warakawakwanzawapaulomtume kwa wakorintho · 1wakorintho1:26 3 1wakorintho2:6 za binadamu. 26...

34
1 WAKORINTHO 1:1 1 1 WAKORINTHO 1:12 WARAKA WA KWANZA WA PAULO MTUME KWA WAKORINTHO 1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene, 2 tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Ko- rintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia. 3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo. 4 Ninamshukuru Mungu wangu daima kwa ajili yenu kwa sababu amewatunukia ninyi neema yake kwa njia ya Kristo Yesu. 5 Maana, kwa kuungana na Kristo mmetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwa elimu yote na uwezo wote wa kuhubiri, 6 kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwa ndani yenu, 7 hata hampungukiwi kipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia Siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae Yesu Kristo Bwana wetu. 10 Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na fikira moja na nia moja. 11 Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu. 12 Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,” mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni

Upload: others

Post on 04-Feb-2020

18 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 1:1 1 1 WAKORINTHO 1:12

WARAKA WA KWANZA WA PAULO MTUMEKWAWAKORINTHO1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo

Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,2 tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Ko-rintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuunganana Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamojana watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu YesuKristo aliye Bwana wao na wetu pia. 3Nawatakieni neemana amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetuYesu Kristo. 4 Ninamshukuru Mungu wangu daima kwaajili yenu kwa sababu amewatunukia ninyi neema yakekwa njia ya Kristo Yesu. 5 Maana, kwa kuungana naKristo mmetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwa elimuyote na uwezo wote wa kuhubiri, 6 kwani, ujumbe juu yaKristo umethibitishwa ndani yenu, 7 hata hampungukiwikipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea kufunuliwakwake Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Yeye atawaimarishaninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia Sikuile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu;yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae YesuKristo Bwana wetu. 10 Ndugu, ninawasihi kwa jina laBwanawetuYesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambomsemalo; yasiwekomafarakano kati yenu; muwe na fikiramoja na nia moja. 11 Ndugu zangu, habari nilizopatakutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyeshawazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu. 12 Natakakusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema,“Mimi ni wa Paulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,”mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni

Page 2: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 1:13 2 1 WAKORINTHO 1:25wa Kristo,”. 13 Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiyealiyesulubiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jinala Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwamba sikumbatizamtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa tu Krispo naGayo. 15 Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwakwa jina langu. 16 (Samahani, nilibatiza pia jamaa yaStefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatizamtu mwingine yeyote.) 17 Kristo hakunituma kubatiza,bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutege-mea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo chaKristo msalabani isibatilishwe. 18Maana ujumbe kuhusukifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwawale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisitulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu yaMungu. 19 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Nitai-haribu hekima yaowenye hekima, na elimu yawataalamunitaitupilia mbali.” 20 Yu wapi basi, mwenye hekima?Yu wapi basi, mwalimu wa Sheria? Naye bingwa wamabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanyahekima ya ulimwengu kuwa upumbavu. 21Maana, kadiriya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungukwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Munguamependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kileambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu,yaani ujumbe tunaohubiri. 22Wayahudi wanataka ishara,na Wagiriki wanatafuta hekima; 23 lakini sisi tunamhu-biri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili nikikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu; 24 lakinikwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ninguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25 Maana kina-choonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busarazaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekanakuwani udhaifuwaMungu, kinanguvu zaidi kulikonguvu

Page 3: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 1:26 3 1 WAKORINTHO 2:6za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa:wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikiraza binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watuwa tabaka ya juu. 27 Ndiyo kusema, Mungu aliyach-agua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu,ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale am-bayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenyenguvu. 28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikiraza dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa,mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutiliembali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo yamaana. 29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochotembele ya Mungu. 30Mungu mwenyewe ndiye aliyewaun-ganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristoawe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa naMungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.31Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenyekutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana.”

21 Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri

ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwahekima ya binadamu. 2 Nilipokuwa kwenu niliamuakutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo;naam, Kristo aliyesulubiwa. 3 Nilipokuwa kwenu ni-likuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi. 4 Hotubazangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno yakuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi nanguvu ya Roho. 5 Nilifanya hivyo kusudi imani yenuipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya bi-nadamu. 6 Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekimakwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si yahapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao

Page 4: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 2:7 4 1 WAKORINTHO 3:1wako katika mkumbo wa kupotea. 7 Hekima tunayotu-mia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika,ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili yautukufu wetu. 8 Ni hekima ambayo watawala wa duniahii hawakuielewa; maana wangalielewa, hawangalimsu-lubisha Bwana wa utukufu. 9 Lakini, ni kama yasemavyoMaandiko Matakatifu: “Mambo ambayo jicho halijapatakuyaona wala sikio kuyasikia, mambo ambayo binadamuhajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliy-owatayarishia wale wampendao.” 10 Hayo ndiyo mamboMungu aliyotufunulia kwa njia ya Roho wake. MaanaRoho huchunguza kila kitu hata mambo ya ndani kabisayaMungu. 11Nani awezaye kujuamambo ya ndani yamtuisipokuwa roho yake mtu huyo? Hali kadhalika, hakunaajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.12 Sasa sisi hatukuipokea roho ya ulimwengu, bali tume-pokea Roho atokaye kwa Mungu ili atuwezeshe kujuayale tuliyojaliwa na Mungu. 13 Basi sisi twafundisha, sikwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya binadamu,bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanuamambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho. 14 Mtu wakidunia hapokei mambo ya Roho wa Mungu. Kwake mtuhuyo mambo hayo ni upumbavu mtupu; yanapita akiliyake; maana yanaweza tu kutambuliwa kwa msaada waRoho. 15 Lakini mtu aliye na huyo Roho anaweza kubain-isha ubora wa kila kitu, naye mwenyewe hahukumiwina mtu mwingine. 16 Maandiko yasema: “Nani awezayekuifahamu akili ya Bwana? Nani awezaye kumshauri?”Lakini sisi tunayo akili ya Kristo.

31 Ndugu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu

mlio na huyo Roho. Nilipaswa kusema nanyi kama watu

Page 5: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 3:2 5 1 WAKORINTHO 3:15wa kidunia, kama watoto wachanga katika maisha yaKikristo. 2 Ilinibidi kuwalisheni kwa maziwa, na si kwachakula kigumu, kwani hamkuwa tayari kukipokea. Hatasasa hamko tayari. 3Maana bado mu watu wa kidunia. Je,si kweli kwamba bado ukowivunamagombano kati yenu?Mambo hayo yanaonyesha wazi kwamba ninyi bado niwatu wa kidunia, mnaishi mtindo wa kidunia. 4 Mmojawenu anaposema, “Mimi ni wa Paulo”, na mwingine,“Mimi ni wa Apolo”, je, hiyo haionyeshi kwamba mnaishibado kama watu wa dunia hii tu? 5 Apolo ni nani? naPaulo ni nani? Sisi ni watumishi tu ambao tuliwaleteenininyi imani. Kila mmoja wetu anafanya kazi aliyopewana Bwana. 6 Mimi nilipanda mbegu, Apolo akamwagiliamaji; lakini aliyeiotesha mbegu ni Mungu. 7 Wa maanasi yule aliyepanda mbegu, au yule aliyemwagilia maji;wa maana ni Mungu aliyeiwezesha mbegu kuota. 8 Yulealiyepanda na yule aliyemwagilia maji wote ni sawa, in-gawa kilammoja atapokea tuzo lake kufuatana na jitihadayake mwenyewe. 9 Maana sisi ni ndugu, wafanyakazipamoja na Mungu; na ninyi ni shamba lake; ninyi nijengo lake. 10 Kwa msaada wa neema aliyonipa Mungu,nimefaulu, kama mwashi stadi mwenye busara, kuwekamsingi ambao juu yake mtu mwingine anajenga. Basi,kila mmoja awe mwangalifu jinsi anavyojenga juu yake.11Hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine badalaya ule uliokwisha wekwa, yaani Yesu Kristo. 12 Juu yamsingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha aumaweya thamani; anaweza kutumiamiti, majani aunyasi.13 Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekanawakati Siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyoitatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonyeshaubora wake. 14 Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingikitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; 15 lakini kama

Page 6: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 3:16 6 1 WAKORINTHO 4:6alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakiniyeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyokakutoka motoni. 16 Je, hamjui kwamba ninyi ni hekalula Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndaniyenu? 17 Basi, mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Munguatamharibu; maana hekalu la Mungu ni takatifu, nahekalu hilo ni ninyi wenyewe. 18 Msijidanganye! Mtuyeyote miongoni mwenu akijidhania mwenye hekimamtindo wa kidunia, heri awe mjinga kusudi apate kuwana hekima ya kweli. 19 Maana, hekima ya kidunia niupumbavumbele yaMungu. Kwani MaandikoMatakatifuyasema: “Mungu huwanasa wenye hekima katika ujanjawao.” 20Na tena: “Bwana ajua kwambamawazo ya wenyehekima hayafai.” 21Basi, mtu asijivunie watu. Maana kilakitu ni chenu. 22Paulo, Apolo na Kefa, ulimwengu, maishana kifo; mambo ya sasa na ya baadaye, yote ni yenu.23 Lakini ninyi ni wa Kristo naye Kristo ni wa Mungu.

41 Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo

tuliokabidhiwa siri za mungu. 2 Kinachotakiwa kwayeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu.3 Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na ninyi, auna mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu.4 Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakinihiyo haionyeshi kwamba sina lawama. Bwana ndiyeanayenihukumu. 5Basi, msihukumu kabla ya wakati wakeacheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichuamambo ya giza yaliyofichika, na kuonyesha wazi niaza mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifaanayostahili kutoka kwa Mungu. 6 Ndugu, hayo yoteniliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezokwenu: kutokana na mfano wangu mimi na Apolo

Page 7: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 4:7 7 1 WAKORINTHO 4:18nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieniyaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyoteanayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine.7 Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani weweambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya ninikujivunia kana kwambahukukipewa? 8Haya,mmekwishashiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalmebila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweli watawala,ili nasi pia tuweze kutawala pamoja nanyi. 9 NafikiriMungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwishokabisa, kama watu waliohukumiwa kuuawa, maanatumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbeleya malaika na watu. 10 Sisi ni wapumbavu kwa ajili yaKristo, lakini ninyi ni wenye busara katika kuunganana Kristo! Sisi ni dhaifu, ninyi ni wenye nguvu. Ninyimnaheshimika, sisi tunadharauliwa. 11 Mpaka dakikahii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi,hatuna malazi. 12 Tena twataabika na kufanya kazikwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakiabaraka; tukidhulumiwa, tunavumilia; 13 tukisingiziwa,tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kamauchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi ni takataka!14 Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha ninyi,bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi.15 Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katikamaisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwanikatika maisha ya Kikristo mimi ndiye niliyewazaeni kwakuihubiri Habari Njema. 16 Kwa hiyo, nawasihi: fuatenimfano wangu. 17 Ndiyo maana nimemtuma Timetheokwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifukatika Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katikakuishi maisha ya Kikristo; njia ninayofundisha kilamahali katika makanisa yote. 18 Baadhi yenu wameanza

Page 8: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 4:19 8 1 WAKORINTHO 5:10kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tenakwenu. 19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi;na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kilewanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kilawanachoweza kufanya. 20 Maana Utawala wa Mungu sishauri la maneno matupu, bali ni nguvu. 21Mnapendelealipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendona upole?

51 Ziko habari za kuaminika kwamba kuna uzinzi mion-

goni mwenu; tena ni uzinzi mbaya ambao haujapatakuwako hata kati ya watu wasiomjua Mungu. Nimeam-biwa eti mmoja wenu anaishi na mke wa baba yake!2Mnawezaje kujivuna? Ingekuwa afadhali kwenu kuom-boleza, na huyo aliyefanya kitu hicho aondolewe mion-goni mwenu. 3 Nami, kwa upande wangu, ingawa kwamwili niko mbali nanyi, hata hivyo kwa roho niko hapopamoja nanyi: na hivyo, kamavile nipohapo, nimekwishamhukumu huyo aliyefanya jambo hilo la aibu. 4 Wakatimnapokusanyika pamoja kwa jina la Bwana Yesu, naminikiwa pamoja nanyi kwa roho, basi, kwa uwezo waBwana wetu Yesu, 5 mkabidhini mtu huyo kwa Shetaniili mwili wake uharibiwe na roho yake iweze kuokolewaSiku ile ya Bwana. 6 Majivuno yenu hayafai! Je, hamjuikwamba chachu kidogo huchachusha donge lote la unga?7 Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpatekuwa donge jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswakuwa; maana, Kristo, Pasaka yetu, amekwisha tolewatambiko. 8 Basi, tufanye karamu hiyo si kwa chachuile ya kale, chachu ya ubaya na uovu, bali kwa mkateusiotiwa chachu, mkate wa usafi na kweli. 9Niliwaandikiakatika barua yangu msishirikiane na wazinzi. 10 Ukweli

Page 9: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 5:11 9 1 WAKORINTHO 6:8ni kwamba sikuwa na maana ya watu wote dunianiwalio wazinzi, wachoyo, walaghai na wenye kuabudusanamu. Maana, ili kuwaepa hao wote ingewalazimuninyi kuihama dunia hii kabisa! 11 Nilichoandika ni hiki:msishirikiane na ndugu Mkristo aliye mzinzi, mchoyo,mwenye kuabudu sanamu, mchongezi mlevi na mlaghai.Mtu wa namna hiyo, hata kula msile naye. 12 Je, nishauri langu kuwahukumu watu walio nje? Hao Munguatawahukumu. Je, ninyi hampaswi kuwahukumu walewalio katika jamii yenu ninyi wenyewe? 13 Mfukuzenimbali nanyi huyo mwovu!

61 Anathubutuje mmoja wenu kumshtaki ndugu

muumini mbele ya mahakama ya watu wasiomjuaMungu badala ya kumshtaki mbele ya watu wa Mungu?2 Je, hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumuulimwengu? Ikiwa basi, ulimwengu utahukumiwa nanyi,kwa nini hamstahili kuhukumu hata katika mambomadogo? 3 Je, hamjui kwamba, licha ya kuhukumumambo ya kawaida ya kila siku, tutawahukumu hatamalaika? 4 Mnapokuwa na mizozo juu ya mambo yakawaida, je, mnawaita wawe mahakimu watu ambaohata hawalijali kanisa? 5 Aibu kwenu! Ndiyo kusemahakuna hata mmoja miongoni mwenu mwenye hekimakiasi cha kuweza kutatua tatizo kati ya ndugu waumini?6 Badala yake, kweli imekuwa mtindo ndugu kumpelekandugu yake mahakamani, tena mbele ya mahakimuwasioamini. 7 Kwa kweli huko kushtakiana tu wenyewekwa wenyewe kwabainisha kwambammeshindwa kabisa!Je, haingekuwa jambo bora zaidi kwenu kudhulumiwa!Haingekuwa bora zaidi kwenu kunyang'anywa maliyenu? 8 Lakini, badala yake, ninyi ndio mnaodhulumu na

Page 10: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 6:9 10 1 WAKORINTHO 6:20kunyang'anya; tena, hayomnawafanyia ndugu zenu! 9Auje, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawalawa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha yauasherati, wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti,10 wevi, wachoyo, walevi, wasengenyaji, wanyang'anyi,hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu. 11 Baadhiyenu mlikuwa hivyo; lakini sasa mmeoshwa, mkafanywawatakatifu, na kupatanishwa na Mungu kwa jina laBwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu. 12Mtuanaweza kusema: “Kwangu mimi kila kitu ni halali.”Sawa; lakini si kila kitu kinafaa. Nakubali kwamba kilakitu ni halali kwangu lakini sitaki kutawaliwa na kituchochote. 13 Unaweza kusema: “Chakula ni kwa ajiliya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula.” Sawa;lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mtusi kwa ajili ya uzinzi bali ni kwa ajili ya kumtumikiaBwana, naye Bwana ni kwa ajili ya mwili. 14 Basi, Mungualiyemfufua Bwana kutoka wafu atatufufua nasi pia kwanguvu yake. 15 Je, hamjui kwamba miili yenu ni viungovya mwili wa Kristo? Je, mnadhani naweza kuchukuasehemu ya mwili wa Kristo na kuifanya kuwa sehemu yamwili wa kahaba? Hata kidogo! 16Maana, kama mjuavyo,anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye—kamailivyoandikwa: “Nao wawili watakuwa mwili mmoja.”17 Lakini aliyejiunga na Bwana huwa roho moja naye.18 Jiepusheni kabisa na uzinzi. Dhambi nyingine zotehutendwa nje ya mwili lakini mzinzi hutenda dhambidhidi ya mwili wake mwenyewe. 19 Je, hamjui kwambamiili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu,ambaye mlimpokea kutoka kwa Mungu? Ninyi basi, simali yenu wenyewe. 20Mlinunuliwa kwa bei kubwa. Kwahiyo, itumieni miili yenu kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Page 11: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 7:1 11 1 WAKORINTHO 7:147

1 Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, nivizuri kama mtu haoi; 2 lakini kwa sababu ya hatariya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wakemwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wakemwenyewe. 3Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe,naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe. 4 Mkehana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo;hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwiliwake, bali mkewe anayo. 5 Msinyimane haki zenu,isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambotu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianenitena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu yaudhaifu wenu. 6 Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, siamri. 7Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo;lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwaMungu;mmoja kipaji hiki na mwingine kile. 8 Basi, wale ambaohawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwambani vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo. 9 Hatahivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana niafadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa. 10 Kwa walewaliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mkeasiachane na mumewe; 11 lakini kama akiachana naye,basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mumewake. Mume naye asimpe talaka mkewe. 12 Kwa walewengine, (mimi binafsi, si Bwana) nasema hivi: Ikiwamwanamume Mkristo anaye mke asiyeamini, na huyomwanamke akakubali kuendelea kuishi naye, asimpetalaka. 13 Na, kama mwanamke Mkristo anaye mumeasiyeamini, na huyo mwanamume akakubali kuende-lea kuishi naye, basi, asimpe talaka mumewe. 14 Kwamaana huyo mume asiyeamini hupokelewa kwa Mungukwa kuungana na mkewe; na huyo mke asiyeamini

Page 12: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 7:15 12 1 WAKORINTHO 7:28hupokelewa kwa Mungu kwa kuungana na mumewe.Vinginevyo watoto wao wangekuwa si wa Mungu; kumbesasa ni watoto wake Mungu. 15 Hata hivyo, ikiwa yuleasiyeamini anataka kumwacha mwenzake aliye Mkristo,basi, na amwache tu. Hapo huyo Mkristo, mume au mke,atakuwa huru. Maana Mungu amewaiteni ninyi muishikwa amani. 16 Wewe mama Mkristo, unawezaje kuwana hakika kwamba hutaweza kumwokoa mume wako?Au wewe mume Mkristo, unawezaje kuwa na hakikakwamba hutaweza kumwokoa mkeo? 17 Kwa vyovyotekila mmoja na aishi kufuatana na vipaji alivyogawiwa naBwana, na kama alivyoitwa na Mungu. Hili ndilo agizolangu kwa makanisa yote. 18 Kama mtu aliitwa akiwaametahiriwa, basi asijisingizie kwamba hakutahiriwa; nakama alipoitwa hakuwa ametahiriwa, basi na asitahiriwe.19 Maana kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; kilichomuhimu ni kuzishika amri za Mungu. 20 Basi, kila mmojana abaki kama alivyokuwa wakati alipoitwa. 21 Je, weweulikuwa mtumwa wakati ulipoitwa? Sawa, usijali; lakiniukipata fursa ya kuwa huru, itumie. 22 Maana yeyealiyeitwa na Bwana akiwa mtumwa huyo huwa mtu huruwa Bwana. Hali kadhalika naye aliyeitwa akiwamtu huru,huwa mtumwa wa Kristo. 23 Nyote mmenunuliwa kwabei; kwa hiyo msiwe tena watumwa wa watu. 24 Nduguzangu, kila mmoja wenu basi, na abaki na Mungu kamaalivyokuwa wakati alipoitwa. 25 Sasa, kuhusu mabikirana waseja, sina amri kutoka kwa Bwana; lakini natoamaoni yangu mimi ambaye kwa huruma yake Bwananastahili kuaminiwa. 26 Basi, kutokana na shida iliyoposasa nadhani ingefaa mtu abaki kama alivyo. 27 Je,umeoa? Basi, usitake kuachana na mkeo. Wewe hukuoa?Basi, usitake kuoa. 28 Lakini ikiwa utaoa hutakuwa ume-tenda dhambi; namsichana akiolewa hatakuwa ametendadhambi. Hao watakaooana watapatwa na matatizo ya

Page 13: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1WAKORINTHO7:29131WAKORINTHO7:40dunia hii, lakini mimi ningependa hayo yasiwapate ninyi.29Ndugu, nataka kusema hivi: muda uliobaki nimfupi. Natangu sasa wale waliooa na waishi kama vile hawakuoa;30 wenye kulia wawe kama hawalii, na wenye kufurahiwawekamahawafurahi; wanaonunuawawekamahawanakitu; 31 nao wenye shughuli na dunia hii wawe kamavile hawana shughuli sana nayo. Maana ulimwengu huu,kama tuujuavyo, unapita. 32 Ningependa ninyi msiwe nawasiwasi. Mtu asiye na mke hujishughulisha na kazi yaBwana jinsi atakavyompendeza Bwana. 33 Mtu aliyeoahujishughulisha na mambo ya dunia jinsi atakavyompen-deza mkewe, 34 naye amegawanyika. Mwanamke asiye-olewa au bikira hujishughulisha na mambo ya Bwana ap-ate kujitoleamwili na roho kwaBwana. Lakinimwanamkealiyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii jinsiatakavyompendeza mumewe. 35 Nawaambieni haya kwafaida yenu, na si kwa kuwawekeeni kizuio. Nataka tumuwe na mpango unaofaa, mpate kumtumikia Bwanakwa moyo na nia moja. 36 Kama mtu anaona kwambahamtendei vyema mchumba wake asipomwoa, na kamatamaa zake zinamshinda, na afanye atakavyo; waoanetu; hatakuwa ametenda dhambi. 37 Lakini kama huyomwanamume akiamua kwa hiari moyoni mwake kutooana kama anaweza kuzitawala tamaa zake na kuamuanamna ya kufanya, basi, anafanya vizuri zaidi asipom-woa huyo mwenzake bikira. 38 Kwa maneno mengine:yule anayeamua kumwoa huyo mchumba wake anafanyavema; naye anayeamua kutomwoa anafanya vema zaidi.39 Mwanamke huwa amefungwa na mumewe kwa mudawotemumewe aishipo. Lakinimumewe akifa, mamahuyoyuko huru, na akipenda anaweza kuolewa na mtu yeyote,mradi tu iwe Kikristo. 40 Lakini, nionavyo mimi, atakuwana heri zaidi kama akibaki hivyo alivyo. Hayo ni maoni

Page 14: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 8:1 14 1 WAKORINTHO 8:12yangu, na nafikiri mimi pia ninaye Roho wa Mungu.

81 Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu:

Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huohuwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendohujenga. 2 Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kwelihajui chochote kama inavyompasa. 3Lakini anayempendaMungu huyo anajulikana naye. 4 Kwa hiyo, kuhusuvyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwambasanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu nimmoja tu. 5 Hata kama viko vitu viitwavyo miunguduniani au mbinguni, na hata kama wako miungu namabwana wengi, 6 hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungummoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwaajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, YesuKristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, nasisi twaishi kwa njia yake. 7 Lakini, si kila mtu anaoujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwishazoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokulavyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwasanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwaunajisi. 8 Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidina Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikilahatuongezewi kitu. 9 Lakini, jihadharini: huu uhuruwenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katikadhambi. 10 Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu,akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyondani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kulavyakula vilivyotambikiwa sanamu? 11Hivyo, huyo nduguyako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapoteakwa sababu ya ujuzi wako. 12 Kama mkiwakoseshandugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu,

Page 15: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 8:13 15 1 WAKORINTHO 9:12mtakuwa mmemkosea Kristo. 13 Kwa hiyo, ikiwa chakulahusababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyamakamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katikadhambi.

91 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi

sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo yakazi yangu kwa ajili ya Bwana? 2 Hata kama kwa watuwengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimini mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwasababu ya kuungana kwenu na Bwana. 3Hoja yangu kwawale wanaonipinga ndiyo hii: 4 Je, hatuna haki ya kulana kunywa? 5 Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristokatika ziara zetu, kama vile wafanyavyomitumewengine,ndugu zake Bwana, na pia Kefa? 6Au ni mimi tu na Barn-aba ambao tunapaswa kujipatiamaslahi yetu kwa kufanyakazi? 7 Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wakejeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shambalake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwaya mifugo yake? 8 Je, nasema mambo haya kibinadamutu? Je, Sheria nayo haisemi hivyo? 9 Imeandikwa katikaSheria ya Mose: “Usimfunge kinywa ng'ombe anapoli-wata nafaka.” Je, ndio kusema Mungu anajishughulishana ng'ombe? 10 Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposemahivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili yetu; kwaniyule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wanahaki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno. 11 Ikiwasisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambokubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia? 12 Ikiwawengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu,je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukui-tumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili kila kitu

Page 16: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 9:13 16 1 WAKORINTHO 9:25ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.13 Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupatachakula chao Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadakamadhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka? 14 Bwanaaliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapateriziki zao kutokana nayo. 15 Lakini, mimi sikutumia hatamojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie hakihizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanyayeyote aone kwamba najisifu bure. 16 Ikiwa ninaihubiriHabari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumunililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!17Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ninge-tazamia malipo; lakini maadam naifanya ikiwa ni wajibu,hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze.18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wanguni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai hakininazostahili kwa kuihubiri. 19 Kwa hiyo, ingawa mimisi mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wakila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.20 Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapateWayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini ya Sheria,nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili niwapate hao waliochini ya Sheria. 21 Na kwa wale walio nje ya Sheria,naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao walionje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko njeya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.22 Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate haowalio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipatekuwaokoa baadhi yao kwa kila njia. 23Nafanya haya yotekwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki baraka zake.24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawawapigambiowote hukimbia, nimmoja tu anayejinyakuliazawadi? 25Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali;

Page 17: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 9:26 17 1 WAKORINTHO 10:13hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisitwafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima. 26 Ndivyobasi, ninavyopigambio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyoninavyopigana, na si kama bondia anayetupa ngumi zakehewani. 27 Naupa mwili wangu mazoezi magumu nakuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi mwenyewenikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine.

101 Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote wa-

likuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wotewalivuka salama ile bahari. 2 Wote walibatizwa katikaumoja na Mose kwa lile wingu na ile bahari. 3 Wotewalikula chakula kilekile cha kiroho, 4wakanywapia kiny-waji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ulemwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwaKristomwenyewe. 5Hata hivyo, wengiwaohawakumpen-deza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani. 6 Sasa,mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisitusitamani ubaya kama wao walivyotamani. 7 Msiwewaabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kamayasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa,wakasimama kucheza.” 8 Wala tusizini kama baadhi yaowalivyozini, wakaangamia siku moja watu ishirini natatu elfu. 9 Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivy-omjaribu, wakauawa na nyoka. 10 Wala msinung'unikekama baadhi yao walivyonung'unika, wakaangamizwa naMwangamizi! 11 Basi, mambo hayo yaliyowapata wao nikielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi,ambao mwisho wa nyakati unatukabili. 12 Anayedhaniamesimama imara ajihadhari asianguke. 13 Majaribumliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Munguni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu

Page 18: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 10:14 18 1 WAKORINTHO 10:28zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvuya kustahimili na njia ya kutoka humo salama. 14 Kwahiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu. 15Naongeananyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayonisemayo. 16 Tunapomshukuru Mungu kwa kikombekile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo?Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili waKristo? 17 Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawani wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkatehuohuo. 18 Chukueni, kwa mfano, Wayahudi wenyewe:kwao, wenye kula vilivyotambikiwa madhabahuni wal-iungana na hiyo madhabahu. 19 Nataka kusema nini,basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu nikitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitukweli zaidi ya sanamu? 20 Hata kidogo! Ninachosemani kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Munguwanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe ninyimuwe na ushirika na pepo. 21Hamwezi kunywa kikombecha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushirikikatika meza ya Bwana na katika meza ya pepo. 22 Auje, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhanituna nguvu zaidi kuliko yeye? 23 Vitu vyote ni halali,lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyotevinajenga. 24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ilafaida ya mwenzake. 25 Kuleni chochote kile kiuzwachosokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu;26 maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomoni mali ya Bwana.” 27 Kama mtu ambaye si muuminiakiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vy-ote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu yadhamiri zenu. 28 Lakini mtu akiwaambieni: “Chakulahiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyoaliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile.

Page 19: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 10:29 19 1 WAKORINTHO 11:929 Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, balidhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwanini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine?30 Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuruMungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwaajili yake nimemshukuru Mungu?” 31 Basi, chochotemfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajiliya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kikwazo kwa Wayahudiau kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu. 33Muwe kamamimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bilakutafuta faida yangumwenyewe ila faida ya wote, wapatekuokolewa.

111Niigeni mimi kama ninavyomwiga Kristo. 2Nawapeni

hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababumnayashikilia yale maagizo niliyowapeni. 3 Lakininapenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kilamwanamume, na mwanamume ni kichwa cha mkewe,na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Basi, kila mwana-mume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Munguhuku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.5 Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe wa Mungubila kufunika kichwa chake, anamdharau mumewe;anayefanya hivyo ni sawa tu na mwanamke aliyenyoakichwa chake. 6 Mwanamke asiyefunika kichwa chake,afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwamwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi,afadhali afunike kichwa chake. 7Haifai mwanamume ku-funika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano wa Munguna kioo cha utukufu wake Mungu; lakini mwanamkeni kioo cha utukufu wa mwanamume. 8 Mwanamumehakutoka kwa mwanamke, ila mwanamke alitoka kwamwanamume. 9 Mwanamume hakuumbwa kwa ajili

Page 20: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 11:10 20 1 WAKORINTHO 11:23ya mwanamke, ila mwanamke aliumbwa kwa ajili yamwanamume. 10 Ndiyo maana mwanamke hufunikakichwa chake, iwe ishara ya mamlaka yaliyo juu yake,na pia kwa sababu ya malaika. 11 Hata hivyo, mbeleya Bwana mwanamke si kitu bila mwanamume, nayemwanamume si kitu bila mwanamke. 12 Kama vilemwanamke alivyotokana na mwanamume, vivyo hivyomwanamume huzaliwa na mwanamke; kila kitu hutokakwa Mungu. 13 Amueni wenyewe: Je, inafaa mwanamkekumwomba Mungu bila kuvaa kitu kichwani? 14 Hatamaumbile yenyewehuonyeshawazi kwambakwamwana-mume kuwa na nywele ndefu ni aibu kwake mwenyewe;15 lakini kwa mwanamke kuwa na nywele ni heshimakwake; nywele zake ndefu amepewa ili zimfunike. 16Kamamtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, naajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisaya Mungu hayana desturi nyingine. 17 Nikiwa badonawapeni maagizo haya, siwezi hata kidogo kuwapa ninyihongera kuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyiwaumini yaleta hasara zaidi kuliko faida. 18 Awali yayote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea ma-farakano kati yenu. Nami naamini kiasi, 19 maana nilazima fikira tofauti ziweko miongoni mwenu, ili walewalio thabiti wapate kutambulikana. 20 Kweli mnaku-tana, lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana!21Maana mnapokula kila mmoja hukikalia chakula chakemwenyewe, hata hutokea kwamba baadhi yenu wananjaa, na wengine wamelewa! 22 Je, hamwezi kula nakunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisala Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Ni-waambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusujambo hili. 23 Maana mimi nilipokea kwa Bwana yalemaagizo niliyowaachieni: kwamba, usiku ule Bwana

Page 21: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 11:24 21 1 WAKORINTHO 12:3Yesu aliotolewa, alitwaa mkate, 24 akamshukuru Mungu,akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwaajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” 25 Vivyohivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: “Hikini kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damuyangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikum-buka.” 26 Maana kila mnapokula mkate huu na kun-ywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpakaatakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo aukunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa nahatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. 28 Basi, kila mtuajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo naanywe kikombe hicho; 29 maana anayekula na kunywabila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula nakunywa hukumu yake yeye mwenyewe. 30 Ndiyo maanawengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wenginekadhaa wamekufa. 31 Kama tungejichunguza wenyewevizuri hatungeadhibiwa hivyo. 32 Lakini tunapohuku-miwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusijetukahukumiwapamoja na ulimwengu. 33Kwahiyo, nduguzangu, mnapokutana kula chakula cha Bwana, kilammojaamngoje mwenzake. 34 Na kama kuna yeyote aliye nanjaa, na ale nyumbani kwake, ili kukutana kwenu kusis-ababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine,nitawapeni maelezo nitakapokuja.

121 Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu

vizurimambo haya: 2Mnajua kwamba, kabla ya kuongokakwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu.3 Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Rohowa Mungu hawezi kusema: “Yesu alaaniwe!” Hali kad-halika, mtu yeyote hawezi kusema: “Yesu ni Bwana,”

Page 22: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 12:4 22 1 WAKORINTHO 12:19asipoongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Vipaji vya kiroho nivya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja. 5Kunanamna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwani mmoja. 6 Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi yahuduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zotekatika wote. 7 Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwafaida ya wote. 8 Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima,na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huy-ohuyo. 9Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpamwingine kipaji cha kuponya; 10humpammoja kipaji chakufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe waMungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyokwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipajicha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzi-fafanua. 11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja,ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyomwenyewe. 12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenyeviungo vingi, na viungo hivyo vyote—ingawaje ni vingi—hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifamengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwaRoho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukany-weshwa Roho huyommoja. 14Mwili hauna kiungo kimojatu, bali una viungo vingi. 15 Kama mguu ungejisemea:“Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili”,je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha! 16 Kamasikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi simali ya mwili”, je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemuya mwili? La! 17 Kama mwili wote ungekuwa jicho,sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwasikio, mtu angewezaje kunusa? 18 Lakini kama ilivyo,Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kamaalivyopenda. 19 Kama sehemu zote zingekuwa kiungo

Page 23: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 12:20 23 1 WAKORINTHO 13:2kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20 Ukweli ni kwamba,sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja. 21Basi,jicho haliwezi kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe”, walakichwa hakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji ninyi.”22Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile zamwilizinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.23 Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahiliheshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifuzaidi; viungo vyamwili ambavyo havionekani kuwa vizurisana, huhifadhiwa zaidi, 24 ambapo viungo vingine hav-ihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuwekamwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kilekilichopungukiwa heshima, 25 ili kusiweko na utenganokatika mwili bali viungo vyote vishughulikiane. 26 Kamakiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamojanacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyotehufurahi pamoja nacho. 27 Basi, ninyi nyote ni mwiliwa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo.28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pilimanabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipajicha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi nawenye kusema lugha ngeni. 29 Je, wote ni mitume? Woteni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji chakufanyamiujiza? 30 Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya?Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wotehufafanua lugha? 31Muwe basi, na tamaa ya kupata vipajimuhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidikuliko hizi zote.

131Hata kama nikinena lugha za watu na hata zamalaika,

lakini kama sina upendo mimi nimekuwa tu kama sautiya debe tupu au kengele. 2 Tena, naweza kuwa na kipaji

Page 24: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 13:3 24 1 WAKORINTHO 14:3cha kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zotena kujua kila kitu; naweza kuwa na imani yote hatanikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendomimi si kitu. 3 Nikitoa mali yangu yote na kuwapamaskini, na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe, kamasina upendo hiyo hainifai chochote. 4 Mwenye upendohuvumilia, hufadhili; mwenye upendo hanawivu, hajidai,wala hajivuni. 5 Mwenye upendo hakosi adabu, hatafutifaida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira; hawekikumbukumbu yamabaya, 6hafurahii uovu, bali hufurahiaukweli. 7Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote,na hustahimili yote. 8 Upendo hauna kikomo kamwe.Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbewaMungu, hivyovitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya kusema lughangeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo itapita. 9Maanaujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangazaneno la Mungu si kamili. 10 Lakini kile kilicho kikamil-ifu kitakapofika, vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.11Nilipokuwamtotomchanga nilisema kitoto, nilifahamukitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtumzima,mamboya kitoto nimeyaacha. 12Tunachoona sasani kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadayetutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakinihapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Munguanavyonijuamimi. 13Sasa yanadumuhayamatatu: imani,tumaini na upendo; lakini lililo kuu kupita yote ni upendo.

141 Jitahidini kuwa na upendo. Vilevile fanyeni bidii

ya kupata vipaji vingine vya kiroho, hasa kipaji chakutangaza ujumbe wa Mungu. 2 Mwenye kunena lughangeni hasemi na watu bali anasema na Mungu. Yeyehunena kwa nguvu ya Rohomambo yaliyofichika. 3Lakini

Page 25: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 14:4 25 1 WAKORINTHO 14:15mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe waMungu, husemana watu kwa ajili ya kuwajenga, kuwafariji na kuwa-tia moyo. 4 Mwenye kunena lugha ngeni anajijengamwenyewe. Lakini mwenye kipaji cha kutangaza ujumbewa Mungu, analijenga kanisa. 5 Basi, ningependa ninyinyote mseme kwa lugha ngeni lakini ningependelea hasamuwe na kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, maanamtu mwenye kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu, niwa maana zaidi kuliko yule mwenye kusema lugha ngeni,isipokuwa tu kama yupo hapo mtu awezaye kuyafafanuahayomambo asemayo, ili kanisa lipate kujengwa. 6Hivyo,ndugu zangu, kama nikija kwenu na kusema nanyikwa lugha ngeni itawafaa nini? Haitawafaa chochote,isipokuwa tu kama nitawaelezeni ufunuo wa Mungu auujuzi fulani au ujumbe wa Mungu au mafundisho fulani.7Ndivyo ilivyo kwa vyombo visivyo na uhai vyenye kutoasauti kama vile filimbi au kinanda. Je, mtu anawezajekuutambua wimbo unaochezwa kama vyombo hivyo hav-itoi sauti waziwazi vinapopigwa? 8 La mgambo likilia bilakufuata taratibu zake, nani atajiweka tayari kwa vita?9Hali kadhalika na ninyi, kama ulimi wenu hausemi kituchenye kueleweka, nani ataweza kufahamu mnayosema?Maneno yenu yatapotea hewani. 10Zipo lughambalimbaliulimwenguni, na hakuna hata mojawapo isiyo na maana.11 Lakini ikiwa mimi sifahamu maana ya lugha asemayomtu fulani, mimi ni mgeni kwake mtu huyo naye piani mgeni kwangu. 12 Hali kadhalika na ninyi, maadammna hamu ya kupata vipaji vya Roho, jitahidini hasakujipatia vile vinavyosaidia kulijenga kanisa. 13Kwa hiyo,mwenye kunena lugha ngeni na aombe apate uwezo wakuzifafanua. 14 Maana, nikisali kwa lugha ngeni rohoyangu ndiyo inayosali, lakini akili yangu hubaki bure.15 Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu, nitasali

Page 26: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 14:16 26 1 WAKORINTHO 14:26pia kwa akili yangu; nitaimba kwa roho yangu, nitaimbapia kwa akili yangu. 16 Ukimsifu Mungu kwa roho yakotu, atawezaje mtu wa kawaida aliye katika mkutanokuitikia sala yako ya shukrani kwa kusema: “Amina,”kama haelewi unachosema? 17 Sala yako ya shukraniyaweza kweli kuwa bora, lakini huyo mwingine haitam-faidia. 18Namshukuru Mungu kwamba mimi nasema kwalugha ngeni zaidi kuliko ninyi nyote. 19 Lakini katikamikutano ya waumini napendelea zaidi kusema manenomatano yenye kueleweka ili niwafundishe wengine, ku-liko kusemamaneno elfu ya lugha ngeni. 20Ndugu, msiwekamawatoto katika fikira zenu. Kuhusu uovumuwe kamawatoto wachanga lakini katika kufikiri ni lazima muwekama watu waliokomaa. 21 Imeandikwa katika Sheria:“Bwana asema hivi: Kwa njia ya wenye kunena lughangeni, na kwa midomo ya wageni, nitasema na watuhawa, hata hivyo, hawatanisikiliza.” 22 Hivyo basi, kipajicha kusema lugha ngeni ni ishara, si kwa ajili ya watuwenye imani, bali kwa ajili ya wale wasioamini; lakinikipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu ni kwa ajili yawale wanaoamini na si kwa ajili ya wasioamini. 23 Basi,kanisa lote linapokutana pamoja, na wote wakaanzakusema kwa lugha ngeni, kama wakija watu wa kawaidaau wasioamini, je, hawatasema kwamba ninyi mna waz-imu? 24 Lakini, wote wakiwa wanautangaza ujumbewa Mungu, akija mtu wa kawaida au asiyeamini, yoteatakayosikia yatamhakikishia ubaya wake mwenyewe;yote atakayosikia yatamhukumu. 25 Siri za moyo wakezitafichuliwa, naye atapigamagoti na kumwabuduMunguakisema: “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi.” 26 Ndugu,tuseme nini, basi? Mnapokutana pamoja, mmoja aimbewimbo, mwingine atoe mafundisho, mwingine awe naufunuo kutoka kwa Mungu, mwingine atumie kipaji

Page 27: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 14:27 27 1 WAKORINTHO 14:40cha kusema kwa lugha ngeni na mwingine afafanueyanayosemwa. Yote yawe kwa ajili ya kulijenga kanisa.27 Wakiwepo watu wenye vipaji vya kusema kwa lughangeni, waseme wawili au watatu, si zaidi, tena mmojam-moja; na awekomtuwakufafanua yanayosemwa. 28Lakinikama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusemalugha ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yakemwenyewe na Mungu. 29 Kuhusu wale wenye kipaji chakutangaza ujumbe wa Mungu, waseme wawili au watatu,na wengine wayapime maneno yao. 30 Ikiwa mmoja ana-posemamwinginewawasikilizaji amepata ufunuo kutokakwa Mungu, basi, yule anayesema anyamaze. 31 Maananyote mwaweza kutangaza ujumbe wa Mungu, mmojabaada ya mwingine, ili nyote mpate kujifunza na kutiwamoyo. 32 Kipaji cha kutangaza ujumbe wa Mungu nilazima kitawaliwe na huyomwenye hicho kipaji. 33MaanaMungu siMunguwa fujo, ila wa amani. 34Kama ilivyo des-turi katika makanisa yote ya watu wa Mungu, wanawakewakae kimya katika mikutano ya waumini. Hawanaruhusa kusema; ila wawe watii kama isemavyo Sheria.35 Ikiwa wanayo maswali ya kuuliza, wawaulize waumezao nyumbani, maana ni aibu kwa mwanamke kusemakatika mikutano ya waumini. 36 Je, mnadhani neno laMungu limetoka kwenu ninyi au kwamba limewajienininyi peke yenu? 37 Kama mtu yeyote anadhani kwambayeye ni mjumbe wa Mungu au kwamba anacho kipaji chaRoho, na ajue kwamba haya ninayowaandikia ninyi niamri ya Bwana. 38Lakinimtu asiyetambua hayo, basi, mtuasimjali mtu huyo. 39Hivyo basi, ndugu zangu, mnapaswakuwa na hamu ya kutangaza ujumbe wa Mungu; lakinimsimkataze mtu kusema kwa lugha ngeni. 40 Lakini yoteyafanyike kwa heshima na kwa utaratibu.

Page 28: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 15:1 28 1 WAKORINTHO 15:1615

1 Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile HabariNjema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimamaimara ndani yake. 2 Kwa njia yake mnaokolewa,ikiwamnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kamakuamini kwenu hakukuwa bure. 3 Mimi niliwakabidhininyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea:kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu ku-fuatana na Maandiko Matakatifu; 4 kwamba alizikwa,akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa; 5 kwambaalimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi nawawili. 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwamara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yaowamekwisha kufa. 7 Baadaye alimtokea Yakobo kishaakawatokea mitume wote. 8 Baada ya wote, akanitokeahata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kablaya wakati. 9 Maana mimi ni mdogo kabisa miongonimwamitume na wala sistahili kuitwamtume, kwa sababunililidhulumu kanisa la Mungu. 10 Lakini, kwa neemayake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yakekwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kulikowote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayokazi pamoja nami. 11 Lakini hata hivyo, iwe wao ndiowahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndichotunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini. 12 Sasa,maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutokawafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakunaufufuo wa wafu? 13 Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi,Kristo naye hakufufuka; 14 na kama Kristo hakufufuka,basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu hainamaana. 15 Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wauongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungualimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua—kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi. 16 Maana,

Page 29: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 15:17 29 1 WAKORINTHO 15:30ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristohakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imaniyenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu. 18Zaidiya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana naKristo wamepotea kabisa. 19Kamamatumaini yetu katikaKristo yanahusu tu maisha haya ya sasa, basi, sisi niwatu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote duniani.20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutokawafu, limbuko lao wale waliolala katika kifo. 21 Maanakama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyohivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa namtu mmoja. 22 Kama vile watu wote wanavyokufa kwakujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwakuungana na Kristo. 23 Lakini kila mmoja kwa mpangowake: Kristo kwanza, halafu wale walio wake Kristowakati Kristo atakapokuja. 24 Baada ya hayo, mwishoutafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu BabaUtawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlakana nguvu. 25Maana Kristo sharti atawale mpaka Munguatakapowashinda adui zake na kuwaweka chini ya miguuyake. 26 Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.27Maana,Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyotechini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema:“Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale”ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo lavitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chiniya Kristo. 28 Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini yaUtawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiwekachini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake;ili Mungu atawale juu ya vyote. 29Kama hakuna ufufuo, jewatu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainiakupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwakwa ajili yao? 30 Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa?

Page 30: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 15:31 30 1 WAKORINTHO 15:4531Ndugu,mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayojuu yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetuinanifanya nitangaze jambo hili. 32 Kama kusudi langulingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu nawanyamawakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kamawafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana keshotutakufa.” 33 Msidanganyike! Urafiki mbaya huhaributabia njema. 34 Amkeni! Anzeni kuishi vema, na achenikutenda dhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa.Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu! 35 Lakini mtuanaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa namwili wanamna ganiwakatiwatakapokuja tena?” 36Hayonimaswali ya kijinga! Ukipandambegu, isipokufa kwanzahaitaota. 37 Unachopanda ni mbegu tu, labda ya nganoau nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokeabaadaye. 38 Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutakamwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee.39 Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu niya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, yandege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia niya namna nyingine. 40 Iko miili ya mbinguni na miili yaduniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na nauzuri wa miili ya duniani ni mwingine. 41 Uko uzuri wajua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafianakwa uzuri. 42Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kamavile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwa katika hali yakuharibika, lakini hufufuliwa katika hali ya kutoharibika.43Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu;huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenyenguvu. 44 Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofu-fuliwa ni mwili wa kiroho. Kuna mwili wa kawaida na ku-takuwa na mwili wa kiroho. 45Maana Maandiko yasema:“Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbemwenye uhai;”

Page 31: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 15:46 31 1 WAKORINTHO 16:1lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima.46 Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ilaulemwili wa kawaida kisha ulemwili wa kiroho. 47Adamuwa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtuwa pili alitoka mbinguni. 48 Wote walio wa dunia wakokama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo; wale walio wambinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni. 49 Kamavile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo,vivyo hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni.50 Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwamwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme waMungu; nachenye kuharibika hakiwezi kuwana hali ya kutoharibika.51 Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ilasote tutageuzwa 52wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nuktamoja, kufumba na kufumbua. Maana mbiu itakapolia,wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, nasisi tutageuzwa. 53 Maana ni lazima kila kiharibikachokijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivaliehali ya kutokufa. 54 Basi, mwili huu wenye kuharibikautakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufakitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimialile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa ushindiumekamilika!” 55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezowakowa kuumiza ukowapi?” 56Ukali wa kifo hutokana nadhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika Sheria.57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwanjia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 58 Basi, ndugu zanguwapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daimakuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazimnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

161Sasa, yahusuulemchango kwa ajili yawatuwaMungu:

Page 32: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 16:2 32 1 WAKORINTHO 16:17fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia. 2 KilaJumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiriya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchangowakati nitakapokuja. 3 Wakati nitakapokuja kwenu,nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenuwapeleke baruana zawadi zenuYerusalemu. 4Kama itafaanami niende, basi, watakwenda pamoja nami. 5 Nitakujakwenu, baada ya kupitia Makedonia —maana natarajikupitia Makedonia. 6 Labda nitakaa kwenu kwa mudafulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wabaridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangukokote nitakakokwenda. 7 Sipendi kupita kwenu haraka-haraka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenukwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu. 8 Lakini nitabakihapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste. 9Mlango uko wazikabisa kwa ajili ya kazi yangumuhimu hapa, ingawa wap-inzani nao ni wengi. 10Timotheo akija, angalieni asiwe nahofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kaziya Bwana kama mimi. 11 Kwa hiyo mtu yeyote asimdha-rau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani iliaweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamojana ndugu zetu. 12 Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihisana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapen-delei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana.13Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari nawenye nguvu. 14 Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo.15Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wakwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya,nawamejitolea kuwatumikiawatuwaMungu. Ninawasihininyi ndugu zangu, 16 muufuate uongozi wa watu kamahao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikiapamoja nao. 17Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunatona Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa

Page 33: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

1 WAKORINTHO 16:18 33 1 WAKORINTHO 16:24kutokuwako kwenu. 18 Wameiburudisha roho yangu nayenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namnahii. 19 Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula naPriskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbanimwao wanawasalimuni sana katika Bwana. 20 Nduguwote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa isharaya mapendo ya Mungu. 21 Mimi Paulo nawasalimuni,nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe. 22 Yeyoteasiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA —BWANA, njoo! 23 Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.24Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na KristoYesu.

Page 34: WARAKAWAKWANZAWAPAULOMTUME KWA WAKORINTHO · 1WAKORINTHO1:26 3 1WAKORINTHO2:6 za binadamu. 26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za

34Biblia Takatifu

Portions of the New Testament in the Swahili Language of Kenya,Mozambique, Somalia, and Tanzania, translation by Dr. Johann

Ludvig Krapf completed in 1850Public DomainLanguage: Kiswahili (Swahili)Dialect: KimvitaTranslation by: Dr. Johann Ludvig Krapf

2014-08-25PDF generated using Haiola and XeLaTeX on 11 Jan 2020 from source files dated 30 Dec201962071dc0-70e6-5b86-b569-c1b45e7771bd