uwezo tanzania 2013 · hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu uwezo....

20
Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea 2 0 1 3 UWEZO TANZANIA

Upload: others

Post on 06-Sep-2019

6 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea2 0 1 3U W E Z O T A N Z A N I A

Page 2: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

ii 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

RATIBA YA MAFUNZO

Muda / Tarehe Mada

Siku ya 1: Jumanne

2:00-2:30 Usajili na Kujitambulisha Wahojaji wa Kujitolea

2:30-03:00 Matarajio na Makubaliano ya Pamoja

3:00-04:15 Kuitambulisha Uwezo

04:15-04:40 Kufafanua Mchakato wa Utafi �

04:40 - 05:00 | Chai ya Kifungua kinywa

05:00-05:20 Kutembelea Eneo la Kuhesabia (Nadharia)

05:20-06:40 Kutembelea Kaya (Nadharia)

06:40-07:30 Upimaji Watoto

07:30-08:30 | Chakula Cha Mchana

08:30-09:30 Ufafanuzi wa Tathmini ya Kusoma

09:30-10:10 Ufafanuzi wa Tathmini ya Kuhesabu

10:10-10:40 Mrejesho wa Papo kwa papo (Nadharia)

10:40-11:00 | Chai ya Alasiri na mpangilio wa Tara� bu za zoezi

11:00 �12:30 | WAHOJAJI WA KUJITOLEA KUTEMBELEA KAYA � MAFUNZO KWA VITENDO

Muda / Tarehe Mada

Siku ya 2: Jumatano

2:00-03:30 Mrejesho na Maswali yatokanayo na ziara ya kutembelea Kaya

03:30-04:15 Kutembelea Shule (Nadharia)

04:15-04:30 Masuala ya Kimaadili

04:30- 04:50 | Chai ya Kifungua Kinywa na mpangilio wa tara� bu za zoezi

04:50 �06:30 | WAHOJAJI WA KUJITOLEA KUTEMBELEA SHULE�MAFUNZO KWA VITENDO

06:30-07:30 | Chakula Cha Mchana

07:30-08:00 Mrejesho na Maswali yatokanayo na ziara ya kutembelea Shule

Wahojaji wa Kujitolea Kuondoka kwenda vijijini kwao

Page 3: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

1Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

YALIYOMO

1

2

5

6

8

11

12

15

16

ZITAMBUE NEMBO ZAKO

SURA 1: KUITAMBULISHA UWEZO

SURA 2: KUELEZEA MCHAKATO WA UTAFITI

SURA 3: KUTEMBELEA SHULE

SURA YA 4: KUTEMBELEA KAYA

SURA YA 5: KUPIMA WATOTO

SURA YA 6: UFAFANUZI WA TATHMINI YA KUSOMA NA KUHESABU

SURA 7: MREJESHO WA PAPO KWA PAPO

SURA YA 8: MASUALA YA KIMAADILI

Zitambue Nembo zako

Dhana muhimuUnapoona picha hii, maana yake ongeza umakini kwa kuwa hili ni jambo muhimu kukumbuka!

Kazi ya kikundiWaka� wa mafunzo, mkufunzi wako atawapanga ka� ka makundi ili kufanya kazi fulani maalum kwa pamoja.

Swali & Jibu Kipindi cha Maswali na Majibu ni muhimu sana. Unahimizwa kuuliza maswali mengi ili kuhakikisha kwamba unaelewa kikamilifu shughuli mbalimbali za mafunzo.

Q ASehemu ya VidokezoSehemu hii ni kwa ajili ya kuandika maelezo na kujipima mwenyewe juu ya yale uliyojifunza.

Page 4: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

2 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka� ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo.

1.2 UWEZO NI NINI?

Uwezo ni….

l Ni neno la Kiswahili lenye maana ya 'kipawa/umahiri'

l Ni ji� hada inayoongozwa na wananchi

l Inafanya kazi kote Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda)

l Inatathmini watoto ka� ka stadi za msingi za kusoma na kuhesabu

l Inakusanya taarifa kutoka shuleni na ka� ka kaya

l Ji� hada ya Uwezo imekuwa inatekelezwa na wananchi wa kawaida ka� ka makazi ya jamii zao

l Inawa� a hamasa wananchi kuchukua hatua ya kuboresha viwango vya kujifunza vya watoto wao

SURA YA 1: KUTAMBULISHA UWEZO

1.1: UTAMBULISHO UNAOFAA

HABARI ZA ASUBUHI MZEE. JINA LANGU NAITWA SARA NA NI

MTAFITI WA KUJITOLEA WA UWEZO. UMEWAHI

KUSIKIA KUHUSU UWEZO HAPO KABLA?

UWEZO NI .......

NA SIJUI UNAWEZA KUNIAMBIA, KAMA

KIJIJI HIKI KINA......KITUO CHA POLISI .....BARABARA YA LAMI.....MAJI YA UHAKIKA YA

UMMA?

USIWE NA WASIWASI, HUU SI KAMA MTIHANI

WA SHULENI. TUPO HAPA KUBAINI JINSI UNAVYOWEZA KUFANYA

VIZURI KATIKA MAJARIBIO HAYA

MAFUPI ....

Page 5: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

3Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

Tafsiri sentensi 5 ka� ka lugha ya asili au lugha utakayotumia ka� ka kaya.

UNAFIKIRI ‘Ji� hada’ maana yake nini?

1.3: NI VIPENGELE VIPI MUHIMU VYA UTAFITI WA UWEZO?

Tathmini ya Uwezo ya Kitaifa ina vipengele muhimu vifuatavyo:

l Ni tathmini ya kikaya

l Ni tathmini ya kiwango kubwa

l Inatumia zana rahisi

l Inaendeshwa na wananchi wazalendo

l Inatoa mrejesho wa matokeo papo kwa papo

l Tathmini hii hufanyika kila mwaka

1.4: JITIHADA NI NINI?

Ji� hada inafafanuliwa kama...

l Ni hali ya wananchi kutathmini ta� zo ka� ka jamii yao ambalo linawahusu, na kuamua kuchukua hatua ya haraka, kulitatua ta� zo hilo ili kujenga jamii bora

Page 6: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

4 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

1.5: MALENGO YA UWEZO NI NINI?

Uwezo inalenga:

1. Kutathmini stadi za watoto ka� ka kusoma na kuhesabu kote nchini Kenya, Tanzania na Uganda

2. Kupata data za kuaminika na za kina juu ya viwango vya kusoma na kuhesabu kila mwaka

3. Kukusanya data ambazo ni mkusanyiko wa takwimu ngazi ya wilaya

4. Kutoa taarifa ya matokeo ya tathmini kwa mapana zaidi - kwa wananchi wazalendo, wazazi, walimu na serikali

5. Kuchochea raia wazalendo kuchukua hatua ili kuboresha viwango vya kujifunza vya watoto ka� ka jamii zao

Kama unataka kuandika kumbukumbu zozote, tafadhali andika hapa: 1.6 1.6 KILE AMBACHO UWEZO SIYO

Uwezo is NOT:

û Asasi ya Kijamii

û Shirika

û Inafadhiliwa na serikali

û Chanzo cha kufi kiri/mawazo

û Kikundi cha kushawishi

û Mradi

Je, unajua?

1. Ni chini ya mtoto mmoja ka� ya watoto watatu walioandikishwa ka� ka Darasa la 3 ka� ka Afrika Mashariki ndiyo wana uwezo wa kufaulu majaribio yote ya Kiingereza na Hisaba� yaliyoandaliwa ka� ka ngazi ya darasa la 2

2. Hata ka� ka darasa la 7, karibu mtoto mmoja ka� ka ya kumi hawezi kufaulu majaribio ya Kiingereza na Hisaba� ya ngazi ya Darasa la 2

3. Kwa wastani, karibu mwalimu mmoja ka� ya walimu kumi anakuwa hayupo mazingira ya shuleni waka� wowote uwao

1.7: MATOKEO YA UWEZO

Page 7: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

5Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

2.1: UTARATIBU WA ZIARA

1. NGAZI YA KIJIJI:1. Mtembelee Mwenyeki� wa Mtaa, siku ya kwanza ya Tathmini 2. Jitambulishe na kuwasilisha barua za utambulisho3. Thibi� sha Mkoa, Kata, Kijiji / Mtaa, Wilaya / Halmashauri, na namba ya Eneo la Kuhesabia (EA)4. Kamilisha kujaza Fomu ya Taarifa za Eneo la Kuhesabia

2. NGAZI YA SHULE:1. Tembelea Shule kabla ya kutembelea kaya2. Tembelea ofi si ya mwalimu mkuu kabla ya kutembelea vyumba vya madarasa3. Jitambulishe na kuwasilisha barua za Utambulisho4. Kamilisha kujaza Fomu zote za data za shule na uchunguzi wa darasani

3. NGAZI YA KAYA:1. Ziara ya kutembelea kaya inapaswa ifanywe mara tu baada ya Fomu ya Taarifa za Kijiji na Fomu ya

Taarifa za Shule kuwa zimekamilika kujazwa.

SURA YA 2: KUELEZEA MCHAKATO WA UTAFITI

NA SIJUI UNAWEZA KUNIAMBIA, KAMA KIJIJI HIKI KINA...... KITUO CHA POLISI

..... BARABARA YA LAMI..... MAJI YA UHAKIKA YA UMMA?

Page 8: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

6 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

SURA YA 3: KUTEMBELEA SHULE

3.1: KUJITAMBULISHA SHULENI

Jitambulishe kwa Mwalimu Mkuu KWANZA. Muoneshe barua za idhini ya kufanya utafi �

Hakikisha unaeleza yafuatayo:

“Uwezo inachukua maeneo ya jamii kutoka kila Wilaya ya Afrika Mashariki itakayo tembelewa. Shule hii ni mionno mwa shule za ka� ka sampuli iliyochaguliwa. Pia kaya ishirini ka� ka Eneo hili la Kuhesabia zitatembelewa leo na kesho, na ka� ka kaya hizo watoto wenye umri wa miaka 7-16, watafanyiwa majaribio.

Uwezo si sehemu ya serikali na hatuchunguzi utendaji wa shule. Tunakusanya takwimu ambazo zitatusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani watoto wanajifunza ka� ka Afrika Mashariki.

UWEZO NI JITIHADA YA MIAKA MINNE INAYOFANYIKA KOTE AFRIKA MASHARIKI

KUTATHMINI WATOTO KATIKA STADI ZA MSINGI ZA KUSOMA NA HISABATI.......... "

Page 9: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

7Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

A

Ofi si ya Mwalimu Mkuu

B

Nenda kwenye chumba kimoja cha Darasa la Pili

D

Chunguza mazingira ya Shule

C

Hesabu vyumba vyote vya madarasa

E

Mshukuru Mwalimu Mkuu kisha nenda kwa

Kiongozi wa Kijiji

Ni muhimu kumuuliza maswali mkufunzi kama huelewi vizuri au kama unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu kipengele chochote cha ziara ya kutembelea shule. Q A

Page 10: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

8 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

SURA YA 4: KUTEMBELEA KAYA

4.1: KAYA NI NINI?

Kaya inahesabika kama kundi la watu wanaoishi ndani ya nyumba moja kila siku. Watu hawa lazima pia wawe wanapika na kula kutoka ka� ka chungu kimoja ndipo waitwe ni watu wa kaya moja.

4.2: KUINGIA KATIKA KAYA

Unapoingia kwenye kaya, zinga� a kufanya yafuatayo:

1. Thibi� sha kwanza kama uko kwenye kaya sahihi, kama ilivyooneshwa kwenye orodha ya kaya zilizochaguliwa kisampuli

2. Jitambulishe kwa mkuu wa kaya 3. Itambulishe Uwezo (Hii ni muhimu sana)4. Eleza sababu ya ziara yako 5. Jibu maswali yoyote ambayo wanaweza kukuuliza wanakaya6. Kuwa wazi, mtulivu na mwenye amani7. Omba idhini ya kufanya utafi � kwenye kaya hiyo. Ni pale tu unapopata ruhusa ndipo unaweza kuanza utafi � 8. Daima uwe mnyenyekevu na mwenye heshima9. Washukuru wanakaya baada ya kumaliza kufanya utafi � wako

UWEZO SI SEHEMU YA

SERIKALI. UWEZO INATATHMINI

WATOTO NA INAKUSANYA

DATA AMBAZO ZITATUSAIDIA

KUELEWA NI VIZURI KIASI GANI

WATOTO WANAJIFUNZA KATIKA

AFRIKA MASHARIKI.

Page 11: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

9Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

Ubadilishaji wa Kaya KAMWE usifanyike pasipo kupata idhini ya Mra� bu wa Wilaya.

Kaya zinazohesabika ka� ka utafi � Kaya ambazo hazipaswi kujumuishwa ka� ka utafi � (Kaya hizi zinatakiwa kubadilishwa)

ü Kaya zisizo na watoto wenye umri ka� ya miaka 3-16. (Taarifa kuhusu mkuu wa kaya bado zinapaswa kukusanywa.)

û Nyumba ambazo zimefungwa kwa sababu wanafamilia wamehama kutoka ka� ka eneo hilo au hawatarudi siku hiyo

ü Kaya anayoishi mtu mmoja aidha mwanaume au mwanamke anakula kutoka ka� ka jiko lake mwenyewe

û Kaya ambayo imekataa kushiriki ka� ka utafi � . Kaya hiyo inapaswa kujazwa "Hakuna jibu"

ü Kaya ambayo imefungwa au hakuna mtu aliyepo nyumbani lakini watarudi baadaye

û Nyumba ambazo kuna watoto lakini hakuna watu wazima wa kutoa idhini kwa watoto kushiriki ka� ka utafi �

MTOTO! WAZAZI WAKO WAPO

NDANI? TUNAWEZA KUZUNGUMZA

NA MAMA AU BABA YAKO?

HAPANA. WAZAZI WETU HAWAPO NYUMBANI LEO.

WANATARAJIA KURUDI NYUMBANI BAADAYE? "

HAPANA. TUMEBAKI NA MAJIRANI NDIO

WANATUHUDUMIA LEO

Page 12: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

10 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Sasa unaweza kujipima wenyewe iwapo unatakiwa ukusanye au usikusanye data kwenye kaya zenye hali zifuatazo:l Binamu ambaye anaishi ka� ka kaya kwa sababu shule anayosoma iko ka� ka kijiji hicho lakini

huwa anaenda kijijini kwao kila mwishoni mwa wiki ili kuwaona wazazi wake. Je, tunachukua taarifa zake na kumpa majaribio?

NDIYO / HAPANAl Mtoto ambaye karudi kutoka shule za bweni kwa sababu ni mgonjwa. Je, tunachukua taarifa

zake na kumpa majaribio? NDIYO / HAPANAl Mama ambaye ana umri wa miaka 16 na ana mtoto. Je, tunamfanyia tathmini? NDIYO / HAPANAl Kaya ambayo bibi kizee anaishi peke yake. Je, tunaihesabu kama kaya ya tathmini? NDIYO / HAPANA

Q A

l Kamilisha kujaza Fomu ya Utafi � KABLA ya kuwapa majaribio watotol Chukua maelezo ya wanakaya wote l Ikitokea watoto hawapo nyumbani (wanaweza kuwa kijijini au shambani), waombe

wanafamilia wamwite uzungumze naye uso kwa usol Kama mtoto hatakuja haraka kwa muda huo, chukua taarifa zake - jina, umri na elimu yake ya

sasa na itembelee tena kaya hiyo baadaye ili kukamilisha tathmini ya mtoto

Ni muhimu kumuuliza maswali mkufunzi kama huelewi vizuri au kama unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu kipengele chochote cha ziara ya Kutembelea Kaya.

Swali: Ni kaya ngapi zitafanyiwa tathmini ka� ka kijiji?

Jibu: Ishirini. (20)

Swali: Je, Wahojaji wa Kujitolea wanaweza kuchagua kaya ambazo wanakutembelea?

Jibu: Hapana. Kaya hizo ishirini zitakuwa tayari zimechaguliwa na Mra� bu wa Wilaya / Mtu wa Mawasiliano. Wahojaji wa Kujitolea watapewa orodha ya kaya za kutembelea zilizochaguliwa kisampuli.

Swali: Nini kinatokea endapo kaya inakataa kushiriki ka� ka utafi � ?

Jibu: Utaiacha kaya hiyo. Kisha utampigia simu Mra� bu wa Wilaya na kupanga kuibadilisha kaya hiyo

7.5: MASWALI AMBAYO HUULIZWA MARA KWA MARA KWENYE KAYA

Swali: Je, Wahojaji wa Kujitolea wanaweza kuchagua kaya ya kubadilisha?

Jibu: Hapana. Unaweza tu kubadilisha kaya ambayo ni aidha imefungwa kwa siku nyingi; inakataa kushiriki au haina watu wazima wa kutoa ridhaa ya upimaji wa watoto. Ka� ka matukio yote Wahojaji wa Kujitolea lazima wawasiliane na Mra� bu wa Wilaya ili kuwajulisha na kupanga kuibadilisha kaya

Swali: Kama wanakaya hawapo nyumbani, lakini watarudi baadaye, Wahojaji wa Kujitolea wanaweza kubadilisha kaya?

Jibu: Hapana. Kama wanakaya watarejea baadaye siku hiyo, Wahojaji wa Kujitolea waendelee kutembelea kaya nyingine zilizo kwenye orodha kwanza, na baadaye kurejea kwenye kaya hiyo mara wanakaya watakapokuwa wamerudi nyumbani. Wanaweza wasiibadili kaya hiyo.

Page 13: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

11Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

WATOTO WOTE WA KWENYE KAYA ZILIZOCHAGULIWA LAZIMA WAFANYIWE TATHMINI WAKIWA NYUMBANI. KATIKA HALI YOYOTE ILE MTOTO WASIPEWE MAJARIBIO TOFAUTI NA YALIYOTOLEWA KATIKA VIJITABU VYA UWEZO.

Umri wa Mtoto Taarifa gani za kujaza Kusimamia majaribio?

Miaka 0-2 û Usimuorodheshe û Hapana

Miaka 3-6

ü Jina Kamili

ü Wasifu

ü Taarifa za Elimu ya Awali

û Hapana. Usimfanyie majaribio mtoto, hata kama anasoma shule ya msingi

Wenye umri wa miaka 7 – 16 ambao aidha

l Wako shulenil Wamewahi kuandishwa shule

kipindi kilichopita

ü Jina Kamili

ü Wasifu

ü Taarifa kusoma

ü Ndiyo. Toa majaribio kwa watoto wote wenye umri wa miaka 7-16 kama wanasoma kwa sasa au wamewahi kuandikishwa shule ka� ka kipindi kilichopita

Wenye umri wa miaka 7 - 16 ambao KAMWE hawajawahi kuandikishwa ka� ka shule. (Hii haijumuishi pamoja na watoto ambao waliwahi kusoma shule ka� ka baadhi ya ngazi na kisha kuacha.)

ü Jina Kamili

ü Wasifu

ü Ndiyo. Wafanyie majaribio hata kama mtoto hajawahi kuandikishwa shule

Zaidi ya miaka 16 û Usimuorodhesheû Hapana. Usimfanyie majaribio mtoto yeyote mwenye umri wa miaka zaidi ya 16, hata kama bado anasoma shule

SURA YA 5: KUPIMA WATOTO

MHUSA HAKUJA S ..... S .....

SHULENI LEO. MUSA ALIVUNJIKA

MGUU WAKE. ALIKUWA ANENDESHA

B ....... B ....... BAISKELI KWA KASI

SANA.....

Page 14: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

12 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

6.1: JINSI YA KUTATHMINI WATOTO

Hatuendi vijijini "kuchunguza" watoto, au kuwa watoa hukumu kwa makosa ya watoto. Tunakwenda kubaini kile ambacho watoto wanaweza kufanya BILA SHIDA ka� ka stadi za kusoma na kuhesabu.

l Fanya mazungumzo ya kirafi ki na mtoto kabla ya kumpima, ili kumsaidia mtoto kubaki mtulivul Kumbuka kwamba hausubiri kuchukua makosa. Unapaswa kupongeza na kuzitambua juhudi

ambazo mtoto anazifanyal Kuwa na subira, tabasamu, na m� e moyo mtotol Kwa usahihi kabisa amua ni NGAZI GANI YA JUU ambayo mtoto huyo anaweza kufi kia bila shidal Usiwatathmini au kuwafanyia majaribio watoto ambao wamekuja kutembea kwenye kaya hiyol Usiwaorodheshe watoto ambao wako shule za bweni. Usiwajumuishe pamoja ka� ka idadi ya

jumla ya kaya

SURA YA 6: UFAFANUZI WA TATHMINI ZA KUSOMA NA HESABU

Mkufunzi atatumia sehemu hii ya mafunzo kuwaelekeza, hatua kwa hatua, mpaka mwisho jinsi ya kuendesha zoezi la upimaji wa stadi za kusoma na kuhesabu kwa watoto, na jinsi ya kuwapanga ka� ka madaraja au ngazi zao sahihi kwenye fomu ya utafi �

Q A

Swali: Kwa nini majaribio ya kusoma yanaanzia ka� ka ngazi ya aya? Je, kwa nini majaribio yasianzie kwenye ngazi ya kutambua herufi na kupanda juu kwenye majaribio magumu zaidi kadri mtoto anavyoweza kukamilisha jaribio?

Jibu: Jaribio la kupima stadi za kusoma huanzia ka� ka ngazi ya aya kwa kuwa watoto wote wanaotathminiwa wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma na kukamilisha ngazi hii ya jaribio. Kuanzia ka� ka ngazi ya aya kwa watoto wote inachukua muda mfupi zaidi kwa mhojaji wa kujitolea ambaye anatakiwa kutembelea jumla ya kaya ishirini.

6.2: MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

Swali: Ninapomsikiliza mtoto akisoma, kuna tofau� ka� ka matamshi na sau� kutokana na lugha ya asili ya mtoto au lugha ya mama. Je, nichukulie tofau� hizi kama kosa?

Jibu: Hapana. Usichukulie tofau� hizi kama kosa. Mwambie mtoto asome tena kwa umakini.

Swali: Ninapomsikiliza mtoto akisoma, anaweza kusoma neno vibaya au kuruka neno. Je, nichukulie hili kama kosa na kumuweka mtoto ka� ka kundi la daraja la chini?

Jibu: Hapana. Kama ilivyo hapo juu, mwambie mtoto asome tena kwa umakini. Aidha atasoma vizuri kwa usahihi au ataendelea kufanya makosa yale yale. Kama ataendelea kufanya makosa yale yale, kukosea maneno au kusoma neno lisilo sahihi, basi hii ina maana kwamba mtoto anapata ugumu wa kusoma ka� ka ngazi hiyo na kwamba inapaswa awekwe kwenye ngazi ya chini.

Swali: Waka� anasoma aya au hadithi, inakuwaje endapo mtoto amefanya makosa 3 au zaidi?

Jibu: Kama mtoto amefanya makosa 3 au zaidi, hana uwezo wa kusoma ka� ka ngazi hii. Anapaswa kuwekwa kwenye ngazi ya chini.

12 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Page 15: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

13Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

UFAFANUZI WA TATHMINI YA KUSOMA

13Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

ANZA

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

HAPANA

HAPANA

HAPANA

HAPANA

Mwambie mtoto asome hadithi. Je, mtoto anaweza kusoma hadithi kwa urahisi na kasi bila

kufanya makosa zaidi ya 2?

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE

DARAJA LA ‘HADITHI’

Weka alama 'Anaweza Kufanya' ka� ka kujibu swali

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE

DARAJA LA 'HERUFI'

Baada ya kusikiliza mtoto akisoma

hadithi, umsomee swali. Je, mtoto kajibu swali kwa

usahihi?

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE

DARAJA LA 'AYA'

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE

DARAJA LA 'MANENO'

Muoneshe mtoto ukurasa wa kusoma

kwa kutambua herufi . Mwambie

asome herufi zozote tano kutoka ka� ka orodha ya herufi .

Je, mtoto anaweza kutambua / kusoma

angalau herufi 4?

Weka alama 'Hawezi kufanya'

ka� ka kujibu swali

Kama mtoto hawezi kutambua/kusoma

herufi nne,MPANGE MTOTO HUYU KWENYE

DARAJA LA 'HAJUI KITU'

Mwambie mtoto asome maneno yoyote matano kutoka kwenye orodha ya maneno. Je, mtoto anaweza kusoma maneno angalau manne?

HAPANA

Muoneshe mtoto moja ya aya mbili ambazo ni rahisi kusoma.Je, mtoto anaweza kusoma aya hii kwa kasi na bila kusitasita, na

bila kufanya makosa zaidi ya 2?

Page 16: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

14 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

UFAFANUZI WA TATHMINI YA HISABATI

14

ANZA

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

NDIO

HAPANA

HAPANA

HAPANA

HAPANA

HAPANA

HAPANA

Mpe mtoto maswali ya kuzidisha. Mwambie mtoto achague na kufanya maswali yoyote MATATU. Angalau maswali mawili afanye kwa usahihi. Je, maswali hayo

mawili ya kuzidisha yamefanyika kwa usahihi?

Mpe mtoto maswali ya kugawanya. Mwambie mtoto achague na

kufanya maswali yoyote MATATU. Angalau maswali mawili afanye kwa usahihi. Je, maswali hayo

mawili ya kugawanya yamefanyika kwa usahihi?

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'KUGAWANYA'.

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'NAMBA IPI NI KUBWA'

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'KUTAMBUA NAMBA'

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA MTOTO WA 'KUHESABU NA KUOANISHA NAMBA'

MPANGE MTOTO HUYU

KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'KUTOA'

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'KUZIDISHA'

MPANGE MTOTO HUYU

KWENYE NGAZI YA

MTOTO WA 'KUJUMLISHA'

Mpe mtoto maswali ya ‘Namba ipi ni Kubwa’. Mwambie mtoto achague na kufanya maswali yoyote MATANO. Angalau maswali MANNE afanye kwa usahihi. Je, anaweza kufanya maswali

MANNE kwa usahihi?

Mpe mtoto maswali ya ‘Kuhesabu idadi na Kuoanisha namba’. Mwambie mtoto ahesabu se� zozote TANO za alama na kuzioanisha na namba. Angalau jozi NNE afanye kwa usahihi.

Je, anaweza kukamilisha jozi NNE kwa usahihi?

MPANGE MTOTO HUYU KWENYE NGAZI YA MTOTO WA 'HAJUI KITU'

Mpe mtoto maswali ya ‘Kutambua namba’.

Mwambie mtoto asome namba zozote TANO. Angalau namba NNE

ziwe sahihi. Je, anaweza kutambua namba NNE

kwa usahihi?

Mpe mtoto maswali ya kujumlisha. Mwambie mtoto achague na kufanya maswali yoyote MATATU. Angalau maswali mawili afanye kwa usahihi. Je, maswali hayo

mawili ya kujumlisha yamefanyika kwa usahihi?

HAPANA

Mwoneshe kwanza mtoto jaribio la kutoa. Mwambie mtoto achague na kufanya maswali yoyote MATATU. Angalau afanye maswali mawili kwa sahihi. Je, maswali

hayo mawili ya kutoa yamefanyika kwa usahihi?

2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Page 17: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

15Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

SURA YA 7: MREJESHO WA PAPO KWA PAPO

7.1: MREJESHO WA PAPO KWA PAPO KATIKA NGAZI YA KAYA

l Mrejesho wa matokeo wa papo kwa papo ni sifa muhimu ya Uwezol Kutoa mrejesho wa papo kwa papo ni muhimu SANA.l Kabla ya kuondoka ka� ka kaya, mtafi � wa kujitolea lazima atoe mrejesho wa matokeo papo kwa papol UNAPASWA kutoa mrejesho kwa uwazi na uaminifu kwa wazazi kabla ya kuondoka kwenye kaya l Toa matokeo kwa ukweli bila kufi cha hata kama hayaridhishil USIWAAMBIE wazazi nini cha kufanya

7.2: USHAURI KUHUSU MREJESHO WA PAPO KWA PAPO

l Majaribio haya yameandaliwa ka� ka ngazi ya Darasa la 2.l Mtoto yeyote ambaye yuko ngazi ya juu zaidi ya Darasa la 2 anapaswa kuweza kufanya majaribio yote bila

shida.l Kama mtoto aliye ngazi ya juu ya Darasa la 2 hawezi kufanya majaribio ya Darasa la 2, unaweza kuwaambia

wazazi kwamba mtoto hana ujuzi ka� ka stadi za msingi za kusoma / kuhesabu. Kama hawawezi kufi kia ngazi za juu kabisa, basi ni dhaifu.

l Usiongeze chumvi au makeke, kwa mfano: “Mtoto huyu ana akili sana na atakuwa profesa.”

15Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

MAJARIBIO YAMEANDALIWA KWA NGAZI YA MAZOEZI YA

DARASA LA 2. ASHA ANASOMA DARASA LA 3, MAANA YAKE

ANAPASWA KUWEZA KUKAMILISHA NA KUFAULU MAJARIBIO

YOTE BILA SHIDA. ASHA ALIFAULU KWA NGAZI YA "HADITHI"

KATIKA KUSOMA NA NGAZI YA "KUGAWANYA" KATIKA

HISABATI. HII INA MAANA ASHA ANAFANYA VIZURI KWA

KIWANGO KINACHOTARAJIWA.

Page 18: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

16 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Hapa mkufunzi atawaongoza kupi� a masuala ya kimaadili yanayohusika ka� ka Tathmini ya Uwezo, na makosa ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara

8.1: MASUALA YA KIMAADILI NA MAKOSA AMBAYO HUJIRUDIA

l USIWAFANYIE majaribio watoto bila ridhaa ya mzazi au mlezi l Kila waka� omba ruhusa kutoka kwa mkuu wa kaya kabla ya kuanza utafi � l Fuata hatua na kanuni zote kama zilivyoainishwa ka� ka mafunzo l USISHIRIKISHANE au KUFICHUA majina ya watoto au wazazi, au taarifa zozote binafsi kwa wanakijijil USITOE ahadi ya msaada wowote au ufadhili kutoka Uwezo. Wewe elezea tu kile kinachofanywa na Uwezol Epuka makosa ya kizembe, uwe nadhifu na aliyejipangal USIBAGUE watoto wa kuuliza maswali kwa watoto wote walio ndani ya kundi la umri wa ka� ya miaka 7-16l Beba barua ya idhini ya kufanya utafi � waka� wote wa utafi � l Hakikisha unaripo� kwa Mwenyeki� wa Mtaa/Kijiji kabla ya kuanza utafi � l Kama nyumba imefungwa, usichukulie unajua vyema taarifa za kaya hiyo na kuamua kujaza bila wahusika

kuwepol Kuwa mkweli ka� ka mchakato mzima wa tathmini na epuka njia za mkatol Omba ridhaa kabla ya kupiga picha zozote l Wahojaji wa Kujitolea wanapaswa kuzinga� a maadili ya kitamaduni na kanuni za uvaaji wa jumuiya

wanayokwenda kutembelea kwa mfano, namna ya kusalimia, na uvaaji nk

8.2: MAKOSA YALIYOFANYWA MARA KWA MARA NA WAHOJAJI WA KUJITOLEA MWAKA 2012

A. Kushindwa kumtembelea mwenyeki� Mtaa au Afi sa Mtendaji wa Kijiji (VEO)B. Kaya inapokuwa imefungwa, walijaza baadhi ya taarifa na wasifu bila kumuuliza mkuu wa kayaC. Kutowafanyia majaribio watoto wote wenye umri wa miaka 7-16 ka� ka kayaD. Kuwafanyia majaribio watoto wenye umri chini ya miaka 7 na zaidi ya miaka 16E. Kutokutoa Mrejesho wa matokeo papo kwa papoF. Kutorudi tena kufanya tathmini ka� ka baadhi ya kaya ambazo watoto hawakuwepo waka� wa tathmini

Wahojaji wa Kujitolea lazima wahakikishe

wanabeba barua za idhini ya kufanya

utafi ti wakati wote wa zoezi la tathmini

SURA YA 8: MASUALA YA KIMAADILI

Page 19: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

17Uwezo | Elimu bora, Jukumu langu!

l Ni neno la Kiswahili lenye maana ya 'kipawa/umahiri'

l Ni ji� hada inayoongozwa na wananchi

l Inafanya kazi kote Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda)

l Inatathmini watoto ka� ka stadi za msingi za kusoma na kuhesabu

l Inakusanya taarifa kutoka shuleni na ka� ka kaya

l Ji� hada ya Uwezo imekuwa inatekelezwa na wananchi wa kawaida ka� ka makazi ya jamii zao

l Inawa� a hamasa wananchi kuchukua hatua ya kuboresha viwango vya kujifunza vya watoto wao

Lengo kuu la Uwezo kwa miaka minne ya kwanza ya utendaji ni kuchangia ka� ka uboreshaji wa angalau asilimia 10 ka� ka viwango vya kusoma na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 7-16 ka� ka nchi za Tanzania, Kenya

na Uganda. Tunalenga kufanikisha hili kwa kuhamisha mwelekeo kutoka kujikita kwenye miundombinu na uandikishaji wa watoto kuelekea viwango halisi vya kujifunza kwa watoto.

Dhana ya Uwezo ni rahisi sana. Tunapeleka watoto shule kwa sababu tunarajia watajifunza stadi za msingi na ujuzi muhimu utakaopelekea ustawi. Hivyo, Uwezo - badala ya kuelekeza nguvu ka� ka idadi

ya kuvu� a ya madarasa yaliyojengwa, walimu walioajiriwa, na vitabu vilivyotolewa inauliza swali rahisi 'Je, Watoto wetu wanajifunza?'

Tathmini ya Uwezo ya Kitaifa ina vipengele muhimu vifuatavyo:

l Ni tathmini ya kiwango kubwa

l Inatumia zana rahisi

l Inaendeshwa na wananchi wa kawaida

l Inatoa mrejesho wa matokeo papo kwa papo

l Tathmini ya Uwezo hufanyika kila mwaka

l Ni tathmini ya kikaya

UWEZO EAST AFRICA

Uwezo ni...

Page 20: UWEZO TANZANIA 2013 · Hadi mwisho wa somo hili, unapaswa kuwa na uelewa wa kina kuhusu Uwezo. Utapokelewa vyema ka ka kaya kama unaweza kuelezea vizuri na kwa kujiamini kuhusu Uwezo

18 2013 • Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea

Mtaa wa Mafi nga,barabara ya Kinondoni

S L P 38342, DSM, TanzaniaE: [email protected]

www.uwezo.net

Mwongozo wa Wahojaji wa Kujitolea2 0 1 3U W E Z O T A N Z A N I A