mwongozo wa mafunzo kazini kwa walimu wa shule za sekondari … · mwongozo wa mafunzo kazini kwa...

50
1 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014

Upload: others

Post on 29-Mar-2021

41 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

Page 1: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI

SOMO LA KISWAHILI

MZUNGUKO WA KWANZA

AGOSTI 2014

Page 2: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

2

1.0 UTANGULIZI

Somo la Kiswahili ni miongoni mwa masomo ambayo yameonekana kuwa na changamoto

katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Katika kukabiliana na changamoto hizi Wizara ya

Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu wamefanya jitihada

za kuandaa miongozo ya masomo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwongozo wa Ufundishaji

wa Walimu Kazini wa Somo la Kiswahili.

Mwongozo huu umeandaliwa ili kuweza kuziba mapengo ya ufundishaji na ujifunzaji wa

baadhi ya mada za somo la Kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Mwongozo

umekusudiwa kutumika katika mzunguko wa kwanza kwa mafunzo ya walimu wa sekondari

wa somo la Kiswahili.

1.1 MALENGO

Mwongozo huu umeandaliwa kwa malengo yafuatayo:

Kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.

Kukabiliana na mada zenye changamoto.

Kuboresha stadi za upimaji.

Kuendeleza masomo yenye kuzingatia ujuzi unaomlenga mwanafunzi kwa kupata

uzoefu katika maisha ya kila siku.

1.2 MWONGOZO WA MAFUNZO

Mwongozo huu mafunzo kwa walimu kazini una jumla ya mada kuu nane (08) na mada ndogo

ndogo ambazo zimeonekana kuwa na mapengo katika kuielewa mada yenyewe, mbinu za

ufundishaji na ujifunzaji pamoja na zana za kufundishia miongoni mwa walimu.

Mada zinazoonesha mapengo husika zimepangwa katika mpangilio ufuatao:

Utangulizi: Hutegemea na mwezeshaji katika kutambulisha mada

Usuli: Huonyesha nia halisi au sababu katika kushughulikia tatizo.

Malengo mahususi: Kuonesha maarifa yanayotazamiwa baada ya kukamilika kwa mada

husika.

Shughuli: Hivi ni vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji.

Tafakuri: Maswali au kauli za kutaka kujua kama washiriki wamelewa mada husika na

jinsi wanavyoweza kuhawilisha maarifa na stadi walizopata katika ufundishaji na

ujifunzaji wao.

Upimaji na tathmini: Maswali yanayotoa mrejesho kuhusiana na shughuli zilizofanyika

kama zimeziba pengo/mapengo husika.

Page 3: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

3

Ufupisho: Maelezo mafupi kuhusiana na mada husika.

Marejeo: Orodha ya vitabu na vyanzo vinginevyo vya taarifa kuhusiana na mada husika.

Namna ya Kutumia Mwongozo

Mwongozo huu umekusudiwa kutumika kwa siku kumi za mafunzo ambapo kila siku ina

vipindi vitatu na kila kipindi kina saa zisizopungua mbili za ufundishaji na ujifunzaji. Urefu

wa mada husika ndio mwongozo wa wingi au uchache wa saa za ufundishaji na ujifunzaji.

Tanbihi: Wawezeshaji wanatakiwa:

Waandae kwanza mafunzo kabla ya uwezeshaji wenyewe.

Wahakikishe kuwa vifaa au zana zinazotakiwa kwa ajili ya mafunzo vinapatikana.

Page 4: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

4

2.0 MAANDALIZI KATIKA UFUNDISHAJI Utangulizi Maandalizi katika ufundishaji ni mpangilio au utaratibu wa ufundishaji kwa muda maalumu. Utaratibu huu unamwezesha mwalimu kupanga na kuchanganua mada kwa namna atakavyofundisha kipindi/vipindi vyake kwa wiki, mwezi au muhula. Maandalizi katika ufundishaji hujumuisha azimio la kazi, andalio la somo na shajara ya somo ambavyo hutumika kama dira ya mwalimu katika tendo zima la ufundishaji na ujifunzaji. 2.1 Azimio la Kazi Azimio la kazi ni moja kati ya zana muhimu katika maandalizi ya ufundishaji. Azimio la kazi huandaliwa kutokana na muhtasari wa somo husika. Azimio la kazi huwa na sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni taarifa tangulizi ambazo huusisha jina la halmashauri husika, jina la shule, jina la mwalimu, muhula, mwaka wa kuandaa, jina la somo na kidato husika. Sehemu ya pili huwa na vipengele ambavyo ni ujuzi, malengo, mwezi, wiki, idadi ya vipindi, mada kuu, mada ndogo, vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji, vifaa/ zana, rejea, upimaji na maoni. Aidha, azimio la kazi humwezesha mwalimu kubuni, kupanga na kutumia njia mbalimbali katika ufundishaji wake kwa kuzingatia mada na vifaa vinavyohitajika. Usuli Utafiti unaonesha kuwa idadi kubwa ya walimu huwa na maandalizi finyu katika ufundishaji. Moja kati ya maandalizi hayo ni Azimio la kazi. Walimu hao wanakosa stadi na maarifa katika kuandaa azimio la kazi na mara nyingine hufikia uamuzi wa kukwepa kuandaa, na kufanya ufundishaji na ujifunzaji kuwa duni. Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze:

(a) Kubainisha vipengele muhimu vya Azimio la Kazi. (b) Kuandaa Azimio la Kazi.

Muda: saa 4 Mahitaji Muhtasari wa somo, kalenda ya mwaka na kalenda ya shule, kalamu, rula, karatasi za kuandikia, manila, bango kitita, kalamu ya wino mnene. Shughuli 1 Katika vikundi vya washiriki kumi kumi:

(a) Waeleze maana ya Azimio la Kazi (b) Wabainishe vipengele muhimu vya Azimio la Kazi.

Page 5: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

5

Shughuli 2. Katika vikundi vipya vya washiriki kumi kumi waandae:

(a) Azimio la Kazi la wiki. (b) Azimio la Kazi la mwezi. (c) Azimio la Kazi la muhula.

Washiriki wanatakiwa kuwasilisha kila baada ya kila shughuli iliyotolewa na mwezeshaji

awaongoze katika majadiliano.

Page 6: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

6

MANISPAA YA MOROGORO SHULE YA SEKONDARI KILAKALA

Jina la Mwalimu……………………….. Somo…………………………………… Darasa…………………………………. Muhula…………………………………. Mwaka…………………………………. MUUNDO WA AZIMIO LA KAZI

UJU

ZI

MA

LE

NG

O

MW

EZ

I

WIK

I

IDA

DI

YA

VIP

IND

I

MA

DA

KU

U

MA

DA

ND

OG

O

VIT

EN

DO

VY

A

UF

UN

DIS

HA

JI

VIT

EN

DO

VY

A

UJI

FU

NZ

AJI

VIF

AA

/

ZA

NA

RE

JEA

UP

IMA

JI

MA

ON

I

Kutumia vitenzi vishirikishi katika miktadha mbalimbali

Mwanafunzi aweze: kubainisha vitenzi vishirikishi katika sentensi

Agosti

2

3 AINA ZA MANENO

Vitenzi vishirikishi

Kwa kutumia njia ya maswali na majibu kuwaongoza wanafunzi wataje na watumie vitenzi vishirikishi katika kuunda tungo mablimbali.

Kushiriki kwa pamoja katika kutaja na kuvitumia vitenzi vishirikishi katika tungo mbalimbali.

Ufaraguzi wa zana, migomba tawi la miti, Matini, chati/kadi za maneno

Kiswahili Kitukuzwe -Kiswahili Sekondari (Taasisi ya Ukuzaji Mitaala) -Kiswahili 1 Kidato

Je mwanafunzi ameweza kubaini na kuvitumia vitenzi vishirikishi katika tungo?

Page 7: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

7

cha 1 (TET)

Tafakuri: Elezea jinsi gani azimio la somo linavyoweza kumsaidia mwalimu katika mchakato mzima wa ufundishaji. Upimaji: Je kutokuandaa azimio la kazi kunaweza kuathiri kazi ya ufundishaji? Kwa nini?

Page 8: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

8

Hitimisho: Kwa kifupi vipengere vya azimio la kazi vinajiainisha kama ifuatavyo:

1. Ujuzi: Stadi, maarifa na muelekeo ambao hutegemewa kujengwa kwa mwanafunzi baada ya kumaliza ujifunzaji wa mada husika.

2. Malengo: Mambo muhimu yanayotajariwa kwa mjifunzaji kuyapata kutokana na mada itakayofundishwa.

3. Mwezi: Jina la mwezi ambao mada husika itafundishwa.

4. Wiki: Wiki katika mwezi ambayo mada itafundishwa.

5. Vipindi: Idadi ya vipindi vitakavyofundishwa kwa mada husika.

6. Mada Kuu: Mada kuu husika iliyopo kwenye muhtasari wa somo.

7. Mada ndogo: Mada ndogo inayotokana na mada kuu ambayo nayo ipo kwenye muhtasari wa somo.

8. Vitendo vya ufundishaji: Taarifa zinazomwelekeza mfundishaji vitendo atakavyofanya ili wajifunzaji waweze kuelewa mada husika inayofundishwa. Mfano wa vitendo hivyo ni kama vile kuuliza maswali, kutoa maelezo, kufanya maonesho na kuwapa kazi katika vikundi.

9. Vitendo vya ujifunzaji: Vitendo vinavyofanywa na mjifunzaji ili kukidhi maelekezo ya mfundishaji. Mfano wa vitendo hivyo ni kujibu maswali, kufanya kazi kwenye vikundi, kuwasilisha, kufanya mazoezi n.k.

10. Vifaa/Zana za kufundishia na kujifunzia: Vifaa/zana mbalimbali zinazosaidia katika zoezi la ufundishaji na ujifunzaji.

11. Rejea: Vitabu ambavyo mfundishaji anavitumia katika uandaaji wa mada husika.

12. Upimaji: Maswali yote yanayoulizwa ili kujua kama mada iliyofundishwa imeeleweka.

13. Maoni: Taarifa inayotolewa na mfundishaji kuhusu mada husika kama imefanikiwa na changamoto pamoja na kutoa mapendekezo katika kuboresha ufundishaji.

Marejeo TET (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya Kujifunzia Ufundishaji wa

Somo la Kiswahili: Dar es Salaam. TET (2013). Diploma ya Ualimu: Moduli: Ufundishaji wa Somo la Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari: Dar

es Salaam. Wizara ya Elimu na Utamaduni (2005). Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini Daraja la IIIC/B –

IIIA: Moduli ya Somo la Ufundishaji: Dar es Salaam Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (2010). Muhtasari wa Kiswahili kwa Shule za Sekondari

Kidato cha I-IV: Dar es Salaam 2.2 Andalio la Somo

Page 9: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

9

Andalio la Somo ni mpango wa kazi wa muda mfupi unaotumika kwa kipindi kimoja au viwili. Mpango huu huandaliwa na mfundishaji ili umwezeshe kufundisha somo lake hatua kwa hatua na kwa mafanikio. Usuli Uzoefu unaonesha kwamba kuna maandilizi na matumizi hafifu ya Andalio la Somo kwa wafundishaji wengi katika ufundishaji, hivyo kupelekea kutokuwa na ufanisi katika shughuli nzima ya ufundishaji na ujifunzaji wa somo husika. Hali hii inatokana na wafundishaji ama kutoelewa umuhimu wake au kutokuwa na maarifa ya kutosha kuhusu uandaaji wa Andalio la Somo. Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada hii, mshiriki aweze:

(a) Kubainisha vipengele muhimu vya Andalio la Somo. (b) Kuandaa Andalio la Somo.

Muda: Saa 3 Mahitaji Azimio la Kazi, kalamu, rula, karatasi za kuandikia, manila, bango kitita, kalamu ya wino mnene. Shughuli 1 Katika vikundi vya washiriki kumi kumi:

(a) Waeleze maana ya Andalio la Somo (b) Wabainishe vipengele muhimu vya Andalio la Somo.

Shughuli 2. Katika vikundi vipya vya washiriki kumi kumi waandae:

(a) Andalio la Somo la kipindi kimoja na kuwasilisha. (Tumia mada ya Aina za Maneno) (b) Andalio la Somo la vipindi viwili na kuwasilisha. (Tumia mada ya Aina za Maneno)

Tafakuri Je, kuna umuhimu gani kutumia Andalio la Somo katika ufundishaji? Upimaji Eleza vipengele mbalimbali vinavyozingatiwa katika uandishi wa andalio la somo. Hitimisho Ili kuwa na ufanisi zaidi katika mchakato wa ufundishaji mwalimu hana budi kuandaa na kutumia andalio la somo kwakuwa humfanya:

(a) Kufundisha kwa mtiririko ulio bora hivyo kufanya somo lieleweke kwa urahisi.

Page 10: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

10

(b) Kujiamini. (c) Kutumia muda vizuri.

MFANO WA ANDALIO LA SOMO

SEHEMU YA KWANZA: TAARIFA ZA AWALI Sehemu hii inajumuisha tarehe ya siku husika ya kipindi, darasa, kipindi, muda wa kipindi/vipindi na idadi ya wanafunzi katika darasa (walioandikishwa -ke/Me, waliohudhuria-Ke/Me).

Tarehe Darasa Kipindi/vipindi Muda Idadi ya wanafunzi

Walioandikishwa Wasiohudhuria

ME KE Jumla ME KE Jumla

Sehemu hii pia ina vipengele vifuatavyo:

i. Ujuzi: Ni kauli/maelezo kuhusu stadi, maarifa na muelekeo ambao mjifunzaji huyapata

baada ya ujifunzaji wa mada husika. Ujuzi unaweza kupatikana baada ya vipindi kadhaa

vya mada husika kulingana na Muhtasari wa Somo.

Mfano: Baada ya kukamilika mada mjifunzaji aweze:

Kutumia vitenzi vishirikishi katika miktadha mbalimbali.

ii. Mada Kuu: Huonesha mada kuu itakayofundishwa kwa siku/wiki au mwezi. Mada hii

inaweza kufundishwa zaidi ya kipindi kimoja.

iii. Mada Ndogo: Mada hii iko chini ya mada kuu husika inayotakiwa kufundishwa.

iv.

v. Lengo kuu: Ni maarifa anayotarajiwa kuyapata mjifunzaji baada ya ufundishaji wa mada

husika.

vi. Malengo Mahususi: Maarifa au stadi mahususi anazotarajiwa kuzipata mjifunzaji baada

ya ufundindishaji. Mfano: Baada ya somo mjifunzaji aweze kubainisha aina ya vitenzi

vishirikishi.

vii. Zana za kufundishia na kujifunzia: Orodha ya zana za kufundishia ambazo zitatumika

katika kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa mada husika.

viii. Marejeo: Orodha ya vitabu vya rejea, ziada na kiada anavyotumia mfundishaji katika

kuandaa na kufundisha mada ndogo husika.

SEHEMU YA PILI: HATUA ZA SOMO

Sehemu hii inajumuisha hatua zifuatazo:

Page 11: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

11

i. Utangulizi: Unaonesha mambo yatakayofanyika mwanzo wa kipindi au somo. ii. Maarifa Mapya: Kipengele hiki kinaelezea shughuli za ufundishaji na ujifunzaji ambazo

zitamjee mjifunzaji maarifa/ujuzi mpya. iii. Kukazia Maarifa: Kipengele hiki kinahusika na shughuli ambazo zitamfanya mjifunzaji

awe na kumbukumbu ya mada iliyofundishwa. iv. Tafakuri: Kipengele hiki kinapima mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji na

kutafakari kile walichojifunza kwa jinsi ya kukitumia katika maisha yao ya kila siku. v. Hitimisho: Kipengele hiki kinamhusu mfundishaji kutoa hitimisho la somo alilofundisha

kama malengo yamefikiwa na ikiwa hayajafikiwa atoe ufafanuzi zaidi.

HATUA

MUDA VITENDO VYA UFUNDISHAJI

VITENDO VYA UJIFUNZAJI

VITENDO VYA UPIMAJI

Utangulizi

Maarifa mapya Kuimarisha maarifa

Tafakuri Hitimisho

SEHEMU YA TATU: TATHMINI NA MAONI

i. Tathmini ya wanafunzi: Mfundishaji anaangalia mabadiliko ya wanafunzi kama wameelewa mada husika.

ii. Tathmini ya Mwalimu: Mwalimu hujitathmini mwenyewe kutokana na tathmini ya wanafunzi.

iii. Maoni: Taarifa inayotolewa na Mwalimu kuhusu mada ndogo kama imefanikiwa au haikufanikiwa na kutoa mapendekezo.

Mfano wa Andalio la Somo la mfano

Tarehe

Darasa Somo Vipindi

Muda Idadi ya wanafunzi

26/08/2014

Kidato cha IB

Kiswahili

1&2 02:00-3:20 asubuhi

Waliosajiliwa Waliohudhuria

KE ME

JUMLA

KE ME JUMLA

20 28 48 15 20 35

Ujuzi: Uwezo wa kutofautisha matumizi ya aina mbalimbali za maneno katika miktadha tofauti.

Page 12: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

12

Mada Kuu: AINA ZA MANENO. Mada ndogo: Ubainishaji wa aina za maneno. Lengo kuu: Kubainisha matumizi sahihi ya maneno katika tungo mbalimbali za Kiswahili. Malengo mahususi: Baada ya kumalizika kwa mada hii mwanafunzi aweze:

a) kubainisha aina saba (7) za maneno. b) kutofautisha aina mbalimbali za maneno katika tungo.

Zana/vifaa: Chati za ukutani za aina za maneno na ufafanuzi wake, vitu halisi, chati ya sentensi mbalimbali. Rejea: Kiswahili kidato cha kwanza, TET (2006)

Page 13: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

13

HATUA ZA SOMO

HATUA MUDA

SHUGULI ZA UFUNDISHAJI SHUGHULI ZA UJIFUNZAJI

TATHMINI

1. Utangulizi Kuuliza maswali mafupi mafupi kwa mdomo kuhusu somo lililopita

Kujibu maswali hayo kwa mdomo

Kuchunguza kama mwanafunzi anaweza kujibu maswali hayo kwa usahihi.

2. Maarifa mapya

a) Kuwaongoza wanafunzi kutunga sentensi mbalimbali kwa kutumia vitu halisi.

b) Kuwaongoza wanafunzi

katika jozi kubaini maneno (yaani: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kihisishi, kiwakilishi na kiunganishi) kwa kutumia chati ya sentensi mbalimbali.

a) Kutunga sentensi mbalimbali kwa kutumia vitu halisi.

b) Kubaini maneno

(yaani: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kihisishi, kiwakilishi na kiunganishi) kwa kutumia chati ya sentensi mbalimbali.

Kuchunguza kama wanafunzi wameweza kutunga sentensi hizo. Kuchunguza kama mwanafunzi wameweza kubaini aina saba (7) za maneno.

3.Kukazia maarifa

Kuwaongoza wanafunzi katika makundi kuchora chati za ukutani na kubainisha aina za maneno.

Kuchora chati za ukutani na kubainisha aina za maneno.

Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kubainisha aina za maneno kwa usahihi.

4.Tafakuri

Kutoa zoezi kwa wanafunzi la kubainisha maneno katika sentensi na kusahihisha.

Kufanya zoezi la kubainisha maneno katika sentensi kwa kuandika.

Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kubainisha maneno katika sentensi.

5.Hitimisho Kuuliza maswali ya mdomo kwa wanafunzi juu ya somo na kutoa ufafanuzi panapohitajika.

Kujibu maswali kwa mdomo, na kuuliza maswali kwa mdomo juu ya somo hasa panapohitaji ufafanuzi.

Kuchunguza kama mwanafunzi ameweza kijibu maswali kwa usahihi.

Page 14: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

14

Tathmini ya wanafunzi: …………………………………………….…………….…………………………………………………………………..

Tathmini ya mwalimu: ………………………………………………………………………………………………………………………………..

Maoni: ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………

Page 15: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

15

Marejeo TET (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya Kujifunzia Ufundishaji wa

Somo la Kiswahili: Dar es Salaam. TET (2013). Diploma ya Ualimu: Moduli: Ufundishaji wa Somo la Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari: Dar es Salaam.

Wizara ya Elimu na Utamaduni (2005). Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini Daraja la IIIC/B –

IIIA: Moduli ya Somo la Ufundishaji: Dar es Salaam Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (2010). Muhtasari wa Kiswahili kwa Shule za Sekondari

Kidato cha I-IV: Dar es Salaam 2.3 Shajara ya Somo Shajara ni kitabu kinachoandikwa kumbukumbu za mada zilizofundishwa kwa siku husika kulingana na Azimio la Kazi. Kitabu hiki ni cha mfundishaji ambamo huandika maendeleo ya somo lake kila mara anapomaliza kufundisha. Matumizi ya shajara ya somo husaidia katika kuepuka kurudia mada ambazo zimekwishafundishwa na kuonesha maendeleo ya ufundishaji. Aidha, shajara humwezesha mwalimu mwingine kuendelea na ufundishaji iwapo mwalimu husika hatakuwapo.

Usuli Katika ufundishaji na ujifunzaji imeonekana kuwa walimu wanafundisha lakini hawazingatii kuweka kumbukumbu za mada walizozifundisha na lini walizifundisha. Tatizo huenda ni kutokana na kutotambua umuhimu wake au kutojua namna ya kuiandaa ikiwa ni pamoja na kujua vipengele muhimu vinavyounda shajara ya somo. Kutokana na changamoto hizo sehemu hii itaeleza umuhimu pamoja uandaaji wake kulingana na azimio la kazi.

Malengo mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: i. Kubaini vipengele vya Shajara ya Somo ii. kubaini vipengele vya Azimio la Kazi vinavyotakiwa kuingia katika Shajara ya Somo iii. kuandaa Shajara ya Somo Muda: saa 3 Mahitaji Kadi za manila, rula, kalamu za wino mnene, matini ya shajara, madaftari, Azimio la Kazi, Andalio la Somo.

Shughuli 1 Katika vikundi vya washiriki kumi kumi wafanye yafuatayo:

Page 16: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

16

(a) Kubainisha vipengele vya Shajara ya Somo na kuwasilisha. (b) Kubainisha vipengele vya Azimio la Kazi vitakavyoingia kwenye Shajara ya Somo na kuwasilisha

Mwezeshaji aongoze majadiliano kwa kila wasilisho. Shughuli 2 Katika vikundi vipya vya washiriki kumi kumi waandae Shajara ya Somo katika mada zifuatazo:

(a) Aina za Maneno. (b) Mawasiliano. Tafakuri Kutokana na shughuli ya uandaaji wa shajara uliyopewa je, kuna maarifa zaidi uliyopata ya kutengeneza shajara? fafanua

Upimaji Je, washiriki wameweza kuandaa shajara ya somo kwa kuzingatia Azimio la Kazi? Linganisha maaarifa ya awali ya kuandaa shajara na maarifa mapya uliyoyapata. Toa maoni yako

Hitimisho Katika uandaaji wa shajara ya somo, mwalimu azingatie yafuatayo:

Mwezeshaji awaelekeze washiriki watumie vifaa rahisi na visivyo na gharama kubwa vinavyopatikana kwenye mazingira yake kama vile madaftari, bila kulazimika kwenda kutafuta katika maeneo mengine ya mbali au vyenye gharama kubwa.

Mshiriki azingatie muundo ufuatao katika uandaaji wa Shajara ya Somo:

Page 17: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

17

Mwezi Wiki Mada Kuu

Mada Ndogo

Tarehe ya Kuanza

Tarehe ya Kumaliza

Ujuzi uliofundishwa

Saini na Maoni ya mwalimu wa somo

Saini na Maoni ya Mkuu wa Idara

Saini na Maoni ya Mkuu wa shule

Agosti 2 Aina za Maneno

Vitenzi Vishirikishi

11 Agosti 2014

15 Agosti 2014

Kubainisha aina ya vitenzi vishirikishi

B.Lyimo Mada imeeleweka vizuri

A. Faustin Mada imefundishwa vizuri

H. Jacob Mada imefundishwa

Ufafanuzi: Mwezi: Mwezi ambao mada imefundishwa Wiki: wiki ya ngapi Mada Kuu: Mada kuu husika iliyofundishwa Mada ndogo: Mada ndogo iliyofundishwa ambayo ni kipengele kidogo katika mada kuu Tarehe ya kuanza: Tarehe ambayo mada ilianza kufundishwa Tarehe ya kumaliza: Tarehe ambayo mada ilimalizika kufundishwa Ujuzi uliofundishwa: Uwezo na stadi zilizopatikana baada ya kufundisha mada husika Saini na maoni ya mwalimu wa somo: Saini na kauli ya mwalimu juu ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mada iliyofundishwa na mikakati ya kuboresha maeneo dhaifu.

Saini na maoni ya mkuu wa idara: Saini na kauli ya Mkuu wa Idara juu ya ufundishaji wa mada husika pamoja na maoni ya mwalimu

Saini na maoni ya mkuu wa shule: Saini na kauli ya Mkuu wa Shule juu ya ufundishaji wa mada husika pamoja na maoni ya mwalimu wa somo na Mkuu wa Idara.

Page 18: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

18

Marejeo TET (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya Kujifunzia Ufundishaji wa

Somo la Kiswahili: Dar es Salaam. TET (2013). Diploma ya Ualimu: Moduli: Ufundishaji wa Somo la Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari: Dar es Salaam.

Wizara ya Elimu na Utamaduni (2005). Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini Daraja la IIIC/B –

IIIA: Moduli ya Somo la Ufundishaji: Dar es Salaam Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (2010). Muhtasari wa Kiswahili kwa Shule za Sekondari

Kidato cha I-IV: Dar es Salaam 2.4 Zana za Kufundishia na Kujifunzia

Zana za kufundishia na kujifunzia ni nyenzo muhimu sana katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ili kurahisisha kueleweka kwa somo. Zinasaidia kuamsha ari ya kujifunza na kujenga kumbukumbu kwa mwanafunzi. Zana hutayarishwa kabla ya kuzipeleka darasani na ni jukumu la mwalimu kusimamia shughuli nzima ya uandaaji wa zana. Aidha, zana hizo zinaweza kuandaliwa na mwalimu au mwanafunzi. Zana zinaweza kuwa za kutengeneza, kufaragua au vitu halisi kulingana na mada ya somo pamoja na mazingira.

Usuli Uzoefu unaonesha kwamba baadhi ya walimu hawatumii zana katika ufundishaji. Jambo hili linaathiri uelewa wa somo hivyo wanafunzi kutopata ujuzi uliokusudiwa. Aidha, Kutotumia zana za kufundishia kunasababisha walimu kutowashirikisha wanafunzi kikamilifu wakati wa somo, hali hii huchangia wanafunzi kutofurahia somo. Hivyo basi, walimu wanatakiwa kutumia zana za kufundishia na kujifunzia ili kufanya somo kueleweka kwa urahisi.

Malengo mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: (a) Kubaini umuhimu wa kutumia zana (b) kuandaa zana (c) kutumia zana kikamilifu Muda: saa 7 Mahitaji: Kadi za manila, tawi la mti, viboksi, kamba, kalamu za rangi, karatasi, kalamu za wino na kalamu za risasi, flip charts, kopo/ndoo, mchanga na gundi.

Shughuli ya 1

Kwa kutumia vikundi vya watu 5 mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kujadiliana kuhusu umuhimu wa kutumia zana.

Page 19: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

19

(b) Kuwasilisha hoja za vikundi. Shughuli ya 2 Kwa kutumia kazi za vikundi mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kufikiria na kufafanua ni zana gani wangetumia katika kufundisha mada zifuatazo: Mofimu, rejesta, ngeli za nomino, insha ya hoja, insha ya wasifu, vivumishi, viwakilishi, vielezi, majigambo na methali.

(b) Kuwasilisha kazi ya vikundi. Shughuli ya 3 Mwezeshaji awaongoze washiriki katika makundi ya watu kumikumi kutoka kila kikundi cha awali:

(a) Kujadili changamoto zilizojitokeza katika kuandaa zana walizotumia. (b) Kuwasilisha kazi walizojadili.

Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo:

(a) Je ulichojifunza katika mada hii kitakusaidia nini katika ufundishaji wako wa kila siku? (b) Baada ya kujifunza mada hii ni mambo gani unataka yaboreshwe? Upimaji Je ni kila mada ina zana za kufundishia? Ufupisho Mfano wa jinsi ya kuandaa zana za kufundishia mada ya vitenzi vishirikishi: (a) Andaa tawi la mti lenye vitawi vidogo 6. (b) Kata vipande vya boksi 6. (c) Chukua kamba za mgomba. (d) Umba herufi mbalimbali kwa kutumia kamba za mgomba. (e) Kila kiboksi andika neno moja kati ya haya yafuatayo, alikuwa, nina, yu, ni, ki na lipo. Paka gundi katika herufi zilizo kwenye kila neno uliloandika kwenye kiboksi kisha bandika herufi zilizoundwa na kamba za mgomba.

(f) Toboa viboksi vyenye maneno sehemu mbili za juu. (g) Chukua kamba na uiingize kwenye matobo ya viboksi. (h) Funga katika kila tawi. (i) Jaza mchanga kwenye ndoo/kopo. (j) Chomeka mti kwenye ndoo/kopo. (k) Andika neno vitenzi vishirikishi kwenye ndoo/kopo. (l) Hakikisha kila neno linasomka vizuri.

Page 20: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

20

Mfano wa jinsi ya kuandaa zana za kufundishia muundo wa shajara ya somo:

(a) Andaa herufi zilizoumbwa vizuri kwa kutumia rula, kalamu ya wino au ya risasi na karatasi.

(b) Andaa boksi na kipande cha gunia la nailoni kinachotosha muundo wa shajara ya somo.

(c) Funika kipande cha boksi ulichokata kwa kipande cha nailoni kwa kutumia gundi ya mbao.

(d) Chora muundo wa shajara ya somo kwa kalamu na zingatia maneno unayohitaji.

(e) Rudia ili kukoleza herufi za maneno hayo kwa kutumia kalamu ya rangi.

(f) Weka gundi kufuatisha maneno uliyoandika.

(g) Weka uwele, ulezi, mchanga au maharage kutegemeana na maneno uliyoyaumba.

(h) Pindua boksi lako ili umwage uwele, ulezi, mchanga au maharage uliotumia kwenye chombo au sehemu nyingine kwa matumizi mengine.

(i) Rekebisha herufi/maneno ili yasomeke vizuri.

Marejeo Taasisi ya Elimu (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya Kujifunzia

Ufundishaji wa Somo la Kiswahili. Dar es Salaam -TET. Wizara ya Elimu na Utamaduni (2005). Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini Daraja la IIIc/B-IIIA:

Moduli ya Somo la Ufundishaji. Dar es Salaam- Wizara ya Elimu. 2.5 MBINU ZA KUFUNDISHIA Utangulizi Mbinu ni njia ambazo mwalimu anazitumia katika ufundishaji. Miongoni mwa mbinu hizo ni kuwagawa wajifunzaji kwenye vikundi, igizo mbinu, ziara, mazoezi ya kurudiarudia, changanyakete, „KWL‟ mhadhara, kumwalika mgeni, masimulizi na ziara tembezi. Njia hizi huwezesha suala zima la ufundishaji na ujifunzaji kufanyika kwa ufanisi. Ili kuweza kukidhi haja na matakwa ya ufundishaji wa mada zozote, mbinu anuai zinahitajika zitakazomwezesha mwalimu aweze kufundisha mada kwa ustadi. Mbinu bora za ufundishaji zinajumuisha uwezo wa mwalimu kutumia mbinu hizo ili kuweza kuwasilisha mada husika vizuri. Mbinu hizo zinatakiwa ziendane na vionjo vya ufundishaji na ujifunzaji ili kuweza kukidhi malengo ya mada husika. Mbinu za kufundishia uandishi wa Insha Insha ni maandishi au maneno yaliyotungwa kwa mtindo wa nathari juu ya jambo fulani. Insha huandikwa katika muundo wa aya mbalimbali ambazo zimegawanyika katika sehemu kuu tatu: utangulizi, kiini na hitimisho. Usuli

Page 21: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

21

Ufundishaji wa mada hii umekuwa ni tatizo kutokana na walimu wengi kukosa mbinu mbalimbali za kuweza kufundisha uandishi wa insha. Aidha imeonekana kuwa, kuna tatizo katika kuteua mbinu sahihi za kufundishia uandishi wa insha shuleni. Kitendo hiki kimefanya ufundishaji na ujifunzaji kuwa mgumu hata kusababisha mada kutofundishwa vizuri. Mada hii itabainisha na kueleza baadhi ya mbinu za ufundishaji wa uandishi wa insha. Malengo mahususi Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze:

(a) Kubaini mbinu za ufundishaji uandishi wa insha. (b) Kufafanua mbinu mbalimbali za kufundishia uandishi wa insha. (c) Kutumia mbinu mbalimbali katika kuandika insha.

Muda: saa 4 Mahitaji Kielelezo cha muundo wa insha, matini za mifano ya insha, zana faraguzi za muundo wa insha, kadi za manila, kalamu za rangi za wino mzito, vigunia vya nailoni, maharage, ulezi, uwele, mtama, gundi ya mbao na karatasi. Shughuli 1 Katika vikundi vya watu kumikumi washiriki:

(a) Wabainishe mbinu za ufundishaji uandishi wa insha na kuwasilisha. (b) Wafafanue mbinu za ufundishaji uandishi wa insha.

Shughuli 2 Katika vikundi vya watu kumikumi washiriki watumie mbinu tofauti katika uandishi wa insha. Tafakuri Je, ni maarifa gani mapya umeyapata katika mbinu za kufundishia uandishi wa insha? Upimaji Je, mshiriki ameweza kufundisha uandishi wa insha kwa kutumia mbinu sahihi? Hitimisho Mbinu za kufundishia insha ni nyenzo muhimu katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Miongoni mwa mbinu zinazoweza kutumika ni kama zifuatazo: Mbinu ya maswali na majibu Njia hii hutumika kufundishia somo kwa mahojiano. Hatua:

kuuliza maswali kuhusu insha. Mf. Insha ina sehemu ngapi? Majibu yatolewa kutegemea uelewa. Maswali mengine yaulizwe kutokana na jibu lililotolewa ili kuendeleza mada ya

uandishi wa insha.

Page 22: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

22

Ikiwa jibu litakuwa tofauti, swali hilo liulizwe kwa njia nyingine. Kuhakikisha kuwa wengi wanashiriki katika kujibu. Kuwepo na fursa ya kujadiliana au kuuliza maswali

Mbinu hii ni shirikishi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji na husaidia kuibua maarifa na ubunifu kwa wanaojifunza. Mbinu ya Majadiliano Hii ni mbinu inayolenga uchangiaji wa mada fulani. Wanaojifunza ndio wanaohusika katika kuchangia mada hiyo na kila mmoja anakuwa na uhuru wa kuchangia kulingana na jinsi anavyoelewa mada. Maoni na maarifa ya wengi yanakusanywa kutokana na majibu ya kila mchangiaji. Majadiliano yanaweza kutokana na picha, mchoro, ziara, tukio fulani, kauli fulani kama vile methali ya asiyesikia la mkuuu huvunjika guu. Mfano 1: Jinsi ya kutumia picha katika kuandika insha

Wachunguze kwa makini picha waliyopewa. Wabainishe mambo muhimu yanayojitokeza katika picha hiyo. Waeleze ujumbe uliowasilishwa na picha hiyo kabla ya kuanza kuandika kwa sababu

wakikosea katika hatua hii kuna uwezekano wa kuandika kisa kisichofaa. Waandike insha ambayo inaweza kuyaeleza matukio yaliyopo kwenye picha hiyo. Hakikisha kuwa mambo yote yanayowasilishwa kwenye picha hiyo kama vile maandishi

au rangi yanashirikishwa katika insha inayoandikwa. Zingatia uteuzi mzuri wa lugha (sanifu) ambayo husaidia kuleta mvuto kwa msomaji. Kufuata kanuni za uandishi wa insha.

Mbinu ya Ziara Ziara ni kutembelea mahali maalumu kwa lengo la kujifunza jambo fulani la kielimu. Ili ujifunzaji ufanikiwe, lazima mshiriki aandae madodoso au maswali ya mwongozo kuhusiana na jambo wanalotakiwa kujifunza. Ziara inaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu- saa moja au zaidi. Mbinu hii ina manufaa katika ujifunzaji kwa sababu huwapa washiriki uwezo wa kudadisi na kugundua mambo mengi wenyewe kutokana na kutumia milango yote ya maarifa ambayo ni kuona, kusikia, kugusa, kunusa na kuonja. Mfano 2: Jinsi ya kutumia mbinu ya ziara katika kuandika insha

Kuteua mada: Mfano mada ya Vyombo vya Kukuza na Kuendeleza Kiswahili Tanzania. Kuteua eneo la ziara: Mfano BAKITA, TATAKI, BAKIZA. Kupata taarifa kabla kuhusiana na eneo la ziara ili kujua kama malengo ya mada husika

yatafanikiwa. Mfano: ili kufanikisha ziara mshiriki aende au awasiliane na uongozi kuangalia kama mada iliyopo hapo juu inaweza kukidhiwa na ofisi za BAKITA, TATAKI au BAKIZA.

Kutayarisha maswali ya mwongozo. Mfano: Je, kuna vyombo vingapi vya kukuza na kuendeleza Kiswahili nchini Tanzania? au Kazi za vyombo hivyo ni zipi?

Kugawanya kundi kubwa katika makundi madogo madogo ya watu wanne. Kila kundi lielekezwe maswali ya kuuliza ili lipate fursa ya kuuliza maswali na

kufafanua jambo kulingana na ziara hiyo:

Page 23: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

23

Tanbihi: Insha iandikwe kwa kuzingatia sehemu kuu tatu: utangulizi, kiini na hitimisho. Marejeo TET (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya Kujifunzia Somo

la Kiswahili. Dar es Salaam. Wamitila, K.W. (2007). Mwenge wa Uandishi: Mbinu za Insha na Utunzi. Vide-Muwa

Publishers Limited. Nairobi

3.0 USHAIRI

Utangulizi Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha ya mkato kuwasilisha ujumbe katika jamii. Ushairi umegawanyika katika Nyimbo, Mashairi, utenzi na ngonjera. Mada hii itashughulikia uhakiki wa mashairi katika kipengele cha muundo na mtindo na utungaji wa ngonjera.

3.1 Uhakiki wa Muundo katika Mashairi. Muundo wa shairi ni mjengo wa shairi yaani mpangilio wa vina, mizani, idadi ya beti, mistari katika beti, vipande na vituo. Muundo unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa. . Usuli Muundo ni miongoni mwa vipengele vya fani vinavyotumika katika uhakiki wa mashairi. Kipengele hivi kinawakanganya walimu wengi katika ufundishaji wa mada ya uhakiki wa mashairi. Walimu kutokuwa na maarifa ya kutosha ndiko kunakosababisha kutofundisha dhana hii ipasavyo na baadhi yao kuegemea katika matumizi ya tahakiki zilizoandaliwa na watu mbalimbali. Mada hii ni muhimu kwani itamwezesha mfundishaji kuwa na maarifa ya kutosha katika kuhakiki muundo wa mashairi.

Malengo mahususi Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze (a) Kubainisha vipengele vinavyojenga muundo wa shairi ambavyo ni idadi ya mistari katika beti

(mishororo), vina, mizani, idadi ya beti, kipande na vituo. (b) Kuhakiki muundo wa shairi kwa kuzingatia idadi ya mistari katika beti (mishororo, vina,

mizani, idadi ya beti na vituo. Muda: Saa 4 Mahitaji: Vitabu vya mashairi, magazeti yenye mashairi, matini zenye mashairi mbalimbali. Shughuli 1 Kwa kutumia makundi ya watu watanowatano mwezeshaji atumie nakala/vitabu mbalimbali

vya mashairi kuwaongoza washiriki:

Page 24: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

24

(a) Kueleza maana ya muundo katika mashairi. (b) Kubaini vipengele vya muundo katika mashairi. (c) Kufafanua vipengele vya muundo katika mashairi. Shughuli 2 Kwa kutumia mbinu ya changanya kete mwezeshaji awaongoze washiriki (vikundi vya watu

watano watano) (a) Kuhakiki vipengele vya muundo kwa kuzingatia mashairi waliyopewa.

(b) Kuwasilisha hoja za majadiliano.

Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo:

(a) Ni maarifa gani mapya umeyapata. (b) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo. (c) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo.

Upimaji Je mshiriki ameweza kubainisha vipengele vya muundo na kuhakiki mundo katika mashairi? Ufupisho Vipengele vya muundo ni kama ifuatavyo:

Vina: Ni silabi/mizani inayofanana ya kati na ya mwisho au pengine ya mwisho tu katika kila mstari wa beti. Yaweza kuwa na vina vitatu au zaidi katika mstari mmoja wa beti.

Mizani: Ni idadi ya silabi zilzomo katika mstari wa beti. Katika shairi ndizo zinazoleta urari wa mapigo. Kwani kila mstari unatakiwa uwe na mizani sawa na mstari mwingine. Wakati mwingine mstari wa mwisho huwa na nusu ya mizani ya mstari.

Mistari (mishororo): Ni mistari inayojitokeza kwa kila ubeti. Shairi lawza kuwa na mistari miwili (tathniya), mistari mitatu (tathlitha), mistari minne (tarbia), mistari mitano (takhmisa) na mistari sita na kuendelea (sabilia).

Beti: Ni kifungu chenye kuleta maana kamili katika jumla ya vifungu vilivyomo katika utungo. Shairi linaweza kuwa na ubeti mmoja, mbili au zaidi.

Kituo: ni mstari wa mwisho katika kila ubeti wa shairi. Kinaweza kuwa, kibwagizo/kituo baharí, nusu baharí au kimalizio. Kinaweza kuwa na vina tofauti na vya mistari ya juu.

Kipande: Ni sehemu mojawapo katika sehemu mbili au zaidi kwa kila mstari

3.2 Uhakiki wa Mtindo katika Mashairi

Page 25: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

25

Mtindo wa shairi jinsi/namna yaani ufundi wa kipekee wa mtunzi ambao utofautiana kati ya mtunzi mmoja na mwingine. Inaweza kusemwa kuwa mtindo ni yale mambo ambayo mtunzi ameyafanya kwa ubunifu wake na si kwa kuwa yapo katika kanuni. Usuli Uhakiki wa mtindo wa mashairi umekuwa na changamoto kubwa sana kwa kuwa walimu wengi wanashindwa kutambua upi hasa ni mtindo wa shairi. Hii ni kutokana na kuwepo kwa tahakiki nyingi zinazoeleza kwa namna isiyosahihi kuhusu mtindo wa mashairi, tahakiki hizo hueleza kuwa mtindo ni wa kimapokeo na kisasa. Hivyo mada hii imeandaliwa ili kuwawesha walimu kupata maarifa yatakayowasaidia kuhakiki kipengele cha mtindo kwa usahihi. Malengo mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: (a) Kubainisha vipengele vinavyojenga mtindo wa shairi ambavyo ni uteuzi wa maneno,

matumizi ya nafsi, matumizi ya picha, matumizi ya taswira, ufupi au urefu wa mistari, uteuzi wa vichwa vya mashairi, vibwagizo.

(b) Kuhakiki mtindo wa shairi kwa kuzingatia uteuzi wa maneno, matumizi ya nafsi, matumizi ya picha, matumizi ya taswira, ufupi au urefu wa mistari, uteuzi wa vichwa vya mashairi, vibwagizo.

Muda: saa 2 Mahitaji: Vitabu vya mashairi, magazeti yenye mashairi, matini zenye nyimbo/mashairi mbalimbali.

Shughuli 1 Kwa kutumia makundi ya watu watanowatano mwezeshaji atumie nakala/vitabu mbalimbali vya mashairi kuwaongoza washiriki: (d) Kueleza maana ya mtindo katika mashairi. (e) Kubaini vipengele vya mtindo katika mashairi. (f) Kufafanua vipengele vya mtindo katika mashairi. Shughuli 2 Kwa kutumia mbinu ya changanya kete mwezeshaji awaongoze washiriki (vikundi vya

watu watano watano) (c) Kuhakiki vipengele vya mtindo kwa kuzingatia mashairi waliyopewa.

(d) Kuwasilisha hoja za majadiliano.

Tafakuri

Page 26: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

26

Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo: (a) Ni maarifa gani mapya umeyapata. (b) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo. (c) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo. Upimaji Je mshiriki ameweza kubainisha vipengele vya mtindo na kuhakiki mtindo katika mashairi? Ufupisho Mtindo wa shairi ni tabia pekee ya mtunzi au uandishi na huhitilafiana kati ya mtunzi na mtunzi. Jambo hili hutegemea ufundi, hisia na unafsi wa mtunzi. Mtindo haufundishiki bali hutokana na uwezo na mazoea na vitabia pekee vya mtunzi (Mulokozi na Kahigi uk 54, 1979). Hivyo mtindo huwa ni upekee wa mshairi katika kujenga kazi yake kifani na kimaudhui tofauti na mshairi mwingine. Katika uchambuzi wa mashairi, mtindo wa mashairi huweza kujitokeza kwa kutumia mifano ya mitindo kama mitindo ya pindu/mkufu, Msisitizo wina au ulalo, Kuchanganya lugha kama matumizi ya methali, nahau na tamathali za semi, kutumia maneno magumu, Kipande cha mwisho katika huwa ni chanzo cha ubeti unaofuata. ujenzi wa vina, idadi ya mistari, matumizi ya taswira, uchaguzi na mpangilio wa maneno Marejeo Mulokozi, M. na Kahigi,K. (1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. TPH: Dar es Salaam. Njogu, K. na Chimerah, R. (2008). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Jomo

Kenyatta Foundation: Nairobi. Mulokozi, M. (1989). “Uchambuzi wa Mashairi” katika Mulika Na.21 uk 48-57. TUKI: Dar-

es Salaam. Massamba D.P.B. (1983). “Utunzi wa ushairi wa Kiswahili” katika Makala za Semina ya

Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III Fasihi. TUKI: Dar es Salaam. Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato cha Tatu Oxford University Press: Dar es

Salaam. Wamitila, K.W. (2010). Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Focus Publications Ltd:

Nairobi.

3.3 Utungaji wa Ngonjera Utangulizi Ngonjera ni mazungumzo yenye muundo wa majibizano baina ya pande mbili au zaidi.

Upande mmoja hutoa ubeti unaojaribu kukinzana na upande wa pili, na hivyo hujenga hali ya kupokezana mazungumzo. Jambo la msingi ni kwamba ngonjera zenyewe husemwa

Page 27: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

27

haziimbwi. Ngonjera mara nyingi hufuata kanuni za ushairi wa kimapokeo ambapo katika fani yake zina vina, mizani, mishororo, beti, vipande pamoja na vituo. Katika utungaji wa ngonjera inapaswa ieleweke kwamba ngonjera huwa ni mazungumzo au majibizano ya kishairi kuhusu mada fulani ambapo jibu, utatuzi au suluhisho hupatikana mwishoni mwa ngonjera.

Kanuni za Utungaji wa Ngonjera

Usuli Imebainika kuwa walimu wengi wanapata matatizo katika kufundisha, kutunga na kutumia kanuni za utungaji wa Ngonjera. Matokeo yake ni kuwa na ufundishaji hafifu na wakati mwingine walimu kutoifundisha kabisa mada hiyo. Malengo mahsusi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: (a) Kubainisha kanuni za utunzi wa ngonjera. (b) Kutunga ngonjera kwa kufuata kanuni husika. Muda: Saa 4

Mahitaji Matini zenye ngonjera, bango kitita, kalamu ya wino mnene. Shughuli ya 1 (a) Wawezeshaji kuwasilisha ngonjera isiyofuata kanuni za ushairi. (b) Wawezeshaji kuwasilisha ngonjera iliyofuata kanuni za ushairi. (c) Washiriki kusikiliza ngongera zinazowasilishwa. Shughuli ya 2 Kwa kutumia kazi za vikundi vya watu kumikumi mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kubaini tofauti za maonesho yaliyowasilishwa. (b) Kubainisha kanuni za utunzi wa ngonjera. (c) Kutunga ngonjera kwa kufuata kanuni husika. (d) Kuwasilisha ngonjera walizoitunga. (e) Kujadili changamoto walizokabiliana nazo katika utunzi wa ngonjera. Mfano wa Ngonjera TUONDOE KUPE Mume Mke wangu wasikia, yasemwayo redioni? Wakubwa wahutubia, na kusema hadharani, Kupe wanatuibia, watutia umaskini, Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani.

Page 28: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

28

Mke Lo! Kaka wamchukia, kisirisiri moyoni? Hana baya katulia, hana kukuru nyumbani, Kazi ajitafutia, tamjalia Manani, Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani? Mume Hivi waniiga kumbe, vile ndugu yumo ndani? Hana mke yu msimbe, nitamtupia nani? Maneno hayo usambe, wanitia ghadhibani, Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani. Mke Wako si mwana mkembe, ni mkubwa mara thani? Kila mara umpambe, na chakula kila fani, Huyu wangu umchimbe, umrudishe nyumbani, Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani? Mume Mjumbe wa nyumba kumi, hukumwona jioni? Alisema kwangu mimi, nitafikishwa bomani, Kwa siasa ya uchumi, tusiweke watu ndani, Kaka yako huyu John, arudi kwao shambani. Mke Hendi aniache mimi, tufukuzwe sote ndani, Kwa nduguyo hungurumi, kwani ana kazi gani? Hana kazi na hasomi, kazi yake ukunguni. Nawe nduguyo yu ndani, vipi haendi shambani? Mume Kaka yako ndiyo kupe, anatunyonya nyumbani, Na kila kitu tumpe, wala hana shukrani, Madeni mengi tulipe, waleta hawa wahuni, Heri watoke nyumbani, wote waende shambani. Mke Na wako pia ni kupe, azimio labaini. Linasema tuwakwepe, wasio kazi mjini, Wanyonyaji tuwatupe, wajitegemee nchini, Heri watoke nyumbani, wote waende shambani. (Ngonjera za Ukuta, uk. 54-55, M E Mnyampala)

Page 29: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

29

Tafakuri (a) Je unafikiri vado kuna umuhimu wa kufundisha ngonjera shuleni. Kwa nini? Upimaji Mbinu gani zinaweza kutumika katika ufundishaji wa ngonjera? Ufupisho Katika utungaji wa ngonjera mwalimu anapaswa kuzingatia yafuatayo:

Ngonjera ni lazima isemwe au kuzungumzwa na watu wawili au zaidi/makundi mawili.

Kuteua mada ya kujadiliwa-kwa mfano masuala ya UKIMWI, jinsia, masuala ya maadili ya jamii, madawa ya kulevya, kilimo na ajira kwa watoto.

Kuweka lengo au nia; lazima kujenga mtafaruku au mgogoro kuhusiana na wazo kuu la mtunzi kwa kuwafanya wahusika mbalimbali kutofautiana na kupingana vikali na hatimaye kuelewana.

Lazima kuonesha wahusika ni akina nani na wana nafasi gani.

Kutumia muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani, vina, vipande, mishororo na beti.

Kuteua mandhari kutegemeana na nada.

Kuwepo kwa wahusika wawili au zaidi/makundi mawili.

Kuwe na matumizi ya lugha ya kishairi: Hii hujumuisha lugha ya mkato, teule, ya picha, matumizi ya methali, misemo na tamathali za semi.

Mbinu zinazopendekezwa kutumika katika kufundishia mada hii ni kama zifuatavyo: (a) Kazi mradi (projekti) ambapo mwalimu huchagua jambo la kufanya kuongoza na kuelekeza namna ya kufanikisha lengo. (b) Majadiliano katika vikundi, ambayo hulenga kuchangiwa mawazo kutoka kwa kila mwanafunzi. Mwanafunzi huchangia kwa uhuru maarifa, stadi na uzoefu. (c) Onesho mbinu ambalo hutumia vitendo katika kuonesha matumizi ya kanuni katika uwasilishaji wa ngonjera. Marejeo Mnyampala, M. E (1970). Ngonjera za Ukuta, Oxford University Press: Nairobi. Mukulu, P na wenzake (2009) Kiswahili Kitukuzwe; Kidato cha Kwanza 1, Longman: England. Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (1988), Kiswahili Sekondari, Kitabu Commercial LTD. Njenge, S (2011) Kiswahili Shule ya Sekondari; Kidato cha Kwanza, Oxford University Press: Dar es Salaam. TET, (2009). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundishaji Muhtasari wa Taaluma ya Kiswahili kwa Stashahada ya Ualimu ngazi ya Sekondari

Page 30: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

30

TET, (1996). Kiswahili kidato cha Kwanza; Oxford University Press, Dar es Salaam, Tanzania.

4.0 UANDISHI Utangulizi Uandishi ni stadi muhimu sana katika umilisi wa lugha ambayo inamsaidia mwanafunzi kuweza kuunda mawazo na kuyapangilia kimantiki. Stadi hii humsaidia mwanafunzi kuwa na uwezo wa kutumia na kuzingatia kanuni za uandishi katika kuandika habari, makala, insha, kumbukumbu za mikutano pamoja na aina mbalimbali za barua. Mjadala huu utajikita zaidi katika uandishi wa kumbukumbu za mkutano, barua rasmi na barua za kirafiki.

4.1 Kumbukumbu za Mkutano Kumbukumbu za mkutano ni muhtasari wa mambo yaliyojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano au ni rekodi zinazoandikwa na katibu/mwandishi wa mkutano ili kuhifadhi yanayojadiliwa na kukubaliwa katika mkutano huo. Ni muhimu kuandika kumbukumbu za mkutano ili kusaidia na kurahisisha utekelezaji wa mambo yaliyoamuliwa na pia kwa ajili ya marejeo.

Usuli Ukosefu wa maarifa ya kutosha kuhusu uandishi wa kumbukumbu za mkutano ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili walimu. Changamoto hii husababisha walimu kushindwa kufundisha ipasavyo mada ya uandishi wa kumbukumbu za mkutano. Mada hii ni muhimu sana kwa walimu kwani itawajengea ujuzi wa kutosha katika kuifundisha ipasavyo.

Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze:

(a) Kubainisha taratibu za uandishi wa kumbukumbu za mkutano. (b) Kuandika kumbukumbu za mkutano kwa kufuata taratibu za uandishi.

Muda: Saa 5 Mahitaji: Bango kitita, gundi ya karatasi, kalamu ya wino mnene. Shughuli ya 1 Katika makundi ya washiriki kumikumi mwezeshaji awaongoze washiriki:

(a) Kubainisha mambo muhimu katika kumbukumbu za mkutano. (b) Kuwasilisha mambo muhimu waliyojadili kwenye vikundi.

(a) Mwezeshaji atoe ufafanuzi wa hoja zilizowasilishwa.

Shughuli ya 2

Page 31: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

31

(a) Kuandaa mkutano (washiriki waigize kuhudhuria mkutano) (b) Kuwaongoza washiriki kuandika kumbukumbu za mkutano uliowasilishwa kwa kuzingatia taratibu za uandishi.

(c) Kuwaongoza washiriki kuwasilisha hoja. (d) Mwezeshaji kutoa ufafanuzi wa hoja zilizowasilishwa. Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo:

(a) Ni maarifa gani mapya umeyapata? (b) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo? (c) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo? Upimaji Kuna umuhimu gani wa kumfundisha mwanafunzi kuandika kumbukumbu za mkutano. Hitimisho Katika uandishi wa kumbukumbu za mkutano mwalimu anapaswa kuzingatia yafuatayo: (a) Kichwa cha kumbukumbu: Kinapaswa kuonesha mkutano unahusu nini, tarehe ya kufanyika kwa mkutano, mahali ulipofanyika na muda.

(b) Mahudhurio: Majina ya waliohudhuria na wasiohudhuria (kwa wasiohudhuria mwandishi anapaswa kuonesha wazi ni wajumbe gani hawakuhudhuria na aoneshe wazi kama mjumbe alitoa udhuru au la) mahudhurio huandikwa kwa kuanzia kwa yule mwenye cheo cha juu hadi wajumbe wa kawaida. Mwandishi anapaswa kuonesha vyeo hivyo. Orodha ya mahudhurio inaweza kuonesha majina ya waalikwa endapo katika kikao hicho kuna watu waliohudhuria kwa kualikwa.

(c) Ajenda: Ni mambo yatakayozungumzwa katika mkutano. Baada ya mkutano mambo yaliyojadiliwa katika kila ajenda huandikwa kwa muhtasari, kwa kila ajenda mwandishi hutakiwa kuonesha kama ajenda hiyo ilikubaliwa au ilikataliwa.

(d) Kufungua mkutano: Mwandishi au katibu aandike saa ya kufungua mkutano na yale yaliyoelezwa na mwenyekiti wakati wa ufunguzi.

(e) Kufunga Mkutano: Baada ya majadiliano, mwenyekiti hufunga mkutano. Mwandishi/katibu azingatie muda kikao kilipofungwa.

NB: Katibu/mwandishi atakapoandika kumbukumbu za mkutano azingatie kuandika jina la mwenyekiti na katibu na kuweka nafasi ya kusaini na tarehe.

Marejeo Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato cha Nne. Oxford University Press: Dar es Salaam.

Page 32: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

32

Njenge, S. (2013). Kiswahili Shule za Sekondari Kidato cha Nne. – Oxford University Press: Dar es Salaam Tanzania.

4.2 Barua ya Kirafiki Barua ya kirafiki ni aina mojawapo ya barua ambayo hutumiwa kufikisha ujumbe kwa ndugu, marafiki, jamaa, wazazi na wapenzi kwa malengo mbalimbali. Barua hii humpa mwandishi uhuru wa kutumia lugha anayoitaka, kwa kuzingatia mahusiano yake na mwandikiwa.

Usuli Imebainika kuwa walimu wengi hawana maarifa ya kutosha kuhusu muundo sahihi wa barua za kirafiki. Hali hii huenda imesababishwa na mabadiliko ya sayansi na teknolojia hasa matumizi ya simu za mkononi, ambazo zimesababisha jamii kupunguza matumizi ya uandishi wa barua za kirafiki. Katika mada hii mkazo zaidi utawekwa katika muundo sahihi wa barua za kirafiki.

Malengo mahususi Baada ya kujifunza mada hii mshiriki aweze: iv. Kutaja mambo muhimu katika za barua ya kirafiki v. kubainisha muundo wa barua ya kirafiki vi. Kuandika barua ya kirafiki kwa kuzingatia muundo sahihi. Muda: saa 3 Mahitaji Matini za barua ya kirafiki, bango kitita, kadi za manila, kalamu za wino mnene. Shughuli ya 1 Katika jozi ya watu watanowatano mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kutaja sehemu kuu za barua ya kirafiki. (b) Kubainisha muundo wa barua ya kirafiki. Shughuli ya 2 Mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kuandika barua ya kirafiki. (b) Kuwasilisha barua walizoandika katika kundi. (Kila mshiriki atawasilisha barua aliyoiandika)

(c) Kubaini changamoto ya kila barua iliyowasilishwa. (d) Kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizobainika katika barua zilizoandikwa. Tafakuri Je, mwalimu ameweza kuandika barua ya kirafiki kwa kufuata muundo sahihi wa uandishi wa barua ya kirafiki?

Page 33: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

33

Upimaji Je, kuna umuhimu wa kuendelea kufundisha uandishi wa barua ya kirafiki. Ufupisho Katika uandishi wa barua ya kirafiki mwalimu azingatie yafuatayo: (a) Muundo ufuatao:

(b) Kanuni za uandishi wa barua za kirafiki zifuatazo: i. Anwani ya mwandishi huwa juu upande wa kulia na isiwe na jina la mwandishi.

Shule ya Sekondari Juhudi, S.L.P 10, TABORA. Au Shule ya Sekondari Juhudi, S.L.P 10, TABORA.

Anwani ya mwandishi

Kiini cha barua

Mwisho wa barua

Jina la mwandishi

Mwanzo wa barua

Tarehe

Page 34: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

34

ii. Tarehe ya kuandikwa barua huwa chini kidogo baada ya anwani ya mwandishi. 12/8/2014 au 12-8-2014 au 12.8.2014 au 12 Agosti, 2014.

iii. Mwanzo wa barua huwa upande wa kushoto wa chini kidogo ya tarehe na huanza na maamkizi kama vile mpendwa mama, mpendwa rafiki na mpendwa baba. Baada ya maneno hayo aya fupi ya salamu hufuata.

iv. Kiini cha barua huanza na aya fupi ya utangulizi. Kwa mfano madhumuni ya barua yangu ni........... au kusudi la barua yangu ni.......... au lengo la barua hii ni...........

v. Mwisho wa barua ni sehemu ya maagano ambayo hutumia maneno machache kwa mfano:

wako akupendaye, rafiki yako mpendwa, baba yako na mama yako. vi. Jina la mwandishi huandikwa mwisho wa barua baada ya maagano na huweza kuandikwa kwa kirefu au kwa kifupi.

Mfano. F. Amani au Furaha Amani au Furaha.

4.3 Barua Rasmi Barua rasmi ni mojawapo ya barua ambayo huandikwa kwa makusudi maalumu. Mfano kuomba kazi, kutoa taarifa kwenye maeneo ya kazi. Mwandishi hupaswa kuandika kwa kutumia lugha sanifu inayoeleweka kwa msomaji. Huzingatia muktadha husika.

Usuli Ufundishaji wa mada hii umekuwa hautilii maanani taratibu zinazotakiwa. Kwa hiyo mada hii itabainisha na kueleza muundo na kanuni za uandishi wa barua rasmi.

Malengo mahsusi Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze; (a) Kubainisha kanuni za uandishi wa barua rasmi. (b) Kuandika barua rasmi kwa kufuata kanuni husika. Muda: saa 4 Mahitaji Matini za barua rasmi, mchoro wa muundo wa barua rasmi, kadi za manila, kalamu za wino mnene.

Shughuli ya 1 Katika jozi ya watu watanowatano mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) kubainisha kanuni za uandishi wa barua rasmi. (b) Kuwasilisha hoja za majadiliano.

Page 35: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

35

Shughuli ya 2 Mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kuandika barua rasmi. (b) Kuwasilisha barua walizoandika katika kundi. (Kila mshiriki atawasilisha barua aliyoiandika)

(c) Kubaini changamoto ya kila barua iliyowasilishwa. (d) Kuwasilisha changamoto mbalimbali zilizobainika katika barua zilizoandikwa. Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo:

(a) Ni maarifa gani mapya umeyapata? (b) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo? (c) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo? Upimaji Je, mshiriki ameweza kuandika barua rasmi yenye kufuata kanuni sahihi? Ufupisho Katika uandishi wa barua rasmi, mshiriki azingatie yafuatayo: (a) Kanuni za uandishi wa barua rasmi: i. Anwani ya mwandishi: Hii huandikwa upande wa kulia wa karatasi. ii. Tarehe: Huandikwa upande wa kulia wa karatasi katika mstari uleule wa kumbukumbu ya

barua kama ipo. Huwa chini ya anwani ya mwandishi. iii. Kumbukumbu namba: Hii huwa kama kitambulisho cha barua. iv. Anwani ya mwandikiwa: Hii hutanguliwa na cheo cha mwandikiwa, na huandikwa upande

wa kushoto wa barua. v. Mwanzo wa barua: Huu huandikwa chini ya anwani ya mwandikiwa upande wa kushoto.

Kwa kutaja maneno kama Ndugu, Mheshimiwa. vi. Kichwa cha barua: huandikwa kwa herufi kubwa kwa kutumia maneno machache na mara

nyingi hukaa katikati ya barua chini kidogo ya mwanzo wa barua. Kichwa cha habari hupigiwa mstari au hukolezwa wino.

Mfano: Yah: MAOMBI YA KUJIUNGA NA SHULE

Au Yah: MAOMBI YA KUJIUNGA NA SHULE

vii. Utangulizi wa barua huwa chini kidogo ya kichwa cha barua. Mfano:

Kichwa cha barua chahusika........ Mada hapo juu yahusika......... Husika na kichwa cha barua hapo juu.......

Page 36: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

36

Tafadhali husika na kichwa cha barua hapo juu……. viii. Kiini cha barua/Barua yenyewe: Iwe na taarifa muhimu na ziandiwe kwa ufupi. ix. Mwisho wa barua: huwa ni hitimisho na huweka mkazo kuhusu jambo lililoandikwa. Baadhi ya mifano; Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litakubaliwa/ litafanikiwa. x. Salaam za maagano: Baadhi ya mifano; Wako katika ujenzi wa taifa. Wako mtiifu. Mwanafunzi mtiifu. xi. Saini ya mwandishi huandikwa mwisho kidogo ya maelezo ya mwisho wa barua. Mfano; F. Amani.

xii. Jina kamili la mwandishi huandikwa chini kidogo ya saini ya mwandishi. Mfano: Furaha Amani.

xiii. Cheo/wadhifa wa mwandishi wa barua huandikwa baada ya kuandikwa kwa jina la mwandishi na huwa inatoa utambulisho kwa mwandikiwa.

Mfano: Mwalimu mlezi, mwanafunzi, mkuu wa shule n.k

Page 37: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

37

Marejeo

Mlyauki, J na wenzake (2009) Kiswahili kitukunze 2: Kidato cha pili, kitabu cha Mwanafunzi: Longman: England. Njenge (2013) Kiswahili Shule za Sekondari, kidato cha pili: Oxford University Press: Dar es Salaam. TET (1996) Kiswahili 3, Kidato cha Tatu: Oxford University Press: Dar es Salaam.

Tarehe

Namba ya Kumbukumbu kama ipo

Anwani ya Mwandikiwa

Kichwa cha Habari

Mwanzo

Kiini cha Barua

Mwisho wa Barua

Maagano

Saini ya Mwandishi

Jina kamili la Mwandishi na cheo chake

Anwani ya mwandishi

Page 38: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

38

5.0 UFAHAMU WA KUSOMA

Utangulizi Ufahamu wa kusoma ni uelewa unaopatikana kwa njia ya kusoma kwa sauti, haraka, kimya na kwa makini. Uelewa huo huweza kubainika endapo mhusika ataweza kujibu kwa usahihi maswali aliyouliza. Miongoni mwa maswali hayo ni kuandika ufupisho wa habari. Ufupisho ni sehemu pana ya ufahamu licha ya kuwa si kila ufupisho unatokana na habari uliyosoma. Unaweza kufupisha habari uliyosikia inayotokana na hadithi, shairi, hotuba au risala. Katika kufupisha mhusika anapaswa kubainisha mawazo makuu na kuyafupisha bila kupoteza maana ya awali. 5.1 Hatua za Kuandika Ufupisho Ufupisho ni muhtasari wa mambo uliyoyasikia au uliyoyasoma. Ujuzi wa kuchanganua na kupanga mawazo kimantiki ndio unaowezesha kubaini kuwa mhusika ameelewa alichokisoma au alichokisikia. Mhusika anapaswa kutumia maneno mengine bila kupoteza maana ya habari ya awali. Usuli Ufundishaji na ujifunzaji wa mada ya ufupisho umekuwa ni tatizo kwa walimu wengi, hii ni kutokana na walimu kutozingatia hatua za ufupisho. Hali hii imesababisha mada kutofundishwa ipasavyo na wanafunzi kutopata ujuzi na maarifa yaliyokusudiwa. Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: (a) Kubainisha hatua za kuandika ufupisho. (b) Kufupisha habari kwa kuzingatia hatua za ufupisho. Makadirio ya muda: saa 4 Mahitaji Vifungu vya habari na nakala za mashairi. Shughuli ya 1 Kwa kutumia jozi za watu wannewanne (4) mwezeshaji awaongoze washiriki: (c) Kubainisha hatua za uandishi wa ufupisho. (d) Kuwasilisha hoja za vikundi. (e) Kufanya majadiliano ya hoja zilizowasilishwa.

Shughuli ya 2 Kwa kutumia jozi za watu wannewanne (4) mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kusoma kifungu cha habari/shairi (b) Kubainisha mawazo makuu.

Page 39: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

39

(c) Kuwasilisha mawazo makuu waliyoyabainisha katika vikundi. Shughuli ya 3 Kwa kutumia jozi za watu wannewanne (4) mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kuunganisha mawazo makuu kwa kutumia maneno yao tofauti na yale yaliyomo

katika kifungu cha habari/shairi. (b) Kuzingatia maelekezo ya idadi ya maneno aliyoelekezwa kuwepo katika ufupisho

wake. Kwa kawaida ufupisho huwa ni theluthi moja ya maneno yaliyo kwenye habari ya awali.

(c) Kusoma ufupisho aliouandaa ili kubaini mapungufu yaliyomo. Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa kuwauliza maswali yafuatayo: (c) Ni maarifa gani mapya umeyapata. (d) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo. (e) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo. (f) Ni mbunu gani zingine zinaweza kutumika katika ufundishaji wa uandishi wa

ufupisho. Upimaji (a) Soma kifungu cha habari/shairi ulichopewa kisha fupisha habari.

5.2 Mbinu za Kufundisha Ufupisho

Usuli Ufundishaji na ujifunzaji wa mada ya ufupisho umekuwa ni tatizo kwa walimu wengi, hii ni kutokana na walimu kutozingatia hatua za ufupisho. Hali hii imesababisha mada kutofundishwa ipasavyo na wanafunzi kutopata ujuzi na maarifa yaliyokusudiwa. Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze: (a) Kubainisha mbinu za kufundisha ufupisho. (b) Kutumia mbinu mahususi katika kufundisha ufupisho. Muda: Saa 4 Mahitaji Vifungu vya habari na nakala za mashairi.

Shughuli ya 1

Page 40: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

40

Kwa kutumia makundi ya washiriki watanowatano mwezeshaji awaongoze washiriki namna ya kutumia mbinu ya majadiliano katika kufundisha uandishi wa ufupisho. (a) Mshiriki mmoja asome habari. (b) Washiriki wabainishe mawazo makuu. (c) Washiriki waunganishe mawazo makuu. (d) Mshiriki mmoja asome ufupisho ili kundi zima lione usahihi wa ufupisho huo. (e) Endapo kutakuwa na dosari katika ufupisho marekebisho yafanyike. (f) Washiriki wawasilishe ufupisho wao.

Shughuli ya 2 Kwa kutumia makundi ya washiriki watanowatano mwezeshaji awaongoze washiriki namna ya kutumia mbinu ya changanya kete katika kufundisha uandishi wa ufupisho. (a) Katika makundi ya nyumbani:

(i) Mshiriki mmoja asome habari. (ii) Washiriki wabainishe mawazo makuu.

(iii) Washiriki waunganishe mawazo makuu. (iv) Mshiriki mmoja asome ufupisho ili kundi zima lione usahihi wa ufupisho huo. (v) Washiriki wafanye marekebisho endapo kutakuwa na dosari katika ufupisho

walioandika.

(b) Katika makundi ya utaalamu: (i) Kila mshiriki awasilishe ufupisho ulioandikwa katika kundi la nyumbani.

(ii) Kuandika changamoto zilizobainishwa na kundi la utaalamu. (iii) Kuwasilisha ufupisho uliofanya na kila kundi.

Tafakuri Ni mbinu gani nyingine unaweza kuitumia kufundishia mada ya ufupisho?

Upimaji Onesha jinsi utakavyotumia mbinu ya onesho mbinu katika kufundisha ufupisho. Ufupisho Katika ufundishaji wa ufupisho mwalimu anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo; aandae vifungu vya habari au mashairi atakayoyatumia. Mwalimu anashauriwa kutumia vifungu vya habari au mashairi ambayo yana mada mtambuka au mada zinazofundishwa katika masomo mbalimbali. Aidha, ili mada ya ufupisho ifundishwe kwa ufasaha na usahihi mwalimu anapaswa kutumia mbinu anuai kama vile; onesho mbinu, changanya kete na majadiliano ya vikundi.

Page 41: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

41

Marejeo Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato cha Tatu. Oxford University Press: Dar es

Salaam. Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (1988). Kiswahili Sekondari. TUMI: Dar es Salaam. Taasisi ya Elimu (2013). Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Elimu ya Msingi: Moduli ya

Kujifunzia Ufundishaji wa Somo la Kiswahili. TET: Dar es Salaam. Wizara ya Elimu na Utamaduni (2005). Mpango wa Mafunzo ya Walimu Kazini Daraja la

IIIc/B-IIIA: Moduli ya Somo la Ufundishaji. Dar es Salaam. 6.0 UPIMAJI Utangulizi Upimaji ni muhimu sana katika maisha ya kila siku ya mwanadamu katika kuleta maendeleo. Mafanikio katika kazi yanatokana na upimaji wa utendaji wa kila mtu katika sehemu ya kazi. Katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji suala la upimaji haliwezi kukwepeka kwa kuwa ni lazima mwalimu afahamu kama malengo ya ufundishaji aliyoweka kabla yamefikiwa au la. Upimaji ni tendo la kutafuta ni kwa kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa na stadi alizofundishwa kufuatana na malengo ya ufundishaji. 6.1 Matumizi ya Vitenzi vya Upimaji Vitenzi vya upimaji ni maneno yanayotumiwa katika upimaji wa nyanja mbalimbali za utambuzi. Maneno hayo hutumika katika kuandaa mazoezi, majaribio na mitihani. Ili mwalimu aweze kupima ngazi fulani ya utambuzi kwa usahihi hana budi kufahamu vema matumizi sahihi ya vitenzi vya upimaji. Usuli Imebainika kuwa walimu wengi hawana maarifa ya kutosha juu ya namna ya kutumia vitenzi mahususi vya upimaji wa ngazi fulani ya nyanja ya utambuzi. Malengo Mahususi Baada ya kujifunza mada hii mshiriki aweze: a) Kutumia vitenzi vya upimaji kwa usahihi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji.

Muda: Saa 4 Mahitaji Kadi za manila, kalamu za wino mnene, bango kitita, gundi ya karatasi. Shughuli ya 1 Kwa kutumia mbinu ya bungua bongo, washiriki katika jozi wabainishe vitenzi vya upimaji vya ngazi mbalimbali za nyanja ya utambuzi

Shughuli ya 2

Page 42: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

42

Katika vikundi vidogo vidogo, washiriki wahusishe vitenzi vya upimaji walivyobainisha katika shughuli 1, na ngazi zote za nyanja ya utambuzi na kufanya uwasilishaji. Lifuatalo ni jedwali lenye ngazi za Nyanja ya utambuzi na vitenzi vya upimaji.

NA. NGAZI ZA KUFIKIRI

VITENZI VYA UPIMAJI

1. MAAARIFA Taja, andika ,onesha, ainisha, eleza, orodhesha,oanisha, fasili, bainisha

2. UFAHAMU Toa, fupisha, endeleza, toa muhtasari, bashiri tofautisha, andika tena, tabiri, jumuisha, husisha,eleza

3. MATUMIZI Badili, onesha,boresha, linganisha,andika, husisha, tumia, zalisha, unda, buni, tunga

4. UCHAMBUZI Dhihirisha, chambua, husisha, changanua, andika kwa ufupi, tofautisha, chora, gawanya, chagua, onesha, tenga, maswali yote yanayo anza na kwa nini?

5. UUNDAJI Husianisha, jenga upya, panga upya, kusanya, fupisha, pangilia, andika upya, unda, vumbua, tunga, eleza

6. TATHMINI Tathmini, elezea, hakiki, fasili, linganisha, hitimisha, kubaliana, tetea, husianisha, toa ufupishao, toa makosa, tenga, eleza, jadili

Shughuli ya 3 Katika vikundi vya watu kumikumi, washiriki watunge maswali mawili mawili ya kupima kila ngazi ya nyanja ya utambuzi kwa kutumia “mada ya sarufi na utumizi wa lugha.” Tafakuri Je, kuna ulazima gani wa mwalimu kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya vitenzi vya upimaji wa ngazi zote za nyanja ya utambuzi? Upimaji Eleza athari hasi za mwalimu kutotumia kwa usahihi vitenzi vya upimaji katika utunzi wa maswali. Ufupisho Kwa hakika, ili mwalimu apime ngazi fulani ya nyanja ya utambuzi kwa usahihi anapaswa kuwa na weledi wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya vitenzi vya upimaji.

Marejeo Taasisi ya Elimu Tanzania (2013). Ufundishaji wa Somo la Kiswahili kwa Elimu ya Sekondari.

TET: Dar es Salaam. 7.0 MAWASILIANO

Page 43: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

43

Utangulizi Mawasiliano ni tendo la upashanaji habari kwa njia mbalimbali kama simu, barua, redio, televisheni na teleksi. Upashanaji habari huweza kufanyika ana kwa ana: kati ya watu wawili, mtu mmoja na hadhira ya watu wengi kwa kutumia lugha ya maneno, ishara na miondoko inayokubalika katika jamii. Mawasiliano hayo huweza kuwa hotuba kwenye mkutano, kwa mwalimu na wanafunzi darasani au kwenye familia. Dhana hii ni muhimu sana kwa binadamu, kwani humwezesha binadamu kupeleka na kupata taarifa mbalimbali kwa kutumia lugha inayoendana na miktadha mbalimbali kulingana na maadili ya jamii husika. Taarifa hizo humwezesha binadamu kuzifanyia kazi na kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali. Katika sehemu hii tutazingatia mada za Matamshi ya Kiswahili na Matumizi ya Kamusi. 7.1 Matamshi ya Kiswahili Matamshi ya Kiswahili ni namna ya kutamka maneno katika hali inayozingatia kanuni zote za kisarufi za maneno ya Kiswahili. Kanuni za matamshi ya Kiswahili hujikita pia katika kiimbo na mkazo. Kila lugha ya binadamu ina kiimbo, kwa hiyo lugha ya Kiswahili ina kiimbo chake ambacho ni utaratibu maalumu wa kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti wakati wa utamkaji. Pia kuna mkazo ambao ni nguvu ya ziada inayotumika kutamka silabi mojawapo ya neno kuliko silabi nyingine. Silabi yenye mkazo huwa inatamkwa kwa nguvu nyingi kuliko isiyokuwa na mkazo. Usuli Imeonekana kuwa baadhi ya walimu hukosa mbinu za kufundishia matamshi kutokana na kuaathirika na lugha mama na hivyo kushindwa kufundisha Kiswahili fasaha ipasavyo. Kazi ya ziada inabidi ifanyike ikiwa ni pamoja na kutoa semina kwa walimu juu ya mada hii ya Matamshi ya Kiswahili. Malengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada hii washiriki waweze:

(a) Kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji wa matamshi ya Kiswahili sanifu. (b) Kutumia matamshi ya Kiswahili sahihi katika mawasiliano. (c) Kusahihisha makosa ya kimatamshi katika mawasiliano.

Muda: Saa 2 Mahitaji Kamusi, manila, kalamu ya wino mnene, bango kitita, chati za maneno. Shughuli 1 Kwa kutumia ziara tembezi washiriki waandae chati ya orodha ya matamshi ya lugha sanifu ya kiswahili. Shughuli 2 Kwa kutumia majadiliano washiriki wajadili faida za kutumia matamshi ya lugha sanifu ya Kiswahili.

Page 44: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

44

Tafakuri

(a) Stadi za mawasiliano zina nafasi gani katika maisha ya kila siku? (b) Mwandishi asiyemudu stadi za mawasiliano ataifanyaje kazi yake? (c) Elezea ni kwa namna gani upotoshaji wa matamshi kwa mwalimu huweza

kurudisha nyuma tendo zima la ufundishaji? Upimaji Ni maarifa gani mapya washiriki waliyoyapata? Je washiriki wameweza kutumia matamshi sahihi katika mawasiliano? Je wameweza kusahihisha makosa katika mawasiliano? Hitimisho Ni dhahiri kuwa kila lugha ina utaratibu maalumu wa kutamka sauti. Utaratibu huo huhusu namna au jinsi ya kuzitoa sauti hizo na mahali ambapo sauti hizo hudhibitiwa. Matamshi hutegemea sana matumizi sahihi ya ala za matamshi kama midomo, ufizi, meno, kaakaa (gumu na laini), koromeo na ulimi. Matamshi ya lugha ya Kiswahili sanifu hayabadiliki kutokana na umbo na kiimbo bali huangalia na kuzingatia matumizi ya lafudhi, umbo, mpangilio na maana.

Lafudhi ni namna ya kutamka maneno ambayo hutambulisha mahali au jamii anayotoka mzungumzaji.

Umbo la neno Huendana na tabia ya lugha inayohusika.

Mpangilio ni namna ya kuyapanga maneno kwa utaratibu maalumu ili kuunda sentensi zinazotoa maana.

Maana ni dhana ambayo hubebwa katika neno au sentensi. Mbinu za kutumia ni pamoja na mazoezi mbalimbali ya namna ya kutamka maneno sahihi. Igizo dhima ikiwa na maana ya kuiga wadhifa au uhusika wa mtu. Pia mbinu ya kutunga hotuba ili kuonyesha kuwa hotuba ni njia mojawapo ya mawasiliano. Njia ya majadiliano, hapo walimu hujadiliana ili kupata stadi za mawasiliano kama, uwezo wa kubadilishana, kushirikiana na kutumia nyenzo zilizopo za mawasiliano ili kufanikisha mawasiliano husika pia itatumika mbinu ya ziara tembezi.

Marejeo Mukulu, P na wenzake, (2009) Kiswahili Kitukuzwe1: Kidato cha Kwanza, Longman Kiswahili Shule ya Sekondari, (2011) Kidato cha Kwanza, Oxford

Wanjala. S, & Kavoi. M (2013) Stadi za mawasiliano na Mbinu za kufundishia Kiswahili:

Serengeti Educational Publishers (T) LTD. TET, (2009). Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Muhtasari wa Taaluma ya Kiswahili

kwa Stashahada ya Ualimu ngazi ya Sekondari. ``TET, (1996). Kiswahili kidato cha Kwanza; Exford University Press, DSM, Tanzania.

Page 45: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

45

7.2 Matumizi ya Kamusi Kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno yaliyopangwa kwa mujibu wa alfabeti na kutolewa kutolewa maana na maelezo mengine. Usuli Utafiti unaonesha kuwa baadhi ya walimu wanakosa maarifa ya kutosha ya mbinu za kufundishia matumizi ya kamusi. Hali hiyo inapelekea baadhi ya walimu kutoifundisha mada hiyo ipasavyo. Mwongozo huu umeandaliwa ili kuwawezesha walimu kupata mbinu mbalimbali za kufundishia mada ya matumizi ya kamusi. Malengo mahsusi Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze: (a) Kubaini mbinu za kufundisha mada ya matumizi ya kamusi. (b) Kutumia mbinu hizo katika kufundisha mada ya matumizi ya kamusi. Muda: Saa 3 Mahitaji Matini mbalimbali, Kamusi ya Kiswahili Sanifu, kadi za manila, kalamu ya wino mnene. Shughuli ya 1 Katika makundi ya washiriki kumikumi mwezeshaji awaongoze washiriki: (a) Kupanga maneno yaliyomo kwenye kadi za manila kwa kuzingatia jinsi

yanavyopangwa kwenye kamusi. (b) Kuwasilisha mpangilio waliokubaliana kwenye kundi kwa njia ya kujipanga mbele

ya darasa kwa kuzingatia herufi zilizoandikwa kwenye sakafu. (c) Kufafanua kigezo walichotumia kupanga maneno katika mpangilio husika.

Shughuli ya 2 Mwezeshaji awagawie washiriki kadi za manila zilizoandikwa maneno mbalimbali na kuwaongoza washiriki hao kujipanga kwa kuzingatia maingizo ya maneno hayo katika kamusi.

Anza, anwani, bakora, zeze, tiba, tezi, desturi, faru, zeituni, matini, akiba, amini, utandawazi, udokozi, marumaru, kiti, nyumba, dhahabu, gari, embe, jicho, lala, uzi, bariki, papai.

Tafakuri Je mwalimu ameweza kupata mbinu za kufundishia kufundisha mada ya Matumizi ya Kamusi.

Page 46: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

46

Upimaji Eleza mbinu zingine ambazo zinaweza kutumika katika kufundisha matumizi ya kamusi. Hitimisho Mwalimu anaweza kutumia mbinu anuai katika kufundisha matumizi ya kamusi kwa kuzingatia mazingira na vifaa vinavyopatikana katika mazingira hayo. Marejeo Mukulu, P na wenzake, D (2009) Kiswahili Kitukuzwe1: Kidato cha Kwanza, Longman Wanjala. S na mwenzake (2013) Stadi za mawasiliano na Mbinu za kufundishia

Kiswahili: Serengeti Educational Publishers (T) LTD. TET, (1996). Kiswahili kidato cha Kwanza; Oxford University Press, DSM, Tanzania.

8.0 UUNDAJI WA MANENO Utangulizi Uundaji wa maneno ni kitendo cha kuzalisha maneno mapya kwa kupanua msamiati ili kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Maneno yanaweza kuundwa kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayotokea katika jamii. Mwalimu anapaswa kujua kuwa jambo lolote jipya linaloibuka au kutokea katika jamii halina budi kuwa na msamiati wake. Maneno kama teknolojia, ujasiriamali na barua pepe ni baadhi ya maneno hayo. Aidha, maneno huweza kuundwa kwa njia mbalimbali zikiwemo kutohoa, kurudufisha, kufupisha, kuambatisha, kuambisha na kunyambulisha. Katika mwongozo huu tutajikita juu ya mada za Uambishaji na Unyambulishaji. 8.1 Uambishaji na Unyambulishaji Uambishaji ni kitendo cha kupachika mofimu tegemezi (vipashio) mwanzoni na mwishoni mwa mzizi wa neno ili kulipa neno hilo hali, tabia au maana ya ziada. Unyambulishaji ni kitendo cha kuongeza mofimu tegemezi mwishoni au baada ya mzizi wa neno. Usuli Uundaji wa maneno kwa njia ya uambishaji na unyambulishaji ni mada zinazowakanganya walimu wengi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Mkanganyiko huu husababishwa na baadhi ya wafundishaji kukosa maarifa ya kutosha juu ya dhana hizo. Hivyo basi, mada hii ni muhimu kwa kupata maarifa yatakayosaidia kuzipambanua kwa usahih dhana hizo. Malengo Mahususi

Baada ya kukamilika kwa mada hii mshiriki aweze: (a) Kubainisha dhana za uambishaji na unyambulishaji. (b) Kutofautisha dhana ya uambishaji na unyambulishaji. (c) Kutumia uambishaji na unyambulishaji katika kuunda maneno.

Page 47: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

47

MUDA: Saa 2 Mahitaji Kadi za manila, kalamu za wino mnene, bango kitita, gundi ya maji na karatasi na matini faraguzi. Shughuli 1 Kwa njia ya bungua bongo, mwezeshaji awaongoze washiriki katika jozi:

(a) kubainisha maana ya Uambishaji na Unyambulishaji. (b) Kuwasilisha mada hizo.

Shughuli 2 Katika makundi ya watu kumi kumi mwezeshaji awaongoze washiriki

(a) kuunda maneno kwa njia ya uambishaji na unyambulishaji. (b) Kuwasilisha mada hizo.

Shughuli 3 Katika makundi ya watu kumikumi washiriki wajadili na kueleza tofauti zilizopo kati ya dhana ya uambishaji na mnyambuliko na kuwasilisha. Tafakuri Je, uambishaji na unyambulishaji una faida gani katika lugha ya Kiswahili? Upimaji Je mshiriki ameweza kutofautisha dhana ya uambishaji na unyambulishaji? Ufupisho Uambishaji ni kile kitendo cha kuongezea viambishi awali peke yake, viambishi awali na tamati kwa pamoja katika mzizi/shina la neno na kubadilisha maana ya awali. Aidha unyambulishaji ni kitendo kurefusha au kuongeza viambishi kwa kawaida baada ya mzizi/shina la neno na kubadili maana/aina ya neno la awali.

Page 48: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

48

Jedwali lifuatalo ni baadhi ya mifano inayobainisha uambishaji na unyambulishaji. MZIZI/SHINA LA NENO

UAMBISHAJI

UNYAMBULISHAJI

Pig-a

Mpigaji, kipigo, Mapigo, anapiga, anapigwa, tunapigwa, zilipigwa.

Pigia, pigwa, pigisha, pigana, piganisha, pigisha, piganisha.

Chez-a Mchezaji, mchezo, michezo, wachezaji, mchezeshaji, anacheza, wanacheza, tunacheza, tunachezeshwa.

Chezeni, chezea, chezwa, chezeka, chezesha, chezeshana, chezeana, chezewa, Chezeana, chezeshwa.

Som-a Msomaji, msomi, somo, wasomaji, tunasoma, wanasoma, msomaji.

Someka, somea, someana, someshana

Refu

Mrefu, warefu, mrefushaji, urefu, kirefu, parefu.

Refusha, refushwa, refushiwa,refushika

Fupi Mfupi, wafupi, kifupi, ufupishaji, ufupisho

Fupisha, fupisheni, fupishwa, fupishuka

Mshiriki ili aweze kufundisha dhana hizi kwa usahihi anapaswa kuwa na weledi wa kutosha juu ya tofauti zake.

Page 49: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

49

9.0 UCHANGANUZI WA SENTENSI Utangulizi Katika uchanganuzi wa sentensi mwalimu anapasa kuwa na weledi mpana kuhusu uainishaji na ubainishaji wa maneno na tungo. Weledi huu humsaidia kutambua hatua zinazotakiwa kufuatwa katika uchanganuzi kwa kuzingatia viwango vya wajifunzaji . 9.1 Hatua za Uchanganuzi wa Sentensi Kuchanganua sentensi ni kugawa sentensi kulingana na vipashio, makundi ya maneno au aina za maneno kwa kubainisha na kuainisha katika viwango mbalimbali. Ubainishaji na uainishaji wa vipashio hivyo hufanywa kwa kuzingatia hatua tano mahususi. Hatua hizo ni: kutambua aina ya sentensi, kutaja sehemu kuu za sentensi, kutambua vikundi vya maneno, kutaja aina za maneno na kuandika sentensi upya. Usuli Ukosefu wa maarifa ya kutosha kwa walimu kuhusu hatua mahususi za uchanganuzi wa sentensi, umesababishwa na mikabala miwili tofauti inayotumika katika uchanganuzi ambayo ni mkabala wa kimapokeo na mkabala wa kisasa. Kila mkabala una hatua za uchanganuzi wa sentensi na hatua hizo zinatofautiana. Kutokana na mkanganyiko, huo walimu wanatakiwa kuzingatia hatua muhimu zinazotakiwa katika kuchanganua sentensi. Mada hii imeandaliwa ili kuwepo na usawa katika kufundisha uchanganuzi wa sentensi. Lengo Mahususi Baada ya kukamilika kwa mada mshiriki aweze:

(a) Kubaisha hatua za uchanganuzi wa sentensi (b) Kuchanganua sentensi kwa kufuata hatua tano.

Muda: Saa 4 Mahitaji: Bango kitita na kalamu za wino mnene, kadi za manila.

Shughuli ya 1

Mwezeshaji afanye yafuatayo: (i) Awaongoze washiriki kutaja hatua za uchanganuzi wa sentensi.

(ii) Katika makundi ya watu watano washiriki wachanganue sentensi ifuatayo: Mwalimu wetu anafundisha darasani.

(iii) Washiriki katika makundi wabadilishane kazi ili kubaini changamoto zilizojitokeza. (iv) Washiriki wawasilishe na kujadili changamoto zilizojitokeza katika makundi.

Shughuli ya 2

Katika makundi ya watu watano Mwezeshaji awaongoze washiriki: (i) Kutunga sentensi zenye muundo wa N+V+TS+T+N+E.

Page 50: MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI … · MWONGOZO WA MAFUNZO KAZINI KWA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI SOMO LA KISWAHILI MZUNGUKO WA KWANZA AGOSTI 2014 . 2

50

(ii) Washiriki wachanganue na kuwaslilisha. (iii) Wabaini na kujadili changamoto zilizojitokeza. Tafakuri Mwezeshaji awaongoze washiriki kutafakari walichojifunza katika mada iliyowasilishwa kwa

kuwauliza maswali yafuatayo: (a) Ni maarifa gani mapya umeyapata. (b) Ni mambo gani hukuyaelewa vizuri katika somo. (c) Nini kifanyike kuboresha mambo hayo.

Upimaji Mbinu gani zitumike katika uchanganuzi wa sentensi. Ufupisho Uchanganuzi wa sentensi usizingatie mikabala bali hatua tano zilizobainishwa katika mwongozo huu. Hatua hizo ni kutambua aina ya sentensi (sahili, changamano, ambatano na shurutia0, kutaja sehemu kuu za sentensi (kiima na kiarifu), kutambua vikundi vya maneno (KN, KT, KE), kutaja aina za maneno (N, V, T, E, U, W), na kuandika sentensi upya. Tanbihi Uchanganuzi wa sentensi uzingatie njia mbili (02) za uchanganuzi zilizobainishwa katika muhtasari wa Kiswahli kidato cha I hadi IV, yaani njia ya majedwali na njia ya matawi. Marejeo Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato cha Tatu. Oxford University Press: Dar es Salaam. Taasisi ya Ukuzaji Mitaala (1988). Kiswahili Sekondari. TUMI: Dar es Salaam. Myauki, J., Mulashan, E., na Ndilime, D. (2009). Kiswahili Kitukuzwe 3. Longman: England John, J. (2011). Kiswahili shule za Sekondari Kidato cha Tatu. Oxford University Press: Dar es Salaam.