annuur-1009

16
ISSN 0856 - 3861 Na. 1009 JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRIL 20 - 26, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu MHESHIMIWA Mohamed Raza aliwahi kutamka hadharani kwamba mfumo wa sasa wa Muungano unaiminya Zanzibar. Raza alitaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kwa madai kwamba ndio suluhisho la matatizo ya Muungano. Hata hivyo, kama ilivyotarajiwa jambo hilo halikuwafurahisha wakubwa ndani ya chama chake. “Hii ni sera ya vyama vya upinzani kama Raza haridhiki na CCM, ni heri akaondoka na kujiunga na wenye sera ya Tanganyika”. Alisema Mapuri. Mohamed Raza aliyetishwa na Mapuri bado ni yule yule? Au kalainika hataki tena Tanganyika Hanga, Twala waliuliwa, isiwe sababu Msitake kuwaziba wananchi midomo Abdalla Kassim Hanga na Abdulaziz Khamis Twalla waliuliwa kikatili. Basi isiwe sababu ya kufunga midomo na kuogopa kusema kweli. (Soma uk. 6) MHE. Mohamed Raza Mauti ya umoja wa kijamii Lawama atabeba “Abu Idd”, Sheikh Mataka Sikiliza nasaha za Profesa Noam Chomsky Wananchi wasimame wazomee, wapinge Shein mahali pake UN Sio Baraza la Bawaziri Bongo Si Waziri, si Makamu wa Rais Utafutwe muundo mpya unaofaa Uk. 9 Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein SHEIKH Mohamed Idd (aliyesimama). Kushoto ni Bw. Idd Simba. Masheikh wapigwa msasa Markaz Uk. 16

Upload: annurtanzania

Post on 31-Aug-2014

508 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: annuur-1009

ISSN 0856 - 3861 Na. 1009 JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRIL 20 - 26, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

MHESHIMIWA Mohamed Raza aliwahi kutamka hadharani kwamba mfumo wa sasa wa Muungano unaiminya Zanzibar.

Raza alitaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kwa madai kwamba ndio suluhisho la matatizo ya Muungano.

H a t a h i v y o , k a m a ilivyotarajiwa jambo hilo halikuwafurahisha wakubwa ndani ya chama chake.

“Hii ni sera ya vyama vya upinzani kama Raza haridhiki na CCM, ni heri akaondoka na kujiunga na wenye sera ya Tanganyika”. Alisema Mapuri.

Mohamed Raza aliyetishwana Mapuri bado ni yule yule?

Au kalainika hataki tena TanganyikaHanga, Twala waliuliwa, isiwe sababu Msitake kuwaziba wananchi midomo

Abdalla Kassim Hanga na Abdulaziz Khamis Twalla waliuliwa kikatili. Basi isiwe sababu ya kufunga midomo na kuogopa kusema kweli. (Soma uk. 6)

MHE. Mohamed Raza

Mauti ya umoja wa kijamiiLawama atabeba “Abu Idd”, Sheikh MatakaSikiliza nasaha za Profesa Noam ChomskyWananchi wasimame wazomee, wapinge

Shein mahali pake UNSio Baraza la Bawaziri BongoSi Waziri, si Makamu wa RaisUtafutwe muundo mpya unaofaa

Uk. 9

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein

SHEIKH Mohamed Idd (aliyesimama). Kushoto ni Bw. Idd Simba.

Masheikh wapigwa

msasa MarkazUk. 16

Page 2: annuur-1009

2 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri/Ujumbe

K AT I K A k i p i n d i hiki ambacho watu wamekuwa wakitumia elimu na taaluma zao katika kujinufaisha kwa namna yoyote, h a t a k a m a k a t i k a hilo kuna kujidhuru mtu mwenyewe au kuidhuru jamii na taifa kwa jumla, ni vyema Muislamu ukakumbuka kwamba Mtume wako Muhammad (s.a.w.) a m e k u f u n d i s h a umuombe Mwenyezi M u n g u k i l a s i k u akukinge uepukane na elimu isiyokuwa na manufaa kwako na kwa jamii.

A m e p o k e a Z a i d Bin Arqam kwamba Mtume (s.a.w.) alikuwa akiomba dua hii: “Ewe

Epuka elimu isiyokuwa na manufaaMola wangu, nakuomba unikinge nisiwe na elimu isiyokuwa na manufaa, na moyo usiokuwa na unyenyekevu, na nafsi isiyoshiba (isiyitosheka), na dua isiyojibiwa”. Ameipokea Hadithi Imam Muslim.

A m e s e m a I m a m Atwibiy kuwa: “Elimu isiyokuwa na manufaa ni ile ambayo mwenye nayo haitumii, hawafundishi wengine na haimrekebishi kitabia na kimaadili”.

Imam Alghazaliy naye anasema kuwa “Elimu isiyokuwa na manufaa ni ile ambayo ina madhara kwa yeye mwenyewe mwenye nayo au ina madhara kwa wengine”.

Kwa hiyo, ni wajibu wako ndugu yangu

M u i s l a m u ; w e w e unayesoma au ambaye t aya r i umeshasoma na tayari una taaluma, kumbuka Uislamu wako unataka elimu na taaluma yako iwe na manufaa kwako na kwa jamii inayokuzunguka.

M u i s l a m u d a i m a jiulize: Je, elimu uliyo nayo ina manufaa gani kwako na kwa jamii yako?

Ikumbuke dua hii na kila siku iombe kama alivyokufundisha Mtume wako:

“Ewe Mola wangu, nakuomba unik inge n i s i w e n a e l i m u isiyokuwa na manufaa, na moyo usiokuwa na unyenyekevu, na nafsi isiyoshiba (isiyotosheka), na dua isiyojibiwa”.

WITO umetolewa kwa wanawake wa Kiislamu kuingia katika shuguli za uchumi kwa juhudi, uvumilivu na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Wito huo umetolewa na maafisa masoko wa benki za NMB na CRDB katika semina ya wanawake wajasiriamali wa Kiislamu iliyofanyika katika ukumbi wa DYCC Kariakoo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Semina hiyo iliyoandaiwa na wanawake wa Kiislamu jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni kwa ajili ya kukumbushana na kuelimishana juu ya utaratibu wa biashara kwa mujibu wa dini ya Kiislamu ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa, ikiwemo mada ya ujasiriamali.

Akizungumzia mada ya ujasiriamali, Meneja Masoko wa benki ya NMB Bi. Shilla Senkoro, alisema kuwa wajasiria mali wengi wanashindwa kutimiza

Benki watoa somo la ujasiriamali kwa kina mama wa Kiislamu

Na Pendo Masasa malengo yao kutokana na kukabiliwa na changamoto nyingi.

Al iz i ta ja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa elimu, hasa ya biashara au shughuli anayoifanya, ukosefu wa mtaji na ujuzi mdogo juu ya masoko, ukosefu wa utafiti na masoko ya uhakika.

A l i s e m a i w a p o mjasiriamali atajiandaa na kumudu kuzikabili changamoto hizo kabla ya kuanza biashara yake, ni wazi kwamba atafaulu.

Aidha Meneja huyo M a s o k o a l i w a t a k a wajasiriamali wanawake wa Kiislamu kuepukana n a b i a s h a r a h a r a m u kwa mujibu wa dini ya Kiislamu.

Alitoa mfano wa watu w a n a o f u g a k u k u w a nyama na kuwapa vidonge vya majira ili wakue na kunenepa kwa muda mfupi, lengo likiwa ni kupata faida kubwa bila kujali madhara makubwa wanayosababisha kwa binadamu.

Katika hali hiyo, japo biashara hiyo ni halali, lakini utaratibu wa kuzinenepesha unaingiza uharamu.

Naye Meneja Masoko benki ya CRDB Amina Muhaji, aliwataka akina mama hao wa Kiislamu kumtanguliza kwanza Mwenyezi Mungu kabla ya kuanza biashara yoyote ile.

A l i w a t a k a k w a n z a wamuombe Mwenyezi Mungu awaongoze katika biashara zao kabla ya kuzianza.

Alisema kuwa kuwa baada ya kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kumuomba asaidie kufikia malengo katika biashara yao, akina mama hao wanapaswa watulie wafikirie biashara ya kufanya kwa kufanya utafiti , kwa kuangalia maisha ya watu wanaoishi nao katika eneo la biashara na kujua mahitaji yao .

Alisema kuwa utafiti huo utamsaidia mjasiria mali kwani mambo yanabadilika kila siku .

JANA Aprili 26 Watanzania wameadhimisha miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano ulioasisiwa na Marais, Hayati Julius Kambarage Nyerere wa Tanganyika na Marhum Mzee Abeid Aman Karume Zanzibar, Aprili 26 1964.

Wa k a t i Wa t a n z a n i a wakiadhimisha sherehe hizo, Muungano wenyewe umeende la kugubikwa na kasoro lukuki, kiasi cha kuzua maswali na malalamiko miongoni mwa Watanzania wa pande zote mbili za muungano. Imefikia hatua kwamba wapo baadhi ya Watanzania ambao kwa kushindikana au kuchelewa kutatuliwa kero hizo za kimuungano, wamediriki hata kutangaza kutouhitaji muungano wenyewe.

Mfano mzuri ni watu 12 waliokamatwa na polisi Zanzibar hivi karibuni kwa kufika katika eneo la Baraza la Wawakilishi kufikisha kero yao juu ya muungano. Wengi wanakosoa muundo wa muungano wa sasa wa serikali mbili , hususan wanasiasa ambao wanataka marekebisho yafanyike na uwe wa serikali tatu au moja.

Wazanzibar kwa upande w a o , w e n g i w a n a o n a kuwa mamlaka ya serikali yao imemezwa na dola ya Muungano, ambayo inaonekana kama ni dola ya Watanganyika. Kwamba Rais wa Zanzibar hana mamlaka kama Rais wa nchi. Anafananishwa na mkuu wa mkoa ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Hata u le mgawanyo wa rasilmali za nchi, nao umeonekana kuwa ni kero kubwa kati ya pande hizi mbili za Muungano na kuzua tafrani ndani ya vyombo vya kutunga sheria husan katika Bunge na kwenye Baraza la Wawakilishi.

Aidha mfumo wa kutoza kodi wa serikali ya Jamhuri na ule wa serikali ya Zanzibar umekuwa ukilalamikiwa, lakini zaidi na watu wa visiwani kwamba sio wa haki.

Gwaride zuri lakini kero za muungano zingalipo

K w a k w e l i h i z i n i baadhi tu ya kero ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu ambazo zinauandama Muungano. Kwa makusudi au kwa bahati mbaya, kadiri muda unavyokwenda ndivyo mvutano juu ya kero hizi unavyozidi kuwa mkubwa.

Licha ya kuwepo juhudi za kuundiwa Wizara ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano, mahsusi kwa ajili ya kutatua kero za Muungano, lakini inasikitisha kwamba hadi leo kero hizi hazijapatiwa utatuzi wa kudumu.

Wala hatuoni wananchi wakipewa taarifa za uhakika kwamba ni kwa kiasi gani wizara hii imefanikiwa kutatua kero za muungano ikizingatiwa kwamba Wizara imeundwa mahsusi kwa ajili ya kazi hiyo.

Tulidhani kwamba kila inapofika siku ya kuadhimisha sherehe za Muungano, basi ungekuwa muda muafaka wa wizara kueleza imefanya nini katika kutatua kero za muungano wenyewe ili wananchi wafahamu, badala ya kutizama magwaride ya majeshi na kushuhudia itifaki za kiserikali wakati baadhi ya wananchi wanatokota juu ya muundo wa muungano wenyewe.

Kutokana na kutopatikana matunda yanayoonekana ya kuwepo hiyo Wizara ya Muungano, ndipo zinapokuja hisia kwa wananchi wa pande zote mbili kwamba, labda Wizara hiyo imeundwa kwa ajili ya kuwapa watu ajira na kuongeza tu matumizi ya serikali.

Kwa mtazamo wetu , hatudhani kwamba serikali inaweza kutatua kero za Muungano wa sasa kwa kupitia hiyo wizara yake. Labda mabadiliko ya kweli yataletwa na huu mchakato wa maoni juu ya katiba mpya.

Na hilo litafaulu iwapo m c h a k a t o w e n y e w e utaendeshwa kidemokrasia na kwa ukweli na uwazi.

Wananchi waruhusiwe kutoa maoni yao juu ya muundo wa muungano na maoni yao yathaminiwe.

Page 3: annuur-1009

3 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Habari

Tiba asili ya malariaNa Bakari Mwakangwale

Shein mahali pake UNIMEELEZWA kuwa hadhi ya Rais Dr. Ali Mohammed Shein ni kukalia kiti katika Umoja wa Mataifa (UN) akiiwakilisha Zanzibar na sio kuingia katika Baraza la Mawaziri Tanzania.

Kuingia katika kabineti ni sawa na kumvunjia heshma Rais huyo wa Zanzibar kwani hana cha kufanya katika Baraza hilo. Yeye si Waziri wala hawezi kuendesha Kebineti inapokuwa Rais hayupo.

H a y o y a m e e l e z w a katika mjadala uliokuwa ukiendeshwa jana asubuhi katika Channel Ten ambapo mada ilikuwa juu ya muungano baada ya miaka 48.

Ak izungumza ka t ika mjadala huo, Bwana Suleiman Kindy aliyejitambulisha kuwakilisha taasisi mbalimbali za Kiislamu amesema kuwa h o j a i n a y o z u n g u m z w a hivi sasa sio kuwepo kwa muungano au la, lakini muundo gani wa muungano.

Akisherehesha hoja yake kwa kunukuu vifungu vya katiba akasema kuwa ilivyo ni kuwa Tanzania Bara ndio serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mtindo huo Zanzibar inapunjwa na kuhisi kuwa imekaliwa, inakabwa haina uhuru.

A k a t o a m f a n o ilivyokemewa na kuzuiwa kuingia katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC).

Lini Rais wa Jamhuri anaapa kwamba sasa anafanya mambo ya Tanzania Bara, na lini anafanya kazi kama kiongozi wa Tanzania Bara? Hakuna.

Yale mambo yanayoitwa ni ya Tanzania Bara ambayo hayatafanywa na serikali ya muungano kama katiba inavyosema, hufanywa na serikali ya muungano, h u f a n y w a n a R a i s w a muungano. Kwa hiyo Tanzania Bara imegeuka kuwa ndiyo Jamhuri ya muungano.

Hayo ndiyo maoni na hoja za taasisi za Kiislamu Zanzibar kama zilivyowasilishwa na Bwana Kindy ambaye alisisitiza kuwa katika hali ya namna hi i Zanzibar inajihisi kuwa imekaliwa, haipumui, inaminywa na kudhalilishwa.

Akizungumzia Baraza la Mawaziri ambalo Rais wa Zanzibar ni mjumbe anasema kuwa, kuingia kwa Rais huyo katika Baraza hakuna maana yoyote, sana ni kumvunjia heshma.

Akasema, kifungu cha 54 (1) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) kinasema kuwa,

Na Mwandishi Wetu

“Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.”

Akirejea 54 (2) akanukuu kwamba: “Rais atahudhuria m i k u t a n o y a B a r a z a l a M a w a z i r i n a n d i y e atakayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza Mikutano.”

Baada ya kunukuu kifungu hicho akahoji, nini nafasi na kazi ya Rais wa Zanzibar katika kebineti, maana yeye si Waziri na hawezi kumwakilisha Rais wa Jamhuri katika kikao hicho, kinyume chake anakuwa chini ya Makamu wa Rais au Waziri Mkuu, inapokuwa Rais hayupo.

Katika watoa hoja waliopiga simu kuna waliosema kuwa inafaa muungano uendelee kama ulivyo maana hiyo ndiyo njia pekee ya kuwafanya Wazanzibari kubaki katika amani.

Akadai kuwa muungano ukivunjika u-CUF na U-CCM uliojaa chuki utasababisha vurugu.

Hata hivyo akijibu hoja

hiyo Suleiman Alkindy alisema kuwa kama ni vurugu zipo Bara ambapo Chadema walishafikia mahali pa kupiga hata viongozi wa serikali kama walivyofanya kule Igunga walipomkwida Mkuu wa Wilaya na kudhalilisha

hadharani.Akataja pia vurugu za CCM

na Chadema katika uchaguzi uliopita Arumeru Mashariki.

A k a s e m a , Z a n z i b a r haijafikia hatua hiyo ya kupiga viongozi wa serikali, wala hakuna ile chuki na vurugu

za ki-Chadema za kutaka nchi isitawalike.

A k i j i b u m a d a i y a mgawanyiko wa Unguja na Pemba akasema kuwa huo ni mgogoro na mpasuko hewa unaopandikizwa na maadui wa Zanzibar.

Alisisitiza kuwa siasa za chuki na hasama zinafanya kupandikizwa kuwatisha wananchi wa Zanzibar ili watishike na wasahau kudai utaifa wao na nchi yao.

Kwa wale waliodai kuwa hivi sasa Wazanzibar wamejaa Bara wakifanya biashara na kwamba wamejenga, alisema kuwa Wazanzibari hawapo Bara pekee.

Wapo London, Canada, Oman na nchi mbalimbali diniani wakitafuta mali na hata kuishi kama ambavyo Wachina wamejaa Tanzania Bara wakifanya biashara.

Kwa hiyo suala la kufanya biashara lisichanganywe na masuala ya muungano.

Aidha a l i s ema kuwa kupitia muundo wa muungano uliopo hivi sasa na nafasi ya TRA, umefanya uchumi wa Zanzibar kudorora. Na hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za wataalamu wa kiuchumi.

Akihitimisha akasisitiza kuwa kinachotakiwa ni muundo huu kutizamwa upya ili nchi zote, Tanganyika na Zanzibar zinufaike na muunganio badala ya sasa ambapo upande mmoja unajihisi kama umekaliwa kooni.

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein

SERIKALI imetakiwa kuwapa fursa wataalamu wa tiba asilia nchini kwa kuzitangaza dawa zao baada ya kuzithibitisha ili waweze kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwamo malaria.

Wito huo umetolewa na mtafiti wa dawa na tiba asilia Jijini Dar es Salaam Bw. Mohammed R. Mkweli (35), akiongea na An nuur Jumatano wiki hii katika kilele cha kuadhimisha siku ya malaria duniani (April 25, 2012).

Mkweli amesema, wakati umefika kwa serikali kutoa kipaumbele kwa tiba asili na kuachana na tabia ya kuomba misaada kwa Wazungu (Ulaya) kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa malaria.

M k w e l i anayejishughulisha na tiba asili kwa kufanyia utafiti dawa asili katika maradhi mbalimbali na kuzipeleka

kwa Mkemea Mkuu wa Serikali kuthibitishwa, alisema badala ya kutumia mapesa mengi na malaria ipo pale pale, ni vyema w a k a j a r i b u k u t u m i a wataalamu wa ndani (dawa asili) katika vita hiyo.

Alisema, yupo tayari kushughulikia ugonjwa wa malaria kwa kutumia dawa zake za tiba asili, katika sehemu zinazojulikana n a s e r i k a l i k u w a zinasumbuliwa na malaria sugu ili aweze kwenda kuthibisha kuwa dawa asili zinaweza kuwa suluhisho la tatizo hilo.

“ N a i o m b a S e r i k a l i iniruhusu au inipe Wilaya tatu zinazosumbuliwa na malaria sugu, nina imani kwa kutumia dawa yangu ijulikanayo kwa jina la Malaria One, inaweza kutokomeza tatizo hilo.” Alisema

A l i d a i , d a w a y a k e h i y o ( M a l a r i a O n e ) imethibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali na kupewa hati yenye kumbukumbu namba 341/VOLXIII/II/42, ya mwezi Septemba 26, mwaka 2011.

Mtaalamu huyo, ambaye hati yake hiyo ilitiwa saini na Naibu Mkemia Mkuu wa Serikali, alisema tiba asili pamoja na kutopewa nafasi na wataalamu na hata wanasayansi ni wazi zina uwezo wa kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

A l i s e m a , j a m i i inakabiliwa na changamoto ya maradhi mengi hivyo alitowa wito kwa wananchi kufika katika kituo chake cha Afya (Bora Herbal Clinic) kilichpo Kigogo, Jijini Dar es Salaam.

A l i s e m a , Wa b u n g e wamekuwa wakisimama Bungeni, wakisema kuwa

dawa ya Kisukari, presha haz i japa t ikana lak in i si kweli kwani al idai maradhi hayo dawa zake zinapatikana kwa dawa za asili (Miti shamaba).

Alisema, ni aibu kwa Serikali kuendelea kuwa ombaomba kukabiliana na malaria nchini sambamba na vifaa kutoka Ulaya badala ya kutoa ushirikianao kwa dawa asili ili wajiridhishe ili na wao watoe mchango wao badala ya kuwategemea wazungu.

Bw. Mkweli alionyesha w a s i w a s i w a k e k w a mamlaka za Serikali kwa kuwa wagumu ku toa vibali kuruhusu dawa asili kuingia katika soko la ndani ili zishindanishwe na zile za Ulaya, akisema huenda kuna mgongano wa kimaslahi ndani yake.

Bw.Mkweli, alisema yeyote anaye hitaji tiba asi l i zi l izothibi t ihwa, awasiliane naye kwa namba za simu 0713 477725/0779 487725.

Page 4: annuur-1009

4 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012Makala/Tangazo

Jumuia ya wanafunzi na vijana wa Kiislamu Tanzania (TAMSYA) inawaalika wanafunzi wote wa Kiislamu kuhudhuria kongamano la semina elekezi ya kiwango cha ufaulu kidato cha pili litalofanyika inshallah.

TAREHE: 29/04/2012. JUMAPILIMAHALI: UWANJA WA MAONESHO SABASABA MUDA: SAA 1:30 ASBH HADI SAA 6:30 MCHANA

Mada mbalimbali zitawasilishwa

Utakapo pata taarifa hii mjulishe na mwenzio.

Katibu Idara ya Habari TAMSYA mkoa0654 290875

Tanzania Muslim Students and Youth Association (TAMSYA)

KONGAMANO LA WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI JUU YA SEMINA ELEKEZI YA KlWANGO CHA

UFAULU

CAIRO – WA K I WA w a n a i s h i k a t i k a m i t a a y a wahamiaji maskini, jamii ya Waislamu Ufaransa imejiandaa kutompigia k u r a R a i s N o c o l a s Sarkozy katika Uhaguzi Mkuu ujao kutokana na sera zake za kudharau shida zao kuwa mpinga Wahamiaji na Uislamu.

“Waislamu wa Ufaransa h a w a t a v u m i l i a t e n a . Wamechoshwa na mijadala hii ya utambulisho wa utaifa, vyakula halali, hijab au kauli za msimamo mika l i k i l a maha l i , ” a l i ie leza Washington Times, Francoise Lorcerie, mtaalam wa masuala ya kijamii wa Institute of Studies on the Arab and Muslim World jirani na jiji la Marseille.

“Maneno ya Uislamu, wahamiaji, na msimamo m k a l i y a m e k u w a yakitumiwa bila kujali, huku watu wakilengwa kudhalilishwa ili kupata kura”.

Waislamu Ufaransa wanakadiriwa kufikia milioni sita, wamekuwa kwenye matatizo miezi kadhaa iliyopita baada ya Uislamu na wahamiaji kuwa somo kuu katika kampeni za uchaguzi z a w a g o m b e a U r a i s kufuatia uchaguzi Mkuu utakaofanyika kuanzia Aprili hadi Mei mwaka huu.

Akijaribu kupata kura za watu wa mrengo wa kulia, serikali ya Rais Sarkozy imezidi kutilia mkazo u jumbe wake dhidi ya wahamiaji na mwezi Januari ilitangaza kuwafukuza wahamiaji wasio halali mwaka 2011.

Sarkozy, mgombea k u p i t i a c h a m a c h a wahafidhina cha Union for a Popular Movement (UMP), ametaka kubanwa wahamiaji kwa sababu ya kile kinachoitwa “kuna wageni wengi” Ufaransa.

Naye Marine Le Pen, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha mrengo wa kulia cha National Front Party, yeye amesema kuwa

Waislam kutompigia kura Sarkozy Ni kwa sera zake za kupinga Waislamu

anashangazwa na “kiasi cha Waarabu aliowaita wa Mohammed Merahs, kuwa wanawasili kwa boti na ndege kila siku na kuijaza Ufaransa na wahamiaji.”

Kauli hizo zimewaudhi Waislamu wa Ufaransa kiasi cha kuzua mijadala juu ya asili na utambulisho wao.

“Wanaoi twa Merah wamezaliwa Ufaransa. Hakuja kwa boti wala ndege, lakini kila mmoja anahoji asili yake licha ya kuwa ni Mfaransa,” alisema Mohamed Mechmache, Rais wa AC Le Feu, Jumuia inayohusika na kuinua hali za wahamiaji wafaransa maskini.

Waislamu walilipuka dhidi ya kampeni za wagombea wahafidhina wa mrengo wa kulia wakisema kuwa wanachohitaji hasa wakazi wa mitaa hiyo ya watu maskini ni elimu na kazi, sio mapambano dhidi ya Uislamu.

Wakionyesha hasira yao dhidi ya sera za wahafidhina wa mrengo wa kulia, wanaharakati wamesema kuwa Waislamu w a n a w a u n g a m k o n o wagombea wa mrengo wa kushoto ambao wanaunga mkono wafaransa wenye asili ya wahamiaji.

Kwa sasa Waislamu wa Ufaransa wanaonekana kumkubali mgombea Urais kwa tiketi ya Socialist, F r a n c o i s H o l l a n d e , m g o m b e a a m b a y e anaonekana kuwa namvuto na mpinzani mkubwa katika uchaguzi ujao wa Mei 6.

Mgombea huyo katika kampeni zake ameahidi atapunguza kodi za pango na bili. Jambo ambalo kila mmoja amevutwa nalo.

Wakati huo huo, habari kutoka Paris Ufaransa, zimeeleza kuwa utawala wa nchi hiyo umemzuia mwanazuoni maarufu wa Kiislam, Sheikh Yusuf Qaradawi kuingia nchini humo kuhudhuri mkutano mkubwa wa Kiislamu mwezi ujao.

“Nimeweka wazi kuwa kuna watu walioalikwa

ka t i ka mku tano huu ambao hawatakaribishwa k u k a n y a g a a r d h i y a Ufaransa,” amenukuliwa akisema Rais Nicolas Sarkozy alipozungumza na France Info radio.

S h e i k h Q a r a d a w i , a m b a y e n i R a i s w a International Union for Muslim Scholars (IUMS), alipewa mwaliko kutoka Union for French Islamic Organizations (UOIF) kuzuru Ufaransa.

Lakini Rais Sarkozy amesema kuwa Qaradawi, ambaye anaishi nchini Q a t a r, h a t a r u h u s i w a kuingia nchini humo.

“ N i m e m f a h a m i s h a Amir wa Qatar mwenyewe k w a m b a m t u h u y u h a k a r i b i s h w i n d a n i ya mipaka ya Jamhuri ya Ufaransa,” alisema Sarkozy.

Hatua hiyo ya Rais Sarkazy imekuja siku chache baada ya kutangaza kupiga marufuku wahadhiri a m b a o a n a d a i k u w a wanasaidia “kuongezeka k w a m i t a z a m o y a “ m i s i m a m o m i k a l i ” kufuatia wimbi la mauaji yalidaiwa kufanywa na Al-Qaeda yaliyotokea jijini Toulouse.

“Mtu huyu hahitaji Visa kwa sababu ana pasi ya kusafiria ya kidiplomasia, lakini hatua zitachukuliwa kumzuia kuingia Ufaransa,” Sarkozy aliieleza French Radio J.

Siku ya Alhamisi ya Machi 29, serikali ya Ufaransa ilizuia wanazuoni wengine maarufu wa Kiislamu wanne kuingia nchini humo kuhudhuria mkutano huo.

Wanazuoni waliozuiwa n i She ikh Ayed B in Abdallah al-Qarni na Sheikh Abdallah Basfar kutoka Saudi Arabia

Wengine ni mhubiri maarufu kutoka Misri Sheikh Safwat al-Hijazi na Mufti wa zamani wa Jerusalem, Akrama Sabri.

M e y a w a z a m a n i wa jiji la London, Ken Livingstone amekuwa ak imwelezea She ikh Qaradawi kama “kiongozi

wa Kiislamu mwenye mtazamo wa kimaendeleo” na kumfanan i sha na mwanabadiliko Pope John XXIII.

Meya huyo wa zamani

amekuwa akisifia misaada ya kidemokrasia ya Sheikh Qaradawi na jitihada zake katika kujenga daraja kati ya Uislamu na watu wa Magharibi.

Rais Nocolas Sarkozy

Page 5: annuur-1009

5 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Kimataifa/Tangazo

Uongozi wa Msikiti wa Istiqama Ngunguti Wilayani Mkuranga, unaomba mchango wako kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa nne (4) ambalo litakuwa Msikiti na shule ya sekondari kidato cha tano na sita.

Uongozi unaomba msaada wenu wa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa jengo hilo.

Unaweza kutuma mchango wako moja kwa moja Msikitini hapo au kwa Account-Msikiti Istiqama Ngunguti Islamic NBC 0542 06005461 au unaweza kuwasiliana na Ustaadh Muhidin 0716 427 842

Wabillah Tawfiq

Tangazo

������� ��� ����� ��� ������� ��� ������������� ��� ����� ������� ��������� ��������������� ��������� ������������� ��������� ����� ��������� ������ ������ � �� � � ������� ����� �������� ������ �������� ��������� ��� ����� ��� ������� ��� ����������� ��� ������� ����������� �������

���������� � � ������� ������������ ������� ��� ����� � �� � � � � � � � � � �� � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � ������� � ���� ���� ��� ������� ���� �����

����� ��� � � � � � � � ����� ���������� ������ ��� ������ ����������� � � � � � � � � � � � � � � � ��� ����� �������� ������� ���������� � � � � � � � � � � � � � � �

����� ��� � � � � � � � � � � ����� ��� ������� ��� ��������� ������������� � � � � � � � ��������� ���� ����� ������ � ������ � � � � � � � � � � � �

� � � � � � � � � � � � � � � � � � � ���� ������ ������

����� ������ � � ����� ����� ������� ���������� � � � � � � � ��������� � � � � � � � � � � � � � � ������������ � � � ������ ��� �������� ��� � � � � � � � � � � � � � � � � �

� � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � ������� �������� � ���������� � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � � ���������� � ���� ����� ��� ������ ��� ��������� ��� � �����

������ � � ����� ������������� ���� ����� ��������� � ������� �� � � � � � � � ������� ���� �� ������ ���������� ������� �������� � � � � � � � � � � � �� � � � � � � � ������� ��� ������� �������� ������ � ������� �� � � � � � � ������� � ������

����� ���������������

����� ������� ��������� ��������

� �������� � ������� ������ ������������� ���� ��� ������� �� ��������������� ����� ���� �������� ����� ���� ������

��� �� �� �� ��� � �� �� �� ��� �� ��

����� ���� ���� ��������� � ���� ��������

��� ���� ���� � �� �� ��� �� ��

��� �

� ��� �

� �� �

� �

� ����� � �

� �� ��

GAZETI la kila wiki linalochapishwa nchini Marekani lijulikanalo kwa jina la Free Press, l i m e a n d i k a k u w a viongozi wa Ikulu ya Marekani White House, w a n a t o a m a f u n z o ya ugaidi kwa watu wanaowaua kigaidi wasomi wa Kiirani.

Gazeti la kila wiki la American Free Press l i m e a n d i k a k u w a , licha ya kwamba Rais B a r a c k O b a m a w a Marekani anazungumzia udharura wa kutumika udip lomasia ka t ika kufanya mazungumzo na Iran, lakini wakati huo huo viongozi wa White House wanaendesha siasa za kutoa mafunzo kwa makundi ya kigaidi kwa lengo la kuwauwa

White House yatoa mafunzo kwa makundi ya kigaidi makamanda wa kijeshi na wasomi wa Kiirani.

Free Press, gazeti la kila wiki linalochapishwa Marekani, limeendelea kuandika kuwa, Rais Obama anaendesha siasa ambazo zilikuwa zikiendeshwa pia na Rais wa zamani wa nchi hiyo George W. Bush na Makamu wake Dick

Cheney. Mwandishi wa gazeti

hilo anayejulikana kwa jina la Simon Harsh, anasema kuwa, serikali iliyopita ya Marekani mwaka 2003 iliruhusu k u p e w a m a f u n z o wanachama wa kundi la kigaidi la MKO katika jangwa la Nevada nchini Marekani.

M A G A Z E T I y a Marekani yamechapisha p i c h a n y i n g i n e z a askari wa nchi hiyo h u k o A f g h a n i s t a n w a k i d h a l i l i s h a n a kuvunjia heshima maiti za Waislamu.

Udhal i l ishaj i huo umezua mjadala mkubwa katika fikra za walio wengi duniani.

M a g a z e t i h a y o yamechapisha picha 18 mpya za askari wa Marekani wakichekelea huku wakidhalilisha mai t i za Wais lamu w a l i o w a u w a h u k o Afghanistan.

Gazeti la Los Angeles Times, limeandika kuwa kuchapishwa kwa picha hizo zinazoonyesha utovu wa maadili ya kibinadamu wa askari wa Marekani huko

Askari wa Marekani wadhalilisha maiti

Afghanistan, kutaweka matatani maisha ya askari hao wavamizi huko Afghanistan.

Miezi mitatu iliyopita, vyombo vya habari vya Marekani vilionyesha m k a n d a w a v i d e o unaowadhihirisha askari wa nchi h iyo huko

Afghanistan, wakikojolea maiti za wapiganaji wa kundi la Taliban huku wakiwatusi.

Picha hizo za dharau na utovu wa maadili ya kibinadamu za askari hao zilizua kulaaniwa na walimwengu duniani kote.

Rais Barack Obama

Page 6: annuur-1009

6 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012Makala

BAADHI ya v iongoz i hutufanyia biashara ya siasa ya kutupotosha ili tusipate kuujua ukweli na viongozi hao hufanya kazi hiyo baada ya wao kupokea rushwa kwenye sekta ya siasa.

Rushwa hii ndio chimbuko la matatizo ya Zanzibar katika mambo ya Muungano. Rushwa inayopokewa na wanasiasa n d i o i n a y o i a n g a m i z a Zanzibar. Eneo la siasa l i takaposafishika ndipo tutakapo kuwa na Serikali safi Visiwani Zanzibar. Lakini kuna rushwa ya Taifa, hii inawafuata wale wenye sifa ya kujikomba na kujipendekeza. Rushwa ya viongozi hao haijali Elimu waliyokuwa nayo. Sana hupokea rushwa ya vyeo na nafasi za juu katika serikali na chama tawala. Hapo ndipo hupokea fedha kupitia vyeo na nafasi walizotunukiwa ndani ya serikali na chama.

Kazi zao hasa hutakiwa kubadili misimamo ambayo haitakiwi kuiunga mkono kwa vile haina maslahi ya wakubwa ndani yake au kuwashawishi viongozi wenzao na wananchi kuachana n a m i s i m a m o a m b a y o itawavurugia mipango yao ya muda mrefu juu ya jambo lolote lile lililokwisha pangwa kwa kusingizia sera au sababu nyengine yeyote ile.

Hapo ndipo tunapojikuta Wa z a n z i b a r i h a t u n a chochote cha maendeleo katika nchi yetu isipokua ugomvi miongoni mwetu na hasama ndio zinatamalaki visiwani. Kumbe katika uhalisi wa mambo, nchi yetu hupata viongozi ambao hawakustahiki kuongoza

Rushwa ya kisiasa inaiangaza Zanzibar

Na Ibrahim Mohammed Hussein

chochote zaidi ya kufanya shughuli zao. Viongozi wanaweza kupangua safu za uongozi kama atakavyo na kuweka watu watakaoitikia hewala kwa kila jambo hata kama linaiangamiza Zanzibar.

V i o n g o z i w a a i n a hii tuwaangalie bila ya kupepesa, siku ya kusema hapana ndio unaanza uadui na kunyang’anywa hicho cheo wal ichozawadiwa maana uongozi unageuka kuwa zawadi , na hapo ndipo zinapoanza siasa za kufadhiliwa.

Mtindo huo unapoteremka hadi chini kwenye ngazi za masheha na udiwani ndio inakua mfumo balaa ambao wananchi hawawezi kuupinga kwa vile nafasi nyingi za uongozi huo zimepatikana kwa kujikomba au kwa kufadhiliwa au kwa kufanya maovu mengi tu ambayo watawala huyaridhia.

Leo kiongozi anathubutu ku te tea mfumo ambao unaimaliza na kuipokonya Z a n z i b a r u w e z o w a kujiamulia na kujitengenezea uchumi wake kwa kisingizio cha “ tumeshazaana au tumejenga huko Tanganyika” huyo natumuangalie bila ya kupepesa.

K i o n g o z i h u y o h i v i karibuni alikua mbogo na ku thubutu kumwambia mwenzake ajiuzulu nafasi yake ya uwaziri kwa sababu anataka kutoa sehemu ya nchi (mipaka ya bahari) iwe chini ya himaya ya Serikali ya Muungano. Leo kiongozi huyo huyo yuko radhi kuiuza nchi nzima sio sehemu tu ya nchi, sijui tumuelewe vipi? Au ndio vyeo vya rushwa ambavyo sio saizi yake hana uwezo na hiyo nafasi aliopewa, lakini kapewa tu kwa kazi maalum ya kuipigia debe sera inayoibana Zanzibar isifurukute katika hali zote za kiuchumi na kisiasa huku akitaka watu wote waseme “Tunataka Muungano”, kwani ni lazima Muungano?.

Akitokea mtu akisema siutaki iwe ni kosa? Basi Karume aliukataa Muungano huu wa mmoja kumtambia mwenzake. Uamsho nao wana haki na nchi hii wana sehemu ya urithi vile vile. Sio viongozi peke yao ndio wenye haki na nchi hii. Wao ni miongoni mwa Wazanzibari wanopenda kuiona nchi yao inapata mafanik io ya kiuchumi na kijamii. Wananchi wake wanaishi kwa amani na upendo bila ya kubaguana. Mimi hivi ndio

ninavyowaona hawa kundi la Uamsho.

Vile vile kwa upande mwengine ninawaona baadhi ya viongozi wa serikali na chama ambao wamedhamiria na kujizatiti kwa gharama yoyote i le , kuendeleza maslahi ya upande wa pili wa Muungano huu.

Sio ugomvi, kuukataa Muungano, wale wanaoukataa Muungano wana sababu zao na hawazifichi wanazisema kwa kinywa kipana. Na wale wanaoutaka Muungano vile vile wana sababu zao vile vile. Toweni sababu za kuukataa na kuukubali, tutazisikiliza mwisho uamuzi tutakuwa nao sisi wananchi.

Wenzetu wa Uamsho wanazo sababu za uhakika na zenye ukweli kuliko viongozi wa chama na Ser ikal i . Wanachodai wao Uamsho ni kitu cha msingi kabisa. Mkataba wa Muungano wa asili uliotiwa sahihi na Karume uko wapi? Ni Mzanzibari gani asiounga mkoni dai hili? Mimi nimemsikia Mh. Aboud Jumbe Mwinyi akisema yeye hakuwahi kuushuhudia mkataba huo kwa macho yake. Mwinyi vile vile amewahi kutamka kwamba yeye hakuwahi kuuona mkataba huo. Sasa viongozi wetu hawakuuona mkataba wa Muungano wal ikua

wakitawala kibubusa hakuna uhakika kama mkataba ule ulikua ni muda wa miaka kumi au ni wa milele hapana ajuwae, isipokua watu wawili waliokua nyuma ya mgongo wa Marehemu Karume alipokua akitia saini yake mkataba huo nao ni Hanga na Twala. Sasa kosa la wazee hawa wa kundi la Uamsho liko wapi?

Tunaelewa wazi kwamba viongozi wetu hawawezi kutueleza chochote kile ki l ichokua cha sir i , na wanaogopa kifungo cha miaka ishirini jela. Kuna sheria ya usalama wa nchi No. 3 ya 1970 kila kiongozi anatakiwa atie saini yake kwenye fomu maalumu isemayo:

“TAMKO RASMI LA KUTUNZA SIRI” Kiongozi huyo ikiwa yumo Serikalini au ameshaacha kazi hatakiwi kutangaza habari hizo kwa njia yoyote, ikiwa kwa maneno, maandishi, michezo ya kuigiza, sinema n.k katika Jamhuri ya Tanzania au mahali pengine popote.

Akifanya hivyo adhabu yake ni miaka ishirini jela. Ndio maana leo hatujamsikia hata kiongozi mmoja kutuelezea kisa cha Marehemu Karume al ipokwenda kumkabil i Nyerere na kutaka baadhi ya mambo ayaondowe ndani ya Muungano.

Viongozi hawatuelezi ukweli kwa hofu hiyo. Hawako tayari kujitolea kusema ukweli ili wananchi waelewe. Hofu imewagubika, wanaogopa kwenda jela, kwa hivyo nchi na itokomee lakini wao wawe salama.

Nakumbuka maneno ya Balozi Mohamed Ramia alipokua katibu mwenezi mpya wa CCM, alisema hadharani kuwa kuna “mabwana w a k u b w a w a n a o t a k a kuwachagulia viongozi wananchi wa Zanzibar Rai June8-14,2000.

Hii ni dhahiri viongozi w a Z a n z i b a r h u p o k e a kutoka Dodoma. Na kweli hilo lina ushahidi kwa lile tokeo la kuondolewa Mzee Aboud Jumbe madarakani huko Dodoma. Viongozi wote wenye akili ndani ya CCM Zanzibar huambiwa wapinzani pale wanapotoa hoja za msingi ambazo wakubwa huko Tanganyika hawazipendi. Ndani ya CCM hakuna mwenye jeuri ya kusema maoni yake ambayo yatakua kinyume na matakwa ya viongozi kutoka Bara basi akitokea kidume wa aina hiyo atakipata cha moto.

Mfano mzuri ni wa Mh. Mohamed Raza (hivi sasa ni muwakilishi wa jimbo la Uzini) aliwahi kutamka hadharani kwamba mfumo wa sasa wa Muungano unaiminya Zanzibar. Raza a l i t a k a k u u n d w a k w a Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano kwa madai kwamba ndio suluhisho la matatizo ya Muungano. Hata hivyo, kama ilivyotarajiwa jambo hilo halikuwafurahisha wakubwa ndani ya chama chake. Akijibu hoja hiyo ya Raza, katibu mwenezi wa CCM, Ramadhan Omar Mapuri, alisema kama Raza haridhiki na hali ya mambo ndani ya CCM ni vyema akaondoka na kujiunga na vyama vya upinzani.

“Hii ni sera ya vyama vya upinzani kama Raza haridhiki na CCM, ni heri akaondoka na kujiunga na wenye sera ya Tanganyika”. Alisema Mapuri, Mwanahalisi Mei 6-9,2006.

Viongozi hawa wapo wengi wamefichwa fichwa katika sehemu mbali mbali kuwapinga wazalendo katika madai yao ya msingi. Hawa ndio wale wanakula rushwa ya siasa, hupewa vyeo au huteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ndani ya nafasi hizo hupokea

RAIS mstaafu wa SMZ, Amani Abeid Karume.

Inaendelea Uk. 11

Page 7: annuur-1009

7 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Makala

KWA jina la Mwenyezi M u n g u , m w e n y e kuneemesha neema kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

Shukurani zote anastahili Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu wote na rehema na amani zimfikie mbora wa Mitume, bwana wetu Muhammad na jamaa zake na Masahaba zake wote. Ama baada ya utanguliza huu.

H a k i k a U i s l a m u u m e s h u g h u l i k i a s a n a matatizo mawili haya na umehimiza katika kuyatibu kabla hayajazuka kwa njia za kuyakinga. Panapozuka umasikini au ukosefu wa ajiria, basi huwekwa njia ya kuyatibu matatizo hayo. Miongoni mwa njia za kuyatibu hayo ni:-

Imani kiasi cha kuamini kwamba Mwenyezi Mungu yeye ndio muumbaji na mtoaji riziki. Anamuhimiza masikini aridhike na kile alichomgawia Mwenyezi Mungu kwake na imani hii inamsukuma mtu kutafuta sababu za riziki, ili kupata kile alichomuandikia Mwenyezi Mungu kwake. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (na hakuna mnyama yoyote yaani kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Mungu na anajua makao yake ya milele na mahali pake pa kupita tu (napo ni hapa duniani). Yote yapo katika kitabu kinachodhihirisha kila kitu.

Ucha Mungu: Hakika ucha Mungu humfungulia mtu milango ya kheri na riziki kwa namna asiyoijua, pale aliposema Mwenyezi Mungu (na anayemuogopa Mwenyezi Mungu humtengenezea njia ya kuokoka katika kila balaa) na humpa riziki kwa namna asiyoitazamia.

K u s h u k u r u : N a kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema zake inakuwa ni sababu ya kuzidi kheri na neema. Amesema Mwenyez i Mungu (na kumbukeni alipotangaza Mola wenu kuwa kama mkishukuru nitakuzidishieni.

Kuomba msamaha:- Hii ni sababu miongoni mwa sababu za baraka toka mbinguni na

Majukumu ya Msikiti katika kupiga vita umasikini na ukosefu wa ajira

Na Sheikh Mostafa Rashad Rushdy

ardhini na ongezeko la mali na watoto. Amesema Mwenyezi Mungu (nikasema muombeni m s a m a h a M o l a w e n u kwani yeye ni msamehevu, anateremsha kutoka mbinguni mengi na anakuongezeeni mali na watoto).

Kuimarisha Misikiti kwa kuswali na kuhifadhi, kwa kutoa huduma mbalimbali na kumta ja Mwenyez i Mungu na kuomba dua, k u m t a k a s a M w e n y e z i Mungu na kumshukuru kwani kwa kufanya hivyo anabubujiza neema zake kwa wanaoimarisha Misikiti yake kwa kheri za dunia na malipo huko akhera. Amesema Mwenyezi Mungu, ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na kusimamisha swala na kutoa zaka.

Kumtegemea Mwenyezi Mungu: Amesema Mwenyezi Mungu (na anayemtegemea Mwenyezi Mungu yeye humtosha , kwa yak in i Mwenyezi Mungu anatimiza kusudi lake, hakika Mwenyezi Mungu amekwisha kiwekea kila kitu kipimo chake). Kutoka kwa Omari (ra), nimemsika Mtume (saw) akiseme (lau mngemtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea angewaruzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaoondoka asubuhi wakiwa na njaa na wanarudi wakiwa wameshiba.

Kutotumia hovyo na kwa fujo ni sababu miongoni mwa sababu za ufakiri katika jamii. Kwa ajili hiyo basi umekataza Uislamu kutumia hovyo. Amesema Mwenyezi Mungu na kuleni na kunyweni lakini msifanye fujo kwani yeye hawapendi wafanyao fujo.

Ya pili: Njia za matibabu ya umaskini na ukosefu wa ajira.

Hakika miongoni mwa njia ya masikini katika kutibu matitizo haya ni:-

Kuhimiza watu katika kufanya kazi kwa uhuru kwa baadhi ya kazi za kujiajiri kama vile ufundi, kama walivyokuwa wakifanya Mitume (a.s) ambao ni kiigizo na mifano bora kwa kujiajiri na kuchuma kwa njia ya halali. Na mfano wa hao ni:-

Nuhu (a.s) amejifunza kutengeneza jahaz i na amemuamrisha Mwenyezi Mungu kuitengeneza katika neno lake (na uundaji jahazi mbele ya macho yetu (yaani katika hifadhi yetu, hawataweza kukuamuru na iwe sawa na amri yetu

(wahyi tuliokuletea) wala usinisemeze kuwasamehe wale walio dhulumu nafsi zao, kwani sitawasamehe kwa yakini wao watazamishwa) na akawa anaunda jahazi na kila wakimpitia maraisi makafiri wa umma wake, walikuwa wakimcheka na yeye husema kama nyinyi mnatucheka nasi tutakuchekeni kama mnavyotucheka (surat hud 37/38).

Daud i ( a . s ) a l ikuwa a k i k u s a n y a v y u m a n a kutengeneza kanzu za chuma kwa ajili ya vita. Amesema M w e n y e z i M u n g u , n a kwa hakika tulimpa Daudi fadhila kubwa kutoka kwetu (tuliyaamrisha majabali yawe yanaitikia dua za ibada pamoja naye, tukayaambia enyi milima rejezeni sauti pamoja naye na nyie ndege, pia na tukamlainisha chuma. Tukamwambia tengeneza nguo za chuma pana na upime vizuri katika kujilinganisha na fanyeni vitendo vizuri bila shaka nayaona yote mnayoyatenda. Na imetolewa hadithi Imamu Bukhari toka kwa Abihurairat (r.a) toka kwa Mtume (saw) kwamba, Mtume Daudi (a.s) alikuwa hali chakula isipokuwa alichokichuma kwa mkono yake (jasho lake). Mussa (a.s) ambaye alijiajiri mwenyewe kwa kuchunga mbuzi kwa miaka minane kwa Mtume Shuibu (as) kwa kulipwa kuozeshwa mmoja na watoto

wawili wa Shuibu. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu (akasema Shuibu mimi nataka nikuoze mmoja wapo katika bint zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane, na kama ukitimiza kumi ni hiyari yako lakini mimi sitaki kukutaabisha utanikuta Mungu akipenda miongoni mwa watu wema. Akasema Mussa (a.s) mapatano hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako, muda mmoja nitakaomaliza basi nisidhumiwe, na Mwenyezi Mungu ni mlinzi juu ya haya tunayosema (Surat Qases 27 – 28).

Muhamad (saw) ambaye alikuwa akichunga mbuzi na kufanya biashara kwa mali za Bi. Hadija (r.a) kabla ya kupewa Utume na katika hadithi ambayo ameitoa Imamu Bukhar toka kwa Abi Huraikat (ra) toka kwa Mtume (saw). Amesema hajapata kumleta Mwenyezi Mungu Mtume ispokuwa alichunga mbuzi, wakasema masahaba zake na wewe? Akasema ndio nilikuwa ninawachunga, basi tuna sisi toka kwa Mitume kiigizo chema na kizuri katika kufanya kazi na biashara na kuchunga mbuzi, na hii ni kazi tukufu kwa kupata riziki na ni njia ya halali kwani kufanya hivyo ni kazi za Mitume na ni vitendo vya Manabii (as). Imehimiza Qur-ani tukufu juu ya kutafuta riziki ya halali na ikajulisha njia za riziki na

sababu za utajiri kwa kutafuta kwa mikono, hivyo kazi ni njia kipato na maendeleo katika jamii kwa upande wa maendeleo ya nyanja zote.

Na miongoni mwa aya ambazo zinahimiza kufanya kazi na kutilia mkazo jambo hili.

Amesema Mwenyez i Mungu nasema uwambie tendeni mambo mazuri, Mwenyezi Mungu atayaona m a m b o y e n u h a y o n a Mtume wake na Waislamu n a m t a r u d i s h i w a k w a mtunzi wa siri na dhahiri, naye atakwambieni yote mliyokuwa mkiyatenda mwenyezi Mungu anayaona pale mnapotenda jambo lolote na Mtume pia na waumini wanayaona duniani. Pia hapa pana himizo la kufanya kazi kwa ufanisi na kuchunga m i p a k a y a M w e n y e z i Mungu katika kazi zote tunazozifanya.

Ameamrisha Mwenyezi Mungu kutawanyika katika ardhi na kutembea kutafuta riziki kwa ajili ya kujiingizia kipato. Amesema mwenyezi Mungu na itakapokwisha sala tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili msipate kufanya mabaya ili mpate kufauli, kwa maana mnapomaliza swala tawanyikeni katika ardhi kwa ajili ya biashara

Inaendelea Uk. 11

Page 8: annuur-1009

8 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012Makala

MNAMO Machi mwaka huu, tuliandika habari kuhusu machine za tiba za VIGEN Medical, ambazo hutibu maradhi kadhaa kwa njia ya jotojoto la masaji (Thermal massage therapy) kwa kupasha moto uti wa mgongo (spinal cord).

Wasomaji wengi sana walipiga simu za pongezi kuhusu makala zile, lakini pia walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua namna ambavyo na wao wanaweza kuanza kupata matibabu haya.

Tu l i w a e l e k e z a t u p o Mtaa wa Matumbi ‘B’ na Nyamwezi, Kariakoo, maeneo ya Faya; wengi wamefika na sasa wanapata matibabu hayo kila siku hapa Vigen Centre bila malipo yoyote—BURE.

Pro fes sa Chung S in J a , n i m w a n a s a y a n s i mwanamke kule Korea Kusini. Mwanamama huyu pia ni Daktar i Bingwa aliyebobea katika magonjwa ya kibinadamu. Lakini kubwa zaidi ni mtu mwenye upendo, huruma aliyetaka sana kuifanya Dunia isiwe na watu wengi wanaougua maradhi yasiyoambukizwa.

K w a m a n e n o y a k e mwenyewe, “..nilitaka sana kutumia elimu yangu kufanya watu duniani wapungukiwe na maradhi na kuishi maisha ya furaha,”anasema msomi huyo.

M a z i n g i r a t u i s h i y o ; makazi ya watu kujengwa kiholela—choo cha jirani yako kajenga dirishani kwako hivyo harufu mbaya yote kuingia kwako — vyakula tunavyokula; kukaa bila kufanya mazoezi au kupima afya kumeathiri sana afya za watu duniani. Leo wengi tumekuwa wagonjwa kwa kuugua maradhi makubwa makubwa. Kumwona au kusikia fulani ana kisukari, presha na kiharusi imekuwa mazungumzo ya kawaida tu.

Baada ya kuguswa na hali hiyo, Professa Chung Sin Ja, ambaye ndiye Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Vigen kule Korea Kusini, kwa kushirikiana na wanasayansi na madaktari bobezi wenzake walifanya kazi ya kitafiti na hatimaye walikuja kubuni vifaa mbalimbali vya tiba kwa wanadamu ambavyo sasa vimeenea ulimwenguni (zaidi ya nchi 70 sasa) kote ikiwamo hapa kwetu nyumbani— ingawa tumechelewa kidogo kuikubali.

Moja ya vifaa ambavyo

Wakazi dar wachangamkia tiba ya vigen—3Na Alhaj Abdallah

Tambaza

v i m e k u w a m k o m b o z i m k u b w a w a m a r a d h i ni VTB 2000. Machine hii imetengenezwa kwa mfumo wa digitali (digital) ikiwa na uwezo wa kutibu maradhi mengi sana ambayo hayatokani na maambukizi ya nje ya mwili – Vigen haitibu magonjwa ambukiz kama Ukimwi, malaria, typhoid, magonjwa ya zinaa.

V T B 2 0 0 0 i n a t i b u magonjwa kama vile kisukari, moyo, vidonda vya tumbo, bawasili, presha, ganzi, kiharusi, nguvu za kike na kiume, nyonga na ganzi. Mengine ni miguu, magoti, uvimbe, kupunguza mafuta na mengineyo mengi sana.

Tiba hii ya masaji jotojoto (thermal massage) haitumii mionzi kama watu wenye fikra finyu wanavyowapotosha watu. Mionzi hufanyika pale Ocean Road Cancer Institute kwenye chumba cha kiza (dark room), lakini machine hizi za Vigen zinafanya kazi barabarani, ofisini na hata nyumbani kwako ukiangalia TV.

Tiba hii haitumii dawa za kunywa. VTB 2000 ina projecta 2 zenye vitufe mithili ya balbu ndogo za taa pamoja na flaps kwa kutibu ganzi mwilini. Vitufe hivi ndivyo vinavyoleta hilo joto linalotakiwa kupasha moto mishipa (nerva) ya pingiri za uti wa mgongo katika sehemu zake 12 kwa dakika 2 kila hatua. Sehemu 3 nyingine huwekwa tumboni kwa kutibu magonjwa mbalimbali yaliyomo tumboni—vidonda

vya tumbo, cholesterol na tezi kwenye kibofu.

Msomaji , ni muhimu kuelewa kwamba uti wa mgongo ndio unaobeba mambo yote kwenda kwenye viungo vya mwili— moyo, figo, maini, macho, miguu, mikono, ngozi (endocrine system), tumbo, ulimi nk.

Inapotokea kwa bahati mbaya, sehemu fulani ya uti wako wa mgongo ikawa haina mawasiliano na kiungo husika—labda kwa mishipa kusinyaa au namna gani — basi bila shaka yeyote ile hapo patatokea tatizo kubwa sana.

K w a m f a n o , m t u anayesumbuliwa na ugonjwa wa kisukari. Tatizo hapo ni utendaji mbovu wa kongosho. Kama kongosho likikosa mawasiliano na virutubisho kutoka kwenye ile pingiri kwenye uti wa mgongo (thoracic vertebrae), basi litashindwa kufanya kazi yake ya kuweka uwiano wa sukari mwilini kama inavyotakiwa. Vivyo hivyo kwa figo, ini, mapafu, tumbo, moyo; kama ile mishipa yake haina mawasiliano na pingiri zake basi magonjwa ya viungo hivyo yatajitokeza.

Mishipa ya uti wa mgongo ya sehemu ya Cervical, inapeleka habari kwenye macho, pua, masikio, uvimbe (goitre), kuhisi chungu na tamu (sweet and sour); kupoteza kumbukumbu nk. Mishipa au mshipa husika ukikosa mawasiliano kwa kusinyaa, basi matatizo hayo hujitokeza kwa mgonjwa.

S e h e m u n y i n g i n e muhimu ya uti wa mgongo ni ile inayojulikana kama Lumber. Pingiri za sehemu hii zinaposhindwa kufanya kazi ipasavyo, basi magonjwa kama vile ganzi, kiuno, magoti, miguu kuchaanga, k u w a k a m o t o , m i g u u kuvimba kila mara; vidole, hasa kidole gumba huvimba (stiff); mgoro na kupooza (paralysis) hujitokeza. Ni matatizo makubwa sana, tumwombe Mungu atuepushe nayo.

Mwandishi huyu ni shuhuda wa matatizo ya Lumber, kwani pingiri zake tatu za sehemu hiyo zina uwaziuwazi, hivyo husumbuliwa na miguu, vidole gumba kuvimba na enka pia. Baada ya kugundua hivyo kutokana na picha za X-ray, mafanikio makubwa sana yameonekana kwa kutumia mashine za VTB2000 na Mkanda wa VTB 102.

U t i w a m g o n g o w a mwanadamu, umebeba mambo mengi ambayo kwayo ndio yanayoendesha mwili wote na shughuli zake zote. Kukatika kwa mawasiliano hayo ni kama vile nyumbani inapotokea hitlafu ya umeme, basi inaangaliwa ni ‘fuse’ gani iliyopoteza mawasiliano na hivyo kushughulikiwa haraka ili kifaa (iwe taa, pasi, frigi, jiko, radio nk) kirudie hali ya kawaida. Fananisha Ut i wa Mgongo kama vile ‘Mkongo wa Taifa’—National Grid— wa Mwili wa Binadamu. Kama njia yenu ya umeme haimo mle basi nyinyi hampati umeme.

Ni kama Ruvu Juu au Ruvu Chini ya Dawasco, ikiharibika basi maji hamna kuelekea eneo fulani na mabomba yatafokafoka tu!

Mashine hizi za Vigen hupasha moto pingiri na hivyo hufanya mishipa kuchangamka na kuufanya mwili urudie hali ya kawaida yake na katika muda mfupi wa kuzitumia, mgonjwa ataona anaanza kujisikia mwenye afya tele kwani mwili mzima huanza kuboreka na siyo ile sehemu isumbuayo tu.

Mkanda wa VTB102, ambao mimi kwa kukosa jina zuri zaidi la kuuita, nimeubatiza na kuupa jina la ‘Mkanda Muujiza’, unafanya marekebisho ya mfumo wa nerva za uti wa mgongo kurudia hali ya kawaida kwa haraka zaidi. Mkanda huo, ulio mithili ya ule wanaovaa m a b o n d i a w a k u b w a duniani, umetengenezwa na kuzungushiwa madini maalumu ya titunum na Hyegea (inatamkwa shugea), ina uwezo mkubwa wa kuponya mengi ya maradhi ya mwili.

Titanum na Shugea ndio siri kubwa ya tiba hii ya Vigen. Madini na vito hivyo hufanya kazi ya kuweka jotojoto sawia (regulate) na pia ni hiyo Shugea inayosababisha uponyaji haraka. Shugea ni mchanganyiko wa aina 19 za dawa asilia. Katika makala zinazofuata, inshaal lah tutapata fursa zaidi ya kuzungumzia kazi za shugea japo kwa muhtasari. (Angalia tovuti: www.vigenm.com)

Saleh Iddi Mkandara, toka Tandika ni mgonjwa anayehudhuria matibabu hayo ya bure hapa Vigen kwa zaidi ya miezi 6 sasa. Amepona kwa kiasi kikubwa lakini bado anaendelea kupata tiba hii ili kuweka sawa afya yake. Hapa chini anasimulia namna alivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa kiafya:

“…Nilikuwa na maradhi mengi tu haswa ganzi . Nilikuwa siwezi kutembea kabisa… nayumbayumba… macho hayana nguvu ; nikisema sieleweki hata kidogo… nikitembea mpaka nipate mtu wa kuongozana naye … hayo yote sasa yameboreka kwa k ias i fulani,”anasema

Mwingine ni Bi. Hindu Shaaban toka Kindondoni, Biafra, Dar es Salaam. Ana haya ya kusema:

“Nashukuru sana tiba hii ambayo imenirudishia ujana wangu… nilikuwa

Inaendelea Uk. 14

Page 9: annuur-1009

9 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Makala

Mauti ya umoja wa kijamiiKATIKA kitabu chake, Myahudi na Msalaba, Runes (1965) anasema ili kuhalalisha ubaguzi dhidi ya Wayahudi, Kanisa kwa makusudi lilipandikiza hadithi zilizowaonyesha Wayahudi kama wauaji wa kishirikina na wawekaji sumu katika visima.

“Aina hii ya propaganda ilifanikiwa sana ilipotolewa na wachungaji kiasi kuwa waumini wanaokwenda makanisani walimtuhumu kila Myahudi kutundika msalabani watoto siku za sikukuu za Kanisa”.

Ushahidi wa kihistoria unaopat ikana hauelekei kuonyesha, hata kwa mbali kuwa Watanzania ambao wametokea kuwa Waislamu na wananchi wenzao

ambao ni Wakristo ni maadui wa kukata na shoka. Tofauti na hapo, licha ya k u w a k a m a w a n a n c h i , Waislamu wana nafasi chache katika nafasi za elimu na ajira, Waislamu hawajawahi kuwaona Wakristo kama maadui zao

ambao inafaa kuwachukia a u k u w a u a . Wa i s l a m u wameendelea kuishi kwa uelewano na Wakristo bila viashiria vya kuleta hofu za chuki za kijamii au za kidini. Kama ni kulalamika wanaikaba koo serikali kama ndiyo adui wa Waislamu. Hawagombani na Wakristo wala Ukristo. Mgovi na adui yao ni mfumo wa kidhalimu unaowapendelea Wakristo na kuwahujumu Waislamu. Huu ndio wanaotaka kuung’oa. U a d i l i f u u w e p o . H a k i ipatikane.

Hata hivyo, Tanzania ambayo hadi hivi karibuni i l i k u w a i n a s i f i w a n a Rasmussen (1993) kama inayoweka mfano mzuri wa uhusiano wa Waislamu na Wakristo katika Afrika, imeanza kuhisi viashiria vya ugomvi vinavyotokana na ‘mauti ya umoja wa kijamii’.

Itakumbukwa kuwa hakuna kipindi ambacho kilikuwa kibaya kwa Waislamu kama ilivyokuwa kati ya miaka ya 1993 na 2005. Hiki ni kipindi kilichoshuhudia kuuwawa Waislamu, kuteswa kwa maana ya kuwekwa ndani muda mrefu bila ya dhamana, kulazimishwa kukufuru na kufungiwa baadhi ya taasisi zao za Ki i s lamu. Hik i kilikuwa kipindi cha kadhia ya mabucha ya nguruwe, mauwaji ya Mwembechai, Mauwaji ya Waislamu Pemba, kukamatwa na kufungwa wahadhiri waliosema Yesu si Mungu, kupigwa marufuku Balukta, kuwekwa rumande kwa muda mrefu Sheikh

Na Omar Msangi

Kassim Juma n.k.Lakini kilichoandamana

na madhila haya, ilikuwa propaganda ya kuwatukana na kuwasingizia uovu Waislamu. Kwa mfano, katika toleo lake la pili, gazeti la Family Mirror (Mei 1993), gazeti ambalo lilikuwa na ushawishi mkubwa na umakini kwa kawaida, liliandika:

“Balukta yatoa mwito wa kumwaga damu wakati vijana 500 wajiandikisha kwa ‘Jihad’. Katika habari hiyo likadai kuwa “kiasi cha vijana 500 wanaaminika kuwa wamejiandikisha jijini Dar es Salaam kujiunga na Jeshi la Kiislamu ambalo l inasemekana kuundwa kupigana ‘J ihad’ (Vi ta Takatifu) iliyotangazwa na kikundi cha siasa kali (Balukta) dhidi ya kinachodaiwa ni uwekwaji kando wa Waislamu unaofanywa na Wakristo, kwa mujibu wa uchunguzi wa Family Mirror.”

Likiendelea likadai kuwa “Uchunguzi umeonyesha pia kwamba makontena mawili yenye silaha yaligunduliwa na maofisa wa forodha. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo mtoaji mkuu wa silaha na fedha kupigana hiyo Jihad.”

Ili kuipa nguvu na uhalali habari yake, mwandishi akasema kuwa, “Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema ambaye pia anasimamia Wizara ya Mambo ya Ndani alithibitisha kuwa serikali imepokea taarifa hizo na inazifanyia kazi.”

Hapa gazeti linawataja Wais lamu kama waas i ambao wameunda jeshi lenye silaha za kivita. Na kwamba wamefanikiwa kuingiza nchini makontena

ya silaha. Kuandika habari kama hii na wakati huo serikali haina habari kwamba kuna makontena ya silaha yameingizwa ni sawa na kutusi vyombo vya usalama vya nchi. Ni kuitukana, kuidhalilisha na kuiumbua hadharani serikali kwamba haina maana yoyote. Ambacho kilitarajiwa ni kuwa serikali ingetoa kauli ya kulitaka gazeti kuthibitisha habari hiyo likishindwa hatua kali zichukuliwe na serikali kutoa kauli ya kuwahakikishia wananchi usalama wao. Hilo halikufanyika.

Sote tunaijua Balukta iliyokuwa ya Almarhum Sheikh Yahya Hussein. Sote tunamjua Sheikh Yahya Hussein. Ndiye huyo Sheikh Yahya Hussein wa Magomeni, tunaambiwa na Balukta yake walikuwa na jeshi la vijana 500 waliopewa silaha kutoka Iran tayari kwa kuuwa Wakris to!!! Mwandishi alijua anasema jambo la uwongo, lakini maadhali anaowatukana ni Waislamu, serikali haitamfanya lolote.

Lakini kabla ya hapo, katika toleo lake lililotangulia, gazeti hilo liliandika kichwa cha habari kinachovuta macho:

“ M v u t a n o w a d i n i Tanzania: Iran yatoa fedha kwa Waislamu wenye siasa kali, Ubalozi wa Vatican kuchomwa moto? Askofu Mkuu wa Dar es Salaam kuuawa?”

Jarida la Tanzania Analysis (July 22, 1995:1) lilijiunga na msafara huu wa ulipuaji huu wa Waislamu ki-aina. Katika toleo lake la kwanza jarida hilo liliandika kuwa Waislamu nchini walikuwa wameazimia

kwa dhati “kuzuia hali ya Mkristo kuchukua urais” na kuwa ‘Rais (Mh. Ali Hassan Mwinyi) yeye binafsi alikuwa amewapa silaha za kutosha kukata makoo ya Wakristo wote katika nchi hii. Ni wazi kuwa jarida hilo lilikuwa linarudia tu tuhuma ambazo makuhani walikuwa wametoa dhidi ya Rais katika mwaka uliotangulia katika taarifa iliyotiwa saini na Mchungaji A. Shila. Pamoja na mambo mengine viongozi wa Kanisa walimtuhumu Rais kwa “kufungulia lango la umwagaji damu kwa kutumia Mujahiddina ambao wamepania kuchoma mashule ya Wakristo na hospitali nchini” (Watu, Agosti 12-16, 1994).

Haya ni madai mazito. Maaskofu wanamtuhumu Rais wa nchi wakati huo Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwamba anashirikiana na ‘mujahidina’ kutaka kuuwa Wakristo. Sote tunajua ilivyo nidhamu ya waumini wa Kikristo kwa wachungaji wao, Mapadiri na Maaskofu. Hebu jiulize, huyu mwananchi Mkristo anayeambiwa na Askofu wake katika misa kwamba achukue tahadhari kwa sababu kuna mujahidina wamepania kuuwa Wakristo na kuchoma shule zao, atamtizama vipi mwananchi m w e n z a k e M u i s l a m u wanayeishi pamoja mtaani? Kutakuwa tena na upendo na umoja wa kitaifa?

Katika makala yangu moja niliwahi kusema kuwa tatizo la Waislamu katika nchi hii, sio la kikatiba. Ni zaidi ya katiba. Kwa maana kwamba hata kama hiyo katiba mpya ikipatikana na

iwe nzuri itakavyokuwa, hali ya Waislamu itandelea kuwa mbaya. Rais wa nchi ndiye mwenye mamlaka ya juu kabisa katika nchi. Akisema leo nimemfuta kazi Waziri Mkuu, hakuna atakaye muuliza kwa nini. Ulilala PM, unaamka raia. Lakini pamoja na hayo, watu walimpuuza kufikia kiwango cha kumtukana na kumbambika kesi ya kula njama za kuuwa Wakristo na kuchoma moto shule zao. Hakuweza kuwafanya kitu, akabakia kulalamika na kutaka ‘mujahidina’ wenzake wamsaidie. Bila shaka tunakumbuka i le hotuba yake aliyomaliza kwa kusema, “Waislamu wenzangu nisaidieni.”

Mzee Mwinyi hakuweza kufanya kitu wakati ule kwa sababu, tatizo halikuwa la kikatiba wala sheria za nchi. Kama ilivyo leo, tat izo l i l ikuwa mfumo. Na mawakala wa mfumo walikuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa mfumo hautetereki hata akiingia nani.

Lakini labda turudi nyuma kidogo. Katika ile kadhia ya mabucha ya nguruwe, mauwaji ya Mwembechai na Waislamu wakitukanwa pamoja na Mwinyi wao, kila Sheikh anayejisikia leo kui twa Sheikh iwe wa Mkoa, Wilaya au hata asiye na vyeo katika hivyo vya Kibakwata na Baraza Kuu ajiulize, alifanya nini wakati ule? Alichukua hatua gani? Alisema? Alichukia? Je, kuna namna yoyote Masheikh walikutana katika mtaa, wilaya au mkoa na kutafakari juu ya madhila yale yaliyokuwa yakimfika Mzee Mwinyi? Waliwahi kukutana Masheikh na Maimamu kujadili na kutafakari kwa pamoja juu ya shutuma zile walizokuwa wakirushiwa W a i s l a m u k w a m b a wanaingiza silaha nchini za kuulia Wakristo? Walichukua h a t u a g a n i k u m k a b i l i Augustino Lyatonga Mrema aliyekuwa ametangulizwa m b e l e n a m a a s k o f u kuendesha ‘Crusade” dhidi ya Waislamu? Kama wakati ule hawakuwa wamefanya kitu, je, leo wamebadilika? Kama hawa jabad i l i ka , n i w a z i k u w a w e n y e vyombo vyao vya habari wataendelea na mtindo wao wa kuwakashifu Waislamu na maaskofu nao wataendelea kuwazulia urongo Waislamu na serikali itachukua urongo wao na kuufanyia kazi kama ilivyochukua wa Paroko L w a m b a n o n a k u u w a Waislamu. Ndio maana ninasema, Masheikh wana

Inaendelea Uk. 14

SHEIKH Khamis Mataka SHEIKH Mohamed Idd ALHAJ Ali Hassan Mwinyi

Page 10: annuur-1009

10 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012

Na Khalid S Mtwangi

Makala

INATAMBULIKA nchi nzima kuwa maendeleo ya Waislamu Tanzania ni duni sana hasa katika nyanja ya elimu na hiyo, kama inavyojulikana, ndio msingi hasa wa maendeleo ya kila aina. Ni muhimu kutambua k u w a k u j i k w a m u a kutokana na janga hilo ni jukumu la Waislamu wenyewe. Inapotamkwa “Waislamu” maana yake ni Waislamu wote popote walipo. Kama vile masheikh na alim wanavyotufundisha Waislamu wote ni ndugu; AL IKHWAN MUSLIMIN ingawa hilo linatafsiriwa vibaya hasa na nchi za Ulaya Magharibi na Marekani kwa maslahi yao wenyewe. Hivi sasa hakuna jambo ambalo linaweza kuwaletea maendeleo haraka bali ni kwa kujitegemea na kusaidiana miongoni mwao. Napenda kurudia kuwa pale inaposhauriwa iwe miongoni mwao ni Waislamu wote duniani.

Wamishionari na makanisa yao wamepiga hatua marudufu sio kwa nguvu tu za waumini wao walio nchini humu bali pia kwa misaada mingi kutoka makanisa dada yaliyo nje ya nchi. Hayo ni kwa makanisa ya kiprotestanti. Wakatoliki wao wana serekali yao kamili iliyotanda katika kila pembe ya dunia na ni makao makuu ya Katoliki yal iyo Vatican ambayo ndio hupanga mipango ya maendeleo takriban dunia nzima. Turudie kukumbusha kuwa inasemekana Baba Mtakatifu Papa ndie mtawala aliyebaki duniani aliye na kauli ya mwisho isiyopingwa (absolute mornach). Mfalme Mswati wa Swaziland hana uwezo alionao Baba Papa wa Vatican. Serekali hii ya Vatican ni tajiri sana hivyo ni rahisi sana kwao kuweza kuleta miradi ya maendeleo

Waislam wasaidiane kuleta maendeleo mikubwa mikubwa pahala popote pale wanapotaka kusimika utawala wao, sio kwa waumini wao tu bali kwa nchi nzima ikiwezekana.

Ya l e m a k a n i s a y a siku hizi ambayo mengi yametokea Marekani, haya ya Pentecost na matawi yao nao hivi sasa wanafanya kwa bidii sana kutawala dunia nzima. Inafahamika kuwa huko Marekani ya Kusini ambako Kanisa Katoliki ndio liloshamiri tangu WaHispania na WaReno walipofika huko na kuleta gharika kwa wenyeji wa huko. Ni Kanisa Katoliki ndilo lilokuwa hata juu ya Serekali za nchi za huko. Leo hii haya makanisa ya Pentecost yameingia kwa nguvu sana kiasi kwamba Kanisa Katoliki linalalamika kuwa waumini wao wengi wanaghilibiwa na hawa Pentecost. Vita kati ya makanisa huko ni kali sana. Tanzania nako tumeingiliwa na haya ya Pentecoste kiasi kwamba wameonyesha uhasama wao dhidi ya Uislamu. Kwa mfano wamekuwa wakitaka kujenga makanisa kila panapokuwa msikiti na liwe katika kiwanja kimoja na msikiti. Wasomaji watakumbuka uchokozi w a l i o u l e t a k u l e K e k o Machungwa walipojenga k i k a n i s a c h a o k a t i k a kiwanja cha msikiti. Hapa Kichangani nako wameleta uchokozi kama huo ilimuradi wamejenga kanisa kubwa karibu ya ule msikiti wa hapo. Walifanya kila jitihada ya kughilibu Wananchi ambao wengine ni Waislamu, na wakaweza kununua viwanja vya pale kwa gharama kubwa, ilimuradi tu wawachokoze Waislamu.

Matokeo ya juhudi hizi za makanisa ni kwamba Wa i s l a m u w a n a z i d i kurudi nyuma tu. Kweli ikubalike kuwa Waislamu nao wamejitahidi kujenga shu le zao kwa wing i . Lakini hawajaweza kufikia kasi wanayokwenda nayo makanisa. Kanisa Katoliki hivi leo limeanzisha na linaendesha Vyuo Vikuu sita nchini humu, hiyo ni kulinganisha na kile kimoja cha Waislamu. Hali ilivyo haijulikani lini Waislamu watakuwa wamepiga hatua kufikia robo ya yale waliyo nayo Wakristo hivi leo.

Hakika kuna sehemu zingine, kwa mfano pale Morogoro kwenye barabara kubwa iendayo Dar es Salaam, ama Same nako kwenye barabara kubwa inayoelekea Korogwe, hawa wamechukua sehemu kubwa ya ardhi kujenga makanisa na majengo mengi mengine yakiwa ni shule na matumizi ya kikanisa. Kanisa limehodhi ardhi takriban kuzunguuka Kigoma/Ujiji yote. Kwa miaka mingi sana Uvinza pamejulikana kama ni mji wa Waislamu, lakini hivi leo pale Kibaoni pamoja na kuwa tayari pana shule yao ya msingi Kanisa Katoliki wamechukua takriban ekari mia moja kujenga kituo kingine. Hakika mgeni anayetembelea mara ya kwanza nchi hii anaweza kab i sa kuamin i k iuwa kweli Tanzania ni nchi ya Kikristo.

K u n a h a j a y a kuwakumbusha Waislamu kwamba pesa za kuanzisha na kuendeleza miradi mikubwa kama hii sio zote zinatoka humu humu nchini. Haya hata kama itakubalika kuwa waumini wa Kikristo wa hapa nchini huwa tayari kuchangia maendeleo yao. Wanapoitisha mikutano ya “harambee” kwa mfano pesa zinazopatikana huhesabika katika makumi ya mamilioni. Ndugu yangu mmoja anayehudhuria sala za Jumapili katika kanisa la Ki-Lutheri pale Tangi Bovu ananiambia kuwa michango

ya sadaka za Jumapili hufikia mpaka shilingi milioni sita. Katika msikiti wetu hapa kwetu Mikocheni B siku ya Ijumaa michango kama hiyo inapofikia shilingi elfu kumi basi siku hiyo hujigamba kweli kweli.

Pamoja na uwezo huo mkubwa miongoni mwa hawa waumini Wakristo wa humu nchini lazima ikubalike kuwa, kama ilivyokwisha dokezwa huko nyuma, bado wanaletewa misaada mingi kutoka nje ya nchi. Wasomaji watakumbuka kuwa wakati pa l ipo tokea mkasa wa kusimikwa askofu shoga huko Marekani baadhi ya maaskofu wa hapa nchini walikasirika kiasi kwamba wal i tangaza wazi wazi kwamba hawatapokea tena misaada kutoka kwa makanisa dada yaliyounga mkono uteuzi ule. Hapa maana yake ni kwamba ni kweli kuwa misaada inakuja humu nchini. Siku nyingine nilipata bahati ya kuzungumza na askofu wa moja ya yale makanisa ya Pentecost naye alikiri kuwa miradi yao mingi inasimamiwa na viongozi kutoka nje, hakika alidiriki kusema kuwa viongozi Wananchi hawaaminiki sana katika kutekeleza miradi mikubwa mikubwa. Pia niliwahi kuelezwa kitu kama hicho na kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki. Haya yote ni kweli kabisa wasomaji, hakuna lilopikwa hata moja. Kwa ufupi n i kwamba

wamishionari na makanisa yao yaliyomo hapa nchini yanapokea misaada mikubwa sana na mingi kutoka Ulaya na Marekani. Misaada hiyo inawapa uwezo mkubwa wa kujenga miradi ya shule, vyuo na hospitali na matokeo yake ni dhulma zaidi dhidi ya Waislamu.

Sua la hapa n i kuwa Waislamu nao wafanyeje kujiletea maendeleo? Itakuwa vigumu kutegemea michango kutoka kwa waumini na michango hiyo iwe mikubwa kama ile inayochangwa na waumini wa Kikristo wanapohudhur ia ibada yao Kanisani. Kwa sababu zinazofahamika wengi wa Waislamu nchini humu wana hali duni kimaisha. Hivyo vile vimichango vidogo vidogo tu kama vile vinavyopatikana kwenye Masjid Abdallah pale Mikocheni B haitatosha kuleta maendeleo yakini na haraka. Kweli waumini hawa wanastahili sifa kwa vile, pamoja na hali kuwa duni, wameweza kujijengea misikiti yao na hata kujenga na kuendesha shule ambazo pia wanaziendesha wenyewe. Maendeleo hayo ni kidogo sana hayatoshi. Sasa tufanye nini?

Mwandishi huyu atatoa maoni yake katika makala nyingine; lakini kwa leo wasomi wanaombwa watoe maoni yao kwa barua ambazo zitumwe kwa Mhariri wa gazeti hili.

AFISA Masoko wa KUTAYBA SACCOS LTD, Salma Yusuph Fataki (kulia) akikabidhi pikipiki wanawake wa kikundi cha Fiiasabillah Kutayba hivi karibuni.

Page 11: annuur-1009

11 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Makala

Rushwa ya kisiasa inaiangaza ZanzibarInatoka Uk. 6asante ya mishahara kwa kazi moja tu: nayo ni kuviza mawazo yoyote yale ambayo yataweza kuharibu mipango iliyokwishapangwa ya muda mfupi na muda mrefu katika ku ikwamisha Zanz ibar isipumuwe.

Mohammed Raza hivi sasa yupo ndani ya Baraza, hatujui kama atakuwa Raza yule yule au naye ashaingia katika anga za akina Omar Ramadhani Mapuri ambao hawako pamoja na mawazo mema ya Wazanzibari. Wao wapo wapo tu kupokea amri kutoka Bara ili waisitiri Tanganyika iendelee kujichimbia ndani ya Tanzania.

Hebu tujiulize, hivi Bara kuna Wizara isiyokuwa ya muungano? Tunaambiwa ipo! Lakini waziri huyo asiyekuwa wa muungano anateuliwa na Rais gani asiyekuwa wa muungano? Bunge la Tanzania Bara linalojadili mambo yasiyokuwa ya muungano ni lipi? Wizara ya Kilimo (Bara) sio ya muungano,

lakini hujadiliwa na bunge la muungano, hupewa fedha kutoka bajeti ya serikali ya muungano, hutafutiwa wafadhili na misaada nchi za nje na Rais wa muungano. Na ile ya Zanzibar je? Nayo hupat iwa fedha kutoka bajeti ya muungano? Nayo huombewa misaada nje ya nchi na Rais wa muungano? Je, kujadili na kuhoji mambo kama haya ni dhambi?

Viongozi hawa wanaelewa v izur i kwamba mfumo halisi wa Muungano hauko wazi . Ni bado mambo yanayosumbua vichwa vya wananchi wa visiwa hivi. Vitu viwili muhimu Mkataba wa Muungano na mfumo wa Muungano. Viongozi wetu hawaoneshi juhudi ya kusimama pamoja na wananchi kwa kudai vitu viwili hivyo vilivyo muhimu sana.

Leo kila wakitokea watu wenye mawazo mapana na kujaribu kusaidia wananchi wenzano kuwakwamua kimawazo yaani kufichua, basi huonekana adui mkubwa.

Ndipo hapo wale viongozi walipokea rushwa ya ki-siasa hujitokeza na kuwabugudhi na kuwatisha ili warudi nyuma.

Nilisema hapo awali kuna mambo mawili makubwa ambayo ni haki ya kila Mzanzibari kutaka kuyajua na kuyatolea maamuzi. Mkataba kwanza na Muundo wa Muungano.

Bahati mbaya viongozi wawili walioshuhudia utiaji sahihi na makubaliano hayo ya viongozi wetu ambao walikuwa wako nyuma ya Marehemu Karume huku wakiangalia kwa makini mkataba huo wameuwawa kikatili nao ni Abdalla Kassim Hanga na Abdulaziz Khamis Twalla. Mungu awarehemu.

Basi isiwe sababu tuliopo leo kuogopa kusema kweli na kutetea haki ya Zanzibar ndani ya muungano. Hata katika dini, wapo waliojitoa muhanga ndio leo tunajifahari kujiita Umma Bora. Tunajifahari kuwa Waislamu.

Majukumu ya Msikiti katika kupiga vita umasikini na ukosefu wa ajira

Inatoka Uk. 7

na kupata mahitaji yenu na tafuteni riziki za Mwenyezi Mungu alikuwa arakibin maliki akimaliza kuswali swala ya Ijumaa husimama kwenye mlango wa msikiti na kusema (ewe Mwenyezi Mungu mimi nimeitikia wito wako na nimeswali faradhi yako na nimetawanyika kama ulivyoniamrisha basi niruzuku kutoka katika fadhila zako kwani wewe ni bora wa kuruzuku. Wamesema watu wa kale atakayeuza au kununua siku ya ijumaa baada ya swala mungu atambariki mara sabini kwa kuali yake inapomalizika swala tawanyikeni katika ardhi mutafute fadhila za Mwenyezi mungu.

Amesema Mwenyez i M u n g u m t u k u f u y e y e ndiye ambaye ameifanya a rdh i nyepes i nendeni katika maendeo yake na kuleni katika riziki yake na kwake ndio marejeo mulku 15. Ameaiwepesishe ardhi Mwenyezi Mungu na ame i r ah i s i s ha kw a ajili ya binadamu quar-ani inawakumbusha watu juu ya neema hii kubwa ameiwepesisha Mwenyezi Mungu ardhi kwa ajili ya kuishi juu ya ardhi na kuhama toka sehemu kwenda nyingine nayo imewepesishwa kwa ajili ya kutembea juu yake kwa meli ambayo inatembea kwenye bahari nayo pia imedhalilishwa kwa ajili ya kilimo na kuvuna na neon lake nendeni ardhini katika pande zake na kuleni katika riziki zake kwa maana ya sehemu za milima.

Na akiwa Mwenyezi Mungu ameruhusu kwenda milimani basi sehemu za tambarale ni ruhusa zaidi na rizikai iliyokusudiwa katika aya sio mali ambayo mtu huitafuta kwa mikono yake ili kupata mahitaji yake na vifaa vyake bali ni kila kitu ambacho alichokitoa mwenyezi mungu katika dunia hii ni miongoni mwa sababu za riziki ni kheri za wazi na zilizojificha na yanaingia hapa madini yaliopo milimini na yaliyojificha chini ya ardhi ambayo amefanya Mwenyezi Mungu kupatikana kwa wepezi kwa sababu ya kuwepesishwa kwake ardhi na kurahisishwa kuvihamisha kutoka hapa kwenda pale an kutembea ktika pembe zake mbalimbali na zimehimza hadithi za mitume juu ya kufanya kazi na zimekataza juu ya kuwa tegemezi na uvivu. Ameitoa imamu al – bukhari toka kwa abi hurairat (r.A) amesema. Amesema mtume (s.A.W) ni bora mmoja wenu akaenda kutafuta kuni akabeba kuliko kuomba watu imawakupe au wakunyime na hadithi hii

naweka wazi juu ya umuhimu wa kufanya kazi na utukufu wa kazi kwani kutafuta kuni na taabu zake na vichache wa faida yake ni bora kuliko kuwa mvivu na kukaa bila kazi na kuomba omba watu.

Kufanya kazi ni moja ya njia ya kuutibu umasikini na kukosa kufanya hivyo basi mtu anakuwa tegemezi kwa watu na jamii. Muhutubu pale anapohimiza watu kufanya kazi katika hotuba za ijumaa au katika mawaidha hapo atakuwa amechangia katika kutatua tatizo la umasikini ambao unaenea katika jamii ya Kiislamu.

Pili: dhamana ya kijamuu kwa maana ya kusaidiana kijamii na mikutano na yanafanyaka haya kwa mtu mmoja mmoja na kwa makundi kiasi ya kuchunga masilahi yamtu mmoja na watu wengi na wala tusijifache wakati wa matatizo.

N a m s i k i t i a m b a o unaanzisha vitengo vya kusaidiana kijamii unachangia k u o n d o a m a t a t o z o y a umasikini na ukosefu wa idara na hii ndio moja ya majukumu ya imamu na muhutubu na waumini wa msikiti na inawezekana kwa imamu wa msikiti na muhutubu wake kusimamia kidete kati kulifanikisha hili pia kuhakikisha mshikamano wa undugu unakuwepo pia kwa upande wa amani na usalama na kuilind ajamii isiwe yenye kujipendelea wenyewe tuu.

Na kung’ang’ania maoni yao ili upatikane umoja na jamii yenye kusaidiana kwa kutumia kuwahimiza waumini kusimamia uhai wa mishikamano kati yao. Na kutengeneza nidhamu

ya kudhaminiana kijamii na majukumu katika jamii yake na afanyekazi kila mmoja juu ya kuikuza maana nzima ya undugu wa ki-imani kwa kubadilisha na mapenzi na huruma na kuzisafisha

roho kutokana na chuki na kuzisafisha kutokana na uadui na dharau na kutekeleza kila mmoja katika kuondoa dharau na bugudha na kutekeleza kuondoa dhiki na kutatuliana matatizo kwa kutumia mali ili wakosekana omba omba mtaani na tuwasaidie kama wapo na tuwahurumie waliopatwa na majanga na tuangalie hali za wagonjwa na wasiojiweza na tuwahurumie. Pia tuwanyooshe mikono ya misaada wale ambao wamekumbwa na menoo ya umaskini kama anavyoweza imamu wa msikiti kutokana na kuaminika kwake awahimize wale wenye mali katika mtaa ili wawe vyanzo vya kuendelea kwa ndugu zao masikini ili kuwapunguzia ukali wa maisha na kuwasaidia kwa kile alichowapa Mwenyezi Mungu juu yao katika mali.

Na kuwatosheleza mahitaji ya masikini na kuwakunjulia mikono kwa kutoa mali zao kwa kuwapa wazee na wajane na malofa (masikini) na mayatima na wale wasioweza kufanya kazi na kuwapunguzia mchungu yao ya maisha yote hayo ni kwa ajili ya kuweka daraja la upole na huruma kwa watu wa jamii ambao yamewakumba wao majanga ya umasikini na ukosefu wa ajira na kusababisha hali zoa za maisha kuwa ngumu na kufikia hali hii.

N a t u w a s a i d i e n a kuwatosheleza na kuwaondoa katika balaa la udhalili n a k u o m b a o m b a n a kudhalilika.

MSIKITI ukiwa katika ujenzi.

Page 12: annuur-1009

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]. Ni kilio na huzuni, vimeikumba CHADEMA, Kwa ya hukumu kortini, ilomuengua Lema, Kutoka pale kitini, bungeni kule Dodoma, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

2. Chanzoche ni kampenini, kumtusi mwanamama, Kwa matusi ya nguoni, jambo ambalo si jema, Si mwingine Buriani, ubini wa huyo mama, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

3. Akaanza ‘mfitini, bayana kwa KULOLOMA, AL-QAIDA kundini, akajapachikwa mama, Kisa ‘skafu’ kichwani, ikawa hoja kwa Lema, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

4.Yu mbunge wa jimboni, alokuwa zile zama, Arusha pale mjini, wa kikongwe kile chama, Uchaguzi ‘hakuwini’, mshindi akawa Lema, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

5. Akafikishwa kortini, kwa kesi dhidi ya mama, Akahisi salamani, kwa kukanyaga Dodoma, Wiki jana si zamani, CHOMBO kikenda MRAMA, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

6. Wanasiasa jamani, wa kale na hizi zama, Nidhamu idumisheni, ange kwa mnoyasema, Mtang’olewa vitini, mithili ya ‘bwana Lema, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

7. Kaditama epukeni, tabia ya KULOLOMA, Kwani hushusha thamani, ya kwenu na vyenu vyama, MAADILI yashikeni, lisiwasibu la Lema, Lililomsibu LEMA, ni DARASA jifunzeni.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

FUNDISHO KWA WANASIASA

1. Malenga napiga hodi, jibu ninalihitaji, Nauliza makusudi, mwenzetu mnifariji, Wasiwasi umezidi MHESHIMIWA haliji, Kuita mheshimiwa, tumepima mabo gani?

2. Mheshimiwa hasidi, na tena ni mfujaji, Ulevi umemzidi, sigara ni mvutaji, Na tena ndiye fisadi, mali ya umma mlaji, Kuita mheshimiwa, tumepima mambo gani?

3. Mheshimiwa kazidi, vyaoza kwenye friji, Uhuni umemzidi, gari lake ni fujaji, Na tunao ushahidi, cheo chake ni mtaji, Kuita mheshimiwa, tumepima mambo gani?

4. Rushwa kwake ni ua ridi, sheria mkorogaji, Hamuogopi Wadudi, mheshimiwa haliji, Watu kwake ni samaki, tena awaona uji, Kuita mheshimiwa, tumepima mambo gani?

5. Au twaita mradi, walopanga ni majaji, Sheria ikishadidi, twashindwa hata kuhoji, Tukawa hatuna budi, twaenda kama bajaji, Kuita mheshimiwa, tumepima mambo gani?

6. Niondoeni baridi, nijibuni wa Rufiji, Ali, Mussa, Maulidi, na wote wenye vipaji, Zabibu mwana wa Iddi, akili ingali maji, Kuita mheshimiwa, tumepima mambo gani?

Z. I. Ng’onda – Mwanza.

12 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MAY 3, 2012

KWANINI MHESHIMIWA ?

Barua/Mashairi

Ndugu Mhariri, Sifurahi kukaa kimya, kuhusu suala hili la mgomo wa madakitari wetu hapa Tanzania. Nianze kwa kumkumbuka msomi wa zama zilizopita aliyetuachia kumbukumbu ya jina lake kwa taa ya kandili iitwayo Aladin. Kutokana na jina lake akiitwa AI-Aladina, kutokana na watu wa enzi yake kukosa kuaminika, alitengeneza taa ya kandili akaiwasha mchana wa jua kali, akaingia nayo m j i n i m p a k a s o k o n i akiwaangaza watu huku akiwauliza kuwa, mbona munaendelea kuuza vitu na giza hili? Kutokana na kuwa alikuwa mtu aliyeaminika sana baada ya mazungumzo mengi nao wakamuuliza kuwa kwa nini anawasha taa ya kandili mchana wa jua kali? Aliwajibukuwa:-”Nina tafutamtu wa kumkabidhi

Bora pesa ni msibaamana yangu ya thamani “ tukiwa wawi l i , b i la shahidi wala maandishi. Na nitakapoihitaji anirejeshee vile ilivyokuwa, lakini kwa mwanga huu wa jua kali simwoni, ndiyo maana nimewasha taa ili iniongezee mwanga huenda ningeweza kumwona akawauliza, je ! Ninyi mnamwona munionyeshe?

Kila aliyeulizwa alisema hamwoni, akamwambia kuwa, basi hivyo ndivyo jamii ilivyofika katika kukosa kuaminika na kuaminiwa. Taa ile ilipewa jina lake, ikaitwa Aladini ukaitafuta madukani unaweza ukaipata. Ni moja ya taa maarufu sana yanye chemli ndefu kama aina ya gilasi.

Kisa hki kinatufahamisha kuwa inafikia mahala ambapo unatafuta mtu wa kumkabidhi amana haonekani. Watu wote mafisadi, waongo, wezi hakuna anayeaminika hata

mmoja.Madakitari kuweka roho

za watu juu katika mizani na pesa ni jambo la kusikitisha. Ni kielelezo kuwa ubinadamu umesafiri, haupo nao tena. Maana yake ni kuwa mizani yao inawaonyesha kuwa fedha ni bora kuliko uhai. Afe mtu wapate pesa.

I n a f i k i a m a h a l i p a kujiuliza kuwa ni mtaala gani unaowafilisi akili na utu wao vijana wetu huko vyuoni wanakopitia? Leo madaktari watu wanaotarajiwa kuwa na huruma na waliokula viapo vya maadili, wapo tayari kutizama wagonjwa wanakufa, ili waapewe pesa. Wanawashikilia mateka wagonjwa ili serikali iwape pesa la sivyo wauwe kwa kuwanyima tiba. Ama kwa hakika huu ni msiba.

Tunalotakiwa tufahamu ni kuwa sera na nadharia inayotuongoza ikishakuwa bora pesa, ilimuradi napata pesa, usije kushangaa mtu akafikia mahali kumshikilia mkewe abakwe ilimuradi atapewa pesa. Ndio haya tunaona binti, ‘changu’ yupo tayari na kulala na wanaume hata hajui wanatokea wapi, wawili, watatu hata kumi kwa siku ilimuradi anapata pesa.

Mziray J KhatibSame

Ndugu Mhariri.Nichukue fursa hii kwa hisani yako ili kuweza kutoa maoni kufuat ia makala i l i yoand ikwa na Nova Kambota, yenye kichwa cha habari ‘WAZANZIBARI WANATAKA NINI’ na kutoka katika gazetini tarehe 6/4/2012.

Ndugu mhariri naomba uniruhusu nisahihishe baadhi ya vitu vilivyoandikwa na NOVA Kambota hasa kwa vile gazeti hili linasomwa na wengi wakiwemo wana wanafunzi wanaochipukia.

Hamad Yusuf Mansour liwe Mh. Mansoor Yusuf Hamad. Aidha Juma Shamhuna liwe Mh. Ali Juma Shamhuna, kadhalika maneno kundi lengine, Kiswahili sanifu ni kundi jengine, mwisho ni maneno, yeye yungali anaimba, iwe yeye angali anaimba au yeye bado anaimba.

Zanzibar ni moja kwa nje na kwa ndani, tena iko imara imetulia na watu wake wanaburudika kwa riha nzuri ya marashi ya karafuu. Pia zaidi ya asilimia tisini ya watu wake ni Waislamu, kwa maoni yangu hilo ni jambo la kheri.

Zanzibar imetuliaLakini nawaasa Wazanzibari wasiwe Waislamu majina, bali wafuate maelekezo sahihi ya dini yetu. Viongozi wawe waadilifu ili wanaoongozwa waige uadilifu wao.

Zanzibar si mila yetu kuwa na uhasama, maadili yetu ni watu wanaopendana, sasa kwa murua tumeshikamana. (PEMBA NA UNGUJA MAKAME KIAZI).

Nashukuru mwandishi k u k i r i Z a n z i b a r h a l i imetulia. Hiyo ni kawaida y e t u y a k u p a t a n i s h w a na kupatana, sasa nasema atakae TUGOMBANISHA CHA MOTO ATAKIONA. Nawaasa ndugu zangu wa bara, hivi sasa kuna watu ndani ya Tanganyika wanajaribu kuchezea amani kwa kufanya fujo, haja yao nchi isitawalike, nasema MTI NA MACHO!

A n a t w a m b i a v y a m a ha l i s i vya Zanz iba r n i majina ya viongozi wetu…shabash! AKUTUKANAE HAKUCHANGULII TUSI… sasa namuul iza , vyama vyenye majina ya watu Mh. John Tendwa amevisajili lini katika nchi hii? Mtu anapotaka kujiunga na chama hicho chenye jina la mtu kadi

akachukuwe wapi? Mashawa namkumbuka mwandishi huyu a l iwahi kuandika makala katika gazeti hili hili tarehe 25/3/2011 yenye kichwa cha habari (ANIL KIJA AMWACHE PENGO AMKOSOE KIKWETE) Nakala ya gazeti hilo ninayo). Mwandishi huyu alimkosoa mwenzake anayeitwa Anil Kija kwa kusema, nanukuu: kwanza kabisa nchi hii ina msajili wa vyama na tena ina sheria na kanuni zinazoongoza kila chama”.

Sasa namuuliza huyu Mh. John Tendwa, iweje ameshindwa kufuata kanuni mpaka akaruhusu vyama vyenye majina ya watu nchini mwetu? Basi kama Mh. John Tendwa aliwahi kufanya hivyo, tuna haja ya kumhoji na ikithibitika, basi yawezekana kumng`oa kabisa.

Na iwapo Mh. Tendwa yuko kimya na hakuna aliyemhoji kulikoni, ni dhahiri kuwa haya malalamiko ni mambo ya kisiasa na ya kichuki tu, za MFUMO KRISTO, hayana ukweli wowote. Ni dhahiri kabisa Zanzibar hakuna vyama

Inaendelea Uk. 13

Page 13: annuur-1009

13 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Makala/Shairi/Barua

MOJA ya mihimili m i k u b w a y a propaganda dhidi ya Uislamu nchini Tanzania ni dhana kuwa kuna uhusiano kati ya dini na uhalifu. Wakati enzi za ubaguzi wa rangi Afrika Kusini na Marekani (na hata katika Tanganyika ya kikoloni) dhana ilikuwa ni uhusiano kati ya rangi na uhalifu, nchini Tanzania juhudi zinafanywa kujenga taswira kuwa Waislamu wana mwelekeo wa uhalifu zaidi kuliko makundi mengine ya dini. Kwa uashiriaji tu, Uislamu unaonekana kuwa ndiyo chanzo cha uelekeo wao wa uhalifu. Katika hali h a l i s i M u i s l a m u

Dini na taaluma ya jinai nchini Tanzaniaanachukuliwa kama m h a l i f u t a r a j i w a a u m w e n y e h a k i kutuhumiwa.

Askofu wa Kikatoliki ka t i ka Tangany ika ya kikoloni aitwaye Cassian Spiss alikuwa a k i z u n g u m z a k w a k u j i a m i n i k u w a “Wais lamu hawana maadili, ni wadanganyifu na wote wana magonjwa ya zinaa. Kuwaelimisha haisaidii kitu, ni marafiki wa Serikali kwa kutaka tu ula j i” (Homsby, 1964:85).

Askofu Steere wa K a n i s a A n g l i k a n a a l i s i s i t i z a k u w a mas h u l e y e j en g w e mbali na maeneo ya Waislamu ili kukwepa “athari zinazozubaisha za wakazi wa pwani”

(Swatman, 1976:108). Hisia hizo za kibaguzi zinajirudia leo lakini katika joho la sayansi.

U h a k i k i s h o unatolewa kutokana na kumbukumbu za polisi kuhusu (a) idadi ya watu wanaokamatwa, (b) idadi ya watu walioko mahabusu, na (c) idadi ya watu wanaotumikia vifungo. Kwa mfano iliripotiwa katika gazeti la Mfanyakazi (Aprili 9, 1997) kuwa asilimia 90 ya mahabusu katika jela ya Keko ni Waislamu. Na kulingana na gazeti la Mfanyakazi (Oktoba 1, 1998) mahabusu 111 wa Keko walikufa kati ya 1984 na 1988. Ni wazi kuwa wengi zaidi kati yao walikuwa Waislamu.

Zanzibar imetuliaKuna adhimu ujumbe, mwapaswa kuufahamuNi wajibu niulumbe, mpate kuufahamuChanzoche Aboud Jumbe, ‘PARTNERSHIP’ fahamu, ‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Kimechambua kimbembe, cha muungano haramu, Ulosheheni upambe, wa kambi mbili hasimZote za nyundo na jembe, japo moja madhulumu, ‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Yatakwa funike kombe, apite mwanaharamuAu ridhaa iombe, kwa mshirika adhimu Nyayoze ‘kibidi’ rambe, kwa khushui na nidhamu,‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

La sivyo wake viumbe, washikezao hatamu, Vinginevyo chembechembe, huingizwa zenye sumu, ‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Uhai sasa wa tembe, muungano mahamumu,Kisa wa watu upambe, waso na yake elimuMithili ya wanywa pombe, waso vichwani fahamu, ‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Umriwe si ukembe, mkongwe ni wa kadimuNilolenga si ubembe, ni kuzindua kaumu,Ile watu wasiyumbe, kwa muungano haramu, ‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Kitabu kina ujumbe, maridhawa kwa kaumuKutoka kwa ‘bwana’ Jumbe, kiongozi muadhamu, Kimelifunua kombe, asipite mwanaramu‘Kitaka kuufahamu, msome Aboud Jumbe.

Kaditamati ujumbe, sina dhima kwa kaumuKadhalika mze Jumbe ashatimiza jukumuMwisho nyote niwaombe, someni zake salamu ‘Kitaka kufahamu msome Aboud Jumbe.

Abuu Nyamkomogi-Mwanza.

Muungano haramuInatoka Uk. 12

vyenye majina ya watu. Huyu rafiki yangu mpenzi Nova Kambota anataka kuandika mambo ya kisiasa ya Zanzibar hata majina ya wanasiasa wa Zanzibar hayajui.

Nakuuliza ndugu yangu Mhariri wa gazeti la hili tukufu, Zanzibar kuna kiongozi wa siasa mwenye jina la Hamad Yusuf Mansour? Kama yupo ninacho kiandika usikichapishe kwani itakuwa uzee unanijia vibaya. Kama hayuko, angalau mpe jina sahihi la kiongozi huyo, hilo ni darsa tosha. Sote si wakamilifu.

Ajabu! Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, a l imdha rau Mzee we tu Ramadhani Haji, eti hajui kitu kwa kuwa kasema 1 + 1=3. (wala hakusema hivyo) Kumbe tukichunguza kwa habari ya elimu ilivyo pana naye hajui kitu. Mimi nilihakikisha kuwa Baba wa Taifa hajui kitu. Mimi nilihakikisha kuwa Baba wa taifa hajui yote pale alipotabiri kumshuhudia Rais wa awamu nyingine (ya tatu) kama aliyeweka ahadi na Mungu (Mungu amuweke pahali anapostahiki kumuweka baba wa taifa hili).

Wazanzibari wamepofushwa macho kwa ushabiki wa Kisiasa. He! Hata Rais wetu kipofu Baleghe changa

nayo! Mtu humtukana kila anayemuona sasa najibu, angalau kipofu kwa vile macho anayo lakini hayaoni akipata daktari mzuri anaweza akapona. Sisi tushapatana. Zamu yenu, Watanganyika kama hamna macho wala masikitiko, fujo, maandamano, mauaji ya vikongwe, migomo ya madaktari haiishi. Ndugu zangu wa Tanzania bara, madakari wasomi, mnajali kitu kuliko utu… hizo si mila za Zanzibar wala Tanganyika na Kote Afrika. Tujirekebishe.

K iongoz i mhaf idh ina anayeimba Mapinduzi daima, anayewachukia Wapemba, sasa yuko Tanganyika kwa matakwa ya chama chake, nani huyu? Mtaje ajirekebishe, usipomtaja tutakuona unazuwa.

Wengine watakuona fitna na mzandiki, basi niambie japo kwa siri, kwa busara nitamtumia watu huenda hajajirekebisha, kwani nijuavyo mie asili yetu ni moja, ADAMU NA MAMA HAWA, vibaya kudharauliana, ndio maana tunaitwa BIN-ADAM (binadamu).

Historia na fani nyingine zote tujifunze Wanzanzibar, Watanganyika Waafrika na watu wote ulimwenguni, h i l o w a l i k u b a l i . N a w e nataka ukubali hivyo, elimu tunaihitaji sote, si Wazanzibari peke yetu. Sasa nasema hata Watanganyika wako wanaodai Tanganyika yao, tena kwenye chombo kikubwa cha kutunga sharia- Bunge (kumbuka Group 57) na Mchungaji Christopher Mtikila.

Watanganyika nao pia w a n a p a s w a k u j i u l i z a , w a n a p o d a i w a n a i t a k a Ta n g a n y i k a y a o , j e n i Tanganyika ipi wanayoitaka? Wanaitaka Tanganyika ya Carl Peters, Mjerumani iliitwa Deutch East Afrika Territory iliyojumuisha mipaka ya Rwanda na Burundi, ambayo babu zetu Watanganyika w a l i p i g w a v i b o k o n a kufanyishwa kazi kinyama wakiitwa swaine, kwa maana ya nguruwe?, Tanganyika ambayo wenye nchi wal ichapwa viboko, kutozwa kodi ya kichwa (Poll tax)? Tanganyika iliyomnyonga Bushiri wa Pangani na kumkata kichwa chake na kukipeleka Ujerumani kukiweka kumbukumbu? Tanganyika ile ambayo babu zetu walilazimishwa kufanya kazi katika mashamba ya mkonge ya Wajerumani… Arbeit, ar- beit, Afrikener Swaine!

A u Ta n g a n y i k a y a uko lon i wa Ki inge reza iliyowagawa watu matabaka na kuwakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wakristo hali iliyozaa mfumoKristo wa sasa? Au Tanganyika ya Mwalimu Nyerere ambayo

wasomi walimwambia mwaka 1966 afadhali ukoloni na akanuna? Au Tanganyika ya Vita vya Kagera, ya sembe la njano (Yanga)? Au hii ya madaktari kuhalifu viapo vyao kuwatelekeza wagonjwa kuwacha wafe ilimuradi wao wapate pesa.

Wanzanzibar i na hata Watanganyika ni haki yao kuamua aina ya serikali wanayoitaka, kama wanataka serikali moja, mbili au tatu. Ndio maana serikali yetu ya Muungano ikaleta mchakato wa maoni ya Katiba ili muda ukifika wananchi watoe maoni yao, hujui hivyo? Itikadi za Watanzania kuhusu mfumo wa serikali ni tofauti, lakini mwisho wake wengi wape. Hivyo kuna kosa gani kwa Wazanzibari kutaka mfumo wa serikali moja, mbili au tatu.

Wapo wanaoona hakuna haja ya kuwepo kwa serikali kama wazee wao wanauliwa huko bara kwa tuhuma za ushirikina, Albino wanachunwa ngozi, kuna migomo ya madaktari na ufisadi wa viongozi, serikali inafanya nini? au iko likizo?

Unataka kujua itikadi ya Zanzibar, swali lako mbona rahisi kulijibu licha ya tofauti zetu za kimawazo na kifkra, lakini Wanzanzibar tunaamini so te n i wamoja . . . Ndio maana huku kwetu madaktari hawagomi kwani wakigoma watakuwa wanawaua ndugu zao. Jawabu langu limfikie na Rais wetu mpenzi Jakaya Kikwete.

NOVA Kambota, uliandika kwenye gazeti la An-nuur tarehe 25/3/2011 ‘ANIL KIJA AMWACHE PENGO AMKOSOE KIKWETE’ lakini ukiwa umeruhusu Pengo amkosowe Rais wetu!

Wazanzibari hawana hisia za kuhoji kwa nini wengi ni Waislamu. Uislamu unakataza watu kubaguana, ndo maana h u k u k w e t u w a g o n j w a wakiumwa tunawatibu pamoja na unyonge wetu.

Jinsi Wazanzibar tulivyo wamoja na tunavyocheza na viongozi wetu wapenzi, naanza kucheza na Mheshimiwa Mohammed Seif Khatib. Mheshimiwa nasikia uko Dodoma unasaka tonge, nasikia mnajilia maposho yenu ya ‘fungate ya uhuru’, nakwambia mbona ng`ombe wetu sote maziwa mnakunywa peke yenu? Hiyo ndio fungate yenu ya uhuru ama mwenye shibe hamjui mwenye njaa!

Hivi ndivyo tulivyo Zanzibar, tuna udugu wa asili, sote letu moja, hatuna uhasama.

Mzee Hassan Mkwenda HassanZanzibar

Page 14: annuur-1009

14 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012Makala

Mauti ya umoja wa kijamiiInatoka Uk. 9sehemu kubwa ya lawama. Niwatake radhi “Abu Idd” na Sheikh Hamisi Mataka kwamba nimetumia majina yao kama kiwakilishi tu. Na nimefanya hivi kwa kuzingatia nafasi wanayobeba katika jamii wakiwakilisha masheikh wenzao vijana.

Wayahudi katika nchi za Kikristo Ulaya walituhumiwa kuua kishirikina na kutia sumu visima. Waislamu katika Tanzania isiyofuata dini yoyote wanaonyeshwa kama maharamia wataka damu. Waliopania kumwaga damu ya Wakristo. Pia wanaonyeshwa kama majuha wasioshikika ambao wanapata kipandauso mashule yakitajwa. Picha hii inajengwa kila kukicha katika burudani za radio na luninga ambako Waislamu na dini yao wanadhalilishwa kwa kutumia mzaha uliojificha.

Katika Ulaya ya kimwinyi Wayahudi walichomwa moto kwa kukataa uungu wa Yesu; katika Tanzania ya kisasa Waislamu wanakamatwa, wanakataliwa dhamana na kusumbuliwa kwa kukataa kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Yesu, mwana wa Maria.

Hivi sasa kuna wimbi kubwa la muziki wa Injili ambao unaonekana ndio kiburudisho cha abiria katika mabasi. Ataonekana kiroja iwapo yupo abiria ambaye atataka baada ya kumalizika kanda ya Folora Mbasha

iwekwe kaswida ya Madrasat Damba au Mawaidha ya Mohammad Idd “Abu Idd”.

Swali ni je, wapo abiria Waislamu walio na ujasiri wa kusimama na kutaka zisiwekwe kanda za muziki wa Injili? Au vinginevyo na Kasida za Yusuf Islam ziwepo? Masheikh hi l i wanaliona? Wanawaimarisha vipi waumini wao kukabiliana nalo? Je, hawaoni kuwa baada ya kusambazwa makanisa k i l a maha l i , h i l i na lo linafanywa kwa makusudi ili izoeleke kuwa Tanzania ni ya

Wakristo? Kwenye basi Injili, hospitali Injili, hotelini na kwa mama lishe wimbo wa Injili, katika daladala wimbo wa Bahati Bukuku, katika ofisi za serikali msalaba na wimbo wa Rose Mhando! Akija mgeni atajua kuwa kuna Waislamu hapa? Mtoto Muislamu anayekulia katika mazingira haya, kisaikolojia tunamtarajia awe vipi?

Profesa Noam Chomsky katika kitabu chake “What Uncle Sam Really Wants” , anasema kuwa katika kila nchi kipo kikundi cha watu

ambao ndio hasa wana nguvu na wameshika madaraka ya nchi. Hawa ndio huamua n in i k i fanyike na k ip i kisifanyike.

Chomsky anasema katika Marekani wenye nguvu hiyo ni matajiri wenye viwanda na makampuni ya kimataifa. Hawa ndio wanaiburuza Marekani kupeleka vijana wao wakafe vitani ili wenye makampuni yao wapate kupora mafuta na rasilimali nyingine kwa urahisi.

Ni siri iliyo wazi kwamba nguvu za kisiasa na mamlaka katika nchi hii yapo mikononi mwa “mawakala wa kanisa” ndani ya serikali. Hawa ndio wanaoshikilia mfumokristo na kuulinda kwa masilahi ya kanisa.

Kama alivyosema Profesa Chomsky, hawa wangependa kuona wananchi wanabaki ‘hamnazo’ wakiimba Tanzania haina dini na wakipiga kimya, hata kama wataona Waislamu wakihujumiwa. Anasema ukitaka kuwatoa raha watu hawa ni kuwazomea bila kuchoka. Ni kusema. Ni kufichua maovu na udhalimu wao wanaofanya ili wananchi wa jue na wahamas ike kusimama kupinga. Usichoke kusema. Sio uandamane leo urudi ukalale ukidhani inatosha. Sema, sema, sema

na wakusanye watu waseme na kukataa. Watu wahoji na wasichoke kuhoji na kusema hatutaki. Hiyo ndio njia ya kuwakera na kupambana nao.

Hivi karibuni Mzee Edwin Mtei alitoa kauli akisema kuwa Tume ya kuratibu maoni juu ya katiba imejaa Waislamu. Ukitizama Tume ile, Mwenyekiti na Makamo wake ni Wakristo. Katika wajumbe 15 wa Bara, kwa kuangalia majina, wajumbe 10 ni Wakristo na Waislamu 5. Wale wa Zanzibar ndio wakafanya idadi ya Waislamu kuwa kubwa.

Labda tujiulize, Waislamu wangapi, Masheikh wangapi w a n a k u w a m a k i n i n a kutizama masuala kama haya na kuhoji nafasi ya Waislamu? Wengi wetu kunakucha linakuchwa, hatuna habari na kinachoendelea. Na wengine hata ikitokea kuulizwa kama ilivyotokea katika suala hili la Mtei, majibu ni yale yale ya kujiona sisi ndio wazalendo sana wa nchi hii na Wakristo ‘haki yao kula nchi’ maana ‘wana sifa za kula’ (rejea majibu ya Mufti alipohojiwa juu ya madai ya Mtei).

K a t i k a h a l i i l i y o p o nchini hivi sasa, kama hali itaenda kama ilivyo hivi sasa na masheikh wetu hawatabadilika: Katiba mpya itakuja, lakini hujuma dhidi ya Waislamu itaendelea na hatma yake ni mgogoro utakaovunja kinachoitwa hivi sasa umoja wa kitaifa ikifuatiwa na kuvunjika kwa amani ya nchi.

Wakazi Dar wachangamkia tiba ya vigen—3Inatoka Uk. 8naumwa presha, kiuno, mgongo umepinda, miguu kutembea siwezi …nasotasota hata kwenda chooni. Nilishindwa kuhudhuria kwenye harusi na misiba pia. Nilipopata habari za tiba hii mume wangu alinikataza kabisa kuja hapa kwani alidhani ni mionzi inayodhuru. Sikukubali ushauri wake nikaja tu kwani nilikuwa nasumbuka sana… niliwahi kulazwa nikapoteza fahamu siku 4 hospitali; nilikuwa na uvimbe sasa umekwisha kabisa kwa tiba hii.

“Leo hii mimi nimepona kabisa matatizo yote hayo… mwil i wangu umeboreka kisawasawa ila naendelea kuja hapa kwa kujiweka sawa tu na mume wangu haamini macho yake kwamba ndio mimi nilivyo sasa, mwanzoni hakuniruhusu kuja kabisa,” anasema Bi Hindu ambaye sasa yuko matembezini Kongo—DRC.

Kwa wagonjwa wa kiharusi (kupooza), kisukari, presha, ganzi, magoti, nyonga, kutoka usiku mara kwa mara kwa ajili ya haja ndogo (kikojokojo) watapata nafuu mara moja

hasa kwa kutumia mkanda wa VTB102, na ile mashine mama ya VTB 2000.

Pia, wachezaji mpira wa zamani na hata hawa wa sasa, ambao wameathirika magotini, enka, mabega, nyonga na sehemu za joints kwa ujumla, wanaweza kupata nafuu kwa kutumia mashine ya VLP200. Mashine hii haina moto isipokuwa inatumia nguvu ya sumaku na madini ya titunam na shugea kuondosha tatizo. Wengi wameboreka na mashine hii.

Sasa kwa wale watu wa mikoani ambao wanaulizia namna ya kufikiwa na tiba hii itabidi wafanye mpango wa kununua vifaa hivi ili wavitumie wenyewe majumbani mwao kwa wasaa. Tiba hii inapendeza kufanyika zaidi ya mara moja kwa siku ili kupata mafanikio ya haraka na uhakika.

Msomaji, kama una uwezo wa kifedha vifaa hivi vyote vinauzwa hapa kwenye kituo chetu. Kwa wale wenye uwezo, wanashauriwa kununua vifaa hivi wawe navyo nyumbani ili wasipate usumbufu maana wengi wa wagonjwa ni wale ambao hawawezi kutembea (bed

ridden). Kwa wale wa mikoani na

Zanzibar, wafanye mawasiliano nasi ili wanunue vifaa hivi wakawasaidie wengine mikoani kwa kuwatoza ada kidogo za uendeshaji. Pia inaweza kuwa ni ajira kwako na watu wengine. Huhitaji daktari wala utaalamu wowote kutumia machine hizi. Maelezo kidogo yanatosha kuanzisha huduma yako hapo ulipo.

Pale Barabara ya 8 jijini Tanga, yupo Mama Mapinda (simu 0715 275 986) Ruhana Vigen massage Centre, anatoa huduma hii kwa ada kidogo tu.

Jijini Dar es Salaam, maeneo ya Tegeta Nyuki kituoni, ipo Micu Vigen Centre (0713 311 876) inayotoa huduma hii kwa ada ndogondogo; na Mama Halima Maganga yeye karibu atafungua ya kwake kule maeneo ya kwendea Gongo la Mboto kwa wakazi wa huko.

(Itaendelea. Simu: 0715 808 864/0719 228 866/068 8384 464 [email protected])

RAIS Mstaafu Benjamin William Mkapa

Bi. Mwasiti Hamisi wa Kigogo Ruhanga anaomba msaada wa kumalizia ujenzi wa Msikiti uliopo katika kijiji cha Kitondwe (B) Kibuta katika wilaya ya Kisarawe. Vifaa vinavyohitajika ni Cementi ya kupiga Floor ndani na nje, Rangi, Mikeka au Mazulia pia Kuchimbiwa Kisima cha Maji, pamoja na Mageti ya Milango.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba hii 0656 092436

Tangazo

Page 15: annuur-1009

15 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012Makala

DK. Tumaini Leo Mtenga, amesema kuwa amekuwa akisoma makala nyingi zinazochapishwa na gazeti hili, zilizobeba maudhui ya kutaka Waislamu nchini kuwa wamoja.

Dk. Tumaini ambaye ni daktari na mwana elimu ya jamii (sosholoj ia)) amesema kuwa amekuwa msomaji mzuri wa makala za mwandishi Mzee Khalid Shaaban Mtwangi, ambaye amekuwa hachoki kuandika m a k a l a z a k u s i s i t i z a umuhimu na ulazima wa Waislamu kuwa na umoja madhubuti na wa dhati kwa ajili ya kusimamia haki na maslahi ya Uislamu na Waislamu nchini.

“Kwa jinsi ninavyopokea ujumbe unaobebwa na sehemu kubwa ya makala za Bw. Khalid Shaaban Mtwangi, anaonekana kuwa anasononeshwa sana na hali ya Waislamu nchini walivyo vipande vipande, kiasi cha kushindwa kuwa na nguvu ya pamoja ya kusimamia na kutetea maslahi yao, hasa dhidi ya dola”. Anasema Dk. Tumaini.

Kwa jinsi hali ilivyo, sio Mzee Mtwangi peke yake anayesononeka , wapo Waislamu wengi wasioridhishwa namna Waislamu walivyochanguka k w a k u k o s a U m o j a madhubuti, jambo ambalo l imewagharimu miaka nenda rudi.

Pamoja na man t ik i ya umoja wa Waislamu kuwasilishwa kwa hisia nzito, lipo tatizo ambalo Jamii ya Kiislamu inapata shida nalo. Kwa Waislamu kama jamii, hawana tatizo, shida kubwa ipo kwa viongozi ambao wanatenganisha Waislamu kwa makundi ya kimadhebu, kitaasisi na kifalsafa. Kwa namna moja au nyingine, utofauti ulioingizwa katika Uislamu umetumika kuwagawa Waislamu.

Tunazungumzia umoja wa Waislamu au umoja wa Uislamu? Kwa miaka mingi, jamii ya Kiislamu nchini imeshindwa kutetea haki na maslahi yake kutokana na kukosekana kile kinachoitwa umoja wa dhati miongoni m wao.

Waislamu Tanzania na kilio cha umojaNa Shaban Rajab

AMIR Sheikh Mussa Kundecha. Ni miongoni mwa wanaosisitiza umoja.

MAALIM Ally Bassaleh. Ni miongoni mwa wanaosisitiza umoja.

Kwanini tunazungumzia umoja? Ni kwa sababu kuna makund i meng i miongoni mwa Waislamu. Kabla ya kupata umoja wa kweli, kwanza Waislamu w a n a l a z i m i k a k u k i r i kwamba makundi miongoni mwao yapo. Baada ya hapo kinachotakiwa kufuatia ni kwa Waislamu na viongozi wao kuyafahamu vizuri makundi miongoni mwao.

K w a k u w a v i k u n d i hivyo vimeanzishwa na kuwepo kwa miaka mingi, ni vigumu kuja na hoja ya kuvifuta au kuviua na kubaki na kikundi kimoja ili kujenga umoja tunaoutafuta. Iwapo zitafanyika jitihada za namna hii , ni wazi kwamba Waislamu watazidi kugawanyika na kupoteza zaidi malengo. Kwa msingi huo, kwa kipindi hiki jambo la msingi na la kuzingatia ni kukiri na kutambua makundi na misimamo yake, halafu kila kundi liheshimu kundi jingine.

Tanzania kuna Waislamu wa madhehebu, makundi kifalsafa za Maimamu na maswahaba na taasisi za namna nyingi.

K a t i k a b a a d h i y a madhehebu na taasisi , taratibu za kimaamuzi na kimamlaka katika mambo ya dini na kisiasa hutolewa na viongozi wa ngazi ya kidunia, viongozi ambao wengine makao yao sio hapa nchini. Taasisi nyingine taratibu na maamuzi yao kutekelezwa na viongozi wa taasisi au dhehebu ndani ya nchi. Na miongoni mwa makundi haya, tofauti zao kubwa zimeegemea zaidi katika tafsiri za Qur’an na hadith.

Inafahamika kwamba Waislamu wote wanakiri na kuifuata Qur’an kama muongozo wao. Lakini tofauti katika kutafsir Qur’an, tofauti katika hadithi na tafsiri za hadithi zimekuwa chanzo cha kuwepo makundi haya . Hawa wanaona hadithi fulani sio sahihi au dhaifu. Wengine hadithi hiyo hiyo wanaiona ni sahihi na yenye nguvu. Wengine wanampa swahaba fulani nafasi zaidi na kumheshimu kuliko wengine. Lakini kwa wengine, swahaba huyo huyo asiyepewa hadhi kubwa, ana nafasi zaidi

na hadi ya juu kwa kundi jingine.

Wa p o p i a a m b a o hawakubali kabisa hadithi b a l i Q u r ’ a n p e k e e . Samahani kama wapo watakaochukizwa na maoni haya, lakini ni katika nia ile ile ya kuitakia mema jamii ya Kiislamu. Ndio maana, litakuwa ni jambo la msingi zaidi kwa viongozi wa taasisi na madhebu yetu, kujali kwanza umoja wa Waislamu ambao kimsingi hawana matatizo, ili kufikia malengo ya kupata nguvu kamili ya kutetea na kulinda haki na maslahi ya jamii ya Kiislamu nchini.

Umoja wa Uis lamu utakuwepo iwapo tu, tofauti hizi za tafsiri katika Qur’an na hadith zitaachwa kama zilivyo kwa kutochukuliwa kama ni jambo linaloweza kuleta athari mbaya kiasi cha kuathiri harakati za kuwa na umoja wenye nguvu kwa Waislamu. Ili kufikia malengo, Waislamu waachane na mijadala ya kutafuta umoja wa Uislamu miongoni mwao, h i lo linaweza kujadiliwa baadae, kwanza wakazane huu wa

Waislamu. Makundi , taasis i na

madhehebu yetu yote, yakuba l i ane kuwa na chombo cha kuwaunganisha Waislamu na kutoa maamuzi na miongozo ya pamoja kwa Waislamu wote, hasa katika masuala ya kulinda haki za Waislamu na maslahi yao husuan dhidi ya dola au imani nyingine.

Kama n i jukwaa la Maimamu nchini, basi liwe ni la Waislamu kwa makundi yao. Kama ni Jukwaa la Maulamaa, hali kadhalika nalo liwe la Waislamu kwa makundi yao. Kama ni Jumuia ya Wahadhiri, nayo iwe ya Waislamu kwa taasisi na makundi yao.

Madha l i k i l a kundi l i nakuba l i uwepo wa kundi jingine na viongozi wake, taabu na hisia za kitofauti katika Uislamu zitafifia. Litakuwa ni jambo la busara na la tija iwapo yatatangulizwa maslahi ya Waislamu kwanza badala ya vikundi vya Uislamu miongoni mwa Waislamu.

Pamoja na chuki za maadui wa Uislamu, Waislamu wameshindwa kujikagua w e n y e w e , k u t a m b u a walipokosea tukarekebisha, k a b l a y a k u w a l a u m u waliotumia mwanya wa udhaifu wetu kutudhuru. Leo inahitajika Mahakma ya Kadhi, Waislamu wanataka serikali kujiunga na Jumuia ya Kiislamu ya OIC kwa maslahi ya k iuchumi, wanataka uwiano wa haki wa kiutawala na kiutendaji katika dola, hapa si jukumu la taasisi wala dhehebu, bali ni kwa nguvu ya Waislamu kusimamia mahitaji yao.

Tubadilike, Waislamu w a n a h i t a j i m s i m a m o mmoja, uongozi mmoja katika kutetea haki na maslahi ya Waislamu na Uislamu kwa ujumla dhidi ya dola, mamlaka au dhidi ya dini nyingine zisizokuwa Uislamu.

Pamoja na kwamba Madhehebu na taasisi zitabaki kama zilivyo,Waislamu wanahitaji Imam, kiongozi wa kuwaongoza Waislamu wote nchini kiroho na kiimani, anayetokana na maridhiano ya madhehebu na taasisi za Kiislamu kwa umoja wao.

ridden). Kwa wale wa mikoani na

Zanzibar, wafanye mawasiliano nasi ili wanunue vifaa hivi wakawasaidie wengine mikoani kwa kuwatoza ada kidogo za uendeshaji. Pia inaweza kuwa ni ajira kwako na watu wengine. Huhitaji daktari wala utaalamu wowote kutumia machine hizi. Maelezo kidogo yanatosha kuanzisha huduma yako hapo ulipo.

Pale Barabara ya 8 jijini Tanga, yupo Mama Mapinda (simu 0715 275 986) Ruhana Vigen massage Centre, anatoa huduma hii kwa ada kidogo tu.

Jijini Dar es Salaam, maeneo ya Tegeta Nyuki kituoni, ipo Micu Vigen Centre (0713 311 876) inayotoa huduma hii kwa ada ndogondogo; na Mama Halima Maganga yeye karibu atafungua ya kwake kule maeneo ya kwendea Gongo la Mboto kwa wakazi wa huko.

(Itaendelea. Simu: 0715 808 864/0719 228 866/068 8384 464 [email protected])

Page 16: annuur-1009

16 AN-NUUR JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 - MEI 3, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR USIKOSE KUSOMA AN-NUUR

KILA IJUMAA16 JAMADUL THAN 1433, IJUMAA APRILI 27 -MEI 3, 2012

WALIMU pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Maramba ‘B’ iliyopo Tarafa ya Maramba, Wilayani Mkinga Mkoani Ta n g a , w a p o k a t i k a wakati mgumu katika kutekeleza wajibu wao kwa kukabiliwa na tatizo la choo shuleni hapo.

Baadhi ya walimu wa shule hiyo waliowasiliana na gazeti hili kuelezea kero hiyo kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini, wamesema hali hiyo inawaondoa katika morali ya kufanya kazi.

Wamesema, tatizo hilo limekuwa kero ya muda mrefu sasa na hawaoni dalili za kumalizwa ndio sababu wamefikia uamuzi wa kupaza sauti ili kero hiyo iweze kuwafikia wadau ngazi za juu baada ya uongozi wa shule, Serikali ya Kijiji na Kata kuonekana kukwama kulishughulikia.

M m o j a w a w a l i m u hao alisema, kwa sasa wanafunzi wao wapatao 500, wanalazimika kutumia choo cha walimu, ambacho hakikidhi haja na kusababisha wanafunzi kujisaidia hovyo hali inayohatarisha afya zao na wakazi wa eneo hilo.

“ K i u k w e l i u t e n d a j i wangu wa kazi unaathirika kila unapofikiria kuhitaji huduma ya choo, inakuwa karaha inatulazimu kwenda kuomba kwa nyumba za wenyeji walio jirani na shule, hii ni aibu kwetu walimu.” Alisema mwalimu huyo.

Mwal imu mwingine alisema, anaomba mamlaka za juu zitupie jicho suala hilo kwani athari yake haitakuwa kwa Shule au Kijiji bali ni kwa Jimbo (Wilaya) na hata Mkoa, akadai wasione kuwa suala hilo ni dogo.

Kwa mujibu wa walimu hao wamedai kuwa suala hilo lina mwaka sasa na kwamba Serikali ya Kijiji, Diwani pamoja na Mbuge wanajua tatizo hilo lakini ufumbuzi wake umekuwa mgumu.

An nuur, ilipowasilina na Diwani wa Maramba, Mh. Said Mjakambu, alithibitisha kuwepo kwa tatizo hilo kwa muda sasa baada ya vyoo vya awali kubomoka.

Al ida i kuwa juhudi zinaendelea kuondosha kero

Shule haina chooNa Bakari Mwakangwale

hiyo lakini tatizo kubwa w a n a l o k a b i l i a n a n a l o ni ugumu wa wanakijiji kuchangia ujenzi wa choo hicho.

A k i j i b u s a b a b u zinazopelekea wanakijiji kuwa wagumu kuchangia ujenzi wa suala hilo lililo muhimu katika makazi hususani katika mkusanyiko wa watu kama shule, alisema ni kutokana na wanakijiji kupoteza imani kwa Serikali ya Kijiji.

“ U n a j u a w a t u w e t u w a m e k u w a w a g u m u kuchangia, kutokana na kipindi cha nyuma uongozi wa Kijiji haikuwa adirifu,

unamchangisha mtu kisha marejesho hakuna, si kwamba hawana pesa bali hawana imani katika matumizi yake baada ya kuchanga.” Alisema Mh. Mjakambu.

Alisema, wanatarajia kuita kamati ya shule kuangalia kiasi kilichopatikana kwa waliochanga ili waweze kuangali uwezekano wa kuanza kwani shimo lipo ambalo lilichimbwa kwa msaada wa wanajeshi (JKT Maramba).

Alikiri kuwepo kwa kero kwa walimu pamoja na wanafunzi kwa kukosekana kwa vyoo kwani alidai hakuna mtu ambaye anaweza kuzoea

matatizo hususani kwa suala muhimu kama la choo katika makazi.

A m a a k i z u n g u m z i a ushirikiano kutoka ngazi za juu, alisema kuna tatizo katika halmashauri zao kwani kila unapopeleka tatizo jibu linakuwa hakuna pesa na kuhusu Mbunge, alidai hawezi kuchangia suala dogo kama hilo ambao linaweza kufanywa na wanakijiji wenyewe.

“Mbuge alikuja na alifanya mkutano na wananchi kuhusu tatizo hilo aliongea hadharani kuwa nguvu kazi ya kijiji ni kubwa akadai wanauwezo wa kulitatua. Sasa hali ndio

kama hivi labda akija tena anaweza kuli tatua kwa sababu si kuna mfuko wa jimbo anaweza kutuchangia kwani hili (Mkinga) ni jimbo lake.” Alisema Mh. Diwani huyo.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo aliyetajwa kwa jina la Leya Zahabu, hakuweza kupatikana ili kupata maelezo yake juu ya kero hiyo baada ya simu yake kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa sababu kubwa inayopelekea wanakijiji kugomea ujenzi wa choo hicho ni kukosa imani na Serikali yao ya Kijiji cha Maramba ‘B’, baada ya choo cha awali kujengwa chini ya kiwango kwa msaada wa pesa za MMEM.

V I O N G O Z I w a d i n i wametakiwa kuwaandaa vijana wa Kiislamu katika misingi ya Kiislamu il i waweze kuwa mfano katika ulinganiaji.

Wito huo umetolewa katika semina ya Maimamu wa wilaya ya Ilala na Temeke, iliyoandaliwa na Kituo cha Kiislamu Markaz Changombe, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanyika chuoni hapo.

Sheikh Osama Mahmoud I sma i l , Mkurugenz i wa Kituo hicho alisema urithi wa elimu kwa vijana ndio pekee utakaomfaa kijana katika dunia na akhera yake, pia ndio utakaopunguza matatizo katika jamii inayotuzunguka.

Alisema, Masheikh na Maimam wana dhima kubwa ya kuwanusuru vijana na jamii inayowazunguka, kwa kuwalingania na kuwajenga kiimani ili kupunguza maovu yaliyokithiri katika mitaa yetu.

Naye Dr. Emad Rabii, ambae ni mwalimu katika kituo hicho amewataka Viongozi hao kuwalingania wasio Waislamu kwa hekma, kama ambavyo alikuwa akifanya Mtume (s.a.w) katika uhai wake na kuwataka kuwa mfano katika matendo yao ya kila siku.

Aliongeza kwamba Uislamu ni dini ya haki na uadilifu, hivyo Waislamu wanatakiwa kuishi katika misingi ya kidini kwa kuwa kwenda kinyume na

Masheikh wapigwa msasa MarkazNa Mwandishi Wetu

mafundisho hayo ni kumkosea Allah na Mtume wake.

Dr. Rabii aliwataka viongozi hao wa dini kwenda na wakati ili kumudu kuwaongoza na kuwapa habari waumini wao, kwani wao ndio walio juu ya wale wanaowaongoza katika Misikiti yao na jamii nzima inayowazunguka.

Kwa upande wake Sheikh Suleiman Amran Kilemile, ambae ni mjumbe wa Jopo la Masheikh na mtoa mada katika semina hiyo, amewataka Waislamu kuzingatia ufahamu sahihi wa dini yao katika kutoa

da’wa, ili hatimaye kuwa Da’i wazuri.

“Ili uwe kiongozi mzuri ni lazima uwe msomi mzuri ndipo utatakapoweza kufanya da’wa na kuwa kiongozi unayejiamini kwa kile unachokisema”. Alibainisha Sheikh Kilemile.

Sheikh Wahid Mansour, mmoja wa walimu wa Kituo hicho ambaye aliwasilisha mada yake ya ‘Umuhimu wa Kulingania kwa Njia ya Wastani na Usawa’, alisema kuwa, kama ambavyo amesema Allah (s.w) kuwa hakuna kulazimishana katika dini, unapomlingania

mtu unatakiwa kufuata misingi na taratibu ili isifike mahala mtu akauchukia Uislamu na kuona kuwa hauna maana wakati Uislam ni dini ya upole.

S h e i k h a l i s e m a k u w a kulingania kwa aya na hidithi ndiko kutakakomfanya mtu aone kuwa dini ya Kiislamu pekee ndio dini ya kweli kama ilivyowekwa wazi katika vitabu vitukufu.

Semina hiyo ilihudhuriwa na Maimamu thelathini pamoja na Masheikh mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salamu.

Sheikh Osama Mahmoud Ismail, Mkurugenzi wa Kituo cha Markaz Chang'ombe (wa pili kulia) akifuatiwa na Sheikh Suleiman Amran Kilemile (wa pili kushoto).