote ile ya Biblia). Kwa upande mwingine kuna wengine wanaoandika

Page 125: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 117 -

kutokana na mtazamo kwamba “Wala haijalishi…sio ya muhimu sana hata hivyo.” Baadhi (kimsingi ni wengi) wanasisitiza dhana kwamba sio lazima kuwa na mamlaka ya Biblia kwa kile tunachofanya na tunachosema katika suala la kidini.Baadhi wanajaribu hata “kuthibitisha” kwa kutumia Maaandiko kwamba Mungu wala hahitaji tuwe na mamlaka ya Biblia kwa kila kitu. Na wengine wanasema kwamba mamlaka ya Biblia inaweza kuthibitishwa kwa misingi kwamba “Biblia haisemi kitu chochote”! Angalia kwa makini hoja ya ajabu na inayojipinga yenyewe kwamba Biblia inatoa mamlaka kwa kutokuwepo kwa mamlaka ya Biblia!

2. Sio tu ni “vizuri” kwa sisi kufanya yale yanayopendeza machoni pa Mungu; ni LAZIMA KABISA kama tunataka kumpendeza Mungu katika maisha haya, na kuishi pamoja naye milele, pale ambapo maisha haya

kama jambo halijaruhusiwa na neno la Mungu, basi halitampendeza Mungu (Waebrania 11:6).

3. Mtunzi wa makala anasema: “…suala la ‘mamlaka’ siku zote huwa haliko wazi sana”. Hili sikubaliani nalo kabisa. Ikiwa suala la mamlaka ya Biblia haliko wazi, basi hakuna kitu kwenye Biblia ambacho kipo wazi. Siku moja, nilipokuwa nikimfanyia usaili mtu mmoja kwa ajili ya kuajiriwa katika chuo cha Kikristo, nilimuuliza swali kuhusiana na matumizi ya ala za muziki katika ibada ya Kikristo: “Uko tayari kutambua na kukubali kwamba hakuna mamlaka

Page 126: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 118 -

ya Biblia kwa ajili ya hilo?” Akajibu: “Ndugu Deaver, sina uhakika na jinsi ambavyo Mungu anatoa Mamlaka.” Jibu langu kwake: “Kama ndio hivyo kwa kweli hatuwezi tukakuajiri, kwa sababu kutokana na hivyo, huwezi kuwa na uhakika na KITU CHOCHOTE!”. Kama “suala la mamlaka” haliko wazi akilini mwa mwandishi wa makala haya, basi hana uhakika kabisa kuhusiana na (1) namna ambavyo mtu anakuwa Mkristo, (2) namna ambavyo mtu humwabudu Mungu kwa kukubaliwa, au (3) majukumu yetu, wajibu wetu na matumaini yetu kama Wakristo. Katika mazingira haya anaiweka roho yake hatarini, na pia anaweka hatarini roho za wale wanaosikiliza kile anachofundisha. Mwanafunzi wa Biblia haachi kujifunza hadi pale atakapoelewa namna ambavyo Mungu hutoa mamlaka. Na pale ambapo hili limewekwa sawa kulingana na Maandiko, linakuwa limewekwa sawa daima – kama ilivyo katika Marko 16:16.

4. Tunasisitiza tena kwamba kanuni ya msingi ya Biblia ni rahisi, na iko wazi kwa mtu yeyote na watu wote wanaotamani kwa dhati kufahamu suala hili. Wakolosai 3:17 inaunganisha: “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.” “Katika jina la Bwana” humaanisha “kwa mamlaka ya Bwana” (yaani, kama Mungu alivyotoa mamlaka [Matendo 4:7-10]). Tumepewa jukumu (na fursa) la “kutembea kwa imani” (2 Wakorintho 5:7). Kipimo kitakatifu cha kiroho ambacho kinamwongoza Mkristo

Page 127: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 119 -

(na ambacho kwacho watu wote wanaojali majukumu wanatiishwa) ni kipimo cha imani. Paulo anasema: “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo ” (Warumi 10:17). Ikiwa imani huja kwa kusikia neno la Mungu, ni wazi kwamba pale ambapo hakuna neno la Mungu basi, HAPAWEZI KUWA NA IMANI! Na, kumbukumbu zinaonyesha kwamba bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6). Kuna maandiko mengi yanayofafanua kwamba MUNGU HAVUMILII MATENDO AMBAYO HAYAJARUHUSIWA AU MAFUNDISHO AMBAYO HAYAJARUHUSIWA.

5. Ni dhahiri kwamba hatuna muda au nafasi ya kujadili kwa kina suala la NAMNA MUNGU ANAVYOTOA MAMLAKA, lakini sisi sote tunaweza kujikumbusha mstari. (1) Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa kwa “mfano.” Tunatakiwa tujifunze kwa makini (na kujifunza kujibu) swali muhimu: Ni wakati gani ambapo tendo huhusisha mfano? (2) Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa kwa kudokeza. Hii inahusisha kufikiri kwetu kwa usahihi, kwa kile Mungu alichomaanisha kwa kauli yake ya wazi. (3) Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa kwa kauli ya moja kwa moja. Nimeruhusiwa kufundisha kuwa mtu anatakiwa abatizwe ili aweze kuokolewa, kutokana na tamko la moja kwa moja katika Marko 16:16. (4) Mungu hutoa mamlaka kwa “ kufanya jambo la manufaa .” Kila jukumu ambalo Mungu alishawahi kutoa huhusisha eneo la manufaa binafsi. Lakini ikiwa “jambo la

Page 128: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 120 -

manufaa” (kulingana na fasili ya kimaandiko ya “jambo lenye manufaa”), basi limeruhusiwa na linatokana na suala la imani.Narudia kusisitiza kwamba huu ni uainisho tu. Sikusema kwamba suala la Mamlaka ya Biblia ni “rahisi.” Ninacho sisitiza ni kwamba suala lenyewe lipo wazi katika Maandiko bila mjadala wowote.

AYA YA PILINeno “mamlaka” linapochunguzwa, kuna baadhi ya mambo ya kuvutia yanayoibuka kama vile; maoni, nguvu, kauli la kuhitimisha, maamuzi yaliyochukuliwa kama matokeo, ushuhuda, na ushawishi (Webster – Toleo la 7 la Wanafunzi).1. Hili tamko (na utaratibu huu) umenishitua kwa kweli!

Mwandishi wa makala hii anaona suala la Mamlaka ya Biblia “haliko wazi siku zote.” Sasa atawezaje kujaribu kufanya suala hili kuwa “wazi kabisa”? Anatafuta maana kwenye kamusi ya Kiingereza! Utataka kujua iwapo “kunyunyiziwa maji” ni “ubatizo.” Utafanya nini? Utatafuta kwenye kamusi! Unataka kujua iwapo “Jumapili” ni “Sabato” au la. Utafanya nini? Utatafuta kweye kamusi! Mtu yeyote duniani anayejua kitu chochote kuhusiana na Kutambua Mamlaka ya Biblia, na ambaye anajua asili na makusudi ya kamusi, anajua kwamba huu sio utaratibu sahihi. Muundo na makusudi ya kamusi ni kuniambia jinsi ambavyo neno limekua likitumiwa wakati ambapo kamusi ilikuwa ikiandaliwa. Na kusudi hili linaweza kuwa msaada

Page 129: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 121 -

mkubwa sana katika kujifunza kwangu Biblia. Lakini, ukweli unabaki kwamba matumizi ya sasa ya neno hili (au hata historia ya matumizi yake) hakuhakikishi kwamba hivi ndivyo hili neno linatumika kwenye Biblia. Sio sahihi kwa taratibu za kimaandiko, kujaribu kutafuta maana yake kwenye kamusi. Kimsingi, kwa kuzingatia uzito wenyewe wa mada inayojadiliwa, kuangalia maana kwenye kamusi, kunaonesha jinsi gani mwandishi wa makala haya alivyolichukulia suala hili kirahisi. Ni mwangalifu katika kuchagua maneno fulani anayokubaliana nayo, lakini hatuambii kamusi inasema nini. Anaonekana kuyaonesha maneno hayo kama “maoni,” “nguvu,” “kauli zenye kuhitimisha,” “maamuzi yaliyochukuliwa kama matokeo,” “ushuhuda,” na “ushawishi wa Kibiblia” yanaweza kuwa sawa katika maana na “mamlaka ya Biblia.” Hebu piga picha: majukumu yaliyotolewa na Mungu yapewe mamlaka na “maoni ya Biblia?” au na “ushawishi wa Biblia?”

AYA YA TATUEndapo tutatumia hayo maneno hapo juu na kuyahusianisha na Biblia, tunapata virai kama, Maoni ya Kibiblia, tamko la hitimisho la Kibiblia, maamuzi ya Kibiblia, ushuhuda wa Kibiblia, na ushawishi wa Kibiblia.1. Ndio, inaweza kuwa rahisi kufuata kamusi na kuja

na maneno haya. Lakini kwa namna gani katika Dunia ya Mungu inaweza kuthibitishwa kwamba haya maneno (Maoni ya Kibiblia, tamko la hitimisho

Page 130: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 122 -

la Kibiblia, maamuzi ya Kibiblia, ushuhuda wa Kibiblia, na ushawishi wa Kibiblia.) yana maana zaidi (yako wazi) zaidi ya neno “mamlaka ya Biblia?” Ninafahamu maana ya swali hili “Je Biblia inaipatia mamlaka?” lakini maneno “maoni ya Kibiblia,” “tamko la hitimisho la Kibiblia,” kiasi fulani hayatoi maana halisi. Ni kwa jinsi gani desturi na tamaduni zipewe mamlaka na “maoni ya Kibiblia?” Ni kwa jinsi gani desturi na tamaduni zipewe mamlaka na “ushawishi wa Kibiblia?”

2. Mara ya kwanza nilipoona makala hii niliyoipitia, niligundua papo hapo kwamba ni Mradi wa Tulsa na fikra za Walegezaji. Mpaka sasa bado nafikiri hivyo. Mtu yuko tayari kuweka dhana kuwa kuna viwango tofauti vya mamlaka ya Biblia – kama “U” kubwa (U)shirika na “u” ndogo (u)shirika. Tutarajie kuona kitu kuhusu (1) mamlaka kwa misingi ya maoni ya Biblia (2) mamlaka kwa misingi ya tamko la hitimisho la Kibiblia, (3) mamlaka kwa misingi ya maamuzi ya Kibiblia, (4) mamlaka kutokana misingi ya ushuhuda wa Kibiblia, (5) mamlaka kwa misingi ya ushawishi wa Kibiblia. Kutakuwa na viwango tofauti vya umuhimu kuhusiana na mada hii inayojadiliwa, lakini kunaweza kusiwe na SABABU ambayo itasababisha KUMFUKUZA MTU USHIRIKA! Lakini, ukweli wenye nguvu na wa wazi usioweza kubadilika ni ama kitu kimepewa mamlaka na Biblia au hakikupewa mamlaka na Biblia, na kama hakikuidhinishwa na Biblia halafu tunakifundisha, tunakuwa TUNAFANYA DHAMBI.

Page 131: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 123 -

AYA YA NNEKwa upande wangu, hivi virai ni rahisi sana kuvifanyia kazi kuliko “Mamlaka ya Biblia” kwa sababu vinaeleweka kwa wazi. Sasa ninapokuwa ninauliza juu ya desturi, ninaweza kuuliza, “Je hayo ni maoni ya Kibiblia?” au “Kuna ushawishi wa Kibiblia kwa ajili ya hiyo desturi?” au “Kuna tamko la hitimisho la Kibiblia?” au “Kuna ushuhuda wa Kibiblia?” au “Maoni ya Biblia ni nini?”1. Mimi naona utaratibu wa hapo juu ni hatari sana, upo

nje kabisa ya hoja, na haukamilishi kitu chochote kile. “Maamuzi ya Kibiblia humaanisha nini?” Mwandishi anatumia maneno haya kumaanisha “Mamlaka ya Biblia.” Kwa hiyo, bado ana tatizo la “Ni kwa namna gani Biblia hutoa mamlaka?” Ni kwa namna gani Biblia inaweka “Maamuzi ya Kibiblia?” Kama anajaribu kutafuta kujua “Maoni ya Biblia” ili aweze kujua mamlaka, bado anatakiwa kushughulika na suala la “Ni kwa jinsi gani Biblia hutoa mamlaka?” Badala ya kufafanua, ukungu unakuwa mwingi kiasi kwamba mwandishi hawezi kuona swali halisi!

2. Kwa nini asiulize tu, “Je Biblia imeidhinisha?” Au, tunaweza kufundisha hili “katika jina la Bwana?” Je, Bwana kupitia neno lake anaidhinisha hii desturi au hili fundisho? Halafu, anaweza kwenda kwa umahususi zaidi na kuuliza: (1) Je, hili limeidhinishwa kwa mifano iliyothibitishwa? (2) je, hili limeidhinishwa kwa “mdokezo?” (3) je, limeidhinishwa kwa “kauli ya moja kwa moja?” (4) je, limeruhusiwa kama

Page 132: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 124 -

3. Ningependa kukoleza wino kwenye kile ambacho mwandishi anaweza kuwa nacho akilini, anapotafakari dhana kwamba KITU FULANI kinaweza kuidhinishwa kwa misingi ya “ushawishi wa Kibiblia” au “Maoni ya Biblia.”

AYA YA TANOVipengele hivi mbalimbali vinafanya iwe rahisi kutafuta majibu ya maswali yangu. Kwa nini? Kwa sababu kunavunja hisia zangu binafsi juu ya neno “mamlaka.” Fasili ya mamlaka ni pana sana kiasi kwamba inaacha maeneo mengi sana ili akili yangu ijaze “nafasi zilizoachwa wazi” kadri inavyokidhi matakwa yangu.1. Kwa miaka mingi nimekuwa nikipata fursa ya

kufundisha (sehemu ya kozi katika Mantiki) “Falsafa ya Lugha.” Sehemu muhimu kabisa katika kozi hii ni kipengele ambacho tunashughulika nacho “utata.” Tunasoma “utata” sio kwa kujifunza jinsi ya kuutengeneza, bali ni kuugundua na kutambua aina ya utata uliopo kwenye maandishi, hii yote ni kwa sababu

kwamba utata ni ushahidi wa kuelewa sana, lakini hiyo sio sababu kabisa. Ni jukumu la msemaji (sawa na jukumu la mwandishi) kujitahidi ili aeleweke.

2. Aya hiyo hapo juu ni kielelezo kikubwa sana cha utata. Ni dhahiri kwamba mwandishi anajaribu kusema kitu fulani bila kukisema. “Muda mwingine kusema

“jambo lenye manufaa?” Ikiwa jibu la maswali haya ni hapana, basi HALIJAIDHINISHWA NA BIBLIA.

Page 133: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 125 -

waziwazi ndio kueleweka.” Anamaanisha nini kusema hisia zangu binafsi juu ya neno “mamlaka.” Je, hii ndio hisia binafsi? Au ni kinyume chake? Je ni majivuno kutumia hata neno “mamlaka?” Ina maana gani kusema “fasili ya mamlaka ni pana sana…?” Je hivi ni vizuri? au vibaya? Nilidhani mwandishi ameshasistiza kwamba kwa “kusoma” amekuja na “fasili” ambayo anaikubali, na kwa hiyo angeanza kushughulika na fasili mpya. Anamaanisha nini anaposema “…inaacha maeneo mengi sana ili akili yangu ijaze “nafasi zilizoachwa wazi” kadri inavyokidhi matakwa yangu?” Kwa hili kunakuwa na

3. Zingatia kwa makini anaposema “makundi vya mamlaka.” Hili linathibitisha kile nilichokisema hapo awali kwamba “Mtu tayari amejenga dhana kuna viwango tofauti vya mamlaka ya Biblia.” Mamlaka ya Biblia ni Mamlaka ya Biblia- rahisi, wazi, imajitosheleza na inaleta maana. Hakuna “vipengele” vya mamlaka ya Biblia (kama ambavyo mwandishi wa makala haya anavyotumia hili neno). Hakuna viwango mbalimbali vya mamlaka ya Biblia.

AYA YA SITAKwa kulizingatia hili, sasa ninaamini kwamba nina nyenzo bora ya kuchunguza maandiko kwa ajili ya maelekezo ya Mungu kwa ajili ya matendo yangu na imani. Mungu atubariki sote kadri tunavyojitahidi kufanya mapenzi yake siku zote.

Page 134: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 126 -

1. Aya hii inaonyesha hamasa nzuri kwa ajili ya kusoma, kujifunza, na kulielewa neno la Mungu. Angalau inaonyesha umuhimu wa kusoma na kujifunza neno la Mungu. Ninaamini na ninaomba kwa bidii ili kwamba mwandishi kwa uaminifu kabisa, atake kufanye kile ambacho ni sahihi, kwamba atake kufanya kile tu ambacho kina mamlaka ya Biblia.

2. Ngoja nisistize tu ninapomalizia haya maandishi kwamba simfahamu mwandishi wa makala hii. Wala jina lake halikuoneshwa. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba, maoni haya sio jitihada zangu binafsi kutoa hukumu au hata kuhoji nia ya mtu husika ninayemfahamu. Mimi najishughulisha na makala yenyewe, na ushawishi inayowezakuwa nayo kwenye eneo inamotoka. Ni makala ya hatari sana. Pia, ninashawishika kuhusika na mtua aliyeandika makala hii, na ningependa kumsaidia kwa namna yoyote ile ambayo ningeweza.Ndugu, Mungu atusaidie kila mtu ili kutambua umuhimu wa mamlaka ya Biblia – kuelewa kwamba kila kitu tunachofanya ni lazima kifanyike “katika jina la Bwana.” Hebu tujitafakari upya kuweka msisitizo katika suala la namna ambavyo Biblia inatoa mamlaka.Ni lazima TUFIKIRI kama washauri wa Mungu (hii ni kama ambavyo Biblia inatufundisha kufikiri). Ni lazima TUZUNGUMZE kama washauri wa Mungu (zungumza kulingana na mafundisho ya Biblia). Ni lazima TUABUDU kama ambavyo Biblia inatufundisha kuabudu. Ni lazima TUTENDE na

Page 135: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 127 -

TUISHI kama ambavyo Biblia inatufundisha jinsi ya kutenda na kuishi. Na hivi vitu vinaamuliwa kwa kusoma Biblia ( zaidi hasa Agano Jipya) kwa juhudi, kwa umakini na kwa maombi. Na masuala haya yanaamuliwa na kile ambacho BIBLIA inasema na sio kile ambacho KAMUSI inasema.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 136: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 128 -

MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Swali la msingi katika somo hili ni nini?

2. Mwandishi wa “aya ya kwanza” ana mtazamo gani kuhusu Mamlaka ya Biblia?

3. Ndugu wengi wamedhamiria kufanya nini?

4. Kwenye #1 tumetaja maoni yenye makosa juu ya mamlaka ya Biblia. Maoni haya ni yapi?

5. Ni lazima tusisitize ukweli gani wa msingi?

6. Mtu ambaye “suala la mamlaka” haliko wazi, hawezi kuwa na uhakika kabisa kuhusiana na ______________, namna ambavyo ____________ Mungu kwa kukubaliwa,; au majukumu yetu, wajibu wetu na matumaini yetu kama ________.

7. Tutatakiwa tujifunze na kufahamu suala gani la msingi?

8. Umuhimu wa Wakolosai 3:17 ni nini?

9. Tunajifunza nini kutokana na Matendo 4:7-10 (kama inavyohusiana na somo hili)?

10. Tunajifunza nini kutoka 2 Wakorintho 5:7?

Page 137: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 129 -

11. Tunajifunza nini kutoka Warumi 10:17?

12. Tunajifunza nini kutoka Waebrania 11:6?

13. Mungu havumilii nini?

14. Orodhesha hoja nne zilizoorodheshwa kwenye “orodha za msingi” za mamlaka ya Biblia.

15. Mwandishi wa makala anajaribu kujifunza maana ya mamlaka ya Biblia kwa kwenda kwenye chanzo kipi?

16. Muundo na makusudi ya kamusi ni nini?

17. Inawezekana kweli desturi zetu na mitazamo yetu imeidhinishwa na “maoni ya Kibiblia?”

18. Tulisema kwamba mtu tayari amekwisha jenga dhana gani kuhusiana na mamlaka ya Kibiblia?

19. Ukweli wa wazi na wenye nguvu ni nini?

20. Mwishowe ni swali gani rahisi linaloweza kuulizwa?

21. Msemaji (au mwandishi) ana majukumu gani?

22. Mwandishi wa makala, hususa ni katika aya ya tano, anatupatia kielelezo gani chenye nguvu?

23. Inatakiwa tujitathmini upya kufanya nini?

Page 138: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 130 -

KIAMBATISHO A

WANAWAKE WAKRISTO NA POCHI NYEKUNDU

(Kutoka Wakorintho 11:2-16)Katika mafungu haya, Paulo –I. Anawasifia ndugu wa Korintho kwa uaminifu wao

kwa mambo aliyowafundisha (“Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa”). Mstari wa 2;

II. Anasisitiza juu ya uongozi ulioanzishwa na Mungu (“Lakini napenda mfahamu kwamba kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu”). Mstari wa 3;

III. Anaonesha madhara ambayo mwanaume atayapata, ikiwa ataomba au kutoa unabii mbele za watu, huku kichwa kikiwa kimefunikwa (“Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake”). Mstari wa 4;

IV. Anaonesha madhara ambayo mwanamke atayapata, ikiwa ataomba au kutoa unabii mbele za watu, huku kichwa kikiwa hakijafunikwa (“Lakini kila mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo

Page 139: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 131 -

kufunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake, kwani ni sawa na yeye aliyenyoa nywele”). mstari 5;

V. Anatoa maelekezo yenye msisitizo kwamba mwanamke anatakiwa kufunika kichwa chake (“Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake”), mstari wa 6;

VI. Anafafanua kwa nini mwanaume anatakiwa kutofunika kichwa chake na mwanamke kufunika kichwa chake (“Mwanaume haimpasi kufunika kichwa chake kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume”), mstari wa 7

VII. Anafafanua kwa kina kwa nini mwanamke ana jukumu la kuonesha utukufu wa mwanaume (“Kwa maana mwanaume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke alitoka kwa mwanaume. Wala mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume. Kwa sababu hii na kwa sababu ya malaika, mwanamke inampasa awe na ishara ya mamlaka iliyo juu yake”), mstari wa 8-10;

VIII. Anafafanua kwamba katika uhusiano wao na Bwana, katika ushirika wao na yeye, mwanaume na mwanamke wanafanana kabisa (“Lakini katika Bwana, mwanamke hajitegemei pasipo mwanaume na mwanaume hajitegemei pasipo mwanamke. Kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanaume, vivyo hivyo mwanaume huzaliwa na

Page 140: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 132 -

mwanamke. Lakini vitu vyote vyatoka kwa Mungu”), mstari wa 11, 12;

IX. Huingia akilini mwao kama jambo zuri kuthibitisha maelekezo waliyopewa (“Hukumuni ninyi wenyewe: Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu bila kufunika kichwa chake? Je, maumbile ya asili hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu? Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake. Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu ili kumfunika”), mstari wa 13-15;

X. Anasisitiza kuwa licha ya ukinzani wa mtu yeyote yule kwenda kinyume chake, desturi za wanawake kutofunika vichwa vyao, haziruhusiwi (“Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu") mstari wa 16.

Hali ya Korintho ilikuwaje?1. KUFUNDISHA. Kufundisha katika mikutano ya

kawaida ya ibada ni aina ya kufundisha ambayo inahusisha mamlaka, ikiwa ni pamoja na mamlaka kuhusu wanaume (Tito 2:15). Kuna aina ya kufundisha ambayo mwanamke Mkristo ameamriwa kufanya (Tito 2:3,4) na kuna aina ya kufundisha ambayo amekatazwa kufanya (1 Tim. 1:12). Aina ya kufundisha ambayo amekatazwa kufanya ni ile ambayo inahusisha kutekeleza mamlaka juu ya wanaume. Mamlaka au utawala huo unaweza

Page 141: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 133 -

kuhusika katika kuhutubia watu katika mkutano wa kawaida wa ibada. Kwa hiyo kakatazwa kufanya aina hii ya kufundisha.

2. KUOMBA. Kuna aina ya kuomba ambayo mwanamke mkristo ameruhusiwa kufanya (1 Wathes. 5:17). Kuna aina ya kuomba ambayo mwanamke Mkristo amekatazwa kufanya (1 Tim. 2:8). Aina ya kuomba ambayo amekatazwa kufanya ni kule ambako kungeweza kuhusisha kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Kuomba au (kuongoza maombi) katika mikutano ya kawaida ya ibada kungeweza kuhusisha mamlaka juu ya wanaume. Aina hii ya kuomba mwanamke Mkristo amekatazwa kufanya.

3. KUTOA UNABII. “Unabii” ni karama ya roho kabisa (1 Kor. 12:1, 10). Hakuna unabii bila ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu (1 Kor. 14:30). “Unabii” ulikuwa ni kipawa cha ajabu ambacho kwacho Mungu alidhihirisha matakwa yake. Huhusisha mamlaka takatifu katika kila neno kwenye Agano Jipya. Kwa kuwa “kutoa unabii” na “kuomba” huhusiana kwa karibu katika 1 Kor. 11:4, 5 na kwa kuwa unabii ni karama ya roho, inawezekana kuwa “kuomba” kunakozungumziwa hapa kulikuwa kunahusisha karama za roho za miujiza. Maombi halisi ya Wakristo wa awali yalikuwa ni kama zao la karama za roho. Kimsingi, karama za miujiza za roho pengine zilikuwa zinahusika katika kila hatua ya kazi ya Kikristo na ibada (Rum. 12:6-8)

Page 142: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 134 -

4. MIKUSANYIKO MAALUMU. Mistari ya (4,5) inaonyesha waziwazi kwamba baadhi ya wanawake kanisani huko Korintho walikuwa katika nafasi ya kufanyia kazi karama ya maombi na unabii. Lakini “unabii” ulikuwa ni karama ya roho kutoka kwa Mungu kwa ajili ya kuliadilisha kanisa (1 Kor. 14:4,22). Lakini mwanamke mkristo asingeweza kufanyia kazi karama yake ya maombi na unabii katika kusanyiko la kawaida la ibada, kwa kufanya hivyo wangekuwa wanachukua mamlaka ambayo walikatazwa kufanya. Kwa hiyo kulilazimika kuwepo kusanyiko lingine ambalo wangeweza kutumia karama zao – mikutano ya wanawake wakristo (pengine na watoto). Hawa wanawake wakristo wangeweza kujengwa kimaadili, na kwa hiyo wangechangia kujenga maadili ya kanisa zima.

5. TATIZO. Kule Korintho kulikuwa na tatizo gani (kwa kuzingatia mistari inayojadiliwa)? Baadhi ya wanawake Wakristo waliokuwa na karama ya kuomba na unabii walikuwa wanaonekana katika mikutano hii maalumu (ya wanawake na watoto) bila kufunika vichwa. Huu ungekuwa sio mfano mzuri: Huu usingekuwa ushawishi mzuri kwa wanawake wengine. Hawakuwa wamenyoa nywele zao; waliacha tu kufunika nywele zao. Kwa kuwa wanaume wasingeweza kuonekana kwenye mikutano hii, pengine kulichangia kutofunika nywele zao. Kwa kutazama hali nzima ilivyokuwa Korintho, na kwa kuangalia umuhimu wa kufunika nywele, ingekuwa ni vigumu kukubali mtazamo kwamba wanawake

Page 143: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 135 -

Wakristo wa Korintho wangeweza hata kufikiri kuacha kufunika vichwa vyao kwenye mikutano ambayo wanaume wangekuwapo. Katika Saiklopidia ya Biblia ya Toleo la Kimataifa(uk.3043) kuna maoni ya kuvutia. “Katika nyakati za ‘Agano Jipya zamani, miongoni mwa Wayunani na Warumi, wanawake wenye heshima walivaa kwa kufunika vichwa mbele ya umma, na kuonekana mbele za watu bila kufunika kichwa lilikuwa ni kosa kubwa; Taso, mji wa nyumbani wa Mtume Paulo, ni mji ambao ulikuwa una sheria kali kuhusiana na suala hili. Kwa hiyo maelekezo ya Mtume. Paulo katika 1 kor. 11:2-16, msingi wake ni utaratibu wa kijamii wa wakati huo.”

Maelekezo ya Paulo yalikuwa ni nini?Paulo alikuwa anasisitiza kwamba mwanamke Mkristo wa Korintho, hakutakiwa kuonekana mitaani au katika mikusanyiko maalumu bila kufunika kichwa. Kufunika kichwa kwa WAKATI HUO na katika ENEO HILO – Ilikuwa ni DESTURI ambayo ilikuwa ni nzuri tu. Kukiuka desturi hii kule Korintho ingeleta madhara makubwa.Paulo anasisitiza kwamba wanawake Wakristo wa Korintho, hawakutakiwa kuonekana bila kufunika vichwa vyao. Alitoa hoja tano:1. Huko kungeonyesha kushindwa kutambua na

kuheshimu ukuu -- uongozi wa mwanaume;2. Huko kungekuwa ni kushindwa kutambua na

kuheshimu ukweli halisi wa uumbaji – ukweli unaoonesha usaidizi wa mwanamke;

Page 144: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 136 -

3. Huko kungekuwa ni kushindwa kuonesha heshima inayostahili kwa malaika, waliopo katika kusanyiko la ibada ya Kikristo.

4. Huko kungekuwa ni kushindwa kutambua wa maadili yao;

5. Huko kungekuwa ni kinyume na desturi za kanisa na mafundisho mahususi ya Paulo.

Vipi kuhusu kufunika kichwa huko Korintho?Haya ndiyo makusudi matatu ya msingi ya kuvaa nguo: kujisitiri, kuwa huru, mapambo. Mtu mwenye “akili timamu” huvaa kwa staha (Marko 5:15). Mkisto hataweza kuvaa kwa makusudi, mtindo ambao utachochea tamaa kwa watu wengine. Mwanamke Mkristo atavaa kwa namna ambayo atajilinda dhidi ya macho ya tamaa ya wanaume wenye dhambi. Mkristo hatavaa kwa mtindo ambao utaleta fedheha katika kanisa la Bwana, tunavaa ili tuweze kupata joto au ubaridi, kulinda miili yetu. Kuvaa kusiwe kwa mapambo sana. Mkristo ataepuka mapambo kupita kiasi. Mara nyingi nguo huhusisha suala la ishara. Kitu fulani huvaliwa kama ishara – kuvuta umakini juu ya tukio fulani, kwa kumbukumbu ya mtu fulani au tukio, kutoa taarifa, kuonesha mtazamo fulani.Pengine sababu hizi zote zilihusishwa kwa wanawake wa Korintho kufunika vichwa katika nyakati za Paulo.Korintho ulikuwa ni mji wa anasa. Ulikuwa ni mji unaoharibu maadili. Katika mji huu kulikuwa kuna hekalu

Page 145: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 137 -

la Aphrodite Pandemos ambalo lilikuwa na wahudumu wa kike elfu moja waliojitoa katika huduma zake. Hawa hawakuwa kitu kingine bali ni Malaya. Waliweza kutambuliwa kwa wazi kwa kuonekana hadharani bila kufunika vichwa vyao. Na inatakiwa ikumbukwe kuwa adhabu ya umalaya ilikuwa ni kunyoa vichwa vyao.Kwa mwanamke Mkristo, kupita katika mitaa ya Korintho bila kufunika kichwa kungemfanya atambulike kama malaya wa kawaida wa Aphrodite Pandemos. Suala hili lingeleta aibu na fedheha kwa kanisa.Zaidi, kufunika kichwa kwa wanawake wa Korintho kunaashiria ukweli kwamba mwanamke anatambua na kuheshimu kanuni ya kujinyenyekeza kwa mwanaume. Kushindwa kufunika kichwa, kungeonesha kushindwa kutambua kanuni hii, na kungekuwa na fedheha kanisani.Mwanamke wa Korintho kufunika kichwa, kulimaanisha:1. Kwamba alikuwa anajali staha, na alitaka aangaliwe

kama mwanamke safi. Hakutaka atambuliwe kama malaya wa kawaida wa Pandemos;

2. Kwamba alitambua na aliheshimu kanuni takatifu ya kwamba mwanamke yupo chini ya mwanaume, na huu ndio uhusiano mtakatifu ulioanzishwa;

3. Kwamba alitamani kuona yuko sawa kwa haki ya asili, tamaduni zenye maana, hakutamani kuwa chukizo kwa watu wengine bila sababu ya msingi

4. Kwamba hakutaka kuleta fedheha katika kanisa la Bwana.

Page 146: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 138 -

5. Kwamba hakutaka kuwa chukizo kwa Mungu na malaika zake.

Kufunika kichwa katika mji wa Fort Worth,Texas, USA – 1969!Lakini kwa siku zetu na utamaduni wetu:

1. Wanawake kwa kawaida au kwa desturi hawafu-niki kichwa;

2. Kufunika kichwa kunaweza kusimaanishe suala la mwanamke kuwa safi na mwenye staha;

3. Kutofunika kichwa hakumtambulishi mwanamke moja kwa moja kuwa ni malaya wa kawaida;

4. Kufunika kichwa hakuwezi kumaanisha moja kwa moja kwamba mvaaji anatambua na anaheshimu kanuni ya kuwa chini ya mwanaume;

5. Kufunika kichwa kusingemaanisha moja kwa moja kwamba mvaaji hakutamani kuwa chukizo kwa wengine;

6. Kufunika kichwa kusingemaanisha kwamba mva-aji hakutaka kuleta fedheha katika kanisa la Bwa-na;

7. Kufunika kichwa kusingemaanisha kwamba mva-aji hakutaka kuwa chukizo kwa Mungu au kwa malaika zake.

Vipi kuhusu Kofia?Inatakiwa izingatiwe kwamba 1 Wakorintho 11:2-16 hujadili wanawake ambao hawakufunika vichwa vyao. Hakuna kitu kinachozungumziwa kuhusu kofia. Kabla

Page 147: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 139 -

kusudi hilo hilo lilohusishwa na utaji, linaweza

siwezi nikasema moja kwa moja kwamba ni mwanamke

anatambua na kuheshimu kanuni takatifu za kuwa

kwamba mvaaji hatamani kuwachukiza wengine kwa

kwamba mvaaji hataki kuleta fedheha katika kanisa la

chukizo kwa Mungu na malaika zake.

Je, haya maandiko hayana umuhimu kwetu?Yanayo. Kanuni takatifu zilizofundishwa hapa zinatumika sasa kama ilivyokuwa kipindi hicho ambapo Paulo aliandika haya maandiko. Tatizo ni kwamba kila mara tunakwama kwenye vielelezo na mazingira ambamo kanuni hufundishwa hadi tunashindwa kuona kanuni zenyewe, kanuni zinashurutisha, desturi hazishurutishi.Hebu tujifunze:1. Kwamba kichwa cha Kristo ni Mungu; kichwa cha

kila mwanaume ni Kristo; kichwa cha mwanamke ni mwanaume;

2. Kwa mwanaume hatakiwi kufanya kitu ambacho kitamkosea Kristo heshima; kwamba mwanaume

Page 148: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 140 -

anatakiwa siku zote kuleta heshima kwa Kristo, kwa maneno, matendo na maisha.

3. Kwamba mwanamke hatakiwi kufanya kitu chochote ambacho kitamkosea heshima mwanaume; kwamba anatakiwa kushikilia tabia ya heshima na kujishusha;

4. Ni vizuri na sahihi kuzingatia desturi ambazo ni nzuri, na kwamba hatutakiwi kuwahukumu wengine kwa kuvunja hizi desturi.

5. Kwamba hatutakiwi kuleta fedheha kanisani kwa kukiuka desturi ambazo ni nzuri;

6. Kwamba hatutakiwi kuvaa kwa mtindo ambao tutatambuliwa kama watu tusio safi;

7. Kwamba hatutakiwi kuvaa kwa mtindo ambao utaleta chukizo kwa Mungu au kwa malaika zake (waliopo wakati wa ibada).

8. Uvaaji wetu ni lazima uonyeshe suala la usafi na staha.

Kama muda utajirudia tena ambapo wanawake wasio safi wa Fort Worth wanaojitambulisha kwa kubeba pochi nyekundu kwenye mkono wao wa kulia, ningepinga vikali kwa kuzingatia 1 Wakorintho 11: 2-16 kwamba ingekuwa ni dhambi kwa mwanamke Mkristo wa eneo hilo kubeba pochi nyekundu kwenye mkono wake wa kulia.

Page 149: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 141 -

KIAMBATISHO BBARUA NAMBA MOJA

Ndugu mpendwa …..:Nimesoma barua yako, na nina furaha ya pekee kusikia kutoka kwako. Furaha – lakini pia huzuni. Nimehuzunishwa kwamba umepata kiharusi, lakini nina furaha kwamba bado unafanya kazi katika huduma ya Bwana.Ni leo hii (Katika darasa langu la Biblia katika chuo cha Biblia cha Tennesee) nilikuwa nashughulika na hoja uliyokuwa unauliza.Ndio, ulikumbuka kwa usahihi. Nilisisitiza na ninaendelea kusisitiza kwamba “amri” haibagui, na kwamba “mfano” hauweki kando. Kama amri inaweka kando basi mfano pia unaweza kuweka kando. Kama mfano hauweki kando basi amri pia haiweki.Mhubiri wa shule ya wapinga-Jumapili, amepata mfano wa kufundisha katika kusanyiko, na anasema hii ndio njia pekee inavyotakiwa kufanyika. Mhubiri mpinga-ushirikiano anaona kile anachofikiri ni mfano kwa kanisa kupeleka moja kwa moja kwa mhubiri, na anasema kwamba hii ndio njia pekee inavyoweza kufanyika (suala la uinjilisti).Kuna maswali mawili: (1) hii ndio njia pekee ambayo Mungu anatoa mamlaka kwa mfano? (2) Je mfano hubagua? Au je huidhinisha kile ambacho kimeonyeshwa kwa mfano?

Page 150: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 142 -

Nimepewa mamlaka (kwa mfano) kusafirikwa kutumia mtumbwi, lakini ni dhahiri kwamba ninaweza kusafirikwa kutumia gari. Kanisa linaweza kuchagua watu wawili kuunda njia moja ya kupeleka baraka kwa wengine, lakini kanisa linaweza pia kutumia huduma za posta kupeleka baraka kwa wengine. Matendo 11:29,30.Nimeamriwa kutoa siku ya kwanza ya kila juma. Lakini ninaamini (kwa kuzingatia Wagal. 6:10) kwamba tunaweza kutoa siku ya Jumatano usiku, kukiwa na mahitaji maalumu. Kama ndio hivyo amri haibagui. Fikiria kama Mungu angetuamuru “tuimbe” katika Waefe. 5:19 na “tutumie vyombo vya muziki” katika Wakol. 3:16, basi ingekuwa ni dhahiri kwamba “kuimba” hakukuweka kando “kutumia vyombo vya muziki.” Kimsingi katika Agano la Kale, Waisraeli waliambiwa kuimba na kutumia vyombo vya muziki. Kwa Waisraeli ambao waliamuriwa kuimba hakukuweka kando kutumia vyombo vya muziki. Mungu alipomuelekeza Nuhu kuhusiana na ujenzi wa Safina,aliainisha kwamba ilitakiwa kujengwa kwa mti wa mvinje. Je, “mvinje” uliweka kando msonobari? Mungu alipomuamuru Nuhu kutumia mti wa “mvinje”, Je, kulikuwa na umuhimu wa Mungu kumwambia Nuhu asitumiemti wa msonobari au asitumie mti wa mwembe? Hapana. Mungu hakuorodhesha aina yote ya miti Nuhu hakutakiwa kutumia. Amri iliamuru nini? Iliruhusu “mti wa mvinje” tu. Je, Nuhu angeweza kutumia msonobari? Hakika hapana. Kwa nini? Hakukuwa na mamlaka kwa ajili ya hilo.Mama anamtuma mwanawe dukani. Anamwelekeza akanunue pakiti moja ya maziwa, na mkate mmoja.

Page 151: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 143 -

Mtoto anarudi nyumbani na; (1) pakiti moja ya maziwa, (2) mkate mmoja (3) kilo moja ya maharage, (4) pipi nne (5) nusu kilo ya viazi, na (6) mfuko wa sukari.Mtoto hakuwa mtiifu kwa maelekezo aliyopewa. Mama hakusema: usinunue hiki na kile. Aliidhinisha kile kilichopaswa kununuliwa. Mtoto alinunua vitu ambavyo hakuruhusiwa kununua.Tunafundishwa kwa amri na mifano kwamba tunatakiwa kushiriki meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya kila juma. Je tunaweza kushiriki meza ya Bwana siku ya Alhamisi usiku? Hakika hapana! Kwa nini hapana! Kwa sababu HAKUNA IDHINI YA KUFANYA HIVYO. Je amri (au mfano) unaweka kando Alhamisi usiku? Hapana. Unafanya nini sasa? Huidhinisha kushiriki siku ya kwanza ya juma.Ndivyo ilivyo sawa na amri ya kuimba. Kuimba hakubagui kucheza. Kuna idhinisha kuimba. Sasa kuna ubaya gani na kucheza? Hakuna mamlaka kwa ajili ya hilo. Sababu ya kuweka kando ni ukosefu wa mamlaka.Kanuni ya msingi kabisa ya Kibiblia ni: Tunatembea kwa imani. Imani huja kwa kusikia neno la Mungu. Pale ambapo hapana neno la Mungu hakuna imani. Na bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Kanuni ya kutembea kwa imani hujumuisha kuheshimu ukimya wa Maandiko.Mungu aendelee kuwa pamoja nawe na akubariki katika huduma yake.Ni wako katika Ufalme,Roy Deaver

Page 152: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 144 -

KIAMBATISHO CBARUA NAMBA MBILI

Ndugu mpendwa …:Asante sana kwa barua yako ya Julai 25, 1975. Nimependezwa na maoni yako kuhusiana na KANUNI ZA UREJESHAJI. Nilisisitiza katika makala ambayo umerejelea kwamba “…mfano hauweki kando.” Ninaamini hili ni sahihi. Mfano unaidhinisha kile kilichotolewa mfano, lakini hivi ndivyo ninaweza kusema kuhusu hili. Mfano wenyewe hauweki kando. Mfano wa mtu kusafiri kwa kutumia mtumbwi huidhinisha mtu kusafiri kwa mtumbwi, lakini hauweki kando kusafiri kwa kutumia gari au ndege. Mfano wa kushiriki meza ya Bwana kwenye ghorofa ya tatu, hauweki kando kushiriki kwetu kwenye ghorofa ya kwanza. Mfano katika (2 Kor. 8:1-5) ambao Paulo aliutoa kwa ajili ya ndugu wa Korintho hakika unaidhinisha wapendwa wa Korintho (na sisi) kutoa zaidi ya uwezo wao. Hata hivyo hii haimaanishi kwamba tutakuwa tunafanya dhambi tukitoa kulingana na uwezo wetu (au kulingana na tulivyobarikiwa). Kwa kuzingatia meza ya Bwana, nilisema: “Hoja inayofanya iwe dhambi kushiriki meza ya Bwana Alhamisi usiku ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mamlaka kwa ajili ya hilo.” Nikaendelea kusema: “Maandiko mengi yanaonyesha wajibu wetu kuimba katika ibada ya Kikristo. Kitu kinachofanya ionekane kuwa ni dhambi

Page 153: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 145 -

kutumia ala za muziki ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mamlaka kwa ajili ya hilo. Kanuni takatifu ya kutembea kwa imani hujumuisha kuheshimu ukimya wa Maandiko.” Hakuwezi kuwepo na imani pale ambapo hakuna neno la Mungu.Kama suala ni kwamba tuna mfano wa watu wanaoshiriki meza ya Bwana katika ghorofa ya tatu, na kama suala ni kwamba tunaweza kushiriki meza ya Bwana kwenye ghorofa ya kwanza kwa mujibu wa maandiko, basi itakuwa inamaanisha kwamba (kuhusiana na sehemu) mfano hauweki kando.Kama suala ni kwamba tuna mfano wa watu waliosafiri kwa mtumbwi, na kama kimaandiko tunaweza kusafiri kwa kutumia gari – itakuwa inamaanisha kwamba mifano haibagui.Kama suala ni kwamba wapendwa wa Makedonia walitoa zaidi ya uwezo wao, na kwa mujibu wa maandiko tunaweza kutoa kulingana na uwezo wetu, basi itakuwa ina maana kuwa mfano (Paulo alinukuu kwa ajili ya wapendwa wa Korintho na sisi) haubagui.Ulisema kuwa mpingaji anaweza kuuliza swali: “Kwa kuwa Agano Jipya linaidhinisha kusafiri kwa mtumbwi, lakini haliweki kando kusafiri kwa gari, huoni kwamba kuruhusu Meza ya Bwana kufanyika siku ya kwanza ya juma, ni kuruhusu kushiriki siku ya Alhamisi usiku? Kama hatuna idhini kwa ajili ya Alhamisi usiku, tunapata wapi idhini ya kusafiri kwa gari? Kama kimoja huwekwa kando, kwa nini isiwe kingine? Nitafurahi kusikia maoni yako kuhusiana na hoja hii.”

Page 154: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 146 -

Nimependezwa sana na umakini wako katika swali hili. Ni swali zuri sana na ambalo linatakiwa kujibiwa kwa umakini.Ninaona katika maandiko wapendwa wanasafiri kwa kusudi kubwa la utume kwa kutumia mashua (Mdo. 13:4; Mdo. 27:16), na ikiwa pia nitagundua kwamba walisafiri kwa kutembea (Mdo. 18:22; Mdo, 20:13), basi ni lazima nihitimishe kuwa Bwana hakukusudia kuweka au kuidhinisha njia mahususi ya kusafiria. Ni lazima nihitimishe kuwa namna ya kusafiri imeachwa bila kuainishwa.Katika maandiko ninaona kwamba wapendwa walishiriki Meza ya Bwana kwenye ghorofa ya tatu (Mdo. 20:7-9), na kama nikikuta katika maandiko kwamba wapendwa walishiriki Meza ya Bwana katika sehemu tofauti na ghorofa ya tatu (1 Kor. 11:17 ), basi najua kwamba Bwana hakukusudia kuweka au kuidhinisha sehemu maalumu. Bwana mwenyewe alisisitiza katika Yohana 4:20-24 kwamba kukubalika kwa ibada hakuamuliwi na eneo.Ikiwa nitapata katika maandiko kwamba wapendwa walishiriki Meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya juma, na ikiwa nitapata katika maandiko kwamba, wapendwa walishiriki Meza ya Bwana Jumatano usiku, basi nitalazimika kuhitimisha kuwa Bwana hakukusudia kuweka au kuidhinisha muda maalumu kwa ajili ya kushiriki. Lakini sipati ushahidi wowote kwamba wapendwa walishiriki Meza ya Bwana Jumatano usiku. Ninapata ushahidi wa kutosha na usiopingika kwamba iliadhimishwa na inapaswa kuadhimishwa kila siku ya kwanza ya juma.

Page 155: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 147 -

Kabla ya Alhamisi usiku (katika uhusiano na siku ya kwanza) inaweza kufananishwa na gari (katika uhusiano na mtumbwi) ni lazima nipate kitu kinachohusiana na siku ya kwanza kinachofananishwa na kutembea katika uhusiano wake na mtumbwi, lakini siwezi kupata kitu hicho. Kuna mamlaka ya wazi kwa ajili ya gari. Kuna ushahidi wa kutosha kabisa kwamba Mungu hakukusudia kuweka au kuidhinisha njia mahususi ya kusafiri. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba Bwana alikusudia kuweka au kuidhinisha muda fulani mahususi (kuhusiana na siku) kwa ajili ya kushiriki Meza ya Bwana.

UKWELI

(1) Bwana alisema “enendeni.” (2) Wapendwa wakaenda kwa mashua. (3) Wapendwa wakaenda kwa kutembea

HITIMISHO Ni lazima nihitimishe kutokana na ukweli huu kwamba (1) Ni lazima niende; (2) ninaweza kwenda kwa mtumbwi (3) Ninaweza kwenda kwa kutembea; (4) Namna ya kwenda, kwa hiyo haijaainishwa, ninaweza kwenda kwa kutumia njia yeyote ile, hiyo iko sawa.

UKWELI (1) Tumeamriwa kutoa kama tulivyobarikiwa. (2) Wapendwa wa Makedonia walitoa zaidi ya uwezo wao.

Page 156: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 148 -

HITIMISHOKutokana na ukweli huu ni lazima nihitimishe: (1) Nimepewa jukumu la kutoa; (2) Ni lazima nitoe angalau kama nilivyobarikiwa; (3) Ninaweza kutoa zaidi ya nilivyobarikiwa.

UKWELI: (1) Wapendwa walipewa jukumu la kushiriki Meza ya Bwana. (2) Walishiriki meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya Juma. (3) Tuna maelekezo maalumu kwamba Meza ya Bwana inatakiwa kushiriki meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya juma (Mdo. 20:7 pamoja na 1 Kor. 16:2). (4) Hatuna mamlaka ya kushiriki Meza ya Bwana katika muda mwingine tofauti isipokuwa siku ya kwanza ya juma.

HITIMISHO Kutokana na ukweli huu ni lazima nihitimishe: (1) Ni lazima tushiriki Meza ya Bwana; (2) Ni lazima tushiriki Meza ya Bwana siku ya kwanza ya juma; (3) Ni lazima tushiriki Meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya juma; (4) Tunatakiwa tushiriki Meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya juma tu.Ngoja nisisitize tena, hoja inayofanya iwe dhambi kushiriki Meza ya Bwana siku ya Alhamisi usiku, ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mamlaka kwa ajili ya hilo – sio wazo kwamba mfano hubagua.Asante tena kwa barua yako. Ni matumaini na maombi yangu ya dhati kwamba fikra hizi zitakuwa za manufaa kwako kwa ajili ya kujifunza na kufundisha.

Page 157: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 149 -

Mungu aendelee kuwa pamoja nawe na akubariki katika huduma yake.Ni wako katika Ufalme,Roy Deaver

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 158: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 150 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 159: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 151 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

Page 160: KUTAMBUA MAMLAKA YA BIBLIA - storage.googleapis.com · Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali hapo akamwabudu Yehova

- 152 -

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI